Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 6/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 6 KATI YA 10

Alfred alivya tua risasi ingine ambayo ilipenya kati kati ya kichwa chake na Joyla kukata kauli pale pale,

Alfred aliitazama kwa muda maiti ya Joyla na kuingalia saa yake ya mkononi ambayo ili onesha ni saa tano za usiku,


Kiukweli maisha ya Alfred yalikua ni ya kuwindwa alikua akiishi kama ndege tunduni hakua na mahali ambapo angekaa kwa amani, alimkumbuka msichana aliye soma nae Chuo kikuu ambae alikua anaishi zanzibar,na kutoa simu yake na kubonyeza namba na kuiweka simu sikioni.

"Amina Shauri,Alfredy Mulawa naongea"

"Khaaa, Alfredy uko wapi?, hupatikani, Hanah hapatikani, alafu ime kuaje una tafutwa kiasi hiko nchi nzima, kama kitu gani sijui"?
"We acha tu, nina matatizo makubwa hapa nilipo YAAANI. nashindwa kuelewa kwanini"

"Pole sana Alfredy, sasa ina kuaje upo wapi?"

"Sikia Amina,. Nataka nije huko zanzibar, nitajie una poishi kuna mambo nataka uni saidie"

"Hakuna tabu,karibu sana , ila kuwa makini sana,."

"Nashukuru sana, sina sehemu ya kwenda huwezi amini, kila sehemu picha yangu ime bandikwa, kesho nitaaanza safari"

"Usijali kesho ukifika zanzibar, njoo mpka FORODHANI, uki fika hapo niambie maana ni karibu na kwangu"

Maongezi yaliendelea kupitia simu hiyo Alfred akimshukuru sana Amina kwa kitendo kile cha kumkubalia., aliweka begi lake sawa la mkanda mmoja na kuondoka huku akiacha damu za Joyla zikiwa zina churuzika.
*********************
Upande wa pili Waziri mkuu ana zidi kuchanganyikiwa baada ya kusikia Alfredy hayupo mikononi mwa jeshi la polisi ivyo ana wafuata waandishi wa habari na kuwaambia kuwa waandike habari kwamba Alfredy Mulawa ni mmoja wa kundi la Al shaabab,
Ivyo habari zile zina rushwa katika vyombo vya habari mbali mbali na kuzidi kutapakaa na kufanya wana nchi wata nzania kuwa makini sana na habari zile ambazo zina wafanya washtuke kupita maelezo.

"Kijana mmoja ashutumiwa kuwa ni miongoni mwa kikundi cha Al shaabab jina lake ana itwa Alfred Mulawa, popote mta kapo muona kijana huyu mtoe taarifa kituo cha polisi kilichopo karibu nawewe"

Ili kua ni taarifa ya habari iki tangazwa siku iyo huku pcha ya Alfredy kubwa kuonekana juu ya kioo cha t,v. Kila stesheni ili kua inatoa habari iyo na kufanya kila mtu awe makini kumtafuta Alfredy,
Kweli zoezi hilo lili fanikiwa huku kila raia wa Tanzania akiwa makini na sura aliyo kua ana iona.
************************
Tayari asubuhi kulikucha na Alfred akiwa bandarini akisubiri boti ya AZAM ambayo inge mpeleka Zanzibar akiwa amevalia Koti kubwa na kofia ambayo aliishusha chini iki mfunika uso wake ili yofanya mtu yoyote asiweze kumtambua,
Alikaa kwenye moja ya viti vilivyo kua ndani hapo maalumu kwa ajili ya abiria wana osafiri,

Kweli Alfred akiwa kama msafiri akiwa na abiria wengine huku akiwa ameshika gazeti alilojiziba nalo ambalo ukurasa wa nje ili kua picha yake kubwa ikiwa ime andikwa kuwa AL SHABAB ANATAFUTWA UKIMUONA PIGA 112

"Sasa al shabab washa ingia bongo, sijui ina kuaje mtu wangu"

Ilikua ni sauti iliyo sikika kutoka kwa nyuma alipo kaa Alfred ambao walishika gazeti lile lilichorwa picha ya Alfred mbele.
"Si una kumbuka waste gate, KENYA unaweza uka kuta hata humu wapo, maana wale tu dakika mbili tu wana lipua acha kabisa"
"Kazi ipo,.mi hapa mavi yanagonga, nasikia haja kubwa kwa kweli sina amani,hakuna amani tena"

Alfred aliwa sikiliza kila wana choongea bila kujua wanae muongelea nae yupo mbele yao tena anawasikia kwa kila kitu.
Alfred alihisi kama kuna mtu ame mgusa begani kuashiria kua ana taka kumwambia kitu, ila alihisi moyo unamwenda mbio baada ya kushusha gazeti na kuona mtu aliye valia nguo za kiaskari,
"Embu naomba tuongozane bwana mdogo"
Alfred hakua na jinsi zaidi ya kusimama na kumfuata yule askari bila kuongea nae chochote na moja kwa moja kwenda mpka MAPOKEZI.
"Kaka samahani naomba tiketi yako"
Alfred alitoa tiketi ile ya boti na kumkabidhi dada yule ambae alionekana kuikagua kiasi fulani na kutoa simu ya mezani huku akiiweka sikioni na kufanya Alfred kuutazama mlango na kujiandaa kwa chochote kile hasa kwa kukimbia.

"Eymer Kway, samahani nili kosea kuijaza hii tiketi yako, naomba niku badilishie samahani kwa usumbufu lakini,"
Dada yule aliongea na kuonekana akiandika tiketi nyingine, Alfred alishusha pumzi ndefu ili yochanganyikwa na uwoga kiasi.
"Samahani sana kaka angu"
"Bila samahani dada"
Alfred ali kabidhiwa tiketi yake ambayo ili kua na jina feki,
Abiria walianza kuingia ndani ya boti hilo la AZAM na safari ya kuelekea Zanzibar kuanza huku likitoa nanga,

Baada ya masaa machache boti lili tia nanga ZANZIBAR, na abiria kushuka ambapo Alfred alichukua bajaji na kumpeleka mpka Forodhani, baada ya kufika alimpatia Dereva yule pesa na kazi ya kuanza kumta futa mwenyeji wake Amina shauri kuanza,
Baadae ana kuja kuchukuliwa na Amina ambae ali mpeleka mpka kwake ,
Hapo ana oga vizuri na kutoa uchovu wote na baadae Amina kumuandalia chakula ili ale., baada ya kumaliza alishukuru na kukaa juu ya kochi kubwa huku pembeni Amina akiwa amekaa
"Amina, una jua sina muda wa kupoteza, kuna mtu namtafuta ana itwa Rodgers Mbita"

"Sasa Alfred, una mtafutaje mtu kama tupo darasani, huu mji mkubwa atiii"
"Sina maana hiyo najua pa kumpata kuna kikundi kinaitwa NO MITEGO, kipo michenzani nime ambiwa"
", ume sema NO MITEGO"?
"ya ndio, una lijua hilo kundi?"
"Ndio nalijua, nalijua ndio,"
"Sasa nita wapata vipi?"
"Si ume ambiwa michenzani ndo wapo ndo huko huko wapo",
"Ujue sasa hivi nata futwa hapa,kwaio naomba msaada wako, mbili mke wangu Hannah huko alipo sijui yupo katika hali gani sasa hivi,"
"Pole sana Alfredy, pole sana, sasa wewe huyo nani sijui Rodgers wanini?"
"Huyu ndo nita jua kila kitu, isitoshe kifo cha dada yangu na ukweli pia ndo ana ujua na wahusika vile vile, mi siwezi kuishi hivi "
Alfred alitoa simu mfukoni na kuiweka sikioni
"Una mpigia nani sasa?"
"Mtu ninae muamini"

"Yes Halloo Jaqlin Nyange,Alfredy naongea"
"Alfredy Alfredy, sitaki kuamini, mbona sielewi jamani, naona picha zako kuwa wewe ni Al shaabab, mara jambazi sugu, Hannah yuko wapi?"
" sikia nikwambie mimi nipo salama, ngoja nikwambie nisaidie kitu"
"Niambie Alfredy, naku sikiliza"
"Hannah yupo Bagamoyo kule kwa bi, zahara nenda kule usimwambie mtu yoyote yule, yaani mtu yoyote yule hata Mumeo Sirloom"
"Hata sirloom asijue,??.. Alfredy kweli hapo una nipa kazi huyu mwana ume alivyo kua mtata, lazima atataka kujua"
"Sikia fanya juu chini asijue mtu yoyote, nenda bagamoyo kwa Hannah kule, hakikisha yupo salama, nisaidie Jaqlin tafadhali"
"Mmhh Alfred sawa usijali"
"Sasa niki fika nimwambie nini?"
"Uki fika niambie please naomba usimwambie mtu yoyote yule"
Baada ya maongezi hayo kuisha Alfred alianza kupanga mikakati ya kwenda MICHENZANI kumtafuta Rodgers ila kabla ya kufanya lolote wali sikia mlango una gongwa wa wote kubaki kuangaliana na kujishauri.
"Nani anagonga"?
Amina Shaur aliuliza huku akiiinuka akiuendea mlango ule
"Sisi polisi"

Amina alisita na kusimama baada ya kusikia kauli hiyo na kumgeukia Alfredy ambae alibaki kumwangalia na kujiuliza maswali maaskari hao walijuaje kama yeye yupo pale.


kweli baada ya Amina kufungua mlango ali kutana na askari wa kipemba wawili wakiwa na virungu mkononi, na kuwa siliamia.
"Sijui niwa saidie nini ndugu zangu?"

Amina aliwa uliza huku akiwa ameufungua mlango nusu na shingo yake akiitoa nje huku kiwili wili kikiwa ndani.

"Kuna mtu tulimuona kaingia huku kwako,.nahisi kama tuna wasi wasi nae"!
"Kwaio ina maana mtu.akiingia humu ndo mna kua na,wasiwasi nae"?
"Hapana si una jua habari zili zotapakaa kuhusu Al shabab kwaio ina tubidi tuweke mashaka kidogo"
"Basi hakuna mtu aliye ingia humu ndani"
"Na hivi viatu hapa nje vya nani?"
Swali lile lili mfanya Amina ababaike kweli,
baada ya kuona viatu vya Alfredy ambavyo alivivua na kuviacha nje ya mlango.
"Hivi vya bwana angu Dibby. bwana eee nime choka na maswali yenu, huku hakuna mtu yoyote yule sawa eeeh kwaherini,"
Amina aliongea kwa sauti kubwa na kutaka kufunga mlango ila askari yule aliuzuia kwa mkono na kuusukumiza, kutokana na Amina kutokua na nguvu alijikuta akisukumizwa na kufanya askari wale kupita ndani, wasi wasi uli mwingia Amina na kugeuza shingo ila cha kushangaza alimuona mtu kavaa baibui aina ya NICAB ambayo hufunika uso mzima na kuacha sehemu ya macho mithili ya NINJA.
"We dada habari yako?"

Wali msalimia yule mwana mke bila kujua alikua ni Alfred ambae wakati huo ali kua ameshika kitabu cha shule na kuji fanya ana kisoma soma.
"Mwacheni mdogo wangu, mna mtisha embu fateni mlicho kifata."
Amina alifoka huku akimwendea Alfred ambae kwa wakati huo alikaa kimnya huku akiwa tazama kwa jicho moja la wizi, maaskari waliingia kuta futa kila chumba baada ya kuridhika wali rudi alipo kua Amina na kusimama.
"Huyo ndugu yako, baadae tuongee vizuri basi, nitunzie basi au sio"?
Kitendo cha Alfred kusikia maneno yale kilimuua sana ila hakua na jinsi ili bidi tu aji kaushe na kuku baliana na yote huku akijihami na kujiandaa endapo kwa yoyote atae jifanya ana msogelea umuoneshe kazi.
".embu mwacheni ndugu yangu, aliye waambia ana shida na nyinyi nani, embu nitoleeni UPUUUZI ovyoo"
Maaskari wale waliondoka huku wakiangalia angalia nyuma,
Kitendo cha maaskari wale kutoka Amina hakuweza kuvumilia kicheko chake,.alicheka mpka machozi yaakanza kumtoka

"Sasa una cheka nini??"
"Hahahahahha. Hahahaha. Alfredy una ua mbavu zangu, hahahahaha, uwiiiii Mtume wee, siku jua kama wewe ni msanii,kiasi hiko hahaha"
Safari hii Amina alicheka na kufanya mpka Alfred nayeye aanze kucheka.
"Alafu yule jamaa kanikonyeza nime m-ynd kweli, yaani laiti angejua mimi dume mwenzake"
"Sasa mimi nilivyooona tu umevaa lile bai bui kidogo nicheke ujue, sasa nikajiuliza huyu mwana mke kaja saa ngapi?, Alfred kumbe hujaacha vituko vyako"
"Iyo michezo ya kimafia ,ndo kazi zetu,. Embu tuachane na hayo nataka leo nimtafute Rodgers ikiwezekana"

Stori zili endelea huku bado Amina akiwa anacheka mpka Alfred akaanza kuchukia.
Jioni ilivyo fika na jua kuzama Alfred alivaa kofia yake kama kawaida na kuishusha usawa wa machoni bila kusahau miwani,.
Alichukua begi lake na kulivaa na kuelekea alipoelekezwa kikundi cha NO MITEGO kinapo patikana,
Aliwasha gari yeye akiendesha huku Amina akiwa pembeni yake ambae wakati huo ndo alikua aki muelekeza .
"Simama hapa, paki hapo pembeni,"
"Ndo hapa"?
"Una paona pale?"
Amina alimuonesha kwa Kutumia kidole cha kwanza na kufanya Alfred afuate kidole chake na macho yake kutua kwa wanaume wawili walioonekana kukaa juu ya gogo huku waki vuta sigara.

"Sasa sikia, Amina wee rudi niachie mimi"
"Mmhh Alfred, nirudi vipi sasa mwenyewe wakati tulikuja wote"
"Wewe rudi nita kupigia simu"

Kweli Alfred alishuka na Amina kuingia upande wa Dereva na hapo hapo kugeuza gari huku akimuacha Alfred akiwa ana waenda watu wale.

"Asaaalam aelekuy".
Alfred aliwa salimia kwa kiarabu watu wale huku akiwa pa mikono.
"Waelekuy muislam, vipi tuku saidie nini?."
"Aaah mbona ivyo ndugu zangu sikuja kwa shali, "
"Sema shida yako yaheee"
Aliongea mwingine aki tumia rafudhi ya kipemba.

"Namuulizia huyu mtu hapa, "

Alfred alifungua zip ya begi alilo livaa na kutoa picha ndogo ambayo waliipokea na kuanza kuiangalia angalia na baadae kumuangalia Alfred machoni.
"Wewe nani?, we askari au, au shushushu"?
Alfred kusikia vile ilibidi avue kofia yake na miwani ili waweze kumtambua, macho yalizidi kumwangalia Alfred kwa umakini wa hali ya juu sana.
"Nadhani hii sura mna ijua, sina muda wa kupoteza kuna kazi nataka kuwapa, nyie si ndo wazee wa kazi sio?"
"Wewe...wee Alshabab"
"NDIO,Naweza nika mpata vipi huyo mtu?"
Alfred aliongea huku akitoa bahasha ya kaki ambayo aliwakabidhi.
"Laki nne hizo, kuna kazi hapa ndogo sana kama kidole cha mtoto mchanga, nataka kuwapa, nawajua nyie NO MITEGO".
"okay sawa, ila kwa sasa hivi Rodgers hayupo, ame shikiliwa na polisi kule Forodhani, na kesi yake ina somwa kesho"
".aaaah, ni mbali na hapa"
"Hapana"
"Twendendeni"
"Wapi huko polisi?"
"Ndio, twendeni"
"Alafu we vipi, ame kamatwa,sasa twende tuka fanye nini?"
"Hahahaha, tuka vamie tumuokoe,"
Watu wale waliangaliana kwa macho ya mshangao, Baada ya Alfred kuongea vile , kweli alikua hana masihala hata kidogo, uchu wa kumtia Rodgers mikononi uli mkaba kooni.,
Walielewana vizuri na Kuondoka na Alfred ambako huko walimpa nguo za kuvaa na sasa safari ya kwenda kuvamia kituo cha polisi kuanza bila kujua nini nia ya Alfred,

Kwa kua kituo hiko kili kua karibu ili wapa kama dakika ishirini na mbili kufika nje ya kituo hiko waki paki gari ndogo aina ya PICK UP double cerben,

Wa kwanza kutoka alikua ni Alfred akiwa amevalia soksi usoni ambayo ili mziba na kuacha macho,
"Sasa Afande Mudi, yule mtoto si nili kutana nae pale kwa siku ile,"

Ili kua ni sauti ya askari aliye kua zamu usiku huo akiwa na mwenzake wana piga stori na kuji sahau ndani ya kituo kidogo cha polisi.
"Enhee, ikawaje sasa Masudi, we nawe humuogopi yule si mtoto wa shek"?
"Bwana weee, si sijali. Mtoto kaja kapendeza ana nukiaa kishenzi, nikaanza kumwagia cheche, mtoto akatae mara akubali, kumbuka hapo nili kua nisha kodi ch..... , we vipi?"
Askari yule alikatisha stori baada ya kumuona mwenzake ana toa macho kama mjusi kafili aliye banwa na mlango,
Aligeuza shigo na kuona watu wamevaa soksi usoni huku wakiwa na bastola mikononi.
"Tulia ivyo ivyo nipe funguo za selo, funguo za sero"
Askari yule alipigwa teke na kudondoka na funguo zile kuchukuliwa,
Baadae wana wafunga kamba na kumfungilia Rodgers Mbita ambae Alfred mwenyewe alim shika na kuingia nae ndani ya gari walilo kuja nalo.
Gari lili pigwa moto kutoka mbio., huku Alfred akiji tambulisha kwa Rodgers.,
Baadae Alfred ana muomba Rodgers watoke wote , bila kukataa na kuweka kipingamizi Rodgers ana jikuta akiingia kwenye mdomo wa mamba,
Wakiwa ndani ya gari Alfred alitoa bastola na kumuwekea kichwani.
"Hahaha, Alfred acha utani na bastola ujue, iyo sio nzuri kwa masihala., embu iweke chini , "
".paaaaaaa"
Aliishusha mguuni kwa Rodgers na kuifyatua juu ya paja la kushoto na kusababisha kelele na damu nyingi.
Alifungua mlango na kumtoa nje.
"SINA MASIHALA,.Nili kua nakuta futa kwa muda mrefu sana, Roselyn Mlawa alikua dada yangu kwanini ulimuuwa".?

Alfred aliikoki bastola na kuiweka tumboni kwa Rodgers bila kufanya mzaha wowote ule,.
"Ongea, kwanini ulimuuwa nani alikutuma?"
"Rose.. Rose,. Sawa nakwambia, aliyenituma waziri Mkuu"
"Kwanini alikutuma?"
" ili siri yake isivuje ya madawa ya kulevya Rose alikua ana jua mengi, na pia alitaka kukuua, na pia ndo yeye aliye fanya mpaka una tafutwa"
"Huwa una wasiliana nae vipi?"
"Kupitia simu ya mkononi"
"Mpigie sasa hivi"
Rodgers alitoa simu yake ya mkononi na kuita futa namba ya waziri mkuu na kuiweka simu sikioni.
"Vipi tena Rodgers, usiku usiku tena, ?"
Uli sikika upande wa pili wa simu ambao wakati huo simu ili kua LOUD SPEAKER,.
"Paaa paaaaa paaaa"
Alfredy alivya tua risasi ambazo zili mpata Rodgers na kudondoka chini,
Alichukua simu ile ambayo ilikua hewani muda ule.
"Waziri mkuu, una ongea na Alfred Mulawa:, sasa ama zangu ama zako,"
"Alfredy Mulawa, kwanini una tafutwa kiasi hiko, mi najua hauna hatia"
"Acha una fiki, sasa nakwambia hivi, nife mimi au WEWE, na nina kuja huko ulipo, damu ya dada yangu haiwezi kumwagika hivi"
"Alfred, ...ila u....., titiii"
Alfred alikata simu baada ya kujua ukweli na kuanza kuingiwa na kibarua kingine kizito cha kumuendea waziri mkuu


baada ya muda mfupi kweli ana rudi nyumbani kwa Amina na kumkuta Amina akiwa yupo jikoni ana pika, aliingia bafuni na kujimwagia.maji huku akitafakari sana jinsi ya kumuendea waziri mkuu, alijua hii ita kua kazi ngumu na nzito yenye kuhitaji akili ya hali ya juu na umakini pia kwa sababu ana ingia serikalini akijua kuwa sio lelemama,

Alitoka bafuni na kurudi kukaa baada ya kuhakikisha mlango ume fungwa vizuri.
Amina nayeye alikuja na kukaa nae pembeni na kumuomba amuhadithie kila kitu,
Kweli Alfred alianza kumuadithia tangu alivyo muacha pale na kwenda kumtoa Rodgers kituo cha polisi.
"Una hatari, kwaio mkaenda kufanya uvamizi, ennhee baada ya hapo ikawaje"?

Amina alikaa sawa huku akimtizama Alfred machoni na midomoni na kuwa sana makini kumsikiliza na kusahau kuwa chakula alikiacha jikoni.

Alfred aliendelea na stori ilivyo kua bila kumficha chochote na kumuelezea jinsi waziri mkuu alivyo fanya mpaka yeye ata futwe na kila mtu.
"Hapa nishaanza kupata pcha Alfredy , ujue kakuzushia ivi ili ukamatwe utiwe ndani ili usitoe siri yake"
"Mimi.mwenyewe ndo nafikiri ita kua ivyo"
"Sasa unadhani uta fanya nini jamani, pole sana, mimi ninge kua wewe aisee sijui inge kua kua je"
"Ina nibidi niende tu, sina jinsi, acha nimalize tu Amina"
"NO Alfredy, huwezi kwenda mwenyewe, tafuta ataeku saidia."
Amina alitoa ushauri huo na kumuomba Alfred asiende mwenyewe.

Kweli Alfred aliwaza sana na kutoa simu yake ya mkononi baada ya kuku mbuka kitu, aliangalia kwa muda na kukosa namba anayo ita futa na kuikosa, ivyoo aliamua kuinuka na kwenda kwenye begi lake dogo na kutoa kitabu kidogo chenye namba za simu, alifungua fungua kitabu hiko kidogo mpka aliipoona jina AMNEY CIA., na kuandika namba za simu ambazo zilijitokeza juu ya kioo cha simu , alivyo hakikisha aliruhusu simu ile iende baada ya kuminya kitufe cha kijani.
"Halloo, Amney,. Unaongea na Alfredy"
"Alfred, Alfred Alfred mhh yupi huyo, jita mbulishe vizuri Alfred wapo wengi"

Upande wa pili wa.simu ulisikika kweli aliijua sauti hiyo ni ya Amney . Aliguna kidogo na kukaa kimnya.
""Alfredy Mulawa, tuli kutana Afrika Kusini , Alfred Mtanzania tukamuuwa Mujuni, kumbuka vizuri"
"Aaaah aaah Alfredy Mulawa nisha kukumbuka, uko wapi?, siku tegemea simu yako leo, niambie wangu"
"Amney uko wapi sasa hivi"?
"Nipo Kinshasa ,Congo DRC huku, nipo likizo"
"Amney nina tatizo kubwa nahitaji msaada wako, naomba uje Tanzania. sina mtu yoyote yule wa kumuomba msaada,yaani wewendo kimbilio langu"
"Una tatizo gani Alfredy tena?"

"Naomba uje kwanza"
"Hapana Alfredy siwezi kuja, mi nipo likizo una jua kabisa,"
"Tafadhali, nina tatizo kubwa Amney,naomba uje Tanzania Zanzibar, nipo chini ya miguu yako"
"Aisee , vipi kwanza Rose mzima"?
"Siku kwambia Amney, Rose alifariki, alipigwa risasi, ndo maana nakuit....."
"Subiri subiri. Amefariki, ?, kivipi, ime kuaje?, aliumwa au?"
Amney upande wa pili aliuza kwa jazba baada ya kusikia habari zile ambazo zili muumiza sana moyo wake na kuguswa sana.
"Naomba uje, walimuuwa ni hii serikali ya Tanzania,hapa napokwambia nata futwa sana"
"Hannah, Hannah, Hannah je mzima?"
"Hannah mzima"
"Okay Alfred nakuja Zanzibar wiki hii nita kua huko nitumie location uliyopo, niweze kujua mpka ulipo Alfred pole sana, kwa hili nita kuwa nawewe bega kwa bega, Alfred nakuja, nakuja Alfredy, ila kwanini hukuniambia, nije hata nimuage Rose?"
", Nashukuru sana Amney nakushukuru sana, nili changanyikiwa Amney samahani kwa kutokukwambia"
Simu ili katwa na kumwa ngalia Amina ambae wakati huo alikua mezani akiandaa chakula cha usiku.,

Alfred tena alichukua simu na kumtafuta Jaqlin Nyange hewani na kutaka aonge na mke wake Hannah.
"Haanah sikia, nenda kaji fiche Moshi. Nenda kwa kina Jaq nakuomba nita kwambia kila kitu."
"Alfred mi naogopa mume wangu"
"Hupaswi kuogopa, Jaq ata kupeleka huko kwao, ni sehemu iliyo tulia hakuna atakae jua ulipo nakuomba tafadhali, niamini"
"Sawa Alfred, nakuamini, kuwa makini. Nakupenda sana"
"Namimi pia nakupenda mke wangu, naomba niongee na Jaq"
Jaquee Nyange alipewa simu na kupewa maaagizo kila kitu jinsi ya kuji ficha mpaka atakapo fika kwao Alipo kulia mkoani Kilimanjaro, kijiji cha Mwika,
, kweli wali kubaliana na simu kukatwa ,

Alijua anaenda kuanza vita nzito ambayo hakuwa na uhakika kama angeenda kushinda hata kidogo ila kilicho kua kina muongoza wakati huo ni ujasiri na kujiamini kwake.
siku zote Alfred alifikiria ushindi tu hakuwahi kufikiria kitu KUSHINDWA katika maisha na ndo maana siku zote huwa ana shinda na kutokata tamaa,
Alfred aliienda mezani ambayo ili kua maalumu kwa ajili ya kula baada ya kukaribishwa na Amina shauri ambae alimtengea kila kitu mezani na kumna wisha mikono yote miwili,.
Na baadae wote kuanza kuka huku waki kumbuashiana mambo mbali mbali ya shule.
*****************************
Kila alicho kishika waziri mkuu Kasanga alikiona kichungu.
Wasi wasi na hofu vilizidi kumtanda moyoni mwake hasa akifikiria vita ambayo aliianzisha chini chini ambayo hakuna mtu yoyote anayo ijua hata raisi wa jamhuri ya Muungano hakuwa anaelewa lolote lile, aliwaza sana maneno aliyo ambiwa na Alfredy, na kumfanya akose raha ya maisha,
Akiwa sebleni kwake huku mkononi akiwa ameshika GLASS ilikua ime jaa pombe aina ya wyne.
Alipiga fundo ndefu mpka akaimaliza na kuongeza nyingine, aliangalia saa ya ukutani ambayo ilionyesha ni saa tisa na dakika arobaini na saba usiku,
Alijiinua huku akibeba GLASS iliyo jaa pombe ile na kupandisha ngazi akielekea chumbani kwake ambapo alimkuta mke wake Flora akitoka bafuni akiwa na taulo lilimfunika maziwa na kuacha mapaja yake nje, alimuangalia kwa kitambo sana.
"Mbona una niangalia ivyo kama CHURA masika, vipi una taka kunimeza"?

Mke wake huyo ambae alikua na sifa ya kuongea maneno mengi alimuuliza Mume wake swali ambalo Kasanga , aliachia msonyo mkali na kukaa juu ya kitanda na kuendelea kupiga fundo la wyne iliyo kuwemo ndani ya glass.
"Nikuangalie una nini?"
"Alafu siku hizi sikuelewi elewi we mwanaume"
"Hunielewi kivipi, embu lala"
"Yaani sijui ume kua kuaje, ume kua mtu wa wasi wasi na.mashaka muda wote, kama jambazi, au ndo ushaiba ela ?"
"Embu we mwana mke nyamaza , nita kuzaba makofi"
"Weeee subutuu, ndo uta jua siku iyo mimi ni nani,,, jaribu uone tuta pigana humu mpka kieleweke"
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)


0 comments:

Post a Comment

BLOG