Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SIHITAJI KURUDI NILIKOTOKA - 5

   

Simulizi : Sihitaji Kurudi Nilikotoka 

Sehemu Ya Tano (5)


" Anaitwa nani?.

" Jenipha. Anafanya kazi mhimbili ni mganga mkuu, kisha nlipoenda pale nlimkuta mkaka mmoja hivi nae ni mfanya biasha mkubwa wa kusafirisha madini ambae nliambiwa ni mtoto wao mkubwa, akitoka yeye anafata wa kike ila huyo wa kike sikuwahi kumuona, wako wawili tu.

" Mh!, mama naomba unielekeze niende uenda hii familia inamhusu huyu mwanadada.

" Masaki maduka mawili.

" Masaki maduka mawili?.

" Ndio, masaki mwisho kule tulipowahi kwenda kwa mwarabu wa dubai.

"Enhe nshapakumbuka.

" Pale kuna sehemu panaitwa maduka mawili, kuna maduka mawili moja la matunda lengine la vyakula, ukifika hapo tu na bahari unaiona, kuna nyumba nyeupe ya ghorofa mbili bati lekundu linang'aa ndo hiyo hiyo. Au ukifika hapo uliza kwa mzee edwad ni wapi? Utaoneshwa.

" Basi ngoja nsichelewe, nachukua gari dingi akija mwambie dogo kaondoka nalo.

" Atakuchinja shauri yako.

" Hawezi, watoto wake wote mimi ndo nimempa heshima ya kufika chuo, rais wa badae.

" Uwe rais wewe!.

" Haiwezeakani?.

" Machachari wewe.

" Hujui kama siasa lazima uwe mashauzi.?

" Yani hao watakao kupa urais itabidi wapelekwe mochwari watakuwa hawana akili. Alisema ashura kumwambia mwanae wakaachia kicheko, alimjua vizuri alivyo hivyo kumwambia hivyo hakukosea, japo alikuwa mtiifu mwenye huruma ila hakuwa ametulia kufaa kutumikia Taifa.

" Mwanangu wewe kwanza kazi za kuajiriwa zitakuwa kero kwako, wee soma tu elim ikubali uje uwe na kazi zako binafs basi.

" Na kweli mama, ngoja niende basi bayee. Alisema akainuka alipokuwa amekaa na kumsogelea mama yake, alimwachia busu akaenda chumbani kuchukua funguo ya gari, alipokuwa tayari anayo alipita seblen akaaga vya mwisho akaondoka zake, safari yake ilikuwa ni ya moja kwa moja masaki, huku akimuomba Mungu analolifata akute ndilo ili isije akaenda mkombo na kukwama.


Lucky nae njaa ilipomkamata alienda restaurant kula wakina amina wakiwa tayari wako room, alipomaliza alirudi ndani akajitupa kitandani akalala na cm mkononi, ile hali ya kulia kila anapokuwa kitandani haikuwepo tena, mwili kidogo ulichangamka mchango wa maryam ulianza kuonekana. deniss aliendelea kupatiwa matibabu katika chumba cha huduma.


Kipigo toka kwa lucky kilikuwa kikali kwake kilichompatia maumivu kila kona, alijiuliza mara kwa mara afanye nini ili amuombe lucky msamaha yaweze kuisha, alijilaumua nafsi yake kwa nini tamaa zake zimempeleka kubaya kusikostahili.

" Sikutegemea kwa uzuri wa yule mwanamke kama atanipatia majeraha haya?. Mwanamke anapiga utafiri anold haloo!. Ila nimekoma kuwashobokea madem nimekoma deniss nimekoma sirudii tena ng'o, sijui nimuingieje ili nimuombe msamaha, ila kwa namna alivyo kila akiniona kabla hata sijaomba msamaha ananitwanga itawezekana kweli?. Hapana..... alijisemea moyoni mwake.


kwa picha aliyovuta aliona sii rahisi na ataendelea kuchezea kipigo kila atapoonekana nae, kibaya zaid tayari watu waliokuwa wanamueshimu hasa watoto wa kike walishamdharau kwa kipondo alichopatiwa bila hata kujitetea.

" Yani sasa hivi sijui kama kuna mwanamke ntamtongoza hapa chuoni anikubalie, heshima yangu imeisha deniss dah.

Aliamini heshima yake imepungua na itaendelea kupungua kila leo chuoni bora afanye utaratibu awasiliane na wazazi wake wamfanyie uhamisho wa chuo aende chuo chengine.


Lucky akiwa chumbani kwake aliyakumbuka maneno aliyoambiwa na profesa, yalimrudia rudia mara kumi kumi kichwani akaona kitu alichoambiwa ni cha kweli, ili ndoto zake zitimie lazima akubali kulipita burungutu la kinyesi lililoko mbele yake, wapo watu walioandaliwa kuwa changamoto kwake kama deniss na ataendelea kukutana nao, ikiwa anataka kutimiza ndoto zake za kusoma anatakiwa awapite kushoto bila kujali wamefanya nini kwake ili yake yasonge mbele.


Aliinuka kitandani akatoa khanga aliyokuwa nayo mwilini na kuvaa nguo zake za kawaida, alijiangalia kwenye kioo kama yuko sawa, wakina amina kila mmoja alikuwa kitandani kwake ameweka mahedphon masikioni kwa ajili ya kula miziki mizito mizito, alipoona yuko sawa alichukua cm yake kitandani akavaa viatu vya simpo na kutoka nje, alienda hadi kwenye chumba ambacho deniss alikuwa anapatiwa matibabu akiwa yuko katika wakati mgumu wa kufikiria juu ya vipondo viwili alivyopewa ndani ya siku mbili dabo.

Madaktari walishangaa kumuona lucky anaingia kwenye vyumba hivyo, hawakuitaji kumuamini na kumuacha asogee sehemu alipo denis wakihisi uenda ameenda kulianzisha upya, walimzuia lakini akawaomba apite hajenda kishari, walimruhusu akasogea hadi sehemu alipo deniss nyuma yake akifatwa na watu wawili ili akilianzisha wamuwahi, hawakumuamini hata kidogo japo alishawaambia hayuko kishari.


Deniss alipomuona mwili wote ulikufa ganzi akaanza kutetemeka, alijua tayari balaa lishamfikia hadi hospitali akahisi haja kubwa kutaka kumtoka ghafla, kijasho kilimserebuka midomo ikapishana, lucky alifika akakaa kwenye kiti na kumwangalia, alipoona hali yake aliachia tabasam kisha akampatia pole iliyoonekana ya kinafiki.

" Unajisikiaje unapolazwa kwenye kitanda cha matibabu kwa ujinga wako wa kushoboka mwenyewe?. Usipende kuyaingilia maisha ya watu usiowafahamu kijana, sio kila tunda lililong'aa unaweza kulila likakuongezea afya mengine yashaoza ndani japo nje yanang'aa ukila tu mara unapoteza maisha, ukitoka hapa kamshukuru sana profesa kwa sababu ndo amefanikiwa kukuombea msamaha lakini ningekupatia vitasa mpaka hiki chuo ukihame, Bora ukorofishane na mvuta bangi mtumia madawa kuliko kukorofishana na mimi ambae sijawai kutumia hivyo vitu ila akili yangu ni zaid ya watu wanaotumia hivyo vitu. Najua ulinitamani kwa sababu mimi ni mtoto mzuri navutia, jicho jicho tako tako na nna vitu vyote vinavyomfanya mwanaume awe chizi, simaanishi wale wasiokuwa navyo hawampati mtu no, ila asilimia kubwa ya wanaume wanapenda mwanamke wa aina hiyo, kama ungenikuta katika enzi zangu ungenipata, ila sasa hivi umechelewa sana na baada ya kunipata ndo kama hivyo unaambulia kipigo, Sorry brother, lile bifu langu limeisha, ila popote utaponiona, nione kama dada yako au mwanaume mwenzako ambae ukinivulia nguo naweza kukutengeneza kama ambavyo mwanaume mwenzako ukimvulia nguo anavyokutengeneza. Good day and!, Samahani kwa maneno yangu kama nimekuboa, but lile bifu letu limeisha. Usimwone kila msichana mzuri unaweza kuupata mwili wake kuuchezea kwa jeuri ya pesa zako au cheo cha wazazi wako, ukiwa hivyo utaumia kwa sababu kuna wanawake wazuri zaid yangu na wao ni vichaa walivuta bangi kabla ya kutoka kwenye matumbo ya wazazi wao zaidi yangu.




Alisema lucky kisha akanyanyuka na kuondoka zake, Deniss alimshukuru Mungu maana alishahisi utumbo ndani haufanyi kazi, maneno aliyoambiwa aliyakariri na kuitaji kuyafanyia kazi, aliukumbuka msemo wa waswahili MTU HUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA nae alitaka kujifunza kutokana na makosa yake binafs aliyoyafanya japo yamempelekea kuumia.

Alirudi room lucky akafungua mabook kwa ajili ya kusoma, moyo wake ulikuwa na morali wa kupitia masomo kutokana na maneno ya profesa aliyoambiwa, aliwaangalia Amina na tunu akawakuta wako bize na mambo yao, kwenye kidole chake cha pili kutoka mwisho kulikuwa na pete mbili tofauti ambazo huwa hazivui kokote anapokuwa, alikisogeza kidole hicho mdomoni akaibusu pete moja ya kwanza kabisa, aliiangalia ndani ya  dakika moja na nusu mpaka mbili machozi yakaanza kumbubujika.

" Kweli hakuna wa kumuamini katika maisha zaidi ya mama, yeye pekee ndo anaweza kukuonea huruma pindi utaponyanyaswa akikumbuka uchumbu aliopata leba, nakupenda sana mamaangu na chozi lako unalomwaga juu yangu mpaka kesho daima Mungu atalilipa. nakukumbuka natamani nije niukumbatie mwili wako, ila nahisi nna alegi na hiyo nyumba pamoja na watu unaoishi nao, wewe ndo ndugu yangu wa pekee kwenye hii dunia, siku ambayo mumeo ( edwad ). Na mtoto wako wa kiume ( brayan ) watakufa nahisi ndo siku ntayocheka mpaka jino langu la mwisho lionekane, hawakufanya lolote baya ila nahisi kupoteza malengo yangu na kamwe sitothubutu kurudi nlikotoka nkaipoteza tena furaha yako mamaangu.

Alisema lucky moyoni mwake huku machozi yakiendelea kumtoka, ilivyoonesha alikuwa anamchukia sana baba yake na kaka yake brayan kwa kitu kisichojulikana, mwisho aliuapia moyo wake kusikoitaji kurudi alikokuwa kwa ajili ya kuzuia chozi la mama yake jenipha, alitamani kifo cha baba yake na kaka yake kifike ili afurahi ( Haijulikani walimfanyia nini kipindi ambacho alikiita ni cha enzi zake, lakini anawachukia kuliko maelezo )...

Maryam muda huo huo alikuwa anafika masaki maduka mawili alipoelekezwa na mama yake. foleni haikuwepo kubwa alitumia saa moja na nusu pekee kufika, maduka mawili aliyaona lakini nyumba za eneo hilo zilimchanganya sana, kulikuwa kuna vijana wa boda boda wawili watatu eneo alilopo ikabidi ashuke kuuliza, walipomuona tu jinsi uzuri wake ulivyokuwa unavutia walijikuta wanabadili mada na kuanza kumzungumzia yeye, hadi alipowafikia akawasilimia wote wakaitikia.

" Nzuri mrembo uko poa.?

" Yah namshukuru Mungu. Alisema akitoa miwani. Naitwa maryam, samahanini naulizia kwa mzee edwad.

" Unaulizia kwa mzee edwad?. Walishangaa kuona binti anaulizia kwa huyo baba.

" Yah.

" Wee ni mgeni maeneo haya.?

" Ndio ni mgeni.

" Yani huyo mzee anavyojulikana hapa kisha ukiulizia kama hivyo aisee inashangaza sana, si yule mkewe ni daktari mhimbili?.

" Ndo huyo huyo.

" Pita bara bara hii hapa moja kwa moja, unauona ule mnazi mrefu kule mbele?. Alisema kijana mmoja akinyoosha kidole kumuonesha mnazi uliokuwa mbali kidogo mwendo kama wa dakika tano kutoka hapo.

" Yah nimeuona.

" Basi ndo hapo hapo nyumba nyeupe, rangi yake bado mpya imepakwa juzi si unajua matajiri tena, alafu bati lekundu.

" Nawashukuru sana Mungu awabariki.

" Akubariki na wewe pia mama ee.

" Asante. Alisema akafungua wallet yake na kutoa elfu hamsini akawapatia.

" mtanunua japo maji mpoze kiu ya jua.

" Asante mama asante. Walimshukuru akarudi zake kwenye gari.

" Eh!, huyu dada ana roho nzuri kama yeye mwenyewe masikini ya Mungu asante mama. Alisema mwenye boda boda.

" Mnadhani nisingekuwepo mimi mungezipata hizo?.

" Kwa nini tusizipate.

" Dem kaangalia face hii, kaona ameelekezwa na kijana mwenye sura nzuri nini chotara la kipemba ndo maana katoa.

" Toka zako mjinga wee msiiu!, mtoto katoa kwa roho yake nzuri inavyomtuma, angeenda kumpa mbuzi basi maana hata yeye sura anayo, mtoto ana roho nzuri wewe yule sii nyie mna roho kama bamia.

Walizozana wakawagawana pesa na kumuombea dua maryam ili Mungu amuongoze, elfu 50 ilikuwa pesa ndogo sana kwake kutokana na maisha ya kishua aliyonayo ila kwao unga unga hasa kwa maisha ya kibongo ilikuwa pesa ndefu...

Alikanyaga mafuta hadi kwenye mnazi alikoelekezwa, alipoangalia kweli nyumba yenye rangi nyeupe bati lekundu aliiona, alisogea kwenye geti akapiga honi na kutokea kijana mmoja aliekuwa mlinzi wa getini.

" Sorry hapa ndo kwa mzee edwad?. Alifungua kioo cha gari akamuuliza kijana huyo aliefahamika kwa jina la kaiza.

" Yah ndo hapa unamuitaji?. Aliuliza kaiza. Kabla ya kujibu kwenye mlango mdogo getini alitokea mwanamama aliekuwa amevalia dela zito na mtandio mkubwa wa kutupia kichwani.

" Unafanya nini huko nje?. Aliuliza mwana mama huyo.

" Kuna mgeni hapa namsikiliza.

" Nani?.

" Simjui ni mwanamke.

" Rudi ndani ntaongea nae.

Kaiza alirudi ndani mwanamama akatoka nje karibu na gari la maryam.

" Binti unasemaje?. Aliuliza.

" Shikamoo.

" Kabla sijaitikia shikamoo yako nambie unasemaje.

" Samahani mama nlikuwa naulizia kama hapa ndo kwa mzee edwad.

" Unamuuliza kwa ajili ya kufanya nae biashara za umalaya sio?. Hivi binti hamjui kama huyu mzee ana mke na familia inamtegemea?. Kwa kuwa mnajua ana mali hamjali hata umri wake mnajiegesha tu kwake sio ee. Alisema mama huyo kumwambia maryam maneno yalimfanya bi dada ajisikie vibaya sana, hakujua kwa nini ameambiwa hivyo ila moja kwa moja akafahamu kuwa huyo ndo jenipha mwenyewe mke wa mr edwad. Na kwa picha iliyokuwepo ilionesha mzee huyo hajatulia anafanya umalaya wa kupindukia kwa vitoto vidogo ndo maana mama yake akamwambia sii mtu mzuri.

" Mamaangu mimi ni kama mwanao, naomba utumie busara za kiumama kunikaribisha kwako. Sii kila msichana utaemwona ana tabia mbaya za kutembea na mume wa mtu, shida ya kuisaidia familia yako ndo imenifikisha hapa, nna moyo mwepesi wa kumsaidia mtu nnapoona ana matatizo, ila nafika tena kwa tabu kubwa ya kuelekezwa kisha unantukana kama hivyo mamaangu kweli?. Nsamehe bure na sikulaumu kwa sababu najua nini una maanisha, Naitwa Maryam ni mwanafunzi wa chuo kikuu dar es salam, nna kitu muhimu naitaji kukueleza kuhusu Mwanao LUCKY, au wewe sio mama yake?. Alisema maryam na kumfanya jenipha ashtuke, alijikuta sura yake inanywea kwa maneno aliyoongea kumtamkia maryam na kitu anachoambiwa muda huo.

" Lucky?. Aliuliza kwa mshangao.

" Yah lucky.

" Lucky huyu huyu mwanangu precious lucky?. Aliendelea kuuliza kwa mshangao jenipha, macho yalibadilika maryam nae kidogo nae akashangaa, jina la precious ndo kwanza alikuwa analisikia kwake hakuwai kusikia kama lucky anaitwa precious, ilibidi amwitikie tu hivyo hivyo, ndipo mamaa jenipha alimuomba bibie amsamehe kisha akamuitaji kaiza afungue geti kubwa ili gari la maryam lipite ndani, alijua uenda kuna mengi kweli anaitaji kuambiwa kwani mwanae ana siku nyingi sana ajamtia machoni..

Maryam alipita kwenye geti hadi ilipokuwa paking, kulikuwa na magari zaidi ya kumi ya bei mbaya macho yakamtoka, alipaki gari lake akashuka ndani ya mchuma na kuongozana na ma jenipha hadi ilipokuwa seble ndogo ya faragha, alikutana na sura nne tofauti wanaume wawili nmmoja mzee mzee ambae alihisi uenda ndo mzee edwad mwenyewe na mabinti wawili, alikaa kwenye sofa akasalimia jenipha akaenda kwenye friji kumchukulia kinywaji.

Baada ya kumletea alimkaribisha sana akamtambulisha watu walioko mbele yake.

" Binti huyu ndo mr edwad mwenyewe uliemuulizia, huyu ni mwanangu anaitwa brayan, na hawa ni wadogo zangu wananisaidia kazi za ndani kutokana na ubize nlionao.

" Ok nashukuru kuwafahamu, mimi kama nlivyokuambia hapo awali naitwa Maryam natokea mbez beach samaki ila niko chuo kikuu. Huruma yangu ndo imenifikisha hapa, na nimeumia sana uliponambia maneno nsiyoendana nayo kabisa mamaangu. Chuoni nna mwaka mmoja na miezi sasa, katika room nnayokaa bweni nna binti naishi nae, tokea niishi nae simjui baba yake mama yake wala ndugu yake yoyote, nkimuuliza kuhusu familia yake anasema ana mama tu duniani hana ndugu mwengine yoyote, maisha yake yako tofauti sana na wanafunzi wa chuo wote, anaweza kuwa amekaa akaanza kulia ukimuuliza kwa nini anasema tuachane nae, so hicho kitu kimeniumiza sana na nimefanya juu chini kuhakikisha nnamsaidia kwa kutumia pesa au njia nyengine aweze kurudi katika hali ya kawaida baada ya kugundua hayuko sawa. Mimi pekee ndo rafiki yake chuo kizima, Anaitwa Lucky na bicha yake hii hapa sijui kama ndo mwanenu au nimekosea nirudi nyumbani. Alisema maryam watu wote wakiwa wanamsikiliza, alikuwa vizuri katika uongeaji kitu kilichopelekea kila mmoja kupenda ongea yake, mwisho alimpatia jenipha cm yake aangalie picha ya lucky kama ndie mwanae au sie..

Lilipotajwa jina la Lucky mzee edwad na brayan waliangaliana, walionekana kupitisha mshangao wakakaa vizuri kuiona hiyo picha kama ndie au hapana.

Jenipha alipoiona picha tu hapo hapo alitoa macho ya mshangao akaweka mkono mdomoni, machozi yalianza kumtoka kilio cha nguvu nacho kikapisha hodi, alimpatia cm mtu mwengine akaangua kilio kilichomfanya mwanae wa kiume brayan amsogelee na kumuitaji anyamaze. Alimuomba mama yake anyamaze akaishika cm na kuiangalia picha, kweli alikuwa lucky mwenyewe akamuangalia baba yake na kumuambia ndie, Mzee edwad alihisi presha kupanda akapata mshtuko kwa kuambiwa hiyo ndo picha ya mwanae, chozi la kiutu uzima lilimtoka akachukua kitambaa cha kujifutia akajifuta..

" Ina maana mwanangu lucky yuko mzima?. Aliuliza mzee edwad akimwangalia maryam.

" Ndio baba. Alijibu. Mzee edwad nae alianza kugugumia kwa uchungu, alionekana kuumia sana.

" Ooooh my daghter uko wapi mamaa siku zote hizo?. Alisema mzee edwad huku brayan nae machozi yakianza kumtoka..

" Ina maana bado uko hai?. Alisema mzee edwad.

" Mwanangu uko wapi mwanangu. Alisema jenipha akiwa analia.. Mwanangu umenifanyia nini mwanangu rudi mama mama yako nakufa mimi, umeniua mwanangu kwa nini umefanya hivyo jamaniiii Hiiiiiiiiiiiiii hiii hii hiiiiiii, Mwanangu najua ulikufa tukakuzika kabisa kumbe uko hai kwa nini walimwengu wako hivi mama jamaniii, kaburi lako kabisa lipo lucky lipo lipo lipo kumbe uko hai uko wapi kama hujafa mwananguu!!,, yuuuuuu mwanangu mimi, binti niambie ukweli mwanangu yuko wapi nimfatee mimi, nakufa mwana wa marehemu mimi jenipha jamaniii huuuuuuuuu, Ukoo wako wote unajua ulishakufa na kila siku tunaenda kaburini kwako siamini mimi siaminiii hiiiiiiiii hihihihiiiiiii..... alilalamika jenipha kwa kilio cha kupanda na kushuka huku mwanae brayan akimbembeleza aweze kunyamaza. >> STORY HAITOENDELEA KWENYE HII PAGE.... whtsapp contact: 0774320110

** Kwa nini familia inajua lucky amekufa?. NINI kilipelekea hadi kujulikana hivyo wakati LUCKY ni mzima wa afya..

** Kwa nini Lucky anamchukia baba yake na kaka yake wakati wao wanaonesha kumpenda na kumkumbuka kutokana na taarifa za uzima wake walivyozipokea?

** Maryam yupo katika hali gani baada ya kupata hizo data za kugundua Lucky kwao anajulikana alishakufa?.

** Kitu gani kilipelekea hadi lucky kujulikana amekufa wkati yuko mzima?.

** Ikiwa wanajua amekufa kwa nini mzee edwad aliwahi kumpigia cm lucky ikaita kisha kuikata..




" Ooooh my daghter uko wapi mamaa siku zote hizo?. Alisema mzee edwad huku brayan nae machozi yakianza kumtoka..

" Ina maana bado uko hai?. Alisema mzee edwad.

" Mwanangu uko wapi mwanangu. Alisema jenipha akiwa analia.. Mwanangu umenifanyia nini mwanangu rudi mama mama yako nakufa mimi, umeniua mwanangu kwa nini umefanya hivyo jamaniiii Hiiiiiiiiiiiiii hiii hii hiiiiiii, Mwanangu najua ulikufa tukakuzika kabisa kumbe uko hai kwa nini walimwengu wako hivi mama jamaniii, kaburi lako kabisa lipo lucky lipo lipo lipo kumbe uko hai uko wapi kama hujafa mwananguu!!,, yuuuuuu mwanangu mimi, binti niambie ukweli mwanangu yuko wapi nimfatee mimi, nakufa mwana wa marehemu mimi jenipha jamaniii huuuuuuuuu, Ukoo wako wote unajua ulishakufa na kila siku tunaenda kaburini kwako siamini mimi siaminiii hiiiiiiiii hihihihiiiiiii..... alilalamika jenipha kwa kilio cha kupanda na kushuka huku mwanae brayan akimbembeleza aweze kunyamaza.


Songa nayo......


Maryam alikuwa katika kipindi kigumu cha mshangao sana kilichoambatana na maswali yasiyokwisha katika kichwa chake, hakufahamu wapi ashike wapi aache kwa jinsi alivyoona mapokezi ya familia juu ya lucky, alijiuliza inakuwaje wanajua amekufa wakati yuko mzima na kipi hasa kilifanyika hadi kujulikana amefariki.

Akili yake ilichanganyikiwa akashindwa la kufanya, aliona cha muhimu bora aage aondoke zake kuliko kwendelea, jenipha alimzua na kumuitaji waende wote chuo akamuone mwanae, mwaka na masiku kadhaa hajamtia machoni kitu ambacho ni kigumu kwa mzazi yoyote juu ya mtoto wake anaempenda.


" Mama brayan tulia kwanza mke wangu, maamuzi ya haraka sii busara inabidi tumsikilize binti kiundani kwanza ndo tuchukuane ikiwezekana familia kwenda huko. Alisema mzee edwad baada ya kumuona mkewe ana munkari wa hali ya juu wa kwenda kumuona mwanae.

" Naomba unyamaze baba brayan hujui kiasi gani naumia juu ya mwanangu, kila siku naenda kaburini kuweka maua kwa ajili yake kumbe namsulubu tu yuko hai?. Binti naomba twende chuoni nikamuone mwanangu siitaji kusikia chochote, awe mzimu, awe ndo yeye mzima, au copy yake, nataka nikamuone mwanangu, Twende binti. Alisema jenipha.

" Mama chuoni kwa kipindi hiki hairuhusiwi kwenda kuwaona wanafunzi bora nije nae nyumbani. Alisema maryam kwa sauti ya chini, macho yake tayari yalikuwa yanabubujikwa na machozi kwa kile alichokuwa anaendelea kukisikia, kichwa kilizingirwa na swali la kwa nini familia inajua lucky amefariki wakati yuko mzima?.

" Mwanangu naomba twende maprofesa wote wa chuo kikuu mimi wananifahamu hakuna anaeweza kunizuia kuingia. Alisema jenipha.nimesoma pale na mimi miongoni mwa wanafunzi wachache wa miaka ya 80 ambao hawawezi kusahaulika, nguvu zangu ziko pale na nina heshima kubwa kwa hilo usijali.


Maryam alitafakari ndani ya sekunde kadhaa, alijua kwenda na mama huyo bila kumtaarifu lucky yanaweza kuwa matatizo kwa upande wa wake mbali na mambo ya kichuo, alishamuelewa vizuri lucky kwa kipindi kifupi alichounga nae urafiki, aliamini anaweza kuchezea mkong'oto wa nguvu mtu mwenyewe akili ni ziro kichwani, lakini aliona potelea kote hawezi kuona kilio cha mama huyo kinaendelea kutoka juu ya kumuona mwanae kisha akaendelea kumgomea, alimkubalia wakasimama na kuanza kupiga hatua za kutoka jenipha akiwa na nguo za nyumbani bila kubadilisha.

" Mama brayan mbona hutumii akili wee mwanamke rudi kwanza tupange namna ya kwenda. Alisema mzee edwad akionekana kusikokubaliana na uamuzi wa mke wake. Maneno yake yalimfanya jenipha asimame kisha ageuke nyuma, alimwangalia mmewe kwa jicho chungu akamwambia.

" Ikiwa huna uchungu na damu yako ni wewe mwenyewe, miezi kumi na nne sasa nateseka juu ya kifo cha mwanangu, sikuruhusiwa hata kumuona alipofariki na kifo chake kilikuwa cha kutatanisha, nimekuwa wa kushinda makaburini kama mjane nlofiliwa na mume, nliomba kila nlipopata nafasi ya kuomba ikiwezekana afufuke aje aniage, niacheni kama nlivyo mkitaka mtakuja msipotaka bakini lakini mimi naenda. Binti twende. Alisema jenipha wakafungua mlango na kutoka ndani, mzee edwad na mwanae brayan waliangaliana wakakunja nyuso zao.

" Kwa nini hakufa?. Aliuliza mzee edwad.

" Hii ishu atakuwa aliifanya mzee mjunile mwenyewe, kumbuka alisema nguvu ni ndogo inabidi tutoe mali afanye uchunguzi mwengine kwa njia nyengine sijui kama ilikuwa ndani ya mkataba.

" Wapigie vijana waende kummaliza huyu binti kabla ya kufika huko chuoni ikiwezekana wamteke na huyu bibie ( jenipha ) kabisa, itakuwa aibu kubwa sana itayopelekea vifo vyetu ikiwa mikakati yote iliyo siri itajulikana. Alisema mzee edwad.

" Inasikitisha sana baba, siamini kama huyu dogo yuko hai kabisa, kwa sababu mbali na mambo ya mzee mjunile nlimtandika risasi mimi mwenyewe tena ya moyo. Alisema brayan.

" mpigie kijana wa getini aangalie namba za gari kabla haijatoka, wapigie wakina Suma waifatilie na kuikwamisha kabla haijafika chuo, na nadhani itakuwa bora zaidi kama tutaenda kumuulia mbali mzee mjunile.

" Ni kweli kabisa baba. Alisema brayan akipiga namba ya kijana wa getini Kaiza. Baada ya kuita na kupokea alimwambia aziangalie kwa makini namba za gari inayotoka muda huo kisha amwambie, kaiza alifanya alichoambiwa akaangalia gari na kuwapatia namba zake T 253 AH, brayan alikata cm akawapigia vijana wengine waliokuwa vijana wa kazi ili waende kuikwamisha hiyo gari isiweze kufika katika makazi ya chuo kikuu cha dar es salam...


Sebleni walikuwepo wawili tu madada wa kazi na wao walishaenda kwendelea na kazi zao, walichoitaji ikiwa lucky yuko mzima basi kisijulikane chochote kile kilichoko nyuma ya pazia, hata kama ni vita wainzishe wafe wao au wengine lakini kuhakikisha siri iliyopo kati yao na lucky inaendelea kuwa siri na mama mtu hajui chochote kwani kujua kwake kutakuwa ni hatari kwao ambapo wanaweza kufunguliwa mashtaka ya hukumu ya kifo kwa mujibu ya kifungo cha sheria namba 901 cha mwaka 1980.


Maryam na jenipha waliingia kwenye gari mbio mbio na kuianza safari ya kuelekea chuoni, kaiza getini alishangaa sana namna gari lilivyotoka huku bosi wake akionekana kuwa rafu rafu.

" Mmh nna wasi wasi huko ndani kishanuka, na kama kimenuka kibarua changu kimeota nyasi. Ila huyu mama aliharibika kisaikologia tokea kifo cha precious kitokee, inaonekana kuna mambo tayari yako nje nje huko. Alisema baada ya kufungua geti na kufunga.


Gari ya maryam iliyokuwa aina ya prado new model yenye usajili wa namba T 253 AH ilipiga masafa ya mbio kuelekea chuo, huku mzee edwad na mwanae walionekana kuchanganyikiwa sana kwa kilichotokea.

" Inakuwaje huyu mtoto hakufa jamani mbona tutauana kwa presha?. Alisema mzee edwad, tumbo lilikuwa joto, sura ilishakunjamana ikakaa kishari, hakuwa mzee sana alikuwa kwenye miaka 50 kamili, meno aliyatafuna mdomoni kwa hasira akapagawa.

" Mimi naamini mambo yote yataenda sawa tu baba, umepita mwaka sasa hakuna alieweza kuijua hii ishu, cha kufanya hapa inabidi tutumie roho ya paka, huyo binti auawe alieleta hizo taarifa na kuamsha vidonda vilivyopona, mama mambo mawili yamkute, kifo, au tumfanyie kitu kibaya kitachomfanya apoteze kumbu kumbu zote za nyuma. Alisema brayan kumshauri baba yake, mbinu aliyoipanga juu ya mama yake ni kama hakuwa mama yake wa kumzaa, aliona bora afe au apoteze kumbu kumbu kuliko mambo yao kuharibika.

" Umeongea point moja nzuri sana, ndo maana huwa nakuaminia jembe langu sikupoteza mbegu nlipokuzaa kijana una akili sana. Alisema mzee edwad akaendelea kusema. Shika funguo Kachukue vifaa vya moto chumbani kwangu, unichukulie na ile kofia yangu tutoke twende kwa huyu mzee mjunile kwanza akatueleze vizuri. Alisema mzee edwad brayan akainuka kwenye kiti na kwenda hadi chumbani kwa baba yake, alipatiwa funguo ya droo ambayo huwa haigusi mtu yoyote zaid yake, alipofika alifungua akatoa silaha mbili aina ya miguu ya kuku bastola, kisha alifunga akachukua na kofia aliyoambiwa na kurudi sebleni.

Kati ya wafanyakazi wawili wa ndani wote hawakuwa wakijua kinachoendelea, walichokuwa nacho ni cha lucky kuwa hai kitu ambacho na wao kiliendelea kuwaumiza akili, mzee edwad alisimama sebleni akaweka suti yake sawa akavaa na kofia yake ambayo huwa anaitumia katika mambo yake ya siri ili kumficha sura, ilikuwa ndefu kidogo anapoivaa hata ukikutana nae huwezi kumjua mpaka aitoe, yeye na mwanae walitoka wakashuka hadi chini ambako waliingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea kwa mzee ambae ilionekana waliongea nae dil na kwa lilivyoenda wakahisi yeye ndo amefanya usaliti...


Ndani ya mchuma wa prado aliyokuwemo maryam na jenipha hakukuwa na mazungumzo yoyote zaid ya huzuni, Maryam alikuwa kwenye hatari kubwa sana ya kupoteza maisha kwa kuyaingilia maisha ya watu kisa kumsaidia mtu, jenipha machozi yalikuwa yanamtoka maryam hakupata chansi ya kumuuliza chochote, aliendesha gari kwa makini akafanikiwa kufika sheri ambako kuna bara bara ya kwenda katika chuo cha ardhi, mafuta tayari yalipungua ndani ya gari ikabidi apinde aingie sheri, aliweka mafuta ya elfu 50 akakanyaga gia na kwendelea mbele, walitumia dakika tano wakitokea bara bara inayotokea mwenge wakafika kulikokuwa na mataa ya kusimamisha gari na wao ikawabidi wasimame zilikuwepo nyekundu, walikuwa wapindie kushoto waifate bara bara inayoelekea chuo hivyo ilibidi wasubiri taa ya kijani itayoonesha mshale wa kuelekea kushoto kukatiza bara bara ya pili ya kutoka ubungo kwenda mwenge iwake.

" Mama pole sana kwa matatizo yaliyoko mbele yako. Alisema maryam baada ya kusimamisha gari na kumwangalia jenipha huku akipiga jicho juu ya mataa kama yashawaka au laa.

" Asante mwanangu, nimekuwa wa kuteseka kwa kipindi cha mwaka sasa mimi!, nali kila leo, mwanangu maiti yake sikuruhusiwa kuiona zaidi ya mara ya mwisho akiwa hospitalini, na jeraha la risasi ambalo sikujua amelipata kwa nini?. Alisema jenipha akiwa ameegamia kiti, rundiko la machozi likiwa usoni mwake.

" Ina maana lucky aliwahi kupigwa risasi?. Aliuliza swali la mshangao maryam.

" Ndio!, sikujua kwa nini ila uenda ni kwa sababu watu wengi walikuwa hawampendi mwananguuu!, na nlimwambia mimi lucky badilika maamaaa utaniweka kwenye matatizo mama yako lakini hakutaka kusikia, Huuuuuuuuuuu mwanangu mimi jamaniiiii!!.


Alisema jenipha na kipindi hicho hicho taa zikawa zinaruhusu, kitendo cha gari yao kuvuka upande wa pili tu kuna gari nyeusi kubwa iliyokuwa inatokea upande wa bara bara ya ubungo, iliwasababishia ajali ya maksud ambayo ni kama tayari ilidhamiriwa, iligonga kioo cha mbele upande aliko jenipha jenipha akapata mshtuko na kuzimia hapo hapo, maryam alifanya utaratibu wa kuirudisha nyuma gari baada ya kugongwa bila kujali nyuma yake kuna nini, lakini kabla ya kufanya hivyo zilimiminwa risasi za kufa mtu katika gari hilo zikitokea kwenye gari lililosababisha ajali, raia walioliona hilo walianza kutawanyika ovyo ovyo kuingia mafichoni, risasi zilimiminika ndani ya dakika moja kisha gari likawasha mafuta na kuondoka zake, haikuwa vyepesi kujulikana kama kuna aliepona kati ya jenipha na maryam, hata baada ya watu waliosababisha kuondoka raia waliogopa kusogea kitu kilichokuwa hatari zaid kwani hata kama alikuwepo aliepona kati ya wawili hao angekufa muda wowote kwa kucheleweshwa kuwahishwa hospitalini...

Mwisho wa Kitabu Cha kwanza. Fuatilia Kitabu cha Pili


TAMATI


0 comments:

Post a Comment

BLOG