Search This Blog

Monday, March 23, 2020

ABEE SHEMEJI SEHEMU YA 4/10


ABEE SHEMEJI
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 4 KATI YA 10
*******

Shinikizo la ndoa ya Ahmed lilipelekwa mputa mputa,nyuma ya yote haya kulikuwa na mwanamke huyu Yusrath ambaye hakutaka kujifungua akiwa nyumbani kwao.Licha ya hayo tumbo lake lilikua kubwa tayari,haikuwa siri kama ilivyokuwa hapo awali,hata Baba yake mzazi alilijua
hilo.Kilichokuwa kinamuumiza Ahmed ni namna ya kuishi na mkewe,angeishi wapi?Kwao?Hapana!Hilo hakuliafiki,kichwa kilimuuma kwa kuwaza sana,isingekuwa ni ghafla kuhama namna hiyo,alichokifanya ni kumueleza baba yake kila kitu akamwambia hali halisi,akampelekea hoja hiyo alikuwa ni mtu mzima lakini alikuwa akiwadekea wazazi wake kwa mbaaaali.
“Hilo pia,linaniumiza kichwa mwanangu.Japokuwa unataka kuoa bado mdogo sana!Anyway,nitafanya utaratibu wa kukupangishia nyumba.Alafu nipe mwaka mmoja,nitakupa sehemu ya kujenga.Hiyo itakuwa kama zawadi yako kutoka kwangu na Mama yako”
Kidogo Ahmed,akapata mwanya.Kuna mzigo fulani aliutua wa mawazo,shukrani alizotoa kwa wazazi wake hazikuweza kuelezeka kiwepesi,Mzee Kajeme hakutaka kuliweka swala hilo kiporo,kesho yake akaanza kutafuta nyumba za kupanga,alitaka kumpangia mwanaye sehemu nzuri tena nyumba nzima.
Mpaka usiku, alifanikiwa kupata nyuma tano!Zote zilikuwa nzuri lakini asingeweza kuchagua,ilibidi Ahmed ashirikishwe ili aridhie mwenyewe.Hicho ndicho kilichofanyika!
“Washa gari,tunaenda Ubungo Kibangu”
Ahmed akapewa funguo asubuhi iliyofuata,baba yake akaketi kushoto!Safari ikaanza na kuishia Ubungo Kibangu,ambapo huko kulikuwa na nyumba nzuri kubwa,walivyotoka hapo wakapita Kurasini wakakagua, bila kupoteza muda wakapitia Mbezi na wakaunganisha na Kimara mwisho wakamalizia na Upanga!Huko kote kulikuwa pazuri.Lakini alipapenda zaidi Ubungo Kibangu,palikuwa pametulia na nyumba ilikuwa na vyumba viwili seble kubwa na jiko.Hakusita,akamueleza baba yake!
“Umepapenda pale Ubungo?”
“Ndio Dad”
“Nitakulipia kodi ya mwaka mzima pale,lakini kuhusu vitu vya ndani.Hapo,utajua mwenyewe.Ushakuwa mtu mzima,haya yote niliyokufanyia sio kazi yangu.Mimi sikufanyiwa hivi,maisha yangu yalikuwa ya shida sana, Mwanangu.Pambana sana,mpende sana mkeo!Muombe pia Mungu,alafu sijawahi kukusikia hata siku moja unaenda Msikitini kuswali”
Baba akaanza kutoa lisala wakiwa ndani ya gari wanarudi nyumbani,maneno hayo yalimuingia vizuri sana Ahmed,akayaelewa na kuhaidi kwamba atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo.Hilo ndilo lilikuwa la msingi,taarifa hizo hakutaka kukaa nazo kifuani,akampasha habari Yusrath kila kitu kilichotokea.
“Mwambie Baba ahsante,mpe shukrani sana.Nitampigia simu nimshukuru”
Yusrath alizungumza kwa furaha siku hiyo,akajua tayari mambo yanaenda kua mazuri na siku za usoni angeenda kuishi na Ahmed,watumie kitanda kimoja na shuka moja kila siku. Ilikuwa ni hatua kubwa sana kwake,aliamini angeishi maisha yenye, furaha na rahaa mustarehe,swali lake likawa ni kila siku ni lini wangeanza kuishi pamoja?
“Baby,mpaka ninunue kwanza kitanda kikubwa”
“Sio kila kitu mpaka ununue wewe mme wangu,nina salio kidogo kwenye akaunti yangu”
“Baby,acha bwanaa”
“No,siwezi kuacha.Nitakutumia laki nne baby.Nunua kitanda love,ama itasaidia kuongezea popote pale”
“Sawa love”
Wakati Ahmed na Yusrath wakiwa na furaha, yeye Kassim alikuwa amepata wazo la kipumbavu,kwamba amtingishe Yusrath ikiwezekana atumie siri hiyo ya mimba kama fimbo ya kumchapia,akili yake ilimtuma amgeuze awe mtumwa wa ngono kwake.Hilo ndilo lilikuwa kichwani kwake na aliamini jambo hilo lingefanikiwa kwa asilimia zote mia moja,alichokifanya siku hiyo jioni akajaribu kumpigia tena simu, Yusrath.
“Yusrath…”
Kitendo cha Yusrath kupokea simu,akaita jina lake.
“Abeee”
“Unajua unaongea na nani?”
“Hapana”
“Mmmh,Kassim hapa”
“Kassim,yupi?”
“Aaaaah,shemeji yako!Mdogo wake Ahmed”
“Ooooh shem,mambo vipi?”
Yusrath,akajifanya kumchangamkia na kuingizia jina la shemeji ili heshima iwepo kwanza.
“Safi tu,umenitupa sana.Namba umebadili hata kuniambia”
“Simu yangu,iliibiwa”
Akadanganya.
“Pole sana,lakini pia hongera”
“Hongera ya nini?”
“Mambo mengi”
“Kama yapi?”
“Kutaka kufunga ndoa,Mama Kijacho”
Hapo Yusrath,akakaa kimya kidogo.
“Ahsante”
“Naona unataka kuniletea anco”
“Tuseme Insa Allah”
“Mmmmh”
Hapo Kassim,akaguna kwa sauti.Akameza mate kidogo ili aanze kumpa Yusrath vidonge vyake.
“Yusrath,hivi unatuchukuliaje?”
“Sijakuelewa,kuwachukuliaje kivipi?”
“Unamchukuliaje Kaka yangu,boya boya eeh?Ama kweli boyaa”
“Kassim a…”
“Subiri sasa,nikwambie kitu.Najua kila kitu,hiyo mimba sio ya Ahmed.Naelewa ukweli wooote,mjinga wewe.Huna akili hata kidogo,sikutegemea na lazima Ahmed nimwambie”
Sio siri,japokuwa habari hizo zilimshtua Yusrath lakini hakutaka kulionesha swala hilo waziwazi,hakuwa ana uhakika kama Kassim anatania ama yupo siriazi.
“Umemaliza?”
Yusrath,akauliza kwa kiburi chote.
“Ndio nishakwambia namwambia”
“Hah ha ha hahahaa,ujuwe unanichekesha,alafu unasikitisha kwa wakati mmoja.Leo umekunywa pombe gani?Chang’aa au mnazi?Au akili zako hazipo sawa au hujameza dawa zako?Unataka nini kutoka kwangu?Nilishakwambia sikutaki achana namimi”
“Ni hivii,kwanza sikutaki cha pili kuhusu ndoa sahau hilo nakuhakikishia,huyo mtoto sio wetu.Walai,sikutegemea kama wewe ni muhuni namna hiyo.Nashindwa kuamini”
“Wewe,unataka nisifunge ndoa kama nani?Subiri nikuoneshe kwamba mapenzi yana nguvu gani.Tambua kwamba nina uwezo wa kufanya kaka yako akuchukie maisha yako yote,hilo liweke kichwani alafu jambo lingine.Chezea vyeupe,vyekundu vitakutia doa”
Yusrath,alizungumza kwa hasira alafu kitu kingine alikuwa anajaribu kujihami ndiyo maana akawa mkali kama mbogo,Kassim hakukubali akaendelea kumsisitizia akimwambia mimba sio ya Ahmed.Kassim,alizungumza kwa jazba na ghadhabu akiwa chumbani kwake,mlango wa chumbani upo wazi bila kujua anayozungumza yote, AHMED aliyasikia sababu alisimama karibu na mlango!


Hakuna siku aliyotibuka kama hiyo,Yusrath alikasirika kwa kiasi cha kutosha kwani Kassim alikuwa amegusa mshono kwa kumwambia ukweli kuhusu Mimba aliyokuwa nayo haikuwa ya Kaka yake Ahmed,alielewa angekaa kimya na kuanza kuomba msamahaa ingekula kwake, ndiyo maana akawa mkali kama pilipili mbuzi,akamfokea Kassim kama mtoto mdogo vile.Akapaza sauti na kumwambia hamtaki, akitumia gia ya kwamba Kassim anasema hivyo kutokana na wivu aliokuwa nao!Alichokifanya Yusrath ni kumuhakikishia kwamba mimba ilikua ya Ahmed,alivyomaliza kumpa vidonge vyake hapohapo akakata simu na kusonya.Usiku huo, alihangaika vya kutosha,akajaribu kuunganisha matukio mbalimbali.
“Stupid na nitamkomesha”
Yusrath,alizungumza maneno hayo kwa ghadhabu, akachukua simu na kuiweka sikioni ili ampigie simu Ahmed!

***

Kama mwanamme jambo hilo alilitafsiri kama dharau,akashikwa na hasira sababu katika maisha yake hakuwahi kutukanwa na kuchambwa na mwanamke namna hiyo,akajiona kama yupo uchi mbele za watu,Kassim alikasirishwa na kitendo hicho.Alivyotaka kusimama kutoka nje, akaonana uso kwa uso na Ahmed,ambaye alikuwa anatabasamu mlangoni.
“Broo,umerudi saa ngapi?”
Kassim,akauliza kwa uwoga kidogo!Hakuwa ana uhakika kama Ahmed aliyasikia mazungumzo yake ama la.Ndiyo maana alibabaika kidogo.
“Nipo muda mrefu,nani anazingua tena kwenye simu?”
Ahmed akaibua swali,lililomfanya Kassim atafakari kidogo.
“Broo,ngoja nikwambie ukweli”
“Nini tena?”
“Si huyo Yu…”
Kabla ya Kassim kumalizia sentensi yake simu ya Ahmed ikaita,ilikuwa ina umuhimu sana kwani ilitoka kwa Yusrath kumaanisha kwamba ni lazima aipokee,hakutaka tena kumsikiliza Kassim, akatoka na kuingia chumbani kwake.
“Baby”
Kitendo cha Ahmed kupokea simu,akaita kimahaba majina kama hayo kwao ilikuwa kawaida, kuitana.
“Darling,naomba nikwambie kitu.Nadhani naenda kurudia tena kwa mara nyingine,sipendi kuwagombanisha lakini naomba umwambie mdogo wako aache kunisumbua awe na adabu”
“Kafanya nini tena?”
“Sio kafanya nini?Nina uhakika wewe ndiye umempa namba zangu”
“Sikatai,amefanya nini?”
“Hujui?Kwani sikuwahi kukwambia ananitaka”
“Uliwahi kuniambia”
“Sasa umechukua hatua gani?Au nimkubalie,sema tu”
“Ngoja subiri ,punguza jazba.Nitamwambia asikusumbue”
“Sasa hivi baby”
“Okay subiri”
Ahmed,akashusha pumzi kidogo nzito ya ndani kwa ndani.Akatupa simu juu ya kitanda na kufungua mlango wake,akamuomba Mungu asije kumvunjia heshima mdogo wake, sababu alizijua fika hasira zake zilivyokuwa chafu.Alivyofika,akagonga mlango na kuingia chumbani kwa mdogo wake!
“Kassim”
“Yes Broo!”
“Kuna kitu nataka kukwambia”
“Kitu gani?”
“Mimi ni nani yako?”
“Kaka”
“Nimekuzidi miaka mingi sana,unapaswa kuniheshimu..Umenielewa?”
Hapo kidogo Ahmed alizungumza kwa ukali huku akimyooshea kidole ingawa alijaribu kuweka tabasamu la plastiki usoni ili asimtishe mdogo wake,japokuwa hasira zilianza kumpanda taratibu, hilo akajaribu kulizuia lakini hakuweza.
“Ndio nimekuelewa”
“Naelewa wewe ni kijana na nafahamu vizuri starehe yako ni mademu lakini sasa nachokuomba,usimsumbue Yusrath.Mwache kama alivyo,anaenda kuwa mke wangu!Muheshimu kama shemeji yako….”
“Lakini br…”
“Nimemaliza,wewe ni ndugu yangu tusitafutiane ubaya.Mwanamke asitufanye tujenge uadui,hawa wapo!Nadhani nimeeleweka”
“Okay,poa”Kassim nayeye akajibu kwa hasira!
Ahmed,akamaliza kuzungumza anayotaka kusema!Akarudi chumbani kwake na kumwambia Yusrath awe na amani kwani kuanzia siku hiyo,ataishi kwa rahaa mustarehee kabisa.

****
Mapenzi yao yalikuwa kama makinda ya njiwa,kila kukicha simu.Yusrath alideka simuni,akawa hali bila kumuuliza Ahmed.Mara ghafla aina ya vyakula vikabadilika,akawa anapenda sana kula vitumbua,mara juisi ya ubuyu,akaenda mbali zaidi na kuanza kula nazi na mchele mbichi.Hiyo haikushangaza watu sababu alikuwa ni mjamzito,wakati siku zinazidi kwenda mbele.Mipango ya harusi ilikuwa imepamba moto.Alichokitaka Yusrath ni kitu kimoja tu, aishi nyumba moja na Ahmed kwa maana hiyo ajifungue akiwa tayari mke halali wa ndoa.
Hiyo ilifanya ampeleke mputa mputa Ahmed,ambaye hata yeye ilibidi awashirikishe wazazi wake,hilo halikuwa tatizo, wazee wakaitwa pamoja na wajomba ili kujadili shauri hilo zito,walivyoteta na kumaliza.Wakamrudia Ahmed,tarehe ikapangwa!
“Sawa,ifanyike tarehe sita mwezi wa nane,itakuwa Ijumaa.Baada ya hapo,sherehe Jumamosi ama Jumapili”
“Hakuna shaka,tutafanya taratibu”
Swala la ndoa ya Yusrath na Ahmed halikuwa siri tena,ndugu jamaa na marafiki walipewa taarifa hizo na walitakiwa kuchanga ili kuudhuria kwenye sherehe.Swala hilo lilivyomfikia Benjamin Ngowi akalipokea kwa moyo mkunjufu kabisa,akalivaa kama lake.
“Sasa best Man,ushampata?”
Benjamin Ngowi siku hiyo akauliza swali.
“Ndio,ni wewe hapo”
“Mimi haiwezekani,mimi mkristo.Wewe ni Muslim,isitoshe mimi bado sijaoa”
“Kwani lazima?”
“Ni lazima,hiyo ni ndoa.Sio Kipaimara ama komnio.Kuwa siriaz tafuta mtu unayeendana naye mkuu”
“Benja,nimekuzoea wewe”
“Sikatai,lakini haiwezekani mimi kukusimamia.Tena ndugu yangu,tafuta mtu mwenye akili zake.Sababu matatizo yako yooooote ya ndoa,yeye ndiye mtatuzi sasa akili kumkichwa”
Hapo Ahmed,akapata kibarua kingine cha ziada.Kichwani kwake akaanza kuwaza ni rafiki yake yupo ambaye angeweza kusimamia harusi yake awe kama mpambe wake,marafiki zake wengi wakaja kichwani kwake akaanza na Ali Mwarabu huyu akaziangalia tabia zake akaona hazifai skendo yake ilikuwa ni chafu,akamkumbuka Hassan Ukwaju mtoto wa Ostadh, akachambua mambo yake na mwenendo wake akagundua ana kasoro fulani na wasingewezana,akatafakari zaidi na sura ya Abdulaziz Kamata ikamjia kichwani kwake,akakumbuka chuoni Makumira,yeye yupo mwaka wa Kwanza Abdulaziz Kamata mwaka wa tatu,akazichuja tabia zake.
Akakumbuka maisha ya chuo,mwanamme huyo alikuwa mstaarabu na alikuwa ana sifa zote kwani alikuwa keshaoa tayari.Usiku huohuo,akafanya mawasiliano na baadhi ya marafiki zake ili apewe namba za mwanamme huyo.Alivyopata hakutaka kumpigia usiku huo,akasubiri kupambazuke.
Alivyotaka iwe,ndivyo ilivyokuwa!Kulivyokucha,akampandia hewani.
“Unaongea na Ahmed Kajeme?”
Ahmed,akaanza kujitambulisha.
“Kajeme?Yupi?Wa Makumira?”
“Ndio Kiongozi”
“Mdogo wangu,umenikumbuka leo?”
“Kila siku nakukumbuka Bratha,sema ndio kutingwa.Pilika pilika”
“Nipe mpya”
“Kuna jambo nahitaji tuzungumze”
“Jambo gani hilo?”
“Upo Dar es salaam?”
“Hapana,nipo Mwanza”
“Duu,lini utakuwa na nafasi uje?Nitakutumia nauli,ni jambo Muhimu sana”
“Ni kitu gani hiko?Mbona unanitisha mdogo wangu”
“Nataka kufunga ndoa,nimekuchagua wewe uwe msimamizi wangu”
“Anhaaaaa…Sasa ungesema hivyo,mbona jambo dogo hilo!Tunaongea hata kwenye simu”
Ahmed,akafurahi roho yake ikawa nyeupe.Hakujua kama mambo yangekuwa marahisi namna hiyo,Akamuelezea Abdulaziz Kamata kila kitu kinavyokwenda, mpaka tarehe ya ndoa,kila kitu akakiweka wazi kabisa,Abdulaziz Kamata hakuonesha kusita akakubali na kumuhaidi asingemuangusha kwenye jambo kama hilo ambalo lingekuwa la kihistoria katika maisha yake.

*****
Tumbo lake lilikuwa kubwa tayari,kila mtu alijua kwamba ana mtoto tumboni.Hiyo haikuwa siri tena,hakuweza tena kutembea kwa mwendo mrefu, sababu alichoka sana!Akawa anajifungia ndani,kama kutoka ni mara moja sana!Japokuwa alikuwa ana tumbo kubwa la mimba,wanaume hawakuacha kumsumbua hata kidogo,waliendelea kumgasi wakimtongoza!Mimba yake haikufanya shepu yake iharibike,zaidi tu alizidi kuwa mnene,akanona vizuri.Mashavu yake, yakawa makubwa kiasi!Hiyo ilifanya kila mwanamme amtolee udenda, mbaya zaidi alikuwa anavaa madera ndani havai kitu jambo lililofanya akipita atingishike yaani ‘tentemente’ kwa Kiswahili cha geto,hakuwa ana makalio makubwa sana lakini alikuwa mwenye nyama laini.
“Wewe ni mzuri sana Yusrath,wakubwa wana faidi.Mbona hutaki kunikubalia?Naelewa una mwanamme namimi nipe nafasi yangu”
“Acha kunielezea huo upupu,unanitia kichefu chefu.Achana na mimi Sangu,nielewe.Nina mwanamme hivi huoni hata aibu hali niliyokuwa nayo?”
“Aibu naona lakini siwezi kuizuia”
“Basi,pambana na hali yako”
“Hali yangu ni wewe ndio napambana nayo”
“Siwezi kuwa nawewe,nampenda Mme wangu”
“Hata mimi nakupenda wewe”
“Lakini mbona mbishi,ngoja nimwambie mwenyewe”
“Ili iweje?Acha hizo habari za kizamani,nifikirie namimi”
“Siwezi”
Yusrath akakata simu,jambo hilo halikuishia hapo.Alizidi kutongozwa kila kukicha,habari hizo aliziripoti kwa Ahmed na kutuma namba za simu ili awaambie waache kumsumbua akiunganisha na swala la ndoa hapohapo.
“Najua baby,ukinioa.Usumbufu utapungua,nitakuwa nakupa simu uongee nao mwenyewe.Darling nimechoka na usumbufu,wanaume ni watu wa ajabu sana.Na mimba yote hii bado jitu linanitongoza”
Malalamiko hayo alishtaki kwa Ahmed,kifupi Ahmed akageuka na kuwa kama kituo kidogo cha polisi!
“Ndio hivyo baby,kuwa makini nao!”
“Nipo Makini my Husband”
“Okay,nipo ofisini.Nikitoka hapa napita kwa Makala.Nimuulize kuhusu kamati yake ya Vinywaji imefikia wapi?Si unajua kikao cha tatu ni wiki ijayo”
“Pole baby,najua umechoka sana”
“Kwelii,sipati hata muda wa kupumzika siku hizi”
“Kila kitu kina mwisho”
“Ahsante Darling nakupenda sana”
Yusrath,akafurahi alivyomaliza kuzungumza na Ahmed.

***
Siku zilizidi kwenda,kuna hali ambayo alishindwa kuielewa kabisa,kila akizungumza na mwanamme anayeitwa Sameer Rajab!Moyo wake ulikuwa ukitulia kabisa,miongoni mwa wanaume waliomtongoza na hakumwambia Ahmed ni Sameer Rajab,hakuelewa kwanini japokuwa alijitahidi kumpiga chenga lakini wapi.Sauti ya Sammer Rajab ilimpagawisha,akawa anatamani azungumze naye kila wakati,mwanamme huyo alikuwa na sauti nene yaani bezi,akiongea ni lazima utamani arudie mara mbili.Licha ya hayo,alikuwa mwanamme mtanashati tena mpole,mara ya kwanza kukutana naye ilikuwa Hospitalini, alivyokuwa anaenda ‘clinic’ hapo ndipo mwanamme huyo akaomba namba,wakaanza mazoea mwisho wa siku akamwambia Yusrath kwamba anampenda na yupo tayari kwa lolote lile.Kwa mara ya kwanza lilikuwa ni jambo gumu sana kwake kulikubali,kadri siku zilivyozidi kwenda mbele ndipo alipojikuta anazama taratibu.
“Njoo basi leo,si ulisema upo Friii?”
Sameer Rajab,alizungumza simuni.Sauti yake ilikuwa sio mchezo,Yusrath alihisi mwili wake unasisimka, mpaka mifupa ya ndani inagongana.
“Leo?Mimi aaah hapana.Ndio ndio nipo Free?Upo wapi kwani?”
“Njoo Sinza”
“Mmmh,Sinza sehemu gani?”
“Gg Hotel”
“Hotelini teena?”
“Ndio”
“Kwanini Hotelini?Kwanini isiwe nje?”
“Tuongee tu,wawili”
“Mmmmh,kuna maongezi kweli hapo?”
Kauli ya Yusrath haikuwa na msimamo,kifupi alikuwa vuguvugu sio baridi sio moto yaani staki nataka!Hapo Sameer Rajab,alishaelewa maaa yake, akatumia ushawishi na porojo za kibongo kumuimbisha!
“Weee njoo,mimi natangulia”
“Sawa”
Yusrath akakubali,kwa utu uzima alishaelewa nini ambacho kingeenda kutokea mbele ya safari.Sio kwamba hakuwa ana uwezo wa kukataa lakini alishindwa kubishana na moyo wake ambao tayari ulidondoka kwa Sameer Rajab.Haikuwa kazi kubwa kumdanganya Ahmed,akamwambia anaenda ‘Clinic’ kuonana na daktari, hivyo akiona simu haipokelewi asiwe na shaka.
“Okay,baby.Kuwa makini mke wangu.Sasa utaenda na nani?”
“Ah baby,kwani siku zote naenda na nani?”
“Nimeuliza tu”
“Nitachukua taxi”
“Sawa nakutumia pesa nyingine,just incase”
“Okay laaziz,nakupenda Mwaa!Mwaaa!”
Maskini ya Mungu,Ahmed hakuelewa kwamba anapigwa changa la macho!Akatuma pesa ili itumike kwa ajili ya Hospitali,hakuelewa kwamba siku hiyo Yusrath anaenda hotelini kuonana na mwanamme mwingine.Hicho ndicho kilichofanyika,baada ya kumaliza kuoga akamtafuta Sameer Rajab, hewani.
“Ndio natoka,ushafika?”
“Mimi nipo Sinza hapa Kumekucha,ni kitendo cha dakika moja”
“Naomba nikukute,utakuwa wapi?”
“Nitakwambia”
“Poa”
Alichokifanya Yusrath ni kuvaa baibui kubwa,akaweka miwani usoni kuhofia barabarani kujulikana na watu,alivyotoka nje akachukua taxi, safari ya kwenda Sinza,Kumekucha ikaanza.Akiwa katikati ya safari ujumbe ukaingia ‘GG Hotel,room no 14’ujumbe huo ulitoka kwa Sameer Rajab,akaufuta na kutulia.
Meseji zote alizokuwa anachat na Sameer alikuwa akizifuta.Walivyofika Sinza Kumekucha,akamuelekeza dereva sehemu anayoenda,wakakunja kushoto na kunyoosha barabara ya vumbi!Haikuchukuwa dakika nyingi,wakawa wamefika nje,akamlipa dereva ujira wake na kuanza kutembea mpaka mapokezi.
“Dada habari,chumba namba 14”
“Panda ngazi,floor ya kwanza”
“Ahsante”
Ki uvivu na uchovu wa tumbo kubwa,akaanza kupandisha ngazi mpaka alivyoufikia mlango uliondikwa kwa juu namba 14,akagonga!Sekunde hiyohiyo mlango ukafunguliwa,moyo wake ukapiga kwa nguvu kidogo upasuke,sura ya mwanamme huyo ilimfanya asisimke mwili wote.Akazama ndani mlango ukafungwa na funguo,huko walikumbatiana.Hapo ndio kabisa,akahisi kama amepigwa na shoti ya umeme.Alichokifanya Sameer Rajab ni kusogeza mdomo wake karibu na Yusrath,ambao ulipokelewa wakaanza kunyonyana ndimi.Taratibu wakasogezana mpaka kitandani,shingo ya Yusrath ikalambwa hapo akawa hoi bin taaban,mwili wake ukalegea hakuweza tena kujigusa,baibui ikatolewa miwani ikatupwa mbali,kwa kuwa ndani hakuvaa kitu chochote ikawa rahisi kwake kulitoa.
“Griii griiiii”
Simu ikawashtua,Yusrath akatulia kidogo.Simu yake ndiyo ilikuwa inaita,akasitisha zoezi kidogo na kuisogelea,aliyekuwa anapiga alikuwa ni Ahmed,moyo wake ukapiga paa kwa nguvu.
“Shiishiiii,usiongee kitu”
Akamnyamazisha Sameer,ambaye tayari mnara wake ulikuwa umesimama dede kwa kufanya tendo hilo,alichukia sababu alikatwa stimu.
“Yes baby..”
Yusrath akapokea simu kwa mbwembwe akijishongondoa!
“Umefika mke wangu?”
“Ndio nimefika hapa baby,nipo kwenye foleni.Ya kuonana na dokta”
“Okay Darling,kuwa makini.Ilove you,msalimie huyo”
“Nanii baby?”
Yusrath akauliza kwa mashaka kidogo.
“Huyo tumboni”
Hapo akashusha pumzi.
“Anakusikia”
“Okay I love you,utanipa majibu ukitoka”
“Okay”
Siku zote maji ukishayavulia nguo sharti uyaoge,kitendo cha kukata simu akamtizama Sameer,wakarukiana mpaka kitandani.Wakaanza kushikana huku na kule,mwili wa Yusrath ulichemka ajabu cha kushangaza ndani ya sekunde tatu,akawa amefunga goli moja!Sameer akazidi kumtomasa kifuani,akamlamba shingo,akamyonya masikioni,akampima oil kila kitu alikifanya ili kumuandaa,ndipo akavua shati lake na kuvuta kaptula yake,akatoa mashine.Kwa kuwa Yusrath alikuwa ana tumbo kubwa, ilibidi watumie kifo cha mende,miguu yake ikachanuliwa huku na kule,Sameer akashika ndizi yake vizuri na kuitumbukiza ndani ya ikulu.
“Aaaashhh mmmh assshhhh”
Yusrath,aliguna huku akiwa amefumba macho yake,yupo sayari nyingine kabisa ya HUBA!


Kitanda kiliendelea kunesa nesa,juu yake alilala Yusrath akiwa chali miguu yake ipo huku na kule, Sameer yupo katikati yake hana nguo hata moja wanazini,wote wapo katika sayari nyingine ya huba!Yusrath hakuweza kugeuka geuka sababu ya tumbo lake kubwa na zito, ndiyo maana alitumia staili hiyohiyo moja,kifo cha mende!Haikuchukuwa dakika nyingi wakawa tayari wamemaliza mchezo,Sameer akajitoa haraka kwani hakutaka kumlalia Yusrath tumboni.
“Una joto sana”
Sameer ndiye aliyeanza kuongea,akiwa pembeni amelala chali anatizama juu ya paa la nyumba.
“Mmmh,sio kweli”
“Unajua sijawahi kugongana na mwanamke mwenye mimba,kumbe mnakuwaga watamu namna hiyo”
“Umeanza Sameer”
“Sio nimeanza nakwambia ukweli”
Yusrath hakutaka kuendelea kupoteza muda mwingi kwa kukaa hapo,alitaka kuwahi kurudi nyumbani ili Ahmed asije kufikiria vitu vingine ama kumuhisi vibaya,sio kwamba hakuelewa alichotoka kukifanya hakikuwa sahihi,alivyomaliza kuvaa akaweka miwani yake vizuri machoni na kuanza kuondoka huku nyuma akimuacha Sameer chumbani,siku hiyo ndipo walipoanza rasmi mchezo wao mchafu wa kukutana sehemu tofauti tofauti ili wafanye ngono!
Yusrath,akabadilika ghafla akanogewa!Kukosa penzi la Sameer kwa siku mbili ilikuwa ni sawa la teja kukosa Unga,Yusrath akapata ugonjwa mbaya wa Arosto baada ya Sameer kusafiri hiyo ilimfanya ahangaike kila kukicha,akakosa raha kabisa ya maisha.
“Baby,leo nakusubiri.Ukifika tu Ubungo,utanikuta pale kwa siku ile”
“Sawa,Mpenzi wangu”
Hakuna siku aliyofurahi kama kusikia Sameer anakuja siku hiyo,akajiandaa vizuri ili akaonane naye wafanye tendo hilo la ngono kama kawaida yao.Na ilikuwa wazi kabisa,hisia zake kwa Ahmed ziliporomoka na kupungua mpaka sitini na tano!Kila Ahmed alipomuhitaji, alimpiga chenga na kumpa kalenda mara kesho mara kesho kutwa.
“Baby,najisikia vibaya.Siwezi kuonana nawewe”
“Kwanini? Unaumwa?”
“Ndio,tumbo,chini ya kitovu hapa”
“Ulimwambia Daktari wako?”
“Nishamwambia,kasema nikamuone leo”
“Uwahi basi uwende tafadhali”
“Sawa baby”
Maneno hayo yalimtoka Yusrath,akiwa ana danganya mchana kweupe!Mambo aliyomwambia Ahmed yalikuwa ya uwongo sababu siku hiyo alipanga kuonana na Sameer,wafanye kama siku zote!Ilivyogonga saa kumi jioni,Yusrath akaongoza mpaka hotelini, ambapo huko alimsubiri Sameer kwa hamu kubwa sana na kwa wakati huo tayari alivua nguo zake,akavaa taulo moja na kujitupa kitandani akitafakari vitu chungu mzima.
“Kwanini sikumjua Sameer mapema”
Yusrath alikuwa akiwaza huku akitoa maelekezo ni wapi Sameer amkute,hilo halikuwa tatizo sababu Sameer alikuwa tayari amefika Kibaha, kumaanisha kwamba baada ya muda mfupi wangekuwa wote chumbani.Muda ulisogea,hatimaye Sameer akafika.Mapigo ya moyo ya Yusrath yalipiga kwa nguvu,joto lake likapanda sana,akamkumbatia Sameer hapohapo wakatupana kitandani huku wakicheza na nyama za ulimi,Shati la Sameer likatupwa mbali.Akavua suruali yake harakaharaka na kuushika mwiko wake vizuri,akaseti vizuri na kuutumbukiza mgodini.Hapo ndipo Yusrath akahisi kama amesimama na ukucha!

****
“Kwahiyo,hutaki kutuambia?”
“Nishasema,sijui mnachoongelea hapa”
“Una uhakika?”
“Uhakika ninao,asilimia zote”
“Nakuuliza tena kwa mara nyingine,huyu binti yuko wapi?Mara ya kwanza ulikataa kwamba hukuwahi kusoma Makumira ukalikana jina lako”
“Siwezi kuongea lolote,nishasema sijui kitu chochote kile”
“Hata mimi naona”
Katika chumba kidogo,ambacho kwa juu kilikuwa na dirisha moja dogo ndipo Florian Fredrick alihifadhiwa humo, akiwa kama mtuhumiwa anahojiwa maswali lukuki,ilikuwa ni lazima ataje ni wapi Hajrath Mpilla alipo vinginevyo angebeba msalaba mzito ama dunia kwake ingegeuka na kuwa Jehanam.
Askari walijawa na usongo pamoja na hasira sababu zoezi la Kumsaka Florian Fredrick liliwapa tabu kidogo,kilichowashangaza ni jinsi Florian Fredrick alivyo,muonekano wake na mambo yake vilikuwa vitu viwili tofauti.
“Wewe ni mrembo sana,una sura ya dada yako.Nakuhakikishia humu ukitoka,hutosahau”
Maneno hayo yalimtoka OCD Ebeneza Mrosso!Aliongea kwa kumaanisha kwani baada ya kutoka ndani ya chumba hiko waliingia askari wawili, wakiwa na vifaa vya kutisha mikononi mwao!Mmoja alikuwa ameshika misumari, mwingine nyundo na mmoja tindo iliyochongoka kwa mbele,picha hiyo ilitosha kabisa kuelezea kila kitu.
“Unamjua Yesu?Yeye alitundikwa msalabani,sisi tunakutundika hapohapo kwenye kiti na misumari”
Hakuna punje ya masihara iliyotoka kwa afande huyo ambaye aliteuliwa kwa ajili ya kazi hiyo,hakukuwa na mazungumzo mengine kuanzia hapo,kilichosikika hapo ni sauti ya Florian Fredrick akipiga kelele na kutaja Miungu yake yote!

****
Taa nyekundu ilianza kuwaka ndani ya kichwa chake kuashiria kwamba kuna hatari mbeleni endapo asingekuwa makini kulinda penzi lake, dalili za kumkosa Yusrath zilikuwa waziwazi,tabia zake zilimfanya akose rahaa ya maisha!Akashindwa kufanya kazi kabisa,Yusrath alikuwa akimzingua isitoshe anamjibu anavyojisikia!Wakati mwingine inapita siku nzima hawazungumzi.Kilichokuwa kinamuumiza, siku zilikuwa ukingoni ili wafunge ndoa wawe mke na mume,hakuelewa kwamba mkandarasi anayebomoa penzi lake ni mwanamme anayeitwa Sameer Rajab!Wiki nzima zilipita,akijaribu kujua nini tatizo la Yusrath kubadilika lakini alikosa jibu lililomridhisha.
“Siku hizi umebadilika?”
Ahmed akasema siku hiyo simuni,akilalamika!Mambo yalimfika shingoni.
“Nimekuwaje?”
“Sikuelewi”
“Mimi mbona najiona nipo kawaida”
“Hapana,umebadilika Yusrath”
“Ahmed,nipo okay sawa.I’m fine,nitakupigia baadaye, tchao”
Yusrath akakata simu,hakutaka kuendelea kuzungumza na Ahmed sababu pembeni yake alikuwa amelala Sameer Rajab wapo uchi wa mnyama,mwanamme aliyetokea kumpenda kwa kasi ya kimondo,hiyo ilimfanya ajishangae mpaka mwenyewe!Hakukuwa na mazungumzo mengine zaidi ya kutupana kitandani na kuanza kunyonyana ndimi,wakageuzana huku na kule.Maziwa ya Yusrath yalitomaswa vizuri,yalilambwa na ulimi,akawa hoi bin taaban.Anatoa mihemo ya ndani kwa ndani,hajiwezi tena!Alichokuwa anakifanya ni kuvuta vuta mashuka huku na kule sababu alikuwa mbioni kufika mshindo,hakuweza kuvumilia hali hiyo, akashindwa kupambana na hali yake alichokifanya ni kumvuta Sameer karibu na kumng’ang’ania kwa nguvu huku akiachia makelele ya rahaa,hapohapo akatulia.
“Baby,tupumzike”
Yusrath alitoa pendekezo akideka,akamsogelea Sameer karibu na kuweka kichwa chake kifuani kwa mwanamme huyo!
“Nani alikupigia?Baba wa mtoto?”
“Baba wa mtoto, waaapi?”
“Sijakuelewa,sasa kumbe nani?”
“Ahmed”
“Sasa Ahmed sindo baba wa mtoto?”
“Sio baba wa mtoto”
“Whaaaaat?!”
Sameer,akapigwa na butwaa akakitoa kichwa cha Yusrath kifuani kwake ili apate maelezo vizuri,habari hiyo ilimshtua kwa kiasi cha kutosha!

*****
“Itakuwa mimba hiyo Ahmed,wala usiwe na presha.Wanawake wenye mimba ndivyo walivyo.Kuna rafiki yangu mmoja mke wake alishika mimba,kulikuwa kuna vurugu.Mbona hiyo cha mtoto”
“Ilikuwaje?”
“Huyo mwanamke mimba yake, ilimpenda chalii mwingine,sio kumpenda kimapenzi lakini.Basi,anatamani kumuona kila wakati,asipomuona siku hiyo vurugu”
“Duuu..”
“Sio duu,jamaa akawa anadhani mkewe anamegwa na huyo Chalii ilikuwa kesi kubwa mzee,kumbe walaa.Mimba ilimpenda,mimba nyingine zinakuja vibaya.Kama hivyo,mkeo hataki kukuona kabiiiiiisa”
“Sasa naenda kufunga naye ndoa,itakuwaje.Nitaweza kweli kuishi hivi?”
“Ungesubiri mpaka ajifungue sasa”
“Yeye alifosi”
“Sio mbaya,wala usiwe na presha kabisa.Ndio walivyo,utaniambia akijifungua,mapenzi yanarudi palepale”
“Ngowi,ahsante sana!Mimi nilidhani labda,kuna boya nakula naye sahani moja.Nikaanza kumuhisi jamaa mmoja hivi,pale Posta”
“Yupi huyo?”
“Alipokuwa anafanya kazi,bosi wake alimtongoza kaka.Juzi nilienda pale nikaanza kudadisi,wala hakuwahi kuonekana tena pale.Sasa nikawa najiulizaaa,anhaaa kumbee ndio walivyo!Daa,ahsante kwa kunifungua akili jembee”
Kelele zilikuwa nyingi katika baa hiyo iliyofahamika kwa jina la Mpumalanga,maeneo ya Tabata Bima.
Hapo ndipo walipoamua kuweka kikao chao bubu ili watete kidogo!Ilibidi bia ziongezwe kwani mazungumzo yalikuwa, yamepamba moto!
“Nampeeenda saaana Yusraaaaath,unajua niniiii Ngowiii,naenda kuoaa!Ooooh mara ndoaa changamoto sijui,Bullshit.Mimi naenda kuenjoy,mambo ya kupikiwa wali naziiiii”
Kichwa cha Ahmed tayari kilianza kupata moto,ndiyo maana alianza kuongea hovyo hovyo.
“Ahmed,ndoa sio wali nazi peke yake.Kuna maisha mengine,baada ya wali naziii weka hiyo kichwani.Changamoto zipooo nyingi.Ndoa it’s all about uvumilivu”
“Kwanini nawewe usiooee sasaaa?”
“Nitaoa,muda ukifikaaa.Bado naweka mambo sawa”
“Ngowiii nawewe,muhuniii muhuuuniiii weweee!Anyway….Mimi wewe ni ndugu yanguuu sana,kila kitu nakwambiaa weweee!Wee, dadaaa psiii psiiiii,njoooo”
Ahmed alikuwa tayari bwii,zilizokuwa zinamuongoza zilikuwa ni pombe tu,weita alivyofika akasimama pembeni yake,Ahmed akamuangalia vizuri kuanzia juu mpaka chini,akambania jicho moja yaani akamkonyeza.Mawazo yake yakahama kwa kasi ya ajabu!
“Weweee,unaitwaa naniiii?”
“Judi”
“Judiiii,unakunywaaaa nini?”
“Savana”
“Nyokooooo,wewe unakunywaga savanna wewe?Alafu mademu bwanaaaa…Ebu tuongezee mbilimbili”
Alivyoagiza,akamuangalia Ngowi ambaye alikuwa akicheka kwa pembeni.
“Nawewe unachekaa niniii?Wananishangaza saana hawa,wakiwa magetoni wanakunywa Konyagiii na virobaaa.Shenziii”
Pombe za Ahmed ziliamia chini,kazi yake ikawa ni kuangalia huku na kule,mbele yake akamuona mwanamke mrembo mrefu,maji ya kunde amekaa mwenyewe!Akamtizama kwa makini,akasimama na kumfuata huku akiyumba.
“Dada mamboooo”
“Safi”
Mwanamke huyo akajibu kifupi,akaendelea kuchezea simu yake.
“Kuna mtuuu?Hapa?”
“Ndio”
“Mimi naitwa Ahmed,Call me Ahmed beibiiiiiii”
“Sawa”
“Wewe jeee?”
“Kaka,achana namimi”
“Ha! Haaa!Haaa!Hahaha,acha hizooo,unakunywa kinywaji gaaaani?”
“Nimefunga,sinywiiii”
Alivyomaliza kuzungumza,kuna mwanamme alitokea nyuma yake.
“Baby vipi?”
“Poa tu”
Mwanamme huyo,akamtizama Ahmed kwa kitambo kidogo na kurudisha macho yake kwa mpenzi wake!
“Baby sorry,karibu kiti”
Hiyo ilimfanya Ahmed amtizame mwanamme huyo kwa dharau,akampandisha juu mpaka chini.
“Okay mrembooo,tutawasilianaaaa”
Ahmed,akaondoka eneo hilo na kurudi kwenye meza yake!Ambapo waliendelea kupiga stori na Ngowi,ulikuwa ni usiku mnene lakini kwao ilikuwa kama ndio kumekucha,jicho la Ahmed lilikuwa mbalii, kwa mrembo aliyekuwa kandokando,mara amkonyeze mara amfanyie ishara ilimradi vurugu tupu.
“Ahmed,achana na mwanamke wa watu!Usitafute balaa”
“Ah wapiii,Yule demuuu..Nimemzimia kinyamaa,alafu kanielewaa”
“Achana nayeee,pombe hizooo sio akili zako.Just stop,usikubali pombe akitoe kwenye reli”
“Sio pombee brooo,Yule mtoto mzuriiii ujue”
Mwanamke aliyekuwa pembeni,alikuwa ni mrembo!Kilichomchanganya Ahmed ni namna mapaja yake yalivyokuwa nje,sketi fupi aliyovaa iliharibu hali ya hewa kabisa.Kitendo cha mwanamke huyo kusimama na kupita mbele ya Ahmed likawa kosa la jinai,akataka kumshika mkono kwa niya ya kumvuta lakini badala yake akamshika, makalio.
“Weweee kaka tuheshimianeee, mseng**** niniii”
Kelele hizo zilimfikia mwanamme aliyekuwa pembeni,akasimama wima kwa hasira na kumuendea Ahmed.Akamshika shati na kumpiga kichwa puani.
“Sameer pleaseeeee stoop”
Mwanamke huyo,akajitahidi kuzuia ghasia hiyo lakini alikuwa amechelewa kwani Ahmed alikuwa tayari amedondokea meza ya vinywaji.Sameer,hakuishia hapo akamuinua tena Ahmed na kumpiga ngumi ya mdomo,tayari wateja waliokuwa eneo hilo wakafika na kuwazunguka.Ngowi hakupendezwa na jambo hilo akatembea kwa kasi na kumshika Sameer kwa nguvu.
“Kaka tuliiia,tuliaaa hivyo hivyo”
Namna Sameer alivyoshikwa mikono yake kwa nyuma,ilifanya ashindwe kuendeleza kipondo.Ahmed alishikwa na ghadhabu damu zilikuwa zinamvuja kichwani na puani,maumivu aliyokuwa anahisi hayakuwa ya kawaida,alivyotaka kumfuata Sameer ili aanzishe varangati akashindwa kwani alishikwa kwa nyuma na wanaume watano.
“Niacheniiii,niachieenii.Nimuoneshe huyu boyaaaaaa”
“Kaka tuliaa,acheni utoto”
“Nimesema niacheee”
Tayari kufumba na kufumbua kulikuwa na vurugu,Ahmed na Sameer walikuwa wamevimbiana kwa hasira, wakitaka kuzichapa!Ilionekana kila mtu alikuwa mwenye usongo na mwenzake.



Kelele zilikuwa nyingi,hakuna hata mtu mmoja kati yao aliyemuelewa mwenzake!Huyu alisema kile huyu alitukana,ilimradi vurugu tupu.Katika watu waliokuwa na hasira ni Ahmed,alichefukwa na kuwa kama mbogo,isingekuwa watu wanne kumshika kwa nyuma angeshamvaa Sameer siku nyingi sana.
“Oya niacheni,okay sawaaa.Nakubali,fine yameisha”
Ahmed alisema maneno hayo ili tu wamuachie niya yake ikiwa ni kumvaa Sameer kwa mara nyingine,wanaume wanne walimuachia. Hapohapo Ahmed akavuta chupa ya ‘Windock’ alivyotaka kumrushia Sameer, akashikwa tena mikono.
“Acha ufala,mpumbavu nini wewe!Ebu msiharibu starehee za wengine”
Jamaa mmoja aliyekuwa na mwili mkubwa wa miraba minne,akachimba mkwara.Hapo Ahmed akatulia lakini alikuwa akihema juu juu,akatolewa mpaka nje ya baa hiyo ya Mpumalanga.Hata alivyotoka nje,hakukubali kazi yake ilikuwa ni kumsaka Sameer popote pale alipo,hiyo ndiyo ilikuwa tabia ya mwanamme huyu katika ugomvi ‘eitha’ kushinda ama ugomvi uendelee.
“Ahmed kausha,kaka”
Ngowi,alikuwa nyuma yake anamtuliza alishaelewa ni kitu gani Ahmed anakitafuta,kazi ya Ahmed ilikuwa ni kuangalia huku na kule,hapo ndipo alipoanza kupiga hatua tano tano baada ya kumuona Sameer ng’ambo ya barabara.Akavuka kwa kasi,akamvaa na bega wote wakadondoka kwenye mtaro wa maji machafu puu.
Huko ndipo alipopata nafasi ya kumshushia misumbwi Sameer,hawakukaa sana watu wakafika na kuingia ndani ya mtaro na kuwatoa.
“Njoeni huku”
Ilikuwa ni sauti kali,iliyowashtua kila mmoja!Hapo ndipo walipogundua kwamba alikuwa ni askari.
“Nyie si mmeshiba sana?”
Askari huyo akazungumza kwa sauti,wenzake wakashuka kutoka kwenye diffenda wakawachukuwa Sameeer pamoja na Ahmed,wote wakaingizwa ndani ya Diffenda,hapohapo safari ya kwenda kituo cha polisi ikaanza mara moja.
Ngowi,hakutaka kubaki nyuma na kumtelekeza rafiki yake,alichokifanya ni kuchukua pikipiki na kuanza kuifuatilia Diffenda hiyo nyuma nyuma, mpaka walipofika Kituo cha Polisi, Tabata Mwananchi.
“Hawa,peleka ndani.Ni wezi,kesho mahakamani”
Afande huyo akazungumza kwa mikwara mikubwa sana,niya ilikuwa ni kuwatingisha kama kawaida yao!
“Afande mimi sio mwiz ni…”
“Nyamaza,vua mkanda.Leo utalala humu,kunguni wewe”
Hicho ndicho kilichotokea,Sameer na Ahmed wakawa wamevuna walichokipanda.Ngowi hakuwa mbali,hapohapo akatokeza na kumvuta askari huyo pembeni ili watete kidogo.
“Nawewe unataka nini?”
“Afande,njoo tuongee pembeni kiume”
Akasema kwa sauti ya chini.
“Uongee namimi nini?”
“Ndugu yangu yupo humu ndani”
“Njoo kesho”
Afande huyo hakumaanisha,aliongea hivyo ili kumtingisha Ngowi na hiyo ndiyo ilikuwa kawaida ya maaskari wote kuwa na mikwara mizito,haikujulikana kama wanafundishwa chuoni ama ndiyo hulka zao.
“Nimekwambia njoo kesho”
“Afande,haina haja ya kuja kesho.Sikia sas..”
“Unataka kusema nini?Ongea harakaharaka nina kazi za kufanya”
Afande huyo aliyefahamika kwa jina la Kidoletumbo,alizungumza kwa sauti nzito yenye ukali kidogo ili kumtisha, Ngowi.
“Kama nilivyokwambia kuna ndugu yangu..”
“Kwahiyo unatakaje?”
“Tuongee”
“Tuongee nini?Nakusikiliza,ebu ongea kiume,tusipotezeane muda aisee.Ongea basi”
Ngowi,alivyosikia hivyo akajua nini maana yake akajiongeza,akasogea pembeni na kutoa wallet,akatoa noti tatu za elfu kumi,akazifinyanga kama ugali wa dona na kumfinyia askari kiganjani.
“Shilingi ngapi hii?”
“Thelathini”
“Kijana,ongeza.Kuna faili limefunguliwa pale.Kuna wenzangu”
“Kuna hiyo tu mkuu”
Mazungumzo yao yaliishia hapo,askari akaingia kituoni, baada ya dakika tano Ahmed akawa ametoka,akatembea mpaka alipokuwa Ngowi.
“Pole Ahmed”
“Ahsante broo”
Akaitikia kwa upole,wakatafuta pikipiki na kuondoka zao!

*****
“Upo wapi umesema Sameer?”
“Kituo cha polisi”
“Umefanya nini tena mpenzi wangu?”
“Nitakwambia,naomba uje kunitoa”
“Kukutoa?Kivipi?Na hali yangu hii?Kwani wanataka nini?”
“Pesa”
“Shilingi ngapi?”
“Laki moja”
“Mungu wangu,nitatoa wapi sasa hivi?Lakini ngoja kidogo,sawa Darling?”
“Okay baby”
Ilikuwa ni simu iliyomfanya Yusrath akae kitandani na usingizi wote aliokuwa nao ukate kabisa,ilikuwa ni asubuhi na mapema!Hakutegemea kupokea simu kama hiyo, iliyomfanya mapigo yake ya moyo yapige kwa nguvu,kitendo cha Sameer kupiga simu na kusema yupo kituo cha polisi kilimnyima raha ya maisha,akalishika tumbo lake lililokuwa kubwa, maana alihisi kama linamuuma kutokana na mshtuko mkubwa alioupata.Akatafakari kwa muda sababu alitakiwa achukuwe maamuzi ya dakika sifuri,hapo ndipo sura ya Ahmed ikamjia kichwani akajua ni lazima angesema tatizo lolote lile, pesa ingetumwa mara moja.Hakupoteza muda,akamtafuta Ahmed hewani ambapo simu iliita bila kupokelewa,alichukia lakini alipiga tena na tena bila kukoma,alivyopiga simu kwa mara ya sita ndipo ikapokelewa.
“Ahmed,mbona hupokei simu zangu?Nina wivu mwenzio.Upo wapi?Upo na nani?”
Kabla ya salamu,aliuliza maswali mfululizo,niya yake ikiwa ni kumtetemesha Ahmed akitumia gia hiyo.
“Bab…”
“Nooo,niambie upo na nani sasa hivi?”
“Nilikuwa naoga ili niende kazini”
“Hapana Ahmed unanidanganya”
“Sasa nikudanganye nini mke wanguu”
“Hunipendi siku hizi kama umenichoka niambie”
“Naanzaje kukuchoka,nakupenda baby wangu!Nilikuwa bafuni naoga”
“Wee sawaa tuuu,wewe nidanganye”
Yusrath,akazungumza kwa sauti ya kudeka kidogo ili kumlainisha Ahmed kwani alishaelewa udhaifu wake ulipo.
Tabia ya Yusrath ilibadilika ghafla ikawa mbaya sana,niya yake ilikuwa ni kumpiga kizinga Ahmed ili amtoe Sameer kituo cha polisi kwa mwanamke kama yeye tena mzuri,hakupaswa kufanya jambo kama hilo,hakuwa na jinsi tayari alikolezwa na Sameer, akakamatika!
“Siwezi kukudanganya baby”
“Nina shida love wangu”
“Shida gani?”
“Nina shida na pesa”
“Ya nini?Kiasi gani?”
Swali hilo lilifanya akili ya Yusrath ichaji kwa kasi ya ajabu, akaanza kusaka uwongo.
“Baby unanipenda?”
“Saaana”
“Ni story ndefu lakini naomba nifupishe,naomba unisamehee”
“Nini Yusrath?!Mbona unanitisha?”
“Nilikula pesa ya Ada ya binamu yangu,nilitegemea ningeipata leo lakini imeshindikana.Pesa yenyewe ilikuwa nimeagiza mzigo al…”
“Yusrath,ngoja nikukatishe”
“Subiri nimalize,alafu naomba unisaidie hili swala likifika kwa Baba,itakuwa msala mme wangu.Sipendi, alafu ukizingatia nina mtoto tumboni,sihitaji stress”
“Yusr…”
“Baby please,naomba unisaidie”
“Nitakusaidia lakini kwanini ule pesa ya ada?Sio vizuri,mimi sipendi.Umeniudhi kwa kwe….”
“Unanipa pesa ama hunipi?Maana unaanza kunisimanga,niambie kama huwezi,nimtafute mtu anayeweza kunisaidia…”
Yusrath,akazungumza kwa ukali tena akifoka,alimkaripia Ahmed kama mtoto mdogo vile hiyo alitaka kumtingisha Ahmed kwani aliamini ni lazima pesa angetoa kwa asilimia mia moja.Ni kweli Ahmed alipoa akawa mdogo kama kidonge cha pilton,mbaya zaidi akakata simu kwa makusudi.Kichwa cha Ahmed,kiliwaka moto sio kitoto,hasira zilimkaba kohoni katika maisha yake,hakupenda dharau tena kama hiyo ya kukatiwa simu katikati ya mazungumzo, alivyotaka kuuchuna akakumbuka kwamba Yusrath ana mtoto wake tumboni hiyo ilimaanisha alitakiwa kuangaliwa na kutunzwa kama yai,alivyotafakari jambo hilo kwa kina zaidi akainua simu kwa hiyari yake na kumtafuta Yusrath hewani,neno la kwanza kulitamka ni ‘I’m sorry baby’ kisha baada ya hapo akamuhaidi kwamba angetuma kiasi chochote cha pesa,hakuelewa kwamba Yusrath sio yule wa kipindi kile,hakuelewa kwamba pesa yake inatumika vibaya tena anatumiwa mwanamme ili atoke kituo cha polisi,laiti angejua hayo yote kwa hasira zake zilivyo angeua mtu.Ilibidi siku hiyo, kabla ya kufika ofisini apitie bank,akachota pesa na kumtumia Yusrath simuni.

****
Shiriki la ndege ya Turkish Airways,lilikanyanga ardhi ya Tanzania jiji la Dar es salaam juu ya uwanja wa kimataifa Mwalimu Nyerere saa 2;45 usiku.Ikakimbia kwa kasi ya risasi na taratibu kupunguza mwendo na kusimama kabisa,magari maalum yaliyokuwa na ngazi kwa juu yakasogea na kukaa mlangoni,mlango wa ndege ukafunguka.
“Pole na safari Honey”
Dokta Sajo,alikuwa ni miongoni mwa abiria waliokuwa wanasafiri siku hiyo akitokea nchini Afrika Kusini,pembeni yake aliketi mpenzi wake, Hajrath Mpilla.Mwanamke huyo alikuwa bado haamini kama amerejea nchini Tanzania kwani nchi hiyo ilimkumbusha vitu vingi sana nyuma,moyo wake ulianza kupiga kwa nguvu, akahisi kama uti wake wa mgongo umepigwa na ubaridi,akatizama nje kupitia dirishani kisha kumuangalia Dokta Sajo,mwanaume aliyetokea kumpenda na kuwa tayari kufunga naye, pingu za maisha!
“Nakupenda Sajo”
“Mimi Pia Hajrath”
Hapohapo wakanyonyana ndimi kisha kusimama,ambapo walianza kuchukua mabegi yao madogo juu ya keria maalum,kisha kuunga foleni ya kutoka nje,ambapo huko walianza kushuka ngazi.Dokta Sajo,alifurahi sana kufika katika nchi hiyo kwani ilikuwa imepita miaka mingi sana,mualiko wa harusi kutoka kwa rafiki yake ndiyo uliomfanya afunge safari hiyo ndefu.
Wakatembea mpaka ‘immagration’ ambapo hapo, walilazimika kupiga ‘passport’ zao mihuri kisha kutembea mpaka sehemu ya kupokelea mabegi,yaliyokuwa yanazunguka.
“Begi langu lile pale”
Hajarth akamwambia Dokta Sajo,lilivyomfikia akalichukua kisha kulisubiria lake.Lilivyopita,akaliokota na wote kuanza kutoka nje.Miwani ya Hajrath Mpilla ilikuwa kubwa machoni tena nyeusi,isingekuwa rahisi kwa mtu yoyote yule kumgundua,mbali na hapo alinawiri.Akanenepa vizuri,umbo lake likajichonga hiyo ikafanya wanaume wakibongo wageuze shingo zao na kumwangalia kwa matamanio.
“Taxiii,hapa Kiongozi.Taxi nzuri,ina ac kila kitu,kuna tivii ndani.Twendeni”
Dereva taxi mmoja wapo alivyowaona wageni hao,aliwakimbilia ili nayeye walau apate mkate wake,wote wakamsogelea.Alichokifanya Dereva huyo aliyejitambulisha kwa jina la Popo,alichukuwa mabegi yao na kuyaingiza ndani ya taxi.
“Tunaenda wapi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa dereva baada ya kuingia ndani.
“Erado hotel”
“Ipi sasa?Ya Posta?”
“Manzese Tiptop”
“Poa”
“Ngoja kwanza, shilingi ngapi?”
Hajrath,akauliza akitaka kujua bei kwanza alielewa sana tabia za madereva taxi wa kibongo,kuweka cha juu.
“Elfu themanini pale”
“Baby tushuke,hauwezi kutuambia bei hiyo.Sisi sio watalii,wabongo wenzako”
“Aaaaah sista,za wapi hizooo.Kwani si tunaongea tuu,alafu dada inaelekea wewe mjanja sana”
Dereva taxi alivyoona amekamatika,ilibidi ajichekeshe kidogo na kulazimisha mazoea.
“Kwa kukuonea hurumaa saaana utapewa thelathini”
“Ongeza kumii”
“Hapana,kuna hiyo”
Dokta Sajo alikuwa kimya,alimuelewa sana Hajrath, linapokuja swala la pesa mwanamke huyo alikuwa ni mchumi, ndiyo maana akanyamaza na kumuacha aelewane na dereva taxi mbali na hapo Dokta Sajo alikuwa ni mgeni,safari ikaanza mara moja.Hajrath alikuwa mwenye mawazo chungu mzima,hakuelewa angeanza vipi kuwatafuta wazazi wake,wangemchukuliaje?Kitu gani angeongea ili wamwelewe,mambo mengi yalipita kichwani mwake.
Ghafla akakumbuka maisha ya chuoni kwao Makumira,akakumbuka siku aliyojaribu kunywa sumu kisa Ahmed,akamkumbuka Necka Golden,sura ya Amney ikamjia kichwani,taswira ikajijenga kichwani kwake akawa kama anatizama picha fulani hivi.
“Baby,nimesahau kuwapigia kwamba nimefika”
Dokta Sajo,akavunja ukimya na kumshtua Hajrath aliyekuwa kwenye mawazo mengi sana.
“Tutawapigia,tukifika.Ama kesho,sasa hivi ni usiku sana mme wangu”
“Sawa love”
Kilichofuata hapo ni Hajrath kulala juu ya bega la Dokta Sajo,safari ikaendelea.Wakakunja kushoto walivyofika Tazara,wakanyoosha Mandela Road,baada ya kufika Matumbi dereva akawasha endiketa na kupandisha Tabata dambo,niya yake ikiwa ni kufupisha njia.Akatokeza Kigogo,baada ya muda mfupi akawasili Mabibo Mwisho,akalala kulia na kunyoosha mpaka mahakama ya Ndizi,hapo ndipo akashindwa kuelewa njia vizuri,akasubiri kidogo na kusimamisha gari.
“Kiongozi,kwema?”
Akamsalimia jamaa mmoja aliyeweka meza anauza mchuzi wa pweza.
“Kwema ndugu”
“Samahani naomba kuuliza”
“Bila samahani”
“Kuna Hotel moja inaitwa Erado,hii ndio njia yake?”
“Erado ipi?Ile ya Tip top?”
“Ndio”
“Nyoosha,pita hapa.Kule mbele utaona njia panda hapo kula kushoto baada ya hapo,nyoosha goti.Utaiona JM hotel,sasa kushoto”
“Poa kiongozi”
“Ahsante”
Dereva taxi akapiga gia na kuingia barabara ya vumbi,akafanya kama alivyoelekezwa.Alivyofika getini akapiga honi,geti likafunguliwa mbele kulikuwa na uwazi mkubwa sana.Taxi ikasimama dereva akalipwa ujira wake,wakatembea mpaka mapokezi.
Kilichofanyika hapo ni kulipia chumba,wakapewa kadi ya umeme iliyokuwa na kazi ya kufungua milango,wakatembea mpaka kwenye lifti.Ilikuwa ni hoteli nzuri yenye hadhi yake,kwa kuwa walipewa chumba namba 406,wakabonyeza namba tatu, lifti ikajifunga ikaanza kupanda juu,ilivyosimama ikafunguka wakatembea mpaka, mlangoni.Dokta Sajo,akatoa kadi na kuiweka mlangoni,akauvuta lakini ukaonekana kuwa mgumu kidogo,wakajaribu tena.
“Baby,usitumie nguvu.Muite muhudumu”
Ilikuwa ni kero lakini hawakuwa na jinsi,muhusika akaitwa!Ilibidi aombe radhi kwani milango yao, ilikuwa katika ukarabati. Walivyoingia ndani tu,kila mtu akamuangalia mwenzake,wakasogeleana karibu na kuanza kunyonyana ndimi.
“Bebiii…Twende bafuuuni”
Hajrath,alisema kwa sauti ya puani huku akirudi kinyume nyume, wakafungua mlango wa bafuni huku wakivua nguo zao,kila mtu akabaki kama alivyozaliwa wakasogea mpaka kwenye bomba la mvua na kulifungua maji yakaanza kumwagika,kilichofuata hapo yalikuwa ni madenda na kuanza kushikana huku na kule,kila mtu alikuwa ana moto mkali,Dokta Sajo akawa ana kazi ya kutomasa maziwa ya Hajrath na kumshika kila idara,akamkunja vizuri na kuuchukua mguu mmoja akauweka kando,akashika mashine yake vizuri na kuingiza ndani ya ikulu.
“Aaaaaashhhh aaaah”
Sauti hiyo alitoa Hajrath Puani huku mikono yake yote miwili, akiwa ameiviringisha shingoni mwa Dokta Sajo,wananyonyana ndimi.



Siku zilisogea kwa kasi,kuliko kawaida.Walikuwa wanazungumzia miezi,sasa waliongelea wiki mbili tu!Harusi ya Ahmed na Yusrath ilikuwa inakaribia kufanyika,hiyo ilimlazimu Yusrath awekwe ndani akiwa kama mwali ili siku ya harusi yake,atolewe!Tukio hilo lilimkasirisha sana na lilimkereketa roho mno akachefukwa kwani alitamani kutoka nje ili akaonane na Sameer wake,alihisi kuna vitu fulani vikubwa alivimisi kutoka kwa mwanamme huyo,hata hivyo hilo halikuwa tatizo waliendelea kuwasiliana simuni,wakizungumza habari nyingi za mapenzi.Na kuhaidiana ya kwamba hata kama angeolewa mchezo wa kuchepuka ungebaki kuwa palepale,kisingeweza kuharibika kitu chochote kile.
Kwa Yusrath, aliamini jambo hilo lingewezekana kwa asilimia zote mia moja,hiyo ni kutokana na Ahmed kuwa bize na kazi, mbali na hapo alishaelewa udhaifu wake ulipo.
“Usijali baby,mimi nawewe mpaka kifo.Hakuna mtu yoyote,atakayeweza kututenganisha”
Yusrath alizungumza maneno hayo akiwa anajiamini kwa kiasi cha kutosha!
“Lakini unaenda kuwa mke wa mtu”
“Hilo lisikutie wasiwasi kabisaaa,najua jinsi ya kumthibiti huyu mwanamme.Kwangu hapindui,ukishajua jina la mbwa siku zote, hakupi shida”
“Sawa Love,lakini nahisi kawivu”
“Usijali kabisa,nachokuomba usione wivu kabisaaaaa just relax”
“Sawa,nakupenda sana”
“Mimi pia Sameer wangu”
Mapenzi tena kwa Ahmed yakawa yamepungua kwa kiasi kikubwa sana,aliyekuwa anamuwaza kwa wakati huo ni Sameer tu,japokuwa alitumia muda mchache sana kuzungumza na Ahmed akimwambia pia anampenda na anaisubiri kwa hamu kubwa siku ya harusi yake.
“Mimi hapa,tumbo linauma.Sijielewi kabisa”
Ahmed alisema kwa hisia,alikuwa ana hamu kubwa na shauku, iliyomjaa.Kazi yake ilikuwa ni kupiga picha halisi siku hiyo ya tukio itakavyokuwa,namna atakavyokaa mbele za watu yaani ‘hightable’hata hivyo hakuamini kama ni yeye kweli, anaenda kufunga ndoa,aliomba Mungu ndoa yake iwe yenye furaha tele.Ndugu,jamaa na marafiki na wao walikuwa katika hekaheka za kutafuta nguo nzuri,kila mtu alikuwa ana hamu kubwa ya kushuhudia tukio hilo la Ahmed, ambalo lingekuwa la kihistoria katika maisha yake,kamati zote zilikuwa makini kupiga hesabu na kukagua bajeti kama ilienda ilivyopangwa!Ahmed alionekana kupagawa kwa kiasi cha kutosha, kwake muda ukawa mchache sana,akahisi kuna vitu hakuvitimiza, hata hivyo alipokea meseji nyingi za pongezi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.
“Kwahiyo ndio umeamua kuoa?Haya Hongera!Mimi Esma Chande”
Ulikuwa ni ujumbe uliomfanya Ahmed,ashtuke kidogo na kuusoma mara mbilimbili,kumbukumbu zake zikarudi nyuma kwa kasi ya mwewe,akamkumbuka msichana huyo Esma Chande, aliyemtoa bikra kipindi wapo kidato cha tano,akakumbuka vitu chungu mzima.Hakuwa ana uhakika kama alishawahi kumpa namba zake mpya,swala hilo halikumtisha sana na kumfanya ashindwe kuendeleza zoezi lake.
“Mama ile suti ipo tayari?”
Ahmed akatokeza seblen baada ya kukumbuka suti yake,ambayo siku ya harusi usiku ukumbini, angeivaa.
“Bado,baba yako ndio katoka sasa hivi.Anaifuatilia.Mwanangu,punguza presha,kila kitu kitakuwa sawa”
“Mama lakini mpaka leo?”
“Leo itakuwa tayari”
“Zuwena ametuma mchango wake,kwenye simu yako, umeuona?”
“Ndio umefika,waambie watume pesa kwa Nurdin!Mimi sipokei pesa jamani,nitaharibu hesabu”
“Sawa Mama,mimi nipo ndani”
Hata Ahmed nayeye hakuruhusiwa kutoka nje,mpaka siku ya harusi ifike.Hakuamini kama siku za usoni angekuwa mme wa mtu,vitu vingi vilipita ndani ya kichwa chake, akaelewa kwamba anaenda kuanza maisha mengine mapya,zaidi na hilo muda mfupi Yusrath angejifungua na familia ingeongezeka.

******
Siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu hatimaye ikafika,siku ambayo Ahmed angefunga ndoa na kuwa mme halali,tukio hilo lilishika hatamu sababu lilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu.Kabla ya kwenda ukumbini ndoa ilipangwa kufungwa nyumbani kwa akina Ahmed yaani kwa Mzee Kajeme,hiyo ilimaanisha Shekh afike mahali hapo bila kuchelewa.Kila kitu kilifanyika kwani saa tatu kamili asubuhi, Shekh Khaleed alikuwa amewasili,amevaa kanzu mkononi ameshika msaafu,shingoni amevaa tasbii.Alikuwa ni shekh maarufu sana jijini Dar es salaam.Mapigo ya moyo ya Ahmed yalikuwa yakimwenda resi,hakuelewa hiyo inatokana na nini hasaaa,alikuwa ana hamu kubwa sana ya kumuona Yusrath akitokea.Pembeni yake aliketi mpambe wake,Abdulaziz Kamata, mwanamme huyu alisafiri na mkewe kutokea Mwanza mpaka Dar es salaam, ili kuhakikisha jambo hilo linaenda salama.Honi za magari zilizosikika kutokea nje,zilimfanya Ahmed atabasamu kwa mbali,vigelegele vilisikika hiyo ilimaanisha tayari bibi harusi mtarajiwa keshawasili.Haikuwa utani,geti likafunguliwa umati wa wanawake ukaanza kuingia,katikati akaonekana mwanamke aliyejifunika mpaka usoni kabisa,mikononi ana michoro ya rangi ya ina,Ahmed aligundua moja kwa moja mwanamke huyo alikuwa ni Yusrath tu.Akatembea taratibu mpaka kwenye mkeka.Siku hiyo Ahmed alionekana mtu wa tofauti kabisa,hakuwahi kuonekana akiwa amevaa kanzu na kibalagashee kichwani, hata hivyo alipendeza na vazi hilo lilimkaa vizuri.Shekh Khaleed,hakutaka kuchelewesha mambo ilikuwa ni lazima afanye haraka ili watu wale ubwabwa,akachoma ubani na kuanza kuzungumza maneno akitoa haya kutoka kwenye kitabu chake cha dini,haikuchukuwa dakika nyingi sana mambo yakawa tayari.Vigelegele vikasikika kila pembe, kumaanisha kwamba Ahmed na Yusrath ni mtu na mkewe kuanzia siku hiyo!Mzee Kajeme,alikuwa mwenye furaha muda wote na alionekana kutabasamu kila wakati, hata hivyo familia nzima ilionekana kukubali kila kitu kilichotokea,isipokuwa Kassim peke yake ndiye aliyeonekana kuilazimisha furaha yake!Ndani ya mtima wake,alichukia tukio hilo kwa ujumla wala hakufurahishwa,kuna mambo mengi sana yalipita ndani ya kichwa chake,nyuma ya yote hayo alihisi wivu sana.
Hata hivyo,hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima akubali matokeo tu,masaa yalikimbia kwa kasi na ilitakiwa siku hiyo jioni wageni waalikwa, wakutane katika ukumbi uliofahamika kwa jina la Mwika Hall,Sinza Makaburini kwani huko ndipo sherehe ilipangwa ifanyike.Wanaokunywa pombe, siku hiyo walitoshekwa,chakula kilikuwepo cha kumwaga!
“Nakupenda Yusrath”
“Hata mimi Mme wangu,nakupenda sana”
Yusrath,alizungumza maneno hayo akiwa analia machozi,alijikuta analia kwa uchungu ingawa hakuelewa ni kwanini machozi hayo yanamtoka kwa siku kama hiyo.

*****
Zilikuwa ni taarifa za kusikitisha mno,kila mtu aliumia moyo kwa namna moja ama nyingine!Ulikuwa ni msiba mzito kwao kuupokea,baadhi ya ndugu hawakutaka kuamini habari hizo,ambazo moja kwa moja waliamini ni polisi ambao walizitengeneza ili wasisumbuliwe tena,haikuwezekana hata kidogo taarifa ya namna hiyo ikawa ya ghafla,kweli waliamini kifo kipo lakini hawakuwa tayari kuamini kama Hajrath Mpilla amefariki kwa kupigwa risasi.Kwa Mujibu wa Kamanda James Edward na uchunguzi aliodai kuufanya, alikuwa ana uhakika asilimia zote kwamba mwanamke huyo alipigwa risasi na kutupwa kwenye mto wenye mamba,hawakuwa wana uhakika japokuwa makachero walitumwa nchini Afrika Kusini kuchunguza,Florian Fredrick alibanwa na kuminywa vya kutosha alipata mateso ya kila aina mwisho wake akaamua kuzungumza ukweli na mipango yote ambayo aliwahi kushiriki lakini mbali na hapo,hakutaka kumtaja Sporah Trevez kama muhusika mkuu,hilo likabaki ndani ya kifua chake na aliapia siri hiyo angeitunza mpaka siku atakapofukiwa mavumbini.
“Haiwezekani!”
Mzee Mpilla,hakuamini alizungumza huku machozi yakimlenga!Juhudi zake zote zikaonekana sio kitu kabisa,akamtizama mara mbilimbili Kamanda James Edward,akiamini wenda angebadilisha matokeo lakini haikuwa hivyo.
“Nahitaji basi nione hata mwili wa binti yangu”
Hapo,hakuweza kuvumilia.Akatoa leso kutoka mfukoni na kuiweka usoni,machozi yalikuwa yakimtoka!
“Pole Mzee Mpilla,tulijitahidi.Jeshi letu,halikulala usiku na mchana laki….”
“Nitamwambia nini Mke wangu,aelewe!”
“Jikaze,sheria itafata mkondo wake”
“Haitoweza kumrudisha,Binti yangu amekufa.Ndio mtoto wa kwanza..Daaaah”
Yalikuwa ni machungu,kumbukumbu mbalimbali za binti yake zikaanza kumpitia kichwani kwake,akaumia ajabu.Hiyo ilifanya agande kituoni hapo,kilichotokea ni askari mmoja wapo kuchukua jukumu la Kumsindikiza Mzee Mpilla mpaka nyumbani kwake,alivyofika na kumtizama Mkewe akashindwa kujikaza kiume akaanza kumwaga machozi,taarifa zilikuwa ni mbaya kwao!Haikuwa siri tena,ndani ya sekunde chache taarifa za kifo cha Hajrath zikaanza kusambaa kwa kasi ya moshi wa kifuu.

******
“Aashsss aaah mmmh aaashss beiibiii aaah aaaashss aaah,yeeees yeees aaashss fuc*** me,like that aaah aaaah ashssss”
Kelele hizo zote zilimtoka Hajrath,akiwa amelala chali yaani amelalia tumbo Dokta Sajo yupo mgongoni mwake,anafanya mashambulizi.Isingekuwa televisheni kuwa na sauti kubwa wenda vyumba vingine wangesikia,siku hiyo Hajrath alitoa sauti za puani huku akiwa amelalia tumbo,hakujiweza tena!Akajiona yupo angani vitu vyote, anaviangalia kwa chini,akasafiri ghafla na kujihisi yupo bahari nyingine ya huba,mambo aliyokuwa anamfanyia Dokta Sajo yalimfanya ahisi raha za ajabu, ndiyo maana akaanza kukinyonga kiuno chake huku akizungumza lugha mbalimbali za kumsifu,siku hiyo maneno yote yalimtoka bila kujijua,Dokta Sajo nayeye hakufanya makosa,kazi yake ilikuwa ni kunyonga kiuno chake taratibu,mara juu mara chini mara pembeni na katikati ilimradi amridhishe mpenzi wake kwani aliamini mapenzi ni kama bia hivyo ilikuwa ni lazima amleweshe!Kashkash ziliendelea,Hajrath akabinuliwa tena na kuwekwa mbuzi kagoma kwenda majanini.Akashika kingo ya kitanda vizuri Dokta akaendelea na kazi yake,mambo yalikuwa ni mazuri kwa wawili hawa,mpaka inafika saa nane ya usiku kila mtu akawa amechoka,hapohapo wakalala fofofo ili kesho yake waamke wajiandae kwa ajili ya harusi.

****
Kivyovyote vile aliamini kusingekuwa na mtu yoyote yule ambaye angemgundua usiku huo,ndiyo maana hakuvaa miwani ya rangi nyeusi badala yake akavaa miwani nyeupe,wigi akaliweka vizuri na gauni refu kiasi lililombana,hiyo ilifanya umbo lake lijitokeze kama kawaida.Kupendeza kwake kulimfanya Dokta Sajo,amtizame mara mbilimbili jioni hiyo walivyokuwa chumbani wanajiandaa.
“Umependeza mke wangu”
Haukuwa utani,Hajrath alipendeza kwelikweli na uhakika ulikuwepo asilimia mia moja ya kwamba ukumbi mzima ungemuangalia yeye.
“Hata wewe Darling,njoo nikuweke tai vizuri”
Dokta akasogea karibu, akarekebishwa tai,ikakaa vizuri kohoni wakasogea mpaka kwenye kioo kikubwa na kukiri kwamba wote wamependeza sana,wakatembea taratibu na kutoka nje ili safari ya kuelekea kwenye harusi ianze!

*********
Magari yalifurika nje ya ukumbi wa Mwika Hall,uliopo Sinza Makaburini.Hiyo ikafanya mpaka magari mengine yakose nafasi ya kupaki,ikalazimika yaegeshwe pembeni ng’ambo ya barabara.Wageni waalikwa walikuwa nje,wamependeza wanawasubiri bwana na Bibi harusi kwa bashasha,ukumbi ulikuwa mkubwa na ulipambwa vizuri.Kamati ya mapambo ilisimamiwa na mwanadada machachali Esther Muganda,mapambo yalikuwa ya kuvutia.Kila meza ilikuwa na bakuli kumaanisha ukiingia lazima ukaribishwe na supu ili upashe utumbo joto.Saa mbili kamili,gari aina ya benzi yenye rangi nyeusi iliyokuwa imepambwa ikiongozana na magari mengine matatu iliingia nje ya ukumbi huo.Kila mtu akasimama waliokuwa nje,wakaanza kupiga kelele za kushangilia.Mlango ulivyofunguliwa akashuka Ahmed,akiwa amenyuka suti kali,iliyombana yaani modo chini kaunyuka moka!Kohoni kanyonga tai,hawakukaa sawa upande wa pili akateremka Yusrath shela lake likawa limeshikwa kwa nyuma,wakaongozana na Ahmed mpaka ndani,hapo ndipo kelele zikaongezeka zaidi.
Kilichowashtua wageni waalikwa ni baada ya kuona baadhi ya waandishi wa habari nje ya ukumbi huo,kwa mara ya kwanza hawakuelewa ni kwanini wapo mahali hapo mpaka walipowaona waigizaji maarufu waliotokea kutingisha nchi ya Tanzania na Afrika Mashariki na kati kwa ujumla, Deo Karekezi na Marietha katika ‘movie’ iliyoitwa Bedroom professionals, waandishi wa habari walivyowaona wakawakimbilia na kutegesha maiki zao.
“Mr.Deo Karekezi,umependeza sana”
Mwandishi wa habari kutoka katika kituo cha Televisheni Sk Tv,alianza kutoa sifa akiwa na maiki mkononi mwake.
“Ahsante,nashukuru”
“Naona umeongozana na Marietha,vipi mna mahusiano yoyote yale ya kimapenzi?Sababu sio mara ya kwanza kuwaona namna hii pamoja”
“Nina mahusiano naye katika kazi tu lakini pia napenda sana kuongozana naye”
“Vipi kuhusu Part 2 ya Bedroom Proffesionals,tumesikia tetesi kwamba inatoka,tunataka kujua lini?”
“Hilo lipo chini ya uongozi lakini tutatoa part 2 nitakuwepo kwenye baadhi ya Scenes!Na pia kuna baadhi ya part atacheza Ramsey Noah na Van Vicker kutoka Nigeria,hivi navyozungumza uongozi ushaanza kufanya mazungumzo nao”
Deo alivyomaliza kuzungumza maneno hayo,akamvuta Marietha na kuanza kuingia ndani kwani hakutaka kuongea mengi zaidi, waandishi wa habari wakaendelea kuwapiga picha,hata walivyoingia ndani kila mtu aliwatizama na wengine wakadiriki kuomba ‘Selfie’ kwao ilikuwa kero lakini hawakuwa na jinsi wakawazoea,kilichowafanya wang’ae zaidi ni namna walivyopendeza.
Wakiwa katikati ya utambulisho wa wazazi mara ghafla Ahmed akapoteza mudi,hiyo ni baada ya kushika simu,alivyoona kwenye grup la chuoni kwao wameandika ‘RIP HAJRATH’ huku picha ya mwanamke huyo ikiwa juu ya group kuashiria kwamba mwanamke huyo amefariki dunia,hiyo ilionekana kumchanganya sana Ahmed.Akabaki ameganda,hata Mc alivyomtaka awatambulishe wazazi hakusikia.
“Ahmed,bebiiii”
Sauti ya Yusrath ilimshtua kutoka katika mawazo aliyokuwa nayo,akakosa rahaa kabisa,moyo ulimuuma ajabu!Kuna vitu vibaya vya kuumiza ambavyo aliwahi kukumbana navyo lakini sio tukio kama hilo lililotokea siku ya furaha yake.Wakati akiwa katika mawazo hayo,taxi nyeupe ikawa imefika nje katika ukumbi huo.
“Inaelekea sherehee hii bab kubwa baby”
Hajrath,alisema akiwa anateremka kutoka ndani ya taxi,magari mengi yaliyokuwa nje!Yalimshtua,picha ilijielezea kwamba ukumbi ulishona,hilo halikumpa shida alichokifanya ni kuuzungusha mkono wake katikati ya mkono wa Dokta Sajo na kuanza kuingia ndani ya ukumbi bila kuelewa ilikuwa ni harusi ya Ahmed.
Kitendo cha kuingia ndani waliketi meza ya mwisho kushoto,mapigo yake ya moyo ghafla yakapiga paa!Baada ya kuangalia kioo kikubwa yaani projekta,sura ya Ahmed ilikuwa imejaa katikati ya Skrin.
“Ahmeeeed!”
Hajrath,akajikuta ameropoka kwa mshangao wa waziwazi huku akijaribu kuangalia huku na kule ili ahakikishe kama ni kweli Ahmed ndiye bwana harusi ama alimfananisha.


Ulikuwa ni mshtuko mkubwa sana na mapigo yake ya moyo yalidunda kama kitenesi ,kila kitu kilichokuwa kinatokea ndani ya ukumbi huo ilikuwa kama kiini macho!Bado,hakuamini. Wakati mwingine alidhani yupo kwenye ndoto kali ya kutisha na baadaye angeshtuka,akageuka pembeni na kumtizama Dokta Sajo ambaye muda wote alikuwa katika tabasamu pana kana kwamba watu waliokuwa ndani ya ukumbi huo anawafahamu wote,sio siri Hajrath alikuwa katika wakati mgumu sana!Akiwa katikati ya dimbwi la Mawazo mengi,yeye Ahmed alikuwa bize anawainua mmoja baada ya mwingine akitambulisha,akamaliza kutambulisha wazazi wake,akafata wajomba,dada zake na jirani zake.Hakuwa ana habari ya kwamba Hajrath ambaye alidhania amefariki dunia yupo hai na isitoshe yupo ndani ya ukumbi huo,hata hivyo alionekana kuchanganyikiwa lakini sio sana kama alivyoingia ndani ya ukumbi huo kwa mara ya kwanza.
Siku hiyo hakuwa mwenye aibu, kutokana na kumaliza Mzinga nusu wa Konyagi ili kukata mshiba wa aibu, ndiyo maana akapata uwezo wa kuzunguka huku na kule.Baada ya utambulisho kuisha,Ahmed na Mkewe Yusrath wakapewa ruksa ya kwenda mbele ya viti na kukaa.Ghafla picha ya Hajrath ikamjia tena kichwani,akakumbuka walivyokuwa chuo cha Makumira,walivyokuwa wanapendana kama watoto mapacha.Ukweli ni kwamba hakuwa sahihi kumuwaza Hajrath siku kama hiyo lakini hakuwa na jinsi, alivyojaribu kujizuia alishindwa kabisa,akatizama huku na kule na kutoa simu yake mfukoni.Akaingia ‘WatsApp’ kwenye grup lao la chuoni na kutizama kinachoendelea,huko aliona namna gani watu walivyoguswa.Kuna comment moja kutoka kwa Amina Mwasomola ,ndiyo ilimfanya machozi yamlenge. ‘Jamani mnamkumbuka Ahmed?’swali hilo liliulizwa kwenye grup na msichana huyo, ambaye pia walisoma chuo kimoja,meseji hiyo ikajibiwa kwamba wanamfahamu ‘Yupi?Ahmed Kajeme.Yule Boy wake Hajrath,hivi yupo wapi siku hizi?’Coment zilikuwa nyingi na zilitiririka, Ahmed alikuwa akizisoma, simu yake ikiwa chini kidogo pembeni ya mguu wake ‘Ndio huyohuyo,leo anaoa.Maskini ya Mungu life’s too short, bado siamini kama Hajrath amefariki’Meseji ziliendelea kumiminika ‘Jamani msimamwambie’….’Yupo humu kwenye Grup,lazima ataona hizi meseji’Hawakuelewa kwamba Ahmed anasoma kila kitu, kilichokuwa kinaandikwa humo.
“Baby,unachat na nani?”
Uzalendo ulimshinda Yusrath,akamsogelea Ahmed sikioni na kumnong’oneza kwa sauti ya chini, hiyo ni kutokana na kumuona Mwanaume huyo alivyokuwa bize anachat.
“Kuna taarifa za msiba nimepewa hapa”
“Please zima simu,utaangalia baadaye”
“Okay baby”
Watu walikuwa wengi,vinywaji vilikuwa vya kumwaga.Saa 5;30 usiku karibia nusu ukumbi mzima walikuwa wamelewa bwii,mbaya zaidi walikuwa tayari wamekula.Kila mtu aliipongeza kamati hiyo ya vinywaji, kilichofuata hapo ilikuwa ni kulisakata rumba katikati ya ukumbi.
Hajrath,hakutaka kuamini akakumbuka ndoto alizokuwa nazo na Ahmed, waje siku moja kufunga ndoa lakini siku hiyo ilionekana kupulizwa na upepo ikazimika,bado aliamini yupo kwenye njozi ya kutisha,ili kuhakikisha hilo akajipiga kofi shavuni ili kama ni ndoto ashtuke lakini haikuwa hivyo,mambo yaliyokuwa yanatokea yalikuwa yana ukweli mtupu.Hata hivyo hakutaka kuliacha jambo hilo liende hivihivi,akapiga fundo refu la glasi ya wine iliyokuwa mezani kwake na kusimama, hiyo ni baada ya kuhakikisha ya kwamba muoaji aliitwa Ahmed Kajeme,kwa mara ya kwanza alidhani wenda duniani wawili wawili lakini haikuwezekana hata kidogo, watu hao wafanane mpaka majina.
“Umeona kisu kilee,mtoto ni motooo.Mtoto anaitaa ona figa ile, bambataaa!Mungu ni fundi bwana”
Sauti hiyo ilitoka kwa jamaa mmoja aliyekuwa kandokando, baada ya kumuona Hajrath kasimama,wezere la mwanammke huyo lilikuwa ni shida ni moto wa kuotea mbali,kila alivyotembea lilitingishika kwa nyuma, walioenda kwenye harusi siku hiyo na wake zao,walipata shida kumtizama hivyo walitumia jicho pembe.
Hajrath alitembea huku akicheza taratibu mpaka alivyofika katikati ya umati wa watu waliokuwa wanalisakata rumba,akamsogelea bibi harusi kwa karibu ili amthaminishe na kumuangalia kama anamfahamu lakini sura hiyo hakuwahi kuiona kabisa.
“Mambooo”
Hajrath,akamsalimia Yusrath aliyekuwa anacheza na ndugu zake,Ahmed alikuwa kushoto kabisa anapiga 'selfie' na washkaji zake, ambao walimpongeza kwa hatua nzito na kwa maamuzi magumu aliyoyachukuwa.
“Poa”
“Umependeza,hongera sana”
“Ahsantee”
Yusrath hakuwa ana habari na Hajrath,yeye alijua ni mwalikwa tu sababu waliokuwa wanampa pongezi walikuwa ni wengi mno!Akaendelea kucheza na kuserebuka,Hajrath alikuwa pembeni yake akaangalia kushoto na kumuona Ahmed, alitamani kumfuata hapohapo lakini akasita kidogo,moyo wake ulimuuma kwa upande mwingine, japokuwa hakuelewa ni kwanini hali hiyo inatokea,akapiga moyo konde,akaanza kupiga hatua za taratibu huku akizuga kucheza, hakuelewa ni kiasi gani Ahmed angeshtuka kumuona,akazidi kusogea karibu, alivyomfikia akamshika begani.
“Baby,njoo tucheze mziki”
Sauti hiyo ilimfanya Hajrath,ashtuke kwani aliguswa begani yeye, alivyogeuka akamuona Dokta Sajo!Moyo wake ukapiga kwa nguvu,akaishiwa nguvu akageuka na kumpa Mgongo Ahmed ambaye hata yeye aligeuka nyuma ili kuangalia ni nani aliyemgusa begani,akamuona mwanammke mmoja aliyevaa gauni refu amempa mgongo,akamtizama kwa sekunde kadhaa kisha kuendelea kuserebuka.Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi sana,aliilazimisha furaha yake lakini hilo lilishindikana.
“Kaka mbona unaonekana huna furahaa,siku yako leoo.Naona kampani ya ubachela inaanza kupunguuua”
Benjamin Ngowi,akatia neno huku wakiwa katikati ya mziki wanacheza.Kelele zilipigwa nyingi baada ya Dj kuweka kwaito hapo ndipo watu wakajipanga vizuri na kuanza kucheza kwa mtindo mmoja,mara waende mbele,warudi nyuma wainame kidogo na kurusha teke.
Sio siri, walikuwa wakicheza vizuri kiasi kwamba ilimlazimu Dj aweke kwaito nyingine.Mambo yakawa yaleyale,wageni waalikwa wakaendelea kufurahia mziki,mambo yaliendelea mpaka Mc alipotoa ruksa ya maharusi waende kupumzika.
Hapo ndipo Hajrath alitaka kuonana na Ahmed macho kwa macho,hata ampe mkono tu ndipo roho yake ingetulia,kuna vitu vingi sana alivikumbuka wakiwa chuoni Makumira,akaamini kwamba isingekuwa Marehemu Gabriel wenda yeye ndiye angekuwa ndani ya shela siku hiyo,lawama zote akamtupia Gabriel kwa kuwachonganisha lakini hilo hakutaka kulipa kipaumbele,akajivuta vuta na kuwapangua watu waliomsonga,siku hiyo kila mtu alitaka kumpa mkono Ahmed na Yusrath,Hajrath akajikaza mpaka mbele kabisa,alivyotaka kutoa mkono Dokta Sajo akawa amefika nyuma yake,akamshika kiuno.Tukio hilo lilimfanya achukie lakini hakuwa na jinsi,kitendo cha kufumba na kufumbua Ahmed akawa tayari ametoka nje na kuingia ndani ya gari lililopambwa vizuri,moyo wake ukabaki unamuuma!
“Tuondoke sasa hivi baby?”
Dokta Sajo,akauliza hakuelewa ni kwa namna gani amemkera Hajrath.
“Aaaah,subiri kidogo”
Hajrath hakutaka kuondoka akiwa hivyohivyo,alichokifanya ni kutembea mpaka kwa Mc,akamshika bega na kuuliza ni wapi Bwana na bibi harusi wataenda kupumzika siku hiyo usiku.
Alivyojua kwamba wataenda kulala Serena,akajua kwake itakuwa rahisi kwenda eneo hilo,akamfuata Dokta Sajo kisha kuondoka zao huku akiapia piga ua, ni lazima usiku huohuo angemuibukia Ahmed hotelini,kwa kitendo alichokuwa anataka kukifanya mpaka yeye akajiogopa mwenyewe.

*******
Kila mtu alikuwa mwenye huzuni na wote walikuwa na mawazo mengi kichwani mwao,Yusrath alimfikiria Sameer,moyo wake ulimuuma ajabu sababu alielewa anaenda kuanza maisha mapya ya ndoa, kumaanisha kwamba asingekuwa huru kwani muda wote ilikuwa ni lazima aage na kuomba ruksa,raha alizokuwa anapewa na Sameeer aliamini zingepungua kwa kiasi kikubwa sana, asingeweza kujiachia tena lakini upande mwingine wa shilingi alijipa moyo sababu alielewa ni wapi udhaifu wa Ahmed ulipo, hivyo alikuwa ana uwezo wa kumburuza anavyotaka yeye,hapo alitabasamu na kujipa moyo kwamba hakijaharibika kitu chochote kile, hakuelewa kwamba hata yeye Ahmed kwa wakati huo alikuwa yupo mbali sana kifikra, akili yake ilisafiri maili zaidi ya mia moja,sura ya Hajrath ilikuwa inapita kichwani kwake bado hakuamini kama mwanamke huyo ameshakufa tayari,aliumia moyoni!Akatamani arudishe muda nyuma walau aonane naye,amuombe msamahaa kwa kila kitu, alichomfanyia lakini hilo aliamini lisingeweza kutokea hata kidogo.Jambo lililozidi kumtesa zaidi ni kitu gani kilichomuuwa mwanamke huyo mdogo kufa,akataka kujua chanzo.Alivyotaka kutoa simu yake, Yusrath akamzuia na kumuegamia kifuani mwake.
“I love you Ahmed,hatimaye ndoto yangu imetimia”
Yusrtah alizungumza kwa sauti ya kudeka huku akijilegeza.
“Hata mimi baby”
Ahmed nayeye akajibu,gari walilopanda lilizidi kutembea mpaka lilipofika Posta katika moja ya Hoteli zilizokuwa na hadhi,hapo walishuka na kusindikizwa mpaka ndani,kitendo cha kuingia ndani wakaanza kushikana shikana kwa furaha,kila mtu akiwa haamini kwamba kuanzia muda huo wangekuwa ni mme na mke.

********
Jambo alilokuwa anataka kulifanya lilikuwa la kimafia sana,kutaka kuondoka usiku huo wa saa sita lilikuwa ni jambo la hatari sana kwa maisha yake na mahusiano yake kwa ujumla!Pembeni alikuwa na Dokta Sajo wanarudi Erado Hoteli,sehemu waliyofikia wakitokea nchini Afrika Kusini.Kichwa cha Hajrath kilikuwa kinawaka moto,akitafakari ni kwa namna gani amtoke Dokta Sajo,alijuwa ya kwamba anaenda kinyume na jambo hilo lilikuwa ni hatari lakini hilo hakutaka kujali ilikuwa ni lazima ausikilize moyo wake ni kitu gani unataka kwa wakati huo.
Walivyofika Hotelini,wakaingia ndani kama kawaida.
“Baby,natoka kidogo”
Hajrath alisema,jambo hilo lilimshangaza sana Dokta Sajo.
“Unaenda wapi usiku huu?”
“Hapo nje”
“Kuna nini?”
Dokta Sajo akahoji,alikuwa ana kila sababu ya kujua ni wapi mpenzi wake anaenda usiku mzito namna hiyo.
“Nakuja sasa hivi,baby..Ilove you mwaa mwaaaa”
Hajrath,hakutaka kujibu swali hilo akambusu Dokta Sajo mdomoni na kuanza kutoka nje, ambapo huko baada ya kufika chini akatafuta bodaboda ili arahisishe safari yake,safari ikaanza hapohapo ambapo haikuchukuwa muda mrefu akawa amefika Serena Hotel,akamlipa dereva ujira wake nayeye kushuka akielekea ndani ya hoteli hiyo.

****
Kilichokuwa kinaendelea ndani ya chumba hiko ni kupongezana,japokuwa kila mtu alikuwa mbali kimawazo wala akili zao hazikuwa katika tendo hilo,Yusrath alivuta picha ya Sameer kichwani kwake Ahmed hakuwa hapo kabisa,alimuwaza Hajrath,moyo wake ulikuwa ukimuuma sana.Japokuwa alikuwa katikati ya miguu ya Yusrath ameipanua huku na kule,ananyonga kiuno chake.Alifanya tendo hilo kwa kujilazimisha sana ili kumfurahisha Yusrath,ambaye tumbo la mwanammke huyo lilikuwa kubwa kiasi, ndiyo maana hakutaka kumlalia kabisa tumboni,alikuwa juu juu.Mbali na hapo Yusrath alikuwa akiigiza kutoa miguno ili kumshawishi Ahmed ajuwe kwamba walikuwa sambamba.
“Aaashss bebii aaah aaah”
Yusrath aliigiza kwa kutoa sauti hiyo puani huku moyoni akiomba Mungu tendo hilo liishe dakika hiyohiyo sababu hakuhisi kama ilivyokuwa awali,akili yake ilishaharibiwa na Sameer, ambaye aliamini ya kwamba ndiye mwanamme mwenye uwezo wa kumkuna mpaka kunako!Akajifanya kutoa sauti kumaanisha kwamba anafika mshindo ili Ahmed amalize,hicho ndicho kilichotokea kwani Ahmed alimaliza na kujitoa,akalala chali.
“Nakupenda Mke wangu,siamini kama nimekuoa”
“Hata mimi baby,siamini kama umenioa hatimaye”
“Nitakupenda,nakupenda.Nawapenda wote na mwanangu”
Ahmed alizungumza kwa hisia zote huku akiligusa tumbo la Yusrath,alikuwa ana kila sababu ya kufurahia maisha yao ya ndoa sababu aliamini huyo ndiye,angekuwa mwandani wake!Akajaribu kuyatupilia mawazo ya Hajrath mbali lakini swala hilo, lilikuwa gumu kwa kiasi chake, bado alitaka kujua nini kimemuua mwanamke huyo.
“Ngooo! ngoo! ngooo!”
Mlango ulisikika ukigongwa wakiwa juu ya kitanda,wametulia.Wakatizamana na kusikilizia tena ambapo uliendelea kugongwa kwa mara nyingine tena,ilikuwa ni usiku sana kugongewa mlango.
“Atakuwa nani?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Yusrath,hiyo ilimfanya Ahmed avute taulo na kuteremka kutoka kitandani,akatembea kwa hatua chache mpaka mlangoni,akanyonga kitasa na kufungua!Mwanamke aliyemuona alimshtua kwa kiasi cha kutosha.
“Samahani,umeagiza chakula?”
Alikuwa ni dada wa jikoni,akiwa na sahani mkononi akimuuliza Ahmed.
“Hapana”
“Itakuwa nimekosea chumba,samahani kwa usumbufu”
“Usijali,anayway.Mna chakula gani jikoni?”
“Tuna kila kitu”
“Sawa,nashuka huko”
“Unaweza kupiga simu mezani,wakuletee”
“Hakuna shida”
Alichokifanya Ahmed ni kufunga mlango,akatembea moja kwa moja mpaka kwenye mkonga wa simu.
“Baby,utakula nini?”
Akamgeukia Yusrath na kumuuliza.
“Nimeshiba,labda nitakunywa Bavaria tu”
“Okay”
Alichokifanya Ahmed ni kuangalia namba zilizokuwa juu ya simu na kupiga jikoni,akajaribu sana kupiga lakini simu iliita bila kupokelewa,uamuzi aliofanya ni kuvaa suruali na shati ili ashuke chini jikoni kuagiza msosi.Akavaa shati na kuanza kutembea,akafungua mlango akiwa na simu yake mkononi,akanyoosha moja kwa moja kwenye lift na Kubonyeza herufi ‘G’ kumaanisha imshushe mpaka chini,lifti ikafunga na kuanza kushuka kwa kasi,ilivyofika chini ikafunguka.Akatembea na kufika mapokezi,kuna mwanamke mmoja alikuwa amempa mgongo hakutaka kuzungumza naye,alichotaka yeye ni kuuliza binti wa mapokezi ni wapi jikoni ili aende kuagiza chakula na vinywaji.
“Nataka niende jikoni,kuagiza chakula”
“Simu hazifanyi kazi?”
“Napiga hazipokelewi”
“Unaweza kuacha oda yako,hapahapa.Tukaandika na namba ya chumba”
Alichokifanya Ahmed ni kusema anachotaka,mwanamke aliyekuwa kandokando yake akageuka na kumuangalia.Mapigo ya moyo ya Ahmed yalipiga kwa nguvu, yakataka kutokeza nje ya kifua.
“Ahmeeed”
Mwanamke huyo alivyolitaja jina hilo,Ahmed akaishiwa nguvu kabisa kwani alimtisha mpaka simu aliyoshika mkononi ikadondoka chini,hakuwa ana uhakika kama aliona mzimu,amemfananisha? Ama ni kweli mbele yake alisimama HAJRATH MPILLA.


Ahmed,aliganda kama barafu mdomo upo wazi.Hakujua ni kitu gani akifanye, kukimbia alitamani lakini wakati huohuo pia alitaka kusubiri,akabaki njiapanda ana muangalia Mwanamke aliyesimama kushoto kwake,bado hakuelewa kama anamfananisha ama ni kweli.Kilichomchanganya zaidi ni sauti ya mwanamke huyo,ilifanana kabisa naya Hajrath, mwanamke ambaye alidhani amekufa masaa machache yaliyopita, isitoshe alikuwa ni mpenzi wake miaka michache iliyopita, walivyokuwa chuoni Makumira, Masomoni.Vitu vingi sana vilipita kichwani akiwa anamtizama bado machoni!
“Ahmed Hongera”
Hajrath akasema kwa mara nyingine,hapo ndipo Ahmed akazinduka kutoka katika dimbwi la mawazo mengi sana!Wakati mwingine alidhani yupo ndotoni,iweje mtu aliyekufa akamuona mbele yake.
“Hajrath ni wewe au?”
“Ndio,ni mimi.Nilikuwepo kwenye harusi yako,hukuniona?”
Ahmed aliendelea kupigwa na bumbuazi.

****
Mawazo yalikuwa mengi sana kichwani mwake,akiwa kitandani, muda wote alitumia kumuwaza barafu wa moyo wake,Sameer.Akawaza vitu vingi sana alivyofanyiwa na mwanamme huyo kwa muda mfupi, wakiwa kitandani akatamani awepo naye wakati huohuo lakini hilo lisingewezekana hata kidogo,wakati anawaza mambo yote hayo Ahmed alikuwa nje anashughulikia maswala ya kula.Hakutaka kuukatili moyo wake,akachukua simu yake iliyokuwa pembeni na kuanza kuzitafuta namba za Sameer ambazo alisave jina ‘Samia’ kumaanisha kwamba hata kama Ahmed ingetokea kuona simu yake inaita, ingekuwa vigumu kugundua,mwanamke huyu alikuwa ana akili nyingi sana hakuwa boyaboya,hapohapo akampigia Sameer simu na kumuelezea ni kwa namna gani amelimisi penzi lake.
“Yusrath,huoni hatari kufanya hivyo?Jamaa yuko wapi kwani?”
Upande wa pili wa simu ulisikika ukiongea,kuonesha ni namna gani Sameer yupo katika wasiwasi mkubwa sana.
“Hilo niachie mimi”
“Sio nikuachie wewe,maisha hayana spea.Hapa ni sawa na kucheza makida makida kwenye nyaya za umeme ujue,mke wa mtu wewe”
“Sameer kumbe wewe muoga hivyo?”
“Mimi sio muoga,lazima nijihami”
“Nimekumisi baby wangu”
“Hata mimi,lakini kawivu kapo”
“Usiwe na wivu,tena ngoja nikuhakikishie hapa ndio nitakuwa huru kuliko unavyodhani”
“Kweli baby?”
“Tutajiachia tunavyotaka,nakupenda Sameer.Sijui lini nitakuona?”
“Mimi nipo Darling”
“Nimemisi penzi lako”
“Mimi hunishindi”
“Kesho tutawasiliana,nakupenda.Nipo tayari kufa kwa ajili yako”
Hisia kali zilimuendesha Yusrath,tayari akawa amekufa na kuoza kabisa!Mapenzi aliyokuwa anapewa na Sameer yalimfanya apagawe kabisa,hiyo akaona haitoshi akafikiria zawadi kubwa ya kumpa.
Wakati akiwa anafikiria hayo,dakika thelathini zikawa zimekatika bila ya Ahmed kutokea,akasubiri dakika nyingine kumi,wasiwasi ukaanza kumuingia alichokifanya ni kutoka kitandani na kunyoosha mpaka kwenye kabati,ambapo huko alivuta dera na kulitia mwilini.Akavaa viatu na kufungua mlango ili kutoka nje huko bado hakumuona Ahmed,akaingia ndani ya lifti ili ashuke chini lakini lifti ilivyofunguka, akamuona Ahmed anatokeza.
“Ilikuwa nikufuate huko chini,ulikuwa wapi?”
Yusrath,akamdaka Ahmed na swali.
“Chakula,chakula nimeenda kukifuata.Ulisema unakunywa?Bavaria,Bavaria nimeagiza tayari”
Jinsi alivyotoka chumbani na alivyomkuta wakati huo vilikuwa ni vitu viwili tofauti kwani alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa,anazungumza kwa kigugumizi.Hiyo ilimfanya Yusrath amtizame mara mbilimbili.
“Ahmed,upo sawa?”
“Nipo sawa Mke wangu,nilikuacha muda mrefu sana?”
“Ndio maana nilitaka kushuka”
“Twende chumbani,niko sawa Darling”
Kichwa cha Ahmed,hakikuwa sawa hata kidogo!Kiliwaza vitu chungumzima kikawa kizito, kama kungekuwa na mzani wa kupima uzito wa mambo aliyokuwa nayo basi mzani huo,ungevunjika!Hakuwa mwenye raha tena,alichokifanya baada ya kufika kitandani ni kuchukua simu yake.
Akaingia kwenye ‘WatsApp’ na kumtafuta Immaculata,akaingia inbox yake na kumwambia Hajrath yupo hai hajafa.Na anavyochat nayeye siku hiyo alitoka kuonana naye lakini kwa bahati mbaya ujumbe wake haukujibiwa kwani ulikuwa ni usiku sana,baada ya hapo akaweka simu pembeni na kuangalia juu ya dari akiwa mwenye mawazo tele.
“Nakuona haupo sawa”
Yusrath,alivunja ukimya hiyo ilimfanya Ahmed apachike tabasamu la plastiki usoni ili amtoe wasiwasi na kuzuga,akamsogelea karibu na kuanza kumtekenya kimahaba ili waanze kucheza mchezo wa kikubwa,hata hivyo Yusrath hakuonekana kuwa tayari kwani aliutoa mkono wa Ahmed uliokuwa unapita kifuani kwake.
“Bebiii,nimechoka bwanaaa.Baadaye”
Yusrath akasema,kiukweli hakuwa tayari kufanya tendo hilo na Ahmed,mawazo yake yote yalikuwa kwa Sameer,mwanamme aliyetokea kumkonga moyo wake!
Kifupi Ahmed alikuwa kama chakula kisichokuwa na ‘Appetite’Yusrath hakutamani kukila.Akili ya Ahmed,haikuwa hapo hata kidogo, alimuwaza Hajrath lakini hata hivyo hakutaka kumpa nafasi sana katika maisha yake, akiamini baadaye ingemletea dosari kwenye ndoa yake,akajitahidi kumtoa katika akili yake sababu tayari alishaanza maisha mengine ya ndoa!Kwanini ni muwaze?Wakati nina mke!
Hayo ndiyo maswali yaliyokuwa yanapita ndani ya kichwa cha mwanamme huyu,kifupi hakulala fofofo,alikuwa akijigeuza geuza.Mara huku mara kule,kwa Yusrath hakuweza kupata usingizi kabisa fikra zake zilikuwa kwa Sameer,alimfikiria mpaka basi.Kichwa chake kilisumbuka sana kikiwaza ni aina gani ya zawadi amtunuku mwanamme huyo wa shoka.
“Vipi,mbona hulali mwenzangu?Unajigeuza geuza tuuu.Kama chavi chavi”
Yusrath akauliza swali baada ya kumuona Ahmed akajizungusha kitandani,hiyo ilimfanya Ahmed pia ashangae kumkuta Yusrath amekaa kitako kitandani.
“Nawewe mbona hulali?”
Ahmed akajibu kwa swali.
“Sina usingizi,mwanao anachokifanya huku tumboni.Anakijua mwenyewe”
“Anafanya nini?”
“Ebu shika”
Alichokifanya Yusrath ni kuuchukua mkono wa Ahmed akauweka tumboni kwake,akasikia kama linacheza hiyo ilimaanisha mtoto anarusha mateke,Ahmed akatabasamu kidogo na kujivuta juu kiasi, akamsogelea Yusrath mdomoni ili ampige busu,Yusrath akakwepesha mdomo wake na kuangalia pembeni kuashiria kwamba hayupo tayari kufanya tendo hilo,Ahmed alivyoendelea kulipapasa tumbo na kutaka kushuka chini kabisa akashikwa mkono.
“Nimechoka bebiii,tulale”
“Lakini nina hamu nawewe”
“Kesho bwaaana,please baby”
Yusrath akachomoa,hakuwa tayari kushiriki tendo hilo ambalo kwao lilikuwa tayari limehalalishwa.Alichokifanya ni kugeukia upande wa pili,akajifunika na shuka mpaka kichwani gubigubi, akimuacha Ahmed katika hisia kali sana,hilo hakujali.
Usiku huo kwa Ahmed ulikuwa mgumu sana,alibaki akimuangalia Yusrath bila kufanya lolote lile,kwake ilikuwa ni sawa na mtu mwenye njaa alafu chakula kipo mbele yake anakatazwa asile.Akatafakari kwa muda mrefu juu ya kitu gani akifanye lakini alishindwa zaidi ya kulazimisha usingizi uje!Kulivyopambazuka,waliletewa chai wakanywa na kushiba hapo Ahmed akataka washiriki tendo,Yusrath hakuwa tayari akampa sababu ileile kwamba amechoka sana anahitaji kupumzika,siku ya kwanza ikapita akakaziwa ya pili akapewa kalenda ya tatu akaambiwa haiwezekani.
Sio siri alikuwa katika wakati mgumu sana,mbaya zaidi Yusrath alikuwa analala bila nguo usiku, haikuwezekana kwa mwanamme rijali kulala bila kumgusa.
“Baby la…”
“Ahmed please niache nimechoka,nini lakiniii”
Ilikuwa ni katikati ya usiku,Ahmed alikuwa mwenye morali, msumari wake umesimama dede, mpaka mishipa ikatokeza pembeni,alikuwa mwenye kiu kubwa siku hiyo na maji yalikuwa pembeni yake.
“Lakini Yusrath mwenzako nina kiu”
“Si ukanywe maji”
“Sio kiu hiyo”
“Sasa kiu gani?Sikia Ahmed,au niende chumba kingine?Maana unanibugudhi”
“Lakini wewe ni mke wangu”
“Kwahiyo kama ni mkeo,ndio kila siku?”
“Sina maana hiyo”
“Sasa basiii,niache nilale”
Ahmed hakuelewa hata kidogo,alichokifanya ni kuendelea kumgasi Yusrath mara amshike huku mara amshike kiuno ili mradi apate haki yake,akili yake haikufanya kazi kabisa.Mambo ya kunyimwa unyumba kipindi anakuwa, alidhani wenda ni stori tu za mitaani na kanjanja za wabongo,siku hiyo aliamini kwamba mambo hayo yapo na isitoshe yamemtokea yeye mwenyewe.Akazidi kufosi,akimvuta Yusrath upande wake.
“Ahmed,usinishike embu niache!”
“Sasa nitakuachaje mke wangu?Nina hali mbaya kidogo tu”
Ahmed alizungumza kwa upole na sauti ya kutia huruma akidhani wenda Yusrath angemuonea huruma lakini wapi,aliendelea kumkazia akidai kwamba amechoka.Hilo likawa gumu kueleweka akazidi kumsumbua huku akimvuta,akavuta shuka.Yusrath akarudisha kwake,Ahmed akalivuta tena wakawa kama watoto wadogo wanaogombania shuka moja,Ahmed akaona isiwe tabu akapanda kwa juu yake na kuishika vizuri mikono ya Yusrath.
“Kwahiyo unataka kunibaka?”
Yusrath akauliza baada ya kumuona Ahmed, amepanda juu yake,amemshika mikono huku na kule, ameikandamiza kitandani.
“Siwezi kukubaka wewe ni mke wangu”
“Unataka kufanya nini?”
Hapo Ahmed hakujibu,akatumia nguvu ikazuka purukushani, kazi ya Yusrath ikawa ni kubana miguu Ahmed anaipanua,kutokana na tumbo lake kuwa kubwa,hakuweza kushindana nguvu na Ahmed aliyekuwa tayari kama mbogo mwenye hasira,hisia zake zilikuwa kali.Kwa kulazimisha sana akafanikiwa kuingiza mashine ndani ya Ikulu,hapo Yusrath hakuwa na jinsi tena, hakuweza kumsukumiza Ahmed akaendelea na zoezi lake mpaka alivyomwaga oili chafu na kutulia,akasogea pembeni na kulala chali,hakutaka kujua Yusrath yupo katika hali gani,alielewa sana amechukia lakini ilibidi atulie na kusubiri mpaka kukuche.

****
Kuanzia usiku huo,hakukuwa na maelewano mazuri tena,Yusrath alinuna kwa kiasi cha kutosha, hakutaka tena kumuona Ahmed mbele yake,hakutaka kumuongelesha.Maisha yao kuanzia siku hiyo yakawa hivyo,siku zikasogea na wiki ilivyofika walitakiwa kuhamia rasmi Ubungo Kibangu ili waanze maisha yao ya ndoa baada ya kutoka fungate.Hapo ndipo Ahmed alipoanza kununua vitu vya ndani kwa kasi,kutokana na kuchangiwa pesa ilikuwa rahisi kwake.Akanunua masofa kabati la vyombo.Baadhi ya vitu kama friji,kabati la nguo,jiko la gesi na kitanda.Haikuwa tabu sababu marafiki zake walimpa zawadi kwenye harusi yake.Hekaheka za kuhamisha vitu zilikuwa nyingi, gari aina ya Kirikuu ilikuwa imejaa wakalizimika kusafirisha vitu hivyo usiku ili wasisumbuliwe na matrafiki barabarani.
“Hivi hapa ndio kona Mlacha eeh?”
Ahmed akavunja ukimya baada ya kufika njiapanda ya Kona hiyo,kulikuwa hakuna lami lakini pamechangamka sana,akaona wamama wapo pembeni wanauza samaki, wengine wanauza sambusa na bagia,akatafakari sana!Alijua kabisa hayo ndiyo yangekuwa maeneo yake ya kujidai.Hata hivyo hakuacha kumpasha habari rafiki yake Ngowi kwamba siku inayofuata angehamia Ubungo Kibangu.
“Ndio hapa,huko mbele Ndio kwa Mchungaji Lusekelo”
Dereva,akamjibu.
“Kwa yule Mchungaji?”
“Huyo huyo”
“Nilikuwa napasikia tu”
Gari lilizidi kunesa, likipita kwenye makorongo,hawakuchukuwa dakika nyingi wakawa wamefika nje ya geti kubwa kiasi.Nyumba waliyopanga ilikuwa yote nzima,ilikuwa na kila kitu kuanzia jiko,seble mabafu na vyumba viwili.Vijana waliokuwa pembeni wanacheza Drafti wakaitwa ili wasaidie kushusha vitu kwenye gari,kazi hiyo ikaanza kufanyika usiku huohuo,kila kitu kikapangwa mahala pake.
“Hiyo,kiongozi”
Ahmed,akatoa shlingili elfu ishirini na kuwakabidhi vijana wa kazi.
“Poa poa Mkushi,amani amani.Sisi ndio mataita hapa mtaani,ndiyo unahamia?Tutakulinda swahiba”
“Freshii”
Kazi ya Ahmed ilikuwa imekwisha,akaingia ndani na kuanza kukagua mazingira ya nyumba hiyo,ilikuwa ni nzuri yenye kila kitu ndani yake,akafikiria namna atakavyoenda kuishi na Yusrath akiwa kama mume.Alivyokuwa katikati ya mawazo simu yake ikaita,akaichukuwa akatabasamu na kuiweka sikioni.
“Ngowi”
Akaita baada ya kuipokea.
“Upo wapi Mzee?”
“Ndio namalizia kupanga vitu”
“Mimi nipo Mikasa hapa,ukimaliza uje”
“Mikaasaa,Mikasaaa,Mikasaaaa.Ndio wapi?”
“Hapa Riverside,ukifika Riverside ukiuliza utaambiwa”
“Poa,nitakuja hapo”
“Haya”
Ahmed alifanya harakaharaka,akafunga nyumba kisha kutoka nje huko alitafuta bodaboda iliyompeleka mpaka Mikasa.Umati wa watu ulikuwa mkubwa sana,magari yalikuwa mengi nje,kelele za mziki zilikuwa kubwa mno.Nje kulikuwa na warembo wanapita huku na kule,Ahmed akaingia ndani na kutizama pande zote,akamuona Ngowi meza ya mwisho kabisa,akamfuata.
“Viiiipii?”
Ahmed akasalimia kwa sauti kubwa ili kushindana na kelele zilizokuwa eneo hilo.
“Poa,karibu.Ndio amekuachia leo,hongera sana”
“Mbona hapa kumechangamka hivi?”
“Leo Ijumaa,hapa ndio pana bamba sana.By the way,nimekutana na jamaa mmoja hivi.Nilisoma naye,atakuja sasa hivi”
“Okay,dada.Niletee Henken ya baridi”
Walivyoagiza vinywaji,dakika mbili baadaye akatokeza mwanamme mmoja mrefu kiasi,kavaa jinsi iliyochanika kwenye magoti,tisheti inayowaka,shingoni ana cheni tatu,masikoni amevaa hereni kifupi hakutofautishwa na wasanii wa bongofleva ama machekibobu.
“Ngowi broo,tsup.I was here long time meeen..Just spoting some bitches,hii baa ina mademuu bombaa Son.Nishang’oa mmoja tayari”
Mwanamme huyo alifika,akazungumza huku akimumunya maneno na kupindisha mdomo kwa swaga.
“Ahmed,huyu ndugu yangu.Au tuseme mdogo wangu,amekaa sana Marekani anaitwa Dedi Mwita”
“Dedi,huyu anaitwa Ahmed.Ni rafiki yangu saana sana sanaa.Tumekuwa kama ndugu sasa”
“Nice to meet you braah,feel free just call me Dayday non other”
Mwanamme huyo, alikuwa mwenye mbwembwe nyingi sana,hakutulia sehemu moja mara ageuze shingo, mara awaite wanawake ilimradi vurugu tupu,waliendelea kunywa pombe nyingi.Ahmed akawa tayari yupo bwii kama kawaida yake, pombe zake huamsha hisia.Akaanza kuangalia wanawake na kuwaita.
“Ahmed,tuondokeee sasa!Mimi tayari”
Ilibidi Ngowi,aseme hivyo ili kuepusha litakalo kuja kutokea, alishaelewa kinachofuata hapo ni vurugu.
“Ngowiiii,huyu mtoto ni kisuuuuu.Bora nisingeoaa,psiii mremboo mremb…”
“Ahmed,tuondokee tuondokee”
“Niache Ngowi,niondoke naye huyu mtotoooo.Ni supaaa,niitie wee dadaa.Yes wewe hapo,njoo hapa nikupakatee”
Tayari Ahmed,alivutiwa na mwanamke huyo aliyevalia kimini kifupi, kilichofanya mapaja yake yawe nje,mbaya zaidi alikuwa anatingishika kwa nyuma,neno ngono ndilo lilikuwa linapita kichwani kwake.Kibarua kikawa kwa Ngowi ilibidi atumie nguvu kumvuta mpaka nje!
“Ngowi unanikoseaa adabu sanaaa ujuwee,kwahiyo hutaki nibaki hapaaa”
“Una mke ujuwe”
“So what?Mwache achukue mzigo akatomb***! Ngowi,mwache mwana akagonge ngozi!Let him fuck,give him freedom son of a bitch”
Dedi Mwita,akaingilia maongezi yao katikati akiwa amemshikilia mwanamke kiuno,hilo halikumfanya Ngowi atulie.
“Dedi,tuache kidogo.Huyu ni ndugu yangu”
“Okay okay boss,fine.It’s not my business,mimi naenda Kutomb****”
Dedi alizungumza kwa sauti kubwa huku akiyumba hatua moja mbele tatu nyuma,pembeni yupo na kimwana.Ngowi hakutaka kumpotosha rafiki yake na kumuacha katika hali hiyo,alichokifanya ni kumpeleka mpaka ndani ya gari.
“Ahmed ingiaa ndani ya gariii twendee nikupelekee”
“Unanipelekaa wapi Ngowiii?”
“Hotelini,Serenaaaa”
“Aaaaaah,niachee”
Ngowi,hakutaka kumsikiliza.Akawasha gari na safari ya kuelekea Posta kuanza mara moja,walivyofika nje ya geti wakaingiza gari ndani.Ulikuwa ni usiku sana!
“Tumefikaa,oyaaa.Oyaaaa”
Ahmed alikuwa tayari amelala,kutokana na pombe.Ngowi akapata kibarua kingine cha kumuamsha!Akamchukuwa na kuanza kumkokota mpaka mapokezi!
“Rafiki yangu,nimpeleke chumba namba ngapi?”
Ngowi,akamuuliza dada wa mapokezi ambapo alimuelekeza chumba namba ngapi,wakaingia ndani ya lifti,walivyofika mlangoni!Ngowi,akasimama nje!Ahmed alivyoingia ndani akatulia kama sekunde mbili na kupiga kelele za nguvu.
“Ngowiiiii,Mke wanguuu hayupooo.Mke wanguu yuko wapiiiiiiii?My wife”
Ahmed alipiga kelele,kumaanisha kwamba Yusrath hakuwepo chumbani.



Yusrath alikuwa amechukia kwa kiasi cha kutosha,kitendo alichofanyiwa na Ahmed cha kumuingilia kimwili bila ridhaa yake kilimfanya aumie mtima.Hakuelewa ni adhabu gani ampe lakini aliapia kutomsamehee kwa kitendo hiko, ambacho yeye alikichukulia kama ukatili japokuwa alikuwa ni mumewe wa ndoa!Mambo mengi sana yalipita kichwani kwake,ghafla akaanza kuchukia uamuzi aliouchukua wa kufunga naye ndoa.Ilikuwa ni mapema sana kuwaza hivyo sababu ndoa ilikuwa bado mbichi,licha ya hayo yote kilichosababisha amchukie Mumewe ni mwanamme anayeitwa Sameer, aliyetokea kumpagawisha kitandani,juhudi za Sameer kwenye sita kwa sita zilimfanya asahau kila kitu cha nyuma,alichofanyiwa na Ahmed.
Akasahau mambo mema yote,alichokuwa anakifanya Yusrath ni kutema ‘big g’ kwa karanga za kuonjeshwa.Vitu vingi sana vilikuwa, vinapita kichwani kwake,muda mwingi alimuwaza Sameer na sio mumewe tena!Kitendo cha kuingiliwa kimwili kilimfanya asuse hata kuongea,hakumuongelesha Ahmed kama wafanyavyo wana ndoa,siku ziliendelea kusogea wakiwa katika hoteli ya Serena ambapo hapo ndipo waliamua kufanya fungate lao.
Wakati akiwa katika hali kama hiyo alitumia muda wake mwingi kushika simu akichati na Sameer,akimueleza ni jinsi gani amelimisi penzi lake,kitu kilichokuwa kinamtesa na kumfanya hisia zimpande ni mwanamme huyo Sameer alivyokuwa anamgusia habari za kufanya ngono,akimwambia kwamba ana njonjo nyingine anataka kumuonesha.Hilo likamfanya Yusrath,asisimke kila siku akitamani atoroke hotelini amfuate Sameer alipo.Hakuna siku iliyomfurahisha kama alivyosikia Ahmed ataenda Mjini Kariakoo, kununua vitu vya nyumba ambavyo wangehamia,akaamini kabisa ni lazima mwanaume huyo angechelewa.
Hakutaka kufanya makosa,siku hiyo Ahmed alivyoaga kuondoka, nayeye akavaa harakaharaka na kumtaarifu Sameeer wakutane Sinza,Kumekucha.Ambapo siku zote walikuwa wanakutana hapo na kufanya, ngono.Siku hiyo akakodi Taxi iliyompeleka mpaka Sinza,njiani alitamani gari hilo lipae sababu alikuwa mwenye haraka sana.
“Huwezi,kupita njia nyingine?”
Yusrath,alizidi kumsumbua dereva, ambapo haikuwa mara moja kuzungumza sentensi hiyo kila alipoona msongamano wa magari.Foleni ilisogea kwa mwendo wa Ajuza, mpaka walivyofika Bamaga,huko pia walikumbana na foleni nyingine.
“Kutakuwa na ajali nini mbele?Hakuna short cut nyingine huko tupite?”
“Dada,hii sio baiskeli ujue.Hili ni gari,tutapita wapi sasa?Kote kumeziba”
Dereva taxi,akamtolea uvivu hata yeye alionekana kuchukizwa na foleni hiyo kutokana na kuchoma mafuta yake mengi,hiyo ilimfanya Yusrath akae kimya sio kwamba hakutaka kujibizana naye aliamua kumezea tu na kumwacha kama alivyo,magari yalizidi kusogea.
Mpaka walivyofika Sinza Kumekucha walitumia zaidi ya masaa matatu,hapo dereva akapewa ujira wake, Yusrath akanyoosha mpaka kwenye moja ya Hoteli ambayo mara nyingi hukutana na Sameer,kwa kuwa alishajua ni chumba namba ngapi,haikumpa shida ikawa rahisi kwake kuuliza mapokezi.Akaingia na kugonga mlango,ulivyofunguliwa akahisi kama damu yake imeacha kutembea baada ya kumuona mwanamme huyo Sameer mbele yake, akiwa hana shati amevaa taulo peke yake.
“Karibu”
“Ahsante,nimechelewa sana kuna foleni”
Yusrath akasema, akijitetea kwani siku zote hakutaka kumkera Sameer,hapo hakukuwa na muda mwingine zaidi,isipokuwa walianza kushikana huku na kule,wakipigana mabusu kedekede.Hawakuwa na haja ya maongezi mengine, zaidi ya miili yao kuzungumza tu,Sameer akazungusha mkono wake nyuma ya kiuno cha Yusrath,akazidi kumvuta kwake na kumsogeza adoado mpaka kitandani akamuweka taratibu,akamvua dera na kulitupa kando!Yusrath,akabaki kama alivyozaliwa sababu ndani hakuwa amevaa chochote kile,hapo ndipo Sameer alipoanza madoido yake, hakutaka kwenda kwa pupa,akaanza kumshika na kupapasa kila sehemu ya mwili wake ili kumpasha joto!Kila kitu kilienda vizuri,mpaka Sameer anavua nguo zake ili waanze mechi, tayari Yusrath alishafika mshindo mara nane jambo ambalo siku nyingi halikuwahi kutokea!Mechi ilianza vizuri,wakiwa katikati ya mchezo huo,Yusrath alikuwa anatoa miguno na kulitaja jina la Sameer kimahaba,akilalamika na kusema ni kwa namna gani anampenda na angetamani kuwa mume wake,siku hiyo Yusrath alizungumza vitu chungumzima kwa hisia kali sana.
“Na...omba uwe Mme wa..ngu aaah aaah shss aah aah”
Sameer alizidi kushungulika na kupeleka makombola,dakika kumi na tisa baadaye kila mmoja akawa amelala chali,wamechoka kwa mbali.
“Baby,umejua kunipatia.Ulikuwa wapi muda wote huo?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Yusrath,alikuwa mwenye kila sababu ya kuuliza hivyo kutokana na mechi hiyo kuwa kabambe!
“Nilikuwepo mbona,wanasema kila jambo na wakati wake”
“I wish ningejuana na wewe mapema”
“Hata mimi”
“Nataka nikupe zawadi,sijui nikupe kitu gani?”
Yusrath alishindwa kufikiria ni kitu gani akitoe,ni aina gani ya zawadi ambayo ingekuwa kubwa na kuendana na Sameer,ilikuwa ni lazima amfanyie kitu kikubwa sana katika maisha ya mwanaume huyo,hakutaka kumpa zawadi ndogondogo tena za kawaida kama Boxa,saa na mashati.Akaenda mbali akataka kumnunulia gari ama kiwanja,lakini alivyofikiria gharama za vitu hivyo akashusha pumzi kidogo.
“Unaniamini mpenzi?”
Yusrath,akauliza swali akimuangalia Sameer machoni.
“Ndio baby”
“Nataka kukupa zawadi kubwa sana,lakini inabidi uwe mvumilivu”
“Nini tena jamani,mbona unanipa kiraruraru?”
“Hapana,usiwe na shaka”
Moyo wa Sameer,ulikuwa ukidunda kwa kutaka kujua ni aina gani ya zawadi anayotaka kupewa.Alikuwa anafikiria vitu vingi sana,akatumia kila njia ili Yusrath amwambie lakini haikuwa rahisi kwa mwanamke huyo kusema chochote.
“Niambie tafadhali, please baby”
“Nitakwambia,sitaki kukuhaidi kwa sasa hivi”
“Nambie tu,sitokusumbua.Nitasubiri”
“Nataka kukununulia kiwanja Sameer wangu,nadhani itakuwa zawadi yako kubwa sana,unastahili.Na hautoweza kunisahau”
Aliongea hivyo akiwa ameleweshwa penzi la Sameer na wala sio kingine,uwezo wa kumnunulia Sameer kiwanja kwa kutumia pesa zake, hakuwa nao,hiyo ilimaanisha ni lazima Ahmed achezewe mchezo mchafu ili atoe pesa hizo za Kiwanja kisha apewe Sameer,hilo ndilo lilikuwa kichwani kwa Yusrath ndiyo maana akasema kwa kujiamini sababu alijua kwa njia moja ama nyingine, angeweza kufanya hilo litokee.
Sio siri,hakuwa ana uhakika kama amesikia vibaya ama masikio yake yana uchafu,jambo la kupewa zawadi ya Kiwanja aliamini lingebadilisha mfumo mzima wa maisha yake,hapohapo akawaza kujenga nyumba kabla ya kupewa kiwanja hiko,hapo ndipo aliamini ule msemo wa watoto wa mjini kwamba ‘Mjini msingi kiuno’ akaunga mkono walionena msemo huo,leo hii kiuno chake na juhudi zake kitandani, kimemfanya atake kupewa kiwanja.Hakuamini hata kidogo, aliendelea kumwangalia Yusrath bila kummaliza akajiona kama yeye ndiye mwenye bahati kupita wanaume wote ambao waliwahi kuishi jijini Dar es salaam.
“Baby,are you serious?”
Sameer,akatumia Ung’eng’e kuuliza swali hilo ili kuonesha msisitizo.
“Ndio,nipo siriazi kwenye hili.Lakini ukiendelea kunifurahisha,inabidi usubiri pia nijifungue.Utapata vitu vizuri mbona Darling wangu”
Yusrath alihaidi vitu akaenda mbali zaidi na kumwambia Sameer kwamba yeye alizaliwa kwa ajili ya kuja kumpa maisha mazuri hapa duniani, hivyo kwa wakati huo ajiandae kula kuku kwa mrija!
“Baby,ahsante sana.Nitakupenda mno”
Sameer,akashukuru na kumbusu Yusrath katika paji lake la uso akajua tayari maisha yake yanaenda kuwa mepesi yaani ganda la ndizi na kwake vyuma vingeenda kulegea.
“Lakini kitu kimoja Sameer”
“Kitu gani?”
“Mimi nina wivu sana,sipendi kushea.Hilo naomba ulijue,sitopenda uwe na videmu demu vingine,sipendi sitaki.Kama utashindwa niambie hapahapa”
“Siwezi kukusaliti Darling,wewe ndio maisha yangu,wewe ndio my oxygen bila wewe siwezi kuishi”
“Nafurahi kusikia hivyo,nakupenda sana”
Kwa kuwa kiuno chake ndicho kilimfanya ahaidiwie vitu vingi vya thamani,ilimbidi akitumie vizuri.Baada ya hapo kilichofuata ni kumuonesha Yusrath utundu,wakaanza kunyonyana ndimi,Sameer akarudi chini kidogo akaipanua miguu ya Yusrath huku na kule na kutoa ulimi,hapohapo kazi ya kudeki bahari ikaanza mara moja!Mambo hayakuwa mazuri kabisa kwa Yusrath,akahisi kila kitu kimebadilika,akajiona kama yupo angani, anaelea juu hana sehemu ya kujishika!Mambo aliyokuwa anafanya Sameer, kwenye ikulu yake yalimfanya azidi kupagawa zaidi na zaidi.

********
Saa nne ya Usiku,kila mmoja alikurupuka kutoka kitandani.Yusrath akahisi kupagawa sababu alielewa ni kwa kiasi gani Ahmed angepaniki na isitoshe angepigwa makofi kwani alimuelewa sana mumewe ni jinsi gani alivyokuwa mwenye hasira za karibu,alichokifanya ni kuingia bafuni harakaharaka na kujimwagia maji, akatokeza na kumuangalia Sameer ambaye alikuwa bado yupo kitandani.
“Baby,utalala humu?”
“Ndio”
“Ah wapi ili ulete mademu zako,vaa twende baby.Nimechelewa,mme wangu hatonielewa”
“Sawa,naenda kuvaa sasa hivi”
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana,Sameer akavaa na wote kuanza kutoka nje ambapo huko Yusrath alichukuwa Taxi iliyompeleka mpaka Posta,akimuacha Sameer Sinza!Saa 5;45 alifika nje ya hoteli,Yusrath akamlipa dereva na kuanza kutembea kwa haraka tofauti na siku nyingine zote,bila kuuliza chochote akapita mapokezi na kunyoosha moja kwa moja kwenye lifti,kichwani akitafakari ni uongo gani atumie ili Ahmed amuelewe.Lakini akili ikamjia haraka,kwa kuwa walikuwa kwenye ugomvi mkubwa ilikuwa rahisi kwake kujitetea,lifti ilivyofunguka akatembea mpaka mlangoni na kusukuma,akatizama huku na kule, hakukuwa na dalili yoyote ile ya Ahmed kuwepo,akanyoosha mpaka bafuni.Kitendo cha kuvua nguo zake ili aoge,akashtuka baada ya kusikia kelele.
“Ngowiiiii,Mke wanguuu hayupooo.Mke wanguu yuko wapiiiiiiii?My wife”
Kelele za Ahmed,zilimshtua kwa kiasi cha kutosha.Akarudisha gauni lake mwilini na kutoka bafuni.
“Wee Ahmed”
Akaita kwa sauti ya ukali kidogo.
“My wifeeeee!”
Ahmed akawa kama mtoto mdogo aliyemuona mama yake,akamsogelea Mkewe na kumkumbatia kwa nguvu.
“Nilijua,umeondoka Mke wangu.Nisamehe sanaaaa,I’m so sorry”
“Mbona unanuka pombee Ahmed,ulikuwa wapi?Kwa wanawake zako eeh”
Chumba kizima,kilitoa harufu ya pombe hiyo ilimfanya Yusrath aulize kwa ukali,akapata sababu ya kuongea hapohapo.
“Shemeeji,hodi kwanzaa”
Ilibidi Ngowi,aingilie kati baada ya kusikia malumbano hayo,ilikuwa ni lazima amkingie kifua rafiki yake ili ainusuru ndoa yao, iliyokuwa changa!
“Karibu Shemeji,mlikuwa wapi na Mme wangu?”
Yusrath akatupa swali,akijifanya amekerwa na kitendo hiko.Sura ya Ngowi haikuwa ngeni kwake,walianza kujuana katika hekaheka za ndoa, hapo ndipo Ahmed alimtambulisha kwake,ndiyo maana alivyomuona tu kidogo akapunguza sauti ya kufoka.
“Tulikuwa Kibangu”
“Bar?”
“Hapana,pale nyumbani.Baada ya kumaliza,tukaagiza palepale na kuanza kunywa foleni ilituchelewesha,isitoshe gari iliharibika njiani,nikamuita fundi aje kutengeneza”
Ngowi,alitoa maelezo hayo akiwa mkavu,yupo siriazi.Usingeweza kudhani kama anadanganya!
“Lakini Shemeji kumbuka huyu ni mme wangu”
“Nalijua hilo shemeji,naomba nisamehee mimi sababu ndiye nilimuhaidi nitamleta,kama unavyojua vyombo vya moto,ndiyo hivyo.Gari ikaharibika njiani”
“Aya shemeji,nashukuru.Lakini siku nyingine,muwe mnatoa taarifa sasa simu zimewekwa za nini?”
“Naelewa shemeji,halitojirudia tena”
“Aya,shem.Huyu amefika tayari,nikutakie usiku Mwema”
Yusrath,akakata maongezi hakutaka kuyafanya mambo kuwa marefu sana!Ngowi akaaga na kuondoka zake.
Hakuna siku ambayo Ahmed alipata kibarua kizito kama hiyo,Yusrath alifoka mno akijifanya amekasirishwa kwa kitendo cha Ahmed kurudi usiku mnene kama huo.
“Mke wangu nisamehee,sitorudia tenaaaa.I’m so sorry,nisamehee.Nilikuwa na Ngowi”
“Sitoweza kuwa na mwanamme mlevi,kumbuka Ahmed unaenda kuwa Baba.Majukumu yataongezeka sasa kama umeanza kulewa mapema namna hii,tutafika?”
“Hapana,nimekuelewa.Nisamehee my wife,sitorudia tena.Haki ya Munguu tena”
“Sawa,kesho tunaondoka saa ngapi?”
“Asubuhi mke wangu,nishapanga kila kitu”
Usiku wa siku hiyo,Kwa kuwa Yusrath alikuwa amewaka na kukerwa,ikabidi Ahmed atulie asimsumbue tena!

*****
Mazingira yalikuwa mazuri,nyumba ilikuwa kubwa ya kuwatosha yeye pamoja na mume wake, ukijumlisha na watoto ambao aliamini hapo baadaye watakuwepo.Hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kufika katika makao yao mapya,mbali na kuoneshwa picha kwenye simu na Ahmed.Lakini siku hiyo ilikuwa ni tofauti kabisa,nyumba ilipambwa na makochi mazuri ya kuvutia.Kushoto kulikuwa na ‘dinning’ yaani meza ya kulia chakula,kulia kuna jokofu kubwa la kampuni ya Samsung,hiyo haikutosha. Yusrath akatembelea jikoni ili ajuwe kulivyo,akaona jiko kubwa la kisasa sambamba na jiko la gesi,akatembea na kuingia chumbani.
Humo ndipo alipopagawa zaidi,akamgeukia Ahmed aliyekuwa nyuma yake!Bado hakuamini kama mwanamme huyo, angepeleka vitu kwa kasi namna hiyo,ki ukweli alistahili pongezi.
“Mme wangu,wewe ndio umefanya haya yote?”
Yusrath,akauliza.Hakutaka kuamini kile kilichokuwa mbele yake.
“Ndio,ni mimi Darling”
“Hongera Mme wangu,You are such a gentleman”
“Thank you baby”(Ahsante mpenzi)
Hiyo ndiyo nyumba yao,waliyotakiwa kuishi kama Mme na Mke!Ilikuwa ni furaha sana kwa Ahmed,kutimiza moja ya ndoto zake,alivyoangalia kidoleni akatabasamu baada ya kuona pete yake ya ndoa inavyong’aa.Siku hiyo waliongea vitu vingi sana,wakapanga mikakati chungumzima kuhusu maisha yao ya baadaye na namna ambavyo watakuja kuishi na watoto hapo baadaye,alichokifanya Ahmed ni kutaka kufungua akaunti ya Mtoto wake aliyekuwa tumboni mwa Yusrath,hakupata picha siku atakayoitwa Baba,alijiona mwenye majukumu mengi sana mbele ya safari,hata hivyo alifurahi kumpata mke mwenye akili na msimamo,hata siku moja hakudhani kama Yusrath angekuja kumsaliti sababu alimuelewa na alijua ni changamoto gani wamepitia mpaka kufunga ndoa.

****
Jumatatu asubuhi,alivyoamka hakutegemea baada ya kukuta chai ipo mezani,akamshukuru mkewe baada ya kunywa.
“Wacha niwahi ofisini”
“Bebi,nitakumisi sana.Jumba lote hili nitakaa mwenyewe?”
“Wala usijali Mke wangu,lazima nitafute.Sasa nikiendelea kukaa humu ndani,tutakula nini?”
“Sawa Darling,Mwaa mwaaaa”
Wakapigana mabusu kama ishara ya kuagana,Ahmed akatoka nje na kutafuta daladala ndogo, ambayo ilimpeleka mpaka Riverside,huko akachukuwa daladala nyingine,ambayo ingemfikisha Posta ofisini kwake.
Ilikuwa ni wazi kwamba Yusrath alimpenda Mumewe lakini vilevile,alimpenda zaidi Sameer,kila mtu alikuwa ana nafasi yake na kama ingetokea siku angeambiwa achague mmoja ili abaki na mmoja angeshindwa, sababu wote aliwapenda kwa nafasi tofauti,ndiyo maana kila kilichotokea, Sameer alikijua na muda mfupi akawa keshajuwa kwamba Yusrath amehamia Ubungo Kibangu.
“Kibangu?”
“Ndio bebi,huku ndio nipo”
“Mbona shamba huko?”
“Sio shamba bebi,ni pazuri wewe hujawahi kufika”
“Nishawahi kufika,kipindi cha nyuma”
“Basi njoo upaone”
“Wapiii?”
“Kwangu,napoishi”
“Hivi,unanitakia mema kweli?”
“Kivipi Darling?”
“Nije kwako,mimi sijitaki au?Mumeo je?”
“Mpaka nakwambia hivyo,najua nachokifanya”
“Bado hujanishawishi,yaani hata niwekewe kisu shingoni.Siwezi kuja”
“Sameer,please.Njoo upaone kwangu,nakuomba”
“Yusrath,hivi unanitakia mema kweli?Unapenda uhai wangu?”
“Ndio bebi,usiwe na wasiwasi wowote ule,nakuhakikishia hilo”
“Mumeo kwani hayupo?”
“Anatoka asubuhi,kurudi usiku”
“Kwahiyo?”
“Njoo,kesho!Saa tano ama saa sita sita hivi”
“Poa,bebi.Mimi nitaibuka”
Mchezo wao,ukaanza kuanzia siku hiyo.Sameeer,alivyofika siku ya kwanza,akatamani kufika siku nyingine pia, sababu Yusrath alimpikia chakula kizuri,wakalala chumbani kama mme na mke.
Mazoea yakajenga tabia,Ahmed akiondoka Sameer anaingia,wakawa wanapishana kama daladala barabarani.
Ahmed,hakuelewa lolote alikuwa bize na kazi.Alitambua majukumu yake ndiyo maana alitakiwa kufanya kazi kwa bidii zote kwani alikuwa ana familia inayomtegemea nyuma,mwezi mmoja baadaye, akapandishwa cheo kutoka Ass.Human Resorce Manager,Mpaka Human Resource Manager.Ilikuwa ni furaha kubwa kwake kwani mshahara ulikuwa unaenda kuongezeka.Habari hizo akampelekea Mkewe.
“Hongera sana Mme wangu,Mungu wetu ni mkubwa sana.Naona pia na mtoto wetu kaleta baraka”
“Aisee,siamini.Nakupenda sana mke wangu,nitakupenda daima”
“Hata mimi mme wangu,vua nguo ukaoge.Ukale chakula mezani,otea nimekupikia nini leo”
“Mmmh,wali samaki itakuwa”
“Muone vile,umekosa”
“Umepika nini sasa?”
“Aaaah,Makange ya Kuku”
“Wacha wee”
“Ndio,mwanamke mapishi bwanaaa”
Ilikuwa ni familia moja yenye furaha sana kwa upande mwingine,Ahmed alimshukuru Mungu kwa kumletea Yusrath,bila kuelewa kwamba mwanammke huyo kila siku analeta mchepuko ndani, hakuwa ana wazo kama hilo,hata angetokea mtu yoyote kumwambia jambo hilo angemkatalia katakata.
Mbali na kupandishwa Cheo,wiki moja baadaye Ahmed alipokea barua iliyomtaka asafiri kuelekea Jijini Mwanza kikazi.Ilikuwa ni furaha sana kwake kwani angeenda kutengeneza pesa nyingi,mbali na hapo hakuwa ana amani sababu angeenda kumuacha mkewe nyumbani peke yake.
“Unatakiwa kusafiri kesho kutwa Ahmed,mipango ya Tiketi ya ndege itakuwa tayari leo.Kazi njema!”
“Ahsante Boss”
Baada ya kuitikia wito huo,akapiga simu nyumbani kwake,ili azungumze na mkewe lakini simu iliita bila kupokelewa,akapiga tena na tena bila kupata majibu,wasiwasi ukaanza kumuingia kutokana na hali ya mkewe.Baada ya dakika moja simu yake ikaanza kuita, alivyoangalia juu ya kioo akaona jina la mkewe,akaipokea kwa haraka.
“Wife,uko wapi?”
Ahmed akauliza simuni,akionekana kama mtu mwenye jazba na wasiwasi mwingi sana.
“Nipo nyumbani mme wangu,nilikuwa jikoni.Simu nimeacha chumbani”Akadanganya,pembeni alilala na Sameer.
“Unanipa Presha,inabidi nikutafutie msichana wa kazi.Kama tulivyoongea”
“Bebi,acha.Mimi sitaki”
Yusrath,alikataa katakata,akiwa ana sababu zake muhimu.
“Sasa na hali hiyo,ukizingatia bado miezi miwili kujifung…”
“Usijali mme wangu”
“Mmh aya bwana,Kesho kutwa nitasafiri”
“Whaaaat?”(Nini)
“Kesho kutwa nina safari ya kikazi”
“Bebiii,please…”
“Nitakuja nyumbani,tuongee vizuri”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa,alivyorejea usiku akamwambia mkewe juu ya safari hiyo na namna ambavyo angeenda kutengeneza pesa nyingi.
Yusrath alifurahi kwa mambo mawili, Mumewe kusafiri ili yeye apate muda mzuri na Sameer na kingine alifurahi sababu aliamini pesa atakazopata Ahmed ni lazima nayeye apewe fungu lake.
“Bebii,nitakumisi sana”
Yusrath,akaanza kudeka.
“Hata mimi mke wangu,niombee nifike salama”
“Kuwa makini huko,tambua umemuacha mke nyumbani,anayekupenda sana”
“Naelewa bebi wangu”
Taarifa hizo hazikuwa siri,akampenyezea ubuyu huo Sameer na kumwambia kwamba ajiandae kujiachia na kupikiwa maanjumati kwani Ahmed,angesafiri.

****
Ahmed,alitakiwa kusafiri na ndege ya saa nne asubuhi,siku hiyo alikuwa mwenye hekaheka kuliko kawaida,alitamani kubaki na mkewe lakini pia safari aliitaka,ndiyo maana alikuwa akiaga mara mbilimbili asubuhi ya saa tatu ili akawahi ndege.
“Bebi,kwaheri.Nakupenda sana,baki salama”
Ahmed,akaaga kwa mara nyingine,wakapigana mabusu na mkewe!Alivyofika mlangoni akageuka na kuaga kwa mara nyingine.
“Bebi,ndege itakuacha”
“Nitawahi”
Ahmed,akatoka akiwa na begi dogo mgongoni,ambapo humo alibeba nguo mbili tatu za kubadilisha akiwa jijini Mwanza,kwa kuwa safari hiyo aliipanga, nje kulikuwa na taxi tayari iliyokuwa inamsubiri,alivyofika akaingia ndani na safari ya kwenda uwanja wa ndege kuanza.Hakuelewa kwamba mbaya wake,Sameer yupo maeneo ya Ubungo Kibangu,anasubiri aambiwe kwamba yeye amesafiri ili ajilie tunda kiulani,kitendo cha Ahmed kuondoka hapohapo Yusrath akaokota simu.Na kumpigia simu Sameer,akimwambia awahi wanywe Chai na Kuku wa kukaanga pamoja na soseji.
Dakika tano baadaye,Sameer akawa amaeingia,akapitiliza moja kwa moja mpaka seblen,akaingia jikoni akampiga mabusu kedekede Yusrath,kabla ya kuanza chochote wakaingia chumbani kwa lengo la kufanya ngono.

****
Ahmed Kajeme alikuwa ndani ya taxi,kiti cha nyuma anapelekwa uwanja wa ndege ili asafiri mpaka jijini Mwanza kikazi,kichwani kwake alikuwa ana mawazo tele, hususani pesa ambazo angepata ukichanganya na salio alilokuwa nalo benki.Kwanza alipanga ampe mkewe kiasi cha shilingi milioni mbili,kisha nyingine atafute kiwanja ama gari.Ilikuwa ni lazima akirudi kutoka jijini Mwanza,anunue kimoja kati ya hivyo.Mara,mawazo ya biashara mbalimbali, yakaanza kupita kichwani kwake,akawaza kufanya biashara ya migahawa lakini akatupitilia mbali wazo hilo,akafikiria kitu kingine cha kufanya.Akamfikiria mtoto wake wa kwanza,atakavyozaliwa.Mawazo,hayo yakafanya safari hiyo iwe fupi kwani alivyoangalia nje akagundua tayari amefika Buguruni,kwenye mataa.
“Shiiiiiiit,Mungu wangu!”
Ahmed,akaachia kelele baada ya kujisachi na kumfanya dereva taxi ageuke.
“Vipi kaka?”
“Nimesahau simu zangu,nyumbani.Embu paki pembeni kwanza”
Ahmed,akaamuru akawa kama mtu aliyechanganyikiwa akaangalia saa yake ya mkononi, akakuta zimebaki dakika 45 ili ndege ipae.Hapo ndipo alihisi kudata zaidi!Gari,likawekwa kando.
Alichokifanya,Ahmed ni kumlipa dereva taxi.Yeye akaanza kukimbia mpaka kwenye pikipiki, zilizokuwa pembeni.
“Naenda,Ubungo Kibangu!Twende tuwahi”
“Poa,twenzetu kiongozi”
Ahmed,akapanda kwenye pikipiki bila kupatana bei hilo halikuwa na umuhimu kwake.Simu zake,zilikuwa zina maana sana sababu zilikuwa na mambo mengi ya kiofisi,hivyo ilibidi amuhimize dereva afanye haraka.

*****
“Ngo! ngooo! ngoooo!”
“Ngoo! Ngooo! Ngoooo!”
Mlango ulikuwa ukigongwa,Yusrath alikuwa akisikia kwa mbali sana!Wakati huo alikuwa yupo chali,uchi wa mnyama, Sameer yupo juu yake,wanafanya usaliti mkubwa sana!Mlango uliendelea kugongwa kwa mara nyingine.


Kwa mara ya kwanza alidhani wenda anasikia vibaya,Sameer bado alikuwa juu yake lakini akajilazimisha kutega masikio yake ili apate uhakika zaidi,maswali mengi yalianza kupita kichwani mwake nani alikuwa akigonga asubuhi hiyo?Hakuwa ana mazoea na mtu yoyote yule na isitoshe mumewe aliaga ili awahi ndege,akiwa katikati ya kujiuliza maswali hayo ambayo alijijibu mwenyewe,mlango uliendelea kugongwa kwa mara nyingine.
“Sam…eeer”
Yusrath aliita,akiwa katikati ya raha huku akimsukumiza Sameer kwa juu atoke, ambapo mwanamme huyo hakuwa tayari kufanya hivyo kirahisi rahisi,aliendelea kumng’ang’ania Yusrath huku akizungusha kiuno hiyo, ilimaanisha alikuwa yupo tayari kukaribia safari yake,alivyomaliza akahema kidogo na kumuangalia Yusrath usoni,ambaye kwa wakati huo alionekana kuwa mwenye wasiwasi mwingi.
“Kuna mtu anagonga!”
“Unasemaje?Nanii?”
“Mimi sijui”
Sameer,alionesha kuchanganyikiwa, hakuelewa kwanini lakini uso wake ulionesha kuwa na wasiwasi mkubwa,akiwa kitandani.
“Atakuwa nani?”
“Mimi sijui Sameer,nisubiri”
“Nikusubiriiii?!”
“Nisubiri ndio”
Alichokifanya Yusrath,ni kutoka kitandani kwa kasi,akaokota dera lake na kuliweka mwilini harakaharaka,akafuta majasho kutumia kiganja chake cha mkononi na kufungua mlango wa chumbani,akanyoosha mpaka seblen,kabla ya kufungua mlango akauliza.
“Naniiii?”
“Tanesco”
Yusrath,akashusha pumzi ndefu ya kuchoka,akafungua mlango uliofungwa kwa funguo na kunyonga kitasa,akamtizama mwanamme aliyesimama nje mrefu kiasi amevaa shati jeusi kwa jicho kali,alikuwa ana kila sababu ya kukasirika sababu alimkatisha katika raha zake.
“Unataka nini?”
Bila salamu,akauliza.
“Nimekuja kuangalia,mita yako”
“Mwenyewe hayupo, Mume wangu kasa…”
Kabla ya kumalizia sentensi yake,ulisikika msukumo wa geti ambapo ulitoa sauti kubwa,alivyoangalia getini ili kujua ni nani,hapo ndipo mapigo yake ya moyo yalipiga kwa nguvu,hakuamini aliyemuona alikuwa ni Mmewe Ahmed,kwa jinsi alivyokuwa mwenye haraka akajua ni lazima kuna majirani walimwambia ndani ana mwanaume na Ahmed alifika hapo ili afumanie.Yusrath alitetemeka akahisi kama damu yake imeacha kutembea!
“Wife,nimesahau simu mezani.Niangalizie haraka,nachelewa ndege”
Ahmed,alizungumza huku akipiga hatua mbilimbili,hiyo ilimfanya Yusrath ashushe presha lakini ilikuwa ni lazima acheze kama pelle,hakutaka kumfanya Ahmed aingie ndani kwani viatu vya Sameer vilikuwa ndani, seblen.
“Simu?”
“Ndio,niangalizie mezani hapo,fanya haraka baby”
“Sawa”
Kwa kasi ya umeme,akaingia ndani akapiga viatu vya Sameer teke vikaingia chini ya meza,akanyoosha mezani,kweli aliziona simu za Mumewe akatoka nazo nje ambapo ilikuwa kidogo Ahmed, azame ndani.
“Hizi hapa baby”
“Sidhani kama nitawahi hii ndege”
“Utawahi baby”
Hakuwa ana muda wa kumsalimia mwanamme aliyemuona mlangoni kwake,ambaye alijitambulisha kama Tanesco,japokuwa alivyofika nje na kupanda pikipiki ndipo picha ya mwanamme huyo ilimjia kichwani,akaanza kujiuliza maswali,akauhaidi moyo wake ni lazima angeuliza akifika uwanja wa Ndege.
“Tuwahi,Airoprt”
Ahmed alisema baada ya kukaa nyuma ya pikipiki,akavaa ‘helment’ hapohapo safari ikaanza.Kichwani alikuwa ana mawazo mengi sana,alichokifikiria ni kuwahi ndege, ambapo zilikuwa zimebaki dakika ishirini na tano.
“Kaka,kimbiza.Ujuwe nawahi ndege”
“Poa”
Dereva wa bodaboda hakuwa na jinsi,akapandisha gia na kuanza kuyapita magari makubwa,ilikuwa ni spidi kali iliyokuwa inahatarisha maisha yao endapo dereva huyo asingekuwa makini,walifika Buguruni na kuanza kuyatafuta mataa ya Tazara,hesabu za dereva huyo ilikuwa ni kuwahi taa ambapo kwa wakati huo umbali wa kama mita ishirini ziliwaka za kijani,alivyosogea karibu zikawaka nyekundu.Ilikuwa ni vigumu kwake kusimama,akavunja sheria kwa kupita katikati ya makutano ya barabara hiyo.
“Pwoooo! Pwooooooooo!”
Ulikuwa ni mlio mkali wa honi ya gari kubwa, yaani lori lililokuwa na mzigo wa mafuta ya Petroli nyuma, linatokea Nyerere Road,lilikuwa katika mwendo mkali,ilikuwa vigumu sana kwa dereva huyo kufunga breki ndiyo maana akapiga honi,kila mtu akatupa macho upande wa lori hilo,hakuna mtu aliyeweza kuamini kilichotokea!
Isingekuwa utundu wa dereva wa pikipiki kucheza na usukani,akatoka nje ya barabara ingekuwa ajali mbaya kwani wangeingia chini ya uvungu na hapo ndipo ungekuwa mwisho wa Ahmed na dereva huyo, kutokana na uzembe wa dereva kutotii taa za barabarani.Kuna baadhi ya watu waliokuwa pembeni,kwao ilikuwa kama sinema lakini wengine walitoa matusi.
“Bodaboda ndio maana kila siku wanakufa,mpumbavu sana yule”
Ilisikika sauti ya Mzee mmoja,ambaye alishuhudia kila kitu.
“Yule jamaa ni kiboko,kama Chuck Noris.Alivyoitoa ile ngoma,kama movie vile”
Baadhi walimpongeza,wakati huo dereva huyo alikuwa tayari amefika Kipawa,wanatafuta uwanja wa ndege ulipo.Mapigo ya moyo ya Ahmed yalikuwa tayari yamehama njia yake,aliogopa kwa kiasi cha kutosha, kwake hiyo ingekuwa ajali mbaya,alivyofikiria hali ya mkewe ilivyo, ndio akaogopa zaidi.
Dereva wa pikipiki hakuwa mwenye habari,wakashuka Uwanja wa ndege langoni Ahmed akalipa na kuchukuwa Bajaj,ambayo ilimpeleka mpaka ndani kabisa,kitendo cha kuweka miguu yake ardhini akaanza kukimbia hatua tatutatu,muda wote alikuwa mwenye haraka na hofu yake ilikuwa ni tayari ndege ilishamuacha,alivyoangalia saa yake ya mkononi,akapagawa zaidi zilisalia dakika mbili tu,ukizingatia bado hajaonesha tiketi na kufanyiwa ukaguzi.Mungu sio Athumani,hakukuwa na foleni mbali na hapo hakuwa na mizigo,kitendo cha kufika getini tu dakika zilikuwa zimeisha,ilikuwa kidogo geti lifungwe.
“Fanya haraka,ulikuwa wapi kaka?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa msichana mrembo aliyesimama kandokando anakagua tiketi,Ahmed akaonesha tiketi yake na kuanza kutembea,akapandisha ngazi zilizowekwa mlangoni,akaingia ndani ya ndege.Kitendo cha kukaa tu,mlango ukafungwa kumaanisha angechelewa kidogo,ingekula kwake.

*****
Hali ya Sameer,ilikuwa mbaya.Kila kilichoongelewa nje,alikisikia.Akatamani aingie chooni ajifiche jasho jembamba lilimtoka kwani alisikia sauti ya mwanamme akihitaji simu,akajuta sana kuingia ndani ya nyumba hiyo kufanya ngono na mke wa mtu.Akatulia kidogo akitafakari ni kitu gani akifanye,ukimya ukatawala.Ghafla mlango wa chumbani ukafunguliwa kwa kasi Yusrath,akaingia.
“Mume wangu huyo,jifiche”
Sameer akaruka kama swala,hiyo ikamfanya Yusrath aangue kicheko mpaka akakaa chini kabisa,machozi yakaanza kumtoka,hakutegemea kumuona Sameer anaruka namna ile kama ngedere mtini.
“Ha! Haa! Haaaa! Haaaa! Haaaaaa!Uwiiiiiii.Kumbee mwanaume wewe,muoga hivyoo..Hahahahahaha”
Yusrath,aliendelea kucheka huku akipigapiga ukutani,hiyo ilimfanya Sameer akunje sura kwa hasira.
“Sasa unacheka nini?Mimi naondoka”
“Baby bwanaa hahahahaha,bado siamini ulivyoruka hahahaha”
“Yusrath,usicheke ujuwe mimi naondoka,siwezi kubaki humu.Kuja hapa,sahau”
“Darling,please.Nimekutania bwanaaa,umekasirika?”
“Huo utani gani sasa?”
“Kidogo tuu”
“Utani mwingine sio mzuri,ningevunjika taya je?”
“Usingeweza”
“Naomba niondoke”
“Baby,umechukia?”
“Hapana,naondoka”
“No pleaseee”
Yusrath,akatoa sauti ya puani na kumsogelea Sameer,bado damu yake ilikuwa inachemka,akitaka kuendelea na mechi.Bado kiu yake haikukatwa sawasawa,ndio maana akasogea mpaka kitandani,akavua dera lake na kumsogelea Sameer mdomoni mwake,wakaanza kunyonyana ndimi kwa fujo.Mawazo ya Sameer ya kutaka kuondoka,yakafutika mara moja, kichwa chake kikasahau kila kitu kilichotaka kutokea,alichokuwa anawaza kichwani mwake ni ngono tu,ndio maana msumari wake ulianza kusimama taratibu,damu yake ikatembea kwa kasi,mwili wake ukamsisimka.

*****
Shirika la ndege ya Precision Air,ilikanyaga Ardhi ya jiji la Mwanza mchana saa 7;40,ikatingishika kidogo na kukaa sawa.Hapo ikachomoka kwa kasi ya risasi kisha taratibu ikasimama mpaka kwenye maegesho yake maalum,miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo alikuwa ni Ahmed Kajeme,alishukuru Mungu kufika salama.Kwakuwa hakuwa ana mizigo mingi,akateremka na begi lake mpaka nje,huko hakutaka kupoteza muda.Alichokifanya ni kumpigia simu mkewe Yusrath akimtaarifu kwamba alifika salama,hivyo asiwe na wasiwasi wowote,alivyohakikisha katoa taarifa hiyo,akatembea mpaka kwenye Taxi zilizokuwa eneo hilo.
“Naenda Malinde,Kijiweni”
“Twende”
“Shilingi ngapi?”
“Twende mkuu,hatuwezi kushindwana.Usiwe na wasiwasi kabisa Kiongozi”
Rafudhi ya dereva huyo,haikuwa ya kisukuma.Sauti yake ilikuwa ya kawaida na alionekana kuwa ni mjanja mjanja,ndiyo maana alitaka kwanza mteja wake aingie ndani ya taxi ndipo wapatane bei.
Gari ikawashwa na safari ikaanza mara moja,hawakuchukuwa muda mwingi wakaingia mjini.Wakafika Posta,wakaipita Iseni wakanyoosha mpaka Pepsi ambapo huko waliunganisha na barabara inayoenda Mkuyuni,walivyofika Nyegezi Kona.Wakakunja na kuacha barabara nyingine wakaelekea Malinde Kijiweni.Ahmed,hakuwa mwenyeji sana,kupitia simu yake alielewa alitakiwa kufika hoteli inayoitwa Nyashizo,alivyofika hapo akauliza na kuelekezwa.
Haikuchukuwa muda sana,kupapata sababu eneo hilo lilikuwa maarufu sana,akamlipa dereva ujira wake kisha kuingia ndani ya hoteli hiyo,ambapo hapo alijielezea na kupewa funguo za chumba.
Alivyojitupa kitandani,akamtafuta Yusrath,lakini simu iliita bila kupokelewa.

*****
Bilionea George Charles,alikuwa katika mawazo makubwa sana ndani ya jumba lake lililofanana na Kasri ya mfalme ama Ikulu ya Rais,kila kitu katika maisha yake kilikuwa hovyohovyo,hakuelewa angeishi vipi.Alivyoangalia jumba lake kubwa na mali zake alizokuwa nazo,aliogopa zaidi kwani aliamini ni lazima siku moja angetangulia mbele za haki,kilichokuwa kinamuumiza moyo ni nani atakayekuja kurithi mali hizo, zilizokuwa nyingi kwa maana hiyo alihitaji mtoto.Sio kwamba hakuwa mwenye uwezo wa kupata mwanamke wa kuzaa naye bali alitaka mwanamke mwenye heshima na adabu zake,moyo wake ukamtuma kwa Yusrath.Akamfukuzia kwa kipindi kirefu sana hatimaye hakutegemea kilichotokea,mwanamke huyo alimkimbia na baada ya siku chache akafunga ndoa!Jambo lililomfanya azidi kumpenda zaidi,isingewezekana hata kidogo kwa mwanamke wa kibongo kumtolea nje wakati yeye alikuwa bilionea mkubwa ndani ya nchi hiyo,wanawake wengi walimsumbua lakini yeye hakuwa tayari,msimamo ulikuwa kwa Yusrath lakini alishaolewa tayari hakutaka kumsumbua tena, sababu aliheshimu hisia zake,hakuelewa ni kwa namna gani angempata mwanammke mwenye tabia kama za Yusrath.
Siku hiyo alikuwa katika mawazo mengi sana,simu zake zote akazima ili atafakari namna ya kufanya kwa kina.Kichwani kwake aliwachambua wanawake wengi, waliomtongoza.
“Dora,hanifai…No,no Manka yule,hapana mbinafsi!Stella,spenda sana anapenda maisha ya sterehe,hapana bado sijaona”
Bilionea George akawa katika mawazo mengi sana,siku hiyo!Hakutoka kabisa nje,hata walinzi pamoja na wafanyakazi wake walimshangaa siku hiyo.Katika kuwaza kwake ghafla ikamjia sura ya mwanammke anayeitwa Lissa Mnzava,mwanammke wa Kimeru!Mwanammke huyu alikuwa ni mrembo wa sura,mwenye mawazo chanya ingawa hakuwahi kukaa naye kwa kipindi kirefu.Mwanamke huyo walikutana ndani ya ndege akiwa anaenda Nchini China jiji la Beijing,hapo ndipo wakabadilishana namba lakini hawakuwasiliana sana kila mtu,akawa bize na mambo yake.
George Charles alikuwa katika presha kubwa ya kupata mtoto,zaidi na hilo alitaka kuwa na familia bora tena ya mfano wa kuigwa.Jicho lake likamuona Lissa Mnzava,akawasha simu na kuanza kumsaka.
Bahati nzuri akampata,mawasiliano yao kuanzia siku hiyo yakaanza kwa kasi,yakakuwa.
Kwa kuwa George Charles alikuwa ana pesa,siku moja akamuomba wasafiri mpaka nchini Senegal,wakafanye mazungumzo yao huko.Ni kweli jambo hilo lilifanyika kwake likawa jepesi,George Charles akagharamia,wakakaa nchini Senegal siku tatu nzima.Walivyorejea nchini Tanzania,kitu cha kwanza kilikuwa ni George Charles kumvalisha pete ya uchumba Lissa Mnzava,kilikuwa ni kitendo cha ghafla tena kilichotingisha nusu ya jiji la Dar es salaam,japokuwa jambo hilo lilikuwa siri kubwa lakini lilijulikana.Lissa Mnzava,alifurahia hakuamini kulala na kuamka angekuwa tajiri,hiyo ilimaanisha mali za George zingekuwa chini yake!Akazidi kumuonesha mapenzi ya dhati George Charles,kila alipotembea aliliringa sio mchezo mwendo wake ukawa wa mikogo,kazi yake ikiwa kutembelea magari ya George Charles,tena yale ya kifahari.Akaona hiyo haitoshi,akataka aolewe na George Charles ili awe mke halali wa Bilionea huyo.
“Baby,nahitaji uwe mume wangu”
Siku hiyo Lissa Mnzava,alisema ya moyoni.Wakiwa kitandani,akimkwaruza George Charles kifuani na kucha zake zilizokuwa fupi kiasi.
“Muda,ukifika nitakuoa Honey”
“Muda gani tena?Ama unataka kunichezea uniache?”
“Siwezi kufanya hivyo”
“Bali?”
“Listen,nitakuoa My love.Nishakuvalisha pete ya uchumba al…”
“No baby,kama hunipendi niambie!”
“Lissa,nakupenda mu..”
“Basi,tuachane.Siwezi kuwa nawewe”
Alichokifanya Lissa ni kutingisha kiberiti kama kilikuwa na njiti.
“Una uhakika na maamuzi yako Lissa?”
George Charles,akaibua swali mwanamme huyu hakuonekana kutingishika hata kidogo,alishayasoma mawazo ya Lissa tayari.
“George hunipendi”
“Nakupenda,kama huwezi kuwa mvumilivu sidhani kama tutafika.Better choose one kuwa namimi uvumilie ama tuachane”
George akahitimisha kwa swali,jambo hilo likamkera sana Lissa kwani hesabu zake zilikuwa kali sana,ilikuwa ni lazima aolewe na George Charles ili baadaye amuuwe kisha arithi mali zote alizokuwa nazo mwanamme huyo.
“Nimekubali,kuvumilia George nakupenda sana,wewe ndio mwanamme wangu wa mwisho,naomba usije kuniumiza”

********

Ulikuwa ni usiku wa saa tano,gari aina ya Pajero ilipiga breki nje ya Hospitali ya TMJ.Dereva akashuka kwa kasi na kufungua mlango wa nyuma,hakukuwa na haja ya maelezo ya kwamba mgonjwa aliyefikishwa usiku huo alikuwa hoi,ndiyo maana manesi walifika kwa haraka ili watoe msaada.Siku za Yusrath kujifungua,zilikuwa zimefika. Ndani ya gari alikuwa akilia tu,jasho jembamba linamtoka kila mahali,anajipiga piga mapajani uchungu umemshika.Mama Ahmed,alichanganyikiwa hakuelewa ni msaada gani autoe lakini alishukuru Mungu kumfikisha mkwe wake hospitalini salama salmin.
“Mshike kwa huko,muweke kwenye kiti”
Nesi mmoja alizungumza,wakaanza kumshika Yusrath,wakamuweka juu ya kiti kilichokuwa na matairi kwa chini yaani 'wheel chair'
Kikashikwa nyuma na kuanza kukimbizwa,mpaka kwenye chumba maalum,ambapo humo kulikuwa na madaktari wawili na wakunga wanne.Mama Ahmed,alikuwa nje ya chumba hiko,anapiga dua zote kwa Mola wake, Mkwe wake ajifungue salama,simu yake ilikuwa ikiita wakati huo.Mpigaji alikuwa ni Ahmed akiwa jijini Mwanza,kivyovyote vile alitaka kujua hali ya mkewe,Mama akapokea simu na kuiweka sikioni.
“Mama,nini kinaendelea?Keshafika hospitali?Keshajifungua?Nambie Mama hali ya mke wangu”
Ahmed,aliuliza maswali mengi mfululizo.Hiyo ilimfanya Mama yake mzazi ashindwe kujua aanze na swali lipi kujibu.
“Mimi nipo nje,usijali.Atajifungua salama tushafika hospitali”
“Huwezi kuingia?”
“Hapana”
“Basi usikate simu,nisikie kila kitu Mama”
“Mwanangu,punguza presha.Mkeo atakuwa salama”Mama,akamaliza na kukata simu,macho yake yote yalikuwa mlangoni,hata yeye alikuwa na kimuhemuhe cha kupata mjukuu.

******
Ndani ya chumba hiko,kulikuwa na hekaheka nyingi sana,Yusrath alilala juu ya kitanda bado alihisi uchungu wa ajabu.
“Sukumaaa,sukumaa mtoto atoke Mama”
Nesi mmoja,alisema.Yusrath akajitahidi kujikaza na kujikamua.
“Sukuma anatoka,sukuma usiache.Sukuma hivyo hivyo,sukuma tena”
Haikuwa rahisi hata kidogo,kichwa cha mtoto kikaanza kutoka taratibu,nesi akakinga mkono, Yusrath akaambiwa azidi kusukuma,mtoto alivyotoka akaambiwa asukume tena.Akatoka mtoto mwingine wa pili.
“Ni mapacha!Wote wa kiume”
Dokta mmoja wapo,akasema huku watoto hao wakianza kulia,wakawekwa juu ya kifua cha Yusrath.
“Ng’aaaa ng’aaaa ng’aaaaaaa”
“Ng’aaa ng’aaa ng’aaa”
Vilio vya watoto kulia kwa sauti vilitawala,walikuwa ni mapacha wawili,hatimaye Yusrath,akajifungua salama akatabasamu bila kuamini huku akiwa amewashika watoto wake, japokuwa alikuwa hoi bin taaban, alijitahidi kuwatupia macho!


Kwake yeye,ilikuwa kama ndoto kubwa siku hiyo.Akaamini ya kwamba muda wowote ataenda kuzinduka kutoka kitandani,kumbe haikuwa hivyo ulikuwa ni ukweli halisi kwamba kuanzia siku hiyo anaenda kuitwa Mama tena wa watoto wawili mapacha,akaona majukumu makubwa sana mbele yake!Kulea watoto,kuwasomesha na kuwafundisha maadili mema.Ndani ya chumba hiko kulikuwa na ukimya, isipokuwa kelele za watoto wake mapacha wakilia tu,Yusrath alikuwa katika mawazo makubwa sana,hasa alivyozidi kuwaangalia watoto hao.Sura ya George Charles ikamjia kichwani,baba mzazi wa watoto hao!Hilo lilikuwa wazi kabisa,akamsikitikia sana Ahmed kwani alikuwa akienda kulea watoto wasiokuwa wake licha ya yote aliapia kubaki na siri hiyo mpaka kifo ingawa wakati mwingine moyo ulimuuma sana.Akajuta na kutamani kila kitu kibadilike,akatamani muda urudi nyuma abadilishe kila kitu kilichotokea,alivyomkumbuka Sameer.Moyo ukamuuma zaidi,akajikuta anashangaa vitu alivyovifanya nyuma wakiwa kitandani na Sameer,akahisi kujuta.Akajiona kama yupo uchi wa mnyama tena katikati ya jiji la Dar es salaam pale Kariakoo shimoni,akakumbuka kipindi cha nyuma alivyokuwa mwenye msimamo mkali dhidi ya wanaume,ikawaje kirahisi akamkubali Sameer, kijana aliyemtongoza kwa kipindi kifupi,moja kwa moja swala la Sameer akalifananisha na ndumba,alikuwa ana uhakika mkubwa kwamba haikuwa akili yake, bali Sameer alitumia kizizi kumpata.
Akiwa katika mawazo hayo mengi,huku watoto wakiwa mikononi mwake,daktari akamfuata na kumuuliza maswali mawili matatu.
Bado alikuwa mwenye nguvu,tofauti na wanawake wengine wanaoishiwa nguvu wakitoka kujifungua,taratibu zikaanza kufanywa mara moja ili abadilishiwe wodi lingine.Taarifa za kujifungua kwa Yusrath,kuanzia sekunde hiyo hazikuwa siri tena.Mama Ahmed,akapashwa habari na manesi waliotoka,akafurahi ajabu hapohapo akampigia simu mwanaye,akimpa pongezi zisizokuwa na idadi kamili.
“Mama,unasema kweli?”
“Ndio mwanangu”
“Mapacha?”
“Huamini au?”
“Wote wa kiume?”
“Wa kiume,jiandae”
“Jamani,Jamani…Ahsante Mungu!Mke wangu je?Yeye mzima?”
“Mzima,bado sijamuona lakini”
“Mama,nitaomba ruksa nije hata kesho huko niwaone wanangu”
“Usijali mwanangu,hawa ni watoto wako.Usiwe na presha”
Mazungumzo yao yasingeisha bila Mama Ahmed kuaga,akaitwa na daktari.Kila kitu kikageuka na kuwa furaha katika familia hizo mbili,wazazi wa Yusrath wakafika muda huohuo pamoja na marafiki.
Kila mtu akataka kumuona Yusrath na kumpongeza,jambo hilo halikuwa gumu sababu tayari alishahamishiwa wodi nyingine, kilichofanyika ni wachache kuingia na kumuona kwa zamu.Wenye zawadi,walimpa,wenye pesa walitoa na waliofika mikono mitupu waliishia kutoa hongera.
“Shem hongera sana”
Benjamin Patrick Ngowi,alifika siku hiyo.Taarifa za kujifungua kwa Yusrath alipewa na Ahmed, usiku huo wa saa sita,akiwa tayari amepumzika.Lakini kwa heshima ilibidi afuatilie mpaka mwisho,ndiyo maana akafika usiku huohuo bila kujali chochote kile.
“Shika hii,utakula matunda Shem”
Ngowi,akatoa shilingi elfu sabini na kumkabidhi Yusrath ili imsaidie kula matunda na kujikimu akiwa hospitalini,hakutaka kuondoka hivi hivi,hapohapo akamtwangia swaiba wake simu.
“Ebwanaa,hongera.Watoto copyright nawewe”
Benjamin Ngowi,akatia chumvi ukweli ni kwamba watoto walikuwa bado wachanga sana, isingekuwa rahisi kujua sura zao zinafanana na nani.
“Hahahaha,embu nipe niongee na wife bwanaa wewe tutamalizana baadaye”
Yusrath,akapewa simu akaiweka sikioni.
“Mke wangu,hongera”
“Nawewe pia hongera sana Mme wangu”
“Natamani ningekuwa hapo,lakini kazi zimenibana Mama watoto!Ushawapa majina sasa?”
“Bado,nakusubiri wewe Baby”
“Nipe niongee nao basi”
“Darling…Usianze hapa,sasa utaongea nao nini?”
“Nitajua mimi,waambie nawapenda sana”
“Wanakusikia,watundu kama wewe”
“Ah,wapi.Wamerithi kwa Mama yao”
“Jibu unalo mwenyewe,mimi siongei hapo”
Wakajisahau kabisa kama simu wameazima, wakaanza kupiga stori.
“Mama Kinyogoli,amekuja leo.Huwezi amini”
“Amekuja kufanya nini?”
“Sijui”
“Mmmh,kazi ipo.Alikuja kukusalimia kwani?”
“Ndio”
“Kuwa makini baby,si unajua mambo yake.Mshirikina yule Mama,asije ikawa ametumwa tu”
“Hawezi,mimi kijukuu cha mtume!Baby,tutaongea baadaye.Simu ya watu”
“Okay Love,nakupenda sana”
Yusrath,akajihisi ni mwanamke mwenye furaha na mwenye bahati kwa wakati mmoja.Ndugu,jamaa na marafiki wakazidi kumiminika,kumpongeza!Usiku wa siku hiyo Ahmed akiwa jijini Mwanza,hakupata usingizi kabisa,alikuwa ni mwenye furaha isiyokuwa ya kawaida.Akatamani siku hiyohiyo arudi Dar es salaam, akajumuike na familia yake lakini jambo hilo lisingewezekana hata kidogo,akasubiri kukuche ili amwambie Bosi wake,kisha aombe ruksa.Kweli kulikucha,akaanza kufikiria namna ya kumuomba bosi wake ambaye alikuwa mkali hasa linapokuwa swala la kazi,akapiga moyo konde na kumpandia hewani,hakutaka kuzunguka akamueleza kila kitu.
“Ahmed,siwezi kukuruhusu.Unajua kabisa,wewe ndio tunayekutegemea kwenye huo mradi.Naomba,usiniangushe!Ndio kwanza,hao wagiriki wanafika leo”
“Lakini bosi in..”
“Hakuna cha lakini,fanya kazi.Kama huwezi niambie”
“Sawa,bosi ahsante”
“Kazi njema”
Hakuna kitu kilichomuuma kama siku hiyo,moyo wake ukachoma kama pasi.Akatamani apige tena simu kwa bosi wake na kumwambia hataki kazi lakini nafsi nyingine ikamwambia punguza hasira,familia yako itakula nini? Ukiacha kazi.Akatulia kitandani,akitafakari vitu chungu mzima.
Akafikiria vitu vingi sana,hapo ndipo wazo la kujiajiri mwenyewe likamjia,akatamani siku moja nayeye awe na kampuni kubwa.Yeye awe bosi,mwenye pesa na mamlaka ya kufanya kila kitu anachotaka, hata hivyo aliamini jambo hilo lisingekuwa rahisi kama anavyofikiria,ingemchukuwa miaka na miaka.Hakuwa na jinsi,isipokuwa ni kuingia bafuni ili ajimwagie maji, asubirie gari la ofisi lije kumchukuwa,akachukuwa simu yake na kumpigia Mama yake,akamsalimia na kumpa maagizo.
“Mama,nitawatumia laki nne,nguo za mtoto ongezeeni.Na mambo mengine”
“Tutanunua,hata hivyo baba yako,katoa milioni moja kwa ajili ya matumizi ya mtoto pia”
“Mwambie ahsante sana”
“Ndio tunajiandaa kwenda hospitalini hapa”
“Ahsante Mama”
“Utakuja lini?”
“Nitakuja siku yoyote tu,kazi huku zimenibana”
Ahmed hakutaka kuweka wazi alichoambiwa na bosi wake,hilo halikuwa na umuhimu sana kwa wakati huo,baada ya kukata simu akaingia benki na kutuma kiasi cha pesa alichohaidi.

****
“LEO NDIO MWISHO,kodi yangunataka utakutavit vyko vipo nje,hiyo sionyumba ya babayako,nataka kodi,leo ndo mwisho”
Ulikuwa ni ujumbe,ulioonesha kwamba muandikaji hakuweza kutumia simu vizuri kutuma meseji, japokuwa ulisomeka kwa shida,Rhoda Denis aliumia moyo na alikuwa katika changamoto kubwa sana.Sio kwamba hakuwa mwenye uwezo wa kulipa kodi ya nyumba anayodaiwa, bali biashara zake zilienda mrama,mzigo wa nguo alioagiza kutoka nchini Kongo, ulishikiliwa na TRA(Tanzania Revenue Authority)Wakitaka shilingi milioni saba,ndipo wauachilie mbaya zaidi walimpa siku saba,awe amefanya muamala huo, vinginevyo ungepigwa mnada,hakuwa tayari kukubali mzigo wake wa milioni kumi na nane,upigwe mnada.Ndiyo maana akachota kiasi alichokuwa nacho benki chote ili apunguze deni,hapo ndipo akajikuta anatumia kodi ya chumba chake.Alihisi kuchanganyikiwa,akaona kama dunia yote ipo kichwani kwake kaibeba,akatafakari kwa muda mrefu na kuwapigia marafiki zake simu akiwaomba msaada lakini wao walimtosa,hakuna hata mmoja kati yao aliyemsaidia.Meseji,aliyotumiwa kutoka kwa baba mwenye nyumba,ilimtisha na ilikuwa wazi kabisa kwamba siku hiyo ni lazima angekuta vitu vyake nje,hakutaka aibu hiyo imkute, ndiyo maana kazi yake ilikuwa ni kuhangaika huku na kule,kutafuta pesa.
Hapo ndipo mwanamke anayeitwa Yusrath akamjia kichwani kwake,hakutaka kujifikiria mara mbilimbili,akampigia simu hapohapo.
“Rhoda,za masiku.Ndio unanikumbuka leo?”Upande wa pili wa simu,ukasikika.
“Mimi mbona nakukumbuka kila siku”
“Sijakuona mbona hospitali?”
“Hospitali?Wapi?Kuna nini?”
“Kumbe huna habari,mwenzako nimejifunguaa mapacha hapa TMJ”
“Weeee,liiiini?”
“Juzi tu,leo au kesho nitaruhusiwa kwenda nyumbani”
“Hongera mwaya,inabidi unielekeze kwako nije”
Baada ya Rhoda kutoa pongezi,akatulia kwa sekunde tatu nzima bila kusema kitu chochote,hakujua aanzie wapi kutangaza shida zake.
“Hallo,Rhoda.Utakuja nyumbani?”
“Nitakuja,lakini nina matatizo mwenzako”
“Una matatizo gani tena?”
“Ni stori ndefu lakini kwa sasa hivi nina shida na pesa”
“Kiasi gani?”
“Milioni nne”
“Mmmmh,mbona nyingi hivyo za nini?”
“Yusrath ni stori ndefu,naomba nisaidie.Nitahadhirika mwenzio,au kama una laki nne ama tano kwa leo,nikopeshe please please”
“Rhoda,kwa sasa hivi.Sina hela kabisa na hii hali niliyokuwa nayo ndio shida,kwa kweli itakuwa ngumu,siwezi kukuhaidi”
“Huwezi kumwambia hata mumeo?”
“Nitaanzia wapi my dear?Hayupo”
“Okay,poa”
Rhoda Denis,akakata simu bila kuaga,ilionekana wazi ni kwa namna gani amechukia.Akili yake ilimtuma kwamba Yusrath,asingeweza kukosa kiasi hicho cha pesa hata iweje kwani alikuwa mwenye mume ambaye ana uwezo kipesa,akakasirika na ili waumie wote akaapia kutoboa siri kuhusu watoto aliojifungua, hawakuwa wa mumewe,hilo ndilo wazo lililomjia lakini upande mwingine ukampiga ‘stop’
“Haiwezekani kama hataki kunipa pesa,nitaongea ukweli.Siwezi kukubali yeye ale bata mimi naumia.Kama mbwai na iwe mbwai tu”
Rhoda Deniss alihaidi, kwake kila kitu kilionekana kuvurugika.

****
“Sameer,nilishakwambia achana namimi.Unataka nini tena kutoka kwangu?Kila kitu sahau fanya kama hujawahi kukutana namimi”
“Aaaaah baby ak…”
“Mimi sio baby wako”
“Yusrath,upo na nani pembeni?”
“Nipo mwenyewe,chumbani”
“Sasa mbona umekuwa mkali hivyo,nini kimetokea?”
“Basi tu,sikutaki.Nimeamua kutulia na mme wangu.Ananipenda sana”
“Namimi je?”
“Tafuta mkeo,yaani nahisi kujuta.NAKUCHUKIAAA”
“Darling,una nini lakini?”
“Sameer,niache.Nimekwambia,achana namimi”
“Nakuja nyumbani kwako”
“Weeee,Mama yupo.Wakwe zangu wapo,mawifi.Usitake kuniharibia”
“Ujue,nitasema ukweli kuhusu hao watoto”
“Ukweli gani?”
“Unajitoa fahamu sio?Kwani hao watoto wa mumeo?”
“Nilikutania,watoto wa Mume wangu kwa taarifa yako”
“Basi sawa”
“Achana na mimi na Mme wangu anarudi Kesho,ukome kunipigia mbuzi wewe kasoro mkia”
Ungeambiwa huyu ndiye mwanamke aliyekuwa analilia penzi la Sameer,habadani ungebisha.Yusrath alibadilika, akawa mkali kama mbogo,hakutaka kumsikia tena Sameer,akili yake ikawa kama imerudi ilipotoka, moyo wake ukaanguka upya kwa Mumewe wa ndoa Ahmed, ambaye hapo kipindi cha nyuma alimfanyia usaliti mkubwa sana,alihisi kujuta lakini hakutaka kukumbuka mambo ya nyuma kwa namna moja ama nyingine.
Kwa kuwa alikuwa ameruhusiwa tayari yupo nyumbani hiyo ilimfanya Mama yake mzazi,achukuwe jukumu la kuishi naye mpaka pale Ahmed atakaporejea.Yusrath hakuweza kufanya kazi yoyote ile,kila kitu alifanya mama kama kuosha vyombo kuangalia watoto na shughuli nyingine za nyumbani,akisaidiana na ndugu wengine upande wa Ahmed.
Kila mtu akiwa mwenye hamu ya kumuona Ahmed nyumbani hapo,siku inayofuata ambapo alikata tiketi ya ndege ya asubuhi,kumaanisha kwamba saa tano ya asubuhi angekuwa jiji la Dar es salaam,Yusrath alitamani kesho ifike. Kwake aliona kama masaa yanatembea kwa mwendo wa kinyonga!

*****
‘NIMEKWAMBIA NINA SHIDA,HUTAKI KUNISAIDIA.KAMA HUTAKI KUNIPA HIYO HELA,NAMWAMBIA UKWELI MUMEO KWAMBA HAO WATOTO SIO WAKE’
Ulikuwa ni ujumbe mfupi wa meseji kutoka kwa Rhoda Denis, uliomfanya Salma atetemeke kwa uwoga, hakuelewa ni kwanini meseji hiyo ilifanya ahisi kama amepigwa na shoti ya umeme,akaisoma mara mbilimbili na kuwaangalia watoto mapacha, waliokuwa kwenye kochi wamelala seblen.
Simu ya Yusrath alikuwa nayo yeye mkononi, usiku huo wa saa tatu.Mapigo yake ya moyo yakapiga kwa nguvu,hakutaka kuamini kwamba binamu yake Ahmed,amebambikiwa watoto na Yusrath yaani sio damu yao, alichokifanya ni kufowadi meseji hiyo kama ilivyo kwa MAMA AHMED,kisha chini akaandika ‘Mimi Salma nakupigia sasa hivi’baada ya hapo akafuta ushahidi, isigundulike kwamba meseji hiyo kaifowadi kwa Mama Ahmed.


Mapigo ya moyo ya Salma yalipiga kwa nguvu sana,akahisi kutetemeka na kuumia mtima kuliko kawaida,hakutaka kuamini kama wifi yake ambaye siku zote alimpenda angekuwa mshenzi namna hiyo,mambo mengi yakaanza kupita kichwani baada ya kutuma ujumbe huo kwa Mama Ahmed,macho yake yote yalikuwa juu ya kioo cha simu akisubiri ipigwe na Mama huyo,ambaye alidhani hao ni wajukuu zake wa damu.
“Tayari,ushawabadilisha?”
Ni sauti ya Yusrath,ndiyo iliyomzindua kutoka katika dimbwi la mawazo,bado alikataa kuamini meseji aliyoiona kutoka kwenye simu ya Yusrath, wakati mwingine alilifananisha tukio hilo na ndoto ya kutisha,akiamini haikuwa hivyo, kila kitu kilikuwa na uhalisia kabisa.
“Ndio,vile visweta viko wapi?Ni baridi kweli sasa hivi”
“Ngoja nikakuchukulie”
Yusrath,akatembea na kunyoosha mpaka chumbani ambapo, baada ya kutoka mkononi alishika vikofia vidogo na masweta ya watoto wake mapacha, ambao kwa wakati huo walionekana kuwa ndiyo kila kitu katika maisha yake,furaha yake iliongezeka maradufu.
Alivyowasili seblen,alimkabidhi Salma ambaye kwa wakati huo, alijifanya haelewi chochote kile,hakuwa tayari kufungua kinywa chake mpaka afanye udadisi wa kina,ndiyo maana wakati huohuo,akaanza kuwachunguza watoto hao wadogo vizuri kuanzia pua,midomo masikio mpaka macho!Hakuna hata kimoja kati ya vitu hivyo vilivyorandana na Ahmed,hapo ndipo akajua kweli Ahmed kauziwa mbuzi kwenye gunia tena mchana kweupe,licha ya watoto hao kuwa bado wachanga aliweza kulipitisha hilo moja kwa moja,hakukaa sawa simu yake ya kiganjani ikaanza kuita,moyo wake ukazidi kupiga kwa nguvu baada ya kioo kuonesha mpigaji alikuwa ni Mama Ahmed.
“Nakuja my wiii”
‘My wii’ndivyo alivyozoea kumuita, kutokana na kuishi sana mjini kulimfanya aweze kuendana na misemo ya masista du wa kibongo,niya yake ilikuwa ni kupokea simu pembeni kabisa, Yusrath asisikie kitu chochote kile,alivyofika chumbani akafunga mlango,akaipokea simu na kuiweka sikioni.
“Shangazi,shikamoo”
“Marahaba”
Mama Ahmed,akaitikia kwa kifupi bila kuongeza kitu kingine chochote kile, kumaanisha kwamba alitaka Salma azungumze kila kitu kilichotokea.
“Shangazii”
“Nakusikia”
“Umeona Meseji niliyokutumia?”
“Salma,ebu nisikilize kwa makini.Chunga sana huo mdomo wako,unaelewa unachokiongea?Huo mdomo wako,utakuponza,nachokuomba kesho sitaki uwepo hapo.Usije ukaleta balaa,umenielewa?Nakuuliza umenielewa?”
Kile alichotaka kukisikia kutoka kwa Mama Ahmed, kilikuwa ni tofauti na alichotarajia,alichokitegemea yeye ni sapoti na wenda Shangazi yake huyo angemwambia waanze kuchunguza lakini haikuwa hivyo,Mama Ahmed aliwaka na alionesha kuchukizwa na tabia ya Salma ya uswahili,hakutaka kukubali, hata simu ilivyokatika ikamlazimu anunue kifurushi kutoka Tigopesa,akampigia tena Salma, akimsisitiza aache mambo ya Kipumbavu ya kutaka kugombanisha familia za watu,akahitimisha kwamba ahame nyumbani kwa Binamu yake Ahmed,haraka iwezekanavyo.
“Uondoke hapo kesho,kwanza mumewe anakuja,hauna haja ya kuendelea kubaki”
“Sawa Shangazi,nimekuelewa”
Hapohapo Mama Ahmed,akakata simu bila kujibu chochote kile.

****
Alishawahi kusafiri sio chini ya mara tano,lakini kwake safari hiyo ilikuwa ndefu kuliko hata ile aliyotokea nchini Tanzania mpaka nchini Malaysia,kutoka jijini Mwanza mpaka Dar es salaam, yalikuwa ni masaa mengi sana kwake kuwasili,kichwani kwake alimuwaza Yusrath na watoto wake mapacha ambao walitoka kuzaliwa siku chache nyuma,Ahmed alijiona ni mwenye bahati sana sababu hata hivyo, ndoto yake kubwa ilikuwa siku moja aje kuwa na watoto mapacha,akiwa ndani ya ndege akamshukuru Mungu kwa kusikia kilio chake.Akaanza kupata picha namna atakavyowatunza watoto wake na kuwadekeza,akawaza kuwasomesha shule nzuri za kimataifa, ikiwezekana hata nje ya nchi wapate elimu bora na wajue kuongea kiingereza kilichonyooka,alitaka wanae wapate malezi bora,ilikuwa ni bora awe maskini kuliko kuwaona watoto wake wanateseka,ndiyo maana siku hiyo alikuwa ana mizigo mingi ya zawadi kwa ajili ya watoto wake,akiwa katika mawazo mengi ndipo aliposhtuliwa na spika zilizokuwa ndani ya ndege ikiwataka abiria wafunge mikanda kwani tayari walikuwa wanatua, uwanja wa ndege wa kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,hapo alitabasamu na kufunga mkanda,utaratibu wa ndege kutua ulieleweka siku zote, mpaka kusimama.Hapo Ahmed akawa wa kwanza kutoka kitini,akasimama wima na kuanza kutoa mabegi yake madogo juu sehemu maalum.
“Kaka naomba kupita”
Msichana mmoja ilibidi aombe njia sababu Ahmed alikuwa ametanda kwenye njia nzima,akavuta begi lake kwa nguvu na kuanza kushusha ngazi,alivyofika sehemu ya mizigo akaanza kuokota begi moja baada ya lingine,akachukuwa kitolori na kuweka mabegi hayo juu yake!Akakisukuma mpaka nje,ambapo huko alikumbana na taxi nyingi,akatizama huku na kule,akamuita dereva mmoja wapo.
“Wapi braza?Karibu sana”
“Ubungo Kibangu”
“Twende,hakuna shida tunafika”
“Bei gani?”
“Utanipa arobaini”
“Shika hilo begi vizuri,lina vitu vya kupasuka”
“Poa poa blazaaa”
Dereva taxi,alionekana kumchangamkia abiria wake,wote wakaingia ndani ya taxi.Kitendo cha safari kuanza mawazo ya Ahmed yakarudi upya,akaikumbuka familia yake kwa mara nyingine,hakutaka kuvumilia, akachukuwa simu na kumtafuta mkewe hewani akimtaarifu kwamba ameshuka kwenye ndege, hivyo yupo njiani ndani ya taxi.
“I can’t wait to see you my Husband”
“Hata mimi,Sweatheart!Hapa natamani gari lipae”
“Ilove you,siamini”
“Niamini baby,nipo njiani”
“Umefika wapi?”
“Tazara hapa”
“Baby,mboona mbaaali?”
Yusrath,akadeka simuni alikuwa mwenye kila sababu ya kufanya hivyo sababu alikuwa ni mtoto wa kike,aliamini kwamba kudeka ni suuuna!
“Nitafika baby wangu”
“Haya love,wanao wanataka kukuona”
“Hata mimi natamani kuwaona”
Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Ahmed,kila kitu kuanzia siku hiyo aliamini kingebadilika kwani jina lake, lingebadilika na kuitwa Baba,hiyo ilimaanisha alitakiwa aihudumie familia yake na si vinginevyo!

****
“Karibu mme wangu,karibu sana”
Yusrath,alikuwa katikati ya mikono ya mumewe amekumbatiwa kwa nguvu tena amejilegeza!Kila kitu kwake siku hiyo, kilikuwa ni furaha kubwa,hususani alivyomuona Mumewe kwa mara nyingine baada ya kusafiri kwa muda mrefu,sio yeye tu hata Ahmed alikuwa mwenye furaha kuliko kawaida, akatamani amnyonye mdomo lakini asingeweza sababu Mama yake mkwe alikuwa pembeni yao,anawatizama.
“Pole na safari Mme wangu”
“Nishapoa,kuna mizigo kwenye gari.Ngoja nikashushe”
Kilichofuata hapo,kilikuwa ni kusaidiana kushusha mizigo ndani ya gari, walivyomaliza dereva akalipwa ujira wake,Ahmed akanyoosha moja kwa moja mpaka chumbani ambapo Yusrath akaunga mkia,mlango ukafungwa hapo ndipo wakapata nafasi nzuri ya kukumbatiana na kupigana mabusu ya mdomo.
“Nilikumisi mme wangu”
“Hunishindi,yaani nilitamani sijui nifanye nini ili nifike mapema,nilikuwa naona siku haziendi al..”
Ahmed,akashindwa kumalizia anachotaka kusema,baada ya kuwaona watoto wachanga wawili wapo kitandani wamelala ndani ya neti ndogo yenye zipu,akasogea karibu na kupiga magoti ili awaone vizuri.
“Wamelala?”
Ahmed akauliza,bado hakuamini kama waliolala mbele yake ni watoto wake.
“Ndio baby”
“Ushawapa majina?”
“Nilikuwa nakusubiri wewe Darling”
“Mmmh,mke wangu!Kwanza kabla sijasahau,nina mazawadi yako mengi kwenye begi”
“Yako wapi?”
“Yote hayo mabegi yenu,wewe na wanao”
“Kweli baby?”
“Sina sababu ya kukudanganya”
Haukuwa utani,swala la kuwapa watoto majina wakaliweka kando kwanza,Yusrath akasimama na kuanza kufungua mabegi,mambo aliyoyakuta yakamuacha kinywa wazi.Zilikuwa ni zawadi za nguo na viatu vizuri.Ahmed hakuishia hapo,akasimama na kufungua begi, ambapo hapo alitoa mikufu na hereni.
“Baby,come geuka nyuma”
Yusrath,akampa Ahmed mgongo akaanza kuvalishwa mkufu ambao ulikuwa unawaka na kumeremeta.
“Dhahabu hizi mke wangu nimenunua pamoja na hizi hereni pia,pure gold.Nakupenda sana mke wangu!Wewe ndiye kila kitu kwenye maisha yangu,sitokubali mtu yoyote aingilie furaha yangu na kututenganisha”
Ahmed alizungumza kwa hisia zote, jambo hilo lilionekana waziwazi sababu machozi yalimlenga,akamkumbatia Yusrath kwa nguvu huku akikumbuka mabonde na milima waliyopitia,haikuwa kazi ndogo mpaka kumuoa Yusrath!
“Hata mimi nakupenda Mme wangu,nitakupenda daima”
Wote wakakumbatiana kwa nguvu!
Zawadi,ziliendelea kufunguliwa mpaka saa tisa ya Usiku bado Yusrath alikuwa akijaribisha nguo,zote zilionekana kumkaa kabisa,walitulia watoto wakaanza kulia hapo Yusrath akawa ana kazi ya kuwanyonyesha.
“Huyu mmoja,tumuite Faisal”
Ahmed,akavunjwa ukimya akimtizama mtoto aliyekuwa kwenye ziwa la kushoto anarusha rusha miguu akifurahia kunyonya maziwa.
“Mmh,baby na huyu?”
“Huyu Faad”
“Kwahiyo?Faad na Faisal?”
“Yes,Yule Faad huyu Faisal.Sasa sijui tutagundua vipi?”
“Mimi mwenyewe wananichanganya”
Hilo halikuwa utani,watoto hao walifanana sio mchezo,walikuwa kama tui la nazi na maziwa.Kila walipojaribu kuwachunguza ili kuwatofautisha,haikuwa rahisi kugundua,siku hiyo walizungumza mambo mengi sana hususani swala zima la maendeleo yao.
“Baby,hapa nina wazo.Nina pesa nimelipwa,naomba nishauri”
“Nikushauri nini Mme wangu?”
“Tununue kitu gani kati ya vitu hivi viwili.Kiwanja ama gari?”
“Baby,vyote vina uzito hivyo!Nikianza kukufafanulia hapa,utashindwa!Kwani wewe unataka kuanza na kipi?”
“Ndio maana nikaleta wazo hili kwako”
“Kiwanja ni muhimu,gari ni muhimu pia.Vyote vina umuhimu”
“Mwisho wa siku inabidi,tununue kitu kimoja hapo”
“Baby,tutaongea kesho.Sasa hivi,tulale kwanza pumzika”
“Okay love”
Kwa Ahmed,alielewa kabisa kwamba mkewe hatakiwi kushiriki tendo la ndoa kutokana na kutoka kujifungua,japokuwa alikuwa ana ugwadu lakini ilibidi akaushe kama hajui chochote,akalala kimya huku damu yake ikichemka kwa kasi ya ajabu.

****
Bado alikuwa ni mwanamke mrembo,aliyekuwa na mvuto wa kumfanya mwanaume yeyote yule amfuate na kumtongoza kwa maneno matamu na kumuimbisha kwa mashairi mazuri ingawa alikuwa tayari amezaa watoto wawili lakini umbo lake lilirudi kuwa vilevile na kuzidi kunenepa,nyuma ya yote hayo kulikuwa na mwanaume anayemgharamia, hakuwa mwingine bali ni Ahmed,juu ya meza ya Yusrath kulijaa vipodozi vya kila aina na manukato mazuri,marashi ndio usiseme.Kila kitu kilikuwa juu ya Ahmed,mwanamme huyo alijuwa kugharamia.Hakuelewa kwa kufanya hivyo,anafanya wanaume waliokuwa nje wazidi kummezea mate mkewe,hilo hakujali ilimradi tu anatimiza wajibu wake.
“Baby,nikuchekeshe”
“Nini tena?”
Siku hiyo usiku,Yusrath ilielekea alitaka kumwambia kitu mumewe.
“Najua utashangaa sana”
“Niambie,ni kitu gani?”
“Unamkumbuka yule mzee tuliyekutana naye siku ile pale getini,wiki iliyopita akaja pia hapa”
“Mzee gani?”
“Baby aaah,si yule mzee Idd ana mvi kichwani,anapenda kuvaa msuli”
“Nishamkumbuka”
“Eti ananitaka”
Ahmed alivyosikia sentensi hiyo,akakaa vizuri kitako kitandani!Akamtizama Yusrath mara mbilimbili kama amesikia vibaya ama masikio yake yana uchafu.
“Yusrath,ilikuwaje?”
Kama kawaida ya Yusrath kuripoti,hawezi kukaa na kitu moyoni hasa akitongozwa,akasema kila kitu kilivyotokea kuanzia walivyoanza mpaka mzee huyo kutamka maneno hayo ya ajabu.
“Mimi nitamvunjia heshima ujue yule mzee,ujue nitamwambia akukome”
“Baby,nakuomba achana naye!Mimi najua nitamfanya nini,niachie mimi hilo”
Sio babu Idd peke yake,wanaume wengi walizidi kumpigia misele ingawa walielewa kabisa alikuwa ni mke wa mtu.

***
Baada ya miezi sita kupita siku hiyo akiwa jikoni anapika uji wa watoto,akasikia mlango wake unagongwa!Akatembea taratibu mpaka mlangoni,ambapo hapo aliufungua,mwanamme aliyemuona alimfanya apigwe na butwaa la waziwazi.
“Sameer,umefuata nini nyumbani kwangu?”
“Nimekufuata wewe mpenzi”
“No!Nooo!Noooo!Naomba uondoke”
“Please,nikaribishe ndani nakuomba sana.Nipe dakika moja ya kuongea nawewe,moja tu.Dakika moja tu”
“Mme wangu,akikukuta je?”
“Hawezi kuja sasa hivi,najua ratiba zake!Naomba niruhusu kuingia ndani”
Ilikuwa kama Sameer alichora mazingira yote vile kwani ndani ya nyumba hiyo,alikuwepo Yusrath na watoto wake tu,kitu alichokifanya Yusrath ni kumkubalia Sameer aingie kwa lengo la wao kuzungumza tu.
“Nakupa dakika moja tu”
“Sawa”
Sameer,akaingia mpaka ndani na kukaa seblen,Yusrath akasimama mbele yake na kumsikiliza shida yake,hapohapo Sameer bila kuongea kitu chochote kile akasimama na kumshika kiuno akamvuta karibu.
“Sameer,niaach…..eee”
Niya ya Sameer ilikuwa ni kulazimisha denda,Yusrath hakuwa tayari ndiyo maana akakwepesha mdomo wake,hiyo haikusaidia kwani Sameer aliendelea kung’ang’aniza huku akimvuta kiuno,mwanaume huyu alikuwa mjanja alifanya hivyo huku akijaribu kuingiza mkono wake ndani ya mgodi wa Yusrath akiamini akifanikiwa hilo,lazima afanye anachotaka.Haikuwa kazi rahisi kama alivyodhani kwani Yusrath alimsukumiza na kuanza kumkwaruza na kucha usoni,hata hivyo Sameer hakuwa tayari kukubali akazidi kutumia nguvu mpaka alivyofanikiwa kumpiga denda Yusrath,hapohapo mkono wake ukazama ndani ya ikulu.Yusrath taratibu, akaanza kuishiwa nguvu,akajisahau damu yake ikaanza kumwenda mbio.
“Aaaashaa mmhhh”
Ndani kwa ndani Yusrath,alianza kuguna baada ya kidole cha Sameer, kufika kwenye mapango,bila kuchelewa akatupwa juu ya kochi, Sameer akapanda juu yake huku akivua shati na kaptula aliyovaa,akamvaa Yusrath na kuanza kumtoa nguo yake moja baada ya nyingine,kwa jinsi alivyompania akaichukuwa miguu ya mwanamke huyo,akaipanua huku na kule akatoa ulimi wake na kuanza kudeki bahari.
“Aaaaah,shhhss aaaah mmmh Sam..eeer aaah st..oooop”
Hiyo ndiyo ilikuwa miguno ya Yusrath,baada ya Sameer kuanza, kupiga deki bahari!



Yusrath alikuwa tayari,amelegea!Hajiwezi tena,kila kitu kwake kilikuwa ni burudani.Kilichosikika hapo,kilikuwa ni miguno na kutamani Sameer aanze mechi hiyo mara moja!Akili yake haikuwa hapo tena,damu yake ilimwenda mbio akawa amelegea kabisa,anauma uma midomo huku akimshika shika Sameer kichwa, akimkandamizia kwenye mgodi wake,raha alizohisi haikuwa rahisi kwa mtu yoyote yule kumuita akasikia,ndiyo maana hata watoto walivyoanza kulia,hakusikia chochote.Aliendelea kujivinjari,sekunde chache baadaye akawekwa vizuri kwenye kochi, Sameer akajipinda na kuanza mechi hiyo kabambe!
Kuanzia siku hiyo,penzi lao likafufuka upya.Yusrath,akaanza tabia yake ya kishenzi na Sameer,hakujali kwamba yupo kwenye ndoa, isitoshe ana watoto wachanga bado,jambo la kuchepuka na Sameer lilibaki kuwa siri kubwa sana na alijificha kwa kiasi cha kutosha, ili kumfanya mumewe asijue,akawa anampa unyumba kila siku ya Mungu!Hiyo ikamuaminisha Ahmed kwa asilimia zote kwamba yupo mwenyewe kumbe alikuwa akijidanganya,mbali na hapo kama mwanaume alikuwa akitimiza wajibu wake wa kumpa pesa Yusrath, ambapo mwanamke huyo nayeye huzituma kwa Sameer moja kwa moja.
“Laki tatu baby,nimekutumia.Ule uvae,upendeze baby wangu”
Siku hiyo Yusrath alizungumza simuni,akimwambia Sameer kwamba amemtumia pesa za matumizi.
“Ahsante Laaziz,nakupenda sana”
“Sasa nikusikie,unaenda kuhonga”
“Nimuonge nani sasa baby?”
“Si,videmu vyako.Nikigundua,nitaua mtu”
“Hawezi kutokea,kwani nakosa nini kwako?”
Yalikuwa ni maongezi ya kuhatarisha maisha na ndoa yake kwa ujumla,endapo Ahmed angesikia na ilikuwa punje tu,Ahmed asikie kwani alikuwa chumbani na kitendo cha Yusrath kukata simu akatokeza seblen.
“Wife,mimi natoka!Pesa,zingine zipo kwenye dro la kabati,droo la chini lile.Utamalizia ile pesa uliyoniomba nadhani nimemaliza deni,alafu itakayobaki nitakwambia cha kufanya,atakuja mtu hapa na gari kuleta viti vya dinning na meza kubwa ya chumbani”
“Okay mme wangu”
Ili kumpumbaza Mumewe,akasimama na kumsogelea karibu kabisa,akaiviringisha mikono yake kiunoni mwake na kumuangalia usoni.
“Nakupenda sana Ahmed,Ahsante Mungu kwa kunipa wewe!Wewe ni mume bora,pia ni baba bora!Ahsante kwa kuja kwenye maisha yangu”
Ungeambiwa kwamba Mwanamke anayezungumza maneno hayo ana mchepuko,habadani ungebisha uso wa Yusrath ulikuwa mkavu hacheki hata kidogo,zaidi na hayo aliongea kwa sauti ya huba huku akiwa amelegeza macho yake,hiyo ilifanya kichwa cha Ahmed kivimbe,kitendo cha kumiminiwa sifa hizo kilimfanya atabasamu na kujiona ni mwanamme mwenye bahati kupendwa na Yusrath,zilikuwa ni sifa ambazo mwanamme yoyote angepewa ni lazima angevimba bichwa.Kilichofuata hapo yalikuwa ni mabusu kwa kwenda mbele!
“Baby,naomba niwahi please”
Ahmed alivyoona anazidiwa ilibidi aage kwani angeendelea na zoezi hilo kwa dakika nyingine mbili ni lazima wangepelekana kitandani.Kiuungwana akaaga na kutabasamu kisha kuondoka zake,kwa kuwa wakati huo alikuwa na pochi nene yaani ana pesa, ilibidi akodi pikipiki mpaka Posta,hakutaka kuchelewa kufika ofisini,alivyowasili akafanya kazi zake zilizokuwa mezani,akaweka sahihi hundi na kuipitisha benki,baada ya hapo akamtafuta Benjamin Ngowi, hewani.
“Ngowiiiiiii,ndugu yangu.Unajua kwamba wewe ni ndugu yangu sana”
“Kwani najua leo hilo?”
“Ndio nakusisitiza sasa”
“Nambie sasa,pole na safari kwanza”
“Nishapoa”
“Vipi familia,haijambo?”
“Wote wazima,leo wikend unajua eeh”
“Naelewa hilo,unataka kusema nini?”
“Hujui au?Nina kiuu ya Ndovuu”
“Ha!Haa!Haaa!Hahaaa,tunafanyaje sasa?”
“Bwana weee,kiwanja gani kinabamba leo Jumamosi?”
“Leo,leoooo.Kwetu Pazuri”
“Ndio wapi?”
“Tabata”
“Basi,sawa.Jioni nitakuwa hapo!”
“Sawa,Chief”

*****
Kilio kilikuwa kikubwa,mayowe yalitawala.Ulikuwa ni msiba mzito sana ambao ulijaza watu wengi nyumbani,ndani nafasi haikutosha.Waliopita nje walidhani wenda aliyefariki ni kizito ama kigogo wa nchi.Kumbe haikuwa hivyo,ni mwanafunzi aliyekuwa ana soma chuoni Makumira.Kilichowafanya ndugu,jamaa na marafiki wajae eneo hilo ni kutokana na mzee huyo kuishi na watu vizuri,hivyo katika tatizo kama hilo zito, ilibidi wawe naye bega kwa bega kushiriki naye.Mzee Mpilla hakuweza kuongea kitu chochote sauti ilimkauka,muda wote kichwa chake kilikuwa chini,ameshika kitambaa kipo usoni,matukio mengi sana yalipita kichwani kwake,kumpoteza binti yake Hajrath kwake lilikuwa ni pigo kubwa sana katika maisha yake,alishawahi kufiwa na kuumia lakini siku hiyo aliumia zaidi.
Muda wote alimuomba Mungu tukio hilo liwe ndoto ili ashtuke na kumuona binti yake kipenzi,Mama Hajrath muda wote alikuwa akipepewa seblen na wakina mama,alishazimia zaidi ya mara tisa na kuzinduka.
Alilia mpaka machozi yakamkauka.
“Mungu,nimekukosea nini mim..iii…Bora ungenichu..kua mi..mi,unirudishi..e mwana..ngu Hajrath”
Hivyo ndivyo Mama huyu,alikuwa akisema maneno hayo kwa uchungu akiwa seblen,pole hazikusaidia hata kidogo,alichotaka yeye ni mwanaye tu!Japokuwa aliamini hakukuwa na uwezo wa mtu yoyote yule kubadilisha kilichotokea!
Wakati ndugu,jamaa na marafiki wakiwa katika huzuni kubwa, taxi nyeupe ikawa imeingia na kupaki umbali wa mita kumi hivi,kutoka kwenye nyumba hiyo yenye msiba na turubai juu yake.
“Kaka,nimefika.Shika pesa yako,nitakupigia uje kunifuata”Dereva taxi,akapewa pesa yake!
Isingekuwa rahisi kwa harakaharaka kumtambua kwani kichwani alivalia kofia kubwa na miwani nyeusi ya jua,mbali na hapo alinenepa kiasi, tofauti na alivyoondoka miaka michache iliyopita,alishangaa kuona watu wengi eneo hilo la nyumbani kwao,juu kuna turubai kubwa.Mapigo yake ya moyo yalipiga kwa nguvu, akimuomba Mungu lisiwe jambo analofikiria kwani aliwapenda sana wazazi wake,akatembea kwa hatua chache mpaka kwa jamaa mmoja aliyevalia shati jeusi.
“Kaka samahani,mambo!Hapa kuna nini?”
Hajrath,akauliza.
“Kuna msiba dada,inasikitisha sana”
“Nani kafa?”
“Mtoto wa Mwenye nyumba hiyo”
Moyo wa Hajrath,ukadunda kwa nguvu.Picha ya kaka yake,ikamjia kichwani akajua ni lazima ndiye yeye amefariki kwani katika familia yao walizaliwa wawili tu hakuelewa kwamba wanamlilia yeye mwenyewe,akazidi kutembea kuelekea mbele zaidi watu wengi walimshangaa baadhi walipigwa na butwaa sababu mavazi aliyovaa yalikuwa tofauti na hali iliyokuwepo,wanaume wengine kazi yao ilikuwa ni kushangaa shundu alilokuwa nalo nyuma,Sio siri Hajrath alivyotembea alikuwa anatingishika makalioni,hilo likawa tatizo lingine.Alichokifanya,ni kuingia ndani ya geti mapigo yake ya moyo yakiwa yanapiga kwa nguvu,nje kulikuwa na wanaume wengi na wazee.Alivyoangalia vizuri akamuona baba yake,ameinamisha kichwa!Akatafakari kwa kina na kusogea karibu zaidi.
“Baba……”
Kitendo cha kuita hivyo,kilimfanya Mzee Mpilla agande kidogo,japokuwa kichwa chake alikiinamisha chini.Si kwamba hakusikia sauti,hakuwa ana uhakika kama ameifananisha ama ni kweli amesikia vizuri,akainua kichwa ili kumuona mtu aliyemuita.Hajrath,akavua miwani yake!Sijui ilikuwaje lakini mzee huyo,aliruka na kuwapiga watu vikumbo kwani alipigwa na mshtuko,mbio alizotoa hazikuwa na kipimo!Watu walimshangaa,kitendo cha kumuangalia mwanamke aliyesimama mbele yao vizuri,wote wakaanza kukimbia huku na kule wengine wakisema jini, baadhi wakipiga yowe na kusema ni mzimu.
“Jamaaani,jiiiiniiiiiii mzimu”
Kila mtu akaanza kutafuta usawa wake wa kutoka,hiyo ilimshangaza sana Hajrath!Wakina mama waliokuwa ndani ilibidi watoke nje ili kujua kuna nini,hata wao walivyomuona Hajrath walikimbia wengine wakidondoka na kukanyagana.Ikazidi kumshangaza sana Hajrath,alivyoingia ndani alimuona Mama yake,amelala analia.
“Mama!”
Hajrath,akaita huku akimsogelea mama yake taratibu.Cha ajabu nacha kushangaza Mama huyo hakukimbia,alibaki akimtizama Hajrath, haikujulikana alikosa nguvu za kusimama ama alidhani yupo ndotoni.
“Mamaaaa”
“Ha..jrath Mwanangu!”
Mama akaita nayeye,akawa kama mtu asiyeamini kitu anachokiona,Hajrath akasogea karibu wakakumbatiana kwa nguvu huku wakilia kama watoto wadogo!

*****
Umati wa watu ulikuwa mkubwa sana,kelele zilikuwa ni nyingi mno!Mziki wa hapo ndiyo usipime,hakuna mtu aliyemsikiliza mwenzake kwa wakati huo,ilikuwa ni lazima uongee kwa sauti kubwa ili usikilizwe, vinginevyo usingesikilizwa na wahudumu ama mtu wa pembeni yako.Licha ya hayo yote,sehemu hiyo kujaza ilikuwa ni kawaida,hususani siku kama hiyo ya Jumamosi,ambapo watu hupenda kwenda kutumbua pesa na kujipongeza kwa kunywa bia ama kula nyama choma.
Hapo ndipo Ahmed alipanga kufika na rafiki yake Benjamin Ngowi,taa za nje zenye rangi nyingi nyingi zilikuwa zinawaka kama ulikuwa ni mtu wa kula bata,usingepita sehemu hiyo hivihivi ni lazima ungepita ili utizame.Zaidi na hayo siku hiyo kulikuwa na bendi maarufu inayoitwa Malaika Band,inayoongozwa na Msaani maarufu Christian Bella,ndiyo maana siku hiyo watu walijaa mno!
“Leta,Heinken mbili.Huyu mwenzangu mletee Ndovu mbili nayeye”
Benjamin Ngowi,alimwambia Mhudumu kwa sauti kubwa kiasi,haikuchukuwa dakika vinywaji vikawa mezani,wakafungua na kupiga cheers,kila mmoja akaweka kinywaji chake mdomoni,walivyoshusha wakaweka mezani.
“Karibu Dar”
Ngowi,akavunja ukimya!
“Nishakaribiaa”
“Vipi,Mwanza huko?Wanasemaje?”
“Jiji lile ni zuri saaaana,hali ya hewa safi haina vumbi.Watu wa kule wakarimu mno”
“Mimi sijawahi kwenda,inabidi niende siku moja”
“Inabidi,fanya hivyo!Utaniambia”
“Ndoto yangu,nataka kuzunguka Tanzania nzima,kila mkoa!Kisha baadaye dunia”
“Safi sana,ni vizuri”
“Nataka kupata exposure,nijue namna watu wanavyoishi na vitu kama hivyo”
Hadithi na stori za hapa na pale,zikazidi kuendelea. Siku hiyo walikuwa na mengi ya kuongea,bia nyingine zikaletwa,muda ulizidi kwenda.
“Yes,nimekuuumbuka kituuu Ngowiii”
“Kitu ganiii?”
“Nahitaji,unishauri kitu kimoja rafiki yangu”
“Kipi hiko?”
“Hivi,ninunue Kiwanja ama Gari?Kipi kianze?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Ahmed,tena akiwa amesogea karibu kabisa ili watu wengine wasimsikie,alitaka ushauri kutoka kwa rafiki yake kwani swala hilo, alivyompelekea Mkewe akaonekana kumpotezea,ndiyo maana akalileta moja kwa moja kwa rafiki yake wa kufa na kuzikana.Swali hilo lilimfanya Ngowi amtizame Ahmed mara mbilimbili,siku zote aliamini kwamba mtu yoyote akikushirikisha kwenye jambo lolote linalohusu maisha yake binafsi ni lazima amekuamini hivyo,usimpotezee! Ndiyo maana akatulia na kutafakari kwa kina, kidogo.
“Ahmed,listen to me”(Ahmed,nisikilize)
Ngowi,akaanza kuongea na kuweka nukta!Alitumia kimombo sababu tayari pombe zilianza kupanda kichwani.
“Nakusikiliza broo,nipo makini”
“This is life ni lazima uchague kitu ambacho,utaona kinakupa furaha.Kiwanja kina umuhimu mkubwa sana,gari pia lina rahaa yake!Cha msingi,nisikilize kwa umakini.Mimi binafsi,nilianza na gari sasa hivi nina kiwanja,kuna wengine wanaanza na kiwanja kishaa yu buy a car!.....”
Ngowi,akaweka pozi na kucheua, akachukua glasi ya bia na kuiweka mdomoni,akapiga fundo moja na kumtizama Ahmed tena.
“Sasa hivi,una familia.Watoto wale wakiumwa ghafla usiku,utafanya nini?Utaenda na kiwanja hospitalini never,mimi ningekuwa wewe.Ningenunua gari kwanza!Kutokana na hekaheka za mjini”
“Nimekuelewa Ngowi,lakini kiwanja piaa kina umuhimu broo”
“Sijakataa,ndiyo maana nikakwambia vyote vina umuhimu.Kutokana na uhitaji wako,sasa hivi kwa hapa mjini huwezi kupata kiwanja kirahisi.Labda huko Kibaha,kaa ukijua hiloo.Anayway follow your mind”
“Ngowi,nahitaji ushauri wako lakini….Niambie nini nifanye”
“Nunua gari”
“Basi sawaaaaa,tupige cheers kidogoo”
Kilichofuata hapo ni cheers kwenda mbele,Ahmed akajiona mshindi sababu alipanga ndani ya siku mbili tatu zijazo akatoe pesa kwenye akaunti ili anunue mkoko,hakuamini kama nayeye ataenda kumiliki gari lake binafsi kwani alichoka kuomba omba lifti,furaha ilikuwa ni kubwa sana,usiku ulikuwa mwingi.
Kama kawaida yake,pombe zikimpanda kichwani ni lazima mwanamke atakayepita mbele yake amuangalie mara mbilimbili.
“Hallooooo,eeeh nani?Dustaaaan.Where are you my friend,nipo hapaa Kwetu pazuriiii.Aisee kuna mabalaaa,njoo njoo you just come.Nipo na jamaa angu mmoja hivi,njoo mzee”
Ngowi,ndiye alikuwa anaongea na simu kwa sauti kubwa ili ashindane na mziki wa bar,akasogea pembeni alivyorudi kwenye kiti akamkuta Ahmed amesimama na mwanamke aliyevalia kimini,mapaja yake yapo nje,akanyamaza na kukaa kimya.
“Namba yangu ndiyoo hii,just call me!Naitwa Ahmeeed,nitakupigiia baadaye ulisema unaitwaa nani tenaa chaurembo?”
“Prisca”
“Una jina zuriii,una mumee?”
“Kaka,tutaongeeaa baadaye kwenye simuuu.Nipo kwenye ile mezaaa”
“Mwaambiee muhudumu,akupe bia tano kwenye bili yanguu mimi hapaaa”
Ahmed akamaliza huku akimtizama mrembo huyo aliyejitambulisha kwa jina la Prisca,kimini cha mrembo huyo kilimfanya asisimke sio kitoto, mbaya zaidi msichana huyo alikuwa ana mguu wa bia,miondoko yake ilikuwa kama twiga.
“Ahmed,vipiii.Umeaanza sasa?”
“Niniiiii?Mtoto nimemuelewa huyuu.Kanipa namba ya simu”
“Achana nao,makahaba hao”
“I don’t care,vipi?Ongeza bia”
“No problem,kuna rafiki yangu namsubiri hapaa.Anakuja sasa hivi,ni Advocate!Ni mtu mmoja safi sana,nataka nikuunganishe naye”
“Mke wangu,atanielewa kweeliii..Usikuu huu?”
“Sasa hivi,hata mimi naondokaaa”
Hawakukaa sana,dakika tano baadaye akatokeza mwanamme mrefu kiasi mweupe.Amechomekea shati jeupe mkanda nje suruali nyeusi,kwa kumuangalia harakaharaka ungempa heshima zake kwani alikuwa msafi kuanzia juu mpaka chini kwenye kiatu,Benjamin akaanza kazi ya utambulisho.Baadaye wakaagiza vinywaji, ilivyotimu saa tano Ahmed akataka kuondoka,lakini Bwana Dustan akamsihi asiondoke anywe bia moja ya mwisho kwenye bili yake.
“Namuwahiii wifeee”
“Moja ya mwishooo,hata mimi nina mke”
“Una mke?”
“Ndioo”
Dustan akajibu na kuonesha kidole chake,kilichokuwa na pete ya ndoa.
“Sasa mkeo utamwambia niniiii?”
“Sikiliiza ndugu,jina lako nani tena?”
“Ahmed”
“Sikia Ahmed,mimi nipo kwenye ndoa huu mwaka wa saba!Wanaume wengi tunafeli,kwenye kitu hiki kimoooja….Unajua,mwanamke ni kama empty disc.Yaani cd ambayo haina kitu,kazi yako wewe ni kurekodi na kumshepu.Mwanamke hatakiwi kujua wewe unarudi saa ngapi.Hata siku moja,usimuwekee mazingira hayo,utaumia vibaya”
Ahmed,akatulia kimya ili asikilize somo.
“Kabla ya kumuoa mke wangu,niliishi naye miaka mingi ndani.Pia kabla ya hapo,nilikuwa naishi naye chuo,nimeanza kuishi naye nipo chuo mwaka wa pili, yeye yupo Form Four,anaaga kwao anaenda shule anakuja Hostel.Namuweka nao,nikaanza kumshepu mwenyewe mpaka amezoea.Lakini kitu kimoja,usimdanganye mkeo.So far,mimi amezoea hata nikirudi saa saba,ataamka atanipashia chakula,tunakula wote!”
“Lakini mke wangu mkorofiii huyoooo”
“Hakuna mwanamke mkorofi hapa duniani na hakuna mwanamke anayependa mumewe achelewe kurudi,mimi mwenyewe mke wangu ni mkorofiii haijawahi tokea ni mtataaa,kuna siku nakumbukla nipo Hostel mwaka wa tatu,alinifumania bwanaaa na demu ilikuwa soo kubwa.Alivunja vunja vitu mule ndani,sio tv sio redio sio vikombe.Hatukuongea mwaka mzima,lakini huyu hapa nimemuoa!Kwahiyo usimwendekeze,mwisho wa siku unatakiwa kujua,wewe ni mwanaume.Lakini kitu kimoja,timiza wajibu wako”
Siku hiyo walizungumza vitu chungumzima wakajuana,hata hivyo Ahmed alifurahi kuunganishwa na Advocate Dustan,wakabadilishana mawazo.Uzuri na kilichomfurahisha Ahmed ni baada ya kusema Advocate Dustan,anafahamiana vizuri sana na bosi wake.
“Kibangala?Wee mwambie siku umekutana na D.k,unamfahamu Anneth?”
Dustan akauliza.
“Aneth,ndiyoo namjuaaa”
“Umuulize unamjua DK,Unajua kwamba ile kampuni unayofanya kazi.Ilitaka kupigwa mnadaa?Unajua hilo?”
“Aaaaah,wacha bwaaanaa”
“Bosi wako,akanitafuta nilikuwa London.Ilibidi nirudi,kutetea.Alikopa milioni mia nane benki,tukaburuzana paaaale mpaka akashinda.Anyawei,hayo tuyaache.Maneno niliyokwambia,sio msaafu kwahiyo wahenga wanasema,lakuambiwa changanya na lako.Usiku mwema,muwahi mkeo”
Dustan,akahitimisha na kuweka glasi ya bia mdomoni,hapo Ahmed akasimama kwa kuyumba kidogo.
“Naenda kupunguza majiii kidogooo”
Ahmed,akasema na kuanza kutembea huku akipepesuka kidogo, akaingia chooni kutoa haja ndogo,baada ya kutoka hakuaga akatafuta pikipiki,ambayo ilimpeleka mpaka nyumbani kwake!Kilichomkuta huko ni kisanga Yusrath alivimba kama chura,hakuelewa somo alinuna na kukasirika kutokana na Ahmed kuchelewa kurudi.
“Nilikuwa naa Ngooowiiiii”
“Ngoowwwiii?Ngowwiii?Ndiyo anakufanya urudi usiku,Ahmed sasa hivi saa saba kasoro.Mme wa Mtu,una watoto wawili wadogo,are you out of your mind?”
“Mkee waaaangu,usiongee kwa sautiii,majiraani wanasikia tunawapa faida al….”
“Waache wasikie,nakwambia ukweli”
Yusrath siku hiyo,aliuwasha moto, akaongea kwa sauti kubwa hiyo ilimfanya Ahmed atembee mpaka chumbani,akaingia ndani ya neti na kujifunika shuka gubi gubi,hakutaka kuongea kitu chochote kile ili kuepusha shari.

*****
Nyumba yao japokuwa ilikuwa ya kupanga lakini ndani ilijitosheleza,makochi yalikuwa ya kisasa televisheni kubwa,friji la gharama.Nyuma ya hayo yote kulikuwa na mwanamme anayejielewa,Ahmed!Kama mwanamme alitakiwa kufanya kila analoweza ili nyumba yake iwe nzuri ya kisasa,kichwani kwake alikuwa ana swala lingine zito la kununua gari.Kisha baadaye kiwanja ili ajenge nyumba,mipango yake aliiweka vizuri na aliamini jambo hilo litakamilika ndani ya miaka miwili tu,hakupenda kuishi kwenye nyumba ya kupanga, alitaka siku moja aishi nyumbani kwake tena kwenye jumba la maana ndiyo maana aliweka bidii kwenye kazi.
Siku hiyo bado hakuamini alivyoingia kwenye ‘showroom’ ya magari,yalikuwa mengi mno tena mapya.Ndoto zake siku zote ilikuwa anunue gari ndogo ya kuanzia maisha na kumrahisishia safari zake za hapa na pale!Gari moja wapo lilimfamya alipende zaidi,akalisogelea na kuliangalia nyuma ambapo aliona limeandikwa kwa maandishi madogo ‘Verosa’,akalikagua vizuri.Gari hilo,alionesha kulipenda.Hakuchelewa zaidi,akamuita muhusika na kumueleza.
Haikuwa kazi ngumu,wakapatana bei kilichofuata hapo ni Ahmed kutoa kiasi cha pesa alichotajiwa,usajili ukaanza mara moja.Kila kitu kilivyokamilika,akakabidhiwa funguo!Bado,hakuamini kama anamiliki gari lake mwenyewe,kitu cha kwanza siku hiyo hakutaka kurudi ofisini alitaka kwenda kumfanyia ‘suprise’ mkewe mchana huohuo,aliendesha gari taratibu sana.Alivyoingia barabaraba ya vumbi yenye mawe na mabonde, akatembeza gari taratibu akiyakwepa mashimo.
“Oyaaa,weka pembeni gari yako ya mkopo hiyo.Au la shemeji?”
Zilikuwa ni kejeli kutoka kwa dereva wa DCM lililobeba abiria wengi,hiyo ni kutokana na Ahmed kuendesha gari mwendo wa bibi harusi,hata hivyo hakuwajali.Aliendesha mwendo uleule,alivyofika kwake akapaki akashuka na kufunga milango,akalitizama vizuri na kuliangalia gari lake hilo jipya.
Akafungua geti na kuingia ndani akiwa ana shauku ya kumwambia mkewe na kumuonesha gari jipya,alivyofika mlangoni alisita!Moyo wake ukapiga paa kwa nguvu,baada ya kuona viatu vya mwanaume nje ya mlango!Kijasho jembamba kikaanza kumtoka,hakutaka kuyapa mawazo yake kipaumbele kwamba mkewe ana mwanamme mwingine ndani,mbali na hapo ilikuwa ni lazima kuna mwanamme ndani sababu ya viatu hivyo vya kiume,hakutaka kujiuliza akanyonga kitasa kwa hasira na kuingia ndani mzima mzima,alichokiona kilimfanya apigwe na butwaa, lisilokuwa na kipimo chake!



Kila kitu kwake kilienda vizuri,furaha ikazidi kuongezeka ndani ya nyumba, watoto mapacha aliotoka kujifungua miezi michache iliyopita,walizidi kuongeza furaha na amani ndani ya nyumba yao!Kizuri na kilichomfurahisha, mume wake Ahmed alikuwa anatoa pesa nzuri ya kutosha, ambayo ingemsaidia kwenye kila kitu,mbali na hapo kulikuwa na akiba chumbani endapo itatokea dharura yoyote ya kwenda hospitalini, basi aingie chumbani na kutoa kiasi cha pesa,kifupi Yusrath alikuwa ni mwanamke mwenye maisha ambayo mwanamke yoyote yule, aliyekuwa ndani ya ndoa, alitamani kuwa nayo!Cha ajabu hakutoshekwa,alikuwa ana mpango wa kando, yaani mchepuko ambao kila siku alikuwa akiuhudumia na kuhakikisha mchepuko huo, ulikula vizuri na kuishi kwa rahaa mustarehe,ilikuwa ni bora mumewe amfokee kuliko Sameer akasirike!Siku hiyo hakuwa mwenye raha hata kidogo,hiyo ni kutokana na Sameer kukasirika,mwanamme huyo alikuwa ana shida na pesa.
“Sameer nitakutumia kesho,mpenzi wangu.Hapa sina hela,sijawahi kukudanganya”
“Kama hutaki,basi sitaki pesa yako”
“Baby,mbona unakuwa hivyo?”
“Nakuaje?”
“Nitakutumia”
“Achana nayo,nitajua pa kuipata”
Kitendo cha Sameer kuzungumza maneno hayo akakata simu,hiyo ilimpagawisha sana Yusrath presha kubwa ikampanda,alichokifanya ni kuingia chumbani na kuanza kuvuta ‘draw’ ambalo aliambiwa kama kuna dharura, basi atoe pesa humo ili imsaidie lakini alichokiwaza yeye ni kumtumia pesa Sameer,bila kujali wala kutafakari kitu kingine zaidi,akachomoa shilingi laki moja na elfu hamsini,akamtafuta Sameer hewani kwa mara nyingine,akamuelezea kwamba amepata pesa, hivyo atamtumia Tigo pesa,hakuishia hapo akamwambia ni kwa namna gani anampenda.
“Wewe ndio asali wa moyo wangu Sameer,sipendi kukuona unanung’unika,vitu hivi ni vidogo sana kwangu”
“Naelewa mpenzi,lakini nina shida leo inatakiwa itatuliwe”
“Basi nakutumia,nimekuongezea na Elfu hamsini nyingine”
“Ahsante baby”
“Nakupenda sana Sameer wangu,utakuja lini nyumbani?”
“Hata leo nitakuja,usijali”
“Okay baby”
Hilo likawa limekwisha,alichokifanya Yusrath ni kujiandaa ili kutoka nje akatume pesa kwa wakala,kwa kuwa wakala alikuwa nje ya geti,akatoka.
Jua lilikuwa kali,linachoma kama pasi mbaya zaidi ilikuwa ni saa saba mchana,watoto walikuwa tayari wamelala.Kwa mara ya kwanza kutoka nje,tangu ajifungue!Kila mtu alimshangaa kwani umbo lake lilikuwa limechanua,amenenepa.Umbo lake likajichora vizuri,kiuno chake kilikuwa chembamba, chini kidogo likajichora na kufanana na kibuyu.Hilo likawa tatizo kwa wanaume wanaopita,hakuwa mwenye habari,mkononi alikuwa na kiasi cha pesa kilichotakiwa kutumwa kwa Sameer.
“Habari”
Yusrath,akamsalimia wakala aliyemkuta kwenye kibanda.
“Safi dada karibu”
“Nataka kutuma Pesa”
“Mtandao gani?”
“Tigo”
“Shilingi ngapi?”
“Laki na hamsini”
“Poa,nipe namba”
Pesa ikatumwa kwa usahihi,akahakikisha imefika ndipo akaanza kuondoka,lakini akiwa karibu na geti akitaka kuingia ndani akasikia ameitwa kwa sauti kubwa,kushoto kwake akamuona Mwanaume mmoja mfupi maji ya kunde.
“Yusraaaath,ndio wewe ama naota?”
Mwanamme huyo akauliza,akionekana kama mtu asiyeamini mwanamke anayemuona mbele yake.
“Haaa!Shotola!”
Mshtuko wa Yusrath,uliambatana na furaha na uchangamfu mkubwa sana!Mwanamme aliyesimama mbele yake,walikuwa ni marafiki wakubwa sana kuanzia utoto na walikuwa wote lakini kilichowatenganisha ni baada ya mwanamme huyo kuhama mitaa ya Ilala,furaha yao ikawa kubwa sana kiasi kwamba Yusrath akaamua kumkaribisha Shotola nyumbani kwake,akavua viatu wote wakaingia ndani seblen.
“Ninaishi huku siku hizi,nimeolewa tayari”
“Mmmmh,acha masihara.Nilisikia hizo habari lakini sikuwa na uhakika,hongera sana.Ujue kuolewa siku hizi ni jambo la kumshukuru Mungu”
“Shotola,unakunywa nini rafiki yangu?Maana nina furaha kukuona,ni muda sana ujuwe!Kipindi hiko tunacheza wote kombolela”
“Usinikumbushe mbaliii,nakumbuka haa!haha,siku ile ulivyoingia kwenye matope ukaanza kulia hahaha”
Kilichofuata hapo,kilikuwa ni kicheko.Kila kitu kikarudi nyuma wakaanza kukumbushana mambo yaliyopita nyuma,utotoni. Namna walivyocheza wote michezo ya ukutiukuti na kula mbakishie Baba na mambo ya nyimbo za akina Amina Kadala,baada ya hapo Yusrath akasimama huku akicheka na kuliendea friji, ambapo alitoa soda kubwa ya coca cola,akatafuta na glasi kisha kummiminia Shotola.
“Hapa ndio kwako?Pazurii Sana.Hujaniambia shemeji nani?”
Shotola,akauliza huku akiweka glasi ya soda mdomoni,alivyoishusha ilikuwa nusu, ilielekea alikuwa mwenye kiu sana.
“Huwezi kumfahamu”
“Kweli?Kwani ni nani mpaka nisimjuwe jamani”
“Huwezi bwana,ulikuwa ushahama tayari”
Kazi ya Shotola kuanzia hapo ilikuwa ni kutizama huku na kule akiangalia mapambo ndani ya seble hiyo,hapo ilibidi Yusrath asimame ili kwenda chumbani kuwaangalia watoto wake kama wameshaamka tayari.Sekunde hiyo, ndipo mlango wa seblen ukafunguliwa ghafla, Ahmed akawa ameingia huku akiwa amevimba,sura ya mwanamme aliyemkuta seblen kwake ilimfanya apandwe na jazba zaidi.
“Wewe ni nani?”
Lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa Ahmed,hacheki kakunja sura anamtizama Bwana Shotola, usoni.
“Shikamoo bla…”
“Nimekuuliza wewe ni nani?”
“Mimi naitwa Shotola ni…”
Bwana Shotola,kijasho jembamba kilianza kumtoka mkojo ukataka kumpenya,akaishiwa pozi.Sura ya Ahmed ilimtisha na alijua muda wowote kuanzia hapo ni lazima lolote baya linaweza kutokea,alichoshukuru ni kutokea kwa Yusrath.
“Mme wangu,umerudi.Leo mbona mapema?”
Yusrath akauliza huku akitabasamu,hakuelewa kwamba ndiyo anachochea moto wa petroli.
“Hapa ni kwangu,narudi muda ninaotaka mimi…Huyu nani?”
Ahmed,akajibu na kuhitimisha kwa swali tena kwa ukali.
“Rafiki yangu”
“Kivipi?”
Kutokana na Ahmed kubadilika rangi,ilimfanya Yusrath aanze kutetemeka, alishaelewa kwa hali iliyokuwepo makofi lazima yahusike sababu alimuelewa mme wake,akaomba Mungu asije kufanya hivyo mbele ya rafiki yake.
“Kijana,unaishi wapi?”
Bwana Shotola akageukiwa na kutupiwa swali,ilibidi asimame ili ajibu kwa adabu.
“Mimi zamani,nilikuwa naishi Ilala jirani na Yusrath, sasa hivi naishi Tandale kwa Tum….”
“Swali langu,unaishi wapi?Sijataka maelezo yako”
“Tandale kwa Tumbo,mkuu”
Bwana Shotola,ilibidi ajibu kwa upole na kutoa heshima kwa kumuita Ahmed ‘Mkuu’
“Kwahiyo huko Tandale,hakuna wanawake wengine.Mpaka mke wangu?”
“Hapana Mkuu,huyu ni rafiki yangu”
“Sasa sikiliza,nakupa dakika sifuri.Naingia chumbani,nikirudi nisikukute”
Ahmed akamaliza na kunyoosha kuelekea chumbani,Shotola hakuaga wala kugeuka nyuma, akatembea mpaka mlangoni,hapo hakutaka kuvaa viatu alivibeba mkononi na kuanza kukimbia mbio ndefu,akihofia wenda mwanamme huyo,kaenda kuchukuwa bastola.Hasira za Ahmed,hazikuishia hapo zilihamia kwa Yusrath chumbani,akawaka akawa kama mbogo,wivu ulimkaa kohoni.
“Kwahiyo,umeanza kuleta wanaume ndani Yusrath?Naongea nawewe”
“Hapana Mme wa…”
“Kumbe nini?Kumbe nini?Alafu mliingia chumbani,mbona kitanda kimevurugika,mliingia kufanya nini huku chumbani?”
Ghafla likaibuka sekeseke lingine, baada ya Ahmed kuangalia kitanda na kukiona kimevurugika,hakija tandikwa kama siku zote akirudi kutoka kazini.
“Baby,sijatandika kitanda leo.Kilikuwa hivyo hivyo”
“Shut up,I said shut up mimi sio fala mimi sio boya..Nyamaza usiongee kitu unakaa na bwana ako seblen watoto umewaacha chumbani! Kwanza nipe simu yako,nipe simu yakooo”
Furaha ya kutaka,kumuonesha Yusrath gari ikapotea hasira zikampanda Ahmed akawa mbogo, anahitaji simu ya Yusrath,hapo ndipo Yusrath alipohisi mkojo unataka kumtoka,alichokumbuka ni kwamba kuna meseji za Sameer,badala ya kutoa simu akaanza kutabasamu na kucheka.
“Nipe simu yako,iko wapi?Usicheke,mimi sicheki”
“Baby,yule ni rafiki yan….paaaaaaaaa”
Kilikuwa ni kibao kikali,kilichomfanya Yusrath ayumbe hakukaa sawa,akapigwa kingine hicho kilimfanya adondoke kitandani puu,hasira za mwanamme huyu zilikuwa mbaya, hakuwa yeye tena wivu ulikuwa kohoni umepanda tayari,akatoka chumbani na kuanza kuisaka simu ya Yusrath,macho yake yakapiga huku na kule, akaiona simu ipo kwenye chaji,akaivuta na kuitoa.
Alivyotaka kuifungua,akashindwa sababu ilikuwa na namba za siri,hapo akanyoosha mpaka chumbani lakini cha ajabu,akakuta mlango umefungwa kwa funguo.
“Yusrath,fungua mlangoo..Yusrath fungua mlangoo”
“Ahm..de sifungui,sitaki.Siwezi kufung..ua na ninajiua,sifungu…i”
Sauti ya kwikwi ilisikika kutokea ndani chumbani,Yusrath alikuwa akilia machozi. Alishajua nini maana ya Ahmed kuingia ndani ya chumba hiko,kipigo kingeendelea, mbaya zaidi alijuwa kivyovyote vile mumewe ana simu na meseji za Sameer, zimeonekana ndiyo maana akajihami.
“Yusrath,nitavunjaa huu mlango.Nitakuuwa nakwambiaaa,Yusrath fungua mlango…Wee Malayaa”
“Mi..mi sio mala…ya,Ahmed kwani..ni unapeda kunipiga?Ma..penzi gani haya?”
“Fungua mlango nakwambia,fungua tuongee sasa”
“Sifungui… Nina..jiua”
Kelele,zilienea na aliyekuwa anapaza sauti kubwa ni Ahmed, hiyo ikafanya mpaka nje ya geti nyumba ya jirani wasikie,kila mtu akatega masikioni.
“Baba Happy,yule Mama atauliwa.Anapigwa,kelele nimezisikia muda mrefu”
Mama mmoja jirani na nyumba anayoishi Yusrath,alimwambia mumuwe kwani alisikia kila kitu.
“Sindo yule Mama aliyejifungua juzi tu?”
“Ndio Baba Happy”
“Aisee,ebu subiri kwanza”
Alikuwa ni mzee wa makamo,umri wake ulikuwa kati ya miaka 40-45! Kichwani ,alikuwa ana mvi,kumaanisha kwamba umri ulikwenda lakini sio sana kutokana na mwili wake kuwa mkakamavu kiasi.
Kelele zilivyoendelea,ilibidi asimame na kutoka nje ambapo huko aliingia mpaka ndani getini,akaingia mpaka ndani kabisa.
“Hodi humu ndani,hodi hodii.Jirani yangu”
Sauti hiyo ilimfanya Ahmed atulie kidogo na kusitisha zoezi lake la kutaka kuvunja mlango.
“Kijana,kuna tatizo gani?”
Baba Happy akawa keshaingia mpaka ndani,akamuona Ahmed alivyokuwa na jazba anahema juujuu.
“Hamna kitu mzee”
“Nasikia kuna kelele”
“Nimekwambia hamna kitu”
“Anataka kuniu..a naomba nisaidie”
Sauti ya Yusrath,ilisikika kutoka ndani ilielekea sauti hiyo aliisikia na kumfanya apaze sauti.
“Kijana wangu,ebu punguza jazba kwanza.Hasira siku zote ni hasara,huyo ni mkeo!”
“Ni mke wangu ndio”
“Kumpiga mkeo hata siku moja,haitakuwa suluisho”
Ahmed,akaona aibu kidogo akamtizama mzee huyo, akapita pembeni yake na kutoka nje ya geti,huko aliingia ndani ya gari lake na kulitoa mbio,akitokomea pasipo julikana.

*****
Ahmed,aliendesha gari kwa kasi ya ajabu.Kwa wakati huo,hakujali tena kama ni jipya,kwenye shimo alipita mzima mzima bila kupunguza mwendo,akaingia barabara kubwa bila kuangalia magari yanayotoka kushoto kwake,ilikuwa kidogo agongwe na gari lingine lililokuwa linakuja nyuma yake,hakujali akaingia ‘high way’ na kunyoosha.
Hakuelewa ni wapi aende lakini alitaka akae sehemu iliyotulia atafakari ni kitu gani akifanye,bado hakutaka kuiruhusu akili yake na kukubali kwamba Yusrath ana mwanamme mwingine, mbaya zaidi kamuingiza nyumbani kwake tena chumbani kwenye kitanda chake,kwake kitendo hiko alikitafsiri kama dharau kubwa sana.Mawazo yalikuwa makubwa,presha ilimpanda akiwa tayari amefika Mikocheni,akanyoosha mpaka Mlalakuwa ambapo huko alikunja kushoto.Ghafla akakumbuka sehemu moja,inayoitwa Kawe Club,akaamini hapo angetulia kabisa sababu kulikuwa na upepo wa bahari.Alivyofika,akapaki gari,akashuka na kutembea kwa haraka mpaka kaunta.
“Niletee bapa,na Ndovu.Nakaa kwenye meza ile pale”
Ahmed,akaagiza na kuanza kutembea kwa kasi kutokana na mawazo aliyokuwa nayo,akajikuta anajikwaa na jiwe lililokuwa chini,akayumba na kukaa sawa,akatembea mpaka kwenye kiti cha mwisho ambacho hakina mtu,akakaa na kutulia.

****
Yusrath,alibaki chumbani akilia kwa uchungu sana na hasira mpaka kamasi nyepesi zikawa zinamtoka puani,kitendo cha kupigwa makofi, kilimuuma kwa kiasi cha kutosha.Japokuwa mlango wake ulikuwa unagongwa lakini hakutaka kufungua,Baba Happy alimsihii afungue kwani Mumewe tayari keshaondoka.Alichokifanya Yusrath ni kutafuta begi lake dogo lilipo,akaanza kuweka nguo moja baada ya nyingine ndani.Akakusanya kila kitu muhimu huku akiwa analia machozi,akatembea mpaka kwenye draw la kabati ambapo kulikuwa na pesa, kiasi cha shilingi laki tisa,akabeba zote na kuweka kwenye mkoba.Akatembea taratibu mpaka mlangoni na kuufungua,akawarudia watoto wake pamoja na mikoba yake,hakutaka kumsemesha Baba Happy aliyekuwa mlangoni,alielewa jirani huyo anataka umbeya,hakuwa tayari kuzungumza chochote kile.Alichoshukuru Mungu ni kuiona simu yake juu ya kiti seblen,akaichukuwa.
“Jirani,unaenda wapi?Punguza hasira haya mambo yapo ni kawaida kwenye ndoa,nini kimetokea kwani?”
Baba Happy,akajaribu kumtuliza lakini haikusaidia, Yusrath akatoka na simu yake,akianza kuangalia namba za simu,akabonyeza bonyeza na kuweka sikioni.
“Ha..llooo Ma..ma shika..mooo”
“Marahaba,vipi?Kuna usalama?Mbona unalia?”
“Naku..ja nyumbani mama,kuna matatiz…o Ahme…d kanipiga”
“Unasemajeeeee?Kakupiga?Kwanini?”
Mama akauliza kwa mshtuko wa hasira.
“Naku..ja Mama,nipo njiani”
“Sawa mwanangu njooo,nakusubiri”
Yusrath alilia kwa uchungu akakata simu na kuanza kutafuta namba nyingine za simu,ambapo hapo alimpata dereva taxi aliyemzoea!Akamueleza sehemu alipo,ndani ya dakika ishirini taxi ikawa imefika nje!
“Twende Ilala,Shauri Moyo”
“Poa,upo sawa?”
“Yes,nina mafua tu”
“Sasa si utawaambukiza watoto?”
“Twende Shauri Moyo,Ilala”
Yusrath,hakutaka kuzungumza kingine zaidi, safari ikaanza mara moja.Lakini akiwa katikati ya safari ghafla sura ya Sameer,ikamjia kichwani akamkumbuka akazisaka namba zake lakini kabla ya kupiga akaingia kwenye uwanja wa meseji na kufuta meseji zote,hakuwa ana uhakika kama Mumewe aliziona meseji ama hakufungua kwani simu ilikuwa na password,hapohapo hakuchelewa akampigia simu na kumuelezea kila kitu kilichotokea kwamba Mumewe kampiga na yupo njiani kuelekea nyumbani kwao,Ilala kwa Mama yake mzazi.
“Sikia Darling,usiende nyumbani”
“Kwanini?”
“Tafuta sehemu,unisubiri tuongee”
“Wapi sasa Sameer?”
“Tafuta hotel hata pale Sinza,mimi nitakuja huko”
“Sawa,nitakwambia nikifika”
Simu ilivyokatwa,dereva taxi akaambiwa wameghaili safari,hawaendi tena Ilala bali Sinza, Kumekucha.
“Poa,sista”
Dereva taxi,akabadili muelekeo hakuwa na jinsi zaidi ya kutii amri ya abiria wake.

*****
Kwa kitendo alichokifanya,alijichukia hasa alivyowakumbuka watoto wake mapacha Faad na Faisal,ulikuwa ni usiku wa saa mbili yupo baa analewa ili kupoteza mawazo,baada ya kuchanganya Konyagi na bia,kusimama ilikuwa ni ngumu sana kwake!Ki ukweli alimpenda sana Mkewe lakini pia alizichukia hasira zake, ambazo alidhani moja kwa moja ni mapepo machafu,ikawa kama akili zake zimekaa sawa sasa baada ya hasira zake kuisha.Akajipiga kibao kwa kitendo alichokifanya,akawaza ni aina gani ya msamahaa amuombe Yusrath,Mama wa watoto wake.
“How could i be so stupid like this?Sijuiii nitakujaaa kuwa Baba ganiiiiii?Ooooh Mungu babaaaaa,haya ni mapepo hayaaa,narudi kwa mke wangu sasaaa.Nakupendaa Yusraaaaath”
Ahmed alizungumza mwenyewe huku akitembea,ungeambiwa mwanamme huyu anaheshimika ofisini kwake,usingekubali.Akatembea kwa kuyumba na kulitizama gari lake jipya.
“My new Caaaaar,hili gari ni letuuuu Mke waaangu,nisameheeeee.Nisamehee popote ulipo my wife”
Alivyozungumza hayo,akaingia ndani ya gari,hapo akatoa simu kwa niya ya kumtafuta Yusrath hewani lakini simu iliita bila kupokelewa,mwisho wa siku haikupatikana hewani.
“My Gooood,kaziiiima simuu.Yusraaath,nisamehee zilikuwaa ni hasira tu mke wanguuuu!Hapana,hii hatokubali,baby ni shetaani tuuu kanipitia!”
Alichokifanya Ahmed ilikuwa ni kujaribu kuigiza ni kitu gani ajielezee kwa Yusrath,ni nyimbo gani amuimbishe ili akubali.Kila kitu kwake,kiliharibika alichokifanya ni kuwasha gari,akafunga mkanda na kulitoa mbio huku kichwani akiwa na mawazo mengi sana,kutokana na barabara kuwa nyeupe,haikumchukua dakika nyingi kufika anapoishi,akashuka na kujifungulia geti mwenyewe,akaingiza gari ndani.Cha ajabu,taa zilikuwa zimezimwa tofauti na siku zote huwashwa usiku.Akaingia ndani, nyumba ilikuwa kimya kabisa,akanyata taratibu na kuingia chumbani huko napo palikuwa patupu,akachungulia bafuni napo hakukuwa na dalili ya mtu yoyote Yule kuwepo.
“Beibiiiiiiiiiiiiiii”
Kimya kilitawala,akaendelea kuita kutokana na pombe akawa ana kazi ya kuinama chini ya uvungu,akaingia jikoni,stoo na kuanza kufungua mafriji.
“Yusrath,mke wanguuuuu”
Akaita lakini hakukuwa na mtu aliyeitikia,hakukaa sawa simu yake ikaanza kuita!Alivyoangalia,akaona mpigaji ni Mama Yusrath,akajikaza kidogo, akijua tayari kimenuka na moja kwa moja akaelewa Yusrath yupo nyumbani kwao na simu hiyo ilikuwa ni wito kwa tukio alilolifanya la kumpiga Yusrath,akakohoa kidogo ili kuweka sauti sawa.
“Halloo Mama angu kipenzi, shikamooo”
Akasalimia kwa adabu zote.
“Marahaba Mwanangu,hamjambo?”
“Sisi wazima”
“Vipi,huyo mwenzako hajambo?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Mama Yusrath lililomfanya Ahmed,asite kulijibu.Hakuelewa ni mtego ama Mama anataka kujua habari ya Yusrath kweli.
“Yes hajambo,sisi wote wazima Mama angu”
“Naomba niongee naye”
“Aaah,aah ametoka kidogo”
“Ameenda wapi?”
“Sasa hivi atakuja”
“Ameenda wapi?Nimekuuliza”
Sauti ya Mama ikabadilika,akauliza kwa ukali.
“Aaah Mama un…”
“Nisikilize Ahmed,tena nisikilize kwa umakini unanisikia?”
“Ndio Mama nakusikia”
“Kama umemchoka mwanangu,tafadhali.Mrudishe,hajaua.Mchana alinipigia yupo njiani,anakuja kwangu,umempiga.Mpaka sasa hivi hajafika na hapatikani kwenye simu,sasa nachokuomba kabla sijakujazia watu,nakupa masaa mawili uniambie mwanangu alipo”
“Lakini Mama al..”
“Hakuna cha lakini,nimekupa masaa mawili.Nakupa masaa mawili,Wallah laazim kama hujampata mwanangu,hutoacha kuona kila aina ya rangi leo,nadhani hunijui mimi ni nani mwana hizaya weweee…tititi”
Mama,akakata simu!Hiyo ikamfanya Ahmed apate kibarua kizito.Hapo ndipo alipogundua amepata Mama Mkwe,pasua kichwa!



Siku zote mtoto wa Nyoka,hafundishwi kuuma!Bilionea George Charles,siku zote alikuwa ni mwanamme makini pengine kuzidi hata baba yake aliyemuachia mali zote na kampuni aziendeshe,kamwe hakutaka kumuangusha, ndiyo maana alichokuwa anafikiria yeye ni kutafuta pesa na kufungua makampuni mbalimbali,kwa muda wa wiki moja nzima alikuwa nchini Ufaransa huko alihangaika kutafuta eneo lingine ili awekeze katika nchi hiyo,kwake jambo hilo halikuwa zito sana kulifanikisha.Akiwa katikati ya jiji la Paris, akakutana na mfaransa ambaye aliyeamini ndiye angekuwa mkandarasi wa kampuni ambayo alitegemea kuanzisha nchini humo.
“Thank you Mr.Mock”
“You are welcome”
Baada ya kikao hicho kizito kufanyika katika jiji la Paris ndani ya jengo kubwa la Arask,matajiri wote wakahafiki!Wakasimama na kupeana mikono,kilikuwa ni kikao kidogo kilichowakusanya mabilionea kumi na mbili kutoka katika nchi mbalimbali,matajiri wengi sana walimshangaa George Charles,aliwezaje kuwa bilionea wakati anaonekana kijana,hiyo ni kutokana na wanaume waliokuwa ndani ya chumba hiko wote walikuwa wenye nywele nyeupe kichwani, yaani wazee!George Charles hakuficha,akazungumza ukweli kwamba baba yake mzazi alimuachia mali zilizo na thamani na dolla milioni mbili,lakini mpaka sasa hivi ana utajiri wa dolla bilioni tatu.Wengi wakamshangaa,haikuwa rahisi kwa kipindi kifupi namna hiyo kupiga mkwanja mrefu.Hilo lilikuwa swali lingine kutoka kwa Mr.Roberty William Jai,alikuwa ni mzee makini akitaka kupata funzo.George Charles hakuwa mchoyo,akawaeleza na kuwaambia ni lazima uamini kwenye kitu unachokifanya,usiogope watu watakisema vipi.Akaongezea na kuwaeleza ya kwamba ukitaka kufanya kitu,usijifikirie mara mbili,fanya kwa miguu miwili.Akazidi kuwapa silaha,baada ya hapo akatizama saa yake ya mkononi.
“I have a flight to catch,take my business card.We gonna jazz mob stuffs!Thank you Mr.Jai,it was nice to see you today”(Nina ndege natakiwa kuwahi,chukua namba zangu.Tutaongea mengi,ahsante Mr.Jai.Nimefurahi kukuona leo)
George Charles,akatoa kadi yake ya mawasiliano kisha kuweka tai yake vizuri kohoni,akatabasamu na kubeba ‘briefcase’ yake ndogo ambapo ndani kulikuwa na ‘laptop’ yake na nyaraka mbalimbali.
Siku hiyo alitakiwa kuwahi ndege,ambayo ingempeleka nchini Marekani jijini Los Angeles,huko alitakiwa kufanya kikao na watu wengine tofauti tofauti,akiwa njiani hakuacha kuwasiliana na mpenzi wake Lissa,ambaye kwa wakati huo mwanamke huyo, alichokuwa analilia ni kuletewa zawadi nyingi sana,katika maongezi yake hakutaka kujua sana kilichompeleka, George Charles Ughaibuni.
“Nasubiri ndege hapa,Baby”
“Safari njema,kipenzi changu.Chunga huko wazungu,wasije kukufanya unisahau”
“Usijali kwa hilo,nakupenda Lissa”
“Usisahau zawadi Darling”
“Nakumbuka mpenzi”
“Utaniletea zawadi gani?”
“Subiri,utaiona”
Walizungumza kupitia mtandao wa ‘Skype’ kumaanisha kwamba walikuwa wakionana,simu ilivyokatwa George Charles akashusha pumzi,mwanamke aliyekuwa naye alimchosha!Lakini alijipa moyo, wenda ipo siku moja,atabadilika.
Wakati George Charles akiwa nchini Ufaransa, yeye Lissa hakutulia,alikuwa akitafuta njia mbalimbali za kumpagawisha George Charles ili aolewe kisha baadaye amuuwe na kurithi utajiri wote, aliokuwa nao mwanamme huyo.Akili yake hakuisumbua kumfanya George Charles,azidi kuwa bilionea ili apande chati akimpa mawazo mbalimbali lakini yeye aliichosha kutafuta njia za kumuaa,jambo hilo la kuua kwake lilikuwa gumu lakini tamaa zilimuongoza,hakuna siku aliyoshtuka baada ya siku moja kuchungulia akaunti ya kampuni ya George Charles na kukuta ina bilioni tatu na ushee,zilikuwa ni tarakimu nyingi kuzisoma lakini alizijua.Moyo wake ukamlipuka,hakutaka kuamini siku moja atalala maskini na kuamka tajiri,hapo ndipo mwanamme mmoja alipomjia kichwani kwake,anayeitwa Degedege!Akaamini kabisa mwanamme huyo anaweza kukamilisha kazi yake kama sio kumpa ushauri,hapohapo akiwa ndani ya jumba kubwa la George Charles tena seblen akachukuwa simu yake na kumtafuta mwanamme huyo hewani.
“Uko wapi Degedege?”
“Maskani,vipi kwani?”
“Kuna kazi”
“Ipi?Toa maelezo.Niingie kazini”
“Sasa nikwambie kwenye simu,ama tuonane?”
“Wewe tu,bi mkubwa!Vyovyote vile freshii”
“Ushawahi kuuwa?”
“Kuuwa nini?Binadamu ama?”
“Sasa unadhani nani,panya?”
“Nakuuliza sababu,nilishawahi kuuwa mpaka Simba nikiwa mwenyewe msituni.Nambie unataka niuwe nini?”
“Binadamu”
“Aina gani ya kifo,unahitaji kichwa chake ama kiungo gani?”
“Nitakwambia,subiri nitengeneze mazingira kwanza”
Ungeambiwa mwanamke huyu mrembo ndiye anapanga unyama wa namna hiyo tena kwa mwanamme anayempenda,usingekubali hata kidogo!
Lakini licha ya kufanya hivyo,hakuelewa kwamba ndani ya jumba hilo kuna CCTV kamera tatu,ndogo sana ambazo zipo juu kabisa kwenye kila kona ya seble hiyo,kumaanisha kwamba kila anachoongea kilirekodiwa kupitia kamera hizo!Bilionea George Charles,alikuwa ana maana kubwa kuziweka kimaficho kwani alielewa ni lazima siku moja atavamiwa kutokana na utajiri aliokuwa nao,ndiyo maana akazitegesha. Siri hiyo ilikuwa ya kwake peke yake pamoja na mwanasheria wake Mr.Kihanga!Ili ikitokea,akivamiwa na kuuwawa basi Camera hizo zitumike kuwasaka wahalifu,sio hivyo tu kamera zilikuwa nyingi ndani ya jumba hilo kwa siri kubwa sana!

*****
Ahmed Kajeme,alihisi kuchanganyikiwa.Pombe alizokuwa nazo kichwani,zilimwisha.Akaingiwa na uwoga,mikwara aliyochimbwa na Mama Yusrath ilikuwa mikali sana, kwamba mwanaye apatikane ndani ya muda mfupi.Hakuelewa ni kitu gani akifanye zaidi ya kuzunguka zunguka chumbani kwake,akifikiria ni hatua gani achukuwe,akajaribu kumpigia tena simu mkewe Yusrath lakini simu haikuwa hewani,kijasho chembamba kilianza kumtoka mbaya zaidi watoto pia hawakuwepo ndani, kumaanisha kwamba kama tatizo limetokea basi ni lazima watoto watakuwa wamedhurika,akajilaumu sana na kujiita mpumbavu kwa jambo alilolifanya la kumpiga mkewe kwani lolote baya lingetokea,yeye ndiye angekuwa mkandarasi wa kila kitu,hilo lilikuwa lipo wazi kabisa sababu mashahidi walikuwepo!Akatafakari zaidi na zaidi,hapohapo akamtafuta rafiki yake na Yusrath anayeitwa Husna Uchullo,ambaye mara nyingi hupenda kuongea simuni na Yusrath,ulikuwa ni usiku mkubwa lakini hakujali!Hapohapo,akaanza kumtafuta.
“Halloo”
Simu ilivyopokelewa tu,Ahmed akawa wa kwanza kuongea.
“Wewe nani?Unapigia wake za watu simu usiku?”
“Mimi naitwa Ahmed,naomba niongee na Husna”
“Mimi mume wake,ongea shida yako”
“Namtafuta Mke wangu”
“Mke wangu sio usalama wa taifa,nenda katangaze msikitini.Alafu kitu kimoja bwana mdogo,nimekufuatilia kwa muda mrefu sana,usizuge ulikuwa unataka kuonge….tititi”
Hapo ilibidi Ahmed akate simu,kuendelea kujibishana na mwanamme huyo kwake ilikuwa kama kupoteza muda,hapo ilibidi amtafute rafiki mwingine wa Yusrath lakini majibu aliyoyapata yalizidi kumchanganya akili,akachoka kabisa.Lisaa limoja,likawa limepita.Simu yake,ikaanza kuita alivyoangalia juu ya kioo moyo wake,ukapigaa paa baada ya kuona mpigaji alikuwa ni Mama Yusrath.Hakutaka kupokea simu hiyo,alichokifanya ni kutulia mpaka ikate,hapo ndipo alipopata wazo la kumpigia simu mjomba wake Mr.Zelyatan.Ambaye aliamini angemsaidia kutatua swala hilo kwa njia moja ama nyingine.
“Ahmed,umefanya nini tena?Mbona usiku namna hiii?”
“Mke wangu simuoni”
“Humuoni?Kivipi?Ametekwa au?Umeenda kuripoti polisi?Tangu lini?”
Yalikuwa ni maswali mengi yakiambatana kutoka kwa Mjomba,akiwa katika sauti ya kukwaruza iliyoonesha kabisa,ametoka kwenye usingizi mzito.
“Ametoweka tu,simuoni”
“Haiwezekani”
“Ndio hivyo anco”
“Katoe,taarifa kituo cha polisi”
Ushauri huo ukamfanya Ahmed,aogope sababu alijua nini maana ya kwenda kituo cha polisi kuripoti.Huko angehojiwa maswali na mwisho wa siku wangegundua kampiga mkewe,hiyo ilimaanisha angefungwa mara moja,kifupi kwa kufanya hivyo ilikuwa ni sawa na kujipalia makaa ya mawe.
“Sawa,lakini anco….”
“Usiogope wewe katoe,taarifa kituo cha polisi.Alafu kesho,nitajua cha kufanya!Wazazi wake wanajua?”
“Hapa…Ndio wanajua!Anco lakini nadhani haina haja ya kwenda kituoni”
“Inabidi ufanye hivyo,watoto wako wapi?”
“Hawapo pia”
“Ahmed,fanya uende polisi al…”
“Aliondoka akiwa na hasira”
“Mbona sikuelewi?”
Hapo Ahmed hakuwa na namna ya kuficha,ikabidi afunguke kila kitu kilichotokea.Alichoshauriwa na Mjomba wake,kukikucha waongozane wote, mpaka Ilala,nyumbani kwao wenda atakuwa huko!
“Hayupo huko”
“Wewe twende”
“Sawa anco”
*******
*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG