Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 5/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 5 KATI YA 10
*******
 *******


ILIKUA NI SIKU YA JUMATANO KICHWA kilimsumbua sana Charles akiwa ana jisomea
darasani, na kuamua kuacha kusoma akitafuta duka la madawa ili aweze kutuliza kichwa chake kiweze kutulia ila alizunguka maduka mbali mbali ya dawa na kukuta yame fungwa, na kuamua kwenda mbali kidogo na chuo, ila alishangazwa siku iyo alipo kua duka la madawa alimuona RAisi okaka akiwa nayeye duka la dawa,
akinunua dawa za usingizi , mwanzo hakuelewa maana yake lakini alipo chungulia nje alimuona anaaingia ndani ya gari , gari hilo alii tambua sana lililkua ni gari la Pamela, hakika alielewa kuna kitu kita kua kinaendelea,
taratibu nayeye alitoka nje na kuchukua boda boda akiwa fuatailia nyuma nyuma. Mwishowe wali fika katika moja mgahawa na kuwa ona wame kaa, kwa macho yake ali mshuhudia Raisi okaka akiweka madawa yale ndani ya juice ya Pamela, baada ya muda mfupi alivyoangalia pembeni alimuona mtu kashika kamera na kuanza kuwa piga picha za mnato, jambo lile lili mshtusha sana.
Alimshuhudia Pamela anavyo bebwa na Raisi okaka huku picha ziki zidi kuchukuliwa na mpiga picha huyo na mwishowe kuingia ndani ya hotel iliyoku pembeni..

************

“IVYO NDIVYO ILIVYO KUA SIKU IYO”
Baada ya kusikia stori hiyo Donald alikua ni kama ameganda na kupigwa na bumbuazi hakuelewa nini afanye, alijiona ni mkosaji mbele ya Pamela,moyo ulimuuma sana alivuta kumbu kumbu kipindi chote cha nyuma jinsi Pamela alivyo kua akimuomba msamaha pengine na kumpigia magoti, alielewa fika alikua ni mkosaji , alihisi mwili wake umepigwa na ubaridi,
“kwanini siku msikiliza”!
Aliwaza Donald
“ina kubidi umta fute Pamela anakupenda sana,”

Baada kuongea maneno yale ambayo yalimuumiza sana Donald na kumfanya ajute Charles aliamua kuondoka zake huku nyuma akimuacha Donald akiwa katika hali ya mshangao sana,

Hakua na wazo zaidi ya kumtafuta Pamela kwa wudi na uvumba bila kujua tayari Alisha chelewa..





SIKU mbili zili pita wazazi wa Pamela walizidi kuingiwa na mashaka kitendo cha mtoto wao Pamela kupotea katika mazingira ambayo yalileta utata na ku leta gumzo , ila hakupitia getini walivyo zunguka uwani walikuta matofali yakiwa yame pangwa pembeni kudhihirisha dhahiri kuwa aliruka ukuta ila hawa kujua ni wapi alienda walitoa taarifa vituo vya polisi lakini hakukuwa na dalili yoyote ile ya Pamela kuonekana. mama yake mzazi alichanganyikiwa sana, hakuelewa nini afanye kwa wakati huo mawazo yake yalifika kikomo,
“yote ume yataka wewe baba Erick”
“nime fanya nini?”
“hujui au”?
“acha kuni laumu cha msingi tumta fute mtoto”
“namtaka mwanangu sitaki kingine”
“ila nina uhakika ata kua kwa Yule kijana, Yule Donald”
Aliongea akiwa usiku huo wakiwa kitandani na kuwa na uhakika wa asilimia mia moja kabisa , na hasira kuanza kumrudia tena, japo kua usiku ulikua umeingia sana aliinuka kitandani na kuvuta droo alichukua bastola yake na kufungua mlango
“unaenda wapi sasa”?
“kwa huyo Donald”
“baba chonde chonde naomba usifanye aina yoyote ya ujinga kwa mtoto wa watu”
“niache nifungwe”!

Alishuka ngazi haraka haraka huku akiwapigia simu walinzi wake pamoja na jeshi la polis ili waweze kuongozana , kweli muda mfupi baadae usiku huo defender tatu zilikua tayari zipo nje ya geti la mzee Deuji.

HAKUTAKA kuamini kama leoo hii kakimbia nyumbani kisa mapenzi , mali zote walizo kua nazo na pesa nyingi walizokua nazo ila aliona dunia ime mpa kisogo, kumkosa Donald ilikua ni sawa na kifo, hakua na wazo lingine zaidi ya kujiua , alitembea bara barani mwenyewe akiwa kama mwendawazimu na mara kibao akikoswa koswa na magari kutokana na mawazo tele aliyo kua nayo kichwani mwake, hakutaka kurudi tena mikononi mwa wazazi wake, ikimaanisha kuwa ni bora afe na kujiua , tayari alikua amefika daraja la
salenda akiyaangalia maji yaliyokua chini ya daraja , aliamini kuji tosa ndani ya maji ange kufa na maiti yake isinge onekana daima, picha ya mama yake mzazi akilia kwa uchungu ili jijenga ndani ya ubongo wake, aliji ona anatolewa ndani ya maji akiwa amekufa tumbo lake limejaa maji,
japo alielewa mfa maji aishi kutapa tapa, lakini aliiona ni bora kuta pa tapa kuliko kuku bali kuishi na mwana ume asiye mpenda kufa wakati huo aliona ni kitu cha kawaida kweli alidhamiria kufa, , alilia sana akiwa daraja la salenda.

“DONALD KUNA SIMU YAKO”!
“KUTOKA KWA NANI”?
“PAMELA”!
Donald aliruka na kuichukua simu ile na kuiweka sikioni haraka haraka
“Donald naomba unisikilize kwa makiini sana, wenda hii inaweza ikawa sauti yangu ya mwisho kuisikia, nisingependa kuchukua uamuzi huu bila kukwambia Donald, nakupenda sana”
“Pamela mbona sikuelewi”?
“uta nielewa ,kwa heri Donald, labda tutaonana ahera au popote pale lakini sio hapa Duniani tena”
“Pamela nime ujua ukweli tayari, nakupenda sana, upo wapi, naimbie tafadhali, nije tuongee!”
“nipo daraja la salenda, siwezi kuishi tena Donald nakupenda sana, hata nikifa leo, naomba ujue kuwa mimi nina kupenda sana, pengine kuliko mtu yoyote Yule chini ya hili jua”
“Pamela sikia nakuja”
“ume chelewa Donald, I LOVE YOU, bye bye…ti tii”
Kwa upande wa pili sauti ya Pamela ili sikika ikiwa inalia kwa uchungu sana, kweli alimaanisha na simu kukatwa , yalikua ni maneno ya kutish nay a kuogopesha kwa Donald, moyo wake ulimwenda haraka na kuzidi kuingiwa na hofu nyingi.
“ halloo halloo Pamela”
Donald alitupa simu chini na kuruka kochi lili lokua mbele yake na kuparamia stuli iliyo mfanya adondoke lakini aliinuka na kuuwendea mlango , alikua kama amechanganyikiwa sana , alichomoka kama mkuki akiwa na wazo moja tu kuelekea daraja la salenda kumuwahi Pamela, hakuwa na uhakika kama angemuwahi kutokana na umbali aliopo…


Mama yake mzazi aliyekua pembeni yake ilibidi ashangae hakuelewa nini kili mkimbiza mwanae alimuitaa lakini alimuona anatokomea akikimbia kama mwendawazimu kabisa,
Alitoka mbio mbio mpaka stendi zilipokua zime paki boda boda ziki subiria abiria wenye haraka, hakuongea chochote zaidi ya kurukia boda boda moja iliyo kua mbele yake kati ya nyingi zilizokua pale na kufanya kidogo piki piki ile idondoke,
“vipi kaka”?!
“twende daraja la salenda”
“elfu saba”
“twende bwana”
Dereva Yule alimsikiliza mteja wake na kutii amri ile, safari ilianza huku mara nyingi Donald akimsisitiza dereva huyo aongeze mwendo kasi wa boda boda hiyo, hakukuwa na sababu ya kumkatalia mteja wake,
gia ili pandishwa na boda boda kuzidi kupea ikienda kwa kasi sana na kufanya upepo mwingi upulize na kusababisha machozi yaanze kumtoka Donald kutokana na upepo ule, mawazo tele yalizidi kusha miri ndani ya ubongo wake alijua

kivyovyote vile Pamela ange kufa au kujiua.
kwa hali yoyote ile alijiona alihusika hakutaka jambo lile litokee . ndani kwa ndani alimuomba Mungu sana ili aweze kumfanya Pamela aweze kubadili maamuzi yake, sababu alimjua vizuri sana Pamela na alikua akiongea kitu alikua akimaanisha ,
“vipi, mbona umesimama”?
“mafuta yame kata,subiri niende sheli pale”
“ una akili wewe MSHENZI nini, mbona mna kua na makusudi”
“broo nisubiri hapa nakuja sekunde chache”
“sina muda huo”
Kitendo cha boda boda ile kuisha mafuta kilizidi kumuumiza sana kichwa na kuzidi kupagawa akiamini kuwa muda unaopotezwa hapo ili pelekea kabisa kifo cha Pamela, alianza kukimbia mbio tena kama mwenda wazimu huku nyuma dereva Yule akilalamika anataka pesa yake ila alizidi kukimbia mbio,

Alivyo fika mbele kidogo alitafuta piki piki nyingine na safari ile kuanza, dakika chache baadae alifika daraja la salenda na kumlipa dereva Yule, moyo ulizidi kumwenda mbio baada ya kumkosa Pamela darajani hapo,
picha mbaya ya Pamela akitolewa ndani ya maji akiwa amekufa kwa kumeza maji

mengi ilianza kupita ndani ya kichwa chake hakuelewa ange pokea vipi habari zile, alitembea taratibu na kuchungulia chini ambapo aliona maaji yanazidi kwenda kwa kasi sana
“Pamela, Pamela!”

Aliita Donald baada ya kumuona Pamela upande wa pili wa barabara, akiwa tayari mguu mmoja upo ndani ya daraja huku mwingine ukiwa nje kumaanisha kuwa kitendo cha kuweka mguu wa pili kilimaanisha kuingia ndani ya maji yenye kina kirefu kwenda chini,

Bila kuangalia magari Donald alivuka bara bara ile , kilicho sikika hapo zilikua ni kelele za matairi kukwaruzana na rami kelele ambazo zili mfanya kila mtu ageuze shingo yake kushuhudia ajali ile mbaya ya gari kubwa la mizigo lililokua linaenda kwa kasi sana, kila mtu aliweka mikono yake kichwani wengine midomoni,

“MUNGU WANGU”!

Ilisikika sauti ya mwana mke mmoja aliye shuhudia gari kubwa lile liki simama ghafla miguuni mwa Donald, kila mtu alidhani kuwa Donald ange kufa pale pale ila dereva Yule alijaribu kuvuta Breki zile huku akiwa na hofu. Nayeye hakuamini kuwa hakumgonga mtu aliye kua akivuka bara bara,

Donald hakutaka kuendelea kusimama pale mbele ya gari lile ambalo lilimkosa kosa kutoa uhai wake, mawazo yote yalikua ni kwa Pamela tu, watu wengi walianza kumshangaa alivyo kua akitembea kama mwenda wazimu na kusogea darajani ambapo Pamela alikua katika hatua za mwisho kuingia ndani ya daraja hilo la salenda , lililo kua na maji yaendayo kasi,
“Pamela nisikilize tafadhali usifanye ivyo, kujiua sio suluisho, nime shaujua ukweli wote kuhusu zile picha, naomba nisamehe PAMELA NAKUPENDA SANA,”
“usinisogelee Donald, siwezi kuishi siwezi, niache tu nife, Donald huna mapenzi na mimi, , umesha chelewa”
Maneno hayo alitamka PAMELA, HUKU Donald akilia machozi jioni hiyo huku watu wakizidi kusogea karibu pengine watu wale waliokua pembeni walidhani kuna maigizo lakini hawa kuona dalili yoyote ya kamera,. yaliyokua yanatokea hapo yalikua ni ukweli mtupu kabisa!
“Pamela nisamehe , nisamehe mpenzi wangu hata wewe siku ile unge oneshwa picha zile hakika usinge kubali , fikiria Pamela , nilikua ndani ya giza nene , kumbuka tuliyopanga nyuma uta kuja kuwa mke wangu, ulini haidi izi ni changa moto tu, kumbuka ulisema uta kua namimi kufa na kupona, usini ache mwenyewe peke yangu Pamela nakupenda sana”!

Donald aliongea kwa sauti sana hakutaka kujali watu waliozidi kumzunguka wakimshangaa. yeye alicho jali pale kwa wakati huo ni jambo moja tu Pamela aweze kumsamehe na warudiane, alijikuta akidondoka chini na kupiga magoti huku akilia sana na kutembea kwa magoti akimuendea Pamela alipokua darajani tayari kwa kujitosa,

Katika maisha yake Pamela udhaifu wake ulikua ni kupigiwa magoti aliamini kuwa anaye pigiwa magoti ni Mungu peke yake, ivyo kupigiwa magoti kwake alijua kuwa kuna maana kubwa sana,

“Donald”!

Aliita Pamela huku taratibu akisogea alipo Donald na kumuinua juu na kumkombatia huku wote wakianza kulia kwa furaha hakika kwao siku hiyo ilikua ni siku mpya katika mapenzi yao, kutokupata kwa muda mrefu.
Watu waliokuwa pembeni walipiga makofi kwa kitendo kile walicho kiona mbele ya macho yao, huku baadhi ya

wadada kuanza kulia machozi na kutoelewa kwa nini walilia,ilikua ni kama filamu ya kihindi iliyo kua anahuzunisha.
“jamani nampenda sana huyu mwanaume”
Aliongea Pamela huku akiwaangalia watu wote waliiokua wakiwa pigia makofi, alimvuta Donald kwa furaha na kumbusu mdomoni bila kujali desturi na damaduni za kiafrika, ilikua ni furaha ambayo alishindwa kuizuia,
“nakupenda sana Donald”!
“nakupenda Pamela”
Waliwa pangua pangua watu ambao wengine walikua na simu zao wakiwa piga picha na kuwaacha pale,.

kilicho kua katika akili zao sio kitu kingine zaidi ya kuta futa hoteli ili waweze kufurahia ushindi wao na kufungua ukurasa mpya wa mapenzi, walipata chumba na kuingia wote kuoga kilicho tokea hapo wote walivua nguo zao na

kusherekea ushindi wao wakifanya tendo la ndoa,
hakika walikua wenye furaha sana usiku kucha waliongea mengi sana, lakini kilicho msumbua Donald bado

hakuelewa mwisho wa mapenzi yao sababu aliamini kua kuna ukuta mkubwa sana na nguvu za kuzuia mapenzi yao,
“usijali Donald, mimi ndiye ninaye kupenda usijali kuhusu baba yangu”
Hayo ndiyo maneno aliyokua akimwambia Donald baada ya kukucha,

Walitafuta taxi na kuelekea kwao sinza ambapo Donald alimkaribisha nyumbani hapo asubuhi, moja kwa moja Pamela aliingia jikoni na kuanza kupika siku hiyo mama yake na Donald hakuingia jikoni aliye kua jikoni ni Pamela kila kitu alifanya na kuosha vyombo,

alikua na furaha sana, wali kula chakula cha mchana wote na vyombo vile kuoshwa na PAMELA hakika alikua ni kama mwana familia,
Jioni ili fika tena na kuingia ndani ya jiko na kuanza tena kupika, kilipo iva kama kawaida aliiandaa mezani na wote

kukusanyika mezani, ila kabla ya kula Mama yake Donald alianza kusali akimshukuru Mungu kwa chakula alicho wapa , ivyo ndivyo alivyo amini kuwa Mungu ndiye kila kitu Duniani hata pia alimfundisha Donald katika misingi imara ya kidini,
“AMEN “
“AMEN”

Wote waliitikia baada ya sala ile ya chakula kuisha na kuanza kula. Ila kabla ya kuanza kula walisikia miungurumo ya
magari kwa nje na milango ya magari ikifungwa, papo hapo walihisi mlango una gongwa kwa upole mama Donald aliuendea mlango na kuufungua,
“Donald yupo”?
Walikua ni maaskari wapatao kumi na moja huku mikononi wakiwa na virungu.
“Donald”?!
MAMA usitupotezee muda yupo hayupo”?
“hei hapo kazi yenu niliyowatuma ni kuingia ndani na kumchukua huyo taka taka sio mahojiano”
Sauti hiyo nzito ili sikika kwa sauti ya juu sana, hakukuwa na haja kuuliza ilikua ni ya nani ili tambulika kuwa ilikua ni ya Mzee Deuji akiwa ndani ya gari huku kioo cha nyuma kikiwa wazi, aliongea kwa hasira
Askari wale kusikia vile walisukuma mlango na kuingia wakitumia nguvu,
“wewe Ndo Donald, ”?
“ndiye mwenyewe huyu, kijana una kesi ya kuteka nyara mwanafunzi wa chuo”
“tuongozane”
“haendi popote, sijatekwa, nili kuja kwa mapenzi yangu”
Pamela alisimama kwa kujiamini sana na kusogea mbele ya askari Yule huku nyuma yake akiwepo Donald alielewa fika kuwa watu wale walitumwa na baba yake sababu alisikia sauti yake.
“binti usituharibie kazi, toa hiko kimwili chako hapa, hatujaja kucheza ngoma ya mdundiko!”
“nichukueni mimi, Donald haendi popote”
Askari Yule ailimsogeza Kwa nguvu Pamela huku wengine wakimshika wakitumia nguvu
Walimpiga virungu miguuni Donald na kumvuta kwa nguvu, mama yake alilia kwa uchungu huku akiwaomba sana wasimchukue mtoto wake, askari Yule bila huruma alimsukumiza Mama Donald na kumfanya adondoke kama mzigo juu ya stuli,
“MAMAAAAAAAAAA”!
Donald aliachia ukulele kitendo cha mama yake mzazi kufanyiwa kitendo kile tena mbele yake ili kua ni bora afe kuliko kumuona mama yake ananyanyaswa tena mbele yake kwa hasira kali ambazo hakujua zime tokea wapi alichomoka kutoka mikononi mwa askari Yule aliye kua amemshika na kumuendea mmoja wa aliye mpiga mama yake na kumtwanga ngumi nzito ya mdomo hakuishia hapo alimvaa na kudondoka nae chini na kumng’ata sikio,
hakuliacha sikio lile japo alihisi maumivu makali aliyo pigwa mgongoni na virungu lakini aliendelea kung’ang’ania sikio la Askari Yule huku akizidi kumshindilia ngumi za mbavu …



Bado virungu vizito viliendelea kutua juu ya mgongo wa Donald tena safari hii askari wote walimpiga sana na virungu, ila baadae walivyomtoa tayari alikua na damu mdomoni na kutema sikio chini la askari

aliyekua akimg’ata, aliiona ni bora kufanya vile kuliko mama yake kufedheheshwa mbele yake, askari Yule alikua hana sikio la kulia alilia sana huku damu ziki mtoka sikioni,waliendelea kumpiga Donald kama mwizi,
“piga piga pigeni huyo, TAKA TAKA, BLOOD FOOL”!
Kauli hiyo ya Mzee Deuji ilizidisha moto wa askari wale na kuendelea na kazi yao ya kutembeza virungu vile , ki ukweli ilikua sio sheria wala haki ila nyuma yake kulikua kuna mkono wenye pesa nyingi na sheria kuvunjwa kabisa! Mama Donald na Pamela walikua wakilia sana kitendo cha kushuhudia Donald kupigwa vile kiliwauma sana lakini hawakua namna ya kufanya,
“Dad I hate you(baba nakuchukia), wewe sio baba yangu, sikupendi mimi sio mwanao, huwezi kufanya unyama huu ,
huyu mtoto wa watu, hivi mfano unge jisikiaje Erick ange kua anapigwa kama ivi una shuhudia ila Mungu yupo, na nina mpenda Donald ,, nampenda sana”
Maneno hayo ya uchungu yalitoka kifuani mwa Pamela akiwa ana toa machozi kama chem chem ya maji ,aliongea maneno mengi ya uchungu yaliyo jaa simanzi nyingi mno, mwana ume anaye mpenda kupigwa kama mwizi tena mbele ya mama yake mzazi
“ingia ndani ya gari upesi”!
“siendi popote”
“pelekeni hiyo taka taka kwenye Deffender haraka sana”
Alitoa agizo hilo Mzee Deuji akiwa na bastola yake mkono wa kulia akimuangalia Donald kwa hasira za wazi wazi na kudiriki kukusanya mate na kumtemea usoni alivyopitishwa mbele yake,
“kacha kacha”!
Alikoki bastola na kumuwekea utosini kumaanisha kuwa anaenda kumuuwa wakati huo huo, zilikua ni hasira zilizo mfanya mpaka apate makunyanzi usoni,
“kwanini una mfanyia ivi mwanangu lakini”?
“tena wewe mama nyamaza, nitaanza nawewe, nilisha muonya mwanao asitembee na binti yangu, tena nahisi wewe ndo uliye mtuma,, nili sha sema ninyi hamna hadhi taka taka nyie , hivi wewe kwa akili yako, mwanao aje kumuoa mwanangu, maskini nyie , kwanza nitokee una nuka!”
Yalikua ni maneno ya kebehi kutoka kwa Deuji maneno ambayo yalimfanya mama Donald ashindwe kuongea lolote na kumuachia Mungu, hakua na la kufanya wala pa kushtaki kutokana na umaskini, aliye ongea naye hapo mbele yake alikua ni tajiri aliye julikana Tanzania nzima ivyo hakutaka kuongea lolote lile, alichotakiwa yeye ni kuwa mpole sana,, alivyo taka kumsogelea Donald ndani ya Deffender alisukumizwa na kudondoka chini ,

Pamela aliingizwa ndani ya HAMMER III huku Donald akipigwa vibaya nyuma ya Deffender, Mama yake mzazi alilia sana na kuanza kukimbilia defender ile iliyokua ina ondoka, aliyekuwemo mwanae Donald lakini mwisho wake alidondoka chini kwenye michanga huku akilia,
ilikua ni picha ya kuuzunisha kwake, alihisi uchungu sana, hakuwahi kulia kama siku hiyo ila yote alimuachia Mungu wake aliye juu mbinguni, majirani waliiokua wakiishudia madirishani huku wame jifungia ndani walianza kutoka mmoja mmoja na kumuonea huruma sana huku waki mfariji kwa yaliyo tokea hapo!,

*****

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG