IMEANDIKWA NA : SAID S MAKAKA
********************************************************************************
Simulizi : Hasna (Mfu Anae Ishi)
Sehemu Ya Kwanza (1)
Anaitwa Hasna ni binti mwenye umri wa miaka kumi na saba.Ni mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mbika kilichopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.Ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto wa nne ana dada zake wawili,na kaka yake ambaye ndio wa kwanza kuzaliwa.Mama yake alifariki kipindi Hasna ana umri wa miaka mitano.Baba yake akuweza kuoa tena na starehe yake kubwa ni pombe tena za kienyeji.Katika familia ni yeye pekee ndiye aliye soma,kamaliza kidato cha nne na kafahuru kuendelea na masoma ya kidato cha tano.Lakini ndoto zake zinakatishwa na tamaa za baba yake.
Baba yake alichukua mahali ya milioni tatu, ng'ombe wa nne,na zawadi kemkem pia ikiwepo ahadi ya kujengewa nyumba ya kisasa.
Sifa kubwa ya Hasna hapo kijijini ni nidhamu na ukarimu wake.Mabinti wenzake walitamani kuwa na ukaribunae.Wavulana wengi walimsumbua lakini hakurusu mwanaume yoyote amsogelee,wengi walimuogopa kwa msimamo aliokuwa nao.
Hasna hakutaka kabisa kuuharibu usichana wake kwa sasa,malengo alio jiwekea mwanaume atakae toa usichana wake,ni mume wake tu.
Hapo baadae atakapo kuwa kamaliza masomo yake.kwani malengo yake yalikua afike hadi chuo kikuu.Hivyo mpaka sasa alikua kautunza usichana wake vema.
Aliyeamua kumuoa alijua hilo ndomana alitoa mali nyingi na kuahidi vitu vya thamani.Ili baba yake Hasna akubali kirahisi,kwasababu walijua ni mtu mwenye tamaa.
Anae muoa Hasna alikua ni mtu mzima mwenye umri wa miak arobaini na mbili.Nimkazi na mwenyeji wa Kahama mjini.Alikua ni mfanya biashara mkubwa wa madini.Na kwa umaharufu wake hakuna asiye mfahamu hii kanda ya ziwa,Anafaha mika kwa jina la Zuberi lakini wengi upenda kumuita Zuberi Madini.
Zilikua zimebaki siku mbili ili ndoa hifungwe,Na Hasna kaka ndani mwezi mzima akiwa na makungwi wakimfunda mwalio wao iliajue jukumu lakue nini kwa mume.
"Dada yani na nyinyi mnafurahia mimi kuolewa,angalieni umri wangu ulivyo mdogo, hata miaka kumi na nane sijafika,naitaji kusoma jamani"
Hasna aliongea kwa uchungu huku chozi likimtoka.lakini dada zake hawakumjali.
"Hivi Hasna kusoma kitu gani,bahati imekuja unataka kuichezea.hebu tuangalie dada zako tuna zeekea hapa hapa hakuna hata mwanaume aliekuja nyumbani kuleta hata hiyo mahali ya shilingi elfu kumi.sasa wewe unaolewa na tajiri ana mwanga mihela unataka kulinga."
Aliongea dada yake na Hasna anejulikana kwa jina la mwanjia.
"Dada wewe unaongea tu.Thamani ya utu wangu ni kubwa kuliko hizo pesa na mali.hivi mmeshindwa kufikilia mtu mzima yule mpaka sahizi hana mke wala mtoto.naona mmeamuwa kunichezea kamali sawa"
Aliongea Hasna huku chozi likiwa likimtilika.Baada ya muda kidogo aliingia shangazi yake na Hasna ,nakuwaambia wote waliokuwemo kwenye chumba wampishe abaki na Hasna
"Mwanangu nakujua vizuri maana mimi ndio nimekulea,nimeshindwa kukusaidia hili lisifanyike,na ukorofi wakaka nadhani unaujua mwanangu"
Shangazi yake Husna alikua anongea hukua akipeleka mkono wake kwenye maziwa yake akatoa kitu alikua kakihifadhi
"Mwanangu kamata hii naomba usiiacha kila sehemu unapokuwepo basi uwenayo.unapokwenda huko ni pazito mwanangu"
Aliongea maneno hayo kisha akatoka nje.Hatimaye siku ilifika watu walikuwa na shamlashamla.
Mara msafara wawaoaji uliingia zilikua gari tano alafu zote za kifahari alishuka Bwana harusi Zuberi akiwa na wapambe wake kumi, alafu wote lika sawa kulikua hakuna hata kijana.
Shangazi yake Hasna alikua kasimama akiwangalia watu walivyo na furaha kupokea ugeni huo.
Kunasehemu kwenye gari miongoni mwa magari hayo yaliokuja Shangazi yake Hasna alikaza macho hadi kaonekana kubadilika kwa hasira, na macho yakawa mekundu ghafla.Aliondoka haraka na kuingia ndani alipo Hasna hakukuta mtu hata mmoja na wote walikua nje bize na ngoma.
"Hasna mwangu ingekuwa ni amri yangu hii ndoa isinge fungwa.na ndoto nilio ota usiku wa kuamkia leo,amani sina mwangu chamsingi hicho kitu nilichokupa fanya kama nilivyo kwambia tunaweza tusionane tena."
Alikua anaongea huku kamshika begani Hasna
"Shangazi naomba uniambie kuna nini mia nogopa"
Ile shangazi yake nataka kuongea mara watu waliingia kumchukua bibi harusi kwa jiri ya kwenda kufunga ndoa.
Ndoa ilifungwa na waoaji walikua haraka haraka,waliomba kuondoka kuelekea kwao Kahama.
Safari ilianza hatimaye walifika kwenye nyumba moja kubwa lenye ghorofa mbili.kulikua na uwanja mkubwa wa fensi na ndani kumepakiwa gari tofauti tofauti na zote za kifahari.
Walishuka pale Hasni alikua mpweke na mnyonge,maana hakuna hata ndugu yake yeyote aliye msindikikaza.
Wale ndugu wake Zuberi Madini hawa kutaka hata kuingia wote walishia nje,walione kama kuwa na hasira ya jambo flani.Zuberi alimpeleka Hasna ndani akamuonesha bafu lililokuwemo mule mule kwenye chumba chao cha kulala.Baada ya kumuonesha Zuberi alirudi kuwa sikiliza wenzanke.
"Jamani naombeni mnielewe mimi mwenyewe sijui kimetokea nini"
Aliongea Zuberi akiwa anawambia wenzake
"Hapana Zuberi kuna kitu utakuwa umefanya jua huyo siyo ndugu yako si tunachojali ni biashara zetu"
Alionge baba mmoja kwa asira
"Sasa tutaonana usiku,tutaongea vizuri"
Waliagana na kuondoka.Zuberi alingia ndani
"Baby kama umemaliza kuoga njoo chakula kipo tayari"
Alisema Zuberi.kidogo Hasna alitoka akiwa ana shangaa shanga.nakuwaza kuona jumba lote hii mtu anaishi peke yake.
"Hivi hiki chakula umepika sangapi"?
Aliuzi Hasna
"Nimeagiza mke wangu,ilituwahi kula tupunzike"
Alijibu Zuberi lakini Hasna muda wote alikua hana amani na akikumbuka maneno ya shangazi yake. walimaliza kula wakawa wamekaa kwenye sofa.Huku Hasna akiwa kaa mbali na Zuberi maana alikua anamchukia.
"Hasna sogea karibu tuongee mawili matatu"
Alisema Zuberi
"Sema tu maana hata huku nasikia"
Alijibu Hasna,huku akiendelea kuangalia tv.Zuberi alinyanyuka mwenyewe na kusogea alipo Hasna.
"Ngoja nisogee maana usije sema huku sikia vizuri nilicho ongea"
Aliongea Zuberi
"Sasa naomba uwe makini kunisikiliza haya nayo kuambia tusije laumiana baadae."
Aliongea Zuberi lakini Hasna macho yake yalikua kwenye tv
"Nyumba yangu hii ina mashariti naunatakiwa uyafuate,kwanza haurusiwi kutoka humu ndani pekeako. mwisho ni getini,pili mwiko kuvaa nguo ya rangi nyekundu,tatu haurusiwi kupulizia marashi yoyote ndani ya nyumba hii , nne hakuna kupika pila zaidi ya siku ya ijumaa tu,na tano hakuna kuchoma udi wala ubani nadhani umenielewa ukienda kinyume tusilaumiane".
Alimaliza Zuberi kutoa mashariti yake.
"We mzee mashariti yote hayo ya nini"
Aliuza Hasna
"Alafu naomba uwe na heshima mimi ni mume wako sio kuniita mzee"
Alisema Zuberi huku akinyanyuka kuelekea chumbani
"Mume hiyo kwioooo"
Alijibu Hasna.ilikua imefika mida ya saa sita za usku Hasna alitamani alale pale pale kwa kuofia usumbu wa mume chumbani. Mara ghafla macho yake yakiwa bize kwenye tv.aliona kitu kama mtu kapita mbele yake.
"Hivi nausingizi au ni chaukweli nilichokiona"?
Hasna akiwabado anatafakari mara alisikia maji yana taka nikama mtu kafungua.alisi hatakua muwe wake kaamua kuoga sababu ya joto.lakini alikuja kushituka alipo sikia kitu kama sufuria limeanguka.
Ndipo alipo nyanyuka nakugundua hizo sauti za maji azitoki chumbani mwao.Alienda taratibu hadi kwenye chumba maji yanaposikaka kutoka alianza kufungua taratibu.Mara kidogo alisikia kitu kimemshika begani Hasna alipiga kelele zanguvu.
"Kumbe ndio muoga hivyo sasa kwenye chumba cha kuoshe dhabu unaenda kufanyanini"
Alikua Zuberi.alikua kamfata mke wake wakalale
"Zuberi kuna mtu humu alikua kafungulia maji"
Aliongea Hasna
"hakuna mtu hofu yako tu twende tukalale"
Zuberi alimwambia Hasna.Hasna alipo fika chumani alipanda kitanda na nguo zake.Hasna alikua na hofu. kama Zuberi akitaka wafanye mapenzi na yeye hajawahi hata siku moja.
Hasna akiwa anawaza hayo Zuberi mwenyewe ana hata habari na Hasna ndio kwanza anakoloma.
Hasna nae alivuta shuka kutafuta usingizi.
Mara usiku wa manane Hasna alishituka na kusikia nje ya chumba chao watu wanaongea kama wanabishana kitu.
Alinyanyuka bila kumshitua mume wake aliyeonekana kalala usingzi mzito. akaenda akafungua mlango taratibu aliwaona wale walio kuja na Zuberi kuoa wakiwa wamejifunga mashuka meupe.Lakini kilichokuja kushitu zaidi ni pale alipo muona Zuberi kule nae kavaa hivyo.karudisha mlango kwenda kuakikisha aliye lala kitandani
Hasna alishangaa sana kumuona Zuberi hakiwa kalala pale kitandani.Alijalibu kumuhamsha lakini Zuberi hakuonesha dalili yoyote ya kuamka.
Upande wa Nje ya chumba hicho Zuberi alionekana kushituka kuna kitu alihisi, alinyanyuka na kuanza kuelekea chumbani.Hasna alihisi kama kuna kitu kinakuja haraka haraka allijifunika shuka na kujifanya kalala.Zuberi alifika hadi pale alipo lala Hasna, akahakikisha kama kweli kalala,halipo jirizisha kuwa kweli kalala alirudi barazani kuendelea na kikao.
Hasna alibaki kalala huku akiwa anatetemeka na aliogopa tena kuinuka kwenda kuangalia nini kinacho endelea.
"Zuberi umetuangusha sana Hasna alitakiwa afe njiani na sio afike hadi huku"
Aliongea mmoja wa washirika hao
"Jamani mimi ndiyo niliyekuwa naongoza zoezi zima la ajari,lakini mlipo fika eneo ajari ingetakiwa itokee nilibonyeza limoti ili gari hiyo ianguke lakini niliona gari ikiendele nilifanya hivyo mara kadhaa"
Aliongea huyo ndio aliyeonekana ni mkuu wao.
"Kwahiyo mkuu unataka kusema nini juu ya hili"?
Aliuliza mmoja wa washilika hao.
"Jamani hapa tuna kazi ya kufanya,huyu binti sio mzuri kwetu kwasasa.kuna kitu anacho ambacho kinafanya zoezi letu kuwa gumu.Tukifanikiwa kwa hilo basi biashara zetu za migodi zitaenda vizuri, kwa sababu damu yake kwetu ina thmaani kubwa na ina nguvu ya ajabu.Zuberi na toa wiki tatu damu ya huyu binti inaitajika.Ikipita tunakupa adhabu kubwa zaidi ya aliyoipata bwana Haule"
Alitoa maagizo hayo mkuu huyo. kisha Zuberi aliongea maneno kwa lugha isiyo eleweka.walitoka mabinti sita kwenye chumba kimoja mule kwa Zuberi wenye umri sawa na Hasna .Wote wakiwa wamevaa magauni meupe yalioka mfano wa kanzu wote wakiwa wamenyolewa vipala.
"Zuberi hawa mabinti uliwaoa sawa ni mabikira lakini hawana nguvu kama za huyu binti mwingine.Mapaka sasa umefisha wake zako sita ,uliye waoa kwa ndoa amba ndio hawa mbele yetu.
Hivi unadhani majirani zako watakufikiliaje endapo na huyu binti akifariki akiwa hapa kwako nakutimiza idadi ya wake saba mpaka sasa, wamefariki kwako.Ndomaana tulipanga ajari itokee njiani iliusije hisiwa vibaya na watu"
Alikua anaongea mkuu huyo.kidogo ililetwa meza kubwa na ndefu kwenda juu. walimpandisha binti mmoja juu ya meza hiyo kisha kikaletwa chungu, kilicho funikwa na kitambaa cha rangi nyekundu.Kisha kikachukuliwa kisu kirefu aina ya jambia, akakishika yule mkuu na kumchoma yule binti sehemu ya moyo kwa kutumia nguvu hadi kikatokeza upande wa pili wa meza.Wakakinga chungu chini yameza ambazo damu zilikua zikitililika kufata kisu hicho.
Zile kelele za maaumivu makali ya binti yule zilimfanya Hasna ainuke tena kitandani na kwenda kuangalia nini kinaendelea.Mtu wa kawaida yeyote hawezi kusikia wala kuona matukio hayo. kwa Hasna anauwezo wa kuona hayo kutokana na kile kitu alichopewa na shangazi yake.Hasna alikuwa kaziba mdomo huku jicho likimtoka kwa mshangao.
"EWE MFALME WETU TUNAOMBA UPOKEE SADAKA HII JAPO SIO ILE TULIO KUAHIDI MCHANA.NA PIA KWANIABA YA MSHILIKA WAKO ZUBERI TUNAOMBA MSAMAHA SANA KWA KILICHOTOKEA"
Yalikua ni maneno ya mkuu huyo,akitoa sadaka kwa mfalme wao wakishetani.Mambo yote Hasna alikuwa hakishuhudia.
walimaliza kufanya mambo yao ilikua ni mida ya saa kumi za usiku.Pia Zuberi alikumbushwa kuzingatia hasifanye mapenzi na Hasna ilikutunza bikira.
Hasna hapo sasa ndipo alipo jua dawa pekee ya yeye kuwa salama ni kufanya mapenzi tu ili bikira yake itoke.
Hasina alirudi kitandani nakujifunika kama kawaida na kujifanya kalala, huku jicho moja likiwa likichungulia.
Zuberi aliingia ndani kisha kuna maneno aliongea na ule mwili uliokua kitandani ulinyanyuka na kwenda kwa mwili mwenzake nakuingia kisha ukawa mwili mmoja.
Hasna alikuwa anatetemeka kwa mambo yote aliyo yaona ndani ya siku hiyo moja tu.
Kesho palivyo kucha Hasna aliwahi kuamka na kwenda kuangalia pale walipo kua wameka wakina Zuberi usiku.Hapakuonesha dalili yoyote kama kulikua na watu,
Kidogo zuberi alitoka chumbani akiwa kajianda kwenda kazini.
"Vipi mke wangu mbona umewahi kuamka"
aliuliza Zuberi.
"Nilikua nafanya usafi tu,kwani vipi"
Aliuliza Hasna.
"Sasa ukingia jikoni kuna kila kitu unatangalia mboga kwenye fliji"
Alimpa maelekezo hayo Hasna kisha Zuberi akaondoka.
Zuberi aliondoka kafunga geti nafungu kaondoka nayo,
Hasna alianza kuingia chumba kimoja kimoja kukagua lakinia hakuambulia kitu chochote.
Ilifika mida ya saa tano asubuhi Hasna alianza kuhisi njaa aliingia jikoni akaangalia lakini hakuona mkaa wala jiko.
"yani huyu Zuberi anataka mimi nishinde na njaa"
Aliwaza Hasna huku akiwa anatoka jikoni.kidogo Hasna alisikia sauti ikiita dada,aliangaza huku na kule.Yule mtu aliye ita baada ya kuona Hasna kageuka alishangaa sana.
"kumbe huyu binadamu ananisikia au na yeye ana mambo ya kichawi"?
Kilikua kikijiuliza hicho kiumbe kisicho julikana na wala hakionekani kwa wakati huo.Hasna alivyo geuka hakuona kitu chochote alihisi ni mawenge yake tu akaendelea kusonga mbele
"Dada samahani naomba usimame"
kiliongea kiumbe hicho tena.Hasna alipogeuka alipiga kelele nakuanza kukimbia baada ya kukiona kiumbe hicho.
Mara kilitokea mbele yake.Hasna alianza kutetemeka jasho lilinzakumtoka kwa wingi.
"samahani dada mimi humu nilikuja kama wewe naomba usiniogope.lakini mbona wewe unauwezo wa kunisikia na kuniona.?wakati tunaonana tu ni sisi tuliokufa au ukiwa mchawi ndio unauwezo huo."
"kwani wewe umekufa"?
aliuza Hasna huku hakiwa anatetemeka.
"Sasa naona unahisi njaa njoo kwanza jikoni nikuoneshe jinsi ya kutumia gesi,alafu nataka tuongee mengi ili nikusaudie yasije kukuta haya yalio tukuta wenzako"
kiumbe hicho kiliongea huku kikielekea jikoni.alikuwa ni miongoni mwa wale mabinti walio kuwepo jana usiku mwenzao alitolewa kafara .
Hasna nae alianza kufata huko jikono.Alikua nawasi wasi lakini alipata moyo kusikia anataka kumpa Masada.Ili aondokana na hilo janaga.
"Hasna naomba,usiniogope Mimi naitwa Mariamu"
Dada huyo kwa sasa inajulikana maisha kufa.Alimtoa hofu Hasna
"Sawa haina shida Mariamu"
Basi Mariamu alimuelekeza Hasna jinsi ya kutumia gesi hiyo.
Hasna alianza kupika huku Mariamu kakaa pembeni wakiwa kimya ana mtazama tu Hasna.Hasna alimaza kupika
"Mariamu chakula tayari njoo tule"
Hasina alimkaribisha Mariamu
"Hasna wewe endelea kula sisi wenzako tuna vyakula vyetu maalumu sio hivyo"
Mariamu alimjibu Hasna.
"Nivyakula gani hivyo "
Aliuliza Hasna.
"Hasna kula kwanza,utayajua mengi tu"
Mariamu alimwambia Hasna.Basi Hasna aliendelea kula .Alipo maliza alikusanya vyombo kwa lengo La kwenda kuviosha.Lakini Mariamu alimkataza kwenda kuviosha.
"Sasa Mariamu kwanini umenikataza kuosha"
Aliuza Hasna.
"Kwani Hasna Jana usiku si ulikula na mume wako na vyombo ukaacha mezani na haukuvikuta na mahali mlipolia palikua pasafi kabisa.Huku wapo wa kuosha wewe viweke tu.ungekuwa hauna uwezo wa kutuona hizi kazi ungefanya lakini sahizi wapo"
Aliongea Mariamu nakumfanya Hasna akumbuke Jana vyombo aliviacha mezani na meza ilikua chafu na yeye ndio alikua wa kwanza kuamka,lakini alikutapasafi na vyombo hakuna.Hakuweza kufatilia hilo kwa sababu ya Yale aliyo yaona usiku ndomaana aliamka nawazo moja LA kuangaria sehemu kina Zuberi walio kua wakifanyia mambo yao.Hasna vyombo aliviacha hapo hapo,kisha Mariamu alimuomba wakakae nje.basi walitoka hadi nje ya nyumba kwenye fansi kulikua kumepaki magari mengi na mazuri.
"Hasna huyu baba mbaya sana,Mali zote hizi ni damu za watu.
Aliongea Mariamu.
"Kwahiyo na nyinyi ilikuaje vifo vyenu sasa".
Aliuza Hasna.
"Hasna Kwa sasa hilo sio LA muhimu .njoo tukae hapa ilituongee LA muhimu"
Aliongea Mariamu kisha wakakaa mahali ndani ya fensi mule mule.
Mariamu alianza kumuhadithia kuwa wenyewe Kwa sasa wamebaki watoto mwemzo mmoja Jana walimtoa kafara.
Na hapo walipo wanaonekana wamekufa kwa upande wa duniani,lakini kumbe ni wafu wanao ishi.Mariamu pia aliendelea kumuhadithia napia akamuambia yeye na wenzake,wanaitaji kumsaidia tena kwa shariti moja tu.Wenzake na Mariamu wa nne walikua kwenye chumba cha kuoshea dhabu.Wakiendekea na kazi ya kuzisafisha na kuzipakia kwenye kifungashio maalumu kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi kwa ajili ya biashara.
Mariamu aliendelea kuongea kabla ya kumpa shariti hilo Hasna.
"Sasa unatakiwa utoke nje"
Alisema Mariamu
"Sasa tatokaje wakati Zuberi kaondoka na funguo."
Alisema Mariamu.
"Usjali kuhusu hilo takupa mbinu,ngoja nimalize nini unachotakiwa kukifanya nje"
Mariamu alimpa maelekezo yote kuwa akitoka nje anatakiwa aende kwenye makaburi yao.Amboyo yanasadikiwa kuzikwa miili yao.
Achukue udongo wa kwenye kila kaburi LA mmoja wao.Pamoja na majani yaliyo chipua kwenye makaburi hayo.kisha amletee Mariamu na wenzake,iliwaweze kuchanganya na vitu wanavyo jua wenyewe warudi kwenye hali ya ubinadamu.
"Hasna hiyo ni kazi ngumu maana hata makaburi yetu yako mbali mbali,makaburi moja la mwenzetu liko Geita.Pia ukitoka hapa haurusiwi kwenda kwenu,wala haurusiwi kuongea na kiumbe chochote kina choitwa binadamu jambo hili.Hukithubutu kuongea jambo hili unakua umejiua mwenyewe.
Aliongea Mariamu.
"Sasa tajuaje makaburi yenu,?pia shariti gani nalotakiwa kupewa"
"Kuhusu makaburi kila mmoja atakuambia kwa muda wake na kukuambia jina lake."Shariti tunalokupa unatakiwa utuachie hicho kitu ulicho vaa shingoni."
Aliongea Mariamu huku akiwa ananyanyuka kwa lengo ka kuondoka na kumuambia Hasna anampa masaa machache ya kufikilia hilo.
Lakini alimkumbusha anatakiwa wafanye zoezi hilo kabla ya wiki tatu.
Hasna alibaki njia panda maana shangazi yake alimuambia asikivue kitu hicho popote anapokwenda.Napia wiki tatu hizo atawezaje kukamilisha swala hilo. Hasna kwa sasa aliona anazidi kuwa kwenye wakati mgumu.
Hasna alirudi ndani na kwenda chumbani kwake kupunzika.Huku akitafakari jambo hilo.
Upande wapili Zuberi alionekana hakiwa nyumbani Kwa wazazi wake.
"Zuberi sisi wazazi wako hatukuekewi kabisa una shida gani. Kila mwanamke unaeoa afikish siku arobaini anafariki Na wewe hata hakuna unacho jali kabisa."
Aliongea baba yake Zuberi aliyeonekana kuwa na hasira.Zuberi alijitahidi kumuelewesha baba yake kwa maneno yauongo.huku akisema jambo hilo analifanyia kazi.Lakini baba yake hakutaka kumsikiliza kwa hilo.
"Yani wewe Zuberi haujui unvyo tuzalilisha huko mitaani,kwamba sisi ni wachawi sasa utake usitake kesho nakuja kwako na shekhe hili tusome dua kwenye hiyo nyumba yako."
Aliongea baba yake Zuberi huku akinyanyuka na kuingia ndani akimuacha Zuberi akiwa kakaa pale pale.Kajiinamia chini akionekana kuna jambo analotafakari.
Baada ya muda aliwapigia simu washilika wenzake na kuwaomba waonane haraka nyumbani kwake.
Zuberi aliondoka bila hata kumuaga baba yake,na kuelekea nyumbani kwake.
Alikuta baadhi ya washilika wenzake wakimsubiri nje ya geti maana alikua kafunga.
"samahani jamani kwa kuwaweka.Mbona wachache wengine wako wapi"?
Ambae alikua anaongea alikuani Zuberi.Alifungua mlango wakaingia,lakini hawa kwenda kukaa sebuleni,walikaa nje kwenye kanyumba kaliko tengenenza mfano wa msonge.
" ndugu zangu nimewaita kuna jambo kidogo limenichanganya,inatakiwa tulifanyie kazi haraka".
Alisema Zuberi.
"Tunaomba utuambie ni jambo gani hilo".
Aliuliza miongoni mwa wale washilika.
Zuberi alianza kuwaelekeza jinsi baba yake alivyo muambia.Nakuomba ushauri.
" Yani nahisi katika watu wanao weza kuja kutuumbua ,mini wewe Zuberi.Maana toka ujiunge na chama chetucha kafara,kumekuwa na matatizo mengi".
Aliongea miongoni mwa washilika huku akuwa amekasilika.
"Bwana Maliki usipaniki,hapa inatakiwa jinsi gani ya kusovu nasio kulaumiana".
Aliongea yule kiongozi wao.Kisha wakapanga wakutane usiku,kama kawaida ili kujadili zaidi na kujua hatima ya hilo.
Walipo maliza kila mmoja alionfoka zake.Alibaki Zuberi akiwa kakaa peke yake,hakiwa kwenye dimbwi LA mawazo.
Hasna alikuja na kumkuta Zuberi akiwa pale nje.
" Jamani mume wangu toka umekuja umekaa huku nje,hata kuja kumjulia hali mkeo".
Aliongea Hasna huku akimshika shika kidevu Zuberi
"Nakuomba unitolee ujinga wako hapa,Mimi na mambo yangu usinichanganye kabisa".
Aliongea Zuberi kwa kufoga.Lakini Has in a aliendelea kumsumbua Zuberi.Zuberi aliona kero zimezidi aliwasha gari na kuondoka zake.Kama kawaida take alifunga geti na funguo aliondoka nayo.
Baada ya Zuberi kiondoka Hasna aliingia ndani haraka haraka,kumbe alikua na lengo lake.Halipofika ndani alimuita Mariamu huku akiangaza huku na kule asijue Mariamu anatokea wapi.
muda kidogo Mariamu alitokea.
Aliuliza Mariamu huku mikononi mwake akionekana na damu zikidondoka chini.Hasna alianza kupatwa na hofu baada ya kuona Mariamu akipeleka mikono yake mdomoni na kuanza kuzilamba zile damu.
"Hasna naomba uniambie ulicho niitia usinipoteze muda wangu Mimi"
Aliongea Mariamu aliwa kwenye Hali tofauti kabisa.
"Nimekubali kufanya hivyo"
Aliongea Hasna.Mariamu alicheka kicheko ambacho kilifanya hadi popo wote walio kuwemo ndani woteke na kuanza kuruka ruka hovyo.
kilikua kicheko cha ajabu.Hasna alikua kaziba masikio kwa kelele ya kile kicheko.
"vua unikabidhi hapa" Aliongea Mariamu huku akipeleka mkono kwa Hasna.Hasna alivua na kumkabidhi Mariamu kitu hicho.
Mariamu alipo kipokea,Mara alikiachia ghafla huku akipiga kelele za maumivu.kilimpiga shoti kitu hicho.
Hasna alibaki kushangaa nini kimetokea.Mariamu alimungalia Hasna jicho Kali hadi Hasna alinza kuogopa.
"Chukua na uvae,utanipa usiku wakati nikikuonyesha njia ya kupita.
Aliongea Mariamu alafu akapotea.
Hasna hakuweza kutambua chochote.Alichukia kitu chake hicho na kukivaa.
Ilikua in majira ya Saa mbili usiku.Hasna alikua kapika na kundaa chakula mezani,akiwa anamsubiri Zuberi waje kula.
Wakati anamsubiri Zuberi aliingia zake chumbani akawa kajilaza kitandani.Baada ya muda usingizi ulimpitia.
Huku nyuma Zuberi alikuja na kumuita Mariamu.Wakawa wanaongea lakini haikujulikana nini walichokua wanaongea.
Na huku Hasna nae alitoka ndani,akiwa anapikicha macho kwa usingizi.
" kumbe umekuja?,mbona nimesikia kama unaongea na MTU."
Aliongea Hasna alafu akamuuliza swali Zuberi.Zuberi alishituka kidogo.
"kwani wewe ulicho sikia ni nini”?
Aliuliza Zuberi huku akionekana na wasi wasi.
“Mimi sijasikia maongezi, lakini nimesikia sauti za watu wawili”
Alisema Hasna huku akimuangalia Mariamu,ambaye kasimama pembeni.
Kwa akili ya Zuberi anajua Hasna amuone Mariamu.Hasna hakua kasikia mazungumzo hayo ya Zuberi na Mariamu.
“wewe umesikia vibaya na mausingizi yako”
Zuberi alimwambia Hasna.Hasna alimkaribisha mume wake chakula,huku Mariamu akiondoka zake.Sijui alikua akipewa maagizo gani na Zuberi maana yeye ndio alionekana na cheo kuliko wenzake.
Basi walimaliza kula kisha wakakaa kuangalia TV.Ilifika mida ya saa NNE za usiku Zuberi aliingia chumbani kulala,huku Hasna akiwa pale pale kwa lengo la kumsubili Mariamu.
Lakini akiwa kaka pale usingizi ulianza kumpitia,aliona no bora akalale.
kama kawaida aliahituka usiku Hasna na kusikia watu wakizungumza.
Alinyanyuka kitandani na kumuona mume wake kalala pale pale kama kawaida.Alienda kufungua mlango taratibu nakuona yote yanayoendea,alimuona Zuberi na wenzake.
“CHIFU TUMEKUITA TENA HAPA TULIKUA TUNAOMBA USHAURI WA KUHUSU BABA WA MSHILIKA MWENETU ZUBERI AMBAYE ANAONEKANA KUINGILIA MAMBO YETU”
Alimaliza kuongea mkuu wa ushirika was kafara.Mara kidogo ulivuma upepo mkali hadi ndani vitu vikanza kuanguka hovyo hovyo.Kidogo ilisikika sauti nzito,ilimfanya hadi Hasna aogope.
“INATAKIWA ADHABU YA KIFO NA DAMU YAKE ATAKUNYWA MTOTO WAKE.KWA SABABU YA KAFARA.NA PIA NIMEMPUNGUZIA ADHABU NILIOMPA JANA.SASA ZILE WIKI TATU NIMEZIFUTA NIMEMPA MIEZI MIWILI DAMU YA HUYO BINTI NIIPATE”
Ilisikia sauti ya MTU asie onekana.Wakati mtu huyo kamaliza kuongea.Kidogo walimleta baba take na Zuberi pale mbele ya washilika.Zuberi alichukua kisu kikubwa na kirefu kisha akamtoboa kidogo kwenye paji la uso baba yake.Akachukua damu zilizo toka na kuziweka kwenye kibuyu.
“Zuberi hapo sawa na dhani unajua hiyo damu unatakiwa uifanyaje”.
Yalikua maneno ya kiongozi waushilika.Damu huyo aliyo ichukua kidogo ni kwa sababu ya kuengeneza kifo cha baba yake.Hayo yote alikua akiyashuhidia Hasna.Mara kidogo nyuma ya Hasna kilionekana kiumbe cha ajabu kikimfata pale alipo simama mlangoni huku yeye akiwa hana habari yoyote.
Kilizidi kusogelea kilipo mfikia kilimshika mgongoni Hasna alitaka kupiga kelele.Lakini akakumbuka yuko sehemu ya siri wata msikia.Na kwa akili yake alijua ni Zuberi yule anae baki kalala Zuberi wa ukweli akiwa kwenye kikao.
Hasna aligeuka taratibu huku akiwa anatetemeka.Alipogeuka alijikuta akizidi kutetemeka zaidi. na alipo jaribu kupiga kelele sauti iligoma kutoka.Kilikua nikiumbe cha ajabu ni kama maiti iliyo fufuka kutoka kaburini.
Mara ghafla aligeuka kuwa Mariamu.Hasna alishangaa sana kumuona Mariamu akiwa kwenye umbo tofauti na alivyo mzoea.
"Mariamu kumbe ni wewe umenitisha.Lakini mbona unafanya mambo ya ajabu sana.Huo uwezo unatoa wapi"?
Aliuliza Hasna huku akiwa na mshangao mkubwa.
"Hasna ni jambo lingine ndio limenileta hapa,hayo mengine baadae
Alisema Mariamu.
"Hasna nadhani umeona kila kitu hapo kama mtu anweza kumuua baba aliye mzaa, sasa wewe ni nani ashindwe kukumaliza"?
Aliongea Mariamu.Huku Hasna kiwa ana msikiliza.
Jambo lililonilita,kesho hapa kuna msiba wa baba yake Zuberi.Hivyo baada ya siku tatu ndio unatakiwa kuondoka,kwenda kufata vitu nilivyo kuagiza"
Aliongea Mariamu.Hasna alikubaliana nae.Mariamu alipo malizana naHasna aliondoka.Hasna nae alipanda kitandani kulala hakutaka tena kuendelea kuangalia kina Zuberi wanafanyafanya.
Hasina alitamani hizo siku tatu zifike haraka iliaweze kutoka.Zuberi nae alimaliza mambo yake na kurudi zake chumbani,alifanya kama kawaida yake na mwili uliokua umelala uliingia kwenue mwili origino uliokuwa nje kwenye kikao,nakua mwili mmoja.
Hatimaye siku iliyofata ilifika .Zuberi aliwahi kuamka na kwenda kwenye chumba kimoja kilicho mule ndani.Lakini chumba hicho huwa akifunguliwi mara kwa mara.
Aliingia kwenye chumba hicho akiwa kabeba ndoo ya plastiki,iliyo kuwa na kitu ndani.
"Nyinyi wapumbavu nimewaletea chakula napia naomba mniskilize vizuri.Leo kuna mgeni atajumuika nanyi sema mgeni huyo ni jinsia tofauti na nyinyi.
Aliongea Zuberi.Walikua ni wale mabinti watano,Lakini walikuwa wamesimama wakiangalia ndoo iliyo kuwa na chakula,walionekana hawajala muda mrefu.
Zuberi aliwawekea chini ndoo hiyo walianza kugombania.Akikuweza kujulikana nichakula gani walicholetewa.
Upande wapili nyumbani kwa kina Zuberi.Baba yake Zuberi alionekana akiwa juu ya mti,akikata matawi ya mti yaliyo onekana yamezidi na kugusa bati.Hiyo baba Zubeli yalionekana yana mkela hasa nyakati za usiku akiwa kala,kukiwa na upepo matawi hayo upiga kelele zaidi.
Baba Zuberi akiwa juu, mama Zuberi alikua chini akimuelekeza mume wake.Mara baba Zuberi alikanya tawi lilivunjika akaanguka chini na kufikia kichwa,mama Zuberi alipiga kelele za kuomba msaada.Walikuja majirani na kukuta baba Zuberi tayari kaisha fariki.
Zuberi taarifa zilimfikia, kwa sababu yeye ndiye alikua mtoto mkubwa.Hivyo aliwaomba msiba huo uwamishiwe kwake.
Basi walimkubalia.Lakini yeye alikua na lengo lake jingine.Maandalizi ya msiba yaliendelea kufanyika.
Zuberi na wenzake wawili waliingia kwenye chumba kilichokua kimeifadhiwa maiti ya baba yake.
Walipo ingia Zuberi alitoa kamkia sijajua kamyama gani.Aliongea maneno aliyo yajua yeye huku akiichapa maiti.Baada ya muda kidogo alinyanyuka baba yake,huku kivuli chake kikibaki kimelala pale pale.
Zuberi alimshika baba yake mkono na kumpeleka kwenye kona ya chumba hicho,kisha akamuambia achuchumae alipo chuchumaa .Zuberi alitoa unga mweupe aliokua kauhifadhi kwenye kibuyu kisha akampaka baba yake usono.
"Nakuomba ukae hapa hapa na wala usitoke hadi tapokuijia"
Zuberi alimwambia baba yake.Baba yake aliitika kwa kutisa kichwa.
Baada ya muda mchache waliingia wazee wawili kwa lengo la kuuanda mwili.Lakini kuna mzee mmoja alionekana akiangaza huku na kule.Lakini macho yake yalipofika kwenye kona ile aliyo wekwa baba yake na Zuberi.Alionekana kakazia macho pale.Kidogo alitoka nje na kumuita Zuberi
"Zuberi nimekuita hapa nje kuna kitu unakosea mwanangu,fanya umtoe baba yako kwenye hiki chumba.Ataingia mtu mwingine mwenye uwezo wakuona mambo yanayoendelea ,haka sababisha uumbuke".
Aliongea mzee huyo.Alikua ni mzee aliyeko kwenye ushirika wa kina Zuberi.
"sawa mzee wangu nimekuelewa ngoja nifanye haraka"
Zuberi alifanya kama alivyo agizwa na mzee huyo,
Hasna alikua chumbani katulia akiwaza haya mambo yanavyoendelea.Hakutaka hata kwenda kujumuika na wenzake nje, wanao omboleza .Sababu Hasna alijua kila kitu kinachoendelea.
Utaratibu wa mazishi ulifanyika na hatimaye walienda kuusitili mwili wa baba Zuberi.
Zilipita siku tatu zoezi la uogaji maji lilikamilika na msiba ukawa umeisha.
Jioni ya siku hiyo mama yake Zuberi alimwita Zuberi.
"mwanangu kifo cha baba yako bado akiniingii akilini kabisa ,minaona bado yuko hai"
Aliongea mama yake na Zuberi.Zuberi alishituka kidogo lakini usoni hakuonesha dalili yoyote ya hofu.
"Mama usifikilie tofauti hiyo nikazi ya Mola.Tukisema mange tutamkufulu mola wetu"
Aliongea Zuberi maneno yakumuaminisha mama yake.kuwa kifo cha baba yake ni mipango ya mungu.
Basi mama yake Zuberi alimkubalia mwane japo kwa shingo upande.
Siku hiyo Zuberi aliuaga Hasna.Alikua ana mpeleka mama yake nyumbani kwake.kwa sababa msiba ulikua umeisha,iliwatu wanaoenda kumuhani wamkute kule kwenye nyumbani yake na marehemu mumewe.
Zuberi alimwambia hasna hato rudi atalala huko huko kwa mama yake mpaka kesho.Zuberi aliondoka na kuelekea nyumbani kwa mama yake.
Ilifika majira ya saa saba usku Hasna akiwa chumbani kwake.Alitokea Mariamu akiwa kabeba chungu kisicho na kitu ndani.Amuamsha Hasna,alipo amka alibaki kitandani kakaa akimuangalia Mariamu.
"Mariamu mbona usiku sana kuna nini"?
Aliuliza Hasna.
"Ndio kazi yetu sasa inaanza,inuka unifuate"
Aliongea Mariamu Hasna a alikua kaisha jua nini kinachoendelea.Hasna alinyanyuka na kuanza kumfuata Mariamu.
"Mariamu unanipeleka wapi mbona hauongei chchote"?
Aliuliza Hasna.
"Hasna naomba unifuate,acha maswali fuata maagizo yangu"
Walitoka hadi nje ile sahemu waliyoekaa siku Hasna anapewa maagizo na Mariamu.
"Hasna naomba uvue hicho kitu na ukiweke humu kwenye chungu."
Aliongea Mariamu kwa sauti ya kibabe.
"Sasa Mariamu ndio navua lakini sio nakupa chotechote"
Aliongea Hasna.
"Hasna nadhani umeona mambo yanayoendelea humu,nawewe umebakiza siku chache za kuishi ,sasa ukiwa mbishi sisi ndio tutakufa kabisa na wewe ndio utakuwa mwisho wako"
Aliongea Mariamu.Hasna alikivua na kuliweka kitu hicho.KIlikua ni kikamba cheusi kilichotengezewa kwa nguo,na kwa chini kulikua na kafundo.Kafundo hako kalikua kagumu kuna kitukilijua kimeshonewa humo.
Na hiyo ndio ilikua kinga pekee.Na mtu yoyote mwenye ushirikina basi hawezi kukigusa lazima kimuunguze.
Hasna alivyo kiweka kwenye chungu .Mariamu alicheka sauti tena ilkua ya ajabu sana.
"Hasna hapo kazi imeisha nenda kalale.Maelekezo yote utayapata"
Aliongea Mariamu kwa sauti yenye mikwaluzo.
"Sasa Mari......"
Hasna alitaka kuongea lakini Mariamu alimkatisha,kabla hata ya kuongea alichotaka kuongea
"Hasna kuwa muelewa"
Aliongea Mariamu kwa sauti ya ukali na ya juu.Kisha akapotea kimaajabu.Alipotoweka tu mara ilisikika sauti ya mtu akiwa analia tena kwa uchungu sana.
Mara na sauti ikasikika ikisema.
"Mwanangu umefanya nini sasa"
Hasna alishituka sana. Na aligundua ile sauti ilikuwa ni ya shangazi yake.
Hasna alikimbia hadi chumbani kwake. Siku hiyo alijiona yuko tofauti sana.
Zilipita siku tano Hasna hajaona wala kusikia kitu chochote, hata vile vikao vya kina Zuberi hakuweza kuviona tena. Na hata alipo jaribu kumuita Mariamu hakuweza kutoka.
Siku moja Hasna akiwa amelala, aliota ndoto yuko chini ya mti mkubwa aina ya msufi akiwa kavishwa nguo nyeupe huku akizungukwa na watu wengi wapatao ishirini hivi huku wote wakiwa wamevalia majoho meusi.
Hasna alianza kuzungusha macho, alianza kumfahamu mmoja mmoja alimuona Zuberi. kugeuza macho upande wa pili alimuona Mariamu, alipatwa na hasira alitaka anyanyuke amfuate lakini nguvu hakua nazo.
Hasna alopo kuja kushangaa zaidi alipo muona baba yake ,akiwa mwa wale watu.Aliita baba lakini sauti haikuweza kutoka.
Baba Hasna alikabidhiwa upanga mkubwa unao ng'aa na kuambiwa aende kuchoma Hasna.Alilishika na kulinyanyua na kuanza kulipeleka kifuani mwa Hasna.
Kabla hajashusha upanga huo kifuani mwa Hasna ilisikika sauti.Iliyo mzuia kufanya hivyo,baba Hasna aliacha na kugeuka alikua ni kiongozi wa juu kwenye kambi hiyo ya kichawi.
Hasna alibaki akishanga na kujiuliza kumbe na baba yake anausika .wakati akiendelea kuyawaza hayo.
Mkuu wa wachawi alisimama mbele ya umati huo mkubwa wa watu hao walio valia majoho meusi.
"Hapa watu mmekuja kwa matatizo mbali mbali ,kuna watu waliotaka Mali nabiashara zao zifanikiwe kwa kiwango kikubwa.hawa wenyewe sio wachawi lakini wana mambo yakichawi,mfano Zuberi na wenzake."
Aliendelea kuongea mkuu wa kichawi huyo naumati huo.Huku Hasna hakiwa kalala tu pale pale chini.
"Pia kuna kundi lingine wenyewe walitaka kuwa wachawi wakubwa kama Mimi. Kama Jafari(baba Hasna),Na wenzake naleo hii tunafura sana, kumuona Jafari hapa akishilikiana na Zuberi, kutuletea Binti Hasna.
Nahili tukio LA Leo linanikumbusha miaka kumi na mbili iliyopita kwenye mti hu Jafari(baba Hasna) aliwenza kumtoa mkewake mpendwa kafara na lengo lake alikua akitaka uchawi mkubwa ili aweze kuwa tishio kwe huu ulimwengu.
Na sasa baada ya kukaa miaka yote hiyo akiwa na uchawi mdogo,sasa Leo tunamskimika rasimi uongozi wa kambii hii ya kichawi na tunampati nguvu za ajabu"
Aliongea hayo mkuu wakichawi na umati wote ulishangilia kwa furaha.Hasna alishindwa hata afanye nini baada ya kusikia yote yanayo muhusu baba yake.lakini lile La kumtoa kafara mama yake lilimuuma sana ,maana mama yake alifariki Hasna akiwa na umri wa miaka mitano.
Aliendelea kuongea mkuu huyo wa kichawi.
"Sasa namkalibisha ndugu Okwami kutoka naijelia aweze kumkabidhi madaraka na kumkabidhi nguvu Ndugu Jafari."
Alimaliza kuongea mkuu huyo wa kichawi na kumpisha kiongozi wa kichawi kutoka kambi ya Naijelia.Ambeya alikuja kama mgeni rasimi wa tukio hilo LA kumuapisha baba yake Hasna.
Baba Hasna alipita mbele na kupiga magoti kisha akakabidhiwa ngao na Okwami mkuu wa kichawi wa Naijelia .Alianza kuomba mizimu ya kwako Naijelia .
"Obinaaaa na Okechiiiii nawaomba mumpokee binadamu huyu kwenye ufalme wenu na mumpe nguvu za ajabu"
Aliongea Okwami kwa lugha ya kinaijelia.
Alimaliza kumuapisha baba yake na Hasna.Zuberi alitwa mbele na mkuu wa kichawi wa kambi ya Tanzania.
"Sasa zoezi linalofata ni kumtoa Hasna kwenye sura ya dunia nakumleta huku kudhimu, nabaada ya siku arobaini basi tutamtoa kafara rasimi .Leo tunamundoa dunia nawote wajue kafa"
Alisema mkuu huyo na kumkabidhi upanga baba ake Hasna.baba Hasna akinyanyuka upanga na kumchoma Hasna kifuani.Hasna alipiga kelele nakushituka kutoka ndotoni
Aliongea kwa sauti ya chini sana Hasna.Mara alishituka kuona kavaa nguo tofauti na alizo vaa Jana wakati wa kulala.Moja kwa moja alifikiria kuangalia kama Zuberi alimuigilia kimwili bila ya yeye kujua.Lakini apoangalia alikua yuko salama.Akiwa bado anajiuliza maswali kuhusu nguo hizo alizo vaa.Alianza kusikia sauti za watu nje wakilia.Hasna alijiuliza kuna nini.Alitoka nje haraka nakukuta watu wengi alimfata dada mmoja aliyekua kasimama pembeni akiongea na mwemwenza.
"Dada samahani hivi kuna nini hapa mbona watu wengi alafu wanalia"?
Aliuza Hasna lakini hakuna aliye mjali wala kumuangali .Aliwasikia tu wakiongea kuwa marehemu kafa ghafla.Jana usiku kasumbuliwa na tumbo hadi kupefekea kufikwa na umauti.
Hasna akawa anajiuliza nani kafa ?.
Aliondoka NA kwenda kuwauliza watu wengine lakini hakuna aliye mjali kabisa. Hasna alipiga kelele kwa nguvu lakini hakuna hata mtu aliye shituka.
Baada ya muda kidogo aliwaona dada zake pamoja na shangazi yake wakiingia mahala hapo .Huku dada zake wakiwa wanalia .lakini shangazi yake macho yalikua makavu Hasna alimkimbilia shangazi yake huku akimwita lakini shangazi yake alikua hana Habari yoyote.Hasna alifika hadi karibu na shangazi yake alipo mgusa hakuweza, mkono ulikua unapita tu kama hakuna mtu Anagusa hewa.
Hilo nalo lilimchanganya Hasna nakuanza kujiuliza nimekuwaje Mimi lakini. Aliondoka hadi mahali walipo kuwa wamekaa wanaume alimuona baba yake wakiwa wanaongea na Zuberi .Baba Hasna alipo muona Hasna alishituka na kumuambia Zuberi .Zuberi aligeuka nakumuona Hasna alienda haraka alimshika mkono na kumrudisha ndani.
"We pumbavu naomba usitoke humu "
Zuberi alimwambia Hasna.
Lakin ilipofika majila ya saa tano za asubuhi yalionekana magari yanaingia na moja lilionekana limebeba mwili wa mtu aliye sadikika kufariki dunia.
Walishusha mwili. Wakati wakiwa wanauingiza ndani ,wa mama waliongeza kulia.
Vilio hivyo vilimfanya Hasna atoke tena chumbani na kwenda kuangalia.Alishuhuduia kuona watu wamebeba maiti.
Aliwafata nyuma nyuma hadi walipo ingiza chumbani.Nia ya Hasna nikutaka kujua ni nani huyo aliye kufa?.
Walipoifikisha chumbani wale walio kuwa wamebeba walitoka nje.
Walibaki wa mama watu wazima ,kwajili ya kuuosha na kuuandaa mwili huo.
Walipo ufunua ilikuupandisha juu ya kitanda kililochotolewa godoro kwajili yakuosha.Hasna alingalia kisha akatabasamu na kuanza kuondoka.
"Yani kuna watu wajinga sana kwenye hii dunia.Wameacha shuguli zao kuja kulia huku."
Hasna alitoka na kurudi chumba alichoambiwa ake na Zuberi .
walifanya maandalizi ya mazishi na kwenda kuusitili mwili huo.
Ilikua ni majila ya saa mbili za usiku alitokea Mariamu na kumkuta Hasna akajiinamia akiwa analia kwenye chumba kile alichombiwa akae na Zuberi.
"Hasna Hasna"
Alita Mariamu kwa sauti ya chini chini.
Hasna aliinua kichwa na kumuona Mariamu.
"Vipi Mariamu hiyo safari naenda au maana umechukua kinga yangu na wewe hauonekani."
Aliongea Hasna.
Mariamu alicheka kwa sauti ya dharau.
"Hasna wewe safari yako imeishia hapa"
Alisema Mariamu.
"Mariamu mbona sikuelewi una maana gani"
Aliuliza Hasna.Mariamu alimwambia.
"Siumeoa huu msiba tuliozika Leo?"
Aliuliza Mariamu.
"Mi nimeona tu watu wengi"
Alisema Hasna.
"Sasa aliye kufa ni wewe"
"Mimi nimekufa kivipi? wakati nimeona wanosha limgomba"
Alisema Hasna.Pale alipoenda kuchungulia aliona ni mgomba.
"Hasna wewe ulitusumbua nikaona nikuingie kwa njia hiyo ili tu unipe hiyo kinga yako ilikua ninatutesa hadi tuna shindwa Fanya mambo yetu.Angalia hapo kwa ukutania kwa makini"
Mariamu alimwambia Hasna.
Hasna alikaza macho.Mara akanza kujiona Jana usiku alipo maliza kula akaingia chumbani kulala .Mara tumbo lilimshika ghafla nakuanza kumuuma akipiga kelele za kuomba msaaa.Zuberi alikuja nakuanza kumsaidia. Lakini ilishindika .
Ikabidi amkimbize hospital ,Madaktari walimpokea wanajianda kumudumia akiwa kafariki. Madaktari waliufunika mwili huo wa Hasna kisha wakatoka nje .Zuberi aliingia kama kawaida yake na kuuchapa mwili huo na mkia.huku aliongea maneno anayo yajua yeye mwenyewe. Na Hasna alianza kunyanyuka na kuacha kivuli chake kimelala.
Hasna alikua ana jiangalia jinsi alivyo kufa.
"Sasa ujanja wako uko wapi ,usinilaumu Mimi Hasna ,wakumpelekea lawama ni baba yako."
Aliongea Mariamu kisha akaondoka. Usiku ulipokuwa mkubwa Zuberi alienda kumchukua Hasna kwenye chumba alichokua kamwambia ake.
Alimpeleka kwenye chumba,walipo kuwemo wale mabinti watano pamoja na baba yake na Zuberi.
Chumba kilikua na Giza watu hawa onani,Zuberi alimtupia Hasna kwenye chumba hicho kisha akafunga na kuondoka.
Nje ya nyumba ya Zuberi shangazi yake na Hasna alimuita baba yake na Hasna pembeni wakawa wanateta jambo.
“Hivi kaka mbona umekaa kimya ,kifo cha Hasna kinakuingia akilini kweli ”.
Aliongea shangazi yake Hasna.
“Dada hivi kwanini unapenda kufikilia mambo ya kishilikina ju ya kifo cha mwanangu?,sitaki kusikia tena ujinga wako utao sababisha mwanangu asipunzike kwa amani”.
Aliongea baba yake Hasna kwa kufoka alafu a kaondoka zake akimuacha shangazi yake na Husna akimuangalia tu.
Zilipita siku tatu.shangazi yake na Hasna aliondoka na kurudi kijiji kwako.
Siku moja akiwa kalala aliona mwanga mkali sana ukiwaka chumba kwake.Shangazi yake Hasna alishituka maana ilikua usiku, lakini paling'aa kama mchana. Kidogo alianza kusikia sauti iliyo ambatana na mwangwi.
“Najua unachungu sana Rehema,Maana Hasna nimekukabizi akiwa mdogo sana.Lakini tambua Hasna yupo hai ,wala hajafa.Nakuomba usiuzunike Wifi yangu,lakini kaka yako sio mtu mzuri kueni nae makini atawamaliza wote ,kwa tamaa za madaraka ya kichawi.
Kaanza na Mimi Leo kamuuza Hasna kwa watu kwa lengo la kafara”
Ilisika sauti hiyo ikiongea kisha ikatoweka.
Ilikua ni sauti ya mama yake na Hasna.Aliyetolewa kafara miaka kumi na mbili iliyopita na mume wake.Nakipindi kaugua kabla hajafa alimuita wifi yake na kumkabidhi Hasna akiwa anamika mitano .Alimkabizi pamoja na kinga ile ili Hasna akifikisha umri wa kujitambua amkabidhi .kwa kujilinda zaidi maana Hasna alikua wa pekee.
Ndani ya kijiji hicho cha Mbika. Mila yao mtoto akizaliwa kwa uparesheni, basi anakua ni mwenye upeo mkubwa wa kufanya mambo.Na anakua na akili ya kipekee.
Watu wengi umpenda na kumuheshimu ,pia anakua kabalikiwa na mizimuu ya kabila lao.
Nahilo ndio lilofanya mama yake Hasna, kumkabidhi wifi yake kinga ile iliakikua amkabidhi.Maana watu wanaojiusisha naushilikina ,wakipata damu ya mtu huyo ufanya mambo yao yanyooke.Ndomaana baba yake alimuuza kwa Zuberi ili wawe kumchukua damu .
Basi turudi upande wa Hasna.Ilikua mida ya mchana akiwa kwenye chumba alicho fungiwa .wale mabinti watano wote walikua hawaongei walikua wamekatwa ulimi .Lakini baba yake na Zuberi pamoja na Hasna walikua bado hawaja katwa ulimi.Hivyo alikua wakiongea
Hatimaye ilifika siku ambayo ,kila mshilika wa kichawi alikua nafura , ni siku ya kwenda kumtoa kafara Hasna .Na kila mshilika anatakiwa anywe damu ya Hasna, ilikujiimalishia nguvu zake pamoja mvuto kwa jamii na mambo yeke.Pia damu hiyo ya Hasna inafanya chama chao kua na nguvu zaid ya Iluminati.
Ilikua ni kwenye ule ule mti mkubwa wa msufi.Viongozi wa chama Hicho walikua wamevaa nguo nyeupe huku wa kiwa waekaa mbele.Waliletwa mbele Hasna na Baba Zuberi. Na kiongozi moja alisimama mbele na kuanza kuongea.
"Hawa watu hatuwaweki msukule ,bali tunawatoa kafara kubwa .Damu yao tutainywa na miili yao tuyakula nyama”
Alivyoongea hivyo umati mkubwa wa washirika ulishangilia kwa nguvu na kwa sauti ya juu.
Alichukuliwa baba yake Zuberi alipelekwa mbele .Kilikua kimeandaliwa kichanja maalumu kwa shughu hii ya leo .Alipandishwa juu ya kichanja akalazwa chali.Alitwa Zuberi kisha akapewa upanga mkali na mshika mwingine alibeba chungu kilichokua kimefunikwa na kitambaa chekundu .
“CHIFU NAMTOA BABA YANGU KWAKO ,ILI KUKUZA BIASHARA ZANGU.NIWE BILIONEA ,NIHESHIMIKE MARA DUFU. TUNA KUNYWA DAMU NA KUMLA NYAMA YAKE.CHIFU BOKEA SADAKA HII.
Aliongea Zuberi kwa sauti ya juu na yenye besi.Kisha akamchinja baba yake .wakakinga damu na mwili wake waka ukata vipande vidogo vidogo,vya kuwaenea washilika .Wote
Hasna alivyo ona vile alianza kutetemeka.Naalinza kuwaza.heshima na thamni yangu ya siku nazaliwa kama mtoto wa oparesheni nakuleta faraja kwenye kijiji chetu sasa iko wapi mizimu ya mababu yote ilinijua sasa iko wapi leo nakufa kifo cha kikatili.
Hasna akiwa kwenye mawazo hayo Mara walikuja kumnyanyua na kumpelka kwenye kichanja.Walimlaza kama kawaida.
Alikuja mbelea akiwa kashika panga mkuu wa wachawi wa Naijelia mzee Okwima.
" Leo tunatoa kafara hii kwa ajili ya chama chetu .kiwe juu kupitia damu hii ya binti Hasna"
Washilika wote walipiga makogo kisha wakaina kama wanasujudu aliinuka NA kuongea lugha walio ijua wenyewe wote kwa pamoja.
Okwami alinyanyua upanga lakiwa kabla hajauwashia shingoni mwa Hasna ulitokea upepo mkali uliopeperusha watu wale na kujipigiza huna kule Mara ilisikika sauti ya ajabu ikifatiwa na mwanga mkali sana.
ITAENDELEA
tigeo0tempbe Andrea Demchuk https://www.cloudypeake.com/profile/peacockeleitahwaikikee/profile
ReplyDeleteonzansofe