Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

RANGI YA CHUNGWA - 2

  

Simulizi : Rangi Ya Chungwa

Sehemu Ya Pili (2)



Aliongea bosi wake kwa ufupi na kumkumbatia Dickson, kiukweli bosi huyo alionekana kuto ridhika kwa kuondoka kwa Dickson na kuonekana kumpenda na kumthamini kama mwanae.

Bosi wake ambae alijulikana kwa jina la Visent alimuacha Dicksoni pale na kuondoka kuelekea ndani ya ofisi yake.


Dickson alirudi nyumbani akiwa hana furaha kabisa, alipofika alishangaa na mazingira aliyo yakuta, nyumba ilikuwa tofauti na siku zote, ilionekana kusafishwa vizuri na kupangwa vizuri. Kilikuwa kitu cha kushangaza maana alijua mpenzi wake hakuwa nanafanya usafi hivyo aliamini siyo mpenzi wake aliefanya ule usafi.


Kila kitu kilikuwa kimepangwa kwa utaratibu maalumu, akiwa sebleni alishangaa kumuona mpenzi wake akiwa anatokea chumbani akiwa amependeza sana, tofauti na siku za nyuma, alihisi yupo kwenye ndoto. Lakini haikuwa ndoto bali ilikuwa ni kweli kwa kile alichokuwa anakiona. Alimwangalia mpenzi wake mara mbili mbili kwa jinsi alivyoongezeka uzuri wake na kuwa kama malaika.


Mpenzi wake alimkaribisha vizuri huku mezani kukiwa kumeandaliwa vizuri, kila kitu kilikuwa tofauti na siku zote, kitu ambacho kilimfanya Dickson kushangaa, hakuwai kuona kitu kama kile tokea ameanza kuwa na mpenzi wake, japo alikuwa hana furaha kutokana na kuamishwa kikazi na kuhisi atamuacha mpenzi wake, likini alijisikia furaha baada kuonana na mpenzi wake.

"Johar mpenzi upo tayari kwenda na mimi Dae es salaam?"

Aliuliza Dickson huku akiwa anamwangalia mpenzi wake kwa jicho la huzuni.


Johar hakumjibu kitu wala kushtuka, aliendelea kumpakulia chakula mpenzi wake. Dickson alibaki akimwangalia huku akiwa anahisi mpenzi wake hakuwa hajasikia yale alio yasema. Alisita kurudia kuuliza maana alijua mpenzi wake asinge mwelewa, maana Johar alikuwa akisoma chuo hivyo ingekuwa ngumu kumweleza lile jambo. Alikaa kimya huku akiwa anajaribu kula chakula alichopika mpenzi wake, mawazo aliokuwa nayo ni mengi, moja ya mawazo yaliokuwa yakimsumbua na kumuweka katika wakati mgumu ni kuamishwa kikazi bila sababu za msingi, hakutaka kumuacha mpenzi wake nyuma. Chakula hakukitamani kabisa alibaki akiwa ameinamisha kichwa chini hadi mpenzi wake akawa anamshangaa.


"Dickson mpenzi mbona upo hivyo leo, vipi kuna tatizo limetokea?"

Aliuliza Johar na kumfanya Dickson kumwangalia Johar kwa jicho la huruma. Ni kweli kabisa uyasemayo, tatizo lipo mpenzi hadi nashindwa nianzie wapi. Ni meamishwa mikazi na wameniambia safari ni kesho, sijajua ni kwanini mabadiliko yametokea ghafla kiasi hiki" Ni maneno ya Dickson yaliomfanya Johar kuangua kicheko hadi Dickson akaanza kumshangaa, Dickson alishindwa kuelewa kwanini mpenzi wake alikuwa akicheka na ni baada ya kumwambia yale maneno.


"Sasa Dickson mpenzi, hicho kinachokufanya uwe katika hali kama hiyo? Eet mpenzi?"

Aliongea Johar na kumfanya Dickson kuzidi kushangaa na kuhisi mpenzi wake hakuwa ameelewa kilichokuwa kinaendelea.

"Johar sitanii ni kweli niyasemayo na tiketi nimeshakatiwa hii hapa" Aliongea Dickson akiwa anatoa tiketi ambayo alipatiwa kwaajili ya safari yake, lakini cha kushangaza msichana huyo hakushtuka wala kuonyesha dalili yoyote ya kushangazwa. Dickson alishindwa kumwelewa mpenzi, Johar alionekana kama mtu aliekuwa analitambua lile jambo, kwa jinsi alivyokuwa amezipokea zile taarifa, msichana huyo alionekana kutoshtuka.


"Johar umenielewa kweli, maana kama vile hujanisikia vizuri?"

"Nimekusikia vizuri na nimekuelewa mpenzi wangu" Alimjibu Johar kwa sauti ya kubembeleza, yale maneno yalimfanya Dickson kufunguka akili yake, alijiuliza maswali mengi kuhusu yeye pamoja na mpenzi wake. "Kama amesika na kunielewa, kwanini asishtuke wakati anajua nikisafiri nitakuwa mbali nae?" Alijiuliza Dickson kwenye akili yake na kuhisi mpenzi wake hakuwa upande wake, hata chakula alichokuwa amepikiwa hakukitamani tena, aliondoka na kuelekea chumbani kwake huku akiwa na mawazo mengi. Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo mengi huku mengi yakiwa juu ya mpenzi wake.


Alipofika chumbani kwake alishangaa kwa kile alichokikuta, alikuta kila kitu chake kilikuwa kimewekwa kwenye sanduku lake la kusafiri, kila kitu chake kilihifadhiwa vema na baadhi ya vitu vyake vilikwa juu ya meza huku kukiambatana na box dogo lililofungwa vizuri. Kile kitendo kilimfanya Dickson kushangaa na kushtuka maana hakutarajia kukutana na jambo kama lile, aliamua kutoka na kwenda kumuuliza mpenzi wake.


Alipofika seblen alishangaa kukuta kiti alichokuwa amekalia mpenzi wake kipo wazi, alishindwa kuelewa wapi mpenzi wake alipoenda, alitoka nje kumwangalia akihisi huenda alikuwa ametoka nje, chakula alichokuwa amepakuwa mpenzi wake kilikuwa vile vule na alivyo kiacha. Alizunguka hadi nyuma ya nyumba huku akiita jina la mpenzi wake, lakini hakufanikiwa kujibiwa chochote zaidi ya kimya kutawala. Alishindwa kuelewa mpenzi wake ni wapi alikokuwa ameelekea kwa muda mfupi alio muacha pale mezani, alibaki akijiuliza bila kupata mjibu.


Aliamua kurudi dani na kwenda kukaa pale mezani alipokuwa ameketi na mpenzi wake hapo awali, alipo keti kwenye kiti na kuangalia sahani ambayo ilikuwa na chakula alichokuwa anakula mpenzi wake, alishangaa kuona karatasi chini ya sahani hiyo, hakusita kulichukua karatasi ilo ambalo lilionekana kuwa na maandishi ndani yake, alilikunjua na kutaka kujua kilichokuwa kimeandikwa kwenye hilo karatasi.


Dickson mpenzi. Kwanza naomba unisamehe kwa haya utakayo yasoma kwenye hilo karatasi, ni kipindi kirefu nimekuwa napigana na familia yangu kuhusu kwenda kusoma nje ya nchi. Kiukweli toka nilipokutana na wewe sikutaka kabisa kukaa mbali na wewe, nilitamani kila wakati niwe na wewe. Nilikuficha vitu vingi sana ila kwa yote nitakwambia nikirudi kutoka masomoni, nasikitika sana kuwa mbali na wewe kwa muda wote nitakaokuwa masomoni.


Nakuomba Dickson usije kunihisi vibaya, kiukweli nakupenda sana na sitamani kukuacha. Nakutakia safari njema ingawa na mimi kesho Asubuhi nitakuwa naanza safari ya kwenda masoni nchini Italia. Nakupenda sana Dickson. Alimaliza kusoma lile karatasi akiwa haamini yale alioyasoma kwenye lile karatasi, alihisi ule ujumbe haukuwa wake. Alijihisi kuchanganyikiwa, kwa jinsi yale maneno yalivyokuwa yanasomeka yalimfanya ahisi kizungu zungu, mwili wake ulionekana kuishiwa nguvu. Hakuweza kuliweka lile jambo kwenye akili yake, kitu ambacho kilimfanya asiweze kuamini ni kuhusu safari yake ya kwenda Italia.



Aliamini safari hiyo si yakweli maana fedha ya kulipia alijua Johar hawezi kuwa nazo maana yeye ndiye aliekuwa akimfanyia kila kitu. Alifikiria vitu vingi na kuanza kuona Johar alikuwa anamtania, alichukua simu yake na kumpigia mpenzi wake ilikujua kama yale alio yasoma kwenye lile karatasi yalikuwa ya kweli.

Alitafuta jina la mpenzi wake na kumpigi, alishtuka na kushangaa baada ya kupiga simu na simu ikawa inaitia pale ndani.



Dickson alibaki akiwa ameishika ile simu asijue nini chakufanya, alishindwa kuelewa mpenzi wake nini kinacho endelea. Kitendo cha Dickson kuona simu ya mpenzi wake ikiwa pale kilimfungua akili na kujiaminisha mpenzi wake alikuwa akitania, hivyo ndivyo aliamini kijana huyo.

"Johar bhana anapenda kunichezea ila ya leo kiboko, lakini mbona hajaniambia kama tutaondoka wote . Alafuu..."

Aliongea Dickson huku kwa sauti ya kufikiria jambo, kabla ya kuendelea kuongea alionekaa kukumbuka kitu katoka akili yake.


"Inamaana hizi taarifa hazijamshitua, au hajasikia vizuri, na mbona nilivyomuuliza alinijibu amenisikia na kunielewa. Mhh!"

Hayo ni maswali aliokuwa anajiuliza Dickson na kumfanya kuwa katika hali ya sintofahamu, mawazo yale yalimsumbua sana katika akili yake, hadi akajikuta anapitiwa pale mezani. Alipokuja kushtuka alishangaa maana ilikuwa tayari ni usiku sana, aligeuka pande zote kumwangalia mpenzi wake lakini hakumuona, alinynyuka na kwenda kuwasha taa za pale ndani.


Alizunguka nyumba hiyo kila kona ya nyumba hiyo bila mafanikio, alishindwa kuelewa kilichomkuta mpenzi wake hadi kushindwa kurejea nyumbani. Aliamua kuchukua simu na kwaajili ya kumpigia rafiki yake na Johar ilikujua kilichomsibu, simu iliita bila kupokelewa alijaribu mara kadha wa kadha bila mafanikio. Nijihisi kuchanganyikiwa, hakutamani kitu chochote kibaya nimkute mpenzi wake, alihisi ali yahewa imebadilika na kuwa joto.


Alijaribu kuunganisha matukio juu ya kile alichokuwa ameambiwa na kuanza kuhisi huenda yakawa ya kweli, maana haikuwahi hata siku moja Johar kulala nje bila kutoa taarifa. Kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza kijana Dickson ni kutofahamu familia ya Msichana huyo, hakutambua chochote kuhusu familia ya msichana huyo, vile vile hata msichana huyo hakuwahi kutambulishwa na Dickson katika familia yao. Kiufupia hawakuwahi kutambulishana kwa wazazi wao, waliishi maisha walio yataka wao, hawakukumbuka wazazi zaidi walijali penzi lao na kulifanya lichanue.


Dickson aliinamisha kichwa chake chini huku akiwa mwenye mawazo mengi alikuwa kama mgonjwa wa ghafla aliekosa huduma ya kwanza, Dickson alianza kuona umuhimu wa kujua familia ya msichana huyo. Hakuwahi kufikiria juu ya matatizo yoyote ambayo yangeweza kujitokeza kwa wakati wowote yangemuweka katika hali gani endapo Kama Johar angepata matatizo.

"Kweli mimi Dickson nina makosa,sasa ona sijui nini kimemkuta mpenzi wangu. "Ee Mungu wangu naomba mpenzi wangu awe salama, asidhurike kwa chochote. Naamini atakuwa salama maana wewe ni muweza wa yote"


Yalikuwa ni maombi ya kijana huyo ambae alikuwa na zaidi ya miezi sita hakuwa anajua kanisa wala hakumkumbuka Mungu zaidi ya kula raha na mpenzi wake, machozi yalimtoka huku akiwa afanya maombi ya kumlinda mpenzi wake. Kiukweli Dickson alimpenda Johar kuliko kitu chochote hapa duniani, alionekana kumjali na kumsamini, hakuwa na utani kabisa na mapenzi yake yeye pamoja na mpenzi wake Johar.


Saa zilisogea hadi ilipofika asubuhi Dickson hakupata usingizi kabisa, saa moja asubuhi Dickson alikuwa mlangoni kwa rafiki yake Johar, alipofika aligonga kwa muda bila mafanikio, alivyojaribu kuzungusha kitasa cha mlango huo alijuta mlango haujafungwa. Aliamua kuingia ndani ya chumba cha msichana huyo aliejulikana kwa jina la Angely, alipoingia alishtuka na kuahangaa maana alimkuta Angely akiwa kama alivyozakiwa.



Ile hali ilimfanya Dickson kushtuka na kuhisi amefanya makosa kuingia chumbani kwa msichana huyo bila idhini yake, alibaki akiwa anajiuliza kuingia ndani au kutoka nje, ile hali ilimfanya abaki ameduwaa asijue nini cha kufanya. Wakati akiwa kwenye hali ya kutafakari alishtukia anavutwa mkono wake na msichana huyo, kilikuwa ni kitu cha kushtukiza na kujikuta anaingia ndani bila kupenda. Alishindwa kujizuia na kujikuta ameangukia kwenye kifua cha msichana huyo, alipotaka kujinyanyua alijikuta anashindwa maana msichana huyo alikuwa amemshika na kumtaiti vilivyo, ile gali ilimfanya Dickson kushangaa na kushindwa kuelewa alichokuwa anakihitaji msichana huyo. Taratibu msichana huyo alianza kumpapasa Dickson huku akijaribu kuonyesha hisia zake kwa kijana, hakikuwa kitu cha masihara maana yote aliokuwa anayafanya msichana huyo alikuwa akifanya kwa kumaanisha. Dickson alimuheshimu msichana huyo maana alikuwa ni rafiki wa mpenzi wake, ilimuwia ngumu kufanya mapenzi na msichana huyo aliejulikana kwa jina Angely.


"Angely embu acha ujinga unaotaka kuufanya"

Aliongea Dickson huku akiobekana kukasirishwa na lile jambo, lakini msichana huyo hakutaka kusikiliza maneno ya Dickson, aliendelea kufanya alichokuwa anakifanya. Hasira zilimshika kijana huyo na kumsukuma kwa nguvu msichana huyo, kile kitendo cha kumsukuma msichana huyo na kuanguka chini kilimshtua sana. Msichana Angely alipoanguka chini alijikuta anaangukiwa kichwa na kujipigiza chini, damu zilitapakaa pale ndani. Dickson alikuwa kama mtu aliegandishwa, baada ya kuona damu zikiwa zimetapakaa huku Angely akiwa amelala chini na kuwa kimya alishtuka sana. Kimya kilitawala huku taratibu machozi yakiwa yanamtoka kijana Dickson, alihisi ameuwa alimsogelea Angely na kumuita bila mafanikio.


Hakuweza kwa kile kilichotokea, katika maisha yake hakuwahi kufikiria jambo kama lile lingeweza kumtokea. Alihisi joto angali kulikuwa baridi, mapigo ya moyo wake yaliongezeka kasi, mwili wake ulionekana kutokwa na jasho jingi hata nguo alizokuwa amevaa zilionekana kulowa kwa chasho. Hofu ilimjaa, alihisi kuishiwa nguvu. Alianza kujilaumu kwanini alifika pale, hakutaka kitu kama kile kitokee. "Angely shosti leo mbona umelala sana vipi leo huendi kazini?" Nisauti ya rafiki wa karibu na msichana huyo, mtu ambae walikuwa wanakaa nae kwenye ile nyumba japo vyumba vyao vilikuwa tofauti. Ile sauti ilimfanya kijana Dickson kushtuka na kuanza kutetemeka kwa hofu akihisi segerea panamuita.


Kwa vile mlango ulikuwa wazi aliamua kutembea kwa kunyata kwenda kuufunga ili rafiki yake na Angely asiweze kujua kilichokuwa kinaendelea, Dickson aliamini kama msichana huyo angegundua kilichotokea basi alijua lazima angeozea segerea. Alipofika mlangoni akiwa tayari kufunga mlango huo alishtukia mlango unafunguliwa na kuingia msicha aliekuwa rafiki wa Angely, kile kitendo cha msichana huyo kuingia ndani na kumkuta Dickson huku rafiki yake kipenzi akiwa amelala chini huku akizidi kutokwa na damu nyingi tena akiwa kama alivyo zaliwa, binti huyo alionyesha mshituko mkubwa. Lilikuwa nu jambo la kushtukiza maana hakutegemea kitu kama kile.


Dickson alizidi kuchanganyikiwa baada ya kuingia kwa rafiki wa Angely, kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, yule msichana alimsogelea Angely akiwa anaogopa hata kumgusa kwa jinsi alivyokuwa ameumia na kutoka damu nyingi, alipomfika na kumgusa aligundua Angely alikuwa mzima, alionekana kulitambua hilo mapema na kumwambia Dickson wasaidiane kumpeleka hospital. Kijana Dickson hakutaka kupoteza muda, alimyanyua Angely na kuanza kutoka nae nje ya chumba chake, walitembea mwendo wa haraka kwa kutaka kuwahi ili ikiwezekana kuokoa maisha ya msichana huyo. Maombi ya kila aina yalipita katika kinywa cha Dickson huku akiapiza kwa kila aina na kutoa ahadi ambazo hakutambua alichokuwa akikisema. Kiukweli Dickson alionekana kuchamyikiwa.


Baada ya muda kidogo walifanikiwa kufika katika hospital ambayo ilikuwa karibu na maeneo yale, walipofika walipokelewa na Angely alichukuliwa na kupelekwa katika vyumba vya wagonjwa mahuti huti, shati la kijana huyo lilibadilika na kuwa jekundu kutokana na damu zilivyokuwa zilivyo mlowanisha. Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo mengi, akili yake haikuwaza jambo lingine zaidi ya kwenda kuozea jela. Akiwa pale alishangaa na kutamani kukimbia baada ya kuwaona polisi wakizunguka maeneo yale, akiwa katika mshangao mkubwa alishtukia pingu zikiwa zinaingia katika mikono yake na kujikuta amekamtwa na polisi bila kujua hatima ya yote. Kilikuwa ni kitu cha kushtukiza, hakukuwa na maelezo yoyote.


Rafiki yake na Angely alionekana kutoshtuka kwa kitendo cha kukamatwa kwa Dickson, ilionyesha dhahiri msichana huyo yeye ndiye alietoa taarifa hizo kwa polisi. Dickson alichukuliwa kwa nguvu huku akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani kwake, mwili wake ulionyesha kutetemeka na jasho lilizidi kumtoka. Alipakiwa kwenye gari la polisi na kufikishwa kituo cha polisi, kitendo cha kufika kituo cha polisi alipokelewa na kipigo kikali. Ndani ya muda mfupi nguo zake zilikuwa zimelowa damu, kila kona ya mwili wake kulikuwa na maumivu



Nyumbani kwa kina Dickson waliandaa vitu vizuri kwaajili ya kumkaribisha mtoto wao ambae ni muda mrefu walikuwa hawajaonana. Familia hiyo ilimpenda kijana wao kupita maelezo, taarifa za mtoto wao kuamishwa kikazi walizifahamu vilivyo maana wao ni moja ya watu waliochangia, mtoto wao kuamishwa. Walijua mtoto wao angeliwahi kufika maana tiketi aliokatiwa ilikuwa ni ya gari za alfajiri, walimsubiri kwa hamu kubwa huku wakiandaa vitu kemkemu kwaajili ya kijana wao.


Masaa yalisogea na kusogea hadi ikawa imefika saa kumi na moja hawakuwa wamemuona kijana wao, walijipa moyo wakihisi pengine gari ndilo lililochelewa kufika. Hadi inafika saa moja usiku bado Dickson hakuonekana, wasiwasi uliwashika wazazi hao hofu iliwashika, ndipo walipoamua kupiga simu kwa gari ambalo alitakiwa kuja nalo kijana wao.


Taarifa walizozipata ziliwashtua sana maana waliambiwa gazi walilokuwa wanalizungumzia lilikuwa jijini hapo toka saa kumi. Zile taarifa ziliwapa mawazo mengi na kujiuliza mtoto wao amepatwa na nini, kimya kilitawala katika nyumba hiyo. Tukija kwa upande wa Dickson hali yake ilikuwa mbaya, kipigo alicho kuwa amekipata kutoka kwa polisi kilimfanya mwili wake kujawa na maumivu makali. Alishindwa kuelewa ni kwanini alikuwa akipigwa namna ile, alijihisi mtu asiekuwa na hatia, alifungiwa kwenye moja ya vyumba ambavyo wengi tunapenda kuita lokapu.


Siku zima kijana alikuwa ndani ya chumba hicho huku akiwa na maumivu makali, hakuna hata mmoja aliekuwa anatambua kilichokuwa kimempata Dickson, wazazi wake walibaki na maswali mengi hata bosi wake alishindwa kuelewa kilichomkuta Dickson. Walijaribu kwenda nyumbani kwa Dickson kumwangalia lakini hakuna walichofanikiwa zaidi ya kukuta vitu vyake vya kusafiria, hali ya kumtafuta Dickson iligonga mwamba. Mateso yaliendelea kwa Dickson kila siku, chakula kwake ilikuwa ni gumnz. Hakufanikiwa kujua kama Angely amepona au la, alibaki mwenye mawazo mengi.


Akiwa pale kituoni aliweza kupata ugeni, ugeni ule ulimfanya Dickson kuona Mungu amejibu maombi yake,ambayo alikuwa akiomba kila kukicha.

"Habari yako kijana?"

Alisalimiwa baada ya kuketi kwenye kiti, alipomwangalia yule mtu alionekana kumfahamu lakini hakukumbuka alikwisha muona wapi.

"Nzuri tu kaka"


Alijibu kiunyonge na kuonekana kama mtu aliekata tamaa.

"Nadhani unanikumbuka vema, ila kumbukumbu zako zisikufanye kuona nimekuja kukupa msaada. Kwa kitendo ulichokifanya hakika lazima ufie jela. Aliongea mtu huyo na kumfanya Dickson kukaa kimya kutafakari yale maneno aliyokuwa ameambiwa, alikumbuka yule mzee alikuwa ni nani. Alipokumbuka kuwa yule mzee ni moja ya wateja wake ambao alikuwa anawasaidia katika kesi zao mbali mbali alishangaa sana.


Yale maneno yalimuweka kwenye wakati mgumu kmna kujiuliza kipi kibaya alichokifanya, kauli ya yule mzee ikimfanya Dickson kuwa kwenye hali ya sintofahamu.

"Yaani wewe mtoto wa malaya unaweza kunipigia mwanangu kiasi kile, mimi mwenyewe unae niona hapa siwezi kumfanyia mtoto wangu au kumpiga kiasi kile. Sasa kaa ukijua endapo mwanangu atapatwa na tatizo lolote jua wewe utawajibika kwa yote, mpuuzi mkubwa wewe" Aliongea mzee huyo, maneno yaliozidi kumfanya Dickson kuchanganyikiwa.


Yalikiwa ni maneno yaliojawa na hasira pamona jaziba nyingi, Dickson alitaka kuzungumza kitu lakini mzee huyo hakuwa tayari hata kidogo, hakutaka kusikia hata sauti ya kijana Dickson. Baada ya kuondoka mzee huyo Afande alimchukua Dickson na kumrudisha ndani, maisha ya Dickson yalikuwa kwenye wakati mgumu sana.


"Inawezekana yule ndiye Baba yake na Angely? Hapana! Inawezekanaje, mbona huyo mzee ni tajiri sana iweje mtoto wake awe kwenye maisha kama yale ya kiswahilini" Alijiuliza Dickson huku akijaribu kujiuliza juu ya Angely, hakukuwa na mtu wa kumjibu maswali yake, machozi yalianza kumtika huku akikimbuka vitisho vya mzee alie semekana kuwa Baba wa Angely.


Taratibu alianza kuwakumbuka wazazi wake, alijutia sana kwa kuwasaliti wazazi wake kwa muda mrefu. Hakuwa na uwezo wa kuwapa taarifa wazazi wake, hali ya pale polisi ilikuwa mbaya, njaa ilimyesa maana chakula alikipata kwa shida. Manyanyaso yalitosha kabisa kumkondesha, siku nne zilipita bila kuwa na msaada wowote au taarifa yoyote kuhusu Angely au wazazi wake, alihisi mambo yale yote na ndoto zake zote zingeishia gerezani.


Alianza kuona Angely ndiye mkombozi wake, alijua endapo Angely angepona basi na yeye angekuwa salama, maombi yake yote yalikuwa juu ya msichana huyo.

"Kijana vipi unayaonaje haya maisha, sizani kama kuna uwezekano wa wewe kutoka humu. Nataka nikuambiekuwa usije ukafikiria kama kuna atakae kuja kukutoa huku, labda nikuulize swali dogo tu. Kwanza uliingiaje ndani kwa mtoto wangu mtu kama wewe, inaonyesha kabisa ulikwenda kwa lengo la kumbaka alivyo kataa ndiyo ukaamua kumpiga na kumuumiza kiasi kile" Ni maneno ya luomfanya Dickson kunyanyuka pale chini alipokuwa amelala na kukuta ni yule mzee, aliesemekana ni Baba wa Angely. Yale maneno yalimshitua sana Dickson na kumfanya ashindwe kuelewa yule mzee alikuwa anamaanisha nini, hakika yalikuwa ni maneno ya kushtusha.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG