Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SEKESEKE (ROHO MKONONI) - 1

IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA

********************************************************************************

Simulizi : Sekeseke (Roho Mkononi) 

Sehemu Ya Kwanza (1)

Familia ya afisa wa jeshi la polisi John Butu inaingia katika hatari inayomweka afisa huyo wa jeshi la polisi katika wakati mgumu wa kuipoteza familia yake,sekeseke hilo lilianza baada ya inspekta huyo kupokea simu ya mtu alojitambulisha kama 'raia mwema' na kumpa taharifa za watu waloingiza madawa ya kulevya,kitendo cha yeye kuamua kulivalia njuga swala lile kuna amsha vita kali ambapo anapoamua kuvikimbia anagundua alishachelewa mapema sana.

Ungana na mtunzi mahiri wa riwaya za kijasusi Zuberi Maruma utiririke nayo....

SURA YA KWANZA

Alikuwa ni kijana mrefu, mwembamba, maji ya kunde, sura yake ya upole ilipendezeshwa na tabasamu jepesi lililoundwa katika mdomo wake kila mara umtazamapo,alikuwa si muongeaji ila maneno yake machache yalikuwa kivutio masikioni mwa wamsikilizaye kwa kujaa busara,hekima na hata kufuraisha pia kwa utani mwingi...

Huyu ndo John Butu Afisa wa jeshi la polisi aliyekuwa na hari,kasi na nguvu ya kulitumikia taifa lake...

SIKU HII

Alijinyanyua kwenye kiti alichokuwa ameketi mbele ya mkuu wake akampigia saluti ya kumuaga,akageuka na kupiga hatua ndefu kuufata mlango huku akisindikizwa na macho makali ya mkuu wake,akashika kitasa akafungua mlango na kutoka akaelekea moja kwa moja mpaka ilipo gari yake binafsi akafungua mlango na kuzama ndani

Kabla ajawasha gari ghafla akashtushwa na mngurumisho wa simu yake,akasitisha kuwasha gari na kuingiza mkono wake mfukoni akatoa simu yake,akaachia mguno baada ya kuitazama namba ilompigia akakata na kurudisha simu yake mfukoni akawasha gari lake na kuliondoa eneo lile,ila akiwa njiani ghafla simu yake ikawa ikiita tena,hata alipoitazama ni namba zilezile '15551' mwanzo akuzipokea baada ya kuhisi labda ni namba za mtandao,kama si zile za kubashiri michezo,ila kitendo cha kupigiwa sana kikamtia khofu mwisho akaamua kupokea ile simu,huu ukawa ni mwanzo wa safari yake ngumu tena ya kutisha ilo ondoka na furaha yake na kumpa maumivu tele katika moyo wake,bila kusahau kumwachia majuto,..

Sauti alokutana nayo ilikuwa geni katika masikio yake,sauti nzito,ilo ongea kwa kujiamini

"bila shaka naongea na inspekta John butu.."

"yah ndo mimi sijui ni nani mwenzangu?!"

Butu akahoji huku uso wake ukionesha wazi wasiwasi na mashaka tele juu ya simu ile

"hakuna haja ya kulitambua jina langu kwa sasa ila waweza nitambua kama raia mwema,na taharifa nzuri tu kwako"

Kwa kuwa Butu alikuwa katika rafu road haraka akapaki gari yake kusudi amsikilize yule jamaa vizuri...mtu yule baada ya kimya kifupi kusudi maneno yale yasikilizwe vyema na amsikilizaye sasa akaendelea...

"Nina habari ambazo zinaweza kuwa njema kwako,pindi tu utakapoamua kuzifatilia,ila kama utoziamini na uka amua kuzipotezea pia ni juu yako"

Mtu yule baada ya kumaliza kuzungumza maneno yale akaweka tuo,bila shaka ili amsikie mlengwa wake angejibu nini,Butu baada ya kuona anasikilizwa ajibu kitu,basi naye akaona akate ukimya,

"Sawa nakusikiliza ndugu"

"Swadakta,ni kwamba kuna kiasi kikubwa cha mzigo wa unga wa madawa ya kulevya yataingia kesho na ndege ya shirika la ndege la Marekani 'British aerway' utaletwa na vijana wa tano wa kiafrika ambao wote wamevaa suti nyeusi na wamenyoa,vijana hao ushirikiana kwa ukaribu na walinzi pamoja na wakaguzi wa uwanja huo wa DIA,watu hao uwa wakishaweka mzigo yao mashine zote uzimwa hivyo kutowezesha kupiga kelele mara nyingine upeana tu ishara na wakaguzi nao uondoka bila kukaguliwa,ni watu hatari na wenye mbinu zote za mapigano..."

Mtu yule alizidi kumfahamisha inspekta yule na mwisho kukata simu,akiacha kazi kwa Inspekta kuamua kufatilia hiyo kesho au kupuuzia.

Baada ya simu kukatwa Inspekta Butu akawaza kwa sekunde kadhaa,mwisho akawasha gari lake na kuliingiza barabarani kuendelea na safari yake,kuelekea nyumbani.

Ila kichwani mwake alikuwa na maswali mengi sana akijiuliza juu ya mtu yule alojitambulisha kama 'Raia mwema' je habari zile alizo mpa ni za kweli au?!,na kama ni za kweli kwa nini mtu yule amwambie na asitake malipo yoyote?!,akakuna kichwa chake kidogo na kuachia tabasamu jepesi,akajua huyo alompigia pengine ana bifu na mmiliki wa huo mzigo ivyo kaamua kumuunguzia makusudi hili kumtia hasara wazo hili akupingana nalo kabisa,yote kwa yote akutaka kujiumiza sana kufikiria swala hilo,alichoamua ni panapo majaliwa hiyo kesho asbuh aelekee uwanja wa ndege na vijana wake wakaweke mtego...

Inspekta wa Jeshi la polisi John Butu anapokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu na kumpa habari juu ya kuingia kwa madawa ya kulevya,mtu yule anamwingiza Butu katika mawazo mazito je unahisi nini kiliendelea?

Tusonge katika sehemu hii ya pili kuzidi kutiririka nayo...

Binafsi alijijua kuwa yeye alikuwa ni afisa wa jeshi la polisi ilikuwa ni lazima kufatilia kila habari atakayopewa iwe ya kweli au lah,kwa kujua ilo akajua kesho lazima atakuwa na kibarua kizito...

Akaliwasha gari lake na kuliingiza barabarani,ulikuwa kama ni mwendo wa dakika 15 ulomfikisha nje ya jumba lake la kifahari maeneo ya Tmk Vetenary.

Alipiga honi mara moja kisha geti likafunguliwa na kijana alovaa nguo za mgambo huyu ndo alikuwa mlinzi wa jumba hilo,Butu wakati anaingia alimpungia mkono mlinzi wake ishara ya kupokea salamu alopewa na mlinzi yule kwa kupungiwa mkono Baada ya butu kuingia mlinzi yule akafunga geti na kurudi eneo lake alilokuwa ameketi akanyanyua kikombe chake cha kahawa na kukiweka mdomoni.

Akapiga funda moja na kukirejesha chini,akazidi kusoma kitabu alichokuwa nacho mkononi,alikuwa ni msomaji mzuri wa vitabu vya riwaya hasa za kijasusi na leo hii kitabu kilichokuwa mkononi mwake ni kitabu cha *KUFA TU (HAKUNA NAMNA) cha mtunzi ZUBERI MARUMA

Inspekta John Butu baada ya kupaki gari lake eneo maalumu la maegesho akashuka na kuelekea upande ulipo mlango wa nyumba yake,alipofika akaufungua na kuzama ndani. Ndani pale sebuleni waliketi watoto wawili wakiangalia tv,watoto wale walifanana 'copyright' kama mapapai,usingeweza kuwatofautisha kwa mfanano ule kiumri walikuwa na miaka 19 walijaliwa sura nzuri,ucheshi kitendo tu cha kumuona baba yao wote wakainuka katika makochi na kumkimbilia baba yao wakamkumbatia.

"Shikamoo dady!"

Wote wakasalimia kwa pamoja huku wakiwa wamemng'ang'ania baba yao,

"Marhaba wanangu amjambo?!"

"hatujambo dady"

"mama yenu yupo wapi?!"

"yupo chumbani" Wakaachiana,na kurejea walipokuwa wameketi Butu akaelekea moja kwa moja chumbani...

"alice,katenge mezani uoni dady kashakuja?!"

Katika wale watoto wawili mmoja akamtuma mwenzake,baada ya kutoa kauli ile Alice aligeuza shingo na kumkata jicho kali dada yake kitendo kilicho mfanya anywee ila hakutaka kubaki kimya,

"Hata uniangalie vibaya ndo nishakwambia katenge mezani!..."

"Bwana eeh,usinipigie kelele hata wewe una mikono waweza kwenda kutenga pia si lazima mimi!"

"Nyie mnabishana nini hapo badala mtenge!" Ghafla wakashtushwa na sauti nyuma yao wote wakageuka,

Alikuwa ni mwanamke alojaliwa kila sifa ya kumwita mrembo,kwanzia weupe,urefu wa wastani umbo na hata sura,huyu ndo mama wa watoto wale na mke wa inspekta John Butu basi wakaandaa chakula mezani,John Butu alipotoka bafuni wakaketi na kula kwa furaha na upendo,hakika yeye na familia yake wali ishi kwa amani na upendo.

Baada ya chakula wakaelekea vyumbani mwao kulala wakitakiana usiku mwema watoto wakilala katika chumba chao,baba na mama nao wakaelekea katika chumba chao. Mngurumisho wa alamu aloitegesha katika simu yake ilimuamsha,alipotupa macho yake ukutani kulipokuwa na saa ilikuwa ni saa kumi na mbili kamili akawasha redio yake kusikiliza bbc hii ilikuwa ndo kawaida yake,baada ya kuamka asikilize amka na bbc kisha kumepambazuka na mwisho taharifa ya habari,ya saa moja,hapo ndipo atoke kitandani akakoge anywe chai saa mbili ndo atoke kuelekea kazini ambapo kwa kuwa alikuwa na usafiri na kituo chake cha kazi hakikuwa mbali muda mfupi tu alikuwa akifika kazini...

Hivyo siku hii baada ya kufika kazini alionana na mkuu wake na kumpa taharifa aloipata jana yake juu ya mtu yule alompigia simu kamishna Nurdin akampa askari kadhaa kwa ajili ya kuelekea huko uwanja wa ndege kuisubir hiyo ndege aloambiwa ingeingia saa tano,wakiwa katika nguo za kiraia kama vile wanasubiria wageni wao pale uwanjani zikiwa zimebakia dakika tano ndege kuwasili ghafla simu ya Inspekta Butu ikaita tena,akaitoa,alishtuka baada ya kuona namba ilompigia,aikuwa namba geni kwake '15551' ni namba ilo mpigia jana jioni kumpa habari ilo mfanya muda ule kuwa pale,haraka akaipokea,Kwanza kilitangulia kicheko kizito!,

"Ha ha ha ha ha Butu nafrah kwa kufatilia kile nilichokwambia bado dakika chache ndege iwasili,kuwa makini na watu hao si wakawaida na wanamtandao mkubwa jipange vizuri na vijana wako,"

Baada ya maneno yale simu ile ikakatwa pasina mtu yule kuhitaji jibu lolote kutoka kwa Butu,kitendo hiki kikazidi kumpa mashaka Butu juu ya mtu huyu,maswali kibao yakatawala katika kichwa chake,je mtu yule alikwepo pale uwanjani au?!,kwa nini ampigie kwa namba maalumu?!,ni nani hasa?,ila hakupata wasaha wa kutafakari zaidi baada ya ndege ile kuwasili,ikatua na kwenda kusimama eneo lake mlango ukafunguka watu wakaanza kushuka,wenyeji wao wakijisogeza kuwalaki wenye kukumbatiana wakikumbatiana,wakati askar wale wakitazama walokuwa wakishuka ghafla akashuka jamaa mmoja kweli alikuwa kavaa suti nyeusi mkononi hakuwa na kitu akaenda na kuongea na mtumishi mmoja wa pale ghafla akarudi ndani.Butu alitazama tu,mtumishi yule alienda akazungumza na wenzake ndani ghafla akatoka,sasa watu wale watano wakiwa katika suti nyeusi wakashuka mkononi wakiwa na mabegi makubwa ya kuwekea nguo,wakaweka katika eneo la kupimia wakaenda kuchukua upande wa pili,yani walikaguliwa kama abiria wengine mwisho wakachukua mabegi yao tayari kwa kuondoka,kabla Butu na wenzake kuwafata na kuwaweka chini ya ulinzi wakaonesha vitambulisho vyao na kuhitaji kukagua mizigo..

Kitendo cha kufungua mabegi yale hawakuamini walichokikuta ndani!,pakiti za unga wa madawa ya kulevya yalijaa ndani ya mabegi yale makubwa,palepale wakawekwa chini ya ulinzi,pamoja na watumishi wa pale 'earport' kwa kuwa gari yao awakupaki mbali wakamshtua dereva akaisogeza karibu watuhumiwa wakaingizwa ndani baada ya kunyang'anywa silaha landrover ile ya polisi ikiwa na watuhumiwa ndani ikaanza kutoka uwanja wa ndege huku waandishi wakipiga picha aikujulikana walifika saa ngapi,ila tayari habari zile zilishazagaa...

Butu hakiwa ndani ya gari ghafla simu yake ikaita tena kucheki namba ni zile zile '15551' haraka akapokea "vizuri sana afande kwa kazi nzuri,ila nyuma yako kuna gari ilotumwa kuja kuwachukua hao watu inawafatilia kazi iliyopo mbele yao ni kuwashambulia,na siyo hiyo tu hata mbele yenu kuna tipa la mchanga linakuja lengo kuwagonga ikiwezekana kuwaokoa wenzao nanyi mko wachache ivyo yatakiwa mfanye kitu haraka tofauti na ivyo amtofika hata hapo kituoni!

Inspekta wa jeshi la polisi John Butu anapokea simu kwa mtu asiyemjua,mtu huyo alotumia namba maalumu '15551' anampa taharifa za watu wanaoingiza madawa ya kulevya,Butu anaamua kufatilia na kweli anafanikiwa kuwakamata ila wakati wakiwa njiani wanarudi kutoka uwanja wa ndege mtu yule anampigia tena haraka Butu anapokea...

Mtu yule kwanza anampa pongezi kwa kazi nzuri aloifanya,ila pia anamwambia awe makini kwani nyuma kuna gari imetumwa kwa lengo la kuwashambulia,na siyo ivyo tu pia mbele yao kuna tipa la mchanga linakuja kwa lengo la kuwagonga,je unadhani nini kiliendelea?! Tusonge katika sehemu hii ya tatu kujua kitakachojiri....

SEHEMU YA TATU

Inspekta Butu alitoa macho ya mshangao pasina kuamini kile alichokisikia wenzake walimwangalia kwa mantiki ya kumsikiliza nao wajue mwenzao alichoambiwa.

Macho yalipotua kwa wale majamaa watano walionesha kuwa katika matabasamu mazito yamkini pengine walijua mkuu wao ndio atakayekuwa kampigia simu Inspekta yule kumuomba awaachie huru.

"Kwa habari nilizopata ni kwamba tunafatiliwa mbele na nyuma,mbele kuna tipa la mchanga linakuja kwa lengo la kutugonga na nyuma kuna gari linakuja kutushambulia hivyo wekeni silaha zenu tayari ngoja nipige simu makao makuu kuomba msaada zaidi"

Butu aliongea huku akishika simu yake tayari ku mpigia mkuu wake ila kabla ajapiga akapata wazo,ni baada ya kukumbuka mita kadhaa mbele yao kuna matrafki na mmoja wapo wa matrafiki walokuwepo pale ni rafiki yake Hamza

Kijana huyo waliwahi kuwa nae katika mafunzo ya upolisi ila mwishoe huyo rafiki yake wakabadilishwa vitengo,yeye akapelekwa 'ffu' mwenzake akapelekwa askar wa usalama barabarani 'trafki' na kituo chake kilikuwa tu mita kadhaa mbele,haraka akashika simu yake na kumpigia,akisitisha kwanza kumpigia mkuu wake,

"Hamza swahiba naomba uzuie kila tipa la mchanga linalokuja huku mpaka tutakapopita,"

Baada ya maelezo yale hapohapo akakata simu na kumpigia mkuu wake kamishna Nurdin,na kumpa taharifa juu ya taharifa aloipokea,kamishna akamuomba asubiri hapo hapo kando ya barabara anatuma askari wa kutosha wakuja kuwapa msaada!

Mpaka dakika kumi zinakata gari tatu zilizojaza polisi wa kutosha wengine wakining'inia wote wakiwa na silaha zilizojaa risasi za kutosha,mpaka wanawasili hiyo gari ya kuwashambulia ikuwa imewasili,ivyo watu wale wakazidi kuwekwa kwenye ulinzi mkali,safari ikaendelea.

Walipofika pale eneo walipo ma trafki hawakukuta tipa hata moja kwa mantiki hiyo hakukuwa na tipa ilopita,maswali yakajizalisha katika kichwa cha Inspekta yule,je habari alopewa ni ya uongo?!,ah! akutaka kuzidi kujiumiza kwa maswali mengi yasiyo na majibu.

Hatimaye baada ya safari ya takribani dakika 20 waliwasili makao makuu ya jeshi la polisi,hiki ndo kilikuwa kituo cha Inspekta huyu akawaingiza watuhumiwa 'lock up' Kisha akaenda kuonana na mkuu wake kamishna Nurdin na kumjulisha kila kilichotokea

Mkuu wake alimpongeza ila alimuomba afanye mahojiano nao na kila kitu akikamilishe siku hiyo hiyo kusudi siku inayofatia watuhumiwa wafikishwe mahakaman ikiwezelana wahukumiwe siku hiyo hiyo kama sheria ilivyosema akutwaye na madawa ya kulevya lazima afikishwe mahakamani na kuhukumiwa kabla ya masaa 48 kukatika toka kukamatwa kwao,ivyo kwa kuwa muda ule ulikuwa ni saa nane na alihisi njaa alipotoka ofisini kwa mkuu wake akaenda kantini kula,aliposhiba sasa akaelekea ofisini kwake,akamuagiza askari mmoja amletee mtuhumiwa mmoja mmoja ndani kwa ajili ya mahujiano

Wakati hayo yakiendelea nje iliingia gari fulani mpaka maeneo ya maegesho,ikapaki pembeni ya gari ya Inspekta Butu zikapita dakika kadhaa bila mlango kufunguliwa Wala kutoka mtu ndani ya gari ile,ila ghafla mlango ukafunguliwa na kwa haraka akashuka mtu na kuzama chini ya mvungu wa gari ya Butu pasina kuonekana na mtu,hata dakika moja aikuisha hakatoka na kuingia ndani ya gari yake,akapandisha vioo juu,akarudisha gari nyuma na kulitoa,akaelekea kunako geti kutoka ndani ya jengo lile,alishakamilisha kazi alopewa

Mpaka inatimia mida ya kuondoka,watu wale wa tano hapakuwa na alodiriki kufungua mdomo wake kusema mzigo ule wa metumwa na nani,hata baada ya vipigo vikali kutoka kwa askari polisi,bado walikuwa kimya wakicheka tu,ni kama walikula kiapo cha usiri,mwisho Inspekta akaamua tu waachwe wakafie segerea,

Baada ya kutoka katika ofisi ya bosi wake kufikisha ripoti akaingia ndani ya gari yake tayari kuelekea nyumbani sasa akakae na familia yake,kimuonekano alionekana wazi kuchoka,dakika kadhaa alikuwa katika barabara kubwa "double rod" na sasa alikuwa katika foleni kama mjuavyo foleni nyakati za jioni katika barabara kubwa jijini Dar

Wakati akiwa hana hili wala lile ng'afla simu yake ikaita,kuangalia ni namba ngeni '0767433106' haraka akaipokea

"Inspekta John Butu,askari ufanyaye kazi yako vyema,na mwenye uchungu na nchi yako,una watu wangu nakuomba uwaachie kwa usalama wa maisha yako,nakupa dakika moja na sekunde 15 tu piga simu kituoni achia watu wangu na mizigo yangu tofauti na ivyo ohooo tusilaumiane hati!"

Palepale simu ikakata,Butu hakuweza kuongea kitu mdomo ulikuwa mzito,mshangao ulimvaa akabaki kaganda...

'tik,tik,tik,tik,tik'

Ghafla akashtushwa na mlio kama wa saa,

"Huu ni mlio wa bomu rimonti ya kulipulia au kutegua anayo huyo ulo ongea naye,ndani ya dk alizokupa fanya kama ulivyo ombwa tofauti na ivyo sina msaada na wewe"

Ghafla ikasikika sauti ambayo bila shaka ilirekodiwa ikasetiwa ndani ya gari yake akujua iliwekwaje,hakuwa na muda wa kuitafuta,kabla ajafanya kitu gari ya mbele yake ikaanza kuondoka hii ilimaanisha gari za upande wao ziliruhusiwa honi zikaanza kupiga nyuma yake,wazo alilopata haraka ni kufungua mlango na kurukia upande ule mwingine gari zilizo simama nyuma kukafatia mlipuko mkali...

Hakika ilikuwa ni hatari

Kelele zikazagaa,gari ilokuwa nyuma yake aikusalimika kwani moto uliruka,dereva akawahi kutoka...

Hali ya sintofahamu ikazuka,wakati hayo yakiendelea kule alipoangukia Butu simu yake ikaita kucheki namba ni zilezile 0767433106 haraka akapokea ila awakuelewana kutokana na makelele,mtu yule baada ya kuona awakuelewana akatuma sms...

"Butu,ongera kwa kuokoa maisha yako,ila niku ulize je vipi utaweza kuiokoa familia yako?!,una dakika 15 tu za kufikiria uzitumie kwa kupiga simu kituoni watu wangu waachiwe,au uwai nyumban kwako ukaiokoe familia yako,maamuzi yapo mkononi mwako'

SMS ile ikaishia hapo...

Inspekta John Butu anapokea simu kwa mtu asiyemjua,mtu huyo alijitambulisha kama 'Raia mwema' anampa taharifa ya watu kuingia wakitokea nje ya nchi wakiwa pamoja na mihadarati ya madawa ya kulevya....

Butu akishirikiana na Askari wake kadhaa wanaamua kufatilia uwanja wa ndege na kweli wanawakamata ila wakati wakirudi Butu anapigiwa simu na mtu yule yule na kumwambia wanafatiliwa ivyo awe makini....

Hatimaye wanafika kituoni salama Butu anamweleza mkuu wake kila kitu,Nurdin anampongeza ila anamuomba amalize uchunguzi wake siku hiyo hiyo na siku inayofatia watuhumiwa wafikishwe mahakamani.

Mahojiano yanafanyika mpaka jioni washtakiwa awakusema chochote juu ya mkuu wao,Butu anaamua kufunga faili lao akiadhimia kesho kuwafikisha mahakamani wakapate hukumu yao

Wakati akielekea nyumbani anapokea namba ngeni nyingine anapewa dakika moja na sekunde 15 za kupiga simu kituoni na kuwaruhusu wale watuhumiwa tofauti na ivyo hana maisha,mlio wa bomu unasikika Butu anawahi kuruka na gari linalipuka.

Akiwa upande wa pili wa barabara aliporukia ghafla simu yake inaita anapopokea kutokana na makelele wanashindwa kuelewana na upande wa pili,simu inakatwa punde inaingia sms

"Butu,ongera kwa kuokoa maisha yako,ila niku ulize je vipi utaweza kuiokoa familia yako?!,una dakika 15 tu za kufikiria uzitumie kwa kupiga simu kituoni watu wangu waachiwe,au uwai nyumban kwako ukaiokoe familia yako,maamuzi yapo mkononi mwako"

SMS ile ikaishia hapo...

Je unadhani nini kiliendelea?!........

Tusonge kuburudika zaidi...

Inspekta Butu akuamini kile alichokisikia kwa sekunde kadhaa aliganda akiwa katika bumbuwazi,ila ghafla akazinduka na kuanza kukimbia hovyo mara aende mbele mara arudi nyuma,Wakati hakiwa katika hali ya kutojielewa walifika askari kadhaa wakamkamata kwa nguvu na kumzuhia kwani kwa wenge alilolipata angeweza hata kugongwa na magari...

"kuna tatizo gani afande mbona ujatulia mara uende huku mara kule kuna nini alafu mbona wahema ivyo?!"

Mmoja wa maaskari alimuhoji inspekta yule,hata ivyo Butu akujibu kitu zaidi ya kuitazama saa ilokuwa katika simu yake

"Butu,ongera kwa kuokoa maisha yako,ila niku ulize je vipi utaweza kuiokoa familia yako?!,una dakika 15 tu za kufikiria uzitumie kwa kupiga simu kituoni watu wangu waachiwe,au uwai nyumban kwako ukaiokoe familia yako,maamuzi yapo mkononi mwako"

Kumbukumbu ya sms aloisoma dakika chache zilizopita ikajirudia katika akili yake akamwangalia mmoja wa wale askari walomshika

"embu niachieni kwanza"

Butu akaachiwa palepale akabonyeza tarakimu kadhaa za simu yake na kuipachika sikioni...

"Hallow mkuu,nimekoswa koswa na bomu hapa nyerere road,..ndiyo,katika gari yangu,nilipigiwa simu na mtu nisiye mjua akanambia niwa achie wale watuhumiwa huru ndani ya dakika moja na sekunde kumi na tano tofauti na ivyo wataniua alipokata simu tu nikasikia mlio wa bomu nikawahi kuruka,..limeleta mahafa bosi,trafki wapo hapa,wakanipigia tena na kunipongeza kwa kusalimika kifo ila wamenipa tena dakika kumi na tano familia yangu itakuwa hatarini sijui nifanyaje mkuu?!"

Wazo alilopata nikumpigia Kwanza mkuu wake na kumjulisha kila kilichomkuta.

"Hizo namba umeshazituma kwa kpl 001?!"

"Ndiyo mkuu!"

"Ok!,wapigie nyumbani Kwanza ujue wanaendeleaje then uwai utanijulisha kila kitakachoendelea,mi nawasiliana na Kpl 001 kujua huyo mtu ni nani ok?!,"

"Sawa mkuu"

Akaitikia Butu sambamba na kukata simu,Kpl 001 kilikuwa Ni kitengo cha mawasiliano ndani ya idara ya jeshi la polisi.

Inspekta John Butu baada ya kukata simu alokuwa akiongea na mkuu wake sasa akaelekea upande zilipo bodaboda akapanda akampa ishara aondoe,wakati huo huo akampigia simu mlinzi wake

"Aloo Sam mpo salama?!"

"Ndio mkuu kwani kuna tatizo gani!"

"Kuna hatari cha kufanya funga geti kwa ndani usimfungulie mtu yoyote mi nipo njiani nakuja sawa?!"

"Sawa mkuu" mlinzi alotambulika kwa jina la Sam akaitikia,baada ya maelezo yale Butu akakata simu muda ule ule akamtumia msg mkuu wake kumjulishs kuwa familia ipo salama

Maskin ni kama akujua muda huo anamaliza tu kuongea na simu wakati Sam analifata geti kwa mantiki ya kubana kitasa kwa ndani ghafla alishughudia kageti kadogo cha lile geti kakifunguliwa,vijana wa tano walokuwa wamevaa maski nyeusi usoni kuziba nyuso zao huku mikononi wakiwa na silaha bastola zile ndogo wakazama pale pale wakamweka Sam chini ya ulinzi

Watatu wakaelekea ndani kuichukua familia,wawili walobakia wakaweka silaha zao vibindoni wakasaidiana kumfunga mlinzi yule kamba Kisha wakambeba na kutoka naye nje,ambapo palikuwa na gari lao wakafungua buti ambapo walitoa kamba nyingine wakamweka huko na kulibana buti lile,

Sasa wakabeba ile kamba na kurudi nayo ndani tayari kwenda kuwasaidia wenzao kuikabili ile familia.

Mama na wanaye wawili....

Inspekta wa jeshi la polisi John Butu anapokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu tena ikiwa ni namba maalumu '15551' ina mtaharifu juu ya watu wanaoingia nchini na madawa ya kulevya hivyo yeye kama afisa wa jeshi la polisi ana amua kufatilia habari ile,

Kitendo cha kuamua kufatilia anajikuta akiyaweka maisha yake hatarini,na si maisha yake tu lah bali mpaka maisha ya familia yake...

Familia yake inatekwa na watu wasojulikana na anaambiwa hili kuipata familia yake ikiwa nzima basi aachiye watu alowakamata pamoja na mzigo wa madawa alokamatwa nao

Je unadhani Inspekta Butu atachukua maamuzi gani?!,ungana nami Zuberi Maruma katika burudani hii itakayokuweka katika hali ya taharuki na maswali mengi ukijiuliza

Hatua ya tano

Inspekta John Butu alifika katika jumba lake la kifahari maeneo ya Msovero,maeneo wanayoishi matajiri,nyumba nyingi zikiwa na fensi,kuta ndefu zenye nyaya za ulizi,pamoja na mageti makubwa yenye cctv camera

Kwanza alishtushwa na giza alokumbana nalo,pale getini kwake palikuwa na taa mbili kubwa zilizo mulika eneo kubwa la nje kivipi pawe giza,wasiwasi ukamvaa,haraka akakaza mwendo kuliendea geti dogo na kulisukuma,mlango wa geti ukafunguka afande akazama ndani...

Kajumba cha mlinzi kalikuwa wazi na ndani hapakua na mtu,haraka akakimbilia ndani ya nyumba walokuwa wakiishi familia yake

Nyumba yote ilikuwa tupu,wakati akiwa bado katika bumbuwazi ghafla simu yake ikaita haraka akaichukua kuangalia ni zilezile namba 0759427653 haraka John Butu akazipokea kwanza akapokelewa na kicheko kikali tena cha majivuni,kicheko kilichotoa sauti ya kukereka kwenye masikio yake...

Sauti ile sasa aikuwa ngeni kwake

"Nadhani utakuwa umeshaijua nguvu yangu ni kubwa kiasi gani,afande wewe ni mtu mdogo sana kwangu usitake makuu ya kushindana nami utaipoteza familia yako nawe kuteketea pia sasa Ni saa tatu kasoto nakupa nusu saa nenda usiku huu kawa achie watu wangu sambamba na kete zote za mzigo wangu tofauti na ivyo tusije kulaumiana"

Sauti ile ikamaliza na simu ikakatwa,Butu akajikuta akikaa Sofani pasina kuamini kile akisikiacho wala akionacho,Ni ukweli usiopingika kwamba aliipenda familia yake na pia aliipenda kazi yake,ni kipi afanye?!....

Akakumbuka alishakula kiapo kulitumikia taifa lake kufa na kupona kutolisaliti hata ikiwezekana kuipoteza familia yake,ila kwa wasaa ule katika hali alokuwa nayo hapana hakuwa tayari japo kulikuwa na baridi iloletwa na 'ac' ilokuwepo pale sebuleni lakini mwili wake wote uliloa jasho

Ghafla akakurupuka,Akasimama kwenye lile kochi na kuelekea ulipo mlango akafungua na kutoka akaelekea kunako eneo anapoegeshea magari yake akaliendea gari moja lililokwepo Pale na kushika mlango kabla ajaufungua akakumbuka gari yake iloteketea masaa machache yalopita,gari yake aloipenda akaliangalia eneo anapoliegeshea akapeleka mkono wake usoni na kufuta machozi yalomtiririka...

Butu alikuwa na gari mbili moja yake nyingine ndo haka ka Artaza cha mke wake,akafungua mlango na kuzama ndani...

Akaliwasha na kuliondoa kuelekea getini alipofika akaanza kupiga honi kusudi mlinzi amfungulie....

Ni wazi alishasahau kuwa muda huu mlinzi wake hayupo,au ni kutokana na kuchanganyikiwa na kujua kuwa kitendo cha kushuka kwenda tena kufunga geti ni kuzidi kupoteza muda katika zile dakika alizopewa.

Alipokumbuka haraka akashuka huku akikimbia akaelekea kufungua geti,akatoa gari na kurudi akafunga geti kwa kurudishia kwa nje akarudi kwenye gari lake akaingia na kuliwasha akaliondoa tena kwa mwendo wa kasi.

Butu saa tatu hii ya usiku alizidi kukanyaga mafuta na katu akuangaika wala kuitilia shaka gari moja nyeusi aina ya pajero ilopakiwa pembeni ya barabara,Butu alipopita tu,aliyekuwa dereva wa gari ile akashika simu yake na kubonyeza namba kadhaa akaweka masikioni akasubiri kwa nukta kadhaa kisha akaongea...

"Ndiyo katoka,katupita hapa kwa kasi ya ajabu bila shaka ndo anaenda kuwaachia"

"Sawa mkuu"

Mtu yule akaitika na kukata simu akawageukia wenzake,ndani ya gari ile jumla na yeye walikuwa watano,siti ya nyuma walikaa wawili,mbele pamoja na yeye walikuwa watatu...

"Mkuu kasema tumsubiri,akiwaachia watu wetu tumpeleke ilipo miili ya familia yake"

Dereva yule aliongea kwa majivuni, wenzake wakatingisha kichwa ishara ya kukubali,nyote wakiwa wameficha nyuso zao kwa kofia maalumu zilizoacha tu macho,kofia hizi utumiwa sana na majambazi kuibia kusudi sura zao kutotambulika kiurahisi, wakaendelea na stori zao huku wakimsubiri mzee wa kazi inspekta John Butu 'JB' kama bosi wao alivyo waagiza...

***

Inspekta alifika kituoni akashuka kwenye gari yake na kuelekea zilipo mahabusu ndogo za watuhumiwa akafungua na kuwatoa wale watano pamoja na wale watumishi wa uwanja wa ndege akawapeleka ofisini kwake...

Akawaambia wasubiri,akaelekea katika chumba kilichokuwa kina ifadhia ushahidi akatoa zile begi za madawa akawapelekea wenyewe

Polisi walokuwa zamu usiku ule walibaki tu wakishangaa kila kilichokuwa kikiendelea hakukuwa na aliye mzuia

"Haya ondokeni"

Palepale akawaruhusu watu wale waka anza kuondoka.

"Mkuu mbona umewaruhusu tena watuhumiwa utaeleza nini kwa kamishna?!"

"Nailinda familia yangu"

"Lakini jua umeenda kinyume cha sheria na utashtakiwa kwa hili....

Kabla Butu ajajibu ghafla simu yake ikaita Kutazama ni bosi wake Cp Nurdin kabla ajapokea ghafla namba nyingine zikaingia 0759427653 haraka akakata zile za bosi wake na kuzipokea zile namba ngeni...

"Vizuri sana kijana kwa chaguo zuri ulochagua sasa nenda nyumbani kwako nje utakuta pajero nyeusi ingia watakupeleka ilipo familia yako wahitajika uende peke yako"

Baada ya maelezo yale simu ile ikakata,

Butu palepale akanyanyuka na kuelekea nje alipopaki gari yake alipofika ile anaingia ndani ya gari yake ghafla nyuma yake akasikia sauti sambamba na milio ya kukokiwa risasi...

"Tafadhali John Butu upo chini ya ulinzi,usiingie kwenye gari na tupa silaha tofauti na ivyo sitosita kutoa ruksa kuusambaratisha ubongo wako ulolala,ikiwa ni amri kutoka kwa kamishna...

John Butu akaganda sauti ile ali ifahamu fika ni ya Inspekta mwenzake aitwaye Jonathan,taratibu akageuza shingo sauti ile ilipotokea akakutana na mitutu mitatu iloshikwa vema na wale askari alokutana nao ndani,walokuwa zamu usiku ule...

Butu akaachia tabasamu,na kutaka kuongea kitu ila Jona akampa ishara kwamba asiongee kitu zaidi ya kufanya alivyoambiwa...

Kweli akatupa silaha yake na kuonesha mikono mbele tayari kwa kufungwa pingu,

Kumbe ile alipoingia tu huku akionekana wazi kuchanganyikiwa na kuelekea zilipo selo Insp Jona alimpigia simu mkuu wao na kumjulisha kuwa Butu anataka kuwatoa wale watuhumiwa wa madawa alowakamata asubuh,haraka Kamishna akampigia Butu,kitendo cha kukataa kupokea akawapa amri wamweke chini ya ulinzi kwenda kinyume na sheria pasina kujali Butu yupo katika hali ya kuikomboa familia yake...

Insp Jonathan akaweka bastola yake ndogo kibindoni na kuitoa pingu taratibu akawa akimsogelea Butu kutaka kumfunga bado bastola mbili za makoplo zikiwa zimemwelekea!

Hakika alikuwa katika mtihani mzito,tena mtihani wa maisha...

Na ilikuwa ni lazima aufahulu kuikomboa familia yake,

Kivipi sasa!....

Lilikuwa ni swali lisilojibika

JE INSPEKTA JOHN BUTU ATAFANYAJE?!,TAYARI YUPO CHINI YA ULINZI....

MKASA HUU UPO MPAKA 30 KWA SASA MWENYE KUTAKA MWENDELEZO TUWASILIANE 0759427653 NIMTUMIE VIPANDE VYOTE KWA BEI CHEEEE

TUONANE J MOSI KWA MWENDELEZORIWAYA YA KIJASUSI&UPELELEZI

SEKESEKE(ROHO MKONONI)

MTUNZI:ZUBERI MARUMA

WHATSUPP:0767433106/ 0759427653

No:0673999120

0655176715

0624408343

No 05

Inspekta John Butu analazimika kuwaachia watuhumiwa kadhaa alowakamata na madawa ya kulevya,lengo la kuwaachia ni ili familia yake ilotekwa na watu

wasojulikana ipate kuwa huru....

Kufanya ivyo ni kwenda kinyume na sheria,wakati anaondoka anajikuta akiwa chini ya ulinzi wa Askari wenzake anasamli amri na Inspekta Jona anamsogelea kwa lengo la kumtia pingu ikiwa ni amri kutoka kwa kamishna wao Cp Nurdin Kyango je unadhani nini kiliendelea?!....

Tusonge ujifunze na kuburudika zaidi...

*HATUA YA SITA*

Inspekta Butu alijua kuendelea kusimama pale ni kupoteza muda hali ya kuwa ajui familia yake ipo katika wakati gani kwa muda ule,machozi yakaanza kutiririka katika macho yake,alijua ndiyo kaenda kinyume cha sheria kuachia watuhumiwa ila sasa angefanyaje,

"Jonathan rafiki yangu,tambua nimefanya hayo kwa ajili ya familia yangu,...

Palepale akatoa ile simu yake mfukoni na kwenda upande aliposevu audio mbalimbali alizorekodi,akaanza kumsikilizishia afisa yule mwenzake,huku akimsimulia toka mwanzo jana alipopokea simu kutoka kwa namba 15551 na leo kuamua kufatilia,jinsi alivyo wakamata wale watuhumiwa,simu za vitisho alizokuwa akipigiwa,mabalaa alokumbana nayo barabarani ikiwemo kukoswa koswa na bomu na hata kuikosa familia yake mpaka kufikia pale kuwa achia wale wahalifu,Inspekta Jonathan kiukweli alijikuta akimuonea huruma askar mwenzake,alijua hata yeye yale yangeweza kumtokea,palepale akawahamuru askar waweke silaha chini,na kumruhusu Butu kuondoka baada ya yeye kukataa msaada wake,Butu akaingia ndani ya gari yake tayari kurudi nyumbani akiacha zogo huku nyuma kati ya inspekta Jona na mkuu wake

***

Inspekta Butu aliwasili nyumbani kwake akaliweka gari lake na kutoka nje ambapo alielekea mpaka kwenye

ile gari aloelekezwa akafunguliwa mlango wa nyuma akapanda gari,akiwa ndani ya gari alisachiwa baada ya kutokutwa na silaha gari ikaondolewa,ndani ya gari hapakuwa na mtu aliye ongea wote walikuwa kimya,safari yao iliishia palipo na msitu mdogo ujulikanao kama pori tasa,walielekea mpaka katikati ya msitu huo,ghafla gari likasimama na taa za mbele ya gari zikawashwa Butu akuamini alichokiona mbele yake,haraka akafungua mlango na kutoka akaikimbilia familia yake ilokuwa imelala chini katika madimbwi ya damu!

Kitendo cha kushuka tu ile gari ikawashwa na kuondoka kwa kasi ikipita pembeni yao kidogo,Butu wala akuangaika nayo,macho yake yalikuwa kwa familia yake mkewe na wanaye wawili walilala pasina uhai,tena walikufa vifo vibaya waliharibiwa macho na kutandikwa risasi,nguvu zilimuisha Butu sauti ikakata baada ya kulia sana,huku akiwa kapiga magoti ghafla giza likamjia akajikuta naye akienda chini!

Tayari alishapoteza fahamu!.

*****

Usiku ule maneno aloambiwa na Inspekta mwenzake kiukweli yalimuumiza roho,japo hakuwa tayari kufatwa kama agizo alilopewa ila Jona aliwapa ishara maaskari wenzake watatu walokuwa zamu usiku ule,wakafunga kituo nao kuingia ndani ya kitara cha polisi na kwa siri sana wakaanza kumfatilia John Butu,baada ya kuona anaelekea mtaa alokuwa akiishi wakiwa mtaa wa nyuma walisimamisha gari wakashuka na kutambaa pembezon mwa barabara,ghafla kwa mbali waliliona gari limepaki,wakasimama palepale kujificha kuto onekana hata na walioko kwenye lile gari...

Wakiwa pale katika ficho lao walishughudia Butu akitoka katika jumba lake akaifata ile gari akaingia na gari kuondolewa waliiangalia ikiondoka wakaiacha mpaka ikatoka kwenye mtaa ule ikakata mtaa wa pili kushoto nao haraka wakarudi kwenye gari yao wakaingia na kuitoa kwa spidi wakamaliza mtaa ule na kuingia huo mtaa wa pili nao wakakata kushoto ila hawakuweza kuiona ile gari, wakanyoosha na hiyo barabara wakaingia lami,kwa kuwa kulikuwa na gari nyingi awakufanikiwa kuiona ila kwa mawazo yao tu wakaona wachukue barabara iendayo pori tasa,kwa kuwa ndo pori linalosifika kuwepo kwa majambazi,na pori hili ndilo linalotekewa watu na kuteswa,safari yao iliendelea hatimaye wakaingia katika pori lile,saa sita za usiku ndipo walipofanikiwa kuikuta miili ile barabarani,inspekta Jona akamjulisha mkuu wao,wakafanya uchunguzi,wakachukua vipimo haraka wakapigiwa simu madaktari usiku ule ule askari na madaktari wakawasili katika pori lile uchunguzi ukaendelea

Mihili ikabebwa na kupelekwa hosptalini kwa uchunguzi zaidi!

Macho yalikuwa mazito kufunguka, kichwa kikawa kikimuuma, akayafungua , harufu ya madawa ndiyo ilo mpokea,ndani ya chumba kile taa ziliwaka kumjulisha ni usiku akagundua yupo hosptal,

Kafanyaje sasa?!,akajaribu kuvuta kumbukumbu ndipo alipoikumbuka familia yake,pale pale akajikuta akipiga kelele na kuinuka,hasira ghadhabu zilishampanda,alichohitaji ni kimoja tu kujua ukweli je ni kweli familia yake imekufa?!

Madaktari kadhaa wakiume na baadhi ya maaskari ndio walokuja kumtuliza na kumchoma sindano nyingine ya usingizi,

"Itahitajika apatiwe daktari wa saikolojia awe hapa karibu asubuh akizinduka tu awekwe sawa tofauti na hivyo itamchukuwa muda akili yake kutulia"

Daktar alokuwa zamu usiku ule alizungumza kwa upole,ni wazi alimuonea huruma askari yule na si yeye tu hata na maaskari walokuwepo pale wakiongozwa na Jona wote walimuonea huruma kijana yule!.

Asubuhi aliwasili kamishna Nurdin na viongozi wengine wa jeshi la polisi pia aliwasili daktari Samson Semkiwa huyu ni daktari bingwa wa magonjwa ya akili na saikolojia,yeye alienda moja kwa moja kwenye kitanda cha Butu akisubiri azinduke kusudi aianze kazi yake rasmi,kamishna yeye alielekea mochwari kuiangalia miili ya familia ya Butu ukweli wote walisikitika baada ya kuiona miili ile ikiwa imeharibika vibaya...

Hatimaye baada ya nguvu ya dawa alopewa kupitia sindano alochomwa kumuisha hatimaye taratibu akafumbua macho yake mbele yake akapokewa na tabasamu jepesi la mtu alokaa pembeni yake...

"Pole sana kijana unajisikiaje sasa?!"

Mtu yule kwa sauti ya upole akauliza huku bado tabasamu lake likiupendezesha uso wake!

"Najiskia vizuri,kwani nimefanyaje na hapa nipo wapi?!"

Ni wakati alipouliza swali lile wakati akijilazimisha kukumbuka Samson akamuwahi

"Hapa ni hosptal ulipata mshtuko wa ghafla ila familia yapo ipo salama!

"Hapana!,imekufa,nani kawaua,kwanin lakin...

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG