Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

SLAVE SEX SEHEMU YA 6/10


SLAVE SEX
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 6 KATI YA 10
*******


Hakuweza kuzizuia hasira zake zilizoonekana waziwazi usoni mwake,kitendo alichotaka kumfanyia
Parston alikichukulia moja kwa moja ni utovu wa nidhamu ama kuvunjiana heshima!
“Hivi unanichukuliaje?Naomba uondoke kabla sijakuchukulia hatua mbaya”
Sonia akazidi kufoka.Partson akaona aibu kupita kiasi akapata kigugumizi cha ghafla,hakutegemea kitu kama hicho kama kingetokea kwa sekunde kadhaa, kichwani akawa anajilaumu.
“Sonia,nisikilize nachotaka kukwambia”
“Huwezi kuniambia kitu chochote, kwanza sitaki na urafiki ufe leoleo”
“Unafika mbali,niwie radhi nimeshindwa kucontrol hisia zangu,ni shetani tu”
“Kama ndo gia zako za kuwatongozea wasichana wako kwa namna hiyo usilitee mimi hizo swaga,naomba uwende unazidi kunikera”
Hakukuwa na namna ya kuyabadili maamuzi ya Sonia kwa kila alichokiongea, Partson alijaribu kumtuliza lakini ilikuwa bure kabisa.Ili kudhihirisha kuwa ni kweli amekasirishwa alitembea mpaka mlangoni na kuufungua.
“Usiku mwema,naomba nipumzike”
Partson akawa mnyonge ghafla,hakutofautishwa na kifaranga kilichomwagiwa maji kweli alijua kwa kitendo hicho amebugi 'step' kwa mjanja au mtoto wa mjini kama yeye hakupaswa kukurupuka.
Kwa jinsi mambo yalivyoenda ilibidi asalimu amri, akatembea taratibu mpaka mlangoni huku akimuangalia Sonia ambaye alikuwa anaangalia pembeni, hakutaka hata kumuangalia Partson usoni.
“Usiku mwema nawewe”
Partson akasema akiwa anatembea, lakini Sonia alibaki kuangalia kando na kuufunga mlango, ambapo Partson alikuwa bado hajatoka nje vizuri akasukumizwa nao mpaka nje.
Sonia akafunga mlango na funguo na kutembea mpaka chumbani kwake, ambapo alianza kuchojoa nguo moja baada ya nyingine mpaka alivyobaki mtupu,akavuta kanga na kuivaa ikawa imeishia juu ya magoti, mapaja manene meupe yakawa wazi kabisa,akatembea mpaka bafuni.
Alivyoitoa kanga akakumbana na kioo.Mapajani bado alijaa makovu yaliyoacha alama nyekundu,sura ya Sebastian ikamjia kichwani, akajikuta analia machozi,mateso aliyoyapata nchini Sweden bado aliyakumbuka,akawa anajiona jinsi alivyokuwa amekalishwa juu ya kiti cha moto anaunguzwa na wazungu,akazidi kuwachukia wazungu kupita kiasi na kupanga ipo siku angewafanyia kitu kibaya akiwemo Sebastian mwanamme mwenye roho ya kinyama.
Alivyotoka kuoga akatembea mpaka kwenye meza yake ya vipodozi akakaa ili kuanza kujiremba,japokuwa ulikuwa ni usiku lakini alipaka baadhi ya mafuta ili kuifanya ngozi iwe laini,akachukua tena dawa nyingine aliyopewa ya kutoa makovu akaanza kupaka mwilini mwake hususani kwenye mapaja,alivyohakikisha kila kitu kipo sawa alizima taa na kujitupa kitandani,akashika simu yake.
Cha kwanza kukikuta ni 'missed call'kumi za Partson na meseji zisizokuwa na idadi,akaanza kuipitia moja baada ya nyingine.
Zote zilikuwa za msamaha,Partson alilia kwenye meseji zake.Mbali na meseji zote wala hakushtuka akazima simu na kujitupa kitandani.
***
“Sio ivyo Nasra,ukweli wangu ndiyo huo kwanini nianze kuzunguka zunguka kama mtoto wa Sekondari,mara sijui nikutumie vocha ya mia tano.Nikutumie maua,sisi watu wazima.Sina haja ya kuzunguka wala nini.Mimi nipo Strait nimekuzimia.Kama hutaki uniambie hapahapa,nifanye mambo mengine,maisha yenyewe mafupi haya,mambo ya kupeana stress ndiyo sipendi mimi”
“Si unajua nina Boyfriend?”
“Naelewa,nani asiyejua hilo swala”
“Sasa akijua?”
“Nani atamwambia unadhani?”
“Paparazi wapo kila kona”
“Hawawezi kutuona,mjini kubwa hii”
Nasra alikuwa akitongozwa ndani ya gari aina ya BMW X6 na kijana aliyefahamika kwa jina la Alex Patrick Mwandambo,jina hilo halikuwa ngeni mdomoni mwake, baba yake alishawahi kuwa mchungaji miaka mingi iliyopita akafariki kwa ugonjwa wa Ukimwi,swala hilo lilitingisha mwaka mzima, kwa kipindi hicho Alex alikuwa masomoni Uingereza na mpaka amerudi nchini alikuwa tayari ana miezi mitatu,alikuwa ni miongoni mwa vijana wadogo matajiri nchini na kujumlisha na sifa za baba yake Mchungaji Patrick aliyeuwa watu kwa virusi vya ukimwi ikamfanya jina lake livume kiasi.
“Mr.Alex una pete ya ndoa lakini”
“Ndio nina mke lakini asikutishe,wewe hutaki kuendesha gari zuri lakini?”
“Nani amekwambia mapenzi ni magari?”
“Gari lina nafasi yake kwenye mapenzi,nipatie jibu harakaharaka”
“Kwa sasa hivi siwezi kukupa jibu”
“Basi shika kadi yangu ya simu”
“Sawa,nitakutafuta”
Kabla ya Nasra kushuka ndani ya gari akavutwa na Alex,midomo yao ikakutana wakaanza kubadilishana mate,lilikuwa ni denda la kama sekunde tano!
“Woow!you are such a good kisser”
Alex alitoa sifa akimaanisha kuwa Nasra ni fundi wa kupigana mabusu.Bado aliendelea kumsindikiza kwa macho ya ngono hata baada ya kushuka ndani ya gari na kuanza kutembea kuvuka barabara kuelekea Chuoni.
***
Alex Patrick Mwandambo aliendelea kumuwinda Nasra kila kukicha,mitego yake yote aliyoiweka ilimnasa mrembo huyo siku chache tu,Alex aliweka pesa mbele, kila siku Nasra alikuwa akikutana na Alex alikuwa ni lazima atoke na laki mbili, hapo ndipo alipopagawa zaidi,hakuna siku iliyomchanganya akili yake kama alivyonunuliwa simu kubwa ya kisasa moyo wake ukanunuliwa kwa siku chache tu.
Chuoni akawa anatesa akawa anatembea na wanaume wawili kwa mpigo,kwa jinsi alivyokuwa mjanja alifanya jambo hilo kwa siri kubwa sana.
“Hii simu umetowa wapi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Partson Ngogo,simu kubwa ambayo hata yeye hakuwa nayo ilimshangaza sana jicho likamtoka,machale yakaanza kumcheza kuwa kuna mwenzake wanakula wote sahani moja.
“Honey,mbona unauliza kwa ukali”
“Hujajibu swali”
Partson alitaka jibu na sio kuchekewa kama alivyofanya Nasra.
“Anti yangu kanitumia kutoka Germany”
“Germany!?”
“Yah,Germany honey”
“Katika kumbukumbu zangu hukuwahi kuniambia kama una anti yako yupo Germany”
“Sio anti yangu kiviiiiile baby, ni kama rafiki tu wa Mama yangu,alienda huko kipindi kirefu sana ndiyo juzijuzi hapa aliniambia mama kuwa anahitaji namba zangu.Akanitumia hii simu”
Nasra alikuwa mkavu,alijitetea kwa umakini na katika maneno yake hakuonesha hali ya wasiwasi, ulikuwa ni uwongo wenye PHD na alivyokuwa anaongea na Partson alimuangalia usoni bila wasiwasi.
“Vitu vingine uwe unaniambia baby,mjini hapa.Alafu wewe ni mtoto mzuri”
Kwa Nasra mpango huo ulikuwa umetiki, tayari aliweza kumdanganya mpenzi wake akamuamini.
“Utakuja basi leo nyumbani”
“No Honey,kesho nina test sitoweza tufanye keshokutwa”
“Sawa baby”
Walivyotoka kuagana na Partson kwa madenda akaingia ndani ya gari na kulitoa, lakini alivyokunja kona akapishana na BMW X6 inayowaka, hata yeye akaitolea macho,ilikuwa ni gari iliyovimba akashindwa kumuona mtu aliyekuwa ndani ya gari kutokana na vioo vya gari hilo kuwa vyeusi yaani tinted.
Akageuza shingo yake na kuzidi kulisindikiza kwa macho.
“Duu,bonge la ndinga.Usikute huyu kaacha familia yake anaenda kwa mchepuko huko,watoto wa chuo hawa nuksi sana,wazazi wao wanajua wanasoma”
Partson akajisemea mwenyewe akaweka gia na kuondoka,hakuelewa kuwa gari hilo la mume mwenzake,hakutaka kuwaza na kutaka kurudi nyuma.
***
Shoping ya kwanza kufanyiwa ilikuwa ya milioni mbili,ilikuwa ni kufuru, Nasra alikuwa keshatekwa tayari na pesa za Alex,bado aliendelea kufanya siri na muda wote alivaa ushungi na miwani kubwa ili sura yake isigundulike kirahisi na waandishi wa habari.
“Tupite na kariakoo kule,nikakununulie viatu”
“Sawa honey”
Kweli pesa sabuni ya roho!wakaingia ndani ya gari kwa safari ya kwenda kariakoo madukani.
***
“Nishakusamehe,tusahau yaliyopita niambie mechi lini tena? ujue umenifanya nipende mpira Partson,nani kakufundisha mpira?”
“Hakuna mtu aliyenifundisha,nilijikuta tu nacheza,tangu nipo Nursery nilikuwa napenda sana mpira,Baba angu akawa ananinunulia mipira,basi ndiyo ikawa ivyo”
“Sio siri,hivi kwenye mpira unakuwa ukicheza unajisikiaje pale uwanjani,Mademu wanavyokushangilia”
“Ha! Haa! Haaa! Haaaa!sio mademu,wana ndio wananipa shangwe,sasa pale ni sawa na kuweka petrol kwenye moto,wananichochea”
“Hapo kichwa kinakuvimba mwenyewe”
“Wananipandishaga mori”
Mazungumzo hayo yalifanyika ndani ya duka la Sonia, lilikuwa kubwa mno wakaona wakae pembeni kwenye kona,kilichomuinua Sonia ni wateja walioingia.
Alianza mwanaume mrefu maji ya kunde akafatiwa msichana mfupi kiasi kavaa ushungi na miwani kubwa.
“Karibuni”
Sonia akasema huku akiachia tabasamu pana usoni.
“Ahsante,hapa unauza nguo za kike peke yake?”
“Ndio Kaka angu”
“Nahitaji vitopu topu jeans,Baby embu chagua nguo unayotaka”
Nasra akawa anazunguka kila kona,alivyoiona sura ya Partson akashtuka mpaka akadondosha pochi.
“Dada vipi?”
Kutokana na mavazi aliyovaa Nasra isingekuwa rahisi kumgundua,Partson akainama na kumsaidia kuiokota.
“Sasa Sonia,wacha mimi niwahi naingia kwenye mazoezi nimetumiwa meseji na kocha”
Partson aliaga,alivyotoka nje akakutana na BMW X6 gari ambayo haikuwahi kumtoka kichwani mwake,akaitizama kwa makini na kutembea mpaka ilipokuwa gari yake Alteza akaingia na kutimka!
****
“Sawa Latifah lakini hupaswi kudeka kiasi hicho,una mimba yangu ndiyo naelewa sasa unafanya mpaka nisinywe maji,mara baby kizunguzungu,baby sijui nina mafua.Mimi daktari? ukiona hali kama hiyo nyoosha kwa daktari au mpigie dereva simu aje kukuchukua.Sio unakuwa kama mtoto mdogo,unaniboa wakati mwingine.Unatakiwa ujiongeze”
“Alex sina maana hiyo,nahitaji ukaribu wako”
“Kwahiyo niache kazi nikae nyumbani namimi nilee mimba?”
“Hapana Mme wangu”
“Ila?”
“Samahani kama nimekuudhi Alex”
“Wala hujaniudhi ni wajibu wako kuniambia,ujirekebishe”
“Sawa Darling,kesho inabidi niende clinic”
“Nitakupeleka ondoa shaka”
Upole wa Latifah ndiyo uliomponza,alimpenda sana Alex na alikuwa tayari ana mimba ya miezi mitano.
Alikuwa msichana mtulivu na mwenye maadili yote ya kiislam, japokuwa Alex alikuwa mkristo lakini walipendana hivyohivyo hata siku moja hakutaka kutoka nje ya ndoa yake,alimuamini Alex kupita kiasi,kwake alikuwa ni kama Mungu wa pili.
Ni kweli Alex alikuwa ni mwanaume mchapakazi lakini mbali na hivyo alikuwa na mchepuko, hakumsahau mke wake.Upendo wake ulikuwa palepale, yaani huduma zote alitoa kama Mwanamme.
Kama ilivyopangwa,Alex alimpeleka Latifah clinic kesho yake asubuhi na mapema baada ya hapo akamrudisha nyumbani.
“Baby upo wapi?”
Nasra ndiye alikuwa akipigiwa simu na Alex.
“Niko Magomeni Mapipa”
“Nakuja kukuchukua nipo karibu”
“Lakini baby usi...tititi”
Simu ikakatwa bila ya Nasra kutaka kumalizia anachotaka kusema,aliipiga simu ya Alex lakini haikupokelewa,alikuwa yupo Stendi na dakika moja tu iliyopita alikuwa ameongea na Partson kuwa ampitie,alikuwa katika wakati mgumu.
Wakati anafikiria hayo ALTEZA ya Partson Ngogo ikawa imefika imepaki mbele kidogo,kabla hajatafakari vizuri BMW x6 ya Alex ikasimama pembeni yake.
Hapo ndipo alipohisi kupagawa mkojo wa ghafla ukawa umem-bana!

****
Nasra alikuwa katika wakati mgumu kuliko siku yoyote ile, wanaume wake wote wawili walikuwa mbele yake na alitakiwa aingie ndani ya gari moja wapo,akabaki ameganda kama barafu.
Akili yake ikafanya kazi kwa kasi ya umeme akatembea haraka mpaka kwenye Alteza ya Partson na kuingia, sababu aliamini kuwa yupo sahihi kwa hatua aliyoichukua lakini kwa mbali alihisi roho yake inamuuma, akalichukulia swala hilo ni sawa na kupiga teke fuko la pesa!
“Vipi mbona una mashaka hivyo?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Partson huku akimtizama Nasra jinsi alivyokuwa akitetemeka kwa hofu.
“Ha..ha haapana nipo sawa,twende tu”
Hata Partson alishaanza kuingiwa na wasiwasi,sio kwamba Bmw x6 hakuiona, kupitia 'site mirror' ya upande wake aliishuhudia,moyo wake ukahisi kitu.Akaunganisha baadhi ya matukio na kushindwa kupata jibu sahihi.
Ghafla akaikwapua simu ya Nasra na kuiwasha lakini akashindwa kuendelea zaidi sababu ilidai namba ya siri.
“Toa code”
“Abe abee”
“Toa code ya simu”
Tayari Partson alishikwa na hasira iliyochanganyika na wivu akili yake ikachezwa na machale.
“Baby ba..by nimeisahau”
“Unasema?!”
“Griii griii grii griiii”
Simu ya Nasra iliita ikiwa mikononi mwa Partson na jina likatokeza ALEX, Partson akaitizama na kupiga jicho nje ya site mirror,bado BMW X6 lilikuwepo na mtu aliyekuwepo ndani alionekana kushika simu.
“Pokea simu na uweke loudspiker,nakwambia hivi pokea simu na uweke loudspeaker.NITAKUUWA humu ndani ya gari Nasra”
Nasra alizidi kutetemeka akahisi kubanwa na haja kubwa,hakuelewa ni kitu gani afanye lakini akapiga moyo konde, akaipokea na kuiweka Loudspeaker sauti ikawa inaenea ndani ya gari.
“We Nasra,unanichelewesha njoo uchukue maagizo yako, sasa mbona unaniweka? nachelewa nataka kusafiri leo na kama una vitu vingine vya kumpa Mama niambie nimpelekee”
Yalikuwa ni maneno ambayo yalimshangaza Nasra lakini kwa ujanja wa mjini alielewa kuwa Alex alitaka kumnasua kwenye hatari, nayeye akajiongeza.
“Sawa nakuja,nipo na shemeji yako”
“Kumbe upo na Shemeji,basi ngoja mimi nije hapo”
Yalikuwa ni maigizo yaliyokwenda shule.
Alex akafungua mlango kwa kujiamini na kusogea mpaka kwenye Alteza tena upande wa Partson, kioo kikashushwa.
“Shemeji habari”
“Poa, vipi ndugu”
“Salama,nina maagizo ya ndugu yangu hapo ya kumpa.Kama hujanifahamu mimi naitwa Alex mimi na Nasra ni ndugu.Sijui unaitwa nani mwenzangu”
“Partson Ngogo”
“Partson Ngogo?yule mcheza mpira?”
Alex akajifanya kuigiza kama hamfahamu.
“Ndio”
“Sasa samahani kidogo,nani Nasra”
“Abee”
“Utaenda pale Ubungo kesho,utaonana na Kasim wa Taqwa ana mzigo wako,upo pale.Kwa maelezo mengine kama hujaelewa nipigie simu maana nina safiri leo”
“Sawa ahsante,safari njema pia”
“Poa,sasa shemeji ngoja niwaache nikapambane na ujenzi wa taifa”
Hata ungekuwa mjanja vipi kwa jinsi walivyokuwa wanaigiza ungekubali kuwa ni ndugu,asilimia mia moja Partson akawaamini hakuelewa kwamba alifanywa bwege na watu hao walikuwa wapenzi,akashusha pumzi.
“Partson,umeniudhi.Siku izi huniamini?”
Nasra akaanza kujihami na kuanzisha maongezi kwa hasira.
“Mimi sikujua,nakupenda ndiyo maana nafanya hivyo.Hata hivyo hukuniambia kama huyo ni ndugu yako”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa.Nasra akaendelea kufanya mchezo mchafu akitembea na wanaume wawili kwa mpigo!
***
“Ah ah shs ah ah ah Ale...x aah aah mmh shss aah aah”
Kiuno cha Nasra kilikuwa kimekamatiwa na mikono miwili ya Alex, wanafanya ngono huku akitoa sauti za puani tena kimahaba na dalili zilionesha kwamba anakaribia kufika mshindo na ndiyo maana alizidi kulalamika akihisi utamu unaongezeka,Nasra alipenda sana Ngono kuliko hata chakula.
Na ndiyo maana akiwa kitandani hujituma kwa bidii zote,akazidi kumkatikia Alex kama aliambiwa kwamba atakufa kesho,akajipindua kama samaki akawa chini ya Alex,kifo cha mende!
“Bab..y si..ku za..ko vipi?”
Alex aliuliza akiwa sikioni mwa Nasra huku nayeye akijitahidi kuamsha popo!
“Usij..ali aah aah aah nipo kwenye si..ku salama”
Kauli hiyo ilivyotoka kwa Nasra ikazidi kumpandisha Alex midadi,akajiachia na kupeleka majeshi majeshi, alivyokaribia kufika mshindo akazidi kwenda mbiombio,baada ya sekunde moja alitoa mguno wa ki-utu uzima akalala kifuani mwa Nasra.
“Nakupenda Nasra”
“Mimi pia”
“Mfano nikikwambia uachane na yule Partson utakubali?”
“Hapana siwezi”
“Kwanini sasa?”
“Nampenda bado”
“Namimi je?”
“Hata wewe nakupenda”
Bado walizungumza wakiwa wamelaliana.
“Baby,nataka tupige picha za kumbukumbu”
“Mh,tukiwa hivi?”
Lilikuwa ni wazo la Nasra.
“Ndio kwani vibaya?tena naomba nitumie simu yako.Yangu haina chaji”
Hicho ndicho kilichotokea,simu ya Alex ikatumika kupiga picha wakiwa kitandani wakiwa katika mapozi mbalimbali, mara wapigane denda mara wamelaliana ili mradi mahaba kwa kwenda mbele.
“Zinatosha sasa”
“sawa honey,nikifika tu hostel utanirushia.Nitakuwa nakukumbuka sana”
“Poa baby,mimi naenda kuoga wewe si bado upo?”
“Mimi bado nipo”
Alex akaingia kuoga,alivyotoka alivaa na kuondoka zake.
***
Uzuri wa Sonia Nickson Shayo ulizidi kutingisha,duka lake likawa maarufu, uzuri wake ukawanyanyasa wafanyabiashara wenzake wa kike waliokuwa na maduka yao pia.
Kila mwanaume alitaka kuingia kwenye duka lake ili mradi tu aweze kuushuhudia uzuri wa ajabu aliokuwa nao msichana huyo mdogo.Kwa mwezi alikuwa anauza sio chini ya milioni kumi na mbili tena kwa hesabu za harakaharaka,mtaji wake ukawa unakuwa siku hadi siku.
Siku moja jioni alivyofunga duka lake akaamua kumtembelea rafiki yake kipenzi Sauda, nayeye alikuwa ana duka jirani yake.
“Hee!Sonia leo makubwa,umeamua kuja kunitembelea!”
“Sisi ni ndugu ujue”
“Ndio lakini muda kidogo”
“Ubize tu,si unajua muda wote unatakiwa uwepo ndani.Wateja wenyewe ndiyo ivyo”
“Enhe lete mpya”
“Hivi,nguo zako huwa unaagizia wapi?”
“Mh,mara nyingi China na India”
“Huwa unaendaga mwenyewe?”
“Ndio,tena nahisi mwezi ujao nitaenda”
“Ukienda basi naomba niambie namimi nataka niende kuagiza nje ya nchi nimechoka kununua Wholesale hakuna faida sana”
“Hakuna shaka”
Wakaendelea kupiga stori za hapa na pale kisha kuagana,Sonia akatembea kuelekea stendi ya basi ili kutafuta daladala apande aende kupumzika.
Kuna kitu alianza kuhisi akiwa anatembea. Ni kweli lilikuwa ni gari aina ya BMW X6 likampita mbele yake na kusimama,alivyolikaribia.Kioo cha gari hilo kikashushwa.
“Dada,Anti..”
Sonia akageuka.
“Samahani,unanikumbuka?”
“Hapana”
“Nilikuja dukani kwako pale,wiki iliyopita”
“Dukani kwangu wanakuja watu wengi”
“Anyway,unaelekea wapi?”
“Nyumbani”
“Wapi?”
“Sinza”
“Ingia nikakudrop,sababu ndiyo njia yangu hiyo”
Sonia hakuwa na tabia ya kukubali lifti kirahisi na isingekuwa uchovu aliokuwa nao asingeingia ndani ya gari.
“Unaishi Sinza Sehemu gani?Soorry mimi naitwa Alex”
Alex akavunja ukimnya na kujitambulisha huku taratibu akikanyaga mafuta.
Kabla ya kuingia barabara kubwa aliangalia pande zote mbili na kuliingiza gari barabarani.
Akageuza shingo yake kumtizama Sonia,udenda ukaanza kumtoka.
“Unaitwa nani?Daada... hey..”
Sonia alikuwa mbali kimawazo,akili yake ilikuwa umbali wa maili mia.
“Sorry akili yangu ipo mbali sana,naitwa Hafuan”
Alidanganya,hakutaka jina lake lijulikane kwa kila mtu.
“Oh Hafuan,vipi biashara lakini?hivi lile duka ni lako au?”
“Ndio”
“Hongera sana,mimi napenda binti mchapakazi wewe ni fighter,mimi ni mfanyabiashara mkubwa tu hapa jijini Dar es salaam,nawasaidia watu wengi sana.Na wengi wanafanikiwa, kama unahitaji msaada wowote usisite kuniambia mimi nitakusaidia”
Alex alizidi kujinadi, akajiongezea sifa nyingine ambazo hazikuwa zake.Sura ya Sonia ilivuruga akili yake aliongea maneno mengi kama redio ya mchina.
Lakini Sonia yeye alikuwa akimjibu kifupi, tayari alikerwa na mazungumzo yake.
“Ahsante kwa kukufahamu”
“Inabidi unipe namba zako za simu”
“Za nini?”
“Tuwe tunawasiliana”
“Namba nilizokuwa nazo zinatosha,nashukuru.Nishushe hapo mbele kwa Remmy”
“Nataka nikupeleke mpaka kwako”
“Ndio nimefika,wewe nishushe”
“Sasa hapa unaishi kwa sehemu gani?”
“Kaka naomba usisamishe gari nishuke,mbona una maswali mengi?Basi nirudishe uliponitoa.Kunipa lifti isiwe tabu sasa”
Sonia akafoka kwa ukali,gari likasimama akashuka na kubamiza mlango.
Akatembea harakaharaka na kuingia ndani ya bajaji,hakutaka kabisa mtu asiyemfahamu ajue anapoishi.
Kilichomshtua Alex ni simu yake ya mkononi kuita,alivyoangalia alikuwa ni Nasra anapiga,akaipokea na kuiweka sikioni.
“Baby”
“Nambie kipenzi”
“Nirushie basi zile picha”
“Sasa hivi nakurushia”
Alex akashuka na simu yake kubwa na kuingia kwenye 'gallery' akachagua picha za utupu walizopiga na Nasra ili kumrushia.
Ghafla kama kifaranga cha kuku kinavyokwapuliwa na mwewe ndivyo simu yake ilivyofanywa na bodaboda iliyopita,akabaki anaishangaa pikipiki inapotelea gizani.
“Haaa!Picha”
Akili yake ilipokaa sawa ndipo akafikiria kitu hicho hatari,picha za utupu!


 Alex alizidi kushangazwa na kupigwa na butwaa la waziwazi,uwezo wa kuikimbiza pikipiki iliyokwapua simu yake alikuwa nao sababu pembeni yake zilikuwa nyingine zimepaki zinasubiri abiria,asingeshindwa kufanya hivyo lakini kwa hadhi yake alijishtukia,kwa mtu mwenye pesa kama yeye kuanza kukimbizia simu yenye thamani ya shilingi laki tisa kingekuwa kitu cha aibu.
“Potelea mbali”
Akatupa mikono yake hewani huku baadhi ya watu wakiwa wanamshangaa,akarudi ndani ya gari na kujiondokea.
Alifika nyumbani kwake akiwa mwenye mawazo chungu mzima,hakutaka kumsemesha mke wake.
“Mume wangu una nini leo?”
Alex alikumbana na swali hilo baada ya kuweka mgongo wake kitandani.
“Niko sawa”
“Niambie tu,ninaweza kukusaidia.Mimi ni mke wako”
“Okay!Simu yangu imeibiwa”
“Sasa Mpenzi ndiyo unawaza kiasi hicho?”
“Ina documents zangu za muhimu sana”
“Pole Mme wangu,kwani si huwa una save kwenye kompyuta yako?”
“Latifah,naomba uniache siko sawa.Niache nipumzike”
Haikuwa kawaida hata kidogo kwa Alex kuropoka kwa sauti kubwa kiasi hicho,alionekana kukerwa na maswali ya mke wake,akavuta shuka na kujifunika gubigubi.
**
Bado Partson Ngogo moyo wake ulimsukuma awe na Sonia kimapenzi,alifanya kila awezalo lakini kila kitu kilishindikana kabisa, uzuri wa Sonia ukamchanganya akili, akashindwa hata kucheza mpira vizuri uwanjani, kichwa chake kilijaa msongo wa mawazo,kocha wake Msafiri alijaribu kumshauri lakini ikashindikana pia, timu ya Tanzania ikawa inafungwa magoli na ikashuka katika chati,jambo hilo liliwaumiza sana akili,kila alipoingia Partson Ngogo uwanjani alibolonga.
Kila mtu alisema maneno yake, watanzania wengi walidhani Partson amerogwa na wengine walisema kuwa amenunuliwa na wazungu ili Tanzania wasifike fainali la kuwania kombe la Dunia.
Hakuna hata mmoja aliyeweza kujua nini kilichojichimbia moyoni mwa Partson.
“Baby una mawazo gani?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Nasra.
“Sina mawazo nipo Normal”
“Sio kweli,kuna kitu kinakusumbua,hata perfomance yako ya mpira sio nzuri”
Partson alikumbana na maswali mengi,sio kwa Nasra peke yake hata waandishi wa habari waliandika vitu wanavyovijua wao.
“KUMBE PARTSON NI FREEMASON,NGUVU ZAKE ZIMEISHA.KIWANGO KIMESHUKA HABARI KAMILI UK.2”
Hiyo ndiyo habari iliyoandikwa kwenye kichwa cha habari cha magazeti,kila mtu alitaka kununua magazeti na watanzania wengi waliamini.
”PARTSON AKUTWA NA IRIZI CHUMBANI,WATU WACHANGANYIKIWA,NA SASA MWISHO WAKE UMEFIKA”
Habari zilizidi kuvuma,kila mabaya yote yalizungumziwa na Watanzania wengi waliamini,kutokana na kiwango chake kushuka ghafla,ilimuuma lakini hakuwa na la kufanya.
***
“Hivi Partson unajisikiaje unavyoandikwa hivyo kila siku?mimi hata sipendi”
“Hata mimi pia sipendi,wewe ndiye unanifanya niwe hivi Sonia”
“Kivipi?”
“Nakupenda,nataka uwe mke wangu”
“Mbona haya tulishayaongea na sidhani kama ndiyo hicho kinakufanya ushindwe kucheza mpira vizuri”
“Sina kingine zaidi ya hicho”
Partson aliendelea kulalamika kuhusu penzi lake,akazipigia debe hisia zake.
Maongezi hayo yaliendelea wakiwa ndani ya duka lake la nguo.
“Naomba ukifunga duka twende sehemu tukaenjoy”
Partson aliomba.
“Sawa,tutaenda wapi?”
“Hata club,popote pale tukaenjoy”
“Poa,leo lini?”
“Jumamosi”
“Kesho hakuna kazi,sawa”
Hatimaye Sonia akakubali.
Ilivyofika jioni wakafunga duka, Partson na Sonia wakaingia ndani ya gari na safari ya kwenda Sinza kuanza.

Walivyofika tu kazi ya Sonia ikawa ni kwenda kujimwagia maji.Alivyotoka hapo alikuwa amependeza kupita kiasi,kikaptura alichovaa kilifanya mapaja yake manene yawe wazi,juu alipigilia topu ya kuwakawaka,kiatu alichovaa kilikuwa 'flat' kilichofanana na rangi ya kofia.
Kwenye mavazi tu alijikubali,kuishi sana nje ya nchi kulimfanya aende na wakati.
“Sonia,woow ni wewe?!”
Partson aliuliza kwa mshangao huku akimkagua kuanzia juu mpaka chini.
“Ndiyo mimi twenzetu”
“Sasa namimi inabidi kidogo,nikajikoki”
“Mbona hapo umetoka bomba”
“Hata hivyo bado mapema”
“Basi twende kwako,ukabadili nguo”
“Hapo freshi”
Katika siku aliyokuwa na furaha Partson ni hiyo, kutoka na Sonia.
Akawasha gari wakaenda mpaka Kawe kituo kinachoitwa msikitini.Wakakunja kona wakasimama nje ya geti kubwa la rangi nyekundu.
“Hapa ndiyo kwako?”
“Hapana,mimi nyumba yangu bado haijaisha bado naishi kwa wazazi wangu”
“Pazuri,inabidi nikusubiri ndani ya gari sasa, maana hizi nguo nilizovaa sio”
“Sawa,ngoja nikuwashie mziki usikilize,nakuja sasa hivi”
Partson akashuka na kuingia ndani ya geti akamuacha Sonia ndani ya gari.
****
Mapenzi ya Alex na Nasra yalizidi kuongezeka siku hadi siku,ni kweli aliweza kumvuta taratibu mpaka mzani wa upande wake ukawa mzito kuliko wa Partson,Nasra akazidi kutanua walifanya mapenzi kila sehemu,iwe ndani ya gari,chooni,jikoni chumbani na popote pale.
Hilo likazidi kumfurahisha Nasra anayependa mchezo huo wa kikubwa,akawa mtumwa wa Ngono.
Kitendo cha Partson kuporomoka na kusemwa vibaya kwenye magazeti ndicho kilimpa sababu ya kumuwekea ukuta,kila akipigiwa simu na Partson anajifanya yupo bize!
“Nakupenda Alex,kama ungekuwa muislam ungenioa tu uwe na wake wawili”
“Hata mimi nilitaka kusema hivyo,umeniwahi”
“Kweli?”
“Ndio Darling”
“Alafu.....!”
“Nini tena?”
“Ile simu hukuifuatilia tena?”
“Hapana,nimeachana nayo”
“Nilikuwa naipenda sana ujue”
“Achana nayo”
Maongezi yao yalifanyika wakiwa ndani ya gari viti vya nyuma,wamelipaki kandokando ya barabara ya Mwenge, usiku wa saa tano.
Mambo waliyofanya ndani ya gari yalikuwa ni kufuru,gari liligeuzwa na kuwa gesti ndogo,kwa maana walianza kushikana kila sehemu ya miili yao wakibalishana mate,wakilana denda.
Adoado mambo yakazidi kuendelea, wakavuana nguo zao zote wakazitupa kando,kilichoendelea hapo ni muonekano wa gari kutingishika kumaanisha kuwa walikuwa wakilana uroda.
***
“Roger Hamy.....Upo wapi?”
“Nipo Mwenge hapa,ndiyo nakungoja”
“Mimi ndiyo natoka”
“Poa,nipo hapa stendi kwenye magari ya makongo”
“Nikukute basi hapo”
Partson alikuwa yupo tayari,keshajipigilia pamba, pembeni kushoto yake alikaa Sonia,ilikuwa ni lazima wampitie mtu aliyeitwa Roger Hamy,rafiki yake kipenzi na Partson.
Walivyofika Stendi wakaonana na Roger Hamy, safari ikaanza mara moja.
“Hivi hili gari huwa lipo moja au?maana kila wakati naliona hii ni mara ya nne kama sikosei”
Partson akavunja ukimnya baada ya kuliona BMW x6 limepaki kandokando ya barabara.
“Lipo moja tu,huyo ni Alex”
“Hivi ni nani?”
“Mfanyabiashara tu”
wakati mazungumzo hayo yanaendelea, Sonia alikuwa amekaa kimnya,anawasikiliza hata yeye gari hilo alilijua vizuri lakini hakutaka kutia neno sababu halikuwa swala lake.
***
“Oya Bakari,sasa mzigo huu hapa si ulikuwa unataka kuuona?”
“Ndio, lakini huo mtonyo sina mwanangu”
“Wewe una ngapi?”
“Jiwe tano tu,hapa nitakupa laki mbili, hiyo nyingine nitakumalizia wiki ijayo”
“Sasa unazingua Beka,Maswala gani hayo?Wewe nipe mzigo wote nijikwatue”
“Hapa nina laki mbili Haruna”
“Kama huna basi,kuna mtu anaitaka”
“Usinifanyie hivyo,kwani huniamini?”
“Nakuamini lakini hii ni biashara,hii yenyewe nimetoka kupiga tukio”
“Poa ilete nikamuoneshe sista”
Simu iliyokuwa imeibiwa ilikuwa sokoni tayari, inapigwa mnada baada ya siku mbili kupita,ilikuwa ni lazima iuzwe kwa bei ya hasara.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa,Bakari alivyochukua simu akawasha pikipiki mpaka nyumbani kwa dada yake ambaye alikuwa ana shida na simu.
“Sista Simu hii hapa”
Bakari alifikisha simu.
“Ndio shilingi ngapi ulisema?”
“Laki saba,mpyaaa haijatumiwa sana hii, kuna mwanangu mmoja katoka nayo Dubai ana shida na pesa”
Bakari alikuwa mjanja nayeye akataka kupiga winga!Simu ilikuwa inauzwa laki tano.
“Ah Bakari!mimi dada yako ujue”
“Hiyo simu Milioni moja dukani sista,jamaa ana shida kweli na pesa, anauza bei ya hasara”
“Sawa,ngoja basi leo Mme wangu arudi nitamwambia,iache hapa kesho upitie”
“Poa haina noma”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Kitendo cha Mume wake kufika na kumpokea alimuonesha simu iliyokuwa inauzwa.
“Umeitoa wapi?Mbona nzuri sana,ni bei gani?”
“Anataka laki saba”
“Itabidi mimi ndiyo niitumie”
Mumewe aliipenda sana simu,haraka kesho yake ilivyofika akatoa pesa akainunua.
Baada ya kukaa nayo siku mbili na kuipekua kuna kitu kilimshtua kupita kiasi,aliona picha za utupu zikiwa zimepigwa.
Akaziangalia vizuri, sura ya kike aliyoiona ilimshangaza.
“Huyu si Nasra huyu!”
Hakuwa na uhakika sana,ili kuthibisha hilo usiku huo huo,akamtafuta Partson kwa njia ya simu!
“Halloo Partson”
“Mr.Kiluswa shikamoo”
“Marahaba,hujambo?”
“Sijambo,Vipi hali?”
“Safi tu”
“Wapi sasa hivi upo?”
“Naelekea Sinza Mara moja,kwenye tafrija kidogo”
“Sasa kuna picha nataka kukutumia uziangalie”
“Za mpira?”
“No! utaziona”
“Poa tuma nitazicheki”
“Okay”
Picha zikatumwa tatu kwa mpigo.
Partson akawa ana zi 'download' mkono mmoja ukiwa juu ya usukani, mwingine umeshika simu.
Moyo wake ukapiga paa! Kwa nguvu,sura ya Nasra ilimshtua akiwa na Alex wapo watupu wanapigana denda.
Hawakuwa mbali sana na Mwenge na gari la Alex alilitambua,bila kusema chochote akaweka gari kando,akawaacha Sonia na Roger ndani ya gari,kila mtu alimshangaa.
Partson akavuka barabara kwa hasira mpaka kwenye BMW x6,akajaribu kufungua mlango wa gari lakini haukufunguka.
Akagonga kioo cha gari.kwa kama dakika moja nzima mlango ukafunguliwa akamuona Nasra na Alex wapo viti vya mbele.
“Shemeji,vipi hali?”
Alex alianza kutoa salamu lakini alijibiwa na ngumi ya uso!
 Partson alizidi kupandwa na hasira kupitiliza,hakutaka hata kumsikiliza Alex aliyedhani kuwa ni shemeji yake tena alimuheshimu.
Akazidi kumpiga ngumi za usoni huku akiwa nje ya gari kwa dirishani,hali ilikuwa mbaya kwa Alex hata kwa Nasra ambaye tayari alianza kuingiwa na wasiwasi,picha ilionesha kila kitu, katika fikra zake alidhani wenda Partson alikuwa anawaona walichokuwa wanakifanya ndani ya gari.
“Partson Mpenzi punguza hasira”
Nasra alipiga kelele nyingi,akijaribu kumtuliza Partson.Hakukuwa na namna ya kuzuia ugomvi huo,Alex hakuwa na jinsi jambo la kumiliki bastola alilifanya siri kubwa,hakutaka afanye ivyo lakini ilimbidi tu,akili yake ilimtuma aichukue silaha yake,akapapasa chini ya kiti na kuichomoa.
“Embu niachie”
Alex aliongea huku akiwa na bastola mkononi tayari,lilikuwa ni jambo la kutisha mno.Mdomo wa bastola ulikuwa kichwani kwa Partson,hakuwa na jinsi zaidi ya kunywea!
“Nitakufumua ubongo huo,Nawewe Malaya shuka ndani ya gari langu, kabla sijachengua utosi wako”
Kibarua kikageuka kwa Nasra,bastola akaekewa usoni,almanusura akojoe,Alex alikuwa amekasirishwa kupita kiasi.
“Ale...”
“Nimekwambia shuka,Moja...mbili..”
kabla ya namba tatu kumaliziwa Nasra akashuka ndani ya gari akiogopa kufa,alijua nini maana ya namba tatu kumaliziwa, hakutaka umauti umkute,kwa hali aliyokuwa nayo Alex swala hilo lingewezekana kabisa.Alex alivyoona ivyo akalitoa gari kwa kasi ya ajabu.
**
Kila kitu alikiweka wazi kwa Sonia,akamwambia kila kitu kuhusu Nasra na kumuonesha picha zote za utupu alizotumiwa,ilikuwa ni simanzi kwake.
Akakosa raha kabisa, tumaini lake likawa kwa Sonia akawa ndiyo faraja yake.
“Usijali Partson,Mungu atakupa Mke mwema.Wanawake mbona wapo wengi”
Sonia alimpa ushauri siku hiyo jioni wakiwa ndani dukani.
“Nashukuru kwa kila kitu,sidhani kama nitakuja kupenda tena”
“Usiseme ivyo”
“Sasa nisemeje?”
“Mungu yupo”
Siku hiyo waliongea sana,Partson akayaacha mambo kama yalivyo akachukua maneno ya Sonia,akaheshimu ushauri wake.
***
Alikuwa ni msichana mdogo tena ni mzuri kupindukia,ungebahatika kumuona kwa macho ungethubutu kusema kuwa hana kasoro ya aina yoyote ile.Asili yake haikujulikana sababu alikuwa na rangi iliyochanganyika.
Ungeambiwa ni Mwarabu usingebisha pia ungekutana naye usingekataa.
Alikuwa na kila sifa ya kuitwa msichana mrembo.Muda wote alikuwa mitandaoni.Picha yake moja akiipost basi ilikuwa ni lazima ipate 'likes' sio chini ya laki moja,wanaume wengi walikuwa wakimsumbua inbox wakitaka japo namba zake,lakini hawakuambulia kitu chochote.Kitu kilichowavutia watu ni macho yake yaliyofananishwa na taa za benzi.
“ADD CAPTAIN,GOOD NIGHT”
Hiyo ndiyo picha aliyopost Samia siku hiyo usiku akiwa amevaa nguo ya kulalia,hazikupita hata dakika tano zikawa na Comments mia mbili,alisifiwa mpaka na wasichana wenzake.Lakini hata siku moja hakuwahi kuandika ni wapi anaishi,hakutaka jambo hilo lijulikane.
Samia alipenda sana michezo hususani mpira na mchezaji aliyempenda siku zote ni Leone Merci.
Akiwa Tanzania alimfurahia sana Partson Ngogo, katika uchezaji wake wa mpira,mara nyingi alikesha Facebook kumchunguza kijana huyo mcheza mpira aliyetokea kutingisha Tanzania nzima.
“HII”
Siku hiyo alijitosa kuingia kwenye inbox ya Partson Ngogo facebook na kumtumia Meseji,lakini zilipita siku mbili hakujibiwa chochote.
Akaachana nayo.
Alitamani siku moja akutane naye macho kwa macho,hakumpenda lakini alitaka tu japo apige picha na mcheza mpira huyo maarufu aliyemfananisha na Leone Merci uwanjani.
Akajikuta ana hamu sana ya kufungua account nyingine Instagram,akafanya hivyo mara moja.
Akawaalika watu kupitia 'facebook' akafanikiwa kupata followers elfu sita ndani ya masaa machache,kila picha aliyoweka ilitingisha mtandaoni,kila mtu alimsifia kuwa ni mzuri,ilikuwa ni kawaida kwake kumiminiwa sifa, hilo alilizoea.
****
Ndani ya 'inbox' yake kulikuwa kuna meseji sio chini ya elfu saba,kwa umaarufu wa kucheza mpira hilo lilikuwa kawaida kwake,hakuwa na muda wa kufungua meseji zote.Alijibu meseji chache tu za mwanzo,nyingine aliachana nazo.
Partson alikuwa katika mtandao wa 'Facebook' siku hiyo usiku akiperuzi vitu mbalimbali,akaingia kwenye picha za Sonia,akamtizama jinsi alivyokuwa mzuri akamkagua na kuendelea kuangalia picha zake nyingine,bado moyoni alikuwa ana kitu kinachomsumbua,hisia zake zilimsukuma awe na Sonia kimapenzi lakini aliamini swala hilo lisingewezekana hata kidogo,kuwa na Sonia kwake aliamini kwamba ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege,alikuwa tayari kuendelea na maisha yake japo aliumia moyoni.
Nguvu zake akazirudisha mpirani akaachana na Sonia,akajaribu kuupiga moyo wake 'stop' kumuwaza binti huyo.
***
Kesho yake asubuhi aliamkia kwenye mazoezi ya kukimbia ili kukusanya pumzi,zilikuwa zimebaki siku mbili ili mechi ya mwisho ichezwe na wakishindwa ilikuwa Tanzania itolewe katika mchuano.
Hakuna hata mtanzania mmoja aliyeweka matumaini kuwa Tanzania itashinda,nguzo yao waliyoitegemea mpirani ilikuwa imedondoka,wachezaji wote waliyumba tena timu ilifungwa magoli kila siku.
Partson akawa anapewa kipindi cha pili aingie wakamdharau,hakupewa nafasi tena kipindi cha kwanza tangu kiwango chake kishuke.
**
Watu wengi walifurika uwanjani,wengi wao walikuwa raia kutoka nchini Ghana,hiyo ndiyo ilikuwa fainali yao katika mchuano huo na Tanzania.
Washangiliaji kutoka Tanzania walikuwa wachache hawakuwa tayari kuona aibu hiyo,kila mtu aliamini kwamba tayari wametoka katika mchuano.
Kama ilivyokuwa kawaida Partson alipangiwa kipindi cha pili na kocha wake,mpira ulianza,ndani ya dakika kumi na tano Tanzania walifungwa goli moja tayari,hawakukaa sawa wakafungwa la pili.
Baada ya dakika Arobaini na tano filimbi ya mapumziko ikalia.wachezaji wakaenda kupumzika, Tanzania tayari walifungwa magoli mawili kwa sifuri.
Katika mchuano huo msichana mrembo Samia alikuwa akishuudia kila kitu,alikuwa ana hamu kubwa sana ya kumuona Partson macho kwa macho tena waongee na kupiga picha,mita kama nane alikuwa ameketi Sonia,hata yeye alitaka kumuona Partson.
Wala hakukuwa na shangwe kama za siku zote akiingia Partson,hakuwa tegemezi tena, kila mtu alimuona ni mchezaji tu wa kawaida,hata mpira ulivyoanza hakupewa pasi kama alivyozoea kupewa, ilimbidi afanye kazi ya ziada kuusaka mpira kwa timu mpinzani.
Ndani ya dakika mbili mpira ulikuwa mguuni kwake akachomoka kwa kasi na kupiga chenga kwa njonjo,akamtoka mchezaji wa kwanza akakimbia mpaka kwenye chaki,akapiga mikasi na kuuzungusha mpira kiutaalamu akampiga kanzu beki akachomoka mbele mpira ukatua juu ya kichwa chake,kitendo cha kuuweka mguuni kwake aliachia shuti kali, mpira ukachomoka kwa mwendo wa upepo,hakuna hata mtu mmoja aliyeweza kutegemea kuwa kitu kama hicho kitatokea,mpira uligonga mwamba ukazama nyavuni.
Partson hakushangilia aliwatizama wachezaji wa Ghana na kuwapa ishara kuwa bado magoli mengine.

Hasira zilimpanda,alitaka chati yake irudi kwenye mstari,ivyo ndivyo alivyoamini,hata mpira ulivyoanza tena bado aliendelea kuusaka, alivyoupata alikimbilia kwenye chaki pembeni,huko ndipo alipofanya maajabu mengine.
Chenga mbili tatu akasogea mpaka kwa kipa akabaki naye.Akamtisha kama anapiga shuti lakini hakufanya ivyo,alipiga mpira taratibu kwa kumuonesha dharau alimpiga 'goalkeeper' tobo, mpira ukaingia nyavuni kwa mara nyingine.
Hapo ndipo Tanzania iliposhtuka na kuanza kushangilia, Partson alikuwa tayari amesawazisha magoli,kila mtu alianza kumshangilia yeye,alipoweka mpira mguuni kelele za fujo zilisikika,beki mmoja alitaka kumvaa amchezee vibaya akamruka,hilo ndilo liliwafanya watanzania wapige kelele nyingi,lilikuwa ni goli la tatu tena yote alishinda Partson Ngogo mwenyewe.
Hazikupita hata dakika tano mpira ukawa umekwisha tayari.Partson alibebwa juu juu kama Mfalme waandishi wa habari walianza kumgasi!
“Parston,Partson,Partson”
Sonia aliita akiwa katikati ya kundi la watu anawapangua ili akaonane na Partson na kumpa pongezi alitumia nguvu sana mpaka kufika mbele kabisa,akamshika bega.
Partson alivyogeuka tu akamfuata mdomoni na kuanza kumla denda,waandishi wa habari walifanya kazi yao,kitendo hicho kilishuhudiwa na Samia vile vile.
Ilikuwa ni furaha ya ajabu kwa Tanzania mara ya kwanza kuingia kwenye orodha ya kuwania kombe la dunia,ilikuwa ni historia.
***
Kila gazeti lilichapa habari za Partson, picha yake ikiwa juu akiwa na Sonia wanapigana denda,kila gazeti liliandika linavyojua ili mradi tu liuze.Mechi hiyo ilishuhudiwa na matajiri wengi na iliangaliwa na makocha wengi nje ya nchi kila mtu alimtaka Partson Ngogo acheze timu yake.
***
Sonia Shayo alihisi furaha ya ajabu sana kumuona Partson amerudi kwenye chati,akazidi kuwa karibu naye siku hadi siku,mara ghafla wakajikuta wapo ndani ya mapenzi mazito,bila kutegemea.
“Nakupenda Partson”
Hilo ndilo neno alilosema Sonia siku hiyo akiwa kwake Sinza,hakuna kilichofuata hapo zaidi ya kupigana madenda mfululizo,damu za watu hawa zilikuwa zikienda mbio kupita kiasi,kila mtu alikuwa mbali kihisia.
Haraka Partson akatoa shati lake akamvua Sonia,akafakamia Maziwa ya mrembo huyu na kuanza kuyalamba huku na kule.Hapohapo juu ya masofa walikuwa wanashikana na kuvuana nguo zao,wakabaki kama walivyozaliwa.Wakazama kwenye sayari nyingine ya huba,wakafanya mchezo wa ngono.
Mguu mmoja wa Sonia ulikuwa juu ya mkono wa Partson ambaye hakutaka kuamini kuwa yupo na Sonia tena kamvua nguo zake zote,bado alidhani yupo ndotoni,akazidi kupeleka majeshi majeshi.
Hata raundi ya kwanza ilivyoisha wakarudia nyingine,kila mtu alikuwa na hamu na mwenzake.Kutokana na mazoezi ya mpira ilimfanya Partson awe na pumzi nyingi,ivyo mchezo huo kwake haukumpa shida.Nusu saa baadaye wakawa wamelaliana wamejifunika shuka moja.
“Sonia”
“Abee”
“Nakupenda sana”
“Kweli?”
“Ndio,tena sitokuumiza”
“Nafurahi Baby wangu”
Kufumba na kufumbua tayari walikuwa wapenzi.
Sonia alikuwa akimpenda sana Partson kupita maelezo yaliyojitosheleza, muda wote akatamani kuwa naye lakini kazi zilimbana,alikuwa hawezi kukaa kidogo bila ya kupiga simu akimuulizia Partson,penzi la dhati likakuwa siku hadi siku,swala hilo halikuwa siri tena,likawa wazi hata kwenye magazeti,walianika mapenzi yao.
“Upo wapi mpenzi?”
Sonia aliuliza simuni kwa sauti ya kudeka.
“Nipo uwanjani, nataka kuingia mazoezini”
“Sawa baby,nimekumisi”
“Mara hii mpenzi!si tulikuwa wote asubuhi?”
“Naelewa baby,mimi kila ipitapo sekunde nakumisi sana”
“Hata mimi”
“Nakupenda partson,nakupenda sana”
“Mimi pia mamii”
Hayo ndiyo yalikuwa mapenzi yao.
Simu za Partson mara nyingi alipokea Sonia na alionekana mkali endapo akisikia sauti za kike.
“Amepumzika,wewe wa nini?Nimekwambia amepumzika elewa kiswahili,hawezi kuongea sasa hivi,kwahiyo?unaniuliza kwahiyo.Okay labda siku nyingine.Uwe na mchana mwema”
Sonia ndiye alikuwa simuni akiongea,alikuwa ni mwenye wivu mno.
Alichukia msichana yoyote yule aliyeonesha ukaribu na Partson,alimpenda kuliko kitu chochote kile duniani,alimkabidhi moyo wake aufanye vyovyote anavyopenda,kila sehemu alijigamba na kumtaja kwa marafiki zake.
“Sonia twende lunch basi”
“Ngoja nimuombe baby ruksa”
Mashoga zake walishangaa,ilikuwa sio penda ya kawaida.Na haikuwa utani Sonia aliinua simu na kuzungumza na Partson akitaka kuomba ruksa ya kwenda kula,siku zote msichana huyo alideka kwa Partson.
“Mh!Makubwa mwenzangu,mwaka huu tutakoma”
Rafiki yake mmoja alishangazwa na jambo hilo,akaropoka.
**
Wakati hayo yanaendelea msichana Samia aliwaza ni kwa namna gani aweze kuongea na kupiga picha na Partson ili apate 'kick' ghafla akapata wazo,akaingia facebook na kuandika ujumbe mzito wenye maneno mengi ya kimapenzi.ulikuwa ni ujumbe alioamini kwamba ungejibiwa siku hiyohiyo sababu aliona Partson yupo online.
Hakukaa dakika moja meseji ikawa imejibiwa,moyo wake ukadunda kwa nguvu taratibu akaanza kuusoma ujumbe huo.


****
“KWA MUDA MREFU SANA NILIKUWA NIKIKUTAFUTA JAPO NICHAT NAWEWE LAKINI NIKASHINDWA SABABU UKO BIZE,NAPENDA SANA MPIRA NA NINAJIVUNIA KAMA MTANZANIA KUPATA MTU KAMA WEWE.NATAMANI JAPO TUONANE”
Huo ndio ujumbe uliosomeka kutoka kwa Samia.
“WEWE NANI?”
“NAITWA SAMIA”
“NASHUKURU KUKUFAHAMU,ULIKUWA UNATAKAJE?”
Ilikuwa ni tofauti kama alivyotarajia,kompyuta ya Partson alikuwa nayo Sonia na ndiye yeye alikuwa akijibu meseji za Samia,alitaka kumchimba ili ajue kila kitu.
“TUONANE”
“SIWEZI,AHSANTE”
Samia akakatwa maini,akavunjika moyo, meseji aliyopokea ikamuumiza kichwa chake,hakuelewa ni kitu gani akifanye alijisikia vibaya sana.Akafunga kompyuta yake na kujitupa kitandani.Akachukua maji na dawa zake akameza kisha kuanza kuutafuta usingizi.
***
Partson na Sonia walizidi kupeta,kila mtanzania aliufahamu uhusiano wao wakawa maarufu.Uzuri wa Sonia ulizidi kutingisha jiji na kila mtu alimsifu Partson kupata chaguo bora,Watu walidiriki kusema kuwa Partson ndiye anamiliki msichana mrembo kuliko wachezaji wote Tanzania.
Kama kungekuwa na kipimo cha kupima mapenzi basi kingeonesha kuwa Sonia ndiye amekolea kupindukia,alimpenda Partson sio masihala,kila alichokifanya kilitoka moyoni mwake.Kwa jinsi paparazi walivyokuwa wakimgasi dukani kwake akaamua kumuajiri mtu asimamie kila kinachoendelea huku yeye akiwa bega kwa bega na Partson,walitembea wote kila mahali,walizuka kwenye migahawa mbalimbali na mikoa tofauti wakisubiri mechi kubwa tena ya kwanza itakayochezwa Afrika Kusini ndani ya jiji la Capetown.
“Partson Baby,naenda msalani”
“Okay Love”
Sonia akasimama kuelekea msalani,sketi fupi aliyovaa iliwafanya wanaume karibia wote wageuze shingo zao nyuma,walimtizama kwa macho ya matamanio!
“Partson, is that you?”(Partson,ni wewe)
Sauti ya binti mmoja ilimshtua,kabla ya kugeuka na kumuangalia tayari alishikwa bega na simu kutolewa,binti aliyetokea nyuma yake akaanza kupiga picha za 'Selfie' nyinginyingi huku akiweka mapozi tofauti.Partson hakuwa na jinsi akabaki ametulia alielewa fika kuwa ni mmoja wa mashabiki zake wa mpira.
“Siamini jamani,upo hapa leo?Martha atanikoma”
Msichana huyo akazidi kuongea kwa pozi huku akiendelea kupiga picha zisizokuwa na idadi kamili.
Kwa mbali Sonia aliwaona, wivu ukamjaa moyoni, akazidi kutembea kwa kasi mpaka karibu na Partson.
“Hapa vipi?”
Hiko ndicho kitu cha kwanza kuuliza.
“Ameniomba nipige naye picha”
Partson akajibu.
“Kwahiyo ukakubali?”
“Sikuwa na sababu ya kukataa”
“Eti eeh!”
“Ndio mpenzi wangu”
“Sawa”
Hilo ndilo jibu alilotoa Sonia na kuondoka zake,hakuwa tayari kubaki eneo hilo.
“Sonia,Soniiia”
Partson akaita na kusimama akamuendea na kumshika mkono.
“Si ukaendelee kupiga picha”
“Usiwe hivyo mpenzi wangu”
“Niache basi”
“Unataka kwenda wapi?”
“Kwani hapa kwangu?naenda kwangu.Kwa staili hii mimi sitoweza kwa kweli”
“Sonia,njoo tuongee”
“Siwezi,i can't please fanya mambo yako”
“Kisa nini sasa?”
“Basi tu nimeamua”
Sonia alikuwa ni msichana mwenye wivu kupita kiasi,hakutaka kuendelea kubaki eneo hilo tena, akataka kurudi nyumbani akalale,kwa jinsi alivyoweka mkazo wake,hakukuwa na namna nyingine za kuzizuia.Wakaingia ndani ya gari na kuondoka zao.Barabara nzima Sonia alikuwa akitupa lawama zake, aliongea na kulia machozi.
“No Partson,mimi sitoweza.Utakubali vipi upige picha na wasichana,tena anakushika kama vile”
“Sonia,sasa unalia nini?”
“Ina..ina niuma.Mimi nakupenda Partson.Najisikia wivu sana,sio ivyo tu.Juzi juzi hapo kuna msichana kakuandikia barua ya. Map..penzi,mimi naumia.Naumia sana,inaniuma”
“Kupiga nao picha haimaanishi chochote,kumbuka mimi ni nani Mpenzi wangu,inakupaswa uwe mvumilivu tu”
Sonia aliendelea kulia tu tena kwa kwikwi,aliumia sana mtima.Na aliamini kulia ndiyo suluisho peke yake, maumivu aliyohisi hayakuwa na mfano wake.
“Sonia”
“A..beee”
Aliitika kwa kwikwi.
“Usilie,sogea karibu”
Huku akiwa anaendesha gari Partson akawa ana kibarua kizito cha kumbembeleza mpenzi wake,akamfuta machozi na kumwambia maneno matamu.
Akamuimbia na baadhi ya nyimbo,hapo ndipo Sonia akaanza kutabasamu kwa mbali,uzuri wake ukachanua.
“Hujui hata kuimba Baby wangu,una lisauti libayaaaa”
Sonia akatania,wote wakacheka akalala kifuani kwa Partson huku wakizidi kusonga mbele.
****
“Baba Samia,inabidi twende tena Marekani,tukabadili damu”
“Kwani si bado mwezi mmoja?”
“Mwezi si unaisha wiki ijayo, au?”
“Naelewa,kuna mambo bado nafatilia nadhani by Jumamosi tutasafiri.Mwambie na Samia aandae mizigo yake,viza zipo tayari, okay?”
“Ndio Mume wangu”
Ilikuwa ni familia iliyoathirika na virusi vya Ukimwi kwa miaka mingi,isingekuwa pesa yao ya kusafiri nje ya nchi na kubadili damu kila baada ya mwezi mmoja wangeshakuwa wafu tayari.
Sio Baba wala Mama na mtoto wote walikuwa wana maambukizi hayo ya virusi vya ukimwi.Jambo hilo lilifanywa kuwa siri kubwa sana.
Afya zao zilikuwa zimenona na hakuna hata mmoja kati ya majirani zao ama ndugu aliyeweza kuchimbua siri waliyokuwa nayo katika familia hiyo.
Mzee Mfaume Bardar aliweza kuitunza familia yake na kuijali,ndiyo maana haikuwa rahisi kwa mtu yoyote kugundua.Na siku zote alimkanya mke wake pamoja na Mwanaye Samia wasije hata siku moja kuuwa kiumbe kisichokuwa na hatia,kumaanisha kuwa wasiwe na mahusiano yoyote na wanaume.
Baada ya mwezi mmoja walikuwa wapo Marekani,washngton DC.Kila mtu alibadilishiwa damu na wote wakarejea nchini Tanzania afya zao zikiwa imara kabisa.
“Am back now,it was very fun”
Samia ali'post' picha akiwa nchini Marekani mara ya mwisho wanakula chakula cha usiku,kila mwanaume aliishobokea picha hiyo wakimpongeza.Baadhi yao walimfuata inbox na kumtongoza, hawakuelewa kuwa wanakimbilia kifo chao bila kujijua.
“SASA UNATAKA KUNIONA ILI IWEJE?”
“BAC 2,NAKUKUBALI SN HUMU FB HAKUNA MSICHANA MREMBO KM WW,UNAISHI WAPI?”
“NP HAPA HAPA DAR”
“TUONANE BASI P'SE,MIMI NAFNY KAZI BANDARI AU NAOMBA NAMBA ZAKO”
“HPN SIWEZI”
“USIWE IVYO KICHUNA,UJUE MIMI SIWEZI KULALA BILA KUPITIA PAGE YAKO,HIVI WEWE UMESHUSHWA AU UMEZALIWA?MAANA MTOTO KM MALAIKA”
Samia alikuwa akitongozwa mtandaoni,sio kwamba hakutaka kuwa na mwanaume lakini hakutaka kuwa muuaji!na alikaa nao mbali akiogopa dhambi,kwa siku alitongozwa sio chini ya mara ishirini.
Haraka akapata wazo akaingia kwenye 'Search' na kuandika Partson Ngogo Jr,picha ya mcheza mpira maarufu ikaja.
Akaanza kuikagua picha moja baada ya nyingine.Akajaribu kumuangalia 'Online' lakini hakuwepo,akatafakari na kutabasamu akasimama na kutembea mpaka Seblen kwa baba yake.
“Baba,nikuombe kitu!”
Samia akaongea,baba yake akashusha miwani na kumtizama.
“Niombe binti yangu”
“Unakumbuka kipindi kile nilikuomba kitu?”
“Kitu gani?”
“Yule msanii anayeimba na kuitangaza Tanzania kuja kula chakula cha usiku nasisi”
“Ndio nakumbuka”
“Safari hii namuhitaji Partson aje,please Baba”
“Mh mwanangu,kwanini?”
“Basi tu napenda aje hapa”
“Sawa Mwanangu,ngoja niongee na mjomba wako afanye utaratibu”
“Sawa Baba nakupenda sana”
“sawa mwanangu”
“Lakini kitu kimoja Baba”
“Kitu gani?”
“Nataka aje mwenyewe,aje yeye peke yake”
“Sawa”
Kwa pesa za Mzee Mfaume na kujulikana kwake swala hilo lilikuwa ni kama kuweka kikombe cha chai mdomoni.
Samia akazidi kumsumbua baba yake kila kukicha.
***
“Ni wapi?Obey?sasa sehemu gani?Ndio tuliongea juzi naelewa.Mimi nimesahau nina mambo mengi ujue.Wiki ijayo naenda South Afrika ndio.Nikwambie mara ngapi Rama,Mzee Mfaume kwake sipajui nilikwambia...sawa nielekeze”
Partson alihitajika nyumbani kwa Mzee Mfaume akale chakula cha usiku na familia yake,jambo hilo aliliheshimu sana sababu katika orodha ya watu matajiri Tanzania Mzee huyo alikuwepo.Kitu kilichomchanganya akili yake alipewa mualiko peke yake bila ya Sonia.
“Sasa kwanini nisije na Mke wangu,hapo ndipo nashindwa kukuelewa”
“Ndio ivyo,mimi sijui ila anza kujiandaa”
“Okay”

****

Siku hiyo nzima Samia alikesha chumbani kwake akiwa mbele ya kioo,kila nguo aliyojaribu aliona haijamkaa sawasawa mwilini mwake,alikuwa ana nguo nyingi lakini aliipania sana siku hiyo.Mgeni aliyekuwa anafika nyumbani kwao kula chakula cha usiku alikuwa ni muhimu kwake,ilikuwa ni lazima afanye juu chini amuweke karibu.
Ghafla akapata wazo,akatembea mpaka kabatini na kutafuta kigauni chake kifupi.
Akavua nguo, akakijaribu.
“Woow!”
Samia akajikubali mwenyewe,akayaweka maziwa yake vizuri akayapadisha kwa juu huku akizungukazunguka akiikagua shepu yake iliyofanana na kibuyu.
“Nakumbuka hii nguo ilimfanya mpaka waziri mkuu anitongoze,hii hii nitaivaa jioni”
Kama alivyopanga. Jioni ilivyofika alizama bafuni kuoga na kujisugua vizuri,akarudi chumbani akavaa na kujipulizia marashi,akanukia kama jini.Akajiangalia mara ya mwisho kwenye kioo,akaweka dole gumba kumaanisha kuwa katoka bomba!
***
Partson aliingia nyumbani kwa Mzee Mfaume usiku wa saa mbili akisindikizwa na walinzi wa Mzee huyo tajiri,kwa jinsi alivyoueshimu mualiko huo,alivaa suti nyeusi na kunyonga tai iliyomkaa shingoni barabara, akashindwa hata kupumua vizuri.
“Hii tai bwana,ikinizingua naitoa”
Partson aliwaza huku akijaribu kulegeza vifungo vya shingoni vilivyokuwa vinamkaba.Gari aina ya Marcedez Benz 520 ilisimama pembeni ya lango kubwa na walinzi kutoka,wakafungua mlango wa nyuma Partson akashuka,siku hiyo alipokelewa kama Raisi.Akaingia ndani ambapo tayari Mzee Mfaume na familia yake walikuwa seblen wamejiandaa kumpokea.
“Shikamoo Mzee Wangu”
Partson akatoa salamu na kupeana mikono na kila mmoja,alivyofika kwa Samia hali ilikuwa tofauti kwani mkono wake uliendelea kushikiliwa tu.
***
Sio kwamba Sonia alimruhusu Partson kuondoka peke yake kwa moyo mkunjufu,alivyoondoka tu yeye alianza kulia machozi ya uchungu.Alilia kuliko siku nyingine yoyote ile, taa nyekundu ndiyo ilikuwa ikiwaka kichwani kwake, akajua ni lazima Partson atakua ana msaliti na wala sio kitu kingine,wivu ndiyo ulikuwa ukimuongoza.
Alijuta kujiingiza kwenye mapenzi kwa mara nyingine.Kila wakati alikuwa akimpigia Simu Partson akitaka kujua kinachoendelea.
“Kweli baby upo kwa huyo mzee?”
Sonia alihoji Simuni.
“Ndiyo Darling,niamini”
“Ninakuamini lakini moyo wangu mbona bado mgumu”
“Usiwe hivyo Sonia,sasa unadhani mimi nipo wapi sasa hivi?”
“Aya basi,Kuwa makini”
“Usijali,nakupenda sana”
Alishaukabidhi moyo wake wote kwa Partson na alimpenda kweli,hicho ndicho kitu alichokuwa anajilaumu,kupenda mazima!
**
Muda wote jicho la Samia lilikuwa kwa Partson wakati wa kula mezani,ndani ya moyo wake alihisi hali isiyo ya kawaida kabisa,alihisi kumtamani kimapenzi.Lakni moyoni mwake alijitahidi kufanya hilo lisitokee, ikashindikana moyo ukazidi kumsukuma, mapigo yake ya moyo yakazidi kudunda,mcheza mpira maarufu alimchanganya akili yake.
Alivyoona hiyo haitoshi akachukua mguu wake taratibu na kuanza kumkanyaga Partson chini ya meza bila mtu yoyote yule kujua,biashara hiyo ikaendelea, kwa mara ya kwanza Partson alidhani wenda kawaida lakini mambo yalikuwa tofauti kwani mguu wa Samia aliuhisi unapanda mpaka katikati ya miguu yake,kunako!
Kitendo hicho kikazidi kumuumiza kichwa,alikuwa katika majaribu makubwa mno ambayo alistaili kuyashinda,alimuhofia sana Mzee Mfaume na kumuheshimu pia,Mzee Mfaume na Mke wake hawakujua ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea.
“Samahani kidogo naenda chooni”
Hali ilimshinda Partson,kwake yeye ilikuwa kero akaona bora atumie sababu hiyo ili mambo mengine mabaya yasije kutokea.
“Acha nikusindikize”
Samia akadakia.
“Hapana,wacha tu.Nielekeze nitafika”
“Utapotea,twende nikupeleke”
“Partson,mwache huyo Samia akupeleke maana hii nyumba ni kubwa sana”
Kauli hiyo ilitoka kwa Mzee Mfaume, kwa Samia kwake ilikuwa ni kama 'Ahsante Mungu'.Partson akashindwa kukataa,akasimama na kutembea huku nyuma Samia nayeye akasimama.
“Sio huko ni huku juu”
Samia akasema na wote kuanza kupandisha ngazi kuelekea juu gorofani.
“Choo cha huku chini kibovu,kipo kwenye ukarabati inakubidi ukatumie cha huku juu chumbani kwangu”
“Sikia...basi kama ndiyo ivyo”
“Twende bwana”
“Hapana mimi narudi,ahsante sana”
Partson akasema na kutaka kushuka ngazi,Samia akamuwahi na kumzuia bila kufanya lolote akamfuata mdomoni na kumla denda,kwa jinsi alivyoelewa ni wapi wanaume udhaifu wao ulipo, akaupitisha mkono wake mpaka juu ya suruali ya Partson na kuanza kuchua mwiko wake.
Partson akatulia kama mtoto mdogo anayeogeshwa,Samia akazidi kufanya mambo ambayo angekutwa na baba yake Partson angekuwa kwenye matatizo makubwa,kwani huku akiendelea kumla denda aliifungua zipu ya Partson na kuutoa kabisa mwiko nje,akapiga magoti na kuanza kuunyonya.
Hapo ndipo Partson alipoanza kupagawa,akasahau yupo nyumbani kwa watu,akafumba macho yake akibubumia kwa raha.
Hakuna kilichofuata hapo zaidi ya Kumvuta Partson mpaka chumbani akambwaga puu.
Nia ya mchezo huo ilikuwa ni Samia apashwe wasifanye ngono sababu aliijua afya yake vizuri.
Kichwani kwake hakutaka kufanya ngono,Waliendelea kushikana shikana huku na kule mpaka wote wakalegea,hapo ndipo Partson akamvuta Samia kwa nguvu na kupanua miguu yake.
“Partson..No ..onoo Pl..ease.tusi.fanye mape..nzi”
Haikuwa rahisi kusikilizwa hata kidogo,ilikuwa ni lazima wafanye mapenzi.Samia aliendelea kusisitiza jambo hilo lisitokee lakini haikusaidia, Partson alikuwa teyari keshazamisha gunzi lake ndani na wanafanya mapenzi.
“Ahh ahh Mhh”
Samia aliguna na wakati mwingine alikuwa akilia,alimsikitikia Binadamu huyu asiyekuwa na hatia na tegemezi kwa taifa,kila kitu kiliendelea.
Kutokana na waliaga kwenda msalani walifanya mambo harakaharaka,Samia akatoka na kuvaa vizuri.Akapita seblen kisha baadaye Partson alifuata mezani.
“Vipi mbona kama unalia,kila kitu kipo sawa binti yangu?”
Mzee Mfaume alikuwa wa kwanza kuligundua hilo.
“Nipo sawa Da..ad”
“Kweli?”
“Ndio,usijali”
Chakula kiliendelea kuliwa,walivyomaliza walipiga picha za kumbukumbu wakiwa na Partson.Mpaka inafika Saa sita za usiku wakawa wamemaliza kila kitu.
***
“Hapana Partson umebadilika,haukuwa hivyo”
“Siku hizi nimekuwaje?”
“Haupo kama zamani”
“Mbona nipo vilevile tu”
“No baby,umebadilika haukuwa hivyo,siku hizi ratiba zako sizielewi hata kidogo”
“Ki ukweli ratiba zangu zimebadilika,nimebakiza siku chache ili tucheze mechi ndio maana niko bize”
“Hapana,ubize huo usiku tu?alafu simu zangu kuzipokea mpaka upende,Partson.. Real?”
“Baby”
“Nooo,usinishike.Kama hunitaki uniambie tu ili nijue cha kufanya sio unanipotezea muda wangu tu”
“Still nakupenda Sonia,haya yanayotokea ni mambo ya kupita.Ipo siku nitatulia”
Sonia alimlalamikia mpenzi wake,tabia za Partson zilimchosha akashindwa kumuelewa.
Mapenzi aliyokuwa akimpa zamani yote yalihama,hilo ndilo lilimuumiza sana Sonia Mtima.

Japokuwa Partson alisemwa sana abadilike lakini haikusaidia,Sonia akawa haishi kulalamika,kila kitu kilichosemwa kilipita sikio la Partson kulia na kutokea kushoto,tayari alishalewa penzi la Samia,hakuwa na haja tena ya kumpapatikia Sonia wakati alishaijua nguo yake ya ndani akamfanya anavyotaka,hicho ndicho kikampa kiburi.
“Sikia Sonia,usiniburuze buruze kama unavyotaka sawa,mbona unakuwa sio mwelewa?mwanamke gani unakuwa hivyo.Usiwe kama mtoto,nimeshakwambia mimi niko bize wewe unanilazimisha.Kama huwezi kuwa namimi chukua time”
Hakuna siku aliyolia kwa kwikwi Sonia kama siku hyo,katika maisha yake tangu amjue Partson hakuwahi kupewa majibu hayo,ndiyo maana akaumia moyo.
“Part..son unanijibu mimi hivyo?”
“Unaboa wakati mwingine”
“Unanipenda?”
“Ndio nakupenda, hilo sio swali la kuniuliza”
“Sasa mbona unanitesa?”
“Sonia embu achana na hizo habari”
“Siwezi,wakati habari zako ninazo”
“Habari gani?”
“Wewe jua ivyo”
“Acha kusikiliza Propaganda za watu,utakuja kujiumiza bure,mimi nakupenda wewe,amini hivyo.Watu hawapendi kutuona tupo pamoja”
Partson alizidi kujitetea,ukweli ulibaki kuwa tayari alipata msichana mwingine.Hakuelewa kabisa anajiingiza kwenye kifo bila kujijua,moyo wa Sonia uliumia lakini hakuwa na jinsi alivumilia tu,kwa sababu aliamua kumpemda kweli Partson na hilo lilijulikana.

Usiku wa siku hiyo Partson alitakiwa kukutana na Samia,tena kwa mara ya kwanza walihaidiana kulala wote yaani usiku kucha wakifanya ngono,kwake siku hiyo ilikuwa haiyendi.
Hatimaye saa mbili ya usiku ikafika,kama walivyohaidiana,wakutane M&K Hotel iliyokuwa Tegeta kwa ndevu,huko ndipo walipanga kujivinjari.
Kama walivyopanga ndivyo ilivyokuwa, kwani hazikupita hata dakika mbili walikuwa ndani ya chumba kimoja,wanapigana madenda.
Ndani ya Moyo wa Samia kulijaa vitu vingi,bado alisikitika na kujiona ni muuaji,alikuwa akimuuwa binadamu mwenzake,alijihisi mkosaji na aliyestaili moto wa shetani.
“Baby wait,umekuja na Condom?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Samia,baada ya kuandaana vya kutosha.
“Condom ya nini sasa?kwani vipi?Siku ile mbona hatukutumia condom,mimi niko freshi nilipima majuzi,unanichukulia kicheche sana nini”
Partson aliongea akijitetea hakujua kwamba anakingwa na hatari inayomkabili,japokuwa Samia hakuwa na uhakika kama alishampa virusi vya ukimwi,bado aliendelea kusisitiza swala la Condom lakini Partson alilipinga.
Akaendelea kumshika shika na kumnyonya maziwa yake,hapo ndipo Samia alipolegea damu ikazidi kumwenda mbio akatamani afanye tendo hilo mara moja,alishayavulia maji nguo ilikuwa ni lazima ayaoge.
Waliendelea kucheza mchezo huo kitandani wakiiburudisha miili yao,kila mtu akajituma ipasavyo,miguno na mitingishiko ya kitanda ndivyo vilivyochukua nafasi kubwa sana usiku huo.
Samia alilia machozi ya majuto,mbele yake aliona ni jinsi gani atakavyoifanya Tanzania ilie na kusaga meno kwa kumpoteza mtu muhimu ndani ya Taifa,kwa Partson yeye aliendelea kukizungusha kiuno chake.Sawa aliona Samia analia lakini hakujali,alijua ni mambo ya mahaba!
“Baby nime enjoy sana siku ya leo”
Partson alitoa sifa baada ya mechi kuisha,lakini Samia aliendelea kulia machozi ya uchungu.
“Vipi,mbona unalia?”
“Naomba unisamehe Partson”
“Nikusamehe kwa lipi?”
“Nisamehe”
“Kwani umefanya nini?”
Baada ya kusema hayo Samia alianza kumwaga tena machozi mfululizo!


*****
Moyo wake ulimuuma kuuwa mtu asiyekuwa na hatia,alijiona ni mkosefu sana mbele za Mungu na alijua fika moto wa shetani unamuhusu Jehanam!
akamtizama Partson kwa macho yaliyojaa machozi akitaka kumwambia ukweli juu ya ugonjwa wake wa ukimwi aliozaliwa nao lakini moyo wake ukampiga 'stop' asifanye jambo hilo kwani siri yake ingevuja na angekuwa mahala pabaya!
“Baby,unalia nini?”
Partson alizidi kuuliza akakaa kitako vizuri na kumtizama Samia machoni.
“Nakupenda sana Partson,nalia kwasababu naamini ipo siku utanisaliti kisa wewe ni maarufu,wanaume wengi walinitesa kwenye mapenzi. Na..omba usiwe I..vyo tafadhali”
Uwongo alioutumia uliendana na kitu alichokizungumza,ulimgusa mpaka Partson mwenyewe, kama kondoo akasogea karibu na kumvuta Samia karibu na kumbusu juu ya paji lake la uso,hakujua ndani ya moyo wa Samia kuna kitu gani,laiti angelijua angekimbia mbali.Kwa nje Samia alionekana mwenye afya nzuri tena kanawiri lakini ndani alikuwa ni mfu.Kutokana na kutoelewa lolote Partson alianza kumshikashika tena Samia wakazama kwa mara nyingine ndani ya dimbwi la mahaba,wakafanya ngono watakavyo,wakazidi kuoneshana ubavu juu ya kitanda, japokuwa Samia alikuwa mkimnya lakini juu ya kitanda alikuwa gwiji,muda wote alicheza na filimbi ya Partson kisawasawa!Mpaka inafika asubuhi walikuwa hoi bin taaban!
kichupa kilichojaa alichokuwa nacho Samia sasa kiliisha,akawa tayari kashapata mtu wa kufanya naye ngono, kutokana na kukaa miaka mitano bila kuzini.
“Baby,amka twende mimi nachelewa mazoezini”
Partson ndiye alikuwa wa kwanza kuzinduka usingizini,akamtingisha Samia aliyekuwa bado amelala.Wote wakaingia bafuni kuoga na kilichoendelea huko walijua wenyewe.
***
Tabia ya Partson ilianza kubadilika siku hadi siku,alimnyanyasa sana Sonia bila sababu ya msingi,kwasabu tu alimpata msichana mwingine mrembo,akaona Sonia hafai,akawa anamjibu anavyotaka yeye na anapokea simu anapojisikia.
“Mbona unanipigia pigia simu ovyo?mtu asipokupokelea simu jua kwamba yupo bize.Kusoma hujui hata picha huoni,ukiona sipokei simu yako,uwe unachuna basi”
Ilikuwa ni simu iliyopokelewa na Partson baada ya kuita mfululizo,tena alipokea bila salamu akaanza kuporomosha maneno mabaya yasiyostaili kwa mpenzi wake Sonia aliyekuwa muda wote anamtafuta simuni.
“Parston mbon...”
“Nipigie kesho..tititi”
Alimkatisha Sonia na kukata simu,hakutaka kusikiliza tena sauti yake,alichotaka kusikia ni sauti ya mtoto wa kichotara Samia,bila kujua yupo kwenye hatari mbaya kuliko nyingine yoyote ile.
Partson aliendelea kutanua akawa muda wote yupo na Samia lakini kwa siri kubwa sana, ndani ya gari lake alizidi kufanya vioo viwe vyeusi ili watu wanaomfahamu samia wasipeleke unoko kwa Mzee Mfaume.

****
“Unataka nini kwangu?”
“Ah baby”
“Baby nini?toka kwangu Partson”
“Nisikilize nachokwambia sasa”
“Siwezi kukusikiliza,nakuuliza umefuata nini kwangu?”
“Nimekufuata wewe mpenzi wangu”
“Uko ulipotoka?”
“Wapi?”
“Partson,achana na mimi”
“Sonia,bado nakupenda na unajua hilo kabisa,mazoezi ndiyo yalinibana nataka twende wote South Africa,ukaone ninavyocheza mpira,tafadhali mpenzi wangu,twende ukanipe kamshange!”
“Siwezi kwenda,muda wote ulikuwa wapi?hukupatikana mwezi mzima”
“Tulikuwa kambini baby,tunafanya mazoezi ndiyo maana kipindi kile sikutaka kabisa unipigie,huko hatukuruhusiwa kuwa na simu kabisa,ndiyo maana ikawa ivyo lakini siku zote nilikuwa natamani mazoezi yaishe nikuone,alafu kuna kipindi niligombana na kocha nikawa na hasira hasira za ovyo”
Partson alijitetea lakini kila alichokuwa anaongea kilikuwa cha uongo,kusafiri kwa Samia kwenda Marekani kulimfanya ajirudi kwa Sonia,alichoelewa yeye kwamba Samia ameenda Marekani kuwasindikiza wazazi wake,hakuwahi hata kuhisi kuwa ameenda kubadilishiwa damu.
“Partson,nakupenda unajua.Muda wote nilikuwa nikilia kisa wewe,hasira zako ukigombana na watu wako usiniletee mimi,sawa mpenzi wangu!”
Sonia hakuwahi kukubali jambo kirahisi kiasi hicho,ni mapenzi ya dhati aliyonayo moyoni ndiyo yalimfanya awe teja,alimpemda Partson kuliko mwanaume mwingine yoyote yule,hata alivyojaribu kuuliza moyo wake kwanini unampenda Partson hakupata jibu lililomridhisha, vituko vyote akavisahau,akaweka kama ni changamoto katika mapenzi.
“Nilikuwa ndiyo napika pika jikoni baby”
“Unapika nini mpenzi wangu?”
“Wali kuku”
“Wacha wee,twende nikakusaidie”
“Kwenda hapa,unajua lini kupika embu kaa hapo”
Sonia alielewa somo akamfuata Partson mdomoni wakaanza kulana denda akiwa mwenye furaha kupindukia,moyoni alihisi ni mwenye amani akazidi kumpiga mabusu mpenzi wake yasiyokuwa na idadi kamili,hakuamini kama Partson amerudi mikononi mwake,fikra zake zilimtuma kuwa ana kimada kingine lakini akaitupilia mbali roho hiyo,akidai kwamba ni shetani ndiye anataka kuharibu mapenzi yake.
“Baby unajua nini?”
Sonia alisema akiwa ametoka mdomoni kwa Mpenzi wake.
“Nini tena Sonia”
“Nilidhani ushapata kidemu kingine”
“Mh,ah wapi uko peke yako,nimpate wapi wakati nimekufa na kuoza kwako”
“Nakupenda Partson na unajua hilo,siku ukiniacha najiua”
“Naanzaje kukuacha labda, mtoto mzuri kama wewe”
“Vipi mazoezi,umejiandaaje?”
“Si unanijua mimi huwa siongeagi,nikifika tu uwanjani nakuwa kama chizi”
“Umeniandalia magoli mangapi kama zawadi?”
“Hahahaha,umenikumbusha mbali sana”
“Wapi?Shule?”
“Hukohuko”
“Baby,alafu leo utalala hapa eeh”
“Mh”
“Baby please say yes”
“Yes”
Hapohapo Partson alipewa denda la nguvu,wakawa wanabadilishana mate kwa njia ya ndimi.Wote walijisikia amani sana.Sonia akaingia jikoni kuendelea kupika,akafanya juu chini chakula kiwe kitamu kuliko siku zote,akaweka kila kiungo kinachostaili,mchuzi wa kuku ukawa mzito akaweka wali jikoni na kuweka tui la nazi.
Baada ya dakika arobaini alikuwa mezani anaweka vyombo.
Kwa heshima ya penzi akamfuata Partson na kumkaribisha mezani kama mke anavyomfanyia mme wake.Wote wakawa wanakula mezani huku wakipiga stori za hapa na pale.
***
Mguu wa Sonia ulikuwa umekunjwa na kuwekwa begani kwa Partson juu kitandani wakiwa kama walivyozaliwa wanafanya tendo lililowaleta duniani,kila mtu alikuwa akielea kwenye sayari ya huba.
Kutokana na Sonia kuwa na kiu kupita kiasi siku hiyo aliwahi kufika mshindo akahitaji tena penzi la Partson,walikuwa wakifanya ngono nyama kwa nyama bila kutumia mpira,ilikuwa ni hatari kubwa mno.
Ukimwi kwao ulikuwa nje-nje na kwa asilimia tisini na mbili zilikuwa kwamba Partson anatembea na mdudu huyo ndani ya damu yake bila kujijua,Sonia alikuwa katika hatihati ya kuupata ugonjwa huo uliomtesa mama yake mzazi mpaka umauti kumfika,katika maisha yake aliuogopa ugonjwa huo sababu alishawahi kuuona unavyotesa kabla ya kumuondoa binadamu duniani,siku zote alikuwa akijichunga na ndiyo maana hakutaka kumsaliti Partson,alitokea kumuamini kupita kiasi,kwa kumuangalia tu alijua ni mwanaume muaminifu,hapo ndipo alipofanya kosa kubwa.
Aliendelea kukinyonga kiuno chake huku akitoa miguno ya puani,kwa raha alizohisi akajiona kama yupo juu angani anatizama viumbe vyote kwa chini.Walifanya tendo hilo la ndoa mpaka kunakucha, asubuhi saa kumi na mbili ndipo walipata usingizi,wakalala na kuamka saa kumi ya Jioni.
Tena wa kwanza kuamka alikuwa ni Partson akachukuwa simu yake kubwa,cha kwanza kukifanya ni kuingia facebook,akazama kwenye picha za Samia,akaona tayari amepost picha aka 'like' na kuingia Inbox ambapo alikuta ujumbe wake.
“BABY NIMEFIKA TAYARI SASA HIVI TUPO WASHINGTON DC NA MY FAMILY,BAADA YA SIKU NNE NITARUDI LAKINI SITOFIKA TANZANIA,NATAKA NISHUHUDIE MECHI UTAKAYO CHEZA SOUTH AFRICA,NAKUPENDA BABY”
Partson alivyotaka kujibu akashindwa sababu Sonia alikuwa akijigeuza,haraka akaweka simu pembeni na kumuwekea mkono kiunoni,Wakalala tena.
***
Maisha kwake yalikuwa yaku tangatanga siku zote akiwa kama Mjane,elimu aliyoipata haikumsaidia chochote kwani alizunguka na vyeti vyake karibia kila ofisi lakini hakuambulia kupata kazi zaidi tu aliombwa rushwa ya ngono na mabosi waliokuwa na tabia za kishenzi!
Mwili wake aliupa thamani aliona bora afe maskini na mwanaye kuliko kupanua miguu yake na kutoa rushwa ya ngono!

Pendo Jonas aliteseka na mwanaye Brenda maisha yake yakawa ya kuunga unga tangu Nickson afariki,msaada kwake alikuwa ni Tito,alikaa nyumbani kwake hivyohivyo kwa vibarua vya kuunga unga huku Brenda akiwa anasoma darasa la saba tayari.
“Tito,niliomba kazi wiki iliyopita Arusha naona wamenijibu hapa,embu njoo mara moja uone”
“Sawa,ngoja nije”
Tito pamoja na Mke wake waliishi na Pendo Jonas kama ndugu yao,waliamini kwamba leo yeye kesho kwao,hivyo waliamua kutoa msaada bega kwa bega na Tito ndiye alikuwa akimsomesha Brenda mtoto wa marehemu rafiki yake Nickson, ambaye hakutambulika kifamilia.
Yeye akamchukua mtoto huyo kama kumbukumbu kwake.Uzuri wa Brenda ulichipua akiwa yu mdogo,uso wake mwembamba ulifanana na watu wa Rwanda,pua yake ilichongoka kama ya kitusi.Mdomo alichukuwa kwa Mama yake ukazidi kuwa na lips nzuri za kuwaka,bado alikuwa mtoto mdogo lakini alipata nyonga iliyojichonga kama nyuki na nyuma kukasambaa na kumfanya awe na nyama pembeni ya hips akatengeneza shepu kama kibuyu,uzuri wake ulitisha na haukuwa mwepesi kuelezeka.
Alimpenda sana Mama yake na alijituma sana darasani ili Mama yake afurahi,katika maisha yake hakuwahi kubahatika kuita baba.Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya mtoto huyu Brenda.
“Hapa hawa wanasema Deadline ni wiki ijayo,duu alafu mbali huko ni Serengeti inabidi ujipange best”
“Kweli,ndiyo nimeona hapa.Wamenitumia Email,Tito niombee Mungu nipate hiyo kazi”
“Utapata tuu,Mungu ni mwema”
“Kweli Tito?ujue sikudhani kama una roho ya ukarimu kiasi hiki Tito”
“Nimekuonea sana huruma,tuachane na hayo.Hii Dunia unajua ni Duara,inazunguka siku zote tuishi kwa kusaidiana licha ya yote mimi nawewe tumetoka mbali sana”
“Nashukuru Tito,sina chochote cha kukupa lakini Mungu atakulipa,sasa si inabidi niende na mtoto”
“No no no no,Brenda atabaki hapahapa wewe nenda tu mambo yakiwa sawa,atakuja.Inabidi uende ukaweke vitu huko viwe kwenye mstari”
Ulikuwa ni ushauri kutoka kwa Tito,habari hizo zilipomfikia Mke wake alizipokea kwa mikono miwili wote wakamtakia mafanikio mema.

Siku ya siku ilipofika wakamsindikiza Ubungo na kumpandisha basi la Arusha huku nyuma akimuacha Brenda nyumbani kwa Tito,kila lililotokea katika maisha yake alidhani ni ndoto tu.
Mkurugenzi msaidizi wa Hotel iliyokuwa Serengeti aliyeitwa Eveline Said alikuwa tayari anamsubiri Pendo Jonas stendi.
Hotel aliyotakiwa kwenda kufanya kazi ilikuwa ni kubwa na ya kitalii.Wazungu waliofika mbuga ya Serengeti walifika kwenye hotel hiyo.Pendo Jonas alikuwa taaban kwa safari.
Alikuwa njiani masaa karibia nane na jinsi basi lilivyoharibika njiani ndiyo akachoka zaidi,kutokana na shida aliyokuwa nayo ilibidi tu ajikaze.
Eveline Said akampokea wakanyoosha mpaka hotelini ambapo kabla ya yote aliingia bafuni na kujimwagia maji.
Kama ratiba ilivyopangwa asubuhi yake akaitwa ndani ya chumba kikubwa kwa ajili ya 'Interview'kiingereza alichokua akiongea kiliwashangaza watu wote,Pendo aliongea ung'eng'e kama hakuwahi kuishi bongo!hiyo ilimfanya azoe pointi nyingi.
Hakukuwa na haja nyingine zaidi ya kuajiriwa ndani ya hotel hiyo akiwa kama muhudumu,akafanya kazi kwa bidii,kila mtalii aliyepewa huduma yake alifurahi sana.
Katika watalii waliopenda huduma ya Pendo Jonas ni Santiago raia wa Marekani,ilikuwa ni kama mara yake ya sita kufika Tanzania ndani ya mbuga ya Serengeti kutalii,matamshi ya Pendo na ukarimu wake ulimvutia mzee huyu.
“No,not you i need the other one,chocolate colour, she is kind tall"(Hapana,sio wewe,namuhitaji mwingine mwenye rangi ya chocolate,ni mrefu kiasi)
Santiago alijaribu kumuelekeza muhudumu aliyefika kwenye meza yake kuwa alimuhitaji Pendo.Hilo lilijulikana na alivyofika kama kawaida alimchangamkia mteja.
“Yes sir.What would you prefer?”(Unahitaji huduma gani)
Pendo alizungumza huku akiachia tabasamu pana na kumtizama mtalii huyo.
“I'm speechless Madam,i want to talk to your boss”(Nimeishiwa pozi,nahitaji kuongea na tajiri yako)
Pendo Jonas alitetemeka kupita kiasi,hakuelewa ni kosa gani amelifanya alijua tayari Mzungu anaenda kutoa unoko kwa bosi wake,aliganda kama barafu akatembea mpaka kaunta na kumkuta mkurugenzi anataka kuingia ndani ya gari lake.
“Bosi”
Pendo akaita kwa adabu.
“Sema Pendo”
“Kuna mtu anahitaji kukuona”
“Nani?”
“Yuko pale,ni mtalii”
“Sawa”
Vincent Towo mkurugenzi wa Hotel hiyo akatembea mpaka kwa Mtalii na kusimama mbele yake.
****
Mkurugenzi wa Hotel ya kitalii alifika mbele ya Mzee Santiago ili kumsikiliza.Baada ya kusalimiana Mzee Santiago hakutaka kupoteza muda wake alimueleza Mkurugenzi jinsi gani mfanyakazi wake alivyokuwa ana adabu na unyenyekevu wa hali ya juu,akam-mwagia sifa kedekede na mwisho akahitimisha kuwa anamuhitaji Pendo angalau kwa siku moja.
“Kwani ulishaongea naye?”
Mkurugenzi Vincent Towo aliuliza,kusifiwa kwa Pendo Jonas hakukumshtua kwa sababu haikuwa mara yake ya kwanza kupokea sifa hizo.
“Hapana sijaongea naye,nimeona bora nikuombe wewe ruksa,ukikubali mimi nitazungumza naye”
“Mimi ndiyo bosi wake,alafu vilevile ni mdhamini.Endapo likimpata jambo baya mimi nitawajibika,utanihakikishia vipi usalama wake?”
“Unahitaji nini kutoka kwangu?”
“Passport yako”
“Hilo halina shida,labda kama una lingine”
“Hakuna shida,basi subiri usiku akiwa Off mtaongea, sasa hivi yupo kazini”
“Nitasubiri,Ahsante kwa kunielewa”
Hatua ya kwanza alikuwa keshaimaliza,lilibaki swala moja la kuzungumza na Pendo Jonas.
**
Uzuri wa Pendo ulizidi kuwaka,angewekwa Madam Wema Sepetu pembeni yake usingebisha ungeambiwa kuwa ni mapacha,walifanana kwa kila kitu,senti mbili tatu alizokuwa anazipata nyingine alituma nyumbani kwa ajili ya mwanaye na nyingine vipodozi mbalimbali,ngozi yake ilikuwa laini, viyoyozi na hali ya ubaridi wa mkoa huo ulimfanya azidi kuonekana maridadi.

Aliendelea kufanya kazi kwa hofu sana akielewa ana makosa na muda wowote atafukuzwa kazi sababu Vincent Towo hakuwa bosi mwenye mchezo mchezo,atacheka nawewe lakini kwenye maswala ya kazi hanaga masihala na ndiyo maana alitandwa na hofu ya kufukuzwa kazi,akakosa raha kabisa.
“Pendo njoo Mara moja ofisini kwangu”
Jioni ilipofika bosi wake akamuita ofisini,kijasho chembamba kilianza kumtoka,akajikagua vizuri na kushusha pumzi akachomekea shati lake ndani ya sketi na kuanza kutembea mpaka ndani, ofisini kwa bosi wake.
“Ingia Pendo”
“Ahsante bosi”
“Kaa chini”
“Ahsante”
“Unaona hiii?”
Vincent Towo aliuliza huku akiwa na hati ya kusafiria yaani passport.
Pendo hakujibu sababu hakujua maana yake.
“Ndio nimeiona bosi”
“Hii ni passport ya yule Mtalii uliyekuwa unaongea naye leo mchana,kesho una frii sasa ameniomba awe nawewe,nimechukuwa passport yake kama dhamana”
“Ameniambia kuwa anahitaji kuwa namimi?”
“Ndio ana mazungumzo nawewe,chochote atakachokifanya kibaya usisite kuniambia”
“Sawa bosi”
“unaweza ukaenda”
Pendo Jonas akasimama na kuuendea mlango.
“Pendo”
Bosi wake alimuita kabla ya kuufungua mlango,Pendo Jonas akageuka.
“Kuwa makini”
“Sawa bosi”
***
Mzee Santiago alifiwa na familia yake mnamo mwaka 1980, mke na watoto wake wawili Celine na Brandon walifariki baada ya bomu kutegwa katika uwanja wa kimataifa Switzealand,wakisafiri kuelekea Brazil,maisha yao yaliishia hapohapo kwenye mlipuko.
Alichanganyikiwa kwa kiasi cha kutosha, lilikuwa ni pigo kubwa sana kwake.
Hakutaka kuoa tena japokuwa marafiki zake walimshauri aoe mwanamke mwingine ili atoe mawazo lakini hakutaka, akaamini kwamba hakuna mwanamke yoyote atakayeweza kuziba pengo la Marehemu mke wake.
Ili kutoa mawazo akaamua kustaaf kazi ili azunguke nchi mbalimbali za Afrika kama Uganda,Kenya,Tanzania,Demokrasia ya kongo akiwa kama mtalii.
Kitendo cha kutua Tanzania kwa mara ya kwanza na kwenda kutembelea Serengeti alikutana na mrembo Pendo Jonas,akamuhudumia vizuri kesho yake akasafiri kwenda Uganda kisha Kenya akarudi tena Tanzania.
Alivutiwa sana na huduma ya msichana Pendo Jonas,lugha ya ukarimu na tabasamu lake vikamkonga moyo wake,akahisi kuna kitu ndani ya kichwa cha Pendo Jonas.
Ndiyo maana akamuombea ruksa ili wakakae sehemu nzuri waongee.Alivyomueleza Pendo hakuwa na kipingamizi.Akavaa nguo za kawaida ambazo alizidi kuonekana vizuri,umbo lake likajikata vizuri akazidi kumpagawisha mzungu huyu.
“You look like an angel”(Unafanana na malaika)
Mzee Santiago alitoa sifa zake,pendo akaishia kutabasamu wakaingia ndani ya basi la kitalii na kuanza kuzunguka,wakafika sehemu na kukodi gari lingine dogo ambalo litakalo wazungusha sehemu tofauti tofauti ili kuangalia wanyama.

Siku hiyo nzima walitumia kujuana kila mtu akatoa historia yake kwa kifupi.Siku zikasogea mbele kila Pendo alipopata muda basi hukaa na Mzee Santiago ili kupiga stori, baada ya siku chache walijikuta wapo katika mapenzi mazito.
“Will you marry me?”
Hilo ndilo swali alilouliza Mzee Santiago baada ya kutoka kunyonyana midomo,hakuwa mzee wa longolomgo alitaka mke wa kumfariji na kumletea furaha maishani, alichoka kuwa mpweke.
“Oh My God!”(Mungu wangu)
“Will you Marry Me Pendo?”(Utakubali nikuoe Pendo)
“Ofcourse yes!”(Ndio)
“Sure!?”(Hakika)
Pendo alimtizama Mzee Santiago machoni akaionekana ana kitu anataka kumueleza,hakutegemea kama mambo yangeenda kiundani kiasi hicho,ilibidi amwambie ukweli uliojificha kuwa ana mtoto anaitwa Brenda!
“Mimi sijali kama una mtoto,nishakupenda wewe.Atakuwa ni mtoto wetu.Tutaondoka naye,tufanye mipango ya ndoa twende Marekani mpenzi wangu”
Pendo Jonas alifurahi kupita kiasi,kwa mara ya kwanza alidhani mzee huyo ni tapeli na lengo lake lilikuwa kumtapeli,hakuamini kama anaenda Marekani.Taarifa hizo akampa Tito, haraka mikakati ya ndoa ikafanyika.Baada ya miezi miwili ndoa ilifungwa na ilihudhuriwa na watu wasiozidi hamsini,ilikuwa ni ndoa ya kizungu.
Mzee Santiago hakutaka kupoteza wakati,haraka Pendo akatengenezewa Passpot pamoja na Viza.Kama utani vile, siku hiyo alikuwa ndani ya ndege na mwanaye Brenda wanaelekea nchini Marekani kuanza maisha mapya ya ndoa.
***
“Mr.Santiago karibu tena Marekani”
“Ahsante rafiki yangu,naona umekuja na familia”
“Nimechoka kuishi mpweke bwana”
“Nimeona una kifaa sio mchezo,sawa basi.Twende kidogo tukale chakula jamani”
Mzee Aidan Waytte ndiye aliyempokea rafiki yake kipenzi Santiago,urafiki wao ulikuwa wa kufa na kuzikana na walishirikiana katika mipango mbalimbali ya kibiashara na katika watu waliomshauri Santiago atafute mwanamke mwinginge ni mzee huyu tajiri, Waytte.
“Huyu Sebastian naye sijui kaenda wapi na gari”
Mzee Waytte alikasirika baada ya kufika kwenye maegesho ya magari na kutoliona gari lake.
Ghafla gari la kitajiri aina ya Escelard ikapiga msele miguuni mwake,Mzee Waytte akaruka pembeni almanusura adondoke.
“Stupid Sebastian, are you out of your mind!”
“Sorry Dad,i was trying to drift like Jason,get in”
Sebastian aliongea akiwa anacheka,akamtizama baba yake aliyekuwa anaendelea kuongea kwa jazba.
“Sasa unataka nani aweke mizigo ndani ya gari?mbona unakuwa huna adabu na ndiyo maana nilitaka kumpigia dereva wangu anilete,hizo bangi unazovuta sijui za wapi”
“Ah dingi,taratibu basi si kwanza naangalia ustaarabu,basi subiri nashuka”
Sebastian akashuka na kumpokea Mzee Santiago pamoja na Pendo Jonas mizigo,akaiweka ndani ya gari kisha baada ya hapo wakaanza salamu.
****
Sonia na Partson Ngogo waliingia jijini Johernsberg saa kumi na mbili ya jioni, baridi lilikuwa kali kiasi kutokana na mvua za hapa na pale kunyesha,zilikuwa zimebaki siku nne tu ili mechi hiyo ianze.
Kwa mara ya kwanza Tanzania walikuwa wameingia katika shindano kubwa lililozungumziwa karibia dunia nzima,karibia robo tatu ya dunia walikuwa wamefika nchini Afrika kusini.
Hotel zilijaa na wageni wengine walikosa vyumba,siku hizo mbili tatu machangudoa walipata soko, walinunuliwa na kugombaniwa kama mpira wa kona,saa saba za usiku hakukuwa na changudoa yoyote, wote walikuwa wamenunuliwa na kwa sababu hiyo na wao wakapanda bei.
“200 Dollar per shot”(Dolla 200 mzunguko mmoja)
“Why?its expensive”(Kwanini?,ni ghali)
“150?”
“ I said 200 us dollar.That is my last price you don't want, just go”(Nimesema dolla 200,hiyo ndiyo bei ya mwisho,hutaki nenda)
Biashara ya uchangudoa ilikuwa ikiendelea ndani ya jiji la Cape town,madada poa waligombaniwa na walitajirika kwa muda mfupi tu baada ya wageni kutoka katika nchi mbali mbali tofauti za kigeni kuingia ndani ya nchi hiyo ili kushuhudia mchuano wa kombe la dunia.
Mambo hayo yalimshangaza sana Sonia akiwa ndani ya Taxi na Partson wametoka club wanaenda kulala.
“Hivi kwanini wanawake wanajiuza kiasi hichi?yule si mtoto mdogo kabisa?”
Sonia aliuliza,msichana mdogo alikuwa ukutani amevaa kimini amesimama anavuta sigara akisubiri mteja,jambo hilo alilichukia mno.
“Maisha Sonia,maisha ni magumu”
“Sasa hawaogopi Ukimwi.Huo ni ugonjwa hatari sana.Nina uogopa kama nini”
“Ni kweli lakini sasa inatokana na hali ya maisha duni.Wanajikuta wanaingia humo.Kuna wengine hiyo kama ajira kwao,wameajiriwa hapo wana mabosi wao”
“Mimi sijui naonaje kuona mwanamke anajiuza”
Sonia alihofia ugonjwa wa Ukimwi,aliwasikitikia sana wasichana wenzake wanaojiuza.
***
Siku hiyo ilisubiriwa kwa hamu kubwa sana,uwanja wa Taifa ulifurika watu.Baadhi ya watanzania walikopa pesa ili kufika Afrika kusini ili kushuhudia mechi hiyo.Sonia alikuwa amekaa V.I.P amevaa jezi iliyoandikwa Partson Ngogo jr nyuma ya mgongo wake,kajichora rangi iliyoashiria bendera ya Tanzania usoni,anashangilia kuliko mtu yoyote yule.
Tanzania kwa mara ya kwanza walikuwa wanacheza na Jamaica,uwanja mzima zilisikika ngoma za 'palanawe' Wajamaica walikuwa wanashangilia na kupiga ngoma za mila zao.
Kama alivyohaidi Samia nayeye alikuwepo ndani ya uwanja huo baada ya kutoka nchini Marekani kubadilisha damu iliyokuwa na virusi vya ukimwi,macho yake yote yalikuwa uwanjani,anataka
kumshuhudia Partson,aliwatizama watanzania wote kwa ujumla na kuwasikitikia,alijua ni kiasi gani watakuwa katika pigo kubwa baada ya mchezaji huyo kufa miaka michache itakayofuata,alijiona ni mkosaji mbele za Mungu.Akavuta picha jinsi gani watanzania watavyolia na kusaga meno!
“Buuuuuu buuuuuuuuuu buuuuuuuu”
watu walimzomea Partson,tena upande wa watu waliokuwa wamekaa wajamaica wanamesuka Rasta wanapiga ngoma,Partson akakosa ujasiri na kujikuta anajikwaa mwenyewe na kudondoka.
Mpira ukachukuliwa kwake na hapo likatokea goli la kwanza.
Tanzania waliwekwa goli moja,ngoma zikazidi kusikika.Hawakukata tamaa,mpira ukawekwa kati,hazikupita hata dakika kumi,ikatokea kona.Nsajigwa akaweka mpira ili achonge kona.Akapiga mpira,kama Mungu ukaingia kati,Partson akaruka kama masai mwenye mori akaupiga mpira kichwa,nyavu zikacheza.
Hakuna hata mmoja aliyeelewa mpira umeingiaje nyavuni,Tanzania wakawa wamesawazisha.

Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha mpira ulikuwa mgumu,Tanzania moja na Jamaica Moja.
“Sasa hivi ni mwendo wa Barcelona,sio mbaya tukitoa droo,Mshana utapanda mbele kumsaidia Partson na Nsajigwa,wewe Kiko utashuka chini na kukaa beki,msiogope.Partson usiogope kuzomewa maana nimekuona ume loose confidence,weka masikio pamba hawa washachanganyikiwa”
Maneno ya kocha Msafiri yakawapa moyo,wakaingia uwanjani.
Mpira wao ulikuwa wa kupigiana pasi mara wapande mara washuke.
Mpaka dakika ya themanini na nane bado walikuwa vilevile.
Partson alivyoangalia muda alikuta zimebaki dakika mbili ili mpira uishe,akataka kujaribu kufanya maajabu ndani ya dakika za mwisho.
“Nsajigwa,Nsajigwa”
Partson aliomba pasi,ikapigwa 'chop' juu kwa juu Partson akautuliza mpira,akachomoka kama risasi,akapiga mikasi akamtoka beki wa kwanza, wa pili akampiga tobo na kumzunguka akatokea nyuma yake na kutembea na mpira,akabaki yeye na kipa,kwa hasira alizokuwa nazo akaachia shuti kali lililojaa hasira,ilikuwa kidogo nyavu ichanike.
“Goooooooooooooooo,pyeeee pyeeee pyeeeeee”
Kitendo cha mpira kuzama nyavuni,hapo hapo filimbi ikapigwa mpira ukawa umeisha.Partson akafunga goli la dhahabu, lililoanza kurudiwa juu ya kioo kikubwa.
Watanzania walishangilia na kulia kwa furaha kupita kiasi.
***
Samia na Partson walikuwa katikati ya bustani kubwa,wanapigana madenda yasiyokuwa na idadi.Walifanya ivyo kwa kujiachia bila kujali watu wanaopita.
“Baby I miss yo...”
Samia alikatishwa na madenda aliyokuwa anapigwa mfululizo,akapiga magoti na kufungua zipu ya Partson,wakasogea mpaka kwenye kona iliyojificha ambapo kulikuwa kuna giza totoro.
Samia akawa ana kibarua cha kunyonya karoti ya Partson akiwa ameibugia mdomoni, akahisi kuna mtu amesimama nyuma yake lakini hakutaka kuyapa nafasi mawazo hayo kwamba sehemu kama hiyo kutakuwa na mtu anayeweza kufika.Ni kweli mawazo yake yalikuwa sahihi sababu hata Partson akiwa sayari ya mbali anahisi utamu unakuja,alihisi sauti ya mtu analia kwa kwikwi.
“Sa..mia na..ku..penda sa..na”
Partson alisema akiwa kwa mbali anahisi raha za ajabu huku mkono wake ukiwa juu ya nywele za Samia anamkandamizia kwenye karoti yake,bado sauti ya mtu anayelia aliendelea kuisikia.
Akajilazimisha kufumbua macho yake,hakuamini mtu aliyemuona mbele yake, analia machozi ya uchungu!

*****
Kelele zilikuwa nyingi uwanjani,watu wengi walimsonga Partson mpira ulipoisha, waandishi wa habari maarufu kama Millad Ayo alikuwepo akitaka kumuhoji Partson juu ya mechi,lakini cha ajabu hakupata nafasi kutokana na msongamano wa watu kuwepo nje ya lango la uwanja.
Wajamaika walikuwa wamefungwa na Tanzania tayari, jambo ambalo hawakulitegemea hata kidogo,ulikuwa ni kama muujiza.
Sonia alikuwa nyuma nyuma anajitahidi kupambana na watu akiwapiga vikumbo ili amfuate Partson mbele lakini akashindwa.
Akamshuhudia anapanda ndani ya basi la wachezaji na kuondoka zake.Nayeye hakutaka kupoteza na kumkosa ili washerekehe furaha yao pamoja.Alivyotizama nyuma akaona taxi nyingi zimepangana.
“Unaweza kulifuata hilo basi?”
Sonia bila salamu akauliza baada ya kuingia ndani ya taxi viti vya nyuma,alionekana mwenye haraka mno.
“Hilo la wachezaji?”
“Ndio kaka,fanya haraka”
“Sawa”
Dereva akakanyaga mafuta wakaanza kulifuatilia basi lililobeba wachezaji.
“Angalia lisitupotee”
“Usihofu”
Dereva taxi alikuwa na kibarua cha kufatilia basi nyuma nyuma.Wakasimama kwenye foleni ambapo basi la wachezaji lilikuwa mbele yao, magari matano.
Sonia alivyotaka kushuka taa zikaruhu,ilibidi aghaili na kurudi ndani ya taxi.
“Dada,embu naomba pesa yangu kwanza”
“Unahisi nitakudhulumu?”
“Hapana,sababu naona hapo ulitaka kushuka”
Ilibidi Sonia aingize mkono wake mfukoni na kutoa dola mia moja,dereva akarizika akazidi kulifuatilia basi alilokuwa amepanda Partson ambalo pia lilibeba wachezaji wa Tanzania.
Moyo wake wakati wote ulikuwa ukidunda kama kitenesi.
Akashuhudia linapaki pembeni ya hotel kubwa na wachezaji wote wakashuka akiwemo Mpenzi wake Partson Ngogo,akaruka kutoka ndani ya taxi kama chura.
Akatembea mpaka mapokezi.
“Dada samahani”
Sonia akaanza kumsalimia dada wa mapokezi aliyemkuta.
“Bila samahani,nikusaidie nini?”
“Nilikuwa nina shida ya kuonana na mtu mmoja anaitwa Partson ni miongoni mwa wachezaji walioingia humu ndani”
“Jina lake nani umesema?”
“Partson Ngogo”
“Okay subiri kidogo”
Dada wa mapokezi akainua mkonga wa simu na kubonyeza namba Fulani.
“Unaongea na mtu wa mapokezi hapa,kuna mtu anaitwa Partson huko?”
Dada wa mapokezi alivyokuwa akiuliza Sonia alikuwa makini juu ya sofa anayafuatilia maongezi.
Lakini hakuweza kusikia upande wa pili wa simu unazungumza nini.
“Ndio yupo,lakini anaongea na simu”
“Akikata mwambie kuna mgeni wake hapa ashuke chini mara moja”
“Sawa nitamwambia”
“Okay”
Kabla ya msichana wa mapokezi kuweka mkonga wa simu,Sonia akamfuata hapohapo kwa kasi ya umeme.
“Ulimpata?”
“Hapana,lakini atakuja sasa hivi”
“Sawa”
Sonia akarudi kitini na kuketi akasubiri kwa hamu, macho yake yakawa kwenye ngazi na kwenye lifti akimtizama kila mtu anayetoka na kuingia,bado alikuwa ana kihoro cha kumuona kipenzi chake.
Muda ulizidi kukatika hakumuona Partson,usiku ukazidi kuingia.
Uvumilivu ukamshinda,akasimama na kwenda tena mapokezi.
“Dada vipi?”
“Bado hajafika kwani?”
“Ndio”
“Ngoja nimpig…”
Kabla ya Msichana wa mapokezi kumalizia maneno aliyotaka kuongea,akatokea msichana mweupe kama chotara kwa mikogo.
“Dada samahani,nimeambiwa niingie chumba namba 102 kwa Partson,naweza nikaenda?”
“Jina lako nani?”
“Samia”
“Sawa,subiri kidogo”
Msichana wa mapokezi akafanya kama mara ya kwanza,akapiga simu gorofani.
Moja kwa moja akampata Partson kwenye laini.
“Umesema jina lake nani?”
Partson akauliza upande wa pili wa simu,kwa jinsi msichana wa mapokezi alivyokuwa karibu na Sonia aliweza kumsikia.
“Eti dada jina lako nani?”
Dada wa mapokezi akamgeukia mteja wake na kumuuliza.
“Samia”
“Mwambie apite”
“Sawa”
Mkonga wa simu ukawekwa mezani,Samia akapewa ruksa.Kitendo hicho kikamshangaza sana Sonia akashindwa kuelewa jambo lililotokea,akamwangalia msichana huyo mpaka anaingia ndani ya lifti kwa madaha.
“Dada samahani,bado hujampata?”
Sonia akauliza tena kwa sauti ya kinyonge.
“Ulikuwa unamuulizia nani tena?”
“Partson Ngogo”
“Huyu dada mbona kaenda hukohuko!”
“Kwahiyo namimi niende?”
“Hapana,inabidi nimpigie simu”
“Sawa,mpigie basi mwambie kuwa nachelewa hapa,namsubiri mwambie Sonia anakusubiri”
Dada wa mapokezi ndiyo ilikuwa kazi yake wala hakuchoka,akainua mkonga na kupiga tena simu,jinsi alivyojibiwa na Partson,akabaki kinywa wazi.
“Mwambie sihitaji kuonana naye”
Hapohapo simu ikakatwa,dada wa mapokezi akamtizama msichana huyu mrembo ambaye bado alikuwa na rangi ya bendera ya Tanzania usoni, amechoka bado hajaoga.
“Dada,samahani Partson amesema uje kesho, sasa hivi amepumzika kidogo”
Dada wa mapokezi alijaribu kupunguza ukali wa maneno,kwa jinsi picha alivyoiona alianza kuhisi kitu kisichokuwa cha kawaida.
“Naweza kuongea naye kwenye simu?”
“Hapana,labda kama una namba zake una weza kumpigia namba zake binafsi”
“Ahsante dada angu”
Moyo wa Sonia,uliumia kupita kiasi.Hakuelewa ni kitu gani akifanye lakini alihisi kuna jambo limetokea tena baya,hivyo ndivyo moyo wake ulimtuma na kumwambia.

Licha ya yote hakutaka kubanduka eneo la hotel hiyo,akatoka nje huku machozi yakimlenga,akaenda kukaa mwenyewe nje kwenye bustani akiwa analia machozi,alijihisi kujuta sana kuingia katika mahusiano ya kimapenzi.
Baridi lililokuwepo nje halikuwa la kawaida lakini alijikaza.Hazikupita hata dakika arobaini akahisi vicheko vya watu,sauti ya kike na ya kiume, haikuwa rahisi kwa mtu yoyote kumuona sababu alikuwa amekaa chini ya kiti ambacho chini kina mti mkubwa.
Hakuamini macho yake mtu aliyemuona,kwa kutaka kushuhudia akasimama ili apate uhakika,alikuwa ni Partson akiwa na msichana mwingine wanapigana madenda.
Bado alizani macho yake yanamdanganya,akazidi kuwafuatilia mpaka wanaingia gizani nayeye akawa nyumanyuma,aliyokuwa anayashuhudia yalizidi kumuumiza moyo akajikuta analia kwa kwikwi,machozi yakaanza kumtiririka kama maji.
Mashine ya Partson ilikuwa nje tena inanyonywa kama koni.
Partson akageuza shingo yake,akamuona Sonia analia machozi,alipigwa na bumbuazi lakini hakutaka kukatisha jambo alilolianza.
Sonia alidhani Partson atashtuka lakini wapi,hiyo ndiyo ilimfanya aumie moyo Zaidi.Akashindwa kupiga moyo wake konde,maumivu aliyoyasikia kwake yalikuwa ni Zaidi ya msiba.
Akatoka akikimbia huku akilia, hakuelewa ni wapi anaelekea,ghafla akasikia kelele za treni la umeme linapita.
Maumivu aliyohisi aliona ni bora afe kwa kujitupa juu ya reli limsagesage abaki nyama na wala mifupa yake isionekane,akashika sketi yake vizuri na kukimbia upande wa reli huku akizidi kulia machozi.
Tayari aliumizwa kwa mara ya pili, hakujiona mwenye thamani tena duniani,akatamani aondoke juu ya uso wa dunia mara moja.
Akatembea mbiombio na kuwapiga watu vikumbo.
Treni ya umeme iliyokuwa inatembea kilomita kumi kwa sekunde yaani kasi yake haikuweza kuelezeka,ilikuwa ikitokea Capetown kuelekea nje ya mji huo.
Mahesabu ya Sonia yalikuwa ajitupe juu ya reli na asagwesagwe kabisa na treni ya umeme, kwa jinsi alivyopanga haikuwa rahisi kwa mtu yoyote kumuokoa.Akasimama juu karibu na reli na kuona treni ikiwa mita kama mia mbili inatokea upande wa Magharibi ikiwa katika mwendo wa ajabu.
Haraka akajitupa na kulala juu ya reli.
“Oh My God!”(Mungu wangu)
Mzungu mmoja mwanamke mtu mzima,alishtuka na kuziba mdomo wake baada ya kuona kitendo hicho kimetokea.
Sonia alikuwa juu ya reli anasali sala yake ya mwisho, tayari alishaelewa muda mchache angeenda kusagwasagwa na treni,akalala kifudifudi huku akisikia mtikisiko wa ardhi.Kila mtu alishika kichwa chake,treni likazidi kutembea kwa kasi,kila mtu aliogopa kutizama kitu kitakachotokea muda mfupi, wengine wakatizama pembeni.
Kufumba na kufumbua kila mtu alishangaa kuona damu zimetapakaa zimeruka,dalili zilionesha kuwa Sonia amechanwachanwa na treni iyendayo kwa kasi ya upepo!

*****
Maisha kwa Pendo Jonas yalikuwa ya raha mustarehe,Mzee Santiago alimuhudumia kwa kila kitu yeye pamoja na mtoto wake, Brenda.
Mzungu huyu alimdekeza na kumpeleka kila kona ya kiwanja anachojua yeye kitamfaa,kazi yake ilikuwa ni kumtambulisha kila rafiki yake anayekutana naye.Kila mtu alimsifia kwa kuchagua kifaa kutoka Afrika.
Mzee Wyatte pamoja na familia yake siku moja waliwaalika Mzee Santiago na familia nzima kwa ajili ya chakula cha usiku.
“Uje bwana hapa kwangu leo”
“Kwanini tusifanye wiki ijayo Wyatte?”
“Hapana kwa kweli,mimi nishaandaa kila kitu, usinifanyie ivyo rafiki yangu,sisi ni ndugu ujue isitoshe mimi nawewe sote wake zetu ni watu kutoka Afrika”
“Naelewa hilo”
“Sasa kwanini usije nae ili akutane na mke wangu nina imani atafurahi sana”
“Basi nitafanya hivyo,leo usiku nitakuwa hapo”
“Sawa,hayo ndiyo maneno.Kuna wisky zako nimekuandalia”
“Hahahaha,okay”
Simu ilivyokatwa Mzee Santiago akamfikishia habari mke wake, Pendo.Swala hilo akalipokea kwa furaha iliyozidi kifani.

Hakukuwa na kipingamizi kingine chochote kile.Mchana wa siku hiyo wakatumia kwenda kwenye maduka ya nguo na kununuwa nyingine mpya za Brenda na Pendo.Baada ya hapo walirudi nyumbani wakiwa na furaha mno.
“Brenda mwanangu,hizo nguo zimekutosha?”
Mama alimuuliza mwana.
“Ndio Mama”
“Umependeza sana,sasa leo vaa hilo gauni jekundu”
“Hili?”
“Ndio hilo hilo”
Yote yalikuwa ni maandalizi ya kwenda kula chakula cha usiku nyumbani kwa mzee tajiri,Waytte. Brenda alikuwa ni mdogo wa umri lakini mwenye umbo kubwa aliloridhi kwa mama yake,ungemwangalia ungedhani ana miaka kumi na tisa lakini alikuwa ni mdogo tu.
Kila kitu alichukuwa kwa mama yake kuanzia umbo mpaka midomo.Vijana wa kizungu walijisogeza karibu na Mzee huyu Santiago ili tu wajenge mazoea na Brenda.
***
Kwa mara ya kwanza Sebastian kumuona Brenda alijikuta amechanganyikiwa kabisa,ulikuwa ni usiku mezani wanakula,akili yake haikuwa kwenye msosi.Alikuwa akimuangalia Brenda wakati wote jinsi anavyokula kwa mapozi tena mara nyingine vishimo vya mashavu vinaingia ndani yaani dimpoz.
Hapo ndipo moyo wake ukawa unakita kwa nguvu.
“You beautiful”(Wewe ni mrembo)
Sebastian akajikuta anaropoka kwa sauti,kila mtu akamtizama.Brenda hakuwa na uhakika kama niyeye anaambiwa maneno hayo akajikuta anainua shingo yake,macho yake yakagongana na Sebastian kwa kama sekunde mbili nzima, kwa aibu akarudisha shingo chini.
Meza ilikuwa imechafuka na kilichokuwa kinasikika ni sahani na vijiko vinagongana,bado Sebastian alikuwa akitumia jicho pembe akimtizama Brenda,bado alikuwa akimtathmini jinsi msichana huyo alivyokuwa mzuri wa sura.
“Wewe Sebastian,embu kula basi”
Mama yake akamnong’oneza masikioni kwa sauti ya chini.Bado akili yake haikuwa hapo hata kidogo, ilikuwa imesafiri siku nyingi sana.
“Jamani,nawashukuru sana kwa kufika hapa leo lakini pia vilevile niliandaa burudani kidogo,tukitoka hapa tunaenda huku nyuma kuna ukumbi, niliamua kumualika mtu maalumu kwa ajili ya kuimba.Shemeji karibu Marekani”
Mzee Waytte alizungumza baada ya chakula kukaribia kuisha.
Hatimaye Wote wakasimama na kushukuru kwa chakula kitamu, wakaelekea nje.
Nyumba hiyo ilikuwa kubwa mno na ilikuwa na ukumbi mpana ambao ulikuwa na uwezo wa kuingiza watu hata elfu moja na kitu!
Hapo ndipo Sebastian alipata muda wa kumkagua Brenda kuanzia chini mpaka juu,akazidi kudata mno rangi ya mrembo huyo maji ya kunde ikazidi kumchanganya akili yake,moyo wake ukazidi kwenda mbio.Hakutaka kupoteza muda na kuendelea kuinyanyasa nafsi yake kiasi hicho.
“Umependeza sana siku ya leo”
Sebastian alianzisha maongezi.
“Oh Ahsante sana”
“Nani kanunulia nguo nzuri kama hizi?”
“Mama yangu”
“Anajua sana kuchagua,mimi naitwa Sebastian,wewe mwenzangu unaitwa nani?”
“Brenda”
“Una jina zuri kama wewe mwenyewe”
Hapo Brenda alitabasamu na vishimo vyake kwenye mashavu vikaingia ndani,uzuri wake ukachanua.
“Napenda unavyocheka”
“Ahsante,hivi wewe ulizaliwa huku huku Marekani?”
Brenda taratibu alianza kumzoea Sebastian na kuanza kumuhoji maswali,rangi ya ngozi ya mwanaume huyo ilimfanya atake kujua chimbuko lake.
“Mimi nilizaliwa hukuhuku Marekani”
“Wale ndiyo wazazi wako?”
“Ndiyo,yule ni Mama yangu na yule ni baba yangu”
Sebastian alisema na kunyoosha vidole ambapo Wazazi wake walikuwa mbele pamoja na Santiago na Pendo.
“Kabisa?kabisa?”
“Ndio”
“Sasa mbona umechukuwa sana rangi ya Mama yako?Ni mtu wa wapi yule?”
“Namibia”
Siku hiyo waliongea mambo mengi mbalimbali wakazoeana,Brenda hakuwa na mwenyeji yoyote yule nchi hiyo, hivyo ikamlazimu azoeane tu na Sebastian.
Wakaingia ndani ya ukumbi na kuangalia maonyesho ya muziki.Brenda na Sebastian akili zao hazikuwa hapo,walikuwa ndani ya stori ndefu, waliongea mambo mengi sana siku hiyo.

****
“Sasa utakuja au?”
“Mimi bado mgeni,sasa nitapajuaje?”
“Ongea na dingi au Mama,mwambie akulete mjini tukutane au nije nikufuate tukatembee beach,tupo Summer bwana lazima tukafurahi”
“Sawa nitajaribu”
Brenda alikuwa kwenye simu akizungumza na Sebastian asubuhi sana.Haikuwa kazi ngumu kwa Brenda kumwambia Mama yake juu ya Sebastian tena walivyokuwa mezani asubuhi wanakunywa chai.
“Hakuna shida yoyote ile,tena itakuwa bora akuoneshe mji huu”
Mzee Santiago ndiye aliyedakia mazungumzo.Jinsi walivyozoeana na Mzee Waytte hakuwa na sababu ya kupinga ombi la mwanaye Sebastian.
***
Masaa mawili baadaye nje lilionekana gari la kifahari aina ya Ferari,ndani nyuma ya usukani alikuwa amekaa Sebastian amevaa miwani nyeusi yaani ‘sunglass’ na nguo ya juu iliyokuwa imebana misuli yake yaani ‘board’,akapiga honi ya gari mara mbili.
Alivyoona hakuna dalili ya mtu kutoka akafungua mlango wa gari ambao ulifunguka kwa juu, raba kali aina ya supra iliyopanda juu ikatangulia na kukanyaga ardhi,akatoka nje mpaka getini na kubonyeza kengele.
“Sebastian subiri kidogo,anakuja”
Mzee Santiago ndiye aliyesema sauti yake ikasikika kupitia kipaza sauti,Sebastian alionekana akiwa nje kupitia camera zilizokuwa juu ya geti.
“Sawa Mzee”
Hazikupita hata dakika tano,Brenda akatokeza akiwa amependeza kupita kiasi.Nywele zake zinawaka sio masihala,Sebastian akabaki ameduwaa.
“Mambo”
Brenda akaanza kutoa salamu.
“Oh,poa.Umependeza”
“Hata wewe sharobaro”
“Hahahaha,twenzetu”
Wote wakaingia ndani ya gari na safari ya kwanza walifika ufukweni mwa bahari.Kila alipopita Sebastian alisalimiwa,hata walinzi pia walifanya hivyo,walimsujudu kama Mungu.
“Sebastian,pita huku”
Mlinzi wa getini aliongea na Sebastian.
“Poa poa,napita na huyu mrembo wangu”
Mambo hayo yalimshangaza sana Brenda,umaarufu wa Sebastian ulimfanya atake kuuliza lakini akasita.

Maisha ya wawili hawa yaliendelea hivyo hivyo,ilikuwa kila siku lazima wakutane na kutembea sehemu mbalimbali.Wakati mwingine Sebastian alifanya Siri wakisafiri miji mingine kama Carlfonia,Washington DC na mpaka New York,mji mkubwa.
Wanamuziki aliokuwa anakutana nao Sebastian ikamfanya Brenda aulize maswali.
“Ulisema yule ni 50 cent?huyu mwanamuziki”
Brenda akauliza kwa mshangao wakiwa mji wa New York ndani ya mgahawa mkubwa wa Chicago inn.
“Ndiyo,mbona kama umeshtuka sana?Hao watu wa kawaida kwangu.Huwa nakunywa nao sana pombe ndani ya huu mgahawa,unahitaji kuonana na msanii gani labda?”
“Mh!”
“Usigune,wewe niambie tu”
“Jamani,hata Rihhana huwa unaongeaga naye?”
“Ile siku niliyokuja kuwapokea Airport na dingi,nilikuwa naye lakini sasa hivi hayupo.Yupo Portland anafanya kazi zake za muziki”
Hapohapo akatokea mwanaume mweusi mwenye misuli,kichwani alikuwa amevaa kofia,hakuwa mwingine bali ni msanii maarufu 50 cent,akarudi kukaa kwenye meza ya Sebastian.
“Yoh Seba,Mimi naondoka sasa hivi Trey songs kanipigia simu niende studio”
“Basi nitakutafuta”
“Poa”
Jinsi msanii huyo 50 cent alivyoongea kwa kumung’unya maneno kulimfanya Brenda amuangalie.
“Brenda vipi?”
“Sebastian,tafadhali naomba nipige picha na huyu mkaka jamani,mwite”
“Mh,kupiga nao picha hawa wanakuwa wanaringa sana,lakini subiri hapa”
Sebastian akasimama na kutembea mpaka kwa msanii huyo,akamuomba.
“Unataka Picha?”
“Ndio Curtis”
“Si unajua noma,nitapiga naye moja basi”
“Haina shida”
“Mimi ni biashara,nadhani unatambua”
“Naelewa”
Brenda akaitwa,akapiga picha na 50 cent akafurahi moyo wake ukazuuzika.

Jioni ya siku hiyohiyo wakapanda ndege ndogo na kurudi Los Angeles,hakuna mtu yoyote aliyejua kuwa watu hao walikuwa wakisafiri.
Sebastian akazidi kumvuta karibu Brenda,mazoea yakazidi na wakaanza michezo ya kikubwa ya kushikana viuno kama masihara,mara wakaanza kupigana madenda.
Brenda kwa mara ya kwanza kushikwa maziwa yake alihisi kama anapigwa na shoti ya umeme,akatetemeka kupita kiasi.

Alikuwa ni mdogo bado kufanyiwa vitu kama ivyo.Sebastian aliendelea kuzitomasa chuchu zake siku hiyo usiku wakiwa kandokando ya fukwe za bahari.
Alizidi kuudidimiza mkono wake akapachua sidiria,akaingiza mkono ndani kabisa akakutana na maziwa yaliyosimama akashika chuchu zake, hapo ndipo Brenda akayafumba macho yake,kuna kitu cha ajabu alianza kukihisi.
Sebastian, hakuishia hapo.
Mkono wake akaupitisha chini tumboni mpaka kwenye kitovu akafungua kifungo cha kaptula ya Brenda akaingiza mkono wake chini akakumbana na vinyasi vilivyoanza kuota,akazidi kuuingiza mkono wake chini kwa chini karibu na maporomoko.
Hapo Brenda akamdaka mkono hakuwa tayari jambo hilo lifanyike siku hiyo.Sebastian akaelewa nini maana yake.Akarudisha gia namba moja na kuanza ‘fresh’.Wakaendelea kunyonyana midomo.
Sebastian akatoa nguo ya juu ya Brenda na kutoa sidiria,akaanza kunyonya maziwa ya Brenda tena juu ya chuchu zake zilizokuwa zimesimama wima kama embe bolibo.
Brenda alikuwa taaban hajiwezi tena,hapo ndipo Sebastian alipoanza taratibu kushusha kaptula ya Brenda chini akafanikiwa kuitoa,akaitoa na chupi yake akabaki hana kitu chini,hapo ndipo Sebastian akaipanua miguu yake na kutoa ulimi,akaweka ulimi wake na kuanza kupiga deki bahari!

****

Ilikuwa ni katikati ya usiku wa manane,mji ulikuwa umetulia, kilichosikika ni milio ya honi za magari.Maaskari walikuwa wakiranda huku na kule kulinda usalama wa raia na kutuliza fujo endapo zitatokea kwa namna yoyote ile.Macho yao yalikuwa makini kwa kila raia anayepita hususani kwa watu waliokuwa wanazurura ovyo.
“Zaid embu tizama”
Sauti ya askari aliyekuwa juu gorofani ilisikika akimshtua mwenzake akionekana ameona kitu cha ajabu.
“Kitu gani?”
Mwenzake akauliza na kugandisha kikombe cha kahawa.
“Mtizame yule binti,mbona kama hayupo sawa?”
“Sasa wewe anakuhusu nini?”
“Hapana,nina mashaka kuna kitu anataka kukifanya”
Maaskari waliokuwa doria upande wa pili,walizidi kumtizama Sonia aliyekuwa analia huku anasogelea reli.Likiwa ni jambo la hatari sana na kilichowashtua zaidi ni baada ya kusikia muungurumo wa treni ya umeme inayoenda kwa kasi.Katika hali ya kushangaza wakamuona amejitupa juu ya reli.
“Mikeeee”
Zaid alishtuka baada ya kumuona mwenzake kajitupa kutoka gorofani,nia ya Mike ilikuwa ni kumfuata Sonia na kuyaokoa maisha yake.
Umbali kutoka alipo na mpaka kushuka ngazi ulikuwa ni mrefu kiasi, aliamini kwa kuruka gorofani na kudondoka juu ya meza ya vyakula ndiyo ingeokoa maisha ya Sonia kwa kufupisha njia.

Bila kuangalia huku na kule askari Mike alianza kukimbia kuelekea relini ili kuyaokoa maisha ya Sonia,treni lilizidi kutembea kwa kasi lilikuwa ni kama mita kumi na mbili na alipo Sonia,kama swala akaruka juu ya reli na kumnyanyua Sonia akamtupa upande wa pili,akashika ukuta mfupi ili ajitoe lakini hakufanikiwa kwani treni lilimpitia hapohapo akapasuliwa kama nyanya na kusagwasagwa kama nyama kwenye mashine,
kilichoonekana hapo ni damu kuruka hewani na nyama.Kila mtu alifumba macho.Watu wa upande wa pili walijua binti aliyelala juu ya reli ndiye kapoteza maisha.Treni likatembea kwa umbali wa mita tano na kupiga breki hapohapo.Ilikuwa ni ajali ambayo haikuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo mtu kugongwa na treni.
Watu walianza kukusanyika mmoja baada ya mwingine,kila mtu alitaka kushuhudia wenye mioyo mepesi walikimbia mbali,hawakutaka kushuhudia utumbo uliochenguliwa vibaya sana na vyuma vya treni,maisha ya askari Mike aliyeokoa uhai wa Sonia yakaishia hapohapo.
Hakuna kitu kilichofanyika zaidi ya magari ya kubebea wagonjwa kufika eneo la tukio dakika hiyohiyo,gari la kwanza likambeba Sonia aliyekuwa pembeni kapoteza fahamu zake, hakuelewa lolote linaloendelea duniani!
****
Kwa mbali alihisi anapigwa na ubaridi na watu wanazungumza,kumbukumbu zake taratibu zikaanza kujikusanya akakumbuka tukio zima alilolifanya, mara ya mwisho alikuwa juu ya reli akisubiri kifo cha kusagwasagwa na treni ya umeme.
Bado aliendelea kutafakari akadhani wenda yupo ahera,taratibu akaanza kujipapasa mwilini mwake,akagusa mguu wake akaukuta.Kwa kutaka kuhakikisha jambo hilo akayafumbua macho yake, hapo ndipo akagundua yupo hospitalini juu ya kitanda pembeni ametundikiwa dripu ya maji.
Akashindwa kujijibu kuwa amefikaje,hakuelewa lolote juu ya kufika eneo hilo.
“Bado sijafa?inakuaje nipo hapa?!”
Sonia akajiuliza swali mwenyewe.
Nesi alivyoona mgonjwa wake amefumbua macho akamsogelea karibu yake.
“Dada unajisikiaje?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Nesi aliyevaa nguo nyeupe na kofia maalum kichwani.
“Imekuaje nipo hapa?”
“Mshukuru Mungu umepona dada,una tatizo gani?”
Nesi alijaribu kumdodosa Sonia wakitumia lugha ya kiingereza.Picha ya Partson ikamjia akiwa na msichana mwingine wanafanya mambo ya kishenzi, machozi yakaanza kumlenga,akawa analia kwa kwikwi,kupitia kitendo hicho Nesi alijifunza kitu.
“Dada mbona unalia?”
“Na..taka kujiua sa..sa hivi.. kwanini mmenioko…a lakini?”
Sonia aliongea kwa kwikwi alijihisi uchungu sana,usaliti aliofanyiwa ulikithiri.
“Hapana usifanye hivyo,mimi ni mwanamke mwenzako niambie tu”
“Wa.naume ni watu wabaya sa..na”
“Kwanini?”
Muuguzi akasahau kazi yake,akajaribu kumtuliza Sonia asilie,alimuonea huruma kupita kiasi.Sonia alijikaza na kumuhadithia kila kitu kuanzia walivyokuja na Partson mpaka jinsi ilivyokuwa na mwisho akahitimisha kuwa anahitaji kujiua.
“Pole sana dada,ivyo vitu vya kawaida usijali sana.Wapo walioteswa na mapenzi.Wewe sio wa kwanza na hautokuwa wa mwisho.Swala mshukuru Mungu umepona”
Maneno ya Muuguzi kidogo yakamuingia akilini.Lakini haikumfanya asiumie moyoni.

Siku zikazidi kwenda, Sonia akiwa hospitalini anapatiwa matatibu,akapewa daktari wa saikolojia.Huyo ndiye akamfanya asahau kila kitu.
“Ili kuhakikisha haya yote yanaisha inabidi tupime afya yako”
“Afya yangu kivipi Dokta?”
“Huwa tunawashauri wagonjwa wetu kufanya hivyo lakini sio lazima,ni hiyari yako”
“Kupima vipi?”
“Kupima damu kubwa”
“Sawa hakuna tabu”
Hapohapo taratibu zikaanza za kuchukuwa damu kubwa ya Sonia,aliyefanya hivyo ni dokta Zahoro Kanyika,akafanya kazi kama alivyoagizwa, damu kubwa ya Sonia ikachukuliwa akanyoosha mpaka maabara akimuacha nyuma Sonia ndani ya ofisi yake.
Akaweka damu kwenye mashine maalumu akatia damu, akasubiri kwa dakika kadhaa,majibu aliyoyaona yalimpa wasiwasi mkubwa kupita kiasi,haikuwezekana hata kidogo kwa binti mzuri aliyemuacha ofisini kwake akawa na virusi hatari vya ukimwi.
Dokta Kanyika alijaribu kuangalia tena vipimo vyake kwa mara nyingine,bado hakutaka kukubaliana na hali halisi.
“Mh!”
Akaguna baada ya kuona majibu ni yaleyale kwamba damu ya Sonia ina virusi hatari vya ugonjwa wa Ukimwi,akasikitika kwa jinsi binti huyo alivyokuwa mdogo mwenye malengo katika maisha yake.
Akavuta kiti nyuma na kurudi ofisini kwake ili kumpa majibu.Lakini cha ajabu hakumkuta Sonia akatoka mpaka nje lakini hakumuona popote pale.
****
Hakuwa mwenye wasiwasi wowote ule alijiamini kupita maelezo,kutolewa damu yake ili ikapimwe ukimwi aliona ni kama upotevu wa muda ingawa alibaki akisubiri ili ajihakikishie kwamba yupo salama na damu yake ni safi,alimsubiri daktari kwa dakika kumi nzima huku akitafakari maisha yake yalivyokuwa,alimchukia sana Partson kwa kitendo alichokifanya na aliapa kuwa hatopenda mwanaume mwingine yoyote kwani aliamini wana roho za kinyama na hawastaili kuishi nchi kavu wala majini.
Juu ya ukuta kulikuwa kuna televisheni kubwa akatupa jicho lake.
Hasira zikazidi kumpanda baada ya kumuona Partson Ngogo anahojiwa kuhusu mpira,bado alikuwa Afrika kusini tena katika stesheni ya WBS.
Sonia alihisi kichefuchefu cha kutapika baada ya kuiona sura ya Partson, hakutaka kubaki tena hospitalini kusubiria majibu,akatoka nje na kutafuta taxi.
“Nipeleke hotel yoyote ile ya karibu”
Alitoa amri baada ya kuingia ndani ya taxi,safari ikaanza mara moja.
Hakutaka kubaki tena ndani ya nchi hiyo akiteseka,alitaka kurudi Tanzania haraka iwezekanavyo,akatafuta tiketi usiku huo huo.
Bahati nzuri alipata ndege ya shirika la British Airways inayotokea nchini Venezuela,ikawa bahati kwake.

Asubuhi sana siku iliyofuata alikuwa tayari Boarding pass kwa ajili ya ukaguzi wa mwisho,baada ya nusu saa ndege ikaanza kutembea na kuachia ardhi, matairi yakaingia ndani,ikazidi kupanda juu angani.
Sonia hakuwa mwenye furaha hata kidogo,alitamani kufika haraka iwezekanavyo.
***
Hakutaka kujiingiza tena kwenye maswala ya mapenzi alikuwa mpole kuliko siku zote,akaendelea kufanya biashara zake za kuuza nguo.Kitu ambacho kilikuwa kinampa changamoto ni usafiri wakati wa kurejea nyumbani kwake.
“Hivi kwanini napata shida wakati pesa ninazo chungumzima kwenye akaunti yangu?”
Sonia akajiuliza swali hilo,kama pesa alikuwa nazo za kutosha, kesi aliyoshinda nchini Sweden ndiyo ilimfanya avune mabilioni ya pesa.
Siku hiyohiyo mchana akafunga duka na kwenda bank CRDB kuchungulia salio lake,pesa alikuwa nazo nyingi mno tena za kumwaga!
Akatabasamu na kutafakari ni aina gani ya gari atumie likatakalo endana naye.Hakupakuwa pesa yoyote ile, akakodi pikipiki mpaka faya karibu na ‘Showroom’ ya waarabu ambapo mara nyingi hupita hiyo njia na kuona magari mazuri ya kisasa.
“Unanidai shilingi ngapi?”
“Buku tatu sista”
“Poa”
Sonia akatoa elfu kumi akampa dereva wa pikipiki na kuondoka zake,kwa furaha aliyokuwa nayo hakukumbuka hata chenji.
Akaingia ndani ya geti na kukumbana na magari mengi ya kifahari,akachanganyikiwa.
“Dada karibu”
“Ahsante,nahitaji gari kali sana”
“Usijali,wewe chagua chagua hapo”
“Kaka embu nichagulie,nataka gari ya juu juu hivi kama Landcruiser”
Sonia akasema huku akipiga macho yake huku na kule.
Akagandisha macho yake kwenye REXAS Landcrusier, iliyovimba nyeusi sana.
“Hii gari nimeipenda,kiasi gani?”
“Milioni tisini nitakufanyia ndiyo gari zilizoingia sasa hivi,ikitoka Landcruiser v8 ndiyo hizi Rexas”
“Inakimbia lakini?”
“Hilo usiulize,inakimbia kuliko risasi nusu saa upo Kigoma”
Muuza magari akatia mbwembwe!
“Nalipa vipi?pesa zangu zipo bank tunaweza tukaenda wote?”
“Bila shaka”
“Lakini kaka,kitu kimoja naomba”
“Kitu gani?”
“Bado sijui kuendesha gari,inabidi unisaidie kuendesha mpaka nyumbani kwangu”
“Hilo halina shida”
Taratibu zilianza kufanyika hapohapo,wakaongozana na Sonia mpaka CRDB bank, akapakua pesa na kurudi tena kwenye ‘showroom’ ambapo alipewa kadi ya gari na kila kitu.Sonia alifurahi sana alivyoingia ndani ya gari,hakuamini kama amemiliki gari kama hilo la kisasa.
***
ILIBIDI tu aanze ‘driving school’ ili ajue jinsi ya kuendesha gari na kupata leseni,baada ya mwezi mmoja Sonia alikuwa ana uwezo wa kuendesha gari yake mwenyewe kwenda kazini bila matatizo yoyote yale.Uzuri wake pamoja na gari alilokuwa akitembelea vilimfanya azidi kupata umaarufu na kupeta,licha ya kuogopeka mtaani mpaka kazini lakini wanaume walimgasi mno,haikupita hata siku moja bila ya kutongozwa mara mbili au tatu.
“Ha!Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! unanichekesha sana Tiko,sasa na yule demu wako utamuachia nani?”
“Yule namuacha Sonia,nakupenda sana.Usitake kuniumiza kiasi hicho”
“Sasa utaacha wangapi?embu acha kuwa mapepe”
“Sio mapepe,mimi nakuzimia.Ukinikubalia nakuoa”
“Ha!Ha! Ha!unaniona mimi mtoto sana eeh ”
Jinsi Sonia alivyocheka kwa mapozi ndiyo kabisa,meno yake yalionekana vizuri yakiwa yamejipanga mdomoni.
“Usicheke sasa”
“Sasa unataka nifanye nini?nyie wanaume mna maneno matamu sana,embu tuwe washkaji tu hivihivi kwangu itatosha,maswala ya love siwezi,yakaushie tu”
“Au kisa wewe matawi ya juu?”
“Sasa hapo ndiyo utanikera Tiko,hayo yametoka wapi?.Sasa hivi utanichefua ohoooo!”
“Basi yaishe”
“Ongea vitu vingine,wakuongeze Konyagi au?”
“Poa tu wacha nilewe”
Tiko alijaribu kutupa mawe akijaribu kumtongoza Sonia lakini alitoswa na kupigwa kibuti,akabaki tu kula kwa macho,siku hiyo wakanywa baada ya lisaa limoja Sonia akawasha gari na kuondoka zake.
***
Ulikuwa ni usiku mnene siku ya Ijumaa ndani ya ukumbi ulioitwa Kibo complex, hapo ndipo Sonia alipochagua kwenda kusikiliza mziki na kunywa pombe,alikunywa huku akicheza mziki,kila alipoingia katikati kucheza wanaume nao walisimama na kutaka kum-bambia lakini hakutaka swala hilo litokee.
“Kaka niache nicheze mwenyewe”
Sonia alisema huku akiwa amesimama,anamtizama mwanaume aliyekuwa nyuma yake.
“Kwani vibaya tukicheza pamoja?”
“Sitaki sasa,kwani lazima?”
“Aya poa”
Sonia akaendelea kukizungusha kiuno chake,kimini alichovaa kiliwakosha watu wengi mno,alicheza na kuendana na mziki unavyokwenda mara kushoto mara kulia.
Mpaka inagonga saa tisa ya usiku bado alikuwa ndani ya Kibo complex anayumba huku na kule pombe zipo kichwani,akawa anapepesuka huku na kule akatoka nje.
“Dada,uko poa?”
“Ndioooooo,what is wrong with youuuuuuuu?”
Sonia aliongea kwa sauti ya kilevi huku akiyumba na chupa ya wisky mkononi mwake akitafuta alipopaki gari lake.
“Njoo basi huku”
Mwanaume mmoja aliyeonekana ana uchu alisema huku akimfuata Sonia na kumshika mkono.
“Niacheeeee tafadhaliiii”
“Dada,umelewa sana njoo kwenye bajaji huku”
“Niache Mse** nini,unadhaaani sijielewi niachieee nitakupigia kelele za mwiiiziiiiiii,nina bastola kwenye pochiiii yanguuuu”
Sonia aliongea kwa ukali,japokuwa alikuwa bwii lakini alijihami, kichwani kwake alielewa kuwa angechekacheka angeenda kufanyiwa kitu kibaya.
Akazidi kuporomosha matusi akatembea haraka mpaka kwenye gari lake.
Akabonyeza rimoti ya gari ikapiga kelele na kuwasha taa kumaanisha kuwa ‘lock’ imefunguka,akafungua mlango na kuweka chupa ya pombe kiti cha kushoto.
“Wanadhani nimelewaaa hawaaaaa,Mse** weweee mimiiii nikoo fiiiiit,Shenzi type Blood fool,stupid boy”
Sonia aliongea mwenyewe ndani ya gari na kulitia moto ili kurejea nyumbani kwake,aligeuza gari kwa kasi na kuingia barabarani.
Kwa mikono miwili aliukamata usukani,kwa jinsi alivyokimbiza gari iliogopesha kwa mtoto wa kike kama yeye,barabara ilikuwa nyeupe hiyo ilimfanya atambe barabarani.
Alizidi kunyoosha mguu na kuzidisha mwendokasi mshale wa spidi ukazidi kuzunguka.
Katika hali ya kushangaza gari likatokea upande wake ghafla lililokuwa linatokea Goba,kwa bahati nzuri aliwahi kulikwepa akazungusha usukani, akahama upande hapo ndipo alipokutana na gari nyingine na kuligonga vibaya sana kwa nyuma,kwa uwoga hakutaka kusimama.
Alikuwa ameligonga gari la kifahari Range Rover Sport, uwoga ukamtanda ukichanganya na pombe alizokunywa ikamfanya asitake kusimama,akaliondoa gari mkuku mkuku,moyo wake ukazidi kupiga kwa nguvu baada ya kuona gari aliloligonga aina ya Range Rover sport linamfuata kwa nyuma!

****

“Oyaa Leythan eeh”
“Nambie”
“Sasa ile cheni yangu unataka kunizima au?”
“Kaka,nitakurudishia bwana,mbona unakuwa hivyo sasa”
“Hapana Leythan,ile cheni niambie ukweli.Nimemuona nayo Tina kwahiyo usitake kunidanganya”
“Sioo kweli,umeifananisha”
“Poa,utanipa lini?Maza anaiulizia”
“Nitakupa”
Ndani ya kijumba kidogo chenye kitanda kimoja na godoro lisilokuwa na shuka zilisikika sauti za watu wawili wakijibishana,walikuwa ni maswaiba wa kufa na kuzikana.

Maisha ya Leythan Jabir yalikuwa mabovu na alikuwa ni maskini wa kutupwa.Maisha yake yalikuwa ya kuunga unga,kutokana na kuwa na mwili mzuri uliopanda juu na rangi yake ya kichotara ilimfanya apendwe na watoto wa kike,alikua ana sura nzuri kama msichana.Sura yake ndogo ya duara na macho ya kusinzia ndiyo ilikuwa ugonjwa wa watoto wa kike kitu kingine kilichowapagawisha ni nywele zake nyingi,hapo ndipo walipo mpachika jina na kumuita ‘Mwisho mwampamba’hata hivyo alifanana na mtu huyo karibia kila kitu,endapo ungemuweka pembeni na mshindi huyo wa Big brother Africa hakika usingeweza kuwatofautisha,wakati mwingine aliwadanganya wanawake kuwa huyo alikuwa ni binamu yake.
Licha na yote hayo alikuwa akitumia gia tofauti tofauti kuwanasa wasichana,hakuna mwanamke hata mmoja aliyejua ni wapi anaishi Leythan Jabir, maisha yake yalikuwa ya kuazima nguo na magari ya kifahari kuwatongozea mademu!
Angevaa suti na kukwambia kuwa ni mkurugenzi wa benki kuu usingepindua na hivyo ndivyo alikuwa akiwaongopea wasichana wa kishua.
Siku hiyo asubuhi alikuwa amelala akaamshwa na rafiki yake, akitaka mkufu wake wa dhahabu.
“Sasa Juma,si nilikwambia nitakupa mshkaji wangu mbona unanikazia,alafu kuna kitu kingine nilikuwa nataka uniazime”
“No Leythan”
“Ah Juma,acha zako basi.Sikia sasa kitu chenyewe, ushakijua?”
“Kitu gani?”
“Kuna modo yako ulikuja nayo juzi hapa,ile nyeupe nyeupe.Nisaidie niitinge leo kuna mtoto mmoja hivi nataka nikamfuate pale Ustawi”
“Ile chafu”
“wewe nipe ivyo ivyo,alafu shati jeusi nitachukuwa kwa Mwiba,Moka atanipa Mzee Ukwaju.Gari naenda kuchukua kwa Demu wangu Roda.Tayari mambo mwake”
Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Leythan Jabir duniani.Ungeambiwa kuwa anachonga vinyago Mwenge usingekubali hata kidogo.
**
Leythan Jabir alipendeza sio masihara,modo nyeupe aliyovaa na Shati jeusi lililom-bana mwilini na kumkaa vizuri vilimfanya aonekane maridadi mno,nywele zake akazibana vizuri kwa nyuma akawa kama Mwisho Mwampamba ‘copyright’.
Kila alipotembea mabinti waligeuza shingo zao na kumnyooshea vidole.
“Baby upo wapi?”
Leythan aliinua simu na kumtafuta mwanamke aliyekuwa akimuhonga na kumgharamia.
“Nipo kazini,njoo basi baby wangu nataka nikuone nimekumisi Handsome boy wangu”
“Acha zako Rhoda,si unajua mimi pia nipo kazini sasa hivi, lakini nimepata dharura hapa ya ghafla,gari yangu ipo gereji”
“Sasa uje tuongelee huku mpenzi wangu”
“Sawa basi nakuja hapo sasa hivi”
“Sawa mpenzi,usichelewe bwana”
“Sasa hivi nachukuwa bodaboda hapa”
Simu ikakatwa.

Mfukoni alikuwa ana shilingi elfu saba na mia mbili tu.Akapiga hesabu zake za harakaharaka anajumlisha na kutoa,akiwa anatembea kuelekea stendi ya mabasi Mabibo mwisho,ghafla akapata wazo.
“Hapa nachukuwa gari la Posta,nashuka Maktaba nachukuwa bodaboda,Hahahahaha”
Leythan akatabasamu na kutembea akiwa anadunda,akafika stendi na kupakia daladala za posta akampigia simu Rhoda,akamwambia kuwa atachelewa bado ana kazi za kiofisi.
“Ndio,nipe kama nusu saa hivi nitakuwa nimemaliza.Okay sawa nakuja Rhoda,acha wivu”
Leythan akauwa Soo,kutokana na msongamano wa magari.
Ni kweli mahesabu yake yalienda kama alivyopanga alivyofika Maktaba kuu ya taifa akashuka na kukodi bodaboda iliyompeleka ofisi za Jiji.Akashuka na kutembea hatua kama kumi na kuingia ofisi hizo.
“Namuulizia Rhoda”
Leythan akaongea alivyofika mapokezi.
“Pita,anakusubiria”
Msichana wa mapokezi alimtizama kwa macho ya matamanio,hata yeye alizimika sio masihala, ‘Perfume’ aliyopuliza Leythan ilikuwa kasheshe.
“Baby”
Rhoda alivyomuona Leythan alitoka juu ya kiti na kumkumbatia hapohapo wakaanza kubadilishana mate wakilana denda.Mkono wa Leythan ukapita mpaka kwenye makalio ya Rhoda akayabinya kibaha-sha.
“Baby,unanukia sio mchezo”
“Ah bwana we,kawaida yangu kunukia,hapa nimekimbia kazi ofisini nimepigiwa simu ya dili moja huko Bagamoyo sasa gari yangu ile kabureta yake inavuja alafu cheki yangu haijatoka na……”
Leythan akanyamazishwa na kidole alichowekewa mdomoni na Rhoda.
“Shhshssss,acha kuongea sana mpenzi wangu.Mbona unaongea maneno meeeeeeeengi.Fupisha love sema unaomba gari nikuazime basi,mengine ya nini? unakuwa kama unatoa ese darasani”
“No najaribu kukuelezea tu”
“Sitaki maelezo yako,nitakupa gari yangu.Utarudi lini?”
“Leo narudi usiku sana”
“Pitia Mbezi basi mpenzi wangu,uje kulala kwangu”
“Baby,nitakuwa nina kazi za kumalizia”
Leythan akajifanya hataki lakini moyoni alitamani Rodha amsisitizie.
“Honey bwaaana ah,nimekumisi”
Rhoda akazidi kudeka akitoa sauti za puani akamuendea Leythan mdomoni na kuanza kumla denda upya.
“Mhh,okay baby nimekubali”
“Daaaarling,ilove youuuuuu,sasa nitakupa laki moja si itakutosha eeh!”
“Ya nini sasa?”
“Basi tu”
Rhoda alitamani afanye ngono hapohapo ofisini lakini aliogopa mno,damu yake ilimuenda mbio hasa alivyoziangalia lips za mwanaume huyu mzuri, zilikuwa nyekundu muda wote.
“Shika pesa hizi hapa na funguo za gari hizi hapa pia.Gari yangu si unaijua?”
“Pajero au?”
“Ile sina siku hizi,njoo nje nikuoneshe”
Leythan na Rhoda wakaongozana mpaka nje kwenye maegesho ya magari,wakasimama pembeni ya gari la kisasa aina ya Jeep.
“Hii ni left hand?”
“Ndio,nimeagiza Germany juzi”
Hakukuwa na ukweli wowote ule kutoka kwa Rhoda,ukweli ni kwamba gari hilo alihongwa na Mwanaume kigogo serikalini na alimtumia mzee huyo kuchuma pesa zake, nayeye alifanya hivyo kumuhonga Leythan kisiri.
“Safi sana”
Bila kupoteza muda Leythan akaingia ndani ya gari upande wa kushoto akawasha na kuliondoa taratibu barabarani.

Jinsi alivyovimba juu ya kiti cha gari na kutanua mikono yake kama kibosile, usingekubali kwamba hapo alipo hana kitu chochote,kuanzia nguo mpaka viatu havikuwa vyake.Mfano kila mtu angetokea na kutaka mali zake hapo angebakiwa na boxa peke yake.
Akiwa kwenye mataa ya Samora akapapasa simu yake pembeni ya gia na kuingia ‘phonebook’ akatafuta majina mpaka alipokutana na jina Christina Macha,mtoto wa kichaga mwanafunzi wa chuo cha ustawi,aliyetokea kumpagawisha kwa uzuri.Akaweka jina vizuri na kuipa simu ‘ok’
“Tina mrembo wa dunia!”
“Nambie Mr.Handsome,upo wapi?”
“Ndio naingia Dar sasa hivi,nimetokea Arusha”
Alidanganya.
“Mbona mapema sana?”
“Nilitoka usiku wa jana baby”
“Jamani karibu,kwahiyo baby utakuja leo hostel au?”
“Lazima nije mpenzi wangu,hilo sio la kuuliza”
“Baby nitafurahi sana,nataka ukija nikutambulishe kwa mashosti zangu”
“Sawa,ndio nipo Kimara mwisho.Kwa kuwa nakupenda breki ya kwanza nitafika kwako”
“Woow!nakupenda sana Leythan wangu”
“Mimi pia”
“Baby take care,usiendeshe gari kwa spidi”
“Sawa”
Simu ilivyokatwa Leythan alitabasamu na kuingia kwenye inbox akakutana na ujumbe wa meseji.
‘LOVE UPO WAPI?NAKUMISI MWEZIO NILIENJOY SANA KUWA NAWEWE’
Leythan akasonya na kuingia kwenye meseji nyingine.
‘SIKUTEGEMEA KAMA UNGEWEZA KUNIFIKISHA,NAKUPENDA NITAMUACHA MUME WANGU KWA AJILI YAKO REI,NAKUPENDA MNO’
Alizidi kusoma meseji.
‘OYAA WE BOYA,SAA YANGU UMEIVUNJA UTAILIPA’
Meseji hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kuisoma,ikamtia kichefuchefu akatupa simu pembeni na kupiga gia baada ya taa za kijani kuwaka.

Lisaa limoja baadaye alikuwa anapaki gari Chuo cha Ustawi Sinza, akampigia simu Christina Macha,msichana aliyekuwa anatikisa chuo hicho kwa urembo na mikogo.Kwa jinsi alivyokuwa akitembea msichana huyo ungedhani kwamba anaogopa ardhi,alitembea kama twiga,alikuwa ana futi nyingi za urefu kwenda hewani.
“Baby upo wapi?”
Tina baada ya kutafuta sana nje hakumuona Leythan ilibidi ampigie simu.
“Nipo upande wa kushoto huku mwisho kabisa”
“Wapi baby?jua linanichoma”
“Nyoosha kuna gari nyeusi kabisa lina rim nyeusi pia”
“Hilo lenye machuma kwa juu?”
“Ndio”
“Ndio nimeliona,sasa upo kwa wapi?”
“Ndani ya hilo gari”
“Mh!”
Christina alishtuka,hilo lilikuwa gari la sita kumuona nalo Leythan moyo wake ukapiga hatua kumi mbele,gari aliloliona mbele yake lilikuwa kali na la kipekee.
Alivyofika tu alifungua mlango na kuanza kumpiga denda Leythan.
“Baby,umenunua gari mpya?”
“Kwani bado hujanizoea?”
“Hili gari kiboko”
“Vipi vipindi vimeisha?”
“Nishamaliza”
“Sasa?”
“Nakusikiliza wewe”
“Twende hostel kwako”
“Poa baby”
Gari likawashwa,Leythan akakanyaga mafuta nia yake ilikuwa kwenda kumpanda msichana huyo mrembo,hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Leythan Jabir ulimwenguni.
Aliwachanganya wanawake kama pilau na kachumbari akawapanda kama farasi, hakujali lolote kuhusu kutumia Condom.
Na katika maisha yake hakuwahi kukataliwa na mwanamke yoyote yule,kwa gia aliyokuwa anaingilia isingekuwa raisi kwa binti yoyote yule kumchomolea.
**
“Na ile nyimbo Rei umeimbiwa wewe”
“Nyimbo gani?”
“Yahaya,yaani hujulikani unaishi wapi,mambo yako kama Yahaya,Jay dee hakukosea, kuanzia leo jina lako Yahaya”
“Embu acha ufala basi Shedu tueshimiane,embu ongea pointi.Mimi ndiyo maana sipendi kutulia nawewe maskani unazogoa sana”
“Mimi nakwambia ukweli,lakini kaka unawatafuna una dawa nini?Alafu watoto unaowamega clasic”
“Amna sikia nikwambie,kwanza niazime hili tisheti lako jioni.Kuna demu naenda kumuona”
“Rei hili tisheti jipya ujue”
“Wewe niazime nitakuletea,kuna maza mmoja hivi naenda kumcheda.Na hizi nywele zangu inabidi leo nikapigwe shampuu kwa Misanya pale”
Leythan hakutania,ungekataa katakata ungemuona jinsi alivyo.Bwanga alilovaa kama puto lilimfanya awe kituko.


*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG