Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 2/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 2 KATI YA 10
*******
 *******




HALI ina endelea kuwa vile vile jambo ambalo bado lina zidi kumuumiza kichwa, kuto kupatikana
kwa Donald kuna jenga wasi wasi mwingi ndani ya moyo wake,

alihisi kuna kitu ambacho haku kielewa, aliji kuta ana kubaliana na hali ile na kurudi darasani ili kuungana na wana funzi wenzake sababu kuna kipindi kilikuwa bado kina endelea DARASANI.

licha ya kulazimisha mawazo yake kuwa darasani ili aelewe kile kina chofundishwa lakini hakuna hata moja alilo lielewa mawazo yake hayakuwa darasani ila ni mwili wake peke yake ndio ulikua darasani, alihama kifikra na kushindwa kabisa kuelewa kile kili chokuwa kinaendelea darasani,! hakuona umuhimu wa kuendelea kubaki darasani.

Alibeba vitabu vyake na kuondoka akielekea hostel,moja kwa moja aliingia na kuji tupa kitandani akiwa mwenye mawazo mengi sana juu ya Donald, tangu waaanze mahusiano na Donald hakuwahi kuumia roho kiasi hiko na

hakuelewa kwanini roho ili muuma kiasi kile, alielewa moja kwa moja kuna jambo baya sana litatokea mbeleni, na kuji kuji kuta ana lia machozi

"EEEH Munguu,naomba umlinde Donald"!

aliiongea huku akibubujikwa na machozi, alichukua tena simu na kuitafuta namba ya Donald ila hali ili kua ile ile, hakukuwa na jinsi yoyote ile ya kubadilisha ukweli kuwa Donald hapatikani,
"Leo una tatizo gani Pamela"?
rafiki yake kipenzi Gloria alihoji baada ya kumkuta Pamela analia anashindwa kuelewa nini kime mpata rafiki yake,
alienda mpaka kitandani na kumuinua na kumfuta machozi.

huku akilia machozi alianza kumuadithia Gloria kila kitu .

"labda simu yake imeisha chaji"
"hapana Gloria! ange niambia kabla, namjua Donald wangu"!
"nisikilize ita kua network tu, ya kawaida , una jua yupo ndani ya basi kuna wakati mwingine netwok ina kua ina sumbua, kuna vijiji vingine vina kua havina netwok, usilie pamela, Donald ni mzima tena ata kupigia sasa hivi"

maneno yale kweli yalianza kumtia moyo pamela na kuanza taratibu kurejewa na furaha tena na kuanza kufuta machozi,

Jioni ili fika bado hali ilikua ile ile kwamba Donald haku patikana, hakuwa na amani kabisa hata kidogo hata chakula hakuona umuhimu wa kula . hamu yote ya kula chakula ili funikwa na mawazo aliyo kua nayo juu ya Donald,

usiku mzima ulipita bila kupata hata lepe la usingizi, taarifa mbaya za msiba zilianza kupita ndani ya kichwa chake na hakuelewa angeishi vipi bila Donald, licha ya hayo yote hakutaka kuyapa nafasi mawazo hayo mabaya ndani ya kichwa chake, masaa yalisogea taratibu mwendo wa kinyonga, huku akitafakari mengi sana mpka kuna kucha hakupata usingizi hata kidogo.

*******

Asubuhi aliamka na mapema alija ribu tena ile namba na hali kuwa vile vile
"Lazima niende kwao niki toka kwenye vipindi, kuna jambo lazima wata kuwa wana nificha"!

aliwaza pamela na kuanza kujiandaa kwenda darasani kweli aliapa endapo vipindi vya mchana vikisha angeenda kwa mama yake na Donald ili ajue kina choendelea aliamini huko ndipo ata jua ukweli, na kujua kuwa angepata majibu ya swali lake.

aliingia darasani katika hali ya unyonge sana huku pia Gloria akizidi kumfariji bila mafanikio yoyote yale,
kili chokua kina fundishwa hakuwa ana elewa hata kitu kimoja, baadae kidogo alihisi simu yake ina ita katika mlio wa vibration, na kuitoa ili ajue ni nani hakuamini macho yake.
baada ya kuangalia juu ya kioo cha simu na kukuta ni Donald,

aliji kuta akishangilia bila kuelewa yupo darasani na kufanya wana funzi wenzake wabaki kumwangalia, alitoka nje akiruka ruka na kuiweka simu masikioni,

"Pamela, suprise mama, nime rudi"
"Donaaaaaald, upo salama, upo wapi?, umefika, niambie mume wangu"!

kwa furaha aliji kuta ana uliza maswali mengi mfululizo
"nipo hapa hapa maeneo ya chuo, njoo kwa huku juu nime rudi salama mpenzi wangu"
"kweli, nakuja sasa hivi".

Pamela alitembea haraka haraka baada ya kuelekezwa alipo Donald na kweli hakuamini macho yake baada ya kumuona Donald mbele yake, alimrukia kwa nguvu sana na kufanya kidogo wadondoke. walikombatiana wakiwa

wenye furaha sana kupita maelezo, kweli yalikua mapenzi ya dhati, na kufanya baadhi ya wana funzi wengine kupita na kuanza kuwa shangaa,

ila kwa Pamela hakujali macho ya watu, alicho jali yeye ni furaha iliyo kua ndani ya moyo wake.

"Lakini baby, mbona ulikua hupatikani muda wote naku tafuta uka nifanya niwe roho juu, kwanini lakini"?
"netwok ili kua ina sumbua hata ivyo, nili taka nikufanyie suprise mama"
"utaniua Donald, una jua nakupenda sana"
"hata mimi, ndo maana mpaka leo tupo pamoja"
"hautoniacha"?
"sitokuacha wewe ndio utakae kuja kuwa mke wangu, niamini"
"nakupenda sana"

yalikua ni maneno yenye hisia kali sana kupita kiasi, kweli kila mtu alimuamini na kumpenda mwenzake hakuna hata siku moja, waliofikiria kuwa wata tengana, ukweli ni kwamba walipendana pengine kuliko watu wengine wote ambao wali wahi kupendana hapa chini ya jua,

baaada ya siku chache tayari Donald alikua kesha jiunga na chuo kikuu akichukua masomo ya sayansi na ndoto zake kuja kuwa mkandarasi, kweli jambo lile lili fanyika na kuanza chuo, Mapenzi ya Donald na Pamela tayari yali kua gumzo

kila mtu aliya jua mahusiano hayo kutokana na wote kuonekana wakiwa wote sehemu mbali mbali,

"shemeji ni mzuri sana, ana mvuto "

ili kua ni sifa kutoka kwa rafiki yake Gloria siku iyo usiku wakiwa hostel ki ukweli ndivyo ilivyo kua Doanald alikua ni kijana mzuri na mwenye mvuto pengine kupita hata wana funzi wote ndani ya chuo hiko, wasichana pia walitamani japo kuongea nae ila waliishia kugombana na Pamela ambae alionesha chuki na wivu kupita kiasi, hakutaka kuona Donald awe na mazoea na jinsia yyoyote ile ya kike, ki ukweli alikua na wivu sana, na Donald alilijua hilo.

"yule ndo ana nifanya niwaone wana ume wote mashetani!, nampenda sana, yaani sana. na ndo wewe ndo nimekuruhusu uwe na mazoea nae"

Pamela aliongea maneno hayo akijiamini sabau ki upande mwingine alimuamini sana rafiki yake huyo kipenzi na kuamini kuwa hakuna chochote kibaya kita kacho tokea....




“Lazima nifanye kitu mtoto mzuri kama Yule iweje atembee na mchimba chumvi, mimi ndo raisi wa chuo ata hama hiki chuo”!
Aliwaza Rais wa chuo hiko aliye fahamika kwa jina la Jackson OKAKA, kweli alitokea kumpenda sana Pamela, ila alishindwa kutokana na kila njia aliyotumia ili gonga mwamba, haku taka kukata tama alitokea kumchukukia sana DONALLD
kuliko mtu yoyote Yule chuoni hapo, alimuona kama yeye ndiye ana muwekea kiwingu na si vinginevyo, hakuta ka kumkosa Pamela, na hilo aliliamini, laiti ange jua msimamo wa PAMELA Pengine hata asinge jaribu kuijiapiza kuwa ata mpata Pamela, hakuelewa wawili hao walipendana sana,

Alicho taka yeye ni kuwa na pamela tu, hakika ali riki kuwa Pamela ni mziki mwingime kwa uzuri

MAPENZI ya wawili hao tayari yalikua gumzo sana sababu kila mwanachuo aliwajua kweli walikua maarufu , maana kila wakati walikua pamoja, hakika walikua ni mfano wa kuigwa kutoka kwao,

Siku hiyo asubuhi sana PAMELA alipokea simu kutoka kwa baba yake mzee Deuji akimuhitaji mara moja nyumbani, kuna jambo ali taka kumwambia,

Wasiwasi mwingi ulitanda juu ya moyo wa pamela na kumfanya awe na hofu sana kupita kiasi, alivyoohoji kwanini ana hitajika nyumbani haku pata jibu kamili,
“baba asije akawa ana jua kuwa Donald nayeye yupo hapa”

Aliwza Pamela huku akijiandaa kwenda myumbani alipo itwa na baba yakre, huku akiwa na wasi wasi mwingi sana sababu haikuwa kawaida ya baba yake kumuita ghafla ivyo,

Alimueleza Donald kila kitu na kumuaga , bila kupoteza mudda alita futa taxi na safari ya kuelekea oysterbay kuanza

Alipatwa na msongo wa mawazo sana juu ya Donald hakuwa na raha hata kidogo, alijua baba yake sio mtu wa kuchezea kweli alielewa kuwa baba yake ana mchukiioa Donald kupita kiasi,ila yeye hakujali hilo alikua yupo radhi hata akosane na wazazi wake lakini sio kumkosa Donald hakika alikua na mapenzi ya kweli.

Baada ya dakika sabini tayari taxi ili kuwa isha fika oysterbay na PAMELA KUMLIPA DEREVA Yule kiasi anacho takiwa kulipa na kuingia ndani akiwa m wenye wasi wasi sana.

Alivyo ingia ndani alimkuta baba yake akiwa seblen huku mkononi akiwa ameshika fimbo yake ya dhahabu,
“Dad Good after noon”(baba habari za mchana)!
“how are you?”(vipi hali)?
“am doing fine dad,(naendelea vizuri baba).

Baada ya salamu mbili tatu mzee Deuji alisimama na kumwambia Pamela amfuate nje , ki ukweli bado hakuelewa nini kinaendelea,
“Pamela mwanangu, mimi na mama yako hatutukupa zawadi,.. hiyo ita kua zawadi yako’, tume kupa iyo zawadi ya gari mwanangu, uli fanya vizuri katika masomo yako”
“Dad!”

Ili kua ni furaha ya ajabu kwa Pamela hakuamini kuwa mbele yake kuna mark II GRANDE ambayo ilikua tayari ime sajiliwa kila kitu, ilikua ni mpya, Pamela alijikuta ana mrukia babayake kama mtoto mdpgo anavyo mrukia mama yake,
“Dad Dad , asante, you’re the best, nakuhaidi sitokuangusha nita soma kwa bidii zote”

Aliongea Pamela akiwa mwenye furaha sana, alikabidhiwa funguo za gari hilo na baba yake, hakika ili kua ni zawadi kubwa sana kwa PAMELA

“hiii gari ni yako mwanangu, sawa”!

*********

“sasa ushajua kuendesha gari, leseni yako hii hapa, uta kua unaniendesha Donald, sitaki kugusa gari wewe upo,”

Yalikua ni maneno yaliyoitoka mdomoni mwa Pamela baada ya kurudi hostel, chini kwa chini alimpeleka Donald Driving school chuo cha kuji funza kuendesha gari na kupata leseni tayari, na leo hii Donald alijua kuendesha gari wakiwa wenye furaha sana siku hiyo,

Mapenzi yalizidi kunoga na kuchepua kana kwamba ndo yaliianza jana,

Siku iyo ya jumapili Pamela alimuomba sana Donald ampeleke nyumbani kwao Oysterbay, ila Donald alikataa na kumfanya Pamela aanze kulia,
“lakini Pamela una kumbuka ile siku yaliyo tokea”?
“hata kama Donald, isitoshe leo baba angu hayupo,”
“mama je?”
“, mama pia hayupo”
“lakini bado moyo wangu ni mzito”
“Donald una nipenda”?
“swali gani hilo una niuliza”?
“aaah aaah nijibu kwanza”
“ndio nakupenda, laki…”
“lakini nini, kama una nipenda naomba nipeleke nyumbani nisha kwambia kuwa, hakuna mtu leo”

****

Kutokana na mapenzi ya dhati aliyo kua nayo kwa pamela aliji kuta analegeza kamba na kuku bali ombi la Pamela ila ndani ya moyo wake ulikua bado mgumu na mzito sana, alikumbuka mara ya mwisho alivyo dhalilishwa kama mwizi, ila yote hayo aliya sahau kutokana na penzi zito alilo kua nalo juu ya Pamela, hakutaka mpenzi wake aka sirike hata kidogo,

Aliendesha gari na baadae kupiga honi nje ya jumba kubwa la kifahari la mzee Deuji ambapo geti hilo lili funguliwa na mlinzi na wote kushuka, na kuingia ndani,
“ngoja hapo baby niku letee juisi”

Badae juisi ili ketwa na Donald kuanza kunywa, ila bado moyoni hakua na amani,
“fanya haraka Pamela tuondoke”
“poa baby”

Kabla ya kuweka Glass ile mezani ghafla ulisikika mlio wa honi ya gari na kumfanya Pamela aruke dirishani na kufungungua pazia hakuamini macho yake baada ya kuona HAMMER III lina ingia ndani, alihisi moyo unaenda mbio.
“mungu wangu baba”!
Aliropoka Pamela na kumfanya Donald kubanwa na haja kubwa, maana alijua kinachofuata hapo sio kitu kizuri, alimuogopa mzee huyo kama ukoma…




Hofu ilizidi kutanda ndani ya moyo wa Donald, hakuona kitu kingine zaidi ya kifo!, hakika alimuogopa sana mzee Deuji baba yake Pamela, hilo hakulipinga hata kidogo, mzee huyo alikua ni mtu wa kutisha ni mtu wa kuogopeka na kila mtu,
hakua mtu wa mchezo mchezo hata kidogo, Donald nayeye alikurupuka haraka ili kweli ahakikishe kama Pamela ana sema ukweli, pengine alitamani iwe utani ila haikuwa ivyo baada ya kuchungulia dirishani na kumshuhudia mlinzi wa getini akitoa unoko kwa bosi wake.
“bosi, Pamela ameingia na Yule kijana humu ndani”?
“kijana yupi”?!
“Yule. Yule uliye mkataza asiingie humu”
“kwanini ameingia nawewe ulikua wapi,? Erick zunguka nyuma, wewe usitoke hapa, hakikisha humu ndani hatoki”
Mzee Deuji aliongea kwa msisitizo huku akishuka ndani ya gari kweli aliongea huku akifoka kwa sauti kubwa sana na
kuonesha hasira za wazi wazi sababu moja kwa moja alijua ni Donald na kupania ata mfanya kitu kibaya endapo ata mtia mikononi,
Aliweka mkono kiunoni na kutoa bastola yake huku akiingia ndani.,

Pamela akiwa ndani na Donald walianza kuta futa sehemu za kuji ficha ila hawa kuona sehemu ya wao kuwa salama, alimchukua Donald na kuanza kukimbia nae wakitokea mlango wa nyuma,
“sasa tunaenda wapi”?
“njee njoo huku”
Huku na kule wali toka nje na kumuona Erick ila wali wahi kutoka geti la nyuma na kuanza kutoka mbio, wakikimbia , hilo ndilo jambo ambalo waliamini kuwa wata toka salama siku hiyo ,
“wale kule”
Aliongea mlinzi wa getini na kuanza kuwa kimbiza nyuma yao huku akiwa na Erick,

Bastola ndogo tayari ilikua juu ya meza huku Mzee Deuji akiwa ame tanda juu ya sofa, mbele yake alisimama PAMELA akiwa ameshikwa na kaka yake Erick huku pembeni akiwemo Donald akiwa ameshikwa na mlinzi, hakujua nini hatma yake kwa wakati huo, hofu ya kifo chake alikiona wazi wazi, aliogopa sana alikumbuka maneno ya mama yake mzazi,

“Pamela, nilikwambia nini”?
Alihoji Mzee Deuji huku akisimama kwa hasira ambazo zili fanya sura yake ichore makunyanzi
“nawewe panya buku taka taka, uli fikiri ungeweza kukimbia huu mkono,!?”
“lakini ba..”
“shut up,(kaa kimnya)”
Alifoka mzee Deuji na kutoa simu yake mfukoni na kuiweka kiganjani, alibonyeza namba namba baada ya kuridhika aliweka sikioni.
“Naongea na MAGUGU, naomba defender nyumbani kwangu, ndio unaongea na Deuji, ni nyumbani kwangu nime vamiwa na jambazi, walinzi wangu wame mkamata, sawa waambie wafanye haraka”

Donald alizidi kuingiwa na hofu alijua nini maana ya simu ile kupigwa alijua ni nani aliye pigiwa simu ile alijua ni polisi na si kitu kingine,
leo hii ana enda kulala polisi kisa Pamela alilaumu sana nafsi kwa kukubali kuingia ndani ya nyumba hiyo, alimuangalia Pamela ambae wakati huo alikua akilia machozi ya uchungu,

Kwa hasira Mzee Deuji alisimama na kumpiga kofi Donald na kumrudisha jingine, haikuwa picha nzuri kwa Pamela hata kidogo roho ili muuma sana kupita kiasi kuona mpenzi wake mwanaume wake, aliye mpenda pengine kupita mwana ume yoyote chini ya jua anapigwa na baba yake hakika haikuwa picha nzuri juu ya mboni ya jicho lake,aliumia moyoni sana, lakini alikua hana la kufanya na kubaki kulia kama motto, alimchukia sana baba yake mzazi pengine fikra zake zili mwambia wenda sio baba yake, kwanini amtese kiasi kile, kwanini amnyime furaha yake.
“kwanini una fanya ivyo baba.”?
“kelele tena nyamaza,usiongee kitu, keep quit, na huyu anaenda kufia ndani, taka taka,MPUMBAVU!”
Kabla ya kutaka kufanya kitu chochote tayari maaskari walikua washa fika ndani ya nyumba hiyo na kuoneshewa Donald.
“pigeni huyu mwizi, aliruka ukuta ame kamatwa na hawa walinzi wangu”
“Dad”!
“nyamaza, peleka polisi , na sitaki dhamana apewe na mtu yoyote Yule, mimi na nyie tutaongea mtoeni hapa”!

Pamela aliangua kilio kama mtoto mdogo akiwafuata polisi wale nyuma na kuwa vuta vuta ili wamuachie DoNALD ILA Kaka yake Erick ana mshika na kumzuia. Asifanye kitendo kile, Erick nayeye aliungana na baba yake , kitendo kile kina mshangaza sana Pamela, hakutegemea kama kaka yake nayeye ali mgeuka
“Erick I hate you,(erick nakuchukia) wewe sio kaka yangu, nawewe sio baba yangu kwanini mnaa mua kufanya hivi, nampenda Donald, ”

Pamela alichungulia Dirishani na kumuona Donald anavyopigwa virungu, alilia sana . maneno yaliyo kua yaki mtoka kweli yalittoka ndani ya moyo wake aliongea kwa hisia kali sana huku machozi yakizidi kumtoka na kulowanisha shingo yake,
“lakini mdogo wangu Pamela, ume mpendea nini Donald”?
“niache Erick, usini shike, usini shike”

Kama umeme haraka haraka aliirukia bastola ya baba yake ambayo iliyo kua mezani nakujiwekea usawa wa kichwa, sio Erick wala baba yake woote hawa kutegemea kama Pamela ata fikia hatua hiyo. Wote waliogopa sana
“mwanangu tafadhali weka hio silaha chini!”
Aliongea Mzee Deuji huku akimsogelea Pamela kiukaribu baada ya kujua bastola ile ilikua tayari ime kokiwa na risasi ipo kwenye chemba ivyo kitendo cha Pamela kuvuta triga inge kua ndio mwisho wake, kibaya zaidi alikua amejiwekea usawa wa kichwa,
alipata kazi nyingine tena ya kumbeleza Pamela ili aasifanye jambo ambalo ana taka kuli fanya, ili kua sio kazi rahisi kumtuliza!.
“Dad usini sogelee nita jiua sasa hivi!, simama hapo hapo, hata niki fa sasa hivi, najua wewe ndio ume changia mimi kufa nampenda Donald mbona hutaki kunielewa”
Maneno aliyokua akiongea Pamela yalikua ni ya kuuzunisha sana sababu alikua akiongea huku akitoa machozi mengi.
“jamani kuna nini Pamela”?

Maneno hayo yalimtoka mama yake akiwa kwenye ngazi na kushudia kitendo kile kila mtu alitetemeka kuona hali ile, walijua kweli Pamela hakuwa katika hali ya utani hata kidogo, ivyo wali takiwa wamsikilize kile anacho taka lasivyo atajiua, na hiko ndiko kilicho kua kina tokea muda mfupi ujao.
“baba naomba umtoe Donald , moja ,mbili, taa...paaaa”

Ulisikika mlio wa risasi na kila mtu alishika kichwa chake hawa kuamini kilichotokea mbele yao..




Wakati huo tayari Donald kashafikishwa kituo cha polisi akiwa ameharibika uso baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa maaskari hao wasiokuwa na huruma wao walicho fuata ni maagizo na si vinginevyo.
“Yani ukitoka humu ndani lazima itakuwa historia yako ya maisha”
aliongea mmoja wa maaskari aliyempokea’ ilibidi aombe simu na kumpigia mama yake kipenzi,alimwambia kila kitu bila kuficha

“lakini baba si nilikwambia huyo mwanamke hakufai, ona sasa mwanangu unaenda kuteseka, ila usijai baba ntakuja”.
aliongea mama yake akiwa mwenye uchungu sababu hakuwa na mtoto mwingine zaidi yake na alikuwa akimtegemea sana .ili baadae aje amsaidie
“sawa mama nakupenda”
Donald aliaga na kuingizwa maabusu na kujutia kwanini alikubali kuingia kwa akina Pamela lakini alijua alifanya yote kwa sababu ya mapenzi ya dhati na wala si vinginevyo na kuamini kuwa ipo siku Pamela ata kuja kuwa mke wake ewatengeneze familia

Kila mtu alishika kichwa baada ya kusikia mlio ule wa bastola, hakuna mtu aliye tegemea kitendo kile, ni baada ya Erick kumrukia Pamela na kuitingisha bastola ambapo bila yeye wenda Pamela angeitwa marehemu, risasi ilyo fyatuka ilitulia juu ya flat skrin na kuisambarisha tv iliyo kua seblen , hakika walijua Pamela hana masihala hata punje!
kweli alicho kiongea alimaanisha , bado akiwa chini alikua na bastola ile mkononi na kusimama tena na kujiwekea kichwani kama mara ya kwanza. Mzee Deuji hakutaka kumpoteza mwanae kiurahisi kiasi kile japo alikua na roho ya ukatili alijikuta akilegea na kutoa simu yake mfukoni.
“ hallo enhe ndio naomba Yule kijana mumuachie ”
aliongea deug kupitia simu ya mkononi.
“kijana yupi Yule mwizi”?
“huyo huyo”!
Mr. Deuji alisalimu amri na kumtaka Donald aachiwe mara moja
“ naomba niongee nao ili ni hakikishe “
, Pamela alikata simu, sababu hakuamini kama ni kweli baba yake alitoa kauli hiyo, alipewa simu na kutaka kuongea na Donald.
Kweli baada ya kuhakikisha Donald kaachiwa huru kabisa, taratibu aliteremsha bastola ile na kuuiweka mezani.

Bado wanaume pia wakiwemo wanafunzi mbalimbali wa chuo hawakukata tama walizidi kumsumbua Pamela japokua walijua ana mahusiano ya kimapenzi na donald , haikuwa tatizo , mmoja wa wanafunzi hao alikuwa ni Jackson okaka alikuwa ni raisi wa chuo hiko alimpenda sana Pamela . akiwa chumbani kwake alifikiria mipango mingi sana ya kuwatenganisha Pamela na Donald.
“nampenda donald , naomba nielewe Jackson “
Maneno aliyo ambiwa na Pamela yalikua yaki pita kama mkanda wa filamu kichwani kwake, siku inayo fuata ali mtafuta PAMELA na kumuomba waongee kidogo, na kumuomba watoke nje ya chuo ili waweze kuzungumza mawili matatu.
“NO sitoweza bila Donald,”
“hapana hakuna sababu ya yeye kuwepo Pamela, mbona una kua kama mtoto?”!
“ndo nisha kwambia siwezi kutoka bila kumwambia”
“aya sawa”

Jackson alisimama kwa hasira na kuondoka sehemu ile huku akiwa na mawazo mengi maana katika historia yake ya hapo chuo hakuna hata msichana mmoja ambae alikua akiruka kwake, ili kua ni lazima akimtaka ampate, isipo kua kwa Pamela , kweli alipata wazo na kuitisha kikao cha wana funzi wote wa kiume wa mwaka wa kwanza siku inayo fuata na kutilia mkazo endapo mtu yoyote akikosa ata kuchukuliwa hatua nia yake ilikua moja tu,
Donald asiende safari wanayo enda na Pamela,

Kweli kesho yake alimuita Pamela na kumueleza kila kitu, alivyo mtafuta Donald kwenye simu alimuimbia kuwa yupo kwenye kikao, bila kumuambia chochote akimini kuwa ange rudi mapema, anaaamua kuchukua maamuzi magumu ya kuondoka na JACKSON OKAKA nje kabisa ya maeneo ya chuo, bila kumtaarifu chochote Donald japokua roho yake ili sita lakini aliona haina sababu ya kumueleza kuto kana nay eye angerudi mapema na kumueleza kila kitu.

Baada ya dakika chache tayari walifika maeneo ya sinza Lego dagaa dagaa na kutafuta viti huku wakikaa na kuagiza vinywaji.
“niambie sasa kwanini nipo hapa”?
“sasa subiri mbona una haraka Pamela”?
“amna zungumza, niambie kwanini ume nileta hapa”

ILIPOFIKA jioni Donald alitoka kwenye kikao na kuamua kumtafuta Pamela kwa njia ya simu na kukuta simu yake haipokelewi, ali jaribu kupiga tena na kukuta hali ni ile ile, ila baadae ana shaangaa alivyo piga tena alikuta haipatikani kabisa, na kuamua kumpigia Simu Gloria rafiki yake mkubwa wa PAMELA Akimini kuwa anajua alipoi ila jibu la Gloria linazidi kumkata maini.
“hakuniaga mimi. Labda atakua amekwenda kwao”
“angeniambia”
“sasa hapo sijui atakua wapi”
“hakuna sehemu nyingine unadhani ata kuwepo”?
“kwa kweli hapana”

Mazungumzo hayo yali katwa huku Donald akiwa bado na mawazo hakuelewa nini kili mpata PAMELA , hakuelewa kwanini aliondoka bila kuaga na haikuwa kawaida hata kidogo. Usiku uliingia alijaribu ile namba na kukuta hali ni ile ile,

Usiku mzima mpaka kuna kucha hakupata usingizi hata kidogo, baada ya kukucha alipiga tena simu na kukuta hali ni ile ile. Kwa mbali alihisi ,mlango una gongwa wa chumbani kwake kuufungua.
“wewe ndo Donald”?
“ndio”
“kuna mzigo wako hapa”
Kijana Yule alitoa bahasha kubwa ya kaki na kumkabidhi nayeye kuondoka zake, alikua na shauku kubwa sana ya kutaka kufungua bahasha ile, hakuamini alichokiona baada ya kufungua bahasha ile ya kaki’, zili kua ni picha za Pamela akiwa na Raisi OKAKA chumbani, alihisi kuishiwa nguvu za miguu na kushindwa kuelewa kile alichokiona juu ya picha zile, Pamela akiwa ame mlalia Raisi Jackson kifuani huku wakiwa watupu. Huku wakiwa wame piga picha nyingine tofauti za kuashiria kua ni wapenzi hakika alihisi mkuki wa moto ume tumbukia ndani ya moyo wake na kuelewa nini maana ya picha hakukuwa na sababu kuuliza moja kwa moja alijua kuwa kuna kitu kili kua kinaendelea...




Ndani ya moyo wake alihisi ganzi wakati mwingine alihisi mapigo yake ya moyo yame simama, hakuwahi kuumia roho kama siku hiyo, mtu anaye mpenda leo hii amekua shubiri! Hakika alidhani anaota kabisa, na wakati mfupi ujao ana enda kushtuka katika njozi hiyo ambayo kwake aliiona ya kutisha mno, bado alikua ameganda kama barafu, akitetemeka sana!
“Pamela!”

Aliiita jina hilo hasa alipooona tena picha nyingine ya Pamela akiwa amelala juu ya kifua cha Raisi Jackson Okaka, alizidi kupekua bahasha ile na kukuta ujumbe mfupi wa maneno
“NITAFUTE KWA NAMBA HIO HAPO CHINI”

, kweli alichanganyikiwa kuliko siku zote maishani!, jasho jingi lili mtoka mwilini, sababu hata siku moja hakuwahi kuwaza kuwa Pamela ange kuja kufanya kitendo cha kuumiza moyo wake kama siku hiyo, alichukua simu na kuipigia ile namba iliyokua juu ya karatasi, baada ya upande wa pili wa simu kupokea sauti ya kijana mmoja ili sikika ikimwambia kuwa wakutane TEMEKE kama akitaka kujua ukweli juu ya PAMELA, alivaa shati haraka haraka na kutoka
kama mwenda wazimu, alitafuta dala dala na baadae kidogo kufika
Temeke na kuipigia tena ile namba.akisubiri maelekezo kupitia simu ni wapi wakutane, kweli alikua alikua na shauku ya kujua ukweli wa mambo, japo alijua ukweli huo ungeweza kumuumiza moyo wake maradufu!

“Donald, si ndio”?
“ndio ndo mimi mwenyewe”!
“asante kwa kuja naitwa MSAGUSA, njo tutafute sehemu nzuri tuweze kuongea”
Walitafuta moja ya sehemu iliyo tulia kabisa na wote kuketi, kwa upande wake, hakika alikua na shauku ya kujua kile ambacho aliambiwa anataka kuambiwa,
“we mwana ume mwenzangu,na nisinge penda kukuona una potea nika baki tu nakuangalia”
“una maana gani”?
“ujue nini kaka!, ngoja nikwambie ukweli kuhusu PAMELA, Yule demu sio ndugu yangu, Yule demu ni mchafu, niamini mimi, kwanza ana mahusiano na Raisi OKAKA, huwa wana penda sana kuja maeneo ya huku, unaona hiyo gest hapo”?
Kijana Yule aligeuka nyuma na kuioneshea gest hiyo kidole.
“ndio”
“huwa wana kujaga kila siku usiku kulala ndo maana nika amua kuwa piga picha ili nije kukuonesha najua ume umia sana, kama ndugu yako, nisingependa kukuona una potea kabisa, nakufahamu muda mrefu sana Donald!,”
“mahusiano yao yalianza lini”?

Donald aliuliza kwa uchungu na kutamani kulia pale pale ila alijikaza kisabuni sana, hakika alizidi kuumia pengine alitamani hata asingekuja Temeke kusikiliza maneno hayo ambayo yalikua yakizidi kuuchoma moyo wake, kijana Yule
alizidi kuongea maneno ya kuchoma bila kujali uzito ,Donald alihisi kuchanganyikiwa hakuelewa nini amfanye Pamela , kilichomuumiza zaidi ni kitendo cha kupotezewa muda na kuzalilishwa mbele za watu kisa pamela leo hiii hataki kuamini kuwa mtu aliyempenda na kuamisha nguvu zote kwake alimgeuka,
Ndoto zake waje kuwa mume na mke zilizimika kama mshumaa uliopulizwa na upepo mkali au kumwagiwa maji,

Mbio mbio aliondoka sababu hakutaka kusikia vitu vingine alia mini ange zidi kusikiliza wenda angezidi kuumia na kuchukua uamuzi mwingine mba-ya, alitembea akiwa na mawazo mengi sana, mpaka alivyo fika Hostel hakutaka kuingia darasani, mawazo yalimsonga sana huku jasho liki zidi kumtoka hakujua kwanini jasho lile lina mtoka.

Alihisi simu yake ya mkononi ina ita alivyoangalia kioo cha simu aliona ni Pamela anapiga hakutaka kuipokea aliitupa kitandani kwa hasira ila simu ile ilizidi kuita na kukata tena.
‘”oyaa simu huisikii ina ita au””?
Alikua ni rafiki yake ambae walikua wakiishi wote ndani ya hostel moja.
“achana nayo”
“kaka yamekuwa hayo”?
“Kway eeeh, achana na hiyo simu”
“ una tatizo gani ndugu, Pamela ndo ana kupigia lakini kumbuka”?
Donald kuona vile alichukua simu ile na kuizima kabisa, kitendo kilie kina mshngaza sana Kway ambae hakuelewa kinachoendelea ila kwa haraka haraka alijua kuwa kuna tatizo kubwa sana, ila kwa wakati huo hakutaka kuuliza chochote,

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG