MCHACHUKO SEHEMU YA 7/10
MCHACHUKO
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 7 KATI YA 10
*******
*******
Moyo wa Jaqlin ulipiga paa! baada ya kupewa habari mbaya ya basi la Abood lililotumbukia Mlima
Kitonga na kuuwa watu karibia wote, mawazo yake yalisafiri haraka kwa kasi ya umeme mpaka kwa Adrian na kuhisi wenda Adrian atakuwa mmoja wa marehemu waliokuwa wamefariki dunia kwenye ajali hiyo iliyotokea wiki tano nyuma.
Mama Oswadi jirani yake aliendelea kutoa habari juu ya ajali hiyo iliyotokea.
“Ndio nimetoka kumzika mdogo wangu hapa juzi alikuwa kwenye hiyo Abood, iliyokuwa inatoka Dar”
“walipelekwa hospitali gani?”
“Kitonga Hospital”
“wacha niende”
Siku hiyo hiyo Jaqlin na tumbo lake kubwa alitembea kwa haraka kama chizi mpaka benki kutoa fedha, bila kumuaga Mzee Mwangenya huko huko alipanda basi mpaka Mjini kisha kupanda daladala inayokwenda kitonga alivyofika kitonga alichukua taxi,
ndani ya ubongo wake alikuwa ni mwenye mawazo mengi sana.
Baadaye walifika Mlima Kitonga Jaqlin alidondosha chozi la uchungu, hakuelewa angeishi vipi bila ya Adrian endapo akiwa amefariki dunia sababu alishalewa na Penzi la mwanaume huyo.
Kwa mbali dereva alisikia king’ora cha gari la kubeba wagonjwa yaani Ambulance na kuweka gari kando baada ya kuvuka mlima kitonga!
“Dereva vipi?”
“Napisha hilo gari”
“bado lipo mbali Bwana tuwahi”
“Hapana Dada linakuja spidi”
Gari la wagonjwa liliwapita kwa kasi na wao kuendelea na safari, Jaqlin hakuelewa kuwa gari hilo ndilo alibebwa Adrian na anawahishwa hospitali ya Jirani!
Walifika mpaka hospitali na kuanza kuulizia.
“Hilo jina sisi hatulijui,ni kweli tulipokea hapa wagonjwa mahututi wanne wawili walifariki jana wamebaki wawili mmoja ana wahishwa hospitalini na ambulance, nadhani mmepishana nalo kama mmetokea njia ya mjini”
“Ndi..io dokta, ni hospitali gani?”
Maelezo aliyopewa Jaqlin yalitosha kabisa kuondoka na dereva taxi mpaka hospitali ya Wilaya aliomba Mungu Mgonjwa huyo walau awe Adrian,
Nusu saa baadaye walikuwa getini ndani ya hospitali ya wilaya wanaingiza gari ndani, kabla ya Taxi kusimama Jaqlin alisharuka nje na kuanza kutembea haraka haraka mpaka ndani ya hospitali.
“Kuna mgonjwa ameletwa sasa hivi hapa na Ambulance amepelekwa chumba gani?”
Jaqlin alimuuliza Dada wa mapokezi bila kumeza mate.
“ingia Wodi namba kumi na mbili”
“Ahsante”
Ndani ya sekunde mbili alikuwa ananyonga kitasa cha mlango wodi namba kumi na mbili, jicho lake moja kwa moja alilitupa kwa mwanaume aliyewekewa bandeji uso mzima na miguu yake kuwekewa machuma huku ikiwa imening’inizwa juu, mapigo ya moyo ya Jaqlin yalimdunda kwa kasi na kudondoka chini hapo hapo.
***
Adrian Mwangenya yu mgonjwa mahututi yupo hospitali ya wilaya, ajalli mbaya aliyopata baada ya basi alilolipanda kutumbukia mlima kitonga, takribani wiki tatu na nusu alilala hospitali bila kufumbua macho yake hatimaye mwezi ulifika ndipo alipopata fahamu.
Hayo yote yana tokea Jaqlin hakuwa anaelewa lolote alishamtafuta Adrian mpaka kuchoka hatimaye kujua ni wapi alipo baada ya kupashwa habari na jirani yake.
Kitendo cha kumuona Adrian tu hapo hapo alidondoka na kuzimia hatimaye kuzinduka masaa manne baadaye!
“Nini kimetokea?”
Jaqlin alimtupia swali daktari.
“Ulidondoka wodini”
Kumbu kumbu zake zilirudi nyuma tena na kuangua kilio baada ya kukumbuka hali aliyomkuta nayo Adrian,
aliumia sana Moyoni na kutaka tena kwenda kumuona, hakukuwa na kipingamizi cha aina yoyote ile madaktari walimsindikiza mpaka wodi alilolazwa Adrian.
“Adri….an”
Kwa tabu na mateso Adrian aligeuza shingo yake, na macho yao kugongana!
hata yeye alivyomuona Jaqlin machozi yalimlenga alijikaza kisabuni asilie lakini mwisho alijikuta akidondosha machozi, japokuwa hakuelewa ni kwanini analia kwa wakati huo, hakuna mtu aliyeweza kumbembeleza mwenzake, ilikuwa ni picha ya huzuni sana mbele ya macho ya madaktari.
Jaqlin alivyomtizama Adrian ndiyo alizidi kulia na kudondoka chini na kupoteza fahamu tena, hapo hapo madaktari walimbeba harakaharaka mpaka chumba kingine ili wampatie matibabu.
“jamani huyo Mwanamke msimlete tena ndani ya hiki chumba,msije mkaleta balaa jingine mnaona kabisa hali yake hatakiwi kuwa na mawazo”
“Sawa Dokta”
Tangu hapo Jaqlin alikuwa chini ya usimamizi wa madaktari hakuruhusiwa kwenda tena kumuona Adrian sababu ya ujauzito alioubeba, walihofia wangefanya kitendo hiko wenda mimba ingeharibika na hawakutaka kitu kama hiko kitokee, Jaqlin kila kukicha alikuwa ni mtu wa kulia machozi, hakuwa na matumaini tena kama kuna uhai kwa jinsi alivyoiona hali ya Adrian, ilimtisha kupindukia.
Picha ya kifo ndiyo iliyomjia kichwani na ndiyo maana muda wote alilia kama aliyefiwa na mzazi wake!
“Dok..ta niambie tu ukweli kama Adr..ian amefariki mbona kufa ni hali ya kawaida”
“Hapana ondoa wasiwasi yupo salama kabisa”
“Hapana mbona hamtaki nikamuone kwani mimi sina haki ya kumuona mpenzi wangu?”
“Hapana siyo ivyo kuna kitu tunaepuka,lakini napenda kukuhakikishia kuwa Adrian yupo salama na atapona tu kuwa na amani kabisa, sisi ndiyo kazi yetu, kama tuliweza kuyaokoa maisha yake mpaka kufikia hali aliyokuwa nayo nina uhakika atapona kabisa”
“Mhh lakini sawa…”
“Wazazi wake wako wapi?”
“Mama yake alishafariki ila baba yake yupo”
“Anaweza akaja hapa mara moja sababu kuna mambo anapaswa kuyajua”
“Dokt…..”
“Adrian hajafariki, yupo sawa ondoa shaka kabisa, fanya mawasiliano na Baba yake”
“Lakini Daktari…….ila nitafanya ivyo”
Jaqlin aliitikia kwa shingo upande lakini hakuwa na uhakika na majibu aliyopewa.
Licha ya kupewa majibu yaliyompa moyo lakini hakutaka kubanduka hospitalini na hapo ndipo alipoamua kumtafuta Baba MZAZI wa Adrian kwenye simu kisha kumueleza ni wapi alipo.
***
Mzee Mwangenya alikaa juu ya benchi la hospitali huku mikono yake ikiwa kichwani mwili wake ukiwa umekufa ganzi, baada ya kupokea taarifa hizo kutoka kwa Daktari, hata yeye hakuamini kama Mwanaye amepona kutokana na historia ya Mlima huo kitonga wenye historia ya kuchukua roho za watu.
“Sasa Mzee nifuate Ofisini”
Dokta Sai na Mzee mwangenya walitembea mguu kwa mguu mpaka ofisini kisha kuanza mazungumzo.
“Nimeamua kukuita hapa mzee ili nikueleze hali halisi ya mambo”
“Nieleze tu mwanangu”
“Sikupenda haya mambo kumwambia mke wake nimeona sio jambo la busara”
“Kabisa…!”
“Mimi ni daktari bingwa wa mifupa,na ndiye nimekabidhiwa huyu Adrian nimfanyie Scanning kila kitu,kule hospitali tuliyotoka ameacha deni la Shilingi laki saba,hapa hospitalini anadaiwa laki nne, pointi yangu ni ipi hapa, kuna mawili yanatakiwa kutokea, nimeshindwa kumtibu mguu wake, na wagonjwa wetu mara nyingi tunawapeleka India…
Daktari aliinamisha kichwa kidogo na kumuangalia tena Mzee Mwangenya kisha kuendelea.
“Na inahitajika milioni nane kwa ajili ya matibabu, usafiri kila kitu inahitajika kama milioni kumi,kama hautakuwa tayari inabidi Mguu wake ukatwe tu,maana tutakuwa hatuna jinsi tena”
Mzee Mwangenya alimtizama Daktari mara mbili mbili machoni, hakuelewa ni jibu gani ampatie.
“Hizo ni pesa ndogo sana kwa Mwanangu, hilo litawezekana tu mara moja, hata kesho nyie anzeni kufanya utaratibu wa safari,kama kuna uwezekano wa kuongea naye naomba mnipeleke kwenye chumba chake ili aniambie utaratibu wa kunituma Dar es salaam nikafuate hizo pesa”
“SAWA hilo halina tatizo kabisa sasa hivi amepumzika tumemchoma dawa za usingizi”
“ basi akiamka inabidi nimuone”
“Ondoa shaka wacha tuanze utaratibu huo”
MZEE Mwangenya alitoa majibu kwa kujitutumua kupita kiasi,
katika maneno aliyoongea alikuwa ana uhakika nayo, hakuwa anajua kilichompata Adrian alipokuwa mjini Dar es salaam, laiti angelijua asingethubutu kufungua kinywa chake na kuongea kwa kujiamini.
Hatimaye jioni ilifika kisha kuruhusiwa na kupewa dakika Thelathini za kuongea na Adrian.
“Adrian mwanangu pole sana”
“Ahsan..te Mzee” Adrian aliitika akiwa kwenye hali ya maumivu.
“vipi sasa hivi unajisikiaje?”
“Mguu na kichwa ndiyo bado vina leta tatizo, vipi Baba .Jaqlin yupo wapi?”
“wamemkataza asije humu ndani kutokana na hali yake kuwa mbaya alafu anazimia tu akikuona”
“Ok…ay”
“Sasa Adrian”
“Naa..m Bab..a”
“Kuna pesa unatakiwa kulipa ili uwende India ukatibiwe huo mguu wako, maana hapa wameshindwa na ndio wamenieleza nije kukuambia”
“wanadai kiasi gani?”
“pesa sikumbuki ni kiasi gani lakini ni mamilioni huko, sasa inanibidi niende Dar uniagizie kwa vijana wako maana hakuna mtu wa Kwenda Mkamwana wangu ana hali mbaya”
Adrian Alikuwa ni kama ametoneshwa kidonda na kukumbushwa mambo yaliyotokea nyuma,
alimtizama baba yake huku machozi yakimlenga ki ukweli benki hakua ana uhakika kama ana salio lililofika Milioni,
alielewa kabisa Baba yake hakuelewa lolote kuhusiana na maisha yake.
Sababu Alivyomtizama aligundua kuwa ni bado anadhani wenda ni tajiri kumbe hakuwa ivyo,alikuwa ni fukara wa kutupa aliyelala tajiri na kuamka maskini, ki ujumla maisha yake yalishuka ghafla hayakutofautishwa na mtu aliyepewa laana za shangazi,
maisha kwake yalibadilika ghafla mno na ndiyo sababu inayomfanya akikumbuka hayo analia machozi mfululizo,ilikua ni picha mbaya sana kichwani kwake tena ya kusisimua,
hasa alipofikiria deni la hospitali.
Hakuelewa aanzie wapi kumueleza baba yake aliyekuwa amesimama wima anasubiri atajiwe ni wapi pesa zilipo kisha aende Dar es salaam mara moja.
“Baba”
“Naaam Mwanagu”
“kuna matatizo nilipata,sikupenda kuja na basi Mzee”
“Matatizo gani?”
Adrian alinyamaza kwa sekunde nane na kuanza kumueleza baba yake tangu alipotoka jela na kukuta nyumba pamoja na Kampuni zake zimefilisifiwa hakutaka kumwambia yote alimuhadithia kwa ufupi kinagaubaga!
Mzee Mwangenya moja kwa moja alirudisha mawazo yake nyuma na kujilaumu kwa kitendo cha kumchagulia mke kutoka kijijini na kufanya Adrian afunge safari ya kwenda Kilimanjaro Moshi ili kumuwahi Jaqlin , na ndipo huko matatizo yalipoanzia,aliamini kabisa isingekuwa yeye wenda Adrian asingefirisika kiasi hiko,Yeye ndiye alikuwa mkandarasi wa mambo yote yanayomtokea mwanaye alijuta!
Alimtizama Mwanaye wa kiume anayemtegemea bila kuamini kwa kile anachokisikia na kulengwalengwa na machozi,Kufirisika kwa Adrian ilimaanisha kuwa hata yeye muhimili wake wa maisha ungeyumba.
“Pole sana Mwanangu,sasa itakuwaje?”
“Sie..lewi Mzee”
“Naomba nisamehe mimi, najua mimi ndiye chanzo”
“Usijali wewe ni baba yangu na kwenye maisha kukosea ni kawaida,mimi nina amini kuwa kila kitu kinatokea kwa makusudi,Kama Jaqlin ana chochote mwambie atoe ili nitoke tu kwanza hapa hospitali, usimueleze kwanza kuhusu hizi habari nataka mwenyewe nimwambie”
“Sawa Mwanagu”.Wote walikubaliana.
**
Kwa BAHATI nzuri Jaqlin alikuwa ana akiba Benki ya shilingi milioni tano peke yake, hakuwahi kuigusa pesa hiyo maana aliamini ipo siku itamsaidia katika matatizo yake,ni kweli Akiba haiozi, na ndipo hapo aliponyoosha mpaka Benki na kutoa pesa, kisha kwenda hospitali kufanya malipo akiwa na wazo kuwa bado Adrian alikuwa ana pesa na pesa kama hiyo haikuwa kitu kwake.
Wiki moja baadaye Adrian aliruhusiwa Hospitali huku nyuma akipewa dawa za kupaka kwenye vidonda vyake na zingine za kumeza ili kutuliza maumivu, japokuwa Jaqlin alikuwa ana maswali mengi ya kuuliza juu ya Adrian kuruhusiwa wakati bado hali yake haikuwa sawasawa!
lakini alikaa kimnya na kusubiri wafike nyumbani kisha amtwange maswali, kilichomshtua zaidi ni mguu wa Adrian uliokuwa bado umevimba sana!
Saa kumi na mbili jioni ilivyogonga walikuwa teyari wapo Mwakaleli na Jaqlin kumlipa Dereva taxi, kisha Mzee Mwangenya na Jaqlin kumshika Adrian huku na kule ili kumsaidia kutembea mpaka chumbani kumlaza.
“Pole Mpenzi wangu”
Jaqlin alisema kwa sauti ya upole wakiwa chumbani.
“Ahsante Jaqlin”
“Vipi sasa unajisikiaje?”
“sasa hivi nina afadhali kidogo”
“jambo la kushukuru ni uhai tu,utapona taratibu,Alafu baby inabidi nikakuogeshe kwanza kisha ule ndiyo upumzike”
“Sawa”
Jaqlin alionesha Mapendo!
Japokuwa alikuwa ana mimba kubwa alijitahidi kumvua nguo Adrian kisha kuingia naye bafuni na kumsafisha kila sehemu ya mwili na wote kurudi tena chumbani, baadaye alimletea chakula na kuanza kumlisha taratibu Adrian alipata faraja.
“Jaqlin Mpenzi wangu”
“Naam baba”
“Nashukuru sana nimeshiba”
“Hapana kula wewe ni mgonjwa”
“Hapana mimi sio mgonjwa,nipo fiti hapa”
“Upo fiti wapi,wakati bado unadeka,huna lolote”
Walitaniana! Lakini Adrian alionekana hana furaha hata kidogo ilielekea kulikua kuna kitu kinamsumbua ndani ya kichwa chake, Jaqlin aliligundua hilo, kisha kumuuliza hakutaka kukaa na dukuduku moyoni.
“una tatizo gani mbona unaonekana haupo sawa Darling?”
“Nina matatizo Jaqlin ningependa nikwambie,ili usipate matatizo baadaye, naomba uwende tu kwenu ili nisikupe mzigo wa kunilea mimi pamoja na kiumbe ulichobeba tumboni”
“una maana gani Adrian kusema ivyo?”
“Ki ufupi sina mali hata moja,nimefilisiwa!”
Adrian aliongea kwa Uchungu sana huku machozi yakimlenga lenga, hakika alimpenda sana Jaqlin na hakutaka huko mbeleni aje kuteseka na ndiyo maana aliamua kumwambia ukweli usiku huo huo ikiwezekana amruhusu aende zake kwao Arusha akapumzike,
alikuwa teyari kwa lolote atakalo sema Jaqlin kwa wakati huo.
Alishaelewa kuwa mwanamke mzuri kama huyo anahitaji matunzo ana hitaji kugharamiwa na kwa wakati huo hakuwa na uwezo ukizingatia alikua mjamzito na muda mfupi angeenda kujifungua!
“Whaaaaat?”(Nini”)
Jalin alishtuka baada ya kusikia historia hiyo, hata yeye hakuamini.
“Ndiyo ivyo Jaqlin, mguu wangu utakatwa kutokana namimi kukosa pesa, Jaqlin naomba uwende”
“Hapana unanitania,hizo ni njama tu umepanga ili uniache”
“Ni kweli Jaqlin,niamini nayosema sina sababu ya kukufanyia maigizo”
Jaqlin aliangua kilio cha kwikwi.
Usiku mzima hawakulala,wote walilia machozi kama watu waliofiwa, kila mtu alishindwa kumfuta machozi mwenzake, ilikuwa ni kama wanaigiza filamu ya kihindi.
**
Kulivyokucha Asubuhi Adrian alipapasa mkono wake upande wa kushoto ili amguse Jaqlin lakini hakumuona, alivyogeuza shingo yake Alichanganyikiwa zaidi, baada ya kugundua kuwa begi la nguo za Jaqlin halipo, alishaelewa nini maana yake,alishaelewa kuwa amekimbiwa na Jaqlin hakuweza kubaki naye tena kwa sababu ya umaskini aliokuwa nao ghafla,
alijikuta amekaa kitandani mashavu yake yamelowana kutokana na machozi yaliyoanza kumtoka ya uchungu aliona maisha yatakuwa bure bila Jaqlin.
***
Hakuamini kuwa Jaqlin mwanamke anayempenda kwa dhati amemkimbia na hayupo naye tena na ndiye aliyedhani atakuwa faraja yake katika kipindi hiko cha dhiki lakini haikuwa ivyo.
Maisha yake alidhani yana mikosa au laana Mali kufirisiwa,kupata ajali na kukimbiwa na mwanamke aliyepanga kuja kuishi naye hapo baadaye kufa na kuzikana.
Alivyokumbuka hayo tu alijikuta akilia kila siku.
Wakati mwingine alidhani yupo ndotoni anaota njozi ya kutisha na baadaye angeshtuka na kukuta analetewa kahawa ofisini kwake, lakini haikuwa ivyo mambo yaliyokuwa yanamtokea yalikuwa yana ukweli halisi kabisa!
Kilichomchanganya zaidi ni kutokupatikana kwa Jaqlin hewani siku tatu mfululizo akizidi kumtafuta,alibaki akisononeka, hakuwa na utofauti na mwanadamu aliyefiwa na wazazi wake wote wawili.Majirani waliokuja kumuangalia walisononeka machoni lakini mioyoni walifurahi sana kuona mtoto wa Mzee Mwangenya kafirisika.
“Mwanangu ndiyo maisha hayo,inabidi tu uchukulie ni sehemu ya historia katika maisha yako”
Baba yake mzazi alimfariji kila kukicha na kumpa moyo.
**
Kila kukicha hali ya Adrian ilizidi kuwa nzuri tu kiafya lakini kilichomtesa zaidi ulikuwa ni mguu, kidonda chake kilikuwa kigumu kukauka na kufanya kitoe maji maji, kwa mara ya kwanza walikitafutia dawa lakini kadri siku zilivyozidi kwenda kilizidi kuchimba ndani kwenye mfupa na kuanza kutoa maji maji yanayotoa harufu kali sana na wakati mwingine mpaka usaa kabisa,
majirani waliwasema vibaya lakini hawakuwa na jinsi yoyote ile.
“Sasa Wewe mzee unafikiri sisi tutaishije hapa kwa hali kama hiyo?”
Mama mmoja wa jirani aliuliza asubuhi kulivyokucha.
“Sijakuelewa Mama Tiko”
“Hamuoni kama mnatia harufu jamani, hatupati usingizi usiku”
Adrian aliyekuwa ndani alimsikia mama huyo kwa masikio yake yote mawili, alilia kwa uchungu, tangu siku hiyo hakuna hata jirani mmoja aliyefika kumwangalia, walimuona kama kinyesi, nzi walitapakaa ndani ya nyumba,Wakati Mwingine alimlaani Mungu wake ni kwanini alizaliwa Duniani, au ni kwanini aliruhusu yeye apate matatizo ya gafla kiasi hiko. Hakuwa kama binadamu wengine!dunia ilimbwaga na kumpa kisogo, mambo yalikuwa kinyume kwake.
Historia yake ya nyuma ilimkumbusha mengi sana, hasa alipowakumbuka marafiki zake waliomtenga na ndiyo hao aliokuwa akila nao maisha siku za nyuma zilizopita!.
“Baba”
“Naam Mwanagu”
“Mimi naona huu mguu ushakuwa kero hata mimi unaniuma utautibu mpaka lini?”
“Una maana gani sasa kusema ivyo?”
“Bora ukatwe tu niondokane na fedhea bora nibaki na mguu mmoja peke yake”
“Hapana Adrian Baba yako nitapambana, nitauza hata mashamba yote ili mguu huo upone”
“Usifanye ivyo mzee, Mashamba hayo ndiyo utajiri uliobaki, unadhani ukifanya ivyo itakuwaje.. mimi nimeamua kwa ridhaa yangu naomba mguu ukatwe, japo sio kwa mapenzi yangu, naona ukikatwa utakuwa umenisaidia sana”
Adrian alisisitiza sana.
Ni kweli maumivu ya mguu aliyokuwa akihisi aliona ni heri auondoe kabisa kuliko kuendelea kuteseka nao.
Mzee Mwangenya hakuwa na jinsi, siku hiyo hiyo alitafuta mteja na kuuza Ng’ombe zake watatu ili Adrian aende hospitalini na mguu ukwate!
Alivyopata malipo, kesho yake aliwaaga majirani,baada ya hapo alimchukua Adrian mpaka kwenye taxi kisha safari ya kwenda Hospitali kuanza.
Adrian njia nzima alikua akilia machozi, hasa alipofikiria kuwa maisha yake yote atakuwa na mguu mmoja peke yake.
Licha ya yote lakini hakutaka kujilaumu sana sababu ndiyo maamuzi aliyoyachukua tayari.
Walifika Hospitali na kupewa karatasi ya kujaza, kila daktari aliyeuona mguu wa Adrian alishika kichwa chake sababu ulikuwa umeshaoza tayari hautamaniki hata kidogo!
Dakika mbili baadaye aliitwa ndani ya chumba maalumu kisha kupandishwa juu ya kitanda ili mguu wake ukatwe na mashine maaulumu ambazo zilikuwa teyari zimeletwa.
“Huyu ana ugonjwa hatari sana kitaalamu unaitwa Osteoporosis ungemsababishia kansa ya damu baadaye, ni bora hata umechukua uamuzi wa kukatwa huu mguu. osteoporosis ni ugonjwa hatari sana wa mifupa”
Alisema Dokta huku akivuta dawa ndani ya Bomba! Adrian alikuwa ametulia yupo tayari kwa kile kitakachotokea, hakuamini kuwa baada ya kufumbua macho yake atajikuta na mguu mmoja.
Alichomwa sindano za nusu kaputi . HAPO hapo macho ya Adrian yalijaa ukungu na kuona giza mbele yake baada ya dawa hizo kali kumchukua alilala fofofo.
***
Njia nzima Jaqlin alilia machozi akiwa ndani ya basi la HOOD akielekea jijini Dar es salaam kisha baadaye achukue basi jingine litakalo mpeleka Mkoani Arusha,
Moyoni aliumia sana kwa kitendo cha Adrian kufirisika na kilichomuuma zaidi mguu wake kutaka kukatwa na zilizihitajika pesa nyingi kwa ajili ya kuzuia mguu wake usikatwe.
“Dada upo sawa?”
Abiria mwezake alimuuliza baada ya kumuona Jaqlin analia machozi huku akiwa ana mimba yake kubwa, Picha iliyomjia abiria huyo kuwa wenda Jaqlin alifukuzwa na mume wake.
“Ndi..o nipo sawa nasumbuliwa tu na kichwa”
“Sasa kwanini usimwambie kondakta, ili upatiwe dawa”
“Usijali nishameza dawa tayari”
“Pole dada”
“Ahsante”
Mpaka basi linafika Ubungo saa tatu ya usiku Jaqlin hakuweka kitu chochote mdomoni isipokuwa maji tu peke yake,
alivuta begi lake na kushuka, hapo alitafuta Nyumba ya wageni kisha kulala ili kesho yake apande basi za Arusha, ilikua ni lazima afike Arusha kesho yake. Hakuweza kulala hata kidogo, alivyotaka kumtafuta Adrian simu yake haikuwa na chaji,
hakulala. ilivyogonga saa kumi ya asubuhi alioga harakaharaka na kunyoosha mpaka ubungo!
Alipata tiketi siku hiyo hiyo ya kampuni za MTEI,Saa kumi na mbili lango la Ubungo lilikuwa wazi na mabasi kuruhusiwa ya mikoani!
Njia nzima ilikuwa kama alivyotoka Mbeya, alilia machozi hasa alipomkumbuka Adrian mwanaume anayempenda, ilikua ni lazima atafute pesa ili arudi na kumuokoa asikatwe mguu, lakini swala hilo ilibidi aliweke siri hata wazazi wake wasijue lolote!
Hatimaye masaa kumi na moja yalikatika ndipo alipofika Arumeru, hapo alichukua taxi iliyompeleka nyumbani, mpaka anafika nyumbani kwa wazazi wake alikuwa hoi bin taaban amechoka.
Mama yake mzazi alipomuona kidogo adondoshe chozi, Jaqlin alikuwa amekonda mabega yamempanda juu lakini mimba ilitokeza na kuwa kubwa.
“Mama Shikamoo”
“Marahaba! Vipi Mwan..angu umefukuzwa?”
“Hapana Mama kwani vipi mbona unalia?”
Katika mazungumzo waliyoongea, Jaqlin hakutaka kuonesha hali yoyote ile ya kuwa ana shida ya aina yoyote, walipo muuliza habari za Adrian aliwaambia yupo mzima wa afya.
“Hongera mwanangu,naona unataka kutuletea mjukuu”
“Ndio Mama,nawewe upate kuitwa Bibi”
Mzee Mshana usiku aliporudi furaha iliongezeka baada ya kumuona Binti yao, ni muda mwingi sana hawakumtia machoni, usiku mzima walikula kwa pamoja na kuongea mambo mengi sana, hawakuelewa kuwa Jaqlin ana matatizo aliyoyaficha na tabasamu lake muda wote.
“Sasa mbona haukuja na Mzee?”
“Kazi nyingi, sasa hivi amefungua tawi jingine huko Mbeya kwao la kampuni ivyo tulikuwa tunasimamia kidogo lakini atakuja amesema, anawasalimia sana”Jaqlin alitoa jibu la uongo.
“Mhh hongereni sana”
“Vipi za kwenu, Mama niliwamisi mjue”
“Hata sisi”
Siku hiyo ilipita!
Kila kukicha Jaqlin alifikiria jinsi ya kupata pesa, lakini ghafla mawazo ya binamu yake yalimjia, alikuwa tajiri sana na isitoshe walikuwa wote,asubuhi kulivyokucha aliwasha gari ya Mama yake mpaka ofisini kwa binamu yake.
“Namuulizia Martin Phares yupo?”
“Ndio lakini ana mgeni”
“Sawa basi akitoka mwambie Jaqlin Mshana anahitaji kumuona”
“sawa,pumzika tu kwenye kiti”
Baada ya mgeni kutoka Jaqlin aliingia mpaka ndani ya ofisi ya mkurugenzi Martin Phares, wote walishangaana, ni miaka mingi sana ilipita tangu waachane, ilikuwa ni furaha kubwa sana kwao, baada ya salamu Jaqlin alieleza shida yake ya kiasi cha shilingi milioni themanini kama ikiwezekana atamlipa.
“Mbona pesa nyingi kiasi hiko?”
Martin Phares aliuliza huku akisimama kwenye kiti chake na kumuendea Jaqlin huku akimtizama!
Jaqlin alivyoyaona macho yake alielewa nini anachotaka Martin kwa wakati huo.
“Lakini nitakusaidia wala usijali,wewe ni binamu yangu lakini nawewe inakubidi ujiongeze”
“Kivipi sijakuelewa”
“WEWE ni binamu yangu naelewa, lakini ni mrembo sana isitoshe sawa ni mjamzito naona hapo,unajua muda mrefu sana nilikua natamani nafasi kama hii itokee lakini Mungu ni Mkubwa umekuja sasa”
“Sijakuelewa Martin”
Mwanaume Martin bila aibu alimsogelea Jaqlin na kuanza kumtomasa Maziwa yake huku akijipigia debe kuwa anataka ngono ndipo aweze kumsaidia.
Hasira zilimkaba kooni Jaqlin hakutegemea kabisa kama angeambiwa maneno kama hayo tena na binamu yake, hakuwa tayari kupanua miguu yake kwa mwanaume yoyote Yule, sababu alishaweka uaminifu kwa Adrian, hapo hapo aliyakusanya mate mdomoni na kumtemea Martin usoni kisha kusimama kwa ghadhabu.
“Stupid,Stupid, hivi unanichukuliaje Martin?…mimi sijaja kujiuza hapa”
Jaqlin alibeba pochi yake mkononi na kuuendea mlango.
“Najua utazunguka kote lakini utakuja hapa”
Jaqlin alishusha ngazi haraka haraka na kurudi ndani ya gari akiwa ana machozi mengi!
**
Wiki mbili sasa zilipita baada ya kuomba msaada kwa marafiki bila mafanikio hakua na chaguo lingine zaidi ya kufanya maamuzi magumu,
siku hiyo asubuhi alinyoosha mpaka mjini kwenye maduka ya Baba yake na kuanza kupita moja kwa moja kwa wafanya kazi wa baba yake.
“BABA amenituma, ameniambia unipe mauzo yote ya duka”
“Sasa si mpaka tumpigie simu jaquee?”
“Huniamini, hivi mfano sasa hivi nikimpigia simu na nikimwambia kuwa huniamini huoni kwamba utafukuzwa kazi?”
“Ndio”
“Sawa.. basi ndiyo amenituma”
“okay sawa”
Alipita kila duka na kukusanya pesa zote za mauzo hatimaye kupata kiasi cha shilingi milioni tisini na tano! Hapo hapo alikwenda benki na kuzihifadhi, alirudi nyumbani haraka haraka na kuanza kupanga nguo zake ndani ya begi tayari kwa safari ya kwenda Mkoani Mbeya Mwakaleli,siku hiyo hiyo!
Alivyohakikisha kila kitu kipo sawa aliandika ujumbe mfupi juu ya karatasi na kutoka nje kwa safari moja tu kurudi Mbeya ili afanye utaratibu wa Adrian asafirishwe mpaka India kwa ajili ya matibabu yake ya Mguu, lakini hakuwa ana uhakika kama angekuta mguu wa Adrian bado upo.
“Wazazi wangu mtanisamehe”
Aliongea Jaqlin akiwa nje ya geti anapanda taxi itakayo mpeleka Stendi.
***
WAZAZI WANGU NAOMBA MNISAMEHE KWANI NAJUA NILICHOFANYA SIO KITU KIZURI LAKINI NAPENDA KUWAHAKIKISHIA KUWA NIPO SALAMA, MSIHANGAIKE KUNITAFUTA,NIMECHUKUA PESA HIZI NINA SHIDA NAZO SANA! MBAKI SALAMA, WENU MUMPENDAYE JAQLIN.
Barua hiyo ilikutwa chumbani kwa Jaqlin ikiwaacha wazazi wake wakiwa wamechanganyikiwa hasa walipoiona laini ya simu ya Jaqlin mezani kumaanisha kuwa hakutaka mawasiliano nao.
***
Safari ya siku mbili ilimchosha sana, japokuwa alifika jioni ya saa kumi na mbili Mbeya Mwakaleli lakini hakutaka kupumzika hata kidogo, alichanganyikiwa zaidi alipoambiwa kuwa Adrian amepelekwa Hospitalini kukatwa mguu, haraka haraka alipanda taxi mpaka Hospitali aliyoelekezwa, kwa shida sana alikimbia mpaka mapokezi kumuulizia Adrian.
“Ndio yupo kwenye chumba cha upasuaji”
“Ndio kipo wapi?”
“Hauruhusiwi kuingia dada”
“Niambie kilipo”
“Nyoosha moja kwa moja kushoto, chumba cha kwanza kulia kwako”
Jaqlin alianza kutembea haraka haraka kwa hatua mbili mbili, lakini alivyokunja kona alikutana na Daktari akitoka ndani ya chumba cha upasuaji huku gloves zake zikiwa zimelowana na damu, dalili zilionesha kuwa Adrian teyari keshakatwa mguu na kusafiri kwa Jaqlin kwenda Dar es salaam na kuiba pesa ilikuwa ni kazi ya kutwanga maji kwenye kinu.
****
Kidonda cha Adrian ndani ya mfupa wake mguuni kiliwaogopesha madaktari sana,hawakutegemea kama kilijichimba kiasi hiko na kufanya wadudu waingie na kutoa usaa,ilibidi wakisafishe kwanza kabla ya kuukata Mguu wake kuepusha kansa ambayo ingesababishwa na wadudu hao baadaye, na ivyo ndivyo alivyoshauri Daktari Bingwa wa mifupa Towo,alivyoona kidonda hiko ndani ya mguu alishika mdomo wake,
kwani kiliharibu mifupa na kusagika.
“Inabidi kwanza tukisafishe hiki kidonda la sivyo hapa tutakuwa tunafanya kazi bure kukata huu mguu, hawa wadudu wataacha bakteria na wataendelea kuzaliana”
Dokta Towo aliendelea kushauri na jambo hilo kufanyika mara moja! Wakati hayo yanaendelea Adrian alikuwa nusu kaputi amechomwa sindano ya kulala takribani masaa Sita,
haelewi kinachoendelea kayafumba macho yake hakutofautishwa na mtu aliyekufa kwa wakati huo.
Madaktari walizidi kuukarabati mguu wake kisha baada ya hapo waukate. Waliupaka spirit na kukata nyama za juu kisha kupaka dawa nyingine aina ya anti biotic ili kuua bakteria walioanza kuzaliana na kusababisha harufu kali kutoka na kusambaa.
Hapo ndipo Dokta Towo alipochukua mikasi tena na kuanza kukwangua mfupa wa Adrian kwa juu karibu na goti, damu nyingi sana zilitoka,kitendo hiko kilidumu masaa matatu peke yake. Baada ya zoezi hilo kukamilika lilibaki sasa kuukata mguu wa Adrian kwa sababu alikosa pesa za matibabu za kuutibu na ndiyo maana leo hii unakatwa, ulisha fika usiku tayari lakini ilikua ni lazima mguu huo ukatwe!
Dokta Towo alitoka chumba cha Upasuaji ili kwenda kuchukua mashine nyingine za kukata mifupa ofisini kwake na ndiyo hapo alipokutana na Mwanamke mjamzito mbele yake akiwa anahema juu juu kama aliyetoka kukimbia riadha za mbio ndefu.
“Dada vipi mbona ivyo unahema juu juu kama Bata?”
“Dokta nina shida nawewe”
“Hapana sio wakati wake, nina mgonjwa anahitaji matibabu subiri kidogo kwenye benchi pale”
“Hapana siwezi kusubiri ni shida ya muhimu naomba unisikilize”
Japokuwa Dokta Towo alikuwa ana haraka lakini Jaqlin alimsihi kuwa amsikilize.
Ni kweli alikuwa ana shida sana yeye peke yake ndiyo kwa wakati huyo alikua ana uwezo wa kuzuia mguu wa Adrian usikatwe na ndiyo maana alienda Mkoani Arusha kuiba Pesa ili kufanya zoezi hilo lisitokee.
Waliongozana na Daktari mpaka ofisini kisha kuketi na kuanza mazungumzo!
Jaqlin aliongea akiwa ana kwikwi nyingi mpaka kushindwa kumalizia anachokiongea kutokana na kulia mfululizo.
Bado daktari hakuelewa nini hasa kina mliza Mwananke aliyekuwa ameketi mbele yake.
“Mimi naitwa Jaqlin”
Alijitambulisha baada ya kujikaza.
“Ndio Jaqlin”
“Kuna mgonjwa nimeambiwa kuwa yupo kile chumba ulichotoka kabla ya kuanza mazungumzo naomba uniambie kama keshakatwa mguu. tayari au bado?”
“Ndio nimekuja kuchukua vifaa hapa,ili niendee kuushughulikia mguu wake mara moja, kama hutojalia naomba unione nikitoka”
“Mimi ni mke wake, hauna sababu ya kwenda kuendelea, nimeleta pesa ili akatibiwe India, tafadhali naomba ufanye mawasiliano na hao madaktari wa huko bila kupoteza muda”
Dokta Towo alishtuka sana na kumuonea huruma Jaqlin aliyekuwa mbele yake anaongea kwa huzuni,alilitizama Tumbo kubwa alilokuwa nalo na kuzidi kusikitika, alijiona ni mtu aliyekwenda kubeba dhambi kubwa kwa kitendo cha kutaka kukata mguu wa Mume wa mwanamke mja mzito.
“Pole sana ngoja nianze kufanya utaratibu huo mara moja”
Dokta Towo alisimama haraka haraka mpaka kwenye chumba cha operesheni kisha kuwa taarifu madaktari wenzake alichoambiwa!
***
Mawasiliano yaliruka usiku huo huo mpaka Nchini India Appolo Hospital na kupewa taarifa ya mgonjwa watakaye mpokea kesho yake.
Lisaa limoja baadaye kila kitu kilikuwa kimeandikwa likijumuishwa na swala la uhamisho wa Adrian kwenda Mumbai.
“Sasa ataenda na nani?”
Dokta Towo alimuuliza Jaqlin baada ya taratibu zote kukamilika.
“Nitaenda naye mimi, nitakuwa namuangalia”
“Na hali hiyo uliyonayo?”
“Ndio! itabidi nifanye ivyo siwezi kukaa mbali naye”
Ki ukweli kwa hali aliyokuwa nayo Jaqlin hakupaswa kuzunguka popote pale,alikuwa katika siku za usoni za kujifungua, tumbo kubwa sana alilokuwa nalo liliwashtua madaktari,walimshauri abaki lakini alikataa katukatu akidai kuwa hakutaka kukaa mbali na Adrian.
“Sawa kama umeamua ivyo hakuna tabu, kuna gari litakuja hapa la wagonjwa litawapeleka mpaka Songwe, hospitali ya pale jirani hapo mtapanda ndege ya Saa moja asubuhi kesho yake”
“Sawa Daktari ahsante kwa kila kitu”
Haikupita hata dakika sitini gari la wagonjwa lilikuwa nje kisha Adrian kupakiwa, bado alikuwa hana fahamu zake,
dawa za nusu kaputi zilikuwa bado zipo mwilini.
Jaqlin nayeye alipanda ndani ya gari la wagonjwa kisha Gari hilo kuanza kupiga king’ora huku likianza safari!
Jaqlin muda wote alikuwa haamini kama alishinda kile alichokuwa amekipanga, alilia kwa furaha huku akimtizama Adrian aliyekuwa bado amelala,
aliinamisha kichwa chake na kuanza kumbusu mdomoni yaani alimpiga denda la kama dakika mbili nzima.
“Nakupenda sana Adrian mume wangu sijui ni kipi kitakuja kututenganisha”
Aliongea maneno hayo peke yake tena kwa hisia kali kutoka ndani ya moyo wake.
Lakini alipokumbuka alichowafanyia wazazi wake moyo ulimuuma,kwa jambo alilolifanya la kuiba pesa za baba yake, licha ya kuumia sana moyoni aliamini kuwa anafanya kitu sahihi na ipo siku pesa hizo zitazaa mara mia tatu zaidi, hiko ndiko alichoamini.
Kitendo cha Adrian kufumbua macho yake, jambo la kwanza aliutizama mguu wake kwa uchungu akiamini kuwa hatoukuta, lakini cha ajabu aliuona, hakuelewa ni kitu gani kimetokea, sababu mara ya mwisho alikuwa chumba cha upasuaji tayari kwa mguu wake kukatwa,
alivyopiga jicho pembeni moyo wake ulilipuka, alivyomuona Jaqlin ameweka mikono yake mashavuni anaangalia dirishani.
Kumbukumbu zake zilikaa sawa na kugundua kuwa yupo ndani ya gari lakini hakujua kwanini na wapi anaenda, hakuelewa ni saa ngapi Jaqlin alifika, ilikua ni kama ndoto kwake kumbe ni kweli!
“Jaqli…n”
Adrian aliita.
“Darling unaendeleaje?” uso wa Jaqlin ulichanua tabasamu.
“Mbona sielewi,umefikaje mahali hapa na imekuaje?”
“Nitakuhadithia mpenzi,lakini kifupi sasa hivi tunaenda songwe kisha asubuhi tunaenda India”
“Kufanya nini?”
“kutengeneza mguu wako”
Mpaka wanafika hospitali ya Songwe Adrian hakuamini hata kidogo,bado alidhani anaota na atashtuka baadaye, akijikuta yupo na mguu mmoja.
Alimtizama Jaqlin kwa umakini bila kummaliza na kuonekana akitafakari vitu vingi, hakuelewa ni kitu gani akifanye.
Madaktari waliopewa taarifa juu ya ujio wa Adrian walifika mara moja na kumtoa ndani ya gari kisha kumuweka kwenye kitanda kingine chenye magurudumu, na kunyoosha moja kwa moja ndani ya chumba cha wagonjwa maalumu yaani V.I.P chenye vitu kama kiyoyozi,televisheni na mengine kadhalika chumba kama hiko hutibiwa wagonjwa wenye pesa au vigogo mbalimbali kama ikitokea wakifika katika hospitali hiyo,
na ndiko hiko chumba alichotaka Jaqlin ili Adrian alazwe.
“Baby mguu unauma kwani?”
“Hapana sio s….”
Kabla ya Adrian kumalizia sentensi yake alinyonywa mdomo na kuanza kubadilishana ndimi zao kama njiwa, ilikuwa ni furaha sana kwa Jaqlin kupita maelezo!
“Jaqlin”
Adrian aliita baada ya kuachiana.
“Abee Mpenzi “
“Samahani kwa kukuwazia vibaya nilijua umenitoroka kisa nimefirisika”
“Hapana siwezi kufanya ivyo maisha yangu yote,nakupenda mpaka kufa Adrian siwezi kukuacha nakupenda kutoka moyoni,nitakuhadithia kila kitu ukishapona”
Siku hiyo hawakulala Jaqlin alitumia muda huo kumfariji Adrian kuwa atapona.
“Lakini Darling”
“Abee”
“Kwanini usingepumzika na hiyo hali huoni kuwa unajitesa?”
“Hapana Adrian,sitaki kukaa mbali nawewe tena,tutaenda wote huko huko”
Wote walikuwa wenye furaha wakisubiri kukuche ili waanze safari.
***
Kitanda cha Adrian kiliburuzwa mpaka ndani ya gari kubwa maalumu la kubebea wagonjwa asubuhi kulivyopambazuka, kisha kuingizwa ndani na Jaqlin kufuatia pamoja na baadhi ya madaktari walioteuliwa kwenda nchini India jijini Mumbai.
Safari ilianza mara moja asubuhi mpaka uwanja wa ndege Songwe na Adrian kushushwa.
Mpaka hapo tayari walikuwa na tiketi zao za Air India pamoja na hati zao mikononi.Kitanda cha Adrian kilipandishwa ndani ya ndege sehemu maalumu kisha Jaqlin kuingia na kuketi siti yake aliyopangiwa, alitamani safari nzima akae na Adrian lakini ilishindikana,
Ilibidi Adrian awekwe chumba maalumu ambapo mguu wake ulifungwa vizuri na machuma ili usiweze kutingishika akiwa amelala juu ya kitanda. Kipaza sauti kilitangaza sauti ikitokea kwa msichana mrembo ili abiria wote wafunge mikanda kwenye siti zao sababu ndege hiyo inaenda kuwa angani dakika kumi na tano baadaye!
Baada ya abiria kufunga mikanda kwenye siti zao.Ndege taratibu ilianza kutembea kisha baadaye kuchanganya mwendo, ilianza kuinuka kwa mbele kisha matairi ya nyuma kufuata, na matairi yote kuingia ndani, ilikwenda juu na kukaa sawa angani, Jaqlin muda wote ndani ya ndege alikuwa ni mwenye furaha na kuchukulia hiyo ni kama ndoto kwake!
Shirika la ndege ya kimataifa la Air India ilizidi kutoboa mawingu na kusonga mbele baada ya kutoka Mkoani Mbeya Songwe.
Jaqlin muda wote alikuwa mwenye furaha kupita kiasi,aliwaza mengi sana akiwa ameketi ndani ya ndege hiyo,mambo mengi sana yalipita ndani ya akili yake akimuwaza Adrian aliyefanya mpaka aibe pesa kwa wazazi wake,aliamini kuwa asingefanya ivyo asingepata pesa kwa sababu ya wazazi wake kuwa wabahili mno, alimuelewa sana Mzee Mshana baba yake, kuiona shilingi mia yake basi umefanya kazi ya ziada, ilikuwa ni lazima achukue pesa kwao kwa namna yoyote ile, hata kuvamia benki, ilimradi mguu wa Adrian usikatwe na ndiyo ivyo alivyopanga endapo swala la kukusanya pesa kwenye maduka ya baba yake lingefeli!.
“it seems your very excited beautiful”(inaonekana una furaha sana mrembo)
Mwanaume mmoja wa kizungu alivunja ukimnya aliyekaa na Jaaqlin ni baada ya kumuona ana tabasamu mwenyewe.
“Yeah! yes why not,your very right”(Ndio,Ni kweli kwanini nisiwe, upo sahihi kabisa)
Jaqlin alizidi kuongea kwa furaha kumaanisha kuwa kuna kitu ndani ya moyo wake kilimfanya awe katika hali hiyo na si kingine bali ni Adrian kwenda India.
“Can you tell me why your excited”(unaweza ukaniambia kwanini una furaha)
“Ohh by the way am Maxmillian Godfrey”(Ohh hata ivyo naitwa Maximilian Godfrey)
Walitambulishana kisha kupeana mikono huku wakitabasamu.
Maxmilian Godfrey alionekana kuvutiwa na Jaqlin hapo hapo na kumtamani, kazi aliyoifanya ni kumsifia sana na kumwambia ni jinsi gani alivyokuwa ni tajiri ana miliki visiwa vya mafuta uarabuni na viwanda mbali mbali.
Alizidi kummiminia sifa za kutosha ambazo zingine aliongeza chumvi zaidi!
“I would like to be with you one day I don’t care either you have a husband or what”(Ningependa kuwa nawewe siku moja sijali kama una mume wala nini).
Maxmilian alizidi kumuimbisha Jaqlin bila kujua teyari maongezi yake yalishakuwa kero muda mrefu na yaliharibu furaha ya Jaqlin iliyokuwa moyoni ya kumpeleka Adrian katika Hospitali ya Appolo ili akatibiwe mguu wake, alijuta kwa kitendo cha kumuonesha mazoea Mzungu huyo.
“I like your skin colour,you look like Alicia keys do you know Angelina Julie? Who is your husband? is he rich than me? Talk to me my angel"(Nimependezwa na rangi ya ngozi yako, unafanana na Alicia Keys, unamfahamu Angelina Julie, nani mumeo, ni tajiri zaidi yangu,sema nami malaika)
Maximilian alizidi kujipigia debe akimsumbua Jaqlin ambaye tayari alipandwa na hasira mno, hakuelewa anazungumza na mwanamke aliyekuwa ana msimamo kiasi gani.
“Stop please, just leave me alone”
Jaqlin alifoka kwa sauti kubwa na kufanya abiria waliolala vitini wageuke nyuma sababu walishtuka sana. Msichana mrembo mrefu kiasi aliyevalia nguo za bluu alifika mahali alipoketi Jaqlin na Maxmiliani ili kujua nini tatizo.
“Am not comfortable here, can I shift to another seat if possible?”
Jaqlin aliomba abadilishiwe siti, hakutaka kukaa kabisa na Maxmiliani ambaye alionekana kuwa msumbufu kwake.
Kwa bahati nzuri nyuma kabisa kulikuwa kuna siti iliyokuwa na mtu mmoja peke yake, hapo alipata ahueni na kutua mzigo wa maneno ya Maximilian.
****
Baada ya kutembea kwa muda mrefu angani Kipaza sauti kilisikika kuwa abiria waweze kufunga mikanda yao kwani Ndege inaenda kushuka mjini Mumbai.
Moyo wa Jaqlin ulichanua tabasamu alijawa na furaha mara zote kwani aliamini kufika kwake salama ndiko kitu pekee alichokitaka,Kichwa cha ndege kilielekea chini kisha kutoa matairi yake na kukanyaga ardhi ya nchi ya India huku ikitingishika kidogo kisha kukaa sawa,hapo ilikwenda kasi na mwishowe kutulia.
Magari maalumu yaliyobeba Ngazi yalifika mara moja kisha abiria kuanza kushuka,ndani ya akili ya Jaqlin alimuwaza Adrian peke yake na kitendo cha kushuka tu alimuendea muhudumu wa ndege ili kujua mpango mzima.
“Subiri abiria wote washuke, kuna gari maalumu litakuja, inakubidi usubiri kidogo usitoke mahali hapa”
“Sawa nitafanya ivyo”
Baada ya kujibu hayo Maximilian alijipitisha mbele yake na kumuaga huku akimkonyeza na kumpiga busu la mbali mbali, ilionekana dhahiri ni jinsi gani mzungu huyo alivyodata na kukolea na uzuri wa Jaqlin asilia.
Hawakukaa sana walisikia king’ora cha gari la wagonjwa kisha baadaye madaktari maalumu kuingia ndani ya ndege na kumtoa Adrian akiwa juu ya kitanda taratibu ili mguu wake uliowekewa machuma usiweze kutingishika.
Jaqlin, Adrian pamoja na wauguzi wa kihindi waliingia ndani ya gari la wagonjwa na gari hilo kutimua mbio huku juu likiwa linawaka taa ya rangi nyekundu, hapo ilikua teyari imetimu saa tatu ya usiku.
Baadaye Gari la wagonjwa liliegeshwa nje ya hospitali ya Appolo kisha wauguzi wengine kutokeza wakiwa na haraka sana na kumshusha Adrian mbio mbio.
Hawakutaka kupoteza wakati hata kidogo, kitanda kiliburuzwa na kumuacha Jaqlin mita kama kumi hivi.
“Subirini kwanza tafadhali nataka niongee na mke wangu”
Alisema Adrian baada ya kumuona Jaqlin anateseka akikifuata kitanda huku akipata shida kutokana na Mimba aliyobeba.
“sawa tunakupa dakika mbili tu”
Kitanda kilisimamishwa, hatimaye Jaqlin kwa Shida alikifikia huku akihema sana kutokana na kukimbia.
“Adriiaaan, nakupenda mpenzi wangu, yote haya nafanya kwa ajili yako, tafadhali katika moyo wako tambua kuwa nyuma yako kuna Jaqlin nikupendaye kwa dhati,sina cha zaidi ila nitahakikisha nitakuwa nawewe bega kwa bega Mungu akutangulie”
Jaqlin aliongea na kumbusu Adrian usoni huku akitokwa na machozi na kulowanisha mashavu yake, hakuelewa ni kipi hasa kilimtoa machozi kiasi hiko, ni mapenzi ya kweli yaliyokuwa tayari yameota mizizi moyoni mwake.
“Jaqlin, usilie mpenzi nitakupenda kufa kuzikana, wewe ndiye mke wangu wa maisha,na ninaelewa unanipenda kwa dhati hakuna mwanamke mwenye mapenzi ya kweli hapa duniani isipokuwa wewe”
Walizungumza kwa kama dakika mbili mbele kisha kitanda kuanza kusukumizwa na manesi kuelekea katika chumba cha upasuaji ili waukarabati mguu wake.
Zoezi hilo lilianza mara moja, lilisimamiwa na Dokta Shamir ambapo nyuma yake walifuata madaktari bingwa wengine tisa wakiushambulia mguu wa Adrian, kila daktari alishika kifaa chake kisha Adrian akachomwa sindano kali za dawa zilizomfanya alale masaa matano zaidi.
****
“Sasa inakuaje shoga yangu, mimi ndiyo ivyo nimeweka matambala tumboni sielewi itakuwaje mwisho wa siku, na miezi tisa ishafika sasa mume wangu akihitaji mtoto nitamuonesha nini?”
“Wewe usijali,usijishtukie wala nini,mimi nitajua cha kufanya wewe andaa mpunga, akitoka huko alipo atakuta mtoto tayari ”
“Kweli?”
“Mimi ndiye mimi kila kitu kitaenda sawa kabisa wala usiwaze”
**
Uchungu wa Kuzaa ulimbana Jaqlin akiwa hapo hapo Hospitali ya Appolo anamfanyisha Adrian mazoezi ya kutembea, Alisha tembelea kiti chenye matairi, sasa alitakiwa kutumia magongo ili mguu wake upate nguvu, Jaqlin alichukua jukumu hilo nayeye akilijumuisha na swala lake la Mimba akisingizia anafanya mazoezi na mpenzi wake,
na ndipo hapo uchungu wa mimba ulimbana na taratibu kwenda chini.
Nesi aliyekuwa karibu alimuwahi Jaqlin na kumdaka kabla ya kufika chini.Madaktari walifika hapo haraka haraka na kumpeleka chumba cha kumzalisha.walimuweka kitandani kwa kasi ya umeme huku Jaqlin akiendelea kupiga kelele za uchungu.
Madaktari walimuweka kati na kukizunguka kitanda chake.
“Bana pumzi Mama! Sukuma mtoto atoke”
Jaqlin alijikakamua huku jasho jingi likimtoka mwilini lakini zoezi hilo la kutoka kwa mtoto lilishindikana.
“Imeshindikana Mama bana Pumzi jitahidi kwa nguvu, sukuma”
Bado zoezi lilikuwa gumu sana, hapo ndipo Dokta Kheri alipotoa wazo kuwa apelekwe chumba cha upasuaji ili ajifunguwe kwa operesheni, jambo hilo lilifanyika wakati huo huo na Jaqlin kupelekwa ndani ya chumba kingine maalumu kisha kuchomwa nusu kaputi.
***
Hakuamini alivyoamka Masaa Manne baadaye alitabasamu baada ya kukuta watoto wawili pembeni yake.
“Hongera dada umejifungua watoto mapacha, mmoja wa kike mmoja wa kiume”.Alisema Nesi.
Jaqlin alitabasamu lakini alionekana hana nguvu mwilini mwake,kingine kilichomchanganya zaidi ni kuhusu watoto hao wawili, alikumbuka vizuri sana alivyobakwa na Manase, hiyo ilimaanisha kuwa watoto sio wa Adrian, licha ya yote hayo ilibidi tu awapende watoto wake wote wawili mapacha, alimshukuru Mungu, kesho yake asubuhi Adrian alifika, alijawa na Furaha mno na kumpongeza Jaqlin.
“Hongera Mpenzi wangu kwa kuzaa mapacha”
“Lakini Adrian ningefurahi zaidi kama hawa watoto wangekuwa wako..”
“No usiseme ivyo,hawa ni watoto wetu”
Waliongea mengi siku hiyo hususani kuwapa majina kila mtu aliumiza kichwa.
“Jovan huyu wa kiume, na Jovana huyu wa kike”
“Hapo baby umeongea majina matamu sana hayo”
Furaha iliongezeka zaidi!
Asubuhi kulivyokucha Jaqlin alishindwa kuelewa kwanini Jovan yupo kimnya ametulia, alivyomchukua ili kumnyonyesha maziwa hakukuwa na dalili yoyote ya mtoto kutikisika, hisia mbaya zilimtawala na ndipo alipopiga kelele kwa sauti na kuwashtua madaktari, na kufika wodini mbio mbio.
“Nini Mama mbona kelele?”
“Jovan Jov…an, hatingishiki”
Daktari alipompima tu mapigo ya moyo alitikisa kichwa chake na kumwambia kuwa mtoto amefariki dunia, Jaqlin alilia hapo hapo na kuzirai…
*********
Ilikuwa ni familia yenye utajiri mkubwa, iliyomiliki viwanda vya kukatia mbao na visima vya mafuta katikati ya jiji la New Delhi nchini India, utajiri huo ulimilikiwa na Mzee wa kihindi Ahsan Rahman na mke wake Hajrath, walikuwa wenye furaha tele kuwa na utajiri huo kiasi kwamba hakuna hata mmoja wao alijua nini maana ya shida.
Licha ya kuwa na utajiri wote huo kitu kilichowanyima raha maishani mwao ni kutobahatika kupata mtoto ambaye atakayekuja kurithi mali zao endapo watafariki Dunia siku yoyote ile, Dada zake na Mzee Ahsan walimchukia sana wifi yao kila siku walimsengenya sana Mke wa kaka yao, Hajrath!
“Hivi kaka ni mwaka wa kumi sasa huu hatusikii chochote, tumechoka sio siri,tunataka kuitwa mashangazi”
Mzee Ahsan aliambiwa na Dada yake mkubwa siku hiyo wakiwa sebuleni asubuhi.
“Lakini huko ni kukoseana adabu kabisa, mambo yangu na mke wangu hayawahusu sawa, Mambo ya mtoto ni kudra za subhana Allah”
Mzee Ahsan alijitetea angali alijua Mke wake ni tasa hana uwezo wa kuzaa, lakini alimfichia siri hiyo,alimpenda sana mke wake na kuamini kuwa ipo siku moja Mungu angetenda muujiza na kuwapa Mtoto lakini hakujua ni lini,alikuwa yupo radhi kusubiri hata kwa miaka mia kuliko kuachana na Hajrath.
“sio ivyo, sisi tumechoka! tumechoka kabisa unadhani hizi mali zako zote nani atarithi kama sio watoto zako?”
“Hata kama nisipopata mtoto kwani watoto yatima hakuna? nitaenda kuwapa watoto yatima, naomba huu mjadala uishe” Mazungumzo hayo yalifanyika kwa lugha ya kihindi,
Mzee Ahsan sasa alianza kufoka.
Hajrath akiwa chumbani alisikia kila kitu juu ya malumbano hayo alilia machozi na kumtupia lawama zote Mungu wake kwa kumfanya awe Mgumba, ni bora angekuwa maskini kuliko kupewa ugumba,kila siku alikuwa ni mtu wa kulia,japokuwa alipewa faraja na Mume wake lakini bado alitamani siku moja apate mtoto kama wanawake wenzake. Ilikuwa kila akipita mawifi zake wanamnyali wakimwangalia kama kinyesi na kudiriki kumwambia kuwa anajaza choo na kumaliza masofa ya kaka yao.
Alilia machozi na kukosa raha ya maisha,faraja yake siku zote alikuwa ni Mzee Ahsan mume wake.
“usilie Mke wangu ipo siku, Allah atatenda miujiza yake, cha kufanya tuzidi kumuomba maana hakuna linaloshindikana kwake”
“Sawa Mume wangu”
Siku hiyo ilipita.
**
Mzee Ahsan alipata dharura ya ghafla, alisafiri kwa muda wa miaka miwili na kwenda Canada kikazi na kumuacha mke wake nyuma.Hali ya Hajrath ilizidi kuwa mbaya mawifi walizidi kumsimanga wakimsema vibaya hakuwa na raha ya maisha, hapo ndipo alipowasha gari mpaka kijijni kwao huku akiliia machozi na kumdondokea dada yake Roshban miguuni na kumueleza ni jinsi gani anavyoteseka na ndoa yake.
“Ndio ivyo da..da yangu naomba uni.saidie”
Roshban alimuonea huruma Mdogo wake nayeye kujikuta analia na kumfuta machozi kisha kufikiria kwa kitambo kidogo.
“Inabidi tufanye kitu, nina wazo”
“Wazo gani dada yangu?”
“Inabidi tufanye usanii”
“usanii gani?”
Hapo ndipo Roshban alipompa mbinu za kuweka matambala tumboni kwake ili yafanane na mimba.
“Sasa itakuwaje Mume wangu akijua,anajua mimi sina uwezo wa kuzaa”
“Si ulisema yupo CANADA mwaka mzima? Lazima atajua ni mipango ya Allah”
“Mhh lakini…”Hajrath aliguna.
“Sasa fanya ivyo, kisha mengine niachie mimi”
Mpango wa Roshban ulikuwa kabambe sana, ulionekana kuwa mpya kwa Hajrath na ndipo hapo alipoamua kuweka matambala tumboni akizuga kuwa ni mimba, jambo hilo liliwashtua sana mawifi zake tangu siku hiyo.
Mzee Ahsan alivyopokea habari hizo alitamani apae siku hiyo hiyo mpaka India ili akae na mke wake mpaka atakapo jifugua mtoto huyo, lakini haikuwezekana hata kidogo.
Mzee Ahsan Alipiga magoti barabarani na kuibusu Ardhi siku hiyo na kumshukuru Mungu wake, wafanya kazi wake walimshangaa sana kwa tajiri kama huyo kufanya kitu kama hiko cha kitoto, siku hiyo hiyo aliita wafanya kazi wake kwa ajiri ya kufanya sherehe kubwa lakini hakutaka kuwa wazi ni sababu gani alifanya ivyo na kuwadanganya kuwa amefurahishwa na uhodari wa kazi.
Tangu siku hiyo simu haikubanduka sikioni mwa Mzee Ahsan akiwa anaongea na mke wake kipenzi kila ifikapo usiku, hakukua na habari nyingine katika maongezi yao zaidi ya kuzungumzia swala la mtoto, licha ya kuongea kwa furaha lakini alishangazwa na jinsi mke wake alivyokuwa akiongea kwa unyonge kadri siku zilivyozidi kusogea mbele, Mzee Ahsan alilitambua hilo.
“Vipi mbona kama hauna raha?”
“Siamini Mume wangu,Mungu ni mkubwa sana”
“Furahi sana mke wangu hupaswi kuwa mnyonge jambo hili ni la Kushukuru sana,nitakupa zawadi kubwa sana ukijifungua”
Hajrath aliweka tabasamu la plastiki usoni, lakini moyoni alijiona ni mkosaji hakuwahi kumdanganya mume wake hata siku moja iendayo kwa Mungu,
hakuelewa itakuwaje endapo Mume wake atagundua siku moja.
**
Miezi tisa ilipokaribia Hajrath aliwasha gari mpaka kijijini kwa Mdogo wake Roshban na kumueleza ni hatua gani waifanye ili kuokoa ndoa yake.
“Kuna hospitali inaitwa Apolo nina shangazi yangu pale ni daktari, una kiasi gani cha pesa?”
“Pesa sio tatizo”
“sawa hakuna shida,niachie mimi ikifika wiki mbili mwambie Mumeo utakuja hapa kwangu kujifungulia kisha nitakupeleka mpaka hospitali,tutaiba mtoto”
“Sawa dada hakuna tatizo, lakini itakuwaje Mume wangu akigundua?”
“HAWEZI niamini mimi”
“Sawa”
Roshban alimuhakikishia Hajrath.
***
Tangu siku hiyo Roshban ilibidi aanze kufanya mawasiliano na Shangazi yake ambaye alikuwa Mkunga katika Hospitali ya Appolo. Baada ya wiki moja kupita walipanga kukutana ili wafanye mazungumzo.Roshban hakuficha hata kidogo, alielewa ni jinsi gani shangazi yake alikuwa na shida ya pesa na mwenye hali duni kupita kiasi, na ndipo hapo alipotumia njia ya pesa.
“Umesema utanipa kiasi gani?”
“Dola laki nne”
“Duu”
Udenda ulimtoka Shangazi! kwa idadi ya pesa hizo neno ‘sawa’ halikuwa gumu kwake.
“Hakuna tabu nitafanya ivyo, lakini inabidi uniingizie nusu ya pesa kwenye akaunti”
“Hilo halina tabu,nadhani unamjua Mke wa Tajiri Ahsan Abrahman”
“si Yule wifi yako umesema”
“Ndio, leo jioni nitakuingizia Dolla laki moja”
Shangazi alipoenda kusoma akaunti yake jioni alikuta keshawekewa pesa,aliruka ruka kwa furaha sana huku mikono yake ikiwa juu.
“Sawa nimeiona,lini mnahitaji mtoto?”
“Baada ya wiki tatu”
“Sawa, mnahitaji mtoto wa jinsia gani?”
“Wa kiume nadhani itakuwa nzuri sana”
Kazi ilianza mara moja.
Baada ya wiki tatu mwanamke mweupe alipandishwa juu ya machela mpaka chumba cha kuzalisha watoto na kujifungua watoto mapacha.
Mkunga Mariam Hakutaka kupoteza muda, akili yake ilifanya kazi kwa kasi ya maporomoko ya maji ya owen falls, aliingia mpaka chumba kingine cha maiti za watoto kisha kusubiri usiku ufike, kichwani kwake alifikiria utajiri,alijua akifanya kitendo hiko atamaliziwa pesa zake na kupishana kando na umaskini.
Usiku ilipofika zamu yake alichukua maiti ya kichanga kisha kwenda kubadilisha kwenye kitanda alicholala Jaqlin aliyekuwa amejifungua watoto mapacha kisha kuweka mtoto aliyekufa na kuondoka naye taratibu.Hapo kazi yake ilikuwa teyari imekwisha.
***
Adrian alijisikia uchungu ajabu!
Alimuonea sana huruma Jaqlin aliyekuwa akilia mfululizo bila ya kunyamaza.
Madaktari walishindwa kuelewa ilikuwaje mpaka mtoto huyo mchanga afariki dunia wakati alikuwa ni mwenye afya nzuri tu jana yake,hawakutaka kufanya lolote zaidi ya kuchukua maiti hiyo na kwenda kuiifadhi.
ILibidi Jaqlin asahau na yote amuachie Mungu wake Kama mtoto watatafuta mwingine, walimuonea huruma sana Jovvana kuondokewa na pacha wake. Siku zilivyozidi kwenda Afya ya Jovanna ilizidi kuwa nzuri maradufu,Jaqlin alishtushwa na jambo moja na lilimchanganya akili yake,Jovvana alifanana sana na Adrian kuanzia midomo mpaka mashavu hili aliligundua baada ya mwezi mmoja kupita,
hakutaka kukaa kimnya alimuita Adrian ili amueleze.
“Adrian, huyu mtoto kafanana nawewe sio siri”
Jaqlin alimwambia Adrian baada ya kutoka kufanya mazoezi mguu wake ulishaanza kupona.
“Hata mimi nililiona hilo juzi,nikashindwa kuelewa”
“Huyu mtoto ni wako Adrian nimekumbuka kitu”
“Kitu gani?”
“Mara ya mwisho tunafanya mapenzi nakumbuka nilikua katika siku za hatari ndipo Yule mpuuzi akanifanyia unyama na kuivuruga akili yangu, nilitaka nikwambie ile ile siku lakini nikasahau”
“Jaqlin, kama ukweli basi itajulikana”
“Nataka tukapime DNA Adrian ili niwe na uhakika zaidi, kama hatakuwa wako basi sawa”
“okay”
Walikubaliana.
Siku hiyo jioni walimuendea daktari na kumueleza shida yao, Damu ya Adrian ilichukuliwa kisha baadaye ya mtoto na kupelekwa maabara.
Baada ya siku mbili Daktari aliwaita ofisini kwake ili awapatie majibu.
Adrian alizidi kupigwa na butwaa Jaqlin aliyatoa macho yake baada ya daktari kutoa majibu ya vipimo vya DNA….
“Majibu tuliyopata kwenye vipimo vyetu yanaonesha kuwa mtoto ni wa kwako na damu za DNA zimeendana kabisa”
Alisema Dokta huku akiwatizama wote wawili.
“Dokta ni kweli?”
Jaqlin hakuyaamini maneno ya Daktari.Adrian alikaa kimnya, hakutaka kusema lolote. Moyoni alikuwa ana furaha ya ajabu na kushindwa kuelewa ni kweli anayoyaongea Daktari au alipewa hongo na Jaqlin ili agushi majibu.
Walitoka ndani ya chumba cha daktari wakiwa wamejawa na furaha mioyoni mwao, walipigana mabusu usoni na midomoni tena mbele za watu bila kujali.
Kitendo cha Jovvana kutokeza Duniani kilizidi kuongeza furaha na mapendo kila siku iliyokatika,lakini walipomfikiria Jovan roho ziliwauma na yote kumuachia Mungu wao,waliamini alifariki kutokana na baridi na ndivyo walivyoambiwa na Daktari baada ya kupewa majibu hayo.
“Darling! naona mguu wako sasa unaendelea vizuri”
“Sasa hivi una ahueni sio kama hapo kipindi cha nyuma hawa madaktari ni mabingwa sana,sasa hivi naweza kidogo kutembea hatua kadhaa bila magongo”
“sasa kesho sitaki utembee na magongo,sipendi mimi, utalemaa”
Ilikuwa jioni ya saa kumi na mbili kasoro robo, baada ya Adrian kutoka kufanya mazoezi ya kutembea na kumkuta Jaqlin akimnyonyesha Jovvana.
Adrian alijiona tayari ni mwanaume mwenye majukumu ya kifamilia hakuwa na namna ya kumlipa Mpenzi wake Jaqlin kwa aliyomtendea, isipokuwa kuwa mwaminifu mpaka milele sababu bila yeye wenda angekuwa kilema.
Hatimaye mguu wa Adrian ulirudi katika hali yake ya kawaida baada ya miezi miwili kukatika. Hawakuwa na sababu ya kuendelea kuishi Nchini India.
wiki moja baadaye walitafuta tiketi zitakazo warudisha mpaka Tanzania walikuwa wenye furaha sababu waliondoka wawili na sasa wanarudi Tanzania watatu akiwemo Jovvana.
ILIKUWA ni siku ya Jumamosi saa nne kasoro dakika mbili asubuhi! ndipo walifika uwanja wa ndege Mumbai wakiwa tayari na mizigo yao mikononi wakisubiri taarifa za ndege ya shirika la Air India itakayo wapeleka moja kwa moja Tanzania Dar es salaam kisha hapo wachukue precision Air mpaka Songwe mkoani Mbeya walipokubaliana kufika na kuanza maisha yao.
Na ndivyo ilivyokuwa, dakika mbili zilivyopita ilisikika sauti ya kipaza sauti kutokea kwenye spika ikiwataka wasafiri waondokao na Air India wajongee kwenye ndege.
Adrian na Jaqlin pamoja na mtoto wao Jovvana walisogea kwenye milango na kuungana na abiria wengine, hapo waligonga mihuri passpot na kuingia ndani ya ndege.Jovvana alikuwa ameshalala teyari haelewi lolote.
**
Saa mbili ya usiku shirika la Ndege ya Precision Air ilikanyaga ardhi ya Mkoa wa Mbeya, Hapo Adrian na mpenzi wake Jaqlin pamoja na Jovvana walishuka,Mzee Mwangenya alishaelewa ujio wa watoto wao aliwasubiri kwa hamu,Ng’ombe wawili wakubwa walikuwa teyari wameandaliwa ili wachinjwe sababu alikuwa ni mwenye furaha mno.
Baada ya kushuka ndani ya ndege walinyoosha mpaka nje zilipojaa taxi kisha kuingia ndani ya moja wapo kila mmoja wao alionekana kuchoka na safari.
Kitendo cha Taxi kufunga Breki zake nyumbani kwa Mzee Mwangenya zilisikika kelele nyingi kutoka kwa mzee huyo akiongea kwa Lugha ya kinyakyusa.
“Wanangu karibuni sana,karibuni jamani ololo ololo Mkamwana huyoo! Mumeniletea na mjukuu wangu?”
“Ndio Mzee,mjukuu wako huyu”
“Huyu wa nyumbani kabisa, naona hata sura yake ilivyo, sisi tuna damu kali barabaraa”
Waliongea mengi sana siku hiyo,nyumba nzima ilijawa na furaha baada ya ukimnya wa muda mrefu.Kesho yake kulivyokucha Mzee Mwangenya aliwaita baadhi ya wazee na Ng’ombe wawili kudondoshwa chini,baadhi ya majirani walialikwa walikula na kusaza!
***
“Baby inabidi tupange, tuanze sasa maisha yetu”
“Tupange?kwani hapa hapatufai Darling?”
“sina maana hiyo Mpenzi wangu,sasa tutaendelea kukaa kwa mzee mpaka lini? inabidi tupange ili tuwe huru tufanye mambo yetu sio kwa nia mbaya lakini,kuna jambo nimefikiria?”
“Jambo gani hilo?”
“Tufungue mgahawa wa chakula kule mjini,hizi pesa nilizokuwa nazo nafikiri zinatosha kuanzia mtaji kuliko kuzitumia tu bila kuzizungusha”
Jaqlin alijaribu kumuelewesha Adrian juu ya kile anachofikiria kichwani, ilielekea ni jambo ambalo lilikuwa ndani ya kichwa chake muda mrefu sana, ilikua ni lazima waanze maisha upya alishakubaliana na Adrian kwa hali yoyote ile kimaisha,kwa ivyo hakutaka kuendelea kubaki kwa Mzee Mwangenya akizidi kutumia pesa zake Benki pasipo kuizungusha kwa kufanya biashara yoyote ile.
Adrian alizipokea habari izo siku hiyo asubuhi na kwenda kumuelezea Mzee Mwangenya Baba yake kile walichokiongea ili wamuage!
“Kwanini msikae hapa Mwanangu?”
Mzee Mwangenya aliuliza kwa unyonge sababu hakutaka kabisa Adrian na Jaqlin wamuache mpweke, kifupi aliwazoea sana.
“Tutakuwa tunakuja Baba,wala hatuendi mbali kila Jumamosi au Jumapili tutakuwa hapa”
“Na mjukuu wangu je?”
“Tutamleta pia”
Mzee Mwangenya hakuonesha hali ya kipingamizi aliwakubalia.
Baada ya usiku kufika na Jovvana kulazwa Jaqlin alimrukia Adrian na kuanza kumlamba mdomoni na hapo ndio ukawa mwanzo wa kubadilishana mate wakitumia ndimi zao kama njiwa.
Walishikana shikana na kutomasana kila sehemu ya miili yao,Mkono mmoja wa Adrian ulikua teyari kwenye ziwa la Jaqlin la kushoto na kumfanya ajinyonge nyonge kwa raha sababu hapo ndipo ulipokuwa udhaifu wake,hakuishia hapo aliushusha mkono wake mpaka juu ya sketi ya Jaqlin na kuanza kuishika sehemu ya juu.
Mambo hayakuwa mazuri kwa Jaqlin sababu alianza kutoa mihemo ya nguvu.
“Taratibu Loove! usipige kelele mzee atasikia”
Alinong’ona Adrian akiwa sikioni mwa Jaqlin kisha baada ya hapo alitumbukiza ulimi wake sikioni huku akizidi kusugua MGODI wa Jaqlin, alivyoona haitoshi aliingiza kabisa mkono ndani yake akijaribu kucheza na nyasi nyasi zilizokuwa zinataka kuota kwa mbali, baada ya hapo mkono ulisogea karibu na ikulu, kwa ufundi wa hali ya juu kidole kimoja sasa kilikuwa ndani ya MGODI.
Jaqlin hakuwa anajiweza tena na kuzidi kupiga kelele huku akiwa ana katika juu ya kidole huku macho yake yakiwa yamejifunga, ni kweli alihisi yupo juu ya dunia anaangalia vitu vyote kwa chini, alihisi kufa kufa baada ya maziwa yake kuanza kunyonywa tena kwa zamu juu ya chuchu zake,
japokuwa alikuwa teyari amezaa maziwa yake yalikuwa bado yamesimama kama mnara yaani bado chuchu saa sita,
Jina la Adrian ndilo lilikuwa likitajwa kila wakati kwa sauti za puani, Adrian alikuwa Hodari kitandani, hata siku moja katika maisha yake akicheza mechi hiyo hakosei, alikuwa ni kiungo mzuri hatari, wachezaji walikuwa wakipasha kwanza kwa spidi zote!
Haikupita hata dakika mbili Jaqlin alizidisha kelele na kumfanya Adrian aweke mkono juu ya kinywa chake na ndio hapo alipokuwa akihangaika kuibana miguu yake kisha kutulia baada ya kufika mshindo,hiyo haikumaanisha kuwa mechi imeisha La!
Adrian aliingia kati na kuipanua miguu ya Jaqlin kisha kuseti mitambo.Mkanda uliingizwa ndani ya deki kisha sinema ya kikubwa kuanza kuendelea! Walienda sambamba kwa kukatika,Adrian alizungusha kiuno chake akiwa juu ya Jaqlin taratibu sana huku ulimi wake ukiwa unanyonya maziwa ya Jaqlin, hapo ndipo Jaqlin alikua kama amepigwa stata,miyemko ilikuja tena na kuonesha ushirikiano maradufu, na hata kudiriki kuweka mikono yake juu ya makalio ya Adrian akijaribu kumkandamiza kwa Ndani.Wote walilifurahia tendo hilo sio masihala, Mpaka inafika saa tisa ya usiku kila mtu alikuwa ameridhika amejitupa upande wake amelala fofofo.
***
Mzee Mwangenya hakuwa na jinsi tena ya kubadili maamuzi ya Adrian na Jaqlin, aliwapa baraka zote katika maisha yao!
Jaqlin akiwa na Jovvana mkononi alitamani kulia machozi sababu tu alimzoea Mzee Mwangenya ,kuagana ni sehemu ya maisha hata ivyo nyumba ya kupanga waliopata hapakuwa mbali sana na nyumbani kwa Mzee Mwangenya, zilikuwa ni kama kilometa nane hivi kutokea hapo! Dalali alikuwa teyari ana taarifa hizo.
Siku hiyo hiyo walipitia mjini ili kununua mahitaji muhimu ya ndani, kama makochi kitanda pamoja na vyombo vya kupikia.
Mpaka jioni inafika zoezi la kutafuta vitu vya ndani lilikamilika,pick up iliegeshwa nje ya chumba kidogo kiasi kilichofanana na geto, hakikuwa kikubwa sana, kilikuwa ni chumba kimoja tu kilichofaa kuweka kitanda, makochi pamoja na kabati! Mpaka inafika saa nne ya usiku walimaliza zoezi la kupanga vitu vyao ndani ya chumba walichopanga,walikamilisha malipo kwa dalali pamoja na Baba mwenye nyumba waliyemtambua kwa jina la Mzee Kinyogoli!
alikuwa ni Mzee mfupi mwenye mvi nyingi kichwani lakini ni mwingi wa maneno.
“Wewe kijana, sasa choo kipo huko nyuma, maji masaa ishirini na nne yapo,hapa maji hayakauki kama ikulu,umeme pia vile vile,mwezi ujao nitakuwa hapa tarehe kama ya leo asubuhi na mapema kabla sijaamka”
“Babu, nataka nilipe kodi ya miezi sita”Jaqlin alisema.
“Sawa Mjukuu wangu, tena itakuwa vizuri sana mtaepusha usumbufu na kero”
Mzee Kinyogoli alipewa pesa yake na kuondoka.
Adrian na Jaqlin kuanzia hapo walianza maisha mapya, hazikupita hata siku saba walifungua mgahawa wa Chakula kama Jaqlin alivyohaidi, wakisaidiana kufanya kazi kwa pamoja,kama Adrian ataosha vyombo basi Jaqlin atahudumia wateja,siku iliyofuata Jaqlin akiosha vyombo Adrian atahudumia chakula au kinyume,
waliendelea ivyo ivyo mpaka miezi mitatu kukatika wakawa wamefungua mgahawa mwingine mbali kidogo.
Jaqlin alijitahidi kufanya migahawa ya chakula kuwa misafi kila wakati,wateja walijazana sio utani, hata wakati mwingine wakawa wanakosa siti za kukaa.
Jaqlin alianza kunga’aa na uzuri wake kurudi upya,alikuwa mrembo kwelikweli! hata siku moja hakuna hata mtu mmoja aliyedhani kuwa ameshazaa mtoto.kuna wengine walikuja kula chakula kutokana na kuvutiwa kwa uzuri wake.
“Dada embu njoo mara moja unihudumie”
Mteja alimuita Jaqlin kwenye meza yake.
“Nakusikiliza kaka”
“Vipi umeolewa?”
“Ha! Haa! Haaa! Haaaaa! kwanini unauliza?”
“Nimeuliza tu”
“Nimeolewa ndio”
“Hapana sio kweli,pete yako iko wapi?”
“kwani lazima kutembea na pete?”
“Lini unakuwa frii?”
“Sina Frii hata siku moja”
“Acha utani basi chaurembo, hivi unajua kuwa wewe ni mrembo sana,na haustaili kuishi mahali kama hapa,wewe unatakiwa kukaa na watu kama mimi,mimi ni tajiri sana nina magodauni mjini Dar es salaam, ulishawahi kufika Dar wewe? mimi nitakupeleka leo hii hii, kitendo cha kukubali kwenda namimi tukalale”
Jaqlin alitabasamu!
Maneno ya mwanamme aliyekuwa anakula yalikuwa ya kuchekesha Kwa Jaqlin sababu hayakuendana kabisa,alikuwa amejawa na vumbi la cement usoni, amechafuka mwili mzima kwa masizi, kwa haraka haraka alikuwa ni mbeba mizigo.
“Usione kwamba hili vumbi namna gani vipi Chaurembo, nimeamua tu kufanya kazi na vijana niwafundishe kazi,nipatie namba yako” kijana alizidi kujipigia debe.
“Nitakupa kesho ukija”
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa wanaume kumsumbua Jaqlin,Kila mwanaume alitaka kupewa penzi japo kwa usiku mmoja tu,wanaume ndiyo walikuwa wakijazana katika mgahawa!
Adrian alipatwa na wivu lakini alimezea, hakuwa na jinsi ya kufanya.
Ilikuwa furaha sana kwao sababu kwa siku waliweza kuingiza kiasi cha shilingi laki saba kila usiku baada ya hesabu kufanyika kutoka katika migawaha miwili waliyofungua.
Walihama walipokuwa wanaishi na kutafuta nyumba nyingine yenye chumba na Seble baada ya miezi sita kuisha.
Macho yao yote yalikuwa kwa mtoto wao Jovvana siku zote aliyeanza kuita “Mama” walimpenda kupitiliza alikuwa mzuri na mwenye weupe wa kung’aa kila mtu alitamani kumbeba!
Siku moja Adrian alishtuka asubuhi na mapema na kutomuona Jaqlin, alivyochungulia nje aliona gari aina ya Landcruiser Jaqlin akiwemo nje anacheka na kufurahi na mwanaume, aliingiwa na wivu ajabu. Alitamani kutoka nje aharibu kila kitu lakini alisubiria mpaka Mpenzi wake Jaqlin alipoingia ndani.
“Yule ni nani?”
Adrian alimtupia Swali Jaqlin akiwa amekasirika,anamtizama kwa macho makali,Moyoni alipata uchungu alishajua nini maana ya gari,alikumbuka kipindi cha nyuma alivyokuwa akiwachanganya wanawake kama pilau na kachumbari,alishajua kuwa ugonjwa wa mwanamke ni gari na teyari Jaqlin atachukuliwa kwa staili hiyo.
“Adrian mpenzi wangu Yule ni mteja tu”
“Mteja gani mpaka majumbani? Na hapa kapajuaje?”
“Adrian, acha wivu basi,najua unaongea kwa sababu una wivu na ninajua hilo lakini huo wivu wako utakufa na presha”
Jaqlin alimaliza kuongea na kutaka kuondoka lakini kabla ya kutembea alishikwa mkono hakuelewa Adrian alikuwa ana hasira kiasi gani.
“Yaani unaondoka sijamaliza kuongea?”
“Adrian naomba niache,hizo hasira mwisho wake hautakuwa mzuri”
“Nikuache? wakati ushaanza umalaya tayari”
“Adrian Mimi siyo Malaya nakuheshimu, naomba ujieshimu na uniheshimu pia. Utamuamsha mtoto ,jiandae twende kazini”
Jaqlin alijaribu kuutoa mkono wa Adrian lakini badala yake alishtukia kofi kali lililotua shavuni mwake na kulia kwa nguvu ‘tasaa’.
Jaqlin hakukubali hata kidogo nayeye alirusha kofi lililomfikia Adrian shavuni kwa hasira.Adrian alitabasamu kama kawaida yake akiwa mwenye hasira sana.
Alimtizama Jaqlin kwa macho makali na kukunja uso wake huku akiwa anatetemeka kwa hasira kama mtu aliyekuwa ana homa ya usiku, hakuelewa amfanye nini Jaqlin aliyekuwa mbele yake tena kampiga kofi kitendo ambacho alichohesabia kama dharau.
Hakuweza kuzuia hasira zake alirusha kofi lililompeleka Jaqlin chini mzima mzima, hakuishia hapo alimuinua na kuzidi kumzaba vibao vikali visivyokuwa na idadi kamili.
****
“Naomba nionane na Meneja”
“Una mihadi naye?”
“Ndiyo, Mwambie Jaqlin Mshana nipo hapa”
“Sawa subiri”
Mwanamke aliyevalia shati jeupe juu na sketi ya rangi ya kijani aliinua mkonga wa simu kisha kubonyeza namba Fulani akisubiri upande wa pili upokelewe.
“Bosi, kuna binti ana kuulizia,yupo hapa,anasema anakuhitaji anaitwa Jaqlin Mshana..,ndio. okay sawa bosi”
Mwanamke aliyevalia sare zilizoandikwa EMBANK alimruhusu Jaqlin aingie ofisini kwa Bosi baada ya maongezi kufanyika.
Jaqlin alisimama na kujikagua vizuri kisha taratibu kuingia ndani ya chumba kilichoandikwa Manager kwa juu, alisukuma mlango kisha mbele yake kukutana na mwanaume mweusi kiasi nyuma ya meza na kukaribishwa akae kwenye viti wakaavyo wageni.
“Karibu Jaqlin”
“Ahsante.Nafikiri wewe ndiye Mr.Mwaipungu niliyekuwa naongea nawewe wiki iliyopita?”
“Ndiye mimi na nilipokea barua yako”
“Ahsante. kama nilivyoandika kwenye barua, nilikua nikihitaji mkopo ndiyo nimekuja leo”
“Ulisema ulitaka kufungua kitu gani?”
“Nataka kufungua nyumba ya wageni yaani gest house nimeona hapa tunapoishi hakuna kabisa huduma hiyo wageni wanalazimika kwenda mbali”
“Itabidi mimi nawewe tuongozane mpaka kwenye biashara zako,kisha kesho nije kwako nione unapoishi, ili nikupe huo mkopo”
“Sawa hilo halina tatizo”
Jaqlin alivutiwa na upole Wa meneja Mwaipungu Hafsa mikopo, pia alikuwa na cheo cha umeneja katika benki hiyo ya EMBANK.
Nia ya Jaqlin kufika hapo alihitaji kupata mkopo wa pesa ili aanzishe mradi mwingine wa nyumba za wageni,akili zake siku zote ziliwaza kutafuta pesa na aliamini siku moja atapata.Hakutaka kumshirikisha Adrian kwanza, alitaka afanye jambo hilo kimnya kimnya na utaratibu wa mkopo ukikamilika ndipo amshirikishe, alijua kivyovyote vile angeweka kipingamizi na ndiyo maana aliliweka swala hilo ni siri kubwa ndani ya kifua chake,
maisha aliyokua akiishi hakuyapenda hata kidogo, ilikuwa ni lazima awe tajiri siku moja,na ndiyo maana kila siku hufanya kazi kwa bidii zake zote! Alitaka siku moja amrudishe Adrian kwenye mstari, tena wawe matajiri zaidi ya walivyokuwa hapo awali.
Meneja Mwaipungu alisimama kitini kisha wote kuongozana mpaka kwenye migahawa aliyofungua. Alionekana kuvutiwa na uchapakazi wa Jaqlin,Baadaye ilipofika jioni walienda mpaka kwenye nyumba anayoishi Jaqlin na kupaona.
“Basi kesho asubuhi nitakuja, ili ikiwezekana nikupitie ukachukue huo mkopo”
“Sawa.Lakini hakuna umuhimu wa kunipitia mimi nitakuja huko”
“Hapana, nitakuja kumsalimia hata shemeji ili ajue kuwa nakupatia pesa, si unajua haya mambo ya pesa,inabidi mashahidi wawepo!”
“Sawa pita Asubuhi”
Jaqlin alishuka ndani ya Landcruiser la Mwaipungu akiwa mwenye furaha sana moyoni, alipanga furaha hiyo aifurahie na Adrian kesho yake wakiwa kwenye mgawaha wao ikiwezekana hata waende mjini kupunga upepo na kuosha macho.
Asubuhi na Mapema kulivyokucha hakutaka kumuamsha Adrian, alitoka mpaka nje baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa Hafsa Mwaipungu aliyekuwa nje amepaki gari.
“Samahani kwa kukusumbua asubuhi”
“Wala usijali”
“Vipi Mista yupo?”
“Amelala sitaki kumsumbua”
“Mke wa mtu sumu ujue,isije ikawa kasheshe hapa,nikapata skendo kazini nikapigwa chini, kazi yenyewe nimeanza juzi tu”
“Ha! Haa! Haaaaaa,acha vituko,basi nitakuja leo kuchukua ule mkopo”
“Sawa,utakuja na leseni zako za biashara na barua ya mwenyekiti wa serikali za mitaa, utapata. kila kitu kitakuwa sawa”
Jaqlin Alijawa na furaha na kufanya ajiachie huku akicheka,hakuelewa Adrian yupo Dirishani anawaona lakini hakuweza kusikia ni kipi wanazungumza.
***
Hasira na wivu ndivyo vilimpelekea ampige mpenzi wake Jaqlin kimakosa,Adrian alizidi kumpiga Jaqlin makofi bila kumpa wakati wa kujitetea, alijiona yupo sahihi na aliamini kuwa atarudisha heshima,Kelele alizokuwa anapiga Jaqlin zilipaa mpaka nje kwa majirani na kuwafanya waingie ndani kuwaachanisha.
“Vipi wanangu mbona mnataka kuleta balaa asubuhi yote hii?”
Mzee Mwenye busara aliuliza baada ya kuwaachanisha Jaqlin na Adrian.
“Babu, ungeniacha tu aendele… kuni..piga Adr..ian ko..sa gani nimefanya mwacheni anipige tu”
Jaqlin aliongea kwa kwikwi ni kweli alipigwa kwa kosa la kusingiziwa, alilia kwa uchungu mbele za watu.
Mpaka zinapita siku mbili hakuna hata mmoja aliyemsemesha mwenzake walinuniana, hata chumbani ilikuwa ivyo ivyo,Jaqlin akiweka kichwa juu basi Adrian anaweka kichwa chini walilala Mzungu wa Nne.!
****
Ujenzi wa nyumba za wageni uliendelea kadri siku zilivyozidi kwenda, Jaqlin alisimamia zoezi hilo na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, mpaka inafikia miezi mitatu nyumba ilikuwa imefika kwenye renta tayari,Adrian ndipo alipobutuka hakutaka kukaa kimnya uzalendo ulimshinda.
“Jaqlin”
Usiku Adrian alimuita Jaqlin lakini hakuitikiwa, na kuita tena mara ya pili lakini ilikuwa ivyo ivyo hakujibiwa kitu sio kwamba Jaqlin hakusikia.
“Jaqlin”
“Sema nakusikia”
“Mama tusahau yaliyopita,geukia huku tuongee kitu naomba nisamehe ni hasira tu”
“Ndiyo unachotaka kuniambia?”
“Sio ivyo Mpenzi wangu”
“Niache nilale basi, wewe si bondia endelea na ubondia wako”
“Mimi sio bondia Jaqlin, hata ungekuwa wewe ndio mimi ungefanya ivyo”
“Wala nisingefanya ivyo”
“Mkono uliteleza Mpenzi, sasa tutaishi hivi mpaka lini?”
“Mpaka hasira zangu ziishe”
“Baby embu tusahau yaliyopita, tugange yajayo”
Ilichukua kama lisaa limoja na nusu mpaka Jaqlin akatabasamu na kukaa kitako,ndani ya moyo wake alihisi amekosa furaha ya maisha kwa kutokuongea na Adrian, aliamini kugombana ni sehemu tu ya mapenzi hakuwa na sababu ya kuendelea kuweka kinyongo, ilikua ni lazima aweke yaliyopita kando ili wasonge mbele, aliamini hayo ndiyo maisha.
“Adriian, nakupenda sana,usifanye ivyo siku nyingine Yule mwanaume uliyemuona siku ile ni meneja katika benki ya EMBANK, sina mahusiano naye,nakupenda mpenzi wangu,hata siku moja sitokuja kumvulia mwanaume yoyote Yule nguo yangu ya ndani!Nimewakataa wanaume wengi sana sababu yako”
Adrian alikua ni kama aliyepigwa sindano ya ganzi mwilini aliganda mwili ulimsisimka,alijiona mkosaji alishuka kitandani na kupiga magoti akijaribu kuomba asemehewe makosa yake, kupitia macho ya Jaqlin aligundua ni kweli alikuwa akicheza na shilingi katika tundu la choo, na alijifunza neno fikiri kabla ya kutenda!
Kweli aliyaamini maneno hayo sababu tu kutokana na hali duni aliyokuwa nayo, angekuwa mwanamke mwingine angeshakimbiwa zamani za kale!
Kilichofuata hapo ni mfululizo wa mabusu na kuvuana nguo zao kisha kufanya tendo lililowaleta duniani kila mtu alifurahia.
Ujenzi ulizidi kuendelea mpaka unafika mwaka tayari Nyumba ya wageni ilikuwa tayari wakaiita A & J Lodge,Mpaka hapo Jovvana alishaanza kutembea na kuwajua wazazi wake kwa sura.
“Tataaaaa”
Jovvana alijaribu kuongea kitu akimaanisha Baba,Adrian aligeuka na kumbeba na kuanza kumrusha rusha kwa furaha.
A & J ilizidi kujaza watu kila kukicha,wageni walipishana na kuisifia, ilikuwa ina kila kitu ndani,Haikupita hata mwezi mwingine pesa zilizopatikana walifungua bar na kuweka kila aina ya vinywaji na jikoni walimtafuta mtu wa chakula,
kumaanisha kuwa mgeni atakaye kuja kulala apate mahitaji.
Mambo yaliwanyookea, miradi waliyokuwa nayo ilibidi watafute gari ndogo aina ya Starlet itakayosaidia kuwafikisha kazini,Jaqlin akiwa anasimamia migahawa Adrian alikuwa kama Meneja katika nyumba ya wageni, maisha yalisonga Mbele!
*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
0 comments:
Post a Comment