Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 1/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 1 KATI YA 10
*******
 *******

 *******

Donald na Pamela ni mtu na mpenzi wake, tangu utotoni walianza mapenzi tena walikua wenye
malengo makubwa sana waliweza kuhaidiana vitu vingi sana, wakiishi jijini Dar es salaam, Donald akiishi sinza na Pamela akiishi oysterbay baada ya kutenganishwa na Donald hii ni kutokana na baba yake pamela Mr,DEUJI kutoku pendezwa na mahusiano ya mwanae na Donald mtoto wa maskini,

Pamela katika maisha yake hakutaka kumpoteza Donald hata kwa sekunde moja, kweli yalikua ni mapenzi ya dhati na mapenzi ya kweli, Pamela hakuku bali mara kadhaa alikua akitoroka kwao na kwenda sinza ili mradi amuone Donald ili roho yake ili ridhike, ali tumia kila njia na wakati mwingine aliwahonga walinzi wa getini pesa nyingi ili mradi atoke nje kwenda sinza, ili amuone mpenzi wake ambae wakati huo moyo wake wote uli dondoka kwa Donald na wala si vinginevyo. aliamini Donald ndie mwana ume pekee katika maisha yake hakujali umaskini wala hadhi ya familia ya Donald kweli alimpenda sana kuliko kitu chochote kile duniani.

kwa upande wa familia ya kina Pamela baba yake Mr, DEUJI akiwa mwenye uwezo mkubwa sana kifedha akichuana na matajiri wengi nchini Tanzania, alikua ana pesa nyingi sana kupita kiasi , bila serikali kujua pesa izo kazitolea wapi na zili tokana na nini.

ivyo serikali ilia mua kuingilia kati na kuanza kumuhoji, ila wali tulia baada ya mr, DEUJI kuwaonesha mali zake pamoja na hotel nyingi alizo kua nazo nje na ndani ya nchi hiyo, ki ukweli alikua na pesa sana, hakuna aliye kua hamjui Mr, DEUJI sababu katika matajiri wa nchi hiyo ya Tanzania nayeye alikua miongoni mwao.,

vile vile utajiri wake uli mfanya awe na jeuri na mwenye nyodo kupita kiasi hakutaka mwanae aolewe na maskini, alipenda angalau aolewe na mtu mwenye uwezo pengine kuzidi yeye, lakini vile vile alibahatika kupata watoto wawili tu,

wa kwanza aliitwa Erick na wa pili aliitwa Pamela. kati ya watoto hao hakuna hata mmoja aliweza kujua kama duniani kuna shida yoyote,
walisikia tu kwa watu. ila kwa upande wao walikua watoto wa kisasa maana kila walipohitaaji kitu chochote kwa wazazi wao, wali fanyiwa mara moja, ndani ya nyumba yao kulikua na wafanya kazi wa kila aina, wali fanyiwa kila kitu hata kufua nguo zao hawa kuwahi kufua,wafanya kazi maalumu kwa ajili ya kufua nguo zao walikuwepo wakilipwa pesa nzuri,

Akiwa nyumbani pamela ana subiri matokeo ya kidato cha sita, alipokea simu na kupewa taarifa kuwa amefaulu na amecha guliwa kuingia chuo kikuu, ili kua furaha sana kwake hasa alipo sikia kuwa amechaguliwa chuo kimoja na mpenzi wake Donald akiamini kuwa anaenda kuku tana na Donald tena ki ukaribu zaidi.

"hakika Mungu ameya sikia maombi yangu"

alijisemea Pamela huku akiwa mwenye furaha sana kupita kiasi,

uzuri na umbo zuri la pamela lili mfanya kila mtu ampende kimapenzi ila hakuna hata mwana ume mmoja aliyeweza kubahatika kuiona nguo yake ya ndani isipokua kwa Donald peke yake, ndiye mwana ume aliyeweza kubahatika kuiona nguo yake ya ndani na si vinginevyo.kwa upande mwingine pia Donald ndie aliye mfanya awe mwanamke sababuu ndiye aliye mtoa bikira yake.

utanashati wa Donald hata uzuri wa kijana huyo ukiendana na sura yake ya upole uli fanya wana wake wengi wamtamani kimapenzi tena wenye pesa zao ila waliambulia patupu na kusimamia msimamo wake kuwa pamela ndie mwanamke wake, ivyo ndivyo ili vyo kua.

Donald aliishi na mama yake, hakuwahi kumjua BABA yake, ivyo alimpenda sana Mama yake hii ni kutokana na Mama yake kumpa historia kwamba baba yake alimtelekeza tangu akiwa na mimba yake, hio haikumuummiza kichwa sababu alipata mapenzi yote kutoka kwa mama yake huyo ambae kwa upande wake alikua ni kila kitu kwake.

ila mara kwa mara aligombana na Mama yake juu ya yeye kuwa na mahusianno na pamela,MAMA yake hakutaka kusikia kabisa habari za Pamela.
"ila Mama mimi nampenda sana Pamela, nampenda sana, unani nyima haki yangu"
"naju una mpenda mwanangu, najua una mpenda sana pamela ila tatizo lipo moja wazazi wake, wana uwezo sana, sio saizi yako yule mwanangu, utapata matatizo mwanangu, kuna tabaka kubwa sana kati yetu na yao"

MAMA Donald aliye itwa Prisca alimkatisha mwanae.

ki ukweli alimpenda sana Donald sababu alikua ni mtoto wa pekee aliongea mengi sana na mwanae siku iyo akijaribu kumsisitiza juu ya mahusiiano yake na Pamela ila Donald hakutaka kuisikiliza habari ile, hakuwa tayari kuachana na Pamela iwe kwa kifo au uhai,

Shamra shmra na nderemo za pamela kuchaguliwa kujiunga chuo kikuu, ili mfanya baba yake Mr, Deuji amfanyie sherehe ya kumpongeza binti yake huyo pamela, huku akiwaalika matajiri wenzake mbali mbali nyumbani kwake oysterbay, magari mengi ya kifahari yalikua yapo nje ya uwanja mkubwa wa mzee huyo .

nyumba kubwa hiyo ili tosha kabisa kwa watu kuingia ndani ya nyumba hiyo kubwa ya gorofa huku sehemu maalumu yakiwemo magari vile vile,

kwa upande wa Pamela hakuona umuhimu wa sherehe hiyo bila kumualika mpenzi wake Donald
"si una jua wazazi wako hawa pendi kuniona niwe karibu nawewe pamela , "

upande wa pili ulisikika wa simu.
"kwa hilo usijali Donald, njoo mpenzi wangu, ita kua vizuri tena wajue mimi nakupenda kwa dhati na nime kuchagua wewe, na baba yangu hawezi kuku fanya lolote siku ya leo, kuna wageni wengi"

Pamela aliweza kumshauri Donald na mwishowe kukubali kwenda kwenye sherehe hiyo ili amridhishe PAMELA mwana mke anaye mpenda kupita kiasi....



Baada ya dakika thelathini tayari Donald alikua nje ya geti akigonga kwa hofu sana sababu hakuwa na uhakika kama ata kubaliwa kuingia ndani ya nyumba hiyo kubwa ambayo ili fananishwa na kasri ya mfalme sababu ili kua ni kubwa kupita kiasi,

"aroo we si ulikatazwa kuingia humu ndani,?! mbona una kuwa king'ang'anizi sana ivyo wewe kijana"?

aliongea mlinzi wa getini akifoka baada ya kumuona Donald nje ya geti hilo akigonga.
"Ebu mwache apite kwanza ukome, kilicho kuleta hapa ni kufunga na kufungua hili geti na sio kufukuza watu wanaoingia humu ndani"
alifoka Pamela baada ya kufika na kukuta malumbano yale, alicho fanya alimshika Donald mkono na kuingia nae ndani.

kelele na vifijo pamoja na nderemo vili pigwa baada ya shampeini kufunguliwa ili kua ni furaha kubwa sana na yenye furaha hasa kwa wageni waaliikwa ambao walikua wakila na kunywa.

"Daddy yule kijana ame kuja na yupo ukumbini na Pamela"

ili kua ni sauti ya Erick akimchongea Pamela kwa baba yake, ki ukweli hata Erick kaka yake pale haku pendezwa na mahusiano yale na Donald,

japo kua Erick alikua ni rafiki wa karibu yake ila hakupenda wala kutaka kusikia dada yake awe na mahusiano na Donald .
nayeye pia ana lipiga vita swala hilo, kutokana na yeye pia kuwa jeuri sababu baba yake alimkabidhi moja ya kampuni zake aziendeshe ivyo ERick alishika pesa na kuzijua akiwa bado kijana mdogo sana.

waliinuka na baba yake huku ERick akiwa nyuma na moja kwa moja kuwa fata wakina Pamela na Donald ambapo walionekana kukaa pembeni ya pembe ya sitting room
"hivi wewe kijana una mtakia nini mwanangu?, nili shakwambia uachane na mwanangu hausikii sasa sijui una taka nini,"?

alifoka mzee DEuji huku akiwa na jazba nyingi sana na kufanya wageni waliokuja kugeuza shingo kuwaangalia, ili kua ni picha mbaya sana kwa Pamela kwa kitendo cha Donald kufokewa vile, na kuanza kujutia maamuzi ya kumuita kwenye ile sherehe,

Mr, DEuji aliogopeka sana si kwa Pamela wala Donald kila mtu aliingiwa na wasi wasi sana, wageni waliokua pale ili bidi wasitishe zoezi la kula na kubaki kuwaangalia, mr, DEuji alizidi kufoka huku akiwasogelea karibu,

"Nawewe Pamela, mara ngapi nime kukataza kukuona na huyu taka taka mbwa!, nikuitie mwizi, kwanza ulipitia wapi?"
"lakini Dady"!
"nawewe kelele nita kulabua sasa hivi"

pale pale waliitwa walinzi na kumtoa Donald kama mwizi aliyeiba kitu, Pamela akiwa analia akimuonea sana huruma Donald kweli roho ili muuma sana kupita kiasi pengine aliji laumu kwanini alikua na baba kama huyo, alilia kwa uchungu sababu Donald hakustaili kutolewa kama mbwa, mwana ume anaempenda , mwana mme aliye jitolea maish yake kufa au kupona leo hii ana dhalilishwa tena mbele za watu vile vile mbele ya macho yake.

Kwa hasira alipandisha ngazi na kuelekea chumbani kwake sababu hakuona umuhimu wa sherehe hiyo, aliingia na kujifungia mlango huku akilia kwa uchungu sana. Mama yake aliliona hilo na kumfuata nyuma , na kumuomba afungue mlango,

kweli mlango ule uli funguliwa na mama yake kuanza kumbeleleza mwanae sababu hakupenda kumuona akiwa katika hali ya majonzi, kazi ya kumbeleleza ilianza amabpo alimchukua na kukiweka kichwa chake kifuani kwake huku akimfuta machozi,

"Mama siwezi kunyamaza nampenda sana Donald, na baba ame fanya kitendo cha kinyama kufanya vile, ina niuma mama, ina niuma sana" aliongea Pamela kwa kwikwi
"usijali nitaongea na Baba yako,usilie mwanangu, nitaongea nae kila kitu kitaenda sawa mamii"

MAma yake amabaye aliitwa Hilder alizidi kumfariji mwanae kwa kipindi hiko kigumu na kumpa moyo huku akimuahidi kila kitu kitaenda sawa, na kumuahidi ipo siku ata kuja kuishi na Donald mwana ume anaye mpenda sana katika maisha yake, habari izo zina mrudisha tena Pamela katika hali yake ya kawaida.
"kweli mama"?
"ndio mwanangu"
"nakupenda sana MAMA"
"MIMI pia mwanangu"

*******
"Hivi wewe Pamela una akili wewe?,na kwa taarifa yako nisha kutafutia mume wa kukuoa, ukimaliza chuo utaenda LOndon ukakae huko huko sio kukaa kaa na taka taka wahuni,huyo sijui Donald ana uwezo wa kuku dumia wewe? nakuliza ana uwezo wa kuku hudumia wewe? na wiki ijayo unaenda chuo sitaki kusikia tena habari za Donald"

bila Mr, DEuji kugundua kuwa pia na Donald wangeenda kuku tana nae chuo kimoja cha UDSM, alizidi kufoka mzee DEuji huku akiandaa vitu vyake ili aende kazini asubuhi hiyo,

Baada ya siku mbili kupita ERick anapanga mipango ya kuonana na donald na kumwambia kuwa kuna jambo angependa kumwambia ,Donald bila kipingamizi chochote ana kubali wito huo sababu alikua ni rafiki yake,
ila kwa upande wa ERick anaanza kumchukia Donald sababu ya mahusiano ya kimapenzi aliyoanzisha na dada yake,

ivyo walipanga wakutane na Donald katika moja ya mgahawa uliokuwa mjini, kweli walikutana jioni hiyo na Donald akitaka kumsikiliza Erick alikua na jambo gani la kumueleza.
"ujue nini Donald, dingi ana maindi sana wewe kuwa na mahusiano na Pamela dada yangu, wewe ni rafiki yangu ivyo nakuonea huruma sana, anaweza kukufanya kitu kibaya sana yule mzee, achana na Pamela tafuta msichana mwingine""
"wewe ni rafiki yangu sana ERick, ila ngoja nikwambie kitu kimoja, sitaki kuku danganya ili niku furahishe, ki ukweli nampenda sana Pamela nampenda sana, naomba unielewe kwa hilo, naomba unipe nafasi hio, naomba umueleze baba yako"
"Donald naona hunielewi, mimi nisinge penda kuona baadae una pata shida yoyote ile, achana na Pamela tu, tafuta mwana mke mwingine"
"hapana siwezi kuta futa mwanamke mwingine.siwezi"

Maongezi yale yana mkera sana ERick na kuamua kuondoka kwa hasira baada ya vitisho vyake kugonga mwamba, na kuapia kwamba ata fanya kila njama ili awa tenganishe wawili hao, aliingia ndani ya gari na kutoa mbio.


*****
Masaaa yali katika siku zilienda pia hata wiki ziliyoyoma hatimae muda wa Pamela kufika wa kuanza chuo uliitimu, kwa upande wake alikua na furaha kupita kiasi, kwa wazazi wake walidhani wenda furaha yake ili changia nayeye kwenda kuanza chuo, ila haikuwa ivyo kwa Pamela Furaha yake kubwa ili tokana na yeye kwenda kuku tana na Donald mpenzi wake, tena watakuwa wenye uhuru na kufanya mambo yao.

Alimtaarifu Donald kuwa yeye angeenda chuo siku iyo ila anapewa jibu kuwa bado ana hangaikia maswala ya ada ivyo baada ya wiiki mbili zijazo ange jiunga na chuo, furaha yake ili zidi maradufu na kufurahi baada ya kukata simu yake ya mkononi,

wazazi wake wakiwa nje wakimsubiri , haraka haraka alibeba begi lake la nguo na kutoka nje ambapo aliwa kuta wazazi wake wana msubiri kwenye maegesho ya magari, huku baba yake akiwa nje ya mlango wa gari la kifahari aina ya HAMMER III,.
Baada ya Pamela kuingiza mabegi ndani ya gari Mr, DEuji nayeye aliingia pamoja na mke wake ambae alikaa kushoto kwake huku nyuma aliketi Pamela na safari kuanza ya kuelekea chuo kikuu cha Dar es salaam.
"mwanangu uki fika huko usome, elimu ndo kila kitu sasa hivi, usome kwa bidii zote mwanangu"
Alivunja ukimnya MAMA yake huku akiongea kwa upole sana, waliongea mengi na mareffu siku iyo, hususani juu ya kumsisitiza Pamela asome kwa juhudi zote, na aepuke vishawishi.
"sawa wazazi nina wahaidi nita jitahidi,!."

alijibu Pamela , tayari walikua bara bara ya mwenge na kuiacha njia kuu na HAMMER hiyo kuingia njia ya chuo kikuu cha Dar es salaam muda mfupi baadae , gari hiyo iliegeshwa nje ya hostel za wasichana, na kufanya kila mtu akodoe macho kuliangalia gari hilo. na kutaka kujua nani atakae shuka ndani ya gari hilo la kifahari na lenye garama nyingi kupita kiasi.

wengi waliokua nje ya hostel walikua ni wana funzi wavulana kwa wasichana walikua wakiongea na kupiga stori ila baada ya gari ilo kupaki ukimnya uli tawala na macho yao yote yalielekea kwenye gari hilo. kili tangulia kiatu cheusi kili chochongoka mbele na fimbo ya dhahabu, huyu alikua ni Mr, DEuji akiwa na fimbo hiyo yenye siri.

amabapo hakuna hata mmoja aliye jua nini maana ya fimbo hiyo hata mkewe pia, ila siri hiyo alikua nayo mwenyewe, baada ya kushuka mzee huyo Pamela nayeye alishuka akifuatiwa na mama yake,
"ume muona mtoto wa kishua!?".

aliongea mmoja wa wana funzi wa kiume baada ya kumuona Pamela akiwa ameshuka ndani ya HAMMER III.

"MOM am gonna miss you!."(mama nita kukumbuka).
ili kua ni sauti ya pamela akiongea kiunyonge sana, kweli ki upande mwingine ili kua ni majonzi kwake, kukaa mbali na mama yake japo kua haikuwa umbali sana, ila alimzoea kumuona karibu yake,
"don't worry my daughter,me and your Dad, we shall be coming to visit you. but incase you have any problem contact us, we love you. be carefull sweetheart(usijali mwanangu, mimi na baba yako. tutakua tuna kuja kuku tembelea. ila kama una tatizo lolote tuwasiliane, tuna kupenda. kuwa makini kipezi)

aliongea mama yake huku akiwa ame mkombatia mwanae,. Moyoni mwa Pamela ulikua kama msiba ila alijipa moyo na kuji fariji kuwa atakua ana rudi nyumbani mara kwa mara.

Baada ya Pamela kuagana na WAzazi wake na kuachiwa pesa za matumizi, mzee Deuji aliiingia ndani ya gari na MKe wake na kuondoka huku nyuma wakimuacha Pamela aanze maisha yake mapya ya chuo kikuu,

**********

Tayari usiku mnene uliingia na kusababisha kiza kinene, kila mtu akiwa amelala ulikua ni usiku wa giza nene, ila kwa Mr, DEuji kwake ili kua kinyume yeye aliamka usiku na kumuacha mke wake amelala fofofo, aliliendea kabati na kufungua kabati la nguo na kutoa nguo nyeusi na kuzivaa na baadae kwenda kuichukua fimbo yake ya dhahabu,

alitembea mpaka kwenye moja ya pembe ya ukuta na kuongea maneno yasioeleweka huku akipiga piga ukuta na ile fimbo na pale pale kupotea, upande wa pili wa mr, DEuji nyuma ya utajiri wake alikua ni mchawi akiwa toa watu kafara kama sadaka ili mambo yake yazidi kuendelea.

akishirikiana na matajiri mbali mbali ndani ya nchi hiyo, jambo hilo alili fanya kwa siri kubwa sana, hakuna mtu aliye jua kuwa Mr, DEuji ni mchawi wa kutisha tena muuaji.

sekunde chache baadae alitokea chini ya mbuyu mkubwa sana ulio kuwa maeneo ya chalinze nje kidogo ya mji wa Dar es salaam hapo ndipo yalipo kua makutano yao kila siku usiku waki panga mikakati ya kuwa toa watu kafara na kunywa damu za watu pamoja na nyama za watu, ivyo ndivyo ilivyokuwa,.

Mmoja mmoja alianza kufika chini ya mbuyu huo wengine wakiwa na ungo na wengine wakija wamekalia fisi na huo ndio ulikua usafiri wao mkuu, vile vile kuna wengine walikua wapo uchi wa mnyama.wakiwa na irizi mikononi na miguuni.

"Naam mshirika, tuna hitaji damu za kutosha na nyama"

aliongea mzee huyo ambae alikua mkuu wao huku akiwa juu ya msukule aki fanya kama kigoda, kila msukule alikua na kazi yake, kuna wengine walikata kuni kuna wengine walikuwa wapishi ili mradi kila kitu kina fanyika kwa mpangalio, waki fahamiika kama ulimwenguni wamekufa kumbe walikua waki fanyishwa kazi ngumu huku wakiteswa sana.

kufumba na kufumbua tayari walitokea kati kati ya bara bara kuu inayo enda mkoani Moro goro. wachawi hao ili kua ni kwa nia moja tu kusababisha ajali ili wawachukue watu misukule na kunywa damu zao,

"Bakari mbona naona vitu vya ajabu!."?

aliuliza Dereva wa gari kubwa lili lobeba matera mawili na kumwangalia utingo wake, gari hilo lili kua katika mwendo wa kasi sana, ambapo mita chache dereva huyo ana ona asivyo vielewa.
"Yohana hao vibwengo, usisimame tutakufa."!
"hakuna bwana sio vibwengo, mbona ni weusi kuanzia kichwani mpaka miguuni, mi nina simamisha gari ili niwaone vizuri"
"usisimame Yohana tuta kufa vigonge, usisimame, tuta hatarisha maisha yetu, uki zingatia ni usiku huu".

sauti ya utingo huyo akiwa katika hofu alimsihi sana dereva huyo asisimame kwani mapigo yake ya moyo yalikua yakienda mbio kupita kiasi huku hofu nyingi iki mtanda..



Mapigo yake ya moyo yalizidi kumwenda mbio kana kwamba ame toka kukimbia mbio za riadha mita mia mbili sababu katika maisha yake hakuwahi kuona vitu vya ajabu kama ivyo, vitu kama vile alishia kuvisoma kwenye vitabu au kuviona kwenye t,v leo hii ana viona kwaa macho yake,
lili kua sio jambo la kawaida kwake hata kidogo, aliviona vijitu vifupi mno vikiwa vina waka moto kichwani,

Dereva huyo baada ya kuona utingo wake ameingiwa na hofu sana tena huku jasho liki mtoka anaamua kupandisha gia na kukanyaga mafuta kwa nia moja tu kuvigonga, maana alijua kweli vitu anavyo viona mbele yake sio vya kawaida, alizidisha mwendo kasi na gari hilo kuwa katika kasi ya ajabu, tayari walikua mita chache na vibwengo vile, ila cha kushangaza walipita UPEPO bila kusikia hali ya kugonga kitu chochote kile,

walizidi kusonga mbele kupitia vioo vya pembeni site mirror ili kuangalia kama kuna kitu nyuma, ila cha ajabu hakukuwa na kitu chochote kile na kufanya wazidi kustaajabu, na kumfanya Yohana aamini kweli wale walikua sio watu wa kawaida.

"nili kwambia mimi vile ni vibwengo, tunge kufa leo.!."
"kweli, leo tunge kuwa nyama yao"

dereva huyo alizidi kusonga mbele usiku huo mnene ambapo hali ya hewa ili kua sio nzuri na kufanya ukungu ulio tokana na baridi kali sana,

ila kwa mbali kidogo wana ona gari kubwa lenye matera na kupunguza mwendo kasi wa gari hilo, alicho fanya alichungulia kama kuna gari mbele ili alipite gari hilo, alivyo hakikisha hakuna gari lina lokuja , alikanyaga mafuta na kuanza kwenda kasi kwa nia moja tu, alipite gari hilo,

ila kwa upande wa pili haikuwa ivyo kulikua kuna basi kubwa la abiria lina kuja kutokana na dereva huyo kupigwa upofu na wachawi ambao bado walikua wana wafuatilia kwa nyuma Lori hilo,.

kufumba na kufumbua wali jikuta wame gongana uso kwa uso na basi hilo la abiria lililo kua lina tokea Mbeya,ambalo lilikua katika kasi ya ajabu sana, na kufanya libinuke mara tatu, ili kua ni ajali mbaya sana kupita kiasi, Matera yote ya lori lile yali dondoka juu ya basi lile la abiria na kufanya basi hilo lipondeke vibaya sana, huku likiwa limebiringika, kili chotokea hapo ilikua ni vifo na watu wengi kupoteza uhai, hakuna hata mmoja aliye pona katika basi hilo,

hata Kwa Yohana na mwenzake huo ndio ulikua mwisho wa maisha yao duniani. Upande mwingine wa shilingi haikuwa ivyo wachawi hao wakiwa wenye furaha sana baada ya zoezi kufanikiwa walianza kuchukua watu pamoja na damu nyingi kutoka kwa abiria ambao walio fahamika kama wame kufa duniani, mmoja wa wachawi hao ambae alikua ni kibibi

kizee alichukua mkia wa jogoo na kuwapiga dawa inayo itwa 'pumbazo' usoni kila mmoja ,na kuanza kuwa pakiza kwenye nyungo zao pamoja na fisi huku wakipaa angani wakiwa wenye furaha waki shangilia kutokana na ushindi walio upata,

WAlichukua misukule hiyo huku msafara huo ukiongozwa na Mzee Deuji akiwa mbele juu ya fisi na huo ndio ulikua usafiri wao mkuu usiku huo, hayo ndiyo yalikua maisha ya mr, deuji akitoa watu misukule ili atajirike , baaada ya dakika chache tayari wali fika maeneo ya Chalinze chini ya mbu-yu mkubwa na kutua na nyungo zao na kuweka mkutano wao huo.

"hahahhhahaha! hakika tume pata damu nyingi, ni jambo zuri sana, embu tujipongeze kwa kunywa"

ili kua ni sauti nzito iliyo kua ina jikwaruza kwaruza na kuji rudia rudia mara mbili mbili kama mwangwi kutoka kwa mkuu wao huyo ambae alikua ni mzee kiasi aliyeitwa Kira,
akiwa amekalia juu ya binadamu waliye kua msukule, kweli ilikua ni dunia nyingine tena ya kutisha, ngoma zili anzwa kuchezwa huku wengine wakiwa uchi wa mnyama , na misukule mingine ikiwa ina pika nyama za watu, kweli ili kua furaha sana kwa wachawi hao siku iyo baada ya kupata watu wengi sana na damu, ambayo nyingine ili tumika kama sadaka kwa mizimu yao

muda mfupi baadae mzee Kira ana funga kikao akiwa taka wachawi wenzake kesho wakutane tena sehemu ile ile, kila mtu alipanda usafiri aliokuja nao, wale waliokuja na ungo walipanda na wale waliokuja na fisi walipanda na kupaa angani, kila mtu akielekea majumbani kwake, huku misukule wakiificha ndani ya mti huo mkubwa.

***********

baada ya kupambazuka vyombo vya habari vilianza kutangaza juu ya ajali mbaya ili tokea maeneo ya chalinze na kuuwa watu wote, ili kua ni habari ya kuuzunisha sana, kila mtu alishika kichwa wengine walilia machozi hasa wale wenye ndugu zao, kili kua ni kilio kikubwa sana jijini Dar Es salaam,

hakuna mtu aliye jua nini chanzo cha ajali hiyo, wengine walisema ulikua ni uzembe wa dereva kwenda kasi, wengine walisikika wakisema breki za lori zili feli, lakini hakuna aliye hisi kwamba ajali hiyo ili sababishwa na nguvu za giza tena aliye sababisha mtu wana emfahamu kama tajiri mr, DEuji,

Habari izo mbaya wana zipokea wana chuo cha UDSM. hasa walipo sikia kuwa mwalimu wao nae alikua ni miongoni aliye kufa katika ajali hiyo akitokea mkoani Mbeya, kila mwana funzi aliguswa na msiba huo bila kujua mwalimu huyo alikua yupo dunia nyingine alikua ame tolewa msukule,

Miongoni mwa wana funzi waliotia huruma ni Pamela muda wotea alionesha simanzi roho ili muuma sana wakati mwingine hakujua kwanini, alichukua simu yake akiwa hostel kitandani na kumtafuta Donald kwa njia ya simu,
baada ya kufikia jina lililo andikwa ONE AND ONLY aliipa simu okay

"baby, umeamkaje"?!.
"nime amka salama mke wangu.vipi wewe?"
"SIPO SAWA,,,baby, umesikia ajali ya leo"?
"hapana mbona sija sikia LOVE"

ilibidi Pamela taratibu kwa upole aanze kumsimulia mpenzi wake, ambae kwa upande wa Donald alipokea habari izo kwa masikitiko sana kupita kiasi, kweli nayeye alionekana kuguswa sana, hakuacha kumuelezea juu ya kifo cha mwalimu wao.
"poleni sana kwa msiba, kazi ya Mungu haina makosa baby wangu, cha kufanya tuzidi kuwaombea marehemu waliotangulia mbele ya haki, maana kifo ni sehemu ya maisha, izo ni kazi za Mungu"
"sawa baby, "
"alafu LOVE nili taka kusahau kukwambia kesho nasa firi naenda Arusha"
Donald aliongea na kumfanya Pamela moyo wake umuende mbio, alitamani kulia ila alijikaza, picha mbaya ya ajali ili yotokea asubuhi iyo inaanza kuji jenga ndani ya ubongo wake tena. alitamani kumzuia Donald asiende ila alisita na kukaa kimnya kwa muda.
"halloo!"
sauti ya Donald ili sikika baada ya Pamela kukaa bila kusema chochote

"naam nime kusikia Donald wangu, lakini mbona ghafla ivyo?"
"siku penda iwe ivyo, shangazi yangu ana umwa sana, itanibidi niende tu kesho, niombee nifike salama pia nirudi salama"
"usijali, uta fika salama mume wangu, Mungu akutangulie"

Maneno hayo yali mtoka Pamela huku akiwa mwenye huzuni sana, baada ya kukata simu aliji tupa kitandani na kuji futa chozi hakujua kwanini analia, ki ukweli alimpenda SANA Donald na wala hakutaka ampoteze , alimpenda
kupita maelezo.
alivuta pumzi ndefu huku akiwa amelala chali akiangalia juu huku bado mapigo ya moyo yaki mwenda mbio hasa juu ya safari ya Donald na kufikiria ajali aliyo sikia asubuhi ya siku hiyo.......




Vyombo vya habari mbali mbali bado viliendelea kutangaza juu ya ajali hiyo mbaya sana ilio uwa watu, mamia ya watanzania kweli waliguswa, kila kona ya pembe ya mkoa walizungumzia juu ya ajali hiyo mbaya sana, iliyo pelekea kupoteza uhai wa watu wengi sana,

magazeti pia mbali mbali yalizidi kuchapishwa na kuuzwa sana siku hiyo.
moja ya gazet la ajali hiyo mbaya alishika pamela na kumfanya alie machozi ya uchungu hasa alivyo jua Donald kesho yake ana safiri, alimuomba Mungu amfikishe mpenzi wake huyo salama salmin, hiko ndicho alicho fanya , alijua kimbilio pekee ni kuweka mambo yote kwa Mungu aliye juu mbinguni na ivyo ndivyo ilivyo kuwa,

aliji futa machozi na kujitupa kitandani akilazimisha usingizi uje tena, taratibu za Mazishi ya lecturer wao Hilary yalianza kufanyika mara moja huku rambi rambi ikipitishwa kwa wana funzi, na baadhi ya wana funzi kuteuliwa kwenda kwenye msiba ili kuwawakilisha wanafunzi wengine.

mawasiliano yalizidi kuendelea baina ya Donald na Pamela. na siku iyo asubuhi Pamela alikuta ujumbe mfupi uki mtaarifu kuwa Donald alikua Ubungo kwa ajili ya safari, bila kupoteza sekunde alimpigia simu ili kumtakia safari njema, kweli jambo lile lili fanyika na kila kitu kwenda sawa,

Baada ya siku nne tayarri mazishi ya Lecturer Hillary yali fanyika tayari na wana funzi kurudi chuoni na kuendelea na masomo kama kawaida,

Pamela tayari alishaanza kuya zoea mazingira ya chuoni hapo akiwa na marafiki tofa uti tofauti.

siku hiyo akiwa maeneo ya chuo peke yake akiji somea vitabu vyake ghafla ana hisi mtu ame simama mbele yake
"mambo naitwa Samir"!

sauti hiyo ili sikika kutokea kinywani mwa mwanaume wa makamo mweupe kidogo ambaye kwa haraka haraka alikuwa chotara.
"Pamela"!

alijibu jibu hilo fupi na kurudisha kichwa chake juu ya kitabu alicho kua ana soma huku peni yake ikiwa mdomoni akionekana kama ana tafakari kitu,
"Nashukuru kuku fahamu"
"Mimi pia"
"sijui naweza kukaa hapa pembeni nawewe"?.
"hapana labda siku nyingine, leo sipo sawa, isitoshe, una ona nasoma kwaio sito taka aina yoyote ile ya usumbufu"

Maneno hayo yalimkata maini SAmir sababu alishindwa kuendelea na mazungumzo kutokana na Pamela kuonesha kuto mjali hata kidogo,

Uzuri wa Pamela ukiendana na sura yake nzuri ya duara, uli beba macho makubwa kiasi na kuzi disha uzuri wake maradufu, si ivyo tu,hata mwendo wake uliendana kabisa nayeye sababu hakuwa na mwili mkubwa sana, kweli alikua ni mzuri, shingo yake nzuri ili shuka mpaka kwenye kifua ambacho kili beba maziwa yake yaliyo kuwa madogo kama embe bolibo,

kweli alikua mzuri na tayari vijana na wana ume walianza kumsumbua wakimtolea udenda wakimtaka kimapenzi ila misimamo wake ulikua mkali sana, hakutaka kusikia neno mapenzi kwa wakati huo sababu alijua yupo mtu ambae ni Donald, pia vile vile alimsihi sana Donald arudi ili wana ume waache kumsumbua.

"baby rudi basi"
"nita rudi mke wangu".
"nime choka kusumbuliwa"
"narudi mke wangu, usijali LOVE"
"mimi nita wakubalia, wewe chelewa chelewa uta kuta mwana sio wako"
Pamela alitania kidogo
"weee Thubutu"
"nakutania baby, ninaanzaje labda kuwa kubali, siwezi kabisa, nakupenda sana Donald"

hayo ndiyo yalikua maongezi yao karibia kila siku, moyoni mwa Pamela kweli aliji apiza hatokuja kumvulia nguo ya ndani mwanaume yoyote yule.

Mazoea baina ya Samir na Pamela yalizidi kukuwa kwa kasi sana huku mwanaume huyo akiwa mwaka wa pili akichukua masomo ya Sheria, ivyo mwanaume huyo alichukuanafasi hiyo ili awe mwenyeji wake maeneo ya chuo huku akimsaidii mambo mbali mbali ya kimasomo sababu hata Pamela nayeye alichukua masomo ya sheria, lakini upande wa pili wa Samir alikua na nia moja tu kumsogeza karibu Pamela, kweli alionesha kumpenda sana Pamela.

siku zilivyo zidi kwenda hakusita kuonesha hisia zake juu ya Pamela, siku iyo wakiwa wana kula chakula cha mchana canteen SAmir aliamua kufunguka na kumueleza aliyokua nayo moyoni siku nyingi.

"ndo ivyo Pamela, tangu siku ya kwanza niliyo kuona, ki ukweli moyo wangu ulivutiwa na wewe naomba niwe wako mpenzi, naomba usiutese moyo wangu, niamini huto jutia kuwa na mimi Pamela, nime shindwa kuji zuia"
"Tafadhali naomba ubadilishe maongezi, sababu hilo unalotaka halitokuja kutokea, na ufute mawazo hayo kichwani kwako, SAmir wewe nakuchukulia kama kaka yangu sasa hivi"

Maneno yale yaliipenya vizuri ndani ya ngoma za masikiio ya SAmir na kuzidi kumbembeleza awe nae akiomba awe mpenzi wake, .Pamela hakuongea chochote alichofanya allinyanyua pochi yake na kusimama huku akiondoka zake sababu hakuona tena umuhimu wa kukaa kwenye meza ile,
ki ukweli katika upande wa pamela hakutokea kuvutiwa na meanaume yoyote yule, alichukizwa na mwanaume yoyote yule aliye mtamkia neno nakupenda,

Neno nakupenda halikua na nafasi kutoka kwa mwanaume yoyote yule isipokua Donald.

Wanaume wengi walizidi kumsumbua huku wengine wakitoka vyuo mbali mbali kuja kumfuata, huku wengine wakija na magari ya kifahari ila kwa Pamela alikaza uzi, alionesha msimamo wake ule ule. katika siku chache tu tayari Pamela alianza kujulikana chuo kizima na nje ya vyuo jirani na kufanya gumzo kwa wana ume mbali mbali,

kweli hakusita kumwa mbia Donald kila kina choendelea chuoni, kila kitu alimwambia mpenzi wake, na jibu alilo kua akitoa Donald ni moja tu avumilie na ajitunze sana.

Alimpata rafiki yake ambaye alitokea kumpenda sana aliyeitwa Gloria sababu waliendana kitabia wakisaidiana mambo mbali mbli huku wakishauriana vitu vingi juuu ya masomo yao , urafiki wao ulifanya wawe karibu zaidi na kushirikiana katika kila jambo sababu wote walioinesha bidii sana darasani na juhudi nyingi.

*****

siku hiyo akiwa mwenye furaha sana hasa alipopokea simu kutoka kwa Donald kuwa yupo njiani anarejea DAr se salaam ili kua ni furaha sana kwake, moyoni alikua na furaha sana akitamani Donald afike mara moja

"nitakaa pale ubungo kuanzia saa moja asubuhi, niki kusubiri wewe mume wangu"
"hahahaha, uta kua chizi Pam"
"potelea mbali, acha niwe chizi kwa ajili yako,"
"aya mama, nikifika ubungo nita kupigia tena"

Pamela alikata simu akiwa mwenye furaha sana,kweli alikua mwenye furaha ya ajabu mno,

alijiandaa kwenda darasani ambapo alibeba mkoba wake na kuelekea chuoni wakiongozana na Gloria rafiki yake kipenzi..

baada ya maasaa sita kupita aliamua kumta futa Donald hewani baada ya kutoka darasani ila cha kushangaza haikuwa hewani, alijaribu na kukuta hali ni ile ile, wasi wasi mwingi unazidi kumuingia moyoni na kuanza kukosa amani tena wakati muda mfupi alitoka kuongea nae, huku picha mbaya ya ajali ikianza kujijenga ndani ya akili yake, ila alijipa moyo wenda ita kua simu yake haina chaji, Lakini licha ya kujipa moyo bado roho yake ina muuma sana..

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG