Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 7/10


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 7 KATI YA 10
*******
 *******

bila kujua wana kiweka kifo chao karibu kwa kitendo cha kumuweka Witness karibu yao, wali panda
Ngazi na Witness kuwa omba waende VIP ambapo pia,

Witnes aliiomba watoe pesa wakodi sehemu nzima, kweli kitendo kile kili fanyika huku Witness akiwa amevaa miwani yake vizuri sana na wigi jekundu kichwani, na kumfanya isiwe rahisi kugundulika.

walianza kunywa pombe kali na kuanza kulewa huku Witness akiji fanya nayeye amelewa akizidi kuwa lewesha kuliko ,maelezo,

baada kuha kikisha kila kitu kimeenda sawa alitoa kisu chake na kumsogelea Shirima ambaye alikua amelewa sana


 Hakutaka hata kupoteza sekunde moja hapo alijua huo ndo muda pekee wa kufanya kazi iliyo mpeleka, aliangalia pembeni na kumuona baunsa wa club ile amewapa mgongo na hatoweza kuona kile kitakachoendelea, kwa nguvu sana alitumbukiza kisu kile tumboni mwa shirima na kufanya damu nyingi ziruke zikiambatana na kelele nyingi sana ila kutokana na mziki mkubwa wa club iyo sauti ile haukuweza kwenda popote pale aliyokua akipiga Shirima,

alichukua chupa ya wyn ili kua mezani na kuipasua na kubaki nusu ambapo upande wa pili kili baki kipisi chenye ncha kali sana. bila kupoteza muda wa aina wowote ule alimfuata mwingine ambaye alikua amelala kwa kunywa pombe nyingi na kuitumbukiza chupa ile shingoni,

kweli yalikua ni mauaji ya kinyama sana ambae bina damu yoyote yule hawezi kufanya ila kwa Witness kutokana na hasira ana jikuta ana tenda dhambi ile ya kuua tena kinyama kupita kiasi, alivyo hakikisha kila kitu kimeenda sawa ana mfuata mwingine na kumvunja shingo na kumchoma kisu tumboni na kufanya utumbo umwagike chini,

kwa hasira sana hasa alipo kumbuka shirima alivyo kua aki mbaka mama yake mzazi alimfuata pale chini kwa hasira na kuya toboa macho yake yote mawili bila huruma yoyote, roho ya kikatili ili muingia na kuhisi kama kuna kitu kime mkaba shingoni hii ni kutokana na hasira aliyokua nayo kupita kiasi,

mambo yaliyo kua yana tendeka juu V,I,P hakuna hata mmoja aliyeweza kujua na hakuna hata mtu mmoja aliye gundua kuwa kuna mauaji ya kinyama yana endelea , alivyo hakikisha kila kitu kimeenda sawa sawia, alienda bafuni na kuvua gloves za mkononi alizo kua amezivaa kwa nia moja tu asije kujulikana pindi wata kapo pima alama za vidole.

baada ya kumaliza kila kitu na kunawa alivua wigi lake jekundu pamoja na miwani na kuviweka ndani ya mkoba wake na kurudia katika sura yake ya kawaida.

amabapo ana tumia upande wa pili kutoka, na kushuka chini ambapo mziki uli kua unaendelea kupigwa kama kawaida bila kujua kuna mauaji ya kinyama sana yame tokea.

aliji changanya kat kati na kuanza kucheza mziki peke yake huku akita futa njia ya kutokea, ana toka na kuingia tena bafuni ila kabla kufanya chochote ana hisi ana shikwa bega na kugeuza shingo na kumuona mwana mke mrefu w wastani na mweusi kiasi,
"dada nime kuona ume tokea kule VIP, nani Shirima, bado yupo kule juu"?
"aaah, nani mimi?, Shirima yupi huyo"?
"alipandisha kule na mwana mke aliye vaa wigi hivi jekundu"
"mi simjui huyo unae muulizia"
"any way ngoja niende"

Dada yule ambae alimuona Witness ana shuka muda mfupi VIP ambapo alimuona mara ya kwanza Shirima kapandisha juu, hakuzoea kumuona Shirima akiingia ndani ya club ile bila kumnunulia kinywaji au kwenda nae kulala nae wote iki bidi, ivyo anaamua kwenda juu kumuulizia kabla haja ufikia mlango Witness ana muita
"ulikua una muulizia Shirima"?
"ndio Shirima"

Witnes alitembea mbele mpaka mlango wa bafuni na kusimama huku akivaa Gloves zake na pale pale kutoa kisu chake.
"sikupenda kuku uaa ila samahani kwa kufanya ivi"

Witness alimsogelea Dada yule na kumchoma kisu tumboni, ambapo alikizungusha zungusha baada ya kuhakikisha dada yule kakata kauli , alivua shati lake na kuonekana akimchora dada yule kifuani kwake, huku kifua kile kikiwa kina toa damu nyingi,

ki ukweli mauaji yale yaalikua ya kinyama sana kupita kiasi, alivyohakikisha kila kitu kimeenda sawa alinawa tena na kutoka mule na kuanza safari ya kuondoka zake, nia ya kumuua dada yule ilikua moja tu kupoteza ushaidi na sio vinginevyo

*********

Mauaji ya hatari yana zidi kutokea nchini Tanzania katika maeneo tofauti tofauti . ulinzi una zid kuimarishwa kila kona ya pembe ili kumdhibiti muuaji huyu ambae mpaka kipindi hiko hawa kujua ni nani na kutokuelewa kwanini ana ua kikatili kiasi hiko,

sababu aliua kiakili na kuonekana ni jasusi, leo hii jeshi la polisi tena wana pokea habari mbaya ya kifo cha Mr, Sombe ambapo yeye na mke wake wote wali uwawa kinyama usiku wa siku hiyo, huku walinzi wote wakiwa wame uwawa nje ya nyumba hiyo kubwa, na kufanya jeshi la polisi wazidi kuchanganyikiwa sana, na kuanza kuka mata kamata watu ovyo ili kuka milisha upelelezi wao,

baada ya siku tatu kupita baada ya kifo cha Mr, sombe wana pokea habari mbaya sana za kukutwa kwa maiti ili yokutwa ime chomwa moto uku ikiwa ime fungwa kamba, ambapo mbele yake kulikua pia na gari lime chomwa moto pia ,

"hapa nashindwa kuelewa Cassimu, hiki kifo, gari hili lime chomwa moto, huyu mtu kachomwa moto alafu kafungwa kamba na hili gari, mbona sielewi aise"

askari mwingine alihoji na kuonekana kama amechanganyikiwa ilikuwa ni pembezoni mwa bara bara ya moro goro rod, ambapo ili kutwa maiti hiyo imechomwa na mafuta ya patrol pamoja na gari hilo,,
"hapa nashindwa kuelewa kabisa, ila una ona hii damu ime tokea kule, huyu ina elekea alikua akiburuzwa nadhani"
"sasa aliye mburuza huyu sawa, sikatai maana hata mimi nimeona damu hizo, na nani kachoma hili gari moto"?
"tusiende mbali sana, subiri niangalie engine ya hili gari na namba zake, nitajua mmliki wa gari hili na tu tamkamata leo hii hiii. embu njoo tuangalie namba zake za usajili"
"una akili sana"

walitembea kwa pamoja na kwenda mbele ya gari na kuangalia namba za gari hiyo. kweli waliziona namba za gari hilo na kutoa redio upepo huku wakitoa taarifa TRA waweze kujua ni nani mmiliki halali wa gari hilo,

katika kutembea pembeni wana okota wallet na kuangalia kitambulisho ambapo juu ya picha kulikua na mwana ume
"Rameck Maduu, nahisi ndo hili lifuzu hapa, jina lake Rameck, ndo hii picha yake"
"ndo jina la marehemu sio"?
"ndio ana itwa Rameck"

picha zili endelea kupigwa huku watu wakizidi kusogea karibu na eneo hilo huku wengi kushindwa kuangalia mara mbili mbili jinsi Rameck alivyokua kuwa ameuwawa kwa kuchomwa moto ambapo lili onekana fuvu la kichwa likiwa lime toa meno, kwa mtu ambae hana moyo wa kinyama asingeweza kuangalia mara mbili mwili huo uli okua chini pale.

"okay, afande mmiliki wa gari hili anaitwa Msabaha HAMISI, "
"ana patikana wapi"?
"hapatikani popote"
"una maana gani sasa, ukisema ivyo"?
"ina onekana huyu mtu alifariki muda mrefu sana, hapa nina maana gani ujue, huyu muuaji kajipanga sana, ana trick sana , na ana mbinu zote ni jasusi, hapa kuna kazi ya ziada"

aliongea polisi huyo huku akimwangalia mwenzake kwa umakini sana ambaye alikua ameacha mdomo wazi maana hakuwahi kuona wala kusikia mambo anayosikia.

******************************************
 Ilibidi safari hii jeshi la polisi kitengo cha upepelezi waingilie kati CRIMINAL INVESTIGATION DEPERTMENT(CID), kutokana na serikali ili yokua madarakani kuona wana chama wenzao wakiuwawa
na wengine kupotea katika mazingira ya kutatanisha sana, jambo hili lina muumiza sana kichwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Steven Alinga na kubaki akichanganyikiwa hasa baada ya kifo kingine cha naibu spika Furaha Moses, ambae alikutwa chumbani kwake amenyongwa kwa kamba ya manira,

mwenyewe kimnya kimnya anaamua kuita kikao kidogo ndani ya ikulu yake, ambapo aliwaita wapepelezi wapatao kumi na moja akiwemo mkuu wao wa kitengo hiko Mr, vicent Towo ambae kila mtu alimuamini kuwa hafanyi makosa katika kazi yake ya upepelezi, Vicent Towo, alitengeneza sana sifa ndani ya Nchi hiyo yab Tanzania hakuna kile kilicho mshinda tangu aanze kazi yake ya upelelezi, leo hii RAisi wa jamhuri ya muungano ana muita na kumpa kazi hiyo ya kumtafuta gaidi huyo anae ua kikatili,

"naamini mtafanya kazi hii vizuri, mki kwama popote pale, msisite kuniambia, haiwezekani huyu mtu auwe watu kikataili kiasi hiki, naomba hili swala lifanyike kimnya kimnya. umakini wa hali ya juu, nafikiri hamto niangusha kwenye hili"

Aliongea raisi Steven Alinga huku akionekana mwenye hofu kupita kiasi. ndani ya ikulu akiwa na jeshi hilo kitendo cha upepelezi,
"muheshiwa Raisi, nadhani una ijua vizuri kazi yangu bila shaka, nakuhaidi ndani ya masaa arobaini na nane, muhalifu ata kua amepatikana, mimi Vicent Towo, nina uhakika nita fanya hii kazi, sija wahi kushindwa hata kidogo"

aliji kweza Vicent Towo, bila kujua mtu anaye mtafuta ni hatari sana kupita maelezo.
"alafu nili sikia muuaji ni mwana mke"?
alihoji Raisi
"muheshimiwa Raisi, sina uhakika kwa hilo, ila sidhani kama ata kua ni mwana mke, au kama ni mwana mke, ata kua ni hatari sana,inaonekana ame jipanga sana"
"sawa! haijalishi ni mwana mke au mwanaume, bibi au babu, swala la msingi nataka atiwe kizuizini mara moja"
"sawa Mheshimiwa Raisi"

Kikao hiko kidogo kiliisha ambapo kili tumia dakika thelathini tu, wapepelezi hao walitoka nje na kuingia ndani ya magari yao na kuondoka zao, huku wakimuahidi raisi ategemee mema na mazuri kutoka kwao

******************

"cheeeerssss"

ili kua ni sauti ya blandina wakiwa ndani ya baa moja ilio kua sinza al maarufu kama dagaa dagaa, walikua wasichana watatu mmoja wao akiwa Witnes Kafifii, akiwa mwenye furaha sana kupata marafiki hao, ambao upande wa pili hawa kujua kama Witnes ndie muuaji,

"Linnah, vipi huongezi kinywaji?"

alihoji rafiki huyo na kumuangalia Witness ambae wakati wote wali jua anaitwa Linnah, hakutaka wamjue jina lake kamili kwa wakati huo,
"noo preciuos, hapa naji fikiria, twende club gani baadae"
"leo sunciro hapo,"
"sunciro nawewe kila siku una kibuzi nini"?
"aaah wapi, kibuzi bongo, bongo kuna wana ume basi, wote wababaishaji, sisi tuna pesa bwana, eti Blandina na Linnah kuna wana ume wa kutu babaisha sisi"?

aliongea Preciuos huku akipiga fundo la Wyn, ki ukweli wana wake hao watatu walikua wakiji weza kupita kiasi, walikua na pesa ivyo, wali tumia kufanya starehe mbali mbali, Precious mjomba wake alikuwa ni waziri mkuu wa Tanzania huku Blandina babu yake alikua mkuu wa Mkoa, nia na lengo la Witness ili kua ni

kuwaweka karibu watu hao , ili kua kwa lengo moja tu amalize kazi yake kiurahisi. aliamini kitendo cha kuwaweka watoto hao wa vigogo karibu, angeweza kuwa pata pia watu aliowatafuta kwa muda mrefu, upande mwingine mkuu wa mkoa ambae ni babu yake na Blandina alikua akimtaka kimapenzi Witnes sababu alijulikana mpaka kwa akina Blandina, siku aliyo mpeleka kwao, na ndo hiyo siku mzee huyo alianza kumsumbua Witnees bila kujua anajiwekea kifo karibu

, ila hakutaka kumwambia Blandina, aliamua kufanya jambo hilo liwe siri na amuuwe babu yake ambae ni mkuu wa mkoa kwa siri kubwa sana tena taratibu mno

kweli alidhamiria kuuwa bila huruma, na kila alilo lifanya aliili fanya kwa umakini wa hali ya juu, alijua bado ana kazi nzito sana mbeleni kupita maelezo, ila alipiga moyo konde na kujua kivyovyote vile ata imaliza,

"Leo sunsiro, Leo sunciro, tuwashe magari yetu baadae tuku tane pale, tunywe tulewe. maisha mafupi haya, YOLO you only leave once(tuna ishi mara moja tu")

aliongea Precious, katika kundi hilo la watatu yeye ndiye aliye onekana mwongeaji kupita wenzake wote, alisikia nyimbo ya kisanola ya Koffi iki pigwa na kuanza kucheza akienda sawa nayo,
"precious kaa chini, usha lewa wewe mwana mke"
aliongea Witness
"aaah wapi, nina furaha tu Linnah"

waliendelea kunywa na kula bata, mpaka ilivyo fika mishale yaa saa nne usiku, na kuagana baadae wakutane Sunsiro waendeleze sterehe yao ya kula bata,

kweli kutokana na kila mtu alikuja na usafiri wake waliwasha magari yao,na kutembea huku nyuma wakiacha gumzo kwa wanaume waliowaona, kutokana na wasichana hao watatu kuwa wazuri na muda wote waliongozana pamoja,

**********

Prado, Landcruiser Rexus na Verrosa, yalikua yame paki nje ya club hiyo kwa pamoja yalionekana yalikua yame ongozana na wote kushuka wakiwa wamependeza kupita kiasi, kila mtu siku iyo alitaka kumfunika mwenzake kwa kupendeza ila mwisho wa siku wali jikuta wote wame pendeza sana,

na kufanya kila mwana ume awakodolee macho, wakiwa tamani japo kwa usiku mmoja,waliingia ndani ya club na kutafuta sehemu nzuri ili yokua tulivu na kuka huku wakiendelea na vinywaji na stori huku wakiwa na furaha sana.

"samahani dada angu"
aliomba muhudumu wa club hiyo huku akiwa masikioni mwa Witness
"bila samahani"
"kuna wakaka pale wame sema mna tumia vinywaji gani, hasa ana uliza wewe hapo, una kunywa nini"?
"hahahahaha"

Witnes alicheka na kuwa geukia wenzake
"nini tena Linnah"?
"msikilizeni huyyu, kuwadi. embu rudia tena kaka"

ili bidi muhudumu yule arudie tena na kuwa fanya wote wacheke kwa dharau,
preciuos alisimama na kumsogelea muhudumu yule
"sikiliza, fanya ivi, bili yao sisi tutalipa, alafu kitu kingine, waambie wanywe mpaka walewe, na nina kupa pesa nyingine ya wattu ishirini wa kwanza kuja kununua vinywaji weka kwenye bili yangu mimi hapa, hakuna mtu mwenye shida hapa, hatubabaiki sisi"

aliongea Precious huku akiwaangalia watu wale ambao kwa haraka haraka walikua watu wa kawaida sana
"hahahahahahaha precious huyoooo, wape wape, namimi natoa laki yangu, uka wape, walewe, hatuna dhiki hapa"

Witness nayeyey aliongea, ki ukweli muhudumu huyo alishangaa sana, pale pale alipewa pesa zile na kurudi huku akiwaacha WAkina Witnes wakicheka sana,

"usijali usijali, wewe nenda tu"

ili kua ni sauti ya mmoja wao kati ya watu waliomba kumpa Witnes kinywaji, ki upande mwingine walikua ni wapepelezi ambapo, kati yao alikua ni Vincent Towo,
"msijali, humu hawatoki wote hawa,"

Aliongea Vincent Towo huku akizidi kuwa piga jicho warembo wale, kwa nia moja tu kuwa tia mikononi mwa sheria ili kuka milisha upelelezi wake...

 "hawa lazima tujuwe wana poishi hasa yule aliye vaa pink yule,"

Aliongea Vincent Towo mkuu wa wapelelezi akiwaambia wenzake ambao wote walibaki kumwangalia Msichana huyo ambae alikua ni Witness,

Witness, Blandina na Precious waliendelea kunywa pombe wakiwa wenye furaha sana bila kujua ndani ya club hiyo kuna wapelelezi , wote waliingia kati kati na kuanza kucheza mziki wakiwa watatu, wana ume waliojisogeza karibu kujaribu kucheza nao wali kataa kata kata na kuendelea kucheza kivyao wakiwa wame tengeneza

duara na mmoja mmoja kuingia kati kati kucheza kwa zamu,

usiku mnene uliingia tayari na mshale wa saa kugonga saa tisa na kuamua kutoka nje ili kila mtu arejee kulala sababu walikua wame choka sana, wali agana na kila mtu kuingia ndani ya gari lake,

wapepelezi wale nao hawa kucheza mbali waliingia ndani ya gari yao aina ya Mark x na kuanza kumfuatilia Witness ambae alikua ana tumia Land cruise RExus, wali mfuatilia nyuma nyuma bila Witnes kujua,

ivyo ndivyo ili vyo kua, hisia kali juu ya Witness japo alikua hana uwa kika kama ni muuaji vina jijenga ndani ya akili ya Vincent Towo, ivyo ana aamua kumfuatilia ili ajue ana poishi akiamini hiyo ndiyo ita kua hatua ya kwanza amabayo ita mpelekea, akamilishe upelelezi wake,

"usi msogelee karibu, endesha mwendo wa kawaida, hakikisha tuna muacha mita kama ishirini hivi"

alitoa maagizo Vincent Towo akimwambia Dereva huo ambae alitii na kupungguza mwendo kasi wa gari, waliona gari ya Witnes ina kata kushoto na wao kukata kona, kila alipo enda na wao wali kua nyuma yake ki umakini sana,

Kila sekunde Witnes hakuacha kupepesa macho yake njee ya vioo vina vyoitwa site mirror kama wafa nyavyo madereva wengine ili kujua nani yupo nyuma, ila kila alipoangalia kioo cha njee aliliiona gari hilo aina ya mark X lipo nyuma yake mita chache tangu muda mrefu, aliangalia tena kioo cha kati kati na kuwaona wana kuja alikunja kona na kuliona pia gari hilo lina kuja nyuma yake.

alichukua simu yake ya mkononi na kuta futa namba ya Precious na kumpigia simu.

"mamii vipi usha fika?"
"aaah bado,! vipi wewe?"!
" nipo salenda bridge, embu angalia nyuma yako hakuna gari yoyote ina yokufuata"?
"mmmh embu ngoja,,, hakuna kwani vipi"?
"kuna , mark x ina ni fuata tangu muda mrefu sana"
"okay nime kumbuka, hilo gari nililiona kabla huja ondoka walianza kuku fuata tangu pale club, mi nika jua wana safari zao, ni jeusi"?!.
"ndio"
"ndo hilo hilo."
"poa asante"

Witnes alikata simu na kuto kuonesha hali yoyote ile ya kuongeza mwendo, alicho fanya aliona U turn na kuzungusha gari na kurudi alipo toka, kweli alivyo angalia tena aliona gari ile ina mfuata,
"hawa wata kua akina nani"?!

aliwaza Witness huku akiingia patrol Station. alivyo simama patrol Station aliliona gari hilo lime paki pembeni kidogo na kupata uhakika kweli wana mfuata,

kwa mwendo wa kawa ida kabisa aliendesha gari huku akiwaangalia, baada ya dakika arobaini aliingia bara bara ya mwenge na kunyosha moja kwa moja mpaka Mlimani City,

ambapo alishuka na kuchukua simu yake huku akiingia mlimani city, bado alili ona gari lile limepaki kupitia kioo cha mlango wa mbele yake, alivyo ingia ndani ali tembea haraka haraka na kutokea mlango mwingine wa kutokea na kutoka nje kwa miguu ambapo aliita bajaji,

"nipeleke Msasani"
"msasani ipi"?"
"twende twende nita kwambia huko huko"

bajaji ili washwa na kuondoka zake na kuliacha gari lake mlimani city.

*****
"shiiit, yuko wapi sasa? tuna msubiri mpaka sasa hivi""?
"atakua alijua tuna mfuata yule"
"ah wapi sio rahisi, sio kirahisi Brian"
"tuendelee kumsubiri hapa hapa, hawezi kuliacha gari hapa, lazima atarudi"
"poa embu tusubiri"

yalikua ni maongezi ya wapelezi hao ambapo baada ya kumsubiri Witness kwa muda mrefu sana bila kutokea, waannaa mua kuingia ndani ya gari na kuondoka zao huku waki haidi kuwa kesho yake wange rudi asubuhi sana.

********

"sasa Linnah, vipi mbona huku niambia ule mpango wetu, eti binti, nataka niba dilishe maisha yako, au hujui wadhifa wangu hapa mkoani"?!

ili kua ni sauti ya Mkuu wa Mkoa kupitia njia ya simu asubuhi hiyo
"najua wewe ndiyo ni mkuu wa mkoa, sasa huoni hatari kucha fua jina lako"?
"tuta fanya siri sana, kwani nani ata sema, na kutumia nauli una enda DODOMA tuna malizana huko huko, we usha kuwa mtu mzima wewe, mtoto mzuri kama wewe una hitaji matunzo kutoka kwa watu kama sisi. bunge litaanza wiki ijayo, cha kufanya wewe uta tangulia kule, mimi nita kuja huko huko mrembo, au sio Mama"?!
"sawa hakuna shida yoyote"!.
"ila usi mwambie huyu rafiki yako Blandina sawa"!
"usijali kwa hilo sito fungua kinywa changu hata siku moja"

Witness alikata simu akiwa upande mwingine ana furaha sababu anaenda kumaliza kazi yake nyingne ya kumuua mkuu wa mkoa Joel Nchwari , jambo lile lina mfurahisha sana, na kuingia bafuni ambapo alijimwagia maji na kutoka,

alienda kwenye kabati na kulivuta pembeni ambapo kulikua na mlango mwingine wa siri, aliufungua na kuingia chini ndani ya andaki ambapo aliwasha taa, na kwenda uku tani ambapo kulikua na picha za watu nyingi,

ambapo watu waliokufa waliwekewa X na moja kwa moja kuweka duara kwenye picha mkuu wa mkoa,
kumaanisha kwamba ndie anae fuata.
"wewe una fuata, hahahaha, kesho uta wasalimia uendako"

aliongea Witness huku akicheka kicheko cha dharau, alitoka ndani ya chumba kile na kurudishia kabati lile na kufanya mtu yoyote yule asiweze kujua kama kuna mlango wa aina yoyote ile. kili kua ni chumba cha siri sana, hata mtu yoyote yule asingeweza kujua kama kuna mlango.

alivaa nguo chap chap na kushuka ngazi,

"we mzee"
"Naam MAMA"
alikua ni mzee wa getini ambapo muda wote alikua na mtutu aina ya SMG begani kutoka katika kampuni ya KK security,
"naomba usi mfungulie mtu yoyote yule geti mpaka ruksa kutoka kwangu"!.
"hata Fr.."
"nime sema mtu yoyote yule, asifunguliwe geti"
"sawa Mama"

Witnes alitoka nje akitembea mpaka dukani ambapo hupenda mara nyingi kununua vitu vidogo vidogo kama chumvi, sukari , vochA n.k

"mangi, nipe sukari kilo mbili, sukari ime niishia"
"sawa mamangu . "
"nipe na kamba ya manira"
"hivi mama lile jumba lote una ishi peke yako yesu na maria""?!.
aliongea mangi wa dukani kwa rafudhi ya kichaga.
"ndio, vipi una taka uje tuishi wote"?
"ndio ni tafurahi sana, yaani nitaa muacha Mama Manka kule moshi. Marangu Mwika"
"hahahaha wewe mangi, uta filisika urudi moshi ukalime, shauri yako"
"nipe iyo nafasi basi"
"huna ela wewe, una uwezo wa kunipa laki tatu kila siku"?
"yesu !yesu !yesu !yesu !yesu!, pesa yote hiyo upeleke wapi?, yesu wangu, laki tatu, yaani laki tatu kila siku, yewomiii, ngashtuka mae laki tatu'"
"hahahahaha"

Witness alicheka sana hasa mangi huyo alivyo kua akitoa macho yake, huku akishangaa na meno yake ya rangi kuonekana, kweli habari zile zili mshtua sana mangi kupita maelezo
"una ona sasa, tatizo nyie wachaga wa kibosho bahili sana, nipe vitu vyangu niende"!
ki ukweli Witnes ali mpenda sana muuza duka huyo sababu alikua aki mchekesha sana na vituko vyake, ivvyo walitokea kuzoeana sana.

Alivyo fika nyumbani kwake alipaki nguo zake ndani ya begi na kuweka ndani ya begi na kamba ya manira, alichukua bastola yake na kuiweka chini ya begi lake na kuweka nguo izo juu yake, kwa ajili ya safari ya Dodoma ambapo mkuu wa mkoa alimwambia wakutane huko, ila upande wake alikua na nia moja tu amuuwe na ampoteze duniani , ivyo ndivyo akili yake ilivyo mtuma.
"Halloo, Beni, gari nimeiacha mlimani city.!"
"gari lipi BMW"?
"hapana RExus, nita muachia funguo huyu mlinzi uende ukalichukue, sikia kwa makini, litumie kwanza"
"yaani sija kuelewa"
"litumie tumie kwanza wiki ijayo uli rudishe, au mpaka nita kapo kupigia simu"
"kwani una safiri?"
"hapana nipo"!.

Maongezi hayo kupitia simu yali katwa huku Witness akiwa ana jiandaa kwa safari moja tuu, kumuua mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, siku chache zijazo, haku taka kumwambia mtu yoyote yule juu ya safari yake hiyo ata kayo anza kesho.....

 Magari aina ya Landcruiser v8 yalizidi kuchanja mbunga, magari takribani sita yalizidi kutembea kwa kasi ya ajabu sana huku magari mengine yakiwa pembeni ulikua ni msafara wa Mh, JOel Nchwari mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akielekea Dodoma huku akisindikizwa na msafara huo na ulinzi mkali sana,

kichwani kwa JOel Nchwari alikua akiwaza mambo mengi sana hususani alimuwaza sana Witness yote hii ni kutokana na kumtamani na kumfanya awe nyumba ndogo, kweli nafsi yake ili kiri kuwa Witness ni mzuri kupita

maelezo yaliyo jitosheleza, hakuona mwana mke wa kumfananisha nae hata kidogo! picha ya Witness ili mjia kichwani kama mkanda wa filamu, , alihaidi vitu vingi ange mfanyia bila kujua upande wa pili, mwana mke huyo ni hatari sana,

hakujua binti huyo sio mtu wa mchezo, hakujua Witness ni gaidi tena commando muuaji na sasa ili kua ni zamu yake kuuliwa, laiti angelijua hilo asingethubutu hata kwenda Dodoma na angegairi safari hiyo mara moja!

gari zili zidi kwenda kasi kama upepo au mshale, madereva wakiwa makini sana wakiwahi mkoani Dodoma, kona walilalanazo, ili onekana madereva hao ni wazoefu sana.
"vipi ushafika Mama"?
"Kitambo sana nakusubiri wewe Laaziz"
"mimi nipo njiani"
"safari njema, nina hamu kweli nawewe wahi basi"
"mimi ni wako usijali"

Ni mazungumzo kati ya mkuu wa mKoa na Witness akiwa bado yupo ndani ya gari, siti ya nyuma kushoto, mkuu wa mkoa alitamani afike siku hiyo hiyo, ili amuone Witness..

Baada ya masaa matano kuka tika tayari wali kuwa wame fika Dodoma na Mkuu wa mkoa kufikia ndani ya Hotel kubwa ya nyota tano yenye ulinzi wa kutosha,

ila ilipo fika usiku kimnya kimnya alitoka baada ya kuwa siliana na Witness wakutane mbali kidogo na sehemu iliyo jificha, kweli jambo lile lili fanyika na kukutana ndani ya baa moja iliyo kua mbali kidogo na mjini.

"sasa ngoja nikwambie ukitaka kuni faidi vizuri subiri bunge liishe"
"jamani uta ni tesa mwenzio!."
"mimi ni wako, huu ni mwili wako muheshimiwa, usijali kwa hilo, nipo Dodoma kwa ajili yako"
"sawa nita fanya nini tena, nita kusubiri tu, lakini hatuwezi kulala wote leo"?
"hapana, subiri ,maliza kwanza kili cho kuleta"
"okay!."

waliendelea kunywa na kuongea bila mkuu wa mkoa kujua kuwa siku zake za kuishi zime fika uki ngoni hakujua kuwa anae ongea nae hapo ni israel mtoa roho za watu, kwa mambo aliyo kua akifanya Witness akicheka na kufurahi na haikua rahisi kujua kuwa ni muuaji mbaya sana tena wa kutisha kupita maelezo,

hata urembo wake pia vile vile ilikua picha tosha kuonesha kuwa alikua mtu safi, vile vile katika maisha yake hakuwahi kuwaza kuja kuwa muuaji alifanya ivyo kutokana na wazazi wake ambao waliuwawa kinyama sana tena mbele ya macho yake, na watu walio fanya unyama ule wapo hai mpaka leo wana vuta pumzi,
kitendo hiko kina muuma sana.

kweli alibeba siri nzito ndani ya kifua chake ambayo hakuna mtu yoyote yule aliye jua chini ya jua, alijiapiazia atamuua yule yoyote aliye husika kwa namna moja au nyingine..

siku zilizidi kwenda huku majuma yakikatika witness alizidi kujipanga vizuri dhidi ya MKuu wa mkoa akitafakari ange muua kwa njia gani. hakuacha kuwasiliana nae mara kwa mara ili amuweke karibu mkuu wa mkoa,

Tayari muda wa bunge uliisha ila Mkuu wa mkoa aliomba akae japo wiki moja akisingizia kua kuna mambo bado ana fuatalia ya kiserikali bila kujua ndo anaenda kuki fuata kifo,

siku iyo alikodi gari kimnya kimnya usiku bila walinzi wake kujua na moja kwa moja kumfuata Witness mwanamke mzuri aliye tamani siku moja afanye nae ngono.

kweli kila kitu kilienda sawa na kukutana Gest house ambayo ilikua kidogo ipo uswahili, Witness alimuelekeza kila kitu na mwishowe kufika mpka ndani na kumkuta Witness akiwa amevaa kanga pekee yake, na kumfanya mkuu wa mkoa

aizdi kuchanganyikiwa, alijikuta ana mvua nguo kifikra na kupeleka mawazo yake kitandani aki fanya mapenzi na Witnes na kufanya damu yake izidi kwenda mbio kwa kasi ya ajabu.

"hakika ume umbika Linnah, sio siri, alafu mbona ume kuja huku uswazi?!"
"asante baby, naogopa paparazi ndo maana nime kuja ili tuji fiche huku , nataka uni faidi mpaka uchoke".!

Witness alimsogelea na kuanza kumfungua vifungo vya shati huku aki mtupa kitanda na kumfanya mkuu wa mkoa atulie tuli, na kusubiri kupewa penzi,
"nataka tufanye mchezo fulani hivi wa Tanga".
"upi huo tena"?
"nataka niku funge kamba miguu na mikono yako ukiwa ivyo chali, namimi nipande juu ya yako, nikuoneshe mambo ya pwani baby"
"leo kazi ipo ruksa, uta niua kwa presha mzee mimi, umri umeenda sana, "

Witness alichukua kamba ya manira na kuifunga mikono huku na kule pamoja na miguu na kufanya MKuu wa mkoa kuwa kama yupo kwenye msalaba.

alikaza zile kamba sana kiasi kwamba haikua rahisi kutoka, Witness alipanda juu ya yake na kuanza kumshika masikio kima haba na kumfanya Joel azidi kupagawa kwa raha alizo sikia na kuhama dunia.

ila GHafla Witness alisimama na kutoka kitandani na kufuata begi lake,
ambalo lilikua chini na kutoa kisu kirefu chenye ncha kali sana, moja kwa moja alienda kwenye kidole cha Joel, na kukikata kidole gumba, na kumfanya Joel apige kelele sana, alimuendea na kumziba mdomo.

"kaa kimnya mshenzi wewe"
"aaaaaaaaaah......"
"kaaa kimnya, utaenda kuniambia kile nachotaka kujua"

Witness alikamata kidole kingine kwa hasira na kukikata tena,
hakuwa Witness tena wakati huo sura yake ili badilika na kufanya macho yake yawe mekundu kupita kiasi , gubu la hasira lili mkaba sana. mkuu wa mkoa hakujua kwanini jambo lile lime tokea, alidhani wenda Witness amepandwa na wazimu, na kuzidi kupiga kelele sana huku damu zikiruka kama chem chem ya maji

Witness alichukua matambala na kuya weka kinywani mwa MKuu wa mkoa Joel na kufanya kelele zisipenye popote pale.
alicho fanya Witness alienda kukaa juu ya kiti kilicho kua pembeni yake.
na kumwangalia Joel ambae wakati huo alikua akiweweseka akiomba msaada huku akilia machozi kama mtoto mdogo wa miaka mitatu

"Joel. hakika una mjua vizuri Dimalia Kafifi,"?
"mmmhhh mhhhh"

Mkuu wa mkoa alitingisha kichwa chake kuashiria kuwa hamfahamu mtu aliye tajjiwa na Witness.

kwa hasira Witness alisimama tena na kushika kidole chake, na kuchukua plies ndani ya begi ya

kukatia waya na kukata tena kidole kingine, ki ukweli Joel alipata maumivu sana. damu nyingi sana zili mvuja na kumfanya alie kama mtoto mdogo, na kumwaga machozi ya uchungu kupita kiasi,

"vikiisha vidole vya mikono, naanza vya miguu. . una mjua Dimalia kafifi"?
"mmmh mmh"

Joel alikataa tena na Witness kuchukua tena moja ya kidole chake na kumtoa kitambaa kile mdomoni,
"nanananana namjua ndio namjua namjuua aaaaaaah"

Kutokana na mateso yale kuzidi ili bidi akubali ili asiendelee kuteswa, maana alijua mtu aliye kua mbele yake hakua na masihala hata kidogo, hakutegemea kama binti huyo angefanya unyama kama ule,
"vizuri, kwanini mlimuuwa, na nani aliye husika"?
"sisi sijui"
"una nitania"?
"hapana nakutajia, baadhi yao walisha kufa,"

Witness kusikia vile alitoa kifaa cha kunasa sauti na kukiweka pembeni kiwe kama ushahidi tosha
ambapo alikua ana rekodi kila kitu,
"Dimalia kafifi aliuwawa ndio, na watu waliomuuwa walitumwa na raisi mstaafu Emmanuel Magessa, na pia wapo baadhi ya watu wapo serikalini wali usika, akiwemo Raisi aliye kua madarakani, sasa hivi"
"bado wangapi"?
"nao wajua mimi ni tisa naomba usiniue, Linnah, "
"wewe ulijuaje"?
"nilihusika pia, tulikaa kikao wote, nia yetu ili kua tumuuwe Mr, Kafifi, yeye mwenyewe sababu tuli hofia ange chukua madaraka na kutaja siri nyingine nzito,"
"kwa nini mliimuwa mke wake"?
"ha ha hakuna, mimi sijui ila , ili kua Mr, kAFIFI NDO auwawe wala sio mke wake, ndo hayo tu"
"una danganya,"

Witnes alichukua tena plies na kuingiza kidole kimoja kati kati ya plies ile na kutaka kukata ambapo kili baki kidole kimoja tu mkono wa kushoto.

"mtafute Ibengwe, IGP Ibengwe yeye ndo ndo alipewa pesa nyingi ili azime kesi ile ya Kafifi, yeye ndo ana jua kila kitu tafadhali ni hayo tu, yeye ndo ana jua siri zote, , siri zote ana zoyeye naomba uni urumie"

Witness alimuangalia Mkuu wa mkoa joel kwa macho makali sana huku akiwa na hasira kupindukia, vifo vya wazazi wake bado vili mtesa sana kichwani mpaka ndani ya moyo wake, hakuona sababu ya kuwaacha watu waliio husika wawe hai, aliona kama hato watendea haki wazazi wake walio lala makaburini.

aliji kuta akilia kwa hasira sana huku midomo yake iki tingishika kwa hasira na kumkata jicho Joel ambae wakati huo akiwa amesha poteza damu nyingi sana mwilini mwake, na kucha fua mashuka na damu nyingine ziki churuzika chini

alichukua begi lake na kutoa bastola ambapo alichukua kiwamba kinachozuia bastola isipige kelele na kukiweka kwa mbele ya mdomo wa bastola

"kacha kacha"

alikoki ba stola ile na kuzidi kulia kwa hasira huku picha za wazazi wake kuuwawa kinyama huku mama yake mzazi kubakwa viki pita kichwani kama mkanda wa filamu .


 Mauaji ya kutiha yanazidi kuliogopesha jiji la Dar es salaam huku viongozi mbali mbali wakizidi kuuwawa vifo vya kinyama sana, Raisi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania anamua kuingilia kati swala hilo nakuitisha kikao kidogo cha siri ili waweze kumtia muuaji huyo kizuizini ila licha ya kutuma wapelelezi wake wa siri bado hali ina zidi kuwa tete! Katika uchunguzi uli ofanyika ana gundua kuwa muuajji huo ana uwa wana chama wote wa YBDP (youth brave democratic party) ambacho kipo madarakani anazidi kuweka walinzi kila kona dhidi muuaji huyo hatari,

SONGA NAYO,

HALI nyingine ya kuogopesha inazidi kuwa mbaya ambapo habari zilianza kusambaa kuwa majambazi wana vamia vituo vya polisi na kuiba silaha za moto, hakika serikali ya Tanzania ilikua kama ime changanyikiwa. Mawazo yao yali

wapelekea wenda watu hao wali taka kupindua nchi hiyo na kuanzisha vita kali!, vikosi vya jeshi la polisi vina mwagwa kila kona ya jiji, na ulinzi wa kuji toshelesha, ambao uliwekwa mara mia, .

Mpelelezi mkubwa kutoka katika kikundi cha CID(central investigation department) ana zidi kumtilia mashaka Witness hii ni kutokana na , kuli fuatilia gari lake ,mpaka nyumbani ambalo lili kua lina endeshwa na kijana mwingine, alivyo enda kumuulizia Witness ali mkosa na kuambiwa kuwa kasafiri,

baada ya siku chache wali pokea Msiba mwingine ulioleta gumzo sana, hapo ndipo Vincebt Towo alizidi kuweka mashaka juu ya mrembo huyo na kuanza kuamua kula nae sahani moja mpka pale kita kapo eleweka, alimpania sana, sababu nayeye pia alihaidiwa donge nono kutoka kwa Muheshimiwa Raisi. Bila kujua kuwa mwanamke anaye eenda kupambana nae ni hatari pengine kuliko hata ukoma, hakuelewa kuwa ana jiingiza kwenye matatizo makubwa ambayo hakaustaili hata kuingia,

Baada ya mauaji yake kutimia tayari alirejea Dar es salaam akitumia gari yake ambapo aliingia usiku sana , kutokana na uchovu mwingi alioga na kujitupa kitandani ili asubiri kesho yake afanye uchunguzi wa kuanza kumsaka IGP IBENGWE akiamini kuwa huyo ndiye ana jua siri nyingine na ange msaidia kuwa taja wahusika wengine,

Mchana kutwa alizunguka akifanya kazi yake kimnya kimnya ya kuisaka nyumba ya IBENGWE, alipata jibu na kugundua kuwa ipo KIGAMBONI Maeneo ya mji mwema,

Jioni ili fika kama kawaida, hakutaka kujulikana sura yake alichukua kinyago na kukiweka ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea kigamboni mara moja, hakuataka kupoteza hata dakika moja, aliji vika sura ya mauaji, kuuwa tena kwake lili kua ni jambo la kawaida sana.

“Mama Maria, nani yupo jikoni”?
“mimi sijui, kwani vipi”?
“nime sikia kama kikombe kime dondoka”
“embu lala usiku huu, hakuna kitu”
“hapana kuna kitu”
Alizungumza IGP ibengwe baada ya kusikia kitu kama kikombe kime dondoka jikoni akiwa amelala usiku na mke wake, alichukua bastola yake taratibu na kuanza kunyata, ila kabla ya kufanya lolote mkono wake uli pigwa tekena bastola yake kudondoka chini, alivyo taka kukaa sawa, alipokea ngumi ya pua na kumfanya apate maumivu makali sana,

aliiona ngumi ina kuja na kuinama kidogo alivvyo inuka alipokea ngumi nyingine ya uso,
Hakika haku mtambua mtu huyo sababu alikuwa amevaa kinyago, alianza kurudi nyuma kwa hofu kubwa, katika kurudi nyuma kule alikumbuka kuwa nyumba yake aliweka kifaa kidogo ambacho akibonyeza angeweza kupata msaada wa usalama. kidude hiko kilikuwa ukutani, alibonyeza, bila witness kujua.
Winess alimsogelea na kumtwanga kichwa puani na kumvuta Seblen, na kumuamuru akae.
“fanya upesi, chukua pingu hii jifunge”
“wewe ni nani”?
“jifunge pingu hiyo”
IGP Yule alitii amri ile na kujifunga pingu ile mwenyewe, na kusubiri nini kinge fuata, tayari alikua mwenye hofu sana na kujua kifo chake kili kua kime fika kutokana na kusikia habari za mbaya za mwana mke muuaji, tena leo hii yupo ndani kwake, hakuwa na ujanja tena zaidi kuona ni kifo tu.

Lakini katika hali ya kushangaza Witnes ana pokea teke la mgongoni lililo mfanya ayumbe kidogo na mwishowe kudondoka chini, alivyo geuka alimuona mtu mrefu kiasi na mwembaba, alikua ni Vincent Towo, baada ya kupokea alam ile kuwa IGP anahitaji msaada moja kwa moja alijua kuwa alikua ni Yule muuaji ambae alikua akimuwinda siku nyingi haku taka kupoteza muda aliamuua kuja mwenyewe ili wapambane, hakika Vincent nayeye alijiamini hasa kwenye maswala ya kupigana,

Alitingisha tingisha miguu yakena kurusha teke ambalo witness aliliona na kuli kwepa

Wiitnes alikunja ngumi na tayari kuanza mashambulizi, aliziona ngumi za Vincent zina kuja na zote kuzikwepa, alizidi kuisoma staili yake ya kupigana na kugundua kuwa ana tumia mchezo wa karate, ambao kwake ulikuwa wa kitoto sana, Vinncent alirusha tena teke ambapo Witness alirudi nyuma ila bahati mbaya aliteleza na kinyago alicho kua ame kivaa usoni kuvuka na sura yake kuonekana,
Na kweli hapo hapo Vincent Towo kupata jibu la swali lake kuwa muuaji ni Yule aliye kua akimuhisi muda mrefu

 Kitendo cha kinyago kile kuvuka kilimkeera sana Witness hakika hakutaka sura yake ijulikane mapema, na ndani ya kichwa chake kuwaza kitu kimoja kumtoa duniani Vincent Towo, akiaimini kuwa akifanya ivyo, ataweza kumfumbisha mdomo na siri ile kubaki nayo yeye mwenyewe, alikunja ngumi ambapo

alimuona vicent anakuja mzima mzima na kuhepa kushoto , huku akimsindikiza na teke la mbavu lili lomfanya ayumbe kidogo, hakutaka kupoteza muda hata sekunde alimfata na kumtwanga kichwa cha
pua, alimvuta na kuanza kumshushia ngumi za uso kwa mara ya kwanza mpelelezi huyo aliji tahidi kuzi pangua ngumi zilizokua zikija ila baadae ana ishiwa ujanja na kutulia tuli akizidi kupokea ngumi nyingi
zinazokuja dhidi yake, Withness alizungusha round kick na kumpiga nalo shingoni na mpelelezi Yule kudondoka mzima mzima huku akiwa tayari na damu nyingi sana,
“shiit”
Alizungumza Witness baada ya kuona maaskari wengi wakipita dirishani wakiwa na mitutu mikononi mwao, kabla hawajaingia mlangoni alirusha kiti na kumpata askari wa kwaza kuingia mlangoni na pale pale kuruka njee.
“griii griii”
Milio ya risasi ilianza kurindima baada ya kumuona Witness akikimbia walimshuhudia akipasua kioo na kuruka nje ya dirisha, haraka haraka wakiwa na mitutu yao walisogea mpaka dirishani lakini hawa kuambulia kumuona Witness
“muheshimiwa upo salama”?
“mkamateni Yule mwanamke!“
“sawa muheshimiwa”
Askari walizidi kuzunguka nyumba hiyo wakitapakaa kila kona wakiamini kuwa Witness bado hajatoka nje ya nyumba hiyo.


0 comments:

Post a Comment

BLOG