Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

THE WORLD HATES ME (DUNIA INA NICHUKIA) - 4

   

Simulizi : The World Hates Me (Dunia Ina Nichukia)

Sehemu Ya Nne (4)




taratibu abdul akaanza kushuka chini hatimae akakaa chini abdul akahisi kuishiwa pumzi akabaki amekondoa macho akiangalia ndugu wa baba yake walio kuwa wanaendelea na shughuli zao bila kumjali abdul. abdul akakumbuka hali ya mama yake hosptal abdul akaudhunika na kujiona yeye ndo msaada mkubwa kwa mama yake hakutakiwa kukata tamaa mapema wazo likamuijia akaangalie hela kwenye kabati chumbani walimokuwa wanalala wazazi wake, abdul akaamka huku kichwa kikimuia wepesi akijihisi kupoteza fahamu abdul alipishana baadhi ya ndugu wengine wakimshangaa abdul, alipo kuwa anakaribia ndani akasikia kama sauti ya watu wakiwa kama wana kikao sebuleni ".,.hapa tukishindwa sana nikugawana mali..." nisauti aliyo isikia abdul kutoka kwa ndugu waliokuwa na kikao sebuleni walikuwa wanaongelea juu ya mali alizo acha baba abdul, abdul aliingia ndani mule na wote wakaonekana kushtuka baada ya kumuona abdul.

"habari zenu" alisalimia abdul bila kusimama akielekea kwenye chumba cha wazazi wake hakuna alie jibu salamu ile! abdul alikuta mlango wa chumba cha wazazi wake ukiwa wazi! abdul akaingia ndani na ndipo alipo kutana na hali tofauti!

kabati lililo kuwemo chumbani mule droo zake zote zilikuwa wazi huku mafaili na baadhi ya docoment zikiwa zimezagaa pale chini na hata suluale za marehemu baba yake zilikuwa chini zikiwa na dalili zote za kupekuliwa zikionekana macho pa abdul "kweli humu nita pata hata mia?...na ni nani amepekuwa hivi" alijiuliza abdul na kuanza kutafuta mule ndani kama atapata chochote ,abdul alitafuta sana hakuona hata shilingi mia kwani ndugu wa baba yake walikuwa wamechukuwa akiba zote za pesa zilizo kuwa pale walikuwa wame sachi mpaka mifuko ya nguo za mama abdul na marehemu baba abdul. abdul alishagundua kilicho endelea mule ndani na alijua walio fanya vile walikuwa ni ndugu wa marehemu baba yake . asira zilimuijia abdul akamka na kuanza kutafuta bastola ya marehemu baba yake abdul alikuwa anataka akawauwe ndugu wale walio jaa roho mbaya, bahati nzuri na bahati mbaya abdul aliikosa ile bastola abdul akaamua awafuate wampe hela walizo chukua ,abdul akaenda mpaka walipokuwepo

"jamani utu ni bora hemu tuziache hizi tofauti tulizonazo....naombeni pesa mlizo chukua zina umuhimu mkubwa na maisha ya mama yangu" alisema abdul kwa sauti ya kuomba iliyojaa majonzi huku akijaribu kuondoa tofauti iliyopo katikati yao kwani mama abdul na abdul walikuwa hawapatani kabisa na ndugu wa marehemu I.G.P ibrahimu hiii ilitokana na....,..

marehemu ibrahim alilelewa na mama yake mzazi na kusomeshwa mpaka kupata kazi baba yake ibrahimu alikufa ibrahimu akiwa bado mdogo kabisa.

palitokea mgogoro mkubwa kati ya ibrahimu na mama yake mgogoro huu ulikuja baada ya ibrahimu kukataa mwanamke aliechaguliwa na mama yake na kumuoa mama abdul ambae hakutakiwa hata kidogo kwenye familia ya ibrahim, mpaka mama yake ibrahim anakufa ule mgogoro ulikuwa bado unaendelea huku ndugu wa ibrahim kila siku wakimshawishi amuache mama abdul lakini ibrahim alikataa kabisa....ndio huu mgogoro ulio kuwa unaendelea kuweka mipaka ya kimahusiano kati ya ndugu wa marehemu ibrahim na mama abdul...na sasa walikuwa na mpango wakumzulumu mama abdul na mwanawe mali zote.....


"tafadharini mama yangu yupo kwenye hali mbaya" abdul aliendelea kusisitiza akitoa machozi huku akijitahidi kuzuia hasira zake

"ebwana hakuna aliechukwa hela... wewe na huyo mama yako msitu zingue tunahitaji mje mchukue kilicho kuwa chenu muondoke kwenye hii nyumba " alijibu baba yake mdogo alie kuwa amekaa kwenye kochi la mtu mmoja akiwa amepakata laptop ya mama abdul,

"bitch mliijenga hii nyumba... pumbavu na laptop ya mama unaishika ..." alisema abdul akiwa ameshindwa kuzuia hasira zake, abdul akainuka na kwenda kumnyang'anya laptop kwa nguvu yule baba yake mdongo

"jamani nikirudi hapa nikiwakuta bado mpo yatakuwa mengine" alisema abdul na kuondoka na laptop ya mama yake kwani abdul aliona anapoteza muda alijua sheria zipo , abdul alikuwa ameamua akauze ile laptop apate pesa za kumsaidia mama yake.

abdul alitembea kwenye maduka ya wahindi akitembeza ile laptop kwa bei ya chini lakini siku ya kufa nyani miti yote huteleza! hakuna alioinunua laptop ile ya thamani kwa bei ya chini kabisa.

abdul alizunguka sana bila kufanikiwa huku mda ukiwa unakwenda kama mshale

mwishowe alikata shauri aende hospatal akaiweke poni ile laptop kwa madaktari na matibabu ya mama yake yakishaanza aende kutafuta mteja atakae nunua kabati au tv ya nyumbani kwao.

jua lilikuwa limemuishia abdul akiwa na laptop alioiona kama ina mkosi matatizo yalikuwa yameamuamulia abdul kwa mara ya kwanza abdul aliianza kuziona hila za ulimwengu uliojaa kila aina ya uovu muda mwigi chozi lilikuwa linamtoka abdul.

abdul akiwa anatembea mara simu yake ikaita kuangali mpigaji alikuwa ni violla mpenzi wake, abdul akapokea na kumueleza kwa kifupi huku akilia na kumuomba violla asimpigie abdul akakata simu na kumuachia violla kizazaa na masimango kutoka kwa wazazi wa violla!


abdul alifika hosptal wodini hakukuta hata ndugu mmoja abdul akajua sasa hata ndugu wa mama yake walimkimbia abdul akaenda mpaka kwa doctor


"samahani doctor laptop hii hapa kaeni nayo anzeni matibabu ya mama mimi naenda kuuza tv na kabati nita waletea pesa yenu" alisema abdul huku akijizuia kulia

"....ah kuna mtu ameshatoa laki tano! bado tano imebaki laki mbili...anaitwa george amesema usiache kwenda kwake leo" alisema doctor na kumshangaza abdul

"hah ...basi laptop hii hapa laki saba iwe imekamilika" alisema abdul huku akiwa haamini kama meja george amekuwa msaada mkubwa kwake kiasi kile

"...hapana hiyo laki mbili mtaileta tu kwakuwa mmeshatoa laki tano sio mbaya" alisema doctor ,abdul akashukuru na kwenda kwenye kitanda cha mama yake ambae alikuwa bado kwenye ileile hali yake iliyo muhuzunisha abdul.

abdul akiwa amekaa kwenye kitanda cha mama yake mara simu ikaita kuangalia violla!

"haloo..niambie" alisema abdul kwa sauti ya huzuni

"...abdul nashindwa hata nisemaje kwani huku wazazi wangu tangu wajue matatizo yenu imekuwa gumzo kwangu...nasimagwa japo nipo hostal... ..wanasema hawana hela za kumlea mtoto ambae familia ya baba yake ni ya biashara haramu" alisema violla kwa masikitiko maskini ya mungu taarifa ya kuwa ibrihimu alikuwa anajihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya zilikuwa zimefika kwa wazazi wa violla, kwani taarifa ilikuwa ni kashfa kubwa kwenye familia ya abdul

"ah...muambie mama tutakuja kuya ongea kwa sasa mniache nipo kwenye matatizo nakupenda violla....baba yangu amesingiziwa " alisema abdul kwa kusikitika akakata simu na kuizima kabisa hakutaka aendelee kuchanganyikiwa.

abdul akambusu mama yake kwenye paji la uso wake na kuanza kuondoka akiwa na mawazo mengi akimfikiria mama yake pamoja na violla na mwanae ambao wameanza kunyanyasika abdul akajikuta akiuona ulimwengu ulikuwa una mtesa.


abdul alienda mpaka kwa george ambae alimkuta akiwa amekaa sebuleni yenye hadhi akiwa anaangalia tv.

abdul aka msalimia meja george na kumshukuru

"usiwe na wasiwasi abdul wewe nikama mwanangu...vipi ulienda nyumbani?"aliuliza george na abdul akasimulia jinsi ndugu wa marehemu baba wake wanavyotaka kuimiliki nyumba yao

"yaani meja nimetafuta hela mule ndani sijaona hata kadi za benki za wazazi wangu" alisema abdul

"achana nao zile nimali zako wewe fuatilia kwanza swala la mama yako...wale watatolewa pale na sheria" alisema george kumliwaza abdul ambae hudhuni imekuwa sehemu kubwa ya maisha yake.


siku zilienda huku hali ya mama abdul ikiwa imepadilika kidogo sana kila kitu alisaidiwa na ndugu aliekuwa anamlea kiukweli ndugu msomaji hali ya mama abdul alikuwa hawezi hata kuongea alitumia mkono wake mmoja kwa kutoa ishara alikuwa hawezi lolote muda wote alikuwa akiendeshwa kwenye beskeli ya walemavu muda wote mdomo wake bado ulikuwa upande kitu ambacho kili mliza kila siku abdul.

kila siku violla alimpigia simu abdul na kumuambia kuwa kila siku amekuwa gumzo kwa wazazi wake kuhusu mtoto alie zaliwa hii ikazidi kumchanganya abdul .


imesha pita wiki tatu mama abdul akiwa hosptal tangu apelekwe hosptal na hali yake ikiwa inakatisha tamaa na kumliza abdul kila kukicha.

ilikuwa ni saa mbili usiku ndani ya nyumba ya george abdul alikuwa amekaa kimya akifikiria hali mbaya ya mama yake, na ndipo george akaona ule ndo ulikuwa muda muafaka wa yeye kumuambia abdul kitu ambacho alikuwa anakitaka kutoka kwa abdul ...

"abdul mama yako yupo kwenye hali mbaya sana na tatizo alilo kuwanalo ni vigumu kupona kwenye hizi hosptal za tanzania" alisema george kwa utulivu wa hali ya juu

"ndio nafahamu..but nitafanya nini kumsaidia mama yangu" alijibu abdul kwa kutia huruma

"huo ungonjwa aliokuwa nao mama yako niugonjwa mdogo sana akipelekwa india!" alisema george kwa utulivu uleule

"yah nafahamu ...ikiwa hela ya matibabu ha mwanza yalinishinda kutoa ndo nitaweza gharama za kumpeleka mama yangu india?" abdul aliuliza akiwa hana matumaini

" uwezo unao naamini hata nia utakuwa nayo...kuna kazi ukiifanya utapata pesa na kumaliza matatizo yote" alisema george na kumshangaza kabla abdul hajauliza swali george akaendelea

"abdul una uwezo mkubwa wakuendesha gari utaiweza hiyo kazi"

"kazi gani?" abdul ikabidi aulize george akashusha pumzi

"unajua sisi watu tunayo itumikia serekali ni watu wenye mshahara mdogo na tuna majukumu mengi... mtu anaeitumikia serekali ni vigumu kujenga jumba kama hili nililo jenga mimi lazima upite njia tofauti...!" alisema george na kutulia kidogo kisha akaendelea

"...me huwa na deal na mambo ya ambush na kuvamia na kupola benki.....nina kama miaka mitatu tangu nimeacha hii kazi kwani dereva nilie kuwa na mtegemea kwenye mambo ya kupola alipigwa risas mwaka juzi tukiwa kwenye harakati ya kukimbia polisi tukiwa na mamilioni ya pesa but sisi kwa kwa bahati nzuri tulikimbia... abdul mi nili ona uwezo wako wa kuendesha gari unawezo mkubwa sana kuna mpango nataka kukushirikisha ...kuna milioni mia nne zipo njenje" alisema george na kumuangalia abdul aliekuwa ametoa macho

"abdul kazi ya siku moja itafanikisha kuokoa maisha ya mama yako nawewe kuweka sawa maisha yako ...jifikirie uamuzi upo mikononi mwako" george aliendelea kumpa nasaha abdul , abdul hakuamini aliyo ambiwa lakini kwakuwa ana ana mzigo wa shida akaamua kuuliza hiyo kazi itakuwa vipi ili aone ugumu wa kazi

" hiyo kazi itakuwa vipi" aliuliza abdul

" siku tano mbele kuna gari litakuwa linaleta milioni mia nne tuta uvamia msafara huo ukiwa unakaribia mjini na kuufanyia ambush then mabingwa tuna sepa na pesa kama za baba yetu weve " alisema george huku akitabasamu

"meja unataka kuniangamiza...kwanza umesha sema dereva wako wa kwanza alipigwa risasi, unataka na mimi nife nimuache mama yangu akiwa kwenye mateso" alisema abdul akiwa ana muhujumu george

"abdul wewe umepitia mambo yote ya jeshi nitakushangaa ukiwa na moyo wakike kiasi hicho na mimi nili uona uwezo wako ...muda mwingine katika maisha inabidi ufanye jambo moja ambalo ukilifanikisha inakuwa rest in peace shida" george aliendele kumpa abdul maneno ya ujasiri

"na endapo nitakufa kama alivyo kufa dereva wako wa kwanza" aliuliza abdul huku akionesha kila dalili ya kumpinga george

"utakuwa umepotea katika harakati missing in mission nenda kapumzike ujifikirie na iangalie hali ya mama yako hosptal anavyo tesaka siku force upo huru kuchagua" alisema george na abdul akaamua aende chumbani alimo lala ili afikirie vizuri.

abdul usiku ule hakupata usingizi alifikiria sana ni kweli akifanya kazi ile ataokoa maisha ya mama yake lakini je kama ikitokea akifa si atamuacha mama yake pamoja na violla mtoto wake katika mazingira magumu

abdul alijifikiria sana usiku ule.

asubuhi ilifika george aliamka na kushangaa kumkuta abdul sebuleni

"meja kazi nitaifanya...lakini kabla ya kazi nataka mama yangu apelekwe india ili hata kama nikifa mama yangu awe amesha pata matibabu itakuwa ndo malipo yangu kwenye kazi hiyo" alisema abdul hata bila salamu alikuwa amesha fanya uamuzi

"sawa haina tabu mama yako ataenda india utaratibu utaanza leo" alisema george kwa furaha.


utaratibu wa kumpeleka india mama abdul ulifanyika huku abdul akiwa kwenye mazoezi ya kuendesha gari kwa mitindo yote.

abdul alifurahi sana siku alio kuwa anampeleka mama yake na mama yake mdogo airpot ili wapelekwe india kwa ajili ya matibabu ya mama abdul na mama mdogo wake ndio angekuwa ana muuguza.

abdul alifurahi kuona mama yake anaenda india huku gharama zote mpaka za matibabu zikiwa zimisha lipwa na george.


ilikuwa ni saa tata usiku ndani ya nyumba ya george kulikuwa kuna jopo lilio shirikisha watu sita akiwemo abdul

"so wazee ndo kama nilivyo wambia gari tuna lishamburia pale kwenye mataa huwa kuna watu wengi najua kutatokea vurumai ambayo sisi itatusaidia" alisema george kuwaambia wale watu waliokuwa na miili mikakamavu abdul alionekana kijana mdogo kwa hawa watu waliokuwa wa makamu.

usiku huo waliongea mengi sana kwani kazi ya uporaji ilikuwa ifanyike kesho yake saa nne asubuhi. hatimae wakaagana na kwenda kulala wakiwa wamesha afikiana juu ya mpango walio panga.


saa kumi alfajiri abdul alikuwa kapiga goti akimuomba mungu amlinde katika kazi iliyo kuwa mbele yake, abdul alikuwa na wasiwasi na ile kazi alijuwa lazima inge gharimu maisha yake, abdul kila alipo kumbuka kuwa anamtoto na mke mtarajiwa abdul alimwaga chozi alijua angeweza kufa na kuwaacha lakini kwa kuwa alimsaidia mama yake abdul alibidi aingie kazini.


******


ilikuwa ni mida ya saa nne mjini mwanza gari aina ya rav4 ilikuwa katika mwendo mkali huku ikifuatiwa na askari wanne wenye pikipiki wakiwa na siraha huku wakiwa wamevalia nguo za kuzuia risasi wakiifuata ile rav4 kwa nyuma walionekana kuwa wanailinda ile rav4 na ndani ya ile rav4 kulikuwa na dereva pamoja na askari.

gari lilikimbia kwa kasi kuelekea kwenye mataa.


george alikuwa kasimama akisoma gazeti pembeni kidogo na ile barabara ambayo kuna rav4 ilikuwa ikija huku ikilindwa na askari.


pembeni kidogo mbali na alipokuwa george kulikuwa kuna tax nyeusi ambayo ndani yake kulikuwa kuna watu watano akiwemo abdul ambae alikuwa kwenye kiti cha dereva tax hii ilikuwa imeangalia kule ilipo tokea ile rav4.

abdul akiwa mule kwenye gari aliiona ile rav4 ikija kwa kasi , hapohapo abdul akaiwasha gari yake iliyo beba watu wa nne, abdul akaiondoa kwa kasi tax ile kuelekea kwenye ile barabara ambayo rav4 ilikuwa inakuja, gari aliondesha mlio wake ilionesha kuwa ni mbovu na hata ilitoa moshi mweusi sana!

abdul akaingiza gari upande ambao ile rav4 ilikuwa inautumia sasa gari ya abdul ilikuwa inakutana uso kwa uso na ile rav4 iliyo lindwa na maaskari!


dereva aliekuwa anaendesha rav4 alishituka kuiona ile tax ikija upande wake huku ikionesha mwendeshaji alikuwa kadhamilia kusababisha ajali dereva akajua kulikuwa kuna hatari.

askari aliekuwa na dereva ndani ya rav4 akatoa bastola yake haraka tayari alishajua ile tax ilikuwa ina majambazi.

askari wenye pikipiki nao walianza kupunguza mwendo ili wasimame waishambulie ile tax.

na muda huo tax ya abdul ilikuwa imesha kalibiana kabisa na ile rav4 , ukasikika mlio mkubwa wa msuguano wa taili za gari na rami ya barabara.....



dereva wa rav4 alihamanika kwani gari ile tax ilio endeshwa na abdul ilikuwa imesha mkaribia kama hatua ishirini dereva alijua kama ataendelea kuendesha gari ni lazima wangegongana uso kwa uso na tax ya abdul na kama wange gongana basi pangetokea maafa dereva wa rav4 akafunga brek kwa nguvu huku mlio wa msuguano wa taili za ile rav4 na rami ukisikika mahali pale, sehemu ilipo simama ile rav4 ilikuwa ni karibu na pale alipo kuwa kasimama george ambae alikuwa ameacha kusoma gazeti akiangalia ile rav4 george alivyoona ila rav4 imesimama alipeleka mkono wake kiunoni na kuchomoa bastola .

yule askari alie kuwa na dereva ndani ya rav4 alishusha kio cha gari haraka kisha akasogea akashika bastola vizuri na kutoa mkono wake wenye bastola kupitia kwenye dirisha la mlango wa gari akawa anajaribu kuilenga ile tax ikiwezekana ampige dereva wa tax ile ambae ni abdul.

lakini hapohapo abdul alikata kona ya haraka na kuhama ule upande kisha hapohapo akakata kona ya nguvu huku taili za nyuma ya ile tax zikivulutwa zikiwa hazizunguki abdul akaendelea kuikata kona ile huku akiwa amekanyaga brek mwishowe tax ile ikawa imeikata ile barabara tax ikawa imeziba robo tatu ya barabara ile .

yule askakari baada ya kuona tax ile imehama ule upande akahamisha mkono wenye bastola na kuelekeza upande ule ambao tax ilikuwa imesimama lakini kabla askari haja fanya chochote pah pah ! ....na damu nyingi zikamrukia dereva wa rav4!.

meja george alimuona yule askari akiwa anataka ashambulie tax ya abdul, hapo hapo george akafyatua risasi mbili huku akikimbia kuelekea kwenye ile rav4 .risasi alizo fyatua george zilimpata sawia kichwani yule askari ndani ya rav4 dereva alishtuka kuona karukiwa na damu ndipo alipo angalia na kumuona askari akiwa katapakaa damu hana uhai tena dereva akataka aichukue bastola iliyokuwa kwenye maiti ya askali lakini alikua kachelewa kwani risasi mbili kutoka kwenye bastola george aliekuwa karibu kabisa na gari zikampata dereva kifuani yowe kubwa la maumivu likamtoka dereva george akasogea karibu na mlango na kuachia risasi moja iliyo mnyamazisha dereva , kwa upande wa george akawa kamaliza kazi kwani kazi yake ilikuwa kuua watu walio kuwa kwenye rav4 yenye milioni mia nne .

wale askari wenye pikipiki walivyoona ile hali wali jitupa pembeni kutoka kwenye pikipiki kila mmoja kwa mtindo wake na kurudi nyuma ambapo walipata cover kwenye roli lililo kimbiwa na dereva baada ya kusikia milio ya risasi, wale askari wakaanza kuitupia risasi tax aliyo kuwemo abdul na watu wa nne.

abdul na wale watu wanne wali jikunja baada ya kuona askari wanawatupia risasi, wale watu wanne wakiwa wamejikunja kwenye gari huku baadhi ya vioo vya gari vilivyo pasuliwa na risas zilizo toka kwa maaskari viki wadondokea na baadhi vikiwakata kioo kimoja kili dondoka na kumchana abdu juu ya jicho abdul akatoa mguno wa maummivu na kuanza kufuta damu kwa shati lake kwa mara ya kwanza abdul akapata kovu kwenye uso wake tangu azaliwe abdul na wenzake walifungua begi lao lilo kuwa na bunduki tano aina ya ak47 zilizo katwa vitako na risas wote wakashika bunduki na hata abdul ambae alikuwa ameanza kuhisi kupoteza uhai wake abdul akiwa kainama akatoa rock ya milango ,abdul na watu wanne wakafungua milango ya upande wa pili huku waki wameinama vilevile abdul akatoka nje akiwa na bunduki yake mkononi na mkono mwingine akiwa na dumu jeusi la lita tano! abdul akapiga goti moja chini na kugeuka kule zilipotokea risasi abdul akaanza kujibu mashambulizi huku kile kidumu akiwa amekiweka chini ya gari karibu na tenki la mafuta la gari, na wale watu wanne walifanikiwa kutoka kwenye gari lililokuwa lina chakazwa na risasi za maaskari na hawa watu wanne wakaanza kujibu mashambulizi huku bundiki zao zilizo kuwa na mikanda ya risas zikitoa sauti kubwa.

milindimo ya risas ililindima huku raia waliokuwa eneo lile wakikimbia ovyo,

"nikinge" alipaza sauti abdul kuwaambia wale aliokuwanao wale watu wanne wakaanza kupiga risasi mfululizo mpaka wale maaskari wakakosa nafasi muda huohuo abdul akatoka mbio akiwa amejikunja kutokea kiunoni huku akifuta damu zisiingie kwenye jicho damu nyingi zilikuwa zinamtoka akielekea kwenye rav4 huku akiwa amekiacha kile kidumu pale kwenye tax yao, abdul akafanikiwa kufika kwenye ile rav4 na kufungua mlango wa upande wa dereva na kuingia ndani ambamo alimkuta george akiwa amesha toa zile maiti huku damu ikiwa imetapakaa ndani ya gari lile .

" shit umeumia abudul pole ndugu ....washa gari tusepe" alisema george aliekuwa amekaa siti ya nyuma kuliko kuwa na mabox ya mamilioni

abdul akafuta damu mikono yake ilikuwa imetapakaa damu akawasha gari akarudi nyuma kido harafu akaanza kupandisha taili za upande mmoja kwenye tuta linalo tenganisha barabara za pande mbili tofauti abdul akaanza kuendesha gari huku taili za upande mmoja zikiwa kwenye tuta na taili za upande mwingine zikiwa kwenye barabara abdul alifanya hivi ili apate upenyo wa kupita kwani tax yao ilikuwa imeziba robotatu ya barabara abdul alifanikiwa kupita kwenye ule upenyo uliokuwa katikati ya tax na tuta lilio tenganisha barabara za pande mbili tofauti abdul alipofika kwenye ile tax alipunguza mwendo kabisa wale watu wanne wakaacha kuwashambulia na kuingia kwenye ile rav4 kila mmoja kwa mtindo wake abdul akaanza kuondoa ile rav4 taratibu, wale askari walianza kuitupia ile rav4 risasi ile rav4 huku wakitoka kwenye lile roli wakisogea kwenye ile tax walioiacha kina abdul, ndani ya gari kina george walilala baada ya kuona rav4 yao inashambulia abdul aliinamisha kichwa chake asije kupatwa na risasi za maaskari zilizoanza kuvunja kioo cha nyuma cha rav4 , abdul bado aliendesha gari kwa mwendo mdogo kana kwamba kuna kitu alisubiri kitendeke, abdul kupitia satimila ya ile rav4 aliwaona wale askari wakiwa wamepata cover kwenye ile tax walio iacha

"fire meja" alisema abdul

"oya nipeni cover" alisema george na hapohapo wale watu wanne kwa kupitia madirishani wakaanza kufyatua risas ovyo ovyo kuelekea kwa wale askari waliopata cover kwenye tax, askari wakakosa nafasi ikabid watulie, muda huo huo george akashika bastola yake na kwa kutumia uwazi uliokuwa kwenye kio cha nyuma cha rav4 kilicho vunjwa na risasi za askari, george akaanza kufyatua risas kukilenga kile kidumu kilichokuwa chini ya ile tax alicho kiacha abdul , kile kidumu kilikuwa na petrol na george alifanikiwa kukipiga risasi ambazo zili sababisha mlipuko mdogo ulio washitua wale askari na kabla hawajafanya lolote walitupwa nyuma na mlipuko mkubwa wa ile tax ukasikika eneo lile, hii tax ilikuwa ndo kazi yake ambayo george alikuwa kaidhamilia na ndomaana ilikuwa mbovu mbovu

abdul alianza kuongeza speed baada ya kuona ile tax imesha lipuliwa na wale askari wakiwa wametupwa kulikuwa hamna upinzani tena, abdul akazidi kuichochea mwendo ile rav4 iliyo kuwa na uwezo mkubwa wa speed , george alifungua box lenye pesa na kutoa burungutu moja la noti nyekundu

"toa pesa ukaribishe pesa "alisema george na kulitupa lile burungutu nje hewani na likasambaa na kusababisha vulumai ya wana nchi walio kuwa eneo lile wakigombania zile noti zilizo peperuka hewani ikawa patashika watu wengi waka miminika katikati ya barabara ili waokote zile pesa wale watu waka wamejaa katikati ya barabara na kuzuia magari mengine yasikatize, george alifanya vile ili hata kama kuna maaskari walikuwa karibu na eneo lile wasiweze kupita kwenye patashika ya watu wale walio gombania pesa katikati ya barabara , gari alio endesha abdul likuwa speed kali huku abdul akiliyumbisha na kuhama barabara mara huku mara kule huku akisababisha ajali kadhaa baina ya boda boda na magari abdul alizidi kuover take na kuzidi kuyoyoma na mara akaingia kwenye bara kubwa iliyokuwa inaelekea nyegezi kiukweli abdul alikwa hatari kwenye uendeshaji wa gari,

george akiwa ndani ya gari alitoa simu na kupiga namba flani "oya sogeza gari haraka....poa changamka" alisema george na kukata simu .

abdul aliendesha gari alivyo fika eneo moja lililo itwa MRUNGUSHI abdul akaicha ile barabara ya kuelekea nyegezi akakata kona na kuingia kwenye barabara ya vumbi iliyo elekea ndani ya ya mtaa wa mrungushi abdul akaongeza mwendo huku akikikata mitaa ya mrungushi kana kwamba alikuwa na ramani ya mtaa ule abdul ali nyoosha kwenye barabara za mtaa ule hadi kwenye uwanja flan ambapo pembeni kidogo ya uwanja ule kulikuwa kuna tax nyeusi iliyo paki, abdul akasogeza gari lake mpaka kwenye ile tax nyeusi .

*** kitu ambacho abdul na george hawakujua ni kwamba ile rav4 ilikuwa nakifaa ambacho kilikuwa kina itrack ile rav4 na kila ilipoenda ilionekana kwenye kompyuta maalumu za benk kwa hiyo kila hatua waliopita walionekana.

<<<wakati kina abdul wanaondoka na gari lenye mamilioni taarifa zilifika haraka kwenye benk ambayo zile pesa zili hitajika kufika kwenye hiyo taarifa ikatolewa kwenye kituo cha polisi pale mjini ..polisi wakaingia kwenye magari ya polisi mawili na kuanza kuifukuzia gari ya rav4 iliyo endeshwa na abdul , haraka haraka mtu mmoja aliokuwa anahusika na mitambo ya benk alitoka nje ya benk akiwa na laptop akaingia kwenye landrover na baadhi ya askari wa benki ile landrover ikiwa inaendeshwa na askari ikaanza kuondoka huku yule mtu wa mitambo akifungua ile laptop, laptop ile kwenye kioo ilionesha picha kama ramani ya mji huku kidude kidogo cha pembe nne chekundu kikionekana kama kina pita kwenye mstari ulio maanisha barabara. yule mtu akawa anaangalia kioo cha laptop ile huku akikifuatilia kwa makini kile kidude chekundu cha pembe nne na hicho kidude kilimaanisha gari rav4 iliyo endeshwa na abdul. ile landrover aliyo kuwemo mtu mwenye laptop ilionesha kina abdul walipo elekea landrover ilikuwa kasi huku nyuma ikifuatiwa na gari mbili za askari.

"kata kushoto" alisema yule mtu mwenye laptop kumuambia dereva, eneo walipokuwa ilikuwa ni MRUNGUSHI na kushoto aliposema mtu mwenye laptop ndipo pale ambapo kina abdul walikatisha na kuingia mtaani .

landrover ikifuatiwa na gari mbili za polisi ilianza kukata barabara kwa kasi kuelekea laptop ilipo waelekeza na ni hakika ndipo walipo kuwa wameelekea kina abdul...




abdul alivyo isogeza ile rav4 yenye mamilioni karibu na ile tax nyeusi wali shuka wote kwenye ile rav4 abdul akiwa katapakaa damu upande mmoja wa uso wake na george akasogea mpaka kwenye ile tax ambamo kulikuwa na mtu mmoja

"oya kila kitu kipo fresh?" george alimuuliza jamaa aliekuwa ndani ya tax

"baridah tu mzee" alijibu jamaa aliekuwa kwenye tax

"oya tuna pakua hayo mabox yenye pesa mnaya fungua napesa mnazimwaga kwenye hii buti ya tax" alisema george na kwenda kufungua buti ya tax ile na kiana abdul wakaanza kupakua yale mabox yenye pesa kutoka kwenye rav4 , kina abdul wakawa wakipakua wanafungua mabox na kumwaga pesa kwenye buti ya tax, na george akawa anazipekua zile pesa walizo mwaga kina abdul, george alikuwa akipekua zile pesa kwa kuzisambaza ndani ya buti kana kwamba kuna kitu alitegemea kukiona kwenye zile pesa.

kina abdul wakaendelea kupakua pesa na kuzimwaga kwenye buti na george akaendele na zoezi lake la kuzipekua pesa , na mara ghafla kipindi george anaendelea na zoezi laki aliona kidude kidogo cheusi kilichokuwa kama kifuniko cha kalamu kikiwaka taa nyekundu

"pumbavu nilijua tu watakuwa wame weke vimitambo vyao.... oya fanyeni haraka wanatufuatilia" alisema george baada ya kukiona kile kidude , haraka haraka kina abdul wakapakua pesa zote na kuanza kuingia kwenye ile tax. george kwa nguvu alikitupa kile kidude ndani kabisa ya mtaa, kisha nae akaingia kwenye tax na kuka kwenye kiti cha mbele abdul kwa mara nyingine aliwasha ile tax na kuiondoa kwa kasi huku ikiwa imejaza watu ambao walibana ndani ya tax hiyo na kwenye buti kukiwa kume furika pesa ,

" oya fanya fasta walikuwa wameweka mtambo wakujulisha wapi pesa zilipo... so wanatufuatilia" alisema george na abdul akazidi kuichochea tax na kukata mitaa kurudi kwenye barabara kubwa inayoelekea nyegezi , hatimae abdul alikamata barabara kubwa na kuanza kuendesha mwendo wa kawaida huku akiangalia nyuma kama alikuwa akifuatwa na polisi.


yule mtu mwenye laptop ndani ya landrover nyuma akifuatiwa na gari mbili za polisi alizidi kusogea kule walipo elekea kina abdul ,na mara laptop ilianza kupiga alam huku kwenye kioo ikionekana kitu kama ramani ya kiuwanja na kile kidude kilicho maanisha ile rav4 iliyo ibiwa kikazidi kuwaka taa nyekundu kikiwa kimesimama sehemu moja,tayari mtu mwenye laptop amesha gundua kitu na ndipo alipo inua mcho na kuiona ile rav4 ikiwa kwenye uwanja umbali kama hatua mia, mtu mwenye laptop akamuambia dereva asimamishe gari na kuwataarifu askari waliokuwa wakimfuata nyuma na magari mawili na kuwaonesha ile rav4 askari wakashika bunduki zao na kuzikoki wakaanza kusogelea kwa tahdhari ile rav4 ambayo imetelekezwa na kina abdul dakika tano zilizo pita .


askari pamoja na mtu mwenye laptop walipigwa butwaa kukuta gari ikiwa tupu!

"ah wameondoka na hela but kwenye pesa kuna kifaa kinachowaonesha walipo...hawawezi kufika mbali tutawanasa" alisema mtu mwenye laptop na kuanza kubonyeza batani za laptop ile akianza kukitrack kile kifaa ambacho alijua kipo kwenye pesa walizo kimbia nazo kina abdul, mtu mwenye laptop alishituka kwani laptop ilionesha kuwa kifaa kile hakikua mbali na pale walipo, kwa akiri ya haraka haraka mtu mwenye laptop akajua kuwa hela zilizo ibiwa zitakuwa zimefichwa mitaa ya hapo karibu "hah washamba kweli kumbe wamezificha ndani ya mtaa huu huu...afande nifuateni kuweni na tahadhari inaonekana jamaa wapo eneo hili na pesa"alisema mtu mwenye laptop na kuanza kuwaongoza maaskari wakifuata laptop ilivyo waelekeza. hawakujua kuwa wanapoteza muda bure kwani kile kifaa george alikitoa na kukitupa kwa nguvu ndani ya mtaa.

askari na mtu mwenye laptop walisogea kwa tahadhari mpaka eneo ambapo laptop iliwaonesha kuwa ile ndo sehemu husika.

mtu mwenye laptop alishangaa kwani laptop ilionesha kuwa eneo walipo ndipo kulipokuwa na kile kifaa lakini cha ajabu pesa hazionekani

"pumbavu ...wametuuza" alifoka mtu mwenye laptop huku tusi kubwa la nguoni baada ya kuona kile kifaa kilicho tupwa na george kikiwa chini ,tayari walikuwa wamesha poteza muda mwingi eneo lile na hawakuju kina abdul walikimbilia sehemu gani na kwa usafiri gani, ikabidi warudi pale ilipokuwa ile rav4 na baada ya kuchunguza ndipo wakafanikiwa kugundua alama za taili ya tax zikiwa zilitoka pale kuelekea barabara kubwa , tatizo nikwamba hawakujua ile tax ilikuwa vipi rangi gani na kibaya zaidi barabarani kuna tax nyingi , askari wakawa wamepotezwa na kina abdul taarifa ikatoka askari wa barabarani wakaanza kukagua kila gari lilio pita barabara ile ya nyegezi.


***Abdul akiwa watu sita kwenye gari pamoja na mamilioni ya pesa aliendasha gari kwa mwendo wakawaida kanakwamba alikuwa hakibizwi na polisi.

aliendesha gari mpaka eneo la mkuyuni abdul akakata kona kulia na kushika barabara ya vumbi na kukamata barabara ilioelekea igoma abdul akaendesha gari huku akiacha vumbi nyuma hatimae abdul akaacha barabara ile na kushika barabara nyingine ndogo na hatimae abdul akasimamisha gari mbele ya gereji flani ambayo ilikuwa mbali kidogo na mji geti kubwa la gereji likafunguliwa abdul akaiingiza gari abdul akashusha pumzi mfululizo... geti likifungwa .

gereji ilionekana kuchakaa kidogo na ilionekana kutotumika mara kwa mara huku mafundi wasio zidi kumi wakiwa eneo lile wakiangalia kwa tabasamu tax alio endesha abdul, geriji ilikuwa na eneo kubwa magari mabovu yalikuwa mengi eneo lile

george alishusha kioo cha gari

"oya muber chukueni piki piki mfuate njia ya mkuyuni mchunguze isije ikawa tulikuwa tunafuatiliwa na polisi" alisema george na vijana wawili wakawasha pikipiki na kuondoka.

tax ilizidi kusonga huku wakiwa wanapita sehemu zenye vifaa vya kila aina ya vifaa vya geriji kana kwamba pale ndo ilikuwa kiwanda cha magari.

hatimae abdul akapaki tax sehemu ambapo kulikuwa na baadhi magari mazima mazuri yasiyo pungua saba na wote wakashuka na kukusanya bunduki zao zote na kuweka kwenye begi moja kisha george akachukua begi lenye bunduki na kusogea nalo mbele kidogo na kwa kutumia jembe alichimba kwa mtindo wa mraba aridhi ya eneo dogo kama nusu futi kisha akapiga goti moja chini na kuanza kutoa udongo hadi akafikia sehemu ambapo kulikuwa na kifuniko cha chuma chenye kufuri kubwa kana kwamba kulikuwa na kisima eneo lile, george akafungua lile kufuri akafunua kile kifuniko na kuchukua lile begi lenye bunduki na kulitupia mule kwenye shimo ambalo lilijengewa kama kisima ndani ya shimo hilo mlikuwa na bunduki nyingine na risas nyingi, george akafunga kile kifuniko na kufukia kisha akakanyaga kanyaga kwa juu. ama hakika kazi ya ujambazi ilikuwa ni sehemu kubwa ya maisha ya george....george alikuwa ameianza hii kazi ya uporaji kwa mda mrefu yeye na na wanajeshi wenzake walio kuwa wanatamaa ya pesa ...george yeye kila siku ali ituhumu serekali na kuamini kuwa uporaji anao ufanya ni halali maana alisema kuwa serekari haiwajali wanajeshi wa tanzania... george aliwahi kwenda kulinda amani nchini uganda ambako walishambuliwa na waasi wa uganda ambapo george alipoteza rafiki yake mpendwa aliepigwa risas na waasi...george alirudi nchini akiwa na majonzi huku akiwa na wenzake saba kati ya wanajeshi ishirini walioenda uganda kumi na mbili wote wali kufa,... kilicho muudhi george ni pale walipo rudi nchini kwao tanzania walipokelewa kwa mapokezi yasiyo heshima ...kibaya zaidi ni pale walipo lipwa pesa ndogo ambayo kwa hakika walitakiwa wapewe hata mara nne ya zile wazo pewa.

hii ndo ilisababisha george kufanya awe msaliti wa nchi na kuanza kufanya kazi ya uporaji wa benk na sehemu nyinginezo ambazo zilikuwa zina mzunguko wa kipesa ...george alikuwa amesha kuwa kundi lake ambao walikuwa ni wanajeshi wakiwemo wale saba ambao alioendaga nao uganda kundi hili walijiita D M yaani dealers money.

george aliendelea na kazi zake huku akizidi kufanikiwa kimaisha na ndipo D.M walipokaa na kuamua waongeze miradi wakaamua kuanzisha gereji na kununua gereji mmoja kwa mwalabu ambayo ilikuwa imefilisika... george akiwa anaongoza D.M wakawa wameanza wizi wa magari na kulitikisa jiji la mwanza ambapo walikuwa wakiiba magari wanapeleka kwenye gereji yao na kuibadilisha rangi na baadhi ya vitu kisha wanaiuza, na hii gereji ilikuwa ndo kama stoo yao ya silaha.


ndugu msomaji hayo ndo maisha ya george na sasa abdul yupo pamoja nao tuendelee


*** ilikuwa ni furaha kubwa ndani ya nyumba ya george tayari walikuwa wamesha fanikiwa kuzitoa pesa gereji na kuzifikisha nyumbani kwa george wale watu wanne ambao ni wanajeshi pamoja na george walikuwa wakinywa na kufurahia ushindi wa pesa walizo iba

abdul alikuwa kimya akifikiria mambo aliyo ya fanya.

baadae wali watu wanne walipewa milioni mia na george

"wazee si mnajua bado sijampa yule informer wetu wa benk bado hatujampa na kuna baadhi ya wenzetu tutawagawia japo kidogo hata kama hawaja fanya kazi... na bado simba wetu abdul aliefanikisha sisi tupate hizi pesa" alisema george akimaanisha hizo milioni mia zina watosha kugawana wale wanajeshi wenzake wanne.

"poa kaka meja hamna tabu" walijibu na kuondoka wale watu wanne akabaki abdul na meja.


abdul alijua hana chake tena maana hela yake ndio iliyo tumika kumpeleka mama yake india

"unaona abdul kazi ndogo isiyo izidi masaa matatu imeweza kufanikisha hitaji lako lenye gharama" alisema meja george

"yah meja but ni hatari"alisema abdul

"usiogope abdul we are born to die"

"mmh"

"... abdul na jua una mpenzi na anamtoto chukua milioni tatu kwa ajili ya matumizi ya mtoto...kesho nakutafutia mwana sheria kwa ajiri ya kuwatoa ndugu wa baba yako kwenye nyumba yenu" alisema george na kumpa abdul milioni tatu.


abdul alikaa siku kazaa kwa george akiwa anauguza jeraha lake lililo kuwa juu ya jicho alikuwa kashonwa nyuzi ,

baada ya kupona abdul akampigia simu violla na kumuuliza hali ya mtoto wao na ndipo kwa mara ya kwanza abdul akauliza jina la la mtoto wake mpendwa

"anaitwa joel jina la baba yangu...but me nili taka aitwe ibrahim wakakataa wazazi" alisema violla na kujitetea

"usiwe na wasisi me nacho penda mtoto wangu awe mzima,..hayo mambo ya majina na imani za kidini sio kitu kwangu.... vp majibu ya chuo" aliuliza abdul

"wow am so happy... nime faulu mlimani city baby...but baba anasema anasubiria muafaka kati yako na huyu joel your son"

"ok ngoja nitakuja dar hukohuko tutayaongea acha nijiandae kwa safari baby nakupenda"

alisema abdul huku machozi yakimlenga kwani alifikiria sana mtoto wake joel mpaka muda huu abdul alikuwa hana hata wazo moja juu ya masomo yake.

"pouwa abdul nakupenda" alisema violla kwa furaha .

abdul akamwambia george kuwa atakuwa na safari ya kwenda dar es salaam

"ni vizuri...but nimeongea na madakatari wa india wamesema mama yako amesha pona na nimzima kabisa ila yupo kwenye mazoezi madogo madogo nafikiri baada ya siku tano atarudi tanzania akiwa mzima" alisema george na kumfanya abdul awe na furaha "sasa kama na safari jiandae kesho uondoke ili ukayamalize then me nitabaki nikifanya mpango wa mwana sheria ambae atawatoa ndugu wa baba yako kwenye nyumba yenu ili mama yako akifika awe huru kwenye nyumba yenu" george aliendelea kuongea maneno yaliyo mfanya abdul amuone george kama muokozi kwake.


abdul akajiandaa kwa safari na kesho yake alipanda basi na kuingia dar.


abdul alifika stend ya mkoa ubungo akiwa na begi lake la nguo akiwa kavaa miwani ya jua huku juu ya jicho lake la kulia akiwa na alama ya mshono iliyo kuwa ipo kama herufi 'i' hii alama ni ile aliyo chanwa na kipande cha kio kilicho pasuliwa na wakiwa kwenye ile tax wakati wakishambuliana na askari kwenye lile tukio la uporaji wa mamilioni .

abdul alienda kupanga kwenye guest iliyopo river side ubungo baada ya kumpuzika akampigia simu mpenzi wake violla na kumjulisha kuwa amesha fika dar abdul akamuelekeza violla guest aliyo kuwepo na vioalla akaanza safari ya kumfuata abdul alipokuwa amefikia violla alikuwa na furaha kwani hakutegemea kama abdul angekuja muda wote aliamini angemkana kwahiyo kuja kwa abdul ilikuwa furaha kubwa kwa violla.

violla alifanikiwa kufika alipofikia abdul na alifurahi sana kumuona abdul

"wow abdul nimefurahi kukuona baby" alisema violla na kumkumbatia abdul

"hata me pia" alisema abdul...

kila mtu alikuwa na furaha kumuona mwezeka

"mwanangu joel ?" aliuliza abdul

"ah yupo home nimemuacha kalala" alisema violla.

waliogea mengi kuhusu uhusiano na badae wakaianza safari ya kuelekea tabata kwa kina violla.


violla na abdul walifika kwenye nyumba ambayo haikuwa ya kifahali sana

abdul hakuamini alivyo muona mtoto wake joel ...mtoto alikuwa kachukua weupe wa wazazi wake huku copy ya sura ya abdul ikidhihirika kwa mtoto yule abdul alimbeba mtoto wake aliekuwa na mwezi mmoja na siku chache ...viola alishangaa kuliona chozi la abdul akiwa anamuangalia mtoto wake joel "abdul mbona una lia" aliuliza violla kwa kushangaa

"nothing baby ..furaha tu"alijibu abdul huku akifuta chozi 'nime pata mtoto nikiwa kwenye matatizo...kibaya nimejihusisha na mambo ya uporaji" alijiwazia abdul na ndicho kilicho mtoa chozi.


siku hiyo abdul aliongea na baba yake violla juu la swala la yeye na violla

"baba mimi nitatoa milioni mbili kwa ajili ya mchango kwenye masomo ya violla" alisema abdul kwa kujiamini

"ah abdul sisi tuta msomesha kwa pesa yetu .....sio siri tulijua utamkana mwanetu ..kwa kuwa umeonesha ushirikiano hizo milioni mbili zitakuwa kwa ajili ya malezi ya mwanao mpaka pale violla atakapo maliza masomo yake" alisema baba violla na kumfanya abdul awe na furaha kwani abdul alijua angepewa garama nyingi .

abdul alitoa zile milioni mbili na wazazi wa violla wakazipokea kwa shukrani. abdul alikaa mpaka jioni na baadae akarudi river side kwenye guest aliyo fikia alisindikizwa na violla ambae alikuwa na furaha iliyo pitiliza na njiani waliongea mengi kuhusu uhusiano wao na malengo juu ya mtoto wao mpendwa joel na abdul akamsimulia violla matatizo yaliyo mkuta mama yake.


abdul alikaa pale river side kwa muda wa siku tatu wakati wote abdul alipomfikiria mwanawe mpendwa joel alitoa machozi 'maskini baba haja muona mwanangu'

ndicho kilicho mliza abdul


abdul alipigiwa simu na meja george na kuambiwa kuwa baada ya siku mbili mama yake angewasili nchini akiwa mzima abdul alifurahi na akaenda nyumbani kwa kina violla na kuwaomba wazazi wa violla wa ruhusu aondoke na violla kuelekea mwanza wakampokee mama yake wazazi wa violla wakakubali abdul akafunga safari na violla akiwa na mtoto wao mpendwa joel wakapanda basi na kurudi mwanza ambapo walifikia kwa george.


ilikuwa ni saa saba mchana abdul na violla na mtoto alie mbeba walikuwa wakipishana na watu walio kuwa wakipita na mabegi yao abdul alikuwa anaangaza kumtafuta mama yake katika eneo lile na ndipo akamuona kwa mbali kidogo !

"mamaaaa" abdul aliita kwa nguvu na kwafuraha huku akipangua watu na kwenda kumkumbatia mama yake

"mwanangu abdul" alisema mama abdul na wote wakakumbatiana

na hapohapo abdul na mama yake walianza kulia abdul alikuwa haamini kama mama yake atapona abdul alipo kumbuka hali ya mama yeke ilivyokuwa alipopata kiharusi abdul alishindwa kuvumilia akaanza kulia.

hata mama abdul pia alianza kulia kwa uchungu wa kumkosa ibrahim walikumbatiana kwa mda mwishowe wakaachiana.

"abdul usilie mwanangu yamesha pita.....hah na hili kovu mwanangu" aliuliza mama abdul akiwa kashika lile kovu ambalo abdul alilipata akiwa kwenye harakati za kupora mamilioni.

"ah niliumia bahati mbaya....mama muone mjukuu wako!" alisema abdul na kumpoteza malengo mama yake abdul hakutaka mama yake ajue kuwa alijihusisha na ujambazi

"wow mjukuu wangu...hah kumbe umekuja na violla" alisema mama abdul kwa furaha ikawa furaha kubwa uwanjani pale...na badae walianza safari ya kurudi nyumbani wakiwa na mama mdogo wa abdul ambae alikuwa anamuuguza mama abdul huko india , mama abdul alikuwa amekonda kiasi na rangi ya ngozi yake ilikuwa imeanza kufifia wakaenda mpaka kwa george ambae alimpokea mama abdul kwa furaha.


george alikuwa ameshafanya kila kitu na ndugu wa ibrahimu walikuwa wamesha tolewa na sheria kwenye nyumba ya akina abdul ila kulikuwa na utata na hasara maana wale ndugu wa ibrahim walikuwa tayari wameshauza baadhi ya vitu vyandani kama tv friji na vingine vya thamani lakini habari njema ni kwamba ndugu wale walikuwa wameondoka na kuicha nyumba, mama abdul hakutaka wachelewe walikaa kidogo na kuanza safari ya nyakato nyumbani kwao na george akampa mama abdul laki mbili na na kumuambia abdul waonane badae(habari za uporaji wa mamilioni zikabaki kuwa siri ya abdul na george]


abdul violla mama abdul na mdogo wake mama abdul baada ya kufika kwenye nyumba yao ambayo ndani kulikuwa ovyo ovyo baada ya kupumzika kidogo mama abdul alikaa na mwanawe kimaongezi "mwanangu mimi nilishangaaa naambiwa eti baba yako amekamatwa akiwa kwenye biasha za madawa ya kulevya na amepelekwa kituoni....cha ajabu ni kwamba hawa kutaka nionane nae ndani ya wiki mbili nilienda kwa r.p.c nikitaka wanioneshe kituo alicho wekwa baba yako lakini walikataa...na baada ya siku kadhaa taarifa ikatoka eti baba yako kajiuwa akiwa kituoni hiyo ni kwel mwanangu" alisema mama abdul huku akilia, kabla abdul haja jibu chochote wakasikia mtu ana gonga hodi mlangoni, abdul akaenda kufungua abdul akashangaa kumuona afande huseni


hussen askari ambae aliagana nae miaka sita iliyo pita huku hussen akimuahidi abdul kuwa atamsaidia beka.


leo kuna jambo lilikuwa limemleta hussen [hussen alikuwa ameshafanikiwa kujua kuwa ibrahimu baba abdul aliuwawa na hii taarifa ndio lilo mpeleKa kwa kina abdul]

nani alimua baba abdul na kwanini alimua ?




abdul alihisi kumfahamu hussen ila hakukumbuka vizuri

"karibu ndani" alisema abdul na hussen akaingia.

hussen alimsalimia mama abdul na kumpa pole kwa yaliyo mkuta , hussen alidai kaja kumsalimia

na alikaa kidoga na kuaga kuwa anaondoka ila akaomba aongee faragha na abdul , abdul na hussen wali toka nje na kusogea pembeni ya geti

"abdul unanikumbuka?" aliuliza hussen

"hapana"jibu kutoka kwa abdul huku akimtazama kwa makini, hussen akamkumbusha kuwa yeye ni yule askari alio muahidi kumsaidia beka,ndipo kwa mara ya kwanza abdul akamkumbuka rafiki yake beka ,abdul tangu aiengie kwenye matatizo ya kifo cha baba yake alikuwa hakukumbuka kabisa kuhusu beka .

"hah afande niambie rafiki yangu beka yuko wapi" abdul aliuliza kwa shauku , hussen ikabidi amweleza utata wa kesi ya beka na alimwambia beka tangu akimbie hakuonekana tena

"abdul leo kuna taarifa nataka kukujuza za kuhusu kifo cha baba yako na nitahitaji maelezo machache kutoka kwa ko ili tujue ni nani alimua baba yako"alisema hussen abdul akawa na hamu ya kusikia mengi kutoka kwa hussen

"baba yako aliuwawa maana kuna ushahidi mwingi unaonesha baba yako aliuwawa"

"please niambie nani kamuua baba yangu" alisema abdul kwa msisitizo huku akiwaza kufanya mauaji pindi akimgundua alie muua baba yake.

" baba yako ameuliwa na drug dealer mwenzake....inaonekana mtu huyo yupo ndani ya serekali" alisema hussen na kusababisha maumivu kwenye moyo wa abdul

"no baba yangu hakuwa mfanya biashara wa madawa ya kulevya" abdul alisema huku machozi yakimtoka..

"abdul usikatae nina ushahidi wa ni nacho kiongea...tuachane na hayo shida yangu nimjue mtu alimfanyia hila baba yako....mazingira yanaonesha muaji ni mtu mkubwa serekalini .... So naomba uniambie ni mtu gani serekalini alikuwa anakuja kwenu mara kwa mara ambae alikuwa na urafiki na baba yako?" aliuliza hussen, abdul alikaa kimya kidogo akifikiria

"hapana sijawahi kumuona then maisha yangu yalikuwa ya boarding mara nyingi sikuwa nyumbani but why unasema muaji ni mtu wa serekalini?" aliuliza abdul

"kipindi vyombo vya habari vinatangaza kuwa baba yako amekamatwa na polisi kwa kosa la kujihusisha na biashara za madawa tayari baba yako alikuwa amesha kufa mwili wake ulikuwa upo hosptal...waandishi wa habari walipo uliza kuwa baba yako centrol gani serekali haikujibu chochote...inamaanisha alikuwa amekufa na mtu anae husika ni mkubwa serekalini na niyeye aliamulu vyombo vya habari vitangaze habari ile bila mtuhumiwa kuonekana ...nili fanikiwa kuona gari ya baba yako ambayo wanadai kuwa alipata ajili kipindi anakimbia maaskari kioo cha mbele cha gari ya baba yako kilikuwa kina mtundu mawili ya risasi hii ina maanisha alishambuliwa kabla hajafa.. gari ime pondekapondeka but ule mpondo inaonesha ni wa nyundo namaanisha ile haikuwa ajali ila wametengeneza mazingira ... abdul nenda umuulize mama ni kiongozi gani alikuwa na urafiki na baba yako" alisema hussen na kuondoka na kumuacha abdul .

abdul alipigwa butwaa aliamini baba yake ameuwawa swali ni nani alifanya vile na kwanini?

abdul alienda kwa george na george alimkabidhi milioni tano kama malipo ya mwisho upande wa george ile kazi ya uporaji wa milioni mia nne ndo ilikuwa kazi yake ya mwisho aliamini mamilioni aliyo pata angeweza kufanya biashara na george alimuambia abdul akiwa na tatizo amfuate.

abdul aliweka zile pesa kwenye akaunti yake na kurudi nyumbani akijiuliza afanye biashara gani.. abdul alijifikiria ajiendeleze na masomo akiri ya abdul haukuwa tayari kurudi masomoni matatizo makubwa aliyo yapitia katika siku chache yalikuwa yameiathiri akiri ya abdul mawazo aliyo kuwa nayo abdul juu ya kifo cha baba yake yalichukuwa nafasi kubwa kwenye kichwa chake asinge weza kumudu masomo ya chuo kwa ufupi abdul abdul alikuwa hana idea na masomo kabisa.

mama abdul na violla alikusanya dokoment zote za kazi ila hakuiona kadi yake ya benk hakuiona

"...kadi ya benk ya marehemu mume wangu aliondoka nayo kabla hajapata matatizo na kipindi anapata matatizo alikuwa nayo na ilipotea..but kadi yangu ilikuwa humuhumu" alisema mama abdul kwa hudhuni . waliendelea kutafuta sana lakini hawa kuipata "itakuwa imechukuliwa na hawa ndugu wa marehemu mume wangu" ndio lilikuwa wazo la mwisho kwa mama abdul ...akaamua aanze kukusanya dokoment ili siku zitakazofuata aanze kufuatilia mafao ya kazini kwake kwani kwa matatizo aliyo yapitia asingeweza kuendelea na kazi

abdul katika milioni tano aliamua kutoa laki kadhaa na kununua friji tv na kulipa madeni ya bili ya maji

"mmh abdul hela umetoa wapi?" swali kutoka kwa mama abdul

"ah nimetoa kwenye akaunti yangu nyingine kaniongeze meja george" huu ulikuwa uongo wa abdul kwa mama yake abdul hakutaka kabisa mama yake ajue kuwa alifanya kazi ya uporaji na hata kufanikisha gharama za matibabu ya mama yake india ..mama abdul alichojua alisaidiwa na meja katika gharama za matibabu hakujua kama mwanae alidiriki kushika bunduki.( siku zote abdul aliishi na siri nzito moyoni.)

abdul aliamua kufungua flem ya M PESA na alimdanganya mama yake kuwa amekopeshwa mtaji na meja

"so my son.. masomo ndio basi tena?" swali kutoka kwa mama abdul

"ah mama matatizo si unayaona nitaendelea vp na masomo...acha niayaanze maisha si unaona sasa hivi naitwa baba" abdul alijibu majibu yenye vigezo vya kumlizisha mama yake.

muda ulifika na violla akafunga safari kurudi dar akiwa na mtoto wake na kumuacha abdul akiwa ndo kwanza anaanza kutafuta maisha violla alirudi dar kwa ajiri ya kuanza masomo ya chuo.

mama abdul aliendelea kufuatilia mafao yake huku afya yake ikiwa sio nzuri kidogo kutokana na msongamano wa mawazo

abdul alimuuliza mama yake kuwa ni kiongozi gani serekalini alikuwa na urafiki mkubwa na marehemu baba yake

"kwa kwel mwanangu baba yako alikuwa na marafiki wengi tu wakubwa" ni jibu kutoka kwa mama abdul ikabidi atulie huku akitafuta njia nyingine za kumjua mtu alie muua baba yake .

siku ya kufa nyani miti yote hutereza ...M PESA aliyo fungua abdul ilikuwa haina wateja wengi kana kwamba zile pesa zilikuwa na mkosi ...na hata mtaji pia ulianza kuporomoka ukizingatia na pesa ya matumizi alikuwa anatoa mule mule kwenye mtaji .

mawazo ya maisha pamoja na maswali mengi kuhusu kifo cha ibrahim ili sababisha abdul awe mtu wa mawazo na ukimya wa kuhuzunisha ukamgubika abdul ama kweli ukimya na huzuni ulikuwa umependa kuweka makazi kwenye maisha ya abdul abdul akawa mtu wa hudhuni na simanzi na mda mwingine alitoa chozi kila alipojua yeye amesha kuwa baba.

hussen nae alimtembelea mara kwa mara abdul na kupanga mikakati ya kumjua muuaji... siku zote hussen aliwaza kama angebahatika kuipata simu ya marehemu ibrahimu kidogo kazi ingekuwa nyepesi lakini simu haikuonekana. pamoja na hayo hussen hakukata tamaa alizamilia kumjua muhusika wa mauaji.

kama ilivyo kawaida ya nchi yetu mtu akianza kufuatilia mafao yake lazima atazungushwa kwa miezi kadhaa ndivyo ilivyo kuwa kwa mama abdul mama abdul aliendelea kufuatilia mafao yake huku akiwa ana pigwa kalenda kila siku kiukweli ilikuwa ni simanzi ndani ya nyumba ya mama abdul. sio abdul sio mama abdul wote walikuwa kwenye simanzi kulikuwa hakuna wa kumbembeleza mwenzake ndani ya nyumba walikuwa wawili tu abdul na mama yake...."mwanangu hii ni mitihani ya dunia usisikiteke yata pita" ni maneno ya mama abdul aliyo kuwa ana mwambia abdul huku hata yeye akijizuia asilie mbele ya mwanawe mpendwa...wimbi kubwa la simanzi lili ipiga nyumba aliyo ishi abdul na mama yake.

abdul alikuwa amekaa kwenye flem yake cha M PESA kajiinamia akiifikiria dunia na akifikiria ni vipi ange weza kurudisha furaha ya mama yake iliyo potea kabisa....mara simu ikaita abdul akaangalia mpigaji alikuwa ni meja george

"hellow meja" aliongea abdul

"ah abdul unaweza ukaja home now" aliuliza george

"ndio"

"basi njoo kuna mchongo" alisema meja na kukata simu, abdul akafunga duka na kuanza safari ya kwenda kwa meja george.

abdul alimkuta meja akiwa na watu wa makamu watatu ambao hawa kuwa wageni kwenye macho ya abdul ,baada ya salaam george alimwambia kuwa wale vijana walimuhitaji walikuwa na dili...abdul ikabidi awa sikilize

"abdul kesho kuna milioni ishirini na tano zinaingia kwenye duka moja la airtel money tuna hitaji uwe dereva wetu"alisema baba mmoja kati ya wale watatu

"na hii ni rahisi sio kama ile ambush mlio ifanya majuzi...sisi tutakuwa ndani ya duka wakati pesa zinaingia...tuta waweka chini ya ulinzi...muda wote wewe utakuwa barabara ya tatu mbali na lile duka ukitusubiri....tuta kupa milioni saba" jamaa mmoja akaongezea.

abdul alijifikiria sana kuhusu ile kazi na alifikiria hali ngumu ya maisha yao nyumbani kwao abdul alihisi zile milioni saba angeweza kuzifanyia biashara na kuweka sawa mazingira nyumbani kwao abdul akawaza afanye ile iwe kazi yake ya mwisho

"hamna shida itakuwa saa ngapi?" alisema abdul,

"kesho saa mbili usiku"

abdul na watu wale watu watatu walipanga mikakati na hatimae kuagana huku wakiwa wamepanga kesho wafanye uporaji ule.

ilikuwa saa mbili kasoro gari moja aina ya tex ilikuwa imeegeshwa pembeni ya barabara, ndani ya tax alikuwemo abdul aliekuwa anajifanya anasoma gazeti ,siku hiyo abdul alikuwa amemuaga mama yake kuwa kaenda kuangalia mpira kumbe alikuwa kaja kwenye uporaji.

abdul muda mwigi alikuwa anaangalia saa yake ya mkononi ..mara akasikia milipuko ya risasi ikitokea kule walipo kuwepo, abdul akawasha gari akawa anasubiria wakifika tu aondoe gari eneo lile.

siku ya matatizo ni siku ya matatizo tu!

wakati abdul anaendelea kuwasubiri wenzake kumbe hatua kama miambili kutoka pale alipokuwa abdul .. kulikuwa kuna balaa kubwa polisi walikuwa kwenye gari lililo endeshwa na afande hussen! kina afande hussen walikuwa wanawakimbiza watu wawili walio kuwa na mabegi migongoni wenye asiri ya kiarabu

watu hawa wawili walikuwa wanakimbia kwa miguu na walikuwa wameiacha gari ya polisi kama hatua mia walikuwa kwenye ile ile barabara aliyokuwepo abdul watu hawa wakiwa wanakimbia kwa kasi ndipo wakaiona tax aliyo kuwemo abdul

watu hawa wakaona ni bora wakaitumie tax ile kukimbia maaskari

watu hawa walikuwa na bastola mikononi mwao na wao walionekana kuwa wa harifu , watu hawa waliisogelea tax ya abdul na kufungua milango, abdul alishtuka kuona watu wawili asio wajua wakiingia kwenye tax yake na kisha waka muwekea bastola kichwani

"endesha gari na ukimbize kabla hatuja kuua" alisema mtu mmoja kati ya wale wenye asili ya kiarabu wawili alie kuwa na mwili mkubwa

abdul alipigwa butwaa na kushangaa wale watu ni kina nani

"endesha gari we malaya au unataka tukuue tuendeshe wenyewe" alifoka mmoja kati ya wale walio ingia kwenye gari na abdul akaanza kuitekenya gari ili aanze kuondoa.

nyuma ya tax ya abdul kama hatua themanini kulikuwa kuna gari la askari likiendeshwa na hussen .

hussen aliwaona wale watu walivyo ingia kwenye tax ya abdul ,hussen akaongeza mwendo wa gari lake aina ya toyota ya polisi ili kuiwahi ile tax aliyo kuwemo abdul.

haya abdul kaingia kwenye majanga..nyuma kuna afande hussen na askari ,..afande hussen ameshawaona wale watu anao wafukuzia wameingia kwenye tax na yupo kama hatua themanini kuifikia tax ile.

ndani ya tax abdul ame shurutishwa awashe gari na waharifu wawili....kumbuka abdul alikuwa anasubiria wenzake ambao wameenda kupola pesa kwenye duka la airtel money ... na hawa watu wawili wenye asirli ya kiarabu wame mshurutisha abdul awashe gari aondoke...je abdul atawaacha wenzake?

kumbuka kuna gari la askari linalo endeshwa na hussen abdul atachomoka hapo?

hawa wenye asili ya kiarabu ni kina nani na kwanini wanakimbizwa na polisi?



abdul alianza kuondoa gari huku akiwa na kihoro kwani alikuwa amesha ona gari la polisi na lilizidi kumkalibia

mara ghafla watu watatu mmoja wao akiwa na box kubwa walitokea kwenye uchochoro wakiwa na bastola mkononi na kuiwahi tax ya abdul walikuwa ni wale watu watatu wenzake na abdul.. abdul alishituka kuwaona wenzake wakija mbio kuifuata tax abdul akatoa rock ya milango .

wenzake na abdul wale watu watatu walishangaa kuona abdul akiwa ameanza kuondoa gari wakati wao walikuwa bado hawajaingia na ndipo kwa kihoro wakaishuhudia gari ya polisi iliyo kuwa karibu kama hatua arobaini

watu watatu hawa kuwa na njia nyingine zaidi ya kufanya maamuzi ya haraka, watu kwa haraka walianza kuitupia risas ile gari ya polisi huku wakirudi nyumanyuma waki iwahi ile tax

"abdul simamisha gari vp we" alisema mmoja wa wale watatu huku wakizidi kufyatua kuelekea kwenye kioo cha mbele cha gari la polisi alilokuwemo hussen... hussen alihamaki sana na kufunga breki ghafla na kulala chini ndani ya gari ili asipatwe na risasi .... abdul aliliona balaa lile na aliwaona wenzake wakirudi kinyume kinyume kuiwahi tax iliyokuwa kama hatua kama tano...abdul akajua maamuzi yalikuwa mikononi mwake kama angefanya kosa dogo tu linge gharimu na kuzikosa pesa walizo iba kwenye duka la airtel ambazo zilikuwa mikononi mwa wale wenzake watatu aliona hakutakiwa kuogopa bastola za watu wawili walio muelekekezea ndani ya tax

abdul alipiga brek ya ghafla na hapo hapo akabadilisha gia ya gari na kuanza kurudi nyuma kwa kasi..."pumbavu nini wewe" alifoka mmoja wa wale walio kuwa wamemshurutisha abdul

abdul haku jibu kitu alikuwa kaisha fanya maamuzi ndani ya sekunde saba abdul alirudisha GARI NYUMA na kuwafikia wenzake wanne ambao waliacha kushambulia gari ya polisi na kila mmoja akafungua milango ya tax ile kwa pande zote mbili mmoja aliingia kwenye mlango wa mbele akaingia na kushangaa kukuta midomo ya bastola mbili ikiwa kwenye kisogo cha abdul ..kwa wepesi usio tarajiwa huyu aliengia kwenye mlango wa mbele aliwalekezea bastola wale watu wawili walio muekea bastola abdul ...wale wenzake na abdul wawili walifungua miliango ya nyuma kila mmoja upande wake na wao wakashangaa kukuta watu wawili wakiwa wamemuelekezea bastola abdul ...wenzake na abdul na wao wakawaelekezea bastola wale jamaa "whats going abdul" alifoka mmoja kati ya wenzake na abdul..."hawa maboya wamenizingua ...ingien haraka tuondoke tukimbie polisi ...hawa tuta malizananao mbele kwa mbele" alipaza sauti abdul sauti ya abdul ilikuwa kubwa na hussen aliisikia na akahisi kuitambua. wenzake na abdul wakaingia wakiwa wamewaelekezea bastola wale jamaa wawili jamaa wawili wakawa wame elekewa na midomo ya bastola mitatu huku wao wakiwa wame muelekezea bastola zao abdul .


walikuwa wamebanana ndani abdul akaindoa gari kwa kasi huku bastola mbili zikiwa zime muelekea kisogoni ...


hussen baada yakuona ile tax imeondoka aliinuka na kuwasha gari lake " jamani mpo wazima"aliuliza hussen kwauliza askari waliokuwa nyuma ya gari toyota body "tuko wazima afande "baadhi ya askari walijibu kwa wakati tofauti "acha tuwafuate " alisema hussen na kuwasha gari huku akiri yake ikifikiria mtu alio hisi ni abdul kwanza amesikia wale watu watatu wakilitaja jina la abdul na kingine aliisikia sauti ya abdul na kuifahamu ,hussen akawa anakimbiza gari kuiwahi tax ya abdul...


*watu wa wili walio muwekea bastola abdul*


hawa watu wawili walio muelekezea abdul bastola ,walikuwa mtu na mdogo wake pia walikuwa wafanya biashara za madawa , walikuwa wamekuja pale mjini kwa ajili ya kufanya biashara baada ya kufanya biashara na kuachana na wafanya wenzao, wao wakiwa na madawa ya kulevya wakaingia ndani ya gari yao iliyo endeshwa na mdogo wao "dogo washa gari tuondoke" alisema mmoja alionekana kwa nimkubwa ...lakini kabla hajawasha gari mara wakamuona trafki akigonga kioo cha gari yao yule mdogo wao akashusha kioo "...jamani nina mashaka nanyinyi sogeza gari pembeni " alisema yule trafki aliovaa nguo nyeupe nadhifu

"ah afande acha tuje tuyaongee " alisema yule alio kuwa mkubwa huku akishuka akiwa na beg mgongoni mwake na mwenzake akamfuata

wakamsogelea trafki na kumsogeza pembeni kidogo trafki akawa amelipa mgongo gari la hawa wafanya biashara...waliongea kwa mda huku wakionekana kuto afikiana ,.."ah hapana yaani nyi warabu kabisa mnafanya biashara then mnipe laki nne...kama hamuongezi pesa hapa acha nipige simu kituoni" alisema trafki kuwaambia watu hawa wenye asili ya kiarabu...trafki aka anajifanya kuchukua radio call ile awatishe hawa watu wenye asili ya uarabu,...yule mdogo wao aliekuwa kwenye gari alimuona yule trafki akitoa radio call ili apige kituoni...huyu mdogo wao akaona kaka zake walikuwa wanamchelewesha yule trafiki mdogo wao akachukua bastola na kumlenga yule trafki ...akatulia kama sekunde tano kisha akabonyeza kifyatulio cha (traiga) na hapohapo yule trafki akahisi kasukumwa na kitu kizito huku akipata maumivu makali mgongoni akageuka huku akihisi maumivu makali lakini alipogeuka tu risas mbili zikapenya kifuani na kumuangusha chini huku akipiga kelele bastola iliyotumika ilikuwa imewambwa kitu cha kuzuia sauti ya risas..."pumbavu harooney umefanya nini" alifoka yule alionekana kuwa mkubwa kumfokea mdogo wake mwenye asili ya kiarabu

"twenden tukimbie ange tusumbua" alisema harooney mdogo wa wale wafanya biashara wa wili...harooney alikuwa kafanya kosa kubwa! kwani wakati yote yanatendeka afande hussen usiku huo alikuwa kwenye gari pamoja na askari wengine akipita barabara ya upande wapili na ndipo alipo muona yule trafki akibishana na wale wafanya biashara wawili na hussen akiwa anajiuliza wanabishania nini ndipo alipo muona yule trafki akianguka na kupiga kelele za maumivu ... hussen aliekuwa barabara ya upande wa pili alishuka na kupiga risas hewani ili wale watu wenye asili ya kiarabu wajisalimishe .

hawa watu wawili wakiwa bado hawajaingia kwenye gari walishtushwa na mlipuko uliopigwa hewani na hussen wakabaki wameduwaa...harooney alivyo sikia mlipuko alihamanika akahisi hatari na hapo hapo akawasha gari na kuiondoa kwa kasi kuwaacha kaka zake kwani alihisi kama ange wasubiri wange mponza "harooney simama" wale jamaa wawili walipaza sauti lakini tayari harooney alikuwa amesha ondoka walikuwa hawana lingine zaidi ya kuanza kukimbia kwa kasi kwa miguu.

"askari wawili shukeni muwakimbize kwa mguu wale wawili mimi ngoja niendeshe gari kuifuata ile gari" alisema hussen na kuingia kwenye gari na kuanza kukata kona akiwa na baadhi ya askari kwenye ile gari ya polisi aiwahi ile tax...askari wawili walianza kuwakimbiza watu wale wawili .

hawa watu wawili walipo ona wanakimbizwa na askari wawili walisimama ghafla wakatoa bastola zao zenye viwambo vya kuzuia sauti na kuwashambulia wale askari wawili kwa kushtukiza , askari wawili walipatwa na risasi na kuanguka chini, wafanya biashara wawili wakaendelea kukimbia kwa kasi .

hussen wakati anakata kona alishudia askari wake walio wakimbiza waharifu wakishambuliwa na kuanguka chini hussen akabadili dhamila yake ya kuikimbiza gari ya harooney na kuanza kukata kona ili awakimbize wale watu wawili,

ilimchuka muda kidogo hussen kukata kona na kushika barabara waliyo kuwepo waharifu wawili lakini alifanikiwa kushika ile barabara na kuanza kuwakimbiza waharifu waliomuacha kama hatua mia moja.

sehemu walipokuwa wanakimbilia hawa waharifu wawili ndio kule alipo kuwepo abdul akisubiria wanzake walioenda kupola pesa kwenye duka la airtel,

wakati watu hawa wawili wenye asili ya kiarabu wakikimbia ndipo walipo iona tax aliyo kuwemo abdul ,watu hawa wakaingia kweny gari ghafla na waka mshurutisha abdul abdul aendeshe gari .....


<<*watu watatu kwenye duka la airtel money*


watu watatu ambao niwenzake na abdul walifanikiwa kuweka ambushi ndani ya duka la airtel wakati gari la kampuni likeleta pesa pale,

bahati nzuri ilikuwa upande wao kwani walinzi wapale walikuwa wachache ,walifanikisha kuwauwa baadhi ya walinzi na

wakachukua box lenye pesa na kuanza kukimbia huku wakipiga risasi hewani wakaingia kwenye uchochoro kuelekea ilipokua tax ya abdul.


ni kweli walifanikiwa kuiba zile pesa lakini tatizo ni kwamba...lile duka la airtel halikuwa mbali na benk flan iliyokuwa inalindwa na polisi wengi...polisi walisikia ile milipuko ya risasi iliyotokea kwenye duka la airtel...polisi kama polisi lile tukio lili wahusu polisi wakaingia kwenye gari na kuwasha kingola wakaanza kuelekea kwenye duka la airtel.


polisi wakaelekezwa uchochoro walio pitia wale watu watatu walio pola pesa kwenye duka la airtel, kwakuwa gari isingeweza kupita kwenye ule uchochoro ikabidi askari watatu washuke wapite kwenye ule uchochoro wakifuatwa na na walinzi wa duka la airtel

gari ka polisi likiwa linapiga king'ora likanyoosha barabara ili likazunguke kwenye barabara kubwa ...



abdul akiwa bado kwenye kiholo hapohapo alishuhudia gari ya polisi ikikata kona na kuja kwenye barabara aliyokuwepo abdul alihamaki na kujikuta akikata kona huku akinusurika kuingia kwenye mtalo kitendo cha abdul kuacha barabara na kuipisha ile gari ndio ilikuwa salama kwao kwani ilikuwa kidogo tu wagongane ,gari ya polisi ili yumba kidogo na hapohapo wale wenzake na abdul kwa kupitia dirishani wakaanza kuifyatulia risasi ile gari ya polisi ovyoovyo wakawa wameacha kuwaelekezea bastola wale watu wawili wenye asiri ya kiarabu .

askari aliekuwa anaendesha alihamanika kwanza amekosakosa kugongana na tax ya abdul pili gari yake inashambuliwa na risasi dereva kosa alililo lifanya ni kuhamanika na na kugeuza macho yake kule ilipo tax ya abdul !

"mamaaa" yowe la hofu lili mtoka dereva baada ya kuona anakutana uso kwa uso na gari..hapo hapo kishindo kikubwa kikasikika eneo lile!.

ilikuwa ajali kati ya lile gari la polisi na gari la hussen.

hussen alikuwa anaendesha gari kwa kasi kuiwahi tax ya kina abdul lakini ghafla akaona gari nyingine ikikosakosa kugongana na ile tax na hapo akasikia milipuko ya risas ...hussen alijaribu kuikwepa ile gari lakini walikuwa wamesha karibiana na walikuwa wapo kasi wote "mtumeee" yowe lilimtoka hussen na hapohapo gari lake likavaana na gari ya polisi puuh!ilikuwa ni bonge la kishindo baina ya gari mbili

"wow yeah wame kula jeuri yao "abdul alipiga kelele kwa furaha baada ya kuona ile ajali ,abdul akairudisha tax barabarani kisha akachochea mwendo na kushika barabara inayo kwenda nyegezi

"uuuh tuna kurespect abduuu" alisema mmoja kati ya wale wenzake na abdul kama kawaida yake abdul aliendelea kuchochea speed kana kwamba mwendo alioendesha ulikuwa mdogo....wale watu wawili wenye asiri ya kiarabu walibaki wamepigwa butwaa hawakuamini mambo yaliyo kuwa yakitokea kwani walishuhudia abdul alivyo kosakosa kupata ajali na walisikia ule mlipuko nyuma na sasa walibaki wanashangaa gari ilivyo kuwa inaendeshwa na abdul kiukweli walihamanika na walijawa na woga...wenzake na abdul waliona hawa wenye asiri ya kiarabu kuwa walikuwa wamezubaa na muda huo bastola walikuwa hawaja muelekezea abdul ..."haya na nyie msijitikise...abdul imekuwaje wamekuteka" alisema mmoja wa wenzake na abdul na kuwaelekezea bastola wale watu wenye asili ya kiarabu .

"...ah hawa maboya me nilishangaa tu wanaingia ndani ya gari na kuniambia niwashe gari...then wanaonekana walikuwa wanakimbizwa na gari la polisi lililopata ajali"alisema abdul huku akiwa makini kwenye uskani

"nyie ni kina nani... hemu lete kwanza hilo beg"alisema mmoja wa wenzake na abdul na kumnyang'anya yule mwenye asiri ya kiarabu na kufungua zipu hapo akapatwa na mshtuko hakuamini alicho kiona ndani ya beg "...wazee safari moja imeanzisha nyingine...hawa wajinga wana madawa ya kulevya... pumbavu kwa kuwa mlituongezea matatizo tuna waua na madawa tuna chukua tukale maisha" alisema yule mmoja wa wenzake na abdul huku akizidi kuwa elekezea bastola...hawa watu wenye asili ya kiarabu walitetemeka na hawakuwa na jinsi walikuwa wameingia choo cha kike ...

*hussen*kwenye*ajali*

ajali ilikuwa mbaya na kubwa gari ya hussen ilipinduka na kusababisha maafa , hussen alipoteza fahamu kabisa na damu nyingi zilimtoka kutokana na majeraha .

baada ya munda kidogo walitokea wasamalia wema na kuwapa msaada kina hussen na kuwapeleka hosptal hussen alikuwa hajitambui kabisa..

*abdul *na* wenzake* ndani *ya* tax*

"nyie ndo kidogo mtuponze sababu ya madawa yenu so sisi tuna waua maana kifo chenu ndo pesa yetu" yule mmoja wa wenzake na abdul aliendelea kuongea huku akionesha kuwa amedhamilia "jaman msituuwe hatukujua kama mlikuwa kwenye mission...tuambieni tuwape shingapi but msituue sisi wote tunatafuta maisha " alisema yule mmoja mwenye asili ya kiarbu alionekana kuwa mkubwa..."wewe lazima mfe"mwenzake na abdul alipayuka

"oya wote watafutaji usiwauwe...hey mtatupa shiling ngapi" sauti ya abdul iliyo sababisha patokee ukimya na wenzake wa kashangaa

"ah abdul hela ya nini haya madawa tu ni hela"alisema mwenzake na abdul

"jamani kama madawa chukueni but msituuwe" alisema mwenye asiri ya kiarabu kwa kutia huruma

"but ujue ni msala kwanza soko hulijui then ni hatari ukikamatwa...we acha watupe hela" alisema abdul huku akili yake ikiwaza pesa, na hata wenzake waliona wazo zuri

"sasa wata tupa shiling ngapi?" aliuliza mmoja wa wenzake na abdul

"tugawane faida tutawapa milioni mbili"alisema mwenye asiri ya kiarabu

"nini we unaona hili box limeja mamilioni huwezi kutupa vimilioni viwili" alifoka yule mmoja wa wenzake na abdul huku akigusa box lenye pesa walizo pora...

mgogoro uliendelea hatimae watu wale wawili wenye asili ya kiarabu waliafikiana kuwa watawalipa kina abdul shilingi milioni tano lakini tatizo ikawa ni kwamba hawa waarabu hawakuwa na pesa muda ule wakawaomba kina abdul wawaamini na kuwa waende mpaka kwao ndo wakawape hizo pesa ikawa utata mwingine kina abdul waliona proses itakuwa ndefu kipindi yote yanaendelea abdul alikuwa anaendesha tax kwa kasi na sasa alikuwa amesha acha barabara ya nyegezi na alikuwa kaingia kwenye barabara ya vumbi " nyumbani kwenu wapi? "abdul aliwauliza hawa watu wawili

"mkolani"alijibu mmoja, abdul akakaa kimya kwa muda mara ghafla akasimamisha gari. "oya nyie shukeni tunawaacha hapa mtusubiri tunaondoka na madawa yenu kama poni but fasta tunarudi mkatupatie hizo milioni tano nasi tutawapa madawa yenu" alisema abdul ,wenzake na abdul waliafikiana na abdul na walimuona abdul ni mtu anae ona mbali kwani hawakutakiwa kwenda na hawa waarabu kwenye gereji yao na maamuzi aliyo yafanya abdul ya kuchukua madawa na kuondoka nayo kisha kuwaacha waarabu wakiwa subiri ilikuwa ni maamuzi mazuri kwani waarabu wasinge ondoka kuyaacha madawa yao ya kulevya.

wale waarabu wakashuka na abdul akawasha gari na kuondoka kwenye gari wakiwa na madawa na bastola za wale waarabu.

abdul aliendesha gari haraka huku kichwa chake kikiwa kinawaza pesa za wale waarabu kwani alijua hata angepata mgao wa milioni moja na nusu ingemsaidia .

abdul aliendesha gari mpaka kwenye ile gereji yao ya D.M wakapaki lile gari na kudhihifadhi zile pesa walizo iba kwenye duka la airtel kisha wakachukua gari nyingine tofauti na ile tax abdul akaingia kwenye gari na kuanza kuiondoa na kurudi kwa wale waarabu .

waarabu walipokuwa wanawasubiri kina abdul walikuwa wamejawa na woga lakini hawakutaka kuondoka kwani madawa yao yenye thamani yalikuwa mikononi mwa akina abdul.

walisimama kama dakika kumi na ndipo wakasikia muungurumo wa gari huku mwanga wa taa ukiwamulika gari ilisimama karibu yao na waarabu wakaingia baada ya kujua walikuwa kina abdul ..safiri ya kwenda kwa wale waarabu ikaanza .

abdul aliendesha gari mpaka mkolani na hatimae wakafunga brek mbele ya mjengo mkubwa wa kifahari

"tumefika acha tukawaletee pesa zenu" alisema yule mwarabu huku wakianza kuinuka lakini hapohapo abdul akatoa bastola na kuwageukia kisha akawaelekezea wale wenye asili ya kiarabu watu hao wakapigwa na butwaa hata wenzake na abdul walimshangaa abdul

" inabidi pesa aendee mmoja mwingine abaki kama poni msije mkatugeuaka mkaja na kundi lenu hapa" alisema abdul huku akiwa amewakazia macho...mambo aliyo kuwa anafanya abdul ni makubwa na alikuwa anajua mbinu na tahadhari kana kwamba alikuwa anamiaka kumi kwenye ile kazi ...abdul alijua wale waarabu wangeondoka wote kuleta pesa kulikuwa na hatari ya kugeukwa na hatimae kupoteza maisha ...hata wenzake na abdul waliona abdul alikuwa na uwezo wa kufikiri mambo ya mbele.

ikabidi yule mwarabu alieonekana mkubwa akaendea pesa kwenye jumba lao,

ndani ya tax wali baki kina abdul wakiwa na yule mwenye asili ya kiarabu.

baada ya dakika kama saba yule aliendea pesa alirudi akiwa na bahasha ya khaki na kuwapa kina abdul, mmoja wa wenzake na abdul akazihesabu na kuzikuta zipo kamili

"oya mkagueni asije akawa na bastola tukiondoka atushambulie" alisema abdul huku akizidi kuthibitisha umahiri wake wakufikiria na kuweka tahadhari ya mambo yajayo wenzake wote mawazo yao yalikuwa kwenye pesa, mmoja wa wenzake na abdul akatoka ndani ya tax na kwenda kumkagua yule mwarabu alieonekana kuwa mkubwa na hakumkuta na siraha... kina abdul wakamuachia yule mwarabu na abdul alianza kuwasha gari aondoke

"samahani abdul umetusaidia sana ... nitajie namba zako kesho nikutumie pesa kwa ajili ya ahsante" alisema yule mwenye asiri ya kiarabu , abdul akataja namba zake za voda na kuondoa gari kwa kasi

muda ulikuwa ni saa nne na kina abdul tayari walikuwa wamesha paki gari gereji na kuchukua gari nyingine na kwenda kwa george wakiwa na pesa zote walizo pora na zile za waarabu.

abdul siku hiyo hakulala kwao ila alimpigia simu mama yake na kumwambia atalala kwa rafiki yake

abdul alikuwa kachoka sana na alihitaji kupata muda wa kupumzika muda wote abdul alifikiria juu ya balaa alilo lifanya.

*nyumbani* kwa *waarabu*

wale waarabu wawili waliingia ndani na kumkuta harooney akiwa ameketi kwenye sofa "pumbavu we mtoto uhame humu ndani so leo ulitaka tufie jela" alifoka yule mwarabu

"hapana kaka mudy we mwenyewe uliona..ni bahati mbaya" alisema harooney

"umemuua trafki halafu umeona haitoshi umeamua kuwasha gari na kutuacha we ungekuwa sio mdogo wangu wa damu leo ningekuuwa" alizidi kufoka mudy

"kaka kama ningesema ni zubae ingekuwa balaa lingine kwani polisi wangetukamata kwa pamoja"harooney alijitetea

"ila kaka huyu dogo kila siku anatuletea matatizo yaani ipo siku atatuletea majanga zaidi ya haya " alisema yule mwingine alioitwa omary kisha akaendelea

"...kaka unajua yule jamaa ni hatari na anaonekana anaweza kama ungempata ingekuwa poa"

"jamaa gani?" aliuliza mudy

"si yule abdala sijui abdul...unajua kwa lile balaa la leo angekuwa mtu mwingine leo tungekufa kwenye ajali...na kingine jamaa anaonekana profession wa mambo ya mafia anafaa sana... kama tukimpata tutafanya biashara bila wasiwasi" omary alifafanua. haya maneno yali mwingia akirini mudy na mudy akaanza kupanga njia za kumpata abdul.

Abdul alikuwa yupo kwao baada ya kuchukua pesa zake swali kubwa na zito lililo muumiza akiri ni kwamba afanye biashara gani ili ajiandae na maisha ya baadae bado hakupata jibu na wakati akiwa anaendelea kuwaza simu yake ikaingia ujumbe abdul akafungua na ndipo akakutana na ujumbe ulio thibitisha kuwa kapokea laki saba kutoka kwa mudy , abdul alishangaa hakujua kuwa katumiwa na nani pesa akiwa bado anajiuliza ndipo simu ikaita kuangalia namba ilikuwa ngeni ikabidi apokee ,

"hellow me mudy tulio kuwa wote jana kwenye majanga..vp umeiona pesa "aliuliza na abdul akajibu "ndio" waliongea kidogo lakini kabla mudy haja kata simu alimuomba abdul waonane sehemu yoyote, mudy akamwambia abdul alikuwa na jambo muhimu

"eh bwana unaweza ongea sitakuwa na muda wa kuonana na wewe" alisema abdul ,ikabidi amueleze kuwa anamuhitaji kwenye biashara zake na atamlipa vizuri

"abdul mi nitakulipa vizuri...na kazi ya madawa sio hatari kama uporaji wenu ambao mnauza roho waziwazi" alisema mudy

"ebwana...jana mimi ilikuwa siku ya mwisho kufanya dili zile so tafuta mwingine" alisema abdul kwa ukali kidogo

"abdul karibia watoto wote wa viongozi nchini wanafanya dili hizi na hata baadhi ya wasanii so nita kushangaa wewe unae kataa kazi itakayo badirisha maisha yako....kazi rahisi kwenda kupokea madawa airpot na kuleta nyumbani kisha tuna ya sambaza..." alisema mudy

abdul akawa anajifikiria

"mara nyingi kila tunapo ingiza tunapata faida si chini ya milioni tano katika milioni tano nitakupa milioni moja na kwa wiki tuna ingiza mzigo mara mbili au mara tatu...jifikirie utakuwa unapata milioni mbili au milioni tatu kwa wiki hemu fikiria kijana" alisema mudy

moyo wa adul uliripuka kusikia milioni tatu kwa weki

"hemu nipe muda nifikirie"alisema abdul na kukata simu

milioni tatu kwa wiki ni pesa ndefu ambayo kwa abdul ingetengeneza maisha "kama niliweza kazi za kuvamia gari ya benk hii kazi ya madawa ni ndogo sana.... nitafanya kwa miezi miwili na nitaacha nitakuwa nimesha pata pesa nyingi na nitafungua miradi mikubwa hapa na nitaacha hizi kazi za haramu nafanya kazi miezi miwili itakayo badilisha maisha yangu " abdul alijiwazia huku akijipa vigezo vingi vya yeye kushiriki biashara zile haramu... tayari abdul alikuwa amesha ingiwa na tamaa.

abdul aliongea na mudy wakapanga abdul aende juma pili kwa ajili ya kuongea mengi.

jumapili ilifika na abdul akaenda kuchukuwa bastola kwenye gereji ya D . M kwa ajili ya tahadhari hakutaka kuwaamini sana wale waarabu.

abdul alikodi tax mpaka mkolani abdul akapiga simu na kumuambia mudy kuwa amesha fika na mara geti likafunguliwa abdul akashangaa kuwaona waschana wawili walio vaa nguo fupi waka mkaribisha abdul na kumuongoza mpaka ndani ya jumba la kifahari, abdul alishangaa kukuta watu wengi wakiwa wamejaa sebuleni wakinywa vinywaji mbalimbali abdul hakuamini kuona kwenye ukuta kuna kitambaa kikubwa cheupe kilicho andikwa kwa maandishi makubwa "YOU ARE WELCOME ABDUL" hii ilimainisha mgeni lasmi alikuwa ni abdul

abdul alivyoingia tu sauti kubwa ya mudy ikasikika "karibu abdul,... jamani huyu ndio THE ROCK abdul" alisema mudy na watu wote wakasimama na kuanza kumpa mkono abdul , mudy alianza kumtambulisha abdul kwa watu hawa wasio pungua ishirini watu hawa walikuwa wafanya biashara wenzake na mudy.

baada ya sherehe ile ya kumkaribisha abdul kuisha mudy na abdul walikaa na kuanza kupanga mipango ya kazi na hatimae abdul akaafikiana na mudy na abdul akachukwa nafasi ya harooney...

Harooney alikuwa kijana mkorofi tena mwenye roho mbaya na kuua kwake alikuwa kitu cha kawaida ni mara nyingi tu aliwahi kuuwa wafanya biashara wenzake na mudy kwa ajili ya tamaa ya pesa.

Harooney hakupendezwa na mapokezi ya abdul nyumbani kwao kibaya zaidi abdul alikuwa kachukuwa nafasi ya harooney, harooney alikuwa ameshaanza kumchukia abdul , abdul alikuwa na jina kubwa kwenye nyumba ya mudy. Harooney akaona njia pekee ya yeye kuwa na amani na kuchukwa nafasi yake ni kumuua abdu....



abdul aliamua kumfungulia mama yake duka la vinyawaji kwa bei ya jumla japo lilikuwa dogo .mama abdul akawa na maswali mengi zidi ya mwanawe wapi kapata pesa? "wewe abdul mimi ni mama yako nimekuzaa nimekulea nakujua wewe siku hizi umebadilika kwanza pesa ya huu mtaji ulio nifungulia umetoa wapi pesa?" swali zito lili mpa maumivu abdul kutoka kwa mama yake

"ah mama kuna rafiki yangu tulisoma nae aliya sikia matatizo yangu akawa kanitafutia kazi kwenye ofisi moja iliyoko geita inahusika na mambo ya madini" abdul alisema uongo ambao mama hakuuamini hata kidogo

"abdul elimu ulioishia ya form six huwezi kupata kazi unayo sema...na pesa ulizo nifungulia huu mradi umetoa wapi?" mama abdul alizidi kuuliza akiwa ana wasiwasi na abdul

"mama unaweza kusoma mpaka chuo but usipate kazi kila kitu kina kwenda kwa mjuano na mimi nimeipata kwa kujuana na rafiki yangu....mama hiyo pesa nilio fungulia huu mradi rafiki yangu kanifanyia mpango nimepewa mkopo" alisema abdul, mama abdul akakubali kwa shingo upande hakuyaamini maneno ya abdul

"mama kuna kitu nataka kukuomba sijui utanikubalia " abdul alimuuliza mama yake kwa upole

"kitu gani?"

"mama nataka nikapange chumba geita maana itakuwa karibu na ofisi" alisema abdul akiwa na mwawazo ya kuishi mbali na mama yake japo alimpenda kuliko kitu kingine!

"mwanangu baba yako kaniacha nikiwa mpweke nimebaki na wewe mwanangu furaha yangu uhai wangu...mwanangu abdul unataka kuondoka na kuniacha kwenye upweke huu...abdul kama ni kazi bora uache kazi but tuishi wote nyumbani bora tulale njaa but usiondoke mwanangu nakupenda wewe ndo furaha yangu ndani ya jumba hili nitaishi vipi bila kukuona mwanangu nakupenda" alisema mama abdul huku machozi yakianza kumdondoka..abdul alikuwa ndo kila kitu kwa mama yake mama abdul alimpenda sana abdul

"mama we ndo kila kitu kwangu nakupenda...yote sababu ya kazi mama nakuahidi kila siku nitakuja hapa mpaka nikuone ndo nilale mama please" alisema abdul akilia na kumkumbatia mama yake, abdul na mama yake wote wakawa wanalia,

mama abdul akaamua kumkubalia mwanawe japo hakupenda.

abdul baada ya kumbembeleza mama yake na kuwa amemuamini abdul akamuaga mama yake kuwa anaenda kulala geita ilikesho awahi ofsini . macho ya mama abdul yalimsindikiza abdul kwa hudhuni mama abdul alitaka muda mwingi awe na mtoto wake kwani alikuwa ndio furaha yake hapa duniani maskini ya mungu mama abdul hakujua kama mwanawe ameshaanza kushika siaraha na kusababisha baadhi ya vifo vya askari...na sasa abdul alikuwa ameingia kwenye mtandao mbaya wa madawa ya kulevya .

abdul alienda moja kwa moja hadi mkuyuni ambapo alikuwa amepata chumba abdul siku hiyo akanunua kitanda kizuri na godoro na kuweka kwenye chumba kile, abdul alikuwa amemdanganya mama yake kuwa ataenda kupanga geita na kumbe ameenda kupanga mkuyuni...abdul alikuwa ameamua kufanya hivi kwa sababu maalumu tena za msingi...abdul aliamua kufanya vile kwani alijua tayari alikuwa ameshaingia kwenye mtandao hatari abdul alijua kama ataendelea kuishi na mama yake ingekuja kutokea tabu siku polisi wakigundua anajihusisha na kingine hakutaka kabisa kina mudy na wafanya biashara wengine wagundue nyumba yao na anaishi na mama yake...kingine abdul alijua kama angeendelea kushi na mama yake ingekuwa rahisi kugundulika kwa mama yake kuwa anafanya biashara ya madawa ya kulevya.

Abdul akawa ameanza kazi kwa kina mudy kazi yake kubwa ilikuwa ni kwenda kupokea madawa airpoti na alishirhkishwa katika maswala ya uuzaji kitu ambacho kikamfanya abdul awe akupata umaarufu kwa wafanya biashara wengi.

kitika biashara ya madawa sio wote waaminifu, wengine huwa katika biashara wanaleta tamaa na kuhutaji wamdhulumu mfanya biashara mwenzao na hata kumuua , mara kadhaa abdul alijikuta akikutana na watu waaina hii na abdul akiwa na omary kwa kutetea maisha yao abdul akajikuta akiua kwa kuji hami abdul akawa anashangaa maana mudy alisema kuwa hii kazi haina hatari "imetokea bahati mbaya"ndo lili kuwa jibu la mudy abdul hakurudi nyuma maana pesa ilikuwa imesha mnogea pesa yake abdul aliweka kwenye akaunti yake, japokuwa abdul alikuwa kapanga chumba chake lakini kila siku alienda nyumbani kwao na kumkuta mama yake akiwa na mawazo mengi pamoja na ukimya mama abdul alikuwa kapoteza kabisa furaha aliyo kuwa nayo, abdul hakupenda kuuona ule ukimya kwa mama yake abdul akatafuta house girl na kumuwekea mama yake awe anamsaidia mama yake kazi ,mama abdul alimshangaa sana mwanawe mama abdul alijiuliza ni ofisi gani alipo fanya kazi abdul na ofisi gani iliyo mruhusu abdul kuondoka maeneo ya kazi kila siku na kusafiri kutoka geita kwenda mwanza swali lilikosa jibu.

Mudy akwa ameanza kufanya biashara na watu wengi wa aina mbali mbali na kuanza kukuza jina kwa wafanya biashara wenzake ,abdul ndo alifanikisha yote yale kwa mudy kwani abdul tangu aanze kufanya kazi na mudy alikuwa hajawahi kukamatwa na polisi japo mara nyingi tu alikimbizwa na polisi lakini abdul aliwatoeka polisi kama mchezo.

Biashara ya mudy ilikua na akawa anaingiza mzigo wa madawa kwa wiki mara nne na kudhidi kukua kibiashara na hata abdul pesa yake iliongezeka akawa anapata milioni tano kwa wiki kitu ambacho kilimfanya abdul aendelee kudumu kwenye biashara ile, abdul akazidi kukuza mradi wa vinywaji vya bei ya jumla aliokuwa amemfungulia mama yake mama yake akazidi kushangaa.

Ujana ni maji ya moto kutokana na abdul kupata pesa nyingi akajikuta akiwa mtumiaji wa pombe kiasi kiasi na akawa mtumiaji mkubwa wa sigara ,abdul akaanzisha mradi wakununua pikipiki na kuwa kodishia madereva wa bodaboda ambao walimlipa kwa siku elfu kumi na tano ,abdul akazidi kununua kununua pikipiki huu mradi ulikuwa ni siri yake mwenyewe abdul.

George alihuzunika sana pale alipojua abdul alikuwa anajihusisha na madawa ya kulevya, george ali msihi sana abdul na kumuambia aache biashara ile lakini ilikuwa bure kwa abdul

"abdul na kusihi acha hizo yasije yakakukuta yaliyo mkuta baba yako" alisema george huku akionesha kujua mengi kuhusu kifo cha baba abdul, lakini abdul hakuonesha hata dalili ya kumkubalia meja "walimsingizia baba yangu kuwa anajihusisha na madawa ya kulevya...sasa walicho msingizia baba yangu ndicho nacho kifanya"abdul alikuwa kamaliza.

Afande hussen alifanikiwa kupona baada ya kupata ajali ile mbaya iliyo sababishwa na abdul, baada ya hussen kupona alienda moja kwa moja hadi kwa kina abdul, hussen alikuwa na uhakika kuwa abdul ndio alie sababisha ajali

Hussen alimkuta mama abdul na kuanza kuulizia habari za abdul "anasema anafanya kazi kwenye ofisi flani geita..but mwanangu amebadilika sana"

Mama abdul alimueleza hussen, hussen ikabidi amsubiri abdul, na ilivyo fika saa tisa mchana abdul akaja

Abdul alishtuka kumuona hussen ambae alikuwa na makovu mikononi na alikuwa na kovu kwenye paji la uso wake abdul alijiuuliza hussen kafuata nini pale kwao, baada ya salamu hussen alimuomba abdul waongee faragha wakaenda nje ya geti

"tazama haya makovu umenitia kovu la maisha....abdul nayapenda maisha yako kwanini umeamua kujiingiza kwenye biashara hatari....ni wewe siku ile uliokuwa kwenye tax na kukimbia na wale waarabu wenye madawa..."

"ebwana afande mbona sikuelewi" abdul alimkatisha hussen kwa ukali

"abdul utanielewa...unaweza kuniambia umepata wapi pesa za kumfungulia mama yako duka.... Abdul hata mama yako anashangaa umebadilika sana...abdul sijaja kukukamata nimekuja kukupa ushauri na kukuonya achana na hizo biashara" alifoka hussen,

"afande tueshimiane una ushahidi gani ..kaa mbali na mimi...wewe ni mnafiki kwa mara ya kwanza nikiwa mdogo ulioiahidi kumsaidia rafiki yangu beka lakini mpaka leo sija muona, juzi umekuja kuniletea umbea juu ya kifo cha baba yangu...narudia afande achana na mimi kabisa" abdul alimaliza kauli yake yenye kiburi cha pesa

"abdul naondoka but sitakuwa nalawama pindi ukikutwa na hatia"alisema hussen na kuondoka, abdul akaona kama hussen alikuwa anatwanga maji kwenye kinu.

Abdul aliendelea na kazi zake huku akizidi kujipatia pesa na hatimae alimpigia simu violla na kumuambia kuwa atafute mfanya kazi wandani na akapange chumba na mtoto wake na mtoto atakuwa anabaki na mfanyakazi wa ndani

"...nahitaji pindi nikija dar nafikia ulipo panga na mwanetu tuna kuwa nae" alisema abdul

"poa baby hata me napenda kuishi na mwanetu joel cozi nampenda"alisema violla kwa furaha,

Abdul akampangishia chumba violla eneo la river side cha bei na kumtafutia house girl ambae angekuwa anabaki na mtoto pindi violla akienda chuo, violla alifurahi lakini swali kubwa kwa violla ilikuwa abdul wapi kapata pesa "ah nipo naendesha miradi aliyo iacha baba" jibu la uongo kutoka kwa abdul.

Harooney kila siku alikuwa akiumiza kichwa nijinsi gani angeweza kumuua abdul na kumnyamazisha milele kwani abdul alikuwa kachukua jina kubwa kwenye mji wa mudy na hata kwa wafanya biashara wengine "abdul nita muua kifaida kifo chake itakuwa pesa yangu...brother mudy atajuta kumfahamu abdul" alijisemea harooney huku akiwa na plan nzito ya kifo cha abdul....

katika aina ya madawa ya kulevya huwa kuna madawa ambayo ubora wake unakuwa upo chini huu unga usio n ubora ndo huu ambao huletwa na kuchakachuliwa na kisha unasambazwa kwa watu wanao wauzia unga mateja wa tanzania hasa dar es salaam unga huu ni unga mbovu na ndomaana vijana wetu wa tanzania wakitumia huathirika.

mudy alikuwa ameshapata wateja dar wa unga ule mbove, na tayari mudy alikuwa ameshaanza kuwa ananua kutoka nje kwa bei rahisi na kuwapa kina abdul na omary kwa ajili ya kwenda kuuza kwa wateja wadogo wadogo dar es salaam.

abdul na omary waliingia dar wakiwa na ule unga mbovu kwa ajili ya kwenda kuwauzia hawa wateja wa dar es salaam.

ilikuwa mida ya saa nane mchana abdul alikuwa ndani ya gari wakiwa na begi lenye madawa ya kulevya, abdul aliendesha gari mpaka ilala ambapo kulikuwa kuna mteja wao wa madawa ambayo yapo chini kwa ubora,

walifika kwenye nyumba iliyopo pembeni ya soko la ilala nje ya nyumba hiyo mateja walipishana na kutoka walikuwa wamekuja kuvuta unga, omary alishuka na lile beg lenye madawa na kuingia ndani ya nyumba ile ,abdul akabaki ndani ya gari, kama ilivyo kawaida ya abdul akatoa sigara kwenye pakti na kuiwasha akaanza kuvuta taratibu ,mara ghafla abdul alishtuka macho yakamtoka abdul akaacha kuvuta sigara na kubaki amekodolea macho kwenye satimila ya gari ambapo kuna mtu mwenye muonekano wa kiteja alionekana kwenye kioo cha satimila ile, abdul hakuamini kumuona yule mtu akiwa ana pita . mtu huyo alipo pita karibu na mlango wagari ndipo abdul alithibitisha kitu alicho kiona "BE..BE BEKA..." abdul alibabwaja .... naamu nikweli abdul kamuona beka.

abdul hakuamini kumuona rafiki yake beka ambae alikuwa anapita nje ya gari "beka" abdul alipaza sauti iliyo mshitua beka huku abdul akianza kufungua mlango wa gari.

beka alishtuka kusikia anaitwa jina ambalo hajawahi kuitwa kama miaka saba iliyo pita beka alikuwa haitwi beka "nani huyu anae lijua jina langu la mwanza" beka alijiuliza na hapohapo akiri ikaanza kumzunguka "au polisi amesha gundua mimi ndio beka nilio kuwa natafutwa miaka sita iliyo pita" alijiuliza beka na hisia zakuwa yupo kwenye hatari zikamzunguka beka akageuka na kumuangali abdul aliekuwa amesha toka ndani ya gari.

"oh mungu mkubwa beka kila siku niliomba nije kukuona rafiki yangu beka mungu mkubwa" abdul alieongea akiwa haamini kilichokuwa mbele yake ,nakuanza kumsogelea ,beka akazidi kushangaa na kuzidi kujiuliza maswali "huyu jamaa kachero nini" alijiuliza beka...abdul akiwa amemkaribia beka na kutaka kumkumbatia mara alisikumwa na kurudishwa nyuma kama hatua mbili!alikuwa kasukumwa na beka

"we chiz nini? mbona tunalushana stym we boya vipi?" alifoka beka na kwa sauti yenye lafuzi ya kiteja na kumsukuma abdul, beka alihisi yule angeweza kuwa ni kachero

"heh beka mbona siku elewi" abdul alisema kwa mshangao sura ilikuwa ni ileile ya beka lakini sema alikuwa ameshakuwa kijana mkubwa

"acha shobo nani beka hapa " alifoka beka kwa sauti ya juu na kulikana jina lake, eneo lile kulikuwa na mateja waliokuwa pembeni na walimsikia beka akifoka na wakasogea kwani wote walimjua beka

"oyaa mista kapelo nani anakuzinguaaa" alisema kijana mmoja kwa sauti ya puani iliyo jaa lafuzi ya kiteja

"ah mwanangu Beda si huyu fala ananiita majina ya ajabu ajabu" beka aliongea akiwa ameanza kufula abdul akazidi kushangaa

"oya we vipi unataka nini kwa mwanetu mista kapelo" teja mwingine aliuliza akiwa na pisi pisi mkononi beka alikuwa haitwi beka eneo lile ila alikuwa anaitwa mista kapelo...abdul alizidi kushangaa na muda huo mateja walikuwa wamefika wanne ukimuongeza na beka wanakuwa watano

",..beka niwewe uliokuwa unaishi mwanza nyakato ulizaliwa nyegezi..." alisema abdul na kabla hajamalizia beka akamkatisha..

"oya wana huyu kachero ...usikute kaja kumpeleleza pusha wetu.. kama vp tumpoteze!" alisema beka akiwa na nia mbaya kwa abdul kwani kitendo cha abdul kutaja nyegezi kilimdhirishia beka kuwa abdul ni kachero na beka alikuwa amewambia mateja wenzake wampoteze abdul yaani kumuua abdul...beka alihisi kuwa abdul ni askari na njia ya kukata mzizi wafitina ni kumuua.

hapohapo yule teja mwenye pisipisi akaanza kumfuata abdul kwa kasi akiwa kashika pisipisi kwa mtindo wa kuchoma...abdul kwa wepesi alirudi hatua moja nyuma kisha kwa wepesi akaachia teke zito lililo mpata teja mweoye pisipisi na kumtupa chini na hapopo mateja wanne akiwemo beka wakaanza kumfuata abdul kwa kasi kwa mtindo wa kuvamia huku mateja wawili wakiwa na kisu na muda huo walikuwa wamesha mfikia abdul..


umuona rafiki yake beka ambae alikuwa anapita nje ya gari "beka" abdul alipaza sauti iliyo mshitua beka huku abdul akianza kufungua mlango wa gari. beka alishtuka kusikia anaitwa jina ambalo hajawahi kuitwa kama miaka saba iliyo pita beka alikuwa haitwi beka "nani huyu anae lijua jina langu la mwanza" beka alijiuliza na hapohapo akiri ikaanza kumzunguka "au polisi amesha gundua mimi ndio beka nilio kuwa natafutwa miaka sita iliyo pita" alijiuliza beka na hisia zakuwa yupo kwenye hatari zikamzunguka beka akageuka na kumuangali abdul aliekuwa amesha toka ndani ya gari. "oh mungu mkubwa beka kila siku niliomba nije kukuona rafiki yangu beka mungu mkubwa" abdul alieongea akiwa haamini kilichokuwa mbele yake ,nakuanza kumsogelea ,beka akazidi kushangaa na kuzidi kujiuliza maswali "huyu jamaa kachero nini" alijiuliza beka...abdul akiwa amemkaribia beka na kutaka kumkumbatia mara alisikumwa na kurudishwa nyuma kama hatua mbili!alikuwa kasukumwa na beka "we chiz nini? mbona tunalushana stym we boya vipi?" alifoka beka na kwa sauti yenye lafuzi ya kiteja na kumsukuma abdul, beka alihisi yule angeweza kuwa ni kachero "heh beka mbona siku elewi" abdul alisema kwa mshangao sura ilikuwa ni ileile ya beka lakini sema alikuwa ameshakuwa kijana mkubwa "acha shobo nani beka hapa " alifoka beka kwa sauti ya juu na kulikana jina lake, eneo lile kulikuwa na mateja waliokuwa pembeni na walimsikia beka akifoka na wakasogea kwani wote walimjua beka "oyaa mista kapelo nani anakuzinguaaa" alisema kijana mmoja kwa sauti ya puani iliyo jaa lafuzi ya kiteja "ah mwanangu Beda si huyu fala ananiita majina ya ajabu ajabu" beka aliongea akiwa ameanza kufula abdul akazidi kushangaa "oya we vipi unataka nini kwa mwanetu mista kapelo" teja mwingine aliuliza akiwa na pisi pisi mkononi beka alikuwa haitwi beka eneo lile ila alikuwa anaitwa mista kapelo...abdul alizidi kushangaa na muda huo mateja walikuwa wamefika wanne ukimuongeza na beka wanakuwa watano ",..beka niwewe uliokuwa unaishi mwanza nyakato ulizaliwa nyegezi..." alisema abdul na kabla hajamalizia beka akamkatisha.. "oya wana huyu kachero ...usikute kaja kumpeleleza pusha wetu.. kama vp tumpoteze!" alisema beka akiwa na nia mbaya kwa abdul kwani kitendo cha abdul kutaja nyegezi kilimdhirishia beka kuwa abdul ni kachero na beka alikuwa amewambia mateja wenzake wampoteze abdul yaani kumuua abdul...beka alihisi kuwa abdul ni askari na njia ya kukata mzizi wafitina ni kumuua. hapohapo yule teja mwenye pisipisi akaanza kumfuata abdul kwa kasi akiwa kashika pisipisi kwa mtindo wa kuchoma...abdul kwa wepesi alirudi hatua moja nyuma kisha kwa wepesi akaachia teke zito lililo mpata teja mwenye pisipisi na kumtupa chini na hapopo mateja wanne akiwemo beka wakaanza kumfuata abdul kwa kasi kwa mtindo wa kuvamia huku mateja wawili wakiwa na kisu na muda huo walikuwa wamesha mfikia abdul... teja wa kwanza alirusha mkono wake wenye kisu ili amchome abdul kifuani lakini abdul kwa umahiri aliudaka ule mkono kwenye maungio ya kiganja na teja akajikuta katulizwa na hapohapo abdul aliunyonga ule mkono kwa nguvu mkono ukatoa mlio wa kama kijiti kikavu kilicho vunjwa yowe kubwa la maumivu lilimtoka yule teja na hapo hapo abdul akamuinua kidogo na kumsukuma kwa nguvu na teja akawaangukia wenzake ambao walisita kidogo na hapohapo abdul aliruka hewani kidogo na kumshindilia teke la kifua teja mmoja ambae alitoa yowe kana kwamba anabweka mateja watatu wakawa chini yote hayo yalifanyika ndani ya sekunde thelathini ama hakika abdul ni kiboko... beka na mwenzake alioitwa beda ndio waliobaki wamesimama wenzao wote walikua chini wakigaragara, beka akajua akileta uzembe basi angenaswa na abdul aliehisi kuwa ni kachero kweli usilolijua ni usiku wa giza beka haku mtambua kabisa abdul, beka kwa haraka alimsogelea abdul na kumrushia ngumi ambayo ilikuwa haina muelekeo wa ufundi wa upiganaji ,abdul alituna chini kidogo ngumi ya beka ikapita hewani na beka akapepesuka kwa kukosa stamina na hapohapo abdul alimsukuma beka aliekosa kabisa stamina beka akajikuta akienda chini bila kutarajia abdul alimsukuma beka tu na wala hakuwa na nia ya kumpiga, pale alipokuwa ameanguka beka kulikuwa na kisu chini na beka akakiogota na kuinuka kwa ajili ya kukabiliana na abdul ! "we maraya utulie nisije nikakua....abdul kuna nini?" sauti kali ya omary ilifoka omary huku akiwa amemnyooshea bastola beka BEDA NA MATEJA WATATU WALIVYO ONA OMARY ANA BASTOLA WAKAINUKA NA KUKIMBIA .. "ah dont shoot muache ni rafiki yangu but kuna some wrong....please beka weka kisu chini mimi ni ABDUL yule rafiki yako wa tangu ALIENCE" abdul alisema kwa utaratibu kwani abdul alikuwa amesha kumbuka kuwa aliambiwa na hussen kuwa beka hana kumbukumbu vizuri na abdul aliona njia nzuri nikumkumbusha beka urafiki wao "beka nikumbuke vizuri mimi ndio nilikuwa rafiki yako pekee kule mwanza mtaa wa nyakato....kumbuka tulivyokuwa beka haunikumbuki mimi ni abdul" abdul aliendelea kumkumbusha beka...beka alibaki kapigwa butwaa jina abdul alilitambua na siku zote lilimpa shida kwenye kichwa chake akiwa ndani ya dar es salaam kila siku jina abdul lilijirudia kichwani mwake lakini alikuwa hakumbuki abdul ni nani.. picha za watoto wawili waliokuwa marafiki wa wakubwa ikaanza kumuijia kwenye ubongo wake beka akabaki ameganda kama sanamu la posta "beka ni wewe uliekuwa unasema wewe ni kama kaka yangu ...kwanini beka hunikumbuki ulipokuwa nafuraha tulifurahia wote nilipo kuwa kwenye huzuni tulilia pamoja...beka kwanini unashindwa kunikumbuka .... hemu kumbuka ni mtu gani aliekuwa rafiki yako mwanza..na uniangalie vizuri mimi ni abdul" abdul alizidi kusema na kutaja mambo waliyo pitia... ubongo wa beka bado ulikuwa kwenye hali ya kumbu kumbu beka alianza kumbuka matukio machache ambayo huwa yanasumbua kichwa chake tangu akimbie mwanza . "beka kumbuka urafiki wetu ulianzia kwenye mpira wa DOBO" alisema abdul na kumsababishia beka mshtuko...kitendo cha beka kusikia mpira wa dobo kilifanya beka ashtuke na mara picha ya mtoto abdul ikapita kichwani mwa beka na muda huohuo matukio na mambo waliyo fanya yeye na abdul yakaanza kupita mfululizo kwenye kichwa cha beka hatimae beka akawa anaiona picha ya abdul akiwa bado mdogo beka akamuangalia abdul aliekuwa mbele yake beka kweli akatambua kweli yule alikuwa ni abdul rafiki yake kipenzi wa miaka mingi "ni wewe abdul ..kila siku jina lako lilisumbua kichwa changu ...abdul ..." beka alibwabwaja huku machozi yakimtoka na hapohapo abdul alimsogelea beka na wote wakakumbatiana huku wakilia , kipindi yote yanaendelea omary alikuwa pembeni akishangaa "abdul nakukumbuka but sina kumkumbu vizuri tafadhari niambie mimi ni nani..abdul mimi sijielewi elewi" alisema beka akiwa analia wakiwa bado wamekumbatiana beka bado kumbukumbu zake zilimwambia kuwa wakati anatoroka bugando alikuwa kwenye tukio la wazazi wake..swali lililo muumiza beka kichwa ni kwamba kama yeye na abdul kipindi wanajuana alikuwa anaishi wapi?kwani kumbukumbu zilimwambia beka wakati siku anajikuta hostal jana yake ndo wazazi wake walipo uwawa...beka hakukumbuka kama aliwahi kuishi nyakato kwa mjomba wake edward ...swali ni kwamba abdul na beka walijuana beka akiwa anaishi wapi? hili swali lili mchanganya sana beka... "beka acha twende tukayaongee sehemu nyingine ..oya ommy inabidi twende river side mara moja" alisema abdul huku akifuta chozi "beka tunaenda river side tukayaongee vizuri niamini"alisema abdul "nakuamini abdul" alijibu beka na wote wakaingia kwenye tax na ikabidi omary ndo aendeshe gari..."oya jamaa kachukua mzigo wote?"abdul alimuuliza omary "ah kachukua nusu ila ulio baki tuta upeleka tandale" alijibu omary walifika river side kwenye nyumba aliyo kuwa kapangishiwa violla alie ishi violla na mwanae joel pamoja na house girl wake , abdul na beka pamoja na omary walishuka na kuingia kwenye nyumba ile na kumkuta violla akiwa kambeba joel "wow abdul ... karibuni wageni" alisema violla na kuwa karibisha kina beka "beka na omary huyu ndo mke wangu mtarajiwa na huyu ndo mtoto wangu...violla hawa rafiki zangu" alisema abdul kwa furaha "aah jamani karibuni" walikaa kama dakika kumi na tano ikabidi abdul amwambie omary apeleke tandale mzigo ulio bakia ili yeye abaki aongee mengi na beka abdul hakutaja kuwa ni madawa alitumia jina la mzigo maana hakutaka violla na wengine wajue kuwa wana madawa ya kulevya... omary akaondoka. "sorry violla unaweza kuondoka kutuacha wawili?"alisema abdul "hamna shida " alijibu violla na kuondoka. "beka ni kipi kimekuta ndugu yangu why ulichukuwa maamuzi mazito kiasi kile ndugu yangu" abdul alimuuliza beka. "ah abdul mimi nilijikuta nikiwa bugando...lakini nikashangaa kusikia kwenye radio eti natafutwa kwa kosa la kuua wakati hata huyo wanae sema nime muua simjui...ikabidi nitoroke na kupanda basi mpaka shinyanga nikapanda treni ya dar lakini nilikuwa na homa kali.....abdul nimepata tabu.." alisema beka huku wingu kubwa la kumbukumbu likitawala kwenye kichwa chake mawazo ya beka yakarudi kwenye treni.......




REJEA MIAKA NANE ILIYOPITA .... BEKA NDANI YA TREN...

saa sita usiku tren ya kutoka mwanza ilifika shinyanga na wasafiri wote wakaingia ndani ya tren akiwemo na beka .

baada ya dakika tano tren ilipiga honi kubwa na kuanza kutoa moshi na safari ya kulekea dar ikaanza,..

beka akawa anaenda dar es salaam akiwa hajui atafikia wapi ...ili mradi alikuwa anaenda mbali na mwanza.....


ENDELEA....


beka hakuwa na koti hakuwa na shuka hakuwa na begi la nguo...baadhi ya watu walimshangaa kwani alikuwa kijana mdogo halafu hakuwa na mzazi beka alipo ulizwa kuwa ana matatizo gani alikataa "...ah sina matatizo ila narudi kwetu dar kwa ajili ya masomo kwani nilikuwa likizo kwa bibi" ndilo lilikuwa jibu la beka

"sasa hauna ndugu hauna begi huna koti sasa safari gani? we mtoto" aliuliza mama mmoja

"ah mama vitu vyangu vyote walitangulianavyo ndugu zangu ambao nitawakuta morogoro wananisubiri"alisema beka na hapakuwa na swali lingine.


siti aliyokuwa amekaa beka mbele yake kulikuwa na kijana ambae alikuwa na makovu sehemu za mwili wake kijana huyu alionekana kuwa mtu wa majanga.


kufikia saa saba baridi na upepo mkali ulizidi kupiga ndani ya tren na watu walikuwa wamejifunika makoti na mashuka mazito kuzuia baridi ile.


baridi kali lilimpiga beka mpaka akaanza kusaga meno homa kali ikaanza kumkamata beka ,beka akawa anatetemeka akiwa hana koti la kuvaa kwa umri aliokuwa nao beka na homa ile ilimpasa beka alie lakini beka hakusubutu kulia kwani kwa kufanya vile angekaribisha maswali mengi kutoka kwa wasafiri wenzake...

yule kijana mwenye makovu aliekuwa mbele ya beka aliona hali ile aliyokuwa nayo beka na kijana huyu ambae alikuwa na umri wa miaka kumi na saba alijua beka aliteseka na baridi, huyu kijana akavua koti lake na kumpa beka "shika dogo koti hilo ...baridi kali" alisema huyu kijana kwa sauti iliyo onesha dhahiri ni mtumiaji wa madawa ya kulevya au kama sio basi bangi , kijana huyu baada ya kumpa beka koti yeye aliinuka na kuchukua begi lake na kulifungua kisha akatoa shuka la kimasai akajifunika kisha akawa ana muangalia beka kwa macho ya kuchunguza ..lile kwa koti kwa upande wa beka lilikuwa ni msaada mkubwa sana na beka alilivaa haraka haraka " ahsante brother" alisema beka

"haina noma...mimi naitwa BEDA we unaitwa nani?" kijana huyu mwenye sauti ya kiteja aliuliza, beka alisita kidogo kutaja jina lake akaamua kusema jina tofauti "naitwa juma "alisema beka kwa ufupi

beda alimuuliza beka maswali madogodogo ambayo yalikuwa kero kwa beka "dah brother nina usingizi sana acha nilale" alisema beka ili kukatisha maswali ya beda"poa dogo" alijibu beda na beka akaanza kujisumanta na kisha kujifanya kasinzia.


kadri muda ulivyo zidi kuyoyoma ndivyo homa ilizidi kumuandama na beda akagundua kuwa beka alikuwa mgonjwa... "we dogo unaumwa na kwanini unaficha ugonjwa" beda alimuuliza beka huku akimtingisha kumuamsha "a nina kahoma kiaina...una panado unisaidie kaka" beka alisema huku akihisi kichwa kikimuuma

"dogo mimi sina tukifika tabora nitakununulia" alijibu beda

"nita shukuru" alisema beka...beda alijaribu kumdadisi beka kwani beda alishakuwa na wasiwasi juu ya beka lakini beka alimchengachenga beka hakuwa tayari kumsimulia matatizo yake.


saa moja asubuhi treni iliingia tabora huku beka akizidi kupata shida kubwa kwani kichwa kilimuuma sana, baada ya tren kusimama beda alimuomba beka ajieleze jinsi anavyo jisikia na ni kipi kina muuma "kichwa kinauma na nasikia baridi sana halafu nasikia maumivu mwili wote...hii hapa buku mbili itatosha kwa dawa" alisema beka na beda akaondoka kwenda kumtafutia dawa beka, beda alitoka nje ya geti la stesheni ya tabora na kwenda kutafuta duka la madawa baridi..beda alimueleze doctor jinsi beka anavyo umwa "dawa zake itakuwa elfu saba"alisema dokta baada ya kusikiliza maelezo ya beda beda alikuwa amepewa elfumbili tu na beka na dawa bei yake ilikuwa elfu saba beda alikuwa amenuia kumsaidia beka ikabidi beda atoe elfu tano yake mfukoni na kumpa doctor ,beda akakibidhiwa kimfuko cheusi kilicho kuwa na dawa nyingi tofauti tofauti " kabla ya kunywa hizi dawa anywe kwanza chai"alisema doctor na beda akaondoka mpaka kwenye behewa alimukuwemo beka beda akamkabidhi dawa beka "usinywe kwanza acha nikatafute kwanza chai ukisha kunywa chai ndo unywe dawa"alisema beda na kuondoka kwenda kutafuta chai, baada ya muda kidogo beda alirudi na chai iliojazwa kwenye chupa ya maji ya uhai ya lita moja pamoja na vitafunwa....walikunywa chai beka na beda huku wakiwa wameanza kuzoeana wakipiga story za hapa na pale huku beka akiwa bado kichwa kinamsumbua , baada ya chai beka alikunywa dawa aina mbili tofauti na beda akamlazimisha beka anywe maji mengi baada ya saa moja tangu beka anywe dawa beka alianza kusikia joto kali na jasho likaanza kumtililika kama maji beka akahisi macho yake yakiwa mazito ,baada ya dakika kumi usingizi mzito ulimchukua beka.

mpaka treni inaondoka tabora kuanza safari ya dar bado beka alikuwa kalala usingizi bila kuamka beda ikabidi amwache rafiki yake beka ajipumzishe.


beka alilala kama masaa manne na [beka kabla hajaamka kichwani mwake akaanza kuona picha za kijana mdogo akiwa na mwenzake wakiwa marafiki wakubwa aliona taswira ile kwa mfumo negative ...beka aliona picha kama watoto wawili wakicheza mpira wa dobo halafu akaona kama akiwa yumo ndani ya gari akiwa na mama mmoja na mtoto mwenzake na yule mtoto akashuka kwenye gari akiwa na begi kisha akasema "beka usisahau tulivyo panga"] "poa abduuuuul" beka alipiga kelele mpaka akawashtua kwenye tren "vipi dogo" beda aliuliza kwa kuhamaki

"ah ndoto tu" alijibu beka na kujiinamia akijiuliza abdul ni nani ,"usisahau tulivyo panga" ni maneno ambayo abdul alimwambia beka siku ile jioni ambayo ilikuwa ni siku yao ya mwisho kuonana...beka alikuwa hamkumbuki kabisa abdul lakini kichwani mwa beka jina abdul lilijirudia rudia huku akiwa anahisi kwamba alishawahi kuwa na rafiki kipenzi lakini beka hakujua rafiki yule walikutana wapi , na hapohapo beka akaanza kuumwa na kichwa na akawa anahisi kuchanganyikiwa mambo mengi yalimchanganya mtoto beka kwanza anatafutwa na polisi kwa kosa ambalo beka anakataa hajafanya na kingine beka alikuwa kaanza kujishtukia na kujishangaa hii ilitokana na kumbu kumbu za beka zinaonesha yupo kwenye tukio la vifo vya wazazi wake na wakati vifo vile vinatokea beka alikuwa na miaka minne sasa hapa beka anajiona nimkubwa wamiaka kama kumi na nne..hili lilizidi kumchanganya beka na kumsababishia maumivu makali kichwani mwake....

"vipi hali yako "beda alimuuliza beka

"kidogo nafuu sasahivi maumivu ya mwili tu " alisema beka kumfariji beda kwani beka kichwa kilimuuma sana ila hakutaka kumuambia beda.


safari iliendelea huku beda akimdadisi beka bila kufanikiwa maana beka hakutaka kabisa kumueleza beda hali halisi beda , wakiwa kwenye maongezi mara simu ya beda ikaita na beda akapokea

"halow..niaambie mwana...eh kamanda wangu,.....dingi miyayusho kumbe hakuniitia kazi wala nini et anaiambia kanitafutia shule...eh hahahahaha mimi nimemuona kavu tu...eh ndo nipo kwenye gogo la moshi nakuja huko huko dizim baridah " aliongea beda maneno ambayo yali mdhihirisha kuwa alikwa muhuni .


tren iliingia dar es salaam saa tatu usiku na abiria walianza kushuka na mizigo yao na mabegi, beka hakuwa na kitu chochote cha kubeba alikuwa yeye kama yeye

"sasa dogo...mi ngoja niingie camp wewe si una mtu wakuja kukupokea?" beda alisema kumuuliza beka

"ah hapana nita songa mwenyewe mpaka home " alisema beka

"basi poa ngoja kwanza mimi nikamcheki stopper wetu ndo niingizane maskani " alisema beda na kuagana na beka rafiki yake ambae wamejuania kwenye treni..

beka akaanza kutoka nje ya geti la stesheni huku kichwa na mwili vikimuuma , beka alivyofika nje ya geti mataa na ghorofa za eneo lile vilimchanganya lakini hakurudi nyuma aliendelea kusonga hatimae akashika njia ya kariakoo .

beka ali kwa mda kama wa dakika kumi na tano kisha akaona ukuta wa ghorofa flani ambao ulikuwa na giza giza na hapakuwa na mtu beka bila uoga akasogea kwenye ule ukuta na kukaa kisha akatoa dawa zake na chupa ya maji beka akanywa dawa na muda huo akahisi usingizi beka akaamua kulala pale huku akijihisi homa kali .

beka alilala kama dakika kumi mara ghafla alishangaa akikanyagwa na mguu wa mtu beka akamka kwa mshtuko na mara alishangaa kuona amesisimiwa na vijana wasio punguwa saba "jamani vipi?" beka aliuliza na hapohapo alikanyagwa tumboni na kuinuliwa na kukamatwa na watu watatu beka alipiga kelele kuomba msaada lakini hakuna aliekuja kumsaidia "kelele boya wewe...hii ndo kariakoo yetu" kijana mmoja kati ya wale walimshika alisema na kumupiga kofi kali la uso beka akaona nyotanyota...hawa watu wakaanza kumsachi beka na kukuta ana elfu tatu tu!

"ah ana buku tatu tu...pumbavu acha tumfanye kama tunavyo wafanyaga maboya kama hawa ambao wanatembea bila pesa kubwa" alisema mmoja wa watu hawa waliomkamata beka beka alijua kuna hatari ilimkabiri na hapohapo beka ghafla alijikakamua na kufanikiwa kuchoropoka na kuwasukuma wale walio mkamata beka akachomoka mbio na muda huohuo wale vijana wakaanza kumkimbiza...beka alikuwa amechoka na hakuweza kuwa kimbia watu hawa kwani wakati anakimbia watu hawa walimfikia na kumpiga mtama beka akaanguka chini kama gunia na hapohapo akiwa chini alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa hawa vijana saba baadhi yao wakiwa wanamkanyaga kama wanapiga mnyama.....



beda alienda kwa mtu aliemuita stopper na alienda kuchukua kete ya bangi na akaanza kurudi akipitia njia ya kariakoo ili aende ilala ambapo kulikuwa na maskani ya mateja , wakati beda anazidi kwenda ndipo alisikia kelele za mtu akiomba msaada beda akaamua kuenda kule alikosikia kelele zikitokea .

beda alitembea kama dakika moja na ndipo akaona kundi la watu pembeni likiwa kama linampiga mtu aliekuwa chini " hawa wana sijui vipi...acha nika wacheki"alisema beda na kusogelea

"oya wana vipi kuna nini" aliuliza beda baada ya kuwasogelea wale watu wale 

"wewe nani" alisema kijana mmoja kati ya wale waliokuwa wanampiga beka na kumgeukia beda

"ah kumbe kamanda beda...tupo tuna muadabisha huyu fala amevamia camp" alisema yule mmoja wa wale waliokuwa wana mpiga beka na alionesha alimfahamu beda....ni kweli hawa watu walikuwa wanamfahamu beda.

beka aliisikia sauti ya beda na alimsikia yule mtu akitaja jina la beda

"kaka beda ni mimi beka ...tuliokutana kwenye tren..."beka alipaza sauti iliyo kauka huku akikohoa na kutema damu , beda alishtuka kumsikia beka " kumbe beka...nyie wajinga mmemfanya nini huyu dogo" beda alihamaki na kuwapangua wale vijana na kusogea pale beka alipokuwa amelala beka "beka pole.... nyie mafala yaani leo mtajuta" beda alifoka akiwa na hasira huku akitaka kuamka ili aanze kuwapa kipigo vijana hawa walio anza kuogopa..

"kaka beda achana nao nipeleke hosptal nakufa"beka aliongea kwa sauti dhaifu.,.beka alikuwa kaumizwa sana na alikuwa anakohoa damu... beda hakutaka kupoteza muda alimnyanyua beka na kumuweka mgongoni kwake na kuanza kukimbia huku nyuma akifuatwa na wale vijana walio mletea balaa beka, beda alikimbia akiwa amembeba beka mgogoni huku akiwa anaangaza huku na huku kama angeona gari ili apate msaada na bahati nzuri akaona gari aina ya toyota, beda akasimama katikati ya barabara kwani alijua angeisimamisha kwa kupungu mkono isinge simama kwa kuhofia ambush, dereva alipiga honi ili beda apishe barabarani lakini beda hakupisha hatimae toyota ikasimama na beda akaisogelea "samahani baba tusaidie mwenzangu anaumwa tunaomba utupeleke amana" beda alibembeleza na dereva wa toyota akakubari kuwasaidia "ingieni kwenye body tuondoke " alisema dereva na haraka beda akampandisha beka na na yeye mwenyewe akapanda, toyota ikaanza kuondoka kuelekea amana, kutokana na ajali alioipata beka akiwa mwanza na ukijumlisha kipigo cha hawa vijana ilimsababishia beka apoteze fahamu huku damu zikiwa zinaanza kumtoka puani ,

toyota ilifika amana na beda akisaidiana na wauguzi walimbeba beka na kuanza kumpeleka kwenye matibabu beda alilalamika sana alipoombwa PF3 beda aliwaomba sana madaktari hatimae wakakubali kumuanzishia matibabu beka...

beka alitindikiwa drip ya damu kwani siku chache zilizopita alipoteza damu nyingi kwenye ajali aliyo ipata mwanza.... beda muda wote alikuwa pembeni ya kitanda cha beka,

baada ya masaa matano tangu beka awekewe drip kichwa chake kilianza maluweluwe kama ilivyokuwa kawaida yake , beka akaanza kusikia sauti za ajabu ajabu kwenye kichwa chake huku akiona picha ya vurugu vurugu isio eleweka 'some time inabidi kumtoa mtu kafala kwa faida ya watu wengi....kamfufue mama yako ambae ni kafara' haya maneno yalijirudia kwa fujo kichwani mwake beka "wewe beka ni kaka yangu na sio rafiki" haya maneno ya abdul yalipita kichwani mwa beka na kumtoa beka kwenye usingizi mzito "abduuuul" beka alipiga kelele na kuamka na kushangaa yupo hosptal na kumuona beda pembeni "tulia mdogo wangu upo hosptal" beda alimwambia beka huku beda akijiuliza abdul ni nani kwani amemsikia akitajwa mara mbili na beka beda alishaanza kuhisi kuna uwalakini kwenye maisha ya beka, beda akamwambia beka kuwa yupo hosptal anapatiwa matibabu..

beka alitulia kitandani pale huku mawazo yakimzonga na hisia zakuwa alishawahi kuishi sehemu na kuwa na rafiki mkubwa ziki mtawala...beka aliumiza sana kichwa huku akiwa hajui hili jina abdul kwanini linajirudia sana kichwani mwake 'some time inabidi umtoe ndugu kafala kwa ajili ya watu wengi..... kamfufue mama yako ambae ni kafala' haya maneno nayo yalizidi kumchanganya beka kwani yalipita kichwani mwa beka na beka akazidi kuumiza kichwa kujiuliza haya maneno aliwahi kuya sikia wapi na kwanini yanapitapita kwenye kichwa chake...beka alikosa jibu kichwa kikazidi kumuuma tu.

ilifika asubuhi na beda akaanza kupanga aende kwenye utafutaji wa pesa ili kukizi mahitaji madogo madogo

"oya dogo mi nakuja muda sio mrefu naenda hapo nje mara moja" beda alimwambia beka "poa beda" beka alijibu na kaka beda akaanza kuondoka.

beda alitembea moja kwa moja hadi ilala sokoni

"ah mwanetu beda umerudi sisi tulijua upo kwa mshua mambo safi vipi tena?" kijana mmoja alieonekana kuchoka na maisha na kuathirika na madawa alimuuliza beda huku akicheka

"ah miyayusho kumbe kaniita ili niendelee na shule na sio kazi...halafu kule village mambo yetu hayapo alosto ya kufa mtu"beda aliongea na wote wakacheka.

huyu beda ni kijana aliezaliwa shinyanga kwenye familia yenye maisha bora...beda alianza kuharibika pale alipo kuja dar es salaam kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuanza masomo ya sekondari ...beda akiwa form two alijiunga na marafiki waliokuwa na muelekeo mbaya wa masomo na kibaya walikuwa wavuta bangi beda nae kwa ulimbukeni akajikuta akivuta bangi na upepo wa shetani mbaya ukampitia akawa mtumiaji wa madawa ya kulevya, ikawa kila pesa anayotumiwa beda na wazazi wake haitoshi yote ilienda kwenye madawa ya kulevya beda akaanza kuuza nguo baada ya kukosa pesa ya kununulia madawa mwisho wake beda akaamua kuacha shule na kwenda soko la ilala ambapo aliamua kuwa anauza mifuko na sigara na pesa aliyo pata  beda yote iliishia kwenye kuvuta unga sehemu aliyo lala ilikuwa ni kwenye maduka . beda ni mtu mcheshi na huo ucheshi ulimletea umaarufu sokoni pale ilala.

na sasa miaka mitatu imepita tangu beda aingie ilala

beda alikuwa kabadirisha kazi sasa hivi kazi yake ilikuwa ni kupakia mizigo na kupakua hapo sokoni ilala...na hata sehemu ya kulala amebadirishe pembeni kidogo ya ilala kuna mzee ana nyumba ya vyumba vinne vya single hapa ndipo walipo lala mateja kila chumba kimoja wali lala mateja nane na zaidi na kila teja alilipia elfu mbili kila siku,! hapo ndipo alipoishi beda. beda alikuwa maarufu sana na ndomaana wale vijana waliompiga beda walimtambua beda haraka sana ..hayo ndo maisha ya beda.

beda alifanyafanya kazi asubuhi ile na kupata elfu nane beda akaenda kuvuta unga na iliyo baki beda akanunua matunda na kumpelekea beka amana.

hatimae beka alipona na kikwazo ikawa pesa ya kulipia gharama lakini beda aliwabembeleza sana madaktari na kuwaambia hali halisi "daktar sisi hatuna baba wala mama wala baba mjini hapa" beda alisisitiza mwishowe madoctor wakaamua kuwa acha waende zao beda na beka wakaondoka...

beda alimsihi beka amueleze ukweli juu ya maisha yake na beka akabidi amdanganye beda "mimi nilikuwa naishi na mama wa kambo ila amenitesa sana nimeamua kukimbilia dar kuja kutafuta maisha" alisema beka na beda akamueleza beka uhalisia wa maisha yake "kama upo fresh twenzetu ukaanze maisha ilala"beda alimwambia beka na beka alikuwa hana njia nyingine zaidi ya kukubali.

beka na yeye akawa anashinda ilala akiuza mifuko na sigara huku usiku ukifika wanaenda kulala geto ambapo walilipa elfu mbili kwa siku marafiki wa beda waliokuwa mateja ndo wakawa marafiki wa beka...

miezi ilizidi kusonga huku beka akisumbuliwa na kumbu kumbu asizo zi elewa .

beka hatimae akaanza kuwa mkubwa na kuanza kubeba mizigo kama beda..beka haku jisumu kuvuta unga hata sikumoja.

mara kwa mara beka aliweweseka usiku akiwa kwenye ndoto na kusikia maneno ambayo alihisi kuwahi kuyasikia sehemu lakini beka hakukumbuka  beka akajikuta akitumia muda mwingi kuumiza kichwa akifikiria mambo yalio muumiza kichwa kitu kingine kilicho muumiza kichwa beka ni swali la nani alie uwa wazazi wake na kwanini aliwaua ...kichwa cha beka kilihisi kumtambua muuaji na alihisi amewahi kumuona sehemu beka akawa katika hali ngumu ya kustahimili mawazo mengi mkubwa na yeye akiwa kijana mdogo... . beka akaanza kujikuta akipoteza upeo mkubwa wa kufikiri na kuwa mzito wa kufikiri na kila muda alimfikiria sana mama yake mpendwa. BEKA alikuwa mtu wa kkuvaa kapelo kila wakati hakutaka ajulikanue sura yake kwani alihofia kujulikana kwa polisi mpaka watum wakaw wana mita kista kapelo

mchana kutwa beka alishinda kwenye jua kali na kazi nzito na usiku ulipofika badala ya kulala muda huo ndo akawa anatumia kuwaza mambo mengi ya maisha yake na kujiuliza kwanini hajieliwe beka akajikuta usiku akilala masaa mawili pekee

mwenendo huu uliendelea kwenye maisha ya beka mawazo mengi yakampotezea kabisa raha ya kuishi beka na hata kukosa usingizi...beka akajikuta akianza kutumia vidonge vya kuleta usingizi ,siku zikasonga huku beda akiendelea kutumia vidonge vya usingizi. hatimae beka akawa hawezi kuvusha siku bila kunywa vidonge vya usingizi. kichwa bado kiliendelea kumpa shida beka kwani kiliuma mara kwa mara ikabidi aombe ushauri kwa rafiki yake beda "tatizo wewe mawazo mengi mno .... lakini kama utabwia mambo yetu nafikiri hata mawazo yata kwisha" alisema beda akimshauri beda avute unga , beka alikataa " wewe nini hayo mavaliamu unayokunywa kwa ajili ya usingizi haya tofautiani na mambo yetu tofauti yake bei na hayo mavaliamu ndo yanakuletea matatizo sasa hivi huwezi kula bila kunywa hayo madawa yako ya usingizi...sikia ni kwambie beka hata mimi nina mawazo mengi na majanga kupita wewe lakini nikitumia mambo yetu yaani mawazo yote kwisha kabisa" beda alisema kumuambia beka... watu wanasema ukitembea na mwizi utakuwa mwizi hapana ni mpaka ukishawishiwa, beka ameishi na beda kwa muda bila kumfuata nyendo zake

, lakini leo beda kamshawishi beka avute unga na kwakuwa beka hajielewielewi ikabidi ajaribuaone kama nikweli mawazo yata kwisha...ndugu msomaji kilevi hakijaribiwi hasa madawa ya kulevya, ni kweli beka alipovuta alijiona tofauti kabisa na kila alipo vuta mawazo yalipotea lakini baadae yalimrudia tena...beka akajikuta hawezi kuacha uteja na kujikuta akiwa mtumiaji mkubwa wa wa sigara na kujikuta akiwa afikirii sana kuhusu maisha yake na mpaka muda huu beka anakutana na abdul bado beka alikuwa hana kumbu kumbu juu ya urafiki wake yeye na abdul ....

*tuendelee*

*abdul na beka* ndani ya nyumba river side.

"nimeteseka sana abdul" alisema beka

abdul chozi lilikuwa linamtoka kusikia mambo yaliyo mkuta beka rafiki yake

"abdul mimi nahisi tu nakujua ila sijui tulijuana vipi na wapi ...tafadhali abdul niambie mimi ni nani ulinijua vipi?" beka aliongea likawa pigo lingine kwa abdul, kwani moyo wa abdul ulimuuma sana kujua beka hakumbuki chochote juu ya urafiki wao...,..abdul akawa na kazi ya kumkumbusha kilakitu beka



abdul akashusha pumzi ndefu na kufuta chozi na abdul akafikiria mambo ambayo angeweza kumkumbusha beka abdul akaona ni vyema aanze na tukio la vifo vya wazazi wa beka

"beka wazazi wako waliuwawa ukiwa mtoto mdogo....na mjomba wako akakuchukuwa na kuanza kuishi na wewe kwake na kuanza kukusomesha na mimi na wewe urafiki wetu ulianza siku ambayo nilikukuta ukipigana na watoto wawili" abdul akaelezea kila kitu , maelezo ya abdul yalikuwa kama dawa kwa beka, kwani kumbu kumbu za beka zilianza kurudi, na beka kichwani mwake akawa kama anaona mtukio yote kwenye ubongo wake kana kwamba anaangalia kwenye tv

"yah urafiki wetu ulikuwa mkubwa zaidi ya urafiki....maraya mwisho tuliachana tukiwa tunatoka shopping wewe na mama mkarudi wote nyumbani...bekakwanini ulimuua binamu yako yona" abdul aliongea maneno ambayo yaliufungua ubongo wa beka....beka akakumbuka alipo achana na mama abdul na yeye kwenda kwa mjomba wake ambapo alifanya balaa ambalo lilikuwa la kihistoria beka akawa amekumbuka kila kitu na jinsi alivyo jua kuwa mjomba wake edward ndie alie waua wazazi wake moyo wa beka ulishtuka kupata kumbu kumbu ya mambo aliyo yafanya mwanza

"abdul mjomba wangu ndie alie ua wazazi wangu" alisema beka huku kilio cha uchungu kikimtoka

"nini? na ulijuaje" abdul akamaka beka akamsimulia abdul juu ya uwiano wa maneno ya muaji na maneno ya mjomba wake na kumuambia juu ya lile kovu kwenye bega la edward ambalo aling'atwa na mama beka kabla ya kifo ".... nilipanga kuiuwa familia ile yote lakini bahati mbaya nikawa nime muua yona pekee" alisemabeka na kusimulia jinsi alivyo fanya lile balaa kwenye mji wa edward . abdul alishangaa kusikia balaa alio lisababisha beka

"...namshukuru mungu nimekuona na umenirudishia kumbukumbu zangu...nilipokuwa mdogo nilimkosakosa kumua mjomba edward... sasa hivi nimekuwa mtu mzima nitamchinja kama kuku lazima nirudi mwanza tena ndani ya wiki hii"alisema beka kwa msisitizo

"ah beka subiri kwanza kila kitu kinaenda kwa mipango na sasa hivi mjomba wako hayupo pale alisha hamaga..." alisema abdul

"nini? na amehamia wapi?" beka aliwaka

"sijajua but niamini nikirudi mwanza nitahakikisha najua alipoamia....sonow unafanya kazi gani"

"ah nipo ilala nabeba beba mizigo... na wewe ulifuata nini kwa stopper wetu?" beka alijibu na kumuuliza abdul ambae alihamanika na kutembeza macho kuagalia kama kulikuwa na mtu pembeni yao

"ah beka tuta yaongea badae...violla njoo nikutambulishe upya" abdul alisema na kupaza sauti kumuita violla, violla akaja

"baby huyu ndo beka aliosababisha nikakosa furaha nikiwa darasa la sita.... ndio yule beka nilie kuambia ni kaka yangu ukimuona huyu jua umeniona mimi kama unavyo niheshimu mimi basi na huyu shemu wako vilele" alisema abdul kwa furaha. beka na violla wakapeana mikono na kufahamiana kwa furaha .

baada ya muda kidogo beka na abdul waliondoka na kumuaga violla kuwa watarudi muda sio mrefu , abdul na beka wakawa wapo njiani kuelekea stend wakati wapo njiani abdul alimsimulia beka juu ya mikasa iliyo mkuta najinsi alivyo ingia kwenye biashara haramu . abdul alimsimulia kila ki2 beka bila kuficha chochote

"pole sana abdul hii dunia mbaya sana"

"nimesha poa... abdul nataka uanze maisha mapya hutakiwi kabisa kurudi ilala...unatakiwa uishi maisha mema uache utumiaji wa madawa" abdul alisema kwa kumsihi beka

"nita shukuru ndugu yangu abdul" alisema beka kwa furaha.

abdul na beka walipanga mipango na hatimae walikubaliana kuwa beka akute anafanya ubodaboda wakati wakiwa wanasubiria biashara gani itakao walipa ...abdul akampa beka laki tano kwa ajili ya kutafuta chumba na kununua, vitu vya ndani vya muhimu, beka hakuamini kupokea laki tano kutoka kwa abdul pesa ambayo hakuwahi kuikamata tangu aanze kuitafuta pesa..."beka najua nikukuambia saivi uache kuvuta madawa najua huta nielewa ila nacho kuomba jitahidi uache unga mbaya sana ...hiyo pesa ya chumba na vitu vya ndani nitakuachia elfu sabini kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale ndani ya siku tatu pikipiki itakufikia na kisha ujishikize" alisema abdul kwa kumsihi beka

"ondoa shaka abdul" alisema beka huku akifikiria ni vipi ataweza kuacha kuvuta madawa ya kulevya beka akapiga moyo konde.

omary alirudi akiwa amesha uza mzigo na na wakapanga safari na kuanza safari ya kurudi nyumbani mwanza.

beka alifanikiwa kupata chumba japo baadhi ya pesa alitumia kwenye madawa na kujikuta akilipia chumba laki moja na elfu themanini na godoro la elfu tisini na pesa iliyo baki yote ikatumika kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

abdul alirudi mwanza akiwa na furaha kupita kiasi mpaka mama yake akashangaa kwani muda wote abdul alikuwa mwenye furaha, abdul hakutaka kumuambia mama yake kuwa amekutana na beka kwani angemwambia angejisababishia maswali mengi na hatamae hata hussen angejua na kumsababishia beka balaa lingine abdul akabaki na siri yake moyoni.

ndani ya siku nne abdul alifanikisha dhamira yake kwani alichukua moja ya pikipiki kwenye mradi wake na kuisafirisha kwenda dar ambapo alifanya mpango rafiki yake beka wa mafunzo ya udreva na sheria za barabarani na baada ya wiki chache beka akawa amefuzu na kuanza rasmi kazi ya ubodaboda kisheria akiwa na reseni huku asilimia kadhaa ya pesa zake akitumia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya japo alikuwa kapunguza kuvuta.

japo beka alipata unafuu wa maisha tangu akutane na abdul lakini kamwe beka hakumsahau beda, mara kwa mara beka alienda ilala akiwa na pikipiki aina ya boxer ,na alipofika ilala alikutana na beda na kupiga stor na wakati wakuondoka alimuachia pesa kidogo ila mradi waligawana umaskini, kila siku beka alimsisitizia abdul kuwa atafute sehemu alipo hamia edward ,beka alitamani sana apajue alipo hamia edward kwani beka alikuwa kadhamiria kuimaliza familia ya edward pamoja na edward mwenyewe.

abdul nae hakuwa nyuma alijitahidi kadri anavyo weza kutafuta na kuulizia sehemu aliyo hamia edward na familia yake, abdul alijitahidi lakini hakufanikiwa maana edward alihama kimya kimya.

siku zilisonga huku abdul akizidi kujipatia pesa na kuwa na jina kubwa baadhi ya maeneo mara kwa mara abdul alienda dar maeneo ya tandika kwa beka abdul alipata matumaini pale alipogundua kuwa beka amepunguza matumizi ya madawa, abdul alizidi kufurahi pale alipo muona mtoto wake joel akikua tena na afya nzuri huku violla akiwa anaendelea na masomo ya chuo.

abdul alianza kuwaza afungue miradi mikubwa na kuachana na biashara haramu kwani kama akount yake tayari ilikuwa inapesa ya kutosha na alikuwa na pikipiki zisizo pungua ishirini ambazo kila moja zilimuingizia elfu kumi na tano kwa siku na abdul alikuwa amesha dumu kwenye biashara haramu abdul akaona ni bora aachane na biashara zile kwani malengo yake ilikuwa nikufanya biashara ile miezi michache lakini pesa mwana haramu abdul alikuwa amesha dumu kwenye biashara ile kwa miezi mingi mara dufu.

abdul akiwa bado anajipanga iliafungue miradi yake siku moja mudy alitembelewa na ugeni mkubwa nyumbani kwake alikuwa ametembelewa na mfanya biashara mkubwa mfaransa ambae alikuja na walinzi wake wafaransa wenzake, mfaransa huyu alikuwa ni mmoja wa wafanya biashara wa madawa ambae alikuwa akifamiana na mudy mfaransa huyu japo alijuana na mudy lakini alimfahamu zaidi abdul kwani abdul alitambulika sana kama mchapa kazi wa mudy .

siku hii kuna biashara kubwa ilikuwa imemleta huyu mfaransa alie itwa paul na biashara ilionekana kuwa ya pesa nyingi kwani mudy na paul walionekana kuwa na furaha abdul hakujua walikuwa wana biashara gani.

siku hiyo mfaransa alie itwa paul alilala nyumbani kwa mudy na kesho asubuh paul na walinzi wake wakiwa na harooney waliingia kwenye hiace ya mudy iliyo endeshwa na abdul kuelekea airpot!

harooney

alionekana kuwa nafuraha kubwa kwani alijua kitu kilichokuwa kinamsumbua akiri yake kila siku sasa alikuwa amekaribia kukitimiza harooney alikiona kifo cha abdul kikiwa kimekaribia na siku za kuishi za abdul zilikuwa zina hesabiwa na harooney kijana mkorofi mwenye roho mbaya, muda wote harooney alimtaza abdul kwa macho yaliyo ashilia ubaya, abdul aliwafikishi kina paul na harooney uwanja wa ndege na kuwaacha wakisubiria ndege ambayo ingefanikisha kuwa fikisha ufaransa, abdul akarudi nyumbani.

ilikuwa ni saa tano asbuhi baada ya siku tano tangu harooney aende ufaransa, abdul akiwa na polisi mwenye cheo ambae huwa anawasaidia kuwa pitisha kwenye block za asakari, abdul na polisi walikuwa uwanja wa ndege wakiwa kuna mtu wanamsubiri , baada ya kusubiri kwa muda ndipo walipo muona harooney akiwa na beg kubwa mgongoni huku akiwa ameshika begi lingine mkononi polisi akaenda kumpokea harooney, abdul hakuwa na muda wa kumpokea harooney kwani abdul alisha jua harooney ana wiVu wa kijinga , abdul akawasha hiace na kusubiri harooney na polisi waingie ndani ya gari, horooney aliingia kwenye hiace na kulitua beg la mgongoni huku akitweta kana kwamba alikuwa amebeba mfuko wa cement, beg lile lilionekana kama ndani yake kulikuwa kuna viji kokoto vidogo vidogo!, harooney akakaa nyuma ya abdul na afande akaka pembeni ya abdul, abdul akawasha gari na kuanza kuondoa hiace kwa kasi.

abdul akiwa amekaribia kushika barabara ya nyegezi abdul alishtuka kuguswa kisogoni na kitu kama chuma cha baridi ...alikuwa amewekewa bastola na harooney!

"haya haraka kamata barabara ya igoma bwege wewe nikakupeleke kuzimu...si unajifanya transporter" harooney alifoka huku bastola yake ikiwa sanjali na kisogo cha abdul, abdul hakuamini na hakujua ni kipi harooney anataka kumtenda, abdul ikabidi aendeshe gari kuelekea igoma...abdul aliendesha gari huku harooney akimshurutisha aendeshe kwa speed

waliipita igoma na kuzidi kuacha mji

"haya kata kushoto"harooney alifoka na abdul akakata kushoto ambako kulikuwa kuna kibarabara kilichokuwa kina manyasi mengi, abdul akazidi kuendesha gari kutokomea ndani ya pori "simamisha gari " alifoka harooney , baada ya abdul kusimamisha gari harooney alishuka akiwa amemuelekezea bastola abdul na kumuambia polisi ampekue abdul, polisi akampekua abdul na kuichukua bastola ya abdul

"haya shuka unyooshe upande huu"alisema harooney na abdul akashuka na kuanza kutembea kuelekea upande alioambiwa, harooney akawa anamfuta nyuma abdul kama hatua sita nyuma tena kwa tahadhari kwani alijua abdul ni mtu hatari.

walitembea kama dakika kumi na mara wakatokea sehemu kulipokuwa na wanaume wanne wenye vifua vya miraba na abdul alipofiki tu alisogelewa na mwanaume mmoja mwenye kifua cha miraba na kupigwa ngumi nzito ya shavu iliyo mpeleka abdul chini "wewe leo lazima ufe si ulijifanya mchapakazi basi leo uende ukachape kazi kuzimu" haroney alifoka huku akiwa amemuelekezea abdul abdul aliekuwa chini akiugulia maumivu ya ngumi aliyo pigwa....



.."kwani harooney kosa langu nini"abdul aliuliza akiwa chini huku akionesha dalili zote za kuto amini kinacho mtokea"wewe kosa lako ni kuwa na jina kubwa kwenye biashara za kaka kupita mimi mdogo wake .... kwanza wewe kifo chako ndio utajiri wangu"harooney aliongea na kumuacha abdul kwenye mabano abdul hakujua kifo chake kilihusiana vipi na utajiri wa harooney. juu ya anga kulikuwa kulikuwa kuna hali ya mawingu na tayari manyunyu yalikuwa yameanza"mbona sikuelewi harooney"abdul aliongea kwa kulalamika"utanielewa sali sala zako za mwisho mimi ndo izlael ninayo yachkua maisha yako..... oya wazee tufanyeni fasta mvua isije ikatu kuta oya niger chukua koleo unifuate tukaandae kaburi la huyu ..."alisema harooney na jamaa mmoja mwenye kifua cha miraba akachukua koleo walio kuwa nalo na kuanza kumfuata harooney"oya afande muelekezee bastola kwani anajifanyaga hatari... wazee mumlainishe ili azikwe akiwa amechoka"alisema harooney akiamaanisha wampige abdul kumlainisha yule polisi akachomoa bastola yake na kumuelekezea abdul aliekuwa bado chini, harooney na mtu mwenye kifua cha miraba wakaanza kumdoka kurudi walipo iacha hiace huku mvua ikiwa imeanza kunyesha . abdul alijua tayari kifo kilikuwa kina mkabili mbele yake , abdul alitembeza macho na kuwaangalia wale mabausa watatu walio jazia vifua wakiwa wanajiandaa kuanza kumuangushia kipigo , bausa mmoja alikuwa amevaa buti na katika buti kulikuwa na kisu kilichochomekwa vizuri kwenye kiatu, polisi alikuwa kama hatua tatu kutoka pale alipokuwa abdul akiwa amemuelelezea bastola abdul. bausa mmoja akamfuata pale alipokuwa abdul akianza kujizoazoa, bausa alivyo mfikia abdulalimtandika teke zito la tumbo lililo mrudisha abdul chini , abdul kabla hajafanya lote na kabla hajainuka bausa alimkamata abdul kwa mtindo wa kumkaba"wewe et gwiji wa kuendesha gari .... chagua tukuue kifo gani"bausa alisema kwa kejeli , abdul akiri yake ilikuwa ikimzunguka afanye kitu gani ili atoke kwenye balaa lile, ni kweli kama abdul angeamua kuleta vurugu angeweza kuchomoka hata kwa kimbia lakini tatizo polisi alikuwa pembeni kamnyooshea abdul bastola , abdul akatulia na kuvumilia kichapo , kwa muda wa dakika kama nane watu hawa walimfanyia abdul mambo mengi ya kudhihaki na muda huu polisi alikuwa mbali na abdul kama hatua mbili na wale mabausa watatu walikuwa wamemsimamia abdul kwa mtindo wa kumzunguka"mtoto mzuri mweupe ulifaa sasahivi uwe jikoni sasa wewe unajifanya mafia sijui tukuue kifo gani?"yule bausa mwenye kisu kwenye kiatu alimuuliza abdul kwa kumdhihaki"wewe ndo ulitakiwa muda huu uwe unamstarehesha basha wako kwenye baridi hili... shoga wewe"abdul alisema akiwa anachuluzika maji usoni na damu kutokana na kichapo kidogo, yule mtu mwenye kisu kilicho chomekwa kwenye kiatu chake alifura kusikia tusi kubwa alilo tukanwa na abdul mtu mwenye kifua kwa wepesi akaachia teke zito akiwa na lengo la kumpiga abdul mbavuni bila kujua alifanya kosa kubwa sana! huyu mtu aliachia teke kwa mguu ule uliokuwa na kisu kwenye kiatu na ndicho alicho kisubiri abdul! abdul kwa ustadi wa hali ya juu aliukamata ule mguu na kwa haraka akakichomoa kile kisu kwenye kiatu cha huyu mtu na abdul bila kuchelewa alinyanyua mkono wake wenye kisu na kumchoma kwa nguvu maeneo ya paja la mtu huyu mwenye kifua cha ubausa yowe kubwa lilimtoka bausa huyo na sauti ya yowe lile ikasambaa mstuni mule huku mwangi mkubwa kifuatia , abdul hakulaza damu kwani aliuona ule muda ndo ulikuwa wakati wa ukombozi wake , abdul alichomoa kile kisu na kumsukuma jamaa kwa nguvu kuelekea upande alipokuwa yule polisi, jamaa alipepesuka na kujikuta akirudishwa nyuma na kuanguka kwenye miguu ya polisi polisi alihamanika kuona kitendo kile na aliyumba kidogo kwani bausa aliemdondokea miguu alimsukuma kidogo polisi, hapohapo abdul aliruka hatua kubwa na kupiga teke mkono wa polisi ulio shika bastola na bastola ikatupwa mbali na eneo lile

polisi alihamanika na kutaka kukimbia lakini abdul alikuwa karibu akiwa na kisu mkononi , polisi alirusha ngumi akitaka kumpiga abdul usoni lakini abdul alikwepa kwa kunepesha kichwa chake upande na ngumi ya afande ikapita pembeni ya kichwa cha abdul , polisi alikuwa katumia nguvu nyingi kurusha ngumi ile kitendo cha abdul kuikwepa ngumi ile kilisababisha polisi akose balansi na kujikuta kayumba kumsogelea kabisa abdul na hapo hapo abdul alirudisha nyuma mkono wake wenye kisu na kupeleka kwa nguvu kwenye tumbo la polisi, yowe kubwa lili mtoka polisi huku damu nyingi zikimtoka tumboni alikuwa kachomwa kisu tumboni!, abdul alikichomoa kisu kutoka kwenye tumbo la polisi na kugeuka nyuma haraka kwani alijua bado kulikuwa na wengine nyuma yake

mabausa walishtuka kwani hawa kutegemea kitendo kile kutoka kwa abdul kilicho fanywa ndani ya sekunde nane tu!na hapohapo walishtuka kumuona abdul akiwa amegeuka kwa wepesi ili akabiliane nao walikuwa umbali kama hatua moja na nusu kutoka pale alipo kuwa abdul , abdul aliona kuwa wamehamanika na alicho takiwa kufanya ni kuwatawanyisha , abdul aliruka hewani kidogo na kumshindilia mmoja wa mabausa kwa miguu miwili kifuani bausa aliepigwa akatupwa nyuma na abdul akibwagika chini kama mzigo na alipo anguka tu akabilingita kwa ustadi kuelelekea pale alipo angukia bausa na abdul alipo mfikiaa bausa abdul aliinuka haraka na kumlukia mzima mzima yule bausa aliekuwa chini akianza kuinuka abdul akawa yupo juu ya mwili wa yule bausa na mkono wa abdul wenye kisu ukaonekana ukipanda juu na kushuka sehemu za mbavu za bausa huku damu ikiruka na kelele nyingi zikimtoka bausa! bausa alikuwa amechomwa na kisu mbavuni. yule bausa wa pili alishtuka sana kuuona wepesi wa abdul na muda huo alishuhudia mwenzake akichomwakisu na abdul , bausa huyu alipatwa na woga na akaona kibao kilikuwa kimewageukia bausa akajua angechelewa tu basi ingefuata zamu yake bausa bila kuchelewa aliamua kukimbia kutokomea porini huku akiji gonga kwenye baadhi ya miti kwa sababu ya woga. abdul alisikia vishindo vikiishilizia kwenye majani abdul akaamka haraka na kuangalia alipo sikia vishindo na kumuona yule bausa akikimbia na hapohapo abdul akamuona yule bausa wa mara ya kwanza alie mchoma kisu kwenye paja bausa huyu alie chomwa kisu pajani alikuwa anainuka ili na yeye akimbie lakini haraka abdul akaenda pale bastola ya polisi ilipo dondokea na kuichukua"haya wewe utulie kama ulivyo"alifoka abdul na kumuelekezea bastola yule bausa"nyie ni nani na mnampango gani na uhai wangu ?"abdul alimuuliza bausa huku akianza kumsogelea, polisi alikuwa pembeni kalala akitokwa na damu nyingi tumboni"kaka sisi tulikuja kumsaidia harooney kazi yake ...hatujui anampango gani"bausa aliongea kwa kulala mika kana kwamba analia"aaah haujui mpango wake...haya weka mikono kichwani na ugeuke haraka"abdul alifoka na jamaa akageuka na abdul akamsogelea na kumpiga kwanguvu kisogoni kwa kitako cha bastola jamaa akatokwa na yowe na hapohapo abdul akampiga tena jamaa akapoteza fahamu abdul harakaharaka akafungua kamba za viatu vya bausa huyu na kwa kutumia kamba zile akaifunga mikono ya bausa kwa nyuma abdul alitembeza macho na kuangalia eneo lile mstuni hakuona watu wengine zaidi ya miili ya mabausa wawili pamoja na yule polisi, abdul akamuangalia yule polisi akiwa chini akigumia maumivu ya kuchomwa kisu tumboni abdul akaona ule ndo ulikuwa muda muafaka wa yeye kuanza kumfuatilia harooney, abdul akaangalia kule walipo elekea rooney na bausa abdul akaziona alama za viatu na abdul hakutaka kupoteza muda akaanza kukimbia kuzifuata zile nyayo huku akiwa ameshika bastola kwa umakini mkubwa,,,, harooney alipoondoka na bausa wakiwa na koleo walienda mpaka kwenye hiace na harooney akachukua yale mabegi mawili huku moja likiwa zito zaidi ya lenzake na wakaanza kutembea kuelekea sehemu ambayo ilionesha kuna kazi wanaenda kuifanya walitembea kama dakika kumi na tano na mara wakafika sehemu iliyokuwa na miti mingi na pembeni kidogo kulikuwa na mlima mdogo wa mawe"oya hapa panafaa anza kuchimba pakufikia huu mzigo!"alisema harooney na bausa akaanza kuchimba shimo muda wote akiri ya harooney ilikuwa inawaza utajiri ulio kuwa mbele yake plan aliyo kuwa kapanga ilikuwa ina kwenda kutumia. wakati bausa anaendele kuchimba harooney alitoa simu yake bila kujali kakijimvua kalikokuwepo muda ule harooney akatufuta namba ya kake yake mudy na kumpigia simu ikaita kidogo ikapokelewa"hellow mbona mmechelewa kufika?"mudy aliuliza kwa kufoka kidogo"ah kaka abdul katusaliti yaani ametuleta mstuni mimi na polisi.. yaani hapa katuacha katufunga kamba .. yeye ametokomea na mzigo wote yaani hapa nimepenyeza penyeza mkono mpaka nimetoa simu mfukoni ndo nimekupigia kaka fanya fasta uje utusaidie"harooney aliongea akijifanya analia nakulalamika kana kwamba alikuwa kwenye mateso ... maskini ya mungu harooney alikuwa amemuangushia jumba bovu abdul

"whaaat...abdul ndo kafanya hivyo .... mpo wapi"mudy alifoka na harooney akaelekeza sehemu waliyo kuwepo


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG