THE PAINFULL SECRET
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
WatsApp…+255718 862176
SEHEMU YA 9 KATI YA 10
"sasa ndo nini kusimama ivyo kama mshumaa wa pasaka? , si uje ulale"
Ili kua ni sauti ya Flora akiwa kitandani baada ya kumuona Mume wake waziri mkuu Joseph Partson Kasanga akiwa dirishani amesimama kama namba moja akionekana akitafakari na kuonekana mwenye wasi wasi kupindukia.
"Lala"
"Hivi we mwana ume siku izi una vitu gani sijui, una matatizo gani lakini,? "
"Sina tatizo nime kwambia nipo sawa Flora"
Waziri mkuu alimgeukia mke wake na kumtazama kwa makini machoni na kusonya huku akielekea kwenye mlango
"We sonya tu, na mpka huo mdomo uende upande, nita jua, "
Waziri mkuu hakutaka kumsikiliza mke wake maana ange msikiliza angeendelea kumuuzi na pengine ange mpiga na ndo huwa suluisho pekee ana lolifanya akiona mke wake yupo katika hali ile,
huwa ana muacha akiongea peke yake,
Alitoka mpka sebuleni na kutoa simu akiwa tafuta FBI kwenye simu na kuzidi kuwapa vitisho vikali endapo hawato mpata Alfred,. Japo wana mpa moyo kuwa angepatikana muda mchache, haiku mzuia kumuwaza Raisi Alphonce Mriba ambae alitaka ripoti, ivyo kuka matwa kwa Alfred alijua ndio lita kua suluisho pekee na wala si vinginevyo,
Baada ya kuwaza na kujiuliza maswali mengi ana shusha pumzi ndefu na kushika kitambi chake huku akiliendea friji na kutoa kileo,
Alichukua glass iliyo kua juu ya friji na kuanza kumimina akiamini kua ndio suluisho pekee la kuta tua tatizo kwa muda ule.
***************************
Upande wa pili Hannah akiwa ame jificha nyuma ya mti mkubwa wa mparachichi baada ya kukimbizwa na watu asio wajua, ana toka na kuchungulia huku na kule kwa uma kini na kuona watu wale wana pita kwa mbali, kwa tahadhari ya hali ya juu ana rudi nyumbani na kumkuta jaqlin Nyange ambaye pia alionekana kumtafuta sana.,
Baada ya kuingia ndani wana jifungia wakiwa na hofu sana huku waki jiuliza maswali mengi tofauti.
************************
Mkono wa Alfred ulizidi kuendelea vizuri baada ya kupata matibabu ya siri sana ndani ya kambi hiyo ya jeshi bila mtu yoyote kujua,
Akisaidiana na mkuu wa jeshi Msangi, kila alicho taka walimpa ivyo ndivyo ilivyo kua,
Leo hii akiwa tayari kwa kila kitu, .
kutokana na vituko vya serikali wana jeshi hao wana muunga mkono kwa kile anachotaka kwenda kufanya na kumuahidi wange mpa silaha zozote ana zotaka na kuwaahaidi kuwa wata msaidia pale ata kapo kwama hata ikiwezekana waanzishe vita,
jambo lile lina wafurahisha wote wawili Amney na Alfred, ambapo wana washukuru kwa kila kitu na kuanza kujiandaa kwa safari moja tu kwenda kumtafuta waziri mkuu.
"Nipatie Rovolver, shot guns, kisu kidogo, mabomu ya Grenade, SMG, na sub mashine gun. Bila kusahau bastola ndogo , na maboxi ya risasi,. "
Maneno hayo aliongea Alfred na kitendo kile kufanyika pale pale, huku wakiwekea vitu wana vyoitaji ndani ya begi kubwa maalumu kwa ajili ya silaha,
Amney alichukua kofia na kuvaa alichukua koti ambamo ndani aliweka kisu, huku bastola ndogo akiiweka ndani ya kiatu kwa juu, alichomeka bastola vizuri nyuma ya kiuno na kufunika na koti alilovaa, alichukua sub mashine gun na kuikoki huku akiikagua kagua kama inge mfaa,
alivyoo ridhika aliiweka ndani ya begi hilo kubwa , alichukua bastola nyingine ndogo na kuiweka pembeni ya kiuno,
jambo lile lina washangaza sana wana jeshi ambapo hawa kutegemea mrembo kama yule angeweza kucheza na bastola
Kweli alijiandaa vya kutosha na kuji koki vilivyo.
Kila kitu kilienda sawa hata kwa Alfred pia.
,"Alfred kila ra heli huko uendako, ila uki kwama, piga simu nita tuma jeshi,., nita kupa na gari dogo la kwenda"
"Asante sana Msangi kwa kila kitu, "
Walipeana mikono huku waki tingishana baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa,
waliaga na kutoka huku kila mtu akiwa ameshika begi mkononi na kuji dhatiti kikamilifu, wali sindikizwa mpka nje ya geti na kutoka nje huku wakiliendea gari dogo aina ya IST waliyo pewa na Msangi.
Alfred alika upande wa dereva na pembeni yake alikaa Amney kabla ya kupiga gia wana shtushwa baada ya kioo kugongwa na kuwekewa bastola na Harris kwaa nje.
"Mikono juu tokeni nje"
Alivyo angalia upande wa pili wa Amney pia alimuona Carlos akiwa na bastola pia,
Alimuangalia Amney kwa umakini na kumpa ishara akimbania jicho kuashiria kwamba awe tayari kwa lolote lile litaka lo tokea wakati huo,
Alfred pale pale alikanyaga mafuta na gari kutoa mbio huku akiwaacha Harris wakirudi ndani ya gari yao na kuanza kuwa fukuza.
"Shiiit, hawa wame juaje tulipo tena?"
"Sielewi Alfred, nahisi kuna mtu wana mtumia,"
"Wata tuharibia hawa, ina bidi tumalizane nao"
Amney alitoa bastola yake iliokua pembeni ya kiuno na kuishika mkononi akijiandaa kwa lolote litakalo mkabili.,
Milio ya risasi ilianza. Kusikika kwa nyuma wakina Harris wakianza kurusha risasi ambazo zili fanya kioo cha nyuma kipasuke cha akina Alfred, Amney aliweka kichwa chini nayeye kugeuka na kujibu masha mbulizi ya risasi, risasi zilendelea kurushwa kama mvua,
.
"Njoo uendeshe, hao niachie mimi"
Gari lili zidi kwenda kasi Alfred alivua mkanda wa gari na kuanza taratibu kuba dilishana siti,.
Baada ya Alfred kukaa vizuri upande wa pili akimuachia Amney aendeshe gari, alivuta begi na kutoa Rivolver ambayo aliikagua baada ya kuchungulia matundu yake ambayo aliona yame jaa risasi,
Alitoa kichwa nje na kupima kwa kutumia jicho moja kwa ujuzi wa hali ya juu, alifya tua risasi na kupiga tairi la gari waliokuwemo.F,b,i wale, na kufanya gari ile ipoteze muelekeo na kuingia ndani ya mtaro,.
"Simamisha Gari Amney,"
Pale pale gari lili simama,
Na Alfred kutoka,
Ila baadae ana rudi kukaa upande wa pili wa gari akijificha baada ya kusikia risasi zina rushwa,,
Wana kaa chini pamoja na Amney na kujibu masha mbulizi ya risasi.
"Alfred subiri, mwenye bastola kabaki mmoja, ana tumia rivolver"
"Ume juaje?"
"Najua mlio wake, rivolver ina kaa risasi kumi na mbili, kapiga kumi, bado mbili zinaisha,"
Amney aliongea akiwa ana hesabu risasi zita kazo pigwa nyingine.
"Una uhakika?"
"Kuliko unavyo dhani"
Kweli baada ya risasi zile mbili kupigwa ukimnya uli tawala na Amney kusimama akiwa na bastola mkononi,
Na kuanza kusogea upande wa gari la akina Harris ambalo lilikua mtaroni.
"Wote mikono juu"
Aliongea Amney na Harris kuta basamu kwa dharau.
"Paaaaa,"
pale pale Amney alivya tua risasi ili yo mpta F,b,i mwenzake kichwani hii kuashiria kua hakuwa katika hali ya masihara, na kufanya kudondoka kama mzigo,
Na kumfanya Harris abaki akishangaa akizema fundo la mate yaliyo changanyika na woga,
"Mikono juu nasema, inayo fuata wewe hapo,"
Harris alivyoona vile aliweka mikono juu na wote kutiii.
", mpigie waziri mkuu mwambie Alfred ume mkamata tayari"
Harris bila kujibu chochote ali toa simu na kubonyeza namba za waziri mkuu.
"Alfred ninae hapa tayari!"
"Safi sana, yaani hongera sana, sasa muwekeni sehemu mtu yoyote asijue vizuri sana, HONGERENI, nyie ni viboko, mimi nawaelewa nyie, "
"Usijali nita fanya ivyo,."
Simu ili katwa na Harris na wenzake kuwekwa chini ya ulinzi huku safari ya kwenda kwa Emilia kuanza,
Baada ya muda mfupi wali fika na kumuweka Emilia chini ya ulinzi, wali waweka chini na kuwa funga wote kamba,
Amney aliingia kwenye computer na kuanza kubonyeza bonyeza ambapo aliingiza namba ya waziri mkuu na kubonyeza bonyeza vitu ambapo picha ya waziri mkuu ili onekana akiwa mwenye furaha sana.
"Alfred, tuanze kazi"
Aliongea Amney na kumgeukia Alfred,
Alfred alipo kaa na kumuendea Amney alipo
"Angalia Ratiba yake iko vipi leo"
Amney alibonyeza ile computer ambapo aliingia ndani ya system ya ofisi ya serikali na kuanza kusoma ratiba.
"Leo ana msafara saa kumi jioni, ataelekea ikulu kuna kikao , sasa sija jua una taka nini"?
"Sawa mimi nitaenda"
"Alfred, una hakika"?
"Niandalie silaha za kutosha"
.
Baada ya kuongea maneno yale Alfred alichukua video camera na kuingia sehemu nyingine ya chumba kidogo na kuta futa kiti,
baada ya kupata alikaa na kuitegesha video kamera ile mbele yake ambayo ili kua iki mtazama kwa kile ana choenda kusema, alivyo hakikisha kila kitu kipo sawa, alibonyeza record ili video ile ianze kumchukua.
"MHESHIMIWA RAISI, NAJUA SURA HII SIO NGENI KWAKO, VITU VINGI VILI KUA VINA ENDELEA CHINI KWA CHINI NDANI YA NCHI YAKO, WATU WASIO KUA NA HATIA WAME KUFA HUSUSANI DADA YANGU ROSELYN,WAZIRI MKUU JOSEPH KASANGA NA VIONGOZI WENGINE WAME HUSIKA LEO HII NAENDA KUFA KWA AJILI YA KUPIGANIA NCHI YANGU, MIMI SIO AL SHABAB KAMA ULIVYO DHANI AU NCHI ILIVYO DHANI, NIKIFA LEO NAOMBA UITUNZE FAMILIA YANGU, MKE WANGU HANNAH......"
kila alicho kua ana ongea Alfred kili jirekodi ndani ya kamera hiyo ndogo, baada ya kumaliza alichukua simu ya mkononi na kumtafuta Jaqlin Nyange ili aweze kuongea na mke wake Hannah.,kweli kitendo kile kili fanyika.
"Ndio Hannah,. Mi nipo salama usijali, kila kitu kipo sawa"
"Ila Alfred, ukija nita kwambia kitu"
Alfred alivyo sikia vile alikaa kimnya kidogo., na kutojua amjibu nini.
"Hallo Alfred"
"Ndio Hannah nime kusikia, Mke wangu, sawa mama nikirudi usijali"
Ki ukweli hakutaka kumwambia ukweli wowote kuhusu jambo ambalo alikua akitaka kuli fanya, Alfred aliji kuta ana dondosha chozi la uchungu na kumuaga Hannah ili asije kuhisi chochote,
baada ya kufanya kila kitu, alitoka nje na kumkabidhi Amney kamera.
"Shika hii uta mpa Raisi, "
"Alfred mbona siku elewi"?
"Uta mpa raisi wa Tanzania, umeelewa sasa, niwekee silaha vizuri, niambie Waziri mkuu alipo."
"Ndo ana jiandaa kutoka, "
"Sawa, tafuta CCTV camera za ikulu uta kua una niambia kila kitu"
"Poa safari njema"
Alfred alivaa begi dogo na kujiandaa vizuri,.
Baada ya kuridhika aliingia ndani ya gari na kutimua mbio na safari kuishia nje ya nyumba ya waziri mkuu ambapo aliona mapiki piki meupe yakiwa na madereva waliovaa ma elment meupe na pia kuvalia sare nyeupe,.
Baada ya kumuona askari mmoja katoka ali mfata nyuma nyuma na kumuona ana ingia chooni na Alfred kuingia.
Alimfata na kumpiga na kitako cha bunduki utosini na askari yule kudondoka,. Haraka haraka alimvua nguo zake na kuzivaa yeye, alichukua pia na elment na kulivaa kichwani, na kumfanya sura yake isionekane,
Kweli alitoka nje na kupanda ile piki piki nyeupe,
Kwa mbali alimuona Waziri mkuu ana kuja na kuwasha piki piki huku mapiki piki mengine yakiwa tayari kwa safari, waziri mkuu aliingia ndani ya gari hilo aina ya benz na piki piki zile kuanza safari akiwemo Alfred Mulawa katika msafara ule.
***************************
Harris akiwa chini ame fungwa kamba taratibu aliinza kuifungua,
ili vyoachia ali mfata Amney na kumpiga teke lili lomfanya ayumbe kidogo na kugeuka, aliona Harris ana tupa ngumi na kuinama kidogo, pale pale Amney alirusha teke hewani aina ya ROUND KICK na kumfikia Harris puani vilivyo, alimuendea kabla ya kupata nafasi yoyote na kumkaba kooni ambapo baadae alivyo hakikisha amelegea aliizungusha na kuivunja shingo ya Harris na kumwangalia Emilia ambae wakati huo alikua akitetemeka,
Amney alirudi juu ya kiti na kukaa,
"Alfred ndani ya Ikulu nje nawaona walinzi sita, sasa hivi waziri mkuu yupo chumba namba 10H.pita kushoto, simama kwanza,. Nenda nenda,"
Yalikua ni maelekezo aliyo toa Amney kutokana na kuona chumba kizima cha ikulu huku akimuongoza Alfred,
*************************
"Wee vipi una taka nini humu"?
Aliongea waziri mkuu baada ya kumuona Askari yule mwenye nguo nyeupe,
Ila baadae ana shuhudia kofia ile iki vuliwa na kuona sura ya Alfred ,macho yali mtoka na kushindwa kuelewa nini kime tokea mbele yake ,
" simama "
Alfred alitoa kauli moja tu ambayo ili ambatana na hasira na kufanya macho yake yazidi kuwa mekundu.
"Aaa aaaa aaalfred,"
"Kelele,"
Alfred ali mfuata Waziri mkuu na bastola na kumuwekea tumboni.
"Kwanini uli muua Rose?"
"Sio mimi, mimi sio mimi , Alfred usiniue tafadhali"
"Ongoza mbele"
Alfred akiwa nyuma huku akiwa ameshika bastola na kumuwekea kwa nyuma, alimuamuru mlinzi aweke bastola chini na mlinzi yule kutii baada ya kuona waziri mkuu kawekewa bastola kichwani.
Kweli ali fanya vile kwa walinzi wengine alio wakuta,
Ila cha kushangaza baada ya kufika nje ana kutana na maaskari wengi wakiwa wame tanda kila sehemu huku wakiwa na bastola mikononi kila askari akiwa tayari kufyatua risasi.
"Weka silaha yako chini, huna sehemu ya kwenda, weka silaha chini"
Alikua ni mku wa Maaskari akitoa kauli iyo huku Alfred akizidi kumsogeza Waziri mkuu karibu yake huku akiwa ame muwekea bastola kichwani.
"Alfred, weka tu silaha chini,"
Aliongea waziri mkuu kwa sauti ya chini,
"Wekeni silaha chini"
Alfred aliongea huku akiikoki bastola yake .
Alfred alizidi kuwa kazia macho mmoja baada ya mwingine aligeuza shingo na kuwaona maaskari wengine wapo nyuma yake huku magari ya polisi yakizidi kufika katika eneo lile huku wakiwa kwa mbali kidogo na kumzunguka Alfred ambae wakati huo alikua katikati na Maaskari wale kutengeneza kama duara au dimba, waandishi wa habari nao hawa kucheza mbali na camera zao wengine wakirusha kitendo kile hewani,
ki ukweli lili kua ni tukio la ajabu ambalo hali kuwa hi kutokea Tanzania.
Macho ya Alfred yali gongana na Raisi Alphonce ambae wakati huo alikua na walinzi wake wakiwa wana mzuia asisogee kwa Alfred alipo.,
"Nani mkuu wenu?"
Aliuliza raisi Alphonce na askari mmoja kugeuga nyuma.
"Bosco, Bosco yule pale."
"Namuhitaji hapa"
Yule askari alimuangalia raisi Alphonce mara mbili mbili kana kwamba haja sikia swali,
"Wewe ndo mkuu"?
"Ndio mheshimiwa raisi"
"Waamuru watu wako waweke silaha zao chini, hizi ni aibu mnatia huoni waandishi"
"Muheshimiwa, la..."
"Kijana waamuru watu wako waweke silaha chini "
Pale pale Bosco alitoa kauli aliyo pewa na Raisi Alphonce na kilicho kua kinaendelea pale wote wali shusha silaha zao chini na kitendo kile kumshangaza Alfred.
"Ongoza mbele"
Alfred aliongea na taratibu kuanza kutembea na waziri mkuu Kasanga,
huku akiwaangalia kila mtu.
"Na mkija ribu kuni fuatilia, nita muuwa"
Alfred aliingia nae ndani ya gari na kutimua mbio,
"Alfr,,,d unataka nini?, nita kupa pesa zozote una zotaka"
Waziri mkuu Alfred aliongea huku kijasho kiki mtoka kutokana na kuto kutegemea kama maaskari wale wange muacha aondoke na Alfred.
"Kaa kimnya, nita sambaratisha ubongo huo dakika moja,"
Aliongea kwa sauti ya ukali Alfred.
"Dada yangu uta urudisha uhai wake kwa izo pesa,? nitaenda kukuua nawewe siwezi kukuachia hata kidogo ukweli ndo huo"
Waziri mkuu alizidi kutetemeka kwa hofu..,
Alfred alisimamisha gari na kuingia katika kimsitu kidogo ambamo kulikua hakuna dalili yoyote ya nyumba wala watu
"Shuka, toka nje"
Alfred alishuka na kuufungua mlango wa upande aliokua Waziri mkuu Kasanga na kumtoa nje huku akiikagua bastola yake kama ina risasi baada ya kuridhika alimuwekea Waziri mkuu kichwani.
"Piga magoti , piga magoti nime kwambia ,"
Alfred aliongea kwa hasira sana huku akiya bana meno yake, na waziri mkuu akitii amri ile huku akizidi kuomba msamaha.
"Al..fred tafadhali, usiniue mimi ni kama baba yako ujue, nisamehe hata maandiko yana kataza, usilipe baya kwa baya, mwanangu"
"Angalia upande wa kule, leo ndo una jua hayo"
"Eeh Mungu baba Pokea roho yangu"
Aliongea waziri mkuu huku akianza kutoa machozi kweli hakuona kitu kingine zaidi ya kifo kwa wakati huo.
Alfred akiwa amesimama nyuma yake ame muwekea bastola kichwani.
Alizungusha mkono wake juu ya shingo ya waziri mkuu na kuanza kumkaba kwa kutumia nguvu nyingi sana,
Baada ya kuha kikisha waziri ametulia, aliingia ndani ya msitu hii ni kutokana na kusikia milio ya magari ya polisi ikija upande alipo.
Ali mtafuta Amney kwenye simu na kumuomba msaada wa kuja kumchukua, ivyoo baadae ana kuja
kumchukua na wote kurudi walipo kua wamewa fanguka mateka wale wakina Emilia
"Ime kuaje Alfred?"
"Nime muwekea recording device kwenye kalamu yake"
"Alafu sasa?"
"Nataka ukweli uju likane wewe subiri"
.
Habari mbali mbali tofauti tofauti zikiwa zime andikwa katika magazeti hata na stedheni za redio zilizidi kutoa habari za Alfred kwa kitendo kile alicho kifanya na kurushwa mpka CNN ,
kitendo hiko kina mkera sana raisi wa Nchi Alphonce Mriba, kutokana na nchi yake kucha fuliwa na picha mbaya iliyo tokea.
"Mme shindwa kumpata, mna fanya nini sasa?, hii ni aibu Tanzania tume itia, mi najisifu nina majeshi kumbe bure kabisa, hakuna kitu hapa, sasa naombeni mumkamate huyo kijana mara moja,"
Raisi Alphonce aliongea huku akipiga meza ndani ya chumba kikubwa cha mikutano akiwa na viongozi mbali mbali wa nchi na baadhi ya jeshi la polisi kutokana na kukerwa na kitendo kile, aliinuka kwa hasira na kutoka nje.
Waziri mkuu akiwa hospitali chini ya uangalizi mkubwa akilindwa na jeshi la polisi ambao wengine walikaa milangoni na getini na wengine wakiwa pembeni yake.
"Embu naomba utoke nje kidogo nipokee hii simu"
Aliongea waziri kasanga huku akisubiri askari yule atoke na yeye kupokea simu ambayo wakati huo ili kua ikiita.
"Eeeh Abdul, sikia asante nisha poa, yule ana tafuta kufanya kisasi nili muuwa dada yake, alafu... Sikia bado naongea Abdul, alafu mambo ya madawa ya kulevya,.
Sasa nisikilize kabla haja tiwa mikononi mwa polisi muuwe kabisa,. Muuwe muuwe , yule ndio Alfred, tafuta vijana shupavu kabisa,. Sawa nita kupa sasa hivi milioni 25 , fanya ivyo"
Waziri kasanga aliongea kwa sauti ya chini chini huku akionekana kuwa na mashaka kuliko maelezo,
Kweli mawazo yali msha mbulia sana kichwani na kukosa raha ya maisha.
Msako wa chini.kwa chini uliendelea huku jeshi la polisi likizidi kuta pakaa kila kona na pembe ya nchi, wali ta pakaa mipakani kote na boda zote za nchi ya Tanzania,
"....KABLA HAJATIWA MIKONONI MWA POLISI MUUWE KABISA...."
Ili kua ni sauti ya waziri mkuu ikijirudia katika kifaa kidogo maalumu cha kurekodi sauti na upande wa pili ambayo simu ya waziri mkuu ili kua hewani na kujisikia kile alochokua ana ongea na Abdul siku chache zilizopita.
"Sasa hii sauti nampelekea Raisi ili kila kitu kiwe wazi"
"Nini una taka kufanya usi fanye ivyo,. Upo wapi tuje tuongee"?
"Tayari tusha ongea hakuna mjadala, "
Alfred alikata simu na kumgeukia Amney ambae wakati huo alita basamu na kumpa mkono Alfred kwa kazi nzuri aliyo fanya,
Mawazo ya waziri mkuu ya kutaka kujihuzuru yali pita katika ubongo wake, na kuzidi kuhaha na kutetemeka huku kijasho kiki mtoka na kumfanya akose raha ya maisha.
Amney na Alfred baada ya kuongea na Raisi Alphonce kupitia simu ya mkononi na kumuelezea kuwa ange taka kuongea nae ivyo anakubaliwa na kuanza kujiandaa ili aweze kwenda ila simu ina ita na kutokuona namba(private no.)
Alipokea na kuweka sikioni.
"Una masaa mawili tu, yaani.mawili mke wako ana kufa leta memori kadi"
Upande wa pili ulisikika.
"Waziri mkuu"
Amney baada ya kuona Alfred ana shtuka ili bidi nayeye asogee karibu na kutega sikio karibu na Alfred ili asikie.
" sikia kwa umakini, na ngoja nikupe taarifa mkeo ni mja mzito, uki fanya masihala nitamuuwa yeye mtoto na huyu Jaquue sijui Nyange"
"Nipe nithibitishe mke wangu hayupo hapa....Alfred mme wangu, usi wape wanacho taka, niache niache nife"
"NO nakuja, nakuja mke wangu, nakuja kuku chukua..........Una masaa mawili njoo uwanja wa UFI , ."
Tayari simu ili katwa na kubaki kumtazama Amney machoni ambaye alionekana kuchoka sana baada ya kusikia habari zile.
"Wacha niende"
"Wapi kwa Raisi au?"
"Kwa Raisi kufanya nini?, naenda kwa Hannah"
Wakati huo tayari Alfred alishika funguo za gari na Amney kufuata nyuma huku akiiweka bastola yake kiunoni vizuri.
Baada ya kutembeza gari alifika alipo ambiwa na kuweka gari pembeni kati kati ya uwanja mkubwa na wote kushuka, baadae waliona magari matatu yana fika kwa mbali na watu wanne kushuka huku waki washikilia Hannah na Jaque
"Iko wapi memory kadi"?
Aliuliza mtu huyo aliye mshikilia Hannah,
na pale pale Alfred kuitoa mfukoni na kuwaonesha,
"Naomba aanze kutembea kwanza."
Aliongea Alfred akiwaangalia watu wale ambao pia walitoa bastola., Amney nayeye hakuchelewa alitoa bastola yake na kujiweka vizuri kwa lolote.
"Nawewe uje huku tulipo, uje na memori kadi"
Alfred alimwangalia Amney na kuanza kupiga hatua.
"Alfred Alfred"
Amney aliita ila Alfred alizidi kupiga hatua kuelekea kwenye magari yale ambapo aliwaona Jaq na Hannah wakija na wao,
ila Alivyo fika kati kati Hannah alimshika mkono na kumzuia
"Alfred,!,"
"Sio wakati wake huu Haanah nenda "
Alfred alimuangalia Hannah na kuwaangalia watu wale ambao waliowaoneshea bastola.,
Na kuanza kutembea na taratibu aliwa fikia watu wale karibu na kutoa memori kadi na kuwa kabidhi,,
Ghafla aliona kundi la watu na magari ya polisi yaki tokea kila upande na kushangazwa na kitendo kile,
Mmoja wao alikuja na kumpiga na kitako cha mtutu mdomoni na Alfred kudondoka chini pale pale,
Wali muingiza ndani ya gari la polisi na kuondoka nae.
Tayari habari mbali mbali zikitoa habari kuhusu kukamatwa kwa Alfred na Waziri mkuu kupewa pongezi kwa kile alicho kifanya bila kujua ukweli uliojificha nyuma ya pazia.,
Kesi ya Alfred ili somwa akiwa hana ushahidi wowote wa kujitetea. Ivyo serikali ina kaa chini na kuamua kifungo chake kihukumiwe GUANTANAMO habari izo ana zipata Hanaah na kulia kama mtoto mdogo ambaye ameachwa na mama yake,
Zili kua ni habari nyingine za kuis kitisha,
Baada ya Alfred kupigwa mbingu akiwa nje ya mahakama hiyo huku akipigwa picha mbali mbali na waandishi
"Alfred mtoto atalelewa na nani?"
Aliongea Hannah akiwa ana lia kwa uchungu sana huku akiwa ame mkombatia Alfred,
Amney nayeye aliji kuta ana dondosha chozi hasa alipo muona na Alfred pia analia kitendo ambacho hakutegemea.,
"Haanah jikaze, usilie mke wangu ndo yasha tokea huna sababu ya kulia, usilie zaidi tu Muombe Mungu auweke ukweli ,mtoto wangu..."
Alfred aliongea huku akimfariji mke wake huku mkono wake mmoja ukiwa juu ya tumbo la Hannah ambae alikua mja mzito ,
Amney ali mfata Alfred na kumkombatia pia na kuanza kulia, uli kua ni kama msiba na simanzi kwao,
"Usijali Amney, kaa na mke wangu, naomba usi msahau kisa mimi nita kua gerezani"
"Usijali Alfred wewe ni kama ndugu yangu sasa hivi,.."
Mambo yali kua yana tokea pale Jaqlin Nyange aliona ni kama sinema ya kihindi na kuji kuta ana toa kitambaa ambapo nayeye alianza kuji futa machozi yaliyo kua yana lowanisha mashavu yake.
Mianga ya camera iliwaka kila mahali ambapo waandishi walizidi kupiga picha za mnato,
Alfred alimuangalia Waziri mkuu pembeni ambapo alimuona ana pewa pongezi sana na viongozi wa serikali.
Maaskari wali kuja na kumsukumiza ndani ya karandika ili ajiunge na wafungwa wenzake walio huki miwa.
Taratibu za Alfred kusafirishwa katika gereza la GUANTANAMO lililopo visiwa vya CUBA ,
ambayo safari hiyo inaaandaliwa na Raisi Alphonce Muriba ambapo mwenyewe kwa mikono yake alitaka aende nae nchini Cuba,
kweli ndege ya Raisi Alphonce ina wekwa tayari.
Na leo hii Alfred akiwa na Raisi pamoja na baadhi ya viongoZi na ulinzi mkali waliingia ndani ya ndege hiyo ya Raisi Alphonce
Baada ya muda mchache ndege hiyo ilianza kupaa angani huku Alfred akiwa na mawazo mengi.
Katika hali ya kushangaza baadae una tokea mlipuko wa ajabu angani ambapo ndege ya raisi ili kua imelipuliwa na bomu aina ya RPG kombola na kuka tiks vipande vipande.,
Masaa mawili kabla.
***********************
Waziri mkuu kasanga akiwa ndani ya ofisi ya Raisi.alichukua makaratasi na kuifoji sahihi ya Muheshimiwa raisi Alphonce juu ya karatasi na kuingia juu ya komputer ya raisi na kuanza kubonyeza kubonyeza na kutuma barua kwa njia ya Fax mpaka makao.makuu ya jeshi nchini kenya kuwa walipue ndege ya raisi akiji fanya ni yeye akiwaambia kua ime tekwa nyara na Alshabaab. Jeshi la kenya lina pokea barua hiyo na bila kipingamizi wana pewa amri ya kuachia mzinga wa kombola., ambayo ndege hiyo ili kua tayari juu ya anga yao.
"Nickson, kuna kombola lime agizwa na lina kuja kuli pua hii ndege"
Alikua ni rubani aliyeekuwemo ndani ya ndege ya raisi . Ndege hiyo ya Raisi ina anza kutoa milio kuashiria kwamba kuna kitu cha hatari kina kuja
"Sasa tuna fanyaje Johnson"?
"Hapa sasa ina bidi tumwambie Raisi"
"Sasa tuki mwambia una fikiri ita kuaje?"
"Kabla ya kumwambia embu kwanza tu jaribu kutumia njia nyingine, maana watu wata panic"
Marubani wa ndege hiyo ya raisi walizidi kushauriana nini cha kufanya ili ndege hiyo.islipuliwe.,
Baadae wana muita muudumu wa ndege na kumwambia kila kitu kutokana na wali shindwa cha kufanya ., kipaza sauti kina sikika kiki tangaza juu ya bomu lina lokuja na wote kusali sala ya mwisho waki jua kwamba hakuna atakae pona.
"Zime baki dakika kumi na sita tu,hakuna la ziada"
Ali toka Rubani Nickson na kuwaambia waheshimiwa walio kuwemo ndani ya ndege hiyo akiwemo raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,
Taaarifa zile zina mfikia moja kwa moja Alfred ambae alikua ndani ya chumba kidogo, anasimama na kuangalia huku na kule na kuona chuma kizito kipo pembeni yake na kukichukua, alivunja mlango wa chumba kile na kutoka ,
Kabla ya kufanya chochote ndege ile tayari ili kua ime pigwa kombola pembeni ya bawa na kufanya moto uwake ivyo kupelekea upepo mkubwa kuanza kuigia ndani na baadhi ya waheshimiwa kutoka madirishani kutokana na upepo ule kuwa mkali sana,
Alfred alimuona Raisi akiwa amejishika na kiti ambapo upepo huo wenye nguvu za ajabu ulianza kumvuta nje, alizungusha mkono wake mmoja na huku mwingine kumshika Raisi Alphonce,
"Muheshimiwa Raisi"
Alfred aliita huku akimwangalia, Raisi Alphonce aligeuza shingo akimsikiliza.
"Jiachie ndege inaanza kulipuka mimi nita kufuata."
"Niache tu nife kijana"
".hapana siwezi kukuacha ufe, wana nchi wa Tanzania bado wana kuhitaji,. Nisikilize nahesabu mpka tatu, uniachie hu mkono alafu nitakuja nyuma yako, niamini"
Raisi Alphonce alianza kurejewa tena na tumaini baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Alfred.
"Sawa. Nime kuelewa"
"Moja, mbili. Tatu"
Pale pale Raisi Alphonce alijiachia na upepo kumvuta nje, na Alfred kufuata ambapo baada ya kujiachia ndege hiyo tayari ilikua ime lipuka na moto wa ajabu kuwaka.
Alfred akiwa ana elea elea angani aliweza kumuona Raisi Alphonce kwa mbali, alichofanya aliiibana mikono yake kwa nyuma na kuwa kama namba moja huku kichwa chake akikielekezea kwa chini na kuanza kushuka chini kwa kasi, muda mfupi tayari alikua amemshika Raisi Alphonce na wote kuanza kushuka chini kwa kasi.
************************
*******
ENDELEA KUSOMA HADITHI NA SIMULIZI ZA MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 1/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 2/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 3/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 4/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 5/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 6/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 7/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 8/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 9/10
- THE PAINFULL SECRET SEHEMU YA 10 MWISHO
0 comments:
Post a Comment