Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SEKESEKE (ROHO MKONONI) - 4

   

Simulizi : Sekeseke (Roho Mkononi) 

Sehemu Ya Nne (4)




Aliyekuwa Inspekta wa Jeshi la polisi John Butu anafatiliwa kwa kila hatua pasina yeye mwenyewe kujua kama anafatiliwa,nyumba yake yote inategeshwa kamera za ulinzi,mambo ayaishi hapo hapana!,nje ya nyumba yake kandokando ya barabara anaonekana binti kichaa,


Na pia mtaa wa pili katika Restraunt moja anaweka makazi mjeda mmoja akiwa na kazi moja tu!....


Kumfatilia Butu kwa kila hatua....


Wakati huo Butu ana gida bia za kutosha ghafla anapata wazo,pale pale anainuka na kutoka,


Binti kichaa anamtaharifu kijana Isack akae sawa Butu anakuja usawa wake palepale Isack anamtaharifu Zidu anaye mwambia amtwange risasi naye atoweke ahakikishe aachi ushahidi,naye Zidu anakwea pikipiki kwenda eneo aliloambiwa!


SEKESEKE LILIANZIA HAPO! JE NINI KILIENDELEA?!...


tusonge katika hatua inayofuata kuzidi kuburudika!


HATUA YA KUMI NA SABA


Ile anataka kuichomoa bastola ghafla akasita baada ya kuona kamera katika jengo moja kubwa kando ya barabara..


"Usalama aupo vizuri watu ni wengi na magari pia ni mengi si vizuri kulianzisha nitalipaka matope jeshi letu!"


"Ina maana upo ndani ya Gwanda?!"


Zidu akamohoji


"Ndio kamanda"


Isack akajibu kwa majonzi


"ooh! Shit,usifanye chochote but endelea kuifatilia ujue inaelekea wapi"


"Sawa mkuu"


Kwa kuwa Isack alishaipita pikipiki ya Butu ikamlazimu apunguze mwendo,Butu akampita


Isack akaanza kumfata nyuma nyuma kwa siri sana ili hata asitiliwe mashaka!


***


Baada ya Butu kutoka tu kichaa yule wa kike alimsindikiza kwa macho baada ya kupotelea mtaa wa pili,akawasiliana na Isack,kisha akanyanyuka,akabeba pochi lake moja chafu na kuelekea kunapo geti,tena alificha uso wake kwa mikono kusudi kamera za pale getini zisinase sura yake.


Alipofika getini akaingiza moja ya funguo alizokuwa nazo,akafungua na kuzama ndani,alitembea haraka haraka juu ya tails zilizopo chini mpaka katika mlango wa nyumba ya ndani,akaingiza pia funguo,akafungua,ile kuingia akakutana na sebule nzuri,akaifata korido,chumba cha kwanza akasimama akashika kitasa akakizungusha kikamtwii,akazama ndani!


Hiki ndicho kilikuwa chumba cha Butu cha kulalia macho ya kichaa yule yakadondokea katika kabati,kwa hatua za taratibu akalifata,alipolifikia akatia funguo kabati likafunguka...


Kwa sekunde kadhaa akabaki akitumbulia macho ndani ya kabati lile!


Nguo zilikaa shaghalabaghala bila hata kukunjwa,binti kichaa akatingisha kichwa kwa masikitiko,akafungua pochi lake chafu cha ajabu ndani palikuwa na pakiti kibao za unga zilizofungwa kidogo kidogo katika vipakiti wenyewe uhita kete,akavitoa na kuvisukumia chini kabisa ya nguo!.


Baada ya kukamilisha zoezi lake,binti akabeba pochi lake lile chafu akatoka ndani ya chumba kile,akafunga mlango kama alivyoukuta,akaelekea getini akafunga,akatoweka mtaa ule,akiacha hatari kwa Butu!


***


Isack alizidi mfatilia Butu,huku akizidi kuwasiliana na Zidu!


"Naona anaelekea uwanja wa ndege mkuu!"


Akazidi kumjulisha!


"Ahaaa sawa,atakuwa anataka kwenda kuonana na wale watu wetu ngoja niwajulishe watoke pale kabisa,kingine badgal kashafanya yake ivyo akirudi home tu dogo hana uhuru!"


Isack alimuelewa Zidu alimaanisha nini,alimuaga akakata simu!


Safari iliendelea mpaka uwanja wa ndege wa Dia,Isack akapitiliza,kazi yake ilishaisha,maana kama angeendelea kumfatilia lazima Butu angemtilia mashaka na kitu hiki akikutakiwa!.


Butu alizikumbuka sura za wale wafanyakazi wa tano alowakamataga siku chache zilizopita.


Pia sura za wale waletaji wenye vipara zilinasa katika fikra zake.


Alienda mpaka mapokezi akajitambulisha na kutoa kitambulisho chake,akaomba apelekwe ofisi ya mkurugenzi wa uwanja ule akaelekezwa.Butu akaingia ndani ya lift kuelekea uko alipoelekezwa.


Baada ya kufika Mkurugenzi alimkaribisha Vizuri Butu akajitambulisha Kama alivyojitambulisha mapokezi

Mkurugenzi akahitaji kumsikiliza.


Butu akaomba 'list' ya wafanyakazi wote na picha zao,lengo pengine wale watano angewatambua angewabana lazima wangemfungulia kumjua mbaya wake,alitazama picha za wafanyakazi moja baada ya nyingine cha ajabu akumuona hata mmoja!...


"una uhakika hii ndo list ya wafanyakazi wako wote wa hapa earport?!"


Alimpachika swali mkurugenzi ambaye alimjibu ndo hao tu katika listi hakukuwa na wengine Butu akarudia kuwatazama tena,ila hakuona sura hata moja kati ya zile tano alizokuwa akizitafuta!


Maajabu!!!...


Utata!


Mashaka yakaanza kumvaa,hofu kumtanda!,akahitaji kuona list ya wasafiri wote walotua tar 4 ya mwez wa 4 mida ya saa tano akataja na aina ya ndege na namba zake,akapewa faili la siku hiyo akakagua,pia cha ajabu akuona picha kati ya watano wale alowakamata kabla ajaja kuwa achia kwa dhumuni la kuikomboa familia yake!...


Iweje picha zao zisiwepo?!...


Alizikumbuka sura zao fika,ila pale azikwepo!,nani anayemchezea?!, akajikuta akikosa raha,Butu akazidi kuchanganyikiwa akakifata kiti na kuketi!...


Macho yake yalikuwa mekundu,wakati akiwa kaketi pale ghafla simu yake ikaita,haraka akaitoa kucheki ni askari mwenzake Jonathan!,alokuwa akiisimamia kesi yake,haraka akaipokea ile simu...


Kwani alishakata tamaa ya kujua angefanya nini kwa kuwa kila upenyo auonao kuwa utamfikisha kumtambua adui yake unazibwa na kumuacha katika tafakuri kuu.


Ila kupigiwa na Jona kukamtia nguvu pengine alikuwa na habari njema kwake ambazo zingemuwezesha kumjua mbaya wake


Ni ule wakati Jonathan alipoamua kumpigia akapokea...


"kuna jambo nimeligundua tuonane muda huu kivulin bar tupate moja baridi,moja moto tuzungumze"


"Sawa!"


Palepale Butu hakakata pasina kupoteza muda akatoka ndani ya ofisi zile tayar kuianza safari,kivulini Bar.


***


18


Kamishna uchovu ulimchovya, alikuwa akisinzia ghafla akazinduliwa na mlio wa simu yake akaitazama alishtuka,ni baada ya kuona 'privet no,'


No za aina ile akuzipendaga kabisa ila akaamua kupokea Kama wajibu wake umtumavyo.


"Nurdin naongea sijui ni nani mwenzangu!?"


Kwa sauti ya utulivu,akijitahidi kutoweka mashaka Nurdin akazungumza...


"Nitambue kama raia mwema inatosha!"


Upande wa pili ukajibu kwa kiburi na dharau ya hali ya juu.


"Ok,nikusaidie nini?!"


Nurdin akaongea kwa hasira ni wazi akupendezwa na dharau za mtu yule


"Aliyekuwa askari wako mtihifu anauza madawa ya kulevya, Butu, kayaifadhi katika kabati lake la nguo chumbani,sasa kazi ni juu yako uamue kufatilia au upotezee juu yako mie nshakupa taharifa hiyoo"


Hapo hapo mpigaji akakata simu!


kamishna Nurdin akashusha pumzi ya kuchoka!


Ndiyo!,alichoka kwa lile aliloambiwa!, ila kama mkuu wa polisi akupaswa kupuuza chochote aambiwacho lazima achunguze mshtakiwa ahukumiwe!


Palepale akashika simu yake,tayari kumpigia Jonathan kijana aliyemwamini kati ya vijana wake wote!.


Upande wa pili baada ya Zidu kukata simu akaachia cheko kuna watu wengine alihitaji kuwa taharifu wakaweke mtego nyumbani kwa Butu ili tu akitolewa wasambaze habari zake!


Waandishi wa habari,...


Alijua polisi wangeweza kuficha jambo lile kusudi kutolipaka matope jeshi lile ila kama waandishi wangeliripoti lazima Butu angeishia pabaya.


Akatabasamu tena palepale akaichukua simu yake tayari kwa kuwasiliana nao,awapange.....


Jonathan akiwa katika kikao alimueleza kila kitu Butu,juu ya kutekwa kwa mama yule,ambaye mumewe ndiyo wao waliyo muua!,wakajaribu kuyaunganisha matukio haya mawili wakapata picha!,kwamba Silivestar familia yake ilitekwa baada ya yeye kugundulika ni msaliti,akajitoa muhanga kufa ili familia yake ipate kuwa huru!,ila sasa je Silvestar ilikuwaje mpaka kutoa siri za watu hao?,je walitapeliana?,ni watu gani wanaukaribu gani na Silvestar?!,bado maswali yakawa mengi kwao!,ila ghafla simu ya Jona ikaita...


"Nakuomba wewe na wenzako mje hapa ofisini mara moja kuna dharura imetokea"


Ikabidi kikao kifungwe,haraka Butu akarudi nyumbani kwake pasina kujua kinachoenda kumtokea.


Inspekta Jona na wenzake wakarejea ofisini!


"Bebeni silaha za moto tuelekee katika cruzer haraka twende kwa Butu,maaskari wale sasa wakawa wakishangaa,ila wakatii amri,wakaingia ndani ya gari ya polisi,Jonathan na kamishna Nurdin wakiwa mbele,huku Patrick,Paul na Isack wakiwa nyuma ya bodi,Jona akaliwasha gari tayar kuelekea kwa ins Butu!


***


Butu alikuwa sebuleni mwake akipitia pitia gazeti ghafla akasikia sauti ya ka kengele cha mlango akasimama na kwenda kufungua,alishtuka kumkuta mkuu wake na walokuwa maaskari wenzake!


"Tunahiji kukagua nyumba yako Butu!"


Nurdin alisema,butu alibaki katika mshangao pasina kuelewa nini kinachoendelea,yote yale Zidu aliyaona,katika simu yake maafisa wale wa polisi wakaingia na kuelekea moja kwa moja chumbani!


"Tunakuomba ufungue kabati!"


Butu bila ubishi pasina kujua kipi kinaenda kutokea akaingiza funguo na kufungua kabati,nguo zikaanza kutupwa chini,punde kete zile za madawa zikaanza kutolewa,palepale Butu akawekwa chini ya ulinzi, akavikwa pingu, na kutolewa nje! Cha ajabu nje waandishi walikwepo wa kutosha aikujulikana walitaharifiwa na nani!,picha zikafatia...


Butu akaingizwa kwenye gari safari ya kwenda kituoni ikafatia!,akiwa chini ya ulinzi mkali!


Tena akiwekwa na wale walokuwa chini yake kicheo!...


Walompigia saluti na kumuheshimu....


Sekeseke linaanza kuya andama maisha ya aliyekuwa inspekta wa jeshi la polisi John Butu,pasina kujua anategeshewa madawa ya kulevya katika kabati lake chumbani sasa yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi ni nini kitakachoendelea?!,


Butu atasalimika kweli?!,tusonge katika hatua hii kujua kilichoendelea!


*HATUA YA KUMI NA TISA NA ISHIRINI*


Habari za kukamatwa kwa aliyekuwa afisa wa jeshi la polisi zilizagaa,vyombo vya habari vyote vilielezea,watu mbalimbali waka andamana kushinikiza askari yule kupewa adhabu kali!.


Wakati hayo yakiendelea Mkuu wa polisi Igp Gerald Uwiyo aliketi ofisini kwake,kichwani kwake alikuwa na mawazo sana,alimkubali sana Inspekta Butu alishtushwa na habari alizozipata,hakuziamini kabisa na alijua lazima kuna mchezo kijana yake yule atakuwa kachezewa,si bure,haraka akachukua simu yake na kumtwangia Cp Nurdin,Nurdin alimuelezea kila kitu,toka kupigiwa simu na mtu alojitambulisha kama raia mwema na kumueleza juu ya kuwepo kwa madawa ndani ya kabati la Butu,walipofatilia na kufanikiwa kuyakuta!.


"Mlikagua cctv camera?!"


"Hapana mkuu hatukufanya ivyo!"


"Ndo kosa mlilokosea,haraka sana uchunguzi uanze mara moja wapatikane hao washenzi wanao mchafua huyu kijana wangu!"


"Sawa mkuu!"


"Ok,ntakutafuta acha niongee na mh Waziri naona anantafuta!..."


Palepale Igp Uwiyo akakata mawasiliano na kamishna akampokelea waziri!


"Umeona habari inayoendelea kwenye vyombo vya habari juu ya kijana wako?!"


"Ndiyo mkuu,lakini kwa hisia zangu Butu kasingiziwa awezi kuwa muuzaji kuna mchezo..."


"Usitake kunifanya nika amini kwamba Raisi alikosea kukuteua mkuu wa polisi,kijana wako kakamatwa na ushahidi,kalichafua jeshi zima la polisi bado unataka kumlinda eti ufanyike uchunguzi nina chokuomba toa tamko katika vyombo vya habari kulahani tabia hiyo na pia uhaidi adhabu kali kwa askari huyo masikio ya wananchi wote yapo kusikiliza serikali itachukua hatua gani,narudia tena apewe adhabu kali iwe fundisho kwa watu wengine hii inaonesha hata siri ya kuipoteza familia yake anaijua..."


Igp alishtuka kwa amri ile,lakini ilipaswa aifate japo moyo wake ulimuuma,haraka kama alivyoambiwa akahitisha mkutano wa waandishi wa habari aka laani kitendo kile cha Butu na kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa!...


Hakika sasa maisha ya Butu yalikuwa hatarini!


Roho mkononi!!...


Jeshi lilimtenga,marafiki walimtenga,alifikishwa kituoni akatupwa rumande na kesho yake akapelekwa mahakamani...


***


Mahakama ilifurika watu,wengi wakitaka kujua ni nini hatma ya polisi yule aliyekutwa na madawa nyumbani kwake.


Hatimaye akapandishwa kizimbani ,akasomewa shtaka lake la kukutwa na madawa ya kulevya alipoulizwa alikubali kukutwa nayo japo alikana kujishughulisha na uuzaji,alisema wazi aliwekewa kimtego,utetezi wake ukakosa nguvu akahukumiwa miaka 35 na kulipa faini,wengi walifuraishwa na hukumu ile,.


Butu mwenyewe binafsi alishangaa kesi yake ilivyopelekwa haraka haraka mpaka kuhukumiwa kwake,hapakuwa na uchunguzi,wala nini,sasa anaelekea gerezani,hakuwa na ndugu wala familia wa kumpigania,hakuwa na rafiki wala hata mpz wa kumfariji,akaingizwa katika karandinga tayari kwa kwenda kuya anza maisha mapya ya gerezani.


*'NA AHIDI NITATOKA MR X SITOKUACHA HAI,SAFARI HII UMESHINDA ILA SAFARI NYINGINE UTOSHINDA NASEMA'*.


Huku akiwa kaji inamia,ndani ya karandinga lile Butu alijiwazia safari ikiendelea.


***


*SURA YA TANO*


*LANGO LA JEHANNAMU:*


Lango la geti kubwa likafunguliwa na wanajeshi walovaa nguo za magereza,karandinga lile lililobeba wafungwa likapita.


Lango likafungwa!...


Karandinga lile ilitembea kama dakika kumi na tano katika njia ndogo huku pembeni ya njia hiyo pakiwa na miti,ilikuwa ni mfano ya hifadhi ya msitu ndo wameingia.


Hatimaye baada ya mwendo ule wa dakika kumi na tano na ushee hatimaye walifika mwisho wa kale ka njia mnyohofu ,mbele yao palikuwa na jengo kubwa sana ambalo juu kidogo ya mlango palikuwa na maandishi makubwa mekundu yalosomeka

'GEREZA LA SEGEREA'.


Mbele ya jengo lile palikuwa na bustani nzuri ambayo katikati yake iliwekwa bendera ya taifa,palikuwa na uwanja mkubwa!.


Hapa ndipo wafungwa waliposimama mistarini pale ilipowabidi kukutana,na jengo lile ndipo zilipokuwepo ofisi ya mkuu wa magereza na askari wake,.


Gari likapakiwa eneo maalumu la maegesho wafungwa wote ambao walikwepo takribani kumi na mbili wakashushwa na kuswagwa kuingia ofisini!.


Walifikishwa mpaka ofisi ya mkuu wa magereza,wakapewa mavazi mekundu yalokwepo katika mfumo wa ma ovaroli,pamoja na namba za miaka yao watakayoishi gerezani pale!.


Butu akipewa namba 35 ikiwa na maana ni miaka 17 na miezi sita,kwa hesabu za kifungwa!,


Mkuu wa magereza kimuonekano alikuwa ni mzee kichwa chake chote kilijaa mvi,ila ukakamavu ulinyonya uzee wake wote,akaonekana ni mtu katili,asiye na roho ya huruma hata chembe,hakuwa mtu wa kucheka hata na askari wake,kugomba ilikuwa hulka yake!...


"Na sikia kuna polisi hapo ni yupi huyo Mshenzi?!".


Mkuu yule wa polisi akauliza kishari,wala Butu akuangaika kumjibu,mpaka askari mmoja alipo muonesha kwa kumnyo oshea kidole!.


"Huyu anao nekana ni jeuri apelekwe kwanza lango la jehanamu akakae huko masaa 24 kesho ndo tutampangia mahabusu kati ya triple a,b au c sawa?!"


"Sawa mkuu!"


Wafungwa wale wakatolewa sasa kupelekwa katika vyumba vya mahabusu yao!,kesho ndo wangeanza kazi rasmi!.


Baada ya wafungwa wale 12 kutolewa,mkuu yule akashika simu yake na kuipiga!.


"Zidu nishamuona mtu wako,masaa 24 ya awali ataishi na siafu nyoka,na wadudu wote watambahao waumao,hana siku mbili atakufa tu kwa mateso tutakayo mpa hapa ndo segerea!".


"Safi sana ancle,kijana mdogo anataka kupambana na watu wakubwa mwache ajionee".


Zidu aliongea kwa furaha,akakata simu!.



Kwa upande wa Butu si kwamba akulijua lango la kuzimu,yeye ni askari,sifa ya jengo lile alilijua,jengo hilo lilitumika kama adhabu kwa kumuua muhalifu aloshindikana,yeye anapelekwa huko,kwa uhalifu gani aliokuwa nao?,kwa kosa gani alofanya yeye mpaka kustahili kupewa adhabu kubwa kiasi kile?!....


Tumaini sasa la kuishi lilimyeyuka, roho mkononi,ilikuwa ni nadra mtu kuingizwa kule na kutoka,hakukuwa na sakafu,palikuwa na mashimo ya nyoka wakali,siafu wa kutosha,mashimo ya panya wakubwa ambao si wakawaida na juu kabisa kulikuwa na popo walotambulika kwa jina la popo mdonoo.


Unajua kwa nini walipewa jina hilo?!


Butu alijua sababu na mbaya zaidi chumba hicho kilichojengwa kwa umbo la duara,kilikuwa ni giza tupu.


Hatimaye ka mlango ka dogo kama cha kuku ila cha chuma kakafunguliwa akapewa amri aingie, akatii, kakafungwa!.


Ghafla baada ya kuzama ndani likasikika yowe!.....


Kunanini?!



Sekeseke lina ya andama maisha ya Inspekta wa jeshi la polisi John Butu roho mkononi,hatari ya kuyapoteza maisha yake anaiona kabisa,anasekwa ndani ya gereza la Segerea mbaya zaidi anajikuta katika selo ijulikanayokwa jina la lango la jehannamu,selo hiyo uki ingizwa aina stori ya kutolewa ukiwa mzima,kwanza ndani kumetawaliwa na kiza,hewa hafifu,na wadudu waumao,je Butu atasalimika ndani ya hayo masaa 24?!


Tusonge katika sehemu hii ya ishirini na moja


HATUA YA ISHIRINI NA MOJA


Baada ya Butu kusukumiwa ndani,kamlango kale kakafungwa,Butu aliachia yowe akijua wazi sasa ndo anaenda kukutana na mateso makali,alipokewa na kiza kikali,nuru ya mwanga aikupata kuwepo ndani ya eneo lile,pua zake zikanusa harufu kali,tena harufu mbaya,ni mizoga ya watu ilooza ghafla akahisi mwili ukianza kumchoma choma,akujua ni saa ngapi alivua lile ovaroli akitoa wadudu wale aina ya siafu waloanza kumtembelea,


Wakati akiwa bado ana angaika ghafla akadonolewa usoni,hakupata tabu kugundua kuwa wale ni popo mdonoo!


Akujua afanye nini,ashike wapi,kati ya mwilini au usoni,ghafla akahisi akidonolewa mguuni,panya nao walisha anza yake.


Ndani ya dakika tano mwili wote ulimvimba,akajikuta akishindwa kuvumilia kuendelea kusimama akaenda chini,hapo ndipo wadudu walipoendelea kumshambulia vizuri,kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo nguvu zilivyozidi kumuisha na hali ilizidi kuwa mbaya!.


Ambacho hakutaka kusahau ni swala la kusali sala zake za mwisho,kumkabidhi Mungu mwili wake!.


Imani kwamba ataendelea kuishi ilishamtoka kabisa.


***


TRIPLE C JAIL


Eneo lingine ndani ya gereza lile la segerea juu kabisa ya lango paliandikwa Triple c,gereza hili la segerea lilijengwa kwa matabaka,na kila tabaka lilijitegemea katika makazi yake,kula kwao,na hata maaskari wake,japo mkuu wa gereza alikuwa ni mmoja,na katika kila tabaka walizungushiwa ukuta mkubwa,lango la kuzimu lilikwepo upande wa triple c,watu walokwepo katika tabaka hili ni wale waloshindikana,majambazi sugu,watu makatili au wenye kesi za kusta ajabisha,kuuana humu ilikuwa kawaida,hata maaskar wao walikuwa nunda vilevile na kila mara walikuwa na mbwa waloijua kazi yao vyema!


Kutoka triple c,kulikuwa na triple B,huku walikwepo watu wa kawaida,wezi wa kuku,wakabaji,wauaji wa kutokukusudia,wezi wa mtandao,na aina nyingine ya wahalifu wadogo wadogo,huku walikwepo askari wakawaida na tabaka la mwisho ni triple A,hawa ni class A,Vip wafungwa walikula chakula kizuri,walilala pazuri waliangalia Tv,walisoma magazeti,hawakupewa kazi ngumu,wengine hawakupewa kazi kabisa,huku walikwepo viongozi wakubwa wa dini,viongozi wa serikali,wasanii,huku ndipo ilipaswa aswekwe Insp Butu naye ndo alijua ivyo ila kitendo cha kupelekwa lango la kuzimu kukamtilia shaka.


Ndani ya ofisi ya mkuu wa magereza Dunga,mbele yake alikwepo askari wake mtihifu,dakika 15 zilishakata askari yule akiwa mbele ya mkuu wake pasina kusemeshwa chochote,dharau ya aina gani hii!,Dunga akijifanya yupo bize na game katika simu yake mguu kauweka mezani,kijana kasimama wima kikakamavu mbele yake,akumjali mpaka alipo kosea na mchezo kuisha ndipo aliposhusha miguu yake chini akaweka simu yake chini na kumwangalia askari aliyekuwa mbele yake!.


"kruta nenda triple c,namuhitaji Manzua haraka ofisini kwangu"


"Sawa mkuu!" Kijana yule akajibu kikakamavu na kujinyanyua kidogo ishara ya kutoa heshima akageuka na kuufata mlango.


Akatoka!.


Alienda mpaka lango la Triple c,akamnong'oneza mlinzi naye akarudi zake,mlinzi akachepuka kuelekea zilipo selo apatikanapo mtu huyo!...


***


Ndani ya selo moja alionekana kijana mmoja alojengeka kimazoezi akiwa kamkamata vyema kijana mwenzake kamnyongea ukutani,kimya kilitawala sauti ya mwamba yule pekee ndo ilokuwa ikisikika.


"Mali ya manzu huwa aipotei, ulinidhulumu uraiani ukajua nimefungwa utanufaika pekee yako wapi sasa leo nakuua kwa mkono wangu sheitwan wewe"


Jamaa yule alomkaba mwenzake aliongea kibabe akizidi kumnyonga mtu yule,punde maaskari wakawasili,ndipo mtu yule alipo muachia yule alo mnyonga hata ivyo hakuwa hata na punje ya uhai tena!"


"Manzu umeua tena?!"


Askari yule alokuja alio ngea kwa ukali,huku akimfata manzu gobole kalishika kwa mbele yani eneo silaha inapo chomokea.


Polisi wengine watano wakiwa nje langoni,silaha wakiziweka tayari!.


Askar yule ambaye ndiye alokuwa langoni na kuambiwa Manzua anahitajika kwa mkuu,alilifikia njemba lile na kuinyanyua gobore lake ile analishusha kichwani kwa sugu,njemba ikapangua na kuudaka ule mkono akauzungusha ukalia kaaa,kilichofatia ni yowe,punde askari wale watano wakazama kumweka kati,ila bila kutegemea jamaa alikuwa mwepesi akafurukuta akimzawadia kila askari teke lake aliye enda kumdondokea mfungwa waliyekuwepo ndani mule,...


Wote wakasimama na kukimbilia gobore zao ila kabla awajafanya kitu ikasikika nje sauti!


"Acheniii!"


Tena ikiwa sauti kali na ya amri maaskari wakasitisha jambo lile, wafungwa wote wakasimama! Kumpa heshima mtu yule,


"Nilituma niitiwe huyu mtu matokeo yake mnampiga ndicho nilicho tuma?!"


Mkuu wa gereza akauliza huku akimwangalia yule mfu alouwawa muda mchache ulopita!


"Lakini mkuu kausika na mauaji tena!"


Askari yule alopigwa wakwanza akajibu huku akishika mkono wake,


"Sicho nilicho tuma mfatilie,chukueni huo mwili mkauzike,jembe langu nifate!"


Mkuu yule akaongea kwa kiburi huku akimwangalia Manzua,aloachia tabasamu,akamfata mkuu wake nyuma,yeye kuwapiga maaskari tena maaskar watukutu ilikuwa kawaida,kuua wafungwa kwake wala akujali...


Maaskari walishindwa kumuua kwa kuwa alipendwa sana na mkuu wao,ivyo kumuua ni kujitafutia kukosa kazi na ikiwezekana kuishia pabaya.icho kikampa uhuru bedui lile kufanya atakalo,hakukuwa na wa kumbambaisha!.


Alifika ofisini kwa mkuu wa magereza akapewa ishara aketi maongezi yakafatia


"Manzu kuna kijana kwa saivi yupo ndani ya lango la kuzimu,sijajua kama atapona,ila akipona kesho atakuwa katika chumba chako mpe mateso uwezavyo hata ukimuua sawa tu!,hii ni kazi ya kwanza nakupa na sitegemei kuniangusha sijawah kukupa kazi kabla,na ukfanikiwa hili ntakupa mwanamke mzuri wa kukidhi haja zako!..."


Dunga akaweka tuo,kwa furaha jamaa yule hakuwa na la kujibu aliishia tu kufurahia,akapewa ruksa aondoke zake,gerezani kupewa mwanamke ilikuwa ni zawadi kubwa alikuwa na miaka zaidi ya mitatu ajawah kukutana na mwanamke,yeye hakuwa na muda mrefu sana gerezani...


Aliomba Mungu huyo maiti wake atoke mzima aje afie mikononi mwake!,japo akujua ni mtu wa aina gani!


BUTU ATASALIMIKA LANGO LA JEHANNAMU,AKITOKA ATAPONA KWENYE MIKONO YA MANZU?!.


TUONANE KATIKA HATUA IFUATAYO KWA MWENDELEZO


RIWAYA YA KIJASUSI&UPELELEZI


SEKESEKE(ROHO MKONONI)


MTUNZI:ZUBERI MARUMA22


WHATSUPP:0759427653


No:0673999120

0624408343


22


Aliyekuwa inspekta wa jeshi la polisi John Butu anaingia katika sekeseke la hatari!


Dalili za kuyapoteza maisha yake zinaonekana dhahiri shahiri!


Anategeshewa madawa ya kulevya anakamatwa anahukumiwa na kuswekwa lupango,mbaya zaidi anaingizwa ndanh ya selo ijulikanayo kama lango la jehannamu,hakuna historia ya kuingia huko na kutoka ukiwa hai naye anajikuta katika mateso makali je atasalimika kweli?! Tusonge kuzidi kuburudika zaidi!


HATUA YA ISHIRINI NA MBILI


Kiza kilitanda ndani ya macho yake,kumbukumbu kwa mbali zikaanza kumjia!.


Akajaribu kufumbua macho yake, yalikuwa mazito kana kwamba yakigoma kufumbuka ila hatimaye yakafumbuka.


Akajaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi hapo alipo,kumbukumbu azikumsapoti,zikagoma kabisa,ila alijua muda ule ni usiku kutokana na kiza kizito,kichwa kilikuwa kizito kwa maumivu makali.


Akatuliza akili!,hapo hapo sasa ndipo kumbukumbu zilipoanza kumrejea maumivu makali ya kausweka moyo wake,akataka kujaribu kusimama pale alipojilaza akashindwa,akatamani hata kukaa pia kwake ikawa ngumu.


Akang'amua hata mwili wake pia umekufa ganzi.


Hapo ndo akachoka kabisa!


Akujua amelala kwa muda gani pale,tumbo liliunguruma kwa njaa angekula nini na uwezo wa kutafuta kwa kipindi hicho kigumu cha kutumikia adhabu alopewa na nchi yake!


Maumivu ya kichwa yalizidi kumgonga,kizunguzungu kikali kikamvaa,ganzi aloipata ilimsaidia kwani hakusikia maumivu ya kung'atwa na siafu wala panya,ikabidi aendelee kulala akiwa kakata tamaa kabisa! na alitamani kufa kwenda kuungana na familia yake kuliko mateso yale mpaka muda ule akujua anapambana na kina nani!,ila alijua ni mtandao mkubwa na ni watu wenye uwezo mkubwa kumzidi hata yeye.


***


Katika jumba moja la kifahari la Zidu alitumihalo kufanyia baadhi ya mikutano yake ya siri,kuhifadhia pia mateka wake,juu ya ghorofa ya tatu katika varanda ya nje kwenye makochi walikaa watu wa tatu,kilikuwa ni kikao cha siri,Zidu akitoa mrejesho wa kazi yake kwa mheshimiwa Raisi na waziri mkuu wake.


"Yule kijana kwa sasa yupo magereza na nimeshaongea na mkuu wa gereza lile mtu yule afe tena kwa mateso makali!"


Walimpongeza sana Zidu kwa kazi aloifanya,alipo yeye hapakuwa na kinachoharibika,waliendelea na maongezi yao wafanyakazi wa jumba lile waka wa andalia chakula wakala hatimaye wakaaga!.


***


BAADA YA MASAA 24


NDANI YA OFISI YA MKUU WA MAGEREZA:


Mkuu wa gereza la Segerea Dunga aliketi katika kiti chake,macho yake yakiwa katika kompyuta yake,mdomoni kulijaa mabuyu alokuwa akiyatafuna na mbegu kuziweka kwenye meza yake,buyu hizo alichukua katika kakopo kadogo!,ambapo alikanunua kakiwa kamejaa na sasa ndo alikuwa anamalizia,macho yake yalidondokea katika saa ilokwepo ukutani hapo ofisini kwake akatabasamu,zilisalia dakika kumi kukamilika kwa masaa 24 toka kuletwa kwa Butu pale,akashika mkonga wa simu yake na kuweka masikioni akabonyeza namba kadhaa simu ikaita!


"Naam afande"


Upande wa pili ukaitika kwa sauti nyororo ya kike,


"Niitie askari yeyote hapo mapokezi"


"Sawa afande,.." Binti yule akajibu na kukata simu


"Mudy unaitwa ofisini kwa mkuu"


Pale pale binti akamlenga mtu alomtaka yeye,na kijana huyo binti alo mpendekeza akijua bosi ka muhitaji akajinyanyua na kuelekea ofisini kwa mkuu wake!.


"Kusanya hizi mbegu ukazitupe kwenye dustbeen hapo nje uje hapa!"


Kijana yule akazikusanya zile mbegu bosi wake alizokula na kwenda kuzitupa kisha akarejea kwa mkuu wake!.


"Nenda kamtoe yule mfu lango la jehannamu kama ni Maiti mwacheni aozee huko,ila kama ni mzima mkamtupe triple c tumeelewana?!"


"Ndiyo mkuu"


Yule askari alijibu huku akionesga wasiwas wa waziwazi usoni mwake,aliushangaa ukatili wa mkuu wake ila kwa kuwa tayari ilikuwa ni amri ilikuwa lazima akaitelekeze.


Akawashtua maaskari wenzake, wakaelekea lango la jehannamu wote walijua wangekuta maiti kwani mtu yule toka awekwe kule akula chochote.kunywa wala kuonja,tena akiwa ndani ya mateso makali!


Leo wamkute hai?!


JE BUTU ATAKUWA MZIMA?! TUONANE KATIKA SEHEMU IJAYO KWA MWENDELEZO


RIWAYA YA KIJASUSI&UPELELEZI


SEKESEKE(ROHO MKONONI)


MTUNZI:ZUBERI MARUMA22


WHATSUPP:0759427653


No:0673999120

0624408343


23


Aliyekuwa inspekta wa jeshi la polisi John Butu bado maisha yake yapo hatarini,ndani ya masaa 24 anafungiwa ndani ya chumba kijulikanacho Kama lango la jehannamo huko apewi chakula, anakutana na wadudu wa uchungu wa kila aina,baada ya masaa 24 kuna mtu anatumwa na mkuu wa magereza akamfate,akimkuta hai apelekwe triple c,akikutwa maiti aachwe tu huko huko,kijana yule alotumwa akifatwa na wenzake wanaenda mpaka kwenye selo ile wanafungua mlango na kuchungulia wana cho ona kinawashtua je wameona nini?!


Tusonge kupata mwendelezo


HATUA YA ISHIRINI NA TATU


vijana wale wakafika,mmoja akachuchumaa na kufungua kale ka mlango kisha akamulika kwa kutumia tochi iliyokuwepo mkononi mwake,akuamini alichokiona,Butu alikuwa kakaa kitako tena akionekana mwingi wa mawazo,.


"Yupo hai,haya toka haraka"


Askar yule aliwa ambia wenzake muda huo huo akimpa ishara Butu atoke kule,Butu alisimama,akajitahidi kupiga hatua akaenda chini,mwili wote bado ulimuuma na tena ulikosa nguvu ikabidi atambae alipotoka akanyanyuka wakamsaidia kumshika mpaka selo,wote walimuonea huruma ila ndo ilikuwa amna namna,walimfikisha katika selo triple c,lango likafunguliwa akasukumiwa ndani!.


Wafungwa wakampokea kwa furaha akiongozwa na nyapara alokwisha pewa kazi na mkuu wa gereza kumtesa kijana yule ikiwezekana hata kumuua amuue tu.


Kabla akijafanyika chochote kengele ya msosi ikagongwa wote wakatoka, Butu akijitahidi kutembea kwa kushika ukuta asidondoke,naye akachukua sagani yake na kujipanga katika msitari,hatimaye zamu yake ikafika naye akawekewa chakula.


Mpaka muda huo hapakuwa na mfungwa alotaka urafiki na yeye,wengi wakisema hakuna urafiki kati ya askar na mfungwa.


"Chezo yule fala si ndo alinikamataga akanipiga sana na kunisweka rumande,akasimama mahakamani kama shahidi mi nikafungwa sasa leo kaingia kwenye kumi na nane zangu ataisoma namba"


Ilisikika sauti ya mfungwa mmoja ikimnong'oneza mwenzake,na palepale akampa sahani yake amshikie taratibu akamfata Butu pale alipo!


"Hoya we fala unanikumbuka!, ulipokuwa kitengo ukajiona afisa utopatwa na matatizo leo umeingia kwenye 18 zangu utaupenda utawala!"


Mfungwa yule alokuwa na namba 15 katika ovaroli lake akaongea kwa kiburi,ila kwa jeuri Butu akawa anakula,alijua mambo kama haya yatajitokeza ivyo alijua jinsi ya kukabiliana nayo,alowatia kule ndani ni wengi hivyo alijua visasi ni vya kutosha,bila uwoga,bila kumtazama usoni yeye akaendelea kula,jamaa akazidi kukasirika.


"Yani wewe boya naongea na wewe nawe waendelea kula nadhani ujanijua vizuri wewe".


Mtu yule akapiga hatua kadhaa na kumfikia Butu akamnyang'anya ile sahani ilikuwa kosa,ndani ya masaa 24 ajala,akajikuta hasira zikimpanda nguvu zikamjia akajiinua akapiga hatua ya kwanza hatua ya pili akamdaka kijana yule namba 15 kola ya ovaroli lake akamgeuza na kumzawadia ngumi moja ya usoni,jamaa akaachia chakula,butu akakidaka.


"Weweeeeee!, tena na usije ukajaribu tena kuingia katika vita yangu sitosita kukuua,usije ukajaribu tena mpumbavu wewe"


Butu alimpa onyo huku akimbana mdomo tena kwa nguvu,alipo maliza akamsukumia kule,akageuka sahani yake mkononi akarejea alipokuwa ameketi awali.


Tukio lile Nyapara Manzua aliliona,hapo akatambua ukorofi wa mtu yule!.


Si goigoi kama alivyodhani,baada ya chakula wakarudishwa katika selo zao.


Butu alienda akatafuta eneo akaketi,akaegemea ukuta,akaji inamia akiyapa nafasi mawazo kukiandama kichwa chake.tayari alishaua viumbe visivyo na hatia,na siyo ivyo tu amejikuta akiwa gerezani kwa kosa ambalo akulifanya,wakati akiendelea kuwaza si ndo Manzu akazama ndani,kwanza alishtuka kumkuta Butu kakaa sehemu yake kwake ikawa kashapata sababu,akamfata akiwa mwingi wa jazba.


"We kijana nani kakuruhusu ukae hapo nadhani ujataka kumjua Manzu ni nani sasa leo utanijua vizuri."


Manzua akapayuka kwa hasira huku akipiga hatua ndefu kumfata pale alipo,Inspekta Butu akanyanyua kichwa chake,akawa tayari kumsubiria mtu yule kweli Manzua alifika,akanyanyua mkono wake aloukunja ngumi akiupeleka alipo Butu,kijana akakinga mkono wake mkono wa Manzu ukapiga mkono wa Butu,ndani ya sekunde ile ile Butu akajinyanyua na kukaa tayari,Manzu akapiga hatua tatu ndefu za chapchap nyuma,akaunyanyua mguu wake kwa uwepesi kumuendea Butu,ila kijana akawa tayari kashaliona lile teke akalipangua kwa mkono wake,sambamba na kurusha konde zito shavuni kwa Manzua likampata sawia,manzu aka achia mguno wa maumivu,ila akajikaza akataka kujaribu kuirudisha usoni Butu akainama ngumi mbili zikapiga hewa wakati alipoji inua akarusha konde jingine la tumbo Manzu chini...


Wakati hayo yakiendelea wafungwa walikuwa wakishangilia kupigwa kwa manzu,aliwaonea sana,si wafungwa pekee hata maaskari nje walichungulia wakifurahia kitendo kile.


Kila pigo Manzu alilopiga aliambulia maumivu,mdogo wote ulitapakaa damu...kelele za ua,ua,ua,ua zilizagaa,


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG