Search This Blog

Sunday, May 31, 2020

BEDROOM PROFESSIONALS SEHEMU YA 2/10



BEDROOM PROFESSIONALS
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 2 KATI YA 10 MWISHO
*******


Ndani ya hotel ya Carajavo kulizuka mzozo mkubwa kupita kiasi,Deo alikuwa anafunga mizigo yake ili arudi jijini Dar es salaam lakini Leila yeye hakutaka kitu hicho kitokee kwani moyoni mwake
alifurahi alivyosikia kwamba Marietha kaondoka,aliamini kuwa hiyo ndiyo nafasi pekee aliyobaki nayo.Ndiyo maana alimsihi Deo waendelee kubaki kisiwani humo,ikawa vuta n’kuvute.
“Leila nishakwambia haiwezekani lazima nirudi Dar es salaam mke wangu ameondoka kwa sababu yako,alafu unaniambia nibaki,haiwezekani”
“Kwanini isiwezekane sasa?kwanini tusibaki wote?”
“Nishakwambia haitowezekana hapa nina kibarua cha kumbembeleza yule mwanamke,nibaki hapa kisiwani nifanye nini?”
“Deo mbona unakuwa hivyo?”
“Leila utanikera sasa hivi,embu niache basi.Kama unabaki wewe baki lakini mimi naondoka sasa hivi”
Kila Deo alipojaribu kuweka nguo ndani ya begi Leila alizitoa,sababu hakutaka aondoke.
“Alafu ulisema kuwa unataka kurudi Dar hapa umepachoka imekujawe?embu acha basi shati langu niliweke kwenye begi.Hivi unataka nini Leila?”
“Mpaka sasa hivi wewe hujui na utu uzima wote huo”
“Alafu kwanza niachie,unanipotezea wakati”
Mara Leila amshike Deo bega mara mashavu ilimradi vurugu tupu,Deo aliona kama jambo hilo ni kero kwake.Akamsukuma Leila kando akaweka nguo zake vizuri ndani ya begi na kulifunga.
“Deo, Real?”
“Unaondoka au unabaki?”
“Sijui”
Leila akajibu kwa mkato akidhani wenda Deo atam-bembeleza lakini haikuwa hivyo kwani Deo alikuwa mwenye haraka ya kumuwahi Marietha hakuwa na muda huo akavuta mlango na kutoka nje,akaanza kutembea.
“Deo Deo..wait for me”(Deo Deo nisubiri)
“Fanya haraka,dakika moja nakupa”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa baada ya dakika mbili Leila akawa tayari amejiandaa na safari ya kurejea jijini Dar es salaam ilianza mara moja,badala ya kufurahi kisiwani kwenye fungate sasa mambo yalibadilika na kuwa karaha.Walitembea na kukodi boti.
“Deo I’m so sorry”
Leila akaongea na kuvunja ukimnya baada ya kumuona Deo akiwa mwenye mawazo mengi kupita kiasi,alikuwa ameweka mikono yake mashavuni yaani ameshika tama.Alikuwa mbali kifikra akimuwaza mke wake Marietha na kuyakumbuka matusi aliyomiminiwa na Leila.Wakati mwingine alijuta kumualika mwanamke huyo wawe wote kwani ndiye aliyesababisha kila kitu kitokee kama asingekuwepo wenda mambo yangekuwa shwari kabisa.
“Usijali”
“Umenisamehe?”
“Ndio”
“Naomba niombee msamahaa kwa mkeo”
“Nitafanya hivyo lakini kwanini ulimtukana?”
“Deo ni hasira tu jaribu kusahau”
“Okay”
Deo alimuwaza Marietha tu mawazo yake hayakuwa hapo hata kidogo na kama ingetokea angepimwa uzito siku hiyo basi ungeonesha kilo kumi zimepunguwa, mawazo yalikula ubongo wake sio masihara na siku hiyo ndiyo aliamini anampenda Marietha kutoka ndani ya moyo wake.

Mpaka wanawasili Zanzibar bado kichwa chake kilikuwa kinatafakari jinsi gani ya kumrudisha tena Marietha,aliomba Mungu asiseme kuwa ndiyo mwisho wao sababu hakuelewa maisha bila yeye yangekuwaje.Walishuka wakachukuwa usafiri mwingine ambao uliwapeleka uwanja wa ndege.
Hata walivyokuwa angani Deo hakuonesha kuwa na furaha, sura yake ilionesha majonzi tu ingawa walikaa siti moja na Leila lakini hakumuongelesha.
“Deo tunakaribia kutua,funga seat belt”
Leila ndiye aliyemzindua Deo katika mawazo,kipaza sauti kilichokuwa kinawataka wafunge mikanda hakukisikia ndiyo maana Leila akamshtua.
“Oh,Thank you”
Alivyofunga mkanda,ndege ikaanza kuelekea chini kutua katika uwanja mkubwa wa kimataifa Mwl.Nyerere.Ilivyokaa vizuri na kusimama Deo alishuka na kuanza kutoka nje ya mlango, Leila akiwa nyuma yake.
“Nadhani unapajuwa Hotelini?”
Deo alimgeukia Leila na kumuuliza sababu hakutaka kuongozana naye kwanza kwa wakati huo,alitumia swali hilo kuzunguka kidogo.
“Ndiyo napajuwa,kwani hatuendi wote?”
“Nitakuja kukuchukuwa, kwa sasa hivi kuna mambo nataka nikafanye kidogo rudi hotelini nitakufuata”
“Deo”
“Naam”
“Upo sawa?”
“Nipo sawa usijali”
“I’m sorry once again”(Niwie radhi kwa mara nyingine)
Leila aliamini kuwa Deo hayupo sawa ndiyo maana akasisitiza kuomba radhi kwa jambo alilofanya.
“It’s okay”
Deo akaingia ndani ya Taxi na kumuacha Leila anamsindikiza kwa macho.Hakuwa ana uhakika kama angemkuta Marietha nyumbani alikuwa ni kama ana bahatisha, jambo hilo akalipa asilimia thelathini chini ya mia.
Alivyofika nyumbani alisukuma geti,ilikuwa ni kama aliotea sababu jinsi alivyoiacha nyumba ndivyo alivyoikuta.
“Shikamoo bosi”
Askari aliyekuwa pembeni alimsalimia.
“Marietha alifika hapa?”
“Hapana bosi”
“Okay”
Majibu hayo yalitosha kabisa kupitisha kuwa Marietha hakukanyaga nyumbani, akapitiliza mpaka ndani na kunyoosha mpaka chumbani,bila kubadilisha nguo akachukuwa funguo za gari na kutoka nje ambapo alizama ndani ya gari na kulitia moto.
“Atakuwa kwa Mama yake tu”Alijisemea mwenyewe.

Hakukuwa na sehemu nyingine ambayo Marietha angeweza kwenda isipokuwa kwa Mama yake swala hilo alilipa kipaumbele zaidi,aliendesha gari akiwa na mawazo chungu mzima.Mpaka anafika nyumba ya Mama yake mkwe bado aliwaza tu.
“Hapana Mama,sio kirahisi hivyo”
Maneno ya Marietha akiwa ndani yalipita kwenye masiko ya Deo bila chenga tena kabla hajaufikia mlango.
Marietha alikuwa akiongea kwa uchungu mno alimueleza Mama yake kila kitu kilivyoenda na jinsi alivyotukanwa na Leila wakiwa kisiwani chakechake wakila fungate.
“Mwanangu embu punguza hasira hizo hasira zako hazitokufikisha popote.Hukupaswa kuchukuwa maamuzi kama hayo ya harakaharaka ya kuondoka”
“Mama ulitaka niendelee kubaki ili nitukanwe?”
“Ha.. Ngo! Ngo! Ngo!”
Mama hakumalizia anachotaka kuongea mlango ukagongwa.Akasimama taratibu na kuuwendea,akafungua.
“Deo Mwanangu!”Mama aliropoka kwa sauti.
Kauli hiyo ilimshtua sana Marietha aliyekuwa juu ya sofa.


Hakuhitaji kitu kingine nyumbani kwa Mama Marietha bali ni kuomba msamaha kwa Mke wake ingawa alielewa hakufanya kosa lolote lile sababu yeye hakumtukana bali ni Leila wakiwa visiwa vya chakechake huko Zanzibar walivyokuwa fungate,Deo alikuwa mnyonge ghafla na sura yake ilitia huruma,akaingia ndani taratibu huku akimwangalia Marietha akamsogelea karibu.
“Naona Mboga inaungua ngoja niwahi jikoni mara moja”
Mama hakuwa na sababu ya kubaki seblen hakukuwa na mboga yoyote iliyokuwa jikoni kwani alishakula tayari alizuga ili awaache Deo na Marietha peke yao.
“Marietha”
Deo akamuita mkewe huku akizidi kumsogelea karibu zaidi,alifunga safari kutoka Zanzibar mpaka Dar es salaam ili kuomba msamaha tu wala sio kitu kingine,Marietha alimgeukia Deo akamwangalia kwa kama sekunde mbili nzima.
“Deo hujanikosea”
“Marietha usiseme hiv…”
“Ni Leila sio wewe”
“Sawa namuombea msamaha.Leila hakuwa vizuri alikuwa amelewa”
Deo alimtetea rafiki yake,hakutaka kuchochea bifu kati ya Marietha na Leila na katika maisha yake alitaka watu waishi kwa amani mbali na hapo wanawake hao wawili kila mtu alikuwa na nafasi yake ndani ya moyo wake,Leila alikuwa rafiki yake mkubwa sana tena waliyesaidiana vitu vingi, Marietha alikuwa mkewe wa ndoa yaani mwandani wake.Kugombana kwa watu hao wawili kungemfanya apate wakati mgumu mno.
“Nakupenda Marietha tafadhali rudi nyumbani,sahau yote yaliyopita.Kumbuka hata maandiko yanasema samehe saba mara sabini”
Deo aliingiza mistari ya Biblia ili mradi kumuweka mkewe sawa.
“Nimekusamehee Deo”
“Kweli?”
“Ndio mume wangu,turudi nyumbani.Samahani kwa kukatisha starehe tuliyoianza”
“Hiyo siyo kitu kabisa”
“Nakupenda Deo”
“Mimi Pia”
Wote wakakumbatiana na kupigana mabusu,Mama akaitwa na alionesha kuwa na furaha baada ya kuwaona wamepatana akaachia vigelegele kwa sauti.
“Mama mbona hivyo?”Marietha akamuhoji mama yake.
“Niache kwa raha zangu”
Mama akarukaruka akaingia chumbani na kutoa begi la Marietha.
“Nawatakia Baraka zote wanangu”
“Amen”
Walitoka nje na kuingia ndani ya gari wakiwa wenye nyuso zenye furaha kupita kiasi.
Ni kweli watu hawa walipendana kupita kiasi hata kingetokea kipimo cha kupima Upendo basi kisingetoa majibu ya kueleweka,Deo alimpenda Marietha na kwa Marietha hivyohivyo,moyoni alijilaumu ni kwanini aliamua kuchukuwa maamuzi ya harakaharaka na kuharibu fungate lao,alijuwa Deo kivyovyote alichukia sababu aliijuwa sana pesa lakini kutokana na nguvu ya penzi hakuweza kufokewa.Wakiwa ndani ya gari Marietha alizidi kutafakari vitu vingi sana.
“Deo”
Marietha akaita Deo akageuka na kurudisha shingo yake mbele sababu alikuwa barabarani anaendesha gari hakutaka kusababisha ajali kizembe.
“Naam baby”
“Naomba unisamehe”
“Kwani umefanya nini?”
“Zilikuwa ni hasira tu kule kisiwani ndiyo maana zikafanya nichukuwe maamuzi bila ya kufikiria”
“Yaliyopita si ndwele tugange yajayo mke wangu”
Deo akatumia Methali kulijibu swali na mkewe,kumaanisha kila kitu kipo shwari na wasahau ya nyuma.
“Nashukuru kusikia hivyo”
Walivyofika nyumbani Deo akapitiliza mpaka jikoni akafunguwa jokofu.
“Baby vitu vimepungua kwenye friji”
“Inabidi nikanunue”
“Noo,nitaenda mimi wewe baki tu Love”
“Deo hizo ni kazi za wanawake”
“Imeandikwa wapi?”
“Mimi ni mwanamke wa kiafrika tambua”
“Kwahiyo?Acha zako niandikie vitu vilivyokosekana niende sokoni”
“Okay lakini ungepumzika basi kidogo”
“Hapana,mwanamme huwa hachoki”
“Kwenda zako wewe mashine kwani”
Hicho ndicho kilichoenda kutokea,Marietha kazi yake ilikuwa ni kuorodhesha vitu vilivyokosekana ndani juu ya karatasi kisha kumkabidhi Deo,akaichukuwa karatasi na kuanza kuipitia.
“Wine hujaweka baby alafu hakuna matunda”
“Nawewe kwa kujipenda”
Kila kitu kilivyoongezwa juu ya karatasi Deo aliichukuwa na kuiweka mfukoni huku nyuma akimuacha Marietha akipanga vitu na kufagia,nyumba ilikuwa na vumbi kiasi sababu hawakuitumia kwa siku kadhaa.Akaanza chumbani kufagia na kupanga kila kitu sehemu yake,akatandika kitanda vizuri na kuingia bafuni kujimwagia maji ili kuuweka mwili wake safi.
****
Lengo la Deo halikuwa kwenda sokoni peke yake,hiyo ilikuwa ni kama gia ya kutoka.Alikuwa akienda kwa rafiki yake kipenzi Leila, alielewa kumwambia Marietha juu ya safari hiyo angechukia, hakutaka kumuumiza moyo alitaka awapatanishe kwanza ndiyo maana aliamua kufanya jambo hilo kimnya kimnya,ilikuwa ni lazima awapatanishe Leila na Marietha ndiyo akae kwa furaha,sababu wanawake hao walikuwa wana uzito sana katika maisha yake.
Ndani ya dakika ishirini na moja alikuwa ubungo mataa anasubiri taa za kijani ziwake aweke gia aondoe gari afike LandMark Hotel ili aonane na Leila.Hapohapo akachukuwa simu pembeni ya gia na kutafuta namba za Leila,alivyozipata akamtaarifu kuwa yupo njiani na anakaribia kufika.
“Umefika wapi?”
Lilikuwa ni swali kutoka upande wa pili wa simu,Leila akiuliza.
“Ubungo mataa hapa ndani ya dakika mbili nitakuwa hapo”
“Poa nakusubiri love”
“Okay”
Simu ilivyokatwa ilimuacha Leila akitafakari kiundani zaidi,alikuwa peke yake chumbani.
Sauti ya Deo ilihamsha hisia zake alijisikia kulala naye na kufanya naye ngono siku hiyo,alielewa jambo hilo lingefanikiwa kwa asilimia mia moja.Hapohapo akatembea mpaka mezani ambapo alichukuwa mkonga wa simu na kupiga namba za wahudumu.
“Niletee Red Label mbili,ndio mizinga miwili chumba namba kumi na tisa yes now please,thank you”
Deo alikuwa anapenda sana kunywa pombe na alitaka kumshawishi anywe alewe alafu apoteze fahamu ndipo afanye tendo alilokusudia,alikuwa amebakiwa na muda mchache kuandaa mazingira,akaingia bafuni akaoga na kujipulizia marashi shingoni.Baada ya hapo akachukuwa kanga akaiweka mwilini tena bila ya kuvaa nguo yoyote ile ndani,kitu ambacho alimlaumu Mungu kila siku ni kutokumpa Makalio makubwa lakini alimpa nyonga ya kuvutia hilo alilijuwa sababu alisifiwa na wanaume wengi.
“Ningepewa wezere.Lakini fine nitaenda China kuchonga niwe na shepu nadhani ndiyo maana anampenda Marietha.Nishakumbuka Deo anapenda wanawake wenye big ass…Subiri dawa yake pia ipo inachemka.Mimi ndiyo Leila”
Alikuwa ni kama anaongea na mtu kumbe alikuwa mwenyewe anajiongelesha huku akijizungusha zungusha kwenye kioo akijikagua.Mlango uligongwa akafunguwa.
“Niandikie bili yangu kisha utanipa”
Alimwambia muhudumu alivyoleta mizinga ya pombe.
“sawa,hakuna shida”
Kitendo cha kuurudisha Mlango mara simu yake ikaita,akatembea haraka kwa furaha na kuikwapua alikuwa ni Deo na alijuwa tayari keshafika,akanyoosha mpaka dirishani na kufunguwa pazia ni kweli alimuona Deo chini ndipo akapokea simu.
“Njoo Deo nishakuona”
“Nije wapi?”
Deo akauliza simuni.
“Room namba kumi na tisa”
“Shuka chini,njoo tuongelee huku nje, siwezi kuja huko mimi”
“Deo please,nimechoka”
“Leila siwezi kuja isitoshe nina haraka kama huwezi kuja mimi naondoka tuonane kesho”
“No! No! No! No! basi njoo unifuate tushuke wote”
“Umesema chumba namba ngapi?”
“Kumi na tisa”
“Sawa nakuja”
Moyo wa Leila uliruka mapigo saba mbele akatabasamu,akaiweka kanga vizuri na kutoa viti vilivyokuwa mbele yake ili Deo afikie moja kwa moja kitandani ingawa kulikuwa na masofa pembeni hakutaka Deo akalie akiamini kwamba kibarua chake cha kumlaghai kingekuwa kigumu.Akafunguwa mzinga wa pombe kali na kuchukuwa glasi mbili ambapo alizimimina na kuziweka mezani,kabla ya kufanya kitu kingine chochote kile mlango ukagongwa.Akauendea na kunyonga kitasa.
“Woow! karibu Honey”
Leila akatoa sauti ya puani huku akirembua, Deo akaingia ndani yeye akafunga mlango na funguo.
“Karibu kitandani”
“Nitakaa hapa kwenye viti,alafu mbona hujavaa sasa?”
“Nitavaa bwana kwani ni dakika ngapi?”
“Vaa basi,kuna mambo nataka kuzungumza nawewe”
“Kwani hapa hapafai?”
“Panafaa sema naenda kununua vi…”
“You are talking too much, embu take this kwanza tugonge cheers”
Leila alizungumza huku akimpa Deo glass ya pombe.
“Not now Leila”
“Deo Real!?”
“Leila nawewe bwana,one shot nitakunywa,okay?”
“Just drink”
Hakukuwa na kipingamizi juu ya kunywa pombe akiamini kuwa atakunywa glasi moja kisha wote waondoke kumbe ilikuwa tofauti na mahesabu ya Leila kichwani kwani yeye alitaka amleweshe kisha wafanye tendo baya la uzinzi!

Alijuwa kwa kutumia pombe ndiyo swala lake lingekuwa rahisi,pombe ni mwanaharamu siku zote,Deo alivyomaliza glasi ya kwanza akahisi kunogewa, mwenyewe akasimama na kuchukuwa chupa akamimina ndani ya glasi.
“Hii ya mwisho niondoke zangu”
“Okay no problem”(Sawa hakuna tatizo)
“Kesho inabidi uje nyumbani kwangu upaone,uonane na mke wangu”
“Na Marietha?”
“Yes Marietha umuone,mpatane mmalize misunderstanding zenu.Muwe kitu kimoja bwana”
“Hakuna tatizo juu ya hilo Love,twende kitandani basi”
“Tukafanye nini? hapa panatosha”
Leila alivyoona Deo anakaribia kumaliza pombe iliyokuwa kwenye glasi akasimama na kuchukuwa mzinga na kumuwekea nyingine,Red Label ilikuwa ni pombe kali mno na ilikuwa inapanda kichwani kwa muda mfupi tu,Deo alianza kurembua na kuanza kuyakaza macho yake,alianza kuhisi kizunguzungu na alielewa kichwa chake hakipo sawa tayari keshalewa,kuepusha hilo alisimama lakini Leila alimvuta juu ya sofa,akapanda kwa juu yake.Akasogeza mdomo wake karibu yake na kuanza kumnyonya ‘Lips’ akachukuwa glasi ya Deo na kuiweka kando.
“Leilaa Sto..p unafanya nini sa…sa..Niachiee Marie..tha Leila leave me”
Ghafla Deo akaanza kuchanganya mafaili ya majina,mdomo wake ulikuwa ukinyonywa akaufungua akaachia meno ulimi wa Leila ukapita kinywani wakaanza kubadilishana mate kwa njia ya kunyonyana ndimi.
***
Ilikuwa yapata saa sita ya usiku bado Marietha alikuwa seblen anamsubiri mumewe wa ndoa,alishampigia simu bila ya kupokelewa tangu alivyotoka mchana akidai kwenda kununua vitu vya ndani tangu muda huo alikuwa bado hajatia maguu.Wasiwasi ulianza kumuingia akaanza kuhisi wenda mumewe amepata ajali njiani akiwa anaendesha gari ingawa wazo hilo hakutaka kulipitisha ndani ya ubongo wake, aliendelea kujipa moyo kwamba wenda angerudi aendelee kumsubiri lakini wapi,muda ulizidi kwenda hakuwa na raha alikuwa mpweke na ‘night dress’ peke yake, hapohapo akakumbuka kitu na kwenda chumbani ambapo alitoa simu kwenye chaji na kuanza kutafuta orodha ya majina,akafanikiwa kupata jina la rafiki wa karibu wa mume wake,Profesa Paul Abel.
Akampigia ili kumuuliza mume wake kama walifanya mawasiliano.
“Samahani kwa kukusumbua usiku shemeji”
Marietha alianza kuomba radhi kwa usumbufu sababu usiku ulikuwa mwingi na kitendo cha kufanya kitu anachokifanya kilikuwa ni usumbufu wa hali ya juu sababu hata yeye hakupenda kusumbuliwa usiku akiwa amelala.
“Bila samahani,vipi mbona usiku usiku.Kuna msiba?”
Profesa Paul Abel aliuliza kwa sauti nzito ya uchovu huku akipiga miayo ya usingizi.
“Hapana,namuulizia Deo kama alifika kwako, leo hukufanya naye mawasiliano?”
“Kwani msharudi tayari?”
Badala ya kujibu swali nayeye akauliza swali likawa swali juu ya swali.
“Ndio tupo Dar,leo hamkuwasiliana?”
“Hapana Deo sijaongea naye tangu majuzi mkiwa Zanzibar na hakuniambia kama mmerudi”
“Okay Ahsante”
Marietha alikuwa na kazi ya kumpigia kila mtu anayemfahamu,kutokana na kuchanganyikiwa alimpigia mpaka mama yake Mzazi kumuuliza Deo alipo.
“Mama Deo hayupo kwako huko?”
Lilikuwa ni swali lililomshtua Mama yake usiku wa saa tisa tena bila ya salamu.
“Hivi wewe umechanganyikiwa?Unamuulizia Deo usiku kwangu?”
“Samahani Mama,ni..”
“Huna adabu mshenzi mmoja”
Mama alilielewa swali na mwanaye vibaya hapohapo akakata simu.
Marietha akazidi kuchanganyikiwa zaidi,akafanya kama bahati kujaribu kumpigia tena Deo,simu iliita kabla ya sekunde moja kupita ikapokelewa,akaanza kuongea harakaharaka kama amemeza makaa ya moto.
“Deo uko wapi Mume wangu? nakutafuta sana nina wasiwasi Love,uko wapi?”
“Amepumzika sasa hivi,acha kusumbua watu”
Moyo wake ukapiga paa!kwa mshtuko sababu alijibiwa na mwanamke kisha simu ikakatwa.

Midomo yao iligandana kama makinda ya njiwa wakiwa juu ya sofa,tayari kwa Leila alijiona mshindi sababu mpaka kufikia hatua hiyo alielewa Deo alikuwa wake na lazima wangefanya mchezo mchafu wa ngono sababu alikuwa keshalegea tayari.Akamlaza Deo vizuri juu akaanza kumvua shati.
“Leilaaaaa..unatakaaa kufa..nya niniii?”
Pombe siku zote haifanyi mtu ashindwe kutambua ni kitu anachokifanya, Deo alijuwa anataka kuvuliwa nguo na sura aliyoiona ilikuwa ya Leila na sio mke wake,alijaribu kuyafumbua macho yake na kuyakaza vizuri hakutaka kuamini kuwa aliyekuwa juu ni rafiki yake kipenzi, Leila.Ni kweli akili yake ilihama na damu yake ilikuwa ikienda mbio ikimsukuma afanye tendo hilo baya lililowaleta duniani tena na rafiki yake,akajaribu kumsukumiza Leila kando lakini haikuwezekana sababu Leila alimshinda nguvu,ikawa purukushani,Leila hakutaka kushindwa na Deo hakutaka kukubali kuvuliwa shati.Alishawahi kuapia kuwa hatomvulia mwanamke mwinginge boxa yake isipokuwa mkewe wa ndoa Marietha,siku hiyo alikuwa na mtihani mkubwa kupita kiasi.Marietha akashika ndizi ya Deo na kuanza kuipapasa hiyo ilimfanya atulie,akaanza kupandwa na midadi akamvuta Leila na kumla Denda hiyo ilimaanisha tayari ameelekea kibra,hapohapo akavuliwa shati wakaendelea kunyonyana midomo,Zipu ya Deo ikafunguliwa taratibu Leila alivyotaka kutoa ndizi ya Deo,akazuiwa. Deo akaweka mkono.
“Leilaaa pleaseee stoooop”
“Deo Nooo,nakupenda naomba unieleweee then I’m horny”
“Pleasee,najuwa umelewa lakini naomba usifanye unachotaka kukifanya”
Deo akasimama kwa kuyumba na kuingia bafuni huku akiyumba huko alienda na kufungua bomba la mvua hivyohivyo bila kuvua nguo zake akalala juu ya malumalu,pombe zikawa zikatoka taratibu na hiyo ndiyo ilikuwa dawa ya kuipunguza pombe kichwani,kuoga maji ya baridi. Alifanya hivyo sababu alijuwa amelewa na asingeweza kuendesha gari aliogopa kusababisha ajali,Deo alikuwa dereva makini barabarani.Kadri sekunde zilivyozidi kwenda mbele ndipo pombe zilipozidi kushuka taratibu.Hakuna siku aliyochukia kama siku hiyo,alihisi kudhalilishwa na alijiona wenda ana kasoro mwilini mwake,Mwanaume kuchomoka kirahisi kama hivyo haikuwa rahisi lakini kwa Deo ilikuwa tofauti kwani aligoma kabisa kufanya naye zinaa.Akakunja sura na kuweka kanga yake vizuri akanyoosha mpaka bafuni,akamkuta Deo amelala kifudifudi maji yanam-mwagikia mwilini mwake.
“Deoo,ndiyo nini sasa?”
Leila akauliza kwa ukali.
“Kichwa kinaniuma”
“Kwahiyo?ondoka basi kwangu unafanya nini bafuni?”
“Sawaaa ninaondoka”
“Sasa hivi,ondoka ondoka”
Leila aliongea kwa hasira huku akitoa amri hiyo, alitanda kwenye mlango wa bafuni akiwa ameganda kumaanisha kuwa anamsubiri Deo aondoke hakujali kuwa nguo zake zimelowa na maji,alitaka aondoke wakati huohuo.Deo akajishika na sink akasimama na kupepesuka kidogo,akamuangalia Leila na kuanza kupiga hatua kutoka nje.
“Itabidi nikanunue nguo nyingine siwezi kurudi nyumbani hivi”
Deo alisema na kuanza kutembea, kauli hiyo ilimfanya Leila aumbuke alijuwa Deo angetetereka na kuomba kidogo hifadhi ili nguo zake zikauke lakini haikuwa hivyo.
“Deo hivi kweli unataka kunifanyiaa hiviii?”
“Kivipi?mbona sikuelewi”
“Wewe mwanaume gani?kusoma hujui hata picha huoni?”
Leila alitumia msemo wa kibongo ili kumzindua Deo akili,lakini wapi! Deo aliendelea kumchukulia mwanamke huyo kama rafiki yake tu ndio maana moyoni alijisikia aibu sana,kitendo kilichotaka kutokea dakika chache zilizopita kilimfanya aone haya licha ya yote alichukulia kwamba Leila alikunywa kiasi kikubwa cha pombe.Hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumuomba Deo asubiri mpaka nguo zake zikauke.
“Nisubiri hapa?”
“Ndio,mkeo hatokuelewa yaani umetoka na nguo hizo alafu unarudi na nguo nyingine.Mimi ni mwanamke naelewa”
“Kweli eeh?”
“Ndio hivyo”
Leila akabadilika akajifanya mpole ili amuweke tena Deo ndani ya kumi na nane zake,akatembea mpaka kwenye meza bila ya Deo kujuwa akachukuwa simu na kuiweka ‘silent’ kumaanisha kuwa hata akipigiwa simu na mkewe asiwe anasikia.
“Ingia bafuni uvue hizo nguo,nikampe muhudumu azianike”
“Poa”
Deo akasimama na kuingia bafuni ambapo alitoka akiwa na taulo peke yake,akampa nguo zake zilizolowa Leila,kilichofanyika ni Leila kupiga simu akawapa maelekezo wahudumu, hazikupita hata dakika mbili akatokeza muhudumu na kuchukuwa nguo ili kwenda kuzianika.

Deo alikuwa na taulo,amekaa kitandani anatafakari mambo mengi sana, alihisi kumuonea sana aibu Leila siku hiyo ingawa walikuwa marafiki wakubwa na Leila alikuwa ana uwezo wa kubaki na chupi mbele yake lakini wasifanye kitu chochote,hakuelewa siku hiyo ilikuwaje, hiyo ikapelekea mpaka kushindwa kumuangalia usoni,hakujuwa kwamba Leila alikusudia.
“Deo,unaweza ukapumzika tu..Usijali inabidi niagize chakula tule”
“Poa”
Chakula kikaagizwa Leila alikuwa bado ana kanga na Deo alikuwa ana taulo, walikula na kushiba na Deo alihisi kuchoka.
“Hizo nguo bado tu?”
Akauliza alitaka kumuwahi mke wake nyumbani licha ya hapo alitaka kwanza apitie sokoni.
“Bado bwana,mara hii zikauke?”
Leila hakutaka Deo aondoke ndiyo maana alisema maneno hayo,bado hakukoma.Kutokana na uchovu wa kukosa usingizi na pombe zilikuwa kichwani ilimfanya Deo ahisi usingizi mzito, akajisogeza taratibu kitandani na kuweka mto vizuri.
“Naomba niamshe baada ya dakika thelathini”
“Fine”
Deo akajitupa usingizini na hazikupita hata dakika kumi alikuwa anakoroma kwa mbali, hiyo ilikuwa dalili tosha kuwa amelala fofofo.
***
Alizinduka kutoka kitandani usiku mnene na giza lilikuwa limetanda,hakuweza kuona kitu chochote sababu taa ilikuwa imezimwa.
“Leilaaa..Leilaaa”
Deo akaita na kupapasa kitandani lakini mkono wake haukugusa kitu chochote,akashika taulo lake vizuri na kutoka kitandani ambapo alianza kutafuta ‘switch’ ya taa ilipo,akaipata ukutani na kuiwasha.Jambo la kwanza kwake lilikuwa ni kutupa macho yake juu ya saa yake ya mkononi.
“Mungu wangu”
Ilikuwa ni saa kumi kasoro kumaanisha kuwa bado lisaa limoja kupambazuke,mtu wa kwanza kumjia katika akili yake ni Mkewe wa ndoa,hakuelewa ni njia gani atumie kujitetea alivyoangalia mezani alipoacha simu yake hakuiona.
“Leilaaa,Leilaa”
Akagonga bafuni lakini hakukuwa na dalili ya mtu yoyote kuwepo, akafungua mlango ili kuhakikisha lakini wapi,Leila hakuonekana.
Alivyotaka kutoka nje alishindwa sababu alikuwa na taulo tu.Alihisi kuchanganyikiwa ajabu,kazi yake ilikuwa ni kuzunguka zunguka huku na kule chumba kizima, hakujuwa ni kitu gani akifanye.Muda ulizidi kwenda ikafika mpaka saa kumi Leila hakuonekana.
“Marietha sijui atanielewaje Mungu wangu”
Deo alihisi kujuta kufika Landmark hotel,dakika nyingine zikapita ikagonga saa kumi na moja kamili.Alitamani kutoka na taulo lakini alishindwa.Mlango ukafunguliwa akageuka.
“Umeamka?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Leila ambalo jibu lake lilikuwa wazi kabisa sababu Deo alikuwa amesimama.
“Nguo zangu ziko wapi?”
“Ndio nimetoka kuziangalia”
“Kwanini hujaniamsha?Alafu simu yangu iko wapi?nataka nguo zangu sasa hivi niondoke”
“Deo la…”
“Nataka nguo zangu bwana,usinikere”
Deo aliongea kwa hasira za waziwazi,akimkaripia Leila.
“Sawa”
Leila alifungua mlango na kutoka nje ambapo huko alitumia dakika nyingine thelathini akikawia kwa makusudi,alifuta ‘missed call’ zote za Marietha na kuchukuwa nguo za Deo akarudi nazo chumbani,alivyomtupia Deo tu,alizivaa kwa kasi ya risasi.Kabla shati hajaweka vizuri akakwapua funguo za gari juu ya meza.
“Nipe nipe nipe simu yangu,fanya fasta”
Aliongea harakaharaka bila nukta,akachukuwa simu na kuanza kushuka ngazi bila kufunga hata kamba za viatu,almanusura adondoke chini sababu alikanyaga kamba,bila kujali alitoka nje na kuingia ndani ya gari ambapo aliliwasha na kuligeuza kwa kasi,akalitoa getini na kuingia barabarani.
Kichwani aliwaza vitu chungu mzima,hakuelewa ni kwa njia gani amshawishi mkewe ili akubali, kila uwongo alioufikiria kumdanganya Marietha aliona haukushiba hakutaka kumpigia simu alitaka aongee naye ana kwa ana,Marietha hakuwa mwepesi kukubali jambo hakuwa mwanamke mjinga ndiyo maana ulitakiwa uwongo wenye ‘masters’aliomba Mungu amkute nyumbani sababu alimjuwa mwanamke huyo kwa kususa, si ajabu akawa keshaondoka kwao,alifika getini na kupiga honi ambapo mlinzi alifungua,akaliweka gari vizuri kwenye maegesho maalum.
Akasubiri kwa kama sekunde tatu ndipo akashuka,akatembea mpaka mlangoni.Akanyonga kitasa mlango ukafunguka,macho yake yakatua kwa Marietha aliyekuwa juu ya sofa amejikunyata analia machozi,ilikuwa ni mara ya pili kutukanwa matusi.
“Ma Ma Mari..etha”
Alipata kigugumizi cha ghafla.Marietha akafuta machozi akitumia viganja vyake akainua shingo, macho yake yalikuwa mekundu tena yamevimba, ilionekana alianza kulia kipindi kirefu.
“Uli..kuwa wapi?”
Aliuliza huku kwikwi ikiwa bado imem-bana.
“Nilipitia kwa marafiki zangu”
“Vitu uli..vyoenda kununua soko.ni viko wapi?”
Marietha alianzia mbali kidogo,mwanamke huyu ndiyo alikuwa ana tabia hiyo,alikuwa kama polisi katika kuhoji maswali hakutaka kukurupuka.
“Kusema ukweli Mke wangu,nilifika sokoni nikakutana na akina Minja pamoja na Mr.Mtui si unajuwa wachaga wale walivyokuwa wanapenda pombe hawakutaka kuniachia.Tukaenda pale DDC Kariakoo,tukaanza kunywa pombe.Najuwa nilifanya kosa sijakutaarifu”
“Mpigie simu Mtui niongee naye”
“Eeeh!”
Deo akatumbua macho kama mjusi kafiri aliyebanwa na mlango,hakudhani kama Marietha angetaka jambo hilo lifanyike.
“Naomba niongee na Mtui, si ulisema ulikuwa naye..Nipe simu yako”
Deo akashindwa kuelewa ni kitu gani akifanye.Angegoma kutoa simu ndiyo ingefanya Marietha aingiwe na wasiwasi.Hakuelewa kuwa Marietha alitukanwa na Leila simuni,kwa uwoga akatoa simu yake mfukoni na kuanza kutafuta namba za Mtui,alitamani kumtumia meseji ili kumtonya amtetee lakini muda ulikuwa finyu.
“Nipe simu Deo”
“Nakutafutia jina”
“Nipe hivyohivyo”
Deo akakabidhi simu,siku hiyo alikuwa mdogo kama kifaranga cha kuku, kifupi alinywea!
“Ume msevu vipi?”
“Mtui,lete nikusaidie kutafuta”
“Niache nitafute”
“Kwani baby huniamini?”
“Ndio”
Marietha kazi yake ilikuwa ni kutafuta majina,akalipata jina la MTUI akabonyeza kitufe cha kijani,simu ikawa inaita upande wa pili.Deo alikuwa akitetemeka kupita kiasi sababu iliwekwa ‘loudspeaker’ aliomba Mungu Mtui asipokee simu lakini haikuwa hivyo kwani ilikuwa bahati mbaya kwake na nzuri kwa Marietha maana simu ilipokelewa,sauti ikaenea chumba kizima.
“Eeh Deo vipi?Mbona asubuhi sana kuna nini?”
“Halloo shemeji Mtui,samahani kwa kukusumbua.Unaongea na Marietha,jana ulikuwa na Deo?”
“Jana?”
“Ndio jana”
“Mh..Ndio nilikuwa naye siku nzima, kwani hajarudi?”
Siku zote katika swala la kuteteana wanaume walikuwa kama ndugu,Kwa akili ya ki utu uzima Mtui alielewa tayari Deo keshaharibu na Mara ya mwisho kuonana ilikuwa kwenye harusi yake na wala hawakuonana kama anavyodai.
“Mlionana wapi?”
Swali hilo ndilo lilimfanya Mr.Mtui akae kimnya kidogo hakuelewa ni kitu gani akijibu.
“Mlikuwa wapi jana?”
“Samaki samaki”
Hapo ndipo Mr.Mtui alipobugi! Maelezo ya Deo na Mtui yalikuwa ni vitu viwili tofauti.



“Kwani mtui jana mlivyotoka DDC mlienda samaki samaki?”
Deo aliingilia mazungumzo hapohapo, maana alielewa mambo yameharibika ndiyo maana akatamka maneno hayo mbele ya Marietha ili kumzuga.
“Ndio Deo,tena pale nikakutana na akina Mbuya pia”
“Aisee”
“Ndiyo”
Marietha alikuwa akisikiliza maongezi hayo kwa umakini, hakuelewa kuwa wanaume hao wanamuigizia na alichokuwa akifanya Mr.Mtui ni kumtetea mwanaume mwenzake.
“Aya shemeji pumzika,samahani kwa kukusumbua”
Marietha akasema.
“Wala usijali”
“Na mwa….tititii”Marietha alitaka kuuliza juu ya mwanamke aliyemtukana lakini simu ilikatwa,ikimuacha Deo akihema ndani kwa ndani,hakuamini kuwa amemtoka Marietha, kimoyomoyo alitamani Mr.Mtui awepo ili ampongeze ama ampe ofa za bia sababu alijuwa mchaga huyo kwa pombe hajambo!
“Nilikutengea chakula mpaka kimepoa,nikupashie?”
“Usijali Marietha,sasa hicho kitakuwa chakula au kiporo?”
Marietha hakuwa na sababu nyingine ya kumshuku Mume wake sababu aliongea na Mr.Mtui, moyoni alianza kujilaumu mwenyewe kwa kumfikiria vibaya na kumkemea shetani ambaye alidhani anataka kuharibu ndoa yake,hivyo ndivyo akili yake ilivyokuwa inamtuma.
****
“Patia mimi pesa kwanza ndiyo matibabu, iko namudai pesa mingi”
“Ndio Dokta tunaelewa tupe muda kidogo tuweze kujichanga”
“No!Laki saba patia ndiyo matibabu yaweze endelea.La sivyo muje chukuwa mugonjwa yenu kesho”
“Dokta..”
“Sisi pata wapi pesa za kununuwa madawa?pata wapi pesa siye za kulipa madakatari? kama hamuwezi patia mimi pesa pelekeni yeye Muhimbili”
Chogo,Mudi pamoja na Kishipa walikuwa ndani ya ofisi ya Dokta Ajei Mohamed Sunil katika hospitali ya Agakhan baada ya kumtafuta sana rafiki yao Issa, walipata fununu kuwa aligongwa na gari hivyo alikuwa mahututi hospitali ya Aghakhan ambapo wasamalia wema walimpeleka ili kuyaokoa maisha yake,ilikuwa ni vigumu kuamini kwamba Issa ni mgonjwa mahututi na tangu afikishwe hospitalini hapo hakuweza kufungua macho,alikuwa ni kama mtu aliyekufa ingawa mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda.
Siku hiyohiyo Marafiki zake walifunga safari mpaka hospitalini ambapo walikumbana na Dokta wa kihindi,hali ya Issa iliwaogopesha kupita kiasi,hakuna mtu yoyote aliyeamini kwamba atapona na pia ndivyo walivyoambiwa na baadhi ya madaktari sababu ubongo wake ulikuwa umevulia damu na hivyo kuendelea kubaki hospitali bila matibabu yoyote kulimaanisha kukisubiri kifo chake akiwa kitandani.

Issa alikuwa maskini hakuwa na ndugu yoyote mkoani Dar es salaam zaidi ya marafiki zake ambao ndio hawa wamekuja kumuona.
“Laki saba tutatoa wapi?”
Chogo alimnong’oneza Kishipa wakiwa bado wapo ndani ya chumba cha daktari.
“Kwani hiyo laki saba ni ya nini?”
Kishipa akajibu kwa swali.
“Ndio anadaiwa ya matibabu waliyokuwa wakimpa tangu afike hapa juzi na hiyo aihusiani na operesheni atakayoenda kufanyiwa”
“Ni pesa nyingi tutatowa wapi?”
“Inabidi tumchangie,mimi nipo tayari kutoa pesa yangu ya mtaji laki moja na nusu”
“Mh,inabidi swala hilo tuongee na akina Sechu pia”
“Tutawaambia,akiendelea kubaki hapa gharama zitazidi”
Kikao cha kimnya kimnya kiliendelea baina ya Chogo na Kishipa,ilikuwa ni lazima wamtoe rafiki yao kipenzi hospitali kwa njia ya kuchangishana mpaka ikamilike shilingi laki saba ingawa hawakuelewa kama itatimia idadi ya pesa wanachokihitaji.
Wote wakatoka nje ili wapate nafasi nzuri ya kuteta,kila mtu alijitahidi kutoa kitu alichokuwa nacho.
“Mimi nitaenda leo kwa mjomba Dick anikope laki tatu”
“Tufanye kesho ipatikane,tujuwe utaratibu mwingine”
“Poa”
Wote walikubaliana lakini kabla ya hapo walitaka kumuona rafiki yao,hakukuwa na kipingamizi mmoja wa wauguzi akawapeleka mpaka ndani ya chumba cha wagonjwa.
Ingawa walikuwa wanaume lakini walihisi kuumia ajabu, Issa alikuwa akipumua kwa msaada wa mashine na alikuwa haelewi nini kinaendelea ulimwenguni,mashine zilizokuwa zimemzunguka ndizo zilikuwa zikipiga kelele kumaanisha kuwa bado mapigo yake ya moyo yanadunda.
“Sasa tukimtoa hapa,tutampeleka wapi?”
Chogo akauliza swali, likafanya kila mtu amwangalie,kuna kitu kilikuwa kina maana kubwa ndani ya swali lake.Kuchomoa mpira unaopitisha hewa ya Oxygen na kumtoa hospitalini hapo ilimaanisha kuweka uhai wa Issa mashakani na kuzisaka shilingi laki saba ingekuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
“Tutafute kwanza hizo laki saba Chogo,Mengine tutajuwa”
Kila mtu aliondoka siku hiyo akitafakari jinsi ya kupata pesa za kumkomboa rafiki yao hospitalini,walikuwa maskini lakini wenye utajiri wa huruma,Issa alikuwa ni zaidi ya rafiki kwao.
***
Siku iliyofuata walifanikiwa kupata kiasi cha shilingi laki sita na themanini,ilikosekana shilingi elfu ishirini ili itimie laki saba,walizunguka sana kuomba pesa siku hiyo ili watimize.Walimshukuru sana Mungu pesa ikapatikana,hapohapo wakaingia ndani ya daladala na safari ya kwenda hospitali ya Aghakhan kuanza mara moja,walivyofika kitu cha kwanza walinyoosha mpaka mapokezi ambapo hawakumkuta mtu yoyote yule.
Bila kufata utaratibu wakaingia chumba cha wagonjwa mahututi alichokuwa amelazwa rafiki yao Issa.Jambo ambalo lililowachanganya akili ni kumkosa rafiki yao,kitandani hakukuwa na mtu yoyote.Wakatizamana wenyewe kwa wenyewe usoni.
“Itakuwa sio chumba hiki”
Kishipa akavunja ukimnya akitaka kujifariji na kuwapa moyo wenzake ingawa alikuwa ana uhakika kwamba chumba ndiyo hikohiko na Issa alikuwa juu ya kitanda amelawza siku iliyopita.
“Ndiyo hiki bwana”
“Sasa Issa yuko wapi?”
Lilikuwa ni swali la kijinga lililoulizwa na Mudi sababu wote walitoka Manzese,hakuna hata mmoja aliyejuwa Issa alipo.
“Ita..”
Kabla ya kumalizia,mlango ukafunguliwa akaingia muuguzi.
“Nani karuhusu nyie kuingia humu?Nendeni nje”
Muuguzi wa Kihindi akafoka kwa hasira, kuingia ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi bila utaratibu ndilo jambo lililomkera kupita kiasi,wote wakatoka nje.Wakashindwa kuelewa wamuulize nani kuhusu mgonjwa wao.
“Dokta samahani”
Chogo akamsimamisha daktari mmoja wapo wa kiafrika aliyekuwa anatokeza ofisini kwake.
“Niwasaidie nini?”
“Tunamuulizia Issa,alikuwa ndani ya chumba hiki jana. Sasa tumekuja leo hatujamkuta”
Katika watu ambao waliweza kujielezea ni Chogo na ndiyo maana siku zote wenzake walimtanguliza mstari wa mbele ingawa alikuwa mkorofi lakini aliweza kutoa hoja na hata kuongea na mtu yoyote yule.
Dokta akawatizama wote kwa zamu, jinsi walivyokuwa wachafu hawajachana nywele tena wamevaa malapa hakuwatofautisha na vibaka ingawa hakutaka kuwaonesha aina yoyote ya kuwanyanyapaa!
“Jina lake nani?”
“Issa”
“Issa nani?”
“Issa Nurdin Mpelembe”
“Yule aliyegongwa na gari?”
“Ndiyo dokta”
Dokta akavua miwani,akawatizama kwa macho ya huruma.
Kuna kitu waliweza kukisoma kupitia uso wa daktari huyu ambacho hakikuwa cha kawaida.
***
Alizidi kuyafurahia maisha ya ndoa,aliamini kuwa ni mwanamke mwenye bahati sababu hakuwa na changamoto yoyote ile.Maneno ya watu waliokuwa wakimwambia ndoa ni chungu aliyaona ni ushuzi mtupu sababu kila alichokuwa anahitaji kwa Deo alikipata hapohapo,kwa maana hiyo miezi ilisogea harakaharaka kutokana na matunzo mazuri akazidi kuwa mrembo,akanawiri.
Marietha hakuwa na shida ndogondogo sababu aliajiriwa na mume wake kwenye moja ya maduka ya vifaa vya ujenzi mjini Kariakoo akawa analipwa vizuri na Mumewe,Deo alikuwa na maduka saba ya vifaa vya ujenzi na kampuni ya usafirishaji mizigo na baada ya mwezi mmoja baadaye akafungua ‘Grocery’ siku zote Deo hakutoshekwa na utajiri aliokuwa nao,alikuwa ana tabia za kichaga ingawa hakuwa kabila hilo.
Siku zote alikuwa akiwaza kesho na hakuwa na mchezo linapokuja swala la pesa,japokuwa alikuwa mfanyabiashara mkubwa lakini aliijuwa shilingi mia.Katika biashara zake alitaka kujuwa pesa zilikwendaje hususani kila baada ya mwisho wa mwezi anapopita kwenye maduka yake kukusanya mauzo,hapo ndipo anapokuaga mkali kama mbogo.
“Wewe Monalisa,sijaelewa hizi hesabu hapa.Umeniambia tu juu juu”
Deo siku hiyo alikuwa ndani ya duka lake la vifaa vya ujenzi anapiga hesabu,Mjini Kariakoo Mtaa wa Swahili.
“Hii milioni mbili nilichukuwa mzigo wa rangi za Sadolin risiti hizo hapo,ambapo kila ndoo inauzwa elfu arobaini na tano”
“Achana nahii milioni mbili,naulizia hapa.Umeandika Expenses sijaelewa hapa.Unakula mara ngapi?”
“Mara tatu”
“Mara tatu!?”
Deo akauliza kwa mshangao mkubwa uliochanganyika na hasira.
“Hapana mara mbili bosi”
“Shilingi ngapi unatumia kwenye kula?”
“Elfu kumi na moja”
“Kwa chakula kipi?ina maana wewe kwa mwezi unakula zaidi ya laki mbili kwa hesabu za harakaharaka?Mimi bosi wako kwa siku nakula shilingi elfu tano,Sikutaki hapa dukani haiweze..”
“Bosi naomba unisame…”
“Nakwambia hivi,nitamtafuta mtu mwingine wa kukaa hapa.Wewe hufai,sikutaki”
Deo hakuwa na masihara,alikerwa kupita kiasi na huyo ndio ulikuwa mwisho wa Monalisa kufanya kazi dukani kwa Deo ‘DK Hardwares’
alivyomaliza maduka yote alimpitia Mke wake Marietha mtaa wa Gerezani, wakapiga hesabu na hakukuwa na shoti ya pesa hata moja,Deo alifurahishwa na umakini wa mke wake wakafunga duka wakaingia ndani ya gari,wakanyoosha mpaka Ukonga na hapo ndipo kulikuwa kuna baa yao waliyoiita DM Grocery,D ilimaanisha Deo na M ilisimama badala ya jina Marietha, kumaanisha kuwa ilimilikiwa na mtu pamoja na mkewe.Walivyofika tu,wahudumu wakaanza kujigonga huku na kule baada ya kumuona bosi wao kafika.
“Niletee Serengeti”
Deo akaagiza,Muhudumu akamgeukia Marietha ili kumsikiliza.
“Mimi Tusker”
“Wewe,sasa unaenda wapi?Nilishakwambia siku nyingine kabla hujaenda kuchukuwa kinywaji udai pesa.Hata mimi nalipa.Pesa mbele”
Deo akainuka kidogo na kutoa pochi mfuko wa nyuma na kumkabidhi muhudumu pesa.Vinywaji vikaletwa wakaanza kunywa na Deo alikuwa mwenye furaha kwa kiasi cha kutosha alikadhalika Marietha.
“Love nimechoka baridi sana,twende tukapumzike”
“Marietha ushaanza,unapenda sana kulala Baby ndiyo kwanza saa tatu”
Hawakuwa na sababu ya kuendelea kubaki na kunywa pombe,Deo alihofia kubaki mpaka usiku sana sababu alikuwa ana pesa nyingi ndani ya gari bado hajaenda kuzihifadhi benki,alivyokumbuka kitu hicho akasimama na kunyoosha mpaka kaunta.
“Nadhani sidaiwi”
“Ndio bosi”
“Kesho akija meneja mwambie anipigie simu,vipi wateja wapo lakini?”
“Hivyo hivyo tu bosi wanakuja na kupotea”
“Aya mimi naondoka”
****
“Baby nikuulize swali?”
IIikuwa ni asubuhi siku iliyofuata baada ya Deo kutoka kitandani anajiandaa.
“Niulize mpenzi”
“Ushawahi kutoa mimba?”
Lilikuwa ni swali lililomshtua sana Marietha kwani hakutegemea kusikia kitu kama hicho kutoka kwa mume wake.
“Kwanini umeniuliza?”
“Nijibu baby”
“Hapana sijawahi”
“Sasa kwanini mpaka leo sioni dalili yoyote ya wewe kuwa na mimba?miezi mitano hii imepita”
“Mtoto ni mipango ya Mungu baby”
“Unasemaaa?Mipango ya Mungu?”
Jinsi Deo alivyouliza kwa ukali na kukunja sura ilimfanya Marietha aogope kidogo sababu hakuwahi kumuona akiwa katika hasira za ghafla.
“Baby lak…”
“Nisikilize nilikuwa nikijaribu kucheza na tarehe zako,lakini naona kimnya mwenzangu hauhisi kichefuchefu wala nini.Nataka namimi niitwe baba”
Deo aliongea kwa sauti ya juu sana tena iliyojaa hasira.


Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya Deo huku akimaanisha kile anachokiongea sababu baada ya hapo alivuta koti la suti na kuliviringisha mwilini, akabeba funguo za gari na kufungua mlango akatoka nje,Marietha bado alidhani kwamba Deo yupo katika hali ya masihara na muda huohuo angegeuza na kumwambia ‘baby nakutania’lakini haikuwa hivyo,alisikia muungurumo wa gari la mumewe kisha likatokomea nje.Haikuwa kawaida ya Deo kuondoka peke yake tangu amuanzishe kazi, ilikuwa asubuhi ni lazima watoke wote na amuache dukani kisha yeye aendelee na majukumu mengine lakini siku hiyo ilikuwa tofauti kabisa kwani Deo aliondoka mwenyewe mbali na hapo alikuwa akifoka kwa hasira akitaka mtoto.
“Kuna lingine au swala la mtoto peke yake?”
Marietha bado alijiuliza kichwani kwake,hakutaka kuamini kuwa Deo alikuwa akitaka mtoto ama alikuwa na sababu nyingine moyoni sababu swala hilo lilikuwa ni lazima waongee kama wenza!lakini haikuwa hivyo bado aliganda kitandani akiwa mwenye mawazo mia moja kidogo.
Akasimama na kutoka kitandani akanyoosha mpaka bafuni ambapo alifungua koki ya bomba la maji ya mvua yakaanza kumiminika mwilini mwake.
****
Ni kweli Deo alitaka mtoto sio masihara hiyo ilifanya akili yake ibadilike ghafla hata yeye alijishangaa ni kwanini amekuwa katika hali hiyo, hata alivyofika ofisini kwake alikuwa akiwafokea wafanyakazi wake bila sababu ya msingi yote hiyo ilitokana na hasira alizotoka nazo nyumbani kwake ingawa haikutakiwa kuzileta kazini.
“Nimeshakwambia siwezi kurudia jambo hilo kila siku,toka ofisini kwangu Eliza haraka sana.”
Deo alifoka ofisini kwake sauti yake ikaenea mpaka nje,wafanyakazi wengine wakasikia.Haikuwa kawaida kabisa kwa tajiri yao kuongea kwa ukali kiasi hicho tena asubuhi tu.
“Niitie Shakira sasa hivi”
“Hajafika bosi”
“Kwanini?”
“Sijui Bosi”
“Akija mwambie anione mara moja aje kuchukuwa barua,simtaki tena ofisini kwangu.GET OUT”
Hakuna siku ambayo aliyotetemeka ofisini kama siku hiyo,Eliza aliogopa na kufanya mpaka adondoshe mafaili aliyoyashika mkononi mwake,alihofia mno akaokota na kufungua mlango kabla ya kutoka nje akaitwa.
“Wewe Eliza..”
“Abee bosi”
Eliza akageuka kwa adabu zote,akasogea karibu na bosi wake.
“Niletee kahawa”
“Sawa bosi”
Hicho ndicho kilichotokea,akili ya Deo ilivurugika kwa kiasi cha kutosha.Mpaka wafanyakazi wake wakamuogopa

“Mpelekee bosi hili faili anatakiwa kujaza”
“Weeee nani aende?Mimi siendi yaani hata uniwekee bunduki,bosi leo hayupo sawa kabisaa ”
“Sasa ndiyo umuogope,alafu wewe ndio umemzoea”
“Nimemsikia kamfokea Eliza huko,sembuse mimi.Peleka mwenyewe”
Ilikuwa tofauti na siku nyingine zote, wafanyakazi siku hiyo walimuogopa Deo kuliko chui ama simba,kazi yao ilikuwa ni kusakiziana mafaili, nani aende.Mwanamke mdogo aliyeitwa Joyce Jackson meneja manunuzi akasimama kwa kujiamini.
“Nipeni hilo faili nipeleke,ni muhimu sana mnazozana tu wakati hizo Quotation zinatakiwa kujazwa sasa hivi”
“Kwahiyo unaenda?”
“Ndio lete”
Joyce Jackson akasimama na kuweka sketi yake vizuri akagonga kidogo na kusukuma mlango wa kioo ambapo alimkuta bosi wake amelaza kichwa juu ya meza,akashusha pumzi kidogo.
“Boss”
“Boss”
“Boss”
Joyce aliita lakini Deo hakuinua kichwa chake ingawa alijuwa kuwa anasikiwa,hakukoma,akazidi kuita.
“Una shida gani?”
Deo alijibu huku kichwa chake bado kikiwa vilevile juu ya meza.
“Kuna mafaili hapa unatakiwa kuj…”
“Yaweke hapo nenda”
“Lakini bosi kuna tatizo lolo..”
“Joyce weka mafaili nenda,nimekusikia”
“Sawa”
Deo hapohapo akasimama,akatembea na kuvuta mlango,wafanyakazi wakaanza kugongana vikumbo.
“Shii shiii shikamoo bosi”
Ilikuwa ni salamu kutoka kwa bwana Gelard Mtabwa katika kumbukumbu zake alikumbuka kuwa alishamsalimia tajiri yake lakini kutokana na uwoga akajikuta anatoa salamu kwa mara nyingine bila kutegemea.
“Shakirah keshafika?”
Deo aliuliza,macho yake yalikuwa mekundu amekunja ndita.
“Hapana”
“Akifika mwambie ninahitaji kumuona”
Alivyosema hayo akatoka nje huku nyuma akiwaacha wafanyakazi wakiangua vicheko kwa sauti.
“Wewe Gerlad kumbe muoga hivyo,jasho limekutoka hahahahahahaha”
“Yaaani mimi hahaha yaaaani nilikuwa nimebana kicheko ilikuwa kidogo nicheke palepale nilivyomuangalia Gerlad alivyokuwa anatetemeka”
Wafanyakazi walicheka,ikawa kama paka kaondoka sasa panya wametawala.
***
Deo aliingia ndani ya gari na kuanza safari ya kwenda asipopajuwa ingawa alitamani kurudi nyumbani kwake akapumzike lakini wazo hilo akaliweka kando,alivyofika maeneo ya Kisutu akaweka gari kushoto baada ya kuona baa,alihisi kunywa pombe akiamini kwamba akili yake ingekaa sawa,haikuwa kawaida yake kunywa pombe asubuhi hata siku moja tena siku za kazi lakini siku hiyo ilikuwa tofauti kabisa kwani alifika viti virefu na kuagiza pombe kali.
“Nipe kisichana kimoja”
“Konyagi?”
“Ndio na coca cola ya baridi”
Muhudumu akafanya alichoagizwa na mteja wake,Deo akashika chupa ya konyagi na kuipiga kwa chini ili presha ipande juu, akafungua na kumimina ndani ya glass ambapo alichakachuwa kwa kuchanganya na Coca cola ili kupunguza uchachu.
Glass ya kwanza ilipoisha ndipo alipoanza kuhisi kizunguzungu kwa mbali,akanywa nyingine.Kichwa chake kilijaa Marietha.Ghafla akaja mwanaume mfupi kiasi mweupe nyuma yake,wakatizamana kwa muda.
“Karekezi,ni wewe au nakufananisha?”
Hapo ndipo Deo alipogeuka vizuri na kumuangalia mwanaume huyo aliyekuwa anaagiza maji ya kunywa ya Dasan.
“Ndioo Mimi,sura yako sio ngeni tulionana wapi?”
“Karekezi Deo,nimeamini kweli milima haikutani lakini binadamu lazima tukutane mimi ni Kway,tulisoma wote shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko pale kariakoo”
“Kwaaaaaay,Aisee.Za siku nyingi?Upo wapi siku hizi?”
“Nipo tu napambana na maisha,ebwana umebadilika kitambi nini.Long time”
“Ni miaka mingi sana zaidi ya miaka kumi na tano nadhani”
“Zaidi ya miaka ishirini bwana”
“Kabisa nakumbuka viboko vya Mwalimu Macha,Ticha Mwakitaluuu”
“Deo tutaonana wacha mimi niwahi shuleni hapo kuna kikao cha wazazi”
“Kumbe una mtoto?”
“Nina watoto wawili sasa hivi,yaani vurugu tupu.Inabidi tuongee nichukuwe namba zako.Kwani vipi wewe bado?”
“Mimi?Mimi?Mimi bado kidogo naweka mambo sawa”Alibabaika kidogo.
Kilichofuata hapo ni kubadilishana namba,Bwana Kway akachukuwa maji na kutoka ambapo Deo alimsindikiza kwa macho mpaka alipoingia ndani ya gari aina ya ‘Spacio’ na kuondoka zake.

Deo aliumia moyo sababu alikuwa na sababu zote za kuitwa baba mpaka wakati huo,alizidi kunywa pombe siku hiyo, mpaka inafika usiku wa saa mbili alikuwa bwii hajiwezi tena.
Ubaya hakula chakula hiyo ndiyo ikafanya pombe zimvuruge zaidi akili yake,akalipa bili anayodaiwa na kuanza kupepesuka mpaka ndani ya gari lake.Haikuwa rahisi kuamini kwamba Deo angefika kwake salama salmin mbaya zaidi alikuwa akitumia chombo cha moto, kivyovyote vile angesababisha ajali mbaya pengine ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yake.
Alilipiga moto na kukanyaga ‘race’gari ikatoa mlio mkubwa akakumbuka kuwa hajaweka gia.
“Ohhh sijafuunga mkaaaanda kumbe”
Alijisemesha mwenyewe huku akicheua,akakaza macho mbele akaweka gia na kuliondoa gari kwa kasi isiyoweza kuelezeka kiwepesi.Ingawa alikuwa amelewa chakali lakini njia ya nyumbani kwake haikuweza kumtoka.
“Pipiiii piiiiii”
Gari ya nyuma yake ilimshtua,alivyoangalia vizuri aligundua kuwa yupo katikati ya barabara akarudisha usukani kushoto.Akazidi kulitoa gari kwa kasi ya ajabu,akakunja kushoto na kuiacha barabara ya lami.Zilikuwa zimebaki kama mita kumi ili alifikie geti lake.
“Piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii”
Deo alikandamiza honi kwa fujo akiwa hata bado hajafika getini kwake,alivyolifikia geti akaweka mguu kati akazidi kufanya fujo za kupiga honi.
Jinsi Mlinzi wa getini alivyokurupuka hakutofautishwa na mgambo aliyepoteza kirungu sababu alikuwa kauchapa usingizi juu ya kiti.Haraka akafungua geti,Deo akaingiza gari ndani ambapo alinyoosha na kukanyaga bustani,matairi yote ya gari yakakanyaga maua.
Bila kuzima gari akashuka akatembea na kuanza kupigapiga mlango.
“Funguaaa mlangoo Mariethaaaaa,Kidume nimerudiiiii.Bepari karudi,fanya upesiii nitavunja huu mlangooo”
Marietha alikuwa juu ya sofa alivyosikia sauti ya Mume wake aliruka na kwenda kufungua.
“Karibu nd..”
Kabla ya kumalizia sentesi akapigwa kikumbo na Deo.
“Karibuuu niniiii?Upo upo tuu kama ling’ombeee…Unamaliza makochi yanguuuu,mara mia ungekuwa kuku ningekunywa maziwaa aaah aaaah Kumbe kuku atoi maziwaa ningekulaaa mayaii,huna faidaaaa USELESS hauna maana”Deo aliongea huku akipepesuka akawa ana tupatupa mikono yake kama mwana ‘hiphop’
Yalikuwa ni matusi makali kupita kiasi,Marietha alikaa chini na kuanza kumwaga machozi.
“Unaliaaaa niniiiiiii?kinyago cha mpapuleeeee..Tena nyamaza nikustiliiiiii….Kesho asubuhi nataka unizalie mtoto,Shenzi!,Nimekutana na marafiki zangu leo wakina Kway wotee wana watotoooo,kasoro wewe.Stupid bustard sikujuwa kama wewe mgumba huzai.Bora ningemsikiliza mama yangu Mzazi alinisihii sana,nisikuoe bila kuzaa nawewe”



Siku zote sumu haijaribiwi kwa kuionja,mbali na Marietha kumpenda Deo lakini siku zote alikuwa akitamani ndoa ingawa kwa mara ya kwanza alionesha kupinga kukubali ombi lake.Hivyo aliingia kwenye ndoa akijaribu, mguu wake mmoja ukiwa ndani mwingine nje,hata siku moja hakuwahi kutegemea kwamba Deo angebadilika kiasi hicho na kumtukana matusi makali kama hayo usiku huo mkubwa, muda huo watu walikuwa wamelala lakini yeye alikuwa anaambulia matusi tu.Alimtizama Deo huku akiwa analia kwa uchungu.
“Naseeeema kwaaamba ninahitaji mtoto,umenielewaaa?Chakulaa kiko wapiiii?Chakula kikoo wapii?”
Deo aliendelea kuongea kwa sauti ya juu iliyochanganyika na ulevi huku akipepesuka huku na kule,haikuwezakana hata kidogo kwa mlevi kumtukana mtu kiasi hicho bila sababu, kwa asilimia mia moja Deo alimnywea pombe Marietha ili amtukane.
“Ki..ko Mez..ani”
Marietha alijibu huku kwikwi ikiwa imem-bana.
“Kilete hapaaaaa,hurry up”
Halikuwa tena ombi bali ni amri tena iliyochanganyika na kiingereza ili kuonesha msisitizo, jinsi Deo alivyosimama macho yake yakiwa mekundu ilimtisha Marietha,akasimama taratibu mpaka meza ya chakula akabeba ‘hotpot’ akaweka seblen juu ya meza akaendea sahani na vijiko, akaweka pia.
“Karibu”Akasema.
Lakini badala ya Deo kukaa chini alimkata jicho kali la chuki lililojaa hasira kali sana,Marietha akarudi kinyumenyume sababu alijuwa kitakachofuata hapo ni kofi kama sio ngumi kwahiyo alijihami.
Deo akakaa na kuanza kufungua ‘hotpot’ ambapo lilikuwa na sehemu maalum ya kuweka mboga pia.Akapakuwa vijiko viwili vya wali na kuweka mchuzi wa kuku juu yake.Akapiga kijiko cha kwanza,akakunja sura.
“Chakulaa mbonaa kina chumvi nyiiingiiii?embuu njoo hapaaaaaa onjaa chakula”
Marietha akazidi kutetemeka na kuogopa zaidi.Hakuelewa ni kitu gani kimempata mume wake wa ndoa sababu kufumba na kufumbua mambo yalibadilika ghafla, hakuwa Deo yule aliyekuwa anamdekeza kipindi cha nyuma hakuelewa ni shetani gani ameingilia ndoa yake tena bado ikiwa changa,wakati mwingine alidhani wenda yu ndotoni.
“Nikwambiaaaa njoooo haapaaaaa”
Deo akasimama ghafla kwa nia ya kumvaa Marietha ili ampige lakini mguu wake uligusa meza ikadondoka chakula chote kikamwagika juu ya malumalu.
“Unaona umemwagaaa chakula”
Deo akasema.Akazidi kukasirika.Ilikuwa ni kama anatafuta sababu.
“Deo, lakini una nini mume wangu?”
Marietha alijikakamua na kuuliza.
“Nina nini?unataka kujuaaaaa,ninahitajii mtoto”
“Ndio ufanye vituko kama hivii,kweli?”
“Vitukooo ganii? mimi najionaa niko fresh,lakini ninachohitajiii ni mtoto nataka kuitwa Dad”
“Unadhani utampata kwa staili hiyo ya kulewa pombe na kunitukana eeh,kama umenichoka uniambie sio unazunguka zunguka Deo,mimi sio mtoto mdogo.Hili ni swala la kuongea mimi na wewe sio unaenda na kunilewea pombe”
Tayari Marietha alikuwa amechemka kwa hasira,aliongea kwa ghadhabu, tabia ya Deo ilimkera sana.Akazidi kuongea huku akilia kwa uchungu,alivyokuja kutahamaki aligundua kwamba Mme wake ameuchapa usingizi tayari tena anakoroma.Akatembea akamvua viatu na kumlaza vizuri juu ya kochi.
****
Alihisi kichwa chake kizito kama tofali,kizunguzungu kikali kilikuwa kimemshika asubuhi alivyoamka na kilichomchanganya zaidi alijikuta yupo juu ya sofa seblen.Hakuelewa amefikaje sababu alivyojaribu kuvuta kumbukumbu zake zikae sawa hakupata jibu sahihi la kumridhisha,akaangalia huku na kule bila kuona mtu yoyote yule.Kichwa chake kilikuwa kinavuta kupita kiasi.Akajitahidi kusimama na kuruka vyombo vilivyokuwa chini vimedondoka,malumalu ilikuwa imechafuka mchuzi wa nyama.Kumbukumbu zake bado hazikuweza kutambua kitu kilichotokea.Akanyoosha mpaka chumbani,alivyofungua mlango alimkuta Marietha analia,macho yake yamemvimba ilionekana usiku kucha alikuwa akilia tu,hilo ndilo lililomchanganya akili zaidi.
“Mariethaaa”
Deo akaita kwa sauti ya chini huku akimsogelea.
“Marietha”
Ingawa alisikia anaitwa lakini hakuitikia,alimtizama Mume wake na kuinama chini akiendelea kulia machozi,ngozi yake ilibadilika rangi na kuwa nyekundu kabisa.
“Kwanini unalia?”
Deo aliuliza, lakini Marietha alitafsiri swali hilo ni kama maigizo.
“Deo,naomba tu nirudi kwetu.Sitoweza kuishi hivi”
“Mbona sikuelewi?”
“Jana umenitukana”
“Mimi?”
Deo aliuliza kwa mshangao wa waziwazi,sababu kitu kama hicho alijuwa hakuwahi kukifanya.
“Jana asubuhi lakini samahani kwa kukuambia ma..”
“Deo jana usiku ulikuja ukanitukana mpaka ukamwaga chakula,ndiyo maana sikutaka kutoa chochote nilijuwa utakataa.Sawa hujanitukana nani kafanya vile seblen?”
Kila Deo alipojaribu kukusanya kumbukumbu zake juu ya kilichotokea usiku wa jana hakupata kitu chochote, kwa maana hiyo maneno ya Marietha yalikuwa mapya kabisa kwake.Alichokumbuka yeye ni asubuhi kuondoka na kumwambia Marietha kwamba anahitajika mtoto kisha kufika ofisini kwake,kila kitu kilitiririka kichwani mwake akawa kama anatizama mkanda wa filamu.Hakujuwa kilichoendelea tangu alivyofika baa kunywa pombe.
“Nyumbani nani alinileta?”
Lilikuwa ni swali la kijinga alilolitupa kwa mke wake.Kichwa chake kilikuwa kama kompyuta iliyoingia wadudu wa ‘virus’maana kumbukumbu zilipotea.Marietha alikuwa amekaa kitandani anamtizama mume wake,hakujuwa ni hatua gani aichukuwe ya harakaharaka.
“Ulikuja mwenyewe”
“Marietha kama nilikutukana naomba unisamehe ni pombe nahaidi sitorudia tena”
Deo aliomba radhi,moyoni alijuta ingawa kila alipojaribu kurudisha mambo nyuma hakuelewa,mbali na hapo hakujuwa alifika vipi nyumbani kwake jambo hilo lilimsumbua sana akili yake na kuamini kwamba pombe kali alizokunywa usiku wa jana zilizidi kipimo chake.
“Griii griiii”
Simu ndiyo iliyomshtua kutoka katika mawazo akiwa bado amesimama,alivyoitoa na kuangalia juu ya kioo aligundua anayepiga ni mmoja wa wafanyakazi wake,akaipokea na kuiweka sikioni.
“Shikamoo bosi”
“Marahaba Sele,vipi?”
“Ile oda tayari imekamilika sasa kuna bei za vitu hapa nashindwa kujaza”
“Nitajie hizo items”
“Makufuli,Mifuko ya cement,Bomba za Ips,Mbao za mninga,makopo ya rangi ya Sadoline na Goldstar,Gatevalve,Vita..”
“Sele”
Deo akamkatisha kidogo.
“Naam bosi”
“Niandikie kwenye meseji,ama piga picha hizo items nitumie kwenye Watsap.Alafu ile profoma invoice uliipeleka TRL?”
“Ndio bosi”
“Sawa,nitumie hiyo picha nikutajie bei fanya haraka.Hivyo vitu vinahitajika leo by ten thirty viwe tayari”
“Sawa bosi”
Siku zote Deo katika biashara zake alikuwa mtu makini sana na hakutaka mchezo kabisa wenda ndiyo maana alikuwa miongoni mwa vijana wadogo wenye utajiri mkubwa jijini Dar es salaama,utajiri wake ulikuwa tofauti na umri wake.
“Marietha si…”
“Nenda kazini Deo nimekusamehe”
“Love una..”
“Nimekusamehe Deo,nenda ofisini kwa amani”
Ili kulipigilia swala lake msumari Marietha alisimama na kwenda mpaka mdomoni mwa Deo na kumnyonya lips zake akiwa mwenye furaha,haikuwa kawaida hata kidogo kwa Marietha kutoa msamaha kirahisi namna hiyo ndiyo maana Deo hakuamini harakaharaka.
“Ingia bafuni uoge,ngoja nikuwashie hita,naenda kukutengenezea supu najuwa bado una hangover”
Deo bado alisimama akimtizama Mke wake,bado alidhani mke wake anamtania na baada ya dakika moja atabadilika ghafla tena ataweka vitu vyake na kuondoka zake kama afanyavyo siku zote akikasirika.
“Marietha naomba nisamehe kama mimi nilifanya mambo unayosema itakuwa ni pombe”
Bado Deo aliendelea kulilia asamehewe na mkewe japokuwa msamaha ulikuwa ushapitishwa tayari.
“Deo nenda kaoge mume wangu”
Baada ya kumwambia maneno hayo mume wake alitembea mpaka bafuni akawasha hita ili maji yapate moto ili baada ya dakika tano kupita Deo aingie bafuni ajimwagie maji kisha aende kazini.
Na hicho ndicho kilichotokea,baada ya dakika sita kupita Deo aliingia bafuni akajimwagia maji alivyotoka alikuta nguo zake zipo kitandani zimeshapigwa pasi tayari,akavaa harakaharaka na kumshukuru mke wake ikawa kama hakuna kitu kilichotokea baina yao.
“Usijali kuhusu supu,ngoja niwahi”
*****
Ingawa alisamehewa lakini hakutaka kulipitisha swala hilo moja kwa moja ndani ya moyo wake,bado aliendelea kufikiria kwamba Marietha wakati huo atakuwa anafungasha virago vyake na kuondoka kabisa,ndiyo maana akawa anampigia simu baada ya kila dakika tano kupita.
“Upo nyumbani kweli?”
Lilikuwa ni swali la Deo,akiwa amelirudia mara ya saba kwenye simu.
“Ndio love,sasa unadhani nitakuwa wapi kwani?”
“Hapana nauliza tu,kwahiyo unafanya nini sasa hivi?”
“Nimetoka kuoga nataka niende jikoni kupika”
“Ooh! okay mimi ndiyo nafika Posta hapa”
“Okay honey,take care”
“Nakupenda”
“Mimi pia mme wangu”
Deo alikata simu na kuendelea na shughuli zake za kila siku ambapo kazi yake ilikuwa ni kujaza bei ya vitu alizoambiwa kuwa vitatakiwa,mbali na kuwa na duka la kuuza vifaa pia alikuwa ana kampuni ya kusambaza vifaa vya ujenzi yaani alikuwa ‘Supplier’.

Hakuna siku aliyokuwa ana furaha kama siku hiyo saa nane ya mchana baada ya kupokea hundi tatu kwa mpigo, moja ilitoka Tazara hiyo ilikuwa ya shilingi milioni kumi na tisa,moja alilipwa kutoka chuo kikuu cha ARDHI hii ilisoma milioni ishirini na moja naya mwisho ilitoka TRL hiyo ilisomeka milioni saba na laki nane,meno yake yote thelathini na mbili yalikuwa nje,akichekelea.
“Wewe nani aah,mpaka nakusahau jina Devotha njoo hapa ofisini”
Deo aliita huku akiwa na tabasamu pana mdomoni mwake,akavimbisha mikono yake, yote hiyo ilikuwa ni furaha.
“Organize na utoe taarifa kwa wafanyakazi wote Jumamosi mchana baada ya kazi wawepo kwenye baa yangu wanywe na kufurahi mimi nitalipa”
“Bosi baa ipi hiyo?”
Devotha hakuelewa kwamba bosi wake ana ‘grocery’.Ilibidi Deo aanze kumuelekeza kila kitu niya yake ilikuwa ni kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa bidii,hiyo ndiyo ilikuwa tabia ya Deo siku zote.Akipata pesa anafurahi na wafanyakazi wake kwa kuwapa ofa.
****
“Baby,Baby…Darling uko wapi?”
Ilikuwa ni sauti ya Deo akimuita mkewe kwa furaha akaingia mpaka chumbani na kumkuta amejilaza anatizama luninga amejiachia.
“Hee!Mbona mapema leo?”
“Baby simama”
“Kuna nini Deo?”
“Simama mke wangu”
Marietha alivyosimama Deo alichukuwa kitambaa cheusi na kumfunga machoni,akamshika mkono na kuanza kutoka naye nje ambapo alivyofika alikifungua.Macho ya Marietha yalitua kwenye gari la rangi nyekundu aina ya Nissan Murano,ilikuwa ni gari nzuri iliyorembwa na maua, juu ya kioo kuna kadi iliyoandikwa’Nakupenda mke wangu’ chini alitizama kadi nyingine iliyokuwa na maandishi ya kuomba msamaha.Mapigo ya Marietha yalizidi kupiga kwa nguvu,bado hakuelewa maana yake.
“Deo umenunua gari mpya?”
Aliuliza huku akimgeukia mme wake.
“Hapana ni gari yako”
“Deoooooo,Oh My God”
Marietha aliruka kwa furaha sababu hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake siku moja kuja kuendesha gari ingawa hakutaka kumwambia mme wake moja kwa moja,alilikimbilia gari na kuanza kulizunguka kama askari anayekagua kitu,bado hakuyaamini macho yake.Gari ilikuwa mpya yaani halina hata ‘plate number’
“Honey ahsante,sasa mimi siwezi kuendesha gari mme wangu”
“Nitakufundisha pia nitakupeleka driving school”
Nusu saa nzima ilipotea wakiwa wanaishangaa gari,ambapo waliingia mpaka ndani na kuanza kuikagua.Ilikuwa ni gari ya kisasa mno na ndani ilikuwa nzuri kupita kiasi.
“Hiki ni kifriji,kama unataka kuweka wine,unafungua hapa kinywaji kinapata baridi.Hapa ni sehemu ya kuweka glasi”
Yalikuwa ni maelekezo madogo aliyotoa Deo,Marietha alibaki kushangaa.Akamsogelea Deo mdomoni na kuanza kumnyonya mdomo.
“Baby unajuwa nini?”
Marietha akasema baada ya kujitoa mdomoni.
“Nambie mke wangu”
“Leo ni siku yetu,nipo katika siku hatari twende chumbani”
Hapohapo Marietha akatoka akamvuta mme wake,wakaanza kupigana madenda walivyofika seblen ambapo waliunganisha mpaka chumbani,wakajibwaga puu! Kitandani, kilichoendelea hapo yalikuwa ni madenda kwa kwenda mbele kila mtu alikuwa mwenye furaha,siku hiyo hawakufanya tendo la ndoa kujiburudisha peke yake,bali kutafuta mtoto na mechi hiyo ilikuwa na malengo makubwa sana.Waliendelea kunyonyana ndimi,mkono wa Deo ulishuka mpaka chini ya kitovu cha Marietha akazidi kuupeleka chini zaidi,akakutana na chupi,akazidi kuudidimiza mkono wake ndani zaidi ambapo alikutana na kitu alichokihitaji,kwa kutumia kidole chake alianza kucheza na mgodi wa mkewe taratibu sana.
Marietha kazi yake ilikuwa ni kujikunja kunja akianza kukatika taratibu,mwenyewe akaanza kuitoa nguo ya juu,akatoa na sidiria Deo akaanza kuyanyonya maembe ki utaalam akawa anatumia ncha yake ya ulimi kulamba chuchu hizi zilizosimama wima,alivyoona haitoshi akashuka chini na kukamata suruali ya Marietha akaivuta chini na Chupi vilevile na hivyohivyo alifanya Marietha alimvua nguo mume wake,baada ya sekunde tano wote wakabaki kama walivyozaliwa,macho yao yalibadilika rangi yakawa mekundu, kifupi wote walikuwa wakichemka,lakini bado waliendelea kupasha Deo hakuwa mshamba wa mapenzi,ndiyo maana alitaka kumuandaa mke wake akamshika kila mahali mwilini mwake,alivyohisi kwenye mgodi kuna hali ya unyevuunyevu hapohapo akaitumbukiza mashine tayari kwa kuchimba madini,akauchukuwa mguu wa Marietha akauweka begani akaendelea kupiga misumbwi.
“Ah aah ah ah ah ah sshsshh”
Marietha alikuwa anatolea sauti puani,Deo akiwa kifuani mwake anamnyonya shingo.Deo alivyoangalia pembeni akapata wazo jipya akambeba Marietha juu juu mpaka ukutani na kumuweka,kutokana na kuwa na mwili mkubwa kazi hiyo haikuwa ngumu,Miguu ya Marietha ilikuwa mikononi mwa Deo,mgongo wake upo ukutani ilikuwa kwa mara ya kwanza kufanyiwa kitu hicho alihisi kufakufa kwa raha za ajabu alizokuwa anahisi akiwa juu juu tena ukutani.
“De…o aaaaah aaaaaah”
“Ba..by have you cumm?”
Deo aliuliza akitaka kujuwa kama mke wake tayari alifika mshindo.
“No ba…by.I don’t wan’t to cumm now,fu*** me hard”
Marietha alitaka kulifurahia tendo kabla ya kufika mshindo na ndiyo maana alimwambia mme wake akiwa juu anabembea,ni kweli mechi hiyo ilidumu kwa muda mrefu sana,sababu Deo alitumia akili,kila alipohisi anataka kufika mshindo,aliitoa akili yake na kuipeleka mbali sana.

***
Saa nne ya asubuhi ndipo walipozinduka kutoka kitandani bado wakiwa wana uchovu, Deo amelala upande wa pili na Marietha hivyohivyo kifupi walikuwa wamepeana migongo na wa kwanza kufumbua macho alikuwa Marietha akamsogelea mme wake na kumkumbatia kwa nyuma,mguu wake mmoja akaupandisha kiunoni mwake.
“Baby,umechelewa kazini”
“Ah nimechookaa,nahisi uchovu.Inabidi twende wote leo,ukaanze kazi tena”
“Sawa love amka basi,achana na usingizi ni umaskini”
“Aya tangulia bafuni nakuja”
“Poa”
Marietha akatoka kitandani na kunyoosha mpaka bafuni,huko alijimwagia maji akapiga na mswaki lakini alivyorudi akamkuta bado Deo kauchapa usingizi.
“Love bwanaaa,wake up”
“Poa poaaa”
Deo akasimama akaingia bafuni nayeye akajimwagia maji,uchovu ukawa umeondoka mwilini,akatoka akakuta tayari nguo zipo kitandani.Marietha nayeye alikuwa anajiandaa ili waongozane na mke wake.
“Leo utani drive,tutatumia gari yako”
Deo akasema.
“Haaa!kama sijakutupa mtaroni leo,baby bwana sijui kuendesha gari”
“Utajuwa tu,kujuwa gari ni rahisi kama ukiweka nia”
Walivyomaliza kujiandaa wote wakatoka kwa pamoja.
Deo alipigwa na butwaa la waziwazi baada ya kufika seblen.Moyo wake ukawa unadunda kwa nguvu,kitu alichokiona kilimuogopesha!


“Leila!”
Deo alishtuka kwa mshangao wa waziwazi,mwanamke aliyemuona mbele yake aliyafanya mapigo yake ya moyo yapige kwa nguvu.Kitu kingine kilichomchanganya zaidi ni jinsi mwanamke huyo alivyokuwa amevaa.kaptula fupi na topu iliyoishia tumboni yaani kitovu chake kilikuwa nje.mbali na hapo hakuelewa Leila alipajuaje nyumbani kwake,sababu hakuwahi kumuelekeza.
“Deo,Long time….No calls no text..Tatizo nini lakini?”
Hilo ndilo swali la kwanza kulitupa Leila,akiwa amechora nne,akamtizama Marietha kwa kitambo kidogo kisha kusimama.
“Wifi naomba unisamehe kwa mambo yaliyotokea kule kisiwani najua umekasirika sana,ndio maana nimekuja hapa.Nisamehee sana”
Leila akatoa mkono wake kwa nia ya kumpa Marietha ili tofauti zao waziweke kando, kwa wakati huo yeye Deo alikuwa kimnya anatizama mchezo unavyoenda alitamani kutia neno lakini hakutaka kuingilia.
“Sawa nimekusamehee usijali”
Marietha akajibu na kutoa mkono wake kumaanisha kwamba mambo ni shwari yaani maisha yaendelee.
“So Deo,wapi sasa hivi?”
“Naenda kazini”
“Poa twende,nataka nipajue kazini kwako pia”
Leila alikuwa mwanamke machepele sana,Deo alitamani kupinga lakini hakuweza, wote walitoka nje na kuliendea gari jipya aina ya NISSAN Murano haikuwa na namba za usajili,Marietha akapanda mbele Leila akapita nyuma.
“New ride?”(Gari mpya)
Leila aliuliza huku akiwa ndani ya gari ingawa Deo alisikia lakini hakujibu kitu alizungusha usukani,akageuza shingo yake nyuma na kurudisha gari kinyumenyume,alivyohisi limekaa sawa mkao wa kutoka nje alivuta gia mpaka herufi D na kukanyaga mafuta,alimnunulia mkewe gari ‘automatic’akiamini kwake itakuwa rahisi sana kuendesha,alivyolitoa gari nje.Leila akauliza tena swali lile lile.
“Gari mpya hii Deo,Umenunua shilingi ngapi?Deo kumbe you have dimes”
“Ni la Mke wangu Marietha”
“Woow!”
“Yeah”
Ilionekana jibu hilo lilimchukiza sana Leila japokuwa alipachika tabasamu usoni mwake,bado alikuwa ana chuki na Marietha sababu alimpenda Deo kupita kiasi,alikuwa akijaribu kumpigia sana simu bila mafanikio yoyote, hiyo ndiyo ikampelekea mpaka aanze kupasaka nyumbani kwake, ilimchukuwa muda kidogo mpaka kupafahamu.
Ndani ya gari Deo hakuongea kitu chochote mpaka walipofika Kariakoo mtaa wa Masasi,akazungusha usukani na kusimamisha gari nje ya duka kubwa la vifaa vya ujenzi hapo ndipo alipotakiwa kumshusha Marietha.
“Sasa,inabidi ili gari nikalikatie namba kisha niende TRA nisajili”
“Okay sawa,kwahiyo leo hutoenda kazini?”
“Nitapita mara moja”
“Okay love take care”
Marietha akamsogelea mme wake mdomoni akamnyonya mdomo na kugeuka nyuma.
“Wifi,tutaonana”
“Aya mwaya”
Leila nayeye akajibu lakini moyo wake ulikuwa unawaka moto.
“Leila”
Deo akaita baada ya Marietha kushuka
“Yes Deo”
“Sijakuelewa vizuri kwahiyo leo utaenda ofisini kwangu?Alafu umepajuaje kwangu?”
Kipindi anauliza hivyo alikuwa anaendesha gari tayari.
“Deo,kwani vibaya mimi kupajua kwako?”
“Sio vibaya lakini umenishtukiza”
“Kwa sababu hupokei simu zangu,ilibidi mwenyewe nipatafute”
“Nilisafiri hata hivyo,nilikuwa nje ya mkoa nimeingia jana usiku”
Deo akadanganya sababu hakutaka kuweka mazoea na Leila kwa maana hiyo alitaka kumpotezea kimtindo ingawa hakutaka kulionesha swala hilo waziwazi.
“Well! pole na safari”
“Thanks”(Shukrani)
Siku hiyo Leila alikuwa kama ruba sababu alimganda Deo kama kitu gani sijui.
Ofisini walikuwa wote hata alivyoenda kula chakula cha mchana alikuwepo pia,hata Deo alivyopitia kwenda kusajili gari Leila alikuwa nyuma yake kifupi siku hiyo hakutofautishwa na mkia.Mpaka inafika jioni ya saa kumi Leila alikuwepo na Deo.
“Leo nime enjoy sana kuwa nawewe,nimekumbuka sana Uingereza tulivyokuwa chuo kikuu”
“Hata mimi”
“Mbona kama hujafurahi?”
“Niko poa,ni uchovu tu”
“Tukapate mbili tatu nini?”
“No hapana,sasa hivi natakiwa kumpitia Marietha,tunaenda nyumbani”
“Oh well,basi mtanidrop Landmark Hotel”
“Hakuna shida”
Deo alishukuru Mungu kimoyomoyo sababu katika hesabu zake alielewa kwamba Leila wenda angetaka kwenda kulala kwake,walivyofika mtaa wa masasi akapiga honi bila ya kushuka.
Akamuona Marietha katokeza nje akafungua mlango na kuingia,Deo akasogeza mdomo wake karibu wakanyonyana midomo kwa kama sekunde mbili.
“Pole na kazi love”
“Nawewe pole na kazi pia,ulifanikiwa?”
“Nilifanikiwa ndio,kila kitu nishalipia.Stika hizo hapo bado tu kubandika”
“Oh,Vipi Leila?”
“Salama tu”
Leila akaitikia na kuendelea kubonyeza simu yake,katika watu aliowachukia duniani ni mwanamke huyu Marietha,alimchukia kuliko kinyesi hiyo ilitokana na wivu, alijishangaa ni kwanini hali hiyo ilitokea ghafla hivyo alishindwa kupata jibu la harakaharaka,hata hivyo moyoni aliapia kwamba ni lazima angempata Deo hata kama ingemchukuwa miaka kumi.
***
Deo na Marietha waliendelea kutafuta mtoto kwa njia ya kufanya tendo la ndoa kila ifikapo tarehe za hatari za Marietha lakini wapi,miezi mitano mingine mbele ilikatika lakini Marietha hakuonesha hali yoyote ile ya kuwa na mimba hilo ndilo likamfanya Deo aanze kubadilika taratibu sababu swala hilo lilimuumiza sana kisaikolojia.
Ghafla akaanza kuleta vituko ndani ya nyumba,mara arudi asubuhi mara amjibu Marietha majibu ya chooni,ilimradi vurugu tupu,licha ya yote Marietha alijaribu kuvumilia.
“Unaongea na nani sasa hivi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Marietha usiku wa saa nane baada ya kutoka Chumbani na kumkuta Deo seblen mwenyewe yupo na taulo anaongea na simu.
“Deo unaongea na nani usiku huu?si nakuuliza”
Lilikuwa ni swali lingine kutoka kwa Marietha,Deo akageuka.
“Subiri nitakupigia baada ya dakika kumi”
Deo akakata simu.
“Naongea na marafiki zangu wenye watoto”
Deo alijibu kwa dharau.
“Sasa ndiyo usiku?”
“Kwani nikiongea usiku wewe shida yako nini?Tatizo ni kitu gani?Kinachokuuma ni kitu gani haswa?”
“Ni muda wa kulala huu”
“Mimi kulala kwangu haikuhusu, sawa”
“Lakini Deo umekuwaje?”
“Kwani wewe unanionaje?”
Yalikuwa ni majibu ya mkato naya choo ambayo mtu yoyote akijibiwa ni lazima akae kimnya lakini kwa Marietha aliendelea kuhoji tu.
“Umebadilika”
“Nimekuwa wa kijani kibichi au?”
Maswali ya Marietha kwake yalikuwa kama kero,akatembea na kupita.Akanyoosha mpaka chumbani kwake ambapo huko alijitupa kitandani.Marietha akamfuata.
“Deo”
“Sikia nataka kulala,tafadhali usinikere.Sasa hivi nitakuharibia usiku wako ohoooo!endelea uone”
Deo aliongea kwa ukali kupita kiasi,ilionesha kuwa alikuwa ana kitu moyoni,Marietha alielewa kosa lake kwamba ni mtoto,alijuwa ndilo linalomsumbua mme wake.
****
Asubuhi na mapema Deo alitoka kitandani,bila kumuaga mke wake alioga na kutoka nje ambapo aliwasha gari na kuondoka zake, kwa kuwa alikuwa ana funguo nyingine za akiba za ofisini kwake aliamua kunyoosha moja kwa moja,siku hiyo alikuwa wa kwanza kufika.
Hata baadhi ya wafanyakazi wake walivyofika na kuliona gari la bosi wao walishtuka sababu haikuwa kawaida hata siku moja Deo kufika ofisini saa kumi na mbili ya asubuhi kama mfanyakazi wa kawaida,muda wake ulijulikana siku zote ni saa mbili kama sio saa tatu asubuhi.Hata hivyo hakukaa ofisini ilivyofika saa saba mchana aliwasha gari na kuondoka zake.
****
“Nipe Red label na coca ya baridi”
Deo alikuwa baa amefika na kuagiza pombe kali.
“Pesa kwanza”
“Okay”
Deo akatoa pochi na kutoa noti ya shilingi elfu kumi akamkabidhi muhudumu na baada ya dakika moja zikaletwa chumba mbili moja ya pombe kali na nyingine ya coca cola.
“Niongeze na Konyagi,Kiroba”
Deo alikuwa akifanya kitu cha hatari kupita kiasi,pombe zote zilikuwa kali,kiroba kilivyoletwa akachana kwa meno, akamimina ndani ya glasi akachanganya na Red Label kisha kumimina soda ya Coca cola, alifanya hayo yote akiamini kwamba atatoa mawazo,hapohapo akakumbuka kitu.Akatoa simu yake na kuonekana kutafuta namba fulani kwenye simu.
“Halloo Mtui,uko wapi ndugu yangu?”
Deo aliuliza simuni.
“Nipo kazini,vipi kwani?”
“Njoo hapa wanapaitaaa,wanapaitaa Kisutu, baa moja inaitwa Kyamba”
“Deo,unakunywa mchana wote huu?Alafu leo ndio kwanza Jumanne?”
“Acha kunipa lisala wewe mchaga,unakuja au hauji?”
“Hapana kwa kweli,mimi siwezi kuja.Nipo kazini.Labda jioni”
“Aya kazi njema”
Deo alivyokata simu,akaachia msonyo.Na kuvuta glasi ambapo aliiweka mdomoni na kuanza kunywa,akajaribu kutafuta namba za marafiki zake lakini wote walikuwa ‘busy’ hakuna hata mmoja aliyemuunga mkono kunywa naye siku hiyo mchana wakidai kwamba ni muda wa kazi.
Deo hakuwa na chaguo lingine sababu alitaka kampani akaamua kumtafuta Leila hewani na kumueleza.
“Umesema upo wapi?”
“Kisutu,tafuta taxi nipe niongee naye mimi nitalipa”
“Okay sawa nakuja My dear”
Siku hiyo Leila alikuwa ana safari zake lakini akaghairi badala yake akabeba mkoba wake na kushuka ngazi ambapo alitafuta taxi kisha kumpigia Deo simu.
“Habari Kiongozi,ndiyo ndiyo kisutu hapo shuleni?Ukipita huo msikiti kushoto.Nishapafahamu okay sawa”
Dereva Taxi alikuwa katika mazungumzo na Deo simuni,akipewa maelekezo,Leila akaingia ndani ya taxi na safari ikaanza mara moja.

***

“Mkeeee waaaangu azaaaaaaai”
“Whaaaaat?”(nini)
“Ninasema hivi Marietha hazaiii ni mguumbaa,nimejaribu mpaka baaasi lakini nothing”
“Deo acha kunitaniaaa basi”
“Kwanini nikutanie wewe rafikiiii yanguuu sanaaaa tu”
“Naelewa sema unajuwa ngojaaa nikwambiee kitu acha kuwaa falaaa”
“Niambieee”
“Anakufanyia tu mchezo,wanawake wengi siku hizi hawapendi kuzaaa na nina uhakika,anatakaaa kukuuuwa yule mwanamke sio mtu mzuri”
Deo na Leila walikuwa bwii,wamelewa pombe na kilichotokea ni Deo kuanza kutoboa siri za chumbani.
Hakuelewa anafanya kosa kubwa sana kwa kufanya hivyo,walizidi kupiga masanga mpaka usiku wa saa tatu.
“Tweeendee kwenyeee baa moja ya Masaweeee,Pale kigogo.Tukaaendeleee”
Deo alishauri,wote walisimama wakiwa wanayumba wakaingia ndani ya gari.
Kwa hali isiyokuwa ya kawaida,Deo alimvuta Leila midomoni na kuanza kumla denda wakiwa ndani ya gari.Mapigo ya Leila yakapiga kwa nguvu.
“Honey”
Leila akaita.
“Yes baby”
“Twende tukapumzike”
“Waaaapi?”
“Tutafute hotel”
“Ndiooo waaaapi?”
“Endesha gari,nikiona nitakwambia,twende Peacock Hotel.Mnazi mmoja”
“Okay,Mwenye ile hotel anaaaiiiitwa Mfugale.Namfahamu poa twendeeeee”
Deo alikuwa bwi yaani tilalila,macho yake yalikuwa mazito mbele anaona giza kwa mbali,aliingia barabara ya mnazi moja na kukunja kulia ambapo baada ya dakika tano alifika baridi,pembeni yake kulikuwa na gorofa kubwa lililokuwa na maandishi makubwa kwa juu yaliyoandikwa PEACOCK HOTEL,akanyoosha na kuzungusha gari alivyofika U turn,baada ya sekunde saba alikuwa nje ya hotel hiyo akashuka na Leila akafungua mlango.
“Vyumba vipo?”
Leila ndiye aliyeuliza baada ya kufika mapokezi.
“Ndio”
“Nahitaji”
Leila akafanya malipo harakaharaka kisha wakatembea mpaka ndani ya ‘elevetor’ ikaanza kupanda juu,walivyofika lifti ikafunguka,wakanyoosha mpaka chumba namba 98 ambapo Leila alitoa kadi na kuweka mlangoni.

Ilikuwa ni hotel kubwa ya kisasa.Baada ya kuingia wakaanza kupigana madenda,bado Leila hakuamini kama alimpata Deo kirahisi namna hiyo,akamtupa kitandani na kuanza kumvua nguo zake nayeye akatupa za kwake,wote wakabaki kama walivyozaliwa.
Leila akapanda juu na kumkalia,wakaanza kufanya tendo baya la kuzini.
****
“Griiii griiiiiii.Griiiiii griiiiiiii.Griiii griiiiiiiii”
Simu ya Deo ilikuwa ikiita mfululizo,hata ilivyokata iliita tena.Kwa mbali alikuwa akisikia ikiita lakini macho yake yalikuwa mazito kufunguka,akajilazimisha.Moyo wake ukapiga paa! baada ya kugundua kuwa hayupo nyumbani na alivyoangalia pembeni alimuona Leila amemuwekea kichwa juu ya kifua chake yupo uchi wa mnyama,alivyojiangalia vizuri akashtuka zaidi baada ya kujikuta hana nguo hata moja,akashindwa kuelewa alifikaje eneo hilo na imekuwaje alilala na Leila,haraka akamtoa na kuingiza mkono ndani ya mfuko wa suruali yake iliyokuwa chini na kutoa simu,jina aliloliona lilimshtua ‘SWEET WIFE’ akaipokea na kuiweka simu haraka sikioni.
“Halloo”
Upande wa pili wa simu ulimshtua,sauti ya kiume ndiyo iliyosikika na wala sio ya mkewe.
“Hallo”
Nayeye akarudisha ili kusikilizia.
“Natumaini naongea na Mr.Deo Karekezi”
“Ndio, wewe ni nani?”
“Naitwa Dokta Bin Paul ,natokea hospitali ya Maranatha.Mkeo ameletwa hapa hospitali. Ana….”
“Niniiii?ana tatizo gani?”
“Sio jambo baya sana,ni mjamzito lakini kuna vitu unatakiwa kujua.Naomba uje hospitali sasa hivi”



Simu ilikuwa bado sikioni mwa Deo,maneno aliyokuwa anaambiwa upande wa pili wa simu hakuyaelewa kwamba ni ya ukweli ama masikio yake yamesikia vibaya,swala la Marietha kushika ujauzito lilimshtua kupita kiasi,ndiyo maana hakujuwa afanye kitu gani.Alikuwa yupo njiapanda.
“Umesema upo hospitali gani?”
Deo akauliza kwa kiwewe.
“Maranatha,Sinza Vatkani”
“Okay nakuja sasa hivi”
Siku zote kwake swala la kuitwa baba ndiyo lilikuwa moja ya ndoto zake na alitaka kuzaa na mwanamke anayempenda kutoka moyoni mwake na wala sio vinginevyo.Kitu kilichoyafanya mapigo yake ya moyo yaongeze kasi ni baada ya kugeuka nyuma na kumkuta Leila amelala kitandani,hakuelewa ilikuwaje mpaka amefika chumbani na Leila,akajaribu kukusanya kumbukumbu zake lakini wapi.Ni kweli alikumbuka alikuwa na Leila lakini hakuelewa ilikuwaje mpaka wakalala pamoja.
“Leila,wewe Leila”
Deo akaita kwa sauti huku akimpiga piga Leila mgongoni.
“Niniiii teeeena jaaamani”
Akaitikia kwa sauti ya uchovu wa usingizi huku akijigeuza upande wa pili,hiyo ikamfanya Deo amtingishe kwa nguvu.
“Wewe Leila,nieleze imekuwaje tupo hapa.Nani katuleta hapa?Naongea nawewe”
“Deooo Mimi sijui”
“Hujui?Hujui kivipi?”
“Mimi mwenyewe sijui,wote tulikunywa pombe”
“Unasema nini?”
“Deo niache nipumzikee”
Leila alitoa majibu ya mkato kwa kiburi chote, tayari alishaijuwa nguo ya ndani ya Deo na alielewa kwamba kwa mambo aliyompa usiku wa jana yangemfanya amrudie kivyovyote vile hilo alijiwekea asilimia mia moja,akajifananisha na kibuyu cha asali.
“Nilikuonjesha tu kidogo,bado yenyewe”
Leila aliongea akitumia misamiati, akageukia upande wa pili.
“Una maana gani?”
“Asiyejua maana haambiwi maana”
Deo Akashindwa kuelewa chochote sababu katika maisha yake hakuwahi kulia uswahilini,kutokana na simu aliyopigiwa kutoka hospitalini juu ya mke wake ilifanya aachane na Leila akaokota nguo zake chini,akiwa bado na shuka mwilini mwake akaliviringisha vizuri na kuingia bafuni akiogopa kuvaa nguo mbele ya Leila,hakuwa ana uhakika kwamba usiku walifanya ngono ama laa.Ingawa alihisi mwili wake haupo vizuri,alijuwa kabisa kuna kitendo kilifanyika lakini hakutaka kulipa swala hilo kipaumbele alichotakiwa kukifanya kwa wakati huo ni kunyoosha hospitalini akaonane na mke wake aliyekuwa mjamzito.

Akatoka bafuni akiwa amevaa tayari,bila kumsemesha Leila akabeba funguo zake za gari na kufungua mlango,ambapo aliingia ndani ya lifti na kubonyeza herufu G kumaanisha kwamba impeleke mpaka chini kabisa,hicho ndicho kilichotokea.Alivyofika chini akatembea mbiombio kwa hatua tatutatu mpaka nje ya hotel ya peacock,akazama ndani ya gari na kulirudisha nyuma,alivyokaa sawa akaweka gia na safari ikaanza mara moja.
Ndani ya kichwa chake kulikuwa na foleni ya mawazo,aliwaza vitu viwili Leila na mke wake.Lakini kwa wakati huo Mke wake ndiyo alikuwa akimfikiria sana,alihisi kujuta,vitimbwi na vituko alivyokuwa anamfanyia vilianza kupita ndani ya kichwa chake na kugundua kwamba siku zote shetani yupo,kifupi alijiona ni mkosaji mbali na hapo hakuelewa atamjibu nini mke wake endapo atamuuliza alilala wapi usiku wa jana.
Siku zote ni hatari sana kuendesha chombo cha moto ukiwa na mawazo hilo alilijuwa hata yeye,mawazo yake hayakuwa barabarani kabisa yalikuwa mbali mno,mkono mmoja akiwa ameshika shavu yaani tama na mmoja usukani,yupo Karume karibia na mataa, anazidi kukanyaga mafuta.
Hata taa nyekundu ilivyowaka kumaanisha magari yanayotoka mjini yasimame yeye hakuona kutokana na msongo wa mawazo.
“Pipiiiiiiiiii”
Honi ndiyo iliyomshtua,gari aina ya Discover iliyokuwa inatokea kigogo ilipiga honi,ikitokea usawa wake ikiwa katika mwendo wa kasi linakuja usawa wake ili kumgonga.Kwa hali ambayo hakuitegemea Deo akakanyaga mafuta mengi,akakosa uelekeo kutokana na hofu gari ikamshinda ikahama barabara,ikaingia pembeni na kuanza kuwasomba wakina mama waliokuwa kandokando wanauza ndizi na maparachichi,gari likagota kwenye nguzo ya umeme na kutulia.
Kila kilichokuwa kinatokea wakazi wa eneo hilo walishuhudia na walijawa na hasira kupita kiasi,wamachinga wakaacha shughuli wanazofanya wakalizunguka gari la Deo.
“Huyu bwege ashuke humu la sivyo tunachoma hili gari moto”
“Hawa wenye magari siku zote wanajiona wapo sahihi sana,leo tutamuonesha,Shuka brooo”
Badala ya watu kutoa msaada wa kwanza kwa majeruhi walilivaa gari la Deo,watu wakazidi kukusanyika.Wanawake watatu walikuwa chini wanavuja damu wameumia vibaya sana.Tangu miaka kumi awahi kuendesha gari hakuwahi kusababisha ajali,hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza.Kama kungekuwa na kipimo cha kupima mapigo ya moyo basi yangeonesha moyo wake unadunda mara sabini kwa Sekunde,Deo alitandwa na hofu alitamani kushuka lakini alihofia uhai wake,wahuni walikuwa wamezunguka gari lake,wanalipiga piga kwa hasira.Kutokana na ajali nyingi kutokea eneo hilo la Karume liliwafanya wawe na hasira kupita kiasi.
“Oyaaa Dulla eeeeeh, kalete petroli pale sheli”
Teja mmoja aliropoka,haraka jambo hilo lilifanyika watu walizidi kukusanyika ukatokea msongamano mkubwa wa magari.
Hiyo ilifanya kila mtu atake kujuwa ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea.
Swala lililobaki lilikuwa ni kulimwagia gari la Deo mafuta ya Petroli kisha walichome moto wakiamini kwamba hilo lingekuwa fundisho kwa madereva wengine waliokuwa wazembe kama yeye,kitendo hicho ndicho kilikuwa kinaenda kufanyika.
Baada ya dumu la petrol kusogezwa eneo la tukio,haraka mafuta yakaanza kumiminwa juu ya gari.Hakuna hata mtu mmoja aliyemuonea huruma.
Deo hakuamini kama hiyo ndiyo ilikuwa siku yake ya mwisho imefika,tena akienda kufa kifo kibaya cha kuchomwa na moto kisha baadaye ageuke majivu,machozi yalianza kumlenga.Alizidi kuwatizama watu waliokuwa nje wana hasira naye,hakuamini kwamba kuna binadamu wana roho mbaya kiasi hicho.
“Leta kiberiti,huyu msimshushe mwacheni humuhumu ndani ya gari si hataki kushuka”
Alizidi kusikia sauti,akaamini kweli.Anaenda kuchomwa moto.Picha ya mke wake Marietha ilianza kujitokeza kichwani kwake,matukio mbalimbali yalianza kupita ndani ya ubongo wake akakumbuka matukio mengi yaliyopita nyuma,akafumba macho ili kusubiri kifo.

***
Ndoa yake ilibadilika ghafla na kuwa shubiri,Deo alimnyanyasa na kumtesa kila siku bila ya kuwa na sababu ya msingi ingawa alijuwa kwamba ni sababu alikuwa anahitaji kumzalia mtoto,hilo ndilo aliamini kwamba lilimbadili Deo akili yake.Mwanaume huyo alibadilika kwa kiasi cha kutosha,Marietha alikuwa ni mwanamke msiri pengine kuliko mwanamke yoyote,siri zake za ndani yakuweza kuzitoa nje hata siku moja.Ingawa marafiki zake walihadithiana jinsi gani wanaume zao walivyokuwa na vituko lakini yeye hakuthubutu kufungua kinywa chake na kusema chochote kinachoendelea badala yake muda wote alikuwa akiweka tabasamu kumbe alikuwa anaumia ndani kwa ndani.
Rafiki yake mkubwa alikuwa anaitwa Prisca Mwakyembe.Ingawa mara nyingi walikuwa wakipishana maneno lakini ndiye huyo aliyemuamini kuliko marafiki zake wote mbali na hapo ndiye aliyemshauri awe na Deo kimapenzi, aachane na Issa.
“Oh Marietha karibu Shosti”
Prisca Mwakyembe alifungua mlango na kutabasamu baada ya kumuona Marietha mlangoni kwake.
“Wapi tena Prisca mbona kama upo haihai?”
Marietha aliongea baada ya kukaribishwa ndani,ni kweli Prisca alionekana kama mtu aliyetaka kutoka sababu alikuwa amevaa nguo za kitenge na kilemba juu.
“Yaani ungechelewa kidogo usingenikuta”
“Safari ya wapi?Alafu hiyo ni wax nimependa sana rangi yake”
“Hii nimetumiwa kama zawadi na wifi yangu kutoka Nigeria”
“Wacha wee”
“Shosti kuna wine hapa kabla sijasahau”
“Hapana usijali nipe tu maji ya kunywa”
“Umekuja na dereva au?”
“Ah mwenyewe”
“Ah,sio kweli”
Prisca akatembea mpaka dirishani na kuvuta pazia ili kuhakikisha kama ni kweli ndani ya gari hakuna mtu,akamgeukia Marietha.
“Siku hizi unajuwa ku drive?”
“Hivi sijawahi kuja na gari hapa kwako?”
“Hapana,mara ya mwisho ulikuja na Deo”
“Kweli,ni kitambo kidogo”
Marietha akajibu akiwa mwenye sura ya uzuni,kuna kitu Prisca alikigundua lakini hakutaka kuhoji kwanza.Akatembea mpaka jikoni na alivyorudi alikuwa ameshika jagi na glasi,akamimina maji ya kunywa kisha kukaa pembeni ya rafiki yake kipenzi, Marietha.
“Vipi Deo mzima?”
Ingawa Marietha alisikia lakini alikaa kimya akahisi kiu yake imekatika hapohapo,jina la Deo lilimkumbusha vitu vingi sana.
“Marietha,kuna tatizo gani?”
Hapo ndipo mwanamke huyo alishindwa kuyazuia machozi yake,akaanza kuvuta kamasi kwa ndani na kulia kwa kwikwi,hiyo ndiyo ikamfanya Prisca azidi kuhoji zaidi sababu alitaka kujuwa nini kinachomliza rafiki yake.
“Marietha”
“A…be..ee”
Akaitikia huku kwikwi ikiwa imemshika.
“Mbona unalia?”
“De..o,Deoooo”
“Kafanya nini?”
“Ameba..dili.ka sana..Ananitu.kana kila si..ku”
Maneno ya Marietha yalikuwa yakushangaza, haikuwezekana hata kidogo kwa Prisca kuamini kwamba Deo amebadilika,alimchukulia ni mwanaume mstaarabu na mwenye heshima zake.
“Marietha umemfanya nini Deo?”
Ilikuwa ni lazima Marietha alifanya kosa hivyo ndivyo Prisca alivyoamini.
“Marietha,usilie basi niambie ili nikusaidie”
“Deoo,kawa mtu wa kulewa pombe na kunituk..na mimi kila siku.Ananitukana ka..ma mbwa,hapana Prisca mimi siwezi ku…ishi naye te..na”
Marietha aliendelea kumwaga machozi,kazi ya Prisca ilikuwa ni kumbembeleza lakini hakufanikiwa kwani aliendelea kulia tu.
Baada ya kulia na kumwaga machozi akiwa begani kwa Prisca aliamua kueleza kila kitu,hakuficha jambo lolote lile.Kila baya alilofanyiwa na Deo aliliweka wazi sababu alihitaji ushauri ingawa swala la kutopata mtoto hakutaka kuliweka bayana sababu hakuwa ana uhakika kama yeye ni mgumba ama la,baada ya kumaliza kila kitu alihitimisha kwamba anahitaji ushauri juu ya kitu gani akifanye.
“Hukumfanya kitu chochote Deo?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Prisca akitaka kujuwa chanzo,bado alikuwa upande wa Deo sababu alijuwa kivyovyote ni lazima Marietha atakuwa amemkasirisha.
Alitaka kuuliza habari za Issa lakini aliupiga moyo wake ‘stop’kwanza kwa wakati huo.
“Sikumfanya kitu chochote”
“Na huyo mwanamke uliyesema rafiki yake vipi?”
“Huyo hausiani na ugomvi wetu Prisca,huyo ni rafiki yake tu”
“Wewe una uhakika?isije ikawa anakufanyia changa la macho”
“Haiwezekani,mimi ningejuwa”
“Basi wewe ndiyo utakuwa mkorofi”
“Hapana”
“Au itakuwa umerudiana na Issa nini?”
Prisca hakutaka kunyoosha jambo hilo moja kwa moja,akalizungusha likawa swali.
“Hapana,Issa sijaonana naye.Nimeamua kutulia na Deo sababu ninampenda kweli sasa hivi”
“Mh,basi makubwa”
Marietha alilalamika mengi kuhusu Deo wakati mwingine alidai kwamba anajuta kuingia kwenye ndoa.
“Usijute,wewe kaa naye chini.Vumilia tu.Hujakutana na vimbwenga vya ndoa,hiyo yako mbona cha mtoto.Bora hata Deo yeye analewa lakini anajielewa,kuna wanaume wengine hawalali ndani kabisaa mabazazi,tena shukuru hata Deo kakununulia usafiri wako,anaacha pesa ndani”
“Prisca hivyo havina maana kama hakuna mapenzi”
Waliongea vitu vingi sana siku hiyo,kifupi walimuwekea Deo kikao sababu walimzungumzia yeye wakati wote.
Ilivyofika saa kumi na mbili jioni Marietha aliaga na kuondoka zake,alijuwa kuendesha gari na alikuwa makini sana barabarani.

*****
Alifika kwake na kuweka gari vizuri kwenye maegesho kisha kuingia ndani.
Ambapo alinyoosha mpaka bafuni na kujimwagia maji.Akatoka na kuelekea jikoni kupika chakula cha usiku,kilivyoiva akaepua akaweka kila kitu sawa.Akapita seblen na kujitupa juu ya sofa.Usiku huo alikuwa akiwaza vitu vingi sana hususani ndoa yake,hakuelewa atazikabili vipi changamoto hizo.Muda ulizidi kwenda mpaka inafika saa saba ya usiku hakukuwa na dalili yoyote ile ya Mumewe kutokeza,akaendelea kujipa moyo kwamba atarudi lakini wapi.
Ghafla akaanza kuhisi kichomi tumboni,kwa mara ya kwanza alipuuzia lakini kadri dakika zilivyozidi kwenda mbele ndipo Kichomi kilizidi kumkata,akahisi kama kuna viwembe ndani ya tumbo lake vinamchana.Akazidi kujikunja na kuanza kupiga kelele.
“Bikoo,Bikooo”
Hakuwa na msaada mwingine zaidi ya kuita jina la mlinzi sababu walikuwa wawili tu ingawa hakuelewa kama sauti yake ilifika nje kutokana na vioo vya dirisha kufungwa.
“Bikooooo”
Biko alisikia sauti kwa mbali akiwa getini juu ya kiti chake anasikiliza redio aliyoishika mkononi,akapunguza sauti ili kusikia kama ni kweli anaitwa yeye ama alisikia vibaya.
Alivyotega sikio vizuri,akasimama wima na kuanza kutembea taratibu mpaka mlangoni,ambapo aligundua kwamba Marietha ndiye anamuita,akafungua mlango na kumkuta yupo chini ana galagala.
“Bosi,Bosiiii,Bosiiii”
“Nipelekee hospitaliii.Bikoo nakufa”
Mlinzi hakuelewa afanye kitu gani,alikuwa mara atoke nje mara arudi.
Hakujua ni uamuzi gani wa haraka auchukuwe,kama angekuwa ana uwezo wa kuendesha gari basi angetoa msaada wa kumpeleka hospitali sababu nje kulikuwa kuna magari matano yamepaki.
Mlinzi akakimbia haraka na kutoka nje ya geti,huko alitembea mpaka kwa majirani na kuomba msaada.
“Kuna nini?”
Mzee mmoja alitoka ndani kwake akiwa ameshika panga mkononi,amevaa kipensi kitambi kipo nje,jinsi Biko alivyokuwa akipiga kelele alidhani kwamba kuna wezi ndiyo maana akatoka na silaha.
“Kuna mgonjwa,tafadhali naomba msaada”
“Wewe kijana embu tulia kwanza,kuna nini?unaomba msaada gani?”
Biko akashusha pumzi,akaanza kuelezea harakaharaka.Hapo ndipo mzee huyu aliyetambulika kwa jina la Mzee Korosho alirudi ndani na kuvaa shati.
Akatoka mbiombio akifuatana na mlinzi mpaka ndani ambapo walimkuta Marietha yupo chini anagalagala,ameshika tumbo.
Wakambeba na kumtoa nje.
“Funguo za gari ziko wapi?”
“Ch…umbani”Marietha akajibu kwa tabu.
Biko akaenda chumbani harakaharaka na kubeba funguo,safari ya kwenda hospitali ikaanza mara moja.

Usiku huohuo Mzee Korosho alikimbiza gari mpaka Kinondoni hospitali ili kuokoa maisha ya Marietha.Baada ya daktari kumpima alishtuka mno.
“Wewe ndio mume wake?”
Dokta alimuuliza mzee Korosho.
“Hapana”
“Mume wake yuko wapi?”
“Huyu ni jirani yangu tu,Wewe kijana embu njoo”
Biko akasogea karibu,Dokta akaanza kumuhoji maswali.
“Bosi bado hajarudi,ndiyo mme wake”
“Nahitaji kuongea naye,una namba zake?”
“Hapana labda niende kufuata simu ya Mama,ili uongee naye”
“Sawa,itakuwa vizuri nenda basi”
“Lakini sina nauli”
Dokta akaingiza mkono ndani ya koti lake na kutoa noti ya shilingi mia tano,akamkabidhi.
“Wahi nyumbani tupate namba za mume wake”
Nauli ya mtu mzima ilikuwa ni shilingi mia nne,kumaanisha kwamba angeenda tu bila kurudi,ndiyo maana alibaki ameganda.
“Haitoshi au?”
Mzee Korosho akauliza.
“Ndio”
“Leta hiyo mia tano”
Mzee Korosho alivyochukua noti ya shilingi mia tano,akampatia noti nyingine ya elfu moja.
“Aya wahi kijana”
***
Asubuhi ya saa tatu ndipo walipompata Deo baada ya kumtafuta usiku kucha bila simu yake kupokelewa.Alionekana kushtuka baada ya kupewa taarifa za mke wake kuwa ni mjamzito akahaidi kwamba angefika baada ya masaa machache. Masaa yalizidi kusogea mbele bila Deo kutokeza,walivyompigia tena simu iliita bila kupokelewa,mpaka inafika usiku hali ilikuwa hivyohivyo simu ya Deo haikupokelewa na kilichomchanganya Dokta Bin Paul ni kutokupatikana kabisa hewani kwa Deo ilivyofika usiku wa saa tatu.




Msongamano wa Magari ulikuwa mkubwa mno na mrefu ukafika mpaka Kigogo ‘round about’jambo ambalo lililowafanya watumiaji wa magari wakasirike kwa kiasi cha kutosha,abiria wanaotumia usafiri wa madaladala ili kuwahi vibaruani ndiyo kabisa.Mpaka zinapita dakika kumi na tano hakuna gari lolote lililosogea.
“Oyaa Tiko”
Dereva wa daladala lenye mstari wa rangi ya udongo lililokuwa linafanya kazi ya kuwatoa abiria Kigogo Luhanga kuwapeleka Kariakoo ama kinyume na hapo,alimgeukia kondakta wake na kumuita.
“Vipi Jumanne”
“Embu kacheki mbele kuna nini”
“Wewe si utanue hapo tupasue jangwani”
“Asubuhi hii,unataka nipigwe bao”
“Poa poa basi ngoja nikadele”
Kondakta aliyefahamika kwa jina la Tiko alijaribu kufungua mlango kwa tabu sababu ya abiria kuwa wengi ndani ya Coaster,hivyo ilifanya mpaka mlango ushindwe kufunguka vizuri.
“Mzee kanyaga hapo juu,nifungue mlango”
“Sasa nitakanyaga wapi?”
“Wewe kanyaga hapo mzee acha ubishi,wewe dada vuta hapo nyuma tufungue mlango”
“Hivi wewe konda una akili wewe?nitasogea wapi?”
“Kwahiyo humu leo hamtoshuka,yaaani ni bora uongoze mbuzi kuliko binadamu.Abiria sijui mnakuwaje”
Kilichofuata hapo ni Kondakta kutumia nguvu huku akilalamika,akauvuta mlango kwa ndani akitumia nguvu,kulivyopatikana uwazi akapenya na kuanza kukimbia na shati lake lililotoboka kwa nyuma,kila alipozidi kwenda mbele dipo alipozidi kuona msongamano wa watu.Akasogea mpaka karibu kabisa na kuona gari aina ya ALTEZA nyeusi watu wanaipiga piga kwenye vioo.
“Kuna nini hapa?”
Kondakta akauliza.
“Kuna ajali,umeona ile Alteza?”
“Ndiyo”
“Bwana wee,imesomba watu hapa.Inaelekea dereva anayeendesha amelewa,kasomba wakina mama.Alafu sasa hataki kutoka nje”
“Sasa si mngelipeleka hili swala polisi”
“Hakuna cha polisi,wamefuata petrol ili kulichoma gari”
“Kwanini mum-chome sasa,ajali ni kawaida haya ni mambo ya magari”
Kondakta alitoa maneno ya busara ingawa hakuwa msomi,alielewa nini maana ya kuendesha vyombo vya moto barabarani,swala la ajali ni kawaida sana kutokea.Mbali na hapo ilikuwa ni lazima awasambaratishe watu ili foleni itembee.
“Kwani trafiki washafika?”
“Hapana bado”
“Sawa”
Hapohapo Kondakta akasogea kandokando kidogo huku akiwa anachungulia gari lililokuwa limezingirwa na raia wanataka kulichoma moto,kutokana na kazi yake ya ukondakta aliweza kujuana na karibia askari wote mjini,hii ilitokana na kupigwa bao karibia kila siku iendayo kwa Mungu.Haikuwa kazi ngumu kwake kupiga simu kituo cha polisi Karume.Hazikupita hata dakika tano Difenda ya polisi ikafika.
“Kuna nini hapa?tunaomba ustaarabu kabla hatuwachukuwa mmoja mmoja kituo cha polisi”
Ilikuwa ni kauli kutoka kwa Kamishna wa polisi aliyeshuka kutoka ndani ya Difenda, mweusi mrefu futi nyingi kwenda hewani.
“Nasema hivi naomba msambaratike mara moja”
Ilikuwa ni kauli nyingine aliyotoa, safari hii akiwa ameweka mkono kiunoni kaikamata bastola ili kusindikiza mkwara wake,hata yeye mwenyewe alihofia umati wa watu ndiyo maana akajihami.
“Marwa”
Akamuita askari mwenzake.
“Yes”
“Mpigie simu Bilali,aje kupima ajali”
“Sawa”
Kamishna wa polisi aliyefahamika kwa jina la kamanda Mwalusambo,akafika mpaka kwenye Alteza ambayo ilikuwa inanuka mafuta ya Petroli,maana kwamba wangechelewa dakika moja mbele gari hiyo ilikuwa inachomwa moto.Deo alikuwa ndani ya gari analia machozi kama mtoto mdogo sababu alijuwa kifo ndiyo haki yake,alivyoona maaskari wamefika bado hakutaka kutoka.Mpaka alivyopewa ishara kwamba ashuke asiwe na wasiwasi.
“Shuka kijana,shuka”
Deo akatoa loki mlango na kushuka akiwa mwenye hofu,alikuwa mwoga na alionesha wasiwasi.Aliwatizama raia ambao walikuwa wanamtizama kwa usongo.Walitamani kumvaa wampige lakini walihofia,wakina mama waliojeruhiwa walishapakiwa kwenye magari na kupelekwa hospitali.
Deo akaingizwa ndani ya Difenda na safari ya kwenda kituo cha Polisi Karume kuanza mara moja,muda wote alikuwa akilia kama mfiwa ingawa alikuwa mtu mzima akiwa haamini kama amepona, hakuelewa kwamba aliyeyaokoa maisha yake ni kondakta kwa kupiga simu kituo cha polisi,mpaka hapo foleni iliruhusiwa kutembea.
Deo alifikishwa kituo cha polisi na kuambiwa atoe maelezo yake.Baada ya hapo akavulishwa mkanda na kutupwa ndani, rumande.
****
Saa tano ya Usiku ndipo akili yake ilipomkaa sawa akiwa ndani ya nondo,bado aliamini kila kilichotokea ilikuwa ni ndoto ya kutisha, habari iliyomjia kichwani kwake ni mkewe.Akasimama kutoka kwenye moja ya kona ya ukuta,chumba alichofungiwa kilikuwa kichafu,sakafu ilikuwa imechoka na kulikuwa kuna harufu kali ya vinyesi na mikojo.Mbali na hapo hewa ilikuwa finyu kutokana na dirisha moja dogo tena lililokuwa juu kabisa,mbu waliokuwa wanaranda kutafuta damu walikuwa wakubwa mithili ya mende tena walikuwa halali yake.
Kunguni walimsumbua,kutokana na utajiri wa pesa alizokuwa nazo hata siku moja hakuwahi kuota kwamba atakuja kulala eneo kama hilo,akatembea na kuziendea nondo, akazishika.
“Afande”Akaita.
“Afande”
“Vipi?Usiku huu ulale acha kupiga kelele”
“Tafadhali nakuomba mara moja”
“Una shida gani?”
“Naomba uje tuzungumze”
“Sawa”
Afande aliyekuwa zamu usiku aliyefahamika kwa jina la Abdallah Mbuya,akatoka mapokezi na kusogea mpaka kwenye nondo ili kumsikiliza mtuhumiwa Deo.
“Sema shida yako”
Walikuwa wametenganishwa na nondo.
“Mimi naitwa Deo Karekezi,nimeletwa mchana hapaa..”
“Najuwa uligonga kwa ulevi wako,ulikuwa unatakaje?”
“Naomba nipige simu mara moja kwa mke wangu ni mjamzito,nakutajia namba.Yupo hospitali”
“Kesho asubuhi sasa hivi lala humo”
“Basi naomba nizungumze na RPC Wilson Kamuhanda,mwambie nipo hapa kituoni Karume”
Moyo wa afande Abdallah Mbuya ukapiga kwa nguvu,akamtizama Deo mara mbilimbili bila kum-maliza sababu alimtaja mtu mkubwa sana mwenye cheo cha juu kutoka jeshi la polisi.
“Unamfahamu wewe?”
“Mpigie mwambie Mpwa wake Deo Karekezi nipo hapa,atajuwa cha kufanya”
Deo Karekezi hakuwa ana tania hata kidogo ingawa hakuwa ana undugu wowote na RPC Wilson Kamuhanda lakini alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana.Na endapo biashara zake zikikwama kidogo alikuwa akimtafuta askari huyo hata hivyo alikuwa akimsaidia katika vitu mbalimbali.
“Nitajie namba za mkeo,nimpigie”
Afande akabadili mawazo.
“0622 862176 Mwambie kila kitu ili umtoe wasiwasi”
“Okay”
Afande akaenda mpaka mapokezi akapiga simu,ilivyopokelewa alijieleza kila kitu kinagaubaga mpaka Deo akawepo kituo cha polisi.

****
Kituo cha polisi Karume siku iliyofuata asubuhi ya saa moja kilijaa watu chungumzima,wafanyabiashara walikuwa wengi kama utitiri,walitaka kumuona rafiki yao Deo Karekezi.Magari yalifurika kuliko kawaida, siku hiyo ilikuwa kama kuna sherehe kumbe walitaka kumtoa rafiki yao rumande.Deo alikuwa kipenzi cha watu.Alijuwa kuishi na wenzake vizuri,ndiyo maana walivyosikia taarifa kutoka kwa Marietha kwamba yupo kituo cha polisi Karume hawakutaka kwenda kwenye biashara zao bila ya Deo kuwa huru siku hiyo.
“Yesu na Mariaa,yaani mimi nakwambia nahitaji kuonana na Deo wewe unareta Mambo ya Kijinga,kiruu wewe chaaa.Aise Meku nadhani huyu hajui mimi ni nani kule Mwika,Kishingoni”
Sauti hiyo ilitoka kwa Mzee wa kichaga aliyeitwa Mushi,akikoromeana na askari.
“Wewe mzee hebu kaa kando kidogo,niache kwanza ninywe chai”
Kilichowafanya askari wagongane vikumbo na kuongea kwa adabu zote ni baada ya mtoto wa mfanyabiashara mkubwa aliyefahamika ndani na nje ya nchi Salim Ali Bakhresa.Walijuwa nini maana yake,kumjibu kiburi kulimaanisha vibarua vyao vingeota nyasi siku hiyohiyo ingawa alikuwa ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka kati ya 25-29 lakini alipewa heshima kubwa sana mjini kutokana na umaarufu na pesa za baba yake, huyu pia alikuwa rafiki wa karibu wa Deo.Alifika kwa mbwembwe zote na dharau juu.
“Naomba Deo Karekezi awe huru mara moja,hiyo kesi mimi nitagharamia.Namuwekea mimi dhamana”
Haikuwa ombi bali ni amri,mtoto huyu alikuwa ana nyodo sio kawaida.Haikuchukuwa hata dakika tano,nondo zikafunguliwa Deo akatoka,akawa huru.Umati wa marafiki zake ulimshtua,hata hivyo alifarijika sana kuwaona marafiki zake wamefika kumkomboa.
****
“Leila,nimekwambia hivi.Kama tulifanya hayo mambo tafadhali naomba usahau.Sasa hivi mke wangu ni mjamzito,naomba upunguze mazoea namimi”
“Lakini Deo,mbona unakuwa hivyo?”
“Nakuwaje?Nishasema maana hunielewi,bora nitumie ukali wenda itasaidia.Utanipigiaje simu usiku wa manane mimi ni mme wa mtu,mke wangu mpaka ananishuku na isitoshe ni mjamzito anahitaji ukaribu wangu zaidi”
“Deo,fine it’s okay.Hutoona tena nakupigia simu”
“Thank you,maisha mema”
Siku hiyo asubuhi Deo alikuwa anaongea kwa sauti ya juu akiwa simuni na Leila nyuma ya meza kubwa ofisini kwake,amevaa suti nyeusi kanyonga tai kohoni.
Tabia za Leila zilimfika shingoni,aliamini kwamba akimuendekeza ipo siku atamshika hata kalio mbele za watu,ndiyo maana siku hiyo asubuhi na mapema akamtolea uvivu,akampa makavu yake bila kukwepesha.

Alikuwa ni mwanaume mwenye furaha pengine kuliko yoyote yule duniani,mke wake kushika ujauzito kwake lilikuwa ni kama miujiza.Alitamani miezi tisa isogee harakaharaka ili mke wake ajifungue apate kumuona mtoto wake.Na siku zote tangu mkewe ashike mimba hakuwahi kuchelewa kufika nyumbani kwake tena akiwa na zawadi tofauti tofauti mikononi mwake,ndoa ilirudi ikawa ya furaha mara mia yake,yote yaliyopita yakabaki kama historia.
“Nakupenda Marietha Mke wangu”
Siku hiyo Deo alisema usiku akimwambia mkewe wakiwa kitandani,Mimba ya Marietha ilikuwa tayari kubwa ya miezi sita.
“Hata mimi”
“Fungua mfuko huu”
Marietha akachukuwa mfuko mkubwa kutoka kwa mumewe na kuangalia ndani,alikuta nguo na mikufu ya dhahabu.
Maisha ya Marietha yalijawa furaha mno.

***
“Shosti”
“Nambie shoga angu”
“Kuna ubuyu nataka nikupe,tena siyo ubuyu ni dili la pesa ndefu”
“Embu kaa kwanza maana upo juu juu kama kitu gani sijui”
“Kuna mtu anatafuta fundi”
“Fundiii?Fundi wa aina gani?”
“Nawewe hujanielewa bwana,kuna mtu anatafuta Mganga wa kienyeji.Ana pesa balaa”
“Sasa wewe ukamwambia nini?”
“Nikamwambia nipe muda,ndiyo nikakufuata wewe”
“Hilo ondoa shaka,mwambie kapata.Ana shilingi ngapi?”
“Kaniambia ana dola mia saba”
“Dolla?”
“Ndio,dolla za kimarekani”
“Hizo ni sawa na shilingi ngapi?”
“Mimi sijui”
“Embu ngoja”
Ndani ya nyumba ndogo ya kupanga wakina mama wawili walikuwa wakiteta.Mmoja akasimama na kufungua mlango akatoka mpaka nje,kwa hatua tatu tatu mpaka kwenye saluni ya kiume.
“Wewe sharobaro”
“Inakuwaje Mama Musa”
“Poa tu,najuwa wewe mjanja mjanja wa town.Dola mia saba ni sawa na shilingi ngapi?”
Kinyozi aliyekuwa kapigilia kofia kichwani akaacha shughuli yake ,akamtizama Mama Musa kwa kitambo kidogo.
“Sasa hivi,reti ni shilingi elfu mbili au buku jero nandani”
“Embu niambie ni shilingi ngapi bwana,reti ndiyo nini wewe?”
“Kwa harakaharaka hapo sio chini ya milioni moja,si umesema dola mia saba?”
“Ndio,Mungu wangu! sio chini ya milioni?”
“Ndio”
“Sawa Ahsante”
Mama Musa akarudi mpaka nyumbani kwake na kutoa jibu kamili kwa rafiki yake.
“Sasa mganga yupo,nina mganga wangu huyo yupo huko Chanika,Dondwe ni kiboko ana uwezo hata wa kuhamisha milima.Hashindwi kitu.Yaani huyo ashindwi kitu kabisaaaaaa,wewe tu”
“Sawa ngoja basi nimpigie huyo dada simu”
****
Leila alikuwa mbele ya kioo anatizama tumbo lake lililoanza kuwa kubwa kiasi,kifupi ni kwamba alikuwa ana mimba, tena ya Deo Karekezi.Kitendo cha kujibiwa vibaya kilimfanya achukie ajabu,kazi yake ilikuwa ni kutafuta watu wanaojuwa waganga wa kienyeji ili amfunze adabu kwanza Marietha kisha baada ya hapo Deo afuate.
“Lazima Marietha aonje joto la jiwe,ile mimba kama hatozaa kunguru labda mimi sio Leila”
Aliapia.


Hata siku moja hakudhani kwamba mapenzi yangempeleka puta kiasi hicho,alishindwa kuyatafakari mapenzi ni kitu cha aina gani mpaka akawaza kutumia waganga wa kienyeji, wakati mwingine upande wa nafsi yake ulimwambia kwamba asifanye vitu hivyo kwani vitamtokea puani ama vina mwisho wake kwani mapenzi hayalazimishwi.Akakumbuka ule msemo unaosema penda unapopendwa,asiyekupenda achana naye.Mbali na kukumbuka vitu vyote hivyo hakutaka kurudisha moyo wake nyuma, akapiga moyo konde.Hakuna siku ambayo alikuwa mwenye furaha kama siku hiyo saa saba ya mchana baada ya kupokea simu kwamba Mganga amepatikana.
“Kwahiyo tutaonana wapi ili twende?”
Leila aliuliza simuni huku akiwa mwenye tabasamu pana.
“Wewe sema,hata ukisema nije hapo ulipo sawa”
“Hakuna shaka,tafuta taxi uje”
“Sawa lakini nipo na mwenzangu”
“Mwenzako?Kivipi?”
“Ni huyu rafiki yangu ndiyo anajuwa pa kumpata fundi mzuri aifanye kazi yako”
“Okay,njoeni Landmark Hotel”
“Sawa,sasa tunakuja.Umesema tupande Taxi?”
“Ndiyo”
“Hatuna pesa ya taxi”
“Mimi nitalipa”
“Ahsante”
Simu ilivyokatwa ilimuacha Leila akishusha pumzi ndefu ya kuchoka,akajitupa kitandani na kuingia ndani ya mawazo mengi sana.
Alichowaza siku hiyo kitu cha kwanza ni kuisambaratisha ndoa ya Deo na Marietha na baada ya hapo mambo mengine yangefuata,alihisi kumpenda Deo kutoka moyoni na njia ya kutumia ndumba alihisi ndiyo ingefanya kazi,sababu alitumia jitihada zote zikagonga mwamba kabisa.

****
Hakuamini kwamba Deo angebadilika na kurudi akawa mtu mwema sababu alikuwa amekata tamaa tayari ya ndoa,aliamini kwamba Mimba aliyokuwa nayo ndiyo ilifanya kila kitu kinyooke.Deo alionesha mapendo kwa mkewe tena akaongeza mara mia moja yake na wakati mwingine hakuenda kazini alibaki nyumbani akishinda na Marietha,sababu aliamini kwamba mwanamke wake anahitaji ukaribu wake kuliko mtu mwingine yoyote yule.
“Dokta amekwambiaje leo?”
“Mtoto ameanza kujigeuza tayari”
“Kweli?”
“Ndiyo baby”
“Leo nataka niingie jikoni nikupikie”
“Mh! Mh! Mh! Mh! Mh!,tangu lini Deo wewe ukapika mpenzi wangu?Unataka tule chakula kibichi leo”
“Subiri uone,wewe tulia hapo weka mguu juu”
Ulikuwa ni mchana wa saa saba,Deo siku hiyo hakuenda popote alitaka kubaki na mkewe siku nzima ampe ukaribu wake.Akaingia jikoni na kuanza kukarabati mambo ya chini ya pua yaani msosi.Akachukuwa sufuria akaweka kwenye jiko la gesi na kuliwasha,akaweka mafuta akakata vitunguu, mafuta yalivyochemka, akaweka vitunguu ili viwe tayari kisha abandike nyama.
Kupika siku hiyo kulimkumbusha maisha ya chuo alivyokuwa nchini Uingereza,huko alikuwa akijipikia mwenyewe ingawa hakuwahi kupika hata siku moja tangu arudi Tanzania.Nyama ilivyochemka akaweka nyanya.
“Bebiiiiiii”
Deo akaita.
“Abeee”
“Royco iko wapi?”
“Hapo juu ya kabati la juu”
Deo alivyosikia hivyo akachukuwa na kuiweka karibu ili kusubiri nyanya ziyayuke.Baada ya dakika moja jikoni kukaanza kunukia,Marietha akatia neno.
“Nasikia huko jikoni,kunavyonukia”
“Leo kamanda nipo mzigoni,acha kuongea utanifanya niunguze baby”
“Hee!yashakuwa hayo.Aya ngoja ninyamaze”
Baada ya kama dakika arobaini na moja kila kitu kilikuwa mezani,Marietha alivyoweka kijiko cha kwanza mdomoni alitingisha kichwa.Chakula kilikuwa kitamu sio mchezo,mwenyewe akakubali.
“Darling,sitaki kuamini kama wewe ndiyo umepika hivi”
“Kula chakula cha mwanaume hiko,wewe unadhani nani kapika?”
“Kumbe unajuwa kupika,tutakuwa tunawekeana zamu”
“Ha! Haa!Haa!Haaa!Haaaa!”
Nayeye akajinadia kidogo na kucheka.
Baada ya kula walishushia na juisi nzito ya machungwa na kuingia chumbani ambapo huko waliongelea swala zima la kumpa jina mtoto na jinsi maisha yao yatakavyokuwa baada ya miezi tisa kuwadia.
“Yaani hapa nishaanza kusave kwa ajili ya mtoto,nishamfungulia akaunti yake tayari.Ina shilingi laki saba”
“Ni vizuri baby”
“Nataka akizaliwa ada iwe kabisa kwenye akaunti yake kuanzia nursery mpaka standard seven”
“Nafurahi kupata mume bora kama wewe”
“Namimi najivunia kuwa na mke mwema kama wewe”
“Aal….”
Marietha hakumalizia anachotaka kuongea,Deo akamrukia midomoni,wakaanza kubadilishana mate,wakanyonyana ndimi na kuwekana sawa ili kupasha.Kutokana na Marietha kuvaa Dera peke yake bila kuwa na kitu chochote ndani hiyo ilimpa Deo urahisi akalichomoa,Marietha akabaki mtupu kabisa.Deo akatoa fulana yake harakaharaka na kuptula aliyovaa pamoja na boxa,akabaki kama alivyozaliwa,mashine yake ilikuwa tayari imesimama dede.
Akaanza kumpapasa mke wake kuanzia kwenye masikio akashuka shingoni mpaka kifuani,akateremka chini akitumia vidole,akaanza kukipapasa kitovu cha mkewe bila papala yoyote ile,akazidi kushuka mpaka chini.Akitumia ufundi wa kidole cha katikati akaingiza kwenye mgodi ili kukagua ni aina gani ya madini yanapatikana ndani ya mgodi,kwa heshima na taadhima akasogeza ulimi wake mpaka kwenye chuchu za Marietha na kuanza kulamba kama paka anayelamba maziwa juu ya kisosi,hapo ndipo Mwanamke huyu alipohisi kufakufa.
Akaona kama moyo wake unaacha mwili,akahisi ameota mbawa yupo angani anaviona vitu vyote kwa chini,kazi yake ilikuwa ni kukunja kunja mashuka,Deo alivyohisi mgodi wa mkewe unaanza kulowana na kuanza kutoa madini ya rubi kwa mbali,akashika Mjegeja wake akamlaza vizuri mkewe chali.Siku hiyo ilibidi watumie staili hiyo ya chali sababu ya tumbo la Marietha kuwa kubwa kiasi na Deo alitaka kufanya tendo hilo la ndoa,moja kumridhisha mke wake lakini mbili alitaka kupanua njia ili siku ya kujifungua mkewe asije kupata shida ya maumivu mengi.

****
Safari ilikuwa ni ndefu mno ilichukuwa zaidi ya dakika hamsini nzima lakini bado hawakufika,Leila akashindwa kuelewa ni wapi anapelekwa.Uvumilivu ukamshinda ikabidi aulize.
“Mbona hatufiki?”
“Karibia tunafika,hapa ni kwa sadala.Bado vituo vichache tu”
“Kweli lakini?”
Leila akauliza tena,bado hakuliamini jibu la Mwantumu anayempeleka kwa mganga wa Kienyeji,huko Chanika,Dondwe.
Taxi waliyokodi ilibeba watu watatu,Mama Mussa,Mwantumu na Leila kujumuisha na dereva wakawa watu wanne.Leila aliwaza vitu vingi sana ndani ya kichwa chake.Alitamani kufika mapema ili aonane na mganga amueleze vitu vingi alivyokuwa navyo ndani ya mtima wake,ilikuwa yapata saa tisa ya alasiri ndipo walipofika njia panda ya Chanika,dereva akakunja kona na kuzidi kusonga mbele.

Mazingira ya Chanika yalimshangaza sana Leila,kilikuwa ni kama kijiji na asilimia nyingi walikuwa wazee tena waliovalia kanzu ama misuli,kilikuwa ni kijiji kilichojaa wazaramo.
Gari ikazidi kupanda milima na kushusha,hatimaye wakafika kituo cha Dondwe,dereva akakata kulia,akaacha barabara ya lami akaingia kwenye vumbi.Njia nzima ilijaa miti ya minazi na muharubaini.Wakazidi kuingia ndani zaidi.
“Dereva umepitiliza,sio huku.Rudi nyuma ni ile kona ya kule”
Mama Mussa alitoa maelekezo baada ya kuona wamepitiliza.Dereva akatii amri ya mteja wake,akaweka gia na kurudisha gari kinyumenyume,akaweka gari sawa na kuingia uchochoro mwingine aliolekezwa.Wakazidi kusonga mbele zaidi.
Gari likaanza kupunguza mwendo kisha likasimama,dereva akashindwa kuendelea mbele zaidi,barabara ilikuwa mbovu aliogopa kuingiza gari lake kwenye mawe.
“Hiyo njia siwezi kupita sista,kama kuna njia nyingine niambie.Lakini hapa siwezi,labda mshuke mtembee”
“Hapana hapana hapana kwakweli,bado ni mbali”Mama Musa akatoa jibu.
“Hakuna njia nyingine?”
“Labda turudi barabarani,tuzunguke kule Kivumbini”
“Mbali kote huko?”
“Ndiyo”
“Mtaongeza pesa la sivyo mshuke hapahapa mnipe pesa yangu”
Dereva akaongea kwa ukali kidogo.Mama Musa akamgeukia Leila.
“Nitalipa,usijali ili mradi tufike”
Kauli ya Leila ikamfanya Dereva arudi tena nyuma na kuanza safari ya kurudi barabarani,iliwachukuwa muda kidogo mpaka kuifikia lami tena.
Dereva akazidi kusonga mbele na baada ya dakika kama thelathini na tano wakaifikia njia ya kivumbini,dereva akakunja kushoto.Njia hiyo ilikuwa afadhali kidogo kuliko ya mara ya kwanza.Wakazidi kuingia ndani kwa ndani,ambapo tangu mita kumi nyuma hakukuwa na nyumba hata moja zaidi ya miti mikubwa na vichaka.Wakapanda milima na kushusha mabonde.
“Dereva,unaona ule mti mkubwa pale wa Mbuyu?”
“Ndiyo”
“Utasimama pale”
“Poa”
Dereva akatii amri na alivyofika kwenye mti mkubwa wa mbuyu akeweka mguu kati,gari ikasimama.
“Shukeni tufanye haraka,tutembee kwa mguu.Huku magari hayapiti”
“Sasa tutarudi vipi?”
Leila akauliza,sababu tangu watoke barabarani hakukuwa na aina yoyote ile ya usafiri.
“Nina namba ya huyu dereva nitampigia aje kutufuata”
“Hapo sawa”
Leila akaingiza mkono ndani ya pochi na kutoa noti tano za shilingi elfu kumi,akamkabidhi dereva kama ujira wake.Kisha wao wakafuatisha kichochoro kinachoingia katikati ya pori lililokuwa na miti mingi.
“Hope tumefika?”
Lilikuwa ni swali la Leila walivyoanza kutembea lakini Mama Musa hakulijibu,jambo hilo likamfanya Leila aishiwe nguvu.
“Twende shoga bado kidogo”
Wakazidi kutembea wakikatiza njia kwa njia,wakafika sehemu yenye mto wa maji.
“Vueni viatu hapa tuvuke hiki kidimbwi”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa,walivua viatu na kupandisha nguo zao juu, wakakanyaga maji na kuvuka mkondo wa maji,wakatokea upande wa pili.
Leila alihisi kuchoka mno lakini alishindwa kuongea swala hilo sababu alikuwa anashida.Si alikuwa anataka cha uvunguni?basi ilikuwa ni sharti ainame! Safari haikuishia hapo,wakazidi kukatiza katikati ya miti ya michongoma.
“Tumefika shoga angu ni paleeee,kwenye kijumba kinachotoa moshi juu”
Leila akaangalia vizuri na kuona kuna moshi kwa mbele unafuka,walivyokatiza katikati wakatokea kwenye kijumba kidogo cha makuti,juu kina kitambaa chekundu na vitu kama mafuvu ya watu kwa nje na kandokando kuna tunguli.
Moyo wa Leila ukaanza kupiga kwa nguvu akaanza kupata hofu ya waziwazi,hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kufika kwa mganga wa kienyeji.
“Hodiiii,Hodiii”
Mama Mussa alianza kusema bila kuogopa,ilionekana alikuwa mwenyeji.Kabla ya kuitikiwa walisikia kelele za manyanga.Mama Mussa akawa wa kwanza kulivuta shuka na kuingia, akafuata Mwantumu,Leila akasita kuingia ndani.
“Usiogope,ingia ndani.Ondoa shaka”Mama Musa alitoka na kumvuta.
Hatimaye Leila akaingia ndani ya kibanda hicho ambacho kwa ndani kilikuwa na giza kwa mbali,alisikia harufu kali ya madawa ya kienyeji.Hazikupita hata dakika mbili akatokeza babu kizee,mwenye mvi kichwani juu hajavaa kitu na mikononi mwake alikuwa amejifunga irizi nyeusi.Akakaa juu ya kigoda,akamtizama kila mmoja wao lakini alivyofika kwa Leila akagandisha macho yake,Leila kwa hofu akaangalia chini.
“Mjukuu wangu ondoa shaka,Deo ni wako”
Mganga huyu alitamka maneno hayo na kuufanya moyo wa Leila ubamize kifua chake kwa nguvu kwani hakuelewa habari za Deo kazijuwa vipi!


****
“Ndio najuwa mimi nishasema hivyo naomba unielewe”
“Sijakuelewa ndiyo maana nakuuliza”
“Nitumie lugha gani?”
“Sina maana hiyo”
“Sasa una maana gani labda?kuwa na adabu basi nikishasema jambo naomba lifuatishwe mara moja”
“Sawa”
“Gharama zinakuwaje?”
“Hilo swala niachie mimi”
“Sawa Dokta Khaila”
Yalikuwa ni mazungumzo baina ya madaktari wawili wa kihindi wakitumia lugha ya kwao.Ilionekana kama vile walipishana kauli ndiyo maana mmoja wao akapandisha sauti ya juu.
Siku zote Dokta Khaila hakupenda kupingwa katika maamuzi yake,alikuwa ni mwanamke mwenye asili ya kihindi lakini maisha yake alikulia sana nchini Tanzania, umri wake ulikuwa kati ya miaka 30-35 ingawa alionekana bado binti mdogo kutokana na uwezo wa kipesa aliokuwa nao.Mbali na hapo yeye na mume wake ndiyo walikuwa wamiliki wa hospitali hiyo ya Aghakhan.Dokta Khaila aliijuwa sana dini,alimuamini Mungu wake ndiyo maana hata siku moja hakuwahi kupitisha bila ya kufanya ibada na alitoa misaada mbalimbali,Mungu hakuwa na hiyana akawa anamfungulia milango mingine ya mafanikio, yeye na mme wake wakafanikiwa kufungua benki mbalimbali nchini Tanzania na matawi mingine nchi za karibu kama Kenya,Uganda,Tanzania,Burundi na Rwanda.
Majina ya wahindi hawa yalivuma kwa kasi ya upepo wa kimbunga wakazidi kujirimbikizia utajiri mkubwa na kila mwisho wa mwezi walikwenda vituo vya watoto yatima kutoa misaada mbalimbali ya vyakula kama mchele,Unga,sukari na kiasi kingi cha pesa.
Mwaka 1991 wakafanikiwa kufungua sheli za kujazia mafuta wakaziita Big Born.Wakafungua moja Kariakoo ikawa inawaingizia pesa sababu walikuwa na visima vya mafuta pia Uarabuni.Walikuwa ni matajiri lakini hata siku moja hawakuwahi kujikweza, waliishi maisha ya kawaida sana kwa nje.Walikuwa wakitembelea magari ya kawaida kabisa.Dokta Khaila alitembelea gari ndogo aina ya Mazda huku mume wake Dokta Kapoor akitembelea Pajero.
****
Siku zote kitu kilichokuwa kinamchanganya dokta Khaila ni mgonjwa aliyeingizwa siku tatu bila kupatiwa matibabu yoyote yale,alikuwa ni mgonjwa wa kiafrika lakini alijikuta moyo unamuuma mno ndiyo maana aliwafokea madaktari wenzake kama watoto.
“Nimesema huyo mgonjwa atolewe hapa mara moja,afanyiwe matibabu.Mmenielewa?Na kama akifa katika hii hospitali nitawafunga”
Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya Dokta Khaila usiku wa saa saba,alikasirika mpaka ngozi yake ya mwili ikawa nyekundu.Hiyo ilifanya madaktari wagongane vikumbo.Wakaingia chumba alichokuwa amelazwa Issa wakiwa wana haha,kauli ya bosi wao iliwaogopesha kupita kiasi.Wakaburuza kitanda cha Issa na kukitoa nje ambapo kilikuwa kinapita mbele ya macho ya Dokta Khaila.
“Mungu wangu!”
Dokta Khaila aliweka mikono yake kichwani hali ya Issa ilimuogopesha mno.Ndiyo maana akakimbia mpaka ofisini kwake na kuvaa koti, akachukuwa vifaa vingine muhimu na kuingia ndani ya chumba cha operesheni,kabla ya kufanya kitu kingine chochote Issa alichukuliwa vipimo vya X ray mwili mzima.
Majibu yalivyotoka yalionesha kwamba Ubongo wake una matatizo makubwa,mbavu pia hivyo hivyo na baadhi ya mifupa ilikuwa imevunjika ndani kwa ndani.Madaktari hawa wa kihindi waliobobea na kucheza na miili ya binadamu wenzao walianza kazi yao mara moja bila ya kupoteza wakati.
“Nipatie huo mkasi mara moja,na hiyo dawa hapo mezani”
Maongezi yaliendelea ndani ya chumba cha upasuaji, juu ya kitanda ulikuwa umelazwa mwili wa Issa Nurdin Mpelembe haelewi ni mambo gani yanayoendelea ulimwenguni,alikuwa ni kama mtu aliyekufa ingawa mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda.
Kichwa chake kilianza kuchanwa kama nguo,kikafumuliwa chote.Kwa kutumia vifaa maaulum kidude kimoja kilichokuwa kina kamera ndogo kikaingizwa ndani ya ubongo wa Issa kwa uangalifu mkubwa na pembeni kulikuwa na kioo kikubwa kama televisheni ambapo ubongo wa Issa ulionekana juu ya kioo hicho,kifaa maalumu kilichokuwa na kamera kikazidi kuingizwa ndani zaidi.Dokta Khaila alikuwa makini sana macho yake kayatumbua juu ya kioo kinachoonesha ubongo wa kijana huyu Mahututi aliyegongwa na gari, hajitambui.
“Stop.”
Dokta khaila akasema baada ya kuona kitu juu ya kioo.
“Look”(Tizama)
Katika taaaluma ya kucheza na ubongo wa binadamu basi Dokta Khaila alibobea kuliko dokta yoyote yule ndani ya hospitali ya Aghakan.Kuna kitu kama uvimbe kilikuwa kimeonekana,Dokta Khaila akaangalia vizuri kwa umakini huku majasho kwa mbali yakimtiririka sababu ya chumba hiko hakikuwa na hewa yoyote ile inayoingia.Ubongo wa Issa ulivyomalizwa kuchambuliwa,Dokta Khaila mwenyewe akaingia kazini kuukarabati.Ndani ya dakika kumi na tano akafanikiwa.Kichwa cha Issa kikarudishiwa kama kilivyokuwa awali.
***
Matibabu ya Issa Nurdin Mpelembe yaliendelea kila kukicha,yakachukuwa zaidi ya miezi sita hospitalini.Ulivyofika mwezi wa saba tangu afikishwe hospitalini ndipo alipofumbua macho yake.
“Mar…ietha ba.d.o nakupenda kwanini umenisali..ti usifunge ndoa tafadhali…Hilo hilo hiloo gariii”
Ulikuwa ni mchana wa saa tisa alasiri ndipo Issa alipoanza kuongea,ingawa kumbukumbu zake hazikukaa vizuri sababu alijiona yupo kanisani mbele yake amesimama Marietha,baada ya hapo akatoka kanisani akikimbia.Akaona gari kubwa linamgonga vibaya sana.Ndiyo maana akayafumba macho yake,akaanza kulia machozi hakuelewa kwamba alikuwa kitandani zaidi ya miezi mitano akipatiwa matibabu.
“Dokta Dokta”
Muuguzi mmoja wa Kihindi alitoka ndani ya wodi mbio mbio mpaka ofisini kwa Dokta Khaila.
“Yule mgonjwa amefumbua macho”
“Mgonjwa gani?”
“Issa”
“Niniiiii?”
Dokta Khaila hakutaka kuamini ndiyo maana akatoka kitini kwa furaha akauwendea mlango akafungua na kutoka,akatembea harakaharaka kwenye korido huku koti lake jeupe likiwa linapea nywele zake ndefu za singasinga zina tingishika.Akasukuma mlango wa wodi alilolazwa Issa,macho yake yakatuwa kitandani kwake.
“Marie..tha kwanini lakini?Nagongwa nagongwaaa nagongwaa gariiii hiloo”
Hivyo ndivyo Issa alivyokuwa anasema maneno hayo tena akiyarudiarudia.Dokta Khaila akamtizama kwa kitambo.
“Issa”Akaita, lakini hakuitikiwa badala yake Issa alizidi kulitaja jina la Marietha huku akilalamika kwamba anagongwa na gari.
“Something is wrong”(Kuna tatizo hapa)
Dokta Khaila akamgeukia muuguzi akiwa ana sura ya masikitiko makubwa sana.
“What is it Doctor?”(Kuna tatizo gani)
Muuguzi akauliza.
“I need to speak to my husband now”(Nahitaji kuzungumza na mme wangu sasa hivi)
Hicho ndicho kitu kilichotokea Dokta Khaila akatembea kwa hatua mbilimbili mpaka mlangoni,ofisi ya mme wake,ambaye hata yeye pia alikuwa daktari bingwa ndani ya hospitali hiyo ya Aghakhan.Akasukuma mlango bila kubisha hodi.
“Kuna nini?”
Mumewe akamuuliza kwa mshangao.
“Tafadhali njoo uone”
Bila kuuliza kitu kingine chochote Mke na mme wakasimama na kutoka nje ya ofisi ambapo walinyoosha mpaka wodi alilolazwa Issa.
“Mari..etha kwanini lakini,nagongwa nagongwa gari garii gariii”
Hivyo ndivyo Issa aliendelea kusema maneno hayo huku akilia machozi.Dokta Khaila akamtizama Mumewe kwa macho yaliyo jaa huruma,machozi yalikuwa yakimlenga ingawa hakujuwa ni kwanini.
“Ndiyo amezinduka sasa hivi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Mume wake akitumia lugha ya kihindi.
“Ndio,kama dakika kumi zilizopita”
“Mh”
Dokta Kapoor akaguna na kutoa miwani yake machoni,akamsogelea Issa na kumtizama kwa kitambo kidogo.
“Wale ndugu zake wako wapi?”
Dokta Kapoor aliuliza akimaanisha wakina Chogo.
Kutokana na kutokukauka hospitalini hapo ikafanya mpaka wazoeleke,Chogo na wenzake ilikuwa kila siku ya Mungu ni lazima wafike hospitalini kumjulia hali rafiki yao,waliapia kufanya hivyo mpaka dakika ya mwisho ama Mungu atakapotoa maamuzi yake.
“Leo hawajafika lakini watafika.Hawawezi kukosa”
“Sidhani kama atapona huyu mgonjwa”
Dokta Kapoor alihitimisha na kurudisha miwani yake machoni.

****
“Mjukuu wangu usiogope,kunywa hii dawa.Huyo kuku kichwani usimtue”
Leila alikuwa akitetemeka siku ya pili yake baada ya kufika kwa mganga wa kienyeji ndani ya kibanda kidogo kilichokuwa kina fuka moshi.
Chini kulikuwa na bakuli lenye maji.Moyo wa Leila ulikuwa ukipiga kwa nguvu alikuwa mwenye hofu mno,mkono wake mmoja ulikuwa umeshika Kuku mweusi aliyekuwa kichwani mwake na mwingine kibuyu anaambiwa anywe dawa iliyokuwa ndani ina majimaji ya rangi nyekundu,akaweka mdomo wake kwenye kibuyu lakini akakirudisha.
“Mjukuu wangu,sio chungu nataka kuangalia mwili wako kama ni msafi ili nikupe dawa nyingine”
Mganga akasema.Leila akainywa dawa iliyokuwa kwenye kibuyu.Kisha kumkabidhi mganga.
“Chakachaka! Chakacha! Chakacha!”
Mganga akaanza kupiga manyanga huku akiongea maneno anayoyajua yeye mwenyewe kwa kama sekunde kumi na tano.
“Mshushe huyo kuku taratibu”
Moyo wa Leila ukapiga paaa!Kuku alikuwa amekufa tayari,jambo hilo likamfanya achanganyikiwe haikuwezekana hata kidogo swala hilo kuliamini sababu alimuweka kichwani kuku huyo akiwa hai,hapo ndipo aliamini kwamba uchawi upo.
“Mwili wako ni mchafu sana hatuwezi kuendelea na zoezi hili kabla sijausafisha”
Mganga huyu Mzee akatamka maneno hayo kisha akatoka nje,akimuacha Leila akiangalia huku na kule kwa hofu kubwa sana.
****
“Deo Deo tafadhali usiniue.Deoo Nooo nimefanya nini?”
“Simama nikikushika nitakuuwa,simama upesi”
Ulikuwa ni usiku mnene,Deo alikuwa amelewa chakali mkononi ameshika Kisu kirefu anamkimbiza Marietha wakiwa ndani seblen.Kutokana na Mimba kubwa aliyokuwa nayo alishindwa kukimbia vizuri, jasho lilimtoka jingi mwilini,alihofia kifo cha kuchomwa na kisu na mwanaume huyu mlevi aliyetoka kunywa pombe usiku wa manane,akashindwa kuelewa nini kilisababisha mpaka akarudi kwenye tabia yake ya ulevi wa pombe uliopitiliza.
“Simama wewe mbwa”
Deo aliongea kwa hasira macho yake yalikuwa mekundu akasukumiza meza ya kioo ikapasuka vipandevipande,akawa anamsogelea Marietha.Kitu kilichokuwa kinamsaidia Marietha ni sofa kubwa la seblen ambapo alikuwa akilizunguka,Deo akipita huku yeye anaenda kule.
“Lak..ini Deooo”
Marietha alipiga kelele lakini haikusaidia chochote,Deo alizidi kumfuata.Kilichomfanya Marietha apate nguvu mpya ni baada ya kuona mlango wa seblen unafunguliwa.Sura ya mwanamke aliyemuona ilimshtua lakini hakuwa na jinsi ilibidi aanze kumuomba msaada.
“Leila tafadhali,naomba nisaidie Deo anataka kuniua”
“Deooo”
Leila akaita huku akimtizama Deo.
“Leila haya mambooo hayakuhusu,umefuata nini kwanza usiku huu kwanguu? tokaaa”
“Unataka kufanya nini?”
“Tokaaaa”
Leila hakukubali akamfuata Marietha alipo kwa nia ya kumsaidia.
“Usiogope Marietha kaa nyuma yangu”
Leila alisema lakini badala yake alimgeuza akamshika Marietha mikono kwa nyuma.
“Deoo njoo umuuwe,mchome kisu tumboni”
Ilikuwa ni kauli kutoka kwa Leila.
Marietha aliangua kilio kikubwa kwa sauti ya Juu,akazidi kumuona Deo anasogea usawa wake na kisu,akafumba macho huku akizidi kulia kwa sauti.Akiwa amefumba macho anasubiri maumivu ya kisu,alishangaa kuona hakuna kitu chochote.Taratibu alifumbua macho yake,kitu alichokiona mbele yake kiliufanya moyo wake upige kwa nguvu.Alikuwa ni mwanaume aliyemsaliti kwa ajili ya Deo ingawa alimpenda miaka ya nyuma,akiwa amesimama mbele damu zinamvuja mwili mzima.Deo yupo chini kisu kipo tumboni mwake.
“Issaaaa”
****
Marietha alikurupuka kitandani usiku wa saa tisa jasho lilikuwa linamtiririka mwilini,ndoto aliyokuwa anaiota ilikuwa ya kutisha mno.Kitu cha kwanza kukifanya ni kupapasa kandokando juu ya meza ambapo kulikuwa na taa ndogo,akaiwasha.Akapiga jicho upande wake wa kushoto ambapo alizoea kulala Deo,lakini hakumuona.
“Deooo…Deooo”
Marietha aliita kwa hofu tena kwa sauti ya chini usiku wa saa tisa huku mapigo yake ya moyo yakizidi kudunda kwa nguvu,ndoto aliyokuwa anaota bado ilizidi kumpitia kichwani kwake.
Akatembea taratibu mpaka mlangoni,akaufungua.Moyo wake ukapiga paa! Baada ya kumuona Deo ameshika kisu anatembea kuelekea chumbani alipo yeye.



Ghafla majasho yalianza kumtoka usoni,akataka kuufunga mlango kwa ndani lakini Deo alikuwa tayari amefika mlangoni,akausukuma.Almanusura umgonge kichwani sababu Deo aliusukuma kwa nguvu,hilo ndilo lilimfanya aogope zaidi.
“Vipi?”
Deo akauliza akiwa ameshika kisu mkononi.
“U..uli ulikuwa wapi?”
Akauliza kwa hofu.
“Jikoni,nilikuwa nakula machungwa karibu tule,mengine yale pale kwenye kisosi”
Marietha akageuka,ni kweli mezani kulikuwa kuna machungwa juu ya kisosi.
Alishindwa kuelewa yalifikaje sababu alivyokurupuka kutoka ndotoni hakuyaona,hata hivyo alijuwa alikuwa ana mawenge ndiyo maana hakuyaona.Akamtizama mme wake vizuri kuanzia juu mpaka chini.Ndoto mbaya aliyoota muda mchache ilipita tena kichwani kwake,akamtizama Deo tumboni.
“’Marietha,are you okay?”(Marietha upo sawa)Deo akauliza.
“Ndiyo”
“Njoo tule machungwa,leo nina hamu nayo kwelikweli.Nilikuwa jikoni huko natengeneza juisi.Machungwa haya ya Chalinze matamu kweli onja”
Deo alikuwa amekaa kitandani,mkono mmoja ameshika chungwa anampa Marietha aliyekuwa bado ameganda kama barafu,ilionekana bado akili yake haikuwa hapo bali imesafiri maili mia moja ingawa mwili wake ulikuwepo.
“Deo”
“Yes”
“Unanipenda?”
“Ndio mke wangu,kuliko unavyodhani.Vipi kwani?”
“Hapana nimeuliza tu”
Marietha alionekana ana kitu anataka kuhoji lakini alimezea,hakutaka kuendelea kuhoji zaidi, alichofanya ni kupanda kitandani na kuvuta shuka ambapo hata hivyo hakuyafumba macho yake.
Aliogopa,sababu Deo alikuwa ameshika kisu,alivyochanganya na njozi ndiyo ikamfanya aogope zaidi, hata hivyo alijipa moyo kwamba Deo hatoweza kufanya kitu kama hicho ile ilikuwa ni ndoto tu hivyo akajaribu kuifutilia mbali,licha ya kujaribu kuisahau ndoto aliyoota usingizi haukumjia hata kidogo.Na Deo usiku huo kazi yake ilikuwa ni kula machungwa tu,akimaliza hili anamenya lile na yalivyoisha alitoka chumbani na kwenda jikoni kuongeza mengine.
***
Deo alikurupuka kutoka kitandani saa nane mchana kutokana na kuchelewa kulala alipata usingizi asubuhi yaa saa moja,kama angekuwa ni muajiriwa siku hiyo kibarua chake kingeota nyasi lakini alikuwa ni mkurugenzi ama bosi.Deo siku zote alichukia swala la kuajiriwa na tangu alivyokuwa mtoto mdogo alikuwa akipenda sana madaraka ndiyo maana hata alivyoajiriwa kwa takribani miaka mitano baada ya kuhitimu chuo kikuu na kupata pesa akaanzisha kampuni yake binafsi ili mradi tu nayeye awe mkurugenzi sababu katika maisha yake hakupenda kuburuzwa ama kumfanyia mtu kazi.

Na ndiyo maana hata alivyokurupuka mchana alijinyoosha bila kuwa na ‘stress’ zozote zile za kazi.Alivyogeuka pembeni hakumuona mkewe,televisheni kubwa ya LG ilikuwa imewashwa kumaanisha kwamba Marietha alikuwa akitizama kabla.Hakutaka kujiumiza kichwa akatembea mpaka bafuni akatoa haja ndogo na kuvuta taulo ambapo alitoka chumbani,akanyoosha mpaka seblen.
“Marietha”
“Abee”
Marietha akasitisha kuandaa chakula mezani akamtizama mume wake.
“Nataka nitafute msichana wa kazi,ili awe anakusaidia”
“Wanini sasa?Yaani utafute msichana wa kazi?Namimi je?Hilo sijaliafiki hata kidogo”
“Sasa na hiyo hali yako”
“Hali yangu imefanya nini?kwani mimba ni ugonjwa?”
“Hapana lakini inabidi upunguze kufanya kazi”
“Hapana Love usijali”
“Leo umepika nini?”
“Ugali,matembele na nyama”
“Sawa naenda kuoga nakuja sasa hivi”
Deo akaingia chumbani ambapo baada ya dakika tano akarudi wakajumuika na mkewe kula chakula cha mchana,akamshukuru mkewe akarudi chumbani kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye majukumu.

Ilikuwa ni lazima siku hiyo aende ingawa alikuwa amechelewa alijuwa kivyovyote vile alikuwa ana vipolo vingi vya kuvifanyia kazi ofisini kwake.
Siku hiyo alivaa kawaida yaani t shirt na Jeans lakini chini alivaa kiatu aina ya mkuki moyoni,mbele kilichongoka kama mshale.
“Mh!”
Mkewe alivyomuona akaguna.
“Vipi?mbona umeguna?”
“Sijawahi kukuona umevaa hivyo hata mara moja”
“Nimekuwaje kwani?”
“Umekuwa tofauti kabisa”
“Lakini nimependeza?”
“Upo simple lakini smart”
“Ahsante sana”
Deo akatoka nje,akaingia ndani ya gari akageuza na kuondoka zake.
****

Ni kweli alikuwa ni kama ametabiri vile,alivyofika ofisini kwake alikuta makaratasi mengi juu ya meza yake ‘documents’ kama Profoma invoice,Quotation,Tender,L.P.O na kadhalika vilikuwa mezani kwake.Kabla ya kuanza kujaza akaanza kupitia moja baada ya nyingine akachukuwa Local Purchasing order(L.P.O) akaitizama kwa umakini,ilionekana ilikuwa imemchanganya kwa kiasi chake,akavuta mkonga wa simu na kuuweka sikioni.Akabonyeza namba fulani.
“Njoo ofisini mara moja”
Sekunde kumi baadaye mlango wake ukasukumizwa akaingia mwanamke aliyevalia sketi ya kijani na shati jeupe,akatembea mpaka mbele ya meza ya Deo.
“Hii L.p.o mbona original yake siioni?”
“Anayo Agness Festo”
“Mwite”
Binti mwingine mdogo aliyeitwa Agness Festo Ng’umbi ambaye aliajiriwa miezi michache iliyopita alifika ofisini kwa bosi wake akasimama kwa adabu zote.
“Agness”
“Abee bosi”
“L.P.O hii original yake iko wapi?”
“Nilimpa Mfaume kwa ajili ya kutafuta bei za vitu madukani bosi,sababu nilidhani kwamba leo hautofika na hiyo L.P.O inatakiwa leo saa kumi na moja jioni”
Deo alimuangalia Msichana huyu mdogo ambaye alimuajiri kwenye kitengo cha ‘Sales’ yaani manunuzi,ni kweli alikuwa sahihi,kuna kitu aliweza kukigundua kutoka kwa binti huyu mdogo aliyekuwa mbele yake ni kwamba alikuwa makini na hata siku yoyote ile asingekuwepo ofisini basi Agness Festo Ng’umbi angeweza kuiongoza pasipo kufanya makosa yoyote yale.
“Nataka kukuamisha kitengo,kuanzia kesho utakuwa Assistance director.Nimekupandisha cheo na mshahara,mtafute Mfaume hakikisha anapata bei za vitu vyote leo hiyo kazi iwe imekamilika”
Deo alihitimisha kila kitu.Agness hakuamini hata kidogo,haikuwezekana hata kidogo kuajiriwa kwa miezi michache na kufumba na kufumbua akawa amepandishwa cheo mpaka mshahara.
“Ahsante bosi,naweza nikaenda?”
Agnes akauliza.
“Kaendelee na kazi, lakini make sure kazi za leo zote zinaisha”
“Ahsante bosi”
Deo akashusha pumzi ndefu ya uchovu na kuvuta laptop iliyokuwa mezani kwake,hakukaa dakika hata moja.Simu yake ya mezani ikaita.Akachukua mkonga na kuuweka sikioni.
“Yes”
“Bosi kuna mgeni wako”
Upande wa pili ulisikika.
“Nani?”
“Amesema anaitwa Leila”
Kuanzia hapo Deo akawa kimnya,hakuelewa ni jibu gani alitoe kwa wakati huo.Akili yake ikarudi nyuma kwa kasi akajiona alivyojikuta hotelini na mwanamke huyo tena chumba kimoja asubuhi wapo uchi wa mnyama.
Jambo hilo lilimfanya apunguze mazoea naye,hakutaka hata kidogo kumsemesha.Uwepo wa Leila ofisini kwake ulikuwa wa ghafla,alitamani amfukuze lakini upande mwingine wa akili yake ulimwambia kwamba asifanye hivyo kwani walitoka mbali sana na msichana huyo isitoshe walisoma wote.
“Bosi”
Upande wa pili ulimshtua kutoka kwenye dimbwi la mawazo.
“Yes mruhusu apite”
Alivyotoa kauli hiyo,akaweka mkonga chini na kutupa macho yake mlangoni,akimsubiri Leila aingie.Akaona mlango unasukumwa kwa ndani,sura ya Leila ikatokeza,macho yake yakatua juu ya tumbo la Leila lililokuwa kubwa kiasi.Moyo wa Deo ukaanza kwenda mbio lakini hakuelewa ni kwanini hali hiyo inatokea.
“Karibu Leila”
Deo akaweka tabasamu la Plastiki usoni.
“Ahsante Deo,za siku nyingi?”
Leila akakaa juu ya kiti huku akitupa macho yake huku na kule anakagua ofisi ya Deo ilivyokuwa kubwa tena ya kisasa.Juu ya meza kulikuwa na picha kubwa ya Marietha anatabasamu.Jambo hilo lilimtia Leila kichefuchefu cha kutapika ingawa hakutaka kulionesha swala hilo waziwazi.
“Nzuri tu za kupotea?”
“Hivyo hivyo”
“Alafu hongera”
Deo akatoa pongezi huku akilitizama tumbo la Leila.
“Ahsante sana”
“Naona umeamua kuhamia mazima Tanzania”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Kwani bwana uliyempata si mtanzania”
“Ndio”
Ujauzito wa Leila ulikuwa wa Deo kwa asilimia zote mia moja sababu tangu alivyotia maguu nchini Tanzania hakuwahi kushiriki tendo la ndoa na mwanaume wa aina yoyote ile isipokuwa Deo Karekezi aliyekuwa mbele yake anampa hongera bila kujuwa.
Leila akamtizama Deo kwa kitambo kidogo hakuelewa ni kitu gani amwambie.
“Wifi yako naye mjamzito”
“Uliniambia najuwa,Deo nina matatizo”
“Una matatizo gani?”
“Kwanza naomba tusahau yaliyopita,naomba unisamehe kwa niliyokufanyia”
“Kwanza niambie una matatizo gani?”
“Baba wa mtoto amenikataa,isitoshe pesa niliyokuwa nalipa pale hotelini imeisha tayari.Sijui nifanye nini?”
“Kwanini kaikataa sasa?”
“Mimi sielewi Deo,nisaidie”
Leila hapohapo akaanza kubadilisha sura yake,akawa kama anataka kulia.Alivyojaribu kuyakamua machozi ili kupigilia uongo wake msumari wa nchi sita ikashindikana machozi yalikuwa mbali.Hivyo akabaki analalamika kwa Deo akidai kwamba amsaidie sababu walitoka mbali.
“Sawa usijali,lakini kwanini usiombe msaada ubalozi wa Uingereza.wewe ni raia wao”
“Hapana Deo wewe hujui,kwanza viza yangu ni invalid.I can’t do that, they can’t help me”
“Sawa basi nitakulipia pesa ya hotelini usijali Leila”
“Deo na hii hali,itakuwaje?”
Hapo ndipo Deo akajaribu kuyasoma vizuri mawazo ya Leila lakini hakuwa ana uhakika baada ya kuelewa ni kitu gani Leila anahitaji,ndiyo maana akahoji.
“Ulikuwa unatakaje sasa?”
“Niishi kwako,angalau hata nikijifungua nitaondoka”
Leila akasema.Alitaka kumuweka Deo karibu yake ili afanye mambo yake ya kishirikina kiurahisi,alitaka kuununua moyo wa Deo na alijuwa Deo kivyovyote ni mwanaume mwenye huruma kuliko yoyote yule aliyewahi kumjuwa.
Swala la kuingia nyumbani kwa Deo na kuishi aliamini kwamba tayari limepita na angeharibu ndoa yake siku chache tu,hivyo ndivyo alivyoambiwa na Mganga na alikuwa tayari ana dawa amepewa za kufanya kazi hiyo.
Deo aliingiwa na huruma mno,ni kweli moyo wake ulinunuliwa na sura ya huzuni ya Leila akajikuta amesimama kutoka kwenye kiti chake na kuzunguka mpaka kwa Leila.
“Leila usijali nitakusaidia,utaishi kwangu mpaka ujifungue, kesho nitakuja kukuchukuwa hotelini”
“Ahsante Deo”
Moyo wa Leila ulipiga sambasoti kwa furaha.
“Basi umekwisha tayari”
Leila akajisemea kimoyomoyo kwa furaha huku usoni akiwa mwenye huzuni.Kama macho ya binadamu yangekuwa yana uwezo wa kuona kilichokuwa ndani ya moyo wa mtu habadani Deo asingekubali kufanya jambo alilokuwa anataka kulifanya,siku zote moyo ni giza nene huwezi kujua yupi mnafki ama yupi muongo.
****

Jambo aliloombwa na Leila akalipeleka kama lilivyo kwa mke wake.Hakuna siku aliyopandisha mori kama siku hiyo alivyoambiwa kwamba Leila atahamia nyumbani hapo tena alikuwa ni mjamzito.Marietha alikuwa ana tabasamu lakini alivyosikia habari hizo alitoka ndani ya shuka na kusimama wima.
“Unasemaje wewe mwanaume?Eti nini rudia tena?”
Marietha aliuliza kwa jazba huku kifua chake kikiwa kinapanda juu na kushuka, pua zake zinamcheza.Maneno aliyoambiwa na Deo yaliyamsha mashetani yake ya kichaga.
“Marietha rudi kitandani basi tuongee,Leila ana matatizo”
“Mimi sio mpumbavu sawa?Usione nacheka cheka nawewe ukanichukulia poapoa.Mimi sio wa hivyo,nasema hivi hapa Leila hakai.Umeona haitoshi unaamua sasa kunionesha waziwazi na nina uhakika hiyo mimba ni yako na….”
“Wife siki…”
“Nisikilize mpumbavu wewe.Deo nimekuvumilia mengi lakini hili siwezi kulifumbia macho,nyumbani kwetu sijaua”
Marietha aliuwasha moto sio kitoto, aliongea kwa kupayuka kwa sauti.Hiyo ilimfanya Deo aogope sababu tangu amjuwe Marietha hakuwahi kumuona katika hali hiyo ya ukali hata siku moja,ndiyo maana akawa mdogo kama kidonge cha pilton.
“Marietha punguza sauti tuongee kama watu wazima”
“Siwezi kuongea tena Deo,this is too much!”
Ilibidi Deo nayeye atoke kitandani,akamsogelea mkewe akamshika bega.
“Usinishike,niache”
Mkono wa Deo ukatupwa mbali.
“Mariet…”
“Chagua kitu kimoja,uishi namimi au Leila?”
Marietha hakukwepesha aliuliza swali na alitaka jibu sekunde hiyohiyo.


“Nakupenda wewe mke wangu”
“Kwahiyo umeamuaje?”
“Leila hakutokuja hapa tena,naomba yaishe”
“Una uhakika?”
“Sina sababu ya kukutania”
Deo akamvuta mkewe karibu akamuweka kifuani kwake,jambo hilo lilikuwa rahisi sababu Deo alikuwa mrefu kwenda hewani hivyo kichwa cha Marietha kikatulia kifuani kwake wakakumbatiana huku Deo akizidi kuomba msamaha kwa jambo alilotaka kulifanya, ingawa Marietha aliombwa msamaha lakini bado aliendelea kumlaumu na kumkanya Deo asirudie tena.
“Hata mwanamke yoyote yule asingekubali kufanya kitu kama hicho”
Marietha alinung’unika akiwa ndani ya shuka.
“Yameisha mke wangu”
“Ndiyo yameisha lakini usirudie tena”
“Sawa Baby”
Mkono wa Deo ukapita akauviringisha kiunoni kwa mke wake na kujisogeza karibu kabisa,akahisi joto wote wakajifunika.
****
Deo aliendelea kufanya kazi kama kawaida siku iliyofuata alionekana akiwa mwenye mawazo mengi sana kichwani kwake,alimfikiria mke wake siku hiyo akijifungua itakuwaje.Alianza kupiga picha hata kabla ya kuitwa baba.Ghafla picha ya Leila ikapita kichwani kwake,hakuelewa ni kwa njia gani amsaidie rafiki yake huyo ambaye walisoma chuo kikuu pamoja,alimuurumia mno kutokana na mimba aliyokuwa nayo tumboni.
“Sijui nitamsaidiaje?”
Aliwaza hasa alipoikumbuka sura ya mkewe.Kama mwanaume hakushindwa kumpeleka Leila nyumbani kwake lakini alimuheshimu mke wake Marietha, ndiyo maana hakuthubutu kufanya kitu kama hicho.Siku ya kwanza ilipita lakini siku iliyofuata asubuhi alivyofika ofisini kwake alikumbana na Leila anamsubiri mapokezi.
“Leila,vipi?Za asubuhi pita ofisini”
Deo alimsemesha Leila.
“Shikamoo Bosi”
“Shikamoo Bosi”
Wafanyakazi walimsalimia mkurugenzi wao kwa adabu zote.
“Marahaba”
Deo aliitikia na kusukuma mlango wa ofisi yake ambapo alimkuta Leila ameshakaa juu ya kiti anamsubiri,akapita na kuketi nyuma ya meza yake.Akavua koti na kuliweka vizuri nyuma ya kiti chake kikubwa cha kuzunguka.
“Leila,niambie”
“Deo,kweli umeamua kunifanyia mimi hivi?Kama hutaki kunisaidia si uniambie tu”
“Sio kwamba sitaki”
“Sasa mimi nikueleweje?”
“Unajua jana alikuja Mama mkwe pale nyumbani,na yupo bado ndiyo maana nikashindwa kukuleta kwangu”
Deo hakutaka kuongea ukweli ilikuwa ni lazima atumie mbinu nyingine ya kupiga 'fix' ili asimvunje moyo rafiki yake,alielewa kwamba angeongea ukweli kuhusu Marietha alivyomueleza asingejisikia vizuri hata kidogo.
“Mbona hukupokea simu zangu?”
“Jana nilikuwa naye siku nzima isitoshe simu nilisahau nyumbani..Mariet.. sorri Leila sikia nitakupa hapa laki nne sasa hivi ulipie hoteli kisha mimi nitajuwa cha kufanya nitakuja kukuona”
“Deo sina shida na pesa”
Kauli hiyo ilimfanya Deo amtizame mwanamke huyu ambaye haeleweki, sababu mara ya kwanza alisema kwamba anadaiwa pesa ya hoteli,hiyo ikamfanya Deo amuangalie kwa umakini zaidi.
“Kumbe una shida na nini?”
“Msaada wako”
“Sikia Leila,embu eleweka.Umeniambia una shida na pesa unadaiwa hotelini nakupa hautaki.Sasa unahitaji nini?Nimeshakwambia nitakusaidia”
“Lakini Deo..”
“Nini?”
“Sawa nipatie hiyo pesa”
Kukataa kitita cha laki nne aliamini kwamba Deo angemfikiria vibaya,ndiyo maana alikubali ili kumzuga.Deo akavuta 'draw' kwa chini ambapo lilikuwa la chuma tena la kisasa, haikuwa rahisi kulifungua bila kuzungusha namba za siri.Lilivyofunguka akahesabu pesa chini kwa chini mpaka zilivyofika laki nne na elfu hamsini,akafunga 'draw' na kuvuta baasha ya kaki.
“Laki nne nakuwekea humu ndani ya bahasha,hii elfu hamsini utafanya nauli.Utachukuwa Taxi na kununua chakula leo na kesho”
“Ahsante”
Jinsi alivyoshukuru Leila ilionekana kabisa hakufurahishwa na pesa alizopewa nia yake ilikuwa ni kuingia ndani ya nyumba ya Deo ili asambaratishe mapenzi ya Deo na Marietha lakini mambo yalikuwa magumu bado kwa upande wake.
Akasimama na kumtizama Deo kwa macho makali yaliyojaa hasira za waziwazi.
“Leila,naomba usinifikirie vibaya.Mama mkwe akiondoka pale nyumbani mimi nitakuja kukuchukuwa.Kama ukiwa na tatizo lolote kipesa usisite kuniambia”
Ilikuwa ni kama Deo anajiongelesha mwenyewe sababu Leila hakutoa jibu lolote lile,akatembea mpaka mlangoni na kuuvuta akatoka zake nje huku akimuacha Deo akimsindikiza kwa macho,moyoni alijisikia vibaya sana, alitamani kutoa msaada lakini alihofia kumkorofisha Marietha ambaye tayari alikuwa keshakataa tayari mbali na hapo aliogopa kuchukuwa maamuzi magumu sababu mkewe alikuwa mjamzito,kumkerakera ovyo ingesababisha matatizo mengine na pengine ingepelekea hata mimba kutoka sababu hiyo hakutaka kabisa jambo hilo litokee.

***
Leila alitoka nje ya jengo,ofisini kwa Deo akiwa amevimba kama chura wa masika,alikasirika kupita kiasi cha kutosha.
“Chanika bei gani?Kutoka hapa mpaka Chanika ni bei gani?How much?”
Ni Leila ndiye alikuwa akiuliza bei kwa dereva Taxi aliyekuwa anapangusa gari yake.
“Mh,Chanika”
Dereva akaguna na kumgeukia mteja wake sababu kutoka Posta mpaka chanika kulikuwa kuna kipande kirefu sio mchezo.
“Chanika sehemu gani?”
“Dondwe”
“Hapo sista,elfu themanini”
“Poa twende”
“Sawa,Oyaaaa oyaaaa wewe Hamisi.Hilo gazeti langu ukimaliza kusoma nitalikuta kwa Bakari hapo”
“Poaa”
Alivyohakikisha ameacha maagizo kwa dereva taxi mwenzake,akafungua mlango wa nyuma Leila akaingia kisha yeye akapita kwenye usukani,safari ikaanza mara moja.
Leila alikuwa anarudi kwa mganga wa kienyeji ili apate njia nyingine ya kumnasa Deo sababu njia ya kwanza ilikuwa ngumu kwake,kuingia ndani ya nyumba ya Deo ulikuwa bado ni mtihani kwa upande wake.
****

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG