Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

RANGI YA CHUNGWA - 3

  

Simulizi : Rangi Ya Chungwa

Sehemu Ya Tatu (3)


"Mimi nimebaka, nime mbaka nani mimi, naomba unielewe Baba yangu mimi sijabaka na wala sikutaka kumbaka mwanao, kweli kabisa hata yeye mwenyewe kama angelikuwa hapa asinge kubaliana na maneno yako"

Aliongea kijana huyo kujitetea kwa mzee huyo, lakini mzee huyo hakutaka kabisa kumsikiliza Dickson wala kumuelewa. Mzee huyo alieonekana kuwa na fedha nyingi ni kwa muonekano wake alivyokuwa, alionekana kutokuwa na roho ya huruma hata kidogo.



Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo mengi, akili yake haikuwaza jambo lingine zaidi ya kwenda kuozea jela. Akiwa pale alishangaa na kutamani kukimbia baada ya kuwaona polisi wakizunguka maeneo yale, akiwa katika mshangao mkubwa alishtukia pingu zikiwa zinaingia katika mikono yake na kujikuta amekamtwa na polisi bila kujua hatima ya yote. Kilikuwa ni kitu cha kushtukiza, hakukuwa na maelezo yoyote.


Rafiki yake na Angely alionekana kutoshtuka kwa kitendo cha kukamatwa kwa Dickson, ilionyesha dhahiri msichana huyo yeye ndiye alietoa taarifa hizo kwa polisi. Dickson alichukuliwa kwa nguvu huku akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani kwake, mwili wake ulionyesha kutetemeka na jasho lilizidi kumtoka. Alipakiwa kwenye gari la polisi na kufikishwa kituo cha polisi, kitendo cha kufika kituo cha polisi alipokelewa na kipigo kikali. Ndani ya muda mfupi nguo zake zilikuwa zimelowa damu, kila kona ya mwili wake kulikuwa na maumivu.


ENDELEA..........................

Dickson alibaki akimuomba Mungu huku akiamini lazima kwenda jela, mtu pekee aliekuwa akimuwaza kwenye akili yake na kuamini ni ndiye msaada wake na mkombozi wake ni msichana Angely, aliamini yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa pale alipokuwa, kwakuwa yeye ndiye anajua ukweli juu ya kile kilichotokea.

"Dickson Michael, umri wa miaka 25 unatuhumiwa na kesi mbili, huku kila kesi ikiwa na sheria zake na adhabu zake. Hivyo kama mahakama imeamua kukupa adhabu ya kwenda jela miaka sit....

"Hapana, hapana nasema, hausiki hata kidogo, msimuhukumu kwa kosa lisilo kuwa lake.

Mimi hapa ndiye mwenye makosa"


Nisauti iliowafanya wengi kugeukia upande ile sauti ilipokuwa inatokea, kijana Dickson alipogeuka hakuamini macho yake. Alikuwa ni Angely alikuwa afungwa na kuzungushiwa bandeji katika kichwa chake, kila mtu alionekana kushangazwa na lile jambo. Dickson hakuamini kile alicho kiona, hata hakimu alionekana kuduwaa na kukosa la kusema. Hali ya pale ndani ilibadilika, Baba yake Angely alikasirika sana kwa kitendo cha mtoto wake kumdhalilisha, maana mzee huyo alidhamitia kumpeleka Dickson jela. Angely alisogea hadi mahali alipokuwa Dickson na kumkumbatia huku machozi yakimtoka, kwa jinsi Angely alivyokuwa ilidhihirisha kuwa alikuwa na hisia kali za kimapenzi kwa Dickson.


"Dickson naomba unisamehe kwa yote yaliotokea, sikutaka iwe vile, nilishindwa kuvumilia Dick. Nakupenda sana Dick. Naongea haya kutoka moyoni mwangu. Nakupenda Dick nipe nafasi katika moyo wako"

Aliongea Angely huku akiwa amemkumbatia Dickson, yale maneno yalikuwa kama utani lakini hakukuwa na utani. Watu wote waliokuwa pale walishangazwa na kile kitendo, aibu iliwajaa kwenye nyuso zao, Baba wa Angely alikasirika sana kwa kitendo kile, lakini Angely hakujali, alichokuwa akikihitaji ni yeye kuwa na Dickson. Baada ya Angely kutoa visibitisho hatimaye Dickson aliachiwa na kuwa huru, japo alikuwa na maumivu makali kutokana na kipigo alichokipata kule kituoni.


Dickson alivyotoka hakutaka zile taarifa zifike kwa wazazi wake wala bosi wake, lakini alikwisha kuchelewa maana taarifa zilikwisha fika kwa wazazi wake, hakuwa na wazo lolote kwa kile kilichotokea, aliamini Angely ndiye aliokoa maisha yake. Aliporejea nyumbani alipokuwa anaishi alishangaa sana kwa jinsi alivyo pakuta, hali ya nyumba yake ilimpa wasiwasi mkubwa. Alibaki amesimama nje huku Angely akiwa pembeni yake, ghafla wakatokea watu wapatao wanne wakiwa wameshikilia chuma zenye mfano wa nondo, Ile hali iliwafanya Dickson pamoja na Angely kushtuka na kutamani kukimbia lakini ilishindikana.


Hawakujua ni kitu gani wamekifanya kibaya hadi kuvamiwa na wale watu, ile hali izidi kumuogopesha Dickson na kuamini ule ungelikuwa mwisho wake, muonekano wa wale watu haukuwa na nia nzuri, ulionekana kutokuwa na nia nzuri. Angely alionekana kuwatambua wale watu, na hata wale watu walipomuona Angely walishtuka na kurudi nyuma hatua kadhaa, lile jambo lilimshangaza Dickson na kujiuliza maswali asipate jibu.

"Najua Baba ndiye kawatuma, ila mwambie endapo Dick ataumia ajue sitomsamehe, bora mniuwe mimi kwanza kabla Dick ajaf.." Kabla hajaendelea liliingia gari la kifahari huku likiwa na milango mitatu kila upande, lilizungushiwa tintedi kila kona, hivyo ilikuwa ngumu kuona kilichokuwa mle ndani, Dickson alibaki akiwa ameduwaa baada ya kumuona Baba yake na Angely ameshuka kwenye lile gari, mapigo ya moyo ya Dickson yalionekana kwenda mbio kitu kilichompelekeaAngely kupeleka mkono wake kifuani kwa Dickson, ile hali ilimuogopesha sana Angely alishindwa kuelewa ni kwanini Dickson alikuwa kwenye hali kama ile.


Dickson alimuogopa sana mzee huyo, ni kutokana na vitisho alivyovipata akiwa kule polisi, alijua mzee yule hakuwa mwema sana kwake. Alipofika pale tulipokuwa tumesimama wale watu walimpa heshima kubwa, kwa jinsi wale watu walivyokuwa wakifanya ilikuwa ni kama muvi "movie" lakini hakuwa na movie. "Dick mpenzi usiogope utakuwa salama, kama ni kufa tutakufa pamoja. Namfahamu vizuri Baba yangu, ila usijali utakuwa salama, ila Dick naomba uniambie unanipenda. Mwenzio sina raha, sitamani kuishi bila wewe" Aliongea msichana huyo maneno ambayo aliyarudia kila saa kwa kijana Dickson, Dickson hakuwa tayari kuamishia mapenzi yake kwa msichana huyo angali alikuwa anajua ana mpenzi aliekwenda masomoni kwa muda.



Baba yake na Angely alipo wafikia alimwangalia mtoto wake kwa jicho lililojaa hasira, mzee huyo alionekana kuwa na hasira sana.

"Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kama ipo siku mtoto wangu kipenzi angekuja kuniaibisha na kunidhalilisha, kama ulivyo nifanyia leo. Hivi unaakili timamu kweli, unaniaibisha kisa huyu mbwa, nahisi hata huko chuoni hakuna chocho unachojifunza"

Aliongea mzee huyo huku huku akionekana kukerwa na kile kitendo. Dickson kwa wakati huo alikuwa amesimama pembeni ya Angely huku akionekana kutetemeka kwa hofu.

"Angely ondoka hapo na uende kwenye gari kabla sijafanya kitu kibay.."

"Baba nipo tayari kufa kwaajili ya Dick, kwanini unanifanyia hivi. Kama kuniuwa niuwe tu Baba, kiukweli Dickson hausiki kabisa mimi ndiye nilie sababisha yote haya. Nakuomba Baba usimdhuru Dick maana nampenda. Nampenda sana Dick, plz Baba"


Aliongea Angely huku akitokwa na machozi na kuonyesha kumpenda sana Dickson, yale maneno yalimfanya Baba yake na Angely kuonekana kumwingia vilivyo na taratibu sura yake ikawa imeanza kukunjuka na hali ya huasira ikawa imepotea katika uso wa mzee huyo, alimsogelea Angely na kumkumbatia huku akiwa anamsihi mtoto wake kuwa wanaume wengi si wakweli. Lakini Angely hakutaka kabisa kusikiliza maneno ya Baba yake, kiukweli alikwa ametokea kumpenda kijana Dickson kupita maelezo. Hatimaye Dickson alisamehewa na kuruhusiwa kuwa na Angely huku akipewa taadhari nyingi, hatimaye Dickson akawa amerejea Dar es salaam huku akifutana na msichana Angely. Nyumbani kwa kina Dickson furaha ulitawala ni baada ya kumuona mtoto wao akiwa na afya njema, penzi kati ya Angely na Dickson liliongezeka mara Dufu, kila siku upendo uliongezeka, na penzi lao kuchanua, kama uwa ridi. Taratibu Dickson alianza kumsahau mpenzi wake Johar. Maisha ya Dickson yalizidi kuwa mazuri siku hadi siku, kila hatu yake ilikuwa ya mafanikio ni kutokana na Baba yake na Angely kuwa na fedha za kutosha, Dickson alijikuta akiinjoi yale maisha na kuhisi pale alipokiwa nipo mahala pake. Siku, miezi na miaka pia vikasogea, maisha nayo yakazidi kuwa mazuri.


"Angely mpenzi si unajua Jumamosi ijayo ndiyo harushi yetu"

"Ndiyo mpenzi wangu, natamani iwe hata kesho, ili namimi niitwe mama, unajua nini Dick mpenzi tumeishi takribani miaka mitatu tukiwa tukiwa kama wapenzi, ila kwa sasa tutakuwa Mke na Mume"

Ilikuwa ni asubuhi tulivu, Dickson pamoja na Angely wakiwa wanajadili kuhusu ndoa yao, walifurahi na kukumbatiana na kupigana babusu ya mdomoni. Kama wasemavyo wengi ya kuwa siku hazigandi, hayawi hayawi siku ya harusi ikafika, kiukweli harusi ilikuwa kubwa, walialikwa wasanii wakubwa, Mawaziri, wabunge na watu wengine wengi. Kila aliekuwa ndani ya ukumbi wa harusi hiyo alikiri ilikuw harusi ya mfano, furaha ilitawala kwa kila mmoja na nyuso zao kujawa na tabasamu.


Dickson yeye pamoja na Mpenzi wake, wao walikuwa wa mwisho kuingia ukumbini, walipoingia ukumini kila mtu aliahangilia na kufurahi. Watu walikunywa na kula na kufurahiya siku ile, baada ya mambo kadhaa kupita Dickson pamoja na Angely waliitwa mbele kwaajili ya kuonyesha visibitisho vyao, havikuwa vingine, ilikuwa ni kuvishana pete. Msimamizi wa harusi hiyo aliamuru Angely amvike pete aluokuwa nayo katika kidole cha pili kutokea mwisho, taratibu na kwa umakini wa hali ya juu Angely alianza kumvisha Dickson pete huku akifuatisha maneno kadhaa aliokuwa akitamkiwa na Msimamizi wa harusi hiyo. Baada ya Angely kumvisha Dickson pete ikawa ni zamu ya Dickson kumvisha Pete Angely, alifanya kama alivyo fanya Angely, wakati ana mvisha ile pete alishangaa kumuona mtu anakuja mbele huku akitoa kelele za sauti ya juu, Dickson pamoja na Angely walionekana kupigwa na butwaa, hawakuamini kile walichokuwa wamekiona.


Dickson alibaki amaduwaa na kuonekana kushangazwa na lile jambo, pete aliokuwa ameishikilia kwaajili ya kumvisha Angely alijikuta anaiachia chini bila kutarajia, ile hali iliwafanya watu wengi kushangaa maana kwa wakati huo kila mtu alikuwa akiwatazama Dickson pamoja na Angely, walipofwatisha macho ya Dickson pamoja na Angely waliweza kugundua walikuwa wakitizama kwenye mlango wa kuingilia. Baadhi ya waliokuwa pale hawakusikia chochote kutokana na sauti kubwa ya kipaza sauti/maiki. Watu walipo angalia walikutana na msichana mrembo akiwa anaingia huku akiwa anakimbia kuelekea mbele, Dickson alimtambua msichana huyo vizuri kwa kuwa alikuwa mpenzi wake kwa kipindi kirefu. Kila mtu alishangaa, kimya kilitawala pale ukumbini huku kila mmoja akitamani kujua nini kilichotokea.


"Dickson? Kwanini umeamua kunifanyia hivi, nikitu gani nilicho kukosea, hizi ndizo ahadi tulizo kubaliana, siamini Dickson kama wewe ndiyo wa kunifanyia hivi. Sikuwahi kufikiria kama ingekuja kutokea jambo kama hili. Angely hili ndilo kubaliano letu, kwanini lakini, nauliza kwanini jamani"

Ilikuwa ni sauti ya msichana Johar, ambae alikuwa masomoni kwa kipindi kirefu. Yale maneno yalisikika kwa sauti kubwa, kila mtu aliekuwa pale aliweza kuyasikia lakini hakuna hata mmoja aliekuwa ameelewa yale maneno, kimya kilizidi kutawala huku Johar akizidi kutokwa na machozi na kilio cha wazi wazi. Kila mtu alishangaa kwa kile kitendo, kwa jinsi Johar alivyokuwa akilia kwa uchungu iliwadhihirishia watu wengi kuwa kulikuwa na tatizo limemsibu msichana huyo. Hakuna alietambua nini kilichokuwa kinamsibu msichana huyo zaidi ya Dickson pamoja na Angely.


Hali ya ukimya iliendelea kutawala, huku kila mmoja akitamani kujua nini kimetokea hadi hali kama ile kutokea. Watu wengine waliweza kusimama ili kutizama vizuri, hali ile ilikuwa kama filamu, lakini hakukuwa na filamu wala igizo pale, kwa jinsi Johar alivyokuwa akilia kwa uchungu ndipo watu walivyogundua kuwa lile jambo halikuwa na utani. Baba yake Angely alisimama kwa hasira ilikujua nini kimetokea, aliponyanyuka alijikuta anarejea kwenye kiti chake taratibu na kukaa kimya. Ni baada ya kumuona Johar pale mbele, haikujulikana ni kwanini mzee uyo alipomuona Johar alikaa kimya na kutamani kuondoka mahali pale.


"Johar naomba unisamehe, shetani tu ndiyo alinipitia, sikudhamiria kukufanyia hivi, Naomba unisamehe. usiponisamehe nitakuwa mgeni wa nani mimi" Yalikuwa ni maneno ya msichana Angely huku akiwa amepiga magoti mbele ya umati mkubwa kama ule, kila aliekuwa pale alishangaa, wengine waliweka mikono yao kichwani kwa kitendo kile. Angely alikuwa ni bibi harusi mtarajiwa na zilikuwa zimebaki dakika chache kutawazwa kuwa mke halali wa Dickson.


Lile jambo lilimshangaza hata Dickson, yale maneno aliokuwa ameyatamka Angely yalimfanya Dickson kubaki akiwa anamwangalia Angely alivyokuwa analia. Johar hakumjibu chochote alichoamua ni kupiga hatua za haraka haraka kuelekea nje huku machozi yakimtoka kwa wingi, Dickson alivyoona vile aliamua kumkimbilia Johar ili ikiwezekana kumtuliza maana alionekana kuwa na hasira sana, lakini alikuwa amechelewa maana Johar alipofika nje aliingia kwenye gari na kuondoka. Hali ya kule ukumbini ilikuwa imebadilika, hakukuwa na harusi tena.


Kila mmoja alikuwa akizungumza lake, Angely alibaki pale mbele huku akitokwa na machozi, alimsubiri na kuwaza pengine Dickson angerudi lakini haikuwa hivyo. Dickson alipoona Johar kaondoka akiwa na hasira na machozi yakimtoka, alitambua pengine Johar angeweza kufanya kitu kibaya. Aliamua kuingia kwenye gari ili ikiwezekana kumzuia Johar asifanye alichokuwa anataka kukifanya. Mwendo wa gari wa Dickson ulikuwa kasi sana, hiyo yote ni kwaajili ya kumuwahi Johar, Akiwa kwenye gari alikuwa akikumbuka mambo aliokuwa ameyafanya na Johar kipindi cha nyuma, machozi yalianza kumtoka pale alipokumbuka ahadi walizopeana kipindi Johar alivyokuwa anaondoka, alijihisi mwenye makosa.


Akiwa kwenye Dimbwi la mawazo juu ya Johar huku speed ya gari ikiwa ni kali alijikuta anaingia upande wa pili wa barabara na kukuta anasababisha ajali mbaya ya gari. Kutokana na mshituko alijikuta anakanyaga mafuta badala ya breki na hapo ndipo alipolivaa lori la mchanga, kwa vile gari la Dickson lilikuwa Dogo liliweza kubinuka vibaya na kubiringita. Ilikuwa ni ajali mbaya sana, kila aliekuwa karibu na yale maeneo aliweka mikono yake kichwani.


Hazikupita hata dakika tatu, watu walikuwa tayari wamekwisha kujaa eneo la tukio, walipofika ndipo walipomkuta Dickson akiwa anavuja damu sehemu za kichwani, kwa jinsi gari lilivyopinduka liliweza kumsababishia Dickson kupoteza fahamu. Wasamaria wema kwenye lile eneo waliweza kumsaidia kumtoa Dickson katika gari lake, hakuna alietambua ya kuwa Dickson ni mzima aua amekufa. Msaada wa wale watu uliweza kufanya Dickson kufikishwa hospital na kupokelewa na madokta, hali yake ilionekana kuwa mbaya sana.


Hata Dokta alionekana kuweka mikono yake kichwani baada ya kuona mwili wa Dickson, Jitihada za Madokta zilionekana kugonga mwamba, kila walipokuwa wakijaribu kwa kila njia ili hali ya Dickson irudi kama apo awali lakini ilishindikana. taarifa zilifika wa wazazi wa Dickson ambao kwa wakati huo walikuwa wakiwaza kile kilichotokea kwenye harusi ya mtoto wao, lilikuwa ni jambo la aibu sana, waliatokea kumchukia sana Johar na kuhisi bila yeye mtoto wao asingeweza kupatwa na ile ajali.


Kilio kilitwala kwenye nyumba ya Dickson, kila siku walikuwa wakimuomba mungu mtotowao awe salama huku wakiapia na kujisemea kama mtoto wao angelipoteza maisha wangeweza kumuuwa Johar, Kwa wakati huo hakuna aligundua Johar alikuwa wapi. Taarifa zilienea karibu kila redio pamoja na tv ukiachia mbali na magazeti pia. wazazi wa Dickson alifanikiwa kupata zile taarifa kutoka kwenye televisheni/runinga, zilikuwa ni taarifa za kushitua na kuwafanya wajiulize maswali mengi.



"Mtoto wa mfanya Biashara mkubwa hapa nchini, Bwana Emanuel Tarimo. Ali maharufu kama Tarimo, amepotelewa na mwanae kipenzi Johar. Taarifa hizi pindi zikufikiapo ukiwa unatambua msichana huyo alipo au alipoelekea utoe taarifa hizi kwenye kituo chochote cha polisi. Kumbuka zawadi nono zitatolewa, kwa yeyote atakaekuwa na taarifa sahihi za msichana huyo. Ilikuwa ni sauti ya redio iliowafanya Baba yake na Dickson pamoja na Mama yake kubaki wameduwa, hawakuweza kuamini jambo kama lile.


"Johar huyu huyu tunaemfahamu au kuna mwingine, tokalini Tarimo akawa na mtoto kama yule. Hapana si kweli kabisa" Aliongea mama yake Dickson huku akiwa aamini zile taarifa. Tarimo alikuwa ni mmoja kati ya matajiri wakubwa mkoani Arusha, ni mtu aliekuwa na mali nyingi. Ukiachilia mali alizokuwa nazo, pia alikuwa na anamiliki viwanda vikubwa vya aina tofauti tofauti. Ni mtu aliekuwa safi, hakuwahi kuwa na kashfa mbaya. Nimzee alieonekana kuwa na busara nyingi sana na mwenye kujali watu, pamoja na maisha yao.


Zile taarifa zilizagaa karibu nchi nzima, ni kutokana na umaarufu aliokuwa nao mtu huyo pamoja na fedha. Wazazi wa Dickson walishindwa kuzielewa taarifa zile, maana Mzee Tarimo ndiye aliokuwa Boss wao na walimweshimu kwa msaada wake kwao. Tukija kwa upande wa Dickson hali yake haikuwa nzuri kabisa, kila siku madaktari waliongeza juudi na maarifa kwa kujitahidi kuokoa maisha ya kijana huyo. Siku,wiki hatimaye mwezi, hali ya Dickson ilianza kurejea na kuonekana kuwa hai tena.


Kutokana na matibabu ya pale hospital na hali ya Dickson,madaktari waliwashauri wazazi wa Dickson kumpeleka mtoto wao nchi India kwaajili ya matibabu ya kina, hakukuwa na jinsi maana madaktari wao ndio waliokuwa na ujuzi wa kuelewa nini kilichokuwa kikimsibu Dickson. Siku tatu mbele Dickson akiwa tayari kuelekea India kwaajili ya matibabu, safari ya kwenda India iliwagharimu fedha nyingi wazazi wa Dickson lakini hawakujali, walichokuwa wakikitaka ni mtoto wao kuwa salama. Walipofika India walipokelewa vizuri na kukaribishwa kwa furaha, walipofika walipumzika na siku iliofuata ndipo walipomchukua Dickson na kumpeleka kwenye hospital kubwa ya nchi hiyo. Wazazi wa Dickson hawakujua ni kitu gani kilichokuwa kinamsumbua mtoto wao hadi kuambiwa wampeleke India, maombi yalikuwa kila mara huku wakizidi kumsihi Mungu kuusuru maisha ya mtoto wao.


Kutokana na kutoifahamu lugha ya nchi hilo ikawalazimu kuwa na mkalmani, kwaajili ya kuwajulisha kile walichokuwa wakikizungumzia.

"Napenda kuwapa pole kwa kuuguliwa na mtoto wenu, ila ni vema mlivyomuwahisha huku maana mngalichelewa tusingekuwa tukiita jina la mwanenu. Kwa sasa maendeleo ya mtoto wenu yapo vizuri, ila kuna tatizo kubwa limejitokeza kwa mtoto wenu na ingekuwa vizuri nyie kulijua kabla muhusika mwenyewe hajalipata, japo itawalazimu kumwambia ukweli wa jambo hilo" Aliongea Daktari aliekuwa anahusika na matibabu ya Dickson kwa lugha ya kingereza, yale maneno yalionekana kuwaingia vilivyo na kuonekana kukaa tayari kutaka kujua nini kilichotokea kwa mtoto wao.


Yule Daktari aliwaangalia wazazi wa Dickson na kutikisa kichwa na kuonekana kuwa sikitikia. "Naombeni muwe wavumilivu kwa hiki nitakacho kisema, kiukweli baada ya mtoto wenu kupata ajali kama mlivyo sema, ajali hiyo imeweza kumsababishia mtoto wenu ulilema, kuwa jinsi ajali ilivyotokea iliweza kumsababishia kijana wenu kupalalaizi maeneo ya kiuno, hivyo basi kwa mujibu wa madaktari wenzangu tunapenda kuwa paarifa hizi japo bado wanajitahidi kumsaidia mtoto wenu" Yale maneno yalionekana kuwa fanya kuduwaa na kuonekana kuhisi kuchanganyikiwa kwa kile walicho ambiwa.



Waliomekana kutomuelewa yule Daktari, walizidi kupiwa na butwaa pale walipoonyeshwa X_ray za mtoto wao. Kile kitendo kiliwaogopesha na kuwapa wasiwasi juu ya mtoto wao Dickson. Kwa upande wa familia ya Angely hali ilikuwa mbaya, kitu ambacho kiliwapa wasiwasi na juu ya kupotea kwa Johar, waliamini kama Johar angepatwa na tatizo lolote wangeweza kuwajibika. Mzee tarimo alionekana kuwa na hasira nyingi na hata wakati mwingine alionekana kushindwa hata kula, alionekana kumpenda sana Johar. Siku zilisogea hadi Dickson akawa amepona ila hakuwa na uwezo wa kutembea kwa miguu yake, badala yake alikuwa akitumia baskeli za wagonjwa ambazo huwa wanatembelea wagonjwa wenye matatizo ya miguu na mengineyo yanayo mfanya mtu kushindwa kutembea.


Daktari waliwashauri wazazi wa Dickson kumzowesha Dickson mazowezi ili kujaribu kunyoosha viungo vyake, ambavyo vilionekana kupalalaizi. Ndani ya wiki mbili Dickson alikuwa tayari anaweza kutembea mwenyewe bila msaadà wa mtu yeyòte. Ile hali hata madaktari walishangaa maana hawakuwa na uhakika wa kupona kwa Dickson. Baada ya Dickson kupona kabisa waliruhusiwa kurudi Nchini Tanzania, wazazi wa Dickson waliweza kufurahi na kuamini Mungu amejibu maombi yao. Kutokana na Johar kupotea kwa kipindi kirefu bila kujulikana ni wapi alipokuwa, mzee Tarimo aliamua kumkamata Angely pamoja na wazazi wake, huku akiwa na hasira na familia hiyo.


Siyo tu wazazi wa Angely bali alikuwa akimsubiri Dickson pamoja na wazazi wake, aliamini na wao ni moja ya watu waliochangia mtoto wake kupotea, hakukuwa na mtu aliekuwa anaweza kumzuwia mzee huyo, hata polisi walimuogopa sana kutokana na kuwa karibu na viongozi wakubwa serekalini. Dickson pamoja na wazazi wake walifika nchini Tanzania wakiwa na furaha huku Dickson akimuwaza sana Johar, walipofika walielekea moja kwa moja nyumbani kwao maeneo ya Mbezi beach. Walipofika nyumbani walikuta tayari mzee Tarimo akiwangoja kwa hamu kubwa. Hawakujua ni kwanini mzee huyo alikuwa nyumbani kwao, hawakuwa na taarifa zozote juu ya kupotea kwa Johar.


Dickson alivyomuona mzee Tarimo alimsalimia kwa heshima maana mzee huyo alikuwa boss wake, lakini badala ya kujibiwa salamu yake, alishangaa anapigwa kibao cha nguvu kilichomfanya kuyumba na kutaka kuanguka. Kile kitendo kiliwashangaza sana wazazi wa Dickson, walionekana kupigwa na butwaa bila kujua nini kilicgomsibu mzee huyo hadi kumpiga mtoto wao kiasi kile. Mzee Michael ambae ni Baba yake na Dickson alisogea pale alipokuwa mtoto wake na kutaka kujua nini kilikuwa kinaendelea.


Aliposogea karibu alishtukia wanaingia askari wawili na kumkamata Dickson na kumfunga pingu mikononi mwake. "Kwa vile nawaheshimu na kuwa thamini, maana tumetoka mbali kimaisha bila hivyo hata nyinyi mngefuatana na mtoto wenu. Mnanifanya nakuwa kichaa, kila ninapo mkumbuka mwanangu nakuwa kawa kama kichaa. Bora ningejua amekufa kuliko hiki kilichotokea, msinione nimewaacha kama wiki hii itaisha sijampata mwanangu kipenzi sinto wasamehe. Nasema sinto wasamehee!" Aliongea mzee Tarimo kwa hasira na jazba nyingi huku akitokwa na machozi kama mtoto mdogo, kiukweli ile hali iliwaogopesha sana wazazi wa Dickson na kuwafanya wabaki njia panda.


Dickson alichukuliwa na kufikishwa hadi kituo cha polisi, hakukuwa na maongezi yoyote juu ya Dickson na polisi, alivyofikishwa alifungiwa kwenye vyumba vya waalifu huku akiwa na pingu zake mkononi. Roho ilimuuwa sana hakujua nini kilikuwa kimemsibu Johar, alimtupia lawama nyingi Angely maana alihisi bila Angely na wazazi wake Johar asingepotea. Asubuhi ya siku iliofuata geti ya chumba alichokuwa amewekwa Dickson lilifunguliwa na Dickson alichukuliwa na kupelekwa kwenye chumba kingine kwaajili ya mahojiano, alipofika ndani ya chumba hicho alishangaa kuwakuta wazazi wa Angely wakiwa kwenye hali ya huzuni, alipoangalia pembeni aliweza kumuona Angely akiwa amepauka mdomo ikwa kama mtu ambae hakuwa ameoata chakula kwa muda mrefu.


Dickson alimwangalia Angely vibaya pamoja na wazazi wake, akiamini wao ndio waliosababisha yeye kuwa pale, hasira za wazi wazi zilionekana kwa Dickson hata yule askari aliekuwa pale aliligundua lile na kubaki akiwa anamwangalia Dickson na kuonyesha kumsikitikia. "Dickson Michael, wewe ni mtu mwenye heshima kubwa kutokana na cheo ulichokuwa nacho, ila kwa sasa inatulazimu kukiweka cheo chako pembeni kwaajili ya kufuata sheria. Nafahamu nyinyi mnamjua vizuri mtoto wa Mzee Tarimo. Kwa taarifa tulizo nazo ni kuwa nyinyi mnahusika na kupotea kwa msichana huyo, hivyo basi endapo msichana huyo hatopatikana basi mtawajibika kwa hilo" Aliongea askari aliokuwa anawahoji na kuwafanya kubaki midomo wazi huku wakijiuliza wamehusika vipi na kupotea kwa Johar.



Dickson hakuwa akimfahamu apo awali kama Johar alikuwa ni mtoto wa Mzee Tarimo. Ile hali ilimfanya Dickson kuwa kimya na kuanza kutafakari jinsi mzee Tarimo alivyokuwa anampenda na kumjali kama mwanae, alishindwa kuelewa kwa nini yale yote yalikuwa yanatokea mbele yake. Yule askari alikuwa akimtizama Dickson na kuonekana kutaka kumwambia kitu, lakini alisita na kuwaambia muda wao umeisha na waweze kurudi walipokuwapo mwanzo. Wazazi wa Dickson walibaki wakiwa hawaelewi waanzie wapi kumtafuta Johar, kila walichokuwa wanajaribu hakukuwa na faida. Walionekana kuwa kama watu walio changanyikiwa, lile jambo lili waumizwa kichwa na kuzidi kuwapa hofu na kuhisi muda siyo mrefu wangeweza kwenda kuanza maisha ya Jela. Walitambua kuwa Mzee Tarimo hakuwa na utani hata kidogo, walijua ni kazima wangepelekwa polisi. Asubuhi ya siku inayofuata wazazi wa Dickson walikwenda kumsalimia mtoto wao.


Walipofika walishangaa baada ya kuambiwa Dickson pamoja na Angely wapo hospital, walihisi wale askari walikuwa wakiwatania na kukumbuka kuwa Dickson hakuwa anaumwa. Kutokana na wale askari kuwa wakali na kudai Dickson hakuwa pale ndipo wazazi wa Dickson walipoamua kufunga safari kwenda hospital waliokuwa wamepewa taarifa. Kama walivyoambiwa ndivyo ilivyo kuwa. "Samahani Dokta kuna kijana kaletwa hapa anaitwa Dickson?"

Aliuliza Baba yake na Dickson baada ya kufika hospital hapo.

"Ndiyo kijana huyo ameweza kuja hapa na ninavyoongea yupo anafanyiwa matibabu, pia ameweza kuletwa na msichana aliekuwa kwenye hali mbaya" Aliongea Dokta huyo na kuwafanya Mzee Michael pamoja na mkewe kubaki wakiwa wamekodoa macho.


Yule dokta aliwaambia waweze kusubiri kwa muda mfupi wakati madokta wengine wakiendelea na matibabu kwa Dickson pamoja na Angely.

"Samahani Dokta unaweza kuniambia nini kinachomsibu mwanangu?" "Mwanao yupi? Huyu wa kike au?"

"Hapana. Huyu wa kiume"

Yalikuwa ni maswali kati ya Baba yake na Dickson pamoja na yule Dokta. Yule Daktari alimwangali Baba yake na Dickson pamoja na Mama yake, alishindwa kuongea na kupiga hatua za kuelekea ofisini kwake. Walipoona yule Daktari ameondoka na kuelekea ofisini kwake na wao wakaamua kumfuata na kuingia katika ofisi ya huyo Daktari. Walipofika walishangaa baada ya kumkuta Dickson akiwa ameketi kwenye kiti pale ofisini, walionekana kushangaa na kuwa kama mtu aliemwagiwa maji ya baridi angali kukiwa na baridi kali. Kimya kilitawala kwa dakika kadhaa na ndipo yule Dokta alivyoanza kuzungumza kile kilichokuwa kinamsibu Dickson.


"Kiukweli naombeni mniwie radhi kwa kuwadanganya, ila sikufanya vile kwa nia mbaya. Kwanza kabisa napenda kumpa pole sana Dickson kwa matatizo yanayo mkabili. Pili napenda kuwashukuru pia na nyinyi wazazi kwa ujio wenu hapa". Aliongea Dokta huyo huku akiwa anachukua karatasi liliwa na maandishi yalioandika kwa kalamu ya blue. Dickson kwa muda wote alikuwa kimya akiwa kama mtu aliekuwa na jambo gumu mbele yake.

"Dickson nakuomba uwe mvumilivu kwa hili, si kwamba hutopona. Haya yote ni mambo ya kawaida na napenda kukupongeza maana muda siyo mrefu utaitwa Baba"


Maneno ya yule Dokta yalikuwa maneno ya mafumbo ambavyo ilikuwa ngumu kuyafumbua, machozi yalianza kumtiririka na kuwafanya wazazi wa Dickson kushindwa kuelewa nini kilichokuwa kinamsumbua mtoto wao. "Dickson mwanangu nini kinakusumbua na mbona unalia?" Aliuliza Mama yake na Dickson huku akiwa anatamani kupata jibu kwa mtoto wake. "Mama bora ningeugua Ukimwi kuliko kuwa kama nilivyo sasa, sina thamani tena maana mimi sinafaida tena zaidi ya kuwa kama makapi tu" Aliongea Dickson kwa sauti kubwa yenye majonzi na hasira nyingi, Mama yake na Dickson alishangazwa na yale maneno ya mtoto wake na kuhisi mtoto wake ameanza kuchanganyikiwa.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG