Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

KILIO CHANGU - 4

   

Simulizi : Kilio Changu

Sehemu Ya Nne (4)



Dula kabla hajajibu kunamzee mmoja akaingia akiwa anahema naitwa juma nimesikia mke wangu na mwanangu wameletwa hospitali hapa wakiwa mahututi bado wazima? Mzee juma aliongea huku jasho linamtoka dokta ikabidi amtulize na kumwambia mke wako na binti yako anaitwa nani.


Aaaaanaitwa mama jeni na mtoto wetu anaitwa jeni

Ile kutaja jeni Dula akashituka kumbe huyu ndio baba yake jeni

Dokta aliweza kumweleza vyema na kumtoa wasi wasi na kuwa wanaendelea vyema ila mtu ambae anaruhusiwa kumwona ni mkewe tyu ila jeni hadi kesho basi mzee juma alienda kumwona mkewe pamoja na akina dula na nasra.


Ndipo dula na nasra walivyomaliza maongezi na mgonjwa waliaga wanaondoka hadi kesho

Mzee juma aliingiza mkono mfukoni akatoa laki mbili akawapa Dula na nasra na kuwashukuru kuokoa maisha ya familia yake

dula alipokea kisha akatoka nje

Ndipo alimgawia nasra laki moja.


Dula hizo hela chukua zote mimi sina shida na hela baba yangu anapesa nyingi nasra alikataa kupokea japo alimlazimisha ila hakupokea

Dula alizitia mfukoni na kumwaga nasra kua yeye anaenda nyumbani

Nasra alimwambia Dula apande gari ili ampitishe anako kaa basi dula alikubali.


Dula na nasra walisogea hadi mahali waliko paki gari nasra alifungua mlango akaingia na kumwambia dula apande

Kitendo cha dula kushika mlango wa gari alishangaa kitu kizito kikatua shingoni puaaa ,dula akayumba kabla hajakaa vyeama akapigwa tena na nondo nzito kifuani dula akayumba na kudondoka nasra akapiga kelele baada ya kumwona mpenzi wake ambae mchana aliwafuma wamekumbatiana na Dula baada ya kumsaidia kurudisha simu yake kwa vibaka.


Jemba ilimtandika Dula balaa mudy akiwa hajielewi yule mwanaume wa shoka akatoa panga na kuliweka shingoni mwa dula kisha sauti nzito ya yule mwanaume ikitetemesha " akasema shenzi boya wewe nakata shingo mchana ulibahatisha kunipiga wasalimie kuzimu.



Tulipoishia jana baada ya Dula kupigwa na jemba kisha akadondoka chini ile njemba ikiwa na kundi lake alitoa panga na kuiweka kwenye shingo ya dula.


Nasra alianza kutetemeka wakati Dula hajielewi anaona marue rue baada ya kupigwa na nondo kifuani na shingoni

Yule jemba alianza kuonge "mimi ndio RAMSONI gaidi wa dar es salam wewe nyau mchana uliniotea ukanizimisha ukajiona wewe ndio hatari kwa taarifa yako nakata shingo wasalimie kuzimu


Ile anashikilia panga ili amkate Dula, Tayari dula kengele ya hatari ishagonga kichwani dula alihisi kichwa kinazunguka alijituliza akakuta panga ipo shingoni.


Alichokifanya aliikamata ile panga kwenye makali , ramso akashtuka kumbe huyu bwege hajafa tyu ramso aliinama ili amkandamize dula asisimame kitendo cha kuinama dula yuko shapu aliinuka kwa stail yake na kumtandika hedi ya maana kwenye utosi ramso akapiga yowe la uchungu yani kichwa alotandikwa ni balaa ikawa zamu yake kuona marue rue,


Dula akafanikiwa kuinuka huku kashikilia panga kwenye makali

Ikawa vuta nikuvute aliachia ile panga akaruka na kudunda juu ya gari akajizungusha na kuachia mateke mawili yaliyompata ramso vyema kichwani ramso akayumba na kudondokea kwenye gari yake

Kabla hajakaa sawa dula katua kifuani na kumtandika makonde ya ngumi nzito.


Ramso ulimi ukamtoka wakati ngumi zikiendelea kurushwa bibie nasra kashikilia mapigo ya moyo na kujisemea" mungu msaidie dula asiuawe nampenda hakika ni handsome anioe mimi walai nimempenda hayo ndio yalikua maombi ya nasra" hakujali kama dula anapambane yeye ombi lake ampate dula.


Ramso nae alijitahidi akarusha ngumi na kumpiga dula shavuni kama karudisha mashambulizi hapo ndipo alipokosea dula aliruka hewani akajizungusha kama kamba na kumtandika mateke ya double kifuani ramso alirushwa na unene aliojazia kwa kunyanyua vyuma na kwenda kujibamiza kwenye mstimu puuu, taya zikapishana akajaribu kuongea hakuweza akajaribu kuinuka hakuweza.


Dula akaenda na kumwambia ramso "kaka yangu mimi staki kukuua huenda utajirekebisha shika panga lako ukipona utaenda kufanya shughuli za shamba na ukiendelea kunifuatilia nitakupoteza kwenye huu ulimwengu nakuheshimu sana "


Dula aliongea na kumtupia panga lake kisha akaondoka na kuingia gari ya bibie nasra ,ramso na wenzake hawaamini kama wamepata mbabe wao ,mwanzo walijua jiji lakwao wananyanyasa watu ile kwa sasa imekuwa tofsuti.


Hospitali ilijaa watu wakishuhudia pambano live simu ilipigwa polis ile dula anatoka akapishana na gari ya polisi

Ramso na wenzake wakawezwa kukamatwa wakati huo dula washaondoka na kuelekea nyumbani ilikua tayari ishatimia saa moja jioni.


Musa nae akiwa getoni kwa Dula alichoka kulala akaamua atoke akatembee ili apunguze mawazo musa alifunga mlango na "kujisemea huyu Dula kaenda wapi?" Au nisitoke huenda atakuja na akikuta sipo atamaindi maana jamaa mwenyewe anajua kupigana kama wachina yaani nishida .


Aliwaza huku akizidi kusonga na kuzidi kufika mbali sehem waliko kulikua na mageti makubwa nyumba za kishua.


Mara kuna mdada mzuri kaumbika balaa akiwa anatembea haraka haraka kashika simu kashika mkoba mkononi kashika pochi ndogo sijui ndo inahela .


Akiwa anaharaka haraka anataka kuiweka ile pochi ndogo kwenye mkoba bahati mbaya hakuiweka ndani yeye alifungua zipu na kuweka kumbe hakuweka ile pochi ikadondoka chini puuuh!.


Kulikua na mwanga wa mbala mwezi na taa za majumbani

Musa aliiona ile pochi wakati huyo dada ashafika mbali kaiacha

Musa akafika mahali iliko dondoka hio pochi akaiokota "mmmmh mbona nzito hii pochi kuna nini?"


musa alijisemea na kufungua akajikuta anatoa macho "mmmmh " akaguna na kusema kumbe watu wanalalamika vyuma vimekaza watu wameweka mahela ivi .


ile pochi ilikua imejaa minoti miekundu tyu musa hakuhesabu aliitia mfukon akaangalia kulia na kushoto hamna mtu

Musa akasema tayari nishakuwa tajiri mimi umaskini bai bai.


Musa akasema hizi hela kazidondosha kwa haraka zake acha nikaziweke geto musa akiwa anawaza. Hivyo mara sauti ya mama yake ikamjia angali mtoto "mama yake alikua akimwambia "


"Mwanangu ukiokota kitu na ukamwona aliyeki,dondosha iwe ka bahati mbaya mrudishie usifsnye dhuluma , usiibe wala kufanya uhalifu ili utajirike,

Utajiri huja taratibu ila sio kwa kuzulumu kuiba na kupora

Yale maneno yalimuuma akasema yawezekana hizi hela alikua anapeleka mahali acha nimkimbilie nikamkabidhi hela zake ,alianza kukimbia kumtafuta yule dada.


Wala hakua mbali aliweza kumwona akiwa anaongea na simu huku anatembea haraka haraka


Musa alimwita "dada nisubiri wee dada nisubiri" musa alimwambia cha ajabu yule dada aligeuka na kumwangalia musa kisha akaendelea kuongeza mwendo ,si unajua ukiwa umebeba pesa nyingi basi kila mtu unaemwona mbeleke yako unahisi ni kibaka


Eneo hilo hapakuwa na watu palikua pametulia sana mageti tu ya nyumba za kishua

Musa alikimbia na kumkimbilia yule dada

Cha ajabu yule dada nae akakimbia huku akiongea na simu ,hufu ya yule dada anajua anapesa hivyo anahofia kuibiwa ama kuporea ndio maana nae akazidi kujihami.


Yule dada akimtizama musa mwonekano alijua ni kibaka anataka ampore simu na hela alizokuwa nazo

Basi dada aliendelea kujihami kukimbia alikimbia na kufika kijiwe cha kahawa akiwa anahema juu juu watu wote walimwambia dada kulikoni mbona unakimbia hivo.


Yule dada akiwa anahema akasema kuna mtu ananikimbiza sijui ni kibaka anataka aninyang'anye simu yangu yule dada aliwaambia vijana kwenye kijiwe cha kahawa


Vijana walisimama kila mtu na zana zake yuko wapi huyo kibaka anataka kukaba saizi mapema saa mbili watu walijiandaa kwa ajili ya kumfundisha adabu huyo kibaka mara musa akajitokeza akiwa anamfuata yule dada akampe pochi yake .


Kitendo cha kufika kijiweni yule dada akamnyooshea musa mkono huyo hapo jamni

Musa alivamiwa na kuanza kupigwa pale pale kijiweni" we kibaka kudadeki zako unataka kuiba ,watu kama ninyi tunawatafuta , musa alishambuliwa na watu wengi vijana kwa wazee wahuni wote wa sinza walimpiga musa na mbao, nondo viti hakika ndani ya dakika tano musa hatamaniki damu kila mahali.


Mimi sio mwizzz musa alijitetea "aah wapi wala watu hawakumwelewa alitandikwa mbaya".


Mara gari ya nasra akiwa na dula, ilitokeza mahali pale dula aliweza kuona rundo la watu wakimshambulia mtu akiwa ana gara gara chini huku wakimpa kipigo kikali dula, alimwambia nasra hebu simamisha gari pale kuna nini mbona kama mtu anapigwa ebu simamishe gari nikacheki kuna nini.


Nasra akakataa kusimamisha gari na kumwambia dula," staki wasije wakakupiga mi nikakukosa bure kwani hujui kama saivi upo moyoni ,yaani natamani nikufungie ndani usitoke nasra aliongea huku akikataa kusimamisha gari".


dula akaona hii tabu kutembea na mwanamke anae waza mapenzi muda wote akajaribu kufungua mlango nasra alikua amelock.


Ikabidi atumie nguvu simamisha gari lasivyo nakufumua sasa ivi nasra alivyoona dula kakasirika ndipo akakanyagw breck gari ikasimama.


Sema walikua washapapita dula,alifungua mlango upesi na kutoka alienda lile eneo alikuta rundo la watu likiendelea kumpiga musa.ki ukweli musa nyota yake mbaya kila mahali yeye wa kupigwa anamkosi.


Musa aliishiwa nguvu damu mwili mzima. Dulaalifika na kusema acheni acheni acheni huku akiwasukuma ili wasiendelee kumpiga huyo mtu kuna kijana mmoja alikua kabeba tofali la block na tayari alijiandaa kumpiga musa kichwani.


Yule jamaa aliachia lele tofali bahati nzuri dula alikua tayari ashafika alilidaka lile tofali kidogo angezubaa musw angepasuliwa wakati huo hajui kama anaepigwa ni musa na alishaambiwa na jeni amlinde musa aishi salama.


Watu wote walimshangaa dula baada ya kudaka lile tofali ,akiwa anahema "aliwiwauliza mnampiga kafanya kosa gani ?" Huku anamwinua mtu aliyekuwa akiipigwa alizidi kushangaa baada ya kuweza kumtambua yule ni musa.


Dulabaliita kwa nguvu musa ndugu yangu kulikoni ,musa alikua hawezi hata kuongea aliongea kwa tabu kaka dula sielewi nimefika hapa wakaanza kunipiga alimwambia dula.


dulw akiwa haamini aliwaukiza watu huyu kafanyeje mbona mmempiga watu wakasema alikua anamkimbiza huyu dada ili amupore simu.


Musa hali yake ilizidi kuwa mbaya wema wake umemponza musa analoa damu kuongea hawezi ukimtizama kama unaroho nyepesi lazama utamwonea huruma.


Musa alijaribu kusimama hakuweza akajikakamua na kusimama aliingiza mkono mfukoni akaitoa ile pochi ndogo ya yule dada musa aliongea maneno machache.


"Dada mimi sio kibaka wala mwizi na hii mara yangu ya pili kusingiziwa mwiz ulidindosha pochi yako na mimi ndio nimeiokota nilikua nakukimbilia ili nikukabidhi pochi yako nasi kukupora simu"


musa aliongea kwa shida yule dada baada ya kuona ile pochi kwa musa akimpa alitumbua macho hakuamini ukweli ilikua pochi yake,

Alifungua mkoba mkubwa pochi haikuwepo ,ndio ile musa alompa


Yule dada alianza kilio nisamehe sikujua kaka yangu nimekuponza umepigwa yule dada alilia kijiwe chote walishangaa na kujilaumu uamuzi waliouchukua

Wote walinza kumwomba musa msamaha


Kwa kipigo alichopigwa musa gafla alidondokea kwa dula na akawa kimyaaa akiwa anavuja damu.

Yule dada aliyepewa pochi yake alilia na kujiburuza chini akiomba msamaha.nimeponza mkaka wa watu anakufa kww ajili ua uzembe wangu.


dula alimwita nasra alete gari upesi amuwahishe hospitali

hatimae musa alifumba macho na kuwa kimyaaaa

yule dada ambae hatujajua ni nani,akasema nimeua ,nimeua akiwa analia,dula nae akamtizama wkamuuliza "unasemaje?



Hakika yule dada alilia sana na kujilaumu kwanini aliwaambia watu kuwa anataka kumpora

Watu kijiwen walimlaumu yule dada na kumwambia usiwe unamhisi mtu tu ukajua ni mwizi ona tulivyompiga kijana wa watu sijui kama atapona yule dada alipewa lawama zote. Watu kijiweni walijilaumu sana , haikuwezekana tena kwa muda ule kuomba msamaha kwa kipigo wapichompiga musa maana alidondoka na kuwa kimya .


Musa alipakiwa kwenye gar na nasra na kuwahishwa hospitalini gafla sim ya yule dada ikaita bila shaka kuna mtu alimpigia aliitoa kwenye mkoba na kuipokea "haloo upande wa pili akaitikia" yes"

mwanangu uko sawa?

Mbona kama unalia yule dada akasema" niko saawa japo alibabaika maana waliwasiliana na baba yake" na kuambiwa awai kinondoni biafra .


yule dada alikodi piki piki akaelekea aliko ambiwa aende dada yule alichanganyikiwa alikua akilia sana aliweza kufika biafra alifuta machozi ili kuzuga baba yake asijue kipi mimemkumba njiani ,aliweza kwenda moja ya baa iliyoezekwa kwa makuti alinyoosha hadi akaunta aliweza kumkuta baba yake .


"Dady shikamoo"

" marhaba mwanangu "

vip mbona kama ulikua unalia?


Yule dada alitikisa kichwa na kusema "hapa "

"Irene mwanangu unanificha ee ok sawa "

kumbe huyo dada alikua anaitwa irene, basi almkabidhi mzigo alioupeleka kisha akamwaga baba yake kua anarudi nyumbani baba yake alimruhusu na kumpa hela ya usafiri .


Irene alirudi nyumbani moja kwa moja alipitiliza hadi chumbani mama yake alikuwa kakaa sebuleni lakin irene aliingia chumbani kwake na kuanza kulia

"Hiiii hiiiii nimeua jamani mungu nisamehe sikujua kwamba yule kijana hakua na nia mbaya na mimi"


Kijana wa watu kaokoa pesa za baba endapo zingepotea baba angeniua mimi wala asingenielewa.


Kijana wawatu kaokoa maisha yangu mimi nimemsababishia kifo

Eeeh mungu muokoe asife nitafanya chochote kwa ajili yake niko tayari kuokoa maisha yake hakika irene alilia na kujilaumu

Mama yake alimwita akale chakula irene alisema ameshiba.


Tukija hospitali ambako jeni na mama yake kalazwa musa nae alipelekwa pale .musw alipokelewa haraka na kupelekwa chumba cha watu mahututi hali yake ikiwa haitambuliki kama amekufa au yu hai madaktari walianza kumshughulikia walimuwekea oxygen na mambo kadha wa kadha

Ilionekana mapigo ya moyo yako mbalii sana dokta alijitahidi usiku kucha

Musa alikesha na nasra.


Nasra alirudisha gari nyumbani kisha akachukua koti na dula nae akampelekea koti

Nasra alikaa pemben ya dula ,wakiwa kimya dula alikua hana ata hamu ya kuongea akifikiria hali ya musa anashikwa na uchungu na kujikuta machozi yanamtoka walikesha wakisubiri majibu.


Ilifika saa nane usiku nasra alichoka akajilaza miguuni kwa dula, alilala huku akipata joto.

dula hakua na hisia zozote , aliingia kwenye msongo wa mawazo nasra alianza kukoroma japo kulikua na feni ila mbu bado walikua wana muuma dula pamoja na nasra.


Hadi pakapambazuka kila akiwauliza madaktari vip anaambiwa cha msingi ni kumwomba mungu kwani hali yake sio nzuri

Palivyopambazuka jua likachomoza


Irene alishidwa kuvumilia irene alilia hadi macho yakamvimba jua lilivyochomoza alitoka na kuanza kumtafuta musa kila hospitali za pale sinza

Hakika irene alichanganyikiwa alijuta alicho kifanya ilifika mida ya saa tatu

Chumba alichokua jeni kilifunguliwq jeni alikua kapona japo sio sana ila aliruhusiwa akaendeleze dozi nyumbani jeni pamoja na mama yake.


Chumba aliko musa alipimwa na ikaonekana damu iliyopo ni chache hivyo anahitaji kuongezewa damu

Dokta aliwafuata dula na nasra ili akawape taarifa za mgonjwa wao kuongezewa dam.


Jeni walitoka na mama yake pamoja na baba yake walishangaa kuwakuta dula na nasra wako pale.


"Hee nyie toka jana hamjaenda nyumbani?" Baba yake jeni alimuuliza ,dula aka wajibu" baba hapana kuna mgonjwa mwingine tumemleta ok baba yake jen akaitikia".


Jeni alivyomwona dula alimkumbatia na kumwambia asante kwa msaada wako kitendo cha jeni kumkumbatia dula, roho ya nasra ikaenda juu na kuhisi jeni anafaidi joto la dula, maana anampenda dula balaa.


Mara dokta akafika na kumwambia dula, mgonjwa wenu anahitaji kuongezewa damu upesi kama kuna mtu atajitolea kumpa damu aje tumpime ili tuweze kuokoa maisha yake anahali mbaya ,dula alisema sawa twende ukanipime jeni akamuuliza dulwla" nani anahali mbaya"? dula akamjibu jeni "musa anahali mbaya jana kapigwa usiku."


Jeni kusikia jina musa akachanganyikiwa na kusema dokta kama damu yangu itafaa kumuwekea musa nitoeni damu yote hata sasaivi haiwezekani kila siku musw wa kupitia mateso hayo nitoeni mimi damu nife musa apone .dunia hii ni mara chache kuona mtu anatoa uhai wake kwa ajili ya mtu mwingine kama bahati aliyoipata musa licha ya kuwa na bahati mbaya kila muda yeye wakupitia mateso.


Jeni aliongea huku analia alikua hawezi kutembea vizuri sababu ya kukanyagwa tumbo, baba yake jeni na mama yake jeni walimshangaa mwanao na kumuuliza huyo musa" unamjua jeni aliwajibu namjua".


Kweli hali ilikua tete jeni kagoma kwenda nyumbani anataka atolewe damu apewe musa si mchezo ,dula alipimwa damu hazikuendana magroupn hivyo haitawezekan.


Jeni alisisitiza yeye apimwe ili damu yake yote apewe musa ,lait anfejua mtu anaeyetaka kumpa dwmu yake tayari keshaonjeshwa tunda bafuni na mpangaji basi asingelisubutu ila kwa kuwa hajui basi alitaman kumsaidia musa apone,


yeye yupo tayari kufa na endapo watakataa kumtolea damu wakasababisha maisha ya musa akafa basi yeye yuko radhi kujiua na yeye endapo tu musa atakufa na yeye atajiua ki vyovyote vile.


Hakika jeni alizidi kuwaacha wazaziwake midomo wazi wakashidwa namna ya kumshauri jeni hakusikiliza chochote anachotaka damu yake ipimwe apewe musa.


Wazazi waligonga mwamba ikabidi wakubali apimwe maana wakikataa endapo musw atakufa na yeye atakufa si mchezo jeni alichukuliwa damu na kupelekwa kwenye vipmo.


Ile dokta anaenda maabara mara irene akaingia wakakutana uso kwa uso na dula .hasira za dula zilipanda baada ya kumwona irene pale hospitalini maana irene ndiye aliyesababisha hayo yote hadi musa kuwa katika hali ile.


Macho ya irene yalikua yamevimba na kulia alivyofika alipiga magoti huku akilia akimwomba dula amsamehe na hakujua kua musa hakuwa na lengo la kumpora irene alilia huku akiomba msamaha,hospitali ilijaa majonzi na kuacha watu vinywa wazi.


Kaka kama yule kijana anahali mbaya anaitaji kuongezewa damu au moyo au mapafu nitoeni mimi ili huyo kijana atibiwe mimi ndiye niliyesababisha awe katika hali ile. irene aliongea mashavu yake yakitiririsha machozi


Irene akiwa analia na kusema kama musa anahitaji kupewa moyo ili asife yeye yupo tayari kutoa moyo wake iwe figo hata damu hakika irene aliwashangaza watu.


Mara dokta alirejesha majibu na kusema damu ya jeni inafaa kwa musa wapo group moja jane akaitwa ili akatolewa damu kama alivyosema awali.


Irene alisimama na kusema hapana wewe dada niache mimi nife dokta pima damu yangu nikamuongezee huyo kijana irene alimzuia dokta dokta nae aliongea kwa msisitizo endapo tutaendelea kuzozana tutampoteza huyo mpedwa.wenu.


Irene akarudia kuongea kama huyo kaka atakua anahitaji moyo chukua wangu kama figo chukua hata damu chukua .


Dokta alichanganyikiwa ikabidi akampime irene endapo damu zitaendana achukue ya irene maana jeni bado anaumwa.


Damu ya irene ikapimwa na majibu yakaletwa kuwa inafaa kumwongezea musa


Dokta akamwita irene akamtoe damu ili amuongezee musa, jeni aliwaza anampenda sana musa na yuko tayari kwa lolote sasa jane alimkaba irene na kusema mimi natolewa damu nimsaidie musa

Irene akamkaba na yeye jeni akasema yeye hastahili kuishi kwani alichomfanyia musa hana thamani ya kuishi kwenye sayari hi kwel ikawa vuta nikuvute mimi natolewa damu jeni anataka irene anataka.


Dokta alitazama saa yake mkononi na kuwambia zimebaki dakika kumi tu endapo mtachelewa basi musa atapoteza maisha




Mwa upande wa jeni ilikuwa ni vigum mno aligoma hadi kufikia baba yake kukasirika kwani ashampinga mwanao vikali asijihusishe na wanaume na hii ndio madhara yake .


Baba yake jeni ikabidi aulize musa ni nani na alipenda aunane nae, akaoneshwe ili amjue hata kwa sura dokta alimruhusu akaenda pamoja na mkewe ile mama ireni kuingia chumba aliko musa na akaweza kuona uso wake akajikuta anakumbatia mdomo kwa hofu kisha yule mama akaanza kutiririsha machozi jambo lililofanya baba jeni ashidwe kuelewa kuna nini kati ya familia yake na huyu musa.


Mama jeni alitoka nje akamvuta mwanaume na kusema hata yeye ashawai kumsaidia huyu kijana mwezi mmoja ulopita alipigwa maeneo ya mwenge mimi nilimchukua na babu mmoja nilimpeleka massana hospital alitibiwa na alikua anaendelea vyema sasa sijui binti yetu wamejuana vipi vipi huyu kijana .


Mama jeni aliongea kisha baba jeni hasira zilipanda alimshika binti yake mkono na kumvuta kwa hasira hakujali yakua jeni anaumwa alimkokota hadi kwenye gari .


Jeni alilia na kusema baba niache hadi nisubiri nione musa anapona ila baba yake aliwaka mbaya alimchukua na kuingia kwenye gari aliongea neno hamna kutoa damu wa msaada wote twendeni nyumbani aliweka kikomo na maneno yake kwenye familiw ni sheria .


Jeni utanieleza huyo kinyago mwizi sijui musa mmekutana vip na nilishakukataza kutembea na wanaume leo ndio utanitambua mimi ni nani mzee aliwaka mbaya, jeni wala hakujali alikua akilia tyu,kupande bwana kunamfanya mtu anakuwa chizi.


Hospitali baada ya jeni kuchukuliwa ki nguvu na baba yake ndipo dokta aliweza kumtolea damu irene haraka haraka na kumpatia musa

Na tayari ilikua zimesalia dakika chache musa apoteze uhai wake kutokana na hali aliyokuwa nayo.


Hapo ndipo musa aliongezewa damu, irene alikua ni mtu wa kulia na kumwomba mungu musa apone amwombe msamaha kwa kweli ilikua ni wakati mgumu kwa irene .


Dula na nasra walikuwa wakikaa pale hospitali walikua wananunua chakula wanakula wote nasra hakutaka kukaa mbali na dula nae moyo ushatawala kwa yule kijana ,sijui kww mwonekano wake ama ujasiri alionao wa kupambana na kuwa mshids ,huenda nasra aliona hio nafasi ndio nzuri kumpenda mwanaume ambae anaweza kumlinda.


Nyumbani kwa irene alianza kutafutwa ,na familia hake haonekaniki kibaya zaidi simu aliacha chumbani alitoka yeye kama yeye mama yake alianza kuwaza huyu binti yangu sasa kaenda wapi maana toka jana simwelewi.


Alijaribu kupiga simu kwa mmewe , "akamuuliza vp irene amekuja huko?" mme akasema" toka jana alivyompelea zile hela yeye aliondoka na yupo mlandizi kwenye shughuli zake za ujenzi ,mama irene alibaki njia panda.muda mwingine kulewa mabinti ni kazi kweli kweli.


Tukirudi hospitalini baada ya jeni kutolewa damu alipewa wosia ale sana mboga za majani na matunda ila irene hakuwa na hamu ya kula

Musa alianza matibabu hatimae hali yake ikawa nafuu.


kila siku irene anakwenda kumtembelea musa hospitalini vile vile dula na nasra wakawa wanamtembelea nao kila siku na kumpelekea chakula musa alikaa miezi miwili hatimae alipona na kurudi katika hali yake.


musa alipona majeraha na mwili ukaimarika ,vile vile alimsamehe irene irene kwa yote yaliyotokea kwake aliona ni sahihi hata asingelimsamehe isingesaidia maana tayari hali ishatokea ,pia kumshukuru kujitolea kumwongezea damu na kuokoa maisha yake.


Musq aliruhusiwa na kwenda kwa nyumbani mwenye geto la dula

nasra na dula tayari walikua wapenzi toka jeni atoke hospitalini hakurudi tena wala hata simu haipatikani sijui kitu gani kilitokea ,kwa upande wa irene akawa kili siku lazima aende kwa akina musa alimfulia musa nguo kumpikia kila kitu alikua anafanya hivyo walau kulipa kew kile alichifw ya ,musa alijaribu kumkataza ila irene hakukubali alilazimisha kufanya vile..


Maisha yaliendelea kama kawaida , kuna siku musa alikaa nje akawa anamfikiria jeni na "kusema jeni nitampata wapi nimemisi nimwone akiwa kakaa kaegemea ukuta" alisikia dula akiongea na simu.


"Halo we nani?"

" Mimi jeni hunikumbuki?"

jeni yupi dula alikua anaongea huku kaweka laudi spika musa aliyasikia vyema maongezi jeni .

pia aliahidi leo anakuja kumwona musa

dula alimwelekeza mahali anamoishi ili iwe rahisi kufika eneo lile.


Ilivyofika mida ya saa nane gari aina ya nissan ilipaki mahali akina dula wanaishi mrembo matata alishuka kwenye gari marashi alopuliza kila mtu aliuliza nani huyo kapuliza hio pafyum nzuri wapangaji walitoka kuangalia huo ujio wa nani? kama mjuavyo wambea lazima waangalie kila kitu.


musa alikua kajilaza kwenye mfuko wa roba na alikua akivuta usingizi wa mchana maana ndani ya chumba dula alikua na bibie nasra wakipeana mavitu roho inapenda ,hio ni kawaida kwa watu wanaoshare chumba ,mwenzako akipata mwanamke basi unampisha unaenda kuzururs hadi atakapomaliza mambo yake utarudi ,ila kwa musa ilikuwa ngumu hana nahali pa kwenda hivyo aliona ni vyema alale.zake nje tu.


Jeni alikua kabadilika kawa mweupe nywele ndefu hadi mgongoni jeni aliangaza macho akatoa simu kubwa akabonyeza namba alimpigia Dula.


Dula alipokea kisha akatoka ndani ya chumba chao huku akivaa vest nyeupe huku jasho likimtiririka bila shaka alikua kwenye shughuli ya kumkuna narsa.


dula alipagawa baada ya kumwona jeni ikabidi aite jeni?

"Yes dula " jeni aliitika na kujibu ni mimi , vipu musa yuko wapi jeni aliitika na kumuuliza".


Dula alicheka na kumwambia inamaana humwoni kweli au unanitania? jeni akauliza tena "yuko wapi "


Dula alimwonesha kwenye ukuta ule pale kalala wala hana habari alikua kajilaza kwenye roba kajikunja vilivyo.


Jeni baada ya kuambiwa ndio yeye musa haraka alienda mahali aliko musa na kukaa kwenye roba hakujali kama linavumbi jeni alikaa kisha akamugusa musa shavuni .


musa alijivuta akiwa usingizini jeni alirudia kumtingisha hapo ndipo musa aliamka ,alishangaa kumwona msichana mrembo sura haikua ngeni alimtambua vyema.


Jeni alimkumbatia kwa nguvu baada ya kumwona mzima wa afya taratibu machozi yakaanza kumtoka musa na jeni nae alilia kwa furaha.siku zote upendo huanzia moyoni hata bila kutamkiana mnapendans,ni dhahiri hisia za muss na mrembo jeni ,mioyo yao ishapendana.


Jeni aliita musa

musa kinywa kilikuwa kizito yote ni furaha ya kumwona msichana ambae kila kwenye majanga amekuwa akiokoa maisha yake .

Musa alimkumbatia jeni na kumshukuru kwa msaada wake.


jeni nae alifurahi kusikia sauti ya musa walikaa nyuma ya nyumba kwenye gunia lenye vumbi jen wala hakujal dula nae walitoka na nasra wake wakaenda kukaa nje pamoja na akina jeni.


Jeni alicheka kidogo akasema samahanini. dula, musa na wifi yangu nasra ngoja niwaletee chakula kipo kwenye gari.


jeni aliongea na kuinuka na kufanya uwazi kwenye mapaja yake ,musa aliweza kuona nguo ya ndani aliyovaa bibie jeni na kusababjsha mjsa ameze mate mengi.


Jeni alifungua gari akatoa furushi kubwa kwenye kapu kulikuwa na sahan hotipot na jagi kubwa la juice ya matunda .


Jeni aliwapakulia chakula wote na yeye akajipakulia kwenye sahan akatoa glass akamimina juice wote walianza kula.


Wapaangaji walianza kubinua midomo na kusema dula anatumia kizizi sio bure apendwe na wadada wenye pesa zao ,kutwa wanapishana ma magari wakati dula ni masikin tu.basi maneno ya wapangaji yalianza chokochoko.


basi wapangaji walilala mika kuona vyakula vitamu mapochopocho tambi kidogo ,pilau nduzi nyama yaani vilikua vyakula vikinukia hata mimi ninaekula wali kisamvu kila siku nami ningeongea tu.


Wakati dula musa , jeni na nasra wakiendelea kula huku wamekalia gunia


Kwa mbali bibie irene alikua anatembea taratibu kwa maringo mkonon kashika kapu bila shaka alikuwa anaweletea musa chakula maana ndio kawaida yake kila siku hua anapika chakula na kumpelekea musa.


Hatimae irene aliweza kufika kwa akina musa maana anakokaa yeye na kwa akina musa hapana umbali.


Ile irene anafika na kuwasalimia wote dula akainuka ili ampokee kapu la chakula jeni aliinua kichwa ili amtizame nani anasalimia


Gaflaa macho ya jeni na irene yakakutana .kama unavyojua mwez ulopita walikuwa wanagombana kumwongezea damu musa leo tena wamekutana kwa , kila mmoja kampelekea musa chakula


jeni alitupa sahan ya chakula ile anainuka amwangalie irene .

Irene nae ile anampa dula kapu ampokee .


mwili wa irene ulikosa nguvu irene alishuka kama gunia na kudondoka chini puuuu na kuwa kimya .

Irene alipata mshituko baada ya kumwona jeni sijui nini ama hawa wanauhusiano upi

Musa akabaki kaduwaa dula alianza kumpepea irene na kanga ambae alipewa na nasra.

Wakati wote wakishangaa kudondoka kwa irene kuna bibi aliingia akijiburuza na makalio .


kucheki mguu wa yule bibi alikuwa kachomwa na msumari kwenye unyayo na kutokeza hadi juu ya mguu

Yaani damu zilichuruzika mno.

Bibi huyo akiwa amechoka alisema wajukuu zangu nisaidien nakufaa msumari umenichomaa huku akitokwa na machozi.


Watu wote walimwangalia bibi ambae alikua akilia ,

Jeni aliwai kwa yule bibi ili akamsaidie kitendo cha kumsogelea tyuu bibi

Gafla bibi alipotea kwa mazingira ya kutatanisha hakuonekana wala ukitizama hamna bata tone la damu,kilichowashangaza zaidi ni mchana kweupe inawezekana vipi bibi atokee na kupotea,au ndio chanzo irene kuzimia?

Hii story nafanya kwa mashabiki zangu tu kama una 500 njoo whatsap unaipata hadi mwisho

Je nini kitaendelea?

Irene akizinduka itakuwaje?

Huyo bibi vp mchawi?




Gafla akaingia bibi akiwa anajiburuza na makalio mguu ukiwa umejaa damu .

Bibi alikua kachomwa na msumari kwenye unyayo hadi kutokeza kwa juu

Jeni aliwai ili akamsaidie yule bibi ampeleke hospitali ile anataka kumshika,Gafla bibi alipotea jeni nae alipata mshtuko pale pale akadondoka akapoteza fahamu.


Kaka vp mbona sielewi mbona jeni nae kadondoka kuna nini musa alimuuliza dula, wakati dula yuko bize anahangaika kumpepea irene nasra alikua kasimama haelewi chochote na yeye.


Kumbe wakati yule bibi anakuja akijiburuza na makalio ni jeni pekee ndiye aliye mwona wengine hawakuona chochote .


Hakika ni jambo la kutisha musa aliinuka nae akaanza kumpepea jeni hawakuchukua muda sana wote walizinduka na wakawa wako poa .


Ilibidi wakae chin wajadili watafanyeje. Ili waishi kama ndugu wasitengane

dula alimuuliza irene ni kitu kipi kilikufanya paka ukapoteza fahamu

Irene alitoa machozi na kusema kitu alichokishuhudia irene alianza

kuongea "dula unafikiri mie nilimwogopa huyu dada sijui ndio jeni mie sikumwogopa tena nilikuwa nataka nimsalimie ila Nilivyomtizama musa nyuma yake kuna bibi kizee alikua kakaa amejifunga masantula kiunoni huku shingoni kachomwa kisu kimetokeza kwa nyuma pia yule bibi alikua analia kwa uchungu huku damu zikimchuruzika ndio aliyenifanya nikashtuka kwani ninyi hamkumwona?"


Irene alimaliza kuongea na kuwauliza swali nasra waliangaliana na dula kisha kwa pamoja wakasema hawakumwona mtu "musa nae akasema hakumwona huyo bibi"


Alibaki jeni ndio hakujibu jeni aliinuka akageuka kulia kushoto akiwa na hofu kubwa jeni alishidwa kujizuia ikabidi akamshikilie dula huku analia

Hali iliyomfanya dula azidi kuchanganyikiwa jeni alilia huku akimwomba dula ampeleke nyumbani maana alichokiona kina tisha .


Ikabidi dula amtulize jeni ili nae aeleze kuna nini ,jeni alitulia kisha akaanza kusimulia

"dula wakati wewe unamapepea irene kuna kabibi kikogwe kalikuja kametokea nyuma ya hii nyumba kakiwa kanajiburuza na makalio mguuni kamechomwa na msumari yule bibi aliomba tumsaidie cha ajabu nainuka ili nikamsaidie ile nataka kumshika yule bibi akapotea".

story na irene na jeni zinafanana ,kulikoni wao wawili wamwone huyo bibi tu halafu bibi anapotea kuna nini nyuma ya hili jambo? bibi ni nani kwanini anajitokeza kwa jeni na irene? swali ambalo halina majibu tuzidi kusonga mbele na story yetu.


Jeni alisimulia na kumfanya irene ashidwa kuelewa

Musa na nasra wao walikua kimya hawajui kinachoendelea

jeni alivyomaliza kusimulia kisa cha huyo bibi,sijui mzimu dula kuna kitu alikumbuka akacheka na kusema sasa mambo yameiva wakuu walichoniambiaga huenda sasa kinatimia dula alijiongelesha kimoyo moyo kisha akatabasam na kusema nimepata msaidizi sasa .


We dula unawaza nini mbona unatabasam mwenyewe musa alimshtua dula na kumuuliza ivo .

Dula alishtuka na kumwambia musa mdogo wangu hawa wadada wanasimulia ndoto tyu .bibi gani kaja hapa wamwone wao tyu na sisi tusimwone kisha dula alicheka na kumwambia nasra amsubiri kuna mahali anaenda dula aliondoka. jeni alimwita dula ila dula hakutaka kusikiliza mtu.


Dul alikimbia na kuingia uchochoron musa akashidwa kuelewa dula ananini.

jeni alimwaga musa na kumwambia anaogopa kukaa tena hapo atamtafuta siku nyingine wapige story jeni aliwasha gari akaondoka

Sasa akabaki musa na irene walikaa tena kwenye roba .


musa akiwa na mawazo tele irene alianza kumuongelesha musa kwa lugha ya upole mbona leo jeni kaja na mambo ya ajabu yameanza kutokea au jeni nimchawi sielewi mim ,Maana kila jeni ukiwa nae lazima upate matatizo itakuwa jeni sio binadamu wa kawaida anakuchezea akili irene alimwelezea musa na kumwambia.


jeni sio bina damu wa kawaida atakua anatuchezea mchezo nishamshtukia baada ya irene kumaliza kuongea musa alisapoti maneno aliyoyaongea irene.


Na kukumbuka mateso aliyeyapitia lazima jeni amwokoe yawezekana jeni ni jini aliyejivika sura ya binadamu au inakuweje? ,


Wakati mazungumzo yanaendelea cm ya irene iliita alipokea sauti mama yake ilisikika akimwambia aende nyumbani hali yake sio nzuri ,pale pale irene alimwaga musa na kutudi nyumbani.


Alibaki musa peke yake alianza kuwaza mambo mengi nae akaamini jeni atakuwa ni jini tyu haiwezekani kila nikipata mkosi jeni anatokea kunisaidia pia mbona haya mambo kama nishawai kuota halafu nashangaa wao wanasema kuna bibi sijui kachomwa na kisu shingoni mara amechomwa na msumari mguuni usiku hii ndoto niliiota iweje waseme wamemwona huyo bibi??.


Bila shaka jeni atakuwa jini tu musa alijiwazia akakunja roba lake vyema kisha kuingiza ndani chumbani musa alifunga mlango alivua shati na kubaki kifua wazi.


Mgongoni kwa musa kulikua na alama "m' imejichora katikati ya mgongo musa aliwaza na kusema hili geto la ndugu yangu bwana halina hata kioo jana niliota ndoto ya haka kabibi ambacho wanasema eti wamekaona leo

Yule bibi aliniambia nina alama mgongoni imeandikwa "m".


Na haitafutika milele sasa nitaonaje na kuniambia nimefuzu mafunzo ya kupigana sasa mie nilikua najifunzaga wapi ndoto zingine bana ni uongo tu.


Ukweli musa usiku aliota ndoto mbaya sana alitokewa na bibi mwenye sura ya kutisha mara ajitokeze amechomwa na kisu shingoni mara amechomwa na msumari mguuni mara tumbo limepasuka hakika yule bibi alikua anatisha bala neno moja alilomwambia musa ni kwamba kuanzia sasa amefuzu mafuzo ya mapigano asaidie kisasi namba yake ni alama M

Ipo kati kati ya mgongo


Musa alivaa shati akafunga mlango na kwenda saloon moja. Karibu na anakokaa, lengo lake alitaka akaangalie kwenye kama ile ndoto inaukweli ili ajue endapo atakuta alama M

Basi ataamini ile ndoto na kama hataikuta basi itakuwa hio ndoto sio ya ukweli .


Musa alifika saloon aliingia akawasalimia watu aliyewakuta mle , alivua shati kisha akajiangalia kwenye kioo hakuona hio alama 'm'

Musa aliguna na kusema lini ndota ya alfajiri ikawa ya ukweli.


Hamnaga ndoto ya ukweli labda mtu uote umekojoa ukiamka asubui mkojo utaushuhudia musw alijiongelesha mle kwenye saloon kisha akatoka na kuwaacha Watu na maswali watu walihisi musa ni chizi maana kaingia saloon kavua shati kaongea halafu katoka bila kuaga.


Watu walijisemea huyu boy atakuwa kalogwa maana sijamsoma ni maneno aliyeongea kinyoz.

Musa alirudi geto akaingia na kulala hadi saa mbili usiku dulq alikua hajarudi bado.


Tukija maeneo ya kawe beach tunamwona dula amekaa pembezoni mwa bahari aliongea maneno yasiyo julikana

Dula aliaanza kuita jina bibi ! Bibiiii

Bibii dula aliita kwa nguvu


Mala gafla upepo mkali ulivuma kwa kasi sana baharini mawimbi yakawa yanapiga kwa kasi Dula aliendelea kuita bibi!!! bibi !!!!


Mara radi ikabiga paaaa na mngurumo ,Juu upepo ukaongezeka dula akiwa ameangalia Bahari inavyozidi kuchafuka.


Nyuma aliko kaa dula kuna kiumbe cha kutisha sijui kimetokea wapi kilisimama nyuma yake kikiwa kimejifunga shuka jeupee miguu yake ni kwato za punda mdomo meno marefu yametokeza macho mekundu kile kiumbe kilikua kinafuka moshi.


dula akiwa haelewi anaendelea kuita bibi kile kiumbe mikono yake ilikua na kucha ndefu kilinyanyua makucha yake na huyo kiumbe alikaa tayari kuyazamisha mwilin mwa dula.,inawezekana ,kile kiumbe ama bibi aliyewatokea irene na jene ,huenda dula anajua kitu kuusu huyo bibi



dula aliendelea kuita bibi sijui anamwita bibi yupi kile kiumbe kilinyanyua makucha yake kikataka kuyazamisha mwilin mwa dula

Mara dula aligeuka nyuma akamwona yule kiumbe akifuka moshi

dula wala hakushituka alimwambia yule kiumbe mbona wewe umekuja bibi yuko wapi?



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG