Simulizi : Hasna (Mfu Anae Ishi)
Sehemu Ya Nne (4)
Mama Zuberi profeshino yake alikua ni nesi akihudumu katika Hospital ya wilaya Kahama.lakini kwasasa anamiaka mitatu tangu muda wake wa kufanya kazi uishe(mstahafu).
Basi mama huyo aliendelea kutoa msaada hadi binti huyo akafanikiwa kukitoa kiumbe hicho.
Basi mama huyo alifanya taratibu zote anazo sitahili kupata mama mzazi pamoja na mmjini
“mama samahani wewe unaonekana ni mgeni eneo hili”?
Aliuliza mama kachanga huyo.
“Ndio mwanangu,Fanya upunzike kwanza.lakini mbona hadi muda wakujifungu umefika hauna maandalizi yoyote wa hakuna mtu karibu wa kuweza kukupa msaada."?
Aliuliza mama Zuberi.
“Mama nistori ndefu, ndomaana nashangaa. hata wewe umefata nini kijijini hapa”
Aliuliza Dada huyo.Mama Zuberi alimuelezea hazima yake ya kufika kijijini hapo.
Yule binti alishangaa kusikia mama yule kamtaja Hasna.
“Mama huyo Hasna ni mdogo wangu.Na kafari miezi kadhaa iliyopita ”
Alisema dada huyo kwa utambulisho wake ni dada yake Hasna. Aliyejulikana kwa jina la Mwanjia.
Mama Zuberi hakutaka kumwambia binti huyo kuhusu Hasna.
“Je Na shangazi yako mwajabu naweza mpata”?
Aliuliza mama yake Zuberi.
“Mama,Shangazi huyo unaemuulizia ndio nilikua namsubiri aje kunichuka kabla sijajifungua.Lakini hata sielewi kapatwa na maswahibu gani”
Aliongea binti huyo.Alianza kumpa simulizi kidogo.
Kuwa baba yake Mtemi Jafari alikua anamtaka mtoto huyo pindi anapojifungua tu.Shangazi yake hakukubaliana na kitu hicho, ndomaana alitaka aje kumchukua mwanjia ili akajifungulie huko.
“Mama nakuomba kitu kimoja ,najua baba yangu aweza kutikea muda wowote.Hivyo mchukue huyu mtoto na uondoke nae kwa shangazi.Baba akimkuta hapa naweza kumla nyama.”
Aliongea Mwanjia Mwanjia.Japo mama Zuberi alionekana kukataa kata swala hilo.Lakini mwisho wa siku alikubali maana nayeye alikua akihitaji msaada wa kina kutoka kwa shangazi yake Hasna.
Mama Zuberi alielekezwa alipo Shangazi yake Hasna.Kilikua ni kijiji cha jirani.
Mama Zuberi akiwa na kichanga hicho njiani alikuta mafuvu ya watu pamoja na maiti.
Aliogopa nakuanza kutembea haraka haraka.Mtoto alianza kulia ,mama Zuberi alisogea pembeni kidogo ya kinjia hicho kilichokua finyu, cha kuelekea huko alipo shangazi yake Hasna.
Mama Zuberi alikua kachoka na mtoto alikua akimsumbua.Aliona nibora apunzika chini ya mti.Na wakati huo upande wa maghalibi kijua chekundu kilikua kikionekana,kuashilia kiza kina ingia muda wote.
Mama Zuberi akiwa pale chini ya Mti huo. Mara alihisi ubichi kwenye bega lake.Alihisi ni umande tu ukimdogokea,lakini alizidi kusikia vikidogoka kwa kasi.Akipopeleka mkono wake akagusa kisha akatiza.Alianza kupeleka macho taratibu juu ya mti huo.
Mama Zuberi baada ya kuona juu ya mti alipaki kanganda kwa butwa huku meno yake yakigongana nikama mtu anae sikia baridi..........
Aliona ilikua ni maiti iliyokua haina ngozi na ilikua ikitililisha damu.Na ilionekana ilikua haina hata muda kutundikwa kwenye mti huo.
Mama Zuberi alirudisha macho yake ,kwa kichanga hicho alichokua kakibeba kwa mbele ya kifua chake.
Akinyanyuka taratibu nakua ananza kupiga hatu.Mara ghafla alisikia sauti ikitokea nyuma yake.Nakumfanya simama.
“Mama usipende kujiingiza kwenye vita hisiyo kuhusu”
Sauti hiyo ilisikika ikisema maneno hayo.
Mama Zuberi aligeuza macho yake nakutazama sauti hiyo inapotokea, lakini cha ajabu hakuona mtu yeyote.
Alitembea haraka hakara kuelekea mbele na kukuta kinjia alichokua akielekea awali.
Alitembea takribani muda wa dakika ishirini hivi.Alianza kumaliza msitu na kuingia kijijini.
Alipo umaliza msitu huo alikutana na mama mtu mzima, mwenye kulingana nae lika alikua kabeba ndoo ya maji kichwani.
“Habari za jioni dada”?
Alisalimia mama Zuberi.
“Salama dada habari yako”
Aliitikia salamu mama huyo.
“Samahani dada nilikua namuulizia dada mmoja anaitwa mwajabu”
Aliuliza mama Zuberi. Mama huyo alicheka kidogo kabla ya kumjibu.
“Dada mtu huyo unae muulizia unamjua vizuri”?
Aliuliza mama huyo.
“Hapana nimeelekezwa tu,sijawahi muona”
Alijibu mama Zuberi.
“Dada yangu naomba twende nyumbani kwangu.Maana kuongelea hapa njiani sio vema.Nakiza hiki kimeingia huwa kuna wanya wakali”
Basi mama Zuberi hakusita .Aliongoza hadi kwa mama huyo.Alifika alikalibishwa kwenye kilago.
“Niambie dada yangu Mimi ndio,mwajabu”
Alisema mama huyo. Mama Zuberi alishusha punzi kidogo.
Alianza kumuelezea kila kitu kumuhusu mtoto mchanga alie mbeba.Kisha akamueleza mambo yanayo msibu mwanae Zuberi.
“Kwanza pole na mitihani dada”
Alisema mama huyo alijitambilisha ndiye Shangazi yake Hasna huku akimchukua mtoto.
“Asante dada,lakini mtoto huyo hajala toka kanyonya kidogo maziwa ya mama yake,"
Alisema mama Zuberi.
“Dada usijali kunamaziwa kwenye kibuyu ngoja nikoke kuni niyatoe baridi kidogo ”
Alisema Shangazi yake na Hasna.Basi aliamuandalia maziwa mtoto.kisha wakaandaa na chakula chao.Ilikua imefika majira ya saa tatu za usiku.
Shangazi yake na Hasna alimuandalia mgeni wake mazingira ya kulala.Na akamuambia kesho pakicha wataona wanafanyaje kuhusu swala la Zuberi.
Mama Zuberi akiwa kalala ,alishituka baada ya kusikia milindimo ya ngoma nje ya nyumba.
Alijaribu kutaka kuchungulia ili aone nini kinachoendea, lakini hakuweza kuona uwazi wowote. Maana nyumba hiyo ilikua haina dirisha.Aliangaika lakini alifanikiwa kuone tundu kwenye ukuta lililokua limezibwa kwa kipande cha kanga kichowekwa kwa kuchomekwa ,basi alifanikiwa kukichomoa kuona nje.Kulikua na mwanga na kulioneka jua linawaka na aliona watu wakicheza ngoma,huku kichanga kile cha Mwanjia kikiwa kimelazwa chini.
“Hivi Mimi nimelala hadi kumekucha au niuchovu.?Alafu mbona hakuniambia kama mtoto leo wanamfanyia matambiko yao”?
Alikua akijiuliza mama yake Zuberi. Aliona bora ache tu kuwasemesha uenda kwenye matambiko yao hausiki.
Alirudi kujilaza maana alijiona bado macho yake mzito kwa usingizi.
Chumba hicho kilikua na Giza Kali sana.Roho yake haikumpa kulala kabisa akapapata mkoba wake kisha akatoa simu yake ya mkononi.Aliiwasha ilipo waka aikuweza kusoma mtandao wowote, maana kijijini huku kulikua hakuna mtandao.
Alishituka baada ya kuangalia muda nakuona ilikua ni saa tisa za usiku .Aliangalia saa hiyo ya simu yake Mara mbili mbili.
Lakini bado ilimuonesha ni saa tisa za usiku.Alirudi tena kuchungulia aliwakuta watu hao wakiendelea kucheza ngoma huyo.
Wakiwa wamevalia vipande vya vitambaa vyeusi. Wanawake wamevaa Shangazi zenye punje kubwa kubwa shingoni.
Huku wamejisiti kwa upande vitambaa kwenye maziwa yao na upande kitambaa mwingine wajisitili nyeti za.Usoni wamejichora chora kwa unga mweupe.
Kwa upande wa wanaume wamevaa shanga hizo zikikatisha mabega yao.Na upande wa kitambaa hicho wamestili maungo yao, huku vifua vyao vikiwa wazi.Nao walikua wamejichora na unga mweupe usoni.
Alivyo angalia vizuri aliona mtu kakaa na alikua kakalia watu waliyo weka migongo yao kama kiti.
Mtu huyo alikua kavaa kichawi kofia kwa juu ilikua wazi na ilikua imewekwa nakshi ya manyoa yaliyo kua marefu.
Alikua kavaa ngozi kama ya chui hivi lakini sidhani kama ilikua ya chui.Iliyokua imemfunika bega moja na lingine likiwa wazi.
Mkononi mwake alikua kashika fimbo,ambayo kwa juu yake ilikua na fuvu la mtu.Alikua akitikisa kichwa akifatiliza mapigo ya ngoma.
Mama Zuberi alianza kutetemeka alivyo muona mtu huyo.Kwa sifa za mtemi Jafari alizozipata na alipo muona mtu huyo moja kwa moja Alikua ndio mtemi wa himaya ya Mbika.
Alijipa ujasi nakuona nibora atoke nje liwalo na liwe.
Alifungua taratibu mlango wa sebureni, uliyotengenezwa kwa matete.Alipo ufungua alikutana na kiza kinene .Alishituka nakuufunga akarudi tena chumbani,moja kwa moja alienda kuchungulia tena kwenye tundu lile.
Alishangaa tena kuona mwanga wa jua.Alirudi kua huku akiwa analia asijue nini cha kufanya alijua ndio mwisho wake alisoma dua na kumuomba mungu kwa lugha zote.
Lakini hakuweza kuona mabadiliko alizidi kusikia ngoma ikipamba moto. Akinyanyuka Na kwenda kuufungua mlango kwa kasi.Mara ngoma ikazima ghafla, alitoka nje kulia kiza kikali,alifanikiwa kuwaona watu kupitia mwanga wa mto waliokua wamekoka.
“Ha ha ha haha ah hah,Binadamu huwa wanapenda matatizo, hata kama hawana basi huya tafuta popote ya yalipo kwa udi na uvumba”
Ilisikika cheko iliyofatiwa na sauti nzito iliyoambatana na mwangwi...
“Mleteni hapa mbele ”
Ilikua ni sauti ya mtemi.Washilika wa mtemi walimkamata na kumpeleka mbele ya mtemi.
“Hivi wewe mwanamke uliona unaakili kuliko mimi”?.
Aliongea mtemi huyo huku akinyanyuka kusogea mahara alipo mama Zuberi.
“Kama nimeweza kumuua mwanangu Mwanjia,Sasa wewe unaanza je kupona”?
Aliendelea kuongea Mtemi.Alimwambia maiti uliyoiona ikining'inia kwenye mti uliopunzi ndiye mwanangu.Nilimuua kisha nikamchuna ngozi yake.
Mtemi aliendelea Na kusema alijibadilisha na kua mwanamke hivyo mama Zuberi aliaminishwa kuwa ni Shangazi yake Hasna.
“Mama nakuomba uchangue kifo chako mwenyewe ”
Aliongea Mtemi huku akiwa anatembea tambea mbele ya mama Zuberi.
Mtemi nia yake nikukipata kichanga cha mwanae Mwanjia kwa ajili ya kafara zaka.Waliingia makubakiano hayo ni baada ya Mwanjia kutoroshwa na mwanaume wa kijiji cha jirani cha ushetu.
Mtemi hakutaka mwanae yeyote aolewe bila kupata faida yeyote.
Hasna alimuoza kwa Zuberi kwa lengo la kupandishwa cheo kwenye himaya ya kichawi pindi damu ya Hasna itakavyo tolewa kafara.
Sasa Mwanjia alipotoroshwa Mtemi alimfata na kumuua kijana aliye mtorosha.Alimchukua Mwanjia na kumrudisha nyumbani kwa lengo la kumtoa sadaka kwenye ushilika wao, ili aendelee kua kiongozi wa wachawi.
Lakini Mwanjia alipo jitete na kusema mjamzito, basi mtemi aliacha kumtoa kafara.
Naaliamua kumsamehe kabisa na wakawekeana makubaliano pindi mtoto atakapo zaliwa basi amkabidhi mtemi,ili yeye awe Salama.
Nahayo ndio makubaliano yalivyo kuwa lakini Mwanjia hakuona vema kupoteza mwanae. Akaona bara amtoroshee kwa shangazi yake.
Mtemi aliendelea kutamba kwa mama Zuberi.
“Nashukuru sana kunipa siri zako zote,mume wako ninae na muda sio mrefu utaungana nae.Pia Zuberi kama ulivyosema wana taka kumuua, upande wa wapinzani wangu nilio wa saliti kutoka kwenye chama cha kafara, na kuunda chama changu kipya kinachoitwa mungu wa ardhi.Zuberi namchukua na tamuua mwenyewe maana kanipa pigo kubwa ambalo sijawahi lipata maishani mwangu”.
Aliongea Mtemi.Huku machozi yakimtoka.
Ilikua hivi pindi Zuberi akiwa hana mwili .alianza kulipiza kisa kwa watu wote waliohusika kwa namna moja au nyingine, yeye kuingia kwenye chama hicho cha kafara na kumshawishi atoe watu wa kalibu ikiwemo familia yake.
Zuberi alijipa kiapo kwa yoyote aliyehusika basi nae atapata machungu na maumivu kama aliyo pata yeye.
Mtoto wa kwanza wa Mtemi alikua anaitwa Said.Na mtemi ndiyo alikua akimtegemea kwa mambo mengi.Na pia alimtangaza ndiye mrithi wake pindi yeye atakapoamua kupunzika .
Said aliuliwa kifo kibaya na Zuberi kwa kukatwa katwa vipande vipande. Mtemi alipopata taarifa hizo na kwenda kuona mwili wa mwanae alichanganyikiwa.
Hivyo ndivyo ilivyokua Mtemi anakisasi na Zuberi na jana kapata habari zake hivyo anafuraha sana.
“Naomba mufuate Zuberi Mara moja,nae aje shuhudia kifo cha mama yake”
Alitoa agizo kwa wafuasi wake,Nao walitoweka kimazingara mara moja.
Azikupita dakika kumi watu walioagizwa walirudi na Zuberi.
“Nimekuleta hapa ili ushuhudie kifo cha mama yako,naili uumia zaidi basi hauwezi kuwa kwenye hali hiyo.nakurudisha kwenye hali yako ya ubinadamu ”
Aliongea mtemi kisha akatema mate kulia na kushoto kisha aliongea lugha aliyo ijua mwenye.Na mate mengine akatemea kwenye vinganja vya mikono yake.Kisha akapikicha akama utu anae taka kupaka mafuta.Aliomba kichupa kilichokua na maji maji akamwangia Zuberi huku aliongea maneno kwa sauti ya chini hayakuweza kusikika hata kwa wafuasi wake.
Zuberi alibadilika nakurudi kama zamani.
“sasa shuhudia vizuri kifo cha mama yako,baada ya hapo utafata wewe na familia nzima mtaitumikia himaya yangu”
Aliongea Mtemi huku akiwa anabadilika nakuanza kuota meno marefu,kucha ndefu pamoja na masikio yakawa marefu.
Alianza kumsongelea mama Zuberi kwa lengo la kumchana chama.Zuberi alikua akipiga kelele kwa lengo la kumzuia Mtemi.
Ile mtemi alivyotaka kunyanyua mkono wake wenye kucha ndefu.Aliona sikadi zimeanza kutua mahali walipo na ziliua badhi ya wafuhasi wake.
Mara zilikata Mtemi akiwa anasha lilitokea kundi kubwa la washilika wa chama cha kafara.
“Jafari tumekulea hadi leo ulipo fikia unatulete dharau sisi.?Umetusaliti umeondoka na baadhi ya washirika tumekukalia kimya.Leo umetuchukulia mtu wetu ambaye tulikua na miahadi nae pindi panapokucha tu”
Aliongea kiongozi wa chama cha kafara kwa jaziba kubwa.Lakini Mtemi Jafari alicheka kwa dharau .
“mmeingia kwenye himaya yangu na hii siku nilikua naitamani sana.Maana nilitaka niwaoneshe uwezo wangu”
Aliongea Mtemi Jafari .kisha akaongea maneno aliyeyajua mwenyewe. Ghafla lilitokea kundi kubwa la watu.
Na upande wa chama cha kafara waliongezeka .Walianza vita ya kichawi kutupiana moto wenye kutema cheche na wengine walikua wakipigana angani bila kushuka chini.
Mama Zuberi na Zuberi alibaki kuwa watazamaji tu.
Mara ghafla angani ilionekana miangaza miwili ikija na hali ya hewa ilianza kubadilika .Upepo mkali ulivuma na mapambano yalishindwa kuendelea kwa watu kurusha huku na kule.
Waliangukiana hakuna cha adui wala nini wote walijikuta wakiwa sehemu moja.
Miangaza ile ikashuka chini ma mwanga mkali uliwaka na kua kama mchana. Nawale wote waliokua wakipigana walianza kuinuka mmoja mmoja.
Walishangaa kuona mabinti wawili wakiwa wamesimama mbele huku macho yao yakitoa mwanga mkali..
Washilika Wa kichawi baada ya kuangalia mbele walishituka kuona kati ya mabinti hao kuna mmoja wanamfahamu .
Waliangaliana Mtemi na yule kiongozi Wa kundi la Washika wa wa kafara walipeana ishala kisha mtemi akacheka kidogo.
“Mwanangu Hasna leo ndio siku yako ya mwisho hapa Duniani ni lazima ufe kwasababu umeshajua siri zangu nyingi sana siwezi kukuacha hai ni lazima ukaungane na mama yako huko kuzimu”
Aliongea mtemi huku akizishikashika ndevu zake.
“Kwanza Mimi sio Hasna Mwanao,Mimi ni Mfu anae ishi na nimetokea kuzimu.kuja kutetea wanakijiji wangu niliokabiziwa na mizimu ya mababu,sijaja pekeangu niko na marikia wangu wa kuzimu”
Alikua aongea Hasna huku akimtazama malikia wa kuzimu kama yeye anavyo mwita.
Mtemi alimtazama kiongozi mwenzake kisha wakongea Kwa pamoja Kwa lugha yao yakichawi.
Makundi hayo yaliungana na kua kitu kimoja walianza kuwashambulia kina Hasna Kwa sikadi za kichawi.
Husna na mwenzake walikua wako vizuri kukwepa na kupangua .
Nao walianza kulusha miale ya moto.Hasna alimwambia mama Zuberi na Zuberi wamchukue mtoto waondoke eneo hilo.
Baada ya muda kidogo kundi la Mtemi lilizidiwa na kina Hasna. na washilika wakichawi wengi walikua wamepoteza maisha.Mtemi baada ya kuona hivyo alipotea kinazingara.
Hasna alivyo tupa jicho hakuweza kumuona baba yake. Alijua wazi atakua kawafata kina Zuberi akakichukue kichanga.
Hasna na alitowe na kumuacha mwenzake akiendelea na mapambano.
Hasna alitokea alipo baba take na kumkuta akiwa na viumbe vya ajabu vilianza kumshambulia Hasna na kumjeruhi Hasna akaona kazidiwa.alipote na kurudi tena Kwa mwenzake.lakini cha ajabu alishangaa kukuta maiti nyingi na mwenzake aonekani.Akiwa pale akiangaza kumtafuta mwenzake huku mkono wake kajiziba tumboni kulikua na jeraha kubwa na damu zikitoka Kwa wingi.
Alishangaa kuona kundi la washilika wa kichawi likija Kwa kasi.Hasna alianza kupambana huku akiugulia maumivu, alijitahidi sana lakini mwisho nguvu zilimuishia akaanguka chini.
Mara gafha alitokea mwenzake na kuanza kupamba na kundi hilo kumnusuru mwenzake.
Nae alipambana nakuanza kuawaelemea kundi hilo. Mara alitokea Mtemi akiwa na kichanga kakibeba,Zuberi na mama yake walikuwa wametobolewa kwenye nyayo zao, nakupitishiwa mti kwenye matundu hayo.Wakibulizwa kuletwa Hasna alipo lala.
Yalitokea Yale majitu ya ajabu na mtemi akawaamuru wammalizie Hasna.yalikua nakucha ndefu na nikali kama kisu.
Basi walichimoa kucha zao nakunyanyua kumchoma Hasna.
Malikia Wa kuzimu akawahi na kujikinga yeye.hivyo akawa kachomwa na majitu hayo.
Alikua yuko hoi sana walinyanyua tena Kwa lengo la kumchoma Hasna
Ulisikika upepo ukipuliza walipo tazama juu waliona ndege mkubwa sana mwenye kufanana na tai.Alivyoanza kushuka alianza kutema cheche zilizo wafanya majitu Yale kukimbia huku nakule .aliwanyakua Hasna na mwenzake Kwa kucha zake na kupaa nao.
Mtemi alikua kashikwa hasira hadi anatetemeka.
Aliwageukia kina Zuberi na mama yake,huku macho yake yakitoka na damu Kwa hasira.
“Sasa nyinyi leo mtanitambua”
Aliongea Mtemi huku akimkanyanga Zuberi sehemu ile aliyo chomwa na mti.Palikua pameanza kupambazuka .Mtemi aliwashika kina Zuberi alafu wakopotea na kwenda kutokea kwenye ngome ya Mtemi Jafari.
Mtemi aliwapeleka hadi kwenye zizi la ng'ombe.kisha aka muagiza mfanyakazi wake atoe ng'ombe mmoja.
Aliingia zizini na kutoa ng'ombe mmoja.walikua ng'ombe wengi wapatao Hamsini.
“nyinyi wapuuzi hawa wote walikua kama nyinyi na sasa nimewashikisha adabu”
Mtemi aliongea hivyo kisha akamtemea mate ng'ombe huyo na kubadilika na kua mtu.
Mama Zuberi na Zuberi wote walipigwa na butwaa baada ya kumuona mtu huyo.Akua mwingine bali alikua ni baba yake Zuberi.
“Mnaona nakila ikifika ijumaa huwa nawapeleka machinjioni ng'ombe sita .nyama mnazokula asilimia kubwa ni nyama za watu”
Aliongea Mtemi kisha akamrudisha baba Zuberi kua ng'ombe tena.
Mama Zuberi alikua analiatu.Mtemi alichukua unga mweupe na kuwapa kina Zuberi usoni ,kisha akaongea maneno Kwa luga aliyo itambua yeye.
Hapo hapo waligeuka na kua ng'ombe. Walifunguliwa na kuingizwa zizini.
Mtemi aliondoka na kwenda kwenye chumba kikubwa kisichokua na kitu.Alikua kakibeba kichanga mkononi,
Alifika akakilaza chini palikua na mfeleji mkubwa uliokua mujaa damu zilizoonekana kuganda.
Upande wapili yule ndege alifika akatua chini ya mti mkubwa .Aliwashusha Hasna pamoja na mwenzake wote walikua hawajitambui.
Alibadilika na kua mama mtu nzima.Alianza kuwatibu Hasna alikua Wa kwanza kupata fahamu na kujishangaa mahali alipo.
Pia alimshangaa mwanamke huyo akiwa bize kuwahudumia.
“Hasna naomba utulie kwanza”
Aliongea mama huyo.
“Hapa wapi na wewe ni nani”
Aliuliza Hasna.
“Hapa ni kwangu na Mimi ni mama yako”
Aliongea mama huyo huku akiwa anaondoka na kuelekea mbele kulikua na kaburi .Alimwambia Hasna muda si mrefu atapata maagizo.Alipofika kwenye kaburi lilipasuka katika mama Hasna akaingia.
Akiwa makini kumuangalia mama yake aligeuka Kwa kasi baada ya kusikia sauti ikicheka Kwa taratibu.Alikua ni malikia wa kuzimu.
“Malikia vipi ,umepata fahamu”
Aliuza Hasna.
“Hasna kuna maagizo kutoka Kwa mama yako"
Alisema malikia wa kuzimu.
“Nimaagizo gani na kakupa sangapi”
Aliuliza Hasna .
“Unamkumbuka yule mzee mliye mkuta porini mkiwa na mama ujugi”
Aliuliza malikia wa kuzimu.
“Ndio namjua kwani vipi”
Aliuliza Hasna.
“kesho mapema inatakiwa uanze safari ya kwenda Kwa mzee huyo.Na maelekezo yote utayapata ukiwa njiani,kaa tambua wewe ndio msada wa wanakijiji”.....
Alisema Malikia wa kuzimu.Alikua bado kalala chini hali yake ilikua bado ni mbaya sana.
Hasna alikua kaka kimya bila kusema chochote akionekana akitafakali jambo.
“Hasna mimi niliamua kuungana na wewe kutetea wanakijiji wanao teseka.Napia nachukia sana watu wenye tabia kama ya baba yako,hata ya baba yangu na mungu akinibaliki nikapona lazima nirudi kigoma na baba yangu atajuta Kwa alichotufanyia mimi na kaka yangu”
Aliongea Malikinia wa kuzimu na kama unakumbuka huyu ndiye binti aliyekua katolewa msukule na baba yake.Na Hasna alikutana nae pale gest.
“Hasna naomba uondoke ukajiandae Kwa safari yako”
Alisema malikia wa kuzimu.
“Sasa mimi naenda wapi?,na wewe unabaki na nani na unaona hali yako ilivyo mbaya”
Alisema Hasna.
“kuhusu mimi usijali naomba ujali jukumu ulilopewa la kutetea wana kijiji”
Alisema Malikia wa kuzimu.Hasna alinyanyuka na kuanza kuondoka huku akimtazama Hasna.
Hasna alifika sehemu moja kulikua na jiwe kubwa ,alikaa chini ya jiwe hilo akiwa anatafakali mambo aliyoambiwa na maliamu.
Ilikua ni mida ya saa sita za asubuhi.Hasna alikaa pale hadi ilipofika usiku.
Hasna akiwa pale alianza kuona macho yake kuwa mzito.
Alipitiwa na usingizi mzito.Alianza kuota ndoto akitembea kwenye msitu mkubwa alitembea bila kujua wapi anapoelekea.Hasna akiwa ndani ya msitu alianza kusikia mlio kama mtu anakata mti,Hasna aliufuta mlio huo hadi akatokea mahala mlio ulipokua kusika.
Alimkuta kijana mmoja akiwa anakata mti.
“Kaka habari yako”
Alisalimia Hasna.
“Nzuri dada,”
Alitikia huku akiendelea kukata mti.
Hakuonekana kumjali Hasna kabisa .
“Kaka naweza kukuuliza”?
Alisema Hasna.
“Weuliza tu”
Alisema kaka huyo huku akiendelea na zoezi lake la kukata mti.
“Nauliza njia ya kwenda Shunga”
Aliuliza Hasna.kijana huyo aliacha kukata mti na kuanza kumtaza Hasna.Hasna hadi aliingiwa na hofu Kwa jinsi kaka huyo alivyo mtazama.
“Dada kwani wewe unatokea wapi,?Na hapa unapajua ni wapi”?
Aliuliza kijana huyo.
Hasna alibaki kumtazama na kukosa cha kujibu.
“dada yangu hiyo njia unayoiulizia ni hatari sana”
Alisema kijana huyo.
“Hatari kivipi kaka yangu”?
Aliuliza Hasna.
Yule kaka hakumjibu chochote alichukua shoka yake na kuiweza begani ,kisha akamwambia Hasna amfate.
Hasna alimfata hadi kwenye pango lililokua linauwazi mkubwa uliokaa kama mlango,Kijana huyo alipita kwenye uwazi huo lakini Hasna aliogopa na kubaki kusimama Kwa nje.
Kijana huyo alimuomba Hasna amfuate.Hasna alisita lakini mwisho Wa siku aliingia ,lakini alipokua akizidi kuingia alianza kuona mabaki ya watu Hasna alianza kutetemeka. Walizidi kusonga ndani hadi wakafika sehemu kulikua na mti mkubwa.
Kijana huyo alifika akaweka shoka yake chini kisha akamgeukia Hasna.
“Karibu ukae kwenye kiti”
Alisema kijana huyo.Lakini Hasna akiangaza aoni hicho kiti.Hasna aliona nibora akae chini,ile anakaa aliona mazingira ya mebadilika.na kujiona yuko kwenye bonge la sebure lenye kila kitu na alipo muangalia yule kijana aliona kavaa suti moja matata.
Hasna alianza kupatwa na Hofu.
“we dada, vipi mbona umepigwa na butwaa kuna nini”
Aliuliza kijana huyo.Na Hasna alionekana kushituka,na alipo muangalia kijana huyo alimuona akiwa vile vile,na alipo angalia mazingira yaliakua yako vile vile.yalikua ni mawazo tu ya Hasna yaliyomfanya kuona pamebadilika.
“Kaka mbona unakaa huku peke yako hauogopi”?
Aliuliza Hasna.
“Tamuongopa nani?,mimi ndio naogopwa”
Alisema kijana huyo.Alianza kumuhadithia Hasna kisa cha yeye kuwa porini hapo.
Nimiaka ishirini na moja iliyopita wazazi wake walifukuzwa kijijini baada ya kupata shutuma ya kuwasumbua wana kijiji Kwa uchawi.Baada ya kijiji kuwa jadili Kwa kuonekana kuwa ni kero kijijini hapo,waliwafukuza nakuja kuanzisha makazi kwenye mstu huyo.
Walianzisha maisha yao na kubahatika kumpata mtoto wakiume ambaye ni huyo kijana.
Nawazazi wake walifariki miaka nane iliyopita.Hiyo kijana huyo kabaki pekeake.
Na chakula chake kilikua ni nyama za binadamu.
Alikua akitaka kupata nyama hizo basi anaenda barabarani, anaotesha mtia au anahamisha jiwe kichawi na kuliweka barabara ,Gari ikitokea kwa haraka madereva wanaweweseka na kupata ajari .Hivyo ndivyo alikua akijipatia kitoweo chake.
Alimaliza kusimulia .Hasna alizidi kuwa na hofi.Mara kijana huyo alianza kubadilika badilika sura za ajabu huku akimfata Hasna .Hasna alitaka kukimbia alikini alishidwa na kijana huyo akiwa kwenye umbo tofauti alimvamia Hasna .Hasna alipiga yowe na kujikuta akishituka kutoka kwenye ndoto.
Lakini aliposhituka alijikuta alishanga,baada ya kuona mazingira yako tofauti na yale aliyokua kakaa, alipoangalia vizuri aliona mazingira hayo alikua akiyafahamu vizuri.
Aliinuka nakuanza kutembea aliona mto mbele na watu walikua wakichota maji.Alianza kuwafata watu hao Kwa lengo la kuwauliza.
Lakini cha ajabu watu hao walipomuona hasina walikimbia na kutupa ndoo zao huku wakipiga kelele......
“Mama weeee ishinga”
(Mama weeee mzimu)
Walikimbia nyumba ya
kwanza kutoka mtoni ilikua ni ya mama Bionce.
“Nyina Bionce,wa mkobwa yahweleye yabhonese kumugezi”
(Mama Bionce,Yule dada aliyekufa tumemuona mtoni)
Waliongea watoto wale waliokua mtoni.Waliongea huku wakiwa wanahema .
“Leka ugutinya mwabana”
(Acheni uongo nyinyi watoto)
Alisema mama Bionce.
“Kweli nyina bionce nditubheha”
(Kweli nyina Bionce nditubheha).
Walimjibu mama Bionce Kwa msisitizo.Mama Bionce aliposikia hivyo alitoka mbio,hadi kwenye nyumba moja alimkuta mzee mmoja kakaa nje.Akiwa anakamua mise ilikupata maweze.
"Ye mutama ndumva lya shinga lya wamkombwa lya bhonese kumugezi”
(Mzee mwenzangu nasikia mzimu wa yule binti ameonekana mtoni)
Alisema mama Bionce,aliye kuja mbio huku kanga yake kaishika mkono.
“Na jewe ndumvise kubhantu ndalimenya nubhubheshi kumbe kweli"?
(Hata Mimi nimelisikia Kwa watu nikajua utani kumbe ni kweli)
Aliongea mzee huyo.Mara ilisikika ngima ikiwaitaji wananchi kuelekea Kwa mwenyekiti.
Watu walikusanyika huku wengine wasijue,walichoitiwa hapo na wengine walikua wameishajua.Wakati mwenyekitia akiwa bado hajafika eneo hilo ,watu walikua wamekaa kimakundi wakiteta jambo.Kila mmoja aliongea anacho kijua.
Baada ya dakika kadha mwenye kiti alitokea akiwa na wajumbe wake,Kwa nyuma alinekana Hasna akiongozana nao.
Watu walishangaa sana baada ya kumuona Hasna.
“Jamani nime waita hapa kuna jambo tuzungumze,nadhani binti huyu mnaomuona mbele yenu mnamfahamu”?
Aliongea mwenye kiti kisha akawauliza swali wanakijiji.
“Ndio tunamfahamu”
Wanakijiji wote Kwa pamoja waliitikia.
“Napenda kuwatoa hofu kuhusu binti huyu.Kwa binti huyu hakuweza kufa kwenye tukio la moto na wala sio mzimu ni binadamu kama nyinyi”
Alisema mwenyekiti lakini wanakijiji wote waliguna,kuashilia kumpinga mwenyekiti.
“Sawa najua hamuwezi kuamini lakini jueni kikulacho kimo nguoni mwenu,binti huyu sio mchawi bali kuna watu wenye tabia hizo za kichawi .walijalibu kumtengenezea mazingira hili wanakijiji mumchukie na mmuondoe hapa kijini,iliwawaze kufanya kazi zao bila kubanwa.”
Aliongea mwenyekiti kisha akamkalibisha Hasna aweze kuwaambia wanakijiji, Hasna aliwaelezea wanakijiji mambo yote yaliyotea na jinsi walivyoweza kutoka kwenye nyumba hiyo iliyo washwa moto.
“Wanakijiji ndiyo ilivyokua.Na leo nataka kuwa umbua mbele yenu ili mwashudie”
Aliongea Hasna huku akiangaza huku na kule. Wanakijiji wote walikua makini kumtazama Hasna kuona nini anachokifanya.
Alimuona mama Bionce akiwa na wachawi mwenzake. Mama Bionce aliupikicha mikono yake hadi ikatengeneza moto,kisha akautupa kwa Hasna.Hasna aliupangua kisha akaanza kucheka Kwa sauti.wanakijiji walibaki wakimshangaa, kwani hakuna aliyejua nini kinachoendea.
Hasna aliangalia juu ya mawingu Kwa muda usiopungua dakika tano.Mara Ilianza kusikika na kuonekana miale ya radi.Hasna alirudisha macho yake chini na kuanza kuwatizama wanakijiji. Ghafla ilianza kunyesha mvua,iliyo nyesha kuwa zunguka wanakijiji washingaa kuona mvua hiyo isio wanyeshea.Bali ilinyesha kama wigo hakuna aliyeweza kutoka eneo hilo.Maana ukitoka unakutana namvua kubwa tena ya mawe.
Wanakijiji waliendelea kushangaa na kuona ni maajabu ya dunia ,mvu kunyesha bila kuwashikia huku ikiwa imewazunguka kama wigo.
Ghafl mvua hiyo ilikata.Mara zikasika kelele za watu katikati ya umati wa wanakijiji.kila mmoja akiomba msaada Kwa aina yake.
Kunabaadhi walikua wakiwasha nakungara gara chi na wengine waliacha kuona.
Wanakijiji wakibaki kushangaa na kunawengine walianza kuwapa Masada.
“Washikeni na muwalete hapa mbele”
Aliongea Hasna.Wanakijiji waliwashika nakuwapeleka mbele.
“Hawa sasa ndio wabaya wa kijijini hapa,Nakila mmoja atongea tukio alilolifanya mbele yenu”
Wanakijiji walishangaa, wengine walishangaa kuwaona wazazi wao,wengine walishangaa kuwaona babu zao na wengine walishangaa kuwaona wapenzi wao.Miongoni mwa kundi hilo alikuwepo Bionce na mama yake......
Kila mwana kijiji alikua kimya akiwatazama Kwa makini,lengo ni kusikia matukio walio yafanya kijijini hapo.
Hasna aliwamwagia unga flani.walio kua wakiwashwa waliacha kuwashwa wale walikua hawaoni basi walianza kuona.
Mwenye kiti alisimama na kuwa ambia wachawi hao waongee Kwa lugha ya kiswahili nasio kiha.Wa kwanza kwenda kuongea alikua ni mama Bionce.
“Jamani naombeni munisamehe sana,nimefanya matukio mengi likiwemo kumuua mume wangu kichawi ”
Aliongea mama Bionce. Wanakijiji wote walibaki mdomo wazi.
“pia yale matukio ya watu kufariki mfurulizo mtoni ni sisi ,na kundi letu la kichawi la hapa kijijini.Tukasema ni Binti Hasna ili mumchukie mmuue maana alikua aki sababisha mipango yetu ikwame”
Akiendelea kuongea mama Bionce,huku machozi yakiwa yanamtoka na macho yake yalikua yakiangalia chini ,huku Mara moja moja analitupia Kwa wanakijiji na kulirudisha haraka Kwa aibu.
Wanakijiji walianza minong'ono ya hapa na pale ambayo ilimfanya mama Bionce akae kimya.
“Jamani wanakijiji tunaomba usikivu samahani”
Aliongea mwenye kiti kisha akamruhusu mama Bionce aendele.
“Tukio li..liingine ”
Aliongea mama Bionce Kwa kigugumizi kisha akawatizama wanakijiji ,akashindwa kuendelea kuongea.
“tunaomba utuambia mwanga mkubwa wewe”
Ilisikia sauti ya baadhi ya wanakijiji wakiongea Kwa sauti ya juu.
Mama Bionce alipata ujasi na kuonza kuongea.
“Tukio lingine ni ile ajari iliyouwa wa... waaatuuu sitini pale mlima wa Nyakitinto.Amboyo timu ya Shule ya Shekondari ya Shunga ilikua ikienda kucheza na Shule ya sekondari ya Nyakitonto.Basi ile ajari tuliitengeneza Mimi na kundi langu mnaloliona hapa mbele yenu.Nakusababisha kijiji chetu kuingia kwenye msiba mzito uliofanya hadi raisi wa jamuhuri ya muungano wa......”
Mama Bionce hakumaliza kuongea wanakijiji waliwavamia nakuanza kuwashambulia.Wangambo Kwa idhini ya mwenyekiti walianza kuwazuia wanakijiji hao,Lakini hakuweza kuwazuia.
Mwisho wa siku wanakijiji waliwaua wachawi wote kisha miili yao wakaichoma moto.
Wanakijiji walianza kuimba nyimbo za kiha wakimsifia Hasna.Japo wengine walikua na udhuni kupoteza familia zao.
Ilikua mida ya jioni kiza kilikua kimeanza kutanda.Hasna alikua kakaa na baadhi ya wazee wakijadiliana jambo,pia alitumia nafasi hiyo kuwaaga,maana alikua na safari ya kwenda Kwa yule mzee kule porini.
“Sasa bibi kwanini usingeenda kesho mapema”?
Mzee mmoja kwenye kundi hilo alimuuliza
“hapana mzee wangu naondoka usiku huu,lakini sitaki wana kijiji wajue maana watanizuia Kwa sasa .hivyo na mambo ya muhimu huko niendako.”
Aliongea Hasna.Basi wazee hao walimruhusu.ilipofika majira ya saa mbili unusu Hasna alianza safari.
Akiwa katikati ya msitu uliokua ni mkubwa na ulikua unatisha hata mchana.Hasna alisikia kitu kimepita nyuma ,aligeuka lakini hakuona kitu.Hasna alianza kutembea Kwa kasi kidogo alisikia kicheko kilicho sikika mara moja alafu kikapotea.
Hasna alisimama kisha akageuka nyuma , Mara kilitokea kitu Kwa juu ya mti kikamnyakua Hasna na kupanda na hadi juu ya mti....
Hasna alianza kupiga kelele,nakujakibu kufanya mambo yake ya nguvu alizo nazo lakini hakuweza kujinasua.Kilipo mfikisha juu kilimuachia Hasna ,alianguka kama mzigo wa kuni alipo anguka chini, alipoteza fahamu kabisa.
Na alipo kuja kushituka alijikuta nyumba Kwa mzee Bungi.Ni mzee ambaye Hasna alikua kafunga safari kuja kuonana nae.
Hasna alipo angaza palikua pameisha pamba zuka.
“Mzee nimefikaje kwako”
Ni swali alilo uliza Hasna.
“Naomba utulie binti takueleza”
Alisema mzee Bungi.Hasna hakuendekea kuongea chochote.Mzee Bungi alinyanyuka na kuingia ndani,Alitoka kabeba chungu kilichokua kikifuka mvuke.
“Binti nyanyuka”
Alisema mzee Bungi.Hasna aliponyanyuka baada ya kujitazama vizuri aligundua alikua hajavaa chochote zaid ya kaniki jeusi alilofungwa.
“mzee mbona sijavaa”?
Aliuliza Hasna huku akijiangalia angalia mwili wake.
“Inuka na ukalie kinu hicho,baada ya kufanya nachotaka kukifanya ndio utakua kwanini ,mzimu wa mama yako umekuambia uje hapa”
Aliongea mzee Bungi huku akifungua shuruali yake iliyokua imefungwa na kamba aliyoitumia kama mkanda.
Hasna alibaki kushangaa tu huku akitekeleza anachoambiwa.Mzee Bungi alivua nguo zote nakubaki kama alivyo zaliwa.
Hasna alikaa juu ya kinu hicho na kuambiwa aangalie jua linapo chomozea.
Mzee Bungi alisimama nyuma ya Hasna ,kisha akachukua kitambaa na kukiloweka kwenye chungu hicho kilichokua na maji ya moto sana yaliyochanganywa na mizizi ya miti tusioyo ijua.
Mzee Bungi alianza kuongea maneno Kwa lugha aliyo ijua yeye pekee.
Baada yakumaliza alimuomba Hasna anyanyuke mahara hapo.
“hiyo ni dawa ya kwanza bado ziko nyingi sana”
Aliongea mzee Bungi.
“Kwani mzee dawa hizi zinahusu nini,?maana Mimi niliambiwa maelekezo tapata huku huku”
Aliuliza Hasna.
“Dawa hizi ni Kwa sababu ya kukuongezea nguvu zaid,ili uweze kupambana na baba yako,maana Kwa sasa ulivyo hauwezi kupambana nae.Na Kwa sasa kapanga kuingamiza Dunia,na mkombozi ni wewe tu kwenye kijiji chenu”
Alisema mzee Bungi.
“Kwani wewe ni nani kwani mzee"?
Aliuliza Hasna.
“Mimi naitwa Shija Maganga Nzwela Bungi,Alimaarufu kama Mzee Bungi,Natokea kwenye kijiji cha Mbika na nilikua ni kiongozi wa kimila lakini sikuweza kutumia nguvu za tamaduni zetu kusaidia wanakijiji bali mimi nilitumia nguvu nilizopewa na mizimu Kwa manuvaa yangu binafsi.Niliwaingilia wanawake usiku bila wenyewe kujijua ,pia nilitumia nguvu za mizimu kuwadhuru watu wataonikosea.
Pia nilijingiza kwenye ushirikina na kuleta machafuko makubwa kijijini hapo.Kifupi nilikua sio mtu mzuri kabisa”
Mzee Bungi aliongea huku akionekana na uzuni.Hasna alimtazama mzee huyo.
“Sasa na huku umefikaje mzee”?
Aliuliza Hasna.
“Huku ,baada ya mizimu ya mababu ilipokasilika ilinipa adhabu ya kuishi pekee yangu, bila kuonana na mtu yeyeto Kwa muda usio julikana.Nilipelekwa kwenye pori la ngamboshi lililoko Kahama.Nauko nilishi miaka saba kama mnyama,nakula mizizi na lala pori kuna wanyama wakali na wadudu wadogo wenye sumu Kali.
Kiukweli maisha yale kwangu yalikua magumu sana.Lakini Kwa kutumia nguvu zangu za giza nilizokuwa nazi niliweza kutengeneza viumbe wa ajabu wa patao ishirini na moja.
Na niliwatumia kwenda kwenye kijiji na kunichukulia chakula na mahitaji yote niliyo yataka.
Mwisho nilichoka kufanya tabia hizo, nikaona bora nitoroke huko ngambushi na kuja kuishi hapa peke angu na hapa namiaka isiyopungua kumi”
Aliongea Mzee Bungi.
“Sasa mzee hao viumbe wako wapi”
Aliuza Hasna.
“Hao viumbe niliwakabidhi kwenye chama cha ushilika wakichawi,alichokuwepo mwanzo baba yako kabla ajaanzisha chama chake cha mungu wa aridhini.Na aliweza kuwachukua viumbe hao,aliweza kuwashinda washilika wenzake na kuwa chukua yeye ni kutokana na kuwapa damu na nyama za watu mara kwa Mara ,maana viumbe hao hawali chochote zaid ya nyama za watu.Na ndio waliokujeruhi kipindi baba yako katoweka kwenye mapambona,na ulipomfuata ulimkuta baba yako akiwa na viumbe hao”
Aliongea Bungi. Hasna alivuta picha kipindi cha mapambano,alipo toweka baba yake nae alimfata Kwa kujua alikua kawa fata kina Zuberi Kwa lengo la kukachukua kachanga .
Basi Hasna alipotokea upande Pili alimkuta baba yake akiwa na viumbe vile vilikua vinatisha na upande wa mdomoni vilikua vinadondosha damu na meno yao yalikua ni marefu.
Walipomuona Hasna pale Mtemi alimuangiza mmoja wa viumbe wale na kumfata Hasna .Hasna alianza kurusha moto kutoka kwenye mdomo wake, lakini kiumbe kile kiliendelea kumfata bila kuteteleka.Kilipomfikia kilichomoa kucha na kumchana Hasna tumboni,ndio Hasna aliona akiwezi na kukimbia kurudi Kwa malikia Wa kuzimu.
Hizi ni kumbukizi ya Hasna baada ya kuambia kuhusu viumbe hivyo na mzee Bungi.
“kweli mzee mi taweza kupambana na hao viumbe ”?
Aliuliza swali Hasna.
“Kwanini usiweze?,Mimi ndio nilio waumba na udhaifu wao na ujua”
Alisema mzee Bungi.Muda huo wote walikua wako uchi wa mnyama.
“kuna sawa moja nahitaji kuitengeneza leo usiku ”
Alisema mzee Bungi.
“sawa mzee kwani dawa ipi hiyo”?
Alikubali Hasna kisha akamuuliza swali mzee Bungi.
“Naitaji damu yako ya kutoka kwenye hiyo bikira yako,na kuipata damu hiyo nilazima nilale na wewe damu itakayo toka ndio nahiitaji kwa jili ya dawa ya maangamizi.......”
Aliongea mzee Bungi akiwa anavaa suruali yake na nyeti zake zilionekana kusimama.
Hasna alivyo sikia hivyo alinyanyuka na kuchukua kaniki na kujifunia na kuingia ndani Kwa mzee Bungi.Alijiuliza maswali bila kupata majibu.
Miongoni mwa swali lililo mchanganya ni pamoja na
“mzee Bungi kajua kua mimi ni bikira?,Huyu mzee atakua kanichezea nilipokua nimepoteza fahamu,au kanifanyia kitu kibaya?.Lakini hapana atakua hajafanya chochote, mbona niko sawa.”
Ni baadhi ya mambo yaliyokua yakizunguka ndani ya kichwa cha Hasna.
“we mzee naomba unipe nguo zangu”
Hasna alitoka nje na kuniambia mzee Bungi.
“Binti acha hasira,fanya kama nilivyokuambia,la sivyo utapata shida sana”
Aliongea mzee Bungi.
“Naomba unikome wewe mzee shida hiyo kwiooo”
Aliongea Hasna akiwa na jaziba.Mzee Bungi alicheka sana kicheko alicho cheka zaidi ya dakika moja.
“Utake usitake utatoa tu kidori wangu”
Baada ya kicheko hicho mzee Bungi alimwambia Hasna maneno hayo.
Hasna alimtemea mzee Bungi mate usoni,lakini mzee Bungi aliyachua Kwa mkono wake kisha akayalamba.
“Unaonekana wewe mtamu sana,kama mate yako yalivyo”.
Alisema mzee Bungi.Kisha akamfata Hasna na kumkamata na mikono yake iliyokua na nguvu kama kijana.alimvuta Hasna hadi ndani alipokua anamvuta kaniki alilokua kajifunga Hasna lilianguka na kubaki kama alivyo zaliwa.Mzee Bungi alimuangushia sehemu alivyoitengeneza Kwa jili ya kulala.alikua katengene Kwa mfano wa kitanda.Lakini alitengeneza Kwa kutumia miti na majani.
Basi alimuangushia Hasna mahala hapo.Mzee Bungi alionekana kua na uchu na binti Hasna,alivua suruali yake Kwa shida iliaweze kufanya anachotaka kufanya.
Upande wa Pili alionekana malikia wa kuzimu akiwa anajitibu jeraha lake alilo jeruhiwa na wale viumbe wa ajabu.
Nae lengo lake alikua apote arudi kwao kigoma kumuadhibu baba yake aliye mueka mzukule kwa miaka miwili ,akiwa muhudumu wa kufua na kusafisha vyumba vya gesti ya baba yake.
Na alisaidiwa na kurudishwa kwenye hali ya ubinadamu na mzimu wa mama Hasna .Ni baada ya kuambiwa akimsaidia Hasna apone, kwa kupata damu ya baba yake Hasna,na kweli alifanya hivyo.
Na sasa ni binadamu wa kawaida,sema alipewa nguvu kidogo za kuweza kufanya miujiza.
Binti huyo kwa jina lake halisi anaitwa Jessica Jacobo .kwàjina alilopewa na Hasna anaitwa malikia wa kuzimu.
Basi alikua akiendelea kujiganga na jeraha lillikua kubwa tumboni mwake.
Malikia wa kuzimu akiwa pale kuna kitu alikihisi na kupotea kimazingara.
Na alitokea upande alipo Hasna na kumkuta mzee Bungi akiangaika kumuingilia kimwili Hasna.
Malikia wa kuzimu alirusha moto Kwa mzee Bungi,ulio mshitua na kuacha kuendelea na zoezi lake la kumtaka kinguvu Hasna.
Mzee Bungi alinyanyuka na kumuacha Hasna akiwa kalala,kaishiwa nguvu kutokana na purukushani na mzee Bungi.
“Leo mungu kanitunuku vigori”
Aliongea mzee Bungi,huku akimsogelea malikia wa kuzimu.
Malikia wa kuzimu alianza kurusha moto,cha ajabu Mzee Bungi alikua akiuzuia Kwa mkono mmoja bila hata kuteteleka.
“Binti hauwezi kufanya lolote kwangu mtu mnae taka kwenda kupambana nae,na nguvu mara mia yake.sasa kuweni wapole na mkubaliane na mimi”
Aliongea mzee Bungi.
“Kwani mzee wewe unashida gani nyingine zaid ya kumpa msaada Hasna,?na ndio maelekezo aliyotupa mama Hasna”
Aliongea malikia wa kuzimu.
“nijambo dogo sana,nilikua nahitaji kulala na binti huyu kwa sababu ni bikira nipate damu yake nitengeneze dawa ya kuangamiza viumbe wale nilio watengeneza mwenye”
Aliongea mzee Bungi. Malikia wa kuzimu alicheka kidogo.
“Kwani lazima damu ya Hasna tu”?
Aliuliza malikia wa kuzimu.
“Hapana ni yoyote kama mkiipata”
Alisema mzee Bungi.
“Mzee naomba unifate,twende huku tunaweza ipata hiyo damu ya aina ya mtu unae mtaka”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment