Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

FATE OF LOVE - 2

   

Simulizi : Fate Of Love

Sehemu Ya Pili (2)


Sawa ulikua unanitafuta lakini sasa hivi kwa miezi hii mitatu iliyopita imekua tofauti kabisa. Ukinitafuta labda mchana tena tunaongea kidogo sana. Usiku hautaki hata kidogo tuongee. Au una mwanamke nini unaishi nae?

Aah aah! Maneno gani sasa hayo unaniambia Agness?

Sema, sasa kama hauna kwanini unanifanyia hivyo? Huo u'busy unaousingizia ni u'busy wa aina gani usiojua kama saa hizi napaswa kuongea na mchumba wangu. Kila siku sio mchana wala usiku wewe upo busy tu. Kweli? Hivi unavyonitumia hela tu mara kwa mara na kukaa kimya unazani mimi shida yangu ni hela?

Mtu mzima nilibaki nipo kimya tu kwani Agness alikua analenga sehemu zile zile muhimu ambazo nilikua nazifanya.

Ina maana umenichoka Alex?

Aah aah! Mbona unaongea maneno yote hayo Aggy, kuna siku niliyowahi kukutamkia hivyo.

Sasa kwanini unanitesa kiasi hiki lakini.

Aggy aliongea hadi akaanza kulia tena mpaka sasa nikaanza kumuonea huruma. Nikamkumbatia na kumbusu kichwani huku nikianza kumuomba msamaha.

Basi mpenzi wangu naomba unisamehe, naelewa kama nimekukosea sana.

Alex utakuja kuniua mimi jamani.

Alizidisha kilio na kunipa tena kazi ya kumbembeleza.

Basi mke wangu yaishe naomba unisamehe.

Agness, Agness, Aggy!

Nilimuita na akainua shingo kunitazama huku machozi yakiwa yanamtoka.

(Sio siri Agness alikua ananipenda sana yani kwani wanawake wote niliowahi kuwa nao hakuna hata mmoja aliyefikia hata robo ya upendo aliokua nao.)

Basi mke wangu tumuache shetani apite nakuahidi sitorudia tena.

( Nilimpa maneno ya kumfariji ambayo nilijua wazi kabisa kuwa ni uongo mtupu maana nikirudi Dar Vanessa ataendelea kunibana kama kawaida na sitokua na muda wa kuwasiliana nae.)


Nikamuona akijifuta machozi na kuanza kurejea kwenye hali yake ya kawaida.Nilimpa maneno mengi sana matamu hadi akaanza kufurahi.

Alex vipi kuhusu suala la matibabu ya baba, umelichukuliaje?

Nitafanya juu chini hadi nihakikishe kuwa baba anaenda nje ya nchi kutibiwa. Siwezi kumtazama baba yangu akiwa anateseka na kufa polepole.

Mhh! Lakini ile hela aliyosema daktari ni nyingi sana.

Sawa lakini mimi ni mtoto wa kiume na sasa hivi najua jinsi ya kuitafuta hiyo hela hivyo nitahakikisha mpaka naipata.

Nakuombea kwa Mungu ufanikiwe katika hilo mume wangu maana hali ya baba ni mbaya sana.

Amina mke wangu, naamini penye kila nia basi pana njia..

Muda huo tulishasahau kila kitu na Agness alikua amenilalia kifuani wakati tunaongea.

Tuliongea mambo mengi sana kuhusu mgonjwa na pia penzi letu na nikamuahidi Agness kuwa ni lazima nije kumuoa kwani yeye ndio mwanamke pekee anayefaa kuwa mke wangu. Agness alifurahi sana na akaniomba niharakishe kwani alikua na hamu sana ya kuishi na mimi kihalali.

Tulipohisi usingizi nilimwambia Agness aende chumbani kwake ila alikataa katakata na kudai kuwa anataka kulala na mimi. Nilimbembeleza sana lakini hakunielewa na ilibidi nimkubalie tu ila nikamwambia awahi kuamka kabla ya mama yangu na mama yake ili wasijue kama tumelala chumba kimoja na aliweza kunielewa.


*************** ***************


Kesho yake asubuhi tuliamka mapema sana na kuanza safari ya kuelekea hospitali na baada ya muda mfupi tukawa tumefika kwani hapakua mbali kabisa kutoka pale nyumbani kwa David. Tulifika na kukuta pilika pilika za watu wengi sana wakiwa wanaingia wodini ili kuwaona wagonjwa wao. Tulishuka kwenye gari na kuanza kuelekea wodini ili tukamuangalie baba. Tulipofika tulipigwa na butwaa baada ya kuona kitanda tulichomuacha baba akiwa amelazwa jana yupo mgonjwa mwengine. Tulitazamana na wote tukawa na alama za kuuliza kwenye nyuso zetu. Nilitamani hata kumuuliza yule mgonjwa kuwa baba yuko wapi lakini alikua yupo usingizini. Nikaamua kumfuata nesi ambaye alikua anahudumia wagonjwa.

Habari za asubuhi nesi.

Nzuri tu kaka, vipi kwema?

Kwema tu. Samahani nilikua namuuliza mgonjwa wangu anaitwa Msare Alex sijui kama una taarifa zake?

Mhh! Samahani kaka naomba uende pale kwenye kile kidirisha kidogo, pale ndo utapata taarifa za wagonjwa wote.

Sawa nesi nashukuru sana.

Kweli sikupoteza muda nikaenda mpaka pale aliponielekeza na kumkuta dada mmoja hivi aliyevalia hijab.

Habari za asubuhi dada.

Nzuri tu kaka, samahani nikusaidie nini?

Nilikua namuulizia mgonjwa wangu anaitwa Msare Alex, jana nilimuacha akiwa amelazwa pale wodini ila nimekuja muda huu sijamkuta hivyo ninaomba taarifa zake.

Si ndo yule mzee anayesumbuliwa na moyo pamoja na kisukari?

Ndio huyo huyo dada yangu.

Yule dada alikaa kimya kidogo kisha akaniambia nisubiri. Aliinuka na kuondoka na baada ya kama dakika 4 alirudi akiwa ameongozana na daktari. Yule daktari alivyofika alianza kunisalimia.

Habari yako.

Nzuri tu dokta shikamoo.

Marahaba. Nimepewa taarifa kuwa wewe unahusiana na mzee Msare Alex.

Ndio dokta.

Ni nani yako?

Ni baba yangu mzazi.

Aanha sawa.


Yule dokta alikaa kimya kwa muda kama vile anatafakari aanzie wapi kunipa taarifa za baba kitu kilichoanza kunipa wasiwasi sana..

Naomba uwe na subira na moyo wa kiume kwa haya nitakayokueleza. Upo mwenyewe hapa au umekuja na mtu?

Nimekuja na mama pamoja na ndugu zangu.

Sawa, sasa taarifa kuhusu mzee ni kwamba.......



Jana usiku mwingi sana yapata saa 8 na nusu usiku mzee alizidiwa sana na ikabidi tumuwamishe na kumpeleka chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na kujaribu kuokoa maisha yake. Ila kwa bahati mbaya...

Dokta, baba yangu amefariki?

Yule dokta alikaa kimya kwa muda akiwa ananitazama kisha akamalizia.

Naomba uwe jasiri katika hili, mzee hatunaye tena kwa sasa. Yapata saa 10 alfajiri mzee alitutoka duniani.

Nilihisi nguvu za miguu zikiniishia na kukaa chini kabisa huku kilio kikianza kuchanganya. Yule dokta alinipa pole sana na kunisihi nijikaze kiume ili nifanye utaratibu wa kuandaa mazishi ya baba. Sikumbuki kama kuna siku niliyowahi kulia kiasi kile kwenye maisha yangu kwani hata manesi waliokuja kunibembeleza walikua wakifanya kazi bure tu. Baada ya muda niliinuka na kuwafuata wakina mama nilipowaacha. Walivyoniona tu na ile hali niliyokuwa nayo wala sikuhitaji kuwaeleza kitu chochote kilichotokea kwani niliona mmoja mmoja akianza kuangusha kilio. Nilienda kukaa karibu na mama na tulilia sana hadi watu waliokua pembeni wakaja kutubembeleza huku wakituuliza maswali.

Poleni sana jamani ndo mitihani yake Mwenyezi Mungu. Akishamuhitaji kiumbe wake basi hakuna namna ni lazima atamchukua tu hivyo naomba muwe na uvumilivu tu. Kaka na wewe naomba uwe na ujasiri maana wewe ndo mtoto wa kiume hivyo wote mkiwa mnalia tu hakuna lolote litakalofanyika. Najua inauma sana ila jikazeni jamani ili mkampumzishe mzee wenu kwenye nyumba yake ya milele.

Kweli yale maneno ya wale watu waliokuja pale yalinifariji sana na kunipa moyo hivyo nikaacha kabisa kulia. Ikabidi niwachukue mama, mama yake Agness pamoja na Agness mwenyewe niwarudishe kule nyumbani kwa David kisha mimi nianze kuhangaika kuupata mwili wa baba na kuusafirisha kuupeleka kijijini kwetu. Tulifika na huko vilio vikaanza upya huku Aggy akiwa analia sana maana walishazoeana na baba kwa kuitana mkwe. Muda huo nilijikaza na ikabidi nitoke nje ili nifanye mawasiliano.


Mtu wa kwanza kabisa kumpigia alikua ni David ambaye alionyesha kusikitika sana baada ya kumpatia taarifa na akaniahidi kuwa ni lazima atakuja na familia yake kuhudhuria mazishi ya baba. Janeth na Happy nikawatumia meseji tu kuwataarifu na baada ya muda wote walinipigia simu na kunipa pole nyingi sana huku Happy akiwa ameshindwa kujikaza kabisa na kuanza kulia maana alikua anamfahamu baba vizuri kwani tulishakaa wote kijijini kwetu takribani wiki mbili. Shida ilikua ni kwenye kumpigia Vanessa na kumpa zile taarifa maana nilijua ni lazima atataka kuja kitu ambacho sikutaka kitokee hata kidogo.

Kweli nikampigia na alihuzunika sana baada ya kumpa zile taarifa.

Kwahiyo mazishi yatakua lini?

Bado hatujakaa kikao ila kwa hali ilivyo inabidi yafanyike kesho tu kijijini kwetu.

Naomba unielekeze Alex mimi nakuja huko.

Hapana Vanessa naomba usije, naheshimu sana juhudi zako na kila kitu ila huu sio wakati sahihi kufika nyumbani kwetu.

Alex, hata kwenye msiba pia hautaki nifike nyumbani kwenu, tabia gani hii? Au umeshaoa una mke huko na unanidanganya?

Hapana sio hivyo Vee ila naomba unielewe kwa hilo.

Hapana Alex mimi sikuelewi hata kidogo. Wewe ni mwanaume wangu tunaoishi pamoja na tunategemea tuje kuoana na kuanzisha familia pamoja. Hivi inaingia akilini kweli wewe ufiwe na mzazi wako halafu mimi nisihudhurie? Hivi hata marafiki zangu wakijua watatufikiriaje?

Kusema ukweli Vanessa alikua anaongea points tupu na nikajikuta nashindwa kabisa kumzuia.

Mimi kesho napanda basi nakuja huko acha leo niombe ruhusa kazini na nijiandae kwa safari.

Kiukweli sikua na jinsi na ilibidi nimuelekeze tu Vanessa kuwa akishafika Tanga mjini apande magari ya kwenda wapi ili afike kijijini kwetu na aliweza kunielewa vizuri sana.

Nikarudi hospitali nikiwa nimeongozana na John na tulivyofika tukaanza taratibu zote na kulipa gharama zote zilizohitajika. Walianza kuuandaa mwili wa baba kwa kuuosha na kuuvalisha nguo nyengine tulizomnunulia kama unavyojua sisi wakristo taratibu zetu wakati wa kumuandaa marehemu ili akazikwe. Hadi inafika jioni saa 12 tulikua tumeshamaliza taratibu zote na mwili wa baba ulikua upo tayari ndani ya jeneza kwa ajili ya kusafirishwa. Tulikodisha gari ndogo ya kubebea maiti na mida ya saa 1 kasoro tukaanza safari. Tuliingia kijijini mnamo saa 2 usiku na kukuta mamia ya watu wengi sana wakiwa wanatusubiri maana tayari walikua wameshapata taarifa ya kifo cha baba.


*************** ****************


Mazishi yalipangwa kufanyika saa 10 jioni na saa 8 mchana Vanessa aliwasili nyumbani baada ya kuwa nawasiliana nae sana na kumuelekeza. Alivalia nguo nyeusi na miwani nyeusi kama wafanyavyo watu wengi pindi wanapohudhuria misiba. David na familia yake walishafika tangu jana usiku mwingi sana kama saa 6 hivi na alikua akiwa yupo yeye, Janeth pamoja na Happy kwa kutumia usafiri wao binafsi. Muda huo nilijikuta nikiwa nimechanganyikiwa kwa mambo mawili. Kwanza msiba wa baba na pili kile kitendo cha wanawake zangu kuwa wapo eneo moja. Muda mwingi nilijiweka busy sana ili tu nisiwe karibu na Vanessa wala Agness maana nilijua kwa upande wa Happy na Janeth mapenzi yetu yalikua ni ya siri sana hivyo wasingeweza kufanya kitu pale. Pamoja na kumkwepa, Vanessa alikua anajiweka karibu yangu mara kwa mara na muda mwingi alikua mara anifute jasho, mara aniweke shati vizuri ilimradi tu kama anatuma salamu kwa mwanamke yoyote ambaye ni mtu wangu na yupo pale. Kwa vitendo alivyokua anavifanya, mtu yeyote mwenye akili timamu ni lazima ajue kuwa mimi na yeye tuna mahusiano ya kimapenzi. Ibada ziliendelea na baada ya watu kula chakula na kumuaga marehemu tulianza kuelekea makaburini. Mama ndo alikua hajiwezi kabisa na alisaidiwa kutembea na wanawake wenzie akiwemo mama yake Agness. Tulimpumzisha salama baba yangu mzee Msare Alex Wegezi kwenye nyumba yake ya milele na baada ya mchungaji kumaliza hotuba yake na maombi watu wote tukatawanyika.


Tulirudi nyumbani huku muda wote Vanessa akiwa ameniganda yupo pembeni yangu akiwa ananifariji. Nikajua kivyovyote vile ni lazima tu Aggy atakua ameona kila kitu na nikajihisi nimejiingiza kwenye matatizo makubwa sana. Hata ndugu zangu wa tumbo moja ambao tulikua hatujaonana siku nyingi sana walikua wamekuja na walinipongeza sana kea kujenga nyumba ya nyumbani kwetu. Kaka yangu mmoja tu ndo tulikua hatujui yupo wapi kwani tangu aondoke takribani miaka mitano iliyopita hatujawahi tena kusikia taarifa zake. Kitu kilichonishangaza ni kuwa baada ya kutoka makaburini sikumuona tena Agness na hakurudi tena nyumbani kwetu na nikahisi huenda tayari nitakua nimeharibu.Muda wote Vanessa alikua anataka kukaa na mimi tu hadi nikawaona Happy na Janeth wakiwa wanamkata jicho la ukali sana. Usiku kulifanyika tena ibada na watu wengi sana tulishiriki. Baba yangu alikua ni mtu wa watu sana na maarufu pale kijijini na ndio maana msiba wake ulihudhuriwa na watu wengi sana. Baada ya kumaliza ibada kila mtu akatafuta pembe yake kwa ajili ya kujipumzisha na wanawake wakalala upande wao huku wanaume tukilala upande wetu.

Asubuhi David na mkewe wakaniaga kuwa wanaondoka kurudi Dar es salaam kwani wameacha biashara zao bila msimamizi huku nyengine wakiwa wamezifunga kwa muda. Kiukweli niliwashukuru sana haswa David ambaye alishiriki kwa kiasi kikubwa sana kwenye msiba ule kwa kutoa pesa nyingi sana. Walienda kumuaga mama aliyekua yupo ndani na wakampatia pesa nyingi sana kama rambi rambi yao. Mama hakuacha kuwashukuru kwani tangu afahamiane na David siku zote amekua mtu mwema sana kwetu. Happy alidai anabaki na ataondoka kwa basi siku ya Jumapili kwani siku hiyo ilikua ni Ijumaa na ndio siku ya mwisho kwa masomo ndani ya wiki chuoni kwao na wazazi wake waliweza kumuelewa.

Watu wengi sana waliondoka na tukabaki mimi, Happy, Vanessa, mama, kaka yangu pamoja na dada zangu wawili ambao walikua wameolewa pale pale kijijini. Kaka zangu wengine wawili walikua wameshaondoka maana wanafanya kazi kwenye viwanda vya wahindi na huko ukikosa kwenda kazini siku 3 tu unakua ni kama umejiachisha kazi wewe mwenyewe hata uwe na dharula ya aina gani.


Kizaazaa kikawa kwa Happy na Vanessa ambao wote kila mmoja alikua anataka kukaa na kuongea na mimi. Happy nae kama alikua anafanya kusudi na ilibidi nimuonye kuwa apunguze kufanya mambo yake kwani Vanessa ni mwanamke wangu ninayeishi nae. Ilifika kipindi hadi Vanessa uvumilivu ulimshinda na kuniita pembeni.

Baby yule msichana ni nani?

Msichana yupi?

Yule mweusi mrefu na amenyoa nywele zake.

Aanha yule ni mtoto wa boss wangu anaitwa Happy, vipi kwani mbona umeuliza?

Mhh! Hapana sio kwa ukaribu huu mliokua nao. Mbona akiwa na wewe anaonyesha anajiamini sana yani kama vile mtu mliyezoeana sana.

Vee bwana hebu acha kuwaza hivyo vitu. Ni kweli tumezoeana sana maana niliishi kwao muda mrefu sana. Lakini kuna kitu gani kibaya tulichokifanya?

Mhh! Haya tu mimi yangu macho.

Hebu kuwa mpole bwana mimi sipo hivyo.

Kusema ukweli Happy alikua mzuri sana na ni mwanamke aliyekamilika kiasi kwamba mwanamke yoyote akiona amesimama na bwana wake ni lazima povu limtoke. Happy alijitunza sana na alijua ni jinsi gani avae ili apendeze.

Nilitamani sana kukutana na Agness ili nijue sababu iliyomfanya aondoke msibani mapema wakati bado tulikua hatujamaliza kila kitu. Japokua nilishaanza kuijua sababu, nilijikuta nataka kujiridhisha tu na kuona amelichukuliaje lile jambo.


Jioni nikawatoroka wakina Happy na Vanessa bila kuwaaga na nikaenda nyumbani kwa kina Aggy ili nikaongee nae. Nilivyofika nikamkuta mama yake nje akiwa anafagia uwanja na aliponiona akabaki ameweka mikono kiunoni huku akinitazama..........



Nilisogea mpaka karibu yake na kumsalimia.

Shikamoo mama.

Marahaba, za tangu jana?

Nzuri tu mama.

Mama Agness wala hakuniongelesha zaidi kwani nilimuona akiingia ndani bila kuniambia kitu chochote. Nikajiuliza imekuaje mpaka anafanya vile na nikabaki nimesimama tu vile vile. Nikaona ukimya umetawala kama dakika 5 na nikajiuliza kwanini mama Agness ananifanyia vile maana sio kawaida yake. Nilisimama karibia dakika 10 ila wakati nilivyokata tamaa na kutaka kuondoka nikamuona Aggy akiwa anatoka ndani kwao kwa unyonge sana huku amejifunika kanga hadi kichwani. Alikuja mpaka mahali niliposimama na kunisalimia lakini akiwa amepooza sana.

Vipi.

Poa mke wangu, mzima?

Mmm! mzima.

Mbona upo hivyo unaumwa au?

Hapana siumwi.

Sasa una nini mbona umepooza kiasi hiko.

Sina kitu.

Aggy alikua ananijibu majibu mafupi tu wakati sio kawaida yake hata kidogo. Nikaanza kuhisi huenda yale mawazo yangu kuwa ameona vituko alivyokua anavifanya Vanessa na vimemkera yatakua ya kweli.

Aggy ndo nini sasa kunifanyia hivyo?

Nakufanyia vipi kwani?

Hauoni jinsi unavyonijibu.

Mbona nakujibu kawaida tu kwani nakosea wapi.

Nilimtazama usoni na kuamini kweli mtu mpole ukimuudhi anaweza kubadilika ndani ya sekunde moja tu maana sikuwahi kumuona akiwa vile hata mara moja.

Aggy hebu niambie nini tatizo sijazoea kukuona hivi.

Si nimeshakwambia hakuna tatizo.

Kwahiyo nimetoka kote huko na kuja hapa kwenu kwa ajili yako ili unijibu hivi, si ndio?

Aggy alikaa kimya akiwa ameangalia chini huku akionekana waziwazi kuwa kichwani amewajaza.

Si naongea na wewe, ina maana kuja hapa kwenu unaniona mpumbavu?

Kidume nikajifanya navimba ilimradi ile shilingi ya makosa niigeuze upande wa pili.

Aggy alinitazama usoni kwa jicho la hasira sana hadi nikaanza kuogopa.

Hivi Alex umeona kufanya mambo yako kote huko haitoshi hadi uje kunionyesha huku?

Mambo gani tena hayo?

Yule mwanamke aliyekua anakushika shika msibani ni nani?

Kwahiyo hiko ndo kimekufanya uwe hivi?

Wewe ulitegemea niwe vipi?

Hebu acha wivu wa kijinga bwana, yule ni mfanyakazi mwenzangu tu.

Alex acha kunifanya mtoto mdogo ulimwengu ndo nauona leo. Hivi ni nani aliyewaona pale akashindwa kuitafsiri ile picha. Ina maana yule ndo anakufanya siku hizi unanidharau na kuniona sina thamani?

Agness alikua anaongea huku ana hasira sana.

Aggy hebu punguza munkari basi tuelewane.

Uelewane na nani? Tuelewane kitu gani, unataka kunidanganya? Alex mimi sio mtoto mdogo yule ni mwanamke wako.

Aah aah! Aggy hebu tulia basi tuongee vizuri.

Sitaki, naomba uondoke kwetu Alex sitaki tena kukuona machoni mwangu.

Akaanza taratibu kutokwa na machozi na kadri alivyozidi kuongea ndo kilio nacho kikaongezeka.

Aggy hebu acha masihara yako bwana.

Ondoka kwetu Alex kabla sijatamka maneno mabaya. Ina maana upendo wangu wote na kukuvumilia kwangu yale ndo malipo ninayostahili? Ile ndo ahadi tuliyowekeana mimi na wewe Alex?

Nikaona sasa Agness yupo serious na nisipokaza kiume ndo nitazidi kuharibu mambo yote.

Agness hebu acha kuongea huo ujinga unaoongea. Mimi sikuachi hata unifanye nini.

Sitaki naomba uniache peke yangu Alex tayari moyo wangu umeshautia kidonda.

Hapana Agness sikuelewi hata kidogo nimesema siwezi kuachana na wewe.

Muda wote huo alikua analia kama mtoto mdogo na nikajiona mkosefu sana kwa mambo yote niliyoyafanya.

Ina maana Agness ahadi zote zile tulizowekeane leo ndo zifikie mwisho? Leo ndo tuachane? Hapana hebu tafuta kitu kingine cha kuniambia lakini kwa hapo sikuelewi.

Kama kweli unanipenda na una malengo na mimi kwanini unanifanyia hivi? Kwanini unautesa moyo wangu? Kwanini unanifanya nipatwe na wivu na kufadhaika kiasi hiki?

Lakini mpenzi mimi nakupenda wewe hawa wengine sina mpango nao.

Kama huna mpango na mtu mwengine kwanini unafanya vile mbele za watu?

Hivi hapa kijijini watu watanichukuliaje mimi, si wataniona kama najipendekeza kwako?

Aggy mpenzi wangu kwanini unapenda kujali watu wengine? Mapenzi yetu mimi na wewe wao yanawahusu nini, waache waseme wanachotaka sisi tuangalie ya kwetu tu.

Sio siri pamoja na mambo yote niliyokuwa nayafanya, Agness ndiye alikua ndani ya moyo wangu na sikutaka kabisa kumpoteza. Tuliongea sana na kugombana ila mwisho nikamuona Aggy anaanza kulegeza kamba.

Sasa Alex kama kweli una malengo na mimi naomba uje kutoa posa nyumbani kwetu, siwezi kuishi hivi mimi na wasiwasi kama nipo vitani.

Basi mpenzi wangu hilo mbona jambo dogo sana. Nakuahidi kabla sijaondoka kurudi Dar nitakuposa.

Kweli?

Niamini mpenzi wangu.

Aggy alinikumbatia kwa furaha na mimi nikampokea huku nikishusha pumzi baada ya kufanikiwa kuimaliza ile kesi.

Nakupenda sana Alex wangu sijui kwanini unakuwa unaniumiza.

Hapana mpenzi wasiwasi wako tu ndo unakuumiza mbona mimi nakupenda sana.

Naomba usizoeane na wanawake wengine kiasi kile mpenzi wangu mwenzio moyo wangu wa makaratasi.

Sawa mpenzi na nakuomba unisamehe sana kwa kukufanya ujihisi vibaya kiasi hiko.

Sawa nimeshakusamehe.

Kidogo sasa nikaanza kupumua na nikaamini kweli sisi wanaume huwa hatuishiwi uongo maana Agness aliniamini kwa vitu ambavyo amevishuhudia kwa macho yake, au labda sijui kwa sababu alikua ananipenda sana.

Kwahiyo utaondoka lini kurudi Dar?

Bado nipo kidogo kama wiki moja hivi, nahisi nitaondoka wikiendi ijayo.

Sawa, basi kesho nitakuja nyumbani maana kwenye msiba baada ya mazishi tu hata sikutaka kukaa, niliondoka kwa hasira nilizokua nazo.

Mmmh! Punguza wivu mke wangu utakuua.

Tulitaniana sana huku Aggy akiwa ananifariji kwa kufiwa na baba yangu mzazi.


*************** ***************


Usiku nilikaa na Happy pamoja na Vanessa tukiwa tunapiga story tofauti za kimaisha.

Hivi Alex ulishawahi kuwa na mwanamke hapa kijijini kwenu?

Vanessa aliniuliza swali ambalo nilihisi ni kama ananitega hivi.

Sasa tangu nipo mdogo mpaka nimefikia hivi nimekulia hapa, hivi nakosaje kuwahi kuwa na mwanamke hapa kijijini.

Huyo mwanamke sijui wanawake bado wapo hapa?

Wengine bado wapo na baadhi wamehama hapa kijijini.

Bado unaongea nao?

Ndio, tunaongea pale inapobidi tuongee.

Basi ndo maana leo mchana ukaondoka na kushindwa japo kuniaga.

Hapana nilipata dharura kuna jamaa yangu aliniita.

Sio kweli kama ni jamaa yako ungeniambia tu mimi nakujua vizuri.

Ina maana hauniamini au?

Ndio, ulienda kukutana na wanawake zako huko.

Vanessa mbona unakua humuamini mwenzio si ameshakwambia alienda kwa rafiki yake?

Happy nae alitia neno kunitetea.

Eeh eeeh! Dada tafadhali, naomba mambo ya mimi na boyfriend wangu usiyaingilie.

Kama wewe ni boyfriend wako basi muulize mimi ni nani kwake tena tumetoka mbali sana sio wewe wa juzi tu.

Happy alikua anatoa majibu mpaka mimi mwenyewe nilishangaa ule ujasiri ameutolea wapi.

Unanijibu nini mimi? Alex huyu ni nani yako niambie ukweli.

Vanessa nae alishaanza kupaniki.

Jamani jamani hebu acheni hayo mambo yenu, kwani tatizo liko wapi?

Niambie Alex huyu ni nani yako?

Eeh eeh! Mbona mtoto wa kike unakua hujiamini?

Happy alikua anaongea kwa kujiamini sana.

Wewe dada unanitafuta nadhani haunijui vizuri.

Sikujui vizuri kuhusu kitu gani, kwani utanifanya nini wewe?

Eeeh! Happy, hebu nyamaza na nakuomba uende ndani haraka.

Alex huyu ndugu yako sijui ni malaya wako ananitafuta nini mimi?

Wewe, mimi nani? Umeniitaje?

Ghafla nikamuona Happy anainuka na kumvamia Vanessa na kumpiga makofi mawili ya haraka haraka ambapo Vanessa nae akaanza kushikana nae kujibu mashambulizi.

Jamani vitu gani hivi mnafanya mbona mnajitia aibu sasa?

Niliwaingilia kati na kuanza kuwatenganisha ambapo kila mmoja alikua anarusha makofi ambayo mengi yaliishia mwilini mwangu.

Wewe Happy si nimekwambia uingie ndani lakini? Vanessa hebu acha bwana, mambo gani haya unafanya?

Niliwatenganisha na nikaona dada zangu wakitoka ndani na kuja pale eneo la tukio.

Jamani kuna nini tena hapa mbona makelele mpaka ndani?

Aliuliza dada yangu mkubwa, mtoto wa tatu kuzaliwa kwenye familia yetu.

Dada zangu kuna nini mbona mnagombana?

Akauliza dada yangu mwengine ambaye alikua ameniachia mimi ziwa.

Hakuna hata mmoja aliyejibu na wakawa wanatazamana kama mbogo waliojeruhiwa.

Wewe, jiangalie sana.

Happy aliongea na kuanza kuingia ndani.

Happy alikua anajulikana na ndugu zangu wote kuwa ni mtoto wa David ila hakuna aliyemjua Vanessa.

Hebu muepusheni shetani jamani, juzi tu tumetoka kumpoteza baba yetu na hapa bado tupo kwenye majonzi, sasa haya mambo gani ya aibu mnayoyafanya watu wazima.

Aliongea dada yangu ambaye alikua ni muongeaji sana na akarudi ndani. Yule dada yangu mwengine nae akarudi ndani na kutuacha nje tukiwa mimi na Vanessa.


Alex mimi naondoka, naomba ukaniletee mizigo yangu ndani.

Aah aah! Vanessa, sasa muda huu unaondoka unaenda wapi?

Narudi Dar es salaam siwezi tena kukaa hapa. Yani yule malaya wako wa kunizalilisha mimi?

Vee yule ni mdogo wangu tu mtoto wa boss wangu.

Hapana sitaki kuamini, mdogo wako aongee kwa kujiamini vile kama anaongea na mke mwenzie.

Hamna bwana, Happy ni mkorofi sana na huwa akikerwa kidogo tu basi ni lazima atagombana.

Sasa mimi nimemkera kitu gani?

Majibu yako sio mazuri Vee, laiti kama ungemjibu vizuri yote haya yasingetokea.

Kwahiyo unamtetea huyo mwanamke wako na kuniona mimi ndo nimekosea eeh?

Hapana sio hivyo ila mimi nasimama kwenye haki.

Sawa, naomba kaniletee vitu vyangu niondoke.

Vee hebu acha utoto bwana. Hivi unadhani saa hizi unapata wapi gari huku.

Alex, tafadhali sitaki tugombane. Mimi siwezi kulala hapa naomba niondoke.

Nikaona sasa hiki ni kizaazaa. Nikapata wazo nimpeleke kwenye guest house iliyopo kwenye kijiji kinachofuata ambacho kilikua na umbali kama wa robo saa kutoka kijijini kwetu. Nikaingia ndani na kutoka na vitu vyake kisha tukaingia ndani ya gari na kuondoka.


Kweli baada ya robo saa tulifika na nikalipia chumba.

Pole sana mpenzi wangu kwa yote yaliyotokea. Naomba upumzike hapa kesho utaondoka Dar.

Vanessa alikua ananiangalia huku akionyesha kuwa na hasira sana............



Hakunijibu kitu na akaangalia pembeni huku akiwa amenuna hataki hata kuniongelesha. Nikaona kuwa nikizidi kukaa ndo kama nitazidi kuharibu kwani zile hasira alizonazo nisingeweza kuongea nae chochote kwa wakati ule akanielewa.

Vanessa mimi naondoka, usiku mwema.

Nenda kwa huyo malaya wako.

Nilimtazama sana ila nikaamua kuepusha shari na kufungua mlango kisha nikaondoka.

Wakati nipo njiani alinitumia meseji mfululizo akiwa ananilaumu kwa kushindwa kumtetea kwenye ugomvi. Sikumjibu kitu na niliamua kuzima simu kabisa. Nilifika nyumbani na kuwakuta dada zangu wakiwa wamekaa sebuleni na Happy.

Umempeleka wapi yule mwanamke wako?

Aliniuliza kwa hasira dada yangu mkubwa.

Dada hebu punguza hasira na sauti ishushe chini ili tuongee vizuri kumbuka tumetoka kufiwa na baba juzi tu hapa sasa hayo makelele yanakua hayaleti picha nzuri.

Dada alikaa kimya na kubaki akinitazama tu.

Ila Alex kwanini unakua na mwanamke mwengine tena mkorofi kama yule wakati unajua tayari una mwanamke wako wa siku nyingi na anakupenda sana.? Ina maana haumuoni Agness jinsi anavyokupenda?

Aliongea kwa msisitizo dada yangu mwengine mdogo.

Muda wote huo Happy alikua yupo kimya na wala hakutia neno. Alikua anachezea simu yake lakini nikimuona wazi kabisa kuwa akili yake ipo makini kabisa kwenye yale maongezi

Wote nikawaona kama wananipigia kelele tu kwani nilikua nampenda sana Vanessa na sikutaka mtu amuongelee vibaya. Nikaamua kuingia kwenye chumba ambacho nilikiteua rasmi kuwa kitakua cha kwangu siku yoyote nitakayokwenda nyumbani. Sio siri wale mafundi waliitendea haki sana ile nyumba kwani ilikua nzuri sana utadhani haipo kijijini. Ilikua na vyumba vinne vya kulala, kimoja kikiwa master ambacho ndo kilikua cha baba na mama ingawa kwa sasa amebaki mama peke yake. Pia kulikua na sebule, sehemu ya kula chakula, jiko, choo cha wote pamoja na stoo. Niliingia ndani na kujifungia mlango kisha nikazima taa na kulala.


*************** ***************


Nilikaa kijijini kwetu takribani wiki moja na nusu huku Happy na Vanessa wakiwa wameshaondoka ile siku ya pili tu baada ya kutoka kugombana. Vanessa tulikua tukiwasiliana japo bado alionyesha kuwa na kinyongo na mimi. Happy nae alikua hachezi mbali na mimi kwani hazipiti siku mbili bila ya kunitafuta. Muda mwingi sana nilikua nipo na mama nikimfariji kwani hakua tena na mtu wa karibu wa kumuangalia usiku na mchana baada ya baba kufariki. Dada zangu wote wawili walikua wameshaondoka kurudi kwa waume zao na sasa tukabaki mimi, mama na msichana wa kazi. Nilimuahidi mama kuwa nitakua na yeye bega kwa katika kila hali. Aggy nae alikua anakuja nyumbani mara kwa mara kumsalimia mama pamoja na kumsaidia kazi. Nikaenda nyumbani kwa kina Aggy kutoa posa kama nilivyomuahidi na alifurahi sana.

Alex hivi ni kweli una malengo na mwanangu?

Mama yake Aggy aliniuliza.

Bila shaka mama, Aggy ndo mwanamke ninayempenda na ninayetaka awe mke wangu.

Sasa kama ndo hivyo kwanini una wanawake wengine?

Mbona mimi sina wanawake wengine mama!

Na siku ile ya msiba yule ni nani yako?

Yule ni mfanyakazi mwenzangu tu mama ila tumetokea kuzoeana sana na kuwa karibu. Hakuna kitu kingine chochote kinachoendelea na hata Aggy nimeshamuelewesha kuhusu hilo.

Mmh! Alex, kuwa makini na mwanangu. Agness namjua mimi huyu anaweza hata akanywa sumu akajiua.

Nipo makini nae mama na nakuahidi nitampenda na kumtunza kwa siku zote za maisha yangu.

Sawa, kama hayo unayosema yanatoka moyoni mimi wala sina neno.

Mama yake Agness alikua ni muongeaji sana ila siku zote alisimama upande wa mwanae kwani hakutaka kitu chochote kibaya kimtokee na ndio maana alikua makini nae sana.

Alex nimefurahi sana leo yani natamani hata ungeufunua moyo wangu uone ni jinsi gani nilivyo na furaha.

Aliongea Agness wakati tukiwa tupo njiani ananisindikiza kurudi nyumbani.

Kweli mpenzi?

Ndio, yani nahisi ahadi yetu ya ndoa inaenda kukamilika muda sio mrefu.

Wala usijali kuhusu hilo, mimi naweka mambo yangu sawa tu kwa sasa ili tuje kuishi maisha mazuri pamoja na watoto wetu. Ndoa ni lazima ifungwe tena nataka iwe kubwa kijiji chote hiki wale ubwabwa wetu.

Sasa wanakijiji wote hawa tutawaweza?

Aggy aliongea huku akiwa anacheka sana.

Kwani tatizo nini? Hela au? Itawezekana tu labda wakatae wao wenyewe.

Sikumbuki kama kuna siku ambayo nilimfurahisha Aggy kama ile kwani nilimuona wazi akiwa ana furaha sana. Nikamuaga kuwa siku inayofuata ninarudi Dar kuendelea na majukumu yangu ya kikazi na Aggy alihuzunika sana.

Tayari nimeshazoea kukuona kila siku nikija kwenu mume wangu.

Usijali mke wangu huu ni muda wa kuyajenga maisha yetu naamini ndani ya muda mfupi tutaishi maisha ya furaha sana.

Sawa mume wangu ila utanipoozesha sana.

Mimi pia ila usijali baada ya kama wiki mbili nitakuja tena mara moja kwa ajili ya arobaini ya mzee kama unavyofahamu.

Sawa mpenzi nimekuelewa, mimi nakutakia kila ka heri tu huko na uwe makini na wanawake kama wale wa siku ile. Hawakawii kumuiba mume wa mtu wale.

Usijali mpenzi siku zote nakuwaza wewe tu.

Tulipigana mabusu na kuagana huku Aggy akionyesha kuwa na huzuni sana. Nikamuahidi kuwa nitamtumia pesa za matumizi nikifika Dar maana pale nilikua nimeishiwa na aliweza kunielewa na kunishukuru sana.


Kesho yake nikarudi Dar es salaam baada ya kumuona mama angalau anaanza kuweza kubandika japo chai jikoni maana mwanzo alikua hajiwezi hata kidogo. Nilimkuta Vanessa akiwa bado kama ana hasira na mimi kwani hata nikimuongelesha alikua hana ushirikiano kunijibu vizuri. Muda mwingi alikua busy kuangalia TV au kuchezea simu yake na nikaona nitafute mbinu mbadala ya kumaliza lile tatizo.

Nilirudi kazini na kuendelea na majukumu yangu kama kawaida na watu wengi sana walinipa pole kwa kufiwa na baba yangu mzazi.

Ilipofika Jumamosi nikaamua kumtoa out na kumpeleka maeneo ya Double Tree ambako kila wikiendi walikua na chakula cha usiku kwa ajili ya wachumba na wanandoa. Ile sehemu ilikua tulivu sana na yenye kupendeza kwani mishumaa ndio iliyotawala eneo lile na kulifanya liwe na mwanga hafifu sana ambao ulivutia kwa kila mtu.Tulikaa kwenye meza yetu ambayo tayari ilishakua reserved kwa ajili yetu kwani nilishafanya booking mapema sana. Ile sehemu ilikua ni nzuri sana kiasi kwamba nilianza kuliona kwa mbali tabasamu la Vanessa.

Tuliletewa chakula na vinywaji na kuanza kula huku kwa mbali tukiwa tunaburudishwa na mziki laini.

Vee najua kama bado una hasira na mimi tangu lile tukio la siku ile kule nyumbani. Najua kama nilikuudhi sana na sijawahi kupata nafasi nzuri ya kukuomba msamaha.

Muda huo alikua akiniangalia kwa macho yake malegevu huku ule mwanga hafifu ukimfanya azidi kuonekana mrembo maradufu.

Sikutegemea kabisa kama kitu kama kile kitatokea na kiukweli niliumia sana. Naomba nichukue nafasi hii mke wangu kukuomba radhi maana sifurahii hata kidogo jinsi tulivyo kwa sasa. Naomba unisamehe sana kwa kile kilichotokea na pia umsamehe Happy kwa yote aliyoyafanya. Ujue usimuone ana mwili mkubwa vile na anapendeza Happy bado ni mdogo kwako ndo kwanza ana miaka 20 kama sikosei. Nisamehe sana mke wangu.

Vanessa alibaki kimya akiwa anaangalia chini kama anachezea kucha zake hivi.

Vee, nakuomba unisamehe mpenzi mimi sifurahii hata kidogo jinsi tulivyo hizi wiki mbili zilizopita. Naomba turudi kama mwanzo mpenzi wangu ili tufurahie penzi letu.

Akaanza kuniangalia usoni huku akianza kutabasamu na alionyesha kama kuna kitu anataka kuongea.

Vipi mpenzi wangu umenisamehe au?

Msamaha gani tena unaoutaka?

Alijibu huku safari hii akiachia tabasamu pana lililopenya vizuri hadi kwenye mishipa yangu ya fahamu.

Nikamtazama kwa macho ya matamanio na kumsogelea karibu na kumpiga busu mwanana mdomoni.

Asante sana mpenzi wangu, hakika nimefurahi sana.

Usinifanyie vile tena Alex.

Kwani mimi nilifanya nini jamani?

Si kunikutanisha na wale sijui wanawake wako wa zamani, sijui wanakutaka maana haiwezekani mtu awe na kiburi kiasi kile.

Basi mpenzi yameisha hayo tusiyaongelee tena na tufurahie huu wakati tulionao.

Sawa mume wangu nimekuelewa, naomba uniagizie wine tafadhali leo nataka nilewe sana.

Kwanini unataka ulewe?

Nilewe kwa ajili yako.

Aliongea huku akiwa anang'ata lips zake na kunikonyeza.

Wanasemaga mtu mzima hapangwi kwani nilishamuelewa alikua anamaanisha nini. Nilitabasamu tu na kumuita muhudumu kisha nikaagiza wine aliyoihitaji. Tulikunywa sana na baadae kucheza mziki laini uliokua unapigwa na DJ wa eneo lile. Kulikua na watu wengi sana kila mtu akiwa na mtu wake na wote walionyesha kuwa kwenye mapenzi mazito sana. Sio siri nikagundua sehemu kama zile zinawafaa sana wanandoa ambao ndoa zao zimeanza kulega lega kutokana na sababu za hapa na pale. Ile sehemu inasaidia kujitafuta tena na kupata zile hisia za wakati mnaanza mahusiano yenu. Mnapata hisia za nini maana ya upendo wa kweli. Tulifurahi sana na Vee alionyesha hakuwa tena na kinyongo na alifurahi kupita maelezo.


Tulirudi nyumbani mishale ya kama saa 7 za usiku na tulikua tumechoka sana. Vee alikua amelewa sana hadi alikua hawezi kutembea vizuri. Tuliingia mpaka chumbani na kujitupa kitandani na muda sio mrefu nikaanza kumuona akinishika maeneo ya kwenye ghala langu la silaha za kivita..



Nikawa nishaelewa nini anataka na sikutaka kuvunga kwani haraka nilimvamia na kuanza kubadilishana nae mate. Vanessa alikuwa amechangamka sana na nikajua tu ni kutokana na pombe tulizokunywa. Tulitomasana sana na nikaona Vee anazidi kulegea. Nilimvua nguo zake zote na kumuacha kama alivyozaliwa kisha na mimi nikavua nguo zote. Nikaanza kumnyonya maziwa yake ambapo alikua anapata raha sana kwa jinsi alivyokua anajikunja kunja. Baada ya kumaliza ikawa ni zamu yake kutuma salama. Alituma salamu kwa umakini sana ili ahakikishe kuwa hakuna mtu aliyemsahau. Hakika ile siku nilipata raha sana kwa jinsi Vanessa alivyojua kuitendea haki mashine yangu. Nikamlaza kifudi fudi na kuanza kumpelekea moto huku nikiwa nayashika shika manyanga yake yaliyokua makubwa wastani. Sio siri Vee alikua ananipa stimu kali sana kila nikikutana nae kwani alikua ni mzuri kupita maelezo. Nilimpa dozi nzito uliyomfanya siku ile aote ndoto nzuri kama yupo peponi vile. Tulipumzika huku tukiwa tumechoka sana kwa kulewa pamoja na ile dozi tuliyopeana maana nilirudia mara tatu mfululizo.


*************** ***************


Ilipita miezi minne tangu baba yangu mzazi afariki dunia na sasa nilikua nimesharudi kwenye hali yangu ya kawaida kabisa. Nyumbani mama alikua yupo na mfanyakazi ambaye alikua akimsaidia kazi zote za nyumbani pamoja na kumpikia. Nilimthamini sana mama yangu haswa katika kipindi kile kigumu cha kutoka kufiwa na mume wake ( baba yangu mzazi ) Mama alikua bado ana majonzi sana kwani nilipokua naongea nae kwenye simu nilimsikia kabisa akiwa hana furaha. Nilijitahidi sana kuwa karibu yake ili angalau awe anafarijika kupitia mimi.

Pia nilikua nimeshaanza kujifundisha lugha ya kiingereza kama nilivyopanga ili niondokane na aibu nilizokua nakutana nazo. Kwa muda huo wa miezi minne nilikua nimeshaanza kujua kuongea japo mdomo ulikua bado mzito na pia maneno mengi nilikua sijayajua. Vanessa alikua akinisaidia sana pindi tunapokua tupo nyumbani kwani alinifundisha maneno mengi sana pamoja na kuwa ananiongelesha mara kwa mara. Janeth na Happy nao kama kawaida yao walikua wakinisumbua kutaka dozi mara kwa mara ila nilikua nawakubalia mara moja moja sana. Happy bado alikua akiishi hostel na tulikua tunapatumia huko kufanya mambo yetu huku Janeth tukiwa tunakutana hotelini au lodge. Wote walishakufa na kuoza kwa raha nilizokua nikiwapa haswa Janeth.

Kwa kipindi chote hiko cha miezi minne nikawa nimeshatengeneza hela nyingine nyingi sana na nikajikuta napata wazo la kujenga nyumba yangu hapa hapa Dar es salaam. Nikaamua nimshirikishe Vanessa kwani niliona ndio amekua mtu wangu wa karibu sana.

Baby hilo ni wazo zuri sana kwani hata mimi ilibaki kidogo tu nikwambie kuhusu hilo jambo.

Sawa baby nafurahi sana kwa kuniunga mkono wazo langu, muda sio mrefu nafikiri nitaanza kulitekeleza hilo kwa vitendo.

Vizuri sana mume wangu na sisi tuishi kwenye nyumba yetu tuepukane na hizi kero za kuhama hama mara kwa mara.

Kweli kabisa hata mimi sipendi hiko kitu.

Nilikua natumia gharama sana kumfanya Vanessa azidi kupendeza kwani alikua ni msichana wa kisasa sana na hakutaka kupitwa na fashion yoyote mpya inayotoka. Naweza nikasema kwa pesa nilizokua nazo nilifanikiwa kabisa kumtuliza msichana mzuri na aliyesoma kama Vanessa maana najua kivyovyote kama hali yangu ingekua apeche alolo asingeweza kunivumilia. Kitu kikubwa kilichonichanganya kwake ni uzuri wake kwani nilijihisi sijawahi kumuona msichana mwengine yeyote mwenye uzuri kumshinda yeye.

Muda mwingi sana nilikua nataka kufanya nae mapenzi tu kwani kila nilipomuona sikuacha kumtamani kwa jinsi alivyo. Vanessa alikua mzuri sana kiasi kwamba natamani ningekua na picha yake nikuonyeshe ili uamini hiki ninachokizungumza.


Siku moja niliamua kwenda kumtembelea Happy hostel kwake na nilimkuta akiwa anapika.

Wow! Alex, karibu sana.

Asante sana Happy, naona nimeingia muda mzuri ndo unakarangiza.

Sana, yani wewe ni mkulima kabisa maana umekuja wakati sahihi wa kupanda mbegu.

Nikusaidie kupika?

Mmhh! Lini ulipika wewe kama sio unataka kuunguza vitu tu.

Eeh! Yani Happy unanidharau sana. Mwenzio nyumbani nilikua nategemewa mimi kutoa dongo.

Aaahh! Alex muongo. Hivyo ulivyo unaweza hata kushika mwiko kweli?

Yani Happy wewe, hebu niachie kwanza ili nikuonyeshe.

Aaah! toka hapa. Utapika siku nyengine leo nimeshaandaa kila kitu na chakula kinakaribia kuiva.

Tulitaniana sana kama kawaida yetu mimi na Happy tukikutana.

Chakula kiliiva na akaandaa tukala. Sio siri Happy alikua ni fundi sana jikoni kwani ndizi nyama alizozipika zilikua na ladha sana kiasi kwamba nilikula hadi nikahisi kuvimbiwa.

Alex, i want to tell you something if you don't mind. ( Alex nataka nikwambie kitu kama hutojali )

Don't you worry, what is it? ( Usijali, kitu gani hiko )

Aliniangalia usoni kwa macho flani yaliyojaa aibu huku akiwa kama anasita kuongea.

Happy tell me, come off your chest. ( Happy niambie, funguka )

Naogopa hata kukwambia maana sijui utanichukuliaje.

Happy hebu acha hizo bwana usiwe kama ndo unanijua leo. Umeanza lini hiyo tabia ya kuogopa kuniambia kitu.

Hapana sio hivyo ila hili ni tofauti.

Tofauti ipi hiyo si ndo uniambie?

Alikaa kimya kidogo kisha akanitazama usoni na kuniambia.

I got a boyfriend. ( Nimepata rafiki wa kiume )

Happy bwana kwahiyo ndo ulikua unaogopa kusema hivyo?

Ndio, niliogopa unaweza kunihisi vibaya.

Kwanini sasa nikuhisi vibaya?

Sikiliza Happy, kiukweli kabisa nimefurahi sana kusikia hivyo maana siku zote nilikua naomba upate mwanaume.

Alex kweli hunipendi, yani hadi unaombea nipate mwanaume!

Hapana sio hivyo unavyofikiria. Ila jaribu kufikiria mimi tayari nipo na Agness na pia kuna mtu mwengine naishi nae kabisa. Hivi nafasi yako wewe iko wapi si nitakua nacheza na hisia zako tu?

Mimi sikujali hilo Alex nilichojali ni kwamba nakupenda tu.

Sawa, sasa unafikiri mapenzi yangu na wewe yatafika kokote kweli? Ni lazima itafika kipindi tutaachane tu, mimi siwezi nikakuoa wewe.

Happy alikua yupo kimya sana ananisikiliza.

Huyo jamaa yupo wapi na anafanya nini?

Nipo nae chuo kozi moja.

Okay, is he a good guy? ( Sawa, ni kijana mzuri )

Absolutely, he is a very good guy ( Kabisa, ni kijana mzuri sana ) na nategemea ukikutana nae utakubaliana na maneno yangu.

Kama ndo hivyo sawa. Mna muda gani tangu muanze mahusiano?

Almost a month now. ( Karibia mwezi sasa )

Have you...eeh? ( Umesha...eeh? )

Nilimwambia huku nikimuonyesha ishara inayomaanisha kufanya mapenzi.

Mmhh! Alex bwana, sitaki hayo maswali.

Nakuuliza hivi nina maana ujue wala usinichukulie vibaya.

Maana gani?

Wewe niambie kwanza halafu na mimi nitakwambia.

Okay, ndio tayari tumeshafanya.

Happy, why are you playing too easy to get? ( Happy, kwanini unakua mwepesi sana kupatikana )

Alex, he is my boyfriend, what would i do? ( Alex, ni mchumba wangu yule ningefanya nini sasa? )

Sawa naelewa lakini ilibidi umzungushe kidogo ili akuchukulie serious zaidi na asikuone mtu rahisi tu. Siongei hivi labda ukahisi nakuonea wivu, hapana. Ila naongea hivi kwa sababu nakupenda sana na sipo tayari kukuona unapatwa na jambo lolote baya. Wanaume sisi tuna mambo mengi sana hivyo usikute mtu alikua na shida ya kutaka kuuona undani wako tu kisha akimbie.

No, boyfriend wangu hayupo hivyo kabisa yani, he is quite different from other guys i've met in my life. ( Yupo tofaut kabisai na wavulana wengine niliokutana nao kwenye maisha yangu. )

Mmhh! kama ndo hivyo sawa mimi sina neno, you take care. ( Kuwa makini )

Usijali Alex na nafurahi sana kuona unanijali kiasi hiko.

Usijali Happy, we are family. ( Sisi ni familia )

Happy alitabasamu kuonyesha amefurahi sana kwa yale maongezi tuliyoongea.

Ila Alex siwezi kukusahau hata siku moja, wewe ndiye mwanaume unayeujua mwili wangu vizuri. Unajua jinsi ya kunipagawisha na kunifanya nijione kama mtoto mdogo.

Happy bwana acha maneno yako hebu muheshimu boyfriend wako.

Wewe mbona humuheshimu girlfriend wako Agness?

Tulitazamana na wote tukajikuta tunacheka tu. Yani siku zote palipo mimi na Happy basi ujue hapaharibiki kitu kwani tulikua tunaelewana kupita maelezo.

Nilivyoona mida imeenda sana nikamuaga na nikarudi nyumbani kwangu.


Nilimkuta Vanessa akiwa amesharudi kazini anaandaa chakula cha jioni. Nilimsalimia na kuingia chumbani kubadilisha nguo kisha nikatoka sebuleni. Muda wote tangu nirudi Vanessa alikua amepooza sana tofauti na nilivyomzoea. Usiku baada ya chakula wakati tunaangalia TV ghafla alipunguza sauti na kuniomba tuongee...........



Vipi kuna tatizo Vee mbona ghafla hivi?

Hapana wala hakuna tatizo .

Sawa niambie mke wangu nakusikiliza.

Vanessa alikaa kimya kwa muda kama vile anafikiria aanzie wapi kuongea.

Vee, i'm listening to you my love. ( Vee, nakusikiliza wewe mpenzi wangu. )

Alex naomba usinifikirie vibaya and don't do any stupid thing. ( na usifanye kitu chochote cha kijinga )

Vee si uniambie jamani mbona unanipa pressure sasa?

Alex nakupenda sana.

Nafahamu hilo na hata mimi pia nakupenda sana.

Promise me ( Niahidi ) kwamba hautoniacha, no matter what happens. ( Haijalishi nini kitatokea)

Vee, nikuache kwa sababu gani sasa mbona hivyo? Hebu bwana usinifanyie hivyo.

Alinyamaza kimya akawa anachezea vidole vyake na kuvigosha gosha.

Alex, i'm...i'm.. ( Alex, nina...nina..)

What? ( Nini?)

I'm pregnant. ( Nina mimba)

Aliongea huku akiwa ameweka sura ya huzuni sana.

Eeh! una nini?

Nina mimba yako Alex.

Vee hebu acha masihara bwana.

Nipo serious Alex, nina mimba ya wiki tatu.

Nilijihisi kama sehemu zangu za siri hazipo kwa jinsi mwili ulivyokufa ganzi.

Vee hebu acha maneno yako bwana, nilikwambiaje lakini?

Sasa Alex unadhani mimi ningefanya nini? I can't control each and everything ( Siwezi kuzuia kila kitu ) Nimejitahidi sana kwa muda mrefu lakini siku hizi wewe mwenyewe unajijua jinsi unavyopenda kusex muda wote. Kuna siku nilikua nakuzuia ukanikatalia na nahisi siku ile ile ndio mimba iliingia.

Vanessa wewe, mbona umenitafutia matatizo makubwa sana.!

Najua baby kama uliniambia kuwa kwa sasa haupo tayari, lakini sio mimi ninayepanga haya yatokee.

No, haiwezekani hiyo mimba haiwezekani iendelee kukua.

Alex unasema?

Hiyo mimba inabidi itolewe.

Alex, are you telling me to do an abortion? (Alex, unaniambia nitoe mimba?)

Yes, i'm not ready to carry that heavyweight. (Ndio, sipo tayari kubeba uzito mkubwa kiasi hiko)

Alex haunipendi. Seriously haunipendi.

Nakupenda sana Vanessa lakini kwa hilo hapana sipo tayari kuona linatokea.

Kwahiyo ulikua na malengo gani na mimi?

Vanessa, please kwa sasa sina muda wa kuongea vitu vyote hivyo ninachohitaji hiyo mimba itoke mara moja.

Hapana, sitoi mimba Alex.

Utatoa, labda kama sio mimi niliyekupa.

Nimesema sitoi mimba fanya unavyotaka kufanya.

Utatoa Vee.

Nimesema sitoi.


Nikaona sasa anataka kuniletea matatizo kwani zile habari zikitokea zikafika kijijini nitakuwa nimeharibu kila kitu.

Lakini Vanessa si nilikwambia usishike mimba kwa sasa?

Sasa mimi ndo niliyepanga? Ina maana haunipendi Alex hadi hautaki kuzaa na mimi?

Hapana sio hivyo ila bado mapema sana mimi na wewe kupata mtoto.

Hata kama ndo imeshatokea sasa inabidi tukubaliane nayo.

Niliona ananiambia vitu ambavyo haviingii akilini mwangu hata kidogo. Nilijua fika kuwa ile mimba ikija kujulikana na Aggy itakua ni tatizo kubwa sana na naweza hata kumpoteza. Sikutaka tena kuendelea kukaa na kulumbana nae, nikainuka na kuingia chumbani. Nilisikia sauti kutoka sebuleni Vanessa akiwa analia na nilijihisi kumkosea sana na kumpa wakati mgumu. Sio kwamba nilikua sitaki mtoto au simpendi Vanessa, hapana. Kikwazo kikubwa kilikua ni Agness. Sikutaka kumpoteza kwa gharama yoyote ile ndo maana niliiona ile mimba kuwa ni kikwazo. Sikutaka kutoka kumbembeleza, niliendelea kukaa chumbani nikiwa na mawazo hadi usingizi ukanipitia.


*************** ***************


David alizindua rasmi kitu alichoniambia kuwa atakuja kuni surprise mara baada ya kurudi safari yake ya Oman na zilikua ni bidhaa zake za nguo za kike na kiume pamoja na viatu vya kike na kiume akiwa anaviita kwa jina la JADA. (yaani Janeth David) David alikua anampenda sana mke wake na siku zote alikua akimuelezea kama ni mtu aliyeshiriki sana kwenye mafanikio yake kwani walianza wote wakiwa hawana hata pikipiki ya kutembelea. Hata Janeth japokua alikua anamsaliti mumewe, bado alikua na mapenzi mazito sana na siku zote aliendelea kumjali na kumuheshimu. Bidhaa zake zilitokea kupendwa sana kwani kwenye duka lake alilofungua kwenye Mall ya Mlimani City, muda wote wateja walikua hawakauki. Nilimpongeza sana David kwa hatua nyengine kubwa aliyoipiga kwani kumiliki bidhaa zako mwenyewe hakikua kitu kidogo. David alikua ananihamasisha sana na mimi nije kufanya vitu vikubwa hapa baadae na ndio maana nilikua makini sana na kazi pamoja na mambo yote niliyokua nayafanya. Kwa jinsi nilivyokua naishi nae kama kaka yangu wa damu, David hakuwahi kunihisi vibaya hata siku moja kuhusu mke wake au watoto wake hata atukute tupo wawili tu tunaongea. Aliniamini kupita kiasi na mimi nilijitahidi kuficha makosa yangu ili nisivunje ule uaminifu na kujiharibia ugali wangu.


Nilinunua kiwanja maeneo ya Mbezi ya kimara ili nianze ujenzi wa nyumba yangu kama nilivyopanga. Muda wote huo bado hatukua na maelewano mazuri na Vanessa kwani bado alishikilia msimamo wake wa kutotoa mimba. Vanessa alishanishtukia kuwa nina mwanamke kijijini kwetu na tunapendana hivyo akajua akikubali ni lazima nitamuacha tu na kuishi na huyo mwanamke wangu. Mara zote alizokua akiniambia nilikua nikimkatalia kuwa sina mwanamke mwengine na nilimuona wazi kuwa haridhiki na majibu yangu. Ilifika kipindi hadi tukawa hatuongeleshani na tulikua tunalala kitanda kimoja. Muda mwingi nikimuangalia huwa namuona macho yake kuwa mekundu sana na nikahisi itakua akiwa mwenyewe huwa analia sana. Mara kadhaa rafiki zake huwa wanakuja kumtembelea na nilikua nawakuta mara kwa mara pindi ninaporudi kutoka kwenye shughuli zangu.

Siku moja usiku baada ya chakula Vanessa alinifata na kuniambia.

Alex shangazi yangu anakuhitaji anataka kuongea na wewe.

Shangazi yako yupi huyo na anataka kuongea na mimi kuhusu nini?

Yule wa Magomeni Mwembechai pale nilipokua naishi mwanzo.

Anataka kuongea na mimi kuhusu nini?

Wewe nenda tu utajua huko huko.

Hapana siwezi nikaenda kama hautoniambia ni kitu gani anachoniitia.

Alex hivi mbona umebadilika kiasi hiki? Ina maana hii mimba ndo imekufanya ubadilike?

Vee tafadhali naomba uniache nipumzike kichwa changu kina mambo mengi sana.

Ghafla nikamuona anaanza kuangusha kilio cha kufa mtu hadi nikaanza kuogopa.

Ina maana mimi kukubali kuwa na wewe ndio kosa langu? Kuacha kila kitu na kukukabidhi moyo wangu leo unaniona sina thamani kiasi hiki?

Niliona kama ananipigia kelele tu hivyo nikainuka na kuelekea chumbani. Vanessa alilia sana mpaka nikawa najihisi vibaya kwanini ninamfanyia vile wakati mimi ndiye niliyempa ile mimba. Ila kwa kiburi nilichokua nacho sikutoka kumbembeleza na nilibaki mule mule chumbani.


*************** ***************


Siku moja nikaamua kwenda nyumbani kwa David kuwasalimia maana ni siku nyingi sana tangu nilivyoenda kwa mara ya mwisho. Ulikua ni wakati wa likizo ya mwisho wa mwaka kwa wanafunzi hivyo nikamkuta Patrick na Winfrida wakiwa wamerudi nyumbani. Happy bado alikua yupo chuo kwani ratiba za elimu ya msingi, sekondari na vyuo zilitofautiana.

Wow! kaka Alex, nimekumiss sana.

Mimi pia Winnie yani nimekumiss sana. majuzi ile nilimsikia mama yako akisema kuwa mmesharudi likizo hivyo leo nimepata nafasi kidogo nimeona sio mbaya nikija kuwaona.

Nashukuru sana, karibu ndani.

Winnie alinikaribisha ndani kwani nilimkuta akiwa nje bustanini akiwa anasoma kitabu.

Nilivyoingia ndani nikamkuta Patrick akiwa anaangalia movie kama kawaida yake.

Eeeh! kaka Alex!

Alinikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu kisha akanisalimia. Patrick alikua ananipenda sana na nilisikia alipojua kuwa nimeondoka pale nyumbani kwao alihuzunika sana kwani alikua amenizoea kupita kiasi.

Kaka Alex baba ameninunulia game jengine.

Aliongea huku akichomeka waya na kuweka CD ya game la magari. Patrick alinifanya kama mtoto mwenzie kwani tukiwa pamoja tulikua tunacheza game muda mwingi sana haswa za ngumi, mbio za magari na pikipiki. Kweli akanikabidhi padi yangu na tukaanza kucheza huku Winnie akiwa pembeni anaangalia. Mfanyakazi wa ndani Grace alikuja na nikasalimiana nae huku akili yangu ikiwa ipo kwenye game. Muda huo wa mchana David na Janeth walikua wapo kwenye shughuli zao. Tulicheza sana game hadi Grace alipotuita tukale chakula cha mchana. Tukaachana na game na kwenda kula tukiwa mimi, Winnie pamoja na Patrick.


Tulimaliza kula na Patrick akarudi kuendelea kucheza game na nikabaki na Winnie tu. Winnie alikua akinitazama kwa macho yake madogo wastani yanayong'aa kama jua la saa sita na akaachia tabasamu pana kisha akaniambia...........




Alex nimekumiss sana hauwezi kuamini.

Hata mimi pia nimekumiss sana Winnie ndo maana nipo hapa leo.

Ina maana upo hapa kwa ajili yangu?

Ndio, wewe pamoja na Patrick.

Thank you so much ( Asante sana )

Usijali Winnie, vipi kuhusu masomo shule?

Namshukuru Mungu masomo yanaenda vizuri tu japo ni magumu lakini napambana nayo.

Pole sana, ila ndo ilivyo kila kitu kizuri ujue kina ugumu kwenye upatikanaji wake.

Kweli kabisa ila nimeshazoea.

Tuliongea mambo mengi sana huku muda wote akiwa amelegeza sana sauti yake tofauti na mwanzo. Ghafla nikamuona akiinuka na kunifata pale nilipokua nimekaa na kuja kunikalia kwenye paja langu.

Alex nimemiss sana mambo yako, please naomba unisaidie jamani.

Mmhhh mmhh! Winnie ushaanza sasa, ina maana hauoni kuwa hapa tupo nyumbani na watu wanaweza kutuona kwa muda huu wa mchana?

Nimezidiwa mwenzako, ni miezi mitano sasa tangu nilivyoondoka shule.

Hebu inuka kwanza na ukae pale, hivi akitokea Patrick au Grace hapa unafikiri watatufikiriaje?

Kweli aliweza kunielewa na kuinuka kisha akakaa kwenye kiti cha peke yake kilichokua karibu yangu.

Kwahiyo tunafanyaje sasa, twende sasa hivi basi chumbani kwangu.

Wewe Winnie unacheza kweli. Hivi unadhani Grace na Patrick hawana akili?

Tunafanya haraka tu, Grace ana kazi jikoni wakati Patrick yupo busy na game.

Sawa hata kama ila haya mazingira hayaruhisi na pia si tulishakubaliana kuwa ile tulivyofanya mara ya pili ndo ingekua mara ya mwisho?

Aah! Alex bwana sitaki mwenzio nimeshanogewa. Raha zote zile unafikiri nitaenda kuzipata wapi?

Ujue Winnie nakuchukulia kama mdogo wangu kabisa wa damu.

Alex bwana mbona hivyo? Kwani ni nani asiyelijua hilo? Mimi shida yangu ni unikate hii kiu yangu na hayo mambo ya kuheshimiana yatabaki pale pale.

Unanitafutia matatizo sana wewe haujui tu. Hivi nikigundulika kuwa natembea na wewe si jela itakua inanihusu? Hivi na umri huu hadi nikirudi panadol si itakua inauzwa shilingi elfu kumi.

Acha uoga bwana hayo hayawezi kutokea mimi nitakulinda.

Mmhh! unadhani muda huo serikali itakua inaelewa tena. Hapo ni kunisukumia ndani tu hakuna namna.

Kwahiyo ndo hautaki eeh?

Sio hivyo Winnie ila naogopa sana mwenzio.

Alex mimi na wewe nani ni mkubwa? Mbona mimi siogopi sasa? Hebu kuwa mwanaume bwana mbona tumefanya mara mbili na hakuna tatizo lolote lililotokea?

Mhh! Winnie ukitaka kitu chako wewe mpaka ukipate.


Nilishangaa sana kuona Winnie ana ujasiri kiasi kile na wala alikua haniogopi kama nilivyodhani kwani mara ya mwisho nilimpa dozi kali sana hadi akashindwa kuendelea na mchezo na alidai nilimuumiza sana.

Kwahiyo umekubali au?

Winnie aliniuliza huku akiwa anang'ata lips zake.

Wewe Winnie wewe, hadi siku uondoke na ch*p* mkononi ndo utaanza kuniogopa.

Winnie alicheka sana hadi akawa anatokwa na machozi.

Kumbe siku ile kuniumiza vile ulinifanyia kusudi eeh?

Wala sikufanya kusudi bwana.

Aanha, ngoja. Safari hii ukinifanya kama vile tena nakung'ata naniu lako hilo.

Jaribu uone kama sijakuvuta kinaniu chako hiko.

Tulijikuta tukiwa tunataniana na kucheka sana utadhani nipo na mtu mzima mwenzangu. Muda mwengine akili zangu zilikua kama za kitoto kwani kwa umri wangu na wa Winnie sikupaswa kabisa niwe naongea nae vitu kama vile. Nilikua nimekosa haya kabisa na niliona ni halali yangu kabisa kwa kuwa alijileta mwenyewe.

Baada ya muda Patrick alikuja kuungana na sisi kupiga story na niliongea nao sana. Nilikaa mpaka jioni na nikawaaga kuwa narudi nyumbani kwangu. Patrick alihuzunika sana ila nikamuahidi kuwa nitaenda kuwatembelea tena baada ya siku chache na nitawatoa out. Nikapanga na Winnie siku ya kukutana na kwenda kumpa dozi na aliniahidi kuwa atanitafuta kwani namba yangu anayo japokua alikua hana simu.


*************** ***************


Maelewano na Vanessa bado hayakua mazuri kabisa na sasa mimba ilishakaribia mwezi mmoja. Vanessa alishikilia msimamo wake wa kutotoa mimba na mimi sikukubaliana nae hata kidogo. Nikirudi kazini ilikua ni kula, kuoga na kulala tu hakuna wa kumuongelesha mwenzie. Kile kitu kilimuumiza sana Vee kwani muda mwengine nilimuona akiwa anataka kuniongelesha lakini alishindwa. Nilimbadilikia ghafla na sababu kubwa ikiwa ni ujauzito alioubeba.


Siku moja ya Jumapili wakati nipo sebuleni naangalia movie, nilimuona Vanessa akiingia ndani akiwa ameongozana na watu wazima wawili, mmoja mwanaume na mwengine mwanamke. Vanessa alinisalimia kama kawaida na kuingia chumbani kisha na mimi nikawasalimia watu wale ambao hata sikuwafahamu. Baada ya salamu wote tulikaa kimya na nikamuona Vanessa akiwa anatoka chumbani na kuja kukaa kwenye sofa nililokaa mimi.

Alex huyu ni shangazi yangu kabisa amezaliwa na baba yangu na yule ni mume wa shangazi yangu.

Sawa, karibuni sana mjomba na shangazi.

Nilijibu huku nikililazimisha tabasamu usoni kwani moyoni nilikua na maswali mengi sana juu ya ule ugeni wa kushtukiza.

Aunty nikuletee kinywaji gani?

Mhh! kwa joto hili maji tu yanatosha mwanangu.

Mhh! shangazi maji tu! Sema kingine bwana kuna juisi hapa, soda na mpaka yale mambo yako ya heineken.

Mwanangu usitake nianze kuzitamani saa hizi hizo heineken. Niletee maji tu yanatosha.

Mhh! sawa!. Vipi mjomba na wewe nikuletee nini?

Mimi pia maji tu yananitosha.

Eeh! jamani yani maji tu? au mmeambizana huko wote mnywe maji?

Vanessa aliwatania kidogo kisha wote akaenda kuwaletea maji. Muda wote huo nilikua nipo kimya tu naogopa hata kutia neno kwani ule ugeni wa bila taarifa ulinitisha sana.

Baba sisi tumekuja hapa tumepata malalamiko kutoka kwa mwenzako jinsi unavyomfanyia. Najua hatujuani kabisa na leo ndo mara ya kwanza tunaonana ila muda kidogo Vanessa alishaniambia kuhusu wewe.

Nilibaki kimya nikiwa ninamsikiliza shangazi yake Vee na aliendelea kuongea.

Vanessa ameniambia kuwa ana ujauzito wako lakini wewe hautaki hata kuusikia na unamlazimishe autoe kiasi kwamba hadi mnagombana. Kwanini unafanya hivyo baba?

Nilikaa kimya kidogo kisha nikaanza kuongea.

Sio kama ninamlazimisha kutoa mimba kwa nia mbaya, nimemwambia kuwa mimi bado sijawa tayari na majukumu yote ya kuwa baba wakati bado haujafika.

Wakati upi huo? na unataka lini ndo uwe tayari?

Wazazi wangu naomba mnielewe vizuri kwa hili. Sio kwamba sina mpango na Vee, hapana. Ila bado muda wa kuanzisha familia kwa upande wangu naona haujafika.

Kwa umri wako unataka lini ndo uwe tayari? Ina maana bado haujakua na hela japo kidogo za kumlea mtoto wako?

Lakini sijamwambia kama akitoa huo ujauzito tutaachana.

Hamna lolote mimi nawajua vijana wa siku hizi yani tabia zenu ndo hizo hizo kuwapa mimba watoto wa watu halafu mnawalazimisha wakazitoe na mwisho mnaachana nao. Sasa nakwambia hivi, hapa hatoi mtu mimba na hautomuacha huyu. Hivi umeshampa mimba unategemea nani mwengine ndo akamuoe?

Shangazi yake Vanessa alionyesha kuwa alikua ni muongeaji sana kwani muda wote aliongea bila kupumzika.

Jamani nafikiri hapa hakuna haja ya kulumbana. Wewe kijana, huyu binti yetu ni lazima utamuoa tu na hiyo mimba haitotolewa. Hivi haumuogopi Mungu wewe? Hivi haujui madhara ya kutoa mimba?

Aliongea mjomba wake Vanessa ambaye alikua ni mume wa yule shangazi yake.

Nilibaki nimekaa kimya kwani sasa nilikua nimeshazidiwa ujanja.

Na kuanzia leo sitaki nimsikie tena mwanangu anakuja kulalamika kuwa hana furaha, mara unamnyanyasa. Kwani shida iko wapi haswa hadi ushindwe kufurahi?

Shangazi mtu alizidi kushindilia misumari.

Kijana umetuelewa vizuri lakini?

Akauliza mjomba.

Nilikaa kimya kidogo huku nikijihisi kama kitu kizito kimenikaa kwenye koo yani nilipaniki sio kawaida.

Wewe Alex umetuelewa lakini?

Shangazi alirudia kuniuliza swali alilouliza mjomba.

Ndio nimewaelewa.

Sawa, naomba haya mambo yawe mwisho leo na muishi kwa amani kabisa kama mume na mke. Pia ufanye haraka umuoe mwenzio, tena umetukosea heshima sana kumchukua binti yetu kimya kimya bila idhini yetu.

Nikaona sasa anataka kuanzisha mambo mengine mapya wakati lile walilokua wanalizungumza bado halijaingia vizuri kwenye halmashauri yangu ya kichwa.

Hilo achana nalo tutaliongea vizuri siku akitaka kumposa, kwa leo tumekuja na hili moja tu.

Aliongea mjomba ambaye alionekana kuwa ni mtu mzima mwenye busara nyingi sana.


Muda wote huo Vanesaa alikua yupo kimya tu huku mara moja moja nikimuona akiwa ananiangalia usoni. Hawakukaa sana kwani baada ya kumaliza yale maongezi, waliaga na kuondoka huku Vanessa akiwashukuru sana kwa ujio wao na kusuluhisha ile kesi.

Kwahiyo ndo umeona ukawaite ndugu zako ili uje kunikomoa hapa na kusemwa kama mtoto mdogo.

Lakini Alex mbona umekua hivyo mpenzi wangu? Sasa unadhani mimi ningefanya kitu gani kingine? Hii hali tunayoishi nayo siipendi na inautesa sana moyo wangu.

Kwahiyo sasa hivi unahisi tayari yameshakwisha?

Alex usinifanyie hivyo tafadhali ujue naumia sana. Hebu niangalie hii hali yangu halafu ulinganishe na mateso ninayoyapata ya kulia kila siku.

Kusema ukweli Vanessa alitia huruma sana ila basi tu na mimi kiburi kilikua kimenijaa ndo maana nikawa sijali.

Niliingia ndani na kwenda kupumzika maana nilihisi kama kichwa kinataka kupasuka kwa mawazo.


*************** ***************


Nikaanza rasmi ujenzi wa nyumba yangu maeneo ya Mbezi ya Kimara na nilipanga kujenga nyumba kubwa sana na nzuri. Siku hizi nilipunguza kabisa mambo ya kwenda viwanja kula bata kwani Vanessa alikua ananibana sana labda kama tutoke twende wote. Marafiki zangu walikua wananitania sana kuwa ujanja wangu wote nimenasa kwenye tundu bovu kwani Vanessa alijua kunimiliki.

Janeth nae hakuacha kuniomba tukapeana raha yani dozi yangu ilimuathiri kiasi kwamba alikua hawezi kupitisha wiki moja bila kutaka tukanjunjane japokua mara kadhaa nilikua nikimkatalia. Siku hizi Hapoy alipunguza kidogo na nahisi ni baada ya kupata boyfriend anayemmalizia shida zake. Mara moja moja alikua akinitafuta na kuniomba nikamkata kiu yake kwani alidai dozi ninayompa huyo boyfriend wake haifikii hata robo. Happy alinogewa sana na kusema ukweli hata mimi nilitokea kumpenda Happy.


Siku moja wakati nipo kazini nilisikia meseji mfululizo zikiingia kwenye simu yangu. Mwanzo nilizipuuzia ila nilipoona zinafululizana sana nikaamua kuitoa simu mfukoni na kuzitazama. Wakati ndo nataka kuzitazama nikaona Aggy anapiga simu na nilivyopokea nikamsikia akiwa analia sana.......



Nilishtuka sana na kujiuliza ni kitu gani kinamliza na ilibidi nianze kuongea nae.

Agness kuna nini tena mbona hivyo?

Alex unaniua mimi. Unaniua.

Nakuua? Mbona sikuelewi.

Alex nakufa mimi, nakufa.

Aggy hebu nyamaza basi uniambie vizuri ujue unanichanganya.

Alex umefanya nini lakini?

Nimefanya kitu gani mimi?

(Agness alikua analia sana kiasi kwamba alikua hawezi kuongea vizuri)

Alex kukuamini na kukupenda kote haya ndo malipo yake kweli?

Mke wangu hebu naomba unieleze vizuri ujue sikuelewi mimi.

Alex umeharibu kila kitu, siwezi mimi tena. Siwezi.

Huwezi nini?

Yule mwanamke wako uliyekua unanikatalia kumbe ni kweli na umempa mimba.

(Sasa hapo moja kwa moja akili ikahamia kwa Vanessa na nikajua tayari ameshapata taarifa)

Mbona sikuelewi Aggy nimempa mimba nani?

Usijifanye haujui Alex tayari umeshampa mtu mimba huko.

Wewe ni nani amekwambia hayo maneno?

Soma hizo meseji nilizokutumia.

Ikanibidi nikate simu na haraka haraka nikaanza kusoma meseji alizonitumia. Kumbe zilikua ni meseji za Vanessa alizomtumia Agness na ndio akanitumia na mimi. Vanessa alimueleza kila kitu Aggy kuwa sisi ni wapenzi na tunaishi pamoja na pia nimeshampa ujauzito. Pia alimtisha Aggy kuwa aachane na mimi haraka kwani tayari yeye ameshanibebea mtoto tumboni na tunataka tuoane. Meseji zilikua ni nyingi ila nilizisoma zote na kunifanya nichanganyikiwe sana. Nilichoka hoi na simu nikaiweka pembeni maana sikujua hata nikimpigia Aggy nitamwambia kitu gani. Nikabaki najiuliza namba ya Agness Vanessa ameipata wapi maana nilikua nimeisave jina ambalo mtu mwengine hawezi akalifahamu na pia huwa hatuna tabia ya kushikiana simu zetu na kuzipekua. Nilijikuta napandwa na hasira sana juu ya Vanessa na nikapanga pindi nitakaporudi nyumbani basi ni lazima achezee makofi mengi sana. Nikahisi hata kazi zenyewe hazifanyiki tena na nikaegemea kiti huku nikiwa na mawazo mengi sana. Baada ya muda mfupi nilisikia meseji zikiwa zinaingia mfululizo na ilibidi niichukue simu na kuzifungua.

"Alex naomba uachane na mimi na usahau kila kitu. Ishi na huyo mwanamke wako na mumlee mtoto wenu. Nilikupenda sana lakini wewe umenitenda. Naomba namba yangu uifute na usinitafute tena"

Nilikutana na hiyo meseji ya kwanza kabisa ambayo nilihisi ikiuchoma moyo wangu mpaka kwa ndani kabisa. Nilifungua na meseji nyengine ambazo pia alikua anasisitiza tuachane na hakutaka tena kuongea na mimi.

Nikaona haiwezekani nimpoteze Agness kizembe kiasi kile na hapo hapo nikampigia simu. Simu yake iliita hadi ikakata lakini haikupokelewa. Nilirudia mara tatu mfululizo na mwisho ikawa haipatikani. Nikaona sasa ujinga wangu wote niliokua naufanya haya ndio malipo yake. Kazi hazikufanyika tena kwani niliinuka na kuondoka zangu kurudi nyumbani ingawa bado ilikua mapema sana mishale ya kama saa nane mchana. Nilifika nyumbani na kupitiliza chumbani ambapo nilijitupa kitandani bila hata ya kuvua viatu. Kichwa kilikua na mawazo sana hadi nikahisi kinaanza kuuma. Nikampigia tena Aggy lakini simu yake bado ikawa haipatikani. Nikawa natamani hata Vanessa arudi muda huo ili nimshushie kipigo kwa ule ujinga alioufanya. Simu nyingi sana ziliingia lakini sikupokea hata moja kwani nilikua sijisikii kuongea na mtu yoyote kwa muda huo. Niliwaza hadi nikapitiwa na usingizi.


Nilikuja kushtuka niliposikia mlango wa chumbani unafunguliwa kwa nguvu na nilipoangalia nikamuona Vanessa akiwa amerudi kutoka kazini huku akiwa anaongea na simu.

Subiri shoga nitakupigia baadae ngoja nisalimiane na shemeji yako.

Alimkatisha mtu aliyekua anaongea nae na nikahisi itakua ni rafiki yake.

Vipi mume wangu mzima, mbona mapema sana leo?

Nikajikuta nilipomtazama usoni tu hasira zikaanza kujijenga tena upya na nilitamani hata nimrukie nimpige vichwa.

Vanessa, hivi ni ujinga gani huu ulioufanya?

Nini tena baby mbona siku hizi ugomvi hauishi?

Kwanini umemtumia Agness meseji za kijinga kama zile na namba yake umeipata wapi?

Vee alikaa kimya kidogo na kunitazama usoni na nahisi alitambua kuwa nimekasirika sana.

Sasa baby kuna tatizo gani ikiwa sasa hivi unaishi na mimi? Nimefanya hivyo ili nihakikishe unakua wa kwangu peke yangu.

Mjinga sana wewe, hivi unajua ni upumbavu kiasi gani ulioufanya? Hivi unamjua vizuri Agness wewe? Unajua mimi na Agness tumetoka wapi?

Alex unaniita mimi mjinga kwa sababu ya huyo malaya wako wa kijijini?

Unasemaje wewe? Nani yule?

Bila kutegemea nilijikuta linanitoka kofi moja zito sana na kutua usoni kwa Vanessa na kumfanya aanguke mpaka chini.

Alex unathubutu kuinua mkono kunipiga mimi kwa sababu ya huyo malaya wako.

Alikua anaongea huku analia sana na nikahisi kama majirani walikuwepo basi ni lazima watakua wamesikia kinachoendelea ndani kwetu.

Kelele! Wewe na Agness nani ni malaya? Si nimekukuta club tu wewe unatafuta wanaume.

Alex ndo unanikashifu kiasi hiko, kweli?

Utajua mwenyewe, tena nasema kuanzia leo sitaki kukuona humu ndani beba kila kitu chako na uondoke.

Unasemaje? Mimi siondoki, na hili tumbo nimpelekee nani?

Utajua mwenyewe kwani nina uhakika gani kama ni la kwangu?

Yani Alex leo ndo unanijibu majibu kama hayo mimi? Kosa langu nini lakini?

Kosa lako nini? Ina maana haujui au? Unanitenganisha na mwanamke wa ndoto zangu kwa sababu ya upuuzi wako halafu unauliza kosa langu nini? Tena nasema uondoke humu ndani leo hii hii.

Alex mimi siondoki nifanye unavyonifanya.

Nikamfata na kumuinua juu kisha nikawa namsukuma kutoka nje.

Nimesema toka ndani kwangu.

Nimesema sitoki

Vanessa alikua analia sana tena kwa sauti kubwa. Sio siri alinikera kupita maelezo na ndio maana nikawa namfukuza kama mbwa.

Vanessa alikua hana nguvu kabisa kwani nilifanikiwa kumtoa mpaka nje na nikarudi ndani haraka kufunga mlango.

Alex nifungulie mlango niingie ndani.

Sikufungulii nenda ukalale huko kwa mabwana zako.

Naomba unifungulie mlango Alex usinifanyie hivyo please.

Usinipigie kelele wewe mwanamke nimekwambia uondoke.

Vanessa alikua anaongea huku analia sana mpaka nikasikia jirani yetu mmoja akiwa amekuja.

Kaka naomba umfungulie mwenzio sio vizuri hivi unavyomfanyia pia kumbuka amebeba kiumbe chako tumboni.

Dada haujui kitu chochote kilichotokea hivyo naomba uniache tafadhali.

Yule jirani alinisihi sana lakini niliendelea kushikilia msimamo wangu.

Mara nikasikia taratibu watu wakianza kuondoka na nilipochungulia dirishani nikawaona Vee na huyo jirani wakiwa wanatoka nje kabisa ya geti.

Nilirudi chumbani na kujitupa kitandani huku kichwani nikiwa nimevurugwa sana. Siku hiyo sikua hata na hamu ya kula kwani nilikaa mpaka saa 5 ya usiku bila kutafuta chakula. Nilirudia kumpigia simu Aggy mara kwa mara lakini bado alikua hapatikani. Siku hiyo nilichelewa sana kulala kwani kila nikijitahidi usingizi ulikua hauji.


*************** ***************


Akili yangu ilikua haipo sawa kabisa tangu Aggy aliponitumia meseji na kutaka tuachane kwani siku iliyofuatia nilikua sina raha kabisa kazini. Nilivyokua nikipiga namba yake bado ilikua haipatikani hivyo nilijikuta nimeishiwa nguvu kabisa.

Alex mbona leo unaonekana kama haupo sawa, unaumwa au?

Alikua ni David akiniuliza baada ya kunikuta nimejiinamia ofisini. Nilishtuka sana kwani sikumuona wakati anaingia.

Hapana kaka siumwi.

Una nini sasa mbona upo hivyo?

Nilikaa kimya kidogo ni nikaona ni bora nimwambie ukweli tu huenda akanipa japo msaada wa mawazo.

Kaka David nina matatizo makubwa sana yanayonisumbua akilini mwangu.

Matatizo gani hayo?

Nilimeza funda la mate kisha nikaanza kumuelezea kila kitu.

Unakumbuka kama nilikwambia kuwa kuna mwanamke ninaishi naye?

Ndio, nakumbuka.

Sasa huyo mwanamke imetokea bahati mbaya nimempa mimba.

Sasa hapo tatizo liko wapi, si umuoe tu kabisa?

Hapana bado sijamaliza ndo maana haujanielewa vizuri. Tatizo kubwa sio kumpa mimba ila tatizo ni kwamba tayari kijijini kwetu nina mchumba wangu wa siku nyingi sana na ndo nimepanga kumuoa. Sasa baada ya kumpa mimba huyu mwanamke wa huku akaamua amtumie meseji chafu mwanamke wangu wa kijijini na kumtaka aachane na mimi huku akimueleza kila kitu kuwa tunaishi wote pamoja na tayari nimeshampa ujauzito.

Mhh! Kumbe mambo mazito hivyo, eenhe! kwahiyo ikawaje?

Jana mchumba wangu akanipigia simu na kulia sana huku akitaka tuachane. Nilijaribu kumuelewesha lakini hakunielewa kabisa na kuonyesha msisitizo alinitumia mpaka meseji na kutaka tuachane. Hapa tangu jana hapatikani kabisa kwenye simu yani hata sijui nifanye nini.

Mhh! Aisee pole sana Alex hayo ni mambo ya kawaida sana kwa sisi wanaume. Kikubwa unatakiwa kusimama imara kuliko wakati wowote ule ili usizidi kuharibu.

Sawa kaka, kwahiyo unanishauri nifanye nini?

Kusema ukweli mdogo wangu siwezi nikakushauri moja kwa moja nini ufanye ila hapo inabidi ufate ndoto zako. Kama huyo wa kijijini ndo unahisi ni mwanamke sahihi kwako basi hakikisha kwa gharama yoyote ile haumpotezi lakini pia huyu wa huku inabidi usimpuuzie maana tayari ameshakubebea kiumbe chako tumboni. Inabidi uwe makini sana kwenye kila kitu unachokifanya ili usizidi kuharibu.

Mhh! sawa kaka nashukuru sana kwa ushauri wako na naahidi nitaufanyia kazi.

Sawa mdogo wangu, be strong (Kuwa imara)

Aliongea huku akinipiga begani kunipa moyo.


Kidogo maneno ya David yalinipa nguvu na kuanza kupata mwanga nini nifanye. Nikaendelea na kazi hadi jioni ilipofika nikarudi nyumbani. Nilipofika nilishangaa kumkuta Vanessa akiwa na shangazi yake nje wakinisubiri mimi.



Nilipaki vuzuri gari na kushuka kisha nikaenda kuwasalimia.

Shikamoo shangazi.

Kama umeona shikamoo mali kua na wewe upate ya kwako. Hivi ni binadamu gani wewe usiye na huruma? Ina maana haumuoni huyu mwenzio yupo kwenye hali gani?

Nikaona yale makelele tutakua tunawafaidisha majirani tu hivyo niliwakaribisha ndani.

Sina shida ya kuingia ndani kwako mimi kilichonileta hapa ni kuhusu kumnyanyasa mwanangu. Hivi unadhani wazazi wake au kaka zake wakizipata hizi taarifa watafurahi? Si watakutafuta wewe wakufanye kitu kibaya. Usimuone hivi huyu kwao anapendwa sana na ndo mtoto pekee wa kike Yani inafikia hatua hadi unampiga! Kweli?

Nikaona sasa shangazi yake Vanessa anataka kuniwashia moto na kunidhalilisha pale nje na ilibidi niwaambie waingie ndani.

Ingieni ndani shangazi sio vizuri kuongelea nje kila mtu ajue nini kinaendelea.

Kama ungekua na busara kiasi hiko usingemfukuza mwanangu kama mbwa tena usiku.

Nilianza kuingia ndani na nikaona wote wakinifata huku shangazi akizidi kunishushia mvua ya maneno.

Tuliingia mpaka sebuleni maana Vanessa aliiacha funguo yake wakati namfukuza jana yake ndo maana alivyokuja na shangazi yake walishindwa kuingia ndani. Nikaenda chumbani kwanza kuvua viatu na kubadilisha nguo kisha nikarudi kuja kupokea maneno mazito ya shangazi yake Vee.

Hivi wewe Alex una malengo gani na Vanessa?

Niliona ni swali gumu sana kujibu kwani Vanessa sikua na malengo nae kabisa zaidi ya kuwa naufurahia ule uzuri wake tu na kuutumia kwa faida zangu. Niliamini kweli uzuri wa mwanamke sio kila kitu kinachomfanya mwanaume amuone ndio chaguo lake kwani mimi akili yangu yote ilikua ipo kwa Agness japokua hamfikii Vanessa kwa uzuri hata robo.

Si nakuuliza wewe, una mpango gani na Vanessa?

Nilivuta pumzi kidogo na kumeza mate kisha nikamjibu.

Nadhani Vanessa mwenyewe ameshakwambia kila kitu, mimi tayari nina mtu wangu na ndo natarajia nije kumuoa.

Unasemaje wewe? Hivi unajisikia kweli hiko unachokiongea? heeh eeeh! Kumbe wewe hautujui vizuri Wagogo eeh! Huyu utamuoa tu baba yangu utake usitake. Yani unampa mimba binti yetu halafu unasema haumuoi!

Jamani huo ndo msimamo wangu na hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.

Nasema hivi huyu utamuoa tu. Umeshampa mimba hiyo halafu unasema haumuoi! Unategemea akaolewe na nani sasa?

Nilimtazama Vanessa ambaye muda wote machozi yalikua yakimtoka tu na nilijihisi kumuonea huruma sana japo moyo wangu bado haukuikubali ile hali.

Tena nasema hivi kuanzia leo nitakapotoa mguu wangu hapa Vanessa aje kulalamika tena kuwa unamnyanyasa au sijui umemfukuza ndo utakapotujua vizuri wagogo kwanini tupo katikati ya Tanzania na sio sehemu nyengine. Nitakuletea ukoo mzima hapa na ndo utakapotujua kuwa sisi ni nani.

Shangazi yake Vanessa alikua anaongea kupita maelezo yani hadi kidume nikaishiwa maneno na kujikuta nabaki kimya sina la kuongea.

Mwanangu Vanessa hapa ndo nyumbani kwako na ishi kwa amani kabisa. Hiyo mimba italelewa, mtoto atazaliwa na huyu ndo mume wako atakayekuoa, full stop.


Nilimtazama sana shangazi yake Vanessa na kujiuliza anajiamini kitu gani hadi aongee kwa kujiamini kiasi kile.

Mimi naondoka nategemea haya mambo hayatajirudia tena na mtaishi kwa amani.

Sawa shangazi asante sana.

Vanessa alijibu huku bado akiwa kama ana sauti ya mtu aliyetoka kulia muda sio mrefu.

Sawa karibu tena.

Nilijibu kishingo upande ilimradi aondoke.

Kweli aliondoka na kutuacha mimi na Vanessa tukiwa tupo wawili tu huku kila mtu akiwa anasita kumuongelesha mwenzie. Nikakumbuka sana maneno ya David aliyoniambia kuwa nifuate ndoto zangu za kuishi na mtu ninayempenda lakini pia nisimsahau na kumtelekeza mtu ambaye alikua amenibebea mtoto tumboni. Nilimtazama sana Vanessa na moyo ukajikuta tu unasema nimuache akae pale nyumbani. Nikaamua niondoke na kuelekea chumbani ila nikashtuka kuona Vanessa amenishika mkono na kunizuia nisiondoke.

Nilimtazama usoni na kuona sura nzuri ya Vanessa ikiwa ina majonzi na kutia huruma sana huku akionyesha anataka aanze kulia.

Vipi una nini?

Alex please naomba unionee huruma mwenzio usinifanyie hivi mimi.

Nilimtazama sana kwa jicho la kuwa serious na sikuonyesha tabasamu hata kidogo.

Unataka nini kwani?

Nataka turudi kama zamani mwenzio siwezi kuishi hivi mimi, nakupenda.

Ile sauti yake na maneno aliyoongea nilijikuta nayasikia yanaingia mpaka kwenye ubongo na mishipa yangu ya fahamu hadi damu ikanisisimka.

Najua nimekukosea sana kwa kitendo nilichofanya cha kumtumia mwanamke wako meseji zile mbaya ila nimefanya vile kwa sababu nakupenda sana na sitaki nikupoteze hata siku moja.

Vee alikua akiongea mpaka machozi yanamtoka na nilijikuta naanza kumuonea huruma sana na kuingiwa na roho ya kibinadamu.

Lakini kwanini ulifanya vile Vee, si ungekaa kimya tu tukailea mimba?

I'm sorry, i'm so sorry! ( Samahani, samahani sana )

Vee alikua anaongea huku akilia kwa uchungu sana na bila kutegemea nilijikuta namvuta kifuani kwangu na kumkumbatia.

She is the woman of my dreams, i have to fight for her. ( Ni mwanamke wa ndoto zangu, inanibidi nimpiganie )

It's fine, i'll be waiting for you. (Sawa, nitakuwepo kukusubiri )

Tulikua tukiongea hayo huku tumekumbatiana. Tuliachiana kisha nikamfuta Vee machozi na kumpiga busu la kwenye paji lake la uso.

Nakupenda sana Vee, ila Agness ni mwanamke wa ndoto zangu. Siku zote ninaota nije kumuoa na kuishi nae na ndio maana nilikasirika kiasi kile na kukutamkia maneno mabaya. I'm sorry. ( Samahani )

Sasa hivi ndio naelewa yote hayo Alex mwanzo nilichukulia mzaha tu. Ila kikubwa kilichokua kinanisumbua ni wivu tu mume wangu ndio maana nikafanya yote hayo.

By the way ( Ukiachana na hayo ) namba ya Agness umeipata wapi?

Vee alitabasamu kidogo kisha akanijibu.

Nimeipata kwenye simu yako. Nilikua nakufuatilia siku nyingi sana ila ulikua haujui tu. Siku nyengine huwa unaiacha simu yako ikiwa haijaingia lock na mimi ndo hutumia muda huo kuipekua na ndo nikagundua yote hayo.

Nilitania kama nampiga kofi hivi na alianza kucheka sana. Jinsi tulivyokua usingeamini kama jana yake palitokea ugomvi mkubwa sana hadi nikamfukuza Vee pale nyumbani. Nikamuahidi kuwa nitailea ile mimba mpaka mtoto atakapozaliwa na alifurahi sana. Tuliingia chumbani na kwenda kuoga kisha Vanessa akapika chakula tukala na kupumzika.


**************** ****************


Kwa siku tatu mfululizo namba ya Agness ilikua haipatikani na nilijikuta naingiwa na hofu sana. Nikajikuta nafikia maamuzi ya kusafiri kwenda kijijini kwetu ili nikakutane nae na kuongea nae. Kweli ilipofika Ijumaa mchana baada ya kazi nilimtaarifu David kuwa naenda Tanga mara moja na kwa kua nilishamueleza kuhusu matatizo yangu aliweza kunielewa. Niliijaza gari mafuta full tank na kuianza safari mida kama ya saa 11 jioni. Nilimtaarifu Vanessa juu ya safari ile na aliweza kunielewa japo kishingo upande. Niliendesha kwa speed kubwa sana hadi sehemu nyengine trafiki walinisimamisha na kunipiga faini lakini sikujali. Kikubwa kilichokua akilini mwangu ni kuwahi kufika na kuonana na Agness. Nilivyofika maeneo ya karibu na segera nilisikia tairi ya nyuma ikipiga mzinga mkubwa hadi gari ikaanza kuyumba na kutaka kupoteza mwelekeo. Nilijitahidi kuiweka sawa na namshukuru Mungu haikuacha njia kwani nilifanikiwa kuisimamisha pembeni ya barabara na kwenda kuangalia. Nilikuta tairi ipo nyang'anyang'a haifai hata kidogo na ilibidi nianze zoezi la kupiga jeki ili kubadilisha na kuweka spair tairi. Giza lilikua kubwa sana maeneo hayo hadi nikaanza kupatwa na wasiwasi wasije wakatokea wezi au majambazi wakanifanya kitu kibaya. Magari yalikua yakipita machache sana kwani muda ulikua umeenda yapata saa 3 za usiku.. Wakati bado nahangaika kufungua tairi kwa bahati nzuri walitokea vijana wawili wakiwa wamepakizana kwenye baiskeli na niliwaomba wanipe msaada.


Kweli tukaanza kushirikiana huku nikiwa namulika na mwanga wa tochi wa simu yangu na baada ya kama dakika 25 tulifanikiwa kulimaliza lile zoezi. Niliwashukuru sana na kuwapatia kiasi cha shilingi elfu 30 ambazo niliwaona wazi kuwa kwao ni ushindi mkubwa sana. Niliagana nao na nikaingia ndani ya gari kuendelea na safari. Nilifika kijijini kwetu yapata saa 5 za usiku na nikaona kwa muda huo siwezi nikaonana na Aggy hivyo ilinibidi nilale nisubiri kesho yake. Mama alishangaa sana kwanini nimeenda ghafla kiasi kile na ilibidi nimueleze ukweli wote japo mengine nilimficha haswa suala la kumpa Vee mimba. Alinilaumu sana kwa mambo yote niliyoyafanya kwani aliona Agness ndiye mwanamke sahihi wa kuwa nae. Ila akanipa moyo kuwa nikajaribu kuongea nae huenda akanielewa kwani alikua ananipenda sana.


Niliagana na mama na kutakiana usiku mwema kisha nikaingia chumbani kwangu kulala. Mawazo yalinitawala sana kiasi kwamba usingizi ulikua hauji hata kidogo. Muda wote niliwaza ni jinsi gani nitaanza kuongea na Agness ili aweze kunielewa na kunisamehe.........



Kesho yake niliamka asubuhi na mapema sana na nilivyotoka nje sikuamini nilivyokuta taa 2 za mbele kwenye gari zikiwa hazipo. Nilishtuka sana na ilinibidi nikachukue funguo ili nikague zaidi kama kuna vitu vyengine vilivyoibiwa. Baada ya kumaliza kukagua kila kitu nikagundua kuwa ni hizo taa tu peke yake ndo zilizoibiwa. Nilikasirika sana na kutamani ningemuona huyo aliyeiba ili nimfundishe adabu. Sikua na jinsi zaidi ya kufanya utaratibu wa kununua taa nyengine na kuzifunga. Nikajiuliza kwanini safari hii imekua na mikosi sana kwani njiani nilipasua tairi la nyuma na mpaka muda ule nilikua nimefunga spair tairi tu. Nikawa najiuliza itakuwaje kuhusu kuzifunga taa maana zilikua zinauzwa Tanga mjini na ilikua haiwezekani kutembea na gari ikiwa haina taa. Nikapata wazo la kwenda kwa gari za abiria kisha nikirudi nichukue fundi ili aje kunifungia. Kiukweli watu walioiba walinipa hasara sana kwani mpaka inafika mchana namaliza lile zoezi lote nilikua nimeshatumia kama laki saba hivi pamoja na kumlipa fundi. Suala la tairi nikaona nitaenda kumalizana nalo nikirudi tena Tanga mjini wakati wa kurudi Dar. Muda wote huo wakati nafanya mambo yote hayo akili yangu ilikua ipo kwa Agness tu na nilikua nawaza sana kama ataweza kunisamehe.

Baada ya kumaliza kula chakula cha mchana nilimuaga mama na kutoka kuelekea kwa kina Aggy.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG