Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SAMAIRAH - 2

 

Simulizi : Samairah

Sehemu Ya Pili (2)


Jesca aliamka na hasira we mbibi ushajizeekea unaniambiaje alitaka kumpiga kofi lakini Samairah aliudaka mkono wa Jesca wakati huo Aryan anashuhudia


Mara gari aina ya prado ikaingia ilipaki pale mahali akina Samairah waliko wakati huo Aryan alitoka kidogo kwenda msalani

Alishuka mama mmoja aliita Jesca ,

Jesca aligeuka nani huyo anamwita alishangaa kumwona yule mama ambae alikuwa anafanya kazi za ndani kwao ambae ndiye mama halisi wa Aryan,

Mara mama yake na Aryan alimwona Samairah alimkimbilia na kumkumbatia ,mama akiwa na furaha aliuliza wewe binti nimetokea kukupenda ulisema unaitwa nani vile ,

Kabla Samairah hajajibu

Sauti nyingine ilisikika ikiita mwanangu Samairah unatafuta nini huku?

Alikuwa ni mama yake na Samairah ambae ndiye alimgonga na gari mama yake na Aryan

Samairah aliita mama niko kwa rafiki yangu,Abbas nae aliita Aryan kwa nguvu ,njoo uone maajabu ya leo.


Aryan anafika pale anamwona mama yake amekumbatiana na Samairah ,Aryan nae alikimbia na kumkumbatia mama yake huku analia

Pale pale Jesca alisema Mungu wangu kumbe huyu mama nilikuwa namtesa ni mama yake na Aryan uwiiiii


*****



Tulipo ishia jana baada ya mama yake na Aryan kukutana na mwanae ,Jesca aliwaza haaa kumbe huyu mama nilimtesa alivyokuwa anafanya kazi za ndani nyumbani ni mama yake na Aryan,uwiii ,mungu wangu je akimwambia Aryan yale mateso ambayo nilikuwa namfanyia Aryan atanielewaje ,

Pale pale alisogea pembeni alimpigia simu baba yake kisha mazungumzo yakaanza


" baba naomba umrudishe yule mama ambae alikuwa anafanya kazi hapo nyumbani na mshahara mlipe hata laki tano baba naomba ufanye hivyo lasivyo mwanao ntakuwa kichaa ,we Jesca una nini leo yule mama si ashaondokana sijui aliko ,Jesca alijibu niko nae huku tegeta au ile nyumba ya mbezi naomba umpe huyo mama lasivyo mwanao ntakuwa chizi ,baba yake Jesca alishindwa kuelewa mwanae ana nini.

Jesca hebu rudi nyumbani uje unieleze vizuri ,Jesca alitoroka pale pale hakumwaga hata Samairah wala Aryan alitafuta piki piki na safari ya kwenda sinza ilianza.


Aryan baada ya kumkumbatia mama yake na kumweleza majanga waliyopata nyumba imeteketea ,mama Aryan alimwambia Aryan nimekuja na mgeni huyu hapa ndio alinigongaga na gari bahati mbaya namshukuru Mungu sikuumia sana akanihangaikia matibabu hatimae nikapona ndipo akanileta na gari hadi nyumbani ,

Aryan anageuza macho amwangalie huyo mama ni nani ndipo nyuso zao zilipogongana na kugundua ndio yule mama ambae alishawahi kununua karanga maeneo ya mwenge ,pia alimnunulia na chakula ,leo hii wamekutana tena ,Aryan alishidwa kujizuia na kumkumbatia yule mama huku akitoa shukrani zake za dhati ,,yule mama alivyomwangalia binti yake aliweza kuona ile bangili na ile bangili anaijua.


Mama aliita Samairah hio bangili umetoa wapi hebu niione ,Samairah kabla hajajibu mtu ambae alimpaga aliitoa na kumwonesha mama yake mama yake na Samairah kosa moja alilofanya ile bangili aliishika na mkono ambao ulikuwa umevalia pete inayofanana na hio bangili.


Unaambiwa miale mikali ilitokea na kuingia machoni mwa Aryan ,Aryan alidondoka chini puuuu,huku akilia kwa uchungu ,kumbe ile bangili haikuwa ya kawaida na mama Samairah na mwanae sio binadamu wa kawida.


Miale ikizidi kubadilika miekundu bluu njano na iliingia kwenye macho ya Aryan ,mama yake na Aryan alikimbilia mahali aliko mwanae lakini kila akijaribu kusogea alishidwa anajikuta anarudishwa kulizidi kutokea nguvu za ajabu ,


tukirudi nyuma kidogo kwenye vipande vya story vilivyopita baada ya mama yake Samairah alivyomgonga mama yake na Aryan na alivyompeleka alirudi kwenye gari ,alilamba ile damu ambae ilidondokea kwenye siti

Leo tutajua mama Samairaha na mwanae ni akina nani na hio bangili ina kazi gani.


Mama Aryan alizidi kulia huku akiita mwanangu mwanangu wakati huo Abbas na Jesca washaondoka,wamebaki wanne tu na ilikuwa tayari ishatimia saa moja usiku.


Mama Samairah kila akijaribu kuitupa ile bangili iling'ang'ania pale ilivyogusana na pete ,mionzi mikali iliingia kwa Aryan,

Pale pale Aryan alipoteza fahamu

Radi zilizidi kupiga kwenye pande kuu za dunia ,mashariki magharibi ,kaskazini na kusini ,

Upepo mkali ulivuma

Mama Samairah alimwambia mwane mfunike mama yake na Aryan macho upesi

Samairah alimfunika mama yake na Aryan macho ,ndipo mama Samairah alianza kubadilika na kuwa kiumbe wa ajabu mama Samairah alizidi kutoka pembe moja ndefu kwenye paji la uso huku akifuka moshi mzito kwenye mdomo wake.


Mama Samairah ule moshi ulianza kupaa hewani na kutengeneza mistari ya rangi mbili ,bluu na kijani ambayo sawa na ile bangili mama Samairah alisema asante mwanangu umefanikisha kunirudisha niliko toka nakuacha mwanangu baki kwenye hii dunia lakini bado niko na wewe leo hii naenda kukutana na baba yako nimepata njia ya kurudi nilikozaliwa.


Mama Samairah alipotea alifuata ule moshi ambao ulitengeneza mistari miwili pale ndipo bibi alifunguka macho yake na kuweza kuona vizuri, bibi alisimama na kuuliza naota ama ni kweli ivi kweli naona ee

Wewe binti mbona umemkumbatia huyo mama macho ,Samairah baada ya kuambiwa vile na bibi alimwachia mama yake na Aryan ,mama hakuelewa chochote aliuliza yule mama yako ameenda wapi,?


Samairah alitabasamu na kusema kaondoka hivyo naomba tumbebe Aryan tumwingize kwenye gari kisha niwapeleke kwenye nyumba mpya kuanzia leo mateso yenu yameisha ,

Samairah alivyoangalia chini aliona ile bangili aliichukua na kuivaa ,

Samairah baada ya kumpakia Aryan alimpandisha na bibi kisha na mama yake na Aryan ,Samairah aliwasha gari ,ndipo alisikia sauti ikimpa maelezo na ile sauti ilikuwa ya mama yake ,


"Samairah najuwa wewe ni binadamu ambae una asili ya kijini naomba uhakikishe hao watu wanaishi maisha mazuri ,naomba uwapeleke mbezi kwenye ile nyumba yetu mpya,

Samairah aliwasha gari hadi maeneo ya mbezi alifika alipiga honi mlinzi alifungua geti kisha gari ikaingia ilikuwa ni nyumba ya kisasa mlango ulifunguliwa na mdada wa kazi kisha Aryan aliingizwa hadi kitandani akiwa hajitambui , Samairah alionekana si mgeni wa hiyo nyumba alienda chumba flani alitoa chupa ambayo ilikuwa na maji meupe alimimina machoni mwa Aryan na kifuani.


Ndipo pale Aryan alianza kuota ndoto "ilikuwa siku ya juma mosi Aryan akiwa na baba yake ,baba alimwambia mwanangu twende leo bahari inatoa utajiri nimeoteshwa ndoto ,Aryan alimuuliza baba ,sasa baba bahari itatoaje utajiri?

Baba alicheka na kusema mwanangu hii story ya bahari kutoa utajiri ni yatoka enzi na enzi ni pale inapotokea mwezi kuvutana na jua na leo imetokea hivyo tukienda baharini tutapata utajiri ,


Aryan alikubali aliondoka na baba yake walifika baharini ndipo walikuta watu wengi wapo baharini wanasubiri kupata utajiri ,siku hio ilikuwa ya tofauti kabisa tofauti na miaka ya nyuma.


Miaka ya nyuma ikitokea kupatwa kwa mwezi basi ukienda baharini utakutana na vito vya thamani lakini leo hii tumekuta na bahari ikiwa na mawimbi makubwa ,


Watu wengi wakiwa wamejaa baharini ,Aryan akamuuliza eti baba hawa watu nao wanasubiri utajiri? Ha ha ha baba alicheka na kusema ndio mwanangu hawa wote wanasubiri utajiri maana leo bahari inatoa utajiri ,lakini baba mbona watu wote wapo wakubwa huku na hakuna watoto wadogo kama mimi kwanini umenileta?

Aryan aliuliza , baba alikaa kimya na kusema mwanangu huu utajiri unaweza ukawa wakweli ama wauongo maana bahari huwa na tabia ya kumeza watu hivyo ikitokea hivyo basi mwanangu naomba uhakikishe unamtunza mama yako na ukikua na wewe usije ukafuata hizi mila ,

Basi siku hio mida ya saa tano mwezi ulianza kupigana na jua ,ila wanasayansi wanasema kupatwa kwa mwezi ,jua lilianza kumeza mwezi ndipo giza lilianza kutanda baba alimkalisha mwanae mbali kabisa na bahari ndipo yeye alisogea kwenye kingo za bahari ili kuangalia kama bahari itarusha madini ama vito vyenye thamani.


Aryan akiwa anamwangalia baba yake akiungana na watu wengine baharini ,Aryan aliwaza ina maana hawa watu wote wakiwa matajiri dunia itakuweje ,lakini wakati anawaza.


Yalitokea mawimbi makubwa ambayo yaliruka hewani na kwenda kuwakumba watu wote ambao walikuwa wamesimama pembezoni mwa bahari wakisubiri utajiri

Ila siku hio ilikuwa ya tofauti watu wote walimezwa na bahari kisha wakazamishwa ndani,


Aryan alisubiri kwa muda huenda atamwona baba yake lakini hakutokea ndipo alipo tokea ndege mzuri mwenye rangi ya blue pamoja na kijani alikuja na kukaa mbele ya Aryan akiwa mdomoni na bangili aliiacha ile bangili kisha akaruka na kutokomea mbali ya upeo wa macho ,


Aryan aliinuka na kuokota ile pete aliipenda kisha alitokea kumpenda yule ndege


Aryan alichukua ile pete na kuiweka mfukoni cha ajabu baharini hapakuwa na njia baada ya wale watu kumezwa na bahari alitokea mama mmoja alionekana akiwa makini akitafuta kitu alipita mahali aliko Aryan lakini hakumwona Aryan,,,,,ila Aryan yeye alimwona alitizama na kusema yule ndege alitua hapa sasa hio bangili iko wapi ,aliitafuta hakuiona ,Aryan alitaka kusema bangili hii hapa lakini kinywa kilikuwa kizito


Hatimae taarifa zilisambaa watu kumezwa na bahari wakiwa wanasubiria kuona utajiri ,Aryan alilia sana baada ya baba yake kutotokea alirudi nyumbani na kumkuta mama yake anaumwa akiwa hoi

,,,Mama mama amka nini tatizo Aryan alimwita mama yake lakini alitoa ile bangili alivyoiweka kitanda cha mama ,Aryan alishuhudia kitanda kikivunjika changa paaa

Mama alidondoka Aryan kwa kuwa alikuwa mdogo alihangaika kumwinua mama yake ,hata hivyo mama nae alijaribu kujikakamua alisema anahisi kifua kimebana


Aryan alimwangalia mama yake kisha akasema mama pole ila nimeokota hii bangili nimeipenda aliiweka kifuani mwa mama yake ndipo mama

Alikohoa kwa nguvu alitoa mwanga mdomoni wa rangi ya bluu na kijani kama rangi ya ile bangili


Ule mwanga uliingia kifuani mwa Aryan na ndipo toka hiyo siku alipata huo ugonjwa wa kupoteza fahamu,"


Turudi upande wa pili kwa Jesca alivyofika nyumbani alikuwa akilia akisema mama baba leo nakuwa chizi Aryan wangu ,namtaka yule mama mmupe hata nyumba Aryan hana nyumba.


Yale maneno yaliwachanganya wazazi wake na Jesca ndipo baba aliuliza unanini? Jesca alipita hadi sebuleni kufika sebuleni

Alibaki mdomo wazi baada ya kuwakuta Kudra na Mussa wamekaa kwenye masofa wameshika visu



Tulipo ishia jana baada ya Jesca kufika nyumbani aliongea na kuonekana kama amechanganyikiwa lakini alivyo tupa macho kwenye masofa aliwaona Kudra pamoja na Mussa wakiwa wamekaa kwenye mikono yao wameshika visu,

Jesca alishituka kidogo kisha akajisogeza hadi waliko akina Kudra na kuuliza kwa upole ,Kudra na Mussa ehe nambie mmefuata nini?


Kudra aliachia kisu kwa dharau kisha akasema "Jesca haiwezekani uaibishe familia yako elewa baba yako na baba yangu ni marafiki inawezekana vipi umpende yule choko ,kinachoniuma eti Mussa humtaki ,halafu baba yangu kasema msimu huu wa mitihani ataenda kuhonga walimu ili sisi watatu tufaulu kwenye mtihani"


Jesca aliwaangalia kwa umakini na kuwauliza kwa nini mmechoma moto nyumba ya akina Aryan ,Mussa alidakia na kusema aaah sisi tuchome moto ili tufaidike nini ,sisi hatuja choma moto ,tulipata taarifa kwenye mitandao kisha tukafika na kuja kushuhudia ,Jesca alikaa kwenye kiti na kusema nikweli baba yako atatoa hela ili tufaulu au mnanidanganya,Kudra alisema sasa tukudanganye ili iweje ,ndio hivyo kama upo tayari useme halafu tupange misheni nyingine,

Jesca alitulia na kusema yaa nakubali ila wakitoa hela waambie waniweke mimi niwe wa kwanza halafu wewe Kudra wapili halafu Mussa watatu vipi hapo si itakuwa poa


Wote waliitikia na kusema ndio itakuwa poa ,"lakini mwalimu Farida jioni nilipita kwake kanambia wanafunzi watatu wa shule ya makongo wamehamia kwetu halafu wote wakike na inasemekana wana akili mbaya,

Jesca kwa mshituko alisema haa wale wadada wamehamia sijui akina Nanaa ,Lusi na nani mwingine , Mudra alisema na Joyce


Okay tutawakalisha msijali sisi tunatumia pesa halafu wao wanatumia akili ,Mussa alisema ,unajua kale kaboya Kiaryan kinajiona kina akili,, baada ya kuanza urafiki na Aryan sasa tunataka tuunde misheni tutakula dawa ya unga utapaka kwenye kitambaa kabla ya kuingia kwenye mtihani utamziba mdomoni akishavuta ule unga , akiingia darasani atasinzia tu ,hivyo akijibu swali moja atalala ,na akilala sisi ndo tunapata nafasi ya kufaulu ,


Jesca alishangilia na kupiga makofi akasema hapo bomba ,kisha akina Kudra waliaga na kuondoka zao ,walimwacha Jesca na mama yake ,Jesca alianza kumuhadithia mama yake "mama yule mmama ambae alikuwa anafanya kazi hapa kumbe alikuwa mama yake na Aryan kijana ninayempenda kuliko kitu chochote ,mama kama kuna uwezekano tumrudishe hapa ili aje afanye kazi halafu mmlipe mshahara mkubwa ,hapo ndipo atamshauri mwanae awe mpenzi wangu ,


Au tuwanunulie nyumba ,maana hawana nyumba ya kuishi,mama Jesca aliwaza ,mmmh mwanangu sikufichi yule kijana sidhani kama ataweza kuwa mpenzi wako maana kwa unyama uliomfanyia yule mama sidhani ,

Yale maneno ya mama yake Jesca yalimfanya Jesca akose amani basi Jesca aliondoka na kuingia ndani chumbani kwake


,tukirudi maeneo ya mbezi kwenye jumba la kifahari baada ya kukumbuka matukio ya nyuma jinsi alivyookotaga ile bangili alizinduka huku akiita mama mama'

Alikurupuka alivyogeuka alimkuta mama yake amejiinamia ,mama alisogea na kuushika mkono wa mwanae kisha akamwinua

Aliita Aryan uko salama? Aryan akiwa anahema alijibu ndio mama lakini nimeota ndoto mbaya sana ,

Mama alimwambia pole mwanangu


Aryan aliuliza hapa tuko wapi? Mama alitabasamu na kusema mwanangu hapa tuko mbezi na hii ni nyumba mpya ambayo tumepewa na mama yake Samairah ,lakini huyo mama kasafiri Samaira alinambia , Aryan aliuliza na bibi yuko wapi ,

"Bibi yuko sebuleni anaangalia tv ,mama alisema na kufanya Aryan acheke ha ha haaaaa mama sasa kipofu anaangaliaga tv ama anasikiliza ,mama alisema anaangalia nenda utamwona,

Aryan aliinuka na kuelekea sebuleni alimkuta bibi kakodolea tv anaangalia move ya kilio changu ,

Aryan alijua labla bibi haoni ,alisimama mbele yake ,bibi alisema Aryan umeamka mjukuu wangu kaa pembeni usinikinge naangalia tv ,pale Aryan alichoka ndipo alipouliza bibi sasa hivi kwani unaona?


Bibi alitabasamu na kusema sijui nimejikuta naona macho yangu yalifunguka sijui baada ya kupata moshi mwingi ndo yakaamua yaone ,Aryan alicheka na kusema kweli haya maajabu.


Ki ukweli Aryan ,bibi na mama yake hawajui kitu chochote kilichotokea ila ukweli kamili Samairah anaujua na mpaka sasa Aryan hajagundua kama Samairah si binadamu wa kawaida ,


Aryan alishangaa kukuta nyumba ina mfanyakazi wa ndani getini mlinzi yupo ,ilibidi aulize ,mama sasa hii nyumba tumepewa kivipi maana sijaelewa ,mama alisema hata mimi sijui ila Samairah ameondoka kasema kesho ndio atatueleza vizuri.


Basi Aryan alirudi kwenye chumba chake aliwasha taa na kujisemea leo hii taa inawaka ntasoma hadi kieleweke na sasa sina mawazo tena nimempata mama yangu sasa ivi ni mwendo wa kusoma ,

Aryan alishika kitabu cha jografia lakini kila akifungua topiki anajikuta anaijua ,yote sasa hadi akawa anajishangaa na kusema kumbe watu wanao soma kwenye umeme wanakuwa na akili ivi Aryan aligairi kusoma na kusema kesho kitaeleweka huko huko ,


Asubuhi yake alizivaa nguo zake za shule kisha akatoka getini alianza kutembea mdogo mdogo ,ile anafika geti la shuleni ,Aryan alishangaa mabinti watatu warembo kupitiliza na walikuwa ni wageni machoni mwake ,

Walimkimbilia na kwenda kumkumbatia huku wakitaja jina Aryan Aryan Aryan ilibidi aogope inawezekana vipi wanafunzi wageni wajue jina lake.


Mimi naitwa Joyce nimehamia hapa shuleni kwenu toka shule ya makongo kiukweli hongera siku ile uliimba wimbo mzuri niliupenda '' Joyce aliongea huku akimgusa gusa mikono Aryan


Mara mwingine akadakia mimi naitwa Nanaa ,naomba nikupokee hicho kitabu halafu leo si ndo tunafanya mitihani ee ,Aryan alisema yaa tunafanya mitihani kisha aliondoka hakutaka kuweka nao ukaribu


Lakini wakati anapiga hatua mbili tatu Aryan alishangaa anashikwa mkono alivutwa kidogo kugeuka alishangaa kumwona Jesca mtoto kaweka lipstick kapendeza mbaya ,Aryan alimkazia jicho na kumwambia nini unataka ,Jesca aliyakwepesha macho yake na kujisemea "Aryan toka mwanzo nakupenda ila wewe hutaki kunielewa halafu leo ninazawadi ya mama yako ,baadae ntakupa" ,


Aryan alimwambia sawa baadae kisha akaondoka ,ile anataka kuingia darasani alikutana na kundi la akina Mussa wamesimama kati kati mlangoni , Aryan alisalimia mambo zenu ,akina Mussa walikausha Mussa alitoa bisi bisi kisha akamwambia oya we boya unaona hii leo lazima izame mwilini mwako kisha akarusha ngumi nzito ambayo ilimpata Aryan maeneo ya kwenye paji la uso.


Uwiiii jamani mkono wangu ni kelele za maumivu Mussa alipiga baada ya kumpiga Aryan aliteguka vidole vyote lakini Aryan wala hakuumia aliondoka zake na kwenda nje ,


Hatimae muda wa kuingia darasani uliwadia Aryan kila akiangalia hamuoni Samairah ,mara Abbas akaja ,"vipi ndugu yangu umemuona Samairah" Aryan aliuliza

Abbas alitabasamu ndio Samairah nimemuona yupo zake kidato cha kwanza amekaa zake kimya , kengele iligogwa wanafunzi walikusanyika mstarini mwalimu alisimama na kuwatambulisha akina Joyce,Nanaa na Lusi na kuwaambia kuwa ni wanafunzi wapya wamehamia kwenye shule yetu.

Wakati wanafunzi wote wapo mstarini Kudra aliwasili akiwa na baba yake waliingia ofisi ya mkuu wa shule.


Baba yake akawa anamaongezi ya siri na mkuu wa shule ,mzee alitoa bahasha tatu zikiwa zimejaa hela ndipo mzee akaongea ,mkuu wa shule nina vijana watatu nataka mhula huu waongoze majina yao yapo kwenye hizo bahasha na bahasha zipo na pesa za kutosha milion moja.


Mkuu wa shule baada ya kusikia kiwango cha pesa kwanza alitabasamu na kusema hilo ondoa shaka wataongoza wala usijali

Baba yake Kudra aliaga na kuondoka ,

Mkuu wa shule aliziangalia zile pesa akajisemea moyoni matajiri mnahangaika sana kama mtoto hana akili si ukubali tu ,kisha akaziweka zile pesa kwenye droo.


Wanafunzi walianza kuingia kwenye madarasa Jesca alitoa kitambaa cheupe ambacho kilikuwa na sumu ya unga alimfunika Samairah kwa sekunde tatu kisha akakitoa

Akina Mussa na Kudra waliona kisha wakamkonyeza Jesca yess kazi nzuri.


Kudra alisema sasa hapa ndio msimu wangu kule mzee ashamaliza kwa mkuu wa shule na haka ka Samairah kanajifanya kana akili leo katalala tu darasani.


Samairah alielewa mchezo alivyoingia darasani aligawiwa karatasi ya maswali na majibu ,alimwangalia Aryan mahali aliko aliona Aryan yuko bize anajibu.


Samairah alijibu mtihani ndani ya dakika kumi ashamaliza maswali yote,tambua Samairah anauwezo wa ajabu ,alivyomaliza alilala

Sasa akina Mussa na Kudra walianza kukonyezana na kusema yeees tumemuweza ,Samairah alijifanyisha anaushingizi lakini ile sumu haikumdhuru hata kidogo.


Hatimae walipo maliza mtihani walitoka nje ,Jesca kwa mbwembwe alimuuliza Samairah mbona ulikuwa umelala? Samairah alimwambia hata sikuelewa nilijikuta na usingizi

Vipi umemaliza mtihani ,Jesca aliuliza ,Samairah alikaa kimia kwa muda kisha alianza kuwaza.


Jesca huna wema nilikuokoa ulivyotaka kubakwa halafu unataka kunifanyia hivyo ila kwangu umechemsha alimjibu hata sijui kama nimemaliza.


Aryan wakati anatoka kwenye mtihani ,alitoka na kwenda kukaa nyuma ya madarasa alishangaa kumwona mrembo Joyce anakuja na kukaa karibu yake ,Aryan vipi mtihani umeuonaje ,Aryan alisema mbona wakawaida.


Joyce macho yake yalikuwa kwenye uso wa Aryan alimwangalia na kusema hakika wewe ndiye mwanaume wakipekee nani kakupa huu mvuto? Mtoto alianza kuwaza mwenyewe mara Jesca nae alitia timu bila hata kuuliza alimpiga mtoto wa watu na jiwe kichwani kisha akaongea nyie wapuuzi mmehamia kwenye shule ili mnichukulie mpenzi wangu hapa hapati mtu,


Masikini Joyce alianza kujihisi kizungu zungu huku damu zinamtoka kichwani alijaribu kuinuka akajikuta anayumba ile anataka kudondoka mtaalamu Aryan aliwahi na kumdaka ,

Ile anamdaka Joyce ,Mussa nae alitia timu ,aliitoa bisi bisi na kutaka kumchoma Aryan

Masikini bisi bisi ilienda moja kwa moja na kuikita kwenye paja la bibie Joyce ,


Joyce alipiga kelele za maumivu jamani nakufaaaaa.



Tulipoishia jana baada ya Mussa kutaka kumchoma bisibisi Aryan,ila kwa bahati mbaya ilimkuta bibie Joyce kwenye paja lake ,Joyce alipiga makele ya uchungu ,huku akiomba msaada jamani nakufa ,nakufaa mie ,walimu na wanafunzi walikimbia na kuwahi nyuma ya shule ,ndipo walishangaa kumwona msichana aliyehamia shule ndo kwanza anasiku moja tayari kaumizwa damu zimeenea mwili mzima ,Mussa wala hakukimbia alisimama pale pale ,ndipo Aryan alitoa maelezo kwa mkuu wa shule ,

Mkuu washule alitoa kauli moja ,we Mussa nifuate ofisini ,kisha akaanza kupiga hatua kuelekea ofisini ,huku,mwalimu wa biology akimchukua Joyce na kwenda kumpatia huduma ya kwanza.


Mussa wewe ni mtoto wa mzee Obote yule tajiri? ,mkuu wa shule aliuliza hilo ,swali ,Mussa kwa kujiamini alijibu ndio ,huku akionesha kiburi ,mkuu wa shule alitabasamu ,aliongea ngoja nimpigie baba yako simu,mkuu wa shule alibonyeza vitufe kadhaa vya simu yake baada ya muda kidogo simu ilipokelewa na mazungumzo yalianza ,

Haloo Mr Obote ,ni mimi hapa mkuu wa shule anaposoma kijana wako Mussa ,upande wa pili sauti nzito ilijibu ,ehe kuna tatizo gani,"mkuu wa shule aliendelea kuongea ,mtoto wako kapiga mwanafunzi mwenzake ki sheria hilo ni kosa kubwa hivyo mtoto wako tunamfukuza shule,

Mr Obote alikohoa kidogo kisha akasema mkuu kwanini unataka kufanya hivyo naomba tufanye yaishe hapo hapo shuleni haina haja ya mimi kuja ,nakutumia laki sita sasa ivi kijana wangu aendelee kusoma ,


Ha ha ha ,mkuu wa shule alicheka huku mkono wa kushoto anagusa gusa kitambi chake alisema ongeza laki moja iwe laki saba ,Mr Obote nae hakubisha alisema sawa ,

Baada ya muda kidogo simu ya mkuu wa shuke iliingia sms ,mkuu wa shule aliitizama simu yake na kuona m-pessa ,alitabasamu alivyohakikisha kuwa pesa imetumwa alimruhusu Mussa akatoka na kwenda darasani kuendelea na mitihani .


Zilipita siku kadhaa baada ya tukio la kuumia kwa Joyce ,huku Aryan kila akimtafuta Samairah waongee ,Samairah alikataa na kusema hajisikii vizuri,ukaribu wa Samairah ulimfanya Aryan kujiona na yeye ni mtu kati ya watu lakini alijikuta anakosa furaha baada ya Samairah kukataa kata kata kuongea nae.


Hatimae walimaliza mitihani Aryan alimfuta Samairah na kumshika mkono,Aryan alimuuliza Samairah kwanini hutaki kuongea na mimi ni kitu gani nimekukosea? ,Samairah hakujibu chochote zaidi ya kudondosha machozi ,kisha akamwambia Aryan niache niende ila ipo siku nitakuambia yanayo nisibu,Aryan hakuwa na la kufanya alimwachia Samairah akaondoka,


Samairah alianza kuwaza ,"Aryan nakupenda lakini kila siku unakuwa kwenye matatizo najaribu kukaa mbali nawe ili nisione ukionewa ,maana nahofia kutumia hasira zangu na kuwadhuru wengine ,.Aryan najua nakupa wakati mgumu ila nitakueleza kwa undani zaidi ,pia ninachohofia muda sio mrefu utapoteza mtu ambae unaukaribu nae na hupendi apotee ila atapotea,"


Samairah alifuta machozi yake kisha akabeba begi lake na kuondoka zake moja kwa moja hadi nyumbani.


Tukija maeneo ya tegeta tunamuona mdogo wake na Abbas ambae anaitwa gwae , alivyotoka shuleni na wenzake moja kwa moja alirudi nyumbani mida ya saa nane ,lakini siku hiyo hakumkuta mtu yeyote nyumbani,


Gwae mwenye umri wa miaka mitano alilitizama kufuli mlangoni ,kisha akashika tumbo lake,alishangaa utumbo wake ukiunguruma kwa fujo yote hayo chanzo ni njaa alikuwa kakabiliwa na njaa mno ,

Mtoto mdogo alikaa pale uani hadi ilivyofika saa kumi jioni alihisi mwili kulegea na njaa

Gwae alianza kuwaza sasa mama kaenda wapi halafu leo hajanipa hela ya kula shuleni nimerudi nyumbani hayupo ,,gwae alibidi aondoke hapo nyumbani hadi kwa mama Ashura akiwa na rafiki yake Rashidi ambae walikuwa wanasoma darasa moja ,


Rashidi ,"mimi nimeenda nyumbani sijamkuta mama yangu sijui kaenda wapi halafu nasikia njaa ,gwae aliongea huku midomo yake kuonekana kukauka yote sababu ya njaa,Rashidi alimuuliza kwani kaka yako Abbas anarudi lini "gwae alitizama jua na kusema huyo hadi jua lizame ,

Gwae alitizama kwa mama yake na Rashidi mama ambae anajulikana kwa jina mama Ashura aliona akipakua wali ,gwae alijikuta akimeza mate na kutamani walau autie kinywani,

Hazikupita dakika mbili ,

Mama Ashura alimwita mwanae ,Rashidi ,njoo ule mwanangu ,Rashidi aliitika naam mama nakuja ,Rashidi alimwambia rafiki yake gwae twende tukale mama yangu tayari ashapakua ,

Gwae alitabasamu maana alikuwa amebanwa mno na njaa halafu kwa umri wake mdogo alikuwa kachoka ,gwae alianza kumwelezea Rashidi ,mimi sijui mama yangu kapatwa na matatizo gani ,jana usiku hata hajatupikia yaani kaja kapika uji bila sukari halafu akasema kunyweni kama hamtaki acheni ,


Mama aliondoka usiku huo huo ,hata sijui wapi kalala natamani hata baba yangu angekuwepo najua angeninunulia maandazi na kachori ,ki ukweli gwae alikuwa mdogo lakini alikuwa na akili sana.


Wakati huo Rashidi na gwae waliingia kwa mama Ashura walikuta kapakua sahani moja ,

Kisha aliweka chini kwenye mkeka ,Rashidi alichukua maji akanawa mikono kisha akampa na gwae anawe ,ile gwae anaanza kunawa mama Ashura alishika bakuli la kunawia mikono kisha kwa sauti ya juu akaongea.


We we we mtoto koma hapa hamna kula ,nasema kale kwenu ,we mtoto inuka kale kwenu ,mama Ashura alimtimua gwae ,Rashidi alidakia na kusema mama mwache ale amesema anasikia njaa halafu mama yake hayupo ,

Rashidi kabla hajamaliza alipigwa kofi zito na mama yake ,masikini Rashidi alilia ,,kitendo cha kulia ndio alizidi kumchokoza mama yake ,

Mama Ashura alishika mpini wa jembe na kusema Rashidi nakupasua kimyaa kaa hapa na ule upesi ,nitakupasua nyau wewe ,"mama Ashura aliongea kwa ukali mno tena kwa sauti ya juu na kumfanya mwanae atulie na kuanza kula huku analia


Wakati huo gwae kasimama anaangalia rafiki yake anakula ,huku tumbo lake likinguruma na njaa ,mama Ashura alimshika gwae masikio alimvuta kwa nguvu hadi gwae akalia kisha akamrusha nje ,

Gwae alikaa hapo njee huku analia maana alivutwa sana masikio ,mama Ashura kaanza kuongea tena "tena wewe mtoto hizi hasira nilizonazo zitakuishia juzi nilimwomba mama yako wigi niende kwenye kitchen party alininyima ,nilimwomba aniazime gauni lake na mkoba lakini mama yako alikataa kata kata ,

Na mimi nasema hapa chakula huli kama mama yako hayupo utakula udongo upo ,hebu toka hapo usinitie kichefu chefu , " mama Ashura aliongea ndipo mama bonge alidakia na kusema hata mimi haka katoto sikapendi ,kalinigombanisha na mme wangu , juzi nilikuwa ile baa ya pale bondeni si nilipata kabuzi flani tukiwa kwenye korido moja kwenye uchochoro wa pale kwa mama pita ,si kale kabuzi changu kalinikumbatia na kuanza kunibusu , haka katoto sijui kalitokea wapi kaliniona ,kakakimbia na kuja kumwambia mme wangu ameniona niko na mwanamme tumekumbatiana ,nakuambia shoga yangu mme wangu aliwaka


Hadi nimetokea kukachukia haka katoto ,kaende zake huo ,gwae aliinuka chini ndipo aliangalia sebuleni kwa rafiki yake alimwona anakula ,gwae alizidi kujisikia vibaya


Mara kuna muuzaji wa mitumba alipita jirani na kwamama ashura ,mama Ashura huwa hapitwi na kitu alimsimamisha na kuanza kuchagua mitumba alichukua gauni mbili kisha alimnong'oneza muuza mitumba ,kaka hapa sina hela halafu hizi nguo nimezipenda baadae uje mme wangu atakuwa hayupo anaenda kazini maana analinda hivyo tutamalizana


Muuza mitumba alijikuta anajilamba midomo baada ya kuona maziwa ya mama Ashura alivyoyapiga jeki na brazia kisha yakajaa vyema huku kavalia dera lake na alivyojaaliwa nyuma ,basi muuza mitumba alijikuta anaitikia sawa nitakuja ,


Mama Ashura aliondoka akiwa ametabasamu ,tukirudi kwa gwae baada ya mama Ashura kwenda kuchagua mitumba ,rafiki yake alimwita walau apate vijiko viwili vya ubwabwa kisha akipata na kikombe cha maji tumbo litatulia,

Rashidi alikuwa anampenda sana rafiki yake gwae maana hata kwenye masomo huwa akishidwa hesabu gwae anamsaidia .


Gwae njoo kula upesi mama kaondoka Rashidi alisema ,japo gwae alikataa ila rafiki yake alimlazimisha akale hakupenda amwone akishinda na njaa

Gwae kutokana na njaa kuwa kali alijikuta anakubali waliingia sebuleni haraka na kukaa kwenye kamkeka kadogo ,gwae alipeleka matonge mawili

Ile anapeleka mkono achukue tonge la pili,mama ashura tayari alikuwa ashaingia


Mama Ashura hakuwa na huruma hata kidogo aliruka na kusema wewe mtoto wa malaya mama yako kaenda kutembea na mabwana zake alimuua mmeo ili apate uhuru wa kutembea na wanaume wawatu ,,wakati huo gwae ndio mkono unafika kwenye sahani alivyoshituka baada ya kumwona mama Ashura alibaki vile mkono ukiwa kwenye sahani.


Mama Ashura aliukanyaga mkono wa gwae na kuukandamiza chini kwa nguvu ,ni sauti ya mfupa ilisikika koooooooh! Huku sambamba na kilio cha gwae

Mama nakufaa mkono wangu ,ndipo mama Ashura aliutoa mguu wake kisha akaangalia mkono wa Gwae tayari ushavunjika

Ha ha ha ha ha ha

Alicheka na kusema hiyo ndo dawa ambayo ulikuwa unaitaka

Masikini Gwae mkono umevunjwa kisa chakula jmn


SONGA NAYO

Episod ya 19

Tulipoishia jana baaada ya mama Ashura kuukanyaga mkono wa Gwae na kuvunjika ,masikini mtoto alianza kulia huku akiita mama mama ,Gwae alipata maumivu makali mno ,njaa yake na rafiki yake kumjali ndo ilomfanya kufikia kuvunjwa mkono ,Gwae kila akiangalia mkono wake ndipo alizidi kulia kwa nguvu ,


" mama Ashura wala hakujali kama kamvunja mkono ,ndo kwanza kainama na kuichukua ile sahani ya ubwabwa na kupeleka chumbani kwake ,,Rashidi alimwangalia Gwae akilia na yeye akajikuta machozi yanamtoka ," mama Ashura alitoka na kumkuta mwanae akilia ,aliita Rashidi kisha akampiga kibao kizito ,kelele ,unalialia nini si nishakukataza kutembea na haka katoto kwanza mama yake anasifa mbaya hapa mtaani,ashaua mume wake ,isitoshe ni ......mama Ashura hakumalizia alisita na kuacha ,kisha alimshika mwanae mkono na kumpeleka chumbani kisha akamfungia.


Mama Ashura alimwendea Gwae na kushika fimbo ,haya geuka ulikotoka nenda kwenu usitupigie makelele kwanza mie nina miahadi na muuza mtumba nijiandae kunengua viuno nimfilisi mtaji wa mitumba si kapenda mwenyewe ha ha .


Hakika mama Ashura aliongea hivyo huku akimwangalia Gwae akiondoka huku analia mkono wake umevunjika ,mamaa mkono wanguu mamaaaaa! Naumiaa !! ,mama panauma

Hakika Gwae alilia kwa uchungu huku akielekea kwao.


"Aryan hebu tulia mbona nasikia sauti kama ya mdogo wangu Gwae akilia " Abbas aliuliza wakiwa maeneo ya kwa akina Abbas ,Aryan nae alisikiliza kweli kama vile sauti ya Gwae itakuwa jino lingine limeng'oka nini maana sasa hivi ndo umri wake wakung'ooka meno, Aryan aliuliza wakati huo tayari kagiza kashaanza kuingia ,

Abbas alisema "hebu twende tumfuate ," walianza kutembea taratibu kuelekea mahali inakotoka hio sauti ya kilio ,

Walikatiza uchochoro mmoja ndipo wakakutana uso kwa uso na Gwae akiwa analia kwa uchungu.


Abbas alivyomuona mdogo wake mkono ulivyolegea alijua huyu tayari amevunjika ,we Gwae umefanyaje mkono wako ,maana wewe kwa utundu haujambo,

Gwae kwa sauti ya kilio alisema kaka mkono umeumia ,hiii hiii "Abbas aliuliza tena umefanyaje wakati huo tayari ameushika mkono ,pale pale Abbas alijikuta akichuchumaa na kusema ulikuwa unacheza mchezo gani hadi ukavunjika mkono ,

Gwae alijibu mama yake na Rashidi kanikanyaga.


Aryan alidakia mama yake Rashidi !,Gwae ilibidi aeleze kilichomkuta,kaka mama Rashidi amenikanyaga alivyonikuta nakula chakula na mwanae ,na kunambia kuwa hataki nile kwako,

Abbas siko zote huwa anahasira mbaya kulikuwa na kibanda flani cha fundi seremala kwa juu alikuwa kaweka miti miti ili kuzuia upepo using'oe bati

Abbas alivuta limti likubwa na kulitia begani alisema mama Ashura kwangu umechokoza nyuki ,leo utaiona kuzimu , basi Abbas akiwa amepandwa na hasira Aryan alimzuia na kumwambia Abbas hapana usifanye hivyo ,


Abbas alimsukuma Aryan na kumwambia niache ,ila Aryan aliinuka upesi na kujikaka mua ,alimzuia Abbas kwa nguvu na kumwambia maneno ambayo yalimfanya Abbas akaelewa,


"Abbas tafadhali nakuomba usifanye hivyo chamsingi tumpeleke Gwae hospitali akapatiwe matibabu ili asiendelee kuuumia sasa ukifanikiwa kumuua mama Ashura na ukapelekwa jela je Gwae nani atamhangaikia kama ujuavyo mama yako siku hizi kabadilika hatulii nyumbani,"

Sawa Aryan nimekuelewa nimeacha twende tumpeleke kwanza dogo hospitalini, Abbas alielewa na kutupa ule mti walimpeleka hadi hospitalini ,maeneo ya tegeta kibaoni njia ya kuelekea madale kuna hospitali moja inaitwa P.K


Walifanikiwa kupokelewa vizuri kisha Gwae akapelekwa kwenye chumba cha kufungiwa p.o.p, yaani lile gamba gumu,watu wengi wanapenda kuita hogo.


Abbas akiwa amejiinamia alimuuliza Aryan ,sasa tumemleta Gwae na matibabu ashaanza kupatiwa hiyo hela tutaipata vipi laki tatu yote hiyo, Aryan alishusha pumzi kisha akasema kuna hela Samairah alinipa laki mbili tutaongea na madaktari wataelewa bana usihofu ,Abbas kidogo akashusha pumzi


" lakini Aryanmama yangu kazidi halafu unasema nimvumilie hadi lini ,ona hadi sasa hivi tumerudi shule hatujamkuta na usiku katulaza na uji daah mama simwelewi hata kidogo",

Aryan alijibu" Abbas elewa huyo ni mama yako hata awe na sifa mbaya kiasi gani atabaki kuwa mama yako hivyo ninachokushauri usisikilize maneno ya watu,"

Sawa Aryan nimekuelewa, Abbas aliingiza mkono mfukoni alitoa karatasi kisha akasema

Oya Aryan kuna karatasi hii hapa nimekuta pale home sijui mama atakuwa ameacha ujumbe.


Abbas alifungua lile karatasi na kukutana na ujumbe aliouacha mama yake " Abbas hakikisha unamtunza vizuri mdogo wako Gwae mimi nipo maeneo ya hapa hapa nyumbani ila nyumbani nitakuwa siji mara kwa mara.


Abbas ule ujumbe ulimfanya achoke ,Aryan alimshika bega Abbas na kumwambia haya mapito tu ,hebu fikiria mimi niliishi mwenyewe hadi nikaachaga na shule lakini sikukata tamaa ninachokuomba kaza moyo.


Akina Abbas walimsubiri Gwae hadi muda wa saa sita usiku ndipo alifanikiwa kufungwa mkono wake kisha Aryan akaingia kwenye chumba cha daktari mkuu kwa ajili ya malipo,

Aryan alimwangalia daktari kwa umakini ,kuna miale midogo ilitoka kwenye macho ya Aryan na kuingia kwa daktari ,

Daktari alijikuna kichwa ,wakati huo Aryan anawaza atamweleza vipi daktari ili akubali kupokea laki mbili ,!


Mara daktari alimwangalia Aryan na kumwambia haya mgonjwa wako tayari kama tulivyokubaliana nipe hio laki moja. Aryan hakuamini ikabidi aulize umesema shilingi ngapi?

Daktari aliseti miwani yake na kusema sina muda wa kuzungumza sana kuna wagonjwa wengi wananisubiria nimesema unipe laki moja,


Aryan upesi alitoa laki moja kisha wakaruhusiwa kuondoka na kupewa dawa za kupunguza maumivu ,walichukua bajaji na kuanza kurudi nyumbani.

Njiani wote walikuwa kimya kila mmoja akiwaza vitu vyake


Walifika kwenye baa flani maeneo ya karibu na nyumbani ,bajaji iliharibika ,ndipo ikabidi washuke dereva achunguze tatizo ni nini,

Walishuka ndipo Aryan alisema Abbas twende pale baa tukachukue walau chipsi za kula maana si unajua nyumbani kuna kufuli tu na mama hayupo.


Walifika baa na kwenda moja kwa moja kwenye jiko la chipsi walimkuta muuzaji kisha Aryan alisema naomba ututengenezee chipsi mayai tatu ,halafu ufunge,

Walikaa kwenye viti vya pale baa huku mziki ukiendelea kurindima kwenye hio baa taratiiibu.


Abbas alimuuliza mdogo wake ,Gwae vipi kwenye mkono bado wasikia maumivu,Gwae alitikisa kichwa na kusema ndio nasikia maumivu

Wakati huo Aryan akiangalia angalia mazingira ya pale baa wakati anaangalia alijikuta anabaki mdomo wazi,


Aliweza kumshuhudia mama yake na Abbas akiwa amepakatwa na kijana mdogo ,kibaya zaidi mama yake na Abbas alikuwa kavalia nguo za utupu naweza sema nguo zinazotumiwa na makahaba, kwa umri alionao mama yake na Abbas haipendezi kwa vitu anavyovifanya

Mapaja yote yalikuwa wazi huku akishikwa shikwa na walevi ,kijana ambae alikuwa amemkalia aliupeleka mdomo na kuanza kunyonya mate huku wengine wakimshika shika makalio yake, mama yake na Abbas mkononi akiwa ameshikilia chupa ya bia huku mkono mwingine kashikilia sigara,

Aryan aliinuka na kutaka kumwambia Abbas ili waondoke asiweze kushuhudia mambo anayoyafanya mama yake baa,

Ile anamwita Abbas,,hebu tuondoke mazingira haya si mazuri

Kumbe tayari Gwae ashamwona mama yake

,Gwae aliita mamaa




Tulipo ishia jana baada ya Aryan kumshuhudia mama yake na Abbas akiwa baa huku kazungukwa na walevi wakiume wakimshika shika kila mahali,Aryan hakupenda Abbas ashuhudie kitu anachokifanya mama yake pale baa.

/////////////////////////////////


Aryan aliinuka upesi kwenye kiti ,na kumwambia Abbas tuondoke lakini kabla hajamalizia kumbe Gwae alishamuona mama yake,Gwae aliita kwa nguvu mamaaa

Aryan alitamani angekuwa karibu na Gwae huenda angemziba mdomo asiite mama lakini ndio hivyo aliita huku akatoka mikononi mwa kaka yake na kukimbia kueleka kwa mama yake huku analia.


Aryan kidogo alisikia aibu maana kitendo anachokifanya mama yake na Abbas si kizuri hata kidogo ,Abbas aligeuka na kumwangalia mdogo wake anaenda wapi ndipo alidondosha machozi taratibu bila kutarajia,


Aryan kwakuwa anajua hasira za Abbas anajua anaweza akatenda kitu chochote kibaya pale baa na angezua matatizo mengine,Aryan alimsogelea na kuita Abbas nakuomba ulichokiona fanya kama hujaona kitu,naomba usichukulie hasira naomba utangulie kwenye bajaji halafu mimi naenda kumchukua Gwae tuondoke nyumbani


Kaka chipsi tayari hizi hapa ,muuza chipsi alikabidhi chips kwa Abbas kisha Aryan alianza kumfuata Gwae ,hatimae alifika kwa mama yake na kumkuta kakumbatiwa na kijana mdogo tena kapakatwa mama anafanya kupiga funda moja la bia kisha akamunywesha yule kijana kisha mama kwa sauti ya kilevi anasema mahaba niueee jamani ,


Kuna mlevi mmoja alisema wewe mtoto unafanya nini baa halafu umeumia mkono,yule mlevi aliongea kwa dharau huku akimshika mama yake Abbas maeneo ya mgongoni ,ndipo mama yake na Abbas aligeuka na kumwona mtoto wake Gwae.


Mama wala hakujali alisema we mbwa umefuata nini huku halafu huna adabu ,pale mama alifusha kofi na kumpiga Gwae maeneo ya mgongoni ,wala hakuangalia kama mwanae kavunjika mkono,masikini Gwae alipepesuka na kwenda kudondoka chini bahati nzuri hakuutanguliza ule mkono uliovunjika ,alitanguliza mkono wa kushoto na kudondoka ,kibaya zaidi alidondokea mahali kulikuwa na walevi wakicheza mziki ,


Mama mmoja bonge alicheza kama anarudi nyuma aliukanyaga mkono wa kushoto wa Gwae,ni sauti kama ya mtu anavunja ukuni ilisikika kooooh! Mamaaa uwiii jamani mkono wangu ndipo yule mama bonge baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia ndipo alitoa mguu wake.


Gwae akajikuta tena anavunjwa mkono mwingine , alilia kilio kisicho elezeka wakati huo Aryan kafika na kumwinua Gwae , hapo ndipo mama yake na Abbas aliinuka na kushusha kimini chake maana kilikuwa kimepanda kwa juu na kufanya sehemu kubwa za mwili wake kuonekana wazi wazi


Wewe mtoto nani kakuambia utembee na mwanangu baa mama wala hakujali alirusha chupa ya bia na kumpiga nayo Aryan usoni paaah! Aryan alihisi kama anaona nyota nyota ,alishika kichwa chake na kuyumba

Ndipo mziki wa baa ulizimwa ,Abbas alivyosikia kishindo cha chupa alikimbia kuelekea mahali yuko mama yake ,ile anafika alishangaa kumwona rafiki yake Aryan ameshikilia kichwa huku damu zinamchuruzika.


Abbas kwa hasira alimkaba mama yake kiblauzi alicho vaa na kuuliza kwa uchungu nini unafanya mama ,mama nambie nini hiki unakifanya? Wakati Abbas kamshika mama yake kwa hasira alivyogeuza macho baada ya kusika kilio cha mdogo wake aligeuza macho pale pale alijikuta anamwachia mama yake na kuelekea mahaki Gwae aliko,

Masikini Gwae alikuwa analia baada ya kuvunjwa mkono kwa mwingine ,kilio cha Gwae kilimfanya na Abbas kulia ,

Yule kijana mdogo naweza sema rika sawa na mwanae Abbas ambae ndiye alikuwa amempakata mama Abbas,


Aliuzungusha mkono kiunoni mwa mama yake na Abbas kisha akaita baby huyu ni nani hadi anakushika blauzi anajua bei yake?,mama Abbas alisema hata mimi nashangaa simjui mimi

,yule kijana baada ya kuambiwa na baby wake kuwa hawa watu hawajui alichokifanya nae alishika chupa ya bia alimtwaga Abbas kichwani na kumwambia wewe boya jiangalia huyu manzi wangu.


Mjinga nini ,kisha akampiga teke shavuni Abbas akajikuta taratibu analala chini na kuwa kimya" mama yake alimfuta yule kijana na kusema baby pole kwa kazi nzito tuondoke kwanza hii baa ishatia gundu".


Waliondoka hamna hata mtu aliyewagusa na kuwaacha wanae wakiwa katika hali mbaya,Abbas ndio kazimika kabisa huku Gwae akipiga ukunga na kulia kilio cha uchungu, kuna jamaa mmoja aliinuka na kusema jamani watu wote hapa tuna akili timamu hawa watoto tuwapeleke hospitalini wakapate matibabu maana yule maza sio yaani anabadilisha vijiwanaume kila dakika ,



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG