Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

FATE OF LOVE - 3

   

Simulizi : Fate Of Love

Sehemu Ya Tatu (3)


Sikukawia na nilivyofika sikukuta mtu yoyote nje kwao. Muda huo nilikua na wasiwasi sana utadhani mwizi kwani nilikua naogopa pindi nitakapoonana na Aggy uso kwa uso itakuwaje.

Hodi! Hodi humu!

Nilipiga hodi lakini hakuna mtu yoyote aliyeitikia. Niliita sana lakini hali ilikua ile ile hakuna anayeitika. Nikatoa simu na kujaribu kumpigia Agness lakini nilikuta bado hapatikani. Nikajiuliza nifanye nini maana shida yangu ilikua ni kuonana na Agness. Nikaamua kukaa pale pale hadi watakaporudi kama wametoka. Nilivyoangalia maeneo ya jikoni kwao wanapopika niliona bado makaa ya moto hayajazima vizuri na nikajua kuwa muda mfupi uliopita maeneo yale kulikua na mtu. Ikanibidi niendelee kusubiri na nilikaa pale karibia dakika 50.


Wakati bado naendelea kusubiri ghafla nikamuona Halima, rafiki yake na Aggy akiwa anakuja. Alivyoniona alifurahi sana na kunifata mpaka nilipo.

Haah! Alex, mambo.

Poa tu Halima, vipi mzima wewe?

Mimi mzima kabisa hofu kwako tu.

Mimi pia nashukuru kama unavyoniona hivi.

Jamani Alex unazidi kupendeza mashaallah! Yani kama haujawahi kuishi hapa kijijini vile.

Nilitabasamu tu na kumshukuru Halima kwa sifa alizokua akinimwagia.

Vipi mbona upo peke yako hapa?

Nimeita muda mrefu sana lakini sijaona mtu hivyo nimeamua kusubiri huenda labda wenyewe watakua wametoka.

Mhh! Aggy ametoka ameenda wapi na mbona hajaniambia? Mama yake ndo hayupo tangu juzi ameenda Monga kwenye harusi hivyo tangu juzi nalala hapa na huyu bibie maana peke yake anaogopa.

Mhh! Sijui maana nimeita sana lakini nimeona kimya tu.

Halima akaniacha na kuanza kuelekea ndani huku akiwa anaita jina la Agness.

Wewe Agness! Aggy! Shoga yangu.! Hivi upo kweli humu ndani?

Alijiuliza yeye mwenyewe baada ya kuona hakuna mtu anayemuitikia. Alifungua mlango ambao kumbe ulikua haujalokiwa kwa komeo na ghafla nikamsikia anaongea kwa sauti kubwa kidogo.

Agness! Una nini shoga mbona hivyo?

Nilishtuka sana nilivyosikia hivyo na ilinibidi niinuke na kwenda mpaka ndani. Nilimkuta Aggy akiwa amejiinamia na analia sana huku jasho jingi likiwa linamtoka kwa joto la ndani kwao.

Agness! Vipi mpenzi mbona hivyo?

Nilimuuliza huku nikimshika mkono wake. Aliutoa mkono wake kwa nguvu akimaanisha kuwa nisimshike na alibaki vile vile akiwa ameinama chini huku analia.

Alex kwanini lakini unafanya mambo yote hayo na unajua kuwa kuna mtu huku anakupenda kiasi hiki? Haya ona sasa ulivyomfanya mwenzio, siku ya tatu hii hana raha kazi kulia tu sio usiku wala mchana.

Maneno ya Halima yalinifanya nijione mkosaji sana na ikanibidi nikae chini karibu kabisa na Agness kisha nikamshika tena mkono wake na kutaka kuuinua uso wake.

Alex niache!

Aliutoa tena mkono wake kwa nguvu na akazidi kujiinamia chini na kulia.

Agness mpenzi wangu tafadhali nakuomba uongee na mimi basi na kunisikiliza nina kitu gani cha kuongea.

Alex nakuomba uondoke kwetu sasa hivi kabla sijafanya kitu chochote kibaya.

Mke wangu hebu punguza hasira basi unisikilize ujue mwenzio naumia sana.

Nani mke wako? unaniita mke wangu halafu unaenda kuwapa mimba wanawake wengine. Kawaite hivyo hao wanawake zako.

Aggy hebu punguza hasira basi tuongee.

Uongee na mimi kitu gani? Kuna kipi nisichokijua? Unataka kunidanganya au?

Sio kukudanganya nataka nikueleze kila kitu kilichotokea.

Sitaki kusikia maelezo yoyote kutoka kwako. Nenda kwa huyo mwanamke wako na mkailee mimba yenu mimi na wewe basi tena.

Aggy hebu usiongee hivyo bwana ujue unaniumiza sana.

Alex, mimi na wewe nani kamuumiza mwenzake? Nimekaa kijijini huku muda wote huu nakuwaza wewe tu na sijawahi kukusaliti hata siku moja japokua natongozwa mara kwa mara. Lakini wewe umeenda mjini huko umeanza kushika shilingi mbili tatu, zipu tena imekua haifungi. Umeona haitoshi ukaamua kumuweka na mwanamke ndani kabisa muishi pamoja hadi umempa mimba. Hivi kukupenda kule Alex hayo ndo malipo yake? Ndo umeamua kunipiga pigo hili Alex..

Aggy alikua anaongea huku akiwa analia sana hadi na mimi nikajihisi machozi yakianza kunilenga.

Lakini ni bahati mbaya tu mke wangu mimi sikupanga kumpa mimba yule, mimi nakupenda wewe tu mke wangu.

Hukupanga kumpa mimba? Na mlivyokua mnavuliana nguo kila siku mlitegemea nini?

Aggy please naomba unielewe mke wangu mimi sijakusudia kufanya yote hayo ni shetani tu amenipitia.

Alex usinifanye mtoto mdogo shetani huyo ni shetani gani unayemsingizia kiasi hiko? Mnatongozana, mnavuliana nguo, mnaingiliana, mnarudia tena, unapanga chumba na mnaishi pamoja, unampa mimba, bado tu ni shetani huyo?

Kusema ukweli niliishiwa maneno kabisa kwani Aggy alikua akiongea point tupu hadi nikajiona mjinga sana.

Sikiliza Alex, kuanzia sasa hivi naomba usahau kabisa na uanze kuishi bila mimi. Siwezi kuwa na mtu ambaye najua ana mwanamke mwengine na wanategemea kupata mtoto, Hivi nitakua mtu wa aina gani mimi?

Lakini mimi sina mpango nae huyo mwanamke mimi nataka kuishi na wewe tu hata hata ukitaka tuondoke leo hii.

Alex usinifanye mimi mtoto mdogo na kunidanganya kwa pipi. Mbona siku zote hizo haukuwahi kuniambia tuondoke wote? Sikiliza, naomba uondoke nyumbani kwetu mara moja Alex sitaki kukuona tena maumivu uliyonipa yanatosha niache niuguze kidonda changu.

Nikamuona sasa yupo serious na suala la kuachana kwani alikua hatanii hata kidogo. Ghafla nikajikuta kidume naanza kuangusha kilio bila kutarajia huku muda wote huo Halima akiwa yupo pembeni anatuangalia tu.

Agness, please naomba usiniache mpenzi wangu, nakuomba.

Alex nimesema ondoka sitaki kukuona.

Sasa mimi niondoke niende wapi Agness, nionee huruma mke wangu bado nakupenda sana.

Alex. Ondoka.

Nikamuona Aggy nae akianza kuangusha upya kilio huku akinisisitiza niondoke nyumbani kwao.

Agness niangalie usoni unione ninavyotia huruma. Nakupenda sana mke wangu.

Alex sitaki nimesema ondoka.

Aliongea huku akiwa ananitazama usoni na kuzidi kulia sana hadi rafiki yake Halima ikabidi aingilie kati.

Alex, naomba uondoke tafadhali hapa hamuwezi mkaelewana kitu.

Naumia sana Halima, naumia.

Naelewa lakini inabidi ukubaliane na hii hali unayoina. Aggy ana hasira na wewe sana hivyo sidhani kama kwa muda huu unaweza kumwambia neno lolote lile akakuelewa.

Niliendelea kulia sana kama dakika tano nzima huku nikiwa siamini kile kinachotokea mbele ya macho yangu. Sikuwa na jinsi, taratibu nikaanza kuinuka na kutoka nje kinyonge sana.

Nitakupenda siku zote za maisha yangu Agness, wewe ndo mwanamke wa ndoto zangu.

Agness alikua analia sana na hakutaka hata kuniangalia. Nikatoka nje na kuanza kuondoka kurudi nyumbani kwetu.


Hakuna siku niliyowahi kuwa na huzuni, kukosa nguvu na kujihisi mpweke sana kama siku hiyo kwani nilivyofika nyumbani moja kwa moja nikapitiliza chumbani kwangu ambapo nilijifungia na kulia sana.............



Nililia sana utadhani mtoto mdogo kwani nilikua siamini kabisa kama ndo nimetoka kuachana na Agness, mwanamke wa ndoto zangu ambaye ndo niliyepanga nije kumuoa. Nililia sana hadi nikamsikia mama akiwa ananiita lakini sikutaka kabisa kutoka. Nikakumbuka sana yale maisha tuliyokua tunaishi kabla ya mimi sijaondoka kwenda mjini jinsi tulivyokua tunapendana. Japo kwa wakati huo nilikua sina kitu na maisha yangu yalikua duni sana, Agness hakuwahi kunichoka hata mara moja na aliwakataa wanaume wengi sana wanaojiweza kifedha kwa ajili yangu. Tulishafanya vitu vingi sana pamoja na ilifika kipindi nikawa naamini hata iweje mimi na Aggy hatuwezi kuachana. Sio siri tulikua tunapendana sana na watu wengi pale kijijini walilifahamu hilo. Hizo kumbukumbu ndo zikazidi kunitoa machozi na kujikuta nimepoteza mtu wa muhimu sana kwenye maisha yangu. Niliwaza sana hadi nikaja kupitiwa na usingizi bila kujitambua.

Nilikuja kushtuka jioni sana jua likiwa limeshazama na giza kuanza kuchukua nafasi yake. Nilitoka nje na kukuta kumepoa sana hakuna kabisa pilika pilika za watu. Nikapata wazo la kutafuta vijana wawili wa kulinda gari ili isije ikaibiwa tena vifaa kwa mara ya pili. Nilienda kwenye maskani ambayo nilikua napenda kukaa zamani na kuwakuta baadhi ya washikaji zangu wakiwa wanapiga story.


Walivyoniona walifurahi sana na nikasalimiana nao wote. Tuliongea mambo mengi sana huku nikijilazimisha kucheka lakini moyoni na akilini nilikua sipo sawa hata kidogo. Nikivyoona nimezuga zuga nao kama robo saa hivi nikawaeleza shida yangu ya kutaka watu wawili wa kulinda gari mpaka asubuhi na walivyosikia kuna elfu 10 kwa kila mmoja wakaanza kugombaniana sana. Nikawachukua wawili kisha wengine watatu nikawaachia kila mmoja shilingi elfu 5 ya soda na walinishukuru kupita maelezo maana maisha ya pale kijijini elfu 5 ilikua ni zaidi ya hela. Nikawaaga na walinishukuru mara tatu tatu kwa pesa ile niliyowapatia. Tulienda mpaka nyumbani na kuwakabidhi jukumu lile la kulinda gari na waliweza kunielewa vizuri. Waliondoka na kuniahidi watarudi baada ya kama lisaa limoja ili wakale chakula pamoja na kuchukua silaha za kwenye lindo lao. Tulielewana wakaondoka na mimi nikaingia ndani ambapo nilimkuta mama akiwa sebuleni anaangalia taarifa ya habari. Nilienda kukaa naye na baada ya muda akaniuliza imekuaje nilivyoenda kwa kina Aggy. Nilimueleza kila kitu kilichotokea na hakuamini kabisa kama ni kweli.

Yani Agness huyu ndo amekufukuza na hataki tena kukuona?

Ndio mama.

Mhh! siamini. Itakua amekasirika sana maana ninavyomjua jinsi anavyokupenda asingeweza kufanya hivyo.

Nimejaribu kila njia kumuomba msamaha na hakunielewa hata kidogo na kunitaka nimsahau kabisa.

Mhh! Pole sana mwanangu. Lakini na wewe umemkosea sana kwanini usingekuwa mvumilivu hadi ukaja kumuoa na mkaishi wote?

Weacha tu mama yani hata sijui imekuaje.

Basi kwa kuwa yameshatokea inabidi kukabiliana nayo tu. Kitu kikubwa inabidi usife moyo tu uendelee kumuomba msamaha maana naamini kwa sasa ni hasira tu ndo zimemtawala.

Sawa mama nimekuelewa na nashukuru sana.

Tuliongea mambo mengi sana na mama akamuulizia huyo mwanamke niliyempa ujauzito kutaka kumjua sifa zake na maisha yake kwa ujumla. Nilimueleza kila kitu na mwisho akanisihi kuwa nisimtelekeze na wala nisimtelekeze mtoto wangu kwani nitakua nimefanya kosa kubwa sana ambalo hata Mungu halipendi. Kiukweli maneno ya mama kidogo yalinifariji na baada ya kula chakula nikaagana nae na kuingia chumbani kwangu. Huko mawazo yote yalikua kwa Aggy yani hadi muda mwengine nikijihisi kuchanganyikiwa Nikaona chanzo cha matatizo yote yale ni Vanessa kumtumia Aggy meseji na nikajikuta namlaumu sana na kumchukia japo tayari nilishamsamehe. Niliwaza sana hadi nikaja kupitiwa na usingizi usiku mwingi sana.


***************** ******************


Kesho yake nilianza safari ya kurudi Dar nikiwa mnyonge sana baada ya Agness kunipiga chini. Nilivyofika Tanga mjini nikanunua tairi na kuifunga maana nilikua natembea na spea tairi. Njiani nilikua na mawazo sana kiasi kwamba ilibaki kidogo sana nisababishe ajali maeneo ya Kabuku. Nilifika salama Dar na moja kwa moja nikaenda nyumbani kwangu. Muda wote huo tangu niende hadi narudi nilikua sijawasiliana na Vanessa kwani nilimpigia marufuku asinipigie simu wala kunitumia meseji nikiwa kijijini kwetu.

Haah! mume wangu, karibu sana.

Nilimtazama huku moyoni nikiwa najisemea angejua alivyoharibu huko.

Sawa asante, vipi za hapa?

Nzuri tu, sijui huko.

Huko hovyo tu.

Kwanini? Nini tatizo?

Uliyoyataka yametimia.

Niliyoyataka yametimia? Una maana gani unaposema hivyo?

Nimeachana na Agness.

Vanessa alibaki akiniangalia tu usoni na kukaa kimya.

Ndio, si ndo ulivyotaka?

Alex! Usiseme hivyo tafadhali. Sawa i was stupid enough ( Nilikua mjinga vya kutosha ) kumtumia Agness zile meseji but i feel bad for this ( lakini najihisi vibaya kwa hili)

Bad? ( Vibaya? ) kwahiyo ulivyotuma zile meseji ulitegemea nini?

Alex, don't be mad at me please (Alex, usinikasirikie tafadhali) naomba unisamehe. I need peace. ( Nahitaji amani )

I'm not mad at you, at all ( Sijakukasirikia, kabisa) ila nilitaka nikwambie ukweli tu.

Vanessa alikua ananiangalia sana kwa sura yake nzuri utadhani chocolate za vanilla.

Nataka nikuahidi kitu Alex.

What is it? (Kitu gani hiko?)

Najua siwezi kuwa Agness na wala siwezi kufanya mambo ambayo Agness alikua anakufanyia kwa sababu mimi ni Vanessa. I'm different kind of person. (Ni mtu wa aina ya tofauti) Ninachokuahidi ni kuwa i'll be the next woman of your dreams (Nitakua mwanamke wako ninayefuata wa ndoto zako) I promise to love you for the rest of my life. (Ninaahidi kukupenda kwa maisha yangu yote yaliyobaki)

Vanessa aliongea maneno ambayo yalikua na hisia sana kitu ambacho hata sikutegemea.

Mmmm! that's very sweet poem (mmmm! shairi zuri sana hilo)

Poem? Are you kidding me? (Shairi? unanitania?)


Tulijikuta tunaanza utani wa mapenzi na Vanessa alinisindikiza mpaka chumbani kuweka mizigo yangu. Tuliongea sana huku akizidi kunipa ahadi nyingi sana juu ya penzi letu huku na mimi nae nikiwa nimeshampokea kwa mikono miwili baada ya kuona Agness hanitaki tena.


************** ***************


Bado hisia za kuachana na Agness zilizidi kuutafuna sana ubongo wangu kwani kuna muda nilijikuta nikiacha kazi zangu na kumfikiria yeye tu. Kwa kauli alizozitoa, Aggy alimaanisha kweli tuachane hivyo nilijikuta nashindwa hata kufanya jitihada yoyote. Sikua na jinsi hivyo ilinibidi nianze kuizoea ile hali na kuanza kuishi bila yeye.

Nyumbani maelewano na Vanessa yalirudi na tukawa tunaishi kwa furaha kama mwanzo huku nikiwa na shauku kubwa ya kumuona mtoto wangu pindi atakapozaliwa. Vanessa alikua ananipenda sana mpaka na mimi nikajikuta nikiwa nimezama kwenye penzi lake bila kutegemea.

Siku moja ya Jumapili nilitoka na Vanessa na kwenda nae shopping kama kawaida yake maana alikua hataki kupitwa na nguo mpya. Tulienda maeneo ya Mayfair Mikocheni na tukawa tunazunguka madukani.

Hiyo usiiache baby itakupendeza sana kwenye mtoko wa jioni.

Kweli eeh?

Yaah!

Vanessa alikua anachagua nguo huku nikiwa namsaidia pamoja na kumpa ushauri ipi inafaa na ipi haifai. Tulikua tunafanya kazi ya kuhama maduka tu maana sehemu nyengine alikua hapati nguo anazozitaka. Tuliingia duka moja ambalo lilikua kubwa sana na lilikua karibia na kila kitu kinachohusika na mavazi na nilimuona Vanessa akikimbilia upande alioona gauni ambalo alikua akilitafuta sana. Nilisimama tu nikiwa namtazama akiwa analipima kwa kulilinganisha na mwili wake. Vanessa alipenda nguo kuliko kitu chochote na kwa hilo alionekana waziwazi.

Wakati bado tunaendelea kuchagua nguo nikasikia sauti ambayo kama naifahamu hivi na ilibidi nigeuke nyuma.

James!

Alex!

Ooh! my God! I can't believe. (Ooh! Mungu wangu, siwezi kuamini) James ndo wewe kweli?

Nilimfata na kumkumbatia kwa nguvu mpaka baadhi ya watu wakawa wanatushangaa.

Alex! Siamini macho yangu, ndo umekua hivi kaka?

Hakika wote tulikua na furaha iliyozidi kifani kwani ulipita takribani mwaka mmoja mimi na rafiki yangu James tukiwa hatujaonana. Mara ya mwisho nilimuacha kijijini lakini nilivyorudi mara tu baada ya kutoka kupata ajali sikukumkuta na nilivyouliza nikaambiwa kuwa aliondoka bila kumuaga mtu. Tangu wakati huo hatukuonana tena hadi tulivyokutana hapo.

Vipi James, habari za siku nyingi rafiki yangu?

Nzuri tu Alex, yani siamini hata kidogo kama tumekutana tena kwenye mazingira kama haya.

Hata mimi pia James, vipi unafanya nini hapa?

Hapa ndo kazini kwangu Alex, nipo hapa takribani mwezi wa nne sasa.

Hebu ngoja kwanza, imekuaje mpaka umefika hapa?

Ni story ndefu sana ndugu yangu ila ni jambo la kumshukuru Mungu sana. Naomba chukua namba yangu nitakutafuta na kuongea.

Kweli tukabadilishana namba na kuisave.

Nilimuita Vanessa na kuja kumtambulisha kwa James.

Vee, meet my very best friend (Vee, kutana na rafiki yangu sana) anaitwa James. Tumekua wote na kusoma wote kule kijijini kwetu.

Okay James, nafurahi sana kukufahamu.

Mimi pia nimefurahi sana kukufahamu.

James, huyu ni mchumba wangu anaitwa Vanessa.

Sawa, nimefurahi sana kukufahamu shemeji.

Mimi pia shemeji, karibu sana kwetu.

Asante usijali nitakaribia.


James alikua anaongea lakini nilimuona waziwazi kuwa ule utambulisho hakuuelewa elewa vizuri maana mara ya mwisho tunaachana nilikua nipo na Agness.

Sawa shem ngoja niwaache bado naendelea kuchagua nguo.

Sawa shem asante sana.

James alijibu huku akiwa anamuangalia sana Vanessa kisha akanigeuzia jicho mimi.

Alex, imekuaje? Vipi kuhusu Agness?

Ni story ndefu sana James nafikiri siku tukikutana tena tukiwa na nafasi ndo tutaongea vizuri.

James hakusema kitu na akarudia tena kuendelea kumtazama Vanessa.

Vanessa alimaliza kuchagua vitu vyote alivyovitaka na nikaenda kuvilipia. Tulimuaga James na kuahidi tutakua tunawasiliana.


Wakati tupo njiani tunarudi nyumbani nilisikia simu yangu mfukoni ikiwa inaita. Kwa kuwa nilikua naendesha gari sikutaka kuipokea hivyo niliiacha iite mpaka ikakata. Mara ikaanza kuita tena na nilipoona nimefika sehemu iliyokuwa na mataa ya trafiki niliamua kuitoa na nilipoangalia nikaona namba ngeni ambayo hata sikuifahamu.......




Muda huo Vanessa alikua yupo busy kujipiga picha pamoja na kuchukua video kwenye simu yake. Nikaipokea na kuanza kuongea.

Hello.

Hello.

Naam habari.

Nzuri, mimi Winnie.

Aanha Winnie, vipi mzima?

Ndio mzima. Upo wapi mbona kuna kelele?

Nipo barabarani naendesha gari nikifika nitakupigia.

Sawa, baadae.

Okay.

Winnie alikata simu na nikaiweka simu yangu pembeni.

Nani huyo uliyekua unaongea nae?

Ni mtoto wa boss wangu anaitwa Winnie.

Mhh! wewe na hao watoto wa boss wako.

Nini sasa, umeshaanza eeh!

Mmm! Wewe haya tu.

Punguza wivu wewe mwanamke.

Vee hakujibu kitu na aliendelea kupiga picha.

Tulifika nyumbani na Vee akashuka kwenye gari lakini mimi nikabaki nikajifanya kama kuna kitu nakitafuta. Nilivyoona ameshaingia ndani nikatoa simu yangu na kupiga namba aliyonipigia Winnie.

Eeh Winnie vipi?

Poa tu. Umeshafika nyumbani?

Ndio ndo nimeingia sasa hivi hapa hata kwenye gari sijashuka.

Sawa. Sasa Alex mimi wiki ijayo naondoka shule, inakuwaje kuhusu ule mpango wetu.

Mmhh! Winnie yani bado hujasahau tu?

Wee! naanzaje kusahau na unajua jinsi gani ny*g* zilivyonijaa.

Wewe mtoto wewe! haya tu. Kwahiyo unataka twende siku gani?

Nakusikiliza wewe tu ndo unakua upo busy mimi muda wote nipo free.

Sawa, kwani hii namba ni ya nani?

Ya kwangu nimenunua simu natumia kwa siri sana baba na mama wasijue.

Angalia Winnie usije ukashikwa, kuwa makini.

Usijali Alex kwa hilo nipo makini sana.

Sawa basi katikati ya wiki hapa nitakutafuta.

Poa, yani ulivyoniambia hivyo hadi mwili nahisi unanisisimka hapa.

Acha maneno yako wewe mtoto. Sasa mimi naingia ndani maana huyu mwanamke ana wivu sana asije akanifata huku huku nje.

Mhh! Huyo nae anajiona kama amekuumba yeye vile.

Nilicheka sana na kukata simu kisha nikashuka na kuilock gari. Niliingia ndani na kumkuta Vee anajaribu nguo alizozinunua na nilimkuta akiwa amebaki na ch*p* tu na sidiria. Ghafla nikajikuta mtalimbo unaanza kuinuka kwani Vee alikua na umbo zuri sana na uzuri wake ulizidi kunogeshwa na rangi yake nyeupe aliyokua nayo. Hapo hapo kidume nikamsogelea na kuanza kumshika shika huku nikimlamba lamba shingoni.

Mmhh! baby, wait. (mmhh! baby, subiri)

Sikumsikiliza na nikaendelea na uchokozi ambapo baada ya muda nikaona Vee nae akinipokea na kuanza kunipa ushirikiano. Tulibadilishana mate kwa hisia sana huku tukiwa tumesimama. Vee alikua mfupi kidogo kwangu na ilibidi achuchumie ili aweze kunifikia vizuri mdomoni. Wote tukajikuta hisia zimeshatuamka na kilichofata baada ya hapo ni kupeana raha tu huku kama kawaida nikimpatia Vanessa dozi yake ya kutosha iliyokua inamfanya awe na wivu kama mnyama Nyegere (Honey Badger) kwani mnyama huyo muda wote hutembea nyuma ya mke wake kulinda sehemu zake za siri na ikitokea hata jani likagusa sehemu za siri za mke wake basi hilo jani litararuliwa mpaka litajuta kwanini liliota. Tulipeana raha sana na Vanessa alifurahi sana.


*************** ***************


Kweli ilivyofika katikati ya wiki nikamtafuta Winnie na kama kawaida tukaenda chaka letu lile lile ambalo tulikua tunaenda siku zote. Tulimkuta jamaa yule yule na kwa bahati nzuri bado alikua hajatusahau kwani siku zote huwa namuungia hela ili aniruhusu niingie na Winnie ambaye alikua yupo chini ya miaka 18. Tuliingia mpaka ndani na kuagiza chakula maana wote tulikua na njaa sana. Tuliletewa na kula hadi tukamaliza. Kumaliza tu nikamuona Winnie anaanza kuvua suruali aliyokua ameivaa pamoja na blauzi. Akabaki na kufuli tu kwani siku zote alikua havai sidiria maana matiti yake bado yalikua hayajakua vizuri na yalisimama barabara. Kama kawaida bwana mkubwa ngobeko akishaona vitu vyake hana stamala kwani suruali ilianza kutuna taratibu. Winnie alinipa mgongo na kuanza kutembea kuingia chooni. Sio siri Happy na Winnie walirithi mgongo kutoka kwa mama yao kabisa kwani walikua na makalio yaliyobinuka sana na malaini kiasi kwamba yalinitoa udenda. Na mimi sikukawia, nikavua nguo zangu zote na kubaki kama nilivyozaliwa na nikamfuata Winnie chooni. Alivyoniona aliachia tabasamu na kuzifanya lipsi zake zizidi kuvutia maradufu. Nilimsogelea na kuanza kubadilishana nae mate huku tukiwa tunapapasana mwilini. Aliishika dunguso yangu na kuisugua sugua na mkono wake. Nilipata raha sana hadi kidume nikawa natoa miguno. Tuliogeshana huku tukiwa tunachezeana sana hadi kila mtu akawa teketeke.


Tulivyorudi ndani tu sikumchekewesha kwani nilianza kumpelekea moto wa kufa mtu hadi akaanza kutoa vilio vya kila aina. Kilichonishangaza ni jinsi Winnie alivyokua fundi tofauti na mwanzo kwani alikua akinizungushia kiuno utadhani mtu mzima vile. Sio siri alinipa stimu sana na kunifanya nizidi kumpa dozi kali hadi akawa anavunja dafu. Alinibadilishia mikao ya kila aina hadi mtu mzima nikapagawa na kujiuliza mtoto kama yule amejifunzia wapi michezo ya hatari kama ile. Baada ya safari ndefu ya kisiwa cha maraha tulifika salama mwisho wa reli na wote tukawa kimya.

Niliinuka na kwenda chooni kujiosha kisha nikarudi tena chumbani.

Winnie hii michezo umejifunzia wapi wewe mtoto mbona umekua fundi kiasi hiki?

Winnie alicheka sana na kunivuta dunguso yangu kisha akanijibu.

Wewe usitake kujua, ila nimejifunza yote haya kwa ajili yako tu maana siku ile ulinionea sana hadi nikaondoka siwezi kutembea vizuri.

Wewe mtoto wewe, aah! hapana. Naona unataka kumzidi mpaka dada yako sasa.

Winnie alicheka sana. Aliinuka na kwenda chooni kujiosha kisha akarudi tena chumbani. Siku ile tulipelekeshana sana huku Winnie akizidi kunionyesha ufundi hadi nikajikuta napiga nyayo nne bila kutarajia.


**************** ***************


Wikiendi nikamuita rafiki yangu James nyumbani kwangu ili aje kunitembelea pamoja na kuongea maana ni siku nyingi sana tulikua hatujakaa pamoja.

James karibu sana mshikaji wangu hapa ndo ninapoishi.

Aisee Alex hongera sana mshikaji wangu, dah! Imekuaje mzee hadi muda mfupi tu hivi unaishi vizuri kiasi hiki?

Acha tu ndugu yangu yani ni jambo la kumshukuru Mungu sana mpaka hapa nilipofika maana sikutegemea kabisa kama ndani ya muda mfupi tu nitapiga hatua kiasi hiki.

Hebu nipe siri ndugu yangu imekuaje?

Aah aah! Ngoja kwanza na mimi nataka kujua imekuaje na wewe mpaka umefika huku Dar na unafanya kazi kwenye duka kubwa kiasi kile.

Acha tu kaka ni kuhangaika pamoja na kumuomba sana Mungu. Siku ulivyoondoka tu kijijini nilijikuta na mimi napata wazo la kuondoka maana maisha yalikua ni magumu sana. Kweli baada ya kama wiki mbili niliondoka na sikumuaga mtu yoyote. Moja kwa moja nikaenda mpaka Tanga mjini kwenye soko la Ngamiani na kuwa mbeba mizigo (Kuli). Niliifanya hiyo kazi huku muda wote huo nikiwa nalala nje tu kwa kutandika mabox na viroba chini maeneo hayo hayo ya sokoni. Kwa bahati nzuri alitokea dada mmoja mtu mzima ambaye tulikua tumezoeana akaniambia kuwa ana ndugu yake anahitaji mtu wa kumuuzia duka lake la nguo na anahitaji mtu muaminifu sana. Nikamuhakikishia kuwa hiyo kazi naiweza na nitakua muaminifu sana. Kweli akanipeleka na kuanza kazi huku nikiwa naishi nyumba ya ndugu yake huyo mwenye duka kwani sikua na sehemu ya kukaa. Nilifanya kazi kwa bidii sana na kwa uaminifu mkubwa kiadi kwamba boss wangu alitokea kunikubali sana. Baada ya kufanya kazi kwa takribani miezi mitano kwenye hilo duka ka Tanga mjini, ndo nikahamishiwa hili duka la sasa hivi ulilonikuta pale Mlimani City na nashukuru nimepanga chumba kimoja maeneo ya Kinondoni Studio.

Daah! Kweli Mungu mkubwa ndugu yangu. Huwezi kuamini ninakuulizia sana kila ninapoenda kijijini hadi nikaanza kukata tamaa kuwa hatutoonana tena. Kwahiyo kijijini ndo haurudi tena.

Hapana, hivi tunavyoongea Jumamosi ya wiki ijayo ndo ninaenda yani hata sijui ndani kwangu pako vipi.

Pako fresh tu ila nahisi kutakua na vumbi la kufa mtu maana ni siku nyingi sana.


Tuliongea mambo mengi sana hadi chakula kilipoiva ambapo Vanessa alikuja kutuita. Nilimkaribisha James na wote watatu tukaungana kula pamoja.

Wakati tunaendelea kula nikaona simu yangu inaita na nilivyoiangalia nikaona Happy ndo ananipigia. Nilimtazama Vee ambayo nae alionekana kuwa makini na simu yangu kusikilizia ni nani anayenipigia..........




Nilitamani hata kuikata ile simu ila nikaona ndo nitazidi kuharibu maana Vee na Happy walikua hawaelewani hata kidogo. Nikaamua niipokee tu na nimsikilize anasemaje.

Hello.

Alex mambo vipi?

Poa tu, mzima wewe?

Mimi mzima sijui wewe.

Niko poa kabisa, niambie.

Uko wapi?

Nipo nyumbani kwangu.

Unaweza kuja huku hostel leo hii?

Kuna nini?

Kuna kazi nataka unisaidie peke yangu siwezi.

Kazi gani hiyo?

Nakuomba njoo tu utakuja kujua huku huku.

Mhh! Sasa hivi nina mgeni nyumbani kwangu siwezi kutoka.

Hata jioni au usiku wewe njoo tu.

Sawa nitakupigia baadae kidogo.


Tulielewana na Happy akakata simu. Nikawa nampiga jicho la wizi Vee huku nikimsikilizia atasemaje. Alijifanya yupo busy na chakula lakini nikajua tu kwamba akili yake yote ipo kwangu. Tuliendelea kula hadi tukamaliza na Vee akatoa vyombo vyote na kusafisha. Akatuaga kuwa anaingia chumbani kupumzika maana alichoka sana kwa kazi ukijumlisha na ujauzito aliokua nao.

Eenhe! niambie sasa ndugu yangu maana mpaka muda huu nipo njia panda kuhusu Aggy pamoja na maisha yako yote hadi umefika hapa.

James ndugu yangu nimeamini kuwa mambo mengi sana yanaweza kutokea ndani ya mwaka mmoja.

Kwanini unasema hivyo?

Hivi tunavyoongea hapa mimi na Aggy tayari tumeshaachana.

Aah! Alex hebu acha masihara bwana.

Kweli James, mimi na Aggy tumeachana.

Daah! Lini na kwanini?

Niliguna kidogo kisha nikaanza kumuhadithia kila kitu kilichotokea na sikuacha hata nukta moja. Pia nilimsimulia jinsi nilivyokutana na David hadi akanisaidia kubadilisha maisha yangu kiasi kile.

Kwahiyo ndo hivyo James nimejitahidi sana kumuomba radhi Aggy lakini hajanielewa hata kidogo.

Daah! Pole sana ndugu yangu naelewa ni jinsi gani inauma kuachana na mpenzi wako wa siku nyingi na mnapendana.

Asante sana James.

Unajua sio mahusiano yote yamepangwa yaishie kwenye ndoa hivyo mkiachana kama hivyo inabidi ukubaliane na ukweli tu na maisha yaendelee.

Upo sahihi sana rafiki yangu. Nimeumia sana na sasa angalau nimeanza kusahau. Siku zote Aggy ataishi moyoni mwangu ila inabidi maisha yaendelee.

Kweli kabisa Alex, pole sana. Changamoto kama hizi ndo zinatufanya tukue na tuzidi kuwa imara.

Kweli ndugu yangu.

Tuliongea sana mpaka jioni ambapo James aliniaga kuwa anarudi kwake anapoishi. Nilimuamsha Vanessa ili waagane kisha tukatoka nje.

Baby ukirudi naomba uje na chipsi kuku pamoja na matunda maana yameisha kwenye fridge. Weka ndimu na ukwaju mwingi sana.

Sawa mke wangu nimekuelewa.


Tuliingia ndani ya gari na nikampeleka hadi kituo cha bodaboda. Nikamkodia bodaboda kisha nikampa kiasi cha shilingi elfu 50 ili afanyie nauli pamoja na kumsaidia siku mbili tatu. James alinishukuru sana na tukaagana kisha akaondoka. Nilitamani sana kumpeleka mpaka kwake na nikapafahamu ila niliona muda umeenda sana kwani nilikua na safari ya kwenda Mwenge anapoishi Happy. Kutoka Sinza Mori hadi Mwenge hapana umbali kabisa hivyo baada ya muda usiozidi robo saa nikawa nimeshafika.

Nilikuta watu kadhaa wakiwa wamekaa nje ya nyumba anayoishi Happy na nikaona nimpigie simu maana nilikua siwafahamu wale watu.

Eeh! Alex vipi?

Poa, mimi nipo nje hapa.

Sasa si uingie ndani!

Njoo unichukue bwana hapa nje kuna watu wamekaa.

Sasa unaogopa kitu gani?

Hebu acha maswali yako nimekwambia njoo.

Happy akakata simu na baada ya kama dakika 3 nikamuona akiwa anakuja.

Yani wewe bwana, sasa unamuogopa nani hapa?

Naogopa nisije nikapigiwa kelele za wizi.

Huyo mtu atakayekuita mwizi si atakua hana akili timamu, yani huo muonekano wako kweli uitwe mwizi?

Nikalock gari kisha tukaongozana mpaka ndani.

Karibu sana Alex, yani nimekumisije!

Asante Happy, mimi pia nimekumiss sana.

Nilikaa kwenye sofa na Happy akaenda kuniletea juisi.

Mbona umenisusa kiasi hiko Alex yani hadi nimekuita ndo umekuja?

Hamna bwana tatizo ni kwamba nipo busy sana yani sipati hata muda wa kutembea.

Mhh! busy hadi wikiendi jamani.

Wikiendi si unamjua wifi yako lakini anavyojua kukaba mpaka penati. Hii sasa hivi yenyewe nimetoka anajua nimemsindikiza mgeni lakini bila hivyo asingekubali au angetaka tutoke wote.

Mhh! huyo nae kazidi sasa anafanya kama kakuumba yeye vile.

Nilicheka sana kwa maneno aliyokua anaongea.

Vipi boyfriend wako hajambo?

Mmmm! tukiwa mimi na wewe naomba tusiongee habari za boyfriend wangu.

Kwanini sasa?

Basi tu sipendi.

Eeh! Haya sawa nimekuelewa. Vipi lakini huwa anakuja hapa?

Anakuja lakini mara chache sana. Mara ya mwisho ni kama wiki tatu hivi zilizopita.

Mmh! naogopa asije akanikuta hapa.

Acha kuwa muoga wewe mtoto wa kiume anatakiwa ajiamini.

Sawa lakini sio kihivyo.

Happy alicheka sana.

Eenhe haya sasa niambie umeniitia nini maana muda unazidi kwenda na yule mwanamke anajua sichelewi kurudi.

Mmhh! huyo mwanamke wako nae unamuendekeza sana yani hata usikae na watu.

Sio hivyo Happy kumbuka amenibebea ujauzito wangu yule na ninaishi naye.

Hata kama ila asikubane kiasi hiko, sisi wengine tutakupata vipi sasa?

Si ndo kama hivi mnanipata!

Nilijibu na wote tukacheka sana.

Tuache utani Happy, niambie ulichoniitia.

Alex na wewe mbona unakua hivyo? Ina maana haunijui au? Sina chochote nilichokuitia ila nilikumiss sana na niliona kila siku nikikukwambia uje kwangu ulikua unanizungusha tu.

Kwahiyo ndo umeamua udanganye kuwa umepata tatizo?

Ndio maana bila hivyo usingenielewa.

Mmhh! Yani wewe Happy wewe.

Happy alifurahi sana kwa jinsi alivyoniweza.

Ila Alex usiondoke hivi hivi tafadhali. Naomba unipe yale mambo yako maana nimeyamiss sana.

Mmh! kwani si una boyfriend wewe ina maana hakumalizii shida zako?

Sawa ninaye lakini ujuzi unatofautiana. Boyfriend wangu kwao wakishua sana yani hata mambo hayawezi vizuri amelelewa kimayai mayai sana.

Happy alinichekesha sana kiasi kwamba hadi machozi yakawa yananitoka.

Kwahiyo anakua hakuridhishi au?

Ndio, yani ananigusa gusa tu wewe ndo unanijulia vizuri Alex.

Tutafanya siku nyegine Happy sasa hivi muda umeenda sana naogopa nisije kuanzisha ugomvi kwa Vee.

Alex bwana usinifanyie hivyo please.

Happy unaelewa lakini jinsi mechi yetu inavyochukua muda mrefu si nitaondoka saa 3 hapa?

Hamna bwana tunafanya haraka haraka hatuchukui muda mrefu.


Nikamuangalia sana Happy na kuamua nimkubalie tu ili arizike niondoke. Niliinuka na kumvamia ambapo alinipokea kwa bashasha sana. Tulianza kubadilishana mate taratibu huku tukitomasana mwilini. Baada ya hapo tukaanza kusaula nguo zetu na wote wawili tukabaki watupu kama tulivyozaliwa. Nikaanza ugomvi wangu wa kumtembezea ulimi kama kawaida kitu kilichomfanya atoe vilio vya raha. Nilimnyonya sana hadi nilivyoona ameiva na kuwa teketeke tayari kwa kuliwa. Sikumpa nafasi hata kidogo afanye mambo yake kwani nilimuweka vizuri na kuanza kumpelekea moto. Happy alikua mtamu sana kiasi kwamba mzuka ulizidi kuongezeka. Alijua kujituma na kunikatia viuno vingi sana hadi nilipagawa.. Akanibadilishia mikao tofauti huku muda mwengine akiwa anatuma salamu kidogo wakati tupo katikati ya mechi. Happy alinifanyia vitu vya kushangaza sana kiasi kwamba sikuamini kama ni yeye ndiye anayefanya. Na mimi kama kawaida nilimpa dozi yangu ile ile ambayo ilikua inamgusa barabara kiasi kwamba alikua hawezi kunisahau hata kidogo. Nilimfikisha pwani ya Mombasa kama mara mbili hivi huku na mimi nikizidi kupata utamu. Baada ya mshike mshike wa muda mrefu kidogo hatimaye tukahitimisha salama pambano letu na kutuacha wote tukiwa hoi jasho linatutoka.


Alex kwanini usiwe mwanaume wangu lakini tukaishi wote?

Happy unajua kabisa kama hiko kitu hakiwezekani. Hivi kwa jinsi nilivyo kwenu ninawezaje kuishi na wewe? Haya ninayofanya tu najiona kabisa kama nakosea.

Sasa kikwazo kipo wapi? Kwani mimi na wewe tumezaliwa pamoja?

Hata kama Happy ila mimi na wazazi wako tunaheshimiana sana na nahisi hata wao watanishangaa sana wakisikia kitu kama hiko.

Mmhh! hamna lolote hutaki tu.

Nilibaki kimya ila kiukweli sikutaka hata kidogo kusikia yale aliyokuwa ananiambia.

Sasa acha mimi nijiandae niondoke maana muda umeenda sana.

Mhh! ina maana haturudii tena?

Kwa leo hapana muda umeenda sana nitajikuta naondoka saa 5 hapa.

Happy alibaki akiniangalia sana huku akiwa amejifunika shuka hadi kifuani. Niliinuka nikiwa vile vile mtupu na kwenda kujimwagia maji haraka haraka kisha nikarudi na kuvaa nguo.

Sasa Happy mimi naondoka tutaonana siku nyengine.

Sawa bwana wewe nitese tu.

Sasa nikutese vipi mbona nimekupa kimoja hiko.

Sawa wewe nenda tu.

Wakati tunaongea nikasikia simu yangu inaita na nilipoangalia nikaona Vee anapiga tena video call ya WhatsApp. Nilishtuka sana na ilibidi nikimbie nje haraka haraka na kuingia kwenye gari. Simu iliita hadi ikakata na akaanza kupiga tena. Nilipoanza kuondoka nikaona niipokee ili aamini kuwa nipo njiani naendesha gari.

Hello mke wangu.

Baby, uko wapi?

Nipo Makumbusho mke wangu nilimsindika James hadi kwake ndo maana nimechelewa.

Wahi bwana mwenzio nina hamu na wewe. Halafu usisahau chipsi nilizokuagiza.

Sawa usijali nafika muda sio mrefu.

Sawa mume wangu take care, i love you ( Kuwa mwangalifu, nakupenda )

I love you too baby. ( Nakupenda pia baby )

Vanessa alikata simu na kunifanya nipumue kidogo.

Nilipitia kumnunulia vitu vyake alivyovitaka kisha nikarudi nyumbani.


*************** ***************


Ilipita miezi 6 na mimba ya Vanessa ilikua kubwa sana kiasi kwamba kila siku nilikua nikimpeleka na kumpitia jioni kazini kwake turudi wote nyumbani. Ilishafikisha takribani miezi 7 na alikua amechoka sana hadi muda mwengine nikawa namsaidia kazi za ndani kama kupika na kuosha vyombo pamoja na usafi. Vanessa alikua ananipenda kupita maelezo na alikua na wivu kumzidi mnyama Nyegere kwani mara nyingi akiona hazielewi nyendo zangu basi ni lazima atanipigia kwa video call. Bado niliendelea na kamchezo kangu ka kujiibia kwa Happy na mama yake na mpaka muda huo hakuna hata mtu mmoja aliyeshtukia. Happy alipunguza kidogo kunisumbua na nikajua ni kwa sababu ya huyo boyfriend wake aliyempata japo mwenyewe alikua anadai kuwa hamridhishi vizuri. Janeth ndo alikua ananisumbua sana na mara kadhaa tulikua tunajiibia na kwenda hotelini kama kawaida yetu. Mjengo wangu ninaoujenga Mbezi nao ulizidi kusogea taratibu na nilikua natunza hela sana ili nitimize lengo langu.


Siku moja wakati nipo kazini James alinipigia simu.

Vipi mshikaji wangu?

Poa tu James ndugu yangu niambie.

Hivi umepata taarifa zozote kuhusu Agness?

Agness? Taarifa gani hizo?....


Agness ameolewa bwana.

Unasema? Amefanya nini?

Agness ameolewa ndugu yangu.

( Niliuhisi mwili kama sio wa kwangu kwa jinsi ulivyonyong'onyea )

Hebu ngoja kwanza James. Unamaanisha Agness yupi?

Agness huyu huyu unayemfahamu aliyekuwa mpenzi wako.

Agness! Aah hapana.

Huo ndo ukweli Alex.

Nani huyo aliyemuoa na wewe umesikia kwa nani?

Ameniambia Dullah yule jamaa kule kijijini anayeuza duka pale kwa mzee Mwadibwa niliongea naye leo hii asubuhi.

Na ni nani huyo aliyemuoa?

Kwa jinsi alivyoniambia alisema yeye hamfahamu huyo mtu ila amesikia tetesi tu juu juu kuwa anatokea Tanga mjini na ndo wameenda kuishi huko.

Hapana siamini, yani Agness aolewe na mtu mwengine kweli na aniache mimi.

Ndo hivyo ndugu yangu inabidi ukubaliane na ukweli tu haina jinsi.

Hapana James, Agness ni mwanamke wangu yule na mimi ndo nilipaswa nimuoe.

Alex hebu punguza munkari. Nakuomba utulie na usifanye kitu chochote cha kijinga. Pumzika na upate muda mzuri wa kutafakari hili.

James unafahamu lakini kama Aggy ndo mwanamke wa ndoto zangu.

Nafahamu Alex ila naomba tulia kwanza kwa sasa. Tangu asubuhi nilitaka kukutaarifu ila nilijua tu kuwa itakuathiri kisaikolojia.

Agness, why? why Agness? ( Agness, kwanini? kwanini Agness? )

Alex hebu jikaze kiume bwana najua ni jinsi gani unaumia. Jikaze ndugu yangu.

Sawa James, asante sana ndugu yangu.


Nilikata simu na kuamua kuizima kabisa kwani sikutaka kuongea na mtu yoyote yule. Nilijiinamia kwenye meza na bila kutegemea nilijikuta machozi yakiwa yananitoka. Nilijilaumu sana kwa ujinga wangu nilioufanya uliosababisha hadi Agness akaachana na mimi. Nilijilaumu sana kwanini nilimtongoza na kumpa mimba Vanessa kwani yeye ndo alikua chanzo cha mapenzi ya mimi na Aggy kuvunjika. Nilijuta sana kwanini nisingepanga sehemu mapema na kumuoa Aggy ili niishi naye. Nilijikuta najuta kwa kila kosa nililolifanya na yote yalikua ni upuuzi wangu mimi mwenyewe.

"Haiwezekani lazima Agness arudi mikononi mwangu".

Niliongea peke yangu kwa sauti. Wakati bado naendelea kuwaza juu ya hilo jambo, nikamuona David akiingia ofisini.

Alex vipi mbona nakupigia simu yako haipatikani nini tatizo? Na mbona unaonekana kama unalia?

Niliinama chini na kutoa leso na kujifuta machozi.

Hapana kaka nipo sawa tu.

Upo sawa wakati nakuona unalia kabisa. Hebu niambie nini tatizo? Nyumbani kumetokea tatizo au?

Ghafla nikajikuta naanza tena kulia mbele ya David.

Alex hebu niambie basi ujue ushaanza kunipa wasiwasi.

Nilitaka kumwambia David ila nikahisi huenda akaliona jambo lenyewe ni la kipumbavu na kuanza kuniona mjinga na mdhaifu sana.

Hapana kaka usijali nitakua sawa tu hakuna tatizo lolote.

Alex si unajua mimi na wewe tuko vipi na wapi tumetoka?

Ndio kaka nafahamu.

Basi naomba uniambie na wala usinifiche kitu.

Nilimtazama David usoni na kuamua nimwambie tu kwani hata nikimficha itakua haina maana kwa sababu mambo yangu mengi alikua anayajua.

Kaka nafikiri nilishawahi kukwambia kuhusu mwanamke wangu wa nyumbani kijijini na nikakuonyesha hadi picha yake.

Ndio nakumbuka.

Sasa yule mwanamke ameolewa kaka.

( Niliongea huku nikiwa nalia kama mtoto mdogo vile.)

Ooh! pole sana Alex, pole kwa yote hayo yaliyotokea. Lakini si uliniambia mapema kuwa ulipata mwanamke mwengine na unaishi naye?

Ndio kuna mwanamke naishi nae.

Kwanini sasa na unajua kuwa una mwanamke mwengine na ndo chaguo lako?

Wewe acha tu kaka najuta sana kwa makosa niliyofanya. Ujinga wangu mwenyewe ndio umenigharimu hadi mwanamke ninayempenda ameolewa na mtu mwengine.

Pole sana mdogo wangu.

Asante kaka ila naumia sana.

Naelewa Alex hata mimi nimeshapitia huko kwenye kuumia. Janeth yule mama yao kina Happy alishanitesa sana kipindi ndo tunaanza mahusiano hivyo naelewa maumivu ya mapenzi yanavyokua.

Kwahiyo nifanye nini kaka?

Kitu kikubwa inabidi ukubaliane na ukweli tu huyo mwanamke umeshamkosa na sio mali yako tena. Makosa uliyofanya ndo yamesababisha yote hayo hivyo inabidi usimame imara na kuendelea na maisha yako sio kujuta.

Sawa kaka nitajitahidi.

Sawa. Nilitaka nikuagize sehemu ila nenda tu nyumbani ukapumzike utaenda hata kesho.

Usijali kaka niagize tu.

Hapana Alex naomba ukapumzike hadi kesho bado nakuona haupo sawa.

Nilimshukuru sana David kwa moyo wake wa huruma na kweli nikaondoka ofisini. Sikuenda nyumbani kama David alivyotaka ila nilienda moja kwa moja hadi kwenye fukwe za Coco beach. Nilifika na kupaki gari kisha nikashuka na kukaa peke yangu sehemu ambayo ilikua tulivu sana na haina watu. Nilianza kutafakari upya lile jambo la Agness kuolewa na lilikua haliniingii akilini hata kidogo.

"Haiwezekani lazima nifanye kitu Agness ni mke wangu mimi"

Nilijikuta napandwa na hasira sana kwa makosa yangu mimi mwenyewe kwani kama ningetulia basi Agness asingediriki kuniacha. Nilikaa sana huko hadi jioni ambapo nilienda kumpitia Vanessa kazini kwake na tukarudi nyumbani.


*************** ****************


Alex mwanangu umepoteza mke bora sana ambaye angekufaa kwa kipindi chote cha uhai wako.

Alikua ni mama akinisimulia kuhusu Agness pindi nilipoenda kumtembelea ghafla siku ya wikiendi ambapo pia iliambatana na sikukuu hivyo nilikua na mapumziko ya kama siku tatu kazini.

Nafahamu hilo mama na ndo maana naumia sana.

Yule mtoto siku ambayo ndo walitaka waanze kumuweka ndani alitoroka kwao usiku na kuja mpaka hapa. Alilia sana na kukulaumu kwa yote uliyoyafanya kwani ndo yamechangia hadi akachukua maamuzi ya kuachana. Pia amesema anaomba radhi sana kwa kuchukua maamuzi hayo ya kuolewa kwani hakua na chaguo jengine baada ya wewe kumpa ujauzito mwanamke mwengine na unaishi nae. Ameomba umuache aishi maisha yake mapya na mume wake na usahau kabisa kuhusu yeye japo amesema hata yeye inamuuma sana na itamuwia vigumu kukusahau.Yule mtoto alikua na upendo sio kwako tu, bali hadi kwangu pamoja na marehemu baba yako.

Maneno ya mama yalinifanya niishiwe nguvu sana kiasi kwamba nilikosa hata kitu cha kuongea.

Usihuzunike sana mwanangu kuwa jasiri tu. Muda mwengine inabidi tulipe kwa makosa yetu wenyewe ya kipuuzi tunayoyafanya na haya ndo malipo yenyewe. Aggy ameshaolewa hivyo inabidi uangalie maisha yako na kutafuta mtu mwengine ambaye unaona atakua sahihi kwako.

Mwanamke sahihi kwangu ni Agness tu mama na hakuna mwengine.

Sawa, lakini tayari ameshaolewa inabidi umsahau.

Maneno ya mama yalikua ni kama mwiba ndani ya moyo wangu japokua yalikua ni ukweli mtupu.

Halafu pia alileta vitu vingi sana ulivyompa vipo huko chumbani. Agness ameolewa lakini amehuzunika sana. Aliondoka hapa akiwa analia sana kiasi kwamba nilishindwa hata kwenda kwenye hiyo harusi yake.

Mama alienda kuniletea hivyo vitu na kuona vitu vingi sana nilivyompa enzi za uchumba wetu zikiwemo picha, nguo, viatu, simu na vitu vyengine vidogo vidogo kama saa. Nilivitazama kwa huzuni sana hadi nikahisi machozi yakitaka kunitoka. Niliingia chumbani kwangu na kujifungia ambapo sikumbuki hata nililala saa ngapi kwa jinsi nilivyolia usiku ule.


Kesho yake kulipokucha baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa nilienda kwa kina Halima rafiki yake na Agness. Kwa bahati nzuri nilimkuta uwani kwao akiwa anatwanga kisamvu.

Eeh! Alex umekuja, karibu.

Asante sana Halima. Mambo vipi?

Poa, mzima wewe?

Mimi mzima, vipi kwenu hapa?

Wote wazima tunashukuru. Karibu ukae kwenye jamvi.

Kweli nilienda kwenye jamvi lililokua chini ya mwembe na kukaa chini.

Alex wewe ulichomfanya mwenzako sio vizuri kabisa. Agness alifikia mpaka akanywa mafuta ya taa anataka kujiua.

Nilishtuka sana kwa maneno aliyoniambia na ilibidi nimuulize vizuri.

Alikunywa mafuta ya taa? Kwahiyo ikawaje?

Yani kwa bahati nzuri kwa yule mzee Akida maziwa bado yalikuwepo kwani tulimnywesha kwa lazima na alitapika damu nyingi sana. Shoga yangu alilazwa Bombo Tanga mjini karibia wiki mbili yani hadi niliogopa na kudhani ndo tunampoteza.

Nilijikuta nazidi kuchoka.

Ina maana ndo kumetokea mambo yote hayo?

Ndio. Yani huku kuolewa ni shinikizo la mama yake tu lakini Agness alikua hataki kabisa kusikia habari za wanaume. Huyo kijana alimfata mama yake na kumwambia anataka amuoe Aggy hivyo mama yake ndo alimlazimisha sana akiamini kuwa ndio njia pekee ya kukusahau wewe na kuanza maisha mapya. Shoga yangu amelia siku ya ndoa utadhani msiba vile yani hata sijui wanaishi vipi huko na huyo mume wake.

Ngoja kwanza, wewe unapafahamu huko wanapoishi?

Ndio napafahamu.

Nakuomba unipeleke Halima, tafadhali sana nipo chini ya miguu yako.

Wee! Yani sithubutu hata kidogo. Nikupeleke ili iweje?

Nina shida sana ya kuongea na Agness.

Aah! hapana bado hujaniambia.

Tafadhali Halima nipo chini ya miguu yako. Nitakupa kitu chochote unachokitaka.

Aah aah! Alex bwana mimi sitaki utanipa lawama.

Nakuomba Halima fanya kwa ajili yangu. Sema unataka pesa kiasi gani?

Alex bwana mbona unanipima imani hivyo?

Sikupimi imani ila shida yangu ni kuonana na Agness.

Utanipa elfu 50?

Nakupa laki moja.

Unasema? Unataka twende lini?

Hata leo hii.

Hapana kwa leo sina nafasi maana mama hayupo, tufanye kesho.

Sawa pia itakua vizuri maana ndo naondoka kurudi Dar.


Kweli nikaelewana nae na kumuaga kuwa narudi nyumbani. Wakati nipo njiani nilishtuka sana kumuona mama yake Agness akiwa anakuja mbele yangu kichwani akiwa na ndoo ya maji. Nilitamani hata kubadilisha njia ila alishaniona muda mrefu.............



Tutakutana na wote tulijikuta tumesimama. Mama Agness alikua ananiangalia kwa jicho la ukali sana huku akiwa na ndoo ya maji kichwani hadi nikaanza kumuogopa.

Shikamoo mama.

Aliendelea kuniangalia na kunibinulia mdomo kisha akanipa sonyo hilo ambalo sitakaa nikalisahau. Taratibu akaanza kuondoka bila kujibu kitu na nikajua nitakua nimeharibu sana. Niligeuka nyuma kumtazama lakini yeye wala hakugeuka na aliendelea na safari yake. Nilijihisi mnyonge sana na mwili kukosa nguvu hivyo moja kwa moja niliongoza njia ya nyumbani na kupitiliza chumbani kwangu ambapo nilijifungia na kupumzika japo bado ilikua ni asubuhi mishale ya kama saa 4 kuelekea saa 5. Kichwa kilikua na mawazo mengi sana kiasi kwamba hata simu zilizokua zinapigwa sikutaka hata kuzipokea. Nilijuta sana kwa yote niliyofanya na kutamani Agness angekua bado yupo mikononi mwangu.

"Haiwezekani, lazima Aggy arudi mikononi mwangu. Yeye ndo mwanamke ninayetaka na anayefaa kuwa mke wangu."

Nilijisemea peke yangu wakati nipo chumbani nikiwaza na kuwazua.


Nililala sana mpaka jioni ambapo simu zilizokua zinaita mfululizo zikaja kuniamsha. Kidogo nilihisi kichwa kimekua chepesi na nikachukua simu ambapo nilikuta missed calls zisizokua na idadi na nyingi zilikua ni za Vanessa. Pia nilikuta meseji kadhaa na niliwajibu wote. Nikampigia simu Vanessa ambapo haikuita sana ikapokelewa.

Mbona ulikua hupokei simu yangu muda wote huo, ulikua wapi?

Ina maana hiyo ndo salamu mpya siku hizi?

Nijibu kwanza usijifanye hujui ulichofanya.

Na wewe nakuuliza ina maana hiyo ndo salamu mpya? Hivi kweli hatujaongea tangu asubuhi unaacha kunisalimia na kuanza kulalamika tu. Unajua nimepatwa na nini huku?

Basi mume wangu nisamehe, habari za jioni.

Sitaki salamu za kulazimishana hivyo.

Sasa unataka nini jamani?

Vee hebu punguza masihara muda huu sipo kwenye masihara hata kidogo.

Kwani kuna nini huko mbona umekua hivyo?

Nimekua vipi?

Nakuona umekua mkali ghafla hautaki hata utani.

Hebu tuachane na hayo, vipi ulivyoshinda leo?

Salama tu mume wangu, hofu kwako tu na ndo maana nimekupigia sana simu hadi nikapatwa na wasiwasi kwanini hupokei.

Mimi sipo sawa hata kidogo.

Kwanini unasema hivyo baby?

Nitakwambia pindi nitakaporudi.

Mhh! baby kwanini usiniambie sasa hivi maana mwenzio ushanipa wasiwasi.

Hapana wala usiwe na wasiwasi nitakua sawa tu. Nikirudi nitakwambia hivyo usiwe na hofu.

Mhh! Sawa bwana, ila kama unaumwa ni bora ukaniambia.

Hapana wala siumwi ni mambo mengine tu.

Mmhh! Sawa.

Niliongea kwa muda na Vanessa na nikahisi kidogo amenichangamsha. Tulimaliza na kukata simu kisha nikaenda chooni kujimwagia maji.


*************** ***************


Kesho yake asubuhi mishale ya kama saa 4 nilitoka na Halima kama tulivyokubaliana ili anipeleke maeneo anaishi Agness Tanga mjini. Nilimuaga mama na kumuachia pesa za matumizi kwani pia ndo nilikua naondoka kurudi Dar.

Hivi unahisi Aggy anataka kuonana na mimi kweli?

Nilimuuliza Halima wakati tupo njiani.

Mhh! kusema ukweli hata sielewi. Ila ukweli ni kwamba mpaka anaolewa Aggy alikua anakupenda sana ila tu alikua hataki kuwa na wewe kutokana na mambo uliyoyafanya.

Sasa kama alikua bado ananipenda kwanini alikubali kuolewa na mtu mwengine?

Mama yake ndo alimlazimisha yeye mwenyewe alikua hataki mambo ya wanaume hata kidogo. Ila wewe ndo mwenye makosa sana kwani tangu ulivyomuomba msamaha siku ile na akakataa basi ndo umeondoka moja kwa moja haujarudi tena. Aggy namjua mimi ni rafiki yangu tangu tupo wadogo, zile zilikua ni hasira tu.

Kwanini unasema hivyo?

Tangu ulivyoondoka nilimuona kabisa kuwa hayupo sawa na alishawahi kunitamkia kwa kinywa chake kuwa amekumiss. Kama ungerudi tena angalau baada ya miezi hata miwili ungeweza kumrudisha tena Aggy kwani hasira zilikua zimekwisha kabisa.

Sasa kama ndo hivyo kwanini lakini ameolewa?

Mama yake ndo kachangia yote hayo kutokea kwani huyo mwanaume mwenyewe Aggy alimuona mara moja tu siku aliyokuja kutoa mahari na ndo alitambulishwa hapo hapo.

Namchukia sana yule mama, amefanya mwanamke wa ndoto zangu aende mbali na mimi na kuolewa na mtu mwengine.

Halima alibaki kimya akiwa anashangaa nje tu wakati gari inatembea.


Tulifika salama hadi Tanga mjini na Halima akanielekeza maeneo aliyokua anaishi Aggy pamoja na mumewe. Tulienda hadi maeneo ya Sahare na kuingia mtaa flani ambao ulikua unaenda kutokea barabara ya kwenda Tanga Beach.

Alex mtaa wenyewe ndo huu na nyumba ndo ile kule mbele yenye bati la blue na michongoma nje. Mimi sifiki mpaka kule naomba nishuke hapa hapa maana nahofia Aggy asije akaniona na alishanionya nisikwambie kitu chochote kuhusu yeye.

Sawa Halima asante sana kwa msaada wako. Kwa hapa uliponifikisha inatosha huko kwengine niachie mimi.

Sawa Alex basi acha mimi niende.

Nilitoa pochi na kumkabidhi kiasi cha shilingi laki moja kama nilivyomuahidi na kumuongeza na elfu kumi ambayo nilimwambia atafanya nauli. Halima alifurahi kupita maelezo kiasi kwamba kama angekua na uwezo angenibeba mpaka mlangoni kwa Agness kabisa. Nilielewa kwanini amefurahi kiasi kile kwani kwa maisha ya kijijini kwetu mtu akipata laki moja tena kirahisi kiasi kile basi anaweza hata kutembea uchi mtaa mzima. Tuliagana na akaondoka zake, kisha na mimi nikasogea hadi karibu kabisa na nyumba aliyonielekeza Halima. Nilishuka kwenye gari na kuanza kutembea taratibu kuifuata ile nyumba huku nikiwa na wasiwasi sana. Moyo ulikua unadunda kwa kasi sana hadi nikajikuta kijasho chembamba kikinitoka. Nilikua na hofu sana Aggy akiniona itakuaje na atanipokea vipi maana mara ya mwisho kuonana tuliachana akiwa na hasira sana kiasi kwamba alikua hataki hata kuniona.

Habari za saa hizi jamani.

Niliwasalimia jamaa wawili niliowakuta wanacheza bao.

Nzuri tu, vipi kwema?

Kwema kabisa. Samahani kuna dada mmoja namuulizia anaitwa Agness nimeambiwa anakaa maeneo haya.

Mhh! Agness! Yupoje huyo?

Mwembamba kiasi maji ya kunde hivi.

Amekuelekeza anakaa mtaa huu?

Ndio, na hana muda mrefu sana kwani ameolewa juzi juzi tu.

Aanha! Au anasema mkewe Shaffih?

Eeh! itakua ndo huyo huyo.

Waliulizana wenyewe kwa wenyewe kuthibitisha.

Hebu ngoja, huyo dada ni mwenyeji wa wapi ndugu yangu?

Anatokea Loko.

Basi ndo huyo huyo mkewe Shaffih. Anaishi nyumba hiyo hapo unayoiona mbele yako ina bati la blue na tena ameingia ndani muda sio mrefu maana nahisi alienda gengeni.

Sawa ndugu zangu asanteni sana.

Sawa karibu sana.

Niliwaacha wale jamaa na kuanza kutembea taratibu ambapo mapigo ya moyo yalizidi kuongezeka mpaka nikawa najihisi kizunguzungu. Nilifika na nikawa najiuliza nifanye nini ili nionane na Agness maana ilikua ni nyumba ya kupanga ambayo ilionyesha ilikua na wapangaji sio chini ya watano


Hodi jamani!

Nilijikuta napata ujasiri wa ghafla na kuanza kugonga hodi mlango wa mbele barazani.

Hodi humu ndani, hodi!

Karibu.!

Alitoka dada mmoja akiwa amejifunga kanga kifuani.

Za saa hizi.

Nzuri dada. Samahani namuulizia dada mmoja nimeelekezwa kuwa anakaa humu anaitwa Agness.

Agness! Mhh! mbona humu ndani hakuna mtu anayeitwa Agness?

Yupo na nimeambiwa muda sio mrefu ameingia humu ndani.

Mhh! yupoje huyo?

Mwembamba hivi kiasi na ameolewa siku sio nyingi.

Au utakua unasema Zulekha wewe? Hebu subiri kwanza.

Zulekha! Zulekha! Zulekha!

Yule dada alikua anaita huku akisogea mlango wa pili kutoka mwisho wa ile nyumba. Nikawa najiuliza ina maana Aggy atakua amebadili dini au hilo jina la Zulekha imekuaje mpaka anaitwa hivyo. Ila nikahisi itakua amebadili dini maana nilisikia huyo jamaa yake anaitwa jina la kiislamu Shaffih.

Zulekha kuna mgeni wako yule kule anakuulizia.

Yule dada aliongea na mtu aliyekua ndani ya kile chumba.

Anakuja kaka.

Sawa dada yangu nashukuru sana.


Yule dada alirudi chumbani kwake na kuniacha peke yangu nikiwa nasubiri kwa nje barazani. Baada ya kama dakika mbili nikasikia miguu ya mtu akitembea ukumbini na alipotokeza nilihisi moyo wangu ukipasuka vipande vipande kwani alikua ni Agness.......



Alex!

Agness!

Umefata nini nyumbani kwangu?

Agness! nimekufata wewe mpenzi wangu.

Tena naomba uishie hapo hapo na uwe na adabu na mimi. Sasa hivi mimi ni mke wa mtu kwahiyo naomba uniheshimu.

Hapana Agness wewe ni mke wangu mimi na sio mtu mwengine.

Alex nimesema sitaki kusikia hayo maneno yako. Kwanza ni nani aliyekueleza kuja mpaka hapa?

Usitake kujua Aggy, ila nimefanya jitihada zote hizi ili nionane na wewe tu.

Uonane na mimi ili iweje? Umesahau nini kutoka kwangu?

Aggy usinifanyie hivyo nakuomba elewa kwamba naumia sana juu yako.

Alikaa kimya akawa ananiangalia tu na kunisikiliza ninayoyaongea.

Kwanini lakini ulikubali kuolewa na unajua mimi nipo?

Upo? Upo wapi? Wewe si una mwanamke wako unaishi naye na umeshampa ujauzito, sasa ulitegemea mimi nifanye nini?

Lakini si nilishakwambia mimi simpendi yule nakupenda wewe tu.

Kwahiyo kama humpendi? Unataka kumuacha na kumtelekeza na mtoto halafu dhambi uje kunipa mimi huku eeh?

Hapana sina maana hiyo mtoto wangu ningemlea tu ila nisingeishi na yule mwanamke.

Alex naona unanichanganya kichwa changu tu kwani hayo maneno unayoyaongea hayana maana kwa sasa. Mimi tayari ni mke wa mtu na mume wangu ananipenda sana.

Tafadhali Agness naomba usiniambie maneno ambayo yananiumiza kama hayo.

Sasa ulitaka niseme nini na huo ndo ukweli? Kwanza nakuomba uondoke maana mume wangu atarudi muda sio mrefu kuja kula chakula cha mchana.

Agness nionee huruma tafadhali, jaribu kufikiria ni kiasi gani natoka mbali na kuacha shughuli zangu kwa sababu yako tu.

Kwani nilikwambia uje na uache shughuli zako?

Agness leo ndo unanijibu hivi kweli?

Alex nakuomba uondoke tafadhali usije ukanigombanisha na mume wangu.

Agness usinifanyie hivyo mke wangu.

Nilianza kuongea huku machozi yakianza kunitoka maana maneno ya Aggy yalikua yananichoma sana.

Eeh eeh! Alex, usinilazimishe nifanye kitu kibaya na ukanichukia mpaka siku unaingia kaburini. Nakuomba kwa amani kabisa uondoke hapa na usirudi tena.

Agness please! please Agness (Agness tafadhali! tafadhali Agness!) bado nakupenda sana.

Niliongea huku nikimpigia magoti na machozi yakinitoka kama mtoto mdogo. Sikujali kama kuna mtu ananiona au kunisikia kwani nilikua nalia kwa sauti kubwa sana.

Alex naomba usiniletee uchuro na majirani zangu wakaanza kunihisi vibaya. Ondoka haraka nyumbani kwangu.

Agness! unanifukuza mimi, unanifukuza mimi Agness. kweli Agness!

Bila kutegemea nikamuona na yeye machozi yakianza kumtoka.

Alex nimesema ondoka na sitaki kukuona.

Agness naomba usikilize moyo wako. Usinifanyie hivyo unanikatili sana. Hebu niangalie jinsi ninavyotia huruma lakini.

Ondoka Alex.

Aliongea huku akiwa analia waziwazi kabisa na nikamuona anakimbilia ndani kwake. Nilibaki nimeduwaa peke yangu huku nikiwa bado nimepiga magoti. Niliinuka na kuanza kuondoka taratibu ambapo ndo nikagundua kuwa kuna watu wengi walikua wanatuangalia ila sikujali. Nilienda mpaka ilipo gari yangu na nikaingia ndani na kutulia kama robo saa nikiwa natafakari kitu gani nifanye. Nikaamini kuwa huenda Aggy atakua bado ananipenda kama alivyosema Halima maana kama hanipendi asingeweza kutoa machozi tena mbele yangu.Nikaamua kuondoka na kuanza safari ya kurudi Dar huku kichwani nikiwa na mawazo mengi sana.


*************** ***************


Ilitimia miezi tisa na hatimaye Vanessa akajifungua salama mtoto wa kiume ambaye tulikuja kumpa jina la Kelvin. Sikua na shaka nae hata kidogo kwani kila nilivyomtazama nilijiona mimi kabisa kwani nilifanana nae sana haswa sura na vidole vya mikono na miguu. Vanessa alikaa kwa shangazi yake takribani miezi miwili akiwa anahudumiwa kama tufanyavyo watanzania wengi sana. Kipindi hiko chote nilikua nipo free sana kwani siku nyengine nilikua naenda sehemu za starehe na kuondoka na wanawake kwenda kulala nao mpaka asubuhi. Nilijitahidi sana kusahau kuhusu Agness lakini nilishindwa kwani muda mwengine nikilewa nilikua najifungia peke yangu chumbani na kuanza kulia. Suala la kwamba agness ameshakwenda na kuolewa na mtu mwengine halikuingia akilini mwangu hata kidogo kwani siku zote niliamini kuwa mimi ndo ningekuja kumuoa.


Alex mume wangu hivi unaishi vipi siku hizi maana nina wasiwasi.

Alikua ni Vee akiniuliza swali siku nilipoenda kumtembelea kwa shangazi yake maeneo ya Magomeni Mwembechai.

Una maana gani kuniuliza hivyo?

Namaanisha kuhusu kunaniliu, unaishi vipi maana nakujua wewe hutaki kupitisha hata siku mbili.

Nilitabasamu kwani swali lake lilinifurahisha sana.

Sasa unafikiri nitafanya nini? Sina jinsi inabidi tu nipambane na hali yangu.

Mhh! kweli? Wewe kweli uweze kuvumilia!

Kwani unanichukuliaje? Au unahisi nina wanawake wengine?

Sina maana hiyo mume wangu.

Kumbe una maana gani?

Eeh! basi yaishe tusije kuzua mengine ambayo hata hayapo.

Acha kunifikiria vibaya bwana, tunaishi vipi sasa ikiwa hatuaminiani?

Basi mume wangu nimesema yaishe.

Nilikaa kimya kuonyesha sijapenda alivyoniuliza kumbe angejua kwa kipindi hiko kifupi tu alichokua kwa shangazi yake, tayari nimeshakutana na wanawake zaidi ya watano. Tuliendelea kuongea mambo mengine kuhusu sisi na mtoto ambapo Vanessa alikua anataka Kelvin akue haraka sana ili akamuandikishe shule.


Ujenzi wa nyumba yangu nao uliendelea vizuri sana japo nilikua najenga taratibu kutokana na kutokua na hela za kutosha. Mpaka wakati huo ilikua imefikia kwenye kuipiga plasta na kuweka tiles nyumba nzima pamoja na kupiga rangi. Nilijitahidi sana kutunza hela japo mara moja moja nilikua natoka out na kutumia.Maisha ya umasikini niliyokulia yalinifunza jinsi ya kulinda hela ili ufanye mambo yako ya msingi uliyoyapanga. Nilikua nahakikisha kuwa matumizi yangu hayafiki hata robo ya pesa ninayoipata ndani ya mwezi mzima hivyo nikajikuta nikiwa natunza hela nyingi sana kila mwezi. Janeth kama kawaida alikua ananisaidia sana pindi ninapokwama na hiyo yote inatokana na dozi nzito ninayompa. Japo siku hizi tulipunguza, lakini mara moja moja huwa tunajiibia na kwenda hotelini kufanya mambo yetu na penzi la Janeth lilininogea sana kwani muda mwengine mimi ndiye nilikua namtafuta. Hata Happy naye tuliendelea na mchezo wetu kama kawaida mpaka akaniambia kuwa boyfriend wake ameanza kumtilia shaka kwani mara nyengine wakikutana Happy anakua hana mzuka kabisa kutokana na mimi kuwa namkata kiu yake yote mpaka ya mwezi ujao.


**************** ***************


Rafiki yake Vanessa anayeitwa Naima alikua amenizoea sana kiasi kwamba nikaona mazoea yamepitiliza kwani alikua ananiambia vitu ambavyo hakupaswa kuniambia mimi shemeji yake. Muda mwengine alikua anakuja nyumbani usiku na anajua fika kuwa rafiki yake hayupo, yupo kwa shangazi yake Magomeni na ukimuuliza anadai amenimiss hivyo amekuja kunisalimia tu. Sio siri mambo yake aliyokua anayafanya yalinichanganya sana na kunipa wakati mgumu kwani nilihisi kama ananitega hivi. Naima alikua ni mzuri sana na ana shepu iliyojazia haswa. Alikua na mwili kiasi na weusi wa asili ambao ulizidi kuchagiza urembo wake. Nilijitahidi kukaza ili tusivunjiane heshima maana Vanessa akija kujua nahisi itakua ni vita ya tatu ya dunia maana alikua na wivu uliopindukia.

Shemeji kesho unaweza kunitoa out?

Aliniuliza wakati tunachat kwa njia ya WhatsApp.

Nikutoe out nikupeleke wapi?

Popote pale utakapopenda maana nimemiss sana kutolewa out.

Sasa mimi kweli ndo nikutoe out?

Ndio, kwani kuna ubaya gani?

Rafiki yako akija kujua?

Hawezi kujua bwana na hata kama akijua mbona ni kitu cha kawaida tu.

Mmhh! Naogopa mimi nisije nikawagombanisha.

Hamna bwana mimi na Vee hatuwezi kugombana tunajuana vizuri.

Kama ndo hivyo sawa tutatoka.

Naima alifurahi sana.


Kweli kesho yake usiku ambayo ilikua ni Jumamosi tulitoka na kwenda sehemu moja maeneo ya Tabata iliyokua inaitwa Kwetu Pazuri. Tulikuta pamechangamka sana na mziki mkubwa ukiwa unapigwa ambapo tulikaa na kuagiza vinywaji na nyama choma za kutosha.Tulikula nyama na kunywa pombe nyingi sana mpaka wote tukawa tumewaka kiasi kwamba tulikua tunacheza mziki na kukumbatiana utadhani sio mtu na shemeji yake. Katika siku nilizowahi kunywa pombe, ile siku nilikunywa pombe nyingi sana kiasi kwamba nilipoteza akili zangu timamu. Muda wa kuondoka ulipofika nikajiona waziwazi kuwa siwezi kuendesha gari kwani hata macho yalikua hayaoni vizuri.

Sasa Naima tunafanyaje mimi hapa nimelewa sana na siwezi kabisa kuendesha gari.

Sijui nakusikiliza wewe tu.

Kuna sehemu ina nyumba ya wageni hapa karibu.

Ndio hapo nje tu niliiona wakati tunaingia.

Basi twende tutajua huko huko tunafanyaje.

Muda huo akili ilikua inaongozwa na pombe tu na kila kitu kwangu niliona sawa hivyo tukaanza kukokotana taratibu mpaka nje maeneo ya kwenye hiyo guest house. Tulifika na kuulizia chumba ambapo tuliambiwa bado vipo hivyo nikalipia chumba kimoja na wote tukaingia na kujifungia. Muda mwengine nilihisi kama akili zinaingia na kutoka kwani kile kitu tulichokua tunataka kukifanya hakikua sahihi hata kidogo. Ghafla Naima akanivamia na tukaanza kubadilishana mate huku wote tukiwa tunanuka pombe. Tukaanza kuvuana nguo na kubaki kama tulivyozaliwa ambapo ndo nikayashuhudia vizuri makalio yake jinsi yalivyo makubwa na kubinuka sana. Naima alivutia sana kwani bwana mkubwa bila kuchelewa aliamka haraka sana kutoka usingizini na kuanza kumtazama kwa uchu mkubwa sana.

Shemeji kumbe una mashine kubwa kiasi hiki? Rafiki yangu anafaidi sana.

Sikumjibu kitu ambapo nilimuona akiikamata na kuanza kutuma salamu. Sio siri Naima alijua kunipagawisha kwani alikua anafanya vitu ambavyo vilikua vinanichanganya sana kiasi kwamba nilibaki nimefumba macho tu. Baada ya kuona nakaribia kuvunja dafu aliniacha na mimi nikaanza kulitawala dimba na kuanza kufanya vitu vyangu.


Nilimtembezea ulimi sehemu zote bila kujali na hiyo yote ilichangiwa na pombe nilizokunywa. Naima alikua anapiga kelele utadhani anakabwa na nilipohakikisha ameiva vizuri nikamuweka sawa na kuanza kumpelekea surundaka za kufa mtu. Naima alikua anatoa vilio vya kufa mtu huku akinionyesha ufundi wa hali ya juu. Kiunoni alikua na cheni moja ambayo ilikaa vizuri sana kutokana na kusapotiwa na umbo lake namba nane. Tulibadilishana mikao tofauti hadi nikajihisi nataka kuandika goli la kuongoza.

Alex jirani anaona wivu.

Eeh?

Jirani anaona gere.

Sijakuelewa, una maana gani?

Nataka nikupeleke kwa Mpalange.

Aliongea huku akinionyesha sehemu yake ya haja kubwa.

Una maana unataka tufanye huko?

Ndio, mwenzio bila kufanya huku sijisikii raha.

Aah! aah! hapana mimi sijazoea.

Sasa si ndo nakufundisha. Kuna raha sana wenzio waliojaribu hawataki kuacha.

Aah aah! Naima mimi naogopa bwana.

Usiogope bwana mbona kitu cha kawaida tu.

Sijui ni pombe zilinizidi au ni Naima ndo alijua kunishawishi, kwani nilijikuta nikikubali kufanya ule mchezo mchafu wa kizazi cha Sodoma na Gomora. Naima alionekana ni mzoefu sana kwani hata maumbile yake yalikua yametanuka sana. Kwa ujinga wangu kweli nilijikuta napata raha za ajabu na baada ya muda mfupi tu nikafanikiwa kufika mwisho wa reli. Nilijitupa chini nikiwa hoi na baada ya muda mfupi nilipitiwa na usingizi mzito.


****************** *****************


Siku moja David aliniita ghafla faragha hadi nikaanza kuogopa. Alionekana yupo serious sana tofauti na mara nyingi ninavyomuona na nikahisi huenda kutakua na tatizo. Tulienda mpaka sehemu moja ambayo ilikua na mgahawa uliotulia sana maeneo ya Namanga......




Tuliagiza vinywaji laini, mimi nikiagiza juisi na David aliagiza maji. Muda wote huo akili yangu ilikua haipo sawa na kitu kilichokua akilini ni kuwa David atakua amegundua mambo yote ninayoyafanya kwa mke wake pamoja na watoto wake.

Alex nimekuita hapa kuna jambo muhimu sana nataka nikushirikishe.

Jambo gani hilo kaka?

Alipiga mafunda mawili ya maji kisha akanitazama usoni.

Kuanzia sasa hivi nataka wewe ndo uwe unafuata bidhaa zangu China. Sasa hivi inabidi niwe karibu sana kufatilia hizi bidhaa za JADA maana mahitaji yanazidi kuongezeka mpaka nje ya nchi hivyo inabidi niwe karibu sana ili niweze kudili vizuri na wateja.

Mmhh! sasa kaka hauoni kama unanipa mtihani hapo?

Mtihani upi tena?

Hata Kenya tu hapo sijawahi kwenda, je huko China si ndo nitapotea mimi?

David alifurahi sana kwa maneno niliyomwambia.

Sikiliza Alex, kwa dunia ya sasa hauwezi kupotea sehemu yoyote ile duniani. Hata mimi mara ya kwanza kusafiri kwenda nje ya Afrika niliogopa sana ila kwa kutumia mawasiliano kila kitu kinawezekana.

Mmhh! Naogopa sana.

Wala usiogope Alex kila kitu kitaenda sawa tu. Tatizo sio kwamba hakuna mtu mwengine aliyezoea kusafiri nje ya nchi, ila tatizo ni kwamba siwezi kupata mtu mwengine mwaminifu kama wewe. Nakuamini sana Alex na ndo maana nakushirikisha kwenye mambo yangu muhimu kama haya. Kipindi nilivyokua nakwambia ujifunze lugha ya Kiingereza nilikua na maana yangu nilijua tu kuwa wakati kama huu utafika na nitakuhitaji kwenye jambo kama hili.

Nashukuru sana kwa uaminifu na imani kubwa uliyonayo juu yangu kaka. Kwahiyo huko China nitakua ninafanya kazi gani?

Swali zuri sana. Kazi yako kubwa itakua ni kuukusanya mzigo kutoka kiwandani na kuuweka sehemu moja maana viwanda vinavyotengeneza bidhaa zangu vipo vitatu hivyo ukusanyaji wa bidhaa kidogo unasumbua.

Sasa hiyo mizigo nikiikusanya nitaiweka wapi na taratibu zote za kuisafirisha zinakuaje?

Kuhusu hilo hata usijali. Nina jamaa zangu Guangzhou pale hao ndo watakaokupokea na kukusaidia mambo yote hayo. Hata mizigo pia wakati unaikusanya utaiweka kwenye godown lao pindi utakapokua unashughulikia taratibu za kuisafirisha.

Hapo sasa nimekuelewa kaka.

Vizuri sana. Itabidi kesho tuanze kufatilia passport yako ya kusafiria haraka sana kwani ndani ya wiki 3 unatakiwa ndo usafiri.

Sawa kaka usijali naahidi sitokuangusha. Nitasimama kwa ujasiri sana na naamini kila kitu kitaenda sawa.

Nafurahi sana kusikia hivyo Akex. Naamini ndani ya mwaka mmoja JADA itakua brand kubwa sana hapa Tanzania na nchi za jirani hivyo kuna mambo mazuri sana yanakuja hata kwako wewe pia.

Maneno yake matamu yalinifariji sana na kuona hakuna linaloshindikana, kila kitu kinawezekanaa ukiwa na nia na kujituma.

Tulimaliza kuongea na tukarudi tena ofisini.


*************** ****************


Mzimu wa kufanya mapenzi kinyume na maumbile na Naima ulikua unanitafuna sana haswa pindi ninapokua nipo peke yangu.Katika maisha yangu sikutegemea kabisa kama ingetokea siku nikafanya ile michezo michafu iliyolaaniwa vikali na Mungu. Nilijikuta nazilaani sana pombe nilizokunywa ile siku kwani ndio zilisababisha hadi nikafanya yote hayo. Nililewa sana ile siku kiasi kwamba nilikua hata sijijui nini nafanya. Nilijuta sana kwanini nilikubali kirahisi mazoea na Naima wakati nilishamuona wazi kuwa ananitaka. Naima naye alihisi kama amenichanganya sana baada ya kunipa hiyo michezo kwani mara kwa mara alikua akinipigia simu na muda mwengine akiwa anataka nimtumie hela hadi nikaanza kumuona kero.


Nilifatilia passport yangu ya kusafiria ambayo David alitumia njia ya magendo kwani kuna watu wa Uhamiaji anafahamiana nao hivyo aliwashikisha hela kidogo ili waniharakishie. Nilifanya vitu vyote nilivyotakiwa kufanya na baada ya kumaliza wakaniambia nirudi baada ya siku 5 ili nikachukue passport yangu wakati utaratibu mzima ulikua unachukua mpaka mwezi mmoja na zaidi. Niliendelea na kazi kama kawaida huku Agness akiwa bado hajanitoka kichwani kabisa kwani muda mwingi sana nilikua nikimuwaza. Niliumia sana pindi nilipokua nikifikiria jinsi kidume mwengine anavyokula tunda langu la thamani ambalo kwangu lilikua ndo kila kitu. Sikukubaliana na ile hali hata kidogo na nikapanga kuwa ni lazima nikaiharibu ile ndoa ili Agness aje mikononi mwangu. Kila nilipokua nikimfikiria huyo jamaa, nilimuona wazi akiwa anaishi maisha yangu, maisha ya ndoto zangu. Nilimuona wazi kabisa kuwa yupo kwenye sehemu ambayo hakustahili kuwepo hata kidogo.

"Haiwezekani lazima ang'oke pale. Aggy ni mwanamke wangu na itabaki hivyo kwa siku zote za maisha yangu"

Nilijisemea peke yangu wakati bado natafakari.


Wakati bado naendelea kuwaza na kuwazua nikaona simu ikiwa inaita na nilipoitazama nikaona namba ngeni ambayo nilihisi kama naifahamu hivi. Mwanzo nilisita kidogo kwa kuhofia kuwa anaweza akawa mmoja kati ya wanawake ambao huwa ninaondoka nao pindi ninapoenda sehemu za starehe kwani kuna baadhi yao wengine huwa ninabadilishana nao namba za simu. Niliamua kuipokea na kuanza kuongea.

Hello.

Eeh hello mambo.

Winfrida!

Ndio, ni mimi.

Haah! umerudi lini?

Nimerudi tangu jana jioni.

Okay, vipi mzima?

Mimi mzima kabisa, nimekumiss sana yani.

Mimi pia Winnie tena juzi tu nilikua nachat na Happy nikakuulizia.

Kumbe na wewe huwa unanikumbuka eeh?

Kwanini sasa nisikukumbuke jamani? Nakukumbuka sana tu.

Nafurahi sana kusikia hivyo. Lini sasa nitaweza kukuona?

Sasa hivi nipo busy sana halafu pia ndani ya siku chache nitasafiri kwenda China.

Heeh! unaenda kufanya nini huko?

Baba yako ndo ameniagiza, kuna mizigo yake naenda kuifatilia na kurudi nayo huku.

Aanha! sawa. Basi naomba kabla haujaondoka tuonane.

Sawa usijali nitajitahidi kutafuta muda.

Tulimaliza kuongea na Winnie akakata simu. Ghafla nikajikuta hisia za Agness zinanijia tena. kila nilipokua nikifikiria kama sasa hivi hayupo mikononi mwangu nilikua nahisi kama kuna kitu kinanichoma moyoni mwangu. Nikapanga niende tena Tanga nikajaribu kufanya kitu labda naweza nikafanikiwa.


Kweli ilipofika Jumamosi mchana nikaanza safari ya kuelekea huko huku kichwani nikiwa natafakari nifanye kitu gani. Mawazo yalinitawala sana kiasi kwamba ilibaki kidogo tu niigonge gari iliyokua mbele yangu nilipofika maeneo ya Lugoba. Nilijitahidi kuwa makini zaidi na nilifika salama Tanga mjini mishale ya kama saa 2 usiku. Nikaamua kukodi chumba kwenye hotel moja maarufu iliyo maeneo ya barabara ya 11. Nikapanga kuwa ifikapo kesho yake ndo niende anapoishi Agness ili nikaonane na mume wake. Siku hiyo nililala mapema sana kutokana na kuwa na mawazo mengi na upweke niliokua nao eneo hilo.


Kesho yake niliamka mapema sana na kwenda kujimwagia maji. Niliagiza kifungua kinywa na ilipofika mishale ya saa 4 asubuhi nilitoka na kuanza kuelekea huko. Kwa kuwa sikua mgeni na Tanga, sikupotea njia kabisa na nilifika hadi mtaa anaoishi Aggy. Niliipaki gari mbali kidogo kisha nikamfuata mtoto mmoja hivi ambaye kwa kumkadiria alikua na umri wa kama miaka 11.

Mdogo wangu haujambo?

Sijambo shikamoo.

Marahaba. Eti unamjua Shaffih?

Eeh namjua anakaa nyumba ile kule.

Akanionyesha nyumba anayoishi Aggy ambapo nikajua anamaanisha Shaffih huyo huyo ninayemuulizia mimi.

Sawa, naomba ukaniitie, mwambie kuna kaka anakuita ana shida na wewe.

Haya.

Nilitoa noti ya shilingi elfu 2 na kumwambia yule mtoto atakunywa soda na alifurahi sana na aliondoka huku akiwa anakimbia kwa furaha sana. Kweli nikamuona anaingia nyumba anayoishi Aggy na ilibidi nianze kujiandaa ni jinsi gani nitamkabili mume wake Agness kwani niliamini kuwa kwa siku hiyo ya Jumapili atakua yupo nyumbani tu.


Kweli baada ya kama dakika nne nilimuona yule mtoto akiwa anakuja ameongozana na kijana wa makamu yangu ambaye niliamini ndo atakua mume wake Aggy. Walifika mpaka pale nilipo na yule mtoto akatuacha akaendelea na mambo yake.........



Habari yako kaka.

Nilianza kumsalimia

Nzuri tu vipi kwema?

Kwema kabisa. Bila shaka wewe ndo Shaffih.

Kweli ndio mimi.

Sawa. Mimi naitwa Alex.

Ooh! sawa Alex nakusikiliza kaka.

Nilikaa kimya kidogo nikitafakari nianzie wapi kile ninachotaka kumwambia.

Sikufahamu na hatujawahi kuonana ila bila shaka wewe ni mume wa Agness.

Unamaanisha Zulekha, ndio ni mke wangu. Unamfahamu vipi mke wangu?

Mimi nimemzoea kwa jina la Agness kwa miaka mingi sana. Ngoja nikupe story fupi halafu uniambie umejifunza kitu gani. Kuna mchungaji mmoja masikini alikua anaipenda sana mifugo yake kiasi kwamba alikua tayari yeye akose chakula lakini mifugo yake ile. Kila siku alikua anaenda kuwakatia majani na kuwaletea zizini na ile mifugo ilinawiri sana. Lakini ghafla ulikuja kutokea ukame wa muda mrefu sana kiasi kwamba yule mfugaji alishindwa kabisa kuihudumia mifugo yake. Akaamua kusafiri akaenda mbali sana ili akatafute majani kwa ajili ya mifugo yake. Huku nyuma ile mifugo baada ya kuona njaa imezidi na yule mchungaji wao anayewahudumia hahamuoni, wakaamua kuvunja zizi na kutoka nje wakajitafutie majani wao wenyewe. Wakati wakiwa wanaranda randa walikutana na mchungaji mwengine tajiri ambaye alikua anaenda kutafuta majani mbali sana lakini kwa kutumia gari yake kubwa. Mifugo ya yule mchungaji tajiri ilikua inapata malisho kila siku na kuzidi kunawiri hivyo ile mifugo ya mchungaji masikini ikaona ijiunge nao ili na wao wapate kula. Kuanzia hapo yule mchungaji tajiri akaanza kuhesabu kuwa na ile mifugo iliyokuja ya mchungaji masikini nayo pia ni ya kwake hivyo akawa anaihudumia yote kwa pamoja. Baada ya siku kadhaa kupita yule mchungaji masikini alirudi akiwa amebeba majani mengi sana kwenye mkokoteni alioununua ila kitu cha kushangaza hakuikuta mifugo yake. Baada ya kuitafuta sana akafanikiwa kuikuta kwa mchungaji tajiri na alipoitaka mifugo yake yule mchungaji tajiri alikataa kumpatia kwa kusema kuwa kwa sasa ni ya kwake kwani yeye aliwatelekeza kipindi wana njaa. Je, unafikiri ni nani hapo anastahili kuwa na hiyo mifugo?


Shaffih alinisikiliza kwa makini hadi mwisho na nilipomaliza nilimuona akishusha pumzi.

Ndugu yangu mbona sikuelewi tangu umeniita hapa unanifumba fumba tu na hauniambii ulichoniitia?

Naomba unijibu hilo swali kwanza kisha nitakuambia kila kitu unachotaka kujua.

Sawa. Mchungaji masikini ndo anastahili kwa sababu mifugo ni ya kwake na aliondoka kwa ajili ya kuitafutia mifugo na sio kuitelekeza.

Vizuri kabisa, umejibu vizuri sana.

Lakini kaka mbona tunazungushana hivi? Wewe ni nani na mke wangu unamfahamu vipi?

Shaffih labda nisikuzungushe sana. Nimekuita hapa kwa sababu moja tu.

Sababu gani hiyo?

Nakuomba uachane na yule mwanamke.

Unamaanisha niachane na mke wangu?

Swadakta! uachane na Agness. Haumjui hata kidogo yule mwanamke na hauyajui maisha yake hata kidogo. Hii story niliyokuhadithia nilikua na maana hii. Wewe ni mchungaji tajiri ambaye umetumia udhaifu wa mchungaji masikini kujimilikisha mifugo ambayo siyo ya kwako. Agness ni mwanamke wangu kwa muda mrefu sana ila tuligombana kwa sababu kadhaa tu. Sikumtelekeza Agness kule kijijini ila nilienda mjini kutafuta maisha ili nije kumuoa na kuishi naye. Kwa maisha niliyopitia na Agness wewe haustahili hata kidogo kuishi nae, ila unaishi maisha ya ndoto zangu. Mimi ndo ninastahili kuwa na yule mwanamke na kuishi nae.

Unasemaje wewe? Yani kumbe umeniita hapa uje kuniambia huo ujinga? Na kumbe wewe ndo unamfanya mke wangu alie kila siku na kunifanya nikose amani na ndoa yangu?

Kwako ni ujinga ila kwangu ni muhimu sana. Leo nimekuja kwa amani kabisa na kuongea na wewe kistaarabu kama hivi. Shaffih wewe bado ni kijana mdogo sana na naamini kwenye familia yako unapendwa sana na kutegemewa. Nakuomba achana na yule mwanamke.

Niliongea huku nikiwa naanza kuondoka kuelekea lilipo gari langu.

Aah! usinitishe wewe, yani mke wa kwangu mwenyewe halafu unitishe kama hivyo.

Sikumjibu kitu kwani niliingia kwenye gari na kuanza kuondoka.


Nilirudi hotelini ambapo nilikua na mawazo mengi sana juu ya Agness. Nikakumbuka maneno ya Shaffih aliposema kuwa Aggy huwa analia kila siku na hana raha na ndoa yake.

"Ina maana Agness bado ananipenda kiasi hiko au kuna kitu kingine kinachomliza?"

Nilijisemea peke yangu nikiwa nimejilaza kitandani. Mara nikaona simu ya Vanessa ikiwa inaingia na ilibidi niipokee.

Hallo.

Yes baby, mambo.

Poa tu baby, vipi mzima?

Mimi mzima tu mume wangu. Uko wapi mbona nimekuja nyumbani sijakukuta?

( Moyo ulinipasuka sana kwani nilisafiri bila hata ya kumtaarifu Vanessa kwani niliamini asingejua kwa sababu kwa sasa yupo kwa shangazi yake.)

Nimetoka mara moja.

Umetoka umeenda wapi?

Nimekuja Bagamoyo huku kuna mambo ya kibiashara nayafuatilia.

Kwanini haujaniaga?

Samahani mke wangu ilikua ghafla sana.

Hata kama, kwani simu si zipo? Ungenipigia au hata kunitumia meseji tu ungepungukiwa na nini?

Nisamehe mke wangu nilipitiwa tu.

Sitaki, najua unanidanganya tangu lini ukawa na kazi Jumapili? Upo kwenye mambo yako wewe. Na mbona kumetulia hivyo? Haupo na mwanamke wewe?

Mmhh! mke wangu mbona unafika mbali sasa na nikudanganye ili iweje?

Sitaki Alex unanisaliti.

Aah aah! Vanessa, mambo gani hayo unaongea?

( Nilimsikia anaanza kulia na mara akakata simu )

Nikajua tayari nishaharibu na nikaona bora niondoke mchana huo wa saa 7 kurudi Dar ili niingie jioni angalau aamini kuwa kweli nilikua Bagamoyo. Nilijiandaa haraka haraka na kukabidhi kile chumba kisha nikaanza safari.


*************** ***************


Kesho yake wakati nipo kazini mida ya mchana nikaona simu yangu inaita na nilipoangalia nikaona namba ngeni. Mimi huwa sipendi sana namba ngeni na ilibidi tu nipokee na kumsikiliza ni nani.

Alex.

Agness.

Hivi unanitafuta nini Alex? Unataka kuitoa roho yangu?

Kwanini unasema hivyo Agness wangu.

Umemfanya nini mume wangu?

Aah aah! Agness hebu ngoja kwanza.

Ningoje nini?

Nisikilize vizuri kwanza usiwe na hasira kiasi hiko.

Hivi si unajua kama mimi ni mke wa mtu na yule uliyemwambia maneno hayo yote ni mume wangu?

Lakini mimi bado nakupenda Aggy na nataka uwe na mimi.

Alex tafadhali. Umeshaniumiza sana na inatosha. Naomba uniache na maisha yangu.

Nikuache vipi sasa na wakati nakupenda? Na hata wewe bado unanipenda sana maana mume wako mwenyewe ameniambia kuwa hauna raha na kila siku unalia tu. Kwanini lakini uishi maisha kama hayo na unajua mimi ninayekupenda nipo?

Alex naomba unyamaze, nyamaza Alex na usiongee kitu. Nakuomba usimfuate tena mume wangu na utuache na maisha yetu.

Siwezi nikakuacha Agness nitakupigania mpaka tone la mwisho la damu yangu. Wewe ndiye mwanamke pekee ninayetaka kumuoa hivyo siwezi nikakubali nikuache tu.

Nilimsikia Aggy akianza kulia na mara moja akakata simu. Ghafla nikajikuta siku yangu imeharibika hivyo nikaona ni bora nirudi nyumbani tu. Nilimkuta Vanessa akiwa anamalizia kupika chakula cha mchana na nilienda kujitupa kwenye sofa.

Vipi mbona mapema sana leo mume wangu?

Sipo sawa najihisi kama nina homa hivi.

Jamani, pole sana baby. Umeenda hospitali?

Hapana sijaenda.

Ngoja nimalize kupika tutaenda mume wangu.

Sawa asante sana.

Niliitikia tu lakini hata nilikua siumwi ila ni mood tu ndo imevurugika.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG