Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SAMAIRAH - 4

  

Simulizi : Samairah

Sehemu Ya Nne (4)



Aryan walivyofika pale walishangaa kusikia sauti za vifijo huku sauti ya mama Ashura ikisikika kwa sana walisogea taratibu na kuchungulia Aryan na Abbas wakajikuta wanafumba midomo yao kwa mshangao.


Walikuta wachawi wakicheza kwenye uwanja wa kwa mama Ashura,huku mama Ashura akiwemo na yeye, walikuwa wamejifunga rubega kaniki na vitambaa vyekundu kichwani lakini kwa chini kulikuwa na mtoto kalala na walikuwa wakiimba na kumzunguka huyo mtoto.

Aryan aliangalia vizuru waliweza kuona ni kitoto kichanga kilimwagiwa unga unga kisha mama Ashura alisema nyofoa hicho kitovu unipe nile

Mama mmoja alikashika katoto na kuvuta kitovu puuu, halafu mama mwingine alimpa mama Ashura na kusema kata haka katoto shingo

..................,.....................



Tulipo ishia jana ,, Walikuta wachawi wakicheza kwenye uwanja wa kwa mama ashura,huku mama Ashura akiwemo na yeye, walikuwa wamejifunga rubega kaniki na vitambaa vyekundu kichwani lakini kwa chini kulikuwa na mtoto kalala na walikuwa wakiimba na kuzunguka huyo mtoto.

Aryan aliangalia vizuri waliweza kuona ni kitoto kichanga kilimwagiwa unga unga kisha mama ashura alisema nyofoa hicho kitovu unipe nile

Mama mmoja alikashika katoto na kuvuta kitovu puuu, halafu mama mwingine alimpa mama Ashura na kusema kata haka katoto shingo ,

Mama mmoja alishika kale katoto kisha akakanyonga shingo ,na kumpatia mama Ashura,yote hayo walikuwa wakiyafanya huku Aryan na Abbas wakishuhudia

Baada ya kunyonga kale katoto ,wale wachawi walimwaga maunga unga yao kisha walipotea ,

"Aryan hivi ndio nimeona wachawi ama naota ,?" Abbas alimuuliza Aryan,na kumfanya Aryan amzibe mdomo na kumwomba atulie maana alijua kuwa yale mazingira si salama walizama kwenye nyumba ya akina Aryan ambayo ilichomwaga moto na akina Kudra , walimkuta Gwae kalala kajikunyata masikini, hakika alikuwa anatia huruma alikuwa kalala usingizi mzito mara anarusha rusha miguu mara mikono ,yote hayo alifanya baada ya mbu wengi kumshambulia.


"Gwae mdogo wangu amka tuondoke",Abbas alimwamsha lakini kitendo cha kumshika mkono alitaka kupiga yowe ila Abbas aliwahi na kumziba mdomo ,

Walimuamsha kisha wakatoka ili waanze safari ya kuelekea mbezi kwa akina Aryan.

Lakini walipiga hatua tatu walisikia kilio nyumba ya tatu ,Aryan aliwaomba akina Abbas wasimame ili waweze kujua nini kimetokea mbona watu wengi ,vilio vilizidi kuongezeka na kufanya watu wa majumba ya jirani waamke na kwenda kuangalia kuna nini mbona watu wanapiga mayowe usiku tena usiku wa manane.


Akina Aryan walisogea eneo hilo ,walivyoangalia vizuri walibaini kuwa kuna msiba umetokea ,mama bonge alifika na kuuliza nini shida? Ndipo mama mwingine alijibu "mama bonge si una habari kuwa mchana waleo Zuhura alijifungua mtoto? Mama bonge alijibu ndio nilisikia hizo habari mama Ashura ameniambia.


Yule mama alimwambia mama bonge kuwa Zuhura mtoto wake amefariki dunia muda si mrefu ,tena Zuhura wawatu alijifungua mtoto mzuri na mwenye afya ,unaambiwa mtaa mzima hamna mtu aliyemuona mtoto huyo kasoro mama Ashura, mchana alikuja wakati Zuhura anapelekwa hospitali kujifungua na alivyojifungua mama Ashura alimpokea mtoto na kucheka kicheko ambacho kiliwafanya manesi washangae.


Pale pale Aryan aligundua kumbe wale wachawi walivyowaona pale wanamnyonga mtoto kumbe ni mtoto wa Zuhura ,Aryan alijikuta akitikisa kichwa na kulaani sana wachawi kwa mambo yao ya kuua watoto wa watu.


Akina Aryan walifanikiwa kuondoka eneo lile na kwenda hadi mbezi mahali wanapokaa kwa sasa waligonga geti na kufunguliwa waliingia ndani ,kisha walilala.


Tukija maeneo ya sinza tunamwona bibie Jesca kaamuka asubuhi na kuingia bafuni kuswaki lakini siku hiyo mawazo yake yalikuwa yametawaliwa na Aryan ,alimuwaza sana Aryan maana anampenda kuliko maelezo ila Aryan hadi sasa hajawahi kuonesha wazi kama nae anampenda ,,Jesca alianza kuwaza mambo ambayo alishawahi kumfanyia mama yake na Aryan alivyokuwa akifanya kazi za ndani kwao ,hasa kumpiga vibao ,kumfulia nguo za ndani,


Jesca alijikuta akipiga piga kichwa chake ngumi na kujikuta analia ,alinawa uso na kuswaki alitoka safari yake moja kwa moja hadi kwa akina Samairah ,bahati nzuri alimkuta Samairah yupo nje ,

"Ooh vipi hali shoga angu" Jesca alisalimu huku akimkumbatia Samairah ,safi za kunisusa , Samairah alichombeza.


Mmmh nani akususe si unajua sasa hivi tumefunga shule hivyo kuonana inakuwa nadra ,ila Samairah mimi na shida ya kitu kimoja ,ehe shida gani Jesca? Samairah aliuliza

"Jesca alikaa kimya kwa muda kisha akaanza kueleza ,"ujue Samaira mimi sikujuaga yule mama ambae anakaa nyumbani ni mama yake na Aryan na tayari nishamfanyiaga vitendo vya ajabu mama wa watu ,alikuwa akishinda ndani akilia yote sababu yangu, muda mwinginge nilikuwa nikikuta kapakua chakula anataka kula mimi nachukua maji machafu namwagia chakula chake ,mama wawatu alishindaa njaa huku nilimdekisha nyumba mara tano kwa siku,,


Huyo mama nilishawahi kumpiga mara kibao kumuunguza moto,je nitafanyaje ili anisamehe na mimi nampenda Aryan kupita maelezo na sitaki nimkose Aryan, nisaidie please", Jesca alihitimisha na kumfanya Samairah awaze

Mimi mwenyewe Aryan nampenda ila nahofia kumwambia kuwa mimi nina asili ya kijini halafu wewe unataka nikupe ushauri mmmmh mbona mtihani ,siku zote Samairah ni mtu anaependa binadamu waishi kwa amani alimuahidi kuwa atampelekea kesho kwa Aryan ili akaombe msamaha kwa mama yake.

Jesca alifurahi kusikia hivyo kisha waliingia ndani kwa akina Samairah na kwenda kuendelea na story zingine;


Tukija maeneo ya tegeta tunawaona tena Abbas na Aryan wanaingia kwa ostadh Othumani ili wakamwombe msamaha kwa kilichotokea jana ili kama kuna njia nyingine ya kumsomea dua mama yake na Abbas apate kupona maana walihisi atakuwa katupiwa jini ,tena jini mbaya, walifika na kumkuta Othumani akifyeka majani kwenye nyumba yake walimsalimia kisha wakamwomba wakae pembeni wazungumze kidogo,

Othumani aliitika wito kisha wakatoka nje ya nyumba na kuanza kuzungumza.


Ostadh nadhani jana ulijionea jinsi huyo mama sasa hivi alivyo tunaomba msaada wako kwa mara nyingine tupate kumnusuru ,aliongea Abbas na kumfanya Othumani awaze kwa kina kisha aliwaambia hilo usijali leo nitahakikisha namaliza kila kitu ,ila kwa sasa twendeni msikitini tukatafute vijana wenye nguvu ili wakamkatate mama yenu kisha wamfunge kamba ndipo tutasoma dua kwa pamoja naimani kwa uwezo wake Allah (Mwenyezi Mungu) atapona Othumani aliongea


Hawakuwa mbali na eneo la msikiti walitembea kidogo hatimae walifika walikuta watu wapo msikitini maana walikuwa wanashiriki katika kujenga msikiti ,ostadh aliomba vijana watano nao waliitikia wito na hatimae walienda hadi kwa mama yake na Abbas.


Kwanza walifika na kukuta akichoma nguo za wanae Abbas na Gwae huku akiongea maneno ambayo yaliwafanya Abbas na Aryan wabaki midomo wazi ,"mama alianza kuongea ,wanangu nimewazaa mwenyewe japo baba yenu nilimuua ,lakini nilimuua kwa maana alikuwa akininyima uhuru sikuwa na njia nyingine zaidi ya kufanya hivyo ,nanyi nimeshiriki kuwauwa ila najua hata tukija kukutana huko mliko tangulia mtaniuliza maswali mengi ambayo sitakuwa na majibu yake .

Wakati anarusha begi lenye nguo za Gwae kwenye moto aligeuka na kumkuta mwanae akiwa na ostadh Othumani ,mama alishituka na kunyoosha mkono na kusema wewe Abbas umefufuka ama umefanyaje ,mama aliinuka kwa mshangao na kuanza kukimbia lakini vijana waliwahi na kumkamata walimfunga kamba kwenye mikono na miguu kisha walichukua mkeka wakatandika na kukaa "tahiyatu" kwa ajili ya kumsomea kisomo ama dua kama kuna jini mbaya aweze kutoka,


Ostadhi aliita pamoja na mashehe watatu akiwemo na yeye walimkalisha kati kati kisha wakamzunguka na kuanza kusoma dua , Othumani alianza kusoma dua ya kutoa majini na kujikinga na majini wabaya inaitwa "AYAT KURUSIY " waliwasha ubani mzuri uitwae ubani maka ,huu ubani waweza utumia hata nyumbani huwa unakinga na kufukuza majini wabaya ,huu ubani maalum si kana kwamba upo sawa na ubani zingine lahasha! mpenzi msomaji na msikilizaji huu ubani ukiuwasha huwa watoa majini wabaya upesi na nia njema ama kutibu husaidia endapo utatia nia na dua ambayo wataka kufanya basi dua yako lazima ifanikiwe

Basi ostadh aliwasha ule ubani

Alianza kusoma

" Allahu lailaha illa huwaalihayuu liqayumu,

Lataaqudhusinatu walaa nauumu,


Lahumafii samawati wamaafil-ardhwi,

Maandhaladhii yashifaghuu ghindahu illa miidhin,


Yaghlamu maabaina aidihimu wamaa khalfahum,

Walaayuhituna bishayiini min ghilmihi illa bimashaa a Wasigha kurusiyu samawati wal-ardhwi,


Walaa yauduhu ihdhuhuma wahuwa lighaliyu lighadhiimu.


Mwenyezi Mungu hakuna Mola ila yeye, Na ndiye mwenye uhai wa maisha,

Msimamizi wa kila jambo,


Kusinzia hakumshiki wala kulala,

Ni vyake vya peke yake vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini,"


"Na nani huyo awezae kuombea mbele ya Mwenyezi Mungu bila ya idhini yake?"


Ayajuwa yaliyo mbele yao viumbe na yaliyo nyuma yao,

Wala hao viumbe hawalijuwi lolote katika yaliyo kwenye Ilimu (elimu)yake,


Ila kwa alipendalo Mwenyezi Mungu,

Enzi yake imeenea mbinguni na ardhini,


Wala kuvilinda hivyo hakumshindi ni yeye peke yake ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu."


**** aalisoma dua hiyo ndefu huku wamemshikilia mama Abbas wamewasha na udi ,gafla mama Abbas alianza kubadilika miguu yake na kuwa kama si ya binadamu ,miguu ilibadilika na kuwa mabaka mabaka kama nyoka aina ya chatu.


Dua hiyo wakati wanasoma nyumbani kwa mama Ashura alianza kuhisi maumivu makali kwenye kichwa chake mara tumbo linamuuma mno ,mama Ashura alianza kuhaha huku akizidi kukabiliwa na kichwa alihisi kinataka kupasuka.


Huku Othumani anazidi kuisoma dua ,kule mama Ashura anazidi kupata maumivu makali ,wakati mama yake na Abbas miguu ilianza kubadilika na kuwa kama chatu ina mabaka mabaka meusi na ya njano iliyopauka,


Mama Ashura alijikuta akitoka kwake mbio na kuanza kukimbia huku akishika kichwa chake na kusema kinauma jamani kichwa kinataka kupasuka

Mama Ashura alizidi kupiga makelele huku akikimbia peku peku alichana dera lake alilolivaa na kulifanya kama mpasuko flani na kuanza kukimbia ovyo huku akisema kichwa chamuuma

Watu walijua mama Ashura kawehuka ama kawa kichaa maana alikua akikibamiza kichwa chake kwenye mashina ya miti ama ukuta alizidi kukimbia watu nao walianza kumkimbiza safari yake ilienda moja kwa moja hadi kwake na mama Abbas alifika pale na kudondoka huku akipigiza kichwa chake chini paaa paaa na kusema sirudiii tena sirudiii tena.


Mama Ashura alianza kugara gara ,huku mama Abbas nae akigara gara na kusema tumbo na kichwa chamuuma ndipo ostadh alizidi kupiga kisomo cha dua

Mama Ashura alipaza na kusema mimi niacheni niacheni mimi, nimemtupia jini mahaba sasa kwanini mnataka kuniua?

Mama Ashura alizidi kuhaha

Huku mama yake na Abbas povu zito likizidi kutoka mdomoni na huku akishikilia tumbo lake na kusema utumbo unataka kunyofoka.




Tulipo ishia jana baada mama Ashura kuzidi kupiga kelele na kujibamiza kichwa chake chini na kusema yeye ndiye alimtupia mama Abbas jini mahaba huku mama Abbas povu zito lilizidi kutoka mdomoni na kushikilia tumbo na kusema anahisi utumbo unataka kunyofoka ,.....

"Mashekhe walizidi kupiga kisomo kizito na kuzidi kuwafukuza hao majini wabaya aliorushiwa ,mama Abbas miguu yake ilichukua muda hadi ikarudi katika hali yake yote hayo yalikuwa yakiendelea Abbas na Aryan walishuhudia kwa macho yao na kuzidi kushanga "

Kisomo kiliendelea ndipo mama Ashura akaanza kuporomosha maneno ," mama Abbas nilitokea kukuchukia pasina sababu ,yote sababu nilimpenda mume wako na mume wako akanikataa mimi ,nilitumia kila njia lakini mume wako alikuwa ni mtu wa dini haswaa ,masaa yote alikuwa wakusoma masihafu ,nilivyoona nimegonga mwamba kumpata ndipo niliamua kukutumia jini ambaye alikuendesha hadi ukamuua mume wako kwa kumkorogea sumu , si wewe uliyehusika bali ni jini niliyemtuma kwako ndio alikuendesha hadi ukafanya hivyo "aliongea huku akilia na kujutia alichomfanyia mama Abbas


"Msiniuee jamani msiniuee

Ostadh alizidi kusoma dua ya kuvunja na kutoa kabisa majini wabaya kwa mama Abbas pamoja na kwa mama Ashura baada ya lisaa limoja wote wawili walikuwa kimyaaa ,hamna hata anaeongea ilibaki tu wakihema kwa kasi.


Ostadh alitoa chupa yenye mafuta ghadhwimu na kuwawekea kwenye nyuso zao huku akisoma na dua kisha alimwambia

Shehe Abbas tumemaliza kazi na sasa mama yako yuko salama

Ila kesho nitarudi kwa ajili ya kumsomea dua nyingine kwa ajili ya kinga zaidi na hata huyu rafiki yake mama Ashura najua mwashangaa kumwona hapa ,huyu kavutwa na dua ambazo tunafanya na ndiye alikuwa mshirikina alizidi kumtupia majini mama yako ili awasambaratishe ninyi ,yote anafanya hivyo kwasababu ya uzinzi alimtamani baba yako ,kibaya zaidi alikutana na baba yako kajikinga ndio kahamia kwa mama yako.


Ila kuanzia sasa mama Ashura tumewatoa majini wake wa kishirikina kuanzia sasa ni mtu mwema kabisa na hatakuwa na uwezo wa kumdhuru mtu.

Abbas alivyogeuka kumwangalia Aryan hakumwona wakati dua inasomwa hata Aryan nae alijisikia kizungu zungu ila alijikaza na kuondoka eneo hilo na kwenda kukaa mbali ndipo alisikia nafuu tambua hata Aryan kuna nguvu flani za bangili zilimwingiaga machoni hivyo mbeleni tutapata kujua zaidi.


Ostadh alimpa Abbas maji ya dua na kumwambia haya utaweza kummiminia mama yako kichwani pamoja na mama Ashura ,ostadhi na mashekhe wengine waliondoka na kumwacha Abbas pale aliendelea kumngojea mama yake hadi aamuke ,kweli ilipita nusu saa mama yake na Abbas aliamka na kukuta kafunguliwa kamba.


Alimwangalia mwanae huku akionekana kama vile kapungua uzito zaidi ya kilo tano,Abbas alimsogelea mama yake na kumuuliza mama uko salama? Mama akiwa haelewi kitu chochote alimwangalia mwanae na kumuuliza Abbas "kwani kitu gani kimetokea mbona sielewi ?"

Abbas alimwinua mama yake na kwenda nae hadi sebuleni ,mezani kulikuwa na chupa za bia nyingi huku glasi moja ilikuwa imejazwa bia ,mama alifika sebuleni na kuuliza mwanangu hizi chupa za bia za nani ? "nani anakunywa pombe ? Kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakipiga ?" Mama Abbas aliendelea kumuuliza mwanae maswali yaliyomfanya Abbas ashangae,Abbas hizi bia za nani ,mama aliendelea kumuuliza mwanae huku akionekana kushangaa sana zile chupa za bia pale mezani.


Ukweli zile bia zilikuwa ni zake lakini alivyosomewa dua na wale majini wabaya wameondoka hivyo pombe ameichukia kupita maelezo , Abbas alianza kuwaza "Ina maana mama yangu kapona? Hadi anauliza hizi bia za nani au atakuwa kapona" ,Abbas alimwambia hizi bia si zilikuwa zako unakunywa pamoja na hizi sigara?

Mama aliwaza kisha akatikisa kichwa na kusema mwanangu muogope Mungu wewe ujue utakuja kuchomwa moto ee lini mimi nimekunywa bia? Mimi sijawahi kunywa bia wala kuvuta sigara hivyo naingia chumbani nisizikute hizo bia hapo

Mama aliongea na kuingia chumbani ,hadi Abbas alishangaa kweli mama yake kapona ,alifurahi mno ,kisha alizikusanya zile bia na kutoka nazo nje moja kwa moja kulikuwa na kigrosary pale nje alimpa mhudumu na kumwambia hizi bia kama utauza sawa kama utakunywa sawa mama kasema hazitaki ,Abbas alimwambia yule mhudumu.


Yule mhudumu alimwangalia Abbas na kumwambia ole wako uniletee kesi hapa za mama yako kama umemwibia pombe zake mi sipo nachukua na naziuza maana nashida na pesa mie ,wakati huo Abbas ashaanza kuondoka ,alimwambia muhudumu we uza pesa ukipata ni za kwako ,

Wakati Abbas anafika nyumbani anamkuta Aryan nae karudi Aryan aliuliza vip mama kafanikiwa kupona ? Kabla Abbas hajamjibu aliinuka na kumkumbatia Aryan na kumwambia hadi sasa mama kanambia hata hajawahi kunywa bia wala bia hataki kuziona.


Ile wanaingia ndani walimkuta mama sebuleni katoa nguo za kiume kila aina ,kisha akamuuliza Abbas

Mwanangu umekuja narafiki yako Aryan,oooh

Aryan habari yako ? Mzima? Na mama yako hajambo?

Aryan kwanza alichelewa kujibu maana haamini kama kweli ile salamu imetoka kwa mama yake na Abbas ambae alikuwa anamchukia aliitikia kisha Mama akauliza Abbas hizi nguo za mume wangu marehemu ama za nani ? "Aryan aliangalia zile nguo na kuzibaini ni za wale wanaume ambao alikuwa anawaingiza nyumbani leo hii hakumbuki ni za nani.


Huko nje mama Ashura nae kazinduka na kujinyoosha aliuliza jamani hapa nipo wapi? ,ndipo mama Abbas alitoka nje na kumwangalia ,alimwona akipangusa mafuta ambayo yalikuwa utosini mwake ,

Mama Abbas aliita wewe si mama Ashura ama

nimekufananisha ,mama Ashura alijiangalia kisha nae akauliza ndio mimi ni mama Ashura ,

Alikumbuka kitu kisha akapiga magoti na kuanza kulia ,mama Abbas nisamehe ni ibilis alinipitia nikakurushia majini nisamehe shetani jamani shetani hiiihihihiii

Mama Abbas alimfuata na kumkumbatia kisha akamwambia yaliyopita yamepita kikubwa tumrudie muumba wetu ,na ijumaa nitakupitia mapema tupate kwenda kuswali ,.mama Ashura nae aliapa kwa mambo anayoyafanya kuanzia leo naachana nayo, ukweli mama Abbas alibadilika na kusahau vibwanga vyake vyote vya baa ,ndipo waliagana baada ya kuongea maongezi marefu.


Mama Ashura aliondoka na kwenda nyumbani alifika kwenye chumba chake ambacho anawekaga tunguli zake alikuta zikiwa zinafuka tu moshi alizitia kwenye kiroba na kwenda nyuma ya nyumba alizifukia na kwenda kwenye begi lake alitoa kitabu kimoja cha Qur'an na kuanza kukifungua ,ndipo alipokumbuka alikuwaga ni ostadhati mzuri aliongoza chuo cha kiislamu cha pale msikiti wa kati na alikuwa akiwafundisha madrasa wabint wadogo,yote aliyarudia akasema kuanzia leo nakuwa mama Ashura wazamani asante Mungu sitaki tena uchawi wala ushirikina nakurudia kukuabudu ewe muumba wangu.


Alifungua kabati lake alichukua mtandio na kujitanda usoni kufunika nywele zake ,hakika mama Ashura alipendezea ushungi ;

Tukirudi katika upande wa pili mama Abbas alimuuliza mwanae Gwae wangu yuko wapi, Abbas wala hakuwa na haja kumficha alimweleza yupo kwa akina Aryan mbezi mahali walikohamiaga nyumba mpya.


Pale ndipo mama Abbas alianza kukumbuka matukio aliyoyafanya nyuma kutembea na wanaume zaidi ya watano kwa siku kukesha baa ,kuwatesa watoto ,aliondoka kimya kimya na kuingia chumbani mwake ,


Akina Abbas na Aryan nao waliondoka kuelekea mbezi kumchukua Gwae nakumlete nyumbani lakini ile wanafika tegeta nyuki walimwona Samairah akishuka kwenye daladala akiwa na Gwae ,ilibidi wasimame kwanza.

Samairah aliwaona na kuwaita Aryan mambo nimewamiss mjue ,alitembea haraka haraka akiwa kamshika Gwae mkono hatimae alifika mahali waliko akina Aryan

Alimwangalia Aryan na kumuuliza vip mmemaliza dua?

Aryan aliguna ilibidi aulize swali kwa Samairah dua? Dua gani hio Samairah ,

"Samairah akacheka na kusema naelewa mbona, Samairah alikuwa na uwezo wa ajabu vitu wanavyofanya akina Abbas na Aryan vyote alikuwa anavitambua "okay tuachane nayo lakini mama yake Abbas si karudi katika hali yake?


Maswali ya Samairah yalifanya Aryan aanze kurudi nyuma taratibu ,huku moyoni akiwaza Samairah kajuaje kama tumeenda kwenye dua ,na nani kamwambia kama walienda kwa mama yake na Abbas ,pale Aryan alipata wasi wasi maana hawakumwambia mtu yeyote zaidi yao sasa ugumu unakuja Samairah kajuaje haya yote.


Samairah alimwangalia Aryan na kumwona ana wasi wasi mkubwa nae alitabasamu na kusema najua bana ila ondoa shaka

Twendeni nyumbani kwa mama Abbas leo nikamwone ,

Mara Hwae alidakia na kuita aunt ulivyokuwa nyumbani ujue niliona miguu yako kama ina kwato kama zile za kwenye movie tunazozionaga za farasi ama pundamili.....


Kabla Gwae hajaendelea kuongea jambo jingine Samairah aliwahi na kumfunika mdomo ,kisha akawaza kwa undani ina maana huyu mtoto aliniona ?

Kisha akamwangalia Aryan na kuendelea kuwaza kimoyo moyo, we Aryan nakupenda ila uwe unaniambia kama unaenda kufanya dua maana ipo siku utaja sababisha nigundulike kwa watu.


Aryan alizidi kumwangalia Samairah na kuishiwa nguvu lakini Samairah alinyosha mkono wake ili amshike Aryan bega lakini kunakitu ambacho Aryan alikiona, alikodoa macho kwa mshangao huku akihisi mwili wake kukosa nguvu

Alijikuta taratibu anafumba macho na kutaka kukimbia...



Tulipoishia jana baada Samairah kupeleka mkono ili amshike bega Aryan ili waondoke ,kuna kitu ambacho Aryan alikiona na kujikuta akifumba macho na kukosa kipi afanye kwa wakati ule ,


Aryan kwa mara nyingine aliitoa mikono yake taratibu na kuanza kuangalia huku akijiuliza ,ni kweli ni yeye? Sauti ya mtu ambae akimkokota baba mmoja kakaa katika baiskeli za walemavu ,

Jamani msaada ,msaaada jamani yule mkokotaji ndio alikua akiongea ndipo Aryan alivyotupa jicho alikutana na yule mkandarasi ambae alitaka kumtoa kafara ,wakati akifanya kazi ya ujenzi moja ya gorofa lilikopo mbezi ,


Leo hii Aryan anamshuhudia yule mkandarasi kwanza alikuwa amekonda huku nguo zake kuonekana chafu na zimefubaa mno ,,mkandarasi àlikuwa hana mikono wala miguu yote ilikuwa imekatwa ,ndipo Aryan alirudisha kumbu kumbu zake na kukumbuka jinsi lile gorofa lilivyo mdondokeaga huyu mkandarasi na yeye alikumbuka jinsi alivyomrushia kwenye nyaya za umeme ili apigwe shoti afe ili mkandarasi aweze kupata tenda nyingi katika kazi zake za ukandarasi,


Leo hii kawa omba omba yote hayo yalikuwa mawazo ambayo akiyawaza Aryan

"We Aryan unashangaa nini?" Samairah aliuliza ,"unashangaa kilema huyu?" Mogy alitikisa kichwa kuashiria ndio anamshangaa ,Samairah alicheka na kusema huyu baba namjua vizuri alikuwa mkandarasi halafu niwaambie kitu ,Aryan na Abbas

Aliwashika mikono na kuwa nong'oneza huyu ni kaka yake na Kudra ,usimwone kachakaa hivi baba yake tajiri ,Samairah aliongea na kumfanya Aryan na Kudra wakumbuke hata Joshua aliwaambia kuwa ana kaka yao ni mkandarasi lakini kwa sasa ni kilema ,leo hii wakaambiwa mkandarasi ndio kaka yake na Kudra.


Gwae alimwambia Samairah ,aunt mpe huyu baba msaada si unaona hana mikono eee ,Samairah alitabasamu na kumwambia Gwae asante nawe usije lipiza ubaya kwa wabaya wako waliokutendea ubaya ,Samairah aliingiza mkono kwenye pochi alitoa noti ya shilingi elfu kumi na kumuwekea kwenye kikombe huyo makandarasi.


Ile Samairah anampa mkandarasi hela ndipo mkandarasi nae aliinua kichwa chake na kumwona Aryan ,alitaka kuruka kwenye kibaiskeli ila hakuwa na uwezo maana hakuwa na mikono ,Aryan alimwambia yule anae mkokota mkandarasi wasogee pembeni aweze kujua nini hatima yake ,mkandarasi japo alikuwa anamwogopa Aryan akijua huenda anaweza kumpiga ama kumjeruhi hasa akivuta kumbu kumbu jinsi alivyotaka kumpigisha shoti ya umeme hadi afe ,mkandarasi alijikuta akichanganyikiwa kisawa

Sawa ,kwakuwa hana mikono na miguu hakuwa na namna tu.


Aryan alimvuta mkandarasi hadi pembeni kisha akachuchumaa na kumwangalia mkandarasi machoni,mkandarasi alikosa cha kufanya na kujikuta machozi yakimbubujika ,kibaya zaidi hana mikono huenda angeyapangusa yale machozi yanayo mtoka wakati akilia na kujutia alichokuwa anakifanya nyuma angali mzima,

"Siku zote Aryan ni mtu wa kutangaza amani na anapenda kuishi na watu vyema, alimwonea huruma kisha alitoa kitambaa chake kipya alikuwa kisha akamfuta mkandarasi machozi huku akiongea maneno mazito


"Najua unahofu na mimi labda wahofia nitakupiga ama kukuua hapana mimi siko hivyo hata kidogo ,ila nakupa pole kwa wakati huu mgumu unaoupitia ,hebu kumbuka ulikuwa na kitambi kipindi wajenga magorofa yako leo hii umekuwa kimbau mbau ,umekondeana wakati wewe bado kijana ila waonekana mzee ,

Wakati huo maneno Aryan anaongea ,mkandarasi alizidi kuangua kilio kisawa sawa na kufanya watu wakusanyike ili kujua huyo kilema anatatizo gani ,pale pale nyuma ya stendi ya tegeta nyuki.


Aryan aliendelea ,natamani ningekuwa na uwezo nikuwekee viungo vyako utembee ujionee mengi ,hii dunia ni duara kila siku tunaambia ,uliwaua wavuja jasho kwenye gorofa yote sababu ya kutaka utajiri na kupata tenda nyingi za ujenzi ,sitaki kujua toka umeanza ujenzi wako umeua wafanya kazi wangapi ,hilo unalijua mwenyewe na roho yako , ila tambua roho ya mwanadamu huwa inakisasi ,ukiua mtu na ukagusa damu yake lazima nawe yatakukuta kama yalivyowakuta wao,


Ndipo pale mkandarasi alianza kuongea ,"nimejifunza leo na kesho natamani miguu yangu na mikono ingekuwepo nitembee niuambie ulimwengu kuwa roho ya binadamu mwenzie ni mbaya mtu asije kuthubutu kumuua mwanadamu ili apate mali nimejifunza" mkandarasi aliongea huku akitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa.


Alimwangalia kijana Aryan kisha akamwambia ,usiniambie sana nimejifunza ,kila nilalapo roho za wafuu ,watu niliowatoa kafara zinanitesa usiku kwenye njozi ,mateso ninayopata siwezi simulia ni mabaya mno ,

Wafu wananinyonga usiku,muda mwingine hadi nakufa kabisa lakini wananirudishia pumzi yangu na kunifanya niendelee kuishi ,

Najiwa na viumbe waajabu mimi ,nachomwa kisu naona kabisa mchana kweupe naugulia machungu masaa matatu lakini machungu yanaisha na kujikuta nipo kama awalii lakini siwezi jilaumu katika familia yetu tumepewa laana mbaya hadi kufa kwetu hivyo wacha niendelee na safari yangu atakae nisaidia anisaidie kama hamna nae aniache.


Sukuma baiskeli twende ,"mkandarasi alimwambia kijana ambae anamsaidia kusukuma hiyo baiskeli waondoke zao ,Aryan alitingisha kichwa kisha akataka kuondoka lakini aliangalia.


Lakini katika ile baiskeli kuna chuma kilikuwa kimekaa karibu na mdomo ili akiwekewa hata chakula ale lakini Aryan aliona kuna unga na hakuweza kuutambua ule unga ni wa nini.


Mkandarasi alimwangalia Aryan kisha akamwambia sogea ni kuambie Aryan alisogeza macho karibu na lile chuma ambalo lina unga ,mkandarasi aliwaza haraka haraka.


Wewe mpumbavu ndio ulinusurika kufa na kunifanya mimi niwe kilema nimezunguka hii dar nzima nikikutafuta nawe nikusababishie ulemavu wa kudumu kama mimi ,

Mimi sasa hivi si mtu wakuishi najua nitakufa kwa madhabi yangu niliyofanya na nitaendelea kufanya hadi kufa kwangu

Aliwaza na wewe kuanzia leo utakuwa kilema kama mimi.


Wakati Aryan hajui chochote anachowaza mkandarasi alimwambia asogeze uso aweze kumwomba msamaha ,Aryan nae alifanya vile alivyoambiwa na mkandarasi

Ki ukweli mkandarasi japo ni kilema hana miguu yote wala mikono lakini bado alikuwa gaidi mno ,


Alichokifanya alimpulizia Aryan ule unga ambao ulikuwa wa bluu na kuonesha kama kuna vimadini vidogo vidogo vikimeremeta , ule unga uliingia machoni mwa Aryan ,kisha mkandarasi alitabasamu na kujiwazia kuanzia leo utakuwa kipofu ,

Kisha yule kijana ambae alikuwa anasukuma kile kibaiskeli alimsukumizia Aryan kile kikombe ambacho watu walikuwa wakitoa msaada wa pesa


Halafu mkandarasi alisema mwiziii jamani mwizi ananiibia mimi japo nikilema ,watu walikuja upesi wakati huo Aryan anahisi macho yake yanawasha kwa uchungu mno alianza kuyapikicha kwa nguvu huku machozi yakimtoka ,watu walianza kumpiga Aryan na nondo,mbao,kuni hakika Aryan huruma yake ilimponza leo hii kageuziwa kibao kuwa ni mwizi,

Alizidi kupewa kipigo haswaa

Aryan alianza kutaka kujitetea wakati huo mkandarasi ndio anasukumwa na kuzidi kutoweka,


Machoni kawekewa sumu ambayo inaenda kuua kiini cha jicho na inafanya kazi dakika moja ,wakati Aryan akiendelea kupigwa kwa nguvu watu wanamrushia mawe na kusema mwizi ,Aryan macho yake yalikuwa hayaoni hata kidogo,


Alijaribu kuita akina Samairah na Abbas lakini walikuwa tayari washatangulia nyumbani kwa mama Abbas,Aryan akiwa hoi mwili mzima umetapakaa damu

Mara kuna gari ilikuja na kupaki pembeni walishuka watu upesi na kusema mwacheni mwacheni msimuue sisi tunaenda kumshughulikia,

Kwa kuwa Aryan alikuwa haoni alijua labda polisi wamekuja kutoa msaada lakini alivyosikia mu-bebeni huyu bwege pakieni kwenye gari tumpeleke masikani kwa kazi ya kumzika akiwa hai.


Ile sauti Aryan aliielewa ni ya Kudra ,mara Mussa alimtandika teke la kwenye taya ,Aryan akajikuta taya la juu na yachini zinapishana

Mussa alisema leo tumekunasa wewe nyumbu ,wakati huo Aryan kapigwa kipigo cha mwizi na vile vile mkandarasi kampa upofu ,sasa yupo mikononi mwa wabaya wake na wanasema wanaenda kumzika mzima mzima.


Hana msaada tena akina mudy na Samairah washatangulia nyumbani



Tulipoishia jana baada yaAryan,kupigwa teke na Mussa kisha wakajipongeza ama kufurahia kumpata Aryan ",we boya afadhali leo tumekunasa kwanza ",waliwaambia raia wasimpige wao wataenda kumshughulikia ,gari ilisogezwa vizuri Aryan alipakiwa kwenye buti ya gari tena kama mzoga vile ,Aryan akiwa anavuja damu, akawa anaita Samaira ,Abbas,mama njooni mniokoe nipo katika mikono ya watu wabaya ,Aryan ndani ya buti ya gari aliendelea kulia na kuichukia huruma yake maana ndio iliyomponza ,alimwonea huruma sana mkandarasi kukosa mikono na miguu ,lakini kumbe mkandarasi bado anakisasi nae leo hii amemtia upofu ,


Ule unga ulikuwa ni sumu mbaya sana uliingia machoni mwa Aryan dakika chache tu alikuwa haoni , akiwa ndani ya buti ya gari aliomba dua za kila aina ,huku akisikia jinsi tairi za gari zikizunguka kwa kasi aligundua yawezekana gari ipo mwendo sana ,alitulia maana hata nguvu za kujitetea wala hakuwa nazo tena ,kipigo alichopigwa kilikuwa cha aina yake,


Huku ndani ya gari Mussa na Kudra pamoja na Issa nae alikuwepo walizidi kujipongeza kumnasa Aryan na wakisema leo ndio mwisho wake ,,walimpeleka hadi maeneo ya bweni ,na kumshusha kwenye nyumba moja ambayo ilionekanika ni ya kifahari

Walimrusha chini kama gunia , hawakujali kama anaweza kuumia au laa ,wao walimrusha chini , walimsogeza hadi kwenye kivuli kwa kumburuza kama gogo ,Aryan alijikuta ngozi yake ikichubuka ,


Kudra alimsogelea machoni na kumwangalia hakika alizidi kucheka kwa nguvu ,baada ya kuona macho ya Aryan yanaanza kumeguka meguka mboni ,vijinyama nyama vinatoka ,

"Khaaa Mussa njoo mcheki huyu zobozo macho yake yanavyoharibika vibaya kumbe kawekewa ile sumu ambayo nilikuambia siku tukimpata tumwekee maana ile inatengeneza upofu kwa haraka.

Kudra aliongea na Mussa kuuliza sasa ni nani ka mwekea hio sumu? ,


Ki ukweli wakati mkandarasi anamuwekea sumu Aryan na kuondoka walipishana na akina Kudra wala hawakuonana ,hivyo hawakujua kama kaka yake na Kudra ndio kafanya lile tukio

Kudra aliagiza tena ile sumu apewe na Issa alimletea upesi na kuweka tena machoni mwa macho ya Aryan,macho ndipo yalizidi kuharibika kumeguka vijinyama ,huku Aryan akilia kwa uchungu ,


Katika nyumba ile ambayo yupo Aryan alikuwepo mama yake na Aryan ambae nae alikuwa katekwa na Jesca na aliingizwa ndani

" we mama nimekuambia unisamehe yale makosa yote niliyokufanyia kwetu na umwambie mwanao Aryan anipende mimi kama mimi ninavyompenda ,unanisikia?" Masikini mama wawatu alifugwa kamba huku akipigwa na kuambiwa atoe msamaha na amwambie mwanae ampende Jesca ,mama alizidi kuchezea kichapo ,lakini kauli yake ilikuwa ni ile ile " Jesca upendo si wa kulazimisha ila wewe ni mbaya toka rohoni siwezi kukusamehe pia mwanangu hawezi kukupenda mwanaharamu kama wewe ," nipigeni mniue ila mwanangu naomba mwacheni asome kiasi anachotaka yeye mama alisema "


Ndipo Kudra aliingia na kumfungulia mama yake na Aryan kisha akamwambia Jesca yule bwege tumemkamata yupo pale nje sijui aliiba maana tulikuta anapigwa na watu ndipo tukamchukua ,Jesca alivyosikia Aryan yupo nje aliachia kisu ambacho alikuwa anamtishia mama yake na Aryan kumchoma tumboni ,alifanikiwa kutoka nje na kumwona Aryan ,mwili wake ukiwa umetapakaa damu


Jesca aliwangalia alivyomchunguza macho ndipo alibaini kuwa Aryan haoni tena ,Jesca aliumia maana alikuwa anampenda mno lakini alivyoona macho yanavyozidi kuharibika alisema Aryan basi tena kwa uzuri wangu siwezi kumpenda kipofu inabidi uzikwe tu ukiwa mzima nisiendelee kukuona tu kwenye hii dunia ,

Mama yake na Aryan alitolewa nje nakufanikiwa kumwona mwanae akiwa katapakaa damu mwili mzima alivyochungulia macho ya mwanae ndipo alizidisha kilio na kuita Aryan ,Aryan mwanangu ,hapo ndipo Aryan aliisikia sauti ya mama yake alinyoosha mkono ili amshike mama yake mkono wake kwa mara ya mwisho ,mama alinyoosha mikono yake na kumshika mwanae akiwa analia kwa uchungu akiwaangalia akina Mussa na Kudra walikuwa hawana hata shida walikuwa wanacheka.


Jesca nae aliumia sana alisimama na kumwambia Mussa na Kudra mmefanya nini sasa kumharibu Aryan macho ,ni bora tungemtesa mama yake yeye akabaki tu ,ila isiwe kesi naomba mmfukie akiwa hai nisiweze kumwona katika maisha yangu ,

Kudra aliita vijana wake wakiwa wanaongozwa na Issa kwanza walimshika mama yake na Aryan walimvuta na kumshika mikono,Aryan alibebwa juu juu na kuzungushwa nyuma ya nyumba palikuwa na shimo ambalo tayari lishaandaliwa Aryan alirushiwa na kwenda kujibamiza kama gogo puu, tambua haoni na mwili wake umepigwa mno.


Kudra aliwaagiza kundi lake wamfukie Aryan akiwa hai walianza kurusha udongo bila shaka huku mama yake na Aryan akishuhudia mwanae akizikwa akiwa hai ,hakika ilikuwa inauma mno alilia mama wawatu hadi sauti ikakauka ,,kwa nje walisikia geti likigogwa na Mussa alikimbia na kwenda kufungua wakati huo Aryan udongo unaendelea kurushwa ile Mussa anafungua geti alishikwa shati na binti wa kike kisha akazama nae ndani huku kijana mwingine akaingia na kufunga hilo geti ,


Mussa jinsi alivyoshikwa alijaribu kujinasua lakini yule binti alikuwa kamshikilia kwa nguvu sana ,Mussa aliita Samairah na wewe pia umejileta ,

Kumbe walikuwa akina Abbas na Samairah hatimae wameingia ndani kutoa msaada kwa Aryan ,Kudra alivyomuona Samairah nae alikuwa anampendaga aliwaamuru vijana wake waache kumfukia Aryan waje wamkamate Samairah ili ambake mchana kweupe pee ,vijana waliacha na kumshika Samairah ki ukweli siku hio Samaira alikuwa watofauti alikuwa akishika mtu mkono ama shati hawezi kumtoa mkono wake.


Samairah akiwa amemkaba Mussa hatimae mama yake na Aryan aliweza kuona ile bangili ambayo yeye alishawai kumpa Samairah kipindi anaondoka kwa akina Jesca ,leo hii mama anaiona ile bangili ikiwa ipo mkononi kwa Samairah ,wakati huo Abbas amekimbia na kwenda kumwinua mama yake na Aryan chini.


Mama vip upo salama? Abbas aliuliza huku akimwinua wakati huo Samairah bado kamshikilia shati Mussa . ,Mussa kila akijaribu kujinasua kwa Samairah alishidwa na kujikuta shati lake likichanika tu, Kudra alichukua kisu na kuanza kumfata Samairah kwa lengo la kumchoma ama kumjeruhi lakini ile anapiga hatua Samaira alimwangalia Kudra maeneo ya tumboni ,pale pale Kudra hata hakusogea hatua nyingi alihisi tumbo linauma tena maumivu yasiyo eleweka japo yeye huwa anajiona mbabe ila kwa maumivu ya tumbo aliyoyapata akajikuta ananywea chini na kushikilia tumbo lake huku akiita watu waje wamsaidie ,jamaan tumbooo ,oooh tumbo ,ni malalamiko aliyoyatoa Kudra na kujikuta akigara gara chini ,kama mtoto


Samairah alimwachia Mussa ,Mussa nae alijikuta anakuwa mpole yaani kama vile mtu punguani asie na akili timamu ,Mussa akawa wakuitika itika ovyo huku akimwogopa sana Samairah.


Samairah alianza kupiga hatua kuelekea kwenye lile shimo ambalo Aryan alianza kufukiwa ,wakati akipiga hatua na mkononi kavaa ile bangili ,ile miale ya lile bangili ilianza kuonekanika machoni mwa Aryan , macho yalikuwa yameharibika na kuurojeka hapakuwa na mboni tena zaidi ya utepe utepe mweusi ,ule unga ulikuwa ni sumu mbaya yaani ukiguswa na maji halafu ukaweka kwenye ngozi,basi ngozi yako itaanza kukatika katika ovyo.


Ndipo macho ya Aryan yalivyoorojeka na kumfanya Aryan kupitia maumivu makali mno na kukata tamaa kabisa ya maisha nakujiona safari yake ya kifo imekaribia ,lakini kadri Samairah anavyosogea kwenye lile shimo ndipo macho ya Aryan yanaanza kurudi kama mwanzo.


Aryan alianza kuona rangi za bluu na kijana kwenye mboni zake,zile rangi ndio zipo kwenye ile bangili aliyoivaa Samairah,,,,,

Mpenzi msikilizaji naomba nikurudishe nyuma kwenye vipande vilivyopita ,tunakumbuka siku mama yake Samaira alivyoishikaga ile bangili ilipogusana na pete ambayo alikuwa ameivaa ndipo kuna mwanga ulitoka wa blue ukiambatana na wa kijani uliingiaga mwachoni mwa Aryan na kumfanya akapoteza fahamu.


Leo hii Aryan anaanza kuona ile miale ,ndipo Samairah alivyofika kwenye lile shimo alimwona Aryan akiwa kajaa udongo , Aryan alifumbua macho yake na kujikuta anaona vizuri sana ,Samairah alinyoosha mkono ishara ya kumsaidia ,ili amtoe kwenye shimo ,Aryan nae aliinua mkono wake taratibu alianza kuvutwa kwenye shimo na bibie Samairah ,


Ki ukweli hapo Aryan hakuamini kabisa macho yake kama yanaona tena ,Aryan alizidi kumwangalia Samairah usoni ambapo Samairah muda wote alikuwa akitabasamu tu ,pale ndipo Aryan aligundua Samairah ni mrembo sana


Samairah alimwangalia Aryan ambae mwili wake ulikuwa na damu ,"Samairah alianza kuwaza ,naweza kuyafuta hayo majeraha na Aryan akabaki kama alivyo awali ila nahofia Aryan ataniogopa na atanitenga nami sitaki kitu hicho kitokee hivyo hakuyafuta majereha ya Aryan.


Aryan alitoka kwenye shimo na kujikuta akimkumbatia Samairah kwa nguvu ishara ya shukrani kwa msaada wake ,ndipo Aryan alivyogeuza macho alimwona mama yake akija mbio huku akisema mwanangu uko salama?

Aryan alivyoangalia alimwona pia Abbas nae alikuwa anakuja ,Aryan alimwachia Samairah kisha akamkumbatia mama yake ,

Mama alimwangalia mwanae machoni na kumuuliza "eti kwa sasa unaona? Ndio naona mama, Aryan alijibu ,mama alishangaa maana alivyoona macho ya Aryan yalivyoharibika alishangaa mno leo hii anaona vizuri tu.

.

Mara Jesca nae alikuja na kumkumbatia Aryan ,huku akionekana mapepe mno ,"Aryan wangu mzima haaa nilijua ushakuwa kipofu ,alimkumbatia kumwambia Aryan nakupenda hata mama yako ameridhia niwe nawe na si huyu Samairah kwanza wanawake weupe wabaya kitu maji ya kunde nakuambia utaona utamu wake ,achana na weupe wa Samairah mimi nakupenda Aryan ,

Hakika maneno ya Jesca yalimfanya mama yake na Aryan agune na kuwaza moyoni mwake utalazimishaje mtu akupende ,mama alitikisa kichwa na kusemea nakuchukia sana Jesca ila mungu anisamehe kwa kukuchukia ulitoa amri mwanangu azikwe angali mzima kwakuwa alikuwa kipofu ili usimwone tena sasa imekuweje?


Aryan nae alianza kuwaza,Jesca ulitoa wazo nifukiwe kwenye kaburi nikiwa mzima maana nishakuwa kipofu nimetoka na naona sasa wasema wanipenda Aryan aliguna kidogo mmmh.

Pale bibie Jesca anaupeleka mdomo wake ili wagusanishe lipsi zao na Aryan,mtoto kaweka lipstick kwenye lipsi zake na alivyo nalipsi nyembamba za kuvutia alihitaji apate denda kwa Aryan.


Lakini Samairah hakutaka kushuhudia kile kitendo alifumba macho ,pale pale Aryan alimsukuma Jesca na kumwambia we Jesca achana na mimi.

Ndipo Aryan alipo angalia vizuri alimwona Kudra kainuka chini ,alikuwa akiinuka kwa tabu na mkononi alikuwa kashika bastola

Alijikaza na kuwanyooshea akina Aryan ,Samairah mama Aryan pamoja na Abbas,,

Kudra akiwa hoi tumbo lilizidi kumkata kwa maumivu nae alijikakamua kwa ubishi aliwanyooshea bastola hasa hasa Aryan aliweka kidole kwenye sehemu ya kubinya ili risasi itoke amtandike Aryan hakutaka tena kumwona akiwa hai,

Aryan aliwahi na kumkinga mama yake ili kama kufa afe yeye mama abaki.


Lakini mama Aryan nae alisema mwanangu acha mimi aniue wewe ubaki wakawa wanagombania nani apigwe risasi mwingine abaki ,

Kudra aling'ata meno kwa uchungu ama maumivu ya tumbo anayoyapata na kuifyatua risasi,,

Wakati huo mama Aryan kamkumbatia mwane asife ,ili risasi impige yeye na tayari risasi ishaachiwa na Kudra kafyatua ile risasi ,na kusema safari njema kuzimu halali yako.


Lakini tayari mama Aryan alikuwa kumkinga mwanae ili asipigwe risasi sasa akawa amemgeuzia mgongo Kudra na tayari akafyatua risasi.


Aryan akajikuta anafumba macho na kusema mama hapaaanaaaaaaa!!!!!!!!



Tulipo ishia jana ,wakati mama na mwanae wanagombania nani amkinge mwenzie ,Aryan hataki mama yake aingie katika matatizo ama kupoteza maisha huku ,mama hataki mtoto wake afe anaona bora yeye apigwe risasi na si Aryan

Wakati wanagombana Kudra alifanikiwa kujikakamua japo tumbo lilikuwa linamuuma alifanikiwa kufyatua risasi ,wakati risasi inakuja kwa kasi Aryan aliiona ,na mama yake ndio alikuwa amemkinga mwanae asipatwe na ile risasi.


Lakini ile risasi Aryan aliiona, cha ajabu hawakujua mahali imepotelea na ilikuwa inaenda kumpiga mama yake maeneo ya mgongoni, kitu kilichomfanya hata Mussa na Kudra wabaki wameduwa.

Halafu Samairah alitabasamu na kumkonyeza Jesca ,ki ukweli ile risasi Samairah aliipoteza kwa kupitia uwezo wake ,aliiangalia ile risasi na macho yake yanauwezo wa kuvuta kitu chochote cha kumdhuru mtu anakifuta kabisa ,ina maana ile risasi iliishia kwenye macho yake lakini yeye hakudhurika ila tu vitone vidogo vya machozi ndio vilitoka tu,


Samaira alimwangalia tena Kudra maeneo ya tumboni tena ,ndipo Kudra alilegea mwili wote na asijue nini chanzo ,akina Mussa waliwahi kwa Kudra na kwenda kumuamusha baada ya kuona kalegea,

Wakati huo akina Aryan Jesca na Samairah bila kuwasahau akina Abbas na mama yake na Aryan ndio walikuwa wanaondoka taratibu kwenda nyumbani japo liliwafanya kundi la Kudra wasiweze kuelewa chochote ,wakati wanaelekea nyumbani basi Jesca alikuwa kimbele mbele mara amshike mkono Aryan mara amshike mama yake na Aryan ki ukweli alikwa anawakera sana akina Aryan ila ndio hivyo Aryan hupenda amani ndio maana alishidwa kumwambia ukweli.


Jesca alianza kuongea " mama Aryan kiukweli nilikutesa ila nisamehe yote hayo niliyafanya sikujua kwamba wewe ndio mzaa handsome Aryan ujue mama nakupenda ee ,Jesca alimkumbatia mama yake na Aryan ,yote hayo anayafanya ili kumshawishi mama yake na Aryan amsamehe makosa yote aliyoyafanya nyuma.


Mama Aryan alimshika mkono Samairah kisha akamwambia Samairah mie nakupenda ila ingependeza kama mwanangu akimaliza shule akuo.... kabla hajamaliza Aryan alidakia na kumwambia mama kuoa tena subiri bana ,nikifika muda wa kuoa nitachagua nimpendae

Basi Jesca kusikia hivyo alidakia na kusema si utanioa mimi ee,hapo Aryan aliona kama wanamkera wakati huo washafika maeneo ya kibo complex ,Aryan aliomba ashuke walau akapate maji ya kunywa maana alikuwa anasikia kiu mno,alishuka na kuvuka barabara upande wa pili alinunua maji lakini watu walimwangalia sana maana nguo zake zilionekana zimechafuka na udongo mbaya halafu mwili wake ukiwa na majeraha ,basi kila mtu alisema lake kila alipo mwangalia Aryan.


Wapo walisema huyu labda walikuwa wanapigana na wengine walisema labda kapigwa na vibaka ,basi Aryan alinunua maji akanywa, pia alirudi na kupanda kwenye gari maana Samairah alikodi gari .

Aryan alianza kumuuliza maswali Jesca

"Jesca kwanini ulimteka mama yangu na kwenda kumtesa huko " Jesca alifikiria na kukosa jibu alimwangalia mama yake na Aryan na kukumbuka alivyompeleka kule kumtesa alimpiga tena makofi na kumlazimisha amsamehe.


Jesca alizidi kuchanganyikiwa na akakumbuka ule ushauri aliupewa na akina Mussa akamteke mama yake na Aryan amtese hadi aseme ametoa msamaha ,pale ndio Jesca akagundua kuwa Mussa huwa anamtaka kimapenzi ila yeye hampendi ,hivyo Musa alitumia njia ya kuzidi kumfanya Jesca achukiwe na mama yake na Aryan ili ampende yeye .


Pale pale alianza kulia na kuomba msamaha na kuwaeleza kuwa hayo mawazo alipewa na Mussa ,Abbas aliwaza na

Wakati huo Abbas alishuka maeneo ya kibaoni na kwenda zake huku akina Samairah ,Aryan,Jesca na mama yake na Aryan waliendelea na safari. Jesca aliendelea kulia na kusema nisamehe huku moyoni anajisemea ,mwenyewe moyoni "utapewaje mawaza na mtu ",


Jesca aliongea kwa hasira"Kama Aryan unampenda Samairah na hunipendi mimi nitahakikisha huyu Samairah nampoteza ili unipende mimi bora nigaramie pesa ili unipende mimi sina kingine alimwambia dereva simamisha gari aliteremka kwenye gari akiwa na hasira na kuchukua boda boda kuelekea kwao.


Mama Aryan alimuuliza mwanae ,hivi utakubali mtu akulazimishe umpende?, Aryan hakujibu ndo kwanza aliangalia majeraha yake aliyopigwa kisa mkandarasi kamsingizia kuwa yeye ni mwizi alijiangalia na kufanya kuwakumbuka akina Kudra jinsi wanavyo yaandama sana maisha yake ,Aryan akajikuta anakosa raha ,vile kumbukumbu za ukaribu wake na bibi ambae tayari ameshatangulia mbele ya haki ,kiukweli Aryan bado alitamani aendeleee kuwa karibu nae.


Aryan aliendelea kukumbuka maneno ambayo bibi alikuwa akimwambiaga kuwa "binadamu akiamua kuyaandama maisha yako hata ufanye wema kiasi gani bado ataendelea kukutesa" yote hayo Aryan alikuwa akiyakumbuka na kujisemea bibi tulijuana juu juu kwa huruma yangu nikaamua kubeba jukumu la kuhakikisha unaishi maisha yenye ahueni lakini alipangalo mungu kamwe mwanadamu hawezi tia kipingamizi.


Hatimae walifika mbezi walishuka na kuingia nyumbani na kumwacha Samairah akielekea kwake , ,Aryanalifika nyumbani na kuoga vizuri kisha akavaa nguo zingine safi ili akatafute dawa za kupunguza maumivu Aryan aliwaza aende moja kwa moja hadi maeneo ya mwenge ili akatafute dawa kisha akamnunulie na mama viatu ,


Tukirudi maeneo ya bweni ,baada ya akina Mussa na Kudra kuachwa na akina Aryan ,Kudra alishangaa tumbo lake limepona tena baada ya dakika tano ,pia kumbu kumbu za Mussa zilirudi maana nae alivyoshikwa shati alijikuta anakuwa kama zezeta flani ,waliungana tena na kuchukua gari lakini walivyowafuatilia akina Samairah na Aryan hawakufanikiwa kuwaona tena .

Hivyo iliwalazimu kila mmoja aende kwao ,


Tukija maeneo ya mwenge tuna mwona Samairah akiwa kapanda bajaji lakini kwa nyuma alikuwa anafuatiliwa na Jesca tena akiwa nyuma yake wakati huo Samairah hana hata habari kama kuna mtu anamfuatilia ,

Walifika mwenge pale kwenye mataa wanapaita makutano ya bara bara wakati huo Aryan nae yupo maeneo yale ya pale pale mwenge, kuna kilema alikuwa anakokotwa barabarani ili avushwe upande wa pili ,lakini gafla yule ambae alikuwa akimsukuma kilema kwenye kibaiskeli kuna mdudu aliingia machoni na kufanya asione ,alikumbatia macho yake ili kumtoa yule mdudu kwenye jicho,


Lakini walikuwa katika eneo hatari mno ,kuna lori kubwa lilifeli breck kwenye mataa na kujikuta likikimbia spidi ya juu kuelekea aliko yule kilema ambae alikuwa kavalia sweta kubwa na alifunika kichwa chake na kofia hivyo Aryan hakufanikiwa kumjua ni nani.


Lile lory lilikuwa linaenda kumgonga yule kilema ,kila raia aliyekuwepo maeneo hayo alifumba macho wengine masikio ili wasiweze kushuhudia jinsi kilema yule anagongwa na lile lory ,sauti za mshangao zilirindima maeneo ya mwenge kila mmoja alisema jamaniii yule mwenye lori anakwenda kumgonga yule kilema masikini !!!


Lakini Aryan alikuwa karibu na eneo hilo ,alichokifanya aliruka na kuishika ile baiskeli ya kilema na kuivuta kwa nyuma pale pale lori likapita mahali alipokuwa kilema lakini tayari alikuwa kaokolewa na Aryan.


Ile kofia ya sweta ambayo yule kilema alikuwa amejifunika sura yake isionekane ilitoka na Aryan kuibaini ile ilikuwa sura ya mkandarasi ,daaaa mkandarasi aliinua kichwa na kumwangalia Aryan kisha akacheka he he he he umeniokoa ,kumbe bado waona ina maana ule unga hujaozesha hayo macho ? Aliuliza


Mkandarasi alicheka na kufanya kila mtu ashangae lakini Aryan akiwa kashikilia ile baiskeli ya kilema ambae alikuwa kakaa mkandarasi alikuwa bado hajaiachia Aryan alishangaa kwa mara nyingine anakutana na mkandarasi na alishagundua mkandarasi si mtu mwema kwake

Aliachia ile baiskeli lakini nyuma yake kulikuwa na yule mtu anae mkokota mkandarasi alitoa kisu kikali cheupe chenye icha kali bila kuchelewa alikikita maeneo ya mgongoni kwa Aryan puuuu!


Aryan alijikuta akicheua damu na kukosa cha kufanya tayari kachomwa kisu na mtu ambae anamkokota mkandarasi inaonekana yule mtu alisetiwa ,ama dili walipanga popote watakapo mwona Aryan wamuue.

Aryandamu zikaanza kumtoka wakati huo Samairah nae anashuka kwenye bajaji ili akamwangalie nani kachokwa na kisu

Maana alisikia sauti ya Aryan akisema jamani kisuuuuuu ,huku mkandarasi akacheka na yule anae mkokota alishika baiskeli na kuendele kumsukuma na kuondoka zao eneo la tukio.


Masikini Samairah nae wakati anaenda kumwangalia Aryan ,nyuma kulikuwa na mbaya wake anamfuatilia bibie Jesca alishika usukani wa gari na kusema ,


"Ngoja nikuuwe wewe unajifanya na weupe wako leo nakuondoa alimwelekezea gari na kwenda kumgonga Samairah ilisikika sauti ya kishindooo paaaaaaaaaaah

Wakati huo Jesca anacheka na kusema nimekumaliza akachochea gia ili aondoke lakini alivyogeuka nyuma alijikuta anaachia usukani na kusema mungu wanguuu uwiii

Nini hiki nimefanya? Jesca alijutia huku akionekana kuchanganyikiwa

.............................


Tulipo ishia baada ya Aryan kumwokoa mkandarasi kunusurika na kifo cha kugongwa na gari lakini mkandarasi bado hakuwa na shukrani hata kidogo yule kijana anaefanya kazi ya kumsukuma kibaiskeli ,mkandarasi walikuwa wamepanga mbinu na mkandarasi nia yao wamuue tu Aryan aondoke katika huu ulimwengu kwa kuwa anajua yeye ni kilema hawezi kufugwa jela ,alitoa kisu na kukikita mgongoni mwa Aryan kisha mkandarasi akaendelea kucheka ha ha ha ha pia na yule naliyemchoma Aryan kisu alikiachia pale pale kisha akaendelea kumsukuma mkandarasi na kuanza kuondoka katika eneo hilo huku Aryan akiwa ameganda pale baada ya kisu kuzamishwa katika mwili wake.


Bibie Samairah nae wakati anaenda kuangalia nani kachomwa kisu ,kumbe nae mbaya wake alikuwa anania mbaya alimwelekezea gari Samaira ,

"Jesca akiwa anatabasamu anakwenda kumgonga Samaira

Ki ukweli gari ilimpitia Samairah juu lakini cha ajabu alichokishuhudia Jesca alijikuta anachanganyikiwa peke yake na kutetemeka mwili mzima.


Alikuta kamgonga mama yake mzazi alijikuta anaachia usukani huku akiita mamaa kwanini mama umefanya hivyooo? Alifunga breki za gari hadi tairi nusu ziwake moto ,

Kila mtu alishangaa ile ajali ,ndugu msikilizaji kama unaroho nyepesi waweza ukapitisha macho juu juu.


"Mama yake na Jesca aliharibiwa mno aligongwa utumbo uliruka mbali na miguu kubakia kwenye tairi, mikono nae ilikuwa ipo na kichwa ,lakini mama alibakia kifua na mdomo alitoa kauli moja tu kisha akayafumba macho,alisema "KWAHERI JESCA" taratibu aliyafumba macho yake ,Jesca akajikuta analia kwa uchungu mno na kujutia kwa nini wivu wa mapenzi unamfanya anampoteza mama yake mzazi ,

Jesca aliinua kichwa ili kumwangalia Samairah yu mahali gani maana yeye ndiye chanzo cha kifo cha mama yake ,

Alimwona Samairah kasimama pembeni huku amemshika Aryan mkono huku akiendelea kutema damu baada ya kuchomwa kisu ,

Jesca kwa hasira alimrukia Samairah ili kumpiga sijui kaokotaje jiwe alitaka kumpiga usoni ,lakini Samairah alikwepa na kumwambia Jesca kweli wewe ni rafiki yangu ngoja nimuwahishe Aryan hospitali nitakuja kukusindikiza tukamzike mama yako

Watu walishangaa ile ajali ilifanya watu wasahau kama Aryan kachomwa na kisu ,watu walikuwa wakishangaa damu zilizotapakaa kwenye lami.


Viungo vya mama yake na Jesca ,kiukweli watu walishidwa kujizuia walijazana pale na kushangaa viungo vimezagaa kwenye bara bara ,polisi waliweza kufika kwenye eneo la tukio ,kumbuka baba yake na Kesca ni mkuu wa polisi kitengo cha usalama wa barabarani aliweza kufika pale na kukuta damu zimezagaa alivyomtazama mwanae ndio alikuwa kakumbatia kichwa na kifua cha mama yake akilia ,

Baba wala hakushangaa alicheka kisha akasema Jesca nani kakupa funguo ya gari?


Jesca hakujua nini amjibu baba yake zaidi ya kuendelea kupiga kilio ,baba yake aliita kitengo maalumu kwa ajili ya kuubeba mwili wa mke wake ili kwenda kuhifadhia kwa ajili ya maandalizi ya mazishi ,baba alimsogelea mwanae na kumwambia ,kweli nimeamini maneno ya mganga ,aliniambia nitatajirika sana ila nitampoteza mke wangu nimpendae shauri ya wivu wa mapenzi na alinambia mwanangu nawe utakufa kwa laana za watu kwa uovu uutendeao watu ,


Baba aliuliza "kwanini umesababisha ajali na kumgonga mama yako?,hapo ndipo Jesca akajikuta akitoa macho na kushidwa nini chakujibu ,alianza kukumbuka matendo aliyoyafanya nyuma na kila mtu alishamwambia utakufa kwa laana ,alishawahi kumwagia mwanafunzi mwenzake chai ya moto ,usoni ,ashawahi kumuunguza mama yake na Aryan ,maji ya moto kwenye mkono wake pasina sababu ,pia na kumteka mama yake na Aryan na kwenda kumtesa ,

Jesca aliendelea kukumbuka ,hata mama yake Aryan alishamwambia hawezi kumpenda hata kidogo maana amejaa uovu hivyo hawezi kuridhia awe mpenzi ama mke wa mtoto wake.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG