Search This Blog

Monday, March 23, 2020

ABEE SHEMEJI SEHEMU YA 7/10


ABEE SHEMEJI
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 7 KATI YA 10
*******

Kelele alizopiga Hajrath akiwa hospitali ziliwashtua wauguzi na wagonjwa waliokuwa kwenye benchi,hiyo ni kutokana na ndoto mbaya aliyoota kwamba Ahmed tayari amefariki dunia,akatizama wodi alilolazwa Ahmed akamuona daktari anatoka,akasimama na kumuendea kwa kasi.

“Vipi hali ya mgonjwa?”
“Bado anaendelea na matibabu,nisubiri pale”
“Kuna matumaini yoyote?”
Swali hilo lilimfanya dokta huyo,amuangalie Hajrath kwa umakini akavua miwani na kumtizama kwa masikitiko bila kumjibu kitu,kuna kitu alijifunza kutoka machoni mwa daktari kwamba hakukuwa na habari nzuri,hiyo ilimfanya aishiwe nguvu kabisa na miguu yake ikafa ganzi.
Sakata la Yusrath kuzaa na Bilionea George Charles, waandishi wa habari walilivalia njuga sababu kwao lilikuwa na maslai makubwa sana vyombo vya habari mbalimbali vilikuwepo nje ya hospitali hiyo wakitaka kuichimba habari hiyo!Haikueleweka ni nani kavujisha fununu kwamba Ahmed alilazwa hapo,lakini hilo halikuwapa shida walichokifanya madaktari ni kutoongea chochote hata walivyoulizwa juu ya tetesi hizo.
Kilichowashangaza zaidi waaandishi wa habari ni baada ya kuona maaskari wamefika hospitalini hapo,walivyotaka kupata za chini ya kapeti hawakufanikiwa kwani askari hao hawakua tayari kuzungumza kitu chochote mpaka usahahidi utakavyokamilika,moja kwa moja wakaingia hospitalini na kutaka kuonana na dokta anayemtibu Ahmed.
“Mgonjwa wako yupo chini ya ulinzi”
Halikuwa swali wala mahojiano,ilikuwa ni amri kumaanisha kwamba Ahmed awekwe chini ya ulinzi.Kufuatia kauli hiyo,dokta akasimama na kuwapeleka mpaka wodi alilolazwa Ahmed.Katika hali ya kushangaza mmoja wa maaskari akatoa pingu,akachukua mkono mmoja wa Ahmed na kuufunga pingu akiizungusha kwenye chuma cha kitanda,kumaanisha kwamba yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi,akiwa hivyo hivyo hajitambui kitandani.

*******
George Charles,aliingia nchini Tanzania Kimya kimya kutoka fungate, akiwa na mkewe Lissa Nzava kushoto kwake,ujio huo ulikuwa wa siri ndiyo maana hakutaka kumpigia dereva wake isipokuwa walinzi wake tu,ndio aliwatumia ujumbe kwamba anarejea siku hiyo, hivyo wasicheze mbali na eneo la uwanja wa ndege.Meseji hiyo alituma bila Lissa kujua,kuna mambo alitakiwa kumshirikisha mkewe lakini kwenye ajenda kama hiyo nzito aliapia kutomwambia mtu yoyote yule kwani katika maisha yake alijifunza kwamba usimuamini binadamu wa aina yoyote ile kwa asilimia mia moja, tena sanasana mwanamke.Alivyofika Mwalimu Nyerere na kutoa mizigo yake akamuona Bruno upande wa kushoto mmoja wa walinzi wake lakini hakutaka kumsalimia,akampotezea kama hamjui.Mbele kidogo akamuona Wiliams yupo makini hao wote walikuwa na bastola viunoni yaani miguu ya kuku na walikuwa makini mno.
Isingekuwa rahisi kugundua kama ni walinzi wa bilionea George Charles kwani walivaa kawaida yaani tshirt na Jeans,zaidi na hilo ndani ya uwanja huo kulikuwa na walinzi wengine kumi na mbili kila mtu amekaa kona yake.Alichokifanya George Charles ni kupitiliza mpaka kwenye texi.
“Nipeleke Masaki”
George Charles alimwambia mmoja wa dereva taxi.Huku mizigo yake,ikiwekwa vizuri kwenye buti.Lisa alionesha kukasirika mno!Jambo hilo lilimchukiza yaani kupanda taxi wakati walikuwa na magari kama utitiri yamepaki.
“What do you mean?”(Una maana gani)
Lissa akaanzisha ugomvi ndani ya taxi.
“What are you talking about?”(Unaongelea nini)
“Haaa!Nishajua,unaogopa waandishi wa habari ndio maana.Kisa yule kahaba wako”
Hapo George alibaki kimya kwani Lissa aligusa mshono,ki ukweli niya ya kupanda taxi ilikuwa ni kuwapiga chenga paparazi ndiyo maana akavaa miwani na kofia kubwa.Hiyo ilimfanya dereva taxi aweke kioo vizuri cha katikati ili awaone abiria wake.
“Lissa,sio mahala pake hapa”
“Ndio,naelewa.Unataka kumtetea kahaba mwenzio!Nambie kilichokufanya uvae huo mkofia na miwani kama jambazi”
“Please....”
Lissa akazidi kubwata,ilielekea bado alikuwa nalo moyoni ndiyo maana akatoa povu sio la kawaida.Akapanga siku moja akaonane na Yusrath macho kwa macho ili ampe vidonge vyake licha na hiyo alitaka apate uhakika kama ni kweli alizaa na George Charles,safari ikaendelea kukiwa na kelele ndani ya gari mpaka walivyofika Masaki,gari likaingia ndani, hapo ndipo dereva wa texi akagundua amempakia Bilionea George kwani jumba hilo lilimshtua mno!
“Kama peponi.Haki ya Mungu mimi nikipata jumba kama hili, walai sitoki nje,sasa nitoke nje kufanya nini?Kuna watu wanaishi bwana,jumba lote hili?Yaani ukikaa humu naamini huwezi kusikia njaa”
Dereva texi alijiongelesha mwenyewe baada ya kurudi ndani ya texi,akapewa dolla mia na kuondoka zake,lakini alivyotoka nje akapishana na gari nyingine mbili,akaziangalia vizuri na kugundua ni lazima wangekuwa wageni wa bilionea huyo sababu gari hizo zilimfuatilia tangu yupo uwanja wa ndege, bila kujua gari hizo zimepakia walinzi wa George Charles!

****
Siku zote damu ni nzito kuliko maji,swala hilo hakutaka kuliachia hivihivi alichokifanya ni kitu kimoja tu kulivyokucha.Baada ya kwenda ofisini akanyoosha mpaka Ilala,alipokuwa anaishi Yusrath huko alitaka kujua nini kinaendelea na alipenda zaidi aelekezwe anapoishi Yusrath, amwambie ukweli kuhusu habari za chini ya kapeti kuhusu watoto mapacha,alivyogonga mlango alikaribishwa na mlinzi.Akapita mpaka ndani, ambapo huko alimkuta Baba mzazi wa Yusrath,mzee Suleiman amevalia msuli, ameshika gazeti pembeni ana kikombe cha kahawa.
“Karibu kijana”
“Ahsante mzee wangu,shikamoo”
George Charles,akaamkia kwa adabu zote kisha kuketi.
“Sura yako,sio ngeni sana.Hivi tulionana wapi tena?”
Kumbukumbu za mzee zikawa zinaingia na kupotea kama saa mbovu!
“Nilishawahi kufika hapa,hata hivyo nilikuwa bosi wa Yusrath pale Posta”
“Anhaaa,basi nimekukumbuka uzee huu.Wewe ndiye George Charles?”
“Ndio mimi”
Mzee akamtizama kwa umakini,akapiga jicho mezani ambapo kulikuwa na gazeti lenye picha yake kwa juu.
“Umefanya vizuri kuja”
“Ahsante”
“Nachokuomba naomba uwe na busara,nina amini wewe ni msomi.Sitaki tupindishe mambo,wewe ni mwanaume mwenzangu.Japokuwa nimekuzidi umri”
Mzee akavuta fundo la kahawa na kurudisha kikombe mezani.Mbali na hapo kuna kitu George alijifunza kwamba Mzee huyo ana busara sana!
“Niliona gazeti,wanasema kwamba wale ni watoto wako.Je,ni kweli?Au porojo tu za waandishi?”
Hapo George Charles,akatulia kidogo na kutafakari akaanza kujibu hoja moja baada ya nyingine na mwisho akahitimisha akisema wataenda kupima DNA lakini alichotaka kujua kwa wakati huo ni wapi Yusrath alipo,hilo halikuwa tatizo Mzee akasema.Na kilichofuata hapo hapo,George Charles kuanza safari ya kwenda Muhimbili.
Akiwa katikati ya safari simu yake ikaita alivyoangalia, akaona jina Bruno mmoja wa walinzi wake,akaipokea na kuiweka sikioni.
“Bruno,nambie”
“Bosi,tumeanza safari nawewe tokea kwako.Lakini kuna gari linakufuata kwa nyuma”
“Linanifuata mimi?”
George Charles baada ya kusikia hivyo,akageuza shingo nyuma.
“Ndio boss,ulivyofika Ilala.Gari hilo likasimama naona sasa hivi limeanza tena,lakini usijali bosi tupo nalo sambamba”
“Okay”
Kuanzia hapo akawa makini sana kuangalia nyuma lakini hakuweza kuliona gari lolote lile hata hivyo alijua yupo salama.
Akanyoosha mpaka Muhimbili, ambapo huko alishuka na kupita mpaka ndani.Alivyofika tu,madaktari waliomfahamu wakamshangaa lakini hakuwa ana habari nao,alichotaka yeye ni kumuona Yusrath.Hilo halikuwa tatizo,akaoneshwa wodi alilolazwa,akaona kitanda kilichokuwa pembeni kabisa kushoto,akakisogelea mpaka karibu.Akamuona Yusrath amelala,kuna vitu alianza kuvikumbuka.Sio siri akaamini bado anampenda Yusrath kwani uzuri wa msichana huyo ulikuwa upo palepale,taratibu akaanza kumshika akimpapasa nywele,hiyo ilimfanya Yusrath afumbue macho yake taratibu.
“Yusrath…”
George akaita,hiyo ilimfanya Yusrath ayalazimishe macho yake kuona,hakuwa ana uhakika kama yupo ndotoni ama ni kweli kwani mwanamme aliyesimama mbele yake alimshtua.
“Georgee…”
“Yes…Unaendeleaje?”
“Kichwa kinaniuma saaana”
“Pole”
George akatoa pole huku akimshika Yusrath mkono.
“Ala..”
“Paaa paaa paaaa paaaaaa paaaaaa”
Sauti ya mtu akipiga makofi,iliwashtua sana wote wakageuka.Moyo wa George ukalipuka kwa nguvu, hakutegemea kumuona Mkewe Lissa mahali hapo!Mbaya zaidi alikuwa akiwapigia makofi.
“Kahabaa wewe,nilijua tu Mme wa mtu unakuwa malaya namna hiyo,nilikufatilia tangu unavyotoka nyumbani.Si ungeniambia unakuja kumuona Malaya wako mbwa…Nawewe mwanamkee,hii dunia utaiona chungu,nakuhakikishia hilo…”
Lissa Nzava aliongea kwa hasira bila breki,alijiamini sababu alikuwa ana kila sababu ya kufanya hivyo kwani alikuwa tayari mke halali wa ndoa!



Moto aliouwasha Lissa Nzava hospitalini hapo haukuwa wa kitoto,mbaya zaidi alitoa maneno machafu, akichanganya kiingereza,kichina na kirusi humohumo.George Charles alivyoingilia akitaka atulie nayeye alijumuishwa na kuogeshwa mvua ya matusi, akiambiwa ni Malaya mbwa.Yusrath akahisi kupona ghafla akatia neno, hapo ndipo kama Lissa alifunguliwa Koki akapandisha mori,Yusrath akatukanwa na kunyambuliwa vibaya sana akachambwa na kuogeshwa matusi ya nguoni.Isingekuwa madaktari kutokea na kumtoa nje, siku hiyo pasingetosha!
“George please,naomba uende”
Yusrath akasema kwa sauti ya mbali,alijisikia vibaya baada ya kutukanwa akiitwa kahaba wa jiji.Jambo hilo lilimfanya George atulie kidogo na kuomba radhi kwa kila kilichotokea, hakutaka kubaki tena wodini,alikasirika na kutoka nje.Ambapo huko akampita Lissa, bila kumuongelesha!
“George,unaenda wapi?”
Lissa akauliza huku akimfuata kwa nyuma.
“Ofisini”
“Sasa hivi ndio unaenda ofisini, sio?”
Kufuatia hapo, George hakujibu kitu chochote kile,akaingia ndani ya gari lake na kuanza safari ya kuelekea posta,alivyofika huko hakufanya kazi kabisa.Zaidi na hilo akawaambia wafanyakazi wake mtu yoyote akiingia kumuulizia waseme hayupo.
“Just waambie sipo.Mwambie Juma gari langu alitoe kule mbele,alipaki huku nyuma”
“Sawa bosi”
Sekretari aliitikia kwa adabu zote na kutoka nje ya ofisi,ilikuwa ni lazima alifiche gari lake ili kuwaaminisha watu kwamba ni kweli hayupo ofisini.Kuanzia hapo alijikita kwenye mawazo makubwa sana,hakuelewa ni kitu gani akifanye lakini alichokuwa anakitaka yeye ni kitu kimoja tu.
Wakapime DNA ili ajulikane kama kweli watoto ni wake,hilo lilikuwa mbioni kufanyika kwani alipanga siku moja azungumze na Yusrath.

*****
Ahmed Kajeme,alizinduka kitandani baada ya masaa 120 kupita,kumaanisha kwamba alilala kitandani siku tano, bila fahamu zake.Huo pia ukawa kama muujiza mwingine kutokea,kutokana na taaluma za wauguzi hao na majibu yaliyotoka vilikuwa ni vitu viwili tofauti, hapo ndipo wakaamini kwamba jaji wa Mwisho katika maisha ya binadamu ni Mungu peke yake na sio madaktari.Kila dokta alidhani wenda Ahmed angepalalaizi ama kupoteza maisha kabisa lakini vyote hivyo havikutokea kabisa.
Hilo likazidi kuwafanya wastaajabu zaidi ukuu wa Mungu na miujiza yake.Mbele yake,aliwaona watu watatu mmoja mwanamme.Huyo alimtambua alikuwa ni Benjamin Ngowi,kushoto kwake akiwa na Mama yake mzazi pembeni yupo Kassim.Wote walionesha kumshangaa yeye,alivyojaribu kujivuta ikashindikana baada ya kuhisi mkono wake umefungwa alivyotupa macho kwenye mkono akaona pingu.
“Usijali Ahmed”
Kabla ya kuuliza swali Benjamin Ngowi,akamtuliza na kumfariji akimwambia kila kitu kipo sawa, hivyo atulie na apunguze ‘stress’hawakutaka kumwambia moja kwa moja kwamba ana kesi ya kujibu baada ya hapo ingawa kwa harakaharaka alilijua hilo, sababu kumbukumbu zake zilirudi akakumbuka mara ya mwisho,alivyokuwa anampiga Yusrath.
“Nipo chini ya ulinzi?!”
Haikujulikana kama lilikuwa ni swali ama anajisemesha mwenyewe ingawa baada ya hapo alishusha pumzi ndefu ya kuchoka,taswira ya milango ya gereza kufunguka nayeye kutupwa jela ilianza kujijenga kichwani,sura ya Yusrath ikamjia ghafla, hakuwa ana uhakika kama yupo hai ama tayari amefariki,akauliza.
“Yusrath yuko wapi?Anaendeleaje?”
“Anaendelea vizuri”
Ahmed hakuweza kuuliza maswali mengine zaidi,dokta alivyofika akaendelea na taratibu zingine hiyo ilimaanisha Ngowi,Mama pamoja na Kassim wakasubiri nje.
Hapo ndipo Benjamin Ngowi,akapata mwanya wa kumfuata kachero mmoja wa jeshi la polisi na kuanza kumzoea,niya yake ikiwa ni kumdadisi ili alegeze makali ya kesi na ikiwezekana, wayamalize kifamilia.
“Hii kesi ni kubwa kijana,kwahiyo hakuna cha mazungumzo hapa”
“Sote tunajua hilo,jamaa bado ni mgonjwa.Linazungumzika hili swala Mkuu, hakuna linaloshindikana”
“Litazungumzika mahakamani”
“Tusifike huko sasa”
“Kwanini tusifike?Yaani huyu kwanza anakesi vilevile ustawi wa jamii huko”
Somo lilikuwa gumu kumuingia kamanda huyo wa Jeshi la Polisi, ambaye alionekana ni mnoko,alichachamaa sio kidogo akidai kwamba yupo kazini na anatekeleza maagizo aliyopewa na mkuu wake wa kazi,vinginevyo hakukuwa na maongezi mengine zaidi,hilo lilikuwa wazi kwamba ni lazima Ahmed Kajeme atupwe gerezani.
Maongezi hayo,yalimfikia Hajrath Mpilla aliyekuwa pembeni kidogo, ilibidi nayeye asogee kusalimia,sura ya Benjamin Ngowi haikuwa ngeni kwake na alimkumbuka sana ni wapi walikutana lakini hakutaka kulikumbushia hilo akielewa ni lazima angehojiwa maswali juu ya Dokta Sajjo.
“Sura yako,sio ngeni wewe dada.Tulionana wapi vile?”
Swali hilo lilimfanya Hajrath Mpilla,apate jibu la harakaharaka.
“Hapana,hatukuwahi kuonana.Duniani wawili wawili”
“Ama kweli”
“Mgonjwa anaendeleaje?”
Lilikuwa ni swali,lililomlenga Ngowi.Hakuwa na jinsi zaidi ya kueleza kile anachokifahamau na mwisho wa maongezi akahitimsha Ahmed yupo chini ya ulinzi.Hakukuwa na maswali mengi ya kuuliza wala siri, kila kitu kilikuwa wazi kwamba kipigo cha Yusrath kilisababishwa na gazeti lililoanika skendo ya kuzaa na Bilionea George Charles!
“Hakuna mwenye uhakika,mpaka sasa hivi kama ni kweli Watoto wa George au wa Ahmed”
“Kwanini,wasipime DNA?”
“Ndio nataka kumshauri Ahmed lakini ana hasira,what if akikuta watoto sio wake kweli,ataua”
“Hilo nalo zito sana”
“He is my friend,lakini ana hasira chafu.Alafu mbaya zaidi anaweka vitu moyoni,ana visasi.Hii vita haitoisha mpaka anaingia kaburini”
Benjamin na Hajrath wakawa marafiki,wakajaribu kumjadili Ahmed pembeni namna ya kumsaidia.Wakasogea kando kidogo ili watete!
“Mimi nitaongea naye”
Hajrath Mpilla,akazungumza kwa kujiamini.
“Utaongea naye?”
“Yes,nitajaribu kuzungumza naye.Niachie mimi yataisha”
Kitendo cha ujasiri huo kilimfanya Benjamin Ngowi,atake kuuliza swali lakini akapiga kimya!Haukuwa mzaha,Hajrath alinuwia akachomoka na kutembea mpaka mlangoni wodini,alipolazwa Ahmed akisubiri madaktari watoke yeye aingie.Hilo likafanyika, akaomba ruksa na kuzungumza na mgonjwa kwa dakika moja ama mbili.
Kwa mara ya kwanza ilikuwa ngumu lakini Hajrath aliwasihi sana akidai kwamba atasafiri, hivyo angependa kuzungumza na mgonjwa.
“Dakika mbili tunakupa lakini kapumzika”
“Nakuomba dokta”
“Ingia,dakika tatu tu.Mbili zinakutosha”
Hajrath hakujibu,badala yake aliusukuma mlango na kuzama ndani, ambapo huko alinyoosha moja kwa moja mpaka kitandani,akamuona Ahmed amefumba macho!Amelala,alichokifanya ni kumsogelea karibu na kumbusu kwenye paji la uso!
“Ahmed, I love you.Bado nakupenda naamini bado tuna safari ndefu.I won’t give up.Die or ride”
Hajrath alijiongelesha mwenyewe,akainama tena kidogo na kumpiga busu lingine la mdomnoni Ahmed.

****
“Umesema yule demu naye,tumuue?”
“Hapana,mwacheni.Watoto ndio nina shida nao”
“Wapo wangapi?”
“Wawili, mapacha”
“Wanaishi wapi?”
“Kuna sehemu mbili,kama sio Ubungo Kibangu.Ilala mtaa wa Shauri Moyo”
“Tukuletee ama tuwauwe hukohuko?”
“Haina haja ya kuniletea sina shida nao,wauwe hukohuko”
“Lini?”
“Leo,kabla jua halijazama”
“Milioni tatu”
“Jambo dogo hilo, hiyo ni kama pesa ya maji kwangu,Minja hajawaambia mimi ni nani?”
“Hiyo haijalishi,tunachotaka ni mzigo”
“Nitawaongezea kama kazi ikienda sawa,nina milioni moja ndani ya gari.Jioni,nitawatumia nyingine”
Ndani ya chumba kidogo,chenye kitanda na stuli tatu, kulikuwa kuna kikao kidogo lakini kizito.Mambo yaliyokuwa yanajadiliwa yaliogopesha.Pembeni kushoto alisimama Minja,kandokando aliketi jamaa anayefahamika kwa jina la Jaquar,mwembamba mrefu na muda wote alikuwa siriazi, sana!Huyo ndiye alikuwa anazungumza na Lissa Nzava!Kitendo cha George Charles kwenda kumuona Yusrath hospitalini kilimuuma, ndiyo maana akaamua kwenda kushtaki kwa Minja,ambaye alimuhakikishia ana vijana wa kazi,hilo likawa rahisi wakaenda mpaka Tegeta huko Bunju karibu! Pembezoni mwa Hospitali ya St.Joseph,Lissa aliamini kwamba watoto, ndiyo wanafanya George awehuke.Moyo wake,ukabadilika kabisa,akataka kuuwa mapema hata kabla ya DNA kufanyika.Kilikuwa ni kijumba kidogo kinachonuka moshi wa Bangi na nje kwenye benchi, kulikuwa na vijana wengine wanasokota karatasi za lisla na kunyonga majani hayo ya bangi.
Akaelewa kwamba hapo lazima kutakuwa na pusha,anayefanya biashara hiyo haramu!Alichokifanya Lissa ni kurudi ndani ya gari.
Chini ya kiti cha dereva alikuwa na shilingi milioni saba na nusu,mwanamke huyu aliijua pesa kama mchaga, hakutaka kuropoka kwamba ana pesa yote kwenye gari.Alichokifanya ni kuhesabu kwa haraka,zilivyotimia milioni moja akachomoa na kuziweka kwenye bahasha,zilizobaki akazificha chini ya kiti.Akafunga mlango wa gari na kurudi ndani.
“Hizi hapa,milioni moja.Ndizo nilikuwa nazo kwenye gari,the rest!Nitawatumia”
“Utampa Minja”
Jaquar,alisema na kupuliza moshi wa sigara ya bangi hewani.Moyo wa Lissa ukawa mweupe,kabisa.Salio lililobaki lilikuwa ni milioni moja nyingine kisha baada ya kazi amalizie nyingine,kila kitu kilivyoenda sawa akaingia ndani ya gari hilo la kifahari, BMW X5 na kuondoka zake!

*****
Saa 12;47 jioni,Noah yenye rangi ya silver ilikuwa nje nyumbani kwa Ahmed.Ndani ya gari kulikuwa na wanaume wanne na msichana mmoja mdogo wa makamo.Wakiwa makini kuliangalia geti la Ahmed kama kuna mtu yoyote angetoka, ilikuwa ni lazima kwanza wahakikishe kama watoto hao wapo kwa Ahmed ama Ilala kwa wazazi wa Yusrath.Hapo walikaa nusu saa lizima,wakiwa makini kabisa.
“Aggy,nenda kagonge”
Kauli hiyo ilitoka kwa Jaquar,Msichana Aggy akavuta mlango na kutoka nje!Alishaelewa ni kitu gani anatakiwa kukifanya,ndiyo maana hakuhoji kitu kingine zaidi na kwenda na kugonga geti.Akagonga,tena na tena.Dakika tatu baadaye likafunguliwa!
“Dada mambo”
Agness akasalimia.
“Salama”
“Mimi naitwa Mona,rafiki yake na Yusrath.Nimetokea hospitalini,nimeagizwa kuja kuwaangalia watoto wanaendeleaje!”
Sentensi hiyo ikamfanya Hadima,amuangalie Agness kwa umakini zaidi, kuna kitu alianza kuhisi lakini hakuwa ana uhakika nacho!
“Ameniambia nije hapa,au Ilala.Nakuwa kama nabahatisha wapo hapa au Ilala?”
“Mbona wapo Ilala tangu muda mrefu,wazima. Ndio nimetoka huko muda sio mrefu.Hapa nimekuja kuwachukulia nguo zao”
“Ooooh,basi ahsante”
Kufuatia jibu hilo Agness akatembea na kurudi ndani ya gari,akawapa taarifa wakina Jaquar.
Hapohapo gari likageuzwa na kuanza safari ya kuelekea Ilala, ambapo njia nzima Minja ndiye alikuwa akielekeza msafara.Haikuwachukua muda mrefu,wakawa wamewasili Mtaa wa Shauri moyo!Wakaweka gari kando!
“Utatutumia meseji”
Agnes akapewa maagizo baada ya kufungua mlango wa Noah.
“Poa”
Alivyoshuka,akagonga geti.Likafunguliwa akakaribishwa ndani.
“Ng’aaa ng’aaaa ng’aaaaa”
Kitendo cha kuukaribia mlango,akasikia sauti ya mtoto mchanga analia.Akapata uhakika ni lazima watakuwepo,hakuwa ana sababu ya kuingia ndani, hapohapo akatuma ujumbe mfupi ‘Njoeni tumalize,wapo’
Ujumbe huo ulimfikia Jaquar,akatoa bastola yake na kuiweka kiunoni tayari kwa kuingia ndani ili akafanye mauaji.



Faad na Faisal walikuwa katika hatari kubwa ya kuuwawa,tayari watu wenye roho mbaya walipewa fungu la pesa ili wafanye kazi hiyo ya kinyama bila kujali kwamba watoto hao walikuwa ni wadogo na malaika wa Mungu,hilo kwao hawakujali kwani pesa ilikuwa mbele kuliko utu.Nyuma ya kila kitu kulikuwa na mkandarasi wa mpango huo mwanamke Lissa Nzava,hakutaka kuwaona watoto hao wakiwa hai akiamini kwamba mbele wangemuwekea kiwingu na ndoa yake ingetingishika!
Roho hiyo hakuelewa aliitoa wapi,hata yeye alivyojiuliza akashindwa kupata jibu kamili,haikuwa roho ya kawaida.Akiwa ndani ya jumba lake alizungukazunguka mara nyingi huku na kule,akisikilizia majibu kutoka kwa watu wake aliowatuma.Siku hiyo hakwenda kazini,alitaka kuhakikisha kwanza kazi yake inanyooka ndiyo roho yake ingekuwa nyeupe kabisa.Aliwaamini vijana wake,hakuwa mwenye wasiwasi hata kidogo!Ndiyo maana akawapa ramani namna watakavyowapata watoto hao mapacha,wakipitia Ilala ama Kibangu.
Timu nzima ya Jaquar ilikuwa imekamilika na walifanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana,ndiyo maana wakaanza Kibangu nyumbani kwa Ahmed,ambapo hapo walikutana na Hadima bila kuelewa kwamba msichana huyo alikuwa makini kuliko wanavyodhani wao.
Baada ya Agness kuondoka na kuingia ndani ya Noah,machale yakamcheza.Hiyo ni kutokana na kuunga unga matukio,kila alipojaribu kumjulisha na kutoa.Haikumuingia akilini,haikuwezekana hata kidogo Yusrath awaulizie watoto wakati alikuwa nao hospitalini muda mfupi uliopita.Hakutaka kulifumbia macho swala hilo,hapohapo akapiga simu hospitalini ambayo ilipokelewa na Mama Yusrath.
“Mama,upo wapi?”
“Hospitali,vipi kwani?”
“Kuna mdada amekuja hapa nyumbani,anawaulizia watoto”
“Mdadaaa,yupi?Anaitwa nani?”
Mama Yusrath,akaonekana kushangaa na kushtuka kwa wakati mmoja.
“Mimi simjui,anasema ametumwa na Dada Yusrath, nikamwambia Watoto wapo Ilala”
“Hapana,ebu subiri”
Japokuwa lilikuwa swala dogo lakini mama huyu hakulifumbia macho,hiyo ndio ilikuwa hulka yake, kulichimba jambo mpaka mwisho,ndiyo maana baada ya kukata simu ya Hadima, akapiga nyumbani kwake,akiulizia kama ugeni wowote ulifika, mwisho akasisitiza kwamba watoto wahamishwe haraka iwezekanavyo eneo hilo.
“Wapeleke kwa Anco Mudi”
Mama akatoa maagizo simuni,aliwapenda wajukuu zake kuliko kawaida na jinsi mambo yalivyotokea, walivyonusurika kuuwawa akajua ni lazima watu waliokuwa wanaulizia wametumwa na Ahmed,wazo hilo alilipa asilimia mia moja kwamba bado wanawindwa ili wauwawe.

****
Jaquar na timu yake nzima walishuka ndani ya gari wakiwa wameficha nyuso zao na vitambaa,wakaingia ndani na kuupiga mlango teke baada ya kusikia mtoto mchanga analia,niya yao ilikuwa ni kuwauwa kama walivyoagizwa ili wamaliziwe salio la pesa yao iliyobaki kwa Lissa Nzava.Kishindo cha mlango kupigwa kwa nguvu kilimshtua mzee Suleiman, aliyekuwa ameshika kikombe cha kahawa, anataka kukiweka mdomoni,hiyo ilimfanya aruke na kukiachia kikombe kikadondoka chini na kupasuka.
“Wotee chiiiini”
Zilikuwa ni sentensi mbili tu,tena nzito za kutisha!Na aliyeongea hivyo alizidi kuwaogopesha sababu mkononi alishika bastola,ndani ya seble kulikuwa na watu watano,wote wakaenda chini bila kuhoji kwani walishaelewa nini maana ya watu hao kuingia.
“Boka,sachi vyumba vyote”
Bado haikufahamika majambazi hao wanataka nini,Mzee Suleiman alikuwa chini anapiga dua zake zote za mwisho!Akielewa kwamba huo ndio mwisho wake,anatetemeka kuliko mtu yoyote Yule!Kilichofanyika ni wanaume wawili kusachi chumba hadi chumba,mwisho wakatoka na mtoto mchanga wa mwaka mmoja,kwa kumuangalia tu na maelekezo waliyopewa vilikuwa ni vitu viwili tofauti.
“Watoto wako wapi?”
Swali hilo lilifanya kila mtu atetemeke,hapo ndipo waligundua walichofuata ni watoto na sio kitu kingine zaidi.
“Wa wa watoto gani?”
Msichana mmoja,aliyefahamika kwa jina la Aisha ndiye alijibu,hakujua lilikuwa kosa kubwa kwani badala ya kujibu swali akauliza swali,akashikwa kwa nguvu na kuinuliwa juu.
“Watoto wako wapi?”
Lilikuwa ni swali lililoambatana na bastola,Aisha aliwekewa bastola kichwani alichotakiwa kujibu ni watoto wako wapi.
“Mi…miii siiijui Siii..juiii”
Kazi waliyoamini ingekuwa rahisi kwao sasa waliioona kuwa ngumu zaidi,hawakuridhika wakazunguka nyumba nzima ili kukagua kila sehemu.
“Oyaa,hawapo”
“Sasa tunafanyaje?”
“Tusepe”
“Hatuwezi kusepa hivi hivi,tutamwambia nini boss”
“Tutakuja tena,hi vita bado itaendelea”
“Shega”
Walikuwa wakijadiliana nje,hawakuwa nala kufanya zaidi ya kurudi ndani kwa mara nyingine.
“Tulieni,mkiinua vichwa vyenu nitaua mtu.Wewe,lala chini mimi nipo hapahapa sitoki leo, mpaka mniambie watoto walipo nakaa hapa navuta sigara,ikiisha nitaanza kuua mmoja mmoja”
Alichokifanya jambazi huyo ni kuwasha sigara,akaitegesha vizuri dirishani ikiendelea kutoa moshi kisha taratibu wakaanza kuondoka.
Wakiwaacha Mzee Suleiman na watu wote ndani wakiwa bado wamelala, vichwa vyao vinaangalia chini.Kila mtu alikuwa mwenye hofu kubwa sana,kilichowafanya wasiinue vichwa vyao ni baada ya kuhisi moshi wa sigara wakijua kwamba jambazi huyo bado yupo,walilala kwa zaidi ya dakika ishirini.
“Hodiii humuuu,hodiii hodiiii”
Sauti hiyo iliwafanya wazidi kutandwa na hofu,walivyosikia mlango unafunguliwa ndiyo wakazidi kutetemeka.
“Hee,jamani kuna nini?”
Sauti hiyo,ikamfanya Aisha atumie jicho moja kuchungulia,japokuwa alikuwa na hofu lakini alijikaza mno!Baada ya kumuona dada yake,ndipo akapata nguvu ya kusimama akawa kama mtu aliyechanganyikiwa, mara aende mara apite vile huku akisema majambazi.
“Aisha kuna nini?”
“Majambaaziiiiiiii”
“Majambazii?”
Kila mtu aliyelala chini baada ya kusikia hivyo aliinuka,Mzee Suleimani akasimama wima kwa mkwara mzito.
“Wako wapi?Wanaharamu wakubwa wale.Wameenda wapi?”
Halikuwa jambo la kuchekesha ingawa ilikuwa kama kibonzo,Mzee Suleiman hakuamini kama amepona kwenye tundu la sindano,alichokifanya ni kuingia chumbani kwake na kujifungia ili kupunguza presha aliyokuwa nayo.

*****
Taarifa za kuvamiwa,zikaanza kusambaa kwa kasi ya moshi wa kifuu mjumbe wa nyumba kumi akapewa taarifa hiyo,wakanyoosha mpaka kituo kidogo cha polisi.Huko waliandika maelezo wakahojiwa maswali,kila mtu akamshtumu Ahmed kwamba ni lazima alihusika kwa njia moja ama nyingine,hiyo ikawafanya maaskari watake kujua ni kwanini walimtuhumu mwanamme huyo!Wakatoa maelezo mengine,hatimaye Ahmed akafunguliwa faili lingine la kushiriki ujambazi RB, ikaandikwa!

******
Matumaini ya kupona kwa Ahmed,yalileta faraja kubwa machoni mwa ndugu jamaa na marafiki!Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele,afya yake iliimarika maradufu,hiyo ilimaanisha madaktari wa hospitali hiyo walifanya kazi yao,kikamilifu.Ahmed,mpaka siku ya sita kufika aliweza kuongea vizuri na kutabasamu lakini hakuweza kusimama kutoka kitandani sababu alikuwa ana pingu mkononi, kumaanisha kwamba yupo chini ya ulinzi,manesi wengi walimuonea huruma na kumpenda pia sababu alikuwa ni mgonjwa mchangamfu na muongeaji kuliko yoyote yule.
“Kaa vizuri,nikuchome sindano”
Nesi aliyefahamika kwa jina la Rebeca,alifika ili kutimiza wajibu wake kwa mgonjwa wake!Huyo ndiye aliyetokea kumzoea Ahmed pia,alisikitika sana sababu alishajua mgonjwa wake anakabiliwa na kesi gani.
“Dozi inaisha lini?”
Ahmed akauliza,ki uchovu.
“Kesho jioni”
“Lakini leo naona kama haupo sawa”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Hujachangamka kama siku zote”
“Niko poa mbona”
“Sio kweli Rebeca,niambie una tatizo gani”
Hapo Nesi Rebeca ilibidi atulie kwanza na kumtizama Ahmed,ilielekea kuna jambo alitaka kumshirikisha lakini akasita kidogo!
“Ni kweli nina matatizo”
“Matatizo gani?Ninaweza kukusaidia hata kwa mawazo unajua”
“Mambo ya kifamilia,kuhusu Mme wangu”
“Mme wako?Amefanya nini?”
“Biashara zake,haziendi vizuri.Hali ni mbaya sana,ameniomba nimsaidie ala…”
“Hayo ni mambo ya kawaida Rebeca,maisha ni kupanda na kushuka.Usijali,anafanya biashara gani kwani?”
Ahmed akataka kudadisi zaidi ili stori ziendelee,sio siri hata yeye alivutiwa na ukarimu wa Nesi huyo.
“Yuko pale Manzese,anachonga majeneza!Analalamika biashara ni ngumu sana siku hizi,ameniomba nimsaidie ki…”
“Ebu su subiri kwanza,anafanya biashara gani?”
Ahmed akauliza kwa mshtuko huku akiangalia sindano ya dawa aliyoshika nesi huyo,hofu ikamtanda.
“Mchonga majeneza,Ahmed tuachane na hayo.Nipe mkono wako nikuchome sindano”
“Thubutuuu umchome nani sindano?Huwezi…yaani kum..”
“Ahmed una nini?”
“Sitaki kuchoma sindano,nimegoma”
Mawazo ya Ahmed yalimpeleka mbali sana,akiamini kwamba nesi huyo anataka kumchoma sindano ya sumu ili afe na mwisho wa siku jeneza liuzwe,jambo hilo likamtisha na kumfanya aweke mgomo mwanzo mwisho!Haukuwa utani ilibidi siku hiyo abadilishiwe nesi mwingine.
Matibabu ya Ahmed yaliendelea kama kawaida,Hajrath Mpilla hakukauka hospitalini,ilikuwa kila siku lazima apeleke chakula na kumjulia hali Ahmed,alihisi faraja kubwa sana baada ya kumuona Mwanamme huyo anatabasamu,hiyo ilimaanisha muda wote angeruhusiwa lakini kilichomuumiza mtima ni kesi iliyokuwa inamkabili mbeleni.
“Pole Love”
Hajrath,akasema siku hiyo akiwa na hotpot mkononi.
“Ahsante”
“Nimekuletea kuku wa kuchoma na Soda,amka ule”
Ulikuwa ni upendo,uliozidi kipimo chake.Hajrath alijitolea kwa hali na mali kumfariji Ahmed na alifanya hivyo kwa mapenzi yote,hakika ilikuwa ni picha nzuri.Ahmed hakuwa na jinsi zaidi ya kukaa na kuanza kula taratibu na wakati mwingine alilishwa.
“Umepika wewe?”
“Ndio”
“Kuku watamu sana,wamenikumbusha mbali”
“Wapi?”
“Makumira,ulivyokuwa unanipikia”
“Ukawa hutulii,kila wakati unakuja kuonja jikoni”
“Hahaha,husahau?Unajua kupika,sio siri”
“Ahsante,kula basi.Unywe soda ili umeze dawa”
Kila kitu kilikuwa faraja kubwa sana,Ahmed alihisi kupona kabisa ingawa bado alikuwa na maumivu makali kichwani, hususani juu ya paji la uso!
Alivyomaliza kutafuna minofu ya kuku,Hajrath akamfungulia soda ya fanta kubwa,akaimimina kwenye glass na kumpa.
“Ahsante”
Kuanzia hapo,hakukuwa na mazungumzo mengine zaidi ya kuangaliana na kukumbushiana stori za chuoni.Wanafunzi waliosoma nao,mara huyu anafanya kazi hii yule amekuwa mwanasiasa.
“Basi pumzika Ahmed wangu,nitakuja baadaye”
Alichokifanya Hajrath ni kukilaza kichwa cha Ahmed kwenye kitanda,akasogeza mdomo wake taratibu mpaka kwenye lips zake,wakaanza kunyonyana ndimi yaani denda!Kila mtu akafumba macho yake,akikumbuka enzi zao zilipendwa!
Ghafla mlango ukafunguliwa,jambo lililowafanya washtuke.Ahmed akachanganyikiwa zaidi sababu aliyesimama mbele yake,alikuwa ni Mama Yusrath yaani mama yake mkwe!
“Malayaa wewe,ushapona sasa!”
Hiyo ndiyo sentensi aliyoingia nayo kwa shali Mama huyu mtata, mbaya zaidi,alimshuhudia Ahmed anapigana denda na Hajrath,jambo lililomfanya azidi kupandisha maruwani!




Lilikuwa ni fumanizi la waziwazi,lililomfanya Mama Yusrath apigwe na butwaa lisilokuwa na kipimo chake!Akawa ameganda,anatafakari vitu mbalimbali kichwani mwake,kila alipotaka kuongezea sentensi nyingine alishindwa sababu ya hasira zilizomkaba shingoni.Haikuwezekana hata kidogo akubaliane na jambo hilo,binti yake kupigwa kipigo mpaka yupo mahututi na Ahmed, alafu anamkuta na mwanamke mwingine wanafanya mambo ya kishenzi,kama Mama mkwe jambo hilo alilitafsiri ni dharau kubwa sana!Kilikuwa ni kitendo kilichomuogopesha mpaka Hajrath mwenyewe,japokuwa hakumjua mama huyo ni nani kwa Ahmed,hiyo ilimfanya arudi nyuma na kuhisi kama amepigwa na ubaridi kwenye uti wake wa mgongo!
“Shikamoo!”
Hajrath akasalimia kwa uwoga,akimtizama Mama Yusrath.Ambapo Mama huyo badala ya kujibu, akampandisha kuanzia juu mpaka chini,akarudisha macho yake kwa Ahmed.
“Sasa kwa taarifa yako,mbinu unazopanga.Haziwezi kufanikiwa!Utaozea jela”
Mama akasema kwa uchungu,hiyo ilimfanya Hajrath atembee taratibu na kutoka nje kwani alishaelewa kosa lake,kubaki kukaa hapo kulimaanisha anasubiri matusi ama vichambo ili kuepusha hilo,ilibidi aondoke eneo hilo tena akiwa mwenye hofu kubwa sana!
“Naomba leoleo uandike talaka,sitaki tena ukae na mwanangu.Umenielewa?”
Ahmed hakujibu chochote,kuna majibu alitamani kutoa lakini kutokana na heshima, akajizuia!
Akabaki anamtizama Mama yake mkwe, ambaye aliendelea kusisitiza kwamba waachane na binti yake,ikiwezekana aandike talaka haraka iwezekanavyo siku hiyo na baada ya hapo alimuhakikishia kwamba angemfunga gerezani kwa makosa aliyoyafanya,habari iliyomshtua Ahmed ni baada ya Mama huyu kumshtumu akisema kwamba alitaka kuwateka watoto na kuwauwa.
“Watu uliowatuma kuuwa watoto,wameshindwa na hawatoweza!Na taarifa zako zipo kituoni,chochote kitakachowakuta wale watoto,utawajibika nina RB yako”
“Mama,mbona sikuelewi?”
“Utanielewa tu,unajifanya una hasira sana eeh?Na ninakuomba tena nakusisitiza kwa mara nyingine kaa mbali na Mwanangu”
Ahmed,alishindwa kutegua mafumbo aliyokuwa anaambiwa na Mama yake mkwe,hakuelewa ni kivipi alitaka kuwateka watoto hao mapacha!Alihisi kujuta na wakati mmoja akagundua kwamba hasira ni hasara,akatamani kuomba msamahaa akashindwa sababu Mama Yusrath aliongea bila breki.
Isingekuwa nesi kuingia wodini na kumwambia apishe siku hiyo Ahmed angepewa vidonge vyake mpaka kunakucha!Jioni ya siku hiyo,askari waliingia na kumsomea Ahmed kosa lingine alilotaka kulifanya la kutaka kuteka watoto na kuwauwa.
“Unaendeleaje?”
Afande aliyejitambulisha kwa jina la Kamanda Mwaka,alianza kwa salamu.
“Naendelea vizuri”
“Kama tulivyojitambulisha,sisi ni makamanda kutoka jeshi la polisi”
Hapo Ahmed,akashusha pumzi ndefu kidogo lakini hakuonesha wasiwasi wowote sababu alishaanza kuwazoea maaskari wanaokuja na kuingia kumuhoji.
“Ndio,nawasikiliza”
“Jana ulikuwa wapi?”
Lilikuwa ni swali la kijinga,ambalo jibu lake lilikuwa wazi kabisa kwamba Ahmed muda wote alikuwa hospitalini,isitoshe alikuwa ana pingu mkononi.Hiyo ilimfanya Ahmed awatizame wote kwa zamu!
“Nyie,mlitaka niwe wapi?”
Ahmed,akajibu kwa swali akionekana kama mtu aliyekerwa!
“Unajibu kiburi?”
“Sio najibu kiburi,mna maswali ya kijinga sana!Hapa nina pingu mnaona kabisa,alafu unaniuliza jana nilikuwa wapi?Mna haki ya kujua nilikuwa wapi sawa,lakini sometimes muulize maswali ya msingi”
“Unatufundisha kazi sio?”
“Vyovyote mnavyofikiria”
Majibu aliyokuwa anawapa askari,hata yeye mwenyewe alijishangaa!Na aliwajibu akiwa mkavu hacheki,hiyo iliwafanya maaskari wapandishe mori sababu walilitafsiri tukio hilo moja kwa moja ni dharau kubwa sana!
“Tupatie simu yako”
“Ya kazi gani?”
“Kuna mambo tunataka tuangalie”
Hilo kwa Ahmed halikuwa tatizo kubwa sana,simu yake ilikuwa mezani akawataka waichukue.Walichokifanya maaskari hao ni kuichukuwa na kuiweka mfukoni,baada ya hapo wakanyoosha mpaka kwa wauguzi na daktari,wakataka kujua ni wakina nani walimtembelea Ahmed,hilo halikuwa tatizo!Wakapewa ushirikiano kisha kuondoka zao ili wakakamilishe ripoti yao ya upelelezi wa awali!

*****
Kama masofa yangekuwa yanasema basi siku hiyo,yangeongea na kulalamika kwamba yanaumia.Haikujulikana shati la Nemesi lilivuliwa saa ngapi lakini alichoshangaa yeye ni kujikuta yupo uchi wa myama,Necka Golden yupo juu yake,anamnyonya ulimi huku akiwa ameushika muhogo wa jang’ombe!Nemesi alibarikiwa kuwa na maumbile makubwa sana,hiyo ilimfanya Necka azidi kupata moto mkali hasa kifua chake kilivyotomaswa,ulikuwa ni usaliti mkubwa lakini hilo hawakujali kabisa!Necka Golden,akatoa nguo yake na kumpandia kwa juu, akaukalia muhogo wa Jang’ombe!Kukaa sana jela na kutoona maumbile ya mwanamme kulimfanya atake mechi hiyo ianze haraka iwezekanavyo,ndio maana kitendo cha kuukalia tu akahisi kama mapigo yake ya moyo yameacha kudunda,akajitahidi kuzungusha viuno vya sotojo hiyo ilimfanya Nemesi nayeye ajibu mapigo, akajitahidi kuzungusha nyonga lakini alishindwa sababu Necka alimthibiti ipasavyo,kila alipotaka kumpindua akae yeye Juu yake,Necka hakukubali, akataka kuendelea kubaki juujuu,haichukuwa sekunde tano.Akawa anakaribia kufika kitonga!
“Aaaaashsss aaaah aaaaa…h yeess aaaaaah”
Hiyo ndio miguno na mihemo aliyokuwa anatoa Necka,akamkumbatia kwa nguvu Nemesi na kumyonya ulimi kwa fujo,alivyofika kitonga akatulia kwa sekunde tatu kisha kuendelea kukinyonga kiuno, hiyo ilimaanisha bado hajakata kiu yake vizuri.Kwa Nemesi alikuwa bado hajafika kitonga lakini alijua fika kuendelea kubaki chini na kumuachia Necka aumiliki mchezo huo,ilimaanisha angetoa boko.Ndiyo maana akamtoa haraka na kumbidua kwa chini,akauchukua mguu wake mmoja na kuuweka pembezoni,hapohapo akaanza kumpelekea majeshi majeshi.Dakika mbili baadaye,mkao ukabadilishwa!Akawekwa chuma kisamvu,hapo ndipo alipoguswa kunako,hakujiweza tena!Sauti za puani ndizo alizotoa mpaka wanamaliza mechi hiyo walitumia masaa matatu,Necka akaingia kuoga, Nemesi akazama chumbani.
Huo ndio ukawa mwanzo wa mchezo huo kuanza!
Ilikuwa ni kawaida kwao,wakafanya kama chakula kila siku wanafanya mchezo huo wa ngono sababu walinogewa.Ilikuwa ni siri kubwa Amney asijue na walifanya kwa uangalifu mkubwa sana, kitu ambacho kilikuwa ni hatari,ilikuwa kila siku Amney akitoka wanasubiri dakika thelathini ndipo wanaanza kufanya yao!
“Siku hizi mbona unachelewa kuondoka baby wangu?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Amney,tabia ya Nemesi ilimtia wasiwasi na mashaka lakini hakufikiria kabisa kwamba ameanza mchezo mchafu na Necka Golden kwani alimuamini sana!
“Pale ofisini kuna ukarabati unafanyika,leo ama kesho ndio unaisha!Wanapiga piga rangi”
“Asa si ungeniambia,we nawee!Anyway,nina zawadi yako mme wangu”
Amney aliongea akiwa juu ya dressing table amevaa kanga,ametoka kuoga anajipaka mafuta.Kila kitu kwake kilikuwa furaha mno na alijiona mwenye bahati kubwa sana,kuwa na mwanamme kama Nemesi, anayejituma na kujielewa akaamini kwamba ipo siku moja angemzalia watoto na kuja kuwa baba bora baadaye,ndiyo maana alifanya kila aliwezalo ili amridhishe!
“Iko wapi hiyo zawadi?”
Nemesi alikuwa bado kitandani,kajifunika na shuka alivyosikia hivyo akakaa kitako ili apewe hiyo zawadi.Haukuwa utani,Amney akasimama na kuendea mkoba wake alivyoingiza mkono akatoa kiboxi kikubwa kiasi!Akamkabidhi,ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Nemesi baada ya kuona saa nzuri ya gharama pamoja na shati zuri la drafti.
“Leo mshahara umetoka,nikaamua kupita madukani.Nikaona hiyo saa ni nzuri baby?”
Shukrani alizotoa Nemesi,hazikuwa na mfano wake!Alimshukuru mpenzi wake,kadri alivyoweza akamsogelea karibu na kum-miminia mabusu kede kede.
“Ahsante wife”
“Usijali,kuna pesa nyingine imebaki.Leo nitapita kununua flat screen kubwa ya LG,ile ya seblen tutaileta humu chumbani baby”
“Mmmh baby,si usubiri namimi nalipwa wiki ijayo.Tuchange,please nakuomba”
“Acha tu ninunue”
“Hapana love,nitanunua usijali”
Msichana huyu alikuwa mdogo lakini aliwaza maendeleo tu,akiamini kwamba siku zote nyumba ni mwanamke.
Ndiyo maana alifanya juu chini ili ahakikishe nyumba inapendeza,alivyomaliza kujiandaa akabeba mkoba wake na kumbusu Nemesi mdomoni!
“Baby,baadaye”
“Natoka sasa hivi love,tutaonana baadaye pia”
“Okay Darling”
Kuondoka kwa Amney nyumbani hapo ilikuwa furaha tele kwa Necka Golden,alivyosikia mlango wa seblen umefungwa akatoka kitandani kwa kasi mpaka kwenye kordo, hapo alitembea na kugonga chumba cha Nemesi,mlango ulivyofunguliwa akataka kuingia.
“Unataka kwenda wapi?”
Nemesi akauliza,akiwa amevaa taulo peke yake ndani hajavaa kitu chochote!Hiyo ilifanya tango lake kubwa lijichore vizuri kwa mbele.
“Ukanipe tamu yangu”
“Hapana sio humu”
“Kwanini baby?”
“Namuheshimu Amney”
“Basii njoo huku”
Necka akatoa sauti ya puani huku mkono wake akiwa ameshika tango la Nemesi,akaanza kulichua huku akimvutia chumbani kwake,wakafunga mlango na kujitupa kitandani!
Kwa kuwa Necka alikuwa na kanga tupu mwilini,akaivuta ikadondoka Nemesi akatoa taulo,Necka alivyoliona tango udenda ukamtoka akasogea kwa kasi na kuanza kulichua huku wakinyonyana midomo kwa hisia kali sana,mkono mmoja wa Nemesi ukapita taratibu mpaka kwenye ikulu!Huko ndipo kukamfanya Necka Golden ajinyonge nyonge,akajiona yupo angani anapaa bila mabawa!Kila kitu kwake kikawa burudani,alichokuwa anakifanya ni kulitaja jina la Nemesi kwa sauti ya puani.Akaona kwanini ajitese,mwenyewe akashika tango na kuliingiza ndani ya ikulu tayari kwa mechi kuanza.
“Ngo ngo ngoooo”
“Ngo ngo ngoooo”
Sauti ya mlango kugongwa,ndiyo iliyosikika, wa kwanza kusikia alikuwa ni Nemesi ingawa hakuwa ana uhakika kama ni kweli ama anasikia mawenge.
“Kuna mtu anagonga!”
Nemesi,alitoa sauti ya chini. Kwa Necka aliona kama kero na hakujali ingawa alianza kusikia pia,mlango ukaendelea kugongwa, hapo ndipo Necka akatulia kidogo!
“Neckaaaaa”
Sauti hiyo iliwafanya wote wawili wapigwe na butwaa kwani sauti hiyo ilikuwa ya Amney,Nemesi akahisi kuchanganyikiwa mbaya zaidi hakuwa ana uhakika kama walifunga mlango wa chumbani kwa funguo,Amney akaita tena na kunyonga kitasa!

****
Ratiba zake hujulikana siku zote na njia zake anazopita,hupanda basi katika kituo cha Magomeni mapipa, ambapo kulikuwa na umbali wa hatua kama sabini na mbili za mtoto mdogo,Amney alifika kituoni lakini akasita kupanda gari kwanza kwani simu yake ya mkononi iliita,alivyoangalia aliona namba ngeni,akajitafakari kidogo na kuipokea!Akaiweka sikioni.
“Amney,mambo?”
Sauti hiyo,ilisalimia upande wa pili!Akajaribu kuvuta kumbukumbu niya nani,sababu haikuwa ngeni.
“Safi tu”
“Upo wapi?”
“Magomeni,sorry nani mwenzangu?”
“Shoga angu,namba yangu umefuta?”
“Nimebadili simu”
“Zahra”
“Oooh kumbe Zahra,za siku nyingi?”
“Sio nzuri lakini nzuri”
“Nini zaidi?”
“Una tabia mbaya,kumbe Ahmed anaumwa amelazwa.Hata kuniambia?”
“Acha masihara”
“Amney,sina utani nawewe”
“Mimi ndio nasikia kwako,anaumwa nini?”
Kwa mara ya kwanza Amney kusikia habari za Ahmed kuumwa,zilimfanya asikitike mno!Mbaya zaidi Zahra alimpa sakata zima la kwenye gazeti lilivyotokea alivyobambikiwa watoto mpaka kumpiga mkewe!
“Zahra,unasema ukweli?”
“Ndio,hapa naenda hospitalini kumuona”
“Basi tutakutana huko,ngoja nipige simu ofisini.Niombe ruksa”
“Madona pale,si unapajua?”
“Ndio”
Moyo wa Amney,ulichoma kama pasi.
Alimuhurumia sana Ahmed akakumbuka chuoni Makumira mbali na kuwa na uadui fulani lakini haikumaanisha ampotezee,alichokifanya ni kupiga simu ofisini kwao ili apewe ruksa,akadanganya kwamba anaumwa tumbo la ghafla,akapewa ruksa!Alichokifanya ni kuanza kurudi kwake ili amuage pia na Nemesi kisha amchukuwe Necka waongozane wote mpaka hospitalini,akatembea kwa haraka.Alivyofika bila kupiga hodi akanyonga kitasa na kuzama ndani,bila kuuliza akapitiliza mpaka chumbani kwake!Huko alimkosa Nemesi,akaachana na hilo kwanza kwani alichotaka yeye ni kuzungumza na Necka,akatembea na kugonga mlango.Akaona kimya,akagonga tena lakini wapi, akaita.Akanyonga kitasa ili afungue mlango lakini alitulia baada ya kugundua,mlango umefungwa na funguo,akaita kwa mara nyingine.
“Neckaaa”
“Abeeee”
Sauti kutoka ndani,ikasikika. Necka akaitikia, jambo hilo lilimfanya Amney atulie kidogo ili afunguliwe mlango!Ndani ya chumba Nemesi alitetemeka kuliko kawaida,hakuelewa ni kitu gani akifanye akawa ameganda,anapiga hesabu ni wapi ajifiche.
“Tulia,ingia uvunguni”
“Siwezi kupita,nitakaa nyuma ya mlango”
“Nyuma ya mlango?Hapana.Njoo kwenye tenga hili la nguo, njoo njoo njooo”
Kwa sauti ya chini tena ya mnong’ono walianza kuvutana huku na kule wakitafuta mbinu ya kujificha,kwa haraka Necka alianza kutoa nguo chafu kwenye tenga kubwa!Nemesi akaingia Necka akaweka nguo juu yake kisha kufunika tenga!
“Neckaaaaa”
“Aaabee abee nafungua Amney”
Alivyohakikisha Nemesi,haonekani akatembea na kufungua mlango lakini badala ya kutoka mzimamzima,akatoa kichwa nje, kiwiliwili kikabaki ndani.
“Huyu Nemesi ameondoka tayari?”
Lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa Amney.
“Sijui,mimi nilikuwa nimelala.Kwani hayupo?”
Necka akauliza swali,akijifanya hajui ni wapi Nemesi alipo.
“Ngoja nimpigie simu nimuulize.Nataka nimuombe ruksa kuna sehemu nataka twende wote!”
Amney akatoa simu,akaanza kutafuta namba za Nemesi.Akairuhusu itoke lakini cha ajabu ikaanza kuitia chumbani,hilo lilimfanya Amney apigwe na butwaa la waziwazi.



Kuendelea kusubiri watoto wafe kwanza ilimaanisha kuchelewa kwa dhumuni lake,alichoamua ni kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja, yaani watoto mapacha pamoja na George Charles kwa wakati huo mmoja!Japokuwa alipata hasira sana lakini haikumaanisha asitishe jambo alilolianza,hiyo ilimpa nguvu ya kufanya haraka haraka ili asije kugunduliwa mapema.Mikakati ya kumuua George Charles, ilianza kupangwa siku hiyo jioni ya saa kumi na moja alivyorejea nyumbani.
Kitu alichokifanya tu ni kuingia ndani,akapitiliza mpaka chumbani kwake.Akaingia bafuni,huko alioga na kubadili nguo!Siku hiyo Lissa Nzava alionekana mtu mwenye haraka sana kuliko siku zote,ndiyo maana baada ya kuvaa taulo akaenda kwenye sofa lililokuwa chumbani, ambapo mezani kulikuwa na simu,akachukua mkonga na kuuweka sikioni,akabonyeza namba fulani.
“Boscow,mwambie Mpenda anisafishie gari”
Mlinzi aliyekuwa getini ndiye aliyepokea simu,ndani ya kijumba chake maalum.
“Gari gani Mama?”
Hapo ikawa kazi nyingine kubwa,kuchagua aina ya gari gani atoke nalo kwani yalikuwa mengi uwani.
“Marcedez benz”
“Ya rangi gani?”
“Ile nyeupe”
“Sawa Mama”
Alivyoweka mkonga chini,akachukua simu yake ya mkononi na kumtafuta Minja ili ampe mpango mzima na jinsi ramani itakavyochorwa.
“Leo atachelewa kurudi,una silaha?”
“Sio jambo la kuuliza,unatakaje?”
“Wait,jambo hili sio la kuongea kwenye simu.Tukutane kwa siku zote”
“Saa ngapi?”
“Right now”(Sasa hivi)
“Okay”
Sijui ni shetani gani alimuingia na kumvaa,pepo la kuuwa lilimtawala kabisa.Akajenga chuki na mumewe akitamani kumuuwa ili apate utajiri mkubwa!Alichokitaka kilikuwa ni lazima kifanyike, mbaya zaidi aliendelea kupanga mikakati ya kuwauwa watoto wa Yusrath,kwa gharama yoyote ile.Ndiyo maana akahitaji afanye mazungumzo na Minja,ampe mchakato mzima jinsi itakavyokuwa.Kwa upande mwingine aliumia sababu aliamini kuanzia siku hiyo,wasingeonana na George Charles, tena!
“Buliani George”
Lissa alisema maneno hayo huku akiwasha gari,akarudi kinyume nyume na kuliweka sawa!Ambapo breki ya kwanza ilikuwa ni Serena Hotel,hapo alimkuta Minja amefika tayari.
“Nahitaji afe leo”
“Litawezekana,ondoa shaka”
“Ndio ulivyo,hata mara ya kwanza uliniambia ondoa shaka.Hivyo hivyo lakini hatimaye mkaniangusha.Bado sijasahau”
“Ajali kazini,lakini amini nachokwambia.Sasa hivi,hatuwezi kufanya makosa!Utaenjoy Show, cha kufanya andaa jeneza na kaburi”
“Tayari,ni wewe tu.Futi zake nazijua kichwani”
Lissa,hakutania kile alichokizungumza alikimaanisha kwa asilimia zote mia moja ni lazima amuuwe George Charles,tena kwa risasi, ndiyo maana akawapanga watu wake wafanye kazi hiyo kwa umakini wa hali ya juu sana!
Alivyoacha maagizo hayo,akaingia ndani ya gari lake akitafakari ni sehemu gani aende, ghafla picha ya Yusrath ikamjia kichwani,akapata wazo la kwenda hukohuko!Aliendesha gari kwa umakini mpaka alivyofika Hospitali ya taifa Muhimbili,kwa kuwa alijua wodi alilolazwa Yusrath,haikumpa shida akatembea na kuingia mpaka ndani ambapo alimkuta Nesi mmoja anamchoma sindano kwenye mshipa wa damu,mkononi.
“Naweza nikaongea na Mgonjwa?”
“Sasa hivi sio muda wa kuona wagonjwa!Njoo saa moja”
Nesi alijibu, hiyo ilimaanisha Lissa atoke nje,alichokifanya Lissa ni kuingiza mkono ndani ya mkoba wake, akahesabu noti tano za shilingi elfu kumi.
“Naomba niongee naye dakika moja”
Nesi akasita kidogo kupokea,akatabasamu. Pesa alizotaka kupewa na kazi aliyotakiwa kuifanya ya kumruhusu Lisa vilikuwa ni vitu viwili tofauti,ilikuwa ni pesa kubwa sana.Akaichukua na kuitia kwenye sidiria vizuri, upande wa kushoto!
“Wala usijali dada,wewe ongea naye tu hata mpaka saa tatu”
“Shukrani”
Lissa akajibu,akipachika tabasamu la Plastiki akamuendea Yusrath.Alichokifanya baada ya kufika ni kumtia Yusrath kibao cha uso,paa!
“Wee kahaba,amka”
Alikuwa anapotelea kwenye usingizi lakini kibao cha uso,kilimzindua alivyofumbua macho yake!Akahisi mapigo yake ya moyo, yameacha njia,sura ya Lissa haikuwa ngeni kwake.
“Dada ha…”
“Mimi sio dada yako!Nisikilize kwa umakini”
Lissa alizungumza huku akiubonyeza mkono wa Yusrath, uliokuwa na dripu kwa nguvu tena kwa hasira na wivu.
“Watoto wale wa naniiii?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Lissa.
“Nakuuliza tena,watoto wa nani?”
Maumivu aliyokuwa anahisi Yusrath yalikuwa makubwa akiwa kitandani,mkono wake ulibinywa kwa nguvu, isitoshe ndiyo ulikuwa umechomwa sindano ya dripu!Hiyo ilimfanya agugumie ndani kwa ndani.
“Wa M…me wa….ngu,A..hmed”
“Muongo,nambie ukweli”
“Wa Geor….ge”
“Alivyokuja hapa,alikwambia nini?”
“Nisi…”
Kabla ya kumalizia kujibu sentensi hiyo,mlango wa Wodi ukafunguliwa.Lissa akatoa mkono haraka na kujifanya anamshika Yusrath, akimpa pole!
“Utapona Mamitoo,sawa!Naenda kukuchukulia chakula hapo nje,narudi sasa hivi”
Isingekuwa rahisi kwa mtu yoyote kujua kilichokuwa kinaendelea,alichokifanya Lissa ni kuchukua mkoba wake na kuondoka zake kwa haraka,akaingia ndani ya gari na kurudi nyumbani kwake.

Siku hiyo alikuwa mwenye furaha kubwa sababu aliamni angeletewa taarifa za George Charles kufariki,hakuna kitu alichokuwa anasubiri baada ya kufika kama simu kutoka kwa Minja,kwamba George Charles tayari amekufa kwa kupigwa risasi.Akapanda ngazi kwa haraka,akafika chumbani na kutafuta Whisky kali,akamimina kwenye glasi na kuanza kunywa huku macho yake yakiwa kwenye kioo cha simu.

******
Kikao kikubwa,kilichowashirikisha wawekezaji kilikula masaa manne na nusu.Ndani ya kikao hiko, kulikuwa na wafanyabiashara wakubwa kumi na sita.Lengo lao likiwa kuwekeza zao la mafuta ya Alzeti nchi za jirani kama Uganda,Kenya na Burundi.Wasingeweza kufanya hivyo bila kuzungumza na Serikali za nchi hiyo.Ndiyo maana wakaitisha Kikao hiko kikubwa na miongoni mwa wafanyabiashara aliyekuwepo ndani alikuwa ni Bilionea George Charles,pembeni yake aliketi Mzee wa Makamo Robert Baseka mzee huyu alijulikana kutokana na kumiliki vituo vingi vya mafuta na maduka ya Jumla Kariakoo na Tegeta!
Pembeni aliketi Kijana mmoja wa kichaga Geofrey Urio,huyu alipata umaarufu kutokana na mabasi yake ya mikoani pamoja na malori ya Mizigo iliyokuwa inafanya safari zake nje na ndani ya Tanzania,mbali na hapo alikuwa ana shule nyingi mikoani,sifa yake kubwa alikuwa ni mzee bahili sana, alifahamika mjini kwa jina la Mangi.
Kifupi kikao hiko kilikuwa na watu wazito na pesa zilizokuwa zinazungumziwa ni kuanzia bilioni kwenda juu!Kikao,kiliisha saa tano ya usiku.Kila mmoja alitawanyika lakini cha ajabu na cha kushangaza kila tajiri alikuwa na dereva wake wengine na walinzi isipokuwa Bilionea George Charles,hakuwa na dereva wala mlinzi, anayelinda usalama wake.
“This is dangerous,huogopi Mr.George?”
Geofrey Urio,akauliza baada ya kumuona Bilionea George Charles, anaingia ndani ya gari lake akiwa mwenyewe.
“What do you mean?Sijakuelewa”
“Hauna walinzi,hauna driver.Unajiamini nini?”
“Mungu ndio mlinzi wangu”
“Hapana,usijiamini hivyo Mr.George!Nitakutafutia walinzi”
Urio alizungumza hivyo kwa utani na kutembea mpaka kwenye gari yake ya kifahari aina ya Hammer III Original, akafunguliwa mlango na mlinzi wake,bila kujua George Charles ana walinzi zaidi ya nane hapo walipo, tena hawapo mbali na kila alipotembea alikuwa nao kisiri!George Charles, alivyoingia ndani ya gari breki ya kwanza tu,alimtafuta mkewe hewani, akimpa taarifa hizo na kumwambia jinsi michakato ya kikao kilivyoenda.
“Baby imiss you.Ni usiku unajuaaaa,naogopa nimezoea kuwa nawewe muda kama huu nikiwa kifuani kwako”
“Usijali,ndio narudi now”
“Huogopi baby?”
“No,siogopi”
“Baby,sijawai kukuona una silaha.Huna walinzi?Unanitisha mme wangu!Mimi ni mkeo nat…”
Lissa alitaka kumuaga George mara ya mwisho,akiamini hatosikia tena sauti yake kuanzia siku hiyo!
“Baby,relax.Narudi nyumbani safely kwa sababu nina wal…”
Ilikuwa kidogo aropoke kwamba ana walinzi lakini akaupiga mdomo wake ‘stop’,alivyokata simu akaingia ndani ya gari.
Kutoka Chalinze kikao kilipofanyika,mpaka anapoishi ulikuwa ni umbali mrefu lakini hakuwa na wasiwasi sababu alikuwa na walinzi nyuma wanamsindikiza kimya kimya,wakilinda usalama wake,hivyo hakuwa na shaka yoyote ile.
Alivyofika Maili moja,akashangaa magari mawili yamempita kwa kasi ya risasi.Hakuwa ana shaka nazo,akadhani wenda madereva wamelewa ama wametoka kumbi za starehe.Akazidi kusonga mbele!Lakini katika hali ya kushangaza,akaiona taa nyekundu za gari limesimama kandokando kidogo ya msitu,akapunguza mwendo kidogo alivyolifikia gari hilo, akaongeza tena mwendo.
Ghafla,kufumba na kufumbua,kuna gari nyingine kati ya zile zilizompita ikachomoka kutokea kwenye kichochoro ambapo kulikuwa na pori,likamgonga kwa mbele mpaka taa zikapasuka.
Watu wanne wakatoka wakiwa na bastola mkononi.
“Tyson”
Ni sentesni moja tu,iliyomfanya Tyson mwanamme wa kigiriki aliyekuwa nyuma ya usukani anaendesha gari, kukanyaga mafuta mengi sana,alishaelewa kwamba tajiri yake yupo kwenye hatari kubwa.
Wanaume hao walianza kuchezwa na machale tangu walivyoona gari hizo zinatembea kwa kasi ndiyo maana wakajihami mapema,kitendo cha kuona gari ya bosi wao imegongwa kiliwafanya watumie sekunde sifuri kuchomoa bastola zao viunoni tayari kwa kufanya ambush!
“Paaa! Paaaaaaa! Paaaaaa!”
Majambazi waliotoka na silaha,wakasikia mlio wa bastola.Hata wao walishtuka mno.Hawakuelewa zinatokea wapi,walichoshtuka ni kuona magari matatu yanakuja kwa kasi nyuma yao!George Charles,alitetemeka akiwa ameweka kichwa chake chini ya usukani anasikia milio ya risasi hakuwa ana uhakika kama walinzi wake wapo karibu tayari.
Kabla ya gari anayoendesha Tyson kusimama vizuri akashuka mwanamme mmoja mrefu futi nyingi kwenda hewani,kitendo cha kutua ardhini akabiringika kama komandoo,akachomoa bastola yake na kuanza kurusha risasi.Mmoja wa majambazi aliyekuwa pembeni ya gari la Bilionea George, akapigwa risasi ya mkono!
“Paa paaaa”
Jamaa huyo,ambaye alibatizwa jina na wenzake Chuck Noris kutokana na uhodari wake,akatembea huku akirusha risasi mpaka lilipokuwa gari la bosi wake bilionea George Charles.Akapasua kioo na kurusha tena risasi!
“Paaaaa”
Jambazi mmoja aliyekuwa kwenye usukani nayeye akapigwa risasi ya bega,Chuck Noriss akafungua mlango na kumsogeza bosi wake kushoto.Alichokifanya ni kupiga gia na kulirudisha gari nyuma kwa mwendo wa kasi,jaribio alilotaka kulifanya kwanza ni kumuondoa Bilionea George Charles kwenye hatari inayomkabili,akaliingiza gari porini na kutulia kwanza ili kuangalia utaribu mwingine!Mirindimo ya risasi iliendelea kusikika,wakazi wa eneo hilo ingawa walikuwa wamelala lakini walitandwa na hofu, wengine walidiriki kuingia uvunguni mwa kitanda,baadhi wakaanza kukimbia tena bila nguo!
Kulikuwa kuna kila dalili za majambazi hao kuzidiwa sababu hawakujipanga na hawakutegemea jambo hilo lingetokea,walichokifanya ni kuanza kurudi kwenye magari yao!Hiyo haikuwa rahisi kwani matairi yalishambuliwa na risasi,wakashindwa kuondoka!Baadhi wakaingia mitini lakini wawili walipigwa risasi za miguu na kudondoka chini.
“Paaaaaaaaaa”
Kati ya wawili waliopigwa risasi za miguu wapo chini wanajiburuza,mmoja akapigwa risasi ya kichwa, mbele ya mwenzake.Tukio hilo,lilionekana wazi kutokana na taa za magari kumulika.
“Unaona nilichomfanya mwenzako,nani kawatuma?”
Lilikuwa ni swali,lililoambatana na kitisho sababu jambazi huyo aliwekewa bastola kichwani.
“Msiniueeee msiniu…e”
Mguuni alivuja damu nyingi sana na alihisi maumivu makali, yaliyotokana na jeraha la risasi.
“Nani kawatuma?”
“Li…ssa Lissa Mnzava na Mi..nja”
Hakuwa na jinsi,zaidi ya kutaja majina kwani kwa wakati huo uhai ndio ulikuwa kila kitu kwake.


Billionea George Charles alikuwa anatetemeka kwa kiasi cha kutosha,japokuwa alikuwa tajiri mkubwa mwenye mamlaka ya kufanya kitu chochote kile anachotaka lakini siku hiyo akaamini kifo kinatisha,tangu azaliwe hakuwahi kusikia milio ya bunduki karibu na masikio yake.Japokuwa alikuwa ndani ya gari na nje kulikuwa na walinzi wake wanne wameshika bastola lakini hakujiamini,akiwa katika hofu kubwa alianza kutafakari ni watu gani walitaka kumvamia?Walitumwa na nani?Sura iliyomjia haraka kwa wakati huo ni tajiri mwenzake ambaye ni mfanyabiashara kama yeye Ezron Kibona.
Akaamini moja kwa moja ndiye yeye aliyechora mchezo huo kwani alikuwa anamdai mwanamme huyo kiasi cha shilingi milioni mia tatu za kitanzania,kumtumia majambazi kulimaanisha atake afe ili asilipe deni.Akaapia kwamba akitoka hapo ni lazima atalifuatilia hilo swala na ikiwezekana amfunge gerezani.Ndani ya gari hakutulia,ilikuwa mara aangalie huku mara kule.Japokuwa gari ilipaki katikati ya miti mingi lakini aliweza kumuona Mlinzi wake mwingine alivyosimama barabarani kwenye lami anatizama huku na kule kulinda usalama!
Dakika kumi na tano nzima walitulia eneo hilo kwa niya ya kuangalia usalama kama upo!
“Boss,upo salama?”
Mmoja wa walinzi wake akufungua mlango wa gari wa mbele na kuuliza.
“Yes,I’m okay”
“Subiri kidogo usitoke”
“Sawa”
Alivyojibu,picha ya mkewe ikamjia kichwani.Na kitu cha kwanza kukikumbuka ni kumpa taarifa ya tukio zima lilivyotokea ili amtoe wasiwasi kwani aliamini kwa jambo kama hilo lingemfanya achelewe kufika nyumbani,kama mwanamme ilikuwa ni lazima atoe taarifa kwa mkewe amueleze kila kilichotokea na kumtoa wasiwasi.
George Charles alikuwa nyuma ya kila kitu,hakuelewa nyuma ya tukio hilo mkewe ndiye kahusika.Akachukua simu ili atoe taarifa,akabonyeza namba za simu kisha kuiruhusu iruke hewani akaiweka sikioni,upande wa pili ukaanza kuita.Kilichomshtua zaidi alivyopiga jicho mbele na kuwaona walinzi wake watatu wanazungumza,haikuwa kawaida kwani waliongea huku wanageuka nyuma ilielekea kuna kitu walikuwa wanajadili.
“Nitamwambia mimi kwamba ni Lissa”
“Nenda kamueleze”
Mmoja wa walinzi aliyefahamika kwa jina la Patrick Mogera,alitaka kueleza kila kitu kilivyotokea!
Japokuwa alielewa ni kwa namna gani bosi wake angeumia lakini hakuwa na jinsi yoyote ile,alichokifanya ni kusogea mpaka karibu na gari kabisa akafungua mlango na kumuangalia bosi wake ambaye kwa wakati huo alikuwa na simu sikioni.
“Patrick,kuna nini?”
Bilionea George Charles akauliza,lakini kabla ya kujibiwa, Mkewe Lissa Nzava akawa tayari amepokea simu yupo kwenye laini.
“Halloo”
Akasikika simuni baada ya kupokea!
“Nakupigia mke wangu,subiri kwanza.Lakini nipo kwenye matatizo”
“Mme wangu una unasema?Matatizo gani tena?”
Lissa akashtuka lakini badala ya George kujibu,akakata simu na kumsikiliza mlinzi wake.
“Boss”
“Yes”
“Kuna kitu unatakiwa ukifahamu”
“Kitu gani Patrick?”
“Anayehusika na hili tukio zima ni…”
Kabla ya Patrick kutoa jibu akamtizama tajiri yake machoni,alielewa ni kwa namna gani habari hizo zingemshtua lakini pia kulikuwa kuna vitu viwili vina pita kichwani kwake,alielewa ni lazima bosi wake angekubali ama kukataa katukatu.
“Pati,talk to me!Usinifiche”
“Your wife,mkeo ndiye kawatuma hao watu wakuuwe”
“Whaaaaaaaaaat?No please,You mean Lissa?Haiwezekani,namfahamau mke wangu!Patrick,stop fooling me”
Patrick alikuwa ni mwanamme makini pengine kuliko yoyote yule na majibu kama hayo kutoka kwa bosi wake aliyategemea,alichokifanya ni kutoa simu ya jambazi waliyempiga risasi.
Akaifungua upande wa meseji na kumuonesha.Meseji zilizokuwa juu ya kioo zilimuogopesha sana George,akahisi joto la ghafla mwilini mwake.Licha ya hayo yote hakutaka kuamini na kulipa swala hilo kipaumbele,akatizama namba za simu ili ahakikishe,akajikuta anaishiwa nguvu baada ya kukuta namba za mkewe!
“Oh My God, Lissa!”(Mungu wangu Lissa)
Japokuwa kulikuwa na baridi kali lakini shati lake upande wa kwapa lilichora alama ya jasho,hiyo ilimfanya azidi kuogopa!Hakutegemea hata siku moja kama Mkewe leo hii alikuwa na mbinu za kumuuwa.Alihisi uchungu ajabu,picha mbalimbali zilianza kumjia kichwani wakiwa kitandani na Lissa wanazungumza na kupewa maneno matamu!Wakati mwingine alidhani yupo ndotoni lakini haikuwa hivyo, yaliyokuwa yanatokea yalikuwa na uhalisia mtupu.
“Boss,kua makini sana!Nikuombe kitu?”
“Patrick I’m not okay.Naomba nimpigie simu ni…”
“Usifanye hivyo,it’s not a smart move”
“What i’m i suppose to do?”(Nifanye nini)
George Charles,hakuweza kufikiria tena!Akili yake ilishindwa kufanya kazi kabisa.Bado jambo lililotokea alihisi ndoto ya kutisha na alitamani ashtuke,alichokifanya Patrick Mogera ni kumtuliza Bosi wake akimwambia kila kitu kitaenda sawa na asiwasiliane na Lissa kwanza.
Akatembea mpaka barabarani ambapo hapo alimuinua jambazi mmoja aliyekuwa anavuja damu mguuni,kuna kitu alikitaka kutoka kwake,akamburuza mpaka vichakani.Kabla ya kufanya chochote, George Charles akawa amefika eneo hilo,walimshauri arudi ndani ya gari,akagoma kwani alitaka kusikia na kuona kila kitu kinachoendelea.
“Unaitwa nani?”
“Ki…de”
“Nani kakutuma umesema?”
“Mmmmmh”
Jambazi Kide,akajifanya kiburi akabenua mdomo.Hakuelewa anaongea na mtu mwenye roho mbaya zaidi yake.
“Paaaaaaaaaaa”
Ilikuwa ni risasi nyingine iliyosikika kwa nguvu na kumfanya Bilionea George Charles aruke na kukaa chini kwa uwoga,Kide alipigwa risasi nyingine ya mguu.Akapiga ukunga wa nguvu wa maumivu!
“Unakumbuka nilichokuuliza?”
Lilikuwa ni swali lingine,mbaya zaidi mlango wa bastola ulikuwa katikati ya jeraha lake linalotoa damu.
“Huwa sipendi dharau,nani kakutuma?”
“M..inja na Li..ssa”
“Nisikilize,shika simu.Mpigie huyo Lissa mwambie kazi tayari,utampigia na huyo Minja pia.Umenielewa?”
Hicho ndicho kilichotokea,simu ikapigwa ikawekwa loudspika na wa kwanza kupewa taarifa hiyo alikuwa ni Minja,baada ya dakika mbili simu ikapigwa kwa Lissa!
“Maa…dam”
“Nani anaongea?”
Upande wa pili wa simu ukasikika kwa sauti,moyo wa George Charles ukalipuka kama bomu kwani sauti hiyo ilikuwa ya mkewe wa ndoa!
“Wale vijana wa Minj..aaa”
“Unasemaje?”
“Nilikuwa nakupa taarifa kuwa,kazi yako tayari”
Hapo aliongea kwa kujikaza!Lissa hakujibu kwanza,akakaa kimya kwa sekunde moja nzima!
“Unasemaje?Wewe nani kwanza?”
“Wale vijana wa Minja,uliotutuma tufanye ile kazi yako”
“Mmefikia wapi?”
“Kila kitu kimeenda sawa”
“Upo siriazi?”
“Sikutanii Madam”
“Kwahiyo?Mmemuua George?”
“Ndioo”
“Kazi nzuri,kazi nzuri saaaana.Excellent,maiti yake mmeitupa wapi?”
“Ndio tumeiweka kwenye gunia,tunaenda Bahari ya Hindi kule feli”
“Make sure hakuna mtu anayewaona.Mkimaliza,mnipigie simu asubuhi.Pesa yenu nitawaongeza mara tatu yake!Hongereni kwa kazi nzuri,next week kila mtu nitamkatia tiketi ya ndege muende mkapumzike nje ya nchi”
Wakati Lissa anasikika akiongea simuni maneno hayo,George Charles alitokwa na machozi.Alilia kwa uchungu sababu aliamini isingekuwa walinzi wake siku hiyo kumkinga,angekuwa kwenye gunia anaenda kutupwa bahari ya Hindi!Akashindwa kuvumilia akarudi ndani ya gari na kutoa kitambaa,huko alilia kwa uchungu kama mtoto mdogo!

******
Mazungumzo baina ya Necka na Amney,aliyasikia kwa masikio yake yote mawili akiwa katikati ya nguo chafu, zinazonuka uvundo lakini kwake hakusikia harufu hiyo,alichowaza yeye ni kutoka salama katika mdomo wa mamba!Alijilaumu sana kwa kitendo alichokifanya,akaapia kama angetoka mahali hapo salama basi asingerudia tena mchezo huo hatari.
Alimpenda sana Amney lakini alimlaumu sana shetani kwa kumuingiza katika majaribu ya namna hiyo!Hakuelewa ni aina gani ya msamaha angeomba mpaka Amney akubali endapo angegundua ana mahusiano ya kimapenzi na Necka Golden!Nemesi alihisi kujuta na kujichukia kwa wakati mmoja.Kila kitu alikisikia jinsi Amney anavyomuulizia mpaka anapiga simu yake!
Mbaya zaidi simu ilianza kuitia chumbani kwake,hiyo ilimaanisha kivyovyote vile Amney angekuwa ana uhakika kwamba Nemesi yupo ndani hajatoka nje!
“Simu yake mbona inaitia chumbani”
Amney aljisemesha na kutembea mpaka mlangoni kwake,ambapo hapo aliikuta kitandani chini ya mto!Akaiangalia vizuri na kushindwa kuelewa ni wapi mpenzi wake alipo,akapata wazo la kutoka nje ili amuangalie kwa majirani kwani nyumba waliyopanga ndani kulikuwa na wapangaji wengine!Huo ndiyo ukawa mwanya wa Nemesi kuchomoka ndani ya tenga la nguo kwa kasi.
“Subiri kwanza”
Necka akamzuia asitoke nje!
“Weee ebu niache”
Nemesi,hakutaka kuelewa akachomoka kwa kasi mpaka chumbani ambapo huko alivaa boxa yake kwa haraka,akarudi seblen alivyotaka kuufikia mlango,kitasa kikanyongwa mlango ukafunguliwa.Amney akapigwa na butwaa la waziwazi baada ya kumuona Nemesi ndani,akashindwa kumuelewa!
“Leo mbona mapema?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Nemesi,akijifanya hajui chochote.
“Ulikuwa wapi?”
Amney,akajibu kwa swali likawa swali juu ya swali.
“Nilikua ndani mbona”
“Nisikuone?”
“Nilitoka,nilikuwa uwani huko narekebisha dishi!Lilikuwa limekaa vibaya”
“Baby,ulipanda juu ya bati?!”
Amney akauliza kwa mshangao.
“Ndio”
“Sasa ungeumia?Ungevunjika je?”
“Thubutuuuu,mimi komando wewe”
Nemesi akaweka utani,akajichekesha kidogo ili abadilishe somo.
“Una ukomando gani wewe?Huna lolote,baby sikia.Nimeomba ruksa kazini nataka niende kumuona rafiki yangu,hospitalini”
“Rafiki yako yupi?”
“Huwezi kumjua Honey,nitaenda na Necka lakini”
Nemesi aliponea chup chup kwenye tundu la sindano,bado hakuwa ana uhakika kama Amney alihisi kitu ama anajikaza hapo alipo!Lakini alijipa moyo kwamba hakuna kitu alichogundua sababu alimjua sana Amney, hakuwa na kifua ni lazima siku hiyo kivumbi kingetimka na pasingetosha hata kidogo!

*****
Shinikizo la Mama Yusrath kutaka Ahmed atoe talaka lilikuwa kubwa mno,kila kukicha alimfuata Ahmed akimtaka afanye jambo hilo haraka iwezekanavyo,hilo halikuwa tatizo kwa Ahmed.Akiwa hospitali alitafutiwa karatasi na kalamu ili aandike.Pembeni akiwa amesimama Mama Yusrath kama mgambo wa jiji ili zoezi hilo likamilike,Ahmed akafanya kama mama huyo anavyotaka, japokuwa aliiandika kwa shingo upande.
“Malizia haraka,bazaazi wewe”
“Mama namalizia”
“Malizia ndio na jela inakusubiri.Nakuchukia sana!”
Mamaa alizidi kuwaka,hakujali Ahmed yupo katika maumivu ya kiasi gani,alivyomaliza kuandika Mama akachukua na kumkata jicho kali la chuki za waziwazi.
“Baada ya hapo,ujiandae kujibu mashtaka”
Mama akasema na kuondoka zake,ambapo baada ya dakika moja akaingia Hajrath,akapitiliza moja kwa moja mpaka kitandani,akambusu kwenye paji la uso kisha kusimama.
“Unaendeleaje?”
“Naendelea vizuri”
Ahmed alijibu.Kupitia macho yake Hajrath alijifunza kitu!
“Una nini?”
“Nipo sawa”
“Ahmed,una tatizo gani?”
“Niko sawa”
“Ahmed,nakuomba uniambie”
Alikuwa ana kila sababu ya kuuliza hivyo.
“Huyo Mama aliyetoka ni Mama yangu mkwe”
“Najua”
“Umejuaje?”
“Nilivyotoka siku ile,niliuliza uliza hapo nje.Ngowi aliniambia”
“Basi ndio hivyo,amefosi nimuandikie mke wangu talaka”
“Kwanini sasa?”
Lilikuwa ni swali la kijinga kutoka kwa Hajrath kwani kila kitu kilikuwa wazi,mbali na hapo moyo wake ulilipuka kwa furaha ingawa hakutaka kulionesha hilo waziwazi.
“Pole sana,mkeo yeye anasemaje?”
“Sijui”
“Kamuombe msamahaa”
“Nikitoka hapa,najua nitafungwa.Moyo unaniuma,naumia sana!Najichukia”
“No please,Ahmed usiseme hivyo”
Katikati ya mazungumzo yao,mlango ukafunguliwa.Hajrath akageuka,moyo wake ukashtuka akaganda akawa kama mtu asiyeamini mtu anayemuona mbele yake,mbaya zaidi pembeni yake alikuwa amelala Ahmed!
Alikuwa ni Necka Golden,msichana aliyetokea kumchukia kuliko mtu yoyote yule katika maisha yake,msichana aliyemtenganisha na Ahmed,msichana aliyemfanya atake kujiua kisa mapenzi.Hakuelewa ni kitu gani akifanye,aliyemzindua kutoka katika butwaa hilo ni Amney aliyetokea nyuma ya Necka Golden,hata yeye alionekana kupigwa na butwaa la waziwazi baada ya kumuona Hajrath Mpilla, eneo hilo.





Ukimya wa kama sekunde kumi na tano ulitawala ndani ya wodi,kila mtu akiwa anatafakari na kukumbuka matukio mbalimbali yaliyopita nyuma!Katika watu walioumia moyo ni Msichana huyu mrembo Hajrath Mpilla,wivu mkali ulimshika.Akashindwa kabisa kuelewa Necka Golden ilikuwaje yupo mahali hapo na ametokaje gerezani,akiwa katika butwaa kubwa, Amney akamshtua akimsalimia huku akionesha tabasamu pana usoni mwake!
“Hajrath,unajua bado siamini kabisa kama ni wewe”
Amney akashindwa kujizuia akajikuta ameropoka,hiyo ikachukua muda kidogo kwa Hajrath kutoa jibu la haraka.
“Ndio mimi”
Hatimaye akajibu,hiyo ilimfanya Necka Golden nayeye atoe salamu lakini matokeo yake haikujibiwa, kumaanisha kwamba bado Hajrath anakumbuka mabaya yote yaliyotokea nyuma.
“Naomba niwapishe”
Hajrath akasema na kuanza kupiga hatua kutoka nje,akampita Necka Golden bila kumsemesha, ambapo huko alihisi hasira zinazidi kumpanda,kuna kama lidudu lilikuwa shingoni kwake linamkaba.Amney akashindwa kuvumilia,akamfuata nje hukohuko ili wazungumze vizuri!
“Hajrath upo sawa?”
Amney akauliza kwa sauti ya chini.
“Ndio,usijali.Za siku nyingi?”
“Salama,mgonjwa anaendeleaje?Pole na kila kitu,hatujaonana siku nyingi”
“Ungetaka kuniona ungenitafuta”
Ilikuwa ni sentensi iliyomfanya Amney ajisikie vibaya,akaona aibu na kuangalia chini kwani hakuwa na hoja ya kujitetea!
“Nilikuwa na matatizo lakini nilipanga nikuone”
“Mimi mzima”
Siku hiyo Hajrath alitoa majibu ya mkato,hakuwa mwenye furaha hata kidogo mudi yote ilikatika ghafla, hiyo ilitokana na sura ya Necka Golden,kifupi alihisi kichefu chefu cha kutapika.
“Huyo rafiki yako,mlitoana wapi?”
“Hajrat….”
“Yaishe,tutaonana baadaye”
Hajrath hakutaka mazungumzo mengine zaidi,urafiki wa Amney na Necka Golden ulimtia mashaka kwani siku zote aliamini ‘Rafiki wa adui yako ni adui yako pia’slogani hiyo ilimfanya amchukie Amney ghafla, ndiyo maana akaanza safari ya kuondoka zake.
Mshtuko aliopigwa nao Ahmed haukuwa na kipimo chake,sio yeye tu!Hata Amney pamoja na Necka Golden walipigwa na butwaa na kilichowafanya washangae zaidi ni kuona mkono mmoja wa Ahmed una pingu, kumaanisha kwamba yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.Licha ya yote hayo fununu walizosikia ziliwaogopesha mno na kufanya wamuonee huruma sana.
“Pole Mme wangu”
Necka Golden,akajitoa mshipa wa aibu!Akaropoka,Amney akashtuka na kumtizama.Ahmed akakunja sura akatamani atoe kauli chafu lakini akajizuia kidogo,akamtizama Amney aliyesimama kando yake.
“Mme wangu,nakupa pole”
Necka Golden akasisitiza kwa mara nyingine,akihisi labda Ahmed hakumsikia vizuri.
“Nishapoa”
Mshipa wa aibu hakuwa nao siku zote msichana huyu mcharuko,alimuacha kila mtu kinywa wazi baada ya kuinama kidogo na kumpiga busu la mdomoni Ahmed,alihisi kumpenda kutoka moyoni na alikuwa yupo tayari kupambana kufa ama kupona!Mapenzi aliyokuwa nayo msichana huyu moyoni yalitisha mno,hakujali lolote kwake ilikuwa, mahaba niue!
“Necka,tuondoke nyumbani tayari tushamuona mgonjwa”
Amney alihisi kujuta kuongozana na Necka sehemu kama hiyo,mbaya zaidi hakua anajua kama angekutana na Hajrath.Historia ya Necka Golden na Hajrath ilijulikana kwamba hawapikiki chungu kimoja.Sinema iliyokuwa inachezwa hapo,ilikuwa ni mbaya mno.
“Neck…”
“Mimi siwezi kuondoka”
Akagoma kuondoka,akitoa sababu kwamba atabaki na mumewe mpaka akipona na ikiwezekana atakuwa tayari kuongozana naye gerezani wafungwe pamoja!Hiyo ilimfanya Amney aishiwe pozi akashindwa kutoa jibu la haraka,alichokifanya ni kuweka mkoba wake na kutoka nje!Hakuwa na jinsi na hakuwa mwenye uwezo wa kumlazimisha Necka Golden, aondoke.
“Amney”
Hatimaye Necka akaita akitoka nje,Amney akasimama.
“Turudi nyumbani tukapike chakula cha mgonjwa”
Necka Golden,akashauri.Kwenye hilo hakupewa sapoti yoyote ile alichokifanya Amney ni kunyamaza, wakaelekea stendi ya mabasi ili kutafuta daladala!

****
Hajrath aliumia mtima,kila kitu kwake akaona kimebadilika kabisa!Hakuwahi kumchukia mtu lakini siku hiyo alihisi moyo wake unauma, baada ya kumuona Necka Golden hospitalini,alimchukia ghafla!Matukio mengi sana ya kuumiza yakaanza kujenga taswira ndani ya kichwa chake akawa kama anatizama filamu ya kuuzunisha.Licha ya hayo yote hakutaka kukata mguu kwenda hospitalini kumuona Ahmed,alihisi kumpenda mara mia yake!Wakati mwingine alitamani yeye ndiye awe kitandani yaani maumivu ya Ahmed ayachukuwe yeye,akiamini Ahmed anaumia sana kitandani.
Siku inayofuata akaamua kumkaangia nyama ya mbuzi,akatengeneza na juisi nzito ya maembe!Akafika navyo hospitali,alivyozama ndani moyo wake ukauma tena, baada ya kumuona Necka Golden pembeni ya Ahmed!Akageuza na kuurudia mlango lakini kabla ya kufika,Ahmed akamuita.
“Hajra..”
Hiyo ilimfanya ageuke,kwa ishara ya mkono akaitwa!Akatafakari kwa kiasi,macho ya Necka Golden yakawa kwake,wakatizamana kwa sekunde kama tatu hivi.
“Hapana,baadaye nitakuja”
Hajrath akasema kwa unyonge akiwa na kapu lililojaa mapocho pocho,hakuwa na jinsi ilibidi arudi nalo alipotoka,awaache Necka na Ahmed, wanazungumza!

****
Kifo cha bilionea George Charles kwake alikifananisha na siku ya sherehe kubwa ya X-mass,siku hiyo alizunguka huku na kule akiimba nyimbo mbalimbali akiwa chumbani.Akaingia kwenye friji na kubeba mzinga mkubwa wa pombe kali,akamimina kwenye glasi na kuanza kunywa kwa furaha huku akicheza bolingo na kutingisha kichwa.Alishaelewa kwamba amelala maskini na kuamka tajiri,akaanza kupiga picha maisha yake yatakavyokuwa,jinsi atakavyokula kuku kwa mrija akitembea nchi mbalimbali duniani.
“Rest in paradise Dear Husband…God needed you home, George”
Siku hiyo Lissa ilikuwa pombe nayeye,yeye na pombe!Alikuwa ana kila sababu ya kufurahia ushindi.Alichojizuia yeye na kukaa kimya ni kutoropoka kuhusu habari hizo za kifo cha Bilionea George Charles,akiamini kwamba angeunguza picha!Aliamini kwamba ni lazima kifo hicho kingetangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa kama CNN,AL JAZEERA na vingine vyote,hilo lilikuwa wazi kabisa!
Ilikuwa ni kama ametabiri vile na aliamini mpango huo ulienda vizuri sababu kulivyokucha tu,alipokea simu kutoka kwa Kamishna wa jeshi la polisi wilaya ya Kinondoni, Kamanda Erick Kyomo!Akimwambia kwamba anamuhitaji kituoni,haraka iwezekanavyo!
“Sawa afande.Kuna nini lakini?Kwema huko?Mbona tunatishana?”
Lissa akajifanya kubabaika simuni,alishaelewa ni kitu gani anaitiwa!
“Ni kwema tu,wala usijali Mama”
“Nakuja,nakuja sasa hivi.Kituo gani?”
“Central,Posta”
“Nakuja Afande”
Mchezo mzima na picha lote lilitengenezwa na mwanaume makini Patrick Mogera mlinzi wa Bilionea George Charles,akamshauri kwamba atulie kabisa ili wamnase Lissa Nzava kiulaini bila kutumia nguvu na hilo lilimfanya bilionea huyu atulie.Walichokifanya kitu cha kwanza ni kwenda kuripoti polisi tukio zima,wakaandika maelezo yote.Hiyo iliwafanya mapolisi wapindue habari hiyo na kilichoandikwa kwenye vyombo vya habari kulivyokucha ni kwamba polisi na majambazi walirushiana risasi.
Walifanya hivyo ili wakamilishe upelelezi wao,wakasubiri mpaka kupambazuke ndipo wakampata Kamanda wa Wilaya ya Ilala Afande Erick Kyomo!Askari huyu alikuwa mrefu mnene,mwenye mwili mkubwa!Muda wote alikuwa makini katika kazi yake,hata alivyozungumza na Lissa Nzava alitumia akili nyingi sana!
“Sasa nishampigia mkeo,atakuja hapa”
Akamgeukia Bilionea George Charles na kumwambia.
“Amesemaje?”
“Atakuja muda sio mrefu”
“Thank you”
“Kwani,mshawahi kuwa na ugomvi wowote ule?Mpaka akutumie majambazi?”
Kamanda Erick Kyomo akahoji kidogo,akitaka kujua inshu nzima.
“Sijawai kugombana naye,ndoa yetu hata miezi mitano.Haijafikisha!”
“Sasa kwanini atake,kukuuwa?Akutumie watu?Au uliwahi kumtishia?”
“I don’t know,nashindwa kupata jibu”
Bilionea George Charles,hakujibu kitu kingine chochote kile zaidi ya kulengwa na machozi ya uchungu, bado taswira ya yeye kuuliwa na kutupwa baharini ilijijenga kichwani na kumtesa sana.
Walichokifanya ni kumtoa eneo hilo na kumpeleka ndani ya gari dogo ili Lissa akifika asimuone kwanza.
lisaa limoja baadaye gari aina ya Range Rover VOGUE yenye rangi nyeupe ambalo kwenye ‘plate number’ limeandikwa jina GEORGE CHARLES,lilikuwa linapaki eneo la kituo cha polisi.George Charles aliliona na akajua ni lazima atakuwa mke wake,akatulia kidogo!Ni kweli,alikua niyeye kwani alimuona akishuka ndani ya gari na kuongoza mpaka kituoni.
“Habari afande”
“Karibu Mama,nikusaidie nini?”
“Namuulizia Afande Kyomo”
“Una miyadi naye?”
“Amenipigia simu muda mfupi uliopita”
“Jina lako nani?”
“Mrs.George Charles”
Hapo afande huyo alitulia kidogo,akamtizama mwanamke huyo kwa umakini kuanzia juu mpaka chini,ilielekea kuna kitu alikuwa anakiwaza.
“Kumbe ndio wewe?Subiri”
Afande huyo,akaingia kwenye ofisi kisha baadaye akamrudia.
“Pita”
Lissa Mnzava kwa mikogo,akatembea na kufungua mlango, ambapo ndani alikutana na Afande Kyomo,moja kwa moja alijua ni huyo sababu mara nyingi humuona kwenye tv.
“Karibu”
“Ahsante sana”
“Pole kwa kukusumbua asubuhi”
“Usijali,kuna nini?”
Alichokitegemea Lissa ni kusikia habari za msiba wa George Charles, ndiyo maana akaanza kuyakamua machozi akayaweka karibu kabisa ili akiambiwa tu,ayatoe hapohapo kwa fujo!
“Mara ya mwisho,kuonana na mumeo lini?”
“Jana”
“Hakurudi tangu jana?”
“Ndio”
“Alikwambia anaenda wapi?”
“Chalinze,kwenye kikao”
“Baada ya hapo alikupigia tena simu?”
“Ndio”
“Saa ngapi?”
“Usiku like kwenye saa nne hivi”
“Akakwambia nini?”
“Hatukuongea vizuri,lakini alichoniambia ni kwamba yupo kwenye matatizo simu ikakata”
“Yupo kwenye matatizo?”
“Ndio”
“Ulijaribu kumpigia?”
“Hapana..Ndi..o”
“Ulijaribu kumpigia?”
Afande,akalirudia swali lake!
“Ndio”
“Akasemaje?”
“Simu haikupokelewa”
“Ukachukua hatua gani?”
“Niliendelea kumpigia bila mafanikio”
“Baada ya hapo?”
Yalikuwa ni maswali ya kiwaki,yaliyomfanya Lissa achukie mno lakini hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima ayajibu ili asawazishe uwongo wake!Baada ya maswali kuisha,akaambiwa anahitajika waende Posta,baharini.
“Kuna nini huko?”
“Tuongozane,kuna mwili umeokotwa tuna wasiwasi ni wa mumeo Mr.Georg…..”
“No no no nooo….Please,afa…”
“Naomba tuongozane”
Kama kungekuwa na usaili bongo movie wa kutafuta waigizaji basi Lissa Nzava angepewa nafasi hiyo kwani alifanikiwa kukamua machozi ya gelesha, mililita mia moja sekunde hiyohiyo,akatoa na kamasi laini huku akimvuta vuta afande shati akimtingisha.
Aliendelea kulia bila kujua anafanya usanii kwenye jumba la sanaa kwani Afande Kyomo akajifanya kumuonea huruma nayeye akiigiza kumbembeleza,wakaongozana mpaka kwenye diffenda ambapo nyuma yao kulikuwa na gari nyingine tatu zinawafuata.
Wakafanikiwa kufika fukwe za Bahari ya Hindi,Kivukoni!Wote wakateremka lakini cha ajabu Lissa hakuona dalili ya mwili wowote ule.
“Nifuate”
Wote wakaongozana mpaka kwenye gari aina ya Corolla,huko buti lilifunguliwa.Kilichoonekana ilikuwa ni maiti ya mwanaume,amelowa damu ana matundu ya risasi.Lissa akaogopa na kufunga macho yake!
“Unaweza ukaitambua hii maiti?”
“Ndio..Hapana”
“Iangalie vizuri”
Lissa hakuweza kuiangalia,aliogopa mno hakuweza kuigundua kwamba aliyekufa ni kati ya wanaume aliowatuma wamuuwe George Charles!Alichokifanya afande huyo ni kumchukua mpaka kwenye gari aina ya Prado.
“Umesema utaweza kuutambua mwili wa mumeo kama ni yeye?”
“Nd..io”Akajibu kwa kwikwi!
Mlango wa nyuma ukafunguliwa,George Charles akaonekana akiwa amekaa, machozi yanamtoka!
Moyo wa Lissa ukalipuka kama bomu akahisi unadundia mgongoni,nguvu za miguu zikamuishia.Hakuelewa kama yupo ndotoni ama mbele yake anauona mzimu!



Mshtuko wa Lisaa Nzava ulikuwa wa waziwazi kabisa,kiasi kwamba akafungua mdomo wake bila kujitambua.Butwaa alilopigwa halikuwa na kipimo chake.Mbele yake ndani ya gari, alimuona Mumewe wa ndoa Mr.George Charles, ilikuwa tofauti na matarajio yake!Alichokuwa anakitarajia kwenye akili yake angekuta mwili wa Mumewe lakini ilikuwa ni kinyume kabisa,kwa sekunde tano nzima akili yake ilikuwa imeganda kama barafu hakuelewa alie ama afurahi, kwake kila kitu kikawa kama kiini macho!
“George Mme wangu,Mz…i.ma Mungu ni mkub..wa.Nilijua umekufa”
Msichana huyu alikuwa ni msanii mpaka askari walipigwa na butwaa kwani alitoa machozi hapohapo na kuanza kuangua kilio cha kwikwi,hakuelewa kwa kuongea maneno hayo ilikuwa ni sawa na kukamilisha ushahidi.
“Mama..Upo chini ya ulinzi.Acha kuleta usanii”
Kauli hiyo ilitoka kwa ASP Peter Machabe,aliyekuwa kando yake!Na katika kauli hiyo hakukuwa na mzaha hata kidogo ndiyo maana akamsogelea na kumvuta kando.
“Kwa kosa gani?”
Lissa akauliza kwa ukali kidogo.
“Utajua,tuongozane kituoni mpumbavu wewe”
“Embu niache”
Lissa kwa kiburi,akabetua mkono wake hiyo ilifanya askari ayumbe kidogo sababu kitendo hiko hakujiandaa nacho!
“George,waambie hawa mbuzi waniache.Hawanijui vizuri”
Uwezo wa kifedha aliokuwa nao George Charles kwa wakati huo alikuwa ana uwezo wa kusema lolote na askari wakatii,ndiyo maana Lissa akahitaji msada huo kutoka kwa Mumewe,lakini cha ajabu George hakujibu chochote akabaki anamtizama!
Machozi yalikuwa yakimlenga licha ya hayo hakutaka kuonesha udhaifu huo,akatoa kitambaa na kuangalia upande wa pembeni,akiamini kuendelea kumuangalia Lissa angezidi kuumia mtima!Hakukuwa na msaada wowote ule,Lisaa Mzava aliwekwa chini ya ulinzi na kupakiwa nyuma ya diffenda,alivyotaka kujua kosa lake hakuna askari yoyote aliyekuwa tayari kuzungumza!Lakini wakiwa katikati ya safari aliyokuwa ana uhakika kwamba wanaenda kituo cha polisi afande mmoja akatoa Laptop akaiwasha,baada ya dakika mbili juu ya kioo ikaonekana sura ya Lissa Mnzava,jambo hilo lilimshtua baada ya kuona sura yake, mbaya zaidi na maneno aliyokuwa anazungumza kuhusu mikakati na harakati za kumuua George Charles akiwa seblen.
Nguvu zilimuishia hapohapo,akaelewa nini kinaendelea!Hakufanya kitu kingine zaidi ya kulia machozi,akaanza kujuta kwa kila kitu alichokifanya,akatamani muda urudi nyuma abadili kila kitu kilichotokea lakini muujiza huo, usingeweza kutokea hata kidogo!Akili ya George Charles,ilishindwa kufanya kazi kwa wakati huo,ikawa kama imeganda japokuwa safari ya kuelekea kwake ilianza lakini hakulitambua hilo mpaka aliposhtuka yupo nje ya geti lake,gari likaingizwa ndani mpaka kwenye maegesho maalum!Mlinzi akashuka na kumfungulia mlango.
“Nipeleke Muhimbili hospital”
George Charles akasema.
“Bosi,unahi…”
“Nipeleke”
Hakuweza tena kupinga kauli ya bosi wake,alichokifanya ni kurudi ndani ya gari na kuliwasha kwa safari ya kuelekea,hospitali ya taifa ya Muhimbili alivyotaka kumuhoji ni kwa ajili gani,akasita kwani jambo hilo halikuwa swala lake!

******
George Charles,alitaka kufika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa jambo moja tu,kumuona Yusrath ili waongee hata hivyo alitamani kujua mkasa mzima wa watoto mapacha kama ni wake kweli,alitamani sana iwe hivyo!Kwani katika ndoto yake moja wapo alitamani itimie ni kuitwa baba,ndiyo maana alivyowasili hospitalini tu, akataka kuonana na Yusrath,jambo hilo halikuwa tatizo.Akaruhusiwa na kuingia moja kwa moja,ambapo huko alimkuta akiwa na watu wamesimama.Hakumtambua hata mmoja lakini aliwasalimia na kumuangalia Yusrath.
“Unaendeleaje?”
Lilikuwa ni swali la kwanza kuuliza!Kila mtu aliyesimama kando ya kitanda cha Yusrath alimtizama George Charles, kwa macho fulani ya viulizo.Sio siri,hapo ndipo walipojua kwamba watoto mapacha ni wa mwanamme aliyesimama,hakukuwa na haja ya DNA.Mbaya zaidi,sura ya George tayari ilikuwa maarufu kutokana na magazeti kumuuzisha sura!
“Georgee”
Yusrath,akaita na kutoa mkono wake kama mtu aliyetaka faraja fulani.
“Naaam”
“Umekuja saa ngapi?”
Sauti yake ilikuwa ya chini lakini ilisikika vizuri sana!
“Nimeingia sasa hivi,nahitaji tuongee”
Sentensi hiyo ilimfanya Yusrath awatizame ndugu zake, waliokuwa makini kuyafatisha mazungumzo yao!Alitamani kusema anahitaji watoke lakini alishindwa,akarudisha macho kwa George!
“Tutaongea baadaye”
“Saa ngapi?”
“Nenda kazini kwanza”
“Sitoweza kufanya kazi,akili yangu haipo sawa.Nitakusubiri hapo nje”
George Charles,hakua na punje ya mzaha hata kidogo!Akatoka nje na kukaa kwenye benchi,ambapo hapo alikaa nusu saa lizima,akitafakari maisha yake kwa ujumla!
“Uncle,samahani.Habari yako”
Salamu hiyo ilimshtua kutoka kwenye mawazo mengi sana!
“Mimi naitwa Salma,binamu yake na Yusrath”
“Ahsante,nashukuru kukufahamu”
“Naweza kukaa?”
“Yes,unaweza”
George Charles akasogea kidogo,hapo akaendelea kujitupa kwenye mawazo!
“Ulikuwa na muda gani na Yusrath tangu mjuane?”
Swali hilo lilimfanya George Charles ashtuke,akamtizama Salma msichana mdogo mwenye asili ya kipemba kwa mbali,hiyo ilitosha kabisa kusema wana undugu na Yusrath, kutokana na asili zao kwani hata nywele zao zilifanana,Salma alikuwa na nywele za singasinga!
Kabla ya kujibu swali la Salma,alianza kutafakari ni kwanini kauliza swali kama hilo.
“Sio muda mrefu sana!Ni rafiki mzuri,pia tulijuana ofisini”
Hapo Salma alitabasamu sababu jibu alilotoa George Charles,lilikuwa tofauti na matarijio yake, hata hivyo hakuona haya kuuliza moja kwa moja.
“Umezaa na Yusrath,hakuna asiyejua!Watoto wale,haina haja ya DNA.Nachokuomba shemeji,usikubali chukua watoto wako,ile ni damu yako”
Maneno hayo yalimfanya George Charles,amtizame msichana huyo aliyekuwa makini na hoja zake!Hakuelewa ni kwanini anayatamka maneno hayo bila uwoga!
“Na ni kwamba majuzi walitaka kuuliwa,wanawindwa.Fanya unavyoweza,watoto watakufa”
“Nani,anataka kuwauwa?”
“Mme wake,anaitwa Ahmed!”
Salma alimaliza na kuondoka zake huku nyuma akimuacha George Charles,asijue ni kitu gani akifanye!

*****
Mguu mmoja ulikuwa begani kwa Kassim,mwingine umenyooka!Wapo uchi wa mnyama kiuno cha Kassim kinapanda juu ya kushuka,kinaenda kushoto na kulia.Anakikoroga taratibu mno!Hiyo ilimfanya mwanamke aliyekuwa chini afumbe macho yake na kuyavuta mashuka.Raha alizohisi hazikuwa na kipimo kamili,ndio maana nayeye alikinyonga kiuno chake ili asionekane gogo na kutoa sauti za puani na mara nyingi, alitoa lugha nzito zisizokuwa na tafsida.
“Aasssshsss bei..biii aashss aaaaah aaaaah naku..upeeeendaaa”
Rhoda Denis,alikuwa na kila sababu ya kuzungumza maneno hayo,kwa jinsi mambo yalivyokuwa!Kwa staili aliyowekwa ilikuwa rahisi kuomba mdomo na kupewa, hapohapo wakaanza kulana denda kwa fujo,hiyo ikamfanya Kassim,achomoke kwake na kumbinua vizuri,akamuweka kwenye kingo ya kitanda.
Rhoda akawa ameshika kitanda, yaani Mbuzi kagoma kwenda majanini.Kiuno chake kikashikwa vizuri na mikono miwili,hapo bila kuchelewa Kassim akaanza kupeleka majeshimajeshi!Kelele zikazidi,Rhoda akageuka kidogo ili wapigane denda tafsiri ya kitendo hiko ilikuwa ni kufika kitonga.Hiyo ikamfanya fundi ama hodari Kassim azungushe kiuno chake kama feni huku mkono wake mmoja akiupeleka kwenye kifua cha Rhoda na kuanza kutomasa chuchu,haikuchukuwa hata sekunde moja,Rhoda akafunga goli hapohapo Kassim akasawazisha kisha wote wakatulia kitandani.
“Darling”
Rhoda akaita huku kwa mbali akiwa anahema,jasho linamtoka!
“Yes”
“Leo umeniweza,umepaka Mundende nini?”
“Ndio kitu gani?”
“Vumbi la Kongo”
“Situmii huo upumbavu,najiamini!Madawa ya nini mimi?Nimekula zangu ugali wa dona na maziwa”
“Nakutania baby,unajua nakupenda sana eeeh”
“Yes naelewa,mke wangu!Asa sikia,mimi naenda sehemu moja hivi.Nawahi,tutawasiliana”
“Wapi unaenda tena?Unaenda kwa videmu vyako au?”
“Hapana,mshua ameniagiza sehemu si umeona mpaka ameniachia ndinga”
“Alafu hujaniambia hali yake”
“Anaendelea vizuri sasa hivi”
“Msalimie”
“Sawa..”
“Baby,twende basi kimoja cha mwisho”
Rhoda Denis,bado alikuwa ana kiu na alihitaji kuipooza lakini hilo likashindikana sababu Kassim alionesha kuwa mwenye haraka kuliko upesi.
Akavaa suruali yake na kubeba funguo,bila kuaga wala kugeuka nyuma akafungua mlango na kuondoka zake!
Rhoda Denis hakuwa na sehemu ya kwenda hata hivyo hakutaka kubaki gesti peke yake,akamkumbuka Ahmed ghafla na kupata wazo la kwenda kumuona hospitalini,taratibu akajizoa kutoka kitandani na kuingia bafuni huko alioga kisha kujiandaa!
Hakutaka kupitia popote zaidi ya kwenda kwenye mgahawa maarufu wa KFC uliopo kariakoo,huko alinunua kuku na chips pamoja na soda, akafunga vizuri.
Kwa kuwa alitaka kufika mapema alichukua pikipiki,ndani ya dakika kumi na mbili akawa yupo nje ya geti anamlipa dereva ujira wake,akashika vizuri mifuko na kuanza kutembea!
Japokuwa alikuwa ni mme wa mtu lakini alimpenda sana na hakuwa tayari kumuacha hata kidogo,ilikuwa ni bora agombane na Yusrath ama akubali kushea naye lakini sio kumuacha Ahmed,ndio maana alifanya juu chini kuhakikisha anaenda hospitalini na kumuangalia,alikuwa mwenye kila sababu ya kufanya hivyo kutokana na upendo wa ajabu aliokuwa nao moyoni.
Ahmed hakuwa mwanaume wake wa kwanza kumpenda lakini alikiri katika waliopita Ahmed alikuwa ni tofauti sana na wengine,kilichochangia kumfanya amuweke kati ya wanaume bora ni uhodari wake kitandani.Licha ya yote aliamini muhogo ni mmoja lakini kila mtu ana mapishi yake na mapishi ya Ahmed yalikuwa yana viungo vingi!Alivyofika mapokezi,haikuwa kazi ngumu kuelekezwa ni wapi wodi alilolazwa Ahmed.Akatembea na kuufungua mlango ambapo ndani alikutana na msichana mmoja,maji ya kunde mwenye mwili mdogo!Sura hiyo haikuwa ngeni machoni mwake,akawa ana kazi ya kurudisha mafaili kichwani kwake akijaribu kuivuta sura hiyo aliwahi kuiona wapi lakini hakupata jibu la haraka,hata hivyo hakutaka kujishughulisha naye!
“Pole Ahmed,nimekuletea chakula”
Rhoda akasema,hakuelewa kwamba Necka Golden alikuwa pembeni nayeye anamtizama.Mapozi aliyoonesha Rhoda na namna alivyotoa chakula kimahaba ilimfanya Necka Golden, asikilizie kidogo,akamtizama Rhoda ambaye alitoa kipande cha kuku na kuanza kumlisha Ahmed.
“Nimeshiba nitakula baadaye”
Hatimaye Ahmed akasema,Rhoda akajitahidi kumbembeleza kwa staili ya kumuwekea paja la kuku mdomoni.
“Amesema ameshiba,atakula baadaye”
Necka Golden akaingilia na aliongea hivyo makusudi ili kupima maji.
“Ndio alivyo Ahmed,hapendi kula bila kumlazimisha hatokula lazima ale ili apate nguvu”
“Wewe ni daktari?”
Necka Golden akauliza kwa shari.
“Yawezekana”
“Una taaluma gani? Hata darasa la saba hujasoma”
Sentensi hiyo ilikuwa ni kejeli kubwa sana kwa Rhoda Denis,tafsiri yake ilikuwa ni dharau kubwa mno!Akakunja sura ghafla,mashavu yakamvimba kama chura,akafura kwa hasira!
“Unasemaje wewe ngedere?”
“Nani ngedere?Ngedere baba yako mzazi al….paaaaaa”
Kilichosikika hapo kilikuwa kibao kikali kilichomfikia Necka Golden usoni, akayumba kidogo na kuona nyota na kuhisi kama sikio lake moja la kushoto lililozibuliwa na kibao limeziba,akaona maluweluwe.
Hata hivyo hakukubali nayeye akarusha kofi likamfikia vizuri sana Rhoda Denis,shavuni lakini hakuyumba kama alivyoyumba yeye.Rhoda Denis nayeye akajibu kwa kurusha kofi safari hii lilimfikia Necka Golden na kumtupa kitandani,akamuangukia Ahmed.Hapo Rhoda Denis,akamvaa kama chui anayemrukia Swala na kuanza kumvuta huku na kule,akalichomoa wigi la Necka lililokuwa kichwani,nywele zake za mabutu zilizokua na vumbi vumbi hazina mpangilio maalum zikaonekana,akageuka akawa kama kituko fulani na badala ya kuendelea kurudisha mashambulizi akawa analitafuta wigi lake,hapo ndipo alishushishwa makonde ya kichwa na Rhoda Denis,waliendelea kumkandamiza Ahmed aliyekuwa kitandani anapiga kelele za maumivu lakini hakuna kati yao,waliomsikiliza!Mbaya zaidi ngumi hizo zilikuwa za kimya kimya, hakuna hata mmoja aliyezungumza,kilichosikika ni vishindo tu!Ghafla mlango ukafunguliwa,mtu waliyemuona mlangoni kashika mfuko mweusi,aliwafanya wasitishe kupigana kidogo ingawa walikuwa wamechelewa tayari kwani kwa picha iliyoonekana hakukua na haja ya kujielezea kwamba walikuwa wanapigana misumbwi!Aliyeonekana kushtuka zaidi alikuwa ni Rhoda Denis,sura ya Kassim ilimuogopesha mahali hapo!
Kilichomjia kwa haraka kichwani kwake ni kuwa Kassim alikuwa akimfuatilia na siku hiyo alimfumania,kumbe haikuwa hivyo Kassim alifika mahali hapo ili kumjulia hali Kaka yake!
“Rhodaaa”
Kassim,akaita kwa staili ya kushtuka hiyo ilimfanya Ahmed aliyekuwa kitandani amtizame mdogo wake na kuanza kujiuliza,amemjuaje mwanamke huyo!



Mikikimikiki aliyopitia Ahmed, tena sambamba ikiambatana ilimfanya atafsiri jambo hilo na mkono wa mtu yaani kuna mtu nyuma ya hilo hapendi maendeleo yake kabisa!Haikuwezekana hata kidogo kwa binadamu wa kawaida, kuandamwa na majanga mfululizo.
Japokuwa alikuwa amesoma mpaka chuo kikuu lakini siku hiyo alianza kuwaza mambo ya Kiswahili,kilichomuaminisha kwamba ni lazima atakuwa amefanyiwa mauzauza ni baada ya kumkumbuka rafiki yake Razaki Kipolio!
Majanga yaliyomkuta rafiki yake mfululizo kama kufiwa na mkewe,kuuguliwa na mwanaye kufukuzwa kazi yalimfanya rafiki yake huyo aende kwa waganga wa kienyeji na huko baada ya mwezi mmoja tu mambo yake yakawa shwari akarudi kwenye chati!
Akaamini kwamba uchawi upo na waganga wanafanya kazi.Lakini nafsi nyingine ya pili ilimwambia aachane na mambo hayo kwani Mganga ni Mungu peke yake,akiwa yupo katikati ya mawazo makali na alivyokuwa akitafakari alikuwa ni kama mtu anayejitazama kwenye kioo kikubwa cha televisheni tena anaangalia sinema ya kusisimua,kila kitu kilijijenga taswira kichwani kwake.Ndio hapo alishtuliwa na Necka Golden, baada ya kuingia na kumsalimia akitaka kujua hali yake,Ahmed alihisi faraja kubwa na kujiona kama amepona,haikuchukuwa muda mrefu akaingia Rhoda Denis!
Akatulia kidogo,wasichana waliosimama mbele yake kandokando ya kitanda wote alishawahi kutembea nao kingono kwa nyakati tofauti tofauti,ilimbidi anyamaze na kuwaangalia wanavyobishana na kubadilishana maneno!Haikuchukuwa hata dakika mbili, wakaanza kupigana na kutupana huku na kule!Necka Golden na Rhoda Denis, waliendelea kurushiana makofi, mpaka mlango ukafunguliwa na wa kwanza kushtuka alikuwa ni Rhoda,kitendo cha kumuona Kassim mlangoni kilimshangaza,jambo hilo lilishuhudiwa na Ahmed.
“Unafanya nini huku?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Kassim,hakutegemea kumkuta Rhoda mahali hapo kwani muda mchache uliopita alimuacha gesti,baada ya kufanya ngono!
“Nimekuja kumuona rafiki yangu”
Rhoda,akajitetea akiongea kwa sauti ya chini ili Ahmed asisikie!
“Rafiki yako gani?”
“Rafiki yako?Kahaba wewe?Kaka samahani,mimi sikufahamu lakini huyu sio rafiki yake,awara wake”
Necka Golden,alipasua jipu akiropoka mbele ya Kassim, hiyo ilimfanya Rhoda Denis ahisi kama amepigwa na shoti ya umeme!
Akabaki ameduwaa asijue ni kitu gani akijibu ili ajitetee kwani lilikuwa ni fumanizi la aina yake,kila kitu kilichotokea hakutegemea kabisa!Katika kutaharuki na mshangao asijue ni kitu gani akifanye,mlango wa wodi waliokuwa ukasukumwa,akaingia mwanamme mmoja mrefu kiasi,amevaa shati jeupe linalombana suruali ya Kadeti na mkononi alikuwa amevaa saa yenye rangi ya ‘Gold’kila mtu alimtambua mtu huyo,haikuwa rahisi kwa mtanzania kutojua sura ya Bilionea George Charles inafanana vipi.
Mbali na hapo,mkasa uliotokea na kumfanya mpaka Ahmed alazwe ndio kabisa ulifanya kila mtu atake kuifahamu vizuri sura ya mwanamme huyo!Nyuma ya Bilionea George Charles, alifuata mwanamme mwingine pande la mtu aliyeshiba kwa mazoezi,kifua kipana kama sokwe na mkono wake mnene kama paja la tembo hacheki yupo siriazi muda wote,macho ya watu wote ndani ya wodi yakawaangalia wao!Sio siri,ujio huo ukafanya kila mtu abaki kimya ndani ya chumba hiko!
“Habari zenu”
Bilionea George Charles alisalimia kwa kifupi huku akimtizama kila mmoja wapo usoni, kwa zamu.
“Salama”
Wakajikuta wanaitikia kwa pamoja huku wakimshangaa Bilionea George Charles,anayetembea taratibu mpaka kilipo kitanda cha Ahmed.
“Unaendeleaje?”
George Charles akauliza lakini Ahmed hakuwa tayari kujibu chochote,hasira zilianza kumpanda taratibu kwani mwanamme aliyesimama mbele yake ndiye mkandarasi wa kila kitu kutokea,ndiyo huyo aliyefanya mpaka amelala kitandani,ndiye huyo aliyevunja ndoa yake na kumnyang’anya furaha yake mbaya zaidi alimzalisha mkewe,haikuwa rahisi kwa mwanamme yoyote Yule kukubali dharau kama hiyo.
Ahmed aliwaza vitu vingi sana kabla ya kujibu salamu hiyo,vitu vingi mno vilipita kichwani kwake, kipindi cha nyuma Yusrath aliyekuwa na misimamo,akamkumbuka namna George Charles alivyomuajiri Yusrath katika kampuni yake!
“Ahmed”
George Charles ilibidi aite,alivyoona salamu yake haijaitikiwa.
“Unataka nini?”
Hatimaye Ahmed akajibu kwa shari,kifua chake kilianza kupanda juu na kushuka kwa jazba akatamani ainuke kitandani aanzishe varangati kwani bado alikuwa mwenye hasira sana!
“Nahitaji tuzungumze kama wanaume”
“Sina muda wa kuzungumza nawewe”
“Ni kwa faida yako lakini il…”
“Broo,naomba uwende sihitaji matatizo mengine.Haya niliyokuwa nayo yananitosha!Tafadhali,mchukue huyo mpumbavu mwenzako muende”
Ahmed alimaanisha baunsa wa George Charles,hiyo ilifanya pande hilo la mtu limtizame Ahmed na kutamani amchomoe kwenye kitanda ampige vitasa kwani Ahmed hata mkononi kwenyewe alikuwa hajai lakini asingeweza kufanya hivyo kutokana na bosi wake kuwa pembeni yake.
“Ondokeni bwana,sitaki kukuona!Na sihitaji kuzungumza nawewe”
Ahmed alifoka kwa sauti, hiyo ikamfanya Bilionea George Charles ageuka na kumtizama baunsa wake ama mtu aliyemwajili kwa ajili ya kulinda usalama wake,akampa ishara ya kichwa kwamba waondoke,pande hilo la mtu likaongoza mbele mpaka mlangoni hapo akafungua mlango na wote wakaondoka huku nyuma wakiwaacha Ahmed,Rhoda,Necka,Kassim wanawasindikiza kwa macho!
“Na nyie,sitaki kuwaona vilevile.Ondokeni”
Hiyo ilimaanisha Necka na Rhoda,hawatakiwi.
“Hee!Yameshakuwa hay…”
“Ondokeni nimesema,Kassim naomba nitolee hawa nzii”
Ahmed alimaanisha kile anachozungumza,hakutaka kumuona mtu yoyote mahali hapo.
Kila kitu kikawa kimevurugika tayari sura ya George Charles ilimfanya ayakumbuke maumivu na kutoneshwa kidonda cha moyoni kilichoanza kukauka.
“Broo,vipi?”
Kassim akarudi ndani baada ya kuwatoa Rhoda na Necka nje!
“Nahitaji kupumzika”
“Sawa,broo!Unamfahamu huyo demu?”
Kassim akashindwa kubaki na dukuduku hilo moyoni.
“Demu gani?”
“Rhoda”
“Rhodaa?”
“Ndio Rhoda”
“Simfahamu,nahitaji kupumzika Kassim!Tutaongea baadaye”
Ahmed,alijibu kwa mkato hakuwa na mudi tena ya kuongea vitu vingine zaidi!Akageukia upande wa pili na kufumba macho yake.

*******
Alichotaka ni damu yake na kuhakikisha kwamba anawachukua watoto na kuwalinda kwa njia yoyote,alikuwa yupo tayari atumie nusu ya utajiri wake ili awakinge na chochote kile, swala la Ahmed kutaka kuwaua lilimfanya apange mikakati ya kuwawekea walinzi na hakutaka kufanya jambo hilo kichwakichwa,ndiyo maana akamshirikisha rafiki yake ambaye siku zote akikwama humwambia.
“Listen to me George,una uhakika wale watoto ni wako?Wewe ni msomi,fanya vitu kisomi vyenye uhakika,usibahatishe”
Siku hiyo kulikuwa na kikao cha watu wawili ndani ya ofisi ya George Charles,wakijadili jinsi ya kufanya na mtu mmoja anayeitwa Gaudence Mgunda,rafiki yake wa karibu na mfanyabiashara mwenzake pia.
Walikuwa ni marafiki walioshibana lakini kutokana na majukumu kuwa mengi,kwao inakuwa sio rahisi kuonana mara kwa mara!
“What do you mean?”(Una maana gani)
George akauliza huku akiikunja mikono yake kwa pamoja kifuani na kuegamia kiti chake kikubwa cha kuzunguka akisubiri wazo kutoka kwa Gaudence!
“Tafuta advocate,fungua kesi.Ukawapime watoto DNA,chif!Hiyo ni kama kesi,umemzalisha mke wa mtu akiwa ndani ya ndoa!”
“Whaaaat,hapana!Mimi sikujua.Nilitembea na yule binti one night stand,sikutegemea kama mimba imeingia,sikua najua”
“Sasa una uhakika gani kama wale watoto ni wako?”
“Nimeambiwa”
Hapo George alisimama kutoka kwenye kiti na kuliendea dirisha la kioo,akatizama chini. Kutokana na kuwa juu ya gorofa akawa anayaona magari kwa chini na watu wanatembea.
Baada ya hapo,akashika meza kwa mikono miwili na kumtizama Gaudence.
“Watoto wale ni wangu,nitafanya juu chini niwapate.Kwa gharama yoyote ile.Alafu kitu kingine Gau”
“Kitu gani?”
“Nataka nimchukue na Mama yao”
“Ebu maliza kwanza jambo moja,tafuta mwanasheria ili mkapime DNA,George hii inshu ni kubwa, sio ndogo kama unavyodhani.Kwa kufanya hivyo naamini utakuwa safe side”
“Fine,nitafanya hivyo”
“Wacha niwahi ofisini kwangu”
Bilionea George Charles akawa amepata wazo jipya,ushauri wa rafiki yake ukawa umemwingia na haraka akaufanyia kazi kwani dakika hiyohiyo akaanza kumtafuta mwanasheria ili mchakato mzima wa kupima DNA uanze!
Mr Yohana Malenda, ndiye mwanasheria aliyemuona anafaa kwa kazi hiyo,hakutaka kupoteza hata nukta ya muda wake, akamtafuta hewani na ndani ya dakika arobaini na tano akawa yupo ofisini!Hakukuwa na maongezi mengine zaidi ya kumpa mkasa mzima na mchakato unavyokwenda.
“Ni jambo dogo sana,huwa napenda kuwashauri wateja wangu.Watume sampuli zao nchini Afrika kusini”
“Mimi nakusikiliza wewe,ilimradi majibu wasichakachue”
“Hawawezi,ndiyo maana nimekwambia hivyo”
“Hao watoto wapo hapa Dar es salaam?”
“Ndio”
“Mama yao?”
“Pia yupo”
“Mme wa huyo mwanamke?”
“Yupo pia hapahapa”
Kilichofuata hapo ni George kutaja ni wapi Ahmed na Yusrath wanapatikana ili barua ichapwe kisha wapelekewe na mchakato mzima uanze mara moja!

*****
Kwa kiasi kikubwa alimpenda sana Ahmed,kwa chochote kitakachotokea alikuwa yupo radhi kujitoa muhanga.Kama aliweza kunywa sumu kwa ajili yake kipindi wapo chuoni Makumira akitaka kufa kwanini ashindwe na mengine.Siku zote akaamini kwamba ‘True love never die’Yaani penzi la kweli haliwezi kufa,hapo ndipo aliamini Mungu alimleta Ahmed duniani kwa ajili yake na sio vinginevyo.
Licha ya misuko suko yote kutokea katika maisha yao lakini aliamini ipo siku moja atakuja kutulia na Ahmed, wajenge familia.Licha ya kukumbuka mambo mengi, bado tukio na unyama aliofanyiwa na Florian Fredrick ulimpitia kichwani na alikuwa na makovu ya risasi mwilini mwake.
Hiyo ilitosha kabisa kutafsiri nini maana halisi ya maisha!Wakati barua kutoka kwa mwanasheria aliyetumwa na George Charles inaletwa hosptalini yeye alikuwa kandokando ya Ahmed,anamlisha chakula.Barua hiyo ikashikwa na Ahmed akaisoma kwa uchungu sana,machozi yalimlenga na alijizuia kulia.
“Ahmed,kuna nini?”
Ilibidi Hajrath aulize,hata hivyo hakujibiwa ikabidi achukuwe karatasi hiyo na kuanza kuipitia!Hata yeye alishtuka kusikia kwamba kuna kesi nyingine ya maswala ya DNA,akamtizama Ahmed kwa macho yaliyojaa masikitiko makubwa sana,alimuonea huruma kwa kipindi kigumu alichokuwa anapitia.
“Ahmed,usijali kila kitu kitaisha.Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”
Hajrath,akasindikizia maneno yake na msamiati wa kibongo ili kupigilia msumari maneno yake!
Siku hiyo Hajrath,alimfariji sana Ahmed akimwambia kila kitu kitakuwa sawa na maisha yataendelea,ili mradi ana uhai!Ahmed akahisi kupona,akamtizama Hajrath kuanzia juu kwenye nywele zake,alizosuka rasta akayaangalia macho mazuri ya msichana huyo ya duara makubwa kiasi,yenye ushawishi mkubwa kwa mwanamme yoyote lijali,akashuka chini zaidi na kutizama midomo ya Hajrath iliyokuwa milaini iliyobeba ‘lips’ pana kiasi,hakuishia hapo.Macho yake yakatua kwenye kifua kilichosimama vizuri ndani ya blauzi, aliyovaa.
Akahisi damu yake inamwenda mbio,akili yake ikahama ikasafiri kwa kasi,akajiona miaka iliyopita alivyokuwa na Hajrath kitandani, wanafanya ngono!Mapendo aliyokuwa anapewa na Hajrath alikuwa kama anayatizama kwenye kioo,akajikuta anajuta kumsaliti kiumbe huyu mrembo!Ambaye alikuwa ni mpole na mwenye moyo wa kipekee,sio siri siku hiyo alikiri kwa mara nyingine kwamba Hajrath Mpilla ni msichana mzuri kuanzia ndani mpaka nje,alivyopeleka macho yake chini akakumbana na shepu iliyojichonga vizuri,ikafanya nyuma awe na mzigo mkubwa.
Hapo Ahmed akashusha pumzi ndefu,hakuelewa kwamba Hajrath alimsoma na alielewa ni kitu gani anawaza kwani hata macho ya Ahmed yalibadilika,mbali na hapo alishawahi kuishi na Ahmed kupika kupakua, akajua kivyovyote vile fikra zake zipo kwenye ngono!
“Utapona mpenzi wangu,nakupenda sana”
Moyo wa Ahmed,ukalipuka kama bomu la nyuklia baada ya kusikia sentensi hiyo,alikuwa ni kama hakutegemea kusikia kitu kama hiko, kutoka kwa Hajrath.
“Nakupenda pia”
Wakiwa katikati ya maongezi yao ya mahaba,kila mtu akivuta hisia na mwenzake,mlango ukafunguliwa wote wakatupa macho mlangoni!
Akaingia Mama mmoja mnene kiasi,nyuma ana maaskari watatu pembeni kuna mwaamme mwingine amevalia koti jeupe huyo alikuwa daktari!Ahmed akajua nini maana yake sababu Mama huyo alikuwa ni mkwewe yaani Mama Yusrath,akatulia kidogo ili ajue nini kitaendelea.
Hakukua na maongezi mengine zaidi ya daktari kufika na kuandika andika maelezo fulani kisha kuwageukia maaskari.
“Huyu mgonjwa,kwa sasa hali yake ni nzuri tu.Labda cha kuongeza,tumpatie dawa za maumivu atameza”
Ilikuwa ni kauli iliyotafsiriwa kwamba tayari ameruhusiwa na askari wapo eneo hilo kwa ajili ya kitu kimoja tu,kumchukua na kuondoka naye!Ni kweli,alikuwa kama ametabiri vile sababu pingu yake iliyokuwa mkononi ilifunguliwa.
“Simama”
Afande mmoja,aliyeonekana ana usongo na Ahmed alitoa amri,hiyo ikamfanya Ahmed atafakari kidogo hakuwa na nguvu ya kusimama ghafla kama wanavyodhani.
“Ebwana,usitupotezee muda!Simama”
“Kwani nimekwambia sisimami?”
Ahmed akajibu kwa hasira,Hajrath alikuwa pembeni anashuhudia kila kitu kinachoendelea machozi yanamlenga ilikuwa ni picha mbaya sana kwake,alijisikia uchungu ajabu!
Kitendo cha Ahmed kusimama,walimshika huku na kule na kumkokota kwa nguvu mpaka nje!
Ambapo huko walimpakia ndani ya diffenda na safari ya kwenda kituoni kuanza mara moja, hilo lilikuwa wazi kwamba ni lazima asomewe mashtaka kisha akafungwe gerezani, labda muujiza utokee!



Diffenda ya polisi iliyobeba askari sita,akiwemo Mama Yusrath pamoja na Ahmed ambaye alikuwa ndiye mtuhumiwa,iliwasili kituoni Tabata,Mwananchi majira ya saa tisa alasiri.
Ahmed,akateremshwa na kupelekwa moja kwa moja mpaka mapokezi,ambapo hapo alipokelewa na askari mwingine aliyekuwa zamu siku hiyo.Kama taratibu zinavyoenda siku zote akaulizwa majina yake na kesi inayomkabili ili faili lifunguliwe.
“Vua Mkanda,toa simu yako andika kila kitu pale fanya haraka”
Kama kawaida ya maaskari wa kitanzania,hawakuwa na kauli na sauti ya chini.Muda wote hufoka kwa sauti ya juu na kupiga mikwara mizito,hiyo ikamfanya Ahmed achukie!Hasira zake zikampanda,mapigo yake ya moyo yakazidi kupiga kwa nguvu hasa alivyokumbuka matukio yaliyotokea,ingekuwa ni bora angeuwa watoto kabisa ili akafungwe vizuri kuliko kuwakosakosa!Akamtizama askari huyo kama mtu anayetafakari kitu.
“Vua mkanda nimekwambia,usinikodolee macho kama samaki changu!”
Ahmed,akatii amri akafanya alichoambiwa akaweka kila kitu sawa,akashikwa begani kwa staili ya kusukumizwa mpaka nje ya nondo ambazo pembeni zilikuwa na kufuli kubwa sana na nzito,likafunguliwa akatumbukizwa ndani ambamo humo alikumbana na hewa nzito,kutokana na watu wengi kujaa!
Ndani ya chumba hiko kidogo kulikuwa na hewa finyu,harufu ya mikojo na majasho,ndizo zilizokuwepo, mbaya zaidi kulikuwa na dirisha moja dogo sana lililokuwa juu,ghafla akatamani kupiga kelele ili atolewe lakini aliamini hata angefanya hivyo,isingesaidia chochote!Akatembea mpaka pembeni na kwenda kujibanza akisubiri,hatma ya kesi yake!

******
Japokuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya Ahmed kuwadhuru watoto wake mapacha ambao hakuwa ana uhakika kama ni wake kweli lakini alijikuta anaingiwa na huruma mno!Moyo wake ulimsuta,kwa kitendo cha Ahmed kutupwa maabusu kilimkosesha rahaa sana!Alielewa maisha ya ‘lockup’ sio mazuri sababu hata yeye alishawahi kuwekwa kwa masaa matatu lakini siku hiyo alilionja joto la jiwe!Asingekuwa muungwana kama angeacha jambo hilo lipite bila kufanya chochote,hata Mungu angemlaani!Alichokifanya George Charles jioni ya siku hiyo ni kuwasiliana na ndugu wa karibu wa Mama Yusrath,kitu alichokuwa anahitaji ni namba ya Mama Yusrath,hilo halikuwa tatizo!
Akapatiwa na siku hiyohiyo akanyoosha mpaka Ilala,akapaki gari lake na kuingia ndani ambapo huko alimkuta Mama huyo akiwa na baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki.Akawasalimia na kuketi,ambapo hapo hakutaka kupoteza muda na kuzunguka mbuyu,akafunguka na kueleza kilichomfanya afike nyumbani hapo.
“George,hili swala naomba usiingilie”
Mama Yusrath,akamkatisha.Kitendo cha George kumkingia kifua Ahmed, kilimtia kichefu chefu Mama huyu.
“Mama,nimemkosea sana Ahmed.Hakustahili,najaribu kuvaa viatu vyake lakini havinitoshi”
“Vitakutosha vizuri tu,hujui alichotufanyia.Yule sio wa kututumia majambazi waje hapa”
“Hapana Mama,sio Ahmed”
George akafunguka,jambo hilo likafanya watu wote wamkodelee macho, wakitaka kujua nyuma ya hayo ni nani kahusika.
“Sasa ni nani?Kama sio Yule mwanaharamu,asiyekuwa na haya!Na nitahakikisha,anaenda jela.Tena kifungo cha maisha”
“Aliyewatuma hao watu ni mke wangu”
George Charles,akaweka kila kitu wazi.Hakuwa na sababu ya msingi ya kubaki kimya,akasema kila kitu kilivyotokea mbaya zaidi akazungumza mpaka mkewe alivyotaka kumuuwa akiwatumia majambazi,jambo hilo likamuacha kila mtu kinywa wazi.
Mama Yusrath akashikwa na aibu akaangalia chini na kuhisi kujuta kwa kitendo cha kumtuhumu Ahmed, ndiye mkandarasi wa kila kitu kutokea!
“Na watoto,alivyotaka kuwauwa je?Au umesahau?”
Mama akaibua hoja ili kuendelea kuweka pingamizi.
“Hasira tu Mama,mimi namfahamu Ahmed.Sijamjua jana wala juzi”
Kwa kasi ya umeme George Charles akakumbuka alivyomwagiwa juisi na Ahmed kwenye moja ya Mgahawa uliokuwa Mwenge, pia akakumbuka Yusrath alivyopigwa mbele yake lakini hilo hakutaka kuliweka wazi,mtu kama yeye kumwagiwa juisi na kuliongelea mbele za watu ulikuwa ni utoto,akabaki kimya na kuzidi kusisitiza kwamba wamuachie huru Ahmed kwani hana hatia yoyote.
“Hata mimi ningekuwa yeye,ningefanya alichokifanya.Wenda ningeua kabisa!Mama mimi ni mwanaume kama yeye,naelewa”
George Charles,akahitimisha!Hakuelewa hata yeye ni kwanini anamtetea sana Ahmed wakati alitakiwa awe mstari wa mbele,kumkandamiza!Juhudi zake zilionekana kufanikiwa kwani Mama Yusrath alilegeza kamba ingawa kishingo upande hata hivyo hakutaka kusema wazi kwamba amekubali moja kwa moja matokeo yake alisema ‘Utajijua mwenyewe’ jibu hilo tafsiri yake ilikuwa George Charles,apambane anavyoweza!
Swala hilo kwa Bilionea George Charles, lilikuwa ni sawa na kumsukuma mlevi kilimani,hapohapo hakutaka kupoteza muda akamtafuta moja kwa moja RPC Juma Mshana,hakutaka kujali kama ingekuwa ni usiku alichotaka yeye Ahmed Kajeme awe huru kwanza ili mambo mengine yaendelee ikiwezekana baada ya hapo waweke tofauti zao kando washikane mikono!
Simu ya Bilionea George Charles ilimkuta RPC Juma Mshana akiwa katikati ya miguu ya msichana mrembo,akifanya naye ngono usiku huo kwenye moja ya gesti,Buguruni Sewa!Alivyotupa jicho,akasitisha zoezi kwani Kamanda huyo alipenda pesa kuliko kitu chochote kile,ndio maana alisitisha zoezi hilo na kuirukia simu yake,akaipokea na kuiweka sikioni!
“Mkuuu”
RPC Mshana,akaita!Kutokana na George Charles kuwa na pesa nyingi ilibidi ampambe na sifa hiyo ‘mkuu’
“Samahani,nimekupigia simu usiku, Mshana nina shida”
Kitendo cha kutaja jina hilo kama anaongea na mtoto mdogo kiliwafanya Mama Yusrath na watu wengine,kutetemeka!
Haikuwezekana hata kidogo RPC aitwe jina lake moja kwa moja bila kupewa heshima kama Kamanda ama RPC na namna alivyoongea naye,alikuwa kama mtu anayeongea na mtu wa kawaida tu,hapo ndipo wakaamini ‘heshima pesa,shikamoo kelele’
“Bila samahani,mkuu”
“Kuna tatizo hapa,kuna ndugu yangu yupo kituoni tangu mchana!”
“Tangu mchana?Kwanini hukuniambia?”
“Sikuwa nchini,ndio nimerudi usiku huu”Akadanganya!Ili kufupisha maelezo yake.
“Yupo kituo gani?”
“Mwananchi,Tabata”
“Jina lake nani?”
“Ahmed”
“Ahmed nani?”
Hapo Bilionea George Charles,alitoa simu yake sikioni na kumtizama Mama Yusrath.
“Anaitwa Ahmed nani?”
“Kajeme”
Baada ya kusema hivyo,akarudi tena kwenye laini na kutaja jina kamili la Ahmed,alichohakikishiwa aende moja kwa moja mpaka kituo hicho cha polisi,Tabata Mwananchi wakamchukue kwani angepiga simu muda huohuo.
Hilo likawa limeisha kirahihsi namna hiyo, bila kutumia nguvu yoyote ile!Pesa ikawa imemaliza kila kitu kwani baada ya hapo Bilionea George Charles alimuhaidi RPC, kiasi cha shilingi lako tano kama Ahsante.

*****
Macho ya Benjamin Ngowi,yalikuwa mekundu na yalikuwa yamelegea mno kutokana na usingizi aliokuwa nao siku tatu mfululizo hakulala!Mbali na kutaka kuhonga maaskari akiwaimbisha nyimbo mbalimbali na kuwatongoza ili amuwekee Ahmed dhamana lakini ilikuwa kazi bure kabisa,hata hivyo hakukata tamaa,aliendelea kubaki kituoni hapo mpaka saa tano ya usiku,hakukuwa tena na matumaini yoyote yale!Kumuacha Ahmed katika mazingira kama hayo peke yake bila kutoa msaada wowote ule,kwake ungekuwa ni usaliti mkubwa sana!
“Vipi?Chakula vipi?Nahitaji nimletee sasa hivi”
“Njoo kesho”
“Ndugu yangu hajala,tangu asubuhi”
“Bwana mdogo,nimekwambia njoo kesho.Wewe ni kabila gani?”
“Mchaga”
“Sasa mbona unakuwa mgumu kuelewa,nimekwambia njoo kesho.Kichaga siwezi”
“Kesho saa ngapi?”
“Saa kumi asubuhi,ukichelewa utamkuta Urafiki ama staki shari.Na huko itakuwa vigumu kumuona”
“Naweza kuongea naye?Japo kidogo”
Afande aliyekuwa zamu siku hiyo,alionekana kukerwa na ubishi wa Benjamin Ngowi.Hiyo ikafanya asimjibu tena swali lake, badala yake akamkata jicho kali, lililoonesha hasira za waziwazi na kero.
“Potea mahali hapa,sasa hivi”
Benjamin Ngowi,alilielewa tukio hilo.Hakuwa na jinsi yoyote ile zaidi yakuwa mpole na kugeuza ili aondoke,wakati anampa mgongo askari akasikia simu ya askari inaita akasita kidogo lakini aliendelea na mwendo sababu aliamini maongezi ya afande huyo yasingekuwa na maana yoyote kwake,lakini alivyoufikia mlango, akasita baada ya kusikia jina la Ahmed Kajeme linatajwa,akahisi kama amesikia vibaya!
Kumbe haikuwa hivyo ulikuwa ni ukweli sababu baada ya dakika moja aliitwa na kuambiwa asubiri kidogo.Hakuamini macho yake baada ya kumuona Ahmed Kajeme anatoka rumande,kilichomuuma zaidi alimuona anatoka tumbo wazi bila shati.
Licha ya yote alishukuru kumuona akiwa huru uraiani bila kujua ni mchakato gani ulifanywa mpaka aachiwe huru ghafla namna hiyo.
“Mchukue mtu wako,tukimuhitaji.Tutamtafuta”
Afande huyo akasema huku akitupa macho yake kwenye daftari,hiyo ilimfanya Ahmed aanze kuchukua kitu chake kimoja baada ya kingine kisha kutoka nje akiwa na Benjamin Ngowi pembeni yake.
“Pole sana kaka”
Benjamin Ngowi akatoa pole lakini badala ya Ahmed kujibu,alilengwa na machozi.Benjamin akalijua hilo akamsogelea karibu zaidi.
“Yote ni maisha,changamoto.Zinakuja na kuondoka”
Ilikuwa ni kama aliyemwambia Ahmed alie,kwani hakuweza kuyazuia machozi yake tena!Alijikuta akilia kama mtoto mdogo,hiyo ilimfanya Benjamin Ngowi amsogelee karibu na kumkumbatia huku akimpiga piga mgongoni akimpa pole.
“Pole sana Ahmed,usilie.Jikaze,wewe ni mwanaume!Mwanaume anakuwa jasiri siku zote”
Ahmed alibubujikwa na machozi,yakalowanisha mashavu yake na kupita mpaka shingoni!Alikuwa ana uchungu vikiambatana na hasira kwa wakati mmoja.Hakuweza kuvumilia kama mwanamme,kazi ikawa kwa Benjamin Ngowi kumfariji.
“Nipele…ke ho…me”
Ahmed,akajibu akiwa na kwikwi kali.
“Tutaenda kwangu”
“Benja…mi..n nipel..eke kwangu”
Hakukuwa na kipingamizi,wakaingia ndani ya gari na safari ikaanza hapohapo.
Ukimya ulitawala na kilichosikika hapo ilikuwa ni sauti ya kwikwi kutoka kwa Ahmed,mikono yake ipo machoni kaziba sura yake,analia kwa uchungu huku akipiga piga kifua chake kama mtu aliyeonewa!
“Nipe..leke kwa Yusrath,nyu..mbani kwao”
“No please,Ahmed punguza hasira rafiki yangu!Usiwe hivyo”
Ahmed akatulia,akatabasamu lakini tabasamu lake lilichanganyika na hasira,Benjamin alilijua hilo na kuna kitu alijifunza kutoka usoni mwa Ahmed,kisasi.
Bado mwanamme huyo alikuwa na kisasi na kivyovyote ilikuwa ni lazima afanye jambo baya kwa Yusrath.Hilo lilikuwa wazi kabisa kwani ni kama alikuwa ndani ya akili ya Ahmed.Ni sifa moja kubwa sana ambayo ni mbaya kwa Ahmed kwake yeye hakukubali kushindwa hata kidogo alichokuwa anakiwaza kichwani laiti Benjamin Ngowi angejua asingekubali kumuachia na kumpeleka kwake Ubungo Kibangu.
“Yes,I’m okay!Nipo sawa,Ngowi.Mimi ni mwanamme,sitakiwi kulia”
Ahmed akasema,akavuta kamasi kwa ndani na kufuta machozi yake akitumia viganja vya mikono.
Safari yao haikuwa ndefu sana kutokana na barabara kuwa nyeupe usiku huo,ndani ya dakika ishirini wakawa wamefika tayari!Ahmed akashuka,Benjamin nayeye akateremka kutoka ndani ya gari.Nyumba ilikuwa kimya taa zote zilikuwa zimezimwa,kumaanisha hakukuwa na kiumbe chochote ndani.Kwa kuwa siku zote walikuwa na utaratibu wa kuweka funguo pembeni ya maua,akafanya kubahatisha!Hata hivyo aliukuta,akafungua mlango.
Ndani alipokelewa na vumbi kali,tafsiri yake ilikuwa kwa muda mrefu hakukuwa na mtu ndani ya nyumba hiyo,akawasha taa!
“Mimi nishafika Benja,unaweza ukaenda!Nataka nikaoge nikalale,ahsante na Mungu akubariki!Tutakuja kuonana siku nyingine”
“Una uhakika,utakuwa sawa?”
“Niamini,nipo sawa”
“Twende ukale basi kwanza hapo nje”
“Niko poa,nitakula tu”
“Pole sana Ahmed”
Benjamin,alimpa tena pole huku akimshika begani akampiga piga kidogo kwa msisitizo na kumuangalia usoni.
“Nitakuja asubuhi,punguza hasira!Naomba upumzike”
Ahmed hakujibu,hakuwa ana uhakika kama wangeonana tena kuanzia siku hiyo!
Kitu alichokuwa anafikiria kumfanya Yusrath na watoto kilikuwa cha hatari sana na fununu alizosikia ni kwamba tayari ameruhusiwa yupo nyumbani kwao Ilala.
Kitendo cha Benjamin Ngowi kumpa mgongo na kufunga geti,akatembea kwa kasi mpaka chumbani ambapo huko alikutana na vumbi jepesi kwani hakukufanywa usafi kwa muda mrefu,akawasha taa na kuvuta ‘draw’ akatoa funguo za gari na pesa kidogo alizoziacha.
Chumba hiko kilimkumbusha vitu vingi sana,hususani mkanda wa suruali uliokuwa chini.Akakumbuka alivyokuwa anampiga nao Yusrath,hakutaka kukumbuka mengi zaidi.Alivyopiga jicho lake ukutani,ilikuwa tayari saa nane na dakika tisa usiku.Akatoka nje na kuwasha gari,akajifungulia geti na kulifunga!Breki ya kwanza ilikuwa ni kituo cha basi,Liverside ambapo hapo aliegesha gari pembeni na kufungua buti la gari.Ndani kulikuwa na dumu kubwa la lita ishirini.Akalichukua kisha kutizama huku na kule ili avuke barabara aende upande wa pili kwenye sheli ya mafuta,kitendo cha kufika tu.
Akakutana na pampu zaidi ya sita,akachagua moja wapo baada ya kumuona msichana mdogo kasimama,aliamini huyo angemuelewa tu.
“Dada mambo”
Ahmed akasalimia huku akisindikizia na tabasamu usoni.
“Poa”
“Nahitaji petroli,lita ishirini”
“Haturuhusiwi kupima kwa vidumu”
“Dada nisaidie,gari yangu imeishiwa mafuta kule Kimara!Nisaidie dada angu,kamata hii”
Haikuwa rahisi kwa msichana huyo kulainishwa na shilingi elfu tano,Ahmed akatoa elfu ishirini na kumpa na kumuomba msaada.Hilo halikuwa tatizo,akajaziwa mafuta ya petroli kwenye dumu likajaa!
“Ahsante”
Kitendo alichokuwa anaenda kukifanya Ahmed,kilikuwa cha kutisha hata yeye mwenyewe alikiogopa mno!Hata hivyo alipiga moyo konde.
Akavuka barabara na kuliendea gari lake,akaweka dumu lenye mafuta ya petrol ndani,akawasha gari na safari ya kwenda Ilala ikaanza mara moja!Haikuchukua muda mrefu,akawa amefika nje ya geti.
Hapo alitulia na kuitizama nyumba hiyo anayoishi Yusrath kabla ya kushuka na kuimwagia petroli kisha kuipiga kibiriti.Alipanga kuwachomea wote ndani,Yusrath na watoto pamoja na ndugu zake wote, hapo aliamini hata angeenda jela na kufungwa kifungo cha maisha ingekuwa sawa tu na halali,roho yake ingekuwa nyeupe.
Bila kufikiria zaidi,akashuka na kulibeba dumu la petroli,akasogea nalo mpaka ukutani!Akafungua,kifuniko chake.Akashusha pumzi ndefu tayari kwa kumimina,akiamini baada ya hapo atawasha kiberiti na mlipuko mkubwa utatokea,isingekuwa rahisi kwa mtu yoyote yule kutoka salama ndani ya mlipuko wa moto, ambao ungetokea sekunde chache zijazo!




Benjamin Ngowi aliingia ndani ya gari lake akiwa hana rahaa kabisa,mbali na uchovu uliochanganyika na usingizi mzito aliokuwa nao lakini moyo wake ulikuwa mgumu usiku huo,hiyo ni kutokana na kumuacha Ahmed peke yake,kila alivyovuta picha hakupata jibu la haraka!Chochote kibaya ama Ahmed angedhurika usiku huo, angejilaumu na urafiki wao usingekuwa wa maana kabisa!Akiwa ameshafika Ubungo mataa akapata wazo la kurudi lakini asingeweza kufanya hivyo bila kumpigia mchumba wake Pendo Jonas akimtaarifu juu ya uamuzi huo,akapeleka mkono kwenye gia akachukua simu na kumtafuta hewani ambapo simu ilipokelewa.
“Ulifanikiwa Darling?”
Upande wa pili wa simu ulisikika sauti nyororo ilioonesha kuchoka kwa mbali iliuliza.
“Ndio,hujalala?”
Ngowi,akajibu na kuibua swali.Mkono mmoja umeshika usukani mwingine simu sikio la kushoto!
“Nakusubiri wewe”
“Mimi nipo njiani lakini kuna jambo naona halipo sawa”
“Jambo gani?”
“Ahmed,nimemuacha mwenyewe!Moyo wangu mzito sana”
Hapo kukatokea ukimya wa kama sekunde tatu nzima.
“Baby,upo siriazi?Kwanini sasa?Kwanini hukumwambia aje hapa nyumbani?”
“Amegoma”
“Darling please,japokuwa simfahamu sana Ahmed lakini kwenye hii situation hatakiwi kuwa peke yake”
Kitendo cha Pendo Jonas,kumsapoti kilimpa nguvu nyingine mpya,bila kuchelewa akazungusha usukani na kuingia barabara ya pembeni, ambapo huko kulikuwa na uwazi kidogo,akapenya penya na kukamata barabara kubwa ya lami kwa niya ya kurudi nyumbani kwa Ahmed ili akae naye na kumpa kampani,akiwa kwenye njia ya vumbi akapishana na gari alilolifananisha na la Ahmed,hakuwa ana uhakika nalo mpaka aliposimamisha gari lake!
Kwa mbali aliona taa nyekundu zinapotelea gizani,akarudi ndani ya gari na kuzungusha usukani tena ili kulifuata,ambapo alishindwa kumaliza kona kutokana na upana mdogo wa barabara,hiyo ilimfanya arudi nyuma na kuliweka sawa.Akakanyaga mafuta na kusonga mbele kwa kasi,umbali wa mita kama kumi aliliona gari la Ahmed,limepaki akamuona anashuka na dumu kubwa.
“Anataka kufanya nini?”
Benjamin Ngowi,alijiuliza na kushindwa kupata jibu la harakaharaka,isingewezekana hata kidogo kwa Ahmed kutafuta maji usiku kama huo ndio maana akabaki kudadisi na jambo hilo lilimfanya azidi kuweka umakini zaidi,dakika ishirini baadaye akamuona anarudi ndani ya gari.Kwa tahadhari kubwa akaanza kumfuatilia kwa nyuma,mpaka wanafika Ilala.
Ahmed,anashuka na dumu hilo ambapo tayari alishaelewa ndani kulikuwa na mafuta ya petrol.Ilikuwa ni hatari kubwa endapo angebaki kumtizama, ndiyo maana bila kusuburi hata nukta moja ya sekunde akavuta kitasa na kushuka, akatembea kwa kasi mpaka kwa Ahmed akamshika.
“Ahmed nini unataka kufanya?”
Lilikuwa ni swali,lililomshtua Ahmed baada ya kufungua dumu la petrol kwani hakutegemea kumuona Benjamin eneo hilo,akaharakisha kumimina petrol ukutani ili amalize zoezi lake.Lakini alishindwa sababu Benjamin alilishika dumu na kulituliza chini.
“Benjamin,tunaheshimiana sana!Nisije nikakuvunjia heshima yako!Nakuheshimu,niheshimu.Tueshimiane”
Ahmed alijibu, macho yake yakiwa mekundu anaongea kwa ukali huku akimtizama Benjamin machoni.
“Siwezi kukuachia”
“Niachie”
“No,siwezi”
Kufuatia hapo Benjamin alisukumizwa na kupepesuka,kutokana na kutojiandaa na tukio hilo alijikuta anarudi kinyumenyume na kuangukia mgongo.Hiyo ilimfany Ahmed aendelee na zoezi lake lakini hakufanikiwa,Benjamin akawa keshasimama tena, kaikamata mikono yake yote miwili.
“Benjamin niachie”
Alivyojitahidi kukukuruka alishindwa kwani alidhibitiwa ipasavyo, akashindwa kufanya kitu chochote kile zaidi ya kujitingisha,hiyo ikamfanya Benjamin amvute kwa nguvu mpaka karibu na gari yake kisha kumsukuma kwa nguvu tena kwa hasira sababu alionekana kuchoshwa na upuuzi wa Ahmed.
“Sikiliza Ahmed,acha utoto na upumbavu.Unataka kufanya nini?Unataka kufungwa?Acha hasira za kishenzi kama mwanamke,wanaume hatupo hivyo!Jambo lishatokea haliweza kubadilika,kuna wanawake wengi.Achana na huyo kahaba,tafuta mwanamke mwingine”
Siku hiyo Benjamin,alizungumza kwa hasira lakini akitoa pointi zilizomuingia Ahmed na kuanza kuzitafakari,hakuishia hapo akazidi kumpa matokeo ya jambo analotaka kwenda kulifanya!
Urefu wa Ngowi na mwili mnene kiasi ambao uliosababishwa na shibe nzuri,uliweza kumdhibiti Ahmed vilivyo.Asingeweza kufanya chochote,jinsi alivyombana kitaalam, hata angefanya nini asingeweza kuchomoka,mbaya zaidi Ahmed alikuwa bado amedhoofika hakula tangu mchana hiyo ilichangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kukabiliana na Benjamin,akabaki anahema kwa nguvu huku akimtizama asijue ni kitu gani akifanye!
“Ahmed,bado una nafasi nyingine ya kurekebisha kila kitu.Tuliza akili yako,changamoto kama hizi ni kawaida kutokea katika maisha.Wewe sio wa kwanza kufanyiwa hivi na hautokuwa wa mwisho”
“No Benja,siwezi nashindwa!Niache”
“Trust me,utaweza tu!Kwanini ushindwe?”
“Inaniuma”
“Punguza jazba,nachokuomba!Kwa heshima yangu,ingia ndani ya gari lako,tuongozane mpaka kwangu”
Hapo Ahmed alitulia kidogo,akionekana kama mtu anayetafakari jambo fulani!Akashusha pumzi nzito na kumtizama Benjamin,akatingisha kichwa kumaanisha amekubali.
“Niahidi”
“Nakuhaidi Benja”
Taratibu Benjamin,akaanza kulegeza mikono yake hapo Ahmed akapata mwanya!Akakaa vizuri na kutembea mpaka ndani ya gari lake,akifikiria kitendo alichotoka kufanya kwa muda mfupi uliopita na kujishangaa mwenyewe!
Akageuza gari na kulipita gari la Benjamin,kupitia kioo cha pembeni akaliona gari la Benjamin, linamfuata kwa nyuma taratibu!

****
Siku zote mchovya kibuyu cha asali,hatosheki!Mbali na kujua kuna nyuki wangemng’ata.Necka Golden na Nemesi,walinogewa haikuwa rahisi kuacha mchezo huo mtamu ambao ulikuwa ni hatari endapo Amney angejua!Mbali na kujua kitendo wanachokifanya hakikuwa kizuri lakini ilikuwa vigumu kuacha.Ilikuwa kama dozi ya dawa sasa, kutwa mara tatu.Necka Golden na Nemesi walifanya ngono asubuhi,mchana na jioni pale ikibidi.Siri hiyo iliendelea kukaa ndani ya vifua vyao na walikuwa makini mno kuliko kawaida.
Ratiba ya Nemesi ilibadilika kadri siku zilivyozidi kwenda mbele,hakuweza kuamka asubuhi kama siku zote kuwahi kazini,hesabu zake zilikuwa kwa Necka!Kwa maana hiyo alikuwa akitega makusudi ili kumsubiri Amney aondoke kisha yeye azame chumbani kwa Necka akachovye kibuyu cha asali.Huo ndio ulikuwa mchezo wao kila siku iendayo kwa Mungu, bila Amney kugundua chochote,alivyojaribu kumuhoji Nemesi juu ya ratiba zake kubadilika majibu aliyopewa hayakuwa na mantiki, hakutaka kuhoji zaidi sababu alimuamini mpenzi wake.
Siku hiyo asubuhi,wingu lilikuwa zito angani ikafanya manyunyu yaanze taratibu, kuashiria kwamba baada ya muda mfupi mvua ingenyesha, mbaya zaidi ilikuwa asubuhi,baridi na upepo vilipuliza kwa wakati mmoja baada ya sekunde moja mvua kubwa ikaanza kunyesha, hiyo ilimfanya Amney,ajivute taratibu na kuanza kumtekenya Nemesi akimpapasa kifuani.Uchu wa ngono ulimshika,akataka wapashe joto lakini alipigwa na bumbuazi baada ya kutupa macho yake ukutani, kwenye saa na kugundua kwamba tayari amechelewa!Jambo hilo lilimfanya ashtuke na kilichotakiwa ni kutoka kitandani na kuwahi bafuni ili awahi kibaruani,kwake yeye alithamini kazi kuliko kitu chochote sababu alijua bila kazi asingeishi.
Ndiyo maana akajikaza bila kupenda na kutoka kwenye shuka,akiwa kama alivyozaliwa yaani uchi wa mnyama.
“Bebiii”
Nemesi akaita,kitendo cha kukatishwa stimu kilimfanya achukie.
“Baby,nawahi kazini”
“Nasikia baridi”
“Hata mimi lakini nitawahi kurudi”
Chumba kilikuwa na bafu ndani,Amney akaingia na mswaki, ambapo huko alifanya kila kitu na kutoka akiwa na kanga moja,akatembea nayo mpaka kwenye kabati huku macho ya Nemesi yakimkagua kuanzia juu mpaka chini,alitamani kumrukia na kumtupa kitandani lakini alivyomkumbuka Necka Golden, akatulia na kuomba Mungu haraka iwezekanavyo Amney aondoke ili yeye ajongee chumbani kwa Necka,akapashe kiporo!
“Na mvua hii,si utaloa mpenzi wangu?”
Nemesi,akatingisha kiberiti niya yake alitaka kujua kama Amney angeondoka ama angesikilizia mvua ikate kwanza!
“Nitabeba mwavuli,wewe leo huendi?”
“Nitaenda baadaye kidogo”
“Acha uvivu,hapo hilo baridi linakudanganya Baby”
Amney hakujua lolote na aliongea akitabasamu kama kawaida yake,akaendelea kupaka mafuta kila asehemu ya mwili wake, kisha kuanza kuvaa,akabeba na sweta na kulivaa pia ili kujikinga na baridi.
Alivyohakikisha amejiweka sawa,akamsogelea Nemesi ambaye bado alikuwa ndani ya shuka kajikunyata,akampiga busu mdomoni kama ishara ya kumuaga,akabeba mwavuli na kuanza kufungua mlango!
Masikio ya Nemesi yalikuwa kama antenna,japokuwa mvua ilikuwa inanyesha nje lakini alifanya juhudi sana kusikilizia mlango wa seblen ukifungwa,alivyosikia akasimama mpaka dirishani akavuta pazia ili amuangalie Amney,akamuona jinsi anavyofungua mwavuli na kuruka mashimo ya maji,akamshuhudia akitokomea kwenye moja ya kona!Hapo akawa mwenye uhakika,hatorudi tena!Bila kujiuliza mara mbili,akavuta taulo lake na kufungua mlango!Akanyoosha mpaka chumbani kwa Necka,ambapo alimkuta amelala chali akakaribishwa na tabasamu mwanana!
“Mbona umechelewa mpenzi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Necka Golden huku akitupa shuka pembeni na kutanua miguu yake, akabaki kama alivyozaliwa.Hiyo ilimfanya Nemesi alitupe taulo na kuruka kitandani.Ambapo hapo alipokelewa na mabusu,wakaanza kunyonyana ndimi kwa fujo huku wakishikana huku na kule.Damu zao,zilienda mbio.Mkono wa Necka taratibu ukawa unapita chini ya tumbo la Nemesi,ukafika na kushika kitu alichokuwa anakitaka,mnara wa Nemesi ulikuwa tayari umesimama wima!
Kwa michejo na madoido ya Necka akashuka kidogo chini akaachama mdomo wake na kuanza kuhutubia bunge,Nemesi hakutaka kutulia hata yeye alijibu mashambulizi kwa kuupitisha mkono wake mpaka kwenye kifua cha Necka, hapo akaanza kuzipapasa chuchu za msichana huyo ambaye kwa wakati huo,hakujiweza tena!Kila kitu kikawa taflani,ndani ya sekunde moja miguu ya Necka ikatanuliwa huku na kule!Nemesi akatoa ulimi wake na kuanza kupiga deki bahari,hiyo ilimfanya Necka aanze kuvuta vuta mashuka,macho yake kayafumba yupo sayari nyingine ya huba!Akakishika kichwa cha Nemesi vizuri,akakikandamizia ndani ya ikulu huku akikinyonga nyonga kiuno chake kumaanisha kwamba hali haikuwa shwari,japokuwa kulikuwa na baridi kali lakini hawakulisikia tena!
“Assshsss aaaah,mmmmh aaaashssssss”
Miguno ya Necka ilimfanya Nemesi,aibuke kama samaki kamongo na kuivuta miguu yake,hapo alijichomeka katikati na kuingiza mjegeja kwenye ikulu tayari kwa vita!Mvua ilikuwa kubwa na upepo uliotokea Magharibi kwenda Mashariki ulivuma kiasi kwamba mvua ilianza kuingia madirishani,hali hiyo ilimpa tabu sana Amney aliyekuwa barabarani anatembea kuelekea kituoni kutafuta daladala awahi kazini,mara kadhaa alishika sketi yake kwani ilikuwa inapanda juu na kuonesha ‘skin tight’ nyeusi aliyovaa ndani yake.
Alivyoona hali hiyo inazidi,akaona atembee mpaka kwenye moja ya kibaraza ili ajikinge na mvua hiyo kubwa,akiwa katika harakati za kuruka dimbwi la maji,mguu mmoja ukateleza akajikuta anaenda chini mzima mzima puu na kutumbukia kwenye mtaro huo,lilikuwa ni tukio la ghafla na lililomtia aibu.
Akatizama huku na kule akiwa na aibu anatetemeka,alivyosimama hakujitamani tena kwani mwili mzima ulikua na matope!Hiyo ilimaanisha asingeweza kuendelea na safari yake tena!Kwa kuwa alikuwa tayari amelowa hakuwa na budi kujikinga na mvua akayakanyaga maji kwa hasira na kuanza kurejea alipotoka!
Alipokuwa anaishi hapakuwa mbali na alipofika,alivyokunja kona ya kwanza akawa amebakiza mita chache kufika,hapo mvua ikazidi kumpiga mwilini,akapiga hatua ndefu na kuendelea kuyakanyaga maji.Alivyofika akauparamia mlango,ukafunguka kwani alivyouacha ulikuwa vilevile,akiwa chapachapa nguo zake zinateremsha maji kwenye malumalu akavua viatu na kuweka mwavuli chini.Akatembea kwa kasi,alivyoufikia mlango wa chumba anacholala Necka, akasita kidogo kwani ulikuwa una uwazi haukufungwa vizuri.
Kwa kuwa hakumsalimia asubuhi ya siku hiyo alivyoondoka kutokana na haraka,akasukuma mlango ili amsabahi na kumuhadithia kilichomsibu!
Lakini alijikuta anapigwa na butwaa la waziwazi,mapigo yake ya moyo yakapiga kwa nguvu!Mshtuko alioupata ulikuwa ni mkubwa sana,mbele yake juu ya kitanda alimuona Necka Golden amekunjwa vizuri,Nemesi yupo kwa pembeni wapo uchi wa mnyama!Lilikuwa ni fumanizi kubwa lililomfanya Amney,aishiwe nguvu kwani alivyotaka kupiga hatua, alishindwa na kuhisi miguu yake imepigwa ganzi,alivyotaka kuzungumza hakuweza, midomo yake ikawa inamcheza akahisi kama damu yake imeacha kutembea, mwili mzima umepalalaizi.



Hakuna mtu yoyote ambaye angeweza kuvaa viatu vya Ahmed,matatizo aliyopitia tena sambamba!Aliyatafsiri kama mkosi fulani,kichwa chake hakikuwa sawa hata kidogo.Akawa kama mtu aliyetoka msukule kwani hakuweza kuongea wala kufanya kitu chochote kile.Benjamin Ngowi,alikuwa naye beneti na kitu cha kwanza kukifanya ni kumpeleka nyumbani kwake ambapo hapo aliandaliwa maji ya kuoga,akaingia bafuni, huko alikaa dakika thelathini nzima bila kutoka.
“Benja,rafiki yako hajatoka mpaka sasa hivi bafuni,kuna usalama kweli?”
Pendo Jonas,msichana makini ilibidi amuulize mpenzi wake.Kukaa sana bafuni kwa Ahmed kulimfanya aingiwe na mashaka,hiyo ilimfanya Benjamin Ngowi asimame himahima mpaka mlango wa bafuni,akagonga!
“Ndugu,ndugu,nduguu…Ahmed….”
Ngowi,akaita. Ukimya wa Ahmed bafuni ukamtisha zaidi, akausogelea mlango na kuanza kuugonga,hata hivyo hakuitikiwa.
Ahmed,alikuwa bafuni machozi yanamtoka, analia kwa uchungu mno machozi yakawa yanapelekwa na bomba la mvua, sio kwamba hakusikia anaitwa lakini alivyotaka kuitikia sauti haikutoka kabisa,vitu vingi vilipita kichwani kwake akawa kama mtu anayetizama filamu ya kutisha.Mambo aliyopitia hata siku moja hakuwahi kuwaza kama yangemtokea yeye,alivyomkumbuka Yusrath moyo ukazidi kumuuma zaidi.Kilichomchanganya ni kitendo cha Yusrath kuzaa na Bililonea George,jambo hilo hakika lilimuumiza ndani kwa ndani.Hakua ana uhakika kama angekuja kusahau pigo kama hilo,moyo wake ulikuwa tayari umeshaingia doa, ilikuwa ni vigumu kutoka!
“Benj….aaaa”
Hatimaye akajitahidi kujikakamua kutoa sauti,mbali na kuitoa lakini alijua kabisa haikufika mbali kwani alijisikia mwenyewe.Alichokifanya ili kumuhakikishia Benjamin kila kitu kipo sawa,akafunga koki ya maji,yakaacha kumwagika kisha akafungua tena!Hapo Benjamin akaacha kumuita, akijua Ahmed yupo salama bafuni, labda tu alikuwa anakata gogo!Yaani anajisaidia haja kubwa,Ahmed hakuishia hapo alitumia muda huo akiwa bafuni kutafakari mambo mengi sana yanaondelea,akajifananisha na kinda la ndege lilioachwa na wazazi wake.Licha ya yote, maji yalivyokuwa yanazidi kummwagikia mwilini, akahisi kupata nguvu mpya,akachukua sabuni na kuanza kujipaka mwili mzima,akajisugua mgongo taratibu, akaja mbele kwa tumboni na kushuka chini kwenye Ahmed mwenyewe,akajisugua vizuri na kuiangalia vizuri ndizi yake,hakuwa ana uhakika kama alikuwa ana ikagua ama anaisafisha vizuri.Alivyohakikisha zoezi hilo limeisha,akarudi katikati ya maji na kujimwagia tena ambapo povu lilianza kushuka,baada ya hapo akachukua taulo na kujifuta taratibu.
Kuoga,kila kitu ukichanganya na mawazo yote kwa ujumla ilimchukua lisaa limoja lizima,akaingia katika chumba alichoonyeshwa, ambapo huko alivaa nguo alizopewa na Benjamin,akapaka mafuta na kutembea mpaka seblen.
“Kuna chakula”
Benjamin,akasema huku akijaribu kumdadisi rafiki yake.
“Hapana nimeshiba”
“Ahmed,tafadhali kula utapata ulcers.Najua hujala,tangu asubuhi nilikuwa nawewe,umekula saa ngapi?”
“Lockup,ulivyoniletea chakula”
“Hapana,njoo mezani tule.Kuna mambo nahitaji tuzungumze”
Ushawishi alioutumia Benjamin ulianza kuzaa matunda,kwani Ahmed alisogea mpaka mezani, ambapo huko alianza kupakua chakula taratibu.Ilielekea chakula hiko aliandaliwa yeye kwa heshima kwani kulikuwa na Kuku wa kuchoma na Wali,ambapo bakuli la pili kulikuwa na maharage mazito yaliyoungwa na nazi za kutosha,akapakua saizi yake na kula,Ki ukweli hakuonesha kuwa mwenye raha hata kidogo!Alijilazimisha,mawazo yote yalikuwa kwa Yusrath, msichana aliyempenda kuliko wote chini ya jua la Mungu.
“Kila kitu kitakuwa sawa”
Benjamin,akavunja ukimya upweke wa Ahmed ulimnyima raha kwani hakumzoea akiwa katika hali kama hiyo.Badala ya Ahmed kujibu,akamtizama kwa sekunde tatu nzima kisha kupeleka kijiko cha chakula mdomoni.
“Ahsante kwa msaada wako”
Hatimaye akajibu,baada ya kula na kushiba akashushia na maji glasi tatu.Hapo,akahisi kama amepata nguvu mpya, akarudi chumbani na kujitupa kitandani kwani usiku ulikuwa mwingi sana!

*****
Japokuwa alichelewa kulala lakini alikuwa wa kwanza kukurupuka kutoka kitandani,jambo la kwanza kulifanya ni kutizama saa yake kwenye simu.Ilikuwa ni saa 12;47 asubuhi,alijisikia yupo tofauti kwani siku zote, alikuwa akiamka ni lazima pembeni yake amuone Yusrath lakini siku hiyo ilikuwa ni kinyume kabisa,hapo akaamini kwamba kila kilichotokea hakikuwa ndoto, ulikuwa ni ukweli mchungu.Akakurupuka kitandani,kuna kitu kilichomjia kichwani kwake na hakikuwa cha kawaida hata kidogo!Katika matukio yote yaliyotokea,hakuna hata mfanyakazi mwenzake mmoja aliyefika hospitalini kumjulia hali, mbaya zaidi hata bosi wake hakumpigia simu,dalili hiyo ilikuwa ni mbaya sana kwake.
Uhakika wa kibarua chake kuota nyasi ulikuwa ni asilimia mia moja,hilo lilikuwa wazi kabisa alivyofikiria hivyo akakosa kabisa raha ya maisha!Mbali na kuamka asubuhi na mapema na kuoga, akakuta kifungua kinywa kipo mezani lakini hakutaka kuweka kitu chochote mdomoni sababu alitaka kujua nini hatma ya maisha yake kwani alijua nini maana ya kukosa kazi.
“Kunywa hata kikombe kimoja basi”
Benjamin Ngowi,alisisitiza akijaribu kumshawishi.
“Hapana,acha niwahi.Kama nilivyokwambia ofisini kule,wacha nikacheki mazingira”
“Make sure unarudi”
“Nitarudi”
“Ahmed,una uhakika?”
“Uhakika waaa….?”
“Kwamba,utafika salama na utarudi”
“Wacha Benja,akusindikize shemeji”
Katikati ya Maongezi Pendo Jonas,aliingilia hakuwa ana uhakika kama Ahmed angefika salama huko anapoenda, hatari aliyotaka kuifanya usiku wa jana yake,ilimfanya aingiwe na wasiwasi mkubwa sana!Hakutaka jambo hilo lijitokeze kwa mara nyingine.
“Usijali shemeji,nitaenda tu mwenyewe”
Hatimaye Ahmed akajibu,alikuwa tayari yupo mlangoni anataka kutoka!
Pendo Jonas hakukubali,akamtizama Benjamin kwa macho yanayosema ‘Msindikize mwenzako’ tukio hilo likamfanya Benjamin ajiongeze na achukue maamuzi hayo moja kwa moja,ndiyo maana akapiga simu dukani kwake kwamba atachelewa ama asingefika kabisa.
“Ndio,kuna oda ya viatu atakuja kuchukua Joseph Marandu,ataenda China next week mpatie ile invoice.Hakikisha unafanya juu chini ananisubiri..Okay sawa,nitakuja hapo au tutawasiliana”
Hakukuwa na haja ya kuuuliza Benjamin Ngowi,anazungumza na nani upande wa pili wa simu maana ilikuwa wazi kabisa alikuwa akiacha maagizo kwa kijana wake aliyekuwa kwenye moja ya duka kubwa la viatu vya ngozi,mbali na kuwa kijana mdogo lakini alikuwa mwingi wa mafanikio.
Benjamin Ngowi,alianza biashara akiwa mdogo sana na siku zote aliamini katika kutafuta,mbali na kuwa mfanyabiashara lakini alikuwa mkarimu na hakupenda dhuluma,hiyo ikafanya Mungu ambariki kadri siku zilivyozidi kwenda mbele.
“Twende Ahmed”
Wazo la Pendo likamuingia,wakaongozana na Ahmed mpaka nje, ambapo huko waliingia ndani ya gari na safari kuanza mara moja!
“Ahmed,katika maisha tambua kitu kimoja!Kuna kupanda na kushuka”
Benjamin Ngowi,akavunja ukimya akitumia busara zake ili amfanye Ahmed arudi katika hali yake ya siku zote.
“Pumzi ndio mtaji wako.Changamoto zinakuja na kuondoka na ndio kipimo cha akili,Ahmed haya yote unayopitia ni marudio tu.Kuna mtu mmoja duniani,anapitia changamoto kama zako!Na hiyo cha mtoto”
“Unataka kuniambia nini Benja?”
“Wewe ni mwanamme,usikate tamaa.Unakumbuka mimi nilivyoanza al..”
“Benjamin,nakumbuka kila kitu.Situation yako na yangu ni vitu viwili tofauti.Mke wangu kazaa na jamaa mwingine,kiwanja changu kimetapelewa na I’m sure kile kiwanja yule kahaba hajaenda kununua kahonga pesa zangu,naanza kupata picha”
“Ahmed,usipende kuhisi”
“Ninaziamini hisia zangu,najaribu kuunganisha picha sasa naanza kupata jibu kamili”
“Sawa,inawezekana unayosema yakawa sahihi.So,unataka kufanya nini?”
“She has to pay for this,haiwezekani”
Ahmed alizungumza akijibu kwa hasira na kupiga dashbodi kwa nguvu hiyo ilimaanisha bado ana kinyongo na Yusrath,moyo bado ulimuuma na kilichokuwa kinazunguka kichwani kwake ni kulipa kisasi na vita iendelee kama mbwai iwe mbwai.
“Ahmed,wewe ni Gentleman.Alafu ni msomi,usifanye mambo ya kitoto.Don’t act like a boy,behave like a man.Acha mambo yaende.Baada ya hayo kuna maisha mengine yanaendelea,shit’s happen life goes on”
Benjamin Ngowi,alijaribu kutoa ushawishi wake mzito,akitoa mifano mbalimbali na madhara ya jambo analotaka kulifanya lakini Ahmed hakujibu chochote mpaka wanafika Posta,jengo la Benjamin Mkapa.
“Paki hapo vizuri,wasije kukufungia gari.Ikiwezekana geuza kabisa”
“Utatumia dakika ngapi?”
“Dakika tano,naenda kucheki ustaarabu”
“Poa”
Ahmed akashuka na kumuacha Benjamin Ngowi,akigeuza gari na kuliweka sawa!Ambapo,alizunguka upande wa pili na kupaki kandokando ya sanamu aliyeshika mtutu,akiwa makini kutizama watu wanaopita barabarani.Hazikupita dakika tano, akasikia kitasa cha gari kimefunguliwa,akageuka na kumuona Ahmed.
“Vipi?”
Lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa Benjamin.Ahmed hakujibu,akafunga mlango na kutoa bahasha ndogo ya kaki!
“Soma”
Bahasha ikafunguliwa, Benjamin akaanza kupitisha macho!Ilikuwa ni barua ya kutisha,iliyomsimamisha Ahmed kazi kwa muda usiojulikana, kumaanisha kwamba kuanzia siku hiyo asingekuwa na kazi tena,jambo hilo lilimsikitisha sana Benjamin Ngowi.
“Usijali Ahmed,hili ni letu sote.Hapa ni sawa wamempiga chura teke”
“Una maana gani?”
“Nahitaji tuanzishe kampuni mimi nawewe,nilikuwa nakuhitaji kwa muda mrefu sana!Sema sikutaka kukwambia,Ahmed.This is serious my friend,nakuamini sana!”
Sentensi hiyo ilimfanya Ahmed amuangalie Ngowi kwa macho fulani yasiyoamini kile anachoambiwa,hakuelewa aseme ahsante ama atie neno gani.
Alichokifanya ni kuitikia kwa kichwa sababu hakuwa ana uhakika kama Benjamin alimaanisha ama anamfariji tu.Baada ya hapo hakuna sehemu nyingine waliyoenda, zaidi ya kwenda kupata kifungua kinywa,ambapo huko walipata muda mzuri wa kuzungumza biashara mbalimbali na jinsi ya kufungua kampuni.
“Nitatoa wapi pesa ya kufungua kampuni Benja?”
“Tutakopa benki”
“Whaaaat,mkopo hapana sitaki kabisa”
“Ahmed,angalia....First listen”
Hapo Benjamin Ngowi,akatoa noti mbili za shilingi elfu kumi na kuziweka mezani kisha kumtizama Ahmed.
“Hii elfu kumi na hii elfu.Zina utofauti gani?”
“Hazina”
“Je,unaweza kutambua elfu kumi ipi ya mkopo na ipi sio ya mkopo?”
“Hapana siwezi”
“Nadhani kuna kitu umejifunza tayari.Mkopo una principle zake Ahmed,ngoja nikupe siri kubwa!Unaona biashara nayofanya,bila mkopo nisingefika hapo!Kama umedhamiria kufanya biashara,usiogope mkopo hiyo ndio principle ya kwanza!Believe me or not mabilionea wote duniani wanadaiwa”
Benjamin Ngowi,alianza kutoa somo!Akimshawishi Ahmed wafanye biashara kisha wafungue kampuni,akamtolea mifano mingi sana juu ya biashara inavyotakiwa kwenda na uvumilivu.
“Tatizo nyie wachaga,mnafundishwa biashara na kuzijua pesa mkiwa wadogo sana.Mtoto wa kichaga ukimuuliza hamsini jumlisha hamsini hajui, sasa muulize shilingi hamsini jumlisha shilingi hamsini,lazima atakwambia shilingi mia”
“Hahahahahaha”
Wote wakacheka kwa utani na kuendelea na stori,walivyomaliza hapo wakarejea nyumbani ambapo huko walimkuta Pendo Jonas,keshapika tayari na chakula kimetengwa mezani.
Furaha aliyokuwa nayo Ahmed ilimaanisha sasa kila kitu kimeenda sawa!Wote wakaingia mezani,kabla ya kula wakasali. Kitendo cha kuitikia ‘Ameeen’wakasikia muungurumo wa gari nje na halikuwa moja,ghafla wakasikia lingine,mbaya zaidi milango ya gari ikawa inafunguliwa na kufungwa.
Kwa mara ya kwanza walidhani wenda ni wapita njia lakini,sekunde moja baadaye mlango ukaanza kugongwa tena bila ustaarabu wowote ule.
“Karibu”
Wa kwanza kuinuka alikuwa ni Pendo Jonas lakini macho ya Benjamin na Ahmed yalikuwa kwake,wakitaka kujua ni nani mgongaji mlango.Kitendo cha mlango kufunguliwa, wakaonekana askari warefu kwenda hewani watano na nyuma yao amesimama Yusrath Suleiman.
“Ndio yule pale afande”
Yusrath alizungumza sentensi hiyo huku akimnyooshea kidole Ahmed.Hiyo ilimaanisha askari wamfuate.
“Kama nilivyowaambia,kirungu kimoja elfu tano nawapa.Mpigeni vya shilingi elfu hamsini ama vya laki mbili”
Kilikuwa ni kitendo cha kinyama kwani Ahmed alishikwa shati na kuvutwa kwa nguvu kama mwizi,Benjamin alivyotaka kuingilia akatulizwa pembeni.
Kirungu cha kwanza kilimfikia Ahmed mgongoni,akajipinda hakukaa sawa akapigwa kingine mdomoni,akachanika vibaya sana na kuanza kuvuja damu,hiyo haikumaanisha wamuachie.
Alichoharibu Ahmed ni kutaka kuleta upinzani kwani alishika kirungu akamsukuma askari na kurusha ngumi ambayo ilimfikia askari huyo puani akapiga yowe kali na ilimpeleka askari huyo mpaka chini puu,hapo ndipo alipokosea sababu alichotwa mtama kimo cha mbuzi na askari wa pembeni,akajipigiza kwenye meza ya kioo na kudondoka kama mzigo,wote wakaanza kumshambulia kama mpira wa kona!


Kilikuwa ni kitendo cha kinyama kwa Ahmed kupigwa kama mbwa aliyedokoa nyama, isitoshe hata polisi walijua kabisa wanaenda kinyume na sheria lakini kwakuwa wao pesa ilikuwa mbele kuliko utu,walifanya kazi yao ipasavyo.
Kitendo cha Ahmed kumpiga ngumi mwenzao wakatumia kama sababu ya kujitetea,ndiyo maana wakazidi kumshambulia wote kwa mateke na Marungu huku wakimtukana matusi ya nguoni,tukio hilo kwa Yusrath alilifananisha na sherehe kubwa sana kwani alifurahi na moyo wake uliridhika kabisa.
Pendo Jonas mpenzi wake na Ngowi,alikuwa akimwaga machozi.Katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mtu anapigwa namna ile na kuvuja damu nyingi sana!
“Simama”
Askari mmoja aliyeonekana ana roho mbaya kuliko wote akatoa kauli hiyo na kumshika Ahmed shingoni kwa nyuma.
“Simama,upesi”
Sio kwamba alishindwa kusimama bali alihisi maumivu makali miguuni na kila sehemu ya kiungo chake kiliuma sana,kwa maaskari tukio hilo wakalifananisha na kiburi.
Mmoja wao,kati ya waliopigwa ngumi ya pua akampiga Ahmed teke kali la tumbo lililomfanya Ahmed apige yowe na kuhisi kichefuchefu cha kutapika.Hapo wakamuinua kinguvu,jambo hilo likamtia hasira Ngowi, sura ya Ahmed iligeuka na kuwa kama andazi lenye amira,iliumuka na kuvuja damu kila sehemu kuanzia puani hadi mdomoni,jicho lake moja la kushoto lilivulia damu, likawa jekundu mno.Hata hivyo hakuna askari hata mmoja aliyemuonea huruma,wakamburuza na kumkokota mpaka nje lakini alipofika huko akajua ni kwanini tukio hilo limetokea na nyuma ya jambo hilo yupo nani.
Gari la kifahari aina ya Hammer III ‘original’ lilikuwa nje pembeni kidogo limeegeshwa,linaunguruma bado.Mlango wa dereva umefunguliwa na mwanamme aliyemuona alikuwa ni Bilionea George Charles,moyo ulimuuma kwa kiasi cha kutosha.Kila kitu kikawa wazi na kilichomuumiza zaidi ni baada ya kumuona Yusrath ameingia ndani ya gari,katika matukio aliyowahi kushuhudia na kumuumiza moyo hilo lilikuwa namba moja!Moyo wa Ahmed,ulichoma kama pasi,kila kitu kikawa kama sinema ya kihindi ya kusisimua.Hakutegemea hata siku moja mwanamke aliyetokea kumpenda leo hii anamtesa namna hiyo,hakuelewa nini kosa lake, kifupi kila kitu kiligeuka juu chini,chini juu akahisi kama amebeba dunia kichwani,bila kutumia utu walimtupa ndani ya gari kama mzigo akajipigiza kwenye kingo ya chuma ya juu,polisi hawakujali ndiyo kwanza walicheka kwa dharau.
Japokuwa alihisi maumivu makali mwilini lakini moyo wake uliuma zaidi kwa dharau aliyoonesha Yusrath mbele yake tena akiwa na George Charles.
“Afande nisubiri,nakuja”
Hiyo ilimaanisha dereva asiondoe Diffenda,askari huyo aliyefahamika kwa jina la Kamanda Mllope alitembea mpaka kwenye Hammer III,akasimama kando ya George Charles akijichekesha,akapewa bahasha ya kaki hakukuwa na swali la kujiuliza kwamba ndani ya bahasha iliyotuna kulikuwa na kitu gani,tabasamu la Kamanda Mllope lilikuwa pana meno yote thelathini na mbili yakaonekana,akarudi kwenye diffenda hapo Benjamin Ngowi akasogea kwa haraka mpaka pembeni ya mlango.
“Mnaelekea kituo gani?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Benjamin Ngowi lakini badala ya kujibiwa maaskari wote wakamcheka kwa dharau.
“Unataka kumsindikiza mwenzako?”
“Nataka kujua kituo gani mnampeleka ndugu yangu”
“Basi,hatukutajiii kashtaki popote!Manyanya washa gari”
Ulikuwa ni utaratibu unaoenda kinyume na sheria,Ngowi akashindwa kuuvumilia kabisa, ndiyo maana akajitoa muhanga na kuwauliza lakini matokeo yake alishindwa kupata jibu,mbaya zaidi ilikuwa kidogo akanyagwe na tairi la gari kwani Diffenda iliondoka kwa kasi,bila kurudisha mguu wake nyuma tairi lingempandia juu yake.
Haikuwa picha nzuri kwake,hata kidogo!Baada ya hapo,akashuhudia Hammer ya George Charles ikiondoka,kwa haraka akaingia ndani ili achukuwe funguo za gari awafuate kwa nyuma.
“Wanaenda kituo gani?”
Pendo Jonas,akamdaka na swali.
“Sijajua,lakini nina uhakika cha hapo karibu”
“Namimi naenda”
“Twende”
Wote wakatoka mpaka nje,wakafunga nyumba na kuingia ndani ya gari.Safari,ikaanza mara moja cha ajabu walivyofika mbele hawakuiona Diffenda,wakatizama huku na kule lakini hakukuwa na dalili ya gari lolote lile.
Jambo lililomuogopesha Ngowi,akajaribu kubahatisha kwa kukunja kulia lakini walitembea umbali wa kilomita moja nzima bila kuona chochote kile.Walivyofika katikati ikabidi waulize wapita njia kama waliona Diffenda ya polisi.
Hakukuwa na mtu yoyote aliyeliona,ikabidi wageuze lakini huko ilikuwa hivyohivyo,walichokifanya baada ya kuwakosa wakaenda kituo cha polisi kilichokuwa karibu na kuuliza jina la Ahmed lakini hawakupata jibu kamili,wakaenda kituo kingine jibu likawa lile lile!Kengele ya hatari ikaanza kugonga kichwani kwake kwamba wenda wale hawakuwa maaskari bali watu wasiojulikana.Mbaya zaidi hakupajua nyumbani kwa Bilionea George Charles,alivyopata wazo la kwenda nyumbani kwa kina Yusrath Ilala,akasita kidogo kwani hakutaka kuchukua maamuzi hayo kwa haraka kabla ya kumaliza vituo vya polisi vyote ama kutoa taarifa kwa ndugu wa Ahmed.

******
“Siku zote anayeua kwa upanga,atakufa kwa upanga.Taarifa zako tunazo,ulitaka kuwachoma watu ndani ya nyumba!Leo,utakiona cha mtema kuni”
Kwa kukadiria na hesabu za harakaharaka walitembea umbali usiopungua kilomita thelathini na mbili,hiyo ilimaanisha walikuwa nje ya mji wa Dar es saalam.Hakuwa ana uhakika sana walikuwa wapi, sababu alikuwa chini ya uvungu,amelalia tumbo,anaugulia maumivu makali mwilini.
Ahmed,alitetemeka na aliingiwa na hofu kwani alijua kama angeenda kituo cha polisi kwa umbali waliotembea hakuna ndugu yake hata mmoja angejua ni wapi alipo!Licha ya yote,akajipa matumaini ni lazima rafiki yake Ngowi atakuwa nyuma anafuatilia kila kitu kinachoendelea.Akahisi gari limesimama na sentensi ya kwanza kusikia kutoka kwa afande huyo ilikuwa kuhusu dumu la petroli,lililokutwa nje ya nyumba ya Kina Yusrath, mbaya zaidi sauti yake ilisikika usiku wa jana yake akitaka kuwachomea ndani watoto pamoja na Yusrath,wakiwemo ndugu pia!
“Mzee,tumefika”
Askari mmoja alifika na kumuinua Ahmed,aliyekuwa amelala kifudifudi alivyoinua kichwa chake, alipigwa na butwaa la waziwazi.
Kila sehemu kulikuwa na kichaka cha miti mirefu,mbele yake kulikuwa na gari ndogo aina ya Corolla.Hakuelewa ni wapi yupo lakini sehemu hiyo aliifananisha na miti ya barabara ya kuelekea Morogoro,katika kujishauri sana akavutwa na kuteremshwa chini,hakukaa sawa akakudwa na kuburuzwa mpaka kwenye Corrola, ndani ya gari hilo alikutana na wanaume wengine watatu,sura zao zilikuwa mbaya kama nyani na hakuna hata mmoja kati yao aliyeonesha kucheka.
Hofu ilimtanda na jasho lilianza kumtoka,hakuwa ana uhakika kama anapopelekwa angetoka salama licha ya hayo yote, hakuelewa sinema hilo limechezwa vipi na ilikuwaje anakabidhiwa kwa watu hao na asipelekwe kituo cha polisi.
“Karibu Jehanam”
Jitu moja wapo likasema huku akimtizama Ahmed, ambaye muda wote alionekana kuwa na hofu nyingi sana,alivyoangalia pembeni chini ya gia akaogopa zaidi, baada ya kuona bastola ndogo,hakika alitetemeka akahisi maumivu aliyokuwa nayo mwilini yote yameisha!Kabla gari hilo kuanza safari,afande mmoja akafungua mlango upande wa Ahmed, akamtizama na kumkabidhi simu.
“Ongea”
Ahmed akapewa simu.
“Ahmed…”
Upande wa pili wa simu ukasikika,sauti ya Yusrath ndiyo ilikuwa hewani moyo wa Ahmed ukapiga kwa nguvu,akapata kigugumizi na kushindwa kuzungumza zaidi.
“Huu ndio upande wangu wa pili,wasalimie marehemu wote!Bye bye,sidhani kama utanisikia tena kwaheri”
Ahmed aliganda,maneno hayo yalikuwa kama mshale na yalizidi kumuogopesha zaidi.Kwa mara ya kwanza, hakuelewa ni kitu gani kilimaanishwa lakini alivyotuliza akili akajua kwamba tafsiri ya maneno hayo ni kifo na sio kitu kingine,alivyojaribu kujibu akashindwa simu ikawa imekatwa!
“Hakikisheni,mnafanya kazi kwa makini.Kama tulivyofanya mara ya kwanza!Asionekane na mtu yoyote yule”
“Najua cha kufanya,labda kama una lingine”
“Mimi sina,nawatakia kazi njema”
Kwa mara ya kwanza Ahmed alihisi roho yake inaacha mwili,ghafla akajifananisha na mbuzi wa pasaka anayepelekwa machinjioni.Alikuwa ana kila sababu ya kuhisi mbele hakukuwa salama kabisa na akaanza kutengeneza taswira ya watu wanavyopotea katika mazingira ya kutatanisha na mwisho wa siku kuuliwa ama wasionekane kabisa,picha hiyo akaifananisha na watu wasiojulikana!
Na ndiyo hivyo alielewa baada ya siku chache watasema ‘Ahmed ametekwa na watu wasiojulikana’ maswali mengi alijiuliza na kugundua jinsi baadhi ya maaskari wanavyoshirikiana na watu hao ili kufanikisha mpango huo!
Kifupi Ahmed alikuwa akilichungulia kaburi,safari ilianza mara moja na hakuna hata mmoja kati yao aliyemuongelesha mwenzake,alivyoangalia pembeni alizidi kutetemeka sababu gari lilikata kona na kuingia katikati ya msitu ambao hakujua ni wapi,wanaelekea!
Ulikuwa ni umbali mwingine wa kilomita nyingine ishirini,ambapo nyuma walivuka mabonde na milima,wakakunja kushoto ambapo huko kulikuwa na miti mingi vichaka vingi,kilichosikika zilikuwa ni sauti za ndege pori na mara kadhaa mbwa mwitu.Walisimama nje ya kijumba kidogo kilichojengwa kwa miti migumu ya mninga!Alivyoangalia pembeni,akaona bwawa kubwa lenye maporoko ya maji.Gari,likawekwa vizuri akashushwa na kupitishwa kwa nyuma,watu aliowaona walimfanya akate tamaa ya kuishi.
Mwanamme mmoja,aliyedhoofika na mrefu kiasi alimuogopesha kwani uraiani alikuwa amepotea na ulipita mwaka mzima wakidai ametekwa na watu wasiojulikana,kando yake kulikuwa na Mwanamke mmoja mwandishi wa habari.Alivyopiga jicho mbele akaona maiti nne,zilizofunikwa hofu ikamtanda zaidi!
“Mwingine huyu,leo ama?”
Mwanamme mmoja mnene mrefu,mkononi ameshika mtutu aliuliza.
“Asiwekwe huyu,asije kuwa ndaza!Zege hailali,si unajua”
Mafumbo waliyoongea watu hao aliweza kuyategua vizuri na alijua kivyovyote vile,walikuwa wakimzungumzia yeye kumaanisha kwamba anatakiwa siku hiyo afe, hapo ndipo akaanza kusali sala yake ya mwisho,akimuomba Mungu aipokee roho yake,hakuacha kuwasamehe watu wote waliomkosea!Ahmed akatumia muda huo pia kuitafakari dunia inavyokwenda na binadamu walivyokuwa na roho za kinyama, ghafla akakumbuka ndoto aliyoota siku moja kwamba Yusrath anamchoma kisu na kumuua,akajaribu kulinganisha na tukio hilo lililopo akagundua kwamba Mungu alikuwa anamuonesha kwa njia ya ndoto!Kwa uchungu,akadondosha chozi moja kwani hakuamini kama Yusrath angefikia hatua hiyo,hapo ndipo alipoamini kuwa WANAWAKE NI WAUAJI.


Kila kitu kilivurugika katika maisha yake,mambo yalimuendea kombo na bado hakutaka kuamini kwamba alipofikishwa ungekuwa mwisho wake duniani.Eneo hilo alilifananisha na Jehanam ndogo kwani aina ya mateso waliyopata watu aliowakuta ilimuogopesha mno.
Moyo ulimuuma sana alivyomkumbuka Yusrath,mkewe aliyefunga naye ndoa. Hakuamini kama mwanamke huyo angekuwa na roho ya kinyama namna hiyo.Akaamini kwamba alikuwa akiishi na nyoka ndani ya nyumba yake sasa aligeuka na kuwa chatu,akammeza mzimamzima!
Hata hivyo kila kitu kilichokuwa kinatokea siku hiyo alidhani ni ndoto ya kutisha lakini haikuwa hivyo.Watu aolizidi kuwaona eneo hilo walizidi kumfanya aingiwe na hofu,mmoja wa wafanyabiashara mkubwa aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha alikuwa mbele yake,amekonda mno kiasi kwamba alishindwa kumtambua vizuri.
Mbele yake kulikuwa na mzee mwenye mvi nyingi.Huyo ndiye aliyemuogopesha zaidi kwani alikuwa uchi wa mnyama na pembeni yake kulikuwa na vitu vyenye ncha kali,alivyomuangalia kifuani vizuri akaona majeraha yaliyosababishwa na kuchanwachanwa na visu.
“Hataki kusema?”
Jitu moja lililotokea upande wa pili likauliza kumaanisha kwamba yule mzee amegoma kuongea mambo wanayotaka kujua.
“Faili liko wapi Jaji Kazungu?”
Ahmed alishuhudia kila kitu kinachoendelea,mateso aliyokuwa anapewa mzee huyo, yaliogopesha kwani alinyanyuliwa kichwa chini miguu juu na kuning’inizwa.Chini wakawasha moto wenye kuni wakawa kama wanachoma nyama.
“Jiokoe mwenyewe kwa kutuambia faili liko wapi?”
“Sito…waambia sababu najua hata nikisema nitakuf..a tu.Siwezi kuwaambia chochote niueni”
Mbali na kuteswa namna hiyo lakini Jaji Kazungu hakuwa tayari kuongea kitu chochote kile,hiyo ilimfanya Ahmed ashangae na kuvutiwa na ujasiri wa mzee huyo, akajiuliza maswali mengi sana kichwani watu hao wanahitaji faili gani mpaka wamtese namna hiyo!
“Wo..te tutakufa,mimi nitatangulia nyinyi mtafuata a…”
Kabla ya kumaliza sentensi yake akapigwa na kitako cha mtutu kichwani,akapasuka vibaya sana, hapohapo akatulia,haikueleweka kama alipoteza fahamu ama amekufa tayari.
Hakukuwa na maongezi mengine kuanzia hapo, zaidi ya Ahmed kushtuliwa na kofi kali la shingo,akadakwa kama kifaranga na kuanza kuvutwa mpaka ndani ya kijumba hiko ambapo kwa harakaharaka kilifanana na hospitali ndogo,ndani kulikuwa na mikasi na madawa kadhaa, kushoto juu kulikuwa na mti ambao juu yake kilichomekwa kichwa cha mtu,ilikuwa ni picha mbaya sana kwa Ahmed na aliogopa na kutetemeka waziwazi,bado hakutaka kuamini kama kuna binadamu wenye roho za kinyama tena wapo, wanaishi Tanzania.
“Tulia hapo”
Kufuatia sentensi hiyo, Ahmed akasukumizwa mpaka juu ya kiti ambapo alifikia mgongo,japokuwa aliumia lakini hakutaka kulionesha hilo.Mwanamme mwingine mmoja mrefu,mwenye misuli kila sehemu mpaka shingoni akatokea,mkononi akiwa na kamba ndefu ya katani.Bila kuzungumza chochote, akaanza kumfunga Ahmed kwa staili ya kumzugushia kifuani na mgongoni,alivyomaliza hapo akaikata na kumfunga miguuni.
“Una masaa machache ya kuishi,muda upo bado wa kufanya toba na kusali.Omba msamaha kwa Mungu wako,uende peponi”
Jamaa huyo akasema,kupitia macho yake tu ilionesha hakuwa na chembe ya mzaha hata kidogo!
“Kaka,kwanini lakini?”
Ahmed akajikakamua kwa hofu akiuliza, jasho nyingi linamtoka usoni.
“Jukumu letu ni kutekeleza amri,sitaki maswali!Tambua tu,kuanzia sasa wewe ni mfu”
Yalikuwa ni maneno ya kutisha,Ahmed akahisi mkojo unataka kumpenya hata hivyo alihisi tayari amelowana lakini hakuelewa kama ni mkojo ama jasho!
Bado hakutaka kuamini kama siku hiyo kwake ingekuwa ya mwisho katika uso wa dunia,akapata muda kidogo wa kuanza kutafakari kifo kinafanana vipi,mtu akifa anaenda wapi?Uwoga ukamuingia hasa alivyomuona Mwanamke mmoja mrembo anaingizwa ndani,kwa macho yake alishuhudia anachaniwa nguo na kubakwa na wanaume watano, wakimuingilia kimwili bila ridhaa yake,kilikuwa ni kitendo cha kinyama sana!Baada ya hapo,akachomwa kisu tumboni ambacho kilitokea upande wa pili.
“Mfungeni jiwe,mtupeni mtoni biashara yake imeisha huyo”
Mwanamme mmoja pande la mtu lilisema huku akifunga mkanda wake,akapandisha zipu baada ya kutoka kufanya kitendo hiko bila uwoga,Mama aliyetoka kubakwa ambaye kwa wakati huo alikuwa marehemu tayari,aliburuzwa na kuingizwa ndani ya gunia na baada ya muda mfupi,wakaanza kuingiza gunia hilo kokoto nyingi mpaka lilipokuwa zito!
“Huyu vipi?”
Jitu hilo likageuka na kumtizama Ahmed,hapo ndipo sura yake mbaya ikaonekana vizuri.Lilikuwa ni jitu linalotisha jicho lake moja lilikuwa na chongo,usoni ana alama kubwa ya nyuzi zilizoshonwa.Kifua chake kipana na kinene kama sokwe,mbaya zaidi alikuwa ni mweusi kiasi kwamba akibeba mtoto mchanga anaweza akalala kwani angedhani giza limeingia!
“Mzigo wa Dasi huu”
“Ana inshu gani?Mwanaharakati au?”
“Hapana”
“Fanyeni haraka,tumalizane naye.Anamaliza hewa ya bure”
Hiyo ilimaanisha Ahmed auwawe mara moja,jitu hilo lilitoa kauli kana kwamba anatoa amri kuku akachinjwe.
Kwa haraka haraka ilielekea kwake kuuwa ilikuwa ni sawa na kuweka kibakuli cha supu mdomoni,Ahmed hakuweza kujizuia tena akajikuta analia kwa uchungu hasa alivyokumbuka kwamba Yusrath ndiye mkandarasi wa kila kitu kinachotokea.
“Unalia nini kama mwanamke?”
“Bra..tha sisi wote ni watanzania unajua”
Kauli hiyo ilifanya chumba kizima waangue kicheko,haikujulikana kama Ahmed aliwachekesha ama wanamkebehi,maana waliangua kicheko kwa sauti kubwa sana huku wakimtizama.
“Kwanini unaogopa kufa?Kufa ni kitu cha kawaida sana,kwahiyo usiogope kutangulia!Nakuhakikishia nitasimamia kifo chako mimi mwenyewe ili usipate maumivu makali,sawa rafiki yangu”
Halikuwa jambo la kawaida kwa binadamu kuzungumza mambo ya kutisha namna hiyo,mbali na kuingiza utani kidogo lakini walimaanisha kile wanachokisema kwa Ahmed.
Akavutwa akiwa na kiti chake mpaka nje,ambapo huko alizidi kuogopa zaidi kwani chini kulikuwa na maiti nyingine saba,zimekatwa katwa vibaya sana na miili mingine ya wanawake haikuwa na nguo kumaanisha kabla ya kuuliwa walibakwa,hakika ilikuwa ni picha mbaya sana katika macho yake,hakuwa ana uhakika kama ingefutika kamwe,tayari alishakata tamaa na alichokuwa anasubiri kwa wakati huo ni kifo tu.Alifikishwa kwenye mti mkubwa ambapo juu yake kulikuwa na kamba ya manira,iliyotengezwa kwa mtindo wa kitanzi.
Moyo ukamuuma zaidi sababu alishajua ni aina gani ya kifo angeenda kupambana nacho,kingekuwa ni kifo chenye mateso makali sana kabla ya kufa.
“Eeeh Mungu”
Ahmed akasema na kuanza kupiga dua zote,anazojua yeye!Hapohapo akasimamishwa, kitanzi kikavutwa!
“Panda hapa”
Ilikuwa ni kauli iliyomfanya Ahmed azidi kutetemeka kwa hofu,mbele yake kulikuwa na kiti kirefu.Kupanda kungemaanisha baadaye kipigwe teke kisha aning’inie kama nyama buchani.
Alikuwa mwenye hofu lakini hakutaka kukubali kufa kikondoo namna hiyo kwani alishaelewa, hata kama asipopanda ni lazima angeuwawa,hilo lilikuwa wazi kabisa lakini kufa kwa kujinyonga mwenyewe ni jambo ambalo hakutaka kulifanya,akasita! Katika kujitafakari,akapigwa ngumi kavu ya shingo iliyomfanya ahisi maumivu makali sana!
“Ebwana panda,unatupotezea muda kuna watu wanasubiri huduma zetu huko”
Maumivu aliyosikia Ahmed shingoni yalikuwa makali akatamani kupanda lakini bado akaonesha kugoma,wakamkamata kwa nguvu.Alivyoona wamemtoa kwenye kiti akajiputa makusudi chini.
“Kiburi sio?”
Ahmed,alipigwa na kiwiko cha mtutu kichwani akahisi kizunguzungu kikali, kabla ya kukaa sawa akatandikwa ngumi ya taya,akahisi kama meno yake ya juu yametoka,alivyoshika mdomo akashindiliwa teke la kifua, lililomchukua yeye na kiti mpaka chini, hapohapo akachotwa na kubebwa juujuu,kuanzia hapo hakuwa na nguvu ya kupambana nao tena,wakamsogeza mpaka kwenye kiti kirefu,kitanzi kikavutwa akavalishwa shingoni kama mbuzi anayepelekwa malishoni.
“Tayari?”
Jamaa aliyeshikilia kamba akahoji ili kiti kisukumwe Ahmed aning’inie mpaka kifo chake.
“Ndio”
Ilikuwa ni kauli iliyofanya kamba ivutwe,kiti kikasogelewa ili kitenguliwe.
“Griiii griiiiiiii”
Simu ikamshtua mtu huyo, mwenye roho mbaya,akasitisha zoezi la kupiga kiti na kupokea simu!
“Ndio mkuu,wapi?Na huyu je?Tumuache?Kesho…Sawa sawa,nakuja hapo”
Simu aliyopokea kutoka upande wa pili,ilimfanya asitishe zoezi hilo!Ahmed akafunguliwa bila kujua sababu hiyo ilitokana na nini,akashukuru Mungu kwa simu hiyo kupigwa pia akajipongeza kwa kitendo cha kuweka ubishi kidogo kwani bila hivyo wakati huo angekuwa ananing’inia.
“Kuna kazi kule,fanya haraka.Huyu tuta deal naye baadaye”

*****
Wakati Ahmed akila mateso na kupambana na kifo ili akishinde, yeye alikuwa kitandani,yupo uchi wa mnyama.Juu ya kifua cha George Charles,anazungusha nyonga zake huku na kule.Mara apande juu,arudi chini.Kila kitu kwake kilikuwa burudani,tendo hilo hakulifanya siku nyingi ndiyo maana akahisi kama yupo sayari nyingine ya huba!
Uzuri wake alikua juu kama anayeendesha farasi, hivyo alikuwa ana maamuzi ya kwenda kwa kasi ama aste aste!Kilikuwa ni kitanda kikubwa kilichokuwa na uwezo wa kubeba watu zaidi ya nane, hiyo ilimaanisha alikuwa mwenye uwezo wa kuzunguka kona zote,ndiyo maana baada ya kutoka juu akajisogeza taratibu mpaka kwenye kingo ya kitanda hapo alishika mbao, kumaanisha George Charles aje kwa nyuma yake,wafanye mbuzi kagoma!Kwa utu uzima aliokuwa nao George Charles,akajiongeza akasogea na kukishika kiuno cha Yusrath kwa mikono miwili,akapeleka mjegeja nayeye kuanza kukinyonga kiuno chake!
“Aaaah asshiii aashiii be..biii aaaashss yeeeh aaaah aaah aashssss”
Hilo lilikuwa wazi kabisa kwamba tayari Yusrath ameguswa sehemu iliyomfanya atoe miguno bila kutarajia,kitu alichokifanya George nayeye kuzidi kupeleka mashambulizi kwa kasi!
Jambo hilo likampelekea Yusrath azidi kukinyonga kiuno chake, mpaka alipofika kitonga. Haikuchukua sekunde moja George nayeye akafika safari yake,wote wakatulia na kulala kitandani.Ilikuwa ni mechi fupi lakini tamu, iliyoongozwa vizuri kabisa!
“Baby, ume enjoy?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Yusrath,alihisi moyo wake ni mweupe kabisa na hakuwa mwenye habari tena na Ahmed,kila kitu kilichotokea nyuma alisahau kabisa!
“Nime enjoy mke wangu”
“Hata mimi,nakupenda sana George”
“Mimi pia,sijui kwanini uliolewa mapema?”
“Naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum,najua ilipangwa niolewe na baadaye nije kukutana nawewe”
“Ahsante kwa kusikia hivyo”
Ghafla sura ya George ikabadilika hakuwa yule,mwenye furaha tena!Kuna kitu Yusrath alijifunza ambacho hakikuwa cha kawaida.
“Mpenzi upo sawa?”
Yusrath akauliza huku akisogea karibu,akalala kifuani kwa George huku akimkwaruza na kucha zake, fupifupi kiasi.
“Sasa itakuaje?”
“Itakuwaje,kuhusu nini?”
“Mumeo”
“Nilikwambia nishaachana naye”
“Naelewa,lakini maamuzi uliyochukua sio mazuri”
“Kivipi George?”
“Mimi nilipenda,tuyamalize kwa amani!Sio kwa staili uliyotumia”
“Mpenzi,nisikilize.Mimi namjua yule kichaa,hatokubali kuniacha hivi hivi,atatuletea fujo ni mtu asiyekubali kushindwa.Ndio maana nikakushauri ufanye vile”
“Kuna njia nyingi lakini”
“Ile ndio halali yake”
“Bado moyo wangu unasita,kumbuka tumeonekana.Itatuletea shida baadaye”
“George,you have deep pocket!Una pesa nyingi,nina aamini hata serikali haiwezi kukugusa kirahisi”
“Lakini na…”
“Hakuna cha lakini George,tunatakiwa tusheherekee kwa kile kilichofanyika na kumshukuru Mungu,tuna watoto wetu mapacha”
Bado moyo wa George Charles ulikuwa mzito kukubali mambo aliyoshawishiwa na Yusrath ayafanye ya kumteka Ahmed kisha auliwe.
Licha ya kuwa na pesa nyingi alielewa nini uzito wa dhambi hiyo ya kumtoa uhai binadamu mwenzake,hata siku moja hakutaka pesa zake ziwe fimbo za kuwachapia maskini,akiwa katikati ya kutafakari akahisi nyoka wake anapapaswa taratibu.Mwili wake ukapigwa shoti ya ajabu baada ya kuhisi amepata joto la ajabu sana,alivyoangalia vizuri akagundua ametumbukizwa mdomoni analambwa kama koni.Raha alizohisi kuanzia hapo,hazikuweza kuelezeka kiwepesi lakini kilichomkatisha ni baada ya kuangalia tv na kuona mwanamme mmoja yupo getini kwake,hiyo ilimfanya asitishe kidogo kwani CCTV kamera alizotegesha getini zilifanya aone kila mgeni anayeingia ndani kwake.Haikuchukua muda mrefu simu ya mezani ikaita!
“Beibiiii please,tumaliziee nina kiuu mwenzioo”
Yusrath akadeka akitolea sauti puani, baada ya kumuona George,anataka kupokea simu.Kitendo cha kuangalia kioo cha tv akapigwa na butwaa baada ya kumuona Benjamin Ngowi getini, kwa akili ya haraka akaelewa nini maana ya ujio huo,ghafla akashikwa na hasira zilizochanganyika na kukatiwa starehe yake ya kufanya tendo la ndoa!
“Mwambie,apite yes!Nipo,ninamfahamu”
George Charles,alikuwa simuni akiongea na mlinzi wa getini,akitoa ruksa Ngowi aruhusiwe kupita.Hilo lilifanyika mara moja!
“Baby,niachie mimi niongee naye.Wewe baki”
Yusrath,akaongea huku akitoka kitandani akavaa dera na kuvuta kitenge kizito akakifunga mwilini, tayari kwa kuanzisha shari.
Akashuka ngazi na kutembea mpaka mlangoni, ambapo hapo kabla ya mlango haujagongwa,akawa ameufikia tayari. Akafungua, macho kwa macho na Benjamin Ngowi.
“Pita ndani”
Yusrath akasema na kuacha nafasi ili Benjamin Ngowi aingie seblen,akamsubiri mpaka akae kabisa.
“Shida?”
Yusrath akatupa swali.
“Shemeji ina..”
“Mimi sio shemeji yako,niite tu jina langu.Au, Mrs George Charles”
Yusrath,akazungumza kwa mashauzi na mbwembwe, akijishebedua!
“Nahitaji kujua Ahmed yuko wapi?”
“Usichekeshe walionuna,sijui alipo.Nenda kituo cha polisi”
“Kote nimezunguka,sijamuona!”
“Kwahiyo,umeambiwa yupo hapa?Kwanza umepajuaje?Mwanaume mmbeya wewe alafu, nakuchukia sana”
“Nimeelekezwa”
“Cha kukusaidia tu,labda nikutafutie pesa ya sanda na jeneza maana..Hahahahahahaha”
Yusrath hakumalizia sentensi yake baada ya hapo alicheka kwa dharau,akasimama na kuliendea friji, ambapo hapo alimimina maji ya baridi na kuanza kunywa taratibu kwa mapozi.
“Karibu maji”
“Sina kiu”
“Kama kuhusu Ahmed,sijui chochote!Alafu kitu kingine,chunga usije ukaingia kwenye matatizo!Achana na haya mambo,utakufa kinywa wazi”
“Yusrath,sikiliza nikwambie a…”
“Sitaki kusikiliza chochote kutoka kwako,toka nje sasa hivi”
Yusrath alimaanisha,baada ya kutamka maneno hayo akatembea mpaka mlangoni na kuufungua,kumaanisha kwamba Benjamin Ngowi, atoke nje dakika hiyohiyo!
“Askari,afandee.Njooo utoe hii takataka nje”
Afande mwembamba aliyekuwa nje,akafika kwa kasi na kuingia ndani ambapo hapo alimshika Benjamin Ngowi, mkono!
“Usinishike,natoka”
Ngowi,alikwapua mkono wake hiyo ilimfanya askari huyo kimbaombao ayumbe kidogo!Benja akasimama na kumtizama Yusrath, kwa macho fulani yanayosema ‘Nitarudi tena’kisha akatembea mpaka nje na kutoka getini kabisa!



Bado hakutaka kuamini kila kitu kilichokuwa kinaendelea kuanzia kupotea kwa rafiki yake mpaka kubadilika ghafla kwa Yusrath,kila kilichotokea siku hiyo alitamani kiwe ndoto ashtuke!Ni kweli, Yusrath alibadilika lakini kwa hatua aliyofikia ilikuwa imezidi kipimo chake,kuna kitu alijifunza kutoka katika sura ya Yusrath kwamba Ahmed hayupo sehemu salama na akichelewa ataweza kumkosa hivyo kama rafiki mkubwa aliyeshibana naye, ilibidi awe mstari mbele kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa!Hakutaka kupoteza muda akiwa eneo hilo,alichokifanya ni kutembea hatua mbilimbili mpaka kwenye gari lake!Akaingia na kuanza kutafakari ni kitu gani akifanye,aanzie wapi?Vituo vya polisi vyote keshamaliza,hapo ndipo alichoka zaidi akiamini kwamba polisi wasingeweza kufanya kitu chochote kile.Wazo la kwenda kwa ndugu zake na Amed lilipomjia akalipuuzia kwanza,lakini baadaye akaliona kama lina mantiki, ilikuwa ni lazima ndugu zake wajue mchakato mzima ulivyokwenda mpaka Ahmed kuchukuliwa na Diffenda ya polisi kisha baadaye kutoonekana popote pale!Kabla ya kuwasha gari simu yake kutoka mfukoni ikamshtua,alivyoangalia akaipokea na kuiweka sikioni kwa haraka!
“Pendo”
“Umefikia wapi?Amekwambia nini?”
“Mambo ni mabaya,hakuna matumaini”
“Kivipi?”
“Nimeonana na Yusrath lakini alichonijibu Mungu anajua”
“Na huyo George sijui?”
“Sijaonana naye lakini nina uhakika yupo”
“Amekwambia nini huyo Yusrath?”
“Kuna maneno ya ajabu,tutaongea nikirudi”
“Benjamin kuwa makini,hili jambo sio la kawaida”
“Nitakuwa makini,sasa hivi naenda nyumbani kwa kina Ahmed kuwapa taarifa ndugu zake.Ili tujue tunafanya nini”
“Ni wazo zuri”
“Sawa baadaye”
Alivyokata simu baada ya kuongea na mpenzi wake,akaweka gia na safari ya kuelekea kwa wazazi wa Ahmed kuanza dakika hiyohiyo.
Kuwapelekea habari kama hiyo nzito aliamini ingeleta tatizo lingine, kutokana na Mzee Kajeme kuuguzwa hospitalini,akiwa ndani ya gari alitafakari vitu chungumzima, alivyoyakaribia mataa ya Mwenge akashtuliwa na simu yake,akatulia kidogo na kuiweka sikioni.
“Benjamin,mambo”
Ilikuwa ni sauti ya kike,kutokea upande wa pili japokuwa hakuangalia ni nani mpigaji lakini alijua ni Hajrath Mpilla.
“Poa,za kwako?”
“Salama”
“Niambie,za siku nyingi?”
“Ahmed mbona simpati?Yuko wapi?Kama upo naye hapo naomba niongee naye mwambie asinifanyie hivyo”
Hajrath hakutaka kuzungumza maneno mengine zaidi,akahitaji kuzungumza na Ahmed dakika hiyohiyo,kukaa kimya kwa mwanamme huyo kulimfanya amsake kwa wudi na uvumba.Ndiyo maana akamuendea hewani Benjamini ili ajue ni wapi Ahmed alipo!
“Hayupo hapa”
“Yuko wapi?”
“Kwa kweli sijui alipo”
“Benjamin,mbona sikuelewi?”
“Ahmed,sijui halipo hata mimi namtafuta”
“Wewe uko wapi?”
“Naendesha gari,nitakupigia mara moja”
Kuzidi kuzungumza na Hajrath maongezi marefu kungemfanya ashindwe kutafakari na kutumia njia nyingine mbadala ya kumpata Ahmed,ndiyo maana akafupisha maongezi na kuaga dakika hiyohiyo.
Sio siri,swala la Ahmed kuchukuliwa na polisi akipigwa kama mwizi bado lilimsumbua kichwani na kitu kama mkanda fulani wa kuuzunisha ulijijenga kichwani kwake.Ghafla picha mbaya ikaanza kumjia kichwani akijua ni lazima Ahmed yupo mahali fulani sio salama na anateswa mno na wala sio kituo cha polisi!Dakika kumi na tisa badaye akawa tayari amewasili kwa wazazi wa Ahmed,hakutaka kuingiza gari ndani ya geti badala yake aliteremka na kugonga geti!Alishukuru baada ya kuchungulia ndani na kuona kuna gari,kumaanisha wenyeji bado wapo!Ni kweli alikuwa sahihi,baada ya muda mfupi geti likafunguliwa na Kassim!
“Karibu Chif”
“Ahsante,Mama yupo?”
“Yupo hospitali”
“Sasa sikia,sina muda wa kupoteza nina haraka.Na nina jambo ninataka kukueleza”
“Jambo gani?”
Kassim,akakaa vizuri kumtizama Benjamin kwa umakini ili asikilize jambo hilo!
“Unajua kaka yako alipo?”
“Ahmed?”
“Ndio”
“Mara ya mwisho,nilionana naye hospitali”
“Baada ya hapo?”
“Sijamuona tena,nilimpigia simu jana haipatikani.Nikajua mtandao”
“Bratha ako,hatujui alipo!Mzee yuko wapi?Nahitaji msaada wake we..”
“No,sijakuelewa hapo”
“Mzee yupo hospitali gani?”
“Lugalo,kuna nini kaka?Niambie”
“Nitakwambia”
Kila mtu alikuwa kama amepigwa na butwaa lakini Kwa Kassim,lilionekana waziwazi.Alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa,akiwa hivyohivyo na malapa yake wakatoka na Benjamin mpaka ndani ya gari,safari ya kwenda hospitali ya Lugalo ikaanza mara moja!
“Imeakuaje?”
Kassim,akavunja ukimya!Alishindwa kuvumilia akitaka kujua ni kitu gani kimemsibu Kaka yake na yupo wapi,kwanini asionekane?
“Wewe ni mtoto wa kiume,acha nikwambie kilichotokea”
Hakuwa na sababu ya kuendelea kubaki kimya,alichokifanya ni kumuhadithia kila kitu kilichotokea mpaka Yusrath alivyofika nyumbani kwake wakamchukua na Diffenda,hata hivyo hakutaka kuweka wazi namna walivyompiga Ahmed ili kuepuka kumuumiza Kassim,baada ya hapo akahitimisha kwa kusema vituo vyote vya polisi hayupo na haonekani.
“Sasa atakuwa wapi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Kassim,usoni akionesha wasiwasi na hofu sana!Kabla ya kujibiwa, simu ya Benjamin ikaita na mpigaji alikua ni Hajrath,hakuwa na swali la kujiuliza msichana huyo anataka nini, alichokifana ni kupokea simu na kumueleza ni wapi wakutane!
“Sawa,nitakuja hapo.Nitachukua pikipiki”
“Utanikuta”
Benjamin akakata simu na muda mfupi wakawa wanaingia kwenye geti la hospitali ya Lugalo,iliyokuwa na ulinzi mkali wa kijeshi,hapo iliwalazimu wasimame kando na kutoa vitambulisho vyao!
“Piteni”
Kamanda aliyevaa jezi za kijeshi,mrefu futi nyingi kwenda hewani, aliwaruhusu baada ya kufanya ukaguzi ndani ya gari.
“Tunapaki wapi?”
“Pale,chini ya ule mti.Amelazwa huku VIP”
Benjamin akapaki gari chini ya mti,angeshukuru sana kama angeonana na Mzee Kajeme sababu aliamini ana cheo kikubwa serikalini kwenye jambo kama hilo angekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mwanaye anapatikana,hakuwa ana uhakika kama wazo lake lingefua dafu lakini ilikuwa ni bora acheze kamali.
Wakateremka na kutembea mpaka kwenye wodi,alilolazwa Mzee Kajeme maalum yaani V.I.P,mbali na hapo alikuwa akilindwa, haikuwa rahisi kwa mtu kuingia kiholela hata kwa Kassim ilikuwa tabu kidogo kumuona,mbaya zaidi alivyosema yupo na Benjamin.
“Hapana huwezi”
Mwanajeshi mmoja alisema,akamgomea katukatu.
“Mwambie nahitaji kuonana naye ni baba yangu”
“Nakufahamu”
“Sasa kuna ubaya gani?Kuna mambo muhimu nahitaji kumueleza”
“Subiri hapo”
Mwanajeshi huyo,akaingia ndani ya wodi alilolazwa Mzee Kajeme, alivyotoka akamruhusu Kassim aingie lakini alivyotaka kupita na Benjamin,akapigwa mkono na kuzuiwa.
“Aingie mmoja”
Hiyo ilimaansiha Benjamin,asubiri nje mpaka utaratibu maalum ufanyike ama apewe ruksa.
Wodi ilikuwa kubwa na muda wote kiyoyozi kilinguruma kikitoa hewa safi ya baridi,pembeni kulikuwa na kochi kubwa aina ya sofa ambapo katikati kulikuwa na meza kubwa sana!Ukutani pembeni kulikuwa na kitanda,hapo ndipo Mzee Kajeme alilala,hali yake haikuwa mbaya sana sababu aliweza kuongea na kutabasamu tofauti na mwanzo,kutokana na kazi yake na usalama ilikuwa ni lazima alindwe kwa njia moja ama nyingine hata hivyo baadhi ya wanajeshi,walikuwa ni marafiki zake wa kushibana yaani kama pete na kidole!Kassim hakuwa na sababu ya kuficha kitu chochote kile,akaongea aliyoambiwa kinagaubaga.
Benjamin,akaitwa ili atoe ushuhuda nayeye akazungumza kila kitu kilivyokwenda mpaka walivyompiga Ahmed na kumuingiza ndani ya Diffenda,Mzee Kejeme aliumia moyo na alisikitishwa kwa tukio hilo.
“Ulisema ni diffenda? Na walikuwa polisi wangapi?”
Mzee Kajema akiwa kitandani,akaanza usaili akitaka kujua picha kamili ili ajue pa kuanzia.
“Zaidi ya sita”
“Walisema wanatoka kituo gani?”
“Hawakusema”
“Shiiiit”
Mzee Kajeme akakema huku akibana meno yake,akarudisha kichwa juu ya paa na kuangalia darini.Akaisumbua akili na kuanza kutafakari vitu fulanifulani.
“Ulisema mkewe alikuwepo?”
“Ndio”
“Na nani?”
“Na yule George Charles”
Kufuatia hapo Mzee Kajeme aliutizama Mkono wake,kujipima kama ataweza kufanya jambo lolote la kijasusi hata hivyo hakua na sababu ya kufanya kitu chochote, alichoamua ni kumuita MP Kiverege na kumueleza kila kitu kilivyokwenda.
“Ahmed?”
M.P Kiverege akauliza kwa upole,alikuwa ni mwanajeshi mrefu aliyejazia kuanzia mikononi na kila mahali,mwili wake ulikuwa wa mazoezi na kombati alizovaa zilimtosha na kumkaa vizuri.Alikuwa na sura nzuri, mweupe kiasi lakini alikuwa ni tofauti kabisa,alikuwa ni mwanajeshi makini mno na mjanja mwenye akili nyingi.
“Nitaongea na George Charles,aniambie kituo gani walimpeleka.Nitaenda jioni nikitoka zamu”
“Ahsante MP”
Swala hilo likahesabika kwamba limekwisha,Mzee Kajeme akajipa matumaini akiamini alilifikisha kwa mtu makini na muda wowote angetegemea majibu mazuri!Alichokifanya MP Kiverege kabla ya kujitafakari akamfuata Benjamin na kumuhoji maswali mawili matatu kama kianzio!
Alivyosikia kwamba Yusrath pia kahusika,akatabasamu!Nusu saa baadaye,Hajrath akafika Benjamin akapata kazi nyingine ya kumuelezea jinsi ilivyokuwa,bila kutegemea Hajrath alijikuta analia machozi akatoa leso na kufunika uso wake, maana alihisi uchungu wa ajabu!

******
Kuendelea kubaki akiwa amefungwa kamba eneo hilo ilikuwa ni sawa na kusubiri kifo,ilikuwa ni bora auwawe akiwa katika harakati za kujikomboa kuliko kufa kikondoo.Mbele yake kulikuwa na giza nene sababu alivalishwa kitambaa cheusi kilichomfunika usoni,kamba aliyofungwa nganganga,haikuwa rahisi kuifungua ndiyo maana akajaribu kutafakari zaidi.
Japokuwa alikuwa mwenye hofu lakini haikuzidi hofu ya kifo chake kilichokuwa mbeleni kutokea endapo angeendelea kubaki kukisubiri.Alichokifanya ni kujaribu kuchezesha vidole vyake kwa nyuma vilivyofungwa kwa kamba,akatumia nguvu nyingi kufanya hivyo na kuhisi zoezi lake linaenda kufanya kazi sababu kamba zilianza kulegea,hatimaye akafanikiwa kuchomoa kiganja kimoja,alivyotaka kuchomoa cha pili ili atoe kitambaa usoni, akahisi hatua za mtu zinakuja,akatulia.
“Sio,napita kuchukua shoka.Yule tumlime nalo utosini,anachonga sana.Tutampelekea baba yake kichwa”
Yallikuwa ni maneno ya kutisha,mapigo ya Ahmed yakadunda kwa nguvu, akijua nini maana ya kugundulika kwamba anataka kutoroka!Alivyohisi hatua hizo,zimepita akatoa mikono yake kwa tahadhari kubwa akaanza kufungua kitambaa,alichokiona mbele yake alimanusura apige yowe,kulikuwa na mafuvu matatu pembeni, nyuma kuna maiti mbili zimekatwa vichwa,ilikuwa ni picha mbaya kwake kushuhudia kwa macho,hata hivyo matukio kama hayo alishaanza kuyazoea!Taratibu akaanza kusimama na kutafuta mlango wa kutokea!
“Namimiii niokoeee”
Ilikuwa ni sauti iliyotoka kwa mbali sana,hakuwa ana uhakika kama ilitokea ndani ya chumba hiko ama nje,alivyoangalia vizuri akamuona msichana mdogo kabisa mwenye umri kati ya miaka 19-25,akiwa amefungwa kamba,hana nguo hata moja mwilini.
Huruma ikamuingia lakini hakuwa na jinsi na wala uwezo wa kufanya ukombozi,akiamini kwamba endapo wangegundulika angezidi kumuingiza msichana huyo kwenye matatizo mengine zaidi pengine kukiharakisha kifo chake,alichokifanya ni kupiga hatua ili kuuwendea mlango lakini moyo wake ukagoma, akageuka nyuma na kumuangalia msichana huyo,ambaye alionekana kukata tamaa ya maisha!Moyo wake ukarudi nyuma,akatembea kwa haraka na kuzifungua kamba zake,akaiendea maiti moja wapo na kuivua nguo na kumkabidhi.
“Vaa hizo,fanya haraka”
Japokuwa yalikuwa ni manguo makubwa,hakujali wala kuona aibu alivaa harakaharaka na kumuona Ahmed kama Malaika vile,tumaini lake lote likahamia kwa Ahmed,baada ya kuvaa akasubiri amri.
“Sogea mbele”
Kwa tahadhari kubwa msichana huyo akasogea mbele karibu na mlango!Ahmed,akaufungua na kutizama huku na kule,hakuweza kuona vizuri mbele, kilichomsaidia ni mwanga hafifu wa mbalamwezi,akaona vivuli vya watu wawili upande wa kushoto!Hiyo ilimfanya afungue mlango akamshika mkono msichana aliyekuwa mateka.
“Unaitwa nani?”
Ahmed akauliza kwa sauti ya chini.
“Ruth”
Japokuwa hakukua na umuhimu wa kulijua jina lake lakini alijikuta anauliza,Mungu alikuwa upande wao wakafanikiwa kutoka nje!Ambapo,walikumbana na miti mingi hiyo ilifanya giza litawale.
“Hawapo,wameondoka watafuteni kila mahali”
Sauti hiyo kubwa iliwafanya watandwe na hofu kubwa,mbaya zaidi wakaona miale ya tochi kali zikimulika huku na kule.
“Hawawezi kutoka ndani ya msitu huu,hawajafika mbali.Wengine wapite kule mkiwapata waueni”
Maongezi hayo yaliwafanya wazidi kutandwa na hofu sana,wakazidi kusonga mbele huku wakiwa wameshikana mikono,hawajui wanapoelekea!



Giza lilikuwa kubwa,halikutofautishwa na mtu aliyefumba macho!Msitu ulikuwa mzito na mara kadhaa ilisikika milio ya wanyama pori.Hiyo ilimfanya Ahmed azidi kutetemeka ukizingatia hakuwa mwenyewe,miale ya tochi iliyokuwa nyuma yao iliwaogopesha zaidi na zaidi.Hiyo iliwafanya wazidi kusonga mbele wakikimbia,waliparamia miba ya miti ya michongoma na baadhi ya miti mikavu lakini hawakusikia maumivu kabisa,japokuwa hawakuwa na uhakika wa kutoka ndani ya msitu huo lakini hiyo haikumaanisha wakae chini na kusubiri kifo,kusimama na kutulia tafsiri yake ilikuwa ni kifo tena cha kinyama.
Picha za maiti zilimsumbua kichwani Ahmed, hiyo ilimfanya apate nguvu mpya ya kusonga mbele,katika kukimbia kwake hakuelewa amekanyaga nini lakini aliteleza vibaya sana na kuanza kubiringika kama mpira,kutokana na kumshika mkono Ruth hiyo ilifanya wadondoke wote na kuporomoka chini kwa kasi huku wakijigonga gonga kwenye miti mikubwa,kilichowafanya watulie ni gongo la mti kubwa, ambapo hapo walijipigiza kwa nguvu.Maumivu ya Ahmed yalikuwa makali sababu alifikia mgongo!
“Ruuuth”
Ahmed akaita huku akipapasa huku na kule akimtafuta msichana aliyetoka kumkomboa mateka,alivyoushika mkono wake akatulia na kuridhika lakini kilichowashtua ni baada ya kusikia sauti za watu kwa juu huku miale ya mwanga ikimulika huku na kule.
Kwa haraka zilikuwa tochi zaidi ya tatu kwani miale ilikuwa ni mingi kutokea kwa juu huku wakisikia vishindo vya watu,hiyo ilimfanya Ahmed arudi nyuma kidogo na kubonyea nyuma ya mti.
“Wapatikane,hawawezi kuwa mbali.Tiko,pita chini kule mimi natulia hapa!”
Ilikuwa ni sauti ya ukali tena kubwa,kumaanisha baada ya hapo utekelezaji ufanyike mara moja.Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwani wawili walishuka bondeni, ambapo Ahmed na Ruth walikuwa wamejificha!
“Mulika huku”
Miale ya tochi ilipita huku na kule,Ahmed alilala Chali, Ruth akiwa juu ya kifua chake anahema kwa mkupuo jasho linamtoka,ametandwa na hofu anasali sala zote.Wanaume wawili kutokea juu walizidi kushuka wakitumia matawi ya miti kujishika vizuri ili wasiteleze,wakazidi kuteremka chini huku wakimulika mti ambao Ahmed na Ruth wamejificha!
Isingekuwa Ahmed kulala vizuri mwanga ungempata kwani kama mara mbili ulimpita juu yake.
“Viiiipiiii?”
Sauti kutoka juu iliuliza.
“Subiriiii”
Jitu hilo moja jeusi,lenye sura mbaya kuna kitu liliona.Ndio maana akainama, kuna majani ya miti aliona yanacheza na alivyoangalia chini akaona mtifuko wa mchanga pamoja na majani kulala,kumaanisha kwamba njia hiyo kuna watu walipita.
Akawa makini kidogo kutizama huku na kule akimulika tochi yake kubwa yenye uwezo wa kuona umbali zaidi ya kilomita mbili,mbaya zaidi Watts za taa hiyo ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba hata angedondosha sindano angeiona hiyo ikafanya msitu mzito uwe na mwanga kama mchana!
Macho yake,yakapiga kwenye mti mkubwa ambapo kwa chini aliona kiatu,akatabasamu kidogo baada ya kujua ni lazima watakuwa nyuma ya mti huo!Alichokifanya ni kusogea taratibu mpaka nyuma ya mti!Akapiga tochi,jambo lililomfanya ashtuke zaidi ni kuona ni kweupe, kiatu kimoja ndio kipo kumaanisha kwamba ulikuwa ni mchezo wa kumzuga!
Ahmed na Ruth walipata mwanya wa kuchomoka baada ya kuona tochi zimepiga Upande wa Mashariki,kuendelea kubaki nyuma ya mti ingekuwa ni hatari kwa usalama wao ndio maana wakaacha kiatu kimoja ili kuwapoteza maboya!Walichokuwa wanakifanya ni kukimbia bila mpangilio bila kujua wangetokea wapi,wakazidi kusonga mbele mpaka walipofika sehemu yenye majani mengi, Ahmed alivyozidi kupiga hatua akahisi amekanyaga tope zito lililomfanya atitie,alivyotaka kurudi alipotoka akazidi kutitia zaidi na kumfunika mpaka kifuani,hiyo ilimtisha sana Ruth.
“Nipe mkono wako”Ruth akasema!
Ahmed,akajitahidi kutoa mkono japokuwa ulikuwa mzito sababu ulikuwa ndani ya tope hilo,katika hali ya ajabu na ambayo hawakuitegemea Ruth akajikuta nayeye kaingia badala ya kumvuta Ahmed atoke akatumbukia nayeye, wote wakawa ndani ya tope!Mbaya zaidi walizidi kutitia,sio siri walikata tamaa kabisa ya kusonga mbele!
“Sitakii kufaaa niokoeee kaka angu”
Wote walikuwa wamekata tamaa tayari,lakini aliyeonesha kushindwa kabisa na safari ni msichana huyu mrembo wa sura,japokuwa ilikuwa ni usiku lakini mwanga wa mbalamwezi uliweza kummulika usoni na uzuri wake kuonekana,rangi yake ilikuwa ni maji ya kunde,mfupi kiasi!
Macho yake yalikuwa ya kulegea,japokuwa alikuwa dhoofu kutokana na kukosa chakula kwa muda mrefu lakini haikumfanya mashavu yake makubwa kuingia ndani!Kila kitu katika maisha yake, kilivurugika baada ya Baba yake kuingia kwenye siasa na kupewa cheo kikubwa serikalini,hawakuishi kwa amani hata kidogo baada ya uchaguzi.Ghafla akaanza kukumbuka maisha yake,alivyokuwa anapelekwa nchi mbalimbali kula kuku kwa mrija,asubuhi anakunywa chai nzito!Mchana,mboga saba. Alikuwa ni mtoto mmoja tu tena wa kishua kwenye familia hiyo na Baba yake alimpenda kuliko kitu chochote kile chini ya jua, mbali na hapo alimdekeza mno!Alivyowakumbuka wazazi wake,machozi yalimtoka alivyokumbuka kwamba mbeleni anaenda kukumbana na kifo cha kinyama alisikitika zaidi sababu aliamini siku moja angezikwa kwa heshima, pengine kupigiwa hata mizinga kutokana na baba yake kumpenda,leo hii anaenda kufa kama mnyama na isitoshe hakuwa ana uhakika kama mwili wake ungeonekana,akiwa katika mawazo hayo Ahmed akamshtua kwa kumtaka ajisogeze pembeni taratibu.
“Sogea kwa huko,taratibu”
“Waaaapi?Niache nife tu,sina sababu ya kuishi”
“Usiseme hivyo,tutatoka salama”
Japokuwa alimfariji Ruth lakini hata yeye hakuwa mwenye uhakika kama angetoka salama ndani ya msitu huo,ambao kwake aliufananisha na kaburi!
“Sogea taratibu,weka mikono kwa juu”
Zoezi hilo likaonekana kufanikiwa,alichokifanya Ahmed ni kumsogeza Ruth kwa pembeni akitumia mikono yake,mbali na kutitia lakini alijitahidi akitumia nguvu,aliamini hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake ya mwisho kuishi, hivyo alitakiwa kuitumia ipasavyo! Hatimaye Ruth akafanikiwa kukanyaga jiwe lililokuwa pembeni,akajishika na tawi la mti akajitahidi kujivuta juu, akafanikiwa kuchomoka alivyofika akamshika Ahmed mkono na kumvuta kwa nguvu,wote wakatoka na kudondoka pembeni kandokando!Hakukuwa na muda wa kusubiri tena eneo hilo,isipokuwa ni kukimbia tu ili kujiokoa, wakazidi kusonga mbele lakini kilichowashtua ni miale ya tochi,hapo walitulia kidogo na kujua kivyovyote vile mtu hatari yupo mbele yao!Miale ikapita upande wa pili, Ahmed akasimama ili akimbie lakini bahati mbaya ikawa kwake na nzuri kwa jambazi huyo kwani alimuona.
“Paaa paaaaa”
Akaachia risasi mbili hewani,hiyo ilimfanya Ahmed atulie na kuhisi haja kubwa na ndogo vinataka kumtoka kwa wakati mmoja,hakuwa na ujanja zaidi ya kutulia kwasababu hata angekimbia asingefika mbali.
“Tulia”
Jitu hilo liliongea kwa sauti yenye amri,Ahmed akaganda kama barafu!Muuaji huyo ambaye kwake alimfananisha na Israeli mtoa roho za watu,akamsogelea karibu zaidi.
“Mwisho wako umefika”
Bastola ilikuwa mkononi mwake,kamuwekea Ahmed usawa wa kichwa ili amuuwe kama alivyoambiwa na mkuu wake wa kazi,kidole kikawa taratibu kinagusa triga ili amuondoe Ahmed duniani ambaye kwa wakati huo alikuwa mwenye hasira naye.Ahmed alikuwa chini kafumba macho yake,anasubiri kifo chake baada ya kukipiga chenga kwa muda mrefu na sasa ameenda kukutana nacho,hakuwa na ujanja zaidi ya kukisubiri tu.
“Paaaaaaa”
Ulikuwa ni mlio wa risasi uliosikika kwa sauti kubwa,mapigo ya moyo ya Ahmed yalidunda cha ajabu hakusikia maumivu yoyote yale,akazidi kuogopa zaidi.
Isingekuwa Ruth kusimama ki ujasiri na kuokota gogo la mti ambalo alimpiga nalo jambazi kichwani, basi Ahmed angekufa siku hiyohiyo,gogo hilo lilimfikia mtu huyo utosini akadondosha bastola ambapo ilijifyatua na risasi kupita pembeni.
Ruth alitetemeka na kulia kwa wakati mmoja,hakuamini bado kwamba ndiye yeye mwenye ujasiri huo!Alichokifanya ni kumvuta Ahmed,wote wakaanza kukimbia kusonga mbele lakini hawakufika mbali wakaonekana baada ya taa kali kuwamulika,kilichosikika hapo zilikuwa ni risasi tena aina ya mtutu wote wakadondoka chini.

********
Mbali na Yusrath kusahau kila kitu kilichotokea lakini hakuweza kusahau fadhila za Ahmed yale mema yote aliyomfanyia akaingiwa na huruma,hata hivyo hakutaka kurudisha moyo wake nyuma akiamini kile alichoamua kilikuwa halali yake,akiamini kwamba Ahmed adhabu yake ilikuwa ni kifo tu kama alitaka kuwauwa watoto wake na mbaya zaidi alitaka kuwachoma na moto kwenye nyumba basi mtu kama huyo kifo ilikuwa halali yake.Hata hivyo,kilichomfanya asahau kila kitu ni baada yua kukutana na George,akampa kila raha ya maisha!Akasahau ya nyuma,pesa ikawa imebadili kila kitu.Yusrath alijiachia sana na alipenda sana ngono,alikuwa akifanya ngono kila wakati na kila saa,ilikuwa kila George Charles akirudi usiku aingie ndani ya gari waanze kupasha!Hata hivyo wakifika ndani anaanza uchokozi kwa kumpapasa George Charles, kila mahali na kuishia kwenye tendo la ndoa!Siku hiyo alikurupuka asubuhi saa kumi na moja,hakuwa nacha kufanya zaidi ya kuupeleka mkono wake kifuani mwa George Charles,akausogeza zaidi na kuushusha kwa chini tumboni,akatumia kidole kimoja kupapasa kitovu,hakuishia hapo. Akazidi kuteremka chini zaidi, ambapo hapo alikutana na Tango,akaanza kulichua taratibu.Akatabasamu baada ya kumuona George Charles,anajigusa kumaanisha kwamba zoezi lake linafanya kazi,hakuishia hapo!Akazidi kumchua nyoka,alivyoona anapata tabu akapinduka upande wa pili na kuanza kumnyonya masikio kwa staili ya kumuingizia ulimi ndani ya sikio,hiyo ilimfanya George nayeye ajibu mashambulizi kwa kuanza kupeleka mkono wake kwenye pachupachu ya Yusrath!Mambo yakaanzia hapo,hakuishia hapo badala yake alimvuta Yusrath akaitanua miguu yake huku na kule,akakusanya mate mengi mdomoni na kuanza kupiga deki bahari,hapo ndipo Yusrath alipoanza kudata mbaya zaidi mkono mmoja wa George Charles ulikuwa kifuani mwake,unachezea chuchu!
“Asshsss aaashshh aaaah”
Hiyo ndiyo ilikuwa miguno ya Yusrath huku akiwa amefumba macho yake,matatizo yote ya dunia akasahau akahisi ameota mbawa,anapaa angani!Kila kitu kwake kikawa burudani,akajiona yupo juu ya dunia vitu vyote anaviona kwa chini!
George Charles alivyohisi kuna majimaji mithili ya utelezi akajua tayari muda wa kusosomola umeanza,hakutaka kupoteza wakati ndizi yake ilikuwa tayari imesimama imara kama mnara!Alichokifanya ni kuitumbukiza ndani ya mgodi,hapohapo kazi ikaanza!George Charles,hakuishia hapo alichokifanya ni kuendelea kucheza na mwili wa Yusrath akimpapasa kifuani na mara nyingine akimlamba chuchu, akitumia ncha yake ya ulimi.Jambo hilo likamfanya Yusrath,ataje majina yote ya utotoni na miguno akiitoa puani, akihisi raha za ajabu!

******
Ndani ya gari aina ya Landcruiser v8,lililokuwa na namba za usajili za kijeshi lilikuwa nje ya jengo kubwa linalomilikiwa na mfanyabiashara bilionea George Charles,ndani ya gari kulikuwa na wanajeshi waliovaa sare za kijeshi wenye nyota zao! Zaidi na hilo, wote walikuwa na vyeo jeshini.Mbele, nyuma ya usukani alikuwa ni M.P Kiverege,kushoto kwake aliketi Luteni Steven Kindolle,nyuma upande wa kushoto alikaa Meja Omary Magugu na kulia alitulia Mkuu wao, Kanali Said Adam Sangu!
“Ndio hapa?”
Swali hilo liliulizwa na Kanali Said Adam Sangu huku akitoa pakiti ya sigara ya Embassy,akaweka kipisi kimoja mdomoni na kuchukua kiberiti cha gesi akawasha,akapuliza moshi nje na mwingine ukatoka puani.
“Ndio mkuu”
“Luteni,tangulia sisi tutakuja”
Kilichowaleta ndani ya jengo hilo ni jambo moja tu,kufahamu ni wapi mtoto wa rafiki yao kipenzi Mzee Kajeme anayeitwa Ahmed alipo na sio maelezo marefu na hadithi nyingi,ndiyo maana walifunga safari kutoka kambini Lugalo asubuhi na mapema.
Mlango wa gari ukafunguliwa, buti kubwa la kijeshi likakanyaga ardhi,Luteni Steven Kindolle akateremka na kutembea mpaka kwenye geti,ambapo hapo alibonyeza kengele!Mlinzi akafungua kidirisha kidogo!
“Nataka kuingia ndani,nionane na bosi wako fungua geti”
Haikujulikana kama lilikuwa ni ombi ama ni amri lakini mlinzi alionesha kubabaika kidogo.
“Fungua geti niingie”
Kabla ya mlinzi kujibu,akaamrishwa hiyo ilimfanya apate kitete.Akaogopa zaidi baada ya kuona gari ya jeshi pembezoni kabisa,akashindwa kutoa maamuzi amruhusu mjeda ama apige simu kwa bosi wake kwanza aulize,jambo hilo likamfanya abaki njiapanda!




Lilikuwa ni jambo la kushtukiza nala kuogopesha kwa wakati mmoja,wanajeshi kufika nje ya jengo la Bilionea George Charles ghafla namna hiyo, kuliwafanya mpaka walinzi wake kuwa makini na kuwatizama,walikuwa umbali wa kilomita moja kurudi nyuma na wengine watatu upande wa mbele,isingekuwa rahisi kuwagundua sababu baadhi yao walikuwa kama wapita njia kumbe walikuwa walinzi maalum tena wenye mafunzo ya kijasusi,macho yao yalikuwa makini sana kutizama gari hilo la jeshi na wakati mwingine kwa mbali walisikia mazungumzo kati ya mlinzi na Luteni!Yalikuwa ni maongezi ya kitemi na yenye amri.
“Fungua geti”
Bado mlinzi alikuwa njiapanda lakini aliamini kwamba wanajeshi hao hawakumpa ajira hivyo ilibidi afuate ‘protocol’ za kazi yake atoe nidhamu ya uwoga,kwenda kinyume na mkataba wake wa getini kulimaanisha kibarua chake kuota nyasi,hakutaka hilo litokee ndiyo maana akapiga simu ndani moja kwa moja ambayo ilipokelewa na Yusrath.
“Waaambie hayupo”
Yusrath alijibu kwa kiburi, pasipo kujua nini maana ya jibu hilo.Kwa kuwa Bilionea George Charles alimfundisha kuwasha televisheni ya CCTV kamera,ikawa rahisi kujua nani yupo getini!Kitendo cha kumalizia sentensi hiyo George Charles aliyekuwa bafuni akatokeza,moyo wake ukadunda kwa nguvu, baada ya kuangalia kioo kikubwa na kumuona mwanajeshi yupo getini kwake,alivyoangalia vizuri nyuma kulikuwa na gari limepaki.Hakuwa limbukeni,kilichomtisha zaidi ni kuona mabega ya mwanajeshi huyo yalivyochafuka kumaanisha kwamba ana cheo kikubwa na lazima kulikuwa na jambo zito sana,hivyo hakutakiwa kufanya mzaha!Hakutaka kutafakari sana,akakwapua mkonga wa simu uliopo sikioni mwa Yusrath.
“Mwambie apite,namsubiri”
Mlinzi,akashusha pumzi nzito iliyoambatana na jasho la pua!Vitimbwi na ukorofi wa wanajeshi alivielewa,akajua kwamba siku hiyo ni lazima angeenda kambini kurushwa vichura ama kujaza maji kwenye tenki kwa kutumia kisoda!Bila kujibu kitu kingine chochote akafungua geti dogo la mtu kupita!Mwanajeshi akaingia ndani na kunyoosha mpaka ilipokuwa nyumba,hapo akapanda ngazi tatu na kugonga mlango,ulivyofunguliwa akaingia ndani na kunyoosha mpaka seblen akiwa na mabuti yake,hajavua hakujali kwamba anachafua!Alichotaka yeye ni kuzungumza na George Charles.
“Mkuu!”
Sauti hiyo ilisikika kutokea kwenye ngazi,hiyo ilimfanya Luteni Steven Kindolle,atupe macho yake kwenye ngazi,akamuona George anateremka!
“Pole na majukumu”
George Charles,akazidi kujisemesha huku akitoa tabasamu la kujilazimisha,akasogea mpaka karibu na Luten Kindolle, akampa mkono kwa heshima,wakapeana mikono huku Luten Kindolle akiwa bado amekaa, tofauti na wengine husimama kutoa heshima.
“Nishapoa,nawewe pole”
“Ahsante,unatumia kahawa au Chai?”
“Hapana nina haraka kidogo,wenzangu wananisubiri hapo nje”
George Charles,akajifanya kushtuka kidogo!
“Waaambie waingie ndani”
“Hapana,haina sababu”
Baada ya kujibu,Luteni Kindole akajivuta kidogo na kumtizama George Charles machoni!Kuna kitu alijifunza kupitia uso wa bilionea huyu kwamba kuna jambo amelificha, ndiyo maana mara kadhaa alikwepesha macho yake na kutizama pembeni ama chini.
“Kilichonileta hapa ni kujua,Ahmed Kajeme anapatikana wapi”
Mapigo ya moyo ya Bilionea George Charles,yakapiga kwa nguvu.Akahisi joto la ajabu sana,japokuwa kulikuwa na kiyoyozi kikali ndani ya seble lakini alihisi jasho la kwapa linamtoka,hakutegemea kusikia kitu kama hiko!Mbaya zaidi halikuwa swali lakini jibu lilitakiwa.
“Ahmed?!”
“Ndio Ahmed Kajeme,alafu naomba napoongea unisikilize kwa makini.Sipendi kuuliza swali mara mbilimbili”
Luteni Kindole,akakunja sura hiyo ndiyo ilikuwa kawaida yake,hakuna kitu anachukia kama kurudia kitu mara mbilimbili ndiyo maana akawaka na kufoka kidogo kwa ukali,hiyo ikamfanya Bilionea George Charles aanze kutetemeka!
“Sijui alipo,mara ya mwisho kumuona ilikuwa hospitalini”
“George….”
Jibu la Bilionea George Charles,lilimpandisha Mori Luteni!Hapohapo akasimama na kumsogelea mpaka karibu kabisa!
“Kabla jua halijazama,nahitaji kujua ni wapi Ahmed alipo!Iwe umemteka,iwe umemfungia sehemu ama popote pale nachotaka,leo apatikane!Vinginevyo,vinginevyooo……..”
Macho ya Luteni Steven,ghafla yakawa mekundu kama mtu anayevuta bangi amesimama wima anamtizama George Charles kwa hasira na chuki za waziwazi,hiyo ilimfanya Bilionea huyu ashikwe na uwoga!Akashindwa kujibu ingawa alitamani kufungua kinywa chake na kuropoka lakini aliogopa kufanya hivyo kwani angeharibu moja kwa moja,hata hivyo hakuwa ana uhakika kama Ahmed huko alipo yupo hai ama tayari ameuwawa,akajuta kwa kitendo alichokifanya!Akaanza kumchukia Yusrath kwa kumshikia akili zake na kumshauri wamteke Ahmed na wamuuwe bila kujua madhara yake mbele yangekuwaje,tayari alishaanza kujuta na alishaelewa baada ya hapo angeingia kwenye kashfa mbaya pengine biashara zake zingeyumba kwa kiasi cha kutosha!Hiyo ilimfanya aogope zaidi,baada ya kumuona Luteni amegeuza na kuondoka,akamsindikiza kwa macho mpaka alipofungua mlango na kutoka nje!
“Mungu wangu”
George Charles,alihisi kujuta kwa kiasi cha kutosha,akaomba Mungu isitokee asikie kwamba wameshamuua Ahmed tayari kwani tafsiri yake ilikuwa ni mbaya sana mbele ya wanajeshi hawa katili,akasimama kwa haraka na kuparamia ngazi,akapandisha mbilimbili mpaka chumbani kwake,akaufungua kwa kasi.Ilikuwa kidogo mlango umpige Yusrath kichwani sababu alikuwa nyuma ya mlango!
“Hee!Tutaumizana wee mwanaume,ndiyo nini sasa?”
Yusrath,akang’aka!Lakini hakujibiwa kitu badala yake George akanyoosha mpaka juu ya meza na kuchukua simu,akabonyeza namba fulani na kuiweka sikioni!
“Halloo,Kamanda!”
“Naam,pole na majaku…”
“Yule Kijana vipi?”
“Kijana gani?”
“Yule nani..Ahmed,yupo wapi?”
“Kama ulivyotuagiza,ndio kilichotokea”
“No,mtoeni.Mambo yameharibika”
“Kivipi?”
“Nimesema mtoeni,haraka sana”
“Sina uhakika,kama yupo hai.Subiri usikate simu….”
Simu ikabaki hewani,mambo aliyokuwa anazungumza George Charles simuni yalimfanya Yusrath amtizame kwa macho ya wasiwasi yenye kutaka kujua kitu gani kinaendelea,ingawa alihisi kuna jambo lisilokuwa la kawaida.Ndio maana akasogea karibu na kuuliza.
“Subiri kwanza”
“George,kuna nini?Unataka kufanya nini?”
“Nitakwambia”
“Niambie sasa hivi”
“Nimesema nitakwambia,kwa sasa hivi niache”
George akafoka kwa ukali,kelele za Yusrath zikageuka na kuwa kero kwani chanzo cha yote mpaka anapigapiga simu za kuomba msaada ilikuwa ni yeye.
“George,unanifokea?”
Yusrath akauliza kama mtu asiyeamini anachokisikia.
“Ndio,wewe ndio umesababisha haya yote so ndio nakufokea!Shut up”
George Charles aliiva kwa hasira,akawa mwekundu uso mzima!
Mishipa ya kichwa imemtoka naya shingo imemsimama tangu Yusrath amjue mwanamme huyo hakuwahi kumuona akiwa katika hali hiyo,akaogopa na kutulia kimya!
“Halloo Kamanda,vipi?”
“I’m sorry George,umechelewa”
“Whaaaaaaat,una maana gani?”
“Wamemaliza kazi”
“Oh My God”(Mungu wangu)
Taarifa alizosikia George Charles,zilimfanya ahisi mwili wake umekuwa mdogo ghafla kama mchanga,nguvu za miguu zikamuishia,akarudi kinyume nyume kama gari na kukaa kitandani,bila kupenda!

*****
Mbele yake,alilala Necka Golden yupo uchi wa mnyama,kushoto yupo Nemesi!Mwanaume aliyetokea kumpenda na kumuamini kuliko mwanamme yoyote yule chini ya jua la Mungu!Bora ufuska huo,angefanya na msichana mwingine kuliko rafiki yake!Akaamini kwamba Kikulacho kinguoni mwako,macho yake hayakutaka kuamini kile anachokiona.Lilikuwa ni fumanizi lisilohitaji maelezo ya aina yoyote ile,moyo wa Amney uliumia vibaya sana!Katika maisha yake,hakuwahi kufumania, alisikia tu stori za watu wakijinyonga na kunywa sumu kisa mapenzi lakini leo hii ilikuwa kwake na alitamani iwe hivyo,maumivu aliyohisi yalikuwa ni zaidi ya kidonda kilichomwagiwa spiriti.Akabaki anamtizama Necka Golden,akahamisha macho yake kwa Nemesi!Wote walikuwa wakimtizama yeye kwa pamoja,hawakuelewa hatma yao!Nemesi alijihisi kujuta,lawama zote akamtupia shetani,hakuelewa alipokuwa kitandani asimame ama aongee nini.
“Nem..esi Ahs.a...nte”
Ilikuwa ni sentensi iliyotoka kinywani mwa Amney huku akibubujikwa na machozi mfululizo,yakapita mpaka shingoni!Kwikwi kali ilimshika,alivyotaka kutia neno lingine akashindwa alichokifanya ni kutoka ndani ya chumba hiko na kuingia chumbani kwake!Mvua ilizidi kupiga na radi ilimulika na mara nyingi ulisikika mlio mkubwa,Nemesi alikuwa kitandani amejikunyata!
Kilichotokea bado alihisi ni ndoto ya kutisha!Hakuwa ana uhakika kama mkataba wake wa mapenzi na Amney tayari umevunjika ama atamsamehe,kubaki kitandani halikuwa suluisho!Alichokifanya ni kusimama akiwa hana nguo hivyohivyo na kutoka kitandani,akanyoosha mpaka mlango wa chumbani kwake ambapo Amney aliingia,alivyoufungua akagundua umefungwa kwa ndani na funguo!Akazidi kuchanganyikiwa zaidi,akabisha hodi lakini hakukuwa na dalili yoyote ile ya mtu kufungua!
“Amney….ngo ngo ngooo!Amney,fungua mlango mke wangu,tuongee”
Hakuwa ana uhakika kama alisikika ama sauti yake ni ndogo,kutokana na mvua kubwa kunyesha nje!Alikaa nje kwa muda wa dakika mbili nzima,ndipo akasikia mlango unafunguliwa!Amney akatoka akiwa na mabegi mkononi,kumaanisha kwamba anataka kuondoka hataki tena kubaki naye kama zamani.
“Amney unaenda wapi?Subiri nikuelezee”
Swala la Amney kuondoka,kwake ingekuwa ni sawa na basi bila konda!Hakutaka hilo litokee ndiyo maana akamshika mkono akimzuia.Lakini badala yake,Amney hakujibu chochote aliupangua mkono wake lakini Nemesi,aliendelea kumshika na kumsihii asiondoke, akimsisitiza abaki wazungumze ili yaishe huku neno ‘I’m sorry baby’ likitamkwa kila wakati!
“Nemesi nia…che,nawaachia nyumba mbaki kwa amani”
“Usiseme hivyo Amney wangu”
“Nia…che niende”
“Amney,nakupenda bila wewe sitoweza!Wewe ndio kila kitu kwangu”
Sentensi hiyo ilimfanya Amney,amtizame Nemesi akatabasamu kidogo,haikujulikana tabasamu hilo lina maana gani lakini Nemesi alilitafsiri na alielewa.
“Baki na Kahaba,mwenzako”
Moyo wake,ulivuja damu kutokana na maumivu makali aliyoyapata ghafla!Picha ya Nemesi akiwa uchi wa mnyama kitandani akifanya ngono na Necka Golden, bado ilimsumbua,akamsukuma Nemesi akaweka mabegi vizuri na kupiga hatua, mbele kidogo,akakutana na Necka Golden amevaa kanga,akamtizama kwa macho makali yalijojaa hasira,bila kumsemesha chochote akatembea mpaka seblen, ambapo huko alifungua mlango na kutoka,mvua ilikuwa kubwa sana!
Kabla ya kufika mbali,Nemesi akawa tayari kamfikia amevaa taulo peke yake,akamshika mkono na kumzuia akimuomba msamahaa hapohapo akadondoka chini kwa magoti bila kujali kama watu wanamuangalia,alichojali yeye kwa wakati huo ni kuokoa penzi lake lililoingia doa tayari!

*******
Risasi tano zilichimba na kutifua ardhi,mchanga ukaruka Ahmed na Ruth wakadondoka chini kusalimu amri,hiyo ilimaanisha wangeendelea kukimbia risasi zingeishia mwilini mwao na wangekufa hapohapo,kwa uwoga na hofu wakatulia huku wakisubiri kifo,baada ya kukipiga chenga kwa muda mrefu!Mwanamme mrefu mwenye misuli mingi akawasogelea karibu akiwa na tochi kubwa sana yenye uwezo wa kumulika umbali mrefu,hakuongea chochote zaidi ya kumpiga Ahmed na kitako cha mtutu kichwani,akadondoka chini huku akivuja damu!Sekunde moja baadaye upande wa kushoto akatokea mtu mwingine mfupi,aliyekomaa mguuni ana vigimbi kama mchimba michanga,mguu wake ulionekana sababu alikuwa amevaa kaptula fupi.Hata yeye mkononi alikuwa ameshika mtutu,jasho linamtoka na alionekana kuchukizwa baada ya kuwaona Ahmed na Ruth wapo hai mpaka wakati huo wakati kifo ndiyo kitu pekee walichokuwa wanastahili nasi vinginevyo.
“Kwanini umewaacha?”
Mtu huyo mfupi,mwenye vigimbi mguuni alihoji kwa hasira huku akimtizama Ruth aliyekuwa chini!Hapohapo akakoki mtutu na kumuwekea kichwani kwa niya ya kumuuwa!
“Tafadhali,usiniue.Nitakupa chochote unachotaka”
“Umechelewa”
Kabla ya kuchukuwa maamuzi ya kumimina risasi,akili yake ikahama baada ya kuona kifua cha Ruth kilivyotuna,mbali na kuvaa shati mpaka juu lakini kifungo kimoja kilikatika,hiyo ilifanya nusu ya matiti yake yawe wazi!Mtu mfupi,akatulia kidogo na kuanza kumtafakari Ruth, kuanzia juu mpaka midomoni,akagundua uzuri wa msichana huyo,mawazo ya ngono yakamjia hapohapo!Aliamini angepata dhambi kubwa kukiua kiumbe kitamu kama hiko bila ya kukifaidi.
“Mlinde huyu kwanza,mimi naondoka naye”
Mtu mfupi alimwambia mwenzake,sentensi hiyo ikawa imeeleweka!Bila kujiuliza mara mbilimbili akambeba Ruth begani lakini kabla ya kuanza hatua,Ahmed akamshika mguu kwa niya ya kumzuia sababu alishaelewa kinachoenda kufanyika ni kitu gani baada ya Ruth kubakwa,hata hivyo juhudi zake hazikumsaidia sababu alipigwa teke moja la mdomo lililomfanya ahisi maumivu makali na kuona nyota nyingi,hapohapo akatulia.
“Niachieee,niache”
Ruth alipiga kelele huku akimpigapiga mtu mfupi mgongoni sababu aliwekwa begani,hiyo haikumsaidia chochote kwani alienda na kutupwa katikati ya kichaka chenye miti mingi.
“Lala chali,panua miguu yako!Sitaki usumbufu.Vinginevyo nitakuua sasa hivi”
Mtu mfupi alikuwa mwenye uchu kuliko kawaida, ndiyo maana alifungua zipu yake na kuanza kuzichana nguo za Ruth!
“Tulia basi mpenzi,mbona una papala hivyo?”
Lilikuwa ni wazo la kiintejensia alilolipata muda mfupi tu,hakuwa ana uhakika kama lingefanya kazi. Jambo hilo akalifananisha na mchezo wa kamali,kupata ama kukosa!Lakini kwake ilikuwa ni bora hivyo kuliko kusubiri abakwe kisha auwawe kinyama kama maiti nyingine alizoziona.
“Nitulie nini?Acha ujanja wako unataka kufanya nini kisura?”
“Najua ukimaliza hapa,utaniua.Sasa kwanini namimi nisi enjoy,namimi nina uchu kama wewe!Unaweza mapenzi lakini?”
Laiti ungemuangalia Ruth alivyojilegeza na maneno anayotoa kinywani ungesema ni kweli ana maanisha kumbe haikuwa hivyo,ndani ya moyo wake kulikuwa na chuki za waziwazi.
Katika mahesabu aliyopiga akaliona jiwe kubwa akajivuta kwa juu kidogo na mgongo ili liwe karibu yake zaidi,jamaa huyo akaweka mtutu kando!Ruth akaanza kuvua nguo taratibu akamsogelea na kuanza kumbusu,japokuwa mdomo wa mtu mfupi ulikuwa unanuka na wenye meno ya njano kama kokwa la embe lakini alivumilia,akateremsha suruali yake na kutoa boxa kwa kasi jambo lililomfanya Ruth apigwe na butwaa la waziwazi,mtu mfupi alikuwa na mashine ndogo kama mbilimbi pori yaani kibamia kama masistaduu wa kibongo wanavyoziita!
Hata kama ingetokea angefanya naye ngono hakuwa ana uhakika kama angemfikisha kitonga zaidi tu angemchafua!
“Njoo basi mpenzi”
Ruth akajilegeza na kuanza kumtomasa kifua huku mkono mmoja akipapasa taratibu jiwe lililokuwa chini pembeni,alivyohakikisha kalishika sawasawa,akazidi kumvuta kwake upande wa chini ili amlalie kifuani, hilo ndilo kosa,alilofanya mtu mfupi!
Jiwe lililokuwa mkononi mwa Ruth lilimfikia utosini,likamfanya apige kelele sana,Ruth akainua tena mkono na kumpiga nalo kichwani akawa kama anayeua nyoka.Alivyotaka kumpiga tena,akapigwa kibao kikali cha usoni kilichomfanya aone nyota,mtu mfupi akawa kama amepata nguvu alivyotaka kusimama Ruth akamshika shingoni na kumng’ang’ania mgongoni!Mtu mfupi,akasimama na kuanza kuzunguka huku akijaribu kumtupa Ruth chini lakini zoezi lake likaonekana kuwa gumu sababu Ruth alimshika shingoni mikono yake na miguu kaiviringisha mwilini mwake kama nyoka anayetaka kumeza Ng’ombe,alichokifanya msichana huyo mdogo akatumia vidole vyake,kwa kasi ya ajabu akavitumbukiza machoni mwa mtu mfupi!Hiyo ikafanya jamaa huyo,apige yowe na kumrusha Ruth kwa nguvu,wote wakadondoka chini lakini bahati nzuri ikawa kwa Ruth sababu alidondoka karibu na mtutu,haraka akaushika!
Japokuwa hakuwa anajuwa jinsi ya kuutumia lakini alikuwa ni mpenzi sana wa kuangalia sinema za kijeshi,akaona kilimi cha kufyatua risasi hapohapo bila kulenga akakivuta.
“Griii griiii griii griiiii”
Zilikuwa ni risasi nyingi zinatoka,zingine zikienda pembeni lakini tatu zilimfikia mtu mfupi kifuani na kumchota hewani,akatupwa pembeni akakata roho.
Kutokana na uzito wa mtutu na mtingishiko wake,ukamfanya Ruth kukosa muhimili akajikuta anadondoka chini chali,sio siri alikuwa akihema mfululizo kama mtu aliyetoka kukimbia umbali mrefu,majasho yanamtoka haamini kinachotokea!Hakutaka kubaki akiwa amelala,akasimama na kuweka nguo yake vizuri,kisha akatoka msituni akiwa na mtutu ili kurudi alipokuwa Ahmed,ambapo alimkuta kapigishwa magoti anataka kuuliwa,bila kupoteza wakati akamimina risasi nyingi zisizokuwa na idadi.Jamaa aliyeshika mtutu akatupwa mbali na risasi,kichwa chake kikawa kimeharibiwa vibaya sana ubongo upo chini,hapo ndipo ukawa mwisho wake!
“Ah..med”
Ruth akaita,ulikuwa ni ukombozi wenye miujiza mikubwa sana baada ya kukata tamaa!Ahmed,hakutaka kuamini,kuna mambo alitaka kuuliza lakini alishindwa sababu haukuwa wakati wake,walichokifanya ni kusonga mbele!Walitembea na kupumzika pumzika bila kukutana na barabara ya aina yoyote ile,mpaka kunapambazuka ilikuwa kazi bure,mwisho ilibidi wakae na kutafakari upya.Baada ya kutulia kwa muda mrefu wakasikia,muungurumo wa gari.Hawakutaka kujiuliza mara mbilimbili wakiamini barabara ipo karibu,wakapata nguvu mpya na kuanza kufuata mlio wa gari hilo,wakatokeza kwenye barabara pana yenye vumbi,wakazidi kusikia muungurumo wa gari unawakaribia,wakashukuru Mungu!Lakini katika hali ya kushangaza,wakaliona gari aina ya Corrola,halikuwa ngeni machoni mwao!Lilikuwa nila watu wabaya wanaowatafuta,walivyotaka kukimbia ikashindikana kwani ndani ya gari waliteremka wanaume wanne walioshiba na kuwaweka chini ya ulinzi.Wote,wakakamatwa kwa mara nyingine na kupakiwa ndani ya gari na hawakuwa na ujanja mwingine zaidi ya kusubiri kifo tu.
Umbali wa kama kilomita tisa,wakawa wamefika kwenye kijumba walichokifananisha na Jehanam,wakashushwa.
“Mkuu,hawa hapa”
“Kwanini,hamkuwaua hukohuko?Nipatie bastola”
Kitendo cha kuongea hivyo kilimfanya Ahmed,ahisi tumbo linamuuma hakuelewa la uwoga wa kifo ama kuharisha,akasali sala zake za mwisho na wa kwanza kuwekewa bastola alikuwa ni yeye,alitetemeka akijua tayari muda wake wa kuishi duniani umefikia tamati,akapata muda kidogo wa kuwakumbuka ndugu zake,ambao aliamini walikuwa wakimtafuta akamuona Yusrath alivyosaidiana na George Charles kuuza roho yake!Akafumba macho ili asubiri kifo chake.
“Kacha kacha”
Jamaa huyo mrefu aliyefahamika kwa jina la Shoki,alikoki bastola tayari kwa kumuuwa Ahmed,hakuwa mwenye huruma hata kidogo roho yake ilifananishwa na Diktekta Carl Peters!
“Griii griiiii”
Kilichomkatisha ilikuwa ni simu,akasikilizia kidogo huku akitafakari amuuwe Ahmed kwanza kisha apokee simu ama apokee simu kwanza!Wazo la pili likawa na nguvu,akatoa simu!Akashtuka sababu ilitoka kwa mkuu wake wa kazi.
“Yes,Halloo”
“Vipi?Yule kijana tayari,au bado yupo?”
“Yupi?”
“Aliyeletwa na Kamanda Jacob”
“Ndio nam-malizia hapa,kazi iishe”
“Kimenuka,achana naye!”
“Sijakuelewa”
“Nimesema hivi,achana naye”
“Unajua madhara yake lakini?”
“Fanya kama tulivyofanya kwa yule msanii mwanamuziki wa hiphop”
“Poa”
Simu ikakatwa,bastola ikashushwa chini!Shoki,akatembea mpaka kwa wenzake,wakaweka kama kikao kidogo wakiteta,Ahmed akabebwa na kufunikwa kitambaa cheusi usoni na kufungwa kamba!
“Tumekuonea huruma sana,mshukuru Mungu!Ole wako,useme ulichokiona huku.Nakuapia,tutakurudisha tena maana hatushindwi kujua ulipo!”
Ahmed alisikia maneno hayo,akiwa na kitambaa cheusi usoni,mikono yake imefungwa kamba hajui anaenda wapi lakini alichojua yeye, yupo ndani ya gari,anapelekwa sehemu fulani isiyojulikana!
Ghafla sura ya Ruth ikamjia kichwani,hakuwa ana uhakika kama yupo ndani ya gari ama ameachwa kule Jehanam amekufa.Kwa haraka walitembea umbali wa kama Kilomita ishirini na saba!Akahisi gari limesimama,katika kutafakari akahisi kapigwa na kitu kizito kichwani hapohapo akapoteza fahamu,walichokifanya watu hao ni kuteremka ndani ya gari,wakambeba Ahmed na kumtupa kandokando ya barabara ya Mbagala bonde la MZINGA,bila mtu yoyote kuwaona, wakaingia ndani ya gari.Namna walivyoligeuza iliogopesha kwani tairi zilizunguka kwa kasi na kutokomea, kusikojulikana!



“Baba Linna”
“Naam”
“Kile nini?”
“Kitu gani?”
“We huoni?Pale chini pembeni ya mti”
“Sioni kitu”
“Baba Lina,ebu angalia vizuri”
Ilikuwa ni barabara ya Mbagala,Bonde la Mzinga!Ndani ya gari kulikuwa na watu wawili,mtu na mkewe asubuhi na mapema!Wa kwanza aliyeona kitu asichokitarajia ni mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Mama Lina!Ni kweli,macho yake hayakumdanganya! Kando umbali kidogo ya mti kulikuwa na mwili wa mtu unacheza cheza,usoni umefunikwa kitambaa.Jambo hilo lilimfanya ashtuke na kumtaarifu mumewe ambaye alionekana kutoona kitu lakini baada ya kutuliza akili,akashtuka sana!
“Unataka kwenda wapi Mme wangu?”
“Unataka mimi nifanye nini?”
“Simamisha gari!”
“Mama Lina,tupo sehemu hatari!Haujui siku hizi majambazi wanatumia mbinu hizo kuteka watu”
“Kwani hauna silaha?”
“Hata kama”
“Sasa unaogopa nini?”
“Wasiwasi ndio akili siku zote”
Mwanamke aliingiwa na roho ya huruma tofauti na siku zote,haikujulikana kama malaika kamshukia ama pepo linataka kumjaribu,kelele zake zikafanya gari aina ya Toyota Surf, liegeshwe pembeni.
“Ni hatari lakini”
“Nenda kaangalie au piga simu polisi”
“Okay subiri”
Alichokifanya Baba Lina ni kujiinua kidogo na kuchomoa bastola iliyokuwa kiunoni mwake,akaikoki na kumtizama Mkewe kwa ishara ya kumuaga na kumwambia ‘Kuwa makini’
“Tia loki,milango”
“Sawa”
Baba Lina akashuka,alikuwa ni mwanamme mwenye rangi ya maji ya kunde,mfupi kiasi na mwenye kitambi cha wastani.Hakuwa mzee sana lakini kwa haraka alionekana ni mtu mwenye pesa zake kwani rangi yake ya ngozi ilikuwa ya kung’aa weusi wake wa kutakata,alivyopiga hatua mbili akageuka nyuma ili kumtizama mkewe,kisha kusonga mbele huku bastola yake ikiwa mkononi lakini mkono ulioshika upo nyuma,akatembea kwa tahadhali mpaka chini ya mti.Kitu alichokiona kilimshtua mno,mtu aliyekuwa chini amefungwa kamba alimuogopesha sababu alikuwa na damu mikononi na baadhi ya majeraha,shingoni.Alichokifanya ni kumkanyaga na mguu ili kujua kama ana uhai.Moyo wake ukapiga kwa nguvu baada ya mtu huyo,kujitingisha!Akatizama huku na kule kisha akatembea kwa haraka kulifuata gari lake.
Alivyofika akagonga kioo,mkewe akafungua!
“Vipi?”
Mke akauliza akiwa na shauku ya kujua kilichotokea!
“Wait”(subiri)
“Nini?Tunaenda wapi?”
Alichokifanya Baba Lina ni kugeuza gari na kurudi walipotoka akisema kwamba anaelekea kituo cha polisi kutoa taarifa ya tukio aliloliona ili baadaye usije ukawa mlolongo mrefu wa maswali,kwa kufanya hivyo aliamini angekuwa upande salama!
Haikuchukua dakika tano walifika kituo kidogo cha polisi,wakatoa taarifa juu ya tukio lililotokea.Difenda ikawashwa na bahati nzuri polisi walionesha ushirikiano mkubwa sana!Walivyofika Bonde la Mzinga!Wakaona mkusanyiko wa watu,kama kawaida ya wabongo jambo dogo hukusanyika na ndicho kilichotokea,askari wakashuka na kuwatoa pembeni!Walichokifanya ni kumsogelea mtu huyo aliyekuwa na kamba mikononi huku amezibwa usoni.
“Sogeeni pembeni”
Askari mmoja akasema,baada ya kuona mkusanyiko wa watu mithili ya nzi wanaofuata kokwa la embe!
“Nimesema kaeni pembeni,sogeeni kule”
Kama taratibu za askari,picha za mnato zikapigwa wakavaa ‘Gloves’ na kuanza kukata kamba za mikononi.
“Msiniue tafadhali,msiniue”
Ni sauti iliyosikika kutoka kwa mtu huyo ambaye bado hawakulifahamu jina lake,wakamfungua usoni.Wote wakamtizama kwa huruma kwani uso wake uliharibika kwa kiasi cha kutosha na ulikuwa na alama sambamba na michirizi ya damu zilizokauka!Umati wa watu uliokuwa mbele yake,ulimshangaza Ahmed watu wengi walimzunguka na kumuangalia, hakuelewa alikuwa kwenye ndoto ama kila kilichotokea kilikuwa na ukweli ndani yake.
“Unaitwa nani?”
Afande mmoja akamuuliza lakini Ahmed akashindwa kujibu chochote,walichokifanya ni kumshika huku na kule na kumpakia kwenye diffenda ili akatoe maelezo!
“Sisi,tunaenda”
“Hapana na nyie twendeni”
Jambo hilo baba Lina alilitegemea,alishaelewa nini kinachoenda kutokea mbele kwani alijua tabia za maaskari wa kibongo kuhoji maswali hivyo alitakiwa kwenda kuisaidia polisi kwa kuandika maelezo jinsi alivyomuona mateka huyo,hilo halikuwa na tatizo akaingia ndani ya gari wakaanza kufuatana nyuma,mbele difenda nyumba Toyota Surf!
Waliingia kituo cha polisi saa 3;12 asubuhi, hakukuwa na maabusu wengi,Ahmed alishushwa lakini alionekana kama mtu aliyepata ugonjwa wa kupooza!Tangu walipotoka mpaka wanafika kituoni, hakuweza kuongea chochote sio kwamba alishindwa bali matukio aliyoyaona masaa machache yaliyopita yalimfanya adate na mdomo wake kuwa mzito!Zilikuwa ni picha mbaya ambazo hakuwahi kuziona katika maisha yake na hakuwa ana uhakika kama zingekuja kufutika,ghafla akaiona sura ya Ruth msichana mrembo ambaye bado kwa wakati huo hakujua yupo wapi na alipatwa na nini!
“Upo sehemu salama,hapa ni kituo cha polisi.Mbagala,jina lako nani?”
Japokuwa afande aliyekuwa zamu siku hiyo aliongea kwa sauti iliyosikika lakini Ahmed hakumsikia,mawazo yake yalikuwa mbali,machozi yakaanza kumlenga akashindwa kujizuia na kujikuta analia, hiyo iliwafanya askari wote waangaliane!
“Usilie,jikaze wewe ni mwanaume.Tunataka kujua,ilikuwaje mpaka ukawa pale?”
Ilikuwa ni kama wamefungulia koki ya maji,Ahmed alilia mno!Kwikwi ikamshika,kila kitu kilichotokea katika maisha yake kilikuwa kama ndoto!Bado hakuamini kama mkandarasi wa kila kitu ni Yusrath mkewe wa ndoa,akatamani kuongea kitu lakini akakumbuka alivyoonywa na watu hatari,wakimtishia maisha yake asifungue bakuli lake! Abaki na siri hiyo mpaka kifo!Hakuelewa ni kitu gani akiseme lakini alichokijua yeye ni kwamba asiseme kitu chochote kuhusu kutekwa kwake!
“Nah..itaji kumpigi..a Baba angu”
“Yuko wapi?”
“Ha..pa hapa Dar”
“Namba yake unayo?”
“Ndio”
Ahmed,alijikaza kisabuni akizungumza kwa tabu na mateso,alichokifanya ni kuzitaja namba za mzee Kajeme!Hapohapo,akapandiwa hewani baada ya simu kuita kwa muda mrefu ikapokelewa,Ahmed akapewa simu ili azungumze.Kwa uchungu na kwa sauti ya kwikwi akazungumza na kusema alipo,alivyomaliza askari akapewa ili atoe maelezo mafupi tu.Kila kitu kwa Ahmed kilibadilika,hakuwa katika hali ya kawaida hata kidogo,picha mbalimbali na taswira za maiti za wanawake waliobakwa na kuuwawa kinyama zilijijenga ndani ya kichwa chake akawa kama anatizama filamu ya kutisha,bado aliendelea kulia mpaka nusu saa baadaye, alivyojitokeza mzee mmoja wa makamo,aliyejitambulisha kwa jina la Kelvin Kibumu,akidai kwamba ameagizwa na Mzee Kajeme.
“Simama kijana,huyu ndio baba ako?”
Afande Chupa,akahoji baada ya kumuinua Ahmed.
“Hapana,lakini namfahamu”
“Nitajie namba za baba ako tena”
Swala hilo likafanyika,namba zikatolewa ili afande ajipe uhakika kama Mzee Kibumu ndiye ameagizwa kweli,baada ya kufanya mawasiliano na Mzee Kajeme na kuhakikisha!Hatimaye Ahmed akaruhusiwa kutoka kituo cha polisi!
*****
Usingizi ulikuwa ni kitu hadimu sana kupatikana usiku,alijilazimisha lakini kwake ikawa kazi bure!Kila wakati alimuwaza Ahmed, akimuombea huko alipo,awe salama ingawa hakuwa ana uhakika kama angemuona tena!Kitu ambacho asingependa kukisikia ama kukipokea ni kusikia Ahmed amefariki,hakuwa ana uhakika kama angeweza kuishi tena duniani matukio ya kutisha ya watu kukutwa wameuwawa na watu wasiojulikana yalimfanya azidi kuogopa zaidi.Alitamani siku wakae chini na amshukuru kwa namna alivyojitolea kumpa pesa ili aikomboe nyumba yao iliyokuwa inapigwa mnada!
Roho ya Ahmed,ilikuwa ni tofauti na watu wengine waliomtenga kipindi ana matatizo,akaamini kabisa huyo ndiye angekuwa mwanaume wake sababu walitoka mbali,Hajrath alienda mbali zaidi na kudiriki kusema kama yeye ni chanda basi Ahmed ni pete kwani siku zote ‘Chanda chema huvikwa pete’Hajrath alikuwa ni mtu wa kushika tama muda wote,chakula hakikushuka tena!Mtu wa karibu aliyekuwa ana mfariji kwa kipindi hiko chote ni Benjamin Ngowi,ambaye muda wote alikuwa bega kwa bega, wakipambana kuzunguka vituo mbalimbali vya polisi,walipita Mabatini,staki shari,Mwananchi,Urafiki,Oysterbay,Buguruni,Mabibo na vituo vingi vikubwa!Mwisho wa siku tegemeo lao likawa kwa Mzee Kajeme ambaye aliwaambia watulie na kila kitu kingekuwa sawa,ni kweli Wanajeshi waliingia kazini na kuanza kupekenyua kila kitu,hayakupita masaa 12 Mzee Kajeme akapigiwa simu kwamba mwanaye kapatikana!
Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake,mtu wa haraka aliyeamini alikuwa karibu ni Mzee Kelvin Kibumu,akampigia na kumuomba aende Mbagala akamchukue Ahmed, hilo likafanyika.

****
“Ahmed kapatikana”
“Muongo,unanitania”
“Nakwambia ukweli,kwanini nikutanie kwenye swala kama hili”
“Yuko wapi?”
“Yupo Mbezi,kwa mjomba wake”
“Nani amekwambia?”
“Baba yake,kanipigia simu”
Moyo wa Hajrath ulipiga kwa nguvu,hakuelewa kwake taarifa hizo zilimshtua ama zilimuogopesha kwani mapigo yake ya moyo yalikita kwa kiasi kikubwa!
“Naomba unipitie twende wote”
“Sawa,jiandae”
Kitendo cha kuambiwa hivyo aliingia bafuni kwa kasi huko alijimwagia maji bila kujisugua vizuri kama anavyofanya siku zote, ilikuwa ni lazima awahi!Picha ya Ahmed ilimjia kichwani,akamshukuru Mungu ingawa hakutaka kuamini moja kwa moja kama ni kweli mpaka angemuona na kumshika, Hajrath akajifananisha na Thomaso siku hiyo!Furaha aliyokuwa nayo ilitisha.
Alivyomaliza,akanyoosha mpaka kwenye meza ambapo hapo alipaka mafuta,akaweka nywele vizuri na kuvaa kwa haraka!Bila kuchelewa akampigia tena Ngowi kwa mara nyingine!
“Umefika wapi?”
“Kuna foleni,Ubungo hapa”
“Nikukute hapo,nachukuwa boda”
“Poa,napaki pembeni hapa sheli”
Hajrath hakutania,kuendelea kumsubiri Benjamin Ngowi ilikuwa ni sawa na kuchelewa kumuona Ahmed wake,alichokifanya ni kutoka nje na kutafuta pikipiki.
Kwa kuwa dereva alizijua njia za panya,akapita kandokando na baada ya muda mfupi akawa amefika Ubungo mataa,akamlipa dereva ujira wake.Gari la Ngowi alilijua,haikumpa shida akatembea mpaka ilipo,akagonga kioo na kufungua mlango!
“Mambo”
Ngowi,alikuwa wa kwanza kusalimia.
“Poa,umesema Ahmed kapatikana?”
“Ndio”
“We,ushamuona?”
“Bado,ndio naenda hapa”
“Mungu wangu,alipatikana wapi?Na alikuwa wapi?”
“Mimi sijui,tutajua huko tukifika”
Hakukuwa na muda wa kupoteza,kila mtu alitaka kumtia Ahmed machoni.Hajrath ndio usiseme,aliapia na kujihaidi safari hii angemwambia Ahmed ‘live’ juu ya hisia zake na ikiwezekana wafunge ndoa kwani tetesi za kupeana talaka na Yusrath alizisikia!
Alikuwa katika mawazo makubwa sana akatamani gari lipae juu wawahi kufika,hakuelewa ingekuwaje siku wanaishi ndani ya kuta nne,wanatumia kitanda kimoja,shuka moja!Aliamini Ahmed ndiye mwanaume wake aliyepangiwa na Mungu na ilikuwa ni lazima kabla ya kufunga ndoa wapitie changamoto mbalimbali na misukosuko!
Iliwachukuwa dakika thelathini nzima,kuwasili Mbezi kwa Msuguli,hapo walipanda juu na kuingia barabara ya vumbi.
“Unapafahamu huku?”
Hajrath akavunja ukimya.
“Napajua”
Haikuchukuwa dakika mbili,wakafika nje ya geti kubwa kiasi lenye rangi nyekundu.
Hakukuwa na umuhimu wa kuingiza gari ndani,wote wakashuka na kugonga geti ambapo walifunguliwa na msichana,kwa haraka haraka na kumuangalia alikuwa ni dada wa kazi,wakasalimiana na kukaribishwa ndani.
“Shikamoo”
“Shikamoo”
Wote walimsalimia Mzee waliyemkuta,wakajitambulisha kidogo na kueleza shida yao!
“Ahmed,yupo lakini amepumzika!Ngoja nikamuangalie”
Mzee alikuwa mkarimu sana na aliwataka wasubiri vinywaji huku yeye akielekea chumbani kumuita Ahmed,ilikuwa ni nyumba kubwa lakini ilielekea ya kizamani sana na wanoishi humo walikuwa wazee kwani viti vilikuwa vya kizamani vya mito na tv ilikuwa ya Chogo.Ukuta wa ndani ulikuwa umechoka kiasi,umepauka!
“Karibuni”
“Ahmed!”
Kila mtu alishtuka baada ya kumuona Ahmed,amesimama mbele yao!Mkononi ana bandeji kubwa,shingoni ana plasta na maeneo ya kichwani kavimba kidogo,Hajrath alishindwa kuzuia hisia zake hapohapo akasimama kwa kasi na kumrukia,akamkumbatia kwa nguvu kama mtoto aliyemuona Mama yake.
Bila kuona aibu yoyote,akasogeza mdomo wake mdomoni mwa Ahmed wakaanza kulana denda,mzee aliyekua pembeni pamoja na Benjamin Ngowi,wakashindwa kuwaangalia, wote wakatizama chini.


Mvua bado ilikuwa kubwa,iliyoambatana na mwanga wa radi!Nemesi na Amney waliloa chapachapa wakiwa nje!Lilikuwa ni tukio la aina yake na halikuwahi kutokea,Nemesi alikuwa chini kapiga magoti mvua kubwa inamnyeshea,kamshika mkono Amney anamsihi asiondoke!Moyoni alijihisi kujuta na moyo ulimuuma kwa kiasi cha kutosha,akamlaumu shetani.Yote aliyoyaongea na kuomba msamahaa hayakumfanya Amney,arudishe moyo wake nyuma, alikuwa akilia lakini machozi yake yalisombwa na maji ya mvua,maneno aliyokuwa anazungumza Nemesi yalipitia sikio la kushoto na kutokea kulia!Hakuwa tayari kumsamehe Nemesi na kwa wakati huo hasira na wivu ndivyo vitu vilivyokuwa vinamuendesha, ndio maana alilia kwa kwikwi,akimtaka Nemesi amuache aende zake ili amuachie Necka Golden.
“Amney,nisamehee!Bila wewe siwezi Mama”
Nemesi,alizidi kuupigilia msumari msamahaa wake,akijaribu kutumia kila nyimbo nzuri kumuimbisha lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,acheze mziki.Tukio hilo liliwafanya wamama wa uswahilini wasogee karibu zaidi ili wasikilize kinachoendelea,hata hivyo hawakuweza kuwafikia karibu, kutokana na mvua kubwa,hiyo iliwafanya waishie vibarazani kwao!
“Nem..si niache tafadhali”
Amney,akasema kwa kwikwi.Moyo wake bado ulimuuma hasa picha ya Nemesi akiwa kitandani na Necka Golden wapo uchi wa mnyama,hasira zikamshika ghafla akamsukuma lakini hakufanikiwa sababu mikono ya Nemesi ilijiviringisha kiunoni mwake,akashindwa kabisa hata kutembea!
“Nisamehe Mke wangu.Kosa sio kosa,kurudia kosa ndio kosa”
“Ndi..o ulale na rafik..i yangu!Umekosa nini kwangu?”
“Sijakosa kitu Amney!Ni tamaa tu,nakiri kwako sitorudia tena”
“Hapana,siwezi Nemesi.Siwezi naomba niache niondoke”
“Siwezi kukuacha,nipo tayari kwenda nawewe popote pale”
Usingekuwa makini ungedhani watu hao wanaigiza,lakini haikuwa hivyo kila kitu kilikuwa halisi kabisa!Nemesi alizidi kutumia ushawishi mkubwa,akimaanisha kile anachokisema, alishaelewa kosa lake na alikiri kwamba hatorudia tena,wakati mwingine alidiriki kusema Necka ni pepo lililotumwa na shetani kuja kuharibu mapenzi yao.
“Mke wangu,naomba tusimpe shetani ushindi.Rudisha moyo nyuma,kosa moja lisikufanye ukafuta mema yote!Kumbuka tulipotoka Amney”
Amney alitulia kidogo,kuna jambo ilielekea alikuwa akilitafakari kichwani kwake!Ghafla akakumbuka matukio mbalimbali yaliyofanywa na Necka Golden kipindi wapo chuoni Makumira,namna alivyotembea na Ahmed kimapenzi!Akawafanya waachane na Hajrath,akaanza kujilaumu ni kwanini kamkaribisha nyoka huyo ndani kwake, akidhani wenda kajirekebisha,alivyotuliza akili akagundua mwenye makosa ni yeye mwenyewe kwani bila Necka kuwepo ndani ya nyumba hiyo,hayo yote yasingetokea!Akatulia kidogo na kumtizama Nemesi,anavyoomba msamahaa huruma ikamuingia,moyo ukamuuma akazilaumu hasira!Mambo mengi yakamiminika kichwani kwake,akakumbuka jinsi walioanza maisha yao kwa pamoja wakiwa na furaha pamoja na ndoto kubwa mbeleni,hiyo ikamfanya ashushe pumzi ndefu akiamini kuachana na Nemesi ingemaanisha Necka Golden ndiye mshindi,akamshika Nemesi mkono na kumuinua,akamkumbatia kwa nguvu huku mvua kubwa ikizidi kuwanyeshea mwilini!
“Nakupenda Nemesi,nakupenda sana”
“Nakupenda pia,mke wangu”
Kila mtu aliguswa na hisia za mwenzake,hatimaye msamahaa ukatoka!Alichokifanya Nemesi ni kuchukua begi la Amney,wakaingia ndani huku ndani ya mtima wake akishikwa na hasira juu ya shetani Necka Golden mwenye mguu mmoja,kitendo cha kufika seblen, akanyoosha mpaka chumbani kwake.
“Sikia,chukua kilicho chako.Ondoka sasa hivi”
Necka Golden,alikuwa kitandani!Haelewi ni kitu gani akifanye kitendo cha kumuona Nemesi,akiingia huku kaloa chapachapa kilimfanya asimame wima na kutaka kujua nini kimeendelea,ingawa alikuwa na uhakika asilimia zote Amney keshaondoka, kwake ingekuwa ni furaha kubwa na aliomba iwe hivyo.
“Hivi,haunisikii?Nimekwambia nini?”
Necka bado,alijibaraguza akitafuta pozi la kuomba msamahaa!
“Nemesi,Darling.Tuyamalize haya,mimi nakupenda kweli nipo radhi kuishi nawewe,ili upooze maumivu yako!Nikubalie tuishi wote,nitajiita mwenye bahati”
Haikujulikana kama yanatoka kinywani tu ama ndani ya mtima wake lakini alikua siriazi hacheki,isitoshe alisimama ili amsogelee Nemesi ambaye bado alikuwa ameduwaa, anashindwa ni kitu gani amjibu,hapo ndipo Amney akatokeza mlangoni.Hiyo ilimfanya Necka arudi nyuma hatua tatu sababu tukio hilo,hakulitegemea hata kidogo!Lilikuwa ni jambo la kushtukiza.
“Necka,wewe ni rafiki yangu!Naomba kwa upole tu,uondoke”
“Amney nisa…”
“Please,sitaki kukuona sasa hivi utoke!Kabla sijakufanyia fujo,nadhani unaelewa mimi nakuwaje,sio mgeni kwako”
Utata wa Amney ulijulikana na Necka Golden,aliufahamu vizuri.Hakutegemea kama siku hiyo angekuwa mpole namna hiyo,Amney alikuwa mkorofi na mwenye hasira mbaya,kitu chochote kitakachokuwa karibu ni lazima angemrushia!Siku hiyo alijishangaa mwenyewe!
“Necka ondoka,tafadhali”
Hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya mwisho kutoka kwa Amney,baada ya hapo alitoka na kuingia chumbani kwake!Ndani ya dakika mbili,Nemesi nayeye akaingia chumbani!
“Keshaondoka?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Amney!
“Bado”
Kitendo cha Nemesi,kumjibu akatabasamu.Na hiyo ndiyo ilikuwa kawaida yake akiwa na hasira kwanza lazima atabasamu kisha akunje sura,hapohapo akasimama wima na kutoka chumbani, Nemesi ilibidi amfuate kwa nyuma sababu alielewa kulikuwa kuna dalili ya damu kumwagika siku hiyo!
“Baby….”
Nemesi,aliita baada ya kumuona Amney kashika chuma kidogo kinachotumika kuvunjia nazi.
“Nemesi,niache.Si hataki kutoka kistaarabu”
“Unataka kufanya nini sasa?”
“Niache utaona,Nemesi nipishe nipite”
Kumruhusu Amney kupita yangekuwa mambo mengine mazito, ndio maana alitanda mlangoni!
“Please punguza hasira”
“Una mtetea Malaya wako,nakuuliza unamtetea Malaya wako?”
Sauti tayari ilibadilika,Amney akapandisha mori na alizungumza kwa jazba!
“Sio hivyo baby”
“Kumbe nini?Basi niache nipite,Nemesi niache nipite!Nemesi sogea nipite”
Haikuwa kazi rahisi kumzuia Amney mwenye hasira mbaya za mkizi,nguvu za ajabu zilimuingia akamsukuma Nemesi pembeni akacholopoka na kuuvaa mlango wa chumba alichokuwa Necka!Kilikuwa ni kitendo cha ghafla na Necka hakukitarajia,kitendo cha kumuona Amney kashika chuma mkononi kilimuogopesha!Akamshuhudia anakuja kwa kasi usawa wake ili amvae lakini hilo halikuwezekana sababu Nemesi alishafika tayari,akamshika mikono kwa nyuma na kumvuta kwa pembeni.
“Amney,stop this!Tulia,nawewe mpumbavu!Ondoka sasa hivi”
Ndani ilitokea vurugu,mtiti alioanzisha Amney haukuwa wa kitoto!
Hasira zilimpanda katika kiwango cha juu kabisa,shida yake ilikuwa ni kumvaa Necka Golden ampasue na chuma cha kichwa lakini alithibitiwa mikono yake,alivyoona kazidiwa nguvu akajikakamua na kukirusha!Bahati mbaya ilikuwa kwake na nzuri kwa Necka Golden sababu chuma kilimkosakosa, kilimpitia karibu na kichwa kikapiga ukutani!Hapo ndipo Necka akajua hayakua maigizo bali ni kweli,alichokifanya ni kubeba dera lililokuwa karibu,akavaa kwa kasi na kucholopoka kupitia mwanya ulioachwa,hapo ilikuwa kidogo Amney achomoke amvae!
“Amney,punguza hasira mama”
“Nemesi,niache!”
Bado Amney,hasira zilikuwa juu!Hapo alifanikiwa kutoka kwenye mikono ya Nemesi na hiyo ilitokea sababu uhakika wa kwamba Necka keshaondoka,ulikuwepo ndio Maana Nemesi,akamuachia!
“Yuko waaapi?”
“Ameshaondoka”
Kifua cha Amney,kilipanda juu na kushuka!Mapafu yake yalijaa hewa,akashindwa kuongea kitu kingine!Ni kweli siku hiyo isingekuwa Nemesi kumshika wangegawana majengo ya serikali,hilo lilikuwa wazi sababu hasira zake zilikuwa mbaya za kutisha!
“Baby relax,calm down!Usilie,tafadhali usilie baby wangu”
Kichwa chake kilitulia kifuani kwa Nemesi na baada ya hapo,alianza kulia machozi kama mtoto mdogo!Kama mwanamme ilibidi ambembeleze,ndiyo maana akafanya hivyo kwa kumkumbatia huku akimpiga piga mgongoni,akawa kama anambembeleza mtoto alale!Hiyo ilimfanya Amney apate nafasi ya kudeka kidogo!
“Baby nakupenda,nimeumia sana”
“Naelewa mke wangu,nisamehee”
“Usirudie tena,nakupenda sana Nemesi”
“Hata mimi”
Baridi lilikuwa la wastani,mvua ilizidi kunyesha na kufanya radi!Mkono wa Nemesi,ukaanza kufanya kazi yake akaanza kuupapasa mgongo wa Amney taratibu kwa nyuma!Akitumia vidole vyake,akaanza kupandisha flana aliyovaa,akaingiza mkono ndani akagusa ngozi,akazidi kumtomasa!Hiyo ilimfanya Amney ajiongeze,akajivuta kidogo na kumsogelea mdomoni wakaanza kulana denda,midadi ikazidi na mvua ilizidi kunyesha, mkono wa Nemesi ukazidi kushuka chini zaidi akaupitisha kwa mbele,ukapapasa kitovu cha Amney,ukazidi kwenda chini kabisa na kuingiza mkono ndani ya sketi hapo alikumbana na nyasi fupi,zinazochoma choma!Kidole chake kimoja,akakilazimisha kukipenyeza!Kikafika mpaka kwenye mapango na hiyo ndiyo sehemu aliyokuwa anaitaka,kidole chake kilianza kufanya kazi!
“Aaaaaaah”
Ulikuwa ni mguno,uliotokea ndani ya kinywa cha Amney,akahisi kama nguvu zake za miguu zinamuishia!Hapohapo akashindwa kuvumilia,akatoa nguo yake ya juu akabaki na sidiria!Hakutaka kuchelewa kutokana na stimu iliyochanganyika na baridi lililosababishwa na mvua akajikuta anavua na sketi yake,hiyo ilimfanya Nemesi nayeye atupe bukta chini,akazidi kumnyonya mdomo na kumtomasa kifua na sehemu za mapangoni!Kwa kuwa mechi hiyo ilikuwa bunda siliga,ilibidi wamalizane hapohapo!Akamshika Amney vizuri akitumia mikono yake miwili na kumsogeza ukutani,hapo alimbeba kitaalamu mikono yake akaizungusha miguuni mwake!Akamuweka ukutani vizuri,mgongo wa Amney ukawa ukutani,wanaangaliana kilichofuata hapo ni Nemesi kuingiza mtambo ndani ya mgodi wakiwa ukutani,ilikuwa ni rahisi kwa Nemesi sababu alikuwa na nguvu za miguu,akazidi kumkunja Amney akiwa ukutani anaelea juu juu miguu yake ipo hewani!
“Asshsss bebiiiii,iloive you”
Amney,alizungumza kwa sauti ya huba,hapohapo akatoa ulimi wake wakaanza kunyonyana ndimi.

*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)

0 comments:

Post a Comment

BLOG