Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 2/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 2 KATI YA 10


Alfred alikanyaga cluch na kubadili gia safari hii alibadili na kufikia gia namba tano, na gari hiyo kuwa katika kasi ya ajabu, kutokana na kutokua na magari katika bara bara hio ili mfanya iwe rahisi kutamba bara barani kama gari ya mashindano, akiwa juu ya usukani akiushikilia kwa mikono yote
miwili aliunyonga na kukata kona ya ubungo bila kupunguza mwendo na kutaka kugonga watu, kwa uma kini aliwa kwepa na kuendelea na safari hiyo, kweli siku hiyo alikimbiza gari kuliko siku zote, huku kila wakati akiwa pigia askari aliowaagiza ili kujua kama tayari walisha fika, ila jibu alilo pewa msongamano wa magari uliowafanya wachelewe,.
*****************************
"Chinga embu weka gari pembeni kwanza".
Aliongea Mujuni huku akiwa ame mshika dereva huyo bega aliyefahamika kwa jina la chinga., na gari kusimama maeneo ya Karakana
"Kwanini tena bosi"?
"Yaani unaendesha gari huangalii vioo vya nje, GARI UME JIFUNZIA WAPI?" chinga aliangalia vioo vya nje huku akizuga zuga.
"Unaangalia nini sasa, PUMBAVU nini,?..kuna Deffender mbili zime tupita hapa, una ona nyingine hizo mbili, hao ni askari, angalia hiyo nyingine ina pita, na zina elekea airpot"
"Kweli bosi hapa kuna kitu"
"Uwe una tembea kima chale, sasa sikiliza, cha kufanya mi nashuka wewe geuza na huyu mwana mke akii shtuka mchome sindano., nita kupa maagizo cha kufanya niki fika airpot":
Kweli Mujuni alishuka na kuta futa TAXI , iliyo mpeleka moja kwa moja mpka uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere uliopo Kipawa na kuona POLISI wame tanda huku mikononi wakiwa wameshika redio upepo., kwa kuwa alikua na ela za kutosha kwenye begi alienda upande wa pili wa ndege za kukodi na kuonana na mwana mke mmoja aliye valia sare za pale na kujua moja kwa moja alikua ni muhusika.
"Nataka kukodi ndege ndogo, ni kiasi gani mpaka Arusha ,KIA?"
"mmmmh milioni tano,kwenda tu"
"Hakuna shida, nataka kwenda tu"
pale pale alivuta begi lake la mgongoni na kutoa pesa hizo, ziliiingizwa kwenye mashine na kuandikiwa tiketi yake,.. Kweli zoezi lilifanyika vizuri na sasa hivi alikua tayari ndani ya ndege hiyo ndogo ya kukodi ambayo muda mfupi inge kua angani.
**********************++*****
Takribani dakika ishirini maaskari walikua eneo la uwanja wa ndege akiwemo Alfred hakukuwa na chochote, wali subiri tena bila kuona ishara yoyote ya Mujuni wala Hanna,
"Sasa Alfred sie tusha choka, mtu mwenyewe hatumuoni ita kua ume danganywa"
"Hapana embu subiri,".
Alfred alionekana kama amepata wazo na moja kwa moja kuondoka bila kuongea chochote aliingia ndani chumba kidogo kilicho andikwa CCTV camera room na kuingia.
"Naitwa Detective Alfred, "
aliongea huku akiwa na kitambulisho mkononi na kuomba kile anacho taka, kweli wali kubali kufanya kazi yake na kwa uma kini aliangalia skrin zile huku akionekana kwa makini aki mtafuta mtu,.
"Embu ngoja kwanza, una weza kurudisha nyuma hapo, yes hapo hapo,"
Alfred aliiona picha ya Mujuni
Na haraka haraka kutoka mbio na kufanya kidogo ateleze aligonga watu vikumbo, huku akitoa bastola yake ili yopo kiunoni, ghafla aliingia ndani ya chumba alichomuona Mujuni kwenye ile skrin ya camera.
"Kuna mtu namtafuta hapa amevaa shati jeusi mrefu alikua hapa sasa hivi, Naitwa Detective Alfred," dada yule alichukua mkonga wa simu uliopo mezani na kubonyeza namba fulani huku akisubiri upande wa pili kusikika.
"Ile ndege KA S4 isha ondoka,?:, okay sawa asante" dada yule alikata simu na kubaki kumtazama Alfred machoni.
"Kaka samahani ile ndege isha ondoka kwenda Arusha na huyo una emuulizia yupo ndani ya hiyo ndege"
" alikua peke yake?"
"Ndio"
Alfred alizidi kuchanganyikiwa na kufanya akae chini na kujiuliza maswali yaliyo kosa majibu sababu hakujua Hanna alipo...


Kilicho muumiza zaidi Hanna alikua ni mjamzito,alitoa simu yake ya mkononi na kutafuta majina kwenye simu na kupata jina lililoandikwa JOYLA,
"Halloo, vipi wale watu wapo kituoni"?
"Ndio nipo nao hapa tuna wahoji"
upande wa pili wa sauti ya kike uli sikika na baada ya kuridhishwa na jibu lile Alfred alitoka na kuwasha gari akielekea oystabay akijua kua huko angejua kila kitu kuhusiana na safari ya Mujuni. Kweli alifika kituoni na kumfuata mtuhumiwa aliyewaambia kuwa Mujuni ana safiri na kumuhoji ana chotaka kujua.
" Mujuni anaenda Afrika Kusini, mengine mimi sijui kusema ukweli".
Alfred alionekana kama ana fikiria kitu na kutoka nje ya chumba hiko kidogo., akitafakari wapi pa kuanzia
*************************

Gari aina ya LANDCRUISER V8 ilizidi kuchanja mbuga ikikata kona ya chalinze na kuiacha bara bara inayoelekea Moro goro, dereva aitwae CHINGA akiwa makini sana juu ya usukani huku nyuma akiwa amekaa mwana ume mwingine mmoja na kushoto mwana mke mweupe mwenye mwili kiasi.Alikua ni Hanna alikua akipelekwa Arusha na huko ndipo walipo panga wampandishe ndege inayoenda Africa kusini ambaye wange kutana na Mujuni,. Wakiwa kwenye gari mwana ume huyo aliye kaa nae alianza kumkagua kuanzia chini mpka juu aliiingalia midomo ya Hana iliyo mizuri na laini macho yake yali ganda kifuani baada ya kuona kifua kilicho beba maziwa ya Hana vizuri, hakuishia hapo alishuka kidogo mpka kwenye mapaja ambayo aliweza kuyaona kidogo sababu ya sketi aliyo vaa kupanda juu kidogo alimwangalia kwa kumtamani sana huku akimeza fundo la mate, Gari lili zidi kuchochea kasi dereva akiwa Chinga,. Kutokana na uwezo mkubwa wa gari hiyo wa kutembea mbio tayari baada ya masaa kadhaa walifika SEGERA na kusimama ili wale, walinunua chakula na chinga kununua chakula kingine cha ziada na kuingia nacho ndani ya gari, wakati huo akiwa bado amelala na kutojua kina choendelea, ila baadae Hanna ana shtuka na kufumbua jicho moja kwa umakini zaidi na kuona kila kitu ,hakutaka wajue kama ameshtuka maana wange mchoma tena sindano alicho fanya alita futa kichupa kile cha dawa ya usingizi na sindano kilichokua chini na taratibu kuanza kuvuta dawa kimnya kimnya huku Chinga akipiga stori na mwenzake aliye fahamika kwa jina la Mnyaru.
"Nakumbuka hapa kuna siku nili kuja na bosi, tulikua na ile gari kubwa canter, una paona hapo,. Ndo tulipo pata ajali siku hiyo,"
"Wacha bana, hakuna aliye kufa?"
"Aaaah wewe, mimi dereva , nili sikia puu, mmmh, ili kua pancha alafu sasa tairi la mbele,ngoma ikaanza kuni vuta, kumwangalia bosi pembeni amelala,. Nikasema usinitanie wewe, nika chomoka dirishani."
"Hahahahahahahahahaha, kama nakuona vile"
"Acha babuuu, ngoma ikaenda kujipiga kwenye mti ndo ili kua ponea , ila la sivyo aaah ange kufa yule"
Zilizukua ni stori waki piga huku wakicheka na mwishowe Chinga akapaki gari pembeni akienda kutoa haja ndogo huku nyuma akimuacha Mnyaru na Hanaa, Mnyaru bila kupoteza muda alianza kumpapasa Hana akimshikashika mapaja yaliyo kuwa malaini sana, alipeleka mkono kifuani na kuanza kumfungua vifungo vya blauzi aliyo vaa, ila Hanaa ana fumbua macho na kushika sindano ile sawa sawa na kuikandamiza shingoni kwa Mnyaru na kuiingiza dawa ile ya usingizi, purukushani zilianza pale shika nikushike na dawa ikaanza kumuingia Mnyaru na kufanya aanze kusinzia kama kuku mwenye mdondo, . Haraka haraka alitoka ndani ya gari huku akiangalia huku na kule na kutoka mbio bila kujua ana poelekea.
Alizidi kusonga mbele asijue ana poelekea alizidi kuchanganyikiwa baada ya kuona hakuna makazi ya watu sehemu hiyo ila eneo zima lili kua ni chaka lililo jaa miti mingi ila kwa mbali ana muona mtu ana kuja na kuanza kumkimbilia kama chizi, mpaka mtu yule akanzani ana kimbizwa nayeye kuanza kukimbia.
"Kaka, kaka. Kaka simama usi kimbie tafadhali"
"Dada vipi, aishee mbona , mi nkajua abda una nikimbiza"
"Hapana kaka angu, nina shida na kitu kimoja tu, nina shida na simu"
Kijana yule aliye ongea kwa rafudhi ya kitanga alitoa mche wa simu na kumkabidhi . Moja kwa moja aliwaza kitu kimoja tu, kumpigia Alfred. ,Maana hakutakataka kuamini kama kweli alfred mume wake amekufa.
"Samahani kaka , hapa tupo wapi?"
"Hii hapa tupo Tanga, pana itwa Mizani"
Aliweka simu masikio baada ya kuibonyeza ila alijihisi kuchoka sana baada ya kusikia namba ile haipatikani, alijaribu tena kuangalia ile namba aliyo ipiga kama ipo sahihi na kukuta ipo sahihi. ,Mawzo ya alfred kuuwawa kinymama na kudhani kweli amekufa yanaanza kuji jenga kichwan.


pale pale alipata wazo na kumpigia simu Jaqlin Nyange, aliipiga na kuanza kuita.
"Halloo, haloo jaq, jaq, mimi Hanaa, mimi Hana. Nipo Tanga mwa........"

Alishindwa kumalizia maneno baada ya Chinga kutokea na kumpora simu ile huku akimpiga na kofi.
" pumbavu zako, "....
Aliongea Chinga


"Uhalifu na uingizaji wa madawa haramu ya kulevya ume kidhiri katika nchi hii, watu hao ni akina nani sasa, tuna wajua, sema tuna wafumbia macho kwa uzembe wetu,embu tufanye kazi bega kwa bega kuli tokomeza janga hili la sivyo taifa litaangamiza vijana wetu wata potea"
Kilikua kikao kidogo ndani ya ofisi ya ma CID kitengo cha upelelezi kiongozi wao akiwa makini kabisa ambaye aliyefahamika kwa jina la Fredrick Momba, akiwa makini sana akiongoza hiko kikao katika meza ya duara ambayo juu ya ukuta ili kuwemo picha kubwa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na picha nyingine za maraisi wa Afrika Mashariki..
"Narudia tena, tufanye kazi bega kwa bega, kuna mwenye swali,?, ndio Alfred, uliza"
"Una sema tufanye kazi bega kwa bega?,Mbona ile kesi huku ifatilia, ?,, wala hukuonesha ushirikiano wowote ule"?
Usione nilivyo kua kimnya ,ukadhani sifwatilii Alfred NO, najua ume umia, kihisia hata kikazi, najua kiasi gani una umia"
"Hapana, muda sana nili kupa taarifa ila ukaniona MPUUZI sijui., uka dharau, na ukategemea nita nyamaza"
"Alfred, kaa chini nakuomba, nime sha kusikia"
"Siwezi kukaa chini ina niuma sana, Fredrick, ."
Tayari Alfred alijikuta ana pandisha hasira na kuwa mwekundu huku akiongea kwa sauti na kuropoka, na kuanza kufanya fujo ,
"Na, sikia na kuanzia leo najiudhuru siwezi kufanya kazi na wapuuzi puuzi, wazembe, ."
Alfred alitoa bastola na kitambulisho na kuviweka mezani na kuuwendea mlango na kutoka nje huku akiubamiza mlango ule kwa nguvu, kweli alikua ana maanisha,
Baadae ana kutana na Jaq na kumueleza kila kitu kuwa muda mfupi alipigiwa simu na Hanna ila ana shindwa cha kufanya baada ya kuipigia namba ile na kukuta haipatikani,
"Hallo Joyla, niambie sasa naweza vipi kumpata Mujuni Kama nikienda Africa Kusini?"
"Alfred ila ulicho fanya pale sio poa, pale ofisini, huku staili kufanya vile".
" sikia, una nisaidia au huwezi kunisaidia, niambie kabisa,"?
"Ana patikana jijini Darban, hua ana penda sana kwenda kwenye casino inayoitwa CASABRANCA ni maarufu sana, pia ana mtoto wake anaitwa Allan, nita kutumia picha yake WATSAP"
"Yote ume juaje haya?"
"Yule jamaa kasema kila kitu"
"Na uki chelewa Hanna uta mkosa,"
"Kivipi, sija kuelewa hapo?"
"Ana mtindo wa kuwa pasua watu na kuweka kete za madawa ya kulevya tumboni, alafu ana tuma Tanzania akizuga ni msiba, na kuwa kodi watu wa kulia,"
"Mungu wangu, una semaje?"
"YES Alfred fanya ivyo, muwahi mapema, mimi nita kusaidia uki kwama niambie "
Maneno yale yalizidi kumpagawisha na kuzidi kumsisimua Alfred Mulawa na kumfanya apigwe na bumbuwazi.

Chinga pembeni akiwa na Hanna tayari wali kua Angani ndani ya ndege inayoelekea Afrika kusini ambamo waki fika wange pokelewa na wenyeji wa huko, na kukutana na Mujuni.


Usiku wa siku hiyo Alfred Mulawa aliandaa baadhi ya nguo zake na kuzipanga vizuri ndani ya begi lake dogo, alisita kidogo baada ya kuiona picha ndogo ya Hanna na kubaki akiingalia, baada ya kuridhika na kila kitu alifunga begi lake akisubiri kukuche na kesho yake aanze safari ambayo kwa wakati huo aliita jeshi la mtu mmoja sababu hakukuwa na msaada wowote,
Kesho yake jioni saa kumi alikuwa tayari amesha wasili uwanjani hapo akisubiri shirika la ndege aina ya KENYA airways, kweli baada ya muda mfupi sauti ili tangaza kwenye kipaza sauti ikiisharia kuwa ndege hiyo ipo tayari uwanjani na abiria waanze kuingia ndani ya ndege, Alfred taratibu aliburuza begi lake dogo na kuliweka ndani ya mashine hiyo iliyo kua hapo kwa ajili ya ukaguzi ambayo ukiweka begi hupelekwa na kutokea upande wa pili, alichukua begi lake lililo kua upande wa pili huku akitoa passpot yake baada ya kufika immagration na kugongewa muhuli wa kuingia,. Kila kitu kilienda sawa kwake, alipandisha ngazi za ndege taratibu na mwishoni kuingia na kukaa siti ambayo aliyo ipata baada ya kuangalia tiketi yake, baada ya muda mfupi sauti nyororo tena ili tangaza na kuwa taka abiria wote wafunge mikanda maana ndege hiyo ikeenda kupaa,.
Mawazo, hasira pamoja na kisasi vili jijenga ndani ya ubongo wa Alfred na kusababisha kama mkanda wa filamu kichwani kwake na kufanya alale kutokana na mawazo,na uchovu.
Kilicho mshtua ni sauti iliyo tangaza kuwa wafunge tena mikanda maana ndege ina enda kutua. Katika ardhi ya Afrika Mashariki.
"Samahani Anti"!
, " bila samahani"
"Tusha fika johnsburg?"
"Ndo tuna ingia sasa hivi, naona ulikua umepitiwa na usingizi kaka"
. "Uchovu, si una jua tena",
Alfred alimuuliza mwanamke aliyekaa pembeni yake.
Ndege ili tua katika nchi hiyo ya Afrika kusini yenye madhari mazuri ya kupendeza sana, na baridi lililosababishwa na ukungu mzito uliotanda juu ya anga, ambao ulifanya kila mtu kutoa Moshi mdomoni . abiria walianza kushuka huku Alfred akijiuliza wapi ataanzia maana bado alikua mgeni ndani ya nchi hiyo........



Kweli Alfred alifika katika nchi hiyo ili yofahamika kama south Afrika, bado akiwa uwanja wa ndege huo ulio mkubwa sana jijini johensburg, alita futa Taxi yaani gari ndogo ya kukodi.
"Nipeleke hoteli yoyote nzuri yenye kila kitu".
Dereva huyo alionyesha kumchangamkia sana mteja wake, haraka haraka alimpokea begi lake na kuliweka nyuma ya boneti nayeye kuingia ndani ya gari akifuatiwa na Afred ambaye yeye ali fungua mlango wa nyuma na gari kuondoka.
" Ako natokea Tanzania?".
Alihoji dereva huyo akiongea kiswahili kibovu.
"Mmmh ndio Tanzania, ume juaje?"
"Mi najuwaga nikiwaona, sura zenyu basi ina nifanya mimi niyuwe, naishi sana na Watanzania wapo huku,."
"Ahaaa, vizuri, hiyo hotel ipo mbali na hapa?"
"Hapa ita pata kama ni kilomita 5 mpaka huko, ipo maeneo ya KIMBERLY, ni muzuri uta ipenda sana, kuna warembo pia wabibi wazuri"
"Fanya haraka tufike maana nime choka sana"
"Huku ume kuya kufanya mambo yepi?"
"Biashara, nime kuja kufanya biashara"
Tayari Taxi hiyo ili egeshwa nje ya hotel iyo kubwa iliyo andikwa MONKAUZI HOTEL, Aliteremka kwanza dereva na kufungua boneti ambamo alitoa begi la Alfred na kumuambia waongozane,
Kweli Alfred alifanya ivyo huku akiangalia mandhari mazuri ya HOTEL hiyo iliyopambwa vizuri kwa vitu vya thamani, upande wa pili aliona Garden iliyo kuwa na viti vilivyo jipanga kwa namna yake, aliangalia juu na kuona urefu wa hotel hiyo, walipanda ngazi ambapo aliona meza za vioo na kushoto aliona pameandikwa RECEPTION , na kumuona dada mmoja aliye valia sare nzuri akiwa ana tabasamu,
ki ukweli alifanana na hadhi ya Hotel hiyo ya kifahari., alimuendea dada yule na kumuuluizia kama angepata chumba kizuri, kweli alipata na kukabidhiwa kadi ya kufungulia chumba.
"Utakaa kwa muda wa siku ngapi kaka?"
"Sija jua, ila izi pesa nita kupa za siku mbili, nikitaka kuendelea kubaki, nita kuongeza."
"Sawa karibu sana twende nika kuonyeshe chumba chako,"
Alfred alimuaga dereva yule taxi na kumuomba arudi tena kesho yake asubuhi huku akiongozana na dada yule ambaye walipanda lifti na kubonyeza namba 14 na lifti hiyo kuji funga huku taratibu ikipanda juu.,
lifti ili funguka kuashiria kua wali fika katika eneo husika na dada yule kutangulia mbele, huku nyuma Alfred aki fuata, wali fika chumba namba 107 na dada yule kuingiza kadi ile kama ana ikwaruza na mlango ule uka funguka, nakuona uzuri wa chumba hiko chenye kitanda kikubwa sana alikagua chumba hiko vizuri.
"Huko ni bafuni, hii simu hapa, ukiitaji huduma yoyote ile ya chakula, uta piga izo namba hapo na kuagiza unachotaka,karibu sana....,"
"Asante sana, usijali," baada ya maongezi hayo dada yule aliondoka na kumtakia Alfred usiku mwema .
Aliangalia simu yake ya mkononi na kukuta ni saa moja jioni, ivyo aliingia bafuni na kujimwagia maji kidogo ili atoe uchovu huku akivuta muda kidogo usiku uingie ili aweze kutoka nje,
Kweli usiku uliingia na Alfred kutoka nje, alitembea mpka kwenye super maket kubwa na kuingia, alionekana kuanza kutafuta anacho kitaka. Alichukua miwani kubwa nyeusi, alisogea mbele na pia kuchukua kisu kidogo ambacho cha kuji kunja, pembeni kidogo alichukua mafuta malaini sana ya kupikia na kuya weka kwenye kikapu , alisogea mbele na kuchukua gundi kubwa pamoja na kamba nyembamba na pia kuviweka ndani ya kapu hilo lenye matairi , alichukua pia na sigara pakiti mbili na kuweka., alichukua vitu vingine vya kula alivyo ridhika na kila kitu alienda kwenye sehemu ya malipo na kulipa kila kitu na kutoka nje.

Upande wa pili huku tayari Hanna alikua kasha fika ndani ya nyumba kubwa hiyo iliyo milikiwa na Mujuni na watu wengine mbali mbali ambao nchini Tanzania walikua matajiri sana,.
"Hahahahhaa, Hanna, si ndio jina lako, ngoja nikwambie kitu, humu huwezi kutoka kamwe, niamini, bora uanze kuzoea mazingira ya humu, , hakuna anaye jua ulipo,... Mumeo kasha kufa, huna msaada wowote ule, UPO KAMA YATIMA,. Cha kufanya uoneshe ushirikiano wako"
Hanaa hakujibu kitu chochote ila aliachia msonyo mkali na kuangalia pembeni, alidondosha chozi baada ya kumkumbuka Alfred mume wake ambaye kwa wakati huo alidhani ame kufa . Ndoto zake na Alfred kuwa baba na mama zili yeyuka kama barafu lililowekwa ndani ya makaa ya moto, ivyo mambo yote alimuachia Mungu aliye juu aamuwe lolote sababu hakua na ujanja wowote wa kutoka ndani ya jumba hilo kubwa lenye walinzi kila sehemu, picha ya Alfred akiwa anahaingaika chini huku akiwa na damu nyingi tumboni vilijenga taswira ndani ya ubongo wake na kuji kuta ana lia kwa uchungu., baadae ana nyamaza baada ya kumuona Mzee mwenye mvi za wastani mwenye kitambi, akionyesha kama ana mjua, ali mwangalia ki umakini sana, akizidi kujiuliza maswali.
" najua una shaanga kumuona mtu huyo mahala hapa, Waziri wako mkuu Huyu wa Tanzania, hahahahaa una dhani nani ata nishika , mimi ndo Mujuni,"
aliji tambia Mujuni huku akiji piga kifuani na kumuendea Waziri mkuu JOSEPH PARTSON KASANGA, na kumpa mkono, kitendo kile kilimshangaza sana Hannah .
Tayari kuli kucha na Alfred akipata kifungua kinywa , kwa mbali alimuona dereva taxi ana kuja na kumkaribisha na wote kuanza kunywa chai ile, walivyo shiba waliingia ndani ya gari na Alfred kumuomba ampeleke kwa mafundi wana otengeneza umeme, dereva alitii amri na gari kuanza safari,. Waliingia mtaa mmoja una oitwa UMTATA na Alfred kushuka,
alienda na kuji ficha kwa mbali na kutoa camera ndogo, aliwapiga picha za mnato , alivyo ridhika aliingia ndani ya gari na kumtaka dereva yule ampeleke mpaka kwa mafundi nguo,
alivyo fika ali waonyesha picha ile na kutaka nguo kama zile za ufundi umeme, kila alicho kua ana kifanya alikua na mahesabu nacho, jioni ilivyo fika alirudi kwenye hotel ile na kubadili nguo,
Alimuendea dereva taxi na kumuomba ampeleke DURBAN kwenye casino inayo itwa CASSABRANCA , humo akiamini ata mpata mtoto wa Mujuni,akiwa na picha ya Allen mkononi,
Taxi hiyo ili anza safari ila Alfred aliomba asimame kidogo alivyoona wana wake wana ojiuza yaani DADA POA, alishuka na kumuona mwanamke mmoja mweupe sana aliye kuwa mrefu kama twiga ambaye aliyevalia sketi fupi inayo mbana na kumchoresha umbo lake lili kua zuri, ali mchukua na kuingia nae ndani ya Taxi.
"Aaaaah bosiii huyo, kumbe ako wewe una pendaga mabibi hao, ila kuanga makini, wana kuanga ni wezi"
"Endesha gari, "
Alfred haku taka kuya unga mkono maongezi yale na kukaa kimnya akionekana kuta fakari kitu, uli kua ni usiku mnene sana, ila kuli kua ni kama mchana kutokana na jiji hilo kuwa na taa kila mahali, baadae gari liliegeshwa kwenye casino hiyo ya CASABRANCA na Alfred kushuka na mwana mke yule aliyevaa viatu vizuri na virefu na kumfanya azidi kua mrefu, aliingia nae mpka casino mule ambamo walionekana wana wake wengi wame vaa nguo za ndani tu huku wengine waki cheza na kuzunguka juu ya machuma, alimununulia mwana mke huyo kinywaji na kukaa wote counter.,
Alfred alitazama tazama huku na kule akionekana aki mtafuta mtu,.
"Twende huku mrembo"
Aliongea Alfred huku akiwa ame mshika kiuno mwana mke yule ambae ni dada poa, wali fika na kukaa kwenye masofa makubwa
, Alfred japokua hakua mvutaji wa sigara ili bidi aitoe sigara na kuiweka mdomoni akiivuta taratibu,
" una tumia cigarete?"
"Yes natumia, nipatie,"
Alfred alimuwekea mdomoni dada yule na kumuwashia kama malkia , kweli dada yule alikua Malikia wa cku ile,
Kuangalia huku na kule Alfred alijikuta ana kaza macho kwa mwana ume mmoja mweusi, mwenye ndevu ambazo zime fugwa na kuachiwa kama beberu,alimuangalia kwa uma kini sana bila kupepesa macho, huku akitoa picha ndogo na kuitazama,.
"Yes ndo yeye". Alijisemea kimoyo moyo bada ya kumuona Allen mtoto wa kiume wa Mujuni na kujua kivyovyote vile inge kua rahisi kupafahamu kwa mujuni., alimshuhudia Allen akisimama nayeye kusimama, ali mfuata nyuma nyuma na kuingia nae mpaka chooni, Miwani nyeusi kubwa aliyo vaa Alfred haikuwa rahisi kwa mtu kumjua,.alivyo toka alitoka nae na kukaa huku akiendelea kumuangalia kila hatua, Kweli Allen alionekana baadae kutoka nje
"Sikia dada asante sana, chukua izi pesa"
"Sasa hatuendi kulala?"
"Kwani wewe shida yako si pesa au,"?
Alfred alimpa pesa dada poa yule ambaye alionekana kushangazwa na kitendo kile,
"Una ona hiyo gari nyeusi, ifuate nyuma nyuma, ki umakini"
"Bosiiii, utaa penda mwenyewe, kaa utulie "

Kweli taratibu kwa mwendo wa taadhali Gari ya Allen Mujuni ikiwa mbele yao, waliweza kuifatilia wakiwa umbali kidogo, ili kata kona na wao kwenda nayo,
Mwishowe gari hilo liliingia ndani ya geti kubwa lililo jifungua lenyewe.
"Niingie mpaka ndani"?
"Tulia simama hapa hapa, una taka kwenda wapi?"
Alfred alitoka nje akionekana kuikagua nyumba iyo kwa mbali ambayo ili kuwa kubwa sana, .


Hannah alimaliza kusali baada ya kumshukuru Mungu kwa kila kitu, hakuacha kuomba ulinzi kutoka kwa Mungu, na ndo ufanya kabla ya kulala kutokana na malezi aliyolelewa akitokea katika familia iliyo mjua sana Mungu baada kusali alichukua picha ndogo ya Alfred na kuanza kulia tena, huku akiwa amelala chali,
Anashtuka na kutoka kitandani baada ya mlango wake kugongwa kwa nje, ivyo alitoka kuufungua.
"Nime ambiwa niku letee maji ya KUNYWA,"
"Asante nashukuru"
"Mbona mnyonge sana?"
Aliongea mwana mke huyo mwenye macho makubwa kidogo kwa ukarimu sana.
"Hapana usijali"
Hanna alitoa kitambaa na kufuta machozi ambayo kwa wakati huo yali kua yana mtoka., alikohoa kidogo na kuvuta mafua yaliyo sababishwa na machozi ya uchungu.
"Samahani naweza nikaingia ndani?"
"Bila shaka karibu ndani"
"Asante nashukuru nimeambiwa wewe ni Mtanzania, sijui una tokea sehemu gani?"
"Mi natokea Dar es salaam"
"Ime kuaje mpka ume fika huku"?
"We acha tu ni stori ndefu sana,"
Mwana mke yule alimuangalia Hanaa akionekana kama ana mkagua kuanzia juu mpaka chini, na kukaa kimnya kwa muda akionekana ana tafakari akitaka kuongea kitu.
"Namimi pia natokea Dar es salaam, maisha yangu nipo huku tangu utotoni, naitwa Roseline".
Hana alishtuka na kubaki akimwangalia machoni vizuri alimuangalia vizuri kiumakini ila aliganda juu ya midomo ya Roseline.
"Una una unaitwa nani umesema?"
"Roseline, wewe je?"
"Mi naitwa Hanna"
"Una itwa Roseline nani?"
"Naitwa Roseline Kenford Mukama,"
Hanaa alihisi kama moyo wake ume pigwa na ganzi haku taka kuamini , kama amesikia vizuri au la, pia hakuamini kama anae ongea nae ni dada yake na Alfred Mulawa, , sababu Alfred alisha muhadithia kila kitu.
"Wazazi wako... Wa....ko wapi?"
"Wote wali fariki, baba yangu mzee Mulawa aliuliwa na watu Wa Mujuni namimi kuni leta huku, kila niki jaribu kutoroka nashindwa'"
"Mlizaliwa wangapi kwenu?"
" tulizaliwa wawili tu, mimi na mdogo wangu, ana itwa Alfred, sijui yuko wapi mpaka sasa hivi, ila ipo siku nita muona Mungu yupo"
Hanaa alijikuta ana lia tena safari hii alipaza sauti ya juu, alilia kwa uchungu sana, Uso wake ulizidi kua mwekundu na kumfanya Roseline amfate na kumpa moyo.
"Usijali, uta zoea tu, cha kufanya ukubali hali ya huku,"
"Siwezi.... siwezi Rose..Alfr...ed, Alfreed,, Alfred alikuwa mume wangu, alikua aki kutafuta kwa muda mrefu sana"
Aliongea Hanaa akiwa ana lia bado
" futa machozi uniambie vizuri, Alfred mzima?, yuko wapi", Mungu ameya sikia maombi yangu.,"
Hanna alibaki akimwangalia Rose machoni na kushindwa amjibu nini.
"Alfred....Al...fred Amekuf......a"
"Whaaaaaaaat(nini)?"
Wali baki wote wakiangaliana kwa kushangaana, na kujikuta wote wakilia, uli kua msiba mwingine kwa Roseline, alilia kwa uchungu, wali kombatiana huku wakiongea maneno ya uchungu, yaliyokua yana tokea mbele ya Hanna alidhani labda wenda anaangalia picha la kihindi, siku iyo Hanna na Rose waliongea mengi sana na Rose kuamua kulala chumba cha Hanna.
Usiku uli fika kwa Alfred Mulawa ili kua furaha sana kwake, akiwa amevalia vizuri nguo za ufundi umeme, huku kichwani akiwa na kofia iliyo mkaa sawa sawia kana kwamba ni fundi kweli, alikodi bajaji ambayo ili mshusha eneo lile karibu na nyumba aliyoingia Allen,
Aliangalia juu na kuona nyaya za umeme zime pita, taratibu alipanda nguzo ya pembebi na kuukata waya ule na kufanya nyumba ile umeme uka tike.
Ali subiri kidogo na baadae kugonga geti lile na kufunguliwa na mlinzi wa geti.
"Niku saidie nini?"
"Fundi umeme, nime kuja kutengeneza umeme, nime pigiwa simu na bosi nije hapa, ni dharura sana"
"Okay pita ndani".
Alfred alipita akiwa na begi dogo mkononi, lilionyesha kuwa na vifaa, ila alisita kidogo baada ya kumuona Mjuni ana kuja mbele yake, alimuangalia vizuri na kugundua kweli ni yeye na kuanza kujitaayarisha kwa lolote lita kalo tokea endapo ata mtambua kuwa ni yeye,
"Wewe, wewe kijana, Embu njoo hapa,"
Sauti ya Mujuni ili sikika na Alfred kuingiwa na hofu kubwa, na kumfanya asite kidogo kutembea.


sauti ile ya Mujuni ili mfanya asite na kuvuta kofia yake kwa chini kuziba sura yake, ila alizidi kusonga baada ya kugundua kua anaeitwa sio yeye ali shusha pumzi ndefu na kuelekea asipo pajua,
Kutokana na ukubwa wa nyumba iyo ambayo aliifananisha na IKULU ya Raisi au KASRI ya mfalme alizidi kuitathimin huku akishindwa wapi aanzie, mkono uliomshika begani ndo uliomshtua na kumfanya ageuka ili kujua ni nani aliye mshika bega.
"Sasa huko unaenda wapi,?, una jua una poenda au unaenda enda tuu,, embu nifuate"?
Alikua kijana mmoja nayeye pia alikua fundi ila wa magari ambayo yame haribika, fundi yule alimpa ishara ya mkono kuashiria kua amfate nyuma.
Alfred alifanya vivyo ivyo huku akizidi kuichunguza nyumba iyo bila fundi magari yule kujua.
"Hii nyumba ni kubwa kweli yaani, humu wana ishi watu wangapi?"
"Watu wengi tu,"
"Huyu jamaa kaji tahidi sana"
"Hivi vyumba vyote vina ishi watu?"
"Hapana, huko una paona hapo, ni stoo tu ya vitu na silaha, ila huko kwengine ndio watu wana ishi.,"
Maongezi yale yaliisha baada ya Alfred kuonyeshwa Main socket na kijana yule kuindoka huku nyuma akimuacha Alfred akitoa vifaa kwenye begi, japokua alikua hajui atoe nini ndani ya begi, alivyo hakikisha jamaa yule kaondoka alichungulia ili apate uhakika kama kweli kaondoka alivyo pata uhakika , taratibu alinyata mithili ya PAKA SHUME anaye nyemelea kitu,
alifika kile chumba alicho ambiwa ni stoo na kuangalia pande zote mbili kama kuna mtu anaye muona, alivyo hakikisha hakuna anaye muona ali fungua begi lake na kutoa vipini viwili na kuanza kukitekenya kitasa kile mpaka kilivyo achia na mlango ule wa stoo kufunguka, aliwasha tochi yake ndogo na kuanza kumulika mulika kila kona, taratibu alianza kusogea baada ya kuona kabati kubwa lenye kioo kirefu na kulifungua huku akiweka begi lake chini,.
Alichoona ndani ya kabati hilo ni silaha za moto, alitabasamu na kuanza kuzipekua kana kwamba ni zake, alichukua bastola ndogo aina ya RIVOLVER na kuiweka kwenye begi, alivyoangalia juu aliona mabomu ambayo yalifanana kama viazi mfiringo alichukua na kuweka ndani ya begi alivyogeuka upande wa kushoto aliona boxi lililojaa risasi hakuliacha na lenyewe alili chukua na kuliweka ndani ya begi, alivyo ridhika alitoka nje na kuuufunga mlango ule kama ulivyo kua,
Alitembea nje mpka uwani na kuku tana na Mwanamke mmoja ambaye wali salimiana na kupishana, ali chunguza mazingira ya uwani na kuona kila aina ya magari ya kifahari yaliyo kua nje hapo, aliangalia vizuri urefu wa ukuta huo na kuupima kwa macho huku akioekana kama akiuwekea alama.
'"Fundi vipi,?, huku una tafuta nini?"
"Aaaah, bado naangalia, ila humu ndani naona hakuna tatizo lolote lile, kila kitu kipo sawa kabisa,"
"Sasa mbona hakuna umeme?"
"Kuna waya nahisi una matatizo ule wa kuingiza umeme ndani"
Alfred alizidi kujijitetea ilhali alikua ana jua alicho kifanya,
Haraka haraka alitoka nje ili wasije waka mgundua baadae,.
Alifika hotelini na kupumzika na kuanza kuta fakari jinsi gani atakavyo ingia ndani ya nyumba ile kubwa, kwa kipindi hiki hakuwa na wasi wasi sababu alisha isoma nyumba nzima na tayari alijua pa kuanzia na wapi angemalizia,
Hanna akiwa bado hataki kuku baliana na hali ile muda wote alikua ni mtu mwenye majonzi, huku akiwa ana tafakari aliitoa picha ya Alfred na kuanza kuitazama .
"Hanna iyo picha ya fundi ume itoa wapi?"
Aliuliza Roseline akimaanisha kuwa picha ya Alfred ambayo kwa wakati ule Hana ndo aliyeekua ameishika mkononi, Hanna alibaki akimshangaa na kushindwa amjibu nini., aliingalia mara mbili mbili ile picha ya Alfred huku akimwangalia Rose na kuona kama amechanganyikiwa
"Picha ya fundi?"
Hana aliuliza kwa mshangao huku akipigwa na butwaa.
"Ndio, fundi umeme, alikuja hapa jioni kutengeneza umeme ulivyo katika"
"Hapana uta kua ume mfananisha, huyu ni Alfred Rose, ina maana hata kwa sura humjui"?
Rose alibaki akishangaa na kuichukua ile picha na kuiangalia kwa makini sana,
"Hapana, huyu nime muona leo, au nili kua naota?, huyu ndo Alfred mdogo wangu?'
"Ndio Rose, huyo ndo Alfred, huoni mlivyo fanana"
Rose alihisi kama amepigwa ganzi mwili mzima baada ya kuendelea kuitazama picha ile huku akikumbuka jinsi alivyo kutana na fundi huyo umeme ambae Hanna anasema kuwa ni Alfred.
"Lakini Hanna, mimi nime muona huyu leo,"
"Alfred ali fariki Rose, usini kumbushe machungu"
Akili ya Roseline bado haiku kaa sawaa alionekana kama haja kubaliana na jambo lile.
Siku inayo fuata usiku tayari Alfred alikua nje tena nyuma ya ukuta wa jumba lile la Mujuni huku akiwa amevalia nguo nyeusi juu mpaka chini, ambapo uso na mdomo aliuficha na kufafana na wale wana ojiita MA-NINJA , kweli alifanana nao kwa kila kitu hadi viatu alivyo vaa vili kua vyepesi sana ambayo vilifanya visitoe kelele ya aina yoyote ile, alisogea katika ukuta ule mrefu na kuweka sikio lake ukutani kana kwamba ana sikilizia mapigo ya moyo ya mtu, alisikiliza kwa muda kidogo, alivyo ridhikika alinyanyua nyayo zake za nyuma,na kuhesabu mpaka tatu na kujivuta juu huku mkono mmoja akiwa tayari kaifukisha juu ambapo alijivuta taratibu na kuchungulia, alivyo hakikisha hakuna mtu, aliserereka na ukuta mpka alivyo fika chini na kuangalia huku na kule,. Alichomoka mbio na kwenda kuji ficha nyuma ya Tank kubwa la maji hii ni baada ya kuona taa za gari zina kuja alipo, alisubiri mpka lipite na kutoa kichwa chake akichungulia kama KOMANDO.
Aliona madaktari wawili wana shuka ndani ya gari hiyo ya wangonjwa yaani AMBULANCE, na kusubiri ili ajue nini kinge fuata, alishuhudia machela ina shushwa huku juu yake kukiwa na mtu amelala, ile machela ili sukumizwa na yeye kufuata nyuma nyuma, huku akiji fi-cha ficha,.
Madaktari wale wali buluza machela ile mpka chini ambamo kuna andaki,
Kabla halija jifunga alibilingika kama tairi akingia ndani mule na haraka haraka alinuuka, huku akiji ficha nyuma ya chuma refu ambamo hata mtu yoyote ata kaye ingia hatoweza kumuona,
Chumba hiko kili kua kina madawa mengi na visu pamoja na mashine nyingi tofauti , waliiwangalia wale madaktari wana chofanya huku akiwa kimnya,
"Sasa tuna mpakia kete ngapi?"
"Ishirini na tano,, tena tufanye haraka,"
"Sawa, Dr, Nico sasa ile dawa ya CALLIPUS usha mchoma?"
Alfred alitoa Camera yake ndogo na kuanza kuchukua mkanda akiwa rekodi na kuwa piga picha za mnato.,
Alivyoona ameridhika aliweka Camera ile ndogo kwenye begi na kulivaa begi lake vizuri.
"Dr. Nico"
Alfred aliongea vile na kufanya madaktari wale wamshangae na kujikuta wote wameacha wana chokifanya huku wakibaki waki mshangaa na kurudi nyuma.
"Wewe ni nani?"
"Mimi ni daktari pia, nataka namimi niwa fanyie operation"
Alfred aliongea huku akikunjua kisu chake kidogo cha kuji kunja na kuzidi kuwa sogelea, daktari mmoja ambae alie kua upande wa kushoto alimfuata Alfred aki taka kumchoma na Mkasi ila Alfred aliona na kupiga hatua mbili nyuma akiukwepa mkasi ule, aliukamata ule mkono wennye mkasi, huku akigeuka na teke ambalo lili mpata daktari mwingine na kumfanya adondoke chini, aliuzungusha mkono ule wenye mkasi na kuutumbukiza kwenye tumbo la daktari yule kwa nguvu na kufanya daktari yule apige kelele sana ila ali mziba mdomo na kuzidi kukandamiza mkasi ule, ali zungusha mkono kwenye shingo yake na kuizungusha mpka mishipa ikalia kumaanisha kua kaivusha shingo yake. alimuendea yule daktari mwingine ambae kwa wakati huo alijawa na uwoga . Akiwa chini pale akimshuhudia mwenzake ameuliwa ivyo alitumia makalio yake kuji vuta vuta nyuma huku jasho likianza kumtoka kwa hofu,
Alfred alimfata na kumuinua na bila kupoteza muda alitumbukiza kisu kirefu tumboni kwake na kukizungusha kana kwamba ana washa gari, alichomoa kisu kile na kukirudisha tena tumboni, alivyo hakikisha daktari yule ameka ta kauli, alichukua kalamu na karatasi na kuonekana kama anaandika kitu juu ya karatasi hiyo na kusokomeza ndani ya mdomo wa daktari.
Na yeye kutoka nje,. Aliungalia ukuta ule ulio kua mrefu, na kujiandaa kuruka ili atoke nje ila kabla hajaruka anazuiwa baada ya mguu wake kuhisi ume shikwa na mkono wenye nguvu alivyogeuza shingo alimuona mtu mrefu na mweusi..



Alfred alijitahidi kujivuta juu ili aushinde mkono ule ila hakuweza tena kutokana na tayari mtu yule alitumia mikono yote miwili na Alfred kuanza kushindwa kujivuta , alichofanya alitumia mguu wake ule mwingine na kuukunja juu ya shingo ya mtu aliye mshika alivyo hakikisha mguu wake ume jishika vizuri juu ya shingo ile alitumia fursa hiyo kuachia ukuta na kujizungusha akitumia nguvu za mguu ule kama mtu aliye kaa juu ya kiti cha ofisini cha kujizungusha na wote kudondoka chini,
Alichomoa kisu chake kidogo na kukidumbukiza shingoni mwa mtu yule ambae kwa wakati huo alikua bado yupo katikati ya miguu yake,
Alivyohakikisha kamaliza lile zoezi alimvuta taratibu na kumuingiza ndani jabali kubwa la uchafu na kumfunika.
"Uta pumzika humo"
Alfred aliongea maneno yale na kuangalia huku na kule na kuruka ukuta ule.
"NIME ANZA NA HAWA ,WEWE UTA FUATA,SIKU ZAKO ZINA HESABIKA, "
Uli kua ni ujumbe uliokuwa juu ya kikaratasi kidogo ambao Mujuni aliusoma mara mbili mbili huku aki fikisha macho na kutoamini,kile kilichoandikwa alichunguza zile maiti za madaktari vizuri,
na kushusha pumzi ndefu kama mtu aliye toka kufumaniwa na baba mkwe wake,

"Bosi, sijaelewa yaliyotokea hapa"
"Pumbavu zako, MJINGA WEWE,we una ona kuna nini, na yote ume yataka wewe,. Tena nyamaza usiongee..."
"Mimi tena, ??"
"Ndio wewe, aliye muombea kazi yule mlinzi ni nani, kwanza yuko wapi?"
Mashaka na wasi wasi vilizidi kutanda kwa Mujuni, kitendo kile haki kuwahi kutokea katika maisha yake, tena ndani ya jumba hilo kubwa lili lolindwa na walinzi kila sehemu., alipiga hatua kubwa na kuendea kibanda kidogo cha mlinzi.
"Askari embu njoo mara moja"
Mujuni aliita kwa kauli ya upole na kumfanya askari yule kuji chekesha huku akikenua meno na kujua wenda ana enda kupongezwa au kuambiwa kitu cha maana ila alijikuta yupo chini ghafla baada ya kutandikwa kofi lili lotua juu ya shavu lake la kushoto.
" pumbavu zako, una linda nini sasa?, una linda nini??, MAKALIO kabisa wewe, ina kuaje mtu ana pita ndani wewe upo hapa getini, NITA KUFUNGA"
Askari yule hakujua kosa lake alibaki chini akiugulia kofi lile ambalo hata hakuji andaa nalo, alibaki aki mtumbulia Mujuni macho kama mjusi alibanwa na mlango wa chuma tena aliyebanwa kwenye mkia.

"Bosi, bosi , bosi njoo haraka sana"
Sauti iyo ili mstua na kuanza kutembea ili kujua nini aliitiwa , hakuamini macho yake alipo kutana na maiti ya Tiko ndani ya Jabali la uchafu, na kumfanya azidi kupagawa.
"Ni kitu gani hiki tena,?,"
Aliangalia maiti ile ambayo ili kua ime toa macho kama samaki wa mwanza aliye kaushwa.
"Fanya uta ratibu wa hizi maiti zitoke, na na na na huyu nita mpata, nasema hivi nita mpata, na niki mtia mikononi mwangu, ATA KIONA CHA MTEMA KUNI, fanya upesi nawewe,"
Kweli kwa namna moja au nyingine Mujuni alionekana kuchanganyikiwa sana kwa tukio lililotokea mbele ya macho yake,.

" This is Mujuni Jumaa,"
" Inspector Msanganya here,
I just heard some troubling news Mujuni am sorry, i want you to know, my offer stands,"
"That wont be neccesary inspector, "
"NO Mujuni, i'm offering you proffesional guards,"
"I said NO, i will fight on my own, dont bother,".
Yali kua ni maongezi mafupi ya kwenye simu kutoka kwa inspector Msanganya akiongea na Mujuni kuhusu tukio lililotokea na kumu ahidi kua ange fanya juu chini ampatie muhalifu.,
Baada ya siku chache kupita ulinzi ulizidi mara dufu ndani ya jumba hilo huku madaktari wengine wapya waki ta futwa ili zoezi lile liendele,
Hanna akiwa chumbani usiku wa siku iyo kabla ya kumaliza sala yake ya usiku ghafla mlango wake alihisi ume funguliwa ila haku taka kufumbua macho mpka ata kapo maliza sala yake., alihisi ameshikwa mkono na kuvutwa juu huku akitolewa nje.
"Ndio, huyo huyo, .pakieni mzigo ule, ukiwa tayari niambieni"
Neno lile kutoka kwa Mujuni Lilipenya ndani ya masikio yake mawili na kushindwa kujua nini afanye maana alijua nini anamaanisha,
Hanaa aliburuzwa huku akiomba msaada ila alizibwa mdomo na kuingizwa ndani ya chumba hiko kidogo cha upasuaji, wali mpandisha juu ya kitanda na kuanza kumfanyia vipimo.
"Mwana mke yule ni mjamzito"
Daktari yule alitoka na kumweleza Mujuni ambaye wakati huo alitegemea kupewa jibu moja tu kua tayari upa suaji ume kamilika.

"Kwa io mimi nika mzalishe au?, "
"Sina maaana hiyo"
"Sasa una maana gani?"
"Nina maana kwamba, hatuwezi kupakia mzigo ule, labda tumtoe yule mtoto tumboni"
"PUMBAVU wewe, naona huwezi kazi,sasa una subiri nini, mambo mengine sio mpka uniulize, tumia akili, MTOE MTOTO tumboni pakia mzigo"
Kauli hiyo ili mfanya daktari yule kugeuka na kuanza safari ya kurudi alipo toka.
Kweli walianza kazi moja tu ya kumtoa mtoto tumboni mwa Hana ambaye kwa wakati huo alikua tayari ametimiza miezi miwili, hawakua na huruma juu ya kiumbe kile kisichokua na hatia, Hana akiwa ame fumba Macho ame kata tamaa kabisa huku akilia sana.,
Kazi ilianza daktari yule alivuta bomba la dawa ya usingizi ili baadae aanze kazi,
aliandaa kila kifaa na kuweka pembeni, alitumia sindano yake kuvuta dawa ndani ya kichupa kidogo ambapo alimaliza na kuanza kuta futa mshipa wa damu wa Hanna kama wana vyofanyaga madaktari wengine,
alivyo upata na kuridhika alichukua sindano yake ila kabla hajaanza kumchoma daktari yule alihisi kitu kizito kime tua kichwani kwake na kumfanya amdondokee Hanaa,
alimshuhudia daktari mwenzake akichomwa kisu mbele yake na mtu aliye vaa nguo nyeusi juu mpka chini,
Kishindo kile kilimfanya Hanna afumbue macho na kumuona mtu aliye jiziba uso akiwa ana kuja usawa wake, alipapasa papasa juu ya meza na kuchukua kisu kidogo, alivyoona mtu yule anae kuja sehemu alipo kwa kujihami aliji kuta Ana mchoma kisu begani.
"Han....naaaa......"
Sauti hiyo iliita na kumfanya Hanna abaki kushangaa huku akishuhudia mtu aliye muita akiweweseka, huku akihangaika kutoa kisu kile..


Ukimnya uli tawala kwa sekunde chache baada ya Hanna kuona mtu yule ana fungua uso wake taratibu, hakuamini macho yake alivyo muona Alfred Mulawa, Mume wake ambae kwa muda mrefu alidhani amekufa,
"Aaa..aaafredy"
Alijikuta anaongea kwa kigugumizi , Alfred alimsogelea pale alipo na kumkombatia.
"Naam Haana, ndo mimi"

Kilichotokea mbele ya macho yake aliouona kama mzimu, au pengine alidhani ana ota tena ndoto kali ambayo baadae angeenda kushtuka na kuji kuta yupo kitandani,
Ila kilicho kua kina endelea pale kili kua ni kweli tena ukweli mtupu sio njozi,
Walitulia kwa muda baada ya kuhisi kuna mtu anakuja, Alfred alisimama nyuma ya mlango na kuanza kujiandaa na yoyote ata kae tokea,
Mlango uli funguliwa na kabla mtu yule kuongea chochote Alfred alimvuta ndani na kumpiga kichwa na kufanya mtu yule akose muhimili wa kusimama, aliyumba ila Alfred almfuata na kumchoma kisu tumboni,.
Alivyo hakikisha mtu yule kakata kauli alichukua bandeji na kujifunga sehemu aliyo chomwa na Hanna kutokana na palikua pana vuja damu,.
"Hanna tuondoke, nime kuja kuku chukua mke wangu"
Hanna alitabasamu na kumshika mkono Alfred, ila walivyotaka kutoka nje Hana alisita kutoka, na kumwangalia Alfred machoni.
"Vipi tena Hanna,?"
"Alfred,.. Rose.,, Rose yupo , nime muona, yupo tafadhali naomba tuka mchukue."
Alfred aliba ki akitumbua macho huku akimuuliza mara mbili mbili yeye ali mfahamu vipi, ili bidi ampe stori kiufupi,
Alfred alitoka na Hana kwa tahadhari huku akiwa ana angalia pande zote, na kumuweka Hana sehemu ambayo mtu yoyote hatoweza kumuona,.
"Usitoke hapa, nita rudi sasa hivi"
Alfred aliondoka akielekea kwenye chumba alichoambiwa yupo Rose,
Alitembea na ukuta taratibu sana, mwishowe akuona ule mlango. Kama kawaida alitoa vitu kama vichuma viwili ambavyo huvitumia kufungulia mlango wowote, na kufanya kama ana tekenya na mlango ule kuachia,
"Shhhs shhhhhsss"
Alfred aliweka kidole chake kimoja mdomoni kuashiria kua aliyepo mbele asipige kelele.
"Rose Mulawa."
"We nani?"
"Alfred Mdogo wako, nime kuja kuku chukua"
Alfred aliongea vile huku akijifungua uso na kumfanya Rose abaki kushangaa na kutokujua nini afanye,
Bila kupoteza muda alimchukua dada yake ambae nayeye pia alionesha kutokiamini kile kina chotokea mbele yake,.
Alifika alipo mficha Hana na kuwa omba wasi pige kelele.
Alivyoona ile hali ya utulivu aliwaacha baada ya kuona kwa mbali mtu anaingia ndani ya gari, aliliendea huku mkononi akiwa ameshika bastola ndogo aina ya RIVOLVER.
Kabla ya yule dereva kuwasha gari alihisi kitu kama kichuma kimemgusa kichwani alivyogeuza shingo alikutana na bastola hiyo na kumfanya adondoshe sigara yake iliyokua mdomoni inatoa moshi kwani hakutegemea kitendo kile, sigara ile ili mdondokea juu ya suruali aliyovaa ila kwa wakati ule haku isikia.
"Una nijua mimi??"
"Aaaahha hap...aa..na"
"Kimnya kimnya fuata nita kacho kwambia"
Alfred aliangalia upande waliopo Hana na Rose na kuwaoneshea ishara kua waende eneo alipo, kweli walifika na kuingia ndani ya gari hiyo aina ya NISSAN PATROL,.
"Sasa washa gari,"
"Tunaenda wapi?"
Alfred aliongea akiwa amelala nyuma ya kiti huku bastola ile ikiwa nyuma ya kichwa cha dereva ambapo mtu yoyote aliye kua nje asinge weza kumuona kiurahisi ivyo ivyo pia Hana na Rose walilala wakiwa hawana uhakika kama wangetoka ndani mule,.
"Tutoke nje, sito shindwa kuweka risasi ndani ubongo wako endapo utaenda kinyume, washa gari twende"
Gari liliwashwa na kuanza kusogea na dereva yule akilisogeza gari lile getini ila mlinzi wa getini ana sita kufungua mlango na kulisogelea gari lile na kufanya hofu kutanda.
"Una kwenda wapi?"
"Maswali gani hayo.?"
"Nakuuliza una kwenda wapi?, sito kuruhusu mpka uniambie"
"Bosi ame nituma nika mpoke mgeni wake bandarini"
"Hapana ngoja nimpigie simu il....."
"Tulia ivyo ivyo fungua geti upesi, kabla sija sambaratisha ubongo,
nipe silaha yako upesi"
Kabla hajamaliza kuongea Alfrd alimuwekea bastola ile kichwani huku akiitolea dirishani, askari yule bila ubishi alivua mtutu wake uliokua kama Rubega na kumkabidhi Alfred aliye kua ndani ya gari.
"Na nina kuona, USINIJARIBU"
Askari yule taratibu alianza kufungua geti,
"Nawewe ingia ndani ya gari,"
"Nani mimi"?
"Wewe ndio, ulidhani nita kuacha"
Yule mlinzi nayeye aliingia ndani ya gari hiyo bila kujua wapi anapelekwa, .
Alfred alimuelekeza dereva yule akate kushoto na yeye kufuata vile anavyo ambiwa, mwishowe waka fika katikati ya msitu na Alfred kumuamuru dereva yule asimame,
"Aya safari yenu nyie ita ishia hapa, shukeni upesi kabla sija badili uamuzi na kuwa uwa, ".
Dereva na mlinzi yule wa lishuka haraka haraka na Alfred kuli tia gari moto.,
Ukimnya uli tawala ndani ya gari hilo huku kila mtu akionekana kutaka kuongea kitu, Alfred akiwa juu ya usukani ila gari hiyo ilianza kupiga kelele kuashiria kuwa mafuta yangeenda kuisha.,
Ivyo ivyo aliendesha ila baadae lilizima na wote kushuka wakitembea kwa mguu,. wali simama bara barani baada ya kuona taa za gari huku wa kisimamisha gari hilo lili lokua lina kuja, taratibu lili simama kulifata,
Dereva yule wa gari lile ali simama na kufungua kioo,
Alfred hakuamini alichokiona baada ya kioo cha nyuma kufunguka na kuona sura ya Mujuni akiwa na bastola mkononi..



Alibaki akimwangalia Mujuni ambaye kwa wakati huo alikua ameshika bastola mkono wa kulia na kuwaamuru wote waingie ndani ya gari hilo.
Hanna na Rose walikua nyuma ya Alfred wakimuweka mbele huku hofu ikiwa tanda kana kwamba Alfred ndie aliyekua msaada wao,
ila kwa wakati huo hata Alfred pia vile vile hakua na la kufanya zaidi ya kuingia ndani ya gari hilo dogo aina ya MARCEDEZ BENZ,
"Detective,... Una maisha marefu sana,.. nakufananisha na Lazaro ulie fufuka,."
Maneno hayo yali mtoka Mujuni akiwa na ile bastola mkononi huku akiongea kwa kejeli,
Aliikoki bastola ile na kuiweka utosini mwa Hannah
"Hauna haja ya kumuuwa huyo mwana mke, niue mimi, Niue mimi Alfred, ndo ninae staili kufa"
"Una dhani nita kuacha, naanza na mwana mke wako, na wote nawaua, kama nilivyo muuwa baba yako Rose, na fikiri una kumbuka"
Maneno yale yana penya moja kwa moja ndani ya ngoma za masikio ya Alfred na kumuangalia Mujuni vizuri, kumbukumbuku za Baba yake IGP Mulawa zina jijenga tena ndani ya ubongo wake na kutengenezwa taswira juu ya mboni ya macho yake,
" kumbe wewe ndo uliye muuwa Baba yangu IGP MULAWA,?, JUMAA, "
Mujuni alimuangalia Alfred na kumuelekezea bastola ile kichwani,
Gari hilo lili zidi kwenda kasi huku Alfred akizidi kutafakari. akili yake ilicheza kama umeme na kukumbuka kuwa mfukoni ana kisu kidogo, kwa kutumia vidole viwili kwa taha dhari sana huku akiwa ame mkazia macho Mujuni na kufanya wote waangaliane kwa macho makali,
Baada ya kuhakikisha kisu kile kimekaa sawa mkononi mwake, alimpiga Mujuni na bega huku akivuta HAND BREAK ya gari iliyo kua pembeni kwa dereva ambalo lili kua lina enda kasi,
Kutokana na mwendo kasi ule wa gari lile ilipelekea gari lile kupoteza uelekeo na kuacha bara bara huku likienda mtaroni ambapo lili pinduka na kufanya matairi ya gari lile kuwa juu,
Alfred aliji tahidi kuvuta mguu wake ambao ulikua ume banwa na kiti na kuupiga mlango teke kwa kutumia nguvu,
uli funguka mlango ule na kutoka huku akiwa toa Hanna na Rose ambao kwa wakati huo walikua wana vuja usoni, aliwa toa na bila kupoteza muda walianza kuingia msituni wakiliacha gari lile.
Wali zidi kusonga mbele baada ya kutembea mwendo mrefu bila kupumzika Hannah ana omba japo wapu mzike kidogo mpka kupambazuke,
kweli wali pumzika na kukaa chini ya mti mkubwa,
Huku kila mmoja aki tafuta sehemu ya kuji egesha ili masaa machache yaliyo baki waweze kuendelea na safari,
Kweli asubuhi kulikucha na mwangaza kuonekana.
"Naomba mni subiri hapa, narudi sasa hivi Hannah kamata hii, nina uhakika una jua kuitumia,"
Alfred alimkabidhi Hannah bastola ndogo ili kwa lolote lita kalo tokea aweze kujitetea , alimpa maelekezo madogo madogo maana sehemu waliyopo hapa kua na usalama wowote.
"Alfred una enda wapi?"
"Nisubirini, naenda kuta futa Kitu chochote cha kuwapa mle"
"Unadhani uta pata wapi chakula huku?"
"Nisubiri hapa, "
Alfred aliongea huku akiwapa visogo nayeye kuanza safari,
alipiga kama hatua kadhaa na kusimama chini ya mti mkubwa sana, ila alishangaa baada ya kukanyaga kitu na kamba kumfunga mguu wa kushoto kwa kasi sana na kumpandisha juu , na kumfanya aning'inie huku miguu yake ikiwa juu na kichwa chake kikiwa chini, na kubaki ana elea elea kama nyama, na kujua tayari ule ulikua ni mtego ambao ume tegeshwa.,
Kwa mbali alihisi kishindo cha mtu kina kuja, na moja kwa moja akijua tayari mwenye mtego huo ana kuja,
Aligeuza shigo kwa shida ili kutaka kujua anaekuja nani ila alishindwa na kuzidi kusikia parakacha parakacha ina zidi kusogea upande wake wa nyuma.
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)



0 comments:

Post a Comment

BLOG