Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 5/10


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 5 KATI YA 10
*******
 *******

kilicho mshtua katika usingizi ilikua ni kipaza sauti kupitia kwenye spika ndani ya ndege iyo,
ambapo ili sikika sauti nyororo ikiwataarifu kuwa ndege hiyo isha fika nchini Rwanda, na sauti hiyo kuji rudia rudia kwa lugha nyingine tofauti ivyo wana oshuka Rwanda waweze kushuka,

baada ya hapo ndege iyo ilianza kuruka na baada ya masaa matano tayari ili kua juu ya ardhi ya Tanzania jijini Dar es salaam katika uwanja mkubwa wa kimataifa wa mwalimu Nyerere,

Witness alisimama na kuvuta begi lake dogo lili lokua juu sehemu maalumu ya kuwekea mizigo na kuanza safari ya kushuka ngazi,

ili kua tayari ime jiri saa kumi za jioni ambapo alishuka moja kwa moja na kuku tana taxi nje,

dereva taxi huyo alimchangamkia mteja wake na kumpokea vitu Witness ambavyo aliviweka ndani ya gari hiyo na dereva yule kuingia ndani ya gari.

"tuna elekea wapi anti?"
"nipeleke hotel yoyote ile nzuri"
"ahaa sawa poa poa,"

Dereva taxi yule alianza safari huku Witness akiwa bado ana ushangaa mji huo wa Dar es salaam ulivyo badilika ki ukweli muda mwingi sana tangu aondoke nchini Tanzania,
"wewe ni mtanzania?"

alivunja ukimnya dereva taxi yule.
"ndio , kwanini ume niuliza"?
"hufananii kabisa anti"
"sifananii kivipi sasa ?"
"rangi yako nzuri alafu anti sio siri wewe ni mzuri sana, mimi nili dhani wewe mjamaica ujue, "
"hahahahaha acha kuni chekesha jamani, mimi mtanzania halisi tena piwa"

dereva taxi ambae aliionekana kuwa ni muongeaji sana alioneakana kumchangamkia Witness ambapo nayeye alionekana kumchangamkia sana na wote kuanza kuzoeana, cheka ya witness ili fanya vishimo viingie ndani ya mashavu yaani dimpoz na kufanya uzuri wake uzidi mara dufu
"hizo dimpoz, mimi hoi"
"acha zako wewe, alafu hujaniambia ni kiasi gani mpaka kwenye hiyo hotel unayo nipeleka"
"pesa ndogo tu elfu sabini, wateja wangu wengi napenda kuwa peleka LANDMARK Hotel pale ubungo river side"
"poa basi fanya upesi tufike nimechoka"

tayari safari hii walikua maeneo ya tabata na baada ya dakika chache walikua katika foleni ya ubungo ambapo baadae gari izo zili ruhusu na mwishowe dereva taxi huyo kuegesha gari nje ya hotel hiyo ili yokua ya gorofa na nzuri,
iliyoitwa LANDMARK HOTEL.

dereva yule alitoa begi la witness na kumpeleka mpaka mapokezi ambapo alipewa funguo za chumba na kumkabidhi dereva yule pesa zake na kuingia ndani ya chumba hiko.

moja kwa moja aliiingia bafuni na kuji mwagia maji na kubadili nguo zake na baadae alipiga simu mapokezi akiagiza chakula ili ale, muda mfupi chakula kili letwa na kuanza kula,

ilivyo fika usiku alitoka nje ya hotel hiyo ili akae na kupunga upepo ambapo alikaa pembezoni kidogo na kuagiza kinywaji na kuanza kunywa taratibu,

"lazima chama kile kipite, mi nakwambia sasa, una jua nini. kwenye siasa una takiwa kuwa muongeaji,ndo maana mi namkubali sana Amani Kabour yaani ana maneno mengi sana yule mzee"

maneno yale yaliipenya moja kwa moja ndani ya ngoma za masikio ya Witness na kumfanya ageuze shingo yake nyuma ili aweze kumuona mtu anae ongea . aliya kaza macho yake sana kwa mtu huyo ambae alikua akiongea na wenzake,

picha mbaya ya wazazi wake wakiuliwa tena hasa baba yake mzazi aki katwa na panga zinaanza kuji jenga tena na kufanya mwili wake uanze kupata ganzi ya ghafla sababu aliye muona mbele yake alikua ni Rameck mtu aliye mkata baba yake na panga na kumbaka mama yake mzazi,

hasira zina zidi kumpanda na kumfanya aanze kutetemeka huku akibana meno yake kwa hasira sana, alishika glass ya kinywaji aliyokua ana kunywa na kuinuka alipo kua amekaa.
kwa nia moja tu kumfuata na kumchoma nayo Rameck glass ile aliyo shika kutokana na hasira alizo kua nazo.....


 "dady MOM is calling you"(baba mama ana kuita)"

ili kua ni sauti ya mtoto mdogo akiwa ana kuja usawa wa Rameck, picha mbaya ya wazazi wake waki uwawa ina jijenga tena hasa alipo kua bado mtoto kama yule aliye muona pale mbele yake, moja kwa moja alionekana kuwa ni mtoto wa Rameck,

hakutaka kufanya kitendo kile cha mauaji tena mbele ya mtoto yule mdogo aliye kua mbele yake,
"where is your MOM"?(Mama yako yuko wapi)"?
"in the Car,(ndani ya gari)

mtoto yule alijibu na kumfanya Rameck asimame na kuanza kuondoka huku akiwa ame mbeba mtoto yule mkononi, alishusha pumzi ndefu sana huku akibaki kumtizama Rameck ambae alimuona akiingia ndani ya gari na kuondoka zake,

aliweka glass juu ya meza na kurudi chumbani kwake ambapo aliji tupa kitandani na kulala chali huku akiwa ana tafakari vitu vingi sana,

baadae usingizi mzito una mpitia na kulala pale pale.

**********

Asubuhi kuli kucha na kuinuka kitandani huku akitembea kuingia bafuni kuji mwagia maji, baada ya hapo Witness alivaa nguo na kuvaa miwani kubwa machoni huku akishuka ngazi akienda chini na kuagiza chai , kweli baada ya kumaliza kunywa chai alita futa taxi moja kati ya nyingi zilizo kuwepo nje ya hotel hiyo,

"nipeleke town , bei gani?
"hapo utanipa elfu thelathini dada angu"
"poa utanipeleka kwenye maduka ya simu na lap top"
"sawa hakuna tabu"

Witnes akiwa nyuma ya kiti cha dereva alitoa maagizo hayo huku taxi hiyo ikianza safari ya kuondoka, kutokana na msongamano wa magari mjini wana jikuta wana chelewa na kutumia takribani masaa matatu kufika k,koo.

alivyo fika alimlipa dereva uyo pesa yake na moja kwa moja kuliendea duka moja la simu lililo kua mtaa wa Congo, na kuanza kupita duka baada ya duka akitafuta simu ambayo itakayo mfaa, baada ya kuzunguka sana mwishowe anaa mua kuchukua simu aina ya iphone ambapo baadae ana nunua laini ya simu na kuiweka ndani ya simu hiyo,

baada ya kuridhika na kila kitu ana ingia tena katika maduka ya lap top na kutafuta Lap top anayo ipenda na kununua pale pale,

alivyo maliza kila kitu na kupata alivyo kua ana tafuta alita futa moja ya mgahawa ulio kua maeneo ya hapo kari akoo ili ale,
alikaa na muudumu yule kuja na kuagiza anachotaka, .
"habari yako"?

ili kua ni sauti ya mzee wa makamo mwenye mvi mvi kiasi ambapo ali msalimia Witnes huku akiwa amesimama.
"nzuri"
"hiki kiti kina mtu"?
"hapana hakina mtu"

mzee yule kusikia vile alivuta kiti kile na kukaa pembeni ya Witness nayeye kuagiza chakula na kuanza kula.
"Naitwa Mr. Sombe"

aliongea mzee huyo huku akiendelea kula chakula na kushushia na soda.
"sawa"

Witness alijibu kiufupi na kuendelea kula
"jina lako nani"?
"Witness"
"unaishi maeneo ya hapa k,koo?"
"No"
"sasa una ishi wapi, by the way una jina zuri sana, hilo jina lina maana kubwa sana unajua,"
"asante"
"huwa napenda sana kuja kula katika mgahawa huu, ila ninge penda siku moja nikupeleke kwenye mgahawa mmoja uliopo kule juu, hapa siku izi sio pazuri sana,"
" hapana nashukuru mimi hapa pana tosha alafu naomba niache nile"
"sawa hakuna tabu shika hii business card"

Witness kuepuka usumbufu wa mzee huyo ambae alionekana kumkera alichukua kadi ile ya namba za simu na kulipa na kuanza kuondoka zake huku mzee yule akibaki kula kwa macho akizidi kumwangalia Witness aliye kua anatembea kwa maringo sana na kufanya umbile lake licheze vizuri.

alita futa taxi kama kawaida na kumrudisha hotelini ambapo baada ya hapo aliweka simu ile mpya aliyo inunua chaji pamoja na ile lap top na kujitupa kitandani,

alivyo jisachi mfukoni alikutana na ile kadi na kuitupa ndani ya kidude cha uchafu na kuiendea rimoti ambapo aliwasha tv na kuanza kuangalia habari ya saa mbili usiku.

"chama kilichokuwa madarakani UNION DEMOCRATIC PARTY bado kina endelea katika mcha kato wa kutoa misaada mbali mbali kwa watoto yatima mwenyekiti wa Chama hiko Mr, Sombe alisema kuwa wata tembelea kila mkoa...."

habari hiyo ili mshangaza sana Witness ambapo baadae ana muona Mr, Sombe akiwa ana hojiwa na waandishi mbali mbali wa habari na kumfanya akae vizuri ili kuha kikisha ni kweli aliye muona kwenye tv au macho yake yana mdanganya,

na kukumbuka sana mchana wa siku iyo alikua nae kwenye moja ya mgahawa picha mbaya sana dhidi ya chama hiko cha UDP kina mfanya Witness apate jazba kubwa sana,

Picha ya baba yake mzazi Dimalia kafifi akiwa chini anavuja damu nyingi huku kichwa chake kikiwa pembeni. inaanza kuji jenga tena upya na kuanza kupata hasira sana hasa alivyoona Mr, Sombe akipongezwa na baadhi ya watu wengi sana.

aliliendea dast bin la uchafu ambapo aliitupa kadi ya namba ya simu ya Mr, Sombe na kuanza kuita futa baada ya kuipata aliiangalia kwa hasira na kuchukua simu yake iliyo kua kwenye chaji na kuiwasha huku akiingiza namba zile zilizo kua juu ya kadi ile........

 Baada ya kuhakiki namba zile aliipa simu okay kuiruhusu iende hewani, ila ana kuta simu ina tumika anapiga tena na kukuta ina tumika tena.

aliachana nayo na kuingia bafuni kuoga alivyo toka hapo aliagiza chakula baada ya kupiga simu ya mezani kwa muuhudumu wa hoteli hiyo wa mapokezi,

baada ya muda kidogo ana letewa chakula na kuanza kula huku akiangalia taarifa mbali mbali za nchi,

habari nyingine mbaya iliyo mfanya akae ki umakini ni baada ya chama kilicho kua madarakani kukutwa na kashfa nyingine ya wizi wa pesa nyingi ambazo zili kutwa kwenye akaunti ya mtu binafsi.

alizidi kuisikiliza habari hiyo ambapo raisi wa chama hiko alijitetea na kusema kuwa ata ongea na watanzania ili kuweza kuweka sawa swala hilo.

"grii griii"

simu yake ya mkononi ndio iliyo mshtua kutoka kwenye habari hiyo alivyoangalia kwenye kioo cha simu alikuta ni namba ya Mr, Sombe haraka haraka aliiipokea huku akitoa sauti ya tv ili waweze kusi kilizana vizuri.
"Mr, Sombe habari yako"?
"salama, naongea na nani"?
"unaongea na Witness, tuli kutana leo mchana kwenye mgahawa fulani hivi kariakoo, ukanipa kadi yako ya namba za simu,"
"ahaa nisha kukumbuka habari yako binti, bado huja lala mpaka sasa hivi?"
"hapana, naangalia angalia habari za nchi alafu ndo nilale"
"unaishi wapi"?
"ubungo naishi ubungo nime panga"
"naweza kukuona kesho "?
"saa ngapi"?
"jioni jioni"
"hakuna tabu, wapi sasa?"
"nita kwambia kesho asubuhi"

bada ya maongezi hayo Witness alikata simu na kufurahi hasa alipoona mpango wake wa kumvuta karibu mr, sombe una enda kufanya kazi ,ivyo ndivyo ilivyokua kutokana na usiku tayari ulisha ingia alizima tv na kuji tupa kitandani.

***********

Asubuhi kulichuka tayari na kuta futa kitu cha kula ambapo baada ya kula alisubiri simu ya mr, sombe. kweli kama alivyo panga simu yake iliita na kuwa hidiana kuwa waku tane MLIMANI CITY bila kipingamizi Witness ana kodi taxi ambayo ili mshusha mlimani city na kumkuta mr, sombe tayari kesha fika ana msubiri

"nafurahi kuwa nawewe leo hii, ila mimi ni mtu wa serikalini embu tutoke hili eneo, si una jua tena paparazi hawa chelewi"
"sawa hakuna shida , sasa tunaelekea wapi"?
"twende ndani ya gari uta ona mwenyewe"

Witness alisimama huku Mr, sombe akiwa mbele na kuingia ndani ya gari aina ya LAND CRUISER V8 nyeusi ambazo gari hizo hupenda kutumiwa na vigogo mbali mbali au watu wenye uwezo kifedha, walikaa viti vya nyuma ambapo tayari kulikua na dereva aliye kua maalumu kwa ajili ya kuendesha gari hilo.
"Ngosha twende blue pearl hotel"

Mr, sombe aliongea huku akimwambia dereva wake huyo na safari ile kuanza .
"unaishi na nani nyumbani kwenu?"
"nipo mwenyewe"
"mwenyewe kivipi, wazazi wako wapi?"
"wapo, nasoma chuo nime panga hostel"
"ahaaa, kumbe bado unasoma"

Witness ili bidi ada nganye ili kufanya Mr, sombe asiweke mashaka yoyote yale juu yake.. gari hiyo ili egeshwa nje ya hotel hiyo ya gorofa na Witness pamoja na mr, sombe walishuka,
ambapo moja kwa moja walienda nyuma na kukaa sehemu ambayo mtu yoyote yule asingeweza kuwaona kirahisi.
waliagiza vinywaji na wote kuanza kunywa,
"naomba uwe mke mdogo, ki ukweli nime tokea kukupenda sio siri, ngoja nikwambie ukweli mimi nina mke na nina watoto pia ila ninge penda uwe mke wangu mdogo"
"No haito wezekana kwanza huja nipenda ume nitamani uta mpendaje mtu kwa siku moja"?
"sika tai ni mapema ila nime shindwa kuvumilia sasa, ndo maana nikawa straight kukwambia hili siku taka kuku anzia mbali, naamini huto juta sababu nita kujengea nyumba yako ili usi pate shida pia nataka baadae uni zalie watoto"
"hahahaha ume data wewe mzee, yaani kuniona jana tu una sema yote hayo. sasa na mkeo je ita kuaje"?
"kuhusu mke wangu niachie mimi, wewe hapa swala ni kusema ndio na kukubali wala sio vinginevyo Witness"

Wiitness ali tafakari kwa muda ki ukweli hakutaka kukubali kirahisi japo kua alitaka kumuweka sana karibu mr, Sombe ili amuangamize taratibu.
"mmmh acha basi nika fikirie Mr, Sombe, maana hili jambo lina hitaji utulivu wa hali ya juu"
"hahahahaha hayo ndo maneno sasa mrembo"
Mr, sombe alicheka huku akipiga fundo la Juice aliyoagiza
'ungejua ninavyo kutamani wewe mzee hata usinge jichekesha ivyo'
aliongea kimoyo moyo Witnes huku nayeye akiweka tabasamu bandia

baada ya kuongea mengi mr, sombe alizama ndani ya koti na kutoa vibunda vya noti za elfu kumi kumi,
"hii laki sita na nusu, uta fanya shopping ndogo ndogo pale hostel kwako, na kesho nataka niije niku chukue twende bagamoyo tuka pumzike"
"kesho saa ngapi"?
"kesho jioni saa kumi kumi nita kupigia simu, vunja vipindi sawa"
"sawa hakuna shida"
bila Kujua Mr, sombe ana jitengenezea kifo chake mwenyewe , baada ya hapo waliagana na Witnes kuchukua Taxi na kumfikisha mpaka LANDMARK hotel ambapo huko ali fika na kuanza mipango ya kumu angamiza Mr, sombe.

kitu kingine ana kumbuka kuwa wata kuja kumjua na kumuhisi .anaamua kuanza kufanya mipango ya kuhama katika hotel hio.
hii ni baada ya kusikia kuna nyumba kubwa ina uzwa maeneo ya msasani, kutokana na kuwa na pesa nyingi sana ndani ya account yake haikumpa shida kununua nyumba yoyote anayo itaka.

alichuukua namba za simu za dalali na kuanza kumta futa ili ajue ina kuaje kuhusu nyumba iyo inayo uzwa. kweli wana panga wakutane siku ili waongee, baada ya maongezi hayo alikata simu na kutoka nje.

ambapo huko anaelekea dukani na kutafuta sumu kali sana ya panya na kisu kidogo pamoja na kamba ya manila kwa ajili ya kazi moja tu iliyo kua mbele yake, alitaka Mr, sombe afe kifo cha kuteseka sana akiamini kuwa ange muwekea sumu iyo kali ya panya ange pata sana shida kabla ya kufa,

kila kitu kilienda sawa alivyo hakikisha mambo yapo sawa, alirudi hotelini ambapo aliomba aletewe chakula cha usiku ili aweze kula,.

********

"Mke wangu kesho nina safari, nina ziara Dodoma, kwenye saa kumi kumi hivi nitaanza safari"
ili kua ni sauti ya Mr, sombe aki mwambia mke wake baada ya kufanya tendo la ndoa wakiwa kitandani. akitumia mgongo wa serikali kumdanganya mke wake ila upande ulio jificha nyuma ya pazia hakuwa na ziara nia yake ili kua moja tu kwenda kuonana na Witness bila kujua anaenda kuku tana na uma-uti ambapo Witnes alipanga kumuuwa.

"mume wangu juzi tu uli toka huko leo tena jamani, si upumzike?"!
"hapana siwezi, tena ita nibidi niende na gari binafsi kimnya kimnya sababu kuna vijana kule nataka nikawaangalie kama wana fanya kazi kweli au wana piga bla blaa"
"mimi sina tatizo mume wangu, najua ni mambo ya kikazi, utaenda mwenyewe"?
"ndio nitaenda mwenyewe"
"hakuna shaka, basi kesho nita kuandalia nguo zako, uki rudi uta kuta tayari"

baada ya kutoa uwongo na mKe wake kuridhishwa ali furahi na wote kulala,

******
baada ya kukucha Witness aliaandaa kila kitu hakusahau sumu ile kali sana ya panya ambapo aliiweka ndani ya mkoba .huku akiweka kisu kidogo pia ndani ya mkoba wake ,
alivaa jins na tisheti aliendea kioo na kuji podoa vizuri alijiangalia vizuri, ila ali ghairi na kubadili nguo ya juu ambapo alivaa top ambayo ina onesha maziwa yake nusu yaani boobs ili aweze kumpagawisha zaidi Mr, sombe,

alijiangalia kwenye kiioo mara ya mwisho, alivyo hakikisha kila kitu kipo sawa aliinua simu yake na kumwambia Mr, sombe kuwa yupo tayari ivyo angeweza kuja kumchukua maeneo ya Mwenge..

baada ya muda mfupi gari aina ya Verossa ina egeshwa pembeni na Mr, sombe kushusha kioo na kumpungia mkono kua aingie ndani ya gari,

"No kaa siti ya mbele Wity"
"okay sawa"

Witness aliketi siti ya mbele na Mr, sombe kuanza safari huku jicho moja likiwa kifuani mwa Witness akimtizama kwa jicho la kumtamani huku akimeza mafundo ya mate.
"ume pendeza sana"
"asante"
"hivi Wity una jua kwamba wewe ni mzuri sana"
"hahahaha NO sijui ndo kwanza unaniambia wewe"
"impossible, mtoto kama wewe una takiwa kuwa na watu kama sisi wenye pesa sana ili tuweze kuku tunza sio unakaa na mwana funzi mwenzako hana hata pesa. wa shit watu kama hao, mimi nakwambia kitu kimoja kwamba nita kufanyia vitu ambavyo hukuwahi kufanyiwa duniani kote, kwanza nina ela za kutosha za kuweza kuku mudu"
"nafurahi sana kuwa nawewe siku ya leo hakika nita enjoy huko napo kwenda"
"yaani we usiongee tulia tulia, nataka unipe mambo yaani uni shawishi pia"
"hilo tu usijali lazima usahau njia ya kurudi kwenu"

Witness aliongea na kuzidi kumpagawisha Mr, sombe na kumfanya azidi kuongeza mwendo kasi wa gari bila kujua ana kiwahi kifo chake, hakujua kama aliye kaa nae pembeni ni Israel na muda mfupi anaenda kutoa roho yake.

baada ya lisaa limoja walifika bagamoyo na kuegesha gari kwenye hotel kubwa sana ya kifahari na kuta futa sehemu ya kukaa ambapo waliagiza vinywaji na chakula huku wakianza kula.
"hivi Wity una mpenzi au boyfrend "?
"yes ninae, kwanini una niiuliza"?
"nataka umwache"
"sasa nitaanzia wapi"?
"si una mtafutia sababu una jua mwenyewe cha kufanya"
"ila lakini nawewe si una mke hapa ngoma droo"
"hahahaha aya bwana umeshinda malkia"

waliendelea kula na kunywa, ili pofika jioni wali tafuta chumba cha kulala na kupata,

witnes ana ingia kuoga ambapo baada ya kutoka ana toka na kanga moja na kumfanya Mr,sombe aanze kupagawa na damu kumuenda mbio hasa alivyo muona Wity yupo ndani ya kanga moja na kufanya umbo lake liji chore vizuri sana, na kuuwona uzuri wa Witnes hasa jinsi alivyo umbika.

alivyo taka kumsogelea Witness alimtuliza,
"tulia kaoge kwanza . ndege wako manati ya nini, leo mpaka asubuhi nipo mzee"
" uzee mwisho chalinze mjini kila mtu baby Witness..,"
"hahahaha sawa baby nenda kaoge"

Witness ali mfuata na kumpiga busu la shavu na kumfanya Mr sombe aingie bafuni kuoga,

nafasi ile hakui lazia damu alicho fanya ali chukua mzinga wa KONYAGI uliokua ndani ya friji na kuumimimina ndani ya glass mbili ambayo moja aliweka sumu iyo kali ya panya,
baada ya zoezi hilo kuisha alirudisha mzinga huo ndani ya friji huku akimsubiri Mr, sombe atoke.

kweli baada ya muda mfupi alitoka na Wity kumrukia na kumtupa kitanda nayeye kupanda juu yake na kuanza kumshika kifuani.
"Witty mbona una kovu kubwa ivvyo hapa mgongoni"

lili kua ni kovu la risasi aliyo pigwa kipindi yupo vitani huku makovu mengine kwa mbali yali yotokana na mateso aliyo yapata kutoka vitani, Wity alimuangalia Mr, sombe machoni huku akirembua macho yake,
"Usinikumbushe mbali, makovu haya yali tokana na shangazi yangu alikua ana nitesa sana kipindi naishi kwake, tuachane na hayo"
"sawa nipe vitu sasa"
"usijali kabla ya hapo nataka kwanza mzinga uishe ili nitoe aibu,"

Witness aliinuka na kuichukua glass ya kushoto ambayo aliikariri kuwa ndo yenye sumu iyo kali sana na kumnyweshwa mr, sombe alimnywesha tena mafundo ya pombe iyo mpaka ilipo isha kwenye glass na kumjazia tena.
"ina tosha"
"noo kunywa, nataka mechi iwe tamu leo yaani hapa bado mchuzi wa pweza tu"
"mambo haya ume julia wapi"?
"mimi mtoto wa kike lazima nijue"

Mr, sombe alizidi kupiga pombe ile bila kujua kua ina sumu kali sana,

baada ya hapo kwa mbali anaanza kuhisi tumbo la kukata la ghafla kuanza kuji kunja ila haku taka kulipa nafasi tumbo hilo, aliji kaza ila baadae linazidi kumuuma sana.
"Wity tu......mmbooo, lina niuumaaa niiitiiiie muuhudumu"

Witness kuona vile alitoka pembeni na kusimama juu ya kitanda.
"Mr, sombe nafikiri una mjua sana Dimalia Kafifi, alikua ni baba yangu mzazi, sina haja ya kukwambia alikufaje ila unajua kifo chake kili tokana na nini na kwa njia moja au nyingine wewe uli husika, sasa leo hii una enda kufa, pombe ulio kunywa nime weka sumu kali sana na muda mfupi una kufa"
"nisaaaaadieeee Witiness nisameheeeeeee..."
Mr, sombe aliongea huku akiwa amejikunja.
"uta fia hapo hapo, mimi naitwa Witness Dimalia Kafifi, uta kufa taratibu sana bila msaada wowote ule"

Witness aliongea huku akivaa nguo zake haraka haraka, baada ya kumaliza kuvaa nguo zake alimuangalia Mr, sombe ambae alikua ame jikunja aki ugulia tumbo lake na kutoa kisu, ila ana ghairi kumuuwa kwa kutumia kisu na kutaka afe ivyo ivyo taratibu sana, ali fungua mlango na kutoka nje akiwa na pochi yake.

aliingia ndani ya lifti na kubonyeza kitufe ambayo lifti hiyo ili mshusha mpaka chini kabisa na kutoka ndani ya lifti.
na kuanza kutembea akiuendea mlango wa kutoka
"dada samahani naomba usimame kidogo"

aliongea mlinzi wa pale huku akiwa ana kuja na mwenzake na kumfanya Witnes asite kidogo na kusimama.


 Witness aliwaangalia wote wawili huku akiwa ana wakagua, alizungusha shingo yake nyuma kwa juu na kuona kamera ndogo ya ulinzi iliyokua juu, na kushusha pumzi.
"samahani anti"
"bila samahani"
"tunaweza kurudi ndani ya chumba ulicho toka?"
"kwanini"?
"kidogo tuna kutilia mashaka maana ume toka kwa kasi sana, kupitia kamera tumeona wenda kuna tatizo"
"hakuna tatizo lolote, nawahi nje kabla maduka haja fungwa nata futa kinga"
"kinga, aah condom"?
"ndo maana yake"
"sasa si unge piga simu mapokezi waku tafutie"
"acha tu, nime amua kunyoosha miguu"

Walinzi wale waliji kuta wana ridhishwa na majibu kutoka kwa Wity bila kujua alikua ame toka kufanya tukio la kinyama muda mfupi uliopita,

alitoka nje haraka haraka na kuita tax, na kuingia ila kabla ya tax iyo kutoka nje ya hotel hiyo Witnes alionekana kama amesahau kitu ivyo alimuomba dereva yule amsubiri kwani atarudi baada ya muda mfupi.
"ila anti pesa ita ongezeka"
"we nisubiri nakuja"

Wity alianza kutembea kwa mwendo wa haraka haraka huku akikata kushoto hii ni baada ya mshale kumuelekeza chumba maalumu cha kamera za CCTV ,

alienda moja kwa moja na kuingia ndani ya chumba hiko, na kukuta tv nyingi ambazo zinaonesha mazingira ya hotel iyo nje mpka ndani isipokuwa ndani ya vyumba vya wateja,

"dada huruhusiwi kuingia humu"

aliongea mlinzi mmoja aliye kua makini ndani ya chumba hiko.
"najua kaka yangu, ila naomba kitu kimoja unisaidie"
"nadhani huja nielewa, hurusiwi kuingia humu ndani mpaka kibali maalumu kutoka kwa meneja"
"kibali ninacho,subiri nikuoneshe"

Witness aliji fanya ana tafuta kitu ndani ya pochi yake.

na kumfanya mlinzi yule azubae bila kupoteza muda alimfuata pale pale juu ya kiti na kuzungusha mkono wake juu ya shingo ya mlinzi yule,

huku akiukaza na kumfanya mlinzi yule atupe tupe miguu huku akihangaika kutoa mkono ule. ila baadae alitulia kimnya na Wity kumuweka vizuri juu ya kiti kile.

"uta pumzika hapo kwa muda"

aliongea Witnes na kuingia kwenye mitambo ile ya komputa ambapo alianza kuta futa video mbali mbali masaa machache yaliyo pita, baadae kidogo anajiona akiwa na Mr, sombe tangu wana poingia na mwishowe kutoka nje,

bila kupoteza muda anazifuta zote ili asiweze kujulikana, alivyo hakikisha kazifuta na kila kitu kimeenda sawa taratibu alianza kutoka nje na kumtafuta dereva taxi yule. ambapo ana mpa agizo moja tu waende LANDMARK hotel,

safari ya kwenda hotelin ilianza huku moyoni kidogo akiwa na amani baada ya kummaliza m-baya wake.
"kaka jaribu kuongeza mwendo, nina haraka tafadhali"
"sawa usijali"

dereva yule alitii amri na kuanza kuongeza mwendo kasi wa taxi ile, ambapo ili kua imeshatimu saa saba usiku.
baada ya lisaa limoja na nusu tayari wali fika maeneo ya Landmark na Wity kushuka, haraka haraka alipandisha ngazi za hotelini na kuingia chumbani kwake huku akiangalia kama kuna mtu ana mfuatilia,

aliiingia bafuni na kujimwagia maji huku akiwasha tv ili ategemee kusikia habari ya kifo cha Mr, sombe ila cha kushanngaza mpaka wakati huo hakuna habari yoyote ile aliyoisikia na kudhani wenda asubuhi ange sikia habari hiyo ya msiba, allijitupa kitandani na kulala.

asubuhi kulivyo kucha alimka na cha kwanza alicho fanya aliwasha tv ambapo alitegemea ange kuta habari ya kifo cha Mr, sombe ila cha kushangaza hakukuwa na taarifa yoyote ile,
"au hakufa"?

alijisemea mwenyewe Witness huku akizidi kutafuta stesheni mbali mbali za tv izo.
alivyoona hakuna dalili yoyote aliingia bafuni kuoga baada ya kutoka bafuni alijiaanda vizuri na kuta futa baibui yaani nicab ambayo ilimziba na kuonesha sehemu ya macho peke yake.

alichukua mkoba wake na kutoka nje ambapo alitoka na kuta futa laini nyingine ya simu, aliiweka kwenye simu na kumtafuta dalali wa nyumba,

ambapo baada ya muda mfupi wana kutana Mwenge kwa jambo moja tu apelekwe kwenye nyumba hiyo ilio kua msasani, jambo lile lina fanyika mara moja na muda mchache tayari wana fika msasani kuoneshwa nyumba iyo iliyo kuwa ya gorofa na ya kisasa,

walianza kuzunguka kila sehemu ya nyumba iyo na baadae Witnes kuingia ndani na kuonekana kupendezwa sana na hiyo nyumba hasa alipoona kuwa ina andaki ndani kwa ndani ambapo hata yeye mwenyewe hakuliona mpka dalali huyo alipo muonesha,
"humu alikua ana ishi nani?"
"mzungu mmoja hivi wa Denmark, ila ameshaondoka sasa hivi"
"ali kua ana jishughulisha na nini"?
"mfanya biashara mkubwa sana alikuwa, ndo karudi huko Denmrak"

**********

baada ya siku mbili tayari malipo ya nyumba hiyo yalikua yame kamilika pamoja na hati za nyumba kukabidhiwa, na kubaki Witnes kuhamia tu,

siku iyo akiwa ana jiandaa akiwa hotelini ili akahamie nyumba yake mpya anahisi mlango una gongwa wa chumbani kwake, kitendo ambacho kina mshangaza sana, sababu ili kua ni asubuhi sana.

"nani?"
Witness aliuliza huku akiusogelea mlango ule ili aweze kusikia vizuri sauti ya upande wa pili.
"fungua mlango polisi"

Witnes alisita kidogo na kuji kagua huku akiji weka sawa na kuufungua mlango ule huku akiji uliza maswali polisi wale wana taka nini.
"niwasaidie nini"?
Witnes alishangaa sana baada ya kufungua mlango

hasa alivyoona mapolisi wale wapo nane wawili aliweza kuwa tambua maana walikua ni walinzi katika hotel ile ya bagamoyo, ivyo bila kusita alijua ni moja kwa moja walikuja kwa kitu kimoja tu kesi ya mr,sombe.
"ndo huyu"
aliongea yule mlinzi akiwaambia wale mapolisi.
"anti tuna kuhitaji"
"sawa nakuja naomba nivae"

Witnes alifunga mlango huku akita fakari kitu, baada ya hapo alivaa na kutoka nje huku akiongozana na polisi wale ambapo nje ana kutana na dereva taxi yule aliye mtoa Bagamoyo na

kujua kivyovyote vile ndie aliye waonesha mahali alipo, waliingia ndani ya gari la polisi na gari izo kuanza kutimua mbio.
mmoja wa mapolisi alitoa simu na kuiweka sikioni.

"ndio muheshiwa tupo nae hapa,"
"sikieni kwa makini naomba iwe kimnya kimnya, mumpeleke sehemu alafu nita waambia cha kufanya kuwa makini na vyombo vya habari, yaani sitaki wajue chochote"
"sawa muheshiwa nita fanya ivyo"

upande wa pili wa simu Witness alisikia kila kitu na kuitambua sauti iyo tena bila chenga ili kua ni ya Mr, sombe na kumfanya azidi kupandwa na hasira.
"mrembo kama wewe una kua gaidi, hufa nanii kabisa"

POLisi mmoja aliongea huku akimuangalia Witness, baada ya muda mfupi gari izo za polisi zili simama ndani ya kimsitu kidogo ambapo Witnes alishushwa na kuanza kutembea huku akiwa ameshikiliwa na mapolisi hao,

walitembea kwa mwendo kidogo ambapo waliishia katika kijumba kidogo kilicho jengwa na matofali na Witness kuingizwa na kufungiwa ndani na mapolisi wale kuondoka

jioni ilipo fika alisikia para kacha za watu zina kuja na ule mlango kufunguliwa ambapo walikua mapolisi wale pamoja na Mr, sombe akiwa pembeni yake.

"Witnes kafifi, mshenzi sana wewe mwanamke, una taka kulipa kisasi,? basi ume chelewa, wewe ni kukuua tu wala sio vinginevyo maana uta niletea shida"
"muheshimiwa tuna fanyaje sasa dhidi ya huyu binti,"?
"muuweni alafu muka mtupe kwenye bahari awe chakula cha samaki, fanyeni juu chini mtumie umakini wa hali ya juu sana....Witness kafifi,"

Mr, sombe aliachia misonyo na kuondoka huku akitoa kauli moja tu Witnes auwawe mara moja.

tayari polisi mmoja alimshika Witness huku mkononi akiwa ameshika bastola yake na kuondoka nae maporini huku akiwa na wenzake kwa lengo moja tu kumuuwa Witnes na kupoteza ushahidi kutokana na kuha idiwa pesa nyingi sana na Mr, SOmbe endapo jambo lile liki fanyika vizuri...

 "Mrembo, chagua una taka kifo chako kiwe cha aina gani,? ufe papo hapo au taratibu eti, naongea nawewe"

polisi huyo aliongea huku akiwa pembeni ya Witness, mkononi alikua ameshika bastola,bila kujua mtu anaye ongea nae

sio mtu wa masihala hata kidogo ni mwanamke ambaye uki chelewa kidogo anaweza kupoteza uhai, laiti ya angejua hayo yote ange muuwa mara moja,
"Naomba usiniue, bado nina hitaji kuishi"
aliongea Witnes huku akiwa ame piga magoti ana muangalia polisi yule.
"hahahaha sisi tuna fuata amri kutoka kwa mkurugenzi wetu, sio kwako, tumeambiwa tukuuwe mara moja,kama una taka kusali sali sasa hivi sala ya mwisho, ili tukupoteze duniani hahahahaha"

Polisi yule alicheka huku akimgeukia mwenzake na wote kuanza kucheka,
ila katika hali ya kustaajabu na kushangaza Witnees ana mvaa na bega polisi yule aliyekuwa na bastola mkononi na kudondoka nae chini pale pale.
bila kupoteza muda alimpiga kichwa puani, huku akiiwahi bastola iliyo kua chini na kumfyatua mwenzake ambae aliye kua ana taka kukimbia,

"simama haraka"

Witness alimuelekezea bastola polisi yule ambae alikua ana hema sana kwa wakati huo huku akionekana kuwa na wasi wasi sana kuliko kawaida maaana kitendo kile hakukitegemea.

"piga magoti mjinga wewe"
"mke mke wangu ni mjamzito usiniue tafadhali"
polisi yule aliongea kwa kubabaika kupita maelezo,
Witness alivyatua risasi ile ambayo ili penya katikati ya mguu wa polisi yule na kumfanya apige kelele sana za maumivu
"mpigie simu mr, Sombe"
"nini ni nini nimwambie nini"?
"mwambie mshamaliza kazi, mwambie mshaniua"

Polisi yule kweli alitii amri ile mara moja kuhofia maisha yake ambayo yalikua mikononi mwa Wity wakati huo,
alitoa
simu na kumpa taarifa mr, sombe kuwa kila kitu kimeenda sawa ivyo Witness amesha kufa tayari.
"safi sana, sasa utupeni huo mwili baharini, alafu kisha tuta ongea uje kuchukua mzigo wako, nime furahi sana kwa kazi yako, hakikisha mna mtupa baharini asiwaone mtu yoyote yule kuweni makini wakubwa"
"sawa bosi tuta fanya ivyo"

baada ya maongezi hayo kuisha ambapo Witness alisikia kila kitu simu ina katwa na polisi yule akizidi kuomba msamaha huku akijishika mguuni kutokana na maumivu ya risasi ile ili yopenya mguuni muda mfupi ulio pita.
"kazi nzuri sana afande, kingine Sombe ana ishi wapi?"
"anaishi Mbezi, Mbezi kule makabe, ukimuulizia tu, uta uta mpata, tafadhali usiniue nisha sema ki,,,,"
"paaaa paaa paaaaa"

Witness alifyatua bastola ile na risasi kupenya kati kati ya ubongo wa polisi huyo, baada ya kuhakikisha kila kitu kimeenda sawa, alienda kwa polisi aliye kuwa amekufa pale chini na kumuwekea bastola ile mkononi,
alivyo hakikisha kila kitu kimeenda sawa,

aliondoka eneo hilo huku akita futa usafiri wa boda boda, ambapo alimuomba dereva endapo aki fika tu hotelini ata mpatia pesa yake,

baada ya dakika arobaini tayari alifika Landmark hotel na kutoka na kiasi cha pesa ambapo alimkabidhi dereva huyo wa boda boda,

Licha ya kuchoka sana usiku huo mnene ana ingia bafuni kuoga na kutafuta chakula, ambapo baada ya kula anaamua kujitupa kitandani na kupumzika huku akitafakari taratibu jinsi ya kwenda kumu angamiza Mr, sombe.

*********


0 comments:

Post a Comment

BLOG