Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 6/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 6 KATI YA 10
*******
 *******



Mwili mzima uli mvimba akiwa maabusu kila sehemu ya mwili wake alihisi una uma hususani
mgongoni, baada ya kupokea kipigo usiku wa kuamkia jana.
“wewe JAMBAZI kuja hapa”!
Aliita mmoja wa maaskari aliye kua nje ya nondo kumaanisha Donald aweze kusimama mara moja, aliiinuka kwa shida, pembeni ya askari huyo alimuona mwanaume ameshika briefcase kubwa, huyu alimtambua vizuri alikua ni Erick kaka yake na pamela tena akiwa ameziba pua zake kwa dharau au harufu mbaya ya vinyesi iliyo kua iki toka ndani ya maabusu humo,, aliye wekwa Donald
“mambo rafiki yangu, ila sikai sana hapa, sababu kuna nuka kishenzi yaani!, nina ujumbe wako hapa, hili begi una liona, lina miliioni mia mbili, nataka nikupe ili uachane na Pamela, hakika uta furahi sana, una weza hata ukahama nje ya nchi, ili mradi ukae mbali na Pamela na asijue ulipo kabisa, kwa sababu yako wewe hataki kula, mzee ame nipa,kwa io una semaje?”
“hapana siwezi kuzichukua nina mpenda sana Pamela, siwezi kumsaliti sababu ya pesa izo Erick, nipo radhi hata nipigwe risasi leo hii sababu yake”

Aliongea Donald akitoa maneno ya kishujaa jambo ambalo lili mshtua sana Erick hakutaka kuamini kuwa zile pesa Donald angezikataa hata kidogo,
“uta kufa Donald, Pamela ata ondoka hivi karibuni, uta kosa vyote nisikilize rafiki yako, utakuja kujutia MY FRIEND!”

Donald hakutaka kujibu lolote alirudi nyuma na kuketi alipo kua ameketi hakuwa tayari kuchukua kitu chochote kile, ili asaliti mipango waliyopanga na pamela tangu utotoni.
Ilikua sio kirahisi kama Erick alivyo chukulia,

******

WALINZI walikaa kila kona ya ukuta ili kumdhibiti Pamela asiweze kutoka au kuruka ukuta , na kuzuiwa katakata kutoka nje ya geti, siku kadhaa sasa hakuweka kijiiko cha chakula mdomoni alilia kila siku mfululizo, mawazo yalikula mwili wake na kupungua uzito yote alimuwaza Donald hakumuongelesha baba yake tena, hakutaka hata kumsalimia alimuona kama ni muuaji au shetani kabisa,
“mwanagu jitahidi basi ule nita ongea na baba yako”
“Mom staki, usiji sumbue nime shiba, wewe nenda tu”
“siku ya nne hii haujala wala kunywa maji, ona ulivyo isha mwanangu”?
“niache hata nikifa yote mta kua mmeya taka nyie, wala msiji sumbue ,”
Yalikua ni maongeazi ya Pamela na mama yake mzazi siku iyo chumbani, ,licha ya mama yake kumsihi ale lakini aligonga mwamba, hakutaka kumsikilza hata mmoja wao, alichotaka yeye ni Donald tu na si vingivenyo,

PHD Graysoon siku iyo asubuhi alikuja baada ya kupigiwa simu na mzee Deuji ili waweze kuya weka mambo sawa na safari ya kuondoka na Pamela ianze mara moja,!
“niwie radhi Mwanangu Graysson Pamela nilishaongea nae hana tatizo kabisa, ana kupenda sana”
Aliongea Deuji wakiwa mezani siku iyo, huku mke wake akiwa pembeni pamoja na Erick, kwa sura ya upole Graysonn aliitikia na kukubaliana na ali amini kua atakuja kuwa mkwe wake,siku chache zijazo
“usijali mzee wangu, wala usijali kabisa, mipango yangu ni kumpeleka ENGLAND na mimi mwenyewe nita msomesha kule, nita mpeleka akamalizie elimu yake chuo kikuu cha OXFORD marekani”
“sawa kabisa PHD Grayson”
“taratibu za kusafiri zita kamilika ivi karibuni nashughulikia mipango ya visa , ikikaa vizuri basi nitaenda nae, nafikiri ni wiki ijayo, ila nil…..”
Kabla ya kumalizia lolote wote waligeuza shingo zao baada ya kumuona Pamela akishuka ngazi mbili mbili kwa jazba na hasira na moja kwa moja kusimama mbele yao,
“NISIKILIZENI HASA WEWE GRAYSON, una danganywa, ukweli ni kwamba mimi sikupendi sija wahi kukupenda hata siku moja, nina mtu wangu nina mpenda sana, usiji potezee muda wako hata kidogo, tena futa mawazo hayo, huyo MSHENZI anaye kudanganya kuwa mimi nakupenda uta muoa yeye mwenyewe,..”!
“Pamela una muita baba yako ni mshenzi…?’”
“ndio MOM, Dad ni mshenzi, tena MSHENZI MPUMBAVU tu, na yeye sio baba yangu wa kuni zaa, Grayson samahani
kwa kuya sikia haya, , chukua pete yako”
Pamela alivua pete ya uchumba aliyovalishwa siku chache zilizopita na kumtupia PHD Grayson usoni, kilichokua kina muongoza Pamela wakati ule sio yeye ni hasira, hakumjali tena baba yake aliye kua pembeni yake, kweli alionekana kuongea maneno ambayo siku nyingi alipanga kuongea na leo hii ndiyo ulikua muda muafaka wa kuropoka kila kitu, alizidi kuongea kwa sauti ya juu sana.



Mr, Deuji ki ukweli hakushindwa kusta himili maneno yale kutoka kwa binti yake isitoshe yupo na mgeni ambaye alimuheshimu sana na sasa hivi anaaambiwa maneno ya ajabu tena na binti yake, kama baba mzazi alitakiwa afanye kitu.
Kwa hasira aliinuka mzima mzima na kumpiga kofi mwanae Pamela ambalo lili fanya limpeleke chini dakika hiyo hiyo na pale pale ukimnya ulitawala alivyo taka kumfata tena tayari Eriick na GRAYSON walimuwahi na kumzuia ili asiweze kumsogelea Pamela,
Tayari Pamela alikua amezirai na kumfanya mama yake mzazi aanze kulia kwa uchungu, msobe msobe walimchukua na kumpeleka hospitali,
“mimi naona mzee wangu sina haja ya kumlazimisha Pamela, sioni sababu yoyote ile ya kuishi na mwana mke asiye nipenda”
“mwanangu niachie mimi”
“hapana mzee, acha tu nimuache ila asante kwa ukarimu wako,”
Alizungumza maneno hayo Grayson wakiwa hosptali hapo na kuanza safari ya kuondoka hakuona sababu ya kushi na Pamela sababu aliamini ndani ya moyo wake kuna kijana mwingine anayempenda kwa dhati, alinawa mikono aliamini kua hayo ndiyo maamuzi pekee japo yalikua ni magumu kwake lakini hakua na jinsi,

*********

“MIMI NAONA MNAMCHELEWESHA TU, NATAKA HATA KESHO AFE”
“HAPANA mambo hayo haya taki haraka, ina kubidi uwe mvumilivu tu”!
“mpaka lini sasa”?
“hivi karibuni ila ina kupasa kwanza umuweke karibu, alafu sisi tuta kwambia cha kufanya hapo baadae”
“nimuweke karibu kivipi”?
“fanya juu chini awe mtu wako wa karibu sana”!
“sawa nita fanya ivyo”
Yalikua ni mazungumzo kati ya Deuji na mkuu wa wachawi ambaye alikua mbele yake amekalia kiti kikubwa huku pembeni yake kukiwa na nyoka mkubwa aina ya chatu mwenye vichwa viwili, ulikua ni uchawi wa kutisha sana, sauti zili kua ziki tokea chini ya mbuyu huo zilikua mithili ya mwangwi, nia ya Mzee Deuji ilikua ni Donald afe mara moja na wamchukue msukule akiamini kua atakua akimtesa sana na kumpa
adhabu nyingi tofauti akiwa huko, ambapo Duniani wangeamini kuwa atakua amekufa tayari, Mkuu Yule ambaye alikua mkubwa wao wote alisimama na kukiendea kioo chake kikubwa , na kama kawaida yake aliongea maneno maneno yasiyo eleweka huku akirusha rusha maji yaliyokua kwenye kibuyu akitumia USINGA mweusi na papo hapo sura ya Donald ilitokea kwenye kioo kile kikubwa ambacho kili kua mbele yao,
“ha! ha! ha! ha! ha! ha! Ha! Ha!, siku zake zina hesabika sasa,. Siku chache atakua na hawa wanyama wenzake. Kama nilivyo kwambia , huyu ina bidi umuweke karibu sana, usioneshe hali ya kumchukia, tuta muua kidigitali zaidi,! “
Aliongea mzee Kira kwa majigambo huku wakicheka pamoja kwa sauti za juu, hakuna mtu yoyote wa kawaida amabye aliweza kusikia kelele hizo za wachawi hao sababu kabla ya kufanya uchawi ili kua ni lazima waweke dawa yao aina ya TAMBIKO hiyo hufanya mtu wa kawaida asiweze kuwaona wala kuwasikia wakifanya mambo yao!
Ivyo ndivyo ilivyokua . yallikua ni mambo ya kichawi sana, mbele yao kulikua kuna misukule ambao hao waliaminika kua Duniani walisha kufa tayari huko wali fananishwa na wanyama kutokana na mateso ambayo yalikua hayana mwisho .
chakula chao kikubwa kilikua ni pumba na Unga usiku kucha walifanya kazi huku wakilimishwa katika mashamba makubwa na wengine waki tumiwa kama CHUMA ULETE katika maduka makubwa, ila ili pofika mchana waligeuzwa na kuonekana mithili ya paka na bina damu wa kawaida.!
ivyo kupitia misukule hiyo waliweza kujiingizia pesa na kipato kikubwa sana, licha ya yote hayo lakini mzee Deuji alitaka Donald auliwe na awe miongoni mwa misukule hiyo,
Wachawi kutoka mikoa mbali mbali walizdi kuongezeka wakitua na nyungo zao wakiwa uchi wa mnyama huku wengine wakiwa na fisi, waliongea mengi sana kuhusiana na uchawi wao na baada ya kikao hiko kuka milika kila mtu alichukua usafiri wake ambao waliuita ndege na kupaa kila mtu akielekea majumbani kwake, hivyo ndivyo ilivyo kua, hakuna mtu aliye kua akijua siri hiyo kuwa nyuma ya utajiri wa Mzee Deuji kuna nguvu kali za giza akitumia damu za binadamu kutajirika.

*********
ASUBUHI YA SIKU HIYO ALIAMKA AKIWA MWENYE furaha sana jambo ambalo lili mshangaza sana mke wake, hakuelewa kwanini sababu usiku wa jana hakua katika hali ambayo ameamka asubuhi ya siku iyo,
“Mama Erick mwanangu Pamela yuko wapi”?
“yupo chumbani kwake, una dhani ataenda wapi wakati ulimkataza asitoke!,”
“anaendeleaje”?
“ana endelea vizuri, vipi kwani?,”
“nahitaji kumuona”!
Mzee DEUJI alisimama alipo kua kitandani na kufungua mlango, alitembea kidogo na kukata kona ambapo baada ya hapo aligonga mlango wa binti yake huyo, alivyoona haitikiwi ilibidi afungue na kuingia,
“ooh my beautiful daughter,(ooh binti ya mrembo)”
Aliita mzee Deuji lakini Pamela alivyomuona baba yake aligeukia upande wa pili wa ukutani sababu hakutaka kumsemesha baba yake, tayari Alisha jenga hali ya chuki ndani ya moyo wake, alimchukia sana ,
“kuna jambo ninge penda nikueleze, nafikiiri uta furahi sana”
Alizidi kuongea na kukaa kitandani hapo ambapo alianza kuzichezea nywele za binti yake Pamela,
“najua una nichukia sana mwanangu, ila naomba unisamehe baba yako, naanza kuamini sasa mapenzi haya chagui tajiri wala maskini, sitaki kukuona mwanangu upo katika hali ya majonzi kiasi hiki, sipendi kabisa, napenda kukwambia kuwa nime ruhusu mahusiano yako na Donald”
Maneno yale yalimfanya Pamela ageuze shingo yake na kutoamini kile alicho kisikia kutoka baba yake ambaye kwa muda mwingi alikua akipiga vita juu ya yeye kuwa na mapenzi na Donald leo hii kakubali tena kirahisi,wakati mwingine alidhani wenda alisikia vibaya au anaota ila ukweli ni kwamba alicho sikia hapo kilikua ni cha kweli kabisa,
“najua ni vigumu kuamini, ngoja niku hakikishie”
Pale pale Mzee Deuji alitoa simu yake mfukoni na kuanza mawasiliano na askari walio mkamata Donald akitoa tamko moja tu , WAMLETE DONALD nyumbani kwake haraka sana na awe huru, alipewa simu Pamela ili aweze kuzungumza na Donald hakika hakuamini kama baba yake leo hii ali kubali ,

Shukurani aliyo mpa baba yake haikuweza kuelezeka kabisa aliruka ruka sana, bila kujua mipango ya baba yake iliyo jificha nyuma ya pazia , baadae kidogo Donald aliletwa nyumbani hapo na Pamela kumrukia kama mtoto mdogo hakuna mtu aliye elewa ni nini kili cho mbadilisha mpaka aka kubali Donald awe na mahusiano na Pamela siri hiyo alibaki nayo yeye mwenyewe kifuani mwake,

Jambo la kumuweka Donald karibu lilizidi kuwa rahisi kwake kama gari kushuka kwenye mlima, alimkabidhi magari yake akiwaacha wawe huru kabisa, ili kuzidi kumuweka karibu sana, siku iyo alifanya mualiko na kumuita mama Donald ili aweze kumuomba msamaha kwa yale yaliyo tokea nyuma, na wamalize tofauti zao.
Siku iyo walijumuika pamoja na kula chakula cha mchana wakiwa wenye furaha sana,
“Leo hii napenda kuwaita wote rasmi mahali hapa, najua mara ya kwanza nilidhani kuwa mapenzi ni pesa, kumbe sikua sahihi kabisa, naomba mnisamehe kwa yaliyo jitokeza nyuma, najua sikua mtu mwema hata kidogo, hasa Mama Donald naomba uni samehe na tuendeleze undugu wetu, watoto wetu washa pendana ivyo hatuna budi kuwapa Baraka zote zile kutoka kwetu, Donald na Pamela naomba mpendane sana, nawapa Baraka zote . mimi kama baba napenda kuwaambia kua mkimaliza masomo yenu tu, nataka ndoa ifungwe na nina wahaidi kuwapa nyumba kubwa ya kifahari kama zawadi. Na nita fanya harusi kubwa ambayo haikuwahi kutokea Tanzania hapa”
Aliongea Mzee Deuji wakiwa kwenye meza ya chakula cha mchana kweli aliongea kwa upole sana, kila mtu aliamini maneno yake,
walielewa kabisa ame badilika na kuwa mtu mzuri,Muda wote Pamela na Donald walikua wenye furaha sana kuliko maelezo , wote walisherekea siku iyo kabisa, hakuna mtu aliyeelewa kuwa ndani ya moyo wa mzee Deuji kuna kitu kizito sana ambacho alikipanga na hivi karibuni kinaenda kutimia,hakuna mtu yoyote Yule aliyeweza kujua kuwa yeye ni nyoka ambaye kajivika ngozi ya kondoo,
“HATUA YA KWANZA IME KAMILIKA TAYARI”
Aliwaza mzee Deuji huku akiweka kijiko cha chakula mdomoni na kumtazama Donald huku akimuwekea tabasamu la bandia,
BAADA ya chakula kile kuisha kama kawaida walitoa vyombo na Mzee Deuji kuwa shukuru akiamini kuwa jambo alilopanga tayari linaenda kukamiliika, usiku wa siku iyo alienda tena kwa wachawi wenzake na kupewa kitu kama irizi ambacho katika hali ya kawaida kwa macho ya kibinadamu linge onekana kama yai ya kuku!,
Kesho yake chakula cha mchana kili pikwa na Mzee Deuji kuomba mayai yapikwe ili aweze kutimiza hadhma yake, irizi ile iliwekwa kwenye sahani ya Donald yeye akidhani kama ni yai kwa mara ya kwanza alisua,
“vipi Donald”?
Aliulza Pamela baada ya kumuona ana sua kuweka yai lile mdomoni,
“amna kitu”
“niku saidie kula hilo yai”?
“wewe Pamela embu kula , acha kuongea ndo tabia gani sasa”?
Alizungumza mzee Deuji alivyoona mambo yanataka kwenda tofauti yeye alitaka yai lile ambalo ilikua irizi ale Donald sio mwanae Pamela, kweli baada ya sekunde chache tayari Donald alikula yai lile,kwa mara ya kwanza aliliona lina radha tofauti lakini aliendelea kula na baada ya kumaliza alishukuru na kuondoka na pamela ambae alimtaka waende shopiing kwa ajili ya kununua nguo,
“sasa mnaenda huko mna pesa”?
“ndio Dad”!
“mna shilingi ngapi”?
“laki tano na hamsini”
“sasa hiyo nayo ni hela, mnaenda kununua maji au kununua nguo”?
“ni nguo tu”
“ni ndogo sana, nawapa milioni mbili,. Mkafanye shopping na nina taka yote iishe Pamela usiweke kwenye account yako,!”
“asante Dad”
“tumieni gari yangu HAMMER. Lakini muwahi kurudi!”
Bado alizidi kumuweka karibu, mambo aliyo yafanya hakika alifanya kwa hatua sana na umakini wa hali ya juu sana, mambo yalikua yakiinyooka kabisa kwa upande wake, aliamini kuwa muda mfupi tu Donald ataenda kuwa msukule kama alivyo taka yeye.

********

“HA HA HA HA HA HA HA HA, naona una fanya kazi nzuri sana , nime furahi , sasa hivi zime baki siku chache, leo ina tubidi twende tukampe dawa zilie ili tuzidi kumsogeza karibu”
“hakuna mashaka kabisa”!
Ulikua ni usiku wa wachawi ambao mzee Deuji alikua na mkuu wao wakiongea usiku huo wa kutisha sana, walikua wachawi wengi wame kusanyika chini ya mti mkubwa, sasa safari ya siku iyo ilikua ni kwenda kuwa chukua watoto wachanga na baadae kumrudia Donald, baada ya kufika hospitali walianza kuwa chukua watoto wadogo kama kafara huku wakiwachaa mama zao wakilia sana hospitalini hapo, wakiamini kuwa watoto wao wamekufa lakini haikuwa ivyo. Waliuwa watoto takribani sitini na mbili, ,

Waliwa pakia juu ya nyungo zao na kupaa angani, kufumba na kufumbua tayari walikua nje ya nyumba ya kina Donald wakiwa wame izunguka nyumba hiyo, na kuanza kumwaga mwaga dawa ili baadae waweze kuingia, waliwekea tambiko nje hapo na dawa aina yaa MCHERA ambayo hufanya mtu alale fofofo na wakati mwingine aote ndoto nzito,
zoezi hilo lili kamilika na wote kugeuka na kuanza kuingia wakitumia makalio na kufanikiwa kutokea ndani kwenye moja ya pembe ya chumba alicho lala Donald, waliingia mmoja baada ya mwingine na mwishowe Mzee Kira kuingia,

Haraka haraka walimuinua Donald na kuanza kumnywesha dawa ambayo ilikua kama damu nyeusi alimuinua na kumzaba kofi zito lililo mfanya azunguke mara tatu,
“rwaa rwaaa, chacharika shwaa shwaa rai rai rai nguurii Donald rii ruuu shali ka”
Ili kua ni lugha ambayo ilikua haileweki hata kidogo ambapo Mzee KIRA mkubwa wao alizungumza huku akimpaka dawa nyeusi usoni, alikuja bibi mwingine aliye vaa nguo za ngozi ya chui, huku akiwa na mvi nyingi kichwani , na kumuwekea kidole chake maeneo ya kichwani, hapo hapo radi kubwa ili tokea ambayo ilikua iki muingia Donald vizuri kichwani…



Asubuhi kulipo kucha kitendo cha kuyafu mbua macho yake alihisi hali ya utofauti kabisa!, uchovu mwili mzima huku kichwa kikiwa kina muuma sana, alivyo toa shuka mwilini, alianza kutetemeka kwa baridi
sana, hakuielewa hali ile ime tokana na nini wakati usiku wa jana, alilala akiwa mzima wa afya kabisa, alichofanya alitembea kidogo ila alihsi kweli maumivu makali ya kichwa pengine alidhani mtu yupo ndani ya kichwa chake ana gonga nyundo ndani ya ubongo wake, alitembea mpaka nje na kutafuta duka la madawa,
Baada ya kununua dawa za maumivu alimeza lakini alikua ndo kwanza kakitibua tena, alifika moja kwa moja na kujitupa juu ya kochi huku akitetemeka kwa baridi lile kali japo kua kulikua kuna jua lililoanza kuchomoza!,
“Donald una tatizo gani baba”?
Alihoji mama yake mzazi na Donald baada ya kumuona mawanae kipenzi hayupo katika hali ya kawaida kabisa,huku akiwa ana tetemeka, kweli mama yake alianza kuingiwa na hofu
“kiiiiichwaa, kinaaaaamua Mamaa”
“kimeanza lini”?
“sasa hivi”
“ume tafuta dawa”?
“ndiii…iiio”!
“pumzika baba, baadae nita kupeleka hospitali, itakua malaria”
Hali ina zidi kuwa mbaya sana, tena safari hiii tumbo lilianza kumuuma vibaya sana alihisi kama viwembe vipo ndani ya tumbo lake, haya kua maumivu ya kawaida tangu azaliwe hakuwahi kupata maumivu kama yale ilo alikiri, hali ile ina zidi kumfanya mama yake aaingiwe na hofu sana. Harakaharaka aliita usafiri wa boda boda huku akijifunga tenge lake vizuri na safari ya kuelekea hospitali kuanza,
Kitendo cha kufika hospitali na kuchukuliwa vipimo kutoka kwa Donald majibu yaliyo toka yalizidi kumchanganya sana mama Donald, hakuelewa nini afanye, hakuamini kile alicho kisikia kabisa kutoka kinywani mwa daktari Yule, aliye kua ,mbele yake.,
“umesema hana ugonjwa wowote?”!
“ndio mama , tumecheki maralia yupo sawa, U.T.I hana, hana ugonjwa wowote ule”
Hakika hakutaka kuyaamini maneno ya daktari Yule alimchukua tena na kumpeleka hospitali nyingine akiamini wenda pale alipo toka walikosea majibu kabisa,
Madaktari walivyo muona Donald walimuonea huruma sana sababu tayari macho yake yalikua meupe na kiini kuonekana na kuongea kwa shida sana. Haraka haraka walianza kumchukua vipimo, na safari hii tayari Pamela alikua kasha fika pamoja na mama yake mdogo na Donald aliiyeitwa Maria,
“mwanangu Donald sijui nini kime mpata ghafla ivi, Maria naumia uchungu nilionao mimi hapa, hakikia hauujui”!
“naelewa uchungu wa mwana aujuae mama, ,ila usijali Mungu yupo,atapona”
pamela aliye kua pembeni mashavu yake tayari yalishaanza kulowana kutokana na machozi aliyo shindwa kuya zuia , alilia kwa uchungu alivyo muona Donald yupo katika hali ile, hakuelewa lolote lile hakuelewa kuwa baba yake mzazi ndiye aliye husika leo hiii na taratibu za kumuuwa zina fanywa, laiti ange lijua hilo ange mchukia sana baba yake mzazi, pengine angemuua hata kwa kumchoma kisu cha utosi, kweli alilia kwa uchungu sana.

Donald akiwa kitandani alihisi upepo uki mpuliza miguuni aliiihisi kiubaridi shingoni mwake alivyo geuza shingo pembeni ya ukuta alimuona bibi kizee aliye kua na kibuyu mkononi, na ghafla kumuona mzee Deuji nayeye akiwa katokea kwenye pembe ya ukuta akiwa na usinga mkononi, kwa mara ya kwanza alidhani anaota au kudhani wenda walionekana ila ki ukweli yeye mwenyewe ndiye aliye kua akiwa ona, sio Pamela wala mtu yoyote Yule aliyeweza kujua kinachoendelea,
alivyo taka kuongea kitu bibi Yule kizee alimpaka dawa aina ya FUNGO mdomoni na kumfanya ashindwe kuongea lolote lile, kweli alichokiona pale aliamini zilikua ni nguvu za giza kabisa hakuamiini kama mzee Deuji nayeye alikua miongoni mwa watu wabaya tena wenye kutumia nguvu za giza,
“nili kukanya usitembee na binti yangu, hukunisikia , ki ukweli nakuchukia sana, na utaenda kujumuika nami siku chache, ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha “
Mzee Deuji alimpiga piga na usinga kichwani huku akicheka na upepo wa ghafla kutokea na wote kupotelea ukutani,
bado Donald alishindwa kuongea na hali yake ilizidi kuwa mbaya sana, alitamani aseme kitu ila alihisi mdomo wake haufunguki hakuwa tofauti na bubu kwa wakati huo.

“ngoja nimpige Dad simu tuone atasemje”
Aliiongea Pamela na kuanza mawasilianao na baba yake mzazi ,baada ya muda mfupi mzee Deuji aliiingia na kumfnaya Donald azidi kuyatoa macho yake kwa hofu ki kukweli alitamani kuongea ila alishindwa kabisa,
“pole mkwe wangu Donald, vipimo madakatari wamesemaje kuhusu Donald,matibabu kasha pewa, kama wana shindwa kumpa matibabu tumbadilishie hospitali”
Aliongea Deuji kwa kufoka na kuji fanya kuwa hausiki kwa lolote lile ki ukweli hakuna hata mmoja aliyeweza kugundua kuwa mzee huyo ndiye alikua akimchezea Donald kwa wakati huo.

“mgonjwa wenu ana onesha kabisa, hana tatizo lolote lile, hapa kuna tatizo kubwa sana, ita kupasa muende kwa waganga wa kienyeji nisiwa fiche kitu chochote kile hapa mtapoteza muda wenu bure”
Kauli ile aliiitoa daktari huku akiwa na majibu yale mkononi, kila mtu alisikitika sana
“hakuna haiwezekani kabisa, siwezi kukubaliana na hilo hata siku moja, hakuna mtu yoyote Yule anaeweza isipokua YESU KRISTO WA NAZARETH aliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, hakika kwake yeye ndiye kila kitu dada yangu, mimi nitaenda nae kwa mchungaji wangu Nathaniel Gabriel msasani , naamini Yesu wagu ata tenda miujiza, na Donald atapona!“
Alifoka sana Maria ki ukweli ndani ya moyo wake alikua ni mtu mwenye imani alimuamini Mungu aliamini kuwa Yesu kristo ndiye msaada tosha,
Mzee Deuji akiwa pembeni ali jua vizuri nini maana ya kauli ile alimtambua sana Mchungaji Nathaniel sababu mara nyingi walimfuata usiku na kuishia kuungua na moto, kutokana na kuwa na nguvu za kiroho,

mchungaji Nathaniel hakuna mtu aliye kua hamjui alikua ni bingwa wa kutoa mapepo na kila kitu alikua mchunganyi mwenye imani sana., mamia na maelfu ya watu hufurika katika kanisa lake.
“hapana mimi nakataa, mta mpoteza huyu,, bora tumpeleke hospitali nyingine”
Alizungumza Deuji huku akionesha kuchukizwa na swala lile la Donald kutaka kupelekwa kwa Mchungajji akiamini kuwa mambo yake yote hayatoenda sawa kabisa.




“ bwana yesu asifiwe mama mchunganyi”?!
“milele AMINA”
“nina haraka mama mchunganyi, nime mkuta mchunganyi?”
“hapana ndo nime toka kumsindikiza uwanja wa ndege ameenda Israel,”
“yesu wangu”!
“kuna nini kwani”?
“hapana hakuna shida, hauna namba ambazo nitaweza kumpata huko alipo?”
“labda tusubiri kesho tukijaaliwa uzima, najua akifika salama ata nipigia simu”
“sawa asante sana mama mchungaji”
Yalikua ni mazungumzo baina ya Maria na MAMA mchungaji ndani ya nyumba kubwa hiyo wakiwa seblen, hakuwa na jinsi zaidi ya kumfata mchungai Nathaniel, akiamini kua angeyaokoa maisha ya Donald kabisa, lakini anashindwa la kufanya baada ya kumkosa alitoka nje na kushindwa kujua cha kufanya, hatua aliyo chukua ni kesho yake aweze kuwa tufa baadhi ya wamuini ili waende hospitaliini pale na kumuombea Donald apone mambo yote alimuachia Mungu wake aliye juu mbinguni,
ili kua ni kama nguvu ndani ya roho yake iki msukuma afanye jambo lile, hakika alikua akiongozwa na roho mtaka tifu hilo aliamini kabisa,

Upande wa pili hali ya Donald inazidi kuwa mbaya tena ya kutisha safari hii alianza kukohoa mfululizo na sasa hata kukohoa damu nyeusi,jambo hilo lili mtisha sana Pamela na mama yake mzazi Donald, walikua wakilia sana, kadri muda unavyozidi kwenda ndipo hali yake inazidi kuwa mbaya tena ya kutisha mno!,
“OOOH Donld mpenzi wangu, nini kime mpata eeh Mungu”!
Alilala mika Pamela huku akitoa machozi na ndo ivyo ivyo ilikua kwa mama Donald uchungu ulimbana sana kumuona mwanae kipenzi akiteseka kitandani pale,

********

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG