Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

RANGI YA CHUNGWA - 1

 

IMEANDIKWA NA : DEOKING PETER 

********************************************************************************

Simulizi : Rangi Ya Chungwa

Sehemu Ya Kwanza (1)



Ni kijana mwenye akili nyingi za kufikiria na kutatua jambo, katika maisha yake hakuwahi kufanya jambo likawa baya mbele za watu. Mungu alimjalia kwa kumpatia wazazi bora wenyekujua majukumu yao, walimjali mtoto huyo ambae alikuwa wa pekee katika familia hiyo, alipata elimu bora hadi kufikia kuwa mtu mkubwa serikalini.


Kazi alioipenda alipenda kuwa hakimu, kitu ambacho hapo awali wazazi wake walikikataa ila kwa kuwa kijana huyo alikuwa na ndoto hizo hawakuwa na namna zaidi ya kukubaliana nae. Kwavile wazazi wake hawakutaka kukaa mbali na mwanao waliamua kumshawishi abaki jajini Dar es salaam ili kuwa karibu na wazi wake, lakini kijana huyo alitaka afanyie kazi zake mkoa Arusha, akiamini hali ya hewa na mazingira ya mkoa huo yangalimfaa.


Wazazi wake hawakuwa na kipingamizi wa walikubaliana nae maana walimpenda sana na kumjali. Kijana huyo alianza kazi mkoani huko akiwa anawasilia na wazazi wake zaidi ya mara mbili kwa siku. Ilipita miezi kadhaa mawasiliano yakaanza kuwa hadimu, ilikuwa asipotafutwa na wazazi wake basi yeye hakushuhulika nao, akiwa mkoani huko alifanikiwa kupata mpenzi ambae alifanikiwa kuuteka moyo wa kijana huyo. Alimjali msichana huyo kuliko kitu chochote, hata kazi aliokuwa nayo aliiona haina thamani kama angelikaa mbali na msichana huyo.


Hakufikiria kama anafamilia alichokijali na kukijua katika akili yake ni Msichana huyo aliejulikana kama Johari, msichana mwenye asili ya kimbulu. Kiukweli kama wanavyosema mapenzi ni ugonjwa basi kwa kijana Dockson ilikuwa ni zaidi ya ugonjwa, naweza kusema ilikuwa kama ulimbukeni wa mapenzi, ni kwajinsi kijana huyo alivyo jitoa kwa mwanadada huyo bila kufikiria.


Familia ya Kijana Dickson ilishindwa kuelewa kilicho mpata mtoto wao kuwa kimya kwa kipindi chote, bila hata kuwatafuta wazazi wake, waliwaza ambo mengi katika vichwa vyao bila kupata jibu kamili. Waliamua kufunga safari kuelekea mkoani ambapo mtoto wao alikuwa akifanya kazi, walikubaliana kwa pamoja kwenda kumuona mwanao bila taarifa, kwa lugha nyingine waliamua kumfanyia "suprice".


Asubuhi na mapema wazazi hao walikuwa maeneo ya ubungo wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Arusha kumuona mtoto wao kipenzi. Dickson siku hiyo asubuhi aliwahi kazini kwake na kufanya majukumu yake ya kila siku, akiwa ofisini kwake alipigiwa simu na mpenzi wake na kumwambia angelimpitia ofisini baada ya kutoka chuo.


Naam! Johari alikuwa ni moja ya wanafunzi wa chuo kikubwa hapo mkoani, chuo ambacho kilikuwa na wanafunzi wengi wa aina tofauti tofauti, na wengine wakiwa wametokea nchi tofauti tofauti. Ni chuo ambacho kilikuwa kikubwa kutokana na wingi wa wanafunzi waliokuwa wakisoma kwenye hicho chuo. Dickson alikubaliana na mpenzi wake kisha kukata simu na kuendelea na shughuli zake za kila siku.


Johar siku hiyo alipotoka chuoni aliamua kupitia kwa rafiki yake kwenda kumsalimia, alipofika kwa rafiki yake alijikuta amepoteza muda mwingi bila kujua kuwa alisha mwambia mpenzi wake amsubiri. Alipokuja kuangalia saa ilikuwa imeshafika saa kumi kasoro, aliamua kuchukua bodaboda ili kuwahi kwa mpenzi wake.


Wazazi wa Dickson safari yao ilikuwa ndefu lakini Mungu aliwasaidia na walifika salama, walipofika Jijini hapo na muda walijua mwanao angelikuwa ofisini maana ilikuwa bado mapema, waliamua kukubaliana kwenda moja kwa moja ofisini kwa mtoto wao. Johar hakuchukua muda mingi kufika kwa mpenzi wake kutokana na kutumia usafiri, alipofika alimkuta mpenzi wake akiwa anamsubiri huku akionekana kumngoja muda mrefu.


"Baby sorry kwa kuchelewa" Aliongea Johar huku akiwa anampiga busu la mdomoni, Dickson nae alimpa ushirikiano mpenzi wake na kunza kupigana mabusu mazito, maarufu kama denda, ile hali ilichukua kama dakika tano na kuwafanya kila mmoja wao hisia kupanda na kujikuta wakitamani kufanya mapenzi pale ofisini, hisia ziliwazidi na kuwakolea na kujikuta wakianza kufanya mapenzi pale ofisini bila kijali.


Tukija huku kwa wazazi wa Dickson nao walikuwa tayari wamefika ofisini kwa mtoto wao, walipofika waliamua kuingia moja kwa moja ofisini. Walishtuka na kutaka kutudi nje, maana walichokikuta kilikuwa hakielezeki.


Wazazi wa Dickson safari yao ilikuwa ndefu lakini Mungu aliwasaidia na walifika salama, walipofika Jijini hapo na muda walijua mwanao angelikuwa ofisini maana ilikuwa bado mapema, waliamua kukubaliana kwenda moja kwa moja ofisini kwa mtoto wao. Johar hakuchukua muda mingi kufika kwa mpenzi wake kutokana na kutumia usafiri, alipofika alimkuta mpenzi wake akiwa anamsubiri huku akionekana kumngoja muda mrefu.


"Baby sorry kwa kuchelewa" Aliongea Johar huku akiwa anampiga busu la mdomoni, Dickson nae alimpa ushirikiano mpenzi wake na kunza kupigana mabusu mazito, maarufu kama denda, ile hali ilichukua kama dakika tano na kuwafanya kila mmoja wao hisia kupanda na kujikuta wakitamani kufanya mapenzi pale ofisini, hisia ziliwazidi na kuwakolea na kujikuta wakianza kufanya mapenzi pale ofisini bila kijali.


Tukija huku kwa wazazi wa Dickson nao walikuwa tayari wamefika ofisini kwa mtoto wao, walipofika waliamua kuingia moja kwa moja ofisini. Walishtuka na kutaka kutudi nje, maana walichokikuta kilikuwa hakielezeki.


ENDELEA.........

Mama yake alipoingia ofisini kwa mtoto wake hakuamini alisho kiona, alishindwa kuzuia macho yake yasione kilichokuwa kinafanyika, waliamua kutoka nje kimya kimya bila Dickson kufahamu, maana wakati wanaingia Dickson hakusikia kitu chchote. Walibaki pale nje ya ofisi ya mtoto wao kwa dakika kadhaa huku kichwani kwao wakiwa hawaamini kilichotokea, walihisi pengine siyo mtoto wao wanaemfahamu, maana walijua wazi Dickson hawezi kufanya ujinga kama ule.


Walikaa kwa muda hatimaye wakaamua kutoka pale ofisini na kuelekea nyumbani kwa mtoto wao, hawakutaka mtoto wao ajue kama wazazi wake wameona ujinga aliokuwa anaufanya. Walipofika nyumbani walimkuta mlinzi wa nyumba ya Dickson, kwakuwa yule mlinzi aliwatambua kuwa wale ni wazazi wa bosi wake aliwaruhusu kuingia ndani.


Waliingia ndani huku lile jambo likawa linawasumbua vichwa vyao, walipofika sebleni hali ilikuwa imebadilika sana, walikuta baadhi ya nguo zikiwa zimetupwa tupwa kwenye viti vya kukalia, kitu ambacho kiliwashangaza walikuta hadi nguo za ndani zikiwa juu ya meza ya pale sebleni. Wazazi hao walibaki wakiwa wanashangaa njinsi nyumba ya mtoto wao ilivyokuwa chafu hadi kufikia hatua kuleta kinyaa, walibaki tu wameduwaa walichokifanya wakaamua kutoka na kumsisitiza kijana wa getini kutimwambia chochote kuhusu ujio wa wazazi wake pale nyumbani.


Mlinzi huyo hakuwa na kipingamizi zaidi ya kuwakubalia maana hakuwa anafaha kilichokuwa kinaendelea, alipomaliza aliwaaga kisha wazazi hao waliondoka na kuelekea nyumba moja kubwa ya kulala wageni, na kuamua kukaa kwa siku hiyo maana hawakutaka mtoto wao awaone. Dickson pamoja na mpenzi wake walipomaliza walikubaliana kurudi nyumbani, huku kula mmoja akiwa anaonekana kuwa na furaha.


Walipofika nyumbani mlinzi wa getini aliwafungulia mlangu wote wakaingia ndani, mlinzi huyo alionekana kutaka kumwambia bosi wake kama wazazi walikuja wakati yeye ambapo hakuwepo, likini kutokana na msisitizo wa wazazi wa Dickson alijikuta analifanya jambo lile siri.


Dickson pamoja na mpenzi wake waliishi kama watoto wasiojielewa, kama ule ulikuwa ulimbukeni wa mapenzi basi Dickson pamoja ba Johar mpenzie walikuwa wamezidi. Kila kitu walichokuwa wanakifanya kilikuwa cha kitoto, hawakuwa na wanajali chochote zaidi ya kunywa kula na kulala.


Dickson hakuwa yule Dickson aliezoeleka kama Hakimu, hata mlinzi wa nyumba hiyo alishangaa maisha ya bosi wake yalivyo badilika, alishangaa kila siku bosi wake alikuwa mtu wa kulewa na kurudi usiku sana tofauti na hapo awali ambapo hakuwa abatumia kilevi chochote zaidi ya juice na vinywaji vingine visivyokuwa na kilevi.


Wazazi wa Dickson walizidi kumfuatilia mtoto wao na kuona mtoto wao alivyo badilika, walishindwa kuelewa kwanini mtoto wao amebadilika kiasi kile. Hawakupata jibu la kuwatosheleza zaidi ya wakijiuliza wafanye kitugani ili mtoto wao kipenzi arudi kama mwanzo.

Waliamua kumfuatilia hatua hadi hatua, walifanikiwa kumfahamfu msichana aliekuwa akitoka na mtoto wao, waliamini msichana huyo ndiye aliekuwa akimwaribu mtoto wao.


Walizidi kufatilia na kufahamu msichana huyo alikiwa ni moja ya wanachuo kikubwa katika jiji hilo, chuo hicho husifika kwa sifa mbaya na kusemekana baadhi ya wanachuo hicho hujiuza kwa watu wa aina tofauti tofauti, na wengi wao huathirika kwa ugonjwa wa ukimwi.


Walijikuta wakipata mawazo mengi juu ya mtoto wao kipenzi, walijaribu kutafuta watu wa kuwasaidia lakini hawakufanikiwa zaidi ya kuzidi kuumia kwa mawazo.

Dickson alizidi kula rahaa na mpenzi wake huku akiwa hatambui kama familia yake ilikuwa pale mkoana, na kibaya zaidi familia yake walikwisha kugundua ujinga aliokuwa akiufanya.



Walizidi kufatilia na kufahamu msichana huyo alikiwa ni moja ya wanachuo kikubwa katika jiji hilo, chuo hicho husifika kwa sifa mbaya na kusemekana baadhi ya wanachuo hicho hujiuza kwa watu wa aina tofauti tofauti, na wengi wao huathirika kwa ugonjwa wa ukimwi.


Walijikuta wakipata mawazo mengi juu ya mtoto wao kipenzi, walijaribu kutafuta watu wa kuwasaidia lakini hawakufanikiwa zaidi ya kuzidi kuumia kwa mawazo.

Dickson alizidi kula rahaa na mpenzi wake huku akiwa hatambui kama familia yake ilikuwa pale mkoana, na kibaya zaidi familia yake walikwisha kugundua ujinga aliokuwa akiufanya.


ENDELEA.........

Siku moja Dickson akiwa ofisini kwake, simu yake ilita na alipoangalia jina lilikuwa ni la mpenzi wake Johar, mtu ambae alikuwa ameuteka wa Dickson, siwezi kujua ni kitu gani alimlisha Dickson. Wakati mwingine Dickson alikuwa akijishangaa kwa jinsi alivyo mpenda msichana, vitu walivyokuwa wanavifanya hakuna hata kimoja kilichokuwa kinaeleweka au kuwa na maana.


Naweza kukubaliana na msemo usemao "Mapenzi ni upofu" Walijisahau na mawazo yao yakawa yanaenda, msichana huyo uwezo wa kuwa kama mwanamke wa kujielewa hakuwa nao, naweza kusema umbo alilokuwa nalo ndilo lililomfanya kuonekana kama msichana mwenye uelewa na uwezo wa kuwa kama msichana.


Baba na Mama wa Dickson waliamua kufaya uchunguzi wa yule mwanamke aliekiwa ni mpenzi wa mtoto wao, walihisi pengine kuna kitu amemlisha mtoto wao, maana mtoto wao alikuwa amebadilika kwa kiasi kikubwa, hakikuwa kitu cha kawaida mtu mwenye kujielewa kufanya vitu kama alivyokiwa anafanya Dickson.


Msichana huyo aliekuwa akitembea na Dickson hakuna alietambua familia yake wala mkoa aliotoka, maichana huyo alikuwa ni kipenzi cha wanafunzi wenzake, kala mwanachuo alimpenda kutokana na ucheshi wake. Kitu ambacho kiliwashangaza wazazi wa Dickson katika uchunguzi wao waligundua yule msihana ni moja ya wanafunzi wanaofanya vizuri pale chuoni, na alionekana kuwa msafi kila wakati, ila kila anapokuwa na mtoto wao alionekana tofauti.


Walibaki wakiulizana na bila kupata jibu. Walishindwa kutambua msichana yule alikuwa na maana gani kuwa katika hali kama ile kila anapokuwa na mtoto wao Dickson. Dickson hata kazi zake aliamini bila kuwa na yule msicha basi asingeweza kufanya chochote, alitamani kuwa nae kila wakati hakutamani kukaa mbali na mpenzi wake.


************

Siku moja Dickson akiwa kwenye miagaiko yake ya hapa na pale, alamua kuingia sokoni pamoja na mpenzi wake, maana walikubaliana kwenda kupika chakula kwa pamoja. Wakiwa wananunua vitu Dickson alishtuka kumuona mtu akiwa amepita mbele yake akiwa anafanana na Mama yake sura mpaka umbo. Dickson alibaki akiwa anajiuliza maswali kuhusu yule mtu alepita mbele yake, mpenzi wake alipomuuliza alinaki kimya maana hakuwa na huakika na kile alichokiona.


Walirejea nyumbani huku kijana Dickson akiwa na mawazo kwa kile alichokiona, ndipo alipoamua kuwapigia simu wazaziwake. Aimu iliita mara kadhaa bila kypokelewa na baada ya muda alijaribu tena na simu iliweza kupokelewa.

"Hellow!!!!!

Ni sauti ya kike iliosika kutoka baada ya ile simu kupokelewa. "Unaongea na Dickson sijui Baba na mama wapo huko"


Aliongea baada ya yule msichana kuanzisha maongezi, yule aliepokea ile simu alimfahamu vilivyo maana alikuwa ni sekretari wa Baba yake. Yule Sekretari alinyamaza kimya kwa muda huku akionyesha ku waza kitu na kunijibu.

"Baba pamoja na Mama yako wametoka muda siyo mrefu, wameelekea kwa shangazi yako"

Aliongea yule sekretar na kunifanya niwaze juu ya yule mtu niliemuona akiwa anafanana na Mama yangu. Dickson alibaki akijiuliza masali mengi kichwani kwake bila kupata jibu kamili, aliamini kile alichokiona alikuwa hajaona vizuri.


Aliendelea na shughuli zake huku mpenzi wake akiwa karibu yake kila wakati. Baba yake na Mama yake waliendelea kuumiza vichwa vyao kutokana na mtoto wao kubadilika hadi kufikia hatua ya kutowafikiria wazazi wake, walizidi kushangazwa na mtoto huyo kwa hali ya maisha aliokuwa anayaishi. Liukweli ilikiwa ni aibu kwa mtu kama Dickson kuishi maisha kama yale. Wazazi wake waliamua kufanya utaratibu wa kumuamisha Dickson pale mkoani ili kuepukana na aibu kutoka kwa msicha yule, maana walihisi yule msichana hakuwa mwema kwa mtoto wao



Ikiwa ni asubuhi kama ilivyokuwa desturi au taratibu alizojiwekea kijana huyo, alijiandaa vema kwaajili ya kwenda kazini kwake. Wakati akiwa anaondoka nyumbani kama kawaida yake aliwasiliana na mpenzi wake na walikubaliana wangeweza kuonana pindi atakapo toka kazini. Dickson alipofika ofisini kwake alikuta utaratibu umebadilika, alishindwa kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea, ofisi yake ilikuwa imebadilishwa huku kukionekana kila kitu kilichokuwamo kwenye ile ofisi si vyake, alizidi kuchanganyikiwa maana vitu vyake vya muhimu havikuwamo ofisini kwake havikuwmo. Wakati akiwa anazidi kukagua na kutafuta baadhi ya vitu vyake.


"Au nimekosea ofisi"

Alijiuliza baada ya kukosa vitu vyake, kiukweli alionekana kuchanganyikiwa, alizunguka huku na huku bila mafanikio. Kwa haraka haraka na kwajinsi alivyokuwa alionekana kuchanganyikiwa.

Alipoona vile aliamua kutoka nje kuangaza kama ni kweli ile ni ofisi yake, alivyotoka na kuangalia aligundua ofisi ni ile ile ya siku zote, alibaki pale nje akiwa anajiuliza maswali mengi, akizidi kujiuliza juu ya mabadiliko ya ofisi yake alishangaa kuona gari aina ya Rav4 nyeusi iliozungukwa na tintedi kila kona, ikiingia na kupaki pembeni ya ofisi hiyo, ndipo aliposhuka mdada mrembo akiwa ameshikilia funguo la gari hilo huku pembeni akiwa na karatasi nyeupe ambazo zilionekana kuwa na maandishi.


Mwana dada huyo alimwangalia Dickson bila ya hata salamu, Dikson kwa haraka haraka alijua yule alikuwa ni mteja, alishindwa kumkaribisha maana aliwaza kuhusu vitu vyake.

"Bila shaka wewe ni Dickson?"

Aliongea msichana huyo baada ya kumfikia Dickson.

"Ndiyo mimi sijui nikusaidie nini?"

Alijibu huku akionekana kutokuwa sawa.

"Vizuri maana nafikiri ujumbe niliopewa umefika"


Aliongea msichana huyo huku akiwa anamkabithi yale makaratasi Dickson, Dickson aliyachuka yale makaratasi na kunza kuyasoma, Alishtuka baada ya kusoma na kumgeukia yule msichana na kubaki akiwa anamshangaa. Ilikuwa ni barua ya kuamishwa kikazi na yule msichana alikuwa ni mtoto wa bosi wake, alibaki akiwa ameduwaa hadi yule msichana akabidi amuullize.

"Vipi Dickson mbona unashangaa hivyo, inaana hizi taarifa hukuwa nazo"

Dickson alitikisa kichwa chake kuashiria hakuwa na zile taarifa, kigugumizi kilimshika ghafla, alishindwa hata kuongea.


"Mbona hizi taarifa kila mtu anazifahamu tena tayari ofisi yako ipo na inakusubiri wewe tu maana vitu vyako vyote vimesha safirishwa na nadhani vitakuwa tayari ndani ya ofisi mpya"

Aliongea msichana huyo ambae na kumfanya Dickson kushtuka kwa zile habari, zile taarifa zilikuwa kama ndoto lakini haikuwa ndoto, zilimwingia akilini ipasavyo hakuwa na uwezo wa kufanya lolote maana alietoa zile taarifa alikuwa ni bosi wake.


Aliamua kuondoka na kwenda ofisini kwa bosi wake kwaajili ya kutaka kujua sababu ya yeye kuamishwa bila taarifa, kwa muondoko aliondoka nao Dickson ulikuwa si wakawaida, alionekana kuwa na hasira kwa kile kilichotoke.

Alipofika ofisini kwa bosi wake alizuiliwa kuingia ikiwa tofauti na siku zote alizokuwa akiingia bila kizuizi, aliwaangalia wale watu na kuhisi wamechanganyikiwa, aliwaamuru wampishe lakini hakuna aliemsikiliza zaidi ya kusukumwa na kutolewa hadi nje ya geti la kuingilia. Kwa bahati nzuri bosi wake ndiyo alikuwa anaingia, Dickson hakufanikiwa kumuona bosi wake lakini bosi wake alifanikiwa kumuona na kushuka kwenye gari na kusogea mahali alipokuwa Dickson.



ENDELEA.................

Dickson alishindwa kuelewa kwanini alikuwa anazuiliwa kuingia kwenye ofisi ya bosi wake, akiwa anataka kuondoka alishangaa kumuona bosi wake mbele yake, alishtuka maana hakutegemea kitu kama kile, kilikuwa kitu cha kushtukiza na kumfanya Dickson kushtuka. Dickson alishindwa kuongea na kuona mdomo wake kuwa mzito kutamka kile alichotaka kumwambia bosi wake ofisini kwake.


"Dickson mbona upo hapa sasa hizi, wakati huu ni muda wa kazi?"

Aliongea bosi wake na kumfanya Dickson kutumbua macho kama mtu aliekanyaga nyoka, kiukweli lile swali lilikuwa kama mtego kwake, maana muda siyo mrefu alipokea barua kutoka kwa Mtoto wa bosi huyo kuwa ameamishwa kikazi na ameamishiwa Jijini Dar es salaam.


"Mbona unaonekana kama mtu anae ekti jambo flani. Unajua Dickson wewe ni kama mwanangu ila huko unapoelekea siko, utakuja kujikuta unaharibu maisha yako kwa mtu asiekuwa na thamani kwako. Kuna muda wa kazi na muda wa mapenzi, embu jiangalie ulivyobadilika hadi nakuhurumia, laiti ningalimjua huyo msichana anaekufanya unakuwa katika hali kama hii sijui nini kingetokea"


Aliongea bosi wake na Dickson ambae alikuwa ni kama Baba kwake, Dickson alibaki mdomo wazi kama ilivyo kawaida yake pale anapoulizwa swali la kumshangaza, au kitu chochote cha kustaajabisha. Dickson alishndwa kuelewa zile taarifa bisi wake amezipata wapi maana muda mwingi Bosi wake huwa ofisini kwake na wakati mwingine huwa kwenye safari mbali mbali za kikazi, alihisi huenda bosi wake alikuwa akimfuatilia kwa kipindi kirefu, ndiyo maana akawa analitambua lile jambo.


"Kama alikuwa ananifutilia mbona anaonekana hamtambui msichana huyo au kaambiwa na mtu"

Dickson alijikuta anazungumza maneno ya chini chini bila kujua sauti yake ilisikika vizuri katika masikio ya bosi wake.

"Nadhani nikija ofisini kwako tutaonge mengi, cha muhimu nakutakia safari njema"


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG