Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 6/10


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 6 KATI YA 10
*******
 *******

Kesho yake asubuhi alianza tena kupakia vitu vyake ndani ya begi kwa ajili ya kuhamia katika
nyumba yake aliyonunua maeneo ya msasani, anaweka kila kilicho chake ndani ya begi kubwa na kufunga mlango wa hotel hiyo, baada ya kufika mapokezi ana mkabidhi mwanamke aliye kua hapo funguo zake na kuta futa taxi moja wapo kati ya nyingi zilizo kua nje ya hotel hiyo.

Safari ya kuelekea msasani ilianza akiwa ndani ya taxi hiyo kwa kazi moja tu kumuelekeza dereva huyo mpaka nyumbani kwake,
baada ya kushuka ana mkabidhi dereva huyo pesa yake na kuingia ndani ya nyumba hiyo iliyo kua kubwa sana,

siku nzima alikua na kazi moja tu, kuweka kila kitu sawa na kufanya usafi wa nyumba nzima, ambayo ilichukua masaa sita mpaka kumaliza usafi wa nyumba hiyo kubwa licha ya kuwa na njaa sana hakutaka aache kiporo cha kazi hiyo,

kweli alimaliza kila kitu na kuamua kutoka nje ili aweze kupata kitu chochote aweze kula, baada ya kutoka nje ya geti anatembea kidogo na mbele yake kuona super maket kubwa na kuingia,

alikagua kile ana chokitaka na kuweka kwenye kikapu aliporidhika alienda sehemu maalumu kwa ajili ya malipo.
"dada samahani nimesahau pesa nyumbani"
aliongea witnes hasa baada ya kujisachi na kuji kuta hana pesa wala kadi ya bank.
"nenda kachukue sasa"
"nita kuletea niamini"
"hapana hatu fanyi biashara hiyo hapa kachukue pesa uje kulipa ndo uondoke na mizigo yako "

dada yule aliongea huku akiendelea na shughuli kupiga hesabu na wateja wengine waliokuwepo pembeni yake.
"kwani huyu dada ana daiwa kiasi gani"?
sauti hiyo ya kiume ili sikika pembeni
kidogo na kumfanya Witness ambae aliye kua ana taka kuondoka asimame.
"elfu thelathini na mia tisa"
"mimi nita lipa, dada njoo uchukue vitu vyako"
aliongea kijana huyo na kutoa kiasi cha pesa nayeye pia kulipia vitu vyake .
"asante kaka"
"usijali , ulikua unaelekea wapi"?
"hapo mbele ndo naishi"
Witness aliongea huku akiwa mbele yake na
kumfanya kijana yule amwangalia kwa nyuma huku akizidi kumtathmin jinsi alivyo umbika na kubinuka kwa nyuma.
"mimi naitwa Frank"
"mmh naitwa Rachel, twende basi nika kulipe pesa yako ile uliyo nilipia"
"hapana usijali uta kaa nayo tu, nime kuja na usafiri twende nika kuache unapoishi"
"usijali nita tembea kaka angu"
"aaah hapana twende Rachel"
Ki ukweli Witness haku taka ajulikane jina lake halisi anaamua kujipa jina bandia,

baada ya kuingia ndani ya gari Witness alikua na kazi moja tu kumuelekeza Frank sehemu anayo ishi mpaka anapo fika,
ila kabla haja fika mbali macho yake anaya gandisha nje ambapo alimuona mtu anaye mfahamu vizuri sana na kufanya shingo yake igande kwa mtu huyo.
"anco Rameck"

alijisemea kimoyo moyo huku hasira kali dhidi ya mjomba wake huyo kupanda huku picha ya wazazi wake wakiuwawa kinyama kujijenga ndani ya ubongo wake, na kumfanya azidi kupandwa na hasira sana.
"Rachel"
Frank aliita huku akimshika bega Witnes ambapo
aliambulia kofi kali la shavu lililo muingia vizuri juu ya shavu, hii ni kutokana na hasira kali na mawazo mengi aliyo kua nayo Witnes.
"samahani Frank"
"usijali, una tatizo lolote?, maana nime kuita muda sana uli kua husikii. niambie una nini? unaumwa?,"
"hapana siumwi na tayari .nime fika, naishi hapo kwenye geti jeusi"

Witnes aliiongea huku akifungua mlango wa gari na kubeba chakula alichonunua na kushuka haraka haraka na kuingia getini akiwa na haraka sana.

alifika ndani kwa hasira na kuanza kubadili nguo kwa nia moja tu amrudie Rameck ambae mara ya mwisho alimuona Ubungo, ambapo alikosa nafasi ya kumuuwa na sasa hivi kamuona tena ivyo hakutaka leo hii ampe nafasi ya kuishi sababu alijua hatoutendea haki moyo wake.

 Hakutaka tena kula chakula ange fanya ivyo ange mkosa mbaya wake ambaye alikua akimuwinda kwa kipindi kirefu sana bila mafanikio ,
alichukua kisu kidogo na kukiweka mfukoni pia na kuji funga kilemba kichwani, alianza kutembea haraka haraka na mwisho kuli fikia geti na kutoka nje,
alizidi kukaza mwendo mpaka alipo fika ile sehemu aliyo muona Rameck iila alivyo angalia pembeni yake aliona gari lina washwa na Rameck kuondoka, alitamani achukue boda boda ila alihofia endapo ata fanya mauaji ata julikana hakutaka kumshirikisha mtu yoyote katika jambo lile, alitaka amalize yeye mwenyewe.

ALibaki akilisindikiza kwa macho gari la Rameck mpaka lilipoishia na yeye kurudi ndani kwake na kuanza kula huku mawazo mengi yaki muandamana kichwani juu kazi nzito itakayo mkabili mbele, ili kua sio kazi ndogo wala lelemama ivyo ili hitaji umakini wa hali ya juu kupita maelezo.

baada ya kumaliza kula ana sikia honi ya gari nje ya geti lake, kwa kua alikua juu gorofani alienda mpka kibaraza cha juu na kuangalia chini ili kujua nani alikua ana piga honi wakati yeye alikua bado mgeni maeneo hayo. ila anashuka ngazi baada ya kuona ni gari la Frank ambalo muda mfupi lili mfiikisha mpaka pale nyumbani kwake.

alili endea geti nakuli fungua geti akimruhusu Frank aingize gari ndani baada ya kuli egesha katika uwanja wa nje mkubwa wa nje hapo FRank alishuka na mfuko mkononi huku akimuendea Witness.
"mambo Rachel?"
"poa tu karibu ndani"
"asante sana"

Wote waliingia ndani na Witness kuwasha tv ambapo habari ya kwanza kuiona ili kua ni siasa na kumuona Mr,Sombe akiwa na vigogo wengine wakitangaza kuwa wana ziara jijini Arusha siku inayo fuata, habari ile ina mgandisha na kusahau kuwa ana mgeni pembeni aliye kuja kumtembelea siku iyo,
"Rachel Rachel!"
"Abee, samahani nili kua mbali sana"
"ina elekea una penda sana siasa"?
"ndio napenda sana siasa, ulijuaje ndo maana muda wote nilikua makini sana kusikiliza hii habari ya ziara"
"aaah mimi na siasa na vitu viwili tofauti Rachel"
"Frank samahani una tumia kinywaji gani, mpendwa"?
"chochote tu, nipe tu maji"

Witness alisimama na kuliendea friji lililo kua pembeni na kutoa maji kwenye jagi huku akiendea glass na kumninia Frank ambae muda wote alikua akimkodolea macho Witness usoni huku akishuka mpaka kwenye shepu yake ili yojigawa,
"mbona una niangalia ivyo Frank"?
"Rachel, sio siri ume umbika sana, ngoja nikwambie kitu kimoja, nime vutiwa nawewe Rachel"
"embu acha visi rani Frank, yaani kuniona leo tu"?
"sikia nikwambie, mimi sitaki kuwa kama mtoto wa sekondari, nime amua kufunguka kwako, tena ukini kubalia nitakuoa, naomba uwe mke wangu Rachel"
"acha masihara Frank yaani kirahisi ivyo, mi sio mtoto mdogo"
"kweli nakwambia"
"aya bwana, tutaongea siku nyingine FRank,nime kusikia"
"ila nataka leo tutoke outing usiku, hivi unaishi peke yako hapa"?
"yaah naishi mwenyewe humu ndani"!
"mmh una nitisha, ila ngoja niende alafu usiku nita kuja kuku chukua twende outing"
"poa, poa"

Witness alimsindikiza Frank mpaka nje na kuingia ndani ya gari
"naomba basi uli fikirie lile swala langu,"
"usijali nita fiikiria"
"hope lita kua jibu zuri"?
"tuombe Mungu"

FRank alitoa gari nje na Witness kufunga geti na kutembea mpaka ndani haraka haraka, nia ya Witnes kumuweka karibu FRank ili kua si kingine bali ni kuujua mji huo wa Dar es salaam vizuri kabisa sababu alikua mgeni, ivyo alikubali hata watoke wote usiku ili aweze kujua vizuri mji huo na wala si vinginevyo, ivyo ndivyo ilivyokua.

bado aliendelea kuangalia habari ile ya chama kilicho kua madarakani ambacho kwa upande wa pili kili husika katika namna moja au nyingine kuwauwa wazazi wake huku akishuhuhudia, kili zidi kusisitiza kuwa baadhi ya wawkilishi serikalini wata enda Arusha kwenye ziara na kukaa huko kwa kipindi cha mwezi mmoja,

*******

tayari ili timu saa 05:30 usiku Witness akiwa ndani ya gari la FRank usiku wa siku hiyo ili kua furaha sana kwa FRank ambae muda wote uso wake ulikua una furaha hasa kitendo cha Witness kumkubalia watoke wote na binti mrembo kama huyo.

"kwani tuna enda wapi FRank"?
"tunaenda club"
"aaah mimi club sija wahi kuingia jamani, nitaanzia wapi"?
"basi leo ndo utaingia namimi FRank ,ndo maana nika kuletea izo nguo uvae, na umependeza kweli Rachel"
"asante sana"

kila kitu kwa Wity FRank alikiona kizuri na kuzidi kumsifia kila saa, kweli gari liliegeshwa nje ya club iliyoandikwa CLUB BILL CANAZ , ambapo nje hapo kulikua kuna foleni ya watu waki kata tiketi ya kuingia ndani ya club iyo iliyo kua maeneo ya posta,
"hii ndo club bill canaz"?
alihoji Wity huku akimtazama FRank aliye kua pembeni na kuonekana akiwa ana juana na watu wengi sana maeneo hayo
"yaah ndo hii, hakuna club inayo bamba kama hiii, sema kuna club nyingine nita kupeleka ina itwa DAR LIVE iyo ndo sasa nayo nahisi ita kuja kufunika hii hapa"
"kipindi nilikua nasoma nilikua nikiisikia, alafu iyo DAR LIVE sindo ya yule mwandishi ERIC SHIGONGO""?
"Ndi huyo huyo, twende tukakate tiketi"

baada ya kukata tiketi waliingia ndani na kusikia kelele nyingi za mziki ambpo ukiwa nje usingeweza kusikia chochote kutokana na club iyo kufungwa mtambo maalumu wa 'sound proof' walifika counter ya vinywaji na Wiitnes kuagiza wyn pia na FRank vile vile aliagiza na kuendelea kutikisa vichwa vyao kutokana na mziki ulio kua ukitumbuizwa ndani ya club iyo, na kila mtu kuonekana kucheza kati kati ya uwanja maalumu kwa ajili ya kucheza.

nyimbo ilio kuwa ikipigwa na dj Nicholus na kufanya wazidi kufurahi na kufanya kila saa arushe jina lake hewani.
"dj Nicholus, dj Nicholus napenda kumkaribisha msanii wa kizazi kipya mta muona"

watu walizidi kupiga yowe sana hasa walipomuona msaani BARNABA akipanda jukwaani, na kumfanya hata Frank nayeye ashangilie na kwenda kati kati huku akimuacha Witness counter ya vinywaji,

ila Witness kati ya watu wengi alio waona macho yake yana ganda juu ya uso wa mtu aliye mfananisha alimuangalia kwa kitambo sana . huku akizidi kuta fakari alimuona wapi mtu huyo, alizidi kuvuta kumbukumbuku kwa muda.
"shirima fanya haraka zamu yangu"

kauli hiyo haukuwahi kumtoka kichwani kamwe, ni sauti ya mwanaume mmoja akimwambia shirima kipindi walikua wana mbaka Mama yake mzazi tena kwa kupokezana,

kumbu kumbu mbaya sana iliyo fanya moyo kumuuma sana baada ya kumuona shirima mbele yake,
uchungu ulimbana sana na kumfanya aheme kwa kasi.

picha mbaya tena inaanza kujijenga kichwani kama mkanda ambayo alimuona mama yake akibakwa tena kwa zamu na kuzirai, ana jikuta anabanwa na hasira na kumfanya atetemeke sana.

pale pale aliweka glass ya wyn chini na kumfuata Shirima ambae aliye kua akicheza kwa nia moja tu kumuua pale pale bila kujali jopo la watu, ila kabla haja mfikia ana shikwa mkono na FRank.
"unakwenda wapi Rachel?"
"niachie FRank, naomba uniachie usije nawewe ukapata matatizo na sitaki hilo jambo litokee"

Witnes aliongea akipaza sauti kutokana na mziki ulio kua uki pigwa ndani ya club iyo uli fanya asisikike vizuri.
aliongea kwa hasira huku akimsukumiza FRank, ila kwa upande wa FRank haku taka kumwachia mkono.
"matatizo gani hayo Rachel, twende nje"

Frank alimvuta Witness mpaka nje na kukaa nae kitako, pale pale hasira za Witness zilianza kupungua na kujua kwamba jambo alolitaka kulifanya muda mfupi ulio pita halikua zuri,
"naomba nirudishe nyumbani"
"sasa hivi?"
"ndio sasa hivi"
"bado lakini muda"
"kama huwezi kuni rudisha nita rudi mwenyewe"

Frank hakua na la kufanya zaidi ya kumrudisha Witnes kwake japo hakutaka kumuuliza kwa nini alifanya vile club hakutaka kumkasirisha Witnes,
baada ya kumfikisha alimuaga na Frank kuondoka zake,
"lazima nilipe kisasi"

aliongea Witness huku akiji tupa kitandani,

*******

kitendo cha asubuhi kuamka alienda moja kwa moja katika show room ambapo yalipaki magar mengi yalikua yanauzwa, alienda kwa muuzaji wa magari na kutaka gari aina ya REXUS,
"hilo anti ni shilingi milioni mia hamsini"
"sawa hakuna tabu nita kupa sasa hivi ngoja niende bank, anza kuli sajili, na kama ikiwezekana kaniwekee full tank"

Witness alitoka pale mbio mbio na kuelekea bank ambapo aliienda kwa keshia na kutoa kiasi cha shillingi miilion mia mbili,

baada ya kila kitu kuka milika,alirudi na kumpa muuza magari yule pesa zile na kuchukua gari ambalo lilikua tayarri lina mafuta ya kutosha,

siku hiyo hiyo alili fanyia usajili,
kwa nia moja tu kwenda nalo Arusha ili aanze na watu wa serikalini,

kweli alipania kuwa uwa mmoja baada ya mwingine, ili pofika mchana saa saba alipakiza mabegi yake ndani ya REXUS na kulitia funguo.

na kushusha pumzi ndefu, na kuanza safari ya kuelekea Arusha akiwa mwenyewe juu ya usukani.

alizidi kutimua mbio za ajabu, kutokana na siku iyo ili kua ni juma pili hakukuwa na vizuizi bara barani hususani askari wa usalama bara barani,

alisimama KOROGWE na kula, baada ya hapo aliwasha gari na kutimua mbio akiwa makini sana huku akiya pita magari mengine ndani ya masaa matano alikua tayari yupo njia panda na kuiacha bara bara ya kwenda kilimanjaro nayeye kukunja kushoto,

ambapo baada ya Masaa matatu aliingia Arusha na kuta futa hotel, kweli alipata Hotel hakutaka kupoteza muda wa aina yoyote ile.

chini ali fanya uta fiti na kujua kikao icho kita kapo fanyika,

siku inayo fuata ali tafuta suti na kuvaa begi lake huku shingoni akiwa amevaa kamera na kuji fanya ni mpiga picha, alingia ndani ya hotel hiiyo uliokua una fanyika mkutano huo na kuona jopo la watu nayeye pia kuji changanya na wapiga picha huku akiwa soma wote waliokua mbele yake huku akijiandaa kumuua mmoja baada ya mwingine.


 "youth brave democratic party, kilianzishwa mwaka 1872, mpaka leo kipo madarakani, sisi tuna weza sana, nime furahishwa sana na utendaji kazi wa serikali hii, ni jambo zuri sana kwa kweli, baada ya muda mfupi ata kuja hapa waziri wa mambo ya nishati na madini na kuongea nanyi kama mgeni rasmi,"

ili kua ni sauti ya Proffesa Mwaipungu mwenyekiti mstaafu wa chama cha YBDP(youth brave democratic party) akiwa juu ya jukwaa. mvi na kitambi cha mzee huyo alionekana dhahiri amekula chumvi kiasi chake,

picha za mnato zili zidi kupigwa tena bila kikomo miongoni mwa wapiga picha hao alikua ni Witness kafifi, akiwa mwenye hasira sana ila hakutaka kuonesha hasira zake, vigele gele na makofi vili zidi kuongezeka viki fuatiwa na yowe za wabunge na viongozi mbali mbali wa nchi hiyo ya Tanzania wakionekana na kufurahishwa sana na hotuba fupi,

baadae kidogo ana panda jukwaani waziri wa nishati na madini mh.Robert Baseka na kushangiliwa na watu wengi sana, huku wengine wakipiga makofi na kusimama kwa furaha.
'leo ndo mwisho wenu sitowaachia hata iweje'

aliwaza Witness huku akiendelea na zoezi lile na kupiga picha feki pale ukumbini, ambapo watu wengi walizidi kurindima na kufanya hata watu wengine wakose siti za kukaa.

Licha ya kukosa siti za kuketi walisimama ili mradi wasikilize hotuba iyo fupi ya mh,Robert Baseka,

baada ya kumaliza hotuba iyo alitoka nje huku akisindikizwa na picha za mnato akizidi kusumbuliwa na waandishi ila wana toka patupu baada ya walinzi kuwa zuia kusogelea,

Witness nayeye hakutaka kucheza mbali alitia gari funguo na kuwa fuatilia nyuma pasipo wao kujua lolote lile, LANDCRUISER v8 alilopanda profesa Mwaipungu .

lilipaki nje ya hotel ya kifahari ya nyota tano, na kuonekana kushuka,Witness alivyo hakikisha ndo ile hotel anayo lala, nayeye aliweka gari pembeni kidogo ili lisiweze kuonekana na kushuka akitumia miguu ambapo alivaa kofia na miwani kubwa na yeye kuingia ndani ya hotel hiyo akimfuata mh, Mwaipung nyuma nyuma akiji fanya nayeye mwenyeji ndani ya hotel hiyo.
"dada samahani"

aliita muhudunu wa mapokezi na kumfanya Witness asimame.
"unaenda wapi?"
"kuna mtu kanipigia simu yupo ndani ya hotel hii"
"yupo chumba namba ngapi"?
"mmh chumba namba mmh chumba nambaa"
Witness alionekana kufikiria huku akijipiga piga kichwani kana kwamba anavuta kumbu kumbu,
"ngoja kidogo basi nimuulize chumba namba ngapi"

Witness alizuga na kuji fanya ana toa simu yake mfukoni na kutoka nje maana alijua ange kaa sana angeweza kugundulika.
"shit"

alijisemea mwenyewe na kulifuata gari lake na kuondoka akielekea hoteli aliyo panga ambapo alipanga kivyovyote vile lazima usiku ange mfuata na kumaliza kazi yake iliyo mleta,

alizunguka madukani baadae na kutafuta GLOVES za mikononi na kununua kisu kikubwa sana na kukinoa na kusababisha makali san, ambapo tena alinunua ushungi na kila kitu alichoona kina mfaa usiku wa siku hiyo, baada ya kuridhika alingia ndani ya gari lake na kurudi tena hotelini.

aliagiza chakula na kula huku akisubiri usiku sana uweze kuingia na kumaliza kazi, kweli katika akili yake alijua kuwa ana fanya kazi ya hatari sana ila hakua na jinsi nyingine ya kulipiza kisasi,

katika maisha yake tangu akiwa utotoni hakuwahi kuwaza kama angekuja kuwa muuwaji, alitamani siku moja aje kuwa mwanasheria na kuwatetea wanyonge ila ndoto yake yote ili yayuka na kumfanya awe gaidi kuliko binadamu yoyote yule, swala la kuuwa kwake aliliona la kawaida sana.

wakati huo, kutoa maisha ya mtu aliona kama kunywa chai ya maziwa, aliona ni kitu cha kawaida sana kutokana na wazazi wake kuuwawa kinyama sana, ivyo hakuwa na huruma hata chembe na kuwa chukia sana baadhi ya binadamu.

hakutaka kuwa na huruma hata kidogo,usiku uliiingia na alivyoangalia saa yake ya mkononi ili kua imejiri saa 05;45 za usiku,

alisimama na kuvaa nguo zake vizuri na kuchukua kisu kile chenye ncha kali na kukiweka ndani ya mkoba wake na safari moja tu kuanza kuelekea kwenye hotel aliyo muacha Proffesa mwaipungu..

baada ya kuingia ndani ya gari alianza kubadili nguo na kuvaa baibui ile ambayo ili mfanya aonekane macho peke yake, baada ya kuridhika aliwasha gari na kuanza safari,

"lazima niwa malize wote"
aliwaza Witness huku akizidi kuongeza mafuta akitimua mbio za ajabu sana, baadae ana egesha gari mbali na hotel hiyo na kushusha pumzi,

ana fungua mlango wa gari na kushuka akiwa na mkoba wake mkononi,

alitembea mwendo wa dakika kumi na kuingia ndani ya hotel hiyo na kumkuta muhudumu yule mapokezi, ambaye alimzuuia kama alivyo mzuia asubuhi kuingia,
"anti embu sogea huku kidogo"

Witness alimuita dada yule wa mapokezi hii ni kutokana na kuona Camera pembeni juu ya muhudumu yule, ivyo alimtoa eeneo lile ili camera ile isi weze kumuona kwa kitendo ambacho amekipanga kukifanya,
"kuna nini"?
"kuna hii picha hapa nataka uni saidie kuniambia kama huyu mtu yupo hapa"?
"hapana siwezi wewe njoo hapa"
"hivi una nijua mimi ni nani, ngoja nimpigie meneja wako simu nimwa mbie unavyo jibu wateja wake"
"dada lak.."
"hakuna cha lakini we subiri uone. tatizo mna kua viburi sana"

Witness alipiga mkwara ule huku akitoa simu yake na kuji fanya akita futa namba za simu na kuzuga.

haraka haraka dada yule wa mapokezi akihofia kibarua chake kisi ote nyasi aliji kuta ana fanya kosa na kutoka pale alipo akimuendea Witness,
"tulia ivyo ivyo, uki piga kelele nakuchinja"

Aliongea Witnes baada ya kumvuta dada yule na kumuwekea kisu shingoni, dada yule aliingiwa na hofu sana kuliko maelezo.
"muheshiwa yupo wapi"?
"yu yu yu yupi"?
"usinipotezee muda, twende nipeleke chumba alicho Mwaipungu"
"sa sa sawa usiue"

Witness aliiingia ndani ya lifti na dada yule kubonyeza namba za floo fulani na lifti hiyo kuanza kupanda juu taratibu. baada ya kufika sehemu husika lifti ili jifungua huku kisu kikiwa juu ya shingo ya Dada yule tena juu ya koromeo na kumfanya aongoze taratibu mbele.
"kwani anti, wewe ni nani?"
"kaa kimnya"

Witnes alizidi kusonga mbele na dada yule ambapo mbele yake kuli kua kuna kona na kusikia parakacha za watu zina kuja na Witnes kukitoa kisu kile shingoni kwa dada yule. na kumuwekea nyuma ya mgongo ili kufanya mtu yoyote asiweze kuhisi chochote wala kuona kisu kile,

"uki fanya upumbavu wowote ule, nita kuua, ume nisikia?"
"ndio"
"aya twende, tembea taratibu"

Walikata kona hiyo na kuwaona askari watatu wakiwa wana kuja, ambao walionekana ndiyo walikua walinzi wa professa Mwaipungu,

Witnes aliwa kazia macho walinzi hao ambao walizidi kuwa karibia walipo, wakiwa wana tokea upande wa mbele yao
"afande,! afande!"
aliita dada yule wa mapokezi na kumfanya Witness aanze kujiandaa na lolote litakalo tokea sababu alijua dada yule ana enda kusema kila kitu,
"sema kuna tatizo?"

dada yule alimgeukia Witness na kumwangalia kwa sekunde kadhaa bila kusema kitu,
"hakuna tatizo, nili kua nawaambia kama kuna shida yoyote msisite kuniambia"
"sawa hakuna shida"

walinzi wale walipita na kumfanya Witnes ashushe pumzi kidogo, na kumuamuru dada yule azid kusonga mbele.
"ndo humu"

dada yule aliongea huku akiwa amesimama nje ya mlango kuashiria kuwa Professa Mwaipungu alikua ndani ya chumba kile,
"gonga mlango"

dada yule kuhofia maisha yake alianza kugonga mlango ule na kuzuga kua kuna mataulo angetaka kuwapa, kweli baadae mlango una funguliwa na Mke wa Profesa mwaipungu ambapo bila kusema chochote alikabwa koo na kuingia nae ndani na muuhumu yule wa mapokezi kuingizwa ndani,

Professa Mwaipungu kuona hali ile alivuta droo yake na kutoa bastola ila kabla kufanya chochote Witness ana upiga teke mkono uliioshika Bastola ile na bastola ile kudondoka pembeni,

mke wake nayeye alivyo jaribu kutaka kupiga kelele alitulizwa na kofi zito lili lomfanya adondoke kitandani na kutulia, hakutaka kupoteza muda hata kidogo aliiwahi bastola ile iliyo kuwa chini na kuwa weka wote chini ya ulinzi,

alimuendea dada yule wa mapokezi na kumpiga kitako cha kichwa cha bunduki na kumfanya dada yule azirai pale pale.

"wewe ni nani?"
alihoji profesa Mwaipungu
"utanijua tu"

Hakutaka kufanya makosa hata kidogo alitoa kisu chake ndani ya mkoba na kuvaa GLOVES alimuendea Mwaipungu amabe alionekana kuwa na wasi wasi mwingi sana, bila huruma alimziba mdomo na kukitumbukiza kisu kile tumboni mwa Mwaipungu na kuki fanya kama ana kizungusha, damu nyingi sana zili tapaaka chini,

ivyo iyo alimfuata mke wake na kumchoma kisu tena shingoni, baada ya mauaji yale kutimia alichukua glass ya pombe na kuiweka sumu ndani yake, alimuangalia dada yule wa mapokezi ambae alikua amezirai haku tgaka kumuacha sababu alijua baadae ange mletea matatizo, ivyo ana mchoma kisu tumboni, na baaadae kumuwekea kisu kile mkononi mwake huku akiiacha Glass ile yenye sumu mezani akiwa na mahesabu yake kichwani.

alivyo hakikisha kila kitu kimeenda sawa alijiaanda kunza kutoka, kabla ya kutoka ana hisi mlango wa chumba hiko una gongwa na kutulia kidogo akionedakana aki tafakari aufungue au afanye nini.....


 Alitoa kisu chake taratibu ndani ya mkoba wake na kukishika vizuri kwa kujiandaa kwa lolote litakalo tokea mbeleni, kweli alidhamiria kuua.

na yoyote atakae muingilia alipanga kumuaa papo hapo,
aliweka kisu vizuri na kuuwendea mlango na kuweka sikio lake mlangoni ili asikilize vizuri.

alitulia kama dakika moja nzima bila kuhisi tena mlango ukigongwa, taratibu ana ufungua kwa tahadhari na kutoa kichwa nje na kumuona mtu ana potelea kwenye moja ya kona ndani ya hotel hiyo.

alirudi ndani haraka haraka na kunawa mikono yake vizuri na kuji futa vizuri, huku akiweka bai bui ile sawa sawa, alivyo hakikisha kila kitu kimeenda sawa, alitoka nje taratibu na kuingia ndani ya lifti ambapo ana bonyeza na lifti kumshusha chini,

baada ya kufunguka ana toka nje na kuelekea bafuni na kutoa baibui ile na kuvaa nguo zake za kawaida ambapo baada ya hapo, alianza kutembea akili fuata gari lake alipo liacha,

********

jeshi la polisi tayari lili kua lime fika ndani ya chumba hiko ambacho kili fanywa mauaji usiku wa jana, tayari walikua wamechelewa maana Proffesa Mwaipungu na mke wake pamoja na mwanamke yule wa mapokezi walikua wame uwawa kinyama ndani ya hoteli ile,
"sasa mnalinda nini hapa?, nani yupo incharge"?

aliuliza mmoja wa mapolisi kati ya wengine nane baada ya kuangalia tukio lile la kinyama sana,
"mimi hapa"
"jana nani alikua zamu"?
"Raphael na Gingi"
"waite mara moja"

Picha za mnato zili endelea kupigwa na jeshi la polisi huku wakizidi kufanya uchunguzi wa kina waki waita baadhi ya watu kutoka ndani ya hotel hiyo na kuwahoji ila walitoka patupu,
"mimi ndo nili kua zamu jana"
"huyu dada una mfahamu"?
"ndio ni mfanyakazi wa hapa mapokezi"
"mara ya mwisho alikua na nani"?
"mmh mara ya mwisho nili muona na mwanamke fulani hivi alikua nae, amevaa baibui, "
"ulimuona sura yake"?
"hapana baibui ile ili mfunika uso mzima sikuweza kumuona sura yake"
"nipeleke chumba cha kamera"

kweli waliongozana mpaka ndani ya chumba cha kamera na kumkuta askari mwingine akiwa ata zama kamera zile na maaskari wale kuji tambulisha, ambapo waliomba wapewe recoding ya tukio la jana kuanzia usiku wa saa moja.

kweli askari yule alianza kubonyeza bonyeza komputa ile na hatimae kupata recoding vizuri ila hawa kuweza kumuona mwana mke yule.
" ina elekea huyu muuwaji aliji panga, ana jua kamera zote zilipo, hapa una ona huyu dada alitoka hili eneo kabisa, na sio kawa ida yake kabisa"
"hakuna camera nyingine"
"zipo"
"fanya uangalie"

ASkari yule aliangalia tena ila aliambulia patupu baada ya kutoona sura yoyote ile, Kweli ili kua ni kazi ngumu sana kumpata Muuaji ambae alikua ni Witness.
"tuta mpata tu, "
aliongea polisi huyo na kutoka ndani ya chumba kile ambapo mlangoni alikuta waandishi wengi sana wa habari, wakiwa wana piga piga picha za mnato.

uchunguzi wa kina unazua utata sana ndani ya chumba kile ambapo daktari aliye kuja kudhibitisha alikuta glass yenye kinywaji chenye sumu kali sana, na kushindwa kuelewa kifo hiko kili sababishwa na nini, ila chini kwa chini walitoka na jibu moja tu, kifo hiko kili sababishwa na mapenzi, mauaji hayo yalisababishwa na mapenzi na si vinginevyo.

habari za kifo cha Proffesa mwaipungu zina washtua watanzia wengi sana kupita maelezo, ivyo viongozi wengi wana ghairi ziara iyo na kurudi mkoani Dar es salaam kwa ajili ya mazishi ya kiongozi mwenzao ambae alikufa katika kifo cha kinyama.

Magari mengi ya serikalini yakiongozwa na msafara huo mrefu ulizidi kuchanja mbunga huku maiti ya Profesa Mwaipungu ikiwa tayari ime wasiri Dar es salaam kupitia usafiri wa anga,

********

Witnees akiwa bado yupo Arusha ndani ya hotel aliyo panga habari zile ana zisikia na kujipongeza kwa kazi nzuri aliyo fanya, alitoa chupa ya wyn na kuimimina ndani glass na kuipiga fundo refu na kuiweka juu ya meza ya kioo na kumimina tena wyn ile ndani ya glass.
"nime fanya kazi nzuri"

aliongea Witness na kupiga tena fundo la wyn huku akitingisha kichwa chake, baada ya hapo aliingia bafuni na kufungua bomba la mvua, ambapo mbele yake kulikua na kioo cha kuji tazama, kumbu kumbu mbali mbali akiwa jeshini kutokana na makovu aliyo yaona zinamjia,

kumbu kumbu za Stuwart zina mrudia na kuanza kumuwaza tena, ambae anajua kivyovyote vile alidhani amekufa,

baada ya kuoga vizuri alitoka na kuvaa vizuri huku akizibana nywele zake kwa nyuma, alitoka nje na kutafuta moja ya sehemu nzuri na kukaa na kuagiza chakula cha mchana,
baada ya chakula kile kuja alinza kula taratibu huku akiutazama mji huo wa Arusha ulio kua mzuri sana na wenye hali nzuri sana ya hewa,

"ndo ivyo sasa mimi ndo nauza ule mgodi arifu"
"sasa mimi sina pesa. sasa ita kuaje"?
"nita futie mteja, mi nataka niende Marekani, ule mgodi nauza"

maongezi hayo yali mfikia Witness moja kwa moja ambae alikua pembeni ya watu hao wawili, na kuwa sogelea.
"samahani kwa kuwa ingilia maongezi yenu,"
"bila samahani tuku saidie nini"?
"nina shida na huo mgodi, nataka kununua kama ikiwezekana"
Watu wale walimshangaa Witness kwa kitambo na kumuomba akae pembeni yao.

kweli walipatana bei na Moja kwa moja kupelekwa Mererani katika mgodi huo ulio kua mkubwa kiasi chake,

alizungushwa kila sehemu na kuanza kupatana bei, baada ya hapo waliandikishana kwa njia ya maandishi na mashaidi kuitwa akiwemo meya wa eneo hilo,

baadae ana mchukua na kwenda nae bank ambapo ana kabadhiwa pesa zake na safari hii Witness ana kua mmiliki mkubwa wa mgodi huo hapo mererani,

alifanya ivyo kutokana na wenda baadae serikali ingeweza kumuhoji na kumuuliza maswali mengi juu ya pesa zake alipo zitoa,

alifanya ivyo ili kuepusha maswali kutoka serikalini akitumia mgodi huo kama mwavuli, kila kitu alifanya kwa mahesabu na mipango, ivyo ndivyo ili vyo kua,

**********

Leo hii Witness alikua njiani akielekea jijini Dar es salaam ndani ya gari aina ya Rexus, kutokana na uwezo mkubwa wa gari hilo kukimbia alitumia takribani masaa matatu kufika maeneo ya same, pia mwendo kasi wake ulichangia. kuendesha gari hilo kwa mwendo kasi usiku huo ambapo kuli kua hakuna hata magari magari njiani, akiwa peke yake

ndani ya gari huku pembeni ya gia kukiwa na bastola ndogo aliyo ichukua kutoka kwa Proffesa Mwaipungu ili mfanya ajiamini na lolote baya litakalo mkuta mbeleni,

baada ya masaa saba tena bila kusimama alikua tayari yupo Mlandizi huku kukiwa kume kucha na mwanga wa asubuhi kwa mbali, ulikua umeanza kuji tokeza taratibu alivyoangalia saa yake ya mkononi alikuta ni saa 12;30 ASUBUHI,

ki ukweli hakula chakula chochote usiku kucha. kweli kama alivyo panga baada ya lisa lomoja alikua nje ya geti lake msasani akili fungua na kuingiza gari ndani, hapo ndipo aliamini ame fika jijni Dar es saalam.

******

Siku hiyo hiyo hakutaka kulaza damu hata kidogo hii ni baada ya kukumbuka kuwa alimuona Shirima ndani ya club bill canaz, alikunja mdomo kwa hasira na kuchukua kisu kidogo sana na kukichomeka ndani ya travota huku akiichomekea suruali yake vizuri,

aliwasha gari yake usiku huo na safari ya kuelekea bill canaz kuanza , japo kua hakua na uhakika kama ange mpata mba-ya wake huyo,ila alijipa moyo na kusonga mbele,

baada ya kufika aliegesha gari yake ng'ambo ya bara bara na kushuka, ambapo alivuka bara bara na kuufiikia mlango wa club hiyo na kukata tiketi,

baada ya kuingia alikaa kaunta huku akiagiza kinywaji na kuanza kunywa,

kweli alianza kusu mbuliwa na kero nyingi kutoka kwa wana ume wakimuomba wakacheze nae ila hakua tayari sababu kilicho mpeleka pale haki kua kucheza bali ni kitu kimoja tu kuuwa na si vinginevyo.

"sorry siwezi kucheza nielewe jamani"

alijibu Witness baada ya kukeerwa na mmoja wa Wanaume wa ndani ya club iyo,

alichukua glass yake na kutoka pembeni na kuingia katikati na kumtafuta Shirima,

takribani masaa mawili yalipita bila kumuona mbaya wake huyo, na kuanza kukata tamaa wenda hawezi kuja leo,
ila baadae ana muona Shirima ana ingia akiwa na wenzake wanne hao wote aliweza kuwa tambua vizuri sababu ndio walio fanya tukio la Kuwa uwa wazazi wake,

jambo hilo lina mfurahisha sana baada ya kuwaona wakiwa pamoja,

alishika glass yake vizuri na kuwaendea ambapo makusukudi ana mwagia wyn Shirima juu ya shati lake huku akizuga kama ame jikwaa,

"we dada vipi"?
"samahani anco, bahati mbaya"
"bahati mbaya nini sasa, wakati ume nichafua tayari"?
"samahani"

"mwache mrembo Shirima, anti achana nae una itwa nani"?
alidakia mwenzake
"naitwa Queen"
" una jina zuri naomba kampani yako"?
"hakuna shida. ata ivyo nime kuja mwenyewe:"


0 comments:

Post a Comment

BLOG