Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 7/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 7 KATI YA 10
*******
 *******


JESHI LA WACHAWI LILIKUA LIPO KASI YA AJABU usiku huo angani wengine wakiwa na
nyungo huku wengine wakiwa juu ya fisi,wakiwa wana piga kelele sana huku wakisherekea safari yao kutimia ya kwenda kumchukua Donald.! Mzee Deuji akiwa juu ya fisi alikua ana furaha sana muda wote,
Hakua tena Yule tajiri ambae ana tikisa Tanzania nzima alikua amevaa kibwaya huku na shanga nyingi kiunoni mwake, ambapo juu aliji funga kitambaa jeusi, kilicho fanana na kilemba, mkononi alishika kibuyu kikubwa , huku akiwa na irizi miguuni

Safari yao iliishia juu ya paa la hospitali ambapo baada ya kufika tuu zilisika sauti za watoto wachanga zikilia sana. Upande Fulani watoto wadogo wachaga huwa wana waona wachawi,

Kelele zile hazikuwazuia wachawi wale washindwe kuingia ndani mule, walianza kumimina dawa zao katika kila kuta ya pembe na kuanza mmoja baada ya mwingine kuingia wakitumia makalio yao,

Upepo mkali ulianza kuvuma huku sauti za bundi zikisikika kila kona ya sikio la Donald alihisi baridi kali sana mwilini mwake, na kumfanya atetemeke kupindukia, alivyoangalia pembeni aliwaona wachawi wakiingia wengine wakiwa uchi wa mnyama na kumuona Mzee Deuji akipita na kumsogelea karibu.
Pamela akiwa pembeni ya kiti na mama yake Donald hawa kuelewa lolote lile linalo endelea baada ya kupigwa dawa za kichawi ambayo hakuna bina damu wa kawaida angeweza kuwaona,
Baada ya wachawi wote kutimia walikizunguka kitanda cha Donald na kuanza kumpaka dawa zao, kila walilofanya walifanya kwa hesabu zao na umakini wa hali ya juu sana.
walimchukua na kumnywesha damu ya nyoka, na baadae kuanza kumvuta ambapo baada ya kutoka kwenye kitanda alibaki Donald kivuli.

Pamela alikua wa kwanza kushtuka baada ya kumuona Donald ana tingisha tingisha miguu kama kuku anayechinjwa aliruka mbio mbio na kutoka nje na baadae kurudi na daktari, , Daktari Yule haraka haraka alitoa kifaa cha kupimia mapigo ya moyo, ila baada ya kupima kidogo Donald alitulia na kufanya hofu kutanda ndani ya chumba hiko.
“dokta kuna nini”?
Waliji kuta wakiuliza swali hilo kwa pamoja Pamela na MAMA Donald huku wakitawaliwa na hofu kubwa sana ndani ya mioyo yao,! kitendo cha Doald kutulia kili washtua sana kabla ya kupokea majibu kutoka kwa daktari walianza kulia,!
“naomba kidogo mtoke nje jamani”
“dokta nini kimempata mwanangu?”
“mama subiri nje kidogo”
Ili mbidi daktari Yule awatoe nje ilii ajaribu kuangalia tena vipimo vyake kwa hali ya utulivu sana, baada ya vipimo vile alishusha pumzi ndefu na nzito huku akitoka nje,

“dokta vipi”?
“Wewe ndiye mama yake”?
“ndiyo”!
“pole Mama mwanao amefariki Dunia, kazi ya Mungu haina makosa, poleni sana!”
Dokta Yule aliongea maneno yale bila kujua yana uzito kiasi gani na kumfanya Pamela aliye kua pembeni adondoke chini mzima mzima sababu ya taarifa zile kuwa mbaya sana kwake,na kumfanya azirai pale pale,
“Donald weeeeeeee Donald mwananguuuuuu, uwiiiiiiiiiiiii. Ume niacha na nani mama yako, Donald wanguuu!?”
Aliliia mama Donald kwa uchungu sana kumpoteza mwanae wa pekee,. bila kujua upande wa pili alichukuliwa msukule…


KILIO KILIZIDI kuendelea ndani ya hospitali hiyo mama Donald hakutaka kuamini kua leo hii mwanae kipenzi kafariki dunia, yaani kwa maana nyingine hatokuwepo katika sura ya dunia , uchungu ulim-bana na kujikuta akilia kwa uchungu sana, daktari aiyekua pembeni yake alikua na kibarua kingine cha kumpa moyo huku wauguzi wengine

wakimuinua Pamela ambaye alikua chini amezirai na kumpeleka chumba maalumu ili wampe huduma ya kwanza,
Pamela baada ya kupewa huduma ya kwanza alianza tena kulia machozi mengi kila alipo mkumbuka Donald hakika ilikua ni siku ya kuuzunisha kwake alitamani iwe ndoto lakini haikuwa ivyo,liliotokea hapo lilikua ni jambo la ukweli kabisa, bila kujua upande wa pili baba yake mzazi ndiye aliye mchukua Donald msukule,
Hakukua na jinsi nyingine zaidi ya kukubaliana na matokeo hayo kuwa Donald alifariki dunia, kulikua hakuna namna nyingine ya kuubadili ukweli zaidi ya kumuachia mambo mengine Mungu aliye juu mbinguni,
Ndugu jamaa na marafiki walianza kupigiwa simu kuhusu taarifa za msiba huo kila mtu aliguswa sababu Donald bado alikua kijana mdogo ambae bado alihitaji kuishi na kufanya mambo mengine ya maendeleo, leo hii amefariki, lili kua ni jambo lililochukua muda mchache tangu aanze kuumwa,

“mama mimi sijafa,, nipo hai usilie mama yangu, usilie mama mimi sijafa!”
Ili kua ni sauti ya Donald ikiongea baada ya kumuona mama yake akiwa ana lia kwa uchungu ila kilicho kua kina tokea hapo hakuna hata mmoja aliyeweza kumuona , alikua tayari kesha chukuliwa na wachawi.!
“Pamela usilie mpenzi wangu,! mimi nipo hai baba yako ni mba-ya sana, baba yako ndiye kaniua, baba yako sio mtu mzuri,.. wewe mzee unalia nini mnafki wewe, wewe mba-ya sana”
Donald alikua akiongea huku akitembea kwenye msiba wake alimfuata mzee Deuji ambae aliji fanya analia na kuanza kumpiga ila ilikua ni kama kivuli sababu kofi alilo mpiga lili pita kama upepo,
“kway rafiki yangu, mimi sijafa mbona ivyo lakini, msilie rafiki zangu, Gloria usilie”
Bado Donald alikua akitanga tanga huku na kule kwa kila mtu aliye kua akilia lakini ukweli ni kwamba hakuna hata mtu mmoja aliyeweza kumuona,

Baadae alisikia kilio sana baada ya jeneza kushuka alivyoangalia aliona mgomba ndio upo ndani ya jeneza na kuzidi kuchanganyikiwa. katika macho ya kawaida waliona ni Donald lakini haikuwa ivyo hata kidogo,.

“uwiiiii mwananguuuuu Donald, Mungu weeeee, nitabaki na nani baba, wewe ndiye ulikua tegemeo langu siku zote mwanangu, ume niacha mwenyewe mwanagu kwanini?, kwanini? Ulikubali kwenda na kuniacha mwenyewe mama yako, basi bora unge niacha mimi nita ngulie, eeh Mungu kwanini ume mchukua mwanangu mapema jamani”
Kilikua ni kilio cha mama Donald baada ya jeneza lile kufika na kuwekwa mbele pale ili waweze kuuaga mwili wa Donald kwa mara ya mwisho., ilikua ndiyo kama watu waliambiwa walie sababu kila mtu alianza kulia,
vilio vilitapakaa kila kona ya pembe, pia hata Deuji alijifanya kulia sana, alijiinamia chini na kutoa kitambaa chake huku akiji futa machozi yake usoni,hakika kilikua ni kilio cha kuuzunisha sana , watu waliizidi kukusanyika sinza kwa Mama Donald , watu walizidi kufurika sababu walikua kipenzi cha Donald kijana aliyekua ana ongea na kila mtu hapo mtaani na mcheshi pia.!,
Pamela alilia kama mwendawazimu kabisa! hakutaka kuamini kuwa hiyo ndiyo siku ambayo asingeweza kumuona Donald mpenzi wake tena, aliilia sana na safari hii machozi yote kumkauka sasa!
Ukweli ni kwamba Donald hakufa kama walivyo dhani duniani au ulimwenguni alikua tayari yupo katika ulimwengu wa kichawi tena ulimwengu wa kutisha sana, uimwengu wa mambo ya giza ambapo ukiingizwa huko hutoki kabisa pasipo kua na nguvu za kiroho za ziada, kulikua kuna hitajika nguvu za kiroho na za Mungu,

Wachawi walianza akushuka mmoja baada ya mwingine na kumfuata Donald pale alipo.
“niacheni niacheni!”
“wakati wako ume fika sasa, tuna hitaji kuondoka nawewe”
“niende wapi?”
“ha ha ha ha ha, uwende wapi mjukuu wangu?, wewe huku ushakufa, tuna subiri wakuzike tu, ili tukuchukue”!
“Mungu yupo”
“yuko wapi Mungu wako?”
Yalikua ni mazungumzo baina ya Donald na bibi huyo kizee aliye kua ameshika kibuyu mkononi hakuna hata mmoja wa watu waliopo hapo aliye gundua kina choendelea ,
Mwili wa Donald ulianza kuagwa na tayari kwa kwenda kuzikwa . waliozimia walizimia waliio lia walipaza sauti zao wa ki-mlilia kijana wao mdogo Donald
“parapanda italiaa, parapanda, watakua wamekwisha nyakuliwa …kweeenda ….”!?
“kumlaki bwana Yesu mawinguni,”
Nyimbo zilianza kuimbwa ndani ya Costa hilo ambapo ndani yake kulikua kuna ndugu waliokua wanalia sana, huku nyuma kulikua kuna gari maalumu kwa ajili ya kubebea jeneza ambapo ndani yake waliamini alikua ni Donald kumbe ni mgomba,
Baada ya dakika chache tayari walikua wamefika sinza makaburini na kushusha Jeneza!,
“tulitoka mavumbini na tutarudi mavumbini,Leo hii tuna mzika ndugu yetu, mwenetu , rafiki yetu Donald Membe, katika nyumba yake ya milele, naamini ata pumzika kwa amani huko alipo, na nina aamini pia Mungu ataenda kuya samehe yale makosa yote aliyo fanya, tulikuja kwa mavumbi na tutarudi kwa mavumbi!”
Yalikua ni maneno kutoka kwa mchunganyi Petro, huku akichukua mchanga ulio kua juu ya chepe na kuurusha ndani ya kaburi, kili cho sikika hapo ni vilio vya chini chini vya uchungu, baada ya hapo vijana walikuja na kuanza kufukia kaburi hilo huku vilio vikianza tena upya!.
“mchunganyi hata wewe una aamini kuwa nime kufa?, mimi sijafa jamani”
Bado Donal alikua akihangaika bila mtu yoyote Yule kujua kuwa yupo mahali pale,
Alitembea huku na kule akiongea na kila mtu lakini jibu ni kwamba hakuna hata mmoja aliyeweza kumuona alilia sana na kuweweseka, !.
“mjukuu wangu muda wako sasa ume fika, tuna weza tukaenda”
Pale pale alipigwa na usinga na kulegea ambapo walishuka wachawi wengine na kumuweka juu ya fisi na safari ya kupaa angani kuanza, walikua wakipishana na magari kabisa bila waendesha magari kuwaona, na kuzidi kutokomea huku wakipiga kelele za ushindi…..


NDOTO ZA AJABU zina zidi kumsumbua Pamela kila usiku ukifika alikua akimuota Donald karibia kila siku iendayo kwa Mungu, bado mpaka leo hakutaka kuamini kuwa mpezi wake Donald amefariki Donald na tayari wamesha mzika, ila ndoto alizokua akiziota zilizidi kumshangaza kabisa!,Alivyokua akijarbu kumueleza mama yake alipewa jibu kuwa apunguze mawazo,
“PAMELA PAMELA, huku nateseka sana, Pamela , Pamela huku nateseka sana, nahitaji msaada wako”
Alikurupuka kitandani baada ya kusikia sauti hiyo kwa mara ya kwanza alidhani wenda ana ota ndoto, ila alishtuka na kufikicha macho yake na kuji piga kofi shavuni, cha ajabu alizidi kusikia sauti ile ikitokea dirishani, ilikua ni sauti ya Donald ikiita jina lake, alitega tena sikio vizuri na kweli alisikia sauti ya Donald ikimuita.
Alishuka taratibu akiwa na hofu nyingi hasa ndani ya moyo wake! alipowasha taa alisikia kishindo cha mtu kiki ki-mbia na kutokomea, taratibu alitoka nje kimnya kimnya na kumuendea mlinzi wa getini,
“masai huja mruhusu mtu yoyote kuingia usiku wa leo”?
“aisee siesi fanya ivyo, mimi nalinda kila saa, nyumba yote mi nasunguka niko vizuri sana, siwesi kulala hata kidogo!”
“embu nisi ndikize huku nyuma”
Masai Yule alishika kirungu chake vizuri huku pembeni akiwepo mlinzi mwingine na bunduki kubwa mkononi, waliongozana mpaka nyuma ya nyumba dirishani kwa Pamela lakini hawa kuona dalili ya mtu yoyote Yule kuwepo, mbali na hapo hakukuwa na dalili yoyote ile ya hata unyayo wa mtu kuonekana,
Jambo lile lii zidi kumchangaya Pamela, na kutoelewa hatua gani afanye.!

MIJEREDI NA FIMBO ZILIZIDI KUTUA mwilini mwa Donald akiwa amefungwa juu ya jiwe kubwa usiku huo, kwa kosa la kutoroka,. misukule waliokua hapo kwa kazi iyo ya kusurubu mtu ambaye ataenda kinyume na kazi hiyo walizidi kumchapa Donald baada ya amri hiyo kutoka kinywani mwa Mzee Deuji,

Damu zilianza kumvuja sasa mwili mzima huku akizidi kupata kipigo kile alilia kwa uchungu lakini hakua na jinsi ingine ya kufanya
“mchapeni nyie, acheni mchezo, au mmeshindwa adhabu iwe yenu”?
Alifoka Deuji.
“ababa baba baba ba ba”
Waliongea misukule hiyo huku wakiendelea kumsurubu Donald bila huruma kilicho tokea hapo ilikua ni picha ya kutisha sana, usiku huo misukule hiyo ilikua haiwezi kuongea sababu tayari walikua wame katwa ulimi, ili kua bado zamu ya Donald ambapo siku arobaini ziki fika tangu afe ndipo wata kapo mkata ulimi na kuungana na misukule hiyo rasmi,na zilibaki siku chache tu! Ili hatua hiyo iweze kukamilika kabisa!.
“hiyo ita kua fundisho kwa mtu yoyote Yule atakaye toroka au kwenda kinyume na matakwa ya humu ndani”
Ivyo ndivyo ilivyokua baada ya adhabu hiyo kuisha Donald alifunguliwa na kuoneshwa shamba kubwa alime huku akipakwa dawa usoni, yalikua ni zaidi ya mateso ambayo hata bina damu yoyote Yule wa kawaida hakuweza kustahimili , hayo ndiyo yaliyokua yakindelea katika ulimwengu huo wa kichawi.

“BWANA YESU ASIFIWEEEEEEE”
“AMEEEEEEEN”!
“AMEEEEEEEEN”
“mshike mwenzako mkono mwambie kuwa upako wa bwana yesu upo mahali hapa leo hiii.shetani ata shindwa katika JINA LA YESU, NILIKUA Israel kule juzi hapa, nili tembelea JERUZALEM, na kuona mambo mengi! , nikaenda mpaka GALILAYA ,amini usiamini kuwa yesu yupo, nili tembelea SAFINA lililojengwa na NUHU, nimeona mabaki yake kwa macho yangu.. bwana Yesu asifiwe sana”!
Yalikua ni maneno kutoka mdomoni mwa Mchunganyi Nathaniel akiwa juu ya madhabau mamia na maefu ya watu walifurika ndani ya kanisa hilo na waumini wengine wakikosa hata viti vya kukaa huku wengine wakiwa nje, ili mradi waweze kusikia neno la mchunganyi huyo jumapili ya siku hiyo.!
Maria nayeye alikua miongoni mwa waumini waliokuwepo ndani ya kanisa hilo kwa nia moja tu mchunganyi akimaliza mahubiri nayeye aweze kumueleza jinsi gani ndoto ya Donald inavyo msumbua hakika aliamini kua kuna kitu au njia ambayo Mungu alimuonesha kwa njia ya ndoto hakutaka jambo hilo aliachie lipite hivi hivi, aliamua kumshirikisha Mchungaji Nathaniel ili aweze kumuelezea ndoto ile ina yomsumbua, kila usiku uingiapo.
Waumini wa kanisa hilo la UPAKO NA UZIMA la mchunganyi Nathaiel lilizidi kufurika watu, wengine wakitoka mikoa mbali mbali hata sehemu mbali mbali kuja Dar es saalam kuombewa na kufunguliwa.
Baada ya kumaliza kuhubiri ndani ya kanisa hilo waumini walianza kuimba nyimbo za kuabudu na kusifu,
“tuna kuabudu bwana ndiwe bwanaaaaaa, kila tuku itapo bwana una shukaaaaaaaa”!!
Baada ya kumaliza kuimba nyimbo za sifa na kuabudu wote walifungua macho ila mchunganyi Nathaniel aliya gandisha macho yake juu ya mwana mke mmoja aliye kua mbele yake amevalia gauni yenye
mpasuo mkubwa huku mapaja yake yakiwa wazi, ili kua ni makusudi sababu mwana mke Yule alijua vizuri sana kuwa mchungaji ana muangalia na kuzidi kuipandidsha sketi ile juu,
Upande wa pili mwana mke Yule alitumwa kutoka kuzimu ili kuja kuharibu maombi ili amfanye mchunganyi ashindwe kuhubiri na aingiwe na tamaa,.! kuzimu kweli huwa wana muogopa sana Mchunganyi Nathaniel huwa akitaja jina la Yesu huliisikia na kuungua moto, leo hii waliamua kumtuma msichana huyo mrembo ili aweze kuya funga maombi yake yasiweze kufika,
Mchunganyi alitabasamu kidogo kisha akachukua kipaza sauti na kukiweka karibu na mdomo.,
“nataka kuwaonesha kuwa leo hii shetani atashindwa katika JINA LA YESU, shetani hana mamlaka juu ya nguvu za Mungu, roho mtakatifu ana niambia kuwa kuna kitu humu ndani ya kanisa, nataka kuwaonesha kitu Diana simama juu”!
Mwana mke Yule alishtuka sana baada ya kutajwa jina lake hakuuelewa jina lake mchungaji kalijuaje,
“Devotha njoo mbele hapa, nataka umpokee roho mtakatifu, na usiwe mtumwa wa shetani kuanzia leo,”
Mchunganyi Nathaniel aliongea huku akishuka ngazi zilizokua juu ya madhabau hayo na kumshika mkono Devotha na kwenda nae mbele ya madhabau,
“kabla sijaamua kukuteketeza na moto wa Yesu kristo, pepo uliye ndani ya huyu mwana mke toka katika jina la yesu,”
“UUUUUH UUUUH TUNA TOKA TUNA TOKA, TAFADHALI USITUUNGUZE”
Aliongea mwana mke Yule kwa sauti ya kiume kuonesha kwamba a liye kua ndani yake ni pepo au aliongozwa na nguvu za giza
“nani kawa tuma?”
“mmmhhh mmhhhhh mhhhhhh”
Dada Yule hakuweza kuongea tena alikua bubu pale pale, na kumfanya Mchunganyi NATHANIEL atabasamu kidogo,
“ha ha ha ha eti wame mfanya bubu hawa taki huyu binti aongee, ila nasema katika jina la Yesuu, muachieni huyu binti”
Pale pale mwana mke Yule alidondoka chini huku akitingisha miguu yake kuashiria kua mapepo yana toka,
Maombi yalizidi kuendelea huku mchunganyi Nathaniel kuzidi kutaja jina la YESU, hakiuchukua hata dakika moja tayari mwana mke Yule alisimama, na waumini kupiga makofi ya ushindi,
“kwa yesu kila kitu kita wezekana, shetani ata shindwa daima,Dada upo tayari kumpokea yesu kristo awe mwokozi wa maisha yako”?
“ndi ndi ndio mchunganyi nipo tayari mchunganyi, ila kuna watu wana teseka sana huko kuz….”
Kabla ya kumalizia maneno dada Yule alianza kutoa mapovu mdomoni huku akifuka Moshi na kufanya waumini na baadhi yao kuanza kushaangaa na kuingiwa na hofu ila ilikua tofauti kwa Mchungaji Natahniel Gabriel yeye alizidi kumsogelea huku akiomba sana…




“hatu toki, hatutoki hautuwezi”
Aliongea mwanamke Yule huku akiwa chini akishushiwa maombi.alionekana kabisa kama ni mtu anaeungua na moto sababu alivyokua akiongea alikua ana weweseka sana. .
“kwa Yesu mtatoka “!
Maombi yalizidi huku mchungaji akizidi kumkemea mwanamke Yule na kumfanya atulie kimnya, bado waumini hawa kutaka kuamini, waliokua hawana imani sasa walikua nje wakitandwa na hofu ila kwa wenye imani imara wote waliungana na Mchungaji Nathaniel wakiomba sana, baada ya hapo mwanamke Yule alisimama na kumshukuru Mchungaji .
“usini shukuru Mimi mshukuru Mungu,!”
Baada ya hapo kilicho tokea ni kuimba nyimbo za ibada na kumsifu Mungu ndani ya kanisa hilo, . baada ya ibada kuisha moja kwa moja nayeye Maria alimuendea mchungaji Nathaniel ofisini kwake , na kumuelezea kila kitu juu ya ndoto ana yoota akiihitaji msaada wa tafsiri ya ndoto ile.
“ulisema una ota kuwa huyo Donald ana omba msaada wako, alafu ukimfuata una shindwa kutokana na mbele yako kuna shimo kubwa”?
“ndio mchungaji, na ni ndoto hio tu huwa ina nisumbua kila siku”
“kuna kitu hapa, najua Mungu ana taka kukuonesha kitu, naomba ufunge na kumuomba Mungu hakika lazima ataifungua ndoto yako na utaielewa tu, mwombe sana Mungu”
“asante Mchungaji”
Baada ya maongezi hayo walisali na Kumshukuru Mungu wakiwaombea watoto yatima na wagonjwa wote ma-hospitali na kuomba ulinzi kwa Mungu nchi ya Tanzania izidi kuwa ya amani, .
Maria aliondoka akiwa na amani ya roho, kweli alipania kufunga na kumuomba Mungu wake akiamini kuwa kuna kitu kime jificha ivyo Mungu anajaribu kumuonesha kwa njia ya ndoto,

Kila kukicha hakuacha kumuomba Mungu akipiga goti mpaka wakati mwingine akinena kwa ndimi na aliamiini kabisa roho mtakatifu ameshuka ndani yake ivyo bado alihitaji kusali sana, hakuacha kulitaja jina la Donald kila wakati na kumuomba Mungu afungue vitu vilivyo jificha..

*****

BADO PAMELA alikua mwenye mawazo mengi sana juu ya sauti ya Donald baada ya kuwaeleza wazazi wake hakuna hata mmoja aliye mjali na kumsikiliza walimuona mwenda wazimu au chizi mapenzi! Kusikia sauti ya mtu aliye kufa, lakini baba yake alielewa fika nini kinaendelea, siku iyo tena usiku alisikia tena sauti ya Donald usiku wa manane alivyo taka kutoka alisikia mtu akikimbia,
“mama nataka leo usiku tulale wote usikie , najua uta niamini”
“Pamela acha mawazo, amesha kufa Donald tayari, najua ulimpenda sana, punguza mawazo mwanangu, ina kubidi tu usahau!”
“hapana mama naomba uniamini, leo lala na mimi uta sikia mwenyewe”
“sawa, nita fanya ivyo”

Usiku ulipo fika kweli mama yake aliamua kulala na binti yake ili aweze kuyaamini maneno yale aliyokua akizungumza mwanae kama yana ukweli, saa saba ili fika na sasa ili timu saa nane za usiku, bado hakukuwa na dalili yoyote ile ya kuwa na sauti ya mtu.
“Pamela Pamela, njoo unisaidie mpenzi wangu, huku nateseka”
Tayari Donald alianza kuita tena , hapo hapo alimuamsha mama yake ili nayeye aweze kusikia kile anacho sikia,
“mbona sisi kii sauti yoyote ile?”
“Mama husikii sauti”?!
“mwanangu ninge kwambia, sisikii sauti ya mtu yoyote Yule, ”

Pamela alizidi kuchanganyikiwa ki ukweli alisikia sauti ile, ila mama yake hakuweza kusikia sauti ilehata kidogo, hakuelewa ni jinsi gani ange mshawishi mama yake aweze kumuamini, mama yake aliogopa sana alijua kivyovyote vile mwanae angeenda kuwa chizi au mwenda wazimu kabisa, ili kua ni lazima afanye jambo ili mambo makubwa yasitokee wakati ule, ikiwezekana ampeleke hata milembe akiamini huko ata patiwa matibabu ya akili yake ambayo aliamini kuwa inaanza kuharibika kabisa!.


*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG