Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 4/10


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 4 KATI YA 10
*******
 *******

Witnes nayeye hakutaka kuchelewa aliingia ndani ya gari dogo lililo kua pembeni yake na kuvunja
sehemu ya chini akitoa Nyaya za hasi na chanya alizigusisha gari kuwaka na kumwambia Miriam aingie ndani ya gari.

gia ili pigwa na gari ile kutoa vumbi huku likienda kwa kasi ya ajabu.

Witnes alinza kurusha risasi tena za kwenye matairi na kufanya magari hayo yapoteze uelekeo na kudondoka mwishowe aliona mbele yake Lori hilo lililo kua lina watoto ndani yake

na kumuomba Miriam akae upande wa dereva nayeye aweze kudandia Lori hilo.

Kweli Miriam alikamatia usukani huku gari hilo likizidi kwenda kwa kasi nyuma ya Lori hilo.

Witness alipanda juu ya gari na kudandia Lori lile na kutembea taratibu juu ambapo alivyo fika usawa wa dereva aliufungua mlango ule na kumtupa nje dereva wa lile Lori nayeye kuingia na kukutana macho kwa macho na Aldolf aliye kua amekaa kushoto kitendo kile kina mshangaza sana Aldolf na kutokuamini aliyekaa pembeni yake ni Witness.

Adolf alitaka kutoa bastola ila Witness alimzuia kwa mkono mmoja huku mkono mwingine ukiwa juu ya usukani wa Lori lile .

Vuta niku vute ile ili fanya Lori lianze kuyumba huku na kule na wakati mwingine kukosa uelekeo. alicho fanya Witness alikanyaga breki na Lori lile kusimama pale pale.

alivuta kichwa na kumpiga Adolf kichwa cha pua ambapo nayeye alirusha ngumi lakini Witness aliizuia na kumpiga teke lililo mfanya Adolf adondoke nje ya Lori lile.

Witness hakukubali nayeye alishuka na kuanza kupambana nae kwa hasira huku aki kumbuka watu mbali mbali walio kufa wakiwemo wazazi wake.

Alimpiga kifuti na kuzunguka nyuma yake na kumvunja shingo pale pale.

Alivyo oona kila kitu kipo sawa alienda nyuma ya Lori na kuwa fungulia watoto wale wa kike ambao wali kua wengi sana.

Waliendelea kusonga mbele waki pita pori kwa pori na watoto wale.

Ila witness baadae ana simama baada ya kuhisi amekanyaga kitu kizito.

Alivyoangalia chini vizuri aliona ame kanyaga bomu ambapo ange toa mguu ule unge tokea mlipuko mkubwa sana na wote kupoteza maisha.

Miriam baada ya kuona vile anaa mua kuwa sogeza watoto wale mbali nayeye kurudi kwenye mguu ule uliokua na bomu ambao Witness alikua ame ukanyaga.
alitoa kisu na kuanza kuchimba chimba.

"Miriam go with the children i will stay here it is okay just go please let me die"
"No i can't leave you here"
"you can and you will"

Witnes alikataa msaada ule na kuku bali kujitolea kufa.

machozi yalianza kumtoka kwa mbali. hasa alivyo mkumbuka Stuwart .

Miriam kuona vile alianza kuondoka na Kumuacha Witness akiwa ame kanyaga bomu lile la kutegwa mchangani huku nayeye akilengwa na machozi.


 Miriam kwa mbali alisimama na kumgeukia Witness huku machozi ya uchungu yakiwa yana mbubujika juu ya mashavu yake sababu alitegemea wange toka wote ndani ya msitu huo wakiwa wenye furaha ila furaha yake ina katishwa hasa baada ya kujua kuwa muda mfupi kifo cha Witness kina fuata sababu hakukuwa na jinsi nyingine.

"MIRIAM GO"(MIRIAM NENDA)."

aliongea Witness kwa sauti huku akitumia mkono wake kumuashiria kua aende huku akitoa tabasamu ili ajaribu kumpa faraja kwa wakati ule

kwa shingo upande Miriam anaendelea kusonga mbele na mwishowe kuwa kuta watoto wale alipo waacha na kuanza safari ya kusonga mbele katika msitu huo ulio kua na miti mingi na mirefu sana.

"Anti Witness yuko wapi?"
Aliuliza mtoto mmoja kati ya watoto wale wengi na kumfanya Miriam ashtuke na kuchuchumaa huku akimshika mtoto huyo mdogo bega.

"jina lako nani?"
"naitwa Jesca"
"una jina zuri. Anti Witness anakuja kasema tukamsubiri mbele"
"mbona alisema ana kuja nasisi?"
"atakuja na sisi cha kufanya tutembee yeye anakuja sawa Jesca"

Miriam alizidi kusonga mbele ambapo alitembea takribani kilomita tatu na kusikia mlipuko mkubwa sana.
"Oooh my GOD. rest in peace Dear Witness"(Mungu wangu pumzika kwa Amani Mpendwa Witness)"

Miriam aliongea maneno hayo huku akiweka ishara ya msalaba baada ya kusikia mlipuko huo ambapo moja kwa moja ulitoka nyuma alipo muacha Witness na kujua kua Tayari amefariki dunia na si vinginevyo.

alisimama kwa muda na kufuta machozi ambayo yali kua yana mtoka huku akiji kaza ili watoto wale wasijue.

Baaa ya kufika juu kilimani anatoa redio kubwa ya mawimbi na kuanza kutafuta netwok ambapo alivuta antenna kwa juu .ambapo redio hio ilianza kutoa sauti kama tv yenye chenga chenga.
"This is area 6.7 i need air support. i reapit this is area 6.7 ineed air support (hili ni eneo 6.7 nahitaji msaada wa anga narudia hii ni eneo 6.7 nahitaji msaada wa anga".

Aliongea Miriam huku upande wa pili katika kitengo cha jeshi la anga kuku bali ombi lake na kumuhaidi asubiri dakika arobaini.

"Shit"

Miriam aliji semea baada ya kuona kikundi cha watu kina kuja na mitutu huku waki zidi kuja kwa kasi eneo alilo kuwepo.
"Tusonge mbele fanyeni haraka"

Miriam aliwa inua watoto wale na kuanza kuondoka nao huku

akisonga nao mbele bila kuwa na uwakika kama wange toka ndani ya Msitu wote salama .
Risasi zilianza

kurindima huku watu wale waliovaa Vitambaa wakizidi kuja kwa kasi sana huku waki tupa risasi .

Miriam alianza nayeye kuwa jibu huku akijificha nyuma ya miti.
kutokana na maadui wale kuwa wengi alishindwa kuwa dhibiti ivyo alivyo kua ana piga risasi alikua akikimbia nayeye pia na kuwa kimbiza watoto wale mbele.
"Motherfuck*****"

Miriam aliji kuta anaropoka hasa baada ya risasi za mtutu ule kuisha na kuuutupa pembeni huku akichomoa bastola ndogo kiunoni na kuendelea kuwa piga risasi ila ana dondoka

chini baada ya kupigwa risasi ya bega ambayo ilipenya na kutokea nyuma upande wa pili wa mkono na kumfanya asikie maumivu makali.

hakuku bali aliendelea kupiga risasi huku akitambaa chini kwa chini ambapo damu nyingi zilianza kumvuja mkononi.

Maumivu makali tena anaya sikia ndani ya mguu wake wa kulia baada ya risasi nyingine kupenya na kumfanya adondoke chini pale pale huku akiwaambia watoto wale wazidi kusonga mbele maana hatoweza tena kutembea.

alitoa kitu kama Kikopo na kuki fungua ambapo kilianza kutoa Moshi wa rangi nyekundu hii ni baada ya kusikia milio ya helikopta kwa mbali sana na kujua kivyovyote vile ni wa Marekani wenzake na ni jeshi la anga lina kuja.

Kweli kama alivyo fikiria ndivyo ilivyokua kutokana na alianza kuona risasi zina tupwa kutoka angani ndani ya Helikopta hizo zikianza kuwaangamiza maadui wale .ambao wengi walianza kudondoka chini na wengine kuja ribu kurusha risasi juu ya Helikopta hizo zili zokua tatu za kivita ila wana shindwa kutokana na jeshi hilo la anga kuji dhatiti vilivyo.

Kitendo cha dakika kumi tayari maadui wale wali kua chini wame kufa wote na Helikopta zile kutua eneo lile lililokua linatoa Moshi Wa rangi nyekundu.

Alitoka mwanajeshi mmoja wa kimarekani huku mkononi akiwa ameshika mtutu wa aina ya Ak 47 na kuonekana kuangalia usalama pande zote alivyo hakikisha kuna usalama aliwa ruhusu wengine washuke walishuka wana jeshi wengi na wengine kumzunguka Miriam na kumuinua ambapo walimshika na Miriam kukaa katikati yao akiwa analia sana kwa uchungu hii ni kutokana na hakuamini kama angepona katika vita ile iliyo kua kali sana.

"Let's go Miriam come on .we are going home.Where are the rest?(tuondoke Miriam tunaenda nyumbani.Wengine wako wapi?)"

"They fuc*****ng DIED have you seen them here?"

Miriam alijibu kwa hasira huku akichechemea na kuingia ndani ya Helkopta iyo na kuanza kupewa huduma ya kwanza watoto wale waliingizwa ndani ya helikopta nyingine na Helkopta hizo kuanza kupaa hewani taratibu huku wakiendelea kumpa matibabu Miriam wakielekea nchini Marekani.

************
MASAA MAWILI KABLA.

"hei hei"

Ilikua ni sauti ya mtoto wa kiume ambae alikua ni mdogo wa makamo ambapo Witness akiwa ame kanyaga bomu lile lililo kua ndani ya ardhi ambapo ange iuna mguu linge lipuka na pengine kumchana na kupoteza maisha yake .

Aligeuza shingo yake na kumuona Mtoto huyo wa kiume akimjia upande ule aliokanyaga Bomu lile Witness.
"wewe ni nani?"
"usinisogelee nitanyanyua mguu tufe wote"
"Hapana usifanye ivyo nataka nikusaidie tulia ivyo ivyo"

Witnes alitulia na kuto jibu chochote hakua na tegemezi wala msaada mwingine wowote .
"naomba ushushe pumzi ndefu na uchuchumae taratibu sana"

Witness alitii na kufuata maagizo yale ambapo baada ya kufanya vile Mtoto yule alitoa kisu na kuanza kuchimba chimba pale chini mpaka alipo lifikia bomu hilo baafa ya hapo alitoa kitu kama chuma kizito na kuweka pembeni alichukua kisu kile na kuanza kufungua nati za lile bomu
"unajua unacho kifanya mtoto?"
"ndio najua nataka kulitegua bomu hili cha msingi naomba uniamini"

Mtoto yule aliendelea kulifungua bomu lile na kukuta chuma mbili zenye spring na kuzikandamiza.
"Toa mguu wako taratibu"

Witness alianza kutoa mguu wake taratibu na mtoto yule kuweka lile jiwe juu ya lile bomu.
"sasa hapa ina tubidi tukimbie mbali sana maana baada ya dakika kumi lita lipuka"

witness na mtoto yule walianza kukimbia ila upande wa pili anashindwa kuelewa kwanini mtoto yule kamuokoa wakati hawa fahamiani na kuanza kumuwekea mashaka.
pale pale alitoa bastola na kumuekea mtoto yule usawa wa kichwani.huku akimuangalia kwa makini sana.

" wewe ni nani?, na kwanini ume nisaidia"?
"hapana usiniue mimi ni mtu mzuri"
"nani kaku tuma?"
"sija tumwa na mtu"
"Kacha kacha. nani kakutuma nambie"
"Hakuna aliye nituma kwe kwe kwe kweli tena"

Witness kuona vile alishusha bastola yake chini na kuirudisha kiunoni.

Baada ya hapo wana usikia mlipuko wa bomu lile na wote kubaki waki shangaa.
"asante sana naitwa Witness"
" Naitwa Abdul Igwe"

Baada ya kuongea ivyo waliendelea kusonga mbele na kuona helkopta za kimarekani ziki pita juu ya anga hilo.
na kujua kivyovyote vile walikua ni wama rekani wana mfuata Miriam ila kwa upande wake hakuwa tayari kurudi.
aliendelea kusonga mbele akiwa na Abdul Igwe.
"Nani kaku fundisha kute gua mabomu?"
"Babu yangu"
"alikua mwanajeshi"?
"Ndio alikua mwana jeshi alinifundisha mbinu nyingi za kijeshi"

Baadae waliingia ndani ya kijiji hiko ambapo Abdul alianza kuwa tambulisha mgeni yule aliye kuja nae.

Baada ya siku kadhaa alianza kuzoea mazingira ya kijiji hiko huku kijiji hiko kutokea kumpenda sana.
ila siku iyo wana ona vumbi kwa mbali sana kutokea bara barani na Witness kuchukua darubini ili ajue nini kina endelea cha ajabu aliona magari takribani saba huku yakiwa na watu wame valia vitambaa usoni

"Hao ni BOKO HARAM wana kuja kuchukua watoto wa kike"

Aliongea Abdul na kufanya amgeukie.
"kuna sehemu ya kuji ficha?"
"Ndio "
"waambie watoto wote waji fiche sasa hivi"

Haraka haraka Abdul alianza zoezi la kuwa ficha wenzake huku jeshi lile likiendelea kuja kwa kasi sana

 vumbi liliendelea kutibuka kwa mbali lililosababishwa na magari kukimbia kwa fujo huku juu ya magari hayo kukiwa na Mijitu iliyo vaa vitambaa usoni huku mikononi wakiwa wame shika mitutu.

"Abdul unaweza kutumia bastola?"

Aliuliza Witness baaada ya Abdul kuja eneo lile na kusimama pembeni yake.

"ndio nina weza"
"Kamata hii"

Witness alimkabidhi bastola ndogo Abdul.
"sasa nawewe je?"
"Usijali kuhusu mimi"
"Hapana ndani kuna gobole na mabomu ya baruti"
"kimbia haraka kayalete"

Abdul alikimbia ndani na kurudi na gobole mkononi ambapo mkononi pia alishika Mabomu ya baruti.

Walijificha nyuma ya kijumba kidogo na kuwashuudia Mijitu ile ikishuka na kuanza kujigawa Witness aliwasha bomu ilo la baruti na kulirusha upande waliopo watu wale na kudondokea juu gari huku mlipuko mkubwa ukitokea na kuwa fanya watu wale waanze kurusha risasi bila uelekeo na bila kujua nani karusha bomu lile.

Witness akitumia gobole lile ambalo lilikua lina uwezo wa kuingiza risasi moja na kukaa sawa sawa ambapo alitumia uma kini wa hali ya juu kumlenga adui aliye kua ana tembea mbele yake.

ana fyatua gobole lile na adui yule kudondoka.
Risasi zilianza kurindima upande aliokua Witnes na kumfanya abiringike na kutembea chini kwa chini mithili ya nyoka akijivua magamba.

"Abdul.Abdul !"

Witness alimuita Abdul ambae nayeye wakati huo alikua chini ya gogo amelala huku akijaribu kurudisha masha mbulizi.
"Una muona yule aliyelala pale?"
"ndio namuona"
"Nataka niende pale"
"Kufanya nini?"
"Ana silaha nahitaji silaha yake"
"Una risasi za kutosha kwenye bastola yako?"

Abdul alichomoa MAGAZINE na kuikagua kama ina risasi na kutingisha kichwa chake bila kusema chochote kuashiria kwamba risasi zipo za kutosha.
"sasa cha kufanya nilinde nataka kuruka upande wa kule. Nitahesabu mpaka tatu. moja mbili tat..."
Abdul aliinua kichwa na kuanza kuwa rushia Mijitu ile risasi na kuonekana kuji ficha ili wasipigwe na ndo palepale Witness alipata mwanya wa Kukimbilia upande wa pili ambapo alichukua mtutu wa jamaa yule aliye kua chini na

kubeba magazine zote ambazo zili kua zime jaa risasi na kurukia upande wa pili huku akimpa Ishara ya dole gumba Abdul

kumuashiria kuwa Kila kitu kimeenda sawa kama walivyo panga.

Witness anamuona mmoja wa watu hao akiwa juu ana chungulia chungulia.

Aliweka mtutu wake sawa na kumfyatua ambapo jitu lile lilidondoka chini na kufanya ivyo ivyo hata kwa wengine na kuzidi kuwa punguza.

"Jitokeze kwa usalama wako la sivyo tuna muuwa rafiki yako"

Sauti iyo ilisikika na Witness kuchungulia kwenye kitundu kidogo na kuona Abdul amekamatwa huku akiwa amewekewa bastola usawa wa kichwa huku jitu lile likiwa na wenzake wakizidi kutangaza.

"Tuna kupa onyo la mwisho.jisalimishe kwa sababu hao watoto mlio waficha tuta wapata na rafiki yako atakufa bila sababu yoyote ile. njoo tu ujisalimishe mwenyewe .. "

Jitu lile lili zidi kuongea huku likitembea kwenye uwanja huo akiwa anaagalia huku na kule ambapo mdomoni alikua na kipisi cha sigara kikitoa moshi.

"Witness usi toke wat..."

Abdul alikatishwa kauli yake baada ya kupokea ngumi kali ya tumbo kutoka kwa jitu hilo na kumfanya ajikunje huku akijishika tumbo lake ambalo alisikia maumivu makali sana na kuhisi ana taka kutapika nyongo au tezi.

"Kacha kacha. muda wako ume isha"

Jitu lile lili koki bastola na kumuwekea Abdul kichwani.
"Tatu. mbili. moo....."
"Subirini msimuuwe:"
Aliongea Witness huku akiji tokeza akiwa amenyoosha mikono yake juu na kusalimu amri huku akiweka mtutu chini.

hakutaka Abdul afe kwa ajili yake.Alitembea taratibu huku mijitu ile ikiwa ime muelekezea mitutu.

"Mimi hapa . mimi hapa haina haja ya kumdhuru huyo kijana"

Witness aliongea huku akizidi kutembea akipiga hatua za taratibu sana.

ana tulizwa na kitako cha bunduki kili chomfikia usawa wa mdomoni na kumfanya adondoke chini ya mchanga huku akiugulia maumivu makali yaliyo mfanya atoke damu mdomoni

sababu ya kujing'ata ulimi.
aliinua kichwa na kuzifuta damu zile mdomoni zilizo kua zina toka kama mchuzi.

"Watoto wako wapi?"
"Sijui mna ongelea nini"
"nakuuliza tena watoto ume waficha wapi?"

Jitu lile lilimpiga kofi zito na kumsindikiza na teke la kifua na kufanya Witness adondoke chali .

alimfuata na kuendelea kumshambulia mateke ya tumbo yasiyo na idadi.
"Hei ina tosha"

Aliamuru mkuu wa kikosi kile cha majambazi na lile zoezi kusitishwa la kupigwa kwa Witness.
"Watoto ume waficha wapi?"

Mkuu wao yule aliingilia na kuchuchumaa ambapo wakati huo Witness alikua amelala chini ana vuja damu nyingi puani na mdomoni.

Jitu lile lilitoa bastola iliyo kua kiunoni na kumuwekea Witnes juu ya utosi na kumfanya afumbe macho huku akisali sala yake ya mwisho

sababu alijua huo ndio ulikua mwisho wake wa kuishi duniani

"Paaa paaaa"

Bastola ile ilifya tuliwa tena bila kupoteza muda pale pale ambapo Witness alisikia vizuri mlio ule wa risasi ila cha kushangaza hakuhisi dalili yoyote ya

maumivu na kumfanya taratibu afumbue macho ili ajue nini kinaendelea.

hakuamini macho yake alivyo yafumbua macho yake alimuona Abdul akiwa amelala chini huku ubongo wake ukiwa ume tapakaa chini kila mahali kutokana na risasi ile kupasua fuvu la kichwa chake.

Walimchukua Witnes na kumburuza ambapo wakati wote hakutoa macho yake juu ya mwili wa Abdul na kumfanya azidi kupata hasira juu ya watu hao waliofanya kitendo cha kumuuwa Abdul walimchukua na kumfunga kwenye mti na kamba ambayo waliizungushia nyuma ya mti na kuikaza vizuri.

" Tunaenda kuwa tafuta watoto. tukiwapata tuna kuuwa. hahahahahaha"

Jitu hilo lilicheka kwa dharau na kuondoka zake huku waki muacha Mlinzi mmoja amlinde Witness.

baadae kabisa wote wana rudi wali pomfunga Witness na kuanza kumpiga ngumi nyingi za tumbo na mdomoni baada ya kuwakosa watoto wale.

"Watoto wako wapi?"
"s.....j.uiii..i"

Waliendelea kutoa kipondo kile huku Witness akizidi kuishiwa nguvu na kulegea kabisa na kufanya apate majeraha usoni huku damu ziki mvuja mdomoni ila hilo halikubadilisha msimamo wake.

"Si..towaambia ni.po. tayari k...ufa bora mniue sababu hamtopata choch..hote kutoka kwangu"

Witness aliongea kwa shida sana huku akiwa amelegea sana.

"Muuwe tu ana tupotezea muda."

Jitu la pembeni lili ropoka na bastola kuko kiwa na kuwekewa Witness kichwani.
" sawa ume chukua uamuzi mzuri . wasa limie uend...."

Kabla haja maliza sentensi ile Witness alishangaa kuona jitu lile lime dondoka chini na wengine walivyo jaribu kutoa bastola zao wote walidondoka baada ya kupigwa risasi huku Witness akijiuliza mara mbili mbili ni nani aliye kuwa akiwa piga risasi.

Kwa mbali sana alimuona mwanamke akija mbele yake . japokua macho yake yalikua yame vimba haya kuweza kuzuia kumuona mwana mke huyo anae kuja mbele yake huku akiwa na silaha aina ya Mak 4 mkononi.

alimfuata na kuanza kumkata kamba aki tumia kisu na Witnes kudondoka kama mzigo.
.
"Naitwa Easher"

Mwanamke huyo alijitambulisha na kutoa bastola kiunoni kama umeme na kulifyatua jitu ambalo lililo kua halijafa vizuri baada ya kuhakikisha lime kufa alirudisha bastola yake kiunoni

"E ..ash..er"
"Tulia usiongee"
Mwana mke yule aliye jitambulisha kwa jina la Easher alimuamuru Witness huku akifungua begi lake na kutoa sindano na kuvuta dawa ndani ya kichupa hiko.

 Ila baada ya Easher kutaka kumchoma sindano kwenye mshipa wa mkono wa Witness ana msukimiza na Easher kudondoka upande wa pili. japo kuwa alikua ana majeraha hakukosa nguvu za kumsukumiza mwanamke huyo pembeni.

"wewe ni nani?"

aliuliza Witness huku akijivuta na kujiegemeza kwenye mti huo uliokuwa nyuma yake.
"nime tokea kijiji cha jirani"
"ume kuja kufanya nini huku?"
"kutoa msaada"
"nipatie silaha yako"
"unasema"?!
"nipatie silaha yako"

Witness aliongea huku akimkazia macho mwanamke yule aliye kuwa mbele yake, ambapo Easher ana chomoa bastola ilio kua kiunoni na kumkabidhi Witness ambae mpaka hapo hakujua ana nia gani na bastola yake, kweli alimkabidhi Witness ambapo alichomoa MAGAZINE na kuikagua kama ina risasi baada ya kukuta ina risasi na kuridhika ana rudisha magazine ile na kuikoki bastola ile.

Ghafla ana muwekea Easher usawa wa kichwa na kumuamuru aweke mikono juu.
"weka mikono juu haraka sana"
"unataka kufanya nini binti?"
"inategemea . nina weza nika kuua pia. wewe ni nani niambie ukweli la sivyo nakuuwa hapa hapa"
"nilisha kujibu tayari, naomba uweke iyo silaha chini tafadhali"

Witness alisimama na kumsogelea karibu huku bastola ile ikiwa ime gusa kichwa cha Easher.
"geuka haraka"
aliamuru Witness na Esher kugeka nyuma ambapo Witness alianza kumkagua na kumsachi kila sehemu ya mwili wake na kumkuta na bastola nyingine ndogo ndani ya kiatu na kisu kidogo. ila baadae ana kutana na kitambulisho cha

kipelelezi na kujua kuwa Easher ni mpelelezi kutoka jijini LAGOS . Anamuachia na kumkabidhi bastola yake baada ya kuridhika kuwa Easher hakuwa mtu mba-ya kwake,

Badae watoto waliofichwa kwenye andaki wana toka pamoja na watu wengine waliokuwa wamejificha. na kumpongeza Witness ambae ame fanya jambo kubwa sana katika kijiji hiko, alirudi katika mwili wa Abdul na kuutzama kwa uchungu sana
"huyu ni nani?"
alihoji Easher huku nayeye akiutazama mwili ule
"anaitwa Abdul aliokoa maisha yangu na watoto pia"
"pole sana"
"nishapoa"

hali ya Witness inaanza kuwa nzuri sana baada ya kuanza kupokea matibabu kutoka kwa wana kijiji hao ambao walimpenda sana Easher hakucheza mbali nayeye alikua nae bega kwa bega na kuomba jeshi lingine kutoka LAGOS lije katika kijiji hiko ili kuboresha ulinzi wa hali ya juu.

CHIF wa kijiji hiko Audu IGBO anaanza kusha mbuliwa na maradhi ya moyo ambayo yana mpelekea kushindwa kutembea hata kufanya kazi pia. Witness ana kua nae bega kwa bega tangu aanze kuugua kuliko mtu yoyote yule. kutokana pia umri wa mzee huyo kwenda sana ana shindwa kupambana na magonjwa yale siku moja akiwa na

Witness akimpa dawa aliweza kumwambia mambo mengi sana kuhusu yeye , kuwa zamani alikua mwanajeshi na kuna pesa nyingi sana alizificha mahali.

"Nenda Abuja ,kuna kijiji kina itwa karu, huko kuna kisima kikubwa pembeni kuna mbuyu mkubwa pia. uki ulizia uta oneshwa"
"CHIF kwanini unasema ivyo?"
"binti yangu sitoweza kuishi sana ivyo ninge penda kukupa izo pesa kama zawadi ili ukirudi Tanzania uweze kuanza maisha mapya. sababu ume fanya jambo kubwa sana katika kijiji changu naomba ukachukue izo pesa ni nyingi sana, ni dollar za kimarekani nili zifukia ndani ya mfuko mweusi ambapo hakuna yoyote atae weza kuziona, naomba ufanye ivyo"
"CHIF utapona usiseme ivyo"
Witnes aliji kuta ana dondosha chozi kusikia maneno hayo kutoka kwa chif huyo amabae alimlea na kumpenda sana alikua ni kama mzazi wake, hakukuwa na jinsi nyingine ya kubadili maamuzi ya CHif huyo ambae aliaweza kukiona kifo chake mbele.

alijifuta machozi Witness na kumshika mkono babu yule ambaye alikua chif
katika kijiji hiko.

"Witness mwanangu nakupa baraka zote , nili bahatika kuwa na mtoto mmoja wa kike kama wewe ila alifariki na ugonjwa mba-ya wa ebola sina mtu mwingine yoyote wa kumpa pesa zile isipo kuwa wewe"

CHif yule alimuomba Witness ampatie begi ambalo lili kua pembeni yake ambapo baada ya kupewa alitoa ramani ndogo na kumkabidhi huku akimpa maelekezo ya pesa zile nyingi sana zili pokua.
"kuwa makini ni pesa nyingi sana hata serikali wakijua una zo wana weza kukuweka kizuizini isitoshe wewe sio raia wa NIGERIA "
mzee yule alizidi kuongea mara kadhaa na kukohoa kohoa.

**********************

"mnasema nini Witness amefariki? hapana haiwezekani kabisa"

zilikua ni kelele kutoka kwa Stuwart akiwa yupo RUSSIA,jijini moscow baada ya kupokea taarifa izo zina zomfanya apige makelele na kumfokea mkuu wake huyo aliye toa taarifa izo kana kwamba yeye ndiye aliye husika katika kifo chake.
"punguza jazba Mr,stuwart. sio peke yako uliye umia watu wote tume umia, tume poteza jeshi kubwa sana una jua"
"mimi sielewi kitu , nataka niuone mwili wake"
"hatu batika kuuchukua sababu aliilipuka na bomu la kutegwa mchangani ili kuokoa maisha ya watoto wasio kua na hatia. leo hii tunavyoongea Marekani ina mkumbuka sana haitoweza kumsahau hata kidogo , ameyaokoa maisha ya mpwa wake OBAMA raisi wa marekani, hakika hatoweza kusahaulika hata mara moja"
"ooh MUNGU wangu Witness, kwanini ulienda?"
"wewe ni mwanajeshi mr,Stuwart tena commando kuji tolea ni kitu cha kawaida sana"

Stuwart jambo lile ana shhindwa kuliingiza akilini na kubaki ana mwangalia mkuu wake huku akiyabana meno yake kwa hasira sana na kushindwa afanye nini. hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo kuwa Witness mwanamke ana yempenda amekufa tayari bila kujua ukweli ulio jificha nyuma ya pazia kuwa alikua hai na wala hakufa. ivyo ndivyo ilivyo kuwa. alipiga piga ukuta kwa hasira huku akitulizwa na mkuu wake huyo.

**************

maradhi yana zidi kumsumbua Audu Igbo chif wa kijiji hiko na kuzidi kumshambulia moyo na kumfanya ashindwe kuhema vizuri, baada ya siku nne Audu alikata kauli na kufariki dunia, pigo lingine kwa witness alilipata na kuzidi kusikia uchungu ila ana muachia Mungu sababu hakua na jinsi ya kuzuia kifo cha mzee huyo,

baada ya mazishi kuisha kila kitu. siku iyo Witness aliwaaga wana kijiji wale na kuwa shukuru kwa kila jambo walilo mfanyia alibeba begi lake kubwa na kuliweka mgongoni.
"uta rudi tena shangazi witness"?

mtoto mmoja mdogo wa kiume alimuuliza Witness huku akiwa na sura ya majonzi sana, Witnees alimwangalia na kuchuchumaa

"ndio nita rudi mwanangu"
"twende wote mi naogopa kubaki"
"hapana usiogope baki na mama . hawa tokuja tena usijali IBU''
"shika hii uta kua una nikumbuka"

Ibu alivua mkufu wake ambao ulikua wa kutengenezwa na kamba pamoja na mawe na pangoni na kumvalisha Witness shingoni.
"Asante sana ni nzuri"
Witness alimkombatia mtoto yule kwa muda kidogo huku wana kijiji wengine pamoja na watoto wakiwa wana mshangaa huku wakiwa wame mzunguka wakiwa katika sura za huzuni,

aliwa pungia mkono na kuanza safari ya kwenda Abuja ambapo alipanga akitoka huko akirudi nchini Tanzania.

 Alitembea mwishowe ali kuta bara bara ya vumbi ila ime chongwa vizuri kuashiria kwamba magari yana pita bila wasi wasi, ali kuwa akitembea huku aki angalia kama kuna dalili yoyote ya gari kuja na kuomba msaada aweze kusogezwa mjini,

alitembea takribani nusu saa zima bila dalili yoyote ya gari kutokea, ila kwa mbali ana hisi muungurumo wa gari na kusimama ili aweze kusimamisha gari hilo, ila ana punga mkono na gari hilo kumpita bila kusimama, ivyo ivyo alifanya kwenye gari la pili la lili mpita na kuamua kuendelea kusonga mbele akitembea kwa miguu huku jasho likianza

kumtoka kuto kana na jua kali hilo la mchana.

kwa mbali tena anahisi GARI lina kuja na kuli pungia japo alikua hana uhakika kama gari hilo linge simama, gari hilo lili mpita tena na kubaki kushangaa akiendelea kusonga mbele ila kwa mbali aliliona likirudi nyuma gari hilo na kusimama pembeni yake ambapo kioo cha gari hilo kili funguliwa na sura ya mwanamke mtu mzima kuonekana akiwa amevalia kitenge na kilemba kichwani.

"habari yako dada"?
mwanamke yule alimsalimia kwa lugha ya kiingereza
"nzuri tu za kwako?"
"ulikua una elekea wapi"?
"hapo mjini,"
"ingia ndani ya gari twende"

Witness aliingia ndani ya gari na mama yule kupiga gia na kuanza safari ya kuondoka tena kwa mwendo wa kasi sana
"huku ulikua una tokea wapi?"
"hiko kijiji cha jirani"
"kijiji cha marehemu Igbo?"
"ndio"
"poleni sana na msiba, yule chif alikua ni mtu mzuri sana, jina lako nani?"
"tusha poa tu Mama angu, naitwa Witness"
"Mimi naitwa Mama Sheila"
walizidi kufahamiana pale kwa kuta mbulishana huku Mama sheila akizidi kwenda kwa kasi sana'
"una jua nawahi bank alafu hii sehemu ni hatari sana kuna majambazi sana watu wana kufa sana maeneo haya, ndo maana nilivyo kupita na gari saa zile nilijua ni jambazi, sema nika ona nikupe msaada sababu nilikuonea huruma jambo baya lina weza lika kukuta"

Mama yule aliongea huku akizidi kukata kona kwa kasi ile ile na kuonekana kweli ana hofu, alikata kona ya kwanza alipandish
a kilima na kukata kona ya kushoto alilala nayo ivyo ivyo bila kupunguza mwendo kasi, ana kata kona nyingine na kuji

kuta ana kanyaga breki ya ghafla na gari kuteleza na kusimama pale pale kutokana na kuona magogo yame pangwa mbele alipiga gia ya kurudi nyuma kama umeme ila ana shindwa kutokana na risasi kupigwa hewani na watu wanne kutokea vichakani wakiwa na silaha mkononi.

wali fika kwenye ile gari na kuanza kugonga gonga vioo na kufanya Witness awaangalie .
"tushuke binti tuta kufa humu"

aliongea mama yule baada ya kumuona Witness ana jiishauri kushuka,
"shukeni shukeni laleni pale chini upesi upesi, pesa toa haraka haraka sana uokoe maisha yako MAMA"
aliongea mmoja wao huku akiwa na panga ambalo alikua akimpiga piga nalo mama sheila Mgongoni kwa kutumia ubapa huo wa panga
"sina pesa msiniue tafadhali"
"hatu jaja kupoteza muda tuna kazi za kufanya toa millioni ishirini izo"

HABARI zile zina mchanganya mama sheila ambaye alijiuliza maswali mengi walijuaje kama ana kiwango cha pesa
"mama wape kama unazo wata tuua hawa"
aliongea Witness huku akimwangalia Jamaa yule aliyeshika panga, hakukua na jinsi yoyote zaidi ya mama sheila kutaja pesa zile zilipo ambapo wanaenda kwenye boneti na kufungua na kukuta begi hilo lenye pesa,

kwa jicho la kuibia Witnes ana muona jambazi mwingine akiwa na bastola ndogo ambaye ndie peke yake alikua na bastola huku akiwa fuata.
"tafadhali msituue tusha wapa pesa jamani ndo izo tulizo kua nazo"

aliongea witness akiji fanya mwenye hhofu nyingi sana huku akiwa omba watu wale wasi waue,
majambazi wale walicheka sana tena kwa dharau huku wakimwangalia Witness ambae alikua na wasi wasi mwingi sana,

akiwa na bastola yake ameishika huku ana cheka Witness kwa nguvu za ajabu alimvaa na bega ambapo wote wali dondoka chini na bastola ile kudondoka pembeni, alimtuliza na kichwa cha pua na kubiringika na kuichukua bastola ile.

"tulieni ivyo ivyo"

mama sheila alibaki akimshangaa Witness ambae alikua muda mfupi ana tetemeka sana na sasa hivi kashika bastola ile vizuri tena kwa mikono miwili.

"paaa,paaa,paaaa,paaaa"

bila huruma Witness alifyatua risasi zile tena kila mmoja alimpata ya kichwa na majambazi wale kudondoka chini pale pale na kupoteza maisha,

alimpa mkono Mama sheila ambae alikua amelala chini huku akiwa mwenye hofu nyingi na kumuingiza ndani ya gari, nayeye kwenda kuya toa mawe yale yaliyo kua yame pangwa na majambazi wale,

safari hii aliingia Witness ndani ya usukani na kuanza kuendesha.
"Mama Sheila ume umia sehemu yoyote?"
"ha ha ha hapana, nipo sawa kwani wewe ni nani??"
"ni mtu tu wa kawaida,"
"imea kuaje umeweza kuwa dhibidi wale watu, nili ogopa saana"
"nacheza karate,"
"piga simu polisi waeleze kila kitu ila usini taje"

Mama sheila alizidi kumshukuru Witness hasa baada ya kumfikisha bank.
"nitakupa millioni moja kama shukrani Witness ume okoa pesa zangu na maisha yangu pia"
"hapana usijali, wewe kaweke bank tu, haina haja ya kunilipa"
"hapana Witness, chukua izi pesa tafadhali nakuomba mwanangu"

Mama sheila aliongea huku akimkabidhi pesa Witness alishukuru na witness kuanza safari ya kwenda Abuja ambapo alichukua taxi pale pale bila kupoteza muda,

ambapo ili mfikisha kijiiji hiko cha kina choitwa karu, alitembea kwa mbali sana anauona mbu-yu mkubwa sana kama aliambiwa na marehemu kuwa pembeni kuana kisima kikubwa cha maji,

aliona watu wakichota maji na kusubiri mpaka usiku ufike ili aweze kuchimba sehemu aliyoa mbiwa kuwa kuna pesa nyingi,

alisubiri mpaka jioni ili pofika ambapo alienda kununua chepe na jembe kwa ajili ya shughuli iyo ya baadae,

kweli alipata na kuanza kuchimba chimba pale takribani lisaa lizima alikua akichimba shimo lile ambapo kwa mbali alihisi kitu kigumu sana na kuendelea kuchimba na kuku tana na mfuko mweusi, na kuutoa mfuko huo mkubwa sana aliendelea kuchimba na kukuta maboxi makubwa sana yaliyo jaa pesa izo za kimarekani alizidi kuchimba na kukuta mfuko mwingine mkubwa, zili kua ni pesa nyingi sana kuliko maelezo,

tayari ili kua imejiri saa kumi na mbili asubuhi ali beba mifuko hiyo na kuta futa taxi ambayo alimuambia dereva huyo ampeleke bank ya barclays sababu alikumbuka vizuri ana account ambayo alifunguliwa na wazazi wake kipindi alipokuwa mtoto, ana ingia bank hapo akiwa na vifurushi ivyo na kufanya kila mtu amshangae

pesa izo hawa kuweza kuzi hesabu pale kumwambia aingie ndani ya ofisi ya meneja huko wali chukua takriba masaa manne na nusu kuka milisha mahesabu yale,

baada ya hapo alitoka nje na kufanya taratibu za kusafiri , ambapo siku iyo iyo alikata tiketi ya shirika la nddege la BRITISH AIRWAYS.

kweli kama ilivy pangwa leo hii alikua ndani ya ndege njiani kurudi nchini Tanzania huku akiwa na mawazo mengi sana.

 shirika la ndege ya BRITISH AIRWAYS ilianza kutembea taratibu ambapo baadae inachochea kwa kasi sana, na tayari kuinua matairi ya mbele huku mengine yaki fuata na ndege iyo kuacha ardhi ya NIGERIA ndani ya ndege hiyo alikua Witness Kafifi akiwa na mawazo mengi sana,

matukio mbali mbali yanaaanza kuji jenga ndani ya ubongo wake na kutengeneza kama mkanda wa movie ,tukio moja wapo ni la wazazi wake kuuliwa kinyama tena akishuhudia kwa macho yake mawili pamoja na mama yake kubakwa mpaka kupoteza fahamu,

kutokana na msongo wa mawazo na uchovu mwingi ana jikuta akipitiwa na usingizi mzito sana huku ndege ikiwa angani ina pasua mawingu,

*******


0 comments:

Post a Comment

BLOG