MCHACHUKO SEHEMU YA 6/10
MCHACHUKO
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 6 KATI YA 10
*******
*******
Alivyohakikisha kila kitu kimeenda sawa alitoka nje kimnya kimnya mpaka kwa shangazi yake,
lakini hakutaka kumwambia lolote, hakuelewa ni mtu gani amwamini kwa wakati huo, kwani polisi wote walikula rushwa na kukingiwa kifua na Mfanyabiashara huyu wa kichaga Manase Shayo.
Siku hiyo hiyo jioni alijiandaa mpaka magereza ya Jakaranda lakini hakuruhusiwa kuonana na Adrian.
“kwanini nisionane nae leo?”
“haiwezekani muda umeshakwenda labda uje kesho”
“nina shida nae tafadhali”
“kwanza ujue binti huwa tuna kufanyia tu upendeleo”
“Naelewa lakini nakuomba tafadhali”
“Ngoja nikwambie ukweli kesho ana hamishwa gereza, anapelekwa Mwanza kwaio nakupa dakika mbili tu za kuongea naye”
“sawa Ahsante afande”
Adrian aliletwa.
Bila kupoteza wakati Jaqlin alitoa simu yake kisha wote kuanza kusikiliza kilichoongelewa.
“Jaqlin”
“Abee”
“hata kama una ushahidi huo unadhani nani atanitoa humu?”
“sheria itakutoa mpenzi wangu, sheria itafuata mkondo wake,sheria ni kama msumeno Darling”
“Hutoweza peke yako”
“Adrian mpenzi wangu, mimi nitaweza nitahakikisha utakuwa huru huu ni ushahidi tosha, isitoshe hii itafanya Yule mwanajeshi aamini kuwa wamekusingizia”
“achana nae”
“naomba namba zake”
“alafu hujanipa habari za Mama vipi mzima?”
“Ndio Mama mzima ndiyo kesho nataka nikampokee uwanja wa ndege hali yake ni nzuri Ahsante mpenzi wangu”
“sawa lakini kesho sidhani kama utaniona tena tuna hamishiwa gereza la mwanza”
Jaqlin alianza kulengwa na machozi lakini sio sana, sababu ushahidi wa kumuweka Adrian huru ulikua wazi wazi.
***
Huo ndio ulikua mwanzo wa Jaqlin kumtafuta Brigedia Saidi Sangu kupitia simu ya mkononi, lakini kila alipompigia simu hakuweza kumpata, mwezi sasa ulisha pita lakini hakuonesha hali ya kupoteza matumaini ya aina yoyote ile.
Hapo ndipo mawazo ya kwenda Dar es salaam yalipomjia, Ni kweli kesho yake asubuhi na mapema aliamka kimnya kimnya na kupanda gari za DAR EXPRESS mpaka Dar es salaam,
licha ya kuchoka na uchovu wa safari baada ya kufika,
Lakini hakupumzika siku hiyo hiyo jioni alitafuta taxi mpaka makao makuu ya JWTZ ili kuonana na Brigedia Sangu amwambie ukweli,
“naomba nionane na Brigedia”
“una shida naye gani?”
Aliuliza mwanajeshi aliyekua getini.
“nina shida naye binafsi nakuomba tafadhali”
“hapana sasa hivi yupo bize”
Jaqlin Hakutaka kubanduka getini kwenye kambi ya jeshi mpaka alipomuona Brigedia sangu anatoka nje usiku, lakini alipomwambia shida yake Brigedia SANGU alimpita akidai kuwa yupo Bize anawahi kikao.
“Ni kuhusu Adrian, nina ushaidi tosha hana hatia tafadhali nakuomba, anateseka sana,sina msaada mwingine”
Aliropoka Jaqlin huku akipaza sauti na kumfanya Brigedia Sangu asitishe zoezi la kupanda Hammer ya Jeshi iliyokua inamsubiri.
Alimwangalia Jaqlin kwa dakika kadhaa.
“Embu ingia ndani ya gari”
Hapo ndipo Jaqlin alipoanza kumuhadithia kisha kutoa simu yake ili wote waweze kusikiliza Mazungumzo ya Manase Shayo.
Brigedia sangu aliyabana meno yake kwa hasira kisha kuchukua mkonga wa simu na kupiga moja kwa moja Mkoani Kilimanjaro jeshi la polisi.
“Naomba niunganishwe na IGP mara moja”
Baada ya dakika tatu IGP Mack Urio alikua hewani.
“unaongea na Brigedia Sangu,naomba nikate rufaa ya kesi ya Adrian Mwangenya leo hii hii nakuja Moshi,na mtuhumiwa wangu wa kwanza anaitwa Manase sijui nani shayu, sijui shivo naomba mumtie ndani”
“Hatuwezi kufanya ivyo bila utaratibu wa protocol mkuu kuna utaratibu, na hauwezi kutuingilia kwenye kazi zetu”
“nafikiri haujui unaongea na nani, sawa ninakuja huko,mwambie kabisa huyo shayo atakiona cha mtema kuni pamoja na RPC Kimario hiyo Moshi ataiona chungu..”
Ni kweli Brigedia sangu alikua mwenye hasira sana alijiona ni mkosaji kwa kumpiga Adrian makofi bila hatia akidhani ni jambazi.
Usiku huo huo alianza kufanya mawasiliano na wanajeshi waliokua mkoani Kilimanjaro mara moja.
Baada ya hapo aliomba helkopta.
“Bunga, nataka helkopta sasa hivi tunaenda Moshi,”
“sasa hivi mkuu?”
“ndio sasa hivi”
Kila kitu kili kamilika ndani ya dakika thelathini.
Brigedia Sangu na Jaqlin walikua wapo ndani ya Helkopta usiku huo kwa safari moja tu kuelekea Mkoani Kilimanjaro ili wakakate rufaa waanzishe kesi upya.
Brigedia sangu alitamani afike haraka hakuelewa ni kitu gani amfanye Manase Shayo pindi atakapo mtia mikononi mwake.
Ndani ya dakika sabini Helkopta ilitua juu ya uwanja mkubwa wa mpira wa majengo, hapo zilikuja gari kumi za Jeshi kumchukua mkuu wao.
***
Tetesi zilishafika teyari Mkoani Kilimanjaro,Wanajeshi walimwaga kila pembe, Manase alivyosikia habari hizo alitamani ardhi ipasuke ili atumbukie ndani sababu tu ya Brigedia Sangu kutoa vitisho vya hali ya juu,
tumbo la kuharisha lilimbana alitamani kila wakati aende chooni kutoa haja kubwa lakini kila akienda chooni hakuweza kutoa haja hiyo.
Brigedia Sangu alikata rufaa na kuanza kufungua faili la kesi ya Adrian upya akiisimamia yeye mwenyewe, maaskari waliokula Njama walianza kubabaika Brigedia Sangu alishalijua hilo lakini alitaka kufanya mambo taratibu ili wote awachukue na kuwapeleka kwanza kambini akawafunze adabu,
Kwa wote waliokuwa na tabia kama hizo,
alijua hakuna mtu yoyote atakaye muuliza juu ya yeye kuchukua hatua hiyo.
“mbona simuoni mtuhumiwa wangu mpaka leo,?”
Aliuliza Brigedia sangu.
“bado bado bado ndiyo tunafanya utaratibu wa kumtafuta”
Koplo Rema alibabaika alivyoulizwa swali.
“okay, Mkuu wenu yupo wapi?”
“hayupo”
Brigedia Sangu alimtizama Polisi aliyekua zamu siku hiyo kisha kuupiga mlango teke wa ofisi ya mkuu wa kituo RPC,na kumkuta yupo ndani na kubaki akimtizama kwa hasira asijue ni kitu amfanye Mkuu huyu wa polisi ambaye teyari suruali yake imeanza kulowana na mikojo kutokana na hofu aliyokuwa nayo!.
Suruali ya Rpc Kimario ilikuwa teyari tepetepe imelowana na mikojo kutokana na uwoga aliokuwa nao,ni kitendo cha kumuona Brigedia Generali Saidi Adam Sangu Mbele yake,alishaelewa maana ya ujio wa mtu huyo ofisini kwake aliyechafuka nyota nyingi mabegani.
“Mwenzako yuko wapi?”
“Abee.. Naam Mkuu”
“Mwenzako Shayo yuko wapi?”
Aliuliza Brigedia Sangu akiwa mwenye hasira za waziwazi na kumsogelea Rpc Kimario, kabla ya kuongea kitu kingine chochote alimtandika kofi aina ya kelbu shavuni, alichukua kichwa chake na kukibamiza mezani,
teyari alikua sio sangu tena zilikua ni hasira ziki mpeleka puta, macho yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu kama aliyekua amevuta cha Arusha,
“unamuweka Ndugu yangu gerezani kisa pesa, sasa leo nakufunza adabu, Umefanya Mpaka mama yake mzazi amefariki kisa wewe na mwenzako inuka sasa hivi”
Sangu aliendelea kutoa kipondo kikali sana hasa alipokumbuka msiba Wa Mama Adrian aliyefariki kwa presha baada ya kusikia mwanae Adrian yupo Gerezani amefungwa miaka Kumi.
Polisi wengine walishafika teyari na kuufungua mlango wa bosi wao baada va kusikia kelele nyingi, licha ya kutokeza kwa wingi haikumfanya Sangu asitishe zoezi la kuendeleza kipigo alichokuwa amekianza!.
“Inuka tuongozane fanya upesi, na nyie sikilizeni mimi naondoka naye huyu nendeni popote mkashtaki”
Alisema Brigedia Sangu huku akiwa amemkunja Rpc Kimario juu ya shati lake mpaka ndani ya gari la jeshi.
**
Mateso yalizidi kuwa makali kambini baada ya kufika, alipelekwa mpaka ndani ya chumba kidogo baada ya kumaliza adhabu ya kubeba Dunia, alilia kama mtoto mdogo wa miaka mitatu,
Walimuingiza ndani ya chumba kidogo kingine na kumwagiwa maji ya baridi kisha kuvuliwa nguo zake zote,
Mikanda ya jeshi ilipita mwilini mwake na kufanya alama zimtoke, kelele alizokuwa akipiga hazikuweza kumuweka huru hata kidogo,
Wanajeshi waliobobea kutoa mateso makali waliitwa na kuanza kumsulubu vya kutosha, mpaka inafika usiku wa saa mbili, RPC Kimario alikuwa yupo hoi bin taaban! machozi yamemkauka hana nguvu mwilini mwake. Asubuhi kulivyokucha alifunguliwa kisha kukalishwa juu ya kiti na Brigerdia Sangu.
“Manase Shayo hayupo nyumbani kwake,yupo wapi?”
“Si..ijui Kwa Kweli Mkubw….a naomba mnisamehe ndugu za..ngu sisi sote ni Watanzania hi..i nchi yetu ya Am…ani”
“sitaki kusikia hizo stori nataka kujua ni wapi Manase alipo”
“kus…sema ukweli sijui”
“Haiwezekani,naongeza tena wiki nzima,ushawahi kulamba mchanga wa choo?”
“Tafa..dhali usifanye ivyo”
Hapo hapo Brigedia Sangu alimuinua kisha kumtoa nje mpaka ndani ya choo,ambacho kilichokua kichafu kina vinyesi na mikojo.
“Deki humu kwa ulimi”
“Mana..se aliniambia Leo leo anaenda Nairobi na Kampala Coach”
“una uhakika?”
“ndio”
“sasa mbona ulikuwa unaleta ubishi,deki choo hiki kwa dakika mbili kiwe kisafi”
Bila kupoteza muda Brigedia Sangu alianza kufanya mawasiliano na jeshi lililokuwa mpakani Namanga ili wazuie basi kubwa la kampala Coach mpaka atakapo fika yeye kwani yeye yupo njiani,
alitaka mwenyewe amtie Manase Shayo mikononi mwake ili amfunze adabu.
Hammer za jeshi zilikua katika kasi ya ajabu sana huku nyuma zikisindikizwa na magari mengine ya Jeshi, ni kweli Brigedia Sangu aliheshimika kila sehemu, hakuwa mtu wa kuchezea hata kidogo.
Gari zote barabarani zilipisha njia.
“Nawewe unaendeshaje gari, nyoosha mguu huo tumuwahi yule mpumbavu”
“Sawa mkuu”
Gia alipandishwa na gari kuzidi kusonga mbele ilikua ni kasi ya ajabu isiyo ya kawaida,
walitembea barabarani takribani masaa manne na kwa mbali waliweza kuliona Kampala Coach likiwa katika mwendo kasi.
“Washa Azadi, nataka huyo dereva asimamishe gari,”
Baada ya taa kuwashwa basi kubwa la kusafiria la kampuni ya kampala coach lilikaa kando,baada ya kusimama
kila abiria alikua na maswali ya kujiuliza kuhusiana na wanajeshi hao waliozunguka gari hilo kama kumbi kumbi.
Kila abiria alimtambua Brigedia Sangu baada ya kuingia ndani ya basi.
“kama unajua ulipewa jina la Manase na wazazi wako,na unajiita Manase Shayo, safari yako imeishia hapa unaondoka na sisi,okoa muda sababu kuna wenzako wanataka kusafiri wawahi kwenye majukumu ya kujenga taifa”
Alisema Brigedia Sangu.
“Nadhani nimeeleweka vizuri na nimetumia Kiswahili fasaha kilichonyooka”
Manase Shayo alibanwa na haja kubwa tumbo lili mbana alitamani afungue dirisha ili atoke nje,kosa lake alishalijua teyari na kujua teyari amekamatwa.
“sitoshindwa kukagua basi zima hata kama yupo kwenye buti nipo radhi kushusha mizigo yote sitojali”
Kitumbua kimeshaingia mchanga, taratibu Manase Shayo alisimama huku akitia huruma sana akitamani kulia.
“Bwana mdogo una mizigo?”
Aliuliza Brigedia Sangu baada ya kumuona Manase Shayo.
“Haa..pana hapana sina nilisahau nyumbani”
“sawa, twende ukaifuate kisha uendelee na safari, Abiria samahani kwa usumbufu nawatakieni safari njema!”
Manase kabla ya yote alikalishwa chini kwenye majani akiwa amezungukwa na wanajeshi wenye hasira kali.
“kabla hatujafika kambini,jichagulie adhabu mwenyewe”
“Nisamehe sa…”
Kabla ya kumalizia sentensi alipigwa kifuti cha mdomo.
“sio jibu hilo,chagua moja utembee kwa Mguu taratibu au ukimbie mpaka Majengo?”
Kati ya hayo mawili hakuna hata moja lililokuwa na afadhali kwake,
hakuelewa achague adhabu ipi kutokea alipo kulikua kuna kilometa Sabini ulikuwa ni mwendo mrefu sana.
Walimpakia ndani ya gari ya jeshi mpaka kambini, alivyomuona RPC Kimario alivyochakaa alichoka sana,
Alishaelewa sasa ni zamu yake.
Walimchukua na kumpaka nywele zake maji ya sabuni kisha kunyolewa kipara ngoto,
Alichukuliwa na kuwekwa katikati ya uwanja wa mpira mchana wa saa saba jua kali tena la utosi.
Jasho lilimtoka juu ya upala, alijuta sana alitamani Adrian atokee ili amuombe msamaha ikiwezekana apige hata magoti.
Wiki nzima RPC Kimario pamoja na Manase walikuwa wakipokea mateso sana,walichakazwa na wanajeshi.
Kisha kuambiwa waende kujitangaza kwenye vyombo vya habari wakimsafisha Adrian Mwangenya ambaye alidhaniwa ni jambazi sugu na kufungwa kifungo cha miaka kumi Gerezani.
Ni kweli siku hiyo jioni walipelekwa kwenye mastesheni ya redio na kuongea ukweli, kila mtu alikasirishwa na kubaki midomo wazi.
Kesi hiyo ilipelekwa mahakamani upya na Adrian kuachiwa huru na kupewa fidia, kiasi cha shilingi milioni thelathini kwa ajili ya kusingiziwa kesi ya ujambazi na jina kuchafuliwa na kupotezewa muda wake pia,
Rpc Kimario na Manase Shayo pamoja na maaskari wengine walioshiriki wote walitupwa gerezani.
Jaqlin alilia machozi ya Furaha siku hiyo baada ya kumuona Adrian yupo Huru,
alimrukia kwa nguvu zake zote kama mtoto mdogo aliyemuona Mama yake huku akimpiga mabusu mengi mfululizo.
“Adrian mpenzi wangu naona kama naota Mungu ni mkubwa sana leo siamini kama umetoka”
“Naomba uamini mpenzi wangu,ndiye Mimi nimetoka”
Baada ya kuachiana alimfuata Brigedia Sangu na kumkumbatia na kumshukuru sana kwa yote aliyomfanyia.
“Ahsante Sangu, nakushukuru sana”
“Huna haja ya kunishukuru ni moja ya kazi yangu kukulinda mdogo wangu ila nisamehe kwa yale niliyokufanyia hapo awali”
“usijali Saidi nipo sawa”
Marafiki na baadhi ya ndugu walikua wapo mahakamani hapo wakiwa wenye furaha Partson Ngogo pia alikuwepo siku hiyo,
“Chif, pole sana ndiyo mitihani ya Dunia”
“Nishapoa sasa”
Waliingia kwenye magari akiwa na Jaqlin pembeni yake viti vya nyuma wakipigana mabusu ya midomoni.
Adrian alitamani afike mapema au apate chumba ili waliridhishane ilionekana wote walikuwa na hamu sana.
Partson Ngogo aliyekua anaendesha gari alishalijua hilo alisimamisha gari kwenye hotel moja wapo kisha kuwaomba washuke.
“Haha Partson hujatulia wewe”
Alisema Adrian huku akiwa amekishika kiuno cha Jaqlin na wote kuingia hotelini na kutafuta chumba.
Kitendo cha kufunga tu mlango walianza kupigana mabusu yasiyokuwa na idadi kamili.
Walivuana nguo zao kwa kasi sana, Adrian alimbeba Jaqlin juu juu na kumuweka ukutani huku wakibadilishana ndimi kwa fujo zote kama watu ambao hawakuwahi kufanya tendo hilo kabla,
ndani ya dakika mbili baadaye kila mtu alikuwa uchi wa mnyama wakisherekea tunda na kufanya mchezo huo wa kikubwa.
Baada ya kumaliza waliingia bafuni kuoga, mmoja kati ya hawa wawili alikuwa mchokozi si mwingine bali ni Jaqlin sababu alianza kumkwaruza Adrian mgongoni akitumia kucha zake taratibu sana, na kufanya KAROTI ya Adrian ianze kupata moto taratibu na kisha baadaye mnara kupanda ukiwa tayari umenasa mawimbi,
alimchukua Jaqlin na kumuweka ukutani kisha kuanza kubadilishana mate huku bomba la mvua likiwamwagikia.
Hakika ilikua ni siku ya furaha sana kwao, mambo yalienda adoado kama gari la mikaa lipandavyo mlima.
Jaqlin alianza kulichua tango la Adrian taratibu kisha kupiga magoti na kulibugia lote mdomoni na kufanya kama analamba koni yenye ice crim juu yake.
Adrian alikuwa hajiwezi tena yupo hoi bin taaban damu inamwenda mbio mapigo yake ya moyo yanadunda mara mia tano kwa sekunde moja.
Ilibidi hata Adrian nayeye alipize, alimuinua Jaqlin na kumsimamisha kisha kuipanua miguu yake kwa chini nayeye kutoa ulimi wake na kuanza kulamba MGODI taratibu sana huku akitumia kidole chake cha katikati taratibu akitafuta madini ndani ya Mgodi,
isingekuwa ukuta basi Jaqlin angeshapiga mueleka na kudondoka chini mzima mzima kwa maana nguvu zake za miguu zilimuishia zote, na kubaki akihema kama Bata mzinga,
alikua akishika mabomba huku akijipinda pinda, Adrian alishalijua hilo na kuzidi kuongeza kasi ya kunyonya mgodi ambao teyari kwa mbali ulianza kutoa madini,
dakika tano zilikua nyingi wote walikua mzigoni wanavunja amri ya sita ndani bafuni.
Juu juu walibebana huku ndimi zao zikiwa zinacheza ndani ya midomo mpaka kitandani puuh ili kuendeleza mashambulizi.
*****
Adrian Mwangenya yupo huru kutoka gerezani, kesi aliyosingiziwa kuwa alivamia na kuwapiga risasi wazazi wa Jaqlin imebainika kuwa alisingiziwa,furaha aliyokuwa nayo ameamua kuimalizia kitandani na mwanamke anayempenda sana kuliko kitu chochote kile.
Ni kweli alipitia mengi sana,na mwanamke huyo ambaye amekiri na kuapia ni lazima wafunge ndoa wajenge familia wawe baba na Mama hapo baadaye!,
tayari sasa wapo uchi wa mnyama wanashikana shikana kila maeneo ya miili yao,
Jaqlin aliyafumba macho yake na kuanza kuhema juu juu ni baada ya Adrian kuanza kudeki bahari huku mkono wake mmoja ukiwa juu ya chuchu ya Jaqlin kwenye maziwa.
Alihisi wenda ana mabawa na ana paa angani,taratibu alianza kukinyonga kiuno chake baada ya kuanza kusikia raha za ajabu sana, walipinduana huku na huku kitandani wakibadili kila aina ya mikao ili mradi raha mustarehe!
Kila mtu alikuwa mbali kihisia kabisa walimiminiana mvua za mabusu kila sehemu ya miili yao, kila mtu alitaka kuwa fundi wa mwenzake siku hiyo,majasho kwa mbali yalianza kuwatoka,
Adrian aliipanua miguu ya Jaqlin na kuingia katikati yake na kuingiza MASHINE yake na hapo mambo kuanza ya kuvunja amri ya sita,
baada ya mkao wa Mbuzi kagoma kumalizika basi walitumia kifo cha mende,
Mguu mmoja wa Jaqlin ulikuwa juu ya bega la Adrian na kuzidi kupeleka majeshi majeshi ndani ya ikulu, Kwenye swala la kuzungusha kiuno basi Adrian alikuwa vizuri, kama ungebahatika kumuona hapo usingeweza kudhani kuwa ndiye yeye anayekatika kiuno, alizungusha kiuno ki ustadi huku MASHINE yake akiipitisha kila pembe ya mgodi kama aliyekuwa akipiga mswaki mdomoni.
“Na….kupenda Adria..n, naomba usije kunichezea na kuniacha”
Maneno hayo yalimtoka Jaqlin katikati ya MChezo tena kwa sauti ya puani bila kujijua.
Tendo lilidumu kwa takribani nusu saa zima kisha wote kulala baada ya kuwa hoi wamechoka, Jaqlin alilala juu ya kifua cha Adrian na wote kuchukuliwa na usingizi mzito.
***
Usiku wa siku hiyo hiyo walinyoosha mpaka Mkoani Arusha kwa wazazi wa Jaqlin ili kwenda kuwapa pole na kuwajulia hali zao ki ujumla, hakuamini walivyomkaribisha kwa furaha Adrian ilikuwa ni kinyume na alivyodhani.
“Karibu Baba”
Alisema Mama mzazi wa Jaqlin huku akimpa mkono Adrian kisha Mzee Mshana kufuatia.
“Ahsante sana”
“pole na matatizo”
“Nishapoa nashukuru Mungu”
“Baba na Mama”
Aliita Jaqlin kisha kuwatizama wazazi wake.
“Huyu ndiye Adrian niliyekuwa naawambia habari zake,naomba mmuruhusu awe mkwe wenu, ndiye chaguo langu”
Jaqlin aliongea kwa utulivu wa hali ya juu, Maana Alishawahi kuwaeleza Wazazi wake juu ya Adrian siku chache zilizopita nyuma, hapo alikuwa anawasisitizia tu.
Ndani ya moyo wake alimpenda sana Adrian hata kama ingetokea wazazi wake wangemkatalia siku hiyo asingewajali, angeusikiliza moyo wake sababu alishakua mwanamke mtu mzima mwenye uwezo wa kuchagua mwanaume anayempenda yeye na wala sio kitu kingine pia aliamini hata angechukua maamuzi hayo asingeyajutia katika maisha yake mpaka anaingia kaburini! Kwani aliamini Adrian ndiye mwanaume wake wa kufa na kuzikana.
“sisi tumekuelewa, basi tuachie Mimi na Baba yako tulizungumzie hilo swala”
“sawa Mama,ila kabla hamjalizungumza naomba muziheshimu hisia zangu”
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Jaqlin kuwasumbua wazazi wake kila kukicha.
Ni kweli kwa wema aliowafanyia Adrian hawakupaswa kuwa na kipingamizi chochote kile,siku hiyo asubuhi ya jumatano wote walikaa kikao na kukubali Adrian aweze kuwa na binti yao,
siku hiyo walifanya sherehe kubwa na kilichokuwa kina subiriwa ni ndoa kubwa sana ambayo Adrian aliipania mno.
Hakuweza kuwa tayari kulifanya swala hilo peke yake ilibidi amtafute Mama yake kipenzi kwenye simu lakini hakua hewani,
alijaribu tena lakini hali ilikua ivyo ivyo.
Alimpenda sana Mama yake alitaka huyo ndiye awe mtu wa kwanza kujua kuhusu ndoa yake atakayo funga na Jaqlin miezi michache ijayo.
“Mama alikua akitaka mka mwana, sasa mbona nayeye amezima simu tena!”
Aliwaza Adrian akiwa bado anabonyeza bonyeza simu yake ya mkononi akimtafuta Mama yake Mzazi hewani, alimtafuta mfululizo bila mafanikio,
Alikumbuka mara ya Mwisho alimuacha Dar es salaam baada ya kifo cha Mama Sikuzani kutokea.
Hapo hapo aliitafuta Namba ya Baba yake mzazi kisha kuipiga.
“Mzee Shikamoo”
Alisalimia Adrian.
“Marahaba Mwanangu”
“Vipi Mzee Unaumwa?”
“Upo wapi Adrian?”
“Nipo Arusha huku Baba nina habari nzuri sana nina imani utazifurahia”
“Niambie Adrian”
Mzee Mwangenya alizungumza kwa sauti ya upole na Simanzi, bado alimkumbuka sana MKe wake aliyefariki Dunia siku chache zilizopita hakika hakuweza kusahau kirahisi kiasi hiko bado alikuwa na kidonda moyoni.
Adrian alishagundua hilo na kuuliza.
“Baba unaumwa?”
“Hapana,njoo nyumbani Mbeya”
“kuna nini, kwanza naomba kuongea na Mama ya…”
Kabla ya kumalizia sentensi simu ilikatwa,Moyo wa Adrian ulimwenda mbio alihisi Baridi linampuliza, alijua kuna tatizo kubwa sana limetokea, machale yalimcheza kichwani kwake,
Fikra zake zilimtuma haraka haraka kwa Mama yake kuwa atakua ana tatizo kubwa sana,kengele iligonga kichwani kwake, tena ya msiba lakini swala la kifo cha Mama yake hakutaka kulipa kipaumbele kabisa,
aliamini Mama yake yupo hai lakini labda anaumwa tu,
Alimpenda sana Mama yake alikuwa ndiye Mungu wake wa Pili, hapo hapo aliinua tena simu na kumtafuta Mama Magesa jirani yake hapo Tegeta.
“Adrian pole sana , umeshatoka Gerezani?, yote ni mitihani ya Mungu lakini Pole sana kwa msiba jikaze Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu, tulimpenda sana Mama yetu na…..”
HAPO hapo Adrian aliikata simu, alishaelewa kila kitu aliserereka na ukuta mpaka chini na kuanza kulia machozi ya kwikwi, alilia kama mtoto alibubujikwa na machozi mengi,
alimkumbuka sana Mama yake , wakati mwingine alijua wenda yupo kwenye njozi ndefu tena ya kutisha na muda mfupi angeenda kuzinduka lakini haikuwa ivyo, yaliyokuwa yanatokea yalikua yana ukweli kabisa, hakuelewa ni kwanini alifichwa na kutopewa habari hizo ili walau aweze kumuona MAMA yake mzazi mara ya mwisho wakati wa Kumuaga!
alichukua simu yake na kumtafuta Jaqlin mpenzi wake hewani.
“Hata hata wewe…?”
Aliuliza Adrian kwa uchungu.
“Darling nini tatizo?”
“Hujui, unajifan…nya haujui?”
“Adrian sikuelewi mpenzi wangu, mbona unalia una tatizo gani HONEY?”
“Mnafiki sana usiniite Mpenzi wala honey.. maana mimi sio mpenzi wako”
“Adrian una nini lakini, ngoja nije”
Jaqlin nayeye alichanganyikiwa sana, hakuelewa ni kitu gani kimemkumba mpenzi wake mpaka azungumze maneno kama hayo tena akiwa analia machozi kama mtoto mdogo,
tangu aanze mahusiano na mwanaume huyo hakuwahi kumsikia akiwa katika hali kama hiyo, alijua kabisa kuna jambo kubwa sana limetokea, hapo hapo alivaa kitenge haraka haraka na kupanda piki piki mpaka hotel aliyokuwa amepanga Adrian kisha kuingia chumbani,
Hakuamini alivyomuona Adrian analia kwa kwikwi amekaa chini juu ya sakafu.
“Honey!”
Aliita Jaqlin huku akipiga hatua za taratibu.
“usiniite ivyo Jaque, ondoka nitakuitia mwizi, toka chumbani kwangu”
“kuna nini Adrian Mpenzi wangu?”
“Nakwambia ondoka, hata wewe umeshindwa kuniambia, kila siku unakuja gerezani umeshindwa kunieleza ukweli, ulidhani sitojua ukweli?”
“Mbona sikuelewi inuka Baba ukae kitandani”
Haikuwa kazi rahisi kumtuliza Adrian aliyekua mwenye machungu, Jaqlin hakuelewa ni kitu gani kili mliza Mpenzi wake, hata yeye alijikuta akitokwa na machozi.
Alimuinua Adrian kisha wote kukaa kitako kitandani.
“Naomba unieleze unazungumzia nini”
“Jaqlin Mama yangu amefariki, Mama amefariki Dunia Jaquee”
Jaqlin aliganda na kubaki mdomo wazi hayaamini maneno yaliyokuwa yanamtoka Adrian, Moyo ulimwenda kasi sana.
HAKUNA hata mmoja aliyeweza kumnyamazisha mwenzake wote walijikuta wakipokezana kulia, mpaka usiku unafika hakuna aliyenyamaza.
Kesho yake asubuhi sana walitafuta Ndege na kupaa mpaka Dar es salaam uwanja wa Mwalimu Nyerere,Safari nzima hakuna hata mmoja aliyemuongelesha mwenzake mpaka walipofika kisha kutafuta Taxi iliyowapeleka Mpaka Tegeta nyumbani kwa Adrian!
Alipoiona nyumba yake tu alidondoka chini na kulia machozi tena, moyo ulimuuma sana.
Hasa alipokumbuka kuwa Mama yake mara ya mwisho alimuacha ndani ya Nyumba yake pamoja na Baba yake kisha yeye kusafiri kuelekea Mkoani Kilimanjaro Moshi kwa Jaqlin.
Alilala chini kifudifudi na kuanza kuipiga piga ardhi,Alimini kuwa hakuna mwanamke yoyote Yule atakayeweza kuja kuziba pengo la Mwanamke huyo ambaye ni mama yake.
“Mama!, nitamuit…a nani tena hilo jina….”
Alisema Adrian huku akiwa analia bado yupo chini anapiga piga kifua chake kwa machungu.
“Mbo..na ma..pema ivyo umenia..cha Mama yangu, Hata Bado huja..muona mka mwana Wako uliye kuwa unamuhitaji siku zo…te kweli Ma…..ma…”
Alilia Adrian huku bado akiwa chini, alimgeukia Jaqlin na kumtizama,mambo mbali mbali yalimiminika ndani ya ubongo wake kama mkanda wa video tena wa kusisimua,na kukumbuka vitu vingi vilivyokuwa vinamtokea kwa ghafla yakiambatana, kupigwa akisingiziwa ni mwizi,kuvamiwa na kuporwa pesa,kufungwa gerezani mpaka Mama yake kupoteza uhai.
Ni hayo tu ndiyo yalimfanya afikirie kuwa wenda mwanamke Jaqlin ndiye amemletea mkosi huo sababu tangu waanze uhusiano hakuwahi kuishi raha mustarehe kama hapo kipindi cha nyuma.
Licha ya kuyafikiria hayo aliyatupilia mbali mawazo hayo sababu alimpenda sana mwanamke huyo na hakuwa na sababu ya kuanza kumfikiria vibaya, aliamini kuwa hiyo ni mitihani ya Maisha.
Alisimama Wima na kuingia ndani bila kusema chochote huku Jaqlin akimfuata nyuma yake mpaka chumbani.
“Unataka kufanya nini Mpenzi wangu?”
Aliuliza Jaqlin.
“Nataka niende Mbeya kuhakikisha kama ni kweli Mama yangu amefariki”
“Tafadhali! Pumzika kwanza kesho tutaenda”
“Hapana siwezi nitapumzika vipi?”
Haikuwa kazi rahisi kuyabadili maamuzi ya Adrian, alisimamia msimamo wake wa kwenda kijijini Mwakaleli, dalili zilionesha wazi kuwa yupo tayari kwa safari sababu alitoa kadi ya benki na kuanza kushusha ngazi.
“Siwezi kubaki peke yangu lazima twende wote” Jaqlin alisema.
Wote walishusha ngazi haraka haraka na kutafuta piki piki mpaka benk ya BOA iliyokuwa Afrikana, kisha kutoa kiasi cha pesa, hapo hapo walitafuta taxi mpaka uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ili kuchukua Ndege itakayowapeleka Mpaka Mbeya usiku huo na kuwafikisha uwanja wa kimataifa wa Songwe kisha hapo wanyooshe mpaka mwakaleli.
Ni kweli dakika thelathini baadaye! Walikuwa wapo Mwalimu Nyerere kisha kukata tiketi ya siku hiyo hiyo, bahati nzuri zilibaki siti mbili tu,
ilikua kama bahati kwao.
**
Dakika Sitini zilikuwa nyingi kufika Mkoani Mbeya wakitumia usafiri wa anga,Walitua Uwanja wa ndege wa Songwe kisha kushuka, hakuna hata mmoja wapo aliyekuwa na mizigo, walienda kama walivyo bila mabegi wala zawadi kama abiria wengine wa kawaida wasafilivyo.
Njia nzima Jaqlin alikuwa ana kazi ya kumliwaza Adrian mpaka wanawasili na kutoka nje ili kutafuta taxi na ilishagonga saa saba ya usiku.
“Darling kwanini tusitafute Hotel ili tulale kisha asubuhi ndio twende huko, huoni kama haitakuwa jambo la busara kuingia usiku usiku namna hii”
Alishauri Jaquee.
Lakini Adrian alimtizama bila kujibu kitu chochote kumaanisha kuwa mawazo ya Jaqlin aliyapuuza, alichotaka yeye ni kufika Mwakaleli hata ingekuwa saa nane ya usiku.
“Tupeleke Mwakaleli kwanza, maelezo mengine nitakupa huko huko”
Alisema Adrian akimpa maelekezo dereva taxi,
Dereva taxi aliondoa gari,Masaa Matatu Baadaye walikuwa Mwakaleli, hapo Adrian alikua ana kazi ya kumuelekeza Dereva huyo mpaka walipofika karibu na nyumbani kwa wazazi wake, lakini ghafla sura ya Adrian ilianza kubadilika taratibu, alihisi mwili wake wa baridi mno, moyo wake ulidunda kwa kasi, alitetemeka kama mtu mwenye homa kali ya usiku, ni baada ya kuona Turubai nyumbani kwao kisha watu kujaa nje ya nyumba ya wazazi wake,
Kama mtu mzima alishaelewa nini maana ya turubai hilo nyumbani kwa wazazi wake, kama Mama yake teyari alishafariki basi ni lazima kuna habari mbaya ambayo ingemshtua tena,
Tarataibu alishuka ndani ya gari hata kusahau kumlipa dereva taxi, watu waliomuona walizidi kuangua vilio walizidi kumuonea sana huruma,
kompyuta ndani ya akili yake ilizidi kuperuzi vitu tofauti vingi,bado alishindwa kuelewa ni nani amefariki tena
Kidogo alipata nafuu japo sio sana baada ya kumuona Baba yake Mzazi Mzee Mwangenya ametoka nje na kumfuata alipo, walipeana mikono na kusalimiana.
“Baba yako mdogo amefariki Adrian, aligongwa na gari”
Alisema Mzee Mwangenya kwa masikitiko sana.
Siku hiyo usiku waliomboleza na kuimba nyimbo za maziko, kisha kesho yake mchana saa tisa ya alasiri walizika,
Adrian bado alikua akimkumbuka Mama yake, alihisi tena maumivu mengine baada ya kuliona kaburi la Mama yake mzazi mashambani, tena limefukiwa tu kwa udongo.
Kwa hadhi aliyokuwa nayo na jinsi alivyomthamini Mama yake hakustaili kuhifadhiwa kama alivyokuwa hata kama alishafariki.
Alisubiri siku nne zipite kisha kuwaita watu maalumu wa kusakafia kaburi la Mama yake.
Ambapo juu yake waliweka malumalu za gharama kisha msalaba kunyooshwa juu,hapo ndipo aliporidhika kabisa,Kila asubuhi huenda kwenye kaburi hilo kuliangalia na kukumbuka mengi sana yaliyopita.
“Adrian Mwanangu” Mzee Mwangenya alimuita mtoto wake.
“Naam Baba”
“Kabla Mama yako hajafariki alikuwa anahitaji sana kumuona mka mwana wake,alipania sana kumuona lakini ndiyo ivyo,nachokuomba umpende sana huyu Binti umtunze ni Mama yako wa pili. Umuheshimu nina imani huko alipo Mama yako atafurahi sana”
“Baba nampenda huyu mwanamke,na ndiye nitakaye muoa nafikiri Mungu ndiye aliyenichagulia niwe naye”
“Nafurahi kusikia ivyo”
Mzee Mwangenya aliwapenda sana Adrian na Jaqlin, upendo aliokuwa nao kwa Mke wake wote uliamia kwao,walifurahi sana, Jaqlin muda wote alikuwa ni mwenye amani.
Hali ya kutapika na kuhisi kichefu chefu ndiyo iliyomfanya Mzee Mwangenya azidi kuwa na furaha sana kwani aliamini kuwa muda mfupi tu ataenda kuitwa babu, hakuelewa ukweli uliojificha nyuma ya pazia!
“Mwanangu hongera”
Mzee Mwangenya alimpongeza Adrian siku hiyo wakiwa shambani.
“Hongera ya nini mzee?”
“Mimi sio mtoto, kusoma sijui hata picha sioni”
“MZEE sijakuelewa”
“Si nitaenda kupata Mjukuu hapa kesho kutwa tu”
Adrian alitabasamu japo sio kwa furaha zote,alimtizama Baba yake machoni kisha kuendelea kutembea bila kujibu chochote.
Mzee Mwangenya kuna kitu alikitafsiri usoni mwa mwanae lakini hakutaka kuuuliza chochote.
***
Mpaka Miezi miwili inakatika Adrian bado alikua mkoani Mbeya Mwakaleli, akiishi na Jaqlin kwa maisha yalijojaa amani tele. Wote walikubaliana kuwa Jaqlin ajifungulie huko huko Mbeya sababu endapo wakienda Dar es salaam hakuna atakaye mtunza vizuri.
“Mimi vyovyote sawa tu Adrian wala usijali”
Alisema Jaqlin wakiwa chumbani siku hiyo.
“Wacha mimi kesho nirudi Dar es salaam kisha ijumaa nitarudi nitakuachia pesa kidogo za matumizi na Mzee”
Jaqlin alikubali kubaki ukweni, aliamini huko alikua yupo salama salmin kabisa tena alishamchukulia Mzee Mwangenya kama Baba yake mzazi hakua na tatizo lolote, kilichomsikitisha ni Adrian kuondoka na kumuacha huku nyuma mwenyewe kwa kifupi alimzoea, hata Kwa Adrian ilikuwa ivyo ivyo lakini hakuwa na namna nyingine ya kufanya.
Siku hiyo asubuhi na mapema Adrian alitafuta usafiri mpaka uwanja wa ndege Songwe hapo waliagana na Jaqlin pamoja na Baba yake wabaki salama kwa maana baada ya siku tano atakua amerudi.
“Mwanangu safiri salama”
“Amen Mzee”
Aliingia ndani ya ndege baada ya kuagana na Jaqlin vilevile.
Dakika sitini baadaye alikuwa yupo Mwalimu Nyerere amewasili salama kabisa, alitafuta usafiri kimnya kimnya mpaka nyumbani kwake Tegeta kisha kushuka na kumlipa dereva Taxi, alifurahi kufika nyumbani salama na kumpigia simu Jaqlin ili kumtaarifu.
“Nafurahi Darling umefika salama,Nina amani sasa”
Upande wa pili wa simu uliongea.
“Hata mimi nafurahi kuongea nawewe lakini nimekumisi sana Laazizi”
“Mimi hunishindi Mume wangu”
“Sio kweli”
“Ndio ivyo, kwaio utaenda ofisini leo?”
“Hapana sitoweza alafu hakuna hata mmoja anayejua kuwa nimefika leo”
“sasa kwanini?”
“Nataka nijue utendaji wa kazi unakuwaje, nataka niwashtukize”
Wote walifurahi kuongea kwenye simu na kupigana mpaka mabusu. waliridhika!
Asubuhi kulivyokucha tu Adrian aliamka na kutafuta Taxi, kwa kuwa gari yake AUDI ilikuwa bado mbovu haina vioo baada ya kuvunjwa na majambazi kisha kutokomea na pesa zake,
lilikua limepaki kwenye maegesho.
“Hili gari kesho nitalirekebisha”
Aliwaza kabla ya kutoka nje ya Geti.
Alipanda Taxi iliyompeleka mpaka Posta ofisi yake na kupanda lift, lakini alipofika kwenye lango kubwa la kioo aligundua kuna mabadiliko, jina la kampuni yake limefutwa kisha kubandikwa RADO Enterprises.
Alisimama na kuyasoma maandishi hayo mara mbili mbili, aliusukuma mlango na kuona sura zote ngeni.
“Kaka tukusaidie nini?”
Aliuliza Mwanamke aliyekuwa mapokezi kwenye meza aliyokua akikaa Martha Msoso kipindi cha nyuma, bado alikua haamini alijua wenda alikosea mlango, alitoka nje na kugundua ni kweli yupo katika ofisi yake lakini jina lilibadilishwa.
Alizidi kutafakari mambo yaliyopita.
“KAKA tukusaidie nini?” Aliuliza tena dada wa mapokezi.
Adrian aliwatizama watu wote waliokuwa ndani sura zote zilikua ngeni,wote walimshangaa yeye.
“Nilikuwa naulizia kampuni ya AMRA sijui ndiyo hapa au nimepotea?”
Adrian aliulizia ili kutaka kujua ukweli kuhusu kampuni yake.
“Hapana siyo hapa,kampuni hiyo ilifilisika na walishindwa kulipa kodi, hivi navyokwambia hiyo kampuni inadaiwa million Mia tatu,mwenye hiyo kampuni anatafutwa sana kaka angu”
Moyo wa Adrian ulidunda mara tisini kwa sekunde moja,alihisi joto kali kwenye uti wa mgongo jasho jembamba lilianza kumtoka na kubaki ameganda kama barafu la shilingi ishirini.
“Vipi kaka?”
“Hakuna kitu, huyu aliyenielekeza hapa nadhani atakuwa hajui ili swala,Asante dada”
“Haya karibu tena”
Adrian alichanganyikiwa zaidi tena vibaya mno! pengine kupita kiasi, hakuelewa deni la milioni mia tatu limetokana na nini,
Mtu aliyemjia kwa haraka kichwani kwake alikuwa ni Partson Ngogo jr, na kumtafuta hewani lakini simu yake haikupatikana hewani kwa wakati huo, alijaribu tena lakini mambo yalikuwa yale yale.
Haraka haraka alitafuta usafiri wa bodaboda mpaka nyumbani kwake Tegeta.
Alikuwa ni mwenye mawazo na alivyofika alijitupa juu ya sofa kama gunia la karanga.
Hakutaka kumueleza Jaqlin swala lolote lile aliogopa sana kumtia katika presha kama Mwanaume ilibidi atafute njia mbadala.
***
Siku Moja akiwa sebuleni alisikia kelele za magari huku akisikia kipaza sauti kinaongea, kwa mara ya kwanza alikipuuzia lakini alizidi kusikia kwa karibu na mtu akitangaza kuwa kuna nyumbna inapigwa mnada,
Alifungua pazia na kuona wanaume watano wanaingia ndani ya geti.
Alitoka nje kwa kujiamini.
“Ustaarabu jamani, mnaingiaje kwa watu bila kupiga hodi, nyie ni akina nani?”
Aliuliza Adrian.
“Tumetoka CRDB Bank,hii nyumba ni mali ya Bank iliwekewa bondi na muhusika na ameshindwa kulipa deni ivyo inapigwa mnada”
Aliongea Mwanaume mmoja aliyevalia shati jeupe amechomekea na kitambulisho cha Bank kikiwa kifuani mwake,
alijitambulisha kwa jina la Michael Frank Katobe.
“Bado sijawaelewa vizuri,hii nyumba ni yangu nilijenga mwenyewe na sijawahi kukopa bank kiasi chochote cha pesa , nashindwa kuwaelewa naomba ufafanuzi wa kina!”
Adrian aliongea kwa kujiamini zaidi kuliko wanaume waliokuja kupiga mnada nyumba yake, lakini ilionekana pia wanaume hao wana kila kithibiti,
“Chale nipatie hilo begi”
Michael Katobe alipewa Begi dogo kisha kuanza kufungua na kutoa makaratasi mpaka hati ya nyumba yake.
Adrian alipoziona tu hati za nyumba alipagawa aliyatoa macho yake kama mjusi aliyebanwa na mlango!
Alikimbia ndani haraka mpaka kwenye madroo kisha kufungua makabati, hakuamini baada ya kukosa hati miliki za nyuma yake,hapo ndipo alichanganyikiwa hakuelewa ni nani aliyemfanyia unyama huo….
Bado alikua haamini ni kitu gani kimetokea katika maisha yake, kwani mikosi ilimtokea kwa ghafla sana tena yakiambatana sambamba!
Nyumba aliibinua juu chini,chini juu na kuikung’uta, alifungua mpaka chini ya makapeti akitafuta hati miliki za nyumba yake.
Alifika Seblen na kutupa tupa makochi huku na kule lakini bado hakuambulia chochote kitu,jasho lilimtoka jingi tayari.
Na kutoka nje kwa kasi.
“Embu nione kwanza hayo makaratasi vizuri”
Alisema Adrian na kukabidhiwa hapo hapo.
“Hapa nani aliyetia sahihi”
“Wewe hapo”
“Mimi kivipi?”
“Si ni sahihi yako hiyo, wewe sindo uliyeandika hapo”
Adrian aliyatumbua macho yake juu ya karatasi, ni kweli alichokiona kilizidi kumshtua moyo wake,mapigo yake ya moyo yalimdunda kwa kasi pengine hata kutaka kutokeza nje ya kifua chake, alipagawa mno.
Hasa alipoona muandiko wake pamoja na sahihi yake yeye mwenyewe kwa chini.
“MIMI ADRIAN MWANGENYA,NI KWELI NILIMTUMA HUYO KIJANA HAPO AJE KUCHUKUA KIASI CHA SHILINGI MILLIONI MIA MOJA,BILA KUWEKEWA KITISHO CHOCHOTE KILE KWANI MIMI NINA HALI MBAYA SANA, NINA AMBATANISHA HATI ZANGU ZA NYUMBA KAMA DHAMANA,IWAPO IYO PESA IKIKOSEKANA NDANI YA MIEZI MIWILI NAJUA NI MICHACHE LAKINI NITARUDISHA PESA YENU HARAKA IWEZEKANAVYO.
NI MIMI WENU MTIIFU ADRIAN MWANGENYA.
Ivyo ndivyo ilivyoandikwa barua hiyo kisha chini sahihi kusainiwa, Adrian alikuwa mdogo na kunyong’onyea kama puto lililopasuliwa au kifaranga cha kuku kilichomwagiwa maji alidata!
Alikaa chini bila kutegemea kabisa, alitizama jumba lake kubwa la kifahari na kudhani wenda anaota ndoto kisha baadaye angeshtuka na kujikuta yupo kitandani analetewa chai ya maziwa asubuhi,lakini haikuwa ivyo mambo yanayotokea yalikuwa ni kweli kabisa.
“Mna picha ya huyo aliyedai kuwa nilimtuma?”
“Ndio, kwanini tukose”
Meneja wa Bank alifungua begi na kutoa baasha yenye picha ndogo aina ya passpot size,Adrian alivyoona picha alishtuka
***
Consolatha alikasirishwa sana kwa kitendo cha Adrian kuukoroga moyo wake,Aliumia pengine kuliko mwanamke yoyote Yule duniani sababu tu alimpenda sana mwanaume huyo na kuzani ndiye atakayekuja kuwa wa maisha yake, isitoshe ndiye aliyemtoa bikira yake kipindi ana miaka kumi na saba.
Ki ufupi alimpenda sana Adrian aliridhia!, wanaume mbali mbali walimpigia misele lakini aliwatolea nje na kuwapiga vibuti!.
Ni kweli consolatha alikuwa ni mzuri kupindukia.
Ngozi yake nyeupe ukiingalia ungedhani labda alijiongezea madawa lakini ndiyo ngozi aliyopewa na Mungu, ki ukweli Mungu alitulia katika kumuumba Binti huyo,Macho yake makubwa yalibeba mashavu mazuri yaliyonona kama Mdoli hasa akicheka vishimo huingia ndani yaani dimpoz,
hakuishia hapo alijua kucheka tena meno yake yaliyojipanga vizuri mdomoni huonekana alikuwa ni mwenye mapozi,
Kiuno chake kilikuwa chembamba kidogo lakini tofauti na nyuma alivyobinuka vizuri na kutengeneza vimlima kama Kibo na Mawenzi,alikua ni mwenye mguu mzuri wenye supu,Hata ungebahatika kumuona usingethubutu kuacha kugeuza shingo yako nyuma kumuangalia,
kilichomfanya azidi kuwa mzuri ni jinsi alivyoyapangilia mavazi yake, alijua kupigilia na pamba akiwa mwanamke wa kisasa, Adrian pia ndiye alimfanya Azidi kuvimba kichwa.
Licha ya Adrian kumfanyia mema yote yaliyopita lakini alimchukia sana kwa kitendo cha kumfumania na Leila rafiki yake kipenzi aliyetoka Marekani,ilikua ni lazima amuoneshe adabu Adrian kivyovyote vile.
“Mimi ndiye Consolatha,nilizaliwa hapa Dar hospitali ya Aghakhan yeye alizaliwa Mbeya Mwakaleli, sasa nitamfunza adabu!”
Hayo yote yalikua ndani ya ubongo wake, alimuwazia mabaya sana Adrian hata ikiwezekana apewe kisu na amchome nacho cha Koromeo amtoweshe duniani,
Katika makosa aliyofanya Adrian ni kumuonesha Consolatha kila kitu hati za nyumba mpaka kampuni yake.
Hakutaka kufanya mambo haraka haraka, aliamini kabisa hatoweza kufanikisha swala hilo yeye mwenyewe ivyo aliitaji msaidizi atakaye msaidia.
SAA mbili ya asubuhi ya siku iyo aliamka mapema sana na kuoga haraka haraka kisha kutafuta daladala za Kariakoo na kushuka mwisho wa kituo hapo alichukua daladala nyingine ya posta mpaka posta Mpya na kushuka kisha kuanza kutembea kuelekea gorofa la PPF Tower anapofanyia kazi Adrian nia yake ilikua ni kuonana na Partson Ngogo jr.
Ni kweli alimsubiri mpaka jioni muda wa wafanyakazi kutoka alilijua gari aina ya Mark II Grande la Partson Jr rafiki yake kipenzi na Adrian kisha kuliendea na kumsubiri.
“Mambo Partson”
“Safi za kwako shemeji”
“Acha unafiki,niite jina langu”
“Mi najua wewe ni shemeji yangu”
“Na Jaqlin je, usinifanye mimi mtoto bwana”
Habari za jaqlin alizijua zote na alishawahi kuwaona sehemu tofauti za starehe ivyo alichoongea alikuwa ana uhakika nacho.
Hapo ndipo Consolatha alipoanza kuonesha mazoea ya karibu na Partson sana kuzidi hapo awali, urafiki ulidumu na kusogea kwa kasi sana, wengi waliowaona walijua ni wapenzi hasa kwa baadhi ya watu waliufahamu uhusiano wa Adrian na mwanamke Consolatha .
“Kwaio umeamua kumzunguka mshakaji, jamaa mbaya sana wewe p”
Marafiki ndiyo umwambia Partson ivyo kila kukicha.
Consolatha alizidi kuonesha ukaribu zaidi kwa Partson na kufanya mazoea ya karibu mno, kichwani alikuwa ana mahesabu yake ya ziada. Laiti Partson angejua kuwa mwanamke huyo ni zaidi ya shetani kuzimu angemtupilia mbali. Ilikua ni bora ukutane na simba aliyejeruhiwa kuliko moyo wa Consolatha uliojaa chuki nyingi za kutisha, laiti kama ungebahatika kuiona sura yake usingethubutu kusema kuwa ndiye anayewaza kufanya malipizi.
Siku hiyo walikuwa wametoka wote club usiku wakiwa wamelewa lakini Kwa Consolatha akulewa sana,walifika mpaka kurasini nyumbani kwa Partson kisha kuingia Chumbani kilichotokea hapo ni kupigana mabusu na kushikana shikana kila sehemu za miili yao, tayari kwa kufanya Ngono.
Consolatha alitaka kufanya kila juhudi ili kumpagawisha Partson na ni kweli alifanikiwa kwa asilimia mia moja kama Delila aliweza kumlaghai Samson kwanini yeye ashindwe?alimpagawisha vibaya mno.
Hapo ndipo mapenzi yalipoanza kati yao.
“Nakupenda Partson”
Alisema Consolatha akiwa kifuani Mwake.
“Sasa muda wote ulikuwa wapi?”
“Si nilikua na Adrian, sikumpenda lakini basi tu alinifosi”
“Sawa nakupenda pia”
Zoezi la Kuteka akili za Partson lilifanyika kikamilifu kwa namna hiyo, Consolataha alijiona ni mshindi sana,Pesa za kodi za kampuni Partson hakulipa tena badala yake alifanya matanuzi na mwanamke mrembo Consolatha, Tena walifurahi walivyosikia Adrian amefungwa jela huko Mkoani Kilimanjaro miaka kumi.
“Baby nataka tuhame huu mji”
“Kivipi?”
“Ni rahisi sana, tukachukue pesa benk kupitia mgongo wa Adrian”
“Sio rahisi”
“Labda kwako”
“Una maana gani?”
“Tutatumia nyumba yake kuchukua pesa benki, naona Kampuni ile ishakwisha,unaonaje tumalize kila kitu tutimue”
Partson Ngogo aliguna guna lakini alivyopewa mapenzi kitandani alikubali kabisa na kumuunga Mkono.
Siku hiyo hiyo Consolatha alinyoosha mpaka Tegeta na kuwakuta wazazi wa Adrian lakini aliwapita bila kuwasalimia kisha kuelekea chumbani kuchukua hati za nyumba.
Alifanya mambo harakaharaka na kwenda kariakoo kwa wahindi ili kufoji Mwandiko wa Adrian mpaka sahihi yake hakuna kitu alichoshindwa muhindi huyo aliyeitwa Rahman kuanzia vitambulisho vya usalama wa taifa mpaka vyeti vya chuo aliweza kufoji na hakuweza kugundulika hata mara moja kutokana na ofisi yake kujificha uchochoroni.
Hapo ndipo Consolatha alipopeleka Mwandiko wa Adrian, kila kitu kilienda sawa.
Dili lao lilivyokaa sawa walienda CRDB bank na kukabidhi barua hiyo wakidai kuwa Adrian anaumwa yupo hoi maututi huko AMANA anaumwa tezi dume na hawezi kutembea kabisa zinahitajika pesa za operesheni aende Marekani kutibiwa.
Consolatha aliigiza na kukamua machozi mililita mbili na kuanza kulia mbele ya mwanamke aliyekuwa akitoa mkopo, akidai kuwa Kaka yake Adrian anaumwa sana anahitajika kufanyiwa upasuaji siku chache zijazo, ni kweli alifanikiwa kuinunua huruma ya mwanamke huyo asilimia mia moja kabisa, ulikuwa ni uwongo uliokwenda shule tena wenye PHD.
Baada ya siku tatu utaratibu ulifanyika akiwa pamoja na Partson Ngogo jr na kukabidhiwa kiasi cha shilingi milioni mia moja taslim! Huku wao wakikabidhi hati za nyumba kama bondi endapo akishindwa kufanya marejesho baada ya miezi mitatu kama walivyoandika kwenye barua waliofoji.
Meno ya Consolatha yote thelathini na mbili yalikua nje anakenua muda wote.Walishauriana na Partson wafanye taratibu za kutoroka na waende mbali, nje ya nchi wakaanze maisha kwani waliamini pesa hizo ni nyingi sana.
“Twende Mombasa Kesho Darling”
Alishauri Consolatha baada ya kutoka kuoga akiwa mwenye kanga moja peke yake akiwa na Partson jr.
“Mimi nakusikiliza wewe Mama watoto” Partson Alijibu.
“Poa ngoja nitafute tiketi za ndege”
Passpot walikua nazo,baada ya siku mbili taratibu za safari zilikamilika kabisa, na siku hiyo usiku walikua njiani kuelekea uwanja wa ndege wakiwa wenye furaha.
“Baby bablish, tafuna tafuna basi ”
Alisema Consolatha kisha kumpa Partson big g, kitendo cha kuitafuta dakika tano baadaye alihisi kichwa chake kizito sana, alijaribu kushindana na hali hiyo lakini ilishindikana, na kulala kabisa, alichofanya Consolatha alimsukuma nje ya gari na kumtupa kwenye mtaro wa maji machafu kisha kukamata usukani kwa safari moja tu uwanja wa ndege ili asafiri na kuelekea Dubai na wala sio Momabasa kama alivyomwambia Partson.
“Mimi ndiye Consolatha,Jini mwanamke”
Alijisifu na kushuka ndani ya gari baada ya kufika uwanja wa ndege wa kimataifa Mwalimu Nyerere, aligonga passpot mihuri na kuingia ndani ya ndege.
**
“Partson…”
Adrian aliita kwa sauti ya uchungu baada ya kuona picha ndogo juu ya karatasi ya mkopo na kuanza kutokwa na machozi japo hakujua kuwa alilia kwa hasira au kusalitiwa na partson.
Hakuamini kwamba kufumba na kufumbua amekuwa maskini wa kutupwa,
mambo mengi sana yalipita ndani ya ubongo wake na kuchambua vitu akiwa anaitizama picha ndogo ya Partson,
hakutaka kuamini kwamba leo hii amesalitiwa na rafiki yake kipenzi, aliumia sana na kupandwa na hasira,
koo lilimvimba na kufanya aangue kilio,hakuelewa angemfanya nini Partson endapo atamtia mikononi mwake wakati mwingine alitamani angekuwepo tu gerezani sababu hakuona sababu ya msingi iliyomleta uraiani, lakini alipomkumbuka Jaqlin aliyatupilia mbali mawazo hayo.
“Blazza mbona unalia kwani imekuaje?”
Mmoja wa wafanyakazi wa benki alimuonea huruma na kumuuliza.
“Kaka nimepigwa….. ki ukweli mimi sikuandika chochote kuhusiana na barua hiyo wala sikuwa naumwa ugonjwa wowote ule”
“Sio kweli”
“Akyanani tena”
“Huyo anadanganya Big! asikulaghai, usijifanye wa mjini, kwanza nenda nje hii nyumba ni mali ya Bank chanja mbuga tu huna chako”
Mmoja wao alidakia maongezi hayo.
“inavyoonekana huyu bwana ana matatizo”
“Anakupiga tu fix hapo, bwana mdogo nenda”
Wakati mabishano hayo yanaendelea Adrian alibaki kimnya na kuomba japo aingie ndani achukue vitu vyake vya muhimu.
“Kila kitu ni mali ya Bank blazza hausikii, yaani ki ufupi wewe sio muhusika kabisa timua zako tafuta ustaarabu usepe,usituwekee kiwingu”
“Naenda kuchukua Passpot zangu”
“Na ukitoka lazima nikupige sachi”
“poa”
Adrian aliingia ndani!
Alivyotoka alikua na kila kitu muhimu alichokihitaji kisha kuanza kutembea taratibu kuelekea getini huku akitizama nyumba yake,
bado alikua haamini kuwa vitu vinavyotokea ni kweli au yupo ndotoni.
Alivyojisachi mfukoni alikua na shilingi elfu themanini peke yake,hiyo ilimtosha kabisa kumpeleka kila tawi la benki ili kuangalia salio, ni kweli alipita benki zote na mwishowe kukuta ana salio la shilingi milioni tatu na laki mbili peke yake,
bado alipigwa na bumbuazi, kiasi hiko kilikua ni kidogo sana kwake kutokana na mali alizowahi kumiliki ikiwemo kampuni ya mikopo na utozaji ushuru.
Hakuamini kuwa amelala tajiri na kuamka Maskini.
Picha ya Partson ilipomjia kichwani alitafuta boda boda hapohapo.
“Psiii psiiiiii Boda”
Aliita Adrian na mwendesha pikipiki kupiga breki ya ghafla.
“Sema blazza”
“Nipeleke kurasini”
“Kurasini kubwa kaka”
“Mnazini pale”
“Poa buku saba”
“Haina noma”
Bodaboda iliondoka akiwa Adrian amepakia nyuma yake!.
Walivyofika tu Adrian alishuka na kumkabidhi pesa Dereva huyo na kupatiwa chenji yake shilling elfu tatu, kisha kuanza kupiga hatua za haraka haraka mpaka nyumbani kwa Partson rafiki yake ambaye alimsaliti kwa kuchukua kiasi kikubwa cha pesa na aliyamini kuwa hata Kampuni yake ndiye yeye aliyeifirisi.
Hakuna kitu alichowaza zaidi ya kuuwa mtu na akafungwe jela, hakuna siku aliyowahi kuchukia kama siku hiyo katika maisha yake yote.
Mambo yalimuendea mbele nyuma-nyuma mbele,au vise versa kama wazungu wasemavyo. Alijiona ni mwenye matatizo kuliko mwanaume yoyote Yule aliyewahi kuishi ulimwenguni!
Kwa hatua za haraka na majasho ya jua la saa saba yalimfanya azidi kupandwa na hasira kama mbogo.
Hatimaye alifika getini na kuingia bila kupiga hodi mpaka mlango mkubwa wa seblen kisha kunyonga kitasa lakini mlango ulikuwa umefumgwa, aligonga kwa fujo na kusikia kuna mtu anakuja kisha unafunguliwa kwa ndani.
“Mbona kaka hauna ustaarabu unagonga kama unadai?”
Alijibu mwanamke mnene, mfupi kiasi aliyevalia tenge mwilini baada ya kufungua mlango.
Adrian alimtizama juu mpaka chini kisha kumsukumiza nayeye kuingia ndani japo hakuwahi kumuona mwanamke huyo hata mara moja.
“Kaka Vipi?”
Alitupa Swali, Mama huyo kwa mshangao.
“Vipi,! vipi ndiyo nini? Ndiyo anavyokudanganya huyo baasha ako mnitapeli,kwanza yupo au hayupo, leo ndiyo nauwa Mtu”
“Kaka umechanganyikiwa au umerukwa na akili.. upo sawa sawa kweli?”
“Nipo sawasawa na nina akili timamu kama binadamu mwingine yoyote Yule,”
Maneno ya Adrian yalimchanganya sana mwanamama huyo hakumuelewa Adrian, Walivyoshindwa kuelewana Mwanamke huyo mnene alitembea mpaka chumbani kwake kisha kusikika minong’ono, Adrian alisikia vizuri ni sauti ya kiume, hasira zilimpanda, alivimba mwili mzima na kuwa kama Chura wa masika macho aliyatoa huku jasho likim-miminika kama maji.
Alivyosikia mlango wa chumbani unafunguliwa alisimama kwa kasi ya umeme na kuuendea, lakini alinywea baada ya kuona pande la mtu lenye miraba minne aliyejazia misuli, alionekana ni mtu wa mazoezi sababu ya kifua chake kutuna mbele.
“Tatizo nini?”
Aliuliza Mwanaume huyo huku akimtizama Adrian.
“Blazza itakuwa nimekosea nyumba,itakuwa nimechanganyikiwa”
“Hujajibu swali bwana mdogo, mbona majasho yanakutoka?,alafu unanuka kama kuku,wewe Mama Vanesa embu nipe maelezo ya kutosha kabla sijamfanya panching begi huyu”
Mwanamme huyu Baunsa mwenye mwili kama wa John Cena alimuuliza Mke wake.
“Kaja hapa anasema maneno ya ajabu ajabu hata sikumuelewa eti kaka shida yako nini?”
Adrian alitamani aeleze matatizo yake lakini aliona hakuna atakaye msaidia zaidi tu ya kupewa pole, lakini ilibidi amuulizie Partson Ngogo Jr.
“Ahaaa huyo jamaa mbona alituuzia hii nyumba ni mwezi sasa umepita”
Adrian alihisi ubaridi kwenye miguu yake, aliishiwa nguvu mwilini na kubaki kinywa wazi.
“Kwaio kwa..io hakusema ni wapi alipo?”
“Hapana hakusema,kwani vipi,imekuaje?”
“Hakuna kitu kaka, naomba maji ya kunywa tafadhali.”
Adrian aliletewa na kunywa glass saba za maji ndipo alipoaga na kuondoka zake akiwa mwenye mawazo mengi sana ndani ya ubongo wake.
Akili yake ilivurugika kabisa wakati mwingine aliongea mwenyewe.
“Kaka unaniongelesha?”
Aliuliza Dada mmoja hapo Stendi baada ya Adrian kuanza kujiongelesha Mwenyewe.
“Hapana Hapana”
Jioni ilipofika alitafuta nyumba ya wageni huko Buguruni Malapa iliyoitwa Sewa karibu na magorofa ya polisi,
hakupapenda lakini hakuwa na jinsi, ilipofika usiku alitoka nje ili kupunga upepo.
Nje kulikuwa kumechangamka machangudoa walijipitisha kila sehemu lakini hakuwahangaikia hata mmoja, alikua mbali sana kimawazo.
“Kaka bei nafuu twende buku mbili tu ukaenjoy usiku”
Changudoa mmoja alisimama mbele yake na kujipigia debe.
“Sawa Ahsante”
“Ahsante ndiyo nini twende tu,bei pungufu tunaongea”
“Nadhani Kiswahili unakielewa Ahsante nimekwambia nenda”
“Au mwenzetu ndiyo vile jogoo apandi mtungi”
Adrian alimtizama kisha kukaa kimnya, Laiti angejua kuwa mwanamme anayeongea naye ana hasira mbaya wala asingethubutu kuendelea kujipigia debe na kumbugudhi ili aondoke naye.
Moyoni mwake alishampenda Jaqlin na kuapa kuwa hatomvulia Mwanamke yoyote Yule nguo yake ya ndani.
Hiko tu ndiko kilimfanya aondoke eneo hilo na kutafuta meza nyingine lakini changudoa huyo alizidi kumgasi.
“Basi buku jero mpaka asubuhi”
“Achana na mimi Dada embu nielewe basi, sitaki hujanivutia peleka kidude chako kichafu huko”
“Mimi kidude changu kichafu Wewe Ku** la Mama yako”
Katika maisha yake duniani alichukia sana kutukanwa na Mwanamke tena kutukaniwa mama yake aliyefariki tayari ametangulia mbele za haki na ndiyo hapo hasira zilimpanda na kukunja sura yake kama mtu aliyekuwa ana kunywa pombe ya Mnazi!
Aliinuka mzima mzima na kumtandika kofi Changudoa aliyekuwa mbele yake. Na kufanya ukelele mkali haikuchukua hata dakika mbili Adrian aliwekwa kati na wahuni na kuanza kumshambulia kama mpira wa kona hakuelewa walitokea wapi.
Sababu changudoa huyo alilalamika kuwa Adrian alilala naye usiku mzima kisha kukataa kumlipa pesa zake, Wahuni walikasirika na kuzidi kumshushia kipigo cha Mbwa mwizi, Mpaka inafika Saa kumi ya usiku alikuwa amechakazwa kabisa na kutupwa nje barabarani akiwa amechaniwa nguo zake mwenye maumivu mwili mzima,
Maisha ya Adrian yalivurugika ghafla tena yalikuwa ni kama yenye mkosi, hakuelewa kabisa ni kwanini matatizo yamemuandama kiasi hiko.
Kitendo cha kupata fahamu zake tu alikaa kitako baada ya kukumbuka yaliyomtokea usiku wa jana, Alihisi maumivu juu ya kichwa upande wa utosi,alivyojisachi mifukoni hakuwa na simu wala pesa alizokuwa nazo, walishamuibia pamoja na viatu,Shati lake lilijaa damu kama aliyekuwa machinjioni.
Alijizoa zoa taratibu na kuanza kurudi nyumba ya wageni aliyopanga jana yake,kwa kifupi alionekana ni kama aliyechanganyikiwa kabisa.
Alienda mpaka mapokezi na kumkuta Msichana aliyempokea alipoenda kukodi chumba.
Hata yeye alipomuona alipigwa na bumbuazi alivyoona tu shati la Adrian limelowa Damu chini hana Viatu.
“Kaka vipi mbona una damu kiasi hiko?”
Aliuliza Msichana huyo kwa hamaki!
“Da!, we acha tu, samahani unaweza kunisaidia kitu?”
“Kitu gani kaka?”
“Nataka niende benki, sasa sina nguo hata moja,kwaio nilikua naomba msaada wa nguo hata nijistili niende benki nikatoe pesa”
“Sasa nitakuamini vipi?”
“Niamini dada angu, maana hata simu wameniibia”
“Itakuwa vigumu kaka kwa hali iliyokuwa sasa”
Ilichukuwa dakika kumi na tano nzima Kwa Adrian kumshawishi msichana huyo ili ampe hifadhi ya nguo ili aende benk kutoa pesa zilizokuwepo na aondoke kabisa eneo hilo.
Alipomkumbuka Partson Ngogo jr Roho ilimuuma kupindukia, bado hakuamini kwa kilichomtokea katika maisha yake,bado alijua anaota njozi ya kutisha tena baadaye angeshtuka ndotoni na kujikuta yupo na Mali zake.
Msichana Marry ambaye walishajuana Majina alikuja na nguo kisha kumkabidhi Adrian, zilikuwa nguo kubwa mno kwake,alivyozivaa na kutoka Marry hakuwa na mbavu kwa kucheka na mpaka machozi kumtoka.
Adrian aligeuka kuwa kituko kwake.
“Sasa unacheka nini?”
“Ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaaa ha ha ha haaaa Kaka unaua mbavu zangu uwiii”
Msichana Marry alicheka mpaka kudondoka chini.
Adrian ilibidi nayeye atabasamu baada ya kujiangalia. Ki ukweli suruali ya kitambaa aliyovaa ilikuwa kubwa mno yaani bwanga! alikuwa kama amevaa puto.
“Hii Suruali Marry umeitoa wapi? Huyo Mtu mwili wake sipati picha anafananaje”
“Ha ha ha ha Adrian naomba uwende utanifanya nife kwa kukosa Pumzi”
Adrian alianza kutembea huku suruali hiyo ikipea pea kama bendera, hata watu walimshangaa.
Alitembea kwa miguu mpaka Buguruni Chama karibu na Sheli ya Oil Com hapo alikuta ATM Mashine kisha kutoa kadi yake ya visa,
alitoa pesa kadhaa kisha kuziweka mfukoni kitu cha kwanza ni kutafuta simu ndogo itakayo msaidia, na nia yake ilikua ni moja tu awasiliane na Mpenzi wake Jaqlin ili amtoe wasi wasi aliamini kuwa huko alipo atakuwa ni mwenye mashaka mno.
Baada ya zoezi la simu kuka milika alienda duka lingine na kununua kadi ya Simu kisha kuiweka ndani yake.
Hapo hapo alibonyeza namba za Jaqlin, kwa kuwa alikuwa nazo kichwani ilikuwa afadhali kwake.
“Hallo naongea na nani?”
Upande wa pili wa simu ulisikia kwa sauti nyororo, Adrian aliitambua kuwa ni ya Jaqlin.
“Adrian, Mimi Adrian”
“Jamani Love upo wapi?”
“Mimi?”
“Kwani naongea na nani?”
“Nipo, nipo nipo nyumbani”
“Sasa leo hujaenda ofisini mpenzi wangu?”
Swali la Jaqlin lilimbabaisha Adrian na kukaa kimnya kwa kama dakika moja nzima akitafakari nini cha kujibu.
“ Aah Mhhh.. sijaenda leo kichwa kinasumbua kidogo, lakini nitaenda Darling” Alidanganya!
“Okay mpenzi utarudi lini?”
“Nitarudi tu wala usijali”
“Nakupenda Mume wangu nakusubiri kwa hamu sana”
“Sawa Honey nitakuja”
“Okay”
Baada ya maongezi hayo Adrian alishusha pumzi ndefu sana. Maneno ya Jaqlin yalimpeleka mpaka katika maisha yake yaliyopita kimawazo,na kuzidi kupata uchungu sana.
Alitembea harakaharaka mpaka kwenye duka la nguo kisha kununua jins na Tshirt,
kila aliyemuona alimshangaa na kucheka kichini chini, hakuwajali alibeba mfuko wake na kulipa pesa kisha kurudi Buguruni sewa nyumba ya wageni.
“Dada Ahsante sana, kamata hii utaseti nywele”
Adrian kwa shukrani alimkabidhi shilingi elfu ishirini.
“Ahsante Kaka,hapana hiyo kaa nayo inaelekea una matatizo sana”
“Tafadhali naomba uchukue tu,alafu nataka niondoke leo leo”
“Sawa lakini hiyo ni kubwa nipe tu elfu kumi”
“Poa”
Aliingia chumbani na kuchukua vitu vyake muhimu na kuanza kutoka nje, alizidi kumpa shukrani Marry aliyekuwa mapokezi kwa msaada aliompa.
Alisonga mpaka stendi ya mabasi Buguruni Sokoni ili kusubiri daladala, japo hakuelewa ni wapi anaenda.
“Ubungo! Ubungo! Ubungo!”
Sauti ya kondakta ilisikika, Baada ya kujishauri kwa muda mrefu aliingia ndani ya daladala, lakini alishuka tena.
“Kaka vipi gari linakaribia kuondoka”
“Nimekosea naelekea Chanika”
“wewe kavu nini”
Adrian hakuangaika na Konda huyo aliyendelea kutukana matusi kwa kitendo cha Adrian kuinguia ndani ya dala dala na kushuka.
Kuna rafiki yake mmoja wa siku nyingi sana alimkumbuka, tena kwa ghafla alipokumbuka kuwa yupo Buguruni, alitembea haraka haraka kuelekea upande wa magari yaendayo kariakoo mpaka alipofika Buguruni Malapa kisha kuanza kuangalia mafremu yaliyojipanga.
“Mafremu ya Mzee Kusa ndiyo haya nafikiri, sasa nyumbani kwake sipajui ngoja nikaulize”
Adrian aliwaza na kuanza kupiga hatua za taratibu mpaka kwa mwanaume mrefu aliyevaa tshirt jekundu ana soma gazeti.
“Blazza za saa hizi?”
“Saalama ndugu”
“Samahani naomba kuuliza”
“Uliza”
“Naulizia nyumbani kwa Mzee Kusa”
“Mzee Kusa? Mzee kusa huyu mwenye mafremu hapa?”
“Ndiyo huyo huyo”
“Sasa sikia,unaona hiyo barabara kubwa, nyoosha nayo moja kwa moja utakuta makutano mbele kule, utakunja kushoto, geti la kwanza, la pili ndio hapo hapo”
“Daa Ahsante Mshkaji”
Adrian alishukuru sana, Mzee Kusa ni Mzee ambaye waliheshimiana sana tena walishawahi kufanya biashara kwa muda mrefu.
Aliamini kuwa hapo angepata hata hifadhi na msaada vile vile, Alitembea na kufuata alipoagizwa kisha kugonga geti kubwa la rangi ya kijivu.
Aliyekuja kumfungulia ni Mwanamke Mnene kiasi, maji ya kunde mwenye mashavu makubwa lakini mwenye sura ya kitoto.
“Karibu Kaka”
Alisema mwanamke huyo.
“Ahsante, bila shaka hapa ndiyo kwa Mzee Kusa”
“Ndiyo penyewe karibu ndani”
“Ahsante”
Adrian alikaribishwa ndani tena mpaka seblen, kwa bahati mbaya Mzee Kusa hakuwepo, lakini mwanamke huyo alimpigia simu ili waweze kuongea na Adrian.
Maongezi ya Mzee Huyo yalimtia Moyo na kuona Nuru nyingine ndani ya moyo wake japo hakuanza kumueleza matatizo yake, alipanga kumueleza jioni atakapo rudi.
“Dada naweza nikapata maji ya kunywa ya baridi”
“Bila shaka”
Adrian aliletewa maji.
Ulivyofika mchana mwanamke huyo alimkaribisha mezani kula, kisha wote kuanza kula huku wakijaribu kupiga stori za hapa na pale, mpaka wanamaliza walishajuana majina.
“usiniite Dada Sakina, niite tu jina langu, maana nina uhakika umenizidi umri”
“Dada haimaanishi kwamba umemzidi mtu Fulani umri, mi ninavyojua ni kama Heshima fulani hivi, kwani una miaka mingapi?”
“Nina miaka kumi na tisa”
“Muongo wewe”
“Kweli tena, au mpaka nikuletee vyeti?”
“Basi!,ndiyo mtoto wake wa kwanza sio?”
“Mtoto wa nani?”
“Wa Mzee kusa”
“Hapana mimi mkewe”
Adrian alishtuka sana lakini hakutaka kuonesha waziwazi, alimtizama binti huyo kuanzia juu mpaka chini akimkagua, ki ukweli alikuwa binti mdogo, aliivuta picha ya Mzee Kusa haraka ndani ya ubongo wake na kuifananisha na ya binti aliyemuona mbele na kudiriki kusema kuwa ndiye mke wa Mzee Kusa mwenye umri wa miaka sitini.
“Mhhh”
Aliguna Adrian.
“Vipi mbona umeguna?”
“Hakuna kitu naomba niongeze maji”
Sakina alisimama!
mwendo wake ulikuwa asilia, nyuma alifungasha na kutembea kwa Madaha, Adrian hakuelewa mwendo huo ulikuwa ni wake au alifanya makusudi.
Waliendelea kupiga stori mpaka baadaye jioni walivyosikia muugurumo wa Gari, Sakina alikimbia haraka chumbani kisha alivyorudi alikua amevaa kitenge juu yake, Mzee kusa alikuwa ni mwenye wivu sana juu ya Mke wake hakutaka abaki seblen bila kitenge kizito au nguo iliyomfunika mpaka chini.
“Karibu Mume wangu, pole na uchovu”
Sakina alipokea mizigo kisha kwenda nayo chumbani.
Huku AKIMUACHA Mume wake anasalimiana na Adrian.
“ Shikamoo Mzee”
“Marahaba vipi kijana wangu?”
“sio kwema kabisa”
“Nini zaidi?”
Adrian aliinamisha kichwa chini,alivyoinuka machozi yalianza kumlenga kisha kuanza kumuhadithia mzee Kusa kila kitu kuanzia alivyowekwa gerezani mpaka kukuta kampuni yake pamoja na nyumba yake kupigwa mnada.
Historia hiyo ilimgusa sana Mzee Kusa, na kuhaidi kumsaidia kwa hali na Mali!
Shukarni alizompa Mzee Kusa hazikuwa na mfano wake.
“Utakaa hapa, mpaka kila kitu kitakapo kuwa sawa”
“Ahsante Mzee sijui nikupe nini”
“Nakumbuka ulishawahi kunisaidia sana kwenye mkopo,Mungu atakusaidia atakupa zaidi ya vitu ulivyopoteza, hiyo ni mitihani tu ya dunia”
Alimaliza Mzee kusa kisha kumuita Sakina ili akamuoneshe Adrian chumba cha kulala.
***
Baada ya kumaliza kula chakula cha usiku kwa pamoja mezani, Adrian aliaga kwenda kupumzika sababu alichoka sana, alivyofika tu alitafuta taulo na kuingia bafuni,bahati nzuri chumba chake kilikuwa ‘self contained’ kama wazungu wasemavyo,
baada ya kutoka kuoga akiwa mwenye mawazo alihisi mlango wake unagongwa alivyofungua alikutana na Sakina mlangoni akiwa na mashuka mkononi.
“Kuna mashuka hapa Adrian, utajifunika usiku”
“Ahsante”
Macho ya Sakina yalitua juu ya kifua cha Adrian kilichojigawa vizuri,udenda ulimtoka ilionekana kuna vitu ana fikiria kichwani kwake.
Hakusema lolote na kuondoka zake.
Adrian alifunga mlango na kujitupa kitandani huku akitafakari mambo mengi sana yanayoendelea.
Kwa kuwa alichoka sana usingizi ulimchukua hapo hapo.
Katikati ya usiku alihisi kuna mtu anamgusa gusa, alivyoyafumbua macho yake alikutana na sura ya Sakina mbele yake,aliyekuwa amevalia night dress nguo za kulalia, iliyoonesha kila kitu na kumchora umbile lake lote kweli alivutia.
“Unataka nini?”
Alifoka Adrian kwa sauti ya chini.
“Hujui au?”
“Embu toka usinitafutie mabalaa usiku usiku, Namuheshimu sana Mzee Kusa”
“Haijalishi.. Mzee kusa huwa hakidhi haja yangu”
“Mimi siwezi Sakina naomba uwende”
“Thubutuu…..humu sitoki”
Sakina Na Adrian waliendelea kubishana huku Sakina akiendelea kumsumbua kuwa anataka kufanya naye Ngono.
Ni kweli Mzee Kusa hakuweza kumkidhi haja zake,Binti mdogo kama huyo aliihitaji penzi motomoto,Kifua Cha Adrian kilimpagawisha hasa alivyoona taulo kwa mbele limetuna dalili zilionesha kuwa ana Mzigo mkubwa.
Kelele hizo za Adrian na Sakina zilipenya mpaka chumbani kwa MZEE Kusa na kumuamsha, kutokana na chumba hiko kukosa Dari kwa juu, alisikiliza kwa umakini na kuisikia sauti ya mke wake, alipandwa na hasira kisha kuchungulia uvunguni na kutoa panga lake lenye makali kotekote ,
Wivu ulimkaba kohoni, alifura!
hakuna kitu alichokichukia kama dharau katika maisha yake haraka haraka alitafsiri Adrian alikuwa na mahusiano na Mke wake siku nyingi ivyo alikuja kwa gia hiyo ili wawe karibu na sio kuomba msaada.
Alitembea kwa kunyata mpaka nje ya mlango wa Adrian kisha kutega sikio na kusikia kitanda kinanesa nesa, dalili zilionesha kuwa Mke wake Sakina analiwa uroda tena ndani ya nyumba yake!
Macho yalimbadilika rangi na kuwa mekundu, alitetemeka kwa hasira na kulishika panga vizuri, alirudi nyumba kidogo na kuupiga mlango teke na kuingia nao mpaka ndani. Hakuamini alichokiona.
“Adrian nakuuwa!”
Hilo ndilo neno alilotamka Mzee Kusa.
Kifua cha Mzee KUSA kilipanda juu na kushuka kwa hasira, mapafu yake yalijaa hewa,Macho yalimtoka majasho yalimtiririka vibaya mno!
hakuamini baada ya kumuona Mke wake Sakina yupo na nguo ya kulalia tena akiwa amemkumbatia Adrian ilikuwa ni picha mbaya sana kwake tena ya dharau.
Alitetemeka akiwa na panga lake mkononi kilichomjia kichwani kwake kwa wakati huo ni kuuwa mtu,Maruwani yake yalimpanda!
Adrian na Sakina walibaki kimnya wanatetemeka walishaelewa kuwa kwa hasira alizokuwa nazo Mzee Kusa ni lazima lolote baya lingetokea.
“Mzee,Mzeee.. Sio Mimi ni ni ni ni Sakina ndiyo aliyonilazimisha, mimi nilikuwa sitaki MZEE wangu, sakina muambie ukweli”
Adrian alijitahidi kuanika ukweli, lakini alikuwa ameshachelewa kwani Mzee kusa alimvaa Sakina na kulishusha panga juu ya bega lake.
Hakukuwa na masihara hata kidogo,Adrian alitetemeka, alihisi Mkojo unampenya na kulowanisha boxa yake aliyovaa! Alimuona Mzee Kusa anakuja usawa wake lakini kabla ya kurusha panga Adrian alimdaka mkono wake na kuanza kushikana huku na huku wakitupata,
wakiwa juu ya kitanda wote walidondoka chini Puu!
Mmoja kati yao alianza kuvuja damu sana na kufanya chumba kizima kinuke kama machinjioni,
Mzee Kusa utumbo wake ulikuwa nje,Panga lenye makali lilitumbukia ndani ya tumbo lake, na kuanza kutingisha miguu yake kama kuku aliyekatwa kichwa taratibu roho yake ilianza kuacha Mwili.
Adrian alichanganyikiwa mno, hakuelewa ni hatua gani achukue,alijua kivyovyote angeenda jela endapo majirani wangeamka usiku huo na kumkuta Ndani.
“Mzee Ku…sa. Mzee Kusa”
Adrian aliita huku akimtingisha Mzee huyo aliyekuwa ameyatoa macho yake ameyatumbua amekufa tayari, kesi ya mauaji ingemkabili endapo akikutwa na maiti hiyo ndani!
Akili yake ilifanya kazi haraka kwa kasi ya Umeme! Alikimbia haraka bafuni na kunawa mikono yake kwa sabuni ili kufuta damu,haraka haraka alibadili nguo na kuvaa nguo za Mzee kusa baada ya kuingia chumbani kwake.
Baada ya kila kitu kukamilika alichukua pesa makabatini na kuziweka mfukoni, hakuwa tayari kubaki na kwenda jela, japo kuwa hakuwa anajua sheria lakini alijua kuwa aliyekutwa na ngozi ndiye aliyekula nyama,hilo alilitambua!
Bila kugeuza shingo yake nyuma usiku huo huo alitoka na kwenda mpaka stendi ya magari kisha kupanda gari lililompeleka mpaka chang’ombe, ndani ya basi alikuwa ni mwenye wasi wasi sana,jasho lina mtiririka japo kulikua kuna baridi la kufa mtu!
“Blazza vipi, mbona una wasiwasi?”
Aliuliza Abiria mmoja aliyekuwa ameketi naye siti moja.
“Nikaushie, sikujui hunijui,wewe unanijua mimi mpaka uniulize, fanya yako”
“Kwani kuuliza ubaya?”
“Ebwana nikaushie, nipotezee temana namimi”
Adrian ilibidi atumie ukali sana,ki ukweli alitoka kufanya mauwaji ivyo hakutaka kuhojiwa na mtu yoyote Yule,kila mtu aliyemuangalia ilimfanya ainamishe kichwa chake chini kwa uwoga.
Alivyofika Chang’ombe alishuka na kutafuta nyumba ya wageni ili atulize akili yake.
Ni kweli alipewa funguo na kuingia chumbani huko hakupata usingizi mpaka kunakucha na kutoka nje.
“Carlos”
Aliita Adrian baada ya kumuona rafiki yake wa kitambo yupo kwenye mgahawa ana kula. Alikumbuka vizuri sana kuwa kila baada ya mwisho wa mwezi ni lazima watoke wote wakafanye starehe.
Carlos alimtizama Adrian kwa macho ya dharau juu mpaka chini na kumkagua jinsi nywele zake zilivyokuwa tim tim hazijachanwa wala shati alilovaa halijapigwa pasi.
“umenifananisha au?”
Aliuliza Carlos huku akibenua mdomo wake kwa dharau.
“Ah Carlos!.. mimi nikufananishe wewe ndugu yangu?”
“Sasa mimi mbona sikufahamu,embu nenda bwana usiniwekee kiwingu kaka”
Adrian hakushangaa sana, sababu huyo aliyekutana naye ni mtu wa tatu kumkana.Habari za Adrian kufirisika zilimfikia kila mtu jijini Dar es salaam, walimtenga wote aliokuwa nao wanakula bata na kwenda kwenye kumbi za Starehe, walimuangalia kama kinyesi,kila aliyemuona alimkana kama Petro alivyomkana Yesu basi ndivyo ilivyokuwa kwake!
Alitamani kudondosha chozi la uchungu, moyoni aliumia alitamani ayabadili mambo yanayomtokea lakini haikuwezekana, mambo yanayomtokea leo hii yalikuwa ni mambo halisi.
“Ebwana nenda nitakuitia Mwizi”
Alizidi kufoka Carlos huku akiendelea kula.
***
Maisha yake kwa ujumla hakuweza kuyatofautisha na ombaomba wa barabarani au mtoto yatima aliyefiwa na wazazi wake wote wawili,
alitangatanga barabarani asijue ni kipi akifanye,ungemuona lazima ungemnyooshea kidole na kudiriki kusema Adrian ni mwendawazimu au mwehu.
Lawama zote alimtupia Partson Ngogo alishaelewa kuwa ndiye mkandarasi aliyeharibu maisha yake yote yakavurugika na kupoteza wadhifa wake, hakuelewa ni wapi alipo! Jaqlin akiwa Mwakaleli Mkoani Mbeya alimpigia simu kila kukicha akitaka kujua kuwa ni lini atarudi Mbeya, tena alimsisitizia arudi na zawadi kubwa.
“Uje na zawadi mpenzi wangu”
“Sawa Honey nitakuja nayo”
“kwani ushatoka ofisini?”
“Ndio nakula lunch sasa hivi”
“unakula nini?”
“Mhhh aaaah, kama kawaida nimeagiza nyama choma ya mbuzi”
“Jamani Love, nimemisi ivyo vitu”
“usijali Mpenzi, nakupenda wacha nikate simu nitakupigia baadaye!”
Jaqlin alikuwa ndani ya giza nene haelewi kuwa Adrian maisha yamemchapa kiasi kwamba alivyokua anaongea naye alikuwa ameshika Mwindi wa kuchoma amesimama kwenye kibanda cha magazeti na wala hayupo mgahawani kama alivyoongea kwenye simu.
“Kaka unaweka kiwingu, mbona umesimama kama mlingoti hununui gazeti? unakula kula tu mahindi kalie basi huko mbele ya safari”
“Wacha nisome some habari za juu juu hapa”
“aah Nenda zako,nyie ndiyo chuma ulete nyie”
Ni bora angekuwa amesoma walau angetafuta vyeti vyake na kuanza kuzunguka ili atafute kazi, lakini ki ukweli hakuwa na elimu, mali zake alizipata kwa kuunga unga kipindi alipozamia Afrika Kusini miaka mingi iliyopita,
alijuta sasa kukataa shule kipindi yupo mdogo baada ya kuona shule inamzingua!
“MAITI YAKUTWA NDANI,IMEKATWA NA PANGA,MKE AJERUHIWA VIBAYA MNO YUPO MAHUTUTI ALAZWA…..”
Kichwa cha habari hiko kilimshtua sana Adrian pamoja na Picha ya Mzee Kusa juu yake na moyo wake kupiga paa! Kwa mshtuko wa ajabu, Mtu aliyekuwa akisoma gazeti hilo la Nipashe alikuwa bize stendi!
“Dada samahani naomba nisome hilo gazeti”
Adrian alivunja Ukimnya tena bila ya kusalimia.
“si unaona nasoma”
“Dakika moja tu chap”
“Acha usumbufu basi, gazeti mia mbili unashindwa kununua, achana na mimi”
Kilichomshtua Adrian ni baada ya kuona polisi Wawili wanakuja upande wa kushoto tena mmoja wao ameshika gazeti la Nipashe likiwa na kichwa cha Habari pamoja na picha ya Mzee kusa amechomwa na Panga.
Alihisi maji maji yanalowanisha boxa yake ya ndani, hakuelewa ni mkojo au majasho!
Polisi hao walizidi kumsogelea huku wakimwangalia usoni na kumkazia macho na kuanza kunong’onezana alishajua teyari amekwisha, maisha yake yalikuwa kwenye matatizo, sababu yeye ndiye alihusika moja kwa moja na kifo cha Mzee Kusa, Akili yake ilimtuma kuwa Sakina ni lazima atakuwa ametaja kila kitu kuhusiana na kifo cha Mzee Ngusa,ivyo askari walikuwa na picha yake.
Nguvu zilimjia haraka haraka na kuanza kutembea kuelekea mbele kwa hatua mbili mbili, lakini kwa nyuma alisikia mapolisi bado wanamfuata.
Alitamani ardhi ipasuke ili atumbukie ndani,Kichwa chake kilipingana na vitu viwili huku kimoja kikimwambia akimbie na kingine kikimwambia atembee tu kawaida kwani hata akikimbia hatofika mbali!
“Potelea mbali wacha nichanje mbuga,kuliko kukamatwa kizembe”
Alivyotaka kuchanganya miguu yake kabla! aliitwa na polisi mmoja wapo aliyekuwa nyuma yake.
“We kijana! Aroo we kijana simama!”
“Aroo Simama”
Adrian alitetemeka lakini alishusha pumzi ndefu baada ya kugundua kuwa polisi hao waliokuwa nyuma yake hawakuhangaika naye, Walimpita huku wakimkimbiza teja aliyekuwa mbele.
Hakuamini kama ameachwa na kutoka kwenye hatari aliyokuwa nayo,alivuka barabara haraka haraka na kwenda upande wa pili kisha kupanda dala dala lingine la Mbagala kutokana na kuchanganyikiwa kwake.
gari liliondoka mara moja huku akiwa mwenye mashaka sana!
Kifo cha Mzee Kusa kilimuogopesha sana hasa alipogunda kuwa Sakina yupo hai na kivyovyote vile angehojiwa basi angekuwa kwenye matatizo makubwa jela ingemuhusu, lawama zote alimtupia Sakina kwani ndiye aliyesababisha mpaka mambo yakavurugika na Mzee KUSA kufarki dunia.
Kwa mara nyingine tena maisha yake yalikuwa kwenye matatizo makubwa,hakuelewa ni kwanini mambo yanamtokea kwa ghafla kiasi hiko tena yakiambatana samabamba!
“Konda shusha hapo”
Aliropoka Adrian kwa sauti ya juu kama aliyetoka usingizini na kuwafanya abiria wote washtuke na kumwangalia.
“ulikuwa umelala au?Sasa mbona husemi muda wote natangaza,ila simu zikiita mnazisikia, mimi sisimami utashuka kituo cha mbele “
Konda alifoka kwa sauti ya juu huku akiwa mwenye hasira,
Ki ukweli Adrian alitaka aruke dirishani kwa hasira alizokuwa nazo dhidi ya mtu aliyemuona,licha ya kupitiliziwa ilibidi akae kimnya na kusubiri kituo kinachofuata.
Hakuwa na uhakika kama angemkuta Partson Ngogo Mtu aliyeharibu maisha yake na kumfanya afirisike na kuwa maskini wa ghafla, alimchukia vibaya, alitembea haraka haraka na kutamani walau apae angani ili aweze kumfikia, katika akili yake hakuelewa kama alimfananisha au ndiye.
Ni kweli macho yake hayakumdanganya alivyofika tu alimkwida Partson shati na kumvuta pembeni kwa hasira huku akikumbuka ni kiasi gani alivyoteseka na maisha yake kuingia katika matatizo makubwa sana.
Partson Ngogo hakuelewa, alipigwa na bumbuazi hakuelewa ni kitu gani lakini,alishaelewa tayari kosa lake alilolitenda, kama rafiki yake wa karibu hakupaswa kufanya alichokifanya alijuta sana na kumlaani sana Consolatha ambaye alitokomea pia na gari yake baada ya kumuwekea madawa makali ya kulevya kwenye big g,
lakini hilo halikuweza kubadili ukweli uliokuwa umetokea.
Hakukaa sawa Partson Ngogo alipigwa ngumi ya shingo na nyingine na tumbo, Adrian alikua na hasira kama Mbogo au simba aliyejeruhiwa na mkuki.
“Chif niachie kwanza nikueleze ndugu yangu”
“unieleze nini sasa?”
“Yaliyotokea aarghh aarghh unaniumzia una…niua Chi..f aaargh”
Partson alipigwa kabali kali na Adrian.
“Ni Consola.tha”
“Nani?”
“Consolatha”
“kafanya nini?”
“Ndio kafanya haya yatokee, naomba unisamehe ndugu yangu ili nikutajie alipo maana hata mimi kaniibia gari na kuuza nyumba yangu vile vile”
Hata angeendelea kumpiga Partson mpaka kumuuwa lakini asingeweza kubadili ukweli na kupata mali zake zote alizopoteza.
Japo alijawa na hasira sana, alikumbuka kuwa ana kesi ya mauaji ivyo anaweza akaua na kupata kesi juu ya kesi!
“Consolatha kafanya nini?”
Aliuliza Adrian akitaka kujua.
Partson taratibu alianza kumuelezea kila kitu lakini hakumwambia kuwa walikuwa wapenzi na Consolatha na walishawahi kufanya Ngono alijiua ni kiasi gani Adrian angeumia sana.
“Kwaiyo kaenda Mombasa?”
“Ndio alivyoniambia baada ya kuniambia una shida sana”
“Kwanini hukunipigia simu,unasema uwongo”
“Kweli Chif,kipindi hiko ulikuwa gerezani”
“Na kuhusu kampuni ilikuwaje?”
“Naomba tukae chini tuongee kwanza”
“Sina muda huo wa kukaa na kuongea nawewe sawa partson, sina muda huo”
“Chif usichukulie hasira sasa,”
“Achana na mimi”
Hakuwa na haja tena ya kubaki eneo hilo aliondoka zake kwa hasira kama aliyechanganyikwa hakutaka tena kuona sura ya Partson Ngogo mbele yake ambaye hapo nyuma walikuwa marafiki wa kufa na kuzikana lakini sasa leo hii wanatenganishwa na Mwanamke.
Alitembea mpaka stendi na kupanda daladala ili arudi Chang’ombe nyumba ya wageni aliyopanga.
Ndani ya daladala alikuwa ni mwenye mawazo mengi sana dunia aliona imemtapika,hakuamini kuwa amelala tajiri na kuamka maskini, ni kweli alikuwa fukara, maisha ya kifahari sasa kwake yaligeuka na kuwa historia tena kabla ya kifo chake kila mtu alisema ‘alikuwaga’. Mambo mengi sana yalipita ndani ya ubongo wake, hakuelewa kuwa Jaqlin angemuelewa endapo akigundua kuwa amefirisika alishaelewa nini maana ya umaskini.
Alishajua kuwa hakuna kitu kibaya kama kuwa fukara alielewa mateso yake kuwa maskini hathaminiki.
Alishuka taratibu na kwenda kwenye mgahawa ili ale chakula cha mchana.aliagiza ugali kisha kuanza kula.
“Jamani duniani kuna watu wawili wawili khaa”
Alisema Dada mmoja huku akimnyooshea kidole Adrian aliyekuwa anakula chakula, aliwatizama na kumtambua mwanamke huyo alikuwa ni Latifa,kumbukumbu zake zilirudi nyuma kwa kasi ya umeme na kumpeleka kitandani walivyokuwa wakifanya Ngono na starehe mbali mbali walizokuwa wakizifanya na kumbi mbali mbali walizokuwa wakitembea, alijisikia uchungu sana.
“kwanini Asha?”
“Yule mkaka namfanisha na Adrian,kaka mmoja hivi anaishi Tegeta ni boyfriend wangu sema tuliachana,jamani wanafanana kweli”
Alizidi kusema Latiffa huku akisisitiza.
Hawakuelewa kuwa huyo ndiye Adrian na wala sio mtu mwingine.
Adrian alipauka kupindukia nywele zake zilikuwa ndefu wala hazikuwahi kupitishwa kitana miezi mingi sana,nguo zake zilijikunja kunja hakuwa Yule wa miaka hiyo aliyekuwa anatesa na AUDI pamoja na JEEP akibadili kama nguo kila wakati akipigwa na kiyoyozi kama sio cha gari basi ofisi kama sio cha ofisi basi ndani ya jumba lake, na ndiyo Maana hata Latifa hakuweza kumfahamu achilia mbali kumtambua, ki ufupi dunia ilimpa kisogo!
***
USIKU wa siku hiyo ndiyo alikuwa akitembea akirudi Chang’ombe kwenye nyumba ya wageni aliyopanga ili akapumzike, lakini ghafla katika hali ya kushangaza gari lilimpita mbele yake na kumwagia maji baada ya matairi kuingia ndani ya shimo.
Alikasirika sana lakini aliishia kusonya hakuweza kufanya lolote zaidi ya kutukana tu, lakini gari hiyo aina ya Landcruiser Lexas haikufika mbali lilifunga breki kisha mwanamke mnene kiasi mweupe mwenye macho ya kusinzia
kushuka na kumuendea.
“Anco samahani”
Alisema Mwanamke huyo.
“Poa usijali”
Sauti ya Adrian ilimshtua Mwanamke aliyeshuka ndani ya Landcruiser Lexus na kumkagua Adrian alionekana ni kama mtu anayekumbuka kitu,
alijaribu kuvuta sauti hiyo na kumtizama Adrian kwa umakini sana usoni.
“Adria…n ndiye wewe au nakufananisha?”
“Ndiye mimi, vipi kwani wewe ni nani?”
“Adrian mimi Natu”
Adrian alishtuka mapigo ya moyo yalimdunda,Kweli pesa haina adabu Natu alibadilika macho ya bandia aliyoweka yalimbadilisha na kuonekana tofauti sana,alinenepa kiasi kwamba haikuwa rahisi kwa Adrian kumtambua kirahisi, marashi aliyopuliza yalisambaa kila sehemu.
Kitendo cha kumkuta Adrian katika hali hiyo kilimshtua sana!
“Mbona sielewi,nini tatizo huku unamfuata nani?”
“kuna mshakaji naenda kumuona hapo mbele”
“Mbona upo ivyo?au ndiyo ubachela”
Natu alimuuliza baada ya kumuona kiasi gani alivyokuwa rafu hajachana nywele.
“Naomba niende”
“No Adrian naomba uingie ndani ya gari”
Adrian alijifikiria kwa kitambo kidogo kisha kuingia ndani ya gari.
Adrian alitia sana huruma na machozi kumlengalenga,aliongea kwa uchungu mno wakiwa tayari wamefika nyumbani kwa Natu, alimuhadithia kila kitu lakini sio yote yaliyotokea.
Alimueleza tu habari za Jela na sio vingine, hakutaka kumwambia ukweli juu ya lolote lililotokea.
“Mhh Adrian pole sana,Mshukuru Mungu tu kwamba umetoka na sasa upo huru hilo ndo la kushukuru”
Natu alimtia Moyo,waliongea mengi sana siku hiyo na kula chakula cha usiku,ilibidi watupe tofauti zao mbali na kuwa marafiki lakini wa kawaida, hawakutaka kukumbushana yale yaliyopita hapo nyuma.
Kila kitu kilikuwa Shwari, siku zilivyozidi kwenda ndipo Adrian alipoanza kubadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida, alipelekwa saluni na Natu ili kumuweka sawa, alinunuliwa nguo na kurudi kuwa mtanashati kama hapo siku zilizopita hatimaye kuanza kuvutia tena,
Kila siku usiku walitoka kwenda kwenye kumbi tofauti za starehe, ulipofika usiku kila mtu alilala chumba chake.
Japo kuwa Natu hakupendezwa na hilo, Bado alikumbuka mapenzi aliyopewa na Adrian miaka mingi iliyopita, hakika hakuwahi kupewa na mwanaume yoyote Yule kamwe hilo alikiri.
Na ndio maana leo hii alifurahi sana kuwa naye karibu tena, na aliamini kuwa lolote atakalo taka kwa Adrian lingefanyikla kwa sababu tu alikuwa ana uwezo kifedha kuzidi yeye!
Usiku wa siku hiyo aliamka na kugonga chumba cha Adrian akiwa na nguo ya kulalia mapaja yake yapo wazi, ki ukweli alivutia sio masihara, weupe wake wenye matunzo uling’aa sana, chuchu zake zilizosimama zilichomoza na kuonekana,chupi aliyovaa ndani nyeupe pia ilikuwa ivyo ivyo,
Aliyalegeza macho yake,damu yake ilimwenda kasi sana akitamani kufanya Ngono na Nguli Adrian, aliamini hilo litafanyika dakika hiyo hiyo, maana Hata mwanaume uwe mbishi kiasi gani ni lazima mtego huo ungenasa na kukubali kufanya Ngono labda tu usingekuwa lijali.
Kugonga mara mbili tu mlango kulimfanya Adrian asimame kitandani na kuchukua taulo kisha kujifunika na kuuwendea mlango.
“Vipi?”
Aliuliza Adrian lakini badala ya Natu kujibu alimtizama kwa jicho la Huba.
“Adrian,njoo chumbani kwangu mara moja”
“Natu chumbani kwako kuna nini?”
“wewe twende tu nikakuoneshe kitu”
“Mhhh”
Adrian aliguna lakini katika akili yake alishaelewa ni kitu gani Natu anahitaji, ni jinsi alivyovaa tu na kuyalegeza macho yake,japokuwa alielewa hilo lakini hakuwa na uhakika sana, aliyatupa mawazo hayo pembeni na kuongozana na Natu mpaka chumbani ,
“Kaa kitandani Adrian”
“kuna nini Natu?”
“Subiri nifunge mlango”Mlango ulifungwa!
Natu alimsogelea Adrian na kuanza kumtomasa mashavu taratibu sana huku akikishika kifua chake.
Lakini Adrian aliitoa mikono na kusimama huku akimtizama kwa macho makali.
“Adrian”
“Nini?”
“Tafadhali naomba ukate kiu yangu kwa usiku tu wa leo”
“Hapana siwezi, kama umeamua kunisaidia kwa lengo kama hili kwa kweli naomba uniruhusu niende, kama nilivyokwambia nina mwanamke wangu tayari, siwezi kufanya kile unachokitaka habadani”
“Adria…n”
Natu alizidi kuwa msumbufu na kutoa nguo zake zote na kubaki kama alivyozaliwa ili tu kumshawishi Adrian, ni kweli damu yake ilimwenda kwa kasi ya ajabu!
Hakuna mtihani mgumu kama aliokuwa nao Adrian siku hiyo,ni kweli alikuwa mwanaume lijali lakini hakutaka kumsaliti Jaqlin Mpenzi wake,alikumbuka alivyomuhaidi Jaqlin kuwa atakuwa mwaminifu mpaka kufa, ivyo alishaupiga moyo wake ‘stop’ kutamani wanawake wengine!
Viungo vya mwili vilimsisimka sana baada ya Natu kumsogelea na kuanza kunyonya masikio yake MTALIMBO wake ulisimama taratibu na kuwa imara kama Mnara,
aliganda kama barafu huku akisikiliza nafsi mbili zikibishana ndani ya moyo wake, nyingine ilimwambia afanye nyingine ikimpinga.ilibidi achague moja kati ya hizo, Ilionekana nafsi ya kwanza ilikuwa na nguvu sana kuliko nyingine.
Hapo ndipo alimvuta Natu na kuanza kumpiga denda kwa fujo na kumtupa kitandani, alianza kumnyonya kila mahali hususani shingoni na kwenye masikio kisha kuanza kumnyonya maziwa juu ya chuchu, Natu alipiga kelele nyingi sana za raha,hasa mkono wa Adrian ulipofika chumvini kwenye nyama ya juu ndogo laini iliyokuwa teyari imesimama wima imetokeza nje.
Mashuka yalikunjwa kunjwa na Natu, weupe wake wote ulibadilika na kuwa mwekundu kiasi kwamba hakuwa na hali, jina Adrian ndilo lilitawala kinywani mwake, hakuwahi kupewa dozi kama hiyo.
Akili ya Adrian ilikuwa imeshahama teyari hakuwaza kingine zaidi ya kufanya Ngono na Natu na ndio maana kwa wakati huo ulimi wake ulikuwa kwenye Mgodi wa Natu anaulamba kwa fujo huku kinywa chake kikiwa kimejaa mate kama fisi aliyeona Mzoga.
Lakini ghafla alijitoa kwa Natu na kusimama wima, picha ya Jaqlin ilimjia kichwani alijiona ni msaliti sana na kukumbuka ahadi aliyemwambia.
Ahadi aliyomuhaidi Jaqlin ilikuwa kama ndoto ni lazima itimie, na ndiyo maana alisimama wima na kushindana na tamaa za mwili wake, hakutaka mwili wake umwendeshe bali akili ndio uendeshe mwili.
Natu alikuwa yupo hoi taaban hajiwezi tayari ameanza kulowana chini kwenye IKULU,
alikatishwa utamu uliokuwa teyari umeanza kunoga, lakini hakujua kichwani kwa Adrian nini anakiwaza.
“Adri…an njoo basi nakufa mwenzio”
Alideka Natu huku akiwa bado kitandani ana kiu sana, Adrian alimtizama na kuvaa taulo lake kisha kuufunga mlango baada ya kutoka nje!
Natu alisimama na kwenda mpaka chumbani kwa Adrian ambapo alianza kugonga bila mlango kufunguliwa,Adrian hakuongea chochote!
Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuingia chumbani kwake na kuanza kujishika shika maziwa huku akivuta picha ya Adrian ubongoni mwake,hiyo ndiyo ilikuwa tiba pekee na wala sio kitu kingine,alitoa miguno ya puani na kuchafua mashuka yaliyokuwa kitandani baada ya kufika mshindo,aliingia bafuni na kujimwagia maji kisha kujitupa kitandani.
***
“NIMEAMUA KUONDOKA HAPA KWAKO ASUBUHI NA MAPEMA, SIO KWAMBA KWA YALIYOTOKEA JANA HAPANA,NINA HOFIA KUENDELEA KUBAKI HAPA NITAKUUMIZA KIHISIA NAMIMI SITAKUWA TAYARI KUMSALITI JAQLIN NAOMBA UNISAMEHE KWA HILO,NAKUPENDA SANA NATU LAKINI NISINGEWEZA KUSHIRIKI TENDO LOLOTE NAWEWE,NAAMINI UMENIELEWA.
NI MIMI ADRIAN.
Hiyo ndiyo barua iliyokutwa na Natu asubuhi chumbani kwa Adrian ikimuacha Natu akilia machozi,alisikitika sana moyoni mwake,kumkosa Adrian alijikuta akilia machozi na siku hiyo hakwenda kazini kama siku zote, alibaki akimuwaza Adrian!
**
Hatimaye Adrian alipata Chumba kingine cha wageni na kuipumzisha akili yake huko, alimuwaza sana Jaqlin na hali yake ilivyokuwa ki ujumla,usiku wa siku hiyo simu yake iliita na kugundua kuwa ni baba yake mzazi Mzee Mwangenya ndiye anapiga, aliitizama na kuiweka Sikioni.
“Shikamoo BABA”
“Marahaba Adrian naomba keho uje kuna matatizo yametokea”
“Matatizo gani hayo?”
“Mkeo yupo Hospitali anaumwa sana, ana hali mbaya mno”
“Ba.. ba baba unasema? Ilikuwaje?”
“Nimemkuta shambani amedondoka anatoa damu puani, hapa tupo hospitali ana hali mbaya”
Adrian alihisi kuchanganyikiwa sana, moyo wake ulimwenda kasi, hakuwa na kingine zaidi ya kuwaza safari kesho yake asubuhi na mapema,
alimpenda Jaqlin kuliko mwanamke yoyote Yule aliyewahi kumpenda chini ya jua la Mungu, na ndiyo maana alikataa katakata kuvua nguo yake ya ndani na kushiriki tendo la ndoa na Natu usiku wa jana yake.
***
Adrian leo hii yupo njiani kwenye basi la kampuni ya Abood kuelekea Mbeya Mwakaleli, amechanganyikiwa mno simu aliyopigiwa na Baba yake Mzee Mwangenya usiku wa jana ilimchanganya akili yake kuwa Jaqlin amekutwa Shambani amezirai hana fahamu zake na yupo Hospitalini.
Laiti angekuwa ana uwezo basi angetafuta ndege mara moja na teyari wakati huo angekuwa Songwe amewasili lakini haikuwa ivyo ndio kwanza yupo Morogoro na basi limesimama,
Wenda dereva angejua ni kiasi gani Adrian ana haraka basi angelitoa gari kwa kasi ya ajabu sana.
“Kaka habari?”
Alimsalimia Msichana Aliyekaa naye kiti kimoja.
“Salama tu”
“Vipi unaonekana una mawazo sana”
“Ndio ni kweli”
“Nini zaidi?”
“Ni mambo tu ya kawaida dada angu,ni mambo tu ya ki utu uzima,naona unasoma soma simulizi hapo”
“Ndio tena imeniteka kweli kweli”
“kinaitwaje hiko kitabu?”
“BIKIRA YANGU”
“Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Bikira ya nani?”
“kinaitwa Bikira yangu,aise hii stori ni nzuri sana haiishi utamu natamani hata safari isiishe kwa kweli”
“kweli imekuteka, inahusu nini?”
“Mambo mengi ki ujumla,huyu aliyetunga hii simulizi kichwa chake kimetulia sana”
“Hakuna kitu, wewe sema hujawahi kusoma simulizi unamjua Joram Kiango?huyo ndiyo moto wa kuotea mbali kabisa hawa wengine wanabahatisha tu hawana lolote kwanza wanaiga iga”
“kama huniamini basi,wacha niendelee kusoma kitabu”
Walizidi kubishana huku Adrian akizidi kukiponda kitabu anachosoma Msichana anayeitwa Godliver,walifika Kitonga hotel ili kupata chakula cha mchana kisha kurudi tena kwenye basi.
Safari ilianza tena huku wakizidi kupiga Stori.Hakuna alichosimulia Godliva zaidi ya kukisifia kitabu alichokuwa akisoma,alimsifia sana Catherine msichana Jasiri na kumchambua tangu alivyotaka kujiua na sumu ya panya kisa mapenzi na baadaye kuwa shupavu.
Adrian alimskiliza kisha kupitiwa na usingizi kilichomshtua ni kishindo,Gari lilikuwa limegonga daraja.
“Kuna nini?”
“jamani tusali Ehh Mungu baba!”
Abiria mmoja alisema na kumfanya Adrian achungulie Dirishani, hakuamini macho yake,moyo wake ulipiga paa!baada ya kugundua kuwa wapo mlima Kitonga na gari limegonga daraja, tairi moja linaelea kuelekea kwenye bonde hilo hatari, kila mtu alisali sara yake ya mwisho Dereva alijitahidi kadri ya uwezo wake na kufanikiwa kulitoa gari kwenye bonde,
abiria walishangilia kama ikitokea manchesta wakifungwa na Arsenal au Arsenal wakifungwa na manchesta, kila mtu alimpongeza na kushusha Pumzi zake, bado waliendelea kupanda mlima huo kitonga wakikata kona kali lakini walipofika mbele basi lilionekana kuyumba yumba!.
Gia za gari zilishindwa kubadilika na kufanya basi lishindwe kupanda mlima huo mkali, na taratibu lilianza kurudi nyuma,Dereva alivyojaribu kupiga Breki haikuwezekana hatimaye gari kuanza kurudi kinyumenyume kwa kasi na kujigonga gonga pembeni.
NA KUGONGA Roli la mafuta lililokuwa nyuma, taratibu lilianza kuelekea kwenye mlima huo mabondeni,
Hakuna abiria hata mmoja aliyeweza kupona isipokuwa dereva ambaye alijitupa nje na kulishuhudia basi lake likiingia ndani ya bonde hilo kali,Adrian alisali sala yake ya mwisho akimuomba Mungu wake amsamehe dhambi zake zote alizozifanya za kuwaza,kunena na kutenda sababu alishazisikiaga habari za bonde hilo,basi lilivyofika chini tu kwenye mawe lilijipiga vibaya sana,kilichosikika ni kelele za abiria basi zima lilitapakaa damu.
Adrian mpaka hapo alihisi maumivu makali yasiyokuwa na mfano wake,damu zilimvuja kila mahali alimtizama Godliva Msichana aliyekuwa anaongea naye wamekaa siti moja, hakuyaamini macho yake baada ya kumuona amekatika kichwa amekufa hapo hapo.
Macho ya Adrian yalijaa ukungu aliona giza kwa mbali,aliutizama mguu wake uliokuwa umebanwa na bati unavuja damu kama maji.
“Nisa…diee”
Sauti hiyo ilitoka nyuma pembeni kwa Mzee wa Makamo aliyekuwa amevunjika mkono amebanwa na viti, baada ya kuongea hayo tu alikata roho hapo hapo!
Mapigo ya moyo ya Adrian yalianza kupungua kasi ya kudunda,macho yake taratibu yalianza kufumba kama redio inayoisha mabetri, alivyotaka kuongea chochote alishindwa,alihisi maumivu mengi sana kila mahali mwa mwili wake,
picha ya mwisho kumjia ni ya Jaqlin Mpenzi wake kisha kwa mbali kuona kiumbe cha ajabu kilichokuwa kina mapembe mawili kichwani,kina mguu mmoja, hakutaka kujiuliza maswali mawili, alishaelewa kuwa huyo ni Israel mtoa roho za watu na ndiye yeye roho yake inatakiwa kuchukuliwa,alikiona kinakuja usawa wake kisha kumshika mkono, hapo ndipo alipoona giza nene na macho yake kufumba!
***
“Dada unajisikiaje sasa hivi?”
“sasa hivi afadhali kidogo,lakini kichwa kwa mbali kinaniuma”
“Hausikii maumivu kwenye mgongo?”
“Hapana Daktari”
“Chini ya tumbo,karibu na kitovu?”
“Hapana pia sisikii”
“Okay, nitakupatia dawa uzitumie kwa muda wa siku kumi alafu urudi tena”
“Sawa”
Dokta Msami alimaliza kuongea na Jaqlin baada ya kuzinduka hospitali hapo masaa matatu yaliyopita tangu azimie siku ya jana yake, ni mimba peke yake ndiyo iliyomfanya mpaka azirai na ndiyo ivyo alivyoelezwa na dokta Msami daktari bingwa wa akina Mama wajawazito.
Baada ya hapo Jaqlin alipewa matibabu kisha kuruhusiwa sababu hakukuwa na kingine cha ziada cha kumfanya abaki kutokana na hali yake ilikuwa imerejea tena na kuwa na nguvu kama kawaida, lakini alisisitizwa na Dokta Msami kuwa asikae kwenye jua au kufanya kazi ngumu.
“Unaendeleaje ,Mwanangu?”
MZEE Mwangenya alimpiga swali Jaqlin baada ya kutokeza ofisini kwa Dokta.
“Niko sawa Baba,Uliongea na Adrian?”
“Ndio niliongea naye jana usiku naona yupo njiani anakuja sasa,maana hapatikani”
“Afadhali maana..”
Kwa kuwa hakukuwa na umbali wa aina yoyote ile ilibidi watembee taratibu kwa miguu mpaka nyumbani kwa Mzee Mwangenya ambaye alimchukulia Jaqlin kama mwanaye wa kumzaa, alimpenda sana na kumtunza vile vile,aliingia jikoni na kumtayarishia chai kisha wote kuanza kunywa, mpaka usiku unaingia Adrian hakupatikana hewani.
Hatimaye kesho yake kukucha, swala lilikuwa ni lilelile, Baadaye walizidi kumtafuta hewani bila mafanikio yoyote yale.
“Kapanda ndege au basi na hata kama kapanda basi,basi gani hilo asifike mpaka leo?”
Maswali hayo yalipita kichwani mwa Jaqlin, alishindwa kabisa kuelewa ni kitu gani kilimkuta Adrian na kumfanya azidi kuingiwa na hofu sana, lakini alijipa moyo kuwa wenda kuna matatizo yalijitokeza na ndiyo maana hakuwa hewani.
Wiki ya kwanza ilikatika na ya pili kupita hatimaye ya tatu mpaka mwezi unafika hakuna hata mmoja aliyesikia taarifa ya Adrian popote pale.
Wasi wasi mkubwa sana ulimuingia Jaqlin alishindwa kuelewa ni kitu gani akifanye, mimba yake ilishaanza kutokeza mbele tena kuwa kubwa sana,alitembea kwa shida, Mzee Mwangenya alihangaika naye kila kukicha mahospitalini.
HAKUWEZA tena kula sababu ya kumuwaza Adrian, kila siku alimsumbua Mzee Mwangenya juu ya yeye kutaka kwenda Dar es salaam ili kujua nini kilimpata Adrian wakati mwingine alihisi wenda alitelekezwa, na Adrian kesharudi katika tabia yake ya kubadili wanawake kama nguo, lakini hakutaka kuyapa mawazo hayo kipaumbele sababu alimuamini sana Adrian na teyari keshampenda, wakati mwingine aliwaza wenda Adrian amemkimbia kutokana na mimba aliyobeba haikuwa yake, ivyo mawazo yake yalimtuma kuwa Adrian hakutaka kulea mimba isiyokuwa yake.
“Nataka niende Dar es salaa Baba”
“Na hiyo hali? hapana mwanangu”
“Kwanini sasa?”
“Siwezi kukuruhusu uwende huko, baki kwanza angalau hata ungekuwa umejifungua sawa, lakini hilo mimi silihafiki kama Adrian yupo atafika, lazima afike mahali hapa, hapa ndiyo nyumbani kwao”
“Lakini hata kama Baba atakuwa ana tatizo wenda”
“sawa sikatai lakini inakubidi uwe mvumilivu mwanangu,Adrian yupo nina uhakika atakuja tu”
“Sasa yuko wapi?”
“Si unajua mambo ya wanaume kutafuta Mwanangu, cha kufanya inakubidi uwe mvumilivu tu”
Mzee Mwangenya ilibidi akae chini kitako akitumia maneno ya busara kumshawishi Jaqlin akubali kubaki kwani hali yake haikuwa nzuri, alikua ni mjamzito sasa wa miezi saba tayari! hatimaye maneno yake yaliazaa matunda kwani Jaqlin alimuelewa na kuamua kubaki akimsubiri Adrian.
****
Machela ilizidi kusukumizwa kwa kasi sana huku manesi wakipiga kelele za kuomba msaada wa haraka sana kwani mgonjwa aliyekuwa juu ana hali mbaya ana vuja damu nyingi sana, Madaktari walipomuangalia tu walitingisha vichwa vyao kuashiria kuwa hakukua na matumaini ya kupona kwa mgonjwa huyo labda pengine utokee muujiza wa Mungu.
Ungeuona uso wake usingethubutu kusema kuwa huyu ndiye Adrian aliyetingisha Jiji la Dar es salaam kwa utanashati, sura yake iliharibika vibaya mno, aliumuka kama andazi lililowekewa Amira,kati ya abiria hamsini waliopona wanne peke yake ambao walikuwa majeruhi wengine arobaini na sita walipoteza maisha baada ya basi la Abood kutumbukia kwenye korongo la Mlima Kitonga,
kilichowasaidia ni gari la kubeba wagonjwa lililokuwa limepeleka wagonjwa teyari na kupita maeneo hayo wakati basi la Abood linapinduka, Wauguzi na wasamaria wema ndiyo walioshuka chini mabondeni kwenye miti kisha kuanza kuwaokoa watu, ilikuwa ni ajali mbaya ya kutisha iliyotangazwa maredioni, kila Mtanzania aliguswa sana,na hiyo ndiyo ilikuwa ponea ya Adrian.
Hakuwa anaelewa lolote linaloendelea ulimwenguni alikuwa nusu mtu nusu maiti.
Haraka haraka kitanda chake kilisukumizwa mpaka kwenye chumba kilichokuwa kidogo chenye mikasi na madawa mengi kwa ajili ya upasuaji, madaktari tisa walizama chumba cha operesheni kila mtu akiwa bize na Mgonjwa huyo aliyekuwa mahututi.
Sindano za kuzuia sumu mwilini zilichomwa kwenye mishipa ya Adrian kisha baadaye kuchomwa sindano za ganzi,
harakaharaka walianza kumsafisha vidonda vyake, mguu wa Adrian ulikuwa haufai kabisa mfupa wa ndani umelika,na kupona ilikuwa asilimia mbili tu.
“Huu mguu wa kukatwa”
Alishauri daktari mmoja wao.
“Hakuna njia nyingine?”
“Hapana, inabidi tuukate ili tuzuie sumu isipande juu”
“Sawa”
Madaktari baada ya kushauriana ndani ya chumba cha upasuaji walikuja na wazo lingine jipya la kukatwa kwa mguu wa Adrian kabisa na abaki na mguu mmoja,
kila daktari aliliunga mkono wazo hilo. Na taratibu za kuanza kukata mguu wa Adrian kuanza.
“Lakini Dokta subiri”
“Nisubiri nini muda unakwenda dawa inaisha nguvu”
“Hakuna haja ya kukata huu mguu, kwani kuna njia nyingine pia”
“Njia gani?”
“Nitakuelezea baadaye, embu tujaribu kumpeleka huyu mgonjwa kwa Dokta Sai mtaalamu wa mifupa wenda anaweza akasaidia kitu au kutoa wazo”
“Sawa”
Hapo ndipo walipoachana na Mguu wa Adrian kisha kuendelea na matibabu mengine.
Masaa Matatu baadaye operesheni ilikuwa teyari imekamilika ivyo walisukuma kitanda mpaka chumba cha wagonjwa maututi na kuwekewa Dripu ya dawa pamoja na mashine ya kupumilia.
Adrian aliendelea kutibiwa chini ya usimamizi wa Dokta Sai daktari bingwa wa mifupi aliyehamishiwa Mkoani Mbeya akitokea Muhimbili hospitali ya Taifa ya Dar es salaam! Kitendo cha kuuwona mguu wa Adrian alitingisha kichwa kuashiria kuwa hakuna njia nyingine zaidi ya mguu huo kukatwa tu,
lakini hakutaka kuyapa nafasi mawazo hayo, hapo ndipo alianza kufanya mawasiliano na Madaktari bingwa wenzake! Alielewa ni kiasi gani mgonjwa huyo angeteseka endapo angekatwa mguu aliingiwa na huruma alishaelewa mateso yake.
Baada ya kutafuta jibu kwa muda mrefu hatimaye alipata ushauri,ilibidi Adrian aingizwe tena kwenye chumba cha upasuaji hapo alipasuliwa na kuingiziwa machuma miguuni ambayo baadaye yangesaidia kuunga mifupa yake, wakati hayo yanafanyika Adrian hakuwa anaelewa lolote linaloendelea, wiki tatu zilishakatika ndipo kwa mbali alianza kufumbua macho yake na kuona mwanaume mwenye mvi yupo pembeni yake amevaa koti jeupe na miwani kubwa ya macho.
“Ni….po wapi?”
Hilo ndilo swali la kwanza kuliuliza baada ya kuvuta kumbu kubu zake nyuma na kushindwa kuelewa ni wapi alipo.
“upo Kitonga hospital?”
“Hospital?,nini kilitokea”
Ilibidi Dokta Sai aanze kumuelezea Adrian kinagaubaga tangu alivyoletwa hospitalini hapo na hali yake ilivyokuwa kwa ujumla, Adrian alilia machozi picha ya kwanza kuikumbuka ni ya kiumbe cha ajabu kilichokuwa kinamvuta kisha baadaye kuanza kukataa hali ya umauti.
bado alikua haamini kama yupo hai anapumua.
“Inabidi wiki ijayo twende Hospitali ya wilaya tukaangalie mguu wako tena”
**
*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
0 comments:
Post a Comment