Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

HASNA (MFU ANAE ISHI) - 5

   

Simulizi : Hasna (Mfu Anae Ishi)

Sehemu Ya Tano (5)


Mzee Bungi alimfata Hasna na kuondoka pasipo julikana.

Baada ya nusu saa  walirudi na wote  walikua na furaha.

Mzee Bungi alingia ndani na hakuweza kumkuta Hasna ndani.

Walianza kumsaka,lakini ghafa mzee Bungi alishituka baada ya kumuona Hasna kuna vitu kashika mkononi.

“wewe m..tooo...tooo”

Aliongea kinyonge mzee Bungi kisha akaanguka chini....



Malikia wa kuzimu alimfata Mzee Bungi pale chini.

Hasna alikua kashika vitu vilivyokua vikiwaka waka  kama rubi.kisha akatoweka alikwenda kutokea  kwenye kaburi la  mama yake.

“asante mama kwa msaada wako,hatimaye nimefanikiwa kupata ulichoniagiza”

Aliongea Hasna kwenye kaburi la  mama yake

Lakini ilisikika sauti ikilia kutoka kwenye kaburi hilo.

“mwanangu nenda  kapambane lakini kaa  ukijua sio kazi  rahisi,”

Ilisikika sauti hiyo iliyokua ya mama Hasna,aliongea kisha akiendelea kilisikika kilio tena.Hasna alishituka sana na kuanza kupatwa  na wasi  wasi.Alinyanyuka nakuanza kuondoka lakini ilisikika sauti ikiongea kwa hasira sana.

“Rafiki kweli anaweza kua adui mkubwa sana mwanangu, sina uwezo tena wakukusaidi mwanangu wameniangamiza,nenda  kapambane hauto nisikia wala kuniona  tena maishani mwako.usioji sana lakini jua  kuna adui mwingine kajitoke ni zaidi ya baba yako”

Ilisikika sauti hiyo alafu ikakaa kimya ghafla.

“Mamaaaaaa”

Aliita Hasna kwa sauti iliyokua kali  na kubwa nakufanya  ndege wote  waliokua  kwenye miti  kuanza kuruka ruka hovyo.

Hasna hakua  na cha kufanya na hakujua vitu alivyochukua kwa  mzee Bungi anavitumiaje.

Aliwaza kumtafuta shangazi yake ili apate msaada.Alianza safari ya kuelekea kijiji alipo shangazi yake.

Hasna alifika na kukutana na shangazi yake, walipokeana kwa furaha sana Hasna alimchukulia shangazi yake kama mama yake mzazi,maana ndiye aliye mlea toka mama yake kafariki,Hasna akiwa na miaka mitano.

“pole sana mwanangu kwa mitihani uliyoipitia naunayoendelea kuipitia"

Alisema shangazi yake Hasna.

"Asante sana shangazi, lakini kuna vitu hivi sijui jinsi ya kuvitumia”

Aliongea Hasna huku akitoa vitu hivyo.

“we mtoto umevitoa wapi vitu hivi ”

Aliongea shangazi yake kwa mshangao.

Hasna alimuelezea kila kitu najinsi ilivyokua.Shangazi yake ali  ahidi kumsaidi na kumuelekeza namna ya kutumia vitu hivyo.

Ilipita wiki moja.Katika kijiji cha Mbika kwa Mtemi Jafari.

Katika Shule ya sekondari Mbika, kuna mwalimu mgeni wa kike  alikua akilipoti ,kwenye kituo chake cha kazi  ni baada ya ajira mpya kutangazwa,katika watu waliochaguliwa nae alikwemo.

Alienda hadi kwenye ofisi  ya mkuu wa Shule.baada ya kuongea nae na kujitambulisha ,mkuu wa Shule alimpeleka kwenye ofisi ya waalimu na kumtambulisha.

Baada ya hapo iligongwa kengele na wanafunzi wote wakakusanyika mstalini.

“Jamani nimewahita hapa kuwatambulisha tumepata mwalimu mgeni,ana itwa madamu helena.Hivyo nilikua naenda kuwaomba nyote mumpe ushilikianao,msimzarau kisa  anaumbo dogo  lakini tambueni kwenye kichwa  chake kabeba maarifa makubwa.Natakua anafundisha somo la  historia vidato vyote,niwaombe tena mumpe ushilikianao. asanteni  sana kwa usikivu wenu"

Alimaliza kuongea mkuu huyo wa Shule.alimuita tena madamu Helena ofisini kwake.

“sasa madamu nimekuita hapa kuna mambo tuzungumze,kwa kuhusu nyumba yakukaa wewe leo  wana malizia  malekebisha hivyo leo  takuombea kwa madamu selina ujisitili”

Aliongea mkuu huyo wa Shule.

“sawa mkuu haina shida kwa hilo”

Alisema madamu Helena.

“Pili kuna jambo linalokihusu kijiji hiki,kuna mambo kwa sisi wasomi hatuyaamini sana lakini inabidi tu.kuna mtemi lazima kila mgeni anapokuaja aende kwake ili amtambue”

Alisema mkuu huyo.

“mkuu mambo gani tena hayo Mimi siwezi kwenda kabisa ”

Alisema madamu Helena.

“nakuomba sana mwanangu,hivyo nakuomba ufanye hivyo kuokoa maisha yako”

Alisema kwa upole mkuu huyo.

“nimesema hapana mkuu”

Aliongea madamu Helena, huku akipiga meza na kunyanyuka kisha akatoka nje...



“Madamu ,madamu”

Aliita mkuu wa shule ,lakini Helena aliendelea  kutembea na kuingia ofisi ya waalimu.

“Karibu madamu Helena”

Alikalibishwa na madamu Selina,na waalimu wate  walimtolea macho.Sio siri madamu Helena alikua kaumbika sana,kila mwanaume alivutiwa pindi amuonapo Helena.

“Asante”

Aliitikia madamu kisha akavuta kiti akakaa nakuina misha kichwa chake kwenye meza.

“Vipi madamu una umwa”?

Aliuliza madamu Selena .Kisha Madamu Helena alinyanyua  kichwa chake alipokua  kakilaza juu ya meza,na kumtazama .

“Siumwi,Lakini mkuu ananichanganyia habari ”

Alisema madamu Helena.

“Nilijua tu ,hawezi kukuacha  salama ,maana asione kichaka lazima haja imbane"

Alisema madamu Selina.Alikua ni mcharuko hatari

“Una maana gani kusema hivyo”?

Aliuliza Helena.

“atakua kakutaka kimapenzi”

Aliongea madamu Selina.

“unaleta habari gani na wewe”

Alisema madamu Helena. Mara walimu wote  walicheka kwa sauti hadi Selina alibaki kipepesa macho yake kwa aibu.

“kweli umbea suna  kwa mwanamke lakini wewe umezidi Selina"

Aliongea mwalimu Abeli.Kidogo aliingia mkuu wa shule na wote  wakakaa kimya.

“Madamu Selina nakuomba ofisi kwangu”

Aliongea mkuu kisha akatoka nje.

“Madamu umeona sasa atakua kakusikia”

Aliongea mmoja wa walimu.Selina alitoka nje akiwa mnyonge.

Baada ya dakiki kadhaa alirudi.Kila mwalimu alikaa kimya kusikiliza  yalio jili.

“waone walivyo wambea hadi mijanaume nayo  tutawavika siketi.Madamu Helena twende huku”

Selina aliwachambua kidogo kisha akamuomba madamu Helena waondoke.

Walitoka hadi kwenye nyumba anayoishi.

“shoga karibu hapa ndio kwangu”

Selina alimkaribisha madamu Helena.

"Asante sana madamu”

Aliitikia madamu Helena.

“Ngoja nikuandalie maji ya kuoga”

Alisema Selina.

“Hapana kwa sasa siwezi kuonga  maana sina nguo ya kubadilisha.Begi langu  kuna sehemu nimeliwekeza”

Alisema madamu Helena. Basi walikaa kidogo wakaondoka kufata begi la  madamu Helena.

Lakini wakipokua njiani waliona kungi la  watu likija,na watu walipisha njiani na kubiga magoti pembeni.

“Madamu mtemi huyo anapita tupige magoti”

Alisema Selina.

“ Siwezi kumpigia magoti mpuuzi yoyote hapa Duniani zaidi ya aliye niumba  tu”

Alisema Helena. Selina alimbembeleza lakini aligoma.Na msafara ulipo wakaribia madamu Helena alikua kasimama tu.

Walinzi wa mtemi walimfata kwa lengo la  kumuadhibu.

“aaaah muacheni msimfanye lolote ”

Alisema mtemi Keisha akashuka walipokua wamembeba.

“Binti mrembo unaevutia unapendeza sana na hicho kiburi chako”

Alisema mtemi huku akimshika shika kidevuni.

Madamu Helena alimtemea mate mtemi.Selina alivyoona tukio hilo aliinama chini kwa kujua lazima Helena auliwe tu.

Mtemi alijifuta mate kwa mikono yake kisha akageuka na kuondoka kwenda kubanda kwenye kiti chake nakuanza safari.

Alipoondoka Selina aliinuka nakumfata.

“Madamu unafanya mambo gani sasa,? Utaniponza mwenzako”?

Alisema Selina.

“ nikuponze kwa kipi,?pambana na hali yako”

Alisema Helena. kisha wakaondoka kuelekea walipokua wanaenda.

Kesho yake palikucha.Madamu Helena aliingia Shuleni kama kawaida,ilipofika saa  tatu alikua na kipindi kidato cha nne.Alipokua  akifundisha Mara mkuu aliingia.

“madamu samaha,”

Alisema mkuu.

“ bila samahani mkuu karibu”

Alisema madamu Helena.

“nilikua nawaomba vijana wakiume wote”

Alisema mkuu huyo.

“ mkuu kuna nini sahizi siunaona wako kwenye kipindi”

Alisema Helena.

“ siumeona na wengine,wale nje ?,kuna kazi  moja wanatakiwa kufanya kwa mtemi ”

Alisema mkuu wa Shule.

“ mkuu hapa hatoki hata mtoto mmoja kwenda kwa huyo mpuuzi”

Alisema madamu Helena.

“hivi wewe unajua Mimi ni mkuu wako wa kazi,sasa nasema wataondoka tu.haya wavulana wote  naomba mtoke nje”

Alisema mkuu wa Shule kwa kufoka.

“kama kuna mtu  kaja hapa kua house boy wa mtu atoke nje,Lakini kama unajijua umekuja kusoma basi kaa  tuendelee na kipindi”

Alisema madamu Helena.mkuu alikaa kimya akimkadilia madamu Helena. Nahisi alitamani hata kumchota mitama.

Mara aliingia mtu  akiwa kutoka kwenye ngome ya mtemi .

“mwalimu niketumwa na mtemi,anasema mbona haupeleki hao vijana”?

Aliongea huyo mtu. Mtemi alimuangalia madamu kisha akanyanyua kidole chake na kukipeleka mdomoni kwake nakukiweka kama ishala ya kumzuia madamu asiseme chochote.

“mkuu una mzuia nani asiongee,?.na wewe kinyago nakutuma kwa kinyago mwenzake kamwambie hata sio sehemu ya kuchukua watu.Asipokuelewa mwambie aje atanikuta mimi”

Alisema madamu Helena. Mkuu wa Shule alikua kabaki mdomo wazi huku mikono yake ikiwa kichwani.

“mwalimu kwani huyu ni nani?.anae mwita mtemi kinyago”?

Aliuliza mtu  huyo.

Mkuu washule alishikwa na kigugumizi na kushindwa kuongea.

“ona msomi mzima unakosa amani  kwa mijitu ambayo ata chekechea ahijaingia”

Alisema Helena. Lakini mtu  yule alionekana  kushikwa na Hasira,alitoweka kimazingara  kulimfanya Madamu Helena kushituka na kupiga kelele.....



“Umeona sasa madamu unajifanya mbabe kumbe na wewe muoga tu.Haya na nyinyi wavulana tokeni ,mjumuike na wenzenu pale nje,kwa ajili ya kwenda kwa mtemi ”

Mkuu wa Shule alimuambia  madamu Helena. Kisha akaamuru wavulana kutoka nje.

“hahahaha hahahhhaha,mkuu kitu alichokifanya hapa, kwetu wanakifanya watoto wa kuanzia miaka mitatu hadi sita,hizo kelele nilizopiga sio za uoga, bali  nilishangaa analeta mambo ya kizamani, wakati sahizi tunafanya mambo kidigital”

Aliongea madamu Helena. Kisha akawazuia wanafunzi wasitike nje.

Alimuomba mwanafunzi mmoja akapige kengelele ya dharula.

Wanafunzi walikusanyika na madamu alipita mbele na kuanza kuwapa matangazo.

“Nilikua nataka kuwaambia kitu kimoja,wazazi wenu wamewaleta hapa kuja kusoma ,nasio kwenda kumfanyia kazi mtemi.Kazi mnazotakiwa kufanya nyinyi zilizozunguka mazingira yenu mnayo ishi,au mazingira yenu ya Shule.sasa nasema sitaki kumuona mwanafunzi yoyote anatoka hapa anaenda kuchota maji kwa mtemi, anatoka hapa anaenda kulima kwa mtemi,ni narufuku.Yangu ni hayo na sitaki maoni ya mtu”

Aliongea madamu Helena .Alipomaliza alimwita mkuu wakaingia ofisini.

“Hivi mkuu unamke”?

Aliuliza madamu Helena.

“Sasa madamu umri huu  ni wakukosa mke,? Tena sio mke tu Na watoto wa tano.Na kwa nini umeniuliza swali la  kishenzi namna  hiyo?,naona madamu unavuka mipaka Mimi ni mkuu wako”.

Aliongea kwa jaziba mkuu wa Shule.

“Nimeuliza kwa nia njema.Mi Na kuona wewe sio mwanaume lijali.Mwanaume akija kwako unauwezo wa kumuachia mkeo tena kwenye nyumba yako ,kwenye chumba  chako kwenye kitanda chako.Na hisi  hata hao watoto sio wako."

Aliongea madamu Helena. Huku mkuu aki  kimya.

“Helena umeamua kunivua nguo sasa”

Aliongea mwalimu mkuu kwa jaziba.

“Wala sikuvui nguo mzee wangu,sema mwanaume anae jiamini hapangiwi cha kufanya kwenye familia yake na jirani ”

Aliongea madamu Helena kisha akatoka nje,mkuu wa Shule alibaki wakimshangaa, hadi alipo tokomea na kuacha kuonekana.

Kuna baadhi ya walimu walikua wamekaa wakiteta jambo akiwepa madamu Selina.

“jamani hivi huyu Helena anajivunia nini ”

Aliuliza mwalimu Jumbe.

“kwa kweli Mimi hata sijui.Tumuulize shoga yake”

Alisema  madamu Happiness.

“Yani hamna  cha shoga yake wala nini.Mi ndio simuelewi kabisa ”

Alisema madamu Selina.Ghafla mazungumzo hayo yalikatishwa, na ujio wa madamu Helena. Kila mmoja alijifanya yuko bize na mambo yake.

Muda wa kutoka ulifika.waliongozana madamu Helena na madamu Selina, walikua wanaelekea kwenye nyumba aliyopewa madamu Helena kuishi.Alikua anaikagua kama iko  tayari kwa kuhamia.

“Helena ilishakamilika hapa kazi kwako”

Alisema Madamu Selina.

“Tahamia wikiendi dear,maana inatakiwa ninunue godoro bado usafi ,inaitaji muda ulio free kabisa sio mambo mengi”

Alisema Madamu Helena.

“Mpendwa tupitie nyama pale Leo na hamu sana”

Aliongea madamu Selina.

“Minyama yenyewe  hiyo unakuta imekaa siku mbili hadi tatu”

Alisema Madamu Helena.Waliondoka hadi buchani.

“Kaka naomba unipimie robo  tatu”

Alisema Madamu Selina.

“Kaka samahani usipime kwanza,kwani huyu ng'ombe gani”?

Madamu Helena alimkatisha kwanza kupima kisha akamuuliza swali ,muuza bucha alibaki katoa jicho  asijue linamaana gani na kwa nini Kali uliza.

“Kaka nimekuambia usipime ,naomba unijibu swali langu”

Aliendea kuongea Madamu Helena.

“Helena wewe mbona mkorofi lakini,? Muache kaka wa watu atupimie tuende tuwahi kupika”

Aliongea madamu Selina kwa ukali.

“Selina kwa tarifa yako hii sio nyama ya ngombe.Kaka kua mkweli umemtoa wapi huyu ng'ombe”?

Aliongea madamu Helena.

“Sema naukweli mtemi ndio huwa anachinya tu naenda kulangua nyama,na sio kijiji chetu tu hadi vijiji  vya jirani".

Aliongea muuza bucha.madamu Helena alimuangalia madamu Selina.

“Hii sio nyama ya ng'ombe bali  ni nyama ya mtu,”

Aliongea madamu Helena. Lakini alipo maliza kuongea madamu Selina alianza kutapika.

Madamu Helena alimshika nakuanza kuondoka nae.

Ilikua mida ya saa  nne za usiku alikua kakaa mtemi na baadhi ya wadau wake.

“Hivi huyu binti ana taka nini?,kumbe kafika  hadi buchani kwako”?.

Aliongea mtemi aliyeinekana kua na hasira.

“Ndio mtemi alikuja. lakini hata wewe tunakushangaa sio kawaida yako,mtu  anakudharau anakuita kinyago, umekaa kimya”

Aliongea kijana yule mwenye bucha.Mtemi aliinamanchi alafu akainua kichwa.

“Sasa zoezi la  kwanza nimuoneshe Mimi sichezewi,Leo usiku mumpeleke akachimbe bwawa kule bondeni”

Alitoa amri mtemi.Na wote walitawanyika na kwenda majumbani mwao ,kusubiri muda ufike wakamchukue madamu Helena kichawi.

Hatimaye kulipambazuka ,muuza bucha alikua kakaa na washika  mwenzake, wakipiga stori  zilizo jili Jana usiku.

“Yani bwawa lote lile  hawezi kuamka kabisa ,na nyodo zitamuisha kabisa”

Aliongea mmoja wa kundi hilo.

“Alafu Jose we noma ulikua  unamtandika fimbo za mgongo hata huruma huna”

Aliongea muuza bucha.

Mara ghafla wote  walitaharuki ,kumuona Madamu Helena akiwa na Madamu Selina,Walikua wanapiga soga na kucheka.

Madamu hakua na dalili zozote za uchovu.Alionekana  mtu  mwenye furaha zote.

“Jamani mtemi ,anaumwa sana yuko hoi”

Alikuja  mtu mbio mbio nakuwapa taharifa hiyo.....


Wote  waliacha kushangaa madamu Helena na kukimbia kwa mtemi.

Walipofika walikuta  watu wa ngome hiyo ya mtemi wakiwa wamemzunguka.

“ Mtemi Mtemi ”

Aliita Jose ,mtemi alifumbua macho na kugeuza shingo yake alimuangalia Jose aliye kua kasimama na wenzake.

“Jose wewe na wenzako mmeniua”  

Aliongea Mtemi kisha akafumba macho yake. Kila mtu  aliyekuepo hapo alishangaa kusikia kauli hiyo.Jose aliangaliana na wenzake  kisha wakapeana ishala wasogea pembeni.

“jamani mmeona kilichotokea,?inaonekana jana tumemchimbisha bwawa mtemi ,unaona mapote yale  yaliyo kaukia miguuni kwake”?

Aliongea José wote walikua awaamini kilichotokea.

“Jose umeona ulivyo muumiza Mtemi lakini,? .Kwa kujifanya unachapia sifa  zile fimbo zimempa hadi vidonda mgongoni”

Aliongea muuza bucha.

“ Jamani tuachane na hayo,hivi huyu mwalimu ni nani hasa  na anakitu gani cha kumzidi mtemi”

Ni swali alilo uliza Jose.

Kila mmoja alibaki hana jibu.Walirudi alipo mtemi walimchukua na kumteleka kwenye chumba  maalum kwaaji ya matibabu.

Walianza kumtengenezea dawa  mbali mbali.

“ Jose Leo andaa mazingira vizuri tumkomeshe huyu mwalimu hadi aone  kijiji kichungu”

Aliongea muuza bucha. Lakini mtemi alimkata jicho  baya sana.

“Kwahiyo vijana mnataka  kunimalizia kabisa sindio”

Aliongea Mtemi kwa kufoka .Wote walikaa kimya.

“ Chochote mtakacho mfanyia kinanirudia Mimi ,kaeni nae huyo mwalimu mbali”

Aliongea Mtemi. Wote walitoa isha  ya kukubaliana nae.

“ pigeni mbiu muwaite wanakijiji wote kwenye uwanja wa mikutano,pia mniitie mzee kingo nimpe maagizo.Pia iwe siri yenu kuhusu kuugua kwangu ,wambieni wana familia wote wa kichawi atakae toa  siri hii namla nyama hadharani"

Aliongea mtemi.Walifata maagizo yote na watu walikusanyika maana walikua wanamuogopa sana mtemi.

“ Jamani leo  sijui kuna maagizo gani.kama alisema tuwe tuna kula mlo mmoja kwa siku,leo  atasema  tuwe tuna kula kwa wiki Mara mbili.”

Walikua wa naongea baadhi ya vijana.Kimya kilitanda ghafla baada ya mzee kingo kufika eneo hilo.Wanakijiji walishangaa baada ya kumuona kingo na sio Mtemi.

“ Jamani nimewaita hapa sito kua na mengi ,ni maagizo kutoka kwa mtemi ambaye kapata  ziara ya ghafla kuelekea Nigeria.Kasema  mmemfurahisha sana kwa juhudi zenu za kulima mashamba yake na kapata  chakula cha kutosha na Leo kimempa heshima ,kwenye mataifa mbali mbali na kaongezewa cheo kwenye Afrika hii.Hivyo basi agizo alilonipa anataka muhishi kama zamani kwa amani  na mfanye chochote kila mnachojisikia kwani kwa sasa mmetoka kwenye kifungo na kua huru". 

Aliongea mzee kingo.Lakini watu walikua kimya hawakuweza kuamini  maneno hayo.Walianza kuamini  baada ya mzee kingo kuondoka .

“ Jamani hivi hili swala mnalionaje,au kuna namna  nyingine kaipanga” 

Ni baadhi ya watu walikua wa naongea .

Zilioita siku mbili kijiji cha mbika kilikua  kimechanga mka sana .watu waliendele na biashara zao kama zamani.

Hali ya Mtemi ilikua bado mbaya .

Siku moja walitokea watu wawili walioonekana walikua ni viongozi wa juu zaidi yake mtemi.

“ Jafari unafanya nini sasa”

Aliongea mmoja kwa kufoka.   

“kwani  nimefanya nini”

Aliuliza mtemi. 

“ Kwanini umewapa watu Uhuru,?”

“Nimewapa kwasababu  mungu katuleta Duniani tukiwa huru  sasa tatizo nini”

Alijibu Mtemi kwa kufoka.

“Naomba usiongee kwa kufoka  jua  sisi tunauwezo zaidi yako”

Aliongea mzee mmoja kati  ya hao.Lakini jafari alicheka sana.

“ Mngekua nauwezo mngeshindwa kuniponesha?,.Hapa Duniani hakuna mwenye uwezo zaidi yake mungu na kamwe kumbuka hakuna aliye juu yake,kila mmoja kwenye mambo yake anamuomba mungu.Nakesho ile zizi nalifungulia na ng' ombe wote na warudisha kua binadamu ”

Aliongea Mtemi. Yale maneno yaliwakasikisha sana viongozi wake.Wakaondoka kwa hasira.

Upande wa Pili alionekana  madamu Helena akiwa Shule.

“mkuu nasikia umeniita”

Aliuliza madamu Helena akiwa ofisi ya mkuu wa Shule .

“ Ndio nimekuita ,naomba uketi chini”

Madamu Helena, alivuta kiti kisha akakaa.

“ hivi wewe unajiamini nini hasa”

Aliuliza mkuu wa Shule

“ Kuhusu nini tena mkuu”?

Aliuliza madamu Helena.

“ wewe unamjua mtemi unamsikia ,kwa majibu yako na kumwita kinyago unadhani kafurahi?,usione kakaa kimya ukajua kakuogopa,lahasa jua  kuna kitu anakiandaa kama sio kwako basi Shule nzima"

Aliongea mkuu,lakini madamu Helena alitabasu tu.

“ Ndomaana nilikuambia  wewe sio mwanaume lijali,mwanaume anaweza kulala na mkeo kwenye kitanda  chako chumbani chako na nyumba yako usifanye chochote kisa  ananyanyua chuma.Acha upumbavu wewe ,subiri taharifa ya mazishi ”

Aliongea madamu Helena.

“yani uliyo yaongea  hata sijaelewa hata moja”

Alisema mkuu kwa hasira .

“ utaelewa nini na wewe ni kichwa maji"?

Alisema madamu Helena. kabla mkuu hajajibu chochote alishangaa kuona kundi LA watu wengi  likiwa  linakuja kwa  mbali ,alipoangaza vizuri mkuu wa Shule aligundua ni watu wa ngome ya Mtemi.

“ Helena umeona sasa,kimbia wanakuja kukuua"

Alisema mkuu wa Shule huku akiwa anatoka nje ,Helena alibaki kakaa kwenye kiti.Walimu wote walitoka nje wanafunzi walisimama na kuchungulia dirishani.

Walipofika walimkuta mkuu wa Shule nje na waalimu wake.

“samaha mwalimu ,tumemkuta mwalimu mgeni”

Aliongea aliyeonekana kiongozi  wa msafara,lakini kilicho wa Sangaza neno samahani.

“ Aaa  huyu mwalimu Leo hajafika".  

Aliongea mkuu wa Shule kwa hofu.

“mnashida gani na Mimi washenzi nyie”

Alijitokeza hela.

Walipo muona wote walipiga  magoti na kuinamisha vichwa  chini,wakiwa na maana kumpa heshima .

Walimu na wanafunzi wote walibaki kushangaa hadi madamu Helena mwenye.....




“Tunakupa heshima zote wewe, Hii heshima huwa tunampa mkuu wetu ambaye ni mtemi”

Kundi zima liliongea  kwa pamoja.

“ Semeni shida yenu,mnatupotezea muda tuko kazini”

Aliongea Madamu Helena.

“ Ujio wetu hapa,tulikua  tumekuja kukuambia kua Mtemi alikua nakuomba ukaonane nae”

Aliongea mmoja katika lile  kundi alioonekana  ndio kiongozi  wa msafara huo.

“ anashida gani na Mimi kinyago huyo”

Aliongea madamu Helena.

“ Helena si uende tu,maswali ya nini tena”

Alidakia mkuu wa Shule.

“ Nakuomba ukae kimya ,huu  mzikii ni wa kiume wewe haukuhusu”

Madamu Helena alimwambia mkuu wa Shule.kisha akawarudi wale washirika wa kichawi.

“ Haya na nyinyi niambieni  shida ya huyo kinyago wenu”

Aliongea madamu Helena 

“Sisi hatujui shida yake, lakini katuomba tukufate tu.”

Aliongea kiongizi  wa msafara huku akiwa bado kainama na kichwa chake kakiinamisha chini.

“ Haya tangulieni mimi nakuja muda sio mrefu”

Madamu Helena aliwambia hao wafuasi wa kichawi.Kisha akaingia ofisini,walinyanyuka na kuondoka.Mkuu wa Shule alikua haelewi nini kimetokea,alibaki kasimama akiwasindikiza kwa macho.

“ Selina si unanisindikiza”?

Madamu Helena alimuuliza .

“ aka mimi  huyo niende huko,nenda mwenyewe mwanakulitafu”

Madamu Selina ,alimkatalia Madamu Helena. Madamu Helena aliondoka.

Alipofika  kwa mtemi palikua  kimya,watu wote kwenye gome  hiyo walikua wanyonge.

Walipomuona madamu Helena walianza kumpisha huku wakiina kidogo kutoa heshima.Wajakazi wa gome  walimchukua hadi kwa mtemi,alikua kalala mwili wake ulikua umeanza kuto  harufu na baadhi ya vidonda vilikua vikitoa funza.

“ tunaomba  mtupishe nataka niongee na mwalimu”

Aliongea mtemi kwa shida sana.Walitoka nje wote walio kuwemo ndani. 

“sijui mtemi anamaongezi gani na mwalimu ”

Huku nje watu waliendelea kuongea.

“ngoja tusubiri yatayo jili"

Aliongea mmoja wa wafuasi hao wa kichawi.

Yalipita Massa mawili ,madamu Helena alitoka ndani. Wote walisimama nakumpa heshima,akusema lolote aliondoka zake.

Wajakazi wa mtemi waliingia ndani haraka haraka.

“ Niitieni mzee kingo”

Alisema Mtemi. Walienda kumwita mzee kingo.

“ Naomba unisikilize kwa makini mzee Kingo, Naomba wote niliowapa Mimi uchawi wa chome  matunguli yao  yote na wasiwe na nguvu tena hilo zowezi liiende sambamba na wale niliowakuta wakiwa wachawi toka mwanzo.Hao wakibisha wafukuze hapa kijijini au wakabidhi kwa Wanakijiji wawa hashibu.Jambo lingine  Inatakiwa ukamwage dawa  hii hapa kwenye zizi,ili hao ng'ombe warudi kwenye uhalisia wao na warudi wakajiungea na familia zao.Pia kumbuka humo  kuna mwanangu pia umtatie na mwanae,”

Aliongea Mtemi kwa kusua  sua nikama mtu  aliyekua akisikia  maumivu makali.

“ sasa mkuu hofu  yangu wale viumbe wa ajabu, alio watengeneza mzee Bungi,wakikosa tu damu kijiji kitachafuka.Napia kama ujuavyo wengi  wanawawinda viumbe hao,maana uliwapokonya kutoka kwenye ushilika wako wa kwanza”

Aliongea mzee Kingo.

“Fata maagizo niliyokupa,kuhusu hao viumbe kuna mtu  nae muuamini nimemkabidhi kazi ya kuwateketeza”

Aliongea mtemi, lakini Kingo kauli ile ya kusema kuna mtu  ninayemuamini,ilimuuma sana nakuona  kumbe yeye haaminiki.Na mawazo yote ya mzee Kingo ,kutokana na kufanya kazi za mtemi kama kaimu wake.

Alijua atakabiziwa kuendesha zoezi la  kuongoza kijiji wakati mtemi akiwa anaumwa.

Lakini umekua tofauti mtemi kaamua kuchoma uchawi wote.

Na wale viumbe ukiwapata wanafanya kazi nyingi sana, popote wanaenda utakapo watuma.Chakula chao ni damu na nyama za binadamu.

Mzee Kingo aliondoka lakini akiwa mnyonge.Aliondoka na kuelekea hadi msituni.

Kulikua kuna mtu  kasimama kavaa nguo nyeusi mfano wa dera ,na uso  wake ulikua umezibwa  na kitu kama mikabu hivyo hakuweza kutambulika .

“Vipi mzee kingo mbona mnyonge ”?

Kumbe alikua ni mwanamke,alivyovaa hauwezi kutambua hadi usikie  sauti.Mtu  huyo alimuuliza  mzee kingo.

“ Mambo magumu,haya jaenda kama tulivyo panga”

Aliongea mzee kingo.

“ Kivipi hebu nieleweshe”

Aliuliza mwanamke huyo.

“leo nilikua najua naenda kukabithiwa madaraka hili mambo yetu yatimie.Madaraka kanikabidhi lakini kwa maagizo mengine.Wachawi wote wachomewe vitu vyao ikiwepo na Mimi na wale ng'ombe tuwarudishe kuwa binadamu. Sasa kitu kilichonichanganya  mimi ,na wale viumbe tunao wahitaji sisi,kuna mtu  kamkabidhi hawateketeze.”

Alitoa maelezo hayo mzee kingo lakini alipoongelea viumbe hao,mwanamke huyo alishituka.

“ Ni nani huyo aliokabidhiwa kuwateketeza hao viumbe”

Aliuliza mwanamke huyo kwa jaziba

“ nahisi atakua ni binti mmoja mgeni  hapa kijijini,walijifungia ndani kwa Massa ya siyopungua mawili"

Aliongea mzee kingo.

“ Au ni binti yake Hasna”?

Aliuliza mwanamke huyo.

“ Hapana sio mwanae,Hasna mimi namjua  huyo ni sura ngeni”

Aliongea mzee kingo .

“ sasa wewe fata  maagizo uliyopewa na Mtemi, lakini kuhusu ng'ombe wale jicheleweshe,mimi ngoja nigatilie hili swala la  huyo mtu  aliye kabidhiwa viumbe”

Aliongea mwanamke huyo, kisha akapotea kimaajabu.Kingo alirudi kijijini kwa lengo la  kuwakusanya wachawi wote ilikuwavua uchawi wao

Lakini alipofika  kijijini,alipata taharifa za kufariki kwa mtemi.

Watu walikua wakishangilia kwa furaha mtaani,walikunywa,kucheza na kuimba.

“ Helena mbona taharifa za kufariki mtemi,haujazifurahia”

Aliuliza Madamu Selina.

“Selina hata usishangilie,bora mtemi asingekufa”

Alisema Madamu Helena.

“kwanini unasema  hivyo”

Aliuliza Madamu Selina.

“ Niache kwanza nipange nguo kwenye bagi,siunajua kesho naondoka saa  kumi na moja alfajili”

Aliongea madamu Helena, ambaye aliomba ruhusa alikua anaelekea kwao kwa matatizo ya kifamilia.

Kesho yake Madamu alipanda basi la  kwanza,na kuanza safari.

Upande wapili .

“leo selina mbona umepoa hivyo,au kifo cha mtemi kimekugusa”?

Aliuzwa na mwalimu mwenzake.

“naomba uniache,maana hampendi kuona mtu  katulia”

Aliongea Madamu Helena.

“kwani wewe haujui sababu ya Selina kua mpole hivyo.!?.Madamu Helena kapata  dharula kaenda  kwa.....”

Kabla hajamaliza kuongea ,aliingia mkuu wa Shule kwenye ofisi hiyo ya waalimu.

“hivi inakuaje mapiga kelele kama watoto ”

Aliongea mkuu wa Shule,na wote walikua kimya.

“ Sasa kuna taharifa nimepata hapa, sio nzuri kwa upande wetu.Basi alilo panda Madamu Helena, limepata ajari mlima Sinai.Na inasadikika Miongoni mwa watu waliofariki na madamu Helena yupo”........



Basi habari hizo zili waumiza sana walimu wote,hasa madamu Selina.

“ngoja tuendelee kupata taratibu tutaendelea kupashana habari,”

Aliongea mkuu wa shule,Kisha aka ondoka.Upande wa kwa mtemi walifanya maandalizi na

kumzika mtemi.

Katika Kijiji cha pili ali onekana mama mtu mzima akimpokea binti yake.

“Karibu mwanangu na pole sana kwa kazi ngumu”

Ali kua Nishangazi yake na Hasna.

“Asnte shangazi"

Alijibu hasna kinyonge sana.

“sasa mwanangu ,mbona umemaliza kazi kubwa sana ,baada ya kufurahi umekua 

mnyonge.Aubkifo cha baba yako kime kuumiza"?

Aliongea shangazi yake Hasna.

“Hapana shangazi Kuna mtihani mkubwa sana unakuja mbele yetu,na unajua SinaTena

msaada,maana mzimu wavmamavmzee bungi kaufungia.Pia Kuna mtu wa karibu na Mimi

kanigeuka na kapewa nguvu nyingi na kupambana nae Ina hitaji kutumia akili"

AliongeaHasna.

“Basi pole twende Kwanza uka pate chochote”

“Lakini shangazi ile ajari umeitengeneza vizuri,hakuna anae weza kujua KamavMimi ndiye

Helena”

AliongeabHasna akiwa kwenye sura yake halisi.Wametengezaajari hili waalimu na wanaKijiji

wasiweze kugundua kua.Madamu Helena ndio Hasna.Na Hasna kafanya kazi ya kummaliza

baba yake kisha karudi kwa shangazi yake.

“Najukumu zito la kwenda kuviua viumbe vile vya ajabu,na vipo kwenye ile ile ngome na

hakuna mtu anaye jua”

Aliongea Hasna.

“Sawa vile vitu uli vyo toa kwa mzee Bungi ndio vina takiwa uende navyo”

Wali jipanga na shangazi yake jinzi ya kuingia pale kwenye Kijiji cha mbika na kufanya

uteketezaji wa viumbe hivyo.

Upande wa mzee Bungi,ali pelekewa taarifa.

“mzee ndio hivyo Sasa sijui ni binti gani huyo, aliye kabidhiwa vitu hivyo"

Aliongea mtoto wakike huyo.Jesca Jacobo.Lakini jina maarufu alilo pewa na Hasna alikua 

aki mwita Malikia wa kuzimu.Maliki wawa kuzimu aliingiwa na tamaa ya kua nauwezo

mkubwa wa kichawi,ili aka muangamize baba yake.Nampaka Sasa kapewa nguvu na uwezo

mkubwa sana na mzee Bungi.Na mzee Bungi alikua ana viitaji viumbe vile ali vitengeneza yeye

miaka mingi iliyo pita.Na akivi pata Basi utawala unarudi na kurudisha heshima yake.

“Yani baada ya kusema Kuna binti kam kabidhi viumbe hivyo ,na baada ya muda mtemi Jafari

kafariki Basi dhahili huyo ni binti yake Hasna.Maana mtemi alikua hakuna wa kumuua zaidi ya

damu yake”

Aliongea mzee Bungi.

“Kwahiyo Sasa mzee kwa hili tuna fanyaje”?

Aliuliza Malikia wa 

kuzimu.

“Tuna kazi kidogo ukiwa makini hii kazi itakua rahisi sana,wasiliana na kingo kwanza”

Basi mzee bungi ali mpa maelekezo ya nini cha kufanya.

Ulipita muda wa takribani mwezi mmoja.Ilikua Ni majira ya saa nane za usiku mzee kingo

alikua na washirika wakichawi.

“jamani nili shindwa kuwaita mapema na kuongea na nyinyi, kutokana na msiba mzito wa

kiongozi wetu.Jambo kubwa nili taka kuwa ambieni,kabla mtemi ajafa ali sema kila mmoja

alete uchawi wake hapa tuu teketeze na Kijiji kibaki na amani.Je mko tayari"?

Aliongea kingo, na wote wali angaliana Kisha waka cheka.

“Sasa kingo? yeye Kaisha kufa sisi tuchome matunguli yetu,tuta ishije na si tuta dhalaulika sana kwa wanakijiji"!?

Aliongea mmoja wa washilika hao wa kichawi.Wali jadiliana kuhusu swala la watu wale 

walio geuzwa kua ng'ombe,waliona Wa waache wasi warudishe kua binadamu.

“Sasa tuchague kiongozi wa kumrithi mtemi Jafari”

Aliongea mzee kingo.

“Kingo wewe unajua Mambo mengi maana ndiye ulikua kaimu wa mtemi jafari.Hivyo wewe

ndio uwe kiongozi wetu mpya"

Aliongea mshirika mmoja wa kichawi.Basi wali mpitisha kingo kua mkuu wao,na usiku huo

huo wali muhapisha”

“Sasa jamani majukumu ndio nayavanza,kuna wale viumbe wa ajabu Mimi sijui wako wapi

mpaka Sasa na ali mkabidhiwa yule mwalimu”

Aliongea kingo.

“Sasa  tuwa tafute lakini huyo mwalimu na sikia kafa kwenye ajari ya Basi ,pale mlima sinai”

Aliongea mshilika mmoja wa kichawi.

“Hivi nyinyi mme shindwa kutumia akili kabisa,uleni mchezo tu”

Aliongea kingo.

“Mchezo kivipi mkuu sija kuelewa"

Aliuliza mshilika wa kichawi.

“Basi Lina tokea hapa kijijini kwetu na asilimia nyingi walio safiri Ni WanaKijiji wa Kijiji hiki.Na

ile ajari imeua watu wengi sana,Je Kuna msiba wowote uliyo usikia hapa kijijini?"

Aliuliza mzee kingo.Na wote wakakaa kimya kwa muda mfupi Kisha wa kacheka,kwamba

waliingizwa mjini na hata mwalimu huyo alionekana feki.

“Hata nyuma wageni walikua Wanaingia kwa wingi Kuna yule alikujanga hapa na kuna balaa

lili tokea,kaja mwalimu ndio kaleta balaa kubwa.Yani kuanzia Sasa mgeni yeyote atakae

jitokeza Nikumuua mapema,awe mbaya kwetu au mzuri kwetu Ni kuchinja tu"

Aliongea mzee

 Kingo,Basi wali kubaliana Mambo mengi na kuupanga utawala wao

vizuri.Kesho yake palipo kucha walipiga mbiu na watu wa kakusanyika.Na mzee kingo ndiye

aliyetangazwa kua mrithi wa mtemi jafari.

“Sasa naombeni mni sikilize kwa makini,najua mlikua mko huru kwa muda mrefu.Kuanzia

Sasa uhuru umeisha na tunarudi Tena kule kule tulipo toka ,mtalima mashamba na chakula

mtaleta kwangua. Hakuna mtu kusafiri  bila Mimi kumruhusu na mtu yeyote atakaye pokea mgeni

Ni lazima amrete kwangu Kwanza."

Aliongea mtemi Kingo.Na wanakijiji walio kua wa meanza kupata furaha,hatimaye wali rudi

kwenye majonzi upya.

Siku moja Basi litokaro Kigoma.Lenye ruti zakebkigoma Gete.lina pita njia ya Uvinza.Ndani ya

Basi hilo kulikua na mzozo wa abiria mmoja na kondakta wa basi hilo.Walikua wakibishana

kwa muda mrefu.Basi lilipofika kwenye Kijiji cha mbika lilisimama ,kondakta huyo alimshika

abiria huyo na kuanguka chini.Alianguka akiwa na begi lake kwa bembeni likiwa chini.

“fala wewe Ni usafiri wa baba yako huu"

Aliongea kondakta huyo.pia aliwapa maagizo abiria kuchimba dawa dakika kumi.

Abiria huyo aliyekua Ni kijana alinyanyuka na kujifuta vumbi Kisha akachukua begi lake.Kuna

mtu alikua mazingira hayo ya karibu akishuhudia kila kitu.Alikua Ni mtu alie vaa mavazi ya 

kiutamaduni,na akiwa na watu nyuma yake.

“Kijana vipi mbona una mfanyia hivyo mwenzako”

Aliuliza mtu huyo.

“mzee mtu Hana nauli nime mpandisha tokea uvinza"

Aliongea kondakta huyo,huku akiwa ana weka mizigo ya abiria ndani ya buti la gari.

“sasa wewe kijana ina kuaje una safiri bila nauli”

Aliuza mzee huyo.

“Mzee wangu Mimi ni mepata matatizo ya msiba na nina enda hapo kahama,nili muambia

nampa hii simu Nikifika Kahama na mpa hela yake”

Aliongea Abiria hiyo.

“hebu ilete hiyo simu niione"

alisema mzee huyo,kijana alimpa simu mzee

huyo ali iangalia huku ana cheka,Kisha akampa mmoja ya mtu aliyenae.

“Umeinunua shingapi kijana”?

Aliuza mzee huyo.

“Nilinunua laki sita mzee,lakini Kama utanipa hela nipe laki nne na nusu ,sababu na matatizo"

Alisema kijana huyo,mzee alimgeukia kondakta,

“Nauliza Ni shingapi alipotoka na anapoenda"?Aliuliza mzee huyo.

mzee elfu kumi na mbili"

Basi alipo ambiwa alitoa elfu kumi na tano kwenye lishuka lake na kumkabidhi kijana

huyo.Lakini alishangaa kuona hela hiyo.

“Mzee wangu elfu kumi na tano kweli,nipe hata laki nne"

Aliongea kijana huyo huku akiwa kaishika hela hiyo.Huku kondakta alianza kuamuru gari

kuondoka.

“Mbona hata hivyo nime kuheshimu hata kukupa hiyo"

“Kaka nisubirini”

Aliita kijana huyo huku akiwa analifata Basi hilo mbio.Basi mzee huyo aliondoka na simu

hiyo hadi nyumbani.

Ilifika majira ya usikua,alionekana mtu katika ngome ya mtemi Kingo.Alikua akitembea kwa

kunyata kutoka chumbani kwa mzee kingo akiwa ana tokanje...



Ali utoa mlango uliokua ume egeshwa, uliotengenezwa kwa miti midogo midogo.Ali utoa akapita Kisha akauegesha Tena ,na kujificha ficha hadi akazunguka nyuma ya nyumba  ya kingo.Kama ujuavyo hapa kwa mtemi Kuna Kaya nyingi ndani ya uzio mmoja.Lakini kwa mbali kwenye msitu,ulionekana Moto mkubwa sana,uki waka .Na ndani ya ngome kulikua kumetukia.Mtu huyo alionekana usiku huo Kuna kitu ana tafuta,alifunga baadhi ya vijumba na kuangalia ndani.Alitafuta kwa muda mrefu bila kupata alichokua ana tafuta.

Kingo na wafuasi wake walikua huko msituni kwenye vikao vyao.

“Kwahiyo kingo hata kumbukumbu zako,azipo Kabisa kua viumbe wale wako wapi"

aliuliza mshilika mmoja wa kichawi.

“Jamani  ningejua si tungekua nao ,Sasa hapa.Shida wale viumbe alikua ana waficha na yeye pekee ndio alikua ajuaye ,mwisho ndio kamuelekeza binti yake awateketeze"

Aliongea kingo.

“basi uenda wapo nje ya hapa" 

Aliongea mshilika mwingene.

“Sio rahisi Kama unavyo dhani,wapo kwenye ngome yetu sema kujua"

Alisema Mtemi Kingo.

“Sasa huyo binti yake hapa ataingia vipi ,Yani akiingia ndio hiyo siku tuna dili nae”

Alichangia hoja mshilika mwingine.

“Yule binti ana mbinu nyingi Sana,kumnasa sio rahisi”

Kingo aliongea hivyo Kisha aka kumbuka kitu .

“Simuuuuuuuuuu"

Alisema kwa nguvu Kisha akapotea,Alitokea chumbani kwake na kukuta mke wake akiwa kalala. 

Na alipo iyangalia simu alipo iweka iko vile vile.Wenzake nao walikuja na kumsubiri nje.Baadae alitoka.

“Vipi mkuu,Simu imefanya je”

Aliuliza mshilika mmoja.

“Leo nimenunua simu Sasa nilivyosema kua ana njia nyingi za kuingia hapa.Ndio nikakumbuka simu ,uenda akawa ndio Hasna."

Aliongea kingo na wote walimcheka.

“Mtemi hakuna kitu Kama hicho ,kweli nimeamini usemi ule usemao kua ,ukiumwa na nyoka hata ukiguswa na Jani unashituka" 

Aliongea mshilika mwingene.

Upande wa Bungi Kuna mbinu walikua wanazipanga na Malikia wa kuzimu

“Hasna ni mtoto mdogo Sana hivyo hawezi kutuzuia sisi”

Alisema mzee Bungi.Palikucha katika Kijiji cha jirani anapo ishi shangazi yake na Hasna.Akiwa anakusanya kuni msituni alishituka baada ya kumuona hasna akiwa ,ana kuja taratibu alipo shangazi yake.

“vipi shangazi mbona umeshituka Sana"

Aliuliza Hasna.

“Mbona umewahi kurudi Sana kwamba Kazi kumbe ilikua nyepesi hivyo"?

Aliuliza shangazi yake.

“Shangazi  Yani nimemaliza kila kitu ,kua na amani "

Aliongea Hasna.Alimsaidia shangazi yake kubeba kuni Hadi nyumbani.Walifika waka andaa chakula ,walika ana kuanza kuongea.

“Sasa vile vitu vya kuangamizia umeviweka wapi mbona ndani sijaviona"?

Aliuliza shangazi yake.Lakini Hasna alionekana kushitushwa kidogo na Hilo.

“Shangazi hata sikumbuki Yani umeniuliza ndio Kwanza nimekumbuka"

Alisema hasna.

“Wewe mtoto mbona una balaa,?.We mwenyewe una jua ,mbele Kuna mtihani mzito"

Alisema shangazi yake.Kisha  hasna haokuonekana kujali aka ondoka zake.Lakini kuna kitu kilimshitua shangazi yake.Ilifika usiku wakiwa wa melala Hasna alinyanyuka na kutoka nje.Shangazi yake alikua kalala usingizi mzito Sana .Hasna alipotoka nje alinza kubadili na kua mtu wa ajabu Sana.Alipo badilika Ali ingia ndani alipo lala shangazi yake na kumtupia kitu kilichotoa sauti mfano wa radi,na kummaliza shangazi yake. kisha alicheka alafu akapotea.Na kutokea kwa mzee Bungi.

“Mzee nimemaliza kazi lakini kuna onekana kua Hasna atakua kwenye hile kazi ya kuteketeza vile viumbe"

Aliongea Malikia wa kuzimu ambaye Aliye kwenda kumuangamiza Shangazi yake Hasna.

“Nenda haraka kwa kingo ,umpe hizi habar"

Aliongea mzee Bungi.kwa msisitizo.Malkia wa kuzimu alipotea na kutokea kwa mtemi kingo ilikua Ni majira ya saa sita za usiku.Mtemi kingo alikua kakaa nje ya nyumba anayo ishi pale ngomeni ,alikua ana chezea simu yake.Alikua anafungua mitandao ya kijamii bila hata mb lakini yeye alikua hata aoni ajabu.

„Malikia wa kuzimu,umenishitua kweli.mbona umekuja Kama Kuna tatizo"

Aliongea mzee kingo.

“Ndio nimeenda kule kwa shangazi yake na Hasna.Alijua Mimi Ni hasna maana nilivaa sura ya hasna.Na ina onekana Hasna hayupo .Yuko huku,sema nimemuua shangazi yake baada ya kusema ukweli"

Malkia wa kuzimu Aliongea ,lakini alipoongea ,simu ya mtemi Kingo iliyokua mkononi ilianguka  ghafla.

“vipi mtemi mbona una angusha simu"

Aliulza Malikia wa kuzimu.

“hapana umenishitua Sana kusema Hasna yupo hapa.Niukweli gani huo aliokuambia"

Aliuliza mtemi kingo.basi alimuambia Mambo mengi,Kisha Malikia wa kuzimu akatoeka kurudi kwao,poli la nyakitonto. Kidogo Mtemi aliwaita washilika wa kichawi Kisha akawapa habari hizo za Hasna.Waliweka ulinzi wa kichawi kila Kona ya Kijiji hicho.

Usiku huo Hasna anarudi kwa shangazi yake akiwa na presha .

“Shangazi , shangazi,"

Hasna aliingia  ndani akiita kwa nguvu ilikua usikua wa manane.Hasn aliacha kuita baada ya Kumuona shangazi yake kalala.

“Vipi Hasna "

Aliuliza shangazi yake.

“Huko salama kabisha shangazi"?

Aliuliza Hasna huku akiwa ana mkagua shangazi yake.

“Kuna mpumbavu  alikuja akajifanya wewe,hatua za mwisho nikamshitukia,sema Sina nguvu za giza ningepambana nae.Lakini Kuna kibuyu cha mizimu ya marehemu baba,nili kiomba kiniweke pembeni, na kitandani akaweka kivuli changu,Mimi nilikua pembeni naangalia .Basi alinyanyuka na kutoka nje alipo Rudi alikua Ni mtu wa ajabu,na alipiga  kitu kilitoa mlio kama radi akajua kaniua"

Shangazi yake Hasna 

Alimaliza kumu hadithia kilichotokea.

Upande wa mzee kingo .Alirudi kutoka kwenye kikao.Aliangalia simu yake inapokaa lakini hakuiona,alianza kuitafuata chumba kizima lakini akuona alimuamsha mke wake...



“Mke wangu Nani kachukua simu hapa,"

aliuliza mtemi Kingo.Kwa kufoka

“Yani toka ununue hiyo simu,hatusikii habari  nyingine ni simu tu"

Aliongea mke wa  Mtemi Kingo.kisha akalala.Kingo aliitafuta kote akuweza kuiona.Alitoka nje kwenda kuwaambia walinza wake.Lakini alipo rudi alishangaa kuikuta pale pale anapoiwekaga.

“Yani mana mke mengine bana sijui yana akili ya aje.sasa uliificha ili iweje"

Aliongea kingo lakini mwanamke hakujibu chochote.Ilikua ni usiku Sana.Mtemi na mke wake walikua wamelala.Usingizi mzito mno.Alionekana mtu akitoka kwenye chumba cha mtemi, kwa mwendo wa kunyata.Alitoka hadi nje nakuingia kwenye kijumba kimoja ndani ya ngome hiyo.

Alivyo ingia kulikua  kume wekwa  mizigo ya nyasi za kuezekea nyumba.Alianza kuto mizigo ya hiyo ya nyasi ,na kuiweka pembeni.Alivyo maliza kwa chini kulionekana Kuna mlango uliotengenezwa kwa mbao na kufungwa kwa kufuli la baiskeli.Alitoa funguo na kufungua,alivuta mlango huo ukafunguka Kisha akaingia na kuurudishia.kulikua na giza toto huko chini macho yake yalitoa mwanga mkali misili ya tochi. Kumbe wakati yeye akiwa anaingia huko chini ,Kuna mtu alikua akimfatilia kila hatua anayo piga. Mtu huyo alizidi kutembea kule chini kulikua na uwazi mkubwa.Alifika sehemu alisikia sauti za ajabu ,zikipiga kelele Kama vile wameona kitu Sasa Wana shangilia.Alipofika happo aliviona viumbe vya ajabu yani Wana umbo Kama binadamu lakini walikua na mikono mikubwa na mirefu kuliko miguu,walikua Wana kucha ndefu Sana ,wana midomo mikubwa na meno marefu yalitokeza mdomoni.  

Viumbe hivyo vilikua vimefungiwa kwenye chumba maarumu.Viumbe hivyo vilionekana kuwa na udhaifu Sana Ni baada ya kukaa muda mrefu bila kupata nyama na damu za watu.

Yule aliyekua anamfatilia alirudi baada ya kushuhudia kila kitu alichokua akikifanya mtu huyo.

Ailitokea chumbani kwa Kingo.Kingo alikua ana koroma tu Hana habari yoyote anayo ijua.

“hivi Ni mtemi gani anaye lala hivi na bila kujua ,kua ngome yake imevamiwa”?

Alikua Ni malkia wa kuzimu,Baada yakuongea hayo mtemi alishituka.

“Yani wewe umelala ,Kuna mtu katoka humu chumbani kwako nimemfatilia hadi alipo enda na Kuna kijumba kipo humu ngomeni ndipo alipo ingia na ndani  ya kijumba hicho Kuna mlango wa kwenda chini.Na mtu mwenye si mwingine ni Hasna."

Aliongea Malkia wa kuzimu ,huku mtemi akiwa ana shangaa kusikia mtu katoka chumbani kwake,alishituka zaidi kusikia mtu huyo ni Hasna.Mtemi Alivaa mavazi yake ya kivita ya kichawi.Na walitokea na  kutokea chini  alipo Hasna.Walishangaa kuviona vimbe vile vikiwa  vina angaika huku vipiga kelele.Hasna hakuonekana mahali alipo.

“Kumbe viumbe hivi vilikua huku"

Mtemi Kingo aliuliza.

“Kingo sio muda wake hayo maswali.Hapa ina takiwa tuangalie jinsi gani kuviokoa viumbe hivi”

Aliongea Malikia wa kuzimu,viombe hivyo kimoja kiomja kilikua kina baki majivu ,vilikua vikiungua ndani kwa ndani.Mtemi Kuna ishala ya mawasiliano aliifanya na baadhi ya wa chawi wenzake na kuweka ulinzi Hasna asitoke nje.Walishinda kuviokoa viumbe hivyo Hadi vyote vikateketea.Malkia wa kizimu alikasilika Sana ,maana alikua akiviitaji Sana viumbe hivyo ili wawe wa kubwa kwenye ulimwengu wa kichawi yeye na mzee bungi.Malkia wa kuzimu alipotea na kutokea nje Na mtemi nae alitotea na kutokea nje.

Hasna alitaka kupotea ili aondoke .gafla palibadilika na kua mchana ndio hapo alipomuona mtemi kingo.

“Binti kamwe hauzi kunikimbia leo umejileta kwenye kifo ,kumbe muda wore naishi na wewe chumbani mwangu,umejibadili kua simu"

Aliongea mtemi Kisha alicheka,Sana kwa sauti ya ajabu iloyo sikika na mwangi.

“Hakuna utakachoweza kunifanya na Leo Kijiji hiki kinarudi kua huru Kama awali,Mimi ndiye mwenye aridhi hii ya mbika na nimebalikiwa  na mizimu ya mababu na pia Allah Yuko na Mimi kwenye Vita hii ya ukombozi”

Aliongea Hasna .Kisha akakaa tayari kwa mapambano.

Mtemi alitema Moto na Hasna aliukwepa Mara kidogo walitokea wafuasi wakichawi wapatao kumi na tano na kumvamia Hasna kwa kasi,wakipaa juu juu Kama mwewe.Alikua wakimparua Hasna kwa makucha yake.

Malkia wa kuzimu,alikua na Mtemi kingo wakiangalia kazi wanayo ifanya vijana wao.Lengo lao wamchokeshe wenyewe waende kummalizia tu.

Hasna alivimba na kuanza kutoa mwanga machoni,ilikua nimiale mikali kila atae mulikwa Basi aliteketea.Nawote waliisha.

Mtemi alinyanyuka ,nakuanza kutema Moto huku akimfata,Hasna alikua ana kwepa Moto ule.Hasna ali zungurusha mikono yake,alikua ana kusanya nguvu na kumrushia mtemi kingo,alianguka chini Kama mzigo .Malikia wa kuzimu alinyanyuka na kujibadikisha umbo na kua kiumbe cha ajabu.Alikua na kucha ndefu na Kali Kama upanga,alimchana tumboni Hasna kwa kucha zake.Mtemi nae alinyanyuka na kujibadikisha ,walianza kumshambuli Hasna kwa pamoja.Hasna alikua na maumivu makali Sana baada ya kukatwa na kucha Kali za malkia wa kizimu.Alijitahidi kupambana lakini,walimshambulia Hadi alizidiwa na kuanguka chini,alikua ana tokwa na damu nyingi Sana tumboni.

“Hasna rafiki yangu ,haya ni maisha na nilazima nikumalizie”

Aliongea Malkia wa kuzimu.Hasna akiwa pale chini alianza kukumbuka jinsi walivyo kutana na Binti huyo Jesca Jacobo(malkia wa kuzimu) ilikua mjini Kigoma ,alifikilia yote na alivyo msaidia kuchukua damu ya baba yake ili amponye.Aliwaza mengi Sana waliyo fanya wakiwa pamoja.

Baada ya muda Mtemi na malkia wa kuzimu ,walirudi kwenye maumbo yao,na hali ya majira ilibadilika na kurudi usiku walimchukua hasna na kwenda kumfungia kwenye chumba kimoja ndani ya ngome hiyo ya kitemi.

Kesho yake palikucha na mzee bungi alikua kafika kutoka nyakitonto Kigoma.

“Kazi nzuri Sana umeifanya Mpenzi wangu"

Aliongea mzee bungi Kisha aka mbusu Malikia wa kuzimu shingoni na kwenda kumpa mkono mtemi kingo.

“Nikazi nzuri,japo tumekosa  viumbe hivyo,lakini kwa sababu huyu binti Yuko mikononi mwetu ,na leo usiku tunaenda kumuua,  takua na nafasi ya kutengeza viumbe vingine na taiteka afrika mashaliki ”

Aliongea mzee bungi.

“Pia leo naufungulia mzimu wa mama yake Hasna uje kushuhudia kifo cha mwanae”

Aliendelea kuongea ,mzee bungi.Walifanya maandalizi ya siku hii ya leo,ambayo kwao ni sikukuu ya ushindi.Ilipofika usiku walikua chini ya mtu kubwa aina ya msufi,kila mshilika alikua ana furaha na wengine walikua bize wakichoma ndafu za nyama ya binadamu.Aliletwa Hasna akiwa kabebwa kwenye kicha na wamemfunga na kamba.Kwenye kiti kikubwa na kirefu kwenda juu alikua kakaa mzee Bungi na pembeni yake mkono wa kushoto kakaa malkia wa kuzimu na upande wa kulia kakaa Mtemi kingo.

   Hasna akiwa kalala pale kwenye kichanja akisubili kifo chake.Mara alisikia sauti ikimnong'oneza sikioni.

“amini hakuna baya lolote liwezalo kukutokea"

Alivyo isikiliza vizuri ilikua ni sauti ya mama yake.Hasna alitabasamu.

       mzee Bungi alichukua upanga mkali na kumsogelea Hasna ,alinyanyua upanga ile anataka kumchinja Hasna ,Ulivuma upepo mkali usio na kifani.Ulinza kuwa rusha wafuasi hao huku na kule .Lakini Hasna hata ukuweza kumgusa.Baada ya dakika kumi hali ili tulia.Na watu karibia wote walikua wamekufa.Hasna aliona kamba alizo fungwa ziki funguka.Alitoka juu ya kichanja hicho,aliangaza huku na kule,alisikia sauti nzito iliyo mshitua hadi yeye.

“Hasna umefanya kazi kubwa na nzito kutetea Kijiji chako .kwa Mambo yaliyokua yakitesa WanaKijiji taribuni miaka ishiriliniiliyo pita.Mungu akusimamie katika Mambo yako na usiache kutembelea mizimu kila upatapo nafasi"

Ilisikia saiti hiyo gafla ikatoweka.Hasna aliangalia pembeni Ali muona mzee Bungi aliwa ana angaika akilia na kuomba msaada,alikua kakandamizwa na gogo lililo vunjika kwa upepo ule mkali.Hasna alienda kuanza kuutoa ule mti ili amsaidie mzee huyo alifanikiwa na kumtoa,alimpa huduma ya kwamza Kisha akaondoka nae.

Ilipofika asubuhi .Alitembea mtu mitaana akipiga ngoya ya kuwaomba wa tu wakusanyike kwa mtemi.

“Jamani sijui leo mtemi ata tupa maagizo gani"

Ni WanaKijiji waliokua wamekusanyika kwenye eneo la mtemi,wakiulizana bila kua na majibu.

Mara walimuona Hasna akipanda juu ya jukwa la kuongelea.

“habari zenu na poleni kwa majukumu.Samahani kwa kuwaita hapa najua mlikua na majukumu tofauti yakimaendeleo.Lakini leo na Mambo machache ya kuongea na nyinyi ,Kwanza kuanzia Sasa mko huru ishini maisha mlio kua mkishi zamani,ya amani na furaha na familia zenu,pili wale wote wachawi wapite mbele hapa na matunguli yao ,tuna taka kuuteketeza uchawi wote hapa kijijini.Maana Kama mzizi wa wachawi tumeuteketeza,na jua yamebaki mashina kidogo."

Aliongea Hasna na wachawi walio salia walipita mbele na kuchoma matunguli yao,na walikili na na kuomba msamaha Wana Kijiji.

“Baada ya zoezi kuisha naombeni wote mnifate"

Aliongea Hasna ,nakushuka jukwaani na wote walimfata.Hasna Alifika kwenye zizi la ng'ombe lililokua kubwa lenye ng'ombe zaidi ya thelathi.

“Jamani naombeni mwenye roho nyepesi asisongee hapa na pia muwe na usamilivu kwa chochote mtakachokiona hapa na muuamini ni ukweli mtupu."

Aliongea Hasna.Alichukua unga mweupe na kuweka kwenye kinganja cha mkono na kuupuliza kwenye zizi. baada ya dakika kumi ng'ombe wale walibadilika na kua binadamu.Wana Kijiji walibaki midomo wazi.Kila mmoja alimuona ndugu yake aliyekufa kifo cha kutatanisha.Hasna alimuona dada yake na kwenda kumkumbatia.Akiwa kakumbatiana na dada yake asikia mtu akimshika bega,ali geuka alimkuta Zuberi . Zuberi Alipiga magoti nakumuomba msamaha.

“Nisamehe Sana Hasna nimeamini mwisho wa ubaya ni aibu nimekilikosa na Nina kilikuikosea jamii.Siku zote analopanga mungu hakuna binadamu anayeweza kulipangu,.Na siku zote tamaa mbaya nimejifunza kulizika na nilichopewa na mungu.Kwel ukitaka maisha kwa njia ya mkato bila kutoa jasho Kuna madhala makubwa Sana."

Aliongea Zuberi Kisha akainuka,zilipita siku mbili kijijini kulikua Shali,na dada yake Hasna alimpata mtoto wake.

Zuberi aliwaomba wazazi wake msamaa na walimsamee.Alikua na hakiba ya hela kidogo kwenye moja ya akaunti zake  za Siri.Alinunua nyumba na aliwaalika mashekhe na baadhi ya watu akiwapo Hasna walichinja mbuzi na walisoma dua nyumbani kwake.

“Hasna Sasa na taka urudi shule uendelee na masomo yako na Mimi tagharamia kila kitu"

Aliongea Zuberi na Hasna alifurahi Sana maana alikua ana penda Sana kusoma.Kutokana na muda mwingi kupotea Hasna hakuweza kuendelea na kidato cha tano,Bali arudia kidato cha nne kwenye shule ya binafsi.

“SIKU ZOTE MAFANIKIO UYALETA MWENYEZI MUNGU PEKEE ,NA HAKUNA MTU HAPA CHINI YA JUA ALIYE NA UWEZO AU NGUVU ZA KUMZIDI MUNGU,KUMBUKA MCHAWI ANA MUOMBA MUNGU ILI AMSAIDIE.HAPO NDIPO UAMINI YEYE NDIO MUWEZA ,NA AKITAKA MUNGU  ITAKUA NA ASIPOTAKA AIWEZIKUA KWAMWE.SIMAMA KATIKA IMANI YAKO NA UMUOMBE HUKU UKIONESHA JUHUDI YA KUTAFUTA MAFANIKIO,NI LAZIMA MUNGU AJIBU"


MWISHO....


0 comments:

Post a Comment

BLOG