Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

THE WORLD HATES ME (DUNIA INA NICHUKIA) - 1

  

IMEANDIKWA NA : IDDI SIRAJI

********************************************************************************

Simulizi : The World Hates Me (Dunia Ina Nichukia)

Sehemu Ya Kwanza (1)


hali ya mawingu ilitawala katika anga ikiambatana na manyunyu yalio sababishwa na mvua kubwa ilionyesha kwa saa zima iliyopipta, mvua ilionekana kumshtukiza kila mkazi wa mji wa dar es salaam hakuna m2 alieitarajia , mvua hii ilionekana kuwa kero kubwa kwa wakazi wa mtaa wa tandika kwa maana barara nyingi za mataa huo zilijaa mtope yakiambatana namaji. wakazi wachache wa mtaa huo walipitapita wakiwa na miavuli ya o wakielekea madukani na sehemu nyinginezo. maderava wa bodaboda nao waliendelea kupita wakibeba abiria wenye haraka.

Hari ndani ya mtaa watandika haikuonekana kuwa nzuri hata kidogo maana maana polisi walioneka kana kila barabara ya mtaa huo watandika, kila aliye kuwa mkazi waeneo lile alione kushangazwa na uwepo wa polisi hao kwani walionekana kuwa na msako usio kuwa wa kawaida na kila polisi aliku amelowa chepechepe huku bunduki zao zikiwa makini katika mikono yao! Wakazi watandika walizidi kuwa na hofu pale walipo ona gari nne zilizo jaza mapolisi ambao waliruka mmojammoja kutoka kwenye gari na kuigia ndani ya vichochoro vya mtaa huo wa tandika, halikuwa gari moja peke yake bali magari mengi ya police yalindelea kupita kila kona ya mtaa huo wa tandika huku yakiendelea na zoezi hilo la kumwaga police katika vichochoro vya mtaa huo,

hofu ilitanda wakazi wa mtaa huo wa tandika hawa kujua nini kilichokuwa kinaendelea japo baadhi ya watu walibahatisha kwa kusema itakuwa ni oparation ya kusafisha wauza bangi na wauzaji wa madawa ya kulevya, lakin kila mtu alisema la kwake wengiwao waliongea wakiwa kwe vibanda vya chips na wengine wakiwa majumbani mwao wakiwa wamesimama mlangoni na baadhi yao wakiwa vibalazani ,

wakiwa wanaendelea kujiuliza maswali yasiyo kuwa na majibu mara ghafla walishuhudia gari mbili za police zikipita mbele yao zikiwa mwendo mkali zikiwa zimejaza watu waliova nguo za police lakini nguo zao zilikuwa tofauti kidogo, kwa muonekano tu watu waliweza kugundua kwamba ni FFU.!

hofu ikaongezaka !

kabla hawaja tanabahi waliona magari hayo yakiwa mwisho kabisa mwa barara yakifunga brek na kupunguza mwendo na kuanza kukata kona kwa kwa muundo wa kuangaliana kisha madereva wa magari hayao wakakutanisha gari hizo zikawa zime funga barara hiyo, na askali wagari la upande kushoto walionekana kushuka huku wakiwa wameshika vitu kama minyororo, na mmojamoja walianza kushuka huku wakiwa wame tanguliza mbwa wakubwa mbele yao!

kufikia hapo amani ilitoeka kwa wa kazi wa eneo hilo walio kuwa milagoni walifunga milango na kuenda madirashani kuchungulia wakisubiri kuona nini kingetokea, na waliokuwa vibarazani walitafuta nyumba za kuji hifadhi kwa wakati huo ,kuna baadhi walikosa pakwenda wakaamua kutulia walipokuwa wakisubiri tukio ambalo kwa hakika hawakujua ni tukio gani lingetokea kutoka kwa askari wale!

wale askali walioshuka na mbwa walikoki bundiki zao nakuondoka kwa mwendo wa mchamchaka mbwa wao wakiwatangulia kuelekea ndani yamtaa, na askari walibakia kwenye gari la pili wao walishuka nakwenda upande mwingine wa magari hayo kisha wakawa wameangalia upande waliko elekea wanzao wenye mbwa!

mudawote bunduki zao zilikuwa zimekaa makini mikononi mwao.****

kufikia muda huo wa saa 7 police walionekana kila kona ya eneo hilo liliopo karibu kabisa na stend i, kila barabara iliokuwa ina tumika kuingia na kutoka ndani ya stand ya tandika ilifungwa kwa magari ya police na hakuna gari hata moja lilo ruhusiwa kutoka ndani ya stendi hiyo ya tandika!, na watu walipo taka kwenye daradara ili watoke ndani ya stend hyo watembee kwa mguu hawakuruhusiwa na polisi waliokuwa wametanda eneo hilo!

hakuna aliejua kuna nini mpaka kufikia hatua ile!

na wingu yalitanda anga yote ikawa giza na mvua kubwa ikaanza kunyesha.

**** je? kuna nini kime ikuta tanzania mpaka kutokea opareshen kubwa kiasi hiki?




watu walitawanyika kujikinga na mvua ile, lakini hakuna polisi hata mmoja alie ondoka sehemu alio kuwepo. ****

Mtaani polisi walijaa wakipita huku na huku mvua ikiendelea kuwa nyeshea polisi hao , polisi wengine waliendelea kusimama sehemu moja ina onekana walia ambiwa wakae sehemu hiyo,

gari moja aina ya rava4 lenye namba za usajili za serekali liingia kwa kasi ya ajabu na kusimama pale kwenye gari ya FFU ilioshusha askali wenye mbwa muda mchache ulio pita, katika gari ya rava4 alishuka mwanaume wamakamu alie kuwa amevaa nadhifu nguo za kiraia za heshima, na bila kujali mvua kubwa iliokuwa ikiendelea kunyesha mtu huyo alianza kuelekea kwenye zile gari za FFU na kabla haja zifikia  zile gari askari mmoja alie kuwa hana bunduki lakini alikuwa na bastola kiunoni alionekana kuwa na cheo flani alimkalibia kabla ya kufika mtu huyo wa makamu na kumpa heshima kwa kupiga saluti,

"nipe taarifa" alisema mtu wamakamu bila hata salamu!kana kwamba aliona salaamu hiyo haina ummuhimu wakati huo!

" tumefanikiwa kufunga barabara zote zinazo toka na kuingia ndani ya stendi na askari wameenea ndani ya stendi hii.." alijibu askari aliekuwa na bastora kiunoni. mtu wamakamu hakusema kitu ila aliendelea kumuangalia kwa macho yaliyo hitaji taarifa zaidi, na yule askari aliendelea kutoa taarifa....

" ...na ndani ya mtaa tumefanikiwa kufunga barabara si chini ya 12, na askari wame tapakaa karibu robo tatu ya mtaa." askari huyo akawa amesha maliza kutoa taarifa yake, na mtu yule wa makamu aliyevaa nguo za kiraia aliingiza mkono mfukoni na kutoa RADIOCALL, na akabonyeza kitufe flani ,na akaisogeza kalibu ya kinywa chake.

"i.s.p robert naongea" aliongea mtu yule wa makamu.

"report please" sauti upande wapili uliongea.

"tumesha dhibiti upande wa stendi hakuna mtu wala gari litakalo toka nje bila idhini,kwa upande mtaani tumidhibiti karibu robo tatu ya mtaa, nita hitaji kuonana wenyeketi wa mtaa ili watulekeze nyumba za kulala wageni pamoja na vichochoro wanavyo vijua , nita hitaji askali zaidi ili oparesheni ianze" ali maliza i.s.p robert.

"sasa mimi nisha fanya mpago baada ya dakika kumi natano vyombo vyote vya habari vitatangaza juu ya oparesheni ilikuwapa taarifa wakazi watandika ili wawe watulivu wakati opareshen ina endelea, baada ya dakika kumi na nane oparesheni ianze" sauti ya upande wapili uli maliza maelezo.

"ok nime kupata and out" robert aliongea kikakamavu, na akashusha mkono wenye radio call na kumgeuka yule askari mwenye bastora kiunoni.

" tuna hitaji mwenyekiti wa eneo hili" alisema robert huku akifuta maji kwenye macho yake alikuwa ameshalowa chapachapa

"hamna tatizo mda mchache uliopita alikuja kuuliza nini kinaendelea, tulimwambia asiondoke ofsini kwake kwa muda huu na alitu onesha ofisi yake ilipo"

"vizuri afande tuma askari wamfuete haraka" alisema na kurudi kwenye gari lake na kuliegemea, dakika kumi badae mwenyeketi wa mtaa aliwasili eneo alilokuwepo robert ****

TAARIFA YA HABARI YA DHARURA! JAMBAZI ALIYE KUWA AKITAFUTWA MKOANI MWANZA KWA KOSA LA KUUWA POLISI, HUKU AKIHUSISHWA NA MAUJI YA MZAZI WAKE, IMESADIKIKA JAMBAZI HUYO AMEFANIKIWA KUINGIA DAR ES SALAM MTAA WA TANDIKA, TAARIFA ZA HABARI ZINA SEMA YAMETOKEA MAUJI YA WATU WASIO NA HATIA NDANI YA TANDIKA AMBAYO YANASEMEKANA YAME SABISWA NA JAMBAZI HUYO NA KUTOKOMEA NDANI YA YA MTAA WA TANDIKA! POLISI WANA WAOMBA WAKAZI WA ENEO HILO WAWE WATULIVU KIPINDI OPARESHEN IKIENDELEA YA KUMTAFUTA JAMBAZI NDANI YA MTAA HUO MPAKA SASA ASKARI WAMESHAFIKA ENEO LA TUKIO .

radio na tv vyote nchini vili tangaza habari hii ya ghafla kwa upande wa wakazi watandika ni wachache walio isikia maana wakati huo hofu ili tawala mtaa mtaa huo watandika wengi hawa kuwasha vyombo vya habari. ***

mwenyekiti aliwapigia simu wanyekiti wenzake na muda mchache badae walikuwa wamekutana na robert eneo la tukiokila mwenyekiti alieleza mtaa wake ulivyo na nyumba za wageni alizozifahamu katika eneo lake,robert katika kufuatilia maelezo ya wenyekiti hao, robert na yule askari waliweza kugundua kwamba upande wa magharibi wa mtaa ule ndio eneo pekee ambalo polisi hawa kuwepo kabisa, na upande huo ulionekana kuwa na vichochoro vingi,..

akili na hisia za robert ziliona upande huo wa magharibi huwenda akawa amejihifadhi jambazi waliemtafuta ambae kwa hakika alikuwa tishio, robert alitoa radio call kisha akaisogeza karibu kabisa na kinywa chake

"OPARESHENI IANZE KWA UPANDE WA STENDI KAGUENI KILA GARI FUNGUENI HATA BUTI ZA GARI , NA UPANDE WA MTAANI INGIINE KILA NYUMBA BAR NA GUEST, MSAKO UWENDE KWA KASI KUELEKEA UPANDE WA MAGHARIBI NINA MASHAKA UPANDE WANAGHARIBI OVER" alisema robert. "nimekupata sir".

oparesheni ilianza ya kumtafuta jambazi huyo.



baada ya robert kutoa maelekezo taarifa zilisambaa kwa maaskari wote waliokuwa eneo la tukio, namsako ulianza kwa kasi na vurugu kiasi ambacho haikuwahi kutokea nchini, upande wa stend askari waliingia kwenye kila gari lililo kuwepo eneo hilo walifungua kila kilicho funguka katika magari hayo , askari wakiwa na picha  ya mtu walie mtafuta waliendelea kumuangalia kwa makini kila mtu alie kuwa eneo hilo, kuna baadhi ya watu waliwekwa chini ya ulizi walio onekana wamefanana na mtu aliekuwa akitafutwa lakini baada ya kuchunguzwa na kufananishwa na picha ya mtu huyo waliachiwa, askari waliendelea kutafuta bila kuchoka japokuwa walikuwa wame lowanishwa na mvua iliokuwa ikiendelea kunyesha lakini miili ilikuwa imechemka kwa kuKIMbia huku na kule, stend yote ilikuwa kimya kilicho sikika kwa muda huo ni sauti ya mvua ikiambatana na ngurumo za mvua, watu waliokuwepo eneo la stendi walibaki wamesimama pembezoni mwa maduka yaliokuwepo eneo hilo wengine walikuwa wakipigwa mvua wao walikosa pakujikinga na mvua hiyo , polisi baada ya kutafuta sana ndani ya magari waliamua kujigawa wengine waliingia kwenye maduka ya eneo hilo la stendi na watu waliokuwa wame jikinga kwenye maduka wali tolewa nakujiunga na wenzao waliokuwa waki nyeshewa mvua!

*****

robert baada ya kuona msako umeanza yeye alichukuwa askari wanne pamoja na mwenyekiti kwajili ya kumuelekeza eneo la upande wa magharibi, ambapo robert alihisi kuwepo na uwezekano wa mtu aliye kuwa akitafutwa kukimbilia eneo hilo, baada askari wanne pamoja na mwenyekiti kuingia ndani ya gari la robert, gari liliondolewa kwa mwendo usio wakawaida hata kidogo gari liliendeshwa na robert , gari ilikatiza mtaani kwamwendo kasi,

ndani ya gari robert alionekana kuwa na hasira iliyo pitiliza mawazo yake yote yalikuwa ni kumkamata mtu huyo aliekuwa anaanza kuwa tishio nchini, akiwa kama umbali wa hatua stini mbele yake aliona gari lililokuwa katikati ya barabara huku likizungukwa na askari kama wanane ,hapo moyo wake ulilipuka na kuhisi ndani ya gari hilo kutakuwa namtu aliye tafutwa, lakini aliwaona wale polisi hawakuwa na tahadhari hata kidogo maana baadhi yao bunduki zilikuwa zimevaliwa migongoni badala ya kuwa nazo mikononi , hakupunguza mwendo alindelea na speed yake na kuwasogelea askali wale , .

askari walishitushwa na muungurumo wagari na wote wali geuka kwa wakati mmoja walishanga kuiona gari yenye namba za usajili wa serekali, wote walihisi ndani yagari hilo kulikuwa na mkubwa wakazi, wote kijasho kili watoka! na muda huo huo gari ilipiga breki kama hatua tatu mbele kutoka kwa wale askari walozunguka gari. na milango yote ilifunguka kwa wakati mmoja na robert alishuka na kutoa bastora yake kiunoni mwake, maaskari alikuwa nao robert ndani ya gari wali weka sawa bunduki zao tayari kwa kuachia risasi, robert alielekeza bastola yake usawa wa gari lile na askari alio kuwa nao ndani yagari walilizunguka gari hilo huku wakielekeza siraha za kwenye gari hilo " NANI YUMO NDANI YA GARI ?" robert ali wauliza wale askari alio wakuta eneo hilo.

* * * *

moses akiwa nyumbani kwake alishangazwa na taarifa ya habari alio kuwa akiendelea kuangalia, macho yake haya kutaka kuamini kwamba jambazi aliekuwa akitafutwa mkoani mwanza sasa yummo ndani ya jiji la dar es salaam. mawazo yake yalikatishwa na mlio wa simu iliyo kuwa mfukoni mwake , aliitoa na kuangalia nani aliekuwa akipiga mara ghafla alikunja uso! kwa sekunde kadhaa alikuwa amesha mtambua mpigaji! alipokea kwa unyonge . " habari afande!" moses aliongea baada ya kupokea.

"uko wapi na sitaki uniambie kwamba uja sikia juu ya tukio linalo endelea tandika" sauti ya upande wapili ilifoka na kumnyong'onyeza moses!

"hapana afande taarifa ndo nimeipata muda sio mrefu" moses aliongea kwa unyonge na hofu,

" baada ya kupata taarifa ukasubiri nikupigiesimu"

"hapana afande"

"sasa sikia mauji yamesha tokea mauaji tangu ABDUL awasili jijini, nenda haraka tandika katika eneo yapotokea mauji kafanye utalatibu wa maiti kupelekwa hospitali? taarifa zote unipe mimi na so mtu mwingine," na simu ikakatwa.

moses alinuka haraka haraka na kuingi chumbani mwake akachukua koti lake jeusi na kulivaa akachukua grove na bastora yake, na kutoka nje bila kuzima tv yake akatoka nje akapanda juu ya pikipiki yenye namba za usajili wa serekari na safari ikaanza.

****

"ndio afande..." alijibu mmoja wa wale askari walioulizwa na robert,

"It's ABDUL!?" robert alimkatisha kabla aja malizia yule askari,

" hapana ila tuna mtilia shaka " askari alijibu kwa kigugumizi!

"kivipi hemu mtoe mlete haraka nje" alisema robert huku akishangazwa na kigugumizi cha yule askari ,

askari mmoja alifungua mlango wagari na kumtoa mzee mweupe mnene, robert alishangaa na hapo aligundua kwamba wale askari walikuwa wanataka rushwa kutoka kwa mzee yule na ndomaana walikuwa wana wasisi mwingi,,ali wageukia wale askari akiwa amekunja uso wake,

"mnamtilia mashaka yapi babu kama huyu mlikuwa mnataka atoe rushwa sio?" aliuliza robert huku aki waangalia mmoja baada ya mwingine.

"hapana afande tusamehe...."alisema yule askari .

"nyie yaani mnaacha kazi muhimu mnaanza kuomba rushwa, au mna ona hii kazi haina umuhimu?" kimya!

"nasema hivi katika hii oparashen nitafukuzisha kazi askari wengi!" alisema huku akirudi ndani ya gari lake na askari wake aliokuwa nao na na mwenyekiti aliekuwa pembeni kidogo walimfuata wakaingia ,

"toeni hilo gari haraka " alisema na baada ya gari kutolewa ali washa gari na kuendelea na safari..

***

kundi la askari kumi na moja wakiwa na gari lao , katika kuulizia ulizia walikutana na kijana aliekuwa na mfuko uliojaa makopo, ni kijana huyu baada ya kudadisiwa na polisi alisema dakika kama kumi zilizopita alikutana na mtu alie onekana kuwa na wasiwasi , polisi mmoja alitoa picha na kumuonesha kijana huyo , kijana alisema ni yeye alie muona aliedakika chache zilizo pita

"...ndio yeye afande lakini ye amevaa miwani ya macho na suti nyeusi, piteni huu uchochoro niliotokea mimi barabara ya tano ndo nilipo kutana nae"alisema kijana huyo muogota makopo huku akielekeza kwa ishara.

askari wali jigawa wanne waliingie kwenye gari hiyo ya polisi, na sita walifuata huo uchochoro, na gari ilindolewa kwa kasi ikizunguka upande wa pili alipokuwepo mtu walie mtafuta.

****

kijana mrefu kiasi mweupe aliekuwa amevaa miwani ya macho mikono yake ikiwa ndani ya mifuko ya koti la suti aliyokuwa ameivaa, na alikuwa amelowa chepechepe, kijana huyo alitembe kwa mwendo wa kasi ajabu, macho yake haya kutilia yale angaza huku na kule alitembea kwa kuchechemea alionekana ku choka sana , alipita kwenye matope bila kujali na ni huyu ndie alie kutana na yule muokota makopo muda mchache uliopita!

****

polisi walio fuata uchochoroni walitembea kwa kasi ya ajabu na kwa umakini wa hari ya juu, ndani ya dakika kumi walikuwa walikuwa wamefikia barabara ya nane ,na kama hatua tisini mbele yao walimuona mtu alikuwa akitembea kwa kasi akisunta mguu mmoja,alikuwa amevaa suti nyeusi waliendelea kumkalibia kwa kasi kubwa huku wakiwa makini asi waone.

****

gari lilo ondoka na askari watano akiwemo dreva lili zunguka mtaa kwa kasi na kuufuata upande walioelekezwa , gari lipopita kama barabara kumi na moja dreva alikata kona na kushika barabara ya kumi na mbili, dreva alikuwa na lengo la dreva ilikuwa kusimamisha gari ili apige simu na kutoa taarifa ili askari waongezwe katika eneo hilo., akiwa mwendo wa kasi mara ghafla mbele yake hatua kama arobaini aliona mtu alievaa suti akiwa anataka kuvuka barara!

****

yule mtu aliekuwa akifuatwa nyuma na askari bila yeye mwenyewe kujua alitembea kwa haraka akisunta ili aivuke barabara alioiona mbele yake, kutokana na waswasi na mawazo pamoja na kelele ya mvua iliyo piga kwenye bati za nyumba za mitaa hiyo, huyo kijana hakusikia kabisa muungurumo wa gari la polisi lilokuwa likija katika barabara aliyokuwa akiiwahi ili avuke,

alipoingia tu barabarani mikono yake ikiwa bado kwenye mifuko wakoti ndipo kwa kihoro kikubwa macho yake yaliishuhudia gari ya polisi ikija kwa kasi alipo simama! huku nyuma akifuatwa na askari sita!

haya mtu alie onekana na muogota makopo yupo katikati ya barabara na gari la polisi inakuja kwa kasi alipo simama na polisi wa sita wapo nyuma yake bila yeye kujua je? nini kitatokea?

jina ABDULI TUMEWEZA KULISIKIA MARA MBILI LIKITAJWA JE? ABDUL NI NANI ?

tukutane kesho tupate kugundua mengi zaidi.

Itaendelea......


"ni abdul"

dereva wa gari alibabaika kumuona abdul akiwa katikati ya barabara na kabla haja fanya lolote, kwa wepesi ambao haukutalajiwa abdul alijitupa pembeni huku akitoa mkono wake wakulia kwenye koti, pah pah , miliyo ya risasi ili sikika huku abdul akijitupa pembezoni mwa barabara,

<*muda wote abdul alipo kuwa anatembea mkono wa kulia ulikuwa umeshika bastola ndani ya koti na kipindi anajitupa pembeni akiwa hewani alichomoa mkono wake kwenye koti na kufyatua risasi mbili akiwa hewani ,

abdul baada ya kujitupa chini akiwa anataka ainuke aangalie sehemu ya kujificha hapo hapo akasikia milipuko mikubwa ya risasi na hapo hapo akashuhudia baadhi ya risasi zikichimba kuta za nyumba za eneo hilo, abdul akabaki pale chini akiwa hana cha kufanya kwani risasi zilikuja kwa wingi eneo alili kuwepo maji yakiwa yamemfika shingoni.

****

robert akiwa anaendesha gari kwa kasi mara alisikia ile milipuko ya risasi ikitokea upande aliokua akielekea moyo wa robert ukaripuka kwa furaha akijua abdul kaonekana"yah hisia zangu zilikwa sahihi upande wa magharibi ndipo alipo kimbilia abdul" alijisemea robert huku akijisifu kwa uhodari wa kuhisia , mara ghafla akasikia milipuko mingine mfululizo ikitokea upande wake wa kulia, robert alipigwa butwaa kwani alisikia milipuko ya risasi pande mbili tofauti hakutaka kuamini kule aliposikia risasi mara ya kwanza ndiko aliko sikia mara ya pili ilikuwa ni sehemu mbili tofauti , robert akiwa anaendelea kujiuliza hapohapo radio call yake ikatoa mlio wa mkoromo,

"inspector robert naongea" alisema robert baada ya kusogeza radio call kinywani mwake,

" ehh afande tumevamiwa huku na wenzetu wa nne wamesha uliwa ndani ya guest walio enda kukagua" sauti iliongea ya upande wa pili ,"unafikiri atakuwa ni abdul" aliuliza robert,

"nafikiri maana wenzetu waliingia kukagua kwenye guest hiyo na mara wakashambuliwa ndani ya guest, na walio shambulia wapo zaidi ya mmoja kwa kifupi tunaomba msaada msaada" taarifa hii ilimchanganya robert robert alijiuliza ina maana abdul alikuwa na kundi lake huko tandika 'yah inaweza ikawa ndomaana aliamua kukimbilia huku' alijijibu robert,

"hemu muulize guest ina itwaje" sauti ya mwenye kiti iliuliza kutokea nyuma ya robert,

"ah wazo zuri.... eti we hiyo guest inaitwaje" robert aliongea na watu wawili kwa wakati mmoja,

"ah eh ni coconut guest"

"washa gari twende na pajua"alisema mwenye kiti,

"sawa lakini acha ni wape kwanza taarifa askari wote" alijibu robert,

robert akawaalifu askari wote waliokuwa kwenye oparesheni waelekee coconut guest kwani huko ndiko waliko shambuliwa wenzao.

robert alipo maliza akawasha gari na kuanza kuondoka .

<<<*****

askari waliokuwa mtaani baada ya kufanya msako bila kufanikiwa waliamua waanze kusogea upande wa upande wa magharibi kama walivyo ambiwa na robert, gari lenye askari kumi na moja lilianza kuondoka kuelekea magharibi na ni hili gari ambalo askari wake walikutana na yule muogota kopo alie waelekeza alipo muona abdul. na gari la pili lili ondoka na askari kumi na mbili gari hili lilipita barabara nyingene, baada ya mwendo wa kasi dreva wa gari lenye askari kumi na mbili alisimamasha gari baada ya kuona bar moja na guest moja pamoja na grocery moja ndani ya mtaa alio kuepo akaona ni vyema washuke na wakague ile guest na bar pamoja na grocery. "oya shukeni tukague eneo hili fasta tuondoke.... wanne muende kwenye ile guest na wanne wengine waende kukagua kwenye ile bar na watatu mnifuate tukakague ile ile grocery", alisema dreva alie onekana kuwa kiongozi wa askari wale. kulitokea ubishi kidogo kwani kuna askari nane wali gombea kwenda kwenye guest kukagua , hii ilitokana na askari hawa kila walipo enda kukagua guest wali vunja milango ya vyumba ambamo wali kuta baadi ya watu wakiwa wakifanya mapenzi na wali wakuta wakiwa kama walivyo zaliwa kitendo hiki kikapelekea askari kupenda kukagua guest kuliko sehemu nyingine , yule askari alie kuwa anaongoza askari hao ali wakemea baada ya kuona wana leta masihara kwenye kazi,

"haya bwana nendeni mkawachungulie vizuri" alisema askari mmoja katika wale wanane huku akijitoa kwenye kundi lile na wenzake watatu wakafuate,

"bwana sasahivi sio zamu yenu tuachieni tukajionee vibwanga" alisema askari mmoja kati ya wale wanne walio baki.

msako ukaanza na wale askari waliokuwa wamepangwa kukagua guest walitembea haraka na kuingi ndani ya guest hiyo iliyo itwa coconut guest, askari wale wakatoa taarifa juu ya msako wao ndani ya guest na wakaanza kukagua,

walivyo fika kwenye korido ya vyumba vya guest wakajigawa wawili wawili ili waanze kukagua vyumba vile,

askari wawili wakagonga chumba kimoja wakafunguliwa wakaingia waanze kukagua, na askari wawili wengine waka gonga chumba kilichofuata ... kimya! hakuna aliitika wala kufungua chumba kile.

askari hawa wawili askari wawili wakaangaliana wakajua mule ndani kilicho kuwa kinaendelea ni mapenzi , askari hao wakapeana ishara kuwa wavunje mlango ili wakajionee mambo, askari mmoja akarudi nyuma na kuurukia teke mlango ukafunguka na ghafla askari alie bomoa mlango akatupwa kwenye ukuta na kuanguka chini kama mzigo! na mlio wa risasi ukasikika! askari wapili alipigwa butwaa hakujua mwenzake katupwa na nini, askari akainua bunduki yake kuelekea kwenye kile chumba lakini alichewa kwani hapohapo risasi mbili zili toboa kifua chake zikitokea kwenye chumba walicho bomoa mlango! askari wawili wakawa chini huku mmoja akiwa na tundu likivuja damu kwenye paji la uso wake. wale askari wengine walioingia kwenye chumba cha kwanza walisikia ile milipuko ya risasi iliyo tokea chumba cha pili wakatoka haraka ili wawa saidie wenzao lakini walikua na bahati mbaya kwani walivyo tokeza tu kwenye korido walipokelewa na risasi mfululizo zilizo toka kwa watu wawili walio simama kwenye maiti za wenzao. watu hao wawili baada ya kuona askari wanne wamesha kufa, watu hawa wawili wakaingia kwenye chumba walicho kuwemo wakachukua mabegi yao mawili yaliojaa wakaanza kukimbia wakitoka nje ya guest askari .

*** wale askari wanane walio kuwa wanafanya msako kwenye bar na grocery walisikia ile milipuko ya risasi kutokea kwenye guest walio ingia wenzao ndipo wakaanza kukimbia kwenda kuwa saidia wenzao,

"itakua ni abdul kashambulia tuwahi tuka wasaidie wenzetu" alisema yule kiongozi huku akitimka mbio.

walivyokua wanaiingia ndani ya guest ile ndipo wakaona wale vijana wawili wenye mabegi wakiwa na bastola mikononi mwao wakitokea kwenye korido walikua kama umbali wa hatua thelasini askari hawa kusita walianza kuwatupia risasi wale watu ambao nao kwa wepesi walijitupa chini waka biringita kuridi kwenye korido ambapo walipata cover na kuanza kuwatupia risasi askari bila kuwa pata kwani askari nao walikuwa wame jikinga kwenye ukuta wa counter, asakari na wale watu wawili wakaendele kutupiana bila kupatana.

yule kiongozi wa askri wale alivyo iona hari ile ndipo alipo amua kumpa taarifa robert juu ya tatizo hilo la coconut guest.

*****>>>

taarifa alietoa robert ilizagaa kwa askari wote ndani ya oparesheni ile askari wakaanza kumiminika kuelekea coconut guest,

robert nae kwa kuelekezwa na mwenye kiti akafanikiwa kufika coconut guest na magari mengine ya polisi yakafika eneo hilo na askari wakazunguka guest hiyo bundiki zao zikiwa makini mikononi mwao, askari wakaanza kujiandaa wavamie ndani ya guest hiyo........

je? hawa watu wawili walio ua polisi wanne ni kina nani? kwani wame ua polisi?

je?nini kitawakuta maana wamezungukwa na asakari.

upande wa pili abdul alijitupa chini na kuachia risasi mbili, lakini kipindi anataka kuamka ana shuhudia risasi zikitua eneo alipo na risasi nyingine zina chimba kuta za eneo hilo je? abdul atapona hapo?



askari wote mtaani baada ya kupata taarifi za tukio la coconut guest walianza kukimbia wakiulizia guest hiyo ya coconut guest.

robert kwenye gari alikuwa akielekezwa na mwenyekiti njia ya kufika kwenye eneo la tukio, na muda mchache gari la robert lilifunga breki mbele ya coconut guest,.

na maaskari wengine walianza kuingia eneo hilo la tukio na wakanza kujipanga kuvamia ndani ya guest .!

yule askari aliekuwa na kumi na mbili  alimueleza robert jinsi ilivyokuwa.

"unafikiri wamo wangapi ndani ya guest " aliuliza robert,

"sifahamu afande ila tulio waona na kuwashambulia ni wawili tu"

"kati ya hao mmoja ni abdul?"

"sikuwaona vizur lakini nafikiri abdul nimmoja kati yao,"

robert akaanza kuumiza akiri jinsi ya kuvamia ndani ya guest hiyo hakutaka kupoteza askari hivyo ilibidi apange mpango wamaana ambao hauta gharimu maisha ya askari wake,

alivyo geuka nyuma yake aliwaona wale ffu wenye mbwa kumi na tatu na hapo akapata wazo zuri alilo liona litafaa.”tuta achilia mbwa waingie ndani ya guest nasisi tutaanza kusogea taratibu kwa taadhari askari wengine zungukeni eneo lote la hii guest" alisema robert na wale FFU waliwapa mbwa ishara ya kuingia ndani ya guest na wakikuta chochote washambulie, mbwa wakatoka mbio wakiwa wameachama midomo yao na kuzama ndani guest hiyo.

wale vijana wakiwa wamesimama kwenye korido hawa kuamini kuona wingi wa askari wale na walijikuta wakijutia kitendo cha kuwa shambulia askari wale wanne.

<<

hawa vijana hawakuwa na uhisiano wowote na abdul! wao waliingia ndani ya guest ile wakiwa na mabegi yao yaliojaa madawa ya kulevya, walivyokuwa ndani ya chumba chao ndipo walisikia mtu akigonga mlango wao kwa nguvu, kijana mmoja aliamka na kwenda kuchungulia kupitia tundu dogo la kitasa na kuona mtu aliegonga mlango alikuwa askari, na hapo hapo alimuona askari akirudi nyuma ili abomoe mlango ,jamaa ali rudi nyuma kidogo yule askari alipobomoa tu mlango ndipo huyu mtu mwenye madawa ya kulevya alimtandika risasi ya kichwa askari yule akaanguka kama mzigo sakafun, mzigo wamadawa walio kuwa nao ulikuwa mkubwa na wathamani ndomaana wali amua kuwauwa wale askari wanne,hawa kutaka hata kidogo madawa yale yakamatwe, lakini kwa kufanya hivyo walikuwa wamejiingiza kwenye janga kubwa kwani mpaka sasa askari walijaa nje wakidhani kati ya watu waliokuwemo ndani na abdul alikuwemo,

>>> vijana hao wakiwa kwenye korido walianza kulaumiana wao kwa wao," wewe usige mpiga risasi wale askari unge acha tukaongea nao " alisema mmoja akimlaumu yule aliemtandika askari risasi ya kichwa, kabla yule kijana ajajibu chochote hatua kama tano mbele aliona mbwa watatu weusi wakija pale walipo kuwa kwa kasi ya ajabu ni wale mbwa kumi na tatu wa FFU!

*************************

<

ABDUL baada ya kuachia risasi mbili akiwa hewani alijitupa chini na kuanza kubiringita akitafuta sehemu ajifiche lakini hapohapo alisikia milipuko mikubwa ya risasi kutokea kule alikotokea na hapohapo alishuhudia risasi ziki chimba kuta za nyumba za eneo alipo angukia abdul alibaki palepale chini akiwa hana la kufanya maji yalikuwa yamemfika shingoni kwani wale askari sita waliokuwa wakimfuatilia nyuma yake ndio walio kuwa wakimtupia risasi mfululizo pale alipo kuwa,

<<zile risasi alizo achia abdul kuelekea kwenye gari ya polisi hazikumpata mtu ila zili pasua kio cha mbele yagari hilo dereva alivyo kosakoswa na risasi hizo alihamanika na gari ilikuwa kasi mno. gari ilimshinda alipalamia nguzo ya umeme gari ikapinduka mara mbili huku mayowe  yakiwatoka askari, gari ilipinduka marambili ikawa imeanguka vibaya mbele ya wale polisi waliokuwa wanamshambulia abdul, gari hiyo ili watenganisha kati ya polisi na abdul ikawa ndio bahati ya abdul kwani askari wale sita waliacha kumtupia risasi, polisi waliacha kupiga risasi na wakaanza kulisogelea gari la wenzao lililo pinduka vibaya, walilisogelea ili wa wasaidie wenzao walikuwa wame umia vibaya mno kutokana na ajali ile, kitendo cha wale askali kuacha kumshambulia abdul na kuanza kulisogelea gari lililo pinduka walikuwa wame fanya kosa kubwa sana!... kwani abdul aliamka harakaharaka akapiga goti moja chini na akainua bastora na kulenga tanki la mafuta la gari , alikuwa ameishika bastola kwa mikono yake yote miwili akatulia kama sekunde tatu akaachia risasi mbili mfululizo!.., wale askari waliokuwa wakilisogelea gari hilo wakiwa kama hatua moja kulifikia lile gari hapo wakasikia milio miwili ya risasi na kabla hawajafanya chochote ,ulitokea mlipuko mkubwa bele yao na wote wali tupwa nyuma na kuanguka kama hatua tano nyuma na hapo waliangukiwa na vyuma vilivyo toka kwenye gari lililo lipulika, hakuna hata mmoja aliinuka eneo hilo, askari mmoja aliendelea kulia kwa sauti ya chini iliyojaa manung'uniko akiomba msaada alikuwa ameangukiwa na mlango wa gari ulio kuwa juu ya mgongo wake. risasi alizo kuwa amepiga abdul zilitosha kabisa kusababisha mlipuko mkubwa uliosikia mtaani kote, maiti za askari walikuwa ndani ya gari hilo zili tawanyishwa na mripuko wagari hilo, miili ya maaskari hao zilizagaa eneo lile huku kitu kama mfano wa gari kikiendelea kuteketea kwa moto, abdul hakutaka kupoteza muda aliamka kutoka pale akiwa na matope nusu ya mwili wake akaanza kusunta kuelekea kwenye uchochoro uliokuwa karibu yake, yule askari aliekuwa akilia akiwa kakandamizwa na mlango wagari kwenye mgongo wake aliacha kulia pale alipo muona abdul akiamka, kama hatua tatu mbele ya yule askari kulikuwa kuna bunduki, askari yule alitamani sana ainuke achukue ile bundiki na amwagie abdul risasi na alianza kujinua lakin akashangaa hawezi hata kujitikisa akageuza shingo yake ili angalie nini kilicho mkandamiza,...haku amini macho yake kwani taili la gari lilo endelea kufuka moshi mweusi lilikuwa limemkandamiza kwenye miguu yake na hapo alianza kusikia maumivu makali kupita kiasi, kwa uchungu alimuona abdul akichechemea na kuingia kwenye kichochoro, moyo ulimuuama sana kumuona abdul akitoweka alikuwa yupo taya kufanya kila njia ili amuue abdul alikuwa yupo tayari hata kufa nae lakini mazingira hayakuruhusu hata kidogo , kutokana na maumivu ya kukandamizwa na taili na mlango ulio mkandamiza mgongoni hasira zili mbana na akaanza kulia kwa sauti kubwa kiasi iliojaa hasira kubwa!

ule mlipuko uli shtusha mtaa mzima na watu waeneo lile walianza kukimbia ovyo, kama ilivyo kawaida ya wabongo ulipotokea mlipuko ndipo walipo elekea watu ili wa shuhudie nini kinacho endelea, abdul akiwa uchochoroni alisikia kelele za watu zikija eneo hilo alilokuwepo na akasikia baadhi ya milango ya nyumba ikifunguliwa ya eneo hilo . ABDUL BADO ALIKUWA KWENYE HATARI.

****************

MOSES aliendesha pikipiki kwa mwendo usio wa kawaida huku kichwani mwake akifikiria jinsi abdul alivyokuwa akisumbua jeshi, moses alivyofika tandika askari wali muonyesha yalipo tokea mauaji , muda mchache akawa amefika eneo yalipo fanyika mauaji eneo hilo la tukio lilikuwa limezungushiwa uzio mwekundu liki zungukwa na maaskari, tukio lilikuwa limefanyika katikati ya barabara ya mtaani, moses alivuka uzio huo mwekundu na kuingia ndani ya uzio huo, moses alipigwa butwaa pale alipoona miili mitatu iliyo lala bila ya uhai pembeni ya gari ambalo lilikuwa limegonga ukuta !, kilicho mshanga moses ni wale maiti ngozi na nywele za maiti wale! nywele zile ndefu laini na ngozi nyeupe yenye wekundu vilitosha kumthibitishia kuwa hawakuwa raia wa afrika, mikononi mwa miili ile kulikuwa na bastora zilizo wekwa viwambo vya kuzuia sauti, moses alizidi kushangaa , 'vyombo vya habari vilisema walio uwawa na raia wa tanzania mbona hawa ni wazungu?' alijiuliza moses huku akitoa grove na kuzivaa, akapiga hatua moja na akachutama karibu na maiti hizo ,eneo walipo lala maiti hao kulikuwa kumetapakaa damu, 'inamaana kabla ya kufa walikuwa wakishambuliana na abdul alie waangamiza au hawa ni FBI?' alijiuliza na kuanza kuwa pekua maiti wale kwenye mifuko ya suruale zao, kwenye kila mfuko wa maiti zile moses alifanikiwa kupata kupata vitambulisho na passpot za kusafilia, alipo angalia vitamburisho vile aligundua walikuwa raia wa ufaransa! alizidi kushangaa 'hawa sio fbi hawa ni raia wa kawaida wa ufaransa, sasa kwanini walimshambulia abdul?' alizidi kujiuliza maswali ya siyo na majibu, alivyo endelea kukagua aliapata tiketi za ndege ,tiketi zilionesha waliwasili nchini saa kumi na moja alfajiri. moses akasimama akaangalia lile gari lililo kuwa limepalamia kona ya ukuta milango yote ya nyuma na wa mbele mmoja ilikuwa wazi alipoangalia ndani ya gari aliona maiti ya mfaransa ikiwa imetapakaa damu kifuani, na hapo akaona matundu madogo mawili kwenye kio cha mbele, na hapo alitambua kabla ya ajali mshambuliaji alimpiga risasi dreva kupitia kwenye kio cha mbele, moses akatoa simu yake mfukoni na kubonyeza batani flani kisha akweka simu sikioni..

"ume maliza kazi niliyo kutuma?" iliuliza sauti kutoka upande wapili,

"afande hii kesi ngumu na ina nichanganya! " alisema moses.

"kivipi? "

"afande hawa watu waliokufa sio raia wa nchini na inaone..."

"wewe mimi nimekutuma kuchukua maiti na na sio kwa ajili ya uchunguzi umeelewe usiniambie upuuzi" sauti ya upande wapili ilimkalipia moses..

"lakini afande mimi ni inspector nina uhuru wa kuchunguza!" alisema moses kwa sauti bila kujali anaongea na mkuu wake wakazi..

"wewe kama huwezi kufanya niambie na nina tuma askari wengine waje kufanya hiyo kazi ok?" na simu ikakatwa.




moses alishindwa kuelewa ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea ,hapo akaanza kuhisi kuna kitu kikubwa mno kilichokuwa kimefichwa, ilionekana wazi kabisa hawa wafaransa walikuja kwa ajili ya mtu alietafutwa na jeshi la polisi 'kwanini wanamtafuta abdul na kwanini I. G. P anaonekana kuwa tofauti' alikosa majibu,

alitoa simu yake akaenda upande wa camera akaanza kupiga picha wale maiti wa ufaransa, akampiga picha na ule mwili kwenye gari aliekuwa dreva,akapiga na sehemu gari ilipo gonga ukuta akatoka kwenye uzio akarudi nyuma aka piga picha moja iliyo piga eneo lote la tukio, kisha zile picha alizopiga akaziamishia kwenye faili flani ndani ya simu yake,

alivyo weka tu simu mfukoni, akiwa amefumbata zile ticket za wale maiti, aliona gari la polisi likiingia , askari mmoja alishuka kutoka kwenye gari hilo na kumsogelea,

"mzee hii ni oder kutoka makao makuu tunachukua maiti hizi na kuzipeleka hospitali ya muhimbili" alisema askari alieshuka kwenye gari,

"sawa endeleeni hamna tatizo" alijibu moses, yule askari alivyo ondoka moses alivua haraka grove na kudumbukiza zile ticket kwenye grove kisha akatia zile grove kwenye mfuko wasuruale yake akashusha pumzi ndefu, wale askari walio kuja kuchukua zile maiti walipakia zile maiti wakaogota vitambulisho vya maiti zile, wakautoa ule mwili uliofia ndani ya gari , moses moyo wake uliuma sana kukosa vitambulisho vya miili ile, kwani kwake vitambulisho vile vilikuwa ushahidi ambao ungemsaidia katika kesi hiyo ambayo aliamua kuifutilia kwa kina, alicho ambulia yeye ilikuwa ni picha za miili ile pamoja na ticket za marehemu wale,

baada ya askari kupakia miili ile kwenye gari, askari mmoja aliingia kwenye gari lile la wafaransa lilo gonga ukuta, askari baada ya kuliwasha gari lile likatoa muungurumo tu .

"afande halitaweza kutembea mzee" alisema askari alie ndani ya gari

"tuta lifunga kwenye gari yetu acha tulisukume tulitoe sehemu hiyo" alisema askari alie toka kuongea na moses muda mchache uliopita,

moses alisaidiana na askari wale, waka lisukuma lile gari na kulifunga cheni kwenye gari lao polisi ,baada ya kumaliza dreva aliwasha gari na kuanza safari ya kuondoa maiti za wafaransa eneo la tukio.

moses alitazama msafara huo wakati ukiondoka, na hapo simu yake ikaita.

"popote ulipo ungana na robert opereshen magharibi mwa tandika over"

"ok sir" alijibu moses akaenda kwenye pikipiki yake akaiwasha na kabla ya kuondoka akampigia robert iliamuelekeze jinsi ya kufika eneo la tukio, baada ya kupata maelekezo akaiondoa pikipiki kuelekea alipo elekezwa na robert..

************

coconut guest...

yule jamaa alivyo ona mbwa watatu wana kuja mahali walipo kuwa alishindwa hata kupiga risasi maana mbwa walikuwa wame wafikia walikurupuka wote kwa pamoja wakitaka wakimbilie kwenye chumba chao lakini walichelewa kwani mbwa waliwarukia na kuanguka,na muda huo mbwa wengine kumi walifika na kuanza kushambulia, bastola za wale vijana zili watoka mikononi bila kutegemea ,mbwa walikuwa wakiwakwaluza na kuwa vuluta, jamaa walipiga kele za maumivu wakiomba msaada,

mayowe ya hao jamaa yalisikika kwa askari wote waliokuwepo eneo la tukio ,

"wamesha anza kushambulia askari tuingie kwa tahadhari abdul ni mtu hatari"alisema robert yeye alijua mule ndani alikuwemo abdul ,kweli robert alikuwa gizani.

askari waliingia kwa style za kuvamia palipo na adui, robert na asakari walivyoingia walikuta vijana wawili wakivulutwa na mbwa huku wakipiga kelele za kuomba wasaidiwe, kwa haraka haraka walijigawa maaskari wengine walienda kuwaweka chini ya ulinzi wale vijana na kukataza mbwa waache kushambulia, vijana wawili walitulia kama sanamu waliona nibora kukamatwa na askari kuliko kularuriwa na mbwa, askari wengine wali angusha msako mkubwa ndani ya guest hiyo , walivanja milango ya vyumba vya guest hiyo ndani walikuta raiya wema waliojaa hofu lakini abdul hawa kumuona, walibinua vitanda vya kila chumba lakini hawakuona mtu alieitwa abdul ,walifunua mpaka makapeti lakini wapi.

robert alifura na kutembea mpaka pale walipokuwa wame wekwa wale vijana walio shamburiwa na mbwa,

alisogea mpaka walipo vijana wale ambao nguo zao zilikuwa zime raluriwa na mbwa,

alichutama mbele yao,

"nyie abdul kajificha wapi?" aliuliza robert kwa sauti ya chini huku akiwatazama mmoja baada ya mwingine,

"abdul? ndio na..." kabla haja maliza kusema kijana huyo, kwa wepesi wa ajabu robert alimtandika ngumi nzito ya shavu kijana huyo yowe kubwa likamtoka akagalagala chini akilia kama mtoto, robert akamka akanyanyua mguu wake wakulia kwa nguvu akamshindilia kifuani yule kijana wapili na kumkandamiza ukutani akatoa bastola yake kiunoni , akaielekeza kwa yule alimpiga ngumi ya shavu,

"nyie mbwa nitawaua kifo ambacho hamtazikwa na mtu ila manispaa, na uliza kwa mara ya mwisho na risasi itafanya kazi yake! ABDUL YUKO WAPI?" aliuliza robert kwa sauti kali,

vijana waliendelea kulia na kushindwa kujua abdul ndo nani,

"mzee usituue sisi tumeingiza madawa ya kulevya kutoka south na kama ni boss wetu anaitwa george na sio abdul" alisema kijana alikanyagwa kifuani na robert, kijana alimtaja boss wake bila kupenda,

"aaah nyie mnaona mi na cheza ! afande leta mbwa hawa wafe kifo cha kuliwa na mbwa" alitamka robert huku afande mmoja akisogeza mbwa, robert hakuyaamini maneno ya wale vijana hata kidogo.

"hapana afande unatua bure we angalia hata mabegi yetu yale yana madawa usifanye hivyo afande" walisema wale vijana huku wakilia na kusaga miguu chini kama kama watoto,

"hemu kagueni hayo mabegi" alisema robert ,na askari mmoja akaanza kufungua mabegi ya wale vijana, walitoa baadhi ya nguo kama tano na kukuta pakti za madawa zilizojaa kwenye mabegi ya vijana hao,

"umeona afande ni hivyo tu na hakuna vingine afande usituue" alisema kijana alie kandamizwa ukutani na mguu wa robert,

"nyie msi tuche..." kabla hajamalizia kuongea robert ,ukasikia mlipuko mkubwa maskio mwa askari wote na baadhi ya raia waliokuwa eneo hilo, ni ule mlipuko wa gari lilio pigwa risasi na abdul,

mlio ulipotokea ni kule robert alipo zisikia risasi kabla ya kusikia zile za hapo coconut guest,

robert akahisi mwili kuingiwa balidi baada ya kusikia mlipuko huo 'dah ina maana hawa kweli hawa husiani na adul? inaweza ikawa matukio yameingiliana , kule nilipo sikia risasi za kwanza ndipo nimesikia mlipuko umetokea! ' alijiuliza maswali mengi abdul,

" hawajamaa watakuwa kweli watakuwa hawana uhusiano, huko ulipotokea mlipuko nilisikia risasi kabla sijaja huku but nikapuuzia, maana niliambiwa huku ndiko abdul ameshambulia na kundi lake, kumbe sio abdul ni hawa vibwengo pumbavu" alisema robert huku akimuangushia teke zito la tumbo yule kijana aliekuwa akigalagala sakafuni,

"afande fanya utalatibu wa kupeleka miili ya askari wetu wanne hospital wakahifadhiwe,na hawa wajinga wapeleke kituo cha polisi kilichopo karibu mimi na askari wengine tunaenda ulipotokea mlipuko"robert alimwambia askari alie pembeni yake,

"sawa afande"

"nyie vibwengo wawili naenda kumsaka abdul ,nikimkosa mtaubeba msalaba wa abdul na mtajuta" alisema robert kuwaambia wale vija wenye madawa ya kulevya, robert alitoka ndani ya guest huku askari wakimfuata nyuma na zile mbwa za ffu, alipotoka nje aliangalia upande alio hisi kutokea mlipuko na kwambali aliona moshi mweusi ukifuka kuelekea mawinguni na ndicho alicho kihitaji,

"hey askari wote tunafuata upande ule unapo onekana ule moshi sio mbali na hapa tulipo" alisema robert akinyoosha kidole chake kulekea alipo uona ule moshi,

kisha akaingia kwenye gari na kuliwasha

" askari wanne ingieni ndani yagari yangu, wenginne ingieni kwenye magari yaliokuwepo, mtakaokosa njooni haraka kwa miguu" alisema na askari walianza kupanda kwenye magari ,pale kulikuwa kuna magari ya polisi sita tu, magari hayo yalijaza askari mpaka wakaisi kubanana,

Robert akaliondoa gari lake kwa kasi huku magari sita yaliojaza askari yakimfuata kwa mwendo uleule,

Hapakuwa mbali sana kufika kwenye huo mlipuko,

Wakiwa wanaanza kukaribia eneo la tukio walianza kuona watu wakikimbia ovyo huku na huku.

*******

UPANDE WA ABDUL.............................

ABDUL alitulia kwanza akiwa ana panga mpango wa kuondoka eneo hilo, na hapo akaona kundi la watu likipita likielekea pale kwenye ili barabara ,ambayo gari la polisi liliendele kuteketea kwa moto,

lile kundi lilivyo fika eneo latukio ikawa patashika!, kwani walipofika hawa kuamini walichokiona, ile miili ya maaskari iliyo onekana eneo lile pamoja na gari lilo endelea kuteketea kwa moto ilitosha kujulisha wale watu kwamba eneo lile halikuwa salama hata kidogo,

hakuna alie vumilia kuendelea kuwa pale ,ni afadhali ile miili ingekuwa ya raia wa kawaida, moja kwa moja kila mtu alijua kilichotokea pale ni vita, watu wakaanza kukimbia ovyo ovyo wakijua vita vimeingia nchini.

yule askari alie kuwa amekandamizwa na taili miguuni pamoja na mlango wa gari mgongoni, alijalibu kuwaita wale watu walio kuwa wana kimbia ovyo waje kumpa msaada, lakini sauti yake haiku sikika kwani kulikuwa na kelele nyingi na vulumai ya wale watu,

akiwa pale chini akiita bila kusikika hapohapo aka muona abdul akitoka kwenye kile kichochoro haraka na akaji changanya na wale watu waliokuwa wakikimbia ovyo , kwa uchungu yule askari akiwa chini kakandamizwa na mlango na taili ya gari alimuona abdul akianza kuondoka akikimbia kwa kusunta akitokomea,..

robert na maaskari wanapo karibia eneo la tukio ,na abdul anajichanganya na watu na kuanza kuondoka eneo hilo lakini kina robert hawapo mbali na tukio je ?abdul atafika mbali?.......



ROBERT alivyoona watu wakitawanyika ovyo aliongeza kidogo mwendo wa gari,

ikiwa bado kama hatua hamsini gari la robert lifike pale kwenye ule moshi robert aliona kama mfano wa gari ukifuka moshi barabarani ,robert alisimamisha gari akashuka pamoja na askari alio kuwa nao, na magari ya polisi yalio kuwa nyuma yake yalisimama askari wakashuka,

"sio sehemu ya kuingia kichwa kichwa nahisi kuna kitu tofauti, tuingie kwa mfumo wa kuvamia" alisema robert huku macho yake yakiliangalia eneo lile kwa makini, sauti za wananchi zilisika zikitokomea eneo lile,

"jamani muhakikishe tuna vamia kwa tahadhari na ndani ya dakika mbili tuwe tumesha zunguka eneo lote lilozunguka la tukio" alisema robert na zoezi lile likaanza,

askari watatu waliondoka kwa kukimbia huku bunduki zao zikiwa makini mikononi mwao, walisogea askari wale watatu kama hatua ishirini waka jibanza nyuma ya nyumba moja iliokuwa karibu na eneo la tukio waka piga goti moja chini na kuelekeza bunduki kwenye lile gari lilokuwa likifuka moshi,

na askari wengine watano wakakimbia na kuwapita wenzao pale walipo jibanza kisha na wao waka chukua cover na kuelekeza bunduki zao eneo la tukio,

zoezi hilo liliendelea kwa muda wa dakika kama mbili na sekunde arobaini, na askari tayali walikuwa wamesha jaa eneo hilo na kulizunguka .

Robert baada ya kuona eneo lote lile lilikuwa lime dhibitiwa akaanza kuhesabu hatua kuelekea pale kwenye gari lilo kuwa likifuka moshi.

***

Moses akiwa kwenye pikpiki yake akielekea alipo elekezwa na robert ,alipo kuwa njiani ndipo alisikia mlipuko ule ulio sababishwa na abdul,

alisimamisha pikipiki yake na kuangalia kule mlipuko uliposikika na hata yeye akauona moshi ukipanda juu, hakutaka kuchelewa aligeuza pikpiki yake na kuindoa kwa speed kuelekea kule alipo uona moshi ukifuka, akiwa kasi aliona watu wakikimbia ovyo wakitoka eneo alipo kuwa akielekea ,alisimamisha pikipiki yake,

"ebwana kuna nini huko?" moses aliuliza wale watu waliokuwa wakikimbia ovyo,

"eh ni vita mwanangu usiende we geuka turudi" alijibu kijana mmoja huku akiendelea kutimka mbio....

moses alishangaa kusikia et vita ,alitaka kusita asiende, lakini yeye kama inspctor lile tukio lili muhusu na istoshe ndio kazi ilio mleta, akaiweka sawa bastola yake kiunoni ambapo angeweza kuikwapua kwa haraka wakati wowote , akawasha pikipiki na kuanza kusogea eneo la tukio,

****

robert hakuamini macho yake pindi alipofika eneo ambalo muda mfupi uliopita abdul na askari walishambuliana,

robert alishika kichwa huku mwilini mwake akihisi baridi likimtembea, maiti nne za askari mbili zikiwa katikati ya barabara na mbili nyingine zikiwa pembeni kidogo mwa barabara, nguo za kipolisi zilizo kuwa mwilini mwa maiti zile zilione kana kuungua ungua , vipande vipande vya vya vyuma vilivyo ruka kutoka kwenye gari lilolipuriwa vilizagaa eneo lile ,

robert aliendelea kuchanganyikiwa hisia zake hazikuamini kwamba askari wale wameshambuliwa na abdul, 'inamaana wameshambuliwa na abdul, au kuna kikundi kime washambulia' wazo la kwamba abduli alikuwa na kundi lake mtaa huo, wazo hilo alianza kuliamini.'duh ni hatari ina maana wame tumia bomu kuwa shambulia askari hawa?' robert aliendelea kuamini kwamba askari walilipuliwa na bomu, hakujua kwamba ni risasi mbili tu za abdul zilitosha kulipua gari lile na kuwasambaratisha askari,

wakati robert anaendelea kuwaza ndipo akasikia muungurumo wa pikipiki alipo geuka alimuona moses akiingia eneo lile,

moses alishuka kwenye pikipiki na kutembea mpaka alipokuwa robert,

moses nae alipigwa butwaaa kubwa baada ya kuona miili ya wale askari,

"ni watu gani wame shambulia?" aliuliza moses,

"hata mimi najiuliza swali hilohio nimefika hapa muda sio mrefu" alijibu robert kwa sauti ya kukwaluza kidogo,

"siuliniambia niambia mpo sijui coconut guest na ukasema mnahisi abdul alikuwemo humo ina maana huku wameshambuli watu tofauti na abdul? , na vp kwenye guest mlifanikiwa kumpata abdul?" moses aliuliza kwa mfulululizo,

" hapana coconut guest hatukumkamata abdul, kuna matukio mawili tofauti yameingiliana kwa wakati moja" alijibu robert,

"kivipi afande?"

"wewe hili sio eneo la kuulizana maswali kinachotakiwa hapa ni kujua nani kashambulia na abdul kakimbilia wapi?" robert alifoka na moses akawa kalifahamu kosa lake pale hapakuwa mahali sahihi pa kuulizana maswali,

"sorry sir"

"usijali acha tujalibu kukagua eneo kwa makini na labda tutapata cha kutu saidia"alisema robert, na moses hakuhitaji kupoteza muda akatoa bastola yake na kuanza kusogea eneo lilipokuwepo gari lilio ungua moto, na robert akaanza kukagua zile maiti alihisi huwenda akawepo mmoja mzima na kuokoa maisha yake.,

Moses alivyofika kwenye gari alitaka kupiga yowe kwa woga lakini alijizuia na kuishia kuguna kwa mshangao kwani hakuamini alicho kiona kwenye gari katika kiti cha dereva aliona maiti nyeusi iliyo kuwa ikifuka moshi kwa mbali ikiwa imekaa kwenye kiti cha dreva, ilikuwa nimaiti ya dereva wagari hilo, yeye wakati gari lina lipuka alikuwa hana fahamu hata kidogo kwani baada ya kuparamia nguzo ya umeme alipoteza fahamu moto wote ulimuishia na akawa maiti yenye kutisha,

moses alibaki kasimama vilevile woga wakibinadamu ukaanza kumuingia,

moses akiwa amesima na bastola yake hapo akasikae sauti ya mtu kuugulia maumivu, sauti ilitokea upande wake wakulia, tangu afike kwenye hilo gari alikuwa hajaangalia kabisa upande wake wa kulia kulipokuwepo na uchochoro mpana kidogo.

moses kwa haraka aligeuka na kuelekeza bastola yake kule kulipotokea ile sauti, na hapo ndipo akaona wale askari sita waliolala kimya kwenye uchochoro huo.. (ni wale askari walio tupwa nyuma na mlipuko wagari).

na hapo hapo moses akamuona askari alEikuwa chini ya taili la gari na mlango akigumia kwa maumivu,

"afande kuna askari mmoja mzimaaa" moses alipiga kelele kumjulisha robert,

robert alishtuliwa na sauti ya moses ,robert alitoka mbio kuelekea pale alipokuwa moses na askari wengine walimfuata nyuma,

moses na robert walifika kwa pamoja kwa yule askari aliekuwa kakandamizwa,

moses haraka haraka aliutoa mlango, kisha waka shilikiana kutoa taili kwenye miguu ya askari yule,

ile wana maliza tu kutoa taili, ya gari yule askari alie tolewe mlango na taili aliamka kwa wepesi akasimama akataka kupiga hatua akachukue ile bunduki iliyo kuwa hatua tatu ,lakini miguu haikumruhusu kwani lile taili zito lilikuwa limemuumiza kwakiasi kikubwa ,askari akashangaa badala ya kupiga hatua akasikia maumivu makali kwenye miguu na akaanguka chini na kudakwa na kina robert , robert na moses waliishangaa hali ile,

"ha inamaana nimevunjika miguu" ali uliza yule askari huku akilia,

"afande tulia tuambie nini kimetokea na nani kawashambulia?" robert alimuuliza askari yule wakiwa wamemshikilia pale chini,

" niachieni nikamue kwa macho yangu nimemuona akiangamiza askari wenzangu na kwa macho ya nime liona likijichanganya na raia na kukimbia likisunta... Moyo wangu unauma sana amekimbia mbele ya macho yangu .,. " yulea askari alisema huku akilia kwa sauti iliyo kauka.

"nani?" aliuliza moses,

"na kaelekea wapi?" akadakia robert,

" kwani tupo kwenye kazi ya kumtafuta nani?" aliwarudishia swali Na akaendelea " nime muona akikimbia kunyoosha barabara ile na kisha kupotelea kwenye vichochoroni, abdul ameua askari wenzangu kama masiara!" alijibu yule askari huku akilia kwa jazba,

kila mtu alishtuka kusikia ni abdul ndie alie shambulia,

"na wenzake waliekea upande upi?" robert aliuliza, akiamini abdul hakuwa peke yake kipindi ana shambulia,

" WENZAKE WA KUTOKA WAPI?, MI NIMEWAMBIA ABDUL AMEKIMBIA KUELEKEA UPANDE ULE, MBONA MNAPOTEZA MDA, BADO YUPO ENEO HILIHILI, HAJA FIKA MBALI ,AMEONDOKA KAMA DAKIKA SABA ZILIZO PITA !, YUPO PEKE YAKE HAKUWA NA MTU MWINGINE?"

askari aliongea kwa kufoka bila kujali alikuwa anaongea na wakubwa wake wakazi,

robert kusikia hivyo alisimama wima,

"askari wote fuateni hilo eneo kagueni kila sehemu " alisema robert na bonge la msako ukaanza kwa kasi upande aliko kimbilia ABDUL.....



MSAKO UKAWA UMEANZA MOJA TENA KWA KASI, MILANGO YA NYUMBA YA MITAA ILE ILIVUNJWA NA MAASKARI ,NA MAASKARI WALIPO INGIA KWENYE NYUMBA ZILE WALIKAGUA KILA KITU KUNA MUDA MWINGINE WALIVUNJA MAKABATI NDANI YA NYUMBA WALIMO INGIA, KILA NYUMBA ASKARI WALIMO INGIA WALIACHA PAKIWA HAPATAMANIKI HUKU, NYUMBA NYINGI ZILIKUWA HAZINA MTU NDANI YAKE KWANI WATU WENGI WALIKIMBIA BAADA YA KUSIKIA MLIPUKO WA GARI,

MBWA WA FFU WALIENDELEA KUHAHA WAKIWA MIKONONI MWA FFU WALIO SONGA MBELE KUMTAFUTA ABDUL.

" Afande fanya mpango wa kuiondoa miili ya askari, na kuangalia ambao bado wazima wawaishe hosptal" nisauti ya robert ilio mwambia moses,

"sorry sir hii kazi inatuhusu ilisha kuwa kazi ngumu, acha tuache askari mwingine afanye utaratibu wa kupeleka hosptal askari wenzetu , na mimi na wewe tuongoze opareshen ya kumsaka abdul" moses alijibu na robert alimuelewa,

" wazo zuri , hey afande fanya kazi hii muaishe haraka afande mwenzetu alieumia miguu haraka" robert alimjibu moses ,na kumpa majukumu yale askari aliekuwa pembeni yao,

"sawa afande" alijibu yule askari alie pewa majukumu ya kusimamia zoezi la kuondoa askari wote walio shambulia,

"tuondoke afande"

alisema robert kumuambia moses,

robert na moses wakaanza kupiga hatua kwenda lilipo elekea kundi kubwa la askari kumtafuta abdul,

walipo fika eneo ambalo msako ulikuwa unaendelea, waligawana maeneo robert akaongoza maaskari waliokuwa upande wa kulia,

na moses aliongoza askari kwa upande wa kushoto.

askari aloachwa kufanya kazi ya kupeleka askari hosptal , akishirikiana na baadhi ya askari walio baki eneo hilo baada ya kukagua vizuri walifanikiwa kutambua kwamba wale askari walio tupwa nyuma kwa mlipuko wagari bado walikuwa wazima ila walikuwa taabani wakipumua kwa mbali,

"afande tuite gari la wagonjwa hawa wanne pamoja na alievunjwa miguu wawaishwe hosptal?" askari mmoja alimuuliza askari alie achiwa majukumu yale ,

"hapana afande muda hautoshi na istoshe hosptal haipo mbali na hapa tulipo acha tuwapakie kwenye magari yetu, mmoja akasogeze gari karibu" alijibu yule afande, na hapohapo askari mmoja alikimbia kuelekea kule yalipo achwa magari yao akaende akaingia kwenye gari lililo kuwa nyuma kabisa na kulisogeza kule karibu ,

kwa uangalifu mkubwa waliwapakia wale askari walio kuwa mahututi na kisha wakambeba yule askari alikuwa ame umia miguu yake kwa kukandamizwa na taili wakamkalisha pembeni ya kiti cha dreva na wakamfunga mkanda , kisha askari wanne wakapanda nyuma ya gari walimowekwa wale mahututi kwa ajili ya kuwashika ili wasijipigepige kwenye bodi la gari, na gari likaondolewa kuelekea hosptal ya temeke, baada ya gari hilo kuondoka likasogezwa gari jingine kwa ajili ya kupakia zile maiti nne, walipakia zile maiti nne kisha wakasogea kwenye gari lilo ungua na hapo wakalazimika watafute mifuko ya laironi wakavaa mikononi ili waishike ile maiti ya mwenzao iliokuwa ndani ya gari ikiwa haitamaniki kuangaliwa mara mbili, walisaidiana kuitoa ndani ya gari huku harufu mbaya ikiwapa shida kuivumilia ,wakafanikiwa kuipakia maiti hiyo iliyo kuwa imekakamaa na gari likaondolewa kupeleka maiti zile.

rober aliendelea kuendesha opareshen hiyo huku akiwa na mzigo mkubwa wa mawazo kichwani mwake, alishindwa kabisa amtafasiri vipi abdul, aliendele kufikiria tukio lile alivyo likuta na askari walivyo sambaratishwa kana kwamba palitokea mapambano ya makundi mawili tofauti alikumbuka alivyo sema yule askari kwamba alieshambulia alikuwa alikuwa abdul peke yake 'au yule afande amechanganyikiwa?' robert aliendelea kujiuliza maswali yasio kuwa na majibu, robert alikilaumu sana kile kitendo cha yeye kubugi kwa kuelekea coconut guest muda ule na kuacha kwenda alikozisikia zile risasi za mara ya kwanza, kama angeenda alipo sikia risasi wangeweza kumdhibiti abdul, robert alilaani kitendo cha lile tukio la wale vijana wenye madawa guest kwa kuingiliana na tukio la msako wa abdul , robert hakuwa na wakumlaumu, yote yaliyo pita kichwani mwake yalikuwa majuto tu! .aliendelea kuendesha msako huku akiwa anatamani abdul afanye tena kosa la kushambulia kwani aliamini kwa muda ule kama abdul ange shambulia hata kidogo ni lazima nayeye abdul ange zikoga risasi za askari waliokuwa eneo hilo.

"LAZIMA ATAPATIKANA TU KWANI YULE ASKARI ALISEMA DAKIKA SABA ZILIZOPITA NDO ABUL ALIKIMBILIA ,BADO YUPO ENEO HILI!" alisema robert na kuwa hamasisha askari waingie kila sehemu hadi mwenye mabafu ya eneo lile.

mawazo aliyokuwa nayo robert haya kutofautiana sana na mawazo ya moses,

moses nae alimfikilia sana abdul ,alishindwa kabisa kujua abdul alitumia umahiri gani kuwashambulia askari 'huyu inaonekana alitumia bomu kushambulia' alijiwazia,

kitu kingine alijiuliza sana kuhusu uwepo wa wafaransa katika swala la abdul, moses alijua majibu yote atajibiwa na abdul pindi watakapokuwa wamemkamata, moses akaongeza kasi katika kuongoza msako huo, huku akitamani kumkamata abduli akiwa mzima kabisa.

***************************^^^^^^

ABDUL alipo jichanganya na watu walio kuwa wakikimbia ovyo, alianza kukimbia kwakasi huku akisunta mkono wake ukiwa umeshika kwenye bega lake la kushuto alikuwa akipata maumivu makubwa kwenye bega lake kwani pale alipojitupa na kuachia risasi mbili kushambulia gari la polisi alipo jitupa aliangukia upande wake wakushoto na kujiumiza bega ambalo kwa hakika lilikuwa limepitia misukosuko mingi,

abdul aliendelea kukimbia huku akikenua na kuuma meno kwa maumivu alikuwa yupo kwenye maumivu makubwa mno lakinI hakutaka kusimama hata kidogo kwani kwa kufanya hivyo alihisi kuyachezea maisha yake, alijua fika baada ya ule mlipuko ulisikika na watu wengi hasa adui zake kichwani mwake alikuwa akihofia sana watu flani waliokuwa wana msakama tangu awasili dar es salam saa tano asubuhi ya siku ile, abdul alihofia sana kwani alijua kwa muda ule alitafutwa na askari pamoja na wabaya wake,

alizidi kuulazimisha mguu wake kukanyaga japo alipata maumivu, wasiwasi mwingi ulitawala hisia za abdul kwani kipindi ana kimbia alipishana na watu wengi alihofia kama ingetokea bahati mbaya wale watu aliopishana nao kama wangemtambua kuwa ni yule anaetafutwa nchini wasinge muacha kwani serekali ilikuwa imetangaza zawadi nono kwa yeyote atakae fanikisha kwa kukamatwa kwa abdul,

bahati ilikuwa kwa abdul kwani watu hawakuwa na mda wa kumtazama mtu usoni kila mtu alikimbia kimpango wake ,

abdul alisimama ghafla mbele ya njia panda alionekana kana kwamba anaangalia apite njia ipi kati ya njia mbili zilizokuwa mbele yake akaangalia eneo hilo alipokuwepo kana kwamba ana vuta kumbukumbu, akatazama nyumba za mtaa ule, na harakaharaka akakata kona kuingi upande wake wa kulia akaacha barabara na kuingi kwenye vichorochoro na mbio zikaendelea, mtaa alioingia ulikuwa kimya na muda huo mvua ilikuwa imeanza kukatika yalikuwa yamebakia manyunyu abdul alikimbia mwendo wa dakika tatu ndani ya kichochoro akasimama nyuma ya nyumba ambayo haikuwa na dirisha nyuma abdul akawa kaegemea ukuta huo huku akitweta na kukohoa alijitaindi sana asikohoe sana kwani alijua eneo lile lilikuwa na baadhi ya watu kama wange msikia anavyo kohoa lazima wange mdadisi, akaendelea kutweta pale kwa muda wa sekunde saba, kisha akajivuta mpaka kwenye kona ya nyumba hiyo aliyokuwa ameegemea,akaawa anachungulia upande wapili wapale alipo kuwa, akatembeza macho eneo lile hakuona mtu yoyote, akageuza kichwa chake upande aliotokea hakuona mtu, alitembeza macho yake eneo lote lile akalizika, akaanza kutembe kwa mwendo wa kawaida akielekea ule upande aliokuwa aki chungulia, akatoa mkono wake uliokuwa begani akaanza kutembea akijitaidi asitunte kwani kwa kufanya hivyo kama kuna mtu angemuona lazima angemtilia mashaka, abdul akaanza kusogea alipita nyumba kadhaa na kuanza kufuata kajumba kaliko kuwa kamejitenge na nyumba zile ,alitembea mpaka kwenye mlango wa ilenyumba ambayo kwa hakika ilitwa chumba na sio nyumba , abdul alipofika kwenye mlango wanyumba hiyo aliingiza mkono wake wakulia mfukoni mwasuluale yake ndani ya suruale aliikamata bastola yake vizuri, na kwamkono wake wakushoto ukanyonga kitasa cha mlango ule, akasukuma ule mlango talatibu na ulivyoa anza kufunguka akaingia ndani kwa haraka na kutoa bastola yake ikawa mkononi baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo.

"we vipi mwanangu abdul mbona unaingia kimagumashi"aliuza kijana aliekuwa amekaa kwenye kochi ndani ya chumba kile,

"ah majanga mwanangu nilihofia kunaweza kukawa kuna ambushi humu ndani" abdul alijibu huku kifungua ndoo ya maji iliyo kuwa pembeni yake akachukua kikombe kilicho kuwa juu ya ndoo hiyo na kuanza kunywa maji kwa mfululizo alikunywa maji mengi sana kisha alivyotosheka akakitupia pembeni kikombe alicho nywea maji kisha akakaa kwenye kitanda kwa kujitupa .

"hah unakaa wakati unajua unatafutwa muda huu na utitiri wa polisi?" aliuliza kwa mshangao yule mtu alikuwemo ndani ya chumba kile,

"sasa nifanye nini beka au unataka niende wapi?"alijibu abdul kwa kukata tamaa,

"et ufanyeje hemu angalia kwenye tv unavyo tafutwa" alisema huyo mtu huku akilekeza kidole kwenye tv iliyo kuwa kwenye kona ya chumba hicho, yule mtu aliamka akachukua stuli mbili na kuzibebanisha kuelekea juu kisha akaenda kufunga mlango uliokuwa umeachwa wazi kidogo na abdul ...PUUH...alibamiza kwanguvu mlango na sauti ya mlango huo ukawa umesikika eneo lile, LILIKUWA KOSA KUBWA MNO!

******

Robert akiwa anaendelea kutafuta bila mafanikio ,aliamlisha askar wakamate baadhi ya raia waliokuwa wana kimbia ovyo na kuwa dadisi kwa ukali ,

na baadhi ya watu walisema nikweli kuna mtu aliwapita na kuendelea kukimbia kwa kusunta.

"alielekea wapi?" aliuliza robert kwa ukali mkubwa,

"alinyoosha na hii barabara alipo fika pale mbele alisimama kidogo na kuingia kulia" alisema baba mmoja wa makamo,

robert alivyo sikia hivyo Ali toka mbio pamoja na askari wenye mbwa,

walikatiza na kuingia kwenye kile kichochoro alicho pita abdul, wakati wana endelea kukimbia mbwa mmoja aligoma kukimbia na kuanza kubweka na kupalamia ukuta uliko pembeni ya uchochoro , ulikuwa ni ule ukuta alio uegemea abdul muda mfupi uliopita,

robert alishangaa kuona mbwa aki nga'ngania kuupalamia ukuta ule, robert akausogelea ukuta huo, na alivyo angalia kwa makini aligundua kuna mtu alieegeme ukuta huo muda mchache uliopita,

wakati anaendelea kutazama ukuta huo, HAPOHAPO WALI SIKIA MLANGO UKIFUNGWA KWA KUBAMIZWA! (niule mlango alimo ingia abdul)




yule mtu alie bebanisha stuli mbili na kuubamiza mlango aligeuka na kumuagalia abdul.

"panda hapo juuya hizo stuli uingie kwenye dali fanya fasta" alisema yule mtu kumuambia abdul,

"sasa beka nitaingia kwenye dali kwa kuyayuka au ? mbona hamna sehemu ya kupitia?" ali uliza abdul huku akisimama kwa mshangao,

" ebwana panda fasta au unataka kunipoza" beka alifoka kwa sauti ya chini, na hapo abdul akaamua kupanda juu ya zile stuli asijue ataingia vipi dalini,

"haya sukuma fasta hiyo kingbodi uisukume pembeni humo humo ndani na uingie fasta" beka alimuambia abdul baada ya kupanda zile stuli, abdul hakuamini kwani kulikuwa na kipande kimoja cha kigbodi kilikuwa kime shikizwa tu na kilikuwa kimefungwa kamba ndani ya dali ili kisianguke, abdul alishika moja ya mbao iliyo kuwa ndani ya dali ile na kuanza kujivuta juu akawa ana ingia ndani ya dali hiyo, alipata maumivu makubwa kwenye bega lake pamoja na kupata maumivu hakulia kwasauti akihofia majilani kumsikia na kujiletea balaa,

beka alivyoona abdul kaanza kung'ing'iniza miguu, alichukua stuli moja akaiweka pembeni kidogo na kisha akapanda kwenye stuli kisha akaishika miguu ya abdul na kumsukuma azidi kuingia, abdul alivyo sukumwa na beka aliingia haraka na kumalizikia kwenye dali ile .

"ahsante partner" alisema abdul kumshukuru beka,

"rudishia hiyo singibodi fasta partner" beka alimjibu abdul bila kujibu shukurani aliyopewa kutoka kwa abdul,

abdul alirudishia ile singibodi vizuri singibodi ikawa imefiti vizuri kama haikutolewa vile,

beka akachukua harakaharaka dekio lilokuwa humo ndani akafuta matope ya abdul na alama za viatu vilivyo baki kwenye stuli, akatazama kwenye sakafu akaona alama za viatu vya abdul mule alimokanyaga abduli akawa anataka kuinama aanze kazi ya kufuta zile alama, lakini kabla hajainama PUUH , beka alisikia mlango ukipigwa na kitu kizio na ukafunguka!


robert alivyo sikia ile sauti ya kubamizwa kwa mlango, aliangalia kule aliko sikia ile sauti,

"afande hiyo sauti itakuwa imetokea kwenye ile pale nyumba ilio jitenga" alisema askari mmoja mkononi akiwa ameshika mnyororo wenye mbwa ,

"yah hata mimi nime gundua hilo, huyu mtu aliye egemea kuwa kwenye huu ukuta ni abdul maana nyayo zake zimetokea tulikotoka na zinaonekana hapa alipokuwa ameegemea ukuta, inamaanisha alivyo fika hapa alivuta pumzi na nyayo za viatu vyake zina onesha zimetoka hapa kuelekea kwenye hiyo nyumba iliyo jitenga, na hiyo sauti ya mlango tulioisikia itakuwa ni baada ya abdul kuingia kaufunga kwa kuubamiza kwasababu amechoka" hisia za robert ndivyo zilivyo mwambia,

"humo ndimo kaingia abdul sasa twendeni tunapo fika mmoja ana piga teke huo mlango ukifunguka askari wanne mnaingia ndani kwa wepesi na kwamtindo wa sarakasi" alitoa amri robert na askari wali koki bunduki zao na kuanza kuifuata ile nyumba alimo ingia abdul,

robert alishikilia bastola yake ki uhakika , huku mawazo ya kumkamata abdul yakitawala hisia zake, robert alijua fika abdul kwa muda huo kamwe asinge weza kutoroka cha zaidi ni kwamba kama abdul akijifanya mjuaji basi risasi za maaskari ingekuwa vazi lake ndani ya mwili wake, ndivyo robert alizidi kuwaza huku akiendelea kupiga hatua kuelekea ilipokuwa nyumba ile ambayo kwa hakika alikuwemo abdul, askari aliokuwa nao robert walikuwa wengi sana baadhi ya askari walihofia kama ingetokea wangepangwa kuwa wa kwanza kuingia ndani ya nyumba ile walijua kabisa kitendo cha wao kuvunja mlango na kuingia ndani ya chumba kile ilikuwa ni kukifuata kifo, kwani kila askari alikuwa na woga baada ya kushuhudia vifo vya askari wenzao,

askari walifika kwenye uwanja wa nyumba ile kwa usiri wa hali ya juu, askari wakaizunguka ile nyumba ndogo kabisa wote walikuwa wameelekeza siraha zao kwenye nyumba hiyo,

robert kwa kutumia mikono yake aliweza kuwapa ishara askari watano kwamba wavamie, askari wanne walisogea wakasimama pembezoni mwa mlango ule wakiwa na hofu kubwa kwa kumhofia abdul, na askari mmoja aliekuwa amejaa mwili aliulikia teke ulemlango kwanguvu ukafanguka na askari walio kuwa pembezoni wakajitupa ndani ya chumba kile,

beka akiwa anataka kufuta zile nyayo za abdul ndipo akasikia mlango ukipigwa na kitu kizo aliinua uso wake kwa haraka,

"simama hapo na utulie ,kabla hatuja kutoboa mwili wako kwa risasi" askari mmoja alimfokea beka huku akimuelekezea bunduki beka , beka akawa ameganda kama sanamu la post, na hapo hapo askari mmoja alimsogelea na kugeuza bundiki yake kisha yule askari alimpiga beka na kitako cha bunduki tumboni, beka alinama na kushika tumbo akiugulia maumivu, na hapo alisukumwa kwa wale askali watatu ambako askari alimdaka na kuanza kumtoa nje alivyo fika mlangoni beka alisukumwa kwa nguvu na askari yule na kuangukia kwenye uwanja uliojaa askari rukuki na mbwa watatu waliokuwa mikononi mwa polisi waliruka na kumzingira beka...


Robert yeye aliposikia sauti ya askari ikimshuritisha beka, yeye alijua alieshurutishwa alikua ni abdul, baadae akamuona askari akimtoa mtu na kumsukuma chini,

"tulia abdul" robert aliongea kwa sauti akidhani alie sukumwa pale chini alikuwa ni abdul, beka akiwa pale chini kazungukwa na mbwa aligeuka kule alipo sikia sauti ile na hapo macho ya robert ya kabibiliana na uso wa beka.!

Rober alimtazama beka kwa mshangao maana alicho tegemea nikwamba yule angekuwa ni abdul,

"nyie mbona sio abdul!" robert aliuliza kwa kuwaka,

"afande sisi ndo tumemkuta huyo huyo" alijibu askari alie msukuma beka,

"ebwana kagueni kwa tahadhari abdul yumo humo humo" alifoka robert kisha akasonya kwa hasira,

ndani ya chumba askari walibinua kitanda kusukumia pembeni godoro,

askari kama wangekuwa wachunguzi wangeweza kutambua kwenye shuka kulikuwa kulikuwa na alama za mtu alie lowanishwa na maji kukaa juu ya kitanda hicho na hiyo ingemaanisha kuwa abdul alikaa hapo muda so mrefu, lakini askari walitumia nguvu sana kuliko kuchunguza, hawa kuweza hata kuona alama za viatu vyenye matope alizo kanyaga abdul, wao walikuwa busy na kubinua kitanda na kochi moja lilokuwa ndani ya chumba kile, zile nyayo za abdul zilitoeka na kufutika kwa kukanyagwa na viatu vya maaskari askari bila kujua walifuta kielelezo cha kuwemo kwa abdul ndani ya nyumba ile ,

askari walitafuta sana ndani ya chumba kile lakini hawa kumuona abdul,

askari walibaki wame simama na wengine wakiwa wameshika viuno hawakujua watafute sehemu gani nyingine maana wamesha angalia kila sehemu ndani ya chumba kile,

"afande abdul hayumo humu ndani" alisema askari mmoja kwa sauti kumuambia robert,

"nini? " aliuliza robert kwa mshangao mkubwa, na hapohapo akainuka na kuingia ndani ajihakikishie mwenyewe..,


******

abdul alipo ingia ndani ya dari akaanza kujisawazisha ili akae vizuri hapohapo moyo wake ulilipuka alipo sikia mlango umevunjwa , alijuafika waliovamia pale walikuwa ni adui zake na sio polisi, na kwanjisi alivyo wajua adui zake alijua kinacho fuata pale ilikuwa ni mateso ya beka ,na alijua kabisa beka asinge vumilia mateso ni lazima beka angetaja mule alimukuwemo yeye,

abdul alianza kusikia ile purukushani, abdul aliingiza mkono wake mfukoni taratibu na kutoa bastola yake, 'wakianza kumtesa tu nawashukia kwa ghafla nimalizane nao' aliwaza abdul,!

robert aliingia ndani kwa haraka alipo angalia chumba kilivyo kuwa alishangaa sana mazingira yalionesha kabisa hapakuwa na mtu mwingine humo ndani zaidi yao aliangalia kwenye kuta zote nne akizania anaweza kuona tundu ambalo alitumia abdul kutoroka lakini hakuona kitu, robert alishindwa kuamini,

"sasa katorokaje huyu?" robert aliuliza bila kujibiwa,

"huyu huyu tulie mkuta humu ataeleza abdul alipo." robert alisema kwa hasira na kuanza kutoka nje kumfuata alipo kuwa beka.



ROBERT alitembea mpaka pale alipokuwa amekaa chini ,akasogelea akachutama mbele ya beka,

"nani jina lako" robert alimuuliza beka kwa sauti ya chini huku akimtazama kwa macho ya kumchunguza,

"beka" beka alijibu mara moja kisha akatulia kimya kama hakujibu kitu, robert aliendelea kumuangalia kwa macho yalio hitaji majibu zaidi kutoka kwa beka,

beka aliendelea kuwa kimya huku macho yake yakitizamana vilivyo na macho ya robert,

"ndio basi umeshamaliza kutaja jina lako?" aliuliza robert baada ya kuona beka hataji jina la baba yake,

"ndio afande au naruhusiwa kutaja na a.k.a?" aliseme beka na hapohapo kofi zito kutoka kwa robert lilitua usoni mwa beka, beka alisukumwa na kofi mpaka chini, kofi alilopigwa beka lilimpa maumivu akatulia pale chini kama sekunde nne akainuka tena na safari hii hakumuangalia robert usoni ila aliangilia pembeni kidogo,

"taja jina la baba yako pumbavu nani umtajie a.k.a hapa?" alifoka robert,

"afande we uliniuliza jina langu na sio la baba yangu, haya anaitwa john" alisema beka kwa kulalamika,

"unamiaka mingapi?" aliuliza robert,

"ishirini na mbili"

robert ndo huwa kawaida yake akiwa ana muhoji mtu humuuliza maswali mengi ilikumchanganya,

"unauhusiano gani na abdul?" robert alimtupia beka swali huku akimuangali kwamacho ya chuki,

" ndio nani huyo" hapohapo beka alipigwa ngumi ya shavu beka akaachia yowe la maumivu ngumi ilimsukuma mpaka chini kwa mara ya pili,

beka maumivu aliyo yapata beka ilibidi atulie kwanza pale chini,

robert alikamata kola ya shati la beka na kumuinua ,

" sijaja kucheza narudia tena abdul yuko wapi" alisema robert huku akimtikisa beka kwa nguvu,

"mzee sikuelewi mbona unanitesa bila kosa?" beka alirudisha swali bila kujibu swali la robert ,

" utanielewa tu nasema hivi muda mchache uliopita abdul aliingia chumbani mwako tuambie alitoka na kuelekea wapi?" robert aliuliza kwa kirefu,

" dah afande umefika mbali huyo abdul mwenyewe mnaemsema bado sijamjua then unasema eti ameingia getto mbona sielewi?" beka alijibu kwa kulalamika,

kwa kusema hivyo beka alikuwa amejipalia moto kwani robert alisimama na kumshindilia teke zito mbavuni kisha robert akachomoa kirungu kilicho kuwa kiunoni mwa askari aliekuwa pembeni yake, na kuanza kumpiga beka kwenye viungo vya mwili wake, beka alipigwa kila mahali kasoro kichwani, kisha robert akasitisha kipigo na kuagiza askari mmoja alete stuli kutoka kwenye chumba cha beka , stuli ikaletwa robert akaiweke vizuri, kisha akamuinua beka aliekuwa chini akiugulia maumivu ya virungu ,beka aliinuliwa na robert kisha akakarishwa kwenye stuli ,uso wa beka ulikuwa umeanza kumuka kwa mbali, mwili mzima alikuwa ametapakaa matope,

" usipende kujiingiza kwenye matatizo ambayo si lazima uyaingie" robert alimwambia beka kana kwamba anampa ushauri nasaha,

" mimi sija jiingiza kwenye matatizo afande matatizo ndo yamenikuta nyumbani kwangu" beka alisema kwa sauti ya chini..

" haya niambie abdul yuko wapi?" robert aliuliza tena,

"abdul wa wapi?" teke la kifua lilimkuta beka na kumtupa nyuma kama mzigo ,ilikuwa niteka la robert ambae kwa muda huo alikuwa akivunja sheria kawa kumtesa raia badala ya kumfikisha kituoni,

robert akamfuata pale alipo anguka beka,

"wewe mi najua kila kitu, abdul aliingia kwenye chumba chako na ndipo mkafunga mlango kwa kuubamiza au na hapo utabisha?" robert alimuambia beka ili kumthibitishia kitu alicho kuwa akimuuliza, angekuwa ni mtu mwingine au mimi na wewe kwa kielelezo hiki robert alicho mwambia beka cha kubamizwa kwa mlango lazima ange babaika na kuingie kwenye mtego, lakini kwa beka haikuwa hivyo,

"hah! afande nikiwa ndani naangalia tv mlango ulisukumwa na upepo ukawa umefunguka, nami nikaenda kuufunga kwa kuusukuma kwa nguvu ukawa umeji bamiza" alimaliza beka kujitetea, hapo moyo wa robert ulishtuka hakutaka kuamini kwamba hisia zake hazikuwa sahihi,

" watu wote wa mtaa huu wametoka na kukimbia ovyo baada ya kusikia mlipuko,imekuwaje wewe kujiamini na kuendelea kukaa ndani ya chumba chako, hii inamaanisha uliendelea kukaa kumsubili abdul, na ulijua ule mlipuko ulisababishwa na abdul" robert aliendelea kumshutumu beka,

"ah mimi niliona kwenye tv kwamba askari walikuwa na msako ndani ya mtaa huu, na nilivyo sikia mlipuko nilijua ni askari wakikikabiliana na mtu walie mtafuta mimi nikaona ni bora kutulia ndani kuliko kutoka nje ambako kwa hakika nyie mliendelea na msako wenu" beka alijitetea kwa point nzuri na nzito , robert alinyong'onyea aliona yale maneno ya beka yalikuwa na ukweli, lakini hisia zake zilipinga vikali maneno yale ya beka, lakini baadhi ya askari walianza kuyasadiki,

"wewe usijitie ujanja hapa bila kusema alipo elekea abdul utajuta kuzaliwa" robert aliendelea kuweka ngumu.,

"ok, afande kwakuwa shelia ya tanzania imefikia hatua ya kumlazimisha mtu aseme kitu asicho kijua, na kumpiga na kumtesa bila ushahidi, pouwa nifanye utakavyo nifanya maana nimejitetea ninavyo uweza." beka alisema kwa manung'uniko mpaka baadhi ya askari wakamuonea huruma,

"pumbavu usijifanye unajua shelia, ushahidi ni alama za viatu vya abdul viliekea kwenye nyumba hii" robert alisema na kumkwida beka kwa nguvu,

"sasa afande kama umeoni nyayo za abdul kuingia geto kwangu na unasema abdul kaingia ndani mwangu, si mkamchukue humo mlimo muona mbona mnaning'ang'ania mimi au mimi ndo abdul" beka alizidi kujitetea,

"inaonesha baada ya kuingia kwako ametoka tuambie alipo elekea abdul haraka" robert alizidi kuwaka,

"afande kama mlifutilia nyayo za abdul kutoka huko mlipotoka , kwani msifuatilie tena nyayo zake kutoka kutoka hapa mlipo ziona na mzifutilie tena huko zilikoelekea" maneno ya beka yalimkosha na kumjaza hasira lakini hakutaka kupoteza mda kwani kitendo cha yeye kuendelea kubishana na beka ilikuwa nikupoteza muda alisimama akashusha pumzi ndefu,

"askari tawanyikeni eneo lote hili ingieni nyumba kwa nyumba" alisema robert na askari wakaanza tena msako wao, robert akabaki peke yake na beka kwenye ule uwanja uliojaa nyayo za viatu vya maaskari,

"upo huru" sauti nzito ya robert ilimuambia beka,

"poa" beka alijibu na kujizoazoa, akainuka akaanza kutembe akichemea na kuanza kuingia kwenye chumba chake, huku macho mawili ya robert yakimsindikiza mpaka anaingia ndani, robert kwa jinsi alivyo ya sikia majibu ya beka hisia zake zili mwambia nilazima beka alikuwa anajua abdul alipo, robert akiwa amesima alitoa radio call yake na kumpigia moses na kumuelekeza eneo alikuwepo ili moses afike eneo hilo haraka, beka nae alipingia ndani alimsikia robert kwa nje akiongea na mtu kwenye radio call,

beka harakaharaka beka akachukua simu iliyokuwa juu ya tv akaenda akafuta namba ya abdul kwenye simu yake akafuta na sms alizowahi kutuma na kupokea kutoka kwa abdul kwa ufupi alifuta kila kitu kilicho kuwa kina husiana na abdul alivyo maliza akaanza kuvua guo zake zilizo jaa matope.


moses alifika akiwa na kundi kubwa la maaskali, robert aliamulu kundi lote la askari liungane na askari waliokuwa wana endelea na msako mkubwa eneo hilo,

robert alibakia na moses pamoja na askari wengine wanne kwenye uwanja ule wa nyumba alioishi beka, robert alimsimulia moses kila kitu kilicho kuwa kinaendele, na alimwambia anamshuku sana beka,

robert ali waamulu wale askali wanne waende majumbani kwao wakabadilishe nguo na wavae za kiraia harafu waje wafanye kazi ya kumfuatilia beka kwa usiri mkubwa, wale askari wakaenda kujiandaa kwa majukumu waliopewa,

robert na moses wakaongozana na kuingia chumbani mwa beka, ambamo walimkuta beka akiwa amevaa pesi fupi akiweka kitanda chake mahali kilipo kuwa mwanzo ,

"karibuni afande" beka alisema kanakwamba hakuna chochote kilicho tokea baina yake na robert

"ah sorry kwa usumbufu uliotokea sisi tunaondoka uniwie radhi" alisema robert akijifanya anaomba msamaha,

"hamna shida karibuni tena" alijibu beka muonekano wa beka hata moses ulimtia wasiwasi,

kina robert wakatoka na kwenda kwenye msako .


msako uliendelea kwa muda mrefu bila mafanikio, mpaka giza la jioni lilianza kuingia abdul hakuonekana machoni pa askari,

robert alikata shauri aliamua aondoke na moses wakatoe taarifa makao makuu na kuacha askari wakiendelea na msako usio kuwa na mafanikio, robert na moses wakaanza kuondoka kurudi walipo acha usafiri wao.


wale askari waliopewa jukumu la kumfuatilia beka walifika eneo hilo kwa usiri mkubwa , wawili walikaa kwenye banda la chips mbele kidogo ya nyumba ya beka, na wawili walikuwa kwenye bar iliyo kuwa pembezoni kabisa lakini kwa hakika waliiona vizuri nyumba alimokuwemo beka, wote wakaanza kufuatilia mienendo ya beka.



wale askari wawili wakiwa pale kwenye banda la chips ambapo kulikuwa na watu wengi wakisubiria chips huku wakiendelea kusimuliana jinsi msako huo ulivyo kuwa wa kushtukiza pamoja na ule mlipuko ulio tikisa mtaa, watu wote waliokuwa kwenye banda lile la chips ni wale waliokuwa wana kimbia ovyo masaa machache yaliyo pita na mda huo ndo walikuwa wakirudi majumbani baada ya kuambiwa na polisi kwamba watulie kulikuwa hamna vita ila msako wa jambazi aliejificha kwenye mtaa wao,

pale kwenye banda la chips kila mtu alikuwa anasimulia la kwake,


wale askari wawili waliovaa kiraia wakiwa wamejichanganya na baadhi ya watu kwenye banda la chips walimuona beka akitoka na maji kwenye ndoo kisha akaendanayo kwenye bafu iliokuwe pembeni mwa nyumba ile, alikuwa ameenda kuoga na badae walimuona akitoka bafuni akirudi ndani ,muda kidogo wakamuona tena akitoka akiwa kavalia nadhifu akiondoka eneo hilo, askari kuona vile wakaamua kuwajulisha askali waliokuwa kwenye bar na askari walikuwa kwenye bar wakaanza kumfuatilia beka huko alikokuwa anakwenda huku askari wa kwenye banda la chips wakiendelea kuangalia kwa makini ilenyumba ya beka kuona kama kuna mtu mwingine atakae ingia mule.

askari wale wengine waliovaa kiraia walimfutilia beka bila beka kuelewa ,walimuona beka akiingia kwenye duka la madawa, wakawa wamejibanza kwa mbali wakimuangalia beka kupitia mlango wa kio cha duka lile, asakali wale wili wakamuona beka akivua shati lake kisha akaanza kufungwa kitambaa cheupe lapstiki kwenye mkono wake wa kulia, na baadae akavaa shati lake akatoa pesa mfukoni na akapewa kimfuko cheusi kilicho jaa dawa akatoka nje ya duka la madawa akanyoosha barabara na kuanza kuendelea na safari yake, wale askari wakaendelea kumfuatilia kwa usiri mkubwa,askari walimfuatilia beka kwa mwendo kama wa dakika nane kasha wakamuona kasimama kwenye kituo cha bodaboda askari wakajificha na kuanza kumuangalia beka aliekuwa akiongea na mtu alikaa juu ya bodaboda ,beka na mtu wa bodaboda waliongea kama sekunde arobaini kisha askari wakamuona mtu wa boboda akisimama wima na kuingiza mkono mfukoni na kutoa noti nyekundu na kumpa beka beka nae akaiweka mfukoni na kugeuza kurudi alipo toka, askali wakazidi kumfuatilia bila beka kujua beka alinyoosha njia na kuanza kurudi mtaani kwake, askari walivyo gundua beka ana rudi nyumbani kwake waliwapa taarifa wenzao ambao bado walikuwa kwenye banda la chips,


beka alivyofika mitaa ya kwake hakuingia nyumbani mwake ila alienda kununua chips kwenye lile banda walipokuwepo wale askari wawili,

askari walivyo muona beka anaelekea walipo kuwa wao walijifanya wanasoma magazeti waliyo kuja nayo ],

"dah hii foleni nitapata kweli chips?" aliuliza beka baada ya kufika kwenye banda hilo la chips, baadhi ya watu waliokuwa hapo walivyo muona beka walianza kucheka inaonekana walikuwa wamesikia balaa lilio mpata beka,

"ebwana mwanangu pole" alisema muuza chips ,

"ahsante bwana nisabishie kwanza chips kavu na mayai manne" alisema beka huku, huku akicheka, na hapo watu wote walicheka watu hawa wote hakuna aliekuwa hamjui beka kuwa ni dreva wa bodaboda na beka na beka alikuwa mcheshi kwa kila mtu mtaani pale na tena alikuwa mtu wa matani sana ,watu waliokuwa pale walibaki wakimsubiria beka awasimulie ilikuwaje akakutwa na majanga yale,

"kwani beka ilikuwaje mpaka wazee wakaja kukusababisha" aliuliza dada mmoja huku akicheka,

"ah wale mazombi hawajielewi wamevurugwa, " alisema beka na kusababisha watu wote waliokuwa pale wakaangua kicheko ,ni watu wawili tu ambao hawa kucheka kabisa.

" oya dogo kanichukulie pakti moja ya embessy hapo kwa mangi" beka alisema huku akichomoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpa mtoto aliekuwa pemdeni kakaa kwenye bechi,

"mi niliona polisi wamejaa kwenye nyumba yako watu tukazania beka ni al-shi abab." alisema muuza chips huku akiendelea na kazi yake ya kuhudumia wateja,

"dah mwanangu kama mkosi vile, nimechezea kichapo then et baadae ananiomba samahani maboya kweli kweli"

"kwanini sasa walikuwa wana kupiga?"

aliuliza yule dada aliuliza mara ya kwanza ,

", wamekuja na bange bange zao eti wanasema abdala sijui abdul kaingia geto mtu mwenyewe wanaemsema sijawahi hata kumsikia" beka alisema huku akisonya,

"Pole jamani wamekuonea bure"

"ah walikuwa wameshiba ugari na dagaa unadhani wangekuwa nanjaa wangekuja kunisumbua kiasi hiki" alisema beka huku kikifuata kicheko kikubwa kwa watu waliokua eneo,

wakati watu wanaendelea kucheka beka alishituka baada ya kuona utofauti mkubwa wa watu wawili, wale watu walionekana kuwa tofauti na wale watu walioendelea kuchekeshwa na beka kwanza walikuwa wana muangalia sana beka kwa kumdadisi, tayari beka akawa amesha tambua tofauti za watu Hao,

"mwanangu eh chips zangu si tayari... hemu nifungie basi nikalale nisikilizie maumivu" beka alisema baada ya kuhisi wale watu wawili watakwa polisi,

"leo hauendishe bodaboda usiku" aliuliza yule muuza chips,

"ah siendi nimemua kumuachia sidebway kwa leo ndo kanipooza buku ten" alisema beka nakuchukua mfuko uliokuwa na chips akatoa sigara moja kwenye pakti akawasha kwenye jiko la kukaangia chips kisha akanunua maji ya uhai akaanza kuondoka huku akivuta sigara yake, alivyo fika ndani aligawanisha zile chips vipande viwili kipande kimoja akatia kwenye mfuko, harakaharaka akabebanisha stuli mbili na akapanda mkononi akiwa na mfuko wa chips na maji ya uhai ,kisha akasukuma ile sinbodi na akaingiza ule mfuko wa chips na yale maji,kisha akashuka akapangua zile stuli, akakaa akatoa simu yake mfukoni na kuanza kubonyeza bonyeza.

*****

Robert na moses walienda walipo acha vyombo vyao vya usafiri wakakubaliana kwamba Moses akapaki pikipiki yake kwenye kituo cha polisi kilichokuwa karibu na eneo hilO nakuicha halafu wapande gari la robert iliwaende kuripot , moses alifanya kama alivyo ambiwa aliendesha pikipiki hadi kituo cha polisi cha tandika akaiacha pikpiki yake na kisha akapanda kwenye gari kuelekea posta kwenye ofisi ya i.g.p .

ndani ya gari robert na moses waliongea mambo mengi sana juu ya kazi inayo wakabili ya kumkamata abdul, robert alishindwa kuelewa abdul alikuwa mtu wa aina gani kwani wamemkosa katika mazingira ambayo kwa hakika kumkamata abdul ilikuwa ni asilimia miamoja, pamoja na kuongea mengi moses hakugusia kabisa juu ya swala la zile maiti za kifaransa zilizo semekana kuwa abdul ndo aliefanya mauji hayo moses alikuwa kaamua kufanya upelelezi wake mwenyewe bila kumshirikisha mtu yoyote,

gari ilikata mitaa hatimae ilikamata barabara ya posta , safari haikuwa ndefu na wali wahi kufika maana hakukuwa na foleni,

gari ilifunga breki mbele ya ghorofa hapo mjini posta na robert na moses walishuka na kuingia ndani ya ghorofa hilo, waliingia kwenye lifti na baada ya muda mchache walikuwa wamesimama kwenye mlango wa ofisi ya i.g.p ahmed, walibisha hodi na kuambiwa waingie ndani, i.g.p alikuwa akisubiri kwa hamu kubwa riport kutoka kwa robert.

robert ali elezea kilakitu kilichotokea huko tandika na jinsi walivyokuta askari wenzao wakiwa wameshambuliwa na abdul,

I.G.P ahmed akawa mkali kama mbogo aliona kilichotokea pale ilikuwa niuzembe, ahmed ali wafokea kina robert na kuwatwisha mzigo wa lawama, ahmed kwa jinsi alivyo chukia aliwaambia waondoke mbele ya macho yake haraka,

ahmed alichukia sana na alimuangalia moses kwa macho yalio jaa chuki maana ndio huyu i.g.p alieonekana kuficha kitu juu ya abdul na wa wafaransa walio uwawa na moses alionekana akitaka kuchunguza kwakina juu ya swala la abdul,

robert na moses waliondoka kwenye ofisi ya i.g.p wakiwa wanyonge , walikubaliana wakapumzeke kwa muda wa masaa matatu na badae warudi tena tandika. robert alimpeleka moses hadi nyumbani kwake na yeye akaelekea kwake.


baada ya masaa matatu robert alitoka nje ya nyumBA yake na kuingia ndani ya ke, na kuanza kuliendesha kwa mwendo wakawaida alienda mpaka kwa moses akapiga honi, moses alisikia ile honi akaziweka zile tiketi za ile miili ya wafaransa kwenye droo ya kitanda chake, alitoka nje akiwa kaisha badili nguo akaingia ndani ya gari la robert na wakaanza safari yakwenda tandika.

ilikuwa kama saa tano na nusu ndio robert na moses walifika tandika.. robert kwa kutumia simu ya mkono aliwapigia wale askari alio waacha wamchunguze beka, askari walimuambia bado hawaja gundua kitu chotechote kutoka kwa beka kinacho husiana na abdul, ila wametambua beka alikuwa dreva wa bodaboda na tena maarufu mtaani humo, robert aliwambia waendelee kuchunguza kwa makini,


msako uliendelea taratibu kwa siku saba mfululizo huku askari wakipeana zamu usiku na mchana, lakini hawa kumpata abdul.

agizo likatoka ngazi za juu kwamba askari wote warudi kazini na kuondoka mtaa huo kwamaana kama kutafuta wamesha tafuta sana,

askali wote walisitasha msako huo na kurudi kwenye vituo vyao,

lakini robert aliamua kufanya kazi yake binafsi alitafuta watu ambao wangekuwa wanapiga patroo usiku ndani ya mtaa ule,


*****

beka na abdul siku zote waliendelea kuwasiliana kwa njia ya sms, abdul akiendelea kuishi ndani ya dari ile huku akipata tabu kubwa kukabiliana na joto kali,

beka nae aliendelea kuwa anampa chakula abdul akiwa darini, beka alikuwa makini sana asigundulike ,

beka alivyoona askari wote wametoeka ndani ya mtaa huo,alijaribu kuangalia kama angewaona wale wapelelezi wawili lakini hakuwaona.


ilikuwa ni usiku wa saa saba baada ya siku nne tangu askali waondoke eneo hilo,

beka alitoka nje kimya kimya akazunguka mtaa ule wote hakuona mtu beka akarudi ndani .

"oya shuka " alisema beka kumwambia abdul aliekuwa ndani ya dari,

abdul alifungua ile singibodi na kushuka ,

"chukua kwanza maji hayo ukaoge" alisema beka huku akisota ndoo kubwa iliojaa maji, abdul akachukua yale maji akaenda kuoga,

abdul alichukua muda kidogo kutoka bafuni,

na badae alirudi ndani na kubadilisha nguo nakuvaa nguo za beka ,

Abdul akavuta stuli na kukaA akiangaliana na beka,

beka akainuka na kwenda kuwasha tv sauti ya juu kidogo kisha akarudi kuka kitandani.

"abdul imekuwaje janga limefikia hatua hii mpaka una tafutwa kama shilingi, mbona mimi uliniambia nitatizo dogo Tu, then nasikia umehusika na mauji ya mama yako, whats going parter" beka aliongea kwa upole huku akimtazama usoni abdul.

abdul hakujibu kitu ila alikuwa analia tu , wingu kubwa la kumbukumbu likakizonga kichwa cha abdul, na abdul akazidisha kulia....



Abdul akavuta stuli na kukaa akiangaliana na beka,

beka akainuka na kwenda kuwasha tv sauti ya juu kidogo kisha akarudi kukaa kitandani.

"abdul imekuwaje janga limefikia hatua hii mpaka una tafutwa kama shilingi, mbona mimi uliniambia nitatizo dogo Tu, then nasikia umehusika na mauji ya mama yako, whats going partner" beka aliongea kwa upole huku akimtazama usoni abdul.

abdul hakujibu kitu ila alikuwa analia tu , wingu kubwa la kumbukumbu likakizonga kichwa cha abdul, na abdul akazidisha kulia....


ENDELEA....


abdul alitoa machozi, kitendo cha beka kusema amesikia kuwa kamua mama yake kili mtoa abdul machozi, beka alibaki akimtazama tuh huku nae machozi yakimlenga.

"beka the world hates me, amini mwanangu hii sayari mi sikupangiawa kuishi ndomaana matatizo yana niandama kiasi hiki , mi nahisi muda mchache utakaofuata nitamfuata mama yangu kipenzi, " alisema abdul na kufikia hapo beka nae alianza kulia beka nirafiki mkubwa sana kwa abdul tena wadhati beka aliingiwa na simanzi baada ya abdul kusema muda mche ujao angemfuata marehemu mama yake, beka alimwaga machozi ,

"so mwanangu nini kimetokea?" beka aliuliza huku akitokwa na machozi..

abdul alikuwa kwenye dimbwi la kumbumbu...


llfe of abdul **maisha ya abdul**


ABDUL alikuwa miongoni mwa vijana walio zaliwa katika familia bora tena tajiri abdul alikuwa mtoto pekee wa I.G.P wa mkoa wa mwanza IBRAHIM,

i.g.p alimpenda sana mtoto wake pekee abdul hakutaka abdul ajekuwa kijana mwenye tabia mbaya zisizo pendeza kwenye jamii,

tangu abdul anazaliwa mpaka anaanza kukua na kufikisha miaka mitatu, alikuwa mtoto wa getini ndani ya mtaa huo wa nyakato jijini mwanza mama yake na baba yake walipinga vikali abdul kucheza na watoto wamtaa huo walimpenda sana mtoto wao abdul,

abdul alikuwa katika mazingira ya upweke,

ni upweke huo ambao uliwafanya wazazi wake wapange kumtafutia shule ya nursery ambayo itakuwa na mabweni ambako abdul angeanzia elimu ya awali na angeishi kwenye shule ile angekuwa akirudi nyumbani siku za likizo, wazazi wa abdul waliafikiana wazo hilo waliamini huko abdul angechangamka na kucheza na wanafunzi wenzake ambao kwa hakika wangekuwa watoto waliotoka kwenye familia zenye uwezo wa kimaisha,


hatimae abdul alifikisha miaka minne, na wazazi walikuwa waki mnunulia vifaa vya shule na sare za abdul.

paka muda huu wazazi wa abdul tayari walikuwa wamesha pata shule ya kumpeleka mtoto wao pekee waliamua kumpeleka shule ya alience .


ALIENCE nishule ilioka jijini mwanza mtaa wa mahina ipo karibu kabisa na shule ya msingi mahina, watoto wengi wanaotoka kwenye familia zenye uwezo hapakuwa mbali sana na mtaa wanyakato ilipoishi familia ya ibrahim ,

shule ilipo funguliwa wazazi wa abdul wali mfungashia mtoto wao vitu vilivyo hitajika, na kumpakia mtoto wao kwenye taxi yao na kumpeleka shuleni pale.

abdul alipokelewa vizuri na akaanza masomo ya awali .

abdul akiwa ndani ya shule hiyo ya alience iliyo nzungushiwa senyenge na kuzungukwa na miti na kwa upande wapili kulikuwa kuna mbuga.

ukimya ulikuwa sehemu kubwa ya maisha ya abdul ndani ya shule hiyo, kitu ambacho mama yake hakukifurahia kabisa ila waalimu walimuambia ukimya unaweza ukawa ni sehemu ya tabia ya abdul na itamchukua muda kuicha na huenda ikawa ndio kawaida yake siku zote za maisha ya abdul, mama yake abdul hakupenda abdul awe mkimya kiasi kile alipenda awe mcheshi kama walivyo mama yake na baba yake.


kuna baadhi ya watoto shuleni hapo walijitaidi kuwa wacheshi kwa abdul lakini abdul hakuwa mtu wa story,kitu kilicho sababisha abdul kukosa marafiki kabisa, abdul muda wake mwingi ilikuwa nikuandika andika na kurudia aliyo fundishwa kitu kilichopelekea madaftari yake ya kujifunzia kuisha kwa muda mdogo sana, lakini walimu walimpenda kwani alionekana mtu alie jali sana masomo akiwa bado na akiri za kitoto..,

siku za michezo watoto wenzake wote walijumuika kwenye michezo kwenye viwanja vya michezo wakicheza michezo mbali mbali lakini abdul ye alikuwa akidaba panzi kwenye eneo lenye manyasi na kukimbiza wadudu warukao juu akiwa na fimbo yake mkono, hayo ndio yalikuwa maisha ya abdul yaliokuwa tofauti kabisa na watoto wingine shuleni hapo.


siku moja ijumaa, wanafunzi waliokuwa darasa la tano ndani ya alience walioukuwa na timu yao ya mpira wa miguu walikuwa wana shindana na wanafunzi darasa la tano wa shule ya mahina ambayo ipo karibu kabisa na shule hiyo ya alience, shindano hilo lilikuwa likifanyaka kwenye kiwanja cha shule Ya msingi mahina,

wanafunzi wote hawakutakiwa kubaki kwenye mabweni wote walitakiwa kuvaa sale na kwenda kuishangilia timu yao ya alience,

hii ikamlazimu abdul kujumuishwa na wenzake japo hakupenda ,

wanafunzi wote walivaa trak suti nyeusi zenye mistari mieupe,

geti la alience lilifunguliwa na wanafunzi waliovaa sale za kupendeza wakatoka wakiimba, huku wasimamizi wakiwa makini na wale watoto wadogo wa chekechea kuwaangali wasitawanyike ovyo, .

mahina ni shule mmoja kidogo ipo nyuma kwa maandeleo, mkondo B madarasa mengi yalikuwa hayana madawati wanafunzi wengi walikaa kwenye mawe yaliyo kuwa kwenye madarasa hayo madarasa yalikuwa na vumbi la kutosha wanafunzi wengi walikuwa wagomvi na watundu kupita kiasi .

tofauti kubwa ilionekana ,kati ya wanafunzi wa alience na mahina kwa usafi na kwa vitu vingi,..

baada ya muda kidogo mpira ulianza,

wanafunzi wa alience walisima upande wa chini kuliko kuwa na mtelemko kidogo na wanafunzi wa mahina walisima upande wajuu kulikokuwa na muinuko kidogo,

Wana funzi wa chekechea walikuwa wamekaa chini kwenye manyasi wakiendelea kutazama mpira,

Abdul hakuvutiwa hata kidogo kutazama mpila ule wa miguu , abdul kwa kujiibaiba alifanikiwa kutoka pale walipo kuwa wamekaa na akaanza kutembea akielekea ambapo alihisi angeweza kuona panzi waki ruka ili aanze kuwakimbiza na kuwa kamata, alitembea kama dakika tatu mbele yake chini ya mwembe kwambali aliona vumbi kubwa chini ya mwembe ule abdul akaanza kutembea haraka haraka akitaka aone nini kilicho sababisha vumbi lile, akiwa anazidi kusogea aliona watoto waliokuwa wamempita umri kidogo, walikuwa wanafunzi wa mahina, akiwa anaendelea kusogea mara ghafla aliona wale watoto wakiacha mpira na kumkimbiza mwenzao walio kuwa wakicheza pamoja, mwenzao huyo alikimbia akielekea kwenye madarasa! ya mkondo B, abdul alishuhudia yule mtoto aliekuwa akikimbizwa akianguka chini na walio mkimbiza wakamfikia na kuanza kumpiga akiwa pale chini, abdul kitendo kile kilimpa hofu hakujua kwanini wale watoto wenzake walikuwa wana mpiga mwenzao, kipindi abdul akishangaa alimuona yule aliekuwa akipigwa akiinuka haraka akiwa amefumbuta mchanga mikononi akawamwagia wale waliokuwa wakimpiga harafu hapohapo akatoka mbio mpaka kwenye ukuta wa darasa moja kisha akagusa ule ukuta kwa mikono yake! na kuanza kurudi pale alipo waacha wenzake alio wamwagia mchanga!

"bwana BEKA sio mchezo mzuri umetumwagia mchanga machoni" alisema mtoto mmoja kati ya wale waliomwagiwa mchanga , Abdul alizidi kushangaa hakujua nikwanini yule mtoto baada ya kugusa ukuta na kurudi wale waliokuwa wanampiga hawa kumpiga tena,

"hah na nyie ndo mchezo gani mi nimeanguka nimeomba poo, lakini nyie mkaendelea kunipiga."

alisema yule alieitwa beka ,huku wakiondoka kurudi walipo acha mpira na wakaanza tena kucheza, abdul aliendelea kuzubaa.

mchezo waliokuwa wanacheza wale watoto ni ule mchezo ambao ikitokea mmoja kati yao mpira ukimpita katikati ya miguu wao waliita dobo basi wote wanaanza kumkimbiza na kumpiga yule ambae mpira umepita katikati ya miguu yake na wanampiga mpaka akashike kwenye ukuta wa darasa kama alivyo fanya yule mtoto anae itwa beka,

abdul alitekewa na ule mchezo akabaki kasimama palepale, kila alipoona mmoja wao akikibizwa na kupigwa abdul alifurahi na kucheka sana, kwa ufupi mtoto abdul aliupenda mchezo ule,

abdul akiwa anaendelea kuangalia mchezo huo, mara mlezi wao alifika na kumvuta mkono,

"hemu muone tumekutafuta kweli, sijui ulitutorokaje" alisema huyo mlezi wa kiume huku akimvuta mkono abdul


Abdul aliupenda ule mchezo alitamani aendelee kuutazama lakini muda ulikuwa umeisha watoto wa alience waliondoka wakishangilia ushindi alience walikuwa wameshinda kwenye mchezo huo, kina abdul walirudishwa mabwenini na kuendelea na mambo mengine,

abdul akiwa shuleni alijaribu kutafuta kama angeona mchezo waliokuwa wakicheza kina beka lakini hakuona watoto wa alience wakiucheza . abdul ikamlazimu kila siku wakitoka mapumziko alienda kusimama kwenye senyenge na kuangalia kama angewaona watoto waliomzidi umri wakicheza mchezo ule, kuna siku aliwaona wakicheza na kuna baadhi ya siku hakuwaona,

abdul akawa kabadilika kidogo akaanza kuwa anatamani sana akacheze huo mchezo lakini mazingira yali mbana, abdul akawa anaisubiri kwa hamu siku ambayo ingekuwa ya michezo ambayo wangetoka nje ya geti alipanga siku hiyo lazima angeeda kucheza na watoto wa shule ya msingi mahina,

abdul aliupenda sana mchezo ule kuliko michezo yote iliyo kuwa bweni..................





Abdul aliendelea na masomo huku kawaida yake ikiwa ni ile ile kila siku wakati wa mapumziko alikuwa akienda kusimama kwenye senyenge za shule ile na kuwaangalia kina beka kwa mbali wakicheza mchezo wao ambao kwa asilimia mia ulikuwa ni vurugu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho vumbi tu,

siku zilienda na hatimae likizo ilifika ambapo abdul alikuja kuchukuliwa na mama yake,

siku hiyo wanafunzi wengi walikuwa wakiagana na rafiki zao kwa furaha ,lakini kwa abdul haikuwa hivyo abdul hakuwa na rafiki hata mmoja wa kuagana nae, yeye abdul alitoka ndani ya bweni akiwa kashikwa mkono na mlezi, abdul alivyomuona mama yake kasimama akiwa kaegemea gari, alitoka mikononi mwa mlezi wake akakimbia kuelekea alipokuwepo mama yake alievaa koti la suti jeusi na suluale ya kitambaa cheusi abdul alikimbia na kwenda kuikumbatia miguu ya mama yake, kitendo hiki kilimfanya mama yake abdul afurahi sana, baada ya abdul kumsalimia mama yake kwa furaha alienda kwenye mlango wa mbele wa gari na kuanza kufungua,

"abdul mbona huwaagi rafiki zako" alisema mama yake abdul huku akitabasamu,

lakini hapo hapo alimuona abdul akikataa kwa kunyenyua mabega yake juu na kujitupia ndani ya gari, mama yake abdul aliagana na waalimu pamoja na walezi kisha akaingia ndani ya gari na kabla hajawasha alitoa choclate kwenye mkoba wake na kumpa abdul ambae mda wote tabasamu lilitawala usoni mwake, mama yake abdul akawasha gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.

gari likiwa linaendeshwa na mama yake abdul aliekuwa na kila sifa za kuitwa mzuri lilipiga honi mbele ya geti jeusi na askari mmoja alifungua geti na gari likaingia ndani ya uwanja ulio kuwa umejaa maua na majani ya ukoka na vitofari vidogodogo vikiwa vimetapakaa kwenye aridhi ya nyumba ile, abdul alitoka kwenye gari pamoja na mama yake wakaingia ndani ya nyumba nzuri iliopendeza katika mtaa huo wa nyakato, abdul alipo ingia ndani ya nyumba yao alikutana na baba yake I.G.P ibrahim ambae nae alimkimbilia na kumrukia ikawa ni furaha kubwa ndani ya nyumba, i.g.p ibrahimu aliamua kumfurahisha mtoto wake alikuwa amenunua computer ambayo alikuwa ameweka game la G.T.A VICE CITY ambalo aliamini abdul angelipenda kwani abdul alipenda sana picha za ngumi,

nikweli baada ya abdul kufundishwa jinsi ya kucheza game lile alilipenda sana, ikawa kila mara abdul una mkuta kwenye computer akicheza game.


siku moja abdul baada ya chakula cha mchana alihitaji juice lakini kwenye friji zilikuwa zimeisha dada wa kazi aliamua kumpa hela akanunue nje dukani abdul alipewa elfu moja akaambiwa atarudisha itakayo baki ,abdul alitoka nje askari alivyo muuliza abdul anaenda wapi abdul alisema anaenda kununua juice askari akafungua mlango na abdul akatoka akaenda kwenye duka lililokuwa pembeni kidogo na nyumba yao, lakini kwenye lile duka hakukua na juice alioitaka abdul, mwenye duka akamuelekeza kwenye duka jingine lililokuwa ndani kabisa ya mtaa huo abdul akaendelea kuzama ndani ya mtaa ule,

abdul akiwa anazidi kwenda ndani ya mtaa ule, mara akasikia vishindo upande wake wa kulia alipo geuza shingo na kuangalia, Aliona watoto wawili wakipigana na mtoto mmoja alivyo angalia alimuona yule mmoja aliekuwa akichangiwa na watoto wanzeke wawili alikuwa kama kuna sehemu, abdul yeye alikuwa haja wahi kuona ugomvi, abdul aliamua kurudi mbio kwenye lile duka la mara ya kwanza na kumuambia muuza duka kuwa kuna watoto wanampiga mtoto mmoja, mwenye duka alitoka nje ya duka na kuongozwa na abdul mpaka pale palipokuwa na ugomvi, walimkuta yule mtoto mmoja aliechangiwa na watoto wawili akiwa amemkalia mtoto mmoja chini huku akimpiga huku mtoto mwingine akijitahidi kumtoa yule aliye mkalia mwenzake,

"pumbavu hili toto litakuja kuniletea kesi ,..... hivi we beka mbona unakuwa mgovi kiasi hiki" alisema yule muuza duka huku akimtoa yule mtoto aliemkalia .


"mjomba wamenichokoza" alisema beka na muda huohuo akapokea kofi la mgongo kutoka kwa muuza duka ambae alikuwa ni mjomba wake,

"wewe beka kila siku una chokozwa wewe tu! twende ndani nika kunyooshe we siunajua kupigana?" alisema mjomba wake beka na kuanza kumvuta beka kuelekea ndani na baada ya beka kuingizwa ndani kilichofuata ilikuwa ni kilio kikubwa kutoka kwa beka,

abdul ali fedheheshwa na kilio kile japo alikuwa mtoto lakini alijawa na huruma sana na alihisi yeye ndo alie sababisha beka achapwe na mjomba wake,

abdul alikuwa bado haja jua kuwa beka ndio yule mtoto alie muona akicheza mpira wa dobo na wenzake kule mahina lakini alihisi tu kama aliwahi kumuona sehemu.

"leo msimpe huyu chakula acha ashinde njaa na alale njaa si anajifanya bondia, leo apigane na njaa." nisauti ya mjomba wake beka, ambayo hata abdul aliisikia,

abdul akaanza kusikia beka akilia kwa kwikwi akitoka nje, abdul akaondoka haraka kwenda dukani kununua juice yake tayari abdul alikuwa ameingiwa na woga juu ya beka,

abdul alinunua juice na kuanza kurudi huku akitamani asipite kule alipomuacha beka akilia lakini abdul hakujua njia nyingine zaidi ya hiyo, abdul alimuona kwa mbali beka akiwa kainamia magoti yake, abdul alitaka apite mbali lakini akiri yake ilimtuma aende kumpa pole beka aliekuwa kajiinamia,

abdul alisogea kimya kimya mpaka kwa beka,

"pole" sauti ya kitoto kutoka kwa abdul, mtoto beka aliinua uso na kumtazama mtoto mwenzake aliekuwa mbele yake ,beka hakumfahamu abdul, akaendele kulia bila kumjibu beka,

huruma ilimuingia abdul na kumsikitikia beka,

"mmh chukua" alisema abdul huku akimpa ile juice beka,

"ahsante " beka alisema huku akipokea na kufungua na kunywa kwani alijua mchana wa siku ile asinge kula zaidi ya juice ambayo aliipata kutoka kwa abdul kama muujiza,


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG