Simulizi : Thamani Ya Fukara
Sehemu Ya Tano (5)
Hadi inafika saa nne na nusu usiku Layla alikuwa bado hajarejea,Gabi alizidi kuchanganyikiwa sana,alitoka nje japo hakujua pa kuelekea usiku ile,alirudi ndani huku akiwa kama mwendawazimu.Saa sita usiku usingizi ulikuwa mbali na mboni zake kila mara alimuwaza Layla,
"Atakuwa kwenye matatizo makubwa sio bure"alijisemea Gabi,alijilaza akipanga kesho yake kwenda kumtafuta.
Layla siku ile alitembea sana,alianzia kimara mpaka mbezi mwisho huko kote alikuwa anaomba omba huku akisingizia kuwa wazazi wake wamepoteza maisha hivyo anatafuta pesa za kuweza kusafiri kwenda mkoani ili akawazike wazazi wake.Watu wenye huruma walimchangia na siku hiyo aliingiza pesa nyingi sana,
"Ngoja nilale halafu kesho niamkie huku huku"alijisemea Layla huku akijiweka kwenye kichaka kilichokuwa karibu na msikiti uliopo kimara,mawazo yake yalimfikiria Gabi lakini alijiambia kuwa akienda na pesa nyingi lazima Gabi afurahi,alizihesabu na kukuta anakiasi cha shilingi elfu kumi na nane ilikuwa furaha kwake.
Asubuhi na mapema Gabi aliamka na kupanda gari za kutoka mawasiliano hadi Kimara, siku ile alivaa mavazi ya kawaida hakwenda kwa ajili ya kuomba omba bali kumtafuta Layla.Ni upendo wa hali ya juu aliokuwa nao Layla,anakubali kulala njaa,kulala nje baridi kali ilihali wazazi wake matajiri sana yote hayo hakujali akaamua kwenda kuanza maisha mapya na Gabi maisha yenyewe ndo haya ya kuomba omba.Kwa siku ile aliamka na kama kawaida yake akanza kuzunguka huku machozi ya uongo yakimtoka mda wote.Majira ya saa mbili na nusu Gabi alikuwa tayari yupo Kimara stend,alibaki kutazama mkusanyiko wa watu eneo hilo huku kila mtu akiwa bize na mambo yake,aliangaza kulia na kushoto na kushindwa pa kuanzia kumtafuta Layla alibaki amesimama huku akiwatazama wapiga debe na watu wengine wakiwa na biashara zao.
Siku hiyo Layla alitembea mpaka Mbezi jogoo huko nako akiwa anaomba,kwakuwa ilikuwa siku ya jumapili alienda mpaka kwenye kanisa la BCIC lililokuwa maneno yale na kuingia mle kanisani,hakuogopa kitu chochote yeye alichotaka ni pesa,alimueleza mchungaji wa kanisa lile kuwa ana matatizo makubwa kutokana na machozi yake ya uongo baadhi ya waumini waliingiwa na huruma na kunyanyuka kwenye viti vyao na kuja kumchangia Layla aliyekuwa amesimama mbele ya kanisa,hata mchungaji naye alitoa noti ya elfu kumi na kumkabidhi Layla,mara baada ya zoezi hilo kuisha Layla aliwashukuru kisha akatoka nje na kwakuwa alikuwa amechoka na njaa kubwa aliyokuwa nayo alikaa kwenye mti mkubwa uliokuwa umbali wa mita sabini kutoka lilipokuwa kanisa,alitoa pesa zake na kuanza kuzihesabu,uso wake uliachia tabasamu alipozihesabu na kukuta ni kiasi cha shilingi elfu sabini na saba na mia tano,
"Mpaka niondoke na laki moja"alijisemea kimoyo kimoyo.Lakini akiwa anazipanga vizuri pesa zake kuna kijana alipita eneo lile na kumkuta Layla akiwa ameshikilia zile pesa, yule kijana alizipiga hatua akasogea mbele lakini alisita na kurudi pale alipokuwa amekaa Layla,
"Habari yako binti,naitwa Dulla"alisalimia yule kijana,
"Salama,naitwa Layla.."Layla alijibu kwa wasiwasi mkubwa,bila kutalajia alimuona yule kijana akitoa noti ya elfu tano na kumkabidhi,
"Kwa kukuangalia tu naona una matatizo makubwa sana,hivyo chukua hii hapa itakusaidia"aliongea yule kijana na ile noti akamkabidhi Layla,
"Asante sana kaka angu, kweli nina matatizo wazazi wangu wamefariki hivyo natafuta nauli ya kuweza kunifikisha nyumbani Bukoba ili nikawazike wazazi wangu"Layla alitunga uongo machozi nayo yakianza kumtoka,
"Pole sana,kwenye lile kanisa umejaribu kwenda kuomba msaada?"aliuliza yule kijana huku mkono wake akiuelekeza lilipo kanisa,
"Ndio ndo wameweza kunipa hizi pesa"Layla naye alimjibu huku akionyesha zile pesa,yule kijana alitafakari kwa sekunde kadhaa,
"Yaani kanisa lile lina watu wengi kiasi kile halafu umepewa pesa hizi kidogo hivi?ila nadhani kwa kuwa walikuwa hawakujui sasa nipe hizo pesa halafu narudi nazo nikawaelezee kuwa mi ni kaka yako,lazima wakiona hizi pesa wataongezea zingine,nitawafanganya kuwa tumeomba tumepata hizi hivyo bado kidogo tukamilishe nauli"aliongea yule kijana.
Layla bila kutafakari alikubali na kutoa pesa zile kisha akamkabidhi yule kijana aliyejitambulisha kwake kwa jina la Dulla,
"Sawa nisubiri hapa nakuja"aliongea Dulla nakuzipiga hatua kuondoka maeneo yale,
"Aya Kaka ang naimani utafanikiwa"alijibu Layla na kubaki kumtazama yule kijana akiishia.Dulla alizuga kuingia kanisani lakini alizunguka kwa nyuma na kupitia kule asionekane.Layla hakujua kuwa alikuwa tayari ametapeliwa.
Gabi alibaki maeneo yale ya Kimara hata alipojaribu kuzunguka hakwenda mbali kwa kuogopa kupotea,alikataa tamaa ya kumupata Layla,
"Kama hajauawa basi atarudi"alijisemea Gabi na kuchukua gari lililomrudisha mpaka Mawasiliano.
Layla usingizi ulimpitia pale pale kutokana na kukaa mda mrefu amemsubiri Dulla aliyesema atarejea mda si mrefu,alistuka usingizini na kuchungulia kanisani lakini alipaona pako wazi kumanisha wauumini wote walikuwa tayari wamemaliza ibada.Hakutaka kuamini kuamini ilimbidi kusogea mpaka na kanisa hilo lakini mambo yalikuwa yale yale,
"Sasa atakuwa ameenda wapi?lakini ngoja niendeleee kumsubiri itakuwa kaenda sehemu nyingine kuongezea zile hela"alijisemea Layla na kurudi pale chini ya mti kisha akaendelea kumsubiri.Njaa kiu vyote vilimuandama lakini hakutaka kutoka eneo lile kuhofia atamkosa Dulla.Hadi inafika saa kumi na moja jioni Dulla alikuwa bado hajarudi,lakini Layla hakukata tamaa hakufikiria kuwa kijana aliyeonekana mkarimu anaweza kumtapeli.Kichwani mwake alipingina na mawazo yake ya kusema kuwa ametapeliwa,
"Yule mkaka mpole sana hawezi kuniibia mimi"alijisemea Layla.Alianza kukata tamaa ilipotimu saa mbili usiku,mbu pamoja na baridi vilimshambulia sana pamoja na njaa kwani kwa siku ile alikuwa hajaweka kitu chochote tumboni mwake,
"Kweli nimetapeliwa?.."alijiuliza huku machozi yakianza kumtoka.
“kweli nimetapeliwa? Ila hapana Yule mkaka mbon alionekana kuwa mpole sana? au ndo zilikuwa mbinu zake?”alijiuliza Layla lakini hakupata jibu lolote,hakuwa na jinsi aliendelea kulala eneo lile.Majira ya saa sita za usiku kuna kijana alikuwa anapita eneo lile na kumkuta Layla akiwa amelala eneo lile,
“Oyaaa!amka hili sio eneo la kulala”alisema Yule kijana,
“Niache mimi”alijibu Layla kwa hasira’
“Umekataa kunisikiliza?haya kitakachokutokea usilaumu”.Aliongea Yule kijana kisha akaondoka eneo lile na kumuacha Layla akiwa bado amelala,katu maneno ya Yule kijana hayakumuingia kichwani.Hazikupita dakika hata thelathini tangu Yule kijana aondoke walikuja vijana wengine wane na walipomkuta Layla amelala walimbeba juu juu,
“Nasema mniache wapumbafu wakubwa nyinyi”Layla alitukana na kujaribu kupiga kelele lakini wale vijana walimuwahi na kumziba mdomo,walimpeleka mpaka kwenye jumba bovu lililokuwa jirani na maeneo yale,walipomshusha chini walimfunga kamba ngumu mikononi,walimvua nguo zake tayari kujiandaa kumbaka,Layla hakuwa na ujanja wowote wa kujitetea zaidi alibaki kuwatazama,
“Naanza mimi hapa”alisema kijana mmoja lakini wale wengine hawakukubali suala hilo,kila mtu alitaka aanze yeye jambo lililozua tafalani,walianza kugombana wenyewe kwa wenyewe,
“Maneno ya mungu yanasema jisaidie nami nitakusaidia”alijisemea Layla huku akijaribu kuruka kupitia kwenye dirisha,juhudi zake zilizaa matunda ambapo alitua nje na kutokomea gizani akiwaacha wale vijana wanaendelea kupigana.Hakujua pa kuelekea usiku ule kamba alizokuwa amefugwa mikononi alizing’ata kwa meno yake mpaka zikakatika,alitembea gizani kwa hatua za haraka haraka,kila mara alijihisi kama anafuatwa jambo lililomfanya azidishe kasi ya kutembea. Hofu ya kubakwa ilimuingia na kumfanya azidi kutembea,akiwa kwenye hali ile ya kutembea haraka haraka mara aliguswa bega,aligeuka haraka huku hofu dhofu ikitawala vyema moyoni mwake,
“Geuka urudi nyuma huko unakokwenda sio salama”ilikuwa sauti ya kiume ikimwambia Layla,
“We ninani kwani?”aliuliza Layla huku akisitisha zoezi la kuendelea kusonga mbele,
“Utanijua kwa badae,ila kama hutakubaliana na mimi unaweza pia kuendelea na safari ila kitakachokukuta huko mbeleni usije kujilaumu”alijibu Yule kijana kisha akageuka kurudi nyuma.Layla aliyafikiria yale maeneo kwa kina kisha akakumbuka kijana wa mwanzo aliyemwambia kuwa asiendelee kulala maeneo yale lakini akawa mbishi ndipo wakatokea vijana waliotaka kumbaka,alipokumbuka hayo alijikuta akimfuata Yule kijana aliyekuwa mita kama ishirini kutoka alipokuwa yeye.
“Kaka basi subiri twende wote naogopa”aliongea Layla,hakujua kuwa ule ulikuwa mtego wa wale vijana aliowakimbia mwanzo,moyo wake uliingiwa na hofu tena baada ya kuona wamerudi tena kwenye lile jumba alilokimbia mwanzo,
“Umejileta mwenyewe hapa huwezi kutukimbia tena”aliongea kijana mmoja huku akimshika Layla na kumvua nguo na bila kuchelewa akaanza kumbaka .Yalikuwa maumivu makali yasiyoweza kuvumilika,Layla hakupewa hata nafasi ya kuongea wale wanaume waliendelea kumbaka kwa zamu,kila aliyekuwa anachoka alipumzika ili kumpa nafasi wenzie huku yeye akivuta pumzi apate nguvu ya kuendelea tena,Layla alilia sana lakini kilio chake hakuna aliyekisikiliza,wale vijana walionekana kuwa wakatili mno.Kila mmoja alipotosheka kufanya kitendo kile walikaa pembeni kidogo na kuanza kupongezana kwa unyama ule,
“Kanaonekana kalikuwa hakajatumika sana”aliongea kijana mmoja na kuwasha sigara akaanza kuivuta,
“Nimepata nguvu mpya ya kuendelea na mchezo”aliongea Yule kijana na kuinuka kumfuata Layla aliyekuwa amelala hajiwezi,alipomfikia alimgeuza na kuendelea na mchezo ule mchafu,wale vijana wa mwanzo walipata nguvu upya na kuendelea kufanya kitendo kile,
“Mabinti kama hawa badala wangelikuwa shuleni lakini wanabaki kuzurula mtaani,vunja mti mdogo hapo unipe”aliongea mwanaume mmoja aliyeonekana kuwa mkubwa kuliko wote lakini hakuwa na huruma,punde mti aliouagiza uliletwa na kijana mwingine,Yule mwanaume aliushika ule mtu na kuuvunja kupunguza kimo chake alipohakikisha umekuwa mfupi aliunza kuungiza kwenye sehemu za siri za Layla,damu nyingi ilimtoka pamoja na maumivu makali alipoteza fahamu,
“Tumeua”aliongea Yule mwanaume aliyekuwa anauingiza ule mti. Wote walitowanyika eneo lile na kumuacha Layla akiwa amepoteza fahamu.
****
Gabi aliendelea na kazi yake ya kuomba omba,kila mtaa aliopita hakuacha kumuulizia Layla lakini hakumpata,mwishowe alikataa tamaa kabisa,
“Ni wanawake wachache sana wenye kujitoa kwa watu wanaowapenda kama ilivyokuwa kwa huyu mwanamke,yaani na utajiri wote wa wazazi wake kauacha kwa ajili yangu?kama hajafa najua ipo siku tutaonana japo sijui ni kipi kilichomkuta huko”alijisemea Gabi wakati akienda kwenye ile kazi yake ya kuomba omba,alibadili muonekano na kuonekana kama kichaa jambo lile lilimuingizia pesa nyingi,kila alipopata hata elfu moja alihakikisha mia tano anaiweka kama akiba.Upendo wa Layla aliuona wa kipekee sana kila mda alikuwa anajisemea moyoni kuwa kama Layla hajapoteza maisha basi ipop siku atamuona na watakuwa wote,
“Wahenga walisema kuwa milima haikutani,naamini upendo wa Layla ntaupata tena”alijisemea Gabi.
*********
Layla alizunduka majira ya saa kumi ma moja asubuhi,aliangaza kulia na kushoto kutokana na mbalamwezi iliyokuwepo aligundua yuko kwenye jumba bovu,alipojaribu kusimama hakuweza kutokana maumivu,alipojiangalia vizuri aligundua kuwa hakuwa na nguo,damu nyingi zilimtoka alikumbuka kuwa mara ya mwisho alipoteza fahamu wakati wale vijana wakimbaka.Mpaka hapo ilikuwa siku ya pili akiwa hajala chochote,njaa kali ilimsambulia asubuhi ile,alijitahidi kuinuka na kuvaa nguo zake kisha akazipiga hatua za taratibu kuondoka kwenye lile jumba,
“Sijui Gabi atanipokea vipi na hali niliyonayo,hii ni aibu siwezi tena hata kumtafuta kama nitakufa sawa tu ila sio haya majeraha eti akayaone Gabi”alijisemea Layla.Kulikuwa kumepambazuka tayari na kila alipokuwaana kutana na watu waliokuwa wanawahi kwenye shughuli zao alisimama ili asiweze kugundulika kutokana na kutembea akiwa amepanua miguu huku matambara akiyajaza katikati ya miguu yake ili damu iliyokuwa inamtoka isiweze kuonekana.Alipitia majalalani na kutafuta angalau chakula kilichotupwa lakini aliambulia patupu,hakika yalikuwa mateso makali aliyoyapata alijilaza kando na mti uliokuwa kando na barabara usingizi ulimpitia,alikuja kushtuka saa sita mchana huku jua kali likimumlika baada ya ule mti kuishiwa kivuli,alijitahidi tena kusimama na alipotazama pembeni kidogo aliweza kuona duka lililokuwa ng’ambo ya barabara,alisimama kwa shida sana kisha akajikongoja kuelekea lilipokuwa lile duka ,
“Kama watanipiga basi lakini siwezi kufa na njaa”alijisemea Layla huku akiwa tayari amelifikia lile duka,
“Kaka habari yako,naoma mirinda nyeusi pamoja na maandazi manne”aliongea Layla mara baada ya kulifikia duka lile.Muuza duka alitoa vile vitu na kumkabidhi Layla.
Sehemu ya ishirini na nne-24.
Layla alikabidhiwa soda pamoja na maandazi,alikunywa taratibu sana licha ya kujua kuwa hana pesa lakini hakuwa tayari kufa njaa ilihali duka analiona,mara baada ya kushiba alitulia kidogo na kuanza kuunda mbinu za kumlaghai yule muuza duka.Baada ya dakika kama tano Yule muuza duka simu yake ilianza kuita,aliitoa mfukoni na kuipokea,alipomaliza kuongea alimfuata Layla na kumdai pesa,
“Nipe pesa yangu nataka nitoke kidogo nimepata dharura”aliongea yule muuza huku akinyosha mkono wake kuuelekeza kwa Layla aliyebaki kushangaa asielewe cha kufanya,hakuwa na pesa alibaki kushangaa,alishusha pumzi ndefu na kuiga mkono akauweka mfukoni na kushtuka kana kwamba kapoteza kitu,aliinuka pale alipokuwa amekaa na kusimama akaanza kutazama pembeni,
“Kaka hela nimezidondosha kabisa sizioni”aliongea Layla kwa wasiwasi mkubwa,
“Acha maigizo binti,naomba pesa yangu kabla sijakufanya kitu kibaya”aliongea Yule muuza duka kwa ghadhabu kubwa,lakini Layla alibaki kumtazama alikumbuka maumivu aliyokuwa nayo kwa wakati ule na alivuta picha kama yule muuza duka atataka kumdhuru,akili ya haraka haraka ikamjia alipitisha mkono wake mpaka kwenye matambara yaliyokuwa yanazuia damu iliyokuwa inamtoka aliyavuta na kuyatoa kabisa,kitendo kile kilisababisha damu nyingi kuanza kumtoka katikati ya miguu yake,muuza duka alisitaajabu kitendo kile,pembeni kidogo kulikuwa kuna mteja mwingine aliyekuwa anakunywa maji,
“Puuuh!!!...”alitema maji Yule mteja aliyekuwa amekaa pembeni,
“Ondoka hapa usituletee mikosi asubuhi asubuhi”aliongea Yule muuza duka kwa jazba,
“Kanatokwa na damu lakini hakajui hata kuizuia,khaa!hata maji hayanyweki tena kichechefu balaa”aliongea na maji aliyokuwa anakunywa akayamwaga kabisa.Layla alianza kutembea sehemu aliyokuwa haijui,moyoni alimshukuru mungu kwa kunusulika na kipigo cha muuza duka,aliendelea kutembea kwa mwendo wataratibu hasa na maumivu aliyokuwa nayo,damu nayo haikuwa mbali iliendelea kumtoka.Kwa mbali alimuona mwanaume mmoja akisimamisha gari na kisha kutoka nje,
“Baba shikamoo”alisalimia Layla mara baada ya kumfikia Yule mwanaume,
“Nani baba yako?humjui baba yako mpaka unite mimi baba?”aliongea yule mwanaume,
“Naomba msaada wako nina hali mbaya”aliongea Layla huku akianza kutokwa na machozi,
“Msaada hapa umeambiwa ni kituo cha kulelea watoto yatima?toka mbele yangu mwanamke hujui hata kuvaa taulo ya kuweza kuzuia huo uchafu halafu eti nikuweke kwenye gari langu,si utahila huu”aliongea Yule mwanaume aliyeonekana kuwa na gari la kifahari lakini hakuweza kumsikiliza Layla,
“Sawa lakini tambua haya ni matatizo yaliyosababisha mi kutokwa na damu si hivyo unavyofikiria wewe”aliongea Layla huku akiyafuta machozi yaliyokuwa yanamtoka na kuzipiga hatua zilizo jaa maumivu kisha akaondoka eneo lile moyoni akimfikiria Gabi ambaye alikuwa hajui kwa wakati huo alipokuwa kuwa.Baada ya kutembea sana nguvu zilimuishia hivyo aliamua kujilaza kando ya barabara kutokana na uchovu aliokuwa nao usingizi ulimpitia.Alikuja kustuka jioni jua likiwa tayari limezama alitazama kulia na kushoto lakini hakuweza kutambua eneo alilokuwepo aliinuka taratibu na kuanza kutembea hakutaka kulala tena eneo lile,licha ya kutembelea sehemu asiyoijua lakini alijipa matumaini kuwa mwenyezi mungu ana makusudi yake kumpitisha kwenye kipindi kile cha mateso.Giza lilipoingia alilala chini ya mti,alishutushwa na mvua kubwa ilikuwa inanyesha,hakupata sehemu yeyote ya kujiegesha alikubali mvua hiyo kumnyeshea,baridi nayo ilimuandama ipasavyo.Mvua ilinyesha mpaka saa kumi na moja asubuhi usingizi hakuupata,akiwa ameloa vya kutosha alisimama lakini alihisi maumivu kuwa makali sana hasa baada ya majeraha yake kutoneshwa na mvua,aliegemea mti na kungoja kupambazuke ili azidi kuomba msaada.Asubuhi kulipambazuka na hali ile ile ya mvua mvua,Layla hakutaka tena kubaki eneo lile alijikongoja na kuzidi kutembea mpaka majalalani ambapo aliweza kupata ugari uliokuwa umetupwa eneo lile,hakujali alianza kuula ili kutuliza njaa iliyokuwa inamuandama tumboni kwake,alipumzika eneo lile na kwa wakati ule ilikuwa yapata saa mbili asubuhi hivyo jua lilikuwa tayari limechomoza na mvua ilikuwa imeacha kunyesha usingizi ulimpitia tena.
***
kulikuwa na vijana wawili ambao kawaida yao ilikuwa kuja pale jalalani na kujipatia chakula kilichotupwa,lakini walipofika eneno lile hawakuweza kupata chochote na haijawahi kutokea wao kukosa chakula eneo lile,walikuwa vijana wa mtaani ambao pia kazi yao kubwa ilikuwa ni kuomba omba mtaani,walimuona Layla akiwa pembeni amelala usingizi mzito,jambo lile liliwatia hasira sana,
“Kamekula chakula chetu tukafanyeje haka ka binti?”aliongea kijana mmoja,wote waliafikiana kumbaka Layla kama kulipiiza kisasi kwa kuwa amekula chakula chao,walimfuata mpaka pale alipokuwa amelala kijana mmoja alimfunua nguo lakini walikutana na damu nyingi iliyokuwa inamtoka,
“Khaaaa! Kapo mwezini lakini hakajui hata kuizuia hii damu”aliongea kijana mmoja,
“Ila kenyewe kana weupe wa asili sema kachafu,tuondoke twende kwenye jalala lingine kabla vijana wengine hawajatuwahi”alidakia kijana mwingine na bila kuchelewa waliondoka eneo lile.Layla alizinduka kutoka usingizini na kunyanyuka kisha akaendelea na safari,alizidi kunyoosha barabara ambayo aliamini inaweza kumfikisha Kimara,akiwa njiani alikutana na mwanamke mmoja wa makamo,
“Shikamoo mama..”alisalimia Layla huku akibana mapaja yake kusudi damu isionekane,
“Marahaba mwanangu hujambo..?”aliitikia Yule mwanamke,
“Sijambo mama ila nina matatizo,nimepotezana na ndugu yangu hapa na sijui wapi alipo halafu mimi mwenyewe hapa nina siku tatu sijala chochote”aliongea Layla,
“Pole sana twende kwanza kwenye lile duka nikununulie taulo ya kuweza kuzuia hizo damu”
“Hapana mama hizi damu zimetokana na maamivu ya kubakwa”aliongea Layla huku machozi yakimtoka.
“Pole sana chukua hii itakusaidia”aliongea Yule mwanaume huku akimkabidhi Layla elfu kumi na tano kisha akaagana naye yeye akaondoka.Layla alifurahi kuona anapata pesa kubwa kiasi kile,alipanga kumtafuta Gabi kwakuwa pesa ya nauli alikuwa nayo tayari,
“Hey yero simama nikupe dawa ya kuweza kuzuia iyo damu inayotoka”ilikuwa sauti ya Mmasai akimsimamisha Layla,alisimama lakini uso wake ulitawaliwa na aibu kubwa sana,
“Hii hapa dawa unapona kabisa,unaipaka sehemu inayovuja kwa dakika kumi damu inaacha kutoka”
“Naomba nisaidie nateseka kweli”aliongea Layla,
“Siwezi saidia mtu ambayo haina pesa ulikuwa hujui kuwa hapa ni mjini,nipe elfu tano”aliongea yule masai kwa lafudhi ya kikwao.Layla alitoa pesa na kumpa Yule mwanaume wa kimasai kisha yeye akapewa ile dawa,aliondoka na kabla hajapanda gari la kumfikisha Mawasiliano alikokuwa anaishi na Gabi kabla yeye hajapotelea Mbezi,aliingia kichakani na kuibandika ile dawa kweli damu ile ilikata mara moja.Aliingia barabarani tena na kwa mbali aliliona gari la abiria,alilisimamisha kisha safari ikaanza,alinunua maji na kuanza kuanza kuibandua damu ilikuwa imeganda miguuni kwake.Hatimaye gari lilifika mpaka Ubungo stend,abiria wote walitelemka akiwemo na Layla,kwakuwa walipokuwa wanaishi alipajua vyema,hivyo alikodi bajaji iliyomfikisha mpaka pale walipokuwa wanaishi,dereva bajaji alimpa ujira wake kisha yeye akazipiga hatua kwenda ndani,licha ya kuweka dawa ya kuzuia ile damu iliyokuwa inmtoka,lakini bado alitembea kwa kuchechemea,kwa wakati huo Gabi ndo alikuwa anatoka ndani kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli yake ya kuomba omba,macho yake yaligongana na Layla,alistuka alipomuona Layla akitembea kwa kuchechemea……
Wote walikumbatiana kwa furaha na kuanza kusimliana maisha waliyoyapitia kila mmoja hasa baada ya kutengana,Gabi alishindwa kuyazuia machozi ya furaha yalimtoka lakini bado hakujua kilichomkuta Layla mpaka atembee kwa kuchechemea,hakuwa na haraka ya kumuuliza alimuacha apumzike kwanza,
“Eeeh nambie mpenzi kipi kimekukuta huko?maana mwenzio nilijua tayari umepoteza maisha”aliongea Gabi,Layla alimeza funda moja la mate kisha akamtazama Gabi kwa sekunde kadhaa,
“Ni story ndefu mpenzi kwanza kabisa tushukuru mungu nimeweza kurejea hapa na tukaonana tena,lakini kiufupi nilipotelea Mbezi na hapa nimefika kwa kuomba msaada,nimetapeliwa pesa zangu nilizokuwa nimezipata lakini tuachane na hayo,vipi lakini mpenzi kazi zinzendeleaje?”aliongea Layla akitaka ile maada ihailishwe.Gabi alikubaliana naye kisha maongezi ya hapa na pale yakashika nafasi,siku hiyo walishinda ndani wote hakuna aliyeweza kwenda kazini
“Lakini si unajua bado tunatafutwa?hivyo hata kama tutaenda kuomba omba lazima tubadili muonekano tusije kukamatwa kizembe”aliongea Gabi,usiku wa siku ile Gabi alihitaji wakumbushie lakini Layla alikataa na kudai kuwa yuko hedhi,basi waliongea mengi sana kubwa zaidi likiwa ni kuanzisha maisha yao upya,Layla ndo alikuwa wa kwanza kusinzia,Gabi alikuwa bado na lengo la kujichelewesha kusinzia alitaka kujua kitu gani kinamfanya Layla atembee vile hivyo alimfunua nguo,hakuamini macho yake alichokiona,yalikuwa ni majeraha mkubwa sana,ndipo alipogundua kuwa Layla kule alipoenda amekutana na mambo mengi sana na yale majeraha yalimfanya atambue kuwa Layla kaingiliwa kimwili,alivuta shuka lake kuu kuu akajifunika akautafuta usingizi.Asubuhi kulipambazuka na hali ya hewa safi Gabi aliamka asubuhi na mapema na baada ya kuhakikisha kila kitu kipo alimuaga Layla kisha kama ilivyo ada aliingia barabarani kuanza kazi yake ya kuomba omba,Layla alibaki nyumbani kwa kuwa hakuwa na nguvu za kutembea,hivyo kazi ilibaki kwa Gabi aliyehakikisha kila kitu kinakuwepo pale nyumbani.Maisha yake yakawa yale yale na mara baada ya mwezi mmoja Layla alikuwa tayari amepona kabisa lakini hakudhubutu kumwambia Gabi kuwa alibakwa hivyo alibaki nayo moyoni bila kujua kuwa tayari Gabi analijua hilo,maisha yao yalisogea walijitahidi sana kubana matumizi.
***
Kijijini Arusha hali ya Doris ilikuwa mbaya sana hasa baada ya kugundua kuwa ana ujauzito wa miezi miwili,jambo hilo baba yake hakulitambua hivyo ilikuwa siri yake na mama yake,waliamua kutafuta dawa za kienyeji na kuitoa ile mimba,Doris hakutaka tena kwenda shule.Bado aliendelea kumuwaza Gabi alipata taarifa kuwa Gabi yuko jijini Dar es salaam alipanga kumtafuta ili ikiwezekana aishi naye kabisa ili kurudisha furaha yake,moja kwa moja alianza kukusanya pesa za kumwezesha kumtafuta Gabi,alijua hakuna lishindikanalo mbele ya pesa,alivuta subira kuwa wiki moja ijayo ndo ajitose jijini Dar es salaam.Wiki moja iliwadia alijipanga vyema na kujitahidi kuulizia kwa majarani na kuambiwa kuwa Gabi anaishi maeneo ya stend,alichokifanya na kuitafuta picha ya Gabi na mara baada ya kuipata aliihifadhi vyema akingoja kesho yake ndo asafiri mpaka jijini.Ilikuwa siku ya juma nne na hiyo ndo ilikuwa siku ya Doris kusafiri mpaka jijini Dar es salaam.Basi la Arusha Express lilikuwa tayari,Doris aliondoka nyumbani akiwa amemuaga mama yake pekee.Saa kumi na mbili kamili gari lilianza safari,njiani Doris alikuwa anawaza ni jinsi gani ya kuweza kumuona Gabi lakini alijipa matumaini kuwa kwa kuwa anapicha hakuna kitakachoharibika gari lilizidi kuchanja mbuga,mwendo wa masaa saba lilikuwa tayari lipo jijini Dar es salaam,Doris alichukua chumba karibu na pale stend kisha akapumzika akisubiri kupambazuke ili aanze kumtafuta Gabi,asubuhi kulipopambazuka Doris aliwatafuta vijana na kuwapa maelezo kuwa anamtafuta ndugu yake hivyo atakayeweza kumpata atampa laki tano,kila kijana aliingia mtaani lakini ilikuwa ni ngumu sana kuweza kumtambua Gabi kutokana na kubadili muonekano,vijana walizidi kuzunguka hasa maeneo waliyoambiwa kuwa Gabi anaishi sehemu ile.Doris naye hakuwa mbali alizidi kuzunguka lakini ghafla macho yake yaliangalia bango lililokuwa limabandikwa kwenye nguzo ya umeme na kukutana na taarifa ya kutafutwa kwa Layla alibaki kuilitazama lile bango,alijua kuwa hata Gabi naye atakuwa matatizoni na alijua fika Gabi atakuwa eneno lile,
“Lazima nimtafute kabla hajapatwa na matatizo”alijisemea Doris,akiwa kwenye hali ile mara alipita Layla mbele yake lakini hakuweza kumtambua kutokana na Layla kuwa na muonekano tofauti,hakuna aliyeweza kumuona mwenzake.Majira ya saa nane mchana simu yake iliita,aliitazama na kukuta ni namba ngeni aliponyeza kitufe cha kijani na kuiweka sikioni,
“Hallow,tayari tumepafahamu anapoishi hivyo njoo tukutane pale stend utupe mshiko wetu”ilikuwa ni sauti ya upande wa pili mara baada ya Doris kupokea ile simu.Baada ya dakika arobaini walikuwa tayari wamekutana,Doris alitoa pesa na kuwakabidhi lakini aliwaambia kuwa ipo kazi nyingine ya kumteka Gabi,vijana hawakuwa na kipingamizi kwani tangu wakae pale mjini hawakuwahi kuwa na pesa myingi kama aliyowapa Doris.Moja kwa moja waliandaa dawa ya kumfanya mtu asinzie pale pale na ndo jinsi walivyopanga kumteka Gabi,jioni ya siku ile Gabi akiwa hana analolijua na kwa wakati huo alikuwa anarudi nyumbani ghafla njiani alikutana na wale vijana waliokuwa wametumwa na Doris,
“Habari yako?pole na mizunguko ya kutwa nzima”alisalimia kijana mmoja lakini Gabi hakuweza kuitikia,
“Okay anyway Hata usipojibu lakini sisi tumeagizwa na mwanamke mmoja hivi,kuwa unahitajika kama utaleta ubishi tutatumia nguvu”aliongea kijana mwingine akionesha kuwa siliasi,
“Yukoje huyo mwanamke?”aliuliza Gabi kwa wasiwasi,lakini wale vijana hawakuhitaji mahojiano zaidi na Gabi hakuwa tayari kwenda sehemu asiyoijua ndipo ilitokea tafalani maeneno yale lakini tafalani hiyo haikudumu sana baada ya kijana mmoja kumpulizia ile dawa Gabi,haikupita dakika moja Gabi alilegea kisha akaenda chini kama mzigo,bajaji iliandaliwa fasta kisha Gabi akapakiwa ndani na kumpeleka mpaka pale alipokuwa Doris.Doris alitabasamu sana alipomuona Gabi licha ya kuwa alikuwa amevalia mavazi machafu,nguo mpya ziliagizwa na mavazi ya Gabi yakabadirishwa mara moja.
“Hongereni vijana kazi nzuri sasa hapa imebaki kazi moja nayo ntawaambia badae shikeni ujira wenu”aliongea Doris huku akiwakabidhi wale vijana,wote walimshukuru kisha wakaagana na kuondoka,
“Hakikisheni simu zenu mda wowote zinakuwa hewani”aliongea Doris na wale vijana wakaitikia kisha wakaondoka.Usiku ule ule Doris alikodi tax na alipanga kwenda Bagamoyo,hivyo tax ilianza safari usiku ule ule,ulikuwa mwendo mkali sana ambapo kabla ya saa nne usiku walikuwa tayari wapo Tegeta kutokana na kutokuwa na foleni njiani.Bado Gabi alikuwa hajazinduka kutoka usingizini hasa hiyo dawa ya Chrolofrom aliyopuliziwa ilikuwa inadumu kwa masaa sita mpaka nane….
Baada ya ile tax kufika Tegeta Doris alimwambia Yule dereva kuwa wanaenda nje kidogo na Dae es salaam,hivyo tax ilianza safari ya kwenda Bagamoyo ulikuwa mwendo mkali sana na baada ya masaa matatu walikuwa tayari wamefika Bagamoyo,Doris alimlipa Yule dereva tax ujira wake kisha yeye akabaki pale stend akiwa na Gabi aliyekuwa bado hajazinduka,alichukua bajaji iliyomfikisha mpaka kwenye nyumba ya kulala wageni iliyoitwa MSAFIRI LODGE,alilipia chumba na kuingia akiwa sambamba na Gabi alipanga kukaa pale kwa wiki nzima kisha ndo asafiri mpaka jijini Arusha ili akafunge ndoa na Gabi,lakini kuna mpango aliokuwa nao kichwani mwake,
“Dada nina mgojwa huyu hapa hivyo nangoja kupambazuke ili niweze kumpeleka hospital”aliongea Doris akimwambia dada aliyekuwa mapokezi ili asishtukiwe,
“Sawa dada haina shida jisikie huru kabisa”alimjibu Yule dada wa mapokezi.
****
Layla alikuwa bado hajasinzia kwa wakati huo alikuwa amemsubiri Gabi kama atarejea lakini kadri mda ulivyokuwa unasogea ndivyo alizidi kuingiwa na wasiwasi,alijua bila shaka kilichomkuta yeye akiwa Kimara basi ndo hicho kilichomkuta Gabi,alipiga magoti na kumuomba mungu aweze kumlinda Gabi huko aliko hakujua kuwa kwa wakati huo Gabi alikuwa na Doris.
“Lakini yeye ni mwanaume hawezi kupotea,mungu amsaidie mpenzi wangu aweze kurudi Salama huko aliko”alijisemea Layla,baada ya kujipa matumaini kuwa Gabi atakuwa sehemu salama basi alivuta shuka na kuutafuta usingizi lakini aliendelea kutega sikio kuwa labda ataweza kurudi mda wowote kutokana na wakazi wa jiji la Dar es salaam kutokuwa na mda maalumu wa kulala.
***
Mzee Gozibert baba yake na Layla hakuacha kufanya mawasiliano na askari wa jiji la Dar es salaam kuwa wazidi kumtafuta Layla lakini mpaka wakati huo hawakuwa na taafifa maalumu zinazohusiana na Layla,uchunguzi wao uliendelea huku picha ya Layla ikiwa mikononi mwao lakini hakuna aliyeweza kumpata,mwishowe walikata tamaa hasa baada ya baba yake Layla kuwanyima pesa za kuendeleza uchunguzi na walijua bila shaka Layla hatakuwa ndani ya jiji hilo.
***
Majira ya saa kumi usiku ndipo Gabi alikuwa anazinduka kutoka usingizini baada ya ile dawa aliyokuwa amepuliziwa kuisha nguvu,alipekecha macho yake lakini hakuweza kuona chochote kutokana na giza lililokuwa mle ndani hasa baada ya umeme kukatika na mvua kubwa kunyesha usiku ule hivyo hata aliyekuwa anahusika na masuala ya umeme alishindwa kuwasha geneletor.Alipopeleka mkono wake kushoto pembeni yake aligundua kuwa kulikuwa na mtu mwingine lakini fikira zake zilikumbuka kuwa alikuwa analala na Layla siku zote hivyo hakutaka tena kufikiria sana alisinzia kwa mara nyingine huku nje mvua ikiwa bado inanyesha.Asubuhi na mapema Doris ndo alikuwa wa kwanza kustuka kutoka usingizini aliangalia pembeni yake na kumuona Gabi akiwa bado yuko usingizini alitabasamu na kutoka pale kitandani mpaka bafuni kwa ajili ya kuweka mwili wake sawa,mara baada ya kumaliza kuoga alibadilisha nguo zake na akiwa kwenye zoezi lile mara ghafla Gabi naye alifumbua macho na kumwangalia Doris moyo wake ulienda mbio sana alijua labda yuko ndotoni hivyo alijaribu kufumba macho yake na kuyafumbua lakini ukweli ndo ulikuwa ule ule,alibaki kutazama Doris ambaye hakuwa na habari kwa wakati ule yeye aliendelea na zoezi lake la kubadili nguo,
“Waaoooh mpenzi umeamka”aliongea Doris huku akiachia tabasamu kwa mara nyingine,
“Nimefikaje hapa na Layla yuko wapi?”aliuliza Gabi kwa mshangao,
“Hapa nimekuleta mimi,nimekaa kijijini bila penzi lako nahisi bado sijakamilika kabisa hivyo nimekufuata tuishi wote au ikiwezekana tufunge ndoa kabisa nadhani unatambua nilivyokuwa nakupenda tangu shule ya msingi nimekataa kwenda shule kwa ajili yako,hivyo baada y a kupata taarifa kuwa upo huku ndo nimeamua kukufuata”aliongea Doris,lakini Gabi bado alionekana kupigwa na butwaa,
“Sasa Layla yuko wapi na atajisikiaje akiyasikia haya unayoyasema ilhali ametoroka na mimi kutoka kijijini kuja huku?ni upendo wa pekee alionao Layla yaani anadhubutu kulala nje wakati kwao zipo mali za kutosha,nilikuwa nimemzoea Layla kama mke wangu nadhani moyo wake unaujua jinsi ulivyo yaani anaweza hata kujiua akiyasikia haya”aliongea Gabi kwa masikitiko,lakini yale maneno yalimkera Doris,”Kwahiyo umataka kuniambia Layla ndo ana thamani zaidi kuliko mimi?na kwa taarifa yako tayari Layla yuko Akhera”aliongea Doris maneno yaliyomshutua Gabi na kushika mdomo kwa mshangao,
“Unasemaje wewe?unataka kuniambia Layla tayari umemuua?”aliuliza Gabi maswali mfululizo,
“Ndo jibu lenyewe hilo,yaani yuko kwa muumba wake ulitegemea nini mimi nikose furaha kwa ajili yako wewe eti kisa yeye?mbona yeye alitaka kuniua kipindi tuko shule ya msingi?nimemuwahisha kabla yeye hajaniwahi”aliongea Doris kwa kujiamini,Gabi alikoswa la kuongea alijua fika tayari mtu aliyempenda ameuawa kwa ajili yake.Machozi yalimtoka kwa kuona Layla ameuawa akiwa hana kosa kabisa lakini hakuwa na jinsi nyingine tena aliufuata msemo wa wahenga kuwa maji yakishamwagika tayari hayawezi kuzoleka tena.Doris alimfuata pale kitandani na kumfuta machozi yaliyokuwa yanamtoka,
“Natambua ni maumivu makubwa uliyoyapata lakini huna ujanja wa kufufua kilichokwisha kuzikwa tayari,lakini usiwe na hofu niko hapa kwa ajili ya kukupa fuaraha zaidi ya huyo unayemlilia”aliongea Doris na kumkumbatia kabisa Gabi wakajikuta wanafurahi asubuhi ile,
“Lakini wazazi wake Layla wakilivalia njuga suala hili hujui kama naweza kwenda jela?”aliuliza Gabi.
“Kwenda jela?kwa sababu zipi hakuna mwenye ushahidi wa kukupeleka jela wewe kwanza utambue kipindi munatoka Arusha hakuna aliweza kuwaona hivyo ondoa shaka kuhusu hilo”aliongea Doris akimwaminisha Gabi kuwa asemacho kina ukweli ndani yake,siku hiyo walishinda ndani kabisa.Jioni ya siku ile walitoka ndani na kwenda kwenye Bar iliyoitwa QX BAR ilikuwa mita mia moja na arobaini kutoka ilipokuwa Lodge waliyokuwa wamefikia,pale walinunua chakula na kunywa vinywaji kama soda na maji lakini Gabi alishangaa kumuona Doris akinywa bia,
“Mpenzi siku hizi unakunywa pombe?”aliuliza Gabi ni dhahiri hakupendezwa na kitendo kile,
“Kwa leo tu mpenzi mara moja moja sio mbaya ila sory kama nimekukera”aliongea Doris,
“Wala hujanikera wewe kinywa tu”alijibu Gabi lakini moyoni akikichukia kitendo kile.Lengo la Doris kunywa pombe alitaka kufanya maamuzi magumu hivyo kila alipokuwa anafikiria kumuua Layla roho ya huruma ilimwingia,na alimdanganya makusudi Gabi ili amsahau Layla wakati ule yeye awe anafanya mchakato wa kumwangamiza Layla ili penzi la Gabi alifaidi vilivyo,hivyo baada ya kunywa pombe ikakolea roho ya huruma aliiweka pembeni na kuivaa roho ya kishetani,alitoa simu yake na kubonyeza namba Fulani na kabla hajapiga kutokana na mziki uliokuwa unapigwa eneo lile ilimlazimu kutoka nje na na kwenda pembeni kabisa na Bar ile akimwacha Gabi mle ndani,baada ya kuhakikisha yuko sehemu salama alitoa simu yake na kuiweka sikioni,iliita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa,
“Hallow,fanyeni kitu kimoja pale alipokuwa anaishi huyu mwanaume mliyemteka anaishi na mwanamke pia,hivyo nataka auawe mara moja na maiti yake itupwe mbali isionekane”aliongea Doris….
“Hallow,fanyeni kitu kimoja pale alipokuwa anaishi Yule mwanaume mliyemteka anaishi na mwanamke pia,hivyo nataka auawe mara moja na mwili wake usionekane ikiwezekana mkautupe mbali kabisa na hapa laki tatu ziko mezani iwapo mkilikamilisha hilo”aliongea Doris kwa msisitizo,
“Sawa bos tupe siku mbili kazi yako itakuwa imemalizika tayari'sauti ya upande wa pili ilisikika ikisema.Baada ya maongezi yale Doris alirudi ndani ya ile Bar na kumkuta Gabi akiwa anaendelea kuwatazama watu waliokuwa wanacheza mziki wengine wakionekana kulewa chakali aliketi pembeni,
“Samahani mpenzi nilikuwa naongea na mama hapa anasema wiki ijayo tufunge ndoa hivyo jiandae mpenzi”aliongea Doris huku akindelea na kunywa pombe,maongezi ya hapa na pale yaliendelea na mda kidogo waliondoka na kurudi pale walipokuwa wamechukua chumba kwa kuwa hapakuwa mbali ndani ya dakika tatu walikuwa tayari wamefika chumbani,Doris alikuwa amelewa sana hivyo alifika anajitupa kitandana mawazo ya Layla hayakuwa kichwani mwake alijua kuwa mda mfupi ujao Layla atauawa.
****
Layla alianza maisha ya kipekee sana mda mwingi alikuwa mpweke lakini alijipa imani kuwa Gabi atarudi hivyo aliendelea na kazi yake ile ya kuomba omba alijitahidi kubana matumizi kama alivyokuwa anafanya Gabi hakuwaza tena wazazi wake alichokiweza kwa wakati huo ni uwepo wa Gabi lakini hadi zinafika siku nne Gabi hakuwa amerudi na jambo lile lilimzidishia upweke Layla.Wiki moja alipita Layla akiwa bado hajamuona Gabi ndipo alipokataa tama kuwa huenda Gabi ameuawa aidha kwa kugogwa na gari hasa mwingiliano mkubwa uliokuwa ndani ya jiji hilo.Hatimaye hali ya upweke aliizoea na kujisemea kuwa kama kweli Gabi atakuwa yuko hai basi atarudi.
****
Ilikuwa siku ya juma tano huko bagamoyo Doris aliamua kuzunguka sehemu tofauti akiwa na Gabi,walienda mpaka baharini huko waliogelea na kutembelea sehemu mbali mbali zenye makumbusho siku hiyo nzima walibaki kufurahi.Mida ya jioni walirudi kule walipokuwa wanaishi na kuendelea kuhesabu siku chache zijazo ili wasafiri mpaka jijini Arusha waweze kufunga ndoa na wayaanze maisha upya,”Natamani sana univalishe pete ya uchumba yaani ntajihisi wa pekee kwenye hii dunia”alisema Doris akimwambia Gabi wakiwa mezani wanapata chakula cha usiku,
“Usijali hata mimi naisubiri kwa hamu ile siku maana nimechoka kuishi mtaani,lakini huko kijijini tutaishi vipi maana mimi sina hata nyumba kama ulivyokuwa unaona nilikuwa naishi na mama yangu,je tukioana huoni kama itakuwa shida hiyo?”aliuliza Gabi,lakini Doris alimuondoa wasiwasi na kumwambia kuwa wataishi kwenye nyumba za kupanga wakati huo wakifanya mchakato wa kujenga,
“Kikubwa ni Baraka za wazazi hayo mengine yatakuja badae”aliongea Doris kwa tabasamu pana.
****
Wale vijana waliopewa kazi na Doris walianza mara moja na waakabahatika kupafahamu alipokuwa anaishi Layla,hivyo walianza kupanga njama za kumuua Layla,walikuwa vijana wawili lakini mmoja wapo alikuwa na hofu sana kufanya tukio lile jambo lililopelekea kujitenga na mwenzake,
“Ujue kaka yangu mpaka sasa yuko jela kwa kosa la kumuua aliyekuwa mama yetu wa kambo,na utambue kuwa siku zote serikali ina mkono mrefu hivyo tunaweza kujulikana, kitakuwa kituko hiki yaani kaka yangu yuko jela kwa kosa la kuua halafu na mimi iwapo ntakamtwa sinitaenda jela niungane na kaka yangu?hapana bora mia mbovu kuliko hamsini mpya lakini kwa hili siko tayari kabisa”alisema kijana mmoja akikataa kazi aliyokuwa amepewa na Doris,kijana mwingine alishindwa kuifanya kazi ile akiwa peke yake na siku mbili walizokuwa wameambiwa na Doris kuweka kukamilisha mauaji yale ilibaki siku moja na hakukuwa na dalili zozote kwani Yule kijana alishindwa jinsi ya kumuua Layla,
“Lakini Kuna haja gani ya sisi kujiita watoto wa mjini?yaani pamoja na kuzaliwa hapa mjini lakini tumeshindwa kumtapeli huyu mwanamke aliyetoka kijijini?hakuna jinsi tena ni kumdanganya kuwa tumeimaliza kazi,
“Wazo zuri sana kuua sio mchezo kabisa toa simu mtumie ujumbe kuwa kazi imemalizika”walishauriana wale vijana na mmoja wapo alitoa simu yake na kumtumia ujumbe Doris alipoupata alifurahi sana kuona sasa hakuna tena wa kumbugudhi,alienda moja kwa moja mpaka kwa wakala na kuwatumia pesa wale vijana alipohakikisha hilo basi alipanga kusafiri siku ya jumamosi ili kwenda kufunga ndoa na Gabi.Wale vijana walipoipata ile pesa waliruka kwa furaha na bila kuchelewa walitoa laini zao na kuzivunja vunja,
“Mjini shule umeona sasa tungepata dhambi za bure wakati njia ilikuwa nyepesi kabisa”aliongea kijana mmoja wote wakagongeana mikono ishara ya ushindi.Doris alifanya mawasiliano na mama yake mzazi kuwa siku ya jumamosi watafika jijini Arusha na ndoa itafugwa siku ya juma pili hivyo maandalizi yawe tayari,na mama yake hakuwa na kipingamizi juu ya mwanaye kwa sababu ile ndo ilikuwa furaha yake,
“Yaani mama sitojali baba anasemaje maana furaha yangu tayari ninayo”alisema Doris akiongea na mama yake kwa njia ya simu.Siku hazigandi hatimaye siku ya jumamosi iliwadia,Doris akiwa sambamba na Gabi walichukua usafiri uliwakisha mpaka Ubungo magari yaendayo mikoani,hapo walichukua basi lililo wafikisha mpaka jijini Arusha.Siku hiyo hiyo Layla anafukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi kwa kushindwa kulipa gharama za maji n umeme huku kodi ikielekea kuisha,baba mwenye nyumba ile hakuwa na msamaha hata kidogo alimfukuza Layla kama mbwa,licha ya Layla kuomba msamaha lakini baba Yule hakuwa tayari kusikia kilio kile cha Layla,kilichomuongeza Layla mawazo zaidi ni pale alipomfikiria Gabi kuwa iwapo atarudi tena pale akikuta Layla hayupo itakuwaje lakini alijipa imani kuwa binadamu hukutana hivyo ipo siku atakutana naye,alichukua baadhi ya nguo ya nguo zake na kuziweka kwenye kijimfuko kidogo cha Rambo kisha akachukua na zile hela alizokuwa amekusanya tayari akaweka na zile za Gabi kwa kuwa alipokuwa anazihifdhi alikuwa anapajua vyema,hakuwa na pa kwenda alichoamua asubuhi ile ni kupanda basi mpaka kurudi kijijni kwao,
“Lakini hizi aibu nitaziweka wapi na vipi nikiulizwa kuhusu Gabi ntajibu nini mimi?”alijiuliza kwa wakati ule akiwa ndani ya basi tayari.
***
Majira ya saa saba mchana Doris na Gabi ndo walikuwa wanafika jijini Arusha,walichukuwa usafiri uliowafikisha mpaka kijijini kwao walipokelewa kwa furaha na maandalizi ya kufunga ndoa kesho yake yalianza mara moja,nguo kwa ajili ya ndoa hiyo yalikuwa tayari,wazazi wa Layla hawakujua chochote labda mama yake Gabi ndo aliambiwa kuwa kesho yake awahi kanisani kwenda kutoa Baraka zake hakuwa na kipingamizi japo alikuwa na mengi ya kuongea na mwanaye hasa kuhusu Layla lakini alingoja ndoa iishe ndo aweze kuongea na mwanaye.
****
Layla alifika stend ya Arusha na kushuka ndani ya lile gari kisha akajifunga kilemba lengo asijulikane na baadhi ya wakazi wa jiji hilo,alipohakikisha hakuna atakayeweza kumtambua alichukua usafiri wa kumpeleka mpaka kijini kwao alikodi bajaji,
“Eeh bhana umesikia kuwa Doris anafunga ndoa hapo kesho na kijana wa kimasikini Gabi?”aliuliza Yule dereva wa bajaji aliyeonekana muongeaji sana huku sigara nayo ikiwa mdomoni kwake.,Layla alistuka sana na kumwamuru Yule dereva asimsmishe bajaji mara moja,dereva Yule hakuwa mbishi,
“Ndoa?itafanyikiwa wapi maana mi sina taarifa yeyote na Yule kijana Gabi ni mtoto wa shangazi yangu lakini hajanambia chochote na hapa nilikuwa naenda kuwatembelea tu”Layla alitunga uongo na yue dereva bajaji akamwambia kuwa ni kesho asubuhi kwenye kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG.Yule dereva hakumjua mtu aliyekuwa anamwambia taarifa zile,
“Basi niache hapa asante kwa taarifa”alisema Layla huku akiingiza mkono kwenye mfuko na kutoa pesa akamlipa Yule dereva huku yeye akianza kuingia ndani ya poli dogo lililokuwa maeneo yale….
Majira ya saa moja asubuhi kanisa la VICTORY CENTLE lilikuwa limepabwa vyema likingoja waliokuwa wanatalajia kufunga ndoa mahali pale,waumini walikuwa wamejaa tayari huku wengine wakikiwa nje kwa kukoswa nafasi za kukaa kanisa lilikuwa limefurika tayari,kwa mbali lilionekana gari lililokuwa limepabwa vyema kwa maua yenye kung’aa,likiwa kwa mwendo mdogo liliegesha sehemu ile na wakashuka wapambe kwanza wakifuatia na wazazi wa pande zote mbili,taratibu walishuka Doris akiwa na Gabi wakiwa wamevalia mavazi nadhifu sana walitangulia wapambe kwa hatua za pole pole wakafuata bibi na bwana harusi ambao ni Gabi na Doris,waumini wengi walishangilia na maua madogo kurushwa juu ishara ya furaha kwa wakati huo walikuwa wanaingia ndani ya lile kanisa.Lilianza neon la mungu na ibada ikaendelea kabla ya kuvalishana pete ya uchumba.
***
Kwingineko mzee Gozibert anapata taarifa kuwa Gabi kaja naaliyetoroka na mwanaye leo hii anafunga ndoa na binti wa mzee Herman ambaye ni Doris,roho inamuingia kama mzazi na kujisemea yeye akiwa na mkewe kuwa huenda mtoto wao ameuwa na ndo maana hii harusi inataka kufanyika kimya kimya,
“Kabla ndoa haijafungwa lazima kwanza nitambue mwanangu alipo vinginevyo hakuna ndoa,ninacho tambua mimi ni kuwa mwanangu alitoroka akiwa na huyu kijana sasa iweje leo hii afunge ndoa na mtu mwingine?nakumbuka kidogo ajiue kwa ajili ya Yule kijana alishinda njaa kwa siku tano halafu leo hii uniambie kuwa mwanangu kamuacha huyu kijana?hapana silikubali hili”
“Ni kweli mme wangu washa gari haaraka sana tuwahi kanisani kabla ya ndoa”
“Wala usiwe na waswiwasi ndoa itafungwa saa nane mchana kwa wakati huu wako wanapata neon la mungu ila jiandae twende,ngoja niwataarifu na police habari hizi”yalikuwa maongezi ya wazazi wake na Layla na moja kwa moja kwa moja aliwapa police taarifa zile kisha wote wakakubaliana kukutana pale kanisani kabla ya ndoa.Majira ya saa sita mchana neno la mungu lilimalizika na matangazo ya hapa na pale yakachukua nafasi ukimya ulitawala sehemu ile.Mama yake Gabi alizidi kumwangalia mwanaye jinsi alivyokuwa amependeza lakini kila mara aliwaza kuhusu Layla na alitamani kuongea na mwanaye ili kumuulizia zile habari za Layla lakini hakupata nafasi,
“Asije kuwa amemuua mtoto wa watu na ninavyomjua mzee Gozibert sidhani kama atalifumbia macho hili”alijisemea mama yake Gabi akiwa anamtazama mwanaye aliyekuwa amevalia suti iliyomkaa vyema.
****
Jopo la maasikari lilifika kwenye kanisa lile wakiwemo wazazi wa Layla waliobaki ndani ya gari,askri walikoswa sehemu y akupitia kutokana na watu wengi waliokuwa eneo lile,
“Sasa umefika mda wa kuvalishana pete na kabla hatujafanya hivyo bwana na bibi harusi kila mmoja anyanyue mkono juu ukiwa na biblia kisha afumbe macho kwa ajili ya kiapo cha ndoa hii”ilikuwa sauti ya mchungaji Joseph aliyekuwa anasimamia ndoa ile,Doris na Gabi walifanya kama walivyoambiwa,
“Haya naanza kwa upande wa mwanaume,je uko taayari kumuoa Doris na unaapa hutakwenda nje ya ndoa?”aliuliza mchungaji Joseph.Lakini Gabi alikubaliana na yote kuwa hatamsaaliti Doris mpaka siku ya kiama.MCHUNGAJI Joseph aligeukia upande wa Doris na kumwambia maneno yale yale ambayo nayo Doris aliyajibu kama Gabi alivyo jibu.Baada ya kumalizia kiapo kile sasa mchungaji alikamatia pete mbili moja akamkabidhi Gabi na nyingine Doris wa kwanza kumvalisha mwenzake alikuwa ni Gabi aliyeushika mkono wa Doris na kuubusu kwanza kisha akakishika kidole cha kati na pete yake akaanza kuipeleka taratibu kwenye kidole cha Doris,
“STOOOOOOP!!!!...”ilikuwa sauti kutoka nyuma ya kanisa na Gabi akasitisha kitendo kile, alipopeleka macho yake yaligongana na Layla aliyekuwa anatokwa na machozi kumbe alifika mapema pale kanisani hivyo kila kitu kilichokuwa kinaendelea alikuwa anakiona.Doris alianguka chini na kupoteza fahamu pale pale alipomtazama Layla alijua labda ni mzimu wake na sio Layla mwenyewe.Gabi alibaki ameganda kama vile ni mtu aliyepigwa na short ya umeme,ile pete aliyokuwa bado ameishikiria ilidondoka na waumini wakabaki na mshangao mkubwa achilia mbali mama yake Gabi aliyedondosha chozi,kanisa zima lilikaa kimya baadhi ya watu waliokuwa wanamfahamu Layla waliendelea kusubiria atakachokifanya Layla,hata wazazi wake walijikuta wakitabasamu kwa wakati huo Doris alipakiwa ndani ya gari kuwahishwa hospitali ilhali Gabi naye akibaki kuduwaa.Layla kwa ujasiri wa hali ya juu alizipiga hatua kwenda mbele na mara baada ya kufika hapo hapo mbele alimkumbatia Gabi aliyebaki kutetemeka,aliikikamata kipaza sauti ,
“Samahani sana kwa kuwaharibia hafla iliyokuwa inaendelea mahali hapa,ila naweza kusema kuwa huyu Doris alikuwa amataka kufunga ndoa na mme wa mtu,yaani mme wangu mimi baadhi yenu mnatambua kuwa niliotoroka na huyu mme wangu nikaenda naye mpaka jijini Dar es salaam,huko tumepata mateso ya kila aina ila nikashangaa huyu mme wangu akawa amepotea ghafla na sikujua kuwa huyu Doris alikuja kumchukua,hivyo basi naomba aongee mbele yenu na mbele za mungu kama hanipendi mimi ili nijue na niweze kuruhusu ndoa hii iendelee asanteni”aliongea Layla na kuketi chini akampa kipaza sauti Gabi.
“Kabla sijasema chochote naomba tumsubiri huyu aliyepoteza fahamu ndo ntaweza kuzungumza”alijibu Gabi na kuketi.Hapo ukimya ukachukua nafasi yake tena hakuna aliyezungumza.
“Kama ni picha basi hili ni la kihindi”alijisemea mwanamke mmoja.Baada ya dakika zipatazo arobaini Doris alizinduka na kukumbuka kuwa alikuwa kanisani akifunga ndoa moja kwa moja alitoa amri kuwa arudishwe haraka kanisani ili akamalizie ndoa yake,
“Siwezi kukubali kupokonywa tonge mdomoni ilihali nami nina njaa”alijisemea Doris, baada ya kufika pale kanisani alishangaa kupakuta kimya huku waumini wakiwa bado wana shauku ya kutaka kujua kitakachoendelea,Gabi alinyanyuka na kukishika kipaza kwa mara nyingine,
“Nachukua nafasi hii kwa mara nyingine tena kuwa watu waliokuwa wananigombania wote wako mbele yenu,tangu shule ya msingi lakini naweza sema kuwa kati ya hawa wawili yupo mmoja ninaye mpenda kwa dhati naye ni Layla,Doris hana mapenzi ya dhati japo analazimisha,nakumbuka Layla alininusuru mimi kwenda jela kwa kesi ya kusingiziwa sio hicho tu bali yapo mengi sana ikiwemo na kutoroka na mimi kwenda mjini lengo apate furaha”aliongea Gabi kisha akamgeukia Layla tena,
“Nisamehe kwa kutaka kufanya kitendo kile lakini ukweli ni kwamba Doris alinidanganya kuwa amekuua tayari na ndo maana nikachukua haya maamuzi”aliongea Gabi.
***
Doris alitafakari na kudondosha chozi,alijaribu kumshawishi Gabi lakini msimamo wa Gabi ulikuwa pale pale.Doris baada ya kumuomba Sana na kuona msimamo wa Gabi ukiwa pale pale hakuwa na ujanja tena waumini wote waliendelea kutazama kila kilichokuwa kinaendelea.Doris alipiga magoti chini kisha akamuomba Layla msamaha pamoja na wazazi wake.
“Asante sana Gabi kwa kuongea ukweli,nilisahau kabisa kuwa MAPENZI HAYALAZIMISHWI,baba na mama pamoja na waumini natubu mbele zake mungu pia naapa kuwa sitawasumbua tena na nawaomba muishi kwa amani na ndoa yenu idumu,labda wangu hajazaliwa”aliongea Doris na kuyafuta machozi yake kisha akaruhusu ndoa aliyotaka kuifunga yeye basi aifunge Layla kwa moyo mmoja.Hakuna aliyeamini maneno yale wengi wao walijua labda Doris ataleta fujo lakini walichokitegemea sicho kilichokuwa.Ndoa iliendelea na Layla akawa amevalishana pete na Gabi wote walifurahi akiwemo mama yake Gabi na wazazi wake Layla.Doris hakuwa na kinyongo tena na neno alilosema mwishoni ni kuwa MAPENZI HAYALAZIMISHWI.Baada ya miezi mitatu Doris alipata mwanaume wa kumuoa na wa kwanza kupokea kadi ya harusi yake alikuwa Layla,ndoa yao ilifanyikia kwenye kanisa lile lile wakaishi kwa furaha.Mwaka mmoja mbeleni Layla alijifungua mapacha kwa wakati huo walikuwa wameshajenga tayari na kuanzisha biashara zao,hawakuacha kukumbushiana matukio ya nyuma waliyoyapitia.Urafiki wa Doris na Layla ukabaki pale pale kana kwamba hakuna kilichotokea..
****MWISHO****
0 comments:
Post a Comment