Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 8/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 8 KATI YA 10
*******
 *******


Kwa upande wa Pamela hakutaka kuishia hapo, asubuhi ya kesho yake aliwasha gari na moja kwa
moja kuelekea sinza kwa mama Donald sababu aliamini hakukuwa na msaada mwingine zaidi ya kumuelezea mama yake na Donald kile alicho sikia, alivyo fika aliweka gari nje na yeye kunyoosha mpaka ndani kwa mama yake na Donald alimkuta akiwa na hali ya uzuni bado usoni mwake!,
Bado alikua na kidonda moyoni, bado alikua akimkumbuka mwanae tangu kifo chake hata siku arobaini bado hazi kufika .
Baada ya kumsalimia alianza kumueleza kila kitu kuhusu mambo anayo sikia kila usiku akilala,
“Binti naomba uende, niachieni mwanangu apumzike kwa amani huko alipo”
“Mama nime kuja hapa ili nikwambie, kila siku Donald ana kuja usiku anaita jina langu dirishani, nime jaribu kuwa eleza wazazi wangu, hawa taki kunielewa nikaamua nije kwako kukueleza , na kitu nacho kwambia ni ukweli , siku danganyi”
Maneno yale yailkua ya ajabu sana ndani ya masikio ya mama Donald ilikua ni stori mpya kwake kabisa, hakutaka kuyapa maneno ya Pamela nafasi, ilikua ni kama ana mtonesha kidonda chake, alicho fanya hapo ni kumfukuza tu hakutaka kumsikiliza tena.
“ondoka ondoka ondoka Pamela, niacheni nipumzike, mwache mwanangu apumzike kwa amani huko alipo, amesha kufa tayari,mwache, mwache, mwache, aaah!”
Pamela aliondoka kwa unyonge sana huku akilia machozi mtu aliye mtegemea sasa ana mfukuza bila kumsikiliza hakuelewa amueleze nani ili amuamini, aliingia ndani ya gari lake huku akilia machozi na kuondoka zake mbio., akielekea chuoni.

“YULE MCHUMBA wake Donald alikuja hapa leo, ana dai kuwa kila siku usiku anasikia sauti ya Donald dirishani kwake”
“mchumba wake yupi”?
“Yule uliye kuja nae siku ile hospitali”
“nani,Pamela”?
“ndio”
“Mungu wangu asante kwa kujibu maombi yangu”!
Yalikua ni mazungumzo kati ya Mama Donald na mdogo wake aliye itwa Maria, siku ya pili sasa alifunga na kuomba hakika aliona maombi yake yanaanza kutimia, alijua kivyovyote vile kuna kitu ivyo ndani ya moyo wake ali panga kitu kimoja tu kumtafuta Pamela kwanza ili aweze kufanya mazungumzo nae.



“MCHUNGAJI, nilikua naomba ile c.d ya Jennifer Mgendi, na Bahati Bukuku kama unazo!”
“sawa subirini hapo nakuja Michael”
Mchungaji Nathaniel alipandisha ngazi kuelekea chumbani na kuwaacha seblen Michael na Bonifasi baada ya kutoka nao kanisani na kutaka nyimbo za dini, ila ki upande Fulani vijana hao waliingiwa na pepo mchafu , Michael alisimama na kutoa kipande cha sabuni kisha akatembea mpaka kwenye meza ya tv na kuchukua funguo za gari la mchungaji, alikandamiza funguo zile, kwenye kipande cha sabuni na upande wa pili alifanya ivyo ivyo, alivyo hakikisha funguo zile zime jichora kwenye sabuni , aliweka ndani ya mfuko na kurudi kuketi kwenyekiti , kile kilicho endelea seblen mchungaji hakuelewa hata kidogo ,
“shikeni hizi hapa”
“asante mchumngaji, Ubarikiwe sana”
“Amen, msisahau kumuomba Mungu, naye atajibu maombi yenu”
“sawa mchungaji”

Vijana wale waliondoka, moja kwa moja walinyoosha mpaka kariakoo mtaa wa Swahili na kupeleka kipande kile cha sabuni kwa mafundi wanaochongesha funguo, ndani ya dakika hamsini tayari funguo zilikua zime kamilika kabisa, baada ya hapo wali mpa kiasi chake cha pesa na wao kuelekea maskani kwao maeneo ya kigogo.!
“oya, kitu kime jipa tusha pata gari washkaji, silaha zile zipo”?
“zipo zipo, jembe langu!”
“sasa kesho mchana, naenda kuchukua ile gari, sawa”!
“sawa”!
Walikua wakiongea na majambazi ambao wali panga kuvamia duka kesho yake , ivyo tayari walisha pata gari ya mchungaji kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo wakiamini kesho yake ata kua kanisani na hakutokuwa na mtu yoyote nyumbani hapo,
Waliandaa silaha za moto na kuziweka tayari kila kitu, na sasa wakisubiri kesho yake kukuche ili waende kuvamia duka la muhindi anaye uza dhahabu maeneo ya K,koo , hazikua akili zao wakati huo Bonifasi na Michael shetani Alisha waingia tayari na kuwaamuru wafanye kile wana cho takakuki fanya.

Kesho yake mchana tayari walikua nje ya ukuta wa mchungaji Nathaniel na kuruka ukuta wakiingia kwa kua kulikua na kila dalili ya ukimnya waliamini kabisa hakukuwa na mtu yoyote Yule,
Haraka haraka baada ya kuingia ndani walisukuma gari hiyo aina ya Benz mpaka nje kimnya kimnya kisha wakaingiza funguo zao za kuchonga na gari kuwaka!,
Walirudishia geti na kutoka mkuku, walifika kigogo na kuwachukua wenzao huku wakiwa na silaha za moto mikononi mwao, dakika chache baadae wali fika nje ya Sonara hiyo ya muhindi iliyo kua na dhahabu na kuingia kama wateja, ila baadae walivaa vitambaa usoni na kuwaweka watu wote chini ya ulinzi, na kuanza kukusanya dhahabu,
“huyo ana kimbia”
“paaa paaaa”
Kijana mmoja aliye kua mateka alitaka kukimbia nje ila alipokea risasi mbili za mgongo na kufa pale pale nje, watu walianza kuogopa na kutanda nje, walichukua dhahabu zile na kuingia kwenye gari lao na kuanza kuondoka,
“kamata namba za gari bana, kamata namba za gari zile, naondoka wale jambazi, lazima nitakamata mimi wale,, wanijui mimi vizuri, ”
Alifoka Muhindi huyo akimuamuru mwanamke aliye kua msaidizi wake, kwa haraka haraka waliweza kuziandika namba za gari lile lili lotoka kufanya mauaji na uvamizi,

Watu walianza kusogea mmoja baada ya mwingine kushudia tukio hilo la mauaji ya kijana huyo aliye pigwa risasi mbili za mgongoni mfululizo na kupoteza maisha yake pale pale chini, hasira kali dhidi ya majambazi wale zilijijenga, haukuchukua muda mrefu tayari jeshi la polisi lili fika na kuchukua maelezo,

Walipewa namba za lile gari na haraka haraka kuanza kufanya uchuguzi juu ya mmiliki wa gari lile ili hatua zifate mkondo wake, ivyo ndivyo ilivyo kua.

Bila kuelewa chochote kile mchungaji Nathaniel asubuhi ya siku hiyo, baada ya kumshukuru Mungu kwa kumuamsha asubuhi hiyo na kuiona siku nyingine kama anavyo fanya kila siku, alianza kujianda kwenda kwenye shughuli zake, wakati huo alikua akiishi peke yake baada ya mke wake kusafiri kwenda nchini Ethiopia kutangaza injili.

Alivyo toa gari nje alishangaa kuona defender tatu ziki simama mbele yake mara ya kwanza hakuelewa kitu ila baadae walishuka askari wanne na kumuendea.
“habari yako mchungaji”?
“nzuri tu, bwana yesu asifiwe”
“Amen mchungaji, una hitajika kituo cha polisi, upo chini ya ulinzi toka nje ya gari”
“kwa kosa gani”?
“usitupoteze muda, mnafki wewe, una jifanya mchungaji, mchungaji gani, toka nje ya gari aisee, uliona haitoshi kuiba sadaka za watu sasa ume amua kuvamia eti”
Mchungaji Nathaniel hakua anaelewa lolote lile ilikua ni hadithi mpya kwake, hakuelewa ni kitu gani cha kujibu, alicho fanya yeye ni kushuka ndani ya gari , pale pale alipigwa pingu kwa nyuma, na kuanza kusukumizwa.
“ita kua mme kosea mimi siwezi kufanya kitu kama hiko, mimi ni mtumishi wa Mung….”
“paaaaaaaaaa”
Kilisikia kibao alicho pokea mchungaji Nathaniel juu ya shavu lake na askari wa kike ambaye alionekana kuwa na hasira sana, na kumfanya atulie kimnya ndani ya moyo wake yote alimuachia Mungu na kujua tu ni hila za shetani lakini aliamini kuwa Mungu yupo na ata fanya kazi yake ivyo hakuwa na ubishi zaidi ya kusali kimoyomoyo akimuomba Mungu wake,
ndani ya nafsi yake alielewa fika wenda Mungu anataka akafanye jambo aka muoneshe kitu,
“hii Dunia bwana, mimi sikuamini Mocha, kumbe izi dini ni unafki mtupu, huyu mchungaji ana jifanya ana toa mapepo kumbe kajambazi aisee, hii kali ya mwaka,”
“wewe ndo unajua leo, hakuna dini siku izi mtu akishindwa maisha anajifanya mchungaji ili apate pesa kiurahisi kabisa, hawa ni magelesha tu, ndo maana yani mimi nawa kubali wazungu, MZUNGU akishindwa maisha ana jitia risasi, lakini huku uta sikia mara ana imba kwaya, mara sijui mchungaji, yaani uwi-zi uwi-zi tu”
Yalikua ni mazungumzo baina ya mapolisi hao huku mchungaji Nathaniel akiwa ndani ya Deffender hakika alikua katika usiku wa giza sana.
Baada ya kufika kituoni moja kwa moja wali mtupa Sello ili asubiri hukumu yake kwa kosa la kuua na kufanya uvamizi wa mali.

“KUMBE SIO MCHUNGAJI NI JAMBAZI SUGU, habari kamili soma ukurasa wa tatu”
Yalikua ni magazeti ambayo yalichapishwa siku hiyo hiyo huku picha ya Mchungaji Nathaniel ikiwa mbele ya gazeti la KAY STALION TZ na kutapakaaa nchi nzima wengine walianza kutoa imani nae ila wengine waliamini kuwa ni Mitihani tu ya Mungu kama Ayubu mtumishi wa Mungu aliweza kuja ribiwa na wanae kuuliwa pia na kuchukuliwa mali zake zote. , waliamini kabisa ni moja ya mitihani ya Mungu hawa kuacha kusali na kuomba sana, ili Mungu aweze kutenda miujiza yake,

Maria akiwa feli kivukoni ana uza samaki wa kuchoma na mwenzake aliye fahamika kwa jina Mama Koku , ghafla ili paki gari ya kifahari na ya gharama aina ya BMW X5 mbele yao na kioo cha nyuma kushushwa.
“habari zenu”?
“salama tu karibu”
“nahitaji samaki”
“kiasi gani,?
“wote hao ni pesa ngapi”?
“elfu ishirini na tano”
“sawa”
Mwarabu Yule alishuka ndani ya gari na kumuomba Maria waongozane sababu hakuwa na pesa hata kidogo hapo alipo, alimuaga rafiki yake Mama Koku na kushukuru Mungu siku iyo aliuza sababu biashara ilikua ngumu sana,
Baada ya hapo aliiingia ndani ya gari na kukuta watu wengine watatu nayeye kuketi kati kati yao, kioo cheusi kili fungwa na gari kuanza kuondoka kuelekea kigamboni upande wa pili, ilikua ni lazima waingize gari ndani ya pantoni kisha wavuke upande wa pili,
Gari lile BMW X5 lili iingia ndani ya pantoni, ila katika hali ya kustaajabu Maria aliona gari lile lina nyanyuka juu mara ya kwanza alidhani ana ona vibaya pengine, alivyo chungulia aliona wana elea hewani alivyo wageukia wale waarabu aliona sura zina aanza kuwa badilika na kuanza kuwa na sura za wanyama wa ajabu sana,
Katika macho ya kawaida ya kibadamu hawa kuweza kutambua kuwa gari lina paa wao waliona ni ndege ana ruka ila haikuwa ivyo,
“maombi yako yame tutesa sana, hautotoka tena huku, ita kua ni zamu yako kuteseka”
Sauti iyo nzito ilizidi kukoroma huku sura iki jibadili na kuwa kama paka na juu pembe kuanza kumuota, ilikua ni picha ya kutisha sana kwa Maria, taratibu gari ile ilianza kuingia ndani ya bahari ile kisha kutokomea kabisa chini ya maji……..


“hiki nini si sabuni hii, ime fata nini chini ya ufungu, hapana nishaanza kupata picha sasa, lazima nipeleke hili suala polisi!”
Ndani ya akili ya Natasha mawazo mengi yalizidi kuji jenga akijaribu kuunga unga mambo ambayo yali endana na Picha halisi ya sabuni ile, alimkumbuka vizuri mpenzi wake alivyokua akiongea na BONIFASI juu ya kutafuta gari, sasa alipata Picha kamili , alijaribu kuunganisha tukio lililo mkuta Mchungaji Nathaniel na kupata jibu la swali lake, hakua na jinsi zaidi ya kuvaa haraka haraka nguo zake kisha kunyoosha moja kwa moja kituo cha polisi kilicho kua buguruni wengi hukiita ngazi mbili.,
Alivyo fika hapo alitoa maelezo ambayo yaliwafanya maaskari wale waweze kuamini kile kilicho zungumzwa na NATASHA,

“umesema huyu Michael ni mpenzi wako”?
“ndio ni mpenzi wangu, tuna ishi wote, lakini kama nilivyo kwambia tangu juzi , alikua anaongelea kuhusu kuiba gari na rafiki yake Bonifasi”!
“asante dada kwa ushirikiano wako, tuta lifanyia uchungizi wa kina swala lako”
Natasha aliwashukuru na kuondoka zake kimnya kimnya bila kumwambia Michael kile alicho kifanya siku hiyo,
Jeshi la polisi chini kwa chini liliamua kufanya uchunguzi na kugundua kuwa kweli funguozile zilichongwa hakukua na sababu ya kuendelea kumuweka Mchungaji Nathaniel mahabusu walimuachia huru kisha kuwa kamata wale waliohusika, siku ya kutoka mahabusu kila mtuhumiwa alisikitika sana, sababu walisha mzoea na wengine kuapa endapo wakitoka katika hukumu yao wangeokoka! , japo alikaa siku tatu ilitosha kabisa kuwapa maneno ya kiroho na maneno ya kumuogopa Mungu, ivyo ndivyo ilivyo kua.

*****

“NYAU NYAU NYAUUUU”!
SAUTI YA paka aliye mbeba Deuji ilisikika baada ya paka huyo kumuona Pamela,

“Dad nime mpenda sana huyo paka, ume mtoa wapi”?
“nime mnunua leo, kwa rafiki yangu”
“pamela Pamela Pamela”!
Donald aliita lakini hakujua kuwa katika hali ya kawaida alisikika kama sauti ya paka , aliita huku akilia na kumuangalia Pamela ambaye alimbeba na kudhani ni paka. alijaribu kufanya kila jambo kumuonesha Pamela kuwa yeye ni Donald lakini ilishindikana kabisa,Alisha geuzwa paka wakati huo na zilisubiriwa siku arobaini akatwe ulimi na kuungana na misukule huko kuzimu,
Pamela hakuelewa kuwa mpenzi wake ambaye alikua radhi kupigwa risasi kwa ajili yake aliye muonesha mapenzi tele leo kageuzwa kuwa mnyama paka, tena na baba yake mzazi!. ,
“haya wewe toka upesi nenda huko jikoni”
Aliongea Deuji huku akimfukuza paka huyo ambaye alikua ni Donald yeye binafsi alilijua swala hilo na maneno aliyo tamka alimaanisha, na paka Yule kukimbia jikoni .
“Mwanangu Pamela, kwanini usikubali uolewe na PHD Grayson,Donald tulimpenda lakini Mungu Kampenda zaidi, naomba ukubali awe mumeo, mbona ni mtu mzuri tu”
“Dad”
“nini mwanangu?”
“bado namkumbuka Donald”
“hapana mwanangu kesha kufa tayari hakuna jinsi nyingine ya kufanya hapo”
“naelewa Dad”
“basi fanya kama niliyo kwambia jitahidi ufikirie!”
Hayo ndiyo yalikua maongezi ya mtu na baba yake kila siku iendayo kwa Mungu, alizidi kumshawishi mwanae aweze kuolewa na Grayson kadri siku zilivyozidi kwenda na kuji kuta ana kubali sababu hakua na jinsi nyingine aliamini Donald wake kesha kufa tayari bila kujua mbele yake kuna giza nene sana, bila kujua kuwa kuna ukweli nyuma ya pazia , bila kujua mpenzi wake ametolewa msukule na baba yake mzazi aliyemzaa akila mateso ambayo walau ange tamani kurudi duniani.!

Maombi yalizidi kupamba moto kanisani, Mchungaji Nathaniel Gabriel alizidi kuomba huku wakati mwingine akinena kwa Lugha aliamini kabisa kuwa roho mtakatifu ameshuka kanisani pale, waumini nao walizidi kuomba na kutaja jina la Mungu baba wa majeshi na Yesu kristo wa Nazareth,.
Maombi hayo hususani walikua wakimuombea Maria ambaye sasa alipotea siku ya sita sasa, mchungaji aliamini

kabisa kuwa kuna nguvu za giza nyuma yake,
“baba wa majeshi navunja vunja nguvu zote , nabomoa nguvu zote na kutangaza nguvu za moto uweze kuwachoma jini MEDUSA aliye juu ana zuia maombi yafike naamuru malaika wako , malaika Gabriel, aweze kupambana., baba wa majeshi , baba wa mbinguni, naangamiza kila hila ya nguvu za giza navunja kila kitu, shetani hana mamlaka, natuma moto kuzimu”!
Alizidi kuomba Mchungaji Nathaniel kwa sauti, kweli kuzimu sauti ile ilisikika na kufika na kufanya moto uwachome .
Katika hali ya kushangaza walihisi upepo mkali sana una vuma kanisani mule na pale pale mbele ya madhabau kutokea watu wanne na kuwa fanya waumini walio mbele watoe mbio na wengine hata kudondoka na kuparamia viti kwa juu, wakita futa mlango wa kutokea kili kua ni kitendo cha miujiza!
, bibi mmoja aliye kua na mvi nyingi huku mikononi akiwa na irizi nyingine pembeni yake alikua amekaa Maria, na wazee wengine wawili walioonekana kuwa na wasi wasi mwingi sana,wakiyatoa macho yao kwa hofu,
licha ya kutokea kwa watu wale mchungaji Nathaniel alizidi kushusha maombi na kufanya wachawi wale kuanza kuji badilisha badilisha sura za wanyama wa ajabu kisha kutulia.
“asante Yesu , asante Yesu!”
Alisema Mchungaji Nathaniel akimwangalia Maria kwa huruma sana.
“Bwana yesu asifiweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!,”
Alipayuka Mchungaji huku akitembea kwa madaha mbele ya madhabau .
“Ameeeeeeeeeeeeen”
“ameeeeeeeeeeeen”
Waumini waliitikia na waliokua nje kuanza kuingia ndani wakistaajabu na kutaka kujua nini kiliendelea mpaka watu wale wakatokea pale.



Swala la Pamela kuolewa na PHD Grayson lilizidi sasa kutiliwa mkazo sana na wazazi wake wote, wakimsihi Pamela aweze kuolewa na mwana ume huyo ambaye wao waliamini kua ange mtunza binti

yao kwa sababu ya pesa nyingi alizo kua nazo , hakukua na haja ya Pamela kukataa sababu aliamini kuwa Donald Alisha kufa tayari na uwezekano wa kurudi duniani ulikua mdogo sana.
Habari za kukubali kuolewa na Grayson zilijenga sura ya furaha sana nyusoni mwao akiwemo Erick ambaye alirudi kutoka uingereza siku chache zilizopita, mawasiliano sasa yalianza kufanywa simu zikiruka nje ya nchi mpaka kwa

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG