Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 1/10


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 1 KATI YA 10
*******
 *******

 Jopo la watu lili zidi kuongezeka baada ya kupambazuka kila mtu akitaka kushuhudia kilichotokea,

tena bila kuadithiwa, waandishi wa habari nao kutoka vituo mbali mbali hawa kucheza mbali kila mtu alionekana akiandika kile anachokiona na wengine kupiga picha tukio la kinyama lililotokea,
japokua uzio wa rangi nyekundu uliwekwa pale na jeshi la polisi huku waki fukuza watu wasisogelee eneo la tukio ila hakuna mtu aliye jali,
Ndani.ya club maarufu nchini Tanzania jijini Dar es salaam iliyo fahamika kama CLUB BILL CONERS zili kutwa maiti tatu zilizo uwawa kinyama sana, huku maiti nyingine zikiwa zime tolewa utumbo na macho nje.
"Huyu katolewa macho,"

Aliongea askari mmoja akiwa amevaa glavs mikononi huki akiiendelea kuka gua maiti ile aliiendea maiti ingine ambayo ili tolewa utumbo na kufanya utumbo huo kuta pakaa sehemu nyingine za chini, ki ukweli yalikua mauaji ya kinyama ambayo haya kuwahi kutokea,
hofu ili tanda sana kwa wana nchi hata kwa jeshi la polisi pia
"Shiiiit,. Haya mauaji sijawahi yaona,"
Aliongea askari yule huku akitingisha kichwa chake akiwa ame chuchumaa bado huku akiwa ameshika kichwa chake.
"Afande James, kuna kitu hapa njoo nikuoneshe"
Askari yule aliinuka na kumfuata mwenzake ambae alionekana kama aliona kitu kingine kwenye maiti nyingine,
"HUO NI MWANZO TU,"
yalikua ni maandishi yaliyo chorwa juu ya kifua cha mwana mke aliye kutwa amekufa kwa kutumia damu, ambayo pia nayo ili kutwa ime tobolewa macho yote mawili.
"Mmmhhh, "
Afande james aliguna baada ya kuona ujumbe ule mzito na wa kushangaza sana,

Zoezi la kupima maiti zile liliendelea alama za vidole ziki pimwa na baadae maiti zile kuchukuliwa na kuingizwa ndani ya magari ya polisi huku picha mbali mbali za mnato kutoka kwa waandishi wa habari zikiendelea kupigwa.,
kweli yali kua mauaji ya kutisha ambayo yali msisimua kila Mtanzania ndani ya nchi hiyo na amani kutoweka.

"Hakuna alama za vidole, hakuna sign yoyote ile, huyu muuaji ni proffesional Killer,"

Aliongea Afande Deoglas ambaye kitengo chake kilikua maalumu kwa ajili ya kupima alama za vidole (handprint).
"Sasa hapa tunaanzia wapi?"
Alihoji askari mwingine huku akiwaangalia wenzake.,
"Mi naona hili swala tuli fanye chini kwa chini bila mtu yoyote kujua, tukianzia pale Bill canas, tukianza kuwa kamata watu wote na kuwahoji"
Ghafla simu ya mezani ilianza kuita pale pale na kila mtu kubaki kumwangalia mwenzake, ila Deoglas ana chukua simu ile na kuiweka loud speaker., ambayo ili fanya sauti isikike ndani ya chumba kile na kila mtu.
"MSIJI SUMBUE HAMTOWEZA KUNI PATA, KAMA MNATAKA NIWAFANYE KAMA WENZENU PALE BILL CANAS ENDELEENI KUNI FUATILIA,NITAWAONESHA"

ili kua ni sauti ya kike ambayo ili sikika upande wa pili wa simu na kufanya kila afande aanze kuogopa na kumwangalia mwenzake
"WE NANI?"
afande Omary aliuliza kwa kuzuga sababu alijua tayari simu ili kata ila ali fanya vile ili aonekane kuaa haogopi chochote,
alisimama na kujifanya ana bonyeza bonyeza simu ile ili hali hajui hata namba gani apige,
"Mwana mke huyu, mimi nita mtafuta"
Afande Omary aliongea na kuwaangalia wenzake ambao wote wali kua waki.mwa ngalia.

 wenzake wali baki waki mwangalia na kushusha pumzi ndefu na nzito.
"Sasa utaanzia wapi Omary?"

Alihoji afande mwenzake na kumkazia macho huku akisubiri jibu kutoka kwa mwenzake huyo ambae aliji amini sana.
"Una niuliza ni taanzia wapi?, wewe subiri uone, alafu huyu ni demu sasa, izi ni dharau . haiwezekani hata kidogo Afande Kapila, naomba Deffender mbili, twende bills pale tuka wakamate vijana pale"

Kweli kitendo kile kili fanyika huku baadhi ya maaskari waki anza kuta wanyika ili kuweza kwenda Posta ambapo club ya bill canas ipo.
****************************
"Witness Kafifi"!!

Sauti hiyo ya mshtuko na ya kustaajabu ili toka kinywani kwa mzee wa makamo mfupi wa wastani mwenye kitambi huku kichwani akiwa na mvi mvi chache,
Mbele yake alikua amesimama mwana mke mrefu wa makamo mweupe mwenye macho makubwa kiasi, Uzuri wa mwana mke huyu uliendana vizuri na rangi yake nyeupe ambapo vile vile alikua na umbo zuri lili lojigawa kama namba nane,
na kumchoresha vizuri na kimini alicho vaa na kuweka mapaja yake laini wazi, ki ukweli ali kua ame umbika hasa akicheka vishimo vyake kwenye mashavu huingia ndani yaani Dimpoz, mzee huyo aliba ki kumtazama Witness Kafifi bila kummaliza, na kuji uliza aliingiaje ndani ya nyumba yake kubwa iliyo kua na walinzi kila sehemu , alivuta pazia na kuchungulia nje na kukuta walinzi wake wote wapo chini wame kufa.
"Uli dhani nili kufa,?!, Mr,Sombe,"?

Aliongea witness Kafifi, na kukaa juu ya sofa la hapo ndani ambapo alikunja nne huku mapaja yake malaini yakiwa wazi na kumfanya Sombe aibie ibie kwa jicho moja.,
"Una taka nini Witi?"
"Well, well , well, nataka nini sio?,"
Witness alisimama pale alipo kua na kufungua friji na kutoa moja ya pombe kali, pia alichukua glass na kuimimina kama ni kwake.
Na kuiweka mdomoni huku akimsogelea Mr, Sombe alipo.
"Nime kuja kulipa kisasi,, ila w..."
Kabla haja maliza maneno alisikia mlango una funguliwa na kutokea mwana mke mnene kiasi ambae alivalia nguo za kulalia huku akiwa ana fikicha fikicha macho kutokana na kutoka usi ngizini, moja kwa moja alionekana alikua ni Mke wa Mr, sombe.
"We ni nani?"
Mke wa Mr, sombe moja kwa moja aliuliza huku aki mgeukia Witness kafifi.
"Muulize baasha ako sijui mumeo,"
"Una semaje wewe kahaba"?
Witnes kusikia vile aliweka glass juu ya meza ya kioo na kumsogelea mwana mke yule, kitendo cha sekunde tatu tayari alikua kavunja shingo ya Mke wa Sombe na kumfanya adondoke chini na kupoteza maisha pale pale,
na kumfanya Mr, sombe jasho lianze kumtoka kwa woga na kutokuamini kile alichokiona mbele yake
.
"Mama yangu ali bakwa mbele yangu niki shuhudia, namimi pia nili bakwa kipindi nipo mtoto, huku nikishuhudia baba yangu ana chinjwa kama KUKU mbele ya macho yangu, Na wewe uli husika Mr, Sombe, so you have to pay for what you have done"

Witnes haraka haraka alivunja chupa ya wyn na kubaki nusu, pale pale kwa hasira alimvuta Mr sombe na kutumbukiza chupa ile tumboni huku akitumia vidole vyake viwili kukamata koromeo la Sombe na kumfanya akose pumzi, damu zili tapakaa maahali pale huku Mr. sombe taratibu kukata roho huku akitupa tupa miguu aki kata roho, alivyo hakikisha kila kitu kipo sawa, ali fungua pochi na kutoa chupa ndogo ya spray maalumu wa ajili ya kufuta alama za vidole na kuipulizia kila mahali ili kufuta alama. Zile, alivyo ridhika aliji futa vizuri na kuondoka zake.

Asubuhi yake kesho yake na mapema kuli kucha na Witnes kushtuka hii ni kutokana na simu yake kumshtua usi ngizini, alivyoangalia kiioo cha simu aliona jina FRANK.,
"Huyu mwana ume msumbufu,."

Aliji semea mwenyewe na kubonyeza simu ile kitufe cha kijani huku akiiweka sikioni.

"Una shida gani wewe mwana ume?"
"Lakini Rachel, yaishe mpenzi wangu, mpaka leo sijaona kosa la wewe kuni tesa kiasi hiki"
Uli sikika upande wa pili wa simu.
"Ndo kili cho kufanya uni pigie simu asubuhi asubuhi"?

"Ndio mpenzi wangu"
"Una chekesha, tena una ni furahisha sio kidogo, mbona una kuwa kama ruba, hakuna wanawake wengine,? nakushangaa mwana ume king'ang'anizi,"
"Nipo njiani nakuja, tuongee"
"Shauri yako,"

Witnes alichukua kanga na kuji funika huku aki toka na kuingia ndani ya chumba kidogo ambapo kulikua kuna picha nyingi zime bandikwa, aliitia x picha ya Mr, sombe kutokana na tayari ali muuwa, na kuweka kiduara juu ya sura ya mtu mwingine akimaanisha kuwa ndo anae fuata.
Alivyo maliza hapo alifunga chumba hiko kidogo kwa funguo ambacho hakuna yoyote anae kijua.

Baada ya hapo aliingia bafuni na kufungua bomba la mvua ambalo lili kua linatoa maji kwa juu, .

Alijiandaa vizuri ipasavyo na kutoka nje ila ana kuja mlinzi n a kumwambia kuwa kuna mgeni wake nje,
Ali toka nje na kukutana Na Frank ambae alikua akiongea nae muda mfupi.,
"Ume fata nini kwangu?"
"Nime kufuata wewe Rachel"
"Nashindwa kuku elewa kwa kweli".
Ukubwa wa nyumba ana yoishi Witness Kafifi haiuku mpasa aishi mwenyewe ili kua ni nyumba kubwa ya gorofa mbili, ambapo nje yake kulikua kumepa mbwa vizuri na bustani,
nje pia kulikua na magari yapa tayo nane ya gharama sana na hadhi yake, uta jiri alio kua nao hakuweza kubaba ishwa na mwana ume yoyote yule, alikua ni mfanya biashara wa madini ya dhahabu na almisi akimiliki mgodi mkubwa jijini.Arusha Mererani ila aliishi maeneo ya Msasani na huko ndipo yalikua makazi yake.
Kabla ya kuma lizana na Frank ghafla mlinzi ana fungua geti na kuona gari nyingine aina ya Mark II lina ingia, na mwana ume mweusi mnene kushuka.
"Ooh baby, mambo vipi?"
Mwana ume yule ali mfuata na kumkombatia na kumfanya Frank ashindwe kuelewa kina cho tokea mbele yake.
"Rachel huyu nani?"
Aliuliza Frank kwa Jazba.
"Maria huyu nani?, we malaya huyu nani, si naongea nawewe?"
waliji kuta wana ita majina mawili tofauti.
"Nisikilizeni nyie wajinga wawili, , tena mni sikilize kwa makini,"
Witnes aliongea kwa sauti ya juu na ukali huku akimwangalia kila mmoja.
"Wote hamnijui, mimi sio Maria wala Rachel hilo moja..,"
"Ujue usini changanye, mimi sio mjinga, hivi una ni chukuliaje wewe demu?"
Dickson nayeye alikuja juu , na kuanza kumsogelea Witness
"Wewe mjinga tena fala mkubwa hapa jijini, una taka kufanya nini?, una taka kufanya nini Dick,, alafu tokeni kwangu, kabla sija waitia wezi, washeni magari yenu mtoke upesi"
Witnes kafifi ali waka na kuzidi kupaza sauti huku maneno aliyo kua aki yaongea kweli alikua akiyamaanisha.
"Babu, wewe mzeee,. Njoo utoe taka taka izi nje,. Haraka, chap chap,. Sitaki kuwaona waki kanyaga humu ndani" ali muita mlinzi wake wa getini ali kuja mbio mbio huku akiki mbia .
Witnes Kafifi aliongea huku aki pandisha ngazi za kibarazi hapo na kuweendea mlango huku nyuma aki waacha Frank na Dickson waki baki midomo wazi....


 Jeshi la polisi kitengo cha upelelezi kili zidi kuumiza kichwa na kusugua bongo zao hii ni kuto kana na mauaji yanayo zidi kutokea ndani ya jiji hilo la Dar es salam,
Umakini wa hali ya juu unazidi huku kila mahali mapolisi kanzu waki tanda kila kona ya jiji na kuta pakaa kila mahali, waliye muhisi wali mchukua na kumweka rumande ili kuka milisha upelelezi,

ila wali ambulia patupu, na kuamua kuita kikao kidogo head qourters ili wapange njia nyingine ya kumdhi biti mwana mke huyo ana e ua kikatili bila kujua kwa nini.anaua.

,Vincent Towo mkuu wa kitengo hiko cha upelelezi aliwaita vijana wake shupavu wapatao nane ambao wali kaa kikao kidogo cha siri sana.

"Nasi kitishwa sana na kitendo hiki cha mauaji,. Huyu mwana mke ni.Proffesional killer, ina bidi tutu mie njia mba dala, kumtia mikononi "

Aliongea Vicent Towo, akiwa ame valia suti nyeusi ambayo kooni alivaa tai ambayo ili mkaa vizuri,.
Ali simama na kuwasha projector, ambapo mbele zili tokea picha za mauaji ya hatari na watu hao wali onekana wame kufa kikatili kuliko maelezo.

"Huyu Mwana mke ndo kafanya haya mauaji, huu ni mwaka elfu mbili na tatu, alimuwekea sumu kali ya DDT poison proffesor Mwaipungu,na kuua familia yake nzima, angalia hapa huyu Mama Katibu mkuu wa chama cha YOUTH BRAVE DEMOCRATIC PARTY(YBDP), alimchoma kisu kifuani"

Alizidi kusogeza picha ambazo picha zile zili zidi kuonekana watu walio uwawa kinyama katika maeneo mbali mbali.

"Nina maanisha nini hapa, hawa wote walio uwawa na huyu mwana mke ni wana chama wa YBDP na juzi Mr.sombe na mke wake wame uwawa pia, kwaio sasa huyu mwana mke mi nadhani ana ua yoyote aliye kwenye hiki chama tawala, mi nafikiri kitu kama hiko."

Vicent Towo aliongea huku akitembea tembea ndani ya chumba hiko cha mkutano huku akizidi kuwa sisitiza wazidi kuweka ulinzi na kupeleleza kwa kina zaidi

************************
MIAKA 12 NYUMA.

chama pinzani UNION DEMOCRATIC PARTY(UDP) kilizidi kupinzana na chama cha YOUTH BRAVE DEMOCRATIC PARTY(YBDP), ambapo chama cha UDP kilizidi kupendwa na watu na kiongozi wa chama hiko kili ongozwa na Dimalia Kafifi, ambapo kili kua na wana chama takribani Laki nane na nusu,

Ambapo chama hiko kili tokewa kupendwa na watu wengi sana na wana nchi wali fanya juu chini ili kiweze kupita na kuweza kuongoza nchi ya Tanzania na wakipindue chama cha YBDP ambacho kili kua madarakani ,
"Ndugu wana nchi mna zidi kunipa moyo sana, naamini tuta shida na niwahaidi nita fanya mengi sana"
"Ndiooooooooo,"
Zili kua ni shangwe kutoka kwa Wana nchi ambao wali openda chama cha UDP ambapo jukwaani ali simama Dimalia Kafifi katika moja ya miku tano,

ila kitu cha kusha ngaza ghafla mabomu yalianza kupigwa na watu kuanza kuta wanyika , askari hao FFU kutoka kitengo cha kutu liza gasia walianza kupiga mabomu ya machozi kila pande ila wana nchi pia walianza kujibu masha mbulizi waki tumia mawe kuwa rushia.

Askari wa kutuliza gasia baada ya kuzidiwa walianza kurusha risasi za moto na mwishowe kuuwa watoto wawili huku waki mkamata Dimalia Kafifi na kumpeleka lupango kwa kosa la kufanya mkutano bila kibali chochote,

Baadae wana muachia huru na kugundua kuwa zili kua ni njama za chama pinzani cha YBDP ivyo hakua na la kufanya kwa sababu ndo chama kilicho kuwa madarakani,

Taratibu za mazishi ya watoto wale walio uwawa kili ongozwa na Dimalia Kafifi na wananchi wengi sana,
Uli kua ni msiba wenye simanzi sana na kutia huzuni , kila mtu ali guswa sana katika Jiji hilo la Arusha,
Dimalia Kafifi akiwa na mke wake Dorika na mtoto wao mdogo Aliyeitwa Witness

ambae wakati huo alikua na miaka tisa,wali kua sebuleni, hasa baada ya uchaguzi mkuu kukaribia,
Ivyo chama kilicho kua madarakani kili onekana kuzidiwa haswa na skendo mbaya za dhuruma na mauaji ivyo wana nchi wengi wali kipiga vita na kutaka chama cha Dimalia Kafifi kichukue madaraka huku yeye waki mchagua awe raisi wa Tanzania,

"Baba Witness, naamini utaenda kushinda maana wana nchi wana vyo kupenda sijui ume wapa nini?"
"Sija wapa kitu chochote zaidi ya kutetea wanyonge na kuwapa haki zao kama watu, una jua wengi hukimbilia siasa ili kupata mapato makubwa ila mimi nipo tofauti na wengine, niombee mke wangu niweze kushinda niingie madarakani, naamini hii nchi ita badilika nina mipango mingi sana, "

Aliongea Dimalia Akiwa na mke wake chumbani wakiwa wanaangalia video huku waki sikiliza hotuba mbali mbali za nchi.

Z ili baki siku saba ili ucha guzi mkuu ufanyike na watu wengi sana wali onyesha kuwa mstari wa mbele kukipigia kura chama cha UDP, ucha guzi uli fanyika vizuri huku kila mtanzania akisubiri majibu huku wakiwa na furaha chama cha UDP kina enda kushinda ila katika hali ya ajabu na kusha ngaza watanzania Chama Cha YBDP kiliiibuka kidedea kwa kupata kura asilimia Themanini huku chama cha UDP kiki fuatia na kura asilimia Sabini na Tano, kitu ambacho kina wa fanya watanzania waanze kufanya fujo wakiamini vizuri sana kuwa kura ziliibiwa, hivyo walianza kuandamana sana na mabango.

Dimalia Kafifi akiwa katika hali ya mawazo na kutokuamini pia siku iyo alipo kea simu kutoka kwa makamu wa raisi wa chama tawala Dr.Amani Kaborou.

"Sikia Dimalia, ngoja nikwambie ukweli,we ndugu yangu, kusema ukweli kura wame iba, ila naomba nikuambie siri, wana kuja kukuua fanya mipango uhame"

Ili kua ni sauti ya makamu. Wa raisi Dr, Amani Kaborou ambaye alikua mbunge wa Afrika Masha riki na sasa hivi ni makamu wa raisi ambae ali chaguliwa muda mfupi, , ana muuwa kumpa siri nzito Dimalia ambayo ina zidi kumchanganya akili yake.
"Sikiliza nikwambie Dr, Amani, mimi siwezi kukimbia popote, kama kuniua acha nife ndani ya nchi yangu, wacha nife tu"
"No Dimalia,. Hapana, tafadhali,. Nenda Turkey kule mimi nita kuja"
"Nime sema siwezi,"
Dimalia alikata simu na kushusha pumzi ndefu,
Ila kabla haja fanya lolote ghafla kishindo cha mlango wake ulilia na mlango kufunguka na watu kuingia na kumvamia na kuanza kumpiga ,
aliweza kumtambua mtu.mmoja aliye itwa Rameck Alikua ni mwana chama wa YBDP,
Walizidi kuingia na kuanza kupasua vitu vya ndani,
Baadae ana muona mke wake ana letwa mbele yake na kuanza kumchania nguo zake wali chana blauzi yake ya juu na sketi aliyo vaa na kuanza kumwingilia kimwili bila ridhaa yake,

walianza kumbaka tena waki pokezana kwa zamu.
"Tayari Shirima zamu yangu"
Mmoja wa watu hao alisema ivyo na pia yeye kuanza kumwingilia kimwili huku wakiwa wame mshika miguu na mikono,

Dimalia alivyo taka kuji toa kwao alishindwa kutokana na Watu walio mshika wali kua wengi,
Kitendo cha kubakwa kwa mke wake kili kua cha kinyama sana,
Aliji kuta ana lia kwa uchungu sana kama mtoto mdogo, alilia kwa uchungu huku akiwa omba wamuachie mke wake, ila ndo alikua kama ana wa chochea, kili cho muuma zaidi ni pale alipo muona mke wake ana vuja damu nyingi sehemu za siri ila wao hawa kujali, waliendelea na zoezi lile Mpka akapoteza fahamu ila cha kustaajabu walizidi kuendelea na zoezi lile,
Dimalia alifumba Macho na kuangalia pembeni ili asione kitendo kile cha kinyamA, ila kilicho muuma zaidi baada ya kuge uza shingo alimuona Mtoto wake Witness akiwa chini ya meza ame jificha huku ana lia kwa uchungu sana,

Witnes Alishuhudia kila kitu, japo kua alikua mtoto mdogo ila alijua ni kiasi gani wazazi wake wali kua kwenye matatizo makubwa sana na wange hitaji msaada,
hasa alipo muona mama yake akiwa uchi wa mnyama huku akiingiliwa kimwili na watu wale ,

aliji kuta ana banwa na hasira na kuanza kububu jikwa na machozi ki ukweli haikua picha nzuri kwake.
Mmoja wao alitoa panga na kumsogelea Dimalia Kafifi baba yake.
"Nawewe tuku bake kama mkeo"?
Lili uliza jitu hilo na kumuwekea panga shingoni huku wenzake wakianza kucheka.

 Dimalia Kafifi aliwaangalia kwa uchungu huku machozi mengi yaliyo changanyika na kwikwi kuanza kumtoka, kweli roho ili muuma sana na kuji kuta ana lia kwa uchungu

Alijitoa kwa nguvu katika mikono ya watu wale walio mshika na kumfata mke wake alipo lala na kuvua shati aki mfunika kwa juu,

Aligeuka na kumtazama Rameck kwa macho ya huruma huku yakiwa na machozi

"Rameck, kwanini ume amua kufanya kitendo hiki cha kinyama, kwa mke wangu, ambae hana hatia"?
"Sisi hapa tuna fuata maagizo na si vinginevyo"

Alijibu Rameck kwa kejeli na kumsogelea Dimalia kafifi pale alipo,
aliomba panga na kuka bidhiwa pale pale,.
Na kuanza kumpiga piga Dimalia Mgongoni kwa kutumia ubapa,
"Tulia tulia, tulia, mkeo mtamu sana, kumbe ulikua una faidi"eee bwana mkubwa?

Maneno yale yali mfanya Dimalia apandwe na hasira na kusimama ili amvae Rameck kwa kitendo cha kuongea maneno yale mbele yake,
ila alizuiwa na kundi lile la watu na kumuweka chini.
Bila kuuliza chochote Rameck aliinua panga na kuli pitisha shingoni mwa Dimalia aliinua na kupiga tena shingo kama ana kata mfupa mkubwa wa nyama,.
Damu nyingi zili ruka kila sehemu na mwishowe kichwa cha Dimalia kili kua pembeni kiki tenganishwa na kiwili wili huku kiki dondoka kama mpira,
damu ziliruka kama chem chem ya maji na baadhi kumrukia Witness Ambaye alikua chini ya meza ya kulia chakula ame jificha,

Alishuhudia mwili wa Baba yake uki cheza cheza kama kuku aliye chinjwa huku uki rusha rusha miguu na mikono, alivyo angalia kichwa cha baba yake ambapo kili dondoka karibu yake aliyaona macho ya baba yake yana mwangalia huku damu ziki zidi kuta pakaa eneo lile.

Hakuamini kama leo hii mtu aliye zoea kumuita Anco Rameck ndo ame fanya kitendo kile cha kinyama,
Kweli ali tamani atoke ili
aweze kupambana nao ila ana jikuta hawezi kutoka alipo jificha aki hofia nayeye ange uwawa kika tili, na kivyovyote asingeweza kupambana na watu wale., hasira zake ziliisha kwa kutoa machozi.

Ali meza fundo la mate huku akiji shika mdomo wake na kububu jikwa na machozi mengi na kufanya rangi ya uso wake uzidi kua mwekundu sana.

"Jamaa si alisema tupeleke kichwa chake, chukua twenzetu, tusha maliza"
Rameck aliongea na kuanza kuchukua kichwa cha Dimalia Kafifi na kuki weka ndani ya mfuko na kuangalia huku na kule, alichukua kile alichokiona kina mfaa na kuondoka nacho,bila kujua kuwa Witness ali shuhudia kila kitu kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Witnes alivyo hakikisha watu wale wame ondoka alitoka mbio mbio na kwenda mpka juu ya mwili wa mama yake mzazi ambao uli kua chini una vuja damu sehemu za siri
"Mama Angu amka, Mom, Mom nawewe ume kufa,? Mama amka mama,"
Alizidi kumtingisha tingisha mama yake akiwa pale chini, alienda pia juu ya kiwili wili cha baba yake na kuanza kulia sana ,
"Dad, Dad, please wake up Dad , dont go Dad, Dad please, Dad(baba , baba, tafadhali amka, usiondoke,baba tafadhali)
Ki ukweli alikua kama amecha nganyikiwa,
machozi aliyo toa haya kuweza kubadili ukweli uli okua ume tokea pale, haukuweza kumfufua baba yake ambaye alikua mbele yake muda ule, haya kuweza kurudisha sauti ya baba yake ambae hupenda kuta niana nae,
hakuamini kama muda mfupi walikua waki cheka wote na leo hii ame lala kimnya ame kufa, aliji kuta ana lia na kupiga kelele.

Majirani walianza kuso gea na kufika ndani ya nyumba hiyo na kusha ngazwa sana na mauaji ya kinyama yaliyo tokea,

Kila mtu ali baki akisha nga sana usiku huo,
Na kumuonea huruma Witness ambae wakati huo alikua ana lia sana,

Ndani ya masaa mawili tayari Mama witnes alikua yupo hospitali akifanyiwa matibabu ya haraka sana ili kuokoa maisha yake, kweli madaktari bingwa wali jitahidi kuokoa maisha ya Mwana mke huyo na kufanikiwa chini ya usaidizi wa Atu Kihaka ,
"Mume wangu yuko wapi?"
Swali hilo lili toka kinywani mwa Dorika , wakati huo akiwa na nafuu ila bado alikua na maji ya dripu mkononi, na baada ya kuamka ana muulizia mume wake.,

Pembeni alikua daktari pamoja na muuguzi wa kike Atu Kihaka,
ila muuguzi huyo alipo taka kujibu daktari yule alimpa ishara na kumbania jicho asiongee ukweli.

"Mama, mumeo ana endelea vizuri, karibia ana ruhusiwa, yupo chumba kina chofuata,"

Muuguuzi yule wa kike ili mbidi aseme ivyo kutokana na hali mbaya aliyo kua nayo Dorika haku taka amtoneshe kidonda kingine,
"Naweza nika muona?"
"Sio kwa sasa hivi, pumzika kwanza, hata ivyo hapa nime toka kumchoma sindano nyingine, usijali ata pona,"
"Mwanangu Witness"?
"Mwanao mwanao yupo,"

Dorika aliji kuta ana rejewa na tumaini na kutabasamu huku akige ukia upande wa pili baada ya kuridhishwa na majibu yale kutoka kwa muuguzi yule.

Jopo la watu lili zidi kuta pakaa ndani ya mahakama kuu iliopo Arusha,
ambapo Kizimbani alipandishwa Rameck akiwa ame shikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuumuaa Dimalia Kafifi,
ambapo baada ya kupanda ana kanusha kila kitu,,na kukataa kata kata , baadae ana,panda mtoto mdogo wa miaka tisa Witness kafifi kama shahidi, japo kua alikua mdogo sana aliweza kuelezea kila kitu tangu mwanzo ilivyo kua.
"Nika muona Anco Rameck, ame shika panga na kuanza kumkata Dad, mimi nili kua nili kua chini ya meza , nili kua naogopa, baada ya hapo Anco Rameck aka chukua kichwa cha Dad, na na na na...."
Pale pale Witness aliji kuta ana lia kwa uchungu baada ya taswira ya picha ya baba yake kuji jenga kichwani akiwa hana kichwa huku,
akitupa tupa miguu na mikono ali shindwa kuongea na kuanza kulia sana kwa uchungu.

"Witnes usilie Mwanangu endelea,"

Wakili Wa upande wake Eveline Mbelwa alimfuata na kumfuta machozi huku aki mpa uja siri na kumpa kitambaa ajifute machozi.

"Ongea kila kitu mwanangu, watu walio muuwa baba yako wata chukuliwa hatua."
"Sawa Anti,"
Witness aliitikia kwa kwikwi na kuzidi kuendelea na ushahidi akiwa juu kizimbani pale. ambapo kila alicho ongea majaji wali kua makini waki andika juu ya makaratasi yao.
Witness aliendelea kuongea kila kitu bila kuogopa,
Watu wenye machozi ya karibu wali jikuta wana lia na kumuonea sana huruma Witness, wali jikuta wana toa vitambaa na kuanza kuji futa machozi,
Kila mtu haku tegemea kama mtoto mdogo kama yule ange weza kuongea mambo mazito kama yale Hakimu Nickodemasi Lazaro Saranga alivua miwani yake na kushusha pumzi ndefu ambapo alichukua makaratasi yake na kumtazama jaji na nyundo kugongwa mezani.
"Kesi ime hairishwa, na ita sikilizwa tena mnamo tarehe kumi na mbili mwezi ujao huku tuki msubiri shahidi mwingine wa pili, "

Jaji aliinuka na huku akiacha mino ng'ono ya chini chini, Rameck na witnes waliangaliana macho. Kwa macho , ambapo wakati huo Rameck ali fungwa pingu na kurudishwa rumande mpaka kesi yake ita kapo somwa. Pia kumsubiri Dorika aweze kutoka hospitali ili aweze kupanda kizimbani ili aka milishe usha hidi.

Ila kile kili choendelea wali mficha Dorika kutokana na ugonjwa mbaya wa moyo pamoja na BLOOD Pressure,
Ivyo mambo haya yali fanyika chini kwa chini na kumzuia hata Witness asiende hospitali kwenda kumuona Mama yake mpka arejewe na hali yake ya kawaida.

Kweli kwa Dorika hali yake ili mrudia kama kawaida na kuba kisha siku moja ili aweze kuruhusiwa,
Akiwa juu ya kitanda alimuona mtoto wake akiwa na daktari,
Ali achia taba samu la uchovu na kumwangalia Mwanae ambae ali mpenda sana.
"Njoo Witness, Dad ume muona, ulienda kumsalimia?"
Swali hilo lili mfanya Witness aanze kulia tena , Na kumshangaza Dorika mama yake ambae alikua hajui kina choendelea kwa wakati huo.
"Mom,. Dad amek...ufa,moo..m"

Daktari ali mvuta Witnes ila alikua kasha chelewa, Dorika alianza kutoa macho huku akihema kwa kasi sana na kutupa tupa miguu kutokana na mshtuko alio upata
,
"Nesi, naku hitaji mara moja,
Upesi upesi, Atu Atu nakuomba,"

Huku na kule madaktari wali jaribu kutumia kila njia,
Alichukua kifaa cha kupima mapigo ya moyo ila baada ya kupima daktari alimuangalia nesi Atu huku aki tingisha kichwa kuashiria kua tayari Dorika kafariki dunia.
"Tume chelewa"
Aliongea daktari yule ila alisahau kama ali funga mlango na kumuona Witness akiwa mlangoni ana waangalia.


 Atu Kihaka alivyo geuza shingo nayeye pia ali muona mtoto yule Witnes ambae wakati huo nayeye alianza kuingia ndani ila alivyo taka kuingia Muuguzi yule Atu alimuendea na kutoka nae nje ya chumba kile.

"Mom amekufa?"
Aliuliza Witnes swali ambalo lili mfanya muuguzi yule amwangalie machoni na kushusha pumzi ndefu.
"Hapana, hajafa"
"Hapana una nidanganya nime sikia Nime sikia, Mom, Mom"

Witnes alianza tena kulia akitoa machozi yaliyo changanyika na makamasi mepesi,

Roho ya huruma ili muingia muuguzi yule nayeye kuji kuta ana dondosha chozi
akimuonea huruma mtoto yule aliye kuwa mbele yake.. alimnyanyua na kumbeba huku kichwa chake akiki weka begani kwake.

Na kumfariji ili anyamaze, kweli Witness aliji kuta ana lala kuto kana na usingizi ulio mpitia huku akiwa ame bebwa na Atu Kihaka.

"Tulikuja kwa udongo, na tuta rudi kwa udongo, Mungu azi raze roho za marehemu mahali pema peponi Amina"

Ili kua ni sauti ya Mchunganyi Petro akiongoza msiba huo na safari ya mwisho ya Mr, Dimalia na mrs Dimalia,

Kilio kilizidi kwa Watu hasa kwa Witnes, ambapo alichukua mchanga uliokua juu ya chepe na kuurusha ndani ya kaburi,
Huku pembeni akiwa ameshikiliwa na watu,
Kweli hakuamini kama leo hii wazazi wake wame fukiwa na hato waona tena, alijua nini maana ya neno kufa, japo alikua mdogo.

Baada ya siku kadhaa kupita kesi ili endelea kuunguruma huku aki saidiwa na Eveline Mbelwa aki mtetea kama wakili wake wakizidi kumkandamiza Rameck.

Ila cha ajabu siku iyo ana pokea habari nzito nyingine zina zo mshtua kwamba Eveline Mbelwa ame uwawa pia,
Aliona kama amepigiliwa msumari wa moto kichwani. Hakuamini kama leo hii nguzo aliyo itegemea nayo ime potea na kuzima kama mshumaa,

"Witness ina bidi uka kae kwangu, Hapa nyumbani sio salama kabisa, Twende nime kuja kuku chukua twende Moshi"

Alikua ni Mjomba wake ambaye alikua ni kaka wa Mama yake Dorika,
aliamua kufanya ivyo hii ni kutokana na kuhisi yupo katika hali ya Hatari sana,
Alipanga nguo zake haraka haraka na kuchukua begi lake dogo na kuingia ndani ya gari la mjomba ake huyo.
"Anco Yona, kwanini wame muuwa Anti Eve?"
"Wana taka asiendelee kuku tetea, Hawa watu ni hatari sana,. Huku una poenda uta kua salama Witnes mwanangu"

Yona aliwasha gari na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwake Marangu Mtoni mkoania Kili manjaro,.

******************************

Gari aina ya Alteza taayari lili egeshwa nje ya Club Maisha,

na mwana mke aliye valia gauni fupi lili lo mchora maumbile kushuka na kuonesha tiketi yake mlangoni ambapo alipita pita mpka kuingia ndani,

na kuagiza kinywaji.
"Nipatie smine off kaka"
Aliongea mwana mke huyo na kutoa pesa ambapo baadae alipewa na glass ,

Aliangalia huku na kule akionekana kama aki mta futa mtu, alivyo hakikisha ame muona aliinuka na kumfata katika sofa kubwa alilo kua ame kas, nayeye alienda na kuketi pembeni yake.

"Samahani Anco,naweza nika kaa pembeni yako"?
"Bila shaka, hakuna tabu mrembo"
Mwana mke yule alikaa huku.aki mdadisi wapi aanze kumuingia.
"Samahani kama na kufananisha ,"
"Nani mimi?"
"Yaah, wewe una itwa Rameck?"
"Yaah ndo mimi,?, ume nijuaje?"

"Aaaah jamani, sasa mimi nisikujue wewe, muda mrefu kidogo , sidhani kama una nikumbuka naitwa Natasha,tulisha wahi kuonana sehemu nakumbuka"

Mwana mke yule ali mpa mkono Rameck ambae pia ali mpa na kumuangalia kwa muda mrefu sana kama akivuta kumbukumbu.

"Any way,. Sio mbaya mi najuana na watu wengi,. Umesema Natasha eeeh?'"
"Ndio, "

Waliendelea kunywa na mwishowe kutimu saa nane za usiku Rameck akiwa amelewa sana haji tambui,

Mwana mke yule ali mchukua na kuingia nae ndani ya gari yake ALTEZA na kuondoka na Rameck.

"Sasa.... Tunaaaakwenda waaapi Naaatashaa,. Where are we going?" Aliuliza Rameck kwa sauti ya kilevi huku akiyumba yumba

Ila Mwana mke yule ali mkata jicho kali na kuzidi kupiga gia.

"Una taka kujua tuna poenda, subiri uta jua sasa hivi"

Baada ya kuona hakuna hata gari moja aliweka gari pembeni na kufungua mlango ambapo alitoka na kumtoa Rameck nje ya gari.

Ali mburuza na kumlaza chini nyuma ya gari na kutoa kamba na kumfunga mguu mmoja ambapo kamba nyingine aliifunga vizuri nyuma ya kichuma cha gari kama wana vyotaka kuvuta magari mabovu.

"Anco Rameck, Mimi ni.Witness,.wala sio Natasha Nili kua nakuta futa kwa muda mrefu sana,. Najua hata wewe ulikua ukini tafuta na kuni winda, sasa leo ndo mwisho wako"

Rameck hakuamini kama aliye simama mbele yake alikua ni Witness Kafifi alihisi pombe zote zili muisha na kuinua kichwa chake huku aki fikicha macho.
"Witness Kafifi"
"Abeee,. Ngoja uone"

Witnes aliingia ndani ya gari na kuli washa ambapo aliingia juu ya lami na kufanya kama ana vuta gari na aliye kua ana mvuta alikua ni Rameck ambaye kwa mikono yake ali mkata baba yake mzazi,
picha ili yo pita kama mkanda ndani ya ubongo ambayo alimuona baba yake akikatwa ili pita taratibu na kufanya hisia za hasira kumkamata, ali kanyaga mafuta akizidi kutoa kasi huku nyuma Rameck akizidi kupiga kelele kutokana na kuchunika ngozi taratibu huku akiji sugua juu ya rami, ali piga sana kelele za maumivu, huku taratibu akiacha nyama nyama na damu juu ya rami hio ambapo gari hilo lili kua lina mburuza kwa kasi...

 kitendo cha gari lile alilo kua anaendesha Witness kafifi kuzidi kwenda kili mfanya Rameck azidi kupiga kelele akipaza sauti kuto kana na maumivu makali sana aliyo sikia juu ya mwili wake ambao tayari nyama za miguu zilitoka zote na sasa hivi kubaki mfupa ambapo uliokua una onekana kwa ndani.

shati alilokua amevaa tayari liliisha na nyama sasa za tumbo kuanza kulika zikibakia juu ya lami.

"Witness wi.....tnes una niiuaa na...kufaaa naku...kukukuufa "
Rameck alizidi kupiga kelele,
Na ghafla gari alilokuwemo.ana endesha Witness kusimama, na Witness kushuka na kumuendea.
"Wit ina tosha , naumia nionee huruma,.nakufa"

Kweli kwa wakati huo Rameck sura yake haiku tambulika kutokana na michubuko na damu nyingi kumta pakaa kila mahali, alikua kama mzoga wa nguruwe au Mbogo,

"NO siwezi kuku samehe, nita endelea hivi mpka uta kapo kata roho Rameck"

Kweli Witness alimaanisha kwa sababu baada ya kuongea hayo alifungua mlango wa gari na kukanyaga mafuta kwa mwendo wa kasi na kuzidi kumburuza Rameck juu ya lami hio ambayo taratibu alianza kuishiwa nguvu na damu nyingi iliyo sababishwa na vidonda vya michubuko.

Witnes alizidi kunyoosha mguu akizidi kwenda kwa kasi sana huku akiwa na hasira sana,

Kwa mbele aliona gari kubwa kwa haraka haraka alijua ni lori kutokana na taa za gari hizo kuwa kwa juu,.
Alizidisha mwendo na baada ya kulikaribia alikunja kona ya ghafla kulia huku akilipitia mbele yake upande wa pili na kufanya matairi ya Lori lile kukanyaga juu ya mwili wa Rameck ambapo matairi yote yali mpandia ,.
Witnes alizidi kusonga mbele na kusi mama pembeni ya kimsitu kidogo na kushuka,
Alimtizama Rameck ambapo wakati huo alikua kimnya tayari amekata roho,

Hakuishia hapo alichukua dumu lenye mafuta ya petroli lililo kua ndani ya gari na kumiminia mafuta ya patrol juu ya mwili wa Rameck na mwishowe kulimiminia gari hilo petroli, ali fanya hivi kwa lengo moja tu kupo teza ushahidi , alivyo hakikisha kila kitu kimeenda sawa,
Aliwasha kibiriti na kutupa juu ya mafuta na kusa babisha mlipuko mkali mithili ya bomu, alikaa kwa muda akitizama gari linavyo teketea kwa moto, na kushusha pumzi nzito,

Alitoka mbio mbio na kuta futa taxi na kuwaza kitu kimoja tu kurudi kwake., baada ya kumaliza moja ya kazi yake.

**************************

Tayari alifika Mkoani
Kilimanjaro ambapo Mjomba wake Yona alimuonesha upendo wote na kumtunza kama mtoto wake wa kumzaa ila hii ilikua tofauti kwa mke wa Yona, Irene
Ambapo haku mpenda Witness mtoto huyo hata kidogo,
"Nani alikwambia uje kula hapa mezani, si nili kwambia kwako ni jikoni wewe mtoto mbona husikii?"
Alifoka Irene mke wa Yona wakati wa kula chakula cha usiku Witnes alimuangalia na kuchukua chakula akielekea jikoni ila alikutaana na mjomba wake Yona
"Rudi mezani"

Aliongea kauli moja tu ila witness alisua sua ila Yona alimshika mkono na kuanza kurudi nae mezani huku akiwa ame kasirishwa sana na kitendo kile. Kweli kitendo cha Witness kuteswa kili kua kina muumiza sana kupita maelezo ila leo hii aliji kuta ana chukia sana .
"Hivi mbona una kuwa ivyo lakini?"
Alihoji Yona akiwa amesimama na kumwangalia Mke wake Irene.
"Nakuaje kivipi?"
"Huyu mtoto ame kukosea nini?"
"Basi tu. simpendi, nawewe kwani vipi?"

"Alafu usini pandishie sauti Irene, nakwambia usini pandishie sauti. Siku izi hauna heshima si ndio?"
"Kwani huyo mtoto wako au, nawewe usini zingue hapa"
"Una semaje,?"

Yona ali msogelea Irene na kumpiga kofi la shavu ila Irene nayeye ali simama na kurudisha kofi lile na kumpata yona.
.
Kitendo kile kina muudhi sana Yona na kuanza kumvaa Irene na kuanza kumsha mbulia makofi na ngumi kwa hasira.

Irene lipapasa pembeni na kushika kisu kidogo kwa hasira alijikuta ana mchoma nacho Yona tumboni na damu kuanza kuvuja eneo lile, taratibu Yona alianza kumuachia Irene na kuanza kudondoka chini huku akiishiwa nguvu.
"Yona"
Irene aliita na kubaki akitoa macho na kubaki kuganda , alimwangalia Witness ambae wakati huo machozi yalianza kumlenga.
"Ancoo Yona'"
Witness aliita huku taratibu aki msogelea huku machozi yakianza kumtoka.

 Akiwa Chini yona Damu zilizidi kumvuja ziki tokea maeneo ya tumboni na kumfanya mke wake Irene kuzidi kuchanganyikiwa na kujutia kwa kitendo kile alicho fanya na kujua kweli hasira ni hasara,
alizunguka huku na kule asijue nini afanye kwa wakati ule, aliji shika kichwa huku akipiga piga miguu chini.

"Yona Yesu wangu. ,yesu yesu wangu"
"Anti tumpeleke anco Yona hospitali"

Aliongea Witness baada ya kuona Irene yupo katika hali ya kuchanganyikiwa,
Kweli wazo lile lina muingia akilini na haraka haraka kuingia chumbani na kutoka na funguo za gari akiwa amezishika mkononi,
"Kamuite mlinzi fanya upesi, ila usimwambie kilicho tokea, usi mwambie mtu yoyote yule"
"Sasa nita semaje anti?"
"Nime kwambia nenda"
Witness hakua na jinsi.zaidi kutoka nje mbio mbio huku mikononi akiwa ame lowa damu,

Haraka haraka Mlinzi wa getini alifika eneo lile na kushangazwa sana na kitendo kile.
"Mama kuna nini?, nini kime mpata bosi?"
"Embu acha maswali nisaidie kumuingiza ndani ya gari"
Mlinzi yule alibaki akitoa macho na kuto kuamini anachokiona mbele yake ,
Alimuona Yona ana vuja damu nyingi tumboni huku bado akiwa na kisu kile juu ya tumbo.

Mlinzi akiwa ame mshika Yona upande wa miguu huku Irene akiwa upande wa kichwa msobe msobe walianza kuliendea gari lililokua nje ya maegesho na Witness kufungua mlango na kumuingiza Yona.

"Sasa nitaenda mwenyewe baki na huyu mtoto."
"Utaweza kwenda mwenyewe"?
Alihoji mlinzi.
"Ndio nime kwambia baki na Wity"
Irene alima liza kuongea huku aki funga mlango wa gari ambapo alichomeka funguo kwenye switch ya gari na kuzungusha ambapo gari hilo lili waka na Irene kutoa gari nje kwa kasi.

Mambo yaliyo kua yanaendelea kwa witness kafifi hakutaka kuamini aliji ona ni mwenye mkosi sana,
Ila furaha ina mrudia tena baada ya kusikia Mjomba wake ame pona na hali yake inae ndelea vizuri na muda mfupi ange ruhusiwa ili.kua ni kama miujiza kwake maana hakuamini kama mjomba wake ange pona

"Shikamoo Anco Yona"
Alisalimia Witness baada ya kumuona Yona akishuka ndani ya gari upande wa pili huku aki mfuata na kumkombatia.
"NO witness uta niumiza hapa nina kidonda mwanangu, ..hujambo"?
"Sijambo Anco , nime furahi kukuona"

Witness alishindwa kuzuia furaha yake na kuji kuta akilia kwa furaha,
"Yona twende ndani"
Upande wa pili.ulisikika ambapo alikua ni Irene mke wake baada ya kushuka upande wa pili wa gari. Wote waliingia ndani na kuanza kula chakula cha mchana,

Siku zilizidi kwenda na miaka kukatika ,Witness akitunzwa vizuri na mjomba wake Yona, ambapo tayari alikua kashamaliza darasa la saba na kubahatika kucha gulia kuingia elimu ya sekondari, ili kua furaha sana kwa yona, Kitendo kile kina mchukiza sana Irene ila ana weka tabasamu la uongo na bandia.
"Hivi witnes ukiwa mkubwa una taka kuja kuwa nani?"
Lili kua swali kutoka kwa Yona siku iyo wakiwa seblen wanaangalia t,v kipindi cha wanyama ambacho witness hupenda sana kuangalia. Ambapo hufurahi sana hasa akimuona simba anavyo kimbiza swala na wanyama wengine.

"Anco Yona mimi nikiwa mkubwa napenda kuja kuwa mwana jeshi. Tena natamani sana nije kuwa komando, "
"Mmmh, witness ?, kwanini una taka kuja kuji tesa ivyo"?
"Sio kuji tesa Anco, mi napenda tu niwe Commando,
Kama Anord, si uliona movie ya Anord?"
"ule ni uwongo usije uka jidanganya mule wana act tu hakuna ukweli wowote."
"Ila mi napenda tu kuwa kama vile, niwe najua kupi gana , kushika silaha."
Upande wa yona alijua wenda ni kutokana na utoto, ivyo alili puuzia jambo lile ila kwa Witness Alizidi kuli sisitiza na kusimamia msi mamo wake.

Alianza kidato cha kwanza katika shule za kata ambapo darasani ana zidi kufanya vizuri sana na kuzidi kuwa shangaza walimu, walimu wali mpenda sana kutokana na upole wake,
Miaka ilizidi kwenda na Witnes kuanza kukua ambapo kifua chake kilizidi kuwa kikubwa na kusa babisha maziwa yatoke mwili wake ulizidi kunona na kuwa mlaini huku uki randana vizuri na sauti yake nyororo sana, hakuishia hapo umbo lake pia lili jigawa vizuri na kumfanya awe na makalio makubwa ya wastani huku akifanana na mwendo wa bata mzinga,. ki ukweli alikua mzuri hasa anapocheka na dimpos kuonekana,
Wana ume hawa kucheza mbali wali anza kumtongoza ila hawa kuambulia chochote.
"Mbona hunielewi Mussa, si ku taki, siku taki , siku taki,mimi na mapenzi ni vitu viwili tofauti"
Maneno hayo yali mtoka Witness akiwa ndani ya mgahawa wa shule akila chakula cha mchana,.
"Lakini wity ,. Jaribu kuni fikiria"
"Mgonjwa kweli wewe, ..mimi sasa hivi ni candidate, niache kufikiria mtihani wangu wa taifa niku fikirie wewe Mussa,.. kwanza nita kuja uni fundishe linear programing,, maana ticha Michael siku muelewa kabisa leo class."
"Sawa nita kufundisha, "
"Hapo ndo una ongea sasa, sio una ongea mashudu yako,.. "
Witness tayari wakati huo ali fikia kidato cha nne tena ili baki miezi michache afanye mitihani ya kumaliza kidato cha nne,

Miezi ili pita na kweli kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne,
Baada ya majibu kutoka ali furahi sana hasa alivyo pata daraja la kwanza ,. Ili kua ni furaha nyingine pia kwa Yona mjomba wake,

Rafiki yake Yona Aliyeitwa Sunday ali fika mkoani kilimanjaro kwa lengo la kumsalimia Yona ,
"Sunday, huyu ana itwa Witness mtoto wa marehemu dada yangu"
"Mmmh, ndo kakuwa hivi?"
"Ni muda umepita sana ndo maana, kamaliza fom four hapa juzi, ame pata one,.Witi huyu rafiki yangu. Uta muita Anco Sunday"
"Shikamoo"
Alisalimia Wity kiufupi na kuigeuzia shingo t,v ambapo kulikua na kipindi cha wanyama.

Basi mazungumzo yaliendelea na Sunday kuchukua jukumu la kuondoka na Witness jijini Dar es salaam ili akaendeelee na elimu ya kidato cha juu,
Kweli jambo lile lina fanyika na safari ya kwenda Dar es salaam kuanza Sunday akiwa ana endesha gari huku pembeni akiwa witnes kafifi akiwa mwenye mawazo sana juu ya kwenda kuanza maisha mapya na mageni, hakua na jinsi zaidi ya kuka biliana na hali,

Witnes alishangazwa sana na hali ya hewa ya joto ndani ya jiji hilo la Dar es salaam ili mlazimu avue koti alilo vaa, kutokana na joto kali na jua la utosi.
"Hapa pana itwa Mbezi tangi bovu:: ndo napoishi"
Alivunja ukimnya Sunday.

"Joto kali sana, mnaishi vipi huku?"
"Uta zoea tu wala usijali"
Gari lili.egeshwa nje ya nyumba kubwa kiasi iliyo pambwa na bustani nzuri na Sunday kushuka ambapo alikuja kupokelewa na mfanyakazi wa ndani.
Baadae witness ana oneshwa chumba cha kulala,
Aliingia bafuni na kuji mwagia maji na baadae kuju muika kula chakula cha mezani usiku huo.
"Kwani Anco Sunday.,anti yuko wapi?"
"Aaah Anti yako amesa firi, ila ata rudi usiwe na wasi wasi, usha onyeshwa sehemu ya kulala'"?
"Ndio"
Aliendelea kula Witness na baada ya kumaliza alishukuru na kwenda kulala, kutokana na mawazo mengi usingizi uli mpitia na kulala fofofo kama mzigo,

0 comments:

Post a Comment

BLOG