Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 3/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 3 KATI YA 10
*******
 *******


Baadae ulisikika mlango una gongwa na Kway kuinuka kwenda kuufungua.
“Donald una itwa”

“na nani”?
“Pam”
Kabla ya kuongea chochote Pamela alisukuma mlango na kuingia ndani,
Na kumfanya Kway atoke nje ili awape faragha wawili hao,
“Donald mbona hupokei simu zangu”?
“ulikua wapi jana”?
“hahahahaha”
Pamela aliji chekesha kidogo bila kujua mtu aliye kua mbele yake alikua na hasira sana laiti angelijua hilo asingethubutu kutoa meno yake nje kucheka.
“usicheke jana ulikua wapi”?
“nilikuwa kwa Rafiki yangu MBEZI beach,alafu simu yangu ilizima chaji mpenzi wangu nisamehe kwa kutokujulisha”
ALizungumza Pamela maneno yale akijaribu kujitetea na kumfanya Donald ageuke na kumwangalia machoni, kwa upande wa Pamela hakujua lolote, hakutaka kuongea ukweli kuwa mara ya mwisho alikua na OKAKA na kujua

angesema ivyo kitendo kile kinge mkera sana Donald ivyo aliamua kudanganya bila kujua Donbald ana jua kila kitu, alizidi kuumiza moyo wa Donald, hakujua kuwa alikua anazidisha ukali wa sumu aliyo tengeneza,
“umeanza lini uongo Pamela”?
“Donald”!
“au kisa mimi maskini, kwetu hatuna uwezo, hatuna pesa, naomba uende uondoke humu chumbani sitaki kukuona tena katika maisha yangu, niache na umaskini wangu baki na matajiri wenzako,”
Yalikua ni maneno ya uchungu na ya kuogopesha sana kwa Pamela, maneno aliyokua akiongea hapo Donald yalichanganyika na hasira za wivu kiasi kwamba alianza kulia machozi kama mtoto mdogo, kweli penzi la Pamela

lilikua chungu siku hiyo, alikumbuka sana maneno ya mama yake mzazi laiti ange msikiliza tangu hapo awali wenda asinge umia kama anavyo umia siku iyo.
“Donald mbona sikuelewi, kosa langu nini usilie”? yote hayo yana toka wapi baba”
“unadhani mimi sijui unayo yafanya,? Subiri hapo”
Donald alisimama na kuliendea kabati la nguo na kutoa bahasha kubwa ya kaki, alichukua na kumtupia Pamela juu ya kitanda, haraka haraka Pamela alifungua ile bahasha, hakuamini alichokiona hata yeye alibaki akilia machozi, hakuelewa ata mueleza nini Donald amuelewe baada yakujiona akiwa na OKAKA wakiwa chumbani wamelala kimahaba.
ki ukweli alionekana kuchanganyikiwa sana , wakati hapo mwazo alidanganya alikua kwa rafiki yake, hakika alikua na kazi nyingine ngumu sana ambayo haikuwa rahisi kuielezea, hakuelewa ataanzia wapi kuongea, nakuzidi kububujikwa na machozi mengi huku akilia kwa kwikwi,

“SIKIA MSAGUSA, UWE MAKINI NA HIYO CAMERA, TUKI FIKA KWENYE HUO MGAHAWA. NITA kua nakupa ishara”
“usini fundishe kazi Jackson”
“poa usiniangushe”
“siwezi bwana!”
Maneno hayo kupitia simu alizungumza Raisi wa chuo Jackson okaka akiwa ana jiaandaa kuondoka na pamela baada ya kukata simu tayari walifunga safari huku mfukon mwa Jackson okaka akiwa ameweka vidonge vikali sana aina ya valium ambavyo huweza kumfanya mtu alale hata kwa masaa kumi na nane bila kuelewa kitu chochote, nia yake ili kua moja tu kumuwekea Pamela kwenye kinywaji chake,

Kweli mahesabu yake yalienda kama alivyo panga sababu baada ya kufika wanaagzia vinywaji , na kuji fanya amesahau simu yake ndani ya gari la Pamela,

Bila Pamela kuelewa nia mbaya ya Jackson aliendea gari lake huku nyuma okaka akiweka dawa izo zilizokua na makali sana ndani ya kinywaji cha Pamela, hakuelewa chochote kile aliendelea kupiga mafundo ya juice, ila baada ya muda ana hisi kichwa chake kizito sana.
“Jack naomba turudi hostel, siji sikii poa,”
“malizia basi kinywaji kwanza ndo turudi, si unajua sio vizuri”
“aah sawa”
Pamela bila kujua anazidi kuipa dawa iyo nguvu alipiga tena fundo refu na kuinywa ile juice yote, na kuanza kuhisi kichwa chake kizito sana kupita kiasi, alianza kurembua akihisii usingizi mzito ambao haukuwa wa kawaida .
“Doo,,naaald aah sori Jack, nipeleke hostel”
“sawa twende”
Jackson alimshika kiuno Pamela ambapo hapo alimpa ishara mpiga picha wake aweze kuchukua picha hiyo ya mnato , hakika Pamela alikua hajiwezi tena hata kidogo, hapo ndipo Okaka alipo chukua fursa hiyo kwenda nae katika moja ya hotel zilizo kua karibu na hapo. Jioni ili kua tayari ishafika na simu ya Pamela kuanza kuita, baadae OKAKA anaizima na kuendelea kupanda ngazi za hotel hiyo huku mpiga picha Yule akizidi kufanya kibarua chake,

Kilicho kua kina endelea hapo Pamela hakua ana jua hata kidogo laiiti angejua hakika angemuua mtu, kili kua ni kitendo cha kinyama sana kwake, baada ya kupata chumba Okaka ana amua kumvua nguo zote Pamela huku picha zikizidi kuendelea kupigwa alikaa pembeni yake na kumkombatia wakiwa kitandani na picha kuendelea kupigwa,

kila hatua iliyo fanywa hapo tukio lili chukuliwa kwa njiia ya picha za mnato, hakika zili kua ni picha mbaya sana kwa mtu yoyote akipelekea hato bisha kuwa wawili hao walikua waki fanya tendo la ndoa.
“naona kazi yako imeisha, nenda mabibo hostel pale, block D kesho, chumba namba 117 jamaa ana itwa Donald uta mpa izo picha na kumuandikia namba yako ya simu, kama nilivyo kwambia cha kumwambia”
“poa usiwaze, uyu demu ni wako, jamaa akiendelea na huyu demu ata kua hana moyo”
“poa kaka,”
“poa”
Jamaa Yule aliondoka na kuwaaacha Okaka pamoja na PAMELA chumbani mule.

Asubuhi kulivyo kucha Pamela alijaribu kuvuta kumbu kumbu ni wapi alipo ila alishindwa kuelewa , alijikuta kitandani lakini hakuelewa kafikaje alijaribu kuvuta kumbu kumbu, lakini zilirudi baada ya kumuona okaka akifungua mlango na kuingia na kikombe cha chai, ,
alivyo jifungua shuka aliji kuta yupo kama alivyo zaliwa hakika alielewa kilicho fanyika usiku uliopita, alielewa vizuri aliingiliwa kimwili pasipo yeye kutaka na aliye fanya ivyo alikua mbele yake alimuangalia kwa hasira kali sana.

“jack, nini ume nifanyia,”?
“karibu chai kwanza”
“sitaki, ume nibaka, jack !”?
Aliongea Pamela kwa hasira sana, hasa alivyoangalia simu yake na kukuta imezimwa moja kwa moja akila yake ili mtuma kwa Donald hakika alijiona msaliti sana.
leo hiii Raisi JACKson kuona nguo yake ya ndani, kitendo kile kilimuuma sana na kujuta kwanini alikubali kutoka na Jackson, alijiona ni mkosaji sana mbele ya Donald, hakujua ita kuaje endapo Donald atajua.
“nguo zangu ziko wapi”?
“za nini”?
“nataka nivae niondoke jack, tena nipishe nivae”

Pamela alisimama akiwa amejifunga shuka mwilini na kuokota nguo zake zilizokua chini na kuingia bafuni kuzivaa, alivyo toka alikua tayari keshavaa nguo zake na kuchukua funguo zake za gari, hakukuwa na jinsi jingine zaidi kukubali kuwa jambo lile tayari limetokea, hakukuwa na njia nyingine ya kuweka hali ile sawa. Ila aliji laumu sana moyoni mwake.!
“sasa hunywi chai”?
Aliuliza okaka ila Pamela hakujibu lolote alitoka zake mbio mbio huku akiwasha simu na kumtafuta Donald na simu ile haikupokelewa alijaribu tena lakini hali ili kua ile ile, alicho fanya ali mtafuta Gloria rafiki yake kipenzi,

Na kuambiwa jinsi gani Donald alivyo kua akimuulizia kila wakati, moja kwa moja baada ya kufika alienda kwa Gloria , hakumficha kile kilicho tokea alimueleza kila kitu ,aliamini kuwa ndiye atakaye mpa ushauri na kumwambia afanye nini.
“sasa utamwambia nini Donald, uta mwambia ulikua wapi”?
“nita mwambia ukweli Gloria sasa ni tafanya nini unadhani”
“weeee, usi fanye ivyo bora umdanganye, we unadhani ukimwambia ukweli ata furahi. Uta mpoteza, tena usijaribu hata kidogo”
“sasa nita mwambia nini”?
“wewe mwambie hata ulikua kwa rafiki yako simu iliiisha chaji, we ni mtu mzima.mengine utaongezea, ila usimwambie kuhusu Jackson. Ata jisikia vibaya sana, na ATA KUACHA”
Ushauri huo kutoka kwa rafiki yake ulimwingia vizuri sana Pamela na kutoka mbio mpaka Hostel ana yo lala Donald ila ana kuta hali ni tofauti kama alivyo dhani

********

“NINI KINA KULIZA PAM, UNALIA KISA leo nime jua ukweli, uliyokua ukifanya na Jackson, sitaki kuamini kama wewe unge fanya mambo kama haya, na ndo maana jana mkapanga mnitoe nje ya chuo mkisingizia kikao, kumbe mlikua na yenu wewe na OKAKA, haki….”
“sio ivyo Donald mpenzi wangu”

Pamela aliji kuta akisesereka chini na kupiga magoti akizidi kulia, bila kuongea ki ukweli alishindwa pa kuanzia pia alishindwa kuelewa picha zile zilitoka wapi., ila katika akili yake alijua ni mipango ya okaka ya kuwatenganisha aliilia sana Pamela,
“naomba utoke, niache na umaskini wangu, toka nje ,Pamela nenda tu”
Wakati Donald akiongea maneno hayo alikua nayeye akilia vile vile, ili kua ni picha ya kuuzunisha sana kwa pande zote mbili, kwelli walitoka mbali sana hawa kuamini kama siku kama iyo inge tokea katika mapenzi yao, ili kua ni siku ya kuuzunisha sana, bila Donald kujua ukweli uliojificha nyuma ya pazia
, Donald alimvuta Pamela na kumtoa nje ya chumba chake nayeye kufunga mlango, huku akimuacha Pamela akilia nje

huku wana funzi wengine waki pita na kumshangaa, aliinuka kwa hasira na jazba kwa lengo moja tu kumfuata okaka,

Alishuka ngazi mbili mbili mpaka alipo fika ngazi za chini na bahati nzuri ali mkuta Raisi okaka akiwa na wana funzi wengine .
“oooh Mrembo wangu”
Alijikweza Raisi okaka ila Pamela alimuangalia kwa hasira na kutojua amfanye kitu gani, alibaki akihema juu juu huku akibanwa na kwikwi la hasira na kumzaba kofi.



Kofi lile lilisikika kwa sauti ya juu sana na kufanya wana funzi wengine kugeuka nyuma, ili kujua nini kinaendelea,k ilikua ni kitendo cha kushangaza sana kwa Raisi wa chuo kupigwa kofi, mara ya kwanza
walijua wenda wawili hao wana utani,ila haikua ivyo haikuwa katika hali ya utani mtu aliye mpiga ukofi alitamani hata amuuwe kama ange kua na uwezo.
“sikiliza Jackson, hivi unadhani mambo uliyo fanya ndio suluisho la kunipata, hilo sahau, nampenda
Donald, najua tume gombana lakini kaa ukijua kuwa sitokuja kutemnbea na wewe hata wana ume wote wafe duniani ubaki peke yako”
Pamela kweli alifura kwa hasira ila hakuna hata mmoja aliye jua nini kinaendelea hawa kujua bado kwanini Pamela anafoka huku akilia kwa hasira sana, wana funzi walizidi kusogea na kutengeneza duara ili wajue nini kinachoendelea, lili kua ni jambo zito sana kwa Rais okaka kudhalilishwa kiasi kile, ila kwa wakati huo hakuweza kuongea lolote kutokana na aibu iliyo mpata, alibaki akimwangalia Pamela jinsi anavyo foka na kuzidi kujaza watu
“bado sija maliza na usifikiri nikimaliza hapa tutaongea tena!, nampenda Donald wangu, sikupendi Jackson nakuchukia sana, nakuchukia nakuchukia”
Laiti kama Pamela ange kua na bastola wakati ule angelikwisha mmaliza Raisi okaka kutokana na hasira kali alizokua nazo .
aliongea maneno mengi sana huku akipayuka wana funzi wenzake walijaribu kumnyamazisha ila walishindwa na kuamua kumuacha aropoke, hakika hakuwahi kuumia kama siku hiyo, alitembea kidogo akiondoka ila alimrudia tena Raisi okaka.
“fuc** you,..! fuc** YOU!, I hate you jackson OKAKA(nakuchukia JACKSON OKAKA.)
Pamela alimaliza huku akitukana matusi na kuondoka zake huku nyuma bado akiacha gumzo hakuna mtu aliye elewa kwanini Pamela aliwaka kiasi kile.

Kila kitu alikiona kichungu kwake, hakika alikua ni mtu mwenye mawazo kupita kiasi alitamani ardhi na mbingu ipasuke, mpaka siku hiyo hakutaka kuamini kuwa Pamela alikua na mahusiano na Raisi wa chuo
kikuu hiko, allihisi ,kila kitu kimeenda juu chini, hakua na kitu kingine cha kufanya zaidi ya kuelekezea nguvu zake zote kwenye masomo yake, akiamini ipo siku ata kuja kumkomboa mama yake maskini ambae ni mfanya biashara ndogo ndogo kama chapatti na chakula cha kupika, akitumia pesa izo kumsomesha yeye,
Pamela alijaribu kuja mara kwa mara kuja kumuomba msamaha ila Donald hakuwa tayari kurudiana nae, hakika hakutaka kupenda tena mwanamke yoyote ,allitokea kuyachukia sana mapenzi kuliko wenda hata shetani mtoa roho za watu.

Leo hii Gloria rafiki yake kipenzi na Pamela alimuita DONALD ili waongee kuhusu Pamela ila Donald alizidi kuweka msimamo wake mkali,
“Gloria kama huna habari nyingine za kuongea bora uniache, sitaki kusikia habari za Pamela, niache nikasome”
“sikia Donald Pamela kuna kitu ana taka kukwambia, hakika uta msamehe. Nakuomba ujaribu kumsikiliza”
“siwezi kuongea nae, nielewe”
Donald aliondoka na kumuacha Gloria pale pale nakushindwa kuelewa atumie njia gani nyingine,

Chuki kati ya PAMELA na Raisi okaka zilizidi mara dufu hakika alimchukia sana okaka, hakutaka h hata kumuona mbele yake akikatiza,
OKAKA kila alipo jaribu kuongea nae Pamela hakutaka hata kidogo, na kumueleza kuwa ipo siku watarudiana na Donald jambo hilo lina muumiza sana akili Raisi okaka bado akiwa ana machungu na Donald akiamini wenda kweli ipo siku watarudiana nayeye kukosa kote kote,

Mitihani tayari ilianza kukaribia ya chuo kikuu wakianza kufanya majaribio mbali mbali ila kwa Pamela hakufanya vizuri katika masomo kutokana na msongo wa mawazo
hakika katika moyo wake aliona ana kidonda ambacho hakitokuja kupona maishaini, aliona dunia ipo juu chini, hakauelewa ataishi vipi bila Donald hakuelewa ata cheka na nani na nani atamfariji akiwa katika
majonzi,hakika leo hii aliumia sana kupita maelezo yaliyo jitosheleza, kila alipomuona Donald kwa mbali aliuzunika sana, ila kila alipojaribu kumfuata aliambulia patupu,
“Donald nisamehe mpenzi wangu naomba tuishi kama zamani, nita kwambia ukweli wote”
“sihi taji ukweli wowote ule Pam., naomba uniache nisha ongea hilo, niache nibaki mwenyewe , sitaki kuwa nawewe”
Hayo ndiyo majibu ambayo alipewa na Donald kila kukicha akiwa ana jaribu kumuomba msamaha,hakika aliumia sana moyoni mwake,

“nime zikuta funguo izi ndani ya begi la Donald na baadhi ya mitihani”
“una maana kuwa ameingia chumba cha kuhifadhia mitihani na kuiba mitihani”?
“ndio profesa”
“call him right now(mwite mara moja)”
Ulikua ni unoko kutoka kwa Raisi okaka akimwambia DC wa chuo hiko, kwa nia moja tu Donald afukuzwe chuo akiamini kuwa akiendelea kubaki chuoni pale ata rudiana na Pamela wakati mwingine aliwaza na kusema bora wakose wote,

Baadae kidogo Donald aliitwa bila kujua nini ameitiwa na kumkuta Rais okaka pamoja na DC Anthony Nagayyi, mzee huyo alisifika kwa kitu kimoja tu roho mbaya, hakuwa mzee wa kubabaisha hata siku moja, upande mwingine alimsikiliza sana Raisi okaka kuliko mtu yoyote Yule, ivyo manenio yale aliyaamnini kwa asilimia mia moja, Donald alivyoambiwa habari zile za kuiba funguo hakika aliona ni habari ngeni sana kwake, hakuelewa nini kinaendelea, na kukataa kuwa hakufanya kitendo kile,
“kwaio huyu Raisi wako ana kusingizia si ndio”?
“hapana, mimi siwezi kufanya kitu kama hiko mzee wangu”!
“naenda kuku fukuza chuoni hapa, unajua hiyo kesi una takiwa ukalale polisi sasa hivi?,sitaki kuendelea kulea majambazi katika chuo changu”

Aliongea DC Nagayi akiwa makini sana na kile anachoongea, na alichoongea kweli alimaanisha, kwa upande mwingine pia yeye alikua na nguvu sana chuoni hapo na mwenye uwezo kumsimamisha mtu chuoni mara moja,

Donald alipiga magoti akilia machozi akizidi kujijitea kuwa hakufanya kitendo kile, lakini machozi yake haya kumfaya DC abadilishe maamuzi yake, pale pale barua ili chapishwa na Donald kuka bidhiwa, hakuamini kile kina cho tokea

mbele yake, alimkumbuka sana mama yake mzazi, katika akli yake aliamini kuwa kivyovyote vile Raisi okaka pamoja na Pamela ndio waliopanga njama ya yeye kufukuzishwa chuoni na kuzidi kuwa chukia maishani..
Hakukuwa na jinsi tena , alikosa kila kitu alimkosa Pamela na pia kufukuzwa chuoni ilikua ni picha ya kuuzunisha sana

na kutisha kwake, hakauelewa ataenda kumueleza nini mama yake, ambae hupta pesa katika hali ngumu sana na leo akamwambie kuwa amefukuzwa chuo, hakuelewa maisha yake ataishi vipi bila elimu ambayo alikua akitegemea,

Alitoka nje huku akitembea kwa unyonge sana, alimuona Pamela mbele yake, roho ilizidi kumuuma sana na kushindwa kujizuia na kuamua kumfata pale pale,
“naona mmeamua kuona haitoshi mmeamua kuni fanya niwe mbali na nyie, “
PAMELA aligeuka na kumwangalia na kushindwa kuelewa nini Donald anamaanisha..


Kweli Pamela hakuwa ana elewa kile anachoambiwa na Donald ila alijua kivyovyote vile Donald alikua kwenye matatizo makubwa sana kutokana na kulia kwake kwa uchungu sana , hakuwahi kumuona Donald nalia kama mtoto jambo lili lokua lina tokea mbele yake, alidhani anaigiza tena picha la kihindi ambapo baadae anaambiwa wame kosea
kipande ivyo waigize tena kwa mara nyingine, ila haikuwa ivyo ulikuwani ukweli mtupu. Tena wenye maumizu yasiyoelezeka.!
“najua Pamela ume husika namimi kusimamishwa chuo, hivi nime kukosea nini, mnge niacha tu japo nisome,nanyi muendelee na mambo yenu, ila yote namuachia Mungu, “
“Donald mbona sikuelewi”?
“maisha mema”
Donald aliongea huku akisononeka sana na kufuta machozi yake yaliyo kua yakimtoka kama chem chem, hakika alitokea kumchukia sana Pamela, alijua yeye ndo aliye haribu msingi wote wa maisha yake, mbali na hapo hakujua ukweli uliojificha nyuma ya pazia,
“Donald , Donald,! Donald”
Pamela aliiita ila Donald alizidi kutembea bila kugeuka nyuma, baadae ana pata habari kuwa Donald kafukuzwa chuo, yote alijua ili kua ni njama ya raisi okaka na wala si vinginevyo. Leo hii ana enda kutenganishwa na Donald hakuelewa ita kuaje, hakuelewa ata mrudisha vipi Donlad mwanaume anaye mpenda kupita kiasi, alizidi kumchukia sana okaka, na kujialumu ile siku ya kwanza kutoka nae nje ya chuo aliamini bila siku hiyo kutoka nje ya chuo wenda yasinge tokea yaliyotokea .

Faraja yote inaamia kwa Gloria rafiki yake kipenzi ndiye aliye kua akimfariji kila siku, ndoto za Donald kuja kuwa mume wake waje watengeneze familia ilianza kuyeyuka na kuzima taratibu hilo aliamini sababu hakukuwa na jinsi nyingine ya kumrudisha Donald tena wawe wote kama zamani,

Walianza mitihani ya kufunga semester na kumaliza na wana funzi wote kufunga chuo, kila mtu akijerejea majumbani kwao kwa ajili ya mapumziko!

******

TAYARI ULIFIKA USIKU MNENE WA KUTISHA, ambapo watu wote walikua wamelala ila kwa upande wa ,MZEE DEUJI na wachawi wenzake hawa kua wamelala, walikua chini ya mti mkubwa wakiwa wame zungukwa na misukule huku

wakinywa damu za watu, pamoja na nyama za binadamu,
hakikia ilikua ni picha ya kutisha, misukule ili teseka sana, chakula chao kili kua ni pumba na unga huku waki fanyishwa kazi nzito bila kupumzika, mzee Deuij hakuacha kueleza duku duku lake juu ya Donald akitaka nayeye wamuuwe ili wamtoe msukule sababu alitokea kumchukia sana na kutamani siku aje amtese akimfanya mmoja wa misukule.
“bado kidogo mpe muda kwanza damu zipo za kutosha na misukule, ipo siku yake”
Aliongea mzee huyo kwa sauti ya kuji kwaruza sana huku pembeni yake akiwepo mmoja wa misukule aki mpepea pepea. Alichukua mkia wa taa na kumtandika mmoja wa misukule ambae alikua akitegea kazi,
“ababaaa abaaa baabaaaabaa”
Aliongea msukule baada ya fimbo ile kumuingia na kuchana mgongo wake, hakika walikua wakiteswa sana. Mzee huyo aliinuka na kukiendea kioo kilichokua mbele yake,
aliongea ongea maneno yasiyoeleweka na gafla picha ya Donald kutokea juu ya kioo kile kikubwa, hakika ulikua ni uchawi wenye nguvu na kutisha, Mzee Deuji alimuangalia kwa hasira sana Donald, na kutaka siku hiyo hiyo auwawe….



Mizunguko aliyoanza kuzunguka takribani juma moja, haya kuonesha dalili yoyote ile ya kupata kazi wala ajira yoyote ile hakika aliumia sana moyoni., jua, mvua na matusi vyote vilimuishia mwilini mwake, kitendo cha kuachishwa chuo aliamini fika kime muharibia ndoto zake, ndoto za kuja kuwa engeneer(muandisi)

mkubwa ndani na nje ya nchi pengine wa kimataifa, vyote vina futika na kuamini kuwa Pamela ndiye aliye tia dosari katika maisha yake, asali ya penzi lake na Pamela liligeuka ghafla na kuwa shubiri , alilaumu sana mapenzi, alijuta sana kujiingiza katika mahusiano na Pamela ambae leo hii alimfanya afukuzwe chuo hakika aliumia sana moyoni! na kuji ona kama yatima asiye na msaada wowote ule, aliona dunia yotekaibeba kichwani,
aliiona Dunia ime binuka chini juu tena imempiga tik taka, akiwa amekaa chini maeneo ya mwenge, bara barani akiwa ameka taa tama kabisa,
aliona jengo kubwa lilioandikwa KAY STALLION ENTERTAINMENT LIMITED,maandishi hayo yalisomeka kwa juu sana
ya gorofa hilo lililo kua upande wa pili wa bara bara chini yake kulikua kuna tangazo la ajira, haraka haraka aliji zoa zoa na kuchomekea vizuri, alivuka bara bara upande wa pili ili akajaribu bahati yake ya ajira,

Aliingia moja kwa moja na kuku tana na wafanya kazi wa hapo ambao waliokuwa wame valia sare za mashati meupe na suruali nyeusi,kila mmoja,
“samahani anti, naulizia ofisi za KAY STALLION, sijui ndo hapa”?
“ndo hapa, una taka kuonana na nani”?
“aaaah na mkurugenzi”
“kikazi au kiofisi”?
“kikazi”!
“una mihadi nae”?
“aaaah hapana, ila nime kuja kuomba ajira, tafadhali naomba uni ruhusu nimuone”
Mwanamke Yule ambaye aliye onekana na dharau sana, alimuangalia kuanzia chini mpaka juu na kubenua mdomo

wake ambao ulikua mkubwa kiasi.
“gorofa namba 12 ingia hapo kwenhye lifti, uki fika mkono wako wa kushoto , mlango wa kwanza ndo ofisi yake ilipo”

Aliongea dada Yule na Donald kushukuru sana, haraka haraka aliingia ndani ya lifti na kubonyeza nambari 12 kama alivyo agizwa, na lifti hiyo kuanza kupanda juu, baada ya kufika ili jifungua na taratibu kutoka nje akikagua mlango ule ambao aliagiziwa, alichomekea tena vizuri na kujiweka sawa kabisa!
Baada ya kugonga baadae kidogo ana ruhusiwa kuingia na kukuta wazee wawili wa makamo kidogo hakika

walionekana kuwa ni mabosi sababu ya vitambbi vya wastani, baada ya kusalimiana nao ana kaa
chini na kuwaelezea shida yake, hakika alikua ana taka ajira yoyote ile hata kufagia vile vile. sababu Alisha zunguka sana na kuchoka pengine alimaliza jiji zima la Dar es salaam kuomba kazi na kuto pata, bado kichwani kwake hakuacha kumlaumu Pamela na kumchukia, ,

“ vyeti vyako nime viona, upo vizuri sana, sema hapa sisi, tuna taka kuanzia digrii na kuendelea”
“naomba nisaidie mzee wangu, hata kufagia nita fagia na kufuta futa hata kiti chako”
“hapana bwana Donald, nenda tu”
Baada ya ubishani ule ghafla simu ya mezani iliiita na mkurugenzi Yule kuuweka mkonga ule sikioni,
“yes una ongea na KIBANGARA, ndio Tumaini kibangara, nili shwa kwambia umlete huyo kijana, si ulisema alipata ziro kidato cha nne!, mlete tu,…….ndio ndio hakuna tatizo ata pata nafasi nzuri tu, .. actually ataongea na Emmanuel Senny ata mfanyia mipango yote, NO NO NO NO JUST BRING HIM TOMORROW (hapana, hapana, mlete huyo kijana kesho).

Wewe ni ndungu yangu, haina haja , mlete tu kijana wako, okay sawa kazi njema, ”
Maneno yale yaliipenya ndani ya masikio ya Donald nakuelewa fika kuwa ajira wana peana watu wana ojuana, hakika aliumia sana, kujua kuwa anaeenda kupewa nafasi ya kazi alipata ziro,
“nadhani tusha malizana una weza ukaenda Mr, Donald!”
Aliongea mkurugenzi huyo kibangara baada ya kukata simu ile na kuendelea kaundika makaratasi yake yali kua juu ya meza,
Kweli alikua kama ame changanyiikiwa kuliko kawaida, hakua na jinsi zaidi ya kukubaliaana na matokeo, kwa kua alikua hana hata nauli mfukoni kutokana na kuzunguka tangu asubuhi, aliamua kutembea kwa miguu mpaka nyumbani kwao sinza, jasho jingi sana lili mtoka kwa wingi, jua kali la saa saba lili zidi kuwaka likimuunguza,

Akiwa amechoka sana alifika karibu na nyumbani kwao kwa mbali sana aliona gari aina ya NISSAN SAFARI, hakua na haja ya kujiuliza sababu alijua moja kwa moja alikua ni Pamela, roho ya chuki dhidi yake ilizidi kumungia mara dufu, na kuzidi kupandwa na hasira, hasa alipo muona kwa mbali anatoka na kutaka kuingia ndani ya gari,
“Donald nili kusubiri sana mpaka nataka kuondoka ,ulikua wapi”?
Donald hakujibu lolote alipitiliza ndani na kukaa juu ya kochi huku Pamela akiwa nyuma yake kwa nia moja tu amuombe msamaha ili waendelee na mapenzi hakika bado alimpenda sana Donald kupita kitu chochote chini ya jua, hakuweza kuishi bila mwana ume huyo…



Bado Pamela hakuweza kuishi bila Donald kweli alikiri alimpenda sana Donald, japo kua kwao alipewa kila kitu kutoka kwa wazazi wake walikua na pesa nyingi za kutosha ila moyoni alihisi kitu kimoja kime kosekana mwanaume Donald, katika maisha yake alijua kuwa pesa ndo kila kitu, ila leo hii msemo huo ana utupilia mbali, alikaa pembeni ya Donald

akiwa mnyonge sana na kumwagalia Donald machoni na kuumia sana ndani ya moyo wake!
“Donald naomba nikuelezee kila kitu, tafadhali naomba uni sikilize sana”
“nakusikiliza”
“Jackson sikua na mahusiano nae yoyote yale niamini,”
“hiko ndiko kilicho kuleta,? Pamela hujui hapa navyo teseka kwa ajili yako maisha yangu yote ume yaharibu wewe, NAKUCHUKIA SANA, mimi ninge kua wewe wala nisinge jisumbua kuomba msamaha, hujui moyoni mwangu nawaza

nini, nenda , siku taki nenda nje, sitaki kukuona tena, sahau kuwa namimi, TOKA PAMELA”
“lakini Donald, hivi ni kosa gani lisilo kua na msamaha mpenzi wangu, sawa naomba uni samehe, nipo chini ya miguu yako”
Pamela alijikuta akipiga magoti huku akilia machozi na kulowanisha mashavu yake, kweli alilia kwa uchungu, ilikua ni bora akose vitu vyote lakini sio kumkosa Donald, hakika alimpenda sana, alimpenda mno,!
Ila japo alipiga magoti na kulia machozi Donald hakuwa tayari kutoa msamaha hakutaka kumuona, alisahau mambo mengi yaliyo pita pengine aliyo fanyiwa na pamela, alisahau kipindi cha nyuma Pamela alishawahi kuwalipia kodi ya nyumba yeye na mama yake walipo taka kufukuzwa, yote mema aliji kuta
akiyasahau, alisimama juu na kumvuta Pamela nje na kumtoa akitumia nguvu, hakika roho ya hasira na chuki vilimuingia kichwani huku akibishana na nafsi moja inayotaka amsamehe Pamela, hakutaka nafsi iyo imteke akili yake
Mama yake akiwa nje alisikia kila kitu na kutoamini kama mwane angeweza kufanya kitendo kama kile,
“sawa Donald, mimi naenda, leo hii nalia kisa wewe, nalia machozi uni samehe, una ni fukuza kama tulianza mapenzi jana, sitaki kuamini, asante Donald, mimi naenda”
Yalikua ni maneno ya kuuzunisha sana, aliongea huku akilia machozi , hakika ilikua ni picha ya kuuzunisha sana, Donald alishindwa kujibu lolote na kuubamiza mlango,
“mwanangu kuna nini”?
“hakuna kitu Mama”
“kanieleza kila kitu mwanangu, , mimi kama mama yako naomba umsamehe”
“hapana mama, hujui tu nakupenda sana mama ila kwa hilo sitoweza”
Hakika Donald hakuwa tayari kumsamehe Pamela, laiti angejua kuwa Pamela hakuwa na makosa ange msamehe mara moja hakika alikua ndani ya penzi la giza ambalo hakuweza kuona mbele wala kupapasa popote pale, aliumia sana.

************

KITENDO CHA PAMELA KUTO FANYA VIZURI katika masomo yake kina mchukiza sana baba yake mzee Deuji kweli alivyopewa matokeo ya Pamela hakika alichukia sana.
“kwanini ume feli Pamela, kwanini ume feli? Najua Yule mwanaume asiye kua na mbele wala nyuma ndo anakufanya ufeli”
Alifoka Mzee Deuji wakiwa katika meza ya chakula usiku wakila mezani ambapo pia alikuwepo ERICK.
“lakini baba Erick , si umuache kwanza mtoto ale. Ndo umseme”
Alizungumza mama yake pamela
“hapana, ale nini, siwezi mimi kulea upuuzi, ame feli sana. . Yule mwana ume Yule Donald ndo anamfanya afeli, ila dawa yake ipo jikoni,”
Ki ukweli hawa kuelewa kwanini Pamela hakufanya vizuri katika masomo yake hawa kuelewa kuwa leo hiii Pamela hakufanya vizuri sababu wali gombana na Donald na si vingivevyo,
Erick akiwa pembeni alimuonea huruma sana MDOGO WAKE hasa alivyo muona akiwa katika hali ya unyonge, alimshuhudia mdogo wake akianza kulia tena kwa kwikwi,

Pamela kwa hasira alisogeza sahani pembeni na kuinuka. chakula hakua na hamu nacho tena, alikiona kichungu alipandisha ngazi na kuelekea chumbani kwake na kuji fungia huku akianza kulia machozi na akilitaja jina la Donald,
“una muona mwanao alivyokua kiburi, mimi naongea yeye kaondoka”?
“sio ivyo , unge muacha kwanza ale”
“una mtetea tu ujinga, na wiki ijayo Grayson ana kuja Yule mtoto wa DOKTA HENRY Mallewo , Yule wa England ana kuja kuji tambulisha rasmi kama mchumba wa pamela, sasa ongea na mwanao”
“ nita ongea nae nini !”?
“uongee nae vizuri, asije kunitia aibu”

******

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG