Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

TRUE VENGEANCE SEHEMU YA 10 MWISHO


TRUE VENGEANCE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 10 KATI YA 10
*******
 *******

Mambo yalizidi kumuendea kombo raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Alinga, taarifa
mbaya za kulipuliwa makao makuu ya CID zilizidi kumuumiza akili yake, Stuwart akiwa ameteguka mkono, kutokana na bomu lililomtupa mbali, isinge kua kuruka nje alikua kesha kufa, Hali ya Ritah ilikua mbaya sana hivi sasa alikua hospitalini ana pumulia mashine ya oxygen,
hiyo ilitosha kabisa kufikisha ujumbe kua bado muuaji hawajaweza kumtia nguvuni, Stuwart ndiye aliye kua mbele yake kumpa habari kuwa hivi sasa mauaji yata tokea kwa Waziri mkuu,
“ulisema Towo katoroshwa”?
“ndio muheshimiwa Raisi”
“ina elekea sasa wameamua kuungana”
“nafikiri kitu kama hiko”
“naomba utume majeshi yako waende kwa Waziri mkuu haraka sana, kabla mambo hayajaharibika Stuwart”
“kwakua nishajua wapi anaenda lazima nita mtia nguvuni, awe hai au amekufa”
Kitendo cha kuambiwa ivyo kilimfaya atume baadhi ya majeshi kwenda kulinda na kufanya ukaguzi kwa kila mfanya kazi wakiamini kuwa ndani mule muuaji huyo kajibadili sura ya mfanyakazi wa ndani,

****

Askari polisi walisha fika nyumba ya Waziri mkuu na kuanza kuwaita wafanya kazi wote wa kike nje ya uwanja wakiwahoji maswali mbali mbali kuhusiana na maisha yao, wafanya kazi wa kike ishirini na mbili walikua katika uwanja mkubwa wa nje wakihojiwa maswali,
“Debora yuko wapi”?
Alihoji waziri mkuu Mfaume Kiboko baada ya kutokumuona Debora na kufanya maaskari wale wapate majibu ya maswali yao,
“sijamuona leo”
“kamtafute”
Haraka haraka walitafuta na kumkuta getini na kurudi nae., hapo hapo walianza kumhoji maswali ambayo aliyajibu ipasavyo.
“umesema ulizaliwa tarehe ngapi mwaka gani”?
“si nilisha kwambia tarehe tisa mwezi wa kumi mwaka mwaka themanini na tano”
“umetokea kijiji gani”?
“Bukoba”
Maswali hayo aliyajibu yaliwaondoa wasi wasi, hawakuelewa nini wafanye sababu alijibu ukweli kabisa,
Baada ya maswali hayo kila mfanya kazi alielekea katika kazi zake,
Lakini Debora alivyofika chumbani kwake alitamani kudondoka baada ya kumkuta mtu anaye fanana nayeye kwa kila kitu mpaka mavazi, alimtizama na kuanza kutetemeka akidhania ni jini.
“wewe ni nani”?
Alihoji Debora.
“naitwa Debora”
Witness alimsogelea na kumziba mdomo wake kisha kukitumbukiza kisu chenye ncha kali tumboni mwake na kufanya Debora aanze kutapa tapa akihangaikia uhai wake,
Baada ya hapo alimburuza na kumpeleka mpaka chooni na kusubiri usiku uingie ili achimbe shimo na kumfukia, ila kabla ya kufanya chochote alihisi Debora akiitwa nayeye kuitika.
“embu njoo mara moja”
Alitoka nje na uso kwa uso kukutana na Waziri Mkuu Mfaume Kiboko na kufanya hasira zizidi kumpanda.
“usisahau niliyo kwambia jana”

Alizungumza waziri Mkuu na kumfanya Witnes ashindwe kuelewa ni kitu gani alicho ambiwa jana Witness bado alizidi kutafakari ni nini ajibu kwa wakati huo, nakujua kivyovyote vile ataenda kukamatwa.

******

Mwandishi wa habari hodari aliyeitwa Rehema Kihaka sasa alikua mikononi mwa polisi wakimuhoji na kutaka mkanda ambao uliorekodiwa na Witness Kafifi kuhusu ukweli wa mambo yanayotokea katika nchi Ya Tanzania kuanzia mauaji ya wazazi wa Witness na mambo mengine mabaya sana kuhusiana na mitandao ya madawa ya kulevya.
Bado hakutaka kutaja ni nani aliye mpa mkanda huo, sio kwamba hakumjua alimjua alikua ni Vincent Towo, mawasiliano waliyokua wakiyafanya yalisikika makao maku ya polisi, hapo ndipo Raisi Alinga aliwatuma askari wamuweke kituoni ili aweze kuutoa mkanda huo.
“binti usitupotezee muda tume kubembeleza naona hutaki kusema, kitakacho fuata hapa naomba usitulaumu hata kidogo”
“mimi sijui mnaongelea nini”
“hujui si ndio,”?
“ndio”
Ilibidi simu ipigwe moja kwa moja kwa Raisi Alinga na mmoja wa mapolisi hao ambaye alionekana kuwa na cheo kikubwa.
“mwanangu unaongea na Raisi wako tafadhali naomba huo mkanda,nina kuhakikishia kuwa utakua salama kabisa”
Rehema Kihaka alitetemeka na kuhaha sana baada ya kuongea na Raisi kwa mara ya kwanza ilimbidi tu asalimu amri na kuamua kutaja wapi mkanda huo ulipo,
Defender ziliwashwa na Rehema kuingizwa ndani ya gari kwa ajili ya kwenda salasala aliposema kuwa aliuhifadhi mkanda huo,
Towo alivuta kofia yake chini na kuanza kufuatilia Deffender hiyo kimnya kimnya mpaka itakapo ishia.

*****

“Grii griii”
Simu ya Alinga iliita na kutabasamu sababu aliona namba ya meja Sangu akiamini kua kazi yake itakua imeshakamilkka tayari na washa upata mkanda wenye ushahidi tosha, alishusha pumzi na kuiweka simu sikioni.
Muheshimiwa Raisi unaongea na Towo, hama zako hama zangu,”
Upande wa pili wa simu ulisikika.

 “TOWO nisikilize kitu kimoja, jisalimishe mapema kabla mambo hayajawa mabaya kwako”
“tayari yasha kua mabaya,hauna cha kuniambia wewe ni muuaji na sheria itafuata mkondo wake”
“tambua unaongea na raisi wako, kukukamata wewe ni kama kumuua mbu ndani ya neti huna pa kwenda Towo”
“haki itatendeka, uachie ngazi au mimi nife ti ti ti”
Towo alikata simu na kuitupa pembeni na kujua fika kupitia simu ile wangeweza kumfuatilia alipo, sababu alikua na mbinu zote za kuwakamata waharifu na kujua ni njia gani atumie ili kukwepa kuingia ndani ya mkono wa sheria,

alishaapa ndani ya moyo wake kufa au kupona ili mradi haki itendeke na wanyonge wapewe haki zao,aliangalia pembeni na kumfyatua risasi polisi mmoja aliyekua akihangaikia pumzi yake pale chini, alishawapiga askari polisi wote na kuwauwa.
“Rehema simama twende”
“kwani mbona sielewi huu mkanda una nini”?
“NDIO NDIO, RAISI ALISHIRIKI KUMUUA DIMALIA KAFIFI, WALIOHUSIKA WENGINE WALISHA KUFA,
NO USINIUE NASEMA KILA KITU,
MADAWA YA KULEVYA NDIYE YEYE RAISI ALINGA NA WENGINE WENGI WANAHUSIKA , HUWA ANA WATUMIA WASANII MBALI MBALI KUINGIZA MIZIGO HIYO HARAMU, NI HAYO TU NAOMBA USINIUE, NASEMA NASEMA, ALISHAUA WATU WENGI SANA ILI APATE MADARAKA. Paaa paaaaaa kishhhhhh”
Mwandishi wa habari Rehema KIHAKA aliyekua akisikiliza sauti ile alipigwa na butwaa sana sababu aliisikia sauti ya Mh.Mrosso alimtizama Towo aliyekuwa mbele yake na kushusha pumzi ndefu sana.
“sasa mtafanya nini, mnanitisha mnaweka maisha yangu hatarini ujue”

“tayari maisha yako yapo hatarini unacho takiwa kufanya ni kumaliza kile ulichoanza, kuna mtu yoyote yule una muamini ofisini kwako”?
“ndio ndio, yupo Gerlad Gerlad anaitwa”
“mpigie simu sasa hivi, umkabidhi huu mkanda”
“poa”
Rehema alitoa simu yake haraka haraka na kuipiga ofisini kwake moja kwa moja,na kusangazwa sana na habari alizopokea zilizo mfanya aanze kutetemeka, baada ya kuambiwa kuwa maaskari wamejaa ofisini wana mtafuta sana,
aliogopa na kukata simu pale pale na kumgeukia Towo huku akitetemeka kwa hofu, tayari maisha ya mwanamke huyu yalisha ingia hatarini alishaanza kutafutwa kwa wudi na uvumba yeye na Towo,
ili mradi tu waweze kuuzuia mkanda huo usivuje ambao ulikua na siri kubwa sana za kumfunga Raisi Alinga, ivyo alitumia njia nyingi tofauti ili mradi watu hao wawekwe kizuizini kabla mambo hayajaharibika kwake.!

Picha mbali mbali zilisha anza kubandikwa zikiandikwa kwa maandishi makubwa WANTED MAJAMBAZI SUGU ambapo mbele ya karatasi hiyo kulikua kuna picha ya Towo na Rehema,
upande wa pili walisha jua kuwa zile zilikua ni hila za raisi Alinga kuwapoteza na kupoteza ushahidi waliokuwa nao mikononi mwao,

Bado walikua na kazi ngumu sana kufikisha ujumbe kwa wananchi ambao walikua ndani ya kiza kinene sana, ilikua ni lazima wafanye jambo ili waweke ukweli wazi ili wao wawe huru na si vinginevyo!
ukizingatia ilibaki miezi michache tu uchaguzi mkuu ufanyike, na hawakutaka taifa la Tanzania liongozwe na chama hiko tena,

***
“baba naomba nikumbushe nimesahau”
“kesho ule uchafu pale nje umpe yule mzee akija Debora”
“sawa”
Aliitikia Witnes kisha kufunga mlango wa chumbani, tayari alisha muhesabia kifo Waziri mkuu sababu ya kujenga ukaribu nae sana ndani ya nyumba hiyo,
Usiku ulipo fika alichukua mwili wa Debora na kutoka nae nje mashambani kisha kuchimba shimo kubwa yeye mwenyewe na kumfukia na kifusi juu yake,
Baada ya hapo alirudi ndani na kujimwagia maji kisha kujitupa kitandani kulala,

Bado alikua akitafakari ni njia gani aweze kutumia ili amuuwe waziri huyo mkuu Mfaume Kiboko,
kwake ilikua ni kazi ndogo sana ila ilimbidi afanye taratibu sana ili aweze kujua vitu vingine vingi.
Asubuhi kulikucha na kuingia jikoni kama wafanyavyo wafanyakazi wa ndani na kuanza kuosha vyombo aliandaa chai huku akizidi kuyasoma mazingira ya hapo,
japo kua wafanya kazi wa nyumba hio walimshangaa jinsi alivyo badilika ila hawakutaka kumuulizia, baada ya siku nne kupita alishaanza kuzoea mazingira ya hapo ndani na sasa kwenda sawa kabisa na kuwa kama Debora mwenyewe.

Mara kwa mara alikua akipishana na Waziri Mkuu Mfaume kiboko na kutafuta ni jinsi gani ataweza kumteketeza waziri huyu aliyeshiriki kuwauwa wazazi wake kikatili sana, ilibidi tu nayeye amuuwe hakua na namna nyingine ya kumuacha awe hai.

***
Hali ya Ritah sasa ilishaanza kuwa vizuri kabisa na kuuruhusiwa kuendelea na shughuli yake ya kumtafuta muaji huyo akisaidiana na commando Stuwart, bado waliweka mashaka ndani ya nyumba ya waziri mkuu muheshimiwa Mfaume Kiboko,

Siku hiyo hiyo waliwasha gari mpaka nyumbani kwake kisha kushuka na kuingia ndani ya nyumba hiyo,
walisalimiana na waziri mkuu na kuanza kumchunguza kila mmoja wa wafanya kazi wa kike ndani ya nyumba hiyo, kweli walikua na kazi ngumu ya kumtambua muuaji kwa dakika hiyo sababu hata wao hawakujua ni aina gani ya sura amejivika,

Walikaa kitako huku wakiwa makini sana kumchunguza kila mfanyakazi aliye kua akipita mbele yao kwa umakini sana huku wakidiriki kuwa simamisha baadhi yao na kuwahoji maswali ya hapa na pale.
“Deboraaa, Deboraaa”
Waziri mkuu aliita
“Abee Baba”
“njoo na wisky na glass mbili kuna wageni”
“sawa Baba”
Waliagiza vileo ivyo huku wakiendelea kuongea mambo mengi kuhusiana na nchi inavyokwenda,
Kila mtu alishtuka baada ya chupa aliyeshika Witnes Kafifi kumteleza mikononi mwake na kudondoka chini, ilionesha kabisa mwanamke huyu jasiri aliona kitu kilichomshtua sana.
“Debora nini unafanya”?

Alihoji waziri mkuu na kumtazama mwanamke huyu ambaye alikua na wasiwasi mwingi sana ndani ya moyo wake huku akitetemeka kwa hofu.
“Stuuuuuwart”!
Witness Alisema taratibu huku akimtizama Stuwart machoni na kutokuelewa kuwa anaota au kweli na kumfanya agande kama barafu.
“are you okay miss(upo sawa binti)?”

Alihoji Stuwart huku akimtizama mwanamke huyo bila kujua kuwa ndiye mpenzi wake kutokana na sura aliyojibadili alishindwa kulijua hilo,
ila kwa upande wa Ritah alizidi kumkazia macho baada ya Witness kuinama akiokota vipande vya chupa na alama ya jeraha la risasi kuonekana begani ambapo yeye mwenyewe alikumbuka ndiye aliye mpiga.
“Stuwart”
Ritah aliita huku akishika kiunoni na kuanza kutoa bastola yake taratibu sana na kumkazia macho Witness. ukimnya ulitawala ndani ya seble hiyo huku kila mtu akionekana akitafakari kitu kichwani kwake…



WOTE wali tizamanakama majogoo, ilielekea kabisa kila mtu alikua akitafakari kitu kichwani mwake, kama umeme Ritah alichomoka na bastola na kimuweka Witness ukutani,
jambo lile liliwashangaza watu wote mule ndani hata kwa Stuwart , sio yeye tu hata kwa waziri mkuu Mh. Mfaume kiboko ilibidi nayeye ashindwe kuelewa ni kitu gani kili cho fanya Ritah achukue hatua ile, lakini hakusema chochote alibaki kimnya na kuamini wenda ndiye muuaji wanaemtafuta siku nyingi.
“Stuwart huyu ndiye mwanamke tunae mtafuta, mimi ndiye niliye mpiga risasi ya bega, angalia hii alama hapa”
Aliongea Ritah huku akilifugua bega la Witnes na kweli alama ile kuonekana begani,
Witness akiwa ukutani ilibidi atulie kimnya hakutaka kujaribu kubashana sababu aliamini kuwa ataharibu kila kitu na kutokumalizia kazi iliyo mpeleka hapo ya kumuuwa waziri mkuu kiboko mfaume.
Jicho lake lilikua usoni mwa Stuwart muda wote alidhani wenda ana mfananisha lakini sasa hivi alipata jibu kamili kutokana na kusikia sauti yake,
“Ritah una uhakika”?
Alihoji stuwart huku akisimama na kumuendea mwanamke Witnes, alimkazia macho na kuangalia jeraha la risasi.
“do you speak English(unaweza kuongea kiingereza)”?
Japokua alikua ana jua kiingereza ilibidi atingishe kichwa kuashiria kuwa hajui kitu, na kuzidi kutetemeka kwa wasi wasi mwingi huku jasho likiwa lina mtoka mwilini mwake,
Machozi pia yalianza kumtoka na kulia kwa kwikwi na kumfanya Ritah aliye kua pembeni yake ashindwe kuelewa nini kina mliza.
Ilibidi stuwart amgeukie waziri ili amuhoji maswali kisha yeye kumuuliza Witness kwa kuwa alisema hajui kiingereza nayeye alikua anajua lugha mbili tu kiingereza na kirusi.
“Deborah unaulizwa hiko kidonda kimetokana na nini”?
“hiki hiki kidon..nda ba..ba…”
Aliongea Witness huku akivuta makamasi na kupangusa pua zake, alionesha uoga wa hali ya juu, hawakuelewa ule ulikua ni usanii hawa kuelewa kuwa mwana mke huyo alikua ni hatari zaidi ya ukoma, lakini hata yeye hakuelewa alipata wapi usanii ule wa kulia.!
“ilikua juzi.. juuzi, nilivyo enda dukani niliteleza na kudondoka kwenye machuma yenye kutu”
Alivyoongea vile ilibidi waziri mkuu atafsiri kwa lugha ya kiingereza kama mkalimani.
“wana kataa wanasema hiko sio kidonda cha chuma ni jeraha la risasi,”
Jibu hilo lili mfanya Witness aangue kilio kikubwa sana huku akiongea lugha isiyoeleweka hata kwa Waziri nayeye alishindwa kuelewa kina choendelea.
“Let her go, I know what to do”(mwache aende najua chakufanya).
Jibu la stuwart lilimshangaza sana Ritah ila alimtuliza na kumuita pembeni kidogo waongee, alimpa wazo jingine kuwa waweze kufunga CCTV camera siku hiyo hiyo chumbani kwa mfanya kazi huyo wa kike waliye muhisi ni muuaji,
Wazo lile lilimuingia vizurisana Ritah na kumfanya atabasamu kidogo, walimuendea wazirimkuu na kumpa habari hiyo.
“cctv camera zipo kila chumba, hilo halina shida kabisa”
Walifurahi wote na jambo lile kulifanya siri sana,
Baadae walitegesha tena camera zao ndogo ndani ya chumba cha Witness bila yeye kujua na kuondoka zao.

Tayari usiku ulifika hakutaka kulaza damu aliamini asipo fanya kazi yake mapema ya kumuuwa waziri mkuu siku hiyo wenda hatoweza kupata nafasi tena.
Ndani ya kichwa chake alijiuliza maswali mengi sana juu ya ujio wa Stuwart Tanzania ambaye alikua ni mwanaume wake kipindi wapo Urusi kwenye mafunzo ya kijeshi.
Bado hakuweza kulitatua swali hilo lililokua likitesa kichwa chake, lakini hakuweza kumtambua baada ya kujibadilisha sura yake.
Alifumbua macho yake taratibu na kutizama huku na kule kisha kuingia bafuni ndani ya sink la maji na kutoa begi lake dogo lililokua na silaha ndogo,
alitoa kisu chenyencha kali na kukiweka vizuri kiunoni na kutoka mlangoni kwa nia moja tu kumuuwa waziri mkuu,
Ndani ya moyo wake kweli alishadhamilia kuua sasa, picha ya baba yake mzazi akiwa chini juu ya bwawa la damu akiwa ame uwawa kikatili huku pembeni kichwa chake kikiwa chini,
ilizidi kujijenga ndani ya kichwa chake ili kua ni picha mbaya ambayo hakuwahi kuisahau ndani ya moyo wake,
Alifika mpaka mlangoni kwa waziri na kugonga mlango
“Baba Baba”
“vipi, wewe nani”?
“Deborah”
“una taka nini”?
“kuna mgeni wako”
“mwambie kesho”
Witness alivyoona vile alitoa vichuma viwili ndani ya begi na kuanza kucheza na kitasa hiko cha kunyonga , baada ya sekunde chache tayari ulifunguka na kuitoa bastola yake ndani ya begi.
“Deborah”
“kaa kimnya mimi sio Deborah”
Witness alifungua ndani ya begi lake nakutoa picha kubwa ya baba yake mzazi Dimalia kafifi kisha kumtupia waziri mkuu aliyekua kitandani ana tetemeka kwa hofu sana.
“Sio..sisi sio mimi, mimi siku muuwa naomba usinidhuru”
“najua kila kitu, nyamaza”

**
“pi piiii piiiiiii”
Stuwart alizidi kupiga honi ya gari akiwa katika mwendo kasi waajabu ndani ya gari huku kushoto kwakeakiwepo Ritah usiku huo mnene.

Tayari walisha mtambua muuaji baada ya kumuona kwenye kamera zao akitoka chumbani kwake, ili kua ni lazima wamtie nguvuni,
mshale wa mwendo uligota mwisho kabisa kuashiria kuwa gari ipo katika mwendo kasi sana, ndani ya moyo wake alidhamiria kumkamata muuaji huyo awe amekufa au hai,
ili apewe donge nono alilohaidiwa na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Alinga,
Hata vile vile alijua ni lazima ingepata sifa kubwa na kuitanganza nchi yao kuwa na jeshi zuri bila kujua upande wa pili mwana mke huyu hatari ni mpenzi wake ambaye alidhani amekufa miaka mingi iliyopita nyuma, wakiwa vitani baada ya kukanyaga bomu lililotegwa mchangani!
Kweli Mark x ilitoka kama mshale baada ya dakika tano tayari walikua nje ya geti la waziri mkuu Mfaume na kila mtu kutoa bastola yake kisha kujigawa kila mtu upande wake,
Waliingia haraka haraka na kutulia nje ya mlango wa waziri mkuu na kuanza kusikiliza,
baada ya kusikiliza vizuri walisikia kishindo cha mtu, mlango waliupiga teke nawote kuingia kwa pamoja wakiwa na bastola zao mikononi wamezishika vizuri teyari kwa kufyatua.
Licha ya kuwahi kote walikua teyari wamesha chelewa hawa kuamini walichokiona baada ya kukuta Waziri mkuu Mfaume kiboko ameuwawa kikatili,
utumbo wake ukiwa njehuku macho yake yakiwa yame tobolewa na kisu chenye ncha kali sana, ndio alikua ana tapatapa kuta futa pumzi yake ya mwisho,
“Ohh my God(ooh Mungu wangu)”
Alihamaki Ritah na kustaajabu mauaji yale yaliyotokea ndani ya dakika saba nyuma yake, taratibu alishusha silaha chini akiwa amechoka akili yake.
Ila kabla hawashauriana vizuri walihisi muungurumo wa gari una washwa walivyo chungulia nje waliona gari aina ya NISSAN mkonge ikitoka nje kwa mwendo wa kasi.
Hawa kutaka kuchelewa na wao walishuka mbio mbio na kuliendea gari lao na kuanza safari ya kumkimbiza muuaji huyo Witnees ambayealikua akikimbiza gari sana yupo mbele yao

“Towo uko wapi”?
“wewe nani”?
“Wity”
“ahaa nipo Magomeni hapa, ulifanikisha?”
“ndio, sasa mimi ndo naingia hapa feli njoo tuku tane kariakoo njoo na shu gang Lee”!
“poa poa”
“ule mkanda vipi uli……”
Kabla ya kumalizia kuongea simu yake ilidondoka chini baada ya kugongwa kwa nyuma na gari lingine aina ya mark X hakukaa vizuri alisikia mlio wa bastola na kufanya kioo cha nyuma kipasuke, alitoa nayeye bastola yake nayeye kuanza kuwajibu.

Alisha jua teyari kuwani Commando stuwart sababu alivyoangalia kioo cha site mirror alimuona akitupa risasi huku akiwa ametoa kichwa chake nje,
alipandisha gia na kuzidi kusonga mbele, ila alishindwa kuuzuia usukani usimpeleke kushoto baada ya tairi la mbele la gari yake kupigwa risasi,
kutokana na gari hiyo kuwa katika mwendo kasi sana pale pale liliacha njia na kupinduka mara mbili huku matairi ya gari la witnesss yakiwa juu,
Hakua na ujanja tena sababu alikua amebanwa na gari ndani huku damu iki mvuja puani mwake

Stuwart na Ritah walipiga msele na kushuka ndani ya gari haraka haraka kama umeme huku wakiwa na bastola zao mikononi mwao walisogea mpaka karibu ya gari hilo Nissan mkonge.
Stuwart alimtoa Witnes ndani ya gari na kumtwanga kichwa kizito puani, na kumuweka kwenye ubavu wa gari, kisha kumuwekea bastola kichwani mwake tayari kwa kumuuwa muuaji huyo ambaye aliye kua akimtafuta kwa siku nyingi sana kwa wudi na uvumba.
“Am gonna kill you, right now, right herebitch(naenda kukuua, sasa hivi, hapa hapa malaya)”


Picha ilijionesha dhahiri tayari Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Alinga kuwa nchi ilisha mshinda, bado mkanda anaoutaka ili kufuta ushahidi alishindwa kuupata kila alipotuma watu wake na jeshi la polisi kisiri siri wote waliuwawa na kumfanya azidi kuingiwa na mashaka ilikua ni lazima ahukumumiwe kifungo cha maisha au kunyongwa kama habari hizo ziki fika UN umoja wa mataifa, alilijua hilo.

Licha ya kuwaza yote hayo bado muuaji hakuweza kumtia nguvuni ilimaanisha kuwa alikua ni muuaji hatari sana, kichwa kilizidi kumuuma kiti cha uraisi alichokalia sasa alikiona hakifai aliona kama kina waka moto wenye petrol,
Akiwa amejiinamia mezani kwake alimuona Mshauri wake Mbetto akiwa mbele yake amekenua meno yake yote nje, alinyazama na kurudisha kichwa chake chini, alikua akikesha ofisini mpaka usiku.
“Muheshimiwa nina habari nzuri sana”
“habari zipi izo”?
“Yule muuaji teyari vijana wameshamkamata na yupo chini ya ulinzi, walikua wana kutafuta kwenye simu ukawa haupatikani”
“una sema ukweli”?
Raisi kwa mara ya kwanza alitabasamu baada ya siku nyingi nyuma, moyo wake ulichanua kwa bashasha na kutokuamini kwa kile anachokisikia mbele yake.
Kabla ya kuongea kitu kingine aliingia mfanyakazi wake mwingine na kumpa simu iliyotoka makao makuu ya jeshi la polisi, alishtuka sana baada ya kupewa taarifa kuwa waziri mkuu Mfaume Kiboko ameuwawa kikatili, .

**
Chama pinzani cha UDP kwa safari hii kilizidi kuchachamaa, kweli kulikua kuna kila aina ya dalili kuwa chama hiko kingekuja kuongoza uchaguzi ujao unaokuja, kilizidi kuwa na watu wengi sana huku wakipinga vikali chama kilichokua madarakani,lakini licha ya yote haikuwa raisi kama wanavyo dhani kutokana na kushikwa kwa mpini.
Mkanda uliokua na siri nzito alikabidhiwa Gerad muandishi wa habari maaarufu sana ili akautoe na kusambaza vyombo vyote vya habari, hata yeye alivyousikiliza aliogopa sana alielewa kufanya ivyo angeingia katika matatizo makubwa hata ikiwezekana kupoteza uhai wake.
Ila alipiga moyo konde ilimbidi tu afuate maagizo aliyopewa na Rehema wakiwa wenye hofu sana siku hiyo.
“mimi naondoka Gerad, fanya juu chini huo mkanda usimpe mtu yoyote Yule.”
Alizungumza Rehema na kutoka nje haraka haraka na kuondoka zake.
Nyumbani kwa Gerad waliingia vijana wawili hao walikua majambazi walitumwa na Raisi kumfuatilia mwanamke huyo ni wapi anapoupeleka mkanda huo baada ya kusikiliza mazungumzo yao kwa njia ya simu,
Walipiga mlango teke na kuingia, bila kuongea chochote walimuweka Gerad chini ya ulinzi na kuchukua mkanda ule wenye ushahidi tosha,
Moja kwa moja walimpigia simu Raisi Alinga nakumpa habari izo nzuri zilizo mfurahisha kuliko siku zote.

***
“mbona nampigia simu hapokei, kuna kitu kuna tatizo embu, tresi simu yake”
Alizungumza Towo akiwa na mchina shu gang Lee na haraka haraka na namba za Witnes kuingizwa ndani ya mtambo maalumu kisha baadae kujua alipo,
waliwasha gari na kuanza kumfuataa alipo, kwa mbali waliona gari limepinduka, kabla ya kukaa sawa walimuona Witnes kawekwa chini ya ulinzi hasira zilizidi kumkaba Towo hasa alivyo muona mwanaume aliye mtesa sana, pale pale alitoa bastola yake na kuanza kurusha risasi. Huku akizidi kuongeza mwendo kasi.
Stuwart alimuachia Witness na kuanza kurusha Risasi ambapo baada ya gari hiyo kutaka kumgonga aliruka pembeni na kujitupa, huku wakiendelea kujibizana na kupigana risasi.
Kitendo cha sekunde chache Witnes aliruka ndani ya gari na gari kuondoka mbio wakiwaacha Stuwart na Ritah wakizidi kuwarushia risasi.
Walifika mpaka kariakoo kwenye mitambo ya shu gang Lee na sasa kazi moja tu kuanza kurudisha sura yake kama hapo mwanzo,
Alipanda juu ya kitanda na Shu gang Lee kufanya kazi yake hiyo.

**
Mbwa wa polisi walizidi kumwagwa ndani ya nyumba kubwa ya marehermu Mfaume kiboko huku wakizidi kunusa huku na kule, na baadae kutulia kwenye kichuguu wakibweka sana.
Hapo ndipo askari walifika na kuanza kufukua chini na kukuta mwili wa Deborah sababu wafanya kazi wenzake waliweza kuitambua nguo yake.
Askari wa Kitengo maalumu kwa ajili ya kupima alama za vidole tayari walisha fika ndani ya nyumba hiyo wakimwaga dawa zao ili waweze kupata alama za vidole waliingia chumba alichokua analala Witnes na kuanza kupiga picha kila mahali,
Mtambo maalumu uliletwa kisha baada ya dakika thelathini walisubiri kompyuta yao ilete picha halisi ya muuaji,
Taratibu picha ilianza kuji fungua na sura nzuri ya mwanamke kuoneka na jina kufuatia.
“Witness Dimali kafifi”!
Askari mmoja alizungumza huku akiwa anashangaa na kumfanya Stuwart aweze kusogea karibu,
Hata yeye vile vile Hakuamini alichokiona baada ya kuona sura ya mpenzi wake juu ya kioo cha kompyuta ile,
alishindwa kuelewa nini kimetokea wakati mwingine alidhani wenda kompyuta ilitoa majibu ya uongo nakuanza kuhakiki yeye mwenyewe upya,
Ila kila kitu kilikuja na kumfanya jasho kuanza kumtoka.
“namfahamu huyu binti ni shemeji yangu kwa kaka yangu anaitwa Austine”!
“huyo Austine yuko wapi”?
“kwa bahati nzuri ataingia leo na ndege ya usiku”
“ni habari nzuri, naomba atiwe nguvuni mara moja Mjuni utaongoza kikosi”
“sawa mkuu”!
Tayari operesheni ilianza na maaskari kujiandaa kwa ajili ya usiku huo kwendda kumkamata Austine mchumba wake na Witnes waliamini kupitia mwanaume huyo ni lazima watamuweka Witnes nguvuni.
“lakini mimi nina wazo”
“wazo gani”?
“Tusimkamate Austine najua kuwa huyo Witnes atakuja kumpokea na ndo hapo tuta mtia nguvuni”
“wazo zuri sana”
Usiku wa saa moja jioni tayari ulikua umefika na defender zilikua zipo njiani ziki toka kasi kuelekea uwanja wa ndegewa Mwalimu Nyerere kwa Lengo moja tu kumkamata mwanamke huyo gaidi ambaye alisumbua serikali ya Tanzania kwa kipindi kirefu sana,
Baada ya kufika uwanjani hapo walijigawa kila askari sehemu yake huku wakiwa makini sana kuwaangalia watu wanaoshuka ndani ya ndege wakitokea mlangoni.
Baada ya dakika kumi kupita walimuona Austine akiwa na mabegi yake mikononi na kuanza kupeana taarifa kupitia redio upepo,
Kila askari jicho lilikua kwa Austine lakini mpaka dakika hiyo hawakuweza kumtia machoni Mwanamke Witnes waliyekua wakimtafuta.
“ova nime muona Ova, unanipata Musa”
“nakupata ova nimeshamuona”
Walipeana taarifa baada ya kumuona Witnes akiwa anampokea mabegi Austine wame kombatiana, bila kuchelewa pale pale waliwazunguka na kutoa bastola zao., walikua teyari washa muweka Witnes chini ya ulinzi mkali huku mbwa wa polisi wakizidi kubweka sana.
Kilikua ni kitendo cha sekunde tatu na kufanya maaskari takribani arobaini kufika eneo hilo sababu walijua ni jinsi gani mwanamke huyo alikua hatari na mafia.
“ganda ivyo ivyo upo chini ya ulinzi”!
Aliongea mkuu wa kikosi akiwa na SMG mkononi mwake. Huku akiuelekezea mtutu huo upande aliopo Witness.


**
Mkanda wenye siri za mauaji ya hatari aliyoshiriki Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Alinga alikua nao mikononi mwake sasa, alichukulia ule ni ushindi tosha aliusikiliza kwa umakini sana huku akitabasamu na kukenua meno yake yote nje huku akiweka tai yake vizuri kooni,
haikupita hata sekunde saba alipigiwa simu kutoka kwa jeshi la polisi kuwa wapo njiani kumpeleka Muuaji aliyekuwa akimtafuta kwa kipindi kirefu kituoni,
alidhani wenda alisikia vibaya alibadilisha sikio na kuiweka vizuri kushoto mkonge wa simu hapo sikioni mwake!.
“unasema kuwa mpo nae sasa hivi?”
Aliuliza Muheshimiwa Raisi
“ndio tupo nae Muheshimiwa”
“njoeni nae ikulu sasa hivi niweze kumuona kabla hamjampeleka kituoni, safi sana sikutegemea kama mngeniangusha kwenye hili!”
“sawa Mheshimiwa, tupo njiani kuja ikulu”
“hakikisha mna ulinzi wa kutosha sana, kama mkihitaji kitu kingine niambieni”
Baada ya mazungumzo hayo kuisha alimtafuta Ritah na Stuwart kwenye simu kuwapongeza kisha kuwaita ofisini kwake hapo ikulu,

walipofika ilibidi tu awaambie kuwa waweze kurudi nchini kwao URUSI sababu kazi waliokuja kuifanya tayari imesha kamilika, hakukua na sababu yoyote ya kuweka kipingamizi, walimtizama Raisi Alinga kisha kupeana mikono, kwa heshima waliandaliwa jeshi maalumu na magari maalumu ili kuwasindikiza mpaka uwanja wa ndege wa kimataifa mwalimu Nyerere.
**
Picha mbali mbali za waandishi wa habari zilizidi kupigwa kila mahali baada ya muuaji aliyetafutwa kwa kipindi kirefu kupatikana hawa kuamini kama alikua ni mwanamke mrembo kiasi hiko,

defender saba zikiwa na ulinzi wa kutosha zilizidi kupiga kelele kuelekea ikulu ili kumfikisha mwanamke huyo hatari na mafia Witness Kafifi mbele ya raisi wao kabla ya kesi yake kufikishwa mbele ya sheria.
Mwendo wa dakika arobaini walikua teyari nje ya ikulu na kuingiza defender zao ndani,

walimtoa witness ambaye alikua amefungwa pingu kwa nyuma na miguuni mwake wakiamini kuwa alikua ni hatari sana,
Maaskari walimzunguka baada ya kujiona ni washindi sana, walipita mpaka ndani ya ofisi ya raisi na moja kwa moja macho yake kutua juu ya macho ya Stuwart alivyomuona tu alianza kutoa machozi na kushindwa kuelewa ni kwanini analia,
Stuwart aliyekua amekaa pembeni ya kiti ilimbidi asimame taratibu na kumsogelea karibu yake.
“Witness kwanini unafanya ivi?”
Hilo ndilo lilikua swali la kwanza kutoka kwa Stuwart akiuliza kwa upole huku akimtizama mpenzi wake aliyefungwa pingu akiwa na tuhuma za mauaji ya watu wengi aliyofanya hapo nyuma,

hata yeye alikua shahidi juu ya hilo.
“Stuwart tafuta mkanda utajua ukweli, sikufanya ivi kwa kupenda mkanda anao Raisi naomba uutafute”
Alisema Witnes akitumia Lugha ya kirusi na kufanya kila mtu asielewe kinachoongelewa,
taratibu Stuwart alirudi kwenye kiti na kutizama mezani kwa Raisina kuuwona mkanda ule, ndani ya kichwa chake ilikua ni lazima ausikilize ndipo ajue ukweli wote kama alivyoambiwa na Witness,
Lakini hakuelewa atauchukua vipi.
“sasa nime kupata, nilikwambia huwezi kufika popote pale, na adhabu yako ni lazima unyongwe mimi raisi nimesema japo sio sheria ya nchi inavyo sema”!
Alizungumza Raisi Alinga akionesha hasira za wazi wazi kabisa. Na kuwaamuru jeshi la polisi wamuweke sero mpaka yeye atakapo toa amri kama raisi wa nchi, na ndo hiko kilicho fanyika mara moja, Stuwart alimtizama Witnes kwa macho ya huruma yenye kujaa ishara sana.
“Muheshimiwa huo mkanda nina weza kuusikiliza?”
Aliuliza Stuwart
“hapana!, safari yako itaanza leo jioni nishaongea na watu wanakata tiketi, utasindikizwa na jeshi la polisi nenda kajiandae Stuwart ahsante!”
Alijibu Mh.Alinga huku akiendelea kupiga simu kwa furaha, kuna kitu kilikua sio cha kawaida kupitia macho ya Mh,Alinga hilo aliligundua tayari Stuwart,
Walipeana mikono tena kisha yeye na Ritah kuondoka mpaka kwenye hotel waliyofikia ili kujiandaa na safari ya kurudi nchini kwao Urusi,
Baada ya kujiandaa alifika nje na tayari magari ya polisi yalikua nje ya hotel hiyo na kuingia ndani na Ritah, na gari izo kuanza kuchapa mwendo jioni hiyo ya saa kumi na mbili ili kuwahi ndege inayoondoka saa kumi na mbili na nusu ya usiku,
Baada ya gari izo kufika mataa ya Shauri moyo Stuwart alitoa bastola yake na kumuwekea dereva aliyekua akiendesha gari nyuma ya utosi,
askari mwingine wa pembeni yake alivyotaka kutoa silaha alitulizwa na kiwiko na kutulia kimnya pale pale na kuzirai.

“Stuwart are you crazy(Stuwart una wazimu)?”
Alihoji Ritah baada ya kuona mambo yame badilika ndani ya gari hakuelewa kuwa ni lazima Stuwart arudi ili kuusikiliza mkanda ule alioambiwa na Witness ambao upo kwa Raisi Alinga ilikua ni lazima afanye ivyo.
“keep Quit(kaa kimnya),”
Alijibu Stuwart huku akimwangalia Ritah kwa hasira, hakuna hata askari mmoja aliyeelewa kuwa teyari wenzao wamewekwa chini ya ulinzi,
safari iliendelea kama kawaida huku dereva akiwa amewekwa mateka, akipewa amri kuwa azidi kusonga mbele aliomba redio upepo yake na baada ya gari kuchanganya alimwambia ajitupe nje,
hakua na ujanja ilibidi aruke nje mzima mzima kisha Stuwart kushikilia usukani wa gari.
“Stuwart”!
Ritah aliita.
“out, get out now”(toka nje sasa hivi)!
“please don’t do this lower your weapon(tafadhali usifanye ivi weka silaha chini)”
Maneno hayo haya kumfanya Stuwart alegeze uzi kweli alimtosa Nje ya gari Ritah, nayeye kuzidi kuchapa mwendo akizidi kukimbizwa na defender zilizo kuwa nyuma yake.!
**
“nini ametoroka”?
“ndio”
“ni lazima atakua anamfuata Yule mwanamke nina wasiwasi huo, ngoja nakuja sasa hivi, wekeni ulinzi wa kutosha hapo kituoni wekeni maaskari shupavu”
Alijibu raisi upande wa pili akiwa amechanganyikiwa sana alisimama na kutoka ofisini kwake mbio mbio akiweka tai yake vizuri na kuingia ndani ya gari.

Benzi aliyokuwemo Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ilifunga breki zake nje ya kituo cha polisi oysterbay, huku defender takribani kumi zikiwa mbali kidogo wakisubiri wamnase Stuwart waliyeamini kuwa nia yake ilikua ni kuingia na kumuokoa Witness,

walisha fanya uchunguzi wa kina na kuona picha walizopiga pamoja wakiwa jeshini, walielewa ni lazima walikua wana uhusiano watu hao hatari sana makomandoo.!
“griii griiii”
Simu ya Raisi ya mkononi iliita na kuitoa mfukoni mwake.
“this is stuwart(mimi ni stuwart)”
Upande wa pili wa simu ulisikika
“don’t make things to be worse than it is, better we arrange the meeting and we sort things out peacefull mr. stuwart(usifanye mambo yawe mabaya kuliko, bora tuandae kikao na tuyamalize mambo haya kwa amani)”
“where are you?”(uko wapi)
“sitting in my office”(nimekaa ofisini kwangu)
“I dought”(nina mashaka)
“why”(kwanini)
“if you were in your office right now, we would be having this conversation face to face”(kama ungelikuwepo ofisini kwako haya maongezi tunayoongea tungekua tunaonana hana kwa hana).
Muheshimiwa Raisi Alinga Alishajua nini maana ya maneno yale, alishaelewa kuwa Stuwart yupo ofisini kwake hisia zilimpeleka moja kwa moja kwenye mkanda wa siri kubwa na kumfanya abanwe na haja kubwa vikiambata na mkojo.
**
“Heiii,!You are going to translate this in English”(hei unaenda kunitafsiria hii kwa kiingereza)
Stuwart alimuita mmoja wa mtu aliye muweka mateka ndani ya ikulu hiyo ya Raisi,
kilichoendelea ndani hakuna hata askari mmoja aliyekua nje anajua baada ya kuingilia ukuta wa nyuma kimafia na kufika moja kwa moja ndani ya ofisi na kuwaweka baadhi ya wafanya kazi mateka.
Tayari mkanda ulianza kusikilizwa na sasa Stuwart kuelezewa nini maana ya kile kilichokua kinaendelea, mambo aliyokua akiyasikia yalizidi kumtia hasira sana.


 Ukweli ulisha kua bayana sasa, Stuwart alishajua ukweli ni kwanini mwanamke komando Witness KAFIFI ambaye alikua ni mpenzi wake na kudhani ni marehemu na leo hii yupo nchini Tanzania ili kumtia nguvuni kwanini anaua kikatili sana.,
hakuelewa ni kitu gani afanye bado akili yake iliendelea kuchanganua vitu vingi tofauti huku akiwa ameshikilia bastola mkononi mwake ndani ya ofisi ya Raisi Alinga haraka sana akili yake ili mtuma afungue mtandao hewani na autume ujumbe huo UN umoja wa mataifa ili sheria ichukue mkondo wake.
ili yeye aende kituoni kumuokoa Mpenzi wake sababu bado alimpenda sana, bado alikua na hisia naye aliamini hana hatia alistaili kuuwa, alikumbuka mambo mengi waliyohaidiana wakiwa jeshini nchini URUSI.

Chuki dhidi ya Muheshimiwa raisi zilimkaba kooni zilishindwa kuelezeka, alivyoangalia tv kubwa ya kamerapembeni yake aliona maaskari wengi wapo nje mlangoni wakijipanga vizuri ili waweze kuingia ndani, ilibidi anusuru roho yake,
Aliangaza macho yake huku na kule na kutizama juu ambapo aliona kitu kama mfuniko alipeleka meza chini yake na kuupiga kwa nguvu,
alipanda juu na kuanza kupita ndani ya tundu hilo lililofanana na bomba. Alitembea na magoti mpaka alipoona uwazi na kutua puh!
Kishindo kiliwashtua askari na kuanza kurusha risasi aliinama na kukimbia huku nayeye akirusha risasi ilikujitetea, alifika mpaka nje na kuchukua gari na kutoa mbio, hakuna safari aliyo waza zaidi ya kufikiria kwenda kumuokoa Witness kituoni.

***
“ni lazima atakua anakuja huku mimi nita mlinda huyu mwanamke nyie nendeni mkalinde nje, namjua Stuwart najua nini anawaza katika akili yake,”
Alisema Ritah akiwa pembeni ya Witness na bastola yake kaikoki tayari, aliamini Stuwart alirukwa na akili zake na anacho kifanya sio kitu sahihi kabisa ili bidi amthibiti mtu huyo kabla hajaleta madhara.
“umesema utakaa na huyu mwanamke?”
“ndio, askari wengine wakae kule mbali, Stuwart ni hatari sana”
“basi sawa!afande panga majeshi kule maili kumi wengine wakae kule fanya juu chini asijue kuwa tuna mlinda huyu mwanamke akiingia tu tuta mkamata kirahisi sana”
“sawa mkuu”
Aliitikia askari mmoja ambaye hata yeye sura yake ilionesha hofu sana mapolisi walijipanga mbali sana jioni hiyo na silaha zao huku wakimsubiri Stuwart atokee ili waweze kumtia nguvuni .
Ili shapita takribani nusu saa tayari bila ya kumuona Stuwart ili bidi wapige simu ikulu ili kujua kama teyari keshaondoka,
Jibu walilopata lilizidi kuwachanganya akili zao baada ya kupewa taarifa kuwa kikosi cha maaskari tisini wote wameuwawa vibaya sana kwa kupigwa risasi na Stuwart na magari matatu kulipuliwa na bomu.

Ili maanisha kabisa mtu wanaetaka kumtia nguvuni ni hatari ni mtu aliye tisha na mwenye mafunzo tosha ya ukomandoo. Licha ya kusikia habari hiyo haikuwafanya waache kumsubiri wakitega SMG zao tayari kwa kuanza vita.

**
Akitumia kipima mbali kidogo cha jicho moja Stuwart aliweza kuwaona askari wote walivyokua wana jipanga, alielewa vizuri sana ni lazima atakua anatafutwa kila kona ivyo ili bidi atumie umafia na kujihami,
Alimtizama kila askari aliyekua na mtutu na kushusha pumzi ndefu kidogo, mbali kidogo alisikia muungurumo wa gari na kuweka tena kipima mbali jichoni mwake alivuta akitumia lenzi kali na kuliona gari hilo Mark X nyeusi yenye vioo vyeusi lime simama,
Hakutaka kupoteza muda alishuka mbio mbio na begi lake dogo mgongoni na kufika mbele ya kioo huku akitoa bastola yake akimuhamuru mpelelezi huyo afungue mlango kisha yeye kuingia ndani ya gari siti za nyuma na kuamuru gari iondoke.

“you do anything I don’t like it, I will send you to hell. UNDERSTOOD?”(ukifanya kitu kisichonipendeza utakua kuzimu,umenielewa!)”
Aliongea Stuwart huku mlango wa bastola ukiwa nyuma ya kisogo cha Derava huyo ambaye nayeye alikua anaenda kituoni hapo hata yeye alishajua ni jinsi gani mtu huyo alikua ni hatari sio wa kuchezea,
“Askari mtu mnaemtafuta yupo kule juu nime muona waambie jeshi lako waende”
Alizungumza mpelelezi huyo akiwa juu ya usukani amefungua kioo huku bastola ikiwa nyuma ya utosi wake bila maaskari kujua kuwa amewekwa mateka tayari na mtu huyu hatari komando Stuwart.
“unasema ukweli?”
“asilimia mia”
“ova ova mna nipata hamisheni jeshi wabaki wachache hapa, twende kule juu kimnya kimnya”
Aliamuru Mkuu wa kikosi na askari kuanza kuingia ndani ya magari yao na kuondoka,
Stuwart alimpiga na kitako cha batola dereva wa gari hilo nayeye taratibu kuzama ndani.
Kitendo cha kupitisha bastola yake mbele ilipigwa teke na kudondoka chini hakukaa sawa alipigwa ngumi ya mdomo huku teke zito likitua kifuani kwake aliyumba kidogo na kurudi nyuma,
alivyokaa sawa nayeye alikunja ngumi lakini alishangaa kumuona Ritah ndiye aliye mpiga,
Ritah alivyotaka kutoa bastola Stuwart alimuwahi na kuipiga round kick na hapo ndipo kila mtu alikunja ngumi ili kupambana na mwenzake,
walikua ni mafahari wawili waliokua na mafunzo sawa.
Ritah alirusha ngumi lakini haikuzaa matunda baada ya Stuwart kuhepa chini na ngumi ile kupita juu yake, akiwa chini alimpiga ngumi mbili za mbavu Ritah kisha kurudi juu na kucheza na uso wake.
Alimfuata na kumtwanga kichwa kizito puani hakuishia hapo aliukunja mkono wake na kumbana ukutani,
Lakini mwanamke huyo pia alikua anajiweza alijibinua pale pale ukutani na kumtandika tekela kifua Stuwart lililomfanya aende chini na kudondoka chali sakafuni!.
Alikuja mzima mzima akitaka kumkanyaga tumboni lakini Stuwart alibiringika na kuukwepa mguu ule na kumkata mtama Ritah ambaye alienda chini,
zilikua ni ngumi za kikomandoo kila mtu akijitahidi kutupa ngumi mpaka walipodondoka ndani ya chumba alichokua Witness.
Hakuwa na la kufanya sababu ya pingu alizo fungwa lakini alijitahidi kusimama na kumvaa Ritah baada ya kusimama na kujizungusha na miguu ya kiti kile kumpiga Ritahna kumtupa ukutani ambapo alijibamiza na kuanza kuvuja damu mdomoni yupo hoi,
Kati kati yao kulikua kuna bastola iliyo kua chini ime dondoka kila mtu aliitizama na kumuangalia mwenzake,
kwa kasi ya ajabu Ritah aliirukia ila alivyotaka kuiweka sawa alipigwa teke na stuwart na kudondoka tena chini na kuendelea tena kupigana vilivyo ndani ya chumba hiko kidogo.
Kwake ilikua bahati sana kudondoka tena upande wa pili na kuifikia bastola ile akiwa nayo karibu yake,
hapo ndipo alipoichukua na kuikoki kisha kumuelekezea Stuwart aliyekua amesimama mbele yake na kushindwa kuchukua maamuzi yoyote yale.
“Ritah usifanye ivyo tafadhali huyo mwanamke hana makosa”
Alijaribu kujitetea Stuwart huku mikono yake akiwa ameibana nyuma ya kichwa chake, taratibu akitoa kisu kilichokua nyuma ya mgongo wake sehemu maalumu kwa ajili ya dharura kama izo.
“kaa kimnya Stuwart!”
“Ritah shusha bastola chini tuweze kuongea vizuri”
Alizidi kukivuta kisu taratibu Stuwart huku akimkata jicho kali Ritah aliyekua mbele yake, Witness alikua kimnya hasemi kitu anawaangalia.

 Alikichomoa kisu chakekama umeme na kukirusha baada ya kukiweka vizuri mkononi ila alikua kasha chelewa sababu kilipishana na risasi aliyoifyatua Ritah na wote kudondoka chini chali upande wake, i
ila mpaka dakika hiyo Ritha hakua na kauli tena baada ya kisu chenye ncha kali kutua juu ya koromeo lake alikua chini chali amelala amepoteza uhai wake amekufa pale pale huku damu nyingi ziki mtoka shingoni!, Stuwart akiwa ameshika bega lake damu nyingi zina mvuja alimuangalia Witness.
Yote hayo Witness aliya shuhudia taratibu alijikokota mpaka kwa Ritha aliyekua chini na kupapasa funguo za pingu, alizishika vizuri kwa nyuma na kujifungua pingu baada ya hapo haraka haraka alimsogelea Stuwart na kumshika begani kwa lengo moja tu waweze kutoka nje.
Kitendo cha kutoa sura zao nje waliona kundi la maaskari wakiwa na SMG zao mikononi wakiwa elekezea walipo wao, hawakua na ujanja mwingine zaidi ya kupiga magoti na kutii amri hiyo iliyotoka kwa mkuu wa jeshi la polisi,walifuatawa na kufungwa pingu mikononi mwao.
Kila askari alijipongeza kwa kuwaweka watu hao hatari kizuizini waliokua wana waumiza vichwa vyao.

Taarifa izo zilimfikia moja kwa moja Towo akiwa ndani ya gari, moyo ulimuuma sana lakini hakua na namna nyingine ya kumuokoa mwanamke huyo Witness aliyekua analindwa na polisi kila kona,
Defender kumi na mbili piki piki nyeupe tisa zilikua zina piga ving’ora vyao ili kusafisha barabara, kila askari alikua na mtutu wake mkononi wakiwa linda Stuwart na Witness,
japo walikua na pingu lakini haikuwafanya waamini pingu izo walizofungwa miguuni mwao na mikononi.

**
“mi naona huyu mwanamke tumchome sindano ya sumu”
“lakini huoni itakuja kuwa shida hapo baadae?”
“subiri nikwambie Mbeto, nita tumia akili mimi ndiye Raisi Steven Alinga, nikitaka kitu lazima kitekelezwe”
“basi hakuna shida yoyote na Yule Stuwart?”
“tuna mrudisha nchini kwao sababu hata yeye ana kesi ya kumuuwa Yule Ritha,”
“hapo sawa!”
Maongezi hayo yalikua yakifanyika ndani ya ikulu ofisi ya Raisi Alinga, kitu kilicho mjia ndani ya akili yake ni kumuua Witness Kafifi, hapo hapo aliinua mkonga wa simu na kumtafuta kamanda wa polisi kanda ya ziwa Msanya na kumpa zoezi hilo,
“fanya chochote huyo mwanamke afe, unajua ni jinsi gani alivyo hatari”
Alifoka kidogo baada ya kuona Kamanda Msanya anahoji maswali
“lakini ina bidi kwanza tumuhoji!”
“kama huwezi niambie, nimtafute mtu mwingine, mimi ndiye natoa amri, fuata maagizo nataka huyo mwanamke afe utajua utafanya nini”
***
Jeshi la polisi la Interpol pamoja na FBI walimiminika kutokea nchini Urusi wakimtaka Stuwart pamoja na mwili wa Ritha aliyekua ameuwawa na Stuwart, kutokana tu na ubishi wake aliye toa taarifa hiyo ni Raisi Alinga,
Walipokelewa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na kusindikizwa mpaka mahakama ya kisutu kumchukua Stuwart ambapo aliwekwa hapo chini ya ulinzi maalumu,
hakutaka kuondoka bila kuongea na Witness ili amuage. Bila kuweka kipingamizi chochote walipewa chumba ili waweze kuongea huku wakiwa na pingu zao mikononi.
“nime fanya haya yote sababu nakupenda sana Witness, nilijua umekufa, sidhani kama tutaonana tena najua huko napoenda nitaenda kunyongwa tu,naaamini ipo siku tuta kutana ahera mimi natangulia, NAKUPENDA SANA”
Aliongea Stuwart kwa sauti ya chini, japo kua alikua komando lakini hakuweza kuzuia hisia zake aliji kuta akidondosha chozi la uchungu, aliamini kile alicho fanya ni haki,
“bado sijamaliza, mkanda nisha utuma UN umoja wa mataifa nina imani wata isimamia kesi yako”
“Stuwart!.....”
Aliita Witnes kwa sauti ya chini pia.
“naam”
“nakupenda sana, nili fanya hivi kulipiza kisasi kwa wazazi wangu walio uwawa kikatili sana siku penda kufanya hivi”
“najua naelewa unachofanya ni kisasi cha kweli naa…”
Kabla ya kumalizia maneno maaskari walikuja na kumuinua Stuwart sababu muda ulikua teyari umekwendana alitakiwa kuondoka na ndege ya saa mbili usiku ya siku hiyo hiyo.
Moyo ulimuuma sana.

***
Chama cha UDP kilizidi kuchachamaa uchaguzi ulikua bado miezi michache sasa, wana chama walizidi kuongezeka kukipa kipaumbele chama hiko ili waweze kukipindua chama kilichokuwa madarakani kilichoitwa YBDP, lakini kila walipo fanya mikutano yao walifukuzwa na jeshi la polisi, hawa kuweza kufanya mikutano yao,
walijua kuwa hawatendewi haki lakini hawakuwa na mahali pa kushtaki, wali mteua mgombea Frank Mayasa ili aweze kugombea uraisi kupitia chama cha UDP waliweza kufanya kampeni na kukubalika karibia mikoa yote ya nchi ya Tanzania, hii iliwapa sana moyo.
***
Watu wengi sana walikusanyika katika mkutano mkubwa ulioandaliwa na mgeni rasmi alikua ni Mheshimu raisi wajamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Steven Alinga, watu wengi walifurika alikua mwenye furaha sana siku hiyo baada ya kutoa agizo kuwa Witness auwawe siku hiyo hiyo.
Kamera nyingi zilipigwa na waandishi wa habari baada ya Raisi Alinga kushuka ndani ya Landcrusier vx akiwa na walinzi wake pembeni ili kuhakikisha usalama wake upo.
Alipita kati kati ya jopo la watu mpaka mbele ya kipaza sauti ili aongee macahche.
“Tanzania ni nchi yenye amani sana, ila kuna watu wachache wana taka kuichafua nchi yetu nzuri, napenda kuwahakikishia kuwa mtoe wasi wasi wenu, kwanza poleni na mambo yaliyokua yakitokea hapo kipindi cha nyuma, mauaji ya ajabu yalikua yaki tokea, ila muuaji mpaka dakika hii yupo mikononi mwa sheria,naa na na….”
Alianza kupata kigugumizi kidogo baada ya kuona magari matatu yame paki nje na watu wenye ngozi nyeupe kushuka ndani ya magari wakiwa na suti nyeusi wame nyonga tai zao kooni,
“Nanana nan a nan a… anpenda kusema kuwa si si kama Tanzania tuta tuta tuta….”
Alizidi kupata kigugumizi sana bila kujua kina tokea wapi ni baada ya kuwaona wanazidi kusogea mbele kwenye kipaza sauti alipo, hapo ndipo jasho jembaba lilianza kumtoka.
“can you come with us sir(unaweza kuja nasisi muheshimiwa)?”
Mmoja wa wazungu alizungumza akiwa masikioni mwa Raisi Alinga.
“no I have to finish this”(hapana inabidi nimalize kwanza)”
“we don’t have much time here, come with us immediately(hatuna muda huo, tuongozane haraka iwezekanavyo)”
Hakua na jinsi nyingine yoyote taratibu aliteremsha ngazi huku bado picha ziki pigwa, kabla hata ya kufika mbali alifungwa mbingu kwa nyuma.
“you cant do this,! am the president of united repuplic of Tanzania, you have no power to arrest me”(hamuwezi kufanya hivi, mimi ni raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, hamna nguvu za kuniweka chini ya ulinzi)”
“sir! no one is above the Law we follow protocols, though your the president, your going with us”(muheshhimiwa, hakuna aliye juu ya sheria tuna fuata protocols, hata kama ni raisi utaenda na sisi)”
Hayo majibu yali mfanya Alinga afunge mdomo wake, mbele yake alimuona Witness kafifi akiwa bado na pingu zake mikononi ana tabasamu akimuangalia, walimchukua moja kwa moja mpaka makao makuu ya umoja wa mataifa na kusubiri hukumu yake.
**
Mahakama ya kisutu ili furika watu wengi mamia na maelfu walimiminika na wengine kukosa siti za kuketi, kila mtu alitega sikio lake kusikiliza kesi ya mwana mke huyo jasiri aliye anza kusimulia kila kitu tangu wazazi wake walivyouwawa kinyama na kuchinjwa,
na mama yake mzazi kubakwa akiwa bado mtoto mdogo,
Wana wake walidondosha Chozi, jaji aliyekua anasimamia kesi hiyo hata yeye alitingisha kichwa chake na kushindwa kuamua kesi.
“napenda kusema kuwa hapa nilipo fikia hata. Hata nikifa ni sawa, Mahakama tukufu ndio hayo tu”
Alimalliza Witness na kumtizama hakimu aliyekua mita chache mbele yake, hapo ndipo nyundo ili gongwa mezani na Witness kufungwa miaka saba Jela badala ya kifungo cha maisha, kila mtu aliye toka hapo alimpongeza sana, hata Towo nayeye alikua mmoja wa watu waliokuwepo ndani ya mahakama akisikiliza kesi hiyo,
alimtizama na kusogea alipo, alimkumbatia na baada ya hapo karandika lilikuja na kumchukua Witnes ili safari ya gerezani ianze.
**
Akiwa gerezani alisikia chama cha marehemu Baba yake UDP kipo madarakani kimeshinda na Raisi Alinga amenyongwa, alitabasamu sana na kupata amani ya moyo, alipiga magoti na kutubu dhambi zake zote alizofanya na kuzidi kuwaombea wazazi wake wapumzike kwa amani huko walipo.

MWISHO.

1 comment:

BLOG