THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 10 KATI YA 10 MWISHO
Waziri mkuu kasanga akiwa chumbani alianza kuserebuka na kuanza kucheza kwa furaha sana, huku akiwa na glass ya wine, jambo hilo lina mshangaza sana mke wake.
"Sasa nina Amani, Raisi amekufa"
Aliji kuta anasema maneno hayo mwenyewe na kufanya Flora akae kitako na kubaki akimshangaa
Mume wake ambae wakati huo alikua ameweka mziki mkubwa wa redio akicheza cheza na kuzunguka ndani ya chumba hiko kikubwa cha kulala.
"Umesema Raisi amekufa?"
"Hahahahahaha, ndio amekufa sasa nina amani "
"Kwaio una shangilia mwenzako kafa,?"
"Naenda kuwa makamu wa Raisi sasa"
Waziri Kasanga aliongea huku akimsogelea Flora na kumshika kiuno.
"Yaaani leo eeeh. Leo nakupiga mambo mpaka asubuhi, mwanzo mwisho bila mapumziko"
Aliongea Kasanga huku akivua koti.
"Hayo mambo utajipiga mwenyewe. Tena usini sogelee nakwambia, sitaki unisogelee"
Flora alijitoa kwa nguvu na kumzaba kofi la shavu mume wake ambalo lili muingia sawa sawa na kufanya Waziri mkuu akasirike na kumkata jicho kali.
Kweli Flora hakuwa tayari kufanya tendo la ndoa na mume wake,
hii ni kutokana na habari mbaya alizo sikia muda mfupi, alivuta shuka na kuji funika mpaka kichwani na kuendelea kuta fakari,
"Patson, una sema kweli Raisi Alphonce amefariki?"
Flora aliuliza kwa unyonge sana baada ya kuta fakari kwa muda mrefu,
Alikaa kitandani huku akiuweka mto nyuma ya mgongo wake,
Ki ukweli mahusiano ya Flora yalikua ya karibu sana na Raisi Alphonce kuliko kiongozi yoyote yule hii ni kutokana kua waliishi kijiji kimoja, ivyo walitokea kuwa marafiki sana na hupenda kutaniana,
"Ndio, subiri kesho uone"
Alijibu waziri mkuu kifupi huku akitabasamu na kupiga fundo lingine la wyn.
"No una nidanganya,!, haiwezekani"
"Sitaki maswali, ume kataa kunipa unyumba alafu una niuliza upuuzi, ndio kafa kasha kufa, ndege yake ime lipuka, "
Flora Kasanga aliumia sana na kubaki kuganda kama barafu huku akimwangalia mume wake ambae wakati huo hakuonesha hali yoyote ya kushtuka wala kuingiwa na wasi wasi wa aina yoyote.
"Alphonce ,. Haiwezekani"
Aliji semea Flora huku machozi yakianza kumlenga.,
waziri mkuu ali furahi pia kwa kuwa Alfred alikuwemo ndani ya ndege ile ya raisi na kujua kivyo vyote vile ange mwambia ukweli, ivyo roho yake ina kua nyepesi sana kufurahi sana kwa kitendo kile.
*****************************
Kwa kasi na kuzidi kwenda chini huku akiwa amemshika vizuri raisi Alphonce huku upepo mkali uki zidi kuwa piga ila hakukata tamaa ya kumuachia raisi wake,
. Walizidi kwenda chini mwishowe walijikita ndani ya maji , ambamo kwa kasi wali zama chini na taratibu Alfred akiwa ana mtafuta Raisi Alphonce chini kwa chini,.
Aliya kata maji ambapo aliweza kumuona raisi ame poteza fahamu, alimshika ubavuni na kuanza kuya kata maji huku akiibuka ibuka kuta futa pumzi nje ya maji na kurudi chini,.
Alfred haku kata tamaa nia yake ili kua moja tu kumuokoa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ivyo alisahau yote yaliyo pita na kuto kujali habari ya kesi yake,. Alizidi kuyakata maji chini kwa chini huku akibana pumzi, mwishowe walitoka nchi kavu ,. Na kuanza kukimbia na kutoka nje ya maji hii ni baada ya kumuona Raisi Alphonce hana fahamu, baadae alirudi na gogo la mti, na kuanza kumvua shati Raisi Alphonce na kumlaza juu ya gogo lile kifudi fudi,
Gogo lile likiwa tumboni alianza kumpa huduma ya kwanza kwa kumkamua maji na maji hayo kuanza kutoka,
Alfred alijiwa na tumaini hasa alipomuona Raisi Alphonce anaanza kupiga chafya nyingi na kutapika maji aliyokua ame kunywa
"Muheshimiwa Raisi, una jisikiaje"?
Alfred alimuuliza huku akimgeuza vizuri Raisi Alphonce.
"Kija...na tupo wapi?"
Raisi Alphonce aliuliza huku akiangalia angalia na kuangaza huku na kule.
"Sijui muheshiwa Raisi,tutoke eneo hili".
Alfred Mulawa alimshikilia vizuri Raisi Alphonce mpka pembeni kidogo ya maji na kukaa kwenye moja ya gogo kubwa,
"Heeei heeeei,. Samahani, eti hapa wapi"?
Alfred alimuuliza mtu aliye kua ana pita mbele yake.
"Entebbe, entebbe,Uganda, Aerial beach"
Alfred alirudisha shingo kwa Raisi Alphonce na wote kuangaliana baada ya kugundua walitua juu ya ziwa victoria upande wa Uganda.
"Muheshimiwa Raisi, naomba nikwambie kitu"
"Kitu gani kijana?"
"Tupo Uganda, ni kwamba hatu kuvuka degrii 85 , hii ndege yako ime lipuliwa na watu wa nchi za karibu sana,"
"Sio kweli,."
"Niamini wewe ni Raisi wangu siwezi kuku danganya,"
Raisi Alphonce alibaki akimwangalia Alfred na kukosa la kumwambia.
"Naitwa Alfred Mlawa,"
Alfred aliongea na kumpa mkono Raisi Alphonce,.
"Nita futie simu"
"Simu ya nini?"
"Nataka nipige Tanzania kwa wananchi wangu wajue nipo salama"
"No usi fanye ivyo,. Mpigie mtu unae mwamini, una wabaya wako wana kuta futa, tafadhali nakuomba"
"Sasa nita mpigia nani,.? Mbunge wa viti maalumu ATU KIHAKA,. Lakini no Ngoja nimta fute Florah Kasanga"
Alfred alimuangalia raisi baada ya kusikia jina lile.
"Flora ni nani?"
"Mke wa Partson Kasanga,"
"Una uhakika na unacho taka kuki fanya mi naona bora umtafute ATU KIHANGA"
Alfred alimchukua Raisi Alphonce pembeni na baadae kuta futa simu na kupiga., ambapo.aliamua kumta futa Flora Kasanga hewani kwa sababu ndie mtu aliye mwamini kuliko mtu yoyote yule Duniani,.
"Halloo Flora, sikia usitaje jina langu, unaongea na Raisi Alphonce"
"Waaaat,.uko wapi Alphonce,. Habari zime tapakaa kuusu ajali ya ndege yako"
"Usijali nipo salama, nisikilize kwa makini, usimwambie mtu yoyote kama nili piga simu au chochote kuhusu mimi,"
"Kwanini Alphonce?"
Upande wa pili uli sika Flora akiwa mwenye furaha sana.
"Kwa ajili ya usalama wako na wangu."
Raisi ali kata simu na kuanza kuongoza na Alfred ambae wakati huo alimvalisha Raisi kofia kubwa ili asijulikane na mtu yoyote yule.
*****************************
Kikosi cha usalama wa nchi kavu kilizidi kuokota mabaki ya ndege ya raisi ambayo baadhi ya vipande vili dondoka nchini kenya,
Ila mpaka dakika hiyo bado hawa kubahatika kuupata mwili wa Raisi Alphonce ambapo kitendo hiko kina zidi kuwa umiza kichwa,
Taarifa za habari kuhusu tukio hilo lina wasikitisha sana baadhi ya wana nchi wa Tanzania,.
Wengine wakilia sana baada ya kusikia kitendo hiko, zili kua ni habari za kusimumua na kuuzunisha ambazo hazikuwahi kutokea katika nchi hiyo ya Tanzania,
Nchi nzima ili kua katika hali ya ukimnya sana na majonzi kupita maelezo.
Taarifa izo zili ugusa sana moyo wa Hannah Mke wa Alfred ambae alibaki kulia kama mtoto hii ni kutokana na kuwa Alfred nayeye pia alikua ndani ya ndege hiyo ya raisi,
Ila baadae wanaanza kuhisi wenda mwili wa Raisi ulilipotelea ndani ya maji na kuliwa na samaki, hii ni kutokana na kuvikuta vipande vipande vya ndege juu ya ziwa Victoria, huku bado pia kikosi cha majini kikizidi kutafuta mwili wa raisi chini ya maji bila kuona dalili yoyote ile.
Upande wa pili wa Waziri alikua mwenye furaha sana akiwa sebuleni akiangalia habari hiyo ambayo bado ili tangaza tukio la Raisi kufariki kwenye mlipuko wa ndege.
"Kasha kufa tayari, mimi sibahatishi,"
"Khaa, una maana gani, kumbe wewe ndo uli yefanya haya yote"? Aliongea Flora akiwa pembeni yake.
". Naenda kuwa makamu wa raisi "
"Ndo kina cho kufanya ukenue meno?"
"Ndio"
Flora hakujibu chochote zaidi aliachia misunyo na kuondoka japo alijua Raisi alikua hai na kutokufa kama watu wanavyo dhani.
*************************
"Raisi nisubiri hapa nika chukue gari"
"Uka chukue gari wapi?"
"Naomba nisubiri"
Alfred alianza kupiga hatua na kwenda maeneo yalipo egeshwa magari, na kuliendea gari moja ambapo alilipiga kioo cha mbele na kupasuka, alingiza mkono ndani ya kioo na kufungua mlango, baada ya hapo ali tafuta kichuma kizito na kupa sua switch ya kuwashia gari ambapo alivuta waya mbili nyekundu na bluu,. Alizichuna taratibu na kuzigusisha na kutoa cheche pale pale gari lilianza kupiga kelele na kuwaka,
Alizifunga waya zile na kupiga gia na kumuendea Raisi alipo.
"Raisi ingia twende"
Raisi Alphonce alimtazama Alfred na kuingia ndani ya gari, na Alfred kutoa mbio, na ukimnya kuta,wala.
"Gari ume toa wapi kijana?"
"Nime iba"
"Hii nchi una ijua vizuri?"
"Ndio naifahamu, nili shawahi kuishi"
Alfred aliendelea kuendesha gari huku akiwa makini.
""Tuna elekea wapi sasa kijana?"
"Kampala,"
"Embu niambie ukweli kijana, wewe ni nani?,. Na ime kuaje ulitaka kumuua Waziri mkuu wako?"
.Alfred alimuangalia Raisi Alphonce kwa uma kini sana na kushusha pumzi ndefu na kutojua aanzie wapi kumwambia ,
Taratibu alianza kumu adithia tangu alivyo kua mtoto alivyo shuhudia baba yake IGP Mulawa ana uliwa , haku mficha chochote,
Raisi Alphonce kwa umakini sana alikua akimsikiliza wakati huo Alfred Mulawa akiendesha gari huku machozi ya kianza kumlenga kweli aliji kaza ila alishindwa na kuanza kudondosha chozi., la uchungu.
"Marehemu Dada yangu Roseline siku bahatika hata kuishi nae, ame kufa bila hatia, muheshimiwa Raisi, kwa heshima yako na kuku heshimu ile siku mbele ya ikulu siku taka kumuua, samahani siku ile najua ili kua picha mbaya sana..."
"Alfred, samahani sana, naona aibu hata kukuangalia, sista hili hata kuwa Raisi wako,No sista hili kabisa, Partson Kasanga, Sijui nimfanye nini huyu mtu?"
Raisi Alphonce aliongea kwa uchungu sana huku akimuonea huruma Alfred hasa kwa hatua aliyo taka kuchukua muda mfupi ulio pita ya kumfunga gerezani , aliji kuta ana jutia sana
"Usijalia utaendelea kuwa raisi wangu,. Huja nikosea chochote uli kua ni wajibu wako, hukua una jua lolote, na muheshiwa Raisi nakuhakikishia kwamba sio wote wana oenda gerezani wana hatia, wengine ni kama mimi leo hii, naamini leo ume jifunza kitu"
Raisi Alphonce alimpa mkono Alfred na kuzidi kumuomba msamaha mara mbili mbili, kweli raisi Alphonce aliji kuta ana jishusha na kumshukuru pia kwa kuokoa maisha yake, katika ndege ile iliyo lipuka...
"Mheshimiwa Raisi, una weza uka fanya juu chini na kutumia njia yoyote ile kesho asubuhi Waziri Kasanga achelewe ofisini?"
"Kwanini una taka iwe ivyo?"
"Kuna kitu nataka kujua kiwe kama ushahidi"
"Usha hidi kivipi"?
"Niambie ita wezekana?"
Raisi Alphonce alifikiria kwa muda kidogo na kumwa ngalia Alfred machoni ambapo hakujua nia ya Alfred ."ndio, ita wezekana, ila mpaka niongee na Flora mke wake"
"Fanya ivyo".,
Kweli baadae ana toa simu na kumta futa Flora na kuongea ambapo ana pewa jibu zuri kwamba asiwe na wasi wasi hata kidogo.
Usiku huo ambao ulifanya kiza kinene ila Alfred alizidi kuchanja mbunga,.
akiwa makini juu ya usukani ambapo wakati huo tayari alikua ame fika maeneo ya Jinja nje kidogo ya mji wa Kampala., ambapo wali tembea na gari takribani kilometa tisini na saba
"Tafuta sehemu tupumzike, naona umeendesha gari kwa muda mrefu sana,"
Alivunja ukimnya Raisi Alphonce.
"Aaaaah hakuna shida usijali,. Nataka asubuhi itukute Kenya,."
. Aliongea huku akiendelea kuangalia mbele ya kioo, baadae anaangalia pembeni na kumuona Raisi Amelala na kutoa simu aki mtafuta Amney .
'"Amney Alfredy naongea"
"Hapana una nitania, haiwezekani, Alfred uko wapi?, Watu wana jua uli kufa tayari na wana fanya taratibu wa msiba wako:, tupo kwako alafu., Raisi nayeye yuko wapi? Amepona?"
"nimepona niamini,nipo nae hapa, nakuomba kitu kimoja, kesho asubuhi uingie ofisini kwa waziri mkuu"
"Kufanya nini?"
"Uki fika uta niambia, sasa siwezi kuongea,vipi mke wangu mzima?"
"Ndio ,lakini amezimia mara tatu, sasa hivi anaendelea vizuri kidogo, yupo na Jaqlin Nyange"
"Amney mtunze mke wangu, ila naomba usimwambie kwanza mpka nimalize nacho kifanya"
"Usijali Alfred"
"Poa nita kutafuta kesho,. Usimwambie mtu yoyote Amney"
"Hakuna tabu"
Alfred aliendea kuendesha gari huku akimfunika Raisi Alphonce na sweta ambalo alili kuta ndani ya gari lile.
***************************
Nchi ya Tanzania ili kua katika hali ya simanzi na majonzi hasa baada ya kutangaza kua baada ya wiki wange tangaza Raisi mwingine wa nchi ya Tanzania,
Asubuhi ilipo fika tayari Waziri Kasanga alianza kuvaa nguo na kuta futa tai yake ambayo alimuuliza mke wake Flora.
Ila baadae Flora ana mletea na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni na kuanza kumvua shati alilo vaa na kumpapasa kifuani.
"Flora wacha niwahi kazini niki rudi basi "
"No baby, hapana mi nina hamu nawewe sasa hivi jamani please, nita kufa, mume wangu"
"Hapana niki rudi"
Flora haku taka kumuachia, alimfata shingoni na kuanza kumnyonya shingo huku mkono wake mwingine akimpapasa kifuani, na kufanya Waziri kasanga damu kumuenda mbio na kuanza kulegea bila kujua lengo la Flora lili kua ni moja tu kumchelewesha mume wake ofisini kama alivyo pewa maagizo na Raisi,
Kweli njia hiyo aliyo itumia ina zaa matunda baada ya kuanza kufanya tendo la ndoa aki tumia kila njia ili Kasanga achelewe.
Upande wa pili tayari Amney alikua nje ya ofisi ya waziri mkuu , akiwa ame valia suti na sketi nyeusi fupi kidogo ili fanya umbo lake liji chore vizuri na makalio yake kidogo kuonekana huku akitembea kwa mikog o na kufanya kila mtu akigeuza shingo, alimpita sectretari wa waziri na mwishowe kuwa kuta walinzi wengine wawili ambao wali mzuia kuingia ndani.
"Naomba nipite nyie watu"
Aliongea Amney kwa kujiamini na kufanya walinzi wale wasogee karibu yake.
"Anti samahani huwezi kuingia bila ruhusa ya waziri mkuu"
"Naona una taka kufukuzwa kazi, si ndio, una jua mimi ni.nani yake?, sasa sikiliza nipe jina lako nimwambie kuwa ume nikatalia kuingia. Wewe jina lako nani nita jie haraka"?
Amney aliongea akitoa simu huku akiji fanya ana bonyeza bonyeza namba,.
"Na ngoja nimpigie huyo waziri wenu, sijui bosi wenu niwa shtaki mna nizuia, nita jie jina lako, nyie nyau mna nijua mimi vizuri, embu subiri niwaoneshe, sio kila mtu mna mzuia zuia"
Amney aliongea na kuweka simu sikioni.
"Halloo Baby..iv....."
"Anti, anti, basi yaishe, ingia tu. Usijali"
Walinzi wale wali jikuta wanamruhusu Amney tena wakimuomba msamaha bila kujua hakuwa hata na namba za waziri mkuu,
Alicho kua ana kifanya Amney hakudhani kama kimgezaa matunda ivyo aliji kuta ana ruhusiwa baada ya kutumia mkwara ule mkali,, akiweka simu sikioni kuji fanya anaongea na Waziri mkuu huku akimlegezea sauti.
Kweli wali mfungulia mlango na kujua Amney ali kua ni awala wa waziri mkuu ivyo wange poteza vibarua vyao na kurudi vijijini kulima
******************************
Tayari kulipambazuka na.Alfred aliegesha gari pembeni baada ya kufika mpakani Busia .mpaka wa kuingia Kenya na kuangalia kwa makini njia gani atumie,
Alimwangalia Raisi Alphonce na kumtingisha aamke,
Baada ya kuamka alimkabidhi sweta kubwa avae na kofia na kuji funika sura.
"Uta weka kichwa chini, na usiongee chochote mpka tuvuke boda hii,"
"Sawa hakuna shaka, sasa na gari ina kuaje?"
"Nita pata lingine, cha muhimu sasa hivi. Tuvuke hii boda"
Raisi Alphonce alimwangalia Alfred na kushusha pumzi na kutokua na uhakika kama wange fanikiwa ila hakua na jinsi zaidi ya kuweka tumaini mbele.
Kweli walianza safari ya kutembea taratibu na kuji changanya na watu wengine ambao walikua waenda kwa miguu
"Haroo eii harooo harooo"
Alfred alisikia sauti iki muita na kutokua na uhakika kama ndo yeye, ila baadae ana shikwa bega na kugeuga, alimuona askari .
"Si nakuita mbona una leta ukora sasa?"
Askari yule aliongea kwa rafudhi ya kikenya.
"Aaah bwana hafsa, ako na shida gani kwani?"
Alfred nayeye alijibu kwa rafudhi ya kikenya na kumfanya Raisi amwangalie kwa jicho la kuibia ibia maana kitendo kile kili mshtua sana kwa sababu hata sauti pia ali badili.
"Una toka fasi gani?"
"Natoka huku kwa juu, ako naelekea home"
"Na huyo nani hapo pembeni?"
"Huyu ni budaa wangu. ako ana matatizo ya masikio huwa aongeagi, hapa na mpeleka kwa manzi yake bwana hafsa, wacha nimu waishe, alafu nakuja tuongee vizuri wacha nika muone nyanya"
Alfred alizidi kumchanganya askari yule na kujua kweli ni Mkenya mwenzake ivyo ana jikuta akimruhusu na Alfred kuanza safari ya kuondoka.
Baada ya kuvuka boda hio Raisi ana vunja ukimnya kwa kucheka sana.
"Alfred, pale kidogo nicheke,., siku amini kama pale tunge pita"
"Usijali raisi, hii ni moja ya kazi yangu,"
Alfred baada ya kuvuka mpka ule anaenda mbele kidogo na kuona gari ainaa ya Range rover na kuisogelea, aliikagua na kuona ina alam ambapo alijua akiigusa tu ita piga kelele, ivyo alichukua vichuma na kukwangua kifaa cha sensa ambacho kipo chini ya gari hilo, alivyo fanikiwa, alivunja kioo na kufungua mlango, hapo alivunja switch ya gari na kugushika waya na gari kuwaka, Raisi Alphonce aliingia na gari kutoa moto,
kutokana na gari hilo ili kua na mtambo wa GPS wa kuonesha ramani ivyo Alfred alibonyeza ramani iyo ambayo ili kua ina waonesha njia, na sasa kuanza safari kuelekea NAMANGA mpaka wa Tanzania, Alfred na Raisi Alphonce wali jikuta wana jenga urafiki wa karibu sana.
walijikuta wakipiga stori za kawaida kama watu wana ojuana ,
. Alfred alizidi kuendesha gari hiyo aina ya RANGE kwa kasi saana.
"Muheshimiwa Raisi, sasa uki fika Tanzania, una tarajia kufanya nini, una mipango gani?"
"Alfred, subiri tufike kwanza, una jua katika maisha yangu, sikuwahi kufikiria kama kuna watu wana utu kama wewe,. Mimi kama mimi binafsi, nime toka katika familia ya kitajiri sana, yaani wana sema wakishua kama mnavyo semaga vijana,. Nili kua niki toka shule ni ndani. , yaani nili kua mbi nafsi sana, siku wahi kuishi na watu tofauti zaidi ya ndugu zangu"
"Sasa ikawaje mpaka ukaamua kuingia kwenye siasa"?
"Baba yangu, Mr,Muriba ndo alipenda sana, mimi niingie japo nili kua sipendi sana, sikuwa na jinsi nili fanya ivo ili nim furahishe, nikuulize kitu Alfred?"
"Uliza tu?"
"Una familia?"
"Nina mke sema hivi karibuni naenda kuwa na familia, "
"Safi sana kijana, lakini..... "
Raisi Alphonce alishindwa kumalizia maneno aliyo taka kuongea hii ni kutokana na kumuonea askari wa usalama wa bara barani kanyoosha mkono kumaanisha kuwa wasi mamishe gari, hiyo.
"Alfred, sasa ina kuaje,?, utasimama?"
"Niachie mimi, hana shida huyu"
Alfred alipunguza mwendo taratibu na kuegesha pembeni huku akimsubiri askari yule aje,
Kweli alikuja na kuanza kukagua kagua gari na mwishowe kuangalia kioo cha mbele akionekana kuka gua makaratasi yaliyo bandikwa.
"Nipatie Driving permit. Na kadi ya gari"
Alfred alimuangalia Askari yule na kukosa cha kumpa, ki ukweli hakua na chochote kati ya vile alivyo ulizwa,
"Tuna haraka Afande"
"Shwain, una haraka?, una nijibu vitu gani, una haraka maana yake nini?, kwani mimi sina haraka, naenda kuku arest. Shuka upesi, yaani teremka ndani ya gari,eti una haraka"
askari yule ali foka kwa sauti sana.
Alfred alishuka taratibu huku akiangalia huku na kule na kumuacha Raisi Alphonce ndani ya gari mwenye wasi wasi sana.
Waliongozana na askari mpaka ndani ya gari dogo la polisi ,
Ambapo baada ya kuangalia angalia makaratasi yake ana gundua kuwa gari lile aina ya Range lilii biwa na lina tafutwa.
"Hapo hapo hakuna kusogea ngoja niwa ite polisi,, hilo gari lina tafutwa"
Alfred alimuangalia Askari yule wa kikosi cha usalama barabarani ambapo wakati huo alitaka kutoa redio upepo, alimu wahi na kumpiga kichwa puani , baada ya hapo ali sogelea na kumkaba shingo, alivyo muona katulia, ali mburuza na kumuweka pembeni ya gari, alichukua redio upepo na kuingia nayo ndani.
"Alfred, upo vizuri,,. Una hatari sana"
Raisi Alphonce alimwambia Alfred,
", mambo madogo haya., ,..Funga mkanda, hapa hatusimami, mpaka tufike Elidoreti"
"Hiyo redio upepo ya nini?"
"Nita kua nawa sikia wana choongea ita kua rahisi mimi kuwakwepa"
Alitembea kwa kasi ya ajabu mpka mshale wa spidi kugota mwisho, na kutokana na gari ile kuwa na uwezo mkubwa wa kutembea kwa kasi,. Ili fanya wakaribie kufika Elidoreti mapema.
*************************
"Alfred, baba,.. Mume wangu, eeeeh Mungu nini nime kukosea Alfred ume niacha na nani mimi, nita baki na nani"?
Kili kua ni kilio kutoka kwa Hanaah baada ya kuzinduka alipo pata fahamu, Hannah alikua ni mtu wa kulia, takribani siku tatu hakula hata kidogo, ki ukweli jambo la kifo cha Alfred aliona ni kama ana ota njozi ndefu ambayo ange tamani iwe ivyo.
Ila ukweli uli kua pale pale, Jaqlin Nyange akiwa pembeni yake aliji tahidi kadri ya uwezo wake ili Hanna atulie ila ili kua ni kama ana chochea kuni au makaa ya mawe., kilikua ni kilio cha ajabu na kumfanya aishiwe nguvu,
Amney akiwa pembeni ambae alijua kila kitu kuwa Alfred yupo hai, alitamani kumwambia Hannah ila aliji kaza, ali msogelea Hannah na kumuweka begani kwake.
"Haanah usilie kila kitu kita kua sawa"
"Hapana, hapana. Alfred wangu namtaka. Mi najiua nipeni kisu, nipeni kisu, nipeni kamba nife nimfuate Mume wangu, jamani, Amney kama una nipenda naomba kisu nimfate Mume wangu. Sitoweza, kuishi mwenyewe"
Watu walianza kujaa na ku mfariji ila kazi ili kua ile ile tu, Hannah hakuacha kulia na kutaja jina Alfred,.
Roho ya Amney ili anza kumsuta na kuji kuta ana taka kumwambia lakini pia nafsi nyingine ina mzuia.
*************************
"Safi sana Abdul, ujue najua kifo cha Raisi Alphonce kime washtua wengi sana,. Sasa hivi najiona mwepesi sana, ngoja niku ahidi. Nikienda kuwa makamu wa raisi, uta kula bata tu, sio bata tu, yaani mpaka MBUNI ndege mkubwa."
Maneno hayo yali mtoka Waziri Partson Kasanga akiwa ndani ya ofisi yake juu ya kiti chake kikubwa huku akiwa ana zunguka zunguka na kuji shika kitambi chake ambacho kili kua kikubwa cha wastani,
"Mi nataka unipe cheo fulani hivi, serikalini Mkuuu"
"Yaani wewe ondoa shaka,. Ongea vitu vingine,.Raisi kushnei, lazima tusherekee leo hiii, tena jioni, huku niki subiri wiki ijayo niwe makamu wa raisi,. Rest in peace Alphonce, nili kua sikupendi"
Waziri Mkuu aliongea huku akicheka kwa furaha sana,. Waliongea mengi na Abdul siku iyo na baadae magharibi kuingia na wote kuondoka wakienda kujiandaa ili baadae waku tane katika kumbi ya starehe, ili washe rekehee kifo cha Raisi Alphonce.
****************************
"Raisi kula chakula hiki nime kuletea"
Alikua ni Alfred baada ya kumletea Raisi chakula na kumkabidhi na wote kuanza kula huku gari likiwa pembeni kidogo ya kichaka ambapo walili ficha ili wasio nekane
"Shika maji haya hapa, Raisi"
"Asante kijana"
Kweli Raisi alikuwa na njaa na kuanza kula haraka haraka na kuya bwia maji yale huku akiendelea kula , baada ya kumaliza wali nawa mikono na Alfred kuwasha gari,
Alfred alitembeza gari kwa kasi vile vile ambapo baada ya masaa tisa tayari waliingia ndani ya jiji la NAIROBI ambapo hawa kusimama hata kidogo,.
Alfred alizidi kucheza na usukani akibadili gia na kuwa makini sana kuliko siku zote akiwa na nia moja tu kumfikisha Raisi Alphonce Tanzania kimnya kimnya na salama salmin,
Kweli baada ya masaa kadhaa waliingia Namanga mpaka wa kenya na Tanzania, ambapo ilikua ime itimu saa kumi za asubuhi, hapo walipita taratibu huku wakiwa wame zima taa gari na kweli wali fanikiwa kupita vizuizi vya hapo, na kuzidi kusonga mbele na kuingia Tanzania Tayari ,.
Wakati huo Raisi Alphonce alikua amelala fofofo wala hakua na habari na kina choendelea ,.
Gari lile lilianza kupiga mlio kuashiria kuwa mafuta yameisha, kitu ambacho kina mshtua Alfred,...
Alfred alichungulia mshale wa mafuta kweli aliona upo chini sana huku taa ya rangi nyekundu ikiwa ime waka, kuashiria kua hawata tembea zaidi ya kilometa moja,
Aligeuza shingo kuangalia nje na kuona hakuna hata dalili yoyote ya kuwa na nyumba wala kijiji, kulikua ni msitu ambao una miti miti mifupi na udongo uli kauka sana,
"Raisi Alphonce,. Hatutoweza kwenda popote, mafuta yameisha,na hapa tupo mbali sana na mji., tupo kwa Babu Loliondo hapa nafikiri."
"Sasa ita kuaje Kijana,?"
"Ngoja niweke gari pembeni kwanza, tuombe msaada"
Alfred aliweka gari pembeni na kushuka, na kumwambia pia raisi ashuke,
Na wote kuingia ndani ya kimsitu ili kuta futa kama kuna kijiji japo waombe msaada wowote ule,
Ila baada ya kusogea ndani kidogo wana shaanga katika hali ya kustaajabu bila kutegemea lina tokea kundi la watu wengi na kuwa zunguka huku wakiwa na mikuki pamoja na mishale, kwa haraka haraka walikua ni wamasai kutokana na mashuka waliyo vaa,
Wamasai wale walianza kupiga kelele kwa lugha ya kimasai ambayo Raisi peke yake ndo alikua ana waelewa.
"Raisi hawa wana semaje?"
"Wana sema tuweke mikono juu"
Kundi lile la wamasai lilizidi kuwa zunguka huku wengine waki anza kupandisha mori na kupiga vigele gele.
Alfred aliwaa ngalia mmoja baada ya mmoja huku akizungusha shingo yake na kukunja ngumi taratibu.
"Kijana usi jaribu kufanya kitu chochote , tuta kufa tuweke mikono juu, tafadhali"
"Unadhani tutatoka hapa Muheshimiwa Raisi"?
"Kijana, mimi ni raisi wako, nisikilize mimi,nita ongea nao, cha kufanya weka mikono juu"
Alfred taratibu alikunjua ngumi aliyo kunja, na kusa wazisha sura yake ambayo ili jikunja kutokana na hasira ya kupambana, na taratibu kuweka mikono yake juu, ambapo wama sai wale walitaka waongoze mbele na huku nyuma wakiwa na mikuki yao wame isimamisha,.
Wali tembea mwendo wa dakika thelathini na saba huku mikono yao ikiwa juu na kuona kijiji kili cho jaa wama sai huku kuki wa na vijumba vilivyo jengwa kwa kutumia nyasi,
na kuwekwa chini na wamasai wale ambao mpaka dakika hiyo hawa kujua nini nia ya wamasai hao., ghafla pale pale wana muona Mtu mwingine aliye valia nguo za kimasai ana kuja, huyu aligundua ni mkuu wao kutokana na walimpa heshima, mkononi alikua ameshika sime na sufuria kubwa sana ambalo aliliweka chini na kuwa sogelea.
Raisi Alphonce alianza kuongea nae kimasai ambapo Alfred hakujua nini wana zungumza maana lugha hio hakuijua.
Mara pale pale wana iuniliwa baada ya amri hiyo kutoka kwa mkuu wao huyo, ambapo Alfred hakujua kwanini tukio lile lime tokea,.
"Raisi, mbona sielewi"?
"Usiwe na wasi wasi, hawa taweza kutu dhuru, ila wali kua wana taka kunywa damu zetu., "
"Ina maana walitaka kutuua"?
"Ndio,"
Baada ya muda mfupi wali letewa viba kuli viwili ambamo ndani yake kuli kua na supu ya ng'ombe na nyama, na kuanza kunywa taratibu, walivyo maliza wali shukuru,
Raisi Alphonce alivua saa yake ya dhahabu ambayo ya gharama sana, na kumkabidhi mmsai yule, ambapo alimwambia aka iuze ili wapate pesa ya mafuta,
Kweli mmsai yule alichukua saa ile na kuondoka nayo na baiskeli.
Baada ya muda mfupi alirudi na dumu kubwa lililo jaa mafuta ya petrol na baadhi ya pesa.
"Hii laki moja na nusu uta kaa nayo rafiki"
Aliongea muheshiwa Raisi na kufanya masai yule aruke ruke kwa furaha maana hakuwahi kuziona pesa nyingi kama zile,
Kwa furaha aliyo kua nayo masai yule aliwa ita wenzake na kuongozana mpaka gari lilipo na kuanzaa kuwa saidi kujaza mafuta kwa kutumia kikopo walicho kata.
Kilicho kua kina tokea pale na wale wamasai wana jikuta wana jenga urafiki na kuomba radhi bila kujua wanae ongea nae na Raisi wao,
Walipeaana mikono baada ya gari kuwaka na Alfred kutia gia na kuondoka zake,.
Alfred alizidi kutoa mbio, na mwishowe kusi mama kwenye mataa ya jiji la Arusha ambapo hapo alisubiri taa ya kijani iwake na azidi kusonga mbele,
Kweli taa za kijani zili waka na kuzidi kusonga mbele baada ya masa mawili na nusu tayari ali kua aki kunja kona ya NJIA PANDA mkoani kili manjaro,
Walizidi kutembea usiku kucha hata bila kuongea chochote,.
" Naomba simu nimpigie Mtoto wangu, najua wata kua na wasi wasi sana,"
Alfred hapo hakua na kipingamizi tena alitoa simu na kumkabidhi raisi ambapo alibonyeza namba za simu na kuiweka simu sikioni.
"Halloo Joyce my daughter, its me your Dad(halloo joyce binti yangu, ni mimi baba yako)"
Raisi Alphonce hupenda sana kutumia lugha hiyo ya kiingereza hasa ana poongeaga na mtoto wake huyo wa kike ambaye yupo kidato cha sita.
"Dad oh My God,. Dad where are you, ?, are you okay Dad?"(baba Mungu wangu , uko wapi? Uko salama baba?".
Mtoto wa Raisi aliongea kwa kutokua mini kile anacho kisikia sababu alimpenda sana baba yake kuliko mtu yoyote na ndo alikua nguzo ivyo baada ya kusikia sauti ya baba yake ambae alidhani ame kufa kwenye mlipuko wa ndege ana furahi sana na amani kumrudia wala si vinginevyo.
"Am coming sweet heart, Dad loves you so much, but honey do not let any one know we talked, (nakuja kipenzi, Baba ana kupenda sana, lakini kipenzi,usi mwambie mtu yoyote kama tuliongea).
"Dad i love you too, i won't tell any one, Dad please come back home, i miss you"(Baba nakupenda pia sitomwambia yoyote, Baba tafadhali rudi nyumbani nime kukumbuka"
Raisi Alphonce aliagana na mwanae huyo ambae ali mpenda kupita maelezo japo alikua na watoto wengi ila Kwa joyce Alimpenda sana na haku taka apate shida aina yoyote ile mpaka ana kufa.
Alfred alizidi kuchanja mbuga akiya pita magari mengine na sasa hivi tayari wali fika maeneo ya Korogwe amabapo ilikua ime timu saa saba mchana.,
"Raisi Alphonce , hakuna mlinzi yoyote wa ikulu una e muamini?"
Alfred alimgeukia Raisi na kumuuliza.
"Yaah yupo pale, Christopher,. Vipi kwani?"
"Mwambie saa kumi na moja jioni tuta kua ikulu,. Asimwambie mtu yoyote yule"
Raisi Alphonce alipiga simu kwa Christopher na kumueleza japo christopher hakuamini kama ana ongea na raisi Alphonce,
Baada ya hapo, Alfred alipiga gia na kwenda kasi ambapo mahesabu yake saa kumi na moja awe ame sha ingia ndani ya jiji la Dar es salaam na kumfikisha Raisi Alphonce salama salmin na hayo ndio yalikua mahesabu yake kichwani si vinginevyo.
Kweli baada ya masaa matatu tayari alikua kwenye msongamano wa mataa ya ubungo Terminal, ambapo baadae zili ruhusu na kusonga mbele.
"Alfred, tume fika sasa jijini,"
"Bado mpaka niku fikishe nyumbani kwako ikulu"
Raisi ali tabasamu na kubaki kumwangalia Alfred ambae wakati huo alikua makini juu ya usukani.,
Taratibu range rover iliingia ndani ya eneo kubwa la ikulu na kusimama nje ya mlango wa ikulu na Raisi kuwa wa kwanza kushuka, ila alivyo shuka Alfred walimuwekea bastola walinzi na huku wengine waki msogelea, na kufanya Alfred aweke mikono yake mbele na kusubiri kufungwa pingu ambayo mmoja wao aliitoa na kumuendea.
"Kuweni na adabu, huyo mnae muona hapo ina bidi mumpe heshima ya hali ya juu, wekeni silaha zenu chini haraka, Alfred karibu ikulu, ",
"Hapana Muheshimiwa Raisi mi nisha kufikisha niache niende kumwangalia mke wangu hajui kama nipo salama"
"Hiyo ni amri kama raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, ingia ikulu, nita mtumia gari nayeye aje"
Alfred aliangalia huku na kule hakua na sababu ya kukataa ivyo alijikuta nayeye anaingia ndani ya ikulu hio ya Raisi, huku akisindikizwa na walinzi, alikua yupo pembeni ya Raisi, moja kwa moja alifungua mlango wake na kuku tana na Mke wake pomoja na mtoto ambao wali mrukia kwa furaha sana raisi Alphonce.
Raisi Alhonce aliomba namba ya Mke wa Alfred na kupewa pale pale Raisi aliiweka simu masikioni na kuongea na Hannah ambapo baadae aliongea na Alfred.,
Raisi Alphonce alituma gari ambalo lilimfuata Hanaah na baadae kuonana na Alfred,
Sio siri haku taka kuamini hata kidogo, aliji kuta aki mrukia na kuanza kulia kwa furaha ,
"Hannah usilie nipo hai"
"Alfred, nakupenda sana"
"Mimi pia"
Hannah alijitoa kwake na kuji finya na kusikia maumivu, alijipiga tena kofi shavuni , hii ni kutokana na kwamba alidhani wenda ana ota, Alfred alimvuta kwake na kumkombatia.
"Haanah haupo ndotoni mke wangu,.Mimi ni Alfred nipo hai".
"Amna Siamini"
.
"Amini ivyo"
Kilicho kua kina tokea pale ili kua ni kweli na wala sio ndoto kama Hanah alivyo dhani,
Baadae Raisi Alphonce ana muomba Alfred waongozane mpka kwenye ofisi ya Waziri mkuu ambapo aliomba maaskari watatu waongozane nae,
"Nime rudi ofisini sasa,. Baadae naomba niandalie hotuba fupi nataka niongee na watanzania wajue kuwa nipo hai ,"
Raisi Alphonce aliongea na mmoja wa mmfanya kazi wake na kumshika mkono Alfred na kuingia nae ndani ya benz iyo ambayo wali funguliwa mlango, Alfred pia siku iyo alikua kama Raisi vile vile,.
Baada ya muda mfupi waliingia ndani ya ofisi ya waziri mkuu.
"Alphonce ndugu yangu, naota au?, sitaki kuamini ndugu yangu, na huyo ana fanya nini humu, Huyo Alfred muuaji"
Waziri mkuu ali msogelea Raisi Alphonce na kumkombatia kombatia huku akizuga ila ki ukweli ali shtuka kumuona mbele yake wakati mwingine ali dhani labda ana ouna mzimu ila alicho fanya aliji kaza.
"Kasanga,. Acha una fiki,, wewe ndo muuaji"
".hapana Alphonce"
Alfred haku taka kuongea chochote ali cho fanya ali pita mpka kwenye kiti cha waziri mkuu na kugusa chini ya meza ambayo kuli kua na kidude kidogo kili cho bandikwa na Amney siku chache zilizo pita, ambacho kili kua na kazi ya kunasa sauti .
Ivyo ali chukua na kuweka mezani na kidude kile kidogo kuanza kutoa sauti ya waziri mkuu kila kitu alicho kua ana ongea, na kufanya waziri mkuu atoe macho huku mapigo ya moyo yakianza kumuenda mbio kama umeme ,alijikuta ana kua mdogo na kukaa kimnya.
"Ongea sasa, nini hiki??, sindo wewe huyu?"
Raisi Alphonce ali ongea huku akimwangalia.
"Uli kua una msingizia Alfred uli taka nichume dhambi bure, sasa huu ndo uta kua ushaidi na uta wa taja wenzako wote"
Raisi Alphonce aliongea huku akiwa ita walinzi wake na kumfunga mbingu na kuondoka nae,
Raisi Alphonce alimwangalia Alfred na kumpa mkono huku akimpongeza na safari ya kurudi ikulu kuanza.
"Sasa Alfred naomba ukae humu ikulu mpka mkeo ata kapo jifungua, wewe ni muhimu sana katika hii nchi, ivyo nita kufanyia sherehe kubwa sana ya kimataifa kwa ajili ya mtoto wako atakae zaliwa, Alfred nita kufanya uwe mtu muhimu katika nchi yangu ya Tanzania, nataka uwe mtu wangu wa karibu sana,"
"Muheshiwa raisi nashukuru sana,"
Ndani ya ikulu waliongea pamoja huku pembeni akiwa na Hannah pamoja na Amney, ili kua ni furaha sana kwao.,
Baada ya miezi tisa kufika kweli Hannah aliji fungua mtoto wa kike na waka muita Roseline jina la maehemu dada yake.
Hapo furaha ili zidi kwa wawili hao na kama walivyo haidiwa na Raisi sherehe kubwa ili fanyika ambapo ili rushwa kila sehemu na viongozi mbali mbali wa nchi kualikwa,.
Ili kua furaha sana kwa Alfred na hanah.
"Alfred, nakupenda mume wangu"
"Hata mimi nakupenda mke wangu,Mama Roseline,"
Wote wali jikuta wana cheka kwa furaha huku picha za mnato zikiendelea kupigwa huku waandishi wa habari wakizidi kuwa sumbua.. .....
Maisha ya Alfred yali kua ya amani ambapo raisi Alphonce ali mpa zawadi ya nyumba kubwa ya kifahari yenye kila kitu ndani na kumkabidhi pia gari la kifahari aina ya BMX X6.,kama zawadi.
Na kupewa kitengo cha kuwa kama muhasibu mkuu wa nchi ya Tanzania ,
MWISHO.
*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 1/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 2/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 3/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 4/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 5/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 6/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 7/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 8/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 9/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 10 MWISHO
0 comments:
Post a Comment