Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SAMAIRAH - 1

 

 

IMEANDIKWA NA : MOGYSHINE 

********************************************************************************

Simulizi : Samairah

Sehemu Ya Kwanza (1)

Aryan aliumia sana na kujikuta anaongea kwa uchungu Mussa nimewakosea nini hadi mfikie hatua ya kutaka kunipa ukilema? Yule jamaa alinyanyua ile sindano ile anataka tu kumchoma sindano machoni alijikuta akiidondosha mwenyewe kisha alishuka chini taratibu na kusema jamani tumbo linaniuma , hakika yule njemba alijaribu kujikaza lakini hakuweza hadi akalala chini huku akihisi mwili wake kukosa nguvu,

Wenzake walivyoona mwenzao kapatwa na homa ya tumbo ghafla ndipo njemba ya tatu alitoa upanga ili amkate Aryan mikono na miguu lakini hata yeye hakufanikiwa alikamatwa na tumbo ,anajikuta anaachia upanga huku akilia kwa maumivu tumboo jamani tumbooo,

Sasa njemba ya tatu ambae alikuwa amemkaba Aryan kwa nyuma nae tumbo likamkamata vile vile wakajikuta wanamwachia Aryan


Walianza kutembea kwa kutambaa na kujiburuza maana waliumwa tumbo kwenye kitovu na walihisi limekaza ,walijiburuza huku Aryan akiwashangaa na kujiuliza hawa watu nini kimewakuta ,"ooh asante Mungu"Aryan alijisemea moyoni.


Aryan hakutaka lile suala alipeleke polisi,wale njemba walijiburuza weee hadi walivyotoka nje walishangaa wanakuwa poa hata matumbo yao hayaumi tena ,

Oya mwamba tumbo langu haliumi tena kwani ilikuwa ni nini? Njemba moja aliuliza huku wakipanda kwenye bajaji ,mmoja aliguna na kusema mmmh kwa leo tuache kumfanyia ubaya yule jamaa maana nilihisi kufa kufa ,waliondoka zao.


Basi siku hiyo Aryan alikaa na bibi wakapakua chakula chao wakaanza kula ,Aryan alimsaidia bibi kumega matonge anampa kwenye mkono halafu anaupeleka mkono wa bibi hadi kwenye chombo cha mboga hakika bibi alijihisi faraja baada ya kufadhiliwa na Aryan walivyomaliza kula bibi alimwita Aryan.


Aryan nae alienda na kukaa karibu yake ,bibi alishika mkono wa Aryan kisha akaanza kuonge"Aryan mjukuu wangu nimekaa hapa japo kwa muda mfupi ila nimegundua kuwa watu wengi wanao kuzunguka hawakupendi wengi wao ,hasa hawa majirani ,jana wakati naenda msalani ,majirani walikuja na kuniambia niondoke huu mtaa ",Aryan alimwangalia bibi ambae goti lake bado halijapona vizuri ,Aryan alisema " bibi nimesema hakuna kuondoka hapa mimi nitahakikisha nakulinda nakuhudumia kwa kila kitu ,

Kisha bibi akaendelea na maongezi ,"usiku nimeota ndoto mbaya mama mmoja kafukuzwa kazi ambayo alikuwa akifanya ,huyo mama alivyofukuzwa wakati ana mawazo ya kufukuzwa kazi alipita kandokando ya barabara aligongwa na gari ila hakuumia sana ,ila kapelekwa hospitali,

.Aryan alitabasamu na kumwambia bibi ndio maana napenda kukaa na wewe story zako bana huwa zinanifurahisha ,sasa hio si ndoto ya kawaida bibi?

Bibi alitabasamu na kumwambia ndio ya kawaida ila nimejisikia kukuambia tu ,yalikuwa maongezi huku Aryan akimsugua bibi miguu na maji ya uvuguvugu,bibi alianza kupendeza na kuonekana safi.


Tukirudi maeno ya mwenge mama yake na Aryan baada ya kufukuzwa kule kwa akina Jesca aliondoka zake akiwa anavuka bara bara hakuangalia gari pande mbili za barabara,


Mama akajikuta anagogwa na gari na kudondoka ,kelele zilisikika watu wakisema ajali ajali ,watu walikimbia hadi kwa yule mama ,bahati nzuri aliyemgonga alikuwa ni mama ,

Yule mama alikuwa na moyo wa kipekee alishuka upesi kwenye gari na kuomba watu wamsaidie kumpakia huyo mama kwenye gari yake ,hakupenda kuchelewesha alimuwahisha hospitali.


Mama alioneka kuchubuka maeneo ya mkono wa kulia na damu nyingi kumtoka sana puani ,

Yule mama baada ya kumpakia yule mama aliyemgonga ,kila akiangalia ile damu inayotoka kwa yule mama anaitamani akitaka kupeleka kidole walau achovye alambe kidogo anasita, mara simu yake ikaita aliipokea na kusema

Haloo ,upande wa pili sauti ilisikika ikisema mama leo sijisikii vizuri nimeenda kwa rafiki yangu Jesca ,nilichokiona kule hata sijapenda Jesca kamfanyia roho mbaya mfanya kazi wao wa ndani


"Samairah mwanangu haya nenda nyumbani nikirudi tutaongea vizuri" kisha mama akakata simu ,kumbe aliyemgonga ni mama yake na Samaira ,ambae samairah alitokea kumpenda huyo mama.


Na tukirudi nyuma ile ndoto ya bibi aliyemsimulia Aryan kuwa ameota mama mmoja kapata ajali ilikuwa ndoto ya ukweli ni mama yake na Aryan kapata ajali.


Tukirudi maeneo ya muhimbili mama aliwahishwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi alipokelewa kisha akaanza kufanyiwa matihabu, lakini mama yake Samairah ambae ndiye alimgonga alirudi kwenye gari na kuanza kulamba ile damu ya mama ambae ilidondoka kwenye siti ya gari.


Mama alilamba ile damu yote ,kisha akasema natamani nirudi katika hali yangu ila binti yangu nitamuachaje? Mama alitikisa kichwa kisha akawasha gari nakuondoka zake

Mama Samairah ni mtu wa aina gani hadi analamba damu za watu na anasema anataka kurudi katika hali yake.


Tukirudi maeneo ya mikocheni zile njemba baada ya kushidwa kumtoboa macho Aryan walirudi kwa akina Kudra na kuwaeleza kila kitu kwamba wameshidwa ile kazi ,Kudra alichukia sana na kuwaambia wakamtafute tena na kuhakikisha wanamtoboa macho Aryan,


Hatimae siku ijayofuata wakiwa darasani Mussa alisimama na kusema jamani nyie wasichana kama mnajipenda nione mtu anamfuata Aryan nitakachomfanyia kitu atajuta ,wasichana wote walitokea kumchukia sana Mussa ,Jesca alisimama na kusema mimi kwa Aryan hunitoi ntamfuata,,, tena pale pale Jesca alichukua kiti na kwenda kukaa karibu yake.


Jesca alimsogelea Aryan na kumnong'oneza "Aryan nakupenda kwanini hutaki kunisikiliza moyo wangu umekuchagua wewe ni samehe hata kwa mabaya yote niliyokufanyia niko tayari kufanya chochote kwa ajili yako",,hayo ni maneno yake Jesca alitokea kumpenda sana Aryan ,ila tatizo Aryan huwa hawapendi wanawake.


Yale maneno ya Jesca yalimfanya Aryan asimame na kumwambia haya nimekusikia nitakujibu baadae kisha Aryan na akaondoka zake ,siku hio Jesca alijisikia amani baada ya Aryan kumwambia atamjibu baadae.


Tukirudi kwa Samairah alikuwa kajiinamia kwa mara ya kwanza alijikuta anaanza kumuwaza Aryan ,"ivi kwa mfano Aryan akiwa mpenzi wangu si itapendeza ee nikiwa njiani twashikana kikono nikienda kwao kujisomea twacheza" Samairah akajikuta anatabasamu.


Aryan baada ya kurudi tena darasani mwalimu aliingia na kuanza kufundisha basi Samairah aliingiza mkono kwenye dawati na kutoa daftari lake lakini kwenye begi aliweka ile bangili aliyopewa na mama yake Aryan


Ile bangili ilidondoka chini kengereee ,ile sauti ya mshido wa bangili baada ya kudondoka kila mwanafunzi akajikuta anageuza macho aliko Samairah

Hata Aryan aliangalia lakini Aryan alipoiona ile bangili alisimama na kuitazama vizuri,Aryan alijisemea ile bangili ya Samairah mbona inafanana na bangili yangu ninayoipendaga ,daa mama angekuwepo ningeenda kuiangalia sasa hata sijui mama alikoiweka ila inafanana sana.


Aryan alipotezea na kuendelea na masomo huku Samairah aliiokota ile bangili na kuiweka kwenye begi kisha masomo yakaendelea,hatimae walimaliza kipindi na muda wa mapumziko uliwadia

Jesca alikutana na Samairah kisha Jesca alimuuliza hivi Samairah ,"ushaniambiaga kuwa Aryan hana mama?" Samairah aliitikia ndio mama yake hajui aliko Jesca alitulia kidogo kisha akasema "ningejua mama yake aliko ningemfuata nimweleze kuwa nampenda mwanae halafu ningempenda mama yake na Aryan ningemnunulia mazawadi naimani Aryan nae angenipenda,,unaonaje wikiendi hii tuende kwa Aryan kujisomea maana wewe si uliniambia unapajua ,


Samaira alitulia kidogo na kumwambia sawa tutaenda halafu si unajua jumatatu tunaanza mitihani ee ,ila kuhusu mama yake na Aryan hata sijui nikushauri vipi maana we mwenyewe hupendi watu wa hali ya chini maana hata majuzi ulinishangaza ulivyomfanyia yule mama aliyekuwa anafanya kazi za ndani kwenu.


Jesca aliongea ,"aah lile limama silipendi tu halafu nishawahi kuliwekea hadi sumu nusu afe sema baba aliwahi kumpeleka hospitali ki ukweli yule mama mmmm silipendi sijui kwa nini sema baba alikuwa anampenda sababu anajua kupika ,nilikuwa nampiga hata makofi ,basi tu nilitokea kumchukia".


Yule ndo mama yake halisi na Aryan na anasema halipendi lile limama halafu anamuulizia mama yake na Aryan ili awe anampelekea zawadi mi sijui akija kugundua kuwa yule ni mama yake na Aryan atafanyaje.


Siku hiyo Aryan alivyoona ile bangili alijikuta anakosa raha na kusema mama yangu angekuwepo ningefurahi mno halafu ile bangili yangu nishawahi kumwambia nitamvisha mwanamke ninayempenda,Aryan wakati anawaza alishangaa warembo wawili wanamgusa kichwa.


We Aryan mbona una mawazo ya nini bana jumamosi tunakuja kwako kujisomea alikuwa ni bibie Samairah wakiwa na Jesca ,Aryan alisema poa karibuni.


Hatimae wanafunzi waliruhusiwa na ilikuwa ni ijumaa walitangaziwa kuwa jumatatu wanaanza mitihani ya kufunga mhula wa pili ,wanafunzi walitawanyika lakini Samairah alimkimbilia Aryan na kumpa kibahasha flani ,Aryan alikipokea na kuuliza kina nini?


Samairah alimkabidhi na kusema utaona huko huko nyumbani ,Aryan alifika nyumbani aliangalia alikuta kuna noti mbili za elfu kumi Aryan alifurahi kama kawaida aliwasha jiko akapika kisha akamwamusha bibi wakala.

Usiku uliingia Aryan siku hiyo hakusoma alilala.


Aryan alianza kuota ndoto yupo ufukweni na bibie Samairah na wanafurahi kwa pamoja lakini wakiwa katika pozi la kukumbatiana , Aryan aligeuza macho nyuma aliweza kuona kundi la akina Kudra wamesimama nyuma yao halafu Kudra ameshika bastola na kumnyoshea,,Kudra alicheka kwa nguvu na kusema huyo Samairah ni mpenzi wangu nampenda kwakuwa wewe hunisikii wasalimie kuzimu Kudra aliinyoosha bastola kwa Aryan.


Aryan akajikuta anapiga kelele ,usiku kisha akainuka "aaah kumbe naota" duu ile anainua kichwa baada ya kutoka kwenye ndoto ukweli Aryan alishangaa kuwaona wanaume watatu wamesimama chumbani mwake ,.Aryan kucheki mlangoni

Mlango umevunjwa mara akamulikwa tochi kisha akaoneshwa shoka.




Tulipo ishia jana baada ya Aryan kuzinduka kwenye njozi alikuta njemba zimesimama tena zimeshika silaha za kijadi ,Aryan aliulizwa aseme kazi ya shoka.


Aryan kabla hajajibu jamaa mmoja alisema leo hatuna muda wa kupoteza kata shingo , Aryan alifumba macho yake baada ya yule jamaa kunyanyua shoka juu, kumbe baada ya kunyanyua shoka juu ,kwenye bati kulikuwa na nyoka katega kichwa chake kwenye ubao nyoka alitema mate kwa fujo wakati huo Aryan huyo kafunika uso

Vile vinyunyu vya mate viliwafanya wale watu wabaya waangalie juu,ni kosa kubwa walilofanya yule nyoka ndio aliongeza kasi ya kutema mate ,kila mmoja alijikuta anafumba macho yao na kusema "nyokaaa" lakini tayari macho yao yashaingia mate ya nyoka ,na nyoka mwenyewe ni yule mweusi,,

Kablaa hawajaa kaa sawa nyoka alimrukia mmoja kwenye shavu alimuuma,kawaida nyoka akiuma mtu lazima ajiviringishe ndo aachie meno yake sasa ,

Alivyomng'ata shavuni jamaa aliruka nje kisha wote wakatoka kila mmoja akijitetea uhai wake ,yule jamaa alitoka nae yule nyoka hatimae nyoka aliachia meno shavuni kwake,kwakuwa ulikuwa ni usiku na mbalamwezi ili pamba vyema walianza kumpiga yule nyoka hatimae wakamuua ,yule aliyeumwa sumu ilipokea haraka uso ukabadilika na kuwa na michirizi mieusii wale wengine wakataka waingie ndani wamuue Aryan lakini na wao sumu tayari ishapokea macho yakajaa machozi huku yanauma hata kuona hawawezi.


Kilichofuata walipiga mayowe kuomba msaada ,majirani walitoka upesi na kuja kuwashuhudia wakiwa wameanza kuvimba macho Aryan nae alitoka alishuhudia kuona wakipakiwa kwenye gari na walipoulizwa huku mlikuwa mnatafuta nini ,walisema tulipotea njia na tulivyofika hapa tulimkuta huyu nyoka tukaanza kumuua ndo katutemea mate namna hio ,

Walibebwa na kupelekwa hosipitani,


Lakini kabla ya kufika hospitalini hali zao zilikuwa tete walizidi kuvimba uso na macho kutoa machozi mfululizo ,yule aliyeumwa na nyoka alifika kwenye lango la kuingia hospitali alipoteza maisha,


Kiongozi wa hicho kikundi alimpigia simu Kudra na kumweleza yaliyo wakuta ,lakini aliongea kwa tabu sana kutokana na ulimi kuwa mzito baada ya sumu ya nyoka kuanza kumtawala , Kudra alimpigia Mussa walichukua gari hadi hospitali ya massana maeneo ya mbezi hakika waliwaonea huruma vijana walio wapa kazi ya kumuua Aryan ,aliyekufa sura yake ilibadilika na kuwa nyeusi kama yule nyoka huku wengine macho na midomo kuvimba hakika sura zao zilikuwa za kutisha,


Kudra alimvuta Mussa pembeni na kumwambia hii siri usimwambie mtu yeyote tumesababisha kifo ujue na mpaka dakika hii hawajafanikiwa hata kumgusa Aryan walau kumpa ngeu moja ,kinachonipa mawazo jumatatu tunaanza mitihani Aryan akitupita tena baba yangu hata nielewa ,Kudra aliongea maneno hayo huku akionekana kuchukia,Kussa alisema ,oya nimepata wazo ,hawa jamaaa kwakuwa tushawapa hela tayari na dili wamefeli sasa kinachotakiwa tuwaruke mita mia moja ,tuachane nao kwanza navunja laini tusiwe na mawasiliano nao halafu huyo Aryan mimi nitamuonesha adabu ,

Mussa aliongea hivyo kisha wakaondoka hospitali na kurudi zao majumbani,


Hatimae siku inayofuata , asubuhi na mapema Aryan aliamka akiwa mchovu alisafisha mazingira ya nyumbani maana alikuwa na taarifa za ugeni wa Jesca na Samairah watakuja ili waje kujisomea kwa pamoja ,hatimae Abbas nae alifika kwa Aryan , siku hiyo Aryan alimnunulia bibi vitumbua na uji akampa bibi akala huku Aryan yeye alienda kula mihogo ,


Aryan mjukuu wangu nimechoka kukaa ndani naomba unisaidie kunishika mkono unitoe nje nikaote jua ,bibi alimwita Aryan,

Haya nakuja bibi ,Aryan aliitikia wito aliacha kazi yake kisha aliingia ndani akatoa kiti nje kisha akaingia tena na kumshika bibi mkono alimtoa nje na kumkalisha vyema ,Aryan aliingia ndani akachukua kitenge na kumfunika bibi miguu ,kisha bibi akaendelea kupata kajua cha asubuhi.


Ilitimia mida ya saa nne bado akina Samairah hawajafika oya Aryan twende pale kwa mangi tukachukue maji ya kunywa si unajua leo tutakuwa na ugeni na watoto wakishua ,Abbas alimwambia Aryan ,

Aryan alitabasamu na kumwambia twende mtu wangu ,waliondoka huku wanapiga mastory yao.


Wakati wanakata tu uchochoro kuna jirani yake Aryan alikuwa anafua alipoona Aryan katoka aliwaita majirani zake na kuwaambia ,haka katoto siku hizi kana jifanya kidume ,tunakaambia kamfukuze huyu bibi ni mchawi hataki kuelewa ona jana usiku watu wameua nyoka hapa mlangoni mwao ,tumeishi miaka mingi hatujawahi ona nyoka sasa leo huyo nyoka katoka wapi ,alisema mama mmoja ambae mwili wake ni mnene,,


Kabla hajamaliza mama Ashura alichukua beseni la mapovu alimwagia yule bibi usoni pwaaa ,masikini bibi wawatu bila kosa anakuta analowanishwa na mapovu ,bibi alipangusa mapovu usoni na kuita Aryan mjukuu wangu nani huyo ananimwagia mapovu ,kabla bibi hajakaa sawa kuna mama mmoja alitoka na sufuria lenye maji machafu sijui alikuwa anaosha sufuria la ubwabwa,


Alikuja kumwagia maukoko ugali maharage ambavyo vyote vilikuwa kwenye matope ,bibi akajikuta analowa ,kibaya zaidi maji aliyomwagiwa yalikuwa yanatoa harufu bibi alinuka mbaya,


Mara bajaji iliingia na kufunga breki kwenye mlango wa akina Aryan walishuka watoto wawili wakike wamewaka mbaya sana si wengine ni bibie Samairah na Jesca marashi yao waliyojipuliza yaliwafanya majirani watoke kuja kuangalia ni nani huyo kapita, wale wamama walio mmwagia bibi mapovu walitoka ,na kuwashangaa warembo akina Samairah,


Wakati huo bibi anaita Aryan njoo nishike mkono niingie ndani ,Samairah alishangaa kumwona bibi aliwahi na kumshika mkono ,Samairah hakujali aliita bibi kisha akamshika mkono na kuanza kumwingiza ndani ,japo bibi alikuwa ananuka mbaya maji aliyomwagiwa na wale majirani


Bibi aliuliza wewe nani ? Samairah alijitambulisha mimi naitwa Samairah rafiki yake Aryan,kwani Aryan kaenda wapi na akina nani wamekumwagia mapovu ,Samairah aliuliza pindi alivyomwingiza bibi ndani ,bibi aliinamisha kichwa chini na kusema mjukuu wangu ,hii dunia tu nimemwagiwa mapovu bila kosa ,kwanza nishazeeka baasi tu ni hivyo ,


Mara Jesca alimfuata Aryan akiwa amefumba mdomo ,Jesca aliuliza we Samairah ,,Aryan ndo anakaa nyumba chafu libibi lake libaya hapa mimi sikai wala sisomi bibi lenyewe lichafu mmmmh.

Kama ni hivi narudi nyumbani ,

Ni maneno aliyoongea Jesca na kumfanya bibi agune mmmm kisha akamuuliza uko na nani wewe mjukuu ,Samairah alimwambia bibi niko na rafiki yangu tu ,tumekuja kwa Aryan hapa kwa ajili ya kujisomea ,

Samaira alirudishia mlango ,kisha akamvua bibi zile nguo zilizochafuliwa na mapovu ,alivyomaliza aliangalia pembeni aliona gauni ,Samairah hakujali alimvalisha gauni lingine bibi kisha akachukua zile nguo zilizochafuliwa na kwenda kuzifua


Jesca alivyoona hivyo alimwambia we Samairah unakichaa nini yaani unashika minguo ya huyo mbibi mmmm zinanuka hivyo bibi mwenyewe mbaya nimemchukia bure kwanza hapa hapanifai kwaheri naondoka zangu ,msalimie Aryan akija tu ,ila siwezi kusoma na yule bibi akiwa yupo hapo


Kwanza mazingira ya hapa mabaya yananuka mikojo halafu mie nishazoea majumba ya mageti niwashe feni nisome kwa raha ila hapa mmmmmmm siwezi, Samairah aliuliza kwahiyo waondoka ?

Jesca alijibu ndio na kusema mimi nampenda Aryan tu siwezi kaa mazingira haya kwaheri

Hakika Jesca alijishebedua kisha akapanda bajaji waliokuja nayo kisha akarudi na kumwacha Samairah


Samairah aliendelea kufua zile nguo za bibi ,alivyomwangalia bibi aliona akidondosha machozi taratibu huku ameinamisha kichwa chini,



Tulipo ishia jana baada ya Jesca kuondoka na Jesca aliongea maneno makali mno,alipanda bajaji na kuondoka zake ,Samairah aliendelea kufua nguo za bibi zilizochafuliwa lakini alivyogeuza kichwa kumwangalia bibi ,alishangaa kuona akidondosha machozi.


Samairah aliacha kufua 1na kwenda kwa bibi alisogea karibu wala hakumnyanyapaa alimshika mkono bibi na kumuuliza bibi kulikoni mbona walia?,kabla bibi hajaongea chochote Samairah aliupeleka mkono kwenye shavu la bibi na kumfuta machozi wakati Samairah akiendelea kufuta machozi ya bibi Aryan na Abbas walirejea ,


Samairah umekuja ,? Mambo ,Aryan alisalimia kwa uchangamfu huku akimtupia bibi macho ,Samaira alijibu poa ,kisha akasimama Aryan aliuliza mbona bibi analia amefanyaje?


Samairah alisita kusema ukweli kisha akamwambia hebu muulize wewe Aryan maana mie nimekuja hapa nimekuta amelowanishwa mapovu ,halafu nimekuta majirani zako wanamcheka ,bibi alikuwa anakuita wewe ndipo mimi nikamshika mkono na kumwingiza ndani nikamvua nguo zake na kuanza kuzifua.


Aryan taratibu alimsogelea bibi ,kisha akaita bibi kulikoni mbona walia?bibi taratibu aliinua kichwa na kusema ,nalia kwa uzee wangu ,upofu wangu ,huenda ningekuwa na macho ningeshuhudia mengi ,kuna msichana yupo hapo nje jamani kaongea maneno mazito sijui itakuwaje na yeye akizeeka ,maana uzee kila mtu ataupitia kama Mungu atajaalia maisha marefu.


Abbas aliuliza msichana gani yupo nje ,Samairah alidakia na kusema Aryan naomba unisamehe mimi ,nimekuja na rafiki yangu Jesca hapa alivyomuona bibi katika hali ile alivyolowanishwa mapovu ,basi akaongea maneno makali kisha akasema yeye hawezi kukaa mazingira haya karudi zake nyumbani.


Aryan akauliza kwa kuhamaki kweli Jesca alikuja hapa? Ndio Samairah alijibu ,Aryan alimshika bibi mkono na kumwambia inuka nikupeleke chumbani ,bibi wala hakubisha aliinuka kisha akaingia chumbani ,

Aryan alitoka lakini bibi alimwita Aryan njoo, Aryan akarudi bibi alimuuliza huyo msichana ni wawapi ambae kanisaidia kutoa nguo nilizolowanishwa ,Aryan alikaa kimya kidogo kisha akasema ni rafiki yangu nasoma nae.


Haya kajisomee nakuombea mfaulu wote wajukuu zangu kisha bibi akajilaza kitandani ,Aryan alitoka kisha wakaingia chumba cha Aryan akakuta Samaira na Abbas washaanza kusoma ,ndipo na yeye akajumuika walianza kujadili baadhi ya topiki kwa pamoja.


Lakini siku hio Samairah alikuwa watofauti alikuwa anamwangalia Aryan usoni kichwani kisha akajisemea moyoni we Aryan ni handsome jamani ,ona anavyoongea ,ona mdomo wake ,macho yake mazuri ,yote hayo yalikuwa mawazo ambayo bibie Samaira akiwaza ,

Mara mlango uligongwa ,Aryan alisema ingia sukuma mlango uko wazi ,kaliingia katoto ,kalivyoingia Aryan alisema aaah Gwae nakuona ona mapengo yako mabaya ha ha Aryan alimtania Gwae ,

Gwae alikuwa ni mdogo wake Abbas mwenye umri wa miaka mitano kama si minne alikuwa anapengo meno ya juu yalikuwa yameng'ooka ,basi alivytabasamu Samaira aliona lile pengo alimpiga Aryan kangumi kadogo kwenye bega na kumwambia bana Aryan usimtanie mtoto hilo jina la mapengo sio zuri,


Gwae alisalimia shikamoo aunt,alimsalimu Samaira ,Samaira akaitikia na kumuuliza unaitwa nani ,Gwae alicheka na kusema naitwa Gwae ,"jina zuri kama ulivyo wewe Samaira alisifia ,

Kisha akauliza ehe Gwae unasemaje?


"Mama kanituma nije nimwite Abbas anataka akamtume kunduchi , mara Abbas akadakia daa maza nae sasa anataka kunituma tena ,jamani kwaherini nikirudi ntakuja tuendelee kusoma

Haya Gwae twende mdogo wangu ,Abbas aliongea kisha wakaondoka ,sasa chumbani walibaki wawili Aryan na Samairah wakaendelea kusoma ,Aryan alikuwa anafanya hesabu ,Samairah basi alikuwa hasikilizi hata kidogo yeye mawazo yake yalikuwa yapo mbali ,

Alianza kuwaza kimoyo moyo,Aryan nakupenda si uniguse tu hata mkono nipate joto lako? Sasa wewe uko bize na mahesabu yako ,ona macho jamani natamani hata busu lako

Mara Aryan alimwangalia Samairah usoni , macho yao yakagongana ,basi Samaira ashampenda Aryan vibaya mno ,mtoto alizifumba mboni zake alikuwa kakaa kitandani halafu kajilaza chali ,


Aryan hakuelewa alishituka na kusogea mahali aliko aliita Samairah nini kimekupata? Samairah alikuwa kimya huku moyoni mwake akiwaza Aryan si uniinue walau uniguse tu mwili wangu.


Aryan alimsogelea na kumshika mashavu alimtikisa huku anaita Samairah,,Aryan nae alipanda kitandani kisha akamwinua na kumlaza mapajani mwake ,huku akiita Samairah ,

Samairah alitabasamu kimoyo moyo akajisemea mambo si ndo hayo alikuwa kavalia sketi fupi sana alivyoipandisha miguu kitandani basi mapaja yake yalionekana meupe pale pale Aryan alivyopiga jicho ,aliona mapaja nae hisia flani zilianza kumwingia

Alimgusa tumbo na kutikisa huku akiita Samairah.


Samairah aliyafumbua macho yake na kucheka na kusema Aryan nilikuwa nakupima je mfano nikipata tatizo utanisaidia? Aryan alitabasamu na kusema kwanini nisikusaidie ,basi mtoto wa kike alirembua na kujisemea kimoyo moyo ulivyonigusa kwenye mashavu nilisikia raha.


Mara simu ikaita kwenye begi la Samairah ,nani huyo ananipigia tena Samairah aliinuka ,kitendo cha kuinuka na kushuka kitandani Aryan aliangalia kiuno cha bibie kilivyokaa vizuri kisha akasemaa aaah wanawake bana.


Samairah alitoa simu kwenye begi kisha akapokea haloo Jesca unasemaje ,upande wa pili simu ilisikika mtu akilia Jesca alisema ,huku sauti yake ikiambatana na kilio ,Samairah nipo huku maeneo ya kunduchi nimetekwa na yule bajaji aliyetupeleka kwa Aryan hivyo nakuomba uje unisaidie maana nampigia mama yangu na baba simu zao hazipatikani.


Kabla Samairah hajajibu bangili ile ambayo Samairah alidondosha darasani ,leo tena ikadondoka na Aryan akaiona Samairah alikata simu na kusema haya nakuja , Samairah akaiokota ile bangili kisha akarudisha kwenye begi.


Aryan akauliza Samairah hio bangili hebu nione? Samaira aliitoa kisha akampa Aryan akaiangalia ,Aryan alianza kuwaza hii bangili mbona inafanana na yangu ambayo nilishawai kuiokota baharini na nilisema nikitokea kumpenda mwanamke nitamvalisha hii bangili ,

Aryan alimrudishia na kusema hii bangili inafanana na bangili ambayo mama yake anayo ,

Kisha Aryan akauliza kwani hii bangili yako umeipatia wapi? Samairah alitabasamu na kusema nimepewa zawadi hivyo naipenda na naitunza.


Sasa Aryan naomba unisindikize maeneo ya kunduchi Jesca kanipigia simu kasema katekwa na dareva wa bajaji ,Aryan aliuliza Jesca huyu ninae mjua ama , ndio Samairah alijibu ,

Kwanini waenda kumsaidia ,Samairah alishusha pumzi kisha akaongea" Aryan yule Jesca ni rafiki yangu halafu mimi ndio nimemchukua kwao na kumleta huku sasa unafikiri akipata matatizo wazazi wake watanielewaje si watasema mimi ndio nimeshirikiana na hao watu"


Okay sawa haya twende ,walitoka na kuacha begi ,walichukua bajaji safari ya kuelekea kunduchi, Aryan alimuuliza Samairah swali ,"hivi yule anae kujaga kukuchukua na gari shuleni ni baba yako?

Samairah alitabasamu na kusema Aryan we nawe huyo si baba yangu ,huyo ni dereva wangu ,mama ka mwajiri kwa ajili ya kunipeleka shule na kunirudisha ,

Ooh mi najuaga ni baba yako ,Aryan aliongea ,na kumfanya Samairah akae kimya kwa muda kisha akaongea.


Aryan mimi sina baba nina mama tu , baba yangu waligombanaga na mama ,hivyo baba yangu ameendaga mbali , na hatoweza kurudi ,maneno ya Samairah yalimfanya Aryan akumbuke hata yeye baba yake ashafariki sasa Samairah nae kasema baba yake kaenda mbali Aryan alisema huenda hata baba yake kafariki.


Hatimae walifika kunduchi mahali waliko elekezwa walifika na kukuta geti jeusi waligonga wakiwa wanasubiria kufunguliwa Aryan aliuliza lakini Samairah unakurupuka kwanini tusingeenda kutoa taarifa polisi sasa unahisi sisi tutaweza kutoa msaada?


Samairah alitabasamu na kusema Aryan mie najua kupiga ngumi tofauti na unavyonifikiria wewe ,nyumbani huwa nina mwalimu ananifundisha masho art hivyo naweza kupiga ngumi mbaya ,Samairah aliongea huku anacheka maana yeye muda wote huwa anacheka.

Baada ya muda geti lilifunguliwa na kijana mmoja mweusi mwenye sura yakikauzu ,aliongea mnatafuta nini? Samairah aliongea rafiki yangu kaletwa huku niambie yuko wapi ,

Yule jamaa alicheka kisha akamshika Samairah mkono na kumvuta akaingia ndani halafu Aryan akampiga teke , Aryan alidondoka chini ,


Kosa moja alilofanya yule jamaa alimpiga Aryan teke maeneo ya kifuani ambako ana ugonjwa wa kupoteza kumbu kumbu,

Aryan aliinuka huku akisikia maumivu makali

Aryan alijikongonja na kukaa kwenye kivuli cha mti huku akiugulia maumivu makali kifuani

Aryan alijiuliza hapa kwani nipo wapi ,masikini tayari kumbu kumbu zake zimepotea.


Tukija ndani baada ya Samairah kuchukuliwa na yule jamaa alimkunja mikono kwa nyuma na kumfunga kamba hatimae alimwingiza ndani ya ile nyumba ,

Ilikuwa nyumba ambayo imeezekwa bati lakini kuta zilikuwa bado hazijasakafiwa.


Ndani kulikuwa na sauti ya kilio cha bibie Jesca ,hatimae Samairah nae aliingizwa ndani kisha akasukumizwa kama mzigo, Samaira alienda kudondoka na mdomo na kufanya damu ianze kumtoka mdomoni ,

Kisha yule jamaa alimwinua na kusema sasa wewe umejileta mwenyewe ,wewe nitakufaidi peke yangu halafu huyu mwenzako atabakwa na hawa jamaa watatu ,


Samairah aliinua kichwa akawaangalia wale vijana kisha akamwangalia Jesca ambae kapigwa uso umevimba na nguo yake kuchanwa alimwonea huruma.

Samairah alicheka kisha akawaambia hivi nyie watu mnajipenda ? Ama hamjipendi.


Yale maneno ya Samairah yaliwakera wale vijana ndipo mmoja aliinuka na kusema we demu unatupima eee sisi alimtandika Samairah ngumi ya usoni Samairah alidondoka chini

Puuuuh!


Samairah alianza kuwaza kimoyo moyo ,"mama ulisema nisitumie nguvu zangu vibaya lakini nitajikomboa vipi hapa pasina kutumia uwezo wangu mama utanisamehe leo navunja masharti uliyoniwekea nimechoka kuona watu wakionewa.


Pale pale Samaira alijikaza kamba alizofugwa mkononi zikakatika akainuka taratibu ,macho yake kwenye kile kiduara cheusi kilionesha alama ndogo nyekundu.


Samairah alisema mwachieni rafiki yangu ,yule jamaa aliyempiga ngumi Samairah hadi akadondoka alikunja ngumi tena na kusema wewe demu hujafunzwa adabu na wahuni mnajifanya watoto wakishua ee sasa ngoja ucheki shoo

Alirusha ngumi Samairah alikuwa mwepesi aliikwepa taratibu jamaa alienda mzima mzima kupiga ukuta.


Uwiiii sauti ya kilio ndio ilisikika mkono wake ulivunjika mara tatu kibaya zaidi hadi mfupa ukatokeza kwa nje

Halafu Samairah alimshika Jesca mkono na kuanza kumfungulia kamba.

Ndipo vijana wengine wawili wakazuia mlangoni




Tulipo ishia jana baada ya Samairah kukwepa ngumi ya yule kijana na kumfanya yule kijana aende moja kwa moja hadi ukutani na kuupiga ngumi ukuta ,ni sauti ya maumivu makali ndio aliyoitoa akilia baada ya mkono wake kuvunjika mara tatu,

Samairah alimwendea Jesca alianza kumfungulia kamba, lakini vijana wengine wawili walizuia mlangoni na kusema we demu hapa hutoki ,yaani unasababisha jamaa yetu anavunjika mkono ehee hapa leo utajijua ,


Jamaa mmoja alitoa bomba la sindano na kumwambia we demu unaona hii ,nakuchoma halafu nakutia dawa ambayo itakulegeza mwili ndani ya dakika moja na utakuwa kama huyo rafiki yako,


Samairah alimtizama Jesca ambae kalegea mwili mzima akiwa amejilaza kwenye kiti huku mikono yake imefugwa ,Samairah aligundua kuwa hawa watu sio wazuri ni wabaya kupita maelezo ,alizidi kuangalia mazingira ya pale aliweza kuona begi la Jesca likiwa pale chini ,


Tayari alifanikiwa kumfungua Jesca lakini Jesca hakuwa na nguvu mwili wake wote ulikuwa umelegea na macho yake aliyafumba ,tukirudi nje ya ile nyumba Aryan alikuwa bado akiugulia maumivu makali kwenye kifua huku kumbukumbu zake zimepotea ,Aryan kila akijitahidi asimame ili aondoke akajikuta anayumba na kujisikia kizungu zungu kikali ,

Kwa mbali kulikuwa na watoto sita wasio zidi umri wa miaka sita ama saba walikuwa wakicheza mpira wakipita eneo ambalo Aryan aliko ,

Katoto kamoja kaliongea we Jimmy kasimame kwenye ule mti karibu na yule kaka halafu nikupigie pasi ndefu tuwe tunarudishiana tuone nani atapoteza nafasi ,

Jimmy alikubali na kusema sawa Dani ila usipige pasi kubwa sana maana wewe unabutuaga mpira ukija kuingia kwa nyumba za watu itakuwa sio poa,


Wakati huo Aryan anajikakamua kuinuka mara Dani akapiga mpira shuti kali ili kumpasia mwenzake Jimmy,,ule mpira ulienda kwa kasi sana na kupita juu juu ,Jimmy alijaribu kuruka ili audake hakufanikiwa ule mpira ulienda moja kwa moja na kutua kifuani kwa Aryan paaah


Aryan alidondoka na povu likaanza kutoka ,tambua Aryan ugonjwa wake wa kupoteza kumbu kumbu ukimpiga kifua anapoteza kumbu kumbu ili uzirudishe lazima umpige tena kifua ,ki undani bado hatujajua yale maradhi kayapataje ila tunavyozidi kusonga mbele tutaelewa ,

Aryan alidondoka chini na kupoteza fahamu kabisa ,alianza kukoroma huku povu jeupe likitoka mdomoni ,wale watoto walivyoona vile ,

Jimmy alisema Dani ,umeua mkaka wawatu ,wale watoto waliwahi na kwenda kumwangalia Aryan walikuta akikoroma huku povu likitoka mdomoni ,rafiki zake Dani walianza kukwambia Dani umeua Dani umeua ,


Dani aliwaambia hapa tukimbie tuondoke lasivyo tukikamatwa ujue tutapelekwa gerezani wale watoto walichukua mpira wao na kuondoka walikimbia ,

baada ya dakika tatu alirudi katika hali yake ndipo kumbu kumbu zake zikarejea

Alianza kukumbuka nilikuja na Samairah hapa sasa kaenda wapi ,mmmh hebu ngoja nikagonge lile geti sijui ndo aliingia hapo ,wakati Aryan anaenda kugonga lile geti ndani yake ya hiyo nyumba.


Yule jamaa alieshikilia bomba la sindano yenye sumu ya kulegeza alimsogelea Samairah "we demu tokea tumeanza kazi za kuteka watu kama ninyi watoto wakishua tuna miaka zaidi ya mitatu sasa wewe leo ndo umenishangaza hebu mwangalie rafiki yetu amevunjika mkono hadi mfupa kuchomoza kisa wewe hakia nani kitu ambacho tunakufanyia utaenda kusimulia ,halafu sisi tuna kambi zaidi ya mia ,tukiteka mtu tunampeleka sehemu mbali mbali usifikirie ni rahisi kutukamata

Sana wacha nikudunge hii sindano kwanza ulegee halafu tukufanyie kitendo cha kinyama


Samairah alimwangalia yule kijana kisha akasema we kijana ungejua mimi ni nani walahi usingejisumbua na ungeomba msamaha mara dufu ,yote hayo bibie Samairah alijisemea kimoyo moyo ,kisha Samaira akasema


Mimi sitaki kupigwa wala kufanyweje nasimama mimi mwenyewe nidunge hio sindano yako ,yule jamaa alisema oya Rama huyu demu analeta ushua kwenye anga za wahuni mkabe , Rama alimrukia Samairah na kumkaba mikono Samairah wala hakuhangaika kujitoa alitulia tuli ,yule mwanaharamu aliishika sindano yake na kumdunga Samairah maeneo ya shingo sindano aliizamisha cha ajabu Samairah hakushtuka alitulia tuli ,yule jamaa alibinya lile bomba na kusukuma sumu ambayo itamlegeza Samairah


Samairah baada ya dakika moja aliachiwa na kudondoka chini ,wakati huo Jesca hali yake bado iko vile vile hajitambui ,yule jamaa aliyevunjika mkono alitoka nje ,sijui aliita bajaji na kuwahishwa hospitali ili akapate matibabu kwanza ,

Wale wenzake waliobaki Rama alitoa mkanda wa suruali na kufungua zifu alivua suruali na kubaki na boxer

Oya shedi hapa hatuna muda wa kupoteza nishikie miguu mie nijilie vitu ,kabla hajakata moto maana ile sumu ni kali halafu mtoto mkali hapa nitapata joto safi ,Rama aliongea huku akipanua miguu ya Jesca ,

Shedi alimuinamia Samairah na kutaka kuanza kumvua nguo huku wakijua tayari sumu ishaanza kufanya kazi


Samairah alianza kuwaza kimoyo moyo ,hawa watu leo ndio itakuwa mwisho wao kufanya upuuzi huu wakati anajifanya kalegea na dawa aliangalia pembeni aliona chupa ya soda ,alijivuta upesi akaishika wakati huo shedi kainama anahangaika kumvua nguo ,alichokifanya Samairah alimpiga nayo kwenye usoo paaa

Ile chupa ilipasukia usoni paaa vipande vya chupa vilipasua uso wa shedi Samairah alikuwa mwepesi mno aliserereka chini huku mkononi kashika vipande viwili vya chupa baada ya ile chupa kupasuka ,alimkita maeneo ya siri Rama kwa nguvu

,Rama alipiga ukunga wa nguvu huku mikono yake kaibana kwenye sehemu za siri alidondoka kama gunia

Samairah alishika tena kipande kingine cha chupa kisha aliruka akadanki kwenye ukuta akakikita kile kipande cha chupa kwenye shingo ya shedi


Halafu akamkonyeza vipi maumivu yake unayasikiaje ,maana wewe umenidunga sindano na haijanidhuru sasa wewe hapo sikilizia usipo wahishwa hospitali unakufa nimekata mshipa wa fahamu ,

Samairah alimwangalia na Rama ambae kadondoka chali damu zinamtoka kwenye sehemu za siri


Samairah alishika shingo mahali alikodungwa sindano alibinya ,

Sumu ilitoka nyeusi kisha akatabasamu na kusema hakika binadamu wanapenda kujiingiza kwenye matatizo

Samairah alimnyanyua Jesca ambae kalegea na wala hajitambui ,Samairah alianza kuwaza hivi Jesca atakuwa kaona kitu kilichotokea na je Aryan akigundua kuwa mimi si binadamu wa kawaida atanielewaje ? Na sielewi ameanza kuingia kwenye moyo wangu ,yote mawazo yalikwa kichwani mwa Samairah alimkokota Jesca hadi walivyotoka nje ya geti walimkuta Aryan amekaa baada ya kugonga geti kwa muda mrefu hakupata msaada aliamua kukaa


Aryan aliita Samairah umemuokoa Jesca aaah umefanyeje? Halafu mbona Samairah yupo katika hali hii,Samairah alitabasamu na kusema amedugwa sindano yenye sumu hivyo tumuwahishe hospitali , Aryan alimsaidia Samairah kumbeba Jesca hadi barabarani walichukua bajaji na kumpeleka Jesca hospitalini ,

Lakini walivyofika maeno ya mbezi afrikana Jesca alizinduka na kurudi katika hali yake . Aliyafumbua macho na kujikuta ameegemea kwenye bega la Aryan ,tena Aryan alimshika maeneo ya tumbo ili asidondoke maana alikuwa kazidiwa na dawa


Jesca kuona amelala kwenye bega la Aryan alianza kuwaza kumbe mimi mzuri ee ona Aryan amekubali kunilaza kwenye bega lake jamani raha ,huyu mkaka mzuri nampenda,,

Si apandishe mkono anishike na kifuani yale yote ni mawazo ya Jesca baada ya kuzinduka ,


Alifanya makusudi akajilaza kabisa kifuani mwa Aryan wakati huo wapo kwenye bajaji ,mara Samairah alimwangalia Jesca alikuta ametabasamu na amejilaza kwenye kifua cha Aryan ,sijui wivu umeanza kili ,Samaira alimwinua jesca na kumuegemeza kwenye siti ,jesca alivyo na makusudi akajilaza kabisa kwenye mapaja ya Aryan.


We Jesca si umeshazinduka hebu kaa vizuri ,Samairah alimwinua ,Jesca alipikicha macho yake akasema nikijilaza kwenye miguu ya Aryan nasikia raha ,Samairah alimwambia hebu acha zako ,


Hapo ndipo Aryan akagundua kuwa Jesca ameshazinduka ,alimshika mkono na kumwambia "unajisikiaje? Kitendo cha kumshika mkono Jesca ndo anasikia raha alitabasamu na kujisemea najisikia vizuri huku anaupeleka mkono wa Aryan kifuani mwake


Aryan alitoa mkono upesi na kumwambia dereva wa bajaji apaki bajaji kuwa yeye anataka kurudi nyumbani ,

Samaira wataka kurudi nyumbani? Aryan alitikisa kichwa na kusema ndio nataka kurudi nyumbani nimechezwa na machale nahisi bibi nyumbani hayuko sawa


Aryan alishushwa na bajaji kisha akachukua pikipiki ili arudi.


Nyumbani ,sasa tukirudi maeneo ya tegeta mahali anako ishi Aryan leo akina Mussa na Kudra waliwasili maeneo haya huku wakiongozana na mtu ,

Kudra "huyo Aryan unae msemea wewe anaishi katika nyumba hii na mlango umefugwa yawezekana ametoka ,Kudra aliangalia nyumba kisha akasema kama tulivyozungumza pitisha hio petroli kwenye hio nyumba halafu tupige njiti nyumba nzima iwake , akikosa mahali pakukaa hata weza kwenda kufanya mtihani na atafanya sisi turudi katika nafasi zetu


Akina Kudra walikuja na mtu walimpa kazi amwagie nyumba anayoishi Aryan petroli halafu waichome lengo lao Aryan asiweze kwenda kufanya mtihani ,


Yule jamaa aliangalia huku na kule hapakuwa na watu alimwaga petroli upesi walivyomaliza walichukua kiberiti waliwasha njiti kisha wakaitupia mlangoni waliwasha piki piki na kuondoka upesi ,

Mussa alijisemea hapa hatakuwa na ujanja tena nguo za shule zikiungua moto na madaftari hata weza kwenda tena shule waliondoka zao


Moto uliwaka maana petroli na moto ni vitu vinavyoshabihiana, nyumba ilianza kuwaka kumbe ndani ya nyumba bibi alikuwa amelala

Baada ya ule moshi kuingia ndani bibi alianza kukohoa ,kibaya zaidi bibi ni kipofu na Aryan hayupo ,, watu walijaaa na kusema moto jamani moto wenyewe wako wapi ,

Majirani wala hawakuhangaika kuuzima moto ndo kwanza wamesimama na simu zao wanarekodi video jinsi nyumba inavyo waka

Bibi alihisi kifua kina mmbana baada ya moshi kutanda ndani



Tulipoishia jana baada ya kundi la wenye roho mbaya akina Mussa na mwenzake Kudra waliweza kuichoma nyumba ya akina Aryan,kisha waliwasha piki piki na kukimbia ,walijisifu kwa kufanikiwa kuwasha ule moto,bibi ndani alipata moshi mzito alianza kukohoa kwa fuju ,lakini sauti yake haikusikika kutokana na moto kuzidi kuwaka ,akina mama Asharua na mama bonge ambae ni majirani zake na Aryan wao ndio walikuwa wakwanza kusema moto jamani moto,

Walisimama na kushika viuno hamna aliyesema waingie wajaribu walau kuokoa mali za Aryan ,


Mama Ashura alisema jamani yule bibi ambae simpendi mungu kasikia kilio changu sijui huu moto umetokea wapi leo huyu bibi ataungua ngoja nikae kabisa nisikie kichwa chake kitakapopasuka paaa aliongea kisha wakacheka na rafiki yake mama kibonge ,watu walizidi kujaa ,wengi wakisema jamani nyumba ndo inateketea hivyo ,mjumbe wa nyumba kumi nae alifika na kusema nini chanzo cha moto ,kila mmoja alisema hatujui ,


Mjumbe aliuliza sasa yule kijana yuko wapi? Mama Ashura alijibu katoka zake siku hizi anajifanya kakua ameenda kutafuta mademu ,ha ha ha ,watu walicheka huku wakiangalia nyumba ikiungua.


Masikini hali ya bibi ndani ilizidi kuwa tete alishindwa kuhema na kujikuta akitapa tapa ,bibi alijaribu kupaza sauti walau kuomba msaada lakini sauti yake haikufanikiwa kusikika maana alikuwa anashidwa kuita sababu ya moshi kutanda ,

Bibi alijikongonja lakini hata mlangoni hakufanikiwa kufika bibi alipoteza fahamu akadondoka


Moto nje na ndani ukazidi kupamba moto ,yaani baada ya bibi kutoka kwenye kile chumba tu kuna kuti lenye moto lilidondokea kitandani kagodoro kalishika moto na kuanza kuwaka


Mlio wa piki piki ulisikika hatimae Aryan alifika nyumbani alikuta mlangoni moto umepamba moto ,masikini Aryan aliita kwa nguvu bibiiiiiiii bibiiii nani kayatenda haya Aryan aliuliza kwa sauti ya juu lakini kila mtu alimcheka mama Ashura alidakia Aryan mimi nipo hapa nasubiri kichwa cha bibi kilipuke ,


Daaah Aryan alitazama mazingira ya hapo nje aliona ndoo ya maji alichukua akajimwagia kisha akaingia ndani huku akiita bibi ,bibiii watu walimkataza asiingie ataweza kufia huko lakini Aryan alizama ndani alimkuta bibi kadondoka chini ,

Wakati Aryan kazama ndani huku nje akina Samairah na Jesca nao wanaingia na bajaji sijui nini wanakitafuta lakini walivyokuta moto umewaka waliuliza Aryan yu wapi

Mama Ashura alitabasamu na kusema Aryan anakitafuta kifo kaingia ndani kutoa msukule wake ule mjibibi , Jesca alisimama mbali na kusema aka na uzuri wangu huu niungue aku ,sitaki mwenzangu,


Samairah nae aliangalia pembeni aliweza kuona kibeseni chenye mapovu ambacho mchana wake alifua nguo za bibi alivyomwagiwa maukoko ,Samairah mtoto mrembo hakujali uzuri wake alijimwagia yale mapovu kisha akazama ndani ,huku akiita Aryan Aryan ,

Alimkuta Aryan yuko sebuleni anahangaika kumnyanyua bibi ili amtoe nje lakini kwakuwa alikuwa peke yake basi alijikuta anakosa namna ya kufanya ,Aryan aliingia chumbani kwake alichukua begi la Samairah ambalo aliliacha mchana ,kisha akaenda kwa bibi ,bibi alifumba macho na kukata tamaa.


Aryan nae moshi ulimzidi kisha akakosa pumzi Aryan alimkumbatia bibi na kusema tutakufa wote,akiwa kapoteza tumaini alishangaa kumwona mtoto wa kike Samairah kanyoosha mkono ,Samairah alimshika Aryan kisha akamwinua alivyofika mlangoni alimsukumiza kwa nje Aryan alidondoka nje na kupoteza fahamu akiwa kakumbatia begi la Samairah


Samaira akiwa kafunika uso wake kaziba kitambaa kwenye pua na mdomo aliingia kwenye chumba cha Aryan alichukua madaftari na nguo za shule baadhi na nguo za Aryan alirusha nje kupitia dirishani

Samairah alimwendea bibi alimnyanyua japo mzito alianza kutoka mdogo mdogo nae alianza kukosa pumzi Samaira moshi ulizidi kumlewesha akajikuta anaanza kuyumba kabla hajadondoka mtaalamu Abbas nae alikuwa ashatia timu ,Abbas alimshika bibi akamtia mgongoni huku mkono mmoja kamshika Samairah mkono,Abbas alijikuta anawatoa wote kwa pamoja


Ile wanatoka tu nyumba ilianguka mabati yakiwa yamewaka moto,yakaangukia mahali bibi alikuwa amelala ,Abbas alivyowatoa Samairah na bibi ,ndipo bibie Jesca alikuja na kumwangalia Aryan ambae anahema juu juu ,alimtizama usoni na kujisemea

Asante mungu handsome wangu hajafa yuko hai lakini kwanini Samairah kamuokoa yule mbibi angemwokoa tu Aryan wangu ninaempenda ,alitoa kitambaa na kuanza kumpepea Aryan

Mama Ashura alikunja sura baada ya kuona ,bibi katoka salama ,

Nyooo ule mbibi umetolewa naona sijui umekufa sijui umezimia kwanza washanikera ngoja nikaepue maharage yangu


Mama Ashura alichukia mno aliondoka na kusema sasa hivi tuone wataishi vipi nyumba hawana imeungua ,mama Ashura ile anaingia kwake tu alipokelewa na kofi zito

Paaaa we mwanamke mshenzi yaani unaacha maharage yanaungua unaenda kushangaa nyumba inaungua hata msaada hamkutoa unapiga tu porojo ,ni maneno ya mume wake ,

Hivi unajua hela zinavyotafutwa? Nakuuliza kwanini umeunguza maharage ,baba Ashura nisamehe ,kabla hajamaliza baba Ashura alivua mkanda alianza kumpiga kama punda uwiiii nakufaaa ,jamani mume wangu nisamehe alianza kupiga kelele za kuomba msamaha lakini hadi watu wanafika walikuta ngeu usoni zimesimama na dera limechwanwa paja moja la kulia lipo nje ,

Mama bonge alimshika mume wake mama ashura na kumbananisha kwenye ukuta na kumwambia


Wewe jiangalie ukirudia tena ntakunyonga lini mwanamke akapigwa kama punda ,alimwachia baba Ashura,ndipo baba Ashura hakukaa tena nyumbani akaondoka zake na kumwacha mkewe akilia


Tukirudi upande wa pili Samairah alikuwa wakwanza kuzinduka alivyofumbua macho alikuta Abbas anamwagia maji kichwani Samairah alitikisa kichwa alivyoyatupa macho kwa Aryan aliweza kumwona akipepewa na bibie Jesca ,yaani Jesca anajikuta anajisahau kupepea na kuanza kuwaza ,Aryan ngoja nikuguse kifua nikupepee lakini Samairah aliweza kufika na kumwekea maji kichwani Aryan alizinduka


Ndipo walikaa kwa muda wa nusu saa ndipo bibi nae alizinduka wote walinusurika ,bibi alijikuta amekumbatiwa mkono ,bibi aliita Aryan mjukuu wangu ,"naam bibi niko hapa ,bibi alitikisa kichwa na kusema watu wabaya dunia haina kosa hata kidogo ,Aryan alimwangalia bibi ambae nywele zake zimekuwa nyupe baada ya kupitishwa kwenye moto, ,Aryan alimwangalia Samairah ambae alikuwa tayari ashavaa lile bangili ambalo alipewa na mama yake Aryan,ila yeye hajui kama ndio mama yake na Aryan ,


Watu waliondoka na kuwaacha akina Aryan baada ya kuona wametoka salama hawakuwapa hata msaada wa mawazo walitawanyika ,Aryan aliangalia madaftari yake aliangalia na nguo zake za shule ,

Aryan aliwaambia Samairah, Abbas na Jesca mimi shule basi tena naacha sina mahali pa kuishii sina hata hela ya kurudishia nyumba ya mama yangu ,Aryan alianza kulia na kuita mama ,mama mwanao nateseka alilia kwa uchungu mno.


Samairah alimwambia Aryan usiseme hivyo nitajaribu kwenda kuongea na mama kama ataweza akusaidie walau hela ukapangishe chumba tumalizie mitihani baada ya muda kidogo kuna piki piki ilikuja wakashuka watu watatu ,

Wakiwa wanacheka ha ha ha wewe si ulijifanya mjanja unapendwa na wanafunzi sasa basi tuone itakuweje


Kumbe walikuwa ni akina Mussa na Kudra walimcheka sana Aryan ndipo Samaira aliwaambia Kudra nyie ndo mmehusika na kuchoma nyumba ya akina Aryan ,Kudra alicheka kwa dharau na kumwambia Samaira tumeanza na Aryan tutamalizia na kwako si unajifanya unaringa na huo uzuri sisi ndo wababe .


Waliwasha piki piki wakaondoka ,Aryan alimwangalia Abbas akamwangalia Samairah pamoja na Jesca Aryan alisimama na kusema shule siachi hata kama ntalala mtaroni ntaenda tu ,

Yale maneno yalimfanya Jesca amkumbatie Aryan kisha akataka kuupeleka ulimi kwenye lips za Aryan ,Samairah alifumba macho ili asione kinachoendelea maana hata yeye anampenda Aryan mbaya ,

Ila Aryan alikwepesha na kumwambia Jesca hapana,Jesca alimkaba Aryan shati na kumwambia Aryan naomba unipe jibu langu toka majuzi hujanijibu swali langu nambie kama unanipenda kama hunipendi niungane na akina Mussa.


Daah Jesca alivombana Aryan namna hio ,Aryan alikuwa na hasira sana alitabasamu na kumwambia usijali bado nafikiria ,Jesca alimwambia juma tatu unipe jibu kama hutaki kuwa na mimi nijue cha kufanya ,lakini Aryan ningependa unieleze mama yako yuko wapi ,maana nikimpata mama yako ataweza kunisaidia kukueleza ili unipende kama mimi ninavyokupenda ,au huyu bibi ni mama yako ,


Aryan alikaa kimya na kumwambia mama yangu sijui aliko ,Jesca alisema pole ntakusaidia kumtafuta ,mama aliyekuzaa handsome wangu ,maneno ya Jesca yalimfanya Samairah kukosa raha maana hata yeye anampenda Aryan

Mara bibi akadakia ," we binti muongeaji sijui waitwa nani ,yaani katika hii dunia hamna mwanaume atakae kupenda kwa mdomo wako wenye maneno machafu ,afadhali huyu binti hata mimi nimempenda toka moyoni ,bibi alimtaja Samairah amempenda na si yeye.



ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

BLOG