Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

BEDROOM PROFESSIONALS SEHEMU YA 1/10



BEDROOM PROFESSIONALS
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 1 KATI YA 10 MWISHO
*******
 *****
“NGO! NGO! NGO!……NGO! NGO! NGO! NGO!”
“Nani?”
“NGO! NGO! NGO! NGO!”
Mlango wa mbao uliendelea kugongwa na ilionekana nyumba hiyo aliishi mtu asiyejiweza
kabisa,kutokana na picha iliyojionesha.Pembeni juu ya mlango kulikuwa na utando wa buibui na mlango ulikuwa umepauka kupita kiasi, mbali na hapo nyumba hiyo ilikuwa vichochoroni,haikuwezekana hata kidogo kwa binadamu mwenye hadhi yake kuishi ndani ya kijumba hicho ambacho juu kulikuwa kuna bati lililokandamizwa na matofali juu yake.
“Nani anagonga?utanivunjia mlango wangu”
Sauti ya kiume iliyotokea ndani ililalamika, ilionekana alikuwa amezinduka kutoka usingizini sababu sauti ilikuwa ya kukwaruza,hatimaye mlango ukafunguliwa.Katika maisha yake hakuwahi kuiona sura ya mtu aliyekuwa nje,alijaribu kurudisha kumbukumbu zake nyuma lakini hazikumpa jibu sahihi.
“Wewe ndio Issa?”
Lilikuwa ni swali lilioulizwa na mwanaume aliyekuwa nje,kwa harakaharaka alionekana ni mtu mwenye uwezo kifedha,suti nyeusi aliyovaa na tai iliyomkaa vizuri kooni vilidhihirisha yote hayo.Ngozi yake ilikuwa tofauti kabisa,ilikuwa nyeupe ya kung’aa mrefu kiasi kwenda hewani,mkononi alikuwa ameshika begi dogo lenye mikanda.
“Ndiyo,nikusaidie nini?”
Issa akajibu huku akimtizama mwanaume huyu kuanzia juu mpaka chini,alizidi kuvuta kumbukumbu zake akikusanya sura ambazo alishawahi kuziona lakini wapi,kompyuta ya kichwani kwake haikuwahi kuhifadhi sura kama hiyo kabla.Akaweka msuli wake vizuri kiunoni.
“Mimi naitwa Mr.Deo Karekezi.Tunaweza tukaongea?”
“Hakuna shaka pita ndani”
Deo alivyoingia ndani hakuelewa ni wapi akae sababu kulikuwa kuna godoro dogo lililokuwa chini hakuna kiti wala meza,chumba kilikuwa kichafu kupita kiasi sakafuni kuna masufuria ya ukoko licha ya kuona yote hayo hakuonesha dharau yoyote ile.
“Samahani sina kiti ndugu yangu,unaweza ukakaa hapo kitandani”
“Usijali nitasimama,sikai sana.Kilichonileta hapa ni kitu kimoja”
Deo alisema na kuanza kukagua chumba cha mwanaume huyu maskini wa kutupwa,alihisi moyo wake unamuuma ajabu kisha akamtizama Issa machoni aliyekuwa mchafu nywele zake zimejaa vumbi.
“Najua kila kitu kuhusu wewe na Marietha mimi ni mchumba wake,sina uwezo wa kumwambia chochote.Wewe ni mwanaume mwenzangu ndio maana nimekufuata.Kuna kitu nimekuja kukuomba,nakupa pesa hizi naomba uhame huu mji kimnya kimnya bila yeye kujua”
Deo alisema na kufungua begi alilokuwa ameshika mkononi,Moyo wa Issa ulipiga kwa nguvu,ni kweli alimfahamu Marietha nje-ndani sababu alikuwa ni mpenzi wake,isingewezekana hata kidogo kuamini kuwa mwanaume aliyesimama mbele yake anazungumza maneno ya ukweli,akachukulia ni kama uwongo na propaganda za matajiri wanaotaka kuwaachanisha.
“Hapana sitaki kuamini”
“Hutaki kuamini nini?”
“Kuwa una mahusiano na Marietha”
“Okay subiri”
Deo hakutaka kuongea maneno mengine zaidi, ilibidi adhihirishe kuwa maneno yake yalikuwa ni ukweli wala hakuwa ana tania,akatoa simu yake kutoka ndani ya koti la suti na kubonyeza namba fulani kisha kuipa simu ‘ok’ ilivyopokelewa akaweka ‘loudspeaker’
“Halloo Darling”
Ilikuwa ni sauti nyororo kutokea upande wa pili wa simu iliyoenea chumba kizima,Moyo wa Issa ukapiga Paa!hakutaka kuamini bado kuwa aliyepokea simu ni Marietha mwanamke aliyempenda kuliko wanawake wote chini ya jua la Mungu!Bado aliendelea kuamini jambo linalotokea ni ndoto,licha ya kusikia hivyo alikaa kimnya ili kuendelea kusikiliza.
“Marietha Mpenzi wangu,bado upo nyumbani?”
“Yes baby nipo ndio natandika kitanda,nimekumisi sana love.Hope utawahi kurudi leo”
“Ndio Mke wangu,si unajua lazima tupange taratibu za ndoa yetu”
“Ndio baby,ushafika ofisini?”
“Nimefika ndio”
“I love you”
“Mee too!”
Hapohapo simu ikakatwa,hiyo ilikuwa ni kama kudhihirisha kuwa katika maneno aliyoongea Deo Karekezi hakukuwa na punje ya utani hata kidogo ndani yake.
“Najua kuwa Marietha anakujaga hapa kwako,ananidanganya kuwa yupo kwa mama yake analala nawewe ananifanya mimi fala.Tuongee kiuungwana chukuwa pesa hizo milioni ishirini hama huu mji,nakuomba”
Deo alizidi kusisitiza,hakuelewa kuwa akili ya Issa haikuwa hapo, ilisafiri maili mia moja,Issa alihisi moyo wake unamuuma kwa kiasi cha kutosha,hakutaka kuamini kuwa ahadi walizopanga na Marietha zilikuwa ni za uwongo na usanii.
Vitu vingi vilipita ndani ya kichwa chake akakumbuka mambo mengi waliyokuwa wanafanya kitandani na mwanamke huyo Mrembo, Marietha. Ambaye kwake alimpa moyo wake, ingawa alikuwa maskini alijitahidi kufanya kila aliwezalo ampe furaha,aliamini kuwa halikuwa kosa lake bali ni yeye kuzaliwa maskini.Ni kweli hadhi aliyokuwa nayo yeye na urembo wa Marietha vilikuwa ni vitu viwili tofauti kabisa.Aliendelea kuyatafakari mapenzi na kushindwa kuyaelewa sawasawa, maumivu aliyoyasikia kifuani mwake yalikuwa ni zaidi ya msiba.
“Mimi naenda,begi hilo hapo”
Deo hakutaka kupoteza muda akatembea mpaka mlangoni na kuvuta mlango ili atoke nje.
“Broo!”
Issa akaita,Deo akageuza shingo ili kusikiliza wito.
“Pesa zako sizihitaji”
“Una maana gani?”
“Nitahama huu mji lakini tafadhali nenda na pesa zako”
Issa aliongea kishingo upande akijikakamua,moyo wake ulimuuma kupindukia.
“Una uhakika?”
“Ndio”
Deo akainama na kuokota begi lililokuwa lina pesa ndani,akamtizama Issa kwa kama sekunde tano kisha kuondoka zake,gari lake alikuwa ameliacha barabarani stendi ya Tiptop, Manzese.
Alitembea akiwa na mawazo chungumzima na kutoa funguo zake za gari,akafungua mlango na kuingia, akaweka begi kiti cha kushoto na kuwasha gari kwa safari ya kuelekea ofisini kwake, Posta.
***
Kichwa chake kilijawa na mawazo kidogo kupasuka, moyo wake ulimuuma kupindukia,hakuwahi kujua maumivu ya mapenzi yanafananaje siku hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza,alihisi mkuki wa moto umekita kwenye mtima wake.Alimuwaza Marietha muda wote akashindwa kutoka nje.Bila kutegemea alihisi mashavu yake yanalowana,alikuwa akilia bila kujua, kisa mapenzi.
“Griii griiiiii”
Simu yake ndiyo iliyomshtua kutoka katika dimbwi la mawazo,alivyoitoa chini ya mto aligundua Marietha ndiye anapiga.Alitamani kuipokea lakini alishindwa,mkono wake ulikuwa mzito mno.Hakuelewa ni kitu gani amwambie endapo atapokea simu ya mpenzi wake.Nafsi moja ilimwambia ipokee lakini nyingine ilikataa,ilibidi achague jambo moja kati ya hayo mawili,ilionekana nafsi ya pili ilizidi kumsisitiza.Akachukuwa simu yake na kuipokea.
“Halloo”
Issa ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza.
“Issa nimekumisi mpenzi wangu”
Maneno hayo ndiyo yalimchoma zaidi Issa na aliyatafakari ni kama kejeli na unafki.
“Umenimisi mimi?”
“Ndio, kwani vibaya?”
“Sio vibaya”
“Mbona unaongea hivyo?unaumwa?”
“Hapana mafua tu yamenibana”
“Yameanza lini?”
“Jana usiku”
“Jana mbona niliongea nawewe vizuri hukuwa na dali…”
“Marietha”
“Abee mpenzi wangu”
“Unanipenda?”
“Hilo sio la kuniuliza,nakupenda zaidi ya sana wewe unajua hilo”
“Una uhakika?”
“Ndio.Nina uhakika.Ninakupenda Issa,kwanini umeniuliza?Unahisi ninakudanganya?”
“Nilitaka nijue,kwani vibaya?”
“Hapana,upo wapi?Nataka kuja kwako”
“Sipo nyumbani”
“Baby upo wapi?”
“Nipo Mbagala”
“Saa ngapi utakuwa umerudi ili nije?”
“Nitakwambia”
Simu ilivyokatwa ilimuacha Issa njia panda,bado alishindwa kumuelewa mpenzi wake alishindwa kutofautisha tui la nazi na maziwa.
***
Ungebahatika kuonana naye ana kwa ana ungekiri kuwa mwanamke huyu ni mrembo kupita kiasi,hakuwa na kasoro yoyote ile.Kitu kilichomzidishia uzuri wake ni miguu yake minene iliyokuwa na supu,kupanda juu ndiyo usiseme alikuwa na mapaja manene meupe ya kuvutia.
Na mara nyingi alipenda kuvaa sketi fupi ambayo ilivuka juu ya magoti,hiyo ndiyo ikawa tatizo zaidi.
Mungu alimpendelea katika uumbaji wake,akamuwekea udongo mwingi kwa nyuma na pembeni vikafanya ‘hips’ umbo lake likawa kama tarakimu nambari nane. Akampa macho makubwa ya kuvutia,kifua chake kilikuwa kimesimama wima,kifupi alikuwa ni mwanamke mrembo kupindukia,na wengi walisema kuwa hana kasoro yoyote ile.
Licha ya yote hayo kuna kitu kilikuwa kinamsumbua akili yake,mapenzi.

Alitokea kutumbukia na kuwapenda wanaume wawili kwa wakati mmoja jambo ambalo lilikuwa hatari,Marietha alimpenda sana Issa lakini alimpenda pia Deo Karekezi vilevile.Hata leo hii angefumaniwa na kuambiwa amchague mwanamme mmoja angeshindwa kutoa jibu la harakaharaka,alitoka mbali sana na Issa lakini hakuelewa ilikuwaje akanasa kwa Deo mwanaume tajiri ambaye alimpa kila kitu anachohitaji,hakuelewa ni tamaa au mapenzi,alishindwa kutofautisha vitu hivyo viwili,akabaki njia panda!
Alikuwa yupo juu ya kitanda kikubwa amevaa kanga peke yake anatafakari mambo mengi sana,akili yake ilikuwa kwa Issa,akakumbuka vitu vingi sana.Akakumbuka miaka ya nyuma jinsi alivyokingwa, na Issa kupigwa risasi mbili za mgongo akijaribu kuyaokoa maisha yake,kwa maana kuwa bila mwanamme huyo leo hii Marietha angeitwa Marehemu,jambo alilokuwa analifanya aliamini hayupo sahihi kabisa,sawa Issa alikuwa maskini lakini hakustaili kumsaliti.
“Pi piiiiiii”
Honi ya gari ndiyo iliyomshtua kutoka kitandani,alijua tayari Deo amefika.Akaendelea kusikilizia muungurumo wa gari.Akasikia mlango wa seblen unafunguliwa,baada ya dakika mbili mlango wa chumbani ukafunguliwa pia,Deo akaingia.
“Darling….”
Deo aliita kwa furaha na kwenda mpaka kitandani,akamvuta Marietha mdomo wakaanza kunyonyana ndimi.
“Hope ili gauni utalipenda”
Deo alitoa mfuko mkubwa,lilikuwa ni shela kubwa la harusi.Moyo wa Marietha ulipiga kwa nguvu.Bado hakuwa na uhakika na jambo analoenda kulifanya kama lilikuwa sahihi ingawa tayari alikuwa amevalishwa pete ya uchumba,alielewa nini maana ya ndoa kwamba ingekuwa vigumu kuonana na Issa tena.
“Yaah ni zuri,ni zuri sana”
Alijibu Marietha na kupachika tabasamu la plastiki usoni.
“Suti yangu bado sijapata, keshokutwa itakuwa tayari”
Deo alimpenda Marietha sio masihara alitaka awe wake peke yake,ndiyo maana alipeleka mipango ya harusi harakaharaka,kadi zikawa tayari zimesambaa na vikao vilikuwa vimefanyika,kitu kilichokuwa kinasubiriwa ni harusi siku ya tarehe 20 september,

zilikuwa zinahesabika siku kumi na tisa ili Marietha na Deo wawe mwili mmoja yaani mme na mke,kitu ambacho kilizidi kumchanganya Marietha akili na kumuumiza mtima.Alimuangalia Deo machoni akiwa kama ana jambo anataka kumueleza.
“Marietha,are you okay?”(Marietha uko sawa)
Deo aliuliza kwa kimombo ili kuonesha msisitizo na kumuangalia Mkewe mtarajiwa.
“Nipo sawa Darling na…”
Kabla ya Marietha kumalizia anachotaka kuongea ‘lips’ zake zilimezwa ulimi wa Deo ukapita ndani ya kinywa cha Marietha,wote wakafumba macho yao.Damu zao zilianza kwenda kasi.Mkono wa Deo taratibu ukaanza kupita chini akatoa kanga na kuanza kuupitisha kuelekea chini.
“Iss…a st..op”
Marietha akasema kwa sauti ya huba akiwa mbali kihisia.
“Issa ndio nani?”
Deo aliuliza na kusitisha zoezi alilotaka kuendelea kulifanya,akijifanya hamjui mwanaume huyo!



Mwili wa Marietha ulikuwa kitandani lakini akili yake haikuwepo hapo hata kidogo, akiwa katikati ya dimbwi la mapenzi alimtaja Issa bila kutegemea mbaya zaidi akiwa na Deo.
“Nakuuliza Issa ndiyo nani?”
Deo akazidi kusisitizia swali lake akitaka kusikia nini angekijibu Marietha.
“Baby ple..ase end..elea”
Kwa sauti ya puani naya kujilegeza alisema sababu hakuwa na jibu la kumpa Deo kwa wakati huo akamvuta karibu yake na kumnyonya mdomo wakaendelea kupigana mabusu yasiyokuwa na idadi kamili,tendo hilo lilidumu kwa sekunde tatu na Deo akaanza kutoa nguo yake moja baada ya nyingine akabaki kama alivyozaliwa,akaendelea kutomasa kifua cha Marietha taratibu,alivyohakikisha yupo tayari.Akamvuta karibu na kuzama katika sayari nyingine ya huba.
***
Kila alipojaribu kuutuliza moyo wake asimfikirie Marietha alishindwa kabisa,ilikuwa ni vigumu bado kuamini kwamba Marietha amemsaliti na mbaya zaidi anaenda kufunga ndoa na mwanaume mwingine,nyuma ya hayo yote aliamini kuwa kuna nguvu ya pesa.Bado alikuwa yupo kitandani, siku hiyo hakutoka kwenda kuuza mitumba kama anavyofanya siku zote.Jambo hilo liliwatia sana wasiwasi marafiki zake,wakaamua kumzukia nyumbani kwake ili kujua nini kimetokea.
“Issa vipi mshkaji,upo sawa.Sikuoni golini.Au mwenzetu umetusua nini,tuelezane?”
Mmoja wa marafiki zake alimuuliza huku akimuangalia.
“Sio hivyo Chogo”
Hivyo ndivyo walivyozoea kumuita kutokana na kichwa chake kuwa kirefu kwa nyuma mithili ya ndizi Bukoba,jina la Chogo ndilo lililozoeleka ingawa jina halisi aliitwa Salumu.Kwa mara ya kwanza alilichukia lakini hakuwa na ujanja ilibidi akubali.
“Kumbe nini sasa?”
“Tuachane na hayo”
“Embu tuambie,ushamtia demu mimba nini kama mwenzako Dulla”
Bwana Kibwe akadakia mazungumzo.
“Si bora ingekuwa hivyo”
“Nini shida sasa”
“Marietha”
“Marietha kafanya nini?”
Wote walimfahamu mwanamke huyo kama shemeji yao.
“Tuachane na hayo”
“Mbona hatukuelewi,Marietha kafanya nini”
Kwa Issa hakuwa na uhakika kwa jambo aliloambiwa ndiyo maana alisita kufungua kinywa chake na kuzungumza jambo lolote kuhusu Marietha ingawa alihitaji ushauri.
“Issa eeh,mbona unakuwa kama demu,embu tuambie”
Marafiki zake walimsisitiza aseme.
“Marietha anataka kuolewa”
Wote walipigwa na bumbuazi isingekuwa rahisi swala hilo kuwa kweli hata kidogo kwa jinsi walivyomfahamu Marietha, haikuwezekana kabisa kuyaamini maneno ya Issa.Waliendelea kuyatafsiri maneno ya rafiki yao ni uzushi.
“Haiwezekani,mimi nakataa.wewe nani kakwambia kuwa anaolewa?”
“Bwana ake sijui mchumba wake kanifuata hapa kwangu,akaniambia niachane nae”
“Sasa hiyo ndio ina…..”
“Subiri nimalize,Nimemsikia marietha mwenyewe kwa masikio yangu mawili anaongea kwenye simu.Hili swala ni la ukweli sio utani”
“Wewe Issa hujakuwa bado,itakuwa anakupima akili Wallah tena hivi umesahau alivyomchomolea yule mzee siku ile pale tena mbele yako.Issa kama umepata demu mwingine achana nae,utapoteza bahati.Marieth anakupenda”
Ushauri aliokuwa anapewa na maneno aliyoambiwa yalim-badilisha akili kwa asilimia sitini na nane,ni kweli alijilaumu sana kumfikiria Marietha vibaya, akamtupia lawama shetani na kudiriki kusema kuwa anataka kumchonganisha na mwanamke anayempenda,ili kudhihirisha hilo akachukuwa simu yake nokia ya tochi iliyofungwafungwa na mipira na kumtafuta Marietha hewani ingawa ilikuwa ni asubuhi sana.
Simu iliita muda mrefu bila kupokelewa akapiga tena swala likawa hilohilo.
“Hapokei simu”
Issa akawaambia wenzake.
“Sasa hivi saa kumi na mbili kasoro asubuhi,atakuwa amelala.Sasa twenzetu basi golini”
“Poa nakuja,ngoja nipate chai kidogo nyie wenzangu mshakunywa?”
“Bado,ndio tunaenda kwa Mama Hamisi”
“Alafu ananidai buku lake”
“Inuka basi”
Issa alivuta suruali yake na kuvaa akachukua shati na kuliweka mwilini wote wakatoka nje.
Biashara ya kuuza nguo za mitumba katika soko la Manzese darajani ndiyo ilimfanya ale na kuishi,Issa hakuwa na elimu yoyote ile wazazi wake walifariki akiwa mdogo sana,hakubahatika kumuona Mama yake sababu alikufa kipindi anamzaa.Maisha yake yalikuwa yakuunga unga na kutangatanga baba yake alivyofariki akiwa na miaka minne aliamua kukimbilia jijini Dar es salaam kutafuta maisha akitokea mkoani Morogoro,akiwa kama ombaomba. Alivyopata ufahamu akajitumbukiza kwenye biashara za kuuza mboga za majani ili mradi aishi.Hata siku moja hakutaka kujichanganya na makundi mabaya ya wavuta bangi,alichokipata alimshukuru Mungu wake aliye juu Mbinguni akiamini kuwa riziki ni mafungu saba,kwa pesa za kudunduliza akafanikiwa kupata chumba Manzese,akilipishwa shilingi elfu saba kwa mwezi.Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Issa duniani!
***
“Mimi sielewi Prisca,akili yangu haipo hapa kabisa”
“Ipo wapi sasa?”
“Namfikiria sana Issa”
“Una akili wewe,hivi Issa kakupa nini kwa mfano! ngoja nikuulize”
“Ninampenda”
“Usinichekeshe mwenzio na usije ukachekesha kadamnasi,sio bure wewe umerogwa.Embu achana na huyo Issa.Deo anakupenda na jamaa ana pesa,hivi unafikiri mpaka mtu anakutangazia ndoa unadhani ni jambo la mchezo”
“Sasa kama ana pesa ndiyo nini”
“Hee!hujui ndio nini,au mimi nikuoneshe”
“Unioneshe nini?”
“Tuachane na hayo,tufikirie hapa tunafanya nini harusi ndiyo hiyo inakaribia”
“Bado moyo wangu mzito sana,sipo tayari”
Moyo wa Marietha haukuwa tayari kuishi na Deo kama wanandoa, bado alitakiwa alifikirie jambo hilo kabla ya kuchukua maamuzi ya mwisho ingawa kila kitu kilishasukumizwa na Deo alishamlipia mahali ili harusi ifungwe,bado alihisi kumpenda sana Issa hilo lilikuwa wazi kabisa.Alimueleza rafiki yake kila kitu ili ampatie ushauri juu ya kitu gani akifanye,mambo aliyoambiwa hakutaka kuyapa nafasi kabisa.
Hakuna siku ambayo aliyokuwa na wakati mgumu kama hiyo.
“Naelewa unampenda Issa,lakini ushawahi kujiuliza.Atakupeleka wapi?Ana malengo gani nawewe?wakati mwingine inakubidi uchukue maamuzi magumu ili maisha yaendelee”
Bado Prisca alijaribu kumshawishi Marietha amsahau mwanaume huyo maskini ambaye hana mbele wala nyuma,alikuwa upande wa Deo sababu alikuwa ana uwezo kipesa yaani tajiri, hata hivyo aliamini maisha ya Marietha yangekuwa ya raha mustarehe kama angekubali kuolewa na Deo.
“Naomba niende nyumbani kichwa kinaniuma”
“Pia ulifikirie hilo swala Marietha,usije ukanitia aibu”
“Nitajaribu kufikiria”
Marietha alichukuwa mkoba wake juu ya meza,akatoka nje na kuchukua taxi ambayo ilimpeleka mpaka nyumbani kwao Kimara,hata alivyofika aliendelea kuwaza na kuwazua.
“Marietha”
Mama yake mzazi ndiye aliyemuita.
“Abee Mama”
“Upo sawa?”
“Ndi..hapana.Ndio Mama nipo sawa”
Hakuelewa ni jibu gani ampe mama yake ndiyo maana alipata kigugumizi,Marietha alilelewa na mama yake peke yake hakuwahi kumjua baba yake hata siku moja.Mama yake alikuwa zaidi ya rafiki katika maisha yake.
“Marietha embu kaa hapo,najua haupo sawa”
“Ni kweli sipo sawa Mama”
“Una shida gani?”
Hakutaka kumficha mama yake,kila kitu alikiweka wazi kabisa juu ya jambo linalomsumbua huku machozi yakimlenga,Mama alishusha pumzi ndefu ya kuchoka.
“Marietha…”
Mama akaita na kumsogelea mwanaye.
“Abee Mama”
“Hata siku moja huwezi kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja”
Mama Marietha alitumia Kiswahili cha geto, kutokana na kuishi sana mjini kulimfanya ajue mipasho ya kibongo ingawa umri wake ulikuwa umekwenda kiasi.
“Una maana gani Mama?”
“Inabidi uchague kitu kimoja,naomba usinitie aibu.Ulikuja na Deo kunitambulisha wewe mwenyewe nikidhani umeachana na Issa,naomba umalize kile ulichokianza”
“Lakini Ma..”
“Tafadhali Mwanangu,unapenda mimi niendelee kuishi maisha ya shida?Embu tizama Deo alivyotufanyia.Angalia vizuri alivyoijenga hii nyumba”
Hilo lilikuwa wazi kwamba Deo aligharamia na kufanya ukarabati wa nyumba yao ikawa nzuri tena ya kisasa,hiyo ilimpa heshima mno.Pamoja na Mama kumshawishi lakini Marietha bado haikumuingia akilini hata kidogo,alimuwaza Issa hakuelewa itakuwaje siku Issa akigundua yeye ana mahusiano na Mwanaume mwingine tena anataka kufunga,alielewa ni jinsi gani mwanaume huyu alivyokuwa na mapenzi mengi juu yake.Hapohapo akasimama wima!
“Unaenda wapi?”
“Kwa Issa”
“Marietha,Marieth…”
Marietha alifungua mlango na kutoka nje bila kugeuka nyuma ingawa alisikia akiitwa,akatoka nje na kutafuta bajaj,alikuwa bado ana pesa alizopewa na Deo kama za matumizi,hizo ndizo alizotumia kama usafiri.Kwa jambo lililotaka kufanyika, Marietha alitakiwa awe ndani kama mwali ili asubiri siku ya harusi yake lakini yeye hakufanya hivyo,alikuwa akipuyanga na kutapatapa huku na kule.
“Nipeleke Manzese darajani”
“Hapo kumi na tano”
“Poa”
Dereva aliwasha bajaj na safari ikaanza mara moja, bado Marietha alitafakari alikuwa bado yupo njia panda.Dakika arobaini baadaye bajaj ilisimama Manzese darajani, akamlipa dereva ujira wake na kushuka.Kivyovyote vile alijuwa ni lazima Issa atakuwa kwenye goli lake anauza nguo,sababu alijua ratiba zake zote.Jinsi Marietha alivyotembea alifanikiwa kugeuza shingo za wauza mitumba walimuangalia kwa macho ya matamanio na uchu hasa alivyokuwa akitingishika kwa nyuma na kimini alichovaa kilichoonyesha mapaja yake ndiyo kabisa,akapenya penya mpaka katikati ya kibanda kilichojaa nguo nyingi za kike na za kiume.
“Kaka hiyo pedo shilingi ngapi?”
Hakuwa na nia ya kununua sababu mtu aliyemuuliza alikuwa ni mpenzi wake Issa.
“Hiyo ni laki mbili sista”
Issa nayeye akaweka utani wote wakacheka,Marietha alijiona mwenye furaha sana, alikuwa na sababu zaidi ya milioni za kumpenda mwanaume huyu Maskini kama angeulizwa ingawa marafiki zake walimshangaa ni kwanini alikuwa na mahusiano na Issa,walimsema vibaya lakini yeye aliweka masikio pamba ilimradi yupo na Issa,aliamini kuwa hakuna mtu yoyote atakayekuja kuwatenganisha ingawa tayari alikuwa amejiingiza kwenye mahusiano na mwanaume mwingine,aliulaumu sana moyo wake.
“Leo mbona umenishtukiza?”
“Nilitaka nikufumanie na videmu vyako unavyovionga”
“Ha! Haa! Haaa! Haaaa! Haaaaa! Umebugi,hutowahi kunifumania”
“Nina mazungumzo nawewe Issa”
“Oyaaa oyaaaa oyaaaa wewe Chogo,natoka mara moja.Nilindie goli langu”
“Poa!”
Issa aliomba ashikiwe biashara yake akamshika mkono Marietha wakaondoka ili wakaongee.
“Leo sina pesa tungekaa hata pale ili tunywe soda”
“Usijali,twende kwako”
Walitembea wakikatiza vichochoro na kuingia ndani ndani uswazi, ambapo kulikuwa na nyumba mbavu za mbwa,hatimaye wakafika nje ya mlango wa mbao uliokuwa umechoka.Issa akatoa kichuma mfukoni na kutumbukiza ndani ya kitasa,akachokonoa mlango ukafunguka,hakuwa na uwezo wa kununua kitasa kipya kichuma alichokitumia kwake ilikuwa ni kama funguo,wote wakaingia ndani wakafunga mlango.
Marietha alihisi furaha ajabu,kabla ya Issa kukaa vizuri akamvuta karibu yake akatoa ulimi wake akautumbukiza mdomoni mwa Issa, ukapokelewa wakaanza kubadilishana mate,Marietha hakuishia hapo alimsogeza taratibu Issa na kumtupa juu ya godoro akampandia kwa juu na kumtoa shati lake huku akiendelea kumpiga madenda kwa fujo,akili yake ilihama kabisa hata kwa Issa vilevile.Issa hakutaka Mpenzi wake akae juu akambinua akamlaza chali,akavuta sketi fupi aliyovaa akaitupa kando.Marietha akabakiwa na chupi tu,hiyo nayo aliitoa vilevile. Marietha tayari alikuwa taaban hajiwezi tena shingo yake ilinyonywa,Issa akapitisha ncha ya ulimi wake masikioni mwake hiyo ndiyo ikamchanganya zaidi akahisi kama amepigwa na shoti ya umeme tena damu yake imeacha kutembea,alivyoona hivyo aliitoa mwenyewe nguo yake ya juu, akaivua na sidiria akaitupa kando.Kazi ya Issa ikawa ni kukilamba kifua cha Marietha kilichokuwa kimesimama sawa sawia,mkono wake mmoja akaupitisha chini,ulivyofika sehemu ambayo alikuwa akiitafuta akatulia na kuanza kucheza nayo huku akiwa anamnyonya maziwa.
“Ahhh ssssh aaaaash Is…a aaaaah ssshs aaaaah”
Marietha alitoa sauti ya puani bila kutegemea huku akiwa ameyafumba macho yake,raha alizohisi hazikuwa na kipimo chake!
***
Kutokupatikana hewani kwa Marietha kulimchanganya sana akili Deo Karekezi,hakuelewa aibu yake angeificha wapi,siku hiyo usiku aliwaalika wageni ili awatambulishe mkewe mtarajiwa.Bado aliendelea kumtafuta hewani lakini hali ilikuwa ileile.Moyo wake ulimuuma ajabu, akakasirika kupita kiasi.
“Naona kidogo huko alipo kuna foleni nimeongea naye muda mfupi atafika,Mr.Ayambo vipi nikuongeze kinywaji?”
Deo alificha ukweli, akizuga.
“Ongeza kiongozi”
Ndani seblen kwake kulikuwa na wageni wapatao watano,wote walikuwa wafanyabiashara wenzake na nia yao walitaka kumuona shemeji yao mtarajiwa.Mzinga wa konyagi uliwekwa mezani,wakazidi kunywa mvinyo.
Kila Deo alipozidi kunywa pombe ndipo akili yake ilizidi kubadilika,pombe ilianza kuingia damuni na kupenya kichwani akajikuta amepandwa na hasira za ghafla.
“Ndugu zanguni nakuja kidogo,kuna mahali naenda dakika mbili nitakuwa hapa”
“Hakuna shaka Deo,sisi tupo”
“Nashukuru,kama kinywaji kikiisha friji liko pale.Ayambo wewe ni mwenyeji”
Macho ya Deo yalibadilika rangi na kuwa mekundu ghafla, akayabana meno yake kwa hasira,akabeba funguo za gari na kutoka nje ambapo alizama ndani ya gari na kulitia moto,aliligeuza na kupiga honi.Geti likafunguliwa na mlinzi.
Jinsi alivyolitoa gari kwa kasi getini iliogopesha.Katika maisha yake hakupenda dharau na aliamini kivyovyote vile Marietha atakuwa Manzese kwa Issa jioni hiyo.Hakuelewa ni kitu gani amfanye mwanamke huyu anayetaka kumtia aibu mbele ya marafiki zake,picha ya Issa ilivyomjia kichwani jinsi alivyokuwa mchafu alihisi kichefuchefu cha kutapika,isingewezekana hata kidogo kwa mtu kama Issa kuwa na mahusiano na mwanamke mzuri kama Marietha tena kushea tundu moja.Aliendesha gari kwa kasi mpaka alivyofika Manzese darajani na kuliweka kando,akashuka harakaharaka na kuanza kutembea kwa hatua mbilimbili,hakupata picha ni kitu gani akifanye,aliomba Mungu asije kufanya kitu chochote cha kijinga, kwa jinsi alivyokuwa ana hasira alielewa kitu gani kingetokea dakika chache zijazo.
Zilikuwa zimebaki mita kama tano ili aifikie nyumba anayoishi Issa,hapo ndipo hasira zilizidi kumpanda zaidi.Alivyoufikia mlango bila kuuliza aliupiga teke ukavunjika,akazama ndani mzima mzima.Kitu alichokiona ndani kilizidi kumfanya apigwe na butwaa!


Chumba kilikuwa cheupe ndani hakukuwa na mtu ,hiyo ilimfanya Deo ashindwe kuelewa mchumba wake Marietha ni wapi alipo ingawa alijuwa kivyovyote alikuwepo eneo hilo.Ni kweli alikuwa sahihi na alichowaza kilikuwa kweli alizidi kuumia zaidi baada ya kuona saa ya kike chini,ilikuwa saa ya Marietha aliyomnunulia yeye mwenyewe kama zawadi,moyo wake ulimuuma kupita kiasi hakuelewa ni kwa namna gani amuoneshe mapenzi mwanamke huyo ili atulie naye.Hakuwa na uwezo wa kumuacha sababu alimpenda sana aliamini kuwa alifanya makosa kumuoinesha kwamba anampenda sana,kichwa chake kilijawa na msongo wa mawazo hasira zikazidi kumpanda,akainama na kuikota saa iliyokuwa sakafuni na kuiweka mfukoni,akatoka nje na kurudi ndani ya gari kwa safari ya kurudi nyumbani kwake.
Yalikuwa ni mawazo makubwa sana kwa Deo,hakuelewa ni kitu gani akifanye nafsi nyingine ya moyoni mwake ilimwambia kuwa ushirikina ulihusika sababu haikuwezekana hata kidogo kwa Marietha kumng’ang’ania mwanaume maskini kama Issa kiasi hicho ambaye hana mbele wala nyuma.Bila pesa mapenzi hapana, hivyo ndivyo alivyoyatafsiri mapenzi kwa upande wake na jinsi alivyomgharamia Marietha ilitosha kabisa kutulia naye.Alikuwa yupo tayari kutumia nusu ya pesa zake kumkarabati Marietha,kitu kilichomchanganya kingine ni siku ya ndoa yake kukaribia,hata siku moja hakutaka kusikia Marietha anamuacha ingekuwa aibu kubwa sana kwake.
“Pipiiiiiii piiiii”
Honi za gari ndizo zilimshtua akiwa ameshika tama ndani ya gari akiwa Sinza,Shekilango kwenye msongamano wa magari,kichwa chake kilisongwa na mawazo mengi.
“Oyaa kaka vipi?endesha gari unaweka foleni bwana”
Dereva mmoja wa daladala aliropoka baada ya kumpita kwa mbele,Deo alipiga gia na kuzidi kusonga mbele macho yakiwa bado mekundu,hakuelewa ni kitu gani awaambie rafiki zake endapo wangemuuliza kuhusu wapi Marietha alipo,hakuwa na jibu la moja kwa moja la kuwapa.Alipiga honi na kuingiza gari ndani.Deo alirejea nyumbani kwake akiwa na mawazo bado kichwani mwake,alitembea kwa hatua za kobe na kupandisha ngazi za kuingia mlangoni,aliyakodoa macho yake kwa mshtuko baada ya kuona viatu vya Marietha nje ya mlango.Akashindwa kuelewa kama ni kweli macho yake yaliona vizuri au alikuwa yupo ndani ya fikra bado.Akanyonga kitasa na kuzama ndani,ni kweli alikuwa sahihi Marietha alikuwa seblen juu ya sofa na wageni anacheka nao.
“Woow,karibu baby.Ulikuwa wapi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Marietha huku akitabasamu.
“Kuna mtu nilienda kumuona umerudi saa ngapi?”
“Muda sio mrefu”
“Simu yako ilikuwa haipatikani uliniweka roho juu”
“Chaji iliisha”
“Okay”
Deo hakutaka kuuliza kitu kingine zaidi sababu ya wageni waliokuwepo ndiyo maana hakutaka kuonesha kukasirika na kumsaili Marietha,aliwaheshimu na aliwasubiri waondoke ili aanze kutupa maswali,alikuwa na maswali zaidi ya mia moja ya kumuhoji mchumba wake,Marietha.
Pombe ziliendea kunyweka na Marietha aliendelea kuwachangamkia wageni wa Deo hata hivyo baadhi yao aliwafahamu.
“Hivi Mudrick nayeye atakuja kwenye harusi?”
“Huyo ndiye wa kwanza kupata kadi”
“Yupo china si ndio”
“Yupo China yah,atafunga safari atakuja ndivyo alivyoniambia.Kasema hawezi kukosa.Huwezi amini hata Lawrence naye atakuja”
“Sitaki kuamini”
“Sikutaniii”
“Hiyo harusi itakuwa kabambe”
Maongezi ya Deo na wageni waliokuja kumtembelea yalimtia Maritha kichefuchefu.Swala la harusi halikuwepo bado kichwani kwake moyo wake ulikuwa ukipiga kwa nguvu, alimsikitikia sana Deo sababu hakuelewa ndani ya moyo wake kuna nini,aliomba Mungu siku zigande.Alishindwa kuuelewa moyo wake unataka nini kwa wakati huo ingawa ilikuwa ni lazima achague kitu kimoja kati ya vitu hivyo viwili,Mbivu au mbichi.
“Baby naenda chumbani mara moja,jamani naomba nikapumzike tuonana, hapa ni nyumbani kabisa”
Marietha alizungumza akiwa tayari keshasimama wima!
“Sawa,usijali mwali wetu”
“Ha ha ha haaaa,aya”
Marietha alitembea na kunyoosha mpaka chumbani na kujitupa chali kitandani,ilikuwa ni lazima afuate moyo wake unachokitaka ndio atoe maamuzi.Baada ya dakika tano kupita akiwa chumbani alimsikia Deo anaagana na wageni wake kumaanisha kuwa sekunde chache ataingia chumbani,hivyo ndivyo ilivyokuwa hazikupita hata sekunde mbili Deo akafungua mlango wa chumbani na kuingia.
“Unaweza ukaniambia ulikuwa wapi?”
Deo alitupa swali,sura yake ikionesha umakini na hasira kwa mbali.
“Kwa Mama ali…”
“Mio sio mtoto mdogo,Marietha usinifanye mimi mpumbavu sina akili.Nakuuliza tena kwa mara ya pili ulikuwa wapi?”
“Kwa rafiki yangu”
“Wapi?”
“Magomeni”
“Marietha ulikuwa wapi?”
“Si nilishakujibu lakini”
“Huo sio ukweli,nambie ulipokuwa”
“Ni kweli baby,nilikuwa saluni nilipita mara moja kutengeneza kucha”
“Saa yako iko wapi?”
Lilikuwa ni swali lingine kutoka kwa Deo,Marietha alivyotupa macho yake mkononi hakuwa na saa.Akababaika kidogo lakini hakutaka kuonesha swala hilo waziwazi.
“Itakuwa nimeisahau saluni,Mungu wangu”
“Una uhakika?”
“Sina sababu ya kukudanganya”
Deo aliingiza mkono mfukoni mwake na kutoa saa,moyo wa Marietha ulianza kupiga kwa nguvu kwake ilikuwa kama mazingaombwe haikuwezekana hata kidogo kwa Deo kufika Manzese kwa Issa.Aliamini mahusiano yake na Issa yalikuwa ni siri kubwa,hakuelewa kwamba Deo anajuwa kila kitu kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi.Marietha alikuwa nyuma ya kila kitu,alijiona mjanja kumbe Deo ni mjanja zaidi yake.
“Sikiliza nikwambie kitu kimoja Marietha,unajua kuwa mambo unayofanya yamepitwa na wakati.Utajiona mjanja kumbe huna lolote,mimi nimezaliwa Dar es salaam ni muhuni kuliko unavyodhani.Vitu vyote unavyofanya navijua.Najua ulikuwa Manzese kwa baasha ako Issa”
Marietha alihisi kuishiwa nguvu mwilini,akahisi uti wake wa mgongo umepigwa na ubaridi,Mambo aliyokuwa anaongea Deo mbele yake yalikuwa yana ukweli mtupu na hakuelewa mwanaume huyu kayajuaje,akabaki anamwangalia tu.
“Ngoja niwe strait,chagua kimoja mimi au Issa?”
“Sijui”
“Hujui kivipi?”
“Naomba nifikirie”
“Ufikirie?what the hell..Ndoa inakaribia alaf…”
“Deo nimekwambia acha nifikirie”
“Ufikirie nini wakati ndoa wiki ijayo,Marietha tafadhali naomba usije kuniaibisha nakupenda.Watu wengi wamepania hii harusi”
Hakutaka kukumbana na aibu mbeleni endapo Marietha angekataa kufunga naye pingu za maisha hakuelewa ni wapi angeificha sura yake,Deo alitia huruna na kuzidi kumsisitiza mchumba wake waweze kufunga ndoa sababu swala la kumuoa Marietha kwake lilikuwa ni kama ndoto ni lazima itimie!
Usiku mzima aliutumia kumuimbisha ili akubali lakini kwa Marietha alizidi kuomba muda zaidi wa kufikiria,bado moyo wake ulishindwa kuchagua kitu kimoja.
***
“Ndio shemeji,ana mwanaume wake anaishi Manzese anaitwa Issa.Utakuwa unamjua tafadhali niambie ukweli”
“Kusema ukweli shemeji,huyo Issa mimi ninamjua lakini nilidhani wameachana muda mrefu sana,unavyoniambia bado wapo pamoja umenishtua kusema ukweli”
“Ndio hivyo,naomba uongee na rafiki yako.Mwambie jinsi gani ninavyo mpenda”
“Mimi nitajaribu kuzungumza naye”
Deo na Prisca walikuwa Blue pearl Garden,wakijadiliana kuhusu Marietha.Malalamiko yote akayapeleka kwa Prisca, alijisikia aibu sana kuzungumza maswala hayo mbele ya Prisca,kama mwanaume ilibidi ayasuluishe mwenyewe.
“Shika hii utafanya nauli mimi naondoka,make sure unaongea na rafiki yako”
Deo aliongea huku akihesabu kibunda cha noti za elfu kumi,zilivyofika noti kumi yaani laki moja alimkabidhi Prisca.
“Ahsante shemeji,ndoa ipo wewe pigia mstari”
Prisca alishindwa kumtafakari Marietha ni mwanamke wa aina gani sababu alitamani kuwa na mwanaume kama Deo na aliamini duniani wanaume kama hao hadimu kuwapata.
“Marietha karogwa nini”
Prisca alijisemea huku akimsindikiza kwa macho shemeji yake akiwa anaingia ndani ya gari,ghafla akamkumbuka Issa hasira zikamkaba kohoni.Hapohapo akasimama,akatoka nje na kutafuta bajaji.
“Nipeleke Manzese Tiptop”
“Sawa, buku nane hapo tunafanyaga”
“Haina shida”
Siku hiyo Prisca alikuwa amejaa tabia yake ya kushusha bei aliitupa mbali,asingekuwa na laki moja alizopewa na Deo basi asingepanda Bajaj ama angemshusha dereva mpaka elfu nne,Prisca aliijua sana pesa ingawa hakuwa mchaga.
“Twende tuwahi kaka”
Moyoni alipanga kumpaka Issa na kumpa vidonge vyake,aliamini mwanaume huyo ndiye anakwamisha kila kitu.Bajaj ilivyosimama Manzese akamlipa dereva na kuanza kutembea kuelekea katikati sokoni wanapouza nguo za mitumba,bahati nzuri ilikuwa kwake alimuona Issa kwa mbali,alitamani apae ili amfikie mapema, amchambe!
“Enheee,Wewe kinyago cha mpapule”
Bila salamu Prisca alitupa maneno hayo ya kejeli akimuangalia Issa akimpandisha juu mpaka chini,kwa dharau.
“Naongea nawewe kibwengo”
“Prisca vipi tena?”
“Vipi! hujui?Hujui?”
Wateja waliokuwa wanachagua nguo baadhi yao waliacha na kumgeukia Prisca aliyekuwa anatoa lugha za kashfa na kejeli,aliongea huku mikono ikiwa kiunoni.
“Prisca vipi mbona una…”
“Kelele wewe,digidigi.Huna hata haya.Sikia nikwambie achana na Marietha ana mtu wake na kwa taarifa yako anafunga ndoa wiki ijayo,umenisikia wewe kiazi mbatata,nywele zile kama mizizi za bangi.Marietha HAKUTAKI”
Issa alijisikia vibaya ajabu,aibu aliyoipata mbele za watu haikuwa na kipimo chake alihisi kudhalilishwa mno,ilikuwa ni kama amevuliwa nguo na kubaki bila kitu mwilini.Prisca alizidi kumpaka kwa kuropoka ndani ya dakika moja watu walikuwa wamewazunguka.
“Prisca!”
Sauti hiyo ilitokea katikati ya watu wengi waliozunguka duara na haikuwa ngeni masikioni mwa Prisca alivyogeuka hakuamini alivyomuona Marietha,amekunja sura amekasirika kupita kiasi!




“Mimi nimempenda hivyohivyo na umaskini wake,Prisca tueshimiane tena tueshimiane.Naona mazoea yamejenga tabia”
“Marietha unatakiwa kujuwa kuwa wew…”
“Kujua nini?kujua nini?Maisha yangu wewe hayakuhusu,umenielewa?”
“Lakini unapaswa kuelewa kitu kimoja Marietha unachezea bahati,wewe ni mwanamke wa aina gani?Deo anakupenda unakuja huku kuhangaika na huyu maskini,umerogwa au?”
“Iwe nimerogwa au sijarogwa wewe sio swala lako”
“Wewe ni rafiki yangu”
“Kwahiyo?Tena ukome,nampenda Issa,nenda kamwambie Deo simtaki sitaki kumsikia.Na harusi hakuna”
“Lakini Ma…”
“Nimemaliza”
Jinsi Marietha na Prisca walivyokuwa wanapokezana maneno hawakutofautishwa na waigizaji waliomezeshwa maneno jukwaani,walikuwa kama wana ‘act’.Watu wengi walikuwa wamezunguka wanawatizama wanawake hawa wawili,Issa alikuwa kimnya hakuweza kuongea chochote.
“Hapa kuna nini?kuna mwizi nini?”
Ilikuwa ni sauti ya mzee aliyevalia kanzu akimuuliza mwenzake baada ya kuona duara limewekwa na kuna watu katikati,alikuwa na kiu ya kutaka kujua kinachoendelea.
“Unamuona yule jamaa pale aliyevaa vest nyeusi”
“Yule wa kule pembeni?”
“Hapana mzee huyu hapo karibu na yule sista aliyevaa pink”
“Pink ndiyo nini nawewe?embu endelea.Imekuaje?”
“Jamaa anagombaniwa na hao magashi kawagonganisha,sasa hapo wamekutana ndio wamemletea varangati”
Maneno aliyoambiwa Mzee huyu yalikwa ni tofauti kabisa,kila mtu alikuwa na neno lake la kuongea hakuna hata mmoja aliyejuwa nini hasa chanzo cha Issa kutukanwa.
“Aaaah bwana!wale mabinti wanamgombania yule kijana?”
Mzee aliuliza kwa uchu.
“Ndio”
Marietha hakutaka kuendelea kubishana alichofanya ni kumshika mkono Issa na kuwapangua watu, wakaondoka eneo hilo wakimuacha Prisca nyuma anawatizama,alihisi kuumbuka na alishindwa kugeuka na kuwaangalia watu usoni,aliweka sura yake chini na kuanza kupenyapenya katikati ya watu na kuondoka zake,swala alilolifuata halikuzaa matunda.
***
“Samahani mpenzi wangu,alafu naomba nikwambie ukweli najua nimekukosea Issa lakini hii isifanye upunguze mapenzi kwangu”
Marietha alililia msamaha walivyofika chumbani kwa Issa,na aliongea huku machozi yakimlenga machoni alishindwa aanzie wapi kumueleza mpenzi wake mkasa mzima,ilikuwa ni lazima siku hiyo aanike ukweli wote nje.
“Issa naomba unisikilize najua itakuuma lakini naomba ujuwe kuwa nakupenda sana,moyo unaniuma nahisi kujuta”
“Marietha nakupenda pia,usijali nieleze”
“Utanisamehe?”
“Ndio”
Bado moyo wake ulisita kuongea,jambo alilotaka kulitoa moyoni mwake aliamini lingemuumiza Issa mtima na pengine huo ungekuwa mwisho wa mapenzi yao siku hiyohiyo, hata siku moja hakutaka swala hilo litokee ndiyo maana alikuwa akisuwasuwa kuongea,alimtizama Issa machoni kwa kama sekunde mbili na kushusha pumzi ndefu.
“Nina mahusiano na mwanaume mwingine”
Bila chenga maneno ya Marietha yalipenya masikioni mwa Issa na kukita ndani ya moyo wake, yalikuwa ni kama mshale wenye moto ingawa kitu kama hicho alishawahi kukisikia, mbali na hapo alifuatwa na kukanywa aachane na Marietha.
Jinsi alivyokuwa anamuamini Marietha hakudhani hata siku moja kama angekuja kuongea maneno kama hayo mbele yake, ndiyo maana hata alivyofuatwa na Deo alichukulia ni fitna na majungu fulani kutoka kwa mapedeshee wa mjini wanaomuwinda Marietha!
“Marie…”
“Issa naomba unisikilize”
Sura ya Issa ilibadilika ikatia huruma,alihisi uchungu ajabu moyoni.Alivyomtizama Marietha kuanzia juu mpaka chini, alivyojikagua nayeye aliona ni vitu viwili tofauti,Marietha alikuwa ni mwanamke mzuri na mrembo kupita kiasi,yeye alikuwa maskini wa kutupwa.Isingewezekana hata kidogo kwa yeye kusimama kifua mbele na kumtambulisha Marietha kama mpenzi wake watu wasingemuamini.
“Nakupenda,niliteleza nikajikuta nipo na huyu mwanaume.Nipo radhi kufanya chochote kwa ajili yako Issa”
“Kweli unanipenda?”
“Ndiyo maana nipo hapa,sitoenda popote nipo radhi kugombana na mtu yoyote yule kwa ajili yako”
Kidogo maneno ya Marietha yalianza kumpa faraja,haikushia hapo Marietha alimsogelea karibu mpaka mdomoni mwake akatoa ulimi na kuutumbukiza mdomoni mwa Issa wakaanza kulana denda.
Damu zao zilianza kwenda kwa kasi ya ajabu kila mtu alihisi joto ndani ya mwili wake,kitu cha kwanza kukifanya Issa ni kupeleka mkono juu ya kifua cha Marietha sababu hapo ndipo alijua ulipo udhaifu wa mpenzi wake huyo,ni kweli hakukosea Marietha alivyoguswa kifua chake alianza kuhema ndani kwa ndani alihisi kama wadudu wa utitiri wanapita ndani ya damu yake akazidi kumshika Issa akavuta kichwa chake wakazidi kupigana mabusu ya midomoni kwa fujo,Issa alishaelewa tayari nini maana yake, akapitisha mkono wake nyuma na kushusha zipu ya gauni alilokuwa amevaa Marietha,zipu ilivyofika chini akapachua vishikio vya sidiria ikaachia kifua cha Marietha kikawa wazi,bila kupoteza wakati akafakamia chuchu na kuanza kuzinyonya taratibu mno bila papara,Mkono wake mwingine ukawa na kazi ya kutoa gauni, lilivyofika miguuni Marietha nayeye alionesha ushirikiano,akatumia mikono yake kulitoa akaliweka kando,akabakiwa na nguo ya ndani peke yake.
Issa hakuwa na sababu ya kuwa na haraka yoyote ile aliujuwa mwili wa Marietha kuliko njia ya kwenda kijijini kwao Matombo,na aliujulia kupita kiasi, sehemu zote za Marietha ambazo akishikwa anapagawa zote alizifahamu alizijuwa kona zote nyeti,akazidi kunyonya kifua cha Marietha akamfuata shingoni na kuanza kuilamba shingo,kazi ya Marietha ilikuwa ni kujikunja kunja kama jongoo aliyemwagiwa maji,kila kitu kwake kilikuwa burudani akajiona yupo juu angani viumbe hai vyote anaviangalia kwa chini,kazi yake ilikuwa ni kuguna na kutoa mihemo ya ndani kwa ndani bila kujijua.Mwili wake ulishikwa mpaka alivyohisi ndani ya mgodi wake kumelowana hapo ndipo alipomvuta Issa na kuanza kufanya naye tendo ambalo lililowaleta duniani,Marietha alimpenda sana Issa na hakuelewa ni lini wangeachana,hakutamani kuondoka kwa Issa.Walifanya tendo la ndoa na kufurahi.
“Baby naomba taulo nikaoge”
Marietha alikuwa juu ya kifua cha Issa alihisi kuchoka lakini alitaka kujimwagia maji,kutokana na joto majasho yalikuwa yanamtiririka.
“Sawa,lile pale”
Bila kuvaa nguo alisimama kutoka kwenye godoro akatembea mpaka kwenye meza ambapo alichukua taulo na kujifunika kuanzia juu ya maziwa,mapaja yake yote yalikuwa wazi na umbo lake likajichora, jinsi alivyobinuka ki ukweli alitamanisha kupita maelezo yaliyojitosheleza.
“chooni kuna maji?”
“Ndio kopo lipo hapo”
“Sabuni iko wapi?”
“Nimesahau kununua Mungu wangu,iliisha juzi.Kuna mshindi hapo sijui utaweza kuogea”
“Ndio nitatumia kwani sio sabuni”
Marietha alichukuwa kopo na sabuni akatoka nje vilipokuwa vyoo huku nyuma akimuacha Issa akitafakari,alikuwa na mawazo mengi na yalitaka mpaka kupasua kichwa chake.

Marietha alivyotoka bafuni alirudi chumbani na kuanza kujifuta,siku hiyo hakutaka kubanduka alitaka kukesha na mpenzi wake Issa na ikiwezekana alale hapohapo chumbani,kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo moyoni alikuwa yupo radhi kulala hata sakafuni endapo Issa asingekuwa na godoro,alikuwa ameridhia kuishi na mwanaume huyu maskini lakini tajiri wa mapenzi.Issa ndiye mwanaume pekee aliyehisi ndiyo chaguo la Moyo wake aliamini ipo siku moja atafanikiwa kimaisha na kuja kuwa tajiri,watu walimtenga na kumsema sababu ya mwanaume huyo lakini yeye hakujali.Ili mradi ana furaha maishani mwake mengine hakujali.
“Kaoge baby,leo tupike nini love?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Marietha akiuliza kimahaba.
“Kuna mihogo hapa”
“Baby hiyo mihogo itaota mizizi tumboni mwako,kila siku hiyohiyo.Kama sio mihogo Ugali.Leo nataka ule nyama”
“Nyama?!Sina pesa baby”
“Mimi nitanunua,una lingine?labda uniambie kama una aleji nayo”
“Nani?Mimi?wala sina aleji nunua kilo mbili basi”
“Baby..Kilo mbiliiiii?Unakula na nani?una sherehe au?”
“Nina usongo na nyama,sijala siku nyingi”
“Basi naona leo utaharisha,tumbo lako litashtuka”
“Haa! Haaa! Haaa! Haaaa! Haaaa!”
Wote walicheka na kugongesha mikono yao,ilikuwa ni furaha sana kwao.Walihisi furaha sana mioyoni mwao,Marietha alihisi amefika kwa Issa na safari yake ya mapenzi ilikuwa imeishia hapo,Issa ndiyo usiseme hakutaka kabisa kuachana na Marietha hata kama ingetokea wangeachana siku yoyote aliamini kuwa asingeweza kupata mwanamke mwingine kama Marietha,kwake aliijita ni mwenye bahati,kifupi Marietha na Issa walikuwa kama chanda na pete!

Siku hiyo usiku kweli Marietha alienda buchani na kununua nyama na mchele na mapochopocho yote kujumuisha na viungo kama iriki,tangawizi,vitunguu maji,binzali na nyanya.Alipania kumpikia Issa chakula kizito.
“Leo utakula mpaka utoe haja kubwa kitandani”
Marietha aliweka utani wote wakacheka,akatafuta jiko na kuweka mkaa na kuliwasha.Wote walikuwa nje,chakula kilivyoiva wakapakua na kuanza kula.
“Wanasemaga karibu mgeni….”
“Mwenyeji apone”
Marietha akadakia wote wakajawa na furaha,siku hiyo Issa alikula sahani na kuongeza mara tatu.
“Hii kachumbari umeweka nini,mbona tamu hivi.Embu nisogezee bakuli hilo”
“Mwanamke upishi babuu”
Marietha akatoa mipasho ya watu wa mwambao!
“Na mwanaume?”
“Malizia mwenyewe”
Walikula siku hiyo na kusaza kilichobaki walifunikia,Marietha akafagia na kuweka kila kitu sawa akapanda juu ya godoro na kulala.Usingizi haukuja, siku hiyo alitaka kumfaidi Issa kisawasawa hakutaka kumpa nafasi usiku,kwa maana hiyo aliomba mchezo wa kikubwa ufanyike.
Issa hakuwa na hiyana wala hakuonesha uchoyo,alimshughulikia mpenzi wake.
***
Kilichomuamsha Issa asubuhi ni mwangaza ukitokea dirishani kulikuwa kumekucha tayari,alivyopapasa kushoto kwake alipolala Marietha usiku wa jana yake hakukuwa na mtu,akafumbua macho yake na kutupa macho pembeni ilikuwa chai imeandaliwa tayari.
“Baby umeamka!”
Marietha alifungua mlango akiwa na taulo,akiwa na maji bado usoni ilionekana alitoka kuoga.
“Nilijuwa umeondoka”
“Nataka leo tukauze wote nguo,viambie videmu vyako kuwa leo mkeo nipo golini nimekaba”
Marietha aliongea kwa utani huku akijifuta.
“Alafu nikwambie kitu”
Issa alikaa sawa kitandani,ilionekana alikuwa na jambo anataka kuzungumza.
“Nini tena?”
“Juzi nilikuta mlango wangu umevunjwa,nikashindwa kuelewa”
“Mh,unasema ukweli?”
“Ndio”
Kumbukumbu za Marietha zilirudi haraka kinyumenyume kama mkanda wa filamu unavyorudi,akamkumbuka Deo alivyomkabidhi saa yake na kivyovyote aliamini yeye ndiye aliyesababisha hayo yote,japokuwa alikuwa ana jibu la kumpa Issa lakini hakutaka kulitoa aliogopa kumuumiza moyo!
“Baby kunywa chai,tuondoke”
Hatimaye akabadili mada.
“Twende wapi?”
“Kazini,nataka namimi leo niuze nguo”
“Hivi upo siriazi?”
“Sitanii”
Issa akasimama harakaharaka na kuchukuwa taulo ambapo alienda kujimwagia maji na alivyorudi wote walijumuika kunywa chai na kipolo cha wali.

Walikuwa ni kama mme na mke ingawa ndoa yao haikuhalalishwa kanisani ama msikitini.Marietha hakuwa na utani hata kidogo ingawa Issa alidhani wenda anatania, isingewezekana hata kidogo kwa Marietha kukaa naye na kuanza kuuza nguo za mitumba,kichwani kwake alitegemea baada ya muda mchache angeambiwa kuwa ulikuwa ni utani lakini haikuwa hivyo,wote walitoka nje na kuingia katikati ya soko la nguo Manzese, wakafika mpaka kwenye goli la Issa,ambapo walimkuta Chogo tayari yupo kibaruani.
“Naona leo upo na kisura”
Chogo akaweka utani kidogo,Marietha akatabasamu na kutoa salamu.
“Mambo vipi Chogo”
“Shwari tu,oya Issa yule maza alikuja hapa tena.Kaja kurudisha lile shati anadai eti kubwa ala…”
Kabla ya chogo kumalizia chochote alihisi kitu ambacho hakikuwa cha kawaida,kushoto kwake aliona lundo la askari, mbaya zaidi walikuwa wameshika mitutu mikononi mwao wakiwa wamejawa na hasira wakawapangua watu.
Hata Marietha na Issa wote wakatupa macho yao hawakuelewa askari hao wanaelekea wapi mpaka walipoiona sura ya Deo Karekezi nyuma yake akiwa amekasirika kupita kiasi macho yake yakiwa mekundu.Marietha alishaelewa nini maana yake, akasimama mbele ya Issa ili kumkinga.
“Afande,mchukueni ndio huyo hapo”
Kauli hiyo ilitoka kwa Deo na aliyetakiwa kuchukuliwa na polisi ni Issa.
“Deo unataka kufanya nini?”
Marietha alihoji huku akimtizama Deo kwa hasira.
“Marietha kaa kando”
“Nitakaaje kando?kwanini nikae kando?”
“Afande nimesema mchukueni huyo mwizi”
Askari walifanya kazi yao,mmoja wao alivyotaka kumsogelea Issa, Marietha akamzuia.
“Binti,embu tuache tufanye kazi yetu.Hatujaja kucheza ngoma za mdundiko hapa tuna kazi nyingi za kufanya”
“Deo una…”
Kabla ya kufanya lolote askari akamtoa Issa na kumvuta,hakujua ni kosa gani amelifanya.
Askari mmoja akatokea kwa nyuma na kumpiga na kitako cha mtutu usoni,Issa akadondoka chini alivyoinuka akatulizwa na kifuti cha pua.Damu zikaruka kama chemchem, alivyoinua shingo yake juu alikuwa hatamaniki usoni,damu zilimvuja mdomoni na puani kama bomba.Hakukaa sawa akapigwa kifuti kingine cha mbavu,yote hayo Marietha aliyashuhudia lakini hakuweza kufanya lolote sababu alikuwa ameshikiliwa na Deo mikono yake kwa nyuma.Askari walikuwa wametembezewa pesa za kutosha ndiyo maana walifanya kazi ya kumpiga Issa ili kumfurahisha tajiri yao.
“Deo De..o tafadh…ali”
“Nyamaza mpumbavu wewe,nyamaza.Askari chukuwa hiyo takataka”
Deo aliongea kwa hasira huku akitetemeka,kauli hiyo iliwafanya askari wamzoe Issa na kumpiga pingu kwa nyuma,watu walimuhurumia na hawakuelewa nini kosa la mtu huyo,jinsi alivyobebwa hakutofautishwa na jambazi sugu.
Marietha alihisi kuumia moyo,alipiga kelele kwa sauti na kulia machozi lakini hakuna mtu aliyemsikiliza,Deo akamvuta mpaka ndani ya gari lake huku akimshuhudia Issa anapigwa virungu visivyokuwa na idadi kamili!





Ilikuwa ni picha mbaya sana mbele ya macho yake, ni bora asingeshuhudia unyama anaofanyiwa Issa mbele yake,mwanaume anayempenda kuliko kitu chochote kile chini ya jua la Mungu leo hii anamshuhudia akipigwa kama mbwa aliyeiba na kudhalilishwa kupita kiasi,hakuwa na nguvu za kumpiga Deo na kufanya lolote alibaki akilia akiwa ndani ya gari, alivyotaka kufungua mlango wa gari ili atoke nje ilishindikana milango ilipigwa ‘lock’gari ya Deo ilikuwa ya kisasa aina ya Subaru ilikuwa ni lazima yeye mwenyewe afungue kwa nje ama upande wake wa dereva ndiyo mtu aweze kutoka ndani ya gari.
Hiyo ilimfanya Marrietha amwage machozi ya kwikwi!
“Deo la…”
“Shut up,i said shut up..Mpumbavu mkubwa wewe unajua ni kiasi gani nimetumia kugharamia hii ndoa sasa nakwambia hivi,utake usitake harusi itafungwa”
Hata Deo nayeye alikuwa amepandisha Mori,mwili wake ulivulia damu kwa hasira ukawa mwekundu kama ubuyu, anaongea huku anatema chembechembe za mate mithili ya mvua,hakutaka kukabiliana na aibu itakayomkabili mbeleni,ilikuwa ni lazima atumie nguvu ya pesa ili kufanya jambo hilo litokee,alikuwa ni mtu na heshima zake kwa maana hiyo isingewezekana hata kidogo kughairi harusi.Kwa hasira akatoa simu mfukoni na kutafuta namba fulani.
“Halloo,afande kama nilivyowaambia pigeni mpaka muuwe”
“Unasema?”
Siyo kwamba askari hakusikia kauli ya Deo simuni,hakuwa ana uhakika kama alisikia vizuri ama masikio yake yalikuwa yana uchafu.
“Nasema hivi pigeni mpaka afe mimi nitakuja kutoa faini si milioni mbili?nadhani umenisikia”
“Sawa”
Deffender bado zilikuwa mbele yao na nyuma ilikuwa imesimama Subaru ya Deo kumaanisha kuwa Marietha alishuhudia tukio zima,baada ya kauli hiyo kutoka aliona kwa macho yake Issa akishambuliwa na virungu kama mwizi,alizidi kulia machozi ya uchungu.
“Nampenda Issa hata ufanye nini,siko tayari kufunga ndoa nawewe labda ufunge na maiti yangu”
Marietha alijikakamua na kuongea maneno hayo huku macho yake yakiwa yamevimba tayari,hata siku moja hakutaka kuamini kama Deo angekuwa mtu katili kiasi hicho.
Hapohapo gari likageuzwa na kuondoka huku Marietha akiendelea kulia machozi na kumtaja Issa,maumivu aliyoyahisi ndani ya mtima wake yalikuwa ni zaidi ya msiba,hakuwahi kulia kwa hasira kama siku hiyo.Ingawa Marietha alikuwa akilia machozi lakini Deo hakujali, aliendelea kuendesha gari huku akifanya mazungumzo na simu yake,aliendelea kupiga simu akiwaalika watu mbalimbali kwenye harusi yake.
“Ndio ni Mwika Hall Sinza itakuwa,kila kitu kipo sawa ongea na yule mkurugenzi wa Konyagi Mr.Mzava maboxi kama ishirini hivi,hayo yatatosha ndio nishaongea nao..nitakupigia baadaye ngoja nipokee simu nyingine”
Akakata simu na kuchukuwa nyingine kubwa juu ya ‘Dashboard’ alivyoangalia kwenye kioo juu alitabasamu,ilionekana mtu aliyempigia alikuwa ni muhimu sana ikapelekea mpaka kupunguza sauti ya mziki.
“Mr.Dominick nimefurahi kupokea simu yako,sawa ndio.No! No! No! No! No! consider it done boss,kila kitu kipo kwenye mstari.Njoo hata na familia yako itakuwa vizuri sana.Yes naoa,nashukuru sana kwa mchango wako.Okay thank you, bye bye”
Moyo wa Marietha ulizidi kumuuma mno,hakuelewa amuweke kundi gani mwanaume huyu Deo ambaye anapanga vitu ambavyo havielewi,kwa hasira aliyokuwa nayo Marietha isingewezekana hata kidogo kukubali harusi ifungwe,hata angewekewa kisu shingoni asingekubali habadani kufunga ndoa na Deo,kitendo alichokifanya dakika chache zilizopita ndicho kilimfanya hata asifikirie kabisa juu ya ndoa!
“Hiyo harusi unaenda kufunga na nani?”
Marietha aliuliza kwa hasira huku shingo yake ikiwa dirishani hakutaka kumuangalia Deo usoni.
“Nawewe hapo”
“Unajidanganya rafiki yangu”
“Wacha tuone”
Jinsi alivyoongea Deo ilionekana alijiamini sana,sababu aliongea bila wasiwasi wowote ule.Na aliongea kwa ujasiri wa hali ya juu,hiyo ilimfanya Marietha ajiulize maswali mengi kichwani mwake.
***
Virungu alivyopigwa Issa havikuwa na idadi kamili,alipasuka vibaya sana usoni mpaka kichwani.Damu zilimvuja zikafanya mpaka nguo zake zichafuke.Alivyofikishwa kituoni sura yake haikuweza kutambulika ilijaa manundu na jicho lake moja la kushoto lilikuwa limevimba na lingine limevulia damu,hakutofautishwa na nyama iliyotundikwa buchani.
Askari hawakuishia hapo,hata walivyofika kituoni walimkaribisha na virungu.
“Afande chukuwa maelezo ya huyu jambazi.Hawa ndio majambazi tuliokuwa tunawatafuta miaka mingi sana”
Maumivu aliyokuwa anayasikia Issa mwilini hakuweza kuyafananisha na kitu chochote kile,alihisi mwili wake wote unamuuma,hakuweza hata kukunja kidole chake kila kiungo chake cha mwili kilimuuma,hakuamini kwamba kuna binadamu wana roho mbaya kama hiyo,hakuwahi kuiba achilia mbali tabia ya udokozi, kwa akili yake ya ki utu-uzima alielewa kuwa nyuma yake kuna swala la mapenzi na yote hayo ni kwa ajili ya Marietha.
Akiwa chini sakafuni alishtuliwa na kirungu kimoja cha kichwa,kikampasua tena damu zikaruka nyingi na kumwagika chini.Umaskini wake ndiyo ulimfanya aonekane kama takataka ama jambazi.
“Aroo jambazi sugu,simama wima”
Hakuwa ana nguvu za kusimama,angezitoa wapi?wakati alipigwa virungu kila sehemu ya mwili wake,alivyojitahidi kuinuka akadondoka chini.
“Jina lako nani?”
Askari aliyekuwa juu ya meza mapokezi, alimuuliza kwa sauti ya ukali.
“Is…”
Alivyotaka kujaribu kuzungumza alishindwa, mdomo wake ulikuwa mzito kupita kiasi na alihisi maumivu makali.
“Ndiyo nini?tamka kwa sauti..Is ndio nini,unajaribu kuongea kiingereza umetusomesha wewe?”
Yote hayo yalifanyika kituo cha polisi Buguruni,walielewa sana kwa mateso aliyokuwa ameyapata Issa asingethubutu kuzungumza hata neno moja.

Issa hakutofautishwa na mtu aliyejeruhiwa na ajali mbaya ya gari.
“Afande Mkude,peleka huyo ndani”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa,Maaskari walimfuata, jinsi walivyotumia kumpeleka Issa nyuma ya nondo ilitisha zaidi,askari walimburuza kama gunia la mkaa,wakamtupa ndani ya selo na kulipiga kufuli.
“Tulia humo ndani ya mgahawa usubiri pizza na baga”
Askari waliongea na kuanza kucheka ingawa ilikuwa picha mbaya lakini wao waliona ni kama kituko fulani.
*****
“Naomba nitoke nje basi”
“Hapana”
“Kwanini?”
“Bosi kasema usitoke”
“Kisa nini?”
“Mimi sijui”
“Lakini mimi ni mchumba wake”
“Hivyo ndivyo alivyoniambia,amesema kuwa usitoke nje ya geti”
Licha ya kunyang’anywa simu yake asifanye mawasiliano hata kutoka nje ya geti hakuruhusiwa kutoka kabisa,Deo ndiye alikuwa akifanya mambo hayo yote.
Hakutaka Marietha atoke nje ya geti na hivyo ndivyo mlinzi wa getini alivyoachiwa maagizo na alisisitiziwa kuwa endapo ataenda kinyume na matakwa ya tajiri yake basi kibarua chake kingeota nyasi,hakutaka kurudi kijijini kwao maporini Mchambawima akacheze na ngedere,ndiyo maana akakaza uzi na kumuwekea Marietha sura ya kazi.
“Alitoka saa ngapi?”
“Asubuhi sana lakini kasema atawahi kurudi”
“Naomba nisaidie na simu yako”
“Simu?”
“Ndiyo simu yako”
“Hapana,hata hiyo pia nimekatazwa”
Marietha hakutofautishwa na mateka ingawa alikuwa huru kutembea ndani ya nyumba lakini hakuruhusiwa kutoka nje ya geti hiyo ilimuumiza zaidi moyo wake,alitamani kujua hali ya Mpenzi wake Issa inaendeleaje,alielewa kwamba alilala kituo cha polisi hivyo alitaka kujua ni wapi alipo.Hasira zilizidi kumkaba shingoni,alirudi ndani na kuanza kutafakari ni kitu gani akifanye,ghafla akapata wazo kabambe.

Akachungulia dirisha la uwani na kuona ukuta.Hapo ndipo wazo lake aliliunga mkono haraka akazunguka uwani,akaangalia pembeni na kuona matofali,kwa kuwa ukuta ulikuwa mrefu ilikuwa ni lazima aweke matofali ili apande na kuondoka zake.Hakutaka kuishi na Deo mwanaume katili kama huyo,aliinua tofali la kwanza akitumia nguvu na kuliweka karibu kabisa,akachukuwa lingine na kuweka juu yake.
Akajaribu kama yamekaa vizuri ndipo alipopanda juu yake,akashika juu ya ukuta na kujaribu kujivuta kwa juu,ilikuwa tabu kubwa kwa ‘sister doo’ na mrembo kama yeye kuruka ukuta.Katika maisha yake hakuwahi kufanya zoezi hilo na hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kutaka kufanya jaribio hilo la kihuni.Akajaribu kujivuta juu akitumia nguvu,huku akijaribu kusukumiza miguu yake,kitu kilichomfanya atoe mkono wake juu ni baada ya kumuona mjusi kapita mkononi mwake hapo ndipo alipofanya kosa,akateleza na kudondoka puu mpaka chini.Kishindo kikamshtua mlinzi aliyekuwa getini,akakimbia haraka mpaka uwani,alishtuka baada ya kumuona Marietha yupo chini chali amedondoka.
“Hee!”
Mlinzi alishtuka,akamsogelea na kumsimamisha wima.Zoezi la Marietha kutaka kutoroka likaishia hapohapo mjusi akawa amemuharibia jambo hilo.
***
Sio kwamba hakuelewa kwamba Marietha alikasirika,swala hilo alilijua na aliamini isingewezekana hata kidogo kwa mwanamke huyo kukubali ndoa,ilikuwa ni lazima atumie akili nyingine ya ziada.Swala hilo alilifikiria kwa upana zaidi,ni kweli yeye ndiye aliyetoa pesa na kumfanya Issa awekwe ndani,askari walikuwa wanasubiri kauli yake ingawa hata wao walijua wanaenda kinyume na sheria lakini kutokana na kulipwa mishahara midogo ambayo haikukidhi haja zao walikuwa wapo radhi kufanya chochote kitu,pesa iliongea.

Deo alitembeza pesa kituo cha Buguruni na Issa akabambikiwa kesi ya miongoni mwa wezi waliovamia sonara ya muhindi mjini Posta na kuiba dhahabu kumaanisha kuwa ilikuwa ni lazima aende gerezani akafungwe,Deo aliona isingetosha kumuweka mbali na Marietha ilikuwa ni lazima afikirie nje ya boxi.Akiwa ndani ya gari lake ghafla akapata wazo,akatabasamu na kutoa simu yake.
“Naongea na Afande Swedi Shauri?”
“Ndio ndiye mimi kiongozi”
“Hakuna kesi yoyote ya kichwa hapo,huyo mwizi abambikiwe?”
“Kesi ya kichwa.. kesi ya kichwa…ukiwa una maana gani kusema hivyo?sijakuelewa kiongozi”
“Kesi ya mauaji,nataka akaozee jela”
“Kesi hizo zipo za kumwaga zinasubiri watu,wewe tu ongea kikubwa”
Afande Swedi Shauri alizunguka kidogo lakini alimaanisha kitu kidogo lazima kitolewe ili mambo yakae kwenye mstari.
“Usijali,naelewa mkono mtupu haulambwi”
Deo nayeye akachombeza akitumia methali.
“Hapo ndiyo tunakuongea sasa unataka huyu mtu apotee kwenye uso wa dunia au gerezani kifungo cha maisha?”
“Embu nifafanulie”
Deo aliuliza akabadilisha simu akaweka sikio la kulia ili azungushe usukani vizuri alikuwa anaelekea Gongo la Mboto, ulongoni.
“Ngoja nikuibie siri,katiba ya nchi yetu tuna kifungo cha Maisha tofauti na nchi nyingine wao wananyonga.Lakini sisi huku tunauwa kisiri,kama jambazi sugu tunamdunga sindano ya sumu anakufa”
“Hiyo ndiyo nzuri,apigwe tu sindano ya sumu”
“Hilo ondoa shaka,embu tuma kwanza hapo ya Soda nisukutue mdomo”
“Nitakutumia,sasa hivi ninaendesha gari nikitulia nakutumia kwenye simu yako”
“Kazi yako tutaifanya vizuri kabisa,yaani itakuwa kimnya kimnya alafu pia kama una jambo lingine yaani ukisumbuliwa na trafiki yoyote yule wewe ongea namimi moja kwa moja….”
Afande Swedi alivyosikia kuhusu swala la pesa alianza kuongea maongezi marefu.
“Okay kazi njema,nitakutumia huo mzigo kidogo ndani ya dakika kumi na tano”
“Ahsante”
Ilikuwa ni lazima Issa achomwe sindano ya sumu ili afe kama Marietha angekataa kufunga naye ndoa,ilikuwa ni bora wakose wote kuliko kukubali kushindwa.
Deo hakuwa na longolongo alivyopaki gari alitoa simu yake na kumtumia Afande Swedi shilingi laki nne.Hapohapo simu yake ikaita na ilitoka kwa Swedi akimshukuru.
“Ahsante sana,unahitaji huyo mtu afariki lini?”
“Hiyo ni nje ya kazi,ni kama ya soda.Subiri kwanza nitakupa jibu kamili”
“Shukrani”
“Usijali”
Simu ilivyokatwa ilimuacha Deo akishusha pumzi ndefu ya kuchoka.
***
“Ngoja nikwambie kitu kimoja,Maisha ya Issa sasa hivi yapo mikononi mwako”
“Kivipi?”
“Kukataa ndoa nitamuuwa kwa njia moja au nyingine.Na sitanii nipo radhi tukose wote,na unanielewa siwezi kufungwa.Sasa hiyo ni juu yako.Nakupa ruksa nenda kamuone kituoni Buguruni lakini kaa ukijua,maisha yake yapo mikononi mwako mwenyewe,wewe ndiye utakaye muuwa”
Yalikuwa ni maneno ya kutisha yaliyotoka kwa Deo na katika hilo hakuwa ana mzaha hata kidogo ingawa hakutaka kufanya hivyo lakini ilimlazimu sababu moyo wake ulimsukuma.
Alichoka kum-bembeleza Marietha,ilibidi atumie njia nyingine ya kibabe.Hayo ndiyo mambo mawili aliyotakiwa kuchagua Marietha,hakuna siku aliyokuwa katika wakati mgumu kama siku hiyo,hakuelewa achague kipi, KUSUKA AU KUNYOA!



Haikuwa kazi rahisi kuchagua kitu kimoja kati ya vitu viwili alivyoambiwa Marietha,alikuwa bado yupo njia panda na ilikuwa ni lazima achague kitu kimoja sababu haikuwezekana hata kidogo ukanyoa na wakati huohuo ukasuka.Ndiyo maana alikuwa katika wakati mgumu kupita kiasi.Na katika maneno aliyozungumza Deo hakukuwa hata na punje ya utani ndani yake,alimtizama kwa macho ya huruma yaliyolengwa na machozi.
“Nenda kamuone bwana ako huku ukiwa unafikiria cha kufanya,nakukumbusha tu katika maamuzi yako angalia usije ukajutia kwasababu sitanii”
Deo alisisitiza sura yake ikiwa makini ana mtizama Marietha machoni bila kupepesa kope, kumaanisha kitu alichokitoa moyoni alikimaanisha,hiyo ilimfanya Marietha aogope zaidi.
“Una nauli?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Deo Marietha alivyoufikia mlango na kunyonga kitasa lakini hakujibiwa,Marietha aligeuka na kumtizama Deo kwa kama sekunde tano akimtafakari na kumchambua mwanaume huyu,moyo wake ulijaa majuto kwa kujitumbukiza ndani ya shimo refu ambalo haikuwa rahisi kutoka hata kama angeshushiwa ngazi, lawama zote alimtupia shetani kuzimu,mpaka siku hiyo alishindwa kupata jibu la moja kwa moja ni kivipi Deo alimuingia na akajikuta yupo naye kimapenzi,moyo wake ulijaa simanzi akatamani siku zirudi nyuma arekebishe kila kitu kilichotokea lakini haikuwezekana hata kidogo,maji yalishamwagika hakuweza tena kuyazoa.Bila kujibu lolote alitembea mpaka getini.
“Unataka kwenda wapi?”
Mlinzi alitanda getini bado hakupewa ruksa ya Marietha kutoka nje ya geti.
“Embu pisha basi”
Marietha aliongea kwa hasira.
“Mpaka nipate ruksa kutoka kwa bosi ndiyo utoke”
“Nenda kamuulize”
Mlinzi akamtizama Marietha,akachukuwa kufuli kubwa la solex na kulifunga getini ili Marietha asitoke kisha akatembea mpaka kibarazani.
“Bosi ku…”
“Mruhusu atoke”
Deo alisema sauti yake ikitokea ndani dirishani, ilionekana kila kilichotokea nje alishuhudia kupitia dirishani.
Hapohapo geti likafunguliwa na Marietha akatoka nje,alitamani kujua hali ya Issa inaendeleaje huko alipo,aliumia mtima kwa sababu mateso anayopata Issa yeye ndiye aliyesababisha kama asingejiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na Deo wenda mambo yangekuwa tofauti kabisa.Hakutaka kuchelewa ndiyo maana alitafuta pikipiki.
“Kaka angu nipeleke Buguruni”
“Buguruni sehemu gani?”
“Kituo cha polisi,kiasi gani?”
“Buku tano tu,tunaenda.Si pale Buguruni sokoni?”
“Ndio”
“Buku tano hapo,twenzetu”
“Naomba Helment nivae”
Marietha alihofia usalama wake,katika maisha yake aliogopa kupanda usafiri huo wa pikipiki lakini siku hiyo ilimlazimu, alijua ni jinsi gani madereva hao walivyokuwa wazembe barabarani na muda wote wanalewa viroba,ingawa alivaa kofia kichwani kwa usalama lakini moyoni alimuomba Mungu wake afike salama amuone Issa wake,bado alitafakari ni kitu gani amwambie.Alishindwa kuchanganua.

Pikipiki ilianza safari na kuanza kupenya penya katikati ya malori.Mpaka wanafika Buguruni Sokoni kituo cha polisi Buguruni bado Marietha alikuwa ana mawazo chungumzima kichwani kwake,alitaka kwenda kumuona Issa kituoni lakini hakujuwa ni kitu gani amwambie,alielewa mambo atakayomwambia Issa yatamchoma moyo licha ya kufikiria hayo yote alihitaji ushauri.Akavua ‘Helment’ na kumkabidhi dereva ujira wake.Akatembea hatua tano na kupanda ngazi akaingia kituo cha polisi.
“Habari za kazi afande”
Marietha alitoa salamu kwa mmoja wa maaskari aliyekuwa mapokezi,mfupi mnene kiasi.
“Nzuri tu,nikusaidie nini binti?”
“Mimi naitwa Marietha,nimekuja kumuona mtu mmoja anaitwa Issa”
“Umekuja kumuona hapa?”
“Ndio”
“Kuja kumuona hapa kivipi?Mbona sikuelewi embu jaribu kunyoosha maelezo kuna Issa wengi humu ndani”
“Ni muuza Mitumba Manzese,alikamatwa na polisi wakidai kuwa ni mwizi anaitwa Issa Nurdin Mpelembe”
“Umesema unaitwa Marietha?”
“Ndiyo”
“Embu subiri kidogo”
Afande aliyefahamika kwa jina la Bakulibovu alitoa simu mfukoni na kutafuta namba za simu,alivyohakikisha namba zipo juu akapiga,akasubiri kwa kama dakika moja ndipo akaanza maongezi na upande wa pili wa simu.
“Ndio Halloo,habari za majukumu ya ujenzi wa Taifa?…Sisi huku tunamshukuru Allah Ha!Haa!Haaa!Haaa!Haaa!Haaaaa! hapana nyie ndiyo mabosi wetu..Leo sawa nitakuwa frii wapi tukutane?Napafahamu hapo,bia natumia bosi wangu…Sasa kuna binti hapa anamuulizia yule kijana..Yes ni Marietha,okay hakuna shaka.Kazi njema.Hahahahaha.. Ahsante”
Ingawa Marietha hakumsikia mtu wa upande wa pili lakini alijuwa ni lazima simu hiyo alipigiwa Deo,hilo lilikuwa wazi sababu aliyafuatilia maongezi yao mwanzo mpaka mwisho!Simu ilivyokatwa afande Bakulibovu akamtizama.
“Pita hapo,kushoto kwako ukaongee na Issa”
“Ahsante”
Kila alivyopiga hatua moja ndivyo mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu,akafika mpaka kwenye nondo zilizochakaa,kutokana na giza totoro, hakuweza kuona vizuri ndani ya chumba hiko kichafu kinachotoa harufu kali za mikojo na vinyesi.
“Issa…Issa”Aliita!
Tangu aingizwe mahabusu hakula wala kunywa maji,mwili wake ulidhoofika kupita kiasi.Ingawa alikuwa amechakaa kabla lakini alichakaa zaidi,ukurutu na wadudu kama chawa na kunguni waliutafuna mwili wake ukawa na vipelevipele na alipauka kupita kiasi.Kwa mbali alihisi anaitwa,sauti hiyo aliitambua lakini hakuwa ana uhakika alidhani wenda yupo ndani ya njozi,aligeuka kwa uvivu na kumuona Marietha nje ya nondo.
“Mari…etha una..fanya ni.ni hapa?”
Hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza kulitupa Issa akijitahidi kusimama na kujikongoja akimsogelea Marietha ambaye tayari alianza kububujikwa na machozi,alimuonea huruma sana Issa alishindwa kujizuia moyo wake ulimuua mno,akahisi kama mtu ameushika anaukamua kama nguo inavyotolewa ndani ya maji.
“Iss…a naomba uni..”
Marietha aliongea kwa kwikwi akijikaza lakini alishindwa kumalizia sentensi yake akaangua kilio cha sauti kama mtu aliyefiwa na wazazi wake.
“We mwanamke hatupo kwenye mazishi hapa,sasa hivi tutakutoa”
Sauti ya polisi iliyotokea mapokezi ilimfikia Marietha na yeye ndiye alikuwa anaonywa.
“Issa naomb..a unisamehee mpenzi wangu”
“Hauna ha..ja ya kuomba msamaha Marietha”
“Mimi ndiye nimefanya haya yote Issa,naomba unisamehe kwa kukudanganya”
“Nimekusamehe Marietha”
“Kuna ja..mbo nataka ulijuwe”
Kufikia hapo Marietha alikuwa akitafakari ni kwa namna gani amueleze Issa,alikaa kwa muda mrefu akijaribu kutafakari, ilikuwa ni lazima Issa ajuwe kinachoendelea kuhusu harusi ingawa alielewa ni kiasi gani moyo wa Issa utaumia.
“Deo anataka kufunga ndoa namimi,nikikataa atakuuwa”
Marietha hakutaka kuzunguka mbuyu kila kitu alikiweka wazi kilichokuwa ndani ya kifua chake.
Kwa maana hiyo ilimaanisha pesa ilitembea na endapo Marietha angeolewa Issa aliamini kwasababu ya umaskini wake,kama angekuwa tajiri wala asingepigwa kama mwizi.Aliamini kwamba maskini hathaminiki,machozi yalianza kumlenga,vitu vingi vilimuumiza moyo, hata siku moja hakuwahi kuota kwamba ataachana na Marietha wake.
“Marietha,mimi sina tatizo nakutakia maisha mema ya Ndoa,napenda uwe na furaha katika maisha ya…”
“Issa usiseme hivyo ndoa siwezi kufunga na Deo, lakini utatoka”
“Una maana gani?”
“Niachie mimi mpenzi wangu.Siwezi kufunga ndoa na Deo”
Wakati anatamka maneno hayo alikuwa anaongea kwa sauti ya chini ili askari wasisikie,kilichowatenganisha kilikuwa ni nondo zilizopita katikati yao.Marietha akapenyeza ulimi ndani ya mdomo wa Issa wakaanza kupigana mabusu.
“Nina kuhaidi sitofunga ndoa na Deo,nawewe utatoka”
Marietha aliongea kwa kujiamini sababu kichwani mwake alikuwa ana mpango kabambe ilikuwa ni lazima autumie kama mwanamke.

Akatoka nje na kuwaaga askari,wazo la kumtoa Issa kituo cha polisi lilimjia ghafla bin vuu!
Alivyotoka nje alitafuta Bajaj ambayo ilimpeleka mpaka nyumbani kwao ambapo alikuwa anaishi na Mama yake mzazi, alivyofika alijibwaga juu ya kochi,alikuwa hoi bin taaban,mawazo yalimfanya achoke!
“Shikamoo Mama”
“Marahaba.Ulikuwa wapi?”
“Kwa Deo”
“Kwa Deo!?”
Mama aliuliza kwa hamaki.
“Ndio Mama”
“Wakati juzi alikuja hapa usiku akakukosa,akaja asubuhi pia anasema haupo nyumbani.Marietha mbona unataka kuniaibisha Mama yako,mbona hutulii kuna wanawake wanatafuta bahati kama yako.Au umerogwa Mwanangu?”
“Mama sijarogwa,nina akili zangu timamu”
“Sasa mbona unakuwa hivyo?Umesahau Deo alichotufanyia?”
“Naelewa Mama kakujengea nyumba na katoa msaada mkubwa sana kwako”
“Sasa unahitaji nini hapa Duniani?”
“Namuhitaji Issa”
Mama alisonya na kumsogelea binti yake kwenye kochi,ilionekana alichukizwa na kauli hiyo.
“Marietha tafadhali usinitie majaribuni mwanangu”
“Mama ninampenda Issa”
“Hivi hicho unachokiongea unakisikia?”
“Nakisikia Mama”
“Deo keshakutolea mahali”
“Najua”
“Mimi hayo mamilioni ya pesa nitarudisha vipi,vitu alivy…”
“Mama….”
Maongezi ya Mama yake yalionekana kuwa kero kwake,alitegemea kuwa ndiye atakaye mpa faraja lakini mambo yalikuwa kinyume.
Akanyoosha mpaka chumbani kwake akizidi kutafakari njia tofauti za kumtoa Issa kituo cha polisi,kama angekuwa ana pesa angewahonga maaskari wote lakini hakuwa na uwezo wa kumfikia Deo.Alielewa ni jinsi gani mwanaume huyo alivyokuwa mwenye pesa na anayejulikana na watu wengi wakubwa jijini Dar es salaam!
Siku hiyo Marietha alijifananisha na mwanaharakati ama mwanajeshi anayeenda kufanya ukombozi,akaiita operesheni hiyo ‘jeshi la mtu mmoja’.
“Mimi ndiyo jeshi la mtu mmoja,inabidi nifanye hili jambo kabla siku ya harusi haijafika.Eh Mungu naomba uwepo namimi”
Hapohapo alitoa simu yake ndani ya mkoba akatafuta namba za Deo na kumpigia.
“Baby upo wapi?”
Hicho ndicho kitu cha kwanza kukiuliza Marietha.
“Sijatoka popote nipo home kama ulivyoniacha”
“Nipo Kwa Mama anakusalimia sana”
“Kweli!?”
“Ndio”
“Nawewe msalimie pia,ushatoka kituoni?”
“Yah”
“Kwahiyo umeamua nini?”
“Tutakuja kuongea Darling,ila juwa kuwa nakupenda”
“Mama kakubalidili maw…”
“Hapana mimi mwenyewe,ni maamuzi yangu binafsi”
“Vizuri,njoo nakusubiri”
“Okay nakuja”
“Chukuwa taxi nitalipa”
“Okay Darling,Nakupenda sana”
“Mimi pia”
Baada ya simu kukatwa Marietha aliachia msonyo mrefu mno na alikunja sura yake kama mtu aliyelamba ndimu,moyo wake na vitu alivyokuwa anaongea vilikuwa ni vitu viwili tofauti kabisa, kifupi alikuwa akimpaka Deo mafuta kwa mgongo wa chupa!

***
Marietha alichukuwa taxi kama alivyopewa maagizo na alivyofika nje ya geti nyumbani kwa Deo dereva alipewa pesa yake, Marietha akaingia getini,ambapo aliachia tabasamu pana hiyo ilimfanya Deo ashindwe kuelewa kama la ukweli au la bandia,isingewezekana hata kidogo kwa Marietha kuonesha tabasamu kama hilo sababu muda mfupi uliopita walikuwa maadui wakubwa ingawa waliongea.
“Baby”
Marietha akaita kwa kudeka,walivyofika seblen.
“Yes”
“Nakupenda sana”
“Kweli Marietha?”
“Sina sababu ya kukudanganya”
“Na Issa je?”
“Issa achana naye,hivi kwa akili ya kawaida mimi niwe na Issa?Hana mpango hana malengo namimi nahisi kuna dawa alitumia kunipata sio bure”
Deo aliyafurahia maneno ya Marietha na siku hiyo mwanamke huyu aliingia jikoni akapika na kukaangiza nyumba nzima ikanukia,kilivyoiva akaenda seblen na kumkalia Deo juu ya miguu yake.
“Darling chakula tayari”
“Sawa nakuja ngoja nimalizie hii movie”
“Baby bwana aaaah!”
Marietha akatoa sauti ya kudeka huku akiweka sura ya kususa,Deo akasimama na wote kuelekea mezani.
“Baby nikuulize kitu?”
“Uliza”
“Honey moon tutaenda wapi baada ya harusi?”
“Utajua hukohuko,ni suprise”
“Mh Baby”
“Usiwe na wasiwasi”
Siku hiyo walikula na kufurahi na baada ya hapo Marietha alitoa vyombo na kusafisha meza,wote wakaingia chumbani kulala.

Huko Marietha hakutaka kufanya makosa ilikuwa ni lazima ampagawishe Deo kwa njia moja ama nyingine,alimrukia Deo mdomoni wakaanza kunyonyana midomo yao kwa fujo,mkono wa Marietha ukapita chini akatoa mkanda wa Deo akafungua zipu akatoa koki,akasogea kwa chini kidogo akajaza mate mdomoni akatumbukiza koki kinywani mwake,Deo alipagawa kupita kiasi ingawa haikuwa mara yake ya kwanza kufanyiwa utundu kama huo lakini alichizika.Kazi ya Marietha ilikuwa ni kucheza na maiki,ilikuwa ni lazima afanye awezalo ili ambadilishe mawazo Deo,alimkumbuka mwanamke aliyeitwa Delilah kwenye Biblia alivyomdanganya Samson.Kwanini ashindwe? wakati Delila alikuwa mwanamke kama yeye,nguo za Deo zilichojolewa moja baada ya nyingine akabaki kama alivyozaliwa yupo chali,siku hiyo alitaka aumiliki uwanja yeye mwenyewe!Alivyoona koki ya Deo imesimama wima nayeye akatoa nguo zake zote akakaa kwa juu,akawa kama anaendesha farasi,akainama kidogo na kuanza kunyonyana ndimi zao.Mpaka Deo anafika mlima kitonga hakuamini,jasho lilikuwa linamtoka kwa mbali,Marietha akiwa juu Deo chini wote walilala na kupitiwa na usingizi.
***
“Baby”
Asubuhi ya saa mbili kasoro ndipo Marietha alikurupuka usingizini alikuwa ndani ya shuka,Deo alikuwa tayari yupo mbele ya kioo anajiandaa kuelekea kwenye majukumu.
“Yes Darling”
“Nikuombe kitu?”
“Niombe tu mpenzi wangu”
“Nimekubali kuwa nawewe kama mkeo,haina haja ya kuendelea kumtesa Issa.Mwache tu huru aende zake”
Kauli hiyo ilimfanya Deo ageuke na kumtizama Marietha kwa umakini machoni.
“Sikiliza nikwambie unajiongopea,mimi sio mjinga na wala sio fala kama unavyodhani.Huo mpango unaotaka kuufanya ufute katika akili yako”



Kauli ya Deo ilimchosha akili,alihisi mwili wake umepungua uzito akaishiwa pozi.Mipango yake ya kutaka kumkomboa Issa kwa njia ya kumlaghai Deo iligonga mwamba na wala haikuzaa matunda kabisa,alimtizama Deo kwa macho ya kujiuliza maswali.
“Nisikilize nikwambie Marietha”
Deo alisitisha zoezi la kuvaa koti la suti akamsogelea Marietha kitandani na kukaa kitako.
“Jua kuwa nakupenda sana wivu ndiyo unanipelekea mpaka nafanya haya yote.Hata siku moja sitokubali mtu yoyote yule akuchukuwe”
“Ndio umtese binadamu mwenzako?”
“Sikutaka kufika huko lakini imenibidi Marietha.You forced my hands,nakupenda ndiyo maana nataka kufunga ndoa nawewe”
“Siwezi Deo,siwezi kuishi nawewe nampenda sana Issa.Tafadhali naomba umuache huru”
“No,tunarudi kulekule kama ukihitaji nimuachie huru basi kubali kuolewa namimi”
Huo ndiyo ulikuwa msimamo wa Deo,Marietha alimjuwa Deo likija katika swala la kuamua jambo, haikuwa rahisi kupindisha msimamo wake hata uwe nani,hivyo ndivyo ilivyokuwa,Marietha akashusha pumzi ndefu na kutoelewa ni kitu gani akifanye.Bado aliendelea kusuka mikakati mingi ndani ya kichwa chake baada ya mpango wake wa kwanza kuharibika.Kila alipojaribu kufikiria njia gani aitumie alishindwa kabisa!
“Nitakuona baadaye,leo kuna wageni wangu wanaweza wakaja hapa nyumbani”
Deo aliacha maagizo na kufungua mlango akatoka zake nje akimuacha Marietha kitandani akiwa katika msongo wa mawazo,kichwa chake kilimfikiria Issa na wala sio ndoa.
Picha ya Issa alivyokuwa kituo cha polisi ghafla ikamjia kichwani akamuona alivyochakaa akiwa anateseka mno,alifikiria vitu chungumzima kuhusu maisha yake.Hapohapo akapata wazo akachukuwa mswaki akaingia nao bafuni,ambapo alivyotoka akawa tayari amaeoga na kuanza kujifuta maji mwilini,alimuwaza rafiki yake wa karibu Dorica na alitaka kumfuata nyumbani kwake ili ampe walau ushauri wa mambo yanayomkabili mbele yake,Marietha alihitaji mtu wa karibu wa kumshauri.

Alivaa gauni lake fupi kama kawaida,hakujali kuwa alitakiwa kukaa ndani kama mwali na kusubiria harusi yake baada ya siku tisa.Alivyotoka nje alitafuta taxi,ikampeleka mpaka Posta,Kivukoni.
Huko akapakia Pantoni akavuka mpaka upande wa pili ambapo alitembea na kutafuta daladala za Mji mwema,safari yake ilikuwa ndefu kiasi.Alivyofika kituo cha mwisho akashuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kama mita kumi na saba,ndipo alipoifikia nyumba ndogo kiasi iliyozungushiwa ukuta, yenye geti la rangi ya kijivu,akagonga.
Baada ya sekunde tatu akahisi kuna mtu anafungua mlango anatembea usawa wa geti akatulia.
“Heee!Marietha!”
Dorika alimshangaa Marietha getini,alikuwa ni mwanamke wa kidigo mfupi mnene, mbali na hapo walikuwa marafiki wa kushibana ingawa hawakuwahi kuwasiliana kwa muda wa takribani miaka mitatu ndiyo maana Dorika akashtuka kidogo.
“Dorika jamani”
“Ulipotelea wapi Shosti?”
Wote walikumbatiana na walionesha furaha kwenye nyuso zao,sio Marietha wala Dorika wote walifurahi kuonana.
“Ingia ndani”
“Ahsante mwaya”
Wote waliingia ndani,Dorika alimkaribisha swaiba wake na juisi ya baridi ya maembe ili apooze koo.
“Shosti,siku nyingi sana.Umezidi kuwa mweupe unakula nini Marietha?Umenenepa mpaka raha”
“Wala sili kitu chochote,nina mawazo sana”
“Sio kweli,mawazo ndiyo unenepe kiasi hicho shoga angu”
“Nakwambia ukweli wewe unadhani nini kimenileta hapa,nina matatizo makubwa sana.Nipo katika wakati mgumu”
“Tatizo nini?”
“Ninaolewa wiki ijayo”
“Unaolewa?mbona kimnyakimnya hivyo?ndiyo uwe na mawazo?nani anakuoa Issa?”
“Hapana”
“Kumbe nani?”
Marietha aliinamisha kichwa chake chini kidogo,Dorika hakuelewa lolote lile ilibidi awekwe wazi kwa kila kitu sababu alihitajika kiushauri,Marietha hakuweza kuamuwa jambo lililokuwa mbele yake pasipo kumshirikisha mtu.
“Marietha…”
“Abee”
“Kuna nini?”
Kuna kitu alijifunza machoni mwa rafiki yake ambacho hakikuwa cha kawaida,akamsogelea karibu ili kujua.
“Marietha,Marietha”
Dorika aliita kwa sauti ya chini,akazidi kumsogelea rafiki yake karibu zaidi.
“Sio Issa,Issa amefungwa. Na nikikataa kuolewa atauliw..a”
Kilichofuata hapo ni kilio kwa kwenda mbele,Marietha alilia kwa uchungu ilikuwa ni kama ametoneshwa kidonda moyoni,jinsi mambo yalivyokuwa yanamtokea hakujitofautisha na Krishna Kapoor ndani ya filamu za kihindi.
Kwa kwikwi na mafua alianza kumuhadithia mkanda mzima ulivyokuwa mpaka Issa akafungwa,akahitimisha kuwa anampenda sana.
“Usilie Marietha,sogea hapa”
Historia ya Marietha ilimuacha Dorika kinywa wazi,akamvuta karibu na kumkumbatia ili kum-bembeleza.
“Ndi..o hi..vyo nifanye nini Dor..ika?nahitaji ush..auri wako”
“Una uhakika kuwa sijui huyo Deo ndiyo kamfunga Issa?”
“Ndiyo,mbele ya macho ya…ngu”
“Mhh!”
Dorika akaguna kidogo,swala la Marietha lilimchosha akili akashindwa kutoa jibu la harakaharaka.
“swala hili umeliripoti polisi?”
“Naogopa”
“Sasa unaogopa nini?waambie ukweli tafuta mwanasheria”
“Hapana Dorika naogopa kufanya hivyo”
“Mimi ndio ninakushauri hivyo kama unaogopa mimi nitakusaidia,au haupo tayari?”
“Nipo tayari nahitaji Issa awe huru”
“Embu subiri kidogo,Mume wangu anajuwana na wanasheria akirudi kutoka kazini nitamwambia kila kitu.Ondoa hofu usijali kwa hilo”
Ushauri wa Dorika kidogo ulimwingikia akilini na kumpa moyo,alijihisi mshindi na moyo wake ulifarijika mno.
“Naomba usisahau kumwambia akija”
“Hilo usijali,usiku nitakupigia simu maana anarudi jioni saa kumi na moja”
“Sawa wacha mimi niwahi”
Marietha aliaga na kuondoka zake, hakutaka kupitia sehemu yoyote ile zaidi, alinyoosha mpaka Kwa Deo ambapo alivyowasili aliingia bafuni na kujimwagia maji,akavaa kanga na kujitupa kitandani.
Kwake siku hiyo masaa yalijivuta kama kinyonga muda ulikuwa hauwendi alikuwa akisubiri simu kutoka kwa Dorika kwa hali na mali,ushauri wa kisheria alioambiwa aufanyie kazi aliuona ni bora na aliamini kivyovyote vile ni lazima Deo angewekwa ndani kama mambo yangeenda vizuri.

Ilivyofika saa nane mchana simu yake ya mkononi iliita na ilikuwa inatokea kwa Deo,akaipokea.
“Marietha,upo nyumbani?”
“Ndio”
“Wageni hawatokuja leo watakuja hapo keshokutwa.Jiandae leo nataka nikutoe outing”
“Hapana Deo sijisikii kutoka”
“Please nakuomba”
“Sina mood ya kutoka”
“Lak…tititi”
Marietha alikata simu hapohapo, hakutaka kuendeleza mazungumzo ya simu na Deo,alimchukia kuliko kinyesi na kitu kilichomfanya awe naye mpaka dakika hiyo ni Issa aliyekuwa kituoni.Maisha ya Issa yalikuwa mikononi mwake, isingekuwa hivyo angetoroka siku nyingi sana na kutokomea mbali kusikojulikana na Issa wake lakini alishindwa.
“Griii griii”
Simu iliita tena na aliyekuwa akipiga ni Deo,Marietha hakupokea mpaka ilivyokata,iliendelea kuita hivyohivyo.Kama angepewa bastola amchague mtu wa kumuondosha duniani angemmiminia risasi Deo nyingi za kichwani ili atoweke duniani,moyo wake ulijaa majuto.
Ni kweli kwa Deo alipewa kila kitu mama yake alijengewa nyumba kubwa ya matofali mbali na hapo kila mwisho wa mwezi akaunti yake iliingizwa pesa,Marietha hakuwa ana shida ndogondogo katika maisha yake hii yote ni kwasababu ya tajiri Deo,ambaye alimgharamia kila kitu ili kununua moyo wake,yote aliyofanyiwa na Deo ilikuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.Moyo wa Marietha haikumpenda na ulitumbukia kwa Issa Nurdin Mpelembe,kijana maskini muuza mitumba Manzese, jambo ambalo liliwaacha marafiki zake vinywa wazi.
“Kwanini lakini?”
Marietha alijisemea mwenyewe akiwa mwenye ‘stress’ nyingi kichwani.Alijaribu kutafuta usingizi lakini haukupatikana,alikuwa akisubiri usiku ufike ili azungumze na rafiki yake Dorika,alimuhitaji mwanasheria ili amkomboe kipenzi chake Issa kituo cha polisi,Buguruni.
****
Saa mbili kasoro na dakika kumi usiku ndipo simu ya Marietha iliita akiwa bafuni anajimwagia maji ili kutoa uchovu,alitoka bafuni akiwa na mapovu mwilini bila nguo sababu kichwani alijuwa ni lazima aliyekuwa akipiga simu hiyo ni Dorika sababu hiyo ndiyo ilikuwa mida ya wao kuongea.Alikuwa ni kama ametabiri kwani juu ya kioo cha simu lilitokea jina ‘DORIKA’,haraka akafuta mikono yake iliyokuwa na maji kwenye shuka akaipokea na kuiweka sikioni.
“Halloo,Dorika.Samahani nilikuwa bafuni naoga”
“Usijali,niliongea na mume wangu.Amesema kuwa ataongea na mwanasheria kila kitu kitakuwa sawa”
“Kweli?”
Bado Marietha hakuamini alichokuwa anasikia.
“Ndio,asubuhi saa mbili nitakupigia simu”
“Ahsante sana Dorika”
“Usiku mwema best,wacha nipumzike”
Marietha alidhamiria kumfunga Deo jela ili amkomboe Issa kwenye mateso,hakuwa na chaguo lingine zaidi.
Siku hiyo Deo alivyorudi hakumchangamkia hata kidogo na aliamini kuwa siku chache lazima sheria itafuata mkondo wake.Alijilaumu ni kwanini swala hilo hakumpelekea Dorika mapema ili wamsweke Deo ndani.
***
Siku iliyofuata Marietha alikuwa wa kwanza kutoka kitandani ilionekana alilala usingizi wa mang’amung’amu na alikuwa akisubiri kukuche haraka!akatembea mpaka seblen na kuwasha luninga ili asukume muda uwende huku simu yake ya mkononi ikiwa pembeni yake.
“Mbona leo mapema?”
Hata Deo alionekana kushangaa,haikuwa kawaida kwa Marietha kudamka asubuhi na mapema kiasi hicho!
“Sina usingizi”
“Sawa,kuna pesa nimekuachia chumbani.Utanunua vitu vya ndani”
“Aya”
Deo alikuwa tayari amevaa suti nyeusi anaelekea kibaruani,moyo siku zote ni giza nene hakuelewa kilichopo ndani ya moyo wa mwanamke huyu Marietha kwa macho,alitoka nje na kuwasha gari akaondoka zake.

Hazikupita hata dakika thelathini simu ya Marietha iliita,moyo wake ukapiga mkambo sababu aliyepiga alikuwa ni Dorika.Haraka akaipokea na kuiweka sikioni.
“Marietha za asubuhi?”
“Nzuri tu,sijui wewe”
“Mungu ni mwema nimeamka salama.Mwanasheria keshapatikana anasema hakuna shida,muonane”
“Wapi?Saa ngapi?”
“Anaitwa Wilvin Munganga,nakupa namba yake sasa hivi”
“Sawa ahsante sana”
Sekunde tano baada ya kukata simu ukaingia ujumbe mfupi wa meseji.
‘WILVIN MUNGANGA 0750 676764’
Ujumbe ulisomeka juu ya kioo cha simu ya Marietha,hapohapo bila kupoteza muda aliinua simu na kumtafuta mwanasheria ambaye atakayeweza kumkomboa Issa.
***
“No Wilvin,inabidi uudhurie kwenye harusi yangu,wewe ni mtu mkubwa sana hapa jijini.Usilete habari zako za sheria kwangu sendoff hukuja.Mwambie na Dustan awepo vilevile na Emmanuel Lukuwi asikose kwenye harusi.Naendesha gari hapa nipo barabarani…Naenda posta ofisini.Njoo basi ofisini kwangu,okay.I’ll appreciate.Thank you.See you soon”
Deo alikata simu na kuiweka pembeni baada ya kumaliza mazungumzo na rafiki yake, mwanasheria MR.WILVIN MUNGANGA!



Simu ya Mwanasheria Wilvin Munganga ilikuwa ikitumika kumaanisha alikuwa kwenye laini na mtu mwingine anazungumza naye,hiyo haikumfanya Marietha asitishe zoezi lake, alizidi kujaribu tena na tena.Hatimaye baada ya dakika tatu ikaanza kuita.
“Halloo”
Sauti nene kiasi ilisikika upande wa pili,Mapigo ya moyo ya Marietha yakaanza kupiga kwa nguvu ingawa hakuelewa hali hiyo imetokana na nini.
“Samahani nazungumza na Mr.Wilvin Munganga?”
“Ndiyo, nani mwenzangu?”
“Naitwa Marietha”
“Naam Marietha”
“Kuna mambo naomba nizungumze nawewe sijui unapatikana wapi?ni kuhusu kesi”
“Ofisi yangu ipo Mikocheni,My fear.Unapahafamu?”
“Ndio”
“Ukifika My fear kuna jengo refu la njano,gorofa ya kwanza, njoo saa kumi jioni”
“Sawa ahsante sana”
“Okay”
Simu ikakatwa.
Moyo wa Marietha ukapiga mkambo,alidhamiria kumfunga Deo kwa kumshtaki, kwa asilimia mia moja ushindi ulikuwa kwake ingawa bado aliogopa kufanya hivyo,hakuelewa watu wangemuonaje kwa hatua atakayoenda kuichukuwa ya kumfunga bwana harusi mtarajiwa.Alielewa kivyovyote vile angehojiwa maswali mengi na watu wengi wangehitaji kujua kisa cha maamuzi yake licha ya hayo angechukiwa kwa kuharibu harusi iliyopaniwa na mamia ya watu,yote aliyafikiria lakini aliyapuuzia na kutojali, alikuwa yupo tayari kufanya lolote ili mradi Issa wake awe huru.

Bado alikuwa seblen akitafakari mambo mengi sana ya nyuma,alimpenda Issa kwa moyo wote hata Deo pia alikuwa ndani ya moyo wake vilevile, alianza kuhisi huruma lakini hakutaka kurudisha moyo wake nyuma.Mwili wake ulikuwa juu ya sofa lakini akili yake ilikuwa mbali mno ilimuwaza Issa na alipanga baada ya Issa kuwa huru watoroke mbali hata ikiwezekana aibe pesa za Deo,hicho ndicho kitu alichokuwa anakiwaza.Alijuwa sehemu zote za Deo anapoweka pesa zake.Hapohapo akasimama na kunyoosha mpaka chumbani,ambapo alifungua kabati na kutoa funguo zilizokuwa chini kabisa,akatembea mpaka kwenye kabati lingine na kuchomeka funguo.Alivyofungua alikumbana na maburungutu ya pesa,zilikuwa pesa za kitanzania pamoja na dola za kimarekani.Marietha alitetemeka kwa hofu,nia yake ilikuwa ni kuhakikisha kama pesa zilikuwepo.Hapo ndipo ziku zote Deo huifadhi baadhi ya pesa zake za mauzo ya maduka yake yote ya Kariakoo na Kinondoni na mwisho wa mwezi kuzipeleka bank.
“Lazima niondoke na hizi pesa kama Issa akitoka nitaondoka naye twende nchi yoyote ile”
Hayo ndiyo mawazo yaliyokuwa ndani ya kichwa chake,pesa alizoziona aliamini zilitosha kabisa kufanya kitu alichopanga.Ilivyotimu saa tisa alasiri juu ya alama akaanza kujiandaa ili saa kumi imkute tayari akiwa amevaa,Marietha alienda na muda na alitaka kufika Mikocheni kuonana na mwanasheria Wilvin Munganga siku hiyo amueleze kila kitu kuhusu Deo,alikuwa anaenda kumshtaki ili sheria ifuate mkondo wake! Tisa na nusu akawa tayari keshavaa akatoa simu yake ili apewe maelekezo kuhusu mpango wa kufika Mikocheni.
“Habari Mr.Wilvin”
“Nzuri tu”
“Mimi ni Marietha ambay…”
“Okay okay,unaweza ukaja sasa hivi nipo Ofisini.Ukifika My Fear upande wa hilo hilo jengo,mita kama kumi kuna jengo la njano,au ukishindwa kufika ulizia ofisi za Law Legal chamber kwa mtu yoyote hapo utakuwa umefika,huwezi kupotea”
“Sawa ahsante”
“Okay karibu”
“Ahsante”
Kwa Marietha ilibaki kazi moja tu,kutafuta usafiri na kuanza safari ya kuelekea Mikocheni kutoa malalamiko yake,kwa kufanya hivyo ndiyo alijuwa lingekuwa suluisho kwake,swala la ndoa kichwani kwake halikuwepo kabisa ilikuwa ni tofauti kwa Deo ambaye alizidi kuwaalika marafiki zake wa ndani na nje ya nchi.
Hakutaka hata kupoteza nukta ya sekunde moja,akatoka nje ya geti na kutafuta bajaji,dakika arobaini na tano baadaye alikuwa anashuka My fear,akamlipa dereva ujira wake na kuanza kutupa macho yake huku na kule akitafuta jengo la njano.
“Sijui ndio lile”
Marietha alijiuliza mwenyewe,hakuwa na uhakika na gorofa aliloliona upande wake wa Mashariki,akatembea kwa mwendo wa taratibu akiwa analitizama jengo hilo kwa umakini,ambapo kwa nje lilikuwa na geti dogo la chuma!akalisukuma na kuingia ndani.
“Samahani kaka”
Akamuongelesha kijana mmoja aliyekuwa anatokea ndani ya jengo.
“Bila samahani”
“Naomba kuuliza”
“Uliza tu”
“Hapa ndiyo ofisi za Law Legal Chamber?”
“Ndio,ndiyo hapa”
“Ahsante sana”
Marietha alivyopata uhakika akatembea na kusukuma mlango wa kioo,mbele yake akakutana na meza kubwa za gharama na makochi ya wageni, kushoto kwake kulikuwa na sehemu ya mapokezi,ilikuwa ni ofisi nzuri kupita kiasi.Kiyoyozi kilikuwa kikali na alihisi ubaridi baada ya kuingia.Akanyoosha mpaka mapokezi ambapo alipokelewa na tabasamu mwanana na mrembo aliyevaa shati jeupe.
“Karibu dada,nikusaidie nini?”
“Nahitaji kuonana na Mr.Wilvin Munganga”
“Advocate Munganga?”
“Ndiyo”
“Pandisha ngazi hizo hapo.Kulia kwako mlango wa pili”
“Sawa Ahsante”
Marietha akafanya kama alivyoambiwa,akapanda ngazi,upande wake wa kulia mlango wa pili akasimama na kushusha pumzi ndefu,akaweka sketi yake vizuri na kugonga.
“Karibu”
Alivyofungua mlango akakumbana na Mwanaume kijana maji ya kunde mwenye umri kati ya miaka 25-30,nyuma ya meza kubwa mezani kukiwa na kompyuta mbili,moja kubwa nyingine ndogo yaani ‘laptop’kwa kimombo.
Hakuwa na uhakika kama ndiyo Mr.Wilvin Munganga aliyekuwa anaongea naye kwenye simu.
“Karibu uketi”
“Ahsante”
Marietha alivyokaa walisahabahiana.
“Namuulizia Mr.Wilvin Munganga”
“Ndiye mimi”
“Mimi ndiye Marietha nilikuwa naongea nawewe asubuhi”
“Sawa Marietha karibu sana,karibu Law Legal Chemba”
“Ahsante nishakaribia”
“Nakusikiliza”
Sentensi ya Mr.Wilvin Munganga ilimaanisha Marietha aseme shida yake.Hilo alilijuwa, kila kitu alitamani kukisema kwa wakati mmoja,alishindwa kuelewa aanzie nyuma au mbele.
“Kama nilivyokwambia naitwa Marietha,nimejikuta nipo katika wakati mgumu sana baada ya kuwa na wanaume wawili kwa wakati mmoja……”
Marietha alihitaji msaada wa kisheria na alitakiwa atoe kila kitu kutoka ndani ya kifua chake ili apatiwe ukombozi na ndicho kitu alichokuwa anakifanya mbele ya Advocate Munganga aliyekuwa makini anamsikiliza kila nukta ya sentensi yake.
Ilichukuwa muda wa dakika sabini yaani lisaa limoja na dakika kumi mpaka Marietha akafikia tamati,ambapo machozi yalianza kumlenga.
“Pole sana Marietha,umesema Issa yupo kituoni na Deo ndiyo kamfunga?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Wilvin Munganga.
“Ndio na amesema atamuuwa endapo nitakataa kufunga naye ndoa”
“Hilo ni jambo rahisi,hiyo kesi ni ndogo sana kwangu.Harusi ni lini?”
“Jumamosi ijayo”
“Jumamosi ijayo?”
“Ndio”
“Unataka nianze lini kazi?”
“Hata leo”
“Sawa lakini inahitajika pesa kama advance ili nianze kazi”
“Kiasi gani?”
“Kwa sasa hivi utatoa milioni mbili.kama nusu ya malipo nyingine utamalizia kesi ikiisha”
Kwa Marietha pesa hizo zilikuwa nyingi mno hakuwa na kazi wala kipato chochote cha pesa,hakuelewa afanye nini ili afanikishe zoezi hilo la kumtoa Issa kituoni na kumfunga Deo gerezani.Kichwa chake kilichanganua mambo mengi sana akawaza na kuwazuwa.
“Ukiwa tayari,utaniingizia humu kwenye hizi account namba EQUITY BANK”
“Sawa ahsante”
Badala ya kuitikia kwa furaha,Marietha akanyong’onyea ghafla hakuwa na nguvu tena.
Maji yalizidi unga na kwa maana hiyo asingeweza kufanya kitu chochote,hakuwa na pesa.Katika kumbukumbu zake alikumbuka kwenye akaunti yake kuna shilingi laki nne peke yake, zilikuwa ni pesa ndogo sana tena hazikuvuka hata nusu ya malipo,hapo ndipo alipochoka zaidi.Wazo likamjia ghafla akam-kumbuka Mama yake mzazi,hapohapo akampigia simu sababu alijuwa ana pesa anazoingiziwa na Deo kila mwisho wa mwezi ukifika!
“Halloo Mama shikamoo”
“Marahaba hujambo mwanangu”
“Sijambo,upo nyumbani?”
“Unadhani nitakuwa wapi na uzee huu”
“Nakuja basi,kuna mambo nahitaji kuongea nawewe”
“Sawa njoo”
Hapohapo Marietha alivyotokeza nje,akapunga mkono.Bajaji ikafika mpaka miguuni mwake.Akaingia na safari ya kwenda kwa Mama yake mzazi ikaanza mara moja,dakika kumi na tisa baadaye akawa tayari amefika akamlipa dereva pesa yake akasukuma geti na kuzama ndani!Akatembea na kufungua mlango.
“Mamaaaa,Mamaaaaaaaa”
“Niniii?”
Mama akaitika akitokea jikoni,alivyomuona Mwanaye akatabasamu lakini baada ya sekunde mbili sura yake ikabadilika,kuna kitu alijifunza kutoka usoni mwa binti yake,Marietha hakuwa na furaha.
“Marietha una tatizo gani?”
“Nina shida Mama”
“Shida gani?Niambie”
“Nina shida na pesa”
“Pesaa!?”
Swala la kifedha aliamini mtu kama Marietha halitampiga chenga kwasababu mkwe wake Deo alikuwa nazo za kutosha haikuwezekana hata kidogo kuwa na shida kama hiyo.
“Pesa za nini?”
“Mama utanisaidia?”
“Inategemea,za nini kwanza alafu ni kiasi gani?”
“Naomba milioni nne?”
Mama akamtizama Mwana kwa umakini zaidi.
“Za nini?”
“Mama naomba nisaidie kwanza”
“Ndio ni za nini?”
Kusema kwenda kumshtaki Deo angeharibu kila kitu,akili yake ikafanya kazi kwa kasi ya mwewe,ilikuwa ni lazima apige porojo kwa mama yake ili apate pesa.
“Mama,nadaiwa”
“Na nani?Deo ulimwambia?”
“Sitaki ajue.Sababu nilivyokopa benki ilikuwa siri kubwa nilitaka nikanunue kiwanja,nikatapeliwa.Mama naomba unisaidie tafadhali”
“Ulikopa benki bila Deo kujua?”
“Ndio Mama”
Mama hakwenda shule hakujua taratibu zozote za benki ndiyo maana akaingia laini,akamtizama binti yake huku akitia huruma alimsikitikia sana sababu alikuwa ni mtoto wake wa pekee.
“Na mbaya zaidi keshokutwa watu wa benki watakuja nyumbani pale kupiga mnada nyumba ya Deo”
Marietha akazidi kulipigilia swala lake msumari ili kuliwekea mkazo.
“Mimi nitakusaidia nitaongea na Deo,nilikuwa na pesa jana nilituma Tanga mjomba wako Sadick anaumwa,anafanyiwa operesheni leo”
“Utamwambia nini Deo?”
“Wewe usijali mimi nitaongea naye,hawezi kukataa kunipa hiyo pesa”
“Mama,lakini usimwambie kuwa nilikuja hapa”
“Usijali lakini usiwe unafanya chochote bila kumshirikisha mwenzako”
***
Zilibaki siku tano ili Marietha na Deo Karekezi wafunge ndoa wawe Mume na mke,kuanzia siku hiyo wageni mbalimbali nyumbani kwa Deo hawakukauka,walipishana wakitoka na kuingia ili kupanga mikakati ya ndoa.Jumla ya bajeti ya ndoa ya Deo ilifikisha shilingi milioni mia moja hamsini,kukodi magari,ukumbi pamoja na mapambo na kuwasafirisha wageni mbalimbali na wazazi wake kutoka mkoani.Deo muda wote hakutulia alikuwa mara ashike hiki aache kile,mbili wala tatu hazikukaa alifikiria harusi yake,aliamini kuwa alikuwa ana muda finyu.
“Mr.Abdul Tore keshafika?nilishakwambia nitalipia Hotel kwa muda wa wiki mbili,mbona hivyo? unadhani nitakutapeli au?No sio hivyo James acha kufanya mambo ya kitoto,mimi nishawahi kukufanyia dhuruma kwani?sawa hiyo hoteli ni yako najua unataka cash lakini kwa sasa hivi sina pesa…sawa nitashukuru hakikisha wanapata huduma zote wakifika okay”
Alivyokata simu,akapokea nyingine.
“Ndio Wilvin,umefika wapi?upo na gari?Okay sikia unaona hilo bango la Tigo hapo..Kuna mtaa unaingia ndani,nyoosha moja kwa moja,utapita baa ya kwanza.Kona inayofuata kushoto kuna nyumba nyeupe hapohapo..Ahsante karibu sana nakusubiri”
Wakati Deo anazungumza na Simu seblen Marietha alikuwa bafuni anajimwagia maji,alikuwa na mawazo chungu mzima,mpango wake wa kutafuta pesa ulidunda na Deo kwa wakati huo hakuwa na pesa hivyo Mama yake alipigwa kalenda,hilo likamchanganya akili zaidi ingawa hakutaka kukubali hata kidogo,ilikuwa ni lazima azipate milioni mbili kabla ya siku ya harusi kufika iwe hata kwa kuiba,wakati mwingine shetani alimvaa na kutamani kujirahisisha kwa matajiri waliokuwa wanamtaka ili akusanye pesa lakini aliogopa kufanya hivyo,aliuthamini mwili wake hakutaka kuvua nguo yake ya ndani kisa shida alizokuwa nazo mbali na hapo aliogopa maradhi hususani gonjwa hatari la UKIMWI.
Alivyokuwa chumbani anavaa alihisi sauti ambayo anaifananisha lakini hakuwa na kumbukumbu nzuri aliwahi kuisikia wapi.
“Mariethaaaa”
Sauti ya Deo ilimuita kutokea seblen.
“Abeee”
“Njoo Mpenzi wangu”
“Nakuja”
Marietha akafungua mlango, kivyovyote vile alijuwa anahitajika kutambulishwa kwa mgeni aliyefika,akatokeza mpaka Seblen Moyo wake ukapiga paa! alivyomuona Wilvin Munganga seblen.
“Marietha”
Wilvin akaita,hapo ndipo Marietha alipozidi kuchanganyikiwa zaidi.
“Mnafahamiana?”
Deo akauliza akitaka kujua, sababu aliamini Wilvin na Marietha hawakuwahi kuonana!



Kila alipojaribu kumtafsiri Deo ni mwanaume wa aina gani alishindwa kupata jibu kamili,kila kitu alichojaribu kukifanya hakikufanikiwa.Njia zote ziligonga mwamba Mwanasheria aliyetaka kumtumia ili amkomboe mpenzi wake Issa leo hii yupo na Deo nyumbani kwake na ilionekana walikuwa ni marafiki wakubwa.Hiyo ilimaanisha kila kitu kitakuwa wazi kabisa, isingewezekana hata kidogo kwa Wilvin Munganga amfunge rafiki yake,hilo lilikuwa wazi.Mambo mengi yalikuwa yakimwagika kichwani mwake.
“Ndio Marietha namfahamu sana,juzi alikuja ofisini kwangu”
Wilvin Munganga alizidi kuropoka hakuwa na koromeo na hakuelewa maneno anayotaka kuongea yangekuwa na madhara gani kwa Marietha.
“Kuna mambo yetu tuliongea bwana”
“Mambo gani?”
Deo alitaka kujuwa ingawa alianza kuhisi jambo,alimtizama Marietha kwa sekunde kadhaa akarudisha macho yake kwa Wilvin.
“Anataka kumfunguka Mumewe mtarajiwa kwahiyo alikuja kwangu nifungue mashtaka”
Wilvin akapasua jipu lakini halikuwa kosa lake hakuekewa lolote mbali na hapo hakujuwa kuwa bwana harusi aliyetakiwa kumfunga ni rafiki yake Deo Karekezi bado alikuwa nyuma ya kila kitu ndiyo maana akajiachia,kaanika kila kitu waziwazi.
“Kwahiyo unataka kunifunga?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Deo,akimuuliza Marietha.
“De..”
“Nijibu swali langu,unataka kunifunga mimi?”
Swali la pili lilisindikizwa na sauti ya juu,Deo alisimama wima na kumsogelea karibu, mambo yalikuwa tayari yameharibika na kitu chochote kilikuwa kinaenda kutokea mkono wa Deo wa kulia ulikuwa ukitetemeka kumaanisha muda wowote Marietha angetandikwa Makofi sababu Deo alikuwa ana mkono mwepesi ingawa alikuwa mpole,Marietha aliogopa akaanza kurudi nyuma taratibu kama gari.
“Deo! Deo! Deo! Deo!”
Wilvin nayeye akasimama akamvuta Deo na kukaa katikati, Marietha nyuma yake.
“Wilvin naomba ukae chini”
“No Deo,ukifanya hivyo utakuwa unakosea,embu njoo tuzungumze hapa kiume”
Wilvin alijaribu kumtuliza rafiki yake,akamvuta mpaka juu ya sofa.
“Deo punguza hasira kwani nini kinaendelea?”
“Kila kitu unakijua”
Picha tayari lilikuwa limeungua kwa Marietha.Deo hakuwa na sababu ya kuficha mambo sababu alielewa Wilvin anajuwa kila kitu,mwisho alihitimisha kwamba anampenda Marietha ndiyo maana akachukuwa maamuzi ya kumfunga Issa.
“Bro,itakuwa haina maana yoyote kumuoa mwanamke asiyekupenda”
“Wilvin asante kwa ushauri,hilo nalijua mambo yangu hayakuhusu.Wewe ni rafiki yangu lakini tutagombana sasa hivi,sasa hivi utaniharibia siku”
Wilvin alipojaribu kutoa ushauri aliumbuliwa na kukatwa maini,Deo aliongea kwa hasira iliyochanganyika na ukali ndani yake.Tayari siku yake ilikuwa imevurugika,hakutaka kumkosa Marietha kwa gharama yoyote ile.Kwa elimu aliyokuwa nayo hakupaswa kufanya vitu kama hivyo vya kishamba lakini ilim-bidi.
Wanawake walikuwa wengi na alikuwa ana uwezo wa kumpata mwanamke yoyote yule amtakaye duniani sababu alikuwa na pesa,hakuelewa ni kwanini Marietha hampendi,aliwakumbuka wanawake wengi waliokuwa wakimtaka kimapenzi.Uzuri wa Marietha ulikuwa wa kipekee na aliamini ndiye atakaye kuja kuwa mke wake wa maisha wajenge familia,swala la kumuoa Marietha siku zote kwake lilikuwa ni kama ndoto lilikuwa ni lazima litimie! Ndiyo maana hakutaka kuiacha ndoto yake ya kumuoa Marietha.
Alishusha pumzi ndefu na kumtizama Wilvin usoni.Wilvin alijifunza kitu kupitia macho ya rafiki yake, kuna kitu aliweza kukisoma.
“Deo….”
“Wilvin naomba unisaidie kitu..Nampenda sana Marietha na ninampenda sana sijamtamani kwamba nimchezee nimuache,nataka awe mke wangu”
Deo alizingumza kwa hisia kali machozi yalikuwa yanamlenga na alichokuwa anakizungumza alikimaanisha kutoka moyoni mwake,hakutaka kumuacha Marietha kirahisi ingawa mwanamke huyo hakumtaka.
“Inabidi uongee naye vizuri,unajuwa wanawake wakati mwingine wanakuwa kama watoto,wanahitaji kubembelezwa,ukitaka kumkera mwanamke wewe mgombeze”
“Hayo yote nimefanya”
“Kaa naye vizuri.Naomba nikuulize kitu”
“Uliza”
“Kabla ya kufikia hii hatua ya ndoa hapo mwanzo ilikuwaje?”
“Alinipenda na hata siku moja sikudhani kama ana mwanaume mwingine,mpaka ikafikia hatua ya uchumba.Nikaja kugundua siku moja aliacha simu yake”
“Enhee”
“Nilivyochukuwa hata mimi sikuamini,sikutaka kumuuliza moja kwa moja nikaanza kufuatilia mwenyewe,iliniuma sana Wilvin,kilichoniuma zaidi ni aina ya mwanaume anayetembea naye,muhuni tu muuza mitumba”
Deo alisimulia kila kitu na wala hakuacha hata kitu kimoja,Wilvin alibaki kimnya anamsikiliza rafiki yake kwa makini kama anayesikiliza kesi kizimbani,alihakikisha aachwi hata na neno moja.Sababu alihitajika kutoa ushauri baada ya kila kitu.
“Deo,najua kinachokuumiza moyo sasa hivi”
“Kitu gani?”
“Ni aina ya mwanaume anayetembea naye Marietha”
“Ndio,Marietha kakosa nini kwangu?sawa angeniambia mapema kuwa ana mtu wake.Imagine hatua za mwisho ndiyo ananieleza mambo hayo na HAKI YA MUNGU nita muua Issa kama hatokubali kufunga ndoa namimi,wewe uwe shahidi.Potelea mbali nifungwe”
Deo alisisitiza swala lake na mpaka hatua hiyo haikuwezekana kumbadilisha mawazo hata kidogo,hakutaka kughairi harusi ambayo iligharimu mamilioni ya pesa licha ya yote alimpenda Marietha aliamini ipo siku atabadilika tu,Deo aliendelea kuufariji moyo wake.

Marietha alikuwa chumbani analia machozi,kila kilichoongelewa kilipenya ndani ya masikio yake.Faraja yake ilikuwa kwa mwanasheria Wilvin na kila kitu kiliyayuka,alilia kama mtoto mdogo,angekuwa na uwezo angesimamisha siku zisiende mbele ama angezirudisha nyuma aweze kubadilisha kila kitu lakini haikuwezekana.Alihisi kujuta kujiingiza katika mapenzi na Deo, shida ndizo zilimfanya awe na Deo na hakutegemea hata siku moja kama mambo yangeenda harakaharaka na Deo kutangaza harusi, katika akili yake alijuwa Deo angekuwa ni mwanaume wa kupita na Issa ni wake wa milele.Kulia kwake machozi hakukufanya mambo yabadilike,alitakiwa afikirie jambo lingine la kufanya,zilibaki siku chache ili ndoa ifungwe,alivyokumbuka hivyo alizidi kuumia zaidi.
“Kwaheri bwana,wewe niachie mimi nitajua cha kufanya Mr.Deo”
“Sawa,ahsante”
Deo na Wilvin walikuwa wakiagana.Yote hayo Marietha aliyasikia na alijuwa baada ya hapo ni lazima Deo angeingia chumbani,ni kweli hivyo ndivyo ilivyokuwa.
“Marietha”
Deo aliita lakini Marietha hakuitikia sio kwamba hakusikia,kwikwi ilim-bana.
“Marietha mpenzi wangu”
“Sema”
“Naomba unisamehee,ni hasira nakupenda tambua hilo naomba unipe nafasi ndani ya moyo wako.Ninakupenda na ninakupenda kweli”
“No De...o hunipendi,kama ungekuwa unanipenda usinge..fanya haya unayofan….”
Machozi yalikuwa yakimbubujika Marietha kama maji,alilia kwa kwikwi.Deo alimtia hasira kupita kiasi na moyo wake ulimchukia vilevile.
“Wewe ndiye unayefanya nifanye haya yote Marietha,niambie nifanye kitu gani ili unipende,niambie chochote nitafanya.Nikujengee nyumba,nikupe kiasi gani cha pesa ili unipende”
“Mapenzi sio pesa Deo,tambua hilo.Na..omba nikwambi..e ukweli leo.Nilikuwa nawewe kwasababu nilikuwa nina shida.Issa alipigwa risasi kwa ajili yangu,alihitaji matiba..bu sikuwa na jinsi”
Ulikuwa ni ukweli uliomuuma Deo lakini hakutaka kuonesha swala hilo waziwazi.
Akasogea karibu na kupiga magoti,katika maisha yake hakuwahi kufanya hivyo na alishawahi kuapa kuwa hatompigia mwanamke yoyote magoti,leo hii mapenzi yanampigisha magoti mbali na hapo machozi yalikuwa yanamlenga,Deo alitia huruma.Marietha alivyogeuza shingo yake alishtuka kuona swala hilo mbele yake.
“Marietha nakupenda sana”
“Deo”
Marietha akaita nayeye akasogea karibu.
“Unanipenda?”
“Zaidi ya sana”
“Na unataka niwe mkeo?”
“Ndio”
“Naomba umuachie Issa huru”
Deo aliendelea kumuimbisha Marietha kuhusu swala lake la ndoa lakini ikawa ni kama kumpigia mbuzi gitaa acheze,Marietha alikazia msimamo wake kwamba ndoa hakuna bila Issa kuwa huru na Deo nayeye hakuwa mwepesi kukubali ikawa vuta n’kuvute.
Kuanzia siku hiyo hakuna mtu aliyemuongelesha mwenzake,Marietha alinuna.
“Ukimuua Issa namimi najiua”
Hivyo ndivyo Marietha alivyosema usiku huo baada ya Deo kumkumbusha kuwa atamuuwa Issa.
“Umesema?”
“Kama ulivyonisikia,sitoweza kuishi bila Issa”
Ulikuwa ni mtihani mwingine mgumu kwa Deo na jinsi mambo yalivyokuwa alielewa kuwa Marietha atajiua haikuwa na maana yoyote kubaki naye,zilikuwa zimebaki siku tatu ili ndoa ifungwe,swala hilo likazidi kumchanganya Deo kichwa chake.
“Sawa”
Jibu la Deo halikueleweka vizuri.
***
Kwa elimu aliyokuwa nayo na mambo aliyokuwa anafanya vilikuwa ni vitu viwili tofauti kabisa,siku nzima aliwaza na kuwazua,akiwa mwenyewe seblen na chupa ya pombe kali aina ya ‘wisky’ tena akinywa bila kuchakachuwa na maji,kwa wadhifa na heshima aliyokuwa nayo ilitakiwa awe ni mwanaume mwenye busara.Alivyofikiria hivyo akajiona mpuuzi na alikuwa akifanya mambo ya kipumbavu.

Aliamini kuwa hata ashuke Yesu Kristo siku hiyo hatoweza kumbadilisha Marietha na wakati mwingine akili yake ilimwambia Marietha hakuwa mke aliyechaguliwa na Mungu.
Hapohapo akapapasa mfukoni na kutoa simu yake ya mkononi,akaingia kwenye orodha ya majina,alivyolifikia jina Afande Bakulibovu akaipa simu ‘ok’ kisha kuiweka sikioni.
“Halloo kiongozi,habari za masiku?”
Upande wa pili wa siku ulisikika afande Bakulibovu alikuwa hewani.
“Nzuriiiii tuuuu,sikilizaaa afandeeee”
“Ndio ndio bosi najua unataka kujua yule mwizi anaendeleaje,nina habari nzuri tushapata kesi tayari.Ya mauaji tushamtengenezea faili mambo yapo ta…”
“Naomba aachiwe huru”
“Unasemaje mkuu?”
Sio kwamba afande Bakulibovu hakusikia anachoambiwa alihisi kama masikio yake yanamdanganya ama amesikia vibaya.
“Naaaaomba aachiwe huru na apelekwe hospitaliii apatiwe matibabuuu sasa hivii please”
“Mbon….”
“Naombaaa nielewekeee”Akakata simu.
Deo alizungumza kwa sauti ya kilevi na ni kweli alimaanisha kwa kile anachokisema,kifupi alinawa mikono na alikuwa tayari kughairisha ndoa.
“Wanawaaake wapo weeengi,bull shit”
Deo alikuwa chakali anabeua pombe,hakutaka kulazimisha mapenzi akiamini kuwa wanawake wapo wengi mjini,tayari mawazo yake yalibadilika!
****
“Mamaaa,Maamaaaaa!,Mamaaaa”
“Mama yako hayupo,ameenda Tanga.Mjomba wako anaumwa sana”
“Mbona hajaniambia?”
“Ametoka amechanganyikiwa asubuhi sana”
Marietha alifika nyumbani kwao mchana,alikuwa na furaha kupita kiasi sababu alitoka kumuona Issa hospitalini,alikuwa yupo huru na Deo aliwaacha waendelee na mapenzi yao kumaanisha kuwa ndoa hakuna ingawa swala hilo halikutangazwa rasmi.Mama zake wadogo walitoka mikoa mbalimbali ili kuja kushuhudia harusi ya Marietha, hawakuelewa kuwa mambo tayari yamebadilika hakuna tena harusi.
“Jaman..”
“Marietha embu subiri kwanza,ongeza sauti ya t.v”
Ghafla kila mtu alitupa macho yake juu ya luninga ilikuwa ni habari ya kutisha.
“MVUA KUBWA YANYESHA MKOANI PWANI MAGARI YASOMBWA NA MAJI WATU WAMEPOTEZA MAISHA”
Mwanamke aliyekuwa anatangaza habari kituo cha ITV alimaliza kisha tukio likatokea,daraja la mto wami lilijaa maji, magari yalikuwa yakisombwa na maporomoko,kitu kilichowachanganya zaidi ni basi la Luxury Coach alilopanda Mama Marietha lilikuwa linasombwa,walilishuhudia.
“Mungu wangu,Chiku yupo kwenye lile basi Eh Mungu”
Kauli hiyo ilimchanganya sana Marietha,akahisi kuishiwa nguvu za miguu hakuelewa ni kitu gani akifanye.Basi la kampuni ya Luxury Coach lilizidi kuvutwa.
“Mama weeeee”
Marietha akapiga ukelele,hakuelewa afanye kitu gani.Msaada ulitakiwa wa haraka,Marietha hakuwa na jinsi akatoa simu mfukoni.Hakuwa tayari kuyaunga mawazo yake mkono lakini hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima ampigie simu Deo atoe msaada wa kukodi helkopta,ikaokoe maisha ya Mama yake mzazi,hakuwa na uhakika kama Deo angekubali.
“Griii griiii griii griiiii”
Siimu ya Deo iliita bila kupokelewa,hiyo ndiyo ikamfanya Marietha achanganyikiwe zaidi.




Mvua ilikuwa ikinyesha mno na ilitishia amani katika mkoa wa Pwani kilomita kadhaa kutoka mji wa Dar es salaam.Sio hivyo tu,iliambatana na upepo mkali na kusababisha miti kudondoka na mabati ya nyumba kupeperushwa hewani.Radi ilipiga sio masihara,ndani ya nusu saa maji yalikuwa yametapakaa kila eneo.Magari yalivutwa na madaraja kuvunjika.Katika watu waliokuwa wamechanganyikiwa ni Mama Marietha,alikuwa ndani ya basi la Kampuni ya Luxury coach kuelekea mkoani Morogoro kwenda kumuuguza kaka yake kisha kesho yake arudi jijini Dar es salaam,mvua kubwa ilimkuta katikati ya safari.Kulikuwa kuna msongamano mkubwa wa magari kwenye daraja la mto Wami ambapo ilisadikika mto huo chini ulikuwa na mamba,abiria waliokuwa ndani ya basi walishuhudia magari madogo yakielea juu ya maji,yanasombwa!
“Eh Mungu baba ziokoe nafsi zetu”
Abiria walianza kusali sara zao za mwisho,wakaweka matumaini yao kwa Mungu, hakuna hata mmoja wapo aliyeamini kama angepona,yalikuwa maji mengi na daraja la mbele lilikuwa limevunjika tayari maji yanasomba magari.
Asilimia za uhai wa maisha yao zilikuwa ndogo sana,Mama Marietha alibaki kuyatizama maji yaliyokuwa yanatembea kwa kasi yanasukumiza basi kuelekea mabondeni,alimkumbuka mwanaye Marietha, hakutaka kuamini kuwa anaenda kufa maji siku hiyo kabla ya kushuhudia harusi ya binti yake ambayo alikuwa akiisubiri kwa hali na mali.Maji yakaanza kuingia ndani ya basi likazidi kusogea na kugota kwenye chuma pembezoni mwa daraja,kitu kilichowachanganya zaidi ni baada ya gogo kutokeza na kuligonga basi,hapo ndipo likaserereka na kutumbukia ndani ya mto.
***
Moyo wa Marietha ulikuwa ukitapatapa mno,kama kungekuwa kuna kifaa cha kupima mapigo ya moyo basi kingeonyesha moyo wake unadunda mara mia mbili kwa sekunde.Deo hakupokea simu yake na ndiyo mtu aliyetakiwa kutoa msaada kwa wakati huo ingawa hakuwa na uhakika kama Deo angekubali,alikuwa akijaribu bahati. Wakati mwingine alijilaumu mwenyewe,kwa sababu wakati kama huo Deo alihitajika kwa wudi na uvumba.Alivyoona simu haipokelewi hapohapo akatoka nje bila kuuliza chochote,akaparamia geti na kutoka nje kabisa,ambapo mbele yake kulikuwa na pikipiki zinazosubiri abiria wenye haraka kama yeye.
“Kaka njoo Mara moja”
Marietha aliongea harakaharaka bila kuweka nukta akionesha kuwa ana dharura,pikipiki ikasogea mpaka miguuni mwake,bila kusema anapoenda akapanda nyuma.
“Wapi tunaenda?”
“Wewe twende nitakwambia”
Dereva hakuwa na tatizo,alimfahamu Marietha sababu alikuwa jirani yake.
“Nipeleke kwa Deo”
“Sawa”
Dereva akatii amri,Marietha alikuwa muoga wa kupanda usafiri wa pikipiki lakini siku hiyo hakuogopa tena, alimsisitiza dereva aendeshe kwa kasi,hivyo ndivyo ilivyokuwa.Upepo ulikuwa ukipuliza na pikipiki ilikuwa katika kasi isiyoweza kuelezeka kiwepesi.Kilichomchanganya Marietha, mbele kulikuwa na msongamano wa Magari.
“Yasin huwezi kupita njia ya minazini tuwahi?”
Marietha alihoji baada ya kuona msongamano wa magari.
“Huko kuna matrafiki wanakamata alafu sina leseni”
“Tupite hiyo njia tafadhali mimi nitaongea nao nina haraka sana”
“Poa”
Dereva akatii amri akakunja kona na kuingia barabara ya vumbi,mwendo ulikuwa ni uleule sababu Marietha alisisitiza uongezwe,wakazidi kuingia ndani ndani vichochoroni njia za panya ili wakatishe njia wawahi kufika.

Dereva alivyotokeza barabarani akashtuka kulikuwa na mapolisi wa usalama barabarani,ilikuwa ni kama ametabiri sababu alipigwa mkono na kuweka pikipiki kando.Marietha alizidi kuchanganyikiwa zaidi.
“Vipi?”
Askari akatoa salamu na kuchomoa funguo za pikipiki.
“Afande tafadhali mimi nina haraka,embu chukuwa hii kanywe soda”
Marietha alikuwa nyuma ya pikipiki akachomoa noti ya shilingi elfu kumi akaifinyanga na kumpa askari.
Askari akageuka huku na kule kuangalia kama wenzake wanamuona.Alivyohakikisha usalama upo vizuri akaichukuwa na kuiweka mfukoni ki utaalam.
“Nawewe dada unaongea kama chiriku!aya wahini upesi”
Afande akarudisha funguo, tangu asubuhi hakupiga bao na kupata elfu kumi kwake ilikuwa shangwe akayakenua meno yake yote nje.
Safari ikaanza hapohapo,ndani ya dakika ishirini walikuwa getini kwa Deo.
“Shika,chenji kaa nayo utanipa siku nyingine.Ahsante Yasin”
Marietha akasukuma geti na kuzama,akatembea hatua mbilimbili na kuingia mpaka ndani.Alichokikuta kilimshtua mno,moyo wake ukazidi kupiga kwa nguvu,ukataka mpaka kutokeza nje ya kifua.Deo alikuwa amelala chali,anakoroma kama kondoo pembeni yake kuna chupa kubwa za pombe kali.
“Deoo,Deooo..Deoooo”
Marietha akaita huku akimtingisha,sura yake ilijawa mashaka.Deo alikuwa bwii yupo mtungi, isingewezekana hata kidogo kuzinduka kwa wakati huo na kuelewana.
“Deooo”
“Siiiikaaaa aaaaah”
Deo aliongea kitu alichokijuwa mwenyewe na kujigeuza upande wa pili.Marietha akatafakari ni kitu gani akifanye akatembea mpaka kwenye friji na kuchukuwa maji ya baridi,akamimina ndani ya jagi.Hakuchelewa akam-mwagia Deo usoni,hapo ndipo alipokurupuka,akageuka akawa kama mtu anayeangalia haamini mtu anayemuona mbele yake.
“Mar..eth..”
“Deo naomba unisaidie ninahitaji msaada wako”
“Mariet…ha”
“Deo wake up!Deo ninahitaji msaada wako”
Ilikuwa sio kazi ndogo kumzindua Deo aliyekuwa katikati ya usingizi wa ulevi, chupa mbili za wisky alizokunywa kutoa mawazo zilikuwa nyingi na zilizidi kipimo,ndio maana ilikuwa kazi ngumu kwa Marietha.
Deo aliona maluweluwe kichwa chake kilikuwa kizito kama kobe, hakuwahi kunywa kiasi kingi cha pombe kiasi hicho mpaka akazima ingawa alikuwa mnywaji,mbele yake alimuona Marietha lakini hakuwa na uhakika, hakuelewa kama yupo ndotoni au kweli,kumbukumbu zake zikawa zinakuja na kupotea kama simu ya kichina.
Marietha akazidi kumpiga piga makofi kwenye mashavu,akam-mwagia tena maji ya baridi usoni,ubaridi ndio ukamzindua tena, fikra zake zikarudi kwa mbali ingawa bado alihisi kizunguzungu kikali.
“Marietha,Unafaanya nini hapa?mimi nishakuruhusu uwendeee kw….”
“No Deo ninahitaji msaada wako”
“Msaada gani?”
“Mama”
“Kafanya nini?”
“Yupo Mto Wami,kuna mafuriko daraja limevunjika”
“Whaaaaaat?”(Nini)
Deo akashtuka akitumia lugha ya kimombo.Akakaa vizuri pombe zikapungua kichwani.
“Ameenda lini?”
“Tafadhali Deo,Leo ndio ameenda”
“Unahitaji msaada gani sasa?”
“Ukamuokoe kama ulivy…”
“Subiri”
Kama mkuki Deo akasimama Wima,alishaelewa ni njia gani aitumie ya haraka,akatembea haraka mpaka chumbani kwake ambapo alitoka na simu na kubonyeza namba fulani,akaiweka simu sikioni.
“Hallo Mr.Ben Moyo,Upo wapi?Ndio nahitaji msaada wako.Helkopta ipo hapo ya kukodi ndio.Imebaki moja?Tafadhali nakuja hapo sasa hivi,okay ahsante”
Simu ilivyokatwa,akamtizama Marietha kwa sekunde kadhaa kuna kitu alikuwa anataka kukizungumza lakini akasita.
“Twende”
Deo mbele Marietha nyuma mpaka kwenye gari aina ya Verosa wote wakaingia ndani, Deo akarudisha gari nyuma,geti likafunguliwa gari likatoka mkuku.

Ndani ya gari hakukuwa na mazungumzo ya aina yoyote ile hakuna mtu aliyemuongelesha mwenzake,ili kufupisha njia ya kuwahi Deo hakutaka kutumia barabara kubwa alitaka kukwepa msongamano wa magari,akapita njia za panya ili awahi kufika Kipawa akutane na Mr.Ben Moyo Mkurugenzi wa kitendo cha usafiri wa anga.
Marietha alikuwa kimnya mapigo yake ya moyo yalikuwa yanaenda kwa kasi,alimtafakari Deo ni mwanaume wa aina gani akashindwa kupata jibu,alikuwa ni mwanaume mwenye roho isiyokuwa ya kawaida.Walikuwa wamegombana na alikataa ndoa,iweje tena amsaidie? hivyo ndivyo vitu vilivyokuwa vinapita ndani ya kichwa cha Marietha,pesa ndiyo kila kitu hapo ndipo alipoamini,bila uwepo wa Deo Mama yake asingeokolewa kama angetokea wangemuwahi,akamfikiria Issa kwa mara nyingine kwa wakati huo hakuwa na msaada wowote ule,hakuwa na fedha mbali na hapo hakuwa na uwezo wa kupata hata shilingi elfu kumi kwa siku.Marietha alikuwa katika wakati mgumu hakuelewa ni aina gani ya shukrani ampe Deo.
“Ulimwambia Mama chochote?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Deo,akavunja ukimnya.Mikono yake yote miwili ikiwa juu ya usukani macho yake kayakodoa mbele.
“Hap...ana hapana hajui”
“Kwani aliondoka leo asubuhi?”
“Ndio”
“Mbona ghafla alienda kufanya nini?”
“Mjomba anaumwa”
“Nani? Bariki?”
“Ndio”
Familia ya Marietha Deo aliitambua sababu wote walimjua kwao,alivyotokeza barabara ya Kipawa akakunja kushoto akazidi kusonga mbele,dakika kumi baadaye alikuwa uwanja wa ndege Mwl.Nyerere, akaweka gari kwenye maegesho akateremka harakaharaka,Marietha akamfuata nyuma kama mkia.
Kwa kuwa alikuwa anajuwa ofisi zilipo haikumpa shida,moja kwa moja akaanyosha na kupanda ngazi.
“Habari,nimemkuta Mr.Moyo?”
Deo alimuuliza Msichana wa mapokezi.
“Ndiyo yupo”
“Mwambie Deo Karekezi nimefika”
“Pita ndani,anakusibiri”
Ilielekea msichana wa mapokezi alijuwa ujio wa Deo ndiyo maana akamruhusu bila kumuhoji maswali.
“Mr.Moyo sina muda wa kupoteza kama nilivyokwambia kwenye simu ninahitaji Helkopta”
“Taratibu ni zilezile”
“Nitakurekebishia,ni kiasi gani tena?”
“Dolla mia saba kwa lisaa”
“Okay hakuna shaka,cheki yangu haija mature naomba nisaidie kwa hilo”
“Kwani unaelekea wapi?”
“Mto Wami”
“Unaelewa kinachoendelea huko?kuna mvua kubwa”
“Najuwa ndiyo maana ninahitaji msaada wako”
Deo alimaanisha kile anachokiongea na alihitaji msaada wa helkopta.
Mr.Ben Moyo akasimama na kutoka nje ambapo baada ya dakika tano alirudi na katarasi ameshika mkononi.
“Nifuate,nimekuombea kwa bosi kwa kuwa wewe ni mteja wetu ndiyo maana kakubali ila amesisitiza baada ya wiki uwe umekamilisha kila kitu”
“Hilo usijali”
Walitoka nje ambapo kulikuwa na uwanja mkubwa uliokuwa na ndege ndogo za kukodi pamoja na Helkopta, walimkuta tayari rubani yupo ndani.
Wote wakaingia na mlango ukafungwa.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Marietha kupanda Helkopta uso wake ulionesha wasiwasi mkubwa.Rubani akabonyeza bonyeza vitu,Helkopta ikaanza kupiga kelele mapanga boi yakaanza kuzunguka taratibu yalivyochanganya,akashika kitu kilichofanana na gia akavuta kidogo kwa juu,Helkopta taratibu ikaanza kupaa angani.
Ni kweli kadri walivyozidi kwenda mbele ndipo wingu lilizidi kuoneka jeusi,mvua ilikuwa kubwa na radi ilipiga.Hatimaye wakafika daraja la mto wami baada ya dakika thelathini.Macho ya Marietha yalikuwa chini anatizama huku na kule.
“Dereve teremsha chini kidogo”
Helkopta ikazidi kushuka chini baada ya Deo kutoa kauli hiyo.
“Basi lile pale Deo”
Bila kujifikiria Mara mbili mbili Deo aliteremsha ngazi,hakujali akashika ngazi vizuri na kujishika akateremka akiwa amejishika vizuri akalifikia basi lililokuwa linaelea juu ya maji chini ya daraja,ilikuwa ni jambo la hatari mno kwake,alifanya hivyo sababu bado alikuwa na mapenzi na Marietha ndiyo maana hakuhofia kitu chochote, alikuwa chapachapa amelowa.
Mungu alikuwa pamoja nao,kupitia dirishani alimuona Mama Marietha akijitahidi kufungua kioo ili atokee dirishani, hapohapo akasogea karibu na kumshika vizuri akamtoa nje.
“Hapana mimi ni mkweo”
Mama Marietha akagoma kushikwa ili iwe rahisi kwa Helkopta kuondoka,ilikuwa ni lazima Deo aiviringishe mikono yake kiunoni mwake ili Helkopta ipande juu.
“Mama hatuna huo muda”
“Nimekwambia mimi ni mkweo,huwezi kunishika hivyo”
“Sawa”
Radi ilipiga na Deo akampa ngazi Mama Marietha, akapanda kuelekea juu,alivyofika ndani ya Helkopta,Deo akashika ngazi.
Katika hali ya ghafla wimbi kali likapita maji yakamchapa kwa nguvu kifuani akapoteza uelekeo akadondoka chali juu ya maji.Mafuriko yalikuwa makubwa, maji yakamsomba yakamzungusha na kumtupa mbali.Marietha aliyekuwa juu ndani ya Helkopta alishuhudia kila kitu,alilia machozi.
“Deooooooo!”
Aliita kwa sauti huku akimwaga machozi!
“Deooooooo!”


“Tuku! tuku! tuku! tuku! tuku!”
Helkopta iliendelea kuzungusha mapanga boi yake,mvua ilizidi kunyesha ikiambatana na radi,Mafuriko yalizidi kusomba mali,magari yaliserereka na kuvutwa na maji.Marietha alikuwa ndani ya Helkopta analia machozi alisikia uchungu ajabu,Deo alikuwa chini anapelekwa na mafuriko ya maji,alitamani kujitosa ndani ya mto ili amkomboe lakini hakujuwa jinsi ya kupiga mbizi, aliogopa kufa maji.Akazidi kuchanganyikiwa zaidi alivyomuona Deo haonekani tena kumaanisha amezama kabisa,hiyo ndiyo ikamfanya Marietha ampigie rubani kelele.
“Sasa tutafanyajeeee?”
Marietha aliuliza kwa sauti ya juu ili ashindane na kelele za radi pamoja na mapanga boi yaliyokuwa yanazunguka,sura yake ilionesha wasiwasi mkubwa na machozi yalikuwa yakimtoka,alitaka Deo aokolewe kwa njia moja ama nyingine.
Mama Marietha alikuwa pembeni hajui ni kitu gani akifanye,kila kilichotokea kwake bado alidhani ni miujiza sababu alikuwa tayari ameikabidhi roho yake kwa Mungu baba!alikuwa hana matumaini ya kupona ndiyo maana mpaka wakati huo akili yake haikukaa sawa.
“Inabidi tuondoke hatuna jinsi”
Rubani akajibu akazungusha kirungu Helkopta ikageuka,Marietha akazidi kupiga kelele.
“Haiwezekani lazima tumuokoe”
“Wote tutakufa”
“Noo,hapana basi mimi nishushe”
Marietha hakuwa na uhakika na kitu anachotaka kukifanya ingawa aliropoka,hakutaka hata kidogo kumuacha Deo nyuma,alikuwa yupo radhi arudi hata na maiti kama Deo angekufa maji.Moyo wake ungemsuta sababu mwanaume huyo alijitolea kuyaokoa maisha ya Mama yake mzazi,alitakiwa kulipiza wema kwa wema na sio wema kwa ubaya, ndiyo maana alimsisitiza rubani wazidi kusubiri.
***
Uwezo wa kuogelea alikuwa nao sababu alijuwa kucheza na maji,Deo alikuwa mpiga mbizi hodari lakini maji yalimzidi nguvu siku hiyo sababu yalikuwa yanazunguka yakamtia kizunguzungu,alivyochapwa na wimbi ndio kabisa akakosa dira,kila alipojaribu kupiga mbizi akijaribu kutumia utaalam wa kuchezesha miguu yake kama chura huku akiyakata maji na mikono ilishindikana maji yakazidi kumpelekesha huku na kule.Mbaya zaidi alikunywa maji mengi, mengine yakamuingia puani,akapagawa!
Akaelewa asipokuwa makini ataenda kufa maji akitapatapa,hakutaka hilo litokee.Akatuliza mawazo na akili yake, akaibua kichwa chake juu na kuvuta pumzi kwa kama sekunde kumi akarudi ndani ya maji na kuanza kuyakata maji chini kwa chini kama mamba.Akazidi kusonga mbele zaidi,alijitahidi mpaka alipoliona gogo la mti linapita mbele yake,akaliwahi na kulishika.Kwa nguvu akajivuta na kulikumbatia akakaa juu yake.Alivyoangalia juu aliona Helkopta inageuza na kuondoka,akajitahidi kupiga kelele lakini sauti yake haikuweza kufika hata kidogo.Ikazidi kuondoka kuelekea Kaskazini Magharibi.
***
“Yule pale,Yule paleeee”
Marietha aliruka kwa furaha na kupiga kelele huku akiangalia kwa chini kwa mbali ingawa hakuwa na uhakika asilimia mia moja,alikuwa ni kama anabahatisha sababu mwanaume aliyemuona alifanana na Deo,shati jekundu alilovaa ndiyo lilimfanya amgundue kiwepesi.Helkopta ikageuka na kurudi ilipotoka.Ni kweli Marietha alikuwa sahihi sababu walivyosogea karibu waligundua kuwa alikuwa ni Deo,kwa haraka Marietha akashusha ngazi, Deo akaikamata na kuanza kupanda,akaingia ndani.Moyo wake ulichanua akamkumbatia Deo kwa furaha.
“Pole sana”
“Ahsante”
Macho ya Deo yalikuwa mekundu sana sababu ya kukaa ndani ya maji kwa muda mrefu ilionekana hata yeye hakuamini kwamba ameponea chupchup kwenye tundu la sindano,hawakuwa na muda wa kupoteza.Rubani akazungusha Helkopta wakaanza safari ya kurudi Dar es salaam.
Marietha akawa na kibarua cha kumpa pole Deo.Walifika Dar es salaam baada ya dakika arobaini na tano.Helkopta ikatua ardhini Deo alioneka kuchoka kuliko mtu yoyote yule,shukrani alizotoa Mama Marietha zilikuwa ngumu kuelezeka kwa maandishi,alishukuru tena na tena!
“Mwanangu nashukuru sana ubarikiwe Baba angu”
“Mama usijali,Mungu ni mwema sote tumetoka salama”
“Ni kweli mwanangu pole sana,inabidi uwende hospitalini,ukapatiwe kidogo matibabu”
“Hapana Mama nipo sawa”
Wakati mazungumzo hayo yanaendelea walikuwa wakitembea kuelekea kwenye lango kubwa la kutokea,Marietha yupo mkono wa kuume wa Deo akimfariji,hata yeye hakuelewa ni aina gani ya shukrani ampe mwanaume huyu mkombozi wa Maisha ya mama yake,alizidi kumtafakari kichwani na kushindwa kupata jibu kamili.Walirudi mpaka ofisini kwa Bwana Moyo.
“Vipi mwenzangu,ulikuwa unapiga kasia?!”
Mr.Ben Moyo alimshangaa Deo jinsi alivyolowa chapachapa,miguuni hana viatu ana soksi peke yake.Ofisi nzima ikawa na maji.Deo alikuwa chapachapa anahema juu juu kama mtu aliyekabwa na ugali wa muhogo!
“Hapana,matatizo tu”
“Shemeji vipi?Ilikuwaje?”
Ilibidi Bwana Moyo amuulize Marietha.
“Alilazimika kuingia ndani ya maji ndiyo maana unaona hivyo”
“Aise poleni sana”
“Ahsante”
Deo hakutaka kuendelea kuchafua ofisi ya watu.
“Naomba funguo za gari”
Mr.Moyo alitembea mpaka kwenye meza yake na kuchukua funguo za gari akampa Deo ambaye pia hakutaka kupoteza wakati,hapohapo akatoka kwenye maegesho ya magari.

Kila mtu alimshangaa,kwa wadhifa aliokuwa nao ilikuwa jambo la aibu lakini yeye hakujali,hivyohivyo akafungua mlango wa gari wote wakazama ndani.Gari likawashwa.
“Nikushushe wapi Marietha?”
Deo aliuliza huku akiwa makini juu ya Usukani,swali alilouliza lilimfanya Marietha apate kigugumizi,hakuelewa ni jibu gani alitoe kwa wakati huo.
“Kwani unaelekea wapi?”
“Nampeleka Mama nyumbani kwanza kisha naenda kwangu”
“Nitaenda kwako”
“Okay”
Deo alimfikisha Mama Marietha nyumbani kwake kisha yeye na Marietha wakarejea nyumbani,walipofika tu kitu cha kwanza Deo aliinyoosha mpaka chumbani kwake,akatupa nguo na kuingia mpaka bafuni ili kujimwagia maji,Marietha nayeye akawa nyuma nyuma,alivyomuona Deo kaingia bafuni nayeye akamfuata pia.Kuna vitu alivihisi ndani ya mwili wake,havikuwa vya kawaida mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu yakasukuma damu yake kwa kasi hasa alivyomuona Deo amevua nguo zake zote,hakujua ni kitu gani akifanye ingawa alijuwa mwili wake ni kitu gani unahitaji.
“Vipi?”
Deo aligeuka na kumuuliza swali lililomfanya Marietha aishiwe nguvu kabisa,Deo alishaelewa nini maana yake,alikuwa ni mwanaume rijali tena aliyekamilika kila idara, akamsogelea Marietha karibu akamshika kidevu akatoa ulimi wake nje,akautumbukiza mdomoni mwa Marietha ambaye hata yeye aliyaachia meno yake ulimi ukatumbukia ndani wakaanza kunyonyana ndimi.Bado Marietha hakuelewa ni kitu gani akichague,kubaki na Deo ama Issa.Alishindwa kuuelewa moyo wake na kutokuelewa ni mwanaume yupi sahihi kati ya hawa wawili,akahisi mkono wa Deo unapita chini ya kitovu,alikuwa amevaa sketi laini.Deo akazidi kupitisha mkono wake chini ukazama mpaka ndani,Marietha siku zote alikuwa mwanamke msafi sana,ndiyo maana Deo hakukutana na nyasi hata moja,mkono wake ukazidi kudidimia chini kabisa mpaka kwenye maporomoko,Mkono ukatulia juu ya pango hapo ndipo Deo alipoanza kuuchezesha.Hapo ndipo Marietha alipochanganyikiwa zaidi,damu ikazidi kumwenda mbio kuliko kawaida,akajiachia na kuzungusha ulimi wake ndani ya mdomo wa Deo akili yake ilihama kabisa,akahisi mkono wa Deo wa Kushoto umepita mgongoni mwake,ukapachua ‘lock’ ya sidiria aliyovaa,mambo hayakuishia hapo ‘top’ aliyovaa juu ikatolewa ikatupwa chini,Marietha akabaki kifua wazi.Akahisi kapigwa na ubaridi mkali baada ya ulimi wa Deo kutua juu ya chuchu zake akiwa analambwa huku chini mkono wa Deo ukifanya kazi yake,haikuwa rahisi kuzikatisha raha alizohisi mwanamke huyu Marietha,ngozi yake ikabadilika rangi na kuwa nyekundu ghafla.Akaona tayari amezidiwa akachukuwa mkono wake mmoja akakamata ndizi ya Deo iliyokuwa tayari imesimama imara kama mnara,akaanza kuichuwa taratibu, mambo yalikuwa mukidemukide kwa watu hawa wawili,Deo alisahau kuwa alitakiwa kuoga,tendo la uasherati lilifanya akili yake ihame mazima!Akam-beba Marietha juu juu akaingia naye chumbani na kumtupa puu,kitandani.Akamfuata kwa juu akaikamata sketi yake kwa pamoja na Chupi akavivuta chini,akatoa na kuvitupa juu ya malumalu,akaipanua miguu ya mwanamke huyu na kutumbukiza ulimi katikati yake,hapo ndipo Marietha alipohisi kufakufa,akahisi moyo wake unaacha mwili,raha zilizidi kipimo chake.Kwa jinsi mambo yalivyoenda,tayari chini alianza kulowana hapo ndipo Deo akamuweka nyoka wake vizuri,akamtumbukiza ndani ya shimo.
“Ah De.o I lo..ve yo..u aaah ssshhh”
***
Issa aliendelea kutibiwa hospitalini akipatiwa matibabu yote akiwa mwenye furaha kabisa,moyoni alimpongeza Marietha na alijiona mshindi.Mpaka siku hiyo aliamini kuwa Marietha anampenda kupita kiasi,bado hakutaka kuamini kwamba wanawake kama Marietha bado wapo duniani,wakati mwingine alidhani yupo ndotoni anaota na baadaye angeshtuka sababu haikuwezekana hata kidogo kwa mwanamke mrembo kama Marietha awe naye kimapenzi aachane na Deo,mwanaume tajiri.
Hakuelewa ni aina gani ya mapenzi ampe kama fadhila ila aliuhaidi moyo wake kuwa atampenda Marietha mpaka kufa kwake na hatokuja kuiona nguo ya mwanamke yoyote yule ya ndani isipokuwa ya Marietha.Hata siku hiyo alivyokuwa anawaadithia marafiki zake walishindwa kuamini.
“Kwahiyo mtoto kakataa harusi,kamkataa mshkaji?”
Chogo aliuliza akiwa ahamini, historia ya Issa ilikuwa ni kama picha la kihindi,haikuwezekana hata kidogo swala hilo kuwa ukweli.
“Ndiyo na alikuja hapa jana kuniona.Harusi hakuna tena,nampenda sana Marietha jamani”
“Ah Issa,sio kwamba umetumia ndumba wewe?tuelezane Mwamba ili nasisi utupe huyo mganga”
“Ah wapi”
“sasa umempa nini mtoto wa watu?”
Bado marafiki zake waliamini kuwa Issa alitumia kizizi kumpata Marietha ingawa walimsihi kwamba asije hata siku moja akamtenda Marietha kwani hatopata mwanamke wa sampuli hiyo popote pale duniani.
“Siwezi kumuacha Marietha hata Mungu atanilaani kwa kweli”
“Ndio usifanye hivyo,vipi lakini kichwa kimeacha kuuma?”
“Kichwa kimeacha lakini upande wa huku pembeni bado unauma”
“Pole sana Issa,kabla hatujasahau tumekuletea chakula hiko hapo,tena ubwabwa na mandondo.Jinsi tunavyokujali”
“Ahsanteni sana”
Issa alijisikia furaha sana siku hiyo akiwa juu ya kitanda amepewa ‘bedrest’ kutokana na kuumizwa sana hiyo ililazimikia madaktari wampe kitanda ili wammchunguze ki undani zaidi.
Kilichomfanya aingiwe na wasiwasi na kukosa raha siku hiyo ni Marietha,hakumuona tena hospitalini alitamani awepo pembeni yake,isingewezekana hata kidogo kwa Marietha kutokufika au kupitisha siku nzima bila kumuona.Alijuwa ni lazima kutakuwa kuna tatizo limempata ingawa hakutaka kuyapa nafasi mawazo yake hasi kipaumbele ila aliendelea kujipa moyo kuwa wenda atafika usiku wa siku hiyo lakini wapi!Marietha hakutokea,siku hiyo ikapita, kesho yake majogoo yakawika Marietha hakuonekana popote pale mbali na hapo alimtafuta hewani lakini namba hazikupatikana.

Mpaka siku hiyo anaruhusiwa hospitalini hakumuona Marietha jambo hilo likamchanganya akili yake.Alitoka hospitalini akiwa ameandikiwa dawa za kupunguza maumivu na zingine za kuuwa bacteria,hali ya Issa iliridhisha sababu aliweza kutembea ingawa kwa kuchechemea.Marafiki zake walikuja kumchukuwa siku hiyo wakampeleka mpaka anapoishi,Manzese!
“Hivi Marietha uliongea naye?”
Lilikuwa ni swali la kushangaza,Chogo alimuangalia na kudhani wenda Issa anaanza kuchanganyikiwa.Issa akalijuwa hilo,akajishtukia.
“Nauliza hivyo kwasababu tangu juzi sijamuona”
“Hatujaonana naye tangu siku ile umeenda polisi”
“Na namba zake pia hazipatikani”
“Issa embu pumzika kwanza,Marietha atakuja. Hapa anapajua hawezi kukosa kuja”
“Nad..”
Ni kweli walikuwa kama wametabiri,mlango wa chumba cha Issa ukasukumizwa moyo wa Issa ukaruka mapigo matano kwenda mbele,chumba kizima kilinukia utuli,Marietha alikuwa ananukia kama jini.Marashi aliyopuliza yalienea chumba kizima.Sio hivyo tu,Marietha alibadilika, shingoni alikuwa amevaa mikufu ya dhahabu nywele zake zimekarabatiwa vizuri,kope amezitinda akawa kama mdoli.
Alisimama mlangoni kwa kama sekunde mbili bila kuongea chochote na hakuonesha tabasamu lolote, sura yake ilionesha umakini,jinsi walivyokuwa wanamshangaa Marietha hawakutofautishwa na watu wanaosoma tangazo.
“Mariethaaa! kweli una maisha marefu mpenzi wangu tulikuwa tunakuzungumzia sasa hivi…Karibu ukae”
Issa alisema lakini Marietha alibaki akimtizama,akashusha pumzi za ndani kwa ndani.Ndani ya kichwa chake vilikuwa vinapita vitu vingi sana.
“Naomba unisikilize Issa,nafunga ndoa Jumamosi.Nimekuja kukwambia kuwa mimi na wewe ibaki historia.Tafadhali sana naomba utambue hilo,ninaenda kuwa mke wa mtu hivi karibuni”
Issa alitabasamu sababu alijuwa Marietha alikuwa katika hali ya utani na mwisho wa siku angemwambia kuwa anampenda na hawezi kumuacha,hilo aliliamini ndiyo maana hakushtuka.
“Marietha,acha utani,alafu nimepewa dawa za…”
“Issa sitanii nipo siriazi”
Marietha hakutania wala hakuwa na punje iliyoonesha kuwa alikuwa katika hali ya masihara,hiyo ikamfanya Issa aanze kuhisi hali ya ubaridi juu ya uti wake wa mgongo ingawa aliendelea kujipa moyo kuwa Marietha anatania.
“Kwaheri,nakutakia maisha mema!”
Hatimaye Marietha akahitimisha,akageuka na kutoka nje.Issa hakutaka kubaki akasimama wima na kuanza kumfuata nyuma.
“Mariethaa,Mariethaa…”
“Issa naomba unielewe.Naomba unisamehe kwa maamuzi niliyoyachukuwa”
“Kwanini lakini Marietha?”
“Sijui”
Marietha akazidi kusonga mbele,Issa akaendelea kumfuata.
Wakatokeza mpaka barabarani ambapo alimshuhudia Marietha ananyoosha mpaka kwenye gari aina ya Subaru, akafunguliwa mlango na Deo ambaye alionekana alikuwa akimsubiri.Issa aliumia sana moyo,wakatizamana na Deo kwa kama sekunde moja,akamshuhudia anazunguka upande wa pili na kuingia ndani kisha gari likaondoka.
Issa alisikia uchungu ajabu,hakutaka kuamini kwamba jambo lililotokea lilikuwa halisi bali ni ndoto ya kutisha!


Ilikuwa ni lazima achukuwe maamuzi magumu ili maisha yaendelee.Jinsi Deo alivyomsaidia na kujitolea isingewezekana hata kidogo kumkatalia ndoa.Moyo wake ungemsuta, hata hivyo aliona ni sahihi kuwa na Deo sababu bila yeye mama yake mzazi angekufa maji,daraja la mto wami.Hakumuwaza tena Issa na tangu siku hiyo alijuwa pesa ina nafasi kubwa sana katika mapenzi na ndiyo ilitumika kuyaokoa maisha ya Mama yake,mamilioni ya pesa yaliteketea ili Helkopta ipatikane.Marietha alikuwa ndani ya gari ametoka kumwambia ukweli Issa juu ya kile alichokusudia alikuwa ndani ya mawazo mengi kupita kiasi,hata yeye alishindwa kuamini kuwa ndiye yeye aliyemtamkia Issa maneno ya kumkataa.Walikuwa na ndoto kubwa sana za kufika mbali na baadaye wajenge familia lakini mambo yalibadilika ghafla.
“Marietha upo sawa?”
Deo ilibidi aulize,Marietha alionekana ameshika tama ana mawazo mengi sana.
“Yeah nipo sawa”
“Kweli?”
“Ndio”
Deo alivyosikia hivyo akabadili gia na kuzidi kusonga mbele,furaha iliyokuwa ndani ya moyo wake haikuwa na kipimo chake.Aliipania harusi sio masihara na alitaka itingishe jiji la Dar es salaam ndiyo maana akawa amewapa kadi mpaka wafanyabiashara mbalimbali na matajiri kama Salim Ali Bakhresa,Dk.Reginald Mengi pamoja na Manji.Hiyo yote ilikuwa ni kutafuta sifa, alitaka harusi yake izungumziwe jiji zima,alitamani siku zisogee mbiombio.Ingawa zilibaki siku tatu lakini kwake ilikuwa kama Mwaka, siku zilisogea kwa mwendo wa ajuza,alitafakari vitu vingi na kujikuta anatabasamu.
“Mbona unacheka?”
Marietha akauliza.
“Nina furaha sana”
“Ndiyo ucheke mwenyewe?”
“Ndio,kwani vibaya love wangu”
“Hapana”
“Nakupenda sana”
“Mimi pia”
***
Ni kweli Deo alikuwa mpenda sifa na kabla ya harusi yake kufanyika alianza kuitangaza katika vyombo vya habari mbalimbali kama Becker T.v,Radio One,clouds tv na TBC1 huko kote alimwaga pesa ili harusi yake ipigiwe debe na ndivyo ilivyokuwa.
“Ndio nataka irushwe online ni kesho,nasema ni Kesho nishaongea na Mkurugenzi wako.Hiyo harusi iruke Becker Tv,nishaongea na Becker mwenyewe.Siongei na mbwa naongeaga na mwenye mbwa siku zote.Usiniletee mambo ya kishenzi,Sawa!”
Ilibaki siku moja peke yake ili harusi ya Deo na Marietha ifungwe,hekaheka zilizidi na wakati wote Deo alionekana kuchanganyikiwa zaidi,aliona kama siku hiyo haikumtosha na bado hakuamini kama siku inayoitwa kesho atamuoa Marietha awe wake wa maisha,aliendelea kuona mambo yanayotokea ni ndoto tu!Alivyokata simu akamtafuta Marietha hewani ambaye alikuwa nyumbani kwa mama yake akiwa kama mwali.
“Baby nishaanza kukumisi tayari,siamini kama kesho ndiyo nafunga ndoa nawewe”
Deo alianza mazungumzo huku akiwa anatembea seblen mara ashike rimoti mara aingie chumbani.
“Inabidi uamini Deo wangu,hapa moyo unanidunda sana”
“Mimi ndio usiseme kabisa,sijui kwanini”
“Punguza presha baba”
“Sidhani kama nitalala leo”
“Inabidi ulale mpenzi wangu”
“Ushaongea na Nandy?”
“Nandy nishaongea naye,anakuja kulala hapa nyumbani”
“Okay vizuri.Nakupenda sana”
“Mimi pia”
Simu ilivyokatwa ilimuacha Marietha akitabasamu alikuwa na furaha, hata yeye hakuamini kama kesho anaolewa,ilikuwa ni heshima kubwa sana kuolewa na aliamini angeeshimika kufunga ndoa akiwa bado ana umri mdogo sana tena na mwanaume mwenye uwezo kifedha,alianza kupiga kesho yake picha atakavyokuwa ndani ya shela akiwa anafunga pingu za maisha na kisha kuvalishwa pete na baadaye kuanza maisha ya ndoa.
Alijaribu kuyafikiria maisha yake ya ndoa yangekuwaje baada ya hapo na kushindwa kupata jibu sababu hakuwahi kuolewa kabla ingawa alishawahi kusikia kwamba ndoa ina changamoto lukuki!
“Hili gauni msambaa yule sijui kalipunguza vipi,embu angalia lilivyokuwa”
“Ha ha ha haaaa,inabidi ulirudishe Mama Sakina.Ndiyo nini hivyo umekuwa kama balanguru”
“Namrudishia leoleo asinichezee akili.Wewe gauni lako vipi?”
“Mimi tayari nishalipiga pasi.Kesho nitakula mpaka basi.Si unajuwa mimi kwenye mambo ya mnuso,silembi”
“Wewe nawe kwa kula hujambo”
“Ah babu wee,nitakunywa balaa”
Ndani ya nyumba ya Mama Marietha kulikuwa na shamrashamra, wakina mama waligongana vikumbo wakijaribisha nguo,mara wavae mara wajaribu ili mradi vurugu tupu.Siku hiyohiyo walianza kunywa na kusubiri siku inayoitwa kesho ifike.
“Marietha mwanangu mbona kama hauna furaha?kesho ndiyo siku yako unaolewa”
Mama alimfuata Mwana chumbani,Marietha alionekana akiwa na mawazo mengi sana,hakuonesha furaha hata kidogo.Ndio maana mama yake mzazi akamuhoji,alitaka kujuwa nini kilichopo ndani ya kifua cha binti yake.
“Mama nipo sawa,usijali ninawaza tu mambo ya ndoa”
“Ndio,ndoa sio kitu cha mchezo.Ina mambo mengi sana inabidi uwe mvumilivu na jasiri.Deo anakupenda sana”
“Najuwa Mama”
“Mimi nakutakia maisha mema,nadhani kila kitu niliongea kwenye Kitchen party uzingatie niliyokwambia.Aibu yako ni aibu yetu”
“Nimekuelewa Mama”
Marietha alimtizama Mama yake kwa kitambo kidogo bila kujibu kitu chochote,bado moyo wake ulikuwa ukipiga kwa nguvu hakuelewa ni kwasababu gani.Mlango wa chumbani ukafunguliwa akaingia Mama yake mwingine mdogo aliyeitwa Veronica.
“Marietha”Akamuita!
“Abee”
“Kuna mgeni wako yupo seblen”
“Mgeni wangu!?”
“Ndio”
“Nakuja”
Marietha akainuka kutoka kitandani,akanyoosha mpaka Seblen.
Hapo ndipo moyo wake ulizidi kupiga kwa nguvu,alihisi kuishiwa nguvu za miguu,Issa alikuwa amekaa juu ya makochi anamuangalia kwa macho yaliyotia huruma.
“Issaa!”
Akajikaza na kuita.
“Marietha”
Moyo wa Issa bado haukutaka kukubali kwamba umeachwa,ndiyo maana alifunga safari mpaka nyumbani kwao ili kutaka kujuwa ukweli wa mambo ingawa ulikuwa wazi,hata hivyo habari za ndoa ya Marietha alizisikia kwenye vyombo vya habari,bado aliendelea kutafakari habari hizo ni kama uvumi wala hazikuwa na ukweli wowote ule.
Hekaheka zilizokuwa ndani ya nyumba aliziona na alijuwa kivyovyote harusi itafungwa,alitaka kujaribu kuizuia ili Marietha arudi kwake sababu alimpenda mno.
“Issa umefuata nini?”
“Nimekufuata wewe Marietha”
“Hujui kuwa naolewa?”
“Naelewa lak..”
“Lakini nini Issa?”
“Tafadhali naomba ufikirie tulipotoka hata kwa nukta moja kumbuka nilipigwa risasi kwa ajili yako,umesahau mara hii”
“Naelewa,bado nakumbuka lakini siwezi kuwa nawewe Issa acha ibaki kuwa historia”
“Hujachelewa lakini”
“Issa,I’m so sorry”(Issa naomba unisamehe)
Uamuzi wa Marietha ulikuwa ni uleule, hakutetereka ilikuwa ni lazima ndoa yake ifungwe sababu maandalizi yalikuwa ukingoni, haikuwezekana hata kidogo kurudisha moyo wake nyuma ingawa alianza kuhisi unamuuma.

Fikra zake zikarudi nyuma kwa kasi ya mwewe akakumbuka maisha ya furaha waliyokuwa wanaishi na Issa,ni kweli walipendana kama mapacha.Na isingewezekana hata siku moja ingetokea mtu kuwatenganisha.Alivyokumbuka hayo machozi yalianza kumlenga, alijizuia kuwaza vitu vingine akiamini kuwa atabadili mawazo.
“Issa naomba uwende tafadhali”
Marietha aliongea huku akibubujikwa na machozi,Mama yake pamoja na ndugu zake walikuwa pembeni wanamtizama,walikuwa ni kama wanaangalia sinema ya kuigiza tena ya kihindi.
“Mar..”
“Iss..a please,naomba uwende siwezi siwezi siwezi nimesema siwezi kuwa nawewe tena.Naomba unielewe”
“Kumbuka japo ki…”
Issa alilia kwa uchungu akateremka chini kwa magoti akamsogelea Marietha na kuishika miguu yake.
“Issa simama uwen…de”
Baadhi ya wanawake waliokuwa pembeni walimuonea huruma na waliguswa,machozi yaliwalenga lakini hawakuwa na uwezo wa kumsaidia.
“Marie..tha”
Issa aliita kwa kwikwi huku akimwaga machozi kamasi zinamtoka,alikuwa akilia kama mtoto mdogo huku akiwa amepiga magoti.
Hiyo ilimfanya Marietha ashindwe kuvumilia akamsukumiza na kukimbilia chumbani akafunga mlango na kuanza kulia machozi,Issa hakustaili kusalitiwa kwa namna moja ama nyingine sababu tangu amjue hakuwahi kumfumania mbali na hapo Issa hakuwa na mazoea ya karibu na Mwanamke wa aina yoyote ile,hiyo ndiyo ilimfanya aumie mtima zaidi.Alitamani mambo yapinduke arudi awe na Issa wake lakini haikuwezekana,maji alikuwa keshayavulia nguo ilikuwa ni lazima ayaoge!
Issa alivyotaka kusimama kumfuata Marietha alizuiwa na kutolewa nje,jinsi picha lilivyoonekana kulikuwa kuna uwezekano mkubwa wa ndoa kuhairishwa ndio maana Issa akafukuzwa kama mwizi.
“Ebwana toka basi.Eboo nywele zile kama mizizi ya bangi,chefuu”
Issa alisindikizwa na matusi mpaka nje ya geti!
******

Kulikuwa kuna msongamano mkubwa wa magari siku hiyo ya Jumamosi jioni ya saa kumi,barabara ya Samuni Joma ilifungwa na mapikipiki yalikuwa yakisafisha njia,baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walidhani wenda kuna msafara wa Raisi.Kama Deo alivyopania kutingisha jiji la Dar es salaam na ndivyo ilivyokuwa,alikodi pikipiki nyeupe saba na askari wote walipewa taarifa juu ya harusi hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashra mbalimbali jijini, ndiyo maana magari yalisimamishwa.Pikipikipi zilitangulia mbele kisha mabenzi matatu kupita ambapo Benzi nyeusi ya katikati alikuwa Deo Karekezi na mpambe wake Junior Saranga,muda wote walikuwa wenye nyuso zenye furaha.
Magari yakasimama nje ya kanisa kubwa la st.Joseph lililokuwa posta ambapo pia kulikuwa na mamia ya watu yanawasubiri.Kitendo cha Deo kuweka mguu wake juu ya ardhi matarumbeta yalipigwa.
Akatembea na mpambe wake na kuingia ndani ya kanisa,wakanyoosha mpaka mbele ya madhabau pembeni ya Mchugaji Elisha Isaya Kalumuna.
Deo Karekezi alikuwa amependeza mno suti yake aliiagiza nchini Canada,ilikuwa ni suti ya kipekee naya gharama.Aliyekuwa anasubiriwa ni bibi harusi Marietha ili ndoa ifungwe.
“Kaka vipi tena?”
Mpambe wake Junior Saranga akiwa nyuma alinong’ona, mpaka dakika arobaini zinapita Marietha hakuonekana na hakukuwa na dalili,Jambo lililowafanya waumini wa kanisa la mtakatifu Joseph waangalie saa zao za mikononi.Moyo wa Deo ulikuwa ukidunda kama kitenesi,akageuza macho yake kwa waumini na wageni.Hakuelewa aibu yake ataificha wapi endapo Marietha asipotokea siku hiyo!



Dalili za kutokutokea kwa Marietha zilikuwa waziwazi,sababu dakika kumi nyingine zilikatika za Bibi harusi kuingia kanisani hiyo iliwafanya waumini waanze minong’ono ya chini kwa chini.Deo Karekezi alihisi kuchanganyikiwa,hakuelewa ingekuwaje endapo Marietha asingetokea siku hiyo ya furaha katika maisha yake,ingekuwa aibu kubwa mno sababu aliwaalika watu wengi wenye heshima zao.Macho yake yalikuwa mlangoni muda wote, uso wake ulionesha kujawa na wasiwasi mkubwa,tayari alikuwa amekata tamaa ya kufunga ndoa.
“Pii pii pii piiii pii piiiiiiii pii piiiiiii”
Kelele za honi zilisikika nje ya kanisa,Moyo wa Deo ukapiga sarakasi kwa furaha,hazikupita hata sekunde tatu akamuona mwanamke mrembo kavaa shela kubwa lililokuwa limeshikiliwa nyuma yake.
Alikuwa ni Marietha akiwa katika nyuso yenye furaha,siku hiyo alipambwa balaa.Wanakwaya walifanya kazi yao vizuri waliinua matarumbeta na kuyapuliza,ndani zilijaa nderemo za vifijo.Tabasamu la Deo lilichanua akazidi kuonekana maridadi,Marietha akasogea mpaka karibu,wote wakamuangalia mchungaji.Ambapo aliongea maneno machache kisha pete zikaletwa.
“Mimi Deo Karekezi,nimekubali kumuoa Marietha kwa pete hii awe mke wangu kwenye shida na raha taabu na mateso mpaka pale kifo kitakapotutenganisha”
Pete taratibu iliwekwa kidoleni mwa Marietha,hapo ndipo waumini walishindwa kuzizuia hisia zao.Kelele za wanakwaya zilisikika pia.Kila kitu kilichokuwa kinatokea kwa Deo kilikuwa kama ndoto, hakuamini kwamba kuanzia siku hiyo Marietha atakuwa wake wa maisha.Pete nyingine ikawa imebaki, zamu ya Marietha ilifika ya kuweka pete kwenye kidole cha mume wake wa ndoa mtarajiwa Deo Karekezi,alimuangalia Deo machoni kisha kuanza kupepesa macho yake kwa waumini.

Ghafla mapigo yake ya moyo yakaanza kubadilika, uti wake wa mgongo akauhisi umepigwa na ubaridi.Akahisi kama mkono wake umepalalaizi,nyuma kabisa alimuona Issa analia machozi ya uchungu moyo ulimuuma mno.Nafsi yake ilimwambia aache kitu anachokifanya amkimbilie Issa kwani bado hajachelewa, akakumbuka filamu ya ON MY WEDDING DAY jinsi Jesca Abel alivyokatisha ndoa ya mtoto wa Raisi Buchanan baada ya kutokeza kanisani,picha zikawa zinamiminika kichwani mwake kama maji,akawaangalia waumini wote.Deo aliyatumbua macho yake akiwa mwenye wasiwasi, uwezekano wa Marietha kughairi kumvika pete kulimaanisha harusi kuharibika siku hiyo na jambo hilo lilikuwa mbeleni kutokea sababu hata yeye alivyogeuza shingo yake alimuona Issa.
“Marietha”
Nandy,mpambe wa Marietha aliita kwa sauti ya chini akiwa nyuma yake baada ya kumuona bibi harusi anasuasua.Waumini wote walibaki kumtizama.Mchungaji aliendelea kurudia rudia maneno yake lakini akili ya Marietha ilihama na kuacha mwili wake,alikuwa akimuangalia Issa asijuwe ni kitu gani akifanye,uamuzi ulikuwa kwake mwenyewe kusuka au kunyoa ingawa hakuelewa kipi sahihi kwa wakati huo,ilikuwa ni lazima achague kitu kimoja kati ya hivyo viwili.Akamgeukia Deo na kumtizama kwa kama sekunde mbili.
“Ndio nimekubali kwa pete hii awe mume wangu kwenye shida na raha tabu na mateso mpaka pale kifo kitakapotutenganisha”
Marietha akamvika pete ya ndoa Deo,kama agano la kuwa mwili mmoja lilivyoandikwa kwenye Biblia.Kuanzia hapo zilisikika tarumbeta kwa kwenda mbele,watu walioudhuria harusi ya Deo ilielekea waliipania sababu wakati wote walikuwa wana kamshange sio masihara!
Deo hakuamini kama tayari Marietha ni mkewe na Marietha kwa upande wake ilikuwa hivyohivyo,ilikuwa kama utani vile kumbe ndiyo kweli.Taratibu wakatoka nje huku matarumbeta yakiwa nyuma yao.Walivyofika nje wakasimama ili kupeana mikono na wageni waalikwa na baada ya hapo waliingia ndani ya magari kwa ajili ya kwenda kupiga picha za kumbukumbu.

*****

Katika siku ambayo hatokuja kuisahau katika maisha yake ni siku hiyo ya Jumamosi Marietha alipofunga ndoa na Deo,bado aliamini yu ndotoni na baadaye atazinduka na kumkuta Marietha wake pembeni lakini haikuwa hivyo,Marietha alikuwa ameolewa kweli nayeye mwenyewe alishuhudia akiwa kanisani,hakutaka kuendelea kukaa ndani ya kanisa sababu angeumia zaidi.Kama ubongo wa Issa siku hiyo ungepimwa CT scan basi angepelekwa milembe sababu akili yake yote ilivurugika,akawa kama mwendawazimu,alitembea kichwa kikiwa chini anaongea mwenyewe huku akilia machozi,akavuka barabara bila kuangalia upande wa pili.
“Huuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu”
Zilikuwa ni kelele za matairi na lami, lori kubwa la kampuni ya Soda Pepsi lilikuwa linapiga kelele,matairi yalikuwa yanajikwaruza juu ya lami,dereva akijaribu kufunga breki ya ghafla.Wakina mama waliokuwa pembeni waliweka mikono yao kichwani,Wengine waliziba midomo yao.Ambao hawakuweza kuangalia walifumba macho.Ilikuwa ni ajali Mbaya, Issa alikuwa anaelea juu kama karatasi ametupwa, aligongwa vibaya sana akadondoka upande wa pili ambapo alifikia kichwa,kikapasua damu zikaruka.
Ilikuwa ni ajali ya kutisha!Damu nyingi zilikuwa zinamtoka mdomoni na puani anatafuta pumzi lakini wapi,watu wakaanza kusogea na kumzunguka.
“Jamani mpeni hewa”Mzee mmoja akasema.
“Hewa tena?Tunahitaji msaada wa gari haraka sana”
“Jamani mwenye gari,huyu mtu atakufa”
“Mimi hapa nina gari”
“Iko wapi?”
“Ile pale kirikuu”
“Kirikuu ndiyo nini?”
“Twende twende twende,utajuwa hukohuko”
Kama Issa angepona basi labda kwa muujiza wa Mungu,alikuwa amepasuka vibaya sana kichwani na mdomo wake umefumuka kama nguo iliyochanwa,uso wake haukutambulika vizuri.
“Gruu gruuu”
Issa ndiye alikuwa anakoroma kama kondoo anayechinjwa,ni dhahiri kwamba Israel mtoa roho za watu alikuwa mita chache kumchukuwa.Alibebwa na wakina baba wenye roho ngumu mpaka kwenye Kigali kidogo cha kubebea mizigo alimaarufu kama kirikuu,akapakiwa nyuma wanaume wanne wakaruka nyuma.Dereva akakimbilia kwenye usukani,jinsi alivyolitoa gari lake haikuwa kawaida, ilikuwa kidogo nayeye asababishe ajali nyingine.
“Kifo eeeh tunatembea nacho kaka”
Dereva alianza stori akibadili gia na kupenya penya katikati ya magari.
“Aisee huyu jamaa sidhani kama atapona,Mungu wangu”
Mwenzake nayeye akatia neno,sababu bado walikuwa maeneo ya Posta kwao ilikuwa rahisi kwenda hospitali ya ‘Ocean Road’gari ikaingia hospitalini,wanaume waliokuwa nyuma wakaruka kabla ya gari halijasimama vizuri,wakaanza kukimbia huku wakipiga kelele mpaka mapokezi.
Wauguzi wa kihindi wakatoka mkuku mkuku mpaka kwenye gari wakiwa na machela,hata wao walishtuka hawakuwa na uhakika na mtu huyo kama alikuwa hai au nafsi yake ilikuwa imechukuliwa tayari.Haraka wakamtoa na kumuweka juu ya kitanda chenye magurudumu kwa chini, wakakisukuma mpaka ndani.
***
Wakati Issa anashindana na roho ya umauti akiwa mahututi siku hiyo yeye Marietha alikuwa na furaha kupita kiasi baada ya kutoka kufunga ndoa na Deo Karekezi, tayari walikuwa studio wakipiga picha za kumbukumbu my fear,Mikocheni.Hakuwa na habari na Issa.Walishikana viuno na kunyonyana ndimi huku picha zikimulikwa,Deo akambeba na picha za mnato zikaendelea.Baada ya hapo walirudi ndani ya magari na safari ya kwenda ukumbini ikaanza hapohapo.
“Marietha nakupenda sana Mke wangu”
“Kuanzia leo usiniite tena Marietha niite mke”
“Okay wife”
“Haha ha ha haaa”
Walikuwa ndani ya gari jioni hiyo ya saa kumi na mbili wakiwa wenye furaha sababu ndoto yao ya miaka mingi ilikuwa imetimia tayari tena bila uchawi wala ndumba,Marietha akamvuta karibu Deo kumaanisha kuwa anaomba denda.Hicho ndicho kilichotokea,wakaanza kubadilishana mate, kila mtu akimsikilizia mwenzake sababu wote waliyafumba macho yao.
“Ah jamani inatosha,mnataka mmalize uroda humuhumu.Bakisheni na baadaye”
Mpambe wa Marietha aliyeitwa Nandy akaweka utani kidogo,Mwanamke huyu alikuwa ana lips pana kiasi, mdomo wake ulimaliza kikopo kizima cha ‘lip shine’mbali na hapo mdomo wake uliendana na matendo yake,Nandy alikuwa mtu wa kuropoka na mchangamfu ndiyo maana Marietha alimchaguwa awe mpambe wake akiamini atachangamka siku hiyo.
“Tuache kwa raha zetu”
Marietha nayeye hakukosa neno wote wakatabasamu,ilikuwa siku ya furaha sana kwake.Tangu azaliwe hakuwahi kufurahi kama siku hiyo ya harusi yake,muda wote alimlalia Deo kifuani.

Kitendo cha magari kuingia ndani ya maegesho ya Mwika Hall maeneo ya Sinza,kelele zilisikika kwenye vipasa sauti, siku hiyo alikuwa Mc maarufu nchini Tanzania aliyeitwa, Swai G. Alikodishwa kwa pesa nyingi sana.
“Haya maharusi wetu wanaingia sasa,Dj Dj Dj Dj Dj tupe nyimbo ya Kwaito”
Kwa mbwembwe na furaha bwana na bibi harusi wakaanza kucheza kwa pamoja huku wakiingia,hiyo iliwafanya wageni waalikwa waungane nao.Ilikuwa ni harusi ya aina yake ambayo pia ilirushwa BECKER TV moja kwa moja.Ilikuwa ni harusi iliyokuwa ya mfano wa kuigwa sababu hata matajiri na wafanyabiashara mbalimbali walikuwepo,hiyo iliwafanya pia mapaparazi wasogee eneo hilo ili kutafuta habari za kuuza siku inayofuata.
Siku hiyo watu walikunywa na kusaza walafi walibeba kwenye mifuko wakale majumbani mwao,wenye uchu wa pombe walikunywa na wengine wakajikojolea lakini hata hivyo chakula na pombe vilibaki.

Saa sita ya usiku juu ya alama ilivyofika Bwana na bibi harusi wakaruhusiwa kwenda kupumzika,wakaingia ndani ya gari lao lililokuwa limepambwa vizuri.Mpaka hapo ilikuwa harusi ambayo imevunja ‘record’na hivyo ndivyo mwanaume huyu mfanyabiashara alitaka iwe.Marcedez Benz nyeusi ikatoka ukumbini ikiwa na maharusi na dakika arobaini na tano baadaye walikuwa nje ya hotel ya nyota tano,Kilimanjaro Hotel,wakapita mapokezi na kupewa kadi za milango.
Kitendo cha kuingia chumbani hapohapo walifuatana midomoni na kuanza kupigana mabusu ya fujo,ilikuwa ni siku yao ya furaha na ilikuwa ni lazima wajipongeze.Wakasogezana mpaka kitandani na kujitupa hivyohivyo na viatu, kibarua kiliendelea cha kunyonyana midomo kwa papala.Shela la Marietha likaanza kuvuliwa taratibu likatupwa kando mwenyewe akapeleka mikono yake akachomoa viatu vyake,akatoa nguo ya juu.Siku hiyo walivua nguo harakaharaka na Deo aliinama na kufungua kamba za viatu akatupa viatu kando akachojoa koti la suti na shati vilevile,akamvuta Marietha wakaendelea kunyonyana ndimi kama makinda ya njiwa,walikuwa wenye furaha kupita kiasi.Damu zilikuwa zinatembea kwa kasi isiyo ya kawaida kila mtu akili yake ilihama.
“Deoo”
“Mhh”
“Nakup...e.nda”
“Mimi pia”
Wakaendelea tena kupigana mabusu huku wakishikana kila sehemu ya miili yao,mkono wa Deo ukapita mpaka juu ya kifua cha Marietha akaanza kuchezea chuchu za juu nyeusi hapo ndipo Marietha alipoanza kuhema juu kwa juu, mbaya zaidi mkono mwingine wa Deo ukapita mpaka chini,katikati ya miguu yake.Sehemu alizoshikwa Marietha haikuwa rahisi kwa mwanamke yoyote yule kuchomoka hata kama angekuwa mke wa mwanajeshi ili kuwa ni lazima apanue miguu hivyo ndivyo Marietha alivyofanya,kwa hiyari yake akatoa ‘skin tight’ aliyokuwa ameivaa akabaki na boxa nyeupe hiyo haikuwa na haja ya kubaki mwilini,akaweka pembeni.Deo nayeye akafanya hivyohivyo akatoa suruali na kubaki na boxa,mambo yalikuwa mukidemukide kwa wawili hawa,Marietha hakutaka kuonekana mzembe, akachukuwa mkono wake na kumtoa nyoka wa Deo nje ambaye tayari alikuwa amesimama imara.Akaanza kumsugua,alivyoona anapata tabu sana akatoa boxa akamkamata nyoka vizuri,akaipanua miguu na kumtumbukiza ndani ya shimo lake.Hapo ndipo mambo yalipoanza,Marietha alikuwa amelala chali,alichofanya Deo ni kuuchukuwa mguu wake mmoja na kuuweka begani mashambulizi yakaendelea,hiyo haikusaidia akampindua, kiuno cha Marietha kikawa juu akawa ameshika pembe ya kitanda yaani akamuweka chuma mchicha,kwa Kiswahili cha uswazi!
“Ahh aaah mmmh De.. aaah I lo..ve u”
Hapo ndipo Marietha alihisi anafikishwa vizuri,Kiuno chake kilikamatwa vizuri na Deo,Mashambulizi yakaendelea.
***
“Baby amka ujiandae,ndege itatuacha”
“Whaaat,ndege?”
“Ndiyo ndege”
“Kwani tunaenda wapi?”
“Fuata nyuki ule asali,usiulize maswali.Utajuwa hukohuko”
Deo alikuwa wa kwanza kudamka siku inayofuata ya Jumapili,ilikuwa yapata saa nne kasoro tisa.Marietha alikuwa bado kitandani kajifunika na shuka anaitizama pete yake ya ndoa kidoleni.
“Tangulia kuoga nakuja”
“Okay baby”
Deo akaingia bafuni.Marietha alitabasamu na kurudi kitandani, bado alikuwa na uchovu.
“Griii griiii,Griiii griiiiii”
Simu ilimshtua ikiwa inaita,ilikuwa ni simu kubwa ya Deo pembeni kwa juu ya kitanda.Akainua kichwa na kuichukuwa.
“Baby simu yako”
“Nani anapiga?”
“Sijui, ni namba ngeni”
“Pokea”
Deo alijibu akiwa bafuni anaoga,akatoa ruksa.
Marietha akaivuta,kwa kuwa ilikuwa simu ya kisasa yaani ‘screen touch’akaweka mkono kwenye kioo na kusogeza mbele alama ya kijani,akaweka simu sikioni.
“Halloo Baby mimi Leila,nipo Mwalimu Nyerere Airport.Guess what?Nimerudi supriseeeee.Njoo unichukuwe”
Marietha alihisi mwili wake umepigwa ganzi,maneno ya mwanamke aliyekuwa anazungumza upande wa pili yalipita ndani ya masikio yake bila chenga!



Mapafu ya Marietha taratibu yalianza kujaa hewa,alihisi kama amepigwa sindano ya kistapen mwilini.Alihisi damu yake imeacha kutembea,akawa kama amepigwa na shoti ya umeme maneno aliyokuwa anayasikia yalimuumiza mtima.Hapohapo akaweka simu kando bila kuikata,akahisi mashavu yake yanalowana,yalikuwa ni machozi ya uchungu.Deo alikuwa bafuni hakuelewa chochote kinachoendelea alivyotoka bafuni alishtuka alivyomuona Marietha analia machozi.
“Marietha vipi?mbona unalia?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Deo lililomfanya azidi kuhisi uchungu,kwake alilitafsiri swali hilo ni kama unafki alimtizama Deo kwa macho yaliyojaa majuto.Nafsi yake ilijuta kukubali kuolewa na mwanaume huyu ambaye alidhani anampenda,alivyomkumbuka Issa ndipo alipoachia kwikwi kwa nguvu huku kamasi nyepesi zikimchuluzika.
“Marietha”
Deo akaita tena lakini Marietha aliendelea kumwaga machozi,hiyo ikamchanganya sana akili,akamsogelea karibu na kukaa kitako kitandani.
“Kuna msiba au?Marietha nieleze basi.Kuna nini mbona unalia?”
Kila alivyotaka kuongea alibanwa na kitu kohoni,zilikuwa ni hasira kali.Marietha alikuwa na hasira mbaya sana,siku zote alikuwa akionywa na mama yake kuwa aweze kujizuia vinginevyo atapata matatizo makubwa sana maishani.Ndiyo maana alijitahidi kwanza kuzishusha kabla ya kuongea kitu chochote,alibaki akimtizama Deo macho yake yalikuwa mekundu na tayari yamevimba,machozi yanamchuruzika yakapita mpaka kifuani kwake.
“Tu..mbo li..nauma”
“Tumbo?”
“Nd..io”
“Limeanza saa ngapi?Vaa twende hospitali”
“Hap..na usijali”
Alishaelewa angemuuliza Deo kuhusu simu iliyopigwa kivyovyote vile angejitetea na asingepata jibu ambalo lingemridhisha sababu alijuwa wanaume hawakosi utetezi,hakutaka kukurupuka ndiyo maana akajifanya kuumwa tumbo.
“Twende hospitali”
“Ha..pana ni la period”
“Linauma sana”
“No”
Alikuwa tayari kuumia ndani kwa ndani kwanza ili baadaye apate ukweli,akatoka taratibu kitandani akiwa amejifunga shuka mpaka bafuni huko alifungua bomba la mvua na kuanza kulia kwa uchungu, akaserereka mpaka chini akitumia ukuta,kifupi alijuta.

Kitu kilichomshtua Deo ni simu yake,ikaita alivyoichukuwa alikuta namba ngeni,akaipokea na kuiweka sikioni.
“Yes Halloo”
“Darling,ni mimi Leila upo wapi?Nimerudi Tanzania tayari Deo i miss you my love”
“Leila,real?is that you”(Leila,kweli ni wewe)
Deo nayeye akajibu kimombo,kutokana na elimu aliyokuwa nayo pamoja na kusafiri nje ya nchi mara kadhaa kulimfanya ateleze nacho kama alizaliwa uingereza vile ingawa hakuwa mzungu.
“Yeah sweatheart”
“Uko wapi now?”
“Niko airport, please come and pick me up”
“Okay nakuja”
“I love you”
Deo alikata simu akiwa mwenye furaha kuliko kawaida.
Alikuwa na kihoro cha kufika uwanja wa ndege dakika hiyoihiyo.Akavaa harakaharaka.
“Marietha natoka kidogo kuna mtu naenda kumuona,nitarudi sasa hivi”
Ilikuwa ni kama amegusa kidonda chake,Marietha alianza kulia machozi sababu maongezi aliyokuwa anazungumza mume wake aliyasikia kwa masikio yake yote mawili,ukaribu wa bafu na chumba ulifanya asikie kila kilichozungumzwa.Marietha hakuwa mwanamke mjinga alielewa Deo anaenda kwa mwanamke aliyempigia simu na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
“Poaaaa”Akajibu,akijikaza.
Alivyosikia mlango umefungwa akajua tayari Deo ametoka,akaendelea kulia machozi ya uchungu.Kilio chake hakikukoma.Alianza kujuta kuolewa na Deo,hakuelewa angeishi vipi mbeleni sababu hiyo ilikuwa siku ya kwanza tu baada ya ndoa.
Hapo ndipo alipojuwa kuwa Deo alikuwa ameficha makucha yake.Marietha alianza kuichukia ndoa yake kabla haijachanganya,alitamani siku zirudi nyuma aghairi harusi lakini haikuwezekana na mbaya zaidi alifunga ndoa ya kikristo,haikuwa rahisi kuachika labda kifo peke yake.Hapo ndipo alipohisi kuchoka akili mpaka mwili.Akatoka bafuni akiwa na mawazo mengi kichwani, hakuelewa ni kitu gani akifanye,akajibwaga kitandani na kuendelea kuwaza,tayari ndoa yake iliingia dosari.Kilichomzindua ni simu yake iliyokuwa mezani,alivyoichukuwa aligundua ni Deo ndiye anayepiga.Akatafakari kwa muda kidogo,akaipokea na kuiweka sikioni.
“Marietha,vipi tumbo?”
Deo aliuliza simuni.
“Sasa hivi ninaendelea vizuri”
“Una uhakika?”
“Ndio”
“Okay ni hivi.Hatutoenda fungate tena kuna mambo yameingiliana kidogo ya kiofisi”
Moyo wa Marietha ukazidi kupiga kwa nguvu,maneno ya Deo yalimfanya aelewe kila kitu.Na hiyo ilimpa jibu la moja kwa moja kuwa Deo yupo na mwanamke mwingine.Alitaka kulia lakini akajikaza kisabuni!
“Marietha umenisikia?”
Deo alihoji tena sababu Marietha alikuwa kimnya.
“Ndiyo”
“Nitakuja kukwambia kitu”
“Sawa”
Uchungu uliom-bana Marietha haukuwa na mfano wake hata kidogo,hakuwahi kuumia katika mapenzi kiasi hicho.Akiwa katika mawazo mengi ghafla sura ya Issa ikamjia,akamuona kanisani alivyokuwa analia,akajiona ni mkosaji mbele za Mungu,alielewa ni kiasi gani alimuumiza moyo,Issa hakustaili kupewa adhabu kama hiyo.Hapohapo akachukuwa simu yake na kutafuta namba za Issa lakini hakuzipata,akagundua kwamba alizifuta ili asiwe anamuwaza sababu tayari alikuwa anaenda kuyaanza maisha mengine ya ndoa.
“No,lazima niende kwa Issa nikajaribu kumuomba Msamaha”
Hivyo ndivyo alivyosema Marietha ilikuwa ni lazima akaonane na mwanaume huyo ingawa hakuwa na uhakika kama angeweza kuzungumza naye,alimfahamu Issa alikuwa ni mwanaume mwenye wivu katika mapenzi, isitoshe ni mwepesi kukasirika.
Hakuelewa ni aina gani ya msamaha amuombe ili mradi awe naye tu hata kwa kumpa furaha sababu tayari alishakuwa mke wa mtu, hilo alijuwa hatoweza kulibadilisha kamwe.Akasimama wima na kuliendea kabati,bahati nzuri alikuta kuna nguo tayari na aliamini kivyovyote vile Deo ndiye aliyenunuwa.Akaziweka mwilini,akavaa kila kitu na safari ya kwenda Manzese ikaanza dakika hiyohiyo.
Nje kulikuwa na taxi akaita moja wapo.
“Kaka,nipeleke Manzese Tiptop”
“Tiptop?”
“Ndio,bei gani?”
“Kule na hii jam.Arobaini hapo”
“Sawa twende”
Marietha akafungua mlango wa nyuma na kuingia,taxi ikaanza safari hapohapo.Kichwani alikuwa ana mawazo mengi sana.Hilo lilikuwa wazi kwamba Marietha alimpenda Issa kutoka ndani ya moyo wake,kuwa na Deo ilitokana na tamaa zake na vishawishi vya marafiki ambao walidhani pesa ndiyo kila kitu katika mapenzi kwa mara ya kwanza alikubaliana nao lakini siku hiyo alilia mwenyewe na moyo wake.Alijuta kutokuusikiliza moyo wake unataka nini,mkumbo ulimponza ndiyo maana alikuwa akimwaga machozi akiwa ndani ya taxi.
“Dada upo sawa?”
Dereva alimuhoji abiria wake baada ya kusikia kilio cha kwikwi,akaweka kioo cha katikati vizuri ili amuangalie mteja wake vizuri.
“Wewe acha tu kaka angu”
“Una tatizo gani?pengine ninaweza kukusaidia”
“Ha..pana usijali”
Dereva hakutaka kuhoji zaidi sababu haikuwa kazi yake ingawa alitamani kutoa msaada kwa mrembo aliyem-beba.

Walichomoza barabara ya Moroco na kuipita kinondoni.Dereva akazidi kuendesha gari huku akizidi kumdadisi mteja wake amwambie ni kitu gani kinamsumbua lakini hakuambulia kitu, ikamfanya asiulize zaidi kwani kazi yake ilikuwa ni kumfikisha abiria sio kuwauliza maswali.Dakika kumi na tisa baadaye taxi ikasimama Manzese,Tiptop.Marietha akatoa pesa na kumlipa dereva ujira wake.
“Nikusubiri ama?”
“Kama hauna haraka unaweza kunisubiri”
“Ndiyo kazi yangu,nitakusubiri tu”
“Sawa”
Marietha akashuka na kufuta machozi,hakutaka watu wamshangae.
Akavuka barabara mpaka upande wa pili ambapo breki ya kwanza alifika Manzese sokoni,sehemu ambayo Issa anauza mitumba yake.Cha ajabu hakumuona,kwa kuwa nyumbani kwake alipajuwa haikumpa shida akanyoosha na kuufikia mlango ambapo aligonga bila mtu yoyote yule kuitikia,hakukata tamaa akaendelea kuugonga mlango tena na tena,lakini wapi!Watu waliokuwa wanapita walimshangaa Marietha ambaye aliendelea kugonga bila kuitikiwa,ghafla akapita mtu aliyemfahamu.
“Chogo!Chogo”
Marietha akaita lakini jinsi Chogo alivyogeuka aliogopa,alikatwa jicho kali la chuki na kumfanya aogope zaidi,alielewa ni lazima marafiki zake na Issa wangemchukia kwa kitendo alichokifanya kwa rafiki yao lakini hiyo haikumfanya ashindwe kueleza shida yake iliyomtoa alipotoka.
“Issa yupo?”
“Unaongea na mimi?”
Sio kwamba Chogo hakujuwa kuwa anaulizwa yeye,alikuwa na hasira na mwanamke huyo.Jinsi alivyotokeza kwa Issa mara ya mwisho kwa mikogo na kumtangazia harusi kulimfanya alitafsiri swali hilo kama kejeli ama dharau,ndiyo maana nayeye akajibu kwa dharau.Chogo alikuwa maskini lakini mwenye kiburi.
“Ndio naongea nawewe chogo”
“Embu acha dharau basi,chukuwa time.Jikatue”
“Chogo”
“Alafu sina utani nawewe jina langu sio Chogo,acha mazoea namimi kabisa jichenge tu”
Chogo alimaliza kuongea na kuondoka zake akiwa na furushi la nguo mikononi mwake.Marietha alimfuata nyuma sababu alitaka kujuwa ni wapi Issa alipo.
“Chogo..Chogoo”
“Wewe demu usinitafutie matatizo ujuwe,ohooo!”
“Nahitaji kuongea na Issa”
“Acha unafki basi”
“Mimi sio mnafki”
“Issa sijui alipo,aliondoka hapa jana jioni”
“Hakusema anaenda wapi?”
“Hakusema ndio na kwenye simu hapatikani”
Bado Marietha hakutaka kuyaamini maneno ya chogo hata kidogo,alitulia kimnya akawa kama anatafakari kitu,aliamini kwamba Issa amekasirika na hakutaka hata kumuona.Kwa jinsi hali ilivyokuwa aliamini kuwa atakuwa amerudi mkoani kwao Morogoro,jambo hilo alilipa asilimia mia moja.
“Kwenye simu pia hapatikani?”
“Ebwana eeh,unaniwekea kiwingu.Nishakujibu”
Chogo alijibu kwa hasira ilionekana alimchukia sana Marietha hakuelewa ni kosa gani Issa kalifanya mpaka mwanamke huyo ampige kibuti na kumuacha,mapendo ya Issa kwa Marietha yalikuwa ni kama kioo aliyaona na swala la Marietha kuhusu kuolewa hata Chogo alilifahamu vizuri.
“Nenda basi,kakae na mumeo”
Hivyo ndivyo Chogo alivyosema, Marietha aliumia moyo kupita kiasi,alimuangalia Chogo akashindwa kujibu kitu.Kuendelea kubaki na kumuhoji maswali Chogo ilikuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu,aliamini kwamba hatopata jibu sahihi la kitu anachohitaji.Akageuka na kuondoka zake.
“Mademu wengine bwana”
Chogo akaropoka makusudi,maneno hayo yakamfikia Marietha lakini hakutaka kugeuka ingawa aliumia,akavuka barabara akiwa na mawazo chungu mzima.Akarudi mpaka kwenye taxi ambapo alimkuta dereva amevuta kiti,ameuchapa usingizi.
“Turudi”
“Hotelini?”
Dereva akakurupuka na kurudisha kiti sawa.
“Ndio”
Marietha akaingia ndani ya gari na safari ya kurudi hotelini ikaanza hapohapo.
***
Hakuna mtu yoyote aliyejuwa ni wapi Issa alipokuwa sababu aliondoka kimnyakimnya bila ya kumwambia mtu yoyote yule.Siku ya kwanza ilivyopita walichukulia kawaida lakini kulivyokucha siku inayofuata watu waliulizana na hakukuwa na mtu aliyejuwa lolote kuwa alikuwepo kanisani na kugongwa na gari na wakati huo yupo mahututi hospitalini.Wengi walidhani yupo kituoni amefungwa na mwanaume mfanyabiashara Deo.Walivyounganisha matukio wakajuwa ndiyo lazima itakuwa hivyo.
“Alitoka hapa siku ya Jumamosi jioni.Na ndiyo hiyo siku ambayo Marietha alikuwa anaolewa.Nina mashaka yupo kituo cha polisi”
Rafiki yake mwingine na Issa aliyeitwa Kishipa alitowa wazo,kutokana na ubishi wake ilifanya wenzake wam-batize jina hilo.
Kishipa alikuwa ana uwezo wa kubishana hata na watu ishirini akashinda,alikuwa mwembamba mwenye afya mgogoro lakini kwenye ugomvi yeye ndiye wa kwanza kuanzisha.Afya yake na vitu alivyokuwa anafanya vilikuwa ni vitu viwili tofauti.
“Kishipa kaongea pointi.Nina uhakika Issa yupo ndani,kafungwa”
“Inawezekana”
“Inabidi mmoja wetu tumchangie pesa ya nauli aende kituoni pale Buguruni akaangalie”
“Poa poa,haina noma!”
Swala la mtu mmoja kuchangishiwa pesa ili aende kituo cha polisi ndilo lilifanyika kwa wakati huo.Ndani ya dakika arobaini ikapatikana shilingi elfu nane na mia saba.
“Hiyo pesa nyingi sana,ukimkosa hapo.Zunguka vituo vingine”
Kaiza rafiki yao mwingine alikabidhiwa pesa akaanza safari yake ya kwenda kumsaka rafiki yao kipenzi, Issa.
***
Miyenendo ya Deo ilibadilika, kuanzia siku hiyo simu zilikuwa hazibanduki sikioni na hakuzungumzia tena swala la fungate.Sio hivyo tu,Deo alikuwa ni mtu wa kutoka asubuhi na kurudi usiku.Marietha alipojaribu kumuhoji alipewa majibu ambayo hakuyaelewa hiyo ilimfanya atake kujenga hoja ya kutafuta sababu kwa maana hiyo ilikuwa ni lazima siku moja amfuatilie ajuwe ni wapi anashinda siku nzima.
“Lazima nijuwe ukweli.Sitaki kukubali,nitaomba talaka yangu hata kama dini hairuhusu acha niwe mkristo wa kwanza kufanya hivyo”Aliwaza!
Ilikuwa ni asubuhi ya saa mbili Deo alikuwa bafuni anakoga,alivyotoka alivaa nguo zake na kujipulizia marashi.
“Baadaye Love”
“Okay”
Deo akafungua mlango na kuondoka zake.
Kama mgambo Marietha akaruka kutoka kitandani,akavuta nguo zake kila kitu akaweka sawa,akatembea mpaka dirishani akatizama chini na kumuona Deo anaingia ndani ya taxi,hakutaka kupoteza wakati,akafungua mlango.
Akashuka ngazi mbilimbili akatoka mpaka nje nayeye akaita taxi.
“Fuatilia hiyo taxi ya nyuma”
“Hiyo ya Dula?”
“Hiyo hiyo”
Kibarua kikaanza mara moja.
“Hakikisha haitupotei”
“Poa sista”
Dereva akatii amri,akawa nyuma yao umbali wa mita kumi na mbili.Wakazidi kusonga mbele,Marietha alikuwa na usongo wa kutaka kujuwa ni wapi mume wake anaenda kila siku.
Wakaingia Mwananyamala wakazidi kufuatilia kwa nyuma,taxi ya mbele ikakunja barabara ya kuelekea Mwenge.Siku hiyo Marietha alijifananisha na mpelelezi ingawa hakuwahi kusomea kazi hiyo kabla.
Dakika kama ishirini baadaye Taxi ya mbele aliyokuwa amepanda Deo ilisimama nje ya hotel kubwa maeneo ya ubungo iliyoitwa Landmark Hotel.
Akamshuhudia Deo anashuka ndani ya taxi.
“Kaka,sikia nikirudi hotelini nitakulipa”
“Sista nipe hata buku tano ya chai”
Marietha akatoa noti ya elfu kumi na kumkabidhi dereva kisha akashuka,akatembea na kusimama pembezoni kwenye kona.
Moyo wake ulizidi kupiga kwa nguvu baada ya kumuona Deo anakumbatiwa na mwanamke mwingine,hapo ndipo alipata majibu kamili ya maswali yake kuwa Deo alikuwa akichepuka!



Ulikuwa ni kama mkuki wenye moto umetua ndani ya moyo wake ukamchoma vibaya sana,Marietha aliumia kusalitiwa uchungu aliohisi ulikuwa hauna kipimo chake.Hapo ndipo alipogundua ni kiasi gani Issa alipata maumivu kama yeye,machozi yalimbubujika.Deo alikuwa na mwanamke mwingine wanafurahi, tena wamekaa kwenye viti wameagiza pombe na kuanza kunywa,walicheka na kugongesha mikono yao.Ilionekana kuwa Deo alikuwa ana mahusiano na mwanamke huyo tangu miaka mingi sana ndiyo maana walifurahi kuonana tena,alijuta kupita kiasi.
***
Moyo wa Deo ulikuwa unakita kwa kihoro,alitamani apae afike haraka uwanja wa ndege ili aonane na Leila ilikuwa ni miaka mingi sana imepita tangu waachane nchini Uingereza kimasomo.Ndiyo maana alimsisitiza dereva akunjuwe goti aongeze mwendo ili wawahi uwanja wa ndege wampokee mtu huyo muhimu kwake,hakutaka kumchomesha mahindi sababu yeye ndiye alikuwa kama mwenyeji wake.Dakika arobaini na tano baadaye taxi ilifunga breki nje ya maegesho ya magari Uwanja wa kimataifa Mwl.Nyerere.
Deo akashuka mbiombio, kwa kuwa alikuwa keshamlipa dereva pesa yake hakuwa na haja ya kusubiri dakika nyingine zaidi,akachukuwa simu yake ili kumtafuta mgeni wake.Haikuchukuwa hata dakika mbili wakawa wameonana,jinsi walivyorukiana kwa furaha na kupiga kelele iliwafanya mpaka wasafiri wengine wawatupie macho.
“Oh My God! Deo, look at you.. you have gained weight,what do you eat?It seems Africa treats you well”(Mungu wangu,embu jiangalie,umenenepa,unakula nini,inaonekana Afrika inakupenda)
Leila aliporomosha ung’eng’e,kuishi sana Uingereza kulimfanya ajuwe kucheza na lugha hiyo.Aliongea kwa mapozi na madoido ya kisista doo huku akitingisha kichwa chake.
“Sio hivyo,nakula tu mboga zetu zilezile ugali dagaa kwa kwenda mbele na matembele”
“Ndio unenepe kiasi hicho rafiki yangu?”
“Ndio”
“Stop kidding”(Acha masihara)
“I’m not,by the way mabegi yako umeacha wapi?”
“Nipo hivihivi na hiki kibegi kidogo”
“Siku izi umekuwa mzungu kabisa”
“Haha ha ha haaa”
Wote walicheka na kufurahi,wakatembea mpaka kwenye maegesho ya magari huko walitafuta taxi na kukodi.

Leila na Deo walikuwa ni marafiki wa kufa na kuzikana,ungewaona ungedhani ni wapenzi sababu walijiachia sana,hata walivyokuwa masomoni uingereza.Leila alikuwa ana uwezo wa kwenda hata na chupi ndani ya chumba cha Deo lakini wasifanye chochote,walikuwa kama dada na kaka ingawa hawakuzaliwa tumbo moja.Mazoea hayo yalikuwa na kukuwa zaidi.Wakawa zaidi ya ndugu,walisoma kwa bidii mno walisaidiana kwenye masomo yao.Mpaka walipohitimu,Deo alipokea shahada ya uchumi na Leila yeye alichukuwa shahada ya mambo ya utalii,ilikuwa furaha kubwa sana kwa watu hawa wawili.Licha ya yote,Deo hakutaka kuendelea kubaki nchini Uingereza ingawa wazungu walimuhitaji,alitaka siku moja arudi Tanzania akaanze maisha yake nchini kwao,hakutaka kuwa mtumwa wa nchi za watu.Kwa upande wa Leila yeye hakutaka kurudi,siku chache alipata bwana wa kizungu,hiyo ikawa kama tiketi yake ya kubaki nchini humo na alirudi Tanzania kama kutembea tu.
“Heee Deo,umeoa?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Leila,baada ya kuona pete ya ndoa kidoleni mwa Deo.
“Ndio”
“Sio vizuri,hata kunialika”
“I was confused ndiyo maana,ila nitakuhadithia kila kitu,upo mpaka lini nchini?”
“Nitakaa kwa miezi miwili tu”
“Usijali,nitakwambia kila kitu sasa hivi inabidi ukapumzike”
Walifika Ubungo Hotel iliyoitwa Landmark na wote kushuka wakiwa wenye furaha iliyozidi kifani,Deo alifurahi kumuona Leila na Leila ilikuwa hivyohivyo kwake.Walikuwa na mengi ya kuongea siku hiyo ndiyo maana hata walipopata chumba walitoka nje kwenye mgahawa ili wazungumze.Hivyo ndivyo ilivyokuwa hata siku iliyofuata Deo alidamka asubuhi na kwenda Landamark Hotel bila kujuwa mkewe anamfuatilia nyuma.
“Nimekumbuka kitu,inabidi nimpigie mke wangu aje hapa,maana sijamwambia kitu chochote ilibidi twende fungate jana.Simu yako imenishtua”
“You are correct,you should tell her to join us..Mwite wifi”
Hapohapo Deo akatoa simu yake na kumtafuta Marietha hewani,simu iliita bila kupokelewa akapiga tena lakini ilikuwa vilevile.
“She is not picking?”Leila akauliza huku akiwa makini anamuangalia Deo usoni.
Akajaribu tena ikaita, Marietha akapokea.
“Marietha upo wapi?”
“Marietha?”
Deo akaita sababu upande wa pili ulikuwa kimnya.
“Ab..ee”
“Vipi mbona kama unalia?”
“Nipo sawa usijali”
“Naomba uje Landmark hotel sasa hivi,kuna mtu anataka kukuona mke wangu”
“Sa..wa nakuja”
Marietha alikata simu akiwa ndani ya taxi anarejea hotelini kupaki nguo zake ili atokomee asipopajuwa hivyo ndivyo moyo wake ulikuwa ukimsukuma uchukuwe maamuzi hayo,hakutaka kubaki na mwanamme msaliti ama Malaya ndani ya ndoa yake,alitaka kumtafuta Issa alipo kwa hali na mali kisha watoroke,bado alikuwa akitafakari ni kitu gani akifanye,siku zote kubali wito kataa maneno,baada ya kukumbuka huo msemo akamuamuru dereva taxi arudi LandMark hotel.Dereva akatii amri akazungusha usukani wakarudi walipotoka.Marietha alivyofika akajitahidi kutabasamu kidogo,sababu hakutaka kuhojiwa maswali,alimuelewa Deo.
“Marietha,umewahi kufika.Ulichukuwa pikipiki au?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Deo huku akichanua tabasamu.
“Leila huyu ndiyo mke wangu”
Kabla ya Marietha kujibu swali Deo akaanza utambulisho.
“Oh,She is pretty.Umejuwa kuchagua”
Leila alimwaga sifa baada ya utambulisho.
“Marietha,huyu ni rafiki yangu.Ni best yangu sana anaitwa Leila,tulisoma wote Uingereza.Ndiyo ameingia jana sorry kwa kutokuambia”
Baada ya utambulisho kuisha,waliagiza mishkaki na kuku wa kukaanga.Pombe kali zikawekwa mezani,wakaanza kujichana.
Mpaka inafika usiku walibadili viwanja kama vitano,Leila hakuwa mtu wa kutulia alikuwa kama popo,yeye ndiye alitaka kutembezwa jijini siku hiyo.Deo hakuwa na kipingamizi chochote kile.
“Mke wanguuuu amechoka Leila,tunahitaji kupumzikaaa bwaanaaa”
“Noooo,I said noooo,twendeee hapaaa wapi hapaaa,nikumbushee Maisha club”
“Siweeezi,siwezii kwenda na hizi nguooo club,kwanza kesho nitasafiriii nataka kwenda fungate na mkeee wanguuu,So please tuheshimianee,let us do it next timee”
“Unasafiri kwenda wapiiiii?”
“Honeymoon”
“Namimi nitaendaaaa,tutaenjoy hukooo hukooo sote”
“Sawa basi,inabidi ukapumzike kwa ajili ya safari”
“Fine”
Deo alikataa katakata sababu alikuwa bwii,pombe zipo kichwani anapepesuka ana ambaa ambaa na ukuta.Marietha ndiyo kabisa,kichwa chake kilikuwa kizito mno.Wakatoka na kuongozana ambapo Leila walimuacha Landmark Hotel na taxi hiyohiyo iliwapeleka Deo na Marietha mpaka Kilimanjaro Hotel, posta.Kitendo cha kufika chumbani kila mtu alijibwaga kivyake hakuna mtu aliyekumbuka kuvua nguo zake,kifupi walilewa tilalila.
****
Kichwa cha Marietha asubuhi kilikuwa kizito kama ndoo ya zege na kizunguzungu juu,mbali na hapo alihisi kichefuchefu cha kutapika,alikumbuka sana hali hiyo ilishawahi kumtokea miaka mingi sana iliyopita,alielewa ilikuwa ni ‘hangover’akasimama adoado na kuchukuwa mkonga wa simu uliokuwa mezani.
“Halloo naomba mchemsho wa supu ya kuku na ndizi mbili,chumba namba 86”
Alikuwa simuni anazungumza na muhudumu.
“Waambie walete mbili”
Deo nayeye akaagiza,ilionekana nayeye kichwa chake kilikuwa kizito vilevile ndiyo maana alihitaji mchemsho wa supu ili akate pombe za usiku wa jana.
Baada ya dakika tano mlango wao uligongwa,alikuwa ni muhudumu wa hotelini.Wakanywa na kuoga hapo ndipo hali zao zilikuwa nzuri kiasi.

Safari ya fungate bado ilikuwa ndani ya kichwa cha Deo na alitaka kufanya hivyo,akaandaa mazingira ya tiketi tatu ikiwemo ya Leila.Hakukuwa na muda wa kupoteza jioni ya siku hiyohiyo zilikuwa tayari na walikuwa wakijiandaa kwa safari.
“Tukutane Mwalimu Nyerere kesho asubuhi”
Deo alitoa maelekezo ya mwisho akimwambia Leila.
“Okay,umesema saa tatu asubuhi”
“Ndiyo tena bila kuchelewa uwahi kabla ya muda,usinywe pombe leo tafadhali”
“Sawa bwana mkubwa”
“Okay,lala salama”
Simu ilivyokatwa ilimuacha Leila akijiandaa na safari,aliweka nguo zake vizuri kwa ajili ya kesho yake.
***
Saa mbili ya asubuhi Deo na mkewe walitoka hotelini na kufika uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kuelekea Zanzibar ndani ya visiwa vya chakechake huko ndipo waliamua kufanya fungate lao baada ya ndoa.Hawakukaa sana Leila akatokeza na hawakutaka kupoteza wakati,wakaingia sehemu ya ukaguzi na muda ulipofika wakawa ndani ya ndege tayari.Haikuwa safari ndefu,baada ya dakika hamsini walikuwa viwanja vya Zanzibar hapo walichukuwa ndege nyingine ndogo ambayo iliwapeleka mpaka upande wa kisiwa.Ujio wa watu hao ulitambulika ndio maana wakaekewa vyumba viwili tayari,kimoja cha Deo na mkewe kingine cha Leila.Hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa na kila mtu aliifurahia.Ilikuwa ni hotel safi iliyotulia tena ya nyota tano.
“Hii sehemu imetulia sana,umepajuaje hapa Deo?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Marietha akiwa amevaa kinguo kifupi wanapunga upepo ufukweni mwa bahari,maisha kwake yalikuwa murua sababu alijuwa Leila na Deo ni mtu na rafiki yake,hakukuwa na kitu kilichokuwa kinaendelea.
Alijilaumu kumfikiria vibaya mwanaume huyo,alimvuta karibu yake na kumnyonya mdomo.
“Nilishawahi kuja huku two years back,nilikuwa na marafiki zangu”Deo akajibu baada ya kunyonyana ndimi.
“Deo nakupenda”
“Mimi pia”
Leila alivyofika waliungana na stori zikaendelea kila mtu alisifia eneo hilo,kifupi waliipenda Zanzibar.
***
“Ahh sssh aaaaah De…o aaah aaaaah aaaah aaaah aaaah”
Hakukuwa na haja ya kuuliza ni kitu gani kinaendelea sababu sauti hiyo ilijidhihirisha waziwazi kwamba kuna mambo ambayo watoto hawaruhusiwi kufanya yanaendelea,Marietha alikuwa akilalamika na ilielekea alikuwa mbali sana kihisia ndiyo maana alitoa kelele hizo kwa sauti,chumba cha Leila kilikuwa pembeni hivyo alikuwa akisikia kila kitu.Alikuwa ni mwanamke aliyekamilika, kwa mara ya kwanza aliona ni kawaida lakini kadri sekunde zilivyozidi kwenda mbele ndipo alipoanza kuhisi vitu vya ajabu mwilini,damu yake ilianza kumwenda mbio.Alikuwa mpweke na hakukuwa na mtu yoyote atakayeweza kukidhi haja yake,hapo ndipo alipoamua kuvua nguo zake zote na kuanza kujipapasa mwilini hususani kifuani mwake,mkono wake ukashuka chini akaanza kuishika ikulu yake huku akivuta hisia za wanaume mbalimbali.
Sauti ya Marietha ilimtia wazimu wakati mwingine alidhani wenda mwanamke huyo anafanya makusudi ili kumuumiza,nayeye taratibu alianza kutoa mihemo ya ndani kwa ndani.Akazidi kuishika ikulu yake huku akijisugua,kila alipoendelea ndipo alizidi kuhisi raha za ajabu sana.Mpaka mwisho akafika mshindo na kutulia.
***
Marietha aliyafurahia maisha akajiona ni mwanamke mwenye bahati kuliko wengine wote duniani,kila kitu kwake kiligeuka na kuwa furaha.Hata siku moja hakuwahi kuota kama angekuja kuishi maisha ya raha mustarehe kama hayo,matanuzi waliyokuwa wanafanya hayakuwa ya kawaida.Walitembea sehemu mbalimbali huku akiwa kushoto kwa Deo,amemshikilia kiuno wamegandana kama gundi,Leila alikuwa nyuma yao,tangu wanaanza kutembea kuangalia wanyama yeye alikuwa kimnya,kimawazo alikuwa mbali sana.Alipata wivu na alitamani nayeye angepata mwanaume wa kumdekea,alimkata Marietha jicho kali la chuki.
“Baby naogopa kusogea karibu”
“Kwanini?”
“Hujui kama huyu ni simba au?”
“Naelewa lakini yupo ndani kafungiwa”
“Akitoka je?”
“Nitapambana naye”
“Kwenda zako kama hujakimbia na kuniacha hapa”
“Siwezi, thubutuu”
Walikuwa katika hali ya utani,walimsahau Leila hawakuwa na muda naye ilikuwa kama wamemtenga.Hiyo ilimkera sana Leila sababu hata yeye alihitaji mtu wa kucheka naye,walivyomaliza hapo walienda kwenye bwawa lililokuwa na mamba wengi chini ya kisima maalum.
“Mh,hawa mamba?”
“Mamba ndiyo”
“sasa mtu bahati mbaya akidondoka huko?”
“Atatafunwa”
Mamba walikuwa chini wametengenezewa bwawa lao,jinsi walivyokuwa wanapanuwa midomo yao ilimfanya Marietha aogope.Leila aliwatizama Mamba na kumkata tena jicho kali Marietha alitamani amtupe ndani ya bwawa aliwe na mamba,hakuelewa kwanini alimchukia ghafla kiasi hicho.
“Leila unaona Tanzania yetu ilivyokuwa nzuri,unang’ang’ania kuishi Uingereza”
“Hata sio kuzuri”
Leila alijibu kifupi kwa hasira,hiyo iliwafanya Deo na Marietha washindwe kuelewa nini kilimfanya awe katika hali hiyo.
“Kwahiyo hutaki kurudi kabisa Tanzania?”
“Ndio,wala sijapapenda”
Jinsi alivyokuwa anajibu maswali haikuwa kawaida kabisa,sura yake ilionesha kuchukizwa kwa kiasi cha kutosha!ikachora mpaka makunyanzi.
“Ni nchi yako lakini”
Deo akazidi kumuongelesha ingawa alijuwa Leila hayupo sawa kabisa,wakazidi kuzunguka eneo hilo na ilipofika usiku walikaa pamoja ili wale chakula cha usiku.
Kuna kitu hakikuwa cha kawaida ndani ya moyo wa Leila,alikuwa akimuangalia Deo kwa macho yaliyojaa huba, hakuelewa hali hiyo imetokea wapi wakati walikuwa ni marafiki wakubwa yaani kaka na dada.Alijaribu kuizuia hali hiyo lakini ilishindikana kabisa,hisia zake zilihama,akakumbuka miguno aliyokuwa anatowa Marietha chumbani,alishindwa kuelewa kama anampenda Deo au amemtamani.
“Honey naenda kulala,mimi nawaacha”
Marietha alisema baada ya kumaliza kula huku akishushia na juisi ya machungwa.
“Si ukae kidogo baby”
Deo alitoa pendekezo.
“Hapana nimechoka,utanikuta chumbani”
“Okay honey”
“Leila,usiku mwema”
“Same to you”(Nawewe pia)
Leila akajibu,Marietha akasimama na kuondoka zake.
“Deo,hivi umempendea nini huyu mwanamke?”
Deo aligandisha uma mdomoni,swali la Leila lilikuwa tata.
“Vitu vingi tu”
“Sio mwanamke wa kuishi naye huyu kabisa”
“Kwanini?”
“Ipo siku utajuwa”
“Mbona sikuelewi”
“Usiku mwema”
“Embu kaa hapa”
Leila alivyotaka kusimama,akashikwa mkono na kurudishwa kitini.


Deo alishindwa kumuelewa Leila alikuwa ana maana gani kutamka maneno hayo ndiyo maana akamrudisha kitini.
“Leila,una maana gani kusema hivyo?”
“I was kidding love,goodnight.Sleep tight”(Nakutania Mpenzi,usiku mwema)
Kitu alichokitamka Leila kinywani kilikuwa tofauti na mambo aliyokuwa nayo moyoni mwake.Hakuelewa ni kwanini mtima wake unahisi vitu tofauti,Deo aliunyanyasa moyo wake ghafla na hata siku moja hakudhani kama mambo yangekuwa kama hayo kwani walikuwa ni kama kaka na dada,kwa kasi ya umeme akamsogelea Deo mdomoni na kumpiga busu.
“Lala salama”
Leila aliaga tena kwa mara nyingine akasimama na kuondoka zake.Hakutaka kulichukulia jambo hilo kiundani zaidi yeye kwake aliona kawaida sana na kuishi kwa Leila nchini Uingereza kwa kipindi kirefu kulimfanya adhani wenda ni tabia za kizungu ndizo alikuwa anamletea ingawa hakuelewa ingekuwaje endapo Mke wake Marietha angeshuhudia tukio hilo.Deo alimalizia kinywaji chake na kusimama wima ambapo alinyoosha mpaka ‘counter’ na kulipa kila kitu.
“Nadhani sidaiwi leo”
Akauliza ili kuhakikisha baada ya kulipa pesa za vinywaji na chakula.
“Ndio hudaiwi kaka”
Msichana wa mapokezi mwenye asili ya kipemba ndiye aliyejibu.
“Okay ahsante”
Deo akatembea mpaka hotelini na kuingia chumbani ambapo alimkuta Marietha ameuchapa usingizi,akasogea karibu na kumfunika vizuri na shuka kisha kumbusu juu ya paji lake la uso.
“Nakupenda mke wangu”
Deo akasema ingawa alijuwa Marietha yupo usingizini.
****
Wakati watu wamelala usiku yeye alitumia muda huo kumtafakari Deo Karekezi, mume wa mtu.Moyo wake ulimuuma mno alikuwa taaban hajiwezi kwa mwanaume huyo.Hakuelewa ni njia gani atumie ili amnase kimapenzi,kichwani kwake alipitisha mikakati mingi lakini yote haikumpa njia sahihi ya kumteka.Hapohapo akasimama kutoka kitandani na kukiendea kioo kikubwa kilichokuwa mbele yake,akaanza kujikagua kuanzia kwenye nywele mpaka chini kwenye unyayo na kuanza kujitathmin mwenyewe,akaziangalia nywele zake zilizokuwa ndefu kiasi,akashuka kwenye shingo yake iliyokuwa ndefu kiasi kama twiga ambayo ilibeba kifua kilichobetuka yakasimamisha maziwa yake madogo kama embe bolibo.Akashusha chini akaikagua nyonga yake iliyokuwa nyembamba kama dondora,japokuwa hakuwa amejazia nyuma lakini nyonga yake ilibinuka kama imepigwa jeki.Hicho ndicho alichojivunia katika maungo yake ya mwili.Alikuwa ana mwili mdogo kiasi lakini wenye kuwatoa wanaume udenda.Leila aliyajuwa mapozi na hilo alilijuwa,hapohapo akatoa nguo yake ya kulalia na kuitupa kitandani akaanza kujikagua tena.
“Deo lazima nikupate hata iweje,lazima twende sambamba tu”
Leila aliapia na hata siku moja hakukubali kushindwa katika maisha yake hata hivyo aliamini kuwa wanaume ni dhaifu mno hivyo swala hilo aliliona ni kama kuweka kibakuli cha supu mdomoni.
“Mimi ni mwanamke kama Marietha,tutaoneshana inabidi niongeze viza yangu ya kuishi hapa nchini”
Leila alizidi kunuwia huku akizunguka zunguka kwenye kioo akiukagua mwili wake.Akili yake yote ilimuwaza Deo na sio tena bwana wake wa kizungu aliyemuacha uingereza Mr.Philips Maclaren.
****
Marietha alikuwa wa kwanza kutoka usingizini akaingia bafuni na kujimwagia maji,akamaliza kila kitu huko huko kama kupiga mswaki na haja nyingine zote.Akatoka bafuni akiwa amejifunga taulo moja ambalo lilifunika maziwa peke yake, kwa maana hiyo mapaja yake yote yalikuwa nje,jinsi umbo lake lilivyojichora ilimfanya Deo amkague kuanzia juu mpaka chini kwa macho ya huba!
“Acha kuniangalia hivyo baby”
Marietha akasema huku akitabasamu, sio siri alikuwa ni mwanamke mzuri ambaye wengi walisema hana kasoro yoyote ile.Alikuwa na mapaja manene meupe yaliyojaa supu hilo alilijuwa pengine ndiyo maana alipenda kuvaa sketi fupi sababu alijivunia.Mbali na hapo alishawahi kumfanya muuza nyama buchani aliyekuwa anakata minofu ya nyama ajikate kidole chake baada ya yeye kupita,ilikuwa sio rahisi kwa mwanaume yoyote yule kutozungusha shingo yake endapo Marietha akipita mbele yake.
Ingawa wanaume wengi walimfuata wakitaka naye ngono huku wakipanda dau lakini haikuwa rahisi kumvua nguo yake ya ndani aliishia kuwachuna na pesa kumpelekea Issa.
Maswali mengi yalizuka ndani ya halmashauri ya kichwa chake ni kivipi Deo aliweza kumpata na kuamini kuwa siku zote ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu!
“Darling nikwambie kitu”
Hatimaye Deo akasema na kuketi akiegemea mbao ya kitanda.
“Enhee leta sera kama kawaida yako”
“Mi napenda hapo ulivyovaa yaani hapa nahisi kama nimepalalaizi mwili mzima”
“Ah!Ah!Ah!Ah! Wewe Deo wewe,mimi mkeo kwahiyo umenitamani?”
“Ningekutamani ningekuoa?yaani hapa natamani hata nikufungie ndani usitoke nje”
“Ha ha ha haaa,una vituko wewe”
“Sio vituko sitaki watu wakuone”
“Punguza wivu”
“Naanzaje kupunguza na uzuri huo”
“Baby saa nne hii,hatujanywa chai alafu mgeni yule itakuwa anatusubiri”
“Nani Leila?”
“Ndio”
“Oh kweli,ngoja nioge fastafasta basi”
“Mimi najiandaa”
“Okay”
Deo akatoka kitandani akavuta taulo na kunyoosha bafuni.

Alivyotoka akaingia kabatini na kuvaa,kila kitu kilivyokuwa sawa wote wakatoka nje na kuelekea kwenye mgahawa ambapo walimkuta Leila tayari ameagiza supu anakunywa,wote wakaungana.
“Morning”(za asubuhi)
Leila ndiye alikuwa wa kwanza kutoa salamu ambapo wote waliitikia wakaagiza supu na kuanza kunywa.Moyo wa Leila ulimuuma ajabu,alishikwa na wivu alivyowaona Deo na Marietha wanalishana nyama kupitia midomo yao kama makinda ya njiwa, walikuwa katika mahaba mazito mbali na hapo baada ya kulishana nyama wakaanza kunyonyana ndimi.Leila alitafsiri jambo hilo kivingine kabisa kwa maana hiyo alilipitisha kama wanamfanyia makusudi,alijiona mpweke na alihisi wivu uliochanganyika na hasira nyingi.
“I love you Deo”(Nakupenda Deo)
Marietha alisema baada ya kutoka kulana denda hawakuelewa ni kiasi gani moyo wa Leila unaumia,walimchukulia ni kama ndugu yao na kufanya vitu kama hivyo ilikuwa kawaida mbali na hapo Deo aliona ni kawaida sababu mwanamke huyo aliishi sana uingereza wazungu kulana madenda ilikuwa kawaida popote pale ndiyo maana alijiachia mbali na hapo walikuwa fungate ilibidi wafurahi.
“Tutarudi lini Dar?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Leila akiwatizama wote wawili huku sura yake ikionesha umakini kidogo.
“Si tumekuja hapa jana tu,bado sana”
“Nyie hamjapachoka tu huku?”
“Mimi binafsi bado,wewe Marietha”
Deo akamgeukia mkewe.
“Naanzaje kuziacha raha hizi,nifuate joto Dar?Baby mimi nataka tuhamie huku huku”
Kitendo cha kusema hivyo,Leila aliachia msonyo mrefu ulioonesha chuki za waziwazi,alioneshwa kukerwa zaidi na tamko la Marietha mbali na hapo jambo hilo lilichanganyika na wivu ndani yake.Sio Deo wala Marietha wote walimwangalia.
“Nyie wapumbavu kweli,wapuuzi wote”
Leila alitoa maneno machafu kwa hasira zilizoonekana usoni na aliongea kwa kumaanisha.
“Leila sa…”
“Tena wewe ndiyo unyamaze Malaya wewe,kahaba mkubwa.Super prostitute wewe ndiye umechafua hali ya hewa hapa”
Ilikuwa ni kama Leila alikuwa akimsubiri Marietha ajibu kwani aliongea kwa sauti huku akitukana matusi, Deo hakuelewa ni kitu gani kimempata mwanamke huyu mpaka akawa hivyo.
“Leila embu tulia”
“Nitulie nini Deo,si naongea ukweli..huyu mwanamke wako Malaya tu”
Deo hapohapo akasimama na kumshika mkono ambapo alimvuta na kutoka naye kando, hakutaka kumuacha aendelee kumdhalilisha mke wake wa ndoa tena mbele yake.
“Wewe Leila una shida gani?embu njoo huku unieleze”
Walikokotana na Leila aliendelea kutoa matusi ya nguoni tena akitaja jina la Marietha maneno kama MALAYA na KAHABA ndiyo yalitoka kinywani mwake huku akisema kuwa aachiwe anataka kurudi jijini Dar es salaam amechoka kuishi kisiwani humo.
“Sitaki,niachie Deo.Niache nirudi Dar niondoke zangu Uingereza wewe huna muda na mimi.Nimekuja kukutembelea wewe upo na Malaya wako”
“Leila yule ni mke wangu lakini”
“Hata kama lakini mimi nawewe kumbuka tulipotoka”
“Naelewa,sasa ndiyo umtukane mbele za watu?Yeye kakufanya nini ungenitukana mimi hapa sio yule”
Deo alikuwa tayari amechukia na hakuelewa ataanzia wapi kumbembeleza Marietha sababu alimuelewa mwanamke wake kwa kudeka na hukasirika kwa jambo dogo tu,alielewa ni kibarua gani angeenda kukumbana nacho kwa Marietha.
“Lakini samahani kwa yaliyojitokeza Leila”
Deo alimvuta Leila na kukiweka kichwa chake begani na kuanza kumbembeleza alijuwa kivyovyote vile yeye ndiye chanzo cha Leila kuropoka kwa kutokuwa karibu naye,alijishusha na kuanza kumpiga piga mgongoni kama Mama anayem-bembeleza mwanaye alale mgongoni.
Leila alihisi faraja sana mapigo yake ya moyo yakaanza kumwenda mbio,alihisi joto mwilini mwake.Akachukuwa mikono yake na kuiviringisha kiunoni mwa Deo,wakawa wamegandana.
“Deo nakupenda sana”
“Mimi pia”
Deo aliitikia sababu neno hilo alilichukulia kawaida, hakuelewa kuwa Leila alimaanisha kitu kingine tofauti ndiyo maana hakushtuka hata kidogo,hakuelewa ni kiasi gani Leila ananyanyasika moyoni mwake.Mikono yake ilianza kutembea mgongoni mwa Deo ikapanda mpaka juu shingoni,akatumbukiza vidole masikioni mwake akawa kama anampapasa,hapohapo Deo akamtoa ingawa Leila alimg’ang’ania hiyo ilifanya atumie nguvu kidogo.
“Wacha nimuwahi mke wangu,atakuwa amekasirika”
“Deo please”(Deo tafadhali)
“Nakuja nakuja”
Deo hakutaka kumsikiliza tena Leila akaanza kurudi alipokuwa Marietha lakini cha ajabu alipofika meza waliyokuwepo hakumuona,akajawa na wasiwasi.
Aliamini kuwa hakuna sehemu nyingine ambayo Marietha atakayoweza kuwa zaidi ya kuwepo chumbani analia, bila kujifikiria aligeuka na kutembea kuelekea chumbani kwao,alivyofika alisukuma mlango.
“Marietha,Mariethaa…Baby”
Marietha hakuwepo chumbani,akatembea mpaka bafuni akidhani wenda atakuwa huko lakini wapi!Marrietha hakuwepo popote pale,alivyorudi chumbani alipigwa na butwaa zaidi baada ya kukuta kabati lipo wazi hakuna nguo za Marietha wala begi lake kumaanisha kuwa mwanamke huyo ameondoka mazima.Hakutaka kubaki,akatoka nje kama mkuki,akatembea mpaka mapokezi.
“Umemuona mke wangu hapa kapita?”
Alimuuliza Mwanamke wa mapokezi bila hata ya salamu.
“Ndiyo kapita hapaaaa saa hii saa hii na mabegi alikuwa akiliaa”
Mwanamke wa mapokezi alijibu kwa rafudhi ya kikwao,Deo alihisi kuchanganyikiwa alielewa ni kiasi gani Marietha atakuwa ameumia moyo,matusi aliyotukanwa na Leila yalikuwa ni mazito mno na yangepimwa kwenye mzani basi ungevunjika.
Alikimbia kutokea nje ingawa hakuelewa aelekee wapi kusini au kaskazini sababu hakujuwa mkewe katumia njia gani.Bado walikuwa wapo kisiwani,Deo alikimbia kuelekea baharini akatokeza na kumuona Marietha kwa mbali ana weka mabegi ndani ya boti.
“Mariethaaaa...Mariethaaaaa”Akaita kwa sauti huku akiendelea kukimbia bahati mbaya akajikwaa na jiwe, akadondoka chini na kubiringika kama mpira,alivyoinua shingo yake aliona boti aliyokuwa ameingia Marietha inaondoka.


****
Machozi ya hasira ndiyo yalikuwa yanamtiririka kwa wakati huo,hakuwa na uwezo wa kufungua mdomo wake kutukana,Marietha hakuwa na tabia za kiswazi,alijiheshimu na ndiyo maana hata jamii ilimuheshimu pia.Matusi aliyokuwa anaogeshwa na Leila hakuweza kuyastahimili hata kidogo sababu mbali na hapo alikuwa akitukanwa mbele ya mumewe wa ndoa isitoshe watu waliokuwa pembeni yao walikuwa wakiwaangalia,alijisikia vibaya sana.Hakutaka tena kukaa eneo hilo tena, alivyomuona Deo kamtoa Leila pembeni hapohapo nayeye akapata mwanya,akasimama na kuingia chumbani ambapo huko alikuwa akimwaga machozi kama chemchem.
“Kwa..ni nimefanya kosa gani mpaka aniite Ma…laya,kosa langu ni lipi?”
Marietha aliendelea kujiuliza maswali huku akilia kama mtoto mdogo,kuendelea kubaki katika visiwa vya chakechake kulimaanisha kuonana na Leila,hakutaka kitu hicho kiendelee hata kidogo.
Wazo likamjia hapohapo akaingia kabatini na kupakia nguo zake harakaharaka ndani ya begi lake dogo.Alivyohakikisha kila kitu amekiweka vizuri alitoka nje,bado aliendelea kumwaga machozi mtindo mmoja,mwanamke huyu alikuwa ana hasira mbaya, hakumfikiria tena Deo alimjumuisha kuwa yeye ndiye walewale tu.Alitoka mapokezi na kuanza kutembea kuelekea kivukoni,bahati nzuri akakuta boti ndogo ambayo hutumika kuwaleta watu kisiwani humo,hakutaka kujiuliza mara mbilimbili,akaiweka mizigo yake na kupakia.
“Tuondoke kaka”
Nahodha wa boti akavuta kamba ya injini,boti ikaanza kuunguruma ikaanza kuyakata maji.Taratibu boti ikaanza kuondoka,Marietha hakukoma kulia alivyoyakumbuka matusi ya nguoni aliyotukanwa na Leila ndiyo alizidi kupandwa na hasira zaidi,akahisi mpaka kuna kitu kohoni kimemkaba mno,zilikuwa ni hasira zilizopitiliza.
“Dada,vipi upo sawa?”
Nahodha aliuliza baada ya kumuona abiria wake hayupo sawa.
“Usi…jali”
“Kweeli?”
“Ndio”
Mawimbi hayakuwa makali lakini kadri walivyosonga mbele ndipo hali ya hewa ilizidi kubadilika,upepo unaotokea Kaskazini ukaanza kupuliza kuelekea Kusini,mawimbi yakaanza kupiga boti.
Hofu ikaanza kumtanda nahodha akajaribu kuzungusha usukani lakini wapi mawimbi yakamshinda,tangu aanze kufanya kazi ya kuwavusha watu kuwapeleka visiwa vya chakechake haikuwahi kutokea mawimbi makali kama hayo.Hiyo ilimfanya Marietha atandwe na hofu sababu maji yalianza kuingia ndani ya boti kumaanisha kuwa yakizidi kuingia boti itazama na wote watakufa maji.
“Dada unaweza kuogelea?”
Hilo ndilo swali lililomfanya Marietha azidi kuogopa pengine alijuta kutoka kisiwani,neno kifo ndilo lilikuwa kichwani kwake kwa wakati huo.Alivyogeuka nyuma hakukuwa na dalili yoyote ile ya makazi ya watu, mbele ndio kabisa.Katika maisha yake hakuwahi kujifunza kuogelea,hasira zote zikamwisha alichokuwa anawaza kwa wakati huo ni jinsi gani atakavyoyaokoa maisha yake.Dalili zilionesha kwamba ni lazima wangekunywa maji na matumbo yao kujaa kisha kufa ama kuliwa na samaki,alisikitika sana sababu angekufa na hakuna hata mtu mmoja angeweza kuiona maiti yake.
“Dada nimekuuliza unajuwa kuogelea?”
Nahodha akauliza tena.
“Hapana”
“Hapa hatuna jinsi hali ishakuwa mbaya sa…”
Kabla ya nahodha kumalizia anachotaka kusema,boti likachapwa na wimbi zito akadondoka chali.
Marietha akazidi kuogopa maji yakazidi kuingia ndani ya boti,alivyoona hivyo akakimbilia ndoo ndogo na kuanza kusomba maji na kuyamwaga baharini.Ingawa alijuwa anaenda kufa muda mchache lakini hakutaka kukata tamaa,alitaka kujaribu kujitetea kwani aliamini bado wana nafasi ya kuokoa nafsi zao.Hapohapo Nahodha nayeye akasimama akaungana na Marietha kuyatoa maji nje,ndani ya dakika nne nzima walikuwa wakifanya kazi hiyo.Ni kweli walifanikiwa kuyapunguza maji, boti haikuwa tena nzito.Ikaanza kuyakata maji taratibu.
Hakuna mtu aliyeamini kuwa walitoka salama salmin,mpaka wanafika Zanzibar bado waliendelea kuamini kitu kilichotokea ni muujiza.Marietha hakutaka kupoteza wakati,alikuwa ana pesa ndani ya begi ingawa zilikuwa zimelowa, akamkabidhi nahodha.
“Hapana dada,wewe nenda.Ngoja niende leo Msikitini nikatoe sadaka”
Nahodha alikataa pesa.Marietha hakuwa na sababu ya kumlazimisha alishuka na kutafuta taxi iliyompeleka mpaka uwanja wa ndege, hapo alipanda na safari ya kurudi jijini Dar es salaam kuanza mara moja.
***

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)


0 comments:

Post a Comment

BLOG