Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 4/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 4 KATI YA 10
*******
 *******


ERICK akiwa juu ya usukani kwenye mataa ya ubungo siku hiyo mchana. huku pembeni kushoto
akiwa amekaa Pamela, wakiwa kwenye msongamano wa magari ,
Pamela akiwa anaangalia nje, ghafla aligandisha macho yake juu ya sura ya mtu mmoja ambae alikua akiuza maji ya kutembeza mkononi hakuamini alikua ni Donald akiuza maji mchana wa jua kali, hakika roho ili muuma sana, alishindwa kuvumilia na kushuka ndani ya gari na kumuendea Donald,
Pale pale alipo hakuogopa macho ya watu,
“Donald, tafadhali bado nakupenda sana, hupaswi kufanya biashara hii”
“Pamela naomba uniache, ndio hadhi yangu mimi, nime ridhika na maisha haya,”
“no Donald please(tafadhali) , naomba tuwe kama zamani”
“hapana siwezi, naomba niendelee na biashara yangu”

“weee pamela, tuna chelewa tuondoke”
Ilikua ni sauti ya Erick kaka yake akiwa tayari ameshuka ndani ya gari na kumsogelea,
“achana na mimi Erick”
“mimi nakuacha”
“wewe nenda niache”
Kweli Erick baada ya kuona vile aliiingia ndani ya gari na kuondoka zake huku akiwaacha Pamela na Donald.
“chukua hii elfu hamsini Donald, nenda nyumbanni kapumzike”

Pamela alitoa pesa izo ndani ya pochi na kumkabidhi Donald , kwa mara ya kwanza alionekana kukataa ila baadae kidogo alikubali, baada ya hapo Pamela aliita taxi na kuondoka zake huku akiwa bado ana msihi aweze kumsamehe yaliyo tokea nyuma,
Bado akiwa katika mawazo ghafla mbele yake tena mbele ya miguu yake lili simama gari aina ya RANGE ROVER SPORT jeusi sana, kila mtu ili bidi ageuze shingo ili kujua ni nani atakae toka ndani ya gari hilo.

Zili pita sekunde 40 nzima bila mtu yoyote kushuka, baada ya mlango huo kufunguliwa katika upande wa dereva harufu nzuri ya marashi ili enea eneo zima, alikua ni mwana mke mnene kiasi mweupe sana, shingoni laivalia mikufu ya gharama mno!
alikua ni mzuri mno! Kila mtu alipigwa na butwaa hasa makalio yakey alivyo tengeneza mlima kwa nyuma na kuji gawa vizuri pembeni, alienda moja kwa moja alipo simama Donald.
“Donald mambo”?
Bado Donald alikua akimuangalia mwana mke Yule sababu ya kushangazwa sana, hakuelewa walionana wapi na alijua vipi jina lake
“poa, una hitaji maji ya bei gani”?
“hapana sihitaji maji, nakuhitaji wewe Donald”
“kwani tuna fahamiana”!?
Aliuliza Donald na kumfanya mwanamke Yule ashushe pumzi ndefu sana…




Bado Donald alizidi kumshangaa mwana mke Yule aliye kua mbele yake akiwa bado ana vuta kumbu kumbu ni wapi walionana, Licha ya kuvuta kumbu kumbu nyuma bado haku mkumbuka kabisa na wala hakuwahi kumuona sehemu yoyote ile japokua Mwanamke Yule alionesha kumfahamu kabisa, jambo hilo lina mshangaza mno!.
“ndio tuna fahamiana, si unaishi sinza,NA ume fukuzwa chuoni?!”
“wewe ni nani”?
“uta nijua tu, usiogope kabisa, tuna weza tuka pata sehemu nzuri tuweze kuongea?”
“ hapana, sasa hivi nipo kwenye biashara zangu, siwezi kutoka popote pale, isitoshe sikufahamu”
“maji una uzaje?”
“haya mia tano, haya makubwa mia sita,haya buku buku, nikupe yapi”?
“nipe hayo ya elfu moja.”
Mwana mke Yule alitoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi Donald, baada ya kupewa maji Donald alianza kuta futa chenji na kumletea,
“NO JUST KEEP IT(hapana hiyo iweke tu).”
Mwana mke Yule aliongea na kuingia ndani ya gari lake aina ya RANGE alilokuja nalo na kuondoka zake huku nyuma akimuacha Donald akiwa katika hali ya maswali mengi kichwani, hata wenzake pia walizidi kumsonga na kuanza kumuhoji maswali juu ya mwana mke Yule huku wakimuona ni mtu mwenye kukataa mazali siku iyo.

GARI YA KIFAHARI na ya gharama aina ya HAMMER III ilikua tayari ime fika katika maegesho maalumu kabisa, ambapo magari hayo yalijipanga vizuri sana, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ndani ya usukani alikua amekaa Erick huku nyuma kushoto akiwemo baba yake,

NI fika kabisa ili onekana walikua waki msubiri mtu muhimu kwao, gari hiyo ili wekwa vizuri na MR, Deuji kushuka akiwa na fimbo yake mkononi huku nyuma akiongozana na mwanae wa kiume Erick, kwa nia moja tu kumpokea Graysson mwanaume ambae aliandaliwa ili aje kumuoa Pamela,

Alikua ni mtoto wa rafiki yake, Grayson alikua ni tajiri sana pia alikua ni msomi akiwa na PHD ya udaktari huku kazi zake akizifanyia INDIA huko alipata jina kubwa sana, na kua miongoni mwa madaktari matariji
jijini MUMBAI, nayeye pia ni mmoja wa watu ambao wali mpenda sana Pamela na kumueleza baba yake MR, Mallewo kipindi cha nyuma sana na habari zile kupewa moja kwa moja Mr , Deuji ila Pamela hakutaka kusikia habari izo hata kidogo,

Majira ya saa kumi tayari shirika la ndege la INDIA, INDIAN AIRWAYS lilitua juu ya ardhi ya uwanja wa ndege huo wa kimataifa iki tanguliza matairi ya mbele huku mengine ya nyuma yaki fuatiwa, ndege hiyo ilizidi kwenda kwa kasi sana baada ya kutua , na mwishowe kupunguza mwendo kasi na kusimama kabisa,

Sauti nyororo kabisa ili sikika kutoka katika kipaza sauti iki waarifu kuwa abiria wana oshuka washuke sababu ndege hiyo ingeruka tena. Ndani ya ndegge hiyo alikuwemo PHD Grayson alishuka ngazi za ndege hiyo akiwa mwenye furaha sana,
furaha yake ili changiwa na kitu kimoja tu, kumpata Pamela, aliapiza kuwa endapo akimpata ataenda nae moja kwa moja ENGLAND makazi anayo ishi au pengine India, hayo ndiyo aliyowaza PHD Grayson baada ya mabegi yake kuka guliwa na kupita katika kifaa maalumu kabisa cha kupitishia mabegi ambapo baada ya kukaguliwa hutokea upande wa pili,
“OOOOOOH Mr, Grayson,welcome back(oooh Grayson karibu kwa mara nyingine)”
Maneno hayo aliongea Erick akiwa mwenye furaha sana na kumpa mkono huku wakiongoza moja kwa moja mpka kwenye maegesho ya magari ili waweze kuanza safari ya kwenda nyumbani kwao oysterbay ambapo pia kulikua kuna wageni wengi sana wakiwa wana wasubiri……



Kelele za vigere gere zili sikika hasa baada ya PHD Grayson kushuka ndani ya gari akiongozana na mr ,Deuji ambae kwa wakati huo alimuita mkwe tayari, hakika alikua na shauku sana ya kumuona Pamela mwana mke ambae alikua

akimtaka kwa siku nyingi sana, leo hii hakuamini kua ame kubaliwa,
hakuuelewa kuwa alimambiwa maneno ya uwongo na Pamela alilazimishwa, Pamela akiwa chumbani kwake kaji fungia alilia sana, alifungua pazia akiwa juu gorofani na kumuona Grayson akisalimiana na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa pale, aliapia kweli hatotoka popote pale hata kama angeekewa bastola kichwani,
alimkumbuka sana Donald moyo ulimuuma kupindukia, hakika alimpenda sana Donald bado roho ili msuta itakuaje leo hii Donald akisikia kuwa ana mapenzi na Grayson japo kua walikua hawana maelewano ila ana aamini kuwa ipo siku wata kuuja kuwa kama zamani,na kurudiana pengine wafunge pungu za maisha.

Mlango wake aliusikia ukigongwa na aliye gonga alikua ni mama yake akimuomba atoke ili aweze kuonana na Grayson Mallewo, kweli alikataa katakata kufungua mlango,
“fungua mlango kwanza mwanangu, mimi mama yako naomba nifungulie”
“mama sitaki, naomba mniache”
“mwanangu nakuomba mimi mama yako, tafadhali”
“lakini naomba mama usiongelee habari za Grayson”
“sawa mwanangu”
Pamela alijikuta akifungua mlango na mama yake kuingia akiwa mpole sana, alimbembeleza sana ila ali kataa kata kata, jiti hada zote hazi kuzaa matunda yoyote yale. Baadae kidogo aliingia baba yake na kumuomba sana ila bado hakutaka kutoka kwenda kumuona Grayson Mallewo mwanaume ambae aliyeandaliwa amuoe , ili kua ni kitendo cha aibu sana , hawa kuelewa wataenda kumueleza nin Grayson aliye funga safari ya mbali kuja Tanzania kumfata Pamela wamueleze kua PAMELA amekataa hakika jambo hilo lili kua na uzito sana.

Kwa macho yake Pamela alishuhudia mama yake akipiga magoti chini kama mtoto jambo hilo lili muuma sana , mama yake kumpigia goti tena mbele ya baba yake, hakika aliumia moyoni, hakua na jinsi zaidi ya kumuinua mama yake, amabe alikiua chini akimsihi akubali kutoka ili aonane na Grayson.
“mwanangu naomba usi tutie aibu wazazi wako”
“lakini mama nafanya hivi kwa kukuheshimu tu, wala si vinginevyo”
Alizungumza Pamela huku akifuta futa machozi na kitambaa na taratibu kuanza kushuka ngazi, baada ya kumuona Graysson alijaribu kutengeneza tabasamu bandia lililo fanya na Grayson nayeye ata basamu vile vile,
“vipi mpenzi wangu, mbona macho mekundu una umwa au”?
“Nop, nipo sawa”!
“leo ni siku yetu, ina tubidi tufurahi”
“naelewa Graysson, ndo maana nikaja kukuona”
“nakupenda Pamela, nakupenda sana, nataka nikufanye uwe mwana mke wa kipekee katika dunia hii,nataka uishi kama malkia”

Katika hali ya kushangaza Graysoon aliomba watu wote wakae kimnya kwani jambo ambalo ana taka kuli fanya , hakuna mtu aliyeelewa nini kitaka chotokea, ili onekana dhahiri kua kitendo kile alikipanga tangu ana kuja, hii ni baada ya kutoa pete mfukoni,

Kitendo kile kwa Pamela hakua tayari kabisa hata kidogo, japo kua Graysson alimuomba mkono ili amvishe pete ile, ukimnya uli tawala ndani hapo, ila alivyo muangalia mama yake alimpa ishara ya unyonge kuwa akubalia kuvaa pete ile ya uchumba,

Hakua na jinsi zaidi ya kukubali kuvalishwa, kelele zilipigwa ziki ambatana na makofi huku mzee Deuji akiwa na furaha sana kwa mwanae kuvikwa pete ile ya uchumba na mtu tajiri na msomi,mwenye PHD ya udaktari halikua jambo la kawaida.
kwa Pamela hakuonesha furaha hata kidogo na kufanya waalikwa wasielewe nini kili mfanya Pamela asiwe katika nyuso ya furaha..

*********

“NAITWA ROSHBAN hata ivyo”
“ume nijuaje kwani”?
“ha ha ha ha ni mapema mno kujua, ila ipo siku uta nijua vizuri Donald”
“kwanini sio sasa hivi”?
“muda bado”
Yalikua ni mazungumzo kati ya Donald na mwana mke huyo ambae alionekana kuwa tajiri sana siku iyo wakiwa wamekaa juu ya benchi na Donald, baada ya mazungumzo hayo kuisha alimpa Donald kiasi cha pesana kumu haidi kuwa ata rudi tena kesho yake, na kuingia ndani ya gari.,

Bado maswali alikua aakiji uliza sana kichwani bila kupata majibu ya aina yoyote yale, aliendelea na biashara yake ya kuuza maji ya kutembeza ila kwa mbali sana alianza kuhisi kichwa kina muuma , ali puuzia ila kadri muda unavyo zidi kwenda na ndo kichwa kili zidi kumuuma, alienda duka la madawa ili ata fute dawa lakini baada ya kunywa alikua ndo kama kakitibua,
Hakuweza kuvumilia alipanda dala dala na kuamua kurudi nyumbani kwao, baada ya kufika nyumbani alihsi kizungu zungu kikali sana, huku kichwa kiki zidi kumuuma sana..




“NAOMBENI MUNISAIDIE, JAMAAAANI, naomba mnitoe humu, jamanii nisadieni”
Ilikua ni sauti iliyosikika ikitokea ndani ya shimo lillilo chimbwa kuelekea chini sana urefu wa futi nyingi sana, mtu huyo aliye kua ndani ya shimo alikua akiomba msaada ili aweze kutoka nje ila cha kushangaza kila mtu alipita na kumchungulia huku akimpita kama haku msikia,bila kutoa msaada wa aina yoyote ile
“NILIKWAMBIA lakini huku sikia, sasa huku hautotoka tena Donald, nilikwambia uachane na mwanangu, hautotoka tena”
Donald akiwa ndani ya shimo hakuamini baada ya kumuona Mzee Deuji akiwa kwa juu amevalia nguo nyeusi juu mpaka chini mithili ya kanzu huku mkononi akiwa ameshika usinga, aliogopa mno alizidi kuomba msamaha huku akilia lakini haku mfanya mzee huyo abadili maamuzi yake, kwa mbali alisikia ngoma ziki pigwa huku zikianza kusogea karibu, akiwa kichwa chake anaaangalia juu aliweza kumuona bibi kizee akiwa na kibuyu kichwani huku akiwa ameji chora usoni, bila kuuliza chochote alijua tayari yalikua ni mambo ya kichawi na wala si vinginevyo.
“ndio huyu”?
“ndio, huyu ndiye Donald”
“sasa una semaje”?
“kama nilivyo kwambia tumchukue sasa hivi”
“sawa twende huku tukachukue dawa”
Walisikika wakishauriana Mzee Deuji na bibi Yule kumaanisha kuwa wamtoe kafara, hakua na la kufanya zaidi ya kumuomba Mungu wake aweze kutenda miujiza yoyote,

Kwa mbali sana alihisi mtu ana kuja hii ni baada ya kusikia parakacha parakacha, alivyo inua shingo yake juu kumungalia mtu huyo hakuamini kabisa macho yake, mwanamke aliye kua akija na magari ya kifahari
“ROSHBAN”
“DONALD”
“naomba nisaidie Roshban,”
“nime kuja kukusaidia nisubiri nakuja”
Roshban alitoka pale na baadae kurudi na kamba ngumu ambapo alimtupia Donald aliye kua ndani ya shimo lile, na kumwa mbia kua aishike vizuri, aliiikamata vizuri na kuweka miguu yake miwili pembeni ya kuta za shimo hilo na kuanza kupanda juu, alivyo fika kati kati allidondoka tena.
“Donald fanya haraka, wana kuja”
“sawa”
Kwa mara ya pili aliji tahidi kupanda juu huku akijishika na kamba ilie iliyo shikwa na Roshban kwa juu, baada ya kufika juu, waliwaona wachawi wengine wakija na huku wakicheza ngoma, walivyo waona walianza kukimbia huku wachawi wale wakianza kuwa kimbiza kwa nyuma na kuanza kupiga kelele, ila baadae Roshban ana teleza na kushindwa kukimbia tena baada ya kupata maumivu ya miguu, Donald ana muinua ila hakua tayari kukimbia,
“Donald kimbia , Kimbia sasa hivi”
“siwezi tuondoke wote”
“wataakuua hawa, kimbia Donald sasa hivi”
Bibi mmoja aliye kua nyuma yao ana kuja alishika vizuri mkia wa joogo na kumuelekezea Donald ambapo ulitoa radi kali, Ila Roshbani alimsukumiza nay eye kukaa mbele ya Donald, baada ya kupigwa na radi lile ROSHBAN alitupwa mbali sana na kuanza kutoa damu nyingi mdomoni,
“Bi, kinyogoli umeemuwa mtoto wa MKUU hatokuelewa”
Wachawi wote waliingiwa na hofu na kumuacha Donald na kumuendea Roshban.

*******

“HAAAAAAAAAA, YESU”
Donald alishtuka akiwa usingizini pembeni yake alikua amesimama mama yake akilia, ila cha ajabu kichwa kilicho kua kikimsumbua kilikua kimepona, hakuelewa nini maana ya ndoto ile,
“Mwanangu Donald, una jisikiaje”?
“kwani nini kili tokea mama”?
“mwanangu nime kukuta ume dondoka mlangoni unatoa mapovu mdomoni”
Kweli alivyo angalia chumba kile aligundua kua yupo hospitali,

Siku iliyo fuata Donald aliruhusiwa kutoka hospitalini, baada ya hali yake kuwa sawa, aliamua kurudi katika biashara zake za kuuza maji ya kutembeza barabarani, siku mbili zili katika akuweza kumtia machoni Roshban hakuelewa nini kili mpata sababu alimzoea sana, na ili kua hawezi kupita siku bila kuja kumuona Donald lakini wiki sasa ili pita tena bila ya kumtia machoni Roshban, na kuzidi kuta fakari ndoto ile wenda ina weza ikawa ya kweli lakini hakutaka kuweka kichwani ndoto ile aliamini kua ni ndoto tu wala si kitu kingine kile,

Siku iyo akiwa ame pumzika pembeni ghafla aliona gari ikiwa imesimama pembeni yake umbali wa maili chache kidogo ila hakushuka mtu yoyote Yule, ki ukweli ilikua ni gari ya garama sana na hakuwahi kuiona mahali popote pale alipuuzia na kuendelea kuangalia pembeni ,
“Donald”!.
Baada ya kusikia sauti ilie ikiiita jina lake aligeuka upande wa pili na kumuona Pamela akishuka ndani ya gari ile aina ya AUDI na kumfuata mpaka alipo,
“Donald mpenzi wangu,”
Pamela aliongea huku akianza kulia hasa alivyo muona Donald jinsi alivyo chakaa ,hakukua na haja kuuliza ni mtu wa hadhi gani sababu jinsi mavazi yake, ndala zili zotoboka chini pamoja na kaptula ya jinis iliyo chakaa vili mfanya Pamela azidi kulia kwa uchungu,
“Hei baby lets move(hei mpenzi tuondoke). Kama una taka maji si ungesema tuta enda kununua supa maketi, maji ya kutembeza sio mazuri”
Alishuka DOKTA Grayson ndani ya gari huku akizungumza maneno ambayo yali mfanya Pamela amkate jicho kali la hasira, laiti ange jua Donald ni nani mbele ya Pamela asingesema maneno hayo hata kidogo, hakuelewa lolote lile, alimuangalia Donald kwa dharau na kumshika Pamela mkono ili waingie ndani ya gari, lililo kua pembeni lina toa muungurumo sababu lilikua bado hali jazimwa,
“don’t touch me,(usiniguse), wewe una mjua huyu, nakuuliza una mjua huyu, ngoja nikwambie kitu kimoja Grayson ambacho labda sijawahi kukwammbia”
Pamela alianza kupaza sauti huku akimsogelea Donald karibu na kumshika mkono,
“una muona huyu ambae yupo mbele yakoo, ndiye mwanaume ninae mpenda sawa Grayson,, kama ulidanganywa na BABA kuwa nakupenda sio kweli……”
“sikia pamela kama kweli una nipenda na mimi ndio mumeo mtarajiwa ingia ndani ya gari tuondoke”
“excuse me!. Una semaje”?
“Grayson siku pendi hata kidogo, samahani kwa kukupotezea muda wako, ndani ya gari siingii. Wewe nenda niache mimi hapa, nampenda huyu mwanaume, ana itwa Donald”
Kwa hasira Dokta Grayson alirudi ndani ya gari nak uondoka zake bila kusema chochote kile
“Donald, nafanya hivi kwa ajili yako nakupenda Donald wana nilazimisha niolewe, Donald sitaki kuolewa, wewe ndo nataka uje kunioa, naomba rudisha moyo wako nyuma Donald, nakupenda sana, siwezi bila wewe”
Yalikua ni maneno ambayo PAMELA aliya zungumza kwa uchungu uliyo mjaa moyoni mwake hakika yalikua ni maneno yaliyo uchoma moyo wa Donald kwa kitendo cha kumkataa mwanaume mbele yake hakika aliweza kuamini kuwa Pamela alikua na mapenzi ya dhati.
Wote walijikuta wakilia kwa uchungu sana, Donald alimvuta Pamela na kumfuta machozi yake akitumia viganja vyake vya mikono, na pale pale kumkombatia, hawa kujali macho ya watu waliokua wakipita mbele yao,
“Pamela nakupenda sana acha kulia, ila ina tubi…..”
“PUMBAVU, zako”!
Ilikua ni sauti ya BABA yake Pamela mzee Deuji ambaye alifoka kwa sauti kubwa yenye hasira huku pembeni yake akiwa amesimama na Dokta Graysson ilionesha dhahiri kua ndiye aliyeweka unoko ule, sauti ile ili washtua sana na kuwa fanya washtuke wote nakuachiana ili kua kidogo Donald akimbie mbio, wasi wasi ulizidi kumtanda, hakuelewa safari hii inge kuaje kwa upande wake.
“we kijana mara ngapi nakuonya juu ya binti yangu,? Usifanye nije kukufanya kitu ambacho utakuja kujuta katika maisha yako, Pamela ingia ndani ya gari sasa hivi, kijana kaa mbali na binti yangu, NAKUPA ONYO LA MWISHO”!
Mzee Deuji alimvuta Pamela akitumia nguvu na kuingia nae ndani ya gari,..




HALI ina zidi kuwa mbaya kwa Pamela leo hii mapenzi yana mtesa sana hakuelewa ni nini afanye ili baba yake au wazazi wake wamsikilize, kila siku alikua ni mtu wa kulia ila machozi yake haya kuweza kubadili uamuzi ambao baba yake aliutoa tayari.
kuwa PHD Grayson ndiye atakaye kuja kuolewa nae, ili kua sio ombi ilikua ni lazima, hakupenda kabisa alimchukia sana Graysoon na kuonesha wazi wazi lakini bado kazi ili kua ni ile ile tu, kua PHD ata kuja kuolewa nae,
hakika alijiona kama mateka ndani ya moyo wake, alimpenda sana Donald , lakini kwa wakati huo Alisha fikiria mengi afanye na kukosa jibu sahihi, chakula kwake kilkua kichungu hakula wala kunywa kwa siku tatu sasa, jambo hilo lili muumiza sana Mama yake lakini hakutaka kumsikilza mtu yoyote Yule, alichotaka yeye ni kurudiana na mpenzi wake Donald na wala sio PHD Graysoon kama baba yake alivyo taka, mipango ya yeye kuchukuliwa na kupelekwa nje ya nchi kuishi na Graysoon ilishaanza kufanyika wakiamini kuwa hiyo ndiyo ita kua fursa pekee ya kuwatenganisha na Donald,
Pamela alilia sana hakuelewa nini afanye mawazo aliyo waza sasa yali fika ukingoni, na kuwaza kitu kimoja tu KUJIUA na si vinginevyo, hakutaka kuishi na mwana ume asiye mpenda hata kidogo, aliliona wazo lile ni bora pengine kuliko mengine, na kumuomba Mungu amsamehe kwa hatua atakayoenda kuifanya wakati mfupi ujao,
alisimama kitandani na kuanza kutafakari atumie njia gani juu ya kupoteza uhai wake, aliamini kua hata ange kua hai asinge kua na furaha sababu wazazi wake walimpiga vita Donald.
“naomba kwenda nje”
“uwende wapi”?
“embu nipishe”
“nime ambiwa wewe usitoke humu ndani”
“una taka kufukuzwa kazi eeh?”
“ndo ivyo nimepewa maagizo na baba yako usitoke humu ndani”
“okay”!
Baada ya kukataliwa na mlinzi wa getini Pamela alirudi ndani na kuji fungia chumbani, bado nafsi ya kujiua ili tawala ndani ya moyo wake.

Bado Donald aliendelea kufanya biashara zake ndogo ndogo alivyo pata pesa kidogo aliamua kufungua genge la nyanya na vitu vingine vidogo vidogo karikoo sokoni, aliona mambo kwake yana mnyookea na kuserereka kama kawaida, alianza kujiiingiziia kipato kidogo ivyo ivyo na pesa zinginea akiziweka ivyo ndivyo ilivyo kua ,
“fungu hapa mia tano, hapa elfu mbili nazi pia zipo na karoti”
Aliongea Donald akimwambia Mteja aliye kua ame simama mbele yake,
“sijui kama nakufananisha kaka”!?
“aah hapana sidhani , lakini ina wezekana kwani ume ni fananisha na nani”?
“na kijana mmoja ivi, ana itwa Donald, Donald, tulisoma wote chuo kikuu Dar es salaam pale”
Donald alimuangalia kijana Yule kwa umakini wa hali ya juu sana huku akivuta kumbukumbu kweli alionekana kama ana mkumbuka,
“ndiye mimi”!
“mimi ni Charles, muda mwingi sana nilikua nakutafuta ndugu, lakini kwenye simu yako hukuwa una patikana, kuna kitu Fulani muhimu sana nilikua nataka kukwambia kipindi cha nyuma lakini sikuwa nakupata”
“kitu gani hiko tena”?
“Pamela vipi lakini mzima”?
“we acha tu kaka matatizo. Niambie hiko kitu”
***********

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG