Simulizi : Rangi Ya Chungwa
Sehemu Ya Tano (5)
Johar alichukuliwa na yule askari na kupelekwa kwenye nyumba ya kifahari iliokuwa na kila kitu ndani, nikiwa namaanisha vitu vyote vulivyokuwa vinastahili katika nyumba. Baada ya kufika katika nyumba hiyo yule afande alimkabidhi funguo na kila kitu na kumwambia asiweze kutoka mahali pale. Johar hakuwa na uoga hata kidogo, kiukweli alikuwa amebadilika kwa kiasi kikubwa sana, hakuonekana kama hapo awali, mwili wake ulikuwa tofauti kabisa, alionekana kuwa na makovu katika mwili wake. Johar alimwahidi yule afande asingeliweza kutoka pale ndani, hakukuwa na shaka tena maana yule askari ndiye aliekuwa masimamizi wa ile kesi.
Johar pamoja na yule askari waliagana na yule askari aliondoka kuelekea kituoni kwaajili ya kazi za kujenga taifa. Johar alionekana kuwa mwenye mawazo mengi sana alionekana kujutia kwa kile alicho kifanya lakini hakutaka Dickson aendelee kuishi, machozi yalimtoka huku yakiambatana na kilio cha chini chini. Johar akiwa pale alijikuta anapitiwa na usingizi mzito na kulala pale sebleni, alijita analala muda mrefu hadi yule afande akawa amerejea na kumkuta Johar akiwa amelala pale kwenye sofa. Kwa jinsi Johar alivyokuwa amelala huku nguo yake ilio funuka na kumfanya mapaja yake meupe kuonekana, kile kitendo kilimfanya yule afande kumkodolea macho Johar na kuonekana kummezea mate.
Tamaa za mwili zikamjaa askri huyo, taratibu alianza kumsogelea Johar na kuanza kumpapasa katika mapaja yake, askari huyo ambae jina lake hakufahamika aliendeleza mchezo wake huku akizidisha na kupeleka mkono wake katima himaya ya Johar. Kabla yule afande hajafikisha mkono wake kwenye himaya ya Johar alishtukia anakamatwa mkono wake na kupigizwa chini. Lilikuwa ni jambo la ghafla lililomfanya yule askari kushtuka na kuhisi kuvamiwa, yule afande alipogeuka na kutaka kujua ni nani aliekuwa amemvamia alishangaa kumuona Johar akiwa mbele yake huku akiwa kama mtu asiye jielewa.
"Mshenzi mkubwa wewe, huna hata haya. Muone vile jitu kubwa lakini hakili hakuna, ulifikiri kila mwanamke ni dhahifu kama wewe. Tena naomba ujiangalie usifikiri kila mmoja ni mpumbavu kama ulivyo wewe"
Aliongea Johar kwa hasira huku akimtizama yule askari kwa ghadhabu. Yule afande hakutaka kuamini kama kile kitendo, hakuamini kama Johar angekuwa na uwezo na nguvu kama zile. Kile kitendo kilimfanya yule askari kukaa muda mrefu akimtizama Johar asipate jibu la kile kilichokuwa kimetokea.
"Hivi wewe unajua unaongea na nani, na unajua ni kitu gani kina kukabili mbele yako. Unaelewa kesi yako inagharimu vitu gani ili isiendelee, embu acha ujinga, na endapo ukajifanya mjuaji nitaweka kila kitu wazi maana mimi pekee ninaejua kuwa wewe ni muhusika wa lile tukio. Na ninavyoongea sasa hivi wazazi wote wawilibwa Dickson wameppteza maisha na msababishaji ni wewe"
Yale maneno yalimshtua sana Johar na kumfanya kurudi kwenye kochi taratibu, roho yake ilimuuma maana aliwauwa watu wasiokuwa na hatia Machozi yalimtoka na kuhisi mkosaji, nia yake kubwa haikuwa kuwauwa wazazi wa Dickson. Nia yake kubwa ilikuwa ni kumuuwa Dickson. Yule afande alipoona Johar analia alimsogelea na kuanza kumbembeleza huku akijaribu kumfuta machozi. Yule askari alipoona Johar akiwa analia ndipo alipopata chanai ya kumshika Johar na kuanza kumtomasa katika mwili wake.
Ile hali iliendelea huku Johar akiwa anajaribu kujizuia kwa yule askari lakini alipokumbuka tukio alilolifanya alijikuta anakuwa mpole na kumuacha yule askari afnye alichokuwa akitaka kukifanya. Johar alikuwa tayari kufanya chochote na yule askari ilimradi kesi yake ifutiliwe mbali.
"Kweli utanisaidia?" Johar alimuuliza yule askari kwa sauti ya mahaba huku askari huyo akiwa kwenye hisia kali za mapenzi kwa Johar, Sauti za kibahaba ndizo zilizo sikika, huku mihemo ya hapa na pale ikiwa imechukukua nafasi yake. Baada ya dakika kadhaa Johar pamoja na askari huyo walijikuta kwenye tendo la kuzini. Baada ya yule askari kumaliza alimchukua Johar na kwenda bafuni kwaajili ya kukoga, kwa jinsi walivyokiwa walionekana kama wana ndoa wa muda mrefu. Waliingia bafuni na kukoga kisha kurudi sebleni ambapo waliweza kupata chakula cha jioni ambacho alikuja nacho askari huyo. "kwa jina naitwa Fabiani wengi hupenda kuniita Fb kutokana na kifupi cha jina langu"
Alijitambulisha askari huyo huku akimtizama Johar usoni, yule askari alibaki akitazama uzuri wa Johar na kushindwa kuelewa nini kilichokuwa kinamsibu yeye kufanya mambo kama yale ya mauaji. "Johar kwani Dickson alikukosea nini mpaka ukaamua kumfanyia kitu kama kile?" Yule askari aliejitambulisha kwa jina la Fabian alimuuliza Johar na kumfanya Johar kunyanyua uso wake na kumtizama Fabian, Johar alionekana kuchukizwa na lile swali ila hakutaka kuonyesha wazi wazi kwa yule askari, alibaki akimtizama askari huyo huku akiwa anafijiri amwambie nini askari huyo. "Johar naomba usinifiche maana nipo hapa kwaajili ya kukusaidia, ila kama hutohitaji msaada wangu uniambie tu, maana kila ninacho kuuliza hutaki kunijibu sijui kwa nini?" Alilalamika askari huyo huku akijaribu kumwambia Johar aweze kumwambia ukweli hadi akaamua kumfanyia ukatili kama ule Dickson. Kimya kilitawala kwa dakika kadhaa huku Johar akiwa ameinamisha kichwa chake chini, alionekana kuwaza vitu vingi katika akili yake.
Baada ya muda kidogo alinyanyuka na kutaka kuzungumza chanzo cha yeye kufanya yale. Kabla hajatamka neno lolote walisikia kengele ya getini ikilia, ndipo yule askari aliponyanyuka na kwenda kungalia kwenye camera za CCTV na kugundua aliekuwa akitaka kufunguliwa alikuwa ni mzee Tarimo. Askari huyo alielekea getini na kumfungulia mzee Tarimo na kumkaribisha kwa heshima. Johar alipogindua ni Baba yake aliekuwa akiingia alijifuta machozi yake na kuachia tabasamu hafifu katika uso wake, mzee Tarimo alipomuona mtoto wake alionekana kuwa na furaha na kuachi tabasamu mwanana.
"Johar mwanangu unaendeleaje?"
"Naendelea vizuri Baba"
"Nimeona nisiende kulala kabla sijakuona mwanangu, hata hivyo mimi sikai sana maana muda nao unakimbia, na kama unavyojua Mama yako atakuwa amenisubiri sana"
Baba yake na Johar alinyanyuka ili kuweza kuondoka maana alihisi mkewe angelikuwa mpweke sana nyumbani. Mzee Tarimo aliponyanyuka Johar alitaka kumwambia kitu Baba yake lakini hakuweza kuzungumza mbele ya yule askari na ndipo walipoagana na Baba yake kisha mzee Tarimo akaamua kuondoka.
Mzee Tarimo alitoka pale ndani huku akimuaga Johar kwa tabasama zuri na lenye kuonyesha kumjali. Baada ya Mzee Tarimo kuondoka yule afande alianza kumsogelea Johar na kuanza kumshika shika, kile kitendo kilimkera sana Johar na kumfanya kujawa na hasira nyingi lakini licha ya kutokipenda kile kitendo bado hakuweza kumzuwia yule askari kutomfanyia kitendo kile, alijua endapo angenkatalia askari huyo angeliweza kupata matatizo makubwa juu ya kesi yake iliokuwa ikimkabili. Askari huyo alieonekana kuwa na hisia kali za kimapenzi juu ya Johar. Baada ya dakika chache wakawa kitandani wote wawili, Johar alikuwa kama ameolewa na yule askari maana kila alichokuwa anaambiwa alikuwa akikifanya. Wakati mwingine yule askari aligundua kuwa Johar hakuwa anapenda kufanya kitendo kama kile, ila kutokana na tamaa za kimwili za askari huyo alijikuta anafanya mapenzi na Johar kila alipokuwa anahitaaji. Johar hakuweza kumzuia wala kumkatalia, hadi ikafika wakati Johar akawa amekwisha kuzowea hali ile.
***********
Dickson hali yake ilikuwa mbaya sana huku siku zikienda, baada ya wazazi wake kupoteza maisha na kukaa kwa muda mrefu bila kufanyiwa maziko ndipo Hospital ilipoamua kuchukuwa jukumu la kuwazika bila Dickson kufahamu. Hali ya Dickson ilikuwa ikibadilika kila wakati, hakuwa na uwezo wa hata kuvuta pumnzi, mipira iliopitishwa katika pua zake ndiyo iloomuwezesha kuendelea kuwa hai. Baada ya wiki mbili kupita hali ya Dickson ilianza kuonyesha matumaini, alionekana kupumua yeye mwenyewe bila uwezo wa mashine. Siku chache mbele Dickson alikuwa katika mazoezi ya kimwili kutokana na mwili wake pamoja na mifupa yake ambayo hapo awali alionekana kupata matatizo makubwa katika mwili wake. Mazoezi yaliendelea huku yakisimamiwa na baadhi ya madaktari wakubwa pale hospital, wiki mbili mbele Dickson akawa anauwezo wa kutembea mwenyewe bila msaada wa mtu yoyote, ile hali iliwafanya baadhi ya madaktari kufurahi sana maana walijua kupona kwa Dickson kungewaletea sifa kubwa katika hospital yao.
"Dickson kwa sasa unaionaje hali yako?"
"Naendelea vizuri na namshukuru Mungu pamoja na madaktari walioweza kunisaidia. Baba pamoja na Mama mbona sijawaona toka nilipona au wamehamishwa hospital?" Dickson alimuuliza Nesi aliekuwa akiongea nae, yule Nesi alipoulizwa lile swali alionekana kupata wasiwasi na kuanza kutizama chini. Hakuwa tayari kumwambia Dickson kuhusu kifo cha wazazi wake bila idhini ya Dokta mwenyewe. Yule Nesi alikaa kimya kwa muda huku akiwa anamwangalia Dickson kwa jicho la huruma, ile hali ilimfanya Dickson kushindwa kuelewa ni kwanini yule Nesi alikuwa akimwangalia kiasi kwa namna ile. "Wanaendelea vizuri kabisa, wao waliwahi kupona maana hawakuumia sana" Alimjibu yule Nesi baada ya kumuona Dickson anamkodolea macho, yule Nesi alikuwa akiongea kwa kubabaika na kumfanya Dickson kujiuliza maswali mengi juu ya yale majibu ya yule Nesi.
Yule Nesi alipoona maswali yale yalikuwa yakimshinda aliamua kuondoka huku nyuma akimuachia Dickson maswali mengi. Dickson alionekana kuwa na mawazo mengi sana na kuhisi yule Nesi alikuwa anamdanganya na kuhisi hali ya wazazi wake pengine ingalikuwa mbaya. Dickson hakutaka kukaa kimya ndipo alipoamua kumfuata Dokta aliekuwa akimuuguza kwaajili ya kumuuliza juu ya wazazi wake. Alipoingia katika chumba cha Dokta alikuta kulikuwa na wagongwa wawili ambae walionekana kama mtoto pamoja na Mama yake, ilimlazimu Dickson kusubiri nje ya ofisi ya Daktari huyo. Baada ya dakika chache mbele wakawa wametoka na Dickson akawa ameingia kwenye ofisi ya huyo Dokta.
"Dokta wazazi wangu wanaendeleaje maana sijawaona toka niweze kuwa na hali nzuri ya kiafya?"
Aliuliza Dickson Baada ya kuingia katika ofisi yake. Lile swali hata yule Dokta lilimfanya kuduwaa kwa muda na kushindwa kuongea na kubaki akimtizama Dickson kwa macho ya huruma kama yule Nesi. Dickson alishindwa kuelewa nini kilichokuwa kinaendelea, yule Dokta alimuonea sana Dickson huruma maana alijua Dickson hakuwa na ndugu yeyote zaidi ya wazazi wake. Alijua kupoteza maisha kwa wazazi wake kungekuwa ni kovu lisilo futika, licha ya kufahamu hayo bado alihitajika kumwambia ukweli juu ya wazazi wake. "Dickson naomba unisikilize kwa makini na unielewe, kwanza kabisa wewe ni mtoto wa kiume unatakiwa kujikaza kwa hili lililo tokea" Maneno ya yule Dokta yalimfanya Dickson kutoa macho na kubaki kama aliekuwa amepigwa na butwaa. Yale maneno yalimfanya Dickson kushindwa kuelewa yule Dokta yule Dokta alikuwa na maana gani kumuambia maneno kama yale.
Dickson aliweka masikio yake sawa ili kumsikiliza yule Dokta kile alichotaka kukizungumzia.
"Wakati upopata ile ajali wewe pampja na wazazi wako mlikuwa na hali mbaya sana, hakuna hata mmoja aliekuwa anajitambua. Mlipofikishwa katika hospital yetu tuliwapokea wote na kuwapeleka kwenye chumba cha wagonjwa nahuti huti, kiukweli mtu aliekuwa na hali mbaya kuliko wote alikuwa ni wewe, kila aliekuona alijua wewe hutoweza kupona. Tukija kwa upande wa wazazi wako hali zao hazikuwa mbaya sana japo walionekana kuwa wenye maumivu makali sana. Naweza kusema Mungu ni waajabu sana maana wazazi wako walipona kabla yako lakini sijui nini kiliwakuta maana siku mbili baada ya kupona taarifa zilifika hospitalini hapa kuwa wazazi wako wamezidiwa na kupoteza maisha"
Yale maneno haya kumwingia Dickson katika akili yake aliona yule Dokta kama alikuwa anaota, hakutaka kuamini kitu kama kile.
Yale maneno yalimfanya Dickson mwili wake kutokwa na jasho jingi, macho yake yalionekana kulegwa legwa na machozi. "Dokta naomba kuwa siriazi na unacho kizungumza maana unavyoongea kama kweli, embu niambie wazazi wangu wapo wapi" Dickson aliuliza huku akiwa hataki kuamini kile alichokuwa anaambi na yule Dokta. Yule Dokta aliyatambua maumivu ya kupoteza wazazi, lakini hakuwa na chakufanya zaidi ya kumwambia ukweli Dickson kwa kile kilichotokea.
Yule Dokta alishindwa kumficha Dickson aliona kama angefanya vile angeliweza kuja kumsababishia matatizo mbeleni, hakuwa na kingine alichoamua alimtolea picha mbili zikiwa zinaonyesha watu wawili wakiwa katika jeneza, zile sura alizoziona Dickson zilimfanya kushtuka na kutaka kuanguka. Picha ya kwanza ilikuwa ni ya Mama yake akiwa katika jeneza, picha ya pili ilikuwa ni ya Baba yake nae akiwa katika jeneza huku pamba zikiwa ndani ya pua zao. Dickson alihisi kuchanganyikiwa kwa kile alichokuwa amekiona, hakuamini kama wale waliokuwa kwenye ile picha ni wazazi wake, alihisi kizungu zungu na kuziachia zile picha chini huku na yeye akizifuata zile picha na kuanguka chini.
Yule Daktari alimuwahi na kumpandisha katika kitanda ambacho kilikuwa pale ofisini kwake, yule Dokta alimuonea huruma sana, machozi yalimtoka na kumsikitikia Dickson. Yule Dokta alipompandisha Dickson pale kitandani alitoka na kuelekea katika chumba kingine katika ile hospital, alipoingia katika chumba hicho alionekana kushtuka na baada ya kuingia katika chumba hicho. Juu ya kitanda kilichokuwa katika chumba hicho kulikuwa na mtoto mdogo amelala huku pembeni kukiwa na karatasi dogo likiwa na ujumbe.
Yule Dokta aliamua kusogea karibu na yule mtoto na kuchuku lile karatasi. Lilikuwa ni karatasi lililokuwa na maneno machache lakini yale maneno halionekana kumshtua yule Dokta na kumfanya azunguke kwenye chumba hicho huku akiwa anaita jina la Angely. Bila shaka Angely aliekuwa akitajwa alikuwa ni mpenzi wa Dickson, kile kitendo cha kuita kwa sauti kikapelekea yule mtoto aliekuwa amelala kuamka na kuanza kulia. Yule Dokta aliamua kumfuata yule mtoto na kumbeba ili kumfanya asiweze kulia, akiwa pale alichukua simu yake na kubonyeza vitufe kadhaa kisha kuiweka simu yake katika sikio la kushoto, sekunde chache mbele maongezi yalianza huku sauti ya upande wa pili ikiwa inasikika kwa shida.
"Naombeni mumtafute Angely maana katoroka hospital na kama mnavyojua yupo kwenye hatihati za kuuwawa. Akikisheni mnampata. Sawa?"
Aliongea Dokta huyo kisha kuirudisha simu yake mfukoni na kuendelea kumbembeleza mtoto, fakika chache mbele mtoto akawa amelala. Yule Dokta alitoka taratibu na kwenda ofisin kwake, alipotoka yule Dokta kumbe Angely hakuwa ametoroka alikuwa uvunguni mwa kitanda alichokuwa amelala mwanae, Angely alipotoka alimchukua mtoto wake na kumuweka mgongoni na kujifunika kichwani na kuanza kutoka katika chumba kile.
Alipotoka alianza kutafuta mlango wa kutokea katika ile hospital ili ikiwezekana kuondoka kabisa, alipokuwa anapita aliweza kumuona yule Dokta anakuja kule alipokuwa ana tokea, alipomuona yule Dokta alificha uso wake na kupishana na yule Dokta bila kujuwa.
Yule Dokta alikuwa anarejea kule chumbani kwaajili ya kwenda kumchukua yule mtoto, alipofika mlangoni alikuta mlango upo wazi, alishangaa maana mlango wakati alipokuwa anatoka aliufunga. Kile kitendo kilimpa wasiwasi na kupata hofu na kuhisi pengine mtoto hayupo salama, aliamua kuingia ndani ilikwenda kumwangalia mtoto. Baada ya kuingia ndani alishangaa sana kukuta kitanda kipo wazi.
Yule Dokta alipigwa na butwaa, alizunguka chumba kizima lakini bado hakiweza kumuona yule mtoto, aliamua kutoka nje na kwenda kuwauliza manesi kama wamemuona mtu aliechukua mtoto yule. Yule Dokta aliamini aliemchukua yule mtoto si mama yake, maana kitu kilichomfanya asiamini ni pale alipokuta ule ujumbe wa kuondoka kwa Angely huku akiwa amemuacha kitandani. Kila aliekuwa anamuuliza alionekana kutotambua kitu chochote juu ya Angely pamoja na mwanae.
Akiwa kwenye harakati za kumtafuta Angely aliitwa na kuambiwa kulikuw na mgonjwa mwenye hali mbaya hivyo alikuwa nahitajika kwa haraka, hakuwa na budi maana ilikuwa ni wajibu wake. Aliondoka haraka haraka kuwahi kule alipokuwa anaitiwa, akiwa anatembea haraka haraka bila kuangalia vizuri alijukuta anmpamia michana aliekuwa amefunika uso wake na kumfanya msichana huyo kuanguka chini huku kile kitambaa alichokifunika usoni kikiwa kimeanguka na kumfanya uso wake kuonekana. Alikuwa ni Johar yule Dokta alimfahamu vizuri Johar na alifahamu Johar ndiye aliemfanyia ukatili Dickson na kutaka kumuuwa Angely pamoja na mwanae.
Bila kuchelewa yule Dokta alimrukia Johar na kumdhibiti kwangu zote huku akiwa anajaribu kuita walinzinwa hile hospital kuja kumsaidia, kabla walinzi hawajafika Johar alijivingirisha kwa nguvu na kumkanyaga yule Daktari kifuani na kumfanya yule Dokta kuanguka chini. Kabla yule Dokta hajanyanyuka alishtukia anakabwa katika shingo yake huku akipigwa ngumi za vichwa. Maumivu aliokuwa anayasikia yule Dokta alijikuta anaomba msamaha bila kurajia, alishangaa ni nguvu gani alizokuwa anatumia Johar hadi kumdhibiti bila kupata jibu.
Akiwa anaomba msamaha huku akiwa anaugulia maumivu ya ngumi alizopigwa na Johar alishtukia anapigwa nyuma ya shingo ngumi nzito na kumfanya kuanza kuona kiza hatimaye alipoteza fahamu. Johar hakutaka kupoteza muda aliondoka pale haraka haraka kuelekea ofisini kwa yule Dokta kwaajili ya kwenda kummaliza Dickson, ambae kwa wakati huo alikuwa amepoteza fahamu kutokana na taarifa za kupoteza maisha kwa wazazi wake. Johar alipofika mlangoni kwa Dokta aliangalia pande zote mbili kama kuliku namtu, alipoangalia hakufanikiwa kuona mtu ndipo alipoamua kuingia kule Dickson alipokuwa.
Alipoingia ndani ya ofisi ya Dickson alimkuta Dickson akiwa amelala juu ya kitanda huku akiwa hajitambui. Nia ya Johar ilikuwa ni kummaliza Dickson, Johar hakutaka hata kumuona Dickson. Hakuna aliekuwa anatambua sababu za msichana huyo kufanya vitendo kama vile vya kinyama angali akiwa ni mtoto wa kike. Bila kuchelewa Johar alitoa box dogo ambalo lilikuwa na sindano ndogo huku kukiwa na kichupa kidogo kikiwa kina mfano wa dawa japo haikujulikana ni dawa ya namna gani. Alichukua ile sindano haraka haraka na kuitumbukiza katika kile kichupa na kukifonza hadi bomba ya ile sindano. Baada ya kuona amefyonza kiasi cha kutosha alimsogelea Dickson kwaajili ya kumchoma. Johar alidhamiria kwa moyo wake wote, alionekan kutokuwa na shaka wala wasiwasi juu ya kile alichokuwa anataka kukifanya.
Akiwa anataka kumchoma ile sindano ambayo haikujulikana ilikuwa na madhara gani alishtukia mlango wa pale ofisini unafunguliwa. Johar aligeuka kwa haraka ili kujua ni nani aliekuwa ameingia pale ofisini, alipogeuka alishangaa kumuona Angely mtu ambae alikuwa anamtafuta kwaajili ya kumuuwa kwa muda mrefu, Johar alishtuka na kubaki akimtizama asijue Angely alifuata kitu gani. Angely mkononi mwake alikuwa ameshikilia kisu, Angely alionekana kumchukia sana Johar huku Johar nae akionekana kumchukia sana. Angely hakutaka kumuonea huruma Johar aliondoka kwa kasi ili kwenda kumchoma Johar na kile kisu alichokuwa amekishikilia mkononi. Kabla hajamfikia Johar alishangaa Johar anamrushia kile kichupa chenye dawa usoni kwaajili ya kumzubaisha ili kuweza kumtaiti, lakini kile kitendo Angely alikiona na kukikwepa na kufanya kile kichupa kuanguka chini na kupasuka.
Kabla Angely hajasogeza hata mguu tayari Johar alikuwa karibu yake na kurukia na kumfanya kuanguka chini. Johar alionekana kuwa nguvu nyingi tofauti na Angely ambae alioneka kurusha rusha miguu kama kuku aliekuwa anataka kukata roho. Johar kutokana na zile purukushani za yeye pamoja na Angely alijikuta anamchoma ile sindano Angely, kile kitendo cha ile sindano kumchoma Angely kwa dakika chache Angely alianza kubadilika mwili wake na kuanza kubadilika rangi na kuwa mweusi kama mkaa. Kilikuwa ni kitendo cha sekunde kadhaa Angely alikuwa siyo yule Angely wa mwanzo, kile kitendo kilimshangaza hata Johar na kumfanya abaki mdomo wazi. Alionekana kutokuamini kile kilichotokea japo yeye ndiye aliemchoma, lakini kwa kitendo kile kilimshtua sana.
Alijikuta anamwangalia Johar alivyobadilika rangi yake ya uweupe na kuwa mweusi, huku akionekana kutokwa na moshi katika mwili wake. Hakujua ile ilikuwa ni simu ya namna gani ya kumfanya mtu kuwa kama alivyokuwa Angely. Akiwa anazidi kumshangaa Angely alisikia sauti nje ya ile ofisi huku wakiwa kama watu waokuwa wanajibizana, aligeuka kwa haraka na kuanza kumsogelea Dickson ili kummaliza maana sindano aliokuwa anahitaji kumchoma Dickson alimchomea Angely, alipomfikia Dickson alichomoa kisu kidogo na kukikamata kwa nguvu kwaajili ya kumchoma Dickson. Akiwa tayari kumchoma Dickson alishtukia mkono wake unakamatwa na kumfanya ashangae sana, alipotupa macho kuangalia ni nani aliekuwa amemkamata mkono wake alishangaa sana.
Alikuwa ni yule Dokta aliempiga nje muda siyo mrefu na kumpiga hadi kumfanya apoteze fahamu. Johar alistaajabu na kubaki akimtizama yule Dokta asijue ameingiaje pale ndani bila yeye kusikia, kile kitendo kilimfanya Johar kuduwaa bila kijua yule Dokta alikuwa na nia ya kumkamata. Johar alishtukia yule Dokta anamnyanganya kile kisu kwa haraka na kuruka na kumzunguka kwa nyuma huku mkono wake wa kushoto ukiwa kwenye shingo ya Johar, Johar alibaki ameduwaa maana hakutegemea kitu kama kile. Yule Dokta alimshikia Johar kile kisu huku akiwa bado amemshikilia kwa nguvu katika shingo yake. Wakati hayo yote yanaendelea Dickson alikuwa bado hajitambui, alikuwa kama mtu aliekuwa kalala usingizi mzito.
Yule Dokta alimdhibiti Johar kwa nguvu hadi kumshinda na kufanikiwa kumumfunga na kamba za pazia kwenye ofisi yake. Johar alijitahidi kujitoa lakini yule Dokta alimfunga kwa nguvu hivyo haikuwa rahisi kujitoa pale.
"Msichana mdogo kama wewe unakuwa na roho ya kinyama namna hiyo, unajua hadi sasa siamini kama kweli wewe ndiye uliefanya mauaji ya kama haya. Kwa mfano ulipo muuwa huyu msichana wa watu ambae hana hatia umefaidika na nini?"
Aliongea yule Dokta kwa hasira huku akimpiga Johar mateke ya miguu, yule Dokta alionekana kutoamini kama msichana kama yule angeweza kufanya unyama kama ule.
"Kwa usalama wako bora ukimbie au uniachie maana naionea huruma familia yako itakapo kukosa wewe angali ikiwa inakutegemea wewe, sinanii nipo siriazi kwa ninachokisema"
Aliongea Johar kwa sauti ya kujiamini na kumfanya yule Dokta kucheka sana. "Wakukusikitikia ni mimi au wewe, sio kila mtu ni wakumtisha kipuuzi au kumpiga mkwara wa kitoto kama huo. Eet Bora ukimbie! Mimi wakukukimbia wewe embu jiangalie kwanza kisha ufananishe na hayo maneno yako" Yule Dokta alimjibu Johar huku akitamani kummeza kwa jinsi alivyokuwa na hasira nae. Johar hakuonekana kuogopa chochote, japo alikuwa amefungwa lakini bado hakuwa na uoga wa aina yeyote, hata yule Dokta alishangaa sana na ndipo alipoamua kuchukua simu yake kwaajili ya kuwapigia polisi ili kuja kumkamata Johar. "Waambie waji na zima moto maana muda siyo mrefu hapa pata teketea kwa moto" Aliongea Johar kwa sauti ya juu na kumfanya yule Dokta kumkanyaga teke la tumbo, Johar alionekana kupata maumivu makali sana.
Baada ya yule Dokta kumaliza kuongea na simu alimsogelea Johar na kuanza kumpiga piga. "Mimi sina tatizo na wewe ila kwa hiki ulichokifanya wacha sheria ichukue nafasi yake. Ingekuwa mimi ndiye hakimu sijui ningekupa adhabu gani, kwa kitendo hichi cha kumkausha mwenzako bila hata huruma" Yule Dokta alikuwa ni mwenye hasira sana kwa kile alichokuwa amekishuhudia kwa macho yake. "Angalia nyuma yako alafu uone kati yangu mimi na wewe nani mjinga" Yalikuwa ni maneno ya Johar yaliomfanya yule Dokta kushindwa kuelewa Johar alikuwa anamaanisha nini kumwambia vile, yule Dokta alimwangalia Johar kwa hasira na kuhisi Johar anamletea utani angali hapakuwa na hata chembe ya utani. Alinyanyua mkono wake ili kumpiga Johar lakini kabla ili ngumi haijamfikia Johar alishangaa anapigwa anakamatwa mkono wake, alipogeuka kutizama nani aliekuwa anamzuwia alishangaa sana kukuta ni Dickson.
Yule Dokta alibaki ameduwaa sana baada ya kumuona Dickson, yule Dokta hakutarajia jambo kama lile. Alimwangalia Dickson bila kupata jibu kamili, alivyotazama kitandani ambapo Dickson alikuwa amelala alishangaa zaidi maana Dickson alionekana kuwa kitandani. Kile kitendo kilimuogopesha sana yule Dokta na kushindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. "Nilikwambia mapema ila hukutaka kunisikia, unafikiri msamaha wangu unarudi mara mbili. Sisi ukiambiwa kitu mara moja usipokiteketeza utakuwa kwenye hali mbaya" Aliongea Johar huku akiwa pale chini, alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote. Alionekana kujiamini kupita kiasi, hakuwa na utani hata kidogo. "Wewe si ndiye ulienifunga? Sasa njoo nifungulie mwenyewe, maana haitakuwa na maana kama watakuja nifungua watu wengine ambao hawahusiki na hili jambo"
Aliongea Johar kumtaka yule Dokta kumfungulia, ilikuwa kama igizo flani ni kwa jinsi Johar alivyokuwa anaongea. Yule Dokta alibaki ameduwaa huku akiwa anamtizama Dickson ambae kwa wakati huo hakutambua Dickson amekuwaje, maana alishindwa kuelewa tofauti ya wale watu wawili. Akiwa kwenye mawazo hayo alishangaa kumuona Dickson aliekuwa kitandani akiwa nae anaamka, Dickson alipoamka alishangaa sana kumkuta Dokta amekamatwa na mtu aliekuwa anafanana na yeye. Alipoangalia chini alifanikiwa kumuona Johar akiwa chini huku akiwa amezungushiwa kamba. Kile kitendo cha Dickson kumuona Johar pale chini kilimfanya kichwa chake kumuuma, alionekana kupatwa na hasira kali kuliko simba mwenye njaa kali. Kitu ambacho kilimshangaza na kumfanya kushangaa sana Dickson ni kumuona yule mtu aliekuwa anafanana nae, yule Dokta aliweza kumtambua Dickson wa kweli baada ya kumuangalia yule aliekuwa amemkamata katika shingo yake, na ndipo alipogundua kuwa alikuwa na sura ya bandia ikiwa inafanana kabisa na sura ya Dickson.
Yule Dokta alifanya kama alivyoo ambiwa kwenda kumfungua Johar, alianza kupiga hatua za taratibu kwenda karibu na Johar kwenda kumfungu kama alivyokuwa ameambiwa, huku akiwa anatambua vizuri Dickson wa kweli ni yupi. Dickson alipomuona yule Dokta anamsogelea Johar alinyanyuka huku akiwa anahasira kumfuata Johar. Kabla Dickson hajanyanyua mguu wake alishtukia ana tokea mtu mwingine akiwa na sura kama Dokta na kumshika Dickson. Dickson alibaki ametoa macho huku akishindwa kuelewa nini kilichokuwa kinaendelea, kila mmoja alionekana kuonyesha mshangao kwa kile kilichotokea. Kimya kilitawala huku kukionekana kuwa na watu wawili wawili wenye kufanana, kile kitendo kilimchanganya sana Dickson na kumfanya kuhisi kuchanganyikiwa. Dickson hakuweza kutambua chochote juu ya wale watu maana walionekana kufanana huku wakiwa na nguo zilizo fanana, ila Dokta alilitambua lile jambo maana yeye alizitambua sura bandia kutokana na yeye kuwa Dokta na mwenye kutambua vitu kama vile Dickson feki alikwenda kumfungua Johar pale alipokuwa amefungwa na kumnyanyua.
Akiwa ananyanyuka ndipo Dickson alipoangalia chini na kuona mwili wa Angely ukiwa umebadilika rangi na kuwa mweusi.
Dickson alishtuka baada ya kumuona Angely akiwa pale chini, kile kitendo kilimpa wasiwasi sana Dickson na kubaki anauangalia mwili wa Angely. Dickson alimsogelea Angely huku machozi yakiwa yanamtoka, hakuweza kuamini macho yake alilia kama mtoto mdogo. Hakufikiria kama na Angely angemuacha kama walivyomuacha wazazi wake. Kiukweli mwili wa Angely ulikuwa unatisha, kwa jisi ulivyokuwa haukutamanika. Dickson alivyotaka kuushika mwili wa Angely yule Dockt alimuwahi na kumshika ili asiweze kuushika maana angeliweza kujilete matatizo baadae kwa polisi. Wakati yule Dokta anamzuia Dickson Johar alitoa Bastola ili kumpiga Dickson. Lakini kabla hajafyatua alishtukia anaanguka chini huku akiwa anatokwa na damu nyingi katika bega lake la kulia, ndipo Dickson pamoja na yule Dockta alivyogeuka na kukuta Johar akitokwa na Damu nyingi. Wakiwa wanashangaa walishtukia polisi wakiwa wameingia huku wakiwa na bunduki zao. wale polisi walipoingia walishangaa sana baada ya kuona watu wakiwa wanafanana.
Kile kitendo kiliwachanganya sana bila kupata majibu, waliendelea kufikiri wafanye nini, wakati wanajiuliza kumbe mmoja kati ya wale waliokuwa na sura za bandia alikuwa anajisogeza karibu na ile bastola. Kilikuwa ni kitendo cha haraka kwa yule mtu maan aaliweza kuichukua ile bastola kwa haraka na kumwelekezea Dickson. Mtu wa kwanza kuona lile jambo alikuwa ni Dokta. Yule Dockta alivyoona vle alimsukuma Dickson ili kuweza kuanguka chini, lakini akati anamsukuma aijikuta anachelewa kufika chi na kujikuta anapigwa na ile bastola katika mgongo wake na risasi kutokea upande wa pili. Baada ya yule Dockta kupigwa risasi ndipo na polisi walivyo shtuka na kumwelekezea yule aliempiga Dickson bunduki zao. Dickson alishtukia damu nyingi ziki miminika katika mwili wake huku mwili wa Dokta ukiwa juu yake.
Yule Dockta alimwangalia Dickson kwa huruma sana na kutaka kuzungumza jambo lakini alishindwa, hali yake ilionekana kuwa mbaya sana, damu nyingi zilimtoka na baada ya muda kidogo kimya kilitawala. Wale polisi walishindwa kuelewa Dickson wa kweli ni yupi ndipo walipowakamata wote na kwaajili ya mahojiano. Mtu aliekuwa anagundua ile siri alikuwa ni yule Dockta ambae kwa wakati huo hakujulikana kama alikuwa hai au amekufa. Mwili wa Dokta pamoja na Angely ulitolewa na kuingizwa kwenye chumba cha wagonjwa mahuti huti huku mwili wa Angely ukiwa unaelekezwa mochwari.
Dickson alibaki akiwa anatokwa na machozi mengi hku uzuni ikiwa imemtawala. Alimtizama yule mtu aliekuwa na sura kama yakwake kwa hasira na kutamani kumrukia na kumtafuna, lakini hakuweza kufanya hilo maana polisi walikuwa nyuma yao huku wakiwa na silaha za moto. walichukuliwa wote hadi kituo cha polisi, baada ya kufikishwa kituoni walipelekwa moja kwa moja katika ofisi ya mkuu wa kituo hicho. Mkuu wa kituo hicho alishangaa sana baada ya kuwaona Dickson wakiwa wawili huku pembeni akionekana dokta ambae alimtambua vizuri. mkuu wa kituo kile alibaki amedwaa na kubaki akiwa anawashangaa..
Lilikuwa ni jambo la kushangaza, yule mkuu wa kituo alishindwa kuelewa yupi mkweli kati ya Dickson wa kweli na Dickson bandia. Dickson alifahamika vizuri kutokana na kazi yake, pia alifahamika kama hakimu japo yeye alikuwa kama mwanasheria katikakesi mbali mbali. Karibia vituo vingi vya polisi na mahakama nyingi Dickson alitambulika.
Kimya kilitawala huku mkuu wa kile kituo akiwa anajiuliza maswali mengi katika akili yake. Akiwa pale simu ya Dckson iliita ndipo yule mkuu wa kituo akaomba ile simu aweze kuipokea. Baada ya yule mkuu wa pale kituoni kupokea alirudisha simu katika sikio la Dickson huku akimwambia Dickson aongee na ile simu.
"Usijifanye mjanja, najua unatambua huyo alioko pembeni yako si Dickson wa kweli. Cha muhimu fanya juu chini hao wasalimike la sivyo mwanao wa pekee nitamuuwa kikatili kuliko mama yake"
Ni sauti ya msichana iliosikika baada ya Dickson kuwekewa simu katika sikio lake. Yalikuwa ni maneno ya kutisha, yale maneno yalionekana kumwingia vizuri Dickson na kumfanya kutoa macho kama mtu aliekuwa anataka kukata roho. Kile kitendo kilimshitua hata yule mkuu wa kituo, na kumfanya kumkodolea macho Dickson ambae kwa wakati huo alikuwa kama mtu asiejitambua. Ile sauti Dickson aliitambua vizuri, na alijua aliekuwa anatamka yale maneno alikuwa ni Johar. Dickson alionekana kuogopa sana kwa yale maneno aliokuwa ameambiwa. Alishindwa kuelewa Johar amewezaje kutoka pale hospital ambali alikuwa mwenye hali mbaya, alifikiria jinsi johari alivyokuwa na kuaanza kumfananisha na yule aliemuona kule hospital.
Alipokumbuka vizuri ndipo alivyoanza kuhisi yule aliekuwa kule hospital si Johar, alishindwa kusema neno lolote na kubaki akitokwa na machozi. Yule mkuu wa kituo aliweza kugundua kitu lakini alionekana kutokuwa na huakika na kile alichokigundua.
Upande wa mzee Tarimo pamoja na mkewe waliendelea kuwa na aman huku wakiwa wanaamini mwanao anaendelea vizuri. Wakiwa nyumbani kwao ikiwa ni asubuhi simu ya mzee Tarimo iliita huku ikiwa ni namba ngeni katika simu yake, baada ya kuangalia na kukuta ni namba ngeni aliipuuzia na kuendelea na mambo yake, simu iliendelea kuita kwa muda na baada ya muda ilikata. Baada ya simu kukata mzee Tarimo aliichukua ile simu kabla hajabonyeza kitufe cha aina yoyote simu iliita kwa mara nyingine.
Mzee Tarimo aliitazama ile simu kisha kuamua kuipokea na kuiweka katika sikio lake.
"Hallo boss huapata taarifa za Johar?"
"Taarifa gani?"
"Johar yupo hospital tena kwenye hali mbaya, hivi ninavyoongea nipo hapa hospital na Johar amelazwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahuti hiti. Na chumba chake kimezungukwa na polisi mlangoni"
Mzee Tarimo alishtuka kidogo kuanguka chini, kwa jinsi alivyokuwa anampenda mwanae alishindwa hata kuongea na kubaki akiwa kama mtu aliekuwa kwenye mshituko mkali.
"Lakini Johar si alikuwa kule pamoja na yule afande, sasa iweje ametoka hadi kuwa hospital?"
Mzee Tarimo aliuliza huku akionekana dhahiri kushtushwa na kile alichokuwa ameambiwa.
"Boss me nipo hapa hospital toka jana jioni, na nimemshuhudia Johar kwa macho yangu mwenyewe akiwa anatolewa katika ofisi ya Dokta huku Dickson nae akiwa anafuata nyuma, akiwa amefungwa pingu katika mikono yake, na polisi wakiwa wanamsukuma kuelekea nje ya hospital"
Aliongea yule mtu aliempigia na kumfanya mzee Tarimo kuzidi kupata wasiwasi na hofu juu ya mtoto wake, hakutamani kitu chochote kimkute mtoto wake. Johar alikuwa mtoto kipekee katika familia ya Mzee Tarimo, hawakuwa na mtoto mwingine katika familia yake zaidi ya Johar ndiyo maana walimpenda na kumthamini. Zile taarifa zilimuumiza sana mzee Tarimo na kumfanya kuhisi kizungu zungu. Alipojaribu kumpigia yule Afande ambae aliambiwa amlinde Johar simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa, hasira na huzuni zilimshika mzee Tarimo. Kiukweli zile taarifa zilimuumiza sana na kumfanya mzee Tarimo kujiuliza maswali mengi katika akili yake.
Kitu cha kwanza mzee Tarimo aliamua kuondoka kuelekea kule alipokuwa amemuhifadhi mwanae Johar, mke wake alishindwa kuelewa nini kilichokuwa kinamsumbua mme wake. Mzee Tarimo aliingia katika gari lake kwa haraka ili kuwahi kule alipokuwa amemuacha. haraka haraka gari lilitoka huku likiwa na spidi kali, kiukweli mzee Tarimo alikuwa amechanganyikiwa. Akiwa bara barani alionekana kuwa na mawazo mengi juu ya kile alichokuwa ameambiwa.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment