Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 8/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 8 KATI YA 10


Baadae wali fika Nyumbani kwa Amina ,
hawa kua na muda wa kupoteza Alfred alichukua begi lake dogo lenye silaha, na kuanza kujiandaa pamoja na Amney vile vile. walimshukuru sana Amina na kumwambia atoe taarifa polisi juu ya maiti
zile,
wali kombatiana na Alfred pamoja na Amney na kuanza safari ya kuondoka,
Wakichukua gari ya Amina,
Gari akiwa anaendesha Alfred safari hii huku Amney akiwa pembeni yake.
"Wale ni F,b,i sijui wali juaje nilipo"
"Ooooh. Pole na kila kitu, sasa hivi tuna enda wapi?"
"Tukaweke mafuta hivi alafu nita jua cha kufanya Amney nashukuru kwa kuja"

Walizidi kusonga mbele.

Ila wana shangaa gari yao kutingishika baada ya kugongwa kwa nyuma, walivyogeuka wanaona jeshi la Harris wakiwa ndani ya gari nyingine aina ya BREVIS.
"Alfred hao hapo nyuma yetu"
"Wame juaje tupo huku"?
"Nipe simu yako"
Alfred alimkabidhi simu ile Amney nakuonekana kubonyeza bonyeza namba fulani na simu ile kutoa mlio.
"Oh my God, wana tumia satelite frequency Stn15, hapa wana tuona kila kitu, Alfred simamisha gari"
" mmmh, sasa ita kuaje,?"
"We simamisha gari tushuke haraka"
Alfred alipiga brek na wote kushuka, na kuingia katikati ya kipori kidogo kilichopo maeneo ya Mbweni,
na kuanza kukimbia kwa kutumia miguu, baada ya kufika mbele, Amney alitoa simu na kubonyeza bonyeza namba fulani na simu ile kuzima na baadae kuiwasha.
"Hapa hawa tuoni tena twende Alfred, nime kata Satelite yao hawa wezi, kutuona sasa",
"Ume kata kivipi,"?
"Kuna code nime andika hapa, najua wana tumia frequency ya aina gani"
Alfred alimwangalia mwana mke yule Amney na kushindwa kummaliza,

Walizidi kusonga mbele ndani ya miti hiyo na kuta futa sehemu wa pumzike ili kukuche waanze safari yao,
Ila baada ya kukaa kidogo wana ona miale miale ya tochi huku wakisikia sauti za watu zina kuja upande walipo.


Alfred alisimama kwa tahadhari taratibu huku akiweka kidole chake mdomoni kumuashiria Amney akae kimnya,
aliitoa MAGAZINE ya bastola yake ndogo na kuikagua kama ina risasi , alivyo ridhishwa na ukaguzi ule alitembea kidogo na kusimama wima nyuma ya mti mkubwa ambapo alitumia jicho moja kuchungulia upande wa mwanga wa tochi una pokuja,.
Baada ya kumfikia karibu , alivuta mkono wa mtu aliye shika tochi na kumuwekea kichwani ile bastola.
"Tulia "
Alfred aliongea neno moja tu na kufanya mtu yule adondoshe tochi ile na kuiweka mikono yake juu pale pale ,

Baadae watu wale waliji tambulisha kama ni wawindaji na Alfred kuwaachia waondoke.

"Alfred ina tubidi tuondoke eneo hili, si salama"
Amney alishauri huku akimuendea Alfred alipo na wote kuanzw safari ya kuondoka.
*************************

Ving'ora vya magari ya polisi vilizidi kupiga kelele huku vikiongozwa na mapiki piki meupe ambayo yaliyo jipanga katika msafara wa aina yake huku katikati yake kukiwa na gari aina ya BENZ jeusi ambamo ndani yake alikuwemo raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.ALPHONCE RENATUS MRIBA magari hayo yakiwa katika mwendo kasi huku madereva wengine wa piki piki wakiwa mbele wakifanya kazi ya kusa fisha bara bara maeneo.ya uwanja wa ndege wakielekea Tazara ambapo safari ya Raisi iliishia katika sehemu anayo ishi Ikulu,

Baada ya kufika ana funguliwa mlango na walinzi maalumu waliowekwa kwa ajili ya kazi hiyo na yeye kushuka huku akipunga mkono na picha mbali mbali za mnato akipigwa na waandishi wa habari huku wengine wakirekodi mikanda,

Baada ya hapo anaingia ofisi yake kubwa ambamo pia alifunguliwa mlango na yeye kuingia.

"Naomba Nizungumze na Partson Kasanga"

Alitoa agizo hilo Raisi Alphonce akimwambia mmoja wa wafanyakazi wake., ambapo bila kipungamizi alitii kauli hiyo.

"Sasa hivi muheshimiwa"
"Ningependa iwe sasa hivi"

Muda mfupi baadae waziri mkuu Partson Kasanga anaingia ndani ya ofisi ya raisi na kutoa tabasamu ambapo walipeana mikono na Waziri mkuu Kasanga kukaa katika kiti kilicho kua pembeni ambacho ni maalumu kwa ajili ya wageni.
"Pole na safari mh, Raisi,"
"Asante nashukuru, Partson Mbona sikuelewi?"

"Kivipi muheshiwa Raisi"
"Wewe ni rafiki yangu sana, isitoshe ni waziri mkuu pia wa Tanzania, mbona una kua una fanya mambo kiho lela olela Partson"?
"Bado sija kuelewa Alphonce"
"Any way, nisikilize kwa makini, naomba uniandikie chini karatasi zisizo pungua tano, unipe sababu ya kwanini F,B,I wapo hapa Tanzania, "
Habari ile kutoka kwa Raisi Alphonce ili mfanya Partson amwangalie ki umakini sana Raisi wake ambae wakati huo aliongea bila mzaha hata kidogo.
"Well, wapo hapa kwa ajili ya assigment muhimu sana, kula al shabaab h....."
"No Alphonce, kwani nchi yangu haina jeshi,;, ?, hauna sababu ya kujitetea, hapa!, ushaharibu, , yaani usha haribu,, "
"Hakija haribika kitu Alphonce, . Nakuhaidi hutojutia"
"Nenda kaendelee na kazi,, ila jua baadae ita kugharimu,, sasa mbona huku nishirikisha mpka napigiwa simu na raisi wa Marekani"?
"Nime ona nisi kusumbue ulivyo kua kwenye ziara"
"Nenda nita kuita baadae"

Raisi hakutaka kuongea mengi ivyo ali mruhusu Partson atoke ndani ya ofisi yake.
***************************
Amney na Alfred tayari walikua bandarini waki kata tiketi ya boti inayoelekea Dar es salaam ,
ambapo wakati huo Alfred kama kawaida alivaa kofia ya Duara kubwa huku machoni akivaa miwani kubwa ili yomfanya asi julikane na mtu yoyote yule.

Walipanga mstari ili kuingia ndani ya boti hiyo,
Baada ya kupata siti na kukaa boti tayari ilianza safari huku ikipiga honi na kuendelea kukata mawimbi,

Baadae Alfred ana simama na kutoka nje kidogo ya boti hiyo ambayo ukikaa kwa nje unaweza kuona maji ya bahari na mandhari yake kwa ujumla.
"He is making a move, stay closer(anasogea, kuwa nae karibu")
Yalikua ni mawasiliano ya simu kutoka kwa Harris akiwa pembeni yao huku akiwa na gazeti mkononi lililo mziba sura yake, akimwambia Carlos nayeye akiwa ndani ya boti hiyo na wenzake, ambao wali wa fuatalia na kuingia ndani ya boti bila wakina Alfred kujua.

"Copy(nime kupata").

Uliitikia upande wa pili ambao alikua ni Carlos aki mfuatilia Alfred mpka mwisho,

Alivyoona Alfred kasimama nayeye alisimama na kumpa mgongo ili kuficha sura yake asigundulike,

Alfred akiwa hana habari ameshikilia machuma akiangalia bahari na mawimbi,
ghafla alisikia sauti ya mtoto ikilia na kugeuza shingo yake ili kumuona mtoto huyo,
Ila macho yake ana yagandisha nyuma ya mgongo wa mtu aliye vaa suti nyeusi kwa muda mrefu sana,

"F,B,I WAPO KWENYE HII BOTI, UKO WAPI?".
ulikua ni ujumbe mfupi kutoka kwa Amney ambao Alfred aliufungua kutoka kwenye simu yake na kuusoma.,.
"NIPO HUKU NJE,TULIA HAPO HAPO USITOKE"
"POA, "
Baada ya kujibu kila kitu Alfred alirudisha simu yake mfukoni na kumuendea yule mtu aliye vaa suti na kumshika bega, kweli alivyo geuka aliiona sura ya Carlos bila kuchelewa alimpiga kichwa puani na ngumi mbili za haraka mbavuni na kufanya Carlos ajikunje na kujaribu nayeye kurusha ngumi ambayo ili pita hewani baada ya Alfred kuinama kidogo.,
aliinuka na kumpiga ngumi ya kidevu ili yomfanya Carlos ayumbe na kudondoka,
tayari watu wali kua wakikimbia huku na kule baada ya kuona fujo zile,
Alfred alikimbia ndani na kumvuta Amney mkono.

Na kuanza kukimbia nae Amney akiwa mbele alikutana na Harris ambae wakati huo alishika mkono wake kiunoni na kutaka kutoa bastola ila ana shindwa kutokana na Amney kumuwahi na teke ambalo lili mfanya adondoke chini,alivyotaka kusimama Amney alimkata mtama na kudondoka tena, purukushani ilianza ndani ya boti ile ya huku na kule , wali muacha Harris akiwa chini na wao kuanza kukimbia kuelekea upande wa juu wa juu ya boti ile ambayo ili kua na uwazi kwa juu.
"Paaaaaaaa"

Ulikua ni mlio wa risasi ambapo Amney alimuangalia Alfred na kumuona ana vuja damu mkono wa kushoto,
ili kua ni risasi ambayo ili penya moja kwa moja ndani ya mkono wa Alfred na kusababisha damu zimvuje, akitumia mkono wake wa kulia kuzuia damu zisi toke nyingi, ghafla ili pigwa risasi nyingine pale pale,

ila ili mkosa baada ya Amney kumrukia na kumkombatia Alfred na wote kujitupa ndani ya maji ya bahari hiyo ya Hindi.
F,b,i wale wali simama juu ya machuma ya boti na bastola zao wakiwa tayari kufyatua risasi tena, waki subiri wawaone wakiibuka ila hakuna hata mmoja aliye ibuka...
Baada ya kuogelea chini kwa chini huku Amney aki msaidia Alfred kutokana na jeraha alilolipata.
.baadae wana ibuka na kutoa vichwa nje wakivuta pumzi hewani ya kutosha na kubana pumzi tena na kuingia ndani ya maji wakiaya kata maji, walifanya zoezi hilo bila kukata tamaa endapo walio nekana kuchoka ,

Baadae wanakaribia nchi kavu na kutokea juu ya mchanga mweupe ambapo hawa kujua walipo,

Kitendo cha kuya kata maji yale kili onekana kuwa chosha sana na kufanya waheme kwa kasi sana,.

Amney alisimama na kuvua shati lake ambalo ndani yake alibakia na vest nyeusi,

alichana shati lake na kufunga jeraha la risasi mkononi mwa Alfred ili kuzuia damu zisi endelee kutoka.

Aliuchukua mkono mmoja wa Alfred na kuuweka begani kwake na kuanza kutembea wote,

baadae wana fika sehemu iliyo jificha na kumuweka Alfred chini na kumuacha lile eneo.

"Samahani kaka habari yako,eti naomba kuuuliza,.hapa tupo wapi?"

"Hapa Msasani"
"Naweza nika pata wapi Grocery au supermaket"?
"Duuu, hapa super maket labda uende kule juuu kule,. Una ona ile nguzo pale, sasa pale pale, nyuma yake kuna super maket, ila kama Grocery ile pale"

Mwana ume yule alimuelekeza huku akitumia kidole chake.
"Asante sana".
Aliangalia ile Grocery na kujua kua hatopata vitu vyote anavyo taka,
Alianza kutembea haraka haraka mpka kuingia ndani ya super maket hiyo na kuchukua pombe kali aina ya JACK DANIEL'S na mikasi midogo,.
Baada ya kurudi alimkuta Alfred akiwa amelala huku damu zikiwa zina mvuja bado.
"Alfred amka kwanza."
Amney alifungua ile chupa ya JACK DANIELS huku akifungua kidonda cha Alfred taratibu sana.
"Una taka kufanya nini?"
"Sikia, nataka kutoa iyo risasi, iki endelea kubaki ita sababisha sumu mwilini, shika hii pombe kunywa"

Alfred alimuangalia Amney kwa uma kini machoni na kufanya anayo taka, kutokana ndo aliyekua msaada wake pekee, alichukua chupa, aliiweka mdomoni na kukunja sura kutokana na uchungu wa pombe ile.

"Kunywa tena"
"Sasa hii ina saidia nini?, iyo ina spirit ina kusaidia usipate maumivu"

Alfred alipiga fundo lingine huku akiji kaza kisabuni.,
Baada ya hapo Amney alichukua chupa ile na kuimimina juu ya kidonda cha Alfred na kumfanya Alfred apige kelele na maumivu makali aliyo yasikia pale,

"Jikaze"

Aliongea Amney na kuchukua mkasi huku akianza kukata nyama ya juu ,
baada ya hapo ali tumbukiza kichuma kidogo na kuanza kuka mua risasi ili yo kua ndani na baadae risasi ile kutoka,
Amney Alichukua kitambaa kingine kisafi na kumfunga,
"Pumzika hapa,"

Maumivu makali alizidi kuya sikia huku akiendelea kupiga mafundo ya pombe ile, ila baadae alihisi kizungu zungu na kulala pale pale,
Kilicho mshtua kili kua ni chuma cha moto kilichokua kiki mgusa shingoni na kufanya akurupuke asubuhi hiyo.
"Tulia ivyo ivyo, na usija ribu kufanya lolote"

Ili kua ni sauti iliyo sikika kutoka kwa mtu aliye kua mbele yake huku mkononi akiwa na mtutu, pembeni yake aliwa ona wana jeshi watano wame mzunguka alivyo geuka nyuma ali muona Amney ana letwa na wanajeshi wengine huku wote wakiwa wame shika mitutu yao.


Kitendo kile kili mshtua sana Alfred na kukata tamaa akijua tayari ame kwisha maana wana jeshi hao hawakuwa na masihala hata punje,
wali muinua kama mzigo na kutokujali chochote, macho yake anayagandisha kwa mmoja wao ambae alionekana kuwa mkuu wao hii ni kutokana na kuona nyota zilizo kua begani kwake wote waliangaliana kwa kiasi sana kana kwamba kila mtu ana mfananisha mwenzake.
"Alfrend"
Yule mwana jeshi mkuu wao aliita huku akimsogelea Alfred kwa karibu.
"Allen Msangi?",
Allen ali msogelea Alfred na kumkombatia huku waki pigana pigana migongoni kwa furaha sana, wote walikua waki cheka kwa furaha, Allen alijitoa kwa Alfred
"Alfred siamini"
Aliongea Allen na kumkombatia tena wakipigana tena migongoni, kitendo kile kina washangaza sana wana jeshi wengine hata pamoja na Amney.,
"Msangi, Msangi,.. sitaki kuamini hata mimi! , yaaani wewe ndo ume vaa haya magwanda,?,"
"Nita kurusha kichura , aaah nakutania Alfred. , "
"Hahahaha,. Hujaacha tu, milima haukutani ila bina damu...."
"Wana kutana"
Allen alimalizia na wote kucheka, urafiki wa Allen na Alfred ulianzia tangu kipindi wapo o, level mpka waka fika A, level pamoja ila Allen ali fukuzwa shule baada ya kukutwa na kosa la kutoroka shule leo hii wame kutana tena kitendo ambacho ambacho hakuna aliye kitegemea.
"Eeenheeee nime kumbuka, hivi yule mdogo wako Rhoda Msangi, yupo wapi siku izi?"
"Yupo Ushirika hapo chuo, Alfred una kumbu kumbu,"
"Huyu nani, ndo shemeji?, ime kua kuaje mpka mmefika hapa na huo mkono vipi ?'"
Allen aliuliza swali lile baadaa ya kumwangalia Amney na kuuangalia mkono wa Alfred,

Safari ilianza ya kuondoka kuelekea kwenye kambi yao ambayo ili kua karibu na hapo.
"Ni stori ndefu sana, huyu anaitwa Amney nita kwambia ni nani., hapa nilipo natafutwa sana Msangi, natafutwa nchi nzima"
"Aaaaaah, nisha kumbuka nili sikia sikia ila sikujua kama ni Alfred wewe, mpka siku moja Rhoda aka niambia aliona picha yako, sikutaka kuamini kama ulikua Alshabab, "

Dakika chache tayari wali fika kambi hiyo kubwa ya jeshi iliyopo maeneo ya MSASANI kambi hiyo iliyo kubwa kiasi na Allen Msangi kupigiwa saluti ambapo wanajeshi walipo muona wali chapa miguu na kuweka mikono karibu na kichwa wakitoa saluti kuashiria kua ana epita mbele yao ni mtu mkubwa sana.
Pembeni akiwa na Alfred pamoja na Amney walipita ndani na kuoneshwa sehemu ya kupumzikia na Alfred kupelekwa chumba kidogo ambacho walianza kumpa matibabu ya mkono wake ulio pigwa risasi.
******************************

Upande wa pili Hanah Mulawa na jaqlin Nyange wakiwa nje asubuhi hiyo wakipiga stori na kuongea mambo mengi sana, hususani walimuongelea sana Alfred kutokana na kutowa pigia simu muda mrefu,
ivyo wana pata wasi wasi sana. Na kujua wenda amepatwa na tatizo au kasha kamatwa tayari.
"Hapana Hannah, naamini Alfred huko alipo mzima tu, wala usijali"
"Moyo una nienda mbio "
Baadae Hannah ana simama na kukimbia pembeni ambapo kuna mashamba na kuanza kuta pika, jaq haku cheza mbali nayeye alikua nyuma na kumshauri waende hospitali, kweli wazo lile lili tia nanga na wote kuanza kwenda hospitali ambapo hapa kua karibu na pale wana poishi.
Wana fika hospitali, Hannah ana pewa habari nyingine ambazo zina mshtusha sana kuwa ana ujauzito wa mwezi mmoja na nusu.
Baada ya kupewa dawa za kutumia ana rudi pembeni akiwa na Jaqlin Nyange ambae ndiye aliye kua mwenyeji wake na kurudi nyumbani.
Ilivyo fika jioni Jaqlin anaamua kutoka nje na kwenda dukani akimuacha Hannah ambae alikua nje nayeye kwenda kuta futa chakula cha kupika usiku ila baada ya kufika dukani ana kutana na wana ume watatu, ambao walimuangalia kwa kitambo na kumsalimia.
"Dada, samahani habari za saa hizi"?
"Sija ziandika"

Jaq alijibu kwa mkato na kuendelea kusonga mbele, na kuonesha kuto wajali vijana wale..
"Simama kidogo kuna kitu nataka nikuulize"
"Nina haraka"
"Mara moja tu"
"Semeni, dakika moja tu nawapa"
Jaq ali geuka na kuwatazama wote watatu na kumsikiliza yule aliye kua ana ongea.
"Kuna mtu tuna muulizia, huyu hapa"
Yule mtu alitoa picha na kumkabidhi Jaq ambapo aliiangalia kwa umakini na kuona sura ya Hannah Mulawa, juu ya picha ile.
"Alafu nisikilizeni,aliye waambia mimi polisi nani,?, kuweni na adabu, yaani mi nilijua kitu cha maana kumbe.... ninge jua nisinge simama, SIMFAHAMU, nendeni msikitini mkatangaze"
Jaqlin Ali foka na kumkana Hannah kama PETROL alivyo mkana Yesu,
kweli aliji fanya hamjui na kuwa chia misonyo mikali na kuendelea na safari yake, huku moyoni akibaki akiji uliza maswali mwenyewe na kuingiwa na hofu.
Haraka haraka alizidi kutembea na kufika nyumbani ambapo baada ya kufika haku mkuta Hannah, alizunguka kila kona na kumkosa, na kuanza kuingiwa na mashaka na wasi wasi, huku akiendelea kutembea huku na kule.
"Maaaaa maaaaaa, Haanah yuko wapi?"
"Alikua hapo nje"

Jaq alijiuliza maswali mara mbili mbili nje wapi wakati yeye yupo nje na hapa kua na dalili yoyote ya Hannah kuonekana,. Wasi wasi ulizidi kumwingia hasa giza lilipo zidi kutanda na dalili ya Hannah kutokuwepo,,
alikaa juu ya ngazi na kuzidi kuta fakari ata aanzia wapi kumwambia Alfred endapo ata piga simu na kumuulizia mke wake........


**************************
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG