Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

THAMANI YA FUKARA - 2

   

Simulizi : Thamani Ya Fukara

Sehemu Ya Pili (2)


"Lakini shida ni moja mpezi,mimi kwetu masikini hatuna chochote nyie kwenu matajiri huoni kuna tofauti?"aliongea Gabi kwa sauti ya chini,

"Ondoa shaka,kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzie wote wataishia shimoni"aliongea Doris,

"Una maana gani kusema vile?"aliuliza Gabi,

"Namaanisha kuwa huwezi kufanikiwa kama umemshika maskini mwenzako,lazima masikini awe na tajiri ili badae yule tajiri amuinue masikini,hivyo shaka ondoa maisha mazuri yatatoka kwetu nitahakikisha ukitakacho unakipata"aliongea Doris,maneno yale yalimpa nguvu Gabi na kuona adhima yake ya kuwa tajiri itatimia siku zijazo,

"Ndo maana nakupenda yaani unaonekana kunijali sana"aliongea Gabi,mda huo ulikuwa mda wa mapuziko,mara kengere iligongwa kumanisha mda wa mapuziko umekwisha,yote tangu mda ule Doris amekaa na Gabi Layla alikuwa anawaona,hakuwa na hofu kabisa,

"Naona mnacheka yaani natamani wewe ndo ningelikuwa mimi kwa mda ule,eehe kasemaje?"aliuliza Layla,

"Si unajua mtu na shemeji yake yaani stori kama zote"alijibu Doris,Layla aliachia tabasamu pana kusikia maneno ya rafiki yake,lakini kila alipokuwa anamwambia amukutanishe na Gabi Doris alikuwa anakataa,kila mda alimwambia kuwa asiwe na papara,

"Simba mwenda pole ndo mla nyama rafiki yangu,Gabi yupo na mpaka utamchoka hivyo usiwe na wasiwasi"aliongea Doris,Layla alizidi kuvumilia kuna mda alikuwa anatamani kumwambia ukweli lakini alijua fika kuwa anaweza kuaharibu hivyo kazi alimwachia Doris.

Baada ya miezi miwili Gabi alikuwa na pesa nyingi bado hakutaka kumwambia mama yake,alihakikisha zile pesa zinakuwa kwenye usalama,hakuwa na ndoto za kuendelea ba shule alijijua mapema kutokana na matokeo aliyokuwa anayapata.

Ilikuwa siku ya ijumaa,siku hiyo Doris alimfuata Gabi na kumwambia kuwa siku ya jumapili waweze kuonana hadi sehemu ya kukutania alimwambia,Gabi hakuwa na kipingamizi,

"Lakini mpenzi mimi siko vizuri yaani nina mawazo kabisa"aliongea Gabi kwa sauti ya upole na kuketi chini kabisa huku akionekana kuwaza sana,

"Shida nini mpenzi lakini siuniambie naweza kukusaidia,na pia utambue kuwa mimi ni mpenzi wako hivyo unaponificha utakuwa hujanitendea haki"aliongea Doris kwa unyonge,

"Doh we acha tu umasikini huu bwana daah!"alisema Gabi,

"Hicho ndo kitu nisichokitaka mpenzi, usiseme kuwa wewe ni masikini labda nambie ni kitu gani kimekunyima raha"alisema Doris huku akimkazia macho Gabi,

"Asee mama yangu anaumwa sana,sijui hela nitatoa wapi mimi"ghafla baada ya kumaliza kusema yale maneno alianza kutoa machozi ya uongo,Doris alijaribu kumtuliza na kumhaidi pesa siku inayofuata,Gabi aliyafuta machozi huku akichekea moyoni,kila alipokuwa anaiangalia hali ya nyumbani kwao ndivyo alivyozidi kupata mawazo ya kutunza pesa,hata shuleni chai alijinyima licha ya kuwa pesa alikuwa anapewa nyingi,

"Kwakuwa tulipanga kuonana jumapili basi tuonane kesho ili nikupe pesa umuwahishe mama hospital"aliongea Doris kisha akaagana na Gabi.

Kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo Layla alizidi kupata hofu juu ya Doris,lakini yale mawazo aliyapuuzia na kujisemea moyoni kuwa rafiki yake yule wa kushibana hawezi kumgeuka,akiwa kwenye mawazo yale mara alifika Doris akionekana kutokuwa sawa,

"Shida nini mbona tangu asubuhi ulikuwa vizuri?aliuliza Layla,

"Shemeji yuko anatoa machozi,yaani analia kama mtoto mdogo"aliongea Doris,"we sema kweli!kapatwa nanini?aliuliza Layla kwa tahamaki kubwa,

"Mama yake anaumwa na yeye hana hela za kumpeleka hospital"

"What!!(nini)mama anaumwa?

"Ndio ndo nilikuwa naongea naye mda si mrefu"aliongea Doris kwa sauti ya kutia huruma,

"Basi mwambie kesho nitakupa pesa umpelekee ili mama akatibiwe"aliongea Layla,Doris alikubali na kumuaga rafiki yake yule kuwa anakwenda kumwambia Gabi,zile taarifa zilimvuruga kabisa Layla,mda wote alikuwa hatulii darasani alitamani mda uende haraka ili akachukue pesa kwa ajili ya matibabu ya mama yake Gabi.Mda wa masomo ulipokwisha wanafunzi wote waliruhusiwa,

"Sasa tukutane kesho saa tatu asubuhi ili umuwahishie hizo pesa"aliongea Layla akiagana na Doris.

Kesho yake asubuhi majira ya saa tatu tayari Doris alikuwa na Layla,mara baada ya kupeana salamu Layla alitoa noti za elfu kumi zipatazo tano ikiwa na thamani ya elfu hamsini na kumkabidhi Doris,

"Ziwahishe ili mama akatibiwe"aliongea Layla,Doris hakutaka kukawia lakini kabla hajapiga hata hatua tano Layla alimsimamisha,

"Unaonaje tukaongozana wote ili tukamuone huyo mgojwa?"Layla alimuuliza Doris...



Unaonaje tukaongozana wote ili tukamuone huyo mgojwa?aliuliza Layla,Doris alinyamaza kimya huku kidole chake kikiwa mdomoni kana kwamba anafikiria kitu cha kujibu,

"Mbona kimya tena au hutaki tuongozane?"aliuliza tena Layla,

"Aaaha,hapana nafikiria jinsi ya kuwakutanisha,yaani iko hivi wewe usiende nyumbani kwao,wacha mi niwahi halafu nitamwambia jioni muonane"Doris aliongea lakini alionekana kuwa hayuko sawa hata katika uongeaji wake,

"Wacha niwahi"punde baada ya kusema hayo alizipiga hatua ndefu ndefu kwenda kule walikokuwa wamepanga kukutana na Gabi,

"Nilikwambia kuwa usiwaze mpenzi ukiwa na mimi"aliongea Doris mara baada ya salamu,Gabi alishindwa kujizuia alijikuta akimkumbitia na kumbusu shavuni, jambo lile liliweza kuziamsha hisia za Doris lakini alijizuia,"vipi lakini hali ya mgojwa ikoje?"

"Kwa leo angalau ila lazima twende hospital ili akafanyiwe vipimo tujue nini tatizo"aliongea Gabi,moyoni alijawa na furaha alijiona mtu mwenye bahati sana,alilazimika kwenda shule sare zikiwa zikiwa zimechanika lakini hakudhubutu kutoa pesa aliyokuwa anapewa.Maongezi yao aliyakatisha Gabi,

"Sasa mpenzi wacha niwahi ili twende hospital"aliongea Gabi,waliagana huku wakihaidiana kukutana siku ya juma tatu shuleni,

"Ukisikia kuokota embe chini ya mnazi ndo huku,yaani pesa zote hizi?ama kweli mungu akitaka kukupa huwa hakupigii simu"alijisemea Gabi huku zile pesa akizikunja vyema,zilikuwa elfu themanini Doris aliongezea elfu thelathini.Baada ya kufika nyumbani Gabi alielekea chumbani kwake na kuzihifadhi zile pesa,alihakikisha mama yake hatambui chochote,

"Siku nikizitoa hizi pesa lazima mimi na mama yangu tuache kuishi haya maisha ya taabu"alijisemea kijana Gabi.Siku ya juma tatu kulipambazuka na hali ya hewa safi iliyokuwa na ubaridi wa wastani,siku hiyo Layla alichoka kumvumilia rafiki yake hivyo alipanga kumtafuta Gabi na kumwambia ukweli uliokuwa unamsumbua kwa mda mrefu,alishuka ndani ya gari kisha akaenda mpaka darasani bahati nzuri aliweza kumkuta Gabi akiwa anayaweka madaftari yake sawa,ikumbukwe hakuna kitu kigumu kama mwanamke kumwambia mwanaume,Layla alibaki amesimama huku akitafakari amuanze vipi,hata Gabi hakunyanyua uso wake kumtazama Layla yeye alibaki kupanga madaftari yake,

"Hivi nitaficha haya maradhi mpaka lini?nasahau kabisa kuwa kidonda cha mapenzi hakitibiki,hapana lazima niuvunje ukimya"alijisemea Layla na kuuvaa moyo wa ujasiri kisha akasogea mpaka pale alipokuwa Gabi,kabla hata hajamwambia chochote mara ilisikika sauti ikisema,

"Nyie mda wa kufanya usafi humu darasani mnafanya nini?hebu tokeni nje kila mtu aelekee kwenye eneo lake la kufanyia usafi"alikuwa mwalimu,Gabi kusikia vile alitoka nje akiwa wa kwanza,kitendo kile kilimkera sana Layla lakini hakukuwa na ujanja,

"Hata hivyo hakijaharibika kitu leo ni leo na hili jambo siwezi kumshirikisha Doris wacha nilifanye mwenyewe,nimechoka kusubiri mvua isiyo nyesha"alijisemea Layla,hakusita kumlaumu yule mwalimu.

Majira ya saa nne asubuhi iligogwa kengere kuashiria mapumziko,Layla kweli siku hiyo alipania kuvunja ukimya,alipomuona Gabi anatoka nje naye hakusita alimufuata kwa nyuma, Doris aliweza kuona tukio lile lakini alijua fika kuwa Layla ni mwoga hivyo hawezi kumwambia Gabi aliendelea na kuangalia mitihani yake akiwa mle darasani,

"Simama mara moja"ilikuwa sauti ya Layla ikimsimamisha Gabi,naye hakuwa na hiana alisimama japo alijiua dhahiri kitakachosemwa,

"Mambo vipi"alisalimia Layla,

"Salama tu"alijibu Gabi,

"Mbona hujanipa jibu langu?alisema Layla,licha ya kujikaza kuongea lakini mapigo ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio,

"Jibu?jibu gani?"aliuliza Gabi kwa taharuki,

"Ina maana Doris hajamwambia chochote?"aliuliza Layla,Gabi alijua tayari kimenuka,alishusha pumzi ndefu kisha akatulia kwa sekunde kadhaa kichwa chake akiwa amekiinamisha chini,

"Labda aliniambia ila huenda nimesahau,nikumbushe basi"alisema Gabi,Layla kabla hajaongea kitu chochote pumzi ndefu alishusha na kuangaza macho kulia na kushoto alipohakikisha hakuna anayewaona alishusha tena pumzi nyingine iliyokuwa na uoga ndani yake,

"Unatambua fika kuwa nakupenda,nimejaribu kukuonyesha kila aina ya vitendo kuwa nakuhitaji lakini mwenzangu huonyeshi ushirikiano wowote,nimefanya vibaya kwenye mtihani haya yote ni kwa sababu yako,naomba ujali hisia zangu"aliongea Layla huku kitambaa kikiwa mikononi mwake akifuta machozi,Gabi alikoswa la kuongea aliinimisha kichwa chini huku akiwaza wale watoto wa matajiri kipi hasa wanachokitaka kwake hakupa jibu kwa haraka,Layla aliendelea kutoa machozi huku kwikwi nazo zikiwa zinasikika,

"Yes (ndio)hii ndo fursa sasa ya kupiga pesa,yaani hapa lazima nicheze kama pele"alijisemea kimoyo moyo,

"Basi yafute machozi jibu lako nitakupa kesho"aliongea Gabi kisha akaondoka akamuacha Layla akiwa bado anayafuta machozi,ila moyoni alifarijika sana na kujuta kuwa kwanini siku zote hizo alishindwa kumwambia,alipohakikisha uso wake ameuweka vyema alirudi darasani na kumkuta Doris aliyekuwa anaendelea na zoezi lake la kupanga mitihani hakuongea naye zaidi aliketi kwenye nafasi yake,

"Ngoja kesho nije na zawadi ili aweze kufurahi"alijisemea Layla.

Gabi alianza kupanga mbinu za kuweza kuwatumia wale watoto wa matajiri,alijipa tahadhari kubwa kuwa anapaswa kuwa makini vinginevyo itakuwa hatari, lakini nia yake alitaka baada ya kumaliza shule awe tajiri tayari,alianza kubuni biashara mbali mbali atakazozifanya baada ya kuhakikisha kuwa mtaji tayari uko mikononi mwake.Siku ilifuata Layla alikuja na elfu ishirini kisha akamkabidhi Gabi,hakuwa na uoga tena kama wa hapo nyuma yote hayo hakumshirikisha Doris,

"Utakunywa chai lakini vipi hali ya mama inaendeleaje?"aliuliza Layla,maneno yale yalimfanya Gabi ataharuki kwa kiasi kikubwa,

"Mama?inamaana Doris alikuwa anamwambia huyu hizi habari?kama ni hivyo basi nimekwisha"alijisemea Gabi.




Gabi baada ya kusikia yale maneno kwa hataruki kubwa alimuuliza Layla,

"Mama?nani kasema kuwa mama anaumwa?"aliuliza Gabi,

"Doris au alinidanganya?aliuliza Layla kwa hali ya kumshangaa Gabi,

"Hapana hajakudanganya usiwaze mama yuko poa kabisa japo hali yake hairidhishi,alisema Gabi lakini moyoni akiwa na hofu,

"Au huu ni mtego nimetegewa?alijiuliza kimoyo moyo lakini jibu hakulipata.

Maongezi hayakudumu sana,Layla aliondoka lakini taratibu akiwa ana jambo lililomtia hofu,alianza kumuona Doris kama msaliti,

"Nahitaji kufanya uchunguzi wa kina na endapo nitabaini kuwa Doris alikuwa ananizunguka wallah sitamuacha duniani"alijisemea Layla,kwanza alikata mawasiliano na Doris,hata alipokuwa anamfuata Layla alikuwa bize na mambo yake,jambo lile aliligundua Doris na kuhisi kuwa mpango wake ushajulikana, siku hiyo hiyo Doris alihitaji kufanya mazungumzo na Gabi,hivyo mda wa mapumziko alimchukua kisha na kwenda nyuma ya darasa maongezi yao yaliendelea lakini Gabi alimuondoa wasiwasi Doris kuwa hakuna chochote,

"Sawa mpenzi nafurahi maana nilianza kuwa na hofu juu yako"aliongea Doris,lakini Gabi kichwani mwake iligonga kengere ya hatari,

"Lakini hapa shuleni mpenzi usizoee kuongea nami kila dakika,tutakuwa tunakutana Kijiji huko ndo tuongee zaidi"aliongea Gabi.Lengo la kusema vile hakutaka mpango wake ugundulike mapema,

"Sawa kuhusu hilo usijali hata nikikuona tu roho yangu inatulia hakika nakupenda sana,kingine kuwa makini na Layla niliona tangu zamani anakufuatilia hivyo usiruhusu mazoea naye"aliongea Doris,

"Hawezi kunipata moyo wangu tayari umeganda kwako usiwe na shaka"aliongea Gabi lakini moyoni alikuwa na lake jambo,

"Halafu ujue yule ameathirika baba yake tangu mdogo alikuwa akiishi na virus vya ukimwi hivyo ndo maana anajipendekeza kwake lengo akuambukize"aliongea Doris huku akijua fika huo uongo hata Layla afanyeje hatampata Gabi.Maneno ya Doris kuwa Layla ni muathirika yalijirudia kichwani mwa Gabi lakini hakuyatia maanani sana,alitambua kuwa zile ni habari za kumchafua mwenzake.

"Layla njoo nikuambie"ilikuwa ni sauti ya msichana mmoja alitekuwa anaitwa Amina,Layla aliposikia sauti ikimuita aligeuza shingo yake kisha akasimama na kumsubiri yule mwanafunzi aliyeonekana kuwa na jambo la kuongea,mara baada ya salamu maongezi yao yalianza,

"Layla huwa sina mazoea na wewe,ila kwa hiki natamani nikifikishe kwako,hivi kweli unampenda Gabi?aliuliza Amina.Kabla Layla hajajibu alimtazama kwa sekunde kadhaa pumzi nayo haikuwa mbali aliishusha,

"Kwanini unauliza hivyo Amina?"

"Hapana unapaswa unijibu kwanza maana kuna hali siielewi hapa"alisema Amina,"hali gani ambayo huielewi?"aliuliza Lalya,

"Uju...."kabla hajamalizia kile alichotaka kukisema mara kengere iligongwa kumanisha kuwa mda wa mapumziko umekwisha,huo ukawa ndo mwisho wa maongezi yao kila mtu alishika njia yake kwenda darasani.Layla alipofika darasani aliangaza upande wa Gabi lakini hakumuona,hata alipogeuza upande wa Doris napo hakumuona,moyo uliingiwa na hofu,wivu ulimjaa aliona mawazo yake kuwa Doris anauhusiano na Gabi yako sahihi,akiwa kwenye ile hali mara alimuona Doris akiingia darasani punde na Gabi aliingia,hapo ndipo Layla alipodhibitisha kuwa wawili hao wana mahusiano,hakutaka kuonyesha hali ya tofauti aliendelea na mambo yake huku moyoni akiwa na lake jambo,

"Nitafune mimi halafu umeze wewe?hivi unajua nilivyoteseka juu ya huyu? hapana sikubali,kumbe ndo maana hapo awali hakutaka nionane naye sasa safari ya kuzimu inamuita huyu Doris"alijisemea Layla,aliyafuta machozi yake kisha akalalia dawati,hakutaka kufanya uamuzi kwa kukurupuka hivyo alienda taratibu kumchunguza Doris na Gabi.Hakika mapenzi yanauma,uchungu wa mapenzi haulinganishwi na kitu chochote,siku hiyo Layla hakuwa sawa hata kidogo alienda mpaka kwa mwalimu wa zamu na kuomba kurudi akisingizia kuumwa.Kabla ya kufika nyumbani alipitia dukani akanunua kisu Kisha akakiweka kwenye mfuko wake wa madaftari,alipofika nyumbani hakutaka hata kula chakula zaidi alijifungia chumbani kwake,alikitoa kile kisu na kukiangalia kwa sekunde kadhaa kisha akakiweka vyema kwenye mfuko wake ule,

"Kama ni kweli Doris ananizunguka,mda si mrefu nakupeleka kuzimu"aliendelea kujisemea hayo maneno hayo huku moyo wake ukiwa na machungu.

Kesho yake asubuhi aliamka mapema sana na kuelekea shuleni hakutaka kwenda na gari kama alivyokuwa amezoea,alitembea kwa miguu mpaka shuleni,baada ya kufika shuleni alitafuta wasichana watano huku kila msichana akimpa noti ya elfu kumi,wote walibaki kutazamana,

"Niwewapa hiyo pesa nahitaji mnifanyie kazi"aliongea Layla,

"Kazi gani?waliuliza wote kwa wakati mmoja,

"Hakikisheni kila mtakapomuona Doris akiwa na Gabi msikilize watakachokizungumza kisha mtaniambia,haya ondekeni"aliongea Layla,wale wanafunzi waliondoka huku kila mmoja akiwa anayatafakari yale maneno ya Layla lakini wote walikubali kuifanya hiyo kazi isipokuwa msichana mmoja aliyekuwa anaitwa Tedi.Tedi alikuwa rafiki yake Doris hivyo zile taarifa alizipeleka mpaka kwa Doris,

"Hahaha,analazimisha maji kupanda mlima jambo ambalo ni gumu,kamwambie kuwa siku zote asiri ya maji ni kushuka na sio kupanda hivyo asilazimishe"alisema Doris kwa kujiamini,

"Lakini huenda huyu mtu kaja kwa shari kabisa"alisema Tedi,

"Hahaahaaha sasa shari atamletea nani kama ni pesa nyumbani zipo tena za kutosha,niko tayari kufa na sio kumuacha Gabi,it's not possible (hii haiwezekani)"alisema Doris. Tedi baada ya kuona rafiki yake hataki kumuelewa yeye aliondoka eneo lile.

Saa nne asubuhi mda wa mapumziko Doris alimtafuta Gabi kisha akaanza kuzunguka naye hadharani ili amuumize zaidi Layla,wale wanafunzi waliotumwa na Layla walihakikisha wako nyuma ya Doris ili kunasa kila kitakachozungumzwa.

"Nakupenda sana Gabi naomba ukae ukilijua hilo"alisema Doris,wale waliokuwa nyuma maongezi yale waliyasikia vyema na kuyapeleka mpaka kwa Layla.

"Hawa wanapendana tumeyasikia yote"alisema msichana mmoja akimwambia Layla..




Tumeyasikia yote waliyoyaongea ni dhahiri hawa wanapendana tena billa ya kificho kabisa Doris anatembea naye mbele za wanafunzi wote bila aibu"aliongea mwanafunzi mmoja aliyeitwa Nasra.Layla alitahamaki,

"Wako wapi?aliuliza Layla,

"Wamepita nyuma ya darasa la pili wakaenda kwa mbele kidogo wakaa"aliongea Nasra.Layla hakutaka kusubiri kwa mwendo wa hatua kubwa kubwa alianza kwenda kule alikokuwa ameelekezwa,lakini alipofika alimkuta Gabi peke yake Doris akiwa hayupo,

"Au Nasra kanidanganya nini mbona namuona yuko peke yake?alijiuliza Layla huku akizidi kumkaribia Gabi.Gabi alipomuangalia Layla usoni aligundua kuwa amechukia sana uso wake ulionyesha,

"Kwanini Gabi unanitesa kiasi hiki? hivi unajua ni maumivu gani nayoyapata moyoni mwangu?ila kama unacheza huo mchezo jua kabisa kati ya mimi au yeye mmoja atatangulia akhera"alisema Layla,

"Kuna nini kwani?aliuliza Gabi huku akijifanya hana analo jua,

"Unajifanya hujui eeh?sawa ila bora niweke wazi japo nakupenda lakini siko tayari kuvumilia haya maumivu"alisema Layla,

"Hakuna jambo baya mpenzi mbona unawaza mengine?nishakwambia toka awali kuwa nakupenda ila hofu yako tu,ujue wivu ni ugojwa ooh shauri yako kama huniamini"aliongea Gabi maneno ya kumtuliza Layla,

"Ndio lakini mpenzi ujue nami nahitaji furaha yako"aliongea Layla,

"Najua ndo maana furaha yangu yote naiweka kwako ila ajabu wewe huniamini,halafu ujue mpenzi sijala hapa nina njaa"aliongea Gabi kwa uchokozi,Layla alipunguza jaziba na kuwa mpole hasa baada ya kusikia maneno ya Gabi,siku hiyo hakuja na hela ila alikuwa na elfu mbili pekee,

"Basi shika hii mpenzi mi nitavumilia halafu kesho ndo nitakupa hela nyingi zaidi"aliongea Layla huku ile elfu mbili akimkabidhi Gabi yeye akabaki mikono mitupu, Gabi aliipokea na kuitia mfukoni,mda wote huo Doris alikuwa msalani hivyo kipindi anatoka na ndo Layla alikuwa akiagana na Gabi, Doris hakuweza kuona kitu kilichoendelea pale,

"Sasa hapa lazima niangalie upande upi unaotoa pesa ndo nitadiri nao"alijisemea Gabi huku ile elfu mbili yake akiikunja vyema kusudi Doris asiione,hata Doris alipofika alimkuta Gabi akiwa ameinama,

"Unawaza nini mpenzi mbona hivyo?aliuliza Doris mara baada ya kumfikia,Gabi alishusha pumzi ndefu kisha akasimama kama kuuweka sawa mgongo wake na kisha akaketi tena,

"Hapana nina njaa hapa sina hata pesa ya kunywa chai"alisema Gabi,

"Hicho tu mpenzi shika hii hapa elfu tano itakusaidia kwa leo kesho nitakupa nyingine"aliongea Doris.Ile elfu tano Gabi aliipokea.Mda wa mapumziko ulikwisha wanafunzi wote walirudi darasani.Siku hiyo Gabi aliondoka na elfu saba hakutumia hata shilingi mia,mara nyingi nyumbani kwao walishindia mihogo ya kuchemsha na magimbi ya kuchoma lakini Gabi hakutaka kuitoa ile pesa alizidi kuiongeza kila alipokuwa anapewa na Layla ama Doris.Kwa kipindi hicho urafiki wa Layla na Doris haukuwepo tena kila mmoja alikuwa na hamsini zake.Hakuna hata aliyekuwa anamwongelesha mwenzake,

"Yaani ninavyo mpenda Gabi nikiwa nina udhibitisho kuwa kweli Doris anampenda naapa mbele za mwenyezi mungu lazima nimtangulize kuzimu najua siwezi kwenda jela baba atanipigania"alijisemea Layla.

Ilikuwa siku ya juma nne,siku hiyo ilikuwa ni sherehe ya wahitimu wa darasa la saba,Layla siku hilo aliipania kumpa Gabi penzi lake,ilipofika jioni ya siku ile ulifungwa mziki mkubwa kama ilivyo ada wanakijiji mbali mbali walikuwa wanalipia hata wanafunzi kuingia kwenye ule ukumbi wa mziki.Layla alimtafuta Gabi kwa udi na uvumba ili angalau acheze naye ikiwa na pamoja kumpa penzi lake,alimtafuta sana lakini hakumuona,alizunguka sana,hadi ndani ya ule ukumbi aliingia lakini hakuweza kumuona,alichoka sana,kwa wakati huo ilikuwa inatimu saa moja jioni,baada ya kuzunguka sana aliamua kuanza kumtafuta Doris lakini naye hakumuona,hapo ndipo alipojua kuwa kwa vyovyote Gabi atakuwa na Doris.Roho ya wivu ilimjaa vyema alienda mpaka darasani kwao akafungua mfuko wake wa daftari na kuchomoa kisu alichokuwa anatembea nacho,alikiweka vyema kwapani kisha akaanza kuzunguka kila sehemu kumtafuta Gabi,hadi inafika saa mbili usiku hakuona mtu,kwa unyonge kabisa alichukua mfuko wake kisha akaondoka ila dhamira ya kumuua Doris alibaki nayo.

Doris alikuwa kwenye vichaka vilivyokuwa karibu na nyumbani kwao na Gabi,siku ile walishiriki tendo huko huko machakani,Gabi alijaribu kukataa lakini Doris alimlazimisha na kujikuta akishawishika.Mara baada ya kumaliza kufanya kitendo kile waliagana kisha kila mmoja akarudi nyumbani kwao, Doris hakuonekana kuwa mgeni wa mambo hayo kama ilivyokuwa kwa Gabi.Usiku ule kabla Layla hajafika nyumbani kwao alihakikisha anapita nyumbani kwao na Gabi,bahati nzuri alisikia Gabi akiongea na mama yake hapo moyo wake ulifarijika.

Kesho yake asubuhi Layla alifika shuleni akiwa wa kwanza,hakukisahau kile kisu chake,alikuwa na jeuri ya kuwa baba yake anapesa hivyo hata akimuua Doris hakuna kitu kitakachoharibika.Mda kidogo wanafunzi walianza kujaa pale shuleni akiwemo Gabi Layla alipomuona alimfuata,

"Mpenzi Jana nimekitafuta sana lakini sijakupata kabisa kwa nini lakini ulinifanyia vile?aliuliza Layla baada ya salamu,

"Ujue mpenzi mama kumuacha nyumbani peke yake hasa nyakati za usiku huwa mpweke sana ndo maana jana nimeondoka mapema"alitunga uongo Gabi"Layla alikubaliana naye hakutaka kumpinga sana kusudi asije kumkasirisha,waliachana kila mmoja akaelekea sehemu yake.

"Layla njoo ushuhudie yaani Doris yuko na Gabi"ilikuwa sauti ya Nasra aliyekuwa amepewa kazi na Layla ya kumfuatilia Doris,

"Wako wapi?"aliuliza Layla,

"Pitia hapa kajibanze kwenye lile dirisha maongezi yao utayasikia vyema"

"Layla bila kuchelewa alifanya kama alivyoambiwa,

"Yaani jana umeniumiza we acha tu nimeondoka kwa kuchechemea"

"Pole sana kwa hiyo ulifika unajikanda au?

"Kujikanda wapi au kidogo wazazi wagundue ila umenipa raha si ya nchi hii"yalikuwa maongezi ya Doris na Gabi ambayo Layla aliyasikia vyema,

"Kumbe hawa jana wamefanya ushenzi? hapana imetosha sasa nahangaika kumtafuta kumbe alikuwa na huyu kahaba?siwezi kuvumilia"alijisemea Layla huku akitoka mbio mbio kwenda darasani kwao kutafuta kisu.Mara baada ya kukiweka kwapani na kuhakikisha hakuna anayeona alitoka darasani akatembea kwa haraka kuelekea kule alipokuwa Doris na Gabi,

"Leo nakuua mshenzi mkubwa wewe"alijisemea kimoyo kimoyo Layla huku akikaza mwendo.

Asee unaanzaje kuikosa hii?usikae mbali.




"We Layla kagonge kengere wanafunzi wote waje msitarini"ilikuwa sauti ya mwalimu aliyemshtua Layla aliyekuwa na dhamira ya kuua kabisa,alisimama huku akijaribu kuuweka sana mkono uliokuwa na umekibana kisu kilichokuwa kwapani.Wanafunzi wote walikusanyika mara moja,bado Layla alikuwa na hasira isiyopimika,alijizuia lakini ilishindikana,

"Lengo la kuwaita hapa ni kwamba mwalimu mkuu kafiwa na mke wake hivyo kila mwanafunzi aende nyumbani kwao tukutane hapa kesho"aliongea mwalimu yule na kuwafanya wanafunzi wahuzunike wengine kutoa machozi kabisa.Layla aliondoka eneo la shule huku bado akiwa na hasira huku moyoni akiwa nawaza tukio alilotaka kulifanya mda mfupi uliopita,

"Una bahati mwanahayawani mkubwa wewe"Layla aliendelea kutoa machozi huku akijitahidi kujizuia ili usigundulike.Alipofika nyumbani aliwakuta wazazi wake wakiwa sebuleni,mara baada ya salamu aliketi kando yao kisha mazungumzo yao yakaendelea,

"Hivi kwenye mtihani ulioisha umeshika nafasi ya ngapi?maana sijaona matokeo yako"aliongea baba yake Layla mzee Gozirbert,

"Aaha!baba matokeo ndo yale yale tu sema nimejitahidi kushika nafasi ya tisa"alisema Layla.Baba yake alionekana kufurahi,

"Nataka mtihani wa mwezi wa kumi na mbili ushike nafasi ya tano,kama utafanya hivyo nitakufundisha gari uwe unaendesha mwenyewe"

"Usijali baba mimi tena navyopenda gari naweza kushika hata nafasi ya kwanza au ya pili"aliongea Layla,yale matokeo yake mabovu aliyaficha.

Usiku mzima Layla alikuwa anaandika barua iliyokuwa na maneno ya vitisho kuwa kama Gabi hata muacha Doris basi uhai wake uko mikononi mwake,baada ya kumaliza kuiandika alijilaza kuutafuta usingizi alioupata kwa taabu.Asubuhi na mapema Layla aliamka na kujiandaa kama kawaida yake,mara baada ya kujiweka sawa alipanda gari kisha kuelekea shuleni,alipofika alienda mpaka alipokuwa Gabi na kumpa barua ile,licha ya kuwa barua ya vitisho lakini Layla hakuacha kuweka pesa,

"KAMA HUTOKUBALI KUMUUACHA BASI UJUE NTAMUUA"yalikuwa maneno yaliyokuwa yameandikwa kwa herufi kubwa Gabi aliyasoma,

"Hahaha,hizo ni kelele za chura ambazo ni ngumu sana kumzuia tembo kunywa maji"alijisemea Gabi alipomaliza kuisoma barua ile,hakujua kuwa Layla kweli alikuwa amemanisha,yeye alichukulia utani ukiwemo na wivu,hakutaka hata kuendelea kukaa nayo ile barua aliichana chana.

Ghafla pale shuleni ulizuka mchezo mchafu kwa wanafunzi ambao hawakuwa na nidhamu,walipomuona Layla kila mara ni mtu wa kuyafuta machozi waliamua kuandika ubaoni ili wamuumize zaidi,

"Mapenzi moto moto kwa Gabi na Dor"maneno yale yalisomeka hivyo yaliandikwa na mwanafunzi mmoja,wanafunzi wote walilipuka kwa kelele za kushangalia kwa kuwa walijua dhahiri yale maneno ni mahususi kwa Layla,hata Doris naye aliachia kicheko cha kebehi.Layla alinyanyuka kwa jaziba na kwenda kuyafuta yale maneno bado wanafunzi walimzomea,mchezo ule uliwafikia mpaka walimu wakatambua,mwalimu wa nidhamu alimuita kiongozi wa darasa na kumwambia kuwa awaandike wote wenye tabia kama zile,kiongozi alianza kazi yake taratibu hakuna aliyetambua,wanafunzi walizidi kuandikana pale ubaoni ukawa mama mchezo waliufurahia.Layla kila alipokuwa anamwangalia Doris alimuona alitabasamu,kuna mda alimwambia Gabi na kukuta akikonyezana na Doris,jambo lile lilimuuama,kuna mda alitamani kumuchoma kisu mbele ya darasa lakini alijizuia akisubiri sababu itakayo pelekea kufanya vile.

Mwalimu Bernard alihamishwa shule na kuletwa mwalimu mwingine aliyeziba nafasi yake,

"Baba ananipenda hivyo hata nikimuua huyu kinyago lazima atanitetea tu"alijisemea Layla.Tukio la kuhamishwa mwalimu Bernard alilifurahia lakini bado lilimnyima furaha ni la Doris kumuona anafurahia na mpenzi wake ilihali yeye kasota sana kumuweka Gabi kwenye himaya yake halafu leo apokonywe tonge alilokwisha kuliweka mdomoni ilhali ana njaa?aibu iliyoje,aliona hicho kitendo kwake hakiwezekani.

Majira ya saa saba mchana kuligogwa kengere kumanisha kuwa ile ilikuwa kengere ya dharula,wanafunzi wote waliwahi msitarini,mara baada ya kukusanyika wote mwalimu wa nidhamu alisimama huku mkono wa kushoto ukiwa umeshikilia karatasi ilihali wa kulia ukiwa umeshikilia fimbo,

"Kumekuwa na tabia mbaya hapa shuleni kwa baadhi ya wanafunzi kuanza kuvunja kanuni na taratibu za shule,hivi hapa shuleni mmekuja kwa ajili ya masomo au kuanzisha mchezo wenu mchafu wa mapenzi?aliuliza mwalimu Deogratus,

"Tumekuja kusoma"wanafunzi wote waliitikia kwa wakati mmoja,

"Vizuri sana,kuna waliokuja kusoma na kuna wengine wamekuja kufanya mchezo,sisi kama walimu hatuwezi kuendelea kuvumilia uchafu huu ambao umepelekea baadhi yenu kufanya vibaya kwenye mitihani,mnashindwa kujisomea kutwa mnawaza ujinga,hii aibu gani?mwanafunzi anashika namba ya sita lakini anajiingiza kwenye vitendo vya namna hii anashika namba ya thelathini,je sisi kama walimu tunalikomeshaje hili?jibu ninalo mwenyewe hapa,hii ni karatasi yenye majina ya watu wenye mchezo kama huu, tafadhali ukisikia jina lako naomba upite mbele ili upate adhabu uweze kuachana na hizi tabia.Wazazi kutwa nzima wanahangaika kuwasomesha kumbe wanasonesha watu wenye vichwa kama vya mbuzi,

"Doris hermani pamoja na Gabi"pita mbele haraka naanza na nyie"alisema mwalimu yule huku Gabi kwa unyonge kabisa akasogea mpaka mbele,

"Je,wewe Gabi kweli unampenda huyu?aliuliza yule mwalimu lakini Gabi alikaa kimya bila kuongea chochote,

"Eeeh na wewe mtoto wa tajiri Herman unampenda huyu?aliuliza tena mwalimu,Doris alishusha pumzi ndefu kisha akajibu,

"Ndio nampenda,kama kuniua niueni tu lakini sio kumuacha huyu"aliongea kwa kujiamini,maneno yale yalimtia kichefuchefu Layla alitoka pale na kwenda mpaka darasani na kuchukua kisu kisha akarudi na kumkuta mwalimu akiendelea kuwahoji Doris na Gabi,wanafunzi wote wakiwa makini kutazama walimuona Layla akisogea mpaka pale alipokuwa mwalimu pamoja na akina Doris na Gabi,

"Nimesikia vibaya we Doris umesema una mpenda nani?aliuliza Layla,

"Kwani hujasikia? nakwambia huyu hapa"alisema Doris huku akimkumbatia Gabi akizidi kumuumiza Layla mbele ya walimu,

"Vizuri sana,sasa hapa tunabadirishana majengo ya serikali,alisema Layla kisha akachomoa kisu na kumkita Doris kifuani,kila mtu alisitaajabu tukio lile,hata mwalimu alibaki ameduwaa,wanafunzi walipiga kelele Doris alienda chini huku damu nyingi zikimtoka kisu nacho kikiwa kifuani kwenye nyama za mwili wake.Layla alimfuata Gabi kisha akamkumbatia,

"Nitakufa na wewe"aliongea Layla.

Doris kwisha habari...Haya mapenzi haya


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG