Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 8/10


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 8 KATI YA 10
*******
 *******

Vincent Towo alisimama akiwa na maumivu makali sana alishika mdomo wake ambao ulikua ukivuja
damu nyingi sana, aliiinuka na kushika bastola yake na kutoka nje kwa hasira kali akimtafuta mwanamke huyo akiamini kuwa ni gaidi sana na wala sio kama alivyo dhani, kupigwa na mwana mke Yule kiasi kile kuli mfanya apate hasira za kumtafuta.
“mta futeni humu ndani”
“lakini, una ona kule geti lime funguliwa, hayupo humu ndani”

Baada ya kugeuka waliona kweli geti kubwa likiwa wazi, na wote kuliendea bila kujua ile ilikua zuga Witness kweli alifungua lile ili wajue alitoka nje, ki ukweli hakua nje, alikua amejificha nyuma ya ua kubwa akiwaona kila hatua wanayo piga. Baada ya kuwaona wame toka alinyata taratibu na kuchunguila dirishani, alimuona IGP Ibengwe akiwa amezungukwa na askari watatu wakiwa na mitutu wakimlinda,
wakiangalia huku na kule, alicho fanya alichukua jiwe kubwa na kuli tupa pembeni yake, baada ya askari Yule kusikia kishindo kile cha jiwe, alianza kuliendea dirisha , na hayo ndiyo yalikua mahesabu ya Witness, kitendo cha askari Yule kutoa kichwa chake nje alivutwa mzima mzima na kutulia juu ya kifuti cha Witnes, alichukua mtutu wake na kutoka maeneo ya dirishani, alimuona askari mmoja akiwa mwenye mashaka sana, ali mfuata na kumtwanga mtutu wa kichwa,na kumfanya adondoke chini, nia yake ilikua moja tu, kutotaka kumuacha IGP Ibengwe alitaka kujua ukweli wa mambo,
ivyo alitaka kufanya juu chini aweze kuondoka nae, aliamini sana kuwa jambo lile lina wezekana, alimuendea askari mwingine na kumpiga kichwa cha pua na mtutu wa bunduki kichwani na kudondoka chini,
“ulidhani nita kuacha, mikono juu ongoza mbele”
Aliamuru Witness huku akiwa na mtutu mkononi mwake, alivyo geuka pembeni chini ya meza alimuona mke wa IGP akiwa ame jificha huku akiwa tayari kamwaga haja ndogo ndani ya sketi yake na kufanya michirizi kutokana na uwoga,
“njoo huku, fanya upesi”
Mke wa IGP alitoka chini ya meza na kusimama huku akiweka mikono yake juu. Hakika hawa kutaka kufanya ubishi wowote na kujua mwanamke aliye kua mbele yao alikua gaidi sana. Waliongoza mbele huku Witnes akiwa nyuma yao.
Ila alihisi kitu kama kichuma kime mgusa nyuma ya utosi wake, hakua na haja ya kuuliza sababu moja kwa moja alijua chuma kile ni bastola.
“binti weka silaha chini usalimu amri kabla sija weka ubongo wako pembeni”
Ili kua ni sauti ya Vincent Towo akiwa ameishika bastola yake kwa mikono miwili na umakini wa hali ya juu sana.

 Hakua na ujanja wowote ule ki ukweli sababu ya bastola hiyo iliyokua nyuma ya kisogo chake ilikua tayari ime kokiwa na risasi kuingia ndani ya chemba tayari kwa kufyatuliwa na kumfikia mlengwa ambae alikua ni Witness, mbele ya Witness kulikua kuna mlango mkubwa mweusi wa kioo ivyo alivyokiangalia kioo kile kilich kua mbele yake aliweza kumuona vizuri mpepelezi Yule Vincent Towo akiwa nyuma yake, ila hakua na la kufanya.
“sogea ukutani”
Alisema Vincent na witness alitiaa a,ri hiyo
Alitii amri hiyo. Na kuufikia ukuta ule na kuushika mikono miwili, Vincent Towo alimsogelea na kuanza kumkagua mifukoni huku akimpapasa papasa, kama alikua na kifaa chochote, alimkuta na kisu kidogo kiunoni na kukitoa
“muheshimiwa kaa hapo juu ya kiti”
Bado alikua makini na bastola yake akiamini kuwa akifanya makosa kidogo tu, ange pigwa mara moja alielewa vizuri mbele yake hakua mtu wa mchezo.alielewa mwanamke huyo ni zaidi ya MAFIA. Kutokana na kuchezea kipigo kikali mda mchache uli opita ,
“stesheni namba tatu, una nipata Towo, kishhhhh Stesheni namba tatu ova, unanipata Towo kishhhh”
Ili kua ni sauti iki tokea kwenye rediio upepo ambayo ilikua kiunoni mwa mpelezi huyo, bado ilikua ikipiga kelele , kuashiria kwamba ange takiwa kujibu, kwa hali ya umakini sana, aliitoa ile Redio upepo kiuoni huku mkono mmoja ukiwa na bastola,
“naku……”
Kabla ya kumalizia kuongea alipokea kiwiko kilicho tua puani kutoka kwa Witness, hakupata nafasi yoyote ile alipigwa teke kwenye mkono wake wenye bastola na bastola aliyokua ameishika kudondoka pembeni,
pale pale alifuatwa na kupigwa teke liillo tua tumboni na kudondoka chini mzima mzima, kweli alitambua kosa la kuijibu rediio hiyo ili mpelekea kumpa adui yake nafasi, alinyanyuliwa akiwa ameshikwa shati na kuwekwa ukutani na Witness, pale pale alipokea kichwa kingine puani,

Akiwa amewekewa bastola usawa wa kichwa aliamriwa amfunge pingu IGP ibengwe na mke wake mara moja. Kweli alitii nay eye kuambiwa aongoze mbele, IGP ibengwe hakua na matumaini tena ya kuokolewa,
“nisikilize kwa makini sana”
“naam”
“chukua hii redio waaambie wenzako, kuwa ume niona geti la uwani, natoka”
“sawa sawa”
Witness aliongea maneno yale na kumkandamiza ukutani na kumuwekea bastola ile kichwani,
“niangalie machoni, nita kuua endapo utaenda kinyume. Aya upesi”
“sa sa sa sawa”
Alibabaika Vincent Towo huku mdomo wa bastola ile ukiwa juu ya kichwa chake, hakua na sababu ya kuongea uwongo wala kudanganya sababu alijua maisha yake yapo mikononi mwake, endapo akienda kinyume na ndipo hapo uta kua mwisho wa maisha yake, kweli aliongea na kuwavuta maaskari wote upande wa pili , uwani baada ya kupokea maagizo ya uwongo, bila kujua mwenzao aliwekwa chini ya ulinzi mkali.!
Alivyo hakikisha zoezi hilo limeenda sawa Witnes alitoka nae nje,
“gari yako iko wapi”?
“ile ile pale ya silver”
“ongoza”
“wewe ibengwe na mkeo mtakaa ndani ya buti”

Witness alimuamuru Vincent Towo akae mbele aendeshe gari huku yeye akiwa nyuma yake akiwa na bastola ile, aliwa amuru IGP ibengwe na mkewe waingie ndani ya boneti la nyuma, baada ya kuingizwa lina fungwa vizuri,

“tunaenda wapi”?
“endesha gari nita kwambia”
“tafadhali mke wangu ni mjamzito usiniue, mdogo wangu yupo maututi wanani tegemea kwetu”
“endesha gari, wewe si kidume”
Gari lili anza kuwashwa taratibu na kuanza safari ya kuondoka huku Vincent Towo akiwa ana tetemeka kupita kiasi, ila katika hali ya kushangaza ana ona magari ya mapolisi mengine yakija nyuma yake na mengine yaki tokea mbele yake,
yakipita mbele yao na kusimama na kuamuriwa waweze kusimamisha gari hilo,

Witness kuona vile alitoa magazine ya bastola na kukagua kama ina risasi, ila ana shangazwa sana baada kugundua kuwa magazine ina risasi nne peke yake, askari wale walizidi kulizunguka gari lile huku wengine wakitoka na mitutu aina ya SMG , Witness aliji vuta chini kidogo huku akimuwekea Vincet Towo bastola ile nyuma ya utosi wake , kutokana na gari hilo kuwa na tinted kali hakuna hata askari mmoja aliyeweza kujua kuwa ndani mule kuna mtu mwingine nyuma ambae walikua waki mtafuta,

kilicho mshtua zaidi alivyo sikia vishindo nyuma ya boneti alipo wa hifadhi IGP Ibengwe na mke wake, aliwa sikia wakipiga kelele za msaada, na kufanya sauti ile isikike

“mkuu upo salama,”?
Aliuliza mmoja wa maaskari huku kiioo cha gari hilo kiki shuka chini, kabla ya kujjibu alikaa kwa muda huku akishusha pumzi ndefu..

 HALI inazidi kuwa mbaya sana nchini Tanzania hasa mkoani Dar es salaam chama kili cho kua madarakani kilizidi kuwakandamiza maskini watu wenye kipato cha chini, wananchi walizidi kulalamika lakini serikali ya Tanzania iliweka masikio pamba sababu ndiyo waliokua wameshika mpini,
safari hii walikaa chini na kuanza kuwa fukuza wauza mitumba na biashara ndogo ndogo karikoo kwa sababu isiyo eleweka japo mara ya kwanza wafanya biashara hao walileta mgomo lakini baadae wana kubaliana na hali kutokana na vipigo vikali walivyokua wakipigwa na jeshi la polisi ambao walioonekana kutokua na huruma hata punje, ivyo ndivyo ilivyo kua,

Walianza kuandamana ila walishia kupigwa mabomu ya machozi na wengine kujeruhiwa na baadhi yao kuka matwa na polisi, kilicho wauma zaidi ni rafiki yao ambae alikua ni mfanya biashara kuuliwa kwa kupigwa risasi, wana kaa chini wakiteta na kuunda kikundi kidogo walichokiita WATOTO WA SIMBA ambacho kilikua na vijana wadogo takribani mia tatu waki tapakaa kila kona ya jiji na kufanya fujo huku wakipora mali nyingi madukani,kweli vijana hao walikua ni watu wa kuogopeka kilikua ni kikundi kilicho tishia sana Dar es salaam, kiliogopeka hata na mapolisi walifyata mikia, wali tapakaa maeneo ya sinza, mwenge, mabibo na tabata na kuanza kuchoma moto vibanda na kuvunja maduka,

Raisi wa jamhuri wa muungano ana ona hali ina zidi kua tete, hakuelewa nini afanye mauaji yana yotokea, silaha kuibiwa na watu kuvunjiwa maduka na kuibiwa malli vina zidi kumchanganya akili yake,
“hivi ina kuaje mnashindwa kudhibiti hawa watoto wanaojiita WATOTO WA SIMBA”?
“Mheshimiwa tuna jitahidi ila naona ndo wana zidi kuwa wengi sana”
“hamuwezi kazi, natumia jeshi sasa, nita futie Captain Mwanguku kwenye simu, mwambie nahitaji wana jeshi wa kutosha naona jeshi la polisi limeshindwa, usiniangalie ivyo , fanya haraka piga simu upesi”

Baada ya kuona mambo yanapoenda sipo aliamua kuwa shirikisha wanajeshi ili litulize gasia, kweli Raisi alionesha hali yakuchanganyikiwa sana……

*******

“mkuu mbona una onesha kama kuna tatizo alafu nasikia kuna kelele kwenye buti?”
Lili kua ni swali kutoka kwa mmoja wa maaskari akimuuliza Vincent Towo ambae wakati huo alikua kama mateka nyuma ya kisogo chake kulikua kuna bastola ambayo tayari ime kokiwa, aliangalia kioo cha kati na kumuona Witness ame weka kidole chake kwenye kitufe kina choitwa triga kumaanisha kuwa,, angesema jambo lolote lile kuhusiana na Witnes ubongo wake unge kuwa chini dakika hiyo hiyo, alihisi mdomo wake mzito sana, alitamani kuongea kitu lakini alijua ange poteza uhai wake dakika ,moja tu, alielewa vizuri sana swala hilo kuwa aliye shika bastola ile hakua na mzaha hata kidogo
“nipo Sawa Denoo,”
“na izo kelele”?
“mziki wa redio”
Vincent aliongeza sauti ya redio nakufanya ipige kelele na kuimeza sauti ya IGP Ibengwe iliyo kua ikipiga kelele nyuma ya buti
“naomba niende, tutaonana kesho, tumalize hii kazi Denoo, waambie vijana wazidi kupiga patroo”
“sawa mkuu”
Walitoa magari yao mbele na kumruhusu Vincent Mkuu wao apite bila kujua alikua katika matatizo makubwa sana na angehitaji msaada mkubwa pale alipo
Witness alivyona wame kata kona na kuwaacha maaskari wale aliinua shingo na kugeuka ambapo hakuona dalili yoyote ya kufuatwa na watu,
“umefanya vizuri sana”
“tunaenda wapi”?
“chanika”!
“chanika?, kufanya nini”!
“endesha gari”

Hakuwa na la kufanya zaidi ya kutii maagizo aliyo pewa na mwana mke aliye amini kua ni hatari sana, usiku huo aliendesha gari bila kujua mwisho wake kujua angeenda kuishia vipi ila aliamni kua kifo ndo kitu pekee kina cho fuata wala sio kitu kingine,
“kwanini una ua”?
“uliza serikali yako,”
“ naomba uni jibu”
“uta jua baadae, endesha gari,”
Gari lilizidi kuchanja mbuga na tayari walivuka kigamboni na kuingia kivukoni huko walizidi kusonga mbele, baada ya muda mfupi tayari walikua wakiiiacha gongo la mboto na kuzidi kwenda mbele, usiku ulikua ni mwingi sana, waliiacha bara bara ya kisarawe na kukunja kuelekea bara bara ya chanika, pembebi kulikua kuna misitu ya miti yenye giza totoro,

Alikunja kona ya kushoto na kuiacha bara bara ya Rami ambapo Witnes ndiye aliye kua akitoa maagizo , vicent alicho kiwaza ndani ya kichwa chake kili kua ni kifo, baadae alishushwa na IGP ibengwe kutolewa ndani ya boneti na kuanza kutembea kwa miguu ndani ya msitu huo uliokua ukitisha kutokana na miti mingi sana, walifika mbele kidogo nakuona nyumba iliyokua haija isha na kuamriwa waingie ndani, IGP iBENGWE na mke wake walifungwa kamba,
“wewe njoo nje”
“usiniue tafadhali”
“kacha kacha”
Witness alikoki bastola huku akimuamuru Vincent Towo apige magoti chini na kugeukia upande wa pili, alijua sana maana ya msemo huo, alijua hapo ange pigwa bastola ya kichwa na kuuliwa pale pale,
“geukia kule”
“hapana nataka uniue huku una niangalia usoni,”
“sawa piga magoti”
aliongeaWitness kwa hasira na kumuwekea Vincent Towo bastola ile kichwani kwa nia moja tu kufyatu a na kumuua


 HALI INAZIDI kua mbaya sana, tena safari hii ilizidi kutisha MNO! watanzania wana zidi kuingiwa na hofu huku Raisi akizidi kuchachawa na kuzidi kutandwa na hofu, licha ya kuweka ulinzi madhubuti kila pembe na kumwaga kikosi cha upelelezi haikufanya mauaji yatulie hata kidogo ilikua ndo kama kamkasirisha muuaji huyo ambaye bado hakujua ni kwanini ana ua kiasi hiko, habari mbaya zili mfikia kuwa maiti ya IGP IBENGWE na mke wake zilikutwa feli pembezoni mwa bahari ya hindi, wakiwa wame uwawa kinyama, matumbo yao yalikua yame fumuliwa na kutapakaa nje, macho yao yakiwa nje na kutobolewa vibaya, huku baadhi ya viungo vyao vikiwa vime tenganishwa, huo ulikua ni ujumbe tosha kwamba muuaji huyo ni hatari ivyo kuweka walinzi ilikua ni kazi bure kabisa!
Baada ya muda mchache anapokea taarifa kuwa mpelelezi aliye mtegemea katika kila jambo MR, VINCENT TOWO

haonekani ilidhihirisha tosha kuwa ata kua ameuwawa kama sio kutekwa nyara lakini hiyo haikumfanya azidi kuweka ulinzi wa kutosha , hakutaka kuonesha mapema kuwa kashindwa kumpata muuaji, iila ki ukweli ndani ya nafsi yake alitamani akimbie mbali sana pengine ahame hata nchi kabisa, mambo haya kwenda sawa katika upande wa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,
“muheshimiwa!, muheshimiwa Raisi, muheshiwa”
“nakusikiliza”
Alishtuka kutoka katika dimbwi la mawazo mengi akili yake ilikua tayari imechoka kufikiria
“muheshimiwa una onekana haupo sawa kabisa”
“we unadhani nita kuaje sawa, mauaji yanayo tokea una taka niwe nakenua meno, lazima niwe na mawazo, “
“lakini lazima tufanye jambo hapa”
“jambo gani?”
“bado tuna muda, tujaribu kushirikisha jeshi la nje ya nchi, huyu muuaji ina elekea ni MAFIA ni jasusi, ni professional killer, ana mbinu nyingi sana, tusijaribu kuli fumbia hili swala macho kabisa muheshimiwa Raisi, hizi ni aibu kwa nchi kubwa kama Tanzania tena ya amani, juzi nili ona habari ilirushwa CNN, kuusu mauaji ya mkuu wa mkoa , wawekezaji waanaanza kuwa na hofu wanaaanza kukimbia hii nchi, wana hofia, uchumi utayumba hapo baadae, nisikilize kwa umakini, niachie mimi hiyo kazi nitajua cha kufanya, tafadhali muheshiwa Raisi”
Wakiwa ndani ya ikulu ofisini mwa Raisi wakiwa katika moja ya mazungumzo , akili na fikra za muheshimiwa Raisi zilionekana zairi kuwa zime gota kabisa, mbele yake alikua ameketi mshauri wake Mr.Isaya Mbetto akiwa amevalia

suti yake, huyu ndiye aliye kua kama kwenye ubongo wa Raisi sababu yeye ndiye alikua akimshauri kila kitu kuhusiana na nchi yake, hakuweza kuweka sahihi yoyote pasipo kumshirikisha MR, Mbetto, licha ya mauaji ya kutisha kutokea bado Mbetto alikua na maana kubwa kwake tena safari hii alimuachia kila kitu mshauri wake jambo ambalo hakuwahi kulifikiria, hakua na jinsi zaidi kukiri kuwa akili yake amefikia kikomo. Bila kujua Mbetto anajiingiza katika jambo la hatari sana ,

********

“WEWE NANI”?
“UTANIJUA TU, nisikilize kwa umakini Mh. MASSATU! Chukua jeshi la polisi nenda bandari leo saa kumi jioni, kuna madawa ya kulevya yanaingia,”
“wewe nani na ume nijuaje”?
“fuata ninacho kuambia, leo saa kumi jioni, na kesho asubuhi kuna madawa ya kulevya yataingia , na huo mtandao ni mkubwa Raisi wako ndiye ana husika , kuwa makini”
“mimi siwezi kufanya jambo hilo bila kidhibiti”
“fanya niliyo kwambia, usipuuze!”
“kwani wewe ni nani”?
Yalikua ni mazungumzo kupitia simu kati ya Witnness Kafifi na waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa MASSATU ELIAS , baada ya IGP ibengwe kutaja kila kitu na kutaja mtandao mwingine wa madawa ya kulevya ambao ulikua ni mkubwa sana, ukihusisha baadhi ya mawaziri na hata pia rahisi, alitokea kumuamini sana Masatu WAZIRI wa uchukuzi, nia ya Witness ilikua ni kuchafua chama hiko ili baadae chama cha marehemu baba yake kiweze kuingia madarakani aliamini hilo lita fanyika bado alikua na kazi ya ziada sana, , alifanya kila kitu kwa utulivu na kwa hatua , haku taka kukubali kushindwa na kujiita yeye ni jeshi la mtu mmoja, na kuapa ata pambana mpaka atakapofikia mwisho,.

JASHO jembamba lilianza kumtoka MH, Massatu hakuelewa aanzie wapi, ki ukweli alihofia uhai wake alijua fika kuzungumza ukweli au kuweka siri za watu wa chama hiko kuwa baadhi yao walijiusisha na madawa ya kulevya kilimanisha kifo kwake, alishusha pumzi ndefu sana akiwa ofisini kwake, ameinamisha kichwa chini juu ya meza, ilibaki lisaa limoja tu kutimia saa kumi kamili,
“lolote na liwe, potelea mbali, nimekula kiapo cha hii nchi, nikifa poa lakini najua nili kua natetea ukweli”
Aliwaza Mh, MASATU na kuinua mkonga wa simu,
“halloo nahitaji Deffender tisa na askari wa kutosha, na mbwa wa kunusa madawa ya kulevya mara moja, niwa kute bandarini”
“sawa mheshimiwa mbwa wangapi?”
“mbwa wa kutosha “
Mh, Masatu alisimama haraka haraka na kumpigia simu dereva wake ili akae tayari tayari, baadae kidogo walikua wapo njiani wakielekea bandarini , huku dereva wake akiwa makini sana juu ya usukani akiendesha gari,
haikuchukua muda mrefu alikua yupo bandarini na kupita moja kwa moja sehemu maalimu yanapo shukia makontena ya mizigo,
Mbwa maalumu kwa ajili ya kunusu madawa ya kulevya walishaachiwa tayari kwa kazi hiyo, wakizunguka zunguka na kunusa, walikua wana mafunzo ya kutosha sana ivyo askari wote walikaa pembeni,
“wu wu wu wu wuwuwuwuwu”!
Mijibwa hiyo ilianza kubekwa kwa sauti sana huku wakirukia rukia kontena hilo , kumaanisha kuwa kuna kitu ndani ya kontena kisicho cha kawaida , hawaku poteza muda maaskari waliingia ndani ya kontena hilo na kuanza kupekua, hawa kuamini walichokiona yalikua ni madawa ya kulevya KETE ELFU NANE kwa haraka haraka, tena na zaidi, Mheshimiwa Masatu alishtuka sana baada ya turubai kufunguliwa na madawa hayo kuonekana,
“hayo ni madawa ya kulevya”?
Aliulza Masatu huku akisogea karibu.
“sina uhakika mheshimiwa!”
“embu hakikisha”
Askari mmoja wapo ambae yeye alikua kitengo hiko cha kunusa madawa alienda mpaka kwenye moja ya kete zilizo fungwa na kuchana kidogo, unga unga huo ambao ulikua mweupe sana ulimfanya apige chafya alitumbukiza kidole na kulamba huku akiwa ana sikilizia,
“ndo yenyewe Mheshimiwa, haya ni madawa ya kulevya aina ya HERROIN ni makali sana”
“niitie A.O.O wa bandari haraka sana”
Pale pale msimamizi wa makontena yale alisogea karibu baada ya kuitwa ,
“huuu mzigo ni wa nani”?
“mzigo upi”?
“nita kufunga, hili kontena ni la nani”?
“la la la”
“la nani, nijibu swali langu , Afande njoo uchukue maelezo hapa, na utumie kinasa sauti kiwe kama ushahidi tosha”
“la muheshimiwa EBENEZA MROSSO ndiyo kontena lake hilo,”
Ebeneza Mrosso alikua ni mtu mkubwa serikalini tena ni waziri wa miundo mbinu, alijua fika ana jiingiza katika jambo la hatari sana, alijua kua kuna mtandao mkubwa mwingine,

“BOSI KONTENNA LAKO LIME KAMATWA”
“NA NANI,”?
“MH, MASSATU yupo hapa na maaskari mambo yame haribika”
“umenitaja”?
“ndio”
“SUBIRI NIMPIGIE SIMU”
Ulikua ujumbe wa meseji ambao walikua waki tumiana na waziri huyo akimpa taarifa hizo pale pale simu ya Massattu iliiita na kuuiweka sikioni,
“MASATU nini una fanya”?
“we unahisi nafanya nini”?
“liachie kontena langu, sio ombi ni lazima”
“sasa sikia kontena hili siliachii na ndo ita kua kithibitisho tosha cha kukuweka ndani, nita hakikisha sheria ita fuata mkondo wake”
“naona unajaribu kujifanya jasiri, ni hivi ume ingia kwenye vita ambayo ita kupelekea upate matatizo makubwa sana, SHENZI wewe,”
Yalikua ni maneno ya kuogopesha sana ila hakutaka kuonesha kuwa ameogopa, aliloanza ili bidi tu amalize alichukua maelezo ya kutosha ili yawe kama kithibithi na kurudi nyumbani kwake KIJITONYAMA ,

****

Baada ya usiku kuingia alishtuka baada ya watu wengi kuingia wakiwa na vitambaa usoni ndani ya nyumba yake, huku wakiwa na silaha za moto mikononi walimuweka chini ta ulinzi,ili onesha kabisa kuwa walikua ni majambazi kabisa
“una jifanya mnoko sana, KUNGUNI wewe, twende ukafe ngedere wa mwituni”

Aliongea mmoja wa mijitu hiyo na kutoa simu mfukoni na kuiweka sikioni, baada ya kuongea maneno kadhaa alimtumpia simu MASSATU ambae alikua tayari ana onesha hali ya hofu kubwa kutokana na kutetemeka,
“ha ha ha ha ha ha , huu ni mtandao mkubwa sasa utaenda kufa na huo mwili wako hautoonekana popote pale, una toa siri za chama”?
Upande wa pili ulisikika hakua na sababu ya kujiuliza sababu alijua ni MROSSO ndiye aliyekua akiongea tena kwa majigambo sana,
“sawa uta niua ila tambua kuwa kila kitu kina mwisho wake”
“kwa heri marehemu”
Simu ili katwa na jitu lile kuichukua simu ile, alikoki bastola yake na kumuwekea Massatu usawa wa uso kumaanisha kuwa risasi moja tu inge chukua uhai wake pale pale
“naombeni nisali sara ya mwisho, eeeh MUNGU wa mbinguni naomba uniepushe na jaribu hili NAOMBA PIA UIPOKEE ROHO YANGU AMEN”
Mh, Massatu aliji kuta akisali baada ya kumaliza sala ile alimeza fundo la mate akisubiri kuuliwa, taratibu kidole cha jitu lile lililokua mbele yake lilianza kuvuta triga ili kuruhusu risasi itoke, katika hali ya kushangaza walihisi kitu kama kimpira kime pasua kioo na kudondoka mbele yao, sekunde chache kimpira kile kilianza kutoa moshi mkalli ambao uliwafanya waanze kukohoa sana na wengine kudondoka chini,
“Mh, Maasatu vaa hiki ”
Mbele yake alimuona Mwanamke aliyebana nywele zake nyuma huku akiwa na kifaa cha kuzuia moshi kupenya puani kwa haraka haraka alitambua kuwa ndiye Yule mwana mke aliye kua akiongea nae muda mchache uliopita, hakua na la kufanya zaidi ya kuweka kitu kile puani, alikua ni Witness Kafifi
Alitoa bastola yake kiunoni na kuwa fyatua watu wale waliokua chini wakikohoa…….

 Upotevu wa silaha za moto zikiibiwa vituo vya polisi zina zidi kutapakaa na sasa hivi majambazi walidiriki hata kuwauwa baadhi ya mapolisi, nao WATOTO WA SIMBA walizidi kutishia mji, raisi wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania muheshimiwa Steven ALINGA bado anazidi kuonesha hali ya kuchanganyikiwa sana, kiti cha uraisi sasa alikiona kina waka moto wana chama wenzake wa chama cha YBDP(youth brave democratic party) wanazidi kuuwawa kikatili kila kukicha , na mpaka dakika hiyo hakuelewa muuaji ni nani na kwanini ana ua, alionekana alishindwa kufikiria nje ya boxi na akili yake kugota na kufikia mwisho wa kufikiria mshauri wake peke yake ndiye aliye kua akijaribu kumrudisha katika hali yake ya kawaida,

Habari za kuibiwa kwa silaha za moto zina mfikia Witness akiwa nyumbani kwake ana sikiliza habari, habari zile zina mfurahisha sana, alijua kivyovyote vile vijana wale kuna kitu wana taka kuki fanya bila shaka! Kesho yake asubuhi aliwasha gari lake na kuanza kuwa tafuta vijana hao mchana kutwa chini kwa chini na kupata fununu kuwa wana patikana MABIBO mwisho, hakusita kwenda aliendesha gari mpaka alipo fika mabibo na kupaki gari yake, alichukua bastola yake na kuiweka kwenye kiatu huku kisu chake kidogo kukieweka kiunoni kwa lolote lita kalo tokea,

Alianza kutembea kwa miguu na kuliacha gari lake maili kadhaa na kuingia ndani ya kichochoro kimoja wapo, na kukuta vijana wengi wakivuta bangi maskani hapo,
“habari zenu”?!
“salama dada”
“namuulizia MAGOLI sijui mna mfahamu”?
“hatumjui”!
“nakuomba pembeni kidogo”
Kijana huyo aliinuka huku akiwa na kipisi chake cha bangi mkononi.
“nisikilize namuulizia magoli, najua una mfahamu, ila mimi sio mtu mba-ya nataka kumpa kazi”
“wewe uki muona uta mjua”?
“hapana sito mjua”
“sasa uli mjulia wapi”?
“ kama nilivyo kwambia awali kuna kazi moja ya pesa ndefu nataka kumpa, niamini”
“poa nifuate, oya washkaji eeh kama vipi baadae”
Kijana Yule aliwaaga wenzake huku akiwapa ishara ya kuwa konyeza, walizdi kuingia ndani ya vichochoro ndani kwa ndani na ghafla kwa hali ya ajabu vijana wale wavuta bangi walitokea na kumzunguka Witness,
“wewe mwanamke, tume kushtukia weewe ni shushushu”!
“jamani eeh, mimi sitaki haya yatokee, nipelekeni kwa magoli, ”
“hauendi popote huyu tuchojoe nguo zake tumbake tu, katoto kazuri kama hivi!”
Kumbu kumbu ya mama yake mzazi kubakwa ilianza kuji jenga kichwani pale pale, na kuanza kupandwa na hasira ambazo hakuelewa zime tokea wapi,alikua ni kama ame chomwa mkuki wa moto juu ya kidonda ambacho kilishaanza kuka uka na sasa kina aanza kutoa damu , baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa kijana aliye kua nyuma yake akiwa na bisi bisi mkononi ,
Kijana Yule alimsogelea na kumuweka ukutani huku akimuwekea bisi bisi ile shingoni,
“vua nguo mwenyewe ili jambo hili lisiwe gumu kwako mrembo”
Laiti ange jua mtu aliyemshikia bisi bisi ni zaidi ya moto wala asingedhubutu hata kumjaribu, hakuelewa aliye kua mbele yake ni commando tena jasusi muuaji katili wa kutisha,
Alizidi kuikandamiza bisi bisi juu ya shingo ya Witness ila baada ya sekunde mbili kijana Yule alikua chini akiugulia maumivu puani baada ya kupigwa kichwa, alimuinua na kumuwekea kisu alichokitoa kiunoni na kumuwekea shingoni, mwingine alivyo taka kumfuata alitulizwa na teke la shingo, alimzungukia mwingine na kum-mtwanga ngumi ya mdomoni, alimuona mwingine ana kuja mzima mzima na bisi bisi huyo alipita pembeni na kutuulizwa na teke la mdomoni, ndani ya dakika mbili wote walikua chini kila mtu akiugulia maumivu yake,
“namuhitaji MAGOLI, msinichezee akili yangu sawa,”
“sawa sawa, twende tuku peleke”
Ili bidi wote wasi mame kwa hofu na kuanza kuongoza mbele na moja kwa kuingia ndani ya nyumba ambayo haija isha vizuri, aliiingia na kuka guliwa na baadhi ya watu,walivyo mkagua na kukuta kisu kiunoni mwake, bila kujua kuwa ndani ya kiatu ana bastola ndogo,

“wewe ni nani”?
“wewe ndio magoli”?
“ndio mimi wewe ni nani, na ume nijuaje , nani kakuelekeza hapa”?
Witnes alikaa chini na kuanza kumueleza shida yake kuwa ana hitaji silaha za moto kama MARK 4,RIVOLVER, mabomu ya GRENADE . RPG kombora na mabomu ya machozi na silaha nyingine tofauti, kwa upande wa magoli bado alimuwekea mashaka Witnes na kudhani wenda ni shushushu au ni mpelelezi,
“kwaio hauniamini”?
“ndio sikuamini, na mimi siwezi kufanya kazi hiyo, tafuta mtu mwingine”
“nifanye nini uniamini”?
“sikia siwezi kufanya iyo kazi”
Witnes alitoa bastola ili yokua ndani ya kiatu na kumuangalia Magoli na kumkabidhi ilebastola,
“nime ingia na hii bastola bila watu wako kujua, kama uniamini au una mashaka na mimi nipige risasi”
Kilikua ni kitendo cha kujiamini sana,sababu aliongea huku akimuangalia MAGOLI machoni
“ila kabla ya kunipiga risasi tambua kuwa una poteza mamilioni ya pesa, chagua haraka kuniacha hai ili upate pesa nyingi au uniue na ukose kila kitu, toa uamuzi mapema”
Witnes alizungumza kwa kujiamini sana huku akibana meno yake ki ukweli bastola ile ili kua na risasi za kutosha , alijua kivyovyote vile kumkabidhi MAGOLI bastola ile alifanya makosa lakini hakua na jinsi aliamini kua hiyo ndiyo itakua njia pekee ya kumshawishi Magoli mtu ambaye alitokea kumuamini kabisa na kujua kivyovyote vile ange mtumia kwenye kazi zake chafu kama mauaji,

Magoli alivuta pumzi ndefu na kuikoki bastola ile huku akimuelekezea usawa wa kichwa,
“MAGOLI muuwe huyo malaya, sio mtu mzuri”
Ilisikika sauti ya kijana mmoja akiwa mlangoni pale.
“Magoli muuwe bwana atatuzingua, huyo mwana mke ni hatari”
“paa paa paa paaa”
Kilichosikika hapo ili kua ni mlio wa bastola na risasi nne kupenya ndani ya ubongo wa kijana Yule aliye kua akiongea,
“kazi yako nita ifanya una kiasi gani”?
“miilioni mia na hamsini,”
“NO ongeza ifike mia mbili kamili, nikuletee mzigo mkubwa, nakuletea mpaka sub mashine GUN”
“ niletee silaha kwanza ziki kamilika nina weza nika kuongeza ,”
“nipatie advance”
“hakuna tabu nakupa milioni kumi cash jioni ya leo”
Tayari wali patana bei huku kijana Yule aliye pigwa risasi mwili wake kutolewa eneo lile,Witness alikabidhiwa bastola yake ,
“sasa una itwa nani binti”?
“niite jeshi la mtu mmoja”!
Witness aliondoka akiwa na amani moyoni, kila kitu kilienda sawa kwake huku akika milisha malipo ya Magoli, baada ya siku chache aliletewa silaha za aina zote alizotaka , na kufanya kazi yake iwe rahisi kabisa.

 Mambo ndani ya bunge mkoani Dodoma yanazidi kuwa mabaya sana, matusi yalizidi kurushwa kweli palikua hapatoshi na safari hii meza na viti vilianza kurushwa hii ni baada ya Mh. Massatu kutaka kuongea ukweli ndani ya bunge hilo , jambo ambalo waheshimiwa wabunge karibia robo yao hawa kutaka litokee kwaio wali tumia kifungu cha ku mbana Massatu kuwa anawadhalilisha, walinzi walitokea na kutuliza gasia ile.
“mimi nina wajua, na hapa ninavyo ongea nina kidhibiti tosha kabisa, EBENEZA MROSSO alini tumia majambazi usiku wa jana. Muheshimiwa spika wa bunge naomba unisikilize”
Alikua akiongea Massatu huku tayari akiwa tayari na hasira nyingi, ki ukweli alijiamini sana baada ya kuhakikishiwa na Witness kuwa aseme kila kitu huku nyuma yeye ata linda maisha yake, alijiamini sana kupita kiasi,
“tunaomba muongozo”
“kaa chini”
“nita kaaje chini una ona kabisa huyu mwenzetu anaongea pumba”
“nime kwambia kaa chini muheshimiwa”
Alifoka spika wa bunge JANETH AUGUSTINO lakini licha ya kuwa tuliza lakini fujo zilizidi na safari hii viti kuanza kurushwa tena na hatimae ngumi kutokea nia na baadhi ya wabunge wa humo ndani wali taka bunge luvunjike kwa wakati huo, kweli waliona bora iwe ivyo na baadae wamtafute Massatu waweze kummaliza chini kwa chini wali fanya mawasiliano na mheshimiwa Raisi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania.
“MPOTEZENI KABISA,”
“KWAIO TUMUUWE”?
“TENA FANYENI UPESI,”
Yalikua ni maneno kwa njia ya meseji baada ya Mrosso kutumiana meseji na muheshimiwa raisi. Ilibidi spika wa bunge JANET AUGUSTINO aaahairishe mpaka jioni ya siku iyo.

********

Witness akiwa Dar es salaam habari zile alizisikia sana kutoka bungeni , ivyo kama alivyo muahidi Masatu kuwa ata mlinda hakutaka kupoteza muda alianza kuandaa silaha za kutosha ndani ya gari kwa safari moja tu , kuelekea Dodoma moja kwa moja aliweka silaha izo ndani ya RANGE akiamini kua gari hiyo ina mwendo kasi wa kutosha ivyo masaa machache ata kua kasha fika tayari mkoani Dodoma,

Ila kabla ya kuwasha gari alitoka nje kwa mguu ili aingie supa maket anunue chakula cha kula njiani, bila kuangalia mbele ana gongana kikumbo na mwana ume mrefu kidogo aliye chomekea, alijikuta yupo kwenye mikono yake yenye misuli ya mazoezi alivyo muangalia kifuani ambapo alivaa body ili mkaa vizuri hii ili mfanya damu izidi kumwenda sana mbio alimuangalia usoni kwa mwana ume huyo hakuelewa kwanini damu ili mwenda mbio, alikua ni mwana ume mzuri aliye jazia kila sehemu ya mwili wake .
“am sorry(niwie radhi)”
Alizungumza kijana Yule huku akiachia tabasamu hakika Witness alishindwa kuongea lolote tayari hisia za mapenzi ziliazna kumtawala ndani ya moyo wake, alihisi moyo wake una joto sana.
“sawa it’s okay”
Alijibu Witnes huku akijitoa mikononi mwa mwana ume Yule, alizidi kumsindikiza kwa macho mpaka alipo toka nje ila hakutaka kumwacha aende ivi ivi, alimfuata mpaka nje na kumuomba namba ya simu .,
Dakika hiyo hiyo alianza mawasiliano nae na kuanza kusahau kuwa ana safari ya kwenda Dodoma bungeni kumlinda Massatu,

Hisia kali za mapenzi zilianza kumsumbua sana Witness na kuji kuta ana shindwa kujizuia hisia zake kweli alijikuta ana muonesha kila dalili za kumpenda kijana huyo ambaye tayari alimfahamu kwa jina a Austine . siku zilivyo zidi kwenda ndipo walipozidi kuzoeana ili kua haipiti siku bila ya Witness kumuona Austine,
hisia kali zilianza kutembea ndani ya mioyo yao mithili ya upepo uendao kasi sana. Na kujikuta wapo ndani ya uhusiano, Witnes alimpenda sana Austine kupita maelezo, muda wote alimganda kama kupe, kila waipoenda walikua wote, japo ilikua ni kipindi cha muda mfupi lakini Witnes alijikuta anampenda sana Austine.

Siku iyo walitafuta Hotel nzuri ili wapumzike na waweze kuongea kuhusiana na uhusiano wao juu ya mapenzi yao ila baada ya kufika chumbani kili chofuata hapo yalikua ni mabusu tu, na wote kuvua nguo zao na kuzitupa chini na kuanza kuvunja amri ya sita, Witnes hakika aliji kuta anaingia katika mahusiano tena alijiona mawanamke wa tofauti sana baada ya kuvunja Amri ya sita, aliamini Austine ndiye ata ziba pengo la Stuwart, ivyo ndivyo ilivyo kua,
“Witness mbona mgongoni una alama kiasi hiki”?
“nita kwambia Austine usijali mpenzi wangu!,”
“wewe ni mzuri sana, Witness nakupenda sana, nataka nikirudi kutoka Botswana tufunge ndoa haraka haraka, then niku chukue tuishi wote, wiki ijayo nasafiri”
“nakupenda sana Austine, nime tokea kukupenda na kukuamini pia, mimi nakutakia safari njema”
Waliongea mengi huku wakipigana mabusu na baadae tena kufanya tendo la ndoa wakiwa wenye furaha kabisa,
Witnes alikua mwenye furaha sana kiasi kwamba alisahau kazi ana yotakiwa kuifanya, kesho yake aliwasha gari mpaka maeneo ya chanika ndani ya nyumba ambayo haija maliziwa kujengwa na kuingia ndani ambapo kulikua kuna mlango mkubwa,

Alivyofungua kulikua kuna kijana ana kitambaa cheusi kichwani huku akiwa juu ya kiti mikono yake ikiwa nyuma ime fungwa,
Alimvua kitambaa kile cheusi nay eye kukaa pembeni alikua ni Vincent Towo alikua ni kama mateka wa Witness .
“chukua chakula hiki kula”
Witnes ali mfungua pingu na kumpa Vincet chakula ili aweze kula.

“NDIO NDIO ALIYE HUSIKA NA VIFO VYA WAZAZI WAKO NI MUHESHIMIWA RAISI, NDIYO MIMI NILIHUSIKA PIA KUWA UWA WAZAZI WAKO VILE VILE, NDIO NA BAADHI YA WABUNGE, NDIO NIAMINI,
RAISI WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA NI MTU MBAYA SANA, MTAFUTE MASSATU NI MTU MZURI SANA, HUYU HANA TATIZO KABISA, USINIUE TAFADHALI……..”
Ili kua ni sauti iliyo kua iki tokea ndani ya kinasa sauti ambapo sauti ile ilipenya masikioni mwa Vincent Towo , na kubaki kumwangalia Witnes machoni,
“wazazi wangu waliuliwa kinyama sana, nili mshuhudia baba yangu ana katwa kichwa kama kuku huku mama yangu mzazi akibakwa kama kuku, nili wapenda sana wazazi wangu, leo hii serikali hii ime nifanya niwe gaidi, niwe muuwaji, wame yaharibu maisha yangu, sikuwahi kufikiria kama ninge kuja kuishi maisha haya kama ndege”
Witnes aliweka kidole chake machoni na kufuta machozi yaliyokua yanaanza kumtoka tayari, kweli ilikua ni historia ya kuuzunisha sana, hata ungekua mbele yake unge dondosha chozi sababu aliongea huku akitia huruma mno, Vicent alimfuata na kumkombatia, hata yeye pia aliguswa hakutegemea kuwa nyuma ya mauji hayo kuna kisa kikubwa sana na kumfanya hata yeye pia aanze kudondosha chozi la uchunngu,
“usilie Witness mimi nita kusaidia katika kila jambo , tuta kua wote bega kwa bega”
“hapana Towo, acha mimi nimalize nilicho kianza sitaki uingie kwenye matatizo makubwa, niachie mimi”
Ila katika hali ya kustaajabu Vincent Towo alichomoa bastola iliyo kua kiunoni mwa Witnes na kurudi hatua mbili nyuma, huku akimuelekezea alipo na kumuweka Witness chini ya ulinzi.
“mikono juu nakuuwa hapa hapa, kacha kacha”
Vincent Towo aliongea huku akikoki bastola kwa nia moja tu kumuuwa Witness aliye kua mbele yake aliamini asipo fanya ivyo alikua ana kufa yeye pale pale. Alikuwa kasha jua tayari Witnes ni hatari kiasi gani. Ivyo hakupaswa kufanya makosa tena
“sogea ukutani”
Witnes hakuamini kitendo cha kubadilikwa ila ilibidi awe mpole na kusubiri kifo chake ambapo ilionesha dhahiri mtu aliye shika bastola safari hii alikua hana masihala, alishika ukuta uliokua mbele yake huku akisubiri risasi ipenye ndani ya mwili wake.

 AKIWA UKUTANI ANASUBIRI kifo chake gafla alimuona Vincent Towo anazungusha bastola ile na upande wa mshikio sasa ukiwa upo upande wa Witness kumaanisha kuwa achukue bastola ile,
“chukua, nimeamua kukusaidia nataka tuwe kitu kimoja ili haki ipatikane na nchi iongozwe na wanyonge wapewe haki zao naitwa VINCENT SANFORD TOWO,”!
Aliongea Vincent huku akimpa mkono Witness pamoja na bastola ile,
“witness Dimalia KAFIFI,”
Kitendo cha kuunganisha nguvu zile zili mfurahisha sana Witness ila ki upande Fulani mwanamke huyo Witness hakutaka kumuingiza Towo ndani ya matatizo makubwa ambayo yeye aliamini kua bado ana vita kubwa na safari ndefu,. Kupambana na serikali tena akiwa peke yake haikuwa kazi rahisi.
“niamini acha niku Sadie, nita hakikisha nitakua nawewe bega kwa bega. Naamini kwa kiasi kikubwa uta nihitaji kwa kazi yako”
“hakuna taizo ingia kwenye gari tuondoke”
“tuna enda wapi”?
“nita kwambia”
Towo aliingia ndani ya gari na Witness na gari hiyo kutoka mbio ambapo baada ya kufika maeneo ya Gongo la mboto Witness alitoa kisu kikubwa na kikali na kuweka gari pembeni, kisu hiko kili wekwa juu

ya dash bod na kumfanya Towo aanze kutokwa na majasho mengi hakuelewa nini Witnes ana waza ndani ya kichwa chake,
“nataka nikuache hapa”!
“uniache kivipi”?
Witnes aliangalia kile kisu chake kilichokua juu ya dash body na kushusha pumzi ndefu.
“okay, nishajua unachotaka kuki fanya usipate shida”
Towo bila kuuliza chochote alichukua kisu na kuanza kuji kata kata nacho mikononi na kuji chana kidogo usoni alisikia maumivu lakini ili mbidi avumilie tu, damu zilianza kumtoka lakini hakujali kabisa, baada ya kujikataka na kisu kile alipewa sindano yenye dawa ya usingizi na kuji choma mkononi, baada ya dakika chache baadae Towo alikua tayari kapoteza fahamu zake , baada ya dawa zile kufaya kazi, Witnes aliwasha gari na kusonga mbele ,

Giza lilikua tayari limeanza kuingia na kufanya usiku kuwa mkali sana, moja kwa moja Witnes aliegesha gari yake koko bich na kumtupa Towo pembezoni mwa ufukwe na kuondoka zake, alitimua kasi na moja kwa moja kurudi nyumbani kwake, alivyo washa simu yake alikuta meseji mfululizo kutoka kwa Austine mpenzi wake.

Mawasiliano ya chini kwa chini yalizidi kufanyika na kuruka nje ya nchi, baada ya Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kushauriana na mshauri wake, baaada ya kupata mawazo na kuyaunganisha ili mb-di amtafute rafiki yake ABRAHAM NOVICH raisi wa urussi akiamini kuwa yeye ndiye ataweza kumpa ,jeshi au kumsaidia aliamini fika kuwa hakuna msaada wowote zaidi ya kumuangukia raisi huyo wa Russia ambaye nchi yake ilisifika kuwa na ulinzi mkali sana.

“mr,president I have your call (muheshimiwa Raisi nina simu yako)”
Alikua ni mwanamke wa kirusi ambaye alimsogelea raisi Abraham Novich ndani ya kikao hiko na kumpa simu iliyokua ime tokea moja ka moja Tanzania, taarifa za kuomba jeshi.
Baada ya mazungumzo hayo kuisha nayeye aliamua kuita kikao kidogo cha wapelelezi ambapo baada ya kukaa kikao hiko wanaamua kuwa chagua watu wawili waweze kwenda Tanzania ili kumsaidia kumkamata muuaji anayesumbua nchini humo,
Ritha Navarah na Stuwart Scottlah, ndiyo waliyo teulia kwenda Tanzania.

Stuwart alivyo tajiwa nchi hiyo roho ilimuuma sana alimkumbuka sana Witness Kafifi alihisi roho ina muuma sana hasa alipokumbuka kuwa alikufa kwa kifo ,kibaya sana huku upande a pili hakujua kuwa ndiye yeye waliye takiwa kwenda kumkamata napengine kumuuwa,
Mikakati ya safari waliipanga akiwa na msichana aliye pewa kama mpelelezi Ritah Navarah, baada ya kupewa maelekezo jinsi ya kufika ndani ya nchi hiyo. Walipelekwa na magari maalumu mpaka uwanja wa ndege mkubwa wa Moscow ili kusubiri ndege hiyo ya shirika la Fly emirates,

Baada ya muda mchache kipaza sauti kili tangaza kuwa wasafiri wana hitajika kwa ajili ya uka guzi wa mizigo na mengime tofauti yakiwemo kugonga passpoti zao mihuri immigration.
,waliburuza mabegi yao na kuya weka juu ya mashine ambapo wao walipita ndani ya kimlango kidogo na kuvua vitu vyote vya chuma,

Magari maalumu ya kuweka ngazi kwenye ndege yalikua tayari yapo mlangoni mwa ndege hiyo na abiria kuanza kupanda akiwemo Stuwart na Ritah, baada ya dakika kadhaa mbele kipaza sauti kilikua kikitangaza na kuwataa rifu kuwa abiria wote waweze kufunga mikanda sababu ndege hiyo inaanza kupaa angani.

Taratibu sana ilianza kutembea kwa mwendo wa kawaida na mwishowe kuchanganya kabisa na matairi ya mbele kunyanyuka juu kisha mengine ya nyuma kufuata.
“sijawahi kufika Tanzania Stuwart, ni masaa mangapi tuta tumia”?
Aliuliza Ritah akitumia lugha ya kirusi.
“masaa kumi nafikiri, hata mimi sikuwahi kufika ila nilisha wahi kuwa na mchumba wa kitanzania, nili mpenda sana, sema ali fariki dunia tukiwa vitani”
“poleni sana Mr, Stuwart”
“nishapoa”!
Waliendelea na mazungumzo ya hapa na pale mwishiowe wote waliji kuta wamelala, kili cho washtua ni kipaza sauti ambapo ndege hiyo ili tua katika uwanja wa Dubai,
Abiria waliokua wame fika walishuka na wengine kuingia na baadae kidogo ndege hiyo kuruka tena ambapo ili fika Nairobi masaa machache na kutua tena, baada ya dakika kadhaa ndege hiyo ili paa tena na sasa kubakisha uwanja mmoja tu wa mwalimu nyerere jijini Dar es salaam,

Maasaa kumi na moja yali katika tangu waaanze safari yao na hivi sasa tayari walikua wame fika nchini Tanzania juu ya uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere, sauti nyororo ya kipaza sauti iliyo tokea ndani ya spika ili wafanya Stuwart na Ritah waanze kusimama na kuchukua mabegi yao madogo yaliyo kua juu sehemu maalumu, kila kitu kilienda sawa na kuanza kushuka ngazi za ndege hiyo wakiwa na abiria wengine,
“nani ata kuja kutupokea”?
“kuna kikaratasi hapa nilipewa SESILIA nafikiri nita ona bango”
“sawa”
Moja kwa moja walitoka nje na kweli walimuona mtu kashika kibango kilicha andikwa jina hilo na kumfuata,
“Am Stuwart”
Aliji tambulisha Stuwart na baadae Ritah kisha walielekea katika maegesho ya magari maalumu na kuingia moja kwa moja ndani ya Landcruiser VX ambapo mwanamke aliye jitambulisha kwa jina Sesilia alianza safari ya kuondosha gari hilo,

Ndani ya akili ya Stuwart aliwaza kitu kimoja tu kumkamata muuaji pengine na kuumuuwa kabisa, bila kujua aliyeambiwa amkamate alikua ni mpenzi wake ambaye katika akili yake alidhani alikufa vibaya kwa mlipuko wa bomu la kutegwa mchangani.


 GARI hiyo Landcriser vx lilizidi kwenda na safari ya kuelekea ikulu sasa kuanza, jambo la kuingia kwa Stuwart na Ritah lilikua siri sana hakuna hata mmoja aliye jua ujio wao wakitokea nchini Urusi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wao, wakumtafuta muuaji huyo ambaye mpaka sasa hawa kujua ni nani hasa, mshauri wa Raisi Issaya Mbetto ndiye aliye towa wazo ilo na kumpa tena nguvu mpya mh, raisi Steven Alinga sababu alionesha kabisa hali ya kuchanganyikiwa na kuonesha nchi kumshinda kabisa, alikiona kifo sasa ni zamu yake,
Ivyo ujio wa Stuwat na Ritah ulimaanisha sana kwake, ila akiwa katika kiti chake alipokea simu ambayo ili mshtusha sana kutoka kwa Vincent Towo.
“kwani ulikua wapi”?
“nitakuja kuku elezea muheshimiwa Raisi ila kwa sasa hivi nipo hospitali”
“sawa fanya uje kuna mambo nataka niku shirikishe”
Bila kujua hata Vincet Towo sasa hakua upande wake tena.


0 comments:

Post a Comment

BLOG