Search This Blog

Monday, March 23, 2020

THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 1/10


THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
 SEHEMU YA 1 KATI YA 10

Giza totoro lilianza kuingia, hii ni kutokana na jioni kuingia na jua taratibu kuanza kuzama.
Hali ya hewa ya mji huo wa Dar es salaam, kidogo ilikua nzuri kutokana na manyunyu ya mvua yaliyoanza kudondoka kuashiria muda mfupi mvua ingenyesha,wingu zito lili zidi kutawala juu ya
anga na kufanya giza kuzidi japo ili kua saa moja jioni ila ilionekana kama ni usiku mnene kutokana na giza totoro.
Jimmy Wiliam na rafiki yake Abdul Karim walikua tayari washafika uwanja wa ndege wa kima taifa Mwalimu julius Nyerere wakionekana wakimsubiri mtu huyo kwa muda mrefu sana bila kutokea, Baada ya muda mfupi anaonekana mtu mmoja mnene wa wastani na mfupi wa makamo, aliyevalia suti nyeusi iliyoendana na miwani aliyovaa alitembea taratibu huku mkononi akiwa ameshika begi.
"Jimmy. Jamaa yule pale, kapita tayari, nili jua tayari wame mkamata"
" Ah wapi, ila nilianza kuingia na wasi wasi hata mimi".
Walimsogolea mtu waliyenda kumpokea na kumlaki wakiwa na furaha sana, walimpokea begi lake dogo na kuanza kuongoza, ila baaada ya kufika mbele kidogo walisikia sauti ikiwaita japo walikua hawana uwakika mpaka mmoja wao aliposhikwa mkono. Walivyo geuka walimuona kijana mdogo wa makamo mweupe aliye chomekea vizuri na kufanya azidi kuwa mtanashati, mtu huyo aliye wasimamisha alionekana kujiamini sana vile vile alionekana aliwafahamu watu hao bila kubahatisha.
"Naitwa Detective Alfredy Mulawa" aliongea Alfred akiwa mkononi kashika kita mbulisho chake akiwa onesha.
"Naona ume potea njia, tuna haraka kijana, "
"Tafadhali, naomba kidogo tuongozane"
"Huyu kavurugwa nini?, anazingua bana, tusepe Jimmy"
"Mwacheni" neno hilo aliamuru mgeni huyo waliye kuja kumpokea akionekana yule ndo aliye kua ana mamlaka juu yao, waliongozana mpaka kwenye chumba kidogo maalumu kwa ajili ya kukagua mizigo, walianza kufungua mzigo mmoja baada ya mwingine huku Alfredy akiwa pembeni akiangalia kila kitu,
" umeona hakuna kitu"
"Humo kwenye boxi kuna nin?i"
" nguo tu"
"Fungua ndani nione," boxi lile lili funguliwa na nguo kuonekana, ila Alfred hakutaka kuishia pale pale, aliamini kile anacho kitafuta ana uhakika nacho na si vinginevyo, aliiinama mwenyewe na kuanza kupekua nguo moja moja, alikutana na kitu kime fungwa fungwa na gundi nzito na kutoboa na kisu kidogo alichokitoa kwenye mfuko wake na kuona vitu kama unga, aliingiza mkono na kutoa aliuangalia unga ule na kuuweka puani na kumfanya apige chafya.
"Aya ni madawa ya kulevya aina ya cocaine, nyie ndo tulikua tuna watafuta kwa muda mrefu, na mtaenda kunieleza mlipita vipi,?, na nani ana husika ," alifungua tena na kukutana nao upo mwingi, baadae aliingiza mkono ndani kidogo ya begi na kutoa mkufu mdogo, na kumfanya asitishe zoezi la kupekua begi na kuanza kumwangalia aliyekua na begi lile usoni kana kwamba kuna kitu kime mkumbusha mbali na kufanya macho yake yabadilike rangi kwa hasira na kufanya sura kujikunja,.......

*****************************
IGP Samwel Mulawa mkuu wa mapolisi,ambaye alifanya kazi yake vizuri ya kuwa tia majambazi sugu mikononi mwa sheria na kutiwa jela.,leo hii ana pokea msiba mzito sana kuwa mke wake Flora Mulawa amefariki dunia baada ya kuuwawa kinyama na watu wasio julikana, lilikuwa ni pigo kubwa pia kwa watoto wake wadogo wawili Alfred na Roselyn,. Mama huyo aliacha watoto wawili wa kwanza akiwa Roselyn akifatiwa na Alfred ambao walipishana miaka michache, kilio kili tawala sana nyumbani hapo, IGP Mulawa japo alikuwa mbishi alijikuta analia kama mtoto mdogo akiwa na watoto wake wawili mikononi hakuweza amewashika, hakuweza kuzuia machozi yake.
"Mama, mbona ume ondoka mapema ?ume tuacha wadogo hivi?, Eeeh Mungu wangu, kwanini Mama yetu", Alfredy alipiga ukelele sana kwa uchungu sababu ndie aliye kua mtoto wa mwisho na muda mwingi alipenda kukaa sana na Mama kuliko baba yake, IGP Mulawa alishindwa kujizuia machozi yake alijikuta nayeye akijumuika akilia tena, ki ukweli lili kua pigo kubwa sana, ndani hata na nje pia kwa majirani zao, kila mtu aliumia kwa namna yake, . Taratibu za mazishi zili fanyika na Flora Mlawa kuzikwa katika makaburi ya kinondoni na mwisho wake kuishia hapo.
Baada ya arobaini kupita kila kitu, taratibu walianza kumsahau Flora ila ilikua vigumu kwa Alfred mtoto wa mwisho.
" Baba, mfano nikifa nitaenda kumuona Mama tena"?
" Alfredy mwanagu,. Mama sasa hivi analindwa na malaika, hapa tulipo ana tuona yupo pamoja na sisi, wote hata na Roselyn dada yako, cha kufanya mpende sana dada yako, maana Mama yako ata furahi muwahi kulala kesho shule Maneno hayo kutoka kwa baba yake yali mfariji sana Alfred na kuamini anacho ambiwa pembeni akiwa na dada yake usiku huo,
Ghafla mlango ulianza kugongwa kwa fujo na kufanya kero nyumbani, na moja kwa moja kuonekana kuwa anaegonga mlango huo alikua amepatwa na matatizo na akiomba msaada, Alichofanya aliwaamuru watot wake wakalale , hofu ilianza kutanda kwa Alfredy na kutotaka kuondoka.
" Nimesema nendeni chumbani upesi, na msitoke fanyeni haraka",
walivyo sikia kauli hiyo walitoka haraka na Alfredy kuvua mkufu aliopewa na Mama yake na kumkabidhi Rose dada yake amshikie,Marehemu mama yao aliwapa mikufu hiyo kabla ajafariki dunia, hivyo walitokea kuitunza sana mikufu hiyo.
IGP mulawa alifungua mlango kwa kujiamini ila kabla ya kujiandaa alihisi ngumi nzito yenye kilo nyingi imetua puani kwake na kumfanya arudi nyuma kidogo, hakukaa sawa alipigwa teke la tumbo na kudondoka chini,.
" hahahahahaha,MJINGA WA WAJINGA Mulawa, hivi ulidhani hii nchi ya baba yako, bwege sana wewe, sasa leo unaenda kufa kama alivyo kufa mkeo, wewe una weza kunifunga mimi?" Mlawa akiwa chini alisimama kusikia maneno yale, watu wengine walizidi kujaa na kufika takribani kumi,
"JUMA,! mnataka nini?",
" Eti, mnataka nini?, leo wewe ni mfu" aliongea Mwanaume huyo aliye kua pande la mtu. IGP Mulawa alishindwa kuelewa JUMA ametoka vipi jela. IGP Mulawa alimvaa jitu hilo na kudondoka nae chini, na kuanza kumpiga ngumi, ila wengine walimvamia na kuanza kumshambulia, alimfata mmoja na kumpiga kichwa puani, Mlawa alikaaa sawa na kukunja ngumi, ki ukweli alikuwa anaziweza japo alijua angezidiwa lakini hakutaka kukubali mapema, alimfata mwingine na kumkata mtama, alizungusha teke na kumpiga mwingine. Alfredy akiwa chumbani kupitia kitundu cha kitasa alishuhudia kila kitu bila kuhadithiwa, alishuhudia baba yake akipambana nao watu wale na kuanza kuogopa,
IGP Mulawa kuona hali ina kua mbaya alijirusha kwenye kochi na kutua na kufungua mto na kutoa bastola yake ndogo,.
" paaaaaa" alivya tua bastola na kumpata mmoja wao ya kichwa pale pale, ila Juma alimrukia na kuipiga teke silaha ile na kufanya idondoke chini,aliichukua mmoja wao na kuifya tua na kumfanya itue begani mwa Mulawa, na kufanya IGP MULAWA apige kelele nyingi za maumivu, Roseline alitoka mbio mbio mpaka sebuleni bila kuhofia chochote na moja kwa moja kumfuata baba yake aliye lala pale chini huku damu zikiwa zina mvuja.
" baba, Baba......, niueni na mimi basi, mume muuwa Mama yangu, na baba yangu pia, nima lizeni na mimi, Tume wakosea nini,?, Mungu atawalipa"
" kacha kacha" bastola ili kokiwa na kuoneshewa Roseline ila hakuonyesha hofu yoyote ile.
" niue niue basi"
"Paaaaaa paaaaaa" risasi ilivyatuka kwenye chemba na kusa babisha kelele nyingine, aliyekuwa amepigwa ni Mulawa ambaye alimsukumiza mtoto wake pembeni na kukaa yeye, risasi mbili zili penya miguuni. Kwa macho yake alimshuhudia baba yake ana pumua kwa shida baada ya kuishiwa na damu nyingi, kitendo kile kinamfanya ainuke na kumsogelea jambazi yule ila ana pigwa na kitako cha bunduki na kumfanya adondoke chini na kupoteza fahamu. Alfredy alitoka na chuma kikubwa kama nondo ili kusaidia, japo alikua hana uhakika na uamuzi anaoufanya, na kumpiga mmoja wao kichwani na kumfanya adondoke chini.
" Alfred...... Ki....mbi.a kimb..ia" bila kuangalia nyuma Alfredy alikimbia na kwenda kujificha, kutokana na ukubwa wa nyumba hiyo wali mtafuta Alfredy na kumkosa na kuondoka. Alirudi na kumkuta baba yake akiwa amelala chini.
" baba, baba, baaabaaa"
"Alfr..edy wame mchukua dad...a yako., mi siwezi t...ena kuishi.., mta..fute dada yako." Alfredy alilia sana na kupiga kelele za msaada ila hazikuweza kuzuia kifo cha baba ake mzazi ambapo kifo hiko alikushuhudia kwa macho yake.pigo jingine lili mpata la kumpoteza tena baba yake
******************************

Alfredy alimwangalia mtu yule kwenye paji la uso na kumuona ana kovu, na kukumbuka lile kovu na kupata jibu la swali lake. Alimkunja shati na kumkandamiza ukutani na kutoa bastola ndogo na kumuwekea mbele ya kichwa chake huku kidole kimoja kikiwa kwenye kitufe kinachoitwa triga ambacho kikivutwa nyuma risasi hutoka.
"Jina lako nani??, jina lako nani?"
" Naaa...itwa Aarafat Arafat, tafadhali usiniue"
Alimkaba koo uku tani akitumia nguvu nyingi kwa hasira. Na picha ya baba yake mzazi iki jijenga ndani ya taswira ya kichwa chake huku akiwa ameushika ule mkufu.
"Rose yuko wapi?"
" Rose yupi,? mimi simjui", alivuta kichwa na kumpiga puani,. Na vurugu kuanza ilibidi askari wa usalama waingie ndani ya chumba hiko ili kutuliza gasia ile na kumuamuru aweke silaha chini kwani anaenda kinyume na sheria, Walifungwa pingu watu wale na Alfred kuingia nao ndani ya gari aina ya Deffender na kuondoka maeneo ya uwanja wa ndege, njiani hakuongea kitu chochote, bali hasira msongomano wa mawazo ulichanganyika na chuki na kisasi ndivyo vili tawala ndani ya akili yake na kusababisha jasho kumtoka, akiwa makini juu ya usukuni wa gari akiendesha gari, simu yake ya mkononi iliita na kuangalia kwenye kioo cha simu na kuona jina WIFE, alitoa simu na kuipokea.
" mke wangu, usiwe na wasi wasi nipo salama, sasa hivi narudi,., ndio , nita kupigia baadae kidogo", alikata simu na kuirudisha mfukoni.
"Una tokea nchi gani. Arafat? Nakuuliza ume tokea nchi gani,?, na nani kakutuma hayo madawa,."? Arafat alikaa kimnya na kuonyesha hakuwa tayari kujibu swali lolote lile.
"Bora uongee na mimi sasa hivi, maana huko una poenda uta pata tabu na vile vile utasema" aliongea Alfred huku mkono wake ukiwa una badili gia baada ya kukunja kona aliyokutana nayo mbele yake,.
"Usi poteze muda wako, niue tu"
"Siwezi kukuuua , ume tokea nchi gani?, una ona nafanya utani subiri nikuonyeshe". Aliminya breki ya ghafla na kuweka gari pembeni na kumshusha Arafat nje ya gari, alimvuta kichwa chake na kukibamiza juu ya boneti la gari, alimvuta na kumkaba.
" Nani kakutuma", nani kakutuma?" alizidi kumshambulia ngumi nyingi na kufanya Arafat avuje damu nyingi puani, Ghafla bila kutegemea gari lili kuja mbele yake na kushuka watu watatu wakiwa na mitutu mikononi, wakionekana kua muda mrefu walikua wana wafatilia kwa nyuma bila Alfred kujua.
" Tulia ivyo ivyo , aya mfungue upesi, fanya haraka sana.Wafungue na wengine" Alfred hakuwa na ujanja wowote ule alimfungua mmoja baada ya mwingine, ila alivyofika kwa jimmy alimkaba na kumuweka mbele yake akawa kama kinga yake hata ikitokea waki vyatua risasi, isi mpate, hapo alipata nafasi ya kutoa bastola yake na kumuwekea Jimmy ubavuni,. Ilikua ni kama movie ya kuigiza tena ya kijasusi. Alfred alirudi nyuma nyuma na kusimama nyuma ya gari, na kutoa simu, walivyoona hali ina kua sio waliwasha gari yao na kuondoka huku wakitimua vumbia kali alimtia pingu Jimmy na kuingia nae kwenye gari, na kuondoka nae na kujua kivyovyote vile angeenda kutaja kile anacho kijua,. Dakika chache alimfikisha kituo kidogo cha polisi oyster bay na kufunguliwa faili.
"Kesho asubuhi nita kuja hapa, naomba hili faili mwenyewe nili simamie lisi fike popote pale, ume nielewa"
"Ndio mkuu"
aliiitikia mmoja wa Maaskari wa zamu na Alfred kuondoka akielekea nyumbani kwake kimara,.
Alimkuta mke wake Hanna akiwa amelala juu ya kochi akimsubiri mumewe.
" Nime rudi Hanna, za kushinda"?
" mmmmh nzuri, otea nataka nikwambie nini?"
"Umeanza mambo yako sasa , niambie alafu nimechoka kweli kweli leo",
Hanaaha alimsogelea Alfred na kumkalia huku akimbusu juu ya paji lake la uso huku akitabasamu, na kufanya uzuri wake uongezeke mara dufu
"Leo nilienda hospitali, Mmmh, unajua nimeambiwa nini?"
"Enheeee".
" Nina uja uzito wa miezi miwili, Alfred ndoto zangu zime timia, hakika Mungu ni mkubwa",
" una nitania, alafu punguza mzaha," aliongea Alfredy akiwa mwenye furaha sana siku iyo, hakutegemea maneno hayo kutoka kwa mwana mke anaye mpenda sana katika maisha yake wote kwa pamoja wali furahi sana. Alfredy kutokana na uchovu aliingia bafuni kuoga na kurudi na kukuta chakula tayari kipo mezani na kuanza kula.
" griii griiiiii"
simu ya mkononi ya Alfred iliita ila haikuonyesha namba yoyote kwenye kioo, kitendo kile hakikuwa kigeni kwake, aliingalia ile simu kwa muda mrefu na kubonyeza kitufe cha kijani na kuiweka sikioni.
"Detective Alfred,"
"We nani?" Hilo ndilo lilikua swali la kwanza kuuliza tena kwa sauti ya kushtua na kumfanya Mke wake Hanna aache chakula na kutaka kusikiliza maongezi yale.
" haijalishi,. Una kijana wangu ulimkamata jana usiku, nakupa masaa saba na awe huru"
upande wa pili uli sikika ukisema tena kwa sauti ya bezi la kukwaruza
" Hilo swala halitowezekana hata kidogo"
" una masaa saba , na nina uhakika uta badili maamuzi yako,USIKU MWEMA DETECTIVE"
"sasa.....tititiititi" simu ile ilikata na kubaki akiangalia saa ya ukutani ambayo ilikua tayari imejiri saa saba usiku ivyo alijikuta akihesabu masaa yaliyo baki., alimwangalia mke wake machoni na kumuona mwenye wasi wasi, alimshika mkono na kumbusu shavuni.
" usiwe na wasi wasi Hanna,"
" ila nilikwambiaga ubadilishe hii kazi ni ya hatari, nakupenda sana Alfred ila kila wakati nakua nakuwaza alafu isitoshe hapa nina ujazito tayari Alfred"
" Hanah nisikilize kwa makini, usiwe na wasi wasi, niamini" Kwa upande wa Alfred hakuwa na wasi wasi hata kidogo maana vitisho ivyo amevizoea, ivyo haikumpa shida yoyote ile aliendelea kula bila wasi wasi.
" Muda mfupi nita itwa baba" aliongea mwenyewe na kufanya Hannah ata basamu na wote kuendelea kula


Asubuhi kulikucha tayari na Alfred akijiandaa kwenda kazini, alivaa shati jeupe na kuchomekea vizuri, shati hilo lilimkaa vizuri kabisa, alichukua bastola yake ndogo na kuhakikisha ila risasi baada ya kuchomoa mkebe una okaa risasi, alivyoridhika alirudisha mkebe huo ndani ya bastola hio na kuiweka kibindoni sawa sawa na kuifunika na shati ili isiwe rahisi kwa mtu yoyote kujua, alimuaga mke wake vizuri na kuingia ndani ya gari yake mwenyewe binafsi aina ya HARRIER, alipiga honi kuashiria mlinzi aliyekua getini hapo afungue geti hilo,
Akiwa ndani ya gari simu yake iliita na baada ya kuangalia alikuta PRIVATE NUMBER, kumaanisha kuwa mtu aliye mpigia hakutaka ajulikane, aliitoa na kuiweka sikioni.
"Detective Alfredy, usha badili maamuzi yako?,
" Maamuzi gani"?
" kumuachia huru kijana wangu, usijifanye umesahau, UTAJUTIA," Alfred alivyoona vile alikata simu yake na kutotaka kuendelea na mazungumzo yale maana hakuona umuhimu wake,. Baadae aliegesha gari yake kituo kidogo cha oysterbay na kushuka na kutaka lile faili la Jimmy, moja kwa moja alipelekwa kwenye chumba alichowekwa Jimmy na kwenda kukaa nae pembeni ili aweze kujua na kumhoji maswali.
" Jimmy Sangu, bado kijana mdogo sana, taifa lina kuhitaji kwa namna moja au nyingine, tusipoteze muda hapa, ushirikiano wako ndo utakua urahisi wako wa kutoka humu"
" una jisumbua"
" Hata mimi naona,!, sawa najisumbua, utaenda kusema kile nachokitaka tena sasa hivi, hunifahamu vizuri naona"
Alfredi hakutaka kubishana ali simama na kutoka ila baadae alirudi na plies inayotumika kukatia nyaya ngumu pamoja na pini na kuviweka mezani.
"Yule uliyekuwa una mpokea jana uwanja wa ndege ni nani"?
" kamuulize maswali hayo mama yako mzazi" Alfred aliinuka kwa hasira na kumzaba kofi,lililo lia kwa sauti, hakuishia hapo, alichukua plies ile na kuanza kumbana nazo sehemu za siri huku akitumia nguvu kana kwamba ana kata waya au chuma kigumu, na kumfanya jimmy apige kelele sana,
"Sema, sema, sitoacha mpaka useme"
"Aaaaaaaaah,. " zilikua ni kelele nyingi ila hakuonesha dalili yoyote ya kuongea.
"Una jifanya una jua maumivu?, hapana hujui chochote kuhusu maumivu, hujui, ? SUBIRI NIKUONYESHE"
alivuta mkono wa jimmy wa kushoto na kuchukua kidole kimoja, alichukua pini moja na kuichomeka chini kidogo ya kucha mpaka ikazama yote, akachukua kidole kingine na kufanya vile vile, na kufanya kelele kali zilizofanya machozi ya jimmy kuonekana .
" Mu.....juuuni, Muu....juni, Mu...juni ndo ndo ndo kanituma,"
"Ana ishi wapi?,ana ishi wapi?"
" anaa ii..shi KIBAMBA": jimmy alijikuta ana ongea kila kitu baada ya adhabu ile kali yenye maumivu makali.

Upande wa pili tayari gari ndogo aina ya MARK II GRAND nyeusi ambayo ilipigwa tinted yaani vioo vyeusi na kufanya mtu aliye kua nje asiweze kuona ndani, lili egeshwa maeneo ya kimara stop over, pembeni kidogo ya geti la rangi nyeusi. Ndani ya gari hilo wali shuka watu wawili warefu kidogo na kuliendea geti hilo na kugonga kengele, Mlinzi aliye kua akilinda hapo, aliacha chakula anacho kula na kukimbilia getini na kufungua mlango mdogo.,na kuwasikiliza watu aliwaona mbele yake.
" samahani Askari, sijui hapa ndo kwa Alfred,"?
"Ndo hapa, wala hamjakosea"
" sijui tume mkuta?"
"Hapana, katoka asubuhi, na kurudi mpka usiku, kwani nyie ni akina nani?"
" basi tuta kuja usiku, ila unaweza kuni saidia na maji ya kunywa ya baridi,"
Mlinzi yule alikubali kuwapa maji ila kitendo cha kugeuka na kuwapa kisogo, watu wale waliingia na kumkaba na kutoa bastola ndogo na kumuwekea tumboni.
" Tulia tuli, bwana Afande, ukifanya fujo ndo mwisho wa maisha yako, ndani kuna nani,?,
" yu.. yuyuyuyupo Mama"
Mlinzi yule aliongea kwa kigugumizi na kutojua kimetoka wapi.
" yuko peke yake?
"Ndio"
" nipe funguo zako" mlinzi alitoa funguo na kuingizwa ndani ya chumba chake akiwa ame fungwa kamba na kuwekwa nguo mdomoni na kufungiwa kwa nje, na kufanya mtu yoyote asijue kama yupo ndani ya chumba chake,. Taratibu walinyata na kugonga mlango mkubwa wa sebuleni na Hannah mke wa Alfred kutoka nje, macho yake yaligongana na tobo la bastola ambayo alielekezewa usawa wa kichwa na kuamriwa asipige kelele,
" pesa zipo nitawapa zo..te, msiniue tafadhali"
"Tuli kwambia tuna taka pesa,? upumbavu wa Mume wako ndo uta kufanya upate shida, ongoza twende" aliamuru aliye shika bastola na bila kuleta utata Hanna aliongoza mbele na wao kufata nyuma bila kujua wapi ana pelekwa., aliigizwa ndani ya gari hilo ambamo kulikua na dereva na gari hilo kuondoka na yeye kufunikwa kitambaa cheusi ili asijue wapi anaenda.
Alfred akiwa njiani ndani ya gari yake anaendesha kuelekea maeneo ya nyumba aliyo ambiwa ghafla simu yake ya mkononi iliita na kuipuuzia baada ya kuona private number na kujua ni wale wale wanaomsumbua., ila baadae alipokea na kuiweka sikioni.
" Alfredy Mume wangu.....'
"Hanna, Hanna, .. titiiii.." simu ile ili katwa na kumfanya Alfred aingiwe na hofu baada ya kusikia sauti ya mke wake, aliweweseka na kutojua nini afanye, alitafuta majina mpaka alipo fika kwenye jina WIFE na kuipa simu okay ili kuhakikisha kile alicho sikia, ila cha kushangaza simu hiyo haikupokelewa, na kujua kivyovyote vile Mke wake yupo kwenye matatizo, hakuwa na wazo lingine zaidi ya kugeuza gari na kuelekea nyumbani kwake KIMARA.


Akilini aliwaza mengi sana, kutokana na mapenzi ya dhati anayo mpenda Mke wake hakutaka ateseke wala kuteswa, alikumbuka kitu na kutoa simu yake akitafuta namba ya mlinzi wa getini, ila jibu lilikuwa lile lile haikupokelewa na kufanya Alfred azidi kuingiwa na hofu, alikata kona ya Kimara stop ova na kuiacha bara bara ya lami akiifuata bara bara ya vumbi, baada ya muda mfupi tayari alifika na kuweka gari kidogo mbali na nyumba yake, alitoa bastola na kuiweka sawa huku akishuka, alichofanya alizunguka nyuma ya nyumba na kupanda ukutani hakutaka kupitia getini hii ni kutokana na kujihami, taratibu alinyata kama paka shume huku bastola yake ikiwa mkononi akiwa amejiandaa na tukio lolote lita kalo mkabili mbeleni, aliingia ndani na kuzunguka kila chumba ila hakuona mtu yoyote, alipiga jicho lake mpka kwenye nyumba ndogo ya mlinzi na kuona kuna kufuli lime fungwa, alisogea taratibu na kuchungulia dirishani alimuona mlinzi akiwa amefungwa kamba huku akiwa na nguo mdomoni, haraka haraka aliingia ndani na kutoka na funguo nyingine za akiba na kumfungulia mlinzi yule.
"Ime kuaje?, "
" hata sijui, wame mchukua Mama watu wawili," mlinzi huyo aliongea kwa kuweweseka,
Alfred alienda ndani ila hakujua ana enda kufanya nini, hii ili tokana na kuchanganyikiwa simu yake iliita na haraka haraka kuiweka sikioni.
" Nyie ni akina nani,? mtu wenu nita wapa"
"Alfred umechanganyikiwa?,"
ilikua ni sauti ya kike iliyo sikika upande wa pili na kudhani anaongea na majambazi wale., ilibidi aitoe sikioni na kuangalia jina kwenye kidogo cha simu yake
" sio hivyo Jaqlin, nina tatizo kubwa hapa,"
" una tatizo gani?"
" nita kwambia usijali, nita kwambia tu, kwa sasa hivi naomba niache kidogo, maana hata kuongea siwezi tena" .

Msongamano wa mawazo uli msonga na kushindwa wapi aanzie,. Kilicho mshtusha ilikua tena ni simu yake iliyo ita tena na kujua ni watu walio mchukua Hanna kutokana namba kaikujionyesha.
"Una dakika thelathini tu, mkeo ana poteza uhai wake, maisha ya mkeo yapo mikononi mwako, na kwa hili wewe mwenyewe ndo ume sababisha"
" Sawa nime kubali, naomba mumuachie nita wapa mtu wenu"
"Vizuri sana,nita kupigia simu muda mfupi, ila nakuomba usimshirikishe mtu yoyote kwenye hili, sababu huta hatarisha maisha mrembo wako" . Simu ilivyo katwa haraka haraka alichukua funguo za gari na kutoka kama mshale, aliingia ndani ya gari na kulitia moto akitoka kwa kasi, kiapo cha polisi kua ata tumikia jeshi la polisi vili muingia kichwani lakini pia vilevile alikumbuka siku yake ya ndoa akiwa na Hanna kanisani kua atamlinda kwa kitu chochote kile. Aliegesha gari nje ya kituo cha oysterbay na kuingia moja kwa moja mpka kwa Jimmy, na kumshika na kuondoka.
" Mkuu una mpeleka wapi?"
"Nita kuja nae usi hofu, kuna mambo ya upelelezi naenda kumfanyia, ila iishie ivi ivi mimi nawewe"
Alfred ificha ukweli huo na kuingia nae ndani ya gari, ila hakutaka kuku bali, alichowaza yeye ni kimoja tu, baada ya kumchukua mke wake na pia asiwape Jimmy, alitamani kuwa shirikisha wenzake ila alihofia maisha ya mke wake ambayo wakati huo alikua katika mikono hatari.,
" una nipeleka wapi?"
Alfred alimwangalia Jimmy na kukaa kimnya, baadae simu yake iilita na kuiweka sikioni akisubiri maelekezo.
" Ndio, nime kuelewa, sipo mbali na hapo, hakuna tatizo, yupo salama, .NAPAJUA NDIO, nita tumia kama dakika ishirini"
aliweka simu baada ya kuelekezwa wapi wakutane na watu hao asiyo wajua, Gari iliacha lami ya Mbezi mwisho na kuingia kushoto kuelekea Makabe huko ndiko walipo panga wakutane, taratibu alipunguza mwendo na kusimama, ali toa simu na kupiga namba aliyopewa akifika na kutoa taarifa.
" Nipo kwenye HARRIER ya kijivu,"
alielekezwa pa kuingiza gari hiyo ndani ya kamsitu kadogo wenye miti mingi, ina onekana watu hao wali kua wana muona sababu walimpigia tena simu na kumwambia afungue milango yote ya gari ili kuhakikisha hakuna mtu yoyote mwingine, alishuka akiwa amemshika Jimmy pembeni na kuanza kufuata maelekezo mengine, akizidi kuingia kati kati ya msitu mpaka alipo kuta piki piki mbili zimeegeshwa na kuwaona watu takribani watano huku mmoja akiwa amemshika Hanna.
"Mfungue izo pingu"
Alfred alitii kila kitu,. Baada ya hapo jimmy aliachiwa na Hanaa kuachiwa wote wakiwa wanatembea kila mtu akienda upande wake na kupishana, Hanna alifika kwa Alfred na kumkombatia.
" Twende Hanna, sio mahala pake hapa",
baada ya kupiga hatua mbili walishtuka na kuona watu wakishuka juu ya miti na kuwa zunguka.
" ha ha ha ha ha ha, Una jifanya YESU KRISTO, una mpenda sana mkeo, aya leo tuna taka tuone,"
aliye kuwa mbele yake alimsogelea huku akiongea kwa kejeli,Alfred aliona ngumi ina kuja na kuinama na kufanya ipite kama upepo, alirudi nyuma na kukaa sawa,alimsogeza Hana pembeni na kukunja ngumi vizuri, aliona ngumi nyingine ina kuja usawa wa mdomo wake na kuhepa kushoto na kuifanya ipite safari hii nayeye alitupa ngumi nzito na kumpata kwenye kidevu mpinzani wake, alimfata pale pale na kumpiga kifuti cha taya, alizungusha teke na kumpiga wa nyuma yake, ki ukweli Alfred kwenye michezo ya kupigana alikua vizuri kuliko maelezo, hii pia ilitokana na mwili kua mwepesi, alitulia na kuanza kumpiga mmoja baada ya mwingine na kuzidi kuwapunguza, alimfata mmoja na kuzungusha mkono wake, na kumvunja na kufanya ukelele mkali, ila baadae alihisi kuna mtu kamshika begani alivyogeuka alihisi chuma kizito kime mpiga utosini na kufanya adondoke chini, kutokana na uzito wa chuma kile pale pale alidondoka chini na kupoteza fahamu.


Ubaridi wa maji aliyo mwagiwa ndo y aliyo mfanya azinduke na kukurupuka akiwa ame fumbua macho,alishindwa kuinuka kutokana na kamba zilifungwa na kukazwa vizuri kwenye miguu na mikono yake juu ya kiti alicho kalishwa.alitazama juu ya chumba hiko na kuona kidirisha kilicho pitisha mwanga wa jua, alivyoangalia pembeni ukuta wake ulikua hauna rangi hata na sehemu ya chini kulikua kuna zege peke yake kuashiria kwamba yupo stoo au nyumba ambayo haiku maliziwa
"Mke wangu yuko wapi?" Hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza kutoka kinywani Mwa Alfred Mulawa,
" uta muona subiri"
"Si nimewapa mtu wenu, mnataka nini tena,?,
"Hivi una jiamini nini mpaka unaongea maneno hayo,PANYA MFU wewe, tulia ivyo ivyo usubiri kifo chako", Alfred alifunguliwa kamba na kutolewa kwenye kiti kile na kuongozana na mtu yule aliye kua mbele yake, alizidi kuichunguza nyumba iyo bila kujua sehemu alipo, Moja kwa moja alimfikisha sehemu yenye uwazi mkubwa na kumuona Hana alivyotaka kumfuata alizuiwa,
Aligeuza shingo na kumuona pande la mtu lenye misuli na kujazia, alionekana kuwa ni mkubwa wao sababu wote walitulia na kusubiri amri yake.
" nileteeni huyo mwanamke hapa"
weusi wa sura yake yenye makunyanzi uliendana na sauti yake nzito yenye mikwaruzo na moja kwa moja Alfred kutambua kua yule ndie aliye kua akimpigia simu wakati wote,
" Kijana Alfred, haya yote yangeisha vizuri, ila kwa UPUUZI WAKO namuuwa mkeo mbele yako ukishuhudia, na sina mzaha" Hanaa kusikia ivyo alimuomba Mungu aipokee roho yake maana hakuwa na ujanja alimuangalia Alfred machoni na kuanza kudondosha machozi., Alfred alichomoka ghafla kwenye mikono ya watu waliomshika na kuanza kumuendea mtu yule mwenye misuli kwa hasira akitaka kumkabili.
". Mwacheni"
kauli ilitoka kwa mtu huyo baada ya Alfred kutaka kukamatwa na kuzuiwa asi mfuate ivyo aliachiwa na moja kwa moja kumfuata,
Alfred alienda na kumrukia teke ila lili dunda baada ya baunsa yule kutunisha misuli, hakuishia hapo alikunja konde na kutaka kumpiga ila ilishindikana alipotaka kurusha ngumi, Alfred alikamwatwa mkono na kupigwa fundo la NGUMI iliyopenya vizuri kwenye taya na kumuingia, uzito wa ngumi hiyo aliifananisha na gunia la zege lililochanganywa na sementi,hakuweza kuvumilia aliji kuta anashika mdomo wake na kuhisi michirizi, alivyoangalia aliona ni damu nyingi, kweli ngumi ile ili muingia vilivyo na kufanya apate kizungu zungu cha ghafla.
" Mimi naitwa Brigedia Mujuni, wewe nakuona kama kunguni, rusha ngumi,rusha ngumi yako,"

Mujuni alimfuata Alfred na kumpiga kifuti na kumnyanyua na mkono aliouweka kwenye koo lake huku akimkandamiza ukutani.Miguu ya Alfred ilikuwa ikining'inia mithili ya nyama iliyopo buchani. Hanna alipiga sana kelele akimuomba Mujuni amuachie mume wake,
" Alfred wewe ni bwana mdogo sana kwangu, leo utafia hapa hapa na tuta zika maiti yako,"
aliongea Mujuni akiwa karibu na kinywa cha Alfred.,kila alipojitahidi kutoa mkono ule wenye msuli alishindwa, Alizidi kumtazama machoni kama joka KOBOKO aliye taka kummeza mtu,. Alidondoshwa chini baada ya kuachiwa kutoka kwenye mikono yenye misuli na kumfanya aweweseke akitafuta pumzi. Mujuni alimsogelea Hanna na kumshika, ila Hana kwa hasira alimtemea mate na kumfikia Mujuni juu ya jicho la kushoto, alipanguza mate na kumzaba kofi lililo mfanya Hanna Mulawa kuteleza
chini.
"Jimmy nigee bastola," haraka haraka aliwekewa bastola mkononi na kumuelekezea Alfred chini pale alipo.
" naomba utuache twende, na umuache mume wangu, tutawapa mna chota , YESU wangu,."
Machozi yalianza kumdondoka Hanna baada ya kuona kitendo kile na kuanza kumuomba Mungu aweze kutenda miujiza yoyote ile.
"Kacha kacha....., rest in peace,",
aliongea Mujuni na kuvuta nyuma kitufe kina choitwa triga,ili kuiruhusu risasi ilikuwa chemba itoke na kumfikia mlengwa.
"Grrraaa graaa,....Jimmy ina kuaje una nipa risasi haina kitu, una nitania mimi Babu yako?,"

ali mfuata Jimmy na kumkunja na kumzaba kofi la shavu., Na kuchukua kisu kilichokua mezani pale, alimfata Alfred pale alipo na kumchoma nacho ubavuni, alikichomoa kisu hiko na kukichomeka tena alikuwa kama ana pima oil kwenye injini gari, Hana akiwa ana shuhudia aliona kama ana ota kitendo kile cha kumuona mume wake anachomwa kisu na kumfanya avuje damu nyingi nyingine ziki tapakaa chini.
" Al.......freeeeeed " kwa nguvu za ajabu Hanna alichomoka na kwenda kulala juu ya mwili wa mume wake Alfred na kulia kwa sauti huku akimtingisha tingisha


Kwa Mbali Alfred alifumbua macho japo aliya lazimisha macho yake kuona aliweza kumuona mke wake Hana akilia kwa uchungu, kwa mbali akitoa tabasamu japo kwa shida ili amfariji mke wake ambaye alikuwa kasha kataa tamaa kabisa.
" Hanna mtu....nze mtoto wan...gu, usi..lie ku.wa jasi......"
Alishindwa kumalizia anachotaka kusema kunyamaza kimnya huku taratibu macho yake yakiwa yanajifumba kama jenereta lililoishiwa mafuta kwa upande wa Hanna ilikua ni kama picha la kuigiza tena la kihindi, kilicho kua kina tokea mbele yake alihisi ni ndoto ndefu ambayo muda mfupi angeenda kushtuka na kujikuta kitandani akiwa na Alfred ila haikua ivyo, mambo yaliyo tokea hapo yalikua ni ya ukweli na wala sio ndoto wala maigizo,na kubaki alishika tumbo lake..
"Uwiiii, Alfred Mume wangu amka baba, Alfred , Alfred,."
Alizidi kuutingisha mwili wa Alfred bila mafanikio yoyote yale.
Mujuni aliamuru mara moja mwili ule uchukuliwe na kutupwa shambani, haraka haraka vijana wanne waliubeba kama wana beba mzoga na kuondoka na mwili huo huku Hanna akiwa ameshikiliwa na Mujuni,.
Kweli waliubeba na kuutupa shambani na wao kurudi.

Maumivu makali ambayo tangu azaliwe hakuwahi kuyasikia alizidi kuyasikia maeneo ya ubavuni mwake na kumfanya ashindwe kuinuka alipo kua amelala, ivyo ili mlazimu atambae kama jongoo au nyoka magamba, alikua ni Alfred baada ya kurudiwa na fahamu ki ukweli hakufa kama wakina Mujuni na mke wake Hanna walivyodhani. Alitambaa kwa shida huku akiitafuta bara bara ya Lami huko akijua angepata msaada wowote, kweli alitambaa bila kujua anapokwenda , chini kwa chini alipita taratibu, kutokana na giza lili kua lishaingia ili mfanya apate shida kuona kilicho kua mbele yake. Baadae anapata tumaini na faraja baada ya kusikia miungurumo ya magari yakipita na kuzidi kusonga mbele maana alijua hiyo ndo njia pekee ya kujinusuru katika mdomo huo wa Mamba, ivyo ivyo alizidi kujivuta na mwishowe kufika bara bara ya lami na kujilaza chali akitegemea hapo angepata msaada wowote ule, magari yali mpita bila kuonyesha msaada wowote ule na kutokumjali, ACE TOWN nyeusi ilionyesha kusimama na mzee wa makamo kushuka ndani ya gari hilo na kumuokota, bila kupoteza muda moja kwa moja ali mpeleka kituo cha polisi na kupewa kibali cha kutibiwa hospitali yoyote ile. Alichofanya mzee huyo alitafuta hospitali ya karibu na eneo hilo na kumfikisha na kuwaomba msaada wauguzi.
************************
"Mzigo nili upata ila ulileta tatizo kidogo, yes bwana Mbuya, si una jua sisi tuna kula na wakubwa wa nchi hii, usiogope, usiogope kuhusu pesa"
sauti Ya MUJUNI ili sikika akiongea na mzee wa makamo mwenye mvi kichwani kidogo, Mzee Mbuya alikua ni mfanyabiashara mkubwa sana ila mbali na hapo alikua akihusika na uuzaji wa madawa haramu ya kulevya aina ya HERROIN na COCCAINE,
"Yule mchungaji kesho ata kuja na mzigo , ana tokea ISRAEL, ana kete sabini, hakuna cha dini pale, alafu waumini wake wana muamini sana, eeeeh Mungu msamehe mja wako, yule jamaa akikaa mbele pale sijui madhabauni sijui wapi pale, yaani khaa, kweli hii dunia ina mambo"
Aliongea Mbuya akicheka na Mujuni huku wakipiga stori kwenye moja ya bustani kubwa nje hapo huku wakiendelea na vinywaji. Waliongea mengi sana huku wakipongezana kwa biashara zao zikienda sawa. Mazungumzo yao yali katishwa na Jimmy aliye kuja mbio mbio huku akihema kana kwamba ametoka kukimbizwa na simba.
" ule mwili wa Alfred siuoni tena"
"Uuuwoni kivipi?, embu nyoosha maelezo yako vizuri, alafu mbona una hema hema ivyo kama swala nini tatizo,?"
" jana nili utupa kule sijauona leo"
"Una taka kumaanisha nini?"
"Hata sielewi,"
Waliinuka na Mujuni na kwenda mpaka eneo alilotupwa na Alfred na kukuta hakuna dalili ya mtu, ila kwa uma kini Mujuni alitazama chini na kuona michirizi ya damu na kuifata taratibu mpka waka tokea kwenye bara bara ya Lami ya Kibamba, na damu hiyo hawa kuiona tena.
"Hata kuwa mbali na hapa, kama hayupo hospitali ya hapa karibu, subiri kidogo, ila nita mpata mimi ndo MUJUNI, ",
pale pale alitoa simu mfukoni na kutafuta namba Mpka alipofikia Dr.Shamiru na kuiweka simu sikioni akisubiri upande wa pili wa simu usikike, baada ya muda mfupi simu ilipokelewa.
" salama tu Doctor, jana uli kua zamu,?"
" ndio nili kua zamu"
" kuna mgonjwa yoyote jana aliletwa hapo"?
" wagonjwa kila siku wana letwa labda ungenitajia jina lake na saa ngapi"
" Ana itwa Alfred, alikua ana majeraha tumboni,"
"Subiri kidogo usikate simu, Alfred, Alfred, Alfred"
Dr. Shamiru alirudia rudia jina lile na kuonekana moja kwa moja ana litafuta jina hilo kwenye kitabu chake.
"Yaaaah Alfred Mulawa, aliletwa jana, na mzee mmoja hivi usiku, alikuwa hana fahamu, yupo thieta sasa hivi,"
"Naweza nikaja hapo sasa hivi tuongee"
" Hakuna shaka njoo"
Kitendo kile cha daktari yule kukubali kilimfurahisha sana Mujuni na nia yake ilikua moja tu kummaliza Alfred na kumuua .



shirika la ndege la BRITISH AIRWAYS, ilianza kutoa magurudumu yake nje taratibu kuashiria kua ingetua juu ya lami maalumu, ndege hiyo iliyokua ikitokea nchini ISRAEL, na kutaka kutua Tanzania jijini Dar es salam katika uwanja mkubwa wa kimataifa wa Mwalimu NYERERE, matairi yalikanyaga ardhi hiyo ya lami na kusababisha makelele mengi kutokana na msuguano, baada ya matairi yote kugusa lami ilianza kutembea kwa kasi sana na mwishowe kupunguza mwendo huku taratibu ikielekea kusimama,.
Sauti nzuri na nyororo ilisikika ndani ya ndege iyo,kutoka kwenye kipaza sauti ikitangaza kuwa wana oshuka, waanze kushuka,maana muda mfupi ujao ndege hiyo ingeondoka tena.
Mchungaji.ANDREW KONDE, miongoni mwa abiria waliomo ndani ya ndege iyo akitokea ISRAEL kutangaza injili, ivyo alivuta begi lake dogo na kuanza kushuka ngazi za ndege ile taratibu, aliweka miwani yake ya macho sawa sawa kana kwamba anataka kuangalia kitu,Jinsi alivyokua akishuka ngazi alionekana dhahiri kua amechoka sana, aliweka mkono shingoni na kuiweka kola yake nyeupe ya kichungaji iliyopita kama mstari mpana shingoni.
Kama kawaida alipitia mlango maalumu ambao hauna usumbufu wala ukaguzi wa aina yoyote ile,.mara nyingi milango hio hupita watu wakubwa pamoja na maraisi mbali mbali., Hakuamini alicho kiona mbele yake, lilikuwa ni jopo la watu wakimsubiri wakiwemo waumini wake na waandishi wa habari pia, walivyo muona wote walianza kuimba na kusifu kwa nyimbo za kuabidu na kufanya kelele nyingi eneo hilo.
"Bwana YESU asifiwe mtumishi"
"Amen,Mtumishi Hakika bwana amefanya miujiza, namshukuru bwana wa Majeshi Jehova, nilipo toka huko mpka hapa nili fika salama, sifa apewe Mungu",
Alikua akiongea na mmoja wa waumini katika kanisa lake, pcha za mnato zilipigwa nyingi nyingi na waandishi wa habari kutoka makampuni mbali mbali,Umaarufu wa mchungaji.ANDREW KONDE ulitokana na roho yake nzuri ya kujitolea na kuwapa watoto yatima misaada mbali mbali ivyo ili mfanya apate umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.
Waliingia ndani ya magari huku wakiimba nyimbo za kusifu na kuabudu. Mpaka walipo mfikisha kwake na waumini kuondoka baada ya kusali na kumuomba Mungu.,
" Hallo....Mbuya nimesha fika, nina kete sabini za COCCAINE na HERROINE"
_"sasa nita kupata vipi mchungaji Andrew"?
"Fanya kama siku ile mtume kijana aje sasa hivi, na aje na cash, bei ile ile, sitaki huu mzigo ulale hapa nyumbani"
Upande wa pili uliojificha nyuma ya pazia mchungaji Andrew Konde alikua ni muuzaji maarufu wa madawa ya kulevya akiyatoa ISRAEL, na kuya leta TANZANIA, hakuna muumini yoyote aliyeweza kujua siri hiyo , alitumia mgongo huo kwa kujifanya ana fanya kazi ya Mungu ili iwe rahisi kwake kusafirisha madawa hayo haramu.
"Alafu Mbuya, nisikilize kwa Makini,naomba uwe makini sana,"
" wewe sio wa kuniambia maneno hayo, mimi ni zaidi ya mtu makini, hii kazi nilianza kufanya tangu nipo sekondari".
Baada ya maongezi yao kuisha Mch. Andrew alikata simu, na kufungua begi lake lililojaa biblia na vitabu vya nyimbo na kutoa madawa hayo ya kulevya yaliyokuwa yame pakiwa vizuri, Kwa mtu yoyote angeona vile asingedhani kama kuna madawa, ki ukweli kulikua hakuna biblia wala vitabu vya nyimbo, ndani mulikua na madawa hayo haramu, njia hiyo hutumia mara nyingi bila kugundulika sehemu yoyote ile.,
***** *************************
"Tiiiii tiiiiiii tiiiiiiiiii"
Mashine ya hewa iyo aina ya OXYGEN ilitoa mlio mithili ya bomu lililotegwa ambalo muda mfupi lingeenda kulipuka, mtu aliyelala kitandani hapo alionekana kuwa haelewi lolote lina loendelea chini ya jua, ki ufupi alikua nusu MFU,.Macho ya Alfred yalikua yamefumbwa kama mtu aliye kufa tangu alale kwenye kitanda hiko hakuonyesha dalili yoyote ya kuamka ila alikua hai.
Mujuni tayari alikua nje ya hospitali hiyo akiongea na Dr, SHAMIRU, na kutaka kujua wana fanyaje ili kutoa uhai wa Alfred Mulawa ambaye kipindi hiko alikua yupo maututi baada ya kutolewa kwenye chumba cha upasuaji.
"Tume mshona tayari, sasa hapa kuna tatizo, ripoti nitaandikaje kuhusu huyu mgonjwa, ita nibidi niandike ripoti, alikufa vipi"
"Hapa pesa ina ongea,utaandika kifo cha ghafla, kwani kuna ndugu yake yoyote aliye fika?"
"Ndio, kuna dada mmoja aliji tambulisha anaitwa Jaqlin Ny...ange, kitu kama hiko, sema hakijaaribika kitu kile, nitajua cha kufanya, nipe cash yangu ili kiki nuka niondoke kabisa"
" hahahahaha hapo umeongea sasa".
Maongezi hayo yaliendelea na Dr, Shamiru kukubali kufanya kitendo kile cha kuua tena bila kupoteza muda, alienda maabara na kuchukua chupa ndogo ya sumu na sindano ndogo na kuweka ndani ya koti,
"Dr, Dr, kuna mgonjwa huku njoo haraka sana ana hali mbaya sana"
"Subiri kidogo nina kazi"
"Tafadhali njoo haraka". Alikua ni muuguzi wa kike akiongea haraka haraka huku akimvuta mkono, na kuacha shughuli aliyotaka kuifanya na kujikuta anaongozana na nesi yule.
Jaqlin Nyange alishuhudia Alfred akitingisha miguu kuashiria kwamba ana tafuta hewa kwa shida, na kufanya atingishe miguu kama kuku aliyechinjwa,
"Alfred Alfred,....Alfred, jamaaani naombeni msaada, wauguzi naombeni msaada tafadhali,".
Aliingia daktari wa kike kumpima mapigo ya moyo na kutingisha kichwa kana kwamba ana siki tika alimwangalia jaqlin NYANGE kwa huruma sana, huku akisikitika.
"Nini tena doctor,?,?" Jaqlin Nyange aliuliza swali hilo lililo lizidi kumchanganya daktari.



Daktari yule alitoka nje haraka haraka na kurudi na wenzake watatu, walivuta dawa kwenye kichupa kidogo na kumchoma kwenye mshipa wa damu wa mkononi na kumuwekea dripu nyingine,
huku mwingine akichomoa mashine ile ya hewa,
haraka haraka walibuluza kitanda kile chenye matairi huku wakipiga kelele kuomba njia kuashiria kwamba mgonjwa aliye lala juu ya machela ile ana hitaji matibabu ya haraka,kweli watu walipisha njia na kuipisha,
Jaqlin Nyange nayeye hakuwa mbali alikua akikimbia kana kwamba nayeye ni muuguzi, hakuelewa nini kinaendelea sababu hakupata nafasi ya kuuliza chochote.,
Machela ile ilifikishwa nje na kuingizwa ndani ya gari ya wagonjwa ambayo hutumika kuwawaisha wagonjwa waliozidiwa ma-hospitalini.,Jaqlin Alivyotaka kuingia walimzuia na kufunga mlango wa gari wa nyuma,kitendo kile kilimuuma sana.
"Pupupupupu",
Gari lile lili pigwa kwa nyuma na mmoja wa wauguzi ili kumuashiria dereva kuwa aaanze safari mara moja maana kila kitu kilienda sawa.
"Boda boda, wewe ndio njoo upesi upesi"
""Naam dada"
"Unaona hiyo gari ya wagonjwa, naomba uifatilie mpaka mwisho"
bila kuchelewa Jaqlin alipanda juu ya piki piki hiyo na piki piki kuanza kufuatilia gari hiyo ya wagonjwa ambamo ndani ya gari hilo alikua Alfred Mulawa.
Gari ya hiyo ilizidi kupiga king'ora na kufanya ukelele mkubwa utokee huku magari mengine yakipisha njia na kulipa gari hilo nafasi ya kutamba bara barani,
.kwa kasi ya ajabu gari hiyo ilizidi kusonga mbele huku dereva huyo akiwa makini na kibarua kile cha kuendesha gari,
kweli tayari waliimaliza Kibamba na sasa walikua Mbezi mwisho, huku nyuma boda boda ile kwa mbali ilifuata kama kawaida.
"Yule Mgonjwa aliye toka thieta jana , yule ....yule.... kijana, aliyeletwa usiku, Alfred yaah, Alfred yuko wapi"?
Swali hilo lilimtoka mdomoni Dr, Shamiru na kuoneka akiwa kama amechanganyikiwa,
"Muulize Dr, Luci Erick"

Haraka haraka bila kutaka kujua mengine aliingia ndani ya chumba kidogo ambacho mezani kulikua kuna kimbao kimeandikwa Dr, Luci Erick Hamisi, japokua alimkuta ana mgonjwa hakujali Dr, shamiru aliingia na tena bila kubisha hodi yoyote.
"Nini tena shamiru,?, huoni kama nina mgonjwa'"?
"Samahani, tunaweza kuongea kidogo"?
"Huoni kuna mtu hapa"
"Ndo maana nina kuomba samahani"
"Hapana sitoweza subiri kwanza nimesema"
"Haya maongezi ni muhimu kuliko unavyodhani"
"Na huyu unaye muona hapa ni muhimu sana kwangu, maana bila huyu nisinge kua hapa, huyu ndo anaenifanya nilipwe mshahara kwaio naomba usubiri nje Dr, Shamiru, tafadhali"
Ki ukweli Dr, Luci Erick alikerwa sana na kitendo kile ivyo alijikuta ana mkatalia kata kata tena akiwa kweli anamaanisha , kweli alitoka na kuwaacha.
"Samahani sana, niwie radhi, ulikua unasema wakati mwingine una pata shida kupumua, sasa huo Ugonjwa unaitwa CALLAPYN RYPHA,kama nilivyo kueleza hapo awali, husabaishwa na mafuta mengi mwilini na kufanya mirija ya VEIN kushindwa kupeleka damu kwenye moyo, ugonjwa huu una tibika, ila uki fuata nita kayo kwambia"
Dr, Luci Erick Hamisi akiwa makini kabisa na miwani yake iliyo mkaa sawa sawia alionekana akiandika kitu kwenye karatasi akiwa ndani ya chumba kile na mgonjwa.
**************************
" para panda ita lia parapanda...ooooh para panda, parapanda ita lia para panda, wata kua wame kwisha nyakuliwa kwenda kumlaki bwana YESU mawinguni"
Zilikua ni sauti za akina mama wakiimbia ndani ya costa lililo jaa watu wengi na huku nyuma gari dogo maalumu ya kubebea maiti lilifuatia huku ndani yake mlikua na jeneza jeupe lenye msalaba juu na picha,kuashiria kuwa kuna mtu amekufa ivyo wana peleka maiti ile sehemu husika katika bara bara inayo elekea Gongo la mboto,
huku nyuma pia kulikua na vigari viwili vidogo alimaarufu kama VIKIRIKUU kutokana na udogo wa vigari ivyo watu huzoea kuviita ivyo, watu walikua wamejaa wengi na kufanya vigari ivyo vibonyee chini, kilikua ni kilio kikubwa sana,Kwa haraka haraka ilionyesha kuwa aliye kufa ni mtu mwenye hadhi kidogo aliye fahamika,Wakina mama walizidi kulia kwa sauti kubwa sana na kufanya hata wengine kulia, si ivyo hata wale waliokua pembeni walikua wakishanga waliingiwa na huruma.
Waliimba nyimbo nyingi tofauti tofauti, kama wanavyoimba kwenye misiba mingine, Msululu ule wa magari uliongozana mpaka kufika UKONGA na costa hilo kuegeshwa nje ya nyumba kubwa ya kifahari sana, na watu kuanza kushuka,
Kelele zilizidi kuongezeka baada ya jeneza lile kushushwa ndani ya gari lile maalumu.
"Uwiiiii uwiiiiiii Mungu weee, kwanini ume mchukua, Mungu weeeee"
Mama mmoja alipiga ukelele sana na kufanya wenzake wamshike na kumbembeleza ila hakunyamaza.
Watu waliingia ndani ya geti lile na kuonekana kushangazwa sana na ukubwa wa nyumba ile ya kifahari ambayo ilikua na uwazi mkubwa sana, waliingia ndani ya geti na jeneza lile kuingizwa ndani.
"Safi sana, sasa fanya utaratibu watu hao waondoke,"
."NO subiri mpka jioni"
"Sio mbaya, bosi anataka mzigo wake jioni," yalikua ni maongezi ya watu wawili wakiwa ndani ambamo kuliifadhiwa jeneza lile jeupe huku msalaba ukiwa juu yake.,

Ki ukweli haukuwa msiba, bali ulikua ni msiba bandia ambao ilikua ni njama ya kupitisha madawa ya kulevya.
Huo ulikua mtandao wa MUJUNI ambaye alifanya vile ili isiwe rahisi kugundulika, nyumba hiyo aliinunua kwa ajili ya kazi hiyo tu, madawa ya kulevya kutokea nchi mbalimbali huku akiwa kodisha watu wa kulia ili kuweka uwalisia, kila kitu alifanya kwa mipango na kuwachukua madaktari huku akiwalipa pesa nzuri ambayo iliwafanya wakae kimnya.
Madaktari wawili waliingia ndani ya chumba hiko kidogo na kuchukua maiti ile ambayo ndani ya mwili huo kulikua kume pakiwa madawa haramu ya kulevya, sio ivyo tu hata nje ya jeneza hilo,
haraka haraka mwana mke yule alipasuliwa tumboni kwa umakini wa hali ya juu ndani chumba maalumu chenye kila aina ya madawa,na madawa hayo kutolewa tumboni na baadae walimshona na kumrudishia kama kawaida, ivyo ndivyo ilivyo kua.
******************************
"Ng'aaaa ng'aaa"
Ilikua ni sauti ya mtoto mchanga aliye kua amebebwa na Hanna Mulawa akiwa mwenye furaha sana huku akimwangalia Alfred machoni
"Alfred hongera",
Ila baadae mtoto yule anadondoka chini ghafla.

"Ha......nna." kwa mbali sana Alfred alitoa sauti baada ya kushtuka kutoka kitandani alipokua amelazwa siku saba bila kushtuka,
alifumbua macho na kumuona mtu aliye valia koti jeupe na kifaha cha kupimia mapigo ya moyo kukiweka shingoni huyu alijua moja kwa moja ni daktari, alivyo angalia pembeni aliweza kumtambua mwana mke aliye kaa pembeni yake Jaqlin Nyange ambaye muda huo alionyesha kutabasamu kwa furaha.,
alivyogeuza shingo upande wa chini alimuona mwanaume aliyejazia mkono mwenye kifua kipana kidogo, alivyo taka kuongea kitu alihisi maeneo mbavu kuumia na kuka kimnya.
" Taratibu, taratibu Alfred,"
daktari yule alimtuliza kwa upole na kumfanya Alfred azidi kumwangalia mwanaume yule.
Hali ya Alfred kila siku zilipozidi kwenda ndipo ilizidi kua nzuri na sasa hivi alinza kuongea vizuri ila kwenye kutembea ilikua shida kidogo, hali hiyo ana ikataa katakata na kuanza kufanya mazoezi,ya kutembea.
"Martin Phares, na Jaqlin nawashukuru sana kwa kuwa karibu na mimi mpka leo naruhusiwa sina cha kuwapa zaidi zaidi Mungu siku moja ata walipa"
Aliongea Alfred siku iyo aliyoruhusiwa huku akipewa dawa ambazo zinge msaidia,
Jambo la kwanza alilowaza ni mke wake Hana ambaye muda huo mfupi alitoka kumuota na kutojua ndoto ile ina mana gani,
"Pole kwa yaliyo kukuta ndugu yangu, kwa hili nita kua nawewe bega kwa bega mpaka shemeji tumpate" aliongea Martin Phares huku akimpiga piga bega Alfred, . Safari ya kurudi nyumbani kwake ilianza na kichwani alikua na jambo moja tu usiku wa siku hiyo, arudi lile eneo la msitu alipookotwa,
Kweli usiku uli fika na sa yake aliyo itegesha ili mshtua na kuanza kuvaa nguo zake haraka haraka
Alivaa haraka haraka na kutoka kimnya
"Alfred unaenda wapi?" Sauti iyo ilimstua Alfred na kusimama..


Alibaki akimwangalia Martin Phares ambae wakati huo alishika kikombe chenye maji alimkata jicho kali lile lililosema niachie niende, aligeuza shingo na kupiga hatua ila alishikwa mkono na Martin akimzuia, Bila kutegemea aliuvuta mkono wa Martin na kuuzungusha na kuukunja mkono ule na kumsogeza ukutani na kufanya ampe mgongo, ila Martin hakukubali kwa nguvu alijitoa pale na kumsukumiza Alfred ambae aliyumba kutokana na kutokujiaanda, yumba ile ili tulia baada ya kuweka mguu kwa kunywa juu ya kistuli na kumfanya akae sawa.
"Unaenda wapi usiku huu"?
Ilibidi aulize tena swali hilo ila Alfred aligeuka na kuuendea mlango,
Martin alimfuata nyuma na kumshika begani safari hii Alfred aligeuka na ngumi ila Martin aliiona na kuizuia akitumia mkono wake wa kulia, Alfred aligeuka na kumkunja shati na kumuweka ukutani na kumpiga kichwa puani kwa nguvu na kumpelekea Martin akasirike.
Alikunja ngumi na kimpiga shingoni, Pata shika lile na mikiki ilizidi na safari hii walishikana mashati kila mtu akijaribu kumshinda nguvu mwenzake mwishowe wakadondoka chini, Martin akiwa chini huku Alfred akiwa juu yake , alikunja ngumi na kumshushia ila ilipiga chini ya malu malu baada ya Martin kusogeza kichwa chake alivyoona ngumi hiyo, Alitupa mguu wake ambae ulifanya Alfred adondoke upande wa pili na wote kusimama, puru kushani zilizidi wakiwa kama majogoo, Alfred alimfata Martin na kumkunja ukutani tena, ila Martin hakukubali, alijitoa kwake na safari hii Alfred aliwekwa uku tani kutokana na nguvu na mkono mkubwa aliokua nao Martin ukichanganya na hali yake alishindwa kujitoa, Martin alikunja konde na kulitupa, ila ngumi iyo ililia ukutani kwa nguvu sana baada ya Alfred kusogea kidogo pembeni,
" Nyie mna matatizo gani?, mbona ivyo usiku huu?, mna kua kama WANGA, mna fanya nini sasa ? Embu acheni utoto"
Ili kua ni sauti ya Jaqlin Nyange akiwa na mwiko mkononi huku mkono mwingine akiwa ameshika kisu kidogo cha kukatia ugali, na wote waki baki kimwangalia huku wakiwa bado wame shikana,
"Embu muulize ndugu yako sasa hivi anaenda wapi usiku huu",
" mi nilidhani sijui kitu gani...kumbe nyie..Kwani vipi Alfred?"
Alfred alikaa kimnya kidogo na kuwaangalia wote wawili kwa umakini, na kuanza taratibu kuwaambia nia na lengo lake, aliongea kwa uchungu huku akijipiga piga kifuani.
"Alfred nisikilize mimi, huwezi kwenda ivyo peke yako,huwezi Alfred, cha kufanya subiri kukuche uwa shirikishe wenzako alafu na hali yako, waachie jeshi la polisi wafanye kazi yao, naamini wata mpata shemeji Hana"
"Hapana, ina niuma, we una jua huko alipo Hanna ana kula nini sasa hivi,?, hapana lazima niende hata nikifa sawa ila najua nilikua najaribu kuokoa maisha ya mke wangu, kuliko kukaa hivi, hapana sitoweza, kwa hilo mta nisamehe,"
" sikia bro Alfred, ina kubidi ushirikishe wenzako Martin yupo sawa, huwezi kwenda peke yako, una hatarisha maisha, hujui wame jipanga vipi hao watu" Alfred aliji kuta ana lainika na kusubiri mpka kukuche ila hakulala alibaki kwenye sofa huku akiwa ameweka mkono wake kwenye shavu yaani akishika tama.
***************************
"Wote kaeni kimnya nime sema kimnya na mlale chini. kama mkifuata hayo yote kila mmoja atatoka salama"
sauti hiyo ili tokea ndani ya benki ya NBC iliyopo posta mtaa wa samora, mtu aliye kua akiongea alikua ameziba sura yake na macho tu ndo yaliyokua yakionekana, mkononi alishika mtutu huku kiunoni aliweka bastola ndogo, kwenye mlango ivyo ivyo alikaa mwingine huyu alivalia nguo za kiaskari huku nje kibao kiliandikwa CLOSED, kuashiria bank iyo ime fungwa.,ili watu wa nje wasijue kina choendelea ndani ya BANK iyo. Kwa haraka haraka walikua takribani majambazi tisa ambo waliiiweka watu mateka huku wakipakua pesa na kuweka kwenye mabegi.
"Wewe mwana mke, wewe ndio, uliyevaa shati nyeusi njoo hapa"
mwana mke huyo aliinuka akiwa na hofu sana huku akitetemeka sana kwa hofu.
"Jina lako nani,?"
"Nani. ,.. mimi , mi..mi naitwa Aneth, naitwa Aneth Kasera, tafadhali usiniue usiniue,."
"Ingia humo ndani msaidie mwenzako kuweka izo ela, fanya upesi," haraka haraka mwana mke yule aliingia ndani mule na kuweka vibunda ivyo vya elfu kumi kumi ndani ya begi kubwa, baada ya kumaliza hapo walichukua yale mabegi na kila mmoja kuvaa na mengine kuyaweka mikononi, ki ukweli zili kua ela nyingi sana. Askari yule alianza kutoka ndani mule na kuingia ndani ya gari waliyo kuja nayo aina ya VIGO na kutimua mbio.
**************************
Deffender tatu ziliegeshwa mbali kidogo na nyumba kubwa iliyopo KIBAMBA na Alfred kushuka kwenye moja ya gari hilo huku akiwa na mwana mke mmoja aliyevalia suruali ya jinsi na tshirt, aliweka bastola vizuri huku wakiongozana na Alfred, Ila walipo fika ndani ya geti hilo Alfred alikaa chonjo ili liki funguliwa asiweze kuonekana.
"Ngongongo"
geti hilo kubwa lili gongwa na mtu kufungua, alionekana ni askari kutokana na UNIFORM alizovaa,
"Nikusaidie nini dada"?
"Niwa kuta wenyewe?"
"Wenyewe wakina nani?"
"Wenye nyumba"?
"We nani?"
"Mbona maswali mengi wewe, kama wapo niambie usinipotezee muda"
"Aaah wee vipi?, kama huwezi kusema jina lako nenda dada,"
askari yule alivyotaka kufunga mlango mwana mke yule aliingiza mguu na kuuzuia, askari yule kuona vile alitoa shingo nje hapo ndipo alipo kutana na mdomo wa bastola
"Tulia kimnya ivyo ivyo, fungua geti haraka sana,"
bila kipingamizi askari yule ali fungua geti na mwana mke yule kuingia akiwa na Alfred.
"Mujuni tume mkuta?" alihoji Alfredy.
"Mujuni ndo nani,?, mimi simjui,"
"Bosi wako"
" aah hapana siju....." Alfred alimpiga na kitako cha bunduki kichwani baada ya kuona hana faida kwao na Askari yule kudondoka chini na wao kuendelea kusonga mbele., walivyo fika kwenye mlango wa mbele kama kawaida Mwanamke yule aligonga mlango huku akiwa ameishika bastola yake vizuri.
" usipige kelele, kimnyaaa".
Baada ya mlango kufunguliwa sauti iyo ilitoka
"Mujuni yuko wapi?"
"Mujuni, tajiri , yupo njiani ana safiri leo".
"Anaenda wapi?"
"Kwa kweli sijui, Sijui,"
"Una mjua Hanna?" Alfred aliimgilia maongezi hayo
"Hapana simjui, ila aliondoka na mwana mke hapa, na anaondoka na ndege ya saa tano".
Haraka haraka Alfred alikimbia nje na huku akiangalia saa yake ya mkononi ambamo kwa hesabu za haraka haraka lili baki lisaa limoja, na kumfanya kuchanganyikiwa, aliingia ndani ya Deffender moja bila kuuliza aligeuza kwa kasi huku akitoa simu yake ya mkononi., hakua na uhakika kama angewahi kutokana na umbali
" hallooo, haloo, upo kazini, sikiliza Mwita, chukua gari hapo na askari wengine muende airpot haraka sana, ndio, sasa hivi, mimi nipo njiani, mkifika nambie"
aliongea Alfred haraka haraka na kuzidi kubadili gia huku akiongeza kasi........


.Taa za kijani ziliwaka maeneo ya ubungo mataa ikiashiria kuwa magari yanayoelekea MANDELA ROAD yaweze kuanza safari ndani ya gari hiyo ndogo aina ya PROGRESS ambamo ndani yake kiti cha nyuma alikaa MUJUNI huku pembeni yake akiwa amelala Hanna,, dereva alivuta gia mpaka kwenye herufi D na kukanyaga mafuta taratibu na mwishowe gari kuchanganya.
"We nani,... Chinga, embu punguza sauti ya redio , alafu jaribu kukanyaga mafuta tuwahi ndege sawa",
Dereva huyo alitii amri na kunyoosha mguu na kuzidisha gari ile kasi,
Hanna alifumbua macho yake na kuanza kupiga kelele ila alizibwa mdomo na kuchomwa tena sindano ya usingizi na kufanya alale tena na kutojua kina choendelea.
**************+*************
 *******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG