Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SIHITAJI KURUDI NILIKOTOKA - 2

   

Simulizi : Sihitaji Kurudi Nilikotoka 

Sehemu Ya Pili (2)


Tunu na amina walisimama wakavaa nguo zao na kutoka nje wakiwa wamepandwa na hasira kwenda kumwangalia mhudumu ambae huwa anawapatia chai, walimtaka maryam avae waende ila akagoma, walitoka chumbani akabaki maryam na lucky, maryam alikuwa ana huruma sana alijisikia vibaya namna mwenzake alivyo lalamika, hakutaka amuaminishe kuwa yeye ni mbaya wake.

" lucky, sijafunzwa kumuacha mtu anaelia akiendelea kumwaga machozi yake na mimi kutoka nje, maneno yako yanaonesha kiasi gani umekasirika juu ya maamuzi yetu, tokea uingie humu sijawai kukuona ukiongea hivyo, naomba unisamehe sana kwa kufanya kitu ambacho hujaridhia, nisamehe mimi na wenzangu, siko happy kiukweli kukuona ukiuzunika japo itanilazimu sasa. alisema maryam.


" Hivi unajua huyu dem simwelewi Amina ee!. Baada ya kuwa wako nje Tunu alisema kumwambia mwenzake.

" hata mimi, eti nna uwezo wa kuchukua room nzima peke yangu msiniingilie, Haa!, huyu wakuja nini.

" linavyoongea sasa kama mdomo umemeza flash, yani hata yale mapozi hana.

" kaniharibia siku asubuhi asubuhi Akyamungu, sijui mudi kama ntamkuta aniletee bia nipoze akili kwanza. Alisema amina akipeleka mkono kichwani kukuna nywele zake zilizokuwa tim tim flan.

" tena sio moja, huyu mtoto mimi nataka nimchangamkie nimkorogee Kiswahili ajione kama kunya, eti hooo mna maisha yenu na mimi nna maisha yangu yani kaniboaaa. Alisema tunu.

" ila kirehe rehe chetu na sisi, ashuo gani hadi midomo ikatupwaya kwenda kusema?.

" kirehe rehe kihere here mwenzangu na nimekoma kuingilia maisha ya watu yasiyonihusu. Alisema tunu. walifika chini walikokuwa wanapatikana wahudumu wakamuona mudi waliemzoea, walimpatia maagizo ya nini awapalekee kisha wakageuza kurudi.


Maryam ndani aliendelea kumuomba msamaha lucky ili amsamehe kwa kumfanya akose raha baada ya kuchukuana na wenzake na kwenda kwa sofia, lucky alimwelewa akamwambia asijali ni mambo ya kawaida.

" Ok my friend, napenda kuiona furaha ya mtu, sipendi kuipoteza maana najua siwezi kuilipa. Nambie ungependa kula nini morning hii!. Alisema maryam mara alipoona tabasam la lucky, aliinuka kitandani akaweka mkono kwenye mfuko wa nguo yake iliyokuwa umetundikwa kwenye henga kuangalia kama kuna pesa.

" Sijisikii hata kula kitu mumy usijali.

" No Lucky, asubuhi lazima kuwepo na kifungua kinywa, kama umenisamehe naomba unambie utakula nini!. Alisema akiachia tabasam, mkononi tayari alishikilia shiling elfu 10 ya kitanzania.

" Unataka kwenda kuagiza?. Aliuliza lucky

" Yes.

" Poa, nchukulie soseji mbili, chai ya maziwa juis na chapati moja.

" Ok poa.

Alitoka maryam kwenda kuchukua chai, alipofungua mlango akakutana na wakina Amina wao wakirudi.

" ulikuwa bado unaongea na huyo mtu?. Tunu alimuuliza.

" yah nlikuwa naongea nae.

" ana jipya gani.

" katusamehe.

" kwani tumemkosea.

" Tunu acha hizo bhana, huoni kama tumemkosea kwenda kwa sofia bila kumwambia?.

" Duh!. Tunu alitoa macho ya mshangao.

" Ujue tunu huyu nae ndo wale wale huruma huruma. Alidakia Amina.

" sio huruma huruma, ili hali hatutukani, tukimsalimia anajibu vizuri, kwa nini tumuingilie katika maisha yake?. Tumuache kama alivyo. Alisema maryam.

walipomuangalia maneno yake wakajua tayari yupo kwa ajili ya kumtetea lucky, walimruhusu aendelee na safari yake ya aendako nao wakaendelea kuwepo nje kupiga umbea kabla ya kuingia ndani.


" Kashakuwa rafiki yake huyu. Alisema amina.

" Muache akizingua na yeye si tunamsheet tu.

" Anajifanya huruma huruma, wee lini paka na mbwa wakakaa pamoja bila kukoromeana?. Jitu liko kama zombie halijua kuongea, muda wote kuvimbisha mashavu tu kama kabugia pili pili urafiki nae wa nini?.

" ndo hapo sasa!, hata mi nashangaa.


Walimaliza kuongea wakaingia ndani na kumkuta lucky yuko kitandani amelala, tayari alikuwa kwenye mkusanyiko wa mawazo, machozi yalikuwa yanamtiririka upande upande, walimuangalia hawakuitaji kumshtua, kila mmoja alipanda kitandani kwake akachukua cm na kuanza kuchart, waliweka phoni maskioni wakawa hawana habari wasijue kinachoendelea, lucky alikuwa katika wakati mgumu sana, hakuacha kukumbuka baadhi ya mambo yaliyomtokea nyumba ambayo yalisababisha mara kadhaa kumfanya akose raha na kuachia kilio cha bila kutaka wala kutaraji.


Maryam alirudi baada ya kuagiza vya kuagiza, akiwa mlangoni aliwaangalia amina na tunu akaona ambavyo hawana habari na mtu wako bize na kusikiliza miziki, alipomuangalia lucky akajua tayari hayuko sawa, alitikisa kichwa chake kumsikitikia, ni yeye pekee alibakia kumuonea huruma, alisogea akakaa pembeni ya alikolala.

" Lucky. Alimuita kwa sauti ya taratibu, lucky alishtuka akafuta machozi yaliyokuwa yanatoka.

" Usijaribu kufuta chozi la kinyonge wakati haiwezekani. Mbona unajaribu kuficha maradhi ya kidonda cha nje ya mwili wakati kila mmoja anakiona?. Sii vizuri lucky unavyofanya, hali yako hainiusu lakini naumia kuona wenzio tunafurahi wewe huna furaha. Alisema maryam katika hali ya huzuni baada ya kuona lucky anafuta machozi, lucky maneno aliyoambiwa na binti huyo yalimuingia akilini, aliinuka akakaa na kumshika pajani.




" Maryam nsamehe, najijua kuliko anaeniangalia, na najionea huruma kuliko anaenionea huruma, hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho, uenda kuna tatizo linalosababisha hali hii kwangu japo hata mi mwenyewe sijui ni kwa nini, samahani kama nakukwanza kutokana na hali yangu ila kiukweli sijui nini kinanisumbua, najiona niko normal tu mimi. Alisema lucky akijaribu kuuficha ukweli ulioko moyoni mwake.

" Lucky bado unaongopa, yani unaongopa hadi uso wako unaonesha kuwa unaongopa, ila siitaji kukukera, jiandae tukanywe chai. Alisema maryam.

" Si analeta ndani?.

" Hapana, twende tukanywee hotel huko huko tukapate na upepo wa asubuhi, ntafurahi kuongozana nawe. Alisema maryam lacky akakubali, alivaa nguo zake za kawaida akaweka vizuri nywele wakatoka nje.


Walitembea taratibu wakiwa wanapiga story za kukatisha, Wawili hao walishindana kwenye maumbo tofauti na Amina pamoja na Tunu waliokuwa modozi, maryam alikuwa black brown ( maji ya kunde ) mnene kidogo mwenye shep hips la kutosha, alipotembea ilikuwa lazima mwanaume aliekamilika kugeuka, aliwamezesha mate wengi chuoni na nje ya chuo, lakini alijiwekea msimamo wa kusikokuwa na mwanaume kipindi chote cha masomo yake, kitu kilichokuwa tofauti kwa amina na tunu waliokuwa wanawachanganya wanaume kama karanga.


Pia lucky rangi yake ilikuwa nyeupe ya asili iliyokuwa inapendeza kwa kila aliemuangalia, shep na hips lake ndo liliwafanya wengi waishiwe mapozi, macho yake yalikuwa legevu ya mvuto, mdomo kidogo Mungu alimnyima lips za kutosha, kiufupi alikuwa beutfull kiasi chake ambacho Mungu alimpangilia na kumuumba.

Walifika hotel wakakaa moja ya viti vilivyokuwa pembeni kidogo, wanaume wengi waliokuwa eneo hilo wakipata brek fast waliwaangalia sana kimatamanio, wengine walibadili mada kabisa na kuwazungumzia wao kama ilivyo kawaida ya wanaume wanapoona kizuri kimepita, walivalia nguo za kawaida tu lakini bado uzuri wao haukujificha, maryam alifurahi mno kuongozana na lucky hadi hotel, haikuwahi kutokea tokea wawe pamoja bweni.


" Leo ni weekend Lucky, kwa nini tusiitumie kutoka out kama beach hivi, sweeming, or sehemu yoyote ya furaha kwenda kubadili hali ya hewa?. Alisema maryam baada ya kupiga fundo moja la chai ya maziwa kumsemesha lucky aliekuwa kimya, aliitaji amtoe out ili akambadilishe mawazo. kutokana na maisha ya binti huyo yalivyokuwa ya kiukimya sana chuoni hapo haitaji kujichanganya na wenzake, maryam aliamua kuachana na fikra za wenzake za kumtenga lucky, na kilichobaki alitaka kutumia elimu yake ya chuo aliyonayo ili amtengeneze kisaikologia uenda akamuwekea wepesi wa kuchangamka na kama alitoka kwenye maisha flan hapo nyuma akasahau.

" Unaitaji twende beach au sweeming!?. Aliuliza lucky kwa mshangao.

" Yeah!, coz to day is weekend, itakuwa so fa ukikaa ndani tu, kukaa ndani ni moja ya kitu kinachokufanya uwe na mrundikano wa mawazo, tafadhali naomba unikubalie ombi langu twende hata beach tu patatosha.

" mh!, beach gani?

" yoyote ile iliyo tamu.

" Ipi sasa!.

" Kama msasani au coco itakuwa good zaid coz kunakuwa na wasanii wa kutumbuiza na vitu vingi vya kuburudisha.

" Una maneno wewe!.

" Hapana Lucky, ujue mimi nimetokea kwenye maisha flan hivi ambayo ni amazing so nnapomuona mtu hana raha naumia kiukweli, nlikuwa najitahidi kukutenga kipindi chote ambacho amina na tunu hawakuwa na muda nawe kwa hali yako, lakini nlijiuliza mara kadhaa hata nlipokuwa Class, inakuwaje nafurahi kuona mtu nnaeishi nae hana furaha na mimi naridhika?. Je kama ingekuwa mimi ndo yeye alafu yeye ndo mimi ingekuwaje?. Nnapojiuliza swali ka hilo najikuta nanyong'onyea na kuwa mpole.

" mh!, kwani umezaliwa wapi?.

" Nimechanganya Arusha kwa mbeya ila nimezaliwa dar.

" Okey

" why umeuliza hivyo?.

" Hapana kawaida, nimekosea?.

" No hujakosea.

" Long time agoo Arusha ngarenaro nlikaa wiki mbili.

" Wao.

"Nlipapenda sana japo....... alisema lucky, kuna kitu alitaka kusema akawa amekikatisha.

" Japo nini?. Aliuliza maryam baada ya kuhisi kuna kitu kimekatishwa.

"Ulimi hauna mfupa mumy, mimi nshashiba nakuwait wewe twende zetu au?. Alipotezea juu kwa juu akabadili mada, Maryam hilo alilishika akahisi kuna kitu ambacho nae aliitaji yaishe, hakuitaji kumkwaza na bahati nzuri alishamjua alivyo dakika mbili mbele.

" Ok poa.


Waliendelea kupiga story taratibu wakinywa chai iliyokuwa sii moto sana, walipomaliza walisimama kwa ajili ya kurudi room, maryam alifanya malipo lucky akiwa pembeni yake, eneo hilo hilo lililokuwa pembeni kidogo na watu walipo, aliingia moja ya vijana ambao huwa hawajiwezi kwa kummezea mate lucky aitwae Deniss.

" Hi Lucky. Alisema Deniss kumsalimia lucky, lucky alikuwa bado hajamuona, aliposikia hi ilibidi ageuke nyuma akakutana na deniss.

" Hii too.

" Mambo?.

" Poa.

" Oooh maryam mambo?. baada ya kumsalimia lucky alimpa hi maryam.

" poa vipi deniss?.

" fresh tu naona uko na lucky kupata chai.

" Yah si unajua asubuhi hii!.

" Kweli kabisa. Uhm! Lucky nambie mbona kimya sana?.

" kivipi?.

" Ila ujue unavyofanya sii vizuri kabisa hata Mungu hapendi, kunipatia namba yako tu ni tatizo kweli?. Alisema denis maryam akawa amelisikia hilo, alijichelewesha acounter makusudi ili aangalie kitachotokea baada ya denis kusema hivyo, aliitaji kwendelea kumsoma lucky kumwangalia kiasi gani ameharibika kisaikology. Deniss alikuwa anaitaji namba ya lucky muda mrefu sana ila hakubahatika kuipata.

" Denis nakueshim nieshim, usilazimishe kitu kisichowezekana sawa friend!. Alisema lucky kwa ustarabu.

" Dah, lucky shika hii cm ebu uniandikie namba zako usiwe hivyo bhna. Mbona mwonekano wako na roo yako haviendani?. Alisema deniss akamkamatisha cm kwa kumlazimisha. Nnachoitaji ni namba yako tu sii chengine, Naomba ka hauko tayari kunipa namba yako kweli hiyo cm uipige chini ntaamini kuwa hutaki. Alisema kimasihara deniss.

" Ooooh niipige chini sio.

" Yah!, tupa chini tu ndo ntaamini kuwa hauko tayari kunipa.

" Ok. Alisema lucky kisha akaibamiza kweli chini bila kujali thamani yake, deniss aliongea kimasihara akijua hawezi, hakufahamu mtu aliemwambia hivyo akili zake ni ziro point sifuri, cm haikuwa ya bei ndogo ilivyoonekana lakini mtoto wa kike aliibamiza na chini kwa nguvu, ulibaki mshangao kwa deniss maryam nae aligeuka, mhudumu wa acounter aliacha alichokuwa anafanya akaangalia kitu kilichobamizwa na kudata.

" Ushaamini au una lengine?. Aliuliza lucky, deniss sura ilibadilika na kukaa kishari, jambo la cm yake kubamizwa chini lilimuuma sana.

" Kumbe we dem kichaa ee!. Alisema deniss, maryam alikuwa anangalia tu sura yake ikiwa imejaa mshangao.

" sina ukichaa wowote. Vichaa wote wako wanaokota makopo.

" Unaijua thamani ya hii cm hadi uitupe chini?. Aliuliza kwa hasira. Maryam aliona tayari deniss ashabadilika yanaweza kuzuka mengine, alisogea akamuomba Lucky waondoke na kumtuliza deniss kuwa wangeongea badae kuhusu cm, aliinama akaiokota, kioo chake kilivunjika vunjika ilikuwa haitamaniki.

" Maryam uache huu ugomvi haukusu, huyu dem anaijua thamani ya hii cm mpumbavu huyu, milioni moja na laki sita anauwezo wa kuilipa wakati chuoni kwenyewe anategemea mabwana wamg*nge ndo wampatie pesa za matumizi?. Aliongea matusi kumtukana lucky.

" Jamani deniss yanatokea wapi hayo mpenzi?, kwani milioni moja ni kitu gani hata zingekuwa mbili sio tatizo, tuache tuondoke mi na wewe tutaongea badae, naomba usiyakuze hivyo wakati we mwenyewe una makosa vile vile.

" kwa iyo na wewe unamtetea?.

" Sii kumtetea. We umesema kama hayuko tayari kukupa namba atupe cm chini, najua umesema hivyo kimasihara ila hukujua mwenzio atapokeaje, fanya yaishe basi deniss. Alisema maryam huku lacky akiwa anamwangalia deniss kwa jicho chungu, tusi alilomtusi lilizidi kumkolea kichwani, siku zote alizokuwa chuoni akili zake zilikuwa ni akili za kuishiwa charj mara kwa mara, sasa mtu inapotokea akamkoroga ndo kabisaaa anamfanya akili zenyewe zikose akili jumla na kuwa zaid ya mvuta bangi.

" Lucky naomba tuondoke achana na deniss.

" Ushamaliza kuongea?. Aliuliza lucky.

" kuongea nini bhana tuondoke dia?.

" nakuuliza tena ushamaliza kuongea na huyo mjinga?.

" Mimi mjinga?. Alidakia deniss.

" Tena ni malaya usiokuwa na bi*** ya nyuma hanis wa kiume wewe, unanijua vizuri au unashoboka tu kwa sababu unamuona lucky kama lucky?. Aliuliza akiwa amekunja mikono, sura yake ilionesha kiasi gani amechafuka rohoni..

" Lucky naomba usiwe hivyo tuondoke utajaza watu hapa why hivyo!?.

" Maryam naomba usinipande kichwani na wewe, niache kama nlivyo naitaji kumuonesha huyu mjinga kati yangu na yeye nani anawategemea mabwana hapa chuoni, tena yeye hategemei mabwana, anategemea wanaume wenzake wamkaze ndo apate vijisent huoni anavyojipodoa?.



" Maryam unamuona rafiki yako asivyokuwa na adabu ee!!. Alisema deniss baada ya kusikiliza maneno ya lucky.

" Eh jamaniii why hiviii lucky pliz dia tuondoke potezea why!!.. Alilalamika maryam akigonga gonga miguu chini akasogea pembeni, miaka yote hakupenda ugomvi kuushuhudia machoni mwake.

" Yani umenivunjia cm yangu bado unantusi matusi ya nguoni namna hiyo. Alisema deniss.

" Hayo sio matusi, kama ni matusi basi umeyaanza wewe...? Alisema lucky akaongea vitu vyengine ambavyo havisemeki, vilivyopelekea denis kushindwa kustahamili na kumbamiza kofi la shavu la kushoto, Lucky ndo alizidi kuvurugika hakuitaji kushindwa, bila kujali kama yuko mbele za watu alimuingia deniss mwilini, denis alijaribu kujibu mapigo huku maryam akiwaomba watu waje kusaidia, lucky alikuwa kama mwanaume, katika hangaika alifanikiwa kumlaza deniss chini na kuanza kumpa ngumi za uso za shingo na masikio, zilikuwa ngumi ngumi kweli sii ngumi za kike kike, kilikuwa kipigo cha fedheha kwa deniss hata nguvu za kujitetea hakupata, alidhani lucky laini kama wanawake wengine au kuliko wanawake wengine wa chuo kutokana na ukimya wake wa muda wote, alichezea kipigo damu zikaanza kumtoka sehemu mbali mbali usoni, watu walisogea kuamlia ugomvi lakini hawakufanikiwa kirahisi kumwondoa mwilini mwa denis lucky, alimkandika ngumi za ukweli bila kumuonea huruma, sura ilikuwa inafuja kwa hasira macho yakiwa yamefinyika.

" Huu mbona ni upumbavu mnafanyiana nyie watu tatizo ni nini hasa?. Aliuliza bwana mmoja aliekuwa na mwili wa kibabe babe aliefanikiwa kumtuliza lucky, Denis alikuwa hoi analia kama mtoto, kidume kizima kilichokuwa kinajulikaana kwa kujinyodoa chuoni hapo kilipigika vya kupigika, ilikuwa ni aibu kubwa sana kwake, watoto wa kike walijaa eneo hilo, hakuna alieweza kuamini kama ni lucky aliefanya shughuli ya kukivujisha kidume damu, wengi walijiuliza imekuwaje kwani walimzoea kwa ukimya wake.

Maryam alieleza kila kitu kilivyokuwa, baada ya ghash ghash ndefu za hapa na pale, lucky aliomba asishikwe na mtu yoyote ugomvi ushaisha, alimsogelea deniss aliekuwa ameharibika usoni.

" Boy!, usione kila dem wa chuo mkimya kimya ukahisi amelegea na unaweza kumpelekesha unavyotaka,  kaa mbali na maisha yangu na nimekwambia mara kadhaa nikome hutaki, kuyaondoa maisha yako na mimi nkatoeka kwenye dunia hii sii kitu cha kushangaza kwangu. Akili zangu ni mbili tu kichwani na nazijua mimi mwenyewe. Usiitaji nije nikupeleke kuzimu ukajuta kwa nini umezaliwa, Mamaangu tu duniani ndo nnamuheshim wengine wote vinyago, usitake kunirudisha nlikotoka wakati sitaki hata kupakumbuka, neno lolote ntalojisikia ntaongea kwa sababu hakuna nnae muogopa zaid ya Mungu, nshadata na maisha yangu na kama una uwezo nipeleke segerea mjinga wewe, umeitaji biff na mimi na nnakuapia Deniss Kokote ntapokuona iwe ndani ya chuo au nje ya chuo, Akkyamungu naapa ntakutembezea kichapo na hakuna wa kunigusa. Aliongea lucky machozi yakiwa yanamtoka kwa hasira alizokuwa nazo, kulishakuwepo umati mkubwa wa watu lakini hakujali, aliongea alichojisikia bila kuhofia, watu wenye heshima zao walifika na kumuitaji Lucky arudi chumbani kwake akatulie, mwisho alimuonesha deniss jeuri ya pesa kama yeye ndo anazoringia.

" Carefull with me deniss, i swea kama ndo hiki ulichokuwa unakitaka sasa umekipata, na kama unaringia pesa ulizonazo nakusikitikia sana, huna pesa una vijipesa, milioni moja na laki sita ni sawa na elfu moja tu kwangu, kama unashida nayo ntakupatia chek ya benk uende kutoa pesa unayotaka ukitosheka zitazobaki ziache. Usilete usupa star chuoni wakati wee ni wa kuja tu mshamba mshamba wa kijijini huko uluga ulugani..

Hakuna aliewahi kumuona lucky akiongea kiasi hicho, kilikuwa ni kindo cha kipekee huku wengi waliokuwa wanamdharau wakaweka heshima kwake, maryam nae hakutaka kuamini kama lucky anaweza kufanya vitu alivyovifanya, alijua labda ana tatizo la pesa kwao lakini ka milioni moja anaiona elfu moja ina maana ni sheedah!, walichukuana wawili hao wakatoka eneo hilo huku lucky akiwa gumzo kwa kila mmoja, Deniss maneno yalimuishia akapelekwa sehemu kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya sura yake, yote yaliyoongelewa na mtoto wa kike ni moja tu alilikumbuka kila wakati. UMEITAJI BIFF NA MIMI NA NNAKUAPIA DENISS KOKOTE NTAPOKUAONA IWE NDANI YA CHUO AU NJE YA CHUO, AKKYAMUNGU NAAPA NTAKUTEMBEZEA KICHAPO NA HAKUNA WA KUNIGUSA. 

" kaka ilikuwaje hadi dem akakubalaguza hivyo ndugu?. Kijana aliekuwa anampatia huduma kwenye chumba cha matibabu alimuuliza.

" Acha tu ndugu yangu.

" Yani umeshindwa hata kujitetea mzee ukakubali kupigika.

" Yule dem atakuwa na mishipa ya kiume, kwa sababu zile ngumi alizokuwa ananipa nlikuwa nahisi napigwa na Anold au rambo. Alisema denis kijana akaachia kicheko. Usicheke Mwita, kama hayajukukuta huwezi kujifunza, nimejifunza kutoka kwake. Ujue ukiwa una elim tofauti na yule asiekuwa na elim. Ameahidi kuweka biff na mimi ila ntamfata nimuombe msamaha yaishe.

" Yaishe au unaogopa kutembezewa kipigo kila ukionekana?. Ila wee boya sana rafiki yangu. Dem kweli anakupiga. Hata meno basi ya kumtafuna umekosa?.

" Wee nipatie huduma bhna hayo mengine potezea, najua umekalia majungu tu. Alisema kisha akakaa kimya, kijana huyo aliejulikana kwa jina la mwita aliendelea kucheka kama mazuri, haikuwa kwake pekee, hata baadhi ya marafiki wa deniss waliishia kucheka kwa lililomkumba mwenzao, Lucky alikuwa midomoni mwa watu wote walioshuhudia tukio, kibaya zaid taarifa za ugomvi zilifika hadi kwenye ofisi za juu.

Lucky na maryam walirudi chumbani kwao wakawakuta amina na tunu nao wanamalizia kunywa chai yao, hawakuwa na taarifa yoyote kuhusu ugomvi uliotokea, waliwaangalia bila kuwasemesha maryam akaingia bafuni kwa ajili ya kujimwagia maji, Lucky alipanda kitandani kwake akachukua moja ya book lililokuwa la history akaanza kujisomea, hakusoma sana alichukua laptop iliyokuwa pembeni ili kuperuzi kidogo. kitendo cha kutoka kwenda hotel kunywea huko chai japo yalitokea maugomvi kilimchangamsha mwili wake, alijihisi nae mtu katika watu mbali na siku za nyuma alizozoea kunywea chai ndani tena bila kampani yoyote, kwa alivyoonekana ni kama mtu ambae hajapigana, na hasira zake zote ziliishia huko huko chini.

Maryam alimaliza kuoga akarudi akiwa na khanga nyepesi mwilini, baadhi ya viungo vyake nyeti vilitokelezea akakaa kitandani kwa kucky, aliangalia kile anachokifanya kwenye laptop ndani ya sekunde kadhaa, alimwangalia usoni moyoni akajiuliza kitu, alidhani uenda atamuona akiwa amevimba amenuna kwa alichokifanya chini lakini wapi.

" Naona uko kwenye bloggas. Aliuliza.

" Yes mamy.

Alipomsemesha na lucky kumjibu, Tunu na Amina walimwangalia kwa jicho zito kisha wakaangaliana, walinyodoa midomo yao wakaendelea kufanya yao.

" Nna wiki sasa hivi sijapitia huko modem yangu iliharibika.

" Ooh pole ilivunjika au?.

" Hapana, kuna siku nlikuwa nafua nkasahau kama ipo kwenye mfuko wa shart nlilovaa, nlipoinama tu ikaanguka kwenye maji, nliianika lakini kumbe ilishakufa.

" Ntakupatia moja utumie nnazo mbili.

" Ntashukuru sana, jiandae basi tutoke au umeghairi?.

Alisema maryam na kuzidi kuwashtua wakina tunu waliokuwa kimya wanasikiliza mazungumzo yao.

" Mbona mapema.?

" Yes nataka nipite home mara moja, nchukue gari twende shoping na mida ya beach itakuwa inafika.

" ok poa, kwa kuwa nimekupromose siwezi kukukatalia.

" kama ungekuwa hujanipromise?.

" ningekuruka futi mia siendi?.

" Ila wewe ujue ni mtu wa ajabu lucky.

" Kwa nini?.

" Kwa yaliyotokea chini huko sikudhani kabisa kama tutaongea hivi.

" Usijali kuhusu hilo.

" Hizo ngumi umejifunza au ni za kuzaliwa nazo?.

" potezea mambo hayo. Maryam aliitaji kujua baadhi ya vitu lakini lucky akamuitaji apotezee, kuna mambo aliyaona kwa binti huyo na kumvumbua sana akili, hasa msemo wake wa usitake kunirudisha nlikotoka, moja kwa moja maryam aliamini lucky kuna maisha flan alipitia yaliyomfanya asiwe sawa kiakili..

Waliendelea kuongea taratibu huku wakiangalia newz mbali mbali kwenye mablogz na website.

" Duh huyu kaka ana sura mbaya kama usiku. Alisema maryam baada ya kuiona picha mbovu ya mtu.

" Anafaa kuwa mmeo huyu!.

" Loh!, ntampitisha wapi mimi huyu muone mdomo wake.

Alisema kisha akaachia kicheko, lucky alitabasam, hiyo ndo ilikuwa cheka yake sana sana pindi anapofurahi. alitoka kitandani akamwachia maryam laptop akaingia bafuni kwa ajili ya kuoga, ilikuwa inakimbilia majira ya saa sita kasorobo, kitendo cha lucky kuingia bafuni kiliwafanya wakina amina wainuke vitandani kwao kuongea na Maryam.





" kumbe na wewe mnafiki hivyo ee!!. Alisema amina.

" kwa nini?.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG