Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 2/10


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 2 KATI YA 10
*******
 *******


Tayari kuli kucha na kupambazuka tayari ambapo
Alishtushwa na mlango baada ya kugongwa na kushuka kitandani kiuvivu Na kuufungua .

"Shikamoo Anco"
Witness alisalimia ila aliona aibu baada ya kugundua alikua na nguo ya kulalia na aligundua hilo kutokana na Sunday aliye kua mbele yake aliya gandisha macho yake juu ya kifua chake ambapo kutokana na nguo iyo kuonyesha kila kitu aliweza kuyaona maziwa ya Witness.
" Marahahab Sasasaamahani nime kuamsha asubuhi, ila chai tayari kule twende mezani"
Sunday aliongea kwa kigugumizi huku akimeza mate ya matamanio
"Sawa, ngoja nika oge kwanza Anco"
"Poa uta nikuta mezani"

Baadae witness alijiunga mezani na kuanza kunywa chai.
"Anco hiki kisu nime kipenda sana, kidogo mpaka raha"
"Kichukue tu, ukiweke chumbani kwako uwe una menya menya nacho machungwa"
"Asante"
Witnes alikiweka kisu kile mfukoni na kuingiza mkate mdomoni huku kiki fuatiwa na kikombe cha chai.

Baada ya kumaliza alishukuru kama kawaida na kurudi chumbani kulala, ila baadae ana hisi mlango wake una funguliwa alivyo geuka alimuona Sunday ana malizia kuufunga kwa ndani na funguo kuzi weka mfukoni.
"Anco nini tena?"
Aliuliza Witness huku akikaa sawa.
"Ssshss shhs usi pige kelele"
Sunday aliweka kidole chake mdomoni aki mzuia wity asipige kelele,
Alimsogelea na kuanza kumvuta kwake kwa nguvu huku akivuta sketi ya wity aliyo vaa
Ila wity kwa nguvu za ajabu ali msukumiza Sunday pembeni ,
Hasira zili muingia na kumpiga kofi wity lili lomfanya atulie , Sunday alimrukia kifuani na kuanza kumtoa nguo ya juu kwa nguvu,
Kwa upande wa wity alijua vizuri sana nia ya Sunday ila alishindwa kufanya chochote kutokana na Mtu aliye taka kumbaka tayari alimshinda nguvu,
Sunday ali mpanua miguu Witnes na kumvua nguo ya ndani na yeye kushusha suruali yake haraka haraka ,
Haraka haraka akili ya wity ili cheza kama umeme na kukumbuka kisu alicho kiweka ndani ya mfuko wa sketi muda mfupi aliotoka mezani na kuanza kugusa gusa sketi yake ambapo hapo ali fanikiwa kutoa kisu kile cha kuku njua ndani ya mfuko wa sketi yake na kwa nguvu za ajabu aliki chomeka juu ya shingo ya Sunday na kukikandamiza kwa hasira sana ndani ya shingo na kufanya damu nyingi ziruke kama kuku aliye toka kuchinjwa........


 Damu zilizidi kuruka kama chem chem tena kwa kasi na kuzidi kumlowanisha Witnes ambae alikua chini ya mwili wa Sunday.
. Kwa nguvu aliji toa na kubaki akitoa macho kwa kitendo kile alicho kifanya, kwa macho yake alishuhudia Sunday aki tupa tupa miguu na taratibu kukaa kimnya aki kata kauli.
"Mungu wangu"
Aliongea kwa mshangao.
,
Alicho kua ana ona mbele yake kili mfanya mwili wake upige ganzi na kutokuelewa afanye nini kwa wakati huo,
Aliangalia mikono yake na kuji tazama na kuji kuta ame lowa damu,

Haraka haraka ali badili nguo na kuanza kuji futa damu zile, alivyo hakikisha kafanya hayo yote, akili yake ili mtuma aingie kwenye kabati lake la nguo na kutoa pesa zake za akiba , alizihesabu na kukuta zipo laki tatu,

Hakuna alicho fikiria kwa wakati huo zaidi ya kukimbia na kupotea kabisa maeneo hayo alijua ange shikwa kivyovyote vile ange fungwa kifungo cha maisha.

Alifungua mlango wa chumbani na kutoka nje ,
Alitembea mpaka alipo fika stendi ya mabasi na kuju muika na abiria wengine walio kuwemo hapo stendi,
Kila mtu aliye muona kituoni pale alidhani wenda alimuona kwa kitendo alicho kifanya cha kuua muda mfupi ulio pita ,ivyo alizidi kuingiwa na wasi wasi.

Ki ukweli hakuelewa wapi ana poelekea kutokana na ugeni ndani ya mkoa huo wa Dar es salaam.

".kariakoo kongo mnazi mmoja, Karikoo Kongo mnazi mmoja"
Mpiga debe aliita abiria wanaoelekea maeneo hayo na kufanya watu wagombanie basi lile kubwa,

Ili bidi witness nayeye ajumuike na kuingia ndani ya basi hilo ambalo lilikua tayari limejaa,
Fikra za kitendo alicho kifanya cha kuua kili jijenga ndani ya ubongo wake na kuanza kujuta kwa kitendo alicho kifanya, basi hilo lilizidi kwenda liki kusanya abiria na kufanya watu wazidi kujaa.
"Dada nauli hapo"
Sauti ya kondakta ili mshtua Witness katika dimbwi la mawazo.

"Sasa dada angu, mbona una visa,?.. ina maana nilivyo kua natangaza pale wenye ela kubwa wanipe niombe chenji huku sikia?"

Konda huyo alianza kufoka baada ya witness kutoa noti ya shilingi elfu kumi.
"Siku sikia"
"Huku sikia wapi bwana, makusudi tu hayo,, ".
"Samahani siku sikia"
Konda yule aliachia misunyo na kuzidi kuongea chini chini huku aki tukana matusi mazito na kutumia lugha chafu.
"We konda , kuwa na heshima basi"
Aliongea mzee mmoja aliye kua ame kaa kiti cha nyuma, ambapo alionekana kukerwa na kauli za konda huyo.
.
"Aaah we mzee kavu nini , we haya kuhusu haya,"
"Kuwa na adabu tuheshimiane, hatu fahamiani sawa"
"Adabu una ijua wewe, usini zingue, sina haja ya kuku fahamu mzee,"

Mzee huyo aliinuka kwa hasira na kumfata konda yule na kumkunja shati lake kwa nguvu sana huku aki taka kumpiga.
"Dereva simamisha gari, sasa nataka nikaku oneshe adabu, . Dereva simamisha gari nime sema"

Konda yule ali jikuta ana kaa kimnya hasa baada ya mzee yule kutoa kita mbulisho cha jeshi.
"Mzee yaishe"
"Yataenda kuishia kambini kule. Nataka twende kambini ukanieleze nini maana ya KAVU, Nipisheni njia nipite, huyu naondoka nae kambini

, "
Mwana jeshi yule alipangua pangua watu ndani ya dala dala ile huku akiwa amem shika konda yule shati na kushuka nae nje ya basi, huku watu wakiwa wame furahishwa sana na kitendo kile.

Baadae gari lili fika mnazi mmoja na witness kushuka akiwa ana shangaa shangaa na kutoelewa wapi aanze,
Aliingia ndani ya mgahawa mmoja na kuagiza chakula,
Pembeni yake kulikua kuna watu wana ongea na kutaja neno Tabata mwana nchi,
Kumbu kumbu zili mjia kipindi yuko shule mkoani Kilimanjaro alikua na rafiki anae itwa Hajrath Mpila ambae mara nyingi alikua akimtaka siku moja afike kwao tabata Mwananchi,

"Samahani kaka. Habari zenu?"

"Salama tu, vipi?"
"Naomba kuuliza eti sijui tabata Mwananchi, nita fikaje?"
"Anhaa,. Una ona pale kituoni, una panda gari za Ubungo, uki panda uta mwambia konda akushushe mwananchi huto potea"

"Asante nashukuru"
Kweli Witness ali tafuta gari la ubungo na kupanda, huku akimpa magizo konda yule ambapo kweli baadae alishuka Mwana nchi na kusimama bila kujua wapi aanzie.

Jioni ilikua tayari ime sha ingia alijisachi mfukoni na kuhesabu pesa alizo bakiza,
Ila bila kutegemea piki piki ili pita na mtu aliye kua ame kaa juu ya piki piki ali kwapua pesa alizo shika na piki piki ile kutoa mbio, kitendo cha sekunde kadhaa hakuona tena ile piki piki ili poelekea., na kubaki kama amechanganyikiwa.

"Pole sana sister,"
Ili kua ni sauti.ya mwana ume mmoja ambae alishuhudia tukio la Wit kuporwa pesa.
"Sister una elekea wapi kwani?"
"Sijui nime changanyikiwa hapa, naomba niache kidogo"
"Hapana nataka niku saidie, Naitwa Mudi, kwani uli kua una elekea wapi?"

"Kuna rafiki yangu namtafuta sasa sijui nita mpata vipi?'
"Anaishi wapi?"
"Mitaa ya huku huku ila sijui wapi kwao"
"Sio mbaya nita kusaidia kwa kua usiku umeshaingia twende kwangu alafu kesho tuta fanya kazi iyo"

Kwa wakati huo Witness hakuwa na ujanja wowote wa kuka taa sababu hakua na pesa wala sehemu ya kulala, ivyo wali ongozana na Mudi ambapo hapa kua mbali na sehemu waliyo kutana,
Ali fika nyumbani kwake na kumkaribisha. Nyumba hiyo ili kua ni chumba kimoja na sebule.
"Karibu jisikie upo nyumbani"
"Asante"
Mudi aliingia jikoni na kuanza kupika chakula kilipo iva ali mkaribisha na wote kuanza kula,
Baada ya chakula kuisha Witness alishukuru na kunawa mikono.
"Sasa utalala humu chumbani mi nitalala sebleni"
Mudi alifungua chumba hiko na kumkabidhi funguo huku yeye akirudi sebleni,

Kwa mbali alihisi mkono wa mtu una mshika kifuani , wakati mwingine alidhani ana ota kutokana na uchovu alio kua nao,ila hali.ile ina zidi na kufumbua macho,
Macho yake yana gongana na Mudi ambaye alikua pembeni yake , aliruka pembeni na kukaa vizuri kitandani.
"Nini sasa Mbona ivyo?," alihoji Mudi.
"Una taka nini"?
"We mtu mzima, hujui nacho taka jamani"
"Kama ndo ivyo naomba niondoke, mi siwezi"
"Sasa huwezi nini?, hivi unadhani nilivyo kusaidia ili kua bure?: usi lete masi hala wewe hapa mjini hakuna cha bure,., "
Mudi alizidi kumsogelea huku aki mvuta shuka. Ila alizidiwa nguvu,
Alicho fanya Mudi alitoka nje na kufunga mlango kwa nje,, na baadae kurudi na watu wapatao watano.
Wana ume hao waliingia chumba alicho kua Witness na kuanza kumshika kwa nguvu huku waki mziba mdomo ili asiweze kupiga kelele yoyote ile.


 Witness alija ribu kutumia kila aina ya nguvu alizo kua nazo kuji toa mikononi mwa wana ume wale ila aliji kuta ana shindwa, Wali mshika miguu yote na kuipanua wali mvua nguo zake na kuanza kumwingilia kimwili bila ridhaa yake ,
wali anza kumbaka kwa kupo kezana mmoja baada ya mmoja. Kila aliye ridhika na kukidhi haja yake alitoka na kumuachia mwenzake bila kujali Witness alikua katika maumivu ya hali gani.
Maumivu makali aliyo sikia sehemu za siri haku weza kuya stamihili alihisi maumivu makali sana kuliko maelezo.
Na taratibu kuanza kuishiwa nguvu akiwa juu ya kitanda kile huku mijitu ile ikiendelea na zoezi lile bila kupumzika.

"Oyaa Ali, we Ali , Ali msala huo, demu mbona katulia?"

Mmoja wa waba kaji wale ali jikuta akishangaa baada ya Witnes kubaki kimnya bila kuongea chochote hali ile ina wafanya washtuke wote na kuanza kuangaliana kwa uwoga na ukimnya kuta wala.

".Sasa ita kuaje mwanangu?"
"Ita kuaje nini?, we si una ona mtu katulia hapo, ?KADEDI huyo"
"Ndio katulia nakuuliza ita kuaje?, kama wote tume mfanya sasa, tusha uriane, , hii kesi ujue Arif"
"Sikieni. Subiri giza liingie, tuka mtupe kule jalalani, maana hapa huu msala mkubwa kaka"

Walishauriana kila kitu na baadae kuubeba mwili wa Witness na kuutupa mbali na pale maeneo ya Dampo la uchafu,

Wali vyo hakikisha hakuna mtu wa aina yoyote yule aliye waona wote wali geuza na kurudi huku waki uacha mwili ule jalalani pale.

********

Maumivu makali aliya sikia sehemu za siri,

Alijaribu kuta fakari ni sehemu gani alipo kwa mbali kumbu kumbu zina mrudia na kutambua alipo hii ni kutokana na kufumbua macho, ali jikuta yupo jalala la uchafu huku watu wakiwa wame mzunguka waki mshangaa,,
alikumbuka vizuri sana jinsi alivyo ingiliwa kimwili kinguvu na kuzidi kuumia alivyo taka kusi mama alishindwa kuto kana na maumivu makali sana aliyo kua aki sayasikia wakati huo.

"Dada habari yako?"
Ili kua ni sauti ya msamaria mwema aliye kua pembeni yake huku watu wengine wakiwa mbali waki wa tazama.
"Nzuuuri"
Aliitikia Witness kwa sauti ya chini sana na kinyonge.

Bila kupoteza muda mwana mke yule msamalia aliomba msaada kwa wengine ili zoezi la kumpeleka hospitali lianze,

Haraka haraka bila kupoteza muda wali tafuta tax na safari ya kwenda hospitali kuanza.

Wali tafuta hospitali ya karibu na maeneo hayo na papo hapo madaktari kuanza kufanya kazi yao,

Walianza kumkagua kila sehemu na matibabu kuanza bila kupoteza muda wa aina yoyote ule,.

Siku baada ya siku hali ya Witness ilizidi kuendelea vizuri akipata matibabu chini ya usi mamizi wa msamaria mwema yule ambae mpka wakati ule hakuweza kumtambua wala kumjua.

"Mwanangu pole na yaliyo kukuta, sasa hivi una endeleaje?"

Alimuhoji Mama huyo na kuji tambulisha huku mkononi akiwa na Hotpot la chakula.

"Naendelea vizuri"
"Mimi naitwa Mama sabrina, sijui mwenzangu una itwa nani?"
"Naitwa Witness"
"Pole sana, nime toka kuchukua vipimo vyako vya mwili hapa kutoka kwa daktari,"

Witness kusikia vile alikaa sawa na kuegemea ukuta, na kumuomba Mungu sana kuwa isije ika tokea ame ambukizwa virusi vya Ukimwi, na alijua aliingiliwa bila kinga yoyote.
Ila hakua na tumaini lolote baada ya kumuona mama Sabrina anaangalia chini huku akionekana ana sikitishwa sana na majibu yale

"Hapa mjini una ndugu yoyote?"
"Hapana"
"Ila hakuna shida, ngoja nikupe majibu yako,. Kutokana na vipimo vya damu ulivyo pimwa na Daktari ina onyesha kuwa ume athirika na Ugonjwa wa Gonorea, ila pia cha kushukuru Mungu damu yako safi, hauku adhirika na maambukizi ya Ukimwi mwanangu,"

Jibu lile lili mfanya Witness akae vizuri kana kwamba haja sikia vizuri au wenda alipewa majibu ya uwongo ambayo yange mfariji katika hali aliyo kua nayo.
Ukweli ni kwamba majibu aliyo pewa yalikua ni ya ukweli mtupu wala Mama Sabrina haku kosea, alimpatia dawa za mati babu ili aweze kuzitumia kwa wakati huo akiwa hospitali na chakula pia ili ale.,
"Uki maliza kula chakula, uta weka mezani vyombo, mi naenda kwenye majukumu, nita rudi baadae mwanangu"
"Sawa Mama sabrina, nashukuru sana Mama angu"

Ali shindwa kuelewa kwanini Mama huyo alitokea kumsaidia kwa kipindi hiko.

Baada ya kumaliza kula chakula,
Alifanya kama alivyo agiwa,
Ghafla fikra za kubakwa akizi changanya na Kubakwa kwa Mama yake mzazi zili mjia kama upepo kichwani,
Na kugundua kiasi gani mama yake alipata maumivu kiasi kile,
Msongo wa mawazo ulizidi kuta wala kupita ndani ya ubongo wake kama kimbunga kikali,na kuku mbuka baba yake Alivyo uwawa kika kitili, alikiona kichwa cha baba yake mzazi kiki dunda ndani juu ya malu malu, mambo aliyo kua akiwaza hapo alihisi anayaona mbele yake.

Kutokana na msongo wa mawazo usingizi uli mpitia na kulala fofofo kitandani.

"Jamani Jafari una endeleaje kaka angu?"

Ili kua ni sauti ili yo kua ina toka pembeni mwa kitanda alicho lazwa witness kafifi,
Sauti hii aliweza kuitambua japo alikua katika usingizi ame fumba macho, aliweza kuitambua sana ila hakua na uhakika sana kama ndo yenyewe , ali hakikisha baada ya kugeuza shingo nyuma na kufumbua macho,

Hakuamini alivyo gonganisha macho yake na msichana wa makamo aliye kua mbele yake ambae kipindi wapo shule wali kua wana pendana kama mapacha hasa kwa maumbile yao yaliyo fanana kupita maelezo,

"Hajra"
Witness aliita huku akiinuka kitandani na kukaa vizuri hii ni kutokana na kutokuamini mtu aliye muona mbele yake
"Witness".....

 Aliji kuta ana rejewa tena na nguvu bila kujua zilipo toka hasa alipo muona rafiki yake huyo ambae aliye mfanya mpaka yeye Afike maeneo ya Tabata,

Sio upande wake pia hata upande wa rafiki yake Hajrath Mpila, aliji kuta ana furahi na kusahau kwamba ana kaka yake mgonjwa alikuja kumuona.

"Witness una jua mpka sasa hivi siamini, ime kuaje upo hospitali?, una tatizo gani?"

Swali lile lili mfanya Witness aangalie chini kwa muda na machozi kuanza kumlenga lenga, ki ukweli alihisi kama kapigwa msumari wenye moto juu ya kidonda kilicho anza kuka uka,

"Nita kwambia kila kitu, ila ki ufupi nili kuja kuku tafuta Hajrath,. Sina ndugu yoyote hapa Dar es salaam kwa sa.."
"Shsss shhs mimi ni ndugu yako Wity, tume toka mbali tuta ishi wote kwa wazazi wangu, pole sana.pole na msiba "

Hajrath alimsogelea Witness na kumkombatia huku aki mpiga piga mgongoni kama ana mbeleleza mtoto mdogo alale,
kweli Hajratha alionyesha moyo wa dhati na mkunjufu na hio ndio ili kua sifa yake kuu,
"Huyu una emuona hapa ni kaka yangu ana itwa Jafary, ana umwa ndo nime kuja kumuona,"
"Jafari huyu ni rafiki yangu tena ni zaidi ya rafiki yangu, ana itwa Witness"

Uta mbulisho huo mfupi aliutoa Hajrath ambapo wawili wale wali peana mikono na kufahamiana , Baadae ana kuja Mama Sabrina na wote kumuaga , Witness hakuacha kumshukuru Mama huyo ambaye ali msaidia kwenye kila kitu tangu yupo hospitali.

Kwa mapenzi ya dhati bila kuji fikiria Hajrath alimchukua Rafiki yake huyo kipenzi mpaka nyumbani kwao ambapo hapo alikua ana ishi na wazazi wake wote wawili,

Mwendo wa dakika kumi tayari wali shafika nyumbani , ambapo ali onyeshwa bafuni huku baadae alionyeshwa sehemu ya kulala, ivyo ndivyo ilivyo kua,.

"Dad, huyu rafiki yangu ana itwa Witness, ana matatizo sana, nili kua naomba akae hapa nyumbani"

Hajrath aliongea usiku huo na baba yake Mr. mpila ambapo pembeni alikua ame keti mke wake ,

"Sija kuelewa mwanangu, una niomba au una niambia?"
"Nakuomba Dad"
"Hapo huja niomba, hapo una niambia maana tayari yu..."
"Aaah nawewe baba Hajrath, mbona una penda kumnyima mtoto raha sasa, kaja na rafiki yake ana matatizo, kakuomba, umsaidie"

Mama Hajrath aliingia malumbano yale.
"Mimi sina tatizo mke wangu,. Wala sina tatizo binti, aya ataishi hapa,ila kama una vita bia tabia vya ajabu ajabu hapa sio mahala pake, sawa binti"

Mzee huyo wa makamo ambae uso wake haukuwa na masihala hata kidogo alimaliza kusema hayo na kuondoka maeneo hayo ya sebleni akielekea chumbani,.

Siku zili enda na majuma kupita huku Witness akiendelea kuishi katika nyumba hiyo kama mwana familia, haku baguliwa wala kunyanyaswa ivyo ili mfanya aanze kusahau kila kitu na asahau mambo yali yopita,

Siku moja Hajrath aliamua kumtoa maeneo ya nyumbani na kumpeleka mazingira mengine ili wakale chakula cha mchana,

"Shemeji yako ana kuja subiri uta muona"

Aliongea Hajrath huku wakiendelea kula chakula,na kumfanya witness awe na shauku ya kumuona Huyo mtu aliye ambiwa kuwa ange kuja muda mfupi.

Baadae muda mchache Witness ana ona gari aina ya Mazda ime eegeshwa pembeni,
na mwanaume mmoja aliye vaa suti nyeusi na kuchomekea shati lake vizuri na kumfanya azidi kuwa mtanashati ,alishuka ndani ya gari hilo dogo huku akiuendea mgahawa huo wa chakula.

Aliwaendea mpka walipo kaa na mwana ume yule kwenda moja kwa moja na kumziba macho Hajrth ambae kipindi ana kuja hakumuona kutokana kwamba alitokea nyuma yake.

"Mmmh baby huyu"
Hajrath aliongea baada ya kushika mkono wa mwana ume yule aliye mshika,
"Hahaha ume nijuaje?"
"Aaaah chezea, sasa mimi nisijue harufu yako"?

Mwana ume yule alivuta kiti na kukaa pembeni yao,

"Baby huyu ana itwa Witness ni rafiki yangu sana,, witness huyu Emma Kway ni boyfriend wangu,"
"Nashukuru kuku fahamu shemeji"
"Na mimi pia"
Wali peana mikono na wote kuta basamu,
"Ila mbona kama hilo jina Emma Kway sio ngeni kwangu?"
Alihoji witnesa baada ya kuta fakari kwa muda kidogo.
"Hilo jina, Emmanuel Kway, wewe ni mtunzi shemeji"?
"Ndio ni mtunzi wa vitabu."
".basi ndo maana, nili kua naji uliza hilo swali, nime kusikia wapi, basi nishapata jibu mimi nili kua mpenzi sana wa vitabu vyako hasa ile stori ya THE PAINFUL SECRET, kwa kweli una kipaji sana, una mpango gani?"

witness alikaa sawa na kuanza kumdadisi mwandishi huyo wa vitabu.
"Nina mipango mingi sana, nina page yangu facebook nime fungua ina itwa Story za KWAY nataka stori zangu zifike mbali na kila mtu asome, na mipango mingi sana ninayo,, sasa hivi nafanya kazi katika kampuni ya KAY STALLION ,"

"Hajrath , shemeji ana kipaji sana,. Alafu pia ni mchanga mfu sana kwa kweli"

"Hahaha, ujue nampenda sana huyu mwanaume basi tu yeye hajui"

Waliongea mengi sana siku iyo na kuzidi kujuana ki ujumla, baada ya hapo Emma kway aliwaaga na kulipa deni la chakula na vinywaji huku aki mbusu Hajrath huku akiishia zake.

Taratibu za nchi ya Tanzania ili kua kila wana funzi wata kapo maliza vidato vya sita waingie jeshini ivyo Hajrth ali kua ni miongoni mwa watu wana ota kiwa kuingia jeshini ,

Upande wa Witness nayeye alitaka kuchukua nafasi hiyo nayeye aweze kuingia jeshini,
Japo kua aliishia kidato cha nne na kushindwa kuendelea ila haku taka nafasi hiyo impite hata kidogo.
Ki ukweli siku moja ali tamani aje kuwa mwana jeshi tena COMANDO, ili aweze kupi gania nchi yake ya Tanzania, upande mwingine uliyo jificha pia alitaka awe mwana jeshi kwa lengo moja tu, kulipa kisasi kupitia mgongo huo.

Taratibu za kuanza kwenda kambini zilianza huku waki tenganishwa mikoa ya kwenda .Witness alicha guliwa kwenda Mkoani TABORA huku Hajrath mkoa mwingine,

Ili kua majonzi sana kwao kutenganishwa tena, ila wali amini kitu kimoja tu wange kutana tena siku yoyote ile.

Siku iyo Witness akiwa ubungo aliingia ndani ya basi kubwa la Tabora akiwaaga wazazi walio mle kwa kipindi hiko na kuwa shukuru huku machozi yakimtoka kwa uzuni sana,

Basi hilo lili ruhusiwa na kuanza safari yake.

Jioni ili fika na tayari alipokelewa na gari la jeshi ambalo lili kuja kumchukua,

Kila mwana jeshi alimshangaa kutokana na urembo wake wali amini kua hatoweza jeshi wala kusta himili mateso ya depo.

"Binti shuka hapa upesi,. Anza kukimbia tukukute kwenye ule mlingoti, ushaingia depo tayari"

Kauli hiyo aliitoa mwanajeshi mmoja, ambapo witnes alitii na kuruka nje ya gari na kudondoka kama mzigo, alijizoa zoa huku wana jeshi wale waki mbeza na kucheka.,"kweli uta weza jeshi wewe, au ume kuja kuuza sura."?

Alipo kua pale mpaka kwenye mlingoti ule, uli kua ni umbali wa kilomita tatu,
Ivyo ivyo aliji kaza maana alijua mbeleni kuna mateso zaidi na zaidi ya hilo, ali piga moyo konde na kuanza kuki mbia,.

Kwa mbali alisikia kelele za watu waki fanya mazoezi,
Akiwa ana shangaa alikuja mtu mwingine na kumchukua na kumuonesha mazingira ya kambini baada ya kuoneshwa kila sehemu, ali ruhusiwa kwenda kupumzika kutokana na uchovu aliji kuta ana lala.

Kilicho mshtua yali kua ni maji ya baridi sana aliyo mwagiwa kitandani ilhali kulikua kuna baridi asubuhi hiyo kupita maelezo,
Alikurupa na kukaa kitandani.

"Mwana jeshi kamili ana takiwa kuwa mkakamavu, mwana jeshi ni mlinzi wa taifa, mwana jeshi halali,,dakika tatu nawapa muwe gwaride"

Sauti hiyo ili sikika kutoka kwa kiongozi wa kambi ambae mkononi ali shika ndoo ya maji.

Pilika pilika za huku na kule zilianza kila mtu alishika kile alichoona kina faa na wote kutoka nje kuelekea uwanjani,

Ambapo dakika chache walianza kukimbia mchaka mchaka huku wakiimba nyimbo.

Baadae kufika kila mtu alinyolewa nywele na kubaki vipara,
Ukame wa sehemu hiyo lililochanga nyika na jua kali sana lili mfanya Witness azidi kuteseka ila haku taka kukata tamaa, upande wa maji ili kua ni shida sana pia, vile vile hata chakula wali kifuata mbali sana,

Taratibu Witnes alianza kuzoea mazoezi ya jeshi hasa ya kubeba dunia, kukwepa ndege,
Yote alivumilia na kujua ipo siku ata fudhu na kuwa commando baada ya kuhitimu,na iyo ndio ilikua ndoto yake.

Ndani ya kambi hiyo Msange JKT, 823 kj usiku wa siku hiyo ali sikia parakacha parakacha za mtu akiwa ndani kana kwamba ana tafuta kitu., mtu huyo alimsikia ana kuja upande alipo na kumfanya Witness akae sawa kijeshi kwa ajili ya kumkabili.

"Witnes, witnes,"
Sauti hiyo ya chini chini ili muita huku iki mgusa mguu,
"Jaqliin una taka nini usiku sasa hivi?"
"Tutoroke twenzetu nje, mi nina hamu na sigara"
Msichana huyo ambae alikua rafiki yake pekee katika kambi hiyo alimuomba Witness amsindikize.
"Sasa tuki kamatwa Jaq?"
"Hatuwezi, twenzetu,. Fanya haraka sasa"
"Basi subiri nita fute kitu cha kuvaa"
"Kamata sweta hili, fanya fasta fasta"
.witness alishuka kitandani na kuongozana na rafiki yake huyo ambae alionekana ni kiburi na mzoefu sana hasa katika maswala ya kutoroka kambini.,

Japo kua giza lili kua nene sana, ila upande wa Jaqlin hakuonesha kuogopa kitu chochote, wali pita pori kwa pori huku akitembea umbali mrefu.
"Hatu fiki tu?"
"Tusha fika"
"Tangu kule una niambia tusha fika, , ila hatu fiki ,Kua mkweli"

Baada ya kuvuka kipori hiko wali fika mjini na jaqlin kununua pakiti za sigara,
Ali washa pale pale na kuanza kuvuta.
"Jaribu hii"
"Hapana mimi siwezi."
"Wacha woga wewe, Mwana jeshi hapaswi kuogopa, embu kamata Embassy, weka mdomoni, namna hiyo"
Jaqlin kiufundi ali muashia sigara ile witness na kuanza kuivuta, ali vuta fundo la kwanza na kuanza kukohoa kutokana na Moshi ule kumpalia.

"Tatizo lako wewe wa kishua sana, vuta taratibu kama hivi navyo fanya"

Jaqlin ali fanya juu chini ili aweze kumshauri rafiki yake huyo aweze kujua kuvuta sigara,
Baadae nayeye witness ana jikuta ana enda sawa na kuanza kuvuta sigara, taratibu za kurudi kambini zilianza huku wakiwa na sigara zao mkononi.

Tayari watu wote wali kuwa gwaride ila cha ajabu wali shangaa kumuona Mkuu wa majeshi ana kuja na kujua kuna kitu kimetokea.

"Kuna watu wali toroka jana waje mbele hapa upesi,"
Aliongea mkuu huyo akiwa ana tembea tembea huku aki kagua gwaride hilo. Moyo wa Jaqlin ulizidi kwenda mbio kuliko kawaida na kumwangalia Witness.
".sitorudia tena, , watoke mbele, kabla sija gairi na kufanya adhabu hiyo iwe ya kambi nzima,. Kama una wa jua uwa taje mara moja, maana mtapata shida sana, "

Jaqlin alizidi kutetemeka maana. ana jua sana adhabu ya kutoroka inavyo kua,
,.
Ila cha kushangaza alimuona Witness taratibu ana pita mbele huku akimwangalia Jaqlini machoni.

"Mwenzako yuko wapi binti?"

Witness alimuangalia Jaqlin na kumuona jinsi gani alivyo kua aki tetemeka kwa uwoga
"Nili kua mwenyewe."
Aliongea Witness kwa kuji amini huku akimuangalia mkuu yyule kwa kujiamini sana...

 "Ulikua na mwenzako yuko wapi?".

Alizidi kuhoji mkuu huyo huku akimsogelea Witness.
"Nili kua peke yangu,"
Mkuu yule alimsogelea Witness na kumpiga kofi zito lili-lo mpelekea Witness adondoke chini.
Alimuinua na kumpiga kofi lingine. Safari hii ili wafanya makuruta wengine waanze kuingiwa na hofu kubwa sana huku waki shuhudia mwenzao ana pokea kipondo kikali sana bila huruma yoyote.

"Twende huku,.. iyo adhabu ya mwenzako uta ifanya,"

Mkuu yule aliondoka na Witness maeneo yale akienda nae sehemu ambayo ili kua kame sana na yenye jua.

Upande wa pili wa mkuu huyo aliye itwa Ndibalema alikua ame kataliwa kimapenzi na Witness ivyo hasira za kunyimwa penzi alizi changanya ndani ya adhabu hio na kufanya juu chini ampe Adhabu kali witness .

"Wewe si una jifanya mzuri, mimi sikuwahi kuka taliwa hapa kambini na msichana yoyote yule, embu roll hapo."

Witness hakua na jinsi alicho fanya alianza kubiringika kama tairi huku akimwagiwa maji machafu , alibilingika huku akimwagiwa maji , mateso yale yalizidi hasa jua lilipo anza kuwaka na kuwa kali mno kupita maelezo,

"Hivo sio ku roll, nimekwambia roll, mpka kule mwisho, haraka sana, leo uta kiona cha mtema kuni"

Witnes ali fanya kile alichoambiwa ila ili kua sio kitu kwa Ndibalema,
Adhabu hiyo iliyo changanyika na mateso yalizidi , ila haku kata tamaa , zoezi lili badilishwa na sasa hivi ilikua adhabu inayo itwa kibatabata, siku nzima ili kua ni chungu kwake.,

akiwa kati kati ya adhabu hiyo ghafla aliishiwa nguvu kutokana na njaa kali iliyo kuwa ina kwangua utumbo wake, kizungu zungu kili kuja na kudondoka chini pale pale huku kichwa kikizidi kumuuma kana kwamba kuna mtu ana kipiga na nyundo.,
"Simama juu, acha kuji fanya"
Sauti hiyo isiyo kua na huruma ili muamuru witness,ila

Alitii na kuendelea na adhabu ile huku akiji kaza, ila upande wa pili alijua kua yote yataisha,

Alipiga moyo konde na kuzidi kupambana na adhabu ile, jambo lile lina mshangaza sana Ndibalema ambapo mahesabu yake alitegemea wenda Witness atabadili uamuzi na kumpa penzi, ila mambo yana kua kinyume na kumuona Witness akizidi kupambana na adhabu ile tena bila kubisha kama wana vyo fanya wengine.

Mazoezi ndani ya kambi hiyo yaliendelea kama ipasavyo, huku makuruta hao wakizidi kupewa mafunzo ya kulenga shabaha,
jambo la kulenga shabaha lina wafurahisha sana Wanajeshi hao ambapo witness ana kua hodari sana katika ulenganyi wa shabaha na matumizi mazuri na bunduki,.
Kila alilo fanya Witness alili fanya kwa umakini sana kwa sababu alielewa vizuri sana nini ana kifanya na kuki tafuta,

Ndoto za kuja kuwa mwana jeshi na baadae kuwa komando ana ziona zina karibia hii ni kutokana na kufudhu tayari mafunzo ya jeshi , na sasa hivi tayari kuwa mwana jeshi kamili baada ya kuka bidiliana na mazoezi yote kambini.

Haku taka kuishia hapo ana omba tena nafasi ya kutaka kuwa Komando,
Ambapo miongoni mwao kulikua na watu takribani kumi waki taka nafasi hio.

Bila kipingamizi chochote kile
Watu hao kumi wali chukuliwa moja kwa moja mpaka nchini CUBA,

furaha ilizidi kutoka kwa Witness baada ya helikopta hiyo kubwa ya jeshi kubwa,.kutua juu ya uwanja wa ndege wa Moscow wa kijeshi,

ambapo hapo wali pokelewa na makomandoo walio shiba walio kua na misuli na kupanda hewani na wote kuingia ndani ya HAMMER za kijeshi ,

Witness ali tabasamu hasa alivyoona ndoto yake ina enda kuchepua.


 Hammer iyo ya kijeshi ili zidi kusonga mbele huku Witness akiwa na kazi ya kushangaa majengo ya nchi hiyo ya Russia. ambapo majengo yake yalipanda juu sana na kumlazimu witness apandishe kichwa juu akistaajabu urefu wa magorofa hayo ndani ya nchi hiyo.

Hammer izo ziliingia moja kwa moja ndani ya kambi ya jeshi mjini Moscow.Ambapo nchi hapo kulikua na helikopta nyingi za kijeshi.
Gari hilo la kijeshi aina ya Hammer lilifunguliwa milango na Witnes kushuka huku wana jeshi wengine waki fuatia.

siku chache zili pita huku akizidi kuzoea mazingira ya kambi hiyo ambapo tayari mazoezi yakiwa yameanza..

Huku katika mitambo ya mawasiliano yaki ongozwa na Mwana mke wa kirusi Aitwae Amina Bulembo ..

Mazoezi makali tayari alianza na mafunzo mbalimbali yakiambatana na mateso ambayo bina damu yoyote hawezi kuvumilia. ila kwa witness Kafifi haku kata tamaa.

siku iyo wakiwa milimani wakiwa na mabegi makubwa migongoni yakiwa na mawe mazito ndani yake akiwa mazoezini

miguu ilizidi kutitia ndani ya michanga mingi ambapo ili kuwepo juu ya mlima huo mrefu sana ambapo alikua ana karibia kufika juu kileleni.

Kila Witnes alipo zidi kupiga hatua kwenda juu ndipo nguvu zilivyo zidi kumuishia,
nguvu zili muishia huku akianza kukosa muhimili wa kusimama na ghafla kuanza kurudi nyuma na kudondoka huku akirudi nyuma kwa kasi akibiringika kama tairi,

ila aliji kuta ameshikwa mkono wake ghafla alivyo geuza shingo alimuona mwanaume mrefu kiasi aliye jazia kifua na yeye pia alikua ame beba begi kuashiria kwamba alikua kwenye mazoezi,
"are you okay"?(uko salama?)
aliuliza mwana ume huyo huku aki mtazama witness machoni.
"yes am okay"(ndio nipo salama)'

Witness alimjibu huku aki pewa mkono wenye misuli na mwana ume aliye simama pembeni yake.
Ila kabla hawa jasimama vizuri Witness aliteleza tena na kumdondokea mwana ume yule na wote kuanza kuporomoka kuelekea chini ya mlima huo uliyo jaa michanga mingi sana.

walizidi kuporomoka kuelekea chini na mwishowe kutulia huku mwana ume yule akiwa juu ya Witness ana mwangalia.
joto kali huku damu ya Witness ikizidi kwenda mbio kuliko kawaida vina mshangaza sana na kuzidi kumwangalia mwanaume huyo aliye kua juu yake akimtazama machoni.

taratibu mwana ume yule alimsogelea mdomoni na kuji kuta wana pigana mabusu ya mdomoni na pale pale kuji kuta wana fanya mapenzi bila kutegemea.

"stop stop. leave me".(subiri subiri niache).
witnes alifoka na kuji toa kwa mwana ume huyo ghafla na kusha ngazwa na jambo lile la ghafla ambalo lili tokea sekunde chache zili zopita. alivuta tisheti yake haraka haraka na kuivaa huku akimpa Mgongo mwanaume yule.
"where are you going? come back"(una kwenda wapi rudi)?
"i said leave me,we haven't done any thing, understood?"(achana na mimi.hatu kufanya chochote. Ume nielewa?"
Witness aliongea kwa ukali huku akimwangalia Mwana ume yule machoni na kwa aibu sana.

"by the way am stuwart"
aliongea huku akimpa mkono Witness .
"witness"

alijibu witnes kwa ufupi na kumpa mkono stuwart. huku akimpa kisogo na kuendelea na zoezi la kupanda mlima ule.

ulengaji wa shabaha kwa kutumia bastola unazidi kuwa shangaza kila mtu ndani ya kambi ile.
Ki ukweli Witness alikua mlengaji mzuri sana wa shabaha kuliko maelezo.

mafunzo ya kutisha ana zidi kuyapata Witness na kumfanya azidi kuwa shupavu na hodari sana kuliko alivyokuja mwanzo. safari hii aliweza kuogelea kwa umbali mrefu sana bila kutoa kichwa nje.jambo hilo lina mpa sana tumaini..

Taarifa mbaya zina wafikia kutoka kwa msichana mrembo ambaye alikua ni mtaalamu katika maswala ya mitambo Amina Bulembo.
ana pokea taarifa kutoka kwa raisi mkuu wa Russia awaandae makomando kumi shupavu.

ambapo kati ya watu hao kumi Witness ana chaguliwa nayeye kuungana na jeshi hilo dogo la makondoo na kufanya azidi kuingiwa na wasi wasi kwa sababu ndo ili kua mara yake ya kwanza kwenda vitani.
"oooh my God"
witness aliji semea hasa alipo muona Stuwart ni miongoni pia katika jeshi hilo. .

 ...hisia kali za kimapenzi haku taka zita wale ndani ya moyo wake juu ya Stuwart.
hakutaka nafasi hiyo itokee kamwe ivyo anaamua kupambana na nafsi hiyo.

usiku wa siku hiyo aliji kuta ana muwaza Stuwart wala si vinginevyo na huku taratibu usingizi uki mchukua uki msindikiza na mawazo ya vita ambayo anaenda kuka biliana nayo siku chache zijayo.

Kikao cha makomandoo takribani kumi na tatu kili kua tayari kipo katika maandalizi ya kuelekea vitani akiwemo Witness Kafifi.

"Mtakwenda Iraq,huko mta pambana na wata li ban kuna huyu mtu anaitwa Said bin Laden ni mtoto wa Osama bin Laden. namtaka akiwa mzima.ivyo basi mta shukia mji mkuu hapa. Brian na kikosi chako mta shukia hapa."

maneno hayo yali mtoka mzee wa makamo mfupi kidogo mwenye kitambi kwa haraka haraka alikua ni mzee wa miaka themanini . nguo zake za kijeshi alizo vaa zili mfanya kabisa ajulikane ndio mkuu wao yaani captain.

aliongea huku akiwa ame simama huku mbele yake kukiwa na ramani kubwa sana . ambapo nyuma yake wali kua wame kaa makomandoo waki msikiliza kwa makini sana kama darasani.

"Amina Bulembo. nina uhakika katika suala la mawasiliano hakuna tatizo lolote?"

"hakuna tatizo lolote captain"

alijibu kwa kiingereza.
.kila kitu kilienda sawa huku maelekezo machache yaki tolewa. na kupangiwa muda kua saa tano usiku wawe tayari washaanza safari ya kuelekea Iraq.

kweli katika saa ya uku tani ili onesha kuwa ni masaa matatu yali baki kwa wao kujiandaa. si vinginevyo bali captain aliwaaruhusu kila mtu akajiandae kwa safari hio ya kupambana.

"upo tayari Witness?"
alihoji Stuwart wakiwa wana toka nje.
"bado nina ka uwoga fulani"

waliongea kwa lugha ya kiingereza ambayo ndo ilikua lugha kuu wakitumia.
"usiwe na uwoga swala ni kujiamini tu.,alafu katika ulengaji wa shabaha uko vizuri sana"
"yaani sipo tayari kabisa naona moyo wangu mgumu"
"niamini tuta shinda."

baada ya hapo kila mtu alienda kuji panga ipa savyo..

Witnes ali badili nguo haraka haraka. na kuvaa nguo za jeshi huku aki chomeka bastola.
kiunoni kwa nyuma na nyingine pembeni ya kiuno.

alitoa kisu na kukiangalia vizuri na kuki sindika vizuri ndani ya buti refu.

aliangalia mezani pale na kuona mtutu na kuunyanyua. aliubeba vizuri akiwa ana ujaribu jaribu, alivyo hakikisha una mfaa aliuweka ndani ya begi kubwa .na kuchukua magazine za mtutu ule ambao ulijaa risasi na kuchomeka mfukoni baada ya hapo alichukua camera na kuweka ndani ya begi.

alivuta pumzi ndefu huku akifumba macho.

"Hei tayari muda ume fika"
"nakuja nakuja. namalizia"

Witnes alijibu na kuanza safari ya kutoka nje ambapo alitembea kidogo na kuona helkopta kubwa ya kijeshi ambayo wakati huo mapanga yali kua yana zunguka kwa kasi sana kuashiria kwamba ipo tayari kwa kuanza safari ya kupaa angani usiku huo..

"tuku tukutukutuku"

helikopta hiyo ili zidi kuunguruma kwa mlio wa juu sana huku vumbi likizidi kuta pakaa eneo hilo.

"fanyeni haraka haraka.,wekeni vichwa vyenu chini.ingieni ndani ingieni ndani"

aliongea kwa sauti ya juu Humprey Novick kutokana na kelele za helkopta hio.

kweli mmoja mmoja aliingia ndani ya helkopta hiyo na taratibu kuanza kuruka huku ikiacha vumbi kali chini.

maasaa mawili yalitumika angani mpaka walipo fika Iraq kati kati ya msitu huo na kushuka na kamba mpka chini ambapo helikopta hio ili kua ina elekea angani .,
wali shuka mmoja baada ya mmoja na mwishowe kuisha huku alikopta hio ikirudi ilipo toka.

Witness tayari aliingia ndani ya msitu huo mnene na mzito tena wenye miti mingi sana.

"Hapa ina bidi tulale kwanza alafu kuki kucha tuanze ambush"
"sasa tuta lala wapi humu una dhani?"
"una maana gani kusema ivo?"
"namaana kwamba hakuna pa kulala"
"una matatizo sana Victor. tuta lala ndani ya msitu huu huu. yame salia masaa machache.kijiji chenyewe kipo kule bondeni"

0 comments:

Post a Comment

BLOG